Simulizi: Jamani Mchungaji

Simulizi: Jamani Mchungaji

SEHEMU YA 45

Ilimchukua mama mchungaji wiki moja tu kuweza kujitambua kwamba tayari ameushika ujauzito kutokana na tendo alilofanya na kijana Deo au Desmund kama yeye alivyomtambua.

Ilimchukua mama mchungaji wiki moja tu kuweza kujitambua kwamba tayari ameushika ujauzito kutokana na tendo alilofanya na kijana Deo au Desmund kama yeye alivyomtambua.

“nilijua tu!! Tayari balaa jingine hili hapa mbele yangu nitafanyaje mie Rehema??” alijiuliza mama mchungaji kwa hofu tele baada ya siku zake za kwenda mwezini kupita bila dalili zozote za hedhi.

“nimekwisha safari hii siujui ujanja wa kuniepusha na hili” aliendelea kujiuliza mama mchungaji.

“mwanangu Rehema,kamwe usije kuwa kama dada yako mkubwa,nilimueleza kuwa ukoo wetu hairuhusiwi kabisa kutoa mimba,yeye akaleta ujuaji na mwisho wa siku tukamzika,narudia tena kwako mwanangu jihadhari sana na wanaume lakini kama ikitokea bahati mbaya ukapata ujauzito japo sitegemei kitu kama hicho kamwe usithubutu kutoa mimba UTAKUFA Rehema,utakufa!!!!!!” Rehema alikaa akakumbuka maneno ya marehemu baba yake aliyomwambia katika msiba wa marehemu dada yake aliyekufa katika jaribio la kutoa mimba baada ya Yule aliyekuwa amempa mimba hiyo kuikataa,damu nyingi iliyovuja ilipelekea mauti yake na hivyo kutimiza neno alilolisema baba yake hata kabla hajapata mimba “ukitoa mimba hakika utakufa”

“nitafanya nini mimi jamani,sipo tayari kufa hapana hapana siwezi kufa nasema nataka kuishi bado……..vipi sasa hii mimba,mchungaji kwa mdomo wake amenieleza kuwa hawezi kuzaa na ni suala ambalo kila siku tumekuwa tukimwomba Mungu kila siku bila dalili yoyote mh! Leo hii nina mimba je? Ataamini kuwa ni majibu kutoka kwa Mungu au? Na hata kama akiamini je? Motto nitakayezaa hawezi kuzua utata? Nimelikoroga “ mama mchungaji alizidi kuumia kichwa asijue nini cha kufanya.
 
SEHEMU YA 46


“nadhani cha msingi ni kuwafata hao wanaohusika na ujauzito huu huenda watanishauri kitu cha kufanya sina la kufanya kwa kweli mimi hadi hapa nilipo” aliamua kufikia hatua hiyo mama mchungaji
****

Shughuli za huduma ya kiroho zilikuwa zinaendelea kama kawaida na safari hii mchungaji tayari alikuwa amejifunza kitu kamwe hakumwacha mke wake nyuma tena,alikuwa anaongozana naye hadi eneo husika na kama ikitokea siku ambayo hawezi kuongozana naye basi waliagizwa watumishi kadhaa waweze kukaa naye pale nyumbani.

Ilikuwa siku ya mwisho kabisa ya mkutano huu wa injili uliokuwa na kauli mbiu ya “kesheni mkiomba”. Mchungaji Marko aliongozana na mkewe katika kuliongoza kundi kubwa la waumini waliohudhuria siku hiyo ya kipekee. Shangwe za hapa na pale zilitawala eneo lile huku watoto wadogo wakifurahia kuangalia sinema mbalimbali zenye mafunzo mengi sana katika maisha yao ya baadae.

Noela,Oscar nao pia walikuwa kati ya watu walioongeza idadi ya waumini;Noela alikuwa katika mstari wa mbele kabisa wa kwaya kuu ya kanisa lake wakiwaburudisha mamia ya waumini eneo lile,Oscar yeye alikuwa akiburudika tu kumwangalia Noela alivyokuwa anan’gaa na kuzidi kuipendezesha kwaya ile,sauti yake haikuwa ya kujiuliza mara mbilimbili kama ni bora au sio bora,sauti ya Noela ilikuwa ya kipekee na madaha yake katika kuimba yalisababisha watu wengi hasahasa wanaume kumuonea wivu Timoth.
 
SEHEMU YA 47


Siku hiyo Timoth aliamka akiwa na mawazo mengi sana na kwa alichokuwa anawaza aliamini ombi lake lilikuwa limepokelewa na lilikuwa limefanyiwa kazi na majibu alikuwa amepewa,roho mbaya na ya kikatili kwa mara ya kwanza yaliumbika kichwani mwake.hakujua yametoka wapi lakini aliamini yalikuwa mawazo sawa kabisa yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Chuki kuu ilikuwa imejengeka dhidi ya mchungaji wa kanisa lake,matatizo na visanga vyote alivyopitia aliamini ni kwa sababu ya huyo huyo mchungaji.
“ni adui wangu namba moja” alisema kwa hasira Timoth wakati akiwaza nini cha kumfanyia mchungaji ili nafsi yake ilizike
“kufanya mapenzi na mke wake tena kwa siri bila kujulikana haitoshi hata kidogo nitakuwa mpumbavu nikijipa kichwa kuwa hicho ni kisasi” aliendelea kuongea peke yake Timoth wakati akifikiria nini cha kufanya.
Jioni ilipofika hakutaka kuongozana na mkewe pamoja na Oscar kuelekea kanisani katika siku ya mwisho ya mkutano ule mkubwa wa injili.

“nyie tangulieni mimi namsubiri rafiki yangu nitakuja nae,si unakumbuka mchungaji alisema kila mmoja alete mggeni!!! We tayari umemchukua Timoth basi na mimi nataka kuja na wangu” alijibu Timoth huku akitawaliwa na tabasamu pana usoni kwake.

“mh!! Nimekuwahi mimi mjanja zaidi yako” alitania Noela huku akiondoka pamoja na Oscar. Timothy alitabasamu na kurejea ndani.
Hakuna aliyejua kichwani mwakeTimoth alikuwa anawaza nini.
 
SEHEMU YA 48



*****

Giza lilitokea ghafla eneo lote lililokuwa linafanyiwa mkutano huo,tayari ilikuwa majira ya saa sita usiku
“aaaaaaaah!” ndio kelele zilizosikika kutoka kwa watu baada ya giza kuchukua nafasi eneo lile la mkutano wakati mahubiri ya mchungaji Marko yakizidi kunoga na kukonga nyoyo za mamia waliohudhuria eneo lile.

“hata pasipo na umeme nina sadiki kuwa sauti yangu itafika hapo ulipo,bwana Mungu alinipa sauti kuu niweze kuipaza mbele yenu na bila kujalisha umbali neno hili litakufikia na ujumbe wake utakuingiaaaaaaa!!! Haleluyaaaaa!!!!!!!!” ilisikika sauti ya mchungaji Marko ikisambaa eneo lile na kusisimua umati.

“ameeeeeeen!!!!” umati ulijibu kwa shangwe kubwa zilizozizima hadi miji ya jirani.
Kelele za furaha kabla hazijaisha vizuri msukumano wa hapa na pale ulianza pale katika umati ule kila mmoja alikuwa anajaribu kutafuta pa kukimbilia,kelele zilitokea jukwaani alipokuwa anahubiri mchungaji Marko,haikusikika tena sauti ile kuu iliyosisimua umati ule kwa shangwe tele. Giza totoro lililotanda pale lilisababisha watu wakanyagane na kugongana hapa na pale vilio vya watoto vilisikika huku mama zao wakipaza sauti kuu wakitaja majina ya watoto wao hao.
 
SEHEMU YA 49

Roho mbaya iliyokuwa imemwingia Timoth ndiyo hiyo iliyomtuma kutenda uovu huu,silaha yake kubwa ilikuwa ni mshale wake aliokuwa nao ndani ni huu pekee aliamini ungeweza kuwa dawa ya mchungaji Marko kwa tabia yake ya kuchukua wake za watu
Timoth kwa mara nyingine aliingia katika vita lakini safari hii alikuwa peke yake bila ushirikiano kutoka kwa Deo.

“mambo vipi Timoth habari za siku nyingi rafiki yangu yaani umekuwa kimya mpaka naogopa” sauti ya Deo ilisikika pale Timoth alipopokea simu yake.

“majukumu mengi tu rafiki yangu,mi mzima nipo tu!!!” alijibu kinyonge Timoth.

“nina ujumbe wako bwana amakweli we mwanaume wa shoka ndugu yangu” alianza kuongea Deo kwa mshawasha mkubwa lakini Timoth hakusikika kuwa na furaha yoyote ile na badala ya kujibu alikata simu kasha akaizima kabisa.
Majira ya saa nne nne usiku tayari alikuwa eneo la tukio pamoja na silaha zake tayari kwa mapambano makubwa yaliyomkabili mbele yake. Hakuna aliyemtambua alijificha mbali kidogo na kundi la watu,kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu walivyozidi kusogea eneo la tukio kutokana na kuvutiwa sana na mahubiri motomoto ya mchungaji Marko,lakini tofauti na hisia za wengine siku hiyo kwa Timoth ilikuwa tofauti sana kwani kadri mchungaji alivyozidi kuhubiri hasira zake zilizidi kupanda na chuki ikaongezeka dhidi ya mchungaji yule.
lilipowadia somo la ndoa ndio Timoth hasira zake zilipanda maradufu kwani aliamini mchungaji anaurubuni umati wote ule uliokuwa pale.
 
SEHEMU YA 50



“……..utasikia mwingine anasema eti nahisi naibiwa mke wangu,tena mbele ya wanaume ambao wametulia na ndoa zao salama kabisa zikiwa na amani tele,anashangaa kwa nini wenzake wanafurahia ndoa zao jibu ni rahisi sana wamezikabidhi ndoa zao kwake mweza wa yote naye si mwingine ni mwenyezi Mungu” sauti nene ya mchungaji Marko ilikuwa inarindima kwa kishindo,Timoth kwa mara ya kwanza akajikuta anashindwa kuzuia hasira zake,sehemu aliyokuwa amejificha ilikuwa jirani na chumba ambacho umeme ulivutwa kutoka pale,kwa mwendo wa kunyata alisogea mpaka katika chumba kile na kuuchomoa waya uliokuwa unatoa umeme pale,giza lililotokea lilimkosesha ramani ya kumwona vizuri mbaya wake.
Hakuna kosa kubwa alilofanya mchungaji kama kuendelea kupaza sauti yake wakati tatizo la umeme likiendelea kushughulikiwa na watu waliowekwa kwa ajili hiyo. Timothy kwa ujasiri alitumia mwanya huo mbio mbio akapanda jukwaani akiwa na mkuki wake mkononi moja kwa moja katika mgongo wa mchungaji hakusubiri kujua nini kitaendelea aliruka kutoka pale jukwaani na kutua chini akimwacha mchungaji Marko akigalagala kwa uchungu pale jukwaani na maumivu hayo yakifuatiwa na kilio kikali sana,harufu ya damu iliyotapakaa eneo lile ndiyo ilikimbiza watu hapa na pale wakijua kuna hali kubwa ya hatari mbele yao. Mkuki ulikuwa umemuingia vyema mchungaji katika mgongo wake kama Timoth alivyokuwa amepanga. Hakuna aliyegundua harakaharaka aliyetenda ukatili ule kwa mchungaji wa kanisa ambaye mamia kwa mamia walimpenda sana kutokana na moyo wake wa kujitolea kwa sababu ya kanisa na wafuasi wake. Mahubiri yake ya siku hiyo ndiyo yaliwavuta wengi zaidi kuamini kuwa mchungaji Marko alikuwa akiifanya kazi ile ya utumishi kutokea moyoni,hakuogopa kusema ukweli hata siku moja.

Sasa alikuwa ameanguka chini damu zilikuwa zinamvuja kwa kasi na alikuwa ameuma meno yake kwa uchungu lakini bado kilio cha maumivu kilisikia. Hadi umeme ulipoweza kuwaka tena baada ya marekebisho madogo yaliyofanywa na wataalamu mchungaji hakuweza kusema neon zaidi ya kunyoosha mkono wake kama vile anaomba kitu huku mkono mwingine ukiwa kama unauzuia mkuki usitoke pale ulipokuwa umejichimbia kwenye mwili wake,hakuwepo mama mchungaji eneo lile kumwangalia mumewe,watumishi walikuwa kama vichaa kwani waligongana hapa na pale bila kufanya lolote la maana hadi waliposhuhudia mchungaji anatulia tuli bila kusema neno lolote.
*****

Kila mtu aliyeshuhudia kilichomtokea mchungaji pale jukwaani na hali iliyojionyesha dhahiri ya kutulia ghafla pale pale alipokuwa huku mkuki ukiwa umezama katika mgongo wake,watu waliamini tayari mtumishi huyu alikuwa maiti na hakuna cha kuzuia jambo hilo hata ilipopatikana gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali lilifanywa jambo hilo kama kutimiza wajibu tu!
 
SEHEMU YA 51


“maskini sijui hata amewakosea nini bwana huyu,kifo chake ni cha uchungu sana yaani kinasikitisha” alisema maneno hayo mtumishi wa Mungu aliyeshuhudia gari likitimua vumbi kuliacha eneo hilo na kwenda hospitali kwa ajili ya kujaribu kuokoa maisha ya mchungaji Marko. Mkuki aliokuwa nao uliendelea kubaki eneo lilelile mwilini kwani alishauriwa kubaki hivyo hivyo kitendo cha kuthubutu kuun’goa pale ilikuwa ni kukamilisha mauti ambayo walisubiri daktari aweze kuyathibitisha kwani macho yao tayari yalikuwa na majibu kuwa mchungaji amefariki dunia,jambo lakushangaza hadi wanafika hospitali bado mke wa mchungaji alikuwa hajaonekana. Noela ndiye alikuwa kama mke wa mchungaji kwani katika kila hatua alikuwepo akiwa pamoja na msaidizi wake katika kazi (Oscar). Uchungu aliokuwanao Noela kila mmoja aliutambua kwa wale waliomshuhudia akihangahika huku na kule baada ya mchungaji kupatwa jambo hilo la kusikitisha na kuhuzunisha sana

Timoth baada ya ukatili ule alioufanya kwa mchungaji wa kanisa lake aliondoka kwa kasi ya ajabu hadi nyumbani kwake bila kutambuliwa na mtu yeyote kuwa huenda anahusika,lilikuwa tukio lake la kwanza kutoa mtu damu lakini hakuwa na uoga wowote aliona amefanya jambo sawa kabisa na lilikuwa halitoshi kuuridhisha moyo wake.
“huo ni mwanzo naamini atakoma sasa kuchezea wake wa watu wakati nayeye ana wa kwake,halafu asivyokuwa na adabu anahubiri kuwa sisi tunaolia kuibiwa hatuna akili haya ameziona akili zetu huo ni ujumbe tosha” aliongea peke yake Timoth wakati akivua nguo alizozitumia kwenye tukio na kuvaa nyingine kasha akajilaza kitandani na kupitiwa na usingizi fofofo uliotokana na uchovu wa kukimbia kwa kasi hadi kwake hadi alipokuja kushtuka asubuhi ya siku iliyofuata.

Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,mchungaji Marko alifikishwa huku sala za waumini zikilipeleka jina lake katika uso wa bwana aweze kumuepusha na janga la kifo lililokuwa linanukia mbele yake,sala hizo ziliweza kumfikisha akiwa hai katika kitanda cha wagonjwa mahututi mbele ya daktari bingwa wa magonjwa yahusuyo mwili wa mwanadamu aliyefahamika kwa jina la dokta Mpejiwa mzaliwa wa Kahama katika mkoa wa Shinyanga. Katika uzoefu wake wa kazi kamwe hakupenda kupoteza maisha ya mwanadamu katika huduma zote za kiafya zinazoletwa mbele yake. Na sasa alikuwa katika mtihani mwingine ambapo mchungaji mkuu wa kanisa lake alikuwa katika hali mbaya sana iliyokuwa inakatisha tama sana na dakika yoyote ingesababisha vilio kwa waumini na watu wote waliomfahamu au kuzisikia sifa kemkemu alizomwagiwa mchungaji huyu. Kwa madaktari wengine mtihani huu ulionekana kuwa mgumu lakini yeye alijiaminisha kuwa ilimradi mchungaji badoanapumua basi ataendelea kupumua tena hadi anavyoondolewa pale hospitalini. Kiujasiri kabisa Dokta Mpejiwa aliingia kijasiri sana katika chumba alichoingizwa mchungaji akiongozana na wauguzi watatu tayari kwa kukumbana na mtihani huo mbele yake.
 
SEHEMU YA 52


Mapigo ya moyo ya mchungaji yalikuwa mbali sana hali iliyopunguza asilimia chache za matumaini ka daktari huyu na kidogo kuanza kuhisi huenda mchungaji alikuwa katika hatua za mwisho za kuvuta hewa chafu ya dunia hii dhaifu. Mashine za kupumulia alizovalishwa zilimsaidia sana kuweza kuongeza dakika za kuishi lakini ubaridi katika mwili wake ulimaanisha mzunguko wa damu ulikuwa katika kasi ya chini sana ambayo ingesimama wakati wowote ule na kulibadili jina lake kuwa maiti halafu marehemu

Ilianza siku ya kwanza,ya pili,ya tatu hadi ya saba bila hali ilikuwa ile ile ya awali mchungaji alikuwa hajafumbua macho wala kusema neno yaani alikuwa hajazinduka bado kutoka katika safari ya usingizi aliyoianza ghafla usiku wa mwisho wa mahubiri ya huduma za kiroho. Hali sasa ilikuwa tata,waumini hawakukoma kufunga na kusali kwa ajili ya kumuombea mchungaji wao aliyekuwa katika usingizi wa kifo,daktari Mpejiwa naye hakukata tamaa aliendelea na jitihada zote za kujaribu kokoa uhai wa mtumishi huyu wa Mungu.

Baada ya kuwa amekaa kimya kwa muda wa siku thelathini sasa mtumishi wa Mungu,mchungaji Marko alikuwa ameweza kupata fahamu zake tena,japo alikuwa ameperaraizi upande mmoja wa mwili wake lakini ule uwezo wake wa kuongea japo kwa sauti ya chini ilikuwa furaha tosha kwa waumini wake na wasiokuwa waumini lakini kwa daktari Mpejiwa ulikuwa ni ushindi na kumbukumbu nzuri katika maisha yake kwani ni yeye alikuwa ameshikilia furaha ya maelfu ya watu,ni yeye aliyekuwa na uamuzi wa kuleta vicheko au vilio na sasa aliamini ameleta tabasamu pana kwa watu.

“unatakiwa uendelee kuwa hapa hospitali hadi hapo utakapopona kabisa” daktari Mpejiwa alimwambia mchungaji Marko masaa machache baada ya kuwa ameshtuka kutoka usingizini.

“hapana hapana,Mungu amenituma kuihubiri injili yake na wakati ndio huu,kwa nini nilale?” alijibu mchungaji huku akishangaa kwa nini yuko pale. Daktari akishirikiana na wauguzi pamoja na wanakanisa wengine walijaribu kumueleza kila kitu kilichotokea na ni kwa muda gani alikuwa kama maiti pale kitandani akilishwa kwa kutumia mipira.

“mwezi mzima??? Yaani sijatoa huduma mwezi mzima hapana ni uzembe wa hali ya juu” alijibu Mchungaji kwa sauti ya chini alijibu. Baada ya maongezi marefu mchungaji Marko akiwa tayari amepooza upande wa kulia wa mwili wake alipata ruhusa ya kwenda kufanya mkutano alioahidi kuwa kuna mengi sana ya kuwaeleza wananchi kuhusu injili. Kanisa bila hiana likaandaa mkutano huo wa hadhara kama alivyohitaji mchungaji Marko.
 
Story mzuri kweli..
SEHEMU YA 12


***
Yalikuwa ni majira hayo hayo Timoth alikuwa anarejea kutoka kazini,tofauti na alivyotegemea kurudi majira ya saa kumi na moja asubuhi sasa alikuwa amerejea mapema zaidi. Huku akiwa na uchovu mwingi sana wa kazi za usiku na mawazo mengi juu ya anachokishuhudia kwa mkewe Timoth kwa kutumia funguo wake wa ziada hakutaka kumsumbua mtu yeyote yule aliufungua mlango wa sebuleni na kuanza kuingia ndani,kituo cha kwanza kilikuwa ni kwenye friji ambapo alichukua maji ya kunywa na kupooza koo lake.Wakati anameza mafunda ya maji yale anasikia kwa mbali kama kelele za malalamiko hivi."ah! Watakuwa ni majirani" alipuuzia Timoth huku akirudisha glasi ya maji mahali pake.
Hatua moja baada ya nyingine Timoth alianza kutembea kukifuata chumba chake,wakati huu sikio lake halikumdanganya katika chumba chake palikuwa na vurumai flani,kitanda kilikuwa kinachezacheza na sauti ya mwanamke ilikuwa inapiga kelele haikumchukua muda kubaini kuwa yule anayepiga kelele hizo alikuwa ni mkewe wa ndoa. Mwili wake ulikuwa ni kama umepigwa ganzi alihisi baridi kali ghafla na hakika imani yake ya dini ilikuwa imeyumba kama sio kutoweka kabisa."naua!" alijiapiza huku akirudi kasi kuelekea jikoni alipotwaa kisu pamoja na mwiko "nasema hivi! Naua leo" alisisitiza Timoth huku akitembea kwa mwendo wa kunyata kuelekea pale chumbani tena.
"safi kabisa funguo za chumbani ninazo" alikumbuka Timoth na kuzitoa funguo mfukoni mwake taratibu akaziingza katika kitasa na kufungua bila tatizo mlango ukakubali,kwa mkono wa kuume huku akiwa amechomeka kisu katika mkanda wake kwa nyuma na mwiko mkono wa kushoto alianza kushusha kitasa.
 
Back
Top Bottom