Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 80


Siku ya leo hii Neema alitoka nyumbani kwake na kwenda kumtembelea rafiki yake, ambaye alimshangaa kwa mabadiliko ya muda mfupi,
“Mmmh nipe siri ya mafanikio shoga maana sio kwa kung’aa huko, halafu pale kwako mbona umehama bila kusema?”
“Ndiomana nimekuja nikuhadithie”
Kisha akamuelekeza jinsi yeye alivyokuta wameshahama na jinsi Ashura alivyomtumia ujumbe,
“Mmmh kumbe Yule mdogo wako ana upendo hivyo!”
“Ndio, nakushangaa tu wewe ulikuwa na mashaka nae”
“Kwakweli nisiwe mnafki, sijawahi kumuelewa Yule mdogo wako na sijawahi kumuamini kabisa. Yani kila alichokuwa akiongea nilikuwa nakitilia mashaka, eti leo hii ndio amekutafutia nyumba nyingine ya kukaa mmmh”
“Na zaidi ya yote baba yake Salome yani Yule alikuwaga mume wangu, amejirudi yani kawa mpole huyo balaa. Aminiomba msamaha na amesema yupo tayari kumlea mtoto wake”
“Ila wanaume bhana, kaona mtoto amekuwa ndio kujifanya yupo tayari kumlea mtoto wake. Ila napo ni vizuri, halafu kitu kingine, mbona Salome simuoni shule?”
“Na hilo ndio jambo lingine limenileta ili unipe ushauri, Salome hataki shule kwasasa, unaweza kuamini hilo? Salome amesema anataka kupumzika kwahiyo nimuombee ruhusa ya ugonjwa, kwa kifupi Salome wangu hataki shule kwasasa”
“Kheee makubwa hayo, utaniletea niongee nae”
“Sawa nitakuletea maana wewe ndio mshauri wangu, na wakina Pendo wako wapi?”
“Wameenda kanisani”
“Kheee watoto wale kwa kanisa loh!”
“Ila ndio vizuri, na hakika hata wakina Salome wangependa kusali sidhani kama angekataa shule”
“Basi saivi hizo ibada ndio kama kituo cha polisi, mtoto hataki kabisa kuongelea habari hizo”
Mara akafika mgeni mwingine pale kwa mama Pendo ila huyu mgeni baada ya salamu kama alionyesha kumfahamu kidogo Neema yani ilikuwa kama kuna tukio ambalo alilifanya Neema halafu yeye analijua.
“Mmh hivi sio wewe ambaye mwanao alitumbukia kwenye kaburi!”
Neema nae alishtuka kuona kuna mtu anagundua kuhusu hilo jambo kwani yeye na Sa
lome kwenye msiba ule hakujua kama kuna watu wangetokea kuwafahamu,
“Kwani na wewe ulikuwepo kwenye ule msiba?”
“Ndio nilikuwepo, na lile tukio lilikuwa la kushangaza sana. Nakukumbuka vizuri sababu mimi ndiye ulinikuta pale njiani na nikakwambieni tunaenda kwenye msiba wa Moza, mkashangaa pale kuwa Moza amekufa kisha tukaaanza kuongozana kuelekea makaburini’
Ndio Neema nae alipoanza kukumbuka hilo tukio na kuona ni kweli kabisa kama ni yeye lazima awe anamkumbuka vizuri,
“Vipi mwanao hali yake maana kila mtu alipigwa na bumbuwazi pale msibani”
“Mwanangu amepona wala sikutaka kurudi tena kule zaidi zaidi kwenda na mwanangu nyumbani”
“Hata mngerudi kule kuna kilichokuwa kinaeleweka basi! Yalitokea makubwa sana, mwili wa marehemu ulitoweka na hadi leo hakuna anayejua kilichoendelea labda ile familia tu. Ulitokea upepo wa gafla pale makaburini na kila mmoja akikimbia na lwake. Kwakweli hali ilikuwa mbaya sana”
“Duh poleni sana, kwahiyo marehemu hakuzikwa?”
“Azikwe vipi na hata mwili wake haujaonekana”
Mama Pendo ikabidi aingilie kati maana haya maelezo hata yeye yalimchanganya kabisa,
“Unataka kuniambia Salome alitumbukia kwenye kaburi”
“Ndio alitumbukia halafu akazimia”
“Yani Neema umekaa tu na mtoto na alipatwa na makubwa kiasi hiko, anakataa shule unakaa nae tu hujiulizi! Mlete nimpeleke kwenye maombi”
“Nitajaribu kumwambia kama atakubali”
“Wewe ni mama yake bhana, atakubali tu”
Neema aliitikia pale ila hakuwa na namna ingawa Salome alimwambia kuwa wafanye siri ila atafanyaje na mambo yameshakuwa kama hivyo yani kuna watu wanamkumbuka vyema. Aliaga muda huo na kuondoka zake.

 
SEHEMU YA 80



Rose alikuwa amevurugwa kabisa akili na gari alikuwa anaendesha ilimradi tu, kitendo hicho kilimfanya afike nyumbani kwake saa tano za usiku, aliingiza gari ndani na kushuka kisha akaenda sebleni kwake ila akakumbuka lile begi lenye hela akaamua kwenda kulichukua kwanza kabla na lenyewe haljachukuliwa. Cha kushangaza muda huu alienda kuliangalia mule kwenye gari hakuliona na kumfanya achanganyikiwe tena,
“Jamani, begi langu limeenda wapi tena?”
Akamuuta mlinzi kwa nguvu na kuanza kumuuliza kama ameona begi ila mlinzi alikuwa akimshangaa tu maana ni muda huo huo ameingia sasa huyo mlinzi alione begi na kulichukua aende nalo wapi.
“Mi sijaona begi mama”
“Inamaana limeibiwa na nani sasa?”
“Labda huko huko ulipotoka mama lakini hapa hakuna hata mtu mmoja anayeweza kufungua gari na kuiba”
“Hebu niondokee hapa”
Rose alijikuta akifoka tu kisha kwenda tena ndani na akiwa na mawazo lukuki kuwa begi limepotea tena kwa mara nyingine, hakukaa sana sebleni kwani watu wote kwenye nyumba yake walikuwa wamelala hivyo akaamua kwenda chumbani kwake na kumkuta mumewe akiwa amelala hoi,
“Huyu nae kalala kama mzigo leo, na wala simuamshi atajijua mwenyewe saivi nina mawazo yangu”
Akawaza pale cha kufanya kwa usiku ule ila hakupata jibu kabisa na alijiona kama sijui kitu gani ila wazo lingine likamtuma kuwa aende chumba alichokuwa analala Moza ili akapekue kitu Fulani, hakutaka kupuuza wazo hilo na moja kwa moja akaenda chumba alichokuwa analala Moza ila alipofungua mlango alimuona mtu amekaa amempa mgonga, kwa mashaka zaidi Rose aliuliza,
“Wewe ni nani?”
“Ni mimi”
“Ni nani wewe?”
Yule mtu akageuka na kumfanya Rose aanguke na kuzimia, na ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha yake kuzimia kwa muda mrefu kama siku hiyo.
 
SEHEMU YA 81


Kulipokucha Rose alijikuta kitandani kwake na kuanza kujiuliza kuwa mara ya mwisho alikuwa wapi na mbona amepatwa na kitu ambacho hakijawahi kumpata maishani mwake,

“Yani na mimi Rose nalogwa? Haiwezekani yani haiwezekani kabisa”

Rose akakumbuka mara ya mwisho alienda kwenye chumba alichokuwa analala Moza na alimuona mtu ila sura ya Yule mtu alipogeuka hakuiona vizuri zaidi ya kuzimia. Hasira zikampanda na kujiuliza kuwa ni nani anayecheza na akili yake, akataka kuita familia yake yote sebleni siku hiyo ili ajue kinagaubaga kuwa ni nani anacheza na akili yake. Akatoka sebleni ila akagundua kuwa watu wake wote bado hawajaamka ukizingatia hata Patrick amemuacha kwenye usingizi wa hali ya juu, alianza kuita mmoja mmoja na waliokuja sebleni kwa muda huo walikuwa ni wale mapacha na Ana, akauliza kwa hasira

“Wengine wako wapi?”

“Wakina nani mama?”

“Sara na baba yenu?”

“Kuhusu Sara sidhani kama amelala hapa nyumbani jana”

“Mnasemaje nyie?”

“Hatukumkuta mama, sidhani kama amelala hapa nyumbani jana”

Rose akashikwa na hasira na kwenda chumbani kwa Sara, akafungua ila hakumkuta Sara na kumfanya apate jibu kuwa ni kweli Sara hakulala nyumbani kwa siku ya jana,

“Huyu mtoto ameanza kunichezea akili eeeh! Atalalaje nje ya nyumbani, atalalaje nje ya nyumba yangu!”

Akarudi tena sebleni kwa hasira, na kuuliza

“Ni nani alilala chumba cha Moza jana?”

“Mmmh mama, nani anayeweza kulala mule zaidi ya Yule binti Salome. Na toka ameondoka siku ile hajaja tena”

Akawaangalia wale wanae mapacha na kuwauliza,

“Ni nini mnajua kuhusu mimi?”

“Hatujui chochote mama”

“Mna uhakika?”

“Ndio hatujui chochote”

“Haya mnaweza kuondoka, na wewe Ana mwanangu unaweza kwenda kujiandaa na kwenda shule najua hata wewe unachukizwa na hali hii mwanangu”

Rose akaondoka na kuelekea chumbani, ila wale mapacha kabla nao hawajaondoka walishangaa kumuona Sara na Salome wakitokea njia ya vyumbani, na kushangaa

“Inamaana dada Sara ulikuwa chumbani?”

“Ndio, jana nililala na Salome chumbani kwa Moza”

Wale mapacha wakatazamana maana mama yao aliwauliza kuwa ni nani alilala kwa Moza jana na hawakuwa na jibu.

Kwa upande wa Rose, aliingia chumbani kwake na kumuamsha Patrick ila la kushangaza leo Patrick alivyoamka aliinuka na kumuwasha kibao Rose kisha akamwambia,

“Yani wewe mwanamke umeniulia mama yangu!”

Kabla Rose ajajitetea, alishangaa akipigwa kofi jingine.
 
SEHEMU YA 83


Wale mapacha wakatazamana maana mama yao aliwauliza kuwa ni nani alilala kwa Moza jana na hawakuwa na jibu.

Kwa upande wa Rose, aliingia chumbani kwake na kumuamsha Patrick ila la kushangaza leo Patrick alivyoamka aliinuka na kumuwasha kibao Rose kisha akamwambia,

“Yani wewe mwanamke umeniulia mama yangu!”

Kabla Rose ajajitetea, alishangaa akipigwa kofi jingine. Kitendo hicho kilimchanganya sana rose na kila alipotazama sura ya mume wake ilionyesha kuwa na hasira za wazi wazi, Patrick aliendelea kwa kusema,

“Mwanamke wewe ni shetani tena shetani mwenye mapembe, yani siku zote hizi nilikuwa sijui kama naishi na shetani, yani wewe wa kuniulia mimi mama yangu!”

“Patrick sikuelewi mume wangu”

Patrick akamzabua kibao kingine Rose, cha safari hii kilikuwa cha hali ya juu hadi Rose akajihisi kizunguzungu na kuanguka chini akaona akimchekea Patrick atamuumiza, vile alivyoanguka Patrick akamsogelea na kutaka kumpiga tena ila kuna dawa Rose akampulizia machoni Patrick na muda huo huo kizunguzungu kikasmshika Patrick na kuanguka chini.

Rose alimuacha Patrick pale chini kisha yeye akatoka sebleni.



Alipofika sebleni akashangaa kumuona Salome akiwa na Sara pamoja na wale mapacha, alimuangalia Sara kwa hamaki na kumuuliza kwa kumfokea,

“Leo umelala nje eeeh!”

“Hapana mama”

“Hapana kitu gani, mbona nimekuja chumbani kwako sijakukuta”

“Nililala na Salome kwenye chumba cha Moza”

“Nini?”

Sara alirudia yale maneno ila Rose alionekana kuchukizwa zaidi, ila wakati huu huu Sara alimuuliza mama yake,

“Kilichonifanya nilale na Salome ni kuwa nilikuwa naogopa peke yangu, mama Ommy yuko wapi?”

Rose hakujibu ila aliwaangalia wale mapacha wake na kuwafokea,

“Nyie, si niliwaruhusu kuondoka”

Nao walitoka haraka haraka kwani waliogopa mama yao asije akabadilisha mawazo maana huwa hakawii. Walivyotoka alimuangalia Salome na kumuuliza,

“Na wewe nani amekuruhusu kuja tena humu ndani?”

“Yani kuja humu sitangojea ruhusa maana ni kwa babangu”

“Wewe mtoto nitakuja nikufanye kitu mbaya sana”

“Najua huwezi kunifanya lolote”

Salome akatoka pale sebleni na kwenda tena chumbani kwa Moza maana muda huo alikuwa amechukia na angeweza hata kubadilika. Sasa Rose alibaki na mwanae Sara kisha akamwambia mwanae atoke tu amuache nae Sara akafanya hivyo na moja kwa moja alienda tena chumbani kwa Moza akazungumze na Salome.

Rose alitoka tena nje kujaribu kuangalia lile begi la hela ila hakuliona bado yani hapo ndio akaamini kweli hadi yeye kafanyiwa kiini macho.

“Atakuwa ni Moza tu, na nitapambana nae. Ila nitaweza kupambana na mzimu? Mmmh! Cha kufanya ni kuwa nihakikishe haingii kwenye nyumba yangu, ngoja nizunguke nyuma”

Rose alizunguka nyuma ya nyumba ili aangalie cha kufanya na mzimu wa Moza usiingie kwenye nyumba yake.

 
SEHEMU YA 84




Sara alienda kumuuliza Salome kwani yeye bado moyo ulikuwa unamuuma sana kuhusu kusalitiwa na Ommy,

“Ni kweli nimeona kuwa Ommy alitoweka, tena inawezekana ni mama kamficha Ommy ila kila ninapotaka kukazana kumsaidia Ommy naiona sura ya Mishi yani naona kama namsaidia Mishi kumpata mpenzi wake”

“Unaongozwa na wivu Sara, yani ni wivu ndio unakusumbua kwenye moyo wako. Kumbuka hata wewe Ommy unampenda, na akirudi atasema ukweli kuwa kati yako wewe na Mishi anampenda nani”

“Mfano akimchagua Mishi je?”

“Sioni kama ni tatizo hilo, atakuwa amekusaidia maana hutojiumiza tena moyo kwa kumfikiria mtu asiyekupenda. Mara nyingine kujua ukweli ni bora zaidi, mfano Ommy akifa huko wewe utapata faida gani? Utasema tu Mishi kakosa na mimi nimekosa, ila kuna faida yoyote unapata? Hakuna, mara nyingine kujua ukweli ni bora zaidi. Kuna watu wanakupenda wanakufataga ila unawakataa sababu upo na Ommy ila ukweli umeujua hakuna tena kusumbuliwa akili badala yake utaangalia unayempenda kati yao na kumkubali. Na hata ukiwa nae usiruhusu mapenzi yatawale akili yako yani akili yako isiendeshwe na hisia za kimapenzi maana ukiendeshwa na mapenzi, sehemu kubwa ya moyo wako itabebwa na wivu na utajikuta ukifanya jambo baya bila kutarajia. Fanya mapenzi ni sehemu tu ya maisha ila sio kila kitu katika maisha”

“Unajua Salome, wewe ni mtoto mdogo sana ila unayachambua mapenzi vilivyo. Kwani ushawahi kuwa na mpenzi na udogo huo?”

Salome akacheka kisha akamwambia dada yake,

“Tuachane na habari hizo ila tuangalie jinsi gani unaweza kumuokoa Ommy, tambua kwamba Ommy anatakiwa kuokolewa”

“Sawa nitafikiria na ushauri ulionipa, nitaongea na mama amuachie Ommy maana mama yangu ni mchawi kabisa ni mchawi sijui nifanyaje aache”

“Unataka mama yako aache uchawi?”

“Ndio, na mdogo wangu Ana aache uchawi tuwe watu wa kawaida tu na tuishi maisha ya kawaida”

“Ila uchawi wanakula viapo, unadhani ni rahisi hivyo kuacha?”

“Sijui”

“Uchawi inatakiwa mtu aache kwa ridhaa yake mwenyewe ila kwa kulazimishwa haachi, nitasaidia na mama yako ataacha uchawi kwa ridhaa yake mwenyewe”

Sara alikuwa anamuangalia Salome bila ya kummaliza, kisha Salome akamuomba Sara ampishe muda huu anahitaji kuvaa. Sara aliondoka na kwenda chumbani kwake, akampisha avae ila akajiuliza ni kwanini Yule Salome hawezi kuvaa mbele yake wakati yeye ni mwanamke mwenzie,

“Mmmh kila akitaka kuvaa anasema nimpishe, halafu Yule mtoto mbona anaongea mambo ya kikubwa sana!”

Akajiuliza sana, na kuamua kwenda dirishani kwake kuchungulia yani akili ilimtuma tu kufanya vile, wakati anachungulia gafla akamuona mama yake kapiga magoti kwenye ua, Sara alishangaa sana na kuamua kutoka ili amfate na kumuangalia vizuri maana uchawi wa mapema vile ulimuogopesha hata yeye kwani aliamini tu kuwa mamake ni mchawi ila hakufikiria kama uchawi unaweza kufanywa peupe vile.
 
SEHEMU YA 85


Rose alikuwa kwenye maua akifanya dawa kwaajili ya mzimu wa Moza usifike kwenye nyumba yake maana alianza kupata hisia kuwa huenda mzimu wa Moza ndio unaosumbua akili yake, basi alipiga magoti kwenye lile ua ambalo moza aliwahi kulifukua na kutoa kile kimpira kilichopelekea mpaka kifo chake, kwa upande wa Rose hili ua lilikuwa na maana kubwa sana kwake na lilikuwa likimsaidia vitu vingi sana kwahiyo alipiga magoti na kuanza kusema maneno ambayo hayatakiwi yakatishwe akianza kuyasema mpaka ayamalize, akiwa katikati yay ale maneno alishikwa bega na Sara,
“Mama, mama”
Rose hakumjibu chochote Sara na aliendelea na kusema maneno yake ila Sara nae hakuacha kumuita mama yake hadi akawa anamtingisha,
“Mama, mama jamani mama ndio uchawi gani huu sasa mpaka umeanza kufanya peupe ili tujue kama mama yetu ni mchawi jamani!”
“Mama, namuhitaji Ommy wangu, nirudishie Ommy mama. Nipo tayari kuachana nae ila nirudishie Ommy mama”
Alipoona mama yake hamjibu chochote zaidi ya kuendelea na kitu anachofanya, akapata wazo la kuchukua maji na kumwagia hivyo akafanya kama wazo lake lilivyomtuma. Akafungua bomba na kukinga maji kwenye ndoo kisha akaenda kummwagia mama yake.
Kwakweli hakuna siku ambayo Rose aliwahi kuchukia kama siku ya leo maana aliinuka kwa hasira halafu alimpiga mwanae hadi alizimia yani kipigo alichompiga haikuwahi kutokea, mlinzi alisikia kelele tu na kumfanya azunguke nyuma ambako kelele zilitokea ila akaona Sara akipigwa na mama yake hadi kuzimia kisha mama yake alimuacha Sara hapo na kwenda ndani, yani Rose hakujali kama mwanae amezimia au nini alikuwa na hasira zilizopindukia.
Mlinzi alijaribu kumuinua Sara pale, sema sababu alikuwa na nguvu kwahiyo aliweza kumuinua na kumuweka pembeni kwenye kivuli kisha akaanza kumpepea ila hakuzinduka kwa muda huo.
Salome nae alitoka ndani na kukuta yale yaliyopo kisha akachukua maji na kummwagia Sara, yale maji yalimfanya Sara azinduke ila alikuwa na maumivu makali sana ya kupigwa na mama yake, kisha Salome na mlinzi wakasaidiana kumshika Sara na kumtembeza hadi chumbani ambako walimuweka kitandani apumzike. Mlinzi alitoka na kumuacha Salome akiwa na Sara chumbani, kwakweli Sara alikuwa na maumivu mwili mzima kiasi kwamba hata alivyopigwa pigwa na mama yake hakukumbuka vizuri huku akijiuliza mwenyewe,
“Hivi kilichonipeleka nyuma kule na kuanza kumfanyia fujo mama ni nini? Hivi kilichofanya nichungulie mama anachofanya ni nini?”
“Usijilaumu kwa chochote Sara, katika maisha kila kitu huwa kinapangwa na kinakuwa na maana yake kwahiyo usijipe lawama za bure”
“Hapana Salome, nimejitakia mwenyewe. Mwili wote unaniuma yani wote unaniuma. Mama yangu hajawahi kunipiga kiasi kile, mama yangu hajawahi kuwa na hasira na mimi kiasi kile. Hata kama mama yangu ni mchawi ila sikutakiwa kumfanyia fujo kiasi kile”
Salome alimuangalia Sara kisha akaondoka na kumuacha Sara mwenyewe chumbani akijilaumu tu kwanini amemfanyia fujo mama yake maana mwili wote ulikuwa unamuuma,
“Eti nampigia kelele mama amrudishe Ommy wa kazi gani sasa Ommy, janaume Malaya vile la nini? Kama limewekwa msukule na liwe tu msukule, ona nilivyopigwa na mama, huyu Salome nae sio wa kumsikiliza ushauri wake. Hivi yeye anaweza kufanya kwa mama yake ujinga kama huu! Mama ni mama hata akiwa mchawi, natakiwa kwenda kumuomba msamaha mama”
Sara aliinuka kwa kujikongoja akajivuta hadi chumbani kwa mama yake ambapo aligonga bila kufunguliwa, ikabidi afungue mwenyewe. Alishtuka na kushangaa mama yake akiwa mtupu kabisa ila Rose alizidi kupatwa na hasira kwa mwanae na kuongea kwa hasira,
“Hivi wewe mtoto una nini wewe? Unataka upate laana yangu au?”
sara aliondoka kwa aibu hata hakuweza kuzungumza na mama yake kwani hakutegemea kama angemkuta mama yake akiwa mtupu kabisa, Sara alirudi chumbani kwake huku akijiongezea makosa aliyomkosea mama yake kwa siku hiyo na kujiona ni mtoto mpumbavu asiye na maadili halafu ndio mtoto wa kwanza wa mama yake halafu maadili hana anafanya mambo ya ajabu kama yale.
“Nimemdhalilisha mama yangu, sifai mimi yani sifai kabisa”
Alikuwa akijilaumu tu kwa wakati huo.

 
Wakuu ningependa kuomba radhi kwa kuchelewa kuituma. Huku kwetu Transformer ilileta shida, so hatuna umeme. Hapa nipo internet cafe ya mtaa mwingine.
Ratiba itabadilika kidogo lakini, umeme ukirudishwa mambo yataenda sawa.
 
Back
Top Bottom