Smart911
Platinum Member
- Jan 3, 2014
- 135,167
- 160,806
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KabisaHii ni kupatwa kwa Rose na Ana.
Najikuta nacheka kwa mikasa inayowapata hasa Rose.Kabisa
Kila wanachopanga Salome yuko hatua 5 mbeleNajikuta nacheka kwa mikasa inayowapata hasa Rose.
Asante mkuu kwa kunikumbusha, mambo mengi nikasahauSaa 3 tayariiiiiiii
SEHEMU YA 120
Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana wamejaa kwa mganga Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya kuwashangaza sana,
“Eti kuna nini?”
“Kwani huna taarifa?”
“Taarifa gani?”
“Mganga amekufa”
“Kheee amekufa? Lini tena jamani wakati jana nilikuwa nae”
“Ulikuwa nae wapi na muda gani wakati kafa usiku wa kuamkia jana!”
Rose alimuangalia mwanae Ana akiwa anashangaa sana. Alishindwa kujibu kuwa alikuwa nae muda gani na wapi kwani kila akikumbuka matukio ambayo kafanya na huyo mganga halafu anaambiwa kuwa amekufa alihisi kuchanganyikiwa kabisa, Yule mwanamke akamuuliza tena,
“Ulikuwa nae kivipi ndugu wakati amekufa jana alfajiri na amezikwa jioni”
“Kheeee na kuzika tayari?”
“Ndio, ila bado nakushangaa ulikuwa nae wapi”
“Ni juzi, nimechanganya siku. Yani kifo kimenichanganya hiko”
Ilibidi ajigeleshe lakini ukweli ni kuwa kifo cha huyu mganga kilimchanganya vilivyo ukizingatia na yaliyotokea baina yake na mganga huyo siku ya jana, kumbe mganga alikuwa ameshakufa na jioni aliyomuaga ndio alikuwa anazikwa kwakweli Rose alijihisi kudata kabisa. Akaamua asogee kwa mke wa mganga ili apate tetesi kuwa hata ilikuwaje maana bado alikuwa gizani. Alimkuta mke wa mganga akiwa kajiinamia kwa majonzi, na kumpa pole pale kisha kumuuliza kuwa imekuwaje,
“Eti imekuwaje tena maana ni gafla sana”
“Kweli ni gafla sana, kazi aliyokuwa anafanya mume wangu ni kazi ya hatari sana yani nilijua tu ipo siku nitamkosa kama leo jamani”
Huyu mama aliinama tena akilia, basi Rose akawa anambembelea huku akiendelea kumsikiliza kuwa ni kitu gani kilitokea,
“Mume wangu aliniambia amepata kazi ya hatari sana, nilimwambia aachane na kazi hiyo ya hatari ila hakunisikia alisema lazima ataifanya. Sasa juzi jioni aliniambia kuwa mteja wake huyo mwenye kazi ya hatari kamzuia asifanye sherehe yoyote maana akifanya hivyo atadhurika yeye kwani nyumba ya huyo mteja alianza kuizungushia dawa huku huku. Usiku wake akaniambia mteja amekiuka masharti kwani amefanya sherehe na kupiga vigelegele, yani alikuwa anaumia sana na kujishika tumbo huku akisema wanamuumiza kwa kupiga vigelegele, nilikuwa naogopa sana. Mara akasema wanamuua kwa kukata keki, sikuelewa kabisa ila gafla niliona kimya na nilianza kupiga makelele ya kuomba msaada. Ila walipokuja kumuangalia waliona ameshakufa”
Yule mwanamke akaangua tena kilio, basi Rose akawa anambembeleza huku akijlaumu moyoni kwani alijiona kuwa yeye ndio chanzo cha mambo yote hayo maana kama watoto wake wasingefanya ile sherehe basi yale yote yasingetokea. Ila hakusema hapo kuwa mteja mwenyewe mwenye majanga ndio yeye kwani aliogopa kusema na kuona kuwa atamuweka hasira huyu mama ukizingatia anaonekana alimuonya sana mume wake kuachana na kazi ya hatari kama yake.
Rose alimfariji fariji pale mfiwa kisha akaaga na kuondoka na mwanae ila siku hiyo hata nguvu ya kusubiri pikipiki hawakuipata waliamua kutembea tu mpaka kwenye gari yao, na kwavile walikuwa na mawazo basi hata hawakuona kama ni mbali kutoka kule kwa mganga hadi walipoacha gari. Waliingia kwenye gari huku akili ya Rose ikiwa haifanyi kazi kabisa,
“Lakini mama nilikwambia kuwa nina mashaka”
“Mwanangu usiongee sana, hapa nimechanganyikiwa kabisa yani kabisa kabisa, unajua nimezini na marehemu!”
“Kheeee umezini na marehemu?”
“Tuache hizo habari, twende nyumbani tu. Nishachanyikiwa hapa”
Rose alikuwa amechanganyikiwa kweli yani akili yake haikufanya kazi kabisa kwa muda huo, Ana alikuwa akimuhurumia tu mama ingawa alimuonya kabla ya yote. Rose alikuwa akiendesha gari kurudi nyumbani ila aligubikwa na mawazo mengi sana.