Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 116


Wakawa wanacheka pale, mama yao nae alitoka sebleni wakamsalimia akaitikia na kutaka kwenda nje. Ila Salome alimuuliza,
“Mama, unataka kwenda wapi?”
“Safari zangu hazikuhusu”
Rose akataka kufungua mlango, ila kabla hajafungua Salome alimwambia,
“Usihangaike, mgeni wako nimekuletea”
Kisha Salome ndio akaenda kufungua mlango na mara akaingia Yule mganga. Kwakweli Rose alishangaa sana alijikuta akikaa chini kabisa kwani hakuelewa kabisa kinachoendelea na aliona kiini macho kikifanya kazi vilivyo, ila Salome akamwambia Rose,
“Sasa umeshtuka nini? Unakosa raha kwanini? Si nio ulikuwa ukimuhitaji huyu! Ulitaka hadi kwenda kutuma dereva wa kumfata, mimi nimekuletea eti unaishiwa nguvu kabisa”
Rose hakujibu chochote ila Yule mganga aliingia na kukaa pia, halafu akamuangalia Rose na kumsalimia,
“Habari za tangu jana”
Rose akajibu,
“Mbaya”
Salome aliwaambia watoto wengine wa Rose wamuache mama yao aongee na mgeni,
“Kwetu nilifundishwa kuwa mama anapopata mgeni natakiwa kuondoka na kumuacha mama anazungumza na mgeni, kwahiyo kitendo cha kukaa hapa wakati mama kapata mgeni sio picha nzuri”
Basi nao wakasikiliza ushauri wa Salome kisha kila mmoja kuinuka na kwenda zake chumbani ila Salome alienda kwenye sebule ambayo wale mapacha walipenda kuitumia kwa sana.
Rose alibaki sebleni na Yule mganga, kisha akamuangalia kwa makini kwani alihisi kama ni kiini macho, akamuuliza
“Hivi ni wewe au ni nini?”
“Ni mimi ndio”
“Umefikaje hapa?”
“Niliona yaliyokutokea usiku wa jana, kwahiyo leo mapema nikaanza safari ya kuja huku. Ni sababu tulishakuja mwanzo kwahiyo nilishika njia”
“Ulishika njia vile tumekuja na kurudishwa kimaajabu?”
“Ndio nilishika njia, kwahiyo huniamini kuwa ni mimi!”
“Nakuamini ila mambo yamenichanganya sana, unajua umekuja kiajabu ajabu mpaka nimeshangaa. Kwahiyo tutafanya dawa siku ya leo?”
“Ndio tutafanya dawa, ila kwanza ukanionyeshe kila kitu ambacho huwa unatumia kwenye mambo yako”
Rose akafikilia kidogo kisha akakubali kwenda kumuonyesha kwahiyo yeye na Yule mganga wakahamia ndani na baada ya muda walitoka na kuondoka kabisa pale nyumbani, na Rose alimuaga mwanae Ana tu kuhusu anapoenda na Yule mganga.
 
SEHEMU YA 117


Baada ya muda watoto wa Rose walirudi sebleni na siku hii Salome aliwaandalia chakula cha kuwafurahisha sana, hadi wakawa wanamsifia haswa wale mapacha,
“Yani wewe Salome ni binti mdogo ila unajua kupika kila chakula jamani halafu unapika vizuri balaa”
Kisha Doto akamuangalia dada yake Sara na kumwambia,
“Dada na wewe ujifunze kupika jamani, kwa staili yako utaolewa kweli wewe!”
“Aliyekwambia anataka kuolewa nani, hebu nitoleeni balaa”
“Basi dada usichukie kiasi hiko jamani, leo wifi yako anakuja. Nishampigia simu kumuelekeza kwahiyo akafika tu nitaenda kumchukua nje na utamuona na hakika utamfurahia”
“Bora uongelee mada za hivyo sio kuniletea mada za upishi upishi kama sijui kupika ni mimi msinilazimishe”
Sara alionekana kuchukizwa kabisa na swala la kuambiwa kuwa atakosa mume sababu hajui kupika, na kujikuta akimkumbuka Ommy ambaye alijua wazi kuwa Sara hajui kupika ila alionyesha kumpenda hivyo hivyo, ila akakumbuka kuwa Ommy kafichwa na uchawi wa mama yake na kujikuta akikumbuka kuwa Ommy alimsaliti na mtu mwingine, kila alipokumbuka Ommy ni msaliti basi huruma yake kwa Ommy ilipotea muda huo huo.
Alikuwa kimya kwa muda hadi Salome akamshtua,
“Unawaza nini dada Sara?”
“Niache tu”
“Pole sana, mapenzi yanaumiza eeh! Ila bado, utaona yanavyoumiza zaidi”
“Kivipi Salome mbona sikuelewi”
“Utanielewa tu, mapenzi yanaumiza sana ila kuna jambo linaweza kutokea ukajihisi labda utapata unafuu wa moyo ila ukashangaa unafuu hupati zaiddi ya maumivu”
Wale mapacha nao wakaingilia hizo stori,
“Jamani achene hizo habari za kuumizwa na mapenzi, wengine hatutaki kusikia kabisa. Ziacheni bhana, kila mtu ashughulike na penzi lake”
Salome alitabasamu tu kisha akaenda tena kwenye ile sebule ambayo mapacha wa Rose huwa wanapenda kukaa.
Kwa upande wa Ana alikuwa chumbani kwake tu toka mama yake katoka na Yule mganga kwani yeye alijikuta akiwaza kuwa ni mtego tu mama yake kawekewa maana hakuwa na wazo kuwa Yule ni mganga waliyoendaga kabisa,
“Na kama ni yeye amewezaje kuja mapema hivi ukizingatia kule anakotoka ni ndani ndani sana? Nina mashaka”
Akajaribu nae kukaa akifanya fanya dawa zake huku akiwa amejifungia kabisa kwenye chumba chake, hakutaka kabisa kuongea na mtu yeyote kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 118


Wakiwa pale sebleni Sara na kaka zake, basi kaka yake akasema kuwa mchumba wake amefika kwahiyo akaenda kumpokea kwahiyo Sara na kaka yake mwingine wakabaki wenyewe wanamsubiri huyo wifi kwa Sara na shemeji kwa Kulwa. Ila Sara alimuuliza kaka yake,
“Vipi unamjua huyo mchumba wa Doto?”
“Hata simjui kabisa, Doto msiri sana hajawahi kunionyesha hata mara moja huyo msichana wake”
“Wewe je umeshawahi kumuonyesha wa kwako?”
“Hapana, mimi mwenyewe sijawahi kumuonyesha hata mara moja ila nimepanga siku nimtambulishe hapa nyumbani. Hata leo nilitamani aje pia ila kaniambia amepata udhuru”
“Sawa”
“Na wewe wako? Najua ni Ommy ila sijamuona siku zote hizi”
“Achana na huyo mtu, kwanza ananiumiza kichwa tu. Yani mapenzi yameniumiza kweli mimi, kumbe Ommy alikuwa ananisaliti, kunionyesha kote upendo kule kumbe amepata kasichana kengine ananisaliti nako. Siku niliyogundua niliumia sana”
“Kwahiyo Ommy yuko wapi?”
“Achana nae bhana, atajijua mwenyewe alipo”
“Mmh dada jamani, unajua mtu akikusaliti unatakiwa kuwa mpole kwanza, ujue ni kwanini amekusaliti sio kuweka hasira mbele”
Sara alianza kukohoa na kumuomba kaka yake huyu akamchukulie maji ya kunywa,
“Mmmh maneno yangu yamekufanya upaliwe, basi pole. Ngoja nikakuchukulie hayo maji”
Basi Kulwa akainuka na kwenda kumchukulia maji ya kunywa Sara, ila muda huu huu Doto nae alikuja na kuingia ndani kisha akamwambia dadake asimame kumkaribisha mgeni maana ameshafika,
“Mmmh kama tunamkaribisha raisi jamani! Kumbe utamu wa mtu”
“Acha maneno yako Sara bhana”
Basi akamkaribisha Yule msichana ndani, ila Sara alipoangusha macho yake kwa Yule msichana alishtuka sana kwani alikuwa ni Mishi, alijikuta akimuuliza kaka yake kwa umakini huku akifikicha fikicha macho,
“Kaka, mwanamke mwenyewe ndio huyo?”
“Ndio, kwani vipi mzuri eeh!”
Sara alifikicha tena macho yake, ila kabla hajasema chochote Kulwa nae alikuwa ametoka jikoni akiwa na glasi ya maji ila alipomuona shemeji yake huyo, alihamaki na kumuita kwa mshangao,
“Mishi!!!”
Mishi aliangalia kwa aibu sana, na hakuongea lolote zaidi ya kufungua mlango wan je na kuondoka kuelekea getini, alifika getini na kutoka ila alivyotoka tu alijishangaa akijikuta tena yupo pale pale sebleni halafu mara Salome nae alitoka kwenye ile sebule nyingine akicheka, na kuwakuta pale sebleni huku Mishi akiwa anashangaa shangaa, kisha Salome akasema,
“Sasa Mishi unashangaa shangaa nini? Unaona kama maajabu eeh! Wakati unatenda vitu vya namna hii hukujua kama ni maajabu ya namna hii yangetokea mbele yako? Unataka kukimbia uende wapi na ukimbie kwasababu ya nini? Kaa hapo ujieleze, ni kwanini umechanganya ndugu hawa”
Doto alikuwa na hamaki tu na kujikuta akimuuliza Kulwa,
“Kwani huyu msichana unamfahamu?”
“Nio huyu nilisemaga mchumba wangu mwenyewe, leo nilitaka anitembelee pia akasema ana kazi kumbe ananichanganya na pacha mwenzangu!”
Sara nae akadakia na kutoa dukuduku lake la moyoni,
“Yote tisa, kumi ni kuwa huyu dada ndio kidudu mtu aliyekuwa anatembea na Ommy hadi moyo umeniuma sababu yake”
Wote wakashangaa kuwa Mishi amewachanganya kiasi kile, Doto akajikuta akimwambia,
“Yani kukuhudumia kote kule Mishi bado ulikuwa unanichanganya na ndugu yangu!”
Mishi alikuwa kimya kabisa kwani aibu aliyoipata leo hakuitegemea kabisa, Salome nae akaongea,
“Yani sio kwamba wewe Doto ulikuwa ukimuhudumia peke yako, ni hivi huyu binti wote mmeshiriki kumuhudumia. Kulwa pia umemuhudumia sana huyu binti, halafu hata Sara umemuhudia sana maana hela zote ulizokuwa unampa Ommy alikuwa anapeleka kwa huyu binti. Haya sasa nirudi kwako wewe fundi wa kuumiza mioyo ya watu, hivi hukuwahi kuwaza kuwa mambo unayoyafanya ipo siku utaumbuka? Hivi ni bahati za watu wangapi umezifunika wewe mmoja? Yani wewe utembee na Kulwa, wewe utembee na Doto na wewe utembee na mwanaume wa dada yao, kwahiyo umechanganya familia vilivyo”
“Nisameheni sikujua kama ni ndugu”
MIshi alipiga magoti, na kumfanya Salome acheke sana na kusema,
“Kwahiyo kama si ndugu ni sawa kuwafanyia hivyo? Mwanzoni nilijua ni Ommy anakudanganya kumbe ni wewe unaewadanganya wenzio, hivi ungefanyiwa wewe hivi ungejisikiaje?”
“Nisamehe jamani, nisameheni”
Sara alikuwa na hasira sana na huyu Mishi, hata wale mapacha nao walikuwa na hasira nao vilivyo wakatamani wote wamvamie na wampige ila Salome aliwakataza na kwenda kumkinga Mishi ili wasimpige.
“Tafadhalini jamani msimpige wala msimuumize, mwacheni jamani nataka huyu atembee na laana yangu”
Doto alikuwa na hasira sana, ila Salome alimzuia kabisa kumpiga mishi yani alijikuta akiganda tu bila kumpiga. Salome alifungua mlango na kumruhusu Mishi aondoke ila akamwambia,
“Kumbuka utatembea na laana yangu siku zote, leo utafurahi sana kuwa umewachanganya ndugu lakini hujafanywa lolote ila utatembea na laana yangu siku zote. Laiti kama ningekuwa wewe nisingeondoka leo ila ningekesha nikiomba msamaha”
Mishi hakutaka kusikiliza sana kwani alitoka muda huo huo na hakutaka tena kubakia kwenye nyumba hiyo kwani alijiona kama anamkosi kwa siku hiyo.
Kwakweli si Sara wala wale mapacha waliofurahishwa na kitendo kile kwani kila mmoja alienda njia yake mule ndani akiwa na mawazo yake, haswa Doto alihisi kudhalilishwa sana na Yule mwanamke, kwahiyo sebleni alibaki Salome peke yake.
 
SEHEMU YA 119


Mishi alitumia muda mrefu sana kufika kwao, hata akashangaa kuwa imekuwaje tena wakati ametoka kule muda mrefu. Wakati akitembea aliona usiku umeingia, mara alikatisha kwenye njia hiyo na kujiona yupo mwenyewe hadi akaogopa na kujiuliza,
“Hii njia leo vipi jamani? Imekuwaje yani sioni watu!”
Mara akashikwa bega, kugeuka ni chizi alikuwa amemshika bega, alishtuka sana na kuanza kukimbia ila Yule chizi alimzidi nguvu na kuanguka chini halafu akapiga kelele lakini hakuna mtu yeyote aliyeonekana kumsaidia hadi Yule chizi akambaka halafu akamwambia,
“Asante sana kwa penzi lako”
Yule chizi akaondoka zake na kumuacha Mishi akilia sana, muda kidogo walitokea vijana wawili ambapo Mishi alipowaona aliwaita na kuwaomba msaada kwahiyo wakamuinua Mishi pale chini huku wakimpa pole
“Pole sana dada, ila saizi saa saba usiku mtoto wa kike unatafuta nini njiani?”
Mishi alishangaa sana kuwa ni usiku wa saa saba wakati aliondoka mapema sana kwakina Doto,
“Jamani nisaidieni jamani, sikujua kama ni usiku sana saa hizi”
Wale vijana waliondoka na Mishi ila njiani nao wakamgeuka na kumbaka, kwakweli siku ya leo ilimfanya Mishi achanganyikiwe kabisa kwani walimbaka kwa nguvu hadi akazimia pale pale.

Rose alirudi nyumbani kwake usiku, na kwenda chumbani kwa Ana moja kwa moja ili ampe habari ya kitu alichofanya na Yule mganga. Ila cha kushangaza kabla hajamueleza chochote, Ana alianza kusema,
“Mama ila sina imani na Yule mganga uliyeondoka nae. Naogopa hata usiniambie ambacho umefanya na Yule mganga maana sina imani nae kabisa. Simuamini Yule mganga mama”
“Usiseme hivyo mwanangu, nimefanya nae vitu vingi sana”
“Ndio mama ila sina imani nae, kwanza ujio wake wa kiajabu ajabu sina imani nae kabisa”
“Mwanangu lakini kanirekebishia vitu vingi sana, utaona mabadiliko kuanzia kesho”
“Kabla ya hayo mabadiliko, naomba kesho asubuhi twende kwa huyo mganga tujue mbivu na mbichi mama manake sina imani kabisa hapa”
“Kwahiyo hutaki nikueleze chochote ambacho kimetendeka leo”
“Hata usinieleze na wala usiniambie ulipokuwa siku ya leo, sina furaha kabisa na sidhani kama ulipokuwa palikuwa ni pema”
Ikabidi Rose akubaliane na mwanae kuwa ataenda nae kesho yake kwa Yule mganga, ingawa yeye binafsi alikuwa ameridhika kwa huduma ambazo alifanyiwa siku hiyo na Yule mganga, kwahiyo akaenda chumbani kwake baada ya kumaliza maongezi na Ana.
Ila siku hiyo Ana hakuweza kulala kabisa kwani alikuwa na mauzauza yaliyopitiliza, hakuweza kufanya chochote na wala hakuweza kulala alitamani tu pakuche ili aende na mama yake kwa huyo mganga, alihisi kwa siku hiyo mamake badala ya kuyajenga yani ndio kayabomoa kabisa. Basi kulivyokucha tu ni yeye ndiye alienda kumuamsha mama yake ambaye alimkuta amelala hoi kabisa, yani siku hiyo Rose alilala hadi alijisahau basi mwanae alivyomkurupua ndio akaenda kujiandaa kisha wakatoka na mwanae na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa mganga.
Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana wamejaa kwa mganga Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya kuwashangaza sana,
“Eti kuna nini?”
“Kwani huna taarifa?”
“Taarifa gani?”
“Mganga amekufa”
“Kheee amekufa? Lini tena jamani wakati jana nilikuwa nae”
“Ulikuwa nae wapi na muda gani wakati kafa usiku wa kuamkia jana!”
Rose alimuangalia mwanae Ana akiwa anashangaa sana.
 
SEHEMU YA 120



Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana wamejaa kwa mganga Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya kuwashangaza sana,
“Eti kuna nini?”
“Kwani huna taarifa?”
“Taarifa gani?”
“Mganga amekufa”
“Kheee amekufa? Lini tena jamani wakati jana nilikuwa nae”
“Ulikuwa nae wapi na muda gani wakati kafa usiku wa kuamkia jana!”
Rose alimuangalia mwanae Ana akiwa anashangaa sana. Alishindwa kujibu kuwa alikuwa nae muda gani na wapi kwani kila akikumbuka matukio ambayo kafanya na huyo mganga halafu anaambiwa kuwa amekufa alihisi kuchanganyikiwa kabisa, Yule mwanamke akamuuliza tena,
“Ulikuwa nae kivipi ndugu wakati amekufa jana alfajiri na amezikwa jioni”
“Kheeee na kuzika tayari?”
“Ndio, ila bado nakushangaa ulikuwa nae wapi”
“Ni juzi, nimechanganya siku. Yani kifo kimenichanganya hiko”
Ilibidi ajigeleshe lakini ukweli ni kuwa kifo cha huyu mganga kilimchanganya vilivyo ukizingatia na yaliyotokea baina yake na mganga huyo siku ya jana, kumbe mganga alikuwa ameshakufa na jioni aliyomuaga ndio alikuwa anazikwa kwakweli Rose alijihisi kudata kabisa. Akaamua asogee kwa mke wa mganga ili apate tetesi kuwa hata ilikuwaje maana bado alikuwa gizani. Alimkuta mke wa mganga akiwa kajiinamia kwa majonzi, na kumpa pole pale kisha kumuuliza kuwa imekuwaje,
“Eti imekuwaje tena maana ni gafla sana”
“Kweli ni gafla sana, kazi aliyokuwa anafanya mume wangu ni kazi ya hatari sana yani nilijua tu ipo siku nitamkosa kama leo jamani”
Huyu mama aliinama tena akilia, basi Rose akawa anambembelea huku akiendelea kumsikiliza kuwa ni kitu gani kilitokea,
“Mume wangu aliniambia amepata kazi ya hatari sana, nilimwambia aachane na kazi hiyo ya hatari ila hakunisikia alisema lazima ataifanya. Sasa juzi jioni aliniambia kuwa mteja wake huyo mwenye kazi ya hatari kamzuia asifanye sherehe yoyote maana akifanya hivyo atadhurika yeye kwani nyumba ya huyo mteja alianza kuizungushia dawa huku huku. Usiku wake akaniambia mteja amekiuka masharti kwani amefanya sherehe na kupiga vigelegele, yani alikuwa anaumia sana na kujishika tumbo huku akisema wanamuumiza kwa kupiga vigelegele, nilikuwa naogopa sana. Mara akasema wanamuua kwa kukata keki, sikuelewa kabisa ila gafla niliona kimya na nilianza kupiga makelele ya kuomba msaada. Ila walipokuja kumuangalia waliona ameshakufa”
Yule mwanamke akaangua tena kilio, basi Rose akawa anambembeleza huku akijlaumu moyoni kwani alijiona kuwa yeye ndio chanzo cha mambo yote hayo maana kama watoto wake wasingefanya ile sherehe basi yale yote yasingetokea. Ila hakusema hapo kuwa mteja mwenyewe mwenye majanga ndio yeye kwani aliogopa kusema na kuona kuwa atamuweka hasira huyu mama ukizingatia anaonekana alimuonya sana mume wake kuachana na kazi ya hatari kama yake.
Rose alimfariji fariji pale mfiwa kisha akaaga na kuondoka na mwanae ila siku hiyo hata nguvu ya kusubiri pikipiki hawakuipata waliamua kutembea tu mpaka kwenye gari yao, na kwavile walikuwa na mawazo basi hata hawakuona kama ni mbali kutoka kule kwa mganga hadi walipoacha gari. Waliingia kwenye gari huku akili ya Rose ikiwa haifanyi kazi kabisa,
“Lakini mama nilikwambia kuwa nina mashaka”
“Mwanangu usiongee sana, hapa nimechanganyikiwa kabisa yani kabisa kabisa, unajua nimezini na marehemu!”
“Kheeee umezini na marehemu?”
“Tuache hizo habari, twende nyumbani tu. Nishachanyikiwa hapa”
Rose alikuwa amechanganyikiwa kweli yani akili yake haikufanya kazi kabisa kwa muda huo, Ana alikuwa akimuhurumia tu mama ingawa alimuonya kabla ya yote. Rose alikuwa akiendesha gari kurudi nyumbani ila aligubikwa na mawazo mengi sana.
 
SEHEMU YA 121


Kwa upande wa Mishi, alishtuka akiwa nyumbani kwao wanampepea na aliposhtuka wote walimpa pole akauliza,
“Nimefikaje hapa?”
“Umeokotwa tu mwanangu na wasamalia wema ndio umeletwa muda sio mrefu, hivi ndio tulikuwa tunakupa huduma ya kwanza halafu tukuwaishe hospitali.”
Mishi alijitahidi kuinuka na kumwambia mamake asiangaike na swala la hospitali, ingawa alikuwa na maumivu makali sana ila alijua ni maumivu ya kubakwa kwani tukio zima la usiku wake lilimjia kichwani mwake. Alijitahidi kwenda kuoga na kwenda kupumzika chumbani kwake ila mama yake alionekana kumuhurumia sana binti yake, ila Mishi alijiinamia tu chumbani kwake huku akikumbuka maneno ya Salome kuwa bora angekesha siku nzima pale akiomba msamaha kuliko kuondoka,
“Kwani msichana anayechanganya wanaume nip eke yangu jamani! Kwanini kunipa laana ya hivi! Kwahiyo nimebakwa ndio furaha yao? Yani kama nimepata ukimwi nahakikisha nausambaza kwao, haiwezekani nikafanyiwa hivi. Kwanza Yule ni mtu wa aina gani wa kutoa laana kwangu? Ila dah nimekoma jana, sijui kama nitarudia. Najipa moyo tu”
Aliwaza sana, hakutaka waende hospitali wala hakutaka kuwaeleza nyumbani kwao kilichompata, kwanza alishukuru Mungu kuzinduka kabla ya kupelekwa hospitali kwani kwa yeye ni aibu kubwa mno kusema kuwa alibakwa. Alitulia kidogo na kumuaga mama yake kuwa anaenda duka la madawa,
“Kwanini usimuagize mtu mwanangu Mishi?”
“Mama, mimi ni mzima, acha tu niende mwenyewe”
Hakutaka kuagiza mtu kwani bado alihisi huenda mtu ambaye angemuagiza angejua tatizo lake, alifika duka la madawa na kununua dawa azitakazo ila wakati anarudi kwao, njiani akakutana na Salome na kumfanya ashtuke sana,
“Mbona unashtuka hivyo Mishi? Umeona mzuka, mzimu au kitu gani?”
“Aaaah hapana kitu”
“Hukutegemea kuniona hapa eeeh!”
Mishi alikuwa kimya tu kwani alianza kumuona Salome kama kidudu mtu kutokana na ile laana aliyompa jana yake,
“Mishi, nimekuja kukupa ujumbe mmoja tu. Acha tabia yako hiyo, kama unahitaji mwanaume basi upate mwanaume akuoe na uwe mke wa mtu na utulie kwenye ndoa yako sio kutwa kucha kiguu na njia. Unawazibia wenzio liziki zao, wadada wenzio wapo wengi tu wakitaka wachumba halafu wewe bila aibu una miliki wote. Aibu umeipata kwa wachache tu wale, ila ukiendelea ipo siku nitakukutanisha na wanaume wote unaowachanganya, tulia upate mume”
Mishi alimuangalia Salome kisha alijiuliza kimoyo moyo kuwa huyu binti mdogo hivi anajiamini nini mpaka kusema yale ila hakujua Salome anajiamini nini, hakumjibu kitu na kuanza kuondoka ila Salome akamwambia,
“Ningekuwa ni wewe ningeuliza kuwa baada ya kubakwa kitanipata nini ili nikijua nianze kuchukua hatua ila kwavile wewe ni kiburi na mjuaji basi utakula jeuri yako”
Salome akaondoka na kumfanya Mishi ajiulize sana, na moja kwa moja akahisi labda ni ukimwi.
“Itabidi nikapime ukimwi, jamani katokea wapi binti Yule? Hata sijui kanijulia wapi”
Mishi alirudi kwao ila akiwa na wazo la kwenda kupima ukimwi tu.
 
SEHEMU YA 122


Rose na mwanae Ana walifika nyumbani, kiukweli Rose alikuwa na mawazo sana.
Walipoingia sebleni tu walimkuta Salome akiwa peke yake pale sebleni, na Walipoingia tu aliwapa pole ya msiba, Rose alimwangalia na kujiuliza kuwa amejuaje, ikabidi amuulize,
"Pole ya msiba wa nani?"
"Si wa mganga wako"
"Halafu wewe Salome, nakuangalia tu muda mrefu. Siku zote nakuangalia tu, na utahama humu ndani mwangu"
Kisha Rose akaondoka na Kwenda zake chumbani ila Salome alikuwa akicheka tu kiasi kwamba alimfanya Ana amuangalie kwa hasira sana, ila Salome alimuangalia pia Ana na kumwambia,
"Na bado, mpaka mtaacha"
Ana aliondoka na kuelekea chumbani kwake pia ila alijiuliza sana kuwa huyu Salome anajiamini kitu gani mpaka awe anacheka kwa dharau vile, kumbe mama yake nae alikuwa alijiuliza swala hilo hilo maana Ana aligundua baada ya kwenda kwa mama yake ili wakajadili vizuri na kumkuta mama yake akiongea,
"Hivi huyu Salome anajiamini nini?"
Ana aliingia na kumwambia mama yake kuwa hata yeye kitu hiko kinampa sana mawazo, na kumuuliza mama yake,
"Tutamuweza kweli!"
"Kwanini tusiweze wakati ni binadamu wa kawaida tu yule"
"Kwahiyo tutafanyaje mama?"
"itabidi tutumie nguvu, yani yule Salome tumtoe kwa nguvu maana bila hivyo atatushinda"
"Sawa mama, ila je umeshajua kinachowamaliza waganga tunaowatafuta! Sio huyu huyu Salome kweli!"
"Atatoa wapi nguvu za kufanya vitu vikubwa hivyo?"
"Mama, hebu jaribu kufikiria kwanza. Unakumbuka jana asubuhi yule mganga alifika hapa kabla hujaenda kumfata halafu Salome akakuambia kuwa ni yeye ndio amemleta mganga yule, ukawa huru na kumuonyesha kila kitu, tumeenda kwake na kugundua alikufa juzi kwahiyo yule wa jana labda alikuwa mzimu au uliletewa marehemu bila kujijua"
"Ana tafadhali mwanangu usiendelee kuongea, unanikumbusha machungu. Unajua yule mganga nimefanya nae vitu vingi sana, hadi nimeenda kumuonyesha ile nyumba yangu ya juu ambayo haikaliwi na mtu. Samahani kwa kukwambia haya mwanangu ila yule mganga nimezini nae"
"Yani mama kwa swala hilo tambua kwamba umezini na marehemu, kuanzia leo hata sitaki tena mazoea na yule Salome, na amesema na bado mpaka tuache. Mama bado nina maswali mengi sana, Salome si mtu wa kawaida. Nitaendelea na dawa zangu mwenyewe nikishindwa basi ila kwa waganga wako siendi tena. Inaonyesha nao hawamuwezi"
"Hutakiwi kukata tamaa mapema hivyo mwanangu, ngoja tutumie nguvu kwanza halafu kuna mganga wangu mwingine ndio kiboko kabisa"
"Mama, siku ile yenyewe tulijaribu mikono ikaganda. Kwakweli sitaki tena"
"Mwanangu naomba tujaribu mara ya mwisho tafadhali na sitokusumbua tena tikishindwa kwasasa"
Rose alitumia muda wa ziada kumshawishi mwanae mpaka akakubali mipango ya mama yake.
 
SEHEMU YA 123


Wale mapacha pamoja na dada yao Sara hawakuwa na raha kabisa yani hata siku ile hawakutoka nyumbani kabisa, walikaa ndani tu kwahiyo hata muda ambao mama yao amerudi hawakumsikia sababu walikuwa na mawazo sana. Walikaa wote kwenye sebule ile nyingine huku wakijaribu kujadiliana.
“Jamani mimi sijapendezewa kabisa na Yule Mishi kuondoka bila kumpiga kidogo”
“Nyie ni wanaume ila wote mmemuogopa Salome alivyo mkingia kifua Yule Mishi, yani msichana simpendi Yule loh alifanya nione mapenzi machungu na nilie siku nzima ila ni Salome huyo huyo aliyenizuia kumpiga”
“Ila hatuwezi jua jamani, labda tujipange namna ya kumshambulia Yule binti ila nitawaachia nyie, sina hamu nae mimi yani ananiambia kuna mahali anaenda kumbe analetwa kwetu kutambulishwa na ndugu yangu! Sina hamu nae Yule msichana kabisa”
“Jamani nyie achene tu, nishapoteza hela zangu nyingi sana kwa Yule msichana na lazima nitamkomesha siwezi kukubali”
Doto alionekana kuwa na hasira zaidi na Mishi sababu amejiona kama mjinga na alipata aibu jana ukizingatia ni yeye aliwaambia wenzie kuwa mchumba wake anakuja kumbe mchumba mwenyewe anajulikana na wote maana kashawaharibia mahusiano yao wote, Doto alikuwa na mpango kabambe kwa Mishi na hakutaka kushirikisha wenzie kwani hakutaka kuzuiwa kufanya anavyotaka yeye, kwahiyo walivyoongea ongea pale akawaaga wenzie kuwa anatoka kidogo nao hawakutaka kumuhoji zaidi.
Doto aliondoka zake na safari yake ilikuwa ya kwenda kwakina Mishi, ambapo alifika na kuambiwa kuwa Mishi kalala ila aliomba kuongea nae, Mishi bila ya kujua kuwa ni nani alitoka ila alipomuona kuwa ni Doto akatamani kurudi ndani ila kwavile hakutaka kupata aibu pale kwao kuwa amegonganisha ndugu ikabidi atoke nae, aliposogea nae tu Doto hakuweza kuzungumza na Mishi kwanza kwani alijikuta akinyanyua mkono wake na kutaka kumzaba kofi ila cha kushangaza kabla ule mkono haujaangukia kwenye shavu la Mishi, Doto alijikuta yupo sebleni kwao halafu Salome akiwa mbele yake. Doto alishangaa sana, akajikuta akiuliza
“Imekuwaje?”
“Imekuwa hivyo hivyo ilivyokuwa, si nishawakataza kumpiga Mishi nyie! Kwanza na nyie mmeyataka wenyewe, wewe unakuwaje na mwanamke halafu pacha mwenzio humuonyeshi? Mnataka nini kama sio kutembeleana? NImesema Yule msichana asipigwe ila atapigwa na laana yangu, na nina maana kubwa sana kufanya hivi”
Doto alimuangalia Salome kwa hasira sana kwani alionekana ni msichana mdogo ila aliyekuwa na amri zaidi, ila bado alikuwa hajielewi elewi hata alivyorudishwa nyumbani na kumuuliza swali Salome bado hakuelewa kabisa, akataka kutoka tena nje ila kabla hajatoka akamuona mama yake akiwa na Ana wakija kwa kasi sana na wameshika sufuria la maji ya moto na kummwagia Salome, ila muda huo huo alishangaa kuona kuwa yale maji kumbe alikuwa anamwagiwa yeye na sio Salome, alijikuta akipiga kelele za maumivu.
 
SEHEMU YA 124


Doto alimuangalia Salome kwa hasira sana kwani alionekana ni msichana mdogo ila aliyekuwa na amri zaidi, ila bado alikuwa hajielewi elewi hata alivyorudishwa nyumbani na kumuuliza swali Salome bado hakuelewa kabisa, akataka kutoka tena nje ila kabla hajatoka akamuona mama yake akiwa na Ana wakija kwa kasi sana na wameshika sufuria la maji ya moto na kummwagia Salome, ila muda huo huo alishangaa kuona kuwa yale maji kumbe alikuwa anamwagiwa yeye na sio Salome, alijikuta akipiga kelele za maumivu.
Rose na Ana walistaajabu pia kwani hakuna aliyedhania kuwa yale maji yangemmwagikia Doto, kitendo cha Doto kupiga kelele kiliwafanya watupe sufuria na kwenda kumshikilia hata Sara na ndugu yake Kulwa walikuja kwa kasi ya ajabu kwani kelele za Doto ziliwashtua hadi mlinzi getini aliingia ndani kuona kuna nini tena maana zile kelele hazikuwa za kawaida. Sara alimkuta mama yake amemshikilia Doto huku nae analia pia, Sara akauliza
“Kuna nini?”
“Nenda kachukue funguo ya gari tumpeleke Doto hospitali”
Sara akaenda chumbani kwa mama yake kuchukua funguo kisha kurudi nazo, ambapo mama yake aliwaomba wasaidiane kumkokota Doto mpaka kwenye gari ili wampeleke hospitali. Wakati huo Salome alikuwa pembeni tu kanakwamba haoni tukio linalotokea ila alikuwepo na alikuwa akiwaangalia tu, walimpakiza Doto kwenye gari kisha nyumba nzima wakaenda kumpeleka hospitali kasoro Salome na mlinzi ambaye anabaki kulinda nyumba.
Walipoondoka, huyu mlinzi alimshangaa sana Salome na kumfata kumuuliza,
“Mbona unaonekana hujali kabisa! Utafikiri kitu hakijatokea ndani, yani kama mtu ambaye hujui kinachoendelea”
“Ulitaka nifanyeje”
“Yani huonyeshi kujali kabisa, wenzio wote wameenda hospitali kasoro wewe”
“Mbona na wewe hujaenda?”
“Mimi ni mlinzi”
“Ila unajua kwamba mimi naweza kufika hospitali kabla yao? Ila wale hawaendi hospitali kwasasa”
“Wanaenda wapi?”
“Wakirudi watakwambia walipoenda”
“Unajua wewe sikuelewi toka siku umefika hapa”
“Na kamwe hutokaa unielewe”
Kisha mlinzi akaamua kwenda kuendelea na kazi yake kwani kiukweli hakumuelewa kabisa Salome na muda wote alimuona kama mtu wa ajabu.
 
SEHEMU YA 125


Wakiwa ndani ya gari kwenda hospitali, walienda mwendo mrefu sana na kuona hospitali kisha wakashuka ila wakashangaa tena hapakuwa hospitali ila ni kwa mganga. Rose alikumbuka kuwa huyo ndiye mganga aliyekuwa akizungumza na Ana kuwa ataenda kwa huyo, watoto wake walimuuliza kwa mshangao,
“Mama vipi tena, mbona hapa sio hospitali? Panaonyesha ni kwa mganga”
“Hata mimi mwenyewe sielewi tumefikaje hapa, ila nadhani ni Mungu katuleta kwani mganga huyu nilikuwa namuhitaji sana bora tuingie tu”
Ana alimuangalia mama yake na kumtahadhalisha,
“Mama tulisema tunampeleka kaka hospitali, ila hatukukubaliana kumleta kwa mganga. Sidhani kama tupo sehemu sahihi”
“Mwanangu Ana, usiwe na mashaka. Acheni mimi niingie kwa mganga maana huu ni uchawi aliofanyiwa Doto”
“Ila mama kumbuka kuwa yale maji tuliyopanga kuyamwaga hayakuwa ya kichawi, tunamuumiza Doto ujue, bora tumpeleke hospitali”
Hapa ndio wengine wote wakaelewa kuwa mama yao na Ana wanafanyaga uchawi ndiomana wamesema maji waliyoyamwaga hayakuwa ya uchawi. Rose alikuwa mbishi sana, kwavile tayari alishafika kwa mganga kwahiyo aliona ni vyema kuingia kwa mganga na kuzungumza nae.
Rose alivyoingia kwa mganga, Ana akawapa ushauri ndugu zake kuwa wampeleke Doto hospitali kwakweli hata wao walishangaa sana kuwa moyo wa Ana umebadilika kiasi kile, Kulwa aliingia kwenye gari kisha wote kupanda kwenye gari na kuanza kuulizia kwa watu waliowaona pale njia ya kuelekea barabara kuu na kuulizia hospitali.
Rose hakujua kama amebaki mwenyewe kwa Yule mganga, kisha akaanza kumueleza matatizo yake,
“Yani hapa nilipo, mwanangu kaungua na maji mwili mzima. Naomba unisaidie, ni kweli maji nimemmwagia mwenyewe ila lengo langu ilikuwa ni kummwagia mtu mwingine ila eti akamwagikiwa yeye, si nifanyiwa mambo yasiyofaa hayo babu”
“Sikia Rose, unajua kwamba wewe ndio chanzo cha wale waganga wawili waliokufa, yani wote walitaka kukusaidia wewe wakafa. Sasa umekuja na kwangu unataka kunimaliza na mimi!”
“Hapana, ila nahitaji maisha yangu yarudi kama zamani. Nahitaji kufurahia tena maisha, ona mume wangu hataki hata kuniona na hata sijui akija siku na hasira zake atanifanya nini, dawa zangu hazifanyiki. Nyumba yangu ila siwezi kufanya chochote utafikiri sio nyumba yangu”
“Kwanza niambie umefikaje leo hapa”
Rose akamuelezea kwa kifupi kuwa walikuwa wakimpeleka mwanae hospitali ila wakashangaa wamefika hapo,
“Hata hukugundua kuwa umebadilishiwa njia, badala ya kwenda hospitali ukaja huku! Na kama ameweza kukubadilishia njia huyo mtu basi ujue kuwa anauwezo wa kuzunguka na wewe kila mahali, kwahiyo tunaweza tukapanga dawa mimi na wewe ila akawa ameshatusikiliza yote. Huyo mtu lazima anajua kuwa unapenda sana waganga ndiomana amekuleta kwangu kwa makusudi kabisa”
“Babu, nahitaji kujua ni mtu gani huyo anayenifanyia vitu hivi?”
“Mfano ukishamjua, utafanyaje?”
“Tumshughulikie”
Basi Yule babu akaanza kupiga ramli zake kwa muda kidogo kisha akatulia na kumwambia,
“Siwezi kukwambia nimekatazwa”
“Jamani babu, umekatazwa na nani?”
“Sikia Rose nikwambie kwa usalama wako, rudi nyumbani kwako na ukiona kuna mtu nyumbani kwako anakuelekeza sana basi fatilia anachokiataka mtu huyo”
“Mtu anayependa kunifatilia nyumbani siku hizi ni mmoja tu, na tangu amefika nyumbani kwangu ndio mambo yamebadilika simpendi hata kidogo ila sidhani kama ana nguvu za kichawi kiasi kwamba aniumize mimi”
“Kwanza unajua kama muda umeenda sana, na usiku umeingia. Huwa sifanyi kazi usiku ila alfajiri ndio muda mzuri kwangu”
“Kwahiyo unanishauri nije kesho”
“Ndio njoo kesho”
“Bora nilale hapa hapa na wanagu ili niwahi kesho”
Rose hakuwa na wazo la haraka haraka kuwa Doto anahitajika hospitali kwani alichowaza yeye ni kutibiwa na mganga tu.
Basi akatoka nje ili akawaambie watoto wake ujumbe wa mganga ila hakuwakuta, alishtuka sana kwani hata gari hakuikuta na vitu vyake vyote aliviacha kwenye gari. Akarudi tena kwa mganga, ila mganga alimshauri alale hapo hadi asubuhi ili waangalie watoto wako wapi, Rose hakuwa na namna zaidi ya kukubali tu.
 
Ila Rose kiboko, anapenda kuzini na kila mtu
SEHEMU YA 120



Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana wamejaa kwa mganga Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya kuwashangaza sana,
“Eti kuna nini?”
“Kwani huna taarifa?”
“Taarifa gani?”
“Mganga amekufa”
“Kheee amekufa? Lini tena jamani wakati jana nilikuwa nae”
“Ulikuwa nae wapi na muda gani wakati kafa usiku wa kuamkia jana!”
Rose alimuangalia mwanae Ana akiwa anashangaa sana. Alishindwa kujibu kuwa alikuwa nae muda gani na wapi kwani kila akikumbuka matukio ambayo kafanya na huyo mganga halafu anaambiwa kuwa amekufa alihisi kuchanganyikiwa kabisa, Yule mwanamke akamuuliza tena,
“Ulikuwa nae kivipi ndugu wakati amekufa jana alfajiri na amezikwa jioni”
“Kheeee na kuzika tayari?”
“Ndio, ila bado nakushangaa ulikuwa nae wapi”
“Ni juzi, nimechanganya siku. Yani kifo kimenichanganya hiko”
Ilibidi ajigeleshe lakini ukweli ni kuwa kifo cha huyu mganga kilimchanganya vilivyo ukizingatia na yaliyotokea baina yake na mganga huyo siku ya jana, kumbe mganga alikuwa ameshakufa na jioni aliyomuaga ndio alikuwa anazikwa kwakweli Rose alijihisi kudata kabisa. Akaamua asogee kwa mke wa mganga ili apate tetesi kuwa hata ilikuwaje maana bado alikuwa gizani. Alimkuta mke wa mganga akiwa kajiinamia kwa majonzi, na kumpa pole pale kisha kumuuliza kuwa imekuwaje,
“Eti imekuwaje tena maana ni gafla sana”
“Kweli ni gafla sana, kazi aliyokuwa anafanya mume wangu ni kazi ya hatari sana yani nilijua tu ipo siku nitamkosa kama leo jamani”
Huyu mama aliinama tena akilia, basi Rose akawa anambembelea huku akiendelea kumsikiliza kuwa ni kitu gani kilitokea,
“Mume wangu aliniambia amepata kazi ya hatari sana, nilimwambia aachane na kazi hiyo ya hatari ila hakunisikia alisema lazima ataifanya. Sasa juzi jioni aliniambia kuwa mteja wake huyo mwenye kazi ya hatari kamzuia asifanye sherehe yoyote maana akifanya hivyo atadhurika yeye kwani nyumba ya huyo mteja alianza kuizungushia dawa huku huku. Usiku wake akaniambia mteja amekiuka masharti kwani amefanya sherehe na kupiga vigelegele, yani alikuwa anaumia sana na kujishika tumbo huku akisema wanamuumiza kwa kupiga vigelegele, nilikuwa naogopa sana. Mara akasema wanamuua kwa kukata keki, sikuelewa kabisa ila gafla niliona kimya na nilianza kupiga makelele ya kuomba msaada. Ila walipokuja kumuangalia waliona ameshakufa”
Yule mwanamke akaangua tena kilio, basi Rose akawa anambembeleza huku akijlaumu moyoni kwani alijiona kuwa yeye ndio chanzo cha mambo yote hayo maana kama watoto wake wasingefanya ile sherehe basi yale yote yasingetokea. Ila hakusema hapo kuwa mteja mwenyewe mwenye majanga ndio yeye kwani aliogopa kusema na kuona kuwa atamuweka hasira huyu mama ukizingatia anaonekana alimuonya sana mume wake kuachana na kazi ya hatari kama yake.
Rose alimfariji fariji pale mfiwa kisha akaaga na kuondoka na mwanae ila siku hiyo hata nguvu ya kusubiri pikipiki hawakuipata waliamua kutembea tu mpaka kwenye gari yao, na kwavile walikuwa na mawazo basi hata hawakuona kama ni mbali kutoka kule kwa mganga hadi walipoacha gari. Waliingia kwenye gari huku akili ya Rose ikiwa haifanyi kazi kabisa,
“Lakini mama nilikwambia kuwa nina mashaka”
“Mwanangu usiongee sana, hapa nimechanganyikiwa kabisa yani kabisa kabisa, unajua nimezini na marehemu!”
“Kheeee umezini na marehemu?”
“Tuache hizo habari, twende nyumbani tu. Nishachanyikiwa hapa”
Rose alikuwa amechanganyikiwa kweli yani akili yake haikufanya kazi kabisa kwa muda huo, Ana alikuwa akimuhurumia tu mama ingawa alimuonya kabla ya yote. Rose alikuwa akiendesha gari kurudi nyumbani ila aligubikwa na mawazo mengi sana.
 
Back
Top Bottom