LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................351 - 355
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY
Sura ya: 351
Baada ya Joel kujionea ‘live’ usaliti wa Nina, alishindwa kuvumilia na kupata mshtuko wa moyo. Lisa alimpeleka baba yake haraka hospitali kuingiziwa dripu ya IV. Ingawa kuona Nina akikamatwa kulimfanya Joel kupumua, afya yake ilidhoofika tena kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa.
Haikuchukua muda Mzee Ngosha na Bibi Ngosha wakakimbilia hospitali. Mara baada ya Bibi Ngosha kuiona hali ya Joel, machozi yakaanza kumlenga lenga. "Nina hana akili. Tulimtendea vizuri sana kwa miaka mingi. Ajali uliyokutana nayo miaka mitatu iliyopita lazima inahusiana naye. Kwa bahati nzuri, mimi na baba yako tulimwomba Lisa akutunze. Vinginevyo...”
Maneno hayo yalipelekea mtetemo kwenye uti wa mgongo wa Mzee Ngosha. Sasa alipofikiria jambo hilo, alitoa shukrani zake za dhati kwa Lisa. "Tuna deni kubwa kwako, mjukuu wangu..."
Lisa alitabasamu na kukaa kimya kwa muda. “Usijali kuhusu hilo, babu. Sikuwahi kutarajia mengi kutoka kwa familia ya Ngosha, kwa hiyo sijavunjika moyo.”
“Wewe...” Mzee Ngosha aliona aibu ghafla.
Bibi Ngosha akamvuta. “Lisa yuko sahihi. Kwa kweli tabia yetu ilimkatisha tamaa tangu mwanzo. Ni kosa langu. Sikupaswa kumzuia Joel kumuoa mama yako. Samahani sana."
Mzee Ngosha alikunja ngumi na kukohoa kwa aibu. “Nakubaliana na bibi yako. Kuanzia sasa jisikie huru kabisa. Unakaribishwa nyumbani muda wowote utakao. Baada ya yote, hiyo ni nyumba yako."
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda na kujawa na hisia mseto. Kwa kweli, alitamani kwamba babu na bibi yake wangemwambia hivyo alipofika Nairobi kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, walimzingua pindi tu walipomuona. Siku zote alilazimika kupambana peke yake ndani ya jiji hilo, jambo ambalo lilimfanya ajisikie kama mgeni.
Wakati huo, kuna mtu aligonga mlango, ambapo Melanie aliingia akimsukuma Damien, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu.
“Mnatafuta nini hapa?” Joeli alipowaona, alianza kupandwa na hasira na kukohoa kwa nguvu.
“Joel, usifadhaike. Ni mbaya kwa afya yako.” Mzee Ngosha kisha akawanyooshea kidole Damien na Melanie, na kusema, “Tokeni nje.”
“Babu tumekuja kukuomba msamaha. Kwa kweli sikujua kwamba Mama alifanya mambo hayo.” Melanie aliinua kichwa chake na kujibu kwa uchungu. Macho yake yalikuwa mekundu.
“Ulikuwa hujui kweli?” Lisa alidhihaki, “Wewe ndiye uliyempeleka Baba kwa uchunguzi wa kimatibabu kila mara. Wewe na Nina mlipanga njama hizi zote pamoja, lakini una bahati kwamba mama yako ndiye aliyebeba lawama zote.”
Baada ya ukimya wa muda, Lisa alihamishia macho yake kwa Damien. “Baba mdogo, ninazungumza na wewe hivi kwa sababu mimi ni mtu mstaarabu sana. Kama ningekuwa wewe, ningeona aibu kujitokeza hapa. Ikiwa baba yangu angekufa kwa sumu, Kampuni ya Ngosha ingeenda kwako na Melanie. Nyote wawili mngefaidika zaidi, na Nina aliyeenda gerezani kwa niaba yenu.”
Uso mzuri wa Damien ulilegea kabla ya kujibu, “Siku zote nimemchukulia kaka yangu kama baba yangu, kwa hiyo ningewezaje kujaribu kumuua kaka yangu? Kaka nitapiga magoti nakuomba msamaha sasa. Kwa miaka hii yote, nilipumbazwa na Nina na nimefanya mambo mengi mabaya dhidi yako, lakini sikupanga kukuua hata kidogo.”
Damien alipokuwa akizungumza, alijilazimisha kutoka kwenye kiti cha magurudumu na kupiga magoti sakafuni. Hata hivyo, miguu yake ilikuwa dhaifu sana kuweza kusimama. Mara miguu yake ikageuka kuwa mlenda, alianguka sakafuni vibaya.
“Baba.” Melanie alilia na kwenda kumshika kwa haraka.
“Melanie, nishike nipige magoti.” Damien aliendelea.
Kwa kuwa Damien alikuwa mwanae wa kumzaa, Bibi Ngosha alishindwa kuvumilia kumuona akipiga magoti. “Miguu yako imelemaa. Utapiga magoti vipi? Fanya haraka ukae kwenye kiti chako.”
"Ndio, miguu yangu imelemaa." Damien
aliinamisha kichwa chini na kububujikwa na machozi. “Tangu nilipozaliwa, watu wengi wamekuwa wakinidharau kwa sababu tu ya ulemavu wangu. Ninamshukuru Kaka, lakini wakati huo huo, ninamwonea wivu. Nampenda Nina, lakini hakuwa anavutiwa nami. Zaidi ya miaka ishirini iliyopita, sijawahi kumpenda mtu mwingine yeyote isipokuwa yeye. Nilimfanyia kila kitu bila kulalamika. Nilidhani angeniangukia hatimaye baada ya kupata Ngosha Corporation, lakini nilikosea. Ni sasa tu ndio nimeelewa utu wake. Baba, Mama, Kaka, ni kosa langu...”
Bibi Ngosha alikuwa kwenye hatihati ya kulia. Hakuweza kupinga kusema, “Yote ni makosa yangu. Sikupaswa kukuzaa na kukufanya uteseke sana na kujidharau.”
“Baba, Mama, mnaweza kunilaumu mimi. Ni sawa. Lakini natumaini hamtamchukia Melanie.” Damien aliinua kichwa chake na kuomba. "Melanie hana hatia. Sijawahi kuoa, na yeye ni binti yangu wa pekee. Yeye pia ni mjukuu wako wa damu.”
“Babu, Bibi, samahani. Nimekuwa mbali nanyi kwa muda mrefu, na imenisikitisha sana. Bado mnakumbuka jinsi mlivyokuwa mkinijali?" Melanie mara moja akapiga magoti karibu na Damien. Alitazama juu na kugeuza nywele zake kuelekea nyuma, akionyesha uso uliopigwa na kuvimba.
"Ni nini kilitokea kwenye uso wako?" Mzee Ngosha aliuliza kwa sauti nzito.
Melanie akasonga na kuuma mdomo. Kisha, Damien akasema kwa huzuni,
“Ni Jerome aliyempiga.”
"Ni mpuuzi sana huyo mwanamume." Mzee Ngosha alipandwa na hasira. "Familia ya Campos ina kiburi sana. Nitakutana na babu yake.
Familia yetu imewanyanyua sana mafukara wale wasio na shukrani, hawakuwa na kitu chochote!”
“Ni sawa, babu. Tayari wewe ni mzee. Hakuna haja ya kusimama kwa ajili yangu, na sitaki wewe kuwa upset kwa sababu yangu. Familia ya Campos sio sawa na ilivyokuwa hapo awali. Jerome alisema kwamba alinioa kwa sababu tu alifikiri nilikuwa...Binti wa Joel. Alichagua kuwa nami kwa sababu ya familia ya Ngosha.” Tabasamu la uchungu likapita usoni mwa Melanie.
“Ni dharau kiasi gani?” Damien alisema
kwa uchungu huku akimpapasa Melanie sehemu ya nyuma ya mkono wake. “Ni kosa langu, sio lako. Ananidharau kwa sababu mimi ni mlemavu na siwezi kumsaidia chochote”
“Inatosha!” Bibi Ngosha hakuweza kuvumilia tena kusikia hivyo. "Sasa kwa kuwa Nina yuko jela, acha yaliyopita yawe yamepita. Damien, bora usiishi peke yako huko nje. Rudi nyumbani. Uwe mtu mzuri na ulete sifa njema kwa familia ya Ngosha pamoja na kaka yako.”
“Naweza kweli kufanya hivyo?” Damien kwa tahadhari akahamishia macho yake kwa Joel aliyekuwa amejilaza kitandani. “Baba, ni sawa. Sitaki Kaka anielewe vibaya.”
Midomo ya Joel ilicheza, lakini kabla
hajazungumza, Melanie alisema, “Baba, msikilize babu. Mimi nakaa katika nyumba ya familia ya Campos. Nina wasiwasi kuhusu wewe kuwa peke yako katika hali yako. Je, ukianguka? Hata iweje, mtumishi wako si sehemu ya familia yetu kamwe.”
“Rudi tu.” Maneno ya Melanie yalimfanya Bibi Ngosha kukosa raha. "Hamia nyumbani leo."
Joel akafumba macho. Muda si mrefu, Mzee Ngosha na Bibi Ngosha waliondoka wakiwa na Damien na Melanie. Lisa alikuwa akitazama tukio zima kimyakimya. Hakuwahi kufikiria kwamba Damien na Melanie bado wangepokea hisani nzuri kwa wazee hao baada ya Nina kufungwa gerezani. Ukiachana na Melanie, Damien hakuwa na haya kama mwanaume.
“Unawaza nini baba?” Macho ya Lisa yakatua kwa baba yake. Ikiwa baba yake naye alifikiria sawa na babu na bibi yake, Lisa angejuta kujiingiza kwenye sakata hilo.
“Unafikiri kwamba mimi bado ni mjinga kama hapo awali? Baada ya kupitia mengi, nimeshajifunza somo langu.” Joel alilalamika. "Damien anatisha zaidi kuliko hata Nina. Anajua kabisa kwamba babu na bibi yako watamhurumia na kumbembeleza.”
“Najua." Lisa akahema. Babu na bibi yake walionekana kuwa wazee, lakini walikuwa na mali nyingi. Ingawa Mzee Ngosha alikuwa amestaafu kufanya kazi, bado alikuwa na nguvu katika Ngosha Corporation na ushawishi katika jiji la Nairobi. Mara baada ya Melanie na
Damien kupata kampuni ya Ngosha Corporation, wangemtumia tena.
Sura ya: 352
“Lisa, kwa kuwa niko hospitalini, nitakuomba unishughulikie mambo fulani kwa sasa.” Joel ghafla akampiga piga Lisa nyuma ya mkono wake. "Nitamwambia msaidizi wangu kuripoti kwako mambo yote ya kampuni kuanzia sasa."
Kichwa cha Lisa kilianza kumuuma. "Baba, unanilazimisha kijanja kusimamia Kampuni ya Ngosha?"
“Ninakulazimisha vipi?” Joel alimkazia macho. "Kama binti yangu na mrithi wa Ngosha Corporation, hutaitwa tena binti haramu. Unastahili kuwa na mwanmke
bora kabisa katika Kenya nzima. Hata Sarah pia hawezi kufananishwa na wewe.”
Nia ya Joel hatimaye ikamwingia Lisa. Hisia ya joto ikaenena ndani yake. Bila kusema, Joel lazima aligundua kuwa Alvin alikuwa akienda kufunga ndoa na Sarah, hivyo alitaka asihizunike. Kwa kuzingatia kwamba Lisa alikuwa mmiliki wa Mawenzi Investments, binti pekee na mrithi wa Ngosha Corporation, Sarah asingeweza kumshinda kwa heshima na hadhi. Haidhuru Sarah alikuwa na jeuri kiasi gani, yeye alikuwa mwanasaikolojia tu. New Era Advertisings, kampuni ya familia yao, ingekuwa imeanguka kwa muda mrefu bila usaidizi wa Alvin, na Thomas angekuwa jela kama si kukingiwa kifua na Alvin.
“Usijisumbue na mambo hayo mwanangu. Utaweza kupata mtu bora zaidi anayekustahili. Binti yangu ni mrembo sana, mwenye uwezo, na tajiri. Hakuna mtu yeyote katika Kenya anayeweza kukuzidi,” Joel alimtia moyo huku akitabasamu.
“Asante, Baba. Ninajiamini kila wakati. Kwa wale ambao hawakunichagua, ni hasara yao.”
"Safi sana." Joel alitabasamu.
Saa kumi jioni, Lisa alipanga foleni kwenye chumba cha pharmacy kilichokuwa chini ili kuchukua dawa. Alipomaliza, alirudi juu na kumuona Maya akitoka nje ya kitengo cha uzazi na magonjwa ya uzazi ya wanawake akiwa na Sarah.
Akiwa amevalia nguo nyeupe, Sarah alionekana kama malaika kiasi kwamba kila mtu hospitalini alimtazama mara mbili mbili. Kwa upande mwingine, Lisa alikuwa rafu kidogo kwani siku nzima tangu jana yake alikuwa akimuuguza Joel hospitalini. Hakuwa hata na chembe ya kipodozi usoni na nywele zake zilikuwa zimetimka kidogo, na alionekana amechoka.
Sarah alilinganisha sura yake ya nje na ya Lisa, akafurahi sana, na akapata nguvu ya kuongea mbele yake. "Hi, Lisa. Nini kinakuleta hapa? Nini tatizo? Hujisikii vizuri?”
Lisa akatoa macho yake na kuendelea kwenda mbele bila kumjali Sarah. Alihisi kuchoka sana baada ya kumtunza Joel kwa siku moja. Hakuwa na nguvu ya kupoteza kuongea upuuzi na
mwanamke yule.
“We mwanamke, mbona huna adabu hivyo?” Maya alipiga kelele, “Bi Njau alikuwa anakusemesha, ina maana hujamsikia?”
“Bi Njau ni nani na kwanini nijibu swali lake?” Lisa aliwageukia kwa jazba na kusimama kwenye korido. Aliwatupia macho wawili hao kwa hasira.
“Wewe...” Maya alikuwa amekasirika kwa hasira.
Sarah alimsimamisha Maya na kusema kwa upole, “Lisa, najua unanichukia, lakini nimejitayarisha kukukubali. Kwa kweli ninampenda Alvin sana, na wewe najua unampenda, kwa hivyo tunaweza tu kushea. Naweza kukubali hilo.”
Lisa alichukizwa. “Oh, asante. Lakini sina mpango wa kushea mume na mtu yeyote. Ninaogopa kuambukizwa maradhi.”
Sura ya Sarah ilibadilika kidogo, kisha akainamisha kichwa chake. “Unathubutuje kutoa maneno ya dharau hivyo? Unapolala naye kila siku haimaanishi kwamba unampenda?” Aligusa tumbo lake huku akisema, “Sawa, unaweza kukaa kando basi uniachie mume wangu. Nimepanga kuzaa watoto wengi kwa Alvinic. Nilikuja hospitalini leo kuangalia jinsi ya kupata mapacha au mapacha watatu kwa njia ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi.”
Maya alitabasamu na kusema, “Ni Bw. Kimaro ambaye alipendekeza kufanya urutubishaji kwa vitro aliposikia kwamba Sarah alitaka kupata angalau watoto
wawili. Aliogopa kwamba angekuwa na wakati mgumu kuwa mjamzito mara mbili. Tayari amemuomba Dokta Choka kuajiri timu bora zaidi ya madaktari wa uzazi nchini kwa ajili yake.”
“Maya...” Sarah alimtazama kwa aibu na kudhihaki.
Macho ya Lisa yalitangatanga na kutua kwenye tumbo la Sarah kabla ya kucheka ghafla. "Ni bora kuwa mwanaume. Ni rahisi kwao kusema kwa vile wana kazi ya kutoa manii tu kwa ajili ya kuingizwa kwenye hiyo ‘artificial insemination’. Lakini wanawake wana kazi kubwa ya kupitia kila aina ya shida. Katika hatua za mwanzo, wanawake wanatakiwa kuchukua sindano na madawa. Nilisikia kwamba mchakato wa kuingizwa mbegu ni mchungu sana pia. Nakushangaa sana. Upendo wangu
kwa Alvin si kama wako.”
Uso wa Sarah ukabadilika ghafla. Kwa kweli, alijua kila kitu ambacho Lisa alikuwa ametaja. Yeye pia alikuwa hataki, lakini hakuwa na jinsi kwa sababu Alvin hakuweza kumgusa hata kidogo.
“Umemaliza? Una wivu tu.” Maya alimshutumu Lisa kwa hasira.
"Nina wivu?" Lisa aliinua mabega yake. “Nina wivu gani? Nimepata mimba ya mapacha hapo awali, kwa hivyo sihitaji kupitia shida hizi zote. Inaonekana nimeweka kiwango cha juu sana kwa Alvin kwamba mtoto mmoja hawezi kumtosha tena.”
“Umezidi sasa Lisa.” Sarah aliuma mdomo wake kwa huzuni, na machozi yakaanza kumlenga lenga.
Lisa alitazama pembeni, na hakika Alvin alikuwa akielekea kwao. Kulikuwa na viongozi wachache wa hospitali pamoja naye.
Alipofika juu na kumuona Sarah analia, alimwangalia Lisa mara moja. “Ulimfanya nini tena? Si tayari tumeachana, kwanini unaendelea kutusumbua?”
Lisa aliongea kwanza kabla Sarah hajafungua mdomo wake. "Nilikuwa nashangaa tu kusikia kwamba umemwambia Sarah akuzalie watoto kwa njia ya upandikizi wa bandia. Kwanini usimruhusu apate mimba kwa njia ya kawaida? Unajua kwamba ni lazima atumie sindano na dawa kila siku kabla ya kuingizwa mimba kwa njia ya bandia? Bi. Njau, sisemi uwongo, sivyo?”
Sarah, ambaye mwanzoni alitaka kulalamika huku akitokwa na machozi, alipigwa na butwaa. Lisa hapo awali alikuwa akimnanga Sarah, lakini sauti yake mbele ya Alvin ilimfanya aonekane kana kwamba alimwonea huruma Sarah. Sarah alipoona hali ya kutofurahi ya Alvin, alieleza upesi, “Alvinic ana wasiwasi kwamba nitakuwa nimechoka sana ikiwa nitaendelea kubeba mimba mara kwa mara.”
"Ikiwa una wasiwasi kuhusu kumchosha, basi inatosha tu hata kubeba mimba mara moja. Hakuna haja ya kuwachukulia wanawake kama mashine za kutengeneza watoto,” Lisa alisema huku akiachia tabasamu. “Kawaida wanandoa wanapoenda kwa ajili ya upandishaji mbegu kwa njia ya bandia, ni aidha hawana uwezo wa
kuzaa au hawawezi kufanya ngono. Lakini ninafahamu wazi kama una uwezo au la. Haiwezekani kuwa ni Bi. Njau ambaye hana uwezo wa kuzaa...” Aliziba mdomo kwa mshangao. “Nakumbuka sasa. Nyote wawili mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, lakini bado hana ujauzito.”
Uso mdogo wa Sarah ulibadilika rangi kwa hasira. Kwa hakika angeweza kupata mimba, lakini Alvin ndiye ambaye hakutaka kumgusa. Lakini, hakuweza kusema hivyo waziwazi, kwa hivyo aliweza kukubali tu macho ya kushangaza kutoka kwa viongozi wa hospitali. Alifadhaika sana hadi machozi yakaanza kumdondoka.
"Lisa, nitakuchana mdomo ikiwa utaendelea kuongea upuuzi." Alvin alimvuta Sarah kwenye kumbatio lake.
Kisha, akasema kwa hasira kwa viongozi wa hospitali, “Mfukuzeni hapa. Sitaki kumuona.”
Akiwekwa katika hali ngumu, mkurugenzi wa hospitali alisema, “Bwana Kimaro, Lisa ni binti wa Bwana Ngosha. Bwana Ngosha kwa sasa amelazwa katika hospitali yetu...”
“Nataka familia ya Ngosha ihamie hospitali nyingine. Sitaki kumuona hapa,” Alvin alifoka na kuondoka huku akiwa amemkumbatia Sarah.
"Alvinic, yote ni makosa yangu. Nilikutia aibu.” Sarah alinung'unika mikononi mwake.
“Sio tatizo lako. Mimi ndiye nina makosa kukuacha uende kupandishwa mbegu kwa njia ya bandia.” Alvin
alichanganyikiwa pia. Maneno ya Lisa yaligusa udhaifu wake, na kumfanya ajisikie fedheha.
“Ni sawa. Ilimradi niweze kuzaa mtoto wako, niko tayari kufanya hivyo,” Sarah alisema kwa utulivu. Alvin akahema. Alijisikia vibaya kwa ajili ya unyonge wa Sarah.
Dakika 15 baadaye, Lisa alipokea taarifa kutoka hospitalini kuwaamuru wabadili hospitali. Joel alikuwa katikati ya matibabu yake, lakini alikasirika aliposikia kuhusu hilo. “Alvin ana kiburi sana. Kwani familia yetu ilikuwa na chuki dhidi yake katika maisha yetu ya zamani? Au, matibabu yangu yalimsumbua kwa namna yoyote?” “Baba si wewe uliyemsumbua, ni mimi.” Mapigo ya moyo wa Lisa yalikuwa chini. Angekumbuka kila kitu ambacho Alvin alikuwa amewafanyia.
“Lisa, usiwe na huzuni. Ni tatizo langu. Sikupaswa kuja katika hospitali ya familia ya Choka. Familia ya Choka na familia ya Kimaro zimetiwa lami kwa brashi sawa. Hebu tuondoke. Nitakumbuka ukatili huu wa leo. Sisi akina Ngosha tutarudisha walichotufanyia huko mbeleni,” Joel alisema huku akitulia.
“Ndiyo. Tutarudisha walichotufanyia.” Lisa aliitikia kwa kichwa.
Sura ya: 353
Siku iliyofuata baada ya Nina kuhukumiwa, Joel alitangaza hadharani kwamba amemfanya Lisa kikamilifu
kama mrithi wake na mrithi wa urithi wake. Zaidi ya hayo, Lisa angekuwa msimamizi wa kila jambo, liwe kubwa au dogo, alipokuwa amelazwa hospitalini.
Hapo ndipo watumiaji wa mtandao walipogundua kwamba utajiri wa Joel ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni tatu. Pamoja na thamani ya soko la kampuni ya Mawenzi Investments, ilimaanisha kwamba Lisa angekuwa mwanamke tajiri zaidi nchini Kenya.
Si hivyo tu, lakini mitandao pia ilisheheni picha mbalimbali za urembo wake na sifa zake za elimu ya juu. Mamia ya maoni yalitiririka kufuatia habari hiyo kusambaa kama upepo mitamdaoni;
[Nimekuwa mmoja wa mashabiki wake. Ni mwanamume gani atastahili mwanamke tajiri, mrembo, na mwenye
kipaji kama yeye?]
[Hivi, hata anahitaji mwanaume kweli? Si bora kwake kuwa single? Anaweza hata kubadili kati ya wavulana wachache na wazuri wakati wowote anaotaka.]
[Ni ukumbusho tu kwamba yeye ndiye mke wa zamani wa Alvin Kimaro.]
[Hivi Alvin Kimaro ni kipofu? Lisa ni dhahiri kuwa ni bora kuliko Sarah kwa sura, thamani halisi na urembo.] Mashabiki wa Sarah ambao hawakuridhika walionekana kumtetea pia.
[Sarah ana shida gani? Yeye ni mwanasaikolojia maarufu. Ana kipaji na mzuri pia. Kando na hilo, yeye ndiye mmiliki wa New Era Advertisings.]
[Kwani ni nini ikiwa yeye ni mwanasaikolojia? Lisa pia ni miongozi mwa wabunifu bora wa Kilimani Group, na mkurugenzi mkuu wa ubunifu wa kampuni hiyo]
[Kilimani Group ni nini? Sijawahi kusikia.]
[Jibu mbele yangu. Ni sawa kama hujui, lakini tafadhali usifichue ujinga wako. Utaiona mara tu unapotafuta kwenye mtandao. Kilimani Group ni kampuni ya ujenzi maarufu na yenye mapato ya juu zaidi Afrika. Watu wengi wenye vipaji katika Kilimani Group ni wasanifu mashuhuri wa kimataifa ambao wamepokea tuzo nyingi, na mapato yao ya kila mwaka yanazidi makumi ya mabilioni kwa urahisi. Ili kuwa afisa mkuu wa kubuni wa Kilimani Group,
lazima awe mmoja wa wasanifu watano bora Afrika, angalau. Lisa alishinda tuzo kadhaa huko Tanzania na hapa Kenya kama vile Grand-Prix award ya Lexus Crowns]
[Hiyo haiwezekani. Lisa bado mdogo sana. Acha kukuza mambo.]
[Naweza kuthibitisha hilo. Siyo ya kujisemea tu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, nilipata fursa ya kufanya mafunzo yangu katika Kilimani Group mwaka jana. Nilitokea kukutana na Lisa, na wakati huo, hata Lorenzo alikuwa akimheshimu.]
[Lorenzo. Unazungumza juu ya mbunifu, Lorenzo, ambaye alichukua Tuzo la ‘AAK Duracoat Awards of Excellence in Architecture’ mwaka jana?]
[Ndiyo, huyo ni yeye.]
Huku kukiwa na mjadala mzito kwenye mtandao, Kilimani Group ilichapisha kimataifa picha ya Lisa: [Bi Lisa Jones, afisa mtendaji mkuu wa kampuni yetu, ambaye alichukua nafasi hiyo mwaka jana.]
Habari hizo zilishangaza Kenya nzima. Watu wengi walitoa maoni kwenye akaunti ya Facebook ya KIM International.
[Bwana Kimaro, hadhi ya mke wako wa zamani imekuwa juu sana. Unajuta?]
[Haha, Alvin Kimaro, asante kwa kumtaliki Lisa wetu. La sivyo, asingekuwa hapa alipo leo.]
[Bwana Kimaro, tafadhali usijute na uje
kumtafuta Lisa wetu siku zijazo.]
Kwa siku moja nzima, mratibu wa ukurasa wa Facebook wa KIM International alikuwa na kazi ya kufuta ujumbe mmoja baada ya mwingine, lakini maoni hayakuwa na mwisho, kadri alivyoyafuta ndivyo yalivyozidi kuingia. Jambo hilo lilimfanya aingiwe na wasiwasi kiasi cha kutokwa na jasho.
Wakati huo, mkutano wa ndani wa ngazi ya juu wa KIM International ulikuwa ukiendelea. Jack alikuwa akitazama chini kwenye simu yake wakati ghafla alifoka. Chumba cha mikutano, ambacho kilisikika sauti ya Alvin pekee, kilikuwa kimya sana. Kila mtu alitazama kuelekea Jack.
Umbo la Alvin la kifahari liliegemea nyuma, na kalamu iliyokuwa mikononi
mwake akaitupa mezani. Macho yake makali yalikuwa ya hasira kali. “Meneja Mkuu Kimaro unajishughulisha na nini? Kwanini haupo pamoja nasi kwenye mkutano?”
Jack aligusa pua yake. “Unataka kujua kweli?” Wasimamizi wakuu walishusha pumzi zao. Waliweza kuhisi hali ya hewa ikiwa imeanza kuchafuka. Wawili hao walipokaa pamoja haikupita hata dakika tano bila chumba kugeuka kama Urusi na Ukraine.
“Ninaangalia akaunti rasmi ya Facebook ya kampuni. Inakaribia kulipuka.” Jack alitabasamu bila kufafanua. "Inahusiana na wewe, Mkurugenzi Kimaro."
Meneja mmoja alicheka na kusema, “Lazima ni watu wanaompongeza Mkurugenzi Kimaro na Bi. Njau kwa harusi yao.”
"Hiyo ni sawa. Hivi majuzi, watu wengi walikuja kwenye kampuni kutoa baraka zao. Mkurugenzi Kimaro ndiye mtu tajiri zaidi wa Kenya.”
Alvin alibaki kutojali, lakini alikubaliana na kile wasimamizi wakuu walisema. Hata hivyo, hakupendezwa na mambo hayo hata kidogo. "Kwa hivyo ... hiyo ndiyo sababu umakini wako ulizunguka kwenye simu yako katika mkutano muhimu wa kampuni?"
“Hapana, umeelewa vibaya. Inahusu... mke wako wa zamani.” Jack aliinua mabega yake. "Huenda hujui kuhusu hilo bado, lakini Joel tayari amemfanya Lisa kuwa mrithi wake. Wanamtandao wanajadili thamani halisi ya Lisa, na kuna mtu hata akafichua madili yake yaliyofichwa. Kumbe yeye ni
mkurugenzi wa ubunifu wa Kilimani Group. Kilimani Group tayari imethibitisha hilo.”
"Kilimani Group?" Baadhi ya wasimamizi wakuu walishangaa. "Ni ukweli? Hiyo ndiyo kampuni ya juu zaidi ya ujenzi Afrika. Wanaofanya kazi huko wote ni magwiji katika uwanja wao. Ni lazima awe gwiji kwa kuwa na cheo kama hicho.”
“Sisemi uongo. Unaweza kujiangalia mwenyewe ikiwa huniamini.” Jack alimtazama Alvin kwa kuchekacheka. “Kaka, ulijua hilo? Hata hukuniambia.”
Alvin alikosa la kusema. Hakujua jambo lolote kati ya hayo. Haishangazi Kilimani Group ilikuwa ya kwanza kushirikiana na Lisa. Mwanamke huyo... alikuwa na uwezo mkubwa, jambo ambalo
hakulitarajia.
Tayari alishangazwa na kazi nzuri aliyoifanya kuwaondoa wanahisa wasiotii wa Mawenzi Investments mara ya mwisho, lakini, hakutarajia kwamba angemshangaza tena.
Alvin alikodoa macho. Hakuweza kujizuia kupendezwa na mwanamke huyo kwa mara nyingine tena. Akivunga hamu ya kuitoa simu yake na kutazama umbea, Alvin alisema kwa ukali, “Tuko katikati ya mkutano. Ondoka kama unataka kujadili mambo mengine."
Kila mtu katika chumba cha mkutano akanyamaza. Jack aliinamisha kichwa chake na hakuongea zaidi.
Mkutano ulipelekwa haraka haraka huku
mada zikipitiwa juujuu tu. Takriban dakika 10 baadaye, mkutano ulikuwa umekamilika. Kitu cha kwanza alichofanya Alvin ni kuitazama simu yake. Alipoona habari kuhusu Lisa, karibu apige namba yake, bila kujua lengo lake ni kumpongeza au kumdhihaki, lakini sekunde moja baadaye, akakumbuka kwamba alikuwa mwanamume aliyeoa.
Alijizuia na kuwasha sigara. Alipitia kila habari hadi mwishowe, macho yake yakatua kwenye picha nzuri ya Lisa. Alipigwa na butwaa kwa muda na hakuweza kupinga kuhifadhi picha hiyo. •••
Mawenzi Investments.
Wakati Lisa alipopita kuelekea ofisini kwake, nusura azime kwa kelele za pongezi kutoka kwa wafanyakazi wake.
"Mkurugenzi Jones, wewe ni wa kushangaza sana."
Kwa kustaajabishwa, Amba alikuwa akihaha kwa kugonga mikono na magoti yake. "Vyombo vya habari vingi vimepiga simu kuomba mahojiano ya kipekee na wewe asubuhi ya leo. Ulifanya nini hasa kubadilisha hali yako katika miaka mitatu?"
'Nilitegemea kitu pekee cha thamani alichonipa Mungu, akili, bila shaka.” Lisa alisema kwa utulivu. “Tafadhali kataa mahojiano yote ya kipekee. Niko busy,”
“Sawa, lakini umealikwa kuhudhuria Starlight Gala na Times Media kesho usiku. Bwana Ngosha awali alitakiwa kuhudhuria, lakini amelazwa, kwa hiyo mwaliko ulikuja kwako.”
Sura ya: 354
Lisa alipokea kadi ya mwaliko na kuichezea mikononi mwake. "Je, kuna maana yoyote kwa aina hii ya mialiko?"
"Watu mashuhuri kutoka kila tasnia watakuwepo. Nilisikia kwamba Cindy, mwimbaji mashuhuri wa kike unayemchukia zaidi, atatumbuiza pia.” Amba alimchombeza Lisa kwani aliogopa asingehudhuria mwaliko huo. “Ikiwa huna shughuli nyingi, unaweza kwenda kumpa wakati mgumu kidogo, si unakumbuka wakati ule alivyokuwa anachonga sana akiwa na Sarah?”
Sekunde chache baadaye, Lisa alicheka. “Wow, Msaidizi wa miye, unazidi kuwa mkorofi zaidi kama bosi wako. Cindy ni mpenzi wa Chester.
Huogopi kwamba nitaingia kwenye matatizo?”
Amba alisema huku akitabasamu, “Wewe ni mrithi wa kampuni ya Ngosha na mbunifu mkuu wa Kilimani Group sasa. Thamani ya kampuni ya Mawenzi Investments imepanda hata maradufu. Watu wengi sana wanajaribu kukufahamu. Ingawa familia ya Chokaina nguvu, wewe pia si haba. Ni lazima wajiulize mara mbili kwa sasa kabla ya kukufanyia ujinga wowote.”
“Una hoja hapo. Kwa bahati nzuri, nina jambo langu na Chester pia.” Lisa alifunga kadi ya mwaliko. Lisa alikuwa bado na kinyongo kwamba hospitali ya familia ya Choka ilimfukuza Joel mara ya mwisho.
•••
Usiku. Kwenye lango kuu la ukumbi wa
mikusanyiko, Ssafu na safu za magari ya kifahari yaliingia. Kwenye zulia jekundu refu, Lisa alishuka kutoka kwenye gari nyeusi aina ya Rolls-Royce Ghost. Alivalia mavazi ya nguva yenye matundu ya almasi, ambayo yalionyesha kikamilifu mikunjo yake yenye umbo la S. Iliyolingana na sifa zake maridadi na rangi ya korosho iliyokoza, alionekana kama binti wa kifalme moja kwa moja kutoka kwenye jumba la malikia. Alikuwa wa kisasa, wakifahari, mzuri, na asiye na mbwembwe. Angeweza kuelezewa kwa kila kivumishi cha sifa.
Wanawake wasomi na watu mashuhuri waliovalia mavazi ya kifahari usiku huo walipauka kwa kulinganisha na Lisa. Si nyuma ya Lisa, Cindy alishuka kutoka kwenye gari aina ya Bentley Bentayga. na kumshika mkono Chester. Hata
hivyo, Lisa alivutia macho sana hivi kwamba hakuna mtu aliyemwona Cindy pindi anaingia.
Cindy akasaga meno kwa chuki. Times Media ilikuwa moja ya makampuni makubwa ya Kenya, kwa hivyo hapo awali alikuwa amepanga kuwa bora usiku huo. Hata vazi alilovaa lilibuniwa na mbunifu wa hali ya juu, ambaye alikuwa ameombwa na Chester kwa muda mrefu. Kamwe hakutarajia kwamba Lisa angemwibia umaarufu tena. Hata alipata nafasi ya kusaini mkataba na Mawenzi Investments kama balozi wao, lakini Lisa aliuvunja.
Kwanini hakufa miaka mitatu iliyopita? Ikiwa angefanya hivyo, Cindy asingekuwa mtu wa kudharauliwa sana. Ilisikitisha zaidi kwamba Lisa alikuwa sasa mrithi wa Ngosha Corporation.
Hakuna kinachomkera mwanadamu zaidi ya mafanikio ya mwanadamu mwingine.
"Chester, sikuwahi kufikiria kwamba Lisa angezingatiwa sana. Ulikuwa unaangaziwa popote ulipoenda." Cindy alificha wivu wake na kumtania yule mtu mashuhuri kando yake.
Chester akarekebisha miwani yake yenye fremu ya dhahabu na kumtazama kwa mawazo. “Kwanini? Unamwonea wivu?”
Cindy alishangaa, lakini hakuthubutu kufsema ujinga wowote mbele ya Chester. “Hilo ni hakika. Ni nani hapa ambaye hatamuonea wivu? Ana bahati sana.”
“Una bahati pia. Unapaswa kujifunza
kuridhika na ulicho nacho.” Sauti ya Chester ilikuwa ya kubembeleza, lakini ilikuwa ya kutisha.
Cindy alitabasamu huku akisema, “Nimeridhika sana kukutana na wewe. Lakini... Alvin Kimaro na Sarah watakuwa hapa usiku wa leo pia. nina wasiwasi sana...”
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu watu wengine. Kila mtu yuko ndani ya jumuiya moja nchini Kenya na hatimaye tutagongana tu. Sarah lazima azoee.”
Baada ya Chester kusema kwa utulivu, Cindy aliweza tu kuinamisha kichwa chake na kunyamaza.
Lisa alipoingia kwenye jumba la karamu, aligundua kuwa kulikuwa na
watu wengi waliofahamiana naye usiku huo, kama vile Jerome na Melanie, Lea na Mason. Pia kulikuwa na Jack, Kelvin, Rodney...
Lisa akacheka. Hata damu katika mwili wake alihisi ikikimbia kwa kasi.
Usiku huo ulikuwa unaenda kuwa wa kuvutia. Baada ya miaka mitatu, watu waliofahamiana wote walikusanyika mahali pamoja.
Kelvin aliinua glasi yake kuelekea kwake kutoka mbali. Punde, alipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwake: [Ninajua unalenga nini, kwa hivyo sikukukaribia. Lakini nitakuwa nikikutazama.] Moyo wa Lisa ukapata joto.
Jack, ambaye alivalia suti nyeupe, alimwendea kwa furaha na kumpa glasi
ya mvinyo. “Sikutaka kuhudhuria mara ya kwanza, lakini niliamua kuja mara moja niliposikia kwamba na wewe ungehudhuria. Usiku wa leo utapendeza sana.”
“Pamechangamka kweli kweli. Nimependa sana.” Lisa alikunywa mvinyo kabla ya mdomo wake kuinua tabasamu la kuvutia.
Mwangaza uliangaza machoni pa Jack. Ghafla akahema kwa majuto. “Usingeolewa na Alvin kwanza, hakika ningekuoa. Lakini nikikutongoza sasa hivi, wanafamilia wa Kimaro bila shaka watanisema vibaya. Hakuna mtu ambaye angeweza kukubali ndugu wawili kuoa mwanamke mmoja.”
“Kwa bahati nzuri, hukunitongoza. ningekubali.”
“Kwa nini?”
"Kwa sababu nina wachumba wengi sana." Lisa aliwatupia macho wanaume waliokuwa wakimtazama kwa pembeni. "Angalia, kuna watu wengi ambao wanajaribu kumrithi kaka yako."
“Ni kawaida. Sasa wewe ndiye mwanamke mrembo, mwenye kipaji, na mwenye thamani ya juu nchini Kenya.” Jack alinyoosha mkono wake kwake. "Unaweza kucheza na mimi? Ninataka kuwa mtu anayeonewa wivu sana usiku wa leo. Nipe furaha hii."
“Sawa.” Lisa aliweka mkono wake kwenye kiganja chake kikubwa, na wote wawili wakatembea kwenye uwanja wa muziki.
Walichukua nafasi kama wanandoa wakamilifu. Mara moja walivutia wivu na porojo za watu wengi, lakini wote wawili walipuuza yote na badala yake wakaanza mazungumzo.
“Sema, kwa nini umekuja leo? Kuharibu sherehe?" Jack aliuliza kwa utani.
Lisa akatumbua macho. "Ni tamasha la Times Media, kwanini niharibu? Nimekuja tu kucheza gitaa na kufurahi na kujumuika na marafiki.”
"Unajua kucheza gitaa?" Jack akakohoa. “Walimwalika Cindy kutumbuiza usiku wa leo. Yeye ni mtaalamu.”
“Ni vizuri. Nataka kutumbuiza baada yake.” Lisa alidhamiria. "Niliandika wimbo mpya, na nahisi watu
wataupenda sana. Unaweza kuusikiliza kidogo?”
Jack nusura apoteze stepbaada ya Lisa kumwimbia sikiono kipande cha wimbo huo. “Lisa, unataka kumchokoza Cindy? Huu wimbo ameuachia hivi karibuni na unafanya vizuri...”
“Ni wimbo wangu.” Lisa alimnong’oneza huku akitabasamu.
“Toka lini umekuwa mwanamuziki?"
“Huniamini?” Lisa alimkazia macho. “Mimi ndiye niliyeandika nyimbo maarufu za Cindy. Nilikuwa nikicheza gitaa na piano kabla hata Cindy hajajifunza kuimba. Ndoto yangu ya kwanza ilikuwa kuwa mwanamuziki lakini mazingira yalinibadilisha kuwa injinia. In fact ni kwamba Cindy alivutika
kuwa muimbaji kupitia mimi.”
Mshangao ulikuwa umeandikwa usoni mwa Jack. “Kwa hiyo huu wimbo mpya ni wewe pia uliuandika?”
“Sio huo tu, hata ule uliomtoa kwenye gemu niliuandika mimi. Ni vile tu kwamba amesahau kushukuru. Ni lazima nimfundishe hilo leo.” Lisa alilalamika.
"Una ujuzi gani mwingine ambao siujui?" Jack alikosa la kusema.
“Mimi ni hazina. Maisha yangu ya utotoni yalikuwa magumu sana hapo awali, na kipaji changu kilizuiwa na wengine. Sasa, ni wakati wangu wa kuangaza.” Lisa aliongea kwa kujiamini. Jack hakuweza kujizuia kuangua kicheko.
Sura ya: 355
Alvin na Sarah walipoingia, mara wakawaona Jack na Lisa wakiwa katikati ya ukumbi wa ngoma. Walikuwa wakicheza pamoja kama wanandoa waliokuwa na ‘chemistry’ nyingi. Mmoja alikuwa mrembo kama binti wa kifalme, wakati mwingine alikuwa amevaa suti nyeupe kama mtoto wa mfalme.
Chini ya mwanga, walizungumza na kucheka. Mara kwa mara, Lisa alikuwa akisema jambo ambalo lililomfanya Jack acheke kwa sauti. Pia alikuwa na tabasamu la kupendeza na tulivu usoni mwake. Tukio lile liliuumiza sana moyo wa Alvin. Wakati huo, alikuwa na hamu ya kukimbilia na kuwatenganisha wote wawili.
Kile Alvin alichohisi kilimfanya amkaze
kwa nguvu mkono Sarah. Sarah akashusha pumzi na kugugumia kwa sauti ya chini. "Alvinic, unaniumiza ..."
“Samahani.” Alvin aliachia mshiko wake kwa maneno ya kuomba msamaha, lakini macho yake hayakutoka katikati ya sakafu ya dansi.
Sarah alikunja ngumi kwa hasira.
Harusi yake na Alvin ilipaswa kuzungumziwa zaidi wakati huu, lakini Lisa alionekana kutawala kila mahali na kuiba umaarufu wake. Si hivyo tu, watu wengi walikuwa wakimlinganisha na Lisa kwenye mitandao. Ingawa alikuwa ameitangaza harusi yake hadi kwenye mabngo ya barabarani, bado alishindwa kabisa kupambana na Lisa.
Hatimaye alipata kuhudhuria hafla hiyo na Alvin, lakini Lisa alionekana kama
mzimu unaowasumbua. Kilichomfanya azidi kuchanganyikiwa ni kuona wivu machoni mwa Alvin. Ilikuwa ni aina ya wivu ambayo mwanaume angekuwa nayo kwa mwanaume mwingine.
“Alvinic, Aunty Lea yuko pale. Twende tukasalimie,” Sarah alisema kwa sauti nyororo ili kumpotezea mawazo ya Lisa.
“Sawa.” Walikuwa familia, baada ya yote, kwa hiyo walipaswa kutendeana vizuri hadharani.
Wote wawili walitembea kuelekea kwa Lea. Lea alikuwa akibadilishana maneno na rafiki wa zamani. Rafiki yake wa zamani alimtania, “Binti-mkwe wako na mwana wako wako hapa.”
“Habari yako, Aunty Lea,” Sarah aliwasalimia wale wanawake wawili.
"Ah, ana tabia nzuri sana." Rafiki wa zamani wa Lea alipoona kwamba familia ya Lea imeingia, alipata kisingizio na akaondoka kwenda kuzungumza na watu wengine.
Lea alimpa Sarah mtazamo wa chuki. Alimchukia sana Sarah, hasa pale kila Mzee Kimaro na Bibi Kimaro walipotaja kuharibika kwa mimba ya Lisa enzi hizo alipokuwa amebeba mapacha. Wanandoa hao wazee wangeizungumzia kila alipoenda kuwasalimia katika miaka hii michache. Kama si Sarah, Lisa asingepoteza ujauzito wake na angekuwa ni Bi. Kimaro zamani sana.
Ingawa Lea hakumpenda sana Lisa hapo awali, alifikiri kwamba Sarah alikuwa mkatili sana. Sarah aliweza hata kujihusisha na mwanaume ambaye
alikuwa ameoa na alikuwa akitarajia kupata watoto. Mwishowe, alisababisha mke halali apoteze mimba. Ilikuwa wazi kwamba Sara hakuwa na hisia zozote za maadili.
Sarah alionekana kuwa na huzuni baada ya kuona Lea anampuuza.
Alvin aliona ni vigumu sana kuvumilia na akasema, “Mama, salamu ya Sarah.”
“Najua. Mimi si kiziwi,” Lea alijibu bila kujali.
Sarah alilazimisha tabasamu na kusema, “Aunty Lea, nitakuletea chakula.” Hakutaka kujaribu kupata kibali cha Lea ili tu kukwepa asikutane na karipio kali.
Alipoona Sarah anaondoka kwa huzuni, Alvin alikasirika. “Inaonekana sikupaswa
kuja kukusalimia. Na kwanini hukumtupia jicho kali kama hilo Jack na kumwacha acheze na Lisa? Shemeji wa zamani na shemeji yake, ni aibu sana.”
Hapo awali Lea alifikiri kwamba haikuwa sawa pia, lakini kwa silika alienda kinyume na maneno ya Alvin aliposikia sauti yake. “Wewe na Lisa tayari mmeachana. Ni muziki tu wanacheza na sio mapenzi. Watu wengine hata hawasemi chochote. Ni wewe tu unayenyoosha vidole hapa. Unajiingiza sana katika mambo ya wengine.”
“Hata ikiwa watu wengine wanasema jambo fulani, hawatalisema mbele yako,” Alvin alijibu kwa ukali.
“Umekosea. Wanafikiria tu njia za kufahamiana na Lisa sasa. Yeye ndiye mrithi wa Ngosha Corporation na mkurugenzi mkuu wa muundo wa
Kilimani Group. Kwa utambulisho huu, hakuna mtu atakayetaka kupitisha nafasi hii ili kumjua. Kutakuwa na manufaa na hakuna hasara iwapo Jack atajenga uhusiano mzuri na Lisa.” Lea alisema kwa hisia ngumu, “Alvin, lazima uelewe kwamba Lisa si Lisa tena wa zamani. Ana uwezo wa kuongeza thamani ya soko la Mawenzi Investments kwa urahisi na kuifanya iingie kwenye orodha 100 bora za Kenya.
"Mbali na hilo, yeye ndiye binti pekee wa Joel Ngosha na mwanamke wa kweli wa familia ya Ngosha. Ingawa alikuwa ameolewa hapo awali, bado kuna wanaume wengi bora kutoka kwa familia tajiri ambao wanataka kumuoa na kufahamiana naye. Ikiwa huamini, jionee mwenyewe.”
Alvin alitazama tena ulingo wa muziki. Lisa alikuwa tayari amemaliza kucheza wimbo na Jack. Baada ya hapo, alialikwa kwa nyimbo nyingine na Erick Malugu mwenye uwezo na mwonekano mzuri, aliyekuwa mkurugenzi wa S.E Group. Alvin alikunja ngumi bila fahamu.
Lea akahema. "Wakati mwingine, huwezi kuwadharau wengine. Wewe unajiona ndiyo mwenye kujua kila kitu? Uvumi niliousikia zaidi leo haukuwa juu ya watu kumcheka Jack, lakini wanazungumza juu ya jinsi ulivyoachana na Lisa na kumuoa na Sarah! Atakuletea kitu gani kizuri? Kila mtu katika jamii ya juu anamuepuka Thomas Njau. Ikiwa sio wewe kuisaidia New Era Advertisings, hakuna mtu ambaye angekuwa tayari kushirikiana nao.”
“Imetosha, usiseme tena.” Alvin tayari alihisi kuudhika, na alizidi kukosa raha kusikiliza maneno ya Lea. “Nilipona kutokana na ugonjwa wangu kutokana na matibabu ya Sarah. Kama si kutiwa moyo na Sarah wakati huo katika hospitali ya magonjwa ya akili, ningekuwa tayari nimekufa.”
“Lisa aliwahi kukutia moyo pia. Ungeniua wakati ule isingekuwa yeye,” Lea alifoka.
Alvin alipigwa na butwaa, akahisi uvimbe kooni. "Je! kitu kama hicho kilitokea hapo awali?"
Lea alikosa la kusema. “Hivi ndivyo Sarah alivyoutibu ugonjwa wako? Umesahau kila kitu kizuri kuhusu Lisa."
Alvin alikuwa ameduwaa kutokana na maneno yake. Hata hivyo, alipojaribu
kutafakari kwa kina, ghafla kichwa kilianza kumuuma. Aliegemeza kichwa chake kwenye mikono yake.
Alvin alipoona kwamba Mason na Jerome walikuwa katika mazungumzo ya kina si mbali naye, alisema kwa upole, “Mtazame Mason. Alisema hakuwa na hatia, lakini bado ana uhusiano wa karibu na familia ya Campos. Bado unamwamini?”
Lea akatazama juu, na sura yake ikageuka kuwa mbaya mara moja. Aligeuka na kuelekea kwa Mason. "Mason, njoo hapa kwa sekunde."
Lakini, alingoja kwa dakika tatu kamili kabla ya Mason kumjia na tabasamu usoni mwake. “Lea, kuna nini?”
Lea akamtazama. Alihisi kwamba
alikuwa akizidi kumsoma vizuri. "Mason, si nilikuambia toka mwanzo kuweka umbali kati yako na familia ya Campos? Hasa Jerome—”
“Lea, jina langu la mwisho ni Campos. Pia ni familia ya wazazi wangu. Siwezi... kutowasiliana na familia ya Campos kwa sababu tu ya mpasuko kati ya familia ya Campos na familia ya Kimaro.” Mason alinyoosha mikono yake. "Mbali na hilo, maendeleo ya familia ya Campos miaka hii hayajazuia familia ya Kimaro kwa njia yoyote ile. Huoni kwamba familia hizo mbili zinaendelea kukua pamoja katika miaka ya hivi karibuni?”
Baada ya mshangao wa muda, Lea alisema kwa hasira, “Haijaizuiaje familia ya Kimaro? Baadhi ya kampuni tanzu za KIM International zilinyonywa faida
mara kwa mara na kampuni ya Campos. Si hivyo tu, kama isingekuwa msaada wa KIM International wakati huo, familia ya Campos—”
”Kwamba Familia ya Campos ingekuwa kama ilivyo leo? Nilijua ungesema hivyo tena,” Mason alimkatisha. "Familia ya Campos ipo kama ilivyo leo kupitia umoja wa wafanyikazi wote katika kampuni ya Campos. Isitoshe, kwani hatuendelei vizuri hata bila msaada wa KIM International miaka hii mitatu?”
"Kama nisingekupa makumi ya mabilioni hapo awali, unafikiri siku hii ingefika kwa Campos Corporation-"
“Sitaki kugombana na wewe, Lea.” Mason alimkatisha. “Siku zote ni sisi, familia ya Campos, ambao tunashutumiwa kwa kupanga njama na
kula njama kila tunapopambana kutoka kwenye dhiki. Ni kana kwamba familia ya Campos inapaswa kuwa na shukrani kwa familia ya Kimaro milele,” Mason alisema kwa kuudhika. Akageuka na kuondoka.
Lea alihisi ubaridi moyoni mwake. Mason hakuwa hivyo hapo zamani. Hata hivyo, alikuwa akizidi kukosa subira naye kadiri muda ulivyopita.
TUKUTANE KURASA 356-360
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)