Chubbylady
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 621
- 1,018
LISA KITABU CHA NANE (10) SIMULIZI...........................LISA
KURASA.....................481- 485
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY
Sura ya: 481
"Acha kuongea ujinga." Rodney alifadhaishwa kidogo na alichosema Pamela.
“Nasema ukweli tu. ” Wakati huo, Pamela aligeuka na kusimamisha teksi.
“Hutaki nikurudishe?” Rodney alifoka.
“Nisingethubutu. Wewe ni mkorofi sana. Ninaogopa kwamba utnaweza kunitupa barabarani. ” Mara moja Pamela aliingia kwenye teksi bila kutazama nyuma.
Rodney alikuwa ameduwaa kwa muda mrefu. Hii haikwenda kama alivyofikiria. Alidhani kwamba Pamela bila shaka angemsumbua. Baada ya yote, asilimia 10 ya hisa za Shangwe Corporation zilimuuma sana.
Subiri! Alikuwa amesahau kumkumbusha kuchukua vidonge vya kuzuia mimba.
Dakika hamsini baadaye, Pamela alishuka kwenye gari na kumuona Rodney akitokea kwenye gari nyuma yake, alikuwa akimfukuzia kwa nyuma tangu uwanja wa ndege.
“Unataka nini tena?” Hali ya Pamela ilizidi kuwa mbaya mara tu alipomwona yule mjinga.
"Kunywa hii." Rodney alimkabidhi boksi la vidonge vya kuzuia mimba kwa macho ya kukwepa. "Siwezi kukuacha uwe na mimba ya mtoto wangu."
Moyo wa Pamela ukatulia. Kwanini hakuwa na bahati katika maisha yake? Kwanza, alikutana na Patrick, na sasa, alikuwa Rodney, wote ni watu wa ajabu tu!
“Usijali. Nilikunywa mara moja nilipotoka hotelini jana. Ningechelewa sana kama ningesubiri uniletee.” Pamela alizuia hasira yake alipomkaribia hatua kwa hatua. “Rodney Shangwe, usiende mbali sana. Mimi ndiye mhanga hapa. Tafadhali kumbuka kwamba kama si kwa sababu nilijiunga na Osher, ubikira wangu usingeharibiwa na wewe. Unaweza kunichukia, lakini unapaswa kunithamini.”
Rodney alishindwa kujizuia kurudi nyuma kutokana na hasira iliyokuwa machoni mwake, mwili wake ukahisi kuishiwa nguvu kidogo.
“Nafanya hivyo kwa manufaa yako, sikupendi! Hata ukiishia mimba ya mtoto wangu utakuwa single mother. Hata hivyo, usifikiri hadhi yako itabadilika kwa sababu tu una mtoto wangu.”
“Usijali. Sitaki kueneza jeni zako duni,
lakini hii ilinitokea kwenye mkutano wako na waandishi wa habari. Si unipe maelezo ni nani aliniwekea?” Pamela aliuliza kwa ukali.
Rodney alishangazwa na swali hilo. Bila shaka, alijua ni Thomas. Hata hivyo, Thomas alikuwa kaka ya Sarah, na Sarah tayari alikuwa amefanya mambo mengi kwa ajili yake. Ikiwa angemwambia, Tomaso angeweza kuingia matatani na hivyokumsononesha Sarah.
“Mimi... Ningejuaje? Lazima uliwachokoza nyuki wa porini kwa kuvaa vile. Nilikwambia ukabadilishe ukajifanya mjanja.” Rodney alitazama pembeni kwa hatia, hakuthubutu kukutana na macho yake.
Lakini, macho yake hayakuweza kukwepa macho ya Pamela. Ilionekana kuwa mawazo ya Lisa yalikuwa sahihi.
Alikuwa ni Thomas Njau usiku huo, na Rodney aliijua, lakini alikuwa akimfichia Sara.
Athari kubwa ya kukata tamaa ilimwangazia machoni mwake. Ingawa hakumpenda, bado alimkubali mtu huyu. Alifikiri tu alikuwa kipofu kumpenda Sarah.
Ilikuwa sawa ikiwa macho yake yangekuwa kipofu, lakini moyo wake ulikuwa kipofu pia, kiasi kwamba asingeweza kutofautisha mema na mabaya. Kulikuwa hakuna kitu cha kuthamini juu ya mtu kama huyo. Bila kumtazama tena, Pamela aligeuka na kuondoka.
"Hey, unaondoka hivyo hivyo tu?" Rodney alipigwa na butwaa kwa muda lakini bila fahamu akamzuia.
"Nini? Utaniambia kuwa alikuwa Thomas? Je, utanisaidia kumkamata?
Ulimsaidia hata kuficha ushahidi.” Pamela alicheka kwa unyonge. "Rodney Shangwe, usinichukulie kama mjinga. Usiku huo, Thomas pekee ndiye angethubutu kufanya jambo kama hilo, akizingatia jinsi alivyothubutu kuingia ndani ya nyumba yangu, kunipiga, na kunishambulia miaka mitatu iliyopita.
“Miaka mitatu baadaye, ana wewe wa kumlinda, kwa hiyo hawezi kufanya nini? Ana maisha mazuri sana. Hata kama hana Alvin pembeni yake, bado ana Rodney Shangwe.”
Kisha, akainamisha macho yake ili kuficha chuki machoni mwake na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Rodney alimtazama akiondoka kwa mwendo wake wa madaha, na uso wake mzuri ukawaka kwa aibu. Hakufikiri Pamela angejua kila kitu. •••
Usiku, karamu ya biashara ilikuwa ikiendelea. Alvin alisimama kwenye kibaraza cha wazi, chini ya anga ya usiku, akiwa na glasi ya divai mkononi mwake. Macho yake ya kina na ya huzuni yalitazama kupitia dirishani kwenye sherehe nzuri na ya kuvutia ndani.
Asingeenda kwenye karamu hiyo ikiwa mwenyeji wake hakuwa mshirika wake wa biashara kwa miaka mingi. Hakupendezwa kabisa na matukio kama haya. Ikiwa asingekuwa na ugomvi na Lisa, angeandamana naye kwenye karamu hiyo. Pamoja naye, karamu isingekuwa ya kuchosha sana.
Labda ni kwa sababu alikuwa amelewa kidogo, lakini akili ya Alvin ilijawa na mawazo yasiyo na huruma. Alim’mis sana Lisa. Alitaka kumvuta mikononi mwake kwa nguvu na kumbusu kwa nguvu.
Ghafla, mwanamume na mwanamke walitoka nje. "Hubby, kwanini umeniuliza habari za mawasiliano ya Nebula sasa hivi?"
“Ni kwa sababu ya Kelvin Mushi kutoka Golden Corporation." Mwanamume huyo alieleza, “Alifikiri kwamba nguo uliyovaa wakati wa harusi yetu ilikuwa nzuri, kwa hiyo akaniomba niwasiliane na Nebula.”
“Mbona mwanaume kama yeye anaulizia gauni la harusi? Je, amepata mpenzi? Lakini sikuwahi kusikia kuwa alikuwa na rafiki wa kike hapo awali. Halo, ulimweleza wazi? Nebula hasa hutengeneza nguo bora kabisa za harusi.”
"Nilimweleza. Hakunijibu nilipomuuliza ikiwa anafunga ndoa, lakini nilisikia kwamba familia yake huko Dar es
Salaam ilikuwa imempangia ndoa, na aliridhika sana nayo.”
“Labda kweli anaoa. Itabidi tuhudhurie harusi hiyo.”
"Alisema haitakuwa harusi ya kifahari, na sherehe itafanyika Dar es Salaam, lakini tayari nimempa baraka zangu."
Kelvin Mushi! Macho ya giza ya Alvin yalijawa na mwanga ghafla, yakatumbuka kama yanataka kuanguka. Ikiwa mtu huyo asingetaja, alikuwa kishalisahau jina hilo.
Miaka mitatu iliyopita, Kelvin aliendelea kumsumbua Lisa na kumtazama kwa kumtamani, lakini sasa alikuwa anaoa. Baada ya yote, miaka mitatu ilikuwa imepita. Hakuweza kumngoja Lisa milele, na umri haurudi nyuma, kwa hiyo ilikuwa kawaida kwake kuoa.
Hata hivyo, kulikuwa na hali isiyoelezeka ya wasiwasi moyoni mwake.
Akiwa amekasirika, akanywa mvinyo. Aliyekuwa akiolewa na Kelvin bila shaka hakuwa Lisa, kwanini alikuwa anawaza sana?
Saa tatu usiku alipokuwa akijiandaa kuondoka, ilitokea tu bahati kumwona Kelvin akitoka kwenye korido ya chumba cha maliwato. Ilikuwa wazi kwamba Kelvin alikuwa katika hali nzuri. Tabasamu tulivu lilining'inia kwenye kingo za midomo yake, na alikuwa amevalia suti na fulana nzuri nyeusi iliyomfanya aonekane mzuri na maridadi.
Alvin alikunja uso na bila fahamu akajihisi kama mtu anayeumwa macho. "Bwana Kimaro." Kelvin alimpa kwa heshima salamu.
“Mh.” Alvin akanyanyua miguu yake mirefu na kuondoka.
Jamaa huyo mwenye kiburi alipoondoka, tabasamu la kejeli lilitanda mdomoni mwa Kelvin, akajiwazia moyoni mwake. 'Alvin Kimaro, wacha tuone ni muda gani unaweza kujivunia! Hivi karibuni, utaanguka kutoka kwenye mawingu, na mwanamke wako nitamuoa. Inasikitisha kwamba bado haujui chochote.’
Baada ya kutoka kwenye karamu hiyo ya biashara, Alvin alimtaka dereva ampeleke kwenye jumba la familia ya Ngosha.
Sura ya: 482
Kwenye dirisha la ghorofa ya pili la jumba la Joel Ngosha, mwili mdogo wa Lucas ulipanda hadi dirishani na kuchungulia nje. "Mama, baba mchafu
yuko mlangoni tena."
Kwa siku kadhaa, Alvin alikuwa akisimamisha gari lake kwenye mlango wa jumba la familia ya Ngosha, na wakati mwingine, alikuwa akiondoka tu baada ya Lisa kuondoka kwenda kazini. Lisa alikuwa tayari ameshazoea.
“Usimjali. Nenda kalale." Lisa alimtoa Lucas kwenye kiti na kuvuta vifunga dirisha huku akihofia macho makali ya Alvin yangemuona Lucas.
"Mama, ikiwa siku zote yuko hapa, itakuwaje akigundua kuwa unafunga ndoa na Anko Kelvin?" Lucas aliuliza kwa wasiwasi.
“Hatajua. Muda ukifika, nitaiambia kampuni itangaze kuwa niko kwenye safari ya kikazi na nitaondoka kwa siku chache.” Lisa alikisugua kichwa chake kidogo kumliwaza. "Lucas, utajali kuwa
mama anaolewa?"
"Hapana. Nimefurahi kwamba mama hatimaye amepata mtu ambaye atakutendea mema,” Lucas alisema kwa umakini. “Na Anko Kelvin ni mzuri sana kwangu na Suzie. Hakika akikutendea ubaya siku moja nitamfundisha somo. Mimi nitajifunza kungfu, na nikiwa mkubwa nataka niwe mwanajeshi. Nitakuwa na nguvu sana hivi kwamba hakuna mtu atakayeweza kumdhulumu Mama tena.”
"Kijana mzuri." Lisa akambusu paji la uso wake.
Siku iliyofuata, Lisa alitoka nje ya Jumba asubuhi. Alipotoka nje ya geti, aliendesha gari moja kwa moja kana kwamba hakugundua uwepo wa Alvin. Alvin alilitazama gari lake kwa mbali kwa uso uliojaa uchungu.
Zamani, alipokuwa akingoja getini, bado alikuwa akitoka kuongea naye asubuhi. Lakini sasa, hakumpa hata nafasi ya kukutana naye. Kwa kuwa Lisa alienda kazini, hakukuwa na haja ya yeye kukaa hapa tena.
Jioni, Alvin akiwa anajiandaa kwenda kwa akina Lisa tena, ghafla Bibi Kimaro alimpigia simu na kumtaka arudi.
Ilikuwa tayari saa kumi na mbili jioni, na Suzie alikuwa akila na Mzee na Bibi Kimaro. Alipomuona Alvin akiingia ndani, moyo ulimchanika kusikoelezeka huku akiuma kijiko. Ingawa alikuwa bado mchanga, aliweza kuona kuwa baba yake mchafu alikuwa amedhoofu na amechoka zaidi. Nywele zake fupi zilizokuwa safi na nadhifu zilikuwa zimekua kidogo na kukosa matunzo. Bado alikuwa mzuri na anavutia, lakini pia alikuwa na huzuni zaidi.
"Kula chakula cha jioni kisha upande ghorofani ukapate usingizi mzuri, nahisi una mwaka mzima hujala wala kulala." Bibi Kimaro alihema. Hata iweje, bado alikuwa ni mjukuu wake, hivyo kumuona hivyo moyo wake ulimuuma sana. “Acha kusubiri kwenye lango la akina Ngosha kila siku. Umemaliza upasuaji juzijuzi hapa. Utaharibu mwili wako tu bure."
“Niko busy. Ikiwa hakuna kitu kingine unachohitaji, nitaondoka."
Alvin alipokaribia kugeuka ili aondoke, Mzee Kimaro alishindwa kujizuia. “Usifikiri kuwa sijui unaenda kwa akina Ngosha tena. Kila mtu hapa Sherman Mountain tayari anajua kukuhusu kusubiri huko kila usiku, na yeye anataka kuondoka. Zamani, sote tulikushawishi umuoe, lakini hukutusikiliza. Sasa kwa kuwa unajuta, unataka kurudi kwake tena. Unafikiri unaweza kumtupa na kurudiana naye
muda wowote unapotaka?”
“Ndiyo, Alvin. Mwache Lisa aendelee na maisha yake, na wewe mwenyewe uendelee na yako. Bado wewe ni mdogo, una safari ndefu mbele yako. Lisa sio mwanamke pekee katika ulimwengu huu." Bibi Kimaro akatikisa kichwa. Alikuwa mzee sana kuelewa mambo ya mapenzi ya kizazi kipya, lakini alihisi kuwa Lisa asingeweza kumsamehe mjukuu wake.
"Sitaki mtu mwingine ila yeye." Alvin alikunja ngumi kwa ukaidi na kwenda mbele.
Suzie alikimbia na kumshika mkono ghafla. “Anko usiende. Unaweza kulala nami usiku wa leo? Baba harudi nyumbani, na sitaki kulala na yaya.” Msichana mdogo akamtazama kwa macho malegevu na ya kusihi, na moyo wa Alvin ukalegea. Hakuweza kuvumilia
kumkataa.
Angeweza kusema kwa wengine, lakini kamwe hakuweza kusema 'hapana' kwa Suzie.
“Baki na Suzie.” Bibi Kimaro mara moja alimshawishi alipoona amesita kuondoka. "Haujarudi kwa muda mrefu, kwa hivyo anaku’miss."
“Sawa.” Alvin alikubali.
Usiku, baada ya yaya kumuogesha Suzie, Alvin alimkumbatia ili alale. Ingawa hakuwa amelala sana katika siku chache zilizopita, hakuweza kupata usingizi alipokuwa amelala kitandani.
Hata hivyo, hakutarajia Suzie angejirusha na kugeuza kifua chake, asipate usingizi pia. “Anko...”
“Mh? Nini tatizo?" Alvin alimtazama kwa upole.
Moyo wa Suzie ulihisi uchungu. Alijua kwamba ndiye baba yake halisi, lakini hakuweza kumwambia kwamba mama yake alikuwa karibu kuolewa na Kelvin baada ya wiki moja. Kelvin alikuwa mzuri, lakini baba yake mchafu alionekana mwenye huzuni sana. Alimchukia wazi siku chache zilizopita, lakini moyo wake ulikuwa umebadilika siku chache zilizopita pia. Alikuwa mnyonge sana!
“Anko, wiki ijayo... Baba atanipeleka safarini kwa siku chache.” Mwishowe, Suzie alishindwa kuvumilia.
“Hiyo ni nzuri. Jack anapaswa kukupeleka nje kucheza. Nitampa siku mbili za mapumziko.” Alvin hakufikiria sana juu yake.
Moyo wa Suzie ulimuuma, akatoa dokezo lingine. “Rafiki ya baba anaoa,
kwa hiyo atanipeleka kwenye harusi."
"Loo, kuna chokoleti nyingi za kula kwenye harusi, lakini usile nyingi sana," Alvin alimkumbusha kwa sauti ya chini.
Ndani ya moyo wake, Suzie alihema bila msaada. Hivyo ndivyo vidokezo pekee ambavyo angeweza kutoa kwa Alvin. Ikiwa angekuwa wazi sana, Mama yake na Lucas bila shaka wangekasirika.
'Baba, ni juu yako kuigundua mapema. Ikiwa huwezi, basi ndivyo hivyo.' Suzie alijisemea kimoyo. Alitamani sana baba yake aingie kwenye kichwa chake na kuyasoma mawazo yake moja kwa moja.
Siku chache zilizofuata, Alvin alikuwa na kazi ya kwenda na kurudi kati ya Jumba la familia ya Ngosha, na kampuni ya Mawenzi. Kwa kupepesa macho, siku sita zilikuwa zimepita.
Alasiri hiyo, kichwa chake kilihisi kizunguzungu kidogo, labda kwa sababu alikuwa hajapumzika vizuri. Katibu alipomkumbusha kwamba kulikuwa na mkutano wa kimataifa kwa njia ya video uliofanyika saa tisa kamili.
Alvin alikasirika na kusema, “Usije kwangu kwa kila jambo dogo. Jack si yupo? Anaweza kushughulikia mambo haya. ”
"Hapana, Bwana Mkubwa Kimaro. Bosi Jack yuko likizo leo na kesho,” katibu huyo alisema.
Alvin aliduwaa na ghafla akamkumbuka Suzie akisema kuwa Jack anaenda kuhudhuria harusi. “Sawa, nimekumbuka.”
Usiku uliofuata, aliendesha gari hadi kwenye mlango wa jumba la Ngosha.
Alisubiri getini hadi saa sita usiku, lakini hakuona gari lolote likitoka wala kuingia getini. Kwa sababu fulani, hali ya wasiwasi ilimpanda, na hakuweza kujizuia kumpigia Hans simu.
“Peleleza ujue Lisa alienda wapi na kwanini hajarudi mpaka usiku huu.”
Hans hakutaka kufanya hivyo, lakini alikuwa chini ya Alvin. Kwa hivyo, alitafuta mtu wa kumuuliza huko Mawenzi Investments na akajibu haraka, "Bi. Jones ameenda Uganda kwa safari ya kikazi.”
Kama bosi wa kampuni kubwa, ilikuwa kawaida kusafiri kwa biashara. Moyo wa Alvin ulishuka ghafla, akiogopa kwamba huenda amepata mpenzi mpya. Ingawa alijua kwamba asingepata hivi karibuni, bado aliogopa.
"Peleleza alipofikia anaishi hoteli gani. Pia, niwekee tiketi ya ndege ya kwenda
Uganda." Alvin mara moja alisema.
Kichwa cha Hans kilianza kumuuma. "Bwana Mkubwa, kampuni ina shughuli nyingi ..."
"Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko yeye. Suzie alisema kuwa wanawake wanapaswa kulindwa. Kwa hali hiyo, nitamfuata popote atakapokwenda. Ninaamini kwamba ataelewa unyoofu wangu,” Alvin alisema kwa sauti ya chini.
Sura ya: 483
Hans alikosa la kusema na akajiwazia kwa siri kuwa mtoto Suzie alijua kweli kuwachanganya wazazi wake. Ikiwa Lisa angedundua kuhusu hila za Suzie, angeweza kupandwa wazimu.
“Sawa, nitashughulikia.” Hans hakuwa na chaguo ila kuwapigia watu wa
Uganda. Hata hivyo, alipata habari kwamba hakukuwa na rekodi ya Lisa katika hoteli yoyote ya Uganda. Je, Lisa alikuwa na nyumba ibinafsi huko? Alipiga simu kwenye uwanja wa ndege uliofuata na kugundua kuwa hapakuwa na rekodi ya ndege ya Lisa kuruka hadi Uganda. Badala yake, alifahamu kuwa Lisa na Pamela walisafiri kwa ndege hadi Dar es Salaam jana.
Kichwa chake ghafla kilihisi ganzi kidogo. Kwa nini Lisa alienda Dar es Salaam wakati huo lakini akadai kwamba alikuwa Uganda kwa safari ya kikazi? Je! ni kwa sababu alikuwa akifanya jambo kwa siri huko Dar es Salaam, na sababu ilikuwa ni kumficha Alvin?
Kufikiria juu yake, kulikuwa na uwezekano mkubwa. Akiwa anawaza tu, Alvin alimpigia. “Umeshakata tiketi?” “Hapana, mimi... sikujua ni wapi Bi
Jones anakaa Uganda. Anaweza kuwa na nyumba binafsi huko. ” Hans alifanya uamuzi mara moja. Kwa kuwa Lisa alikuwa akijaribu kujificha, angemsaidia. “Bwana Mkubwa, usiende. Jamaa kutoka Mawenzi alisema kuwa Bi Jones atakuwa nje kwa siku mbili hadi tatu pekee. Anaweza kurudi kesho.”
“Basi naweza kurudi naye. Ngoja nitafute watu wa kumfuatilia.”
Mara Alvin alimpigia Master Ganja kutoka ONA baada ya kukata simu. Kwani, ONA ilikuwa na macho kila mahali.
Takriban nusu saa baadaye, Ganja alipiga akiwa na habari njema. “Bwana Mkubwa, taarifa za ndege zilionyesha kuwa Bi Jones hakwenda Uganda kwa safari ya kikazi. Alikwenda Dar es Salaam na Pamela Masanja.”
"Anafanya nini huko Dar es Salaam? ” Macho ya Alvin yalififia. "Hans aliangalia na kusema kwamba alikwenda Uganda."
"Aliiambia kampuni kwamba alikwenda Uganda, lakini hakwenda," Ganja alisema. "Hakuna rekodi inayoonyesha hoteli anayokaa huko Dar es Salaam, lakini Dar es Salaam ni nyumbani kwao, kwa hivyo anaweza kuwa anakaa katika nyumba yake ya zamani.”
Alvin akazidi kuwa na mashaka. Kwanini Lisa alilazimika kusema uwongo ikiwa anarudi Dar es Salaam na Pamela? Kweli, Jack alichukua siku ya kupumzika siku hiyo pia. Je, ilikuwa ni bahati tu? Watu hao watatu waliondoka Nairobi kwa wakati mmoja, na ilionekana kana kwamba Joel hayupo nyumbani kwake pia.
“Peleleza pia Jack na Joel Ngosha
walienda wapi.” Aliamuru ghafla.
Punde, Ganja aligundua mahali alipo Jack. “Bwana Mkubwa, Jack na Joel pia wamekwenda Dar es Salaam.”
Suzie alisema kwamba Jack alikuwa akimpeleka kwenye harusi ya rafiki yake. Watoto hawakusema uwongo. Jack, Pamela, Lisa, na Joel. Je, walikuwa na rafiki gani wa kufanana kwamba wangehudhuria harusi pamoja? Haikuwa na maana.
Subiri... Ghafla akakumbuka kwamba alipohudhuria karamu siku kadhaa nyuma, alisikia kwamba Kelvin Mushi alikuwa akioa, bibi-arusi alikuwa ni nani? Hata hivyo, Jack na Joel hawakulazimika kuhudhuria harusi ya Kelvin. Hawakumjua Kelvin vizuri, isipokuwa kama Bi harusi alikuwa ni mtu waliyemfahamu kabisa, lakini ...
Wazo hilo lilipojitokeza, mwili wake wote ulitetemeka. “Niandalie helkpota yangu mara moja. Ninataka kwenda Dar es Salaam. Sasa hivi.”
Ganja alishtuka. "Lakini Dar es Salaam iko mbali kidogo, na utahitaji kutuma maombi ya njia ya ndege kwenda Dar es Salaam..."
“Sijali. Tumia njia yoyote ya haraka iwezekanavyo. Sijali ni pesa ngapi inachukua kuhonga watu wa uwanja wa ndege. Fanya hivyo sasa.”
Alvin alikuwa akichanganyikiwa kutokana na wasiwasi. Alitumai kuwa huo ulikuwa ni uvumi tu na kwamba haikuwa kweli. Je, ikiwa mtu ambaye Kelvin alikuwa anamuoa alikuwa ni Lisa kweli?
Alvin alishikwa na mshikemshike kabisa akidhani Lisa anaenda kuolewa na mtu
mwingine ghafla. Wakati huo huo, moyo wake ulionekana kushikwa kwa nguvu na nguvu isiyoonekana, iliuma sana akatamani kufa. Ikawa kwamba hisia zake kwa mwanamke huyo zilikuwa za kina kuliko vile alivyowazia. Afadhali kumwangamiza kila mtu kuliko kumwacha aolewe na mwanaume mwingine. Alipokuwa akiwaza hayo, aliendelea kumpigia simu Lisa, lakini hakuweza kumpata.
Upande wa pili, huko KIM International, Hans aliposikia kwamba Alvin alikuwa akiandaa helkopta yake kibinafsi haraka, alisita kwa muda mrefu kabla ya kupiga nambari ya Lisa bila raha.
"Hans, kuna nini?"
Hans alitabasamu kwa uchungu wakati sauti ya Lisa ilipotoka. “Bi. Jones, kwanini ulitoroka kwenda Dar es Salaam? Alvin aliogopa na kuamua kukufuata.”
“Baaasi.” Pamela, ambaye alikuwa kama kijakazi kando ya Lisa, alishtuka sana hivi kwamba viatu virefu mikononi mwake vilianguka chini.
"Hans, ninafunga ndoa leo." Lisa alisema kwa sauti ya chini.
"Nini?" Hans aliruka kutoka kwenye kiti chake kwa mshtuko. “Wewe ... unaolewa na nani? Kwanini hapakuwa na habari yoyote kuhusu hili?” Alipiga uso wake kwa nguvu, akishuku kuwa ni ndoto mbaya.
"Kelvin Mushi.” Sauti ya Lisa ilikuwa laini. “Nimeteswa sana na Alvin kwa miaka mingi sana. Baada ya tukio la mwisho, hatimaye nilielewa kuwa Kelvin ndiye bora kwangu. Nataka kumuenzi, lakini naogopa Alvin angegundua, kwa hivyo tulipanga kwanza harusi ya hali ya chini. Nadhani huenda Alvin ameona
kitu. Hata asipofika, atajua akifika.”
Hans alikosa la kusema kabisa na habari hizo za kulipuka. “Bi. Jones, unafanya jambo kubwa huku ukimzuia jamaa asijue?” Alitabasamu kwa uchungu. "Ikiwa Bwana Mkubwa atagundua, hakika atachukia. Anaweza hata kufanya jambo la ajabu sana.”
Wazo la kugundulika na alvin lilimfanya Lisa ashtuke na kutaka kughairi harusi.
“Bi. Jones, ninakadiria kwamba itachukua saa mbili na nusu kufika Dar es Salaam kwa mwendo wa kasi zaidi.” Hans angeweza tu kumkumbusha.
Ilikuwa ni ukweli kwamba Lisa na Alvin hawakuweza tena kurudiana pamoja, hivyo hakuweza kumshawishi. Mbali na hilo, Bi Jones alikuwa ameteseka sana miaka hiyo michache.
"Asante kwa kuniambia, Hans." Lisa
alimshukuru kwa dhati. Kama si Hans alimsaidia kwa siri miaka yote hiyo, asingekuwa mahali alipokuwa muda huo.
"Sitamwambia Bwana Mkubwa kuhusu hili, lakini nadhani atajua mara tu atakapowasili Dar es Salaam." Hans alisema na kukata simu.
Katika chumba cha hoteli, Pamela alimtazama Lisa kwa wasiwasi. "Tunapaswa kufanya nini? Masaa mawili na nusu itakuwa karibu saa saba na nusu machana atakapofika Alvin. Ikiwa atafanya haraka, sherehe ya harusi inaweza kuwa bado haijaisha.”
“Basi tutaiwahisha mapema. ” Kelvin akaingia ghafla. “Nitaarifu hoteli kwamba itafanyika saa tano na nusu asubuhi.”
Lisa alishtuka. "Lakini wageni bado
hawajafika."
“Ndugu zetu wote wanakaa katika hoteli hii, kwa hiyo tunaweza kupiga simu na kuwaomba waje mapema. ” Kelvin alikandamiza mikono yake kwa upole begani mwake, akimhakikishia, “Pia nitapanga baadhi ya waandishi wa habari waje. Hapo awali nilipanga kuiweka chini ya rada, lakini Alvin anaweza kuwa amegundua kitu, kwa hivyo ni bora kuiweka hadharani. Siamini kwamba atampokonya mke wa mtu mwingine bila kujali sifa yake.”
Lisa aliitikia kwa kichwa. Kusema ukweli, Alvin alikuwa mtu wa kutisha. Hakujua kama angevumilia jambo kama hilo.
Pamela alikuwa na huzuni. “Ulitaka kusubiri hadi upate ujauzito ndio utangaze. Habari zilivuja wapi hasa? Oh, nakuonea huruma sana.
Ulimchokoza mtu tajiri zaidi nchini.” Pamela alipumua.
Karaha kubwa ilitanda machoni mwa Lisa huku akisikiliza. Alichukia wanaume ambao hawakujua jinsi ya kuthamini wengine kama Alvin Kimaro zaidi. Ikiwa angeweza kufanya hivyo tena, hakutaka kukutana naye tena.
Sura ya: 484
Saa tano asubuhi,
Ndugu wa familia ya Mushi walikuja mmoja baada ya mwingine kumuona bibi harusi. Lisa alivaa viatu vyake virefu na kusimama, na kuwaona Sonya Mushi, Ethan Lowe, na Tracy Laizer wakiingia pamoja.
Akiwaza hayo, ilikuwa imepita miaka kadhaa tangu Ethan na yeye kuonana. Mwaka huo, alipoondoka Dar es
Salaam, Ethan alilazimika kumfanya Tracy Laizer, mtoto wa Bilionea wa madini, kuwa mpenzi wake ili kusaidia familia ya Lowe, na walikuwa pamoja tangu wakati huo.
"Lisa, ni muda mrefu." Ethan alimtazama kwa macho magumu. Baada ya kutomuona kwa miaka mitatu, alizidi kuwa mrembo, haswa leo. Akiwa na vazi la harusi lenye weupe wa theluji na uso wake mdogo wa kushangaza ulioguswa na mpambaji kwa usanii mkubwa, alionekana mrembo kama wa kwenye hadithi. Alipokuwa mdogo, alizoea kufikiria mara nyingi kuhusu kuolewa naye, lakini hakufikiri kwamba angeolewa na mjomba wake hata siku moja.
“Ethan, huyu ni mkeo, sivyo? Yeye ni mrembo sana. ” Lisa alitabasamu kwa unyonge na kumsalimia Tracy.
“Habari, Bibi.” Tracy aliitikia kwa kichwa. Bila shaka, alijua kwamba mumewe alikuwa ameshikamana na mpenzi wake wa zamani, lakini kwa bahati mbaya, Lisa alikuwa karibu kuolewa na Kelvin. Hakuwa na maoni mazuri ya Lisa, lakini hakukuwa na kinyongo pia.
Lisa alipigwa na butwaa katika salamu hiyo. Hakuweza kujizuia kufikiria mawazo yake ya zamani. Mara nyingi alifikiria kuhusu Lina kumwita Shangazi, lakini bila kutarajia, Lina na Ethan walitengana.
“Sonya, huyu ndiye bibi harusi, sivyo? Ni mzuri." Baadhi ya jamaa wa familia ya Mushi walikusanyika ghafla karibu na Sonya na kuzungumza.
Sonya alimtazama Lisa kwa dharau kidogo. "Kweli yeye ni mrembo, lakini ni aibu kwamba yeye ni bidhaa ya mtumba."
Maneno ya jamaa zake yalikuwa tofauti. “Kwanini Kelvin anaoa mtu ambaye aliolewa hapo awali? Kelvin wetu ni mmoja wa wajasiriamali wa juu nchini na kijana mashuhuri. Wanawake kama yeye hawastahili.”
“Oh, haikuweza kusaidia. Kelvin alirogwa naye.” Sonya alipumua kwa muda mrefu na kwa nguvu.
Baadhi ya jamaa wa familia ya Mushi mara moja walimtupia Lisa macho kwa dharau. Lisa alikunja uso kidogo aliposikia. Sonya alikuwa hampendi na bado hakumpenda.
Pamela alikasirika na kutaka kuongea wakati Ethan alipomtazama mama yake bila furaha, akisema, "Mama, kwanini Lisa hastahili kuwa na mjomba? Yeye ni mwenyekiti wa Mawenzi Investments na ana utajiri wa mabilioni, bila kusahau
hadhi yake kama mbunifu bora, na babake ni Bw. Joel, miongoni mwa watu mashuhurinchini Kenya na watanzania waliofanikiwa zaidi nje ya nchi. Kwa mawazo yangu, ni Mjomba ndiye anayepata daraja la kijamii kwa kumuoa.”
“Wow, huyu bibi harusi ni wa ajabu sana. ” Macho ya wale jamaa walipomtazama Lisa yalibadilika tena ghafla.
"Hakuna mtu atakayefikiri wewe ni bubu ikiwa hauongei." Sonya alimtazama Ethan kwa ukali.
“Mama, fanya haraka uende kuwasalimia wageni. Kuna jamaa wengine nje.” Ethan alimkumbusha bila kujali, akimfukuza mwanamke huyo kijanja.
"Mwishowe, amani na utulivu. Ethan
Lowe, hatimaye uligundua jinsi ya kufanya kitu kizuri.” Pamela akacheka.
Uso wa Ethan ulipooza kidogo kwa maneno hayo lakini alihuzunika alipofikiria mambo ya nyuma. “Hapo zamani, nilitapeliwa na Lina. Hata hivyo, mmemwona Lina hivi karibuni?"
Moyo wa Lisa yalizama baada ya kutajwa kwa mtu huyo. "Miaka mitatu iliyopita, alikuwa Nairobi baada ya kufanyiwa upasuaji wa plastiki ili kubadilisha sura yake ili kupata mwonekano mpya, na akatoweka baada ya kugundulika. Siku zote nilihisi kwamba kulikuwa na mtu mwenye nguvu sana anayemsaidia kutoka nyuma yake.”
Ethan alionyesha kutoridhika na maneno yake. "Natumai hataonekana tena."
“Naam, ndiyo.” Pamela alidakia. “Sarah peke yake anatosha kutuumiza kichwa. Itakuwa shida ikiwa Lina atatokea pia."
Lisa alikunja uso. Siku zote alifikiri kwamba Lina alikuwa mjanja zaidi kuliko Sarah, na alikuwa na hisia kwamba bila shaka Lina angetokea tena.
“Lisa, hii ndiyo namba ya mawasiliano yangu. Katika siku zijazo, tutakuwa jamaa tuliounganishwa kwa ndoa ya mjomba.” Ethan alimkabidhi kadi ya biashara kwa uchungu. "Nilifanya makosa hapo awali na niliyarudia kila wakati na kukuumiza. Katika siku zijazo, ikiwa Mjomba atakuonea, au ikiwa mama yangu anakukashifu, unaweza kuja kwangu wakati wowote. Hata kama sina uwezo, nitakuwa ndugu yako kila wakati. Zaidi ya hayo, nitakuja Nairobi baada ya siku chache.”
Lisa alipigwa na butwaa. Je! Kampuni
ya Lowe itapanuka hadi Kenya?"
“Hapana, niliachana Lowe Enterprises?” Ethan alisema huku akitikisa kichwa. "Nilijiunga na kampuni ya mjomba, Golden Corporation Kwa sasa inapanuka na tayari ndiyo kampuni inayoongoza ya dawa, kwa hivyo mama yangu aliniambia nitengeneze kampuni hiyo na Mjomba katika siku zijazo."
"Kila la kheri." Lisa alichukua kadi ya biashara.
Baada ya Ethan kuondoka, Pamela alitikisa kichwa chake. “Kabla ya hili, ulitaka kuwa shangazi yake. Sasa, si wewe ni shangazi yake, hata anafanya kazi kwa ajili ya mumeo.”
"Sahau. Imekuwa miaka mingi sana. Haijalishi tena.” Lisa alitabasamu kwa unyonge.
Baadaye kidogo, sherehe ya harusi ilianza. Wakati wa matembezi ya kujongea, Joel alimshika mkono Lisa na kumsogelea Kelvin taratibu. Nyuma yao, Suzie na Lucas wakarusha maua kutoka kwenye kikapu. Ingawa harusi ilikuwa ndogo, ilikuwa ya kifahari na ya gharama, na kila ua lililorushwa lilinunuliwa kutoka nje ya nchi.
Harufu ya maua ilijaza chumba. Lisa alimtazama Kelvin mbele yake. Akiwa amevalia suti nyeupe, alionekana mzuri na mpole kama mwana mfalme. Hapo awali, alifikiria juu ya harusi ya kimapenzi na Alvin, lakini mtu huyo alishindwa mara kwa mara. Katika maisha haya, kuna mtu hatimaye alimpa harusi nzuri. Alijisikia furaha kweli.
"Kelvin, mtunze binti yangu vizuri siku zijazo." Joel akamkabidhi Kelvin mkono wake.
“Nitafanya, Baba.” Kelvin aliushika mkono wa Lisa.
Punde, Padri alianza ibada ya ndoa. "Bwana. Kelvin Mushi, je, unamchukua Lisa Jones kuwa mke wako, katika hali nzuri au mbaya zaidi, katika ugonjwa na afya, wakati wa furaha na wakati wa huzuni, kumpenda bila kipingamizi na kuwa mwaminifu kwake milele?”
Kelvin alisema kwa upendo, "Ndiyo, nakubali."
Padri akatabasamu na kumgeukia Lisa. “Bi. Lisa Jones, je, unamchukulia Kelvin Mushi kuwa mume wako, katika hali nzuri au mbaya zaidi, katika ugonjwa na afya, nyakati za furaha na huzuni, kumpenda bila kipingamizi na kuwa mwaminifu kwake milele?”
Lisa alitikisa kichwa na kunong'ona, "Ndiyo, nakubali."
Padri akasema, “Kisha, tafadhali badilishaneni pete zenu, na bwana arusi anaweza kumbusu bibi arusi.”
Baada ya wanandoa kubadilishana pete zao za harusi, Kelvin alibusu midomo ya Lisa kwa upole kupitia pazia la shela. Wakati huo, waandishi wa habari mara moja walichukua picha.
Sura ya: 485
Suzie aliuma midomo yake na hakuweza kujizuia kulia. Lucas alimtazama, na uso wake wa baridi ulionyesha ulaini adimu. "Nini tatizo? Huwezi kuvumilia kumuacha mama aolewe? Usijali, mama bado atatupenda kama zamani.”
“Usinidanganye. Mama na Anko Kelvin hakika watatuletea wadogo zetu katika siku zijazo. Mama hatatupenda sana
wakati huo.”
Suzie alifuta machozi na kunung'unika kwa sauti ya chini, akijisikia vibaya sana.
Ingawa Kelvin alikuwa mzuri sana kwake, hakuwa Baba yake halisi.
Yote hayo yalikuwa makosa ya baba yake. Kwanini alikuwa mjinga sana? Tayari alimuashiria, lakini bado alikuwa hajafika.
Sasa, mama yake alikuwa tayari ameolewa. Ilibidi akubali ukweli.
“Hilo halitaftokea.” Lucas aliminya midomo yake myembamba na kumshika mkono wake mdogo. “Mama si mtu wa aina hiyo na utakuwa dada yangu mdogo sikuzote nitakunza."
“Lucas...” Suzie alilia tena. Baada ya kuishi kwa miaka mitatu, hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lucas kusema maneno ya joto kama hayo.
Baada ya sherehe hiyo, wanahabari walichapisha picha hizo nzuri za harusi mtandaoni. Kelvin naye alimshika mkono Lisa na kupiga picha wakiwa wamevalia pete zao za ndoa, na kuiweka kwenye Facebook.
[Kushika mkono wako, mpaka kifo kitakapotutenganisha. Nimekuwa nikikusubiri tangu siku ya kwanza nilipokutana nawe. Siku 1257. Ninafurahi kwamba sikukata tamaa.]
Kama bosi wa Golden Corporation, mara chache alichapisha mambo yake kwenye mitandao ya kijamii. Siku zote amekuwa mtu wa faragha machoni pa umma, kwa hivyo chapisho hili adimu lilizua hisia.
[Oh Mungu wangu, Bwana Mushi! Sijawahi kumwona kabisa akitupia vitu
mtandaoni, leo ni ajabu, inaonekana kweli amefurahi!]
[Mke wa Bwana Mushi lazima atakuwa na bahati ya upendeleo katika maisha haya. Amebarikiwa sana. Bwana Mushi ni kiongozi wa biashara ambaye ni mzuri na tajiri na wa chinichini. Wanaume kama yeye ni vigumu kuwapata.]
[Je, hujui bado? Vyombo vya habari tayari vilitoa picha za bibi harusi hapo awali. Bibi harusi wa Kelvin Mushi ni Lisa Jones.]
[Lisa Jones? Hiyo haiwezi kuwa.]
[Ni yeye, mke wa zamani wa Alvin Kimaro na mpenzi wake wa zamani.]
[Kelvin alimalizana vipi na Lisa? Mbona wamefunga ndoa kwa ghafla?]
[Hakika ni kweli. Waandishi wengi tayari walichukua picha kwenye harusi. Lisa ni kweli mshindi katika maisha. Alvin Kimaro alimfanyia ujinga, lakini aligeuka na kuolewa na tajiri mwingine mkubwa, mfanyabiashara wa dawa za binadamu. Inashangaza.]
[Ni ajabu gani kuhusu hilo? Lisa ni mrembo na mwenye kipaji. Nani hataki kumuoa? Anastahili kupendwa.]
[Si ajabu Kelvin hajawahi kuwa na kashfa na wanawake hapo awali, na sijawahi kusikia kuwa ana mpenzi. Kwa hivyo ni kwa sababu amekuwa akimngojea mtu ambaye amekuwa akikaa moyoni mwake. Wanaume wazuri kama yeye ni wachache.]
[Lisa anaweza kuwa aliumizwa sana na Alvin na akageuka na kuona kwamba Kelvin amekuwa akimngoja kimyakimya kila wakati.
Lazima hatimaye aliguswa.]
[Nashangaa kama Alvin Kimaro anajua kuhusu jambo hili. Hata alichapisha kwenye Facebook kwamba atamsubiri Lisa maisha yake yote.]
[Pengine amejificha kwenye kona na analia sasa hivi. Ni kosa lake kwa kutojua jinsi ya kumtunza.]
Majadiliano motomoto kati ya wanamtandao yalisukuma papo hapo sherehe hii ndogo ya harusi hadi kilele cha habari zinazovuma.
•••
Katika helkopta kibinafsi.
Alvin aliendelea kuangalia muda kwenye simu yake. Ilikuwa tayari saa sita mchana Moyo wake ulionekana kushikwa muda wote, ikabidi ashushe pumzi ndefu kila mara. Aliendelea kujipa
moyo kuwa ni mawazo yake tu. Lisa angeolewa vipi na Kelvin? Hawakuwa wameonana tangu miaka mitatu iliyopita, na tangu Lisa arudi, hakuwahi kuwaona pamoja hapo awali. Ilikuwa haiwezekani wao kuoana ghafla.
Alichukua funda kubwa la maji, na kugundua kuwa mkono wake ulikuwa ukitetemeka vibaya.
Chester alimpigia simu ghafla, akajibu kwa hasira.
"Ikiwa una jambo la kusema basi liteme haraka."
"...Uko wapi sasa?" Chester aliuliza baada ya kimya cha muda.
"Kwenye helkopta kwenda Dar." Chester akahema. “Bado hujasikia?” "Nimesikia kuhusu nini?" Moyo wa Alvin
uligonga kwa hofu na sauti ya Chester.
Ndiyo, aliogopa. Ilikuwa ni mara ya pili akipata tena aina hiyo ya hofu. Mara ya kwanza ni pale alipomsukuma chini Lisa ambaye wakati huo alikuwa mjamzito. Ni uoga uleule alioupata alipompeleka hospitali.
Ni kana kwamba alikuwa akipoteza polepole kitu cha thamani kwake.
"Lisa na Kelvin walifunga ndoa huko Dar es Salaam," Chester alisema kwa unyonge. “Harusi imekamilika. Kelvin tayari amekiri hadharani na waandishi tayari wamepiga picha za tukio hilo. Ikiwa huniamini, tafuta tu habari zinazovuma sasa hivi mitandaoni. Kila mtu tayari anajua."
Alvin akasugua kichwa chake na kucheka kwa uchungu. “Unanidanganya. Leo ni Aprili Fools, sivyo?"
"Hapana, Alvin. Lisa aliolewa kweli. Nenda kwenye hisi zako na urudi. Mimi na Rodney tutakunywa pamoja sasa hivi, tunahudhunika pamoja nawe.”
"Nyamaza. Hawezi kuolewa. Haijafika hata saa sita sasa.” Alipiga kelele, akikataa kuamini ukweli.
"Hakuna mtu anayesema kwamba ndoa lazima iwe baada yas saa sita." Chester alimkumbusha. "Tulia. Ni wewe mwenyewe ulilazimisha talaka na kuachana na Lisa hapo awali. Kwa kweli, makosa yote ni ya kwako...”
“Bam.” Alvin akakata simu.
Bado alimpenda Lisa na hakuwa na hamu ya kusikia kuwa ameolewa. Ingawa upendo huu ulikuja kwa kuchelewa sana na ghafla, alimpenda tu. Alitaka kupata watoto naye. Alitaka
kuwa naye maisha yake yote. Ndiyo, aliwahi kumuumiza, lakini alijuta. Tangu waachane tena, yote aliyofanya ni kujuta tu. Hakuweza hata kulala usiku kwa sababu ya majuto yake. Kichwa chake kilikuwa kitupu kwa muda mrefu hadi hatimaye akawasha simu yake na kugusa habari hiyo.
Hakuhitaji kutafuta hata kidogo. Habari za harusi ya Lisa na Kelvin zilijadiliwa na watumiaji wa mtandao kote nchini. Mtandao ulikuwa umejaa picha za harusi yao. Alivaa mavazi ya meupe ya harusi na tabasamu tamu. Alijua kwamba alikuwa mrembo, lakini hakutarajia kwamba angekuwa mrembo zaidi katika vazi la harusi.
Akasogea chini. Kulikuwa na picha za Kelvin na Lisa wakibadilishana pete zake za harusi, na picha za Kelvin akimbusu.
Kila picha ilikuwa kama kisu moyoni
mwake. Maumivu yake yalikuwa yanashindikana. Mwili wake mzima uliganda na macho yake yakibubujikwa na machozi yasiyozuilika. Angewezaje kufanya hivyo? Walikuwa wameachana kwa siku chache tu, lakini aliolewa na mtu mwingine kwa kufumba na kufumbua? Alijua alikuwa katika makosa, lakini kwanini hakumpa nafasi? Macho yake yakawa mekundu ghafla, kama mnyama anayekaribia kupoteza udhibiti.
Hapana. Hapana, alikuwa mwanamke wake. Asingemruhusu kamwe awe mali ya mtu mwingine. Kwa hivyo ikiwa alikuwa ameolewa? Asingeweza kukubali. Lisa angeweza tu kuwa wake. Angemfanya yeyote aliyethubutu kumchukua kutoka kwake aishi maisha mabaya zaidi kuliko kifo.
Alitazama juu kwa kasi na kumfokea rubani. "Tutafika Dar es Salaam lini?"
Hakuweza tena kusubiri.
“T... Dakika kumi.” Nahodha alitetemeka kwa hofu kwa kuangalia kwake.
“Nipeleke hotelini kwa mwendo wa kasi zaidi.” Kisha akapiga namba ya Ganja. "Mtaarifu kila mtu wa ONA anayepatikana Dar es Salaam haraka iwezekanavyo."
Kwa hivyo ikiwa Lisa alikuwa ameolewa? Kwa vile alikuwa amemfuata, angemchukua hata iweje.
TUKUTANE KURASA 486-490
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)