Simulizi, Mikasa, Vitimbi na Visa vya wasanii wa zamani wa bongo fleva - A special thread

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636
20250123_080724.jpg

Hii ni thread maalum ya simulizi mbalimbali pamoja na visa, mikasa na vitimbi vya wasanii wa zamani wa bongo fleva.

Stay tuned....
 
20250123_172739.jpg

Taji Liundi mtoto wa kishua ambaye alinisurika kifo baada ya kunyweshwa sumu na mama yake mzazi.

Ndio mtangazaji wa kwanza kupiga nyimbo za wasanii wa Bongo kwenye radio mwaka 1994 akiwa Radio One.

Neno “Bongo Flava” lilitajwa kwa mara ya kwanza na Mike Mhagama 1996 kupitia kipindi cha “DJ Show” ili kutofautisha harakati za wana hip-hop na RnB wa Bongo, na wale wa Marekani.

Respect kwa Master T
 
20250123_154327.jpg

Mwaka 2001 kundi la Gangwe Mob kutokea Temeke wanazindua brand yao ya nguo, iliyoitwa Gangwe Gear. Walitengeneza T-shirts, full jeans na kofia zenye chapa yao.

Gangwe Mob iliundwa na wasanii wawili Inspecta Harun na Luteni Kalama na wimbo wao wa kwanza kuwatambulisha kwenye game ni Mtu Bee kabla hawajatoa Ngangari wimbo uliokuwa hit mtaani.

Gangwe Mob ni kundi lililopata bahati ya kuwa na management nzuri ya Sebastian Maganga ambae kwa sasa ni mfanyakazi kwenye Clouds Media.

Waliuza album yao Simulizi la Ufasaha kwa MAMU shilling Million 30 na ilibidi wapokee cash sababu hawakuwa na akaunti ya benki wakabeba pesa kwenye kikapu na wakatembea peku kuofia kuvamiwa.

Pia Gangwe Mob wana historia ya kukataliwa Mpwapwa kwa kuwa mashabiki walihisi ni Gangwe Mob feki walifanyiwa fujo na show yao iliharibika, zamani wasanii hawakuwa na video hivyo usipotokea kwenye magazeti inakuwa ni ngumu mashabiki kukufahamu.
 
20250123_174721.jpg

Mr Nice ndio msanii wa kwanza bongo kusafiri kwa private jet.

Ilikuwa hivi Nice alikuwa na show Marekani lakini kabla ajaenda Marekani kuna promota kutoka Comoro akamvutia waya…Hello Mr Nice nakuhitaji kwenye show hapa Moroni, Mr Nice akamueleza haiwezekani kwa sababu siku chache zijazo natarajia kwenda Marekani kupiga show na nikitoka huko ratiba yangu imejaa weekend zote nimeshafanyiwa booking.

Promota akamwambia nakutumia ndege unakuja kupiga show ndege inakusubiri, baada ya show unageuza Bongo unapanda ndege unaendelea na ratiba zako za USA.

Haya ndio yalikuwa maisha ya Mr Nice kupanda private jet na kujaza show nchi za watu alikuwa jambo la kushangaza enzi zake. Alikuwa yupo on top, show zake anapanda na dancers na Wabogojo yupo pembeni.

Alikuwa na videos kali (kwa standard za wakati huo) alikuwa na kila kitu.

Nchi nzima ilikuwa imetegea sikio kusikiliza mikwaju ya Mr Nice.
 
FB_IMG_1737639959093.jpg

Wimbo wa Tutakukumbuka unatoka mwaka 2001, King Crazy GK amemshirikisha TID.

Ni wimbo maalum kwa mshikaji wake anaitwa D Rob aka Zomba.

Mwana FA kwenye ngoma yake ya Ingekuwa Vipi anatuuliza, Ingekuwa Vipi angekuwa hai D Rob?

Huyu D Rob ni nani?

Marehemu D Rob aka Zomba ambaye jina lake halisi ni Robert alikuwa moja ya rappers wakali kabisa wakati huo, akiwa member wa Kwanza Unit (Mimi namuweka kwenye top ten ya rapaz wakali bongo wa muda wote). Ni moja ya marapa waliokuwa wanakubalika sana mtaani haswa kwenye concert za wakati huo.

Watu wanasema ni time traveller sababu alitabiri kifo cha kwenye wimbo wa Msafiri, classic song ya Kwanza Unit.

Mimi ni naupenda wimbo wa Lady JayDee unaoitwa Nakupenda sababu ya verse ya D Rob.

M.A.P Zomba!
 
Attachments

View attachment 3211330

Ni yupi kati ya hao kwenye picha?
 
Eazy B, D Rob, Chief Rhymson, Fresh G, na mwanangu mwenyewe Y-Thang.

Kwanza Unit.
 
View attachment 3211330

Wimbo wa Tutakukumbuka unatoka mwaka 2001, King Crazy GK amemshirikisha TID.

Ni wimbo maalum kwa mshikaji wake anaitwa D Rob aka Zomba.

Mwana FA kwenye ngoma yake ya Ingekuwa Vipi anatuuliza, Ingekuwa Vipi angekuwa hai D Rob?

Huyu D Rob ni nani?

Marehemu D Rob aka Zomba ambaye jina lake halisi ni Robert alikuwa moja ya rappers wakali kabisa wakati huo, akiwa member wa Kwanza Unit (Mimi namuweka kwenye top ten ya rapaz wakali bongo wa muda wote). Ni moja ya marapa waliokuwa wanakubalika sana mtaani haswa kwenye concert za wakati huo.

Watu wanasema ni time traveller sababu alitabiri kifo cha kwenye wimbo wa Msafiri, classic song ya Kwanza Unit.

Mimi ni naupenda wimbo wa Lady JayDee unaoitwa Nakupenda sababu ya verse ya D Rob.

M.A.P Zomba!
D Rob alijywa pia mtoto wa kishua mara waseme alkuwa na ngoma sijui sijui
 
Maisha yanakwenda kasi Pfunk kwa sasa anaitwa Babu mtu.

Mkuu huyo Mamu alikua Promota?
 
Back
Top Bottom