Simulizi, Mikasa, Vitimbi na Visa vya wasanii wa zamani wa bongo fleva - A special thread

Simulizi, Mikasa, Vitimbi na Visa vya wasanii wa zamani wa bongo fleva - A special thread

Alafu mkuu wewe nishakufaham....

Ndo wewe walikua wanakutaja kwenye taarabu wanakuita faza mauji...

Mauji mauji... Mauji anachana nyuzi
Hao kama Sio jahazi modern basi ni tot na Khadija khopa "mimi nilikuaga napiga remix mauji mauji🤣mauji Yanachapa chupi
 
Una uhakika Richard makala bado yupo hai🤔
View attachment 3218820

Yamenikuta, yamenikuta, yamenikuta mzee mwenzangu

‘Yamenikuta’ ni moja ya nyimbo kubwa kuwai kutokea kwenye kiwanda cha muziki Tanzania.

Huu wimbo ulikuwa hit mitaani bila msaada wa social media wala promo ya radio. Ulilia kila kona ya nchi vijana walikuwa wanaimba mashairi yake.

Wimbo ni wa kundi la GWM lililohasisiwa na masela watatu kutoka Temeke, Easy Dope, D Chief na KR. Kundi hili lilianza rasmi mwaka 1993 likiwa na ndugu wawili ambao ni mapacha Richard Makala [Easy Dope] na Robert Makala [D Chief]. KR alikuja kuongezeka baadae .

Yamenikuta ni wimbo wao maarufu Zaidi ambao walimshirikisha 2 Proud kwa sasa Mr II aka Sugu ulirekodiwa na Bon Luv. Ila wana nyimbo nyingi zilizokuwa maarufu kitaa na mainstream kama ‘Cheza mbali na kasheshe’ na ‘Kamua’.
Lilikuwa ni kundi lenye exposure kubwa ya muziki kuanzia kwenye kuandaa catalog, videos na shows.

Kama waswahili wanavyosema maneno uwa yanaumba, inawezekana yameumba kwa vijana awa wa GWM, Easy D na D Chief maana kwa sasa wote wamepatwa na ugonjwa wa kurukwa akili.

Inasikitisha sana story yao maana wanavyosema mtaani ni kuwa chanzo cha matatizo yao ni ugomvi wa nyumba ya urithi iliyopo Temeke hivyo kuna ndugu zao wamewachezea.
 
Na ndiyo maana siku moja anahojiwa "ni kitu gani unajutia katika maisha yako ua muziki" Chuma kilijibu "sina cha kujutia maana kila kitu nimekwishafanya" Kifupi mwamba hana cha kupoteza👀
 
Chief hapa umeshinda sana uko full details kongole sana. Mwamba huo ugonjwa wa usingizi ulimpelesha sana
 
Hao kama Sio jahazi modern basi ni tot na Khadija khopa "mimi nilikuaga napiga remix mauji mauji🤣mauji Yanachapa chupi
Ndo huyu jamaa ndo mauji mwenyewe alafu anajifanya kama hajui kitu hivi ahahahha
 
Back
Top Bottom