Solo Thang AKA Ulamaa anatekwa na Kikosi cha Mizinga
Kuna wimbo wa Solothang unaitwa Ndugu Zangu, Solo anasema, ‘’Nishatekwa na Kikosi na sitolipa kisasi’’.
Ni stori ya kweli, Solo alitekwa na kundi la Kikosi cha Mizinga lilikokuwa linaonngozwa na rapa mbabe Kalapina.
Unaweza kuwa unajiuliza ilikuwaje Kikosi cha Mizinga wakamteka Solo? Tumezoea siku hizi kusikia stori za wasiojulikana ndio wanafanya utekaji.
Lakini enzi hizo ubabe, undava, uhuni na vurugu zote ilikuwa ni jambo la kawaida kwa makundi ya wasanii wa rap.
Sababu haswa ya Solo kutekwa ni bifu alilokuwa nalo P Funk na Kikosi cha Mizinga na chanzo cha bifu ni ubabe tu hakukuwa na sababu ya maana sana iliyofanya Kikosi wapishane na Majani.
Solo alikuwa ni msanii wa Bongo Records ya P Funk Majani na alikuja na style iliyokuwa inafanana na Hashim Dogo member wa Kikosi.
Mtaani kukazuka maneno kwamba P anamtengeneza Solo kama replacement ya Hashim Dogo aka Mwendawazimu.
Wakati huo Hashim alikuwa ni rapa anayeheshimika sana mtaani na anakubalika na mashabiki wa gangsta rap ila hakuwa anatambulika sana kwenye mainstream.
Bongo records waliachia wimbo unaitwa ‘Bongo Chelea pia’ ambao ndani ya huo wimbo kuna mistari Solo Thang anasema ‘Tunasonga kama Dogo na Pina’.
Huu mstari ndio ulikuja kuleta tafarani ya kutafutana mtaani mpaka kutekwa kwa Solo.
Kwa nini? Kalapina na Hashim walikuwa na wimbo wamerekodi muda mrefu kwa Majani unaitwa Tunasonga.
Huu wimbo P Funk aliuzuia kutoka sababu ya mgogoro wake na Kikosi.
Sasa Solo kutumia wimbo wao ambao haujatoka kwenye mistari yake, Kikosi walitafsiri anafanya kusudi ku-pre empty wimbo wao na kuondoa exclusiveness.
Walichukulia hii kama vita na Bongo Records na Solo ndio anatumika kuwashambulia.
Hii bifu ilikuwa mbaya ila ilikuja kumalizwa kindugu. Baadae katika kutunishiana misuli Solo na Pina walikuja kugundua wao ni ndugu kabisa na wakaitwa kupatanishwa na familia.