MIMI NA MIMI
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Lakini, nikajaribu tena kuikwapua simu yangu na kusema, "Madam, leta hapa simu yangu... ni muhimu."
Akaweka kizuizi zaidi, na ndipo akasema, "Hebu acha kutusumbua na wewe! Maswali yote hayo ya nini? Yupo na mke wake hapa, acha usumbufu wako, kwani hujaoa? Muda unapotea, muda unapotea wapi, kwenda huko!"
Akasonya kabisa na kukata simu utafikiri ilikuwa yake!
Dah! Nikabaki nikimwangalia kwa mkazo sana, naye akanitazama na kusema, "We' naye, mbona unakuwa unafanya madili na watu washamba tu?"
"Washamba? Unajua huyo ni nani?"
"Ni nani?"
"Umeona? Haujui. Utapokeaje simu yangu halafu uongee hivyo na mtu usiyemfahamu bila kujua ana uhusiano gani nami? Je kama ni baba yangu?" nikamuuliza hivyo.
"Ba'ako ndo' ana lisauti libaya kama amemeza ngoma ya gwaride?" akauliza kwa kutojali.
Nikamnyakua simu yangu na kusema, "Acha mambo yako madam. Huyu ni ba' mdogo wangu."
"Ndiyo ume-save jina lake kwa kichina?
"Si style tu? Na-save wengi kitofauti kutokana na jinsi navyofahamiana nao, asa' hapa ushaniharibia CV, hujui huyu ni mzazi?"
"Kwenda huko! Hajachangia hata kidogo kukupa damu uliyonayo kwa hiyo usijipe presha," akasema hivyo kwa kutojali.
Nikashusha pumzi kiutulivu, kwa sababu ilionekana nilichokuwa nimehofia hakikutokea, kisha nikamuuliza, "Alikuwa anasemaje kwani?"
"Eti oh, mbona hupatikani... sijui muda unaenda na haumpi mrejesho... ndiyo nikamwambia aache kukusumbua," akajibu hivyo.
Naikaiangalia simu yangu kwa umakini.
"Ni mrejesho wa ninI anataka umpe?" Bertha akaniuliza.
"Ni... masuala ya kifamilia tu. Kuna mchango wa kutoa sasa mimi bado sijawatumia kwa hiyo ndiyo...."
"Wanaomba hela. Ndugu nawaelewa vizuri sana, wala hata usiseme zaidi..." akaniambia hivyo.
"Ngoja nimtumie ujumbe, asije aka...."
Bertha akaikwapua simu yangu na kusema, "E-eeh achana naye..."
Nikamtazama usoni kwa umakini.
Akaweka simu yangu pembeni na kunigeukia tena, kisha akanisogelea huku akikishika kidevu changu kwa makucha yake na kusema, "Focus kwenye kitu kimoja tu hapa. Mimi. Masuala ya ndugu zako utadili nayo ukiondoka, sawa?"
Nikiwa namtazama kwa umakini, nikamwambia, "Yes madam."
"You're mine now," akaniambia hivyo kwa sauti ya chini huku akinitazama mdomoni.
Nikalazimisha tabasamu na kusema, "All yours."
Akatabasamu kiasi kwa kiburi, kisha akalaza mguu wake mmoja juu ya paja langu kwa mtindo wa kupiga nne, kalio lake likiwa nje na likitoa tangazo kuu la biashara, nami nikalikamata shavu moja na kuliminya.
Akatabasamu na kusema, "Uko vizuri kijana. Kama King Nassir."
Nikiwa naelewa aliyemmaanisha, nikamuuliza, "Ndiyo nani huyo?" kwa kujifanya sijaelewa.
Akacheka kwa furaha kabisa, akiachia kidevu changu na kunishika shingoni, naye akasema, "We' ni mjanja kweli, lakini siyo kwenye pande zote unahusika."
"Oh, you have no idea," nikamwambia hivyo.
"Kwa lipi lingine ambalo bado sijaona?"
"Mengi tu. Maana yangu ni kwamba... sasa hivi umenielewa zaidi na hautaniona kuwa mwanaume sura nzuri tu. Uliposema nimeumbwa kwa ajili ya mwanamke hukukosea, ila najua bado ulikuwa unanidharau. Sasa ndo' nimekuonyesha, na bado mengi hujayaona kutoka kwangu," nikamwambia hivyo.
"Kwa hiyo kumbe ulikuwa unanitamani tokea mwanzo?" akauliza hivyo.
Najua alikuwa anataka sifa tu, hivyo nikamwambia, "Tokea ulipomuua Joy. Nilikuelewa sana. Huwa siyo mtu wa kunyenyekea sana mimi, ila kwako hata kama ukiniambia niilambe miguu yako sitosita kabisa."
"Miguu tu? Na nikikwambia unyonye mpalange wangu je?" akasema hivyo.
"Aa wee... ahahahah..." akanifanya nicheke kidogo.
Akawa ananitazama kwa hisia fulani ya furaha.
"Kama chooni kusafi, sawa. Ila siyo kitu yangu..." nikamwambia hivyo.
"Mmm..." akafanya hivyo huku akianza kukitelezesha kiganja chake kuelekea kwenye mashine yangu.
"Nikuulize kitu?" nikamwambia hivyo.
Akawa ameishika mashine yangu iliyokuwa imeanza kuvimba upya, naye akasema, "Uliza tu."
"Hivi... pale tulipoenda juzi..."
"Mm-hmm..."
"Red Room, si ndiyo?"
Akatikisa nyusi kukubali huku akiniangalia kizembe na akiendelea kuchua mtambo wangu.
"Nandy anajua kuhusu hiyo sehemu?" nikamuuliza hivyo.
Akasitisha kunichua na kutulia kidogo, kisha akaanza kucheka kwa furaha sana.
"Nini sasa?" nikauliza hivyo.
"Ahahahah... kwa nini umeuliza hivyo?"
"African Princess casino ni ya kwake kama sikosei. Ni lazima awe anajua biashara zote za pale. Ama?"
"Haujakosea. Lakini yeye ni mmiliki tu wa casino, siyo watu. Watu wanaweza kuingia kwako wakaamua kuongezea vyumba au mapambo mengine na siyo lazima mpaka uyaone. Ilimradi anapata faida yake, basi. Sisi ndiyo tunawanunua mameneja na kuendeleza biashara zetu bila kubughudhiwa. Nandy, Nandy anajua nini kama siyo tu kuimba na mtungi ukiwa wazi mbele ya camera utafikiri kushika mimba ni kitu anachojua peke yake duniani?" akaongea hayo.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "That's a good one."
"You know it," akasema hivyo na kuishika mashine yangu tena.
Nilikuwa nimeshasimama kwa nguvu zote tena, naye akaanza kunisogelea karibu zaidi tukiwa bado tumelalia mbavu zetu, kisha akaupitisha mguu wake mmoja juu kiasi kunipita ili aweze kujiwekea mtambo kwa chini.
"Kidogo tu umeshanyanyuka tena. Ama unatumia mkongo?" akaniuliza hivyo karibu na mdomo wangu.
"Situmii hivyo vitu... na sikuwa na wazo la kufika huku pamoja nawe leo," nikamwambia.
Akajiingizia na kuanza kusugua kiuno chake kwa kukatika taratibu, naye akawa amenishika begani huku akionekana kupata raha sana kwa namna ambavyo alipumua, kisha akauliza, "Ulitarajia kufika huku pamoja na mimi lini?"
"Haikuwa akilini mpaka ulipovua nguo mbele yangu jana," nikamwambia hivyo.
Akacheka kidogo na kusema, "Kumbe ulipagawa?"
"Sikudhani ingekuwa na maana yoyote."
"Mmh... una maana gani?"
"Nilifikiri msimamo wako upo kwa Chalii tu, I mean... mpaka ukamuua Joy ili tu unionyeshe jinsi unavyompenda," nikamwambia hivyo.
Akasitisha kujisugua na kunitazama tu usoni, huku bado tukiwa tumeingiliana.
"Kwa hiyo... sikufikiria kwamba ingefika siku ungeniruhusu nile utamu wako... madam," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini karibu na mdomo wake.
"Unajua unapoongelea hilo suala huwa unaniboa sana?" akasema hivyo.
"Kwa nini? Inakukwangua wapi vibaya?" nikamuuliza hivyo.
Kisha nikaanza kumsugua tena kwa mwendo ule ule wa taratibu na kufunua titi lake moja, nami nikawa nainyonya chukuchuku yake na kuivuta kwa meno.
Akawa anavuta nywele zangu na kunichoma kwa makucha yake shingoni, naye akasema, "Unakuwa unanikumbusha... sss... nisivyotaka kukumbukahh..."
"Kwani kumuua Joy ilikupa ndoto mbaya kihivyo?" nikamuuliza.
"Siyo Joy... ila Charles..." akasema hivyo.
Nikaona nimkolezee utamu kwa mara nyingine tena ili aendelee kufunguka. Nikawa nalamba shingo yake huku nikiendelea kumkuna tu, naye akalaza kichwa kwenye mto huku akipanua mguu wake zaidi na kufumba macho.
"Chalii alikufanyaje?" nikamuuliza hivyo.
"Aahh... ni mpumbavu sana. Kwa sababu ya kupenda mno kula k(...) za nje... akasababisha.... hhh..."
"Akasababisha nini?" nikauliza tena.
Akafumbua macho yake na kuniangalia kilegevu, nami nikawa nimeona badiliko dogo usoni mwake kutoka kwenye raha kwenda kwenye huzuni. Huzuni ile ya ndani sana.
Akaweka kizuizi kiasi kwa kunishika kifuani ili nisiendelee kumpa raha, naye akajitoa kwangu kabisa na kugeukia upande mwingine wa kitanda, akikaa kwa kunipa mgongo na kuweka miguu chini. Kuna jambo zito lililokuwa linamsumbua sana katika mahusiano yake pamoja na Chalii Gonga, na kama ndiyo lilichochea mpaka mauaji ya Joy yakatokea, nilihitaji kujua ni nini.
Nikasogea usawa wa sehemu aliyokaa nikiwa nimejilaza bado, nami nikamwambia, "Madam... niambie nini kinakusumbua."
Hakutoa jibu, na badala yake akavuta kiboksi kidogo cha sigara na kuchomoa moja, kisha akavuta na kiberiti cha mafuta na kuiwasha.
"Madam.." nikamwita na kumgusa mgongoni.
"Tuachane na hayo... tuanze kuongelea nilichokuitia hapa," akasema hivyo bila kunitazama.
"Tutaongea tu, lakini kwanza...."
"Hujaelewa nilichokwambia au?" akanikatisha.
"Nimeelewa. Ila sometimes madam... huwa ni vizuri kukitoa kitu kinachoisumbua nafsi hata kwa kuzungumza tu... ni nzuri kiafya," nikamwambia hivyo.
"Ahahah... kiafya. Afya gani? Huoni navuta sigara?"
"Ya kihisia."
"Sihitaji kujisikia vizuri kwa lolote. Na, wewe siyo daktari wangu, wewe ni mwajiriwa wangu kwa masilahi mengine. Hayo usitake sana kuyachokonoa kisa tu umeni(.....) leo," akasema hivyo.
"Hiyo siyo sababu yangu," nikamwambia hivyo kwa upole.
"Ila ni nini? Kwamba... nini, unataka kuonyesha unanijali sana ama? Acha unafiki bwana," akaniambia hivyo.
Nikajinyanyua na kukaa, nikiwa karibu zaidi na mgongo wake, nami nikamwambia, "Ndiyo. Nakujali Bertha."
Akageuka na kuniangalia machoni, mimi nikiwa namwangalia kwa njia ya hisia ili aweze kuona kwamba nilikuwa namaanisha nilichokisema, kisha akatazama pembeni tena.
Nikasogea usawa wa bega lake na kumshika mkono huku nikisema, "Ongea na mimi. Naweza nikakuelewa kuliko unavyoweza kudhani."
"Acha maigizo yako HB...."
"Niite JC. Na siigizi. Ninataka tu kukujua. Kukuelewa," nikamwambia hivyo.
Akanitazama usoni na kupuliza moshi pembeni, naye akauliza, "Ili iweje?"
Nikamsogelea karibu zaidi na mdomo wake na kusema, "Ili ni-connect nawe. Utanitumia jinsi unavyotaka, sawa, lakini mimi nakutaka tu wewe. And I mean it. Wewe tu."
Haya yote yalikuwa majaribio kuona ikiwa mwanamke huyu alikuwa na udhaifu kwa sehemu hii ya kuonyeshwa hisia-mwenzi, na kutokana na jinsi ambavyo alinitazama baada ya mimi kumwambia hivyo, ilionekana wazi kwamba nilikuwa nimeanza kumwingia.
Nina maana kwamba, sawa, alikuwa ameshanikubali mpaka kunipa mchezo lakini hiyo ilikuwa ni mchezo tu, hii ya sasa hivi ilikuwa ni njia ya kumvuta zaidi na kujua udhaifu wake unakaa wapi, maana inaonekana ni huo huo udhaifu ndiyo uliokuwa unampa nguvu yake.
Akiwa bado anaendelea kunitazama, nikaanza kupitisha vidole vyangu kwenye nywele zake fupi, kisha nikamwambia, "Tell me. Charles alifanya nini? Kwa nini unaonyesha kwamba unampenda sana lakini... lakini moyo wako unamchukia?"
"Acha kujifanya unajua sana kusoma watu. Unaongea upuuzi tu," akasema hivyo kisha kutazama pembeni.
"Nayoongea ni kweli, na wewe unajua hilo. Najua pia sababu inahusiana na G... mtoto wako," nikamwambia hivyo.
Akanitazama usoni tena, zamu hii kwa macho makali kiasi, naye akauliza, "Umemjuaje G?"
"Nilimsikia siku ile Chalii alipokuita mama G... na ulikasirika alipokuita hivyo. Nilianza kuelewa kiasi kwamba jamaa alikuwa amekukosea na lazima ilihusiana na... mwanao," nikamwambia hivyo.
Akaendelea tu kuniangalia, nami nikawa naona macho yake yakitengeneza wimbi la machozi.
Nikamshika kiunoni taratibu na kuishika shingo yake pia, kisha nikamwambia, "Usijali. Ongea tu. Niko hapa kwa ajili yako... nitakusikiliza."
Akavuta pumzi na kuishusha kama vile anajikusanya kifikira, naye akasema, "Yaani unataka nizungumze nawe kuhusu maisha yangu? Kabisa, unafikiri inawezekana?"
"Kwa nini isiwezekane? Wewe umeshakuwa wa muhimu sana kwangu. Na huwezi jua... naweza nikaja kuwa ndiyo future husband wako, au naongopa?" nikasema hivyo.
"Wewe huyo? Unioe mimi?" akauliza kikejeli.
"Sasa je!" nikasema hivyo.
Akacheka kidogo na kuangalia chini, akionekana kuzama zaidi kwenye fikira za mambo hayo.
"Niambie Bertha. Kwa nini unaishi hotelini ingawa unaweza kuwa na nyumba kubwa kabisa...."
"Nyumba ninayo. Na ni kubwa," akasema hivyo kwa kunikatisha.
Nikatulia tu na kuendelea kuisugua shingo yake taratibu.
Akasema, "Unajua nini mdogo wangu? Maisha ya mapenzi kupendana ni usenge mmoja mkubwa sana. Yaani... mmoja akijitahidi kubaki njia kuu lazima mwenzake apotee tu. Ni ngumu sana kupata mahusiano kama ya Beyonce na Jay-Zee, na tena hata na hao wanaongezewa tu chumvi na media lakini wanajitahidi. Mwanamke akikupenda mwanaume kwa moyo wote, atafanya chochote kwa ajili yako yaani, na ndiyo hapo huwaga mnavimba sasa na kuanza kuleta dharau..."
"Ni kweli. Naelewa," nikamwambia hivyo.
"Nimekutana na Charles akiwa hana kitu, nikampenda, nikamwinua mpaka akawa mwanaume unayemwona amekuwa sasa... lakini bado tu hata na yeye hakuridhika na niliyompa. Sawa, sikatai, nyie wanaume kutulia na mwanamke mmoja ni ngumu, utafanya sub za mara moja moja kuonja ladha za wengine, siyo mbaya... lakini usiishushe heshima ya yule mwanamke aliye mke wako kabisa eti kwa sababu tu jiti lako limeshaingia kwenye mashimo mengi. Nimemzalia Charles mtoto mzuri sana, mrembo kama mama yake... lakini kwa ujinga wake, akasababisha mtoto wangu afe..." akasema hivyo huku machozi yakimlenga.
"Aisee... pole sana Bertha," nikamwambia hivyo kwa upole.
Akapiga ulimi mdomoni mwake kwa hasira na kuangalia pembeni.
"Alimfanyaje?" nikamuuliza.
"Si ni mpumbavu? Giselle alikuwa shule huku, wakati huo Chaz ashaanza kuendesha biashara zangu kibao, si ndiyo akafanya upuuzi wa kuiba pesa za benki?" akasema hivyo.
"Wewe! Wapi?"
"Huko Musoma. Alikuwa amekula dili na mhasibu mmoja wa huko, waziibe kupitia yeye, milioni 240 kabisa, ndiyo wakadakwa. Sasa, Chaz ni mjinga, alikuwa anatumia viambata vyangu kwenye hilo dili bila me kujua, ili wakishagawana pesa ziingie kwangu. Alikuja kusema eti alitaka kuni-surprise, ajionyeshe alivo' mjanja pia kwenye wizi... ujanja gani huo ukanitia mimi hatiani?" akaeleza.
"Kwa hiyo walipokamatwa, wakafikiri wewe ndiyo ulihusika?"
"Eeh! Na tena hata hawakuweza kuziiba hizo hela, upumbavu tu... ndiyo me nikaja nikashikiliwa..."
"Ikawaje?"
"Huyo mhasibu alisondekwa jela, na mimi nikapelekwa mahabusu pia. Mwanasheria wangu alisaidia tu wakaona kwamba niliingizwa kwenye hilo janga bila kupenda, lakini kuwaambia kivipi ndiyo ingekuwa na utata. Kama wangemkamata Charles, labda hata wangefatilia na kujua haya mambo yetu mengine, kwa hiyo nikawaacha wanipe adhabu... wanifungie tu," akaongea hivyo kwa hasira.
"Huko huko Musoma?"
"Eeh."
"Na Chalii je?"
"Alikuwa amejificha. Alikuwa anaogopa, akaja kujificha huku... mimi nikajitoa nifungwe badala yake. Miezi kumi na nane... yaani mwaka mzima na nusu," akasema.
"Aisee! Haukupitia shida sana huko?"
"Hamna. Pesa ilikuwepo, kwa hiyo niliishi kama malkia wa gereza," akasema hivyo.
Nikatabasamu kidogo. Bertha kama Bertha.
"Ndiyo baadaye palipokuwa pametulia, akawa anakuja mpaka kule nilipofungiwa, ananiomba msamaha, na ananihakikishia biashara zinaenda fresh. Nilikuwa nimetoa kisingizio kwa mwanangu kwamba niko safarini, hata wazazi wangu walifikiri nimesafiri kwenda nje ya nchi wakati nilikuwa nanyea debe alilotakiwa kunyea Chaz... waliojua ilikuwa ni yeye tu... na Festus..." akaeleza.
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Sasa kumbe mimi kufungwa na kumwacha jamaa asimamie mambo mengi kukamwongezea bichwa la kufanya lolote kwa jinsi alivyotaka. Unajua yaani mwanzoni hakuwaga na kifua, yaani ile nimetoka tu, me si ndiyo nilikuwa "madam" mkalia kiti cha ofisi? Yeye ndiyo akawa "sir" sasa na kukikalia hicho hicho kiti. Akawa ndiyo boss sasa, kiburi kikamjaa, wanawake hao, akafikiri sitakuja kutoka labda. Nilikuwa nawaza sana kuhusu mwanangu. Kila mara tulipoongea... hhh... Charles alifanya nifikiri mtoto anaishi kwa upendo sana, kumbe hata nusu ya robo kwenye muda wake alikuwa hampi. Anampelekea tu mama wengine pale kwenye nyumba yangu yaan... ah!" akaongea kwa hisia sana na machozi yakimtoka.
Mpaka nikaanza kumwonea huruma. Ni kweli nilikuwa soft.
Akaendelea kusema, "Mimi kwa sababu ya resource zangu... maisha yangu tu kiujumla... nilijua ningetoka na kukuta hali iko poa, maana... sikufikiria kwamba Charles angekuwa punguani namna nilivyokuja kumkuta. Mimi sikuwa na noma hata kama angekuwa anatoka na mwanamke mwingine, mwanaume ana mahitaji yake bwana na mimi nilikuwa mbali sana, inaeleweka. Lakini huyu shemeji yangu Dotto, alipokuja kuanza kuniambia yanayoendelea? Nilichoka."
"Dotto alikuwepo huku na mwanao?"
"Ndiyo, ni ndugu yake Charles, na tulimwajiri awe mlinzi wa mtoto wetu. Alikuwa limited lakini, kwa sababu angemwangalia mtoto alipokwenda shule na kumrudisha, ila akiwa ndani isingekuwa rahisi kumwangalia muda mrefu. Sasa... hhh... kuna wakati huyu mpumbavu... nilipokuwa nakaribia kutoka... alikuwa na limwanamke lake lililokuwa linaishi hapo nyumbani. Sijui siku wamezinguana kisa nini, Chaz akampiga, hajamwacha na mtoto huyo mwanamke akampa sumu?" akasema hivyo kwa sauti kali.
Nikawa nimebaki kumtazama usoni kwa mshangao makini.
"Yaani nimebakiza mwezi mmoja... mwezi mmoja, nitoke... mwanangu akanyweshwa sumu?" akasema hivyo kwa hisia sana na kupiga ulimi mdomoni.
Nikaendelea kumtazama tu. Yaani sikujua hata nilipaswa kuhisije.
"Umeona sasa Charles alivyokuwa mjinga? Kwa hiyo akapeleka magomvi yake kwenye nyumba yangu, ambayo ingekuja kuwa ya mwanangu, halafu akamwacha naye ili amlipizie... yaani... hhh... sikuwa nimewahi kuua mtu kwenye maisha yangu yote, ila nilipotoka, huyo mwanamke ndiyo akawa wa kwanza," akasema hivyo.
"Ulimuua?"
"Yeah. Yeye, pamoja na wasichana wa kazi waliokuwepo wakati huo. Ni upumbavu gani kumwangalia mwanangu akauliwa tu kipuuzi namna ile?" akasema hivyo na kusonya kwa hasira.
"Kwa hiyo ukawaua na wadada wa kazi? Dah! Uko vizuri."
"Hakukuwa na lolote la kufurahia hata nilipokuja kumuua huyo mwanamke mshenzi. Haingemrudisha mwanangu... lakini kumlipizia kisasi ilikuwa lazima," akasema hivyo.
"Kwani hakuwa amekamatwa mpaka ulipokuja kutoka jela?" nikamuuliza.
"Alikuwa amekimbia! Polisi wazembe tu, miezi miwili yote walikuwa wanamtafuta tu eti, mimi nilipotoka wiki mbili tu nikawa nimempata," akasema hivyo.
"Ulimpataje?"
"Festus alinisaidia," akasema hivyo.
Mh! Huyo Festo huyo?
Nikamuuliza, "Kwa hiyo... Chalii yeye...."
"Alikuwa anajuta, lakini haikusaidia kwa lolote. Mwanangu... mwanangu alikuwa mzuri! Angekuja hata kuwa miss dunia... angalia..."
Akasema hivyo na kuchukua simu yake, naye akaniwekea picha za aliyekuwa binti yake. Na ni kweli kabisa, Giselle alikuwa mzuri kupita hadi mama yake, na mdogo mno kwenye miaka ya kindergarten.
"Hii ndiyo picha ya mwisho nimepiga naye... ahahh... alikuwa ndiyo anaingia la pili..." akasema hivyo huku akinionyesha picha ya selfie aliyokuwa anambusu binti yake shavuni.
Nikamfuta machozi taratibu tu, naye akasafisha pua yake na kuvuta pafu moja ya sigara.
"Ni mzuri," nikamwambia hivyo.
"Alikuwa. Alikuwa mzuri. Ni kwa sababu ya baba yake sasa hivi natumia neno "alikuwa". Yaani... nimetoka kufungwa kwa sababu yake halafu nikakuta kaniharibia furaha yangu... eti, mpaka watu wakawa wanafikiri mimi siyo mama anayejali maana kwenye mazishi ya mwanangu sikuwepo. Sikutaka kwenda huko huku maaskari wakiwa nyuma yangu, ilinibidi nisubirie mpaka siku ya kutoka... can you imagine, yaani sikuwepo kwenye msiba wa mwanangu niliyemzaa mwenyewe? Na hiyo yote ilikuwa kwa sababu ya Charles! Nilimchukia sana," akasema hivyo.
"Mbona yeye hukumuua sasa?" nikamuuliza hivyo.
"Oh, kuna adhabu nzuri zaidi ya kifo, na utamu wake unakuwa kwenye mtu kuwa hai, usinichukulie simple," akasema hivyo.
"Ulimfanyaje?" nikamuuliza.
Akaangalia pembeni na kusema, "Dotto alipounganishwa na Festus kumpata huyo hawala yake Chaz, alimleta kwangu... nikamchinja kwa kisu bila kuikata mishipa yake yote!"
Nikamwangalia usoni kwa umakini, nami nikamwambia, "Ili afe kwa kuteseka polepole."
"Maana yake. Chaz alikuwa ananipigia sana kelele kuwa nisimchukulie hatua kama niliyochukua kwa hawala yake, eti tumetuoka mbali, tunaweza kuzaa mtoto mwingine tena, nimpe adhabu yoyote lakini nisimuue... yaani alikuwa anafikiri kuzaa huwa ni simple sana sijui? Kwa hiyo nikaamua kumwonyesha nini maana ya uchungu wa kuzaa. Nilimpa viungo vibichi vya huyo mwanamke avitafune..."
"Na akavila?!"
"Vyote! Nilimpa macho, zile goroli zile, nilikata na puchi la huyo mwanamke nikampa ale... kidole kimoja... na ulimi. Alitapika alipoanza kuutafuna ulimi, lakini aliendelea na vingine mpaka akamaliza," akasema hivyo kwa kutojali.
"Eh! Bertha? Unayosema ni kweli au unanipiga fix tu?" nikaonyesha kushangazwa.
"Nini? Hauamini? Nilichukua na video, ninavyo humu vipande... ngoja nikuonyeshe," akasema hivyo na kuanza kubofya kioo cha simu yake.
Aloo! Alikuwa hatanii. Nilimwona Chalii Gonga kwenye video akiwa anakula nyama mbichi, pembeni yake wakisimama wanaume wenye nguvu sana, na bila shaka video ikiwa inarekodiwa na Bertha mwenyewe.
Nikamwangalia usoni kwa mkazo sana na kusema, "Aisee! Bertha we' ni mkatili!"
"Mkatili? Kwa hiki nilichofanya? Hapana. Siyo kama ukatili waliofanya kwa mwanangu," akasema hivyo.
Nikaangalia pembeni na kusema, "Dah!" yaani nilichoka.
"Basi watu wanafikiri mimi ndiyo nalishwa, navishwa na Chaz, wakati yeye ndiyo mbwa wangu. Anatembea na baunsa wanafikiri ni mtu wa kumlinda lakini huyo ni mtu nimwemweka amchunge... huwa ana katabia ka kujisahau sana. Nikiamua kumwondoa muda wowote anapotea faster tu, sema kuna ka-amount ka heshima nilikonako kwa wazazi wetu ndiyo kanafanya nimwache tu... ila hata hapo wakija kuvuruga nitakata nyuzi zote bila kuchelewa," akasema hivyo na kuiweka simu pembeni.
"Kwa hiyo wazee hawajui kuhusu hii kutengana kwenu?"
"Ndiyoo... mbele yao sisi ni power couple, kuna... mengi tumefanya kusaidiana, mama yangu aliumwa sana wakati niko ndani wakamuuguza mpaka nilipotoka, hata mimi kujifungua walinisaidia wazazi wake pia, kwa hiyo... mutual respect ipo. Ila wananijua nikibadilika navyokuwa... na ninahisi wanajua mimi na Charles hatuko fresh sana ila wanakuwa wapole tu kutojiingiza kwenye mambo yetu ili nisichafue hali ya hewa... labda hata Chaz aliwaambia nilichomfanyia kwa hiyo... wananiogopa fulani hivi..."
Nikamwangalia na kusema, "Unapenda zaidi kuogopwa na kila mtu, eti?"
"Siwezi kujuana na kila mtu mdogo wangu. Ila kama wale wanaonijua wakishindwa kuniheshimu, ndiyo ninawafundisha jinsi ya kuniogopa," akasema hivyo.
"Kweli. Nimeamini."
"Hakuna lolote alilonalo Charles, ama ambalo ameongeza bila mi' kuhusika. Hiyo Masai, pale Buza, zote ni mimi. Namwacha tu atambe mbele ya wengine, ila kwangu mimi ye' ni kitambaa cha kufutia jasho. Nilimwondoa kwenye masuala yetu ya unga, nikamwachia tu Masai na Buza ili azipanue, lakini hajui lolote isipokuwa ku(.....) tu manamake na kunywa pombe..."
"Ahahah... eti manamake..."
"Ndiyo hivyo. Siku ile amekuja pale Masai katukuta VIP, akawa anaigiza kwamba inamuuma sana kuniona na mtu mwingine, alikuwa anaitafuta tu... cool ya ndoa, akifikiri labda atapata sifa, ila ndo' ilishapotea... yaani sina habari naye tena. Hiyo nguvu unayoona anaitumia kukoromea watu jua inatoka kwangu, na simnyakui kwa sababu tu ya heshima ndogo niliyonayo kwa mama yake na baba yake. Nachotaka ni kuunda tu empire yangu, niwe juu zaidi, nisimame peke yangu bila deni kwa yeyote... kilichobaki kati yetu mimi na Charles ni reputation tu," akasema hivyo.
"Kwa hiyo... kumbe sababu ya kumuua Joy... siyo mume wako?" nikamuuliza hivyo.
"Nini, kwamba nampenda saaaana Charles ndo' maana nikamuua Joy? Ahahaha... hapana. Nilimuua Joy kumpa onyo Charles. Huyo mwanamke hakunijua vizuri, kwa hiyo akawa analeta nyodo zake mpaka kwenye mambo yasiyomhusu. Siku kanifata kunisemesha kifala, ehe... akasema siwezi kumfanya lolote lile, kwanza hampendi Chalii, na ana mpenzi mzuri zaidi... wewe yaani..." akaelezea hayo.
Nikawa nimeweka umakini wangu wote kwake.
"Nilipokuja Masai nikakuita, nilikuwa na hasira... kwa sababu inaonekana tayari Joy alikuwa anajua mambo mengi kuhusiana na biashara zetu kupitia kwa Charles, na mimi sikutaka aendelee kujichomeka ndani zaidi. Nilimwonya Charles amzuie, lakini demu akawa anajifanya mjuaji, ndiyo maana nikaja kwako kukusihi umwonye aachane Chaz. Me nilijua nyie ni wapenzi kweli, ndiyo maana nikaja na gia ya 'mwambie mpenzi wako aachane na mume wangu,' maana wewe hukujua kuhusu haya mengine. Sasa si na wewe ukanipandisha midadi? Nikamweka huyo malaya sehemu yake. Na wewe yaani ulikuwa umebaki kidogo tu yaani...."
"Ungeniua," nikasema hivyo kwa sauti ya chini.
"Maana yake," akasema hivyo na kuweka mdomoni ile sigara iliyokuwa inakaribia kuisha.
Dah! Picha kamili nikawa nimeanza kulipata, na mzunguko wake ulikuwa unatatiza sana fikira. Ile kwamba mambo yanayokupata maishani ndiyo yanakusukuma uishi kwa njia nzuri ama mbaya, ndiyo iliyokuwa kitu ya madam Bertha. Mtu mbaya mwenye sababu nzuri za kuwa mbaya.
"Vipi, mbona solemn?" akauliza hivyo baada ya kuona niko kimya.
"Hamna, niko poa," nikamwambia hivyo.
"Si ulikuwa unataka kunielewa? Ndiyo mimi sasa huyo... niite malkia wa Shetani, mkatili, mwongo, utajua hujui. Maisha yangu yamefosi nikaufata huo mkondo, na siwezi juta kwa sababu ndiyo yananipa faida zote nilizo nazo. Unanielewa pretty boy?" akaongea hivyo.
"Sana tu. Umefanya nimekuzimikia zaidi," nikasema hivyo.
Akanitazama usoni kwa mkazo kiasi, kisha akaangalia pembeni na kucheka kidogo kwa pumzi.
"Umenisaidia mno ujue?" nikamwambia hivyo.
"Kwa kipi?" akauliza.
"Sitakufanyia mchezo wa kipuuzi maana sitaki kujikuta ndani ya pipa nikichemshwa mzima mzima," nikamwambia hivyo.
"Hahaa... usinifurahishe. Ila haujakosea. Ukiniletea za kijinga tu..."
"Najua, najua. Una moto kweli," nikakuza kiburi chake namna hiyo.
Akawa ananitazama kwa umakini, naye akasema, "Mpenzi wako alipokufa... ilikuumiza sana?"
"Ndiyo hicho Bertha, Joy hakuwa mpenzi wangu. Yaani tumekutana siku moja tu, akaniomba one night stand, ndo' sijui akaja kuzagaza kwako kwamba sisi wapenzi? Ila hakuwa mtu wangu kabisa," nikamwambia hivyo.
"Kwa hiyo alijiroga mwenyewe? Akasababisha nikufate, ukanitukana na kuniongezea hasira mpaka nikamuua. Ama tuseme tu wewe ndiyo ulinipa moto zaidi mpaka nikamuua. Mara ya kwanza nilikuwa nataka tu kuwatuma watu wamdundee ili akae sawa, lakini we' ndo' ukanipa wazo la kummaliza kabisa. Bravo," akasema hivyo huku akitabasamu kiasi.
Nikatazama chini kwa kukosa amani kiasi. Aliyokuwa amesema yalijaa ukweli fulani ndani yake, na kuona kwamba hakujutia kumuua Joy ndiyo kitu ambacho kikanikumbusha lengo la mimi kuwa hapa kwa mara nyingine.
"Lakini tuachane na hayo. Ya marehemu ni shauri ya kaburi. Niambie. Mpenzi wako wa sasa hivi yuko wapi?" akaniuliza hivyo.
"Yupo hapa Dar," nikamwambia.
"Anaitwa nani?"
"Madam Bertha."
"Mm?" akafanya hivyo huku akikunja midomo yake kikejeli.
"Nini sasa?"
"Wewe, me siyo mpenzi wako, mimi ni boss wako. Kama ulivyosema, me nakutumia jinsi ambavyo nataka, usifikiri hii kitu tuliyofanya ni I love you... sahau," akasema hivyo.
"Ahahah... kwa hiyo kumbe tumeifanya kiajira? Mshahara wangu lini sasa?"
"Mshahara wa nini?"
"Si nimekutoa mchuzi mara nne kabisa?"
"Toka hapa! Kazi ndogo sana hiyo. Mpaka uje kunikojolesha mara kumi na tatu ndiyo utalipwa," akasema hivyo.
Akanifanya nicheke kidogo, kisha nikasema, "Unafuga mipira ya DAWASA humo ndani, au?"
"Ahahaaa... matenki kabisa, na bado hujafikia hata robo ya moja. Jiandae, nataka nije juu sa'hivi," akasema hivyo na kukitoa ki-T-shirt chake chote.
"Bado hatujaongea chochote kuhusu ulichoniitia," nikamwambia hivyo.
"Agh, ni ishu za madawa, hatumalizi sa'hivi... tutaongea baadaye bana. Kuwa mtoto mzuri unipe action," akasema hivyo na kupanda kitandani.
Nilikuwa nimeegamia mto, yeye sasa akawa ananifata mdomoni kwa ule mtindo wa kutambaa taratibu huku akibinua kalio lake na kunyonga mwili wake kimadoido. Nilikuwa sitaki tena kurudia hili tendo, lakini, lakini, ilinipasa kuigiza tu kwamba kweli kilikuwa kitu cha kawaida na chenye kupendeka kwangu.
Akanikaribia mdomoni na kusema, "Ulishawahi kunyonywa mshedede mpaka ukachubuka?"
"Siyo kitu ambacho nataka. Ukiamua kufanya hivyo, usinichubue," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu kiasi kwa kiburi, kisha akalaza kichwa chake kifuani kwangu kwa upande na kuanza kulamba titi langu lililojaa kiume. Akawa ananing'ata-ng'ata ili kunipandisha mzuka zaidi, na tayari nilikuwa nimeshaamka maana pamoja na ubaya wake wote kiutu, huyu mwanamke alikuwa wa moto mno. Akawa ananitazama huku akiendelea kunilamba na kuiweka mashine yangu kiganjani kwake, na alipokuwa anataka tukutane mdomoni kwa ajili ya denda, simu yangu ikaanza kuita.
Nikatazama pale ilipokuwa kwa ufupi na kuweza kuona mpigaji alikuwa nani, lakini Bertha akaugeuzia uso wangu kwake ili niipuuzie na kuanza kunibusu moja kwa moja mdomoni. Fikira zangu zote zikavutwa na aliyekuwa ananipigia kwa wakati huu, nami nikamkatisha kwanza Bertha ili nipokee.
"We' naye vipi?" akaniuliza hivyo kwa kuudhika.
"Subiri," nikamwambia hivyo kwa sauti tulivu.
Nikamtoa juu yangu na kusogea mpaka simu yangu ilipokuwa, na kiuhakika nikaona kwamba kweli aliyekuwa akinipigia si mwingine ila Bi Zawadi, mrembo wangu. Sijui alitaka kunisalimu tu, ama labda kuniambia jambo lingine muhimu? Kale kahisia ka 'kuna tatizo' kakawa kanagongesha kengele ya hatari moyoni mwangu kunisukuma nitake kujua alichotaka kusema mwanamke huyo, nami nikapokea na kuweka simu sikioni.
"JC mwanangu..." akasikika.
"Naam mama, shikamoo?" nikajibu kwa salamu.
"Marahaba baba. Uko wapi?" akaniuliza hivyo.
Kabla sijatoa jibu, Bertha akaja nyuma yangu na kuichukua simu yangu kwa nguvu, nami nikamgeukia na kumtazama kwa umakini. Alikuwa anaangalia jina la aliyenipigia, na nilikuwa nimetunza namba ya mwanamke huyo kama "Zawadi mweupe," naye Bertha akaniangalia kwa macho yenye umakini.
Nikasema kwa sauti kuielekea simu, "Nimetoka... nimetoka kidogo mama..." huku nikiwa namwonyesha Bertha ishara kwa kuuliza anataka nini mpaka anikwapue simu.
Bertha akaweka mfumo wa kipaza sauti kwenye simu, na sauti ya Bi Zawadi ikasikika ikisema, "...eh? Eti baba? Njoo tu hata tuongee kidogo, na kuna suala la Mamu kama unavyojua, sasa... kutokea jana hapajakaa sawa kabisa hapa. Nakuomba uje tafadhali..."
Nikatulia tu nikimwangalia madam Bertha usoni, ambaye alikuwa akinitazama kama vile anadadisi hali hii ilihusiana na nini.
Sauti ya Bi Zawadi ikasema, "JC? Unakuja mwanangu? Ama upo mbali sana?"
Nikaacha kutafakari sana na kusema, "Hapana mama, siyo mbali sana. Nimekuelewa, niko njiani... nakuja."
"Sawa mwanangu, nashukuru sana. Jitahidi uwahi wahi, eh? Kabla Mimi haja...."
"Yeah, yeah, naelewa. Niko njiani, sikawii," nikaongea hivyo upesi.
"Haya baba," Bi Zawadi akasema.
Kisha akakata simu. Nikatazama pembeni kiufupi nikiwa nawaza kuhusu uzito wa ishu hiyo ya kutakiwa kwenda huko, maana ni wazi kwamba ningepaswa nizungumze na mama wakubwa kuhusu chanzo cha ugomvi uliotokea jana baina yangu na Miryam.
Nikamwangalia madam usoni na kukuta amenikazia macho yake kama anasubiri maelezo, nami nikasema, "Inabidi nikuage madam."
"Unaenda wapi?" akauliza hivyo.
"M... nanii... Mabibo. Huyo ni mama mkubwa, kuna tatizo na ninahusika..." nikamdanganya.
"Watu wako wa ukoo hawaishiwi na matatizo, eti? Halafu wewe ndiyo wanakuona kama four figure ya kutoa solution, ama?"
Nikatoka kitandani na kuanza kuvaa nguo zangu na viatu huku nikimwambia, "Ni muhimu sana, kama unavyojua... familia. Sema... ni kitu cha muda mrefu yaani, kwa hiyo naona bora kwenda kumalizana nayo sa'hivi... ndiyo maana nikaja hapa nikiwa sina raha. Ni hiyo ishu."
"Kuna mtu anawasumbua? Huyo Mamu ni nani, mdogo wako? Kama kuna mtu kamtia mimba huko, we' sema tu tummalize," akaniambia hivyo.
"Ahahah... siyo kila kitu kinasuluhishwa kwa kuua tu madam. Acha nikalimalize kwanza," nikamwambia hivyo na kusimama.
"Kwa hiyo unaniacha mtupu peke yangu kitandani?" akauliza.
"Hamna, kuna mito hiyo hapo, kuta unachezea," nikamtania hivyo.
Akanikata jicho la kukerwa.
Nikatabasamu kidogo na kurudi kitandani, nikikaa kwa ukaribu naye zaidi, halafu nikamsogelea usoni na kusema, "Usijali. Nikimaliza hiyo ishu nitakwambia kwa simu ili kama utakuwa bado unanihitaji... unaniita tu..."
"Siyo kama nitakuwa. Ukimalizana na watu wako, geuka uje huku... leo leo. Unanielewa?" akaniambia hivyo.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Yes madam."
Nilikuwa namwangalia kwa njia ile ya uvutio, kimakusudi tu yaani, naye akasema, "Unaangalia nini?"
"Si ulivyo karembo! Halafu katamu!" nikamwambia hivyo kizembe.
Akatabasamu kiasi na kusonya kidogo, kisha akaugeuzia mwili wake upande mwingine wa kitanda na kufungua droo la kitanda, huku mie nikitabasamu tu kichokozi. Akatoa kitu fulani na kisha kujirudisha upande wangu tena, na kiganja chake kilikuwa kimeshika manoti ya elfu kumi kama yote. Akaanza kuhesabu moja baada ya nyingine taratibu tu, huku nikitembeza kiganja changu kwenye mguu wake polepole mpaka kufikia pajani, kisha akazielekeza pesa hizo kwangu kama kusema chukua.
"Hii ya nini?" nikamuuliza.
"Nauli," akasema hivyo.
"Laki moja? Umeshasahau kwamba tayari unanidai laki nyingine? Ndo' unaniongezea mkopo wakati bado kazi sijaanza?" nikamwambia hivyo.
Akawa ananiangalia macho yenye upendezi, ikionyesha kwamba alikuwa ameanza kuvutiwa na mimi.
Nikaipokea pesa hiyo na kusema, "Sijui hata kanatoa wapi haya mahela yote... eti nauli."
Akacheka kidogo akiwa amefumba mdomo, naye akasema, "Em' ondoka haraka. Ole wako uchelewe kurudi sasa."
Ha! Bertha akawa amezama!
Nikajinyanyua kutoka hapo kitandani na kuanza kuelekea sehemu yenye kioo na vifaa vyake hapo chumbani, nami nikachukua chanuo ili kutengeneza nywele zangu vizuri, na baada ya hapo nikaenda mpaka mlangoni. Nilipomwangalia madam, nikakuta amelala kwa ule mtindo wa kuegamiza kichwa kwenye kiganja kilichonyanyuliwa kwa kiwiko chake kitandani, huku akilalia ubavu wake na miguu kuipishanisha na kubinua kalio lake kisawasawa.
Najua alitaka nimpe sifa kidogo, hivyo nikasimama usawa wa mlango na kuendelea kumwangalia tu, naye akawa ananiangalia kwa yale macho ya kimalaya na kisha kulitandika shavu moja la kalio lake kofi la nguvu, nami nikaigiza kuuzuia mtambo wangu usinyanyuke kwa kuukandamizia upande mmoja; kitu kilichofanya acheke kimadaha na kulamba midomo yake. Kimalaya kabisa.
Nikamtolea ishara kuonyesha kwamba ngoja niwahi kwenda ili nikirudi ndiyo nije kumkarabati vizuri, kisha ndiyo nikatoka hapo na kuondoka. Maisha yangu haya! Na hapo ilikuwa bado.
★★
Nikaingia mwendoni kurejea Mbagala. Kwa masaa machache niliyokuwa nimetumia pamoja na madam Bertha ilionekana ni kama nilikuwa nimepasahau huku kabisa kutokana na vitu vingi ambavyo mwanamke yule alikuwa ameniambia kuhusu maisha yake, na bila kusahau mechi ya kiadui niliyocheza pamoja naye.
Sisemi kwamba hakuna mwanamke ambaye amewahi kukataa kutoka na mimi kimwili kabla, ila kuna kiwango kikubwa cha imani nilichokuwa nacho kwamba mwanamke huyo alinitamani pia kwa muda fulani sasa ingawa mwanzoni alionyesha kutopendezwa nami.
Kwa kuwa nilifanikiwa kuelewa zaidi sasa nia kuu nyuma ya mauaji ya Joy, nikawa nimepanga kuongea na askari Ramadhan ili nimweleweshe kuhusu suala zima, pia kuhusiana na kilichotokea alipopiga simu muda mfupi nyuma na Bertha akamtolea nje kwa maneno makali.
Nikamwandikia ujumbe mrefu kiasi ili kumwelewesha nilikuwa na nani, taarifa mpya kuhusu maendeleo ya "upelelezi" wangu, na kumwomba aniambie siku ambayo aliona ingefaa kukutana, kisha nikamsihi anijibu kwa ujumbe maana nilitaka kuzima simu yangu, ndiyo baada ya hapo kweli nikaizima.
Nilikuwa najaribu kuhakikisha nakuwa salama endapo ikiwa Bertha angefatilia simu yangu kwa njia yake ajuayo mwenyewe. Si unajua nilikuwa hadi nimepewa na laki kabisa kama nauli ya kwenda Mabibo na kurejea kwake tena? Najua tu angejaribu kufatilia, kwa hiyo kuzima simu ingekuwa na faida moja kama siyo nyingine.
Nikawa nimefika Rangi Tatu hatimaye, mida ikiwa ni ya saa kumi na moja jioni, nami nikashuka na kuanza kutembea kwa mwendo mfupi mpaka kufikia sehemu ambayo ningechukua daladala za kwenda Mzinga. Nilikuwa nikipita kwenye njia yenye shughuli na biashara za wapambanaji, kama kawaida kusikosekane wauzaji na wapita njia walionitazama kwa uangalifu, lakini akili yangu ilikuwa mbele tu zaidi kujali sana macho ya walioniangalia au waliokuwa bize.
Ndipo nilipokuwa nimekaribia kulifikia jengo la ghorofa la Amazon College, nikahisi mkono wangu ukivutwa nyuma kiasi na mtu ambaye nilikuwa nimepishana naye lakini sikuwa nimekazia uangalifu kwake, nami nikageuka kukuta ni mwanamke. Kwa sekunde chache nilibaki nikimwangalia kwa mkazo kutokana na mwonekano wake kumfanya aonekane kama mgeni kwangu, lakini nikatambua upesi kwamba ndiyo, ilikuwa ni yule Khadija, mke wake Joshua.
Wazungu husema 'well, what do you know?' Kile ambacho hujatazamia kitokee ndiyo kinatokea, na kinakuwa ni kitu chenye faida. Mwanamke huyu angekuwa hiyo faida.
Alionekana tofauti kabisa wakati huu, akiwa amevaa T-shirt nyeusi yenye mikono mifupi ambayo ilichomekwa ndani ya suruali ya jeans ya samawati iliyobana sana umbo lake la chini, pamoja na viatu vya kuchuchumia vyenye rangi ya kahawia. Nafikiri ni miwani yake ya urembo machoni hasa ndiyo iliyofanya nisimtambue upesi mwanzoni, lakini akawa amefahamika kwangu bila hata kuitoa.
"Mambo?" akanisalimu namna hiyo.
Nikaachia tabasamu hafifu na kuangalia kifuani kwake, na hapo ningeweza kuona namna ambavyo matiti yake yalizitunisha chukuchuku mpaka kuchoreka kwenye T-shirt lake, nami nikasogea pembeni pamoja naye ili kuacha nafasi kwa ajili ya wapita njia.
"Poa tu. Niaje?" nikamwambia hivyo kistaarabu.
"Safi. Huonekani," akasema hivyo.
"Umenitafuta wapi ukanikosa?" nikamuuliza.
"Sijakuona leo pale kwa Miryam. Nilienda," akasema hivyo.
"Ahaa... sawa. Mizunguko, si unajua? Ila nipo. Umedamshi. Wapi hiyo?" nikamuuliza.
"Ahahah... asante. Niko namsindikiza rafiki yangu Kariakoo mara moja," akasema hivyo huku akinionyesha huyo mwenzake.
Alikuwa ni mwanamke kijana, na baada ya kumwona akiwa amesimama mbele zaidi kwa kusubiri, nikasema, "Okay, sawa. Me ndo' narudi kitaa. Tutaonana lini tena?"
"Wewe tu," akasema hivyo.
Nikatulia nikimwangalia kwa macho yenye uchokozi kidogo, naye akatabasamu na kuangalia chini. Si ile kukumbuka tulivyokuwa tunachezeana ile majuzi kwenye nyumba ya watu mpaka mume wake mnafiki akatushtukiza? Yaani hii kitu kuicheza ilikuwa na utata mwingi sana kwangu, basi tu.
Nikamwambia, "Sawa. Chukua namba yangu. Uni-text halafu nitakucheki badae."
"Poa," akajibu hivyo.
Hapo hapo fasta nikampa namba, huku tukiwa tunaangaliwa na yule rafiki yake, kisha Khadija akaanza kuelekea kwa mwenziye. Alikuwa na kalio huyu mwanamke!
Najua alichokuwa anakitaka kwangu ilikuwa kuonyesha ufundi wake kwenye kuchepuka mbele ya mwanaume mwenye mwonekano mzuri, ikionekana alikuwa na akili zile zile kama za mume wake, isipokuwa tu huyu alipenda zaidi kukitoa nje; na labda alifikiri nina hela mno. Nilikuwa na lengo maalumu kumsogeza karibu zaidi na mimi japo ni yeye ndiye aliyekuwa amenirushia kamba ya kunivuta kwake. Muda tu ndiyo ungeonyesha ikiwa wazo langu lingefanikiwa ama la.
Nikapanda gari na moja kwa moja kwenda Mzinga. Nilikuwa nahisi kuchoka-choka tu nafikiri hasa shauri ya mechi niliyocheza na Bertha, na hata sikuwa nimeoga nilipotoka huko kwake kwa hiyo nikaamua kupanda bodaboda ili niwahi kufika kwa Ankia, kisha nijimwagie halafu ndiyo niende kuonana na Bi Zawadi.
Nikafika hapo maskani na kumlipa boda, kisha nikataka kuelekea kwa Ankia. Lakini, nilipoangalia upande wa mbele zaidi kutokea kwenye geti lao Bi Zawadi, nikaona gari ambalo lilitambulika upesi sana kwangu likiwa limeegeshwa, nami nikapatwa na hisia za hofu kiasi. Niliwaza kwamba bila shaka mwenye nalo angekuwa huko ndani, na kilichonitia hofu ni kutojua alikuwa hapa kwa dhumuni gani.
Ile hisi ya kutenda kwa uharaka ikaniingia, nami nikaelekea mpaka getini kwao Tesha na kufungua mlango mdogo wa geti kisha kuingia, nisijali tena kuhusu suala la kwenda kujimwagia. Gari la Miryam halikuwepo hapo, kwa hiyo nikaenda mpaka kufikia mlangoni na kuufungua kana kwamba ilikuwa naingia kwangu, nami nikakuta kweli; kile nilichofikiria ndicho kilichokuwa hapo.
Bi Zawadi pamoja na Bi Jamila walikuwa wamekaa kwenye sofa lao, wakiwa wananiangalia kwa umakini sasa baada ya mie kuingia ndani humo upesi sana, na kwenye sofa lingine alikuwa amekaa mtu niliyetegemea kumkuta, Mr Festus mwenyewe, a.k.a Festo.
Hakuwa hata ameangalia upande niliosimama baada ya mimi kuingia namna hiyo, kisha ndiyo akageuka taratibu na kuniangalia machoni. Nilikuwa namtazama kwa umakini sana, nisijue ameleta jambo gani kwenye nyumba hii ghafla namna hiyo, naye akaachia tabasamu hafifu huku akiniangalia kwa umakini pia.
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Full Story WhatsApp or inbox
Whatsapp +255 678 017 280