The Legacy
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 5,879
- 11,318
Tony kamla BerthaTony kawa kivuruge simtak tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tony kamla BerthaTony kawa kivuruge simtak tena
Eiii mamaa na simulizi tutaikosa sasa Tonny masikio yake hayasikii akisikia vibesi ila akisikia sauti tamu ya kwako atapost tu hata kama yuko kwenye mwendokasiTony kawa kivuruge simtak tena
Ni story inayotouch halafu mpangilio wa matukio uko vzur ndo Mana nmeulizaKwa nn umeuliza hivyo rafik yangu?
Ndo nimetoka mizururo, Bertha huko😂Tony kawa kivuruge simtak tena
Sikuzote ili story iweze kutouch ni muhim iwe na vitu vinavyoipa uhalisia hata kama ni fiction. Kwa hiyo unakuta mwandishi ataandika na Mambo ambayo yeye mwenyew ameona ama kupitia, ili we ukisoma uhisi kile anachotaka uhisi kama yeye tu. Najiongelea mimi yeah 😂.Ni story inayotouch halafu mpangilio wa matukio uko vzur ndo Mana nmeuliza
Kama Vini Jr 😂😂Eiii mamaa na simulizi tutaikosa sasa Tonny masikio yake hayasikii akisikia vibesi ila akisikia sauti tamu ya kwako atapost tu hata kama yuko kwenye mwendokasi
Na akiliwa ataacha hizo mbwembwe zake maana inaonekana ana ugwadu wa siku nyingi huyo mdadaHaya bwana mimi Ndio niko siti ya mbele kila siku,Amebaki Mimi kuliwa.
Akili zenu nyie kama za tesha tuNa akiliwa ataacha hizo mbwembwe zake maana inaonekana ana ugwadu wa siku nyingi huyo mdada
Mkuu wanawake wakitaka hiyo kitu wanakuja na mood ya makasiriko sijui wakoje yaani, kwa hiyo huyo mimi akipata ile kitu safi kama aliyopata madam Bertha atatulia tuliAkili zenu nyie kama za tesha tu
Kabisa yan..nataman hako kasehemu..tena ajipeleke yeye mwenyew kwenye mnyaduoNa akiliwa ataacha hizo mbwembwe zake maana inaonekana ana ugwadu wa siku nyingi huyo mdada
Basi nitajikaza nimwiteEiii mamaa na simulizi tutaikosa sasa Tonny masikio yake hayasikii akisikia vibesi ila akisikia sauti tamu ya kwako atapost tu hata kama yuko kwenye mwendokasi
Nmelia sanaaaaaaNdo nimetoka mizururo, Bertha huko[emoji23]
Bertha Ana show tam sana sikufikiria.Nmelia sanaaaaaa
Akili anazo na shoo tamu anayo.Bertha Ana show tam sana sikufikiria.
Front seatMIMI NA MIMI
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI
★★★★★★★★★★★★★★★
"JC..."
Bi Zawadi kuniita kukanifanya niache kumtazama Festo na kuwaangalia wanawake kwa pamoja.
"Naam mama, shikamooni?" nikawasalimu upesi.
Wote wakaitikia, naye Bi Jamila akasema, "Karibu... ila... vipi, mbona kama umetoka kukimbizwa baba?"
Wengine wakatabasamu kidogo, nami nikiwa naanza kuelekea sofani nikasema, "Ah... si mrembo wangu kanipigia akasema niwahi kuja kuwatembelea, ndiyo maana nikakanyaga mafuta haswa."
Mama wakubwa wakacheka kidogo, nami nikamwangalia Festo, aliyekuwa amekaa hapo kwa utulivu tu.
"Vipi kaka?" nikamwambia hivyo huku nikikaa.
Festo akanitazama na kusema, "Safi tu. Habari yako?"
"Ni poa," nikamjibu.
"Huyu ndiyo daktari wake Mariam tuliyekuwa tunamwongelea," Bi Jamila akamwambia hivyo Festo.
"Ahaa... sawa," Festo akasema hivyo.
Nilikuwa nahisi kuwekwa utatani kiasi maana sikujua ni yapi yaliyokuwa yamesemwa na wanawake hao kumwelekea huyu jamaa, nasi tukatazamana kwa yale macho ya kujuana japo haikuwa wazi kwa mama wakubwa.
"JC, unamkumbuka Festo?" Bi Zawadi akaniuliza hivyo.
"Aaa... eeh, namkumbuka. Mara ya kwanza tumekutana ilikuwa ule usiku nimefika hapa kwa mara ya kwanza," nikasema hivyo.
"Eeeh," akasema hivyo Bi Zawadi.
"Yeah, hata me ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza... lakini sijakusahau," Festo akasema hivyo.
Mama wakubwa wakacheka kidogo kuineemesha hali ya kirafiki kwa sehemu hii, nami nikalazimisha tabasamu pia huku moyoni kukiwa na jambo zito.
Bi Zawadi akaniambia, "JC, nakuomba uje mara moja... umwangalie Mamu."
"Okay, sawa," nikaitikia mwito wake.
Tukasimama kwa pamoja, Bi Zawadi akimwambia Festo kuwa tunarudi ndani ya muda mfupi, naye akaanza kuniongoza kuelekea chumbani. Lakini ilikuwa ni chumbani kwa Tesha na siyo kwenye vyumba vyao wanawake, nami nikawa nimeelewa nia yake. Baada ya kuingia ndani humo, upesi Bi Zawadi akanigeukia huku akitabasamu kiasi kama vile kwa wasiwasi, nami nikarudishia mlango na kumtazama kwa umakini usoni.
"JC baba, kwanza samahani maana nimesema tunaenda kumwona Mariam lakini..."
"Usijali, ninaelewa. Hukutaka mgeni ajue tuna maongezi private, umetumia akili," nikamwambia hivyo kwa upole.
"Ahah... asante," akasema hivyo.
"Mariam?"
"Amelala... muda siyo mrefu sana. Anapenda usingizi wa jioni kama unavyojua," akajibu hivyo.
"Okay. Aa... huyu, Festo... amefika hapa muda?" nikamuuliza.
"Hapana, siyo sana. Huyo mwanaume inaonekana bado anamfatilia Miryam... alimpenda," akasema hivyo.
"Ahah... naona ndiyo," nikasema.
"Eeeh, sasa hivi ni marafiki navyoona. Amekuja kusalimia, na tunajua bado ana matumaini ya kuwa mkwe wetu," akaniambia hivyo kwa sauti ya chini.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Sawa. Mnaendeleaje lakini?"
"Ndiyo maana nimekuita... njoo, kaa," akasema hivyo huku akikaa kitandani.
Mimi pia nikakaa na kumtazama kwa utulivu.
"JC... wewe ni kijana mzuri sana. Siyo wa sura tu, ila hadi moyo," akasema hivyo.
Nikatoa tabasamu hafifu.
"Umetusaidia sana hasa kuhusiana na Mamu, na hatujawahi kukulipa kwa chochote ingawa unastahili malipo makubwa sana. Utu wako ndiyo uliofanya hata mimi na dada tukuamini mno hadi kukueleza mambo mengi ya familia yetu ambayo hatujaongea na yeyote yule, kwa sababu unaaminika. Sawa?"
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Sasa... jinsi ambavyo mimi na dada, Tesha, na hata Shadya... jinsi ambavyo tunakuamini, ni kitu ambacho kwa matazamio ya haraka tunaweza tukafikiri hata Miryam anacho... kwa hiyo kwa kile kilichotokea baina yako na yeye jana... kinakuwa ni kitu chenye kushtua kwa sababu kinaonyesha kwamba hakuamini... mpaka kuamua... kukufokea... kukupiga kofi, kusema hataki akuone hapa, yaani... Miryam kufanya hivyo... huwa ni ngumu sana. Hebu fikiria, pamoja na yote ambayo Joshua amefanya, yote mabaya kamsamehe, sasa hivi anajirudi tena hapa... lakini wewe umekuwa ni mzuri sana kwetu. Najiuliza, ni kitu gani ambacho unaweza ukawa umemfanya Mimi mpaka kufikia hatua ya kuukatisha msaada unaompa huyu mtoto... Mamu?" akaongea hivyo kwa hisia.
Nikawa nimetazama tu chini kwa kukosa la kusema.
"Sikuoni kuwa... mtu mbaya, JC. Nataka kujua tu kwa nini Miryam akuone kuwa namna hiyo. Tukimsemesha aseme tatizo ni nini, hataki kusema, maana ndiyo alivyo, sikuzote atafanya anachoona kinafaa kwa ajili yetu hata kama tusipoelewa... tunajua tu kwamba anafanya kwa mazuri yetu. Lakini kwa hiki kilichotokea baina yako na yeye JC... sioni njia ya kusema nikae nitulie tu, sisi wote hapa imetuchanganya sana yaani... Mamu hana furaha toka asubuhi, anamuulizia tu JC, 'atakuja saa ngapi?' Natafuta tu amani baba'angu. Nakuomba unieleweshe tu..."
Nikamwangalia usoni kwa ufikirio, nikiwa nawaza kumwambia upande fulani wa kisa changu na Miryam bila kuhusisha mambo mengi ambayo yangemchanganya zaidi mama wa watu. Ni wazi kwamba alitaka tu kujua tatizo lilikuwa wapi, na mimi nilikuwa nataka nihakikishe nahimilisha vyema suala hili.
Nikaanza kumwambia, "Pole mama... kwanza, yaani samahani kwa yale yaliyotokea jana kwa sababu yametokea hapa, na hayajaacha picha nzuri... naelewa. Ila naomba tu ujue kwamba Miryam hana shida... shida iko kwangu mimi..."
"Una maana gani?" akauliza.
"Kukutana kwangu na yeye, mara ya kwanza kabisa... haikuwa ideal, yaani, niseme... mazingira tuliyokutana ndiyo yalifanya anione kuwa mtu tofauti na jinsi ambavyo nyie mnanijua... ndiyo maana hajaweza kuniamini sana kama nyie," nikamwambia hivyo.
"Kukutana? Ile mlipokutana hapa mara ya kwanza, tukafikiri we' ni Festo, ndiyo maana anakuona kama hauaminiki?" akauliza.
"Hapana, siyo hapo. Miryam na mimi tumekutana...."
Kabla sijamaliza kumwelezea, wote tukasikia zile kingili-kingili za geti kutokea kule nje kuashiria kwamba lilikuwa linafunguliwa. Bi Zawadi akanitazama usoni kwa umakini huku akisikilizia sauti hizo, nami nikasikia pia muungurumo wa gari ukivuma kuingia upande wa nyumba hii.
"Eh! Miryam?" Bi Zawadi akasema kwa sauti ya chini.
Nikashusha macho na kutulia tu.
"Mbona kawahi? JC... sikujua kama angerudi mida hii, yaani..."
"Haina shida, usiwaze mama," nikamwambia hivyo kwa upole.
"Labda kawahi shauri ya Festo, labda wamewasiliana..."
"Huenda. Itabidi kutoroka kupitia dirishani asije akanitimua kwa panga," nikatania.
Bi Zawadi akacheka kidogo na kusema, "Hawezi kufanya hivyo bwana. Twende sebuleni, uchachu wa jana utakuwa umeshapungua. Twende baba."
Nikatabasamu tu na kisha kusimama pamoja naye, nikimruhusu atangulie ili tuelekee sebuleni.
Hakukuwa na kitu kilichofanya moyo wangu uwe na amani kwa wakati huu zaidi ya kuona hali nzuri ya kihisia kwa wanawake hawa watu wazima, na ijapokuwa nilijua Miryam asingekuwa mwenye urafiki sana na mimi kwa jinsi tulivyotibuana jana, nilitaka tu kuona itikio lake lingekuwaje kunikuta hapa kwake leo hii tena.
Ile tumefika sebuleni, nikakuta Tesha akiwa ameingia ndani hapo huku dada yake, bibie Miryam, akiwa ndiyo anarudishia mlango baada ya kuingia ndani sasa. Alikuwa amevaa nguo kama gauni refu na pana, lenye rangi ya maziwa (cream) na urembo wa maua ya kijani, na alikuwa amezivalisha nywele zake kilemba cha hiyo nguo juu ya kichwa ila zilionekana wazi kwa nyuma, hereni ndefu za rangi ya dhahabu masikioni, mkoba mweupe mkononi, na tabasamu hafifu usoni kumwelekea Festo; aliyekuwa amekaa sofani akimwangalia kwa shauku kiasi.
Tesha akawa wa kwanza kuniona, naye alikuwa amevaa nguo nzuri kimtoko, ikionekana walikuwa pamoja na dada yake sehemu fulani ama walikutana tu na kurudi pamoja, naye akatabasamu kiasi na kuanza kunielekea nilipokuwa nimesimama.
"Vipi Festo, umefika zamani?" Miryam akamsemesha jamaa huku akivua viatu vyake vyenye mtindo wa ndala nzito, kwenye usawa wa kona ya mlango.
"Siyo zamani sana. Na umeniwahi, yaani ndiyo nilikuwa nataka kupaa sasa hivi," Festo akasema hivyo kirafiki.
"Umekuja na ndege, eh?" Miryam akamuuliza hivyo.
Festo akacheka kidogo.
Tesha akanifikia, naye akagongesha kiganja chake kwenye changu na kusema, "Vipi kaka?"
"Fresh," nikajibu kwa sauti ya chini.
Miryam akaangalia upande wa Bi Zawadi na kumwamkia, ikionekana alikuwa ameshamsalimia Bi Jamila, ndiyo akawa ameniona sasa. Alinitazama kwa njia ya kawaida tu, mimi pia nikiwa namwangalia kwa utulivu, nami nikaamua kujaribu mitambo.
"Za jioni dada?" nikamsalimu hivyo.
Akaacha kuniangalia, naye akasema, "Salama," kisha akaenda kukaa kwenye sofa alilokaa Festo na kuanza kuongea naye. "Vipi, biashara zinakwendaje?"
Wakaendelea na story. Alionekana kutojali uwepo wangu hapo, nao mama wakubwa pamoja na Tesha wakanitazama usoni kwa kuelewa uzito wa hali hiyo. Bi Zawadi bado alikuwa amesimama usawa wa sofa alilokalia Bi Jamila.
Nikamwambia kwa sauti ya chini, "Wacha me nikimbie. Tutaonana tena."
Bi Zawadi akatikisa kichwa kukubali.
"Ulikuwa wapi kaka?" Tesha akauliza.
"Mizunguko," nikamjibu.
"Sawa. Si unaingia kwa Ankia sa'hivi?" Tesha akauliza tena.
"Ee, ndiyo," nikajibu.
"Poa. Nakuja. Usilale," akasema hivyo.
Nikatikisa kichwa kukubali, kisha nikampita na kuanza kuelekea mlangoni. Nikiwa nimeufikia na kuufungua, nikamtazama Festo kwa ufupi, aliyekuwa anamsimulia Miryam jambo fulani lililovuta umakini wa mwanamke huyo, nami nikaona niachane nao tu na kutoka ndani humo. Si nilitaka kuliona itikio la Miryam kunielekea? Nikawa nimeliona.
Mwanamke huyo alikuwa na kahasira fulani hivi kunielekea ambako kweli kabisa kalimfanya asione hatari halisi zilizoelekea kumwangusha, kwa kufikiria mimi ndiyo hatari. Yaani nahisi hako kahasira kake kalichochewa na hisia fulani nyingine kutoka kwa mwanamke huyo, na nisingeweza kujua ni nini tu. Lakini nilikuwa najua kwamba Joshua ni hatari sana kwake, na hata huyo Festo pia, ijapokuwa yeye ilikuwa ni hadithi nyingine.
Bila shaka suala la mwanamke huyo kunikuta hapo tena wakati alinikataza kwenda lingeweza kuzua hata utata mwingi baina yake na mama zake, ila haikuwa na shida sana maana sikuwa na mpango wa kwenda tena hapo. Ikiwa Bi Zawadi angehitaji tuongee zaidi, ningemwita tu hata kwa Ankia ili kuepuka shari yoyote ile kutoka kwa bibie Miryam, na roho iliniuma sana kwa kufikiria namna ambavyo Mariam angeathirika vibaya kutokana na haya yote.
Nikaenda zangu tu kwa Ankia, nami nikamkuta akiwa ametulia tu ndani pamoja na wale marafiki zake wawili vijana, wale wavaa pini puani, isipokuwa tu wakati huu hawakuwa wamevaa hizo pini. Nikawasalimu, Ankia akiwa amefurahia sana kurejea kwangu, nami nikaelekea chumbani na kubadili mavazi na kuvaa nguo nyepesi kwanza, kisha nikaelekea nje ili kujisafisha kwa kuoga. Mwili ulikuwa na joto kali sana.
Niliporudi ndani tena, nikakuta Tesha akiwa hapo tayari, nami nilipoelekea chumbani akawa amenifata pia. Kijana akawa ananisemesha kwa uchangamfu kiasi kuhusu mambo aliyofanya kwa leo na kuuliza ikiwa nilienda pale kwao kumwangalia mdogo wake, nami nikakubali. Akauliza kama nilikuwa na mpango wa kuzungumza na dada yake ili kurejesha amani kati yetu, lakini nikaepuka kumjibu na kumwita Ankia kwanza.
Mwanamke huyo aliitika kwa ile "abeee" utadhani ameitwa na mume wake yaani, na baada ya sekunde chache akawa amekuja hapa chumbani, mimi nikiwa nimeshamaliza kuvaa nguo zingine safi. Akanisifia kwa kung'ara wakati ambao nilikuwa nimeanza kutengeneza nywele zangu vizuri, nami nikamuuliza ikiwa alikuwa huru ili tutoke kwa pamoja.
Akakubali na kuuliza tunaenda wapi, nami nikamwambia twende tu hapo Masai kupiga mbili tatu pamoja na Tesha, na awaambie marafiki zake waje pia kama wangetaka. Akasema hao hawakuwa wa kukataa, tena na hivi walikuwa wametuelewa mimi na Tesha yaani na wenyewe hata wangetoa hela kutununulia bia. Akatoka ili kwenda kujiweka vizuri zaidi kabla hatujaondoka.
Tesha alikuwa ananiangalia kwa njia ya utathmini sana, akiona jinsi ambavyo nilikuwa makini zaidi wakati huu, nami nikamuuliza ikiwa kuna jambo alitaka kusema. Akasema tu nikiwa serious ninatisha kweli, na kuuliza ikiwa labda nilipoondoka leo ile asubuhi nilienda kusaka pesa ambayo ndiyo nilikuwa nimerudi nayo kuja kuwabariki. Nikajitahidi kuacha kukaza sana na kusema mawazo yake ni kweli kabisa, na nilikuwa na mpango wa kuondoka tena baadaye ndiyo maana nikaamua kujiburudisha na marafiki zangu isingekuwa mbaya sana.
Sikuwa nimesahau kwamba dada yake aliniambia niache mazoea na watu wa familia yake, lakini ningefanyaje ikiwa Tesha alikuwa ananifata yeye mwenyewe na kuendelea kunionyesha urafiki? Ningemfukuza? Hapana.
Nilimwambia Miryam jana kwamba hawezi kuendesha kila kitu kwa namna atakayo kwa sababu hana uwezo wa kubeba yote peke yake, na Tesha ilikuwa mojawapo. Ikiwa mwanamke huyo angeendelea kunikasirikia kwa kujua bado namwonyesha mdogo wake na familia yake kwamba nawajali, hiyo ingekuwa ni juu yake, ijapokuwa nami ningepaswa kujitahidi kuweka mipaka kadhaa katika njia yangu ya kushughulika na hawa watu.
Baada ya hapo, jamaa akawa ameomba manukato yangu ajinukshishe kidogo, naye Ankia akaja tena na kusema yupo tayari. Alikuwa amevaa gauni lake lile fupi lenye muundo kama shati, pamoja na suruali ya skinny jeans nyeusi, nasi kwa pamoja tukatoka huku marafiki zake wawili wakiwa tayari kuondoka pamoja nasi. Saa kumi na mbili hiyo.
★★
Basi, tukawa tumeingia Masai na kukaa sehemu yenye nafasi iliyotutoshea sisi wote watano, vinywaji vikaletwa na sisi wote kuanza kunywa. Nilikuwa natumia hela aliyokuwa amenipa Bertha kuwanunulia pombe marafiki zangu hawa, na ukijumuisha na Bobo aliyekuja hapo baada ya muda mfupi, tukawa sita.
Sikuwa nimemwona huyu jamaa muda sasa, na ile juzi tu nilipojikuta nalazimika kulala hotelini kwa Bertha, mmoja wa watu waliokuwa wamenisalimia kwa jumbe ile asubuhi ilikuwa ni yeye, akiwa aliniulizia mchina kutoonekana Masai kuzimua. Ndiyo sasa tukawa tumekutana tena, nami nikamnunulia bia alizopendelea na jamaa kukaa pamoja nasi kuchangamsha meza.
Mpaka inaingia saa tatu usiku, bado tulikuwa hapo, angalau pakiwa pameanza kuchangamka zaidi na watu kuongezeka. Muda mwingi nilikuwa nimetulia, nimetulia tu, nikiwasikiliza wenzangu walipokuwa wanafurahia maongezi zaidi yenye utani hasa kutoka kwa Tesha na Bobo, na mimi nilikuwa naongezea maneno ya hapa na pale kutia chachu ya ucheshi iliyowafurahisha wanawake.
Ilikuwa wazi kwamba wale marafiki zake Ankia walitaka nielekeze fikira zangu kwao, maana pombe ilipoanza kuwaingia, walikuwa wanacheza muziki wakiwa wamekaa huku wananiangalia kwa utongozi na kunionyeshea ishara za njoo, njoo, njoo. Bobo alikuwa amemwelewa mmojawapo na kuniambia mpango wake wa kutaka "kusababisha" ili aweze kuingia naye chumba cha Lodge ya hapo hapo Masai, huku Tesha naye akiwa na shabaha nyingine aliyoiona upande mwingine.
Nafikiri wengi wa watu waliokuwa hapo walidhani Ankia ni mpenzi wangu daima damdam, hasa kutokana na jinsi ambavyo alijiweka karibu nami, kwa hiyo ilikuwa ni kutazamwa sana. Angalau kuwa hapa na kujiweka katika mazingira haya kulifanya nihisi wepesi wa moyo, siyo kulemewa sana na hisia zenye kuvuruga moyo nilizokuwa napambana nazo ndani kwa ndani. Sikuwa nimesahau kuhusu kutakiwa kurudi kwa madam Bertha, lakini nikaona nijiachie tu hapa hapa na mengine yangefuata baadaye.
Inakaribia kufika saa nne usiku ndiyo akawa ameingia mwanamke fulani mwenye mwili huo, na mweupe. Alikuwa amevaa T-shirt jeupe kama tu yale ya kiofisi ama taasisi-taasisi na matamisemi, na suruali ya skinny nyeusi iliyoonyesha nyama zake zinakaaje ndani ya nguo za kubana. Alikuwa amevaa wigi jeusi na fupi kichwani, na ndala nzuri tu za kike miguuni.
Kwa kumwangalia tu upesi nikatambua huyu alikuwa ndiyo moja kati ya ile "mishangazi" yenye hela hela, na alikuwa pamoja na wanawake wengine wawili waliovaa magauni mafupi yaliyoacha mipaja yao wazi, kope za bandia machoni, wenye maumbo na makalio manene, pamoja na jamaa mweupe na mrefu mwenye ndevu nyingi aliyevaa kibishoo, na ndiyo akawaongoza kwenda upande mwingine ili waweze kukaa. Walitoa ujumbe wa kuwa kama wa kishua yaani, na walitazamwa sana pia.
Ankia alikuwa amenionyeshea hao wanawake, eti niangalie hayo makalio, nami nikacheka tu kidogo na kuendelea kutulia. Huo upande waliokaa ulikuwa mbali kutokea kwetu, lakini kwa jinsi walivyokuwa wamekaa, huyo jamaa na huyo mwanamke wangeweza kututazama moja kwa moja, japo kulikuwa na kaugiza kalikowaficha kwa sehemu hiyo. Bobo alikuwa ni wa kutoka na kurudi tena, hasa kwa kuwa alihusika na uendeshaji wa biashara hapo, kwa hiyo kwa wakati huu hakuwa nasi.
Ni hapa sasa ndiyo nikawa nimeamua kuiwasha simu yangu, kwa kuwa sikuona haja tena ya kuiacha ikiwa imezimika maana ilikuwa wazi kwamba nisingekwenda kwa Bertha. Ningetoa tu kisingizio, maana kwenda huko tena ingemaanisha kupigishwa zoezi hatari, na mimi nilikuwa nimechoka. Kama kukasirika angekasirika tu, ila ndiyo ingekuwa hivyo. Baada ya kuwasha simu, ikanibidi nitulie kwanza ili kuruhusu iingize taarifa zote zilizokuwa zimetumwa wakati ikiwa imezimilka.
Nilipotazama kule walipokuwa wamekaa wale waja wapya, nikakuta yule mshangazi akiwa anaangalia upande wangu, nami nikamkazia macho. Alikuwa mkubwa, mtu mzima yaani wa miaka arobaini na kitu huko, lakini kutokana na jinsi alivyokuwa ananitazama ilionekana wazi kwamba alikuwa amenielewa, na huenda alipenda vijana wenye umri mdogo.
Akawa ananitazama kwa kuibia, yaani anajifanya kama vile siyo umakini wake wote upo kwangu kwa kuangalia pande zingine, lakini angerudi tu tena kuniangalia na kukuta nimemkazia jicho. Ankia na Tesha wakawa wameelewa ishu hiyo na kila mmoja kuniambia wazo lake; mwanamke akisema limama linanitaka ila nilipuuzie tu, na jamaa akiniambia likija kwenye kona yangu nilibamize tu. Nikawa wa kutabasamu tu na kupotezea, nami nikarudisha umakini wangu kwenye simu.
Jumbe kadhaa zilikuwa zimeingia; Bertha akiwa ametuma mbili kuuliza kwa nini sipatikani na ikiwa nimeghairi kwenda, namba ngeni ikiwa imetuma salamu na kumtambulisha mwenye nayo kuwa yule Khadija, ujumbe kutoka kwa askari Ramadhani akisema kwamba itakuwa vizuri tukikutana kesho, jumbe kadhaa kutoka marafiki zangu wengine, na hatimaye, jumbe za salamu kutoka kwa Soraya na yule mwanamke mwislamu aliyeitwa Ibtisam.
Hao wanawake wawili walinifanya nitabasamu tu, maana ni katika pindi ambazo sikuwa nikiwafikiria ndiyo walikuwa wanatokea, na Soraya ilikuwa imepita muda, ila nikaamua tu kuendelea kuwaweka benchi kwanza.
Nikaanza kumjibu Bertha, nikimwambia kwamba ile shida niliyokuwa nimeenda kutatua ilinila muda na pia simu ilikuwa imenizimikia njiani, kwa hiyo ningejitahidi kufika kwake mapema kesho endapo kama ingekuwa sawa kwake. Nikahamisha upande wa sms na kuweka kwa askari Ramadhani, nikijibu kuwa sawa, tutaongea kesho tukikutana, na ile tu nataka kumjibu Khadija, Bobo akawa amerejea hapo mezani.
Kwa wakati huu, Tesha alikuwa bize kuongea na mmoja wa wale marafiki zake Ankia, wakiwa wamezoeana vyema kwa nguvu ya pombe, na mwingine alikuwa anacheza muziki wakiwa wamekaa na kuonyesheana na Ankia. Bobo alipofika na kukaa, akanisogelea kwa ule mtindo wa kutaka kuninong'oneza, nami nikasitisha kutuma ujumbe kwa Khadija na kuweka umakini wangu vizuri ili niweze kumsikiliza jamaa kwanza.
Lakini kabla hajaongea, akanionyesha ishara kwa kidole kumwelekea Ankia, nami nikamwangalia kukuta mwanamke huyo amebinua kalio lake huku akiwa amekaa bado, na akikatika taratibu kwenye kiti huku macho yakiwa yamelegea. Tukaendelea kumwangalia, huku nikitabasamu kiasi, naye alipoona tunamtazama, akaacha na kuanza kucheka kwa furaha pamoja na rafiki yake, akiwa ameshika chupa yake ya bia mkononi. Raha ya pombe hiyo!
Bobo akanisemesha sikioni hatimaye, "Oya, hili lidada linajua, utalilamba lini?"
Nikasogeza mdomo usawa wa sikio lake na kusema, "Kulamba? Nishalitafuna mbona mapema tu!"
"Dah, kweli unapata raha sana kuyakojolea haya mapipa matamu we' fala!"
Nikacheka kidogo pamoja naye.
Ankia alikuwa anatuangalia kwa njia ya kudadisi ikiwa tunamsema, nami nikamrushia busu kwa ishara ya mdomo.
Bobo akaniambia, "Oya, sa' s'kia. Umelicheki lile mazeli limekaa kule na yule jamaa white?"
"Yale matatu kule mbele?" nikamuuliza hivyo bila kuangalia huko.
"Eeh... ila lile limevaa T-shirt nyeupe," akasema hivyo.
"Eeh mwana, na penyewe linanicheki kweli! Toka limefika."
"Linakuelewa... afu' muda sana. Si unalikumbuka?"
"Kumkumbuka? Sijawahi hata kumwona mpaka leo," nikamwambia hivyo.
"Aaa? Sikia, mara ya kwanza kabisa umekuja hapa, kipindi hicho hatujuani bado, sawa?"
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Si unakumbuka kuna mtu alikuwa anawaongozea bia hapa? Mliwekewa bia arobaini kabisa," akaniambia hivyo.
"Eeh... nakumbuka," nikamwambia.
"Ndo' hilo lilikuwa linakununulia," akasema.
"Kumbe? We' umejuaje, kwanza si hukuwepo hiyo siku?"
"Me si unajua meneja kaka? Nilikuwa nimetoa guu, ila niliporudi aliyewahudumia ndo' akaniambia... maana aliwawekea bia mpaka nyingine mkaziacha."
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Anafahamika kitaa kama mama Hanscana, anakaa pale hivi... hii njia ukiwa unaelekea road... pale sijui kama ushaiona ile nyumba yenye geti, kuna ma-V8 mule... kabla hujafikia ile nursery pale mbele..."
"Eeh, napapata. Ndo' mji wake?"
"Ndo' kwake. Mwana... huyu anti anakuelewa sana..." Bobo akasema hivyo.
Nikacheka kidogo.
"Sema haukuwa wa kukaa sana hapa, na yeye yuko hivyo hivyo. Akijaga hapa, huwa tu anawa-bless watu wake, anakunywa, wanasepa. Asa' amekuona leo... muda fulani nilikuwa nimetoka... na yeye akaingia toilet, ile ametoka tukakutana. Ndo' akanipanga. Amenipa namba yake nikupe ili myajenge..." Bobo akanisemesha sikioni namna hiyo.
"Ahahah... Bobo bana! Umefanya bonge la advertisment, amekupa nini?" nikamuuliza hivyo.
Akachomoa noti ya elfu kumi kutoka mfukoni na kunionyeshea kwa chini, naye akasema, "Ndo' maana nakwambia anakuelewa sana. Siku ile bia arobaini, leo kanitoa hii eti kumuungia tu kwako... unapagawisha wanawake wengi fala wewe!"
"Ahahahah... me napenda zaidi wale wanaonifata kabisa siyo mpaka watumie madaraja," nikamwambia hivyo.
"Hamna, anatumia akili. Hii Masai si unaijua? Ana mume huyo halafu hapendagi figisu, kwa hiyo yuko care. Changamka baba, tako la sugar mama hilo!" akasema hivyo huku akipiga mguu wangu kwa msisitizo.
"Ahahah... dah! Umelewa wewe," nikamwambia hivyo.
"Usizingue, me nakutumia digit yake kwa sms. Yuko hapo anazuga tu ila jua mwamba unasubiriwa..."
Bobo akaanza kucheza na simu yake, nami nikawa nimetazama upande wa yule mwanamke.
Alikuwa anakunywa taratibu tu na kuwa bize na wale mashosti zake wengine, kisha kwa mpigo mmoja wa macho akawa amenitazama pia. Hatukuacha kutazamana, na nafikiri alikuwa anatarajia labda nitoe ishara fulani, lakini nikaacha kumwangalia hatimaye baada ya kuhisi mtetemo kwenye simu yangu; ujumbe wa Bobo ukiwa umeingia.
Ankia na wenzake walikuwa wamelewa sasa. Walijiachia, wakicheza muziki kwa kusimama hapo hapo kuungana na watu wengine waliokuwa wakiserebuka kule penye uwazi uliojaa watu zaidi kwa wakati huu. Vibe lilikuwa juu.
Nikamuuliza Bobo, "Kwa hiyo huyo jamaa ndiyo mume wa huyo mwanamke?"
Akashusha chupa ya bia kutoka mdomoni na kusema, "Hamna, huyo ni shemeji yake tu. Mume wake hata sijawahi kumwona anakuja hapa."
"Inawezekana na shemeji anakula hapo," nikamwambia.
"Wapi! Huyo bwege hana hela... yule demu alovaa brown, ni mdogo wake na huyo anti, ye' ndo mke wake..."
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Mazeli ndo' anawatoa hao, wako broke kama kuzimu," akasema hivyo.
"Unavyomsifia utadhani ushaiona. Me siwezi kula kama ni ya kizee," nikamwambia hivyo.
Akacheka na kusema, "Ndiyo ukafunue sasa uone. Ukikuta ni zile za kumeza kichwa chote cha mtoto we' kimbia tu..."
Akanifanya nicheke kidogo, kisha kweli nikaamua kumtumia huyo mwanamke ujumbe mfupi wa salamu. Nilihisi kulewa, maana na mimi nilikuwa nashusha bia nyingi, kwa hiyo ubongo na macho yalikuwa mazito kiasi na ndiyo maana mpaka nilikuwa nasindikiza maongezi yetu na Bobo kama sina akili yaani.
Kidogo tu na ujumbe ukawa umeingia kutoka kwa huyo mwanamke, akiwa amejibu salamu yangu na kuuliza ikiwa niko poa, nami nikamwomba aniambie jina lake. Akasema anaitwa Rukia, naye akaomba kujua langu pia. Nikamtumia ujumbe kumwambia anifate mpaka upande wa VIP ili aweze kujua naitwa nani, na kwa kuelewa hiyo lugha akawa amejibu 'sawa.'
Nilikuwa nahisi namna ambavyo wenge la pombe kichwani lilikuwa likiwekea wingu zito njia yangu bora ya kufikiria mambo mengi vizuri na hivyo kuiruhusu iongoze matendo yangu kwa njia hii ya kujiachia, isiyo ya busara yaani. Mimi sikuwa wa kulewa mpaka kuanza kuyumba nikitembea, lakini hata kama ningelewa kiasi cha kuweza kufikia hatua kama hiyo, bado nilikuwa na uwezo wa kujiongoza vizuri ili nitembee bila kuyumba, kwa midundo ya kujiamini tu. Ndiyo ilivyokuwa hata kwa mara mbili nilizoenda chooni mida fulani nyuma.
Kwa hiyo na sasa nikasimama, nikihisi vibe linanivuta hatari maana nilikuwa nimeweka bia saba tumboni tayari, nami nikaanza kuondoka hapo nikielekea pande za vyoo. Sikuwaangalia wale wanawake wala yule jamaa wakati nilipopita usawa wao lakini nilijua wote walikuwa wananitazama, na kabla sijafikia vyoo nikawa nimevutwa na jamaa mmoja aliyekuwa amelewa, akitaka kunisalimia na kuanza kunisifia-sifia jinsi ambavyo mwonekano wangu ni mzuri.
Nikiwa bado nimesimama naye, yule mwanamke, Rukia, akawa amenipita na kuelekea vyoo vya wanawake, wanaume wengine wakiwa wamejaribu kumchokoza lakini akiwapuuzia, nami nikamwambia huyo jamaa anisubiri nikakojoe kwanza halafu ningerudi. Nikamwacha na kwenda kweli kutoa haja ndogo, ndefu kinoma, kisha ndiyo nikatoka.
Lakini sikutoka mpaka kukiacha choo kabisa, nikisimama usawa wa kuta ndogo iliyokikinga kuelekea upande wa choo cha wanawake kupitilizia mpaka njia iliyoelekea VIP, nami nikawa nimemwona "shuga mami" akiwa anaelekea huko taratibu. Nikapiga hatua chache kuvuka vyoo na kuingia upande huo, nami nikasogea mpaka usawa aliokuwa amesimama sasa karibu na kamba zilizoanikiwa nguo chache.
Nikalishika kiunoni kutokea nyuma, nalo likageuka na kunitazama usoni huku likitabasamu kiasi. Kwa ukaribu huu ndiyo niliweza kuona namna lilivyokuwa na weupe ulioling'arisha vizuri usoni kuufanya uwe wenye kuvutia, yaani kwa ile kawaida ya matunzo mazuri wanayojua kujipa wanawake wa aina yake.
Natumia "li" kwa sababu lilikuwa na mwili tepetepe ingawa siyo kama kibonge, makalio yakiwa manene na kuchoreka vizuri mno kwenye skinny liliyovaa, na kifua kikiwa kimetuna kwa ujazo wa maana hapo mbele, na macho yake yakiwa lege kiasi shauri ya kunywa. Halafu lilikuwa linanukia vizuri sana.
Bila kusema lolote, nikamshika mkono na kumvuta mpaka kufikia ukuta uliotenganisha upande huu na kule tulikotoka, nyuma kidogo ya VIP kuelekea kule kwenye geti la nyuma ya jengo hilo, ambako hakukuwa na watu, nami nikaegamia ukuta na kumvuta karibu zaidi na mwili wangu. Hakuwa mzembe maana alipitisha mikono yake kiunoni kwangu na kuukandamizia mwili wake mbele yangu, huku akiniangalia usoni kwa macho yaliyopiga kelele ya "nataka."
Sawa nilikuwa nimesusia kwenda kwa Bertha kwa kutaka kuiepuka shughuli, lakini hapa, nilikuwa nataka nifanye ujinga. Basi tu yaani, pombe na huyu mwanamke vikawa vimeiamsha mood hata ingawa mwanzoni nilihisi kuchoka, na tayari nilikuwa nimeshaamka.
Mule VIP kulikuwa na watu, nami nikaona siyo mbaya nikimtekenya huyu shuga kidogo hapa kisha tupange hata kutimka, maana alikuwa anaonyesha amenielewa sana bila hata maneno kusemwa, na pia sikutaka figisu za Masai zituandame ikitokea bwege mmoja akawa ametuona.
Alikuwa na midomo minene huyu mwanamke, mashavu makubwa pia, nami nikiwa naongozwa vizuri kwa tamaa ya mwili nikaanza kuinyonya midomo hiyo. Piga denda haswa. Ilikuwa kama vile tunapeana ladha za pombe kwa mate yetu, nami nikawa nalivuta-vuta kalio lake kwa viganja vyangu huku nikiwa nimesimamisha mtambo ndani ya suruali mpaka ukatia maumivu shauri ya mwanamke huyo kuegemea mwilini kwangu.
Inaonekana lilikuwa limekolea mahabani maana lilianza kunipapasa sehemu ya siri kuihisi vyema, lakini nikakatisha busu yetu na kulitazama machoni. Uso wake ulikuwa umelegea.
Nikamwambia, "Hapa jau. Tutafute kitanda."
Akafumba macho na kufumbua kwa kurembua, naye akauliza, "Nilipie room?"
"Hamna, hapa Masai siyo. Tukaingie room location 'ingine... ama unasemaje?"
"Mmm... poa. Nipeleke popote unapotaka... nitalipia," akasema hivyo, sauti ikilegea pia kilevi.
"Tukutane nje..." nikamwambia hivyo.
"Poa. Hujaniambia unaitwa nani lakini..." akasema hivyo.
"Niite JC," nikasema hivyo.
"JC. Nataka leo niimbe jina lako... nikupe mapenzi usiku mpaka kukucha..." akaniambia hivyo kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Twende tukaonyeshane sasa."
Akaniachia taratibu huku macho yake yakiwa kwangu kwa matamanio ya hali ya juu yaani, nami nikawa nahisi kiburi kiasi kuona namna alivyokuwa amepagawika. Hakuonekana kuwa na baya, na mimi nilikuwa nataka tu kula hii nyama nyingine huku pombe ikiwa kichwani, basi, mengine yangefuata baadaye. Yaani ndiyo uliokuwa mpango mzima kutokea hapo.
Kwa hiyo nikawa nafikiria kumwambia atangulie kule tulikotoka kisha mimi ningekwenda huko kwa kupitia huku nyuma, yaani nizungukie kule mbele ili kuepuka macho na midomo ya wafitini, lakini ndiyo hapo akawa ameingia mwanaume fulani kijana aliyekuwa amevaa sweta la kijani, suruali nyeusi, na kofia kichwani.
Alikuwa ameingia kupitia geti la nyuma pale na kuanza kuja upande wetu, lakini akasimama umbali mfupi kutoka hapo tulipokuwa na kuniangalia kama vile alitaka kunisemesha. Nikamtazama kwa umakini.
"Vipi kaka?" akanisemesha hivyo.
"Fresh," nikajibu kwa sauti makini.
"Sorry, naomba kuongea na wewe, mara moja tu," akasema hivyo.
Nikaendelea kumpa utizami makini sana, nami nikamtazama Rukia pia, ambaye alikuwa akinitazama kwa macho yenye utulivu lakini wa pombe.
"Dakika zero tu kaka, hapa hapa," huyo jamaa akasema hivyo.
Ijapokuwa sikumjua, sikuona noma kumkubalia maana hata hivyo nilikuwa na mpango wa kwenda kutokea kwenye geti hilo hilo, kwa hiyo nikamwambia Rukia, "Tangulia. Me napitia huku, halafu tutatekstiana..."
Akatikisa kichwa kukubali, naye akaelekea upande tulioingia nao pande hii.
Nikatoka hapo na kumwelekea jamaa, na nilipomfikia karibu ilikuwa ni usawa wa meza za kuchezea pool upande wetu wa pembeni, zikiwa wazi na bila nafsi nyingine zaidi ya sisi wawili kuonekana, nami nikamwangalia jamaa usoni. Alikuwa wa rika langu, mweusi, na wakati huu alikuwa ananitazama kwa umakini kiasi.
"Nambie," nikamsemesha namna hiyo.
Akasema, "Eti ushawahi kuona hii?"
Alisema hivyo huku akivuta sweta lake juu kiasi kufunua bastola aliyokuwa ameficha, nami nikamwangalia usoni kwa umakini.
Akaitoa kabisa na kuishika kiganjani kwake kwa chini akiielekezea kwangu, chuma chenyewe kabisa, naye akasema, "Usijibu. Najua ushawahi kuona hii, na unajua kazi yake, kwa hiyo kama hutaki kazi yake ifanyikie tumboni kwako, toka nje hapo... sasa hivi."
Eh!
Nilibaki nikimwangalia kwa macho yenye mkazo sana, kwa sababu alikuwa amenishtukiza sana kwa wakati ambao sikudhani ingekuwa rahisi kushtuka. Mwanaume huyu alikuwa nani? Sikumfahamu, kwa hiyo ni wazi kwamba alikuwa ametumwa, na hivyo cha muhimu kujiuliza ingekuwa ni kwamba alikuwa ametumwa na nani?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Full Story WhatsApp or inbox
Whatsapp +255 678 017 280