Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Ukimya ukaendelea kuijaza sehemu hiyo ya sebule kana kwamba hakukuwa na watu, maana mimi na Festo tuliendelea kuangaliana na kisha kubadilishana macho na bibie Miryam pia, ikiwa kama vile sote tunasubiri mmoja wetu ndiyo aseme kitu fulani. Na Miryam ndiye akaona avunje hali hiyo yenye utata.

"Karibu Festo," akamwambia hivyo na kutoa tabasamu nililoona lilikuwa la kujilazimisha.

Festo akatabasamu kiasi na kusema, "Asante. Nimefikia pazuri leo, mambo yako moto."

Miryam akatabasamu kiasi pia na kuangalia chini.

"Nani anazaliwa?" Festo akamuuliza hivyo.

"Ni mama," Miryam akamjibu.

"Oh, ni nzuri... sema sikuwa nimepata mwaliko, ningekuja kwa utayari ahah..." Festo akasema hivyo.

"Haina shida. Tayari umeshafika," Miryam akamwambia hivyo.

Jamaa akatabasamu tu, na yeye Miryam akawa ameweka uso ulioonyesha hisia za uajabu-ajabu tu.

Festo akanitazama na kusema, "Habari yako?"

"Safi. Karibu," nikasema hivyo kiutulivu.

"Asante," akaniambia hivyo, huku akikaza macho yake kwangu kama kunipa maana fulani ambayo sikuielewa, ila kama ananiambia 'ondoka.'

Nikamtazama Miryam, yeye akiwa anasogelea sofa ili akae, nami nikasema, "Miryam, me naenda."

Miryam akasitisha kuketi kwanza na kunitazama tu usoni.

"Nitarudi baadaye kidogo, ngoja nikupishe we' na mgeni," nikamwambia hivyo.

Miryam akatikisa kichwa kukubali na kutazama pembeni tena, bado akionekana kutatizika yaani, naye akamwambia Festo, "Karibu ukae Festo."

Nikamtazama Festo, naye akakaa kwa raha zote pamoja na bibie hapo sofani kwa kilichoonekana kuwa maongezi ambayo yangeenda vizuri baina yao, nami nikaamua kujiondokea hapo tu kama sina maana yaani. Kumwona jamaa hapa kulikuwa kumenizidishia hisia mbaya zaidi ya ile iliyokuwa imeniingia muda mfupi nyuma, lakini sikutaka kujiumiza mno kwa kuwaza juu yake, sema ni ile tu kujua kuhusu mambo mengi kumwelekea ndiyo kuliipa akili yangu mkereketo kiasi ulioendelea... yaani kunikereketa. Ilikuwa nje ya uwezo.

Nikafika ndani kwa Ankia na kukaa tu sofani, nikijaribu kujituliza kiakili na kihisia, lakini fikira zikawa zinalazimisha niwaze kuhusu nini ambacho mwanaume huyo angekuwa amekuja kuzungumza na bibie. Maana hakuwa amealikwa. Hata kale kahisia ka wivu kalikuwepo kabisa, nikitamani nirudi huko kujipitisha tu ili nijue ama nione yaliyoendelea, lakini huo ungekuwa ni upuuzi kwangu.

Nikaona tu nifanye mambo mengine ili kupisha muda kwanza, na jambo la mwanzo ikawa kuchukua simu yangu na kumpigia mama.

★★

Baada ya dakika kadhaa za kuongea na mzazi wangu, nikaona ni busara nikiingia bafuni kujimwagia kidogo, shauri tu ya kuhisi joto mno. Katika maongezi niliyofanya na mama nilikuwa nimemjulisha kwamba kesho ndiyo ningekwenda huko nyumbani ili kumsalimia, na ningeambatana na Mariam pamoja na kaka yake. Kwa hilo mama akakubali, na bila shaka angejiandaa kutupokea vizuri maana alikuwa mpenda wageni sana.

Nilipotoka bafuni na kurudi ndani nikakuta Ankia akiwa amerejea hapa kwake tayari. Tena alikuwa pamoja na rafiki yake mwingine aliyetoka naye huko Mzinga, mwanamke mtu mzima kama mama Chande tu aliyependeza kweli kwa namna ambavyo alivaa, nami nikawasalimu vizuri na kwenda kuvaa nguo safi na kujiweka vizuri zaidi. Katikati ya muda huo Ankia pia akawa ameenda kuoga ili ajiandae vizuri kwenda kwa kina Miryam.

Mimi nilipomaliza kujiweka fresh nikarudi tu kukaa sebuleni pamoja na huyo rafiki yake Ankia, akiwa anamsubiri mwenziye amalize kujiandaa. Haikuchukua dakika nyingi sana nasi tukaanza kusikia muziki mnene ukipigwa kutokea hapo kwa kina Miryam, na Ankia akatoka chumbani huku akiwa anacheza taratibu na kuja kunielekea. Nikawa namwangalia tu kwa umakini, naye akaja mpaka nilipokaa na kumwonyeshea rafiki yake jinsi ambavyo alikuwa na ukaribu nami kwa kutikisa kalio lake karibu na mapaja yangu.

Wanawake hawa wakacheka kidogo, nami nikaendelea kutulia tu kama vile sitaki yaani. Ndiyo Ankia akaniuliza ikiwa alikuwa amependeza, na alivalia kawaida tu; gauni fupi la kitenge, yaani fupi sana, na miguuni ndiyo alivaa suruali nyeusi ya skinny iliyobana umbo lake tenteme vizuri mno. Nikamwambia yuko poa, na yeye akaniasa tuelekee hapo kwa Miryam maana mida ya kupachangamsha ndiyo ilikuwa hii, lakini nikamwambia atangulie tu kwanza.

Ilikuwa imeshaingia saa kumi kuelekea saa kumi na moja. Ankia na mwenzake wakaondoka haraka huku akiniambia nisikawie kwenda, nami nikakubali. Alikuwa amekosa kufika mapema kusaidiana na wenzao kutengeneza nini na nini, ndiyo maana alitaka kuwahi hapo kwa ajili ya mengine yaliyokuwa yamebaki. Mimi bado nilikuwa nafikiria kuhusu Festo, sijui kama bado alikuwepo ama la, na sikutaka kwenda tena yaani mpaka niwe na uhakika ikiwa ningekwenda na kumkuta ama kutomkuta.

Siyo kwamba niliogopa. Ni ile tu kuwa na utayari wa kiakili kushughulika na hali tata kama hiyo ndiyo nilichokuwa nahitaji. Naona bado jamaa alikuwa akininyima amani sana kichwani, hata kama ningempuuzia vipi, kuwa kwake huru tu na kuendeleza ukaribu na Miryam japo alikuwa amekataliwa ni mambo yaliyonitatiza sana kichwani. Ni kama vile pamoja na yote niliyokuwa nimefanya, bado jamaa alikuwa amenishinda kwa asilimia kubwa, kwa hiyo ningeendelea kumwona kama mshindani wangu mkuu zaidi aliyebaki haijalishi alikuwa ameniambia nini kuhusu yeye kutaka kubadilika.

Inaonekana shamra hapo nje ilizidi kupanda, maana sauti za watu wakifurahia zilizidi kuongezeka. Nikiwa nimetulia tu, Tesha akanipigia simu kuuliza nilikuwa wapi, mbona siendi wakati watu walikuwa wameanza kuongezeka, nami nikamwambia nilikuwa nimetulia kwanza ila ningefika tu hapo kwao si muda mrefu sana. Akasisitiza niende, kwamba Bi Zawadi alikuwa amesharudi, na yule Doris alikuwa amefika pia pamoja na Dina. Akaniambia mambo yalikuwa yameanza kuiva, na mimi tu ndiye niliyekuwa nimebaki kufika hapo ili yapakuliwe.

Dina pia akaanza kunitumia jumbe za kuuliza mbona sitokei huko, lakini sikujibu hata moja. Yaani nikaendelea tu kukaa sofani kama mtu aliyeishiwa raha, ama labda ungesema walikuwa wamenifukuza. Nilikuwa natamani ninyanyuke tu niende, lakini miguu ikawa kama imeng'ang'ania sakafu la hapo ndani. Nikaanza hadi kujiona kama mtoto aliyezira kula bila sababu yoyote, tena kwenye siku ambayo mapilau na makuku ndiyo yalipikwa sasa, ila haikuchukua muda mrefu sana kwa hilo kuweza kubadilika.

Tesha akawa amekuja hapa kabisa, pamoja na Bobo, wakifikiri kwamba kuna kitu kilikuwa kinanisumbua yaani labda niliumwa, ila nikawaambia nilikuwa poa tu sema kuna jambo lilinivuruga kidogo. Tesha alikuwa mwepesi kunielewa, na bila kumhusisha Bobo, akawa ameniambia kwamba "yule" jamaa alikuwa ameshaondoka, akimaanisha Festo, kwa sababu nadhani aliona kwamba uwepo wa Festo pale kwao ndiyo uliofanya nikaamua kujiweka pembeni.

Taarifa hiyo ilinipa ahueni kidogo ingawa haikuwa sababu pekee iliyofanya niendelee kujichimbia huku kwa muda huo wote, maana hata kama Festo angekuwa hajaondoka bado, nisingeahirisha kabisa kwenda kusherehekea na Bi Zawadi. Kwa hiyo baada ya wana kuwa wameniomba tukajumuike huko, nikajiweka vizuri tena, kisha kwa pamoja tukaenda. Na sasa saa moja ilikuwa inavizia kuingia.

★★

Ile tumeingia tu hapo getini kwao Tesha, nikakuta watu wakiwa wengi-wengi, wadada wale sanasana waliopendelea kuvaa madera wakiwa kwa huku nje pamoja na wanaume vijana, na hapo varandani kulikuwa na ile meza yao Tesha ya dining, kiti kimoja ambacho alikalia rafiki mwingine wa Bobo, huku spika ya muziki ikiwa imewekwa kwa hapo juu ikishusha muziki mnene. Jamaa alikuwa ameunganisha tu simu yake kwa Bluetooth ya sabufa yao wakina Tesha, ambayo ndiyo iliungwa kwenye spika hiyo ili muziki uliotoka kwenye simu yake udundie hapo.

Milango yote ilikuwa wazi, mapazia pia yaliachanishwa ili ndani paonekane vizuri, nasi tukaelekea mpaka hapo ndani. Bobo akabaki nje hapo kwa mwenzake kwa ufupi, na sisi tulipoingia tukawakuta wenyeji na wageni wakiwa wamekaa sebuleni pamoja na watoto wengi wa majirani wa mtaani waliokuwa wamekaa kwenye uwazi ulioachwa pale sehemu ya dining.

Yaani sebule ilipanuliwa kwa kulisogeza pembeni sofa lililoukinga upande huo wa dining, kwa hiyo palionekana kama ukumbi mdogo uliopambwa kwa njia nyeupe na nyekundu, pamoja na watu waliopendeza pia. Baada tu ya mimi kuingia, mama Chande akatoa kama sauti za shangwe kunielekea mimi na wakina Tesha, na mashosti zake waliotufahamu wakaiga. Hizo ndiyo shobo nilizokuwa sifagilii, basi tu. Tesha naye akaanza kuongea kama MC fulani hivi kwa kusema mwarabu na mchina wa kitaa nimefika.

Nikawa nimetuliza tu hisia nikionekana kuchukulia hayo kuwa kawaida, na umakini wangu ukavutwa na Doris, Dina, pamoja na wanawake wengine wawili watu wazima waliokuwa wamekaa pamoja nao. Doris aliniangalia kwa shauku ya kirafiki, na mimi nikamfata hapo na kumsalimia kirafiki pia. Alifanya hadi kusimama na kunikumbatia, na Dina naye akafanya hivyo hivyo, kisha ndiyo wakawa wamenitambulisha kwa mwanamke mmojawapo hapo kuwa mama yao mzazi.

Nikamsalimu pia kwa heshima, huyu akiwa kama vile mama mdogo wake Miryam maana ndiye aliyekua pamoja na marehemu mama yake, na alionekana kuwa aina ya mwanamke aliyependa kuhukumu vitu yaani, kwa kumwangalia tu, saikolojia ya kidaktari ikawa imeniambia hivyo. Kwa hiyo nikaona niachane naye na kwenda kumsalimu Bi Jamila pamoja Ankia, waliokuwa hapo sebuleni pia.

Yaani hii sehemu yote ilionekana kubanana kabisa kutokana na jinsi palivyojaa watu, hapo chini watoto walikaa huku wakinywa juice na biskuti walizopewa, kule jikoni kukiwa na wanawake baadhi walioshughulika na msosi na kuja tena sebuleni, na sikuwa nimemwona Mariam, Bi Zawadi, wala Miryam; bila shaka wakiwa huko chumbani. Inaonekana Tesha alikuwa anataka kumkaribisha mama mkubwa wake kiaina, kwa hiyo akaelekea huko chumbani kama kuwashtua, kisha akarejea akiwa pamoja na Miryam. Ah!

Malkia wa moyo wangu alikuwa amevalia kwa njia ya kawaida tu, lakini alipendeza sana. Sikuwahi kumwona akiwa amevaa nguo yenye rangi ya maroon, na kiukweli hili gauni alilolokuwa amevaa sasa lilimfanya atamanishe mno macho na hisia zangu. Yaani alikuwa kama chakula ambacho hakikuwahi kuguswa, kumwangalia tu kulinisahaulisha shida zote za kichwani maana alinifanya nifikiri ni mimi tu ndiye niliyepaswa kuja kula hicho chakula!

Bibie mwenyewe akawa anajitahidi kuwatendea watu vizuri tu hapo, na inaonekana wakati niko kule kwa Ankia walikuwa wameleta na makreti kama matatu ya bia, bila shaka likiwa ni wazo la Tesha na Bobo, lakini yaliwekwa tu huko chumbani kwa Tesha na hakukuwa na wengine waliokunywa bia taratibu isipokuwa mama yake Doris, rafiki yake, Doris mwenyewe, Ankia, mama Chande, na wanawake wengineo hapo. Najua Miryam asingekunywa, kwa hiyo Ankia aliponipa ofa ya kufata moja ili nipoze koo, nikawa nimekataa. Leo ningeenda kwa mabiti ya bibie.

★★

Baada ya dakika kadhaa, Bi Zawadi, Shadya, na Mariam wakawa wametoka huko chumbani, kwa pamoja wakija sebuleni taaratibu kama vile mwanamke huyo alikuwa kimwanaharusi. Alipendeza kweli kwa kuvaa gauni refu jekundu lenye mistari myeupe hapa na pale, likiwa na muundo kama wa batiki, lakini ikiwa ni kitambaa kizito tu, na mtindo wa nywele za rasta zilizobanwa juu ya kichwa ulimpendezesha hata zaidi.

Alionekana vizuri sana, yaani alipendeza mno, na najua Shadya ndiye aliyekuwa amehusika kumpendezesha namna hiyo yeye na Mariam pia. Binti alivalia gauni la blue-bahari lisilo refu sana, na alikuwa amesuka nywele za kizungu za mawimbi zenye rangi ya brown, huku mbele ya mwanzo wa nywele zake akivaa tiara nyeupe. Walipendeza kama vile wasingekuja kupendeza tena!

Tukaanza na kuwapigia makofi, Tesha akiendelea kufanya u-MC kuwakaribisha na kumtambulisha Bi Zawadi kuwa kama "birthday girl," na Miryam alikuwa akichukua video kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya mambo mengi yaliyotokea hapa. Haikuwa ajabu kwangu kutambua kuwa wanawake waliokuwepo hapo, hasa ambao hawakunifahamu, walionyesha kuvutwa zaidi na uwepo wangu, wakinitazama sana na hata mara nyingine kusimama karibu nami nilipokuwa nimetulia tu kuwaangalia wapendwa wangu.

Lakini sikujishughulisha nao. Yaani nilitulia. Nilitulia kweli. Dina alikuwa akinitumia jumbe fupi kwenye simu na kutarajia tufanye ile kuchat ya kisiri, lakini nikampiga chini kama vile simjali. Yaani mpaka wakina Ankia, Bobo, mama Chande walinifuata kuniuliza vipi, mbona sichangamki bwana, na mimi nikawa natabasamu tu kwa kuwa niliamua kuitathmini kwanza furaha ya wote niliokuwa nawapenda sehemu hii. Hasa Miryam.

Kila mara nilipomwona akitabasamu pale wengine walipokuwa wakiburudika aidha kwa muziki, ama utani wa Tesha, nilihisi amani zaidi ya vile ambavyo nilikuwa kabla ya Festo kuja hapa muda ule. Ikawa wazi zaidi kwangu kuwa hiki ndiyo kitu nilichokuwa nahitaji zaidi ili kuepuka kujishusha moyo kisa huyo jamaa, na haingejalisha tena alikuja hapa kuongea na Miryam kuhusu nini; nisingeacha kuendelea kumwonyesha mwanamke huyo upendo wangu kamwe.

Kila mara ambayo Miryam angetazama upande wangu na kukuta namwangalia tu, angeacha kutabasamu na kufanya aidha shughuli nyingine ama kwenda jikoni, au wapi, akiwa bado analazimisha kuniepuka eti. Nikawa najikuta natabasamu mwenyewe tu kwa sababu hali hii nilikuwa nimeshaanza kuizoea, na ilifurahisha, kwa sababu najua ingeendelea kunizidishia motisha ya mbio zangu za kuufikia moyo wake mpaka kuukamata. Na matumaini ya kuwa pamoja naye bado yalikuwa chanya, kwa hiyo nisingekata tamaa.

Sherehe ikaendelea. Nikapata na juice ya embe ambayo nilimiminiwa na bibie mwenyewe kwenye glasi, na alifanya hivyo mbele yangu kama hataki yaani. Kwa muda huu nilikuwa nimeamua kutulia ndiyo, lakini jambo fulani likafanya niamue kwamba kuchangamka zaidi ingefaa, hasa kwa ajili yake Miryam. Kuna mara ambazo nilikuwa nikimwona mama yake Doris alipokuwa akimtazama Miryam, yaani, alimwangalia kwa njia isiyo rafiki. Miryam angepita hapo mara kwa mara na kusemeshana pamoja na watu wengine kirafiki, hata Doris pia, lakini huyo mama alimwangalia vibaya tu kana kwamba walikuwa na ugomvi.

Mpaka ikafikia hatua nikaona Miryam alipotaka kumwongezea kinywaji, mwanamke huyo akakataa, lakini Shadya alipotaka kumwongezea kinywaji hicho hicho, akakubali. Wengine hawakuwa wakitambua jambo hili, lakini niliona likimnyima Miryam amani kiasi. Huyo mwanamke alitakiwa kuwa kama mzazi kwake pia maana alikuwa na uhusiano wa karibu pamoja na marehemu mama yao wakina Miryam, sasa sijui alikuwa na shida gani mpaka akaona amtendee bibie namna hiyo.

Ikafika muda wa kukata keki sasa, nayo ikaletwa na kuwekwa hapo mezani, lakini haikufunguliwa kwanza. Yaani ilikuwa ndani ya kifaa kama boksi lakini lenye muundo mzito kama ubao, au hizi bodi za dari zinavyokuwaga ngumu (ceiling board), likiwa jeupe na lenye kishikio kwa juu ambacho kikivutwa ndiyo lote linafunguka na kuiachia keki iwe wazi.

Ikiwa imewekwa hapo, Tesha akasema, "Sawa sawa. Sasa... unajua... birthday girl wetu hapa anatimiza miaka 62, na amezaliwa kwenye tarahe 11 ya leo hii, mwezi wa 11 huu, na mwaka wa 61 ule. Lakini hebu mchekini kwanza! Sura na mwanya uoneokanao kama vile binti mbichi mbichi ambaye bado yuko kwenye miaka ishirini vile!"

Tesha akampamba Bi Zawadi namna hiyo.

Sote kwa pamoja tukacheka kidogo, naye Bi Zawadi akasema kwa maringo, "Jamani, me mwanya nimeutoa woopi..."

Tukafurahishwa zaidi na utani wake wa kuigiza kama mwanadada mdogo, naye Tesha akasema, "Upo kwenye loading huo mwanya, maana leo utakula keki mpaka meno ya mbele yatayeyuka!"

Bi Zawadi akacheka kidogo.

Tesha akasema, "Okay, okay. Sasa... umefika wakati maalumu wa bibi wetu kushika kisu na kuchinja keki. Jamani, fungua keki hiyo... watoto msiangalie nyuma, hakuna yai bovu huko, keki safi hii hapa, kwa hiyo macho yote yawe mbele..."

Ankia alikuwa karibu yake Bi Zawadi, kwa hiyo akamsaidia kukivuta kishikio cha boksi la keki, nayo ikawa imefunguliwa. Kweli ni keki moja nzuri sana ikawa amefunuliwa hapo mezani, ikiwa kubwa, yenye rangi nyeupe kwa nyekundu, ambayo mimi na Tesha tuliagiza ipambiwe na kamdoli ka mwanamke aliyeshika namba 62 wakati ule tumeenda kuitafuta. Vyote vilikuwa ni keki.

Miryam, Doris, Shadya, na wengine baadhi walikuwa wakichukua video kwenye simu zao, huku Ankia akimsaidia Bi Zawadi kuweka flare ndogo juu ya keki (vimshumaa vinavyowakaga kwa kutoa cheche kama fataki vile), tayari kwa kuwasha ili tumwimbie Bi Zawadi wimbo wa 'birthday' kwa pamoja kabla ya kuikata. Huu ndiyo ukawa wakati sahihi wa mimi kuanza kuchangamka.

Tesha akasema, "Sawa, sasa tunawasha hapo, simameni jamani watoto na watu wazima ili tumwimbie birthday girl wimbo wake mtamu sana wa...."

"Tesha, ngoja kwanza," nikamkatisha.

Watu wakaniangalia.

"Enhe, JC ana neno. Leta mambo handsome wa Kijiji..." Tesha akaongea hivyo.

"Ahah... wa kuleta mambo ni Mamu. Ana zawadi special kwa ajili ya birthday girl," nikasema hivyo.

"Wooow! Mamu jamani!" Bi Zawadi akasema hivyo na kuanza kumpigia makofi Mariam, ambaye alikuwa pembeni yake.

Akiwa na tabasamu mwanana usoni, Mariam akaniangalia na kunitikisia kichwa chake kama kuuliza kitu, nami nikamtikisia nyusi kukubali. Akatoka hapo upesi na kwenda chumbani huko kwanza, kisha akarudi akiwa na kile kinanda chake mkononi. Watu wakahisi binti alikuwa amekuja kujaribu kumpigia muziki Bi Zawadi, na hawakukosea. Akakaa kitini na kukunja mguu wake huku kinanda kikiwa katikati, nasi sote tukawa tunamwangalia kwa subira.

Mariam akaanza kupiga kinanda, yeye mwenyewe, akipiga ile midundo iliyotokeza sauti ambayo sote tuliifahamu kuwa ya wimbo maarufu utumiwao kwenye sikukuu za kuzaliwa. Yaani kinanda kilitengeneza melody ya 'happy birthday to you, happy birthday to you,' na hakukosea hata mara moja! Kwa waliokuwa wanafahamu juu ya tatizo alilokuwa nalo, walionekana kushangaa sana. Mama yake Doris akajisogeza mbele zaidi kwenye sofa ili asikilize kwa makini, na Mariam akaendelea kupiga kinanda tu kwa utaalamu wa hali ya juu sana.

Nikamtazama Miryam na kuona jinsi ambavyo alimwangalia mdogo wake kwa hisia sana, kisha akaniangalia usoni kwa umakini. Nikampa tabasamu hafifu huku nikimwangalia kwa hisia, naye akarudisha umakini wake kwa mdogo wake tena. Tesha akaanza kumsifia kweli Mariam na watu hapo kupiga makofi. Ankia akamwambia binti arudie tena kupiga midundo hiyo, halafu watu wote wafatishe na kuanza kumwimbia Bi Zawadi wakati ambao flare ingewashwa ili apulize na kutoa ombi lake kwa Mungu. Ikawa hivyo.

Mariam akaanza tena kupiga kinanda, nasi tukawa tunaimba kwa kufatisha sauti hiyo, na tukipiga makofi pia. Bi Zawadi alionekana kufurahi sana, akiwa amefunika mdomo wake kwa viganja huku akimtazama Mariam kwa hisia, naye Tesha akazidisha mbwembwe za maneno ili wimbo uendelee kuimbwa tu. Ankia akawasha mshumaa wa kwenye keki, huku bado tukiendelea kuimba, na Miryam alikuwa akichukua video tu kwenye simu yake huku akitabasamu kwa furaha sana.

Bi Zawadi akaendelea kuenjoy kwanza muziki aliopigiwa na Mariam kabla ya kuinama na kupuliza mshumaa wa keki kwa nguvu, nasi sote tukampigia makofi na wakina mama Chande kutoa sauti kwa shangwe. Ankia akampatia kisu laini Bi Zawadi ili aanze kukata keki, na mama huyu akajitahidi kukata vizuri vipande vya mwanzo, halafu Ankia akachukua kikopo cha stiki na kuanza kuzichomekea keki kipande kimoja-kimoja.

Bi Zawadi akataka wa kwanza kabisa kumlisha iwe ni Mariam, naye binti akanyanyuka na kwenda kula keki kwa furaha, kisha naye akamlisha mama mkubwa wake na kumkumbatia kwa upendo. Akafata Bi Jamila, kisha Miryam, ambaye alikumbatiwa na Bi Zawadi kwa karibia dakika nzima kabisa. Baada ya hapo akafuata mama yake Doris, Doris mwenyewe, Dina, Tesha, Ankia, Shadya, Bobo, mama Chande, na karibia wote walikuwa na kitu kizuri cha kumpa mama huyu kama zawadi, iwe ni kaelfu kumi, mkufu, kitenge kizuri, ama zingine zilizotiwa ndani ya maboksi, halafu ndiyo nikaja mimi sasa.

Bi Zawadi alikuwa ananiita kwa shauku sana kuwa niende kulishwa naye, nami nikamfikia na kula keki yangu, kisha nikamlisha yake pia. Halafu, nikaingiza mkono mfukoni na kuchomoa wallet yangu iliyokuwa imetuna, nami nikaanza kutoa elfu kumi moja baada ya nyingine. Nilikuwa nazitoa kwa madoido yaani, nikiziachia karibu na kichwa cha Bi Zawadi zimmwagikie tu kama mvua, na wanawake wakawa wanatoa sauti za shangwe kunishabikia yaani.

Bi Zawadi akawa amefumba mdomo huku akicheka kwa aibu, Bi Jamila naye akishangilia eti, nami nikamtazama Miryam kutokea pale alipokuwa amesimama. Aliniangalia kwa jicho makini sana, kama hataki eti, nami nikamtikisia nyusi kiuchokozi, na yeye akazungusha jicho na kuangalia pembeni, kitu ambacho kikanifanya nicheke kidogo na kumalizia kummiminia cheupe wangu pesa ya zawadi. Hapo nilikuwa nimemmwagia laki mbili kamili, wanawake wakiwa wamehesabu na kumshangilia cheupe wangu, naye akanikumbatia kwa furaha sana.

Nikaenda pembeni tena na kusimama karibu yake Mariam zamu hii, na ndiyo watu wengine wakaendelea kulishwa keki, na Tesha kuchangamsha sherehe kama ilivyotakiwa baada ya Bi Zawadi kuokotewa pesa zake na Ankia. Angekuja kujinunulia tuvitu tuzuri mwenyewe ahisi raha hata zaidi, cheupe wangu huyo. Ilikuwa siku yake!

Nilijikuta napenda sana hii kitu. Ilikuwa sherehe ya kawaida tu, mambo yasiwe mengi wala ya gharama za ajabu, lakini ushirika wa hawa watu na jinsi walivyoonyeshana upendo ulipatajirisha sana hapa. Halafu pia nikaanza kuona kwamba mama yake Doris alinifatilia sana baada ya hako kakitendo kangu muda mfupi nyuma, yaani aliniangalia mno mara kwa mara, nafikiri akiwa ameona kitu fulani ndani yangu kilichomfanya agundue mi' wa maana. Chezea!

Mariam akawa amemwomba Bi Zawadi alishwe keki tena, kale kamdoli eti, nasi kwa pamoja tukacheka kidogo. Bi Zawadi akamwita na kumlisha taratibu huku watoto wakimkodolea, halafu na yeye akamwomba Mariam ampigie kinanda kwa mara nyingine tena. Mariam akafurahi kufanya hivyo. Akaanza kumpigia kinanda tena, na watu wakaungana naye kuimba wimbo wa birthday kwa kufatisha sauti. Wakina Ankia na mama Chande walikuwa wameelekea jikoni pamoja na wadada wengine, nafikiri kuweka mambo ya msosi sawa zaidi.

Nikamwangalia Miryam. Alikuwa amesimama pembeni tu, akiwatazama Bi Zawadi na Mariam kwa hisia sana, nami nikasogea upande wake na kusimama karibu naye bila yeye kutambua kwamba nilikuwa nyuma yake. Doris, Dina, na wageni wengine walikuwepo hapo sebuleni pia, na niliona umakini wao ukielekea kwangu mara kwa mara, lakini sikuwajali sana wakati huu.

Nikamwambia Miryam kutokea pembeni, "Hiyo hapo."

Akageuza shingo yake kuelekea upande wangu, lakini hakunitazama kabisa.

Nikasema, "Unakumbuka tulivyoongea siku ile? Kuhusu Mamu?"

Akionekana makini zaidi sasa, akamtazama tena mdogo wake.

"Nilikwambia kuna ishara zingejionyesha Mamu akianza kuwa imara zaidi kiufahamu. Hiyo hapo moja, Miryam. Kumbukumbu yake inazidi kuwa imara. ASD inaondoka hivyo," nikamwambia.

Akaniangalia machoni kwa hisia makini.

Nikampa tabasamu hafifu la uhakikisho, naye akaacha kuniangalia na kumtazama Mariam tena, kisha akashusha pumzi na kunipita kuelekea jikoni bila kusema asante wala nini. Lakini najua kutoka ndani ya moyo wake kwamba alikuwa amefurahi sana kusikia hivyo, ni basi tu eti hakutaka nione hilo moja kwa moja.

Nikajisogeza tu pembeni tena baada ya hapo, na Mariam alipomaliza kupiga kinanda chake, Tesha kama MC akasema, "Haya, umefika wakati wa kuhalalisha rasmi kabisa umri wa bibi wetu mrembo. Mko tayari?"

Wanawake na watoto wakasema 'ndiyoo' bila hata ya kuelewa alichomaanisha, na Tesha aliponiangalia, tukajikuta tunacheka kidogo kwa kuwa ni mimi na yeye tu ndiyo tuliokuwa tunaelewa kilichokuwa karibu kutokea. Miryam akawa amerejea tena. Tesha akaomba kiti ili aweze kupanda usawa huo hapo katikati, na baada ya kufanya hivyo, akayafikia maputo huko juu na kuichukua kwa uangalifu ile kamba iliyobaki mwishoni, kisha ndiyo akashuka. Halafu akamvuta Bi Zawadi usawa wake na kusimama karibu yake.

"Hii ni zawadi nyingine kwa mrembo wetu Zawadi. Makofi kwake na vilegelege kwa kutimiza miaka 62!" Tesha akaongea hivyo kwa shauku.

Watu wakacheka na wakina mama Chande kupiga hivyo "vilegelege," halafu Tesha akaniangalia huku akijikaza asicheke. Nikamtikisia kichwa kama kumwambia aache tu, naye Miryam akaniangalia kwa macho yaliyoonyesha alikuwa ameshashtukia dili. Tesha akaivuta hiyo kamba na kumkimbia mama mkubwa wake ghafla, na yale maputo hapo juu yakaanza kupasuka moja baada ya lingine. Kila moja lililopasuka lilitoa vikaratasi vingi vidogo-vidogo vilivyomeremeta, halafu maputo mawili ya mwisho yakamwaga maji!

Miryam akafunika mdomo wake kwa kiganja. Bi Zawadi alikuwa bado amesimama hapo kati, kwa hiyo hivyo vikaratasi na maji yakawa yamemwagikia. Wakati maputo yalipokuwa yanapasuka na kutoa hivyo vikaratasi, watu walikuwa wanashabikia eeeeh, lakini maji yalipommwagikia Bi Zawadi, wengine wakaonekana kushangaa na kubaki kimya. Tesha akaanza kucheka, Mariam pia, huku Bi Zawadi akiwa amefumba macho, kisha naye akaanza kucheka.

Watu wengine wakaanza kucheka pia, Bi Jamila ndiyo alikufa mbavu yaani, naye Tesha akasema, "Maji ya baraka ya sikukuu ya kuzaliwa! Ulifikiri tungekuacha salama ma' mkubwa?"

Bi Zawadi akasonya kidogo na kusema, "Shenzi wewe!"

Wengine ndiyo wakazidisha vicheko, na maongezi kuhusu hicho kitendo yaanza hapa na pale. Nilikuwa nikijizuia nisicheke, lakini nilipomwona Miryam anatabasamu huku akitikisa kichwa chake, nikashindwa kujizuia tena. Ankia akaja karibu na kunilalia begani huku akicheka, na Doris akawa amemsogelea Miryam kumnon'goneza jambo fulani lililofanya kwa pamoja wacheke kwa furaha sana.

Bi Zawadi alipouliza nani aliweka hayo maputo yenye maji huko juu, mimi na Tesha tukanyoosheana vidole kama kulaumiana, naye Bi Zawadi akatikisa tu kichwa na kuanza kuelekea chumbani ili akajikaushe. Miryam akanikata jicho kali kweli eti kama vile hakupenda, maana alijua ni mimi ndiye niliyekuwa nimeyafunga maputo huko juu, nami nikabana tu tabasamu langu na kuamua kwenda uani kwanza kabla hajanitafuna. Lakini naelewa alikuwa ameburudika sana. Ilikuwa wakati wenye kiburudisha kwa kweli!

DJ Bobo pale varandani akawasha muziki tena. Tukawa tumemwomba Bi Zawadi samahani ya kummwagia maji bila kumwandaa baada ya yeye kurudi tena sebuleni, na alituvuta masikio mimi na Tesha, lakini akasema alikuwa ameburudika sana leo kwa kweli.

Akatushukuru sisi wote kwa kuifanya siku hii iwe murua mno kwake, na akaombea uzima wetu sote ili tuendelee kuwa pamoja kwa mazuri na magumu yote ya maisha. Na alimshukuru mno Miryam kwa kuwatunza wote vizuri kwa upendo, akimwombea mafanikio zaidi kwenye maisha yake. Na huyu mama alikuwa na maneno mazuri sana yaliyogusa hisia, mpaka nikajikuta nampigia makofi na wengine kufanya hivyo pia.

Baada ya hayo ndiyo wanawake wakaanza kusambaza upendo wa misosi kwetu sisi wote. Kwa watoto waliokuwepo, waliketi sehemu ya chini pale dining na kuwekewa kwenye masinia, wanawake wakila pamoja hapo sebuleni, na sisi wanaume tukawa kwa huku varandani tukila na kunywa pia taratibu. Wakina Bobo na Tesha walipiga bia mbili tatu, lakini mie sikunywa hata kidogo. Tesha ndiyo akawa ameniambia kuwa yule mpenzi wake, Happy, alibanwa na kazi hata kwa siku hii, ndiyo maana hakuweza kuja kujiunga nasi leo.

Kwa hiyo muda ukaendelea kusonga tu. Hakukuwa na nafasi ya fujo hapo, kila kitu kilikwenda kwa utulivu na utaratibu mzuri kabisa mpaka sote tulipomaliza kula na kunywa, kisha tukamalizia muda wa masaa machache kwa kuoiga story na nini, na watu wengi waliokuwepo wakawa wanaaga na kurudi makwao.

★★

Ikiwa imeshaingia mida ya saa tano, umati ukawa umepungua, hapo kwa Miryam tukabaki siye tu tuliokuwa na ukaribu zaidi na familia hii, yaani hata wanaume tuliokuwepo ilikuwa mimi, Tesha, Bobo, na jamaa wengine wawili waliokuwa na ukaribu na Tesha. Basi. Kule ndani walikuwepo wanawake, Doris na familia yake wangelala hapa leo, na ili wapate nafasi ya kutoshea ya vyumba, Tesha angekuja kulala pamoja nami pale kwa Ankia, na hata Shadya angelala pamoja na Ankia huku kwake. Haikuwa na noma.

Wakati huu nikawa tu hapa varandani pamoja na Bobo na hao jamaa wawili, muziki ukiwa umeshushwa sauti, na Bobo tayari alikuwa ameshaniambia kwamba alimtokea Ankia kimapenzi, na mwanamke huyo alimkubalia lakini alitaka jambo lao liwe la chini-chini kwanza; wengine wasijue. Zilikuwa ni taarifa nzuri, kujua kwamba Ankia alipata mtu wa kumpenda aliyetaka kutulia naye, nami nikampa pongezi Bobo na kuahidi kutunza siri yake.

Tesha alikuwa ameenda huko ndani ili arudi pamoja na chupa zingine za bia, na hata wakina Doris na Dina hapo sebuleni walikuwa wakinywa huku wanapiga story na Miryam, Bi Zawadi, Ankia na mama Chande. Inaonekana Bi Jamila na Mariam walikuwa vyumbani, na hata mama yake Doris na yule mwanamke waliyekuja naye hawakuwepo sebuleni pia.

Nikiwa nimeegamia tu ukuta huku nakula story za kuchorwa tattoo na nini kutoka kwa hawa wasela, Miryam akawa ametoka ndani na kuja hapo varandani pia, nami nikamwangalia kwa umakini. Akasemeshana na Bobo kiurafiki na kisha kuvaa ndala na kutupita sote kuelekea ule upande wa nyuma ya nyumba uliokuwa na stoo. Inaonekana alitaka kwenda kuchukua kitu fulani huko. Kwa hiyo kwa kuzuga, nikajivuta-vuta tu na kuelekea upande huo pia ili nikajaribu kumchokoza kidogo.

Uzuri hakukuwa na watu wakati huu ambao wangekuja kwa huku maana na sherehe ilikuwa inaelekea kuzimika hapo mbele, na nilipofika huko kwenye chumba cha stoo, nikamkuta bibie akiwa ndiyo anatoka humo na kutaka kurudi tena huku tulikotoka. Lakini akasitisha hatua zake baada ya kuniona nimefika mbele yake, naye akanishusha na kunipandisha kwa mtazamo wa kawaida tu. Ile 'na huyu naye vipi?'

Hakuonekana kuwa amechukua chombo wala kitu chochote kutokea humo stoo, kwa hiyo kwa sauti ya chini nikamuuliza, "Ulikuwa unatafuta nini?"

Akaendelea tu kuniangalia kimkazo kiasi.

Nikatabasamu na kusema kimchezo, "Hakuna kilichokuleta kuchukua, eti? Ulikuwa tu unataka nikufate..."

Bila kunijibu, akageuka tu na kuanza kuelekea huko nyuma zaidi, nadhani ili akapitie kwenye mlango wa huko nyuma ili kuniepuka. Nikatabasamu zaidi na kumwahi ili nimsimamishe kwanza.

"Miryam, sikia... usikimbi...."

Nilikuwa nimeanza kumfata huku nikisema hivyo kwa sauti ya chini sana, na yeye kusimama ghafla ndiyo kukafanya maneno yangu yakatike. Alikuwa amefikia kwenye kile kikona chenye nafasi nyembamba, pale pale ambapo nilimnyuka Dina siku ile, na kutokana na yeye kusimama ghafla yaani ikawa imefanya nikaribie kabisa kumgusa kutokea nyuma, na kabla sijajirudisha, nikatambua upesi kwa nini alisitisha kuelekea mbele zaidi.

"Kumbe?"

"Eeh, zilikuwaga za nondo, sa'hivi naona wameweka na chupa-chupa. Ni vizuri, hapa wezi hawaruki ukuta. Nimekuja sana hapa kipindi cha nyuma..."

Nikasikia sauti mbili za wanawake zikisema maneno hayo kutokea huko nyuma, na upesi nikatambua kwamba moja ilikuwa ni ya mama yake Doris pamoja na yule rafiki yake aliyekuja naye, ndiyo waliokuwa wakiongea hivyo. Inaonekana walikuwa wamekuja kwa huku nyuma ili kupaona, na labda kuzungumza kidogo.

Miryam akageuka na kutaka kurudi tena kwa upande wangu, sijui ili awaepuke, lakini nilikuwa karibu zaidi na yeye kwa hiyo akaishia kuniangalia usoni kwa kutotarajia niwe karibu naye namna hiyo. Kisha ndiyo akaashiria kutaka kunipita kwa kulazimisha mwili wake upite kwa kujibana sana hapo ukutani, na mimi nikajikuta natulia tu na kumwangalia alivyokuwa anahangaika kutaka kupita kwa lazima.

Hii ikafanya nyuso zetu ziwe karibu zaidi, na kwa makusudi nikakaza mwili wangu ili kuzuia yeye asisonge mbele zaidi, yaani abaki hapo hapo. Miryam akanitazama usoni kwa ile njia yake ya kuudhika, akiwa anajua nimemfanyia makusudi kabisa, nami nikajitahidi kubana tabasamu langu na kuamua kulegeza mwili ili apite, mwishowe angenimeza kweli!

Maongezi ya wanawake wale yakaendelea.

"Hivi ni kweli kabisa ulivyosema kuhusu huyo dada?"

"Nikudanganye kwa lipi sasa?"

"Hmm... basi ana lake jambo..."

"Siyo siri, me nakwambia. Na tena... hiyo siyo tangu Maimuna alipofariki tu, wala kwa sababu ya vurugu za Joshua na nini hapo juzi... ni tokea muda sana, mpaka me huwa nashangaa...."

Sauti ya mama yake Doris akisema hivyo ikasikika vizuri sana kwetu, na mkazo uliokuwepo usoni mwake Miryam ukafifia baada ya jambo hilo lililosemwa kuonekana kuteka zaidi umakini wake, na hakuacha kunitazama usoni. Mimi pia nikaendelea kumwangalia Miryam usoni kwa utulivu, nikiwa nimeweka umakini wangu kwake kwa sababu ya jambo hilo.

"Kwani tayari alikuwa ameshakuja huku?"

"A-aah, huku amekuja wazazi wake walipofariki... Maimuna alipofariki nimekwambia," mama Doris akasema hivyo.

"Ahaa, sawa. Eh! Mbona sasa anachelewa jamani? Mwanamke mwenyewe mzuri kweli, shida itakuwa wapi?"

"Ndo' maana nakwambia nashangaa. Tumeshamshauri sana, mimi na Shadya tumeshamtafutia wachumba wenye hela, lakini wote kawakataa. Mwanamke heshima ndoa, kuzaa, uwe na kwako na familia yako... yeye mpaka anataka kuzeeka ndo' aje kushtuka eti! Yaani sijui amekuwaje jamani..." mama Doris akaongea hivyo kwa sauti ya chini.

Ilieleweka kwamba wanawake hao walikuwa wanamwongelea Miryam, naye bibie akashusha macho yake kutazama chini huku akionekana kuanza kuhuzunishwa na jambo hilo. Kwa mara ya kwanza leo nikawa nimetambua kuwa marehemu mama yake na Miryam aliitwa Maimuna, na mama Doris kumsema hivyo bila shaka kulimtia simanzi kuu Miryam. Nikawa namtazama kwa hisia.

"Hakuwaga hivyo? Alikuwa na wanaume?"

"Ndiyo, alikuwaga tena anatoka na mtu wa maana nakwambia. Eti akaachana naye, kisa nini sijui. Sasa hivi amekuwa mfungwa kwa hii familia, Doris ni mdogo kwake lakini anatangulia kuolewa.... nakwambia ataendelea kukaa hivyo hivyo hadi huyu mdogo wake wa kike ataolewa ye' anakodoa tu. Sijui anafikiri atakuja kuazima ndoa ya mtu? Labda kwa sababu tu ya huo uzuri?" mama Doris akasema hivyo.

Miryam akafumba macho yake na kutikisa kichwa taratibu, akionekana kutoamini.

"Usiseme hivyo ila, tusimwombee mabaya. Ni vizuri ametulia, labda uje tu ujaribu tena kuongea naye. Atakusikiliza," rafiki akaongea hivyo.

"Ah, me nilishachoka. Ameshakuwa mtu mzima, tumemjali mno, imetosha. Sa'hivi tunajali hawa makinda waliobaki. Yeye kama kaamua kujilaani eti kisa ameachiwa familia ya kutunza... ni yeye. Atakapokuja kujuta baadaye lakini, atakuwa ameshachelewa. Na amechelewa mno. Yaani hataolewa huyu. Ndoa isimame kabisa? Haipo. Me nakwambia, atabaki kudandia ndoa za watu kama siyo kutumiwa na wanaume ambao watamwacha na mamichango tu..." mama Doris akasema hayo.

Aisee!

Rafiki yake akasikika akisema, "Basi turudi ndani, tukikutwa hapa tunapiga umbea!"

"Ahahahah... siongei kwa ubaya, ni ukweli tu. Tushamshindwa. Loh! Twende tukale tu keki tena..." mama Doris akaongea hivyo.

Inaonekana wanawake hao wakawa wamerudi ndani tena, bila kujua kuwa sehemu ndogo ya maongezi yao kumhusu mwanamke mwenzao ilikuwa imemwachia hisia mbaya na nzito sana maana aliwasikia. Najua Miryam aliumizwa na maneno ya mama yake Doris. Yaani mtu aliyemwona kama mama mdogo ama shangazi yake, ndiye aliyekuwa akimsema namna hiyo kabisa, tena hapa hapa nyumbani kwake? Lazima iliuma.

Miryam akawa bado ameinamisha uso wake kiasi, akionekana kuhuzunishwa na utambuzi wa jambo hilo, nami nikapatwa na hisia ya simanzi kumwona namna hii. Nikaweka tu kiganja changu kimoja usawa wa shavu lake na kuligusa, kisha nikalishika lote kwa njia yenye kumpatia faraja ya bila maneno. Akapandisha macho yake na kunitazama usoni kwa macho yaliyojaa hisia zilizovurigika kiasi, na najua aliweza kuiona hisia yangu ya uelewa wa hali yake ndani ya macho yangu kwa jinsi nilivyomtazama pia.

Nikataka nimwambie kitu chenye kufariji ili asiwazie sana kuhusu maneno ya mama yake Doris, nami nikasema, "Miryam... hayo yote siyo kweli. Sawa? Haujajilaani popote. Hawa hawakujui, hawawezi kuelewa kwa nini una...."

Akaacha kuniangalia na kuweka kiganja chake kwenye kifua changu kama kunizuia nisiendelee, kisha taratibu akautoa mkono wangu kutoka usoni kwake na kuondoka hapo; akielekea kule mbele tulikowaacha wakina Bobo. Nikajihisi vibaya kweli.

Sasa ndiyo ikaeleweka vizuri zaidi kwangu kwa nini mama yake Doris alimtendea Miryam kwa njia fulani ya masengenyo. Lilikuwa tu ni suala la mwanamke huyu kukataa wanaume wengi waliokuwa wametafutwa kwa ajili yake ili aolewe, yaani ile tu kwamba aliwapiga chini ndugu zake katika harakati zao za kujaribu kumshurutisha aolewe. Walikuwa wanataka kumpeleka sana, lakini yeye kuendelea kuwa na msimamo ndiyo kitu kilichowafanya wakerwe naye mno. Si wanaukoo ndiyo huwa wako hivyo?

Kwa sekunde chache nikabaki tu sehemu hiyo nikimfikiria kidogo, maana ilikuwa wazi kwamba alibeba mambo mengi mazito moyoni yaliyomsumbua mno kihisia. Ilikuwa ni vita kwake akiwa kama mwanamke kupambana na jinsi jamii ilivyomchukulia, ingawa najua haikuwa lazima kujali hilo, lakini matokeo ya maamuzi yake yaliathiri kwa njia nzuri au mbaya jinsi ambavyo alionwa na jamii nzima mpaka kufikia kwenye familia yake, na watu aliowajali.

Katika hilo pia, ningetakiwa kumsaidia. Najua nisingeweza kubadili jinsi ambavyo watu walimfikiria, lakini ningeweza kufanya jambo fulani ili kubadili jinsi mambo yalivyokuwa kwake yeye. Hapo mbele naelewa kungekuwa na mengi magumu kwenye uhusiano wangu pamoja naye kuendana na yote yaliyokuwa yakimzunguka, lakini ningehakikisha anaipata heshima aliyokuwa akiistahili kutoka kwa watu wote waliokuwa wameishusha. Na huyo mama yake Doris angeisoma!

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI

★★★★★★★★★★★★★★

Asubuhi ya siku ya Jumapili ikawa imefika. Nilikuja pamoja na Tesha, Ankia, na Shadya hapa hiyo jana baada ya kuondoka kwake Miryam, na nililala pamoja na jamaa chumbani kwangu. Nilipoamka kwenye mida ya saa mbili hiyo, nikamwamsha na Tesha pia, nasi tukakaa kuongea kidogo kuhusiana na sherehe ya jana, hususani kummwagia mama mkubwa wake maji, ndiyo mada ikageukia kwenye suala la sisi na Mariam kutakiwa kwenda kumtembelea mama yangu leo hii.

Tesha alidhani kwamba kwa mama yangu ilikuwa ni huko Sinza, lakini leo ndiyo nikamwambia kwamba nyumbani kwa mama palikuwa ni kule Goba, maeneo waliyoyaita Goba Center. Akauliza ugeni wetu ungetegemewa saa ngapi huko, nami ndiyo nikamwambia ingefaa tukiondoka mapema kabisa ili kufikia saa saba tuwe tumeshafika kule, hivyo muda bora wa kuondoka ungepaswa kuwa kwenye saa nne hivi. Kwa hiyo akaamua kuwahi kutoka hapa ili aende kujiandaa na kumwandaa Mariam pia. Sote tulikuwa na hamu na hii ishu.

Kufikia wakati ambao Tesha aliondoka hapa kwa Ankia, mwenye nyumba wangu pamoja na Shadya walikuwa wameshaamka pia, Shadya akitangulia huko kwao pia, na Ankia ndiyo alikuwa kwenye harakati za kuanza maandalizi ya kiamsha kinywa. Alikuwa amekula pilau na nyama nyingi sana jana, lakini kwa sababu fulani akaamka ana njaa kali. Kwa hiyo ikawa ni yeye kwenda dukani kufata mkate, nami nikaona nifanye usafi wa mwili mapema na kisha kuvaa vizuri kabla ya kwenda kwa Miryam hapo.

Bado nilikuwa natafakari kuhusu mambo niliyotakiwa kuendelea kufanya ili kumvuta Miryam karibu nami zaidi, maana hata usiku wa jana niliweza kuona kwamba sehemu fulani ndani yake ilihitaji mno mtu wa kushiriki naye furaha na huzuni zake, na wonyesho wa huyo mtu kuwa mimi mwenyewe haukuwa mbali sana. Bado alikuwa ananisukuma kutoka karibu naye, lakini hiyo ni kwa sababu tu aliogopa. Na najua aliogopa nini, hivyo ningepaswa kuja kumwonyesha kwamba hangetakiwa kuogopa hata kidogo, maana sikuzote ningekuwa pamoja naye kuhakikisha hilo.

Nikapiga pamba kali, T-shirt na jeans, kiatu cheupe chini, mwonekano mkali mwilini yaani, nami nikanywa chai ndogo tu pamoja na Ankia na kisha kumuaga, nikimpiga mabusu mengi shavuni kutokana na raha tu niliyohisi ya kwenda kumwona mama pamoja na Mariam. Na Ankia alikuwa ananiambia naenda kudeka leo, eti mie mtoto wa mama! Nikaachana naye tu hapo na kwenda moja kwa moja mpaka getini kwa majirani zetu pendwa.

Nilikuta gari la bibie likiwepo hapo nje, na pia kulikuwa na hali nzuri ya usafi, ikionekana ulifanywa mapema, na kabla sijafika huko ndani, akawa ametoka Dina na kusimama hapo varandani. Alikuwa amevaa dera ambalo nilielewa lingekuwa la Mariam, na alishika kimfuko ambacho nadhani kilikuwa na uchafu wa vyombo vilivyokuwa vinaoshwa naye maana mikono yake ilionekana kulowana, tayari kwenda kuwekwa kwenye fuko la uchafu.

Nikamsalimu, naye akaitikia vizuri, kisha nikasimama hapo kumsubiri aende kuutupa uchafu na kurudi, na aliponifikia tena, nikamwambia, "Naona umempa Mamu Gucci yako."

"Ahah... ameniazima tu hii, kulala na nguo inayobana sijazoea," akasema hivyo.

"Ooh, sawa. Kameshaamka?"

"Eeh, wote tuko macho. Mariam anajiandaa, mnaenda kutembea sijui..."

"Yeah, tunatoka," nikamwambia hivyo.

"Haya. Me naenda kumalizia kazi. Karibu ndani," akasema hivyo.

"Ona, Dina..." nikamshika mkononi taratibu.

"Bee?" akaitika.

"Naomba usichukulie vibaya kwa ile jana. Mambo yalikuwa mengi, halafu... pia, kuna kitu kingine nataka nikwambie," nikasema hivyo.

"Usijali JC. Me naelewa," akaniambia hivyo.

"Unaelewa?"

"Kabisa."

"Unaelewa nini?"

"Najua utakuwa na mpenzi wako, JC. Tulifanya tu siku ile kwa sababu nilikuomba... ila nahisi ni kama ulijuta," akasema hivyo.

"Siyo hivyo. Nilifurahi... ila..."

"Haitajirudia tena," akasema hivyo.

"Itakuwa vizuri tukiwa marafiki, kawaida tu. Maana...."

"Wala haina shida, usiwaze. Siyo kwamba labda nilikuwa natarajia tuwe wapenzi, ila kama ungependa hata mara nyingine... tuwe wote... me nakuwa tayari," akasema hivyo.

"Kwa nini sasa? Si una boyfriend?"

"Tuliachana. Na me nilikuwa nakukubali sana, mpaka sasa hivi. Ila naona umeamua kutokuwa msaliti kwa mwenzako, so..." akasema hivyo na kupandisha mabega yake kidogo.

"Usijali Dina. Utapata tu mtu mwingine wa kuwa naye, we' ni mwanamke mzuri sana," nikamwambia hivyo.

Akatabasamu kiasi na kuuliza, "Na me mwanamke?"

"Ee. Unajionaje?"

"A-ah, bado bwana..."

"Unapenda ubinti kisura zaidi eh?"

"Eeh, me bado binti."

"Ahah... haya bwana. Mnavyopendaga tusiwazeeshe!" nikasema hivyo.

Akacheka kidogo kwa shau, naye akasema, "Ndo' bado sijazeeka sasa."

"Hata me naona," nikamwambia hivyo.

"Mpenzi wako yuko wapi? Na ndiyo uko kwenye harakati za kuoa au?"

"Ahahah... kwa nini unauliza hivyo?"

"Well... naona umekuwa serious. Inamaanisha unampenda mwenzangu sana. Tena sa'hivi nisijihesabu kuwa mwenza, na usijali, naelewa. Me niko poa kabisa," akasema hivyo.

Kalikuwa kastaarabu kiutu ila katukutu kwenye mahaba haka!

Nikamwambia, "Asante mwaya. Nitakutafutia bonge la chocolate ule mpaka uvimbewe."

"Ahahaaa... ndiyo pole ya kuikosa ya kwako kuanzia sasa hivi, au?" akauliza hivyo kiutani.

"Ih, we... usiongee hivyo," nikamwambia hivyo kwa njia ya tahadhari, nasi kwa pamoja tukacheka kidogo.

Kutokea hapo mlangoni, Tesha akawa ametoka na kusimama varandani, nasi tukamwangalia usoni kwa pamoja.

"Oya!" jamaa akasema hivyo kama vile amepatwa na saibu.

Nikatabasamu kiasi na kuuliza, "Vipi?"

"Mwana nimesugua meno na huu ulimi mpaka cheche zimetoka, lakini nahisi harufu ya pombe haijakata. Sa' itakuwaje?" akaniambia hivyo.

"Mnaenda wapi kwani?" Dina akauliza.

"Kumsalimia mama yangu," nikamwambia.

"He! Huyu asiende, nenda tu na Mamu. Mama yako anaweza kudhani wote walevi huyu mburula akiwasindikiza," Dina akasema hivyo.

"Afu' wewe! Oya, tuko fiti kwenda, usimsikilize huyu anataka tu kunikosesha bata," Tesha akasema.

"Sa' kama mdomo unanuka pombe ndo' hauji. Mama hapendi," nikamtania.

"Aaaa..." Tesha akajifanya kuhuzunika.

Dina akasema, "Eeeh, hakuna kwenda... kama ni bata atakula Mamu tu."

Kisha akaanza kuelekea ndani na kumsukuma Tesha kidogo, na baada ya yeye kutokomea, Tesha akaniangalia na kunipandishia nyusi kwa njia makini, nami nikaelewa kwamba alikuwa ameyasikia maongezi yangu pamoja na Dina hapo mwishoni, na kuja kwake na hayo maigizo ilikuwa kwa ajili ya kuyakatisha upesi ili mambo mengine yaendelee. Kwa hilo nikawa nimempa tano.

Tayari Tesha alikuwa ameshavalia kwa njia nzuri kwa ajili ya matembezi, kasoro tu viatu, nasi kwa pamoja tukaelekea hapo ndani. Bi Jamila, Bi Zawadi, Shadya, pamoja na Doris, mama yake, pamoja yule rafiki yake, wote walikuwa hapo sebuleni, nami nikasalimiana nao vizuri na kukumbushiana na Bi Zawadi mazuri ya jana yaliyoburudisha sana.

Karibia wote walinisifia kwa kuwa na mwonekano mzuri sana, Bi Jamila na hata Doris wakinitania kuhusu mie kuteka mioyo ya wanawake, nami nikatania kwa kusema tayari nilikuwa nimeshaiteka ya warembo wangu wa hapo, na sikuhitaji kuongeza idadi. Walicheka kwa furaha, na hata mama yake Doris alikuwa akijaribu kutaka kuunda mazoea fulani ya kiutani na mimi, lakini nikawa nampuuzia. Angesema kitu na kutarajia nijibu kwa njia yenye kufurahisha, lakini ningetoa tu jibu la mkato na kuendeleza maongezi na wengine vizuri zaidi.

Sikuwa nimesahau aliyosema kuhusu malkia wa moyo wangu huo usiku wa jana, na nilikuwa na nia ya kuja kuhakikisha nayathibitisha maneno yake kuwa ya kibatili. Yeye na watu wote waliofikiria kama yeye. Kwa dakika chache baada ya mimi kukaa hapo, Mariam ndiyo akaja kutokea chumbani, tena akiwa amevaa lile lile gauni lake jipya alilokuwa amevaa Jana kwenye sherehe, mwonekano wake wa nywele za kizungu ukimfanya apendeze zaidi kwa asubuhi hii, na bibie Miryam akawa amekuja sebuleni pia.

Alikuwa ndani ya ule mwonekano wa nyumbani yaani, kwa kuwa leo ilikuwa Jumapili bila shaka asingekwenda kazini, lakini kwa macho yangu bado niliona kama alipendeza mno. Nikawa namwangalia kwa utulivu tu hadi alipotufikia karibu na kusema Mariam yuko tayari, na binti alikuwa ameshakunywa chai pia, hivyo Tesha akawahi kwenda kuvaa viatu. Miryam alijitahidi sana kutuliza hisia zake kutokana na kile ambacho kilitokea jana, akiwa mkimya tu mwenyewe, na kwa sasa nisingeweza kujaribu uchokozi wowote ule kwa hiyo nikatulia tu.

Mariam akaambiwa ajigeuze ili tumtazame vizuri, naye akafanya hivyo kwa njonjo na kurusha nywele zake kwa kiganja huku akiweka pozi. Wote tulifurahia namna ambavyo Mariam alizidi kuchangamka, na huu ndiyo utu wake halisi uliokuwa umeanza kurudi taratibu. Ingekuwa ni wakati mzuri sana kwake leo kwenda kumtembelea mama maana najua ingemwachia "experience" murua ambayo ingeendelea kumsaidia apone zaidi.

Tesha akawa amerejea kwa utayari wote, nasi ndiyo tukaaga hatimaye ikiwa ni mida ya saa nne na nusu hivi. Kwa mwendo wa kujiamini tukaelekea mpaka Mzinga kuchukua daladala, moja kwa moja mpaka Rangi Tatu, na kisha tukapanda gari iliyoelekea Makumbusho na safari ndefu kuanza.

★★

Tukawa tumefika Makumbusho stendi hatimaye ikiwa imeshaingia saa sita mchana. Nikamwambia Tesha tuelekee sehemu ambayo tungesimama kusubiria gari ambalo lingetufikisha Goba, nasi tukaambatana pamoja mpaka hapo.

Tukiwa tunasubiria nikatambua kuwa Mariam alivutiwa na bisi zenye kuchanganywa rangi, kwa kuwa alizitazama sana pale ambapo kulikuwa na muuzaji, nami nikamuuliza ikiwa alitaka nimfatie. Akatikisa kichwa kukubali na kutabasamu, hivyo nikaenda kumchukulia mfuko mmoja.

Likawa limekuja gari ambalo tungepanda sasa, yaani daladala, nami nikawahisha kuchukua bisi huku nikimwonyesha ishara Tesha kuwa awahi kuingia kwenye hiyo daladala ili kupata nafasi ya kukaa, maana waliivamia watu wengi kiasi. Nikaielekea pia na kuingia, kukuta Tesha na Mariam wakiwa wamekaa, lakini kwa kukosa nafasi ikanibidi nisimame. Nikampatia binti bisi zake, na haikuchukua muda mrefu gari likaanzisha mwendo.

Ulikuwa umepita muda wa wiki kama mbili tatu toka nimekwenda huko nyumbani kumwona mama na Jasmine, kwa hiyo nilikuwa nina hamu ya kuwaona tena hasa nikiwa na marafiki zangu hawa. Hapo Makumbusho hakukukosekana wanawake wazuri kila kona, iwe nje, iwe ndani ya majengo ama barabarani, pote walikuwepo, na ndani ya hii daladala walikuwepo wanawake wawili waliovutia sana kwa sura zao.

Niliona wazi kwamba Tesha alikuwa amevutiwa na mmoja kutokana na kunitumia jumbe kuniambia nimwangalie kila mara na nihakikishe nafanya kitu ili kuondoka na namba yake, lakini nikampiga jamaa chini. Yeye alipenda "kula" bado, na najua alifanya hivi kama sehemu ya kujaribu uaminifu niliokuwa nao kwa upendo wangu kumwelekea dada yake.

Ila hata kama isingekuwa ya Miryam, mimi binafsi sikupenda kujichoresha hata kama ningekuwa nataka kumtokea mtu, isingekuwa kwa namna ambayo rafiki yangu alitaka. Sasa zaidi kwa wakati huu kutokana na hisia zangu kuwa kwa dada yake pekee, hawa wengine niliwaona kuwa wa kawaida mno. Kwa hiyo nikamwambia atulize boli la sivyo ningemwambia Happy ikiwa angejitoa akili kumwomba namba demu yeyote yule. Jamaa akatulia. Nilikuwa nimeshaanza kuizoea hali fulani ya ushemeji kabla hata ya kuwa shemeji rasmi!

Dakika zaidi ya ishirini zikakatika mpaka tulipofika Goba Center hatimaye, nami nikampa ishara Tesha kuwa tushukie hapo. Nilikuwa nimesimama muda wote toka tumeondoka Makumbusho, kwa hiyo baada ya kushuka nikajihisi ahueni. Nikiwa nawasubiria Tesha na Mariam waje niliposimama pembeni ya barabara, nikaamua kuita bodaboda wawili. Wakafika karibu nami baada ya Tesha na Mariam kunikaribia pia.

"Oy, tupelekane hapo mitaa ya Steve Nyerere," nikamwambia hivyo bodaboda mmoja.

Baada ya bodaboda kukubali, Tesha na Mariam wakapanda kwenye moja, mimi nyingine, na safari ikaanza. Tukaiacha Goba Center ya lami na kuingia ya changarawe kuelekea mitaa iliyotunukiwa jina la mtu maarufu aliyeitwa Steve Nyerere, kutokana na nyumba yake maridadi kuwa katika maeneo hayo, nasi tukaipita na kusonga mbele zaidi.

Tulikuwa tukikaribia kufikia kanisa moja kubwa la ibada kwenye eneo hilo, lakini nikamwelekeza boda ashushe usawa wa nyumba moja kabla ya kufika huko. Wote tukashuka, na baada ya bodaboda kuondoka, nikaanza kuielekea nyumba hiyo taratibu nikijua Tesha na Mariam wananifata. Lakini nikageuka na kukuta Tesha amebaki kusimama huku akiitazama nyumba hii kwa umakini, kisha ndiyo akaniangalia.

"Vipi? Twendeni," nikamwambia hivyo.

Tesha akaanza kuja mpaka niliposimama na kusema, "JC, hapa ni wapi?"

"Nyumbani," nikamwambia.

"Eh! Hapa ndiyo kwenu JC?" akauliza eti kama vile haamini.

"Ah... unazingua," nikasema hivyo na kumshika Mariam mkono.

Nikasogea pamoja na binti mpaka kufikia geti la nyumba hiyo, iliyokuwa imezungukwa na uzio wa ukuta mrefu na mweupe, chini pembeni yake kukiwa na bustani ya nje yenye ukoka na miti-maua mizuri iliyotunzwa vyema, nami nikabonyeza kengele hapo ukutani na kusubiri. Tesha akawa ametufikia.

"Kaka, acha masihara basi. Hapa ndiyo kwenu? Tusije tukafukuzwa na mbwa," Tesha akaniambia hivyo.

Nikacheka tu kwa pumzi na kuendelea kusubiri, nalo geti likaanza kutoa sauti kama ya kubipu, halafu likaanza kufunguka lenyewe kuelekea upande mmoja na kusimama baada ya kuacha nafasi iliyotosha mtu kupita. Nikaingia pamoja na Mariam sehemu hiyo, Tesha akifata nyuma, nasi tukawa tumepokelewa kwa salamu nzuri sana na mlinzi aliyekuwa eneo la nje la nyumba hii. Kilichokuwa kimefanya Tesha asiamini kwamba hapa ndiyo maskani ilikuwa kutokana na ukubwa wa hii nyumba.

Ilikuwa kubwa. Sana. Ilikuwa nyeupe, pana, yenye ghorofa lenye vyumba vikubwa pia, na iligawanyika mara mbili, yaani ilikuwa kama vile nyumba ziko mbili lakini sehemu moja. Mazingira ya nje hapo yalipendeza kwa usafi wa hali ya juu, kukiwa na bustani za mimea na miti iliyotunzwa vyema, nyumba ndogo ya mlinzi, eneo pana la nje la kuegeshea magari na lingine la ndani kama gereji, na ardhi yote hapo ilikuwa ya matofali madogo-madogo yaliyopangiliwa kwa ustadi.

Tulipomaliza kusalimiana na mlinzi, nikawaongoza marafiki zangu mpaka kufikia mbele zaidi ya nyumba, nami na ndugu hawa tukalipita bwawa maridadi la kuogelea pembeni zaidi kuelekea malango ya nyumba, lililokuwa na maji safi sana. Kulikuwa na miti-maua mengi ambayo ilipangiliwa vizuri kufanya vivuli viwe vya kutosha. Kufikia mlangoni, hapo nje ilikuwa ni uvaranda mpana ambao uliwekewa masofa upande mmoja na viti na meza upande mwingine kwa ajili ya kupumzikia nje ama kutumia kwa ajili ya mlo, na milango ilikuwa myeupe, mtindo wa chuma laini na vioo virefu katikati kuruhusu kuona sehemu ya ndani.

House 2.jpg

Tukafika hapo varandani, na wanawake wawili waliokuwa wamevalia kwa njia rasmi ya kikazi wakatusogelea kutusalimia kwa heshima, wakiwakaribisha wageni kwa njia nzuri sana, halafu wakaelekea pande zingine kwa ajili ya kazi. Nikamwelekeza Mariam kubonyeza kengele ya mlangoni, naye akafanya hivyo na kutabasamu. Tesha alipendezwa sana baada ya kuona magari mawili aina ya Range Discovery modeli ya 2022 nyeupe,

IMG-20240817-WA0015.jpg
pamoja na BMW X1 new model ya brown,

BMW.jpg

zote zikiwa zimeegeshwa na ziking'aa utadhani ndiyo zimetoka dukani.

Akanishika bega na kuuliza, "Oy, BMW ya nani hiyo?"

Nikaiangalia na kumwambia, "Jasmine."

Akasema, "Dah! Na hiyo Range ya mshua?"

"Mama," nikamwambia.

"Kama mama'ako anatumia hiyo, mzee wako anatumia ipi sa'? Afu' na we' mwanangu una gari, eti? JC una gari?" Tesha akawa anauliza kwa msisitizo.

Nikacheka kidogo tu, na ndiyo mlango ukawa umefunguliwa.

Hapo mbele yetu alikuwa amesimama mwanadada mweusi wa maji ya kunde, rika lake likiendana na rika la Tesha. Alikuwa amesuka nywele fupi na nyembamba za mawimbi-mawimbi kama tambi vile, akiwa amevaa blauzi nyeusi yenye mikono mirefu na yenye kubana sana mwili wake wa juu kukichoresha vyema kifua chake chenye matikitiki maji makubwa. Chini alivaa kikaptura kifupi sana kilichoyaacha mapaja yake manene wazi, naye akatabasamu kwa furaha sana baada ya kuniona.

"Jay!" akasema hivyo kwa sauti tulivu lakini kwa shauku.

Nikatabasamu pia na kusema, "Vipi Nuru?"

Akanifata na kunikumbatia taratibu kwa furaha, kisha akaniachia na kuwaangalia marafiki zangu. Alikuwa anatafuna jojo.

"Tesha, Mariam, huyu ni mdogo wangu, anaitwa Nuru..." nikawaambia.

"Mambo?" Nuru akamsemesha Tesha hivyo.

Tesha akasema, "Poa."

"Mariam ndiyo huyu? Jamani mambo?" Nuru akamsemesha na Mariam pia.

"Poa," Mariam akamjibu huku akiwa amenishikilia mkononi kwa nguvu.

"Karibuni... nakwambia leo mama ameingia jikoni..." Nuru akasema hivyo.

"Usiniambie..." nikasema hivyo na sisi wote tukaingia ndani huku Nuru akiendelea kuzungumza pamoja nasi.

Huyu alikuwa ni mdogo wangu pia, na habari zake zitaeleweka mbeleni. Alikuwa mwanadada mtulivu sana hasa mbele ya watu asiowafahamu. Yaani kwa mtazamo wa kwanza, kila kitu kumhusu kilipiga kelele ya neno "utulivu," lakini kumzoea yeye kama yeye kabisa ungetambua alikuwa mchangamfu, mtundu, na nikisema mtundu namaanisha mtundu haswa. Nadhani karibia kila kitu alikuwa ameshafanya huyu, mtoto wa kishua aliyekuwa yeye, kama unaelewa namaanisha nini.

Upande wa ndani wa hii nyumba ulikuwa maridadi vibaya mno, vitu vingi vikiwa vya gharama na kupangiliwa kwa ustadi, na usafi ulikuwa wa hali ya juu. Tukawa tunaelekea sehemu iliyokuwa na masofa marefu meupe ambayo yaliwekewa mito mingi, huku katikati kukiwa na meza fupi ya kioo yenye bakuli lenye matunda. Kwenye sofa moja, alikaa mwanamke mweupe kama kaka yake hapa, yaani Jasmine. Alikaa kwa njia ya kulala akiwa ameipandisha miguu yake yote sofani, na aliegamia mto huku akitutazama kwa utulivu.

Dada yangu huyu hakuwa mtu wa kurukaruka sana yaani, ile kwamba wageni wamefika ndiyo aanze kutabasamu 'eh jamani karibun...' hamna, hakuwa wa hivyo. Tena sasa hapo ukijumuisha na jinsi tumbo lake lilivyokuwa kubwa mno, ilikuwa sababu tosha ya yeye kuona amepewa mateso kama yote, kwa hiyo muda mwingi alikuwa yupo kama vile hataki tu.

Na pia Jasmine alikuwa mwanamke mkali, yaani mwenye fujo hasa akichokozwa, lakini toka tumezaliwa, hatukuwahi kutendeana kwa ujeuri uliopita kiasi kama ndugu wengine wanavyokuwaga. Tulipendana, na wakati mwingine ingeweza hata kuonekana mimi namzidi umri shauri ya kuwa mtu ambaye nilisuluhisha mengi ya matatizo yake mara nyingi kwa kipindi cha zamani, hivyo aliniheshimu sana.

Tulipofikia upande wake, Tesha, Mariam, na Nuru wakaketi kwenye sofa la pembeni, nami nikamsogelea Jasmine karibu na kumwangalia usoni kwa umakini, na yeye akiniangalia huku akitafuna tunda eti kama vile anaona kinyaa. Nyodo tu yaani zisizoeleweka. Nikaanza kumfanyia mzaha kwa kuigiza kulipima tumbo lake ukubwa nikitumia ishara za vidole kama nalikuza, nalipunguza, halafu natikisa kichwa na kupiga makofi kama kumwambia kazi anayo.

Akasonya kidogo na kusema, "Shenzi wewe!"

Nuru, Tesha, na mimi tukacheka kidogo kwa furaha, kisha nikachuchumaa karibu yake Jasmine na kumpa kumbatio, naye akalipokea kwa mkono mmoja kisha kuniachia.

"Unaendeleaje?" nikamuuliza kistaarabu.

"Ah... kubeba mapacha kazi! Libaba lao lenyewe limekimbia kisa umalaya tu," Jasmine akasema hivyo.

"Jas, hebu acha kuwaza hayo bana. Halafu kuna wageni... manners," nikamwambia hivyo.

Jasmine akatabasamu na kuwaangalia marafiki zangu, naye akasema, "Karibuni jamani."

Tesha akasema, "Asante."

Nikasimama.

"Huyo ndiyo mgonjwa wako?" Jasmine akaniuliza.

"Mariam. Anaitwa Mariam," nikamwambia.

"Ahaa... hujambo Mariam?" Jasmine akamsemesha.

Mariam akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Shikamoo dada?"

"Marahaba. We' mzuri kweli mdogo wangu. Ukipona kafanye u-miss," Jasmine akamwambia hivyo.

Tesha na Nuru wakacheka kidogo.

Wakati huo huo, akawa amekuja mwanamke mwingine mweupe aliyekuwa amevalia nguo nadhifu za kikazi, akiwa ni msaidizi wa kazi za nyumbani, naye alibeba sahani pana sana ya plastiki iliyokuwa na glasi sita zenye juisi iliyoonekana kuwa ya embe, akija nazo taratibu tu mpaka alipoifikia meza na kuziweka hapo. Kisha akaniangalia na kutoa ishara ya kupiga magoti kiasi huku akitabasamu, nami nikatabasamu pia.

"Imelda, uko poa?" nikamsemesha.

"Niko poa. Karibuni jamani," Imelda akasema hivyo kuwakaribisha na wageni.

Tesha akatoa shukrani, kisha Imelda akaanza kuwapatia wote hapo glasi moja moja yenye juice.

Aliponipatia yangu, nikamuuliza, "Mama?"

"Yupo jikoni," Imelda akajibu.

"Jay, kaa utusimulie mambo ya huko Mbagala. Sijawahi kufika. Hata dada hajawahi," Nuru akasema hivyo kwa sauti tulivu.

Nikamwambia, "Sawa, ngoja nimwone mama kwanza. Nakuja. Tesha wape hawa ubuyu wa Mbagala kidogo."

Tesha akatabasamu kiasi.

Nikawapa ishara Tesha na Mariam kuwa ninarejea muda si mrefu, nami nikaelekea upande wa jikoni pamoja na Imelda akiwa na sahani yake pana. Kufika hapo jikoni, nikatabasamu baada ya kumwona mama yangu akiwa bize kuonja-onja mapishi aliyokuwa anaandaa, nami nikaegamia ukuta huku nikimwangalia kwa hisia.

Mama yangu alikuwa na mwili ulionawiri vyema, siyo mnene sana wala mwembamba, na alikuwa mweupe. Hapa alivalia gauni refu la blue bahari, na kile kinguo wanachovaaga wapishi kifuani ili wasichafuke alikuwa amekifungia mwilini mwake pia, huku kichwani akiwa amesuka rasta za rangi nyeusi-nyekundu alizozibana juu ya kichwa. Mapishi yake yalinukia kwelikweli mpaka nikaanza kuhisi mtetemo wa njaa ndani yangu.

Alipogeuka na kuniona, akasema, "Jamani, mmewahi! Nilikuwa nataka mfike kila kitu kiko tayari."

"Hahah... unawekaga makolokolo mengi mno kwenye kupika ndiyo maana," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo na kumwambia Imelda, "Acha hii ichemke dakika kama tano sita, afu' ndiyo uzime jiko."

Imelda akasema, "Haya."

Mama akaja mpaka nilipokuwa nimesimama, naye akavishika viganja vyangu kwa chini na kusema, "Hujambo?"

"Sijambo, shikamoo?" nikamsalimia.

"Marahaba. Wageni wako wako comfortable?"

Nikachungulia upande wa kule sebuleni na kumwona Nuru anazungumza na wakina Tesha, nami nikamwangalia mama tena na kusema, "Yeah, Nuru anawafanya wajisikie wako nyumbani. Tuombe tu Jas asiamshe majini yake for no reason."

Mama akacheka kidogo na kusema, "Amepoa sasa hivi. Nataka nimwone huyo Mariam, nimemsikia Jasmine anasema ni mzuri."

"Ahahah... eeh twende," nikamwambia.

Nikiwa nataka kugeuka, mama akasema, "Frank anakuja pia."

"Mzee? Anatoka kazini mapema?" nikauliza.

"Ee. Sijui sasa kama atawahi kabla ya siye kula, ila nataka afike kabla hamjaondoka," akaniambia hivyo.

"Fresh. Ila kwa nini?"

"Nataka tuongee, Jayden. Seriously yaani... suala lako nataka tulizungumzie," akaniambia hivyo.

Nikashusha pumzi kiasi, kisha ndiyo nikatikisa kichwa kishingo upande tu na kuanza kuelekea naye sebuleni.

Najua kuna jambo zito kuhusu mimi ambalo mama alikuwa akitaka sana kuzungumzia pamoja kutokea kitambo sasa, na tena kuona kwamba mzee alihusika pia inamaanisha walikuwa na mtazamo ule ule kulielekea, kwa hiyo kama sikosei walikuwa wanataka kuja kunipa somo kwa pamoja. Nilikuwa nimejaribu sana kuikwepa ishu hii hadi wakati ambao likizo ingeisha, lakini kutokea hapa isingekuwa rahisi tena. Ningetakiwa kuipa za uso tu.

★★

Basi, mama akawa amekutana na Tesha pamoja na Mariam kwa mara ya kwanza, naye akafurahi mno kuwajua. Mama yangu alikuwa mtu aliyependa kufikika kiurahisi sana, hata akakaa karibu na Mariam na kumshikilia kwa njia ya kumkumbatia huku akizilaza-laza nywele zake kama vile anamdekeza. Alimfanya Tesha pia ajiachie vizuri kwa ajili ya maongezi, na baada ya Jasmine na Nuru kutambua kwamba alikuwa mcheshi, walimfurahia sana. Ilikuwa imeshaingia saa nane mchana.

Baada ya dakika chache tu, Imelda akaonekana kuandaa meza ya chakula kwa kuiwekea vyombo mbalimbali vya ulaji pamoja na vile vyenye vyakula, naye Nuru akaenda kusaidizana naye mpaka mambo yalipokamilika. Kisha sote tukaelekea hapo ili kuweza kupata mlo. Kulikuwa na vyakula vizuri kweli, kila mmoja akijipakulia kivyake, lakini ni Mariam tu ndiye aliyekuwa ametulia. Tesha akagusia kwamba Mariam alikuwa ameshazoea kupakuliwa na hata kulishwa na dada yao au mama zao, hivyo mama yangu akaamua kumpakulia na kukaa karibu yake, halafu akawa anamlisha. Hadi raha!

Nilifurahia sana wakati huu, chakula kitamu, maongezi yenye kufurahisha na kujenga, na baada ya kumaliza msosi, sote tukarudi tena kukaa masofani pamoja; Imelda akiwa ameenda kufanya kazi ya usafi wa vyombo jikoni, kisha naye pia akaja kujiunga pamoja nasi. Wafanyakazi wengine wa hapa wangekuja kula baadaye nadhani. Nuru alitokea kumpenda sana Mariam, kale kautoto kake kalikomfanya aonekane mgeni kwa mambo ya hapa na pale ndiyo kalimvutia zaidi, kwa hiyo aliburudika sana kumwonyesha hiki na kile.

Ikiwa inaelekea mida ya saa kumi jioni sote tukiwa hapo bado, gari lingine jeusi likawa limeingia huko nje ya nyumba, yaani kupita geti la nje, nalo likaonekana likiegeshwa. Tesha kama kawaida yake kwa kupenda magari alitambua upesi sana aina ya gari hilo, akiniambia kwa shauku kwamba hiyo ilikuwa ni Toyota LandCruiser 300, gari nzuri yenye ufanano na V8 lakini kwa muundo mzuri sana kulitazama.
LandCruiser.jpg
Tesha alijua hilo kuwa la gharama mno, kwa hiyo akakisia kwamba huyo alikuwa ndiyo mzee wangu. Na hakukosea.

Bwana Frank Manyanza akawa ndiyo amefika, naye Imelda akampokea mizigo kadhaa alipokuwa ameingia ndani, kisha mzee akaja upande wetu na sisi wote kumpa salamu. Alikuwa nadhifu sana ndani ya suti na tai, saa ya gharama na briefcase mkononi, kiatu cheusi cha aina yake, na nywele zake zikiwa fupi kuzungukia kichwa chake alionekana kuwa mtu aliyependa hadhi yake ya hali ya juu ijielezee kwa waliomwona, siyo yeye ndiyo awaambie.

Tukawa tumemtambulisha kwa Mariam na Tesha. Akawakaribisha vizuri, naye mama akamfata na kubeba briefcase lake, kisha wakazielekea ngazi na kwenda chumbani kwao kwanza. Nuru alikuwa amepatana vyema na Tesha pia, na baada ya jamaa kugundua kwamba Nuru alipenda kucheza ma-game, akasema yeye pia hupenda. Kulikuwa na chumba huko ghorofani chenye TV na ving'amuzi vya chaneli na game, PlayStation yaani, naye Nuru akawaalika Tesha na Mariam waende pamoja naye ili wakajiburudishe.

Vijana hao wakapanda ngazi pia, huku Nuru akimwambia Imelda jikoni kwamba akimaliza kazi zake na yeye aende kujiunga nao. Nikawa nimebaki na dada yangu hapo sebuleni, Jasmine, ambaye alikuwa bize na mitandao ya kijamii kwenye simu yake huku akitafuna embe dogo bichi kidogo-kidogo alilokuwa ameweka kwenye sahani pembeni.

Nikamuuliza, "Huyo Kevin hajakutafuta tena toka alipokuacha, Jas?"

Akasema, "Eerr, correction... mimi ndiyo nilimwacha. Sijaachwa mie."

Nikatabasamu na kutikisa kichwa, kisha nikasema, "Haya sawa. Lakini hajakutafuta? Kuulizia hali yako."

Jasmine akaonekana kukerwa tu na kuendelea kujali simu yake.

"Jasmine... talk to me. Niko hapa," nikamwambia hivyo.

Akashusha simu yake na kuangalia pembeni, naye akasema, "Ameshanitafuta. Anatuma sms kuulizia naendeleaje, katika maana ya kwamba hili tumbo lake linaendeleaje, ila sizijibu, na akipiga sipokei."

"Ni hivyo tu?"

"We' unataka kipi kingine J?"

"Nataka tu kujua kama, labda kama ameomba msamaha, au anataka yaishe..."

"Agh... hakuna kitu kama hicho. Yaishe, yaisheje wakati aliyeyaanzisha ni yeye mwenyewe? Aende huko na dharau zake. Nitajifungua, na nitawalea hawa me mwenyewe," akasema hivyo kwa kuudhika.

Najua Jasmine alikuwa amemchukia sana baba watoto wake, ila nikamwambia, "Unajua wakati mwingine... mwanamke anapokuwa mjamzito, zile tabia zake za kawaida kwa vitu anavyopenda au kutopenda, huwa zinabadilika. Na... unakuta anakuwa anapatwa na hisia tofauti-tofauti kuelekea vitu fulani, labda alikuwa hali hata maembe lakini ndiyo anaanza kuyapenda kama wewe hivi, ama labda alikuwa anampenda sana mtu lakini akivurugana naye kidogo, upendo huo unageuka kuwa chuki kali sana... lakini...."

"Ndiyo unataka useme kwamba ni makosa yangu?" akanikatisha kwa kusema hivyo.

"Sina maana hiyo..."

"Ila?"

"Nafikiri tu unatakiwa kujitahidi kutuliza hisia. Sawa, mmekorofishana, lakini... watoto wako watamhitaji baba yao wakizaliwa. Kevin ni mkaidi sawa, lakini anakupenda. Hiki kipindi tu kipite, halafu labda baada ya kujifungua mambo yakae sawa..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Akaniangalia kwa umakini sana, naye akasema, "Umeongea na Kevin wewe."

Nikatulia tu na kuendelea kumwangalia.

"Si ndiyo?" akauliza.

"Ndiyo. Alinipigia tu kuuliza hali yako, maana umem-block, na alikuwa anahofia kwenda moja kwa moja kwa mama..." nikamwambia.

"Enhee, kwa hiyo akakuambia maneno gani kuhusu mimi?"

"Jasmine nisikilize. Mimi ni kaka yako tu, siyo mwamuzi wa unachotaka kufanya kwenye maisha yako. Najua una hasira, lakini unaenda kuwa mzazi sasa. Kumbuka me na we' tulitupwa na baba yetu mzazi na jinsi mama alivyohangaika kutulea..."

"Si ndo' na Kevin anachotaka kufanya pia?"

"Hapana. Jasmine, kukorofishana kupo, tatizo linakuja zaidi msipopeana nafasi ya kusikilizana na kujaribu kutatua mgogoro. Kevin anakujali, aliniambia siku mmegombana alikuwa amekunywa, na maneno mliyotoleana hayakuwa mazuri ndiyo maana anajutia. Alifikiria labda akikuacha kwanza baadaye mambo yangekaa sawa, ila anaogopa kukupoteza wewe ndiyo maana anataka mrudi sehemu nzuri..."

"Alikuwa anakwambia hivyo kwa sababu anajali tu sifa yake iliyo humu tumboni. Basi! Unafikiri me siwaelewi wanaume? Katembea na wengi, lakini watoto wake wa kwanza wako hapa, ndiyo maana anajing'ata. Yaani kanipata mwanamke ambaye nitamzalia, tena mapacha, halafu anaendekeza umalaya, anitukane, halafu eti aje tu kusema 'nyoo,' 'nyoo,' na mimi nijionyeshe mpumbavu kurudi kwake?" Jasmine akaongea kwa makasiriko.

"Sauti... Jasmine, tulia. Nisikilize. Huyo ni mwanaume wako. Atakuwa baba wa watoto wako. Kumbuka umeanza kukutana na yeye kabla hilo tumbo halijawa hivyo, na mmeishi pamoja mpaka hiyo juzi mlipozinguana. Anataka muwe pamoja tena, siku utakayojifungua awe pamoja na wewe, na mwalee watoto wenu pamoja. Hautaki hilo kweli?" nikamuuliza kistaarabu.

Akanikazia macho yake, naye akasema, "Hivi J, mbona naona na we' umeanza kuwa mnafki? Mwanzoni si uliniambia kabisa niachane naye, halafu sasa hivi unampamba tena?"

Nikatikisa kichwa kwa kusikitika. Hakuwa amenielewa.

"Wewe ndiyo wa kunishauri hivyo mimi? Hautaki kudili na ishu ya Stella mpaka leo, halafu ndiyo uje uniambie hivyo?" Jasmine akasema hivyo.

Nikawa makini na kusema, "Usimwingize Stella kwenye haya."

"Umeona? Wewe a-ah, ila mimi ndiyo eeeh. J... naomba tu uniache sasa hivi, usimtaje Kevin tena kabisa. Nataka kuzaa kwa amani, akijisogeza kwangu nitazaa kwa mateso, zaidi ya mateso ambayo nitapitia. Imeisha," akaongea hivyo na kuirudia simu yake.

Nikawa nimenyoosha mikono. Hiyo ndiyo iliyokuwa adhabu ya kumchokoza Jasmine, na akawa ameifanya ikonge nyoyo haswa. Alikuwa na hasira huyo!

Ni ndani ya muda huo huo ndiyo wazazi wetu wakawa wamerejea sebuleni tena, mama akimtangulia mzee, na mzee mwenyewe akiwa amevaa nguo nyepesi tu baada ya kuonekana kumaliza kujimwagia, kisha akaongozana na mama mpaka sehemu ya meza ya chakula na kumwekea msosi, naye mzee akaanza kuushusha taratibu. Mama akaja kujiunga na sisi watoto wake mpaka mzee alipomaliza kula, na baada ya hapo jamaa akapanda tena kuelekea chumbani.

Nilikuwa nimeshamwambia mama kwamba vijana wengine walikuwa kwenye chumba cha TV huko juu, kwa hiyo kwa muda huu sasa ndiyo akaniambia tuelekee huko chumbani kwake ili kuzungumza pamoja na mzee. Nilikuwa nafikiri jamaa ameenda kujipumzisha kidogo, lakini mama ndiyo akaniambia kwamba tayari alikuwa amempanga, na alisema baada ya kumaliza kula ndiyo twende tukaongee kabla hajasinzia kutokana na uchovu wa kazi nyingi kwa wiki, maana ijapokuwa na leo ilikuwa jumapili bado alikwenda kazini. Nikaona hakuna noma.

Tukamwacha Jasmine na maembe yake hapo, nikiwa nimekisukuma kichwa chake kidogo kwa kidole na yeye kuniwasha kofi pajani, fujo za kaka na dada, nami nikaongozana na mama mpaka kufikia chumba chake. Akaingia kuhakikisha kwamba mazingira yalikuwa sawa kuniruhusu kuingia pia, kisha ndiyo akanikaribisha.

Sikukumbuka mara ya mwisho kuingia kwenye chumba cha wazazi ilikuwa lini, lakini kilikuwa kikubwa, na kila kitu kilichokuwemo yaani kilifanya paonekane kuwa kama chumba cha hoteli ya nyota tano. Sitaelezea mengi, vuta picha kwa taswira yako mwenyewe, ila kitanda kilikuwa kipana mno kutoshea watu wanne kulala kwa kujiachia. Kama hawa wawili wangenuniana basi ndiyo ingekuwa mzungu wa nne na bonge moja la nafasi katikati!

Tukamkuta mzee akiwa amekaa kitandani huku akipitia jambo fulani kwenye tablet yake ndogo, nami pamoja na mama tukaelekea mpaka karibu kabisa na alipokuwa amekaa mzee, kulikokuwa na masofa mawili madogo na meza, kisha mama akakaa kwenye sofa moja, lakini mimi nikakaa chini kabisa karibu na miguu yake.

Mama akatabasamu na kusema, "Nilifikiri ungekuwa umeshasahau kufanya hivyo."

"Hamna, hili ni zoea ambalo halitakufa," nikamwambia.

"Hivi alianza kukaa chini kama hivyo toka yuko la ngapi?" mzee akauliza.

"Hata sikumbuki... mdogo. Ila huwa napenda akikaa hivi, anakuwa anaonekana kama mtoto bado," mama akasema.

"Kwani amekua sasa?" mzee akauliza hivyo, nami na mama tukacheka kidogo.

"Huyo Mariam haonekani kama anaumwa, yaani mtu akimwangalia anaweza kufikiri yuko sawa kabisa. Umemsaidia sana. Hongera," mama akaniambia hivyo.

"Asante. Familia yake ni watu wazuri, wanasaidiana sana pia..." nikamwambia.

"Na hawakulipi?" mzee akauliza.

"Hamna. Namsaidia tu. Akikaa sawa zaidi itakuwa fresh sana, iko beyond pay grade yangu, sijawahi kudili na mgonjwa wa namna hiyo. Ni challenge nzuri sana na kuona inafanikiwa inaniongezea confidence," nikawaeleza.

"Vizuri sana. Hivi likizo uliyoomba inaisha lini?" mama akauliza.

Nikasema, "Umebaki mwezi kama mmoja. Krismasi ikipita tu, na mwaka mpya..."

"Unarudi kazini," mama akamalizia.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Hivi huwa hata unaenda kulicheki condo lako? Litakuwa limeshajaa vumbi kama siyo mtu kuingia kuiba vitu vyako..." mama akasema.

"Aa wee... nani aibe? Hapo siyo pa mchezo. Kuna walinzi, na pia kuna utaratibu wa kwenda kufanya usafi wa ndani kila wiki. Niliyemwachia funguo kwa ajili ya utunzaji namwamini, kwa hiyo pako sawa," nikamwambia.

Mzee akasema, "Halafu... huyo binti ndiyo Mariam Constantine?"

"Eee, ndiyo huyo," nikamjulisha.

"Kumbe? Ndo' ulisema dada yake anasimamia ile ishu yake?" akauliza tena.

"Ndiyo," nikajibu.

"Ni ile ile ishu yake uliyoniambia?" mama akauliza.

"Eeh. Mariam aliachiwa shamba na marehemu wazazi wake. Kuna mtu alikuwa anataka kumwibia halafu aliuze kwa mzee, ndiyo mimi na dada yake Mariam tukamzuia," nikamfahamisha.

"Oooh, masikini! Walikuwa wanataka kumwibia kwa sababu ya hali yake, eti?" mama akauliza.

"Mmm," nikakubali kwa mguno.

"Dada yake yupo huku?" akauliza tena.

"Ee, wanaishi wote. Yeye ndiyo anawasimamia," nikamwambia hivyo.

"Sawa. Uje umlete na yeye atutembelee," akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kwa kuhisi furaha ndani ya moyo wangu, kwa kuwa nilikuwa natazamia kwa hamu siku ambayo ningekuja kumtambulisha Miryam kwa wazazi hawa. Ikiwa ingefika. Lakini kwa sasa, kulikuwa na suala zito la kuzungumzia hapa, na najua walikuwa tu wananipoza shavu kidogo kabla ya kulitandika kofi zito.

Mama akasema, "Jayden, unajua ni nini tunataka kuongea. Sijui ikiwa uko tayari kutusikia?"

"Amekaa na chini, unataka afanyaje sasa ili ujue anakusikiliza?" mzee akamtania kidogo.

Mama akamkata jicho la kukerwa, nami pamoja na mzee tukatabasamu kidogo.

"J, tunaenda tu kwenye point. Mama yako na mimi tunafikiri itakuwa vyema sana ukianza kudili na suala la Stella... vizuri zaidi. Ikiwa unanielewa," mzee akasema hivyo.

Nikasema, "Ndiyo naelewa. Ila... sioni sababu ya ni kwa nini mnaumiza sana vichwa juu ya hilo... nitalishughuli...."

"Jayden, hapana. Umeshaimba hayo maneno mara ngapi?" mama akanikatisha.

"Mama..."

"Wakati nakuja huko chini nimekusikia vizuri tu wakati unamshauri Jasmine kuhusiana na Kevin, na alikuwa na point kukwambia kuhusu Stella. Kwa nini bado una hiki kinyongo? Unajua kitamwathiri nani zaidi mbeleni ikiwa hautakiachia? Wewe mwenyewe Jayden..." mama akaniambia hivyo.

Nikashusha pumzi na kuangalia chini.

"Siku ile nimekupigia simu kukwambia Stella kaja hapa, nilihisi namna ulivyokasirika, ulinifokea kabisa yaani baada tu ya me kumtaja," akasema hivyo.

"Mama... sikukufokea, nili... nilikuwa tu...."

"Najua unakuwa sensitive sana ukisikia tu nimemsema Stella, lakini Jayden... hii siyo kuhusu Stella. Ni kuhusu mwanao," akaniambia hivyo.

Nikatazama pembeni tu.

"Nimeshasikia baadhi ya watu wanasema kwamba ukiulizwa kama yule ni mwanao, unakataa kabisa. Kwa nini lakini? Yule ni mtoto wako J. Utaendelea kukimbia mpaka lini? Inajalisha chochote kile ambacho kimetokea baina yako na mama yake? Itafuta ukweli kwamba yule ni damu yako? Na tena usifikiri 'ah mama bana, nitashughulikia hilo baadaye,' unasemaga tu hivyo lakini hufanyi lolote..." akasema hayo kwa hisia.

Nikawa tu nimeshusha macho yangu, nikimsikiliza kwa utulivu.

Akasema, "J... kaa chini utafakari. Yule ni mtoto wako, ni mjukuu wangu, ninataka uwe baba kwake. We' siyo mtoto tena, unatuongoza mpaka na sisi mara nyingine kwa sababu umeshakuwa mwanaume. Kuwa mwanaume basi, kiondoe hicho kinyongo, umfate mwanao Jayden..."

"Na... isiwe tu kwamba utafanya hivyo ili kumridhisha mama, au mimi, unatakiwa ufanye hivyo kwa kupenda. Feel it. Hakuna hisia nzuri kama kuwa pale kwa ajili ya mwanao," mzee akasema hivyo.

Mama akasema, "Yes, ni kweli kabisa. Anatakiwa akujue, akupende, akue akijua ana mama na baba. Haitakuwa nzuri akikua kama nyie na Jasmine ilivyokuwa..."

"Mama... basi, inatosha. Nimekuelewa," nikamwambia hivyo kistaarabu.

Akashusha pumzi kiasi na kuendelea kunitazama.

"Nilikwambia nitalifanyia hilo kazi. Yote mliyoyasema nayaelewa, ila tambua kwamba siyo rahisi kwangu. Na mnajua ni kwa nini..." nikamwambia hivyo.

Mama akanishika begani na kusema, "Najua. Lakini Jayden, jifunze tu kuachilia mapito. Unajua hayana faida kwa ajili ya wakati ujao. Samehe mwanangu... ndiyo utakuwa na amani zaidi."

"Najua. Usijali mama. Nitashughulika na hilo. Lakini kwa sasa hivi, acha tu nimalize likizo hii vizuri... haya mengine yatafata," nikasema hivyo kwa upole.

Akaniangalia kwa uelewa, naye akasema, "Haya. Me yangu ni hayo tu. Jasmine anaenda kujifungua huku tayari ameshaachana na mzazi mwenzake, we' pia ndiyo iko kama hivyo, yaani... nataka tu wanangu muwe sehemu nzuri, msiishi kwa njia itayowaathiri watoto wenu vibaya... lakini naona kama hilo linafeli tu."

"Usiseme hivyo mama. Kila kitu huwa kinatokea kwa sababu fulani, ila la muhimu ndo'... ndiyo kujua tu namna ya ku-handle mambo vizuri... ingawa sometimes mengine yanakuwa magumu sana," nikamwambia hivyo.

Mama akajisawazisha na kukaa vizuri huku akinitazama.

"Just... nipeni muda. Nawaahidi nitafanya jambo fulani, lakini bado tu sijajua lini... ila nitalifanya. Msijali," nikamwambia hivyo.

Nadhani waliona kwamba nilikuwa natoa ahadi hiyo bila kupenda sana, kwa hiyo mama akasema, "Haya. Me yangu macho. Nitasubiria kuona utakachofanya."

"Mama yako kayasema yote J. Kazi kwako," mzee akasema hivyo.

Nikanyanyuka tu baada ya hapo na kuanza kuondoka kuuelekea mlango, kisha nikatoka humo na kusogea mpaka sehemu yenye kingo za vioo kuelekea upande wa ngazi, nami nikasimama hapo kwa kuegamia. Kama ni kitu ambacho kwa muda fulani sasa ndiyo kilikuwa kikinikosesha amani sana, basi ndiyo kilikuwa hiki.

Mama, mzee, Jasmine, Nuru, baadhi ya ndugu zetu wengine, marafiki, labda hata na yule mwanamke mchungaji niliyepelekwa kwake siku ile na Bi Zawadi, wote walielewa kwamba hiki ndiyo kitu ambacho nilikuwa najitahidi sana kukwepa, na kulikuwa na sababu zilizofanya JC afikie uamuzi kama huo. Hata Soraya aliwahi kuniuliza ikiwa nina mtoto na nikakataa, kwa hiyo ieleweke kwamba hiyo sababu ilikuwa nzito.

Ila kutokea hapa, hili suala kweli lilionekana kuwa gumu mno kuepuka tena, na najua ilitakiwa kufika siku ambayo kweli ningetakiwa kulipa za uso hasa kwa sababu nilitaka maisha yangu yabadilike na kuwa bora zaidi ya nilivyokuwa naishi hapo awali. Ningetakiwa kukubaliana na ukweli kwamba nilikuwa baba, na mtoto huyo alinihitaji kwa wakati sahihi, ila ndiyo bado sikujua, na labda tu sikutaka kujua wakati huo ungekuwa lini. Lakini ungepaswa kufika. Yaani maisha yangu haya, aliyajua mimi mwenyewe tu!

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or DM

Whatsapp +255 678 017 280
 
Ninashauku sana ya kusikia story inayomuumiza mtaalamu wetu JC mpaka akiambiwa habari za Stella anakuwa mkali kama pilipili😋😋😋😋
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Tesha na Miryam wakafika nyuma yangu, naye Miryam akatoa sauti ndogo kuonyesha mshtuko, huku Tesha akinionyeshea upande ambao nyoka yule alielekea ili kumwonyesha kwangu. Inaonekana kelele alizopiga Soraya zilifanya baadhi ya watu waliokuwa sehemu za karibu na hapo waanze kuja, hivyo kuna baadhi yao wakawa wamekutana uso kwa uso na huyo nyoka. Wee! Wakageuka na kurudi walikotoka, labda hata mpaka kufikia sehemu ambazo hawakutakiwa kufika.

Katika hali hiyo yenye mshtuko wa ghafla sana, huyo nyoka alisimama, yaani kwa mtindo kama wa Cobra, akionyesha ubabe wake, nami nikaingiwa na hasira kali sana na kutoka hapo nilipokuwa.

"We' JC!"

Tesha akaniita hivyo kwa tahadhari, nami nikawa nimefikia sehemu ambayo ilipandwa maua pembezoni mwa jengo hilo na kuyalinda kwa kuzungushia mawe magumu ardhini. Nikatoa jiwe moja na kulirusha kwa nguvu sana kumwelekea huyo nyoka, na aisee ilikuwa ni shabaha ya bahati!

Hilo jiwe likamponda nyoka mgongoni, sijui tumboni, sijui kiunoni, naye akaanza kuhangaika hapo chini. Tesha akaja kuniunga mkono kwa yeye pia kuokota mawe ili kuja kuanza kushughulika na hilo dude. Ah siyapendi hayo madude!

Baadhi ya wanaume waliokuwa karibu nao wakasogea pia ili kuungana nasi kummaliza huyo ibilisi, nami nikamgeukia Soraya. Hasira iliyoniingia ilikuwa imenifanya nipumbazike na kumfata nyoka badala ya kumjali huyo mwanamke hapo chini, na wakati huu alikuwa amelalia mapaja ya Miryam, ambaye alikuwa ameushika mkono wa Soraya huku akidondosha machozi kwa huzuni pia.

Nikaachana na nyoka na kwenda hapo. Nikapiga magoti na kuutazama mkono wa kushoto wa Soraya, na hapo nikaona uvimbe mdogo sehemu ya kuvalia saa lakini kwa chini, ukiwa na matundu madogo mawili. Nikamtazama Soraya kwa huruma sana kwa jinsi alivyoonyesha kuumia mno, naye Miryam akanigusa begani.

"Nenda ofisini kwangu, kachukue... nimeacha funguo mezani... za gari... wahi..." Miryam akaniambia hivyo.

"Hauna boksi la huduma ya kwanza?" nikamuuliza.

"Hapana... hamna... nenda kachukue funguo tumwahishe hospitali..." Miryam akasema.

Nikabaki kukitazama kidonda cha Soraya mkononi, nikitafakari njia ya haraka ya kumpa msaada kwa sababu hakukuwa na vifaa vya huduma ya kwanza, nami nikaukaza kwa nguvu sehemu ya kiwiko chake.

Miryam akanipiga begani kwa nguvu na kufoka, "Wahi! Kazifate..."

Nikasikia hatua zikifika nyuma yangu, na sauti ya Tesha ikasema, "Tumpeleke Tausi hospitali! Dada... JC... tumnyanyue..."

"Hapana," nikamkatisha.

Kuna watu waliokuwa wameanza kusogea sehemu hiyo baada ya kumuua nyoka nafikiri, naye Miryam akawa ananitazama kimaswali sana.

"Tesha... hospitali ya karibu zaidi na hapa ni ipi?" nikamuuliza hivyo.

"Aa... kuna Dispensary hapo hivi nanii...."

"Hapana, siyo Zahanati. Hospitali," nikamwambia hivyo.

"Ipo ile Epiphany hapo nyuma... si unaikumbuka?" Tesha akasema.

"Epiphany imefungwa," mmoja wa watu waliokuwepo hapo akasema hivyo.

"Kwa nini? Kufungwaje yaani?" Tesha akamuuliza hivyo.

"Sijui sana. Wamesimamisha kazi kwa wiki... zimebaki kama siku tatu ndiyo watafungua," huyo jamaa akamjibu.

"Nyingine kubwa? Bora yaani?" nikamuuliza Tesha.

"Hospitali kama... Rangi Tatu pale ya goverment, ila wana mambo slow mno... sijajua sana, me... labda ya Temeke kule ndo' kubwa na nzuri, ama Uhasibu..." Tesha akawa anasema.

"Temeke? Ile ya rufaa? Huko ni mbali Tesha," nikamwambia.

"Sina wazo la haraka bro..." Tesha akasema hivyo.

Soraya akawa anaendelea kulia.

"Tunapoteza muda jamani... tumwahishe hospitali yoyote..." akasema hivyo Miryam.

"Hapana, tutaenda hiyo hiyo ya rufaa..." nikasema hivyo.

"Ama sumu inyonywe..." akasema hivyo mtu mwingine hapo.

"Unaweza kuinyonya?" akaulizwa hivyo na mwingine.

Nilikuwa naangalia eneo hilo nikitafuta mti au kichaka chenye vijiti, nami nikaona mti mmoja kwa mbele kidogo.

"Tesha... njoo, mshike Soraah mkono kama hivi... mkaze kama hivi..." nikamwambia hivyo.

Tesha akatii na kuchuchumaa, akiukaza mkono wa Soraya kama nilivyosema.

Miryam akajifuta machozi na kuniangalia kwa mkazo.

Nikasimama na kuwaambia wanaume wawili waliokuwa wamesimama hapo, "Kaka, tafuta... nisaidieni nyote kunitafutia kamba ama waya wowote mtakaopata... harakisheni tafadhali..."

Wawili hao wakatii na kuondoka hapo, nami nikakimbia mpaka kwenye ule mti na kupanda. Mvua ndogo ikaanza kunyesha, yaani manyunyu. Matawi yalikuwa juu kiasi kwa hiyo nikapanda na kukata mti mnene wenye matawi mengi kisha nikaruka na kutua chini. Nikaparua vizuri matawi hayo na kukata jiti nene lenye urefu kama fimbo, iliyonyooka vyema, nami nikarudi pale kwa Soraya.

Nikakuta mmoja wa wale wanaume amepata waya mrefu kiasi wa cable, na yule mwingine wa hivyo hivyo pia, nami nikachuchumaa na kuanza kupima fimbo ile na mkono wa Soraya. Nikaikata kwa kupima urefu kutokea usawa wa kidonda chake mpaka kukaribia bega, kisha nikauliza ikiwa kuna mtu alikuwa na kitambaa chenye urefu.

Nafikiri wengi hawakuelewa nilikuwa nataka kufanya nini, na nilipoona hamna jibu ikabidi nishike T-shirt langu kwa chini na kulichana, nikifanya hivyo kwa mzunguko kutokea tumboni kupitia mgongoni mpaka kuikata tumboni tena, nami nikapata urefu niliohitaji.

Nikaushika mkono wa Soraya na kupitisha nguo hiyo kwa chini, kisha nikaanza kuifunga hiyo nguo pembeni kidogo kwenye mkono kutokea pale alipokuwa ameng'atwa.

"JC... vipi?" Tesha akaniuliza.

"Hii itazuia mzunguko wa damu kwenye mishipa midogo zaidi... ili sumu isifikie moyo au misuli ya mapafu yake," nikatoa jibu hilo huku nikiendelea kufunga.

"Wewe, ona mkono wake... kidonda kinavimba. Kata hiyo sehemu sumu itoke..." mmoja wa watu waliokuwa hapo akasema hivyo.

"Si salama..." nikajibu hivyo.

"Siyo salama? We' vipi? Wengi huwaga wanatolewa hivyo..." akasema hivyo huyo jamaa mjuaji.

Nikataka kuikaza nguo hiyo mwishoni vizuri, na kutokana na utelezi kiasi uliofanya vidole visiivute vizuri, nikatumia meno kuivuta kwa nguvu zaidi karibu kabisa na uvimbe wa sehemu aliyong'atwa Soraya.

"We' kijana, unapoteza muda. Atakufa huyo! Tafuteni wembe... kata hiyo sumu itoke nje..." huyo jamaa akasema hivyo.

"Unaangalia movie nyingi za kipuuzi mzee wangu," nikasema hivyo na kuishika ile fimbo ndogo.

"Nini? Hivi huyu mchina wa wapi huyu? Unajifanya daktari au?" jamaa akauliza hivyo.

"Ni daktari ndiyo. Mwache, anajua anachokifanya," Tesha akamzimisha namna hiyo.

Sikuwa nawaza kelele huyo mjinga, bali nikawa naiingiza hiyo fimbo kwenye fundo la kwanza mpaka kuufikia msuli wa juu wa mkono wake Soraya, ukiwa umenyooka na kutoweza kujongea, halafu nikamwomba yule mwanaume mmoja anipe ule waya wa cable, nami nikaikaza fimbo hiyo hapo zaidi.

Nilijua hiyo ingezuia zaidi mzunguko wa damu kwa upande huo wa mkono wake Soraya kwa sababu misuli haingetendeshwa hata kidogo kuzuia sumu isiwahi kufika kwenye sehemu kama figo, ama misuli inayotumka kusaidia suala la upumuaji.

"Tesha, kazifate funguo za gari la dada tumpeleke Soraya hospitali. Upesi," nikamwambia hivyo.

Akatoka sehemu hiyo haraka na kwenda upande wa ndani humo dukani.

Nikamwangalia Soraya na kukuta ananitazama huku akilia kwa hisia, nami nikamshika kwenye paji lake la uso kupima joto. Hakuwa amechemka sana.

"Soraah... kichwa kinauma?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa kidogo kukanusha.

"Unahisi kichefuchefu? Koo inawasha?" nikamuuliza tena.

Akatikisa kichwa kukataa.

Nikashusha pumzi ya utulivu kiasi na kufumba macho kwa ufupi, kisha nikamshika shavuni kwa kujali na kumwambia, "Pole. Utakuwa sawa. Tunaenda hospitali, sawa?"

Akawa analia tu huku akikaza macho yake, nami nikamtazama Miryam. Mwanamke huyu alikuwa ananiangalia kwa mkazo usio wa chuki, bali huzuni, nami nikamwona Tesha akitoka kule ndani na kuanza kuifunga milango ya duka la dada yake upesi sana.

Akatoka hapo na kukimbilia upande ambao gari la Miryam lilikuwa, huku mimi pamoja na wanaume wengine tukianza kumsaidia Soraya anyanyuke taratibu, na nikihakikisha mkono wake haushtushwi kwa chochote. Yaani ulitakiwa kunyooka hivyo hivyo kama mbao, na kidonda chake kikaendelea kuvimbia pale pale alipoumwa.

Tesha akaligeuza gari na kulileta usawa wetu, nasi tukamwingiza Soraya siti za nyuma akiwa pamoja na Miryam, na mimi pia nikakaa nao huko huko nyuma kuhakikisha usalama zaidi wa mwanamke huyo, halafu ndiyo Tesha akatuondoa hapo upesi. Alikuwa anaombea tusikutane na msongamano wa magari la sivyo kuchelewa kungeleta shida, lakini nikamwambia asijali kuhusu hilo, yeye aendeshe tu kwa uangalifu mpaka tuifikie hospitali.

★★

Vuuu tukatoka Kijichi, Zakhem, tukaivuka Rangi Tatu, mpaka huko mbele wapi sijui kuelekea Sabasaba, lakini hatukufika huko kabisa tukawa tumekula kona kwenye barabara iliyoelekea maeneo ya Tandika, kwa kuwa ni hizo pande ndiyo hospitali ya Temeke ilikuwepo.

Muda wote niliokuwa nimekaa nyuma pamoja na wanawake hawa wawili, nilimbembeleza Soraya kwa kumsugua taratibu shavuni na kumsemesha mara kwa mara. Alikuwa amekaa katikati yetu mimi na Miryam, akiwa amelaza kichwa chake begani kwa Miryam, huku mkono wake nilioufunga ukiwa umenyookea kwangu na mimi kuhakikisha unatulia hivyo hivyo.

Ningeona jinsi Miryam alivyoniangalia kwa ufikirio mwingi mara kwa mara, na nilielewa wazi hilo kutokana na namna nilivyomtendea Soraya kwa huruma sana. Labda alihisi wivu kidogo, sikujua. Lakini huu haukuwa muda wa kukazia fikira hayo. Afya ya Soraya ndiyo lingekuwa suala la kipaumbele kwa wakati huu.

Lilikuwa jambo la busara kwa Tesha kutupeleka kwenye hospitali kubwa zaidi japo kuna zingine tulizokuwa tumezipita, jambo zuri kabisa. Akatufikisha kwenye hospitali ya Temeke Hospital, ikiwa ndiyo hospitali bora kwa hapo kwa hiyo bila shaka vifaa vilivyohitajika kumpatia msaada Soraya vingekuwepo; dawa na masindano na mavisu kwa ajili ya mgonjwa wa dharura.

Jengo hilo lilikuwa na ukubwa wa aina yake, maghorofa kadhaa upande mmoja, wodi nyingi za wanawake, wanaume, na watoto upande mwingine, nasi tukafika huko pa kuingilia na kuegesha gari baada ya kupita kivuko cha geti. Nikasaidiana na Tesha kumtoa Soraya kwenye gari, nasi tukaanza kuelekea huko ndani tukiwa tumembeba.

Hii ikiwa ni saa tano kuelekea saa sita usiku kama sikukosea, hakukuwa na watu wengi sana lakini walikuwepo, na kwa jinsi tulivyoingia pamoja na mgonjwa aina ya Soraya, macho mengi yalitupa "karibu" ya kustaajabu.

Hiyo hasa ilitokana na mkono wake kuvimba mno sehemu ya kidonda, ikifanya watu wamwangalie Soraya kwa huruma sana, na baada ya wauguzi wa hapo kutuona wakawa wameleta kiti cha magurudumu kilichokuwa karibu, nasi tukamkalisha mpendwa wetu hapo na kuanza kuongozana nao kuelekea kwenye chumba cha matibabu.

Nikawa nimejitambulisha kuwa daktari pia, na baada ya kumwona daktari aliyekuja kumshughulikia Soraya, nikamweleza kilichotokea, aina ya nyoka aliyemuuma Soraya, muda uliopita toka ameumwa, na pendekezo dogo la dawa ya kumpa haraka. Kwa hiyo sisi watatu tukaachwa nje ya chumba alichopelekwa Soraya baada ya hapo, na baadhi ya watu wakawa wanatuuliza yaliyotokea na Tesha kuwaelezea.

Dah! Soraya alinitia simanzi sana. Huyo Cobra wa kishetani alikuwa ametokea wapi ghafla vile? Unajua naelewa nyoka huwa hawaumi mtu mpaka wajihisi kuhatarishwa, sasa sijui Soraya alimfanya nini huyo kichaa mpaka akaona amng'ate dada wa watu mzuri na mtamu kweli, wakati alikuwa amejikalia tu pale nje akitusubiri!

Basi, tukaendelea kusubiria, huku simu zikipigwa kutuma taarifa kwa waliojali hali iliyotokea. Miryam alimjulisha mume wake Soraya, ambaye akasema angefika hapo hospitali upesi. Ankia alikuwa amenipigia simu pia kuuliza niko wapi, nami nikamwelezea hali halisi ya kilichotokea, nikisema tungerudi huko nyumbani masaa yakiwa yameenda, kwa hiyo yeye apumzike tu.

Kwa kuwa Soraya aliishi Sabasaba na familia yake, nilielewa kwamba haingechukua muda mrefu sana na mume wake angekuwa amefika hapa hospitali. Ningetakiwa kutuliza noma zangu jamaa akishafika la sivyo angejua kwa njia fulani kwamba mke wake nishagapita naye. Niliomba Mungu Miryam asije kunitibulia hiyo ishu aisee, la sivyo ningekimbilia Sinza leo leo! Tesha akawa amewajulisha wa nyumbani kwao pia kuhusu haya, hivyo kwa pamoja tukakaa kuendelea kusubiri.

★★

Dakika chache kupita na mume wake Soraya akawa amefika. Alikuwa mbaba wa miaka kama 40 hivi, mweusi na mrefu kiasi cha kunifikia mimi, na alikuwa na mwili mkubwa, yaani unene wa kadiri. Alivalia miwani ndogo ya macho, nywele zake zilikuwa fupi, na alivalia nguo ndefu kama kanzu lakini yenye muundo wa satini nzito ya kijani.

Alionekana kujuana vizuri na Miryam kwani alifika tu hapo na kuanza kuzungumza naye haraka, nami nikawa namwangalia tu huku nikikumbukia jinsi Soraya alivyoniambia kipindi kile kuwa mume wake ana mahaba ya kuku.

Tesha akanipiga kidogo kwa kifuti ili kunionyesha huyo mzee, maana naye alijua dili nililofanya na mke wake wiki kadhaa nyuma, nami nikaendelea kujituliza tu. Mwanaume huyo akatusalimu mimi na Tesha pia, nasi tukamwitikia vizuri, kisha tukaendelea kusubiri.

Haikuchukua dakika nyingi sana na daktari akawa ametoka, pamoja na wauguzi wawili, naye Miryam akamsogelea karibu.

"Vipi... anaendeleaje?" Miryam akamuuliza hivyo daktari.

Sisi pia tukasogea karibu nao.

Daktari alikuwa mwanaume mtu mzima vya kutosha kunizaa, naye akasema, "Ametulia, atakuwa sawa. Tumempa dawa, sa'hivi amelala."

"Eh, asante Allah jamani! Ah! Nilikuwa nawaza sana dokta. Mke wangu huyo," mume wake Soraya akajinadi.

Tesha akanipiga tena kwa kifuti, nami nikamrudishia kwa nguvu zaidi na kumfanya atoe cheko ya kujikaza na kisha akajikausha.

"Aaa... we' ni mume wake?" daktari akamuuliza hivyo.

"Ndiyo. Nimepewa taarifa na bosi wake huyu ndo' nimekuja. Kwa hiyo... yuko sawa kabisa sasa hivi?" mume akauliza.

"Ndiyo, usijali, yuko sawa. Tumemsafisha," daktari akasema.

"Sumu mmeitoa?" Tesha akauliza.

"Eee... tumeitoa. Mmefanya vizuri sana kutumia IPM, imemsaidia mno na imeturahisishia kazi," daktari akasema.

"IPM ndiyo nini?" Miryam akauliza hivyo na kuniangalia.

"Pressure Immobilization Method. Njia niliyotumia kuizuia sumu kwenye mkono wa Soraya," nikamwambia hivyo Miryam.

Miryam akabaki kunitazama kwa umakini.

"Kwa hiyo kama tusingemfunga hivyo?" Tesha akamuuliza daktari.

"Angekufa haraka. Aa... sumu zinatofautiana ikitegemea na nyoka, ila ya huyo aliyemng'ata ilikuwa kali. Mgekiacha tu kidonda chake angekufa ndani ya dakika 20," daktari akasema.

"Eh!" mume wake Soraya akashangaa.

"Lakini kwa kutumia IPM mkawa mmempunguzia kasi ya kuenea kwa sumu kwenye mwili wake kwa masaa 24. Unajua... utagundua kwamba mtu aliyeng'atwa huwa haonyeshi dalili za sumu kumwingia ikiwa atapewa huduma kama hii, lakini akishafikishwa hospitali tu na kufunguliwa, ndiyo dalili zinaanza kuonekana. Tumemfungulia tu ndiyo akaanza kukohoa na kutapika, lakini tukamsafishia na kumtia dawa, zitaleta matokeo mazuri zaidi ndani ya masaa 72 yatakayofuata. Anatakiwa kuendelea kuzitumia. Sawa?" daktari akasema hivyo.

"Sawa. Tunashukuru. Nitagharamia dawa zake... aa... mtanipa maelekezo..." mume akamwambia hivyo daktari.

"Haina shida," daktari akasema.

"Halafu kuna watu walikuwa wanampigia kelele JC hapa eti hiyo njia haifai. Eti kukikata kidonda na kuinyonya sumu ni njia salama?" Tesha akauliza.

"Hapana, siyo salama. Sumu ikinyonywa inaweza kumwingia anayeinyonya na yeye akaambukizwa. Na kidonda kikikatwa haimaanishi sumu yote itatoka, ila ndiyo utamwongezea tu maumivu aliyeng'atwa. Mlitumia nguo na waya badala ya bendeji lakini..." daktari akasema hayo.

"Ndiyo, hapakuwa na bandeji, na mazingira hayakuruhusu kuzitafuta. JC ndiyo akatumia hiyo njia," Tesha akamwambia hivyo.

"Safi sana kiongozi. We' ni daktari mzuri, umetupa sifa sana," daktari akaniambia.

"Asante," nikashukuru.

"Star TV wangekuwepo hapa, ungekuwa maarufu," Tesha akatania.

Sote tukacheka kidogo kwa kuhisi ahueni, isipokuwa Miryam mnunaji, naye mume wake Soraya akaniambia, "Kumbe we' ndiyo umemsaidia mke wangu? Nakushukuru sana. Allah akuzidishie baraka maishani mwako."

Nikakosa hata cha kusema na kubaki kutikisa kichwa tu kuonyesha uelewa, naye Tesha akaniambia, "Sema ishaallah wabarakatuu..."

Nikajitahidi kuibana cheko kwa kuwa maneno hayo hayakusikika kwa wengine isipokuwa mimi, naye daktari akaondoka pamoja na Miryam na mume wake Soraya baada ya hapo.

"Ila Tesha, mbona unakuwa hutulii?" nikamuuliza hivyo tukiwa tumebaki peke yetu.

"Ahahahah... dah! Kaka haya mambo yanafurahisha sana, basi tu. Alikuwa anakushukuru kumsevu na kumnyandulia mke wake," akasema hivyo.

"Acha basi mwanangu, utakuja unichomeshe ujue..."

"Ah wapi, sisi watoto wa mjini bana. Huyo unafikiri atakufanya nini hata kama akijua?"

"Wanajuaga tu ya kufanya, afu' anaonekana anampenda kweli. Me sitaki hiyo kitu ilete shida sa'hivi, si unajua nayajenga kwa dada yako?"

"Na da' Mimi akijua, utafanyaje?" akaniuliza.

"Anajua," nikamwambia hivyo.

"He! Miryam anajua ulimla Soraya?!" akashangaa.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Ahehee... JC? Tatizo hilo..." akaniambia hivyo.

"Usiniambie..."

"Yote niliyokwambia kuhusu umri na nini, sahau. Hapo tu tena kwenye kuwa Playboy ndo' uhesabu umeshafeli kwa Mimi. Ikiwa bado unamtaka," akasema hivyo.

"Ndiyo, sijaacha kumpenda Miryam. Hayo mambo ndiyo maana nataka niachane nayo, nimwonyeshe niko serious," nikamwambia.

"Ikoje lakini sa'hivi? Dada anafunguka?"

"Bado, Tesha. Bado mapema, taratibu tu. Haya masuala ya u-playboy we' ndo' uendelee nayo tu mpaka yakuue, me kwa dada yako ndiyo nataka nimalize. Na ishu ya Soraya, nataka niisahau..."

"Aaa, unajiongelesha tu, wewe uisahau tamu ya Soraya?"

"Kwa nini nishindwe?"

"Aa, wewe... sisi wanaume tunajuana vizuri, hunidanganyi. Tena ushamkariri hadi kumwita unamwita 'Soraah' ... yaani we' mwenyewe ndo' utakuja kujikamatisha kwa mume wake. Afu' kwanza utaachana vipi na hiyo mali wewe? Mke wa mtu sumu, na ni sumu tamu, sasa kwa mtoto kama Soraya jumuisha na sumu ya Cobra, wee! Anakuwa mtamu vibaya mno!" Tesha akasema hivyo na kucheka.

Akanifanya nicheke sana, lakini kwa sauti ya chini.

"Dhambi hizi mwanangu, ila ndo' tushaumbiwa kuzipenda hahahah..." akasema hivyo.

Nikapiga ulimi mdomoni na kutikisa kichwa kidogo, nami nikaendelea tu kusimama hapo kwa utulivu. Tesha angenionyesha jinsi ambavyo baadhi wa wauguzi wa kike kwenye hospitali hiyo walituangalia sana, huku wengi wao wakiwa ni warembo, lakini mimi mrembo wangu mmoja tu aliyekuwa akilini ni yule ambaye sote tulimsubiri arudi hapo tena; bibie Miryam.

Nilimkubali sana huyo mwanamke. Fikira za siku ambayo ningehitaji kuja kumwambia Miryam ukweli wote wa maisha yangu hasa baada ya kuzungumza na mama yangu leo, zilikuwepo, lakini kwa wakati huu nilitaka kwanza kuhangaika na Miryam mpaka nimthibitishie kwamba upendo wangu kwake ulikuwa wa kweli, ndiyo mengine yangefuata ikiwa siku ambayo angenikubali ingefika. Na najua ingefika tu.

★★

Miryam na mume wake Soraya wakawa wamerejea hatimaye, nasi tukapata kujua kuwa masuala ya dawa na utunzaji kwa ajili ya Soraya yalikuwa yameshughulikiwa tayari wawili hao walipoenda na daktari huko mbele.

Mume wa Soraya aliitwa Arafat, naye akatupa shukrani kwa mara nyingine tena huku akisisitiza twende nyumbani kupumzika, kwa kuwa yeye ndiye angekaa hapo na kuna ndugu zake wengine waliokuwa wanakuja. Baada ya hilo kueleweka sisi tukamuaga jamaa na kuanza kutoka ndani ya jengo hilo kwa pamoja.

Tesha angetoa komenti za jinsi tukio hilo lilivyokuwa limetengeneza aina fulani ya msisimko wa hali ya juu kama aupatao kwenye kuangalia filamu alizopenda, naye akamuuliza dada yake ikiwa kesho angekwenda kazini kwake na kufanya kazi bila uwepo wa msaidizi wake. Miryam akamwambia kwamba kwa siku ambazo Soraya asingeweza kwenda kazini ni kweli angehitaji kufanya kazi zote yeye mwenyewe, na ndiyo Tesha akaomba apewe ajira ya muda mfupi.

Aliomba kuwepo pale dukani kwa Miryam kumsaidia na mambo ambayo Soraya ndiyo alisaidia kufanya, lakini dada yake akamwambia asiwe na hofu; kila kitu angeweza kushughulika nacho mwenyewe mpaka kufikia kipindi ambacho msaidizi wake angekuwa fiti kurudi kazini. Na alimpenda kweli Soraya, maana alikuwa mwanamke mpole na mwenye bidii.

Kwa hiyo tukalielekea gari ili tuweze kurudi nyumbani hatimaye, Tesha akiwa anataka kuendesha tena. Ile mvua ndogo iliyokuwa imeanza kunyesha muda fulani nyuma ilikuwa imeshakata, na ile tu nimeufikia mlango wa nyuma wa gari na kutaka kuuvuta ili niingie, nikapigwa na kizunguzungu kikali kilichokuja ghafla sana na kusababisha nirudi nyuma kama vile nimesukumwa!

Nikajitahidi kujituliza na kuinama kidogo, nikikaza meno na kushika upande mmoja wa kichwa kwa kiganja changu, na nafikiri Miryam na Tesha waliliona hilo na kusitisha kuingia garini.

"Oy JC, vipi?"

Nikasikia Tesha akiuliza hivyo, nami nikainua uso na kuwaangalia wote. Walikuwa wamesimama pande za milango ya mbele kwenye gari huku wananiangalia kwa umakini, na sijui ni nini tu, lakini kichwa changu kikaanza kuwa kizito, kama vile nimelewa, lakini nikajikaza zaidi na kuusogelea mlango ule wa gari tena.

"Ni kizunguzungu kidogo," nikamwambia Tesha hivyo.

"Usingizi ama?" Tesha akauliza.

"Labda," nikajibu hivyo.

"Dah, twende tuwahi, mi' mwenyewe nisije nikasinzia huku naendesha," Tesha akasema hivyo na kuingia ndani ya gari.

Nikamtazama Miryam usoni, naye akashusha macho yake yaliyokuwa yakinitazama kwa umakini bado, kisha akaingia ndani ya gari kimya kimya. Nikaiga hilo pia, naye Tesha akatuondoa hapo. Bado niliweza kuhisi kizunguzungu hicho kikiwa kinacheza kichwani kwangu kwa mbali kiasi, na mwanzoni hata mimi nilidhani labda ni uchovu, lakini muda si mrefu ningekuja kutambua kwamba ilikuwa ni tatizo.

★★

Mwendo wa dakika kama thelathini kutokea huko hospitali ukatufikisha makwetu, uzuri hakukuwa na misongamano kwa muda huo wa usiku, na tukawa tumefika mtaani kwetu kwenye mida ya saa nane iliyoikimbilia saa tisa. Tesha alipolifikisha gari nje ya geti lao, nikataka kushuka ili niwaache na kwenda kwa Ankia, naye akaniaga vizuri kabla ya kuwa wa kwanza kushuka ili akafungue geti lao.

Alikuwa amemtania dada yake kwamba akae tu kama Malkia na yeye ndiyo afanye kila kitu hapo, na baada ya yeye kutoka ndani ya gari, nikafungua mlango pia huku nikimwangalia Miryam kutokea nyuma. Kioo cha juu hapo mbele kiliuonyesha uso wake vizuri sana kwangu, akiwa ametulia tu na kutazama getini kwao, nami nikamwambia...

"Usiku mwema Miryam."

Hakutoa jibu, bali nikaona macho yake yakitazama yangu kupitia kioo hicho, kisha akaacha kunitazama tena. Nikaona nijitokee nje tu, na kabla sijatoka nikasikia...

"Asante."

Nikageuka na kukitazama kioo tena, kukuta macho yake yamerudi kunitazama. Sauti yake tamu ilikuwa imetoa neno hilo zuri, nami sikujua ikiwa upana wake ulielekea suala la kumsaidia Soraya ama kumwambia yeye usiku mwema, hivyo nikamwonyesha tu tabasamu na kisha kutoka.

Nikaelekea upande wetu wa nyumba na kufungua geti la nje, kisha nikalifunga na kuelekea ndani. Muda ulikuwa umeenda, na kiukweli, bado kile kizunguzungu kilinisumbua. Nilipoingia sebuleni nikawasha tu taa na kuufunga mlango vizuri, kisha nikakaa kwenye sofa, nikihisi hali hii ni kama inanisukuma kuumwa, yaani kupatwa na ugonjwa au homa labda.

Nadhani Ankia hakuwa mbali sana kiusingizi au alisikia sauti za milango kufungwa ndiyo akaamka, kwani alitoka chumbani na kuja hapo nilipokuwa, akiwa ndani ya khanga moja na macho yake yakionekana kuwa mazito kiasi. Akakaa karibu nami.

"JC... T-shirt lako vipi? Mbona limechanika?" akaniuliza hivyo.

"Aa... nilikosa bendeji ya kufungia uvimbe wa Soraya, ikabidi nichane tu hapa," nikamwambia.

"Ahaa... sawa. Vipi lakini... Soraya anaendeleaje?" akaniuliza.

"Anaendelea vizuri. Ata... atakuwa sawa zaidi... ndani ya siku tatu au nne..." nikajibu hivyo na kushika paji la uso wangu.

"Vipi? Mbona hivyo?" akaniuliza.

Sikutoa jibu, bali nikafumba macho kwa kuwa na kichwa nacho kilianza kuniuma sasa.

"JC... ni nini? Kichwa kinauma?" Ankia akaniuliza na kunishika mkononi.

"Na kizunguzungu. Sijui homa inanivizia?" nikasema hivyo.

"Eh... unahitaji kupumzika wewe. Sina hata Panadol ndani... ngoja nikuletee maji," akaniambia hivyo na kuelekea jikoni.

Hii hali ilinikera. Ilikuwa kama vile nimelewa lakini kwa njia isiyofurahisha kama pombe ifanyavyo, muulize mnywaji atakuelewesha.

Ankia akarudi tena na glasi yenye maji na kunipa ninywe, naye akauliza, "Ulikula?"

Nikatikisa nyusi kukubali tu japo ni mishkaki tu ndiyo iliyokuwa ya mwisho kuliwa, na ile nimekunywa na kumeza maji kidogo tu, nikakunja sura na kuyaangalia maji hayo kimshangao.

"Nini tena?" Ankia akauliza.

Nikamwangalia na kuuliza, "Mbona maji machungu?"

"Nini? Yana... yana uchungu gani?"

Akauliza hivyo na kuyachukua ili aonje, maji yaonjwe eti, naye akaniangalia baada ya kuyanywa kidogo.

"Maji yana uchungu gani haya JC?" akaniuliza tena.

Nikamtazama kwa mkazo kiasi, kisha nikaichukua glasi na kuyamaliza yote yaliyobaki. Mwanzoni yalipita bila uchungu wowote kusikika, lakini mwishoni ndiyo nikasikia uchungu. Hapo nikagundua kwamba siyo maji, bali mate yangu ndiyo yalikuwa machungu. Ohohoo!

Nikawa nimeelewa kilichokuwa kinaendelea, nami nikaiweka glasi mezani na kufunika mdomo kwa kiganja huku nikitikisa kichwa kwa kutoamini.

"Wewe... JC... mbona sikuelewi? Una shida gani?" Ankia akaniuliza hivyo.

Nikamwangalia na kusema, "Nitakuwa nimeingiwa na sumu, Ankia."

"Sumu?! Sumu ya nini?" akauliza.

"Ya huyo nyoka," nikasema.

"Eti?!" akauliza kwa sauti ya chini kimshangao.

"Ah... aisee! Ningejua mapema ningebeba hata dawa, asa' hapa mpaka kesho tena..."

"We' JC em' acha masihara basi, sumu gani imekuingia? Kwani huyo nyoka alikung'ata na wewe? Au amekurushia mate?" Ankia akaniuliza kwa kujali.

"Usijali, nitakuwa sawa. Asubuhi nita... nitatafuta dawa. Nahitaji kulala, naomba uni...."

"JC siwezi kuacha kujali wakati unaongelea masuala ya sumu. Ukiingia huko chumbani kulala afu' ukapitiliza?"

"Ankia..."

"Unafikiri utaniweka wapi mimi? Utaniachaje? Watu wa huko nje watanielewa? We'... em', kama vipi twende turudi huko hospitali maana haiwezekani..."

"Ankia... nisikilize," nikamkatisha kwa kumshika mikononi.

Sauti yangu ilikuwa imeanza kuwa dhaifu, naye akatulia na kuendelea kunitazama kwa kujali.

"Sijang'atwa... ni kiasi kidogo cha sumu ndo' kimeniingia... kidogo sana... ndo' dalili zinaonekana sa'hivi," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Imekuingiaje?" akauliza kwa sauti ya chini.

"Nafikiri... wakati namfunga Soraya... nilitumia mdomo kukaza nguo karibu na... uvimbe wake, kwa hiyo..."

"Ukawa umeilamba sumu bila kujua?"

"Labda midomo iliigusa kidogo tu, au ilikuwa rahisi kunirukia shauri ya mvua, sijajua ila... usijali. Ninajua dawa za kutumia. Hii itanipa tu homa kwa hiyo... nakuomba... kesho utanisaidia kutafuta dawa nitakazokuelekeza, sawa?" nikamwambia hayo.

"Lakini JC... me naogopa..." akasema hivyo.

"Usijali Ankia. Niamini. Me si ndiyo mganga mfawidhi hapa, au? Umesahau?"

"Acha masihara yako... hii ni kitu serious..."

"Ahah... usijali mwaya... ngoja tu nikalale..."

"Nalala na wewe chumbani kwako leo. Twende," akasema hivyo na kusimama.

"Hamna haja Ankia, kwanza..."

"A-ah... hapana. Twende, nalala karibu yako. Ukifia humo je? Hapana. Nyanyuka," Ankia akasisitiza.

Dah! Sikuwa na namna yoyote ila kumkubalia tu maana alionyesha kunijali sana, na kiukweli nilihitaji msaada wake kwa sababu hata ingawa nilikuwa nimejaribu kuonyesha wepesi katika hilo suala, maneno yake yalikuwa sahihi; lilikuwa jambo serious.

Sumu ya nyoka kidogo tu kuniingia na kukaa huo muda wote mwilini mwangu kulikuwa kumeshadhoofisha maeneo mengi ya ndani kwenye kinga mwili, na nilijua ingeendelea kunidhoofisha zaidi hasa kwa sababu masaa mengine yangepita mpaka kufikia wakati ambao ningepata dawa za kutumia kuikata. Na hakukuwa na namna, subira tu ingehitajika hata kama sikutaka kufa mapema.

Ankia akaniingiza chumbani kwangu na kunisaidia kuzitoa nguo zangu mwilini, kisha nikapanda kitandani na kulala. Ningeweza kuhisi namna alivyoufunika mwili wangu kwa shuka, huku feni ikiwa imewashwa na kupuliza upande niliolaza mwili wangu. Nilikuwa hadi nimeanza kuona maruerue kichwani shauri ya kizunguzungu kilichokuwa kinaongezeka, na pole kwa pole usingizi ukanivuta na kuniingiza mahala pazuri pa pumziko la muda mfupi, endapo kama sumu isingelifanya kuwa refu.

Dah pole sana Mwamba JC
 
Back
Top Bottom