Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Nimekuja kuamshwa na Ankia kukiwa kumeshakucha, na kiukweli niliweza kuhisi namna gani hali ya mwili wangu ilivyozidi kuwa mbaya. Kichwa kiliuma, nilihisi kichefuchefu kizito, na mikono haikuwa na nguvu za kutosha. Koo ilisugua vibaya mno kiasi kwamba nikaanza kukohoa kwa nguvu sana, naye Ankia akaniletea maji ya kunywa.

Inaonekana alikuwa ameshaamka hiyo asubuhi na kwenda kufata dawa za kupunguza maumivu ya kichwa, kwani akanipatia Panadol ili nimeze kwanza, kisha baada ya hapo akaniuliza ni dawa zipi ambazo ningepaswa kutumia. Nikafikiria dawa nzuri za kunisaidia kuondoa madhara ya sumu iliyoniingia, nami nikamwomba karatasi na kalamu ili nimwandikie. Nilipomaliza nikampa, kisha nikamwelekeza ilipo wallet yangu ili achukue pesa na kwenda kunifatia. Huyoo akaondoka.

Sikutoka kitandani kabisa, nilikuwa nimejilaza tu huku nikiendelea kukohoa. Nikawa nachukua maji na kunywa kidogo kidogo, mate yakiwa machungu kinoma, ndiyo baada ya dakika chache simu yangu ikaanza kuita. Ilikuwa kwenye meza ile ndogo hapo chumbani nadhani, lakini sikuweza hata kujinyanyua na kubaki nimejilaza tu. Baridi lilikuwa limeuingia mwili wangu kwa kasi kubwa, lakini wote ulikuwa umechemka kama pasi.

Ankia akawa amerejea hatimaye, na wakati huu hakurudi na dawa pekee, bali akawa amekuja pamoja na Tesha. Inaonekana walikutana huko nje na kuambiana kuhusu hali yangu, na kijana ndiyo akawa amekuja kuniangalia. Ankia akanipatia dawa, nami nikanywa kwa mtindo wa mpangilio uliotakiwa kwa kila dawa, kisha nikajikalisha kitandani hapo na kumwangalia Tesha. Alikuwa amevalia kwa njia iliyoonyesha alitaka kutoka ama ndiyo alikuwa amerudi kutoka sehemu fulani.

"Vipi kaka... unatokea wapi?" nikamuuliza.

"Ah... sitokei sehemu, nilikuwa ndo' nimejiandaa, naenda na da' Mimi hospitali kumcheki Tausi," Tesha akaniambia.

"Miryam haendi kazini?" Ankia akamuuliza.

"Anaenda. Ataniacha hospitali, ye' atapitilizia kazini, maana leo atakuwa huko peke yake," Tesha akasema hivyo.

"Aaa.... sawa..." Ankia akajibu hivyo.

"Mwanangu, unaonekana kutafunwa sana na hiyo sumu. Twende hospitali," Tesha akasema.

"Me mwenyewe namwambia hivyo, ila hataki. Ona anavyonyong'onyea," Ankia akasema hivyo kwa kujali.

"Ahhah... msijali, nitakuwa sawa. Ona... hizi dawa zitanisafishia hiyo kitu... kufikia kesho-kutwa... naamka fresh," nikawaambia.

"Kweli mwanangu?" Tesha akauliza.

"Uhakika," nikamwambia.

"Dah... haya bana. Ila unajua nini? Ngoja nikaongee na ma' mkubwa hapo... huwa anajua dawa dawa anaweza akakutengenezea nyingine ikakusaidia," Tesha akasema.

"Za mitishamba?" Ankia akamuuliza.

"Eee. JC... pole mwanangu. Ngoja me niende, nikitoka tu huko nakuja tena, sawa? Zamu hii na chips," Tesha akasema.

Nikacheka kidogo kwa kukohoa, naye akatuaga tena na kuondoka.

Ankia akakaa karibu nami na kunishika shingoni kwa kiganja chake, naye akafanya, "Sss... Mungu wangu! JC unachemka! Me naogopa jamani..."

Nikatoa tabasamu hafifu na kuangalia chini.

"Kwa nini hutaki kwenda hospitali?"

"Kwa sababu najua nitakuwa sawa. Ni homa ya moto tu, itaisha, wala usi-panick..."

"Siyo ku-panick... em' chukulia labda tuseme sumu imekuingia nyingi, we' unachukulia ni kidogo, ikiyakata maini je? Unatakiwa uende hospitali uangalie... hata kama we' ni daktari bwana..." akaniambia hivyo.

Nikatabasamu na kusema, "Kama ningeenda hospitali, ningepoteza muda maana hata na huko wangenipa hizi hizi dawa ulizoleta... kwa hiyo usijali. Amini hii ndiyo hospitali bora zaidi, na we' ndiyo muuguzi wangu."

Nikamfinya shavu kidogo, naye akatabasamu na kukishika kiganja changu.

"Unaenda dukani?" nikamuuliza.

"A-ah, sitaenda. Nataka kukaa kukuangalia," akasema hivyo.

"Ah, nenda tu kafungue. Nitakuwa sawa."

"Hapana JC. Unaumwa mno, na hapa hamna mtu. Lazima nikae kukuangalia..."

"Ankia..."

"Unaweza ukazidiwa. Ama, niende dukani halafu nimwambie mama Chande aje asimame badala yangu?"

"Aa wee... usifanye hivyo. Basi tu, baki," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo na kusema, "Sawa. Nilipopita hapo kwao Tesha nikawaambia kuhusu hali yako. Na Miryam pia."

"Amesemaje?"

"Hajasema kitu. Wengine wametuma na pole, watakuja kukuona, ila yeye... hana habari. Ameonyesha kama hajali yaani," akaniambia hivyo.

Nikatazama chini kwa huzuni kiasi.

"Labda usiendelee kumfosi wala nini..." akasema hivyo.

"Sijamlazimisha kwa lolote. Ana hisia kwangu, hilo nalijua. Anajipinga tu ye' mwenyewe... akhh... kwa sababu anaogopa," nikamwambia.

"Mh? Haya. Usimtetee sana lakini, huwezi kuwa na uhakika," akaniambia hivyo.

Nikafumba macho tu na kuegamia mto.

"Ngoja nikakuwekee chai. Ule upate nguvu," akaniambia hivyo.

Ni hapa ndiyo nikajihisi vibaya zaidi kifuani, kichefuchefu kikitaka kutoa kitu fulani kwa kasi, nami nikaanza kuhangaika na kujivuta mpaka upande mwingine wa kitanda huku nikiukaza mto kwa kiganja changu. Ankia akauliza vipi, na bila kutoa jibu nikajikuta naanza kutapika chini kwa msukumo wenye nguvu sana!

Nilijihisi vibaya mno nilipomaliza, naye Ankia akaja na kuanza kunisafisha. Akaniweka katika mkao mzuri kitandani tena, nami nikamwona akitoka na kurudi tena chumbani humo na vitu vya kusafishia matapishi. Nikamwomba samahani kwa kuchafua chumba lakini akaniambia nitulie tu, naye akaja tena kwangu na kuangalia hali yangu.

Nilijihisi vibaya kweli ila nilijua hiyo ndiyo iliyokuwa hatua ya mwanzo ya usafishaji wa sumu mwilini mwangu, naye Ankia akanifatia chai ili nije kunywa. Nikajitahidi kunywa kavu, taratibu tu mpaka kumaliza kikombe, kisha nikajilaza tena. Kifua kilizungusha uchafu hapo katikati kwa njia iliyojaza mate mengi, na Ankia akawa ameleta ndoo na kuiweka pembeni ya kitanda ili nikijisikia kutema mate au kutapika basi niachie kila kitu humo. Dah! Leo na mimi daktari nikawa mgonjwa. Sikuwa nimeumwa kwa kitambo sasa, kwa hiyo hii hali ilikera kupitiliza.

Mara mbili, mara tatu hivi tena nikawa nimerudia kutapika, kwenye ndoo, naye Ankia hakutoka pembeni yangu hadi usingizi wa kigonjwa uliponichukua tena; ikiwa bado ni asubuhi.

★★

Nikaja kuamka tena ikiwa imeshafika mchana, na bado nilijihisi vibaya na mzito sana, lakini nikajikalisha kitandani hapo na kutulia tu. Wakati huu nilikuwa ndani ya T-shirt nyeusi ya mikono mifupi na bukta yangu ya michezo, nikiwa sina kumbukumbu ya kuzivaa nguo hizi, lakini ikawa wazi kwamba ni Ankia ndiye aliyenibadilishia bila shaka. Hakuwemo chumbani humo wakati huu, nami nikajitoa kitandani ili niende kukojoa.

Mwili ulikuwa dhaifu kiasi, lakini nikafanikiwa kutoka chumbani na kufika sebuleni. Hapo nikamkuta Ankia akiwa amekaa sofani, akichambua mchele kwenye ungo, na baada ya kuwa ameniona akanifata na kuniuliza kwa kujali ikiwa nilihitaji chochote. Nikamwambia ninaenda tu uani, naye akaona anisindikize kabisa ili kuhakikisha siangukii huko huko.

Mambo yakaenda vizuri mpaka niliporudi ndani tena, naye Ankia akasema ananiletea chakula nilipokuwa naelekea chumbani. Kwa jinsi nilivyojihisi vibaya sikudhani hata ikiwa chakula kingepita, lakini nilijua kula ilikuwa muhimu. Dawa nilizotumia zilikuwa kali, na ningehitaji kunywa maji mengi sana.

Nikajikalisha kitandani tena mpaka mwenye nyumba wangu alipoingia ndani hapo, mikononi mwake akiwa ameshika sahani yenye chips mayai iliyochanganyiwa tomato. Kilionekana kutoka kupashwa sijui ama labda alipika yeye mwenyewe, lakini harufu yake ilinipa shida kwa sababu iliongeza kasi ya kichefuchefu nilichohisi kifuani; mayai hayo.

Akakileta karibu nami na kukaa kitandani pia, nami nikamtazama machoni kwa njia iliyoonyesha hisia mbaya.

"Vipi... unajihisi kutapika?" akaniuliza.

Nikatikisa kichwa kukanusha.

"Kula basi. Haujala toka asubuhi," akaniambia.

"Saa ngapi?" nikamuuliza.

"Saa tisa."

"Ulinibadilishia nguo eh?"

"Ndiyo. Ulikuwa una-sweat kweli..."

"Hata sikumbuki..."

"Ulikuwa umezidiwa wewe... ndiyo maana unatakiwa kula..."

"Mhm... na wewe haukuzidiwa ulipomwona huyu mshkaji wangu?"

"Ahahah... acha basi JC! Unaumwa lakini huachi utani jamani... hebu kula..." akaniambia hivyo.

Akawa amekata kipande cha chakula na kunipa nile, nami nikakipokea na kuanza kutafuna. Ilikuwa kwa shida kweli, lakini sikuwa na jinsi. Dawa nilizotumia ningepaswa kunywa mara mbili kwa siku kwa hiyo za mrudio wa mara ya pili ningekunywa jioni, na hivyo mwili ungetakiwa kuwa na kiwango fulani cha nishati ili zifanye kazi vizuri.

Wakati nikiendelea kulishwa taratibu na Ankia, akawa ameniambia kwamba kwa muda huo niliokuwa nimelala kutokea saa tano mpaka kufikia hii saa tisa, Bi Jamila, Bi Zawadi, pamoja na Mariam walikuja kuniangalia. Tesha pia alirudi na kunijulia hali baada ya kutoka kumsalimia Soraya kule hospitali. Akasema Bi Zawadi alikuwa nyumbani wakati huu akinitengenezea dawa ya mitishamba kwa hiyo angekuja baadaye tena.

Nikauliza kuhusu Miryam, naye Ankia akaniambia kwamba mwanamke huyo hakuonyesha utayari wa kuja kuniona, ama tu kunitumia pole hata mara moja ingawa alikuwa anajua ninaumwa kutokana na kumsaidia Soraya. Yaani, Ankia alimpigia simu Miryam kumweleza kuhusu hali yangu, na baada ya Miryam kuonyesha hajali kutokana na kuwa na mambo mengi, Ankia akawa amemwambia anajua kuhusu mimi kumpenda huyo mwanamke. Alimsihi aje kuniona angalau, kwa kuwa uwepo wake ungenifariji, lakini Miryam akamkatia simu.

Taarifa hii ikanifanya nijihisi vibaya kiasi. Ankia akasema hana uhakika sana ikiwa Miryam alifanya hayo makusudi tu ili kunivunja moyo ama alimaanisha, nami nikamwambia hapana, hayo yalionyesha tu kwamba bado moyo wake haukuwa tayari kuamini hisia zake yeye mwenyewe, kwa hiyo kupisha muda ili utayari huo umwingie bado lilikuwa jambo muhimu.

Nikamwambia ila haikuwa na haja ya kufanya hayo yote mpaka kumwambia huyo mwanamke kwamba anajua nilimpenda, lakini Ankia akasema alikuwa amepandwa tu na hisia ndiyo sababu maneno yakamtoka. Alionyesha kunijali sana, na nilithamini hilo.

Basi, baada ya kujitahidi kwingi kula nikawa nimehisi kutosheka nilipomaliza robo tatu ya hiyo chips, nami nikamwomba Ankia anipe tu maji mengi ili ninywe. Akatoka hapo na kwenda sebuleni huko, nami nikaanza kusikia sauti za maongezi ya kukaribishana, ikionekana kuna mtu kaingia.

Nikaendelea kukaa tu huku nikihisi mapigo yangu moyoni yalivyotimka haswa, na hapo chumbani akawa ameingia mama mkubwa mweupe; Bi Zawadi. Alikuwa ameshikilia bakuli lenye muundo kama hotpot ya plastiki, naye akafika karibu na kitanda.

Nikamwangalia na kuachia tabasamu hafifu, naye akasema, "Mgonjwa... umeamka. Unajisikiaje?"

"Hivyo hivyo tu. Ila najua umekuja na zawadi kwa hiyo nitajisikia vizuri zaidi. Shikamoo?" nikamwambia hivyo na kumwamkia.

Akatabasamu na kusema, "Marahaba."

Ankia akawa amefika ndani humo tena huku akiwa ameshikilia chupa yenye maji ya kunywa, naye akamuuliza Bi Zawadi, "Ndiyo hiyo dawa?"

"Eee... ndiyo yenyewe. Nimetengeneza hii... ilikuwa ngumu kweli kuyapata haya majani, ila kuna rafiki yetu kule Chamgando, yule mama mchungaji, unamkumbuka JC?" Bi Zawadi akaniuliza.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Eeh, huyo ndiyo akawa ameniambia huko yapo... ndiyo nikaomba yaletwe. Yamefika muda siyo mrefu ndiyo nikayachemsha," Bi Zawadi akasema.

Harufu ya hiyo dawa ikaanza kunichokonoa vibaya puani, nami nikakohoa na kisha kupiga chafya kwa nguvu.

"Ahah... ona, imeshaanza kufanya kazi hata kabla hajainywa," Bi Zawadi akasema hivyo na kukaa kitandani.

"Siyo chungu sana?" nikamuuliza hivyo huku nimekunja sura.

Akapiga ulimi kidogo na kusema, "Acha kudeka bwana. Ina uchungu ndiyo lakini ni nzuri sana. Ukishakunywa itasafisha uchafu wote wa hiyo sumu... utabaki kama umepigwa deki mwilini."

Nikiwa naonyesha manung'uniko usoni, nikamwambia, "Cheupe jamani... me uchungu wapi na wapi?"

"Hakuna dawa tamu. Hizo za hospitali zinachukua muda. Hii ni leo leo tu... utaanza kuona. Inakata kichefuchefu, kuharisha, kutapika, ila ni baada ya kuwa umeyamaliza hayo mambo," akasema hivyo.

"Iih... kumbe hadi na kuharisha... mbona me siharishagi?" nikamtania.

Ankia akacheka kidogo, naye Bi Zawadi akaniangalia kwa macho ya kukerwa, lakini kiutani.

Nikatabasamu kidogo na kusema, "Sawa. Nitakunywa. Au natafuna na hayo majani?"

"Hamna, unakunywa tu. Ni nzuri sana, utaona. Mimi mwenyewe anaijua ndiyo maana akahangaika hivyo kuitafuta mpaka ikaletwa," Bi Zawadi akasema.

Nikamwangalia machoni kwa umakini baada ya yeye kusema hivyo.

"Miryam ndiyo amefanya kuitafuta kwa ajili ya JC?" Ankia akamuuliza Bi Zawadi.

"Eee... nilipowasiliana na huyo rafiki yangu, akaniambia anaweza kuitoa huko Chamgando lakini kuna gharama. Ndiyo Mimi akazishughulikia mpaka ikafika haraka," Bi Zawadi akamwambia.

Nikamtazama Ankia machoni na kuachia tabasamu hafifu, na nafikiri akiwa ameelewa nilimpa tabasamu la furaha, yeye pia akatabasamu kidogo.

"Kwa hiyo jitahidi uinywe yote iishe. Sawa?" Bi Zawadi akaniambia.

"Sawa. Nitaimaliza yote kabisa... maana imeletwa kwa upendo," nikamwambia hivyo.

"Umeona eh?" Bi Zawadi akasema.

Ankia akatabasamu, nami nikatikisa kichwa kukubali.

"Haya anza kuinywa sasa hivi. Umalize bakuli lote," Bi Zawadi akasema hivyo kwa uchangamfu.

Nikatabasamu na kuanza kuinywa dawa hiyo, mwanamama huyu akiwa ananinywesha taratibu.

Nilikuwa nimehisi kufarijika kiasi moyoni baada ya kujua kwamba dawa hii ilifika hapo kwa jitihada za Miryam pia, kwa hiyo hata sikukazia fikira uchungu wake kabisa na badala yake kuiona kuwa tamu sana. Baada ya Bi Zawadi kuninywesha yote, Ankia akanipa maji, nikanywa mengi kiasi, kisha akaniambia nijilaze tena ili kupumzika kwa mara nyingine, nami nikaridhia hilo.

Nikamshukuru Bi Zawadi kwa msaada wake, naye ndiyo akanyanyuka na kunivutia shuka ili lifunike miguu yangu mpaka kiunoni; ule upendo tu kama wa mama. Nikajilaza tena nikiwa nimefumba macho, nikiipa akili na mwili utulivu zaidi baada ya kunywa dawa na kula chakula.

Amani ya akili niliyopata kwa kujua kwamba Miryam alionyesha kunijali ilifanya nijikunje tu kitandani hapo huku nikivuta taswira ya sura nzuri aliyokuwa nayo, na masaa yakazidi kusonga nikiwa nimejilaza tu kitandani mpaka siku ilipoanza kulikaribisha giza.

★★

Ankia akawa amerejea tena baada ya kutoka kufanya kazi zake, naye akanishauri kwenda kuoga ili kuushusha zaidi uchovu wa mwili. Sikuwa nimetapika tena ingawa kichefuchefu kilikuwepo, nami nikatii agizo lake na kujiandaa kwa ajili ya kuoga. Alikuwa na nia ya kuchoma dawa za kuua mbu kwa wakati huu, hivyo nilipotoka kwenda huko bafuni akawa ametimiza kusudi lake. Yote kwa ajili yangu.

Ankia alikuwa anafanya mambo mengi ambayo nilitamani sana kuyapata kutoka kwa Miryam, kiasi kwamba ningeweza hata kuhisi vibaya moyoni kwa kuwa upendo wangu haukuwa kwa Ankia, aliyejitoa sana kwangu, na badala yake moyo wangu ulikuwa umetekwa nyara na mwanamke ambaye bado aliukimbia. Ila si ndiyo maana nimesema "bado?" Ningemkamata tu. Yaani Miryam ningemshika tu.

Mbu walipouawa, chumba kikawa chenye amani zaidi, kwa hiyo niliingia tu na kujilaza kitandani kama mgonjwa awaye mimi. Usiku ulikuwa ukizidi kuingia, na sikuwa na hamu ya kushika simu maana hata kama ningebeba kalamu ingeonekana kuwa nzito. Ankia kama kawaida yake aliendelea kunionyesha ananijali sana kwa kuleta chakula kwangu tena, nami nikala kiasi na kutosheka, kisha nikapitisha muda mfupi na kunywa dawa za hospitali.

Akaendelea kukaa pamoja nami chumbani hapo kunipigisha story, na wakati huu kilichokuwa kikisumbua kiasi ilikuwa ni kikohozi cha mara kwa mara, lakini kichefuchefu kilikuwa kimefifia. Ndani ya muda huu, ikiwa ni saa tatu, Bi Jamila, Bi Zawadi, Tesha, Mariam, pamoja na mama Chande na yule Fatuma wa pale dukani pia, wakawa wamekuja kunisalimia tena na kunipa pole, nami nikafurahia uwepo wao pamoja nami. Bi Zawadi alikuwa na imani ningeamka vizuri sana kesho, ila kama nisingeamka vizuri, basi angenichemshia dawa tena.

Baada ya mgonjwa kutembelewa na wapendwa wangu, nikaagwa hatimaye kwa kusisitizwa nilale mapema usingizi kama wa mtoto, na Ankia akiwa muuguzi wangu angetakiwa kuniangalia kwa umakini. Wapendwa wakaondoka na kutuacha mi' na Ankia hapo, ikiwa ni mida ya saa nne sasa. Nikamuuliza Ankia ikiwa Miryam alikuwepo kwake, naye akasema ndiyo, alikuwepo.

Ankia alikuwa ameshaanza kuwaza kwamba huenda Miryam hakuhisi vile nilivyohisi, na labda niwe makini kile nilichodhani kuwa upendo kumwelekea mwanamke huyo kikawa ni uraibu tu (obsession) ambao ungekuja kuniachia maumivu mengi. Nikamwambia naelewa, lakini yaani inaonekana Miryam alikuwa akipambana sana na hisia zake, kwa kujitahidi kuonekana hanijali, lakini najua alikuwa ananijali.

Nilijua alikuwa amenipenda, lakini tu hakuwa ametambua hilo, au alilitambua lakini hakutaka tu kulikubali. Nisingekata tamaa mapema namna hii kwa sababu ndiyo kwanza kuanza nilikuwa nimeanza kumwonyesha kwamba simtanii, kile nilichohisi kwake kilikuwa cha kweli. Nikamwomba tu Ankia asiwe na hofu juu yangu, kwa sababu moyo wangu uliridhia kwa asilimia zote kumpenda yule mwanamke, na ningeendelea kumwonyesha hilo.

Ankia akawa hana neno, naye pia akanisisitizia kulala mapema. Alikuwa anataka kukaa kuniangalia lakini nikamwambia hakukuwa na haja, kwa sababu nilijisikia vizuri kiasi, hivyo naye pia aende kupumzika. Alikuwa na wasiwasi, lakini nikasisitiza akapumzike, mimi ningekuwa sawa. Kwa hiyo dada wa watu akaniacha na kuzima taa ya chumba changu, huku akisema angekaa kidogo sebuleni kisha kuja kuniangalia, halafu ndiyo angeenda kulala.

★★

Haya, nikavuta shuka. Sikutaka kuwa mzigo sana kwa Ankia, ila bado sikujisikia vizuri kivile. Nilikuwa nausaka usingizi, huku nikikohoa mara kwa mara, nao usingizi ukawa unakuja ule wa kuniliwaza kidogo halafu unapotea tena kunifanya nihisi jinsi mwili wangu ulivyoshikwa na baridi kali, lakini sikufumbua macho na kuendelea kujikunyata kitandani hapo.

Muda ulionekana kuzidi kutembea, nilihisi kama vile masaa mengi yalikuwa yanapita ila usiku ukatulia pale pale. Nikaendelea kuvumilia tu, nikikohoa mara kwa mara, baridi likiwa kali mwilini, ndipo nikahisi shuka langu linapandishwa juu kwenye mwili ili kuufunika vizuri. Nilikuwa nimelalia ubavu, na kwa kujua huyo alikuwa Ankia, nikajigeuza taratibu ili nimsemeshe, kumwambia tu akalale.

Akanishika na kwenye paji la uso, nami nilipofumbua macho kumtazama, nikaona taswira ya uso wa Miryam, akiwa anaonekana kuwaza sana juu ya hali yangu baada ya kunishika pajini. Nikafumba macho na kufumbua kivivu, na taswira yake ikabaki kuwa hivyo hivyo.

Nikasema kwa sauti ya chini, "Ankia... akh.. kweli mapenzi yataniua. Nimeanza hadi... akh... kumwona Miryam usoni kwako ahh..."

Akanifunika vizuri zaidi na kuondoka hapo, nami nikafumba macho tu. Baada ya muda mfupi, nikaanza kuhisi kitu chenye kulowana kikipita kwenye paji la uso wangu, usoni, na shingoni, kama kitambaa, nacho kikawa kinatembezwa mpaka mikononi mwangu pia. Nikafumbua macho taratibu ili nimwangalie Ank.... si ndiyo kumwangalia usoni vizuri nikawa nimetambua kwamba haikuwa Ankia!

"Miryam?"

Nikaita hivyo kwa sauti dhaifu na kukohoa kidogo, naye akaonekana kuniangalia usoni kwa umakini.

"Miryam? Ni wewe... au naota?"

Nikauliza swali hilo huku mapigo ya moyo wangu yakianza kwenda kasi, yaani pamoja na baridi niliyohisi mwilini lakini bado msisimko uliotokana na kujua Miryam yuko hapo niliuhisi pia vizuri sana.

Akaendelea tu kunikanda hapa na pale, mimi nikiwa nimeingiwa na furaha tele moyoni, lakini hali yangu ikanizuia kuonyesha hilo kikamili.

"Ahh... hii surprise nzuri Miryam..." nikasema hivyo huku nikimtazama usoni.

Niliweza kuona kwamba alikuwa amevaa kale kaPunjabi kake ka zambarau, huku nywele zake akizibana nyuma ya kichwa chake, nami nikatoa tabasamu hafifu. Alikuwa anafanya nini hapa sasa hivi? Kwanza aliingiaje humu usiku wote huu? Ikiwa alikuwa jini, basi moyo wangu ulikuwa umependa jini la maana sana!

Niliweza kuona stuli karibu na kitanda, ikionekana ndiyo alikuwa akikaa hapo na kuniangalia, kisha angeanza kunikanda upya tena. Si unajua usiku homa ndiyo huwa zinavuta zaidi? Kwa hiyo nilikuwa najihisi mzito mno wakati huu, lakini niliridhika mno kujua mwanamke huyu alikuwa kando yangu kuonyesha namna alivyonijali. Kila kitu nilichomwambia Ankia muda ule kilizaa matunda upesi sana!

Baada ya kuhisi ameacha kunikanda kwa sekunde chache, nikafikiri labda alikuwa anataka kuondoka, hivyo nikaita, "Miryam..."

Nikatazama pale kwenye stuli na kukuta amekaa huku akinitazama tu, nami nikapata ahueni.

"Akh... Miryam... usiniache... usiondoke... please..." nikamwambia hivyo huku nikijaribu kujinyanyua.

Akanisogelea na kuulaza mwili wangu tena, naye akasema, "Usijali. Siondoki. Lala tu."

Sauti yake ilikuwa ya wimbi tamu sana lililopiga kona za masikio yangu mpaka kufikia moyo na kuutuliza, nami nikatulia kweli na kumwangalia. Nilikuwa hadi nataka kuuliza muda huo ni saa ngapi, lakini sikujali tena.

Akakaa kwenye stuli yake huku akiniangalia tu, na mimi bado nilikuwa napambana na hali yangu mbaya kiasi, ila niliweza kutulia kila dakika niliyofumbua macho na kuona kwamba bado alikuwepo. Chumba kilikuwa na giza lakini kwa mwanga hafifu wa taa kutokea nje ulifanya nimwone vizuri usoni.

Nikamwangalia tena, kisha nikamwita, "Miryam..."

"Bee..." akaitika.

Nikakohoa kidogo.

"Unahitaji nini? Maji?" akauliza hivyo kwa sauti yenye kujali.

Nikameza mate kidogo na kusema, "Hapana... hhh... wewe..."

Nikamwona akiangalia pembeni tu.

"Ninakuhitaji wewe..." nikamwambia hivyo.

Akaniangalia usoni kwa hisia.

"Miryam nakupenda... nakupenda sana we' mwanamke..." nikamwambia hivyo kidhaifu.

Akafumba macho yake taratibu na kuutazamisha uso wake pembeni.

Nilihisi kama vile maneno yangu yalikuwa yakimgusa kwa kiwango cha hali ya juu, lakini bado alikuwa anazikimbia hisia zake tu. Ningekuwa na vitu vingi sana vya kumwambia katika pindi kama hii, yaani tukiwa peke yetu tu kama hivi, lakini hali yangu nzito ikawa inanirudisha nyuma. Na kwa sababu ya uzito huo nikawa nimefumba tu macho tena, na usingizi wa moja kwa moja ukawa umenibeba.

★★★

Nimekuja kufumbua macho chumba kikiwa kimeangazwa kiasi kwa kitu kilichomaanisha kwamba palikuwa pamekucha, nami nikaanza kujinyoosha taratibu na kufikicha macho yangu mazito. Nilihisi hali ya uafadhali wa hali ya juu, ikiwa kama vile gonjwa lote lilikuwa limeniondoka, nami nikatulia kidogo kutafakari. Jana usiku, kama siyo kuota kwamba Miryam alikuwa hapa, labda nisingeamka vizuri namna hii. Nilikuwa nimehitaji sana mwanamke yule awe karibu nami kivile mpaka taswira yake ikanijia kwa....

Ile nimeshusha mkono mmoja usawa wa paja langu, nikagusa kitu kilichonifanya nitazame hapo upesi. Ih! Kulikuwa na mtu. Mwanamke. Alikuwa ameulaza uso wake usawa wa kiuno changu hapo kitandani, huku akikalia stuli iliyokuwa chini, na nywele zake laini na ndefu zilikuwa zimefumuka na kufunika kichwa chake chote. Miryam!

Kumbe haikuwa ndoto? Nikamtazama kwa hisia sana na kuachia tabasamu hafifu, kisha nikajivuta taratibu na kujilaza kwa ubavu ili nimwangalie vizuri. Alionekana kuchoka, na sababu ya kuchoka hivyo ilikuwa kukaa pamoja nami usiku wote mpaka kufikia sasa. Nikazigeuza nywele zake kutoka upande wa uso wake na kuzilaza kwa nyuma, nao ukaonekana vizuri zaidi.

Alikuwa anapendeza sana akiwa amefumba macho, uso wake mzuri ukitoa maana kamili ya neno "amani" kwa jinsi ulivyokuwa wa utulivu sana. Nikaanza kupitisha vidole vyangu kwenye nywele zake kupitia sikio lake moja, huku nikimtazama kwa upendo mwingi, naye akawa amefumbua macho yake taratibu.

Sikuwa nimeacha kutembeza kiganja kwenye nywele zake, kwa hiyo ile tu aliponyanyua uso wake ili anitazame, kiganja changu kikawa kimelishika shavu lake, na kidole gumba kikaugusa mdomo wake wa chini (lip). Hiyo ikafanya awe ananitazama huku nikiwa nimemshika usoni kwa wororo, halafu nikafanya umakusudi wa kukishusha zaidi kidole changu, na hivyo mdomo wake wa chini ukavutika kuelekea chini na kisha kurudi juu kwa kutikisika kiasi. Ah! Yaani... sexy as hell!!

Baada ya hicho kitendo changu, akaacha kuniangalia na kuutoa mkono wangu usoni kwake kwa kasi, kisha akajitoa kitandani na kuketi vizuri kwenye stuli huku akirekebisha nywele zake na macho.

Nikajivuta na kukaa kitako kabisa ili uso wangu uwe sawia na wake, nami nikasema, "Nimeamka nikifikiri usiku ilikuwa ni ndoto tu... kumbe kweli ulikuwa hapa..."

Akaendelea kujiweka sawa zaidi bila kuniangalia hata kidogo, uso wake ukiwa wa 'kununa' kama ilivyo kawaida ya mtu aliyetoka usingizini. Akaanza kuzibana nywele zake.

Nikamwambia, "Kidogo ulinifanya nikafikiria labda haunijali, au labda sitafika popote na jitihada ya kukuonyesha hisia zangu. Ila sasa hivi nitaacha kufikiria sana. Kila kitu umeshaonyesha wazi. Imebaki tu we' kuniambia... 'nakupenda pia.'"

Niliposema hivyo, akanitazama usoni hatimaye, nami nikawa namwangalia kwa utulivu tu.

Aliniangalia kwa macho makini sana, kisha akanishusha kidogo na kunipandisha, eti kiunoni mpaka usoni, halafu akanyanyuka na kugeuka ili aanze kuondoka. Lakini kwa sababu ya kutoangalia chini, akajikuta anakipiga kwa mguu chombo ambacho aliwekea maji ya kunikanda ile usiku, naye akatulia kidogo kwa sababu ya kutotarajia hilo. Hicho kibeseni kiliruka mpaka mlangoni!

"Nakupenda pia. Hayo ni maneno rahisi sana kunena Miryam, sema wewe ndiyo unajilazimisha kuyaona kuwa mazito. Niruhusu nikufundishe jinsi ya kuyatamka, na utakapoyatamka, iwe ni mimi tu ndiye utakayeniambia, na utapenda kuyasema kwangu..." nikamwambia hivyo kwa njia ya kishairi.

Alikuwa amesimama tu kwa kunipa mgongo wakati nilipokuwa nasema hivyo, kisha akaanza kuuelekea mlango. Akashika kitasa na kuufungua, lakini kabla hajatoka...

"Uko shuta kweli kuzikimbia hisia zako mwenyewe mpaka umesahau simu..." nikamwambia hivyo.

Akasimama, lakini hakugeuka upesi. Akiwa amenipa mgongo, najua alikuwa anajishauri kuhusu kurudi tena maana ni kweli alikuwa amesahau simu yake hapa kitandani, nami nikaichukua na kuinyoosha kumwelekea.

"Njoo uchukue," nikamwambia hivyo kwa upole.

Akageuka taratibu, akiwa ananiangalia kwa yale macho ya kujihami kwelikweli, kisha ndiyo akaanza kuja tena upande wangu. Akafika karibu na kuishika simu yake niliyokuwa nimemnyooshea, lakini akapata shida kuitoa kwa sababu niliikaza kwa vidole vyangu. Akanitazama usoni, mimi nikiwa namwangalia kiuchokozi kiasi, naye akajaribu tena kuivuta lakini akashindwa.

"Usishindane sana, wakati unajua moyo wako umeshashindwa na wangu tayari..." nikamwambia hivyo.

Akatulia kidogo na kunitazama machoni.

"Huwa naambiwa wewe siyo msahaulifu, Miryam. Lakini siku hizi eti umeanza kuwa msahaulifu sana. Na unajua ni nini kimekufanya mpaka umesahau simu?" nikamuuliza hivyo.

"Nini?" akaongea hatimaye, kwa sauti ya chini.

"Mapenzi," nikamjibu.

Akabaki kunitazama machoni kwa njia ilyojaa maanani ya hali ya juu sana.

Najua hilo neno halikuwa geni kwake, lakini nilipolisema ni kama lilikuwa likimwamshia hisia fulani hivi, kwa kuwa angezubaa kiasi katika kunitazama kama alivyofanya wakati huu. Nikaiachia simu yake, naye akawa ananiangalia machoni bado huku mimi nikimpa tabasamu hafifu, kisha akageuka na kuondoka zake.

Basi nikabaki kuutazama mlango hapo alipotokea huku nikihisi raha kweli yaani, kisha nikajivuta taratibu ili nitoke kitandani na kwenda kusafisha kinywa. Eh! Toka ile juzi tulipompeleka Soraya hospitali leo ndiyo ningetoka ndani nikiwa najihisi nafuu angalau, ilikuwa vita mbaya kupambana na sumu hata kama iliniingia kidogo.

Nikiwa ndiyo nimejitoa tu kitandani, nikasikia sauti ya Ankia ikiita jina la Miryam kutokea hapo sebuleni. Kisha ikaonekana kwamba wawili hao walianza kuzungumza, nami nikasogea mpaka mlangoni ili nisikilize maongezi yao. Mlango huu wa chumba uliachwa wazi kwa hiyo sauti zilisikika vizuri.

"Anaendeleaje sasa hivi?" sauti ya Ankia ikauliza.

"Homa imepungua... nenda kamwangalie..." Miryam akamjibu.

"Hakuna haja. Najua yuko poa maana umekaa naye usiku wote," Ankia akasema hivyo.

Sikusikia Miryam akitoa jibu, nami nikatabasamu kidogo.

"Unajua Miryam... nilikufikiria vibaya mwanzoni. Nilidhani haumjali kabisa, lakini wewe kuja jana usiku wa saa sita ili kuangalia hali yake na kukaa naye mpaka kukucha... kumenifunulia mambo mengi..." Ankia akasema.

"Mambo gani nawe Ankia? Nilikuja tu kumwona... si anaumwa? Kuna uajabu gani hapo?" Miryam akamuuliza.

"We' huuoni uajabu uliopo? Ndugu zako wote wamekuja kumwona mapema, lakini wewe ukasubiri mpaka baadaye ndiyo ukaja, na umekaa naye mpaka asubuhi. Hakuna cha ajabu hapo rafiki yangu?"

"Hakuna uajabu wowote. Nilikuja tu kumwona mgonjwa. Basi."

"Mm... kweli?"

Miryam akabaki kimya.

"Hebu litoe hilo pazia lililofunika macho yako Miryam. Upendo ulionao kwa huyu kaka unajionyesha kabisa. Unaukataa kwa nini? Hauoni kwamba siyo yeye tu ndiyo unayemwonea, ila na wewe pia unajionea?" Ankia akamwambia hivyo.

"Ankia jamani... mimi simpendi. Mbona unalazimisha? We' ni Mungu uuone moyo wangu?" Miryam akamuuliza hivyo.

Nikatabasamu zaidi na kuangalia chini.

"Ahahah... mimi siyo Mungu kweli, lakini ni mwanamke mwenzako. Nimekuchungulia jana. Nimeshaona jinsi unavyomwangalia, ni kama tu yeye anavyokuangalia... na macho yako yanaonyesha namna gani unavyomhamu huyu mwanaume. Em' uje kujaribu kumwangalia kwa mara nyingine machoni halafu umwambie humpendi... ndiyo nitakuamini," Ankia akamwambia hivyo.

Nilipenda sana jinsi ambavyo Ankia alionyesha kuniunga mkono kwa moyo wake wote kama rafiki, nami nikaona niyape maneno hayo aliyoyasema mwishoni uthibitisho zaidi. Nikatoka chumbani hapo na kuielekea sebule, nikiwa natembea taratibu tu, nami nikawaona wanawake hao wakiwa wamesimama usawa wa masofa kuukaribia mlango.

Miryam aliponiona nawafata, akanitazama machoni kwa ile njia ya 'kuendelea kunitazama,' yaani kwa kila hatua niliyopiga kuwaelekea hapo, aliniangalia machoni kwa njia yenye mzubao kiasi, kana kwamba amepotea kifikira kwa kunitazama tu.

Nikafika karibu yao zaidi huku mimi pia nikimwangalia Miryam kwa yale macho yangu yenye ushawishi, naye Ankia akaachia tabasamu la furaha baada ya kuona Miryam amezama katika kunitazama. Bibie akawa kama amejishtukia, naye akamwangalia Ankia kidogo, kisha akainamisha uso na kuuelekea mlango; akitoka ndani ya sebule hiyo.

Nikaangaliana na Ankia, nasi tukapeana tabasamu la kirafiki kwa pamoja.

"Uko poa mkubwa?" Ankia akaniuliza.

"Yeah... niko zaidi ya poa. Nahisi kupona kabisa... siyo mwilini tu, ila moyoni pia," nikamwambia hivyo.

"Hata me naona..."

"Leo siku gani?"

"Ahah... Jumanne."

"Ahaa... ulimwita mtoto jana?"

"Alikuja mwenyewe. Naona dawa imemwingia kabla hajainywa..."

"Na bado..."

"Ahahahah... endelea tu kumchokoza... chuma kitayeyuka," akaniambia hivyo kwa utulivu.

"Asante Ankia. Kwa kila kitu," nikamwambia hivyo.

Akasema, "Usijali. Jiweke sawa, unywe dawa, chai tayari. Unahitaji nguvu unajua..."

"Yeah, nahitaji nguvu nyingi sana. Ngoja nikaswaki... nikimaliza chai, naenda kuwaona warembo wangu," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo na kukubali, nami nikarudi chumbani tena.

Furaha mpya ilikuwa imenitawala moyoni, nami sikutaka kitu kingine zaidi ya kuendelea kuiongeza. Mwanamke aliyekuwa ameuteka moyo wangu kwa asilimia zote sasa alionekana kuanza kunielewa pia, nami ningeendelea kumchokoza kweli mpaka awe tayari kuukaribisha upendo wangu kufikia kwenye uvungu wa moyo wake.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana 😉
 
Fupi jamani
 
Mwamba JC pointi za mbinde umechukua lakini sio mbaya endelea kupambana
 
Mr captain to day hamna kabisa hat ep moja haaa😲 😮 😮,we are believe you,so usitufanyie hivo 😀 😄
 
Back
Top Bottom