Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

Baada ya kumaliza usafi wa kinywa na mwili, nikarudi chumbani tena na kuvaa kwa njia nadhifu na kujiweka vizuri kama ilivyokuwa kawaida yangu, mtu yeyote ambaye angeniona huko nje asingedhani nilikuwa nimetoka kupambana na sumu ya nyoka kabisa. Nikachukua simu na kuangalia yaliyonipita kwa huo muda wote ambao sikuwa nimeishika, na yalikuwa mengi, lakini moja ndiyo ikateka fikira zangu zaidi.

Watu kadhaa walikuwa wamenitafuta, na mmojawapo alikuwa ni askari Ramadhan. Nikaona alikuwa amenipigia hiyo juzi, mara kadhaa, na baada ya kunikosa akanitumia ujumbe ambao sasa ndiyo ukateka fikira zangu. Alitaka kunifahamisha kwamba madam Bertha angepelekwa mahakamani Jumatano, katika ile kusimama mbele ya hakimu na kuulizwa ikiwa alikiri kuwa na hatia au la, na kama angesema hakuwa na hatia, basi ndiyo taratibu za kumfungulia mashtaka na wanasheria kupambania kesi yake zingeanza.

Kwa hiyo Ramadhan alikuwa ananijulisha hivyo ili kama nikitaka kwenda kuona yaliyotokea huko, basi niende, maana akawa ameniambia kwenye ujumbe kwamba kwa njia moja ama nyingine uwepo wangu huko mahakamani ungeweza kuwa na manufaa. Siyo kwamba ningeenda kuapishwa ama kuongea ama nini, hapana, ningeenda tu kuwa mtazamaji, ikiwa ningetaka kufanya hivyo.

Kiukweli nilikuwa nimeshaanza hadi kusahau hayo mambo kabisa, maana nilikazia fikira zangu kwa Miryam zaidi kwa wakati huu. Hivyo ujumbe huu ukaniingizia jambo zito akilini maana yale matukio yote yaliyotokea kumhusu mwanamke huyo, yaani Bertha, yakaanza kujirudia kichwani, nikihisi kama ameacha kovu fulani moyoni. Ningetaka kwenda kumwona tena? Sikutambua la kufanya kuhusu hilo bado. Mimi ndiye niliyemfanya mpaka akawa chini ya hiyo hali, na aliistahili, ila bado sikuweza kujizuia kujisikia vibaya.

Kwa hiyo nikafanya tu kumtumia ujumbe mfupi askari Ramadhan nikimwomba radhi kwa kunikosa maana nilikuwa nikiumwa, nami nikamwambia ningempa mrejesho kuhusiana na jambo hilo. Aliisema Jumatano kama kesho-kutwa, lakini sasa najua ingekuwa ni kesho. Hivyo nikamwambia pia anitumie muda wa kusimamishwa kwake Bertha na mahali hususa pa hiyo mahakama ili ikitokea nikawa na uhakika wa kwenda, basi niende bila shida. Nikaweka simu mfukoni baada ya hapo na kuliacha hilo liwe la baadaye.

Nikaelekea sebuleni tena, na hapo nikapata chai tamu ya karafuu pamoja na chapati tatu za mayai nilizoandaliwa na Ankia, na nikajitahidi kabisa kuzimaliza zote na kumshukuru mwanamke huyo aliyenijali sana. Kisha ndiyo nikatoka kuelekea kwa majirani zetu ili kujumuika nao. Kama kawaida, Ankia angeelekea dukani kwake pia, na leo angetumia muda mwingi huko maana jana hakwenda, kwa hiyo wa kwanza kutoka akawa mimi, na wakati wa kurudi ningekuta mwenye nyumba wangu akiwa ashasepa.

Hii ikiwa ni mida ya saa tatu asubuhi, nikapita getini hapo kwa majirani zetu wapendwa na kukuta gari la bibie Miryam likiwepo bado, kumaanisha hakuwa ameondoka. Ile tu ndiyo nauelekea mlango wa kuingilia ndani, ukafunguliwa na wa kwanza kutoka akawa ni Mariam, huku nyuma yake akifuata Tesha. Mariam alinifata akiwa anafurahi sana, naye akanikumbatia kwa nguvu kiasi, huku mimi nikiweka mkono wangu mmoja mgongoni kwake.

Tesha alifurahia pia kuona nimepata nafuu, na baada ya salamu hapo sote tukaingia ndani. Warembo wangu kama kawaida yao walikuwa wameketi kwenye sofa moja huku wakiniangalia kwa furaha, nami nikawapa salamu na wao kuitikia vizuri. Nikakaa sofani, Mariam akiwa karibu nami huku amenishikilia mkononi kama vile ameambiwa nataka kumkimbia, naye Tesha akakaa kwenye sofa lingine pia.

Inaonekana wote walikuwa wametoka kumaliza kupata kiamsha kinywa, kwa kuwa Bi Zawadi alipendekeza niwekewe chai na mkate, lakini nikamshukuru na kusema nilikuwa nimeshakunywa. Wakaniambia kwamba Shadya alituma pole yake kwangu baada ya kusikia ninaumwa, nami nikawaambia waitume shukrani yangu kwake kwa niaba. Nikamuulizia na Miryam pia, kama alikuwa hajambo, nao wakasema ni mzima, alikuwepo akijiandaa kwenda kazini.

Tesha akagusia kwamba dada yake leo alikuwa amewahi sana kuamka na kwenda mazoezi ya kutembea sijui, maana ameshtukia tu hiyo asubuhi Miryam anatokea nje. Mimi nikashona tu mdomo nikijifanya sielewi somo hilo kabisa, wakati mwamba nilikuwa nimetoka kuhudumiwa na huyo mwanamke usiku mzima. Ah, huduma ya muuguzi tu, ile nyingine-nyingine ndiyo bado ilikuwa 'pending!'

"Ila JC baba, unajisikia vizuri kabisa? Hauhitaji kwenda hospitalini kweli?" Bi Jamila akawa ameuliza hivyo kwa kujali.

"Hamna, niko full nafuu. Kama ni hospitali basi itakuwa tu kwenda kumwona Soraya na kumsalimia," nikasema hivyo.

"Sasa je, si nilikwambia? Umeona nguvu ya mitishamba?" Bi Zawadi akasema hivyo.

"Ah, nimeamini cheupe wangu. Unaweza ukanigeuza mganga wa kienyeji na siyo wa hospitali tena," nikamwambia hivyo.

Bi Zawadi akacheka kwa furaha, naye Bi Jamila akatikisa kichwa huku akitabasamu.

Mariam akaniuliza, "Tutaenda kwa Nuru lini tena?"

Nikatabasamu na kumwambia, "Siku siyo nyingi Mamu, tutaenda. Umem-miss?"

Akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Nampenda. Ananipenda. Na ana simu nzuri."

Nikatabasamu kwa kuhisi furaha.

"Nuru ndiyo mdogo wake JC uliyetuambia?" Bi Zawadi akamuuliza Tesha hivyo.

"Eeh. Halafu mwana, mama hapa anabisha eti kwenu hapafanani na ikulu. Hebu mpe mawaidha," Tesha akaniambia hivyo.

Nikamkata jicho na kisha kumwambia Bi Zawadi, "Anakurusha tu huyu. Ikulu ya wapi?"

"Yaani Tesha ni mwongo! Kaisifia nyumba yenu, eti anasema kubwa kama Ikulu, milango na kila kitu cha vioo, hadi masofa ya vioo, sijui mna magari kumi, yote ni ya kuanzia milioni 300 na kuendelea, eti kweli?" Bi Zawadi akaniuliza hivyo.

"Ahahahah... ila Tesha..." nikamwambia hivyo.

"Hahahaha... mwanangu unaficha nini? We' wa kishua kweli, afu' uko poa, hata hauringi. Mamu huyu hapa shahidi ma' mkubwa, hivyo vitu vipo... muulizeni tu, hata simkonyezi," Tesha akasema hivyo.

"Ndiyo utuambie hadi makochi ya vioo? Eti kweli Mamu?" Bi Zawadi akamuuliza.

Mariam akamwangalia tu.

"Nyumba ya kaka JC... kwa kina Nuru kule mlipoenda, pakubwa sana?" Bi Zawadi akamuuliza tena.

Mariam akasema, "Eee. Kubwa... kuna TV... kubwaaa, halafu ghorofani. Tukaangalia na mchezo, Nuru akanifundisha kubonyeza... ku... kubonyeza..."

"Kucheza game," nikamsaidia.

"Eeeh, kucheza game. Kuna ngazi, tukaenda juu, kuna sehemu ya kuoga, iko chini..."

"Swimming pool?" Bi Zawadi akauliza.

"Eeeh," Mariam akakubali.

"Na magari Mamu?" Tesha akauliza.

"Eeeh, magari. Mawili moja la rangi hii, na lingine la... kama ile pale rangi," Mariam akajitahidi kuongea kwa uharaka zaidi.

Nilifurahia namna ambavyo alijitahidi sana kukumbuka vitu kwa usahihi, naye Tesha akamwonyesha Bi Zawadi ishara kwa mikono kama 'sasa je?'

Nikasema, "Ni kawaida tu, wala hata siyo Ikulu. Na Mamu amesema magari mawili, acha kuwadanganya wenzio Tesha. Utakuja uue mtu kwa uwongo."

"Umeona? Mwambie huyu," Bi Zawadi akasema hivyo.

Ni wakati huu ndiyo Miryam akawa ametoka chumbani kwake baada ya kumaliza kujiandaa kwa ajili ya kazi, naye alipokuwa akija hapo sebuleni akawa ameniona na kusimama kwa ufupi kunitazama, nami pia nikawa namwangalia kwa yale macho yangu ya ushawishi kwa makusudi. Nilitaka aione wazi ile kitu ya sisi kujuana sana, naye akaacha kuniangalia na kuja upande wetu akiwa amebeba mkoba na kwenda usawa wa sofa alilokalia Tesha.

Alikuwa amevaa blauzi kama T-shirt la mikono mifupi jekundu, pamoja na suruali nyeupe ya jeans laini iliyobana umbo lake la chini kwa umaridadi. Yaani alionekana vyema sana kwa huko nyuma ingawa hakuivuta blauzi yake juu kidogo kama wafanyavyo wengi, nami nikawa najishaua kama vile sijamcheki vile. Alikuwa amezitengeneza nywele zake kwa mtindo wa kuzibana kisogoni na kuziachia zimwagikie mgongoni kama mkia mrefu, huku chache zikiwa mbele ya paji la uso lake. Nywele zake kabisa. Na alipendeza sana usoni.

Tesha akampisha kwa kukaa kwenye mkono wa sofa, na bibie akaketi sofani huku akifungua simu yake kuangalia mambo fulani.

"Ah, ma' mkubwa siyo siri. Brother hapa ndo' ana maisha. Yaani, ukiiona nyumba yao, hii utaiona kama ya mabati," Tesha akasema hivyo.

"Tesha!" nikamwambia hivyo kiukali wa kimasihara.

"Mbona una wivu sana we' mtoto?" Bi Jamila akamuuliza Tesha hivyo.

Bi Zawadi na mie tukacheka kidogo.

"Siyo wivu, nawaambia ukweli. Yaani hamna punje hata moja ya mchanga ndani. Nyumba kama imetoka dukani yaani. Aisee... tumtafutie JC mke kwenye ukoo wetu. Kuwa mashemeji nao itatu-save sana," Tesha akasema hivyo.

Miryam akamtazama kwa macho fulani makali kiasi baada ya Tesha kusema hivyo, nami nikatabasamu, huku mama wakubwa wakicheka.

"Au uwongo da' Mimi?" Tesha akamuuliza hivyo, na najua ilikuwa ni makusudi.

Miryam akamuuliza, "Kwamba tuna shida sana?"

Nikacheka kidogo kwa pumzi.

"Aaa... yaani itakuwa fursa... kuna vi-BMW na vi-Range kwa mashemeji, tutakuwa tunauzia sura mara moja moja... badala ya... kukomaza sura na Mistubishi..." Tesha akasema hivyo huku akimwangalia dada yake kwa kujihami kiasi.

Miryam akasonya kidogo na kuirudia simu yake, kitu ambacho kikafanya mama zao pamoja na Mariam wacheke kwa furaha.

"Ila pazuri mno. Natamani turudi hata leo," Tesha akasema hivyo.

"Mtakuja tu. Tena ipo siku... nitawaleta wote," nikaongea hivyo na kumwangalia Miryam.

Mwanamke huyo akanitazama kiufupi eti kama hataki, nami nilipotabasamu, akairudia simu yake.

"Ah, tutafurahi kupaona kwenu kwa kweli. Jinsi Tesha anavyopasifia? Hata me nitakuja," Bi Zawadi akasema.

"Uhakika cheupe wangu," nikamwambia.

"Lazima kutakuwa na mbwa mkali. Hatatung'ata?" Bi Jamila akauliza.

Nikacheka kidogo pamoja na Tesha, naye Mariam akasema, "Hamna mbwa. Hamna."

"Fensi lote limewekewa hizi nyaya za umeme, yaani hata mbu hawaiingii. Ah, hiyo mitaa ina nyumba kali! Ma' mkubwa usipime," Tesha akasema hivyo.

"Yupo Nuru, Jasmine, Imelda, mama JC, na... na wengine... na baba JC," Mariam akasema hivyo.

"Wewe! Wote wazuri eti?" Bi Zawadi akauliza.

"Eeeh..." Mariam akajibu.

Tesha akasema, "Sana. Yaani unavyomwona JC hivi, huyo Jasmine, na mama yao... eh! Wazuri! Tena wanafanana, yaani..."

"Eh, umeshasifia sana Tesha, inatosha. Mama, umekunywa dawa?" Miryam akamkatisha na kumuuliza hivyo Bi Jamila.

"Tayari. Leo utawahi kurudi si eti?" Bi Jamila akamuuliza pia.

"Ee, kama mambo hayatakuwa mengi, mapema tu," Miryam akasema.

"Lazima yawe mengi. Si Soraya hayupo? Nani kwanza anakusaidia sa'hivi?" Bi Zawadi akamuuliza hivyo.

"Nakaa kwenye meza yake, haina shida," Miryam akamjibu hivyo huku akiwa makini na jambo fulani kwenye simu.

"JC..." Mariam akaniita.

"Naam?" nikaitika na kuacha kumwangalia bibie.

"Picha. Niwaonyeshe mama... Nuru na Jasmine," Mariam akasema hivyo.

"Ee hebu tuonyeshe basi, maana Tesha anawasifia sana wa kwenu," Bi Zawadi akasema hivyo.

Nikatoa simu yangu na kufungua sehemu za kutafutia picha, kisha baada ya kupata moja niliyopiga pamoja na Jasmine na Nuru, nikampa Mariam simu, naye akawasogelea mama zake ili kuwaonyesha. Wakati huo nikamtazama Miryam tena, ambaye alikuwa anampa Tesha maelekezo fulani ya mambo ya nyumbani, nami nikatulia tu nikimtazama kwa hisia kutokana na kuvutiwa sana na urembo aliokuwa amebarikiwa kuwa nao.

Nikamsikia Bi Jamila anauliza kwa nini Nuru hakuwa mweupe kama sisi, nami nikamwangalia na kusema, "Aa... Nuru ni mdogo wetu kwa upande wa mama. Yaani... baba yetu me na Jasmine ni mwingine, na wa kwake Nuru ndiyo mume wa mama sasa."

Bi Zawadi na Bi Jamila wakatikisa vichwa vyao kuonyesha uelewa, naye Mariam akasema, "Nuru ana simu nzuri!"

Nikatabasamu maana inaonekana binti Mariam alikuwa ameikubali mno simu ya mdogo wangu, naye Bi Zawadi akauliza, "Si ulisemaga mama yako... na nyie, ni... mnatokea Mwanza?"

"Yeah," nikakubali hilo.

"Hebu tuwekee picha ya mama yako na ye' tumwone," Bi Zawadi akaniambia hivyo huku akitabasamu.

Mariam akanipa simu tena, kisha nikaweka picha ya mama na kumrudishia ili awaonyeshe mama zake wakubwa.

"Hee! Kweli jamani, mama yako mzuri!" Bi Zawadi akaongea hivyo baada ya kuiona picha.

Nikatabasamu tu kwa hisia.

Miryam akawa amesimama na kuweka simu yake mkobani, naye akasema, "Me naenda sasa. Tutaonana baadaye."

Tesha akasema 'haya,' naye Mariam akatoka upande wa mama zake wakubwa na kwenda kumuaga Miryam kwa kumkumbatia.

Bi Zawadi akamwambia Miryam, "Haya Mimi, baadaye. Halafu usisahau kumcheki na Doris kwa ile ishu, eti?"

"Sawa," Miryam akamjibu.

"Hivi kitchen party ya Doris ni lini kweli?" nikauliza hivyo haraka.

"Alhamisi. Kesho-kutwa," Bi Zawadi akanijibu.

"Ahaa... mambo mazuri ya wanawake hao," nikasema hivyo na kumwangalia Miryam.

Bi Zawadi akacheka kidogo.

Miryam akanitazama usoni kwa macho makini, kisha akaacha kuniangalia na kusema, "Mama, me naenda. Mbaki salama."

Alikuwa akimwambia Bi Jamila hivyo, lakini mwanamke huyo hakujibu, kwa sababu alikuwa ameshika simu yangu huku akiitazama kwa umakini wa hali ya juu.

"Mama..." Miryam akamwita tena.

Bi Jamila hakunyanyua uso wake, yaani akaendelea tu kuiangalia picha kwenye simu. Nikamtazama kwa umakini.

"Ma' mkubwa?" Tesha akamwita pia.

Hakuitika. Nikamwangalia Miryam machoni, naye pia akaniangalia kwa kutoelewa shida ni nini, kisha sote tukamwangalia tena Bi Jamila.

Bi Zawadi akamtikisa kidogo kwa bega na kusema, "We' Jamila... vipi?"

Bi Jamila akawa kama ameshtuka kiasi na kututazama wote.

Miryam akamuuliza, "Kuna tatizo mama?"

Bi Jamila akaniangalia usoni kwa umakini, kisha akaniita, "JC..."

"Naam..." nikaitika.

"Huyu ndiyo mama yako? Mzazi?" Bi Jamila akauliza hivyo huku akinionyeshea simu yangu.

"Ndiyo," nikakubali.

"Anaitwa nani?" Bi Jamila akaniuliza.

"Leah," nikamwambia.

Bi Jamila akamtazama Miryam usoni.

"Mama, vipi?" Miryam akamuuliza kwa kujali.

"Kuna shida gani Jamila?" Bi Zawadi akamuuliza pia.

Bi Jamila akashusha macho yake kuiangalia tena hiyo picha kama vile anaitafakari mno. Mh? Sikuelewa kabisa shida ilikuwa nini. Alifanya sebule ijae umakini ghafla.

Nikamuuliza, "Unamfahamu mama yangu?"

Akawa ameniangalia, kisha akasema, "Ha-hapana... sidhani. Nahisi kama nimeshawahi kumwona, ila... sijui wapi..."

"Umewahi kuishi Mwanza?" nikamuuliza tena.

Bi Jamila akabaki akinitazama kama vile kakosa cha kujibu.

"Eeh, Mwanza alishafika. Ni kitambo ila, eti? Labda aliwahi kumwona mama'ako huko kwenye hekaheka," Bi Zawadi akasema hivyo.

Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa, nao wakawa wamenirudishia simu.

Miryam akasema, "Haya basi, baadaye."

Wote wakamwambia 'haya,' na Tesha akamfungulia mlango bibie eti kama malkia ili atoke ndani, ndiyo Miryam akaelekea nje.

Mariam akanifata na kusema, "Nafata kinanda JC. Tufanye mazoezi."

Nikatabasamu na kumwambia 'sawa,' naye akaenda zake chumbani kukifata.

Tukio dogo la muda mfupi nyuma iikawa limenifanya nimwangalie Bi Jamila tena kwa umakini, na bado alionekana kama kukosa amani kiasi baada ya kuiona picha ya mama yangu. Nikawaza sijui labda kweli aliwahi kukutana naye, na labda hata haikuwa kukutana kuzuri maana alionyesha kuishiwa raha, au kushangaa yaani. Ila hamna, labda tu nilikuwa nawaza vitu vingi vibaya. Hata hivyo na uzee na nini, huenda alijichanganya tu na kumfikiria mtu mwingine.

Nikawa nasikia geti kule nje lilipokuwa likifunguliwa na bibie Miryam, naye Tesha akasema anaelekea chumbani kujiandaa kutoka pia na ili alifunge na geti dada mtu akishaondoka, hivyo akatuacha hapo na mama wakubwa. Mariam akawa amerudi upesi na kinanda chake, nami nikamwomba anipe muda mfupi ili nikamsemeshe dada yake pale nje kwa kitu fulani nilichokuwa nimekumbuka kumwambia, na binti akaniachia niende.

Nikatoka humo ndani na kukuta Miryam akiwa hapo nje bado, na geti lote lilikuwa limefunguliwa ili aweze kulitoa gari kwa hiyo huko kwa nje palionekana vyema sana; watu-watu na fujo zao za asubuhi. Alikuwa ndiyo ameufikia mlango wa gari upande wa usukani na kuufungua, lakini aliponiona nimetoka ndani, akatulia na kunitazama tu usoni. Nikampa tabasamu la wazi kuonyesha namna ambavyo nilipenda sana kumwangalia, naye akajikausha tu na kuuingiza mkoba wake garini, lakini yeye hakuingia kwanza.

Nikatoka hapo varandani na kusogea mpaka gari lake lilipokuwa, nikisimama upande wa pili wa mlango wa siti ya pembeni, naye akanitazama usoni kidogo na kushusha tena macho yake kama vile anayaficha eti, na hilo likanifanya nikatabasamu kiasi na kuegamiza mkono mmoja juu ya mgongo wa gari.

Bila kuniangalia, Miryam akasema kwa sauti tulivu, "Unajua kwamba huwa unazungumza sana ukiwa unaota?"

Nikamuuliza, "Kumbe? Na uliona jinsi inavyosimama nikiwa naota?"

Akaniangalia upesi na kusema, "A-ah, sija...."

Akaishia hapo baada ya kuonekana kujishtukia kutaka kusema kitu kilichoonyesha kwamba aliyaelewa maneno yangu vizuri, nami nikatabasamu kimchezo huku nikimtazama kwa hisia machoni. Akakwepesha macho yake na kuonekana akibabaika kiasi, naye akaushika mlango wa gari akiashiria kutaka kuingia ndani.

Nikamwambia, "Asante sana kwa jana."

Akaniangalia kiufupi, kisha akasema, "Ila bado... unahitaji kuonana na tabibu... uende hospitali kuhakikisha afya yako iko salama."

Kwa sauti tulivu, nikamwambia, "Wewe ndiyo tabibu wangu Miryam..."

Akaitikia maneno hayo kwa kukaza vidole vyake taratibu kwenye mlango wa gari huku akianza kuniangalia taratibu.

"Uwepo wako usiku mzima pembeni yangu ndiyo umefanya niamke nikiwa salama, kwa kuwa sikuwa tu naumwa mwilini kutokana na sumu, ila kuna gonjwa la ndani sana kwenye moyo wangu ambalo lilikuhitaji wewe tu ili kulitibu... na umeshaanza kufanikiwa kulitibu..." nikamwambia hivyo kwa sauti tulivu.

Alikuwa akiniangalia usoni kwa macho laini yaani, mdomo wake ukiwa wazi kiasi, ikionyesha dhahiri kwamba kuna sehemu ndani yake ilipenda sana kuyasikiliza maneno yangu hata kama ningeongea utumbo, hivyo ni wazi kwamba alikuwa ameanza kunizoea haswa.

"Kwa hiyo, asante sana tabibu wangu. Sitahitaji kwenda hospitali tena kwa sababu yako," nikampamba namna hiyo.

Akafumba mdomo wake na kuangalia pembeni, kisha akasema, "Nenda sasa uka... ukacheze na Mamu."

"Poa. Tutaonana baadaye. Uwe care na uendeshaji, sawa ee?" nikamsemesha kwa njia fulani kama vile nambembeleza.

Akanitazamaaa, yaani kama vile akiwa ananitafakari sana, huku mimi nikiwa nampa kale kasura ka kupendeka na macho yangu yenye kushawishi, naye ndiyo akaingia kwenye gari lake na kuliungurumisha. Hadi raha! Yaani nilimwambia hayo yote na hakutoa neno hata moja kupingana nayo kama alivyokuwa akifanya awali, na kiukweli hiyo ilikuwa ni alama moja nzuri sana kwangu. Alikuwa anakaribia kuingia huyu.

Nikasogea nyuma na kuendelea kumwangalia kupitia kioo cha mbele, akionekana kuingiza magia na manini, na ni hapa ndiyo Tesha akawa amekuja nje hatimaye. Nikamuuliza ikiwa angeondoka pamoja na dada yake, lakini akasema hapana, anaenda tu pale Kongowe mara moja kisha anarudi baadaye kidogo. Mimi pia nikamwambia kwamba nikimaliza kumpa Mariam twisheni kidogo, nitaelekea kule hospitali ya Temeke kumsalimu Soraya, kwa hiyo tungeonana baadaye.

Hilo lilipoeleweka, ndiyo tukaagana na jamaa akaenda kufunga geti lote baada ya Miryam kuwa ameshasepa, kisha na yeye Tesha akaondoka. Nikarudi pale ndani ili kudili na binti Mariam, nikiwa nahisi furaha na amani zaidi moyoni.

β˜…β˜…

Nilitumia muda wa kama saa moja na nusu hivi pamoja na binti Mariam, nikimfundisha mambo mapya na kupiga naye kinanda kwa njia yenye ustadi zaidi, na alikuwa akiendelea kujitahidi kufika kule nilikotaka afike, ila bado hakuwa amefika kwa asilimia zote. Lakini angalau alinipa matumaini kwamba haingechukua muda mrefu sana, nilikuwa na uhakika kwamba ugonjwa wake ulikuwa umeanza kumkimbia taratibu.

Hivyo ikiwa inaelekea kufika saa sita mchana, nikawa nimewaaga wa hapo nikisema ninaelekea kule hospitali ili kumsalimia Soraya, kwa kuwa saa saba ingekuwa muda wa kuwasalimu wagonjwa. Nikawaacha mama wakubwa na Mariam katika hali nzuri ya amani, nami nikarudi pale kwa Ankia na kuvaa vizuri kwa ajili ya kutoka; T-shirt la blue-nyeusi lenye mikono mirefu, suruali ya jeans ya samawati, na sneaker zangu nyeupe, huyooo nikaingia barabarani baada ya kupafunga hapo vizuri.

Kama kawaida yangu, 'handsome' niliyejitambua kabisa, lakini sikuwa wa kujivuna kupita kiasi. Walionitazama ndiyo wangetoa komenti walizoona zinafaa kunielezea maana sikuzote kuonekana kwangu mbele ya wengi kuliinua macho na mawazo tofauti-tofauti kunielekea, na ndivyo ilivyokuwa na wakati huu. Yaani niliangaliwa kama vile bado nilikuwa mgeni huku.

Kutokea hapo Mzinga baada ya kupanda daladala, safari ikawa yenye kukawiza sana kutokana na msongamano mrefu kuanzia darajani, na uzuri tu ni kwamba nilikuwa nimepata nafasi ya kukaa la sivyo kama ningekuwa nimesimama basi ningeshuka na kuchukua bodaboda. Gari likawa linajivuta taratibu tu hadi tulipofikia maeneo yaliyoikaribia Rangi Tatu, kisha likasimama kwa dakika kadhaa hapo. Watu baadhi waliamua kushuka na kutembea tu, hivyo nami pia nikalipa nauli yangu na kushuka.

Mdogo mdogo tu nikatembea pembeni ya barabara, na huo msongamano ulikuwa umesababishwa na magari kuwa mengi eneo lenye roundabout isiyokuwa na taa za barabarani wala askari wa usalama, kwa hiyo nikapapita hapo na kuendelea kusonga mbele mpaka kufikia Mbagala stendi. Nilielewa kuwa magari ambayo yangeelekea hospitali ya Temeke yangeingia kwanza hapo stendi na kisha kuibukia tena barabarani ili kuongeza abiria na kusonga mbele, kwa hiyo nikaona nisogee mbele zaidi kuipita stendi mpaka eneo waliloita Dar Live ili niwahi kupanda gari moja ambalo lingekuwepo, ama kama kuna ambalo lingenikuta basi nisombwe nalo.

Nikiwa naelekea eneo hilo, nikawa nimepigiwa simu na Adelina, nami nikapokea na kuzungumza naye. Mwanamke huyo alikuwa akinisalimu, na kwa wakati huu niliongea naye kwa njia yenye kumfurahisha ili urafiki wetu uweze kukolea hata zaidi. Nilikuwa nimeamua kumalizia maongezi na Adelina kwanza kabla sijapanda daladala, na kwa upande huu hakukuwa na msongamano, kwa hiyo nyingi zikawa zikinipita tu.

Wakati ndiyo namalizia kuongea naye, katika kupishana na mtu fulani eneo hilo nikawa nimepamiana naye kwa nguvu kiasi. Ile nimemwangalia, nikakuta ikiwa ni mwanamke mtu mzima vya kutosha kunizaa, yaani tena rika la akina Bi Zawadi kabisa, ambaye alikuwa amebeba kitu kama kisado kikubwa chenye nyanya nyingi, na hivyo zikawa zimemwagika chini.

Kwa ile hali ya uharaka kutokana na kutotarajia hilo, nikamwomba mmama huyo samahani huku nikiweka simu yangu mfukoni upesi sana kabla hata sijaagana vizuri na Adelina, na niliiweka mfuko wa nyuma wa suruali, kisha nikaanza kumsaidia mwanamke huyo kuokota nyanya zake zilizokuwa zimezagaa huku na kule. Alionekana kuudhiwa kiasi na hali hiyo, na mimi nilielewa, kwa hiyo nikawa namsaidia kuziokota na kumpatia ili azirudishe mahala pake huku nikimwomba samahani ya kutoka moyoni.

Nikawa nimeona nyanya kama tatu ambazo zilielekea usawa wa barabara kabisa, nami nikazifata upesi sana. Ile nimeinama kuokota moja, mbili, tatu, kwa kasi ambayo sikutarajia nikahisi simu yangu ikivutwa kutoka mfukoni mwa suruali! Kasi hiyo iliambatana na muungurumo wa pikipiki iliyopita karibu kabisa na mimi, nami nikashtuka kiasi na kutazama barabarani.

Hapo nikaona pikipiki iliyokuwa imebeba watu wawili, ikiwa upande huu wa barabara ulioelekea Temeke, lakini yenyewe ikielekea huko Mbagala, ikipishana na magari kwa kasi sana. Nikajishika mfukoni ili kuthibitisha, na simu yangu haikuwepo. Aisss! Hapo nikawa nimeporwa. Watu baadhi wakaanza kuniangalia na kuangalia kule pikipiki ilipoelekea, na mimi nikabaki nimesimama hapo nikiwa siamini. Yaani haijawahi kutokea nikaibiwa simu hata mara moja, tena mchana kweupe.

Hao jamaa walinipatia kwenye wakati wa udhaifu nilipokuwa namsaidia mama huyo na nyanya zake, na inaonekana walikuwa wamenipigia hesabu maana nadhani pikipiki hiyo ilikuwa imetulia tu upande wetu wa barabara, na huenda simu yangu ilitokeza sana kwa nyuma. Dah! Simu ilikuwa na vitu ile! Kumbukumbu, mambo mapya, mawasiliano, yaani simu yenyewe tu ilikuwa kama sehemu muhimu sana ya viungo vya mwili wangu, na sasa ikawa imenyofolewa. Nilihuzunika mno moyoni, lakini ningefanyaje?

Watu kadhaa wakasogea upande wangu na kuanza kunipa pole ama kuwasema wezi wale, nami nikawa naitikia kistaarabu tu, kisha nikamrudishia mama wa watu nyanya zake. Zamu hii na yeye akanipa pole, lakini akaniambia kwamba nisijali, simu yangu ningeipata tu. Niliona hiyo kuwa kama faraja isiyokuwa na faida, lakini nikaithamini hivyo hivyo na kumshukuru pia, nami nikaenda tu kupanda daladala. Kabla moja halijaisha lingine likawa limezuka tena, yaani!

Hakukuwa na jinsi tena. Simu ningetafuta nyingine, na jambo zuri ni kwamba sikuzote huwa ni busara kuwa na 'plan B,' yaani njia ya ziada ya kutatua tatizo ili likitokea, unakuwa hujapoteza kila kitu kabisa. Nyingi ya kumbukumbu kama picha, mafaili muhimu, na taarifa za kisiri nilizitunza kwenye email yangu, hivyo endapo kama ningenunua simu nyingine basi ningezirudisha kihivyo. Kuipoteza simu kizembe namna hiyo iliuma, lakini isingeuma tena baada ya muda.

β˜…β˜…

Basi, nikafanikiwa kufika hospitali ya Temeke baada ya dakika kadhaa, nami nikaenda kumwona Soraya. Ilikuwa imeshaingia saa saba, hivyo nilimkuta mwanamke huyo kwenye wodi ya wagonjwa akiwa ametembelewa na ndugu zake watatu, wote wanaume, na marafiki zake watano ambao walikuwa wanawake, waislamu, nami nikajitambulisha kwao na kumpa Soraya pole yake.

Soraya alikuwa ameshaanza kujihisi vizuri zaidi, hapa alitakiwa kumalizia tu matunzo kisha kesho ndiyo angeachiliwa na kwenda nyumbani kumalizia dozi zake. Alifurahi sana baada ya kuniona, na akanishukuru kwa kuwa aliambiwa mimi ndiye niliyemsaidia usiku ule ili sumu isimdhuru haraka mno, nami nikazipokea shukrani zake kwa kumwambia asante pia kupambana mpaka kupata nafuu. Alikuwa anajua kuhusu sumu ile kunidhuru mimi pia kutokana na msaada niliompatia baada ya kuambiwa na Tesha, naye akanipa pole pia.

Kwa hiyo nikaendelea kukaa hapo pamoja nao, nikiwa nimepatana zaidi na ndugu zake wale wanaume ambao walipendezwa sana na ishu ya mimi kuwa daktari na kufanya maongezi ya kitiba zaidi, na ile imeingia saa nane mchana ndiyo nikamuaga 'beauty Soraah' na kusema tungeonana tena. Huyu mwanamke alionyesha wazi kuvutiwa na mimi bado, tofauti na rafiki zake ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana nami, yeye alionyesha uvutio wa kina sana.

Lakini kwa wakati huu, nilikuwa nimeshaamua kuweka kituo kikuu kufanya michezo niliyokuwa nimeshafanya naye hasa kwa sababu ya Miryam, na pia kwa sababu niliona namna ambavyo mume wake alimpenda. Ningekuwa sifanyi kitu poa kama ningejikuta narudi kule kule nilikopaacha, kwa hiyo macho yangu kuwaelekea wanawake hawa wote yalikuwa ya urafiki. Nilikuwa sukari ya warembo sikatai, lakini hiyo haimaanishi kwamba wote walitakiwa kunilamba. Huo mchezo ulikuwa umefikia kikomo!

Bwana, nikawa nimeondoka hatimaye kutoka hospitalini na kuanza kurudi tena Mbagala. Nilikuwa nimeanza kuhisi njaa tayari maana mpaka tunafika Rangi Tatu muda ulikuwa unaisaka saa tisa, lakini mawazo yangu yalikuwa kwenye kutafuta simu nyingine upesi. Na kulikuwa na suala la laini pia.

Nikaona tu niende moja kwa moja mpaka Mzinga, na tulipokuwa tumekaribia kufika, nilisikia maongezi baina ya dereva na abiria kuhusu ajali iliyohusisha Costa ndogo kama hii daladala, na bodaboda, iliyokuwa imetokea maeneo ya hapo hapo darajani na kuua watu wawili, na hata tukapapita na wenyewe kuonyeshana kwamba ilikuwa ndiyo hapo. Lakini kwa wakati huu, magari yalipita vizuri tu baada ya vyombo hivyo vya usafiri kuwa vimeondolewa, na hatimaye nikawa nimeshuka tulipotua kituoni.

Nikaanza kutembea kuelekea upande ambao duka la Ankia lilikuwepo ili nikamsalimie kwanza, lakini nikakuta pamefungwa. Nikafikiri labda angekuwa amefunga mapema na kurudi nyumbani, hivyo nikaendelea na mwendo hadi nilipokuwa nakaribia usawa wa ile nyumba ya Rukia, nami nikamwona Tesha akiwa anakuja upande wangu upesi sana. Yaani alitembea haraka-haraka huku uso wake ukielekea simu yake kiganjani, mpaka nikamshangaa.

Ikabidi nikatize barabara na kwenda upande wake, nami nikasimama mbele yake kumzibia njia. Aliponyanyua uso na kuniona, akashtuka kiasi na kusimama, huku akiniangalia kimaswali sana.

"Oya, vipi? Ahahah... mbona unasafisha vumbi lote la barabara?" nikamuuliza hivyo kiutani.

Lakini Tesha akabaki kunitazama kimshangao sana, mpaka nikashangaa.

"Nini, mbona unaniangalia hivyo?" nikamuuliza.

Akanyanyua kiganja chake chenye simu kunielekea huku akitaka kusema kitu, lakini akasita kwanza, kisha ndiyo akasema, "Mwanangu michezo gani hii mnafanya?"

"Michezo? Me na nani?"

"We' na Ankia!" akaongea kwa mkazo.

"Unamaanisha nini?"

"Katoka kunipigia simu, anasema uko mochwari eti, sijui kapewa taarifa kwamba umekufa!" akasema hivyo.

"Nini?!" nikamuuliza utadhani sikumsikia vizuri.

Akapiga ulimi mdomoni na kutikisa kichwa chake kwa kukerwa.

"Umeenda huko Kongowe ukanywa nini, mbona sikuelewi?" nikamuuliza kiumakini.

"Sikutanii bro. Nimeambiwa umekufa!" akaniambia hivyo kwa mkazo.

"Naonekana kama nimekufa hapa?" nikamuuliza kistaarabu tu.

"Ah..." akafanya hivyo na kupiga ulimi tena akionekana kuudhika, kisha akaanza kubofya-bofya kioo cha simu yake.

Nikabaki nikimwangalia kwa umakini tu, yeye akaweka simu sikioni akiwa anampigia nani sijui, halafu akaishusha tena.

"Nampigia, hapokei," akasema hivyo.

"Nani?"

"Ankia!"

"Shida ni nini? Kakwambia nimekufa ili iweje... leo siyo sikukuu ya wajinga, acheni ujinga basi!" nikamwambia kimkazo pia.

"Sikiliza. Haya siyo masihara. Ankia kasema amepewa taarifa... yaani mwili wako uko mochwari hapo Mbagala, katuambia sisi wote, akaharakisha kwenda huko. Na yeye ka-panick kichizi, hakuna detail za maana, ila si umeondoka wote tunajua ulitoka kupambana na sumu? Presha ilikuwa juu, ndiyo sababu na me nilikuwa naenda huko sasa hivi. Ah, aisee! Hiiii... unaona tunavyokupenda JC?" Tesha akasema hivyo.

Mimi hapo nikawa natafakari jambo hili kwa kina. Haya yote yalimaanisha nini? Labda nilikuwa nina pacha ambaye sikumfahamu huko wapi wapi, na sasa akawa amekufa, halafu kesi ikauziwa kwangu? Au ni mtu ambaye alikuwa amenifanana? Na ni nani aliyekuwa amempa Ankia hizo taarifa mpaka akaja juu namna hiyo? Tesha akajaribu tena kumpigia, lakini ikaonekana Ankia hakupokea.

"Alisema anaenda hospitali ya Mbagala?" nikamuuliza Tesha.

"Eeeh... ndiyo mwili wako ulipo eti! Hajasema hata imekuwa vipi ukafa, yaani alikuwa anaongea kama analia vile. Hawa wanawake!" Tesha akasema hivyo.

Hisi ya tahadhari ikaniingia bila kujua sababu, nami nikamuuliza, "Mariam yuko poa nyumbani?"

"Ee, yupo nimemwacha anaangalia TV. Hata wakina mama wameshtuka kuhusu hili," akasema hivyo.

"Haya, twende," nikasema hivyo na kugeuza.

"Wapi?" akauliza.

Nikaendelea tu kutembea nikiwa na mawazo kiasi.

Tesha akanikaribia na kusema, "Kwa hiyo tunaenda kuuangalia mwili wako uliokufa huko hospitali? Fantastic!"

"Kutakuwa na tatizo lingine tu. Twende tukahakikishe," nikamwambia hivyo na kuendelea kusonga.

Safari ya kurudi maskani ili nipate mlo wa mchana ikawa imekatikia hapo, hata njaa sikuihisi tena kabisa. Kufikia wakati huu, mwili haukuwa dhaifu sana kama ilivyokuwa jana, na najua chapati tatu za asubuhi zilitosha kunipa nishati niliyohitaji kurudi huko Mbagala tena, ingawa najua nilitakiwa kula sana.

Lakini kwanza nilitaka kugundua huu utata ulitokea wapi na ulinihusu vipi hasa, kwa hiyo tukafanya kupanda bajaji na Tesha upesi, na kwa mara nyingine tena ndani ya muda huo huo ikawa ni kurudi Mbagala. Ilikuwa ni safari yenye kutatanisha, kwa sababu nilikuwa naenda kuthibitisha maiti yangu mwenyewe. Hii ingekuwa balaa.

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana πŸ˜‰
 
##Ilikuwa ni safari yenye kutatanisha, kwa sababu nilikuwa naenda kuthibitisha maiti yangu mwenyewe. Hii ingekuwa balaa##.........🀣 🀣 🀣 Mr angalia usije kuwa mzuka tayari,halafu ukawa hujui 😁 😁 😁
 
bibi kafanya yake
 
Okay ,,, najaribu kuwaza katika angle tofauti kidogo ,,,

Wote tunakumbuka pasipo na shaka kuwa ,, baada ya Jc kuibiwa simu na wale wezi (vibaka ) waliokuwa kwenye pikipiki .. sasa ikawa zamu ya J.C kupewa pole na yule mama

Lakini,, kuna kitu yule mama alimwambia J.C ,,, alisema hivi
" Mwanangu usiwaze simu yako utaipata " na J.C maneno haya uliyasikia sasa ,, huyu mama hawezi kuwa ndiyo sababu ya wale vijana wawili kupata ajali ??.. kama jibu ndiyo

Je ,, nikisema huyu mama ni mwanga /mchawi nitakuwa nakosea ??..

Lakini je huyu mama hataendelea kuleta uchawi wake hadi kwa mwananetu J.C ??..
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

Tumekuja kufika Mbagala Rangi Tatu hospitali ya serikali ishafika saa tisa na nusu, kwa kuwa kutokea eneo la stendi ya Mbagala mpaka hapo hospitalini tulitembea kwa mguu, nasi tukaelekea mpaka ndani na kwenda moja kwa moja kwenye meza ya maulizo. Watu walikuwa wengi; wafanyakazi, na wagonjwa waliosubirishwa kwa ajili ya huduma, wakiwa aidha wamekaa, wamesimama, ama kupanga foleni ndefu kwenye madirisha ya huduma huku na kule.

Tesha akaulizia kuhusu mwili, au maiti yoyote ambayo ilikuwa imeingizwa kwenye mochwari ya hospitali hii majira ya mchana wa leo, na aliyeulizwa kwenye meza hapo alikuwa ni mwanamke. Mdada yaani. Badala ajibu, yeye akawa ananikodolea tu macho utadhani alikuwa mshamba, hivyo Tesha akaniambia labda mimi ndiyo nimuulize ndiyo atajibu sasa. Nikamuuliza vyumba vya mochwari viko upande gani, naye akasema angetuelekeza upande huo kwa kutupeleka yeye mwenyewe.

Akasimama na kuiacha meza kwa jamaa mwingine, naye akatutangulia. Alikuwa mrefu kiasi cha kunifikia, paja na kalio la maana, rika kama langu tu yaani, na akiwa ndani ya nguo ya kijani ya kikazi, alitembea mbele yangu kwa kujibinua mgongo kiasi na kutikisa kalio lake makusudi kabisa yaani. Mpaka nikawa naangaliana na Tesha na jamaa akanipa ishara kama kuuliza 'huyu vipi,' nami hata sikujali sifa za huyo "nesi" alizokuwa anafanya mbele yangu kwa makusudi. Yaani sura yangu kwa wanawake ambao hawakutulia ilikuwa kama hirizi ya kuwaroga sijui!

Akatufikisha upande wa ndani ya hospitali hiyo ambako kulikuwa na korido refu lililoelekea kwenye vyumba vya mochwari, na kutokea hapo akatuambia tungepaswa tu kukunja kona kulia kwetu ndiyo maiti ambazo zilikuwa zimeletwa zilihifadhiwa, na maaskari bado walikuwepo. Mh? Maaskari? Ambazo? Yaani kumbe haikuwa JC mmoja aliyekufa, ila wengi?

Kabla hatujauliza chochote, akaonekana daktari mmoja upande ambao tulitokea na kumwita huyu dada kwa jina 'Anyesi,' naye akamwitikia na kutuacha hapo hapo. Tesha akatania kwa kusema wanawake wenye majina kama vinyesi huwa hawana akili kabisa, nami nikashindwa kabisa kujizuia kucheka, kisha tukaelekea huko mbele kama tulivyokuwa tumeelekezwa.

Ile ndiyo tunakaribia kukunja kona, Tesha akasimama baada ya kuwa amepigiwa simu, sijui na nani, ila mimi hapa nilikuwa nimeshafika mbele kidogo ndiyo nikageuka kumwangalia. Akanionyesha ishara kuwa nitangulie ili azungumze kwanza na huyo mtu, nami nikaendelea kutembea.

Upande huu sasa ndiyo ambao haukuwa na watu wengi sana, kukiwa tu na mabenchi yaliyo na mtu mmoja mmoja au wazi kabisa kwa pande za ukuta, na mbele zaidi ndiyo kulikuwa na milango miwili mipana ambayo ilionekana kuingia ndani ya chumba kikubwa chenye majokofu ya kutunzia maiti. Kwa milango ya pembezoni mwa hizi kuta sikujua sana ikiwa na yenyewe ilifungia vyumba vyenye majokofu, na kwa watu waliokuwepo hapo, alionekana mwanamke fulani akiwa amesimama usawa wa mlango wa pembeni kukaribiana na ile mipana kule mbele, akitazama huko, kwa hiyo nilimwona kwa nyuma.

Nikaendelea kwenda taratibu, kukiwa na ka hali fulani ka ugiza huku mwanzoni, lakini kuelekea huko mwishoni kulikuwa na taa iliyoangaza vyema. Nilipokuwa nikikaribia huko, umbile la mwanamke huyo aliyekuwa amenipa mgongo likaanza kufahamika kwangu. Alikuwa amevaa blauzi nyekundu yenye mikono mifupi pamoja na suruali nyeupe ya jeans laini, vilivyobana umbo lake na kulichoresha vizuri sana, huku nywele zake zikiwa zimebanwa na kuacha kimkia kwa nyuma. Ilikuwa ni Miryam!

Mh?

Nikakunja uso wangu kimaswali kiasi kwa sababu sikutarajia kwamba ningemkuta hapo, na alionekana kuegamia kitasa cha mlango wa pembeni huku akiwa amejishika shingoni kwa kuinamia upande mmoja kama vile mtu aliyechoka sijui, nami nikageuka nyuma kuangalia ikiwa Tesha alikuwa akija, lakini jamaa bado hakutokea.

Nikasogea mpaka nyuma yake Miryam na kuanza kumsikia akiwa anatoa kilio cha chini, yaani akilia huku anavuta pumzi bila kutoa sauti kwa mdomo, na kwa kweli nikashindwa kuelewa nini kilikuwa kikiendelea.

Nikamshika begani kutokea nyuma na kuita, "Miryam..."

Akageuza uso wake na kuniangalia. Yaani, alikuwa ametokwa na machozi mengi yaliyoulowanisha uso wake haswa, nadhani shauri ya kujifuta mara nyingi kwa kiganja chake shavu na shavu na hivyo kujipakaa zaidi. Akanigeukia vizuri zaidi na kunishusha kwa macho yake, kisha akanipandisha tena huku akinitazama kama vile ananishangaa sana.

Nikamuuliza, "Vipi? Kwa nini uko... mbona unalia?"

Akatoa kile kicheko cha mara moja kwa pumzi, akionekana kufurahi kuniona, na bila mimi kutarajia, Miryam akanikumbatia hapo hapo!

Nilisisimka. Sikulirudisha kumbatio lake haraka, huku yeye akinibana hata zaidi, nami nikatazama huku na kule nikiwa sielewi kwa nini alinikumbatia hivyo. Akawa analia kwa kutikisika mwilini kiasi, kisha akaniachia mgongoni na kunishika shingoni kwa mikono yake yote, akiniangalia kama vile haamini yaani, halafu akanikumbatia tena.

Nilikuwa nimeshangaa, lakini hiki kitendo chake kikanifanya niachie tabasamu hafifu tu lililojaa hisia nzuri sana kutoka ndani ya moyo wangu. Nikamkumbatia pia na kuikaza mikono yangu mgongoni kwake mpaka nyuma ya shingo yake ili niuhisi vyema zaidi mwili wake, na ulikuwa unatoa joto zuri ajabu lililoipa nafsi yangu utulivu wa hali ya juu sana.

Sijui tu ikiwa na yeye labda alikuwa anafikiri nimekufa? Subiri, inawezekana alikuwa anafikiri nimekufa ndiyo. Nikawaza labda huu ungekuwa ni mchezo uliofanywa na Ankia, au hata Tesha pia, ili kumsogeza Miryam karibu nami zaidi, lakini sidhani sana; mpaka kwenye masuala ya vifo na maaskari na mahospitali, ilikuwa mbali mno kuwa mpango tu.

Miryam akaendelea kunikumbatia tu, akiwa na namna fulani hivi ya kusugua taratibu kichwa chake shingoni kwangu yaani kama anadeka eti, na mimi nikaendelea kumshikilia huku nikitabasamu kwa furaha tele.

Akiwa amening'ang'ania bado, akasema kwa sauti yake tamu yenye mideko, "Oh God... nilifikiri umenipotea Jayden..."

Aah! Muziki!

Nikatabasamu zaidi na kusema, "Utajuaje kwamba sijapotea? Je kama umeukumbatia mzimu?"

"Ahh... acha masihara yako bwana..." akasema hivyo huku akining'ang'ania zaidi.

Dah! Yaani alikuwa amejisahau kabisa! Kule kukaza kooote kukawa kumepotea, na aisee hii ndiyo pindi iliyofunua zaidi kwamba nilikuwa sahihi kabisa toka mwanzo. Huyu mwanamke alinipenda! Kama hakuwa ametaka kukubaliana na hilo, leo ndiyo angekuwa amekamatika zaidi.

Akawa analia begani kwangu, kile kilio chenye pumzi zenye deko, yaani eh! Sikuwa nimeelewa haya yote yalisababishwa na nini lakini matokeo yake yalileta tunda zuri sana kwangu. Na lingekuwa tamu haswa!

Nikaanza kuzilaza-laza nywele zake na kumwambia, "Basi Miryam... usilie. Niko sawa."

Akageuzia kichwa chake kwenye bega langu lingine na kuendelea kunikumbatia tu, naye akanena, "Ahah... ahh... silii kwa huzuni... nimefurahi tu Jayden..." akasema hivyo kwa sauti yake tamu sana.

"Ahah... hujui ni jinsi gani hata me nafurahi pia Miryam," nikamwambia hivyo kwa sauti yenye kubembeleza.

Ni hapa ndiyo nikawa nimemwona Ankia akiwa anakuja kutokea kwenye ile milango mipana, na tabasamu langu likapanuka zaidi. Baada ya yeye pia kuwa ameniona nikiwa nimemkumbatia Miryam, akasimama umbali mfupi kutoka hapo tulipokuwa, akionekana kushangaa kwa furaha. Nilijihisi vizuri sana moyoni ingawa nilikuwa nimekula hasara kwa kuibiwa simu yangu leo. Huu ulikuwa ni ushindi wa aina yake.

Nafikiri sekunde chache zilizopita nikiwa nimemshikilia Miryam namna hiyo zikafanya awe amemwona Ankia pia, labda alikuwa amefumba macho yake kabla ya kumwona, na taratibu akaanza kujitoa kifuani kwangu. Nikaitoa mikono yangu kutoka mgongoni kwake na kuipitisha shingoni mpaka kuushika uso wake kwa viganja vyangu, na bado nilikuwa nikimwangalia kwa furaha nyingi sana.

Lakini wakati huu, Miryam alinitazama kama vile alikuwa ameshtuka, naye akaviangalia viganja vyangu kama vile haelewi-elewi kinachoendelea sijui, na jambo hilo likanitatiza kiukweli. Nikamtazama Ankia kimaswali kiasi, naye pia alikuwa akiniangalia kwa macho yaliyojaa alama ya kuuliza, na kabla sijamuuliza Miryam tatizo lilikuwa ni nini, akaitoa mikono yangu karibu na uso wake. Tena yaani hadi akajisukuma nyuma kama vile anataka kuniepuka kabisa, kisha akaanza kujifuta machozi.

Nikamuuliza kiupole, "Miryam... tatizo nini?"

Akaanza kutikisa kichwa kama anakataa kitu fulani, kisha akaanza tu kuondoka. Aya?!

Nikaanza kumfata huku nikimwambia, "Miryam, ngoja kwanza. Subiri, usiniambie unataka kuanza kuzikimbia hisia zako tena. Umetoka tu sasa hivi kunionyesha kwamba.... Miryam..."

Ikanibidi nimsimamishe kwa kuuvuta mkono wake kwa nguvu kiasi, naye ndiyo akasimama na kunigeukia.

"Miryam, mbona unakuwa hivi? Kwa nini unaendelea kuukimbia ukweli ulio mbele ya macho yako mwenyewe?" nikamuuliza hivyo.

Akaanza kubabaika, akitazama huku na huko huku midomo yake ikitetemeka.

"Ujitese kwa nini kushindana na hisia zako mwenyewe? Eh? Ninaona wazi kwamba unatamani kunionyesha kina kirefu cha upendo kilichomo kwenye bahari ya moyo wako... kwa nini unajizuia? Kwa nini uzame peke yako wakati niko hapa?" nikamwongelesha kwa hisia.

Akaniangalia machoni.

"Nakuomba Miryam... niruhusu niingie..." nikamwambia hivyo kwa hisia.

Akatazama chini kwa huzuni.

"Maana kiukweli inaniua kukuona namna hii... sana," nikasema hivyo.

Nikaona anajikaza kwa kumeza mate na kuzuia macho yake yasimwage machozi, nami nikamshika pande za kichwa chake kwa wororo, naye akaniangalia machoni kwa hisia.

Nikamwambia, "Acha kuogopa Miryam. Dunia haitakuona kuwa Shetani ukikubali kwamba unanipenda... hicho ni kitu unachofikiria wewe mwenyewe, lakini hakipo. Tafadhali Miryam... fungua moyo wako na uniruhusu nikuonyeshe jinsi ambavyo kupenda ni kuzuri..."

Nilimwambia hivyo kwa kubembeleza sana, naye akalegeza shingo yake kiasi na kubaki akinitazama kama vile ameishiwa nguvu yaani, na chozi likimtiririka. Alikuwa na hisia huyu!

Nikapitisha kidole gumba changu shavuni kwake na kumwambia, "Niruhusu..."

Nadhani kutoka kwenye kona ya jicho lake akawa ameona kwamba Tesha alikuja upande wetu. Akafumba mdomo wake kishupavu na kuitoa mikono yangu usoni kwake kwa mara nyingine tena, naye akaanza kuondoka haraka-haraka kutokea hapo huku akijifuta machozi. Akampita Tesha kama vile hamjui, huku mdogo wake huyo akimwita mara kadhaa, lakini Miryam akatokomea konani kabisa.

Nilibaki nikiuangalia sana upande alioelekea, nikiwa nafikiria tu ni namna gani nilivyokuwa nikihitajika bado kuendelea kuupiga huo ukuta wake Miryam uliomfanya awe mgumu mno kukiri upendo wake kwangu mpaka ubomoke, nami nikatazama chini tu na kutabasamu kiasi. Nikahisi bega langu likipigwa kutokea mgongoni, nami nikageuka kukuta ni Ankia ndiye aliyekuwa amesogea karibu yangu hatimaye.

"We' JC... ndiyo michezo gani hiyo jamani?" akauliza hivyo.

"Nilikuwa najaribu kumwingia binti maringo, ila kanisukuma tena... mhm," nikamwambia hivyo huku nikitabasamu.

Tesha akawa ametufikia, naye akauliza, "Na dada alikuwa amekuja hapa?"

"Ndiyo, tumekutania hapa. Kwa hiyo kumbe haya yote ilikuwa ni plan JC, au?" Ankia akaniuliza hivyo.

"Hapana... yaani... kuja hospitali?" nikamuuliza pia.

"Eeh... na ajali... na kila kitu," akasema Ankia.

"Hamna, me mwenyewe nimekuja hapa na Tesha kwa sabab.... subiri, nani amepatwa na ajali?" nikamuuliza tena.

"Yaani JC ndiyo apange ajali yake yeye mwenyewe?" Tesha akamuuliza.

"Tulijua ni yeye ndiyo amefariki!" Ankia akamwambia hivyo.

"Nani kakwambia hivyo wewe?" Tesha akamuuliza.

"Adelina..." Ankia akasema.

Nikawa makini zaidi.

"Taarifa ilikuwa ya maaskari, ila aliyenipigia simu ni Adelina. Akaniambia maaskari wamepiga namba yake kumtaarifu... yaani, maaskari wakasema 'ooh, tumempata mwenye simu hii, kapatwa na ajalii, kama we' ni ndugu yakee, njoo mochwari uone mwili.' Ndiyo me nikaogopa, nikawaambia na nyie, ndiyo tukaja kuthibitisha," Ankia akasema hivyo.

Tesha akanitazama kimaswali.

Nilikuwa najaribu kuelewa vizuri suala hilo, naye Ankia akaniuliza, "We' ulimpa nani simu yako, JC?"

Ohohoo! Hapo nikawa nimeelewa mchezo.

Bwana, inaonekana wezi wa simu yangu walipatwa na ajali, kwa hiyo waliombeba wakambeba pamoja na simu yangu wakifikiri ni yake, ndiyo hao maaskari wakaitumia kuwatafuta watu wa karibu na mwenye simu; nafikiri Adelina akiwa ndiyo wa kwanza shauri ya kuwa mtu wa mwisho niliyeongea naye kwenye simu kabla haijaporwa. Kwa hiyo nikawa nimepata faida ya kutopoteza simu yangu kumbe!

"Hiyo ajali unayoongelea ndiyo ile imetokea pale Mzinga?" nikamuuliza hivyo Ankia.

Ankia akasema, "Eeeh. Me ndiyo nikampigia na Miryam kumpa hiyo taarifa, na yeye akaja hapa haraka..."

Nikasema, "Aisee! Kwa hiyo... huyo jamaa wa kwenye ajali ame...."

"Ame-dead! Tena ni wawili, walikuwa kwenye boda sijui wanawahi wapi, wakapamiana na daladala hapo Mzinga si mbali na darajani. Sisi tulikuwa tunafikiri ni wewe, tumekuja hapa na Miryam... kashindwa hadi kuingia huko ndani, imebidi niende mwenyewe kuthibitisha ndiyo nikakuta siyo wewe. Natoka kuja kumwambia Miryam, ndiyo nakukuta hapa..." Ankia akasema hivyo.

Nikapiga mluzi kidogo na kutazama pembeni.

Tesha akaniuliza, "Oya, ulikuwa umempa nani simu? Si ulienda kwa Soraya?"

"Eti? Kwani imekuwaje? Hawa waliofariki unawajua?" Ankia akauliza.

Nikamwona askari mmoja akitoka ndani ya hicho chumba, nami nikawaambia hawa, "Ngojeni niongee na jamaa, nitawaelezea."

Nikamsogelea askari huyo na kumpa salamu, naye akasimama na kuanza kunisikiliza nilipokuwa namwelezea kisa changu. Yeye alinijulisha kuwa wamekosa kujua haraka watu hao waliokuwa wamepoteza maisha walikuwa ni akina nani, na hata ndugu zao pia haikufahamika haraka walikuwa wakina nani. Kwa hiyo nilipomwambia kuhusu marehemu hao kuwa wezi walioniibia simu na kusababisha mpaka hawa marafiki zangu waitwe, akaonekana kuelewa vizuri sasa.

Nikaomba tu niweze kurudishiwa simu yangu kwa sababu nilidhani ilikuwa imeshaenda, ndiyo akaniambia ningetakiwa kuifata kwa mtunzaji wa vifaa vya maiti, sijui walikuwa wanavitunzia kwenye chumba gani kati ya hivyo vya pembeni.

Haya bwana, askari akawa ameenda zake, nami nikajiunga na marafiki zangu kwenda kumsaka mtunzaji wa... huyo huyo, ili nirudishiwe simu yangu, na nikafanikiwa kurudishiwa ingawa ilikuwa kwa mbinde. Inaonekana tayari Miryam alikuwa ameshaikimbia hospitali zamani, kwa hiyo na sisi tukaondoka hapo pia hatimaye; nikianza kuwaelezea Tesha na Ankia kuhusu mkasa uliotokea muda ule niko Dar Live hadi tukajikuta ndani ya kisa hiki.

β˜…β˜…

Ndani ya dakika kadhaa, mimi, Tesha na Ankia tukawa tumerudi Mzinga hatimaye, na moja kwa moja tukaelekea makwetu. Tulikuwa tumeshampigia simu Adelina pia kumwondolea hofu juu yangu huko alikokuwa, na niliongea naye kwa urefu juu ya yaliyotokea hadi tukajikuta ndani ya suala hilo lenye kutatanisha. Akanisihi sana niwe mwangalifu zaidi maana mambo mengi yalikuwa mabaya mno mijini, ndiyo tukaagana akiwa amepata amani.

Ilinibidi ninunue chakula na kukibeba ili kwenda kukamulia kwa Ankia, maana njaa niliyokuwa nahisi iliongezeka ukali. Lakini pia furaha niliyokuwa nikihisi baada ya kilichotokea baina yangu na Miryam pale hospitali ilipita maelezo yaani, na nilijitahidi sana kujizuia lakini kila mara ningejikuta natabasamu tu mwenyewe utadhani kuna mtu alikuwa ananitekenya. Ila ni Miryam ndiye aliyekuwa akiutekenya hasa moyo wangu, hakujua tu ni namna gani kunikumbatia vile leo kulinifanya nijihisi kuwa mzawa mpya kabisa, na ningehakikisha ni yeye pekee ndiye ambaye angenilea.

Tulipofikia nyumba zetu, Tesha akasema angekwenda kwao kwanza kwa sababu alitaka kuwaona mama zake na kuwaeleza yaliyotokea, na mimi na Ankia tungeenda upande wetu pia ili tukale pamoja. Tukaachana hapo nje, nikiwa nimemwambia Tesha ningekwenda kwao nikimaliza kula, na yeye akasema angeweza kuja huku kwetu kama bado ningekuwa sijamaliza.

Tukaingia ndani na Ankia, akaleta sahani na maji, kisha tukaweka vyakula hapo na kukaa sofa moja, tukishusha msosi taratibu huku tukiongelea ishu ya leo. Alikuwa akiniambia namna ambavyo wakati amefika hospitalini na Miryam, mwanamke huyo aliongozana naye kuelekea mochwari akiwa anadondosha machozi lakini kwa kujikaza sana asionyeshe huzuni yake kuu, ikionyesha ni namna gani ambavyo taarifa ya kifo changu ilimuumiza sana.

"Kwa hiyo, yaani... akagoma kabisa kwenda kule kuangalia mwili?" nikamuuliza Ankia hivyo.

"Yaani alishindwa! Tumekokotana mpaka hapo, alikuwepo daktari sijui, akatuuliza 'mmekuja kuthibitisha mwili?' Nikamwambia 'eeeh...' 'haya, njooni muuangalie,' nikaanza kwenda namvuta Miryam, lakini akaishia pale mlangoni..."

"Ulikuwa unamvuta?"

"Tulikuwa tumeshikana, me mwenyewe nilikuwa nimeshaanza kulia, mapigo ya moyo yanadunda kishenzi... nikawa namwambia 'twende,' akagoma, akabaki hapo hapo anajipangusa tu machozi, yaani hata kuongea akashindwa. Me nikamwelewa, nikajikaza tu nikaingia. Hee! Panatisha humo!" Ankia akasema.

"Ahahah... kumbe una roho ngumu?"

"A-ah, yaani siji kurudia tena JC. Nilikuwa najikaza tu yaani, ila miguu ilikuwa inatetemeka! Alipofunua uso wa huyo jamaa hadi nikafumba macho, sikumwangalia usoni..."

"Ulijuaje siyo mimi sasa?"

"Niliona tu mikono na miguu yake, ilikuwa ni myeusi, we' ni mweupe. Nikakataa siyo wewe, akanionyesha na yule mwingine... na yeye alikuwa mweusi. Nikakataa. Baada ya hapo..."

"Ukachomoka!"

"Aaah!"

"Ahahahah... haki ya Mungu," nikasema hivyo nikiwa nahisi furaha sana.

"Eh bwana ee... si nikakukuta umemkumbatia Miryam? Em' niambie kwanza ilikuwaje?" Ankia akauliza.

Nikacheka tu kidogo na kuendelea kula.

"Si usemee?" Ankia akanishurutisha.

"Yaani Ankia... sijui hata nisemeje tu. Miryam ananipenda sana, ni dhahiri, lakini ni mwoga mno. Anaogopa mambo mengi yasiyokuwa na maana," nikamwambia hivyo.

"Alikukumbatia yeye mwenyewe?"

"Eeh. Alikuwa anaogopa kuna kitu kibaya kimenipata yaani... alikuwa ananililia... ah! Yaani hadi raha jamani. Kwa nini tu hataki kuiachia?" nikaongea kwa kuigiza njia ya deko, naye Ankia akacheka kidogo.

"Hahahah... yaani kama msemo wa mama Chande, huyo ni mpaka arogwe," akasema hivyo.

"Aa wapi, kama kurogeka asharogeka kwangu zamani sana. Kilichobaki ni kumfanya tu akiri kwamba pendo langu limemmaliza... na hana ujanja," nikamwambia hivyo.

"Wacha we!"

Nikaweka nyama mdomoni na kuanza kuitafuna kwa madoido.

"Ahahahah... ila kuna mtu amekufa JC ili tu we' ufurahi hivi, tambua siyo mazuri sana..." akaniambia hivyo.

"Siyo mazuri? Nani alimwambia aibe simu yangu? Kwa hiyo ye' kuniibia ilikuwa sawa tu?" nami nikamuuliza pia.

"Ila we' JC..."

"Hakuna. Hayo ndiyo matokeo. Hivi kwanza yaani mtu una... unaibaje, yaani... unaishika simu ya JC kuiiba... yaani, kivipi? Kifo!" nikamwambia hivyo kimasihara.

Ankia akaniangalia kwa njia ya kuhukumu, kisha sote tukacheka kidogo. Nilikuwa najihisi raha sana yaani hata ujinga ningeongea tu ili kuineemesha furaha ya kina niliyokuwa nahisi, ila najua bado kulikuwa na kazi zaidi ya kufanya.

Kwa kweli yaani hadi nilikuwa napenda sana hii vuta-nikuvute niliyokuwa naipitia kutoka kwa huyo mwanamke, Miryam yaani, kwa kuwa kadiri na jinsi ambavyo aliendelea kuzikimbia hisia zake, hakujua kuwa ndiyo alizifanya ziwe na nguvu zaidi kutokana na moyo wake kunizoea kwa kiwango cha juu. Nisingekoma hata kidogo kushinda tuzo ya kuunasa moyo wake. Hazikuwa mbali kutimia, angeyeyuka bila kupenda kwa kupenda.

β˜…β˜…

Basi, muda wa kama saa moja hivi ukawa umepita tokea mimi na Ankia tulipomaliza kula, na Tesha akawa amekuja hapa kwetu ili kujiunga nasi. Ilikuwa imeshaingia saa moja tulipoendelea kukaa na kupiga story, huku nikiwa na lengo la kwenda hapo kwao pia ndani ya muda mfupi, ndipo tukasikia honi ya gari huko nje. Ilieleweka upesi kwamba huyo alikuwa ni bibie Miryam, na Tesha akaonelea vyema tukitumia nafasi hiyo kwenda kwao hatimaye ili akamfungulie na dada yake geti; kuepuka kuwasumbua mama zake wakubwa kwa sababu alimwacha Mariam akiwa amelala.

Hivyo, tukamwacha Ankia hapo na kuelekea mpaka kwao jamaa, na kweli dada yake ndiyo alikuwa amefika. Tesha akaenda upande wa ndani ya geti na kuanza kulifungua, akiniacha hapo nje namwangalia tu dada yake. Miryam alikuwa amekaa ndani ya gari na kutazama tu mbele kwa umakini, na najua alikuwa ameshaniona lakini hakutaka kunitazama. Nikatabasamu tu kwa kukumbukia namna ambavyo alinikumbatia leo kule hospitali, na najua angejitahidi sana kunikwepa shauri ya hilo suala, lakini kuanzia hapa yaani ndiyo nisingemwacha. Ningemsumbua mpaka angechoka.

Baada ya Tesha kumfungulia geti, bibie akaliingiza gari eneo la ndani ya geti lao, kisha nami nikaingia pia na kusimama usawa wa uvaranda. Tesha akafunga geti na kuja usawa wangu, na Miryam alipotoka ndani ya gari, akatupita tu na kuelekea ndani huko bila hata kutusemesha, nami na Tesha tukaangaliana na kucheka kidogo. Tesha akasema nijitahidi kuwa mwangalifu sana kwa lolote ambalo ningejaribu kufanya maana alijua dada yake akiudhika haiwi poa hata kidogo, nami nikamwambia asiwaze.

Tulipoingia ndani kwao, nikawakuta warembo wangu wakiwa wamekaa hapo sebuleni pamoja na Miryam pia, nao wakanisalimu vizuri na kunikaribisha. Story za moja kwa moja zikawa ni kuhusiana na yaliyotokea leo hadi tukafikishana hospitali, na nikawaelezea jinsi Hali halisi ilivyokuwa mwanzo mpaka mwisho. Miryam pia alikuwa hapo akinisikiliza, na baada ya kuwaelewesha mengi vizuri ndiyo bibie akanyanyuka na kuelekea upande wa chumba ili akabadili mavazi. Alikuwa amechoka mwenyewe.

Bi Zawadi akawa ananiambia kwamba inaonekana kilichotokea leo kilikuwa ni suala la "mrejesho," au niseme "malipo," yaani ile karma kutokana na mie kuibiwa simu. Nilikuwa nimewasimulia kuhusu namna ambavyo nilimwangushia mwanamke fulani nyanya zake ndiyo mpaka nikaibiwa simu, na huyo mwanamke aliniambia kwamba ningeipata tu hiyo simu tena, hivyo Bi Zawadi aliamini kuwa maneno ya huyo mwanamke ndiyo yalisababisha huo mrejesho ukatokea. Kwamba maneno yanaumba.

Mimi sikuwa naamini sana kwamba maneno ya huyo mmama niliyemwangushia nyanya ndiyo yalifanya mpaka wezi wakapatwa na ajali ili tu niweze kuipata simu yangu, lakini yaliyotokea yalikuwa yameshatokea. Mama wakubwa wakanisihi tu niendelee kuwa mwangalifu maana walinipenda mno, hawakutaka kusikia tena taarifa mbaya kunielekea. Ikawa imeeleweka, na ni muda mfupi tu kutokea hapo ndiyo Miryam akawa amerejea sebuleni, zamu hii akiwa na Mariam.

Mariam ndiyo alikuwa ametoka kuamka, akiwa ndani ya dera nakwambia, naye akaja kukaa karibu yangu na kasura kake kalikonuna. Miryam alikuwa amebadili mavazi kwa kuvalia T-shirt nyeusi ya mikono mifupi, huku akivaa na khanga iliyofunika umbo lake la chini vizuri, naye akaelekea jikoni kushughulikia mapishi pamoja na kwamba alitoka kazini. Ila ndiyo akakaa huko huko kabisa, yaani hakuja sebuleni hata mara moja mpaka chakula alichokuwa akipika kuanza kuiva.

Alikuwa ananikwepa, yaani nilielewa hilo vizuri. Ilikuwa inakimbilia kuingia saa nne, sisi wengine tukiwa hapo sebuleni tunaangalia tamthilia na mara kwa mara Mariam akienda jikoni kwa dada yake kuangalia kama angeweza kumsaidia, lakini Miryam akawa anamwambia arudi tu kukaa. Nilikuwa nawaza sijui nimfate huko jikoni, sijui nimtumie sms, lakini nikaendelea kutulia tu. Labda ningemchokoza zaidi muda wa msosi ukifika.

Katika kutulia huko, bibie akawa amepita hapo sebuleni hatimaye, huku akibeba ndoo na kuelekea nje kwa kilichoonekana kuwa kwenda kuchukua maji pale nje bombani. Tulikuwa tunaangalia tamthilia ya waturuki nakwambia, sijui Golden Boy, na baada tu ya Miryam kutoka, nikamwangalia Tesha usoni. Jamaa akanionyesha ishara kwa macho kichini-chini kuwa nimfate dada yake, nami nikatikisa kichwa kidogo na kutoa simu yangu mfukoni. Nikaiweka sikioni na kujifanya nimepokea, tena hadi nikaongea kabisa 'hallo,' kisha nikanyanyuka na kuelekea hapo nje. Mapenzi haya! Utafanya upuuzi wowote yaani.

Nikiwa varandani, sikuweza kumwona bibie hapo, nikielewa alikuwa kwa huko bombani, hivyo nikavaa malapa yangu na kwenda upande huo, mpaka karibu kabisa na alipokuwa amesimama kusubiri maji yaijaze ndoo. Nikasimama tu na kuendelea kumtazama kutokea nyuma kwa hisia.

Taa ya hapa nyuma haikuwa imebadilishwa bado shauri ya uzembe wa Tesha, yaani palikuwa na ule ugiza uliofaa kujificha na mtu wako na kufinyana wee, lakini weupe wake bibie ulionekana vyema sana kufanya isiwe rahisi kwake kujificha hata kama angetaka kufanya hivyo. Shingo yake laini ilitamanisha sana kugusa yaani, hadi nikawa nakumbukia jinsi nilivyoishika kule hospitali. Na ni usawa huu wa ukuta wa uzio ndiyo nyumba ya Ankia hapo pembeni ilionekana vyema hadi mlangoni, kwa hiyo kama taa ingekuwa inawaka hapa tungeweza kuonwa.

Nafikiri shauri ya sauti ya maji kutoka kwa kasi hakuweza kusikia ujio wangu sehemu hiyo upesi, lakini alipoinama kufunga tu bomba nadhani akaweza kuhisi uwepo wangu nyuma yake, naye akageuka hapo hapo na kuniangalia usoni kwa umakini kiasi. Mimi nikawa namwangalia kwa hisia sana machoni pia, naye akaacha kunitazama na kuirudia ndoo yake ili aibebe. Ile kwamba hakujali uwepo wangu kabisa.

Akaibeba, na akiwa anataka kunipita, akasema, "Nipishe."

Lakini nikaendelea tu kusimama hapo hapo mbele yake kama vile sijamsikia.

Akanitazama usoni kwa macho makini sana, naye akasema kwa msisitizo, "Nipishe."

"Subiri. Nataka tuongee," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

"Sitaki kuongea na wewe. Em'... pisha bana..."

"Kwani unawahi wapi? Si upo nyumbani tayari?"

Akataka kunipita kwa nguvu, lakini nikamzibia njia kwa kusimama karibu na sehemu aliyotaka kupita. Akataka kutumia upande wangu mwingine lakini akashindwa shauri ya ndoo kubana njia. Akaniangalia usoni kwa macho makali.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Ndani utaenda tu. Nataka tuongee kuhusu saa zile."

"Tuongee nini... Jayden, nakuomba kistaarabu nipishe...."

"Ama?" nikamuuliza hivyo kimchezo.

Akanikazia macho yake.

"Shusha hiyo ndoo kwanza mkono usije ukachoka..." nikamwambia hivyo na kujaribu kuishika ndoo yake yenye maji.

"Em' niache!"

Akasema hivyo kwa sauti ya chini lakini kiukali, na aliuvuta mkono wake uliobeba ndoo kwa nguvu, hivyo maji yakawa yametikisika na kummwagikia kiasi miguuni na kwenye khanga. Nikang'ata meno yangu na kumwangalia kwa ile njia ya kujihami nikijua hilo lingemuudhi, naye kweli akaiweka ndoo chini na kuanza kutikisa viganja vyake utadhani alikuwa amelowana sana, kisha akaniangalia machoni kwa hisia kali.

"Usiniangalie hivyo, umejimwagia we' mwenyewe," nikamwambia hivyo.

Akaninyooshea kidole na kusema, "Jayden..."

"Naam..." nikaitika kizembe.

"Naomba hii ndiyo iwe mara ya mwisho kuni...."

"Unajua kwa nini ulinikumbatia leo?" nikamkatisha.

Akashusha kidole chake na kuendelea kunitazama usoni.

"Ama haikuwa wewe uliyenikumbatia? Nilikuwa naota?" nikamuuliza hivyo.

Akasema, "Cha ajabu ni nini kuhusu mimi kukukumbatia?"

"Ih? Huyu ni wewe unauliza hivyo?" nikamuuliza hivyo kimchezo.

Akabaki kimya tu.

"Si ni wewe tu ambaye hata nikikugusa kidogo, kiunoni... unanifokea, unasema hutaki mazoea, hupendi ujinga, lakini mimi kunikumbatia leo hukuona noma," nikamwambia hivyo huku nikimtazama kwa umakini.

"Nili...." akaishia hapo na kuendelea kuniangalia kama vile amekosa cha kujibu.

"Nini? Unakosa hadi cha kusema kujitetea. Umenikumbatia kwa sababu ulikuwa unaogopa nimekufa. Uwongo? Na kwa nini uogope? Ni kwa sababu unanipenda," nikamwambia hivyo kwa uhakika.

Akafumba macho yake na kutikisa kichwa, kisha akaniangalia usoni na kusema, "Jayden, naomba uniache. Unanichanganya..."

"Lazima uchanganyikiwe. Unafikiri mapenzi mchezo?"

"Usiniambie hivyo, nimeshakuzuia..."

"Kwa nini unakuwa mkaidi hivi? Eh? Just be honest with yourself. Shida ni nini? Umeshaonyesha kwamba unanipenda, waziwazi... yaani ulikuwa unanililia leo, tena unasema... 'nilidhani umenipotea Jayden...'" nikamwambia hivyo.

Akafumba macho yake taratibu na kuinamisha uso.

"Ahah... utasema nini kingine kukataa?" nikamuuliza hivyo.

"Okay. Sawa. Uko sahihi," akasema hivyo.

Kauli yake ikanifanya nimwangalie kwa matarajio mengi.

"Nilikukumbatia ndiyo, na hiyo ni kwa sababu sisi wote tulifikiri umepatwa na masaibu. Wewe ni... ni rafiki yetu... hiyo ndiyo sababu," akajitetea namna hiyo.

Nikazungusha macho kiasi kumwonyesha siamini hayo maneno.

"Ndiyo hivyo. Usifikiri mengine. Sijakukumbatia kwa sababu unazofikiri, tena ile imetokea tu kwa sababu nili-panick... basi," akasema hivyo.

Nikamsogelea karibu zaidi na kusema kwa sauti ya chini, "Acha uwongo."

Miryam akarudi nyuma kidogo, huku akinitazama machoni kwa njia fulani yenye hisia, na kwa sauti ya chini akasema, "Sidanganyi."

"Hata ukisema hivyo unadanganya, we' mwenyewe unalijua hilo," nikamwambia hivyo kwa sauti yenye kubembeleza.

"Ah..." akasema hivyo na kupiga ulimi kiasi, kama vile amechoshwa nami.

Nikamwambia, "Kuna vitu vingi tu umeshafanya kunionyesha kwamba unanipenda, ila naona hutaki kukiri hilo kwa sababu unapenda haka kamchezo ka kumkimbia jogoo. Na si ndiyo mpaka nikukamate?"

Akashusha pumzi kiasi na kunitazama, naye akasema, "Jayden..."

"Mm..." nikaitika huku nikimwangalia kizembe.

"Naona umeshakuwa obsessed na mimi, na hicho ni kitu ambacho kitakuumiza usipoangalia. Nakwambia hivi me kama dada yako. Achana na huu upuuzi, hautakusaidia kwa lolote maana hautafanikiwa..." akasema hivyo.

"Eti eh?"

"Eeh. Ninakuheshimu kama mdogo wangu Jayden, umenisaidia kwa vingi, ndiyo maana nakuwa nakuacha tu. Lakini mimi... nimeshakwambia, sipendi michezo isiyo na faida, sipendi... sipendi haya mambo. Nina... nimekukumbatia leo kwa sababu ninakujali ndiyo, siyo kwamba nakupenda... hata Ankia au ma' mkubwa angeweza... angeweza kukukumbatia hivyo hivyo, ungesema wanakupenda... au wanakutaka?"

Nilikuwa namwangalia kwa hisia makini tu, lakini aliposema hivyo akanifanya nicheke kidogo kwa pumzi.

"Usicheke, niko serious. Naomba uache kunisumbua. Sina... sina hisia kwako, nina... ninakujali tu, basi. Elewa hivyo," akaniambia hayo.

Nikamsogelea karibu zaidi tena na kumshika mkono, nami nikamwambia, "Bado unadanganya."

"E-eh... em' niachie..." akajaribu kuutoa mkono wake kwangu, lakini nikaukaza zaidi.

"Unakumbuka alichosema yule mama mchungaji?" nikamuuliza hivyo.

"Sijui bwana. Nimesema niachie," akaniambia hivyo huku akiniangalia usoni kwa kutatizika.

"Una nguvu Miryam, na moyo wako ni mzuri sana. Lakini bado kuna sehemu ndani ya hatma ya maisha yako imefichwa ndani ya gamba gumu kama la kobe, na wewe unaogopa kwamba ikitoka nje... utaumia..." nikamwambia hivyo.

Miryam akaacha kujaribu kujinasua na kunitazama machoni kwa umakini. Najua alielewa maneno hayo yalikuwa ya yule mama mchungaji aliyoambiwa siku ile tumekwenda huko kanisani pamoja, kwa hiyo nafikiri umakini wake ukavutwa kutaka kuelewa zaidi kwa nini niliyaongea sasa.

"Hata huyo mama na upako aliobarikiwa nao aliona kwamba unaogopa Miryam, lakini unakumbuka alivyokwambia?" nikamuuliza hivyo kwa upole.

"Sikumbuki, na sijali. Niachie Jayden," Miryam akasema hivyo kwa sauti tulivu.

"Alikwambia uache kuogopa. Maana ukiendelea kuogopa, unakuwa mfungwa... mfungwa wako wewe mwenyewe..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Akatazama upande wa ukutani na kutikisa kichwa kuonyesha amekerwa.

Nikamwambia, "Alisema Mwenyezi Mungu amekuandalia njia itakayokusaidia ili uwe huru, na... ahah... kiukweli Miryam sikuwa nimefikiria maneno yake vizuri siku hiyo, lakini alikuwa sahihi... upako or no upako. Hakuna mtu aliye kamili kwa lolote Miryam, na ndiyo maana huyo mama akasema tumeumbwa wawili-wawili ili tusaidiane, kukamilishana... na unafikiri ni kwa nini alienda moja kwa moja hapo?"

Akaniangalia usoni kwa utulivu.

"Ni kwa sababu ndiyo kitu ambacho wewe unahitaji zaidi ili uwe na furaha, siyo kwa kuwa tu nani anataka, au nani amesema nini... ni kwa sababu unastahili kuwa na furaha. Niko hapa sasa... niko hapa ili nikupe hiyo furaha Miryam," nikamwambia hivyo kwa sauti yenye kubembeleza.

Alikuwa ananiangalia machoni kwa utulivu wa hali ya juu, nikiona wazi jinsi ambavyo alitamani sana kuendelea kusikiliza maneno yangu. Nadhani ni kitu ambacho kilimvuta zaidi kihisia, kushawishiwa kwa maneno mazuri kama hivi, na nilikuwa najitahidi sana kumwambia yote niliyohisi kuwa kweli moyoni mwangu, na itikio lake lilionyesha kweli yalimwathiri kwa njia bora.

Nikamwachia mkono na kusema, "Napambania nachojua kuwa sahihi Miryam. Sioni ubaya wowote ule wa mimi kukupenda wewe, kwa hiyo sitaacha... kama unavyosema, kukusumbua. Nitaendelea kukusumbua mpaka utambue ni namna gani ulivyo na thamani kubwa kwangu. Nitafanya kila kitu yaani. Na mama mchungaji alisema Mungu amekuandalia zawadi ya kukueletea furaha na amani... ndiyo utambue kuwa hiyo zawadi ni mimi, nimeshafika sasa... na siendi popote tena."

Nilimwambia maneno hayo huku nikimwonyesha wazi kwamba nilikuwa sitanii, naye akaendelea kunikazia macho yake tu na kuanza kunishusha na kunipandisha.

Nikaichukua ndoo yake na kuiweka bombani tena, kisha nikafungulia maji ili ijae vizuri na kumwambia, "Labda unawaza mama mchungaji alikuwa anaongea bullshit tu. Tutaona. Ila siyo kwamba hisia zangu kwako zina-base kwenye maneno ya mtu, hiyo ni motivator tu..."

Nikainama tena kufunga bomba, na Miryam alikuwa ametulia kweli wakati huu, yaani ilikuwa kama vile naongea na msichana mdogo aliyetuliza boli kusikiliza maelekezo.

Bila kumwangalia usoni, nikasema kwa sauti tulivu, "Nakupenda, Miryam. Haitapita siku sitakwambia hivi."

Kisha nikamtazama usoni na kukuta ametazamisha uso wake ukutani kama kuonyesha hajali, nami nikageuka tu na kuamua kuondoka hatimaye. Mapenzi hayo!

Na ni ya namna hii ndiyo ambayo hata mimi nilikuwa nahitaji kwa kweli. Kumbembeleza namna hiyo huyo mwanamke yaani kulinifanya nijisikie vizuri sana, maana aliitikia ushawishi wangu kwa njia iliyoonyesha alikubali, haijalishi alikuwa akiigiza vipi kukataa. Sikutaka kutumia mbinu za kibabe kwa Miryam, yaani niende na swaga zangu zile za zamani, hapana. Hizi pigo za kitamthilia ndiyo zilimfaa.

Moyo wake ulikuwa umeshanikubali, najua alinipenda, lingekuwa ni suala tu la kufanya midomo yake ikiri hilo. Ingekuwa ni ishu ya kungoja tu siku hiyo ifike, na baada ya hapo ndiyo ningemfanya atambue ni mengi mazuri kadiri gani aliyokuwa anayakosa kwa kuepuka kupendwa.

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana
 
Manzi ameshakuelewa kitambo yani sema tu analeta ile SITAKI NATAKA.Mwanangu mnang'ang'anie kama ruba vileeeeeeπŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°
 
Sema sitaki nataka huwa inanogesha sana MAPENZI sema siku hizi ndo hivyo MAPENZI ya hivi hayapo imebaki kuuziana NGONO tu.
 
Respect rana kiongozi, tuachie nyingine midnight ndugu kipenzi chetu Elton Tonny....
 
πŸ‘‹ πŸ‘‹ πŸ‘‹ πŸ‘‹ Mr captain 😊 😊 😊 😊 Tumemmiss sana Jc na MIMI....pls tupatie basi raha Mr captain πŸ™πŸ™πŸ™ sanaaaa
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

Asubuhi ya siku ya Jumatano ikawa imefika hatimaye. Siku iliyotangulia nilikuwa nimepitia kisa chenye utata kiasi nilipoibiwa simu na kuirejesha tena baada ya marafiki zangu kudhani nilipatwa na ajali, na matokeo yake kwa kweli yalinipa manufaa mengi zaidi tu ya simu kurudi kwa kuwa Miryam alionyesha wazi zaidi kuwa alinijali kupita kiasi. Hata nikamsemesha kidogo pale bombani kwao na yeye kuonekana akivutwa na maneno yangu, hivyo bado kumshawishi awe wangu lingetakiwa kuwa pambano endelevu.

Yaani nilikula pale pale kwake bibie hiyo jana usiku na kuja tu kupumzika mapema hapa kwa Ankia, kwa sababu leo nilitaka kutoka. Ndiyo, kuna sehemu muhimu ningeenda leo, na hiyo ilikuwa ni huko Kivukoni katika jengo la mahakama kuu ili nikahudhurie kusimama kwake madam Bertha mbele ya hakimu. Askari Ramadhan alikuwa amenitumia anwani ya hilo eneo, akisema mahakama ingefunguliwa kwenye mida ya saa tatu asubuhi na usikilizwaji wa mwanzo wa kesi za Bertha ukifanywa saa nane mchana, nami ndiyo nikamwambia ningefika huko kuona jinsi ambavyo mambo yangekwenda.

Zilikuwa zimepita siku chache tu tangu madam Bertha alipokamatwa, lakini nilihisi ni kama vile sikumwona kwa muda mrefu. Nilitaka sana nimwone. Yaani nilikuwa nimeshamzoea mno akiwa ndani ya hali yake ya uhuru, kwa hiyo nilitaka kuangalia namna ambavyo angekuwa chini ya ulinzi, na nini kingefuata baada ya maoni yake kuwasilishwa kwa hakimu.

Kwa hiyo nikaamua kujiandaa vizuri, nikavaa T-shirt langu jeupe lenye mikono mirefu na jeans ya blue, kisha nikanywa chai pamoja na Ankia na mama Chande rafiki yake, aliyekuwa amekuja kunisalimia tena tokea juzi nilipokuwa mgonjwa. Ndiyo akakuta nimeshapata nafuu, tena sasa nilikuwa tayari kutoka, na uamuzi ukawa kwenda kwanza hapo kwake Miryam kuwasalimia wapendwa wangu na kutumia muda pamoja na Mariam kabla sijaanza safari ya kuelekea Kivukoni huko. Nilitaka tu kufika huko mahakamani mapema sana.

Nimekuja kuondoka hapo kwa Ankia ikiwa imeshafika mida ya saa nne, nami moja kwa moja nikaenda hadi kwake Miryam kama vile mwenyeji wa maisha. Gari la bibie halikuwepo kwa hiyo ni wazi alikuwa ameshatimkia kazini kwake, na nadhani leo tungekuja kuonana jioni. Nikaingia hapo sebuleni na kuwakuta mama wakubwa wakiwa wamekaa kwenye sofa lao, na Mariam akiwa pembeni anatazama marudio ya tamthilia kwenye TV.

Baada ya kuwasalimu, nilitambua kuwa kulikuwa na tatizo fulani, hasa kwa upande wa Bi Jamila. Mariam na Bi Zawadi waliniitikia kwa uchangamfu kama ilivyokuwa kawaida, ila Bi Jamila alionekana kama amekoseshwa raha na jambo fulani, kwa hiyo uso wake ulionyesha karaha. Hii hata ikanikumbusha namna ambavyo jana mwanamke huyo alionekana kutatizika sana baada ya kuiona picha ya mama yangu, na sijui kwa wakati huu tatizo lingekuwa nini, ila nilihisi kuwa na budi ya kuuliza. Hiyo inamaanisha sikutakiwa kuuliza!

Nikakaa tu sofani pembeni yake Mariam, na umakini wake wote kwa wakati huu ulikuwa kwenye katuni fulani baada ya kuwa amebadili chaneli, katuni iitwayo Zig na Sharko, kwa hiyo najua ningemkatishia uhondo endapo ningeingiza masuala ya kuanza kucheza naye. Nikaona nimwache kwanza mpaka amalize.

"Vipi maandalizi?" nikawauliza mama wakubwa.

Bi Zawadi akaniangalia na kuuliza, "Ya harusi?"

"Eeh. Ni kitchen party lakini kesho, si ndiyo?" nikamuuliza pia.

"Eeeh. Kitchen party ya Doris, halafu wanafanya na send-off Jumamosi, yaani hakuna kuchelewa. Maandalizi ya kitchen party kesho inaonekana yako mbioni kukamilika kabisaa. Sisi tutaenda kwenye send-off lakini, hayo ya kitchen party tunawaachia wakina Mimi hahahah..." akasema hivyo na kucheka kidogo.

"Ahahah... ungeenda tu kama mlikuwa mmealikwa," nikamwambia.

"Hamna, hizo ni za kwao zaidi. Shadya anawaletea nguo hawa baadaye jioni, watachagua za kuvaa. Na Mariam anaenda pia," akaniambia hivyo.

"Ahaa... safi. Shadya ataleta nguo kutoka dukani kwake mwenyewe?" nikamuuliza.

"Eeeh. Ila japo sisi hatuendi lakini tutachukua na nguo nzuri zikiwepo za kutufaa ili tuvalie send-off... na Krismasi," akasema hivyo na kucheka kidogo.

Nikacheka pia na kumtazama Bi Jamila, ambaye bado alikuwa na uso makini tu kama vile hajali lolote la hapo. Nikaona haingekuwa vyema kumchokoza kwa yale masuala ya 'mrembo wangu.'

"Unataka kumfundisha Mamu? Tuzime TV?" Bi Zawadi akauliza hivyo.

Mariam akamwangalia kiumakini.

"A.. hapana, ahahah... acha tu amalize kwanza kuangalia," nikasema hivyo.

Bi Zawadi akanionyesha kwa ishara ya mdomo wake nimwangalie Mariam, nami nikaona binti alivyokuwa ameweka uso wa kununa eti kisa kasikia TV inataka kuzimwa.

"Basi mama, we' angalia tu. Nilikuwa natania," Bi Zawadi akamwambia hivyo Mariam.

"Si na Ankia atakuja kwenye kuchagua nguo?" nikamuuliza Bi Zawadi.

"Ee, atakuja. Ankia, Mimi, Shadya, na Mamu. Halafu Shadya amemwita na Dina, kwa hiyo labda na kenyewe katakuja baadaye," akanijibu hivyo.

"Okay sawa," nikasema.

"Kaka yuko chumbani," Mariam akasema hivyo.

"Tesha? Yupo chumbani?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa kukubali.

"Kumbe Tesha yuko ndani? Hata sina habari. Leo pako kimya kweli nikafikiri ametoka," Bi Zawadi akaongea hivyo.

"Ngoja nimcheki," nikamwambia.

"Ee, mwangalie..."

Baada ya Bi Zawadi kusema hivyo, nikanyanyuka na kuelekea upande wa chumba chake Tesha, nami nikaufikia mlango na kuufungua.

Nikakuta jamaa akiwa amelala kitandani kwake kwa kuegamia mto, simu yake ikiwa mkononi, earphones masikioni, akionekana kuangalia jambo fulani humo. Aliponitazama na kuona ni mimi, akajinyanyua na kugeukia upande mwingine wa kitanda, huku akiendelea kutazama simu yake na kuongea kwa sauti ya chini sana. Nikawa nimeelewa kwamba alikuwa akiwasiliana na mwanamke fulani kwa njia ya video call, naye akanionyesha ishara nikae kitandani kusubiri amalize.

Nikaenda tu na kukaa kitandani kweli, nikimsikia alivyoongea na huyo mwanamke. Kusikiliza kwa umakini maongezi yake kukanifanya nitambue kwamba alikuwa anaongea na mpenzi wake wa kule Tandika, yule aliyeitwa Happy, na inaonekana alimkubali sana. Hapo sasa ndiyo nikawa naona jinsi bukta ya jamaa ilivyotuna kuelekea juu, ikionekana huyo mwanamke alikuwa anamkatia viuno humo kwenye video ama kufanya mambo mengine yenye kusisimua, nami nikatabasamu tu na kutoa simu yangu pia kuangalia nini kipya.

Baada ya dakika mbili tatu hivi, akawa ameagana na huyo mwanamke hatimaye kwa kumpa kisingizio cha kwenda kuoga ili atoke ndani, ndiyo akakata simu.

"Oya!" akasema hivyo huku akitikisa kichwa kuonyesha furaha.

Nikamwambia, "Hata me naona."

"Ahahah... dah! Happy wa ukweli sana mwanangu. Yaani anafanya yote ili nifurahie kuwa naye. Hadi nguo ananivulia kwenye simu!" akaongea hivyo kwa sauti ya chini.

"Anakupenda. Yuko wapi hapo?"

"Kwake. Hajaingia kazini leo."

"Si ungeenda sa'?"

"Ah... naona jau. Nilikuwa nataka nitulie tu ndani leo mpaka jioni."

"Na Dina anakuja nimeambiwa..."

"Ee, demu wako anakuja," akaniambia hivyo.

"Ah, usimwite hivyo bana," nikamwambia hivyo, nasi tukacheka kidogo kwa pamoja.

"Umeshamtema, najua. Na wanakuja na Shadya baadaye kuchagua manguo ya hiyo harusi. Sijui hata kama patachangamka kihivyo maana kuna wengine wamenuniana," akasema hivyo.

"Ahahah... nani tena?"

"Ma' mkubwa na da' Mimi," akasema.

Kauli yake ikanifanya niwe makini zaidi na kuuliza, "Dada yako amemnunia ma' mkubwa?"

"Siyo hivyo, ila... yaani, kama tu ka amani kametikiswa. Jana walivurugana," akasema kwa sauti ya chini.

"Ma' mkubwa yupi?"

"Mkubwa."

Nikaelewa huyo kuwa Bi Jamila, nami nikamuuliza Tesha, "Wamevurugana kisa nini?"

"Ah, sijamaanisha wamepigana..."

"Naelewa bana..."

"Ee, yaani... ma' mkubwa anamsisitizia dada awe na familia yake. Anataka da' Mimi apate mume, atulie kwenye ndoa, azae. Umri unaenda, ukimwangalia dada unaona kabisa huu ndiyo wakati wake yaani... lakini bado kakaza. Sasa... jana usiku ndo' kwenye kuongea naye, hisia za ma' mkubwa zikapanda. Akamwambia hatapumzika kwa amani endapo atakufa kabla hajawaona watoto wa mjukuu wake..."

"Aisee..."

"Da' Mimi naye akajisikia vibaya... ma' mkubwa kumwambia vitu vya namna hiyo, inaonekana ni kwa sababu ya shinikizo," Tesha akasema hivyo.

"Kutoka kwa nani?"

"Shangazi. Mama yake Dina na Doris, yule?"

"Ndiyo..."

"Huwa ana maneno. Hapo juzi inaonekana waliongea na ma' mkubwa kuhusiana na ishu ya dada kutotaka kuolewa, ndo' maana hadi akaongea hayo jana. Si unajua huwa wanamtafutia mume na nini, yaani bro kwenye hii familia yetu wanaonaga ndoa ndo' kila kitu. Da' Mimi ye' akamwambia ma' mkubwa wakati wa hiyo ishu utafika tu maana sasa hivi mambo ni mengi kwake. Sa' ndo' kuni zikachochewa moto mwanangu, ma' mkubwa akamwomba dada aapie kwa jina la mama yetu mzazi kuwahi kuolewa na kuzaa... ili eti ma' mkubwa akifa, afe kwa amani," Tesha akasema hivyo.

Nikaangalia pembeni tu kwa utulivu. Hilo lilikuwa jambo zito.

"Me hata siwaelewi-elewi. Ila kaka, hata mimi naona dada anajiweka nyuma sana. Wanaume kibao wanamtaka, hawataki. Festo ndo' kajitahidi sana, lakini na ye' hamna kitu. We' mwenyewe kakukataa... sijui labda anataka kuwa kama ma-sister wa roma? Au labda ana mtu wake huko ila ndo' kamficha... lakini ma' mkubwa yuko sahihi. Huu ndiyo wakati wake. Sijui tu sa' ye' anataka nini, maana ma' mkubwa anamtakia mazuri, lakini ndiyo hivyo," Tesha akasema hayo.

"Hayo yote waliyaongea na nyie mkiwepo?" nikamuuliza.

"Hamna, ni da' Mimi na mama hawa. Waliongea mpaka saa saba, Mamu alikuwa amelala. Wenyewe walikuwa wanaongea hapo sebuleni, me nikatoka kuchungulia ndiyo nikasikia. Leo dada ameondoka mapema kweli, hajaongea na mtu. Ma' mkubwa anamtakia dada mazuri, I know... ila najua da' Mimi na yeye atakuwa anahisi pressure sana, kila mtu anataka aishi hivi au vile, yaani dah!" Tesha akasema hivyo

Baada ya kuelewa sasa sababu iliyokuwa imefanya Bi Jamila aonekane kukwazika, nikawa nimeelewa pia kuwa kwa wakati huu Miryam hakuwa sehemu nzuri kihisia. Ni lazima maneno hayo ya mama yake yalikuwa yamemchoma sana, nami nikahisi uhitaji wa kufanya jambo fulani kujaribu kumfikia Miryam kidogo.

"Fanya fanya mambo umwoe dada yangu basi, JC," Tesha akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Ili hiyo pressure imtoke, eti?"

"Ee. Ama na we' ndo' ushakubali kushindwa?" akauliza hivyo.

"Hapana. Ngoja tu niendelee kumjaribu, mengine tutaona," nikamwambia hivyo.

"Haya. Nilikuwa nafikiria kuhusu kuondoka hapa, nikakae na Happy huko Tandika mpaka nikipata kazi, lakini hii ni moja ya hali zinazofanya nisichukue huo uamuzi. Sitaki kuondoka yaani... mpaka nione dada yuko sawa. Na Mariam pia," Tesha akasema hivyo kwa hisia.

Haya yote yalinigusa sana. Tesha akawa amenisifia kwa kuvaa vizuri na kuuliza nilikuwa naenda wapi, nami nikamwambia nilikuwa naelekea Kivukoni mara moja kufatilia ishu muhimu huko mahakamani. Sikumweka wazi kwamba ilihusiana na Bertha. Nikaona ingekuwa bora kuondoka hapo sasa hivi, kwa sababu nikawa nimeamua kwenda sehemu nyingine kwanza kabla ya kufika mahakamani. Mazoezi yangu na Mariam ningeyapangia muda wakati mwingine.

Nikamwambia Tesha mimi ndiyo naondoka sasa, tungekuja kuonana jioni. Hakuwa na neno, na baada ya kumwacha hapo chumbani, nikaenda kuwaaga mama wakubwa pamoja na Mariam pia, nikiwaambia ningerudi baadaye kabisa na kutumia muda pamoja nao wote, nao wakanitakia safari njema.

β˜…β˜…

Nilichukua usafiri wa daladala mpaka Rangi Tatu, kisha nikaelekea Zakhem na kupanda bajaji za kunipeleka huko Kijichi. Ndiyo, niliamua kwenda huko kazini kwa bibie Miryam kwanza, maana nilitaka kwenda kumpa faraja ambayo sidhani kama alijua aliihitaji. Miryam alikuwa anapenda kubeba kila kitu yeye mwenyewe, na ndiyo nilikuwa naenda kumwonyesha kuwa hakuhitaji kuendelea kufanya hivyo hata kama matatizo yalikuwa yake tu. Nilikuwa hapa kwa ajili yake.

Nikawa nimefikia kituo cha Upendo, na wakati naenda kuvuka barabara, nikasogelewa na mdada mmoja mfupi, aliyekuwa na makalio makubwa kweli halafu akiyaficha kwa sketi fupi iliyoacha mapaja yake wazi, eti akasema anataka nimvushe barabarani asije kugongwa na gari. Dah! Nikasema poa, kakanishika mkono nakwambia ili tuvuke, na baada ya kufika upande wa pili nikakatelekeza kabisa maana kalikuwa kanaonyesha nia ya kutaka kunisemesha zaidi. Kweli mtu mzima anaogopa kuvuka barabara na macho yote anayo, au basi tu!

Nikashuka zangu mpaka kulifikia duka kubwa la bibie. Nje palionekana vizuri kama palivyokuwa sikuzote. Gari lake Miryam lilikuwepo hapo nje, na nilipokaribia milango ya kuingilia huko ndani nikaona kibango kidogo kilichoning'inizwa kwa ndani sehemu ya kioo kilichokuwa mlangoni, ambacho kiliandikwa "CLOSED." Najua Miryam alikuwepo, lakini bila shaka aliamua kuweka hivyo ili wateja wasije hapo kwa wakati huu. Nadhani alihitaji muda wa kuwa yeye kama yeye, labda 'focus' nzuri ya kikazi hakuwa nayo.

Nikasukuma mlango na kuingia ndani, na hapo kwenye meza ambayo Soraya angekaa sikuzote palikuwa tupu, na mlango wa kuelekea ofisini kwake Miryam ulikuwa wazi. Yaani hapa hata kama mtu angeingia mida hii na kuamua kuiba bidhaa zilizokuwepo upande huu, ingekuwa ni rahisi sana, kwa hiyo kweli palimhitaji Soraya arejee maana Miryam asingeweza kujigawa mara mbili. Nikatembea kuielekea ofisi yake na kufikia mlangoni, na hapo nikawa nimemwona bibie.

Miryam alikuwa amesimama karibu na dirisha pana upande wa pembeni zaidi wa ofisi yake, akitazama huko nje kwa njia tulivu tu, lakini niliona wazi kwamba alijawa na mawazo mengi sana. Alikuwa amevaa vizuri, nguo kama shati refu sana yenye rangi nyeupe, pamoja na suruali pana ya kitambaa ya aina hiyo hiyo, na nywele zake alikuwa ameziachia na kuzilaza upande mmoja wa bega lake kwa mbele, chache zikifunika sikio la upande mwingine wa bega. Yaani nywele zake zilikuwa laini na ndefu kweli, ungefikiri ni mzungu. Alijua kuzitunza, sijui hata alikuwa anatumia shampoo gani, nilipenda sana.

Ni kama alikuwa ametekwa kwelikweli na fikira za mambo mengi kiasi kwamba hakutambua uwepo wangu sehemu hii, hivyo nikafanya kuugonga mlango pembeni yangu mara mbili. Akageuza uso wake na kupata kuniona sasa hatimaye, naye akaonekana kushangazwa kiasi na mimi kuwa hapo muda huo.

Nikiwa namwangalia kwa hisia, nikaingia kiasi ofisini humo na kumwambia, "Habari za saa hizi, Miryam?"

Akaonyesha uso wenye kukosa amani na kusema kwa sauti ya chini, "Jayden, tafadhali... sitaki uniletee mambo yako sasa hivi..."

Nikasimama na kumwambia, "Nimekuja tu kukusalimia."

Akafumba macho na kisha kusogelea sofa-kiti dogo pembeni yake na kuketi, nami nikaanza kwenda hapo.

"Unapaswa uwe makini. Mwizi anaweza akaingia hapa," nikasema hivyo kwa upole.

Akabaki kimya na kuangalia chini tu.

"Unaonekana kama huna raha," nikamwambia hivyo baada ya kumfikia na kukaa kwenye sofa lililotazamana na lake.

"Jayden nakuomba uniache. Tafadhali na tafadhali sana, sitaki usumbufu wako sasa hivi..." akasema hivyo kwa hisia za kushuka moyo.

"Sijaja kukusumbua Miryam. Nimekuja tu kama rafiki... kukuona," nikamwambia hivyo kiupole.

Akawa hataki kunitazama usoni na kuonekana kuudhika.

"Siyo kwamba nitakuwa sababu ya wewe kukosa raha kila ukiniona, usinichukulie hivyo. Me ndiyo nataka kuwa sababu ya wewe kupata amani, kwa lolote lile naloweza kufanya... maana naelewa vizuri pia tension za kwenye familia zinavyokuwa..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Hatimaye akaniangalia machoni, nikiona wazi kuwa kauli yangu ilivuta umakini wake.

Kwa ustaarabu, nikamwambia, "Najua kuhusu Bi Jamila. Nilimkuta yuko grim leo... Tesha ndiyo akawa ameniambia yaliyotokea jana."

Akaendelea kuniangalia machoni kwa hisia.

"Anakutakia mazuri, kama watu wengine wote. Ila siyo makosa yako kwamba umechagua kuwapenda ndugu zako kwanza badala ya kujitanguliza wewe mwenyewe, na muda mwingine tu inakuwa ngumu kwao kuelewa hilo kutokana na misingi iliyopo kwa familia yenu..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Miryam akaonekana kuguswa kiasi na maneno hayo, na machozi yakaanza kujaa machoni mwake huku akijitahidi kuzuia yasimwagike, lakini akashindwa. Kweli hiki ni kitu kilichokuwa kimemkwaza sana. Nikamfuta chozi upande mmoja wa jicho lake, naye akaniangalia machoni kwa hisia.

Nikamwambia, "Wanakupenda... ila hali kama hizi zitatokea maana siyo wote wataweza kukuelewa vizuri."

Akashusha pumzi kiasi ili kujipa utulivu, naye akajifuta machozi na kusema, "Kwa hiyo bado pamoja na kila kitu ninachofanya... mimi ni mbinafsi? Kwhh... kwa sababu tu sijataka kufanya wanachonilazimisha nifanye?"

Nikaendelea kumtazama tu kwa utulivu.

"Hhh... mimi ni mtoto mdogo? Kwamba sijui ninachotaka kwenye maisha yangu mwenyewe? Kweli mimi naambiwa... nitoe kiapo cha kuolewa juu ya maisha ya marehemu mama yangu?" akaongea kwa hisia sana.

Nikaangalia chini kwa huzuni kiasi.

Akashusha pumzi kiasi na kusema, "Mama mkubwa ameenda mbali sana. Yaani sikutegemea. Kutakiana mazuri ndiyo mpaka.... kweli anaruhusu maneno ya watu yamfanye aniambie mimi vitu kama hivyo? Anataka kunipeleka mimi kama wakina Shadya walivyokuwa wanafanya, utafikiri nimekuwa ng'ombe sasa?"

"Nadhani tu mama yako anataka ujitangulize ili uwe na furaha Miryam... siyo kwamba anataka kukuendesha...."

"Hapana... hapana..." akanikatisha huku akitikisa kichwa chake kukataa.

Nikaendelea kumwangalia kwa hisia.

Akajifuta machozi na kusema, "Huyo hakuwa mama mkubwa nayemfahamu. Toka tumalize birthday... nimegundua kuna mambo mengi amewekewa akilini kumfanya mpaka aniambie hivi vitu.
Wameipika akili yake vibaya... yaani... haijawahi kutokea nikahisi ananipinga. Yeye ndiyo huwa ananipa moral support... muhimu... kila mara napohitaji, halafu leo... hhh... ahhh..."

Akashindwa kuendelea kuzungumza na kilio cha pumzi kumteka kwenye sauti. Nikaingiwa na simanzi zaidi kumwona namna hiyo, na yeye akajitahidi kukaza moyo na kukizuia kile kilio chenyewe kuja.

Nikamwambia, "Nafikiri unatakiwa kuongea naye."

Akaniangalia usoni kwa hisia.

"Ongea naye vizuri. Aone uhalisia kwa point of view ya kwako pia, siyo yake tu. Ana moyo mzuri kama wako... ataelewa. Tena... nafikiri itakuwa vizuri ukifanya initiation, maana anaweza akawa anajisikia vibaya, au kuogopa kwamba umemkasirikia baada ya kuwa amekwambia hayo jana..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Akashusha macho yake taratibu kwa huzuni.

"Usilie Miryam. Tafadhali..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Akaniangalia kwa ufupi, kisha akaanza kujifuta machozi tena.

Nilikuwa namwonea huruma, nikitamani hata kuendelea kuwa hapa, lakini hili ni suala ambalo lingehitaji awe na uhuru wa kiakili wa peke yake kulitafakari na kujua ya kufanya zaidi, kwa hiyo nikamwambia, "Kila kitu kitakuwa sawa. Mambo yataenda vizuri."

Akaonekana kuzama tu ndani ya fikira zake mwenyewe.

"Basi... wacha me niende. Nafika Kivukoni mara moja. Tutaonana baadaye," nikamwambia hivyo.

Akaniangalia na kutikisa kichwa kukubali hilo.

Yaani hapa tulikuwa tumeweka zile kesi zetu pembeni kabisa, na angalau nikafarijika baada ya maneno yangu kuonekana kumgusa kiasi mpaka niliposema asilie, akawa amejifuta machozi hapo hapo kama vile kunitii. Kwa hiyo nikaamua tu kusimama na kuanza kuuelekea mlango, na ile nimeukaribia, nikageuka na kumtazama tena. Alikuwa ameangalia upande wa dirisha wakati huu.

Nikasema, "Najua hujala Miryam..."

Akaniangalia usoni kwa njia makini.

"Na hivi Soraya hayupo, ndo' najua utakaa mpaka jioni bila kula. Fanya kuiba mkate hapa hapa, ule wote mkavu bila soda wala maji, halafu ushushie na ream paper ushibe kabisa... ndiyo uendelee na kazi," nikamwambia hivyo.

Nilikuwa najaribu kumtania, na itikio lake likawa kunitazama kimaswali, kisha nikaona tabasamu hafifu sana likitaka kujengeka usoni mwake.

Nikatabasamu na kumwambia, "Eeh, ream paper zinaliwa kama ulikuwa hujui. Tafuta bunda lote la A4 ule, afu' nitakuja kulipia."

Miryam akatabasamu kwa mbali sana na kufumba macho taratibu, halafu akaangalia pembeni tena na kutikisa kichwa kama vile ananiona bonge moja la fala.

Nikiwa natabasamu, nikamwambia, "Na ole wako usile sasa. Nitajua tu."

Akarudisha macho yake kwangu na kunitazama kwa hisia makini.

Nikasema, "Baadaye basi."

Niliona wazi namna ambavyo alipata ahueni kutokana na kukaribia kutabasamu tena, nami ndiyo nikageuka na kutoka ofisini kwake hatimaye.

Nikaondoka hapo dukani kwake huku nikiwa natabasamu kiasi, nikijisikia vizuri kuwa angalau nilifanya uvutano baina yangu na yeye uzidi kuwa na nguvu taratibu tu. Ilipendeza kuona kwamba ule mguso wangu wa kirafiki pamoja naye haukuwa umepotea bado, na ningeendelea kuuimarisha hata zaidi ili kuchochea hisia za kimapenzi kati yetu zing'atane kwa wakati uliofaa. Nikatafuta usafiri tena ili nianze safari ya kuelekea Kivukoni hatimaye, ikiwa ni mida ya saa sita mchana sasa.

β˜…β˜…

Nilichukua daladala za kuelekea mpaka huko Toangoma, kisha nikapanda za kwenda Kigamboni, halafu ndiyo nikapanda bajaji ambayo ilinipeleka mpaka kwenye barabara ya Kivukoni. Nilikuwa nimepitisha muda tokea mara ya mwisho kuja maeneo ya Kivukoni huku, yaani mara ya mwisho ikiwa wakati fulani kipindi cha nyuma nilipokuja kwenye mizunguko, kwa hiyo sikuwa mgeni wa upande huu wa jiji uliokuwa maskani ya vitu vingi bora zaidi vya nchi hii.

Yaani niliyapita majengo ya makumbusho yaliyotunzia hazina za kale za nchi, nyumba na miundombinu ya ukweli, mpaka nafika eneo la mahakama kuu ilikuwa imeshaingia saa nane kabisa. Hakukuwa na muda wa kupoteza zaidi kwa kuwa nadhani tayari Bertha alikuwa ameshafikishwa hapo mahakamani, hivyo nikalipia usafiri haraka na kuelekea huko upesi.

Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwangu kuja kwenye hii mahakama. Jengo hilo lilikuwa kubwa, pana lenye maghorofa kama manne matatu hivi, kukiwa na kumbi na vyumba maalumu kwa masuala ya kisheria na stakabadhi rasmi za kitaifa. Sijui kama hilo ndiyo neno sahihi, lakini palikuwa na ule u-rasmi kwelikweli. Nilielewa hii ilikuwa moja kati ya mahakama kubwa ndani ya divisheni tatu muhimu za mahakama kuu na rufani, kwa hiyo mambo yalikwenda kwa utaratibu ulionyooka. Kama walisema kesi inaanza saa nane, ilikuwa ni saa nane, kwa hiyo kuwahi lilikuwa jambo muhimu.

Hapo nje ya jengo kulikuwa na magari kadhaa, na moja lilikuwa la maaskari. Nikapata kuliona na gari lake askari Ramadhan, kwa hiyo bila shaka alikuwa huko ndani. Nikamfikia afisa mmoja wa usalama usawa wa malango ya kuingilia, ambaye akanipima kuhakikisha sijabeba silaha, nami nikauliza ukumbi mkuu wa mahakama ulikuwa ghorofa ya ngapi, ndiyo akaniambia ya kwanza. Nikamshukuru na kuzielekea ngazi, nikapanda mpaka huko juu, na kweli nikafikia korido lililoelekea moja kwa moja kwenye milango miwili iliyokuwa imeachwa wazi, ndani ya ukumbi wa mahakama yenyewe.

Nikaelekea huko taratibu hadi nilipofikia malangoni, nami nikaona jinsi ambavyo ndani humo palikuwa na mwonekano mpana na wa kimahakama kama nilivyotarajia. Mabenchi marefu kadhaa kwa pande mbili, sehemu za kukaa wanasheria na watuhumiwa wao ama watoa mashtaka pale mbele, sehemu ya vizimba vya watuhumiwa na majaji (jury), na ya hakimu mwenyewe katikati huko juu-juu. Kulikuwa na watu wasio wengi sana, wakikaa na wengine kusimama, na nilitambua upesi waliosimama kuwa madam Bertha mwenyewe, maaskari wawili wanawake pembeni zaidi kutokea aliposimama Bertha, na askari Ramadhan pia.

Sikuweza kumwona Bertha usoni, lakini nilijua ni yeye. Alisimama katikati kabisa hapo mbele kutazamana na hakimu, na huyo hakimu alikuwa ni mwanamke mtu mzima, akikaa kwa utulivu huku akiwa amevaa shuka jeusi. Ah, joho! Hakimu huyo alikuwa ameshaanza kusoma maelezo aliyopewa kuhusiana na kesi zilizomkabili Bertha, akiorodhesha tuhuma za madai na makosa ya jinai ambayo mwanamke huyo alikuwa ametuhumiwa kuhusika nayo.

Nilikuwa nimesimama mlangoni bado, na askari Ramadhan akawa ameniona kutokea huko mbele. Akanifanyia ishara kwa kichwa kuwa niingie, nami nilipoanza kuingia tu, Bertha akawa amegeuka nyuma pia. Nilikuwa nimeanza kuingia kwenye sehemu ya benchi-kiti la kukalia, na macho yake yalipokutana na yangu, nikaishia kusimama na kuendelea kumwangalia tu kwa utulivu. Yaani kama siyo kwamba alikuwa na machale ya hali ya juu, sijui tu alihisije kwamba nimefika hapo mpaka kunigeukia!

Mwonekano wake ulikuwa tofauti kabisa. Alikuwa amevalishwa nguo ya karoti tayari, na nakumbuka mara mwisho kumwona alibeba manywele ya rasta nene nyekundu, lakini sasa hivi nywele zake zilikuwa zimefumuliwa na kuzagaa kichwani kwa njia isiyo ya matunzo. Sehemu ya juu kwenye shavu lake ilionekana kuvimba, nami nikawa nimeelewa kwamba kuna matendo ya kijeuri yaliyokuwa yamempata baada ya kuwekwa ndani na maaskari kwa hizo siku chache. Yaani... alionekana kuchoka, kama vile mtu wa hali ya chini sana asiyekuwa na msaada.

Taratibu akaacha kuniangalia na kutazama mbele tena, nami nikakaa tu hapo hapo benchini, tena huku mwishoni kabisa peke yangu. Kuna blah blah blah nyingi ambazo hakimu alikuwa akisema, na hata mwanaume fulani hapo mbele alikuwa akijibu maswali yake mafupi kwa ajili ya madam, akiwa ni msemaji wa hakimu, nami nikamwona jamaa mwingine aliyevalia joho na kuketi upande wake madam na kutambua alikuwa mwanasheria wake. Ndipo hakimu akawa ameongea na Bertha moja kwa moja, akimwambia ajibu ikiwa madai hayo yote yaliyosomwa yalikuwa ya kweli, au uwongo. Akiri ikiwa ana hatia, ama hana hatia.

Ukimya ukafuata kwa sekunde chache, Bertha akiwa ametulia tu kwa kuinamisha uso wake, naye hakimu akaona amuulize tena. Kulikuwa na hali fulani nzito hivi, yaani hakimu akarudia kwa mara ya tatu tena kumuuliza Bertha swali hilo, na hata mwanasheria wake alipojaribu kumwongelesha, msemaji wa hakimu akamnyamazisha mwanasheria huyo na kusema ni nafasi ya mtuhumiwa pekee kuongea.

Ndipo Bertha akanyanyua uso wake na kusema, "Ndiyo mheshimiwa. Nakiri kuwa na hatia."

Nilihisi ni kama vile sikuwa nimemsikia vizuri, maana jibu lake halikuonekana kuwa lake kabisa! Mwanasheria wake akasimama na kujaribu kuongea kitu kupingana na hiyo kauli aliyotoa Bertha, lakini akanyamazishwa tena. Hakimu akamwambia Bertha afikirie kwa umakini kile ambacho alinena, asiogope kushinikizwa na mtu, akisema jibu lake litaamua ikiwa atahukumiwa kwenda jela, ama atapata nafasi ya kupigania uhuru wake. Yaani alikuwa anamtia moyo kwamba anaweza kujitetea, lakini Bertha akarudia jibu lile lile bila wasiwasi.

"Sijashinikizwa. Nina hatia, mheshimiwa. Yote hayo uliyosema, nimeyafanya."

Mh?

Nikatazamana na askari Ramadhan kwa umakini kiasi, halafu akaendelea kumwangalia mwanamke huyo kwa utulivu. Upande wa pili wa mabenchi haya huko mbele, walikaa wanawake wawili pamoja na mwanaume mzee kiasi, wakiwa na mionekano nadhifu tu, nami niliweza kuona mwanamke mmoja wao akianza kulia na mwenzake kumpa kama bembelezo.

Sikutarajia kabisa kwamba madam Bertha mwenyewe angekiri kuwa alifanya matendo yale. Yaani, ilikuwa kinyume na utu wake kabisa, mpaka nikawa najiuliza ni kwa nini aliamua kufanya hivyo. Ni kwamba labda aliona hizo kesi zingemshinda tu hata hivyo ndiyo sababu akakata tamaa mapema, ama labda alifanya hivi kwa sababu kweli alihisi hatia kwa mambo mengi aliyokuwa amefanya? Nilifikiria jambo hili la pili kuwezekana zaidi, huenda alitaka kulipia mabaya yote aliyokuwa amefanya. Lakini bado nisingeweza kujua kiuhakika.

Baada ya Bertha kutoa jibu lake hakika, hakimu akawa ameshushiwa mzigo kiurahisi. Hapo ingekuwa ni kumpa Bertha hukumu ya moja kwa moja, hakuna masuala ya majibizano ya wanasheria wala nini, yaani hata na huko ingekuwa ni kujisumbua sana na kupoteza wakati maana ushahidi ulikuwepo wa kutosha kuthibitisha kwamba kweli alikuwa na hatia. Hivyo hakimu akatoa tu hitimisho, akisema mtuhumiwa angetakiwa kurudi hapa kwenye tarehe 22 hapo mbele, yaani Jumatano ijayo, ili hukumu yake isomwe. Pah, pah, nyundo ikagongwa.

Hakimu aliposimama ili asepe, nikasimama pia, na watu wengine wakaambiwa wasimame, ndiyo hakimu akaondoka zake hapo. Ilikuwa kama kuchoshana tu yaani. Bertha akawa amefatwa na mwanasheria wake pale pale aliposimama, na askari Ramadhan akamsogelea pia. Niliendelea kuwaangalia, nikiona namna ambavyo mikono yake Bertha iliunganishwa kwa pingu, mwanasheria wake akiwa kama anaongea naye kwa kuuliza kwa nini ametoa jibu hilo, ila najua hata Bertha aliona jamaa alikuwa anajishaua tu kwa sababu alilipwa, siyo kwamba alimjali sana.

Wanawake wale waliokuwa wamekaa huko mbele kabisa, wakasogea mpaka hapo alipokuwa Bertha, na yule ambaye nilimwona analia akamtandika kofi zito sana usoni kwa hasira! Wale maaskari wanawake wakaenda hapo na kuwarudisha nyuma hao wanawake watu wazima, huku Bertha akiwa ameinamisha tu uso, nami nikaelewa kwamba walikuwa na ukaribu fulani; yaani walijuana. Huenda walikuwa ni ndugu zake, ama familia ya mtu ambaye Bertha alimuumiza. Ilikuwa taswira fulani mbaya sana.

Askari Ramadhan akawa amemshika Bertha mkono na kuanza kutembea naye ili bila shaka amtoe hapo, huku akifuatwa na maaskari wenzake, na watu wengine wakaanza kuondoka pia. Nilisimama tu huku nikimwangalia Bertha kwa hisia makini sana, na walipokuwa wamekaribia usawa wangu, akawa amenitazama machoni kwa umakini. Yaani... macho makini. Alinipa hisia fulani mbaya sana, sijui kwa nini tu, lakini ile hatia yake aliyoionyesha machoni hadi mimi nikaihisi. Si ile kwamba nimekuja kumwona sasa akipelekwa matesoni? Alikuwa kama ananiuliza 'umefurahi?'

Ramadhan na wenzake wakapita, lakini walipofanikiwa kumtoa Bertha hapo ndani, jamaa akamwachia kwa wale maaskari wanawake ili wampeleke huko nje zaidi. Sasa hivi kulikuwa na kama waandishi wa habari wa vyombo vya mitandaoni na magazeti zaidi, wakimpiga picha Bertha na maaskari walipokuwa wakielekea huko kwenye ngazi. Nikatoka hapo ndani mpaka kufikia korido, askari Ramadhani akiwa amesimama tu hapo kama vile alikuwa ananisubiria, nami nikamfikia karibu huku nikiona jinsi Bertha alivyokuwa anaishia konani mwa ngazi.

"Habari mkuu?" nikamsalimu.

"Safi. Uko salama?" askari Ramadhan akaniuliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kukubali. Hapo hapo tukawa tumepitwa na wale wanawake, ambao walikuwa na uchungu sana na Bertha, wakiondoka pamoja na mzee wao huku wanaongea kwa njia yenye jazba kiasi.

Nikamuuliza askari Ramadhan, "Huyo mama aliyempiga kofi Bertha ni nani?"

"Ni mama yake na yule jamaa... aliyekuwa mume wake," askari Ramadhan akanijibu hivyo.

"Ahaa... Chalii?" nikasema hivyo kwa utambuzi.

"Yeah," akakubali.

Tukawa tunawaangalia wale maaskari wakiwa wameshafika kwa huko chini, Bertha akiwa katikati yao, wakimpeleka nje taratibu huku wakifuatwa na baadhi ya watu kwa nyuma.

"Hiyo ilikuwa simple," askari Ramadhan akasema hivyo kwa sauti tulivu.

"Sana," nikaongea kwa sauti makini.

"Ni wa kuangalia mno huyo. Anaweza akawa anapanga jambo fulani," akasema hivyo.

"Kwa hali yake, unafikiri anaweza akafanya jambo gani?" nikamuuliza.

"Tumemshikilia ndiyo, lakini bado ana pesa. Anaweza akaingia jela lakini bado akaendelea ku-control vitu vingi huko nje. Ni kuwa makini," akaniambia hivyo.

Nikaingiwa na utambuzi mkuu kutokana na kauli yake, nami nikamuuliza, "Hata akiamua kutuma watu waniumize, anaweza?"

"Usihofu kuhusu hilo. Mimi mwenyewe nitahakikisha hafikiwi na njia za kufanya mipango ya hila akiwa huko ndani. Muda wake wa kucheza umeisha, ila sitaacha kumwangalia," akaniambia hivyo.

"Yeah. Yeah... uko sahihi. Sitakiwi kuwa paranoid, lakini umakini unahitajika," nikamwambia hivyo.

"Umakini ndiyo. Kaenda kwenye trouble yote kumleta mwanasheria ampiganie, halafu afike hapa ghafla tu akubali ana hatia? Kuna vitu anawaza huyo. Na nitahakikisha navizimisha kabla hajavifanyia kazi. Najua ana hila sana," akasema hivyo.

Hayo maneno yalikuwa kweli kabisa.

"Basi, ndiyo imeishia hapo. Ni vizuri umekuja. Angalau umepigilia msumari kwenye moyo wake," Ramadhan akasema hivyo.

"Kwa sababu ameniona niko huru, na yeye yuko ndani ya pingu?"

"Ndo' maana yake..."

Nikatabasamu kiasi.

"Festus alikuaga?" akaniuliza hivyo.

Nikamwangalia kwa umakini na kusema, "Hapana. Ameenda wapi?"

"Ameondoka nchini. Ameenda Nairobi kwanza, baadaye sijui ataenda wapi," akanijulisha.

Nikiwa nimeshangaa kiasi, nikasema, "Kwa hiyo... amekimbia."

Askari Ramadhan akaangalia pembeni na kutabasamu, kisha akaniangalia tena na kusema, "Unawaza mengi mno wewe. Nenda nyumbani ukapumzike."

Akanishika begani na kisha kuniacha nimesimama hapo, nikiwa na jambo jipya la kutafakari kwa mara nyingine.

Festo alikuwa ameondoka? Ndiyo iliyokuwa maana yake ya kutaka kuanza maisha upya? Inaonekana hakuwa na njia nyingine ya kuepuka yale yote ambayo aliyafanya hata kama aliwasaidia vipi maaskari, kwa hiyo bila shaka kuondoka ndilo lililokuwa jambo sahihi kwake kufanya. Na nadhani angeepuka kurudi tena nchini kwa muda mrefu sana, lakini sijui kwa nini badala ya taarifa hiyo kunipa ahueni, ikawa inanifanya nijihisi vibaya.

Si ile hali ya kutoamini mtu? Ilikuwa rahisi kuwaza kwamba huenda jamaa alifekisha kuondoka lakini kihalisi bado angekuwepo huku huku nchini na kwenda tu mkoa mwingine ili kusubiri mambo mengine huku jijini yatulie, halafu arudi kujaribu kuitwaa tuzo yake kivingine. Yaani Miryam. Ningetakiwa kuhakikisha kwamba wazo langu ni sahihi ama si sahihi, kwa sababu sikuhisi amani kabisa bado.

Bertha kufungwa haikumaanisha mabaya ndiyo yalikuwa yamekwisha, kama Ramadhan alivyosema, ila yalipungua tu. Sasa Festo kuendelea kuwa huru na tena kwenda "mafichoni" ndiyo kulinipa hisia za mambo mengine mabaya kuja tena hata na baadaye. Sikutaka kuridhika kabisa. Yaani sikumwamini kabisa yule mwanaume hata kama alikuwa amemshawishi vipi askari Ramadhan. Ningefatilia ishu hii kwa umakini ili nijue kama kweli usalama ungekuwepo kwangu mimi kutokea hapa, na kwake Miryam pia.

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana
 
Back
Top Bottom