Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

Elton Tonny wewe ni Mbuzi 😅😅😅
I meant GOAT
Naomba ep ya 35 kwenye pdf format nirushie whatsapp mwanangu kumbe baba yake JC ndio Mimi 🤣🤣🤣
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Tumesimama hapo kwa sekunde chache tu baada ya kubonyeza 'ding dong,' nao mlango ukawa umefunguliwa. Mbele yetu alisimama Nuru ndani ya tracksuit nyepesi yenye rangi ya pink na mandala manene ya manyoya miguuni, akiwa amefungua mlango huku anatabasamu kwa furaha sana, nami pia nikatabasamu na kuingia ndani bila kumwachia Miryam kiganja.

"JC... karibuni!" Nuru akasema hivyo kwa hisia na kunikumbatia kwa upande mmoja.

Nikarudisha kumbatio lake huku nikimwambia, "Asante mwaya. Nakuona. Unazidi kunenepa tu."

Akaniachia na kumtazama Miryam, halafu akamwambia, "Shikamoo dada?"

"Marahaba," Miryam akamwitikia vizuri.

Tukaanza kutembea taratibu kuelekea ndani kwa pamoja baada ya Nuru kurudishia mlango, na nilipenda sana namna ambavyo Miryam alikuwa akitembea kwa mwendo fulani kama wa mwanamitindo ili ahakikishe viatu vyake visimfanye ateguke, nasi tukawa tunaelekea upande wenye masofa hapo kati ambapo Jasmine alikuwa amekaa kwa kujilaza kwenye sofa huku akituangalia kwa njia ya kawaida tu. Alikuwa amevalia T-shirt pana la Mackenzie jekundu kwa juu, huku miguuni akitia suruali skinny ya kijivu kama za wanamazoezi wa yoga.

Kabla hatujafikia hapo kwa Jasmine, kutokea juu ya ngazi tukaanza kuwaona mama na mzee wakiwa wanashuka kuja huku chini, na mama alikuwa amemtangulia zaidi jamaa huku akionyesha tabasamu hafifu usoni mwake. Mama yangu alivaa gauni jepesi la kushindia tu nyumbani, na mzee yeye alikuwa ndani ya T-shirt la mikono mifupi la blue-bahari pamoja na bukta pana nyeusi, mionekano ya kawaida tu yaani kwa wote wakati huu wa kutulia nyumbani. Na kutokea upande ulioelekea jikoni nikawaona wasaidizi wa kazi wa hapa, Imelda na wenzake wawili, wakija sebuleni na kusimama usawa wa ngazi ya kwanza huku wakitutazama kama vile kamati ya wakaribisha-wageni.

Ikabidi nisimame pamoja na Miryam na Nuru kwanza kuwasubiri wazazi watufikie, na mama alipokuwa amekaribia upande wetu, umakini wake ukawa kwa Miryam zaidi. Alipiga hatua taratibu na kufikia mbele yetu huku akimwangalia Miryam kwa macho ya kisomi yaani.

Nikamwamkia, "Mama shikamoo?"

"Marahaba," akaniitikia vizuri.

Miryam akatoa ishara ya kupiga magoti kiasi na kumwambia, "Shikamoo mama?"

"Marahaba mwanangu. Karibu," mama akamjibu hivyo.

"Asante sana," Miryam akajibu na kasauti kake katamu.

Nuru akaenda kusimama pembeni yake mama, na mzee alipofika karibu nasi, nikamwambia, "Mkubwa, shikamoo..."

Akaja na kuunganisha kiganja chake na changu huku akitabasamu kiasi, naye akasema, "Marahaba."

Miryam akatoa ile ile ishara tena huku akimwambia mzee, "Shikamoo?"

"Marahabaa. Karibu sana mama," mzee akamwambia hivyo.

Nikaona Jasmine akiwa amenyanyuka kutoka sofani na kuvaa ndala zake, naye akaanza kuja upande wetu taratibu huku akijishika kiuno chake kwa mikono yote, yaani hilo tumbo lilikuwa kubwa! Nikamwangalia mama na kukuta anamtazama Miryam kwa macho makini sana, yaani kama anamtathmini vile, nami nikamwangalia bibie usoni huku nikitabasamu kiasi. Miryam akaniangalia pia, na bila kuonyesha hisia yotote akamtazama tu mama tena huku nikihisi namna ambavyo alikikaza kiganja changu kwa nguvu zaidi.

Mama akasema, "Sura yako siyo ngeni sana. Tumeshawahi kukutana?"

Miryam akasema, "Sidhani. Hii ndiyo mara ya kwanza."

Mama akaniangalia usoni kiudadisi.

Nikamwambia, "Unafikiria hivyo kwa sababu umemfananisha na mtu mwingine ambaye nimeshakuja naye hapa."

Mama akamwangalia Miryam tena, naye akasema, "Yes! Mariam!"

Nikatabasamu kiasi, na ni hapo ndiyo Jasmine akawa ametufikia.

"Ni kweli, nimekufananisha na Mariam, ndiyo maana nikafikiri... ahah... Mariam ni mdogo wako eh?" mama akaongea hivyo.

Miryam akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Ndiyo."

Mama akasema, "Okay," na kuweka kiganja chake kimoja shavuni huku akimwangalia Miryam kwa macho yaliyoonyesha hisia nzuri.

Jasmine akiwa amesimama mbele yake Nuru, akamnyooshea kiganja Miryam na kusema, "Karibu sana wifi."

Miryam akatabasamu kiasi na kukiachia kiganja changu, naye akakipokea cha dada yangu na kumwambia, "Nashukuru Jasmine."

Jasmine akapandisha nyusi kimshangao na kusema, "Kumbe unanijua?"

Miryam akasema, "Yeah. Anakuongeleaga huyu."

Jasmine akakiachia kiganja cha bibie na kuuliza, "Kwa mazuri, au mabaya?"

"Mabaya," nikasema hivyo, na wengine wakacheka kidogo baada ya Jasmine kutoa kicheko cha mguno.

Sote tukamwangalia mama tena na kukuta bado akiwa ameweka kiganja chake shavuni, na akimtazama Miryam kwa macho yaliyoonyesha upendezi wa hali ya juu sana. Najua wote hapo walikuwa na yao ya kuwaza, lakini mimi nilitaka kujua maoni ya mama yangu kwanza. Akaliachia shavu lake na kuviweka viganja vyake mbele, akivifungua kwa chini kumwelekea Miryam kama kumwita. Miryam akanipatia pochi yake na kumsogelea mama kidogo, naye akavishika viganja vyake huku wote wakiangaliana machoni.

Mama akamwambia, "Mariam alipokuja, nilimwona mzuri sana. Ila wewe... ndiyo umebarikiwa zaidi. Ni mzuri sana wewe mwanangu."

"Asante mama," Miryam akasema hivyo huku sauti yake ikikatika kiasi.

Sijui alikuwa karibu kulia? Ile furaha yaani kutotegemea apokelewe vizuri namna hiyo. Mama akakumbatiana naye taratibu, akionyesha zaidi kwamba alitokea kumpenda Miryam, na akiwa ananitazama kutokea mgongoni kwa bibie, mama akanikazia macho kama kusema 'wewe!' yaani ile kwamba nimeweza vipi kumkamata mwanamke kama huyu na kumleta hapa? Siyo kwa sababu tu ya sura wala nini, yaani najua mama kwa kumtazama tu Miryam alikuwa ameshaelewa aina ya utu ambao huyu mwanamke angekuwa nao, hasa baada ya kujua ni dada yake Mariam, ndiyo sababu alipendezwa naye upesi sana.

Wakaachiana taratibu, naye mama akiwa anazilaza-laza nywele za bibie upande mmoja wa kichwa, akamwambia, "Jayden aliniambia anakuja na surprise, na nilijua tu lazima iwe mkwe wangu ila hakutaka hata kusema jina lako jamani..."

Sisi wengine tukatabasamu kwa kauli yake.

"Unaitwa nani, mpenzi?" mama akamuuliza hivyo huku akiendelea kuchezea nywele zake taratibu.

"Miryam," akamwambia hivyo.

Nikatabasamu kiasi.

"Miryam. Majina yenu na Mariam yanaendana, halafu mnafanana. Karibu sana mama. Jisikie uko nyumbani," mama akamwambia hivyo.

"Asante mama," Miryam akaonyesha shukrani kwa heshima.

Mama akamshikilia mkono kwa ukaribu huku akianza kutembea naye kuelekea masofa, nami nikasikia anamuuliza, "Atakua alisota sana huyo mpaka kukukamata, eh?"

Na Miryam akamwambia kwa sauti ya chini, "Eeh, alihangaika..." nao wote wakacheka kidogo huku Jasmine na Nuru wakifuata nyuma yao.

Nikasogea karibu zaidi na mzee, sote tukiwa tunawaangalia wanawake, na kwa sauti ya chini akasema, "Dada yake Mariam... imeeleweka vizuri zaidi sasa kwa nini milioni kumi ilikuchomoka."

Nikatabasamu kiasi tu na kumwambia, "Nilikuwa nimeshampenda hata kabla sijafika huko kwenye milioni kumi. Na hiyo siyo sababu yuko hapa sa'hivi."

"Naona. Ila mbona kama amekuzidi sana?"

"Ndo' nachohitaji. Ametulia zaidi. Ananisaidia nitulie pia," nikamwambia hivyo.

Mzee akapandisha nyusi kwa njia ya kusema 'haya,' kisha tukasogea mpaka kufikia masofa na kukaa pamoja na wanawake wote, wakina Imelda wakiwa wamesimama pembeni ya hapo pia baada ya kumsalimu bibie.

Mama alikaa kwa ukaribu sana na Miryam, wakiwa wameanza kufanya maongezi ya mwanzo ya kujuana wao kama wao, kisha ndiyo bibie akaanza kuelezea maisha yake kiujumla baada ya mama kuongelea ishu ya Mariam. Yaani alizungumza na mama kuhusiana na wakati alipokuwa Dodoma, mpaka ilipombidi aje Dar baada ya wazazi wake kupoteza maisha kwenye ajali, na changamoto alizopitia mdogo wake alipoanza kuumwa.

Akawaambia nilikuja kwenye maisha yake kwa wakati ambao alinihitaji zaidi, nilimsaidia sana yaani, na mwanzoni nilipokuwa najitahidi kuukamata moyo wake alijaribu kweli kunikwepa kwa sababu ya kuogopa vikwazo, ila mwishowe hakuweza tena kujizuia kuonyesha upendo wake kwangu.

Mama yangu alikuwa anapenda sana hizi hadithi za safari ya maisha ya mtu, akiwa mtu ambaye alipitia maisha magumu sana pia hivyo sikuzote alikuwa msikivu juu ya hali za wengine na kutaka kuwaelewa vyema pia. Alipenda ustaarabu wa Miryam, na hata Jasmine na Nuru waliona kwamba Miryam alikuwa mtu mwenye roho nzuri, hivyo ilikuwa rahisi sana kwao kupatana naye haraka. Ile trend ya Jasmine kumwita Miryam "wifi" ndiyo ikakita mizizi sasa, yaani ikawa kama vile nimeshamwoa kihalali kabisa.

Mzee alipoongea kidogo na Miryam, ilikuwa kuhusiana na ishu ya Joshua kwenda jela baada ya yote aliyomfanya apitie, akimpa pole na kumtia moyo kwa kusema sisi wote ni familia moja sasa, hivyo hakupaswa kuhofia lolote tena. Miryam hangeweza kufikiri kwamba mapokezi ya familia yangu nzima kumwelekea yangekuwa mazuri sana namna hiyo, yaani akawa na ujasiri zaidi ya jinsi ambavyo alikuwa ndani ya gari muda mfupi nyuma.

Mimi na mzee hatukuwa tukiongea sana, zaidi ni kuwasikiliza wakina mama, Jasmine na Nuru walipoendelea kujitahidi kumfanya Miryam ajisikie huru, na ndiyo meza ya chakula ikawa imeandaliwa vyema baada ya muda mfupi ili twende kujinoma. Kulikuwa na vyakula vizuri, mama alihusika zaidi kwenye upishi wa nyama za kuku na kitimoto nakwambia, nasi sote tukaenda kukaa hapo pamoja na kuanza makamuzi. Wote yaani tulikaa kwenye meza moja kula, hadi wasaidizi wa kazi.

Nilifurahia sana wakati huu kwa kweli. Haikuwa kwamba labda nimekuja kumtambulisha Miryam kama mchumba rasmi aliyevalishwa pete, ila familia yangu ilimtendea kana kwamba alikuwa mke wangu wa ndoa kabisa. Tena na mama JC alivyokuwa mpenzi wa kujali hivyo, yaani alimtendea Miryam si kama mgeni kwake, na hiyo ilimfanya mwanamke wangu astareheke zaidi. Maongezi yalikuwa mazuri wakati tukila, mimi na Jasmine tukikumbushia nyakati za miaka yetu ya utineja kwa jinsi zilivyokuwa na vituko vingi, na meza ikajaa vicheko vya furaha kwa burudani nzuri ya kifamilia tuliyopeana.

★★

Tulimaliza kula na kurudi kukaa masofani tena kuendelea kupatana, mpaka inafika saa nne usiku. Mama kama kawaida aliketi sofa moja na Miryam, Jasmine akikaa kwenye lingine na Nuru, na mimi upande mwingine na pamoja na mzee. Wasaidizi walikuwa huko ndani zaidi labda wakiwa wameshapumzika. Mazungumzo hapa yalitawaliwa zaidi na mama, Nuru na Jasmine, ambao walimsemesha Miryam kuhusiana na mambo mengi mchanganyiko, yaani story ndogo ilikuwa ikifa inaamshwa nyingine, na mimi na mzee tungechangia hapa na pale kuwaburudisha zaidi wapendwa wetu.

Mzee akawa amepigiwa simu ya kikazi na kuamua kwenda huko juu chumbani mara moja. Sekunde chache tu kutokea hapo mimi pia nikawa nimepigiwa simu, na tabasamu liliniponyoka baada ya kuona ni Tesha. Nikawapisha wanawake na kwenda pembeni kidogo, nikaongea na huyo dogo. Alikuwa analalamika eti, nimempeleka wapi dada yake, maana aliona hatukuwepo huko Mbagala ndani ya siku moja kwa hiyo alielewa ni lazima ningekuwa nimemtorosha dada mkubwa. Nikamwambia aache kulia-lia, dada yake na yeye anastahili matembezi kidogo, naye akasema ni vizuri sana.

Akawa anataka eti nifanye kukaa na Miryam huku wiki nzima ili dada yake ale bata mpaka anenepe zaidi, nami nikamwambia ikiwa hilo lingewezekana ningelifanya, sema Miryam asingekubali. Kesho tu angetaka turudi, kwa hiyo wangetuona. Akasema haina noma, alikuwa ameshazoea mno Miryam kuwepo kwao ila huu mwanzo wa mabadiliko ulimfanya ajione kuwa kama faza hausi pale nyumbani, asipate picha itakuwaje dada yake akishaolewa, nami nikamwambia kimasihara asianze kuota mapema kuichukua na nyumba maana dada yake bado angeendelea kuwepo kwa muda mrefu tu. Akacheka mno na kunitakia bata njema, akinisihi nisiache kumpelekea mabaki kidogo.

Tukakatisha maongezi baada ya kuongea kwa karibia dakika kumi na tano, nikiwa nimehakikisha kutoka kwa Tesha kwamba Mariam alikuwa poa tu huko kwao, nami ndiyo nikarudi kwa wengine. Wakati huu mama na mabinti zake walikuwa wameanzisha mchezo mdogo wenye kufurahisha sana wa "chemsha bongo," wakiulizana maswali mmoja baada ya mwingine na kuyatatua ili kuona nani kichwa eti. Najua hili lilikuwa wazo la Jasmine maana aliupenda sana huu mchezo tokea zamani, nami sasa nikafika karibu na sofa walilokalia mama na Miryam, nikisimama kwa nyuma na kuegamiza mikono hapo kwa kuwainamia kiasi katikati yao.

Wakawa ndiyo wameniambia kwamba wote waliulizana chemsha bongo, na za Nuru, mama, na Jasmine, zote aliwahi kujibu Miryam na kupatia, halafu ya kwake Miryam aliyouliza akawa amepewa jibu sahihi na Jasmine. Walionekana kufurahia kweli, na sasa hivi alitaka kuuliza Nuru, lakini mama akasema na mimi wanipe nafasi niulize chemsha bongo. Huu mchezo mimi na Jasmine tuliufanyaga sana zamani, enzi hizo tuko na mama tu wakati tukiwa wadogo na kujiburudisha kwa maswali ama hadithi za uwongo njoo utamu kolea, kwa hiyo ni kitu ambacho kiliwapa starehe sana, hasa Jasmine. Alichangamka kweli yaani, furaha yake yote ilionekana hapo.

Kwa hiyo ili kufanya burudani iwe nzuri zaidi, nikawapa wazo. Ningewapa chemsha bongo, halafu yeyote kati yao ambaye angepatia jibu basi ningempa zawadi ya pesa, ila kama wote wangeshindwa, basi kila mmoja wao angetakiwa kunipa hela. Walihisi nilikuwa nataka kuwapiga bonge moja la swali ili wote washindwe halafu niwale hela, lakini nikawaambia waache kuwa waoga na waonyeshe akili zao. Jasmine akakubali hiyo challenge upesi baada ya mimi kusema hivyo, akiwaambia wengine kwamba, ikiwa watashindwa kunipa jibu, basi kila mmoja wao atoe elffu kumi, yaani zichangwe halafu nipewe elfu arobaini. Ila kama mmoja wao angepatia jibu, mimi ndiyo nitoe elfu arobaini ya kumpa mshindi.

Nikaanza kumwambia hiyo siyo fair, lakini Jasmine akasema niache kuwa kama kuku ikiwa nina uhakika swali lilikuwa zito. Nikamwambia ahaa? Mimi kuku? Ngoja sasa. Nikawaambia wajiandae, na wakikosa jibu hakuna kukamia hizo hela, yaani walipaswa kunipa sasa hivi, naye Jasmine akiwa ndiyo kapteni akasema sawa, nilishushe swali. Miryam alikuwa ameshaweza kujiachia kiasi mbele ya wengine sasa, akiwa na ule utulivu wake lakini mwepesi wa kuitikia furaha za wengine pia, nami nikamtikisia nyusi kidogo kama kumwambia 'naona una-enjoy.'

"Uliza sasa. Tuko tayari," Nuru akaniambia hivyo.

"Sawa. Ila msije kulia nikiwakomba hela zenu," nikawaambia hivyo.

Jasmine akapiga kiganja chake kinyume huku akisema, "Wewe uliza!"

Nikasema, "Haya. Chemsha bongo, chemsha bongo..."

Wote wakaitikia kwa kusema, "Chemsha bongo."

"Neno lipi lina herufi nne, mara nyingine herufi kumi na mbili, lakini ina herufi sita?" nikauliza hivyo.

Mama akaguna, Jasmine akakunja uso kimaswali na kucheka kidogo, naye Nuru akatazamana na Miryam kama kutaka apewe dokezo. Nikacheka kidogo maana najua niliwachanganya.

"Wee... em' rudia tena. Kwamba?" Jasmine akauliza.

Nikaacha kuegamia sofa na kusema, "Ah... kwani hujasikia nini? We' jibu bwana."

"A-ah, ili tutatue chemsha bongo, lazima iwe imeeleweka vizuri, uwongo?" Jasmine akasema hivyo.

"Ni kweli, hata me sijaelewa," mama akasema hivyo.

"Si ndiyo point yenyewe? Msielewe ili mtatue swali sasa," nikawaambia.

"Swali lenyewe limeshapotea kichwani," Jasmine akasema.

"Amesema neno gani lina herufi nne... halafu muda mwingine lina herufi ngapi sijui? Rudia bwana JC..." Nuru akaniambia hivyo.

"Eeh, rudia," Miryam akasema hivyo pia.

"Hata nikirudia, hamwezi kupatia," nikawaambia hivyo.

"We' rudia! Tutapatia tu, kuna mkate mgumu mbele ya chai bwana?" Nuru akaniambia hivyo.

"Anajishaua na bichwa lake, maana anajua akirudia tutaelewa," Jasmine akasema hivyo.

"Ahaa, sawa. Sasa sikiliza wewe captain kitumbo..."

Nikamwambia Jasmine hivyo, nao wote wakacheka kwa pamoja.

Nikaegamia sofa tena na kusema, "Neno lipi lina herufi nne, mara nyingine herufi kumi na mbili, lakini ina herufi sita?"

Wakaanza kuangaliana, wakitafuta jibu kwa kutoleana macho tu, nami nikamwonyeshea Jasmine ishara ya umbumbumbu kwa kejeli.

"Hee, hapo kweli pagumu. Me nimeshindwa," mama akasema hivyo.

Miryam akacheka kidogo kwa pumzi.

"Aaa... mama! Don't accept defeat so early namna hiyo," Nuru akamwambia.

"Neno lipi lina herufi nne, muda mwingine herufi kumi naaa...." Jasmine akaendelea kuchekecha ubongo.

Na Miryam alionekana kutafakari mambo kwa utulivu.

"Neno linaweza kuwa na herufi nne, halafu tena likawa na herufi kumi na mbili?" Nuru akauliza hivyo.

"Ah, ndiyo maana me nimesema nimeshindwa. Nasubiri tu wakati wa kumpa mji," mama akamwambia Nuru hivyo.

"Mama hayo mambo ya children's corner hapa hamna. Tukishindwa, ni kumpa hela. Lazima tukaze... ni kuumiza ubongo kweli asipate hata senti. We' kiazi hii ndiyo challenge sasa. Subiri nikupe jibu lake," Jasmine akasema hivyo.

"Haa, unalo! Kama utalipata jibu sasa..." nikamwambia hivyo kikejeli.

"Vipi Miryam, we' umepata jibu?" mama akamuuliza hivyo.

Nikamwangalia Miryam usoni, na yeye alionekana kutafakari bado, ndiyo akamwambia mama, "Hamna. Ila linakuja, linapotea. Kuna kitu ameficha hapo."

"Mm? Linakuja, linapotea wapi?" nikamuuliza hivyo kikejeli.

Miryam akaniangalia kwa macho makali eti na kisha kuyazungusha kidogo, kitu ambacho kikafanya mama acheke na kupiga viganja vyake kwa furaha.

"Ahahah... semeni tu mmeshindwa, mnipe hela," nikawatania namna hiyo.

"Hakuna. Wifi, komaa. Na me siachi. Mpaka kielewekee," Jasmine akaongea kwa uchochezi.

Dada yangu aliupenda huu mchezo!

Miryam akaniambia, "Hebu rudia kwa mara ya mwisho."

"Eeh, JC rudia," Nuru akasema hivyo pia.

"Mihogo bado michungu?" nikawaambia hivyo.

Miryam akanikata jicho kali tena, nami nikacheka kidogo.

"Wape ya mwisho, wataweza tu," mama akaniambia hivyo.

"Okay, naenda taratibu, na sirudii tena. Neno lipi lina herufi nne, muda mwingine herufi kumi na mbili, lakini ina herufi...."

Kabla sijamaliza, Miryam akacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "Ni hapo."

"Enhe! Miryam kakukamata," mama akasema hivyo.

"Umelipata jibu?" Jasmine akamuuliza hivyo Miryam.

"Usimuulize mwenzako, we' umelipata?" nikamuuliza hivyo kiutani.

"Tulia wewe, mbona mihemko?" Jasmine akaniuliza hivyo.

"Wifi, tuvunjie," Nuru akamwambia hivyo Miryam.

"We'... em' tulia kwanza. Waanze kujibu hao," nikamwambia hivyo Miryam, nikiwa naelewa angekuwa ameshatatua hiyo ishu maana alikuwa na akili nyepesi.

"A-aaah, unaogopa nini? Limekushuka eh? Wifi huyoo! Wifi muumbue ye' ndo' atoe hizo hela, tutanywea wine!" Jasmine akaongea hivyo kwa furaha.

Sote tukacheka kidogo.

Nikamwambia Jasmine, "Unywe wine wapi na hilo tumbo?"

"Si litashuka tu? Kwani nilikuwa hivi sikuzote? Hapa lazima uumbuliwe..." akaniambia hivyo.

"Nani alisema kwani hii ni ya kuumbuana? Si tunacheza tu..." nikamwambia pia.

"Kwenda huko! Tunacheza hiyo kwioo," Jasmine akaniambia.

Miryam na mama wakacheka kwa pamoja.

"Yaani hawa kama Kulwa na Doto mambo yao," mama akamwambia hivyo Miryam.

Miryam akatikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Jibu la swali ni nini eti wifi?" Nuru akamuuliza Miryam.

Miryam akasema, "Ni... ni chemsha bongo, lakini siyo swali, ni kauli. Yaani alikuwa hatuulizi... alikuwa anatuambia."

Nikatabasamu na kuwaangalia wengine kwa furaha.

Jasmine akasema, "Kumbe? Kwa hiyo jibu ni... a-ah, yaani kauli yake, ni kwamba...."

"Neno "lipi" lina herufi nne, "muda mwingine" lina herufi kumi na mbili, "lakini" ina herufi sita," Miryam akawaambia.

"Oooh... sawa. Ahahahah... eh! Nimeelewa," Jasmine akasema hivyo.

Miryam akacheka kidogo.

"Me bado sijaelewa," mama akasema hivyo.

"Hata mimi," Nuru akadakia.

"Yaani, eti alikuwa anatuambia tu kwamba maneno 'lipi,' 'muda mwingine,' na 'lakini' ndiyo yana hizo herufi. Ukihesabu herufi moja moja yaani. Umeelewa?" Jasmine akamwambia hivyo mama.

Ikabidi Nuru aanze na kumhesabia mama ili wawe na uhakika, na kwa pamoja wakacheka baada ya kuona ilikuwa kweli.

"Jamani! Miryam safi sana," mama akamwambia hivyo.

"Asante mama," Miryam akamshukuru.

"Umemshtukiaje?" Jasmine akamuuliza Miryam.

"Si hizo sehemu alikuwa anasema neno lina herufi, LINA herufi, halafu kwenye lakini akasema INA herufi. Hapo asingeweza kuweka lina, ndo' nikamdaka," Miryam akasema hivyo.

Nikatabasamu tu kwa furaha.

"Hee, wifi una akili! Yaani me nisingeweza kujua kabisa. Hadi raha," Nuru akasema hivyo.

"Kweli. Na unajua J katukamatia wapi? Kutufanya tufikirie ni swali, kumbe ni kauli," Jasmine akasema hivyo.

"Na mpaka ungeenda kulala usingeweza kulipata jibu. Ishu yenyewe ilikuwa rahiiiisi, ila ukapuyanga. Bado unaniona kiazi?" nikamuuliza hivyo.

"Aa wapi wewe! Nani kapuyanga? Na tena usijahaulishe, toa hela hapo. Chap!" Jasmine akaniamuru.

"Aliyeitoa jibu hajaiomba bado, we' ndo' masikio yako juu," mama akamwambia hivyo.

"Eti!" nikamuunga mkono.

"Hakuna, sisi tuko timu wifi, mama. Usimtetee huyo. Hey you? Weka mkwanja hapo, wii... aweke hapo huyo," Jasmine akaongea kwa shauku.

"Eeh, weka hapa," Miryam akaniambia hivyo pia.

Nikajifanya kununa na kuchomoa wallet, kisha nikatoa elfu arobaini na kuibamiza kwa nguvu katikati ya uwazi ulioachwa sofani walipokalia mama na Miryam, nao wakacheka kidogo. Miryam akanitazama usoni kwa njia ya kejeli, nami nikamkata jicho la kuudhika kimasihara.

"Hahaaa... aina hiyo! Wifi wahi kuiweka pochi asije kuikwapua tena, si unajua wanaume kwa majungu?" Jasmine akasema hivyo.

Miryam akatabasamu na kuichukua pesa hiyo.

"Imenoga jamani. Tuendelee?" Nuru akaniuliza hivyo.

"Mm? Sichezi tena na nyie, mpaka Miryam asiwepo," nikaongea kwa kujifanya nimenuna.

"Nyoo..." Jasmine akasema hivyo.

Wote wakacheka kidogo kwa furaha, naye mama akasema, "Si ndiyo utaenda naye lakini? Yaani Miryam hakikisha unamla hela za chemsha bongo huyu mpaka afilisike."

Miryam akacheka tu kwa furaha, naye mama akagonga kiganja chake pamoja naye kwa njia ya kirafiki kama wanawake wafanyavyo. Ushosti wa mama mkwe na binti mkwe ukawa unazidi kukolea, na nilihisi furaha sana kwa kweli. Pindi kama hii ndiyo ilifariji hata zaidi, mambo kwa upande huu yalikuwa mazuri sana. Ingebidi kusubiri kuja kuona upande wake bibie wa familia yote ungeitikia vipi pia.

Nuru akawa anataka tuendelee na mchezo huo, nasi tukakubaliana kufanya wa mara ya mwisho kutokana na muda kuwa unakaribia kufika saa sita sasa, maana mdogo alikuwa na hamu ya kutuchemshia ubongo kwa swali fulani. Nuru akiwa ameanza kuongea, mzee akaonekana anashuka kutoka ngazini, nami nilipomwangalia, akanionyesha ishara kwa kichwa kuwa nimfate, halafu akaelekea upande wa dining na kusimama usawa friji ndogo ya hapo.

Nikawaacha wanawake wakiendelea na story zao na kumfikia jamaa, na sasa alikuwa ametoa chupa yake ndogo ya maji baridi kutoka kwenye friji na kuishika kiganjani, kwa hiyo nikawa nimesimama karibu yake huku yeye akiniangalia kwa utulivu tu.

"Vipi mkubwa?" nikamuuliza kistaarabu.

Akatazama upande wake Miryam, kisha akasema, "Miryam wako ni mzuri. Naona ana akili, mstaarabu, halafu anaonekana kuwa na heshima sana hata kwako ingawa amekuzidi umri. Umejitahidi, huo ndiyo uanaume."

Akanipiga na kifuani kidogo kwa kiganja chake, nami nikatabasamu na kusema, "Asante. Yaani Miryam ndiyo kila kitu nachohitaji ili niwe na furaha."

Akaniangalia kwa njia fulani ya utafakari kiasi.

"I figure umeniita pembeni ili unipe somo la maisha kuhusu wanawake, eh?" nikamuuliza.

Akasema, "Mwanamke wako ni mzuri..."

"Lakini?"

"Ahah... I'm offended..."

"Usijali, niambie tu unachowaza," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Ninawaza tu ikiwa huyo ndiye ambaye unamwona kuwa mwenyewe... ikiwa tayari umeshamwandaa kwa ajili ya maisha atakayokuwa nayo pamoja nawe," akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kumtazama Miryam kule alipokaa, nami nikamwambia mzee, "Unapotaka kumzungumzia Stella sikuzote huwa unaanza kutumia mafumbo."

"Siyo kuhusu Stella tu..." akaniambia hivyo.

Nikamwangalia na kusema, "Najua ni kuhusu mtoto wangu, ndiyo. Sioni shida yoyote."

"Miryam anajua kuhusiana na hilo?"

"Yes, anajua. Tunaambiana kila kitu. Wakati utafika atakutana na mwanangu pia, nitamtambulisha kwake, kama ambavyo Stella akiwa na wanaume wengine ni lazima atawatambulisha kwa mtoto, ama asipowatambulisha ni yeye, lakini... Miryam nitamtambulisha kwa mwanangu pia," nikasema hivyo.

"Unamwita mwanao wakati bado hujawahi hata kukutana naye?" akaniuliza hivyo.

Nikaangalia pembeni tu.

"Unajua... sifahamu sana Stella ana maisha yapi ya kibinafsi, lakini... niliona kwamba alikuwa anakuja kutengeneza mazingira mazuri ili mrudia...."

"Nampenda Miryam!" nikamkatisha namna hiyo.

Akatulia na kuendelea kunitazama machoni.

"Siwezi kurudia kitu ambacho hakikuwahi kuwepo. Unapomwongelea Stella, maanisha mtoto, hilo ndiyo litakalokuwa la muhimu. Mengine ni no," nikamwambia hivyo kwa uthabiti.

Akanywa maji yake kidogo na kisha kuendelea kunitazama tu.

Nikajihisi vibaya baada ya kuruhusu hisia zangu zipande mpaka kumsemesha namna hiyo, nami nikamwambia, "I... I'm sorry, nime... nimeenda mbali."

"Usijali. Nakuelewa. We' ni mtu mzima, fanya unachoona kinakufaa... siyo kama vile tunaweza kukuzuia kwa lolote unaloamua," akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kuuliza, "Kwamba ungefikiria kunizuia nisiwe na Miryam, au?"

"Ahahah... hata kama ningewaza hivyo, najua ingekuwa kazi bure. Ukishagakuwa na msimamo ndiyo hautakagi kubadilisha. Na... sisemi kwamba naona hampendezeani na huyu mwanamke. Nitakwambia ukweli. Miryam anakufaa. Nimeshaona hilo siyo kuwa leo tu, ila huyo mwanamke ni gem nzuri sana, Jayden. Itunze. Atakulea vizuri sana pia... yale mambo ya... 'yuko wapi huyuu....'" mzee akasema hivyo.

Nikacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "'Simuni sipatikanii...'"

"Ole wako usije kupatikana sasa," akaniambia hivyo.

"Oh trust me, ashaanza kunipoteza..." nikamwambia hivyo kiutani.

"Ahaa, sawa..." akasema hivyo, nasi kwa pamoja tukacheka kidogo.

Nikagongesha tano na mzee wangu mwelewa sana, kisha tukaelekea tena upande uliokuwa na warembo muhimu zaidi wa maisha mwetu.

Saa sita ilikuwa inaelekea kugonga, na bila kukawia nikatoa heri ya kuaga sasa ili nimepeleke bibie kupumzika. Mama alitamani sana tulale hapa hapa, na najua Miryam angeweza hata kumkubalia, lakini nikasisitiza tu kuondoka kwa kusema bibie ana kazi kesho, hivyo tungepanga muda wakati mwingine mzuri sana akiwa huru aje wakae pamoja kwa muda mrefu zaidi. Wote wakaachiana namba za mawasiliano, nakwambia Jasmine akiwa amepata shosti mpya, nasi ndiyo tukaongozana hadi nje ili hatimaye tuweze kuondoka.

Mama hakuacha kumtendea Miryam vizuri, yaani kama jinsi tu ambavyo alimtendea Mariam siku ile nimemleta, Miryam ndiyo ilikuwa mara mbili zaidi. Hadi tumefikishana sehemu ya kuegeshea magari bado wakawa wanapiga umbea tu na Jasmine, mimi na mzee tukiwa pembeni pia kuzungumza mambo mawili matatu, kisha ndiyo baada ya hapo tukaagana ya moja kwa moja kwa usiku huu na kuingia garini. Tukayaacha makao ya wazazi tukiwa tumeridhishwa sana, na Miryam akiwa na furaha isiyo na kifani moyoni mwake.

★★

Basi, ukawa ni mwendo wa dakika zisizozidi ishirini kutokea huko Goba hadi kufikia Bamaga, na tulirudi kwenye nyumba yangu tukiwa tunafurahika sana. Miryam kiukweli alijihisi kuneemeka, yaani hakutarajia angerudi huku akiwa amefurahi namna hiyo, na nikamwambia huo ulikuwa mwanzo tu. Akasema yaani aliona ni kama vile naichukulia mambo mengi kuwa rahisi sana, lakini sikujua kwamba kwake jambo hilo lilikuwa zito mno. Alithamini mno wonyesho huu wa upendo wangu kwake ingawa nilikuwa sitabiriki, naye akaapa kuja kunionyesha wakwake pia hivi karibuni.

Hiyo ilikuwa ni ahadi niliyotaka aanze kuifanyia kazi tukifika kwangu, na baada ya kufika kweli, bibie akaona aingie bafuni kwanza kuuondolea mwili wake fukuto haraka, huku mimi nikiwa nahakikisha geti na milango imefungwa vizuri na kisha kuingia chumbani ili nikajimwagie pia. Tulikuwa tumekunywa wine kidogo wakati tupo huko kwa wazazi, so kuna kauchangamfu kalikokuwepo kichwani pia ambako nadhani ndiyo kalinisukuma mpaka kucheza chemsha bongo pamoja nao wote.

Nikavua tu T-shirt na saa na kuviweka pembeni, kisha nikakaa kitandani na kuanza kuvua viatu pia. Ni wakati huo huo ndiyo Miryam akawa ametokea bafuni, akijifunika kwa taulo nyingine safi (zilikuwepo kadhaa hapa chumbani), naye akawa anazikausha nywele zake zaidi na kuniambia niende kujimwagia pia. Lakini nilivutiwa zaidi kumtazama akiwa namna hiyo, nami nikamnyooshea kiganja kama kumwita aje kwangu. Taratibu tu akaanza kunifata, akizunguka kitanda kutii mwito wangu mwana-mume wake, naye akaja na kukishika kiganja changu huku taulo ikiwa imefungwa vizuri kifuani kwake.

Nikamkalisha pajani kwangu, nikikishikilia kiuno chake kwa mkono mmoja, naye akasema, "Ntakuchosha hapa. Me mzito."

"Hiyo haiwezi tokea," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Akiwa ananiangalia kwa macho yenye upendo, akapitisha mkono wake mmoja mgongoni kwangu na kuanza kuzichezea nywele zangu huku akisema, "Si ukajimwagie kwanza haraka?"

Nikamwambia, "Nimeahirisha kwanza. Nataka ulihisi joto langu vizuri."

Akatabasamu kilegevu na kuendelea kuniangalia kwa hisia.

Nikiwa makini kiasi wakati huu, nikamwambia, "Kuna kitu nilikuwa nimefikiria."

Akajibu, "Niambie tu."

"Ushawahi kufikiria kubadili lile gari lako labda?" nikamuuliza.

"Pickup yangu nayotumia?" akauliza pia.

"Yeah..."

"Kwa nini unauliza hivyo?"

"Ninajua lile gari umelitunza hasa ili kumuenzi baba yako Mimi, ila... unaonaje tu ukiliuza halafu ukachukua lingine?" nikamwambia hivyo.

Akatazama chini kwa utafakari kiasi.

"Sijaribu kukunyang'anya uhuru wako wa kuamua, ila naona tu unahitaji change. Halafu ninajua sehemu nzuri na ya haraka ambapo unaweza ukaliuza kwa gharama nzuri tu, na baada ya hapo nikakutafutia lingine zuri... ambalo utalipenda pia," nikamwambia hivyo.

Akaniangalia akiwa ameanza kutabasamu kiasi, naye akauliza, "Unataka kuninunulia gari?"

Nikatabasamu pia na kusema, "Ikiwa itakuwa sawa kwako, fresh. Nakutafutia."

"Ahahah... yaani wewe! Kwamba una hela chafu sana..."

"Hahah... siyo chafu, ila ipo. Na mimi nikiamua kukupa kitu chochote kile, haitakuwa kwa sababu nina pesa ama sina pesa, bali itakuwa ni kwa sababu nimeweza kukupa, na nimependa kufanya hivyo. Najua hupendi shortcut na nini, lakini... ukiniruhusu nifanye vitu kama hivi, mimi itanipa furaha sana maana... ninataka kuvifanya," nikamwambia hivyo huku nikisugua kiuno chake taratibu.

Akiwa anazisugua nywele za shingo yangu taratibu, akaangalia chini na kusema, "Ni sawa. Na ni kweli unavyosema. Labda tu itakuwa vizuri nikiliuza, ila sijui sana kama nitaweza ku-adapt na gari jipya. Kwanza ya siku hizi si yana gharama sana?"

"Mhmhm... Miryam bana! Yaani unavyoekti, kama vile we' siyo mwanamke unayestahili hizo gharama!"

"Unamaanisha nini?"

"Miryam hivi haujui kwamba wewe ni mwanamke unayeangaliwa kuwa na thamani ya kuendesha magari ya kifahari, au kuishi maisha ya starehe kwenye majumba ya dhahabu?"

"Ah, kwenda huko..."

"No, I'm serious," nikamwambia hivyo.

Akaniangalia usoni kwa macho yenye hisia.

"Ahah... Ni wanaume wengi ambao wana pesa kupita maelezo wangezimwaga kwa ajili yako Miryam. Ungekuwa mwanamke mwenye roho ya pupa, ungekubali haraka sana kuolewa na mtu kama... Festo. Jamaa alikuwa nazo, ila najua wapo hata zaidi yake ambao wange-give anything ili kukupata na kukuonyesha thamani yako. Unajiona kuwa wa kawaida tu, lakini sisi hatukuoni hivyo. Ningekuwa na uwezo wa kukununulia jumba, ama gari la gharama kuliko la mastaa wa Bongo wanaopenda kujishebedua, ningefanya hivyo..."

Miryam akacheka kidogo na kutikisa kichwa chake.

"Kwa hiyo unapowaza sijui kuhusu gharama, unanishangaza sana. Wewe tu ni gharama Miryam, ambayo bado najitahidi kupiga mahesabu ikiwa nitaweza kuimudu..." nikamwambia hivyo.

Akanirembulia kidogo na kusonya kiasi huku akiangalia pembeni.

"Ahahahah... ni muda sasa wa wewe kurudi kwenye kutambua thamani yako, na mimi niko hapa kujitahidi kukuonyesha hiyo," nikamwambia hivyo na kumshika shingoni.

"Kwa hiyo unamaanisha kwa kuendelea kuendesha gari lililokuwa la baba, thamani yangu unayoisemea... haionekani?" akauliza hivyo.

"Hapana, simaanishi hivyo. Thamani yako kila mtu anaiona Mimi. Ila ni wewe tu ndiye ambaye umejitahidi mno kuificha. It's time for you to stop doing that," nikamwambia hivyo.

"Niache kuificha kwa sababu umenipata sasa?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini, akisogea karibu zaidi na mdomo wangu.

"Yeah. Nimeiona hata ulipokuwa unaificha, na ninataka watu wote waione nitakapoweka wazi kwa walimwengu kwamba wewe ni wangu... na sina nia wala mpango wa kukuacha," nikamwambia hivyo huku nikisugua shingo yake taratibu.

Akafumba macho yake taratibu na kusema, "Oh Jayden... napenda sana maneno yako..."

"Oh Mimi... naipenda sana sauti yako... na wewe zaidi," nikamrudishia.

Akatabasamu kivivu na kufumbua macho yake, akiwa ananitazama mdomoni kwa njia legevu, na kwa kunong'oneza akasema, "Kiss me."

Ah! Kwa raha zote!

Yaani hapa suala la kwenda kujimwagia lingesahaulika upesi sa-na. Kwa njonjo za wazungu, nikaanza kumdendesha bibie taratibu kwa hisia sana, huku akiwa ananitekenya kwa makucha yake shingoni kwangu, nami nikaanza kumpandishia hisia zaidi kwa kucheza na viungo vyake vya utamu bila kumkawiza. Hisia zikampaisha mwanamke wangu, moja kwa moja akaanza kushughulika na suruali yangu ili nimpatie penzi murua, na sikumnyima hilo.

Nikamgeuzia kitandani na kuja juu yake, nikianza na kuendelea kumpa mahaba matamu sana, na baada ya dakika nyingi za kufurahia mapenzi yetu usingizi ukawa umetubeba hatimaye, tukilala ndani ya makumbatio ya mikono yetu tukiwa tumeshibana kwa upendo. Na ni kama tu nilivyosema, hadi bafu lilisahauliwa kwangu yaani! Mafanikio zaidi kwenye safari ya mapenzi yangu na Miryam yangekuwa halisi kadiri siku zingesonga, na niliyatazamia kwa hamu sana.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana
 
🔥🤝🤝
 
Nimependa the way Jasmine na mama walivyokuwa mchangamfu 😂
Mawifi wote wangekua kama Jasmine, ndugu wasingehusika kuvunja ndoa zetu bali kuzitengeneza kuwa imara zaidi
Au hayo ni mambo ya ushuani tu, uswahilini kwetu aah 😂 🙌
 
Kuna watu wanasubiri issue ya JC na Madam wa jela lakin mimi nasubiri mwendelezo wa wale wamama walipoona picha ya mama ake JC wakapata na mashaka......

Nahisi kuna kitu hakipo sawa ila tusubiri tuone
 
Wapenzi wa Simulizi za Elton Tony huyu Jamaa anajua na ndio maana nikamuita Mbuzi au kwa kiingereza GOAT (Greatest of All Times) yaani ni kipaji unaisoma story mpaka unai feel kama maisha halisi sio Waandishi wengine huwa wanarukaruka kama mahindi ya bisi kwenye sufuria. Jamaa anaelezea mpaka vitendo vinavyofanywa na character mmoja mmoja yaani haichoshi hii simulizi.
Hongera sana Elton
 
Thanks a lot brother 👊💪
 
Back
Top Bottom