Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TISA

★★★★★★★★★★★★★

Siku ikaja mpya, Jumatano. Baada ya kuondoka huko Mzinga hiyo jana nilipotoka kumwona Bi Zawadi, moja kwa moja nilielekea hospitalini tena kuendelea na majukumu. Hakukuwa na longolongo lolote, kazi ziliendelea tu mpaka mida ya saa tano ambapo Adelina alinitafuta hatimaye kujibu ujumbe wa salamu niliomtumia awali. Kiuhakika alikuwa amebanwa na kazi sana jana na alichoka, akitoka huko kazini kwake baada ya kumaliza masaa ya ziada. Kwa hiyo nilimsihi tu apumzike, na huenda leo tungeonana kwa kuwa ningeweza kupata mbadilishano wa zamu na daktari mwingine ambaye angefanya kazi kwa upande wangu kuanzia jioni.

Sasa ikiwa ni alfajiri tu, baada ya kuamka na kujiweka safi kuelekea jukumuni, simu yangu ikaita, na baada ya kutazama mpigaji nikatulia kidogo. Ni kutotarajia kabisa kwamba askari Ramadhan angenipigia, siyo kwa sababu ya muda, bali kwa kukumbukia mambo mengi tuliyopitia wiki chache nyuma. Mwanaume huyo alinisaidia kwa vingi, na hasa kwa sababu vingi hivyo vilihusisha mambo mabaya, mwito wake kwangu sasa ukaniwekea hali makini. Hakuwa amenitafuta wala mimi kumtafuta tokea mara ya mwisho nimeongea naye kuhusiana na mdogo wake yule madam Bertha, aliyeitwa Beatha, hivyo udadisi wa akilini juu ya nini angetaka kuniambia wakati huu ulikuwa mwingi.

Nikapokea, na upande wa pili sauti yake Ramadan ikasikika akisema, "Hallo..."

"Yeah, kaka... habari?" nikajibu.

"Safi. Za siku?"

"Mungu anasaidia. Vipi wewe?"

"Kwema kabisa. Mambo yamekaaje huko kwenu?"

"Ah, kwa kipindi hiki mambo mengi yamebadilika ndugu yangu. Nilishatoka kule, sasa hivi niko Muhimbili," nikamwambia.

"Oooh, umerudi hospitali?"

"Ndiyo, likizo imeisha..."

"Okay..."

"Vipi harakati za usalama zinakwendaje?"

"Bomba tu."

"Eti eh? Mission mission kama zote mnamaliza bila shida kabisa?"

"Ah, hamna. Pamepoa sana sasa hivi toka tulipomalizana na yale ya Bertha, ndiyo maana nikaona nikucheki tujue kama umepata mkate mpya uturushie..."

"Ahahahah... hamna, hata mie kwa upande wangu ni utulivu tu sa'hivi," nikamwambia.

"Mwezi umepita sasa, nimeona nikusalimie kijana wetu wa faida," akaniambia hivyo.

Aliongea kwa njia iliyoonyesha hakukuwa na lolote zito, nami nikasema, "Asante mkubwa. Ila alfajiri yote hii, mwanzo nikadhani kuna case mpya."

"Haapana... ni kujuliana hali tu. Ulitusaidia sana kwa zile ishu, we' ni kama comrade hapa," akasema hivyo.

"Asante sana," nikamwambia.

"Basi, tutawasiliana wakati mwingine, ni vizuri kujua uko poa. Wasalimu familia," akaniambia.

Nikasema, "Sawa sawa. Halafu hivi, kuna na...."

"Ndiyo?" akaitikia.

"Ile ishu nilikwambia kuhusu mdogo wake Bertha..." nikamkumbusha.

"Ooh, sawa. Yule mweupe... uliniambia anaitwa...."

"Beatha."

"Sawa. Ndiyo, tulifanya research kuwahusu, na inaonekana hilo siyo jina lake," akaniambia hivyo.

Nikawa makini zaidi.

"Huyo mdogo wake Bertha anaitwa Tamiah Celestine. Hiyo Celestine ni surname yao wote, na wametoka kwa watu wa ukabila fulani wa huko Kenya," akaniambia hivyo.

Nikashangazwa kiasi na taarifa hii, nami nikamuuliza, "Unataka kusema Bertha alikuwa mkenya?"

"Ni watu wa huko, ukoo yaani, wenyewe wamezaliwa Tanzania na sijui sana kama walikuwa na uhusiano na wanaukoo wao, ila hawa wawili wamezaliwa na mwanamke mtanzania," akasema.

"Kwa hiyo ni kusema baba yao, ukoo wa baba yao... ndiyo wa huko nje?"

"Ndiyo. Detail zao nyingi zipo derailed, kwa mambo aliyofanya Bertha huku na wenzake hayakuhusiana na familia yake iliyo huko nje..."

"Wanaukoo wake wapo Kenya?"

"Kwa inavyoonekana, ila sina uhakika. Hakuwa na tie zozote na watu hao."

"Aliwahi kuniambia alipofungwa jela hakutaka wazazi wake na familia ijue kuhusu hilo, nilichukulia ni huku huku Tanzania. Labda alimaanisha wa huko Kenya," nikamwambia.

"Tutajuaje? Hakuna chochote kinacho-suggest kwamba alikuwa na mawasiliano na watu wa huko, na hata huyu Tamiah tumemcheki ila haonekani kujihusisha na biashara alizokuwa akifanya dada yake," akaniambia hivyo.

"Kabla Bertha hajafa kalinifata kunionya kabisa... kana ule moto kama wa dada yake, sikuona ni busara kumchukulia easy maana you never know... wanaweza kuwa na ishu zao mahala pengine na njia tofauti na zile tulizotibua," nikamwambia.

"Ahah... uko makini sana JC. Yote unayosema ni kweli, lakini kama nilivyokwambia... hatujaona lolote tena. Huyo Tamiah... mara ya mwisho najua alikuwa spotted huko Arusha... anasoma, kwa pesa za dada yake. Siyo muda mrefu atasahau yote hayo na kugeuka jiko la mtu huyo. Kama walikuwa na mipango wamebakiza kufanya, sa'hivi imeshindikana tena maana wameogopa tulipoporomosha himaya zao. Kwa hiyo usiwaze. Vile vitisho na nini... chukulia kama upepo tu, havitakuumiza..." akaniambia hivyo kiuhakika.

"Tamiah..." nikasema hivyo kwa sauti ya chini.

"Usimuwaze sana, yaani sasa hivi yale mambo yote yameshakufa na Bertha, tunaangalia vingine," akaniambia.

"Sawa sawa mkuu, asante sana. Hujaacha kuwa baraka kwangu," nikamwambia.

"Hah... kama wewe tu. Take care, wacha tuingie kazini," akaniambia.

"Likewise," nikamjibu kwa kuaga.

Simu ikakatwa, na kwa sekunde chache nikatafakari mazungumzo hayo mafupi niliyofanya na askari huyo. Uhakika alionipatia kuelekea suala la Beat... oh, hapana. Ni Tamiah. Jina la mdogo wake Bertha ndiyo lilikuwa hilo, ikiwa ni mara ya pili napata kujua kwamba majina yake niliuofahamu mwanzo yalikuwa ya uwongo. Hii ilikuwa sababu tosha kunifanya nihisi kwamba kuna kitu zaidi kilifichika kuelekea mwanamke yule, tofauti kabisa na mambo yote askari Ramadhan aliyonijulisha leo hii. Ingeonekana kama upepo wa Bertha kwenye bahari ya maisha yangu ulikuwa umekatika, lakini bado sikuwa na uhakika wa kutosha kama upepo wa Tamiah ulitoweka kabisa. Ulianza kidogo siku ambayo alinisemesha kwa kitisho, na ungeweza kugeuka kuwa mkubwa na kusababisha dhoruba kali sana kwenye maisha yangu wakati ambao nisingetarajia. Nilikuwa mpaka nimeshaanza kuyaweka pembeni kabisa mambo hayo baada ya kifo cha Bertha, lakini sasa ningejitahidi kutafuta mwanga zaidi juu ya huyu Tamiah ili niondoe hasara yoyote ambayo angeweza kuniletea; endapo kama ingekuwa hivyo. Hii tunaita tahadhari kabla ya hatari.

★★

Basi, kazi zikaanza, taratibu muda ukisogea mpaka kwenye saa sita mchana nikapigiwa simu na mama. Akanijulisha kuhusu Stella, akisema aliongea naye jana na kuhisi furaha yake baada ya mimi kuanza kumhudumia mtoto na hata kwenda kwake, na ni jambo ambalo lilimpa furaha mama pia. Ushauri wote aliokuwa amenipatia kuhusiana na hilo sasa akaona umezaa matunda mazuri, na akaomba nafasi ikipatikana tuje tukutane wote kwa pamoja nyumbani kufurahia ushirika na mwanangu Evelyn. Nikamwambia ningeutafuta muda huo, na siku siyo nyingi tungeonana kutimiza hilo.

Maongezi yalipoingia kwenye kujua hali zetu binafsi zilikuwaje, mama akataka kujua endapo kama nilishaongea na Miryam kwa lolote tena lililohusiana na zile ishu zilizozuia mipango ya ndoa, na ndiyo nikawa nimemtaarifu kwamba kwa sasa hatukuwa pamoja, wala kufikiria kuwa pamoja tena maana tuliachana kwa urasmi. Nikamwambia hatukuhitaji kuongelea chochote zaidi maana Miryam alitaka kusonga mbele, na mimi tayari nilikuwa nimeshaanza kusonga mbele pia, kwa hiyo yale yote yangebaki kuwa historia.

Mama alifikiri kwamba kuna sehemu ndani yangu bado iliumizwa sana na haya yote na akataka nije niende tuongee kwa mapana zaidi, lakini nikamwambia hilo halikuwa na haja kabisa. Kuwa sawa nilikuwa sawa, na ningeendelea kuwa sawa zaidi kwa kutojilazimu kurudi-rudi nyuma kuyaangalia hayo tena. Kwa hilo akasema haikuwa na shida, na kwamba kwa wakati huu alijihisi yuko sawa hata zaidi kuja kuzungumza na mama mkubwa wa Miryam, Bi Jamila, kuhusu yaliyopita, na akiwa anataka kusawazisha hali baina ya familia zetu iwe nzuri. Jambo hilo likaonekana kuwa jema sana kwangu, nami nikamwambia tungepanga kuja kuonana na mwanamke yule ili kwanza afanye maongezi naye, halafu baadaye familia kiujumla. Amani na mpangilio mzuri ungefuata bila shaka.

Baada ya kumaliza maongezi na mama, nikawa nataka kwenda kupata chakula kwanza maana asubuhi yote sikuwa nimetia chochote tumboni, lakini ni hapo hapo tu Ankia naye akawa amenipigia. Nikapokea, na baada ya kujuliana hali mwanamke huyo akafanya maongezi kuhusu jinsi nilivyofika pale kwao jana kumsalimia Bi Zawadi ndiyo yawe dhumuni kuu la kunipigia. Ankia alitaka kujua ni kwa nini nilitenda kwa jinsi nilivyotenda kumwelekea Miryam. Mh? Nikamuuliza alimaanisha nini, naye akasema nilimtendea vibaya kwa kutomsemesha na kumwacha akijisikia vibaya sana.

Alikuwa akinilalamikia yaani, kwamba Miryam aliishiwa raha kabisa kwa sababu yangu, nami nikamwambia Ankia ishia hapo hapo. Alitaka niongee nini na yule mwanamke? Nilikuja kwa ajili yake ama Bi Zawadi? Na kumsemesha, sikumsemesha? Alikuwa anataka nimbebe au hayo mawazo Ankia alikuwa anayatoa wapi? Nikamwambia Ankia kama amenipigia kunitibua ni bora akate simu na asinipigie tena ikiwa hana jambo lingine la kusema. Ndiyo akaanza kuja chini et ooh... siyo hivyo, nilimwonea tu huruma, hakusema chochote lakini yeye ni rafiki yangu namwelewa.

Nikamwambia sikufanya chochote kibaya pale, labda kama kibaya kwa Miryam ilikuwa mimi kufika hapo kwake, ndiyo sababu sikutaka hata kuingia ndani. Nikamweleza kwa ufupi kwamba mawazo ya namna hiyo hayakufaa, kwa yeye Ankia, kwa sababu tayari Miryam aliweka uamuzi wake mbele ya watu wote kuhusu mahusiano yetu wiki chache nyuma, na ni kwamba tumeachana, sasa sijui angekuwa na matarajio yapi kwa sasa hivi tena wakati alinibwaga yeye mwenyewe. Mimi hata kujenga hali ya urafiki na Miryam sikufikiri ni jambo ambalo lingewezekana, kwa hiyo nikamwomba Ankia aweke hizo mada pembeni kabisa; akitaka tuongee mambo, yawe mambo yaliyonyooka. Akawa anaguna-guna tu na kusema sawa, ila ikitokea nafasi ya mimi kuongea na Miryam, eti nisikwepe maongezi na nijaribu kumsikiliza mwanamke huyo.

Ankia alinishangaza kwa kweli, ni kama vile alikuwa akitaka kusema jambo fulani hivi, lakini akajizuia, mpaka nikahisi labda hapo aliweka simu kwa mfumo wa sauti ya juu na Miryam mwenyewe alikuwa pembeni yake, kwa hiyo nikaamua tu kumuaga na kukatisha mazungumzo hayo. Yaani nilikuwa nimetoka tu kwenye hali ya amani baada ya kuzungumza na mama halafu Ankia naye akaja kunivutugia mambo. Sasa mimi na Miryam kwa wakati huu tuongelea nini? Tuanze kuongea na kujichekesha kinafiki utadhani hakukuwa na damu mbaya kati yetu, ndiyo walitaka hivyo? Sikuhitaji hayo mambo tena. Na sikutaka kuendelea kuyafikiria. Nikaweka namba ya mpenzi wangu Adelina na kumpigia hapo, nami nikatoka ofisini kwenda kutafuta chakula kwanza huku nikiwa nimeanza kuzungumza naye. Araah!

★★

Siku ikaendelea kutembea vyema, na hata Ankia kunipanda kichwani muda ule kukasahaulika. Nimekuja kumaliza kazi zangu saa moja jioni na kuachia wengine ili nikapumzike, lakini tayari nikawa na mipango mingine kwa usiku huu. Muda ule nimeongea na Adelina, tulipanga kutoka baadaye kwenda kujifurahisha kidogo, yeye akiwa na nafasi kutoka kazini saa mbili, hivyo nikamwambia ningempitia kule kwake akishafika. Alikuwa amenikosa mwenyewe, akitaka kweli tufurahie usiku huu hata kwa masaa machache, kwa hiyo nisingemvunja moyo. Moja kwa moja nikarudi kule kwangu, na tayari rafiki yangu Simba alikuwepo akifurahia kutazama mechi kwa utulivu. Tukasalimiana vyema na kujuliana hali, nami nikatulia pia kwa muda mfupi kisha nikamwambia ningetoka tena kwenda sehemu fulani na mtu.

Simba kama Simba akataka kujua ni nani, na nilipomfahamisha kuwa ni Adelina, akataka kuja pamoja nami pia ili amwone kwa mara ya kwanza. Ilitakiwa kuwa kitu ya mimi na mpenzi wangu pekee, lakini Simba akasisitiza kuja, akisema angekunywa mbili tatu tu pamoja na "shemeji mpya" kisha angetuacha baadaye tuwe pekee. Sikuona shida kwa hilo. Kwa hiyo tukajiandaa kikawaida tu, ikiwa inaelekea saa tatu, tukaondoka hapo nyumbani nikiwa naelewa Adelina tayari angekuwa ameshaondoka kazini. Simba akawa ananipigisha story kama zote wakati tuko njiani kuelekea huko Kinyerezi, na katikati ya safari Adelina akanipigia kuniambia kuwa aliningojea huko kwake tayari hivyo niwahi kabla muda haujayoyoma mno.

Kweli, nikajitahidi kuwahisha, mpaka tumefika kwake mrembo ilikuwa inaelekea kuingia saa nne, shauri ya umbali. Nikamwita, kwa sababu tayari alikuwa amejiandaa ingepaswa kuwa atoke, apande kwenye gari, twende. Simba alikuwa ameketi siti ya mbele pembeni yangu, lakini hapo akashuka na kwenda kukaa ya nyuma ili Adelina akija akae ndiyo pembeni yangu. Baada ya dakika chache, kweli mwanamke huyo akatoka, tukimwona namna alivyopendeza kwa kuvalia kiblauzi chekundu chepesi na suruali nyeusi ya skinny iliyoling'ata umbo lake nono vyema, na Simba akawa amekubali. Kwamba kweli nilijua kuchagua wanawake. Sikumwambia kihalisi ni mimi ndiye niliyekuwa nimechaguliwa na mwanamke huyo, ila hiyo ikaishia hapo. Adelina kusifiwa ilikuwa jambo zuri kwangu. Alikuwa ameumbika kweli.

Kwa hiyo akaja mpaka ndani ya gari, akiwa amependeza kweli usoni, nasi tukapiga busu ya kinywa akiwa hajamwona Simba huko nyuma. Ndiyo ile nimemwonyesha, akacheka kwa haya na kufunika mdomo wake, nao wakatambulishana sasa mmoja na mwenzake; nikimwambia Adelina kwamba huyo Simba ndiyo rafiki aliye "best" katika marafiki wote nilionao. Nikageuza gari, mwendoni tukaingia tena, na Adelina akiwa ameniuliza tunakokwenda, nikamwambia leo tungeenda kujiburudisha club. Hakuwa ametarajia hilo, hasa kwa kuwa alipitisha muda mrefu kwenda sehemu kama hizo, kwa hiyo nikamwambia ajiandae kupagawa na burudanj leo mpaka asahau uchovu wowote wa kazi. Akaonyesha utayari wa hilo. Simba alikuwa mtulivu tu.

Basi, tukafika na kuegesha gari mbele ya jengo la club moja kubwa kwenye maeneo ya Mbezi Luis, sijui ndo' panaitwa hivyo, nasi tukaingia huko na kukuta tayari watu wameshajaa na kufurahia muziki na vinywaji. Aisee watu walijua kujitumbuiza. Yaani ulikuwa unaingia club unahisi ni kama umefika nyumbani. Palichangamka sana. Nikamwambia Adelina tucheze, lakini kwa jinsi alivyokuwa, mwanzoni aliona uzito na hata kudai hajui kucheza. Ahaa? Nikamvuta mpaka sehemu tuliyoweza kusimama na kuagiza vinywaji, hapo tukaanza kupiga pombe sasa. Mwanamke alitaka kuwa mstaarabu kwenye kunywa lakini nikamshinikiza anywe mpaka ahisi kichwa kimebondwa japo kidogo, na hilo lilipofanikiwa, ndiyo nikamwingiza sasa kati. Simba hakuwa nyuma.

Hali ya hewa ikiwa imechangamka, watu wakijirusha, kunywa, kula, kulana, tukaanza kucheza muziki. Adelina alijirusha pia, kila mara muziki mpya uliopendwa na wengi ukipigwa alikuwa akirukaruka na kunichezea kwa ukaribu kwa mitindo iliyonisisimua sana, na kadiri muda ulivyokwenda nikazidi kufurahia sana pindi hii. Watu hata ambao sikuwafahamu walikuja kujichanganya na sisi, wakicheza na mimi, wakicheza na Adelina na Simba, na pombe ikiendelea kunyweka kila nafasi ndogo ilipopatikana ya kupumua. Kuna wakati nikawa nikiangalia simu na kukuta namba ngeni kabisa ikiwa imenipigia mara kadhaa, lakini mvutano wa burudani hapo club ukanizuia kuijali na kuweka simu mfukoni tu. Nikawa nahisi muda umeanza kwenda sana, na nilitaka kujirusha hapa club lisiwe jambo la mwisho kufanya mimi na mpenzi wangu mpya. Leo nilitaka tuvaane angalau kidogo.

Nikataka nimfate, nimshike ili kumvuta pembeni na kumwambia tuondoke kwenda kujilia bata yetu faraghani, na nilipomkaribia alikuwa akicheza pamoja na Simba kwa shangwe nyingi. Nikamsemesha, lakini hakunielewa, macho yake yakiwa yamelegezwa na pombe kiasi, hivyo nikawaomba wote wawili tusogee usawa wa kaunta moja ili tupumue kidogo. Wakatii, na tulipokwenda upande ambao haukuwa mbali sana na kaunta, nikamwambia Simba kimasihara kuwa muda uliisha, hivyo abebe virago vyake asepe ili mimi na Adelina twende kwingine. Wote wakacheka sana, utani na masihara zaidi yakianza hapo huku Adelina akinishikilia kiunoni na kusikiliza maneno ya Simba, nami nikazungusha macho huku na kule kwanza kabla sijawaambia tuondoke kwa pamoja; ilhali Simba hakutaka kuondoka. Pisi nyingi amwachie nani eti? Si ndiyo ile nimepiga jicho hivi tena nikawa nimemwona Miryam pale usawa wa kaunta! Heel

Nilishtuka. Niliganda. Nilihisi pigo zito kiasi moyoni mwangu kutokana na kutotarajia kabisa kumwona sehemu hiyo, na nikajikuta nimeendelea kutulia na kubaki nimemtazama kwa umakini. Yaani alikuwa amesimama umbali mfupi kutokea sehemu ambayo sisi tulikuwa, pale kwenye kaunta la tender wa vinywaji, akitazama kwangu moja kwa moja kabisa. Alikuwa amevaa vizuri, T-shirt nyeupe na suruali jeans yenye kubana, na macho yake yaliniangalia kwa njia iliyoonyesha wazi kwamba alitegemea kabisa kuniona, yaani hakushtuka, ni kwamba alikuwa ameshaniona kwa muda mrefu tangu tumefika sehemu hiyo. Sikuwatazama wenzangu tena baada ya macho yangu na Miryam kukutana namna hiyo, lakini nilielewa wao pia walikuwa wameshaona nilikoangalia, na najua Adelina akabaki kusubiri jambo fulani litokee.

Nilimwangalia Miryam kwa mkazo, lakini kihisia, nikiwa nahisi mapigo yangu ya moyo yanadunda kwa kasi zaidi kumwelekea yeye. Sijui kwa nini tu, ni kama bado alikuwa na athari kubwa moyoni mwangu. Kuna kitu nilianza kuhisi kinanitia msukumo, yaani msukumo wa kama kutaka kumwelekea pale alipokuwa amesimama, na hata nyendo za mwili wake zilionyesha hivyo pia, sema ikawa kama vile sote tunasubirishiana. Ndipo kikatokea kitu ambacho kikafanya msukumo huo uvurugike kabisa. Kutokea upande wake wa kulia akamfikia mwanaume ambaye nilimfahamu vyema sana, Festo mwenyewe! Tarajio lolote ambalo kona ndogo ya sehemu ya moyo wangu lilikuwa limeanza kujengwa likatokomea papo hapo. Nilijisikia vibaya sana kuona picha hiyo.

Festo alikuwa ameshikilia bia mbili za kopo, akimfikia Miryam na kuonekana kutaka kumpatia moja, jambo lililonihakikishia kwamba walikuja sehemu hiyo pamoja. Ah, kudadeki! Sijui kwa nini, lakini nikahisi nikichomwa kweli na jambo hilo. Si nilijiambia nisingejali tena? Lakini bado nikahisi kuumia. Sikutoa macho yangu kwao, na najua wenzangu pia walikuwa wakitazama upande wake Miryam. Simba akawa akinitikisa kuniita 'oya, vipi?' lakini sikumwitikia hata kidogo. Miryam hakupokea kinywaji ambacho Festo alitaka kumpa kwa kuwa aliendelea kunitazama tu, na hilo likafanya jamaa atazame upande wangu. Aliponiona, hakuonyesha hisia zozote za kushangaa na kutulia tu, nami nikaacha kuwaangalia wao kwa pamoja na kumtazama Adelina na Simba pembeni. Adelina alinitazama kwa hisia makini kiasi.

"Tuondoke," nikamwambia Adelina hivyo.

Na sikusubiri anipe jibu, hapo hapo nikageuka nikiwa nimeushika mkono wake na kuanza kuondoka. Simba akaniomba nisubiri kwanza, akiuliza tunaenda wapi, lakini sikukatisha hatua zangu, na hata nilipouachia mkono wa Adelina najua wote kwa pamoja walinifuata kwa nyuma. Ingekuwa kwamba nimemwona Miryam pekee hapo basi labda ningevunga tu na kuendelea na mambo mengine, ila kumwona akiwa na Festo, kulinikata stimu kabisa. Tena yaani hata sijui ilikuwa vipi eti na wenyewe wakawa ndani ya club moja na sisi kwa muda huo huo. Hapa pasingekalika tena kwangu, ila najua bado wenzangu walihitaji kuendelea kupata wakati mzuri, na mimi nisingeacha matatizo yangu yawavurugie furaha yao. Hivyo nikawaza tu tukiondoka sehemu hiyo tuelekee nyingine eneo tofauti, na huko tungesaidiana zaidi kusahau mikazo yetu; yangu sanasana.

Nikiwa nimetangulia, tukazifikia ngazi kupitia mlango wa nyuma wa jengo hilo na kuanza kuelekea chini, pale niliposikia jina langu likiitwa na sauti niliyoifahamu vyema kabisa.

"Jayden..."

Ilikuwa ni Miryam. Sikugeuka, na hatua zangu zikafifia kiasi lakini sikuacha kutembea. Kwa jinsi ilivyosikika, sauti yake ilionyesha kwamba alikuwa akitufuata kutokea kule ndani, bado akiwa hajazifikia ngazi, nami nikaona niongeze kasi ya kushuka ili nimwepuke upesi.

"Jayden..." sauti yake ikasikika tena.

"JC... kuna mtu anakuita..." Simba akanisemesha kutokea nyuma yangu.

Sikujibu wala kugeuka na kuendelea kuukata mzunguko wa ngazi ili niwahi kutoka sehemu hiyo, na sasa ikawa wazi kwamba Miryam alikuwa ametukaribia, akishuka ngazi upesi pia kama vile anakimbia.

"Jayden... subiri..."

Ih! Alikuwa anataka nini? Yaani, wakati huu niliokuwa najitahidi kusonga mbele bila yeye, yeye tena akaanza kunikimbiza ili kunirudisha nyuma, siyo? Tena alinionyesha wazi kwamba na yeye alikuwa ameshaanza kusonga mbele na huyo Festo wake, sasa sielewi alihitaji nini zaidi kutoka kwangu. Mizinguo, ama? Sikutaka kabisa kusimama, na ikiwa ndiyo imebaki mistari miwili kuzimaliza ngazi kufikia chini, Miryam akawa amefanikiwa kuwapita Simba na Adelina na kunishika mkononi upesi, jambo lililofanya nigeuke kwa kasi kumwangalia. Alishikilia mkono wangu kwa nguvu, akiuvuta fulani hivi yaani kunizuia, ili nisimame, huku akipumua kwa kasi kiasi, na macho yake yakinitazama kwa hisia nyingi za huzuni.

"Jayden..." akaita.

Nikaendelea kukaza macho yangu usoni kwake kwa umakini.

"Samahani..." akaniambia hivyo huku machozi yakimlenga.

Nikaendelea tu kumwangalia.

"Tafadhali... naomba unisamehe mpenzi wangu..." akasema hivyo.

Sauti yake tamu aliyotumia kuniambia hivyo ilifanya nihisi kuyeyuka moyoni, yaani aliongea kwa hisia huku akikikaza zaidi kiganja changu, nami nikajikuta nalengwa na machozi kwa sababu ya hisia nilizokuwa nikificha kulazimisha kutoka.

Machozi yake yakamwagika, akikinyanyua kiganja changu kukikaribisha na uso wake, na kwa sauti tetemeshi akaniambia, "Nakuomba... naomba tuongee... tafadhali..."

Alionekana kutaka kusema kitu fulani muhimu sana zaidi tu ya kuomba samahani kwa maneno aliyoniambia ule usiku. Nikakosa hata cha kumjibu, hapo tukiwa tumesimama sehemu ambayo watu na wapenzi wao wangepita na kututazama kwa kudhani tunatengeneza sinema, na ndipo kutokea ngazini kuelekea juu nikamwona Festo akiwa amefika hapo na kusimama. Alisimama kwa huo umbali akitungalia, nami pia nikimwangalia, na Miryam pamoja na wengine wakamwangalia. Miryam akiporudisha macho yake kwangu, nikamwangalia pia, kisha nikakivuta kiganja changu kutoka kwake kistaarabu tu, yeye akiwa kama hataki kukiachia, na nilipofanikiwa kukiondoa, hapo hapo nikamwacha na kuendelea kushuka ngazi.

Bila kugeuka nyuma wala nini, nilisikia sauti yake ya chini ya kilio, akionekana kuhuzunika sana, nami nikakaza hisia zangu kiume na kuelekea moja kwa moja mpaka garini kwangu; Adelina na Simba wakiingia pamoja nami. Sikutaka hata kuzungumza, nikawasha tu gari, na hapo ndiyo hisia zikanilemea zaidi na kujikuta tu naishia kuukaza usukani kwa mikono yangu. Miryam bado alikuwa anaudundisha mno moyo wangu, mpaka sasa nikawa sielewi kile nilichotaka au kuhitaji mimi binafsi kuelekea suala langu na huyo mwanamke. Nadhani Adelina aliona namna ambavyo nilikuwa nimevurugika kihisia, naye akiwa kwenye siti pembeni yangu, akakishika kiganja changu na kukikaza kama kunitia moyo bila maneno. Sikumwangalia, bali nikashusha tu pumzi kujipa utulivu, kisha ndiyo nikaliondoa gari sehemu hiyo.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 678 017 280
Dah
We Mimi 🌝
Sema utulivu wa Festo ni moto 🔥
Jamaa ana akili sana, Huwa hatumii hisia kwenye haya mambo
 
Elton Tonny, mwendelezo Mkuu, ikikupendeza wikiendi hii iende poa
 
MIMI NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI

★★★★★★★★★★★★★

Baada ya kuwa tumeondoka club, niliamua tu kumrudisha Adelina nyumbani kwake kutokana na muda kuwa umeenda sana na hamu ya kufanya mambo mengine zaidi ikiwa imevurugwa. Adelina alikuwa mwelewa, na akanisihi niendelee kuendesha kwa mwendo wa taratibu sana kwa kuwa nguvu ya pombe ilikuwa nyingi kichwani, na Simba ndiyo alikuwa kabisaa. Nilijihisi vibaya kiasi kumwacha mwanamke huyo na taswira mbaya kutokana na kilichotokea huko tulikotoka kumhusisha Miryam, lakini sikugusia lolote na kufanya ionekane ni jambo lililosahaulika. Nikamwambia kesho ningemtafuta kama kawaida na kuangalia kama ratiba zingeruhusu kukutana tena, naye akaridhia na kunitakia usiku mwema.

Mwendo wa kurejea kwangu ungekuwa na umbali mrefu, kwa hiyo kuendesha taratibu mno haikuonekana kuwa sahihi kwa maeneo ya barabara ambayo hayakupita magari mengi. Umakini nilikuwa nao hata kama pombe ilikuwepo kichwani, lakini hasa ni kwa sababu bado akili ilikuwa imekazia fikira jambo lililotokea club. Miryam, alinifata yeye mwenyewe, machozi yakimtoka, akanishika na kuniomba msamaha, akiniita "mpenzi wangu" wakati ambao mpenzi wake wa kipindi hiki alikuwa pale pale pia. Sikuelewa vizuri. Hisia zake za majuto kuachana na mimi zilimlemea kiasi kwamba akashindwa kujizuia kufanya kile kitendo mbele ya Festo?

Niliwaza, ikiwa ingekuwa ni hivyo, hiyo ingemtia Festo hasira, kwa sababu angeona kwamba moyo wa Miryam bado ulikuwa kwangu licha ya yeye kujaribu sana kujiondoa maishani mwangu majuzi hapo. Sasa kufikria ni gani itikio la huyo jamaa kwa kitendo hicho ndiyo jambo lililofanya niwaze, nikijua alikuwa mtu wa aina gani kihalisi, huenda angechukua maamuzi mabaya kwa kuhisi kuwa Miryam alimchezea. Pamoja na yote yaliyotokea, bado nilijali usalama wa Miryam, na bado sikumwamini kabisa Festo. Moyo wangu uliniambia kwa njia moja ama nyingine mwanaume huyo angekuja kufanya jambo baya kama si kwangu, basi kwa Miryam na familia yake. Hayo yote ya yeye kuwa mwema kipindi hiki yalisikika kuwa upuuzi tu kwangu. Lakini ningefanya nini? Niwe sahihi au la, ningefanya nini juu ya hili suala la Miryam? Kwa nini bado alinivuta sana?

Ukimya uliokuwepo ndani ya gari ukavunjwa baada ya Simba kunisemesha kwa sauti ya chini, tukiwa bado mwendoni. "Kaka..."

Nikajitahidi kumwangalia na kuona kuwa alinitazama kwa hisia makini, akiwa siti ya pembeni, nami nikatazama mbele na kuitika kwa kuguna.

"Huna mpango wa kuniambia yule alikuwa nani?" Simba akauliza.

Nikabaki kimya tu nikiendelea kuendesha.

"Okay. Ile mode ya Aisha naona imerudi tena. Isipokuwa sa'hivi tutaiita Miryam mode," akasema hivyo.

Nikatikisa kichwa kwa kukerwa.

"Sijui una nini tu na wanawake waliokuzidi umri, boy. Ukiondoa Stella. Ila sikulaumu. Huyo Miryam ni pisi la aina yake! Mtoto alikuwa anakulilia kabisa mpaka nikasema eeh... kumbe dawa imemwingia! Hahah... alikuwa anadengua nini? Kuna wakati wanawake...."

Maneno ya Simba yakazidi kunichanganya, nami nikakosa utulivu na kusababisha mikono itetemeke, jambo lililofanya gari liweweseke baada ya usukani kutikisika.

"Hey, oya! Vipi?"

Simba akashtuka namna hiyo, maana tulikosa-kosa kuingia mtaroni aisee, nami nikajisawazisha na kujitahidi kulituliza gari pembeni ya barabara. Nikainamishia kichwa kwenye usukani nikiwa nimeishiwa pozi yaani.

"Mambo gani hayo mwanangu, unataka kutuua?" Simba akauliza hivyo.

Nikiwa bado nimeinama, nikasema, "Sorry."

"Ah, sore kitu gani bana? Tungekufa bwege wewe! Hayo mapenzi yasiku...."

"Simba, naomba utulie, yaani nakuomba usiseme jambo lingine kutoka kwenye huo mdomo wako nisije hata nikakutukana kaka! Umenisikia?" nikaongea kwa ukali na kumwangalia.

"Unitukane? Kisa nakwambia ukweli?"

"Ukweli gani? Ukweli unajua wewe?"

"Usinipandishie bangi JC..."

"Asa' unafikiri me unanikuna wapi labda?!"

"Acha ujinga JC!"

"Mjinga mwenyewe!"

"Kama ulikuwa huwezi kuendesha si ungesema..."

"Ningesema nini, we' unaweza kuendesha hapo? 'Akati umekunywa viroba kama...."

"Unanipandishia jazba kisa wanawake, una wazimu?"

"Oya, kama vipi shuka, sitaki unitibue sa'hivi..." nikamwambia.

"Ooh, okay," Simba akasema hivyo.

Rafiki yangu akafungua mlango wa gari na kushuka, akiwa hata hajui tuko wapi, naye akaanza kuelekea mbele huko akiniacha namtazama kwa umakini. Hisia zilikuwa zimevurugika mno, na kwa sekunde chache nikimwangalia hivyo nikatambua niliruhusu hasira yangu iniongoze vibaya.

Nikashuka pia, na baada ya kutembea kumwelekea, nikasema, "Oya, Simba... tulia basi..."

Simba akasimama na kuniangalia.

Nikamkaribia, nami nikasema, "Oya, swagger gani sasa hizi tunaanza kuleteana?"

"Si umeniambia nishuke, nimeshuka..."

"Tusiwe kama watoto wadogo, hizi... ni tension tu bro, and... I'm sorry... yaani..." nikakosa hata namna ya kuendelea.

Simba, akiwa anaangalia upande mwingine, akatikisa kichwa kuonyesha amekwazika na kusema, "Mambo gani haya sijui..."

"Oya, twende turudi kwenye gari. Kuna mambo muhimu kesho, twende tuwahi..." nikamwambia hivyo.

Nilianza tu kutangulia kulifuata gari, naye Simba akafuata tu hivyo hivyo nasi sote kuingia tena.

Tukiwa tumekaa sasa, Simba akatikisa kichwa tena na kusema, "Miryam mode ni kali kuliko nilivyofikiria."

Nikalaza kichwa kwenye siti huku nikifumba macho na kusema, "Ni kali mno. Sijui na me tu nakuwaje. Afanye hiki, ama kile... bado tu nitavurugwa, nitahangaika, nitayeyuka yaani... dah!"

Simba akasema, "Wanawake ni matatizo tu bro. Toka walipompa mzee wetu tunda, hawatakagi kutuacha salama."

"Okay, labda tusiende mbali sana, siyo wote wako kama mama yao," nikamwambia.

Akaniangalia usoni, mimi pia nikiwa namtazama, naye akasema, "Kwa hiyo Miryam anataka mrudiane, si ndiyo?"

Nikatazama tu mbele kumwonyesha sina uhakika.

"Utafanya nini kuhusu Adelina?" akaniuliza.

"Si... sijui Simba. Miryam amenichanganya. Yuko na mtu wake hapo club, nimemwona naye, wako wote, halafu ananifata kuanza kuniambia hivyo..."

"Yule jamaa tall aliyekuwa amesimama kwa pale juu..."

"Eeh. Anaitwa Festo. Ndiyo kalisema katampenda huyo, na sa'hivi naona wanapeta, sa' sa'hivi sijui anatak...."

"JC nisikilize," akanikatisha.

Nikamwangalia kwa umakini.

"Achana na hizo habari. Tulia upande mmoja. Unanielewa?" akasema.

Nikabaki nikimtazama usoni tu.

"Amua unapotaka kubaki, baki hapo hapo. Naongea kilevi, lakini naelewa nachosema. Ushanisoma? Masuala ya kuanza kuwaza ooh sijui nini.. a-ah! Unajiumiza kichwa ili iweje? Wewe fuata moyo wako, sijui kama ni bandama yako ndiyo inapenda, wewe ifuate... simama sehemu moja, utulize kichwa. Adelina... pisi! Miryam... matatizo! Full stop," akaniambia hivyo.

Nikatazama pembeni kwa ufikirio.

"Kwa hiyo ni juu yako. Me sijui mengi, lakini nakushauri kama mwana. Chagua pisi, iliyotulia, safi. Chagua matatizo, uendelee kuonja maafa, good. Ni juu yako, lakini simama sehemu moja. Umenipata?" Simba akaongea kwa mkazo.

Nikatikisa kichwa kukubali kinyonge tu.

"Endesha gari," Simba akasema hivyo na kujiegamiza kwenye siti.

Hakutaka mjadala zaidi, kwa upande wake hapo alimaliza. Kilichokuwa kimebaki ikawa mimi kufanya kweli kile ambacho moyo wangu ungenituma kufanya, na matokeo yake ningetakiwa kuyakubali na kusonga nayo hivyo hivyo. Ni mengi sana yalihusika. Nikageuza gari tu tena na kulirudisha mwendoni, safari hii kuelekea kwangu bado ikiendelea kukijaza kichwa changu na mawazo mengi sana.

★★★

Siku ikakucha. Niliamshwa mapema kabisa kwa kengele ya simu, na maandalizi yakaanza ili niweze kuelekea hospitalini. Tulipofika kwangu na Simba hiyo usiiku ilikuwa ni kulala tu, hali bado ikiwa yenye utata kihisia hakukuwa na jambo lingine la kufanya kutokea pale. Lakini hata wakati huu nimemaliza kujiandaa, bado sikuweza kuacha kutafakari kisa cha jana. Ilinifanya niikose amani kiasi kwamba wakati nimeingia kwenye gari ili niondoke, nikajikuta nimetulia tu humo humo nikiendelea kuwaza na kuwaza. Niliwaza mno nifanye nini. Haingekuwa na maana tena kujaribu kuepuka mikazo ya kwenye maisha yangu maana ilikuwa na njia za kujirudisha tu hata nikifanya nini. Na Miryam ndiye aliyekuwa mkazo mkuu kwa kipindi hiki.

Nikiwa nimeona sasa kwamba kuyaepuka haingekuwa na faida, nikachukua simu yangu na kupiga huko hospitali. Nikatoa kisingizio kupatwa na dharula fulani ambayo ingefanya nichelewe kufika, nikiwa nimeongea na daktari wangu mkuu hapo, na kumwomba atafute njia ya kufidishia muda wangu siku hii ili mimi nije kufanya mara mbili ya kazi nitakazokosa kufanya kwa leo. Hakuwa na neno, lakini akaniambia nisichelewe mno kufika maana alikuwa akiniachia sana kutumia muda mwingi nje ya hospitali, nami nikamshukuru na kuagana naye. Baada ya hapo, nikatafuta namba ya mtu fulani kwenye simu yangu na kumpigia. Alipopokea, nikaongea naye kwa ufupi kumwambia tukutane mahali fulani asubuhi hii hii ili tuweze kuzungumza juu ya ishu muhimu sana, naye akakubali. Simu ikakatwa, mwendo wa gari ukaanza.

★★

Nilifika eneo hilo nililompangia mtu huyo kukutana kwenye mida ya saa moja tu, hii hii asubuhi, nami nikaegesha gari. Ilikuwa ni kwenye jengo moja la biashara lenye ghorofa kama tano hivi maeneo ya Kariakoo Fire, na nilimwelekeza kuwa akija akutane nami huko juu kabisa ya jengo. Kwa misingi hiyo mimi tayari nikawa nimejipeleka huko juu na kusimama tu kwenye hilo dari (terrace) la ghorofa, ambapo kulikuwa na wamasai kama wawili hivi waliohusika na ulinzi nadhani. Nikawaambia nilikuja tu kuonana na mtu, aliyekuwa njiani kuja, na hata niikawapatia pesa kidogo ili kuniruhusu nikae tu hapo maana walionekana kunihukumu fulani hivi. Ah, ya soda haikuwa mbaya, nilitengeneza mazingira rafiki tu. Kwa hiyo wakaanza kuondoka kwa kusema wangeenda kuangalia mambo fulani ya kwenye jengo, nami nikawakubalia na kubaki nikingojea.

Nikiwa kwa hapo juu ningeweza kuyaona majengo mbalimbali kuzungukia eneo hilo, watu, na vyombo vya usafiri vikizunguka huko na huko. Fikira zangu zikitekwa zaidi na jambo lililonileta hapa, nilikuwa nimesimama kwa subira tu nikiendelea kutazama mbele, na hatimaye, ikiwa imeingia mida ya saa mbili sasa, nilichokingoja kikafika. Kusikika kwa hatua zilizokuja upande wangu kukanifanya nigeuke, na kwa hakika ilikuwa ni mtu niliyemtarajia, bibie Miryam mwenyewe.

Ndiyo, muda ule niliamua kuchukua simu na kumpigia, maongezi yakiwa ni mafupi tu kugusia mahali pa kukutana ili tuje kuyarefusha zaidi ana kwa ana. Mwanamke alivalia T-shirt nyeupe yenye kubana, suruali ya kitambaa ya blue iliyochora umbo lake zuri vyema, na alivaa miwani pana myeusi ya urembo kwa ajili ya kukinga macho jua. Hata kabla hajanifikia karibu zaidi tayari harufu yake tamu ikazitekenya pua zangu kwa makusudi ya kuamsha hisia, nami nikajikuta nashindwa kuzizuia na kuendelea kumwangalia kwa uvutio wa wazi. Athari aliyokuwa nayo kwangu bado ilikuwa nzito sana, lakini nikajitahidi kuondoa fikira zangu kwenye urembo wake na kuangalia pembeni tu.

Miryam akafika mpaka mbele yangu na kusimama, naye akaitoa miwani yake machoni. Sikumwangalia, lakini najua alikuwa akinitazama kwa hisia sana, na alingoja niseme kitu fulani labda kumkaribisha. Nikajitia ugumu tu kwa kuendelea kuangalia upande mwingine huko, naye akasafisha koo kidogo na kutazama nilikokuwa natazama pia.

"Samahani kama nimechelewa sana Jayden," akasema hivyo.

"Haina shida. La muhimu umefika," nikamwambia hivyo bila kumtazama.

Akaniangalia usoni.

"Siyo mimi ndiyo nitakuchelewesha kazini?" nikamuuliza hivyo.

"Hapana. Leo sitaingia," akaniambia.

Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa, kisha nikashusha pumzi kiasi na kumwangalia. Alikuwa ananitazama kwa njia fulani yenye imani sana, nami nikasema, "Ile jana pale... tulipoonana... ulipotaka tuongee, nili...."

"Haina shida, Jayden. Usiwaze," akanikatisha.

Nikaangalia pembeni na kusema, "Usifikirie vingine. Sikutaka kuomba samahani, nilitaka kusema hisia zilipaa tu ndiyo maana sikuweza kukusikiliza."

Miryam akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, naye akaangalia chini.

"Kwa hiyo sa' hivi niko poa, unaweza kuongea," nikamwambia.

Akanitazama usoni kwa njia yenye hisia sana.

"Niambie, ikiwa kuna jambo la muhimu kweli. Najua una mambo mengi, na... si vyema tucheleweshane. Mm?" nikaongea kwa njia ya kutojali.

"Jayden, naomba unisamehe..." akaniambia hivyo.

"Oh, Miryam kama una...."

Akanishika kiganjani na kusema, "Tafadhali Jayden."

Nikatulia kidogo, nami nikamwambia, "Tuko past kuombana samahani Miryam. Haijalishi tena kwangu."

"Jayden..."

"Ulimaanisha kila kitu ulichosema, siyo? Ulikuwa unajua kabisa yale uliyokuwa unayaongea, shida ni nini sasa hivi?"

"Jayden please... nisikilize..."

Akaongea kwa kubembeleza na kunishika mikononi huku akisogea karibu zaidi na uso wangu. Nikabaki nikimtazama kwa njia ya kawaida.

"Nilikosea Jayden. I know, I know nimekuumiza kwa niliyosema siku ile, ndiyo maana nakuomba unisamehe. Ninakupenda sana, naku-miss mno mpenzi wangu..." akaongea kwa hisia hadi machozi kumlenga.

Nikatazama pembeni tu kwa kuudhika.

"Please. Nakuhitaji sana Jayden, now more than ever... sijui nitafanyaje kuhusu hili bila ya wewe," akaniambia hivyo.

Nikamwangalia machoni.

Akashusha pumzi kujikaza, kisha akaniambia, "Nina ujauzito."

Kauli yake ilisikika vyema sana kwangu, nami nikakaza hisia na kumtazama kama vile sijashangazwa nayo.

Akaniambia, "Jayden, acha kufanya hivyo. Siyo fresh."

Kweli, ikanibidi tu niondoe ukaidi huu wa kipuuzi, nami nikamuuliza, "Unasema kweli?"

Akatikisa kichwa mara moja kukubali. Hisia fulani nzuri ikaanza kujijenga ndani yangu, nikimtazama tumboni kwa hisia za furaha zaidi sasa, naye akawa anabana tabasamu lake la hisia. Lakini hapo ndipo lile wazo la jambo lililokuwa limetupata likanijia akilini, nami nikatazama pembeni kwa kutatizika kiasi.

"Jayden..." Miryam akaniita.

Nikaendelea tu kuangalia pembeni.

Akanishika mkono na kunitikisa kiasi huku akisema, "Jayden, vipi? Una..."

Nikamwangalia na kusema, "Ngoja. Kuna sehemu nataka twende kwanza."

"Wapi?" akauliza.

"Twende," nikamwambia tu hivyo na kumshika kiganjani.

Pamoja na kutonielewa, Miryam hakuweka kipingamizi chochote na kunitii, akinifuata hadi tuliposhuka na kufika chini. Nikaona gari lake alipoliegesha, nami nikamwambia akaingie na kulifuata langu nitakapoelekea. Niliweka umakini wa aina fulani ambao ulimfanya Miryam aniangalie kwa njia ya kuumia kiasi, nami nikamwacha tu na kuelekea kwenye gari langu. Nilipoingia, nikamwangalia kwa huko nje na kumwona anaingia kwenye lake, nami nikageuza upesi kuondoka eneo hilo huku bibie akinifuata.

★★

Mwendo wa dakika chache tu, nami nikafanikiwa kumwongoza Miryam kufikia hospitali ya Muhimbili. Najua hakutarajia nimlete huku, na tulipofanikiwa kuegesha magari huko ndani, tukakutana na kuanza kuelekea upande wa majengo ili kwenda kufanya vipimo. Miryam hakuhitaji kuniuliza chochote, alitulia tu. Najua akili yake ingemfanya afikiri tumekuja kupima mimba yake, ndiyo maana akaniacha tu bila kuuliza chochote, lakini hilo halikuwa lengo langu.

Tumefika upande fulani wa vyumba vya vipimo vya damu, nami nikamwongoza kuingia chumba kimoja kilichoandikwa DNA testing. Hapo ndiyo Miryam alianza kunitazama kwa utambuzi zaidi, naye akasimama kwanza akinitazama kwa subira. Nikamwangalia tu pia na kumtikisia kichwa kumwambia tuingie baada ya kuwa ameelewa lengo langu sasa, naye akaingia pamoja nami.

Hakukuwa na wasubiriaji sehemu hiyo kabisa, na baada ya kuingia humo, tukamkuta daktari mmoja, mwanamke kijana aliyeitwa Rita, na kwa kuwa tulifahamiana vyema nikamsalimu vizuri, naye pia akaitikia vizuri. Nikamtambulisha kwa bibie pia, nao wakasalimiana, kisha nikamwambia Rita kwamba nilihitaji vipimo vya DNA chap.

Rita akasema, "Oh J, nilikuwa nataka kutoka..."

"Najua, lakini nakuomba tu. Vial mbili, faster tu," nikamwomba.

"Muda wa kusubiri ndo' sina. Tufanye kesho..."

"Kesho? Hapana, Rita nahitaji unisaidie sasa hivi. Bado mapema. Usijali. Nitakufidishia with something, I promise. Ni muhimu sana, maana... ni kwa ajili ya dada hapa, na mimi. Inahitajika leo leo. Please Rita," nikamwomba.

Rita akalegeza kidogo na kuingia ndani ya chumba kidogo ndani humo humo.

Miryam, akiongea kwa sauti ya chini, akasema, "Kwa hiyo unataka kusema huamini kwamba hii ni mimba yako?"

Nikamwangalia.

"Unataka tupime DNA ili uthibitishe?" akauliza.

"Hamna. Hii ni ya mimi na wewe," nikamwambia hivyo.

Miryam akaniangalia kama anatafakari maana yangu, kisha ndiyo akaonekana kunielewa sasa.

"Vipi, ulidhani ninashuku kwamba siyo yangu?" nikamuuliza.

Miryam akaniangalia kwa njia ya kukwazika kiasi.

Nikafanya kukaza tena, nami nikasema, "Lakini ngoja. Nitakuwaje na uhakika?"

"Uhakika wa nini?" akauliza.

"Kwamba ni ya kwangu?" nikamuuliza tena.

"Ni ya nani sasa?" akaniuliza kiumakini.

Nikaangalia pembeni na kutikisa kichwa tu.

Bado hali tata baina yetu ilikuwepo, na yeye alilihisi hilo, hivyo naona alikuwa akijisikia vibaya. Hapa tulikuja kupima kama mimi na yeye kweli ni ndugu, maana suala la ujauzito lingekuwa zito zaidi endapo kama hilo lingine lingekuwa kweli. Nilikuwa na wasiwasi sana, na doctor Rita alipotoka na vifaa vya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo, tukakaa na jambo hilo kufanyiwa utaratibu, naye akatuambia tungojee kwa dakika kama thelathini kwa ajili ya majibu. Kulikuwa na kifaa kipya kilichowahisha jambo hilo tofauti na ilivyokuwa zamani; kupima DNA kungehitaji kungoja kwa siku au hata wiki, lakini sasa, dakika mpaka saa. Kwa hiyo Rita alipoweka vyombo mahala pake, akatuambia tungojee, naye akaondoka kwanza.

Mimi na Miryam tulikaa kwenye viti vya kusubiria, na hatukusemeshana chochote kile. Ningeangalia upande huu na ule bila kumtazama yeye, nami ningeona namna alivyokuwa akiniangalia kwa kutarajia hata nimsemeshe, lakini haikuwa hivyo. Kuna muda akawa anajaribu hata kugusisha kiganja chake kwangu, na mimi nikiona hilo wazi, nikawa namwachia tu. Alikuwa na hamu kubwa sana ya mimi kuirudisha ile... hamu yangu kwake, sana inaonekana. Alikuwa amenikosa. Lakini nilihitaji kutuliza hisia aisee. Tayari nilikuwa nimeanza uhusiano na Adelina, na sikatai, bado nilikuwa nina hisia kwake Miryam. Kwa hiyo nilitatizika kwa kuwaza haya yote yangeelekea wapi kutokea hapa. Nilijiuliza ikiwa yangeishia pazuri ama pabaya, ikitegemea na matokeo ya kipimo cha DNA, na yale ambayo tungeamua kufanya baada ya hapo.

Lilipita saa zima tukiwa hapo, doctor Rita akiwa hajarejea, nami nikaona nimpigie. Alipopokea akasema anakuja hivyo ningoje kidogo, nami nikatulia. Adelina alikuwa ameanza kunitumia jumbe kadhaa kwa simu, lakini sikujibu yoyote na kuendelea kutulia tu. Hatimaye Miryam akawa amefanikiwa kugusisha kidole chake kwenye changu, akianza kukikaza taratibu, nami nikamtazama usoni. Aliniangalia pia, kwa hisia sana, nami nikajihisi kuyeyuka sana moyoni kumtazama namna hiyo. Hakuogopa tena kunionyesha namna alivyonikosa, lakini mimi ndiyo bado nikawa najizuia. Ni wakati huo huo ndiyo Rita akawa amerejea, akiwa na daktari mwingine, nao wakaingia mule ndani na kutuacha tukingoja kwa utulivu.

Dakika chache tu kupita naye Rita akawa ametoka tena, akiwa ameshika karatasi iliyochapishwa. Tukasimama, na baada ya kunipatia karatasi hiyo, Rita akaniambia tu hongera, kana kwamba alikuwa ameshaelewa kilichokuwa kikiendelea baina yangu na Miryam, naye akarejea humo ndani akiniacha nimeweweseka kiasi moyoni. Nikamtazama Miryam usoni na kuona jinsi alivyokuwa akinitazama kwa subira, nami nikaiangalia karatasi hiyo. Nikayasoma majibu. Taratibu kushusha macho mpaka chini, nami nikaliona jibu pekee nililohitaji kulijua. Hisia zikapanda hata zaidi kutokea hapo, nami nikamwangalia Miryam mbele yangu kwa macho yaliyojaa simanzi kubwa.

"Vipi?" Miryam akaniuliza kwa kujali.

Nikampatia karatasi hiyo, naye akaiangalia kwa hisia makini, kisha uso wake ukageuka kuwa wa simanzi pia na yeye kuuziba mdomo wake kwa kiganja kuonyesha hisia kali iliyomwingia. Akaniangalia usoni tena, machozi yakiwa yameanza kumjaa machoni, nami nikamkumbatia kwa nguvu nikiwa nahisi furaha tele moyoni!

Miryam akarudisha kumbatio langu na kujibana kwangu kwa nguvu pia, akianza kulia wa sauti ya chini, naye akasema, "Jayden..."

"Dah! Miryam, yaani hizo fujo zote, kumbe sisi siyo...." nikaishia hapo tu na kucheka kidogo kwa hisia.

"Ahh... nisamehe Jayden... yote ni makosa yangu..." Miryam akasema hivyo.

Nikamwachia na kumwangalia usoni kwa hisia, nami nikasema, "Hapana. Usijlaumu."

"No, ni lazima niseme ukweli. Nilikuwa tu... hh... najifanya mgumu, najifanya najua, ona sasa hayo yote yametokea mpaka... nimekuumiza sana," Miryam akasema kwa hisia.

Nikamshika usoni kwa mikono yote.

Akavikaza viganja vyangu na kusema, "Naomba unisamehe tu. Sasa hivi nimejifunza kuwa tayari kupambana kwa ajili ya penzi letu Jayden, kwa sababu sikuzote ni wewe ndiyo umefanya hivyo kwa ajili yangu. Hili ni jambo zuri sana kwetu, hata kama vikwazo vingi havitaki tuwe pamoja, kwa sasa haipaswi kuwezekana tena kututenganisha..."

Nikatabasamu kwa furaha.

"Ninaomba turudi kuwa kama mwanzo mpenzi wangu. Na nakuahidi, zamu hii ni mimi ndiyo ambaye sitaruhusu lolote litusambaratishe tena..." akaniambia hivyo huku machozi yakimtoka.

"Hata wewe mwenyewe?" nikamuuliza hivyo.

"Hata mimi mwenyewe," akanijibu kwa hisia.

Nilipenda sana maneno yake, mtazamo wake mpya kuelekea hali yetu uliifariji sana nafsi yangu, na kutokana na burudisho jipya ambalo mwanamke huyu alikuwa ametoka kunipatia kwa alichoniambia, nikahisi maumivu yote ya kihisia kuisha ghafla. Sikuweza kujidhibiti tena, nikapitisha mikono yangu mgongoni kwake, na yeye vilevile akapitisha yake kwangu tena na sote kukumbatiana kwa upendo. Nilijihisi uafadhali wa hali ya juu, ile kukiachilia mbali kinyongo na kuirudia amani ya penzi la mwanamke huyu, kulinipa uradhi mkubwa sana. Sikujali kingine tena. Miryam alionekana kufurahi sana mpaka akashindwa kuzuia kilio chake.

"Mbona unalia sasa?" nikamuuliza huku bado akiuficha uso wake kifuani kwangu.

Akasema, "Nalia kwa furaha tu."

"Utakuwa na undugu na K-Lynn wewe," nikamtania.

"Ahah... itakuwa. Na we' ndiyo Bushoke wangu," akasema hivyo.

Nikatabasamu na kumwachia taratibu, huku miili yetu bado ikiwa kwa ukaribu, lakini Miryam akanivuta na kuning'ang'ania zaidi ndani ya kumbatio lake. Nikatabasamu zaidi na kumkumbatia tena.

"Usiniachie Jayden. Naomba usije kuniachia tena tafadhali," akaongea kwa kasauti kake ka mideko.

Nikawa nambembeleza kwa kiganja taratibu, nami nikasema, "Usijali Mimi. Zamu hii sitakuacha kamwe, hata nikihitaji kusimama dhidi yako mwenyewe."

Akatoa mguno ulioonyesha hali ya mridhiko.

"Dah, mahusiano yetu haya ni sinema!" Nikasema hivyo.

Akacheka kidogo na kusema, "Na ma-starring ndiyo sisi."

"Ahahah... kabisa," nikamwambia.

Kisha nikamwachia tena taratibu na kumshika usoni kwa wororo, nikimpangusa chozi lake la furaha pia, na yeye akawa amenishika kiunoni huku akiniangalia kwa hisia.

"Sahau bullshit yote iliyotokea hapo kati, Mimi. Kutokea hapa tunasonga mbele, na tunasonga mbele strong," nikamwambia huku nikiitomasa shingo yake taratibu.

Akatikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Lakini kwanza... kuna mambo nahitaji kurekebisha," nikamwambia.

"Mambo yapi?" akaniuliza kwa kujali.

Nikashusha pumzi kujipa utulivu, hapo nikijua uhitaji wa kuanza kumwelezea kuhusiana na Adelina ulikuwa wa lazima.

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

Whatsapp +255 678 017 280
 
Nampenda sana Mimi ila kumfanya Adelina alie ni jambo linalohuzunisna kiasi chake
Ila ngoja kwanza..we JC, mbona hujamuuliza kuhusu Festo? Una uhakika mahusiano yalikuwa hayaanza? Mwamba atakuacha salama kweli? 😂
 
Daah… afadhali nilikuwa siupendi uhusiano na Adelina basi tu, yaani kwenye sehemu za Adelina nilikuwa nasoma huku nimenuna
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Ysiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA PILI

★★★★★★★★★★★★★

Mshtuko mfupi niliopata ukanifanya nimeze juice na kuvuta pumzi puani kwa wakati mmoja, nami nikapaliwa. Nikakohoa na kudondosha juice kiasi kutoka mdomoni mwangu, kitu ambacho kilifanya wale wanawake wakubwa washtuke na kunitazama kwa kujali. Nikaendelea kukohoa kwa nguvu, nami nikasimama kabisa nikijitahidi kujizuia lakini nikawa nashindwa.

"Hee... pole kijana wangu... umepaliwa?" akaniuliza yule mwanamke mweusi.

"Akh... kkhh... koh... koh..." nikaendelea kubanja.

"Zawadi, mfatie maji..." akasema hivyo mwanamke huyo.

Nafikiri Zawadi ndiyo lililokuwa jina la mwanamke huyu mweupe, naye akaenda upesi kule jikoni huku mwenzake akinisogelea na kunipiga juu ya mgongo kwa kiganja chake. Aisee nilikuwa nimepaliwa vibaya. Machozi yalinitoka, kooni nikihisi kama vile kimiminika kimeunganisha bomba la pua na mdomo kwa pamoja, nami nikawa namwangalia yule mwanamke mlangoni pale aliyenikata jicho la hasira.

Maji yakaletwa, huku binti yule aliyelala sofani bado akiwa anatafuna tu vidole vyake kama vile hayupo. Nikaanza kunywa maji, na kikohozi cha kupaliwa kikawa kinafifia japo kooni palivurugika sana. Nikamwangalia yule dada pale mlangoni, aliyekuwa amesimama kwa utulivu tu, nami nikahisi aibu na kuangalia pembeni.

"Uko sawa baba?" Zawadi mweupe akaniuliza.

"Akh... ndiyo... niko sawa..." nikajibu huku koo imenibana.

"Pole sana baba... pole..." Zawadi akanibembeleza.

"Miryam... karibu mwanangu. Za huko?" yule mama mweusi akamuuliza mwanamke aliyesimama mlangoni.

Ke! Huyo ndiyo alikuwa Miryam? Nimekwisha.

Miryam mwenyewe alionekana kutaka kunipasua kabisa kwa jinsi alivyokuwa ananiangalia, lakini akaacha kunitazama na kumwambia mama huyo, "Ni nzuri. Shikamooni?"

"Marahaba," wakajibu wanawake hawa kwa pamoja.

Mpaka sasa nilikuwa nimesimama kwa ukaribu na Zawadi mweupe, akiwa anausugua mgongo wangu taratibu, nami nikamtazama mwanamke yule aliyetakiwa kuwa ndiyo mwenye nyumba wangu. Kufikia hapa ningeweza kutambua tu kwamba dili lilifeli, na alikuwa na kila haki ya kunikasirikia maana nilimtendea kama mtoto mdogo vile kule tulipotoka. Ah yaani mambo mengine haya! Eti ilipaswa tu kuwa yeye kati ya maelfu ya watu wote walioishi Dar!

Mwanamke huyo ambaye sasa nilijua aliitwa Miryam, akafunga mlango na kusogea usawa wa sofa alilolalia yule binti, nami nikamwona akimshika sehemu ya shingo taratibu na kuibonyeza kidogo. Binti huyo, Mariam bila shaka, akanyanyuka upesi huku akiwa anatabasamu kwa furaha na kumkumbatia Miryam kwa nguvu sana, utadhani alimpamia. Huyo Miryam akatabasamu pia na kukishika kichwa cha mdogo wake kwa upendo.

Kuwaangalia namna hiyo kukanifanya sasa nitambue kwa nini mwanzoni binti huyo aliponitazama nilifikiri sura yake haikuwa ngeni sana. Ni kwa sababu kwa kadiri kubwa alifanana na dada yake, mtu ambaye nilikuwa nimemwona siku hiyo.

Binti akamwachia dada yake na kumwangalia usoni huku akicheka kwa pumzi za kujirudia-rudia kama mtoto vile, na dada yake akaingiza mkono ndani ya mkoba aliokuwa amebeba na kutoa boksi refu la biskuti na kumpatia. Akalipokea kwa furaha sana na kukaa kwenye sofa, naye akaanza kulifungua ili ale biskuti zake.

Macho ya Miryam yakarudi upande wetu tena. Kiukweli, kiukweli, huyu mwanamke alikuwa mrembo. Hata mara ya kwanza tulipokutana niliona hilo lakini hasa baada ya kujua sasa kwamba alikuwa mrangi ndiyo ikawa wazi zaidi ni kwa nini. Alikuwa mrefu kwa kadiri iliyomfaa mwanamke, mwenye mwili mzuri ulionawiri, kiuno chembamba na miguu mirefu yenye unene wa chupa ya Dompo. Alibeba mapaja manene kiasi yaliyoitesa sketi aliyovaa kwa kuivutisha zaidi kila pande, na hapo bado sikuwa nimemchora huko nyuma vizuri ila nilijua kuna hazina matata iliyokuwa imetunishwa huko.

Alionekana kuwa mwanamke makini sana asiyependa mchezo, na ndiyo jambo ambalo lilifanya nisikazie fikira sana masuala ya uanamke wake zaidi ya masuala yaliyonileta huku; ukitegemea tayari nilikuwa na kesi ya mkosaji kwake.

"Tesha amerudi?" Miryam akauliza.

Sauti yake nzuri ikanifanya nikumbuke namna alivyoniongelesha kwa kujali sana kule tulikotoka.

"Hapana, bado hajaja," mwanamke yule mweusi akamwambia.

Kwa jicho la pembeni, niliweza kumwona Zawadi mweupe akimwonyesha Miryam kwa ishara ya macho kuwa niko hapo, na mwanamke huyo akaniangalia. Alinitazama kwa umakini sana, naye akapiga hatua tatu nne kunielekea huku bado nikiwa nimesimama. Nikaweka uso tulivu tu, nikihisi labda hata natakiwa kusema "shikamoo."

"Ndiyo wewe?"

Miryam akaniuliza hivyo, na kama angekuwa ni mtu ambaye amefika akiwa na malengo mengi ya kumfikisha hapo, basi nisingeweza kujua aliuliza hivyo kuelekea lengo lipi. Lakini langu lilikuwa ni moja. Kuja kupangishwa hapo, basi.

Hivyo nikielewa swali lake lililenga ishu hiyo, nikajibu, "Ndiyo."

Sikuendelea kukohoa tena, na wakati huu nilijivika tu ujasiri wangu wa kiume ingawa bado nilihisi vibaya kwa nilichokuwa nimemfanyia. Baada ya kumpa jibu hilo alinishusha na kunipandisha kama kuonyesha haamini vile, nami nilielewa sababu kuwa yeye kutopendezwa nami. Haingejalisha tena kuhusu yaliyotokea ikiwa tu ningemwomba samahani, na kama asingeikubali basi fresh, ningetafuta tu sehemu nyingine ya kukaa.

Nikawaangalia mama zake kwa ufupi, ambao walitutazama sisi wote kwa umakini, nami nikamwangalia Miryam usoni na kusema, "Naomba kuongea nawe Miryam... kibinafsi."

Aliniangalia machoni bila kukwepesha hata kidogo, na wanawake wale wawili wakaendelea kunitazama.

"Kama ni sawa. Twende chumbani, halafu tuzungumze," nikamwambia hivyo kwa sauti yenye uhakika.

Akanikazia macho yake na kuuliza, "Unataka... nikupeleke chumbani?"

"Ndiyo. Nionyeshe chumba... ili tuongee pia," nikamwambia hivyo.

Nilikuwa namwonyesha kwa lugha ya macho kwamba nilihitaji tuzungumze kuhusu tatizo letu, lakini aliniangalia utadhani amechanganyikiwa. Akawatazama wale wanawake kwa mshangao fulani hivi, na hata mimi nilipowaangalia nikaona wananitazama kimaswali kiasi.

Lakini Zawadi mweupe akaachia tabasamu na kusema, "Ni sawa tu... nyie nendeni mkaongee... sisi tutakuwa hapa hahah..."

Nikamwangalia Miryam usoni na kuona ni kama vile anashangazwa na mimi, na nilichukulia hiyo kuwa kwa sababu labda hakutaka kunipeleka chumbani. Lakini akaangalia pembeni kiasi na kushusha pumzi, kisha akaanza kutembea taratibu kuuelekea upande ambao bila shaka ungefikia vyumbani.

Sikuhitaji kupewa agizo, hiyo ilikuwa ishara tosha kwangu. Nikawapa tabasamu hafifu wanawake hao wawili na kubeba begi langu, kisha nikaanza kumfata mwanamke yule. Sijui ni kwa nini lakini eti wakawa kama vile wanashangaa kuona nimelibeba na begi kabisa. Ah ugeni huu! Bora nisingelazimisha kutafuta huduma ya aina hii maana hali yote ya hapa ilizidi kunichanganya.

Kumfata mwanamke yule kulinipeleka upande wa nyumba hiyo uliokuwa na korido fupi lenye milango mitatu ya vyumba vya kupumzikia, na kona nyingine iliyopeleka mtu kwenye choo na bafu. Angalau sasa niliweza kulichora umbo lake huko nyuma, na alikuwa amebarikiwa kubeba mzigo wa maana!

Yeye akaingia ndani ya mlango wa chumba cha mwishoni, na nilipofika hapo nikakuta amesimama mlangoni kama kuniruhusu niingie, nami nikampita na kuingia. Bado alikuwa akinitazama kimashaka fulani hivi, lakini baada ya mimi kuingia ndani humo mashaka yangu ndiyo yakapanda zaidi.

Chumba hicho kilikuwa kizuri; kizuri mno. Lakini ulikuwa uzuri ambao ulimfaa mwanamke, si mwanaume. Vitu vingi sana vilikaa kimaua-maua tu, kuanzia mashuka yaliyotandikwa mpaka kabati la nguo lililopambwa kwa maua, na hata upande mmoja kulikuwa na dressing table, yaani meza ya kujipambia mwanamke iliyo na kioo kirefu pamoja na vipodozi na manukato!

Nikatembea na kuingia ndani zaidi nikiwa nakiangalia kwa umakini, fikira zikiwa kwamba huenda kuna mwanamke aliyekuwa akikaa humo na sasa hakuwepo, ndiyo mimi ningechukua nafasi yake. Siyo kuchukua nafasi ya kuishi kike, ila nafasi ya kulala kwenye chumba!

"Umekuja na begi kabisa?"

Sauti yake Miryam iliyouliza swali hilo ikanifanya nimgeukie na kumtazama. Bado aliniangalia kana kwamba hanielewi hata kidogo, na mimi kiukweli nilikuwa nimeanza kuchanganyikiwa.

"Chumba ndiyo hiki?" nikamuuliza.

"We' unakionaje, ni sebule?" na yeye akaniuliza.

"Hapana, namaanisha... kina mwonekano wa kike sana. Ama ndiyo mnavyopamba siku hizi kwa ajili ya wageni? Nikilala humu nitajihisi kama princess," nikasema.

"Kulala kivipi?" akaniuliza.

"Kulala kulala. Si ndiyo nitalala humu?"

"Hakuna chochote kilichopangwa, unanielewa? Huwezi kulala humu..."

Njia aliyotumia kunisemesha ilijaa kisirani sana, na tayari nilijua sababu kuwa nilimuudhi kwa hiyo nikachukulia yote hayo kuwa majungu tu. Nikaweka begi chini na kusogea mpaka kufikia aliposimama, naye alikuwa ananitazama usoni kwa umakini mno.

"Sikiliza dada. Najua hatujakutana kwenye mazingira mazuri, na ndiyo maana nimeomba uje nami humu ili nikuombe tu samahani. Huna sababu ya kuendelea kunikasirikia, mimi siyo mtu mbaya... muda ule nilihitaji tu msaada, lile eneo sikulifahamu, na usiku ulikuwa unaingia... ndiyo maana nikafanya vile..." nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Akaangalia pembeni na kubana midomo kwa njia fulani ya kukerwa kiasi.

"Hayo ya saa zile tuyasahau. Me napenda amani, halafu na hapa nimepapenda. Nataka nikae hapa," nikamwambia.

Macho yake mazuri yakarudi tena kwangu, akinitazama kama vile bado hanielewi, naye akasema, "Na wewe nisikilize. Sipendi michezo isiyo na faida. Umeanza kunifanyia michezo huko nyuma, na umeileta mpaka hapa. Kuna lolote lililopangwa kukuruhusu ulale chumbani kwangu?"

Nikakunja uso kimaswali kiasi. Chumbani kwake? Sikuelewa vizuri.

Akashusha pumzi kiasi kama kujipa utulivu, kisha akaanza kusema, "Nisikilize Festo..."

A-ah! Festo gani tena? Mbona alikuwa ananichanganya?

"Mimi sitakuwa mwongo kwako. Hili suala haliwezi kufanikiwa. Ni sawa wakubwa wetu wanataka kutusaidia lakini siko tayari kuanzisha mahusiano na wewe, achilia mbali kuolewa..."

Eh! Nikabaki kinywa wazi kiasi huku namwangalia kwa umakini, kwa sababu kiukweli alikuwa ameniacha Mbezi.

"Kama wewe ni mtu mzima naweza kuamini kwamba utanielewa, na ndiyo maana niliyaruhusu haya yote ili tukutane, niweze kukwambia wewe kama wewe. Ndoa ni jambo zito, na bado... bado siko tayari. Sijui hata Shadya aliwaza nini kudhani mimi na wewe tungeendana kwa kweli... kwanza unaonekana kabisa ni mdogo kwangu. Mimi kwa ombi hilo... makubaliano yote ambayo amefikiri tunaweza kufanya... siko tayari. Nadhani inaeleweka kaka'angu..." akayasema hayo kwa sauti tulivu.

Niliinamisha uso kiasi nikiwa natafakari yote aliyosema, na sasa kila kitu kikawa kimeeleweka kwangu.

Hawa wanawake walikuwa wanamsubiria mtu mwingine tofauti na mimi, ambaye labda alikuwa na mipango ya kuja kumchumbia huyu dada. Shadya ndiyo alikuwa mshenga, muunganishi wao. Kwa hiyo mimi nilipofika hapa, wale wanawake wawili walifikiri mkwe ndiyo kafika, na kwa kweli hali nyingi zilikuwa zimeingiliana kwa njia iliyofanya nijikute natendewa kwa njia ambayo aliistahili huyo Festo aliyetarajiwa kufika. Mpaka wali wake na nyama niliula!

Nikajikuta naachia tu tabasamu na kutikisa kichwa kwa kutoamini jinsi hali hii ilivyonifikisha mbali namna hiyo.

Miryam alipoona natabasamu, akaniuliza hivi, "Nilichokisema kimekupa furaha, au?"

Nikamwangalia, nami nikashindwa kujizuia kucheka kidogo kwa pumzi, kisha nikasema, "Ndiyo, ndiyo, sawa."

"Usiseme sawa, nimekwambia hapana," akasema.

"Ndiyo, sawa imemaanisha hapana..." nikasema hivyo.

Akaniangalia kama vile hanielewi.

"Pole dada. Kuna mwingiliano umeingiliana hapa... mimi siyo unayemdhania," nikamwambia.

"Nini?" akauliza kwa sauti ya chini.

"Mimi nimekuja huku kwa...."

Maneno yangu yakakatishwa baada ya kumwona Zawadi mweupe akiwa amefika nje ya chumba hicho, na Miryam akageuka kumtazama pia. Uso wa mama huyo ulionekana kutatizika kiasi, naye akaendelea kusimama hapo huku akiniangalia kimaswali.

Miryam akamsogelea karibu na kumuuliza kuna nini, naye akamwambia kwamba Shadya alikuwa amefika, pamoja na wageni. Wote kwa pamoja wakanitazama tena usoni, nami nikalifata begi langu na kulibeba tena, kisha nikawasogelea na kuwaomba turudi pamoja sebuleni, nao wakakubali.

Tulipofika pale sebuleni, watu walikuwa wameongezeka, isipokuwa binti yule mdogo niliyemwacha akila biskuti ndiye ambaye sikumkuta kwa wakati huu. Wageni niliowakuta hapo walikuwa watu wazima wanne, wanawake wawili, wanaume wawili. Wanaume walikuwa watu wazima kwa pamoja kufikia miaka 40 hivi, pamoja na mwanamke mmama mwenye kama miaka 60 hivi. Wote walisimama kukaribiana na masofa baada ya kumwona Miryam. Ukijumuisha na yule mwanamke mweusi pia, sasa kila mtu hapo akawa amesimama.

Kwa wale wageni waliofika, mwanamke mmoja mwenye umri mkubwa kufikia miaka 45 hivi aliyevalia baibui na ushungi, aliniangalia kiudadisi sana, kama kujiuliza mimi ni nani. Kila mmoja wao alielekeza umakini wake kwangu isipokuwa Miryam, ambaye alisimama tu kwa utulivu baada ya kuwaamkia wawili wa wageni wale ambao walimzidi kiumri. Mimi pia nikawaamkia wote, nao wakanijibu vizuri kasoro mwanamke huyo aliyevaa ushungi.

"Huyu ni nani?" mwanamke huyu aliyevaa ushungi akauliza.

Wanawake wale walionikaribisha wakanitazama tu kama vile wanasubiri mimi ndiyo nitoe jibu, na kwa kutumia akili ya haraka, nikamuuliza mwanamke huyo, "Wewe ndiyo Shadya, eti?"

Huyo mvaa ushungi akatikisa kichwa kukubali.

"Aaa sawa. Aisee... kuna mabiti yamemix vibaya sana hapa ahah... nimejichanganya kidogo," nikawaambia.

Wote sasa wakawa wananiangalia.

"Mimi natokea Sinza, nimekuja Mbagala leo kuna hii nyumba nilikuwa natakiwa kufikia, sasa... ramani imenileta mpaka hapa, nikafikiri ndiyo penyewe, sijui nimekosea wapi..." nikawaambia.

"Ulikuwa unaenda kufikia wapi kwani?" Shadya akaniuliza.

Ongea yake ilikuwa sharp, akionekana kuwa mswahili mkomavu, nami nikasema, "Kuna nyumba inafanyiwa upangishaji mpya wa vyumba... niliwasiliana na aliyetoa tangazo, sasa tukakubaliana nije ili... nikae hapo."

"Lakini ramani ikakuleta hapa?" akauliza mwanamke yule mweusi, ndugu ya Miryam.

"Ndiyo," nikamjibu.

Zawadi mweupe akaonekana kutafakari kitu fulani, naye akaniuliza, "Umesema nyumba ya kupangishwa?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Ahaa... hiyo nyumba ni hapa hivi pembeni, kwa huyu jirani yetu. Ankia si alikuwa ameshatuambia anataka kupanga na mtu juzi juzi?" Zawadi akawasemesha wakina Miryam.

"Eeeh ndiyo..." akajibu yule mwenziye nisiyemjua jina, la sivyo labda na yeye ningemwita Zawadi mweusi.

"Baba ni hapo hivi... ukivuka huu ukuta wetu," Zawadi mweupe akaniambia.

"Hii nyumba ya pembeni kumbe?" nikauliza.

"Eee..." akaitikia.

"Ina maana hukuwa umewasiliana na Ankia akwambie nyumba yake ilipo?" Shadya akaniuliza.

"Tuliwasiliana kwa WhatsApp, nikamwambia nitakuja siku yoyote wiki hii, sema nimechelewa tu kidogo leo... kuna katatizo kalitokea," nikasema hivyo na kumtazama Miryam.

Alikuwa ananitazama usoni kwa umakini, nami nikaangalia pembeni.

"Kwa hiyo alipofika hapa mkafikiri ndiyo Festo?" Shadya akawauliza wale wamama huku akimwonyeshea huyo Festo kwa kiganja chake.

Nikamwangalia jamaa. Alikuwa mmoja wa wale wanaume wawili waliosimama hapo, mrefu kiasi kunipita, mweusi, na mwenye mwonekano nadhifu wa kiutu uzima. Alikuwa na sura tulivu tu, na ndevu nyingi kidevuni pekee, na kwa kumtazama upesi ningeweza kukisia alikuwa mtu mwenye pesa. Bila shaka wale wengine waliokuwa naye walikuwa ndugu zake ama wazazi, nami nikamwangalia Miryam na kuona ameangalia chini tu.

"Eee ndiyo, tukafikiri ni yeye. Jamani! Haya ni makubwa... naombeni radhi sana," Zawadi mweupe akasema hivyo.

Nilijisikia vibaya kiasi ukitegemea na ukweli kwamba wanawake hao walinitendea kwa ukarimu sana. Shadya akawa ananiangalia kama vile hanitaki, yaani hataki niwe hapo, na kiukweli sikutakiwa kuwa hapo. Huenda hata ningesababisha wadhani mchumbiwa ameshaliwa!

Nikalivuta begi langu vizuri mgongoni na kusogea usawa wa Zawadi na mwenzake, nami nikasema, "Asanteni sana, japokuwa tumekutana katika mazingira yenye kuchanganya lakini... nashukuru kwa ukarimu wenu. Msosi ulikuwa mtamu sana."

Zawadi mweupe akatabasamu kiasi na kunishika begani, na mwenzake akatikisa kichwa tu kuonyesha uelewa.

Nikawatazama wageni, ambao bado walikuwa wamesimama wakiniangalia, nami nikasema, "Jamani, msiendelee kusimama, kaeni. Karibuni mkae."

Shadya akaanza kuwaambia wageni wakae kweli, na nilipomwangalia Miryam nikakuta amenikazia sura. Najua alikuwa ananishangaa kwamba mimi si mwenyeji hapo lakini nawaambia wageni wakae kana kwamba palikuwa kwetu, nami nikatabasamu kidogo na kisha kuuelekea mlango.

Nikaufungua na kuwapungia mkono kuwaaga, nikisema ningefika tu kwenye nyumba ya huyo Ankia na kukutana naye kama mwenye nyumba wangu halisi hatimaye, na akina mama wale wakanipa heri na usiku mwema.

Nilipomwangalia Miryam tena, alikuwa amenikazia tu jicho lake kwa umakini, na sijui ni nini tu lakini njia yake ya kununa ilimfanya apendeze sana kiasi kwamba sikuweza kujizuia kutabasamu kila nilipomwona namna hiyo, nami nikafungua tu mlango na kutoka nje.

Nikaanza kuondoka hapo huku nikiwaza jinsi bahati ya leo ilivyokuwa ikipingana sana na mimi, kuanzia kuharibikiwa na daladala mpaka kuingia kwenye sebule ya mhusika nisiyetakiwa kukutana naye. Ila huyo Miryam alikuwa ameifanya jioni hii iburudishe sana siyo siri.

Nikatoka zangu mpaka nje ya geti, na hapo nje lilikuwepo gari aina ya Volkswagen Touareg nyeusi, bila shaka ikiwa ni ya mchumba Festo. Nikawaza ikiwa Miryam alimaanisha kweli kile alichokuwa ameniambia alipofikiri mimi ndiyo nimekuja kumchumbia, basi hata huyo Festo angerudi kwao mikono mitupu. Ila kuna kitu chochote kile ambacho pesa haiwezi kubeba siku hizi? Aa wapi!

Nikavuka tu nyumba hiyo na kwenda ya pembeni. Kwa nje, kulikuwa na duka la bidhaa, na ndani niliweza kumwona mwanamke mwislamu akiwa ameketi huku akinyanyua kichwa chake kunichungulia kutokea ndani humo, nami nikampuuzia tu na kuingia ndani ya geti jepesi la vyuma vyembamba kama milango ya gereza.

Lilikuwa wazi, nikaelekea ndani zaidi ya upande huo, na ukuta ule uliozitenganisha nyumba hizo ulikuwa na... niseme urembo labda, urembo wa matundu manene kuuzungukia ulioruhusu kuiona nyumba ya akina Miryam kwa nje, pale ndani ya geti lao. Yaani kwa hapo ningeweza kuliona lile gari la pickup la Miryam, na bila shaka wao pia wangeona upande huu wa nje wa hii nyumba niliyofikia.

Nikaenda mpaka kwenye mlango wa nyumba hii sasa. Ilikuwa pana pia, lakini si sana kama ya akina Miryam. Kulikuwa na ubaraza mpana uliojengewa matofali madogo-madogo ya simenti yenye mtindo wa urembo, nikaona jengo lingine dogo kwa nje lenye milango miwili kwa ukaribu; bila shaka choo na bafu, sinki fupi la kuoshea vyombo bila shaka likiwa limejengwa kutokea ukutani, na kamba za kuanikia nguo kwa juu.

Hakukuonekana kuwa na watu wengi hapa na inawezekana aliye ndani tayari alikuwa amejifungia kwa ndani maana ilikuwa saa nne hii, ila nisingeweza kujua. Nikaugonga mlango mara tatu na kusimama kwa kusubiri. Haikuchukua muda mrefu sana na mlango ukafunguliwa, na hapo mbele yangu alisimama mwanamke mtu mzima ambaye kwa haraka ningeweza kukisia alikuwa kwenye miaka ya 30 hivi.

Alikuwa na mwili ulioukimbilia unene, mwenye uso wa duara na midomo mikubwa ya denda nzito. Macho yake yakiwa ya kungu kiasi, sura yake ilipendezeshwa kwa weupe fulani hivi uliotokeza sana, aidha wa mapodozi ama kujichubua, kwa kuwa rangi ya mikono yake haikuwa nyeupe namna hiyo. Alivaa kilemba kilichofunika nywele zake ama labda kipara, dera pana mwilini, lakini bado liliuchora mwili wake vyema kuonyesha kwamba alikuwa na mapaja na miguu minene, na puani aliweka pini ndogo ya urembo.

Alinitazama kwa macho fulani... laini, kama vile hajiulizi nilikuwa nani, lakini tena akisubiri kujua mimi ni nani.

Ingawa alionekana kuwa mkubwa kwangu, nikamwambia, "Mambo vipi?" kwa sauti tulivu.

"Poa," akajibu hivyo na kubana midomo yake.

"Wewe ndiyo mwenye mji?" nikamuuliza.

"Ndiyo. Wewe ni nani?" akaniuliza.

"Mimi ni yule kijana tuliyewasiliana WhatsApp, kuhusu ile ishu ya kuishi kwa kulipa kodi kwenye nyumba yako..." nikaeleza.

"Aaaa, ndiyo wewe?"

"Ndiyo."

"Sawa. Karibu, karib... karibu ndani," akanikaribisha.

Aliacha uwazi zaidi ili nipite, nami nikaingia mpaka sehemu ya sebule huku nikisikia anaufunga mlango.

Sebule hii haikuwa pana sana, lakini ilipambwa vizuri mno. Vigae sakafuni, vilivyofunikwa kwa kapeti zito jekundu lililobeba meza ndogo ya kioo, masofa mawili marefu na moja lingine dogo yaliyopangwa kuizunguka meza hiyo, feni kwenye kona moja ya ukuta, na TV ndogo ya flat screen iliyobebwa kwa vyuma vyake vilivyounganika na ukuta juu kiasi. Kulikuwa na mapambo ya midoli kwenye meza ile ya kioo na masofa yalipambwa kwa kutunikiwa vitambaa; bila shaka kuficha zaidi ngozi zake zenye nyufa nyingi kutokana na kuchanika.

Niliona upande mwingine wa mbele zaidi wenye ukuta uliokuwa umetenganisha milango miwili, bila shaka ya vyumba, na upande mwingine ulionyesha sehemu ya jikoni ambayo haikuwa na mlango. Palinukia ile harufu ambayo wanawake waislamu hupenda kuivaa, sijui manukato ya kuchomwa, kitu kama hicho. Lakini huyu hakuonekana kuwa mwislamu.

Nikamgeukia mwenyeji wangu, ambaye alikuwa anasogea upande wangu huku amevibana viganja vyake kwa mbele, na akiniangalia kwa macho yenye subira. Nikamwangalia kwa macho yenye upendezi, naye akatabasamu kwa haya kiasi na kuangalia chini. Athari niliyonayo kwa wanawake!

"Kwa hiyo... nimefika sehemu sahihi?" nikamsemesha.

"Eeee... ndiyo hapa," akajibu.

"Najua hukutarajia nije leo, halafu usiku sana..."

"Hapana, mbona bado mapema? Hamna shida. Karibu sana," akasema kwa sauti yenye kuvutia.

"Asante. Uko mwenyewe?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa kukubali mara moja, kwa njia ya shau.

Nikatabasamu kidogo na kusema, "Poa, basi... nionyeshe chumba af'... tuongee mengine."

Akanipita tu na kuuelekea mlango wa mbele zaidi kati ya ile miwili, nami nikamfata. Ningetaka kumuuliza upesi kwa nini aiishi peke yake kwenye hiyo nyumba, ikiwa alikuwa na familia labda, ama kama haikuwa yake yeye na alikuwa mtunzaji tu, lakini hayo yangepaswa kuja baadaye.

Hapa suala lililokuwepo ni kwamba ningeishi kwenye nyumba hiyo pamoja na mwanamke bila mtu mwingine kuwepo, kwa hiyo ya kutegemea yalikuwa mengi. Yale mambo yetu yale! Mwanamke mwenyewe alikuwa anatembea kwa kutikisa kweli maana na yeye alikuwa na zigo tenteme, nami nikaingia pamoja naye ndani ya chumba hicho.

Kilikuwa na mwonekano safi na mpangilio mzuri wa vitu vichache tu vilivyokuwemo. Kulikuwa na kitanda chenye ukubwa wa nne ya sita, kilichotandikiwa shuka jeupe na safi sana. Mito miwili ilikipendezesha zaidi, na neti ilifungwa juu kwenye ceiling board kukielekea, ama kwa kiswahili tulivyozoea kuiita, basi ni singibodi. Kulikuwa na kabati la kuwekea nguo ukutani, na uwazi mpana kiasi sakafuni kutokea mwisho wa kitanda ambao ungeniruhusu kuwekea vitu vyangu vingine kama viatu. Na palinukia harufu yake huyo mwanamke.

Nikapatazama kwa kuridhishwa sana kwa kuwa palifanana na jinsi nilivyotaka pawe kabisa, kawaida, patulivu, angalau kwa jinsi palivyoonekana. Nikamgeukia mwenyeji wangu na kukuta ananiangalia tu usoni, lakini ndiyo akakwepesha macho yake baada ya yakwangu kugongana na yake.

Nikashusha pumzi na kusema, "Pazuri. Pametulia."

"Ndiyo. Huku hamna makelele yaani unalala vizuri kabisa," akasema.

"Na mbu kama wote..."

"Ahahah... unachoma tu dawa, af' unashusha neti. Hawasumbui. Hata usiposhusha neti, ukishachoma tu dawa wanaisha, unalala kwa amani."

"Sawa. Tutakuwa tunaishi kinyumbani zaidi kwa hiyo mengi ya hapa utanielekeza ili niendane vizuri na mazingira, au siyo?"

"Hamna neno."

"Kwa hiyo, utataka nikulipe kila tarehe ya mwanzo wa mwezi, ama mwishoni?" nikamuuliza.

"Wewe tu," akaniambia hivyo huku akiangalia pembeni.

"We' ndiyo uniambie, si ndiyo mwenye nyumba wangu?"

"Ahah... ni wewe tu, me... hata ukilipia sa'hivi au mwishoni mwa mwezi sawa tu."

"Mh! Mbona kwenye tangazo ulisema malipo kwanza? Je nikikwambia nitakulipa mwishoni halafu nikakimbia kabla mwezi hujaisha?" nikamuuliza kichokozi.

"Hahaah... hapana, huwezi. Kesho tunapaswa kwenda kwa mwenyekiti ukasaini pepa tulani la makubaliano. Kwa hiyo ukikimbia jela inakuhusu," akasema hivyo na kuniangalia kwa ufupi.

Alionekana kunionea aibu, yaani hakutaka kunitazama usoni kwa muda mrefu, nami niliona furaha fulani ndani yake iliyotokana na matarajio mengi ya kupata mteja mwenye sura nzuri. Najua mnaelewa, siyo kwamba najisifu sana!

Nikamwambia, "Aaa, basi poa. Uko makini kumbe."

"Eee... lazima kuwa makini. Hapa mjini, ukizubaa unaachwa kweli," akaniambia huku akitabasamu.

"Safi sana. Ila usijali sitakukimbia. Na... nataka nikulipe sasa hivi ya miezi miwili kabisa," nikamwambia.

"Siyo lazima sasa hivi kaka, wewe... pumzika tu. Mengine hata kesho," akaniambia kwa njia fulani yenye kubembeleza hivi.

Dah! Haya bwana. Nikamwambia, "Asante. Jina lako Ankia, si ndiyo?"

Akaniangalia kimaswali kiasi huku akitabasamu, naye akauliza, "Umejuaje? Hatukuambiana majina WhatsApp. Ama umesoma kwenye namba jina la usajili?"

"Hamna, nimelijua leo, muda sio mrefu. Wakati nakuja nikapotea njia, nikaingia kwenye nyumba hiyo jirani nikifikiri ndo' kwako..." nikasema.

"Wewee!" akanena hivyo kimshangao kiasi.

"Ndiyo. Wakaniambia nimekosea, wakanielekeza hapa na jina lako ndo' nimelijua kutoka kwao."

"Aisee... hahaha pole mwaya," akaniambia huku akitabasamu.

"Sijui ingekuwaje kama ningeingia kwenye nyumba ya wanoa visu," nikamtania.

Akacheka kidogo na kusema, "Wangekunoa. Huku wahuni wengi unajua..."

"Na wewe ukiwemo?"

"Akhaa... mie nakulaga zangu za kistaarabu tu, hayo maisha ya waswahili tunawaachia wengine ndiyo wanayawezea..."

"Eti ehh..."

"Eeeh..."

"Wewe na nani mwingine?"

"Mimi na hao majirani zangu uliotoka hapo kwao, yaani hatuna zile shobo na watu wengi. Tunaishi kivyetu sana. Watu wa huku wakikuzoea mno ni mpaka nguoni..."

"Hahah... hiyo iko kila sehemu," nikasema.

"Yeah, sioni kama inafaa. Kwa hiyo... wewe unaitwa nani?" akaniuliza.

"JC," nikamwambia.

Akatabasamu kidogo na kusema, "JC. Jina zuri."

"Asante."

"Ni kifupi cha?"

"Jina Chafu," nikamwambia kiutani.

Akacheka kidogo na kusema, "Sawa. JC ndiyo inafaa zaidi."

Nikaweka begi kitandani pale, na huwezi amini mpaka kufikia hapo bado nilikuwa nimelibeba.

"Kuna joto," nikasema hivyo.

"Usipime yaani. Tunajimwagiaga kabla ya kulala angalau mwili unakuwa fresh," akasema hivyo.

Sikutoa itikio lolote kwa kauli yake, bali nikawa nafungua zipu ndogo ya begi ili nitoe baadhi ya vitu vyangu. Bado akawa ameendelea kusimama hapo hapo mlangoni kama vile kuna kitu alikuwa anasubiria, nami nikamtazama usoni.

Akaibana midomo yake na kuangalia pembeni kama vile anajishauri hivi, kisha akauliza, "Nikakuwekee maji... bafuni ujimwagie?"

Swali hilo likanifanya nitabasamu kwa mbali huku nikimwangalia kiumakini, naye akatabasamu kwa haya na kuangalia chini. Kiukweli... au basi tu!

Pigo zake za kischana zilieleweka vizuri sana kwangu ingawa alikuwa mkubwa, na hayo madoido aliyoweka yalinifanya nijihisi kweli ni kama nimefika nyumbani kwetu kabisa. Chakula cha nguvu nilikula pale kwa akina Zawadi mweupe, na muda huu nikapewa ofa ya kutengewa maji bafuni. Hayo ndiyo mambo sasa!

"Utakuwa umenisaidia sana, asante," nikamwambia.

Akatabasamu na kuibana midomo yake, kisha akaondoka kwenda kukamilisha zoezi hilo.

Nikacheka kidogo kwa pumzi na kutikisa kichwa, nami nikaendelea kutoa vitu vyangu. Ilikuwa wazi kwamba Ankia alivutiwa na mimi. Sidhani sana ikiwa kama angepata mpangaji mwanamke ama mzee angemtendea kwa njia kama aliyonionyeshea, lakini kwangu hilo lilikuwa jambo la kawaida sana.

Nilitoa vitu kama vyote na kupangilia vingi kabatini, nikiweka viatu vyangu pea mbili sakafuni na kisha kuvaa sendo (sandals) ngumu za kimasai miguuni. Nilikuwa nimeshavua nguo za safari na kubakiza kaushi nyeupe na kaptura ya mazoezi, nami nikaweka taulo yangu ndogo begani ili niweze kuelekea bafuni kupunguza fukuto mwilini. Kabla hata sijafungua mlango kutoka kwenye chumba hicho, ukagongwa taratibu, nami nikimjua mhusika aliye hapo nikasema tu ingia, na Ankia akausukuma na kupita ndani kiasi.

Nilipomwangalia niliona akinitazama mikononi, ikiwa wazi alipendezwa na uimara aliouona, naye akasema, "Nimeshakuwekea maji bafuni."

Nikamwambia, "Asante."

Kisha nikachukua simu yangu pamoja na chaja na kusogea alipokuwa, naye akaanza kuelekea sebuleni huku nikimfuata nyuma. Tulipofika hapo, nikamwomba aniwekee simu ipate chaji, naye akaipokea na kwenda kuichomeka kwenye moja ya matundu ya 'extension' yake.

Mimi nikaenda zangu bafuni, nikatumia dakika chache kujisafisha vizuri maana sabuni ilikuwemo mule mule, kisha nikarejea tena ndani. Nilimkuta mwanamke huyo akiwa amekaa sofani tu, akiikunjia miguu yake kwa pamoja huku akiwa makini kutazama tamthilia ya Ottoman.

Sikumsemesha na kwenda tu chumbani, nami nikajikausha maji, nikajioaka mafuta mazuri ya mwili na kutengeneza nywele vizuri, kisha nikaenda sebuleni tena huku sasa nikiwa nimebadili mavazi kwa kuvalia T-shirt ya njano yenye mikono mifupi pamoja na bukta ya mazoezi.

Nikamtazama mwanamke huyo. Aliniangalia pia upesi na kutabasamu kwa mbali, kisha akasimama na kusema angekwenda kuniwekea chakula. Lakini nikamzuia na kumwambia nilishiba, hivyo labda tu anipatie maji ya kunywa. Akatii kwa kuyafata na kuniletea, kisha akakaa tena huku mimi nikiyashusha kooni taratibu.

Angalau maji ya kunywa aliyachemsha, ingawa bado yalikuwa ni ya chumvi na mimi sikupendelea maji ya chumvi, lakini nikayanywa yote na kumtazama tena. Alikuwa amekaa kama vile ameshika tama, yaani akisikiliza kwa makini tatsiri za kiswahili kwenye tamthilia ile, nami nikamsemesha hatimaye.

Tulianza kwa kuiongelea Ottoman, kisha kuhusu kilichofanya nichelewe kufika huku hadi kuingia kwa jirani yake, na mambo ya mitaa iliyozunguka eneo lote la Mzinga na tabia za watu, na nilijitahidi kufanya maongezi yaburudishe kwa kumchekesha kwa utani wa hapa na pale. Hatukuwa tumezungumza kuhusu maisha yetu ya kibinafsi, na ni kitu kilichofaa kwa mwanzo wa kujuana.

Alikuwa ana nia ya kunichomea dawa za mbu chumbani lakini zilikuwa zimemwishia, na akasema kwa muda huo tayari duka la pale nje lingekuwa limefungwa hivyo asingeweza kwenda kununua zingine maana maduka mengine yalikuwa mbele huko. Nikamwambia aondoe shaka, ningelala ndani ya neti tu, kama yeye vilevile.

Tamthilia ya Ottoman ilipokwisha, akanyanyuka na kusema yeye pia angekwenda kujimwagia maji kabla ya kulala, kisha akaenda chumbani kwake. Hazikupita dakika nyingi sana naye akawa ametoka huko, nami nikamwangalia jinsi alivyokuwa. Alivaa khanga moja kutokea kifuani mpaka kufikia magotini, na mwili wake tepetepe ulinyumbulika kwa makusudi mengi sana alipopiga hatua kuja upande wangu ili atoke mlangoni na kwenda bafuni.

Nikatazama tu runinga na kujitahidi kuweka utulivu, lakini tumawazo twingi twa kihuni tulikuwa tunanisumbua-sumbua sana kichwani. Akanipita na kutoka nje, nami nikajikaza tu nisicheke maana niifurahia sana mchezo wa hapa. Ile kitu unayojua inaweza kutokea lakini unajifanya kama huelewi somo, ndiyo iliyokuwa kitu yangu. Kweli nikaendelea kujifanya kama somo halieleweki kwa kutulia tu.

Simu yangu ikaanza kuita, nami nikaichukua na kuona niibebe tu ili nikazungumzie chumbani; aliyekuwa ananipigia alistahili maongezi ya faragha zaidi, yaani mama yangu. Nilipenda sana kuonngea naye nikiwa sehemu tulivu. Nilitumia dakika nyingi kuzungumza naye kiasi kwamba sikutambua kama muda ulisonga mpaka nilipoona taa za sebuleni zikizimwa, nami nikaelewa bila shaka Ankia alikuwa amesharudi na sasa alijiandaa kwenda kulala.

Nikamaliza maongezi ya kwenye simu na kuamua kutoka chumbani ili niifate chaja maana nilihitaji kuiweka simu ipigwe moto usiku mzima mpaka majogoo. Taa ya upande wa jikoni bado iliwaka kwa hiyo ndani hapo kuelekea sebule palikuwa na mwanga hafifu ulioruhusu kuona mambo vizuri, na ndiyo nilipofika sebuleni tu nikasimama ghafla baada ya kumkuta Ankia akiwa bado hapo.

Nilifikiri labda tayari angekuwa chumbani kwake, lakini haikuwa hivyo. Sasa nilithibitisha kwamba alikuwa na nywele za kusukwa kichwani maana hakuwa na kilemba tena. Alikuwa amesimama usawa wa TV yake akionekana kuifunika kwa kitambaa.

Kwa sababu TV ilikuwa juu kiasi, alinyoosha mikono yake kuiwekea kitambaa hicho huku akiinyanyua nyayo zake za miguu, na hivyo khanga fupi yenye kulowana aliyokuwa amevalia iliyaacha mapaja yake wazi na kulichora umbo lote la nyuma kwa njia iliyoamsha hisia zangu ghafla, na kwa nguvu mno.

Inaonekana hakujua niko nyuma yake, ama labda alijua, lakini hakugeuka upesi, na alipomaliza tu kuifunika TV yake, bila kugeuka akawa ameifungua khanga yake ili airekebishe vizuri na kuifunga tena mwilini, na alipokuwa tu ndiyo anafanya kuirudisha akawa amegeuka.

Kuna kitu chenye kusisimua kiliruka ndani yangu baada ya kuuona mwili wake wa mbele kwa kifupi sana, naye akaonekana kushtuka kiasi baada ya kukuta nimesimama hapo!

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
Daaaah Leo nimerudia kusoma sehemu ya 1 sio Kwa kucheka huku [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwann lakini 😂
Mtoto na shape lake kabsa
Ila JC buana, kwahyo kapiga mtu na dada ake
Eti jamani😃😃 halafu hamkatai mtu, alijitahidi kwa Mariam tu na yeye ilibaki kidogo amkule angekoma angekua kala mdogo ake sijui angemuangaliaje baada ya kujua wameshare baba
 
MIMI NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Nilihitaji muda zaidi kumeza haya yote yaliyokuwa yametokea leo, na niliona kazi hazingefanyika kwa utimilifu wote hata kidogo. Nikiwa na Miryam hospitalini bado, nikaamua kwenda kuongea na daktari wetu mkuu kumwambia kwamba nilikuwa nimefika mimi mwenyewe hapo kumpa taarifa kwamba nisingeweza kuwepo kazini leo, kwa sababu ya safari ya dharura iliyonihitaji kuondoka jijini haraka sana. Yaani ilinibidi nidanganye tu, na utaratibu mwingine wa kufidishia muda ambao nisingekuwepo ungetakiwa uwekwe.

Nilionwa kuwa muhimu kwenye kitengo changu na masuala mengine, lakini siyo kwamba nilikuwa daktari pekee hapo. Walikuwepo wengine pia, na mimi kusema kweli nilihitaji sana kuielekeza akili yangu kwa Miryam angalau kwa muda fulani kwanza, kisha kazi zingeendelea. Mkubwa wangu akasema hiyo ingeweza kuniletea shida hata kwenye masuala ya malipo na nini, lakini nikamwambia haikuwa na tatizo kabisa; yaani hapo ndiyo nilikuwa napita tu kumtaarifu hilo, na moja kwa moja ningeelekea stendi kupanda basi. Mh?

Hakuwa na namna ila kukubaliana nami, nikiwa nimemwambia ni tatizo tu la kifamilia nje ya jiji lililonihitaji kwa uharaka, na kwa misingi hiyo akawa amenipatia kibali cha kuondoka. Ilikuwa kama shule yaani. Kwa hiyo nilipomaliza hilo, nikamrudia Miryam wangu, ndiyo, "wangu," nami nikaondoka pamoja naye tukiwa na furaha isiyopimika ukubwa yaani. Nilihitaji kutumia muda pamoja naye, na mpango ukawa kwenda kule kwangu ili tutulie kwanza na kuzungumzia mengi yaliyotokea na yaliyohitajika kufanywa kutokea hapo. Nikamwongoza kwa gari langu, naye akanifuata kwa lake.

★★

Tulifika kwangu ikiwa ni mida ya saa tano sasa, hii hii asubuhi, na sikumkuta Simba hapo maskani. Inaonekana alitoka, na hiyo kwangu ikawa ni jambo zuri kwa kuwa ningehitaji kuwa na muda wa kibinafsi zaidi na Miryam. Tulipoingia ndani, Miryam akasema kitu kama 'pamebadilika, umeongeza nini?' lakini mimi sikujali maneno yake na kumshika mkononi, kisha nikamgeuzia kwangu na kumkumbatia kwa nguvu kiasi. Nilimkumbatia kwa njia ya kushtukiza kwa hiyo hakurudisha kumbatio langu haraka, naye ndiyo akacheka kidogo kwa pumzi na kunikumbatia pia.

Nilihisi kuridhika, hisia ya mwanzo tu maana ni kama vile yale yote mabaya yaliyotokea baina yetu yalifutika ndani ya sekunde moja tu, na matazamio yakawa mengi kutokea hapo. Nilipitisha kama dakika mbili nzima nikiendelea kumshikilia namna hiyo hiyo, nikimbembeleza taratibu kwa kuyumbisha miili yetu, na yeye akinibana kwake hata zaidi kufurahia upendo wangu. Haukuwahi kutoweka. Hilo nililijua. Na kama maneno ya Simba jana, ikiwa Miryam alikuwa ni matatizo tu kwangu, basi niliamua kuyachagua matatizo haya kwa moyo mkunjufu. Sikujali kingine tena. Suala la sisi kuwa ndugu lilifutika, na sasa ingekuwa ni kurudisha kile tulichodhani kilipotea jumla baina yetu.

Miryam akaguna kidogo na kusema, "I missed you so much..."

Nikamwambia, "Me hata kidogo."

"Mhmhmhm... huna lolote..."

"Dah! Naweza kukushikilia hivi hivi mpaka usiku uingie," nikasema hivyo.

"Ningependa sana. Sema mwenzio nawahi kuchoka kweli sa'hivi," akaniambia.

Nikamwachia taratibu na kumwangalia usoni, miili yetu bado ikiwa imegandana, nami nikamwambia, "Bado hata mwezi haujaisha, tayari ushaanza mideko? Eti 'nachoka sana sa'hivi...'"

Miryam akatabasamu na kukilaza kichwa chake kifuani kwangu.

"Ahah... mahusiano yetu yanahitaji check-up, siyo kwa hivi visa na mikasa aisee," nikamwambia.

Akaniangalia usoni tena na kusema, "Na me ndiyo nimechangia sana kufanya iwe hivyo. I'm sorry."

Nikazilaza-laza nywele zake na kumwambia, "Usijali. Na... me pia niombe samahani. Nilikutia pressure sana."

Miryam akatikisa kichwa kukubali samahani yangu.

"Nitakuwa nimepitwa na mengi kwa hizo siku eh?" nikamuuliza hivyo.

Akatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Hamna. Labda wewe ahah..."

"Ahahah... yeah. Vingi vimetokea," nikamwambia.

"Nisimulie basi," akasema hivyo kwa sauti ya chini.

"Sawa."

Nikaonyesha nia ya kumtaka akae ili tuongee vizuri, naye akalisogelea sofa na kuketi hapo, mimi nikikaa karibu naye pia.

"Kuna mambo mengi yaani... nakosa kujua hata nianze na lipi," nikamwambia hivyo.

"Niambie chochote mpenzi wangu. Niko tayari kukusikiliza," Miryam akasema hivyo kwa hisia.

Nikatabasamu kiasi, nikiwa nimekishika kiganja chake, nami nikamwambia, "Unajua... nimeshakutana na Evelyn."

Akakunja uso kimaswali na kuuliza, "Evelyn ndiyo nani?"

Nikatabasamu na kusema, "Mwanangu."

"Ahaa... kwa Stella?"

"Ndiyo. Ulifikiri naongelea demu, ama?"

"Ahah... wala."

"Mmm?"

"Mmm. Mie siyo wa namna hiyo kabisa," akasema hivyo.

"Mhm, haya bana."

"Umekutana naye lini?" akauliza.

"Kama mwezi unaenda kuisha. Yaani... ni siku chache tu kabla sijaja pale home kwako, mpaka yale kutokea na nini..."

"Eeh..."

"Yeah, ndiyo nilimwona kwa mara ya kwanza. Tulikutana restaurant," nikamfahamisha.

"Okay. Yuko poa?" akauliza.

"Ndiyo, kapo fine sana."

"Nionyeshe picha yake basi..." Miryam akaniomba.

Nikatoa simu na kuweka picha ya Evelyn, niliyopiga siku ile tumekwenda kutembea, naye Miryam akatabasamu.

"Hee! Mnafanana!" akasema hivyo.

Nikacheka kidogo kwa pumzi.

"Ulihisije ulipokutana naye?" akauliza.

Nikaweka simu pembeni na kumwambia, "Vizuri mno. Mwanzoni nilikuwa sijui hata namna ya ku-handle hiyo hali, ila mtoto alifanya iwe rahisi sana kuzoea..."

"Alikuzoea haraka?"

"Yaani ni hiyo hiyo tu mara ya kwanza tumekutana and she was all over me! Huwezi amini, ilikuwa kama vile ananijua vizuri kuliko hata navyojijua..."

"Mm? Lakini Jayden..."

"Ahahah... siyo siri, nilipenda sana hiyo hali. Ndiyo nikagundua ni namna gani nilikosa mengi mno kwa kujiweka kando muda mrefu," nikaongea kwa hisia.

"Naona Stella alifanya kazi kubwa kumwambia mwanao kukuhusu," Miryam akasema hivyo.

Nikabaki kimya na kumwangalia kwa utulivu.

"Ni mama mzuri. Wazazi wengine walio single huwa hawajisumbui kuwaambia watoto juu ya wazazi wao, ama wanawafundisha kuwachukia," akasema hayo.

"Yeah, siku hizi Stella kapunguza ujeuri. Yuko tofauti na nilivyomwelewa zamani," nikakiri hilo.

"Kwa hiyo ni mara moja tu hiyo ndiyo ulikutana na mwanao?" akauliza.

"Hapana. Tangu hiyo siku, naweza kusema karibia mara tatu kila wiki. Yaani mara chache sana hatujaonana, hasa shauri ya kazi, ahah... anajua kulalamika huyo asiponiona!"

"Eeh... daddy yuko wapi?"

"We! Akianza timbwili kisa hajaniona mpaka mama yake anachoka, inabidi nikache kazi nimpigie video call, ama nitimue kwenda kumwona hahahah..." nikaongea kwa furaha.

"Kwake Stella?" Miryam akauliza.

"Yeah. Basi akiniona eti anaanza maringo, halafu na me nikianza maringo ananibembeleza eti nimsamehe. Ana akili fulani hivi yaani... pamoja na kwamba ni miaka mitatu kasoro lakini... sijui hata nielezeeje..."

"Ana kile kitu nilichokwambia unacho pia," Miryam akasema.

"Kitu gani?"

"Inaonekana ana sense nzuri ya direc...."

"Good sense of direction, yes! Umepatia. Hivyo hivyo yaani. Kama baba yake hapa," nikajitutumua.

Miryam akatabasamu na kusema, "Haya bwana. Napenda sana unavyofurahi. Kumpata mwanao naona imekuridhisha sana. Nitapenda kukutana naye pia."

Nikakiunganisha kiganja changu kwenye chake, nami nikamwambia, "Kumjua Evelyn kumenibadilisha sana. Yaani... nimekuwa tofauti kimtazamo, Mimi. Natamani zaidi kuwajibika kama baba, ndiyo sababu nina hamu kubwa zaidi na zaidi kwamba unamleta kijacho wetu wa kwanza."

Miryam akacheka kidogo kwa kufumba mdomo.

"Seriously yaani, I'm so happy," nikamwambia kwa hisia.

"Nafarijika kujua hilo. Asante Jayden," Miryam akasema hivyo kwa hisia.

Nikatikisa kichwa kwa uthamini pia, nami nikamwambia, "Tuongelee upande wako pia."

Miryam akasema, "Kuhusu..."

"Nilikuwa najaribu tu kufanya hali iwe na sss... wepesi kidogo ahah... ila hiki kitu bado kinazunguka sana akilini," nikamwambia hivyo.

"Kitu gani?" akauliza.

"Kuhusu ule usiku. Huwa haiko mbali na fikira zangu kila nikikumbuka namna ulivyoongea, yaani... najua mambo mengi yalichangia, ila... bado nilikuwa... nahisi kama vile haikuwa akili yako, au... kama kuna la ziada lililofanya mpaka ukaniambia haunihitaji tena, na utampenda mtu mwingine..." nikaongea kwa upole.

"Naelewa, Jayden. Najua ulishangaa, na uliumia sana mimi kukwambia vile... hata mimi ni kitu kilichoniumiza pia," Miryam akasema hivyo na kuangalia chini.

Nikaendelea kumtazama kwa hisia.

Akasema, "Niliyoyasema ule usiku yalikuja vibaya si kwa sababu tu ya mambo yaliyotupata, yaani... nilitaka tu kila kitu ambacho nilihisi kingeendelea kuniumiza, kiache... na... labda..."

"Kuniondoa mimi maishani mwako ndiyo kungekuondolea hayo maumivu?" nikamkatisha.

Akapindisha shingo kiasi huku akiniangalia kwa hisia, naye akasema, "Ndiyo. Ni.. nilifikiri hivyo."

Nikaangalia pembeni.

"Lakini haikutoka moyoni. Siyo baada ya siku, wala wiki... ni baada tu ya wewe kuondoka pale ule ule usiku nilibaki na majuto makubwa sana moyoni... lakini... nikawa sina namna ya kufanya mambo yarudi kuwa sawa tena. Hakuna kitu chochote kilichoweza kunifanya niache kukupenda. Sema..." akaishia hapo.

Nikiwa namwangalia sasa, nikamuuliza, "Ila?"

Akabaki kunitazama kwa hisia.

"Niambie. Nataka kujua," nikamsihi kwa upole.

Akaangalia chini kwa ufupi na kusema, "Nilikuwa tu nimeumia."

"Uliumizwa na nini kingine?" nikamuuliza.

Akaniangalia usoni kwa hisia.

"Ni mimi?" nikamuuliza tena.

Akaangalia pembeni.

Nikakikaza kiganja chake na kusema, "Niambie Miryam. Nilikosea wapi? Kwa sababu uko sahihi, nilijua kabisa kuna kitu kingine kilikuwa kinakusumbua, lakini... labda kilikuwa kizito kusema. Ila, sasa hivi unaweza kuniambia. Ikiwa ni jambo ambalo naweza kurekebisha...."

"Hapana, Jayden... hauhitaji kurekebisha lolote," akaniambia kwa upole.

"Basi nakuomba uniambie tu. Nilifanya nini kilichokufanya... usiache kunipenda, lakini upoteze imani?" nikamuuliza hivyo.

Akatulia kwanza, kisha akasema, "Ni Mamu."

Nikamwangalia kiumakini.

"Aliniambia kuhusu... kuhusu mlichofanya," akasema hivyo.

Nikafumba macho na kuinamisha uso.

"Na, siyo kwamba mlifanya, anasema... ilikuwa karibu mfanye siku hiyo, ila... ukamzuia, na..."

"Nilifanya makosa Miryam, nisamehe," nikamkatisha kwa kusema hivyo.

"Hapana, wala usi...."

"No, kiukweli haikuwa sahihi hata kidogo. Nili... nilishindwa tu kujua... njia rahisi ya kumsaidia Mamu aongoze hisia zake siku hiyo, na me nikajikuta nashindwa kuongoza zangu, yaani...."

Miryam akanishika usoni na kusema, "Jayden, usijali. Najua."

Nikamtazama kwa hisia.

"Mamu hakuniambia hayo kwa sababu ya hisia zake kwako, alikuwa tu ameogopa... tulipojua kuhusu haya ya undugu. Alijihisi vibaya kulazimisha mapenzi kwako wakati ungeweza kuwa kaka yake, lakini hayo siyo makosa yake, wala yako. Ni kitu ambacho hamna aliyeweza kuona," akaniambia hivyo.

Nikaendelea tu kumwangalia.

Akaniachia na kusema, "Na... mimi tu kusema kweli ilinichanganya. Nilianza kufikiria kuhusu jambo hilo mno, nikawaza kama ni kweli tuna undugu halafu ungekuwa umelala naye... ingekuwaje? Vitu kama hivyo, lakini siyo kwamba...."

"Miryam najua uliumizwa na tendo langu la kutoweza kujizuia haraka. Hata kama isingekuwa Mariam, najua ungeumia endapo ungetambua nimetoka na mwanamke mwingine wakati tukiwa na mahusiano," nikamwambia hivyo kwa upole.

Akaendelea kunitazama kwa hisia.

"Kwa hilo naomba unisamehe tu. Na sikuwa nimekwambia kuhusu Mamu kwa sababu... sikutaka tu kuchanganya mambo baina...."

"Naelewa Jayden, hilo halina shida. Kama nilivyokwambia, hauhitaji kurekebisha lolote, limeshapita. Sawa? Kuwa na amani mpenzi wangu," akaniambia hivyo kwa uhakikisho.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Asante."

Yeye pia akatabasamu.

Nikatazama pembeni na kushusha pumzi, kisha nikamwambia, "Hivi vitu vimesababisha mambo mengi ku-change ndani ya muda mfupi sana."

Miryam akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Yeah. Mambo mengi."

"Nilidhani... baada ya huo usiku nikadhani kweli ulimaanisha ulichosema, kwa hiyo..." nikaishia hapo.

Nikamwangalia na kukuta ananitazama kwa njia yenye subira.

Nikashusha pumzi na kusema, "Nimeanza kutoka na Adelina, Miryam."

Miryam akaangalia chini kwa ufupi.

"Ilikuwa haraka, I know, yaani... nilipondeka sana moyoni, nikajua tayari una kitu na Festo, sasa... Adelina akawa sehemu kubwa ya comfort kwangu. Siyo kusema hisia zote kwako ziliondoka... ila..."

"Na yeye ukampenda," Miryam akasema hivyo bila kunitazama.

Nikamwambia, "Siyo kitu kilichokaza mizizi, Mimi. Nitaongea naye, nita..."

"Ni makosa yangu hata hivyo..."

"... zungumza... naam?" nikaitikia kauli yake.

Akaniangalia usoni tena na kuniambia, "Sitalaumu. Ni makosa yangu mpaka ukafikia hiyo hatua."

Nikatazama pembeni kwa kutatizika.

"Heey, usijali. Naelewa. Sema... kwa jinsi mambo yalivyo sasa hivi, sijui kama Adelina ataweza kuelewa ukimwambia..." akaishia hapo.

Nikasema, "Nitaongea naye. La muhimu ni kuongea naye. Nitarekebisha hilo."

Akatikisa kichwa kukubali.

"Ni hivyo hivyo na kwako pia I suppose," nikamwambia hivyo.

Akaniangalia kwa njia ya kutoelewa.

"Bila shaka utahitaji kuongea na Festo wako... maana sioni ya kwetu yakisonga bila upande wako kuwa clear pia," nikamwambia.

Miryam akatabasamu kiasi na kusema, "Hapana Jayden. Mimi sikuwahi kutoka na Festo."

Nikakunja uso kimaswali.

"Alirudi tu kutoka huko kwenye biashara zake, akawa amenitafuta, kirafiki tu. Hakuna chochote baina yetu zaidi ya urafiki..." akaniambia.

"Seriously?"

"Ndiyo."

"Urafiki... yaani, kuna usiku nilikuona unashuka kwenye gari lake, kabla hata hatujagombana yaani, tena ulishukia pale Mzinga barabarani, ukachukua boda, ndo' ukaenda nyumbani. Hiyo ilikuwa nini?" nikamuuliza.

"Ooh, hiyo siku... subiri, ulikuwa wapi?"

"Nilikuwa hayo hayo maeneo, hiyo siku nimekuja kukuona tuongee ndo' sikukukuta kwako," nikamwambia.

"Sawa. Yaani... ndiyo alikuwa amerudi, akanitafuta, akaomba tukutane. Alitaka tu tufurahie kinywaji, na me bado nilikuwa na stress, yaani jana yake ndiyo tumetoka kwenu eh... na yale mambo yote, kwa hiyo nikaenda tu kuwa kwenye company mpya. Basi," akanifahamisha.

"Ndiyo alikuwa ameanza kujisogeza eh? Ili arudishe romance?"

"Ahh, Jayden hakukuwahi kuwa na kitu kama romance baina yangu mimi na Festo. Amekuwa rafiki mzuri tu kwangu... ame... amenisaidia kwa vitu fulani, ushauri... hata ule usiku umemkuta pale nyumbani ni kwamba alikuja kuwasalimia tu akina mama. Hakuna kingine baina yetu, ni rafiki tu," akasisitiza.

Nikamuuliza, "Na jana?"

Miryam akanikazia macho.

"Namaanisha... mlikuwa wote club. Hiyo ni...."

"Ilikuwa kwa sababu yako," akanikatiza.

"Kwamba?"

"Nilishindwa kujizuia tena. Nilitaka kukuona, nikwambie kuhusu hali yangu, lakini sikujua namna gani ya kushika simu... nikupigie. Nilijua hata usingepokea. Lakini Festo ndiyo akanisaidia. Alinishauri ni vyema nikikutana na wewe ana kwa ana, ndiyo tuongee. Alikuwa na njia fulani aliniambia, ya kuweza kumtrack mtu ili kumpata, na akanitia moyo nikutafute kwa njia hiyo ili niku-surprise... halafu ndiyo tuongee..." akaeleza.

Nikaendelea kumwangalia kwa umakini.

"Jana... alikuja nyumbani. Akaniambia tu tutoke mara moja, na ilikuwa kama anitembeze kidogo. Tena alikuwa amesema angenionyesha kwa rafiki yake wa muhimu, lakini bila me kutarajia, akanileta mpaka pale tulipowakuta we' na wenzako. Akaniambia uko humo, na akanitia moyo twende nikuone... tuyajenge," akaeleza.

Mh? Nilishindwa kuamini. Huyo alikuwa ni Festo aliyefanya hayo yote?

"Na tena hata hapo sikuwa na uhakika ingekuwaje... bado masuala yetu, na ya ma' mkubwa na mama yako, yaani... pamoja na yote nilitaka tu kukuona pia. Niliku-miss mno, na Festo ndiyo alinipa ujasiri hadi nikaweza kukufata pale. Nilikuwa na wasiwasi mwingi," akaniambia.

Nilibaki nimetulia tu, nikiangalia pembeni kwa umakini.

"Kwa hiyo usiwaze kuhusu huyo mwanaume. Ni rafiki tu, na ukimjua vizuri, we' mwenyewe unaweza ukajenga naye...."

"Hapana, Miryam. Hapana," nikamkatisha.

Akabaki akiniangalia kwa hisia makini.

"Siyo... Festo siyo mtu unayemdhania, Mimi. Si mtu mzuri," hatimaye nikamwambia.

Alichanganywa kiasi, naye akauliza, "Kwa nini useme hivyo?"

"Festo ni mtu aliyehusika na... ah, yaani hata sijui nikwambieje..." nikasema hivyo na kutulia kidogo.

Miryam hakuacha kunitazama kwa subira.

Nikamwambia, "Unakumbuka kipindi kile nimefanya kazi na yule askari Ramadhan kuwakamata wale wauzaji wa madawa ya kulevya? Yule mwanamke, Bertha, ambaye alimuua mdogo wake Adelina..."

Miryam akatikisa kichwa kukubali.

"Sasa Festo... ndiyo alikuwa partner wake," nikamwambia.

Miryam akakaza macho kwa njia ya kushangazwa na maneno yangu.

"Tena, alikuwa kama boss wao. Yaani yeye ndiyo alitengeneza njia za wao kuyapata hayo madawa na kuyasambaza, na hata walikuwa na kundi la watu waliokaa kama... kama majambazi, walikuwa wanafanya kila aina ya unyama Mimi. Hata kuua watu," nikamfahamisha.

Miryam akaangalia pembeni, akionekana kushangaa kweli.

"Festo aliwageuka wenziye mwishoni hapo, wakati tunakaribia kuwakamata, eti akawa amefanya kama dili na maaskari kuwafichua wenziye, halafu akawa kama amelipa fidia sijui... ili yeye asiwekwe hatiani nao. Yaani, mambo yalienda faster sana, me mwenyewe nilishangaa sana alipokuja kuonekana yuko upande wa mazuri, wakati mabaya mengi aliyofanya niliyaona. Kuna siku alimpiga risasi tatu mwanaume mmoja, mbele ya macho yangu!"

Miryam akaniangalia kwa umakini.

"Na sijui yapi zaidi amefanya ili kuhakikisha yuko huru mpaka sasa. Lakini sidhani yako kwa njia nzuri. Hiyo safari yake kuondoka nadhani ilikuwa kama kukimbia kwa muda mfupi, hali itulie, na sasa hivi Bertha amepoteza maisha ni kama Festo hana tati..."

"Huyo Bertha alikufa?" akanikatiza kwa kuuliza hivyo.

"Ndiyo Mimi. Bertha alipatwa na ajali kabla hawajampeleka magereza. Festo alikuwa anadai kwamba, alitaka kubadilika, kwa sababu anakupenda... kwa hiyo aliachana na hayo yote ili aweze kuwa mtu ambaye wewe utamtaka. Miryam..."

Mwanamke akabaki kuniangalia kwa mkazo.

"Festo ni muuaji. Anaweza akasema sa'hivi ameacha, lakini kwa huo muda mfupi nilioshiriki meza pamoja naye, nimemjua. Nimemsikiliza. Nimemwelewa. Siyo mtu wa kuachia mambo kirahisi. Maaskari wanaweza wakawa labda wanamwangalia, wakaona ah sa'hivi yuko safi, lakini nia zake unakuta hazijabadilika. Na ninajua... nia yake ya kukupata wewe bado iko pale pale," nikaongea kwa njia yenye mkazo.

Miryam alionekana kuchoka. Aliishia kuniangalia tu kana kwamba bado hakuelewa chochote kati ya mambo yote niliyomwambia.

"Kwa hiyo kwa kweli... sielewi kwa wakati huu itakuwaje. Yeye kurudi namna hiyo, sidhani kama ilikuwa ghafla. Nahisi alijua kabisa kwamba me na wewe tuna mahusiano, na akajua tulipoanza kutengana. Yaani alingojea wakati mwafaka kwake ili arudi na kuingia katikati yetu, sawa? Halafu sasa ameanza kufanya mambo fulani ili kukuaminisha kwamba yuko upande wako kama rafiki. Mpaka anaangalia ninakokuwa, ili akulete kwangu, hiyo inamaanisha ana-monitor maisha yangu na yako kwa njia fulani... na lazima ziwe za gharama, na illegal. Sijui hiyo inampa faida gani, lakini nahisi anaweza kuwa anapanga kitu Miryam. Na sasa hivi tunarudiana... naanza kuona kama kuna jambo baya atalileta upande wetu," nikamweleza.

Miryam akatikisa kichwa kwa kusikitika sana, na kwa sauti ya chini akaniuliza, "Kwa nini hukuniambia haya Jayden?"

Nikafumba macho na kuinamisha uso, nami nikasema, "Mambo yalikuwa mengi sana. Sijui hata... sijui niseme sababu nini, lakini... lakini hiyo ndiyo hali halisi."

Miryam akaniangalia kwa njia yenye huzuni mno.

Nikamshika shingoni na kumwambia, "Lakini usijali, Mimi. Sitaruhusu huyu mtu atuingilie vibaya. Nitafanya kila kitu kuhakikisha penzi letu linabaki salama. Sawa?"

Miryam akaushika mkono wangu na kuniambia, "Bado sielewi. Yote uliyosema... yanaonekana kuwa impossible yaani."

"Ndiyo hivyo, najua. Lakini niamini. Festo siyo mtu wa kuweka karibu, hata asemeje kwamba amebadilika...."

"Point ya yeye kunisaidia ili nirudiane na wewe ni ipi sasa?" akanikatiza.

Nikatulia kwanza.

"Ikiwa... ana nia ya kulazimisha mapenzi kwangu, si angetumia advantage hata ya sisi kuachana kujaribu kunitongoza labda... au..." Miryam akaonekana kutatizika.

Nikabaki nikimtazama kwa hisia.

"Naogopa," akasema hivyo.

"Mimi..."

"Naogopa nisije kukupoteza Jayden..." akaniambia hivyo.

"No, usiogope. Kama nilivyokwambia, nitafanya jambo fulani kuhakikisha haji kutusumbua tena. Hasa wewe," nikamwambia hivyo.

"Yaani haonekani kabisa... ah... singefikiria angeweza kuwa mtu wa aina hiyo," Miryam akasema.

"La muhimu sasa umejua. Jitahidi tu kuweka distance, endapo kama ana mpango fulani, ni vyema uwe tayari kiakili kupingana nao. Anajaribu kuthibitisha kitu fulani naona, na labda angedhani hatutaweza kurudiana kwa sababu ya suala la undugu, ama tu jinsi nilivyokutendea jana. Lakini sasa hivi ndiyo tutapaswa kusimama imara Miryam, lolote atakalorusha upande wetu, kwa pamoja tutalishinda," nikamtia moyo namna hiyo.

Miryam akaniangalia kwa hisia sana, naye akajilaza begani kwangu kujipa ahueni kidogo.

Hapo tayari tulikuwa tumeanza kujenga kitu fulani imara baina yetu, kwa kumfungua macho Miryam juu ya hatari zingine zilizozunguka mahusiano yetu ingekuwa njia bora ya kujitahidi kuyalinda kadiri ambavyo tungesonga mbele. Na kama nilivyomwambia, ningehitajika kutafuta njia ya kumwondoa Festo kutoka maishani mwetu, mwanzo mwisho. Huyo kwetu najua angekuwa kama kupe asiyetaka kung'oka, na mimi ndiyo ningekuwa dawa yake kuhakikisha anatutoka milele.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Whatsapp +255 678 017 280
 
Back
Top Bottom