Simulizi: Mpaka Kieleweke

Simulizi: Mpaka Kieleweke

51319990_743887862662890_3304133317363761152_n.jpg
 
SEHEMU YA 18

Asubuhi tulipelekwa mahakamani nikiwa na askari yule ambaye nilimvika kesi, tukasomewa kesi ya kujaribu kutoroka nguvuni mwa polisi, tukakana shtaka..

Nilishangaa kukuta hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yetu akiwa yule bwana ambaye alinijia nyumbani akiwa amempoteza binti yake na kuniachia business card.

Baada ya kukana shtaka tukapelekwa kwenye mahabusu ya gereza kuu huku tukipangiwa kesi ile kusikilizwa tena baada ya wiki mbili.



Niliyaona maisha ya jela yakiwa magumu ndani ya siku moja tu. Nilikuwa nimekaa muda mrefu, tena chini mpaka makalio yakawa yanauma sambamba na maumivu ya kipigo cha kule polisi hali ikawa mbaya. Nilijiona wazi wazi kuwa siyawezi maisha ya mule gerezani.. wiki mbili za kuwemo mule mpaka siku ya kusomwa tena kesi nilianza kuziona kama mwaka mzima.



"Abubakar Saireee, kuna mgeni wakooo" ilikuwa ni sauti ya askari ikinishtua kutoka katikati ya dimbwi kubwa la mawazo. Nikasimama na kumfuata askari yule..





Safari yangu na askari yule ikatuchukua mpaka kwenye chumba kidogo ambamo niliingia nikamkuta bwana Filbert Tago ambaye alikuwa ni hakimu na bwana ambaye alipotelewa na binti yake akiwa ananisubiri. Alikuwa amekaa juu ya kiti kimojawapo katika chumba kile chenye viti viwili na meza. Nikaenda na kukaa kwenye kiti kile kingine tukawa tukitizamana. "Nataka uniambie ukweli juu ya jambo hili" alisema bwana yule kufungulia maongezi. Nilibaki kimya nikiwaza, kama huyu bwana amenifuata mpaka huku basi ana nia ya kunisaidia kwa maana sio jambo la kawaida hakimu kumtembelea mshtakiwa, sidhani hata kama inaruhusiwa kisheria "sii sio kesi ndogo, iwapo utashindwa utafungwa miaka mingi sana. Na iko wazi kuwa utashindwa maana kuna ushahidi wa kutosha kuwa ulitoroka" aliongeza bwana yule nami nikamueleza kuwa nilitoroka kichawi, jambo ambalo aliliamini mara moja kinyume na mategemeo yangu.

"Sikia, mimi najua kuwa unayo mbinu ya kumpata mkeo. Unaonaje kama nitakusaidia ili na wewe unisaidie kumkumbuka binti yangu wakati wa kumsaidia mkeo?". Hii ni fursa pekee ya kuharakisha zoezi la kumpata mke wangu ambaye anakabiliwa na mambo mawili mbele yake ambayo mpaka sasa sijui lipi litampata au limekwishampata, kuna uwezekano wa kuolewa Magugi lakini pia nilielezwa juu ya kufa kwake baada ya kijifungua. "Sina muda wa kutosha hapa" niligutushwa na sauti ya bwana Tago kutoka kwenye mawazo ambamo nilipotelea humo. "Sawa bwana, tushirikiane katika hili" nilijibu kisha kumuelezea bwana yule kila kitu juu ya mipango yangu na Mnaro naye akaahidi kunisaidia ila akinitaka kuhakikisha kuwa namrudisha binti yake kutoka Muifufu, tukakubaliana ba mimi kurudi mahabusu nikiwa na matumaini mapya.

Ile siku ikaisha mahabusu ndani ya jela ile.



"Huyu mwingine analala kama vile yuko kwake, aisee amkaaa" nilisikia mtu akizungumza huku akinitikisa kuniamsha. Nikaamka na kukutana na bwana mmoja mkubwa sana wa umbo. "Twende ukafanye kazi kumekucha" alisema bwana yule akinikabidhi fagio nami nikatii haraka kwakuwa sikutaka kujenga chuki ndani ya mahabusu ile kuhofia kuwa na maisha magumu zaidi. Nikaongozana na bwana yule hadi kwenye eneo la vyoo akanitaka kufanya usafi humo. Nilichungilia ndani ya vyoo vile na kwakweli hali ilikuwa ikitisha. Kulikuwa ni kuchafu mno, sidhani kama vyoo vile viliwahi kusafishwa. Kinyesi kilikuwa juu juu kikielea juu ya maji ambayo sikujua yametoka wapi ndani ya vyoo vile.

Nikawaza kubishia kazi ile, ila nilipomuangalia bwana yule ambaye inaelekea alikuwa kiongozi ndani ya mahabusu nilimuona fika kuwa amejiandaa kukabiliana nami iwapo nitakataa kazi ile.

Nikaamua kuwa mpole, nikainama na kuanza kukunja suruali yangu ambayo kama ningeingia bila kuikunja bila shaka ingecheza na kinyesi.

Wakati nikiendelea kukuja suruali yangu mara nikasikia sauti ikiita "Jafariii, namuomba huyo jamaa" nikageuka na kumuona askari wa magereza akimuagiza bwana yule.

"Kamsikilize afande kwanza ila mkimalizana tu urudi haraka, kazi inakungoja hii" alisema bwana yule nami nikaondoka na kumfuata askari yule tukaongozana "una bahati mbaya sana bwana" alisema askari yule nikashtuka na kujiuliza nini kilikuwa kinakwenda kunipata tena "yani umekuja jana tu leo unaondoka? Bado hujajifunza maisha wewe, ilipaswa ukae angalau miezi miwili bwana" alisema askari yule kiutani huku akicheka.

Nivuta pumzi nyingi nikaiachia yote. Nikamshukuru mungu kimoyomoyo kwa wema ambao amenitendeat.

Tuaenda mpaka mapokezi ya gereza lile ambapo nilielezwa kuwa wamepokea hati ya dhamana kutoka mahakamani hivyo natakiwa kwenda nyumbani lakini nihudhurie mahakamani tarehe ambayo ilipangwa kesi yetu isikilizwe tena.

Nikapewa vitu vyangu ambavyo walinihifadhia na kwenda nyumbani.

Nilifika nyumbani na kukimbilia bafuni kabla ya chochote, mwili wangu nilikuwa nauona kama wa ambae alilala jalalani kutokana na mazingira machafu ya ndani ya magereza.
 
SEHEMU YA 19

Baada ya kuoga nikakaa nikijiuliza nawezaje kumpata Mnaro, nilikuwa nikimuhitaji sana lakini sikuwa nikijua namna ya kufika kwake ingawa nimeenda mara kadhaa, hii ni kutokana na yeye kuwa ananichukua kiuchawi kwenda huko kila wakati ambao alitaka twende, hivyo sikuijua njia ya kwenda huko.

"Hii ni mara ya mwisho kukufuata, wakati mwingine utakuwa unakuja mwenyewe" niliikumbuka kauli hii ya Mnaro nikajikuta nimetoa msonyo mkubwa sana.. alitegemea nitakuwa naenda mwenyewe ikiwa sipajui? Niliwaza nikijilaza kitandani na usingizi haukuwa na hiana, ukanipokea vizuri nikalala fofofo.



Niliposhituka ilikuwa ni majira ya saa saba usiku lakini Mnaro hakuwa amekuja. Nikaamua kutoka na kwenda kufanyia mazoezi ambacho alikwishanifundisha. Nikamchukua yule paka, ambaye sasa nilikuwa nimemuweka kwenye banda kubwa nyuma ya nyumba yangu ambalo lilitengenezwa kwaajili ya kufugia kuku lakini halikuwa likifanya kazi hiyo kwa wakati huu.

Nikaingia mitaani nikiwa namuendesha paka yule, nilikuwa nimejua kila kitu kuhusu namna ya kumuendesha paka yule na nilikuwa nikifurahia sana utendaji wake hasa uwezo wa kwenda umbali mrefu ndani ya muda mfupi tu.



Nikawa nimeenda mbali zaidi ambapo hata sikuwahi kufika kabla nikaona kwa mbali nyuma yangu kuna mtu anakuja uelekeo niliopo akiendesha mnyama ambaye kwa umbali ule sikuweza kumtambua. Nikaamua kujificha nyuma ya mti mkubwa wa mbuyu ambao niliuona mbele yangu ili kumpisha mtu huyo apite kwamaana sikujua kama alikuwa ni mwema kwangu ama laah!..

Nikiwa nachungulia nyuma ya mbuyu ule niliona mtu yule akija juu ya mnyama ambaye sasa niligundua kuwa alikuwa ni paka kama huyu wakwangu akija mpaka mbele ya mbuyu ule kisha akasimama, tukawa tumetenganishwa na mbuyu tu, mimi nikiwa nyuma na yeye akiwa mbele. Nikapatwa na uoga kidogo nikijiuliza mtu yule alikuwa na lengo gani kusimama pale? Au atakuwa ameniona? "Umejificha lakini uoga unakuumbua, unapumua kwanguvu mpaka nakusikia" ilisikika ikisema sauti ya mtu yule nyuma ya mbuyu nikagundua mara moja kuwa alikuwa MNARO.

Nikatoka nyuma nyumauyu mbuyuanikiwarahafurahao sikujusikujuakkwa maana nilkwawa nikasirishwailitoka mnharamno na mwenendo wa Mnaro na kutamani angalau ningekuwa na uwezo wa kumchapa hata kibao tutakapo onana

"Ulikuwa wapi siku zote hizi aisee? Nimekusubiri sanaaa" nilisema huku nikishindwa kuzuia tabasamu la furaha.. "mimi ndo nikuulize wewe ulikua wapi? Ulikuwa unaningoja kwani tulikubaliana kuwa nitakuja?" Aliuliza Mnaro nami nikabaki kumshangaa kwa maana wakati wote aluokua anaingia chumbani kwangu bila hodi kama kwake hatukuwa tumekubaliana kama atakuja. "Nadhani mara ya mwisho kukufuata nilikwambia waziwazi kuwa ilikuwa ni mara ya mwisho kukufuata na baada ya hapo ungekuwa unakuja mwenyewe" aliongeza maelezo Mnaro. "Sasa nawezaje kuja ikiwa sipajui pa kukupata?" Niliuliza swali ambalo nililiona ni la msingi lakini Mnaro akanitizama kama ambaye naongea ujinga "leo ndo unauliza hilo swali? Nadhani ulipaswa kuuliza wakati nakwambia kuwa sitokufuata tena. Tatizo lako unaishi kwaajili ya leo tu wala hujisumbui kuiwaza kesho" alisema Mnaro nami nikajiona kweli nilikuwa "juha" nikaamua kuwa mpole.

"Nilipatwa na matatizo bwana" niliamua kubadili mada baada ya kuona lawama zangu zinanirudia mwenyewe. "Ninajua kila ambacho kilikupata. Najua ulitegemea nikusaidie lakini sipo kwaajili ya kukusafisha kila ukijichafua, huko ni kukulemaza. Kumbuka Muifufu hautomwenda na mimi" alisema Mnaro nami nikabaki bila hoja.

"Kwakuwa tumekutana nadhani tugange yaliyopo na yajayo, bora tuanze mafunzo" nilisema kumwambia Mnaro ambaye alitabasamu na kisha akajibu "sielewi kwanini huoni kama hapa tunajifunza, maisha yote ambayo unaishi toka nianze kukufundisha ni mafunzo sio kushika matunguri tu" alisema Mnaro ambaye niliona kama leo ameamua kunionesha ni jinsi gani mimi sijui kufikiria.

"Umejifunza mambo mengi sana ndani ya muda mfupi, tena kwa vitendo. Kapumzike uyafanyie kazi hayo kisha tukutane keshokutwa kwaajili ya kumalizia mafunzo" alisema Mnaro ambaye nilianza kumuona kuwa amekwishazoea hali ya mpenzi wake kuishi Muifufu huku yeye akiwa huku. Anaachaje kuzoea ndani ya miaka yote ambayo amekuwa mbali na huyo mpenzi wake, niliwaza. Ambacho hakielewi ni kuwa mimi siko tayari kuandamwa na tatizo hili kwa muda mrefu kiasi hicho.

"Tukutane keshokutwa" alisema Mnaro akianza kuonda.. "sasa nitakupataje hiyo kesho kutwa?" Niliuliza Mnaro akaniangalia akitabasamu "unaona bwana, vitendo vinafunza zaidi ya maneno. Sasa unajua kuiwazia hata keshokutwa" alisema kisha akatoa kakioo kadogo kutoka kwenye ule mkoba wake wa ngozi na kunikabidhi.

"Sema na hicho kioo ukinihitaji nacho kitanileta" alisema Mnaro na kupotelea mbali na yule paka wake akiniacha nikikitalii kioo kile ambacho kilikuwa chakavu kikiwa kimefungwa na mipira kukizunguka.
 
SEHEMU YA 20



Nikaondoka kuelekea nyumbani kwa usafiri wa paka yule ambaye hakuchukua muda kinifikisha mtaani kwetu lakini nilisita nikaangalia kwa mbali na kuona nnje ya nyumba yangu kukiwa na kikundi cha watu wakiwa busy kufanya shughuli ambazo sikuzielewa.

Nika shuka juu ya paka yule huku nikimnong`oneza kuwa nimkute hapo ninapomuacha.

Nikasogea karibu na nyumbani kwa mwendo wa kuchuchumaa kukwepa watu wale wasinione. Nikafika karibu kabisa mpaka nikaweza kuwaona watu wale.

Nimgundua mmoj wa watu wale ambaye ndiye aliyeonekana kuongoza kundi lile, alikuwa ni mwanamke yule ambaye alikuja kuniwangia nikamkimbiza na kukimbilia kwa wachawi wenzake..









Niliwatazama kwa muda watu wale ambao walikuwa wachawi ambao bila shaka walikuja kupambana na mimi baada ya kujenga ugomvi na mmoja wa wachawi wa kundi lile...

Wachawi wale waliendelea kuwapo pale kwa muda huku wakiihama eneo kila baada ya muda fulani, waliendelea kufanya hivyo kwa muda mpaka wakiizunguka nyumba mpaka kurudi pale ambapo walianzia. Wakatulia hapo na kuanza kuzungumza lakini sikuweza kusikia wanaongea nini, nikaamua kusogea zaidi mpaka sehemu ambayo niliweza kusikia ambacho wanaongea. "Tumeshajikinga vizuri, kama akitushinda tutakimbi nnje ambako hatoweza kutoka,zindiko tulilofanya litamzuia" alikuwa akielezea mchawi yule huku wengine wakimsikiliza kwa makini..

Wachawi wale walikuwa ni kundi lisilopungua watu kama kumi na mbili, kwanini wanafikiria kuzidiwa na mimi?, nilijiuliza na kupata jibu kuwa walikuwa ni waoga na hivyo hawana uwezo wa kunidhuru. Nikaamua kutoka pale mafichoni na kuwafuata wachawi wale pale walipo.

Wachawi wale waliponiona wote wakakimbilia kwenye ukuta wa nyumba ambapo niligudua walikuwa wamechora mstari chini mduara kuizunguka nyumba hivyo wao na nyumba walikuwa ndani duara hilo la kuchora huku mimi nikiwa nnje ya duara hilo.

Nikazidi kusogea lakini wakaanza kurusha vitu kama vitenesi ambavyo nilijaribu kuvikwepa lakini vingine vikanilenga, nikashangaa kuona vile ambavyo vilinilenga havikuwa na maumivu yoyote hivyo nikaamua kuacha vinipige mimi nikisonga na safari ya kuwafuata, jambo ambalo lilionekana kuwashangaza sana.

"hebu acheni ujinga! ondokeni haraka kabla sijavunja mtu mguu" nilichimba mkwara baada ya kufika na kusimama mbele ya mstari ambao waliuchora kuzunguka nyumba nikihofia kuuvuka kwakuwa nilikuwa nikijua kuwa walikuwa wameuchora kujikinga na mimi na sikujua madhara ya kuuvuka.

"kama unataka kutuvunja miguu we tuvunje tu, hakuna ambaye anaondoka hapa" aliongea yule mwanamke mchawi, nadhani alikuwa anajaribu kunishawishi nivuke mstari ule. Nikaamua kujita ujasiri na kuvuka mstari ule ingawa nilikuwa na hofu kidogo. nikajikuta ndani ya mstari ule bila kudhurika na chochote, wachawi wale wakaanza kukimbia kila mmoja na uelekeo wake! lakini nilifanikiwa kumkamata ambaye nilimkusudia, alikuwa ni yule mwanamke ambaye bila shake ndiye chanzo cha ujio wa wachawi wote wale. Mwanamke yule alifurukuta akipambana kujitoa mikononi mwangu lakini nilikuwa kama ambaye nimekamata panzi, hakuwa na uwezo wa kutoroka mikononi mwangu. Akawa analia akiomba nimuachie lakini nilikuwa kama simsikii "kaka naomba unisamehe, sirudi tena haki ya mungu" alijitetea mwanamke yule lakini sikujali maneno yake, nikambeba kwa mkono mmoja nikimbana kwapani kama ambavyo kuku hubebwa nikawa natembea naye kuondoka eneo lile la nyumbani kwangu.

Nikaenda moja kwa moja mpaka nilipouacha usafiri wangu (paka) nikawa napanda juu ya paka yule nikiwa nimembeba yule mwanamke ambaye alizidi kupambana, hakutaka kipanda juu ya paka yule. Baada ya kunikwamisha mara mbili nilizaba kofi zito la uso akazimia papohapo nami nikapanda juu ya paka yule na nikiwa na mwanamke yule, tukaanza safari ambayo sikuwa hata nikiijua. Nilikuwa nikifanya matendo yote kama ambaye ninaongozwa na sauti fulani ndani ya ubongo wangu nami nikawa nikitii bila kuhoji.

Safari ikaenda mpaka kwenye kijumba fulani kidogo na cha kizani kwenye eneo ambalo sikulijua kabla. Baad ya kusimama kwa sekunde kama 10 akatoka Mnaro ndani ya nyumba ile akionekana mwenye furaha sana.

"Sasa safari ya Muifufu imeiva" alisema Mnaro katika hali ya tabasamu huku akinipokea mwanamke yule ambaye nilikuwa nimembeba mapajani juu ya paka yule.

"Kwa muda mrefu nimejaribu kukutumia kama silaha yangu ila ilishindikana kwakuwa ulikuwa na hofu hivyo hukuweza kufanya kama ambavyo nilikuwa nakuagiza, ila sasa umeiva" alisema Mnaro lakini sikumuelewa vyema, hivyo nikauliza "una maana gani?" Akawa amempokea mwanamke yule tukawa tumeongozana kuingia kwenye kajumba kale "huwezi kupambana ndani ya Muifufu kama mimi sitokuwa nyuma yako, lazima nikutumie kama silaha yangu kwakuwa wewe huna mbinu za kutosha" alisema Mnaro, tukawa tumefika ndani tukakaa huku akimlaza chini yule mwanamke.

"Nimekuwa nikijaribu kuunganisha ubongo wangu na wako ili uweze kufanya kama ambavyo ningefanya mimi lakini uoga wako umekuwa ukinikwamisha, mfano nilifanikiwa kukuwezesha kumkimbiza huyu mpuuzi mpaka kule shule na nilikusudia kuwaadhibu wachawi wote waliokuwepo kule lakini uoga wako ulipelekea kushindwa kukuongoza zaidi, ukarudi" alizidi kutoa maelezo Mnaro, nikapata jibu la uwezo ambao nilikuwa naupata bila kujua ulikuwa unatoka wapi.

ITAENDELEA
BURE SERIES
 
SEHEMU YA 21

"Siku zote tambua kuwa niko na wewe na siwezi kuacha udhurike na chochote kwakuwa wewe ni silaha yangu, hupaswi kuwa na uoga wowote ndani ya Muifufu pia kwakuwa nitashiriki mapambano kutokea hapahapa" alizidi kunielezea Mnaro, nikawa nimeelewa vyema.

"Sasa safari ya Muifufu iko tayari, ni wewe tu kuamua unataka kwenda lini" alisema Mnaro lakini kitu cha ajabu ni kuwa siku ile sikuwa na usongo sana wa safari ile kama ambavyo ulikuwa siku za nyuma ingawa bado nilitaka kwenda na ilikuwa lazima niende.

"Hebu nieleze kidogo kuhusu Muifufu na ambacho napaswa kufanya nikiwa huko" nilisema na Mnaro akaanza kutoa maelezo "huko Muifufu yuko mwanamke anaitwa Sauda, mwanamke ambaye nimekueleza sana kumuhusu. Wakati natoroka Muifufu nilikubaliana na mwanamke yule kuwa nitaandaa mtu ambaye nitamtuma kwenda kumchukua. Mwanamke huyo amebaki akijifunza juu ya namna ambavyo yeye na mtu huyo watafanikiwa kutoroka Muifufu. Unachotakiwa Kufanya ni kuingia Muifufu na kuishi kama ambavyo wanaishi watu wengine, mpaka ambapo utakutana na Sauda ambaye atakueleza zaidi nini cha kufanya" aliweka kituo Mnaro. Nikatafakari vizuri maelezo yale kisha nikapata swali na kuuliza "sasa nitamtambuaje huyo mwanamke?" Mnaro akanijibu "sio wewe ambaye unapaswa kumtambua, yeye ndiye atakutambua wewe. Unachopaswa kufanya ni kuweka ishara kuwa umeingia Muifufu kwenye sehemu ambayo tuliku aliana kuwa ataikuta ishara hapo naye kila siku hudamka na kwenda kuangalia hapo jambo ambalo hulifanya pia kabla ya kwenda kulala" alimaliza kunieleza Mnaro nikawa nimeelewa. Sasa ilikuwa imebaki mimi kuamua ni lini niende Muifufu.

Mama yangu anaumwa na sijamuona, sijaaga pia na kupata baraka za wazazi. Siwezi kwenda kwanz mpaka niende nyumbani, niliwaza. "Leo ni jumaa nne, naomba safari iwe jumaa nne itakayofuata baada hii ijayo" niliomba nikiamini wiki mbili zingetosha kujiandaa na Mnaro akakubali bila ubishi hata kidogo. "Vipi kuhusu huyu?" Niliuliza nikimuoneshea mwanamke yule mchawi ambaye alikuwa amelala pale chini akiwa hajitambui. "Huyo niachie mimi" alijibu Mnaro kwa kifupi.

Nikaondoka kurudi nyumbani kwa usafiri ule wa paka.

Nikafika nyumbani, nikalala nikipanga kuwa asubuhi ningeanza safari ya kwenda kuwaona wazazi nyumbani.



Kulipokucha niliamka nikiwa na mawazo mengine.

Kwanini nisafiri kwa basi safari ile ambayo ingenichukua masaa karibu kumi? Nikaamua nisubiri usiku uingie ili nisafiri kwa kumtumia paka yule ambaye bila shaka angenifikisha mapema sana.

Nikaendelea na maisha ya kawaida mpaka ukafika usiku wa kama saa tatu hivi, nikachukua begi dogo ambalo niliweka kila ambacho ningekihitaji na kuanza safari.

Ilinichukua kama masaa mawili nikawa nimefika nyumbani, nikamuhifadhi paka wangu nyuma ya nyumba na kuingia ndani ambako nilipokelewa na ndugu zangu kwa furaha sana "mbona umechelewa hivyo kaka? Uliondoka saa ngapi? Aliuliza mdogo wangu akinipokea begi langu "aaah! Niliondoka saa sita kwa magari ya kuungauunga" nilijibu nikikaa ambapo ndugu zangu wengine ambao walikuwemo vyumbani mwao, kila mmoja akitoka kuja kunilaki kwa furaha, hata baba ambaye alikuwa ameingi kulala tayari akatoka na kunipokea.

Nikauliza juu ya afya ya mama ambaye bado alikuwa hospitali akiuguzwa na dada yangu, nikaambiwa afya yake ilikuwa ikiendelea vizuri sana na walitegemea kesho yake angeruhisiwa.

Nikaongea mengi na ndugu zangu wale ambao hatukuwa tumeonana ndani ya muda wa kama miezi nane hivi lakini ilikuwa ni mingi sana kwani hatukuzoea kukaa mbalimbali kwa muda mrefu kiasi kile.

Tukaingia kulala mida ya saa saba.



Asubuhi tulikwenda hospitali kumuona mama ambaye alifurahi sana kuniona. Afya yake ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba ungemkuta nyumbani ungehitaji kuambiw kuwa alikuwa mgonjwa.

Tukaongea mawili, matatu na baadae tukaongea na daktari ambaye alituruhusu kuondoka naye, tukarudi nyumbani.



Nilikaa pale nyumbani mpaka zikabaki siku mbili kwaajili ya safari ya Muifufu.

Usiku wa siku hiyo nikawaita wazazi wangu, nikakaa nao nikiwaeleza juu y safari ya Muifufu ambayo ilipaswa kuwepo siku mbili zijazo.

Pamoja na wasiwasi ambao walikuwanao, wazazi wangu walinipa baraka zao na kuniombea mafaniko katika safari ile.

Nikawaaga kuanza safari ya kurudi kwangu ambayo niliwaambia ni lazima niondoke usiku ila sikuwaambia kuwa natumia usafiri wa paka kuhofia kuwaacha kwenye wasiwasi mwingi nikiwa safarini.

Nilifika nyumbani haraka kama ambavyo ilikuwa safari ile ya kwenda.

Nikalala nikijua kuwa kesho yake nilitakiwa kuamkia mahakamani ambako kesi yetu ingesomwa.



Niliamka napema nikajiandaa na kwenda mahakamani ambapo ziliendeshwa kesi kadhaa na majira ya saa tano ndipo nasisi tukaitwa na kesi yatu kusomwa.

Nilikataa kuwa mimi sikuwahi kukamatwa na kuingizwa mahabusu kisha kutoroka kama ambavyo askari wale walieleza (melezo ambayo hakimu yule alinifundisha niyaseme).
 
SEHEMU YA 22

Nikaulizwa juu ya kukubali kwangu kuwa askari yule ambaye ni mshatakiwa namba mbili alinitorosha, nikajibu kuwa sikuwa na kingine cha kusema kwakuwa askari wale walikuwa wakinipiga nikubali kuwa nilitoroka.

Hakimu yule akawataka askari wale kuleta ushahidi ila askari wale wakomba wapewe muda kuendelea na upepelezi.

Ikapangwa tarehe nyingine ya kusikilizwa kesi ile ambayo ilikuwa ni miezi miwili ijayo.

Nami nikaondoka kwakuwa tayari nilikuwa na dhamana.

Nikaenda mojakwa moja nyumbani ambapo jioni ya siku hiyo hakimu yule alikuja kunitembelea tukazungumza mengi.

Nilimjuza kuwa safafari ya kwenda Muifufu ilikuwa kesho yake ingawa siijui siku ya kurudi, naye akanitaka niende kwa amani tu ya huku mahakamani nimuachie yeye hata kama nitachelewa.

"Hii kesi itakusubiri tu mpaka urudi, ukija na binti yangu nitahakikisha unakuwa huru ila usiporudi naye nitahakikisha unafungwa miaka mingi sana bwana Saire" aliongea hakimu yule akionesha msisitizo mkubwa ukiashiria kukimaanisha akisemacho. Nami nikajitahidi kumtoa hofu "usiwe na shaka bwana Waisaka, umenisaidia pakubwa sana nami lazima nilipe fadhila" nilisema.

Tukaagana na bwana Waisaka akaondoka na kuniacha nikipanga mipango ya kumtafuta Mnaro kwaajili ya mipango ya safari ya kwenda Muifufu.



Nikaenda ndani, nikachukua kale kakioo ambacho toka Mnaro anipe kwa kwaajili ya kukatumia kumtafuta nikimuhitaji nilikuwa bado sijakatumia.

Nikakishika kioo kile kwa mikono yangu yote miwili na kuanza kusema nacho kama ambavyo alinielekeza "nakuagiza kioo, niletee Mnaro haraka" nilisema nikiwa kama ambaye najarubu kwa maana sikuwa na uhakika na mabacho nakifanya lakini hakikutokea kitu, nikawa narudia rudia kauli ile.

Baada ya kurudia kama mara ya saba hivi kioo kile kikatoa mtetemeko mkubwa sana mpaka kuutingisha mwili wangu, kitu cha kushangaza ni kuwa sikuogopa lakini kioo kile kilikuwa kilianza ghafla kuwa kizito mpaka nikafikia kishindwa kukizuia na kuamua kukiweka chini ambapo kilianza kutoa moshi ukipanda juu na kutengeneza duara fulani mbele yangu.

Moshi ule endelea kuwa mwingi na kujikusanya kwenye lile duara ambalo ulitengeneza na baada ya muda mfupi nikamuona Mnaro katikati ya duara lile.

Mnaro alikuwa akionekana vizuri kabisa kama ambaye nilikuwanaye pale chumbani.

"Sasa niko tayari kwa safari, nakusikiliza wewe tu"

Nilianzisha maongezi. Mnaro aliniangalia akatabasamu na kusogea pembeni akachukua ule mkoba wake wa ngozi na kutoa kila ambacho kilikuwemo ndani na kuanza kunionesha kimoja baada ya kingine.

"Mikufu hii utakwenda nayo na baada tu ya kuingia muifufu utauacha mmoja ambapo nitakuelekeza na kuondoka na mmoja, Sauda atakapouona mkufu ambao utakuwa umeuacha atakutafuta na itakuwa rahisi kukupata na kukuamini iwapo utakuwa umeuvaa mkufu ambao utabakinao" alinielezea akinionesha mikufu miwili ambayo ilikuwa ikifanana sana.

"Kipande hiki cha mkate ni kipande ambacho kimeishi kwa miaka zaidi ya 600, mkate huu ulikuwa ukitumiwa na mchawi wa zamani sana wa Kijerumani ambaye kama angekulisha kipande kidogo tu basi ungefanya chochote ambacho angekwambia, uchawi huu una nguvu mpaka leo, kitunze kipande hiki huenda kikakusaidia huko Muifufu" aliendelea kunielezea akinionesha kimkate ambacho kilikuwa kimekauka sana, kisha akachukia kichupa kidogo sana na kunipa maelezo kukihusu "iwapo utapaka mafuta yaliyomo ndani ya kachupa haka, wachawi hawawezi kukuona, labda kama mchawi huyo ana nguvu kubwa sanaa ila wa kawaida hawawezi" kisha akanionesha vimayai vitatu vidogo kama vya njiwa "haya ni mayai ya bundi wa zamani sana, mayai haya yana thamani sana kwa mchawi kwa maana humuwezesha kuwa na nguvu sana, mchawi yuko tayari kufanya biashara yoyote na wewe kama malipo ni mayai haya"

Aliendelea kunielezea Mnaro huku akirudisha kila kimoja ndani ya mkoba ule baada ya kukamilisha maelezo kukihusu..

"Hii ni dawa ambayo inaweza kukusaidia iwapo utapata maumivu au hata kuvunjika wakati wa kupambana na wachawi" alisema akinionesha majani makavu nami nikayatambua kuwa ndiyo ambayo alitumia kutibu kifundo changu cha mguu mara baada ya kuumia siku nilipopambana naye alipokuja nyumbani kwangu na kunijaribu.

Sasa mezani pale kulibaki kopo moja tu, akilbeba na kulifungua kisha anakionesha ndani yake kulikuwa na kama vikokoto vidogo vinavyotumika kwenye zege..

"Magugi anaweza kukugundua kama una nia mbaya kwake kupitia pumzi yako, njia pekee ya kumzuia kukusoma iwapo utakuwa mbele yake ni kutopumua, dawa hii itakuwezesha kukaa muda wa dakika arobaini bila kupumua, hivyo hakikisha unameza dawa hii kabla ya kuonana naye kama ikitokea ukapaswa kuonana naye" alikuwa amemaliza kuelezea kuhusu vitu vile ambavyo alikuwanavyo ndani ya mkoba ule.

"Ni muda mrefu sana toka niondoke Muifufu, pengime kuna mambo mengi yamebadilika, pengine nguvu za baba yangu ni kubwa kuliko ambavyo nilimuacha.
 
SEHEMU YA 23

Jambo la muhimu ni kukutana kwanza na Sauda ambaye atakupa muongozo wa namna ya kushinda vita hii" alielezea Mnaro na hapo nikajikuta najiuliza swali "Sauda ameshindwaje kutoroka huko Muifufu kwa miaka yote hiyo kama kweli anao muongozo?" Niliuliza nikijiambia kama ni kazi ngumu namna hiyo kuondoka Muifufu mbona yeye Mnaro aliweza na kama haiwezekani mimi nitawezaje kuwatoa. "Njia ya kutokea Muifufu ina amrishwa na mtu mmoja tu kufunguka naye ni Magugi, mimi nilikuwa na uwezo huo ambao nilipewa na Magugi kama msaidizi wake ambaye alikuwa akiniamini, baada ya kumuasi nilifutiwa Mamlaka hayo. Nimeishi nikijifunza namna ambavyo naweza kuingia Muifufu mpaka nimefanikiwa lakini namna ya kutoka bado mtamtegemea Magugi ambaye tukishirikiana na kutumia nyenzo ambazo nimekuonesha lazima tumlazimishe awafungulie njia, najua Sauda pia atakuwa amepata udhaifu ambao tunaweza kuutumia kwa Magugi kwa maana ndio kazi pekee ambayo amekuwa akiifanya huko" alimaliza kunielezea Mnaro nikagundua kuwa nina kibarua kizito sana huko Muifufu lakini sikuwa na budi kwenda kwani ndiko aliko mke wangu kipenzi ambaye nilijiona pungufu bila yeye.

"Lazima pia nikwambie kuwa hakikisha mpenzi wangu anatoka Muifufu. Kama ukifanikiwa kutoa wawili basi ni wewe na yeye, kama akitoka mmoja ni yeye na kama akitoka nusu basi ni nusu yake, sitokuelewa ukirudi hapa bila Sauda na nakuhakikishia furaha unayoitafuta hutoipata kama Sauda hatofanikiwa kutoka, nitayaharibu kabisa maisha yako" alisema Mnaro kwa sauti ya msisitizo mkubwa kiasi cha kuogopesha.

"Sawa mkuu, nitahakikisha Sauda anakuwa na wewe hivi karibuni" nilijibu huku nikitetemeka. Ukweli niliujua moyoni mwangu mwenyewe kuwa kama akitoka mmoja basi ni mke wangu Samia na kama ni wawali basi ni mimi na mke wangu.

"Ninaamini tutafanikiwa kuwatorosha wote, mungu atuwezeshe" alisema Mnaro.

"Sasa safari itakuwa sangapi na itaanzia wapi?" Niliuliza.

"Safari itakuwa alfajiri na nitakufuata na kukusindikiza mpaka ambapo ufanikiwa kuingia" alijibu Mnaro, tukaagana na moshi ule ambao ulikuwa unatoka kwenye kioo kile ukakoma mara moja na Mnaro hakuonekana tena.

Nikabaki nikijaribu kulala lakini sikupata hata usingizi, nikawa nikitizama saa kila wakati kuona kama muda wa safari ulikuwa umefika.



Majira ya saa kumi za alfahiri Mnaro akaja na kunitaka tuanze safari, tukaondoka tukitumia wale paka wetu kama kawaida.

Tukaenda mwendo wa kama nusu saa kisha tukaingia kwenye pori kubwa ambalo sikuwa nimewahi kuliona kabla tukaenda mpaka katikati mwa pori lile kisha tukashuka kwenye usafiri ule wa paka na kusimama pembeni ya mti mkubwa sana. Mnaro akanikabidhi ile Mikufu miwili na kunitaka kuuvaa mmoja na kuutunza vizuri ule mwingine.

"Ukifanikiwa Kuingia utatembea kuelekea mbele kisha utafika kwenye njiapanda ambapo utachagua njia ya kushoto kwako ambayo atapita katikati ya pori, wewe endelea kunyoosha na njia hiyohiyo ambayo itakutoa mpaka nnje ya pori, lakini kukikaribia kutoka nnje ya pori utaona miti ikiwa imepangwa kwa mistari kushoto na kulia kwako wewe ukipita katikati, hakikisha mkufu huyo unauvisha kweye tawi la chini la mti wa kulia kwako ambalo limekatwa na ni fupi tu. Kisha utaendelea na safari mpaka utakutana na makazi ya watu ambamo na wewe utajichanganya na kuishi kama mkazi wa huko mpaka utakapoonana na Sauda" alielezea Mnaro kisha akanikabidhi ule mkoba wake wa ngozi "nadhani unajua kila kilichomo humo na matumizi yake, utatumia kila ambacho unaweza kukuhitaji ukiwa Muifufu. Watu wa huko hawaujui uchawi wa kutumia vitu hivi, wanayajua tu hayo mayai ya bundi" alimaliza kunieleza Mnaro, akiongea kwa upole sana siku hiyo, hata sura yake ilionesha kuwa alikuwa na mtu mwenye hudhuni.

"Wewe ni silaha yangu ya mwisho, ninakutegemea sana katika hili. Tafadhali usiniangushe" alisema Mnaro nami nikamuitikia kwa kichwa tu kisha akapiga magoti chini, akatoa mishumaa minne kutoka mifukoni mwake, akaisimamisha vizuri pale chini, mmoja kulia, mmoja kushoto na mingine mbele na nyuma kisha yeye akawa katikati, akanyoosha mikono juu huku na uso wake akiuelekeza juu lakini alikiwa amefumba macho yake kwanguvu sana, akawa anatamka maneno kwa kunong`ona ila kwa msisitizo sana.

mara mishumaa ile ikawaka, kadri alivyozidi kunongona maneno yale ndivyo mishumaa ile ilivyozidi kutoa mwanga mpaka eneo lote likawa kama mchana, Mnaro nae alikuwa akitokwa jasho jingi sana lakini hakuacha, aliendelea kutamka maneno yake kwa kunong`ona. Ile mishumaa ikaanz kutoa moshi mkubwa ambao uliungana kutoka katika kila mshumaa na kutengeneza uwazi mkubwa kama mlango.

Mnaro akasitisha zoezi lake, akafumbua macho na kunitizama, kisha akatizama ambapo moshi ule ulitengeneza mlango nami nikajikuta nikitupia macho yangu kuangalia mlango ule wa moshi, mlango ule ulionekana kuanz kupungua ukubwa kwa kasi.. "KIMBIAAAAAAAA, PITA HAPO UENDEEEE" alipiga kelele
 
Back
Top Bottom