Simulizi: Msegemnege

Simulizi: Msegemnege

Tupio la XV – Afande akubali matokeo

Ilipoishia...


Baada ya mazungumzo marefu pale, mama Omari alihitimisha kuwa mwanawe atumie tu zile hela kujianzishia biashara na wala asifikirie kusafiri kwenda huko ughaibuni isije ikawa mtego wa kuishia kwa maharamia, wakamdhuru mwanawe.

“Usije ukaenda huko ukaishia kuwa mtumwa, ama kunyofolewa figo zako ama kudhuriwa kwa namna yoyote ile, baki hapa hapa, tafuta biashara nyingine nipatie na mie niongezee mtaji wa genge langu maana hali halisi ya nyumbani si unaiona?!”


Omari akajibu…

Sawa mama, nimekusikia, ngoja nitafakari kwanza.


Sasa endelea…


Siku hiyo Afande Juma, akawahi kurudi nyumbani, wala haikuwa kawaida yake maana huwa anatumia muda mwingi huko kilabuni ama kwenye baa, alikuwa habagui sehemu ya kunywea na hurudi nyumbani kwake mida mibaya siku ikiwa tayari imeshapinduka.

Kabla ya saa tatu usiku alirudi, lakini tayari akiwa amelewa na aka kaa sebuleni na kuomba chakula. Ikabidi mama Omari amsongee ugali harakharaka maana hakuwa na ratiba ya kula nyumbani usiku.

“Leo nimefurahi sana…” kwa sauti ya ulei baba Omari alisema…

“Mwangangu Omari leo amenivisha nguo…” Alifungua kinywa baada ya kimya fulani hivi kile cha kusubiria chakula.

Kwa muda mrefu tangia aliporudi kutoka Dafur Sudan afande Juma hakuwa na kawaida ya kula chakula cha jioni pamoja na familia yake, hivyo siku hiyo ilikuwa si jambo la kawaida kwa Omari hata kwa mama yake kumuona afende cha pombe huyo muda huo akiwepo pale sebuleni.

Wakati baba Omari anaenda kwenye fatiki huko Dafur, mke wake alimuacha akiwa mja mzito. Ulikuwa ni ujauzito mchanga ambao pia uligubikwa na sintofamau nyingi afande Juma akimtuhumu mkewe kuwa amebeba mimba nje ya ndoa.

Alivyorudi kutoka Sudan ndipo tabia za ulevi zikakithiri kiasi kilichopelekea baba kutokuwa na mapenzi na mtoto wake Omari. Hali hii ilidumu hadi siku hiyo baba Omari alipowahi kurudi nyumbani na kula chakula huku familia yake yaani mkewe na mwanawe Omar wakiwa sebuleni wakifuatilia tamthilia kwenye runinga.

“Mwanangu Omari leo umenivesha nguo…” alirudia tena ile kauli yake kwa sauti ya kilevi huku akiwa na chakula mdomoni.

Pakawa na ukimya tena, na afande Juma akamalizia kula kisha akasema…

“Mwanangu Omari, nisogezee maji ya kunawa…”

Omari kwa unyenyekevu kabisa akamsogezea maji ya kunawa kisha akamwagilizia ili baba yake anawe. Wakati huo mama Omari alikuwa kimya kama akisubiri kitu kwa shauku kutoka kwa mumewe. Mumewe ambaye aliolewa naye kwa ndoa ya kiislamu mama Omari akiwa binti mdogo kabisa wa miaka 18 na Private Juma wakati huo alikuwa ana miaka minne tangia aajiriwe jeshini.

“Leo mwanangu amenivesha nguo!” akarudia tena kusema maneno yale na kuendelea...

“Nilikuwa nadaiwa deni la muda mrefu pale Jambo Lee Bar, nimelipunguza sana lakini zikabakia elfu hamsini tu ambapo mimi leo nilikuwa nina shilingi elfu 20 tu mfukoni. Sasa nilipofika pale nimekuta meneja wa bar amechachamaa akisema nisimpomlipa leo basi suala langu atalifikisha kazini…”

Akatulia kidogo kisha akaendelea…

“Sasa kazini ‘osii’ wangu sipatani naye juzi tu ametoka ‘kunipiga gadi’ wiki kwa sababu zisizo za msingi. Sasa nilikuwa sipendi suala hili lifike kazini ndio maana nilirudi kuja kukuomba mke wangu elfu ishirini ili nikiongeza na zangu ningekuwa na elfu arobaini ningepooza kidogo labda na hiyo elfu kumi ningepata pale pale bar kwa jamaa zangu…”

Akakaa vizuri kwenye kochi kisha akaendelea…

“Sasa zile elfu nne ulizonipatia wala zisingefaa kitu, hivyo nilirudi kwa unyonge pale bar huku nikiwa na mawazo tele, kule meneja akinsubiri kwa hamu maana wakati natoka nilimwambia ngoja nikachukue hela nyumbani…”

“Nilifika pale nikiwa na elfu 24 tu mfukoni, nikawa nimejiinamia ingawaje rafiki zangu walikuwa wananipa ofa za bia lakini nilikunywa kidogo tu na nikawa nimeinama nikitafakari…”

“Nilikuwa nawaza miaka zaidi ya 22 niliyotumikia jeshi, kupanda vyeo hadi kufikia sajinitaji lakini kutokana na sababu za kinidhamu nilivuliwa vyeo na kubakishiwa mbavu moja, Koplo usu mimi naenda kudhalilika kwa sababu ya shilingi elfu 50!...”

“Yani mimi niliyefanya fatiki kadhaa katika nchi mbalimbali pamoja na utaalam wangu wa milipuko niliosomea huko ughaibuni ndio elfu hamsini inidhalilishe ofisini!?...”

“Nilikuwa nimejiinamia nawaza mengi sana ikiwemo hii hali iliyosababisha hadi mimi kuwa mlevi wa kupindukia, hii hali ya kutokuwa na uwezo wa kutungisha mimba…”

Mama Omari akashtuka na kutoa macho Omari yeye akiwa anasikiliza tu kwa makini…

“Ndiyo mke wangu, ninajuwa kuwa Omari si mwanangu, hata baba yake mzazi namjua, lakini niliamua kulewa tuu ili nisifanye jambo baya…”

“Lakini, kuanzia leo natamka hapa mbele yako mke wangu na mbele ya Omari na mbele za Mungu kuwa kuanzia leo hii Omari ni mtoto wangu, nitamlea vizuri na kumsaidia katika kuanzisha maisha yake, na wewe mke wangu nakupenda sana ndio maana licha ya kujuwa ukweli huo ambao umeniumiza siku nyingi sijakupa talaka wala kukufukuza sana sana ni maneno ya kilevi tu nikiwa nimelewa sana…”

“Leo sijalewa, nimekunywa bia tano tu tena zote za ofa. Sasa katika hali ile ya mawazo ndipo nikahisi kuguswa begani na kushikishwa kitu kama karatasi mkononi, nikafumbua macho na kuangalia mkononi ndio nikakuta noti mbili za elfu kumi kumi…”

“Nikageuza shingo na kuangalia nani aliyenipa zile hela ndipo nikamwoma mwanangu Omari amechuchumaa…”

Pakawa na ukimya na afande Juma akawa anatoa machozi… kisha akasema…

“Sikutegemea kama Omari anaweza kunifanyia wema wa namna hii… nimekuwa baba mbaya kwake, sikumjali tangia utoto wake licha ya yeye kusaidia sana katika bajeti za humu ndani, usifikiri mimi sijui…”

Akatoa leso akajifuta machozi kisha akaendelea…

“Nilivyorudi kutoka Sudan niliamua kwenda maabara kupima afya yangu ya uzazi, ndipo afande Seba akaniambia kuwa mbegu zangu za uzazi hazina uwezo wa kurutubisha mayai, kwa maana ya kwamba mimi ndiye mwenye tatizo la uzazi kwenye ndoa hii…”

“Licha ya majibu hayo sikuridhika, nikaamua kupekua kepua hapa mtaani na huko kazini lakini wapi, hata wa kusingiziwa sikupata nikaamua kunywa pombe ili nipoteze mawazo, kumbe ni balaa, nikaanza kuona ‘duble duble’…”

“Sasa kuanzia leo, kama nilivyopsema, mimi sijalewa hapa, naongea nikiwa na akili zangu timamu, wewe Omari ni mtoto wangu na nimeamua kuacha pombe rasmi.”

Akaweka kituo, pakawa na ukimya wa sekunde kadhaa kabla mama Omari hajainua kinywa chake na kusema…

“Omari, nenda chumbani kwako kapumzike, tutaongea kesho…” kisha mama Omari akasimama pale alipokaa na kumkabili baba Omari na kupiga magoti mbele yake na kusema…

“Nisamehe mume wangu…” machozi yakaanza kumtoka…

“Mawifi na ndugu upande wenu walianza maneno, eti najaza choo, sasa katika hali ya kutapatapa nikasema ngoja nimkubalie rafiki yako maana amekuwa akinisumbua kwa miezi mingi…”

“Nikavizia siku za hatari nikashiriki naye mara moja tu, miezi mitatu baadaye ndio ukaniambia kuhusu safari yako kwenda Sudani…”

Mama Omari alikuwa anaongea kwa kwikwi na kwa uchungu sana…

“Nakupenda sana mume wangu na ndio maana hujaona nikiwa na mimba nyingine tena baada ya Omari maana nilishajuwa kuwa kumbe tatizo halipo kwangu, nimekutunzia heshima muda wote na wala huyo Saidi hajui kama Omari ni mtoto wake na imekuwa bora alivyohamishiwa Kigoma.”

“Inuka mke wangu kipenzi, nimekusikia. Afande Saidi na wenzake walifariki kwa ajali ya gari huko huko Kigoma, usiwe na wasi wasi wewe ni mke wangu halali…”

Wakakumbatiana pale kisha wakabebana msobemsobe kuelekea chumbani ambako huko waliendelea kuombana msamaha kiutu uzima.
---


Usiku huo, Omari hakupata usingizi mzuri, alijawa na mawazo mengi…

“Bora niende tu huko ughaibuni…” alijisemea baada ya kutafakari kwa muda mrefu.

Akachukuwa ile barua iliyotafsiriwa na kuisoma mara kwa mara…

“Kesho nitaipeleka hii orijino kwa mtu mwingine anitasfirie nione kama Frank alinitafsiria sawa…” hatimaye akapitiwa na usingizi…


Itaendelea...
KItanda hakizai Haram
 
(Nusu) Tupio la XVI - Nasreen

Nasreen ni mtoto wa pekee wa kike aliyezaliwa katika familia ya kitajiri huko mjini Manama nchini Barhain. Ana kaka zake wanne .

Nasreen ni mtoto anayependwa sana kwa baba yake pamoja na mama yake ambapo kila mwaka huwa wanamchuka safarini kuizunguka Dunia.

Miaka michache liyopita Nasreen alifikisha miaka 18 na siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa ilisheherekewa ndani ya ndege binafsi iliyokodiwa kwa ajili ya safari ya kutoka Bahrain hadi Afrika kusini ambao walikuwa na mapumziko ya siku 14.

Utajiri wa familia hiyo unatokana na hisa kubwa waliyonayo katika moja ya makampuni ya uchimbaji mafuta huko Uarabuni. Ni moja ya familia inayoishi kifahari sana hapo mjini Manama, wana kasri kadhaa hapo mjini ambayo wamepangisha kwa baadhi ya watu na pia wao wanaishi kwenye kasri kubwa ambalo lina bustani nzuri, kwa ujumla maisha yao yalikuwa yenye hadhi ya kifalme ingawaje katika mji huo juo kuna matajiri wengine wenye maisha ya kifahari zaidi yao.

Sasa katika kusheherekea kulikuwa na vinywaji kadhaa na ikafika kipengele cha yeye kuweka kitu kama nadhiri hivi (wish)

Kwa mshangao mkubwa Nasreen akasema, (aliongea kwa kiarabu)

“Nikimaliza kinywaji hiki, nitaitupa hii chupa baharini, na atakayeiokota akiwa kijana yoyote rijali wa kuoa basi nitakubali kuoelwa naye, akiwa mtu wa aina nyingine basi nitakuwa rafiki naye na nitamzawadia baadhi ya neema hizi ambazo Mwenyezi Mungu ametujaalia…”

Baba yake, mama yake na kaka yake ndogo anayemfuatia wote walishangaa kwa maneno yale, pakawa na ukimya lakini hatimaye baba mtu akasema…

“Na tunywe kwa urafiki mpyaaaa”

Wote wakashangilia kisha wakaendelea na kuburudika kwa vinywaji na nyimbo mbalimbali za kufurahisha.

Nasreen baada ya kumaliza kile kinywaji, akaikausha chupa kwa joto la kukaushia mikono lililopo kwenye kifaa maalumu maliwatoni humo kwenye ndege kisha akaandika kwa Kiingereza kwa kutumia kalamu yake ya gharama kubwa yenye wino mzuri wa bluu…

Assalaam alaykum.

My name is Nasreen, I am from Manama Barhain.
Whoever will bring this original writtings to me inperson will be my friend. Use dinar bill attached as transport fee, add yours if fare is not enough and I will refund you. Do NOT forget to bring also one note bill attached.

Eager from seeing you, my ideal lucky friend.

May God Almighty bless you.

Nasreen. (+973xxxxxxxxx)


Alipomaliza kuandika hivyo, akachukuwa noti kadhaa akazifungia na ile karatasi aliyoandika kisha akatumbukiza kwenye ile chupa ya kinywaji alichokunywa kisha akafunga mfuniko wake vizuri halafu akamwamuru rubani alishushe ndege chini uswa wa bahari na kupunguza mwendo…

Chupa iliachiwa ianguke baharini kwa msaada wa rubani kupitia sehemu maalumu rubani aliyomwonesha…

Waliendelea na safari yao kuelekea Capetown ambako walikaa siku kumi na tatu kisha wakarudi Bahrain kuendelea na majukumu yao.

Nasreen ni msomi aliyebobea kwenye fani ya upishi na mapambo lakini ni fani ambayo hatoitumikia ili kujipatia fedha bali itamsaidia katika kukuza ustawi katika familia yao.

Miaka mitatu sasa imepita tangia ile chupa itupwe baharini na kufanya watu wote katika familia yao kusahau upuuzi ule isipokuwa yeye ambaye dhamiri yake ndani ilikuwa inamuambia ipo siku atajitokeza mtu.

Katika kuandika aliweka vipimo ili ajue kama kweli atakaye leta ndiye aliyeiokota kwa kuweka sharti la kuja na ile barua halisi na moja ya noti iliyokuwemo mule ambapo note zote alizoziweka alizinakili namba zake. Hivyo kama mtu akija na barua orijino lakini na noti nyingine atakuwa amevunja sharti au mtu akija na barua iliyodurufiwa pia atakuwa amevunja sharti hivyo Nasreen hatofungwa na nadhiri yake.
---

Itaendelea…
 
Tupio la XVII – Deliverence

Ilipoishia...



“Naomba maji ya kunywa…” Yalikuwa maneno ya kwanza kumtoka mama Mchungaji baada ya kuinuliwa…

“Mpeni kiti sasa akae na sisi sote turudi kwenye viti vyetu tukakae tumsikilie..”

Aliongeza Zawadi baada ya kuona mama mchungaji ameshakunywa maji lakini pia waumini walijazana eneo la mbele kiasi cha kufanya kuwe na hewa nzito na nafasi finyu.

“Bwana Yesu apewe sifaaa!...” mama mchungaji alianza kufunguka…


Sasa endelea…


“Bwana Yesu apewe sifa!...”

“Bwana Yesu apewe sifa!...”

“Tumsifu Yesu Kristu…!

Alirudia rudia kusema maneno hayo huku kila aliporudia alikuwa akiongeza sauti… kisha akaendelea…

“Wapendwa katika Bwana, leo ni zamu yangu ya kuleta ushuhuda na kutubu…”

Waumini walikuwa kimyaaaa isipokuwa wale wachache ambao ni kundi mhemko likiongoza na dada mmoja asiye na simile katika kuyaendea mambo.

“Hakika leo nimeona utukufu wa Mungu wa Mbinguni, Mungu aliye umba mbingu na nchi, Mungu wa Isaka, Mungu ya Yakobo…”

“Nilifungwa katika maagano ya kishetani lakini leo namshukuru Mungu kwa kumleta yule binti…” akanyoosha mkono na kidole kumuelekezea Zawadi…

“Binti amakuja kuvunja maagano niliyokuwa nayo…”

“Nilikuwa namtumikia shetani…”

Mama mchungaji alikuwa anaongea kwa kukata kata maneno kama vile akipata tabu ya kuvuta pumzi, ingawaje alikuwa ameketi kwenye kiti lakini ile hali ya mhemo ilikuwa dhahiri wa waumini wote…

“Mwaka fulani (aliutaja) nilimaliza masomo katika chuo cha Biblia Mwanza na huko nikakutana na bwana mmoja ambaye ndiye alinishawishi baada ya kumaliza mafunzo yale tuende Nigeria kusoma zaidi ili tuwe na nguvu nyingi za kimiujiza ili kuwaaminisha waumini juu ya nguvu za Mungu…”

“Ilinichukuwa miezi kadhaa hadi kuandaa nauli pamoja na masurufu ya safri kwa ajili ya kwenda huko Logos ambako kwa maelekezo ya bwana yule tungepata nguvu za miujiza nyingiii”

“Kweli siku ya siku tulifunga safari na tukakaa huko kwa miezi 18 tukipata mafundisho mbalimbali ya kiroho na kisha ndipo nilipojikuta nimetumbukia katika maagano ya nguvu za giza ambapo mimi nilpatiwa nyoka aina ya chatu pamoja na makolokolo mengine nikawa na uwezo wa kufanya miujiza mbele za watu na kuvutia watu wengi katika huduma yangu niliporudi nchini…”

“Huduma yangu kwanza ilikuwa ndani ya makanisa mengine, nikifanya miujiza kidogo basi watu wanaamini na kuanza kuniletea pesa kuniomba niwaombee mambo mbalimbali hadi mwaka juzi nilioamua kuanzisha kanisa langu hili…”

“Kwa kushirikiana na baadhi yenu, tumefanya udanganyifu mwingi wa kuleta ushuhuda wa uongo ili tu ninyi waumini muone nguvu nilizonazo, nimetoa mapepo ya uongo mengi tu na kuendelea kujineemesha kupitia sadaka zenu...”

“Lile kapu mlilokuwa mnaliona halikuwa kikapu, lilikuwa ni joka kubwa aina ya chatu ambalo ndilo lilikuwa likihifadhi zile hela na usiku likiniamuru kwa njia ya ndoto kufanya makafara mbalimbali ili nguvu zangu zisipotee…”

“Ni mabaya mengi sana nimeyafanya, lakini leo hii nimefunguliwa, Haleluyaa!”

“Haleluya!” alirudia kusema neno hilo baada ya kuona uitikio ni hafifu kutoka kwa waumini.

“Binti yule sijui ametokea wapi, maana hata siku ile ya kwanza kumuona humu kanisani nilitamani anisaidie katika kuondosha hali hii niliyonayo lakini nilikuwa sina namna…”

“Leo hii namshukuru Mungu Baba kwa kupitia huyu binti, nimevuja lile agano na lile joka limekufa kwa maana wakati nakabidhiwa niliambiwa siku joka lile likifa ama kupotea basi nguvu zangu nazo zitakufa na ikitokea hivyo basi haraka niwahi kuwenda Logos kwa ajili ya ku-update maagano…”

Aliendelea kuongea pale weee akisimulia mengi aliyokuwa nayo, mengine ya hiyari maengine hakuwa na hiyari nayo na kuonesha kujuta kwa kitendo alichofanya…”

“Leo hii niko hapa mbele yenu, lakini sina zile nguvu tena za miujiza bali nina mafundisho sahihi kama tulivyofundishwa kule Nyakato chuo cha Biblia, na kwa heshima ninaomba binti huyu aniongoze sala ya toba ili nitubu mbele za Mungu na mbele zenu…”

Zawadi akasogea mbele kwa kupanda pale madhabahuni na kuanza kusema kwa sauti nyembamba kali huku mkono wake mmoja akiinua juu…

“Niwakaribisheni nyote kumpokea YYesu kama BBwana nna MMwokozi wa maisha yako…”

“Na kufanya mana hiyo unapokea upendo wa Mungu na kumiminwa ndani ya mioyo yetu kwa uwezo wa Roho mtakatifu…”

“Inawezekana umepoa, inawezekana upendo wako kwa Mungu umepoa, unaomba tu kwa sababu una tatizo ama shida fulani, lakini shida ama tatizo hilo likiisha utaacha kuomba…”

“Warumi 5 tano inatuambia… ‘Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu’…”

“Basi na tutumie muda huu kufufua imani, turudishe tena ule moto kama alivyosema habakuki katika kitabu chake sura ya tatu mstari wa pili… ‘Ffufua kazi yako katikati ya miaka…’, sasa hebu fuata maneno haya, sema…”

“Eee Mungu Baba...,

Nimekuja mbele zako…,

Naomba unirehemu…,

Naomba unisamehe…,

Zambi zangu zote…,

Nilizokukosea…”

“EE Bwana Yesu…,

Nimefungua moyo wangu…,

Nakukaribisha sasa…,

Ingia ndani yangu…,

Kwa uweza wa roho wako…,

Uwe Bwana na mwakozi na kiongozi wa maisha yangu…,

Ee Bwana Yesu…,

Ingia kwa upya…,

Fufua upendo wako ndani yangu…,

Fufua kwa upya…,

Katika JJina la Yesu…”

“Asante kwa kunihesabia haki…,

Katika Jjina la Yesu…,

Unisaidie…,

Niingiapo na nitokapo…,

Katika Jina la Yesu…,

Dhambi zisinishinde, Majaribu yasinishinde…,

Shetani asinishinde…,

Nipe mabadiliko…,

Kutoka kwenye uzima wa milele…,

Unayoyataka kwangu…,

Na shughuli ninazozifanya…,

Katika jina la Yesu…, Amen”


Wakati Zawadi akiongoza sala ile ya toba, waumini wote walifuatisha, tena kwa sauti za kutetema na kujuta na kutoa machozi…

Zawadi aliendelea…

“Kama umefuatisha sala hii kwa dhati, basi Mungu amekusamehe, na nguvu za Mungu zimeingia ndani yako, roho wa Mungu ameingia ndani yako tangia sasa, pendo la Mungu limeingia ndani yako….”

“Sasa tumejenga msingi mpya wa Imani katika maisha yetu ya kiroho. Kwa heshima kubwa kabisa sasa nimkaribishe mchungaji aendelee…”

Wakati wote huo, mpiga kinanda wa kanisa alikuwa naye akichombeza kwa mirindimo ya sauti za kuhanikiza matukio yaliyokuwa yanaendelea…

Mama Mchungaji akasogea katikati ya madhabau na kumgeukia mpiga kinanda akimwashiria kama aanzishe kitu hivi mara…

Melodi za wimbo wa kusifu zikapigwa na kwa kuwa melodi ya wimbo ule ulikuwa unajulikana kanisa zima likaitikia kibwagizo wakiongonzwa na kwaya ya kanisa…

“Ninamjua…, aliye mwamba…., ameyeniokoa… ni Bwana Yesu…”

Waumini waliimba kwa furaha na kucheza…

Kabla wimbo haujaisha, Zawadi aliwaashiria akina Vai waondoke warudi kule nyuma kwenye siti zao, walipokaribia kwenye siti, Zawadai akawaambia twendeni nyumbani hivyo wakatoka mle ndani wakati bado watu wakiimba kwa furaha kumsifu Mungu.



Itaendelea...
 
Tupio la XVII – Deliverence

Ilipoishia...



“Naomba maji ya kunywa…” Yalikuwa maneno ya kwanza kumtoka mama Mchungaji baada ya kuinuliwa…

“Mpeni kiti sasa akae na sisi sote turudi kwenye viti vyetu tukakae tumsikilie..” Aliongeza Zawadi baada ya kuona mama mchungaji ameshakunywa maji lakini pia waumini walijazana eneo la mbele kiasi cha kufanya kuwe na hewa nzito na nafasi finyu.

“Bwana Yesu apewe sifaaa!...” mama mchungaji alianza kufunguka…


Sasa endelea…


“Bwana Yesu apewe sifa!...”

“Bwana Yesu apewe sifa!...”

“Tumsifu Yesu Kristu…!

Alirudia rudia kusema maneno hayo huku kila aliporudia alikuwa akiongeza sauti… kisha akaendelea…

“Wapendwa katika Bwana, leo ni zamu yangu ya kuleta ushuhuda na kutubu…”

Waumini walikuwa kimyaaaa isipokuwa wale wachache ambao ni kundi mhemko likiongoza na dada mmoja asiye na simile katika kuyaendea mambo.

“Hakika leo nimeona utukufu wa Mungu wa Mbinguni, Mungu aliye umba mbingu nan chi, Mungu wa Isaka, Mungu ya Yakobo…”

“Nilifungwa katika maagano ya kishetani lakini leo namshukuru Mungu kwa kumleta yule binti…” akanyoosha mkono na kidole kumuelekezea Zawadi…

“Binti amakuja kuvunja maagano niliyokuwa nayo…”

“Nilikuwa namtumikia shetani…”

Mama mchungaji alikuwa anaongea kwa kukata kata maneno kama vile akipata tabu ya kuvuta pumzi, ingawaje alikuwa ameketi kwenye kiti lakini ile hali ya mhemo ilikuwa Dhahiri wa waumini wote…

“Mwaka Fulani (aliutaja) nilimaliza masomo katika chuo cha Biblia Mwanza na huko nikakutana na bwana mmoja ambaye ndiye alinishawishi baada ya kumaliza mafunzo yale tuende Nigeria kusoma zaidi ili tuwe na nguvu nyingi za kimiujiza ili kuwaaminisha waumini juu ya nguvu za Mungu…”

“Ilinichukuwa miezi kadhaa hadi kuandaa nauli pamoja na masurufu ya safri kwa ajili ya kwenda huko Logos ambako kwa maelekezo ya bwana yule tungepata nguvu za miujiza mingiii”

“Kweli siku ya siku tulifunga safari na tukakaa huko kwa miezi 18 tukipata mafundisho mbalimbali ya kiroho na kisha ndipo nilipojikuta nimetumbukia katika maagano ya nguvu za giza ambapi mimi nilpatiwa nyoka aina ya chatu pamoja na makolokolo mengine nikawa na uwezo wa kufanya miujiza mbele za watu na kuvutia watu wengi katika huduma yangu niliporudi nchini…”

“Huduma yangu kwanza ilikuwa ndani ya makanisa mengine, nikifanya miujiza kidogo basi watu wanaamini na kuanza kuniletea pesa kuniomba niwaombee mambo mbalimbali hadi mwaka juzi nilioamua kuanzisha kanisa langu hili…”

“Kwa kushirikiana na baadhi yenu, tumefanya udanganyifu mwingi wa kuleta ushuhuda wa uongo ili tu ninyi waumini muone nguvu nilizonazo, nimetoa mapepo ya uongo mengi tu na kuendelea kujineemesha kupitia sadaka zenu...”

“Lile kapu mlilokuwa mnaliona halikuwa kikapu, lilikuwa ni joka kubwa aina ya chatu ambalo ndilo lilikuwa likihifadhi zile hela na usiku likiniamuru kwa njia ya ndoto kufanya makafara mbalimbali ili nguvu zangu zisipotee…”

“Ni mabay mengi sana nimeyafanya, lakini leo hii nimefunguliwa, Haleluyaa!”

“Haleluya!” alirudia kusema neon hilo baada ya kuona uitikio ni hafifu kutoka kwa waumini.

“Binti yule sijui ametokea wapi, maana hata siku ile ya kwanza kumuona humu kanisani nilitamani anisaidie katika kuondosha hali hii niliyonayo lakini nilikuwa sina namna…”

“Leo hii namshukuru Mungu Baba kwa kupitia huyu binti, nimevuja lile agano na lile joka limekufa kwa maana wakati nakabidhiwa niliambiwa siku joka lile likifa ama kupotea basi nguvu zangu nazo zitakufa na ikitokea hivyo basi haraka niwahi kuwenda Logos kwa ajili ya ku-update maagano…”

Aliendelea kuongea pale weee akisimulia mengi aliyokuwa nayo, mengine ya hiyari maengine hakuwa na hiyari nayo na kuonesha kujuta kwa kitendo alichofanya…”

“Leo hii niko hapa mbele yenu, lakini sina zile nguvu tena za miujiza bali nina mafundisho sahihi kama tulivyofundishwa kule Nyakato chuo cha Biblia, na kwa heshima ninaomba binti huyu aniongoze sala ya toba ili nitubu mbele za Mungu na mbele zenu…”

Zawadi akasogea mbele kwa kupanda pale madhabahuni na kuanza kusema kwa sauti nyembamba kali huku mkono wake mmoja akiinua juu…

“Niwakaribisheni nyote kumpokea YYesu kama BBwana nna MMwokozi wa maisha yako…”

“Na kufanya mana hiyo unapokea upendo wa Mungu na kumiminwa ndani ya mioyo yetu kwa uwezo wa Roho mtakatifu…”

“Inawezekana umepoa, inawezekana upendo wako kwa Mungu umepoa, unaomba tu kwa sababu una tatizo ama shida fulani, lakini shida ama tatizo hilo likiisha utacha kuomba…”

“Warumi 5 tano inatuambia… ‘Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu’…”

“Basi na tutumie muda huu kufufua imani, turudishe tena ule moto kama alivyosema habakuki katika kitabu chake sura ya tatu mstari wa pili… ‘Ffufua kazi yako katikati ya miaka…’, sasa hebu fuata maneno haya, sema…”

“Eee Mungu Baba...,

Nimekuja mbele zako…,

Naomba unirehemu…,

Naomba unisamehe…,

Zambi zangu zote…,

Nilizokukosea…”

“EE Bwana Yesu…,

Nimefungua moyo wangu…,

Nakukaribisha sasa…,

Inhia ndani yangu…,

Kwa uweza wa roho wako…,

Uwe Bwana na mwakozi na kiongozi wa maisha yangu…,

Ee Bwana Yesu…,

Ingia kwa upya…,

Fufua upendo wako ndani yangu…,

Fufua kwa upya…,

Katika JJina la Yesu…”

“Asante kwa kunihesabia haki…,

Katika Jjina la Yesu…,

Unisaidie…,

Niingiapo na nitokapo…,

Katika Jina la Yesu…,

Dhambi zisinishinde, Majaribu yasinishinde…,

Shetani asinishinde…,

Nipe mabadiliko…,

Kutoka kwenye uzima wa milele…,

Unayoyataka kwangu…,

Na shughuli ninazozifanya…,

Katika jina la Yesu…, Amen”


Wakati Zawadi akiongoza sala ile ya toba, waumini wote walifuatisha, tena kwa sauti za kutetema na kujuta na kutoa machozi…

Zawadi aliendelea…

“Kama umefuatisha sala hii kwa dhati, basi Mungu amekusamehe, na nguvu za Mungu zimeingia ndani yako, roho wa Mungu ameingia ndani yako tangia sasa, pendo la Mungu limeingia ndani yako….”

“Sasa tumejenga msingi mpya wa Imani katika maisha yetu ya kiroho. Kwa heshima kubwa kabisa sasa nimkaribishe mchungaji aendelee…”

Wakati wote huo, mpiga kinanda wa kanisa alikuwa naye akichombeza kwa mirindimo ya sautu za kuhanikiza matukio yaliyokuwa yanaendelea…

Mama Mchungaji akasogea katikati ya madhabau na kumgeukia mpiga kinanda akimwashiria kama aanzishe kitu hivi mara…

Melodi za wimbo wa kusifu zikapigwa na kwa kuwa melodi ya wimbo ule ulikuwa unajulikana kanisa zima likaitikia kibwagizo wakiongonzwa na kwanya ya kanisa…

“Ninamjua…, aliye mwamba…., ameyeniokoa… ni Bwana Yesu…”

Waumini waliimba kwa furaha na kucheza…

Kabla wimbo haujaisha, Zawadi aliwaashiria akina Vai waondoke warudi kule nyuma kwenye siti zao, walipokaribia kwenye siti, Zawadai akawaambia twendeni nyumbani hivyo wakatoka mle ndani wakati bado watu wakiimba kwa furaha kumsifu Mungu.



Itaendelea...
nimetubu bila kutarajia
 
Tupio la XVIII - The Gold Digger

Ilipoishia


“Lakini hata hivyo, itanibidi ni-maintain hali hii hii niliyo nayo hadi hapo baadaye sana au hadi nikigraduate, nataka watu wasione tofauti kubwa iliyopo kati ya jana na leo…” niliendelea kujisemea na wakati huo nilikuwa naelekea maeneo ya IFM.
---

Queen kwa upande wake aliamua kuwakomesha wote waliokuwa wanamdharau, aliamua kufanya kwanza shopping ya maana ya nguo azitakazo, za kiofisi, za mitoko mbalimbali nk.


Sasa endelea…


Chuo kilifungwa, wanafunzi walitawanyika makwao isipokuwa wale ‘waliokamatwa’ ili wamalizie vipolo vyao, Alex alikuwa ni miongozi wa waliorudi likizo. Yeye na dada yake walitumia muda huo kupanga mambo mbalimbali, maisha yakawa yanaendelea vizuri.

Mwezi wa kwanza mwishoni chuo kilifunguliwa na wanafunzi wa mwaka wao katika tahsusi aliyokuwa anachukuwa walikuwa wamerejea wote chuoni.

Alex hakuacha kuuza biashara yake ya vocha za kurusha na wala hakubalika sana kimavazi yani kifupi alikuwa ni Alex yule yule wa siku zote ingawaje safari hii alikuwa mwenye sura iliyokujuka kwa furaha na kufanyiwa usafi na salon zilizopo Shekilango ambako alikuwa akipitisha muda wake wa ziada maeneo hayo hususani Robo Green View ingawaje hakuwa mnywaji wa vileo.

Katika mwaka huu wa masomo, Alex alionekana akiwa ni mmoja watu wanaocheza Kamari za mipira mara kwa mara.

“Mwanangu, hali ngumu inabidi kubeti ili siku ya siku ukipata zari mambo yanakaa sawa…” Alex alimuambia Bony ambaye alikuwa anashangaa rafiki yake kuwa bize na kubeti badala ya kukazania masomo.

“Alex mwanangu utalosti, kwenye mademu umefaulu lakini huku sasa unapojiingiza utapoea mazima…” Bony alisema akimtahadharisha Alex

“Kubeti ni kama madawa ya kulevya mwana, utajikuta huwazi jambolingine zaidi ya kubeti…” Bony alisisitiza.

Alex alianza kubeti kwenye kila kipidi cha redio, kwenye vipindi vya runinga kwenye mipira hadi akaanza kubeti kwenye kampuni za nje ya nchi zijihusishazo na mipira.

Mara kala kilo, mara elfu 50, mara laki 2 ilimradi alikuwa anabeti na akipata lazima wagawane na rafiki yake Bony.

Hali iliendelea hivyo hadi wanafunzi wenzie wakawa wanajuwa kuwa Alex amepata uraibu (addict) wa kubeti.

Bahati nzuri Alex alikuwa yupo vizuri darasani hata kwenye kazi kwa vitendo, hivyo kucheza kwake Kamari hakukumuharibia masomo.

Siku moja Alex akatangazwa mshindi wa milioni 10 kwenye jackpot iliyochezeshwa na kwenye kituo kimoja cha runinga. Nchi nzima ikajua kuwa Alex amepata milioni kumi, na wadada wa pale chuoni wakaanza kujisogeza.


Alex anasimulia…


Baada ya kutafakari kwa muda nilipopata urithi ule, nilitaka nisibadili maisha yangu kwa haraka bali nitafute sababu itakayosaidia kuonekana kwa kubadilika kwangu kimaisha. Lakini pia kwa kuwa bado nilikuwa nampenda Emmy nilitaka nimpate kwa hali na mali.

Kwa bahati nikaona tangazo wa kuuzwa kwa nyumba za mamlaka ya bandari zilizopo masaki, hivyo nikafanya kila linalowezekana kwa kutumia jina la Kampuni anayosimamia dada Queen nikainunua ile nyumba na Dada Queen akanunua nyumba mbili za kawaida ambazo alizivunja zote na kuanza ujenzi wa kasri lake matata na wakati huo yeye tayari alikuwa amepanga kwenye apartment nyingine huko huko Masaki. Hayo yote yalitokea kati ya mwezi Disemba mwanzoni na Januari katikati. Tulikuwa fasta hatari dada akitaka kuonesha rangi zake zote na mie nikiwa vile vile lakini kichwani nikiwa nina yangu.

Ingawaje nilishainunua ile nyumba yetu tuliyofukuzwa zamani, lakini niliendelea kuishi Manzese na nikaanza ukarabati kidogo kidogo wa ile nyumba kwa kutumia kampuni ya kuziboresha nyumba.

Sasa baada ya kushinda ile milioni kumi, nikawa nimepepata sababu ya mimi kuanza kubadilika kimavazi na kimuonekano kwa ujumla.

Kwakuwa wenzangu wengi walikuwa wanajuwa nacheza sana kamari za kubashiri kuhusiana na mipira, nilihakikisha kila nikishinda watu wanajuwa na nikawa nawatoa wana kwa chakula na vocha kiaina.

Hali iliendelea hivyo hadi nilioanza kupunguza kugawana ushindi na wana ingawaje wao walikuwa wanajuwa nimekula. Kuna siku nilidanganya watu kuwa nimeshinda milioni hamsini kwenye Admiral Bet na Eurobet milioni 7, nilifanya hivi ili watu wajue chanzo cha hela zangu ni kubeti lakini ukweli haukuwa hivyo. Kweli nilishinda kiasi fulani kwenye hizo kampuni lakini hakikuwa kingi kihivyo.

Mwezi wa tatu nikanunua Harrier mpyaa (kibongobongo), niliagiza kutoka japani, ilikuwa ni hybrid, rangi nyeusi. Mwezi wa nne nikaanza kuonekana nalo pale chuoni.

Nikaanza kula good time na washikaji kuwatoa out siku za weekend na kufurahia maisha lakini wakati wote huo sikuwa na demu permanet ingawaje nilikuwa naenda kule Sinza kupata wa kuchaguwa nikizidiwa, nafanya starehe zangu mambo yanaisha bila kufungana minyororo.

Nikawa na jina kubwa sana pale shuleni kwa ukarimu kwa wana na matokeo mazuri, hali ile ilimvutia tena Emmy na kujisogeza kwangu akimtema John ambaye sasa alikuwa apache alolo kwakuwa baba yake alifilisiwa kutokana na utakatishaji wa pesa na yuko chini ya uangalizi wa Takukuru.

Pamoja na Emmy kujisogeza kwangu, sikumfukuza (nilikuwa nampenda) lakini pia sikumshobokea maana nilikuwa na uwezo wa kupata pisi kali yoyote mjini iliyopo sokoni. Siku moja akiwa kwenye harrier yangu, ijumaa jioni tukiwa maeneo ya Ocean Road upande wa baharini tukila madafu, Emmy aliniuliza…

“Babe, milioni sitini zako zote ndio umenunua gari hii?”

Nikamjibu…

“Hapana, hii kila kitu imenigharimu milioni 37 hivyo bado nina milioni 30 ndani…”

Emmy: “Oh baybe, I love you so much, unajuwa John yule ni mshamba, hajui mapenzi halafu gari lake sio zuri kama hili, lako lipo kimya kama zimezimwa vile hata likitembea…”

Moyoni nikawaza, huyu wala hajabadilika, yuko vilevile mpenda pesa. Nikaona ni vyema nimpe mtihani wa mwisho kabla sijafanya maamuzi ya kumrudia rasmi.

Siku hiyo usiku tuliupitisha pamoja na Emmy katika moja ya Hotel alizopenda kwenda na John, niliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumuonesha jinsi moto unavyopelekwa mtu akiwa hana stress za hela…

“Oh Alex, you are killing me!”

Kiingereza kingi wakati nampelekea moto kwa hasira zilizojikusanya, nilidhani namkomoa kumbe ndio nampa raha…

“You are the one Alex, No one does like you not even John…” alikuwa akilalama

Kesho yake nikiwa na Emmy nilienda Ocean Road Hospital, lengo lilikuwa kuwatembelea wagonjwa wa pale. Kuna wagonjwa wanapitia changamoto nyingi sana, kwa wale wenye utaratibu wa kutembelea hospitali watakubaliana nami.

Kwenye droo ya gari kulikuwa na bahasha yenye shilingi milioni kumi. Emmy alikuwa hajui na droo ilikuwa imefungwa na funguo.

Nikampa funguo, nikamwambia…

“Emmy, chukuwa hiyo bahasha tuingie nayo hospitali…”

“Ina nini hii babe, isije ikawa madawa ya kulevya!...” alisema huku akiwa anacheka lengo lake tu afunue aone kuna nini, ila wanawake na pesa! Maana dalili zote ile bahasha iliashiria kuna pesa ndani.

“Wow! “ kwa mshangao Emmy alisema

“Ziko ngapi hizi..” aliuliza

Nikamjibu “Hizo ni milioni kumi” kisha tukatoka kwenye gari na kuelekea mapokezi ambapo niliomba kuonana na nesi wa zamu kitengo cha kuhudumia wagonjwa wa saratani.

Muda wa kuwaona wagonjwa asubuhi ile ulikuwa umeisha, hivyo isingekuwa rahisi kwenye wodini bila kufuata utaratibu wa ziada.

Baada ya salamu niliomba kuwajuwa wagonjwa wenye changamoto za kiuchumi kwenye wodi anazozisimamia.

“Wote mdogo wangu waliolazwa humu wana changamoto za kiuchumi, wenye nazo hawalali humu labda siku ya kufanyiwa tiba za miozi au kemo (Chemotherpy), wenye uwezo kwa hapa Dar wapo kule mwenge kwenye Hospitali ya familia ya Dr. Ngoma. Hivyo wote humu wana hali ngumu tu mdogo wangu, kimaradhi na kiuchumi… umewaletea nini leo wagonjwa wangu…”

Nesi yule mcheshi na muongeaji aliongea pale mfufulizo, nahisi atakuwa mzaramo yule, ila ana roho ya upendo sana kwa wagonjwa.

Hii imekuwa mara ya pili kukutana naye hapo hospitali ingawaje tayari nimeshafanya ziara hapo mara sita na mara zote nikija nilikuwa nampa kila mgonjwa elfu kumi na pia huwa nawapa mafuta maalumu kwa baadhi ya wagonjwa. Sikuwa nabeba vyakula. Tangia nimepata ule urithi niliamua kufanya kawaida ya kutembelea hospitali moja wapo kila jumamosi na kugawa elfu 10 kumi kwa wodi iliyobahatika siku hiyo.

Nesi yule hivyo hakuwa mgeni kwangu…

“leo umewaletea nini wagonjwa wangu..” aliuliza tena alipoona nimezubaa kwa kutafakari.

“Eee leo mimi na mchumba wangu tumewaletea pesa wagonjwa, wako wangapi waliolazwa?” niliuliza kisha nikamwangalia Emmy nione sura yake itaniambia nini hata kama hatosema kitu…

“Leo wapo wagonjwa (akataja idadi ) ila kuna wale wanaokuja na kutoka ni wengi kuliko hawa waliolazwa…

Baada ya maelezo ya nesi na kupata idadi ya timu nzima ya siku hiyo na kwa vilelelezo vya maandishi kwenye jedwali maalumu kwa nesi wa zamu, niliridhika nikaomba tuongozwe wodini manesi wakiwa wawili, mimi na Emmy pia.

Emmy nilimpa kazi ya kuzifungua zile hela zote maana zilikuwa zimefungwa kwa barabendi (rubberbend) ili zisiwe zimetenganishwa. Kwa idadi ile niliyoambiwa na nesi kwa hesabu za harakaharaka nikaona hapa nikigawa noti tano za elfu kumi kwa kila mmoja hela zitakaribia kuisha ambapo ndio lengo langu.

Tukaanza wodi ya kwanza, nikawa nachukuwa mkono mmoja wa hela, kisha nagawa kwa mgonjwa husika, bahati nzuri wote walikuwa wenye kuongea wenyewe…

“Pokea hii elfu 50 itakusaidia…” hiyo yalikuwa maneno yangu kwa kila mgonjwa baada ya kumpa pole na kumtia moyo…

“Asante kaka.., asante mwanagu, asante mjukuu, asante… asante…” yalikuwa maneno yaliyofutia baada ya kuwapa hela kisha waliniombea na dua Mungu anibariki nami sikusita kuitikia amina, amina, amina…

Tulifanya hivyo kwa muda mrefu, siku nyingine huwa kazi hiyo nawaachia manesi lakini na wao pia nawaachia za kwao ili kuondoa tamaa.

Sura ya Emmy muda wote haikuwa sawa, alikuwa amenuna kiasi, ingawaje alijitahidi kutoa tabasamu. Lakini Emmy mimi namjua vizuri tangia utoto. Hakufurahia kitendo kile kana kwamba namaliza hela. Kwa hesabu zake baada ya hapo nitabakiwa na milioni ishitini pekee nay eye hajapata hata senti moja zaidi ya chakula cha hotelini kule, malazi basi.

Baada ya takribani saa moja hivi na ushee zoezi zile lilikuwa limeisha, hatukuingilia raundi za madaktari maana tuliongozwa na nesi wa zamu kwa kuhepa sehemu tulizokuta kuna raundi inaendelea na kuingia sehemu nyingine kisha kurudia pale tulipoishia awali hadi zoezi zikaisha.

Tulivyomaliza lile zoezi, kulibakia hela kiasi kilichotosha pia kuwapa motisha manesi wote na madaktari wote waliokuwepo siku hivyo kiasi kama tulichowapa wagonjwa. Ilikuwa furaha sana kwangu lakini kwa Emmy haikuwa hivyo…

“Mchumba wako anaumwa?!” aliuliza yule nesi muongeaji sana…

“Mimba changa tu hiyo inamsumbua…” nilijibu kuficha ukweli.

Emmy tangia alivyonipiga kibuti kwa dharau, jana ndio ilikuwa siku ya kwanza kulala naye na sikuuza mechi. Hivyo suala la mimba wala halipo kabisa na jibu lile lilimfanya Emmy akunje uso zaidi.

Hatimaye zikabakia pesa chache ambazo nikamwambia Emmy…

“Hizi tutaenda kujazia mafuta…”

Tuliondoka eneo la Hospitali huku tukipungiwa na kuoneshwa tabasamu na manesi waliokuwepo pale jirani.

Kwenye gari kukawa na ukimya hadi tulivyofika kituo cha mafuta.

“Jaza full…” nilimuamuru yuke mhudumu pale kito cha mafuta…

Tukaletewa risiti ikionesha shilingi laki moja na ishirini na tano…

“Mpatie hizo hela…” nilisema bila kumjuza tunatakiwa tulipe kiasi gani.

“Zote?!” aliuliza Emmy.

“Ndio mpe zote kwani zimebaki kiasi gani…” niliuliza

Hata hakujibu, akachukuwa bahasha nzima akampatia yule mhudumu…

Nikamwangalia Emmy sikummaliza…

“Boss, bado elfu kumi na tano…” sauti ya mhudumu ilisikika huku akiinama usawa wa dirisha.

Nikatoa noti tatu za elfu tano zilizokuwepo kwenye droo ndogo iliyo karibu na ‘gear lever’ na kumkabidhi Emmy ili ampatie yule mhudumu.

Tulivyoondoka tu pale, Emmy akanyanyua mdomo…

“Yani umegawa hela zote hata hujanipeleka shopping sasa si utaishiwa, halafu mie hujanipa hata shilingi hebu nipeleke nyumbani kwanza nikapumzike…”

Majibu ya awali nikapata kuwa Emmy bado yupo ’after money’ na wala hana mapenzi ya kweli. Nikaivurumisha gari hadi Masaki kwao , nilipita pale kwangu kama sipajui.

Akashuka kwa hasira na kuondoka bila kuaga wala kufunga mlango. Nikashuka na kuufunga mlango kisha nikarudi kwenye gari na kwenda pale site kuangalia maendeleo.
---


Itaendelea wakati mwingine panapo majaaliwa.
 
Tupio la XIX - Learning English

Ilipoishia…


Usiku huo, Omari hakupata usingizi mzuri, alijawa na mawazo mengi…

“Bora niende tu huko ughaibuni…” alijisemea baada ya kutafakari kwa muda mrefu.

Akachukuwa ile barua iliyotafsiriwa na kuisoma mara kwa mara…

“Kesho nitaipeleka hii orijino kwa mtu mwingine anitasfirie nione kama Frank alinitafsiria sawa…” hatimaye akapitiwa na usingizi…



Sasa endendelea…



Kulivyokucha tu, Omari akamuaga mama yake ambaye tayari alikuwa ameamka, baba yake alikuwa bado yupo ndani amelala, alitoka moja kwa moja kuelekea mjini posta.

Omari alikuwa analekea kwenye kituo kiitwacho ‘English Fountain College’, aliona tangazo kwenye nguzo za umeme zilizopo Kawe na kupata shauku ya kwenda kutafsiriwa ile karatasi yake.

“Pale ni chuo, sidhani kama watanitafsiria uongo…” alikuwa anawaza alipokuwa ameshuka kwenye daladala na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea mtaa wa Samora.

“Samahani dada, habari? eti chuo hiki kiko wapi… “Omari alimuuliza dada aliyekutana naye maeneo ya Twiga mtaa wa Samora huku akimuonesha ile karatasi aliyoibandua kwenye nguzo ya umeme…

“Poa, ahaa, hawa wapo hapo ‘Mata Salamat Mansons’ jirani na stendi ya mwendokasi…” yule dada alijibu na kuonesha uelekeo na kuendelea na safari yake…

Baada ya kona na kuulizia ulizia hatimaye akafika alipokusudia.

Alieza shida yake na akatatuliwa vizuri lakini pia alishawishiwa kujiunga nao ili asome kozi ya muda mfupi. Hakukubaliana moja kwa moja kuhusu suala la kusoma hapo lakini alishukuru kwa kutafsiriwa ile karatasi yake ambapo haikutofautiana na tafsiri iliyotolewa na Frank wa Kawe.

Moyoni alifurahi sana kwa kujuwa hajalishwa ‘matango pori’, na wazo wa kusoma kozi fupi likawa linatembea kwenye akili yake.

Alirudi maoja kwa moja nyumbani, akamkuta baba yake yupo nyumbani ambapo si kawaida yake, akamsalimia kisha akaenda kuchukuwa kapu lake na kuelekea pwani.
---

Leo mke wangu sikwenda kazini, nimemuomba afande Kesi akaniombee ruhusa kombaniani. Nataka leo nifurahie maisha ya kuwa nyumbani, kama nilivyosema jana kuwa nilikuwa sijalewa na nilichokisema nilimaanisha, hivyo leo mchana nitakuwepo hapa, usonge ugali tule na jioni pia sintotoka kwenda popote.

Yalikuwa maneno ya afande Juma, baba yake na Omari aliposema wakati akinywa chai nyumbani kwake kitu ambacho pia haikuwa kawaida yake kwa muda mrefu.

“Omari anajituma sana, kumbe kazi za pwani zinalipa eee!” alimdadisi mkewe.

“Hivyo hivyo zinamsaidia, na wakati mwingine husaidia sana kuinua genge langu linapoporomoka kibiashara, tumuombee dua tu mambo yake yamnyookee…” Mama Omari alijibu.

Siku hiyo Omari aliwahi kurudi nyumbani, kazi haikuwa nzuri sana ingawaje alileta kitoweo cha samaki mchanganyiko.

“Leo upepo wa kusi umefanya yake, hamna samaki…” alisema Omari kumwambia mama yake pale gengeni kwake.

“Mama, nimepata wazo la kutumia pesa hii kidogo kujisomesha, kuna sehemu niliona kule Mwenge wanaita kwa Ras Simba wanafundisha kiingereza cha kuongea kwa haraka, kesho mapema nitaenda kuulizia utaratibu na kujiunga…”

Omari aliweka wazo lake mbele ya mama yake, asijue baba yake yupo tu sebuleni amejilaza kwenye kochi akifuatilia taarifa za kwenye runinga.

“Nenda kamshirikishe baba yako pia yupo sebuleni, mie wala sina kipingamizi midhari huendi huko ughaibuni…”

“Ha!, baba yupo, hakwenda kazini leo?” Omari aliuliza kwa mshangao kisha akapanda ngazi (ya tofali moja) kuingia sebuleni.

“Shikamoo baba…” alisamilia Omari.

“Marhaba mwanangu. Isingekuwa wale wajinga kukubania, leo ulitakiwa usalimie jambo afande baba…”

Afande Juma alijibu na kufanya masihara na mwanae.

Omari alivyomaliza darasa la saba, baba yake alimfanyia mpango kuingia jeshini. Kwenye mchujo wa kwanza tu aliandikiwa ‘UBS’, yaani hafai kuwa mwanjeshi. Baada ya majibu yale Omari hakutaka tena kusoma wala kazi nyingine zaidi ya kazi za daladala.

“Ningejiendeleza sasa hivi wewe ndio ungekuwa unanipigia saluti…” Omari alijibu masihara yale kwa baba yake.

“Aaa wapi, ningekuwa navaa kiraia, wewe na minyota yako bado ungenisalimia kwa heshima…” afande Juma alijibu kisha wote wakawa wanacheka.

Ilikuwa ni wakati mzuri sana kwa baba na mwanawe kuwa pamoja na kufurahi siyo kama ilivyokuwa siku nyingine mambo ya amri amri tu.

“Baba leo hukwenda kazini? Si kawaida yako kuwepo nyumbani mida hii..” Omari akapata pa kuchomekea…

“Sikwenda mwanangu, sijisikii vizuri, leo niliona nipumzike nyumbani niwe na familia yangu…” alijibu afande Juma.

Punde si punde, mama Omari akaingia na vipande vya embe dodo akiwa ameviandaa vizuri na kuweka pale mezani. Familia ikawa inafurahia kuwa pamoja kwa amani huku wakiburudika kwa tunda la embe.

Waliendelea kuzungumza pale mambo mbalimbali, mama Omari naye akiwepo lakini alihudumia wateja wake pale gengeni wakifika…

“Gengeni!, Samaki fungu moja!” ni moja ya aina ya uitaji wa wateja wakihitaji huduma, hivyo mama Omari alikuwa akiwahudumia mahitaji yao kisha anarudi kuungana na familia kuzungumza.

“Baba, leo nimefikia uamuzi wa kujifunza kiingereza, fursa nyingi zinanipita kwa sababu ya kutokujuwa kiingereza…” Omari alichomekea hoja yake…

“Fursa gani mwanangu zinakupita…” Afande Juma aliuliza kwa upole…

“Nimewaza kazi za kutembeza watalii yani beach boy, naona kuna watu kule pwani wanatembea na wazungu wanapewa midola na maisha yao yanakuwa mazuri..”

“Umewaza vizuri mwanagu, sasa utajiunga na shule gani uanze form one, si itakuwa ya kulipia!!” Baba Omari alidadisi

“Hapana baba, sijiungi na sekondari, bali nataka kesho niende pale Mwenge kwa Ras Simba wanafundisha kuongea kiingereza…” Omari alijibu.

“Ok, basi wewe kesho nenda, ukishajuwa utaratibu mimi nitakulipia ada mshahara ukitoka maana hii ya ‘resheni’ ameandikwa mama yako kwa ajili ya kuendeshea maisha ya kila siku hapa nyumbani.” Afande Juma alijibu na kumuunga mkono hoja yake.

“Mwanangu, usije ukaanza kufuga rasta tu maana nasikia wazungu wanapenda vijana wenye rasta wawatembeze…” Mama Omari aliasa pale kwa kukwepesha pointi kiaina.

“Sifungi nywele mama, mie mnyoo wangu huu huu wa nywele za kuota, hazinipi tabu kuzisafisha, hazinichukulii muda kuzihudumia na pia gharama za kuzihudumia ni ndogo, kwa wiki natumia jero tu…” alisema Omari akijitetea kwa pointi zenye mashiko kiaina.

Waliendelea na maongezi yao hadi jioni kabisa, wakala chakula pamoja na kuendelea kuangalia vipindi kwenye runinga pamoja hadi muda wa kulala ulipowadia.
---


“Kujiunga na masomo ya kuongea kiingereza bei gani…?”

Aliuliza Omari alipofika pale kwa Ras Simba baada ya kusalimia na kukaribishwa.

“Shilingi milioni moja na nusu utafuatwa popote pale utafundishwa na kwa program ya miezi mitatu hapa hapa ni shilingi laki tano tu…” alijibiwa na yule mhudumu aliyemkuta.

“Du! Laki tano miezi mitatu!” Omari alishangaa

“Mbona kidogo hiyo kaka, kuna faida nyingi ukijuwa kuongea Kiingereza na wala hiyo laki tano siyo ghali, maana ukishajuwa itakulipa zaidi ya hiyo uliyotoa…” aliongea yule dada wa mapokezi.

“Sawa, ngoja niwasiliane na mlipa ada kwanza nitarudi nikiwa tayari…” Omari alijibu na kuaga.

Kutokea pale Mwenge akachukuwa daladala hadi Stesheni ambapo alitembea kwa miguu hadi pale English Fontain na kuuliza ada ya kozi fupi ya kuongea kiingereza.

“Hapa tuna kozi nyingi na bei zetu ni nafuu sana, shika hii bronchure uone…” mhudumu akampatia karatasi iliyo ainisha kozi watoazo…

Wanaoanza 150,000 kwa miezi miwili

Wakatikati ngazi ya kwanza 170,000 kwa miezi miwili

Mara ghafla macho ya Omari yakaangukia kwenye kozi fupi maalumu…

Kiingereza 150,0000 kwa mwezi.

Hakutaka hata kusoma kwingine, akauliza...

“Hii ya kusoma mezi mmoja naweza kuanza lini!?” aliuliza na kuonesha pale aliposoma

“Ni wewe tu, hata kesho njoo uanze…” alijibiwa Omari kisha akaondoka.

“Da! Laki moja na nusu hata mjeda akizingua nitajilipia, ngoja kesho nije nianze…” Omari alijisemea.



Inaendelea…
 
Tupio la XX - Kipaji maalum Darasani

Ilipoishia...


Waumini waliimba kwa furaha na kucheza…

Kabla wimbo haujaisha, Zawadi aliwaashiria akina Vai waondoke warudi kule nyuma kwenye siti zao, walipokaribia kwenye siti, Zawadai akawaambia twendeni nyumbani hivyo wakatoka mle ndani wakati bado watu wakiimba kwa furaha kumsifu Mungu.

Akina Vai walirudi nyumbani wakiwa wamefurahi, walimkaribisha Zawadi ili wapate wote chakula cha mchana kisha ndio arudi kwao.

Nyumba ya Vai ilikuwa ni sehemu ya watu kukutana sasa, kila jumamosi asubuhi kwa ajili ya jumuiya na jumapili jioni kwa ajili ya maombi ya kusifu na kuabudu.




Sasa endelea…




Watu wengi wakawa wanakuja pale kupata maombezi kutoka kwa yule mtoto Zawadi na habari zikaanza kuenea Kihonda. Nyumba ikawa maafuru na watu wajao wakatoa wazo la kuweka uzio, michango ikapitishwa na baada ya wiki kadhaa uzio ukawa umekamilika, mazingira yakawa yana stara.

Nyumba aliyokuwa anaishi Zawadi ilikuwa ni ya familia ya kiislamu, waislamu wale ambao sio wenye misimamo sana inagwaje mtoto wao mkubwa alikuwa anahudhuria madrasa na muda mwingi alikuwa anavaa kanzu na kofia hadi watoto wenzake mtaani wakampachika jina la ‘Ustadhi’ na mama yake akawa anaitwa mama Ustadhi na baba yake alikuwa anaitwa baba Ustadhi.

Ratiba za huduma zilifahamika vyema kwenye familia hiyo ambayo Zawadi alikuja kuwasaidia kulea mtoto kama yaya! Hawakuwa na kipingamizi juu ya Imani yake wala huduma azitoazo maana ilifikia mahali waumini walianza kutoa asante katika huduma yake, awali alikuwa anakataa lakini baadaye akawa anachukuwa na kuzipeleka nyumbani anapoishi baada ya kuzigawa nusu akiwaachia akina mama Rose na mama Vai ambao nao walikuwa wanachukuwa sehemu ya fedha hizo na kuimarisha sehemu za maliwato kwani sasa watu walikuwa wanakuja wengi kwa mara moja siku za jumamosi na jumapili.

Walifanikiwa kujenga matundu mengine matano ya vyoo na kufanya matundu kuwa sita hivyo kuweza kuhudumia vizuri wageni wajapo. Pia waliimarisha sakafu na kufanya mandhari kuwa nzuri.
---


Siku zilienda na Onesmo (Junior) akawa mkubwa kwenye kuanza kuongea maneno. Mle kwao walishasahau kabisa lile suala la kimiujiza la mtoto kuhudumiwa na asiyejulikana.

Onesmo na Rose wote waliandikishwa katika shule ya awali ya karibu maeneo hayo na wakawa wanashinda huko wakati wazazi wao wakifanya biashara zao za kuuza matunda barabarani lakini ikifika siku ya ijumaa hadi jumapili huwa hawaendi kwenye biashara zao ingawaje huwaachia wenzao wawauzie.

Walikuwa na kibarua kikubwa cha kuandaa mazingira ya huduma pale nyumbani kwao kwa wao kwanza kujikumbushia vifungu katika biblia na pia kuandaa maakuli kwa ajili ya wageni wa jumuiya kesho yake na jioni kuandaa vyakula vidogo vidogo kwa ajili ya wana maombi kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristu.

Junior alionesha uelewa wa haraka akiwa shule hiyo ya chekechea kwa kuweza kutambua tofauti za rangi, sauti za milio mbalimbali, upangiliaji wa vitu yani kwa kifupi alikuwa amezidi kile kiwango tarajiwa cha wanafunzi wa ngazi yake.

Akiwa na miaka mine tu ilibidi walimu wamjaribishe kufanya mtihani ambao kama angefaulu basi wangemhamishia darasa la kwanza katika shule ya Saint Anne Marie. Mtihani ule aliufanya vizuri kiasi cha kuwaridhisha walimu wa shule ile ya chekechea kuwa mtoto huyo ataweza kumuda masomo ya darasa la kwanza bila tabu.

Mwaka uliofuata, Onesmo alihamishiwa kwenye shule ya msingi ya kulipia hapo St. Anne. Wala haikuchukuwa muhula kwa walimu wote shule hiyo kutambua kipaji cha mtoto huyo. Alikuwa anafanya vizuri sana licha ya utundu aliokuwa nao katika kucheza michezo mbalimbali ya kitoto.

Sister mmoja ambaye ndiye alikuwa mwalimu wake wa darasa, aliamua kumpa elimu ya darasa la pili ili ikifika mwisho wa muhulia siku ya kufanya mtihani apewe mitihani yote ya darasa lake na ya darasa la pili.

Walimu wote walishangazwa na uwezo wa Junior maana mitihani yote alifaulu kwa kiwango cha juu na huo wa darasa la pili alishika nafasi ya pili nyuma ya mtoto mmoja wa mwalimu ambaye yeye alipata mia kwa mia masomo yote.

Shuleni ikawa gumzo, na siku ya kufunga shule mhula wa kwanza walimu walitaka kuwaona wazazi wake na kuwapongeza kwa malezi mazuri ya Onesmo Onesmo.

“Mmh, Junior yupo hivo hivo, ukimfundisha kitu anashika mara moja, jaribuni kumfundisha mtaala wa darasa la tatu muone…” Vai aliongea mbele ya kikao cha Mwalimu mkuu, mwalimu wa darasa na mwalimu wa taaluma siku alipoitwa shuleni.

“Mtoto huyu ana kipaji maalum, hebu ngoja tumuandalie program maalum itakayoenda sanjari na masomo yake ya darasa la kwanza muhula wa pili.

Mwisho wa muhula wa pili Junior alipata mia kwa mia mitihani ya darsa lake na kuwa wa kwanza darasani, pia alipata alama ‘A’ kwenye mitihani yote ya darasa la pili na kushika nafasi ya pili tena ingawaje yeye alikuwa darasa la kwanza na pia alifanya vizuri mitihani ya darasa la tatu akiwa ameshika nafasi ya nne kama vile angekuwa darasa hilo la tatu.

“Baba yake yuko wapi?” aliuliza mkuu wa shule ya St. Anne…

Ilikuwa siku ya kufunga shule ambapo wazazi wa wanafuzi walialikwa kuhudhuria mkutano maalum na swali hilo liliulizwa hadhrani baada ya kuona zawadi karibia zote za kitaaluma za darasa la kwanza , la pilli na la tatu akipokea yeye.

“Baba yake alishafariki siku nyingi kwa ajali ya gari…” Vai alijibu kwa huzuni na aibu kiasi…

Alivyosimama kujibu lile swali, wazazi wengine ndio wakamuona sasa mama Junior na minong’ono ikaanza chini kwa chini…

“Ni yule mama wa maombi…”

“Ni yule dada wa Zawadi wa miujiza…”

“Ni yule mwenzake na mama Rose kule kwenye nyumba ya maomi”

“Ni yule aliyekuja na aliyemuumbua mama mchungaji kabla hajamuokoa…!”

Yani ilikuwa ni minong’ono iliyokuwa na hisia kali na kwa nia njema kabisa na wote wakajikuta wanapiga makofi kumpongeza mama Junior pale aliposema…

“…Hivyo tangia utoto nimemlea mwenyewe tu.”

“Baada ya mkutano huu nakuomba wewe na Onesmo mje ofisini kwangu…” Mkuu wa shule alisema pale kisha akaendelea na ratiba za mkutano wa wazazi.

Mkutano ulivyoisha, wazazi wakatawanyika lakini mama Junior, mama Rose na wanawe hawakuondoka, kukaandaliwa kikoa cha dharura cha walimu wote na mkuu wa shule wakijumuishwa Vai na Onesmo, mama Rose alikuwa nje akisubiri mwenzake ili warudi wote.

Kikao kilijadili kipaji maalumu cha Junior na kisha wakajadili maisha ya wazazi wake ambapo sasa baadhi wa walimu waliosikia ile minong’ono ya kwamba mama Junior ana huduma ya maombezi nyumbani kwake wakitaka kujua zaidi…

Hitimisho la kikao hicho ikawa ni St. Anne kuamua kumfadhili mtoto katika masomo yake kwa programu maalum watakayo muandalia.

Mama Onesmo alifurahi kupunguziwa mzigo wa kugharamia ada na pia kutambuliwa kwa uwezo wa mtoto wake kitaaluma.

Waliondoka pale eneo la shuleni na kuwahi kurudi nyumbani ambapo jioni hiyo kulikuwa na kuandaa kwa ajili ya jumuiya asubuhi.



Inaendelea…
 
Tupio la XXI – Ofisi Ya Jumla

Ilipoishia…


Tulivyoondoka tu pale, Emmy akanyanyua mdomo…

“Yani umegawa hela zote hata hujanipeleka shopping sasa si utaishiwa, halafu mie hujanipa hata shilingi hebu nipeleke nyumbani kwanza nikapumzike…”

Majibu ya awali nikapata kuwa Emmy bado yupo ’after money’ na wala hana mapenzi ya kweli. Nikaivurumisha gari hadi Masaki kwao , nilipita pale kwangu kama sipajui.

Akashuka kwa hasira na kuondoka bila kuaga wala kufunga mlango. Nikashuka na kuufunga mlangu kisha nikarudi kwenye gari na kwenda pale site kuangalia maendeleo.


Sasa endelea…


Alex anasimulia…

Dada Queen yeye kama nilivyosema awali aliamua kujipambanua kwa mabadiliko makubwa, alinunua gari ya kutembelea, alinunua Rav4 mpya ya kisasa kabisa, mpya yani zero kilomita, aliagiza kupitia Toyota motors Tanzania na ilikuwa ni hybrid pia. Ilikuwa na rangi nyekundu na ‘full option’ ndani. Kule Tabata walikopanga na rafiki yake Mourine walihama na kuhamia kwenye apartment mpya aliyopanga Queen maeneo ya Masaki, na aliendelea kusimamia ujenzi wa kasri lake alilokuwa analijenga maeneo hayo hayo ya Masaki jirani na bahari ingawaje hapakuwa jirani na ufukweni.

Baada ya kumaliza kufuatilia mambo ya kampuni aliorithishwa na baba na mambo mengine yote ya mirathi ndipo siku hiyo akiwa peke yake chumbani kwake Masaki akapiga ile namba iliyotuma meseji.

“Hallow…!” upande wa pili wa simu ulijibu…

Queen akasema… “kumi na moja kumi na mbili moja…”

“Owh”, hatimaye umeripoti…” sauti ya upande wa pili ilimjibu kisha ikasema…

“Ok, jitambulishe kwa majina yako matatu tafadhali…”

Queen akajibu “Naitwa Queen Jonathan Ngonyani”

Sauti kutoka kwenye simu ikasikia: “Mwambie Mourine akulete ofisi ya jumla.”

Queen: “Mourine yupi?!”

Sauti kutoka kwenye simu: “Mourine rafiki yako mnaye ishi wote” kisha simu ikakatwa.

Queen akabaki na mshangao mkubwa… “…yani siku zote hili jambo ingawaje sikumshirikisha Mourine lakini kumbe anahusika!...”

“Sijui ni watu gani hawa, isje kuwa Mourine ameshaniuza kwa watu bila mie kujua…” alijiuliza na kushangaa bila majibu.

“…Sasa kwanini siku zote hizi hata haniambii…” aliendelea kujiuliza maswali mengi pasipo majibu.

“…Okay, njia moja tu ya kupata majibu sahihi, ngoja nimpigie Mourine…” aliamua.

Alimpigia na kumwambia kuwa ana dharura ili Mourine akatishe mishe zake awahi kurudi nyumbani.

Mourine alirudi mida ya jioni wakati jua ndio linazama na kumkuta Queen akiwa na mawazo huku akiwa anakujwa mvinyo taratibu.

“Shoga, zipi kuna shida gani?...” Mourine aliuliza baada ya kuwasili

Mourine na dada Queen ni marafiki wa siku nyingi ambao walikutana kule Ambience Sinza katika harakati za kujitafutia riziki kwa njia ya kuuza miili yao. Na ni yeye aliyemshawishi wahame sinza ili wapange Tabata nyumba nzima wagawane upande na kusongesha maisha kwa njia hizo bila ya kuwa na bughuza na wapangaji wengine mara umeme siju umeisha mwenye zamu hataki kuchanga, mara maji yamechaa kwnye choo hivyo mchango wa kuyavuta unahitajika, mara kugombana na wapangaji wenzao kwa sababu zisizo za msingi yani zile kero zote za kupanga nyumba wapangaji wengi walitaka waziepuke ili wawe huru zaidi…

“Tukiwa kwenye nyumba yetu, tutakuwa huru hata kuleta madanga yetu home na kuinjoi nayo huku tukifaidika na mihela yao kuliko huku uswahilini…” hii ilikuwa ni moja ya sentensi zilizomshawishi Queen kuchangia nusu pango huko Tabata.

Na kweli tangia wahamie kule, mambo yao yalikuwa safi zaidi, ustaarabu zaidi, kujiachia zaidi hadi siku ile nilipoenda kumkuta pale kitambaa cheupe Tabata.

“Yani wewe shoga ndio wa kuniuza mimi kwa madaga nisiyoyajua?!...” Queen alimvaa rafiki yake

“Madanga gani tena dada!...” Mourine aliuliza kwa mshangao…

“Unajifanya hujui!!! Haya sasa nimeambiwa unipeleke ofisi ya kuuza jumla jumla…” Queen alijibu.

Ghafla Mourine akabadilika! Akavuta pumzi na kutulia.

“Hebu nisogezee hiyo wine kwanza!” alisema Mourine.

Queen akamsogezea chupa ya dompo na glass kisha akamiminia kisha akasema…

“Enhe, lete umalaya wako sasa, nakusikiliza …”

“Uliambiwa ofisi ya kuuza jumla jumla au ofisi ya jumla!” Mourine alisema kisha akapiga funda lingine refu la mvinyo ule.

“Hata sikumbuki, lakini neno jumla lilikuwepo, ndio umeniuza jumla nini!” Queen alijibu na kuongezea kautani kidogo…

“Ni ofisi ya jumla wewe na siyo ofisi ya kuuza jumla jumla hahahah! Mourine naye akajibu na kucheka kidogo…

“Haya shoga niambie, danga gani lipo hapo, inaonekana amenisubiria sana…!” Queen alijifariji…

“Skiza shogaangu…” Mourine alianza maelezo…

“Hakuna danga wala nini, ni suala muhimu sana la kazi, kwa muda mrefu ulikuwa unahitajika kusaidia lakini ilikuwa kwanza itoke ndani yako baada ya kupitia mpango fulani ambao mimi nimeshiriki..”

Akapiga funda mbili za fasta kisha akaendelea…

“Kwa sasa muhimu ni wewe kufika hapo ofisi ya jumla na maelekezo mengine utapata hapo…” akatulia.

“Mbona unanichanganya shogaangu kipenzi, sikuelewi ujue?!” Queen aliuliza.

“Utaelewa tu dada, siwezi kukutosa mimi na wala mpango huu haukuanzishwa na mimi, muhimu ni kwenda kesho asubuhi na mapema maana ofisi saa moja asubuhi inakuwa wazi.” Mourine alijibu.

Waliendelea kuongea pale mazungumzo ya kawaida na kufurahia maisha, kisha wakatoka kuelekea viwanja kama kawaida yao baada ya kuvalia nguo za kazi na safari hii walijiachia zaidi kwa kuwa walikuwa na gari.

Mapema asubuhi saa moja na robo hivi Mourine na Queen walifika ofisi ya jumla.

Ilikuwa ofisi ya kawaida tu ambapo mapokezi waliwakuta watu wawili waliovalia kawaida tu wakiuza vocha, kuchaji simu na miamala ya kifedha ya mitandao.

Wakakaribishwa kwenye viti vichakavu vilivyokuwepo hapo pembeni. Kulikuwa na wateja walikuwa wanasubiria huduma, hivyo Mourine ikabidi atumie lugha za kazi…

“Nataka niingize floti mtandao mpya…” Mourine alisema

“Nisubirini hapo ndani nakuja sasa hivi ngoja niwahudumie hawa wateja waliowahi kwanza…” alijibiwa na kaka aliyekuwepo pale ambaye alionekana si mgeni kwa Mourine, yule dada mwingine mhudumu wa pale alikuwa bize na wateja wa vocha.

Mourine akasimama na kufungua mlango ulioonekana mbovu mbovu hapo kisha akamuashiria Queen naye amfuate waingie ndani…

Ndani hapo walikuta kuna meza ya mbao moja yenye kiti kimoja upate wa pili na viti vitatu upande wa mwingine, hapakuwa na karatasi aina yeyote wala peni isipokuwa kulikuwepo na mashine ya POS ya kufanyia miamala nayo ilikuwa inaonekana ipo ipo tu kama vile haitumiki au haijawashwa.

Hapo walimkuta kaka mwingine aliyekuwa ameiinamia simu.

“Habari Jaki?” Mourine alimsalimia Jackson aliyekuwa ameinamia simu lakini alitambuliwa

“Poa tu, mambo zenu?!” Jackson alijibu huku akiinua kichwa kuangalia…

Queen naye alijibu na Mourine akasema…

“Namuonesha msalani huyu ni mgeni anaitwa Queen…”

“Dada Queen Karibu sana…”

Mourine akafungua mlango mwingine ulioandika ‘toilet’ na kumuashiria Queen amfuate, na walikuta kuna milango mingine mine yote iliandikwa toilet (ME) miwili na (KE) miwili na mmoja ulikuwa umeandikwa toile (walemavu) lakini kiliongezewa neno kwa maanishi ya chaki nyeupe iliyokolea vema ‘KIBOVU / HAKITUMIKI’

Ajabu, Mourine alazimisha kufungua ule mlango wa choo kibovu…

“We Mourine, huo si mbovu huo!” Queen aliongea kwa kuning’ona…

“Najuwa ni choo kibovu, wewe nifuate…” Mourine naye alimjibu kwa kunoing’ona

Queen akiwa hajui nini kinaendelea akajikuta yupo kwenye choo kilichoonekana ni cha walemavu, mazingira ya mle yalikuwa ni machafu, vumbi mtindo mmoja dalili zote zilikuwa zinaonesha hakisafishwi maana nyayo za viatu zilikuwa zinaonekana hususani kuelekea kwenye ukuta upande mmoja.

Mourine akapekenyua sehemu fulani ya ukuta ya ukuta kisha akabofya namba kadhaa zilizosikika kwa mbali sana kisha booom! Mlango mwingine wa siri ukafungua na haraka haraka Mourine akamuashiria Queen aingie na yeye akafuata kisha akabofya zile namba tena mlango ukajifunga.

Walitokelezea kwenye kichumba kidogo kama cha lifti hivi kilikuwa na milango migumu mitatu, mbele, kulia na kushoto ambapo kila mlango ulikuwa na sehemu za kufungulia za vitufye vya namba zakubofya.

Mourine akasonga kwenye mlango wa kulia na kubofya namba kadhaa kisha akasukuma mlango na akamuashiria Queen amfuate na mlango ukajifunga tena wenyewe.

Hapa wakatozea kwenye ofisi safi iliyasaminishwa kwa samani maridadi zenye thamani kubwa, ofisi ilikuwa yenye hewa nzuri ya kiyovyozi, kulikuwepo na kochi moja zuri, viti vya ofisi na meza moja ilionekana ndiye ya mhusika wa hapo lakini hapakuwa na mtu.

“Karibu shoga uketi, hapa ndio ofisi ya jumla….” Alisema Mourine

Queen hakujibu kitu alikuwa anashangaa tu mazingira ya pale na mlolongo mzima wa kufika eneo lile.

Wote wakaketi kwenye viti vilivyokuwepo pale na kusubiria. Kulikuwa na magazeti yote ya siku hiyo hivyo wote wakashika magazeti kupotezea muda, wala haikuwa kawaida yako kusoma magazeti.



Itaendelea Jumamosi ijayo panapo uhai na afya.
 
Back
Top Bottom