Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 258

Wakati baba Angel na Erick walipokuwa wakirudi nyumbani, basi baba Angel alimpa Erick hela kama ambavyo alikuwa ameahidi kufanya hivyo naye Erick alimshukuru sana baba yake kisha baba Angel alimuuliza.
“Utaenda kununua nini na hiyo hela?”
“Aaah zawadi baba ila nyingine naiweka kwanza”
“Oooh haya mwanangu, kwahiyo hiyo zawadi unaenda kununua lini?”
“Kesho baba’
“Je mama yako yupo kwenye watakaopata zawadi au ni za kwako mwenyewe? Au mama yako utampa zawadi ya pipi? Yani zawadi wewe unanunua kwaajili ya nani?”
Erick akacheka kwanza na kumwambia baba yake,
“Mama, nitamnunulia zawadi ila sina tatizo sana na mama sababu huwa anapata zawadi kutoka kwako, ila zawadi ninayopanga kununua napanga kumnunulia Erica”
“Wow, mwanangu ni vizuri sana kumpenda dada yako, kumbe huwa unamkumbuka eeeh! Oooh ni vizuri sana, nina uhakika Erica atafurahia sana zawadi utakayomnunulia”
Erick akatabasamu tu, kisha baba yake akasema,
“Unajua mwanzoni nilikuwa najiuliza kuwa unapanga kununua zawadi ya nani? Nimejiuliza sana, nakumbuka mimi jamani wakati nimeanza mahusiano na mama yenu basi katika swala la zawadi ni yeye tu aliyekuwa akinijia kichwani mwangu”
“Na kabla ya hapo baba?”
“Kabla ya hapo, sikuwa mzuri sana kwenye swala la zawadi ni mpaka mtu aniambie kuwa nataka zawadi, kama dada yangu alikuwa na mtindo wa kuniambia nataka zawadi, basi ndio naenda kumnunulia. Badae nilipoanza na mama yenu alinifundisha umuhimu wa zawadi basi hata mama yangu nikaanza kumpelekea zawadi, dada yangu nae na ndugu zangu wengine. Nafurahi mwanangu umejua umuhimu wa zawadi ukiwa mdogo hivi, kwakweli dada zako wamepata kaka wa kujivunia haswaa”
Baba Angel alionekana kumfurahia sana mtoto wake na waliongea mengi sana hadi wanaingia nyumbani.
Basi kutokana na uchovu uchovu wa siku hiyo walikula tu na kwenda moja kwa moja vyumbani maana hakuna aliyekaa kuongea na wengine zaidi ya kuoga na kulala tu.

Usiku wa leo, Junior alikuwa chumbani kwa Vaileth huku akijaribu kuweka sawa baadhi ya mambo,
“Ila kwanini Junior ulinidanganya mpenzi? Yani umesema mama yako anaumwa wakati haumwi jamani Junior!”
“Kwanza naomba unisamehe sana, yani hata sijui nisemaje. Unajua mama alinidanganya pia kuwa anaumwa kumbe shida yake ilikuwa kuniona tu, si unajua huwa siendi mara kwa mara! Halafu kitu kingine, hata mamdogo kanisema sana nilivyorudi, jamani kitoto Erica ni kimbea hadi kimeshindikana. Kweli kwa sauti ile jikoni ni ya kusikiwa jamani!”
Vaileth alicheka kwa muda na kusema,
“Hujamzoea tu Erica, ila kumbuka katufichia siri”
“Kwanza tujiandae wakati wowote ule litabumburuka, katoto kambea kale wala sio ka kukaamini sana”
“Je ikibumburuka itakuwaje?”
“Yani hapo ni kukataa tu hakuna namna”
“Mmmh unajua kuwa Erica ni mbea ila sio muongo ndiomana anaaminiwa sana! Hapa ni kuombea tu asije kusema ukweli”
“Ila sijapata kuona mtu mbea kama yule mtoto, yani akija kuolewa mumewe atapata shida, hao mawifi zake na mama mkwe wajipange maana kanauwezo wa kusambaratisha ukoo mzima kwa umbea wake, atatoka kwa mama mkwe na hili na kupeleka kwa wifi hili, katoto kambea hadi kameshindikana”
“Sasa karithi wapi?”
“Aaaah sijui kwakweli, ila Vaileth kwakweli nimekumiss sana mke wangu yani nilikuwa na mambo mengi ila mawazo yote ni juu yako”
Moyo wa Vaileth uliridhika sana kwa maneno yale ya Junior na kujikuta akitabasamu tu kisha wakalala kama kawaida yao.

Mama Junior akiendelea na kazi zake za hapa na pale, mara alipigiwa simu na rafiki yake daktari, basi alitabasamu na kupokea ile simu,
“Bite, habari. Jana ndugu yangu hata hatukuongea vizuri kwani ulikumbwa na nini rafiki yangu”
“Mmmmh nini tena!!”
“Unajua nilivyopokea ule ujumbe wako tu nikaamua kutuma muda ule ule na hata sikukuuliza ndugu yangu”
“Ujumbe gani tena!”
“Khee Bite, si wewe jana umenitumia ujumbe wa kuazima laki mbili!”
“Mmmh jamani Maimuna, mimi nimekutumia huo ujumbe!! Muda gani?”
“Ngoja nikutumie zile jumbe kwanza tulizokuwa tukiwasiliana”
Basi Daktari alikata ile simu na kumtumia mama Junior zile jumbe za jana, kwakweli mama Junior alikuwa akishangaa tu maana hakumbuki kabisa kuwasiliana na huyu daktari kuhusu maswala ya hela, kwahiyo alikuwa na mshangao, kisha daktari akampigia tena simu,
“Unajua nini Maimuna naomba unipe muda tafadhari, mimi na wewe hatuwezi kujivunjia heshima kwa vitu vidogo kama hivi. Ngoja tu nitapata ukweli”
“Duh! Ila inashangaza, au uliibiwa simu?”
“Hapana, simu ninayo mwenyewe muda wote, ngoja tu Maimuna nitakujibu”
Basi mama Junior alikata ile simu, kiukweli hakuelewa kabisa aliamua kujiandaa na kwenda moja kwa moja kwenye kwenye ofisi za mtandao wa simu ili apate taarifa za akaunti yake ya simu.
Alipopewa alistaajabu sana kuona kweli alitumiwa laki mbili na yule daktari tena sio laki mbili tupu ila ilikuwa laki mbili na elfu kumi, halafu akaona yote ilirushwa kweye namba ya Junior, kwakweli alichoka kabisa na kusema,
“Kheee tuzaege tu jamani, mambo yenyewe ndio kama haya loh! Huyu Junior angebaki tumboni kwangu si angenipatia uvimbe huyu jamani! Khaaa mtoto gani huyu!!”
Basi aliondoka zake kurudi nyumbani kwake ila alikuwa na hasira sana.

Baba Angel leo hakwenda ofisini ila alienda kwenye ujenzi wake kuangalia tu mwenyewe, na pale yule fundi wake mkuu alimwambia,
“Kwakweli hongera sana”
“Hongera ya nini tena?”
“Una kijana mwenye akili sana, yani mtoto wako ana mawazo ya kikubwa hatari tofauti na umri wake”
“Erick huyo!”
“Ndio, Erick yani akiwa hapa anasimamia utadhani ni mtu mkubwa sana yani anauelewa wa kila kitu, nakwambia karibia utaacha kutembelea kweye hizi saiti na kumuachia yeye tu afanye hivyo. Kwakweli una kijana mwerevu sana, hongera kwa hilo”
Baba Angel alifurahi sana na kujisifia zaidi,
“Yule ni mwanangu pekee wa kiume, na amechukua jina langu maana Erick ni jina langu”
“Aaaah kumbe! Yani nimemtamani hata awe ni mwanangu, jamani mtoto ana akili yule na yupo vizuri sana kichwani nina uhakika hata maendeleo yake shuleni ni mazuri. Yule mwingine sasa, na yeye ana akili sana ila asione mwanamke kapita uwiii macho juu juu mpaka namuhurumia kwakweli, ila Erick yupo makini sana”
Baba Angel alizidi kufurahi sana na kufanya upendo wake kwa Erick uwe maradufu kwani aliona fahari sana kwa kila aliyekutana nae halafu akamsifia Erick.
Basi siku hii hakukaa sana kule kwenye ujenzi na kuamua kuondoka tu sababu hakukuwa na mambo mengi sana wala nini.
Moja kwa moja baba Angel alirudi nyumbani kwake, na kumkuta mkewe akiwa chumbani muda huu akimlaza mtoto basi alisalimiana nae pale na kumuuliza,
“Erick yuko wapi?”
“Nilimuona anaenda bustanini kukaa, naona siku hizi anapenda sana lile eneo”
“Sawa, ngoja nikaongee nae”
Basi baba Angel aliondoka na kwenda bustanini ila muda huo huo mama Angel alipigiwa simu na mama Junior,
“Mdogo wangu unajua alichokifanya Junior?”
“Kafanya nini tena?”
“Ngoja tukionana nitakueleza vizuri, yani huyu mtoto ni pasua kichwa hatari”
“Ila kafanyaje dada?”
“Nitakuelezea tu hakuna tatizo”
Basi mama Junior alikata simu na kumfanya mama Angel kujiuliza kuwa tatizo ni nini ila hakupata jibu.
 
SEHEMU YA 259

Mama Junior muda huu alishindwa kumueleza mdogo wake sababu ya mume wake kumkataza, yani alipotaka kuongea basi mumewe alikuwa karibu na kumkataza, kwahiyo alivyokata simu alianza kumsema,
“Ila nawe mke wangu umezidi jamani, sasa unataka kumuelezea mdogo wako wakati hata muhusika mwenyewe hujamuuliza”
“Nimuulize nini sasa wakati inaonekana wazi kitu gani amefanya jamani, nilikuwa nataka nimueleze mdogo wangu ili anisaidie kulipa hii pesa unafikiri mimi natoa wapi laki mbili na elfu kumi kwasasa?”
“Ila mke wangu, unajua kama wale ndio wanaishi na Junior kwasasa, na ukiwaambia juu juu swala hilo hivi huoni kama watamtimua mtoto pale kwao? Mara nyingine uwe unafikiria kwanza, yule Erick usimuone vile, anacheka na kufurahi ila yule ni ana hasira sana tena hasira za karibu hata nashangaa mdogo wenu kamuweza vipi yule na kumtuliza tuli kabisa. Sasa unataka kumcharusha, Erick atataka kuishi na mtoto tapeli? Si ataona kuwa atawafundisha wanae tabia mbaya, yani atamtimua tu na kumrudisha hapa nyumbani. Huoni kama kwasasa tunaishi kwa amani hapa!”
“Kumbe humtaki mwanangu hapa eeeh!”
“Sina maana hiyo mke wangu ila nakwambia tu kuwa sio vizuri kuanza kumtangazia mtoto wakati hata hujaongea nae bado, sikia mimi nitakupa laki moja ili upunguze deni halafu nyingine mwambie tutammalizia”
“Oooh asante sana mume wangu”
Mama Junior aliona nafuu sasa, kisha muda huo huo alimpigia simu mtoto wake na kumwambia,
“Junior, tayari nimejua ujinga ulioufanya kwenye simu yangu, kwa hakika sijapenda kabisa jambo hili”
“Nisamehe mama”
“Yani wewe mtoto hufai kabisa hata kwa kulumangia hufai wewe, kesho uje nyumbani kwangu mara moja”
“Sawa mama, ila kesho naenda Kanisani”
“Kwani huko Kanisani utakaa milele? Nakwambia uje nyumbani, usiniletee ujinga mie”
“Sawa mama, nitakuja”
Mama Junior alikata simu ila kwa kiasi alikuwa amechukizwa sana na tabia ya Junior.

Baba Angel alikaa kwenye bustani na Erick na kuanza kuzungumza nae,
“Ila mwanangu mbona kama umejitenga hivi, kwanini umekaa mwenyewe?”
“Kuna mambo natafakari baba”
“Mambo gani hayo?”
“Yani nawaza maisha yangu ya badae yatakuwaje na nitafanya nini”
“Sawa mwanangu, hayo usiyawaze ila waza zaidi masomo yako maana kuhusu maisha yako ya badae mimi nayaandaa mwanangu hatausijali, ndiomana nakushirikisha mambo mbalimbali mwanangu. Haya hizo zawadi ulishanunua?”
“Ndio, nilishanunua baba”
“Umenunua nini?”
“Nimemnunulia gauni na viatu”
“Oooh mwanangu huyo, najivunia sana kuwa na wewe. Kwahiyo ushamkabidhi?”
“Hapana, sijampa mkononi ila nimemuwekea chumbani kwake kitandani, yani akiingia tu atakumbana navyo halafu badae ndio nitamwambia kuwa ni mimi”
Baba Angel alifurahi sana kiasi kwamba hata hakumuuliza kama na mama yake kamnunulia au la, yani yeye alifurahi tu kusikia Erick kamnunulia Erica zawadi.
Basi waliongea sana pale na mwisho wa siku waliingia ndani maana usiku ulishaingia na wote walielekea mezani kupata chakula cha usiku ambacho kwa siku hiyo kiliandaliwa na Vaileth pamoja na Erica kwahiyo muda mwingi Erica alikuwa jikoni siku hiyo.
Walianza kula pale na baba Angel akauliza,
“Hizi njegere kapika nani jamani!”
Vaileth akajibu,
“Mambo ya Erica hayo”
Baba Angel alitabasamu na kusema,
“Hakika mume atakayekuoa mwanangu atakuwa na furaha sana kama mimi baba yako, yani hiki chakula umepika vizuri sana. Hongera sana”
“Asante baba”
Erica alikuwa akitabasamu tu, na mama yake akaongea
“Naona huyu Erica kafata upishi wangu”
“Kweli kabisa mama Angel ila katoto kamekuzidi haka”
“Aaaah mimi ndio fundi wake bhana”
“Ila kumbuka vya kurithi vinazidi”
Wote wakacheka tu pale na kila mmoja alisifia kuwa chakula kilikuwa kizuri na mboga ilikuwa ni nzuri sana.
Basi alimaliza kula pale na kila mmoja alienda kwenye chumba chake.

Erica ndio aliingia muda huu chumbani ambapo cha kwanza alienda kuoga kwanza, ila alipotoka bafuni alishangaa kuona mzigo kitandani kwake, basi akafungua ule mzigo na kushangaa sana kukutana na gauni zuri sana na viatu vizuri sana halafu alikuta na nguo za ndani mpya kabisa, basi akajaribisha lile gauni, lilimpendeza sana alijiangalia mara mbilimbili kwenye kioo chake kikubwa, akajaribu na viatu navyo vilimpendeza sana kwakweli alishangaa mno aliyemuwekea hizo zawadi, akataka kutoka kwenda kumuuliza mama yake ila alipofungua tu mlango wake alikutana na Erick ambaye alikuwa akitabasamu na kuingia mule chumbani kwake.
Erick nae alivyomuangalia Erica ndani ya ile nguo alifurahi maana ilimpendeza sana,
“Eeeeh Erica umependeza sana”
Erica alitabasamu na kusema,
“Ila sijui ni nani kaniletea”
“Aaaah Erica jamani, nimekuletea mimi”
Erica alifurahi sana na kwenda kumkumbatia kaka yake kwa furaha na kumbusu, kwakweli ile ilikuwa ni furaha sana kwa Erick pia maana aliona raha kwa Erica kuipenda zawadi yake, kisha Erica akamwambia,
“Asante sana Erick”
“Ni wajibu wangu Erica kufanya hivi, kwanza mimi ni kaka yako na rafiki yako kwahiyo ni wajibu wangu kufanya hivi kwako”
“Nashukuru sana Erick, nimeipenda sana hii nguo”
Basi Erick alivyoona kuwa Erica kaipenda sana ile zawadi ndipo alipomuaga usiku mwema na kuondoka zake kwenda kulala.
Jumapili hii, Erica alivaa zile nguo alizoletewa na Erick na wote pale nyumbani kwao walimsifia kuwa kapendeza sana na alipenda na kufurahi maana yeye licha ya umbea pia ni binti ambaye anapenda sana kupewa sifa, yani akisifiwa huona ufahari mkubwa sana.

Junior alipotoka Kanisani tu siku hii, aliwaaga na moja kwa moja kwenda nyumbani kwao ili akaonane na mama yake na alijua kuwa atasemwa sana siku hiyo ila alivyofika tu alimkuta mama yake kajiandaa na alisema,
“Yani ungechelewa tu kidogo ningekupigia simu, haya twende”
Junior alimfata mama yake tu bila kujua kuwa anaelekea nae wapi, wakapanda daladala mpaka walipokuwa wakielekea, basi Junior akamuuliza mama yake,
“Mama, ni wapi huku?”
“Wewe mjinga, umeniingiza madeni makubwa sana, nimepata laki moja ndio nimekuja kumlipa hapa mwenyewe, kwahiyo hapa ni nyumbani kwa daktari”
“Jamani mama”
“Hakuna cha jamani”
Basi mama Junior alimshika mkono Junior hadi kwenye ile nyumba na kugonga, walikaribishwa vizuri tu na daktari alikuwepo, walisalimiana pale na mama Junior alimtambulisha Junior kwa yule daktari kisha akamwambia Junior,
“Huyu ndio rafiki yangu daktari, anaitwa dokta Maimuna, ndio uliyemuongopea ile hela”
Basi mama Junior alianza kumueleza huyu rafiki yake kilichotokea, mara alifika mtoto wa yule daktari na kuwasalimia pale ila Junior na mtoto huyu walibaki kuangaliana kwa mshangao kwani mtoto huyu alikuwa Samia.

Basi mama Junior alimshika mkono Junior hadi kwenye ile nyumba na kugonga, walikaribishwa vizuri tu na daktari alikuwepo, walisalimiana pale na mama Junior alimtambulisha Junior kwa yule daktari kisha akamwambia Junior,
“Huyu ndio rafiki yangu daktari, anaitwa dokta Maimuna, ndio uliyemuongopea ile hela”
Basi mama Junior alianza kumueleza huyu rafiki yake kilichotokea, mara alifika mtoto wa yule daktari na kuwasalimia pale ila Junior na mtoto huyu walibaki kuangaliana kwa mshangao kwani mtoto huyu alikuwa Samia.
Ila kiukweli Junior alionekana na sura ya kuchukizwa sana, basi daktari aliwatambulisha pale,
“Jamani huyu ni mtoto wangu wa mwisho, anaitwa Samia”
Kisha daktari alitambua jicho baya la Junior na kufanya amuulize,
“Mbona unamuangalia mwanangu kwa jicho baya hivyo!!”
Junior hakusema kitu ila aliinuka na kutoka nje yani kitendo kile hata mama yake alishangaa sana kuwa Junior amekuwaje vile, ila alivyofika nje alisimamisha bodaboda na kuondoka zake.
Kwahiyo daktari na mama Junior walibaki wakishangaa huku daktari akimuuliza mwanae,
“Samia, kwani unamfahamu Junior?”
“Hapana, simfahamu”
Samia alikataa halafu akaenda zake chumbani kwahiyo mama Junior na daktari walibaki kushangaa, basi mama Junior alianza kuongea na yule rafiki yake daktari,
“Jamani watoto wana mambo sana, ila tuachane na habari hizo ndugu yangu, unajua nini siku ile kumbe ni mwanangu ndio alichukua simu yangu na kukuandikia ule ujumbe”
“Kheee jamani, watoto hawa!!”
“Kisa tu aliniomba hela nikamnyima, basi akaniomba simu ili apige mahali kumbe jamani ana mambo yake ndio kama vile ndugu yangu, nisamehe sana nakuomba. Halafu naomba nitangulize hii laki moja kwanza, ila nyingine nitakutafutia ndugu yangu kwenye siku mbili hizi”
“Eeeh kwanza pole sana Bite, ndio mambo ya Junior hayo!! Pole sana”
Basi mama Junior akawa anataka kuchukua pochi yake ndogo ilia toe hela yake ila hakuiona na kushangaa,
“Jamani pochi yangu ilikuwa hapa, iko wapi tena?”
“Pochi gani hiyo?”
“Pochi ndogo ndogo nyekundu”
“Mmmh mbona mtoto wako alitoka nayo”
“Kheee Junior jamani, kwanini lakini jamani uuuh!”
“Kwani vipi?”
“Ile pochi ndio niliyoweka hela”
Kisha mama Junior akaamua kumpigia simu Junior ili kumuuliza kwanini ameondoka na pochi, na kweli Junior alipokea ile simu yake,
“Wewe Junior kwanini umeondoka na pochi yangu!”
“Mama, sina mengi ya kuongea ila mwambie huyo Samia amlipe mama yake”
“Kivipi sasa?”
“Mtoto mjinga sana huyo, ile laki mbili ni yeye ndiye aliyesababisha nikamuomba huyo rafiki yako, tena ni vizuri sana ni mama yake kwahiyo yeye ndio amlipe mama yake”
“Wewe Junior wewe una kichaa au?”
“Sina kichaa, nina akili zangu timamu, mwambie huyo Samia amlipe mama yake”
Kisha Junior alikata ile simu, basi mama Junior alimuangalia rafiki yake na kumwambia,
“Unajua hata sielewi yani sielewi kabisa ujue, huyu mtoto sijui kakumbwa na nini?”
“kwanini rafiki yangu?”
Mama Junior akamueleza vile ambavyo aliongea na Junior kwenye simu, kuna kitu Fulani yule daktari alikigundua na kusema,
“Mama Junior, kwakweli watu tunazaa ila muda mwingine tunazaa vitu visivyoeleweka sababu ya kuzaa na watu wasioleweka. Bite acha tu, nitajua cha kufanya kuhusu hiyo hela, si amesema Samia anajua? Basi acha tu najua ni jinsi gani nitambana huyu mtoto”
“Jamani ila hata sijui imekuwaje?”
“Usijali rafiki yangu, niachie mwenyewe tu halafu tutawasiliana, aaarggh watoto hawa jamani dah!”
Kwakweli mama Junior hakuelewa kabisa, kwahiyo aliamua kumuaga tu rafiki yake na kuondoka ake kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 261


Baba Angel alipofika tu ofisini kwake, alikutana na ujumbe toka kwa mtu wake wa mapokezi,
“Bosi kuna mzigo wako huu”
“Asante”
Basi baba Angel aliingia na ule mzigo mpaka ofisini kwake, akauweka pembeni na kuanza kufanya kazi zake, ila mara simu yake ikaita na kumfanya kuipokea kwani aliyekuwa akipiga alikuwa ni madam Oliva,
“Baba Erick, umepata ujumbe wako?”
“Ujumbe gani tena?”
“Kuna mzigo nimeacha hapo kwa mtu wa mapokezi”
“Oooh nimeupata”
“Uangalie basi”
Ikabidi baba Angel afungue ule mzigo, na kukuta ni viatu vizuri sana, kwahiyo madam Oliva alikuwa amemnunulia zawadi ya viatu, kwakweli vilikuwa ni vizuri na madam Oliva akampigia tena simu,
“Umeona?”
“Ndio nimeona, asante”
“Jaribisha kwanza, nakuja muda sio mrefu”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi akakata ile simu na baba Angel akataka kujaribu vile viatu ila kwa muonekano tu vilikuwa ni viatu ambavyo vingemtosha kabisa, ila alipotaka kuweka mguu akajikuta akijiwa na maneno ya Sia kuwa kuna zawadi analetewa na madam Oliva na asiijaribu hiyo zawadi, basi akajisemea,
“Ila Sia nae kama kachawi kale kamwanamke jamani! Inawezekana kweli asemayo mmmh! Ila huyu madam nae kasema anakuja muda sio mrefu, ngoja niondoke ili asinikute”
Baba Angel alifunga kazi yake na kuondoka zake ambapo moja kwa moja alienda tu kule kwenye ujenzi kwani aliona kama siku yake imeharibika na hata kwenye ujenzi hakukaa sana na kuwataka watoto wake warudi nae tu nyumbani kwa muda huo.

Siku ya leo pale nyumbani kwao Erica alitembelewa na rafiki yake Samia na kufurahi sana, basi kwa siku ya leo alienda kukaa nae bustanini huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Kheee leo Junior na Erick hawapo au wanaangalia mikanda?”
“Hawapo, baba kawapeleka huko kwenye ujenzi”
“Oooh sawa, sasa bhana kuna jambo nataka nikwambie shoga yangu”
“Jambo gani hilo?”
“Si kuhusu Junior, ni kwamba Junior alinitongoza”
“Mmmh jamani!”
“Ndio hivyo, na mimi nikamwambia kuwa bila laki tano siwezi kukubali, sijui Junior kapata wapi zile hela maana akaniletea laki tano kamili, akataka kulala na mimi basi nikamwambia kuwa akatafute hoteli ya chumba laki moja, akatafuta halafu mimi sikwenda, si ndio amechukia hivyo! Wakaja nyumbani na mama yake, kumbe Junior katumia simu ya mama yake kumkopa mama yangu hela, basi imebidi nimwambie mama ukweli”
“Mmmh Junior alitaka kulala na wewe!!”
“Ndio, alitaka kulala na mimi”
“Kwahiyo ungekubali Samia?”
“Nisingekubali ndiomana nilimdanganya”
“Ila umepata wapi ujasiri wa kumwambia akuletee hela?”
“Ndio nilivyofundishwa, baba huwa ananiambia kuwa mimi ni wa gharama sana na mwanaume anayenitaka anatakiwa kunigharamia ndio anipate, sasa Junior ni mjinga hata kama alilipia hoteli si ndio sehemu ya kunigharamia, alitakiwa kuendelea kunifatilia tu sio kuja kuniabisha nyumbani vile”
“Kwahiyo Junior anakupenda wewe! Mpaka akakuletea laki tano! Aliipata wapi?”
“Sijui, ila Junior kaniletea laki tano kamili. Na Bahati yake hayupo leo, kanikera sana kwanza mimi simpendi yeye yupo mwingine nimpendaye”
“Nani huyo?”
“Yupo kwenye nyumba hii hii ila simtaji”
“Jamani nitajie!”
“Aaah natakiwa kuwahi nyumbani leo, kwaheri Erica”
Basi Samia aliinuka na kuaga, kwakweli Erica aliwaza vingi ila kwa muda huo kikubwa alichowaza ni Junior kumpa laki tano Samia, na kujisemea,
“Kumbe Junior sio muaminifu kabisa, atampendaje Samia wakati anampenda dada Vai!!”
Basi akaingia ndani huku akijifikiria kidogo na muda huo huo alitaka kumwambia mama yake,
“Ngoja nikwambie kitu mama”
“Eeeeh kitu gani hiko”
“Basi, Samia kaniambia kuwa….!!”
Mara baba Angel na wakina Junior walikuwa wamewasili, kwahiyo Erica ilibidi asiseme tena kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 262

Usiku wa leo, mama Angel na baba Angel walikuwa wakipanga namna ya kesho yake kwa mama yao watakachokifanya,
“Kwanza kabisa tutapika chakula hapa cha kwenda nacho”
“Sawa mke wangu, hilo ni jambo zuri, halafu mimi niliwaza kuwa labda tununue chakula cha kwenda nacho”
“Aaaah tununue cha nini wakati kupika naweza, nipo mimi, yupo Vai na yupo mpendwa wetu Erica yani hakuna kitu kitakachobadilika”
“Oooh mtoto wetu Erica yupo vizuri, yani hawa watoto wananifurahisha sana, huko kila ninapoenda na Erick wanamsifia kuwa ni mtoto mwenye akili sana yani hadi najihisi ufahari kuwa baba wa Erick, halafu huku Erica ni binti mwenye tabia nje na yupo vizuri”
“Ila umbea wake ndio unamuharibia sifa zake zote”
Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, na mama Angel alikuwa wa kwanza kuitumbulia macho simu ile na jina liliandikwa ‘Madam Oliva’
“Mmmh madam Oliva huyo anakupigia”
“Aaaah achana nae”
“Mmmh unanipa mashaka sasa, nipe niipokee”
Baba Angel hakutaka kurumbana na mkewe kwahiyo alimpa aipokee ambapo muda ule ule madam Oliva alianza kuongea,
“Mbona simu zangu hupokei leo nimekukosea nini? Nilikuja ofisini ila uliondoka, hujapenda zawadi yangu?”
“Zawadi gani?”
“Oooh samahani mama Erick, kwaheri”
Kisha madam Oliva alikata simu na mama Angel alimuangalia mume wake na kumuuliza,
“Ni zawadi gani hiyo ambayo madam Oliva kakuletea?”
“Kaniletea zawadi ya viatu, ila usijali mke wangu hata sivihitaji na nimeviacha kule kule ofisini”
“Aaaah ila leo siongei mengi sana, tulale tu muda huu”
Baba Angel hakuelewa ni kwanini mkewe leo hajalalamika sana wakati ni kawaida yake yani alishangaa jinsi mkewe alivyokuwa muelewa vile maana huwa inachukua muda mrefu sana kumuelewesha.

Kulipokucha walianza kujiandaa wote huku wakiandaa chakula cha kuondoka nacho, muda huu baba Angel alikuwa chumbani akijiandaa pia ila ukaingia ujumbe kwenye simu yake,
“Samahani baba Erick, sina nia mbaya mimi mwambie mkeo asinifikirie vibaya, leo nitakuja ofisini kwako ili tuongee vizuri”
Baba Angel hakujibu ule ujumbe wala nini zaidi zaidi ya kuufuta na kumalizia kujiandaa tu na alipomaliza, mkewe nae alifika na kujiandaa kwaajili ya safari ambayo walikuwa wameipanga.
Basi kila mmoja alipomaliza kujiandaa wakatoka na kuingia kwenye gari ambayo iliwatosha wote kisha safari ilianza ila njiani kuna kijana walimuona na Erica alimuona vizuri na kusema,
“Jamani, Elly yule pale. Tumsalimie basi”
Mama Angel alimuangalia Erica na kumwambia,
“Una kiranga sana wewe, muone vile. Hamna kusimama baba Angel”
Basi baba Angel akaendelea kuendesha gari yake bila hata kusimama ila Erica alikuwa akiangalia tu hadi alipomuona Elly ametokomea.
Walifika kwa bibi Angel na kupokelewa kwa furaha sana yani bibi Angel aliona raha sana kwa mshtukizo ule aliofanyiwa, basi walikaa wote na kufurahi na muda ule ule walipakua kile chakula ambacho walikibeba ili waje kula kwa pamoja.
Wakati wanakula, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni dada wa mama Angel yani Mage ambaye walimkaribisha vizuri tu naye ila baada ya salamu tu alikaa na kusema,
“Eeeh ni vizuri leo nimewakuta wote, mwambieni Angel ukweli sasa”

Wakati wanakula, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni dada wa mama Angel yani Mage ambaye walimkaribisha vizuri tu naye ila baada ya salamu tu alikaa na kusema,
“Eeeh ni vizuri leo nimewakuta wote, mwambieni Angel ukweli sasa”
Kwakweli mama Angel alishtuka sana na kuhisi ubaridi ukipita katika mwili wake sababu hakutaka mwanae apewe siri yake kwa wakati ambao hajaupanga yeye, basi akainuka na kumshika mkono dada yake kisha kutoka nae nje kabisa halafu ndio akaanza kuongea nae,
“Dada Mage, nakuheshimu sana ila sipendi unachotaka kunifanyia, kwanini vitu vidogo kama hivi vikatuondolea heshima kwanini? Unajua niliambiwa ila sikuchukulia kwa makini ila leo ndio nimeelewa sasa, kitu gani unachotaka kuifanyia familia yangu?”
“Erica, nisikie mdogo wangu si kwa ubaya, unajua Angel amekuwa mkubwa sasa nahofia kisije kutokea kitu kama wewe”
“Kitu gani?”
“Leo umesahau Erica, si ulitembea na Derrick sababu mlikuwa hamfahamiani!! Nahofia isije kutokea kwa Angel nae akatembea na kaka zake?”
“Kwani mwanangu Angel umemuonaje? Haya nilitembea na Derrick kitu gani kilitokea sasa?”
“Erica jamani, unakumbuka hadi tulienda kufanya tambiko kwasababu hiyo!!”
“Basi ikitokea na kwa Angel tutaenda kufanya tambiko pia, ila usiniharibie familia yangu.”
“Sikia nikwambie Erica, kosa kubwa tunalolifanya wanawake ni kumficha mtoto baba yake halisi, halafu huwa tunaona kuwa tumefanya sawa kabisa, ila kuna umuhimu mkubwa sana wa mtoto kumfahamu baba yake halisi, mtoto huyo mmemdanganya akiwa mdogo hadi leo jamani! Mnamkosesha mtoto haki yake”
“Kwani akishamjua baba yake halisi ndio inakuwa nini sasa? Dada tafadhari niache, kwanza kabisa unatakiwa umuheshimu mume wangu, ni yeye ndiye amefuta aibu yangu, mlikuwa wa kwanza hapa kunisema kuwa nimezalia nyumbani, mlikuwa wa kwanza kusema nimkubali yoyote wa kunioa, ila akatokea Erick mwenye mapenzi na mimi, sasa nimefanya kosa lipi kumzawadia mtoto? Angel nitamwambia ukweli siku ambayo Erick atasema kuwa tumwambie Angel ukweli ila sio kwa maneno yenu. Halafu dada, katika vitu vyote ukifanya unachotaka kufanya kuhusu Angel kwa hakika tutaonana wabaya, mimi mdogo wako nina roho mbaya sana nikitaka, naomba uniache na familia yangu, nitajua mwenyewe inapoelekea”
“Eeeeh yamekuwa hayo, hadi kuonana wabaya kisa kumwambia Angel ukweli!! Yani tatizo lako wewe huyo Erick kakushika masikio sana nadhani huoni kama kuna mwanaume zaidi ya Erick duniani”
“Ndio hakuna”
“Hahahah sasa ngoja siku moja mumeo akuletee mke mwenzio ndio akili itakukaa sawa, kumbuka mwanaume sio ndugu yako na sio mama yako wala baba yako anaweza kubadilika wakati wowote haijalishi mmeishi kwa amani kwa muda gani. Ila siku akipatikana mwanamke mjanja mbona utabaki kulia tu, usijiamini kupata kiasi”
“Kiukweli dada unanichefua”
“Kheee kukwambia ukweli ndio nakuchefua!!”
“Ndio unanichefua sana yani nahisi kichefuchefu kukuangalia”
“Kheee haya kwaheri, fanya unachojisikia”
Mage aliondoka zake yani hata hakuingia ndani kuaga wala nini na wala mama Angel hakuona kuwa ni tatizo ila aliona akili yake ikielemewa tu, akikumbuka mambo ya zawadi ya madam Oliva kwa mumewe na vile dada yake alivyosema akipatikana mwanamke mjanja alihisi kizunguzungu tu na yale mambo ambayo dada yake anataka kuyazindua alihisi kuumia kichwa, basi alifikiria kidogo jambo la kifanya kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 263

Mama Angel alirudi ndani ila walimuuliza kuwa imekuwaje, na Angel ndio alikuwa wa kwanza kuuliza basi akamwambia,
“Mwanangu, nikirudi nitakueleza vizuri”
Wote wakamuangalia na bibi Angel akamuuliza,
“Kwani unataka kwenda wapi?”
“Mama, wakati nipo nje na dada Mage hapo alipita mdogo wake Johari na kaniambia kuwa Johari yupo kwao. Kwakweli nahitaji kumsalimia maana ni muda mrefu sana, ila sitakawia kurudi”
Basi alimuangalia mume wake pale na kumuaga halafu akamwambia,
“Tena ni vizuri niende na gari ili niwahi kurudi, sio mbali kutoka hapa”
Basi baba Angel akampa funguo ambapo mama Angel alitoka nje na kuingia kwenye gari na kuondoka zake.
Safari ya mama Angel ilikuwa ni kwenda ofisini kwa mume wake, kwani alitaka kwenda kuona hiyo zawadi ya viatu ambavyo mumewe aliletewa na madam Oliva, alikuwa akiendesha gari huku akiwaza moyoni,
“Nikishachukua hivyo viatu naenda kuvitupa baharini, sitaki ujinga mie au navichoma moto”
Yani maneno ya dada yake yalimfanya kuhisi kuwa ndoa yake kwasasa haipo sehemu salama.
Alifika ofisini kwa mumewe kama kawaida, mtu wa mapokezi alimruhusu kuingia kwani anatambua kuwa ni mke wa bosi wao kwahiyo walimkabidhi tu funguo, basi aliingia moja kwa moja na kukuta boksi likiwa pembeni ya meza ya mume wake na alipofungua akakuta kuna viatu vile ambavyo vililetwa na madam Oliva, basi aliviangalia kwa makini sana ila muda huo wazo lake la kuvitupa baharini au kuvichoma moto lilipotea na kusema,
“Mmmh viatu hivi ni vizuri sana halafu vinaonekana ni vya gharama, nikienda kuvitupa au kuvichoma moto nitakuwa natenda dhambi, ila sitaki mume wangu avae hivi viatu. Kwahiyo cha muhimu nikampe tu mtu mwingine kama zawadi pia”
Basi akavichukua vile viatu na kutoka, halafu akafunga mlango wa mume kwenye ile ofisi vizuri kabisa na kurudisha funguo kwa watu wa mapokezi kisha akaondoka zake, alikuwa akiondoka na gari huku akiwaza kuwa vile viatu akampe zawadi nani ila kuvichoma moto roho ilimuuma maana vilikuwa vizuri sana.
Wakati yupo njiani alimuona madam Oliva akitembea basi akasimamisha gari ili kumsalimia tu aone anaichukuliaje salamu yake,
“Madam habari”
Madam Oliva alishtuka kidogo kwani inaonyesha hakufikiria kukutana na mama Angel kwa muda huo, basi akasimama na kuitikia,
“Salama, mama Erick”
“Unaenda wapi nikupe lifti?”
“Aaah hamna, usijali kitu naenda hapo mbele halafu nipo kufanya mazoezi”
“Ila mbona hujaja tena kunitembelea?”
“Nitakuja tu, kwaheri”
Yani madam Oliva alionekana kama ana haraka sana ila mama Angel alihisi kuwa madam Oliva anajishuku tu kwa tabia yake ya kumtaka mume wake.

Mage alivyoondoka kwao, moja kwa moja alienda ofisini kwa mdogo wake Tony kwa bahati nzuri siku hiyo alimkuta mdogo wake yupo ofisini basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae,
“Mmmh dada leo ofisini kwangu kuna jema kweli! Au yale yale ya kuhusu Derrick”
“Mmmh umasikini mbaya sana jamani!”
“Kwanini dada, ni mambo ya kuhusu Derrick au kitu gani?”
“Hayo, pia yapo ila cha zaidi kilichonileta ni kuhusu Erica”
“Kwani Erica kafanyaje?”
“Erica, hataki kumwambia Angel ukweli.Wanamnyima mtoto haki yake ya kumtambua baba yake wa ukweli”
Kisha akamuelezea vile ambavyo aliongea na mama Angel na ambavyo mama Angel alimjibu, kwakweli Tony alisikitika na kumuuliza dada yake,
“Ila dada, kwani Angel kadai hiyo haki ya kumjua baba yake wa ukweli?”
“Hapana”
“Unajua mtoto hufikia hatua ya kudai kufahamu kuhusu baba yake mzazi ikiwa yule baba anayeishi nae hamjali, hampendi, hamuangalii ndio pale mtoto hujiuliza hivi sina baba mwingine kweli! Sasa kama Angel maisha anayoishi na anayopewa na huyo Erick anaanzaje kudai kumfahamu baba yake halisi? Ikiwa Erick anampenda na anamjali kama mtoto wake kabisa?”
“Ndiomana nilianza na kauli ya kusema umaskini mbaya sana”
“Sasa umasikini unauhusiano gani na hayo?”
‘Nilijua tu utawatetea Erick na Erica kwani ndio waliyokupa maisha hayo uliyonayo”
“Sikia dada, unajua mara nyingine unaweza kufanya kitu na kuona unapata faida kumbe ilitakiwa upate faida kubwa zaidi ila tu sababu huna muongozo unaofaa inakuwa ni ngumu sana kwako, ukipata mtu wa kukupa muongozo unatakiwa kumshukuru sana. Mimi nilikuwa nafanya kilimo, sio nilikuwa nib ado nafanya mpaka sasa ila kilimo changu cha kipindi hiki na kipindi kile ni tofauti, Erick kanisaidia kupata ofisi hii na kanisaidia niwe na masoko makubwa kawahiyo kilimo changu kimekuwa bora sana na ninamshukuru kwa hilo, ila wewe ni nani usiyekuwa na shukrani upo hapa tu kulalamika umasikini mbaya kisa umekataliwa kusema yasiyokuhusu!”
“Mbona maneno mengi yanakutoka! Hiyo ipo wazi kwasasa mnamuheshimu sana Erica na mumewe Erick, tena mmeacha hata kunisikiliza dada yenu”
“Yani dada maneno mengine unayataka tu, wenyewe washakwambia kuwa hawataki umwambie mtoto wao sasa wewe kinakuuma kitu gani? Tena mimi ingekuwa wewe hata wakina Erica nisingewasumbua kabisa”
“Ndiomana nasema umasikini mbaya, kwahiyo unataka niwanyenyekee wakina Erica?”
“Sio kuwanyenyekea, ila unatakiwa kuwaheshimu pia. Dada kumbuka, mlikuwa mnaishi kwenye nyumba ya urithi na mumeo ila Erica kawapigania hadi sasa mnaishi kwenye nyumba yenu na alifanya kwa upendo tu, alikupa hela ya biashara ila ukaitumia yote, bado Erica hakulalamika bali alikufungulia biashara, hivi unataka mtu akufanyie nini? Na haya mambo uliyoyaanza naanza kuingiwa na wasiwasi”
“Wasiwasi wa nini?”
“Nahisi biashara uliyofunguliwa umeshaiua na kama bado basi unakaribia kuiua ndiomana umeweza kupata nguvu ya kutaka kuharibu familia ya wenzio na nguvu ya kumfatilia Derrick”
“Nilijua tu kuwa nitaonekana naongea porojo sababu tu Erica kawawezesha kwa kupitia mume wake, haya kwaheri”
Mage aliamua kuondoka pia kwa Tony ila Tony hakutilia maanani kabisa maneno ya dada yake kwa zaidi zaidi aliendelea tu na kazi zake.
 
SEHEMU YA 264

Leo Steve alitembelewa dukani na rafiki yake wa muda mrefu sana ila rafiki yake huyu alimkuta Steve yupo muda wote akiangalia simu yake na kumuuliza,
“Mmmh hivi na kazi zako unafanya muda gani?”
“Kama hamna wateja ndio unanikuta hivi na simu halafu unafikiri huwa nawasiliana na mtu basi!! Huwa naangalia picha tu”
“Picha gani?”
“Kuna mama mmoja hivi ni mwalimu, jamani huyu mama napenda sana misimamo yake basi huwa naangalia sana picha zake yani nampenda jamani, angenikubali ningemuoa”
“Aaaah wewe nawe, hujaoa hadi leo, unatakiwa kutafuta wasichana wadogo, sasa hao wamama si utakuta ni wake za watu!”
“Huyo sio mke wa mtu”
“Una uhakika gani?”
“Kwenye ukurasa wake wa facebook kaandika hivi, ngoja nikusomee ‘single and happy’ umesikia inamaana hana mahusiano yoyote ila huwa anaandika maneno yenye busara sana”
“Ushawahi kuwasiliana nae?”
“Mmmh yani kila nikiMtumia ujumbe hanijibu, yani nishamtumia hadi basi ila hajawahi kunijibu hata mara ila sichoki”
“Basi ngoja nikufundishe njia rahisi itakayomfanya akujibu”
“Njia gani hiyo?”
Mara Steve akafikiwa na mke wa bosi wake pale dukani yani mama Angel kwahiyo ilibidi aende nae ofisini kuzungumza nae,
“Unafikiri Steve nakaa basi!!”
“Karibu mama”
“Sasa nimekuletea zawadi,ilikuwa ya mume wangu ila havimtoshi ndio nimekuletea wewe”
Basi mama Angel akampa Steve vile viatu ambapo Steve alivyoviona alivipenda sana yani na muda huo huo alivijaribisha na vilimtosha vizuri kabisa basi alikuwa akifurahia na kumshukuru sana mama Angel.
Muda huo huo mama Angel alimuaga kuwa anaondoka zake, basi aliagana nae pale na kuendelea kumshukuru sana.
Alipofika kwa rafiki yake nje akamwambia,
“Ona sasa tunaopendwa na mabosi zetu, kaniletea kiatu kizuri sana”
“Halafu ni cha gharama sana hiko, nimewahi kuvikuta duka flani hivi nikaulizia bei yake nikaambiwa ni laki tatu na elfu tisini”
“Duh!! Hebu nipige picha nijiweke facebook leo”
Basi rafiki yake alichukua simu na kumpiga picha Steve ambaye alifurahi sana kupigwa ile picha na muda huo huo aliiweka facebook ila pia alihisi akili yuake kutotulia kabisa na vile viatu alitamani wengi waone kuwa kavaa viatu vya gharama, yani alifunga biashara na kuondoka zake kwa muda huo.

Nyumbani kwa bibi Angel walikuwa wakijiuliza sana kuhusu mama Angel hata bibi Angel alijaribu kwenda hadi kwakina Johari ila mama Angel hakumkuta na hakuna aliyesema kuwa alikwenda pale, basi bibi Angel alirudi huku asijue hata cha kumjibu mkwe wake, basi baba Angel akamuuliza,
“Eeeh mama, na huko wamesemaje?”
“Mmmh!”
Mara ndio wakasikia honi ya gari na kujua kuwa mama Angel amerudi kwa muda huo, na kweli muda kidogo tu aliingia ndani ila muda ulikuwa umekwenda sana kiasi kwamba hata hakuelezea alipokuwa zaidi ya kuwaambia kuwa wajiandae ili waondoke halafu alienda kuongea na mama yake ila kama kawaida yake sababu alikuwa na tabia Fulani ya kutokusema ukweli aliweza kumdanganya mama yake na kumfanya mama yake amuamini maana aliona akimwambia vile mama yake basi hatomuelewa kabisa.
Walijiandaa pale na kufanya safari ya kuondoka kuelekea nyumbani kwao, ila kwakweli baba Angel hakufurahishwa kabisa yani na alikuwa na hasira sana kwa kile alichokifanya mke wake ila aliona ni vyema akifika nyumbani waanze kuongea na mke wake.
Na kweli walivyofika nyumbani tu, walipoingia chumbani baba Angel alitaka kumuuliza mama Angel ila kabla ya hapo mama Angel alianza kumuelezea,
“Mume wangu nisamehe sana najua nimekuudhi mno naomba unisamehe, ni hivi mume wangu kwakweli mimi toka jana kuhusu zawadi aliyokupa madam sikuwa na amani nayo kabisa moyoni, nilichokifanya leo nilienda ofisini kwako na kuichukua, nia yangu ni kutoka kuchoma moto vile viatu ila niliona ni vya gharama sana na ni vizuri basi sikuona vibaya kumpelekea mtu mwingine kama zawadi”
“Kwahiyo ukampelekea nani?”
“Nimempelekea Steve, naomba unisamehe mume wangu”
“Ila kwanini unapenda kufanya mambo bila kunishirikisha? Hivi ungeniambia ningekataa kwani? Kwanini mke wangu unakuwa hivyo jamani eeeh! Ungeniambia nisingekataa, na kesho tungeenda wote ofisini kuvichukua ila nadhani ingekuwa ni vyema sana ungenishirikisha kwanza kabla ya kufanya maamuzi yote hayo”
“Naomba nisamehe mume wangu”
“Unajua una mtoto mdogo ila mke wangu jamani kwanini unafanya haya!! Kwanini huna imani na mimi jamani, nakupenda Erica, kwanini huniamini? Hao wakina Oliva wanini mimi jamani, unajua mtu ukifanya sana uhuni kuna muda unafika unakuwa umechoka na huwezi tena kutenda maovu wala kutamani wanawake tena, jamani mke wangu nakupenda tena sana, kwanini huniamini Erica?”
“Nakuamini mume wangu”
“Hapana, huniamini hata kidogo laiti kama ungekuwa unaniamini basi usingekuwa unafanya mambo bila kunishirikisha kama leo, kiukweli sijapenda kabisa”
“Nisamehe mume wangu”
“Unajua umeniabisha mbele ya watoto mke wangu maana wote walikuwa wakiuliza mama yuko wapi? Halafu sina jibu lolote la kuwaambia, umenitia aibu sana leo Erica”
Ikabidi mama Angel ambembeleze mume wake kwani alijua ni wazi kafanya makosa ila hakuwa na namna kwa muda huo zaidi ya kufanya vile.
 
SEHEMU YA 265

Madam Oliva kwa muda huu alikuwa amekutana na rafiki yake Fetty na walikuwa wakiagana sababu alikuwa akirudi nyumbani kwake, ila alishika simu na kushtuka pale pale Fetty alimuuliza basi alimuonyesha kilichomshtua na pale Fetty akamshangaa na kumuuliza,
“Sasa umeshtuka nini?”
“Viatu alivyovaa na kupiga picha huyu kijana vimenishtua sana”
“Kwanini jamani, au sababu ni vizuri sana”
“Licha ya uzuri wake, ni hivi yani unajua yule mume wa mtu nilikwambia nampenda basi ndio nilienda kumtafutia zawadi ya viatu kama hivi ndio vimenichanganya akili hapa”
“Mmmh na wewe una kilanga, yani mume wa mtu ushaanza kumgharamikia hadi viatu!”
“Jamani, nampenda, yani nampenda sana na nahitaji kumpata ila kwa hivi viatu hachomoki”
“Kivipi?”
“Nitakwambia shoga yangu hata usiwe na wasiwasi, ila huyu kijana inaonekana hali yake ni ya kawaida sana hivi amejigharamikia kweli kununua kiatu kama hiki!!”
“Soma kwanza alichoandika juu”
Madam Oliva akaanza kusoma,
“Zawadi kutoka kwa madam le boss”
Basi madam Oliva akaguna,
“Mmmmh! Eti zawadi”
“Ndio, kwani yeye hawezi kupewa zawadi!! Mbona anaonekana ni kijana mzuri sana halafu mstaarabu”
“Aaaah usiku saivi, kwaheri shoga yangu tutaonana tena tu”
Basi madam Oliva alirudi nyumbani kwake ili alikuwa na mawazo sana kama baba Angel alivaa vile viatu au la, tena hakufikiria kama viatu alivyokuwa anaviona kwenye mtandao ndio hivyo hivyo alivyompa baba Angel.

Kulivyokucha tu, baba Angel leo aliamka na kujiandaa ila alipoondoka kwake hakwenda kwanza ofisini zaidi ya kwenda dukani kwake na kumkuta Steve akiwa tayari ameshafika, cha kwanza bila hata salamu alimuuliza,
“Viatu alivyokuletea jana mama Angel viko wapi?”
“Vipo nyumbani bosi”
“Aaaah naomba kesho uje navyo”
Kisha baba Angel akaondoka zake na kuelekea ofisini kwa muda huo, kwakweli Steve alishangaa sana kwani aliletewa vile viatu kwa uzuri kabisa na mama Angel ila alishangaa sana baba Angel kuvihitaji tena akatafakari kwa muda na kumpigia simu mama Angel,
“Mama, kuna tatizo kidogo huku”
“Tatizo gani hilo?”
“Sijui ni kwanini ila baba kaja hapa anahitaji vile viatu ulivyonipa jana”
“Mmmh!”
“Ndio, kasema kesho nije navyo ofisini ili nimpatie”
“Sasa sikia usifike navyo wala nini ila mimi nitakuletea kesho asubuhi viatu vya kufanana na hivyo umpatie, sawa!”
“Sawa mama hakuna tatizo”
“Na kama kuna lingine atasema niambie mapema, ila usimwambie kama umeongea na mimi. Nikiweza kuvileta leo basi nitakuletea leo leo ila nikishindwa basi nitakuja kesho asubuhi”
Kisha mama Angel alikata ile simu huku akitafakari kuwa kwanini mumewe ameamua kufanya vile!alifikiria sana kwani siku hiyo hata mumewe hakumchukua Erick na Junior kuwa aende nao kwenye ujenzi kumbe alikuwa amepanga kwenda dukani kwanza, alijiuliza ila tu hakuhitaji kumuuliza mumewe wala nini, na moja kwa moja alienda kwa dereva wao na kumuelekeza aina ya vile viatu ili akamtafutie dukani ambapo yule dereva aliondoka muda ule ule.

Baba Angel alifika ofisini kwake na kuwa kama mtu anayetafakari jambo Fulani na kuchukua simu yake huku akiangalia ujumbe wa simu ambapo kulikuwa na ujumbe wa madam Oliva, na ujumbe huu ndio uliomchanganya na kumfanya ile asubuhi kabisa aende kwenye duka lake, basi alisoma tena ule ujumbe,
“Baba Erick kama zawadi yangu huitaki basi nitakuja ofisini kwako kuichukua”
Muda kidogo alifika madam Oliva na kusalimiana nae halafu walianza kuongea,
“Hujaniambia chochote kuhusu ile zawadi nilikupa, viko wapi vile viatu?”
“Vipo nyumbani kwangu”
“Ila kwanini baba Angel hutaki zawadi yangu jamani!! Ungeona nilivyojikakamua kuitafuta zawadi ile dah!”
“Naelewa madam, na zawadi yako ni nzuri sana ila vile viatu havinitoshi”
“Jamani, si nilikwambia ujaribu ukakataa siku ile, unadhani mimi sijui namba unayovaa? Kabla sijakuchukulia kiatu nilichunguza kwanza namba unayovaa, sema tu hujapenda kiatu changu. Kikowapi sasa?”
“Njoo kesho uchukue, maana nimeviacha nyumbani”
“Sawa, ni zawadi gani nikuletee ambayo utaipenda?”
“Mmmh labda saa ya mkononi”
“Basi nitakuletea hakuna tatizo, ila naomba yani naomba ukubali zawadi yangu”
“Usijali madam, hivi shule bado wakina Angel hawajapangiwa?”
“Bado, ila wakipangiwa tu nitakuja kukwambia kwani una mpango wa kuwapeleka shule za Serikali? Kesho nitakuja tuongee shule nzuri za kuwapangia watoto”
“Sawa madam, hakuna tatizo”
Basi madam aliaga na kuondoka zake, ila siku hiyo baba Angel hakukaa sana ofisini pia kwani muda kidogo tu aliamua kurudi nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 266


Yule dereva alirudi nyumbani na viatu ambapo mama Angel alipoviangalia akaona vile viatu havifanani na vile anavyovitaka,
“Duh! Umenunua bei gani hivi?”
“Nimenunua elfu hamsini mama”
“Mmmh sio hivi kwanza havifanani na vile nilivyokuelekeza kabisa, vile sidhani kama vinauzwa chini ya laki tatu. Naelewa viatu vya aina ile. Ila ngoja niende mwenyewe basi”
Mama Angel akaenda ndani kujiandaa ili aende mwenyewe ila muda huo huo mumewe alirudi nyumbani na kumfanya ashindwe kutoka tena na kubaki tu na mumewe ila hakumuuliza chochote kuhusu kwenda dukani zaidi zaidi alimuuliza ratiba ya kesho,
“Mume wangu, leo naona hujaenda kabisa kwenye ujenzi, tatizo ni nini? Na kesho je ratiba yako ikoje?”
“Aaaah leo, sijui hata ila akili yangu haikuwa sawa nadhani. Halafu kesho ni lazima niende kwenye ujenzi, tunaenda kumalizia ujue, halafu kuna vitu natakiwa nikaangalie vizuri, kwahiyo kesho nitaondoka na wakina Erick asubuhi na kwenda nao kwenye ujenzi halafu nitaondoka na kwenda kazini mara moja”
“Oooh sawa mume wangu, kwahiyo inabidi niwaambie wakina Erick wajue eeeh kama kesho mtatoka”
“Ndio, ni vizuri ukawaambia”
Basi mama Angel alienda kuongea na wakina Erick ila baba Angel alishangaa sana moyo wake ukimuuma sana yani hakuwa na amani kabisa, viatu vile aliona vikimkosesha amani basi akajisemea kuwa kesho yake akitoka kwenye ujenzi ndio ataenda dukani kuchukua viatu halafu ataenda navyo ofisini,
“Yani nikishafanya hili nahisi moyo wangu utaridhika, sijui kwanini nimekosa amani kiasi hiki jamani! Sio kawaida yangu yani sielewi”
Aliamua tu kujilaza huku akitafakari mambo mbalimbali.

Siku hii kulivyokucha tu baada ya baba Angel kuondoka na wakina Erick, basi mama Angel nae alijiandaa na kuamua kuondoka nyumbani kwake kwenda dukani, kwahiyo mtoto alimuacha chini ya uangalizi wa Vaileth.
Alifika duka kubwa la viatu na kuangalia vile viatu avitakavyo, basi akaviona na kuvichukua kisha akaenda kulipia hela, ila wakati anatoka hapo dukani alikutana na rafiki yake wa muda mrefu sana Fetty na kufurahi kumuona na kuanza kuongea kidogo,
“Umebeba nini Erica?”
“Mmmh wewe nawe, umbea huachi jamani ni viatu hivi”
Fetty alichukua ule mfuko na kuviangalia kisha akasema,
“Kheee ndio umeamua kuja kumnunulia shemeji, naona viatu vimeingia hivi ila wanavaa wenye hela zao. Kuna shoga yangu kanunua kama hivi kumpelekea mume wa mtu huko”
Mama Angel alacheka na kusema,
“Umeanza sasa, yani yote yanakutoka wewe, hata kama hayupo utasema yupo”
“Kweli nakwambia, sasa kwanini nidanganye? Shoga yangu anaitwa Oliva”
Mama Angel akashtuka kidogo na kuamua kumvuta pembeni Fetty ili waongee vizuri, kisha akamuuliza,
“Sijakuelewa, yani kanunua kumpelekea mume wa mtu?”
“Ndio, yani Oliva anampenda huyo mwanaume kufa na kupona na amesema akivaa tu vile viatu basi kampata”
Mama Angel alihisi kama tumbo lake kuunguruma kidogo.

Mama Angel akashtuka kidogo na kuamua kumvuta pembeni Fetty ili waongee vizuri, kisha akamuuliza,
“Sijakuelewa, yani kanunua kumpelekea mume wa mtu?”
“Ndio, yani Oliva anampenda huyo mwanaume kufa na kupona na amesema akivaa tu vile viatu basi kampata”
Mama Angel alihisi kama tumbo lake kuunguruma kidogo.
Fetty alihisi kitu kwa mama Angel na kumuuliza,
“Vipi tena shoga yangu ndio unaibiwa mumeo nini?”
“Hata sielewi, hebu muulize vizuri huyo Oliva kuwa ameweka nini kwenye hivyo viatu hadi aweze kumteka kirahisi huyo mume wa mtu!”
“Basi hivyo huniamini wewe, nakwambia ukweli huniamini. Oliva nimesoma nae sekondari ni rafiki yangu mkubwa sana, yeye kila leo kuponda tu wanaume yani hakuna mwanaume ambaye huwa anasifiwa na Oliva, sasa siku nimekutana nae na kuanza kumsifia huyo mume wa mtu kwa hakika nilishangaa sana ila ndio hivyo anampenda huyo mume wa mtu kufa na kupona”
“Unajua nini Fetty, wewe ni rafiki yangu na sio rafiki yang utu ila upo kama ndugu yangu kwani ni mengi sana umenisaidia, hebu tuingie kwanza kwenye gari halafu nikueleze kidogo”
Basi waliingia kwenye gari, na muda ule mama Angel hakuona kama ni vyema kumficha Fetty kwani alijifunza pia kuwa mambo mengine ni vyema kusema ili uweze kupata msaada kuliko kukaa nalo moyoni peke yako likakutesa tu, basi alianza kumuelezea,
“Unajua ulivyoniambia Oliva nimeshtuka maana kuna mtu anaitwa madam Oliva, kwakweli nina mashaka nae sana kwa mume wangu. Huyo Oliva ni mwalimu?”
“Ndio ni mwalimu, tena ana vituo vyake vya kufundisha kozi mbalimbali na ana saluni yake”
“Mmmh ndio huyo huyo wala sio mwingine”
“Kwahiyo mwanaume anayemnyemelea ni shemeji?”
“Ndio, ngoja nikuelezee kidogo”
“Eeeh niambie”
Basi mama Angel alimueleza vile ambavyo madam Oliva kaweka ukaribu na mume wake, na ambavyo alivyompelekea zawadi ya viatu na yeye kwenda kuvitoa na ambavyo mumewe alivyobadilika,
“Duh! Pole sana, unajua hata siamini kama Oliva kaanza mambo ya ushirikina sababu ya mwanaume tena mume wa mtu!! Dah siamini, tena mume mwenyewe ni mume wa shoga yangu kipenzi, jamani! Ila dunia duara bhana, unayemfahamu wewe kumbe anamfahamu mtu mwingine. Sasa Erica shusha presha shoga yangu, namuendea Oliva hewani muda sio mrefu halafu nitaweka sauti kubwa kama yupo sehemu nzuri basi ataongea tu vizuri”
Basi muda huo huo Fetty akachukua simu yake na kumpigia madam Oliva ambaye hakuchukua muda aliipokea ile simu,
“Kheee shoga yangu uko wapi?”
“Nipo kwangu”
“Nataka kuja kwako leo”
“Aaaah sio leo jamani, nitakuja kukuchukua siku nyingine”
“Mmmh jamani kwanini?”
“Yani ni hivi, yule mume wa mtu nilikwambia basi leo nitamuweka mikononi mwanangu na kuja nae nyumbani kwangu yani sitamuachia wiki nzima”
“Mmmh Oliva jamani, humuonei huruma mke wake?”
Yani wakati huo mama Angel alikuwa akihisi tumbo kumuunguruma tu na akitetemeka kwa hasira, basi madam Oliva aliendelea kuongea,
“Nimuoneehuruma ya nini sasa wakati hata yeye mwanaume huyo alimuiba kwa mwanamke mwenzie? Mbona yeye hakumuonea huruma yule mwanamke?”
“Mmmh kwahiyo hata yeye alivuruga ndoa ya watu? Ila Oliva huyo mume wa mtu imekuwaje hadi umtake?”
“Yani siku moja nilikumta huyo mwanamke wa kwanza wa huyo mwanaume akilalamika sana kuhusu huyo mwanaume na kusema hawezi kumfanya kitu sababu anampenda sana, nikamuuliza kwanini ila alidai hakuna mwanaume kama huyo duniani, kiukweli na mimi nahitaji mwanaume wa tofauti kwahiyo nikaona huyu ndio atanifaa”
“Haya sasa utampataje?”
“Mwanzoni si nilikwambia kwenye viatu nilivyompelekea kuna siri kubwa sana, sasa leo nampelekea saa na lazima ataivaa tena nitamvisha mwenyewe maana kuna siri nzito sana na baada ya hapo nitaondoka nae, hapa naweka mambo sawa kwanza hapa nyumbani ndio niende”
“Kheee sikuwezi, basi utaniambia hiyo siri”
“Tukionana nitakwambia hakuna tatizo, ila leo ni siku yangu muhimu sana”
Basi Fetty alikata ile simu na kumuangalia mama Angel ambaye alikuwa akitoa machozi tu kwa muda huo, akamwambia
“Sasa shoga yangu kwasasa kulia hata hakusaidii, cha msingi unatambua mumeo alipo basi fanya juu chini ukamfate na urudi nae nyumbani na ujaribu kumueleza kila kitu ili uokoe ndoa yako ila kulia hakutakusaidia ndugu yangu”
“Yani nimechanganyikiwa ujue”
“Najua ndio, inauma na lazima ikuchanganye ila chukua hatua sasa, muda ni huu nenda kamfate mumeo kabla huyo Oliva hajamfikia, unajua tatizo ni rahisi kuingia ila ni gumu kutoka, utatambua ukweli mume wangu karogwa ila kila siku utaomba na kulia, mpaka siku akiachiwa ni umehenya sana, shukuru Mungu umeonyeshwa ni kitu gani kinaendelea juu ya mume wako, basi chukua hatua ili umuokoe mapema”
Basi mama Angel aliagana na Fetty ambaye alishuka kwenye gari na muda ule ni moja kwa moja alienda ofisini kwa mume wake.
 
SEHEMU YA 267

Mama Angel alivyofika ofisini hakumkuta mume wake, yani hapo ndio tumbo joto kwani alihisi pengine huyo madam ndio kashamchukua, basi akampigia simu,
“Uko wapi mume wangu?”
“Kuna mahali nipo nakunywa supu”
Mama Angel aliumia pia, akakumbuka kipindi wakienda kazini na mumewe basi mambo mengi mumewe alimwambia kabla ya kuyatenda yani baba Angel kama akitaka kunywa supu lazima amwambia mkewe na ampitie ofisini kwake waende pamoja, na muda wa kutoka mara nyingi alikuwa akirudi na mumewe nyumbani, kwahiyo aliona kama shughuli za uzazi zimemzuilia yeye kufanya mambo mengi sana, akaamua kumpigia tena simu,
“Mimi nipo hapa ofisini kwako mume wangu, niambie ulipo nije”
“Kheee mama Angel, umekuja ofisini!! Basi nakuja muda sio mrefu”
Na kweli muda sio mrefu baba Angel aliwasili, basi mke wake akamwambia,
“Kuna jambo nahitaji kuongea na wewe ila sio hapa inatakiwa tukaongelee nyumbani”
“Jambo gani hilo mama Angel, mimi nina kazi nyingi sana leo”
“Nakuomba sana mume wangu, nipo radhi kesho tuje wote ofisini nikusaidie kazi zako”
“Na mwanangu utamuacha na nani? Kwa mfano leo mtoto umemuacha na nani?”
“Erick, hebu kumbuka uliwahi kuniambia kuwa watoto hawabadilishi chochote katika maisha yetu maana sisi ndio tunaopendana zaidi, nitabaki kuwa Erica wako na utabaki kuwa Erick wangu, unakumbuka hilo!! Ulisema watoto ni sehemu tu ya kuchangamsha familia, sasa leo kwanini uchukie sababu ya mimi kumuacha mtoto!!”
“Kwanza umenielewa vibaya mke wangu, sijachukia ila nimekuuliza maana mtoto yule bado mdogo sana, nakupenda mke wangu na hilo halitabadilika”
“Basi twende nyumbani, nakuomba Erick”
Ingawa Erick alikuwa na kazi nyingi ila kwa hamasa za mke wake aliona kweli mkewe anahitaji kwenda nae nyumbani, ikabidi tu akubali na wakatoka nje ya ofisi, kisha baba Angel akamuuliza,
“Tutaondoka na gari yangu au yako?”
“Tutaondoka na gari yangu halafu gari yako tutamtuma dereva aje kuifata, nakuomba usikatae mume wangu”
Baba Angel alikubali na kupanda kwenye gari na mke wake ila wakati wanaondoka tu mama Angel alimuona madam Oliva akifika kwenye ofisi ya baba Angel lakini lile tukio la kufika madam Oliva wala baba Angel hakuliona na kumfanya mama Angel kutokuliongelea wala nini.

Nyumbani nako, Ester alikuwa akilia sana na kila walichokuwa wakijaribu kumpa alikuwa akikataa na kuendelea kulia, basi Erica na Vaileth wakashauriana kuwa wapi simu ila muda wanapiga simu tu na wazazi wao walikuwa wamefika hivyobasi mama Angel akamchukua mwanae na kwenda kumbembeleza na kumnyonyesha, mumewe aliingia chumbani na kumlalamikia,
“Unaona mke wangu, nilikwambia kuwa mtoto huyu bado mdogo na anakuhitaji sana kwa ukaribu ukaona sijui naongea nini, hivi ungenipigia simu nisingerudi nyumbani jamani hadi unifate!”
“Sio hivyo mume wangu, kuna matukio yamefanya mimi niwe hivi leo unajua nakupenda sana na pia naogopa sana kukupoteza mume wangu”
“Ooooh leo umeniambia neno tamu sana mke wangu, haya sasa malizia kumnyonyesha mtoto tuweze kuongea sasa”
Basi mama Angel aliendelea kumnyonyesha mtoto huku akifikiria kwanza jinsi ya kuanza kuongea nae mpaka mumewe amuelewe, Ester alilala basi mama Angel alimlaza na kumsogelea mumewe kisha akamtaka wasimame na kumwambia,
“Naomba tushikane mikono na tuombe”
“Kheee mama Angel, tuombe kuhusu nini sasa?”
“Nahitaji tuombe na tuvunje hila za shetani ila nitakachoongea na wewe kwa muda huu upate kunielewa”
“Jamani, inamaana mimi sielewi mpaka maombi!”
“Sina maana hiyo mume wangu, ila hili swala kabla hatujaliongelea inahitajika maombi kwanza”
Ilibidi tu baba Angel akubali ila kiukweli yeye binafsi hata hakujiandaa kwaajili ya maombi halafu alikuwa akilna uvivu sana, yani mwili wake ulikuwa na uzito sana kufanya maombi kwahiyo pale aliyekuwa akiomba ni mama Angel mwenyewe.
Baada ya maombi yale ndio alianza kuongea na mume wake,
“Unajua Mungu anatupenda sana sisi, kwanza kabisa katuvusha vikwazo vingi sana, kama milima na mabonde kwakweli tumevuka, penzi letu limepigwa vita sana ila tuliweza kufanikisha hadi mwisho wa siku tukaoana na leo ni mke na mume, nakupenda na unanipenda mume wangu. Mungu bado hajatuacha na anaendelea kulinda penzi letu ndiomana ikiwa kuna mtu mbaya anataka kujiingiza kwetu basi Mungu atatufunulia mtu huyo”
“Mtu gani sasa mbaya kajiingiza kwetu”
“Madam Oliva”
Baba Angel akashtuka, ndipo mama Angel aliamua kumwambia baba Angel mlolongo mzima yani kwa muda huo hakumficha kitu chochote kile, kwakweli baba Angel nae alibaki akishangaa sana kuwa ile kitu inakuwaje kwa namna ile, mara gafla ujumbe ukaingia kwenye simu yake baba Angel alipouangalia ulikuwa umetoka kwa madam Oliva, basi akampa mkewe ile simu ilia some ule ujumbe,
“Uko wapi Erick, nimekuletea ile zawadi ya saa ni nzuri sana maana ina jina lako katikati, uko wapi muda huu?”
Kisha mama Angel akamuangalia mume wake na kumwambia,
“Ndio ningekuwa nakukosa hivi mume wangu!!”
Baba Angel aliinuka na kumkumbatia mkewe kisha akamwambia,
“Asante kwa kunijali, unajua sikuelewa kuwa huyu mwanamke ana akili mbovu kiasi hiki! Ukimuona ni mwanamke mwenye akili timuma kumbe ana akili mbovu kabisa, mimi nakupenda wewe mke wangu na hilo halitabadilika”
Mara madam Oliva alianza kupiga simu baada ya kuona kuwa ujumbe wake haujibiwi, na mama Angel ndio alipokea simu ile na kuanza kuongea nayo,
“Madam, nakuomba kwa amani kabisa muache mume wangu, mimi ndio ninayejua kuwa huyu mwanaume nimetoka nae wapi, naomba niachie mume wangu. Hila zako zote unazozifanya ili umteke mume wangu nimezijua, mara umtegeshee kwenye viatu na sasa kwenye saa, tafadhari niachie mume wangu”
Madam Oliva hakuweza kuendelea kusikiliza kwani muda huo huo alikata ile simu, basi mama Angel na baba Angel walianza kuongea vizuri sasa kuhusu maisha yao.
 
SEHEMU YA 268

Kwakweli madam Oliva hakupendezewa kabisa na kujiuliza kuwa ni mtu gani ambaye anafanya kazi ya kutoa siri zake, kwani hakupenda yale mambo yamfikie mama Angel bila hata kufanikiwa, kwahiyo alichukia sana na muda huu alitafuta mtu wa kuongea nae na moja kwa moja alimpigia simu Fetty,
“Uko wapi muda huu?”
“Nipo nyumbani kwangu”
“Naomba nije nikuchukue tuje wote nyumbani kwangu”
“Kheee yule mgeni vipi tena shoga yangu?”
“Dah! Sijui hata nikuelezeje ila nitakuelezea tukifika nyumbani, nahitaji mtu wa kuongea nae kwa wakati huu”
“Sawa, hakuna tatizo njoo tu unichukue”
Basi madam Oliva akaamua kwenda kumfata Fetty nyumbani kwake.
Madam Oliva alifika nyumbani kwa Fetty na kumchukua Fetty kwenda nae nyumbani kwake ili kuongea nae kiasi, basi walivyofika akaanza kumwambia,
“Unajua sielewi yani sielewi kabisa, sijui nani kamwambia mke wa yule mwanaume jamani! Sielewi mimi”
“Kwani imekuwaje?”
“Mke wake kaja juu, yani nimempigia simu yule baba kapokea mke wake na kusema nimuache mumewe, dawa ninazotaka kumfanyia ameshazigundua. Sijui nani kamwambia”
“Pole, kwani ni dawa gani hizo? Halafu Oliva umeanza lini mambo ya madawa hayo shoga yangu?”
“Sikia nikwambia, nilitokea kumpenda sana huyu mume wa mtu na hata sikujua kama nitaweza kumpata, basi nina shoga yangu mmoja hivi anafanya kazi kwenye shirika flani la kifedha huwa naongea nae mambo mengi sana, nikamwambia akasema kuna bibi mmoja ana dawa za asili, sio limbwata la kumfanya mwanaume bwege sijui hapana ila ni dawa za asili hata yeye alizitumia kumpata mume wake, basi nikaona ni vyema anipeleke kwa huyo bibi na mimi ili niweze kupata hizo dawa za kumteka huyu mume wa mtu. Basi nikaenda nae na huko nikajifunza mambo mengi sana”
“Eeeeh mambo gani?”
“Ni hivi, yule bibi aliniambia kuwa inatakiwa kwanza nijue udhaifu wa huyo mke wa huyo mwanaume ili iwe rahisi kwangu kumteka mumewe maana udhaifu wake ndio nitautumia kama fimbo, ila nikamwambia udhaifu wa huyo mwanamke mimi siujui maana sijamzoea basi akasema ngoja afanye dawa zake za asili na kweli aliniambia udhaifu wa yule mwanamke”
“Udhaifu gani?”
“Basi aliwasha moto na kutupia dawa kwenye moto huo akaniuliza jina la huyo mwanaume nikamwambia anaitwa Erick basi akaanza kuniambia kuwa mke wa huyo mwanaume anaitwa Erica halafu huyo mwanaume ni anampenda sana mke wake tena sana ila mkewe ana udhaifu mwingi sana sema huyu baba anamvumilia tu mkewe, aliniambia udhaifu mmoja tu ambao ndio nilikuwa nataka kuutumia kwasasa kumteka mumewe kwani alisema nikishamteka basi udhaifu mwingine wa huyo mwanamke ningeujua kwa kupitia mkewe na hapo ndio ningeboresha zaidi na kufanya anipende mimi zaidi maana hizi dawa ni za muda tu”
“Sasa alikwambia kuwa huyo mwanamke ana udhaifu gani?”
“Nasikia huyu mwanaume ana upendo sana halafu anajua kujali ila mkewe sio mtu wa kujali, kitu kidogo tu nasikia huyu mwanamke hana kawaida ya kumnunulia mumewe zawadi kabisa ila yeye anapenda kuletewa zawadi na mume wake. Yule bibi akaniambia kuwa, yule baba anapenda mtu awepo wa kumpatia zawadi ila hayupo, yule mwanamke hana tabia hiyo sababu anahisi mumewe hana uhitaji, basi ndio akaniuliza zawadi gani nzuri ninayoweza kumpatia huyo mwanaume? Basi nikafkiria na kuwaza vile viatu, alisema nikatafute nimpelekee kwanza, basi nikanunua na kumpelekea yule bibi ambapo alivinuizia kuwa huyu baba akiviona tu kwanza awe anatamani kuvivaa na asipovivaa ahisi kichwa chake kumvuruga sana, akivivaa basi mawazo yote ni juu yangu kiasi nikimwambia twende nyumbani anakubali bila ubishi na anaanza kunipenda sana, na vile mimi nampenda basi inakuwa maradufu. Ila viatu hata sijui imekuwaje, nilimuuliza nimpelekee zawadi gani nyingine akasema nimpelekee saa basi nayo ndio nikaipeleka kwa bibi na akainuizia na kusema nifanye juu chini nimvishe na baada ya hapo angeondoka na mimi na kurudi nami nyumbani, basi hapa ndio ningemfanyia makeke yote sababu kuna dawa nishanawa sehemu za siri ambapo lazima angeomba mechi na hapo asingeganduka kwangu, unajua hapa nimechanganyikiwa sana”
“Duh pole, kwahiyo na dawa yenyewe ushaitumia hiyo ya sehemu za siri?”
“ndio kwani nilijua leo hapindui nilijua lazima nitarudi nae tu na tungekuwa wote, sijui ni nani ananizunguka jamani”
“Pole sana shoga yangu, nakuhurumia sana sijui hata utafanyeje?”
“Yani acha tu, hebu nishauri ndugu yangu sielewi kitu hapa”
“Sasa, ngoja nirudi nyumbani pia nitulize akili yangu halafu nitakupigia simu ili tuongee vizuri zaidi ndugu yangu na nitakwambia cha kufanya”
Sababu muda nao ulikuwa umeenda ikabidi tu madam Oliva amruhusu Fetty kuondoka, kwakweli akili yake ilikuwa imechanganyikana kiasi kwamba hata kumsindikiza hakumsindikiza.

Fetty aliondoka huku akifikiria mambo mengi sana na kujiuliza,
“Jamani, sasa Erica anashindwa kumnunulia mumewe zawadi jamani!! Ila simshangai sana ni kawaida ya wanawake wengi tukiolewa tunasahau jambo hili ni dogo ila huwa tunasahau ni kama baadhi ya wanaume nao huwa wanasahau jambo hilo. Zawadi ni kitu kidogo sana ila kumbe zawadi inaweza kufanya ukaribishe mchepuko ndani!! Nitamwambia shoga yangu ajirekebishe halafu na mimi pia nimejifunza jambo jamani, kesho nitaenda kumtafutia mume wangu zawadi mmmh makubwa haya ya leo”
Basi Fetty alivyofika nyumbani kwake tu alimpigia simu mama Angel na kuongea nae,
“Kuna mambo nahitaji kuzungumza na wewe, kwahiyo tukionana nitakwambia rafiki yangu”
“Mambo gani hayo?”
“Tukikutana tutazungumza, ikiwezekana kesho tuonane ndugu yangu”
“Sawa, hakuna tatizo basi njoo nyumbani maana si unajua ninalea!”
“Sawa, nitakuja. Utanilekeza basi”
Wakaongea pale ila alivyokata ile simu tu muda huo huo alipigiwa simu na madam Oliva na kuanza kuongea nae,
“Tatizo nini Oliva?”
“Jamani, mwenzio sipo sawa yani sipo sawa kabisa”
“Kwanini?”
“Nahitaji mwanaume, kiukweli nahitaji mwanaume jamani!”
“Kheee pole jamani, zile dawa ulizotumia”
“Yani acha tu, dawa zinanitesa hizi, nahitaji mwanaume kwasasa hata sijui nifanyeje? Yani nimejikuta nikimtamani hata mlinzi wangu, Eeeh Mungu anisaidie jamani nisifikie hatua ya kujidhalilisha namna hii”
“Pole ndugu yangu, sasa ngoja nikushauri kitu”
“Kitu gani?”
“Chukua simu yako, ingia kwenye mtandao wa kijamii halafu angalia picha za watu, matukio mbalimbali, tafuta zile kurasa za vichekesho ucheke humo hadi siku ipite, pole sana”
“Mmmh huo ushauri wako jamani sijui kama utanisaidia, nipo na hali mbaya sana mwenzio”
“Pole, kesho nitakutafuta ili tuongee kidogo”
“Asante, ila sipo sawa kabisa yani”
Alikata ile simu kiukweli Fetty hakujua ni njia gani ya kumsaidia Oliva ila alimuhurumia sana na kusema,
“Ila huyu nae ni kilanga chake, hivi mwanaume hata hamjakubaliana unaenda kutumia dawa jamani!! Si ndio mwanzo wa kutembea na mbwa mmmh!! Halafu ni mwalimu, kwakweli Oliva kajiharibia sifa kwaajili ya ujinga wa kutaka kuiba mume wa mtu”
Alimsikitikia sana maana hakujua ni kitu gani rafiki yake angekitenda.
 
SEHEMU YA 269

Steve alikuwa ametoka zake kuoga na akijiandaa kulala ila alichukua simu yake na kutembelea kwenye mtandao kidogo, ila alivyoingia tu alibambana na picha ya madam Oliva hapo moyo wake ukalia paaa na kuzidi kumpenda huyu madam, aliona kabisa kuwa anashindwa kuzuia hisia zake, basi aliamua kumfata sehemu ya ujumbe na leo alimuangikia ujumbe,
“Nakupenda sana”
Ila hakufikiria kama madam Oliva angemjibu kwani ilikuwa ni kawaida yake kutokujibu jumbe za huyu mtu ila alishangaa kuona madam kama anaandika vile alijikuta akiwa na hamu sana ya kupata jibu la huyu madam,
“Wewe nawe kila leo naona jumbe zako, kwani unataka nini kwangu?”
“Nakuhitaji, kwakweli nakupenda sana. Natamani uwe mke wangu na tuishi pamoja”
“Unamaanisha hayo unayoyasema?”
“Ndio namaanisha, nakupenda sana yani sijielewi juu yako”
“Unaweza kuja nyumbani kwangu muda huu?”
“Naweza ndio, nielekeze nije”
Basi madam Oliva alimuelekeza na muda huo huo Steve alijiandaa haraka haraka na kutoka kwao na moja kwa moja alipanda pikipiki na kwenda hadi alipoelekezwa na madam Oliva, hakujali umbali ila alichojali yeye ni kuonana na madam Oliva.
Na kweli alifika na kumtumia ujumbe,
“Tayari, nipo nje ya nyumba uliyonielekeza”
“Mmmh upo serious kumbe, gonga hapo namwambia mlinzi akufungulie”
Ni kweli Steve aligonga na kufunguliwa na mlinzi na moja kwa moja akaingia kwenye ile nyumba na kukaribishwa na madam Oliva ambaye jambo la kwanza alimuuliza,
“Hivi wewe umejiamini vipi kufika kwa mtu ambaye humfahamu tena kwa muda kama huu?”
“Ni sababu ya upendo nilionao juu yako, nimejikuta nikijitoa muhanga tu na kuja”
“Halafu umenishangaza ujue, hata namba yangu ya simu hukuwa nayo?”
“Nilisahau kabisa kuhusu simu jamani, yote sababu nakupenda sana”
“Ulipanga ukifika na kuniona ufanye kitu gani?”
Basi Steve hakutaka kupoteza muda kwani alimsogelea madam na kumkumbatia kisha akambusu na wote kwa pamoja waliingia chumbani na kulala huko hadi asubuhi kabisa kwahiyo wakawa wamefungua ukurasa mpya wa mapenzi, kilishomshangaza madam Oliva ni kuwa alijikuta akimpenda huyu Steve kupita

Leo Fetty alienda nyumbani kwa rafiki yake yani mama Angel kama ambavyo walipanga jana yake kuwa waonane na waweze kuzungumza, na alipofika pale wanaenda kukaa bustanini na kuongea mambo mbalimbali ambapo Fetty alimueleza kila kitu ambacho kaambiwa na Oliva kisha alimuuliza rafiki yake,
“Ila na wewe unashindwa nini kumnunulia mumeo zawadi?”
“Mmmh sijui ni kwanini jamani, huwa naona mume wangu ni mtu wa kuzunguka sana, kwahiyo huwa nahisi kama akitaka kitu chochote basi lazima atakiona kwenye mizunguko yake na atakinunua”
“Ila kama ukimtafutia wewe zawadi inakuwa vyema zaidi, anazunguka kweli ila zawadi kwenye mahusiano ni muhimu sana haijalishi ana pesa kiasi gani”
“Ni kweli usemayo, kwanza umenifungua akili na mawazo rafiki yangu, kwakweli nitaanza kumtafutia mume wangu zawadi pia nitaanza kupeleleza ni tabia gani ninazo ambazo mume wangu hazipendi ili nizirekebishe, ni kweli ananivumilia kwa mengi sana”
“Ndio hivyo, mumeo anakupenda na usitake kuwa sababu ya mumeo kutoka nje ya ndoa halafu uje usingizie shetani. Mpende mumeo, mjali, mthamini na umuone kama kitu cha thamani kubwa sana katika maisha yako”
Kwakweli yale maneno yalimuingia sana mama Angel na aliona kuwa anapaswa kujirekesbisha ili kutetea ndoa yake, basi waliongea mengi ila Fetty sababu alitaka kwenda pia kwa madam Oliva kwahiyo aliamua kumuaga mama Angel.
Ilibidi mama Angel amsindikize kidogo Fetty, ila wakati wanatoka nje ya geti gafla akatokea Sia, ni kwavile hawakumtarajia walibaki kumshangaa kwa muda ila gafla Sia akamzaba kibao mama Angel.

Kwakweli yale maneno yalimuingia sana mama Angel na aliona kuwa anapaswa kujirekesbisha ili kutetea ndoa yake, basi waliongea mengi ila Fetty sababu alitaka kwenda pia kwa madam Oliva kwahiyo aliamua kumuaga mama Angel.
Ilibidi mama Angel amsindikize kidogo Fetty, ila wakati wanatoka nje ya geti gafla akatokea Sia, ni kwavile hawakumtarajia walibaki kumshangaa kwa muda ila gafla Sia akamzaba kibao mama Angel.
Kile kitendo kiliwashangaza sana Fetty na mama Angel, basi Sia alinyoosha tena mkono wake kutaka kumzaba kibao kingine mama Angel ila Fetty alimkamata ule mkono na kumshusha chini halafu alienda katikati ya Sia na mama Angel na kumuuliza Sia,
“Tatizo ni nini? Unafika kwenye mji wa watu na kuanza kunasa vibao wenye nyumba!”
“Hata na mimi ni mwenye nyumba hii”
“Khee makubwa haya”
Fetty alifikiria kidogo na kumuuliza mama Angel,
“Erica, kwahiyo huyu ndio Sia?”
“Eeeeh ndio huyo!!”
Sia nae akajibu,
“Kumbe unanifahamu eeeh! Nilitaka nishangae unaacha vipi kunifahamu wakati mimi nakufahamu kila kitu na familia yako nzima, kwahiyo ndio mnajitia mashoga na huyo Erica, kuna ushoga kati yenu au unafki tu”
“Kheee jiheshimu wewe mwanamke, wengine na utu uzima huu huwa hatupendi kugombana kabisa, kwani tatizo lako nini?”
“Huyo Erica, kwenda kumvesha mume wangu viatu vya limbwata la yule madam ni nini mpaka muda huu yule madam kamuweka Steve ndani kwake”
Mama Angel alicheka na kutikisa kichwa, kisha alimuuliza Sia,
“Huyo mumeo ni nani jamani! Mbona una mapya kila siku lakini!”
“Inamaana hujui kama mimi na Steve tulifunga ndoa!!”
Fetty akasema,
“Sasa wewe nishakuelewa vizuri, kumbe wewe ndio uliyesababusha mdogo wake Dora akakuoa, na ndio ukamfanyia visanga, kwanza hukuwa na aibu mtu mzima wewe kuwa na yule mtoto!”
“Kwani huyo madam ni mtoto!!”
“Hata kama, naomba uende maana hata sioni kama una maneno yanayoeleweka. Erica rudi ndani tu, huyu mimi nitamalizana nae”
“Utamalizana na mimi kitu gani mnafki mkubwa wewe, hivi kweli marafiki wa damu wanaweza kushea mwanaume? Yani mwanaume anayeachwa na rafiki yako ndio wewe unaenda kujipeleka ili akuoe wewe, kwa mtindo huo si ndio nyie mnaoweza kuolewa hata na mume wa dada yako wa damu! Hivi Erica unafikiri huyu anashindwa kutembea na mumeo? Subiri uone picha, unaruka jivu unakanyaga moto”
Fetty alimuangalia Sia na kumsikitikia kisha akamgeukia mama Angel na kumwambia,
“Ndugu yangu rudi ndani, huyu humuwezi, nitawezana nae mwenyewe”
Na kweli mama Angel alijiona wazi kuwa hamuwezi Sia kwani mama Angel hakuwa mtu wa kuweza kujibishana sana ndiomana mara nyingi alikimbilia kulia, basi aliamua tu kurudi ndani ila Sia alitaka kuingia pia ambapo Fetty alimshika mkono na kumvuta kisha akamwambia,
“Njia ya kuondokea ni hii hapa, haya niambie hilo dukuduku lako ulilonalo. Kwani wewe inakuuma nini mimi kuolewa na mwanaume aliyeachana na Erica? Katika dunia hii ni wapi utampata mwanaume wako peke yako? Akiwa na wewe ujue kuna mtu kaachana nae, ni wapi utampata wako tu! Hebu tumia akili muda mwingine”
“Ila sijapenda kwa alichokifanya Erica, mimi ananifahamu akili zangu zilivyo nitamfanyia kituko hicho hatasahau maisha yake yote”
“Sasa wewe hujapenda kitu gani, yani kitu gani kimekufanya uchukie hivyo?”
“Steve haelewi kitu hatambui kitu, nimeenda dukani sijamkuta, nimempigia simu anasema yupo kwa Oliva”
Ndio hapa kidogo Fetty alishtuka yani mwanzoni alikuwa kama haelewi vile, ndio hapa kajua kuwa rafiki yake Oliva kamuopoa Steve ila hakuelewa ni sababu ya viatu ambavyo Sia anasema au ni sababu ya nini? Basi wakati akifikiria yale ni sauti ya mtoto wa kiume ndio ilimshtua, mtoto huyu alikuwa ni Elly ambaye alisogea kumuita mama yake na alivyofika pale alimsalimia Fetty na kuongea na mama yake ambapo Fetty alikuwa kasimama tu akiwaangalia na walipomaliza kuongea alimuuliza Sia,
“Huyo ni mtoto wako kweli?”
“Kwanini?”
“Umepata wapi mtoto mstaarabu na mwenye heshima kiasi hiko!”
“Mbona hapa bado, ukimuona wangu wa ukweli nadhani ndio utapagawa na kustaajabu zaidi”
Muda huu Sia aliondoka na mwanae na kumfanya Fetty amuangalie tu huku akitikisa kichwa na kusema,
“Hivi kuna mwanaume mwenye akili zake timamu kabisa aamue kuwa na huyu Sia kwasasa!! Labda ampe limbwata kama huyo mdogo wake Dora”
Kisha aliondoka zake kuelekea kwa madam oliva.
 
SEHEMU YA 270

Fetty alifika nyumbani kwa madam Oliva, ila mlinzi getini alimwambia kuwa madam Oliva hayupo,
“Kheee kaenda wapi kwani?”
“Sijui, ila kuna kijana alikuja jana usiku hapa na leo madam kanitambulisha kuwa yule ndio baba wa mwanae yani ndio mumewe, na muda ule walikuwa wanaenda kuchukua mizigo ya yule mwanaume maana anahamia hapa”
“Kheee yamekuwa hayo!! Jamani Oliva sio mzima mmmh!”
Fetty aliamua kuondoka zake, ila alipokaribia kufika nyumbani kwake alikutana na Dora na kuanza kusalimiana pale,
“Umetokea wapi Dora?”
“Nimetokea nyumbani huko mama aliniita mara moja”
“Vipi tena?”
“Unajua mdogo wangu tokay ale majanga ya Sia hadi kuoana nae na kuishi nae pamoja, walivyoachana basi alirudi nyumbani na mama alimuomba jambo moja kuwa akipata mwanamke wa kuishi nae basi aje kuishi nae nyumbani maana tuna nyumba kubwa tu kwasasa. Cha kushangaza nasikia jana usiku kaondoka tena bila hata ya kumuaga mama yani mama kamuona tu akitokomea na pikipiki akanipigia simu basi leo nimeenda, loh muda kidogo Steve kaja na huyo mwanamke na wamefika pale na kusema wamekuja kuchukua nguo za Steve kwani anaenda kuishi na huyo mwanamke, jamani mdogo wangu lini akili yake itamkaa sawa? Atalelewa na wanawake hadi lini? Mwishowe wanamdhalilisha, ila nadhani yule mwanamke kampata mdogo wangu kwa madawa tu ila nitajua mchezo wote nadhani kuna watu wanataka kutibua akili yangu”
“Mmmh jamani, mbona haya mapya?”
“Ndio hivyo”
Simu ya Dora ikaita alikuwa akiitwa tena kwao kwahiyo ilibidi aagane na Fetty, yani hapo Fetty ndio akaelewa wazi kuwa kitu gani kinaendelea kati ya madam Oliva na Steve ila ambacho hakuelewa ni kitu gani kimewakutanisha pamoja watu hawa ni vile viatu na malimbwata ya Oliva au ni kitu gani, hakuelewa kabisa.

Kuna mambo Angel alikuwa akijaribu kuyaunganisha kwenye kichwa chake bila ya kupata jibu, kwanza alikumbuka maneno ya mama yake mkubwa pindi alipomuona na Ally, akakumbuka na siku ambayo wazaziwake walikuwa hapo halafu mama yake mkubwa akaenda hapo, kwahiyo aliwaza kitu ambacho mama yake mkubwa alisema na kujiuliza,
“Sasa ni ukweli gani ninaopaswa kuufahamu?”
Alitamani kujua, basi muda huu alimfata bibi yake na kumuuliza,
“Bibi samahani, eti ni ukweli gani ambao mimi napaswa kuufahamu ila nyie hamtaki nifahamu?”
“Sikia Angel, unajua vitu vingine sio vya kujiumiza kichwa wewe kama wewe, ukiona jambo ambalo wazazi wako wameamua kukuficha basi tambua kwamba hutakiwi kulijua jambo hilo na pengine ukilijua linaweza kukupa madhara makubwa”
“Jamani bibi!”
“Ngoja tubadili kidogo mada, hivi kati ya baba yako na mama yako unampenda zaidi nani?”
“Mmmh wote nawapenda”
“Ndio wote unawapenda ila unayempenda zaidi ni nani?”
“Nampenda zaidi baba”
“Kwanini?”
“Sijui jinsi gani ya kueleza ila nampenda zaidi baba, naamini kuwa baba ananipenda sana, ananijali na kunithamini”
“Hivi gafla ukaletewa taarifa kuwa baba yako amekufa utafanyaje?”
Kwanza Angel alishtuka sana na kumwambia bibi yake,
“Bibi usiseme hivyo jamani, mimi nitakufa ujue. Naomba umpigie simu baba yangu niongee nae, nakuomba bibi”
Bibi Angel akakumbuka tabia ambayo alikuwa nayo Angel wakati mdogo alipenda sana kuongea na baba yake kwenye simu kiasi kwamba wasipopiga simu anaweza kugoma hata kula, alifikiria kidogo na kumpigia simu baba Angel ambaye kwa muda mfupi tu alipokea na moja kwa moja bibi alimpa Angel,
“Shikamoo baba”
“Marahaba mwanangu”
“Unaendeleaje baba, ni mzima kabisa wewe?”
“Salama mwanangu, mimi ni mzima kabisa. Naona umenikumbuka leo, nitakuja kukuchukua mwisho wa wiki nikupeleke matembezi kidogo binti yangu”
“Asante sana baba”
Kisha alikata simu halafu Angel alimuangalia bibi yake na kumwambia,
“Unaona bibi, yani baba atakuja kunichukua anipeleke matembezi, jamani huyu baba ananipenda mimi tena ananipenda sana nadhani katika watoto wote basi mimi ndio namba moja ndiomana huwa anasema nimefanana na nyanya yake”
Basi bibi yake alimuangalia Angel, yani malezi ambayo Erick alimpa huyu mtoto yaliwafanya kupatwa na uoga kidogo kumwambia Angel ukweli kuwa yule sio baba yako maana walikuwa wakijifikiria je Angel ataichukuliaje ile hali ya kugundua kuwa Erick sio baba yake wa ukweli na ikiwa kila mahali anajitapa kuhusu baba yake huyo!! Yani hata bibi ilibidi ake kimya kwa muda kwani kuzungumza ukweli kwa wakati huo ilimuwia vigumu sana.
Angel ndio alimshtua bibi yake kutoka kwenye yale mawazo,
“Bibi zimebaki siku mbili halafu baba yangu anakuja kunichukua kunipeleka matembezi, hivi bibi kwa hali hii kwanini nisimpende baba yangu! Kwakweli baba ni kila kitu katika maisha yangu”
“Na Samir je!”
“Jamani bibi, mbona umebadilisha mada. Ila bibi nyie hamjanigundua vizuri, hakuna kitu napenda kama kukatazwa kufanya jambo Fulani na baba sababu yeye sio kwamba ananikataza kila kitu, shughuli kwa mama kila kitu anakukataza, jambo kidogo tu anafoka, siku moja niliunguza mboga uwiii mama alisema sana ila baba hakuongea jambo zaidi ya kwenda kununua mboga nyingine na kuileta nyumbani, tena mboga iliyopikwa, kisha akaniambia usijali mwanangu hiyo ni Bahati mbaya, nampenda sana baba yangu kuliko kitu chochote duniani”
“Unajua wewe ni mtu wa kwanza kusema hivyo, katika dunia hii kila mtu anampenda mama yake kuliko kitu chochote. Wewe Angel vipi wewe?”
“Mama nampenda tena sana tu ila baba nampenda zaidi”
Bibi akapumua tu na kuamua kwenda kuendelea na mambo mengine huku akifikiria mambo mbalimbali ila muda kidogo Angel alienda kumuomba simu ili aweze kuwasiliana na rafiki zake, siku hiyo bibi hakukataa wala nini kwani alimpa tu ile simu akawasiliane nayo.
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi


4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma

Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

💥💥💥NEW 💥 💥 💥

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma

NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 271

Leo usiku baba Angel alimwambia mama Angel namna alivyowasiliana na Angel na vile alivyomwambia,
“Wewe nawe unamuendekeza sana huyo Angel”
“Ila mke wangu unajua kuna muda huwa sikuelewi kabisa, nikifanya hiki kwa mtoto huyu unasema nampendelea huyu, jamani mbona mimi nalea watoto kwa usawa? Hebu siku moja muulize Erica, unamuonaje baba nae atakwambia halafu siku nyingine muulize Erick halafu useme kama kuna mtoto yoyote nampendelea”
Mara simu ya mama Angel iliita naye aliyepiga alikuwa ni dada yake Mage, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,
“Mdogo wangu unajua leo nimekutana na nani?”
“Nani huyo?”
“Nimekutana na Rahim”
“Kheee dada nawe!”
“Na nimemuuliza kuhusu Angel kasema anamkumbuka, yani kwa kifupi ni kuwa Rahim anamkumbuka vizuri kabisa mtoto wake, tena anasema akikutanishwa nae atafurahi sana maana ni damu yake”
Mama Angel alikata hii simu na kuizima kabisa, basi mumewe alimuuliza,
“Tatizo ni nini mke wangu? Nani huyo aliyekuwa anakupigia?”
“Ni mtu kakosea namba sasa akawa anongea sana”
“Mmmh Erica umeanza uongo tena halafu hapa hapa tuko wote, nimekusikia kabisa hapo ukisema dada nawe inaonyesha wazi ni dada yako halafu saivi kusema ni mtu kakosea namba kweli jamani mkwe wangu ndio aina ya maisha tunayotaka kuichagua hiyo!!”
“Nisamehe mume wangu, ni hivi dada Mage kanipigia simu na kuanza kunikumbusha zile zile mada za kutaka Angel aujue ukweli kuhusu baba yake”
“Kwani Mage yeye cha zaidi nikipi kwake yani kitu gani kinamuumiza akili sana? Ni Angel kutokumjua baba yake au ni maisha ya Angel?”
“Yani yeye anakazana kusema kuwa Angel anaweza kuolewa na kaka yake halafu ikawa balaa kwetu”
“Hivi Angel akiolewa na kaka yake balaa ni kwetu au kwa Rahim maana si ndio ukoo wake? Mimi nasema tu ila ukiona umuhimu wa Angel kufahamu ukweli basi mwambie tu”
“Unadhani ni rahisi hivyo! Kumbuka wakati Angel akiwa mdogo kipindi tunamruhusu Rahim kuja nyumbani kucheza cheza na Angel ili amzoee ni nini kilitokea? Mtoto alikuwa akilia muda wote ambao Rahim atafika nyumbani halafu na ule ujinga alioufanya ndio kabisa ukafanya tujifiche wasijue tulipo ila najua familia haielewi ni yapi nimepitia ni yapi huyo Rahim kanitendea, najua hawaelewi ila siku moja nitakayomwambia Angel ukweli basi nitamwambia na ujinga wote ambao baba yake kanifanyia”
“Mmmh ila naiogopa hiyo siku naiogopa sana, nilimwambia Rahim mapema sana, unatakiw auje mtoto akuzoee hata akiambiwa ni baba yake mtoto anakuwa hana mashaka yoyote na anakuwa na furaha, hivi kwa ile tabia ya Rahim kama utaamua kumueleza Angel atataka kweli kumfahamu baba yake? Atataka Rahim kuwa baba yake? Sijui lakini ila kuna umuhimu wa mtoto kumfahamu baba yake mzazi”
“Ila ngoja mwanangu akue vizuri hata nikimueleza anielewe na asichukie kwanini nilimficha kwa kipindi chote hiki”
Walibaki tu kuongea ila hawakuweza kuelewana kuwa wakati sahihi wa kumwambia Angel ukweli kuhusu baba yake ni wakati gani.

Kulivyokucha tu, Erica aliamka tena siku hiyo aliamka mapema sana kutokana na ndoto aliyoota ambapo alitaka kwenda kumsimulia kaka yake ili waweze kushauriana juu ya ndoto hiyo, basi moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kufungua mlango ambapo bado Erick alikuwa amelala ule usingizi wa asubuhi, basi aliaenda kumtikisa,
“Erick, Erick”
Erick alishtuka na kuanza kufikicha macho, mara Erica alianza kucheka na kumfanya Erick amuulize,
“Nini unacheka?”
“Nini hiko kimetuna kwenye kaptula yako?”
Aliuliza huku akiendelea kucheka basi Erick akavuta shuka na kujifunika vizuri kisha akasema,
“Yani wewe Erica dah!! Una mambo ya ajabu ujue, kwahiyo unataka kujua nini kimetuna kwenye kaptula yangu kweli!! Aaah tuachane na hayo, hebu niambie kilichokuleta asubuhi hii maana lazima una jambo”
“Ni kweli nina jambo, mwenzio leo nimeeta bhana”
“Umeota nini?”
“Ndoto yangu ilikuwa hivi, nilimuona dada Angel anaolewa halafu yule mwanaume aliyekuwa anamuoa dada Angel kama namfahamu vile ila sijui simfahamu, mara nikamuona mama na baba halafu akatokea mama mwingine sijui ni mama wa bwana harusi akasema, sikufahamu kama huyu ni baba yake Angel, kwamaana hiyo Angel na huyu kijana ni ndugu yani mtu na dada yake. Nikashtuka sana kutoka kwenye ile ndoto, nimetafakari bila ya kupata jibu ndiomana nikaona nije nikushirikishe, eti au baba ana watoto wengine nje?”
“Mmmh hapana bhana, sidhani kama baba ana watoto wengine”
“Sasa kwanini niote hivi kuwa dada Angel anaolewa na mtu ambaye inasemekana ni kaka yake! Lazima baba atakuwa na watoto wengine nje”
“Na wewe Erica, kwani umeambia hiyo ni kweli? Hiyo ni ndoto tu kama ndoto zingine, kama baba angekuwa na watoto wengine nje basi angekuja kusema kuwa hawa ni watoto wangu, kwanza baba ana upendo sana kwahiyo hawezi kuacha watoto wake sehemu nyingine wahangaike, sidhani kama baba ana watoto wa nje”
“Ila sisi tuna Bahati ujue, yani Samia anasema kuwa kwa baba yake ana watoto hao hadi wengine hawafahamiani, yani na wewe Erick usiwe kama babake Samia”
“Sasa mimi nitakuwaje kama huyo jamani wakati hata wazo la kuoa halipo kwenye akili yangu, wazo la kuwa kwenye mahusiano halipo kwangu kabisa sasa nitaanzaje kufikiria kuwa kama babake Samia!”
“Sawa, hapo utakuwa kijana mzuri. Ila niambie kilichotuna muda ule kwenye kaptula yako ni nini?”
“Unajua wewe ni chizi sana, ngoja nikaoge kuna siku nitakuonyesha hiko unachokiulizia”
“Mmmh!”
“Sasa unaguna nini? Si umeuliza mwenyewe? Kuna siku nitakuonyesha”
“Haya bhana”
Kisha Erica akainuka na kutoka chumbani kwa kaka yake.

Leo baba Angel hakwenda ofisini wala hakwenda kwenye ujezi sababu ujenzi alikuwa amemaliza karibu kila kitu kwahiyo alikuwepo nyumbani tu, muda huu alikuwa ameshika simu ya mke wake mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu hii basi aliufungua na kuusoma,
“Sasa umeamua kumfanyia hivi mume wangu ilihali unajua wazi kuwa mimi na Steve tulifunga ndoa ya uhalali kabisa, basi nakwambia hivi mimi nitaendelea kumng’ang’ania mumeo mpaka mwisho wangu”
Yani baba Angel alijihisi kucheka na kutikisa kichwa kisha akasema,
“Ndiomana huwa nasema huyu mwanamke ni chizi, hivi mtu mwenye mume kweli anaweza kupoteza muda wake kukazana ili ampate mume wa mwanamke mwingine! Halafu bila aibu yupo kulalamika kuhusu Steve, jamani huyu Sia ni wa kumsamehe tu”
Akacheka pale na kuweka simu ile pembeni na moja kwa maoja aliinuka na kwenda kwenye chumba chake cha kujisomea na kuanza kusoma magazeti mbalimbali ambayo yaliletwa. Wakati baba Angel akisoma yale magazeti, akapigiwa simu na rafiki yake mmoja,
“Uko wapi Erick?”
“Aaaah leo nipo nyumbani tu, sijaenda popote”
“Kuna jambo la maana sana nahitaji kuongea nawe kuhusu ile ofisi yako mpya”
“Mmmh sasa utaweza kuja nyumbani kwangu!!”
“Sawa, nielekeze nakuja”
Basi baba Angel alimuelekeza yule rafiki yake ambaye aliahidi baada ya muda mfupi kufika mahali pale.
Alipofika aliwasiliana na baba Angel ambapo alitoka nje kumkaribisha na moja kwa moja alienda nae kwenye kile chumba cha kujisomea kwani aliona hata maongezi kama watafanyia humo ni vizuri zaidi, muda huo mkewe likuwa yupo na mtoto chumbani kwahiyo hata hakujua kama kuna mgeni amefika pale kwao.
Basi baba Angel akaanza kuongea na yule mgeni,
“Kwanza Erick, yule mwanao uliyekuwa unaendaga nae kwenye ujenzi yuko wapi?”
“Nilikuwa naenda na wawili ujue, kuan Junior na kuna Erick”
“Mmmh siwajui kwa majina ila naweza mtambua kwa sura”
Basi baba Angel aliwaita Junior na Erick kuwatambulisha kwa yule mgeni,
“Jamani, huyu ni rafiki yangu anaitwa Juma, halafu hawa ndio Junior na Erick”
Yule mgeni alifurahi kuwafahamu kisha baba Angel akawaruhusu waendelee kwenye shughuli zao ambapo waliondoka, basi yule mgeni akamwambia Erick,
“Niliyekuwa nataka kumsema ni yule Erick, kwakweli umepata kichwa kile ni hatari nadhani ndiomana umempa jina lako. Sasa sikia nikufundishe ujanja, yani Erick unampeleka pale kiwandani na umwambie tunahitaji kufanya moja mbili tatu ila itakuwa chini ya uangalizi wako, halafu muache ashughulike na hiyo kazi mwezi mmoja tu utaona matunda yake yani utafurahi na kusema kweli una mtoto mwerevu”
“Mmmh ila bado anasoma”
“Anasoma ndio, ila weka utaratibu Fulani hivi hata kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ni siku za yeye kushughulika na biashara tu, matunda yake utaniambia kuwa nilisema. Ila kuna jambo nataka kukuuliza”
“Jambo gani?”
“Huyu mtoto mwingine Junior, mbona kafanana na James?”
Baba Angel alicheka kidogo na kusema,
“Kumbe James ulimfahamu, basi yule ni mtoto wake kabisa”
“Jamani!! James alikuwa ni rafiki yangu sana. Kumbe ni mtoto wake yule!! Nitakuja kufanya kitu kwaajili yake kama ukumbusho kwa baba yake!”
“Itakuwa vizuri sana ndugu yangu kumbe ulifahamiana sana na James!! Inawezekana hata mke wangu unamfahamu maana mke wangu ni mdogo wa aliyekuwa mke wa James”
“Aaaah kumbe!! Basi inawezekana namfahamu”
Ikabidi baba Angel aende kumuita mke wake ili waonane na rafiki yake, na kweli mama Angel alifika pale na kutazamana na huyu mgeni kwanza alimshangaa kidogo kufahamiana na mume wake maana alikuwa akimfahamu huyu mtu, basi alisalimiana nae pale,
“Kumbe ni wewe ndio mke wa Erick!!”
“Ndio ni mimi, karibu sana. Rafiki yangu hajambo?”
“Hajambo kabisa, atafurahi sana nikimwambia kuwa nimekutana na wewe”
Ndio baba Angel nae akauliza kwa makini,
“Kumbe mke wako na mke wangu ni marafiki!!”
Ndio mama Angel alipomjibu,
“Ndio, kumbe humfahamu mke wa huyu Juma? Mke wake ni Johari”
“Kheee kumbe Johari, yule tuliyesoma nae!!”
“Ndio huyo huyo”
“Kumbe mlisoma na mke wangu!! Halafu sikujua yani hata urafiki wa mke wako na mke wangu nilijua tu ni urafiki kwavile wanaishi sehemu moja kumbe mmesoma wote, ngoja siku moja nimlete mke wangu hapa nadhani atafurahi sana”
Basi ikawa ni furaha na waliongea mambo mengi sana, basi maam Angel ilibidi aende kuandaa chakula ili wale pamoja na mgeni wao maana yeye hakujua kama kuna mgeni amefika kwao kwa siku hiyo.
Basi kwa pamoja walienda kula chakula huku wakiongea mambo mbalimbali ya maisha na jinsi mambo yalivyo, akamkumbusha pia jinsi alivyomtafutia leseni ya udereva,
“Unakumbuka nilikutafutia leseni ya udereva!”
“Nakumbuka vizuri, unafikiri naweza kusahau hilo Juma!!”
Basi wakacheka pale na kuendelea kula.
 
SEHEMU YA 272

Kwa upande wa Sia alizidi kuwa na hasira yani yeye alichukia kuona kwanini mama Angel alimpelekea vile viatu Steve, aliona kamavile amemfanyia makusudi wakati mama Angel hakujua ukweli wa jambo lolote lile, basi siku hiyo alijiandaa tena na kwenda dukani ili ajaribu kuongea na Steve vizuri na aweze kumzindua ufahamu wake.
Ila alivyofika dukani hakumuona Steve yani duka lilikuwa limefungwa, na kuwaona tu wale walinzi pale nje basi aliwafata na kuwauliza,
“Ila wewe mwanamke si uliambiwa usifike hapa!”
“Hiyo sio sababu, hivi nyie mnajua kuna mambo mnafanya halafu hamjifikirii mnakumbuka siku mliyonizaba kibao halafu nikaanguka? Mnakumbuka alivyofika mwenye mali alifanyaje?”
“Alikupakia kwenye gari lake na kukupeleka hospitali”
“Unajua kwanini alifanya hivyo!! Sababu anajua umuhimu wangu katika maisha yake, anaijua thamani yangu ni kitu gani ndiomana hamjawahi kumuona hata akinyoosha mkono wake kunizaba kibao. Haya huyu Steve yuko wapi jamani! Hadi leo hajafungua duka!”
“Katupigia simu kuwa hafungui leo, na hapa tuliambiwa tumsikilize Steve kwahiyo ndio hivyo mpaka atakapoamua yeye kufungua hata wale wafanyakazi wengine wa kawaida wale wawili walifika na kuondoka maana Steve hajafungua duka”
“Duh!! Yani huyu mwanamke kamshika sana Steve, ila yote haya ni Erica ndio kayataka”
Basi akaondoka pale bila hata ya kuwaaga wale walinzi, muda huo alikuwa akienda tu nyumbani kwa Erica ili akaonane na Erica,
“Yani leo ndio atanitambua vizuri, nimeachana na Steve ndio ila sio sababu ya kumfanya Steve awe na mwanamke mwingine, sitaki hilo jambo kabisa. Na leo lazima nikamdhalilishe Erica”
Basi moja kwa moja alienda kupanda pikipiki ili awahi kufika huko kwa Erica na kufanya fujo anazotaka kuzifanya.

Muda huu Juma alikuwa ameaga kwani aliona kama muda umeenda kiasi halafu kuna mahali alitaka kwenda, basi walitoka pale nje na hakuwa ameenda na usafiri basi baba Angel alitaka kupanda nae kwenye gari lake ili amfikishe hata stendi ila alikataa,
“Aaaah hapana, unajua mimi huwa sipendi sana kutumia usafiri kuna muda huwa napenda tu kupanda daladala na kutembea, kwahiyo nitaenda tu stendi hakuna tatizo”
“Ni vizuri lakini maana ni mazoezi pia hayo”
Basi waliamua kutoka na kumsindikiza kidogo muda huo walikuwa wameongozana mama Angel, baba Angel pamoja na mgeni wao Juma.
Wakati wametoka tu nje ya geti, walikutana macho kwa macho na Sia ila gafla kitu ambacho hawakukitarajia ni Sia kuanza kutimua mbio tena alikimbia sana kama mtu aliyeogopa kitu Fulani, kwakweli mama Angel alibaki kushangaa sana.

Wakati wametoka tu nje ya geti, walikutana macho kwa macho na Sia ila gafla kitu ambacho hawakukitarajia ni Sia kuanza kutimua mbio tena alikimbia sana kama mtu aliyeogopa kitu Fulani, kwakweli mama Angel alibaki kushangaa sana.
Yani baba Angel ndio alimtoa mama Angel kwenye mshangao,
“Hivi yule sin i Sia jamani!!”
“Ndio mwenyewe, sijui alikuja kufata nini na kitu gani kilichomkimbiza!”
Basi Juma nae akauliza,
“Kwnai yule mwanamke aliyekimbia ni nani? Maana hata sijamuangalia vizuri”
“Ni historia ndefu sana, ila anaitwa Sia na hata sijui ni kwanini amekimbia”
Kisha baba Angel akamuangalia mkewe na kumtaka arudi ndani tu, ila kama kawaida ya wivu wa mama Angel kwahiyo hakutaka kurudi ndani peke yake ukizingatia kamuona Sia mahali hapo ilibidi baba Angel aagane tu hapo na mgeni wake huyo ambaye aliamua kumuitia pikipiki ili impeleke stendi halafu yeye alirudi ndani na mke wake.
Basi baba Angel na mama Angel walipokuwa ndani waliulizana kwanza kuhusu Sia ambapo mama Angel aliuliza,
“Ni kwanini kakimbia sasa?”
“Sijui na alikuwa anafata nini?”
“Nikuulize wewe ambaye huwa unampa hela, unajua unampa kiburi sana huyu mwanamke, halafu sikukwambia tu alikuja na kunikuta getini nikimsindikiza Fetty akaninasa kibao, yani huyu Sia unampa jeuri sana na hela”
“Yani alikunasa kibao wewe!”
“Ndio”
“Mbona hukuniambia kuhusu hilo mke wangu!! Yule mwanamke ni kichaa sana, ila tusimfatilie wala nini tuendelee na mambo yet utu”
Baba Angel alikuwa ameongea hivyo ila alikuwa ameumizwa sana na kusikia kuwa Sia alimnasa kibao mke wake, yani kitu ambacho huwa hapendi ni kusikia kuna mtu kamuonea mke wake ndiomana hata dada yake aligombana nae alipomnasa kibao mke wake.

Mama Junior leo alitembelewa na rafiki yake daktari na kufurahi sana halafu akamkaribisha vizuri sana nyumbani kwake kisha walianza kuongea,
“Unajua siku ile hatukumaliza vizuri maongezi yetu yani kuna mambo hatukuyaweka sawa, najua hukuelewa inakuwaje kwa mwanao kusema hela zipo kwa mwanangu, sasa nimepata ukweli wote”
“Eeeh ukweli gani huo?”
Daktari alimueleza mama Junior kuhusu swala la Junior kumtongoza Samia na jinsi Samia alivyomwambia na vile Junior kutekeleza,
“Kheee jamani, huyu Junior jamani. Hiyo laki tano aliitoa wapi sasa?”
“Sijui, mwanangu anasema alimpelekea laki tano keshi kabisa”
“Ila mwanao duh!! Au ndio watoto wa siku hizi jamani, mjanja huyo balaa, nimempenda bure, enzi zetu tulikuwa wajinga wajinga, utakuta mwanaume anamdanganya mwanamke kwa kitu kidogo tu na anampata ila huyo Samia duh nimempenda jamani, yani Junior na laki tano yake haijafua dafu!”
Wakacheka kidogo kisha daktari akamwambia,
“Unajua mwanangu hiyo tabia hata sijui kaitoa wapi jamani maana nishamsema hadi basi na siku zote huwa anasema anafundishwa na baba yake, kwakweli yule mume ananiharibia mtoto jamani!!”
“Kheee anamfundishaje hivyo mtoto?
“Yani usione watu tunavumilia ndoa, ila huwa tunavumilia mambo mengi sana, kiukweli mimi ile ndoa naivumilia kwa mikiki mikiki mingi sana, kwa kifupi yule mume wangu najua humjui sababu hujawahi kumuona ila alikuwa ni muhuni hatari kiasi kwamba ana watoto yule baba hata wengine hajui wako wapi, basi huwa namwabia hadi watoto wako wataoana, ila huwa anasema hilo haliwezi kutokea, na yeye anaamini kwamba kuna siku watoto wake wote watamtafuta alipo, yani huwa hana muda wa kutafuta mtoto. Ukimuona mtoto wake ujue mama wa huyo mtoto kapambana hadi mtoto amfahamu baba ila asipopambana basi na yeye hana hata habari”
“Mmmh huyo mumeo kiboko, yani mimi nilikuwa nahisi wangu tu ndio hatari maana nimemkuta na watoto watatu halafu wengine wawili kumbe walikuwa bado wadogo ndio mama zao wakawaleta nilivyoanza tu kuishi nae kiasi kwamba hata nimeona ni vyema nisizae tena, sasa wewe mwenangu wangapi?”
“Sijui ni wangapi, ila kwa wanaofahamika hadi kwao na wanaendaga kwa bibi yao wapo kumi ila sijui hao wengine sasa. Naona uhuni wake anaogopa watoto wake kufanywa kama yeye alivyokuwa akiwafanya watoto wa wenzie ndio anamfundisha ujinga mwanangu, unajua nahofia siku anaweza akala hela ya mwanaume chizi na kupelekea kubakwa maana wanaume wa siku hizi akili zao wanazijua wenyewe”
“Kweli hapo umeongea, ila bado nipo kwa mwanangu Junior alipata wapi hiyo laki tano ya kumuhonga Samia? Naona Junior atakuwa anampenda sana binti yako”
Daktari akacheka kwanza na kusema,
“Junior ana maisha?”
“Maisha kivipi?”
“Unajua siku hizi hata sisi wazazi tunatakiwa kuamka, tukisikia kuna kijana anataka kuwa na mwanao lazima tuangalie ana maisha ya mbeleni sio kumpa shida tu mtoto wangu”
“Jamani Junior wangu yupo vizuri si unaona alipata hiyo laki tano kiurahisi tu”
“Unajua mwanao kazitoa wapi hizo laki tano!! Hebu fatilia na ukumbuke kuwa mwanao hana kazi yoyote, ila naona anampenda sana binti yangu sema pole yake maana Samia hana mambo ya mapenzi kabisa”
Basi waliongea mengi sana na mwisho wa siku daktari alimuaga tu mama Junior na kuondoka zake, ila mama Junior alikuwa anawaza jambo kuwa ni lazima apange siku aende kwa mdogo wake ili kuuliza kwa makini hiyo laki tano Junior aliitoa wapi.
 
SEHEMU YA 273

Usiku wa leo, Vaileth alikumbuka jambo na kuamua kumuuliza Junior kuhusu lile swala ambalo alilikumbuka,
“Samahani Junior, hivi ile laki tano ambayo uliichukua kwangu ulienda kufanyia kitu gani?”
“Aaah ile hela, kuna jambo Fulani hivi nimefanya ni la muhimu sana katika maisha yetu ila sikwambii kwasasa na siku ukiligundua utaamini ni kiasi gani nakupenda”
“Basi mwenzio nilishindwa kujieleza kuhusu hiyo hela wakati nimeulizwa, yani nilihisi kupata kizunguzungu kabisa yani, ila nashukuru kama umefanya jambo la maana”
“Sasa unafikiri mimi naweza kwenda kufanya ujinga jamani Vai!! Nichukue hela kwako halafu nikafanye ujinga! Hapana sipo hivyo na siwezi kabisa kufanya hivyo. Niamini mke wangu, amini kuwa Junior anakupenda sana”
Vaileth alikuwa akihisi raha sana moyoni mwake kila Junior alipomwambia kuwa anampenda sana.
Basi waliamua tu kulala kwa muda huo, ila palivyokucha tu Vaileth alisikia akiitwa mlangoni na sauti ilikuwa ya mama Angel basi alikurupuka na kumkurupua Junior,
“Mmmh nasikia sauti kama ya mama Angel, kajifiche”
Kama kawaida, Junior alienda kujificha chooni, basi Vaileth alienda kufungua mlango na kumsalimia mama Angel ambapo aliuliza,
“Hivi maji kwenye choo chako yanatoka?”
Mama Angel alipouliza vile alikuwa kama anataka kwenda chooni kuhakikisha ila Vaileth aliwahi haraka haraka na kumwambia,
“Yanatoka mama”
“Aaaah maana kuna fundi anarekebisha mabomba, jana usiku kuna vyumba vilikuwa havitoi maji chooni”
“Kwangu yanatoka mama”
Basi mama Angel akaondoka na kumfanya Vaielth apumue kidogo kisha alimfungulia Junior mlango na kuongea nbae,
“Unajua presha ilikuwa inapanda balaa, nikawaza hivi angekukuta chooni ingekuwaje jamani!! Sijui yani sipati picha”
“Naona chimbo la chooni limeanza kuzoeleka”
“Ndiomana mimi nilikwambia kuwa ni bora ujifiche uvunguni, ila haya mapenzi dah!!”
“Usijali mke wangu ila naamini kuwa hakuna siku watakayotubamba”
“Mmmh ila tuwemakini sana”
Kisha Vaileth akatoka nje ili kwenda kuanza kazi mbalimbali muda huu, huku Junior naee akitoka ila wakati anatoka tu akabambana na Erica ambaye alisema,
“Nilijua tu, muda huu utatokea humo ndani”
Junior alikuwa akimnyamazisha kwa kidole ili asiendelee kusema, huku akitoka na kufung mlango halafu akawa anaondoka ambapo Erica akasema,
“Kwani ukitoka humo ndio huruhusiwi kuongea?”
Junior akaendelea kutembea huku akielekea chumbani kwake, basi Erica akamwambia,
“Junior kama hunijibu nakusemea”
Junior akasimama ila muda huu mama Angel nae alikuwa anapita pale na kuuliza,
“Kumsemea kitu gani?”
Junior akamsalimia mamake mdogo na kusema,
“Aaaah mimi na Erica huwa tuna mtindo wa kutaniana, si eti Erica eeeh!”
“Ndio”
Basi kila mmoja akaelekea kwenye sehemu yake ila mama Angel alikuwa akijiuliza na kuhisi kuwa lazima kuna kitu maana hakuelewa kama ni kawaida tu kufanya vile.

Leo baba Angel alivyotoka asubuhi kwenda kazini, hakwenda kazini moja kwa moja ila alienda nyumbani kwa Sia kwani alichukia sana kwa kile kitendo cha mkewe kusema kuwa alizabwa kibao na Sia, na alipofika tu alimkuta Sia yupo kufagia nje ya nyumba yake ila Sia alivyomuona baba Angel kwakweli alifurahi sana alijikuta akiwa na furaha mno na kumsogelea karibu ila baba Angel akanyoosha mkono wake kama kumzuia kuwa asimsogelee karibu sana,
“Kheee jamani hata kukukumbatia?”
“Sasa unikumbatie ili iweje? Jiheshimu wewe, tambua kuwa mimi ni mume wa mtu”
“Ila kumbuka kuwa ulikuwa mpenzi wangu, wapenzi huwa hawaachani hata kama mtu akioa na kuolewa”
“Kwa mtindo huo mtu si utakuwa kwenye ndoa na msululu wa watu, mfano mimi kama unavyosema kuwa nisiachane na wapenzi ni wangapi wangekuwepo sasa? Wengine hata majina siwajui”
“Achana na hao ambao ulikuwa nao siku mbili na kuachana nao, kuna wanawake hata mwezi hukuweza kufika nao, hata wiki ilikuwa ni ngumu, katika mahusiano yako ya kimapenzi kabla ya ndoa kuwa muwazi tu kuwa mimi ndiye niliyekuwa mwanamke niliyedumu na wewe, nilikupenda, nilikujali na nilikuheshimu bila kujali chochote kile, nilikufumania na bado nilikusamehe na kufanya penzi letu liweze kustawi. Unajua mara nyingine ambavyo unanifukuza mimi uwe unakumbuka na mazuri yangu ambayo nimefanya kwako sio unakumbuka mabaya tu, laiti kama ungejua mimi nilivyo na siri nyingi basi ungekaa karibu yangu ili nikuambie mengi ninayoyafahamu”
“Hata sina haja ya kujua unayoyafahamu, ila kilichonileta leo ni kukuuliza wewe kitu gani kimekuleta tena nyumbani kwangu wakati tulikubaliana kuwa hutokuja tena kwangu, na kwanini ulikuja na kumzaba kibao mke wangu? Unajua mimi huwa sipendi kuongea sana, katika wanawake zangu wote basi sijawahi kumpiga mke wangu, kama kupiga basi wewe nishakupiga sana na unaelewa kabisa jinsi nilivyo ila ukaja na kumpiga mke wangu kwanini? Na ushukuru sana nimekuja na kukuuliza kwa ustaarabu hivi”
“Kwanza naomba unisamehe sana, haikuwa dhamira yangu kuja kumzaba mkeo kofi ila ni hasira tu. Ngoja nikueleze kwanza, unajua wewe ni mwanaume nikupendaye sana ila sijaweza kukupata sababu ya mkeo licha ya kuwa kwenye mahusiano na wewe kwa muda mrefu sana, nakiri wazi kuwa nilifanya dawa ili nikupate ila dawa zangu zilimpata Steve na mwisho wa siku nikaishi nae hadi kuamua kuzaa nae nakuoana kabisa, unajua kilichomfanya Steve aondoke kwangu sio kuisha kwa dawa maana dawa ziliisha na Steve sababu aliamua kuishi na mimi na kunioa inamaana alinipenda kweli, kilichonifanya niachane na Steve ni ndugu zake ambao walianza chokochoko baada ya mtoto kuzaliwa na kusema kuwa mtoto sio wa Steve, yani pale ndio walianza kuniachanganya akili na kusababisha mimi na Steve kutengana ila nilivumilia tu na kuchukulia ni changamoto maana mengine nilijitakia mwenyewe. Haya unajua mkeo alichokifanya nae?”
“Kafanyaje?”
“Steve alikuwepo tu hana mwanamke yoyote na Steve namfahamu fika kuwa asingeweza kuwa na mwanamke yoyote yule, sababu nazijua mwenyewe, ila mkeo kaenda kumpa Steve viatu ambavyo madam Oliva alikuletea wewe sijui, kaenda kumpa na vile viatu vimechanganya akili ya Steve kwa maana hiyo Steve yupo kwa madam Oliva, yani Steve sio yule Steve uliyemfahamu mwanzoni maana kawa mwingine kabisa”
“Kheee kwahiyo hivyo viatu vya madam Oliva vilikuwa na mambo?”
“Ndio, Oliva alikukusudia wewe, ila mkeo nilijua ataenda kuvichoma moto ila nilivyogundua kampelekea Steve wangu nimeumia sana”
Baba Angel akacheka kidogo na kusema,
“Ila unajua wewe mwanamke unachekesha sana, sasa ulikuwa unanipenda mimi au Steve? Maana hizo nguvu ulizokuwa ukitumia kwangu nina uhakika ungezitumia kwa Steve basi angekubali na mngeishi pamoja tena, ila kweli wewe ni chizi”
“Sikia Erick,kumbuka Steve ni baba wa mtoto wangu”
“Unaendelea kunichekesha, baba wa mwanao kumbe ni Steve ila kila siku kunisumbua mimi na familia yangu kuhusu mtoto wako, jamani wewe mwanamke ukweli wote unaufahamu ila kila siku kunishikilia kuwa mimi ni baba wa mwanao, leo Steve anakuumiza kichwa, unajua wewe ni mgonjwa wa akili!”
“Nadhani hujanielewa Erick, ila ipo siku utanielewa. Mimi nakupenda sana wewe, nilitamani pia awepo mtu wa kunipenda sana mimi yani ambaye hawezi kufanya kitu bila ya kunifikiria mimi”
“Kwahiyo mtu huyo ndio ulitaka awe Steve?”
“Nilitaka Steve anipende sana na niwe kila kitu katika maisha yake”
“Wewe mwanamke ni mgonjwa, ulitaka akupende wakati unajua wazi alikupenda kwa madawa? Halafu kwanini utake kumtesa mtu kwa upendo, unatakiwa kumpenda akupendaye ndio uishi salama. Haya leo nakupa onyo la mwisho, kwakweli nikisikia tena umekuja nyumbani kwangu na kufanya fujo kwa mke wangu nakwambia wazi utanifanya niwe vile nilivyokuwa kwa muda halafu utajutia kitendo chako cha kuamua kufanya ujinga kwa mke wangu”
“Ila hujui tu, laity ungejua huyo Steve hayupo kazini hadi leo sababu ya Oliva hata usingesema hayo, ni kweli nakufatilia na familia yako ila nakusaidia kwenye mambo mengi sana ili kukuokoa wewe na familia yako. Nakupenda sana Erick”
Baba Angel hakusikiliza zaidi kwani kwa muda huo akili yake iliruka kusikia kuwa Steve hajaenda kabisa kazini, kwahiyo aliingia kwenye gari yake na muda huo alikuwa akielekea kwenye ile biashara yake.

Kwa muda huu yani ilikuwa ni tofauti kwa Steve kabisa kwani alisahau shida zake zote, alisahau kila kitu kinachohusiana na yeye sijui kazi, sijui vitu gani alisahau kabisa kwahiyo muda mwingi alikuwa akikaa na madam Oliva ndani ya nyumba, kisha walianza kuongea,
“Unajua tutaishi hivi kwa wiki nzima, kisha ndio itawezekana kufanya mambo mengine”
“Sina tatizo mimi, nakubaliana nawe kwa kila kitu”
“Kwanza, ulikuwa unafanya kazi gani awali”
“Oooh umenikumbusha, Mungu wangu sijui itakuwaje. Nilikuwa nauza duka la nguo za watoto na mimi ndio nilikuwa nimeishika biashara ile kwahiyo siku zote hizi sijafungua”
Mara simu ya Steve ilianza kuita na alipoiangalia akaona ni bosi wake anampigia simu basi aliogopa kupokea ambapo madam Oliva alimuuliza,
“Kwani nani anapiga?”
“Ni bosi wangu”
Madam Oliva akachukua ile simu na kuangalia akaona jina bosi Erick, basi akamuangalia vizuri Steve na kumuuliza,
“Kwani huyu Erick ni nani? Ni yule ninayemfahamu mimi au? Watoto wake wanaitwa kina nani?”
“Ana watoto wanne kwasasa, kuna Angel, Erick, Erica na Ester”
“Oooh ndio huyu huyu ninayemjua mimi ila imekuwaje jamani! Mbona sielewi”
Kisha akakumbuka vile viatu ambavyo alimuona Steve amevaa katika facebook, akamuuliza sasa,
“Kwahiyo vile viatu ndio huyo bosi wako Erick alikupatia?”
“Hapana, ni mke wake ndio aliniletea alisema mumewe havimtoshi kwahiyo aliona ni vyema kuniletea mimi”
“Dah!! Kuna kitu naanza kuelewa sasa, hivi wewe ulianza kunipenda kipindi gani?”
“Mimi, ni siku nyingi sana nilikuwa nakupenda”
“Basi mimi toka siku nimekuona umepiga picha na vile viatu, nikajua na wewe umeanza kunipenda baada ya vile viatu?”
“Hapana, ni siku nyingi sana ila kwasasa ndio sijielewi kabisa maana nakupenda kupitiliza”
Madam Oliva alitikisa kichwa tu kwani alielewa kinachoendelea, kisha simu ya Steve ilianza kuita tena na kufanya Steve aogope maana alikuwa ni bosi wake anapiga ila madam Oliva alimwambia acha apokee yeye basi Steve alimpatia ile simu ambapo madam Oliva aliipokea,
“Wewe Steve uko wapi kwa siku zote hizi jamani hujafungua biashara yangu!!”
“Erick, samahani sana. Steve yupo kwangu, naomba umsamehe bure maana sio kosa lake”
“Nani wewe?”
“Mimi madam Oliva”
“Kheee madam olive!! Sasa Steve anafanya nini kwako?”
“Mimi na mwanamke na Steve ni mwanaume unadhani atakuwa anafanya nini kwangu? Nitakuja ofisini kwako na tutaongea vizuri ila naomba umsamehe bure tu Steve”
Baba Angel alikata ile simu kwani alionekana kuwa na hasira ila kwa upande wa madam Oliva ilikuwa kawaida kabisa maana hakuwa na mashaka na jambo lolote lile, kisha alimwambia Steve,
“Usijali, maana hata ukikosa kazi kwake basi nitakupa kazi kwenye ofisi zangu, najua bado hunifahamu vizuri ila mimi ni mwanamke ambaye najitosheleza”
Steve alikaa kimya tu akimuangalia madam Oliva kwani kila muda alijikuta akizidi kumpenda madam Oliva kupita kawaida.
 
SEHEMU YA 274

Baba Angel alikuwa ofisini kwake huku akisikitika sana, kwanza alikumbuka maneno ya Sia ambayo alimwambia awali akimtahadharisha kuhusu madam Oliva, alikumbuka pia maneno ya mke wake, na kile kilichotokea kuhusu Steve basi aliwaza sana na kusema,
“Inamaana muda huu isingekuwa Steve bali ingekuwa ni mimi ndio nipo nyumbani kwa madam Oliva na kuisahau kabisa familia yangu, dah nauchukia uchawi jamani. Sasa ndio mambo gani haya, yani mtu anaweza kukupa dawa hadi unasahau familia yako!! Ka jinsi ninavyompenda mke wangu, kwa jinsi ninavyowapenda watoto wangu halafu leo hii niwakimbie na kwenda kwa mwanamke mwingine sababu ya madawa kweli! Aaaarghh nauchukia uchawi, nani huyo kaweka dawa za mapenzi jamani!!”
Akitafakari hayo alimuona Oliva akiingia ofisini kwake, kiukweli kwasasa baba Angel alikuwa akimuogopa madam Oliva yani alimuogopa na kumuhofia sana kiasi kwamba hata hakuweza kumkaribisha ila madam alifika na kukaa kisha akaanza kuongea,
“Mbona unaonekana kuniogopa sana baba Erick? Mimi sio mtu mbaya kama ambavyo unafikiria, usiniwazie vibaya, mimi nilikufanyia tu kile ambacho mke wako alishindwa kukufanyia na si vinginevyo”
“Kwani nilikuomba usaidizi?”
“Hapana, ila sikuwa na nia mbaya. Nataka ujue kwamba sikuwa na nia mbaya, na hili nitalidhihirisha kwako kwa kupitia huyu Steve, sikuhisi kama ningeweza kumpenda ila nashangaa kuona nikimpenda sana kiasi cha kutokutaka awe mbali na mimi. Twende nje ukamsalimie maana yupo kwenye gari yangu”
“Hapana madam, nenda tu”
Yani baba Angel hakuwa na amani na madam Oliva hata kidogo, hivyo ilibidi tu madam Oliva aondoke zake yani baba Angel hakuwa na amani na madam huyu hata kidogo kabisa.

Jioni ya leo Angel alienda kumuomba simu bibi yake ili aweze kuwasiliana na rafiki zake mbalimbali, ila bibi yake anampatia na kumwambia,
“Kesho si ndio unaenda matembezi na baba yako, unikumbuke tu kwenye zawadi”
Angel alicheka na kuchukua simu kisha alienda chumbani kwake ambapo alipofika tu akaanza kumtafuta Samir maana ni muda hakuwasiliana nae,
“Jamani Samir ndio toka siku ile unashindwa tena kufika kwetu kuniona, au hujanimiss”
“Nimekumiss sana Angel, ila huyo bibi yako humjui vizuri”
“Kwanini sasa?”
“Huyo bibi yako hashindwi kummwagia mtu maji ya moto”
“Jamani, bibi yangu hana roho mbaya ya kiasi hiko, kweli kabisa ammwagie mtu maji ya moto jamani kwa lipi sasa?”
“Sikia nikwambie Angel, huyo bibi yako ni rafiki mkubwa sana wa bibi yangu kwahiyo namfahamu vizuri sana. Muone hivyo hivyo ila huyo bibi yako ana roho mbaya sana”
“Mmmh jamani!! Kwahiyo nikikaa kwa bibi basi hutokuja kabisa kuniona?”
“Nitakuja tu, ila siku nikijitoa muhanga kufanya hivyo. Halafu vipi kuhusu shule, mimi nilitafutiwa shule ila nimekataa maana nataka kusoma shule utakayosoma wewe”
“Mmmh tusome tena pamoja Samir?”
“Ndio, tena itakuwa vizuri maana kwasasa mimi na wewe tuna mahusiano, tofauti na pale mwanzoni tulikuwa tunasumbuliwa akili tu ila kwasasa tutaishi vizuri sana shuleni”
“Hapo nimekuelewa kabisa, ngoja nikijua ni shule gani wamenitajia nitakwambia Samir”
“Tena itakuwa raha sana kama itakuwa ni shule ya bweni halafu mbali ili kipindi cha likizo tuwe tunarudi wote”
“Mmmh jamani Samir unawaza mambo ya mbali sana, ila mimi sipendi kusoma bweni, naona sitaweza napenda sana kukaa nyumbani”
“Naomba kwaajili yangu kubali utafutiwe bweni mpenzi”
Basi Angel alikubali kwani alihisi kumpenda sana Samir na alitamani mno kuwa nae pamoja kama wapenzi, basi wakati ule akatumiwa tena ujumbe na Ally, ujumbe ule ulisema,
“Angel, ushaulizia vizuri kuwa undugu wangu mimi na wewe ukoje?”
“Ooh bora umenikumbusha, ngoja kesho nitamuuliza baba yangu kama ana mtoto mwingine”
“Kwani baba yako anaitwa nani?”
“Baba yangu anaitwa Erick”
“Hata hivyo hatuna undugu maana mimi niliambiwa kuwa baba yangu anaitwa Rahim, kwahiyo haiwezekani tukawa ndugu nadhani yule sijui mamako mkubwa atakuwa amesema vile ili tusiwe pamoja”
“Ila hata hivyo mimi nina mtu wangu”
“Angel, naongea na wewe kwa kawaida kabisa. Sikia hunitaki ndio nimekubali, una mtu wako ndio nimekuabali ila kuna siku mimi na wewe tutakuwa pamoja tena mke na mume labda mimi Ally nife ila nikiwa hivi mzima basi tambua hilo”
“Mmmmh!”
“Usigune, ndio ukweli huo”
“Kwahiyo utafanyaje?”
“Tena Angel lazima utanizalia watoto mapacha”
Angel akaogopa kidogo na kuamua kuzima ile simu na kwa muda huo aliamua kulala tu maana usingizi ulimshika muda huo.
Kulivyokucha Angel aliamka na kumkabidhi bibi yake simu kisha yeye alianza kufanya kazi mbalimbali huku akijiandaa kwaajili ya kutoka na baba yake.

Leo mchana, ndipo mama Junior alienda nyumbani kwa mama Nagel ili kuongea nae kwahiyo alivyofika alimkuta yupo kwakweli mama Angel alifurahi sana na kuanza kuongea nae mawili matatu kwanza kabisa aliwaulizia wakina Junior,
“Junior yuko wapi?”
“Junior hayupo, yeye na Erick kuna mahali wameenda”
“Wapi tena jamani!!”
“Sijui, wameniambia tu wanaenda kwenye matembezi”
Kisha mama Angel akamuita Vaileth na kumtaka amletee Juisi mgeni, basi alimsalimia pale na kwenda kumletea juisi, basi mama Junior akamwambia sasa mama Angel,
“Yani umemuachia Junior aende matembezi na Erick kweli, ujue Junior anatabia mbaya sana. Sikukwambia haya mdogo wangu ila natakiwa nikwambiae sasa”
“Yapi hayo tena?”
“Junior kuna binti anampenda bhana, sasa huyo binti kamwambia Junior ampelekee laki tano”
“Kheee Junior atatoa wapi hiyo hela sasa?”
“Sio atatoa wapi, kwa kifupi Junior kampa huyo binti laki tano taslim”
Mara gafla walisikia gafli ikianguka chini na kupasuka, walipogeuka ilikuwa ni Vaileth ambaye alikuwa akileta ile juisi.


Kisha mama Angel akamuita Vaileth na kumtaka amletee Juisi mgeni, basi alimsalimia pale na kwenda kumletea juisi, basi mama Junior akamwambia sasa mama Angel,
“Yani umemuachia Junior aende matembezi na Erick kweli, ujue Junior anatabia mbaya sana. Sikukwambia haya mdogo wangu ila natakiwa nikwambiae sasa”
“Yapi hayo tena?”
“Junior kuna binti anampenda bhana, sasa huyo binti kamwambia Junior ampelekee laki tano”
“Kheee Junior atatoa wapi hiyo hela sasa?”
“Sio atatoa wapi, kwa kifupi Junior kampa huyo binti laki tano taslim”
Mara gafla walisikia gafli ikianguka chini na kupasuka, walipogeuka ilikuwa ni Vaileth ambaye alikuwa akileta ile juisi.
Basi walimshangaa sana kisha mama Angel akamuuliza,
“Wewe Vai una matatizo gani wewe?”
“Samahani mama”
Kisha Vaileth akaenda kuchukua tambala na kutoa zile chupa na kufuta ile juisi kisha kwenda kuleta juisi nyingine, basi muda huu mama Angel alimwambia,
“Hebu kaa chini kwanza nikuulize maswali”
Ilibidi Vaileth akae kwenye kochi na kusikiliza maswali ya bosi wake,
“Eeeeh kilichokiustua hivyo ni kitu gani hadi kuangasha kikombe!”
“Samahani mama, sijui ni vipi mkono umeteleza tu”
“Hapana, lazima ulikuwa na mawazo yaliyofanya mkono wako ukateleza”
Ilibidi mama Junior amtetee pale,
“Hapana jamani,kuna wakati huwa inatokea tu, kwahilo namtetea”
“Haya, kaendelee na kazi zako”
Vaileth aliinuka na kurudi jikoni ila hakuwa na raha kabisa ukizingatia ni yeye aliyetoa laki tano na kumbe laki tano hiyo imeenda kupelekwa kwa mwanamke mwingine kwakweli roho ilimuuma sana.
 
SEHEMU YA 275

Junior na Erick wakiwa kwenye gari, Erick alimuuliza Junior,
“Kwani tunaelekea wapi?”
“Utaona tu, ila kuna jambo nataka unisaidie”
“Jambo gani hilo?”
“Kuna mwanamke namuhitaji halafu kashakula hela yangu kwakweli, leo nahitaji kuwa nae karibu”
“Kivipi?”
“Ngoja twende”
Walifika mbele ya nyumba moja hivi na kusimamisha gari, kisha Erick alimuuliza Junior,
“Kwahiyo hapa ni wapi?”
“Hapa ni kwa mtu mmoja hivi unamfahamu, hebu shuka halafu ukimuona muite na akija panda nae kwenye gari”
Basi Erick alishuka chini, na alivyoshuka tu baada ya muda kidogo alishangaa kumuona Samia akipita kuelekea kwenye ile nyumba, basi alimuita
“Samia, Samia”
Samia aligeuka, kwakweli hata Samia hakuamini kama aliyemuita ni Erick, yani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha huku akimuongelesha ila Erick alikuwa kama anamshangaa vile,
“Jamani Erick, kweli unanipenda umefika kwetu bila hata kukuelekeza”
“Kheee kwani unaongelea kitu gani Samia, njoo kwenye gari”
Basi Erick alifungua mlango na Samia akapanda kisha na yeye akapanda ila alishangaa kuona Samia alivutwa siti ya nyuma kwenye gari, mwanzoni hakujua ni kwanini Junior alikaa siti ya nyuma ila muda huo ndio akaelewa. Samia alikuwa amezibwa mdomo na Junior ambaye alikuwa akimwambia,
“Wewe si mjanja, ukaamua kula hela zangu sasa na mimi leo lazima nipate changu. Erick ondoa gari sehemu hii”
Erick alikuwa akimshangaa na kumuuliza,
“Kwani Junior tatizo ni nini? Unataka kufanya nini na Samia?”
“Nataka kumbaka”
“Kheee kumbaka? Kakufanya nini kwani?”
“Kala hela zangu mjinga huyu”
“Sasa na wewe si umdai tu hizo hela zako, kwani ukimbaka ndio utakuwa umelipwa hizo hela?”
“Erick hujui tu”
“Najua vizuri, ila sipo tayari kushiriki na wewe katika hili, ukitaka kufanya huo ujinga wako basi uje ufanye peke yako ila sio ukiwa na mimi, naomba muachie Samia ashuke”
Junior hakutaka kusikia hivyo kabisa zaidi zaidi alianza kumpapasa Samia kifuani na kumvuta blauzi kisha akaanza kumnyonya maziwa, kitendo kile kilimchukiza sana Erick ambaye alifungua mlango na kwenda kufungua mlango wa nyuma na kumshusha Samia kisha akamwambia,
“Kimbia nenda kwenu”
Halafu akarudi ndani ya gari na kuondoa gari na hakuongea chochote na Junior ila Junior ndio akaanza kulalamika,
“Yani wewe kama sio mwanaume vile”
“Kwani mwanaume anatakiwa kuwa vipi? Kama kubaka ndio uanaume basi nakubali ni kweli mimi sio mwanaume”
“Nakushangaa sana, ndiomana ulikula kiapo na dada yako kuwa yeye ndiye atakuwa rafiki pekee wa kike katika maisha yako yani hujawaza hapo mbeleni utahitaji mpenzi au utahitaji mke, yani wewe wa ajabu sana, mambo yako hayaendani na ulivyo”
“Ongea tu ukimaliza tutakuwa tumeshafika nyumbani”
Aliendele tu kuendesha gari wakielekea nyumbani kwao ila Junior alimuomba jambo,
“Sikia Erick nakuomba kitu kimoja tu, unajua akili yangu haipo sawa, naomba nipeleke hata ufukweni basi nikapate kidogo upepo wa bahari”
Erick alikubali na kwa muda huo safari ilikuwa ni kuelekea ufukweni tu.

Angel akiwa na baba yake siku hiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwahiyo aliamua kumuuliza pia kuhusu shule ambayo atatafutiwa,
“Baba, ni shule gani nitaenda kusoma kidato cha tano na cha sita?”
“Kuna shule nishakutafutia binti yangu, ni shule nzuri nina uhakika utaipenda”
“Inaitwaje baba?”
“Nadhani utaijua siku ya kufanya usahili ingawa usahili wenyewe hatufanyi kwenye shule, kwahiyo usiwe na wasiwasi bingti yangu amini lazima baba akupeleke sehemu nzuri inayokufaa”
“Asante baba, ndiomana nakupenda sana”
Basi Angel aliongea mambo mengi sana na baba yake hadi muda ulipofika wa baba yake kumrudisha nyumbani ambapo aliingia nae kwenye gari yake na kuelekea kwa bibi yake ila njiani Angel alikumbuka jambo,
“Nimekumbuka zawadi ya bibi”
“Oooh vizuri sana, unataka kumpatia zawadi gani?”
“Mmmh sijui, ila nataka kumnunulia kiatu”
“Unajua anavaa namba ngapi?”
“Najua baba”
Basi moja kwa moja baba Angel alienda na Angel kwenye duka la viatu na kuchagua kiatu cha kumpelekea bibi yake ila wakati wanaondoka hapo, baba Angel alishtuliwa na mtu ambaye alikuwa akimfahamu basi walianza kusalimiana pale,
“Johari, za siku nyingi?”
“Nzuri tu, yani mume wangu ndio akaniambia kuwa kaonana nanyi dah nikatamani sana nije kuwaona jamani, rafiki yangu Erica hajambo!!”
“Hajambo kabisa, karibu sana nyumbani”
“Asante, oooh nimekumbuka. Unamkumbuka Manka?”
“Manka yupi?”
“Mmmh wewe nawe, yani wewe usimfahamu Manka kweli? Leo hii humkumbuki Manka jamani!! Ila wanaume mna mambo sana, nilikutana na Manka ana mtoto mkubwa wa kike, nikamuuliza tu pale mtoto umezaa na nani kacheka nina mashaka ni mwanao”
Baba Angel alimuangalia Angel ambaye alikuwa amesimama pembeni yao kisha alimuangalia Johari na kumwambia,
“Acha maneno hayo hakuna kitu kama hiko kwangu, karibu nyumbani. Kuna mahali nawahi na binti yangu hapa”
Basi muda ule ule baba Angel alipanda na mwanae kwenye gari ili kuelekea kwa bibi wa Angel, ila wakati wanaondoka Angel alimuuliza baba yake,
“Kwani baba una watoto wengine tofauti na sisi?”
“Aaaah kumbe ulikuwa unamsikiliza yule! Hapana bhana mwanangu, sina mtoto mwingine mimi zaidi yenu”
Angel alitabasamu tu huku safari nayo ya kurudi kwa bibi ikiendelea.

Mama Junior hakuwa na mambo mengi zaidi ya kumueleza mdogo wake kuhusu hiyo laki tano ila mama Angel aliwaza pia kuwa hiyo hela Junior aliitoa wapi? Alikosa jibu kabisa, basi wakati wanaendelea na maongezi simu ya mama Junior iliita ambapo alipokea maana mpigaji alikuwa ni dada yao Mage,
“Ndio dada?”
“Uko wapi?”
“Leo nilikuja huku kwa Erica”
“Oooh sikujua jamani, unajua mimi nipo huku kwako”
“Aaaah jamani, basi nisubiri nakuja muda sio mrefu ngoja nichukue pikipiki”
Basi mama Junior aliamua kumuaga mama Angel ambapo mama Angel alimuuliza,
“Kwanini usimwambie yeye ndio aje huku?”
“Unadhani angekuja? Hawezi kuja, ngoja niende na nitajua kilichokuwa kimemleta nyumbani kwangu maana lazima ana maneno”
“Nimekumbuka kitu, unajua hapa nyumbani kuna kiumbe wangu huyu wa kuitwa Erica ni mbea hakuna mfano ila naanza kuhisi umbea Erica kautoa wapi, naona kwetu kuna asili Fulani ya umbea maana dada Mage nae dah ni mtihani sana”
Mama Junior alicheka tu na kuondoka maana alitaka kumuwahi dada yao ajue ni kitu gani ambacho kimempeleka kwake.

Junior na Erick wakiwa ufukweni, kuna mahali wanaona watu wamezunguka kwahiyo nao wakaona ni vyema waende kushuhudia kuna nini, wakakumbana na sauti ya mtu aliyekuwa akichezesha karata tatu,
“Jamani ukipata basi umekula na ukikosa basi umeliwa, ni mchezo mrahisi sana unaoweza kukufanya uondoke na pesa nyingi za kutosha”
Wakaangalia watu waliokuwa wakicheza, kuna wengine waliliwa hadi viatu walivyovaa, wengine hadi nguo walibaki tu kuondoka na kaptula, waliangaliana kwa makini na kuona kuwa ule mchezo ni mchezo wa kitapeli, ila aliyekuwa akichezesha mchezo ule ndio alikuwa akiwashangaza, basi walisogea pembeni kidogo ambapo Erick alimuuliza Junior,
“Hivi yule sio mjomba Derrick!!”
“Ndio, mwenyewe yule ila ngoja tukahakikishe”
Basi wakati akiendelea kuchezesha ule mchezo, ni Junior ndio alienda kumshtua na kumfanya ashtuke sana, kisha alisogea nao pembeni na kuwauliza,
“Nyie watoto mnafanya nini huku?”
“Sisi tupo kutembea tu, ndio tunakushangaa wewe mjomba”
Derrick aliwacha hapo na kama kuwatonya rafiki zake aliokuwa nao pale na uondoka kabisa eneo lile, kwahiyo Junior na Erick walibaki tu wakimshangaa hata wao waliamua tu kuondoka.
Basi wakiwa kwenye gari Junior alianza kusema,
“Mimi ndiomana mara nyingine hata sitaki kusoma, unajua huyu mjomba ni amesoma sana tu ila saivi kawa tapeli”
“Ila utapeli sio kusoma au kutokusoma ni tabia ya mtu tu.”
Basi wakarudi zao moja kwa moja nyumbani kwa wakati huo.

Usiku wa leo, Vaileth alikuwa na mawazo sana na uchungu wa pesa yake kugundua kuwa ameenda kupelekewa mwanamke mwingine, basi alikuwa kajiinamia tu,mpaka Junior alipoingia bado Vaileth alikuwa akilia tu na kumfanya Junior ahisi lazima kuna jambo,
“Vai nini tatizo?”
“Umenifanya mjinga Junior tena umenifanya mjinga wa kwanza, kweli jamani wewe wa kuja kuchukua laki tano kwangu na kwenda kumpelekea mwanamke mwingine jamani Junior hivi hata hukupata haya katika kunifanyia jambo kama hilo!!”
“Jamani, nani huyo kakwambia maneno ta uongo Vai!”
“Maneno ya uongo eeeh! Wakati mama yako kaja kuelezea hapa mwanzo mwisho halafu unasema ni uongo. Kwakweli umenishinda tabia, hivyobasi kuanzia leo mimi na wewe basi”
Junior akafikiria na kujiona ni kweli ametenda makosa kwa Vaileth, ila kwa wakati huo alishindwa kusema lolote na hata kumbembeleza sana Vaileth hakummbembeleza zaidi ya kuinuka na kurudi chumbani kwake, hiko kitendo kilimuumiza sana Vaileth, aliwaza jinsi alivyojitoa kwa mwanaume huyo, jinsi alivyomuhudumia kama mke na mume, kwakweli roho ilimuuma sana na kumfanya akose raha kabisa, kilichotokea kwake ni kujikuta akilala na dukuduku moyoni mwake.
Kulivyokucha tu, Erica alienda chumbani kwa Vaileth ila leo alifungua tu mlango na kuingia kisha akamuuliza,
“Kheee leo hukufunga mlango dada!! Junior yuko wapi?”
“Nadhani yupo chumbani kwake”
“Mbona unaonekana umevimba Macho dada?”
“Aaaah macho tu yalikuwa yakinisumbua ila usijali nipo sawa”
Erica alimuangalia na kutoka na wala hakusema jambo lililompeleka kwahiyo hataVaileth hakutambua ni kitu gani kilimpeleka Erica chumbani kwake kwa muda huo.
 
Back
Top Bottom