Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 221


Siku hii baba Angel aliamka na uchovu kiasi na asubuhi hii aliongea kidogo na mke wake,
“Eeeeh mke wangu, kuna mahitaji gani ambayo yanatakiwa humu ndani?”
“Hamna mume wangu, yangekuwepo ningekwambia kabla ya kuuliza, ila umenikumbusha kitu kumbe ulimnunulia Erick simu!!”
“Ndio, sababu Sia alikuwa akimfatilia nikaona vyema nimnunulie simu ili akiwa anamfatilia aniambie”
“Jamani mume wangu, mfano shuleni atakwambiaje wakati wanakatazwa simu shuleni! Mimi nimempokonya maana Erica nae alinunuliwa simu na Junior sababu tu Erick anatumia simu”
“Sijakuelea hapo, Erica alinunuliwa simu na Junior kivipi?”
Ikabidi mama Angel amsimulie baba Angel vile alivyomkamata Erica na simu, basi baba Angel alielewa ile hoja ya mke wake na kuamua kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kazi yao.
Alipomaliza kujiandaa alimuaga mke wake na kuondoka, ila wakati anatoka getini muda huu alimuona Sia akiwa amesimama na mtoto wa kiume mwenye umri kama wa Erick, kiukweli baba Angel hakumpenda mwanamke huyu kwahiyo alimpita kamavile hamuoni wala nini, yani baba Angel alikuwa akienda kazini huku akiwa na mawazo sana kwani aliona huyu mwanamke anamchanganya akili yake, ila akiwa barabara kuu kuna mtu alisimamisha gari yake ikabidi asimame na alipomuangalia vizuri mtu yule akamuona kuwa ni madam Oliva, basi yule madam aliingia kwenye gari ya baba Angel na kukaa kwenye siti huku akisema,
“Yani nilivyoona gari yako tu nikahisi moyo wangu ukidunda ndio nikakusimamisha”
“Oooh jamani, sasa moyo wako umedunda kwanini madam?”
“Aaaah tuachane na hayo, unaenda wapi muda huu?”
“Naenda ofisini”
“Basin i vyema nikafahamu ofisi yako ilipo”
“Sawa, hakuna tatizo lolote. Karibu sana”
Basi baba Angel alienda na madam Oliva hadi ofisini kwake na kumkaribisha, kwakweli Oliva aliipenda ofisi ya baba Angel kwani ilipangwa vizuri sana, kwahiyo aliingia nae ofisini na kuanza kuongea nae mawili matatu,
“Nimeipenda ofisi yako baba Erick jamani”
“Oooh asante sana”
“Halafu mke wako natamani sana kumfahamu jamani! Naamini nitamfahamu tu, ila baba Erick unaonekana ni mwanamke mstaarabu sana wewe, kwakweli mkeo ana bahati kubwa sana ya kukupata. Sema itakuwa ni vyema sana mimi na wewe tukiwa tunaonana na kuongelea maendeleo ya watoto shuleni au unasemaje?”
“Ni kweli kabisa, sina usemi kuhusu hilo”
“Basi, nitapenda upafahamu nyumbani kwangu pia”
“Sawa madam, nitapafahamu tu”
“Hata leo ukitaka”
“Hapana, kwa leo kuna kazi imenitinga labda siku nyingine”
“Basi tutawasiliana na nitafurahi sana juu ya hilo, maana ni vyema sana kwa wazazi kubadilishana mawazo”
Kisha Oliva alimuaga baba Angel kwani alitakiwa pia kuwahi kwenye kazi yake ambapo alikuwa akifundisha kwenye shule aliyosoma Erick.

Mama Angel akiwa katoka kumuogesha mtoto wake ambaye mara nyingi sana akioga tu analala, alishangaa mlinzi kufika sebleni na moja kwa moja aliitwa yeye na Vaileth,
“Samahani mama, nje ya geti kuna mgeni wako nimemwambia aingie ila alikataa”
Basi mama Angel akajiuliza ni mgeni gani huyo? Ila akatoka kwenda nje kumuangalia, alishtuka sana baada ya kukuta mgeni mwenyewe ni Sia na Elly yani Sia alikuwa kamshika mkono Elly basi mama Angel alipofika pale Sia alimkabidhi mama Angel mkono wa Ellyn a kumwambia,
“Mtoto hajaenda shule huyo leo sababu anaumwa na mimi sina pesa ya matibabu, kwahiyo ukamtibie”
Halafu Sia alimuacha pale Elly na mama Angel kwakweli mama Angel hakuwa hata na la kusema kwani Sia alikuwa kama kaongea na dereva wa bodaboda sababu alipomaliza tu kuongea hayo, ilifika bodaboda na kumchukua halafu akaondoka nayo.
Basi mama Angel alimuangalia Elly huku akimuangalia na Sia anayeishia na bodaboda kisha akamuuliza Elly,
“Kwani unaumwa nini?”
“Kichwa ndio kinakuuma”
“Huyu mama yako huwa unamuelewa!”
“Namuelewa ndio”
“Kakwambia anakuleta hapa ndio hospitali?”
“Hapana, ila kasema sababu naumwa na yeye hana pesa ya kunipeleka hospitali basi amesema ni bora anilete hapa kwa ndugu zetu”
“Ndugu zenu!! Huyu mwanamke ana wazimu eeeh! Kuna ndugu zenu hapa? Si unafahamu hapa ni kwakina Erica?”
“Nafahamu ndio ila Erica ni dada yangu, nimeambiwa hivyo na mama na nyie ni ndugu zetu”
“Jamani huyu Sia jamani! Ana nini lakini aaarhg!”
Ila mama Angel alipomuangalia Elly vizuri aligundua kuwa Ellyn i mgonjwa, basi aliingia nae ndani ila kwenda nae hospitali hakuweza zaidi zaidi alimpatia pesa na kumwambia kuwa aende hospitali kisha akamwambia,
“Huyu mama yako ni chizi’
“Ila ndio mama yangu, na mama ni mama nampenda na yeye ananipenda sana”
“Mama anayekupenda hawezi kuja kukubwaga sehemu kama hivyo, mfano na mimi nikakutimua ingekuwaje? Huyo mama yako hakupendi wala nini, haya nenda kawahi hospitali huko, upande bajaji hapo ikusaidie kufika haraka hospitali”
Basi Elly alimshukuru pale na kutoka nje ya ile nyumba.
Ila alipotoka tu, alimkuta mama yake nje ya geti lile na kuondoka nae ambapo alimuuliza,
“Amekupa pesa ngapi mwanangu”
Elly akampa mama yake hela ambayo kapewa na mama Angel, basi Sia aliihesabu na kutabasamu maana ilikuwa laki moja, basi akasema,
“Nilijua tu, maana huyu mwanamke ana kisirani na kila kitu huchukulia hasira tu! Haya twende mwanangu, shule utaenda kesho, kama unavyonijua mama yako ni mtu wa…”
Elly akamalizia,
“Mtu wa ukipata tumia ukikosa jutia”
“Ndio mwanangu, Mungu anipe nini mimi eeeh! Anipe zigo la misumari nijitwike na kichwani nina kipara kisa nini!!”
Elly akacheka pale, ila kwa muda huo Elly na mama yake walipitia kwenye mgahawa ili wapate supu kidogo halafu ndio waende nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 223

Wakati mama Angel amekaa na mawazo pale, Vaileth alisogea kumuuliza,
“Mama, kwani yule mtoto alikuwa na shida gani?”
“Anasema eti anaumwa”
“Mmmh mbona haonekani kama mgonjwa?”
“Alikuwa anatoa na machozi, ndiomana sikuwa na budi zaidi ya kumsaidia”
“Ila bora hata ungeniambia mimi nimpeleke hospitali maana naona kama anaweza fanya mchezo sababu anajua unatoa pesa tu, yani wakigundua watakuja kujifanya wanaumwa watu wengi hapa”
“Vaileth mwanangu na mdogo wangu, kuna mambo makubwa sana yapo nyuma ya pazia usiyoyafahamu. Huyu mtoto ana mama yake ni msumbufu hatari, yani akiingia hapa ni anaongea kama kameza cherehani, huyo mama yake ni hafai ila kipindi hiki mwache kanipata maana nina mtoto mdogo ndani kwahiyo siwezi kutoka toka hovyo, ila kitu kingine ni sababu nina huruma ila acha tu”
“Pole mama jamani!”
Mara walisikia kama mlango wa sebleni ukigongwa, basi Vaileth alisogea na kufungua ila aliyeingia alikuwa mama mkwe wa mama Angel pamoja na Mr.Peter kiukweli mama Angel hakupenda kumuona tena huyu mzee kabisa.

Mara walisikia kama mlango wa sebleni ukigongwa, basi Vaileth alisogea na kufungua ila aliyeingia alikuwa mama mkwe wa mama Angel pamoja na Mr.Peter kiukweli mama Angel hakupenda kumuona tena huyu mzee kabisa.
Ila hakuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuwakaribisha tu, ambapo baada ya salamu kitu cha kwanza kabisa mama mkwe wa mama Angel alimuulizia kwanza Angel,
“Mjukuu wangu Angel yuko wapi?”
“Mama samahani, Angel aliondoka na bibi yake”
“Nilijua tu ndiomana ulimtoa nyumbani kwangu”
Mama Angel aliinama chini tu kwani alijua wazi kuwa jambo lile limemuumiza mama mkwe wake, basi Mr.Peter akasema,
“Yani Angel hapokei kabisa simu zangu wakati mimi ni kama babu yake au umemkataza?”
“Aaaah hapana, ila Angel hana simu”
Mama mkwe akajibu,
“Anayo, kwani Angel hajakuonyesha? Mr.Peter alimzawadia Angel simu nzuri ya gharama nay a kisasa, unataka kusema kitu gani au umeichukua wewe”
“Ningeiona kweli ningeichukua ila sijawahi kumuona Angel na simu”
“Oooh nimekumbuka, hata hivyo mjukuu wangu alisema kuwa hana simu sababu wewe unamzuia kutumia simu. Kwanini upo hivyo jamani Erica? Hujui kama karne imebadilika hii! Huu ni wakati wa mitandao na mawasiliano, sasa binti kama Angel asitumie simu jamani kwanini? Unataka kumfanya nini mtoto?”
“Mama nisamehe tafadhari, ila mimi niliona kuwa kwasasa simu ingemchanganya tu Angel na niliona ni vyema asiwe nayo ndiomana ipo hapa simu ya mezani ili kama kuna mawasiliano mengine yafanyike”
“Yani kuna watu mmesoma ila elimu haijawakomboa kabisa, hizi siku hizi ni nyumba ngapi unatembea na kukuta kuna hizo simu za mezani? Kila mtu anakuwa na simu yake hadi watoto, pesa mnayo mnashindwa nini kutumia kwa watoto wenu? Kwanini unawafanyia hivi watoto lakini Erica? Kwani wewe uliharibiwa na simu!”
“Mmmh mama, tusifike huko jamani! Basi nitamruhusu Angel kutumia simu”
Mr.Peter akasema,
“Mwambie apokee simu zangu ili nikamuonyeshe mtu aliyefanana nae”
Yani mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa wakati huo na kuamua kukatisha zile habari kwanza kwa kumuita Vaileth ili awapatie vinywaji ila waligoma na kuaga halafu wakaanza kutoka huku mama mkwe akimwambia mama Angel,
“Safari ijayo ndio nitakuja rasmi sasa kwaajili ya mjukuu wangu, leo nilimleta huyu mzee mara moja”
Basi wakaondoka na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa yule mzee alikuwa amefata nini nyumbani kwake maana hakuelewa lengo la mama mkwe wake kumpeleka yule mzee pale.

Basi bibi Angel na Mr.Peter wakati wanaondoka, wakiwa njiani kuna mwanamke ambaye bibi Angel alimuona na kumwambia kuwa Mr.Peter asimamishe gari basi alisimamisha gari karibu na yule mwanamke ambaye alirudi nyuma kisha yule mwanamke alimkimbilia bibi Angel na kumkumbatia kwa furaha, kisha walisalimiana halafu bibi Angel alianza kumuuliza,
“Kheee jamani kumbe Sia upo!!”
“Nipo mama, za siku nyingi”
“Nzuri tu, jamani umepotea halafu hubadiliki wewe binti jamani! Sema kwasasa umepungua”
“Shida hizi mama ndio zimefanya nipungue”
Basi akamuona Elly akimsogelea Sian a kumsalimia huyu mama ambapo huyu mama alimuuliza Sia,
“Ndio huyu mwanao?”
“Ndio mama, ndio huyu mjukuu wako anaitwa Elly”
“Oooh nafurahi kumfahamu, na yule mume bado unaishi nae?”
“Mume yupi mama? Mimi sikuwa na mume, hivi unajua kuwa huyu mtoto ni mjukuu wako kabisa, yani ndiye niliyezaa na Erick”
“Jamani Sia, bado una zile hoja za kuzaa na Erick!!”
“Sasa mama, kwanini nipinge wakati hii ni damu ya Erick. Hakunioa ndio ila huyu ni wa kwenu”
“Mmmh Erick anayo hiyo habari!”
“Anayo ndio ila Erick alinikataa kipindi nina mimba hadi sasa nina mtoto hanitaki mimi wala mtoto, ila mimi namuachia Mungu tu ila hii ni damu yenu”
“Wewe Sia wewe jamani, unakumbuka nilikubamba kwenu na yule mwanaume wako!”
“Mama, ile ni historia ndefu sana ila ipo siku utasadiki haya niyasemayo”
“Haya, nipe mawasiliano yako. Nitajaribu kuongea na Erick”
Basi Sia alimpa bibi Angel namba yake na kisha kuagana nae, na yule mama kurudi kwenye gari halafu Sian a mwanae kuondoka.
Basi Elly alimuuliza mama yake,
“Mama jamani si ulisema baba alinikimbia nikiwa mchanga kabisa, mbona hapo nimekusikia kuwa baba alinikataa toka tumboni! Na huyo Erick ndio yupi mama?”
“Sikia mwanangu, mambo mengine sio lazima uelewe. Muda wa kuelewa ukifika basi utaelewa tu, ila tumeonana na huyu mama hesabia maisha yetu kubadilika na ukimuona mahali uwe unamuita bibi na kumpa heshima zote”
“Sawa mama”
“Nakuandalia maisha mema hata kama baba yako hataki ila najua kuna siku utakumbuka kuwa mama alinipenda sana na aliniandalia maisha mema, mwanangu usijali, utapata kila kitu, yani kila unachohitaji utakipata halafu mimi na wewe tutaishi raha mustarehe”
Elly alitabasamu na kufurahi kisha waliendelea na safari na mama yake ya kurudi kwao.
 
SEHEMU YA 224

Jioni ya leo mama Angel alikuwa nyumbani akitafakari mambo mbalimbali, ila akakumbuka jambo kuwa Angel ana simu, kwakweli hakupenda kabisa kitendo cha Angel kuwa na simu kwa kipindi hiko kwani aliona wazi simu itavuruga akili ya Angel ukizingatia kuna vitabia ambavyo anaviona kwa Angel na havipendi kabisa, basi akaamua kumpigia mama yake simu na kumuelezea tukio zima la siku hiyo la kufikiwa na mama mkwe wake pamoja na Mr.Peter,
“Mama, huyo Mr.Peter ni mume wa mrs.Peter yule mama mzazi wa Rahim”
“Kheee yule Mwajuma?”
“Ndio huyo huyo”
“Sasa kama wamefika hapo si inamaana kila kitu kitakuwa wazi, mwanangu ni wakati wa kumwambia Angel ukweli”
“Hapana mama, naona kama tutaichanganya akili ya Angel tu kwasasa”
“Ila mwanangu, mfano Angel akaja kusikia kwa watu baki itakuwaje?”
“Unajua mama, nina mawazo mengi unadhani itakuwaje pale Angel atakapogundua kuwa Erick sio baba yake mzazi? Naona kama mwanangu nitamuharibu kisaikolojia, tuache tu mama. Sasa hilo swala la simu itakuwaje?”
“Kuhusu simu hata usijali, mimi nitajua cha kufanya”
“Sawa mama, asante”
Wakaagana pale na mama yake ila leo baba Angel aliwahi kurudi maana muda huo huo aliingia nyumbani na kuanza kuongea na mke wake,
“Ulikuwa unaongea na nani mama watoto?”
“Na mama”
Kisha alianza kumueleza kuhusu mama yake alivyofika siku hiyo na Mr.Peter na jinsi walivyomuulizia Angel,
“Kwahiyo Angel ana simu?”
“Ndio, hapa ndio nimetoka kumpigia mama na kumtaarifu”
“Ila mke wangu, hivi tutambana mtoto hadi lini? Kwa karne hii watoto wanavyotumia simu, tutaweza kweli? Tutamnyang’anya halafu atapewa na wanaume”
“Mmmh umeanza mume wangu jamani!! Tunatakiwa kumchunga mtoto bila kujali kitu chochote”
“Kwasasa Angel anatakiwa aambiwe kuhusu utumizi mzuri na mbaya wa simu, maana najua kwa karne ya sasa kuna madhara makubwa sana, tutamkataza halafu atanunuliwa na mwanaume tutamjengea nini Angel? Mwishowe tutasema bora hata Samir maana anaweza kukutana na wakina Rahim”
“Umeanza sasa baba Angel, hayo mambo si yamepita jamani! Haya, leo kaja mwanamke wako Sian a mapya kabisa, kaja kumleta Elly kuwa anaumwa halafu akamuacha kwangu”
“Ila mke wangu naomba heshima ifate mkondo wake, Sia sio mwanamke wangu na hawezi kuwa mwanamke wangu, ningemtaka Sia basi ningemuoa yeye ila sijawahi kumtaka”
“Sasa kwanini Sia anatusumbua sana kwenye hii familia”
“Na tukimjali atatusumbua zaidi mke wangu, lengo la yule mwanamke ni kuona sisi tunakosa amani kwaajili yake, hebu tuishi kwa upendo wetu kama zamani jamani mke wangu, tena ule upendo uliokuwa kwetu tuuzidishe maradufu, kwakweli mke wangu sitaki kuona kidudumtu kama Sia akijisifu kuwa kafanikisha kuharibu nguvu ya mapenzi iliyokuwa kati yetu, hebu tushikane na tusiteteleke kwa chochote kile”
Basi mama Angel alienda kushikana mikono na mume wake na kusema kwa pamoja,
“Mungu tusaidie, amen”
Kisha wakaendelea na maongezi mengine tu.

Angel alia chumbani kwake baada ya kutoka chuo, alishika simu yake na kuanza kuwasiliana na Samir,
“Sasa Angel nahitaji kuonana nawe ila najua jinsi ilivyongumu kuonana nawe kwasasa”
“Kwahiyo tutafanyaje?”
“Aaaah hakuna tatizo, nimegundua kitu. Huyo bibi yako kuna chama flani yupo na bibi yangu, ngoja nifatilie ratiba zao, halafu nitajua kwa undani zaidi”
“Aaaah nilisikia kuwa Ijumaa ndio wanaenda kwenye chama”
“Basi hakuna tatizo, Ijumaa tutaonana mpenzi na tutakuwa pamoja”
Angel alitabasamu na muda huo huo bibi yake aliingia chumbani kwake ambapo Angel alificha simu yake, basi bibi yake alianza kumuuliza,
“Angel unaficha nini?”
Angel alikuwa kimya tu, ambapo bibi yake aliendelea kuongea,
“Angel, lete hiyo simu unayoificha huko”
“Sina simu bibi”
“Sio wakati wa kunificha huu ujue! Mama yako kashaambiwa kila kitu kuwa una simu, halafu mimi bibi yako nina hasira sana”
“Sina simu bibi”
“Umetoa wapi hiko kiburi Angel? Mbona mama yako alikuwa muoga sana kupigwa?”
Angel alikuwa kimya tu na ameinama chini, kwakweli huyu bibi huwa hapendi kumwambia mtoto kwa kumbembeleza muda wote, basi muda ule ule alitoka nje na aliporudi alikuwa na bakora ambayo alianza kumchapa nayo Angel mpaka Angel alimpa ile simu bibi yake,
“Mjinga sana wewe, unadhani wote tuna akili mbovu kama zako, kisa cha kuniletea mimba nyumbani nini jamani! Hebu nitolee matatizo mie”
Bibi aliichukua ile simu na kuondoka nayo ila Angel alibaki akilia tena alilia sana, aliona kuwa ameonewa mno na bibi yake, hakupenda kitendo cha bibi yake kumchapa bakora wakati alikuwa ni msichana mkubwa, yani Angel alilia kiasi kwamba usiku ule hakwenda hata kula chakula kwani alikuwa akilia huku akimuwaza Samir kuwa lazima kamtafuta halafu hajampata hewani.
 
SEHEMU YA 225

Kulipokucha, Angel aliamshwa na bibi yake ila macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia kwakweli bibi yake alisikitika sana na kusema,
“Yani hadi macho yamevimba sababu ya simu hii tu jamani Angel, umegoma hadi kula usiku sababu ya simu tu!”
Angel alikuwa kimya tu na kumfanya bibi yake aongee tena,
“Kwani wewe umetoa wapi hiko kiburi Angel, kwanini unataka makosa yajirudie? Unataka na wewe uzalie nyumbani kama mama yako alivyofanya”
Angel akashtuka kwani hakuwahi kufikiria kama alizaliwa nje ya ndoa, basi alimuuliza bibi yake
“Kwahiyo mimi nilizaliwa nje ya ndoa?”
“Siku utakayoona kuwa unaanza kuwa mtoto mwema ambaye ukiambiwa unasikia, basi nitakueleza mambo mengi sana, ila mtoto ambaye nikimuadhibu kidogo tu analia usiku kucha huwa sipendi hiyo tabia. Inuka hapo uje unywe chai mjukuu wangu, sina ubaya na wewe ila nakufundisha tu”
Basi Angel aliinuka pale na kwenda kuoga ila alikuwa na hasira sana kiasi kwamba siku hii hakuweza hata kwenda chuo kwani macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia, basi alikaa tu na bibi yake wakitaniana pale ila bibi yake hakutaka kumwambia ukweli kuhusu yeye kuzaliwa nje ya ndoa maana pale aliropoka tu sababu ya hasira aliyokuwa nayo.

Baba Angel leo akiwa ofisini kwake, alitembelewa na mama yake, hata yeye alishangaa kwani hakutegemea kutembelewa na mama yake ofisini kwake,
“Naona umeshtuka maana hujaamini hiki unachokiona!”
“Kweli sijaamini mama”
“Toka jana nipo hapa mjini, leo nikasema ngoja nipitie ofisini kwako mara moja. Halafu mjukuu wangu nitakuja kumuona na zawadi hivi karibuni”
Basi baba Angel alimsalimia pale mama yake na kuanza kuongea nae ambapo mama yake alianza kumwambia,
“Jana wakati nimetoka kwako nikakutana na Sian a mtoto wake”
Baba Angel alichukia kwani alijua ambacho kingeendelea, basi mama yake alitambua na kumuuliza,
“Mbona umeanza kuonyesha chuki mapema hivyo mwanangu?”
“Aaaah mama jamani, huyo mwanamke ni pasua kichwa hadi sitaki hata kumuona”
“Na ni pasua kichwa kweli, nakumbuka kipindi kile alidai kuwa na mimba yako, na hadi sasa kaendelea kusisitiza kuwa yule mtoto aliyenaye ni mtoto wako kwahiyo ile ni damu yako Erick”
“Mama, siwezi kukataa mtoto tu bila sababu za msingi ila kwa kipindi kile Sia hakuwa na mimba yangu kwahiyo ni muongo yani nitasimamia neno langu hilo hadi mwisho”
“Ila mwanangu jamani! Inawezekanaje Sia awe muongo! Basi tukampime yule mtoto”
“Tukampime nini sasa?”
“Tukapime DNA na wewe”
“Mama, hizo hela za kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia kama hazina kazi ni bora kwenda kuzitupa ili wenye shida waziokote, yani mama siwezi kujisumbua kufanya chochote kile. Hakuna kitu chochote ninachomuamini Sia, nampenda sana mke wangu”
“Naelewa hilo, naelewa ni jinsi gani unampenda Erica hata Erica pia anakupenda sana wewe ila hiki ni kitu kingine, inatakiwa kama yule mtoto ni damu yetu basi apate haki zote kama wengine”
“Mama, huko sipo tafadhali. Ukitaka tuelewane mimi na wewe basi tuzungumzie mada zingine na sio hizo mada za Sia, tafadhali mama yangu nakuomba”
“Sawa, mwanangu nimekuelewa”
Ilibidi mama yake abadilishe stori na kuanza kuongea nae kuhusu mambo mengine tu kwa muda huo.

Leo wakati wa kutoka shule, kama kawaida Sarah alikaa karibu na Erick basi alianza kuongea nae,
“Ila Erick kwanini unanifanyia hivi jamani! Yani naona kama unanikwepa hivi siku hizi”
“Hapana sikukwepi”
“Maana toka useme simu kaichukua mama yako, basi siku hizi unanikwepa kabisa yani hata huongei vizuri na mimi”
“Kwani unataka niongee vipi jamani Sarah!”
“Mimi nakupenda, unatakiwa uonyeshe kunipenda pia”
Yani Erick hadi alikuwa akijihisi aibu kabisa kwa wakati huo kwani Sarah aliongea kwa ujasiri mkubwa kabisa kuonyesha kuwa ni kweli anampenda sana Erick, basi akamshtua na Erick akamwambia Sarah,
“Ila sisi bado wadogo Sarah!”
“Kwani wadogo kitu gani Erick? Mimi nakupenda bila kujali kitu chochote kile, sijali kuhusu udogo wetu ila ninachojali ni kuwa nakupenda sana, yani Erick unavyonifanyia sio vizuri ujue, kumbuka tunafunga shule! Nikubalie Erick jamani ili moyo wangu uwe na amani”
“Unanipa wakati mgumu sana Sarah, naamini mama yangu atapenda kuona mimi na wewe tukiishi kama dada na kaka na si vinginevyo”
Basi gari ilifika kwakina Erick naye Erick alishuka kwakweli Sarah hakuwa na amani kabisa, basi alikaa kimya tu hadi alipoingia nyumbani kwao na siku hiyo alienda kulalamika kwa mama yake,
“Mama, nampenda Erick ila kwanini ananikwepa na anasema kuwa sisi ni wadogo eti upendo hauangalii ukubwa au udogo”
“Ila wewe Sarah, umepata wapi ujasiri wa kumtongoza huyo Erick?”
“Nakumbuka mama ulisema nikiwa na hisia na chochote niwe huru kusema, nami hisia zangu zipo kwa Erick, natamani mno awe wa kwangu. Mbona wazungu wanaanza mahusiano wakiwa wadogo kabisa, sembuse mimi na Erick!”
“Aaaah usijali mwanangu, kama Erick ni wako basi atakuwa wako tu hata usijali, kuna mambo sio ya kulazimisha sana. Kuna siku nitakaa nawe na kukufundisha kuhusu mapenzi, hakuna kitu kibaya kama kumlazimisha mtu akupende, yani kama hakupendi basi itakuwa ni tatizo kwako, ila mwanangu huwa napenda kukwambia kuwa usikate tamaa sema kuhusu swala la kumpenda Erick subiri kwanza”
“Sawa mama”
Basi alienda chumbani kwake, yani mama Sarah alimlea mwanae katika maisha ya tofauti sana ambayo wazazi wengi wa kiafrika wasingeweza kulea mtoto kwa staili hii, ila yeye alijionea kawaida tu, na alikuwa akiongea na mwanae karibu kila kitu.
 
SEHEMU YA 226

Erick na Erica wakiwa nyumbani, kipindi hiki walipatana yani Erica aliona rah asana vile yeye hana simu na Erick nae hana simu maana mwanzoni roho ilimuuma sana kuona kuwa mwenzie ana simu na nay eyena, basi muda huu Erick na Erica walienda bustanini ambako alikuwa amekaa Junior kwa muda huo basi Erica alianza kusema,
“Eeeeh haya sasa, leo mbele ya Erick naomba Junior ukubali kuwa utamuoa dada Vaileth”
Basi Junior na Erick walikaa kimya kidogo, kisha Junior akasema,
“Mmmh na wewe Erica, kumbe umeshamuelezea Erick!”
Erick akajibu,
“Hapana hajanielezea, yani na mimi ndio nashangaa hapa”
“Haya, ngoja basi nikuridhishe mdogo wangu Erica”
“Sio uniridhishe, nataka umaanishe”
“Sawa, mimi namaanisha haya niyasemayo kuwa hapo badae nitamuoa Vaileth yani Vaileth ndio atakuwa mke wangu wa maisha”
Muda huu Vaileth nae alitokea nyuma yao kwahiyo alitabasamu aliposikia maneno yale yakitoka kwa Junior, yani alihisi rah asana moyoni mwake, basi aliwasogelea pale karibu na kusema,
“Jamani na nyie msiseme kwa nguvu, hadi mama asikie!!”
Basi Erick akasema,
“Yani ndio mmeweka siri kabisa na Erica, mimi nawatahadharisha tu kuwa msiamini sana maana siku isiyokuwa na jina basi atayabwaga yote hayo”
Erica akachukia muda huu ikabidi Junior ampooze na kusema,
“Erick, unavyomfikiria Erica sio hivyo alivyo kuna maneno ambayo Erica hawezi kuyasema wala nini moja wapo ni jambo hili. Tafadhari usimchukize mdogo wangu mpendwa, maana mimi na Erica ni damu damu”
Hapa Erica alitabasamu maana alipenda sana kusifiwa, ikabidi naye Erick amsifie kidogo ila bado hakuwa na imani kwani alijua lazima hayo mambo ya Junior na Vaileth yatafika tu kwa wazazi wao.

Muda wa kulala ulivyofika, Angel alikaa kwanza na bibi yake kabla ya kwenda kulala ambapo bibi yake alikuwa akimpa habari nyingi za maisha,
“Unajua nini mjukuu wangu, kuna kaka mmoja alikuwa akimpenda sana mdada ila yule mdada alivyokubali kuwa naye, wee yani mdada ndio alimpenda sana yule mkaka na mwisho wa siku yule mkaka alimpa mimba mdada na kumkimbia”
“Khee bibi, hivi mwanaume akimpa mimba mdada na kumkimbia inakuwaje kwa mdada?”
“Yani hapo ndio unaujua umuhimu wa mama katika maisha, unajua mjukuu wangu mama ni wa kumuheshimu sana, ni mengi kapitia, ukikuta mama kakupatia mwanae baba bora anayekulea na kukuhudumia, usidhani imetokea tu ila ujue mama yako alipiga goti na kulia mbele za Mungu. Kwanza kuzalia nyumbani ni aibu, fedheha halafu heshima yako inashuka, yani hutambuliki vizuri na mbaya zaidi uzalie nyumbani ukiwa na umri mdogo eeeh ! Mbona utakuwa unalia kila siku, maana kila mtu analeta lake, huyu atauliza, baba wa mtoto yuko wapi na amekukimbia yani utaona dunia haitamaniki kwako”
“Mmmmh bibi jamani unanitisha”
“Sikutishi ila nakupa ukweli halisi wa maisha ulivyo mjukuu wangu, usikubali kudanganywa na wanaume”
“Ila bibi, utakuwa unaniruhusu mara moja moja niwasiliane na marafiki zangu kwenye ile simu!!”
“Ungekuwa hivyo muda wote mbona tungeelewana Angel mjukuu wangu jamani!! Hakuna tatizo, nitakuwa nakuruhusu ila kwa muda wangu mimi”
“Sawa bibi yangu”
“Haya, ni muda wa kulala huu na leo utaenda kulala chumbani kwangu ili tulale wote”
Angel alikubali tu, bibi alifanya hivi ili Angel asijihisi mpweke na kuanza kuwaza mambo mengine yasiyofaa kwahiyo aliona ni vyema kuwa nae karibu zaidi ili kumsahaulisha mawazo ya kijinga.
Basi walienda kulala, ila wakati wamelala usingizi mzito, bibi aliamka usiku kwaajili ya kufanya maombi, na alifanya maombi yake pale vizuri kabisa ila alipomaliza alimuona kama Angel akiweweseka huku akimtaja Samir,
“Samir, Samir, Samir”
Bibi alimuangalia na kusikitika sana, kisha akamshtua Angel na kumwambia tu alale vizuri, alishaelewa kuwa mjukuu wake amemuweka Samir kwenye mawazo yake ndiomana ameanza hadi mchezo wa kupatwa na ndoto za kumuhusu Samir.
Kulipokucha, bibi alimuamsha Angel na kutoka nae nje ili kufanya nae kazi za usafi,
“Ila bibi bado sijaoga”
“Kheee Angel, yani kwenda kufagia uwanja na kusafisha nyumba ni mapaka uoge? Twende jamani mjukuu wangu”
Ilibidi Angel akubali na kutoka nje na bibi yake ambapo walikuwa wakifagia fagia uwanja kisha bibi yake alitoka nae nje ya geti kabisa ambapo walianza kung’olea majani kwenye maua ya nje na kumwagilia yale mauwa yani hadi wanamaliza kazi ile Angel alijihisi kuchoka sana hadi alimwambia bibi yake,
“Jamani bibi nimechoka”
“Eeeeh huo ndio uanamke, hapo sasa nenda kaoge upate nguvu tuje kunywa chai”
Basi Angel alienda kuoga na kwenda kunywa chai, na walipomaliza tu bibi akampa Angel simu sasa ili akawasiliane nayo kwa muda kidogo.
Angel aliingia chumbani kwake, kiukweli alikuwa amechoka, kiasi kwamba alishika ile simu na kutuma ujumbe mmoja tu kwa Samir na alipokawia kumjibu alijikuta ameshalala kwa muda huo.

Mama Angel leo akiwa nyumbani kama kawaida yake ya siku hizo, ila siku hiyo pia baba Angel hakwenda popote kwani alijihisi kuwa anahitaji kupumzika kwahiyo kwa muda huo alikuwepo tu nyumbani akipumzika, basi waliongea na mke wake pale na kusema,
“Unajua nini mume wangu, nimekumbuka kipindi kile ambacho tulikuwa tukienda ufukweni kufurahi!”
“Hata mimi nimekumbuka sana mke wangu, ila tumngoje Ester akue kue kwanza. Ila twende sebleni tukae kidogo tuangalie Tv yani leo nimekumbuka tu kushinda nyumbani na wewe mke wangu”
Mama Angel alitabasamu kisha yeye na mumewe wakatoka kuelekea sebleni ambapo walikaa na kuanza kuangalia Tv, ila muda kidogo tu mlango wa pale sebleni ulisikika ukigongwa basi Vaileth alienda kufungua ule mlango ila aliyeingia kwa muda huo alikuwa ni Sia.
 
SEHEMU YA 227

Mama Angel alitabasamu kisha yeye na mumewe wakatoka kuelekea sebleni ambapo walikaa na kuanza kuangalia Tv, ila muda kidogo tu mlango wa pale sebleni ulisikika ukigongwa basi Vaileth alienda kufungua ule mlango ila aliyeingia kwa muda huo alikuwa ni Sia.
Kiukweli furaha ya mama Angel ilikatika muda ule hata baba Angel aliona hali hiyo kwa mke wake na hakupenda kile kitu kabisa ila alichokifanya alimsogelea mke wake na kumshika bega kisha akalaza kichwa cha mke wake kwenye bega lake na kumbusu halafu akamwambia,
“Nakupenda sana mke wangu”
Kitendo kile kilimkera sana Sia, ambaye alisema,
“Yani nyie ni watu wa ajabu sana kanakwamba hamnioni!”
Baba Angel akamwambia,
“Tusiendelee na starehe zetu sababu ya kukuona wewe! Kwani ni nani wewe katika maisha yetu?”
Baba Angel akambusu tena mke wake, safari hii alimbusu mdomoni na kumfanya Sia aumie zaidi kwani hakupenda kabisa ile kitu na alijua wazi muda huo akifika humo ndani basi ataharibu hali ya hewa kabisa, ila yeye mwenyewe alishindwa kuvumilia, kwani baba Angel alikuwa kama ndio kafunguliwa kufanya mahaba kwa mke wake pale sebleni, basi Sia alifungua mlango na kutoka ambapo baba Angel na mama Angel waliinuka na kwenda chumbani.
Kiukweli hii ilikuwa ni mbaya sana kwa upande wa Sia, alijikuta akidondosha chozi pale nje huku akisema,
“Najua wanafanya, ila ndio hadi wanionyeshe!!”
Akafuta machozi yake na kutoka sehemu ile na moja kwa moja kuondoka kabisa.

Moja kwa moja Sia alienda nyumbani kwa Tumaini, ambapo leo alimkuta nyumbani tu na kuanza kuongea nae,
“Ila Tumaini kwanza kabisa unafanya kazi gani maana kila siku nakukuta nyumbani!”
“Oooh ninafanya kazi mimi ila kazi yangu haina masharti kivile, nimejiajiri mimi. Haya na wewe unafanya kazi gani maana nikisikia hili kwa huyu nasikia lile kwa yule”
“Aaaah hata mimi nimejiajiri”
“Umejiajiri kugombanisha nyumba za watu? Umejiajiri kuharibu ndoa ya watu? Hivi Sia unajua wazi kuwa mimi na wewe tunajua ukweli wa mtoto wako! Kwanini bado ukutane na mama Erick umwambie kuwa mtoto wako umezaa na Erick?”
“Ukweli wa kuhusu mtoto naujua mimi na si mimi na wewe maana mimi ndio niliyebeba mimba”
“Hata kama Sia, nakumbuka wazi kipindi umeenda kusema una mimba ya Erick ilikuwa ni lengo la kuvuruga penzi la Erick na Erica, nakumbuka wazi kuwa kipindi kile tulikuwa tukisaidiana kwenye mambo mengi tu na nilikuwa nikikupeleka sehemu nyingi, ila ukanigeuka na mimi na kwenda pamoja na Dora kwa mganga wenu sijui wa Bagamoyo kwa lengo moja la kumroga mdogo wangu, ila Mungu si Athumani kwani dawa yako akala kijana mdogo asiye na hatia Steve na alianza kukufata fata nyuma kama bata na watoto wake, na mwishowe ukapata mimba yake kweli, kwanini uendelee kung’ang’ania kuwa mtoto uliyezaa wewe ni wa Erick? Unajua mwanzoni sikumuelewa Erick wakati anasema kuwa unamsumbua na kusema Erick ni mtoto wako na hata hivyo uligoma kuniambia hiyo siri, haya umeibua mengine kuwa mtoto umezaa na Erick, swali langu ni mtoto yupi sasa? Yule Erick au huyo wako au na wewe ulizaa mapacha kama Erica?”
“Usilolijua litakusumbua, tena litakusumbua sana. Kwanza jua kuwa yule mtoto anaitwa Elly, na unapomuongelea jua kuwa hapo umemuongelea Elly, Erick na Erica yani hiki kitu hutoweza kukitenganisha, kila ambacho Erick na Erica wanakipata inapaswa na Elly nae akipate, hutonielewa kwasasa namaanisha nini ila kuna muda utanielewa kuwa nazungumzia nini. Ila kwa muda huu sikuja kuongelea kuhusu watoto nimekuja kuongelea kitu kingine kabisa”
“Kitu gani?”
“Mapenzi yangu kwa Erick, sijui nimpate nani aweze kuokoa moyo wangu au aweze kuokoa fikra zangu, nampenda sana Erick na nitampenda hadi kufa kwangu, hakuna mwanaume nitakayeweza kumpenda kama Erick”
“Ila Sia kuna mambo kwakweli unachekesha, haya umeshamwambia Erick hivyo!”
“Nishamwambia sana, ila hataki kunielewa, kwakwlei Erick ni mwanaume ambaye alinifanya nione kama naimiliki dunia, leo hii kumkosa kwakweli sipo tayari, nampenda sana jamani.”
“Haya, nimekusikia mama ila nakusaidiaje?”
“Najua Tumaini hutaki kuwa upande wangu sababu mimi sina pesa, ila najua ningekuwa na pesa ungekuwa upande wangu. Leo ukiona hadi nimekuja kukwambia haya basi nimeumia sana, ila maumivu yangu huwa yana madhara makubwa sana, ukionana na Erick na huyo mjinga mwenzie Erica waambie wajipange”
“Kheee jamani, kwanza ngoja nikwambie kitu Sia, ukija kuongea nami uje na mada zingine ila mada zako na Erick sizitaki kabisa, kwanza hazinisaidii na pili siwezi kufanya lolote lile. Natumai kwasasa umemaliza ulichokuwa unataka kuongea, kwaheri”
Kwa kifupi kwasasa Tumaini hakuhitaji ukaribu sana na Sia kwani kaona kuwa mwanamke huyu atamgombanisha na ndugu yake bure, kwahiyo aliamua kuwa nae mbali mbali, basi Sia alichukia pia kuambiwa vile kwani aliinuka na kuondoka zake tena bila hata ya kuaga.

Sia alipotoka tu nje ya nyumba ya Tumaini aliona bajaji na kuiita basi ile bajaji ilisogea na akapanda na kuondoka nayo ila yule mwenye bajaji alianza kumuongelesha,
“Mama, samahani kuna binti mmoja mzuri mzuri anaitwa Angel, alikuwa anaishi kwenye ile nyumba uliyotoka ila siku hizi simuoni”
“Kheee unamuulizia Angel! Wa nini? Au unamtaka?”
“Samahani mama, nampenda sana yule binti yani hata ningekuwa namuona tu basi roho yangu ingeridhika”
“Oooh sawa, yule yupo kwao kwasasa, ila unampenda kweli?”
“Ndio nampenda sana”
“Unaitwa nani wewe?”
“Naitwa Ally”
“Ooooh basi sawa, nipe mawasiliano yako, nitafatilia kujua Angel anaishi vipi kwasasa halafu nitakuwa nakuelekeza cha kufanya, hata usijali ila ukiwa nae usimwambie kama kuna mama anakusaidia”
“Dah! Nashukuru sana mama yangu. Yani nampenda yule binti balaa, ni kweli sina hadhi, mimi ni masikini ila nina mapenzi ya dhati yani moyo wangu unampenda sana Angel, natamani hata ningekuwa namuona tu”
“Usijali kitu, ilimradi umeonana na mimi basi andika kila kitu kimepita”
Basi Ally alifurahi sana kukutana na huyu mama kisha walipeana mawasiliano pale na alimfikisha hadi alipoenda na wala hakumdai hela yoyote sababu tu kaahidiwa kumpata Angel.
 
SEHEMU YA 228

Muda wa kutoka shule, kama kawaida Erick alikaa pamoja na Sarah hata alipojaribu kukaa siti nyingine ilikuwa ni lazima Sarah amtoe mtu aliyekaa pembeni ya hiyo siti ili yeye akae na Erick, basi alianza kuongea nae ila leo aliongea nae kawaida kabisa kiasi kwamba hata Erick alimshangaa kwani hakusema zile mada zake za kumpenda kabisa bali aliongelea vitu vingine,
“Ijumaa, shule inafungwa Erick. Ila safari hii likizo nitaenda kwa bibi yangu”
“Oooh hongera sana, mimi nitakuwa nyumbani tu”
“Ila kipindi cha likizo ni vizuri kutembelea ndugu jamaa na marafiki ili kufahamu vizuri ukoo wako”
“Umenishauri vyema, nami kipindi hiki cha likizo nitafanya hivyo unavyosema Sarah”
Yani mpaka Erick anashuka nyumbani kwao hakuletewa mada za mapenzi kabisa na Sarah, kiukweli alijihisi vizuri kwenye moyo wake.
Basi aliingia ndani na kumkuta muda huu baba yake akiwa sebleni na kumsalimia, kisha baba yake akamwambia,
“Kumbe huwa unatangulia kurudi wewe halafu ndio anafatia Erica?”
“Hamna baba, huwa inategemea na siku”
Mara Erica nae alifika na kumsalimia baba yake pale ila kama kawaida ya Erica huwa akitoka na jambo shuleni basi anahitaji kuliongea, basi alimsogelea baba yake pale yani kabla hata hajatua begi lake na kuanza kuongea nae,
“Basi leo baba, wakati tunatoka shule sijui nani kamuelekeza Elly shuleni kwetu ila nikamuona, na kwenda kumsalimia”
“Mmmh, ila shule yenu sin i shule ya wasichana tupu?”
Ndio, ila nilimuona kwenye kibanda cha mlinzi naye akiwa ametoka shuleni kwao, basi niliongea nae kidogo ila unajua kaniuliza nini?”
“Eeeeh kakuuliza nini?”
“Kaniuliza kuwa, eti dada Angel siku hizi anaishi wapi? Basi nikamwambia kwa bibi, sijui ni kwanini kaniuliza vile!”
“Hivi huyo Elly si ndio mtoto wa Sia! Yani mama yake Elly si anaitwa Sia?”
“Mmmh mimi sijui jina la mama yake”
“Haya mwanangu, kabadili sare za shule sasa”
Basi Erica ndio akainuka na kwenda chumbani kwake kubadili sare sasa.
Muda ule ule baba Angel aliinuka na kwenda chumbani kwa mke wake, ila alijua wazi kuwa akimpa taarifa ile mke wake lazima atapaniki, ila alimuuliza tu,
“Hivi mtoto wa Sia anaitwa nani?”
“Kafanyaje tena!! Anaitwa Elly”
“Hamna kitu mke wangu, nilitaka tu kufahamu jina la huyo mtoto ila hakuna mengine wala nini”
“Nimekuelewa mume wangu, yani ndiomana huwa unasema Sia ana wazimu, sasa anavyosemaga Erick ni mwanae, je huyo Ellyn i mtoto wa nani?”
“Mjinga yule, tena mjinga kabisa, tufanye yet utu mke wangu”
Basi waliendelea na mambo mengine ila baba Angel alikuwa na maswali mengi sana kwa muda huo, kwanini huyo Elly aulizie anapoishi Angel kwa kipindi hiko? Akahisi kuwa lazima Elly katumwa na Sia tu, kwakweli akasikitika na kusema kuwa atafatilia swala hilo kimya kimya ili asimpe presha mke wake.

Usiku ulipofika, Erica alienda chumbani kwa Erick ili kumpa pia taarifa ambayo alikuwa akimpa baba yake, ila ile taarifa ilimchukiza sana Erick na kusema,
“Yani simpendi Elly jamani simpendi kabisa, na mama yake simpendi”
“Kwanini sasa? Kwnai Elly kosa lake nini?”
“Elly ananikera, kwanini anakubali kutumwa ujinga na mama yake? Yani hapo ni mama Elly ndio kamtuma Elly kufanya hivyo, namuhurumia dada yangu jamani maana kuanza kupatwa na mawazo ya huyu mama kwasasa dah!”
“Kwani mama yake Elly ana ubaya gani? Maana hata baba nimeona alivyochukia na kumsema mama yake Elly”
“Huyo mama ni mtu mbaya sana, kumbuka vile visheti ambavyo baba alikula na kuanza kuumwa, je alikuwa na maana gani kufanya vile? Kwakweli yule mama hatufai kuanzia Elly na mama yake wote hawatufai katika familia yetu”
“Ila kwanini?”
“Erica na wewe kama huelewi basi endelea kutokuelewa hata hivyo ukielewa ni balaa maana sijui utayapeleka wapi”
Halafu Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake, na muda ule Erica pia aliamua kulala tu.
Kulipokucha kama kawaida, Erica aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda shule.
Leo, baba Angel nae alienda mapema kwenye ofisi yake kwani alipanga kuwa akitoka tu basi moja kwa moja aende kwa mama mkwe wake ili kuongea nae kidogo kuhusu Angel kwani alihitaji awe nae makini zaidi kwani hakuelewa kuwa Sia ana lengo gani kwa binti yao
Ila wakati Erica anatoka kwenda shuleni alimuona mwanamke ambaye alitambulishwa na Elly kuwa ni mamake, kwahiyo alimuona mamake Elly, na alimuona kama anaelekea kwao, pale hakuelewa kuwa yule mama anaenda kufanya kitu gani pale kwao.

Basi muda huu, mama Angel aliamua kurudi kulala tu kwani watu wote waliokuwa wanatoka walikuwa tayari wameshatoka ile asubuhi, basi wakati anajilaza tu akafuatwa na Vaileth na kugongewa mlango,
“Ndio Vaileth kuna nini?”
“Kuna mgeni wako sebleni mama”
Kwakweli mama Angel alishangaa kidogo kuwa kwa muda huo ni nani yupo sebleni kumsubiri, basi alitoka ili kumuangalia akamkuta Sia ndio amekaa sebleni, ila kiukweli mama Angel aliona kuongea na Sia mahali hapo ni kujipa ugonjwa wa moyo tu basi moja kwa moja alienda kufungua mlango na kumwambia Sia,
“Naomba uondoke”
“Niondoke kitu gani? Siwezi kuondoka mimi kama hujanisikiliza”
“Sihitaji kukusikiliza, kama unahitaji kuongea na Erick mfate ofisini kwake”
“Hapana, sijaja kwaajili ya Erick hata mimi najua kama yupo ofisini muda huu ila nimekuja kuongea nawe mke mwenzangu”
Mama Angel alipatwa na hasira muda huo ila akajituliza tu hakujibu kitu, sema muda huo huo akarudi ndani na kuchukua simu yake na kumpigia mumewe,
“Yule shetani Sia kaja na leo, yani hapa tu kashaanza kunichefua”
“Usijali mke wangu nakuja”
Basi baada ya muda kidogo tu baba Angel alikuwa amewasili, na alivyoingia tu pale sebleni alionana na Sia, moja kwa moja baba Angel alimshika Sia mkono na kumtoa nje na alitoka nae hadi nje ya geti na kumwambia mlinzi,
“Sitaki tena uruhusu hii takataka kwenye nyumba yangu tafadhali”
Kisha baba akamsukumia Sia nje na kurudi ndani, moja kwa moja alienda kwa mke wake na kumkumbatia huku akimwambia,
“Usijali mke wangu, hii kitu haitotokea tena”
“Ila kwanini ananifanyia hivi jamani! Sia ananikosesha raha kabisa na amani”
“Achana nae mke wangu, utakosaje amani sababu ya mjinga mmoja!!”
Basi baba Angel alienda na mama Angel chumbani, kwakweli siku hiyo aliamua kutokutoka tena yani alishinda tu pale pale na mke wake, ingawa alijua kuwa kuna kazi zake zinakwama ila kwake ilikuwa sawa tu kuliko kumuona mke wake akihudhunika.
 
SEHEMU YA 229

Muda huu Sia alienda moja kwa moja kwenye lile duka ambalo linasimamiwa na Steve na kumwambia Steve,
“Nimetumwa na mwenye mali, kuwa unipatie laki mbili”
“Aarrgh usinichanganye wewe mwanamke kabisa, nadhani unafikiri mimi ndio bwege lako”
“Kheee mbona umekuwa na hasira kiasi hiko? Nini kimekukera? Unapata shida kupata mwanamke? Ila mimi bado nipo?”
“Yani wewe mwanamke sikukujua tu na dawa zako ndio zilinichanganya kipindi kile hadi nikakuoa, ila laity kama ningejua una akili mbovu kiasi hiki basi nisingethubutu”
Mara simu ya Steve ilianza kuita, alitoka ofisini na kwenda kuongea nayo basi Sia alifungua droo na kuchukua kiasi cha pesa alichokitaka na kumuachia ujumbe mezani tu halafu akaondoka zake, yani Steve aliporudi alikuta tu ujumbe,
“Nimechukua laki tatu”
Yani Steve alijishika kichwa, kwakweli hakuelewa kabisa, kwanza hakuelewa kwanini ameenda kuongea na simu bila kufunga droo ya pesa, na pili hakuelewa ni kwanini aliamua kumuacha Sia ofisini, yani hakuelewa kabisa mahali hapo basi alikaa na kutafakari kisha aliamua kumtumia bosi wake ujumbe kwa kile ambacho kimetokea kwa siku hiyo, kiukweli alikuwa akisikitika sana kwa kilichofanywa na Sia kwa muda huo.
Alipotuma ule ujumbe kwasasa alitulia kwani aliamini kuwa ujumbe umefika na bosi wake ataufanyia kazi.

Muda huu Erica na Erick walitoka shuleni, yani siku ya leo walirudi pamoja ila wazazi wao walikuwa sebleni wakiangalia tv tu na moja kwa moja Erica baada ya salamu tu akawaambia kuwa asubuhi alimuona mama Elly kama anaelekea nyumbani kwao, basi baba yake alimkatisha pale kwani alijua kuwa atayasema nay a jana yake bure. Alimuuliza tu,
“Hivi kesho ndio mnafunga shule eeeh!”
“Ndio baba, kesho ndio kufunga shule”
“Haya, mwanangu”
Kisha Erica sasa alienda chumbani kwake, ila muda huu baba Angel alipata wazo na kuona ni vyema kupiga simu kwa Tumaini, basi akainuka na kwenda chumbani, ila alipochukua simu yake ndio alibambana na ujumbe wa Steve, kwakweli alishangaa sana na kujiuliza kuwa Sia ana maana gani kufanya vile dukani kwake, mama Angel nae alipoingia alimuonyesha ile meseji ya Sia,
“Sasa kwanini kafanya hivyo!!”
“Najua basi mke wangu? Kwakweli sijui huyu mwanamke anahitaji kitu gani kutoka kwangu! Ngoja nimpigie Tumaini nimueleze na jambo hili”
Baba Angel alimpigia Tumaini kwa muda huo na alimueleza yale aliyoyafanya Sia,
“Jamani mimi nimetoka kumtimua nyumbani kwangu hapa, nadhani sasa sio wakati wa kumchekea zaidi huyo mwanamke, sasa laki tatu kachukua kwa kazi gani jamani! Mimi naenda kumpokonya”
“Aaah muache tu dada, ila naenda kuongeza ulinzi kwenye duka langu”
“Hivi Sia wa sasa unamuelewa lakini! Kwakweli sijawahi kufikiria kama ipo siku Sia atakuwa wa aina hii, pole sana mdogo wangu ila fundisha vijana wenzio sasa wasifanye kama wewe maana wewe nawe ulikuwa muongo sana kwa wanawake na uliwaaminisha mno ndiomana huyu Sia kawa kichaa, fundisha wenzio ila pole”
Baba Angel aliona kuwa dada yake hana ushauri, kwahiyo aliamua tu kukata simu ile na kufikiria mambo mengine kwa wakati huo.
 
SEHEMU YA 230

Wakati wa kulala, baba Angel alikuwa na mawazo sana ila hakutaka mkewe agundue jambo hilo, alichokuwa akiwaza ni namna ya kufanya na huyu Sia, yani alitamani kupata kitu cha kumfanya Sia, ila muda ule alipigiwa simu na mama yake na kuipokea halafu akaanza kuongea nayo,
“Hujambo mwanangu”
“Sijambo kabisa mama”
“Sia kanipigia simu, kasema mtoto anaumwa”
Baba Angel hakuwahi kumkatia mama yake simu ila siku hii alimkatia na kuizima kabisa, mkewe alimuuliza kuwa tatizo ni kitu gani ila alimgeresha tu pale kwahiyo hakumueleza ukweli wowote ule.
Basi waliamua tu kulala na kulipokucha kwa siku hiyo ilimbidi baba Angel ajiandae kwaajili ya kwenda ofisini kwake ambako hajaenda kwa siku mbili na alikuwa na kazi za kufanya.
Alifika ofisini kwake na kuanza tu kazi zake, ila muda huu mama yake alimpigia tena simu na kupokea,
“Erick, ndio nini jana kunikatia simu?”
“Mama, kwa kifupi sitaki uniambie habari za huyo Sia, yani sitaki kabisa tuwe tunaongea mambo mengine tu”
“Kweli mwanangu huyu Sia kakutoka loh! Ila kasema mtoto amelazwa”
“Mama jamani, nakuomba mama yangu nakuomba sana, habari za Sia sizitaki kabisa mimi”
Baba Angel alikata tena ile simu aliona na mama yake akimchanganya tu, basi akaendelea na kazi zake kama kawaida.
Mchana wa siku hiyo, ofisini kwake alifikiwa na madam Oliva, basi alimkaribisha na kuanza kuongea nae,
“Nilikuwa napita maeneo haya ya karibu, nikaona ni vyema kama nikija kukusalimia baba Erick”
“Oooh nashukuru sana mwalimu”
“Unaonekana kuchoka sana na kazi, hivi umekula kweli!”
“Sina hata hamu ya kula, halafu muda sina kwanza nimechoka hapa najilazimisha tu”
“Jamani, ungekula hata matunda”
“Naona hata uvivu kuyaagiza”
Basi madam Oliva aliinuka na kutoka na baada ya muda kidogo alirudi na matunda na kumuwekea baba Angel mezani ili aweze kula,
“Asante sana, unaonekana ni mkarimu sana wewe”
Madam Oliva alitabasamu na kusema,
“Unajua maisha huwa yanatufundisha mambo mengi sana, nilikuwa napita hapa ila moyo ukaniuma hadi nimekuja kukuona, na nilipokuona nimehisi kuwa umechoka sana na hujala kitu ndiomana nikakuuliza”
“Nashukuru sana madam”
“Unakaribishwa muda wote baba Erick, shule zimefungwa leo kwahiyo nitakuwa huru muda mwingi sana. Siku ukiwa upo tu huna wa kuongea nae jua nipo”
“Aaaah madam nitakosaje wa kuongea nae!! Yupo mke wangu kipenzi ambaye huniliwaza wakati wote”
Kiukweli madam Oliva alihisi wivu kwa muda huu ila alijikaza tu na kusema,
“Hongera sana kwa kupata mke anayejua nini maana ya mume, ila huwa natamani sana ningeolewa maana mume wangu angepata kila kitu kutoka kwangu”
“Usikate tamaa, muda bado upo wa kutosha tu, usijali utaolewa madam”
“Umri umeenda jamani, yani saivi sina mvuto tena!”
Baba Angel alisimamisha kidogo kazi zake na kumuangalia madam Oliva kisha akamwambia,
“Nani anakuongopea kuwa huna mvuto tena!! Wewe ni mzuri sana madam, usisikilize maneno ya watu walioshindwa”
Kisha baba Angel aliendelea na kazi yake, ila kile kitu cha baba Angel kumuangalia kilimfanya madam Oliva ajihisi vyema sana katika moyo wake, kisha aliongea ongea nae na kumuaga pale huku akimuuliza,
“Jumatatu si utakuwa hapa ofisini?”
“Ndio nitakuwepo, hata kesho pia nitakuwepo ila mara nyingi Jumamosi huwa sikai sana”
“Oooh basi, tutawasiliana”
Kisha madam Oliva aliondoka na kumuacha baba Angel aendelee na kazi zake.
Kwakweli ingawa alipanga kwenda kwa mkwe wake ila aliona kuwa kazi zake zilihitaji muda kumaliziwa kwahiyo alikaa mpaka jioni kabisa ndio aliondoka nakurudi nyumbani kwake.

Leo usiku wakati wa kulala, kama kawaida Junior alikuwa chumbani kwa Vaileth na walianza kuongea mambo mbalimbali kwanza, ambapo leo Vaileth alimwambia Junior,
“Unajua mama na baba humu ndani wanapendana sana, hadi raha kuwaangalia. Natamani na sisi maisha yetu yawe hivyo!!”
“Usijali Vai, mimi na wewe tunapendana sana yani tunaweza tukawa zaidi yao”
“Yani nikawa nawaonea raha sana”
“Jamani mke wangu, ona raha na kwenye haya mapenzi yetu”
Basi Junior alianza kumpapasa pale Vaileth na mwisho wa siku kulala nae kawaida.
Ila leo asubuhi kulivyokucha tu, Vaileth ndio aliwahi kuamka ila simu ya Junior ilikuwa ikiita basi Vaileth aliisogelea na kukuta namba mpya akaipokea ile simu na kuiweka sikioni,
“Mpenzi, jamani mwenzio toka tumetoka kutoa ile mimba basi natokwa na dam utu hadi leo. Nakupigia simu hupokei, nashukuru leo umepokea, meseji zangu hujibu, ni kwanini unanifanyia hivi Junior?”
Kiukweli Vaileth alihisi kama moyo wake umekumbwa na mripuko vile, kisha alimshtua Junior na kumuwekea ile simu sikioni huku akimsikilizia amalize kuongea nayo,
“Nani wewe? Sikufahamu bhana”
Kisha Junior alikata ile simu na kumgeukia Vaileth na kumuangalia kwa muda, wakati huo Vaileth alikuwa kajiinamia huku akilia.

Kiukweli Vaileth alihisi kama moyo wake umekumbwa na mripuko vile, kisha alimshtua Junior na kumuwekea ile simu sikioni huku akimsikilizia amalize kuongea nayo,
“Nani wewe? Sikufahamu bhana”
Kisha Junior alikata ile simu na kumgeukia Vaileth na kumuangalia kwa muda, wakati huo Vaileth alikuwa kajiinamia huku akilia.
Basi Junior aliamua kumuuliza,
“Kwani umeongea na huyu mtu mke wangu?”
“Toka hapa, nani mke wako? Wewe Junior ni mchafu sana sikujua tu”
“Jamani Vai kwani tatizo liko wapi?”
“Hivi Junior wewe ndio wa kukaa na kuniongopea mimi? Unaniambia unanipenda kumbe unawanawake zako wengi tu, mpaka wengine umewapa mimba na kwenda kuzitoa? Haya sasa damu zinawatoka huko hadi leo”
“Sikia Vaileth, huyo mtu atakuwa amekosea namba”
“Aaaah kakosea na jina lako eeeh kusema kuwa Junior kumbe ni Junior mwingine. Hivi Junior unaniona mimi mtoto mdogo eeeh!”
Mara Vaileth alisikia akiitwa na mama Angel kwahiyo aliacha kuongea na Junior pale na kwenda kumsikiliza mama Angel,
“Jamani Vaileth siku hizi unachelewa sana kuamka sijui ni kwanini?”
“Samahani mama”
“Haya, asubuhi hii kuna mahali nataka kukuagiza maana kuna kitu nakihitaji mapema hii basi nenda kajiandae nikuagize”
Vaileth alienda kujiandaa na bila ya kuongea na Junior wala nini na alipomaliza tu alimwambia Junior,
“Na utoke chumbani kwangu, sitaki hata kukuona”
Halafu Vaileth alienda kuchukua maagizo kwa mama Angel na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 231

Vaileth alipofika alipoagizwa, wakati anasubiria alimuona kuna mwanamke ameshuka kwenye gari na kukutana na mwanamke mwingine pale walikumbatiana na kusalimiana kisha walikaa karibu na Vaileth ila hawakumtilia maanani, basi walianza kuongea pale,
“Ila mwenzangu mbona siku hizi upo hivyo yani kuna muda unakuwa na mawazo sana”
“Mwenzangu, yani sijui nikwambiaje, unajua sijawahi kumpenda mume wa mtu ila safari hii nampenda mume wa mtu balaa”
“Kwahiyo upo nae?”
“Mmmh sipo nae wala nini, yani huyo mume wa mtu mwenyewe anajifanya anampenda mke wake balaa ila na mimi nampenda sana”
“Sasa shoga yangu kama swala ni kumpenda mume wa mtu na hujui jinsi ya kumpata si ungeniambia mapema! Ila ana pesa?”
“Kheee yani ana pesa uchafu ila sio kwamba nahitaji pesa zake ila mimi ninachohitaji nilale nae hata mara moja tu”
“Aaaah mbona kazi rahisi hiyo shoga yangu, kumdaka mwanaume ni rahisi sana. Kwanza anaitwa nani?”
“Anaitwa Erick”
Hapo Vaileth alishtuka kwani hakujua ni Erick gani anazungumziwa ila alipatwa na hisia kama anayezungumziwa ni baba Angel, ila alishaletewa alichokifata ikabidi tu aondoke zake huku akitamani kufahamu zaidi kuhusu Erick anayetajwa mahali pale ni nani.
Vaileth alirudi nyumbani na kumpatia tu mama Angel alichomuagiza ila aliogopa kumwambia kuhusu wale wanawake ukizingatia hakujua ni Erick gani aliyekuwa akizungumziwa na wale wanawake.

Leo baba Angel alipokuwa ofisini na akikaribia kufunga ofisi yake kwani siku hii alitaka kuondoka mapema ili kwanza aende dukani akaelewane na Steve na kuangalia kama kuna uwezekano wa kwenda kwa mkwe wake, ila wakati anafunga ofisi tu alishangaa kumuona madam Oliva akiwa ameenda kumtembelea na kuanza kuongea nae,
“Ila ndio nilikuwa nafunga ujue”
“Kwani huwa unafunga ofisi yote!”
“Hapana, huwa nafunga ofisi yang utu na wengine wanaendelea na kazi kama kawaida hadi muda wa kufunga”
“Oooh sawa, sio tatizo basi nimekuja muda mzuri”
“Aaah sio muda mzuri huu sababu naondoka muda huu huu”
“Unaelekea wapi kwani”
“Kuna duka langu mahali ndio nataka niende huko”
“Basi, twende wote”
“Kheee kwani ndio ratiba yako ya leo”
“Hapana, ila nilikuwa nimeboreka na nilikuwa nahitaji mtu niongee ongee nae kidogo kwahiyo ndio nikaja huku ofisini kwako, kwahiyo ni vyema kama tukienda wote huko dukani kwako”
Basi baba Angel hakutaka kumkatalia kwani hawezi kujua kuwa pengine Oliva nae akapenda bidhaa za duka hilo na kununua.
Basi walitoka nje na kuingia kwenye gari ya baba Angel kwani madam Oliva alisema kuwa kwa siku hiyo hakwenda na gari na safari ilianza huku madam Oliva akiongea vitu mbalimbali na baba Angel,
“Unajua napenda sana vile unavyopendana na mke wako, mlianzia wapi nay eye hadi kufahamiana vizuri na kupendana hivyo”
“Unajua upendo mwingine ni mpaka mzoeane ila mimi jamani siku ya kwanza kabisa kumuona mke wangu nilimpenda ten asana, nakumbuka ilikuwa kidato cha pili”
“Kheee kidato cha pili? Mliweza vipi sasa kutengeneza mapenzi na kutengeneza shule?”
“Yani kulikuwa na vikwazo vingi sana, ila Mungu ni mwema kwani mwisho wa siku nikampata mke wangu na kumuoa. Kwakweli huyu ni mwanamke wa ndoto zangu, na kama ningeoa mwanamke mwingine mbali na yeye basi huyo mwanamke mwingine ningemuacha na kumuoa yeye nampenda sana mke wangu”
“Kheee hadi raha jamani, natamani mimi. Natamani sana hata ningepata mpenzi tu wa kuniambia kuwa mimi ni mwanamke wa ndoto zake, napenda sana kupendwa jamani kwakweli mwanamke mwenzangu huyo ana bahati sana, hivi anatambua kweli?”
“Anatambua ndio, na uzuri ni kuwa hata yeye ananipenda sana”
“Ila katika maisha yako hujawahi kufikiria kuwa na mwanamke mwingine?”
“Mwingine wa nini sasa wakati mke wangu ananitosheleza, sijawahi kufikiria na wala siwezi kufikiria hilo maana mke wangu ndio maisha yangu”
“Duh! Watu wanasema hapa duniani wanawake ni wengi kuliko wanaume, ndiomana wanaume wanakuwa na mahusiano na wanawake wengi wengi ili wasiwepo wanawake watakaokosa wanaume. Je wewe unasemaje kuhusu hiyo dhana ya wanawake wapo wengi kuliko wanaume?”
“Hiyo dhana mimi naona ni dhana ya kujitetea tu ili mtu aendelee kufanya uhuni, hakuna cha wanawake wengi kuliko wanaume wala nini sababu kama ni hivyo kwanini ukifatilia asilimia kubwa ya wanawake utasikia nina mtu wangu halafu asilimia kubwa ya wanaume utasikia nimeachwa au sina mtu! Tatizo la wanawake wengi wanachagua sana, yani kuna wanaume wengine hawapati kabisa wanawake sababu tu ya muonekano wao, au sababu hawana pesa ya kutosha au sababu ni walemavu yani wanawake mnachagua sana. Mimi naamini Mungu katuumba wote kwa idadi kamili, kwahiyo yule ni mke wangu na kama nikiamua kuwa na mwanamke mwingine sio kwa kigezo mpo wengi hapana ila ni tamaa tu. Ila mimi naamini na nitaendelea kuamini hivi, tupo kwenye idadi sawa kabisa”
“Mmmmh kwahiyo wewe hufikiriii kabisa kuchepuka?”
“Nakwambia nichepuke ili iweje wakati mke wangu yupo!”
“Mfano mkeo kapatwa na ulemavu je!”
“Ningempenda na ulemavu wake kwani mimi upendo wangu kwa mke wangu upo moyoni na sio muonekano wake, yani yeye akiwa mwembamba au bonge bado nitampenda ten asana tu, akiwa mweusi au mweupe bado nitampenda, akiwa mfupi au mrefu bado nitampenda sana tu. Upendo wangu kwake upo moyoni, vingine hivi ni ziada tu”
“Hivi wanaume kama wewe Erick wapo kweli kwenye dunia hii?”
Baba Angel alicheka na kusema,
“Kwani mimi naongea toka mbinguni!”
Walikuwa wamefika dukani, ila kiukweli madam Oliva alizidi kumpenda baba Angel yani alizidi kuvutiwa nae kila alipokuwa akiongea nae, alimtamani sana.
 
SEHEMU YA 232


Baba Angel na Oliva waliingia dukani, basi Oliva alikuwa akiangalia angalia bidhaa za pale huku baba Angel akienda kuongea na Steve kuhusu tukio la Sia.
“Kwahiyo ilikuwaje Steve maana ule ujumbe sijauelewa hata kidogo”
Basi Steve alianza kumueleza vile ilivyokuwa mpaka Sia alipochukua hiyo pesa na kuondoka nayo,
“Yule mwanamke ana wazimu”
“Ni kweli ana wazimu hata sijui cha kufanya nae”
“Ila akija tena mwambie kuwa Erick anasema nahisi umesahau akili zake za zamani. Maana nahisi yule mwanamke kanisahau ila mimi ni chizi zaidi yake, nikiamua kumfanyia uchizi atalia kwakweli, mwambie asitake kunirudisha nilikotoka kabisa, hili ni duka langu na hizo ni pesa zangu na huo ujinga wake iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho maana sitarajii tena kuusikia. Sitamfatilia kwasasa wala nini andika tu kwenye kitabu kuwa hizo pesa tumeingia hasara ila kitu kama hiki asifikirie kukifanya tena maana nitamfanyia kitu kibaya, mimi huwa nacheka ila nina roho mbaya sana. Ukimuona Sia mkanye juu ya hilo”
Kisha baba Angel akapitia pitia vitu vya duka lake hili na vitabu vitabu vya pale na aliporidhika sasa alimfata Oliva ili waondoke ambapo bado Oliva alikuwa akiangalia bidhaa za duka hilo na kwa wakai huo alishanunua nguo kama mbili, basi alimwambia baba Angel,
“Kwakweli duka lako lina bidhaa nzuri sana nimelipenda bure, hadi nimechukua nguo”
“Oooh vizuri sana, umeona zitamfaa mwanao eeh!”
Madam Oliva alitabasamu kisha aliongoza hadi kwenye gari la baba Angel na kupanda, basi baba Angel alipanda pia na kumwambia,
“Kwasasa nahitaji kwenda kwa mama mkwe wangu ila kama muda umeenda hivi!! Itabidi tu nirudi nyumbani, je nikuache wapi au unataka kwenda nyumbani kwangu?”
“Ni kweli nahitaji kufika nyumbani kwako, nahitaji kuona mke wako ila hatonipiga kweli?”
“Aaah akupige kwa lipi jamani! Kwani umemkosea nini?”
“Kuna wanawake huwa wakiona mumewe kaongozana na mwanamke mwingine basi huwa wanahisia mbaya”
“Oooh hawajiamini hao ila mke wangu anajiamini, hawezi kuwa na hisia mbaya na wewe ila kama una shughuli zingine basi useme nikuache wapi?”
“Hamna sina shughuli yoyote, nifikishe tu kwako”
Basi baba Angel alienda na madam Oliva hadi nyumbani kwake.

Muda huu mama Angel alikuwa amekaa sebleni na kwavile shule zilikuwa zimefungwa basi Erica alienda kwa mama yake na kumtaka mama yake aanze kumsuka suka nywele zake yani azitonee maana Erica alikuwa akinyoa ila kipindi hiko alitamani kusuka,
“Mama, na mimi nataka kuwa na nywele ndefu kama za dada Angel si zitakuwa eti eeeh!”
“Zitakuwa ndio, ila mimi nitakuwa hata sikusuki vizuri, nitakupeleka saluni huko mwanangu wakakusuke vizuri upendeze”
“Nitafurahi sana mama”
Basi mama Angel alikuwa akijaribu pale kuzisuka suka nywele za Erica, na muda huo huo baba Angel pamoja na madam Oliva waliwasili pale nyumbani na kumkuta mkewe wakiwa sebleni akijaribu kumsuka suka Erica, basi waliwasalimia pale na baba Angel alikaa kwaajili ya utambulisho,
“Samahani mke wangu, huyu anaitwa madam Oliva, ndio mwalimu wa nidhamu shuleni kwakina Erick. Halafu madam, huyu ndio mke wangu, kwahiyo mama Erick ndio huyu sasa”
“Ooooh nimefurahi kumuona”
Basi madm Oliva aliinuka na kupeana mikono pale na mama Angel, kisha alikaa na kuanza kuongea mawili matatu, basi akamwambia Erica aende kumwambia Vaielth alete juisi waweze kunywa na mgeni wao yule.
Baada ya muda Erica alirudi na madam Oliva akawa anamwambia mama Angel,
“Jamani unahangaika na vinywele vifupi hivyo vya mtoto!”
“Yani acha tu, anataka urembo, nifanyeje sasa”
“Mimi nina saluni yangu kwaajili ya watoto na wakibwa, yani hizo nywele wanamshika vizuri tu, atasukwa rasta na kupendeza sana huyo”
Erica aliposikia alifurahi sana na kumgeukia mama yake,
“Mama, nahitaji kusuka rasta”
Basi mama Angel alicheka sana na kumwambia yule madam,
“Hakuna tatizo, basi ataletwa na baba yake”
Baba Angel nae akadakia,
“Lini tena jamani, mimi nipo na kazi nyingi sana”
Basi madam Oliva akadakia,
“Hata msijali, Jumatatu nitakuja kumchukua hapa na kumpeleka huko saluni halafu nitamrudisha au nikiona mbali huku nitamrudisha ofisini kwako baba Erick ili urudi nae nyumbani maana saluni kwangu sio mbali na ofisini kwako”
“Kama ndio hivyo sawa, na wewe Erica unataka urembo wa nini si uwe tu kama kaka yako!”
“Jamani baba, nataka kuwa tofauti. Mimi ni mtoto wa kike na Erick ni mtoto wa kiume”
Basi Vaileth alileta juice na kuwamiminia pale, ila alipomuona madam Oliva alishtuka kiasi sema hakutaka kuonyesha mshtuko wake, basi alimimina tu ile juisi na kuwakaribisha halafu akaenda kuendelea na shughuli zake, ila baba Angel alisema kuwa anahitaji kupumzika kwa muda huo na madam nae aliaga ila kwavile hakuwa na usafiri basi baba Angel alimuita Erick ili aongozane na Erica waweze kumsindikiza yule madam kwa muda ule nao walifanya vile na kuanza kumsindikiza ila mama yao aliwaambia kuwa wasifike mbali.
Pale nyumbani baba Angel aliamua muda huo kwenda kuoga tu na kwenda kulala kwani alijihisi uchovu sana, basi Vaileth alienda sebleni kutoa vile vikombe vya juisi na kumuuliza mama Angel ambaye bado alikuwa pale sebleni,
“Kwani yule madam unamjua vizuri mama?”
“Hapana, ndio leo siku ya kwanza kumuona”
“Oooh nilidhani unamfahamu”
“Kwani kuna nini?”
“Hakuna kitu mama, nimeuliza tu”
Bado Vaileth aliogopa kusema, kwahiyo alitoa tu vile vyombo na kurudi jikoni kusafisha vyombo huku mama Angel nae akienda chumbani.
 
SEHEMU YA 233

Basi Erick na Erica walimsindikiza madam Oliva hadi kwenye stendi ya daladala huku wakiongea nae mambo mbalimbali tu, na madam aliendelea kumsisitiza Erica kuwa ataenda kumchukua Jumatatu kama alivyosema. Basi hadi yule madam alipanda daladala ndipo na wao wakaanza kurudi nyumbani huku wakiongea,
“Jamani leo bahati hii! Sijui baba kafikiria nini kusema tumsindikize huyu madam!”
“Yanileo tunaweza kuangalia vizuri mandhari ya sehemu mbalimbali ilivyo, hivi wewe huchokagi kukaa ndani Erick! Mimi nachoka jamani, natamani mama angekuwa ananiruhusu nizunguke kila sehemu ninayoitaka”
Basi njiani karibia na stendi waliona watu wengi wamesimama wakiangalia kitu, ikabidi na wao waende kuangalia walikuta kuna watu wakitangaza vitu vynye madhara na dawa za kutumia,
“Mayai hayo ya kisasa mnakula ila hamjui ni sumu katika miili yenu, leo tutawaonyesha jinsi sumu kwenye yai la kisasa inavyofanya kazi, soda hizo ni sumu kali sana, hayo mafuta ya kupikia mnayotumia ni sumu, hizo soseji mnazokula ni sumu, hizo permpers mnazowazalisha watoto ni sumu na zina madhara makubwa sana, hizo pedi mnazotumia dada zetu zina madhara makubwa sana, leo tutawaonyehs jinsi sumu inavyoingia mwilini na namna ya kuitoa sumu hiyo”
Kwakweli Erick na Erica walikuwa wakishangaa sana, maana yule aliyetangaza alisema karibia kila kitu ni sumu na kuwafanya wabaki pale kushangaa tu mara Erica akavutwa bega, alipogeuka nyuma alimuona mtu anayemfahamu ambapo alimuona Bahati basi akamshtua Erick ambapo walisogea kidogo na Bahati akawasalimia kisha akawaambia,
“Nyie mmesimama kuwaangalia hao, wengi wao ni matapeli, msijisumbue wala nini”
“Matapeli kivipi? Mbona wanasema vitu vya ukweli?”
“Ndio wanasema vitu vingine vya ukweli ila kwa njia zisizo na ukweli, msiwasikilize mtaharibu fikra zenu. Kwanza nyie mkiwasikiliza mtajiona mmekula sumu tupu na kununua dawa zao ambazo hamna kitu zitafanya kwenye miili yenu zaidi zaidi mtaharisha tu basi”
“Wewe umewajulia wapi?”
“Mama yangu ni mnene, aliwasikia hawa wakitangaza sumu na dawa mbalimbali, basi walitangaza na dawa za kupunguza mwili na mama alinunua, ila nini kilitokea aliharisha tu siku nzima na hakuna kupungua mwili wala nini”
Erica na Erick walibaki wakimuangalia kisha akasema,
“Kwani mnaenda wapi muda huu?”
“Tunarudi nyumbani”
“Basin i vyema nikapafahamu hata nyumbani kwenu”
Erica alianzisha safari ila Erick hakupenda kabisa kwani alimuhisi Bahati kumnyemelea mdogo wake na hakupenda kabisa kile kitu.
Basi walifika hadi kwakina Erica ila Bahati hakuingia ndani ila aliwaahidi tu kuwa ipo siku ataenda kuwasalimia.

Mama Angel alichukia sana kwa ambavyo watoto wamechelewa kurudi, na moja kwa moja kwenda chumbani na kumuamsha mume wake,
“Hivi leo kitu gani kimekutuma uwaambie wakina Erick wamsindikize yule mgeni!”
“Kwani bado hawajarudi! Nimechoka sana mama Angel, niache nipumzike”
“Unapumzikaje na watoto hawajarudi”
“Hapo kidogo palimshtua baba Angel na kumfanya akae kwanza, na kusema,
“Jamani, wamepitia wapi hawa watoto?”
“Mimi sijui ila hawajarudi na kumbuka niliwaambia wawahi”
“Ila mke wangu naamini watarudi tu”
“Watarudi muda gani?”
“Kwahiyo unataka niende kuwatafuta kweli jamani mama Angel?”
Mama Angel alikaa kimya kidogo na kurudi sebleni, baada ya muda kidogo Erick na Erica walirudi kwakweli mama Angel alikuwa na hasira nao kiasi kwamba hakuwauliza kuwa wamechelewea wapi wala nini zaidi zaidi aliwavuta na kuanza kuwatandika na fagio kiasi cha baba yao kufika na kuwaamulia pale kupigwa kwahiyo Erica na Erica walikimbilia tu vyumbani kwao.
Basi baba Angel alimchukua mke wake na kwenda nae chumbani kuongea nae,
“Mke wangu, watoto hawafundishwi hivyo”
“Sitaki mtu wa kunielekeza namna ya kufundisha watoto wangu”
“Mmmmh haya mke wangu, ngoja mimi niendelee kupumzika ila usiende kuwapiga tena watoto”
Basi baba Angel aliendelea kulala tu.

Kesho yake jioni, familia nzima ilikuwa nyumbani baada ya kufanya ibada kwa siku hiyo kwahiyo muda huu walikuwa wametulia tu nyumbani ila kwa upande wa Junior hakuwa na raha kabisa kwani tangu alipogombana na Vaileth basi Vaileth hakutaka kabisa kulala nae wala hakumuhitaji tena aende chumbani kwake kwani muda wote alifunga mlango wake kwahiyo Junior alikuwa hafunguliwi mlango.
Basi muda huu wakati wamekaa wote, baba Angel aliwaambia pale,
“Wanafunzi wamefunga shule, ila napenda wote humu ndani mchague sehemu ambayo tutaenda kutembelea kwa kipindi hiki, basi Vaileth akasema
“Jamani mimi naomba twende ufukweni maana sijawahi kutembelea huko”
Basi wote wakacheka sana kwani walikuwa wakiona ufukweni ni kitu cha kawaida kabisa na wao walitaka kitu kingine, basi Erick akasema,
“Bora twende mbugani tukaangalie wanyama”
Mara simu ya baba Angel ikaita na kumfanya aipokee kwani mpigaji alikuwa ni mama yake,
“Kesho nitakuja ofisini kwako maana nina maongezi na wewe”
“Sawa, hakuna tatizo”
Baada ya kuongea nayo aliwaangalia wanae sasa na kuwaambia,
“Jamani, hatujafika muafaka sasa ni mbugani au ufukweni?”
Wote walisema mbugani kasoro Vaileth tu aliyedai ufukweni basi baba Angel akasema,
“Jamani, mbugani tutaenda siku nyingine ila kwa siku hiyo twendeni ufukweni ili Vaileth nae afurahi”
Kisha mama Angel akasema,
“Hivi katika hizo safari zenu mnanifikiria na mimi jamani! Naona mnapanga tu mara mbugani sijui ufukweni, na mimi naendaje na huyu Ester? Au baba Angel utawapeleka tu kisha mimi na wewe na Ester tutashinda nyumbani hadi muda wao wa kurudi”
“Aaah mama Angel kwanini nijisumbue hivyo! Erick na Junior wanaweza kuendesha gari, basi nitawapatia gari moja na pesa na kuwaelekeza ufukwe wa kwenda halafu wataenda huko na kurudi hapa nyumbani halafu mimi na wewe tutashinda hapa nyumbani”
“Oooh hapo sawa mume wangu, halafu Vaileth utafanya kazi ya kuangalia wadogo zako hawa”
Vaileth aliitikia tu, laiti kama angejua Junior huwa anamuita Vaileth mke wangu hata asingejisumbua kumwambia Vaileth kuwa aangalie wadogo zake maana kuna mume wake pale, kuna shemeji yake na wifi yake ila hakujua ukweli tu.
Basi kwa siku ya leo familia hii ilifurahi sana na kupanga siku ya hiyo safari, kiukweli walikuwa na furaha hasa watoto kwani waliona rah asana kama wataenda kwenye hiyo safari bila ya wazazi wao kwani huwa wanaona kuwa wanawafatilia sana.
Siku hii waliongea ongea kwa pamoja, na muda wa kulala ulipofika, kila mmoja alienda zake kwenye chumba chake kulala.
 
SEHEMU YA 234

Asubuhi kwenye mida ya saa tatu hivi, madam Oliva alifika pale nyumbani kwa ahadi yake ya kumchukua Erica ili ampeleke saluni na uzuri ni kuwa alimkuta Erica ameshajiandaa kwahiyo akaaga pale na kuondoka nae.
Siku hiyo alikuwa na usafiri kwahiyo walitembea kwenye gari la huyo madam huku akiongea na Erica mambo mbalimbali,
“Erica, kitu gani cha kutafuna tafuna huwa unapenda?”
“Napenda sana chokleti”
“Nadhani baba huwa anakuletea kila siku!”
“Alikuwa ananiletea ndio ila toka mama kamleta mdogo wangu imekuwa basi tena, baba haniletei tena yani haniletei kabisa”
“Oooh basi mimi nitakuwa nakuletea”
Muda huo akapita nae dukani na kumnunuliza chokleti ambapo Erica alifurahi sana kununuliwa ile chokleti na madam Oliva. Basi walirudi kwenye gari huku madam Oliva akiendelea kumuuliza maswali mbalimbali Erica kisha akamwambia,
“Mimi na wewe Erica tutakuwa marafiki, tutakuwa tunaambiana vitu vingi sana ila itakuwa siri yetu”
“Sawa madam”
Basi madam akampa mkono Erica kama ishara ya urafiki wao na kumfanya Erica afurahi sana.

Leo Angel aliachiwa simu na bibi yake halafu bibi yake alitoka, kutokana na Samir kumwambia kuwa ana hamu sana ya kumuona ilibidi amtumie ujumbe kuwa siku hii bibi yake katoka,
“Oooh Angel unaniambia ukweli? Yani katoka na kukuachia simu!”
“Ndio, nadhani kajisahau”
“Basi jiandae, nakuja hapo kukuchukua ili twende mahali Angel, nahitaji tuwe mahali wawili tu”
“Mmmh wapi hapo Samir lakini? Bibi je akirudi?”
“Atakuwa kaenda kwenye kikundi chao maana hata bibi yangu nyumbani nimeulizia na kuambiwa hivyo na huko huwa wanachelewa sana kurudi, nakuomba Angel jiandae”
Basi Angel alijiandaa haraka haraka , na kweli baada ya muda tu Samir alikuwa amefika mahali pale na kutoka nje na Angel.
Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao.

Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao.
Kwakweli kile kibao kilimuingia Samir, kiasi kwamba aliamua kukimbia tu kwani angeendelea kusimama mahali hapo basi angepigwa tena na huyu bibi na alimtambua vizuri mambo yake, hivyobasi alikimbia, basi bibi alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, kwakwlei kwa wakati huo Angel alijiandaa kupigwa tu kwani alijua wazi kuwa atapigwa sana na bibi yake huyu, ila walipoingia ndani bibi alimkalisha Angel chini na kumuuliza,
“Una uhakika kuwa huyo Samir anakupenda?”
Erica alinyamaza kimya tu huku akiangalia chini kwa aibu, kisha bibi yake akamwambia tena,
“Mjukuu wangu, huyo Samir hakupendi wala nini hebu jiulize anayekupenda kweli anaweza kukimbia sababu ya kupigwa kibao kimoja? Mtu akikupenda huwa tayari kwa lolote lile, kuna kijana mmoja aliitwa Bahati basi alikuwa akimpenda dada mmoja hivi na kumfatilia sana, yani yule kijana alikuwa tayari hata kumwagiwa maji ya moto sababu ya mwanamke, yule kijana aliwahi kukaa rumande sababu ya mwanamke, hakuwa na kosa ila alikaa rumande sababu ya upendo wake tu kwa mwanamke”
“Kheee bibi, sasa kwanini aliwekwa rumande?”
“Ndugu wa mwanamke hawakumtaka, kwahiyo alivyokuwa hataki kuondoka hadi aonane na mwanamke ndipo walipomuweka rumande ila badae walimuhurumia sana na kumuachia huru. Kijana huyo alikuwa akihudumia familia ya mwanamke kama familia yake akiwaletea kuku na samaki, kijana huyo alikuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine ambaye huyo dada alimzaa kabla, yani huyo kijana alikuwa na upendo wa dhati tena upendo mkubwa sana”
“Bibi, vijana kama hao wapo?”
“Wapo ndio, msubirie wa kwako ila sio huyu Samir anakuongopea tu, kibao kimoja kakimbia vile, hata hajali kuwa nitakupiga wewe au nini! Nakwambia ingekuwa huyo Bahati angetaka apigwe yeye badala yako, usimfikirire Samir mjukuu wangu hakupendi wala nini. Haya nipe na simu nikaiweke”
Basi Angel aliitoa ile simu na kumpa bibi yake ili aiweke, kisha bibi aliinuka yani Angel kwakweli hakuamini kama kapona kipigo toka kwa bibi yake maana alihisi muda huo angepigwa vibaya sana ila hakupigwa wala nini zaidi ya kuambiwa kuwa Samir hafai kabisa kwake.

Basi madam Oliva alifika na Erica saluni na kumuweka pale huku akiwaelekeza wasusi namna ya kumsuka nao walianza jambo lile, huku muda huo madam akiwaaga kuwa anaenda kwanza kuangalia chuo chake, kisha alimuuliza Erica,
“Nikirudi nikuletee nini? Maana leo itabidi ule huku”
“Chochote tu”
“Sawa, nitakuletea chips kuku basi”
“Sawa, asante”
Erica alitabasamu halafu madam Oliva alitoka. Alipotoka tu wale wasusi waliokuwa wakimsuka Erica walianza maongezi, kwanza kabisa walimuuliza Erica,
“Huyu madam ni ndugu yako?”
“Hapana, ila ni mwalimu wa kaka yangu”
“Ooooh sawa”
Kisha mwenzie akasema,
“Jamani, huyu madam leo alivyo na furaha utafikiri kitu gani. Halafu naona huyu mtoto kampenda sana”
“Inaonekana, maana sio kawaida yake. Asubuhi kapita kuwa anamleta mtoto tumsuke, alivyokuwa anatuambia kuhusu huyo mtoto basi nikajua mtoto mdogo sana kumbe binti tu. Sijui muusuke taratibu, msimsumbue, msimvute nywele, mpeni anachotaka”
Wakaanza kucheka huku mmoja akisema,
“Kwani jamani yule madam ana mume yule?”
“Mume hana, eti anasema yeye yupo kutafuta pesa tu hana shida na mume wala shida ya kuolewa”
“Ila ana mpenzi au?”
“Yani kwa kifupi yule madam hana mpango kabisa na wanaume, yani yeye anasema anawaza pesa tu ndio ya muhimu kwake.”
“Na kama pesa ni anaitafuta kweli, maana yule kaajiriwa halafu ana biashara zake. Ana chuo chake cha kompyuta, ana hii saluni na ana shule yake ya kujifunza ushonaji”
“Kweli yupo vizuri ila kuna umuhimu wa kuwa na mwanaume katika maisha, mtu anaishi vipi jamani bila mwanaume! Tamaa zake za kimwili anazimaliza vipi?”
“Hapo sasa, au mwenzetu hana tamaa za kimwili jamani! Kuna mambo mengine ndiomana mtu unakuwa na hasira muda wote, kwanza toka nimfahamu huyu madam ndio leo namuona anacheka”
Mwingine akadakia,
“Usikute kashaonja tamu ya asali”
Mmoja akawanyamazisha wenzie,
“Badilisheni mazungumzo jamani, kumbukeni mnayemsema katuajiri na anafanya turinge mjini”
“Kheee bwana eeeh anasemwa raisi sembuse yeye!!”
Basi wakacheka na kuendelea na maongezi mengine.
 
SEHEMU YA 235

Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa muda huo, akaja mama yake kama ambavyo aliongea nae kwenye simu jana yake basi alimkaribisha na kumsalimia pale kisha kuanza maongezi nae ambapo mama yake alianza kuongea,
“Mwanangu sikia, naomba niache niongee kwanza halafu zamu yako ikifika ndio utasema yani usinikatishe wakati naongea”
“Sawa mama”
“Ni hivi, Sia alinipigia simu kuwa mtoto anaumwa, kwakweli na mimi ni mama halafu na mimi nimepitia mazingira ya kulea mtoto bila ya baba kwahiyo najua uchungu wake na ninajua ni hali gani inakuwa. Nimekulea wewe, nimehangaika na wewe kipindi hiko baba yako hana hata habari hata wewe mwenyewe unakumbuka wazi kuwa baba yako umefahamiana nae ukiwa mkubwa kabisa unajitambua tena ukiwa unatangatanga huko baada ya kufukuzwa shule. Kiukweli nilipatwa na uchungu kusikia mtoto mdogo anaumwa na mama yake hana pesa, ilibidi niende. Nilipofika pale nilimkuta mtoto kalala, yani nilienda kwa kuelekezwa na Sia mwenyewe, na nilivyofika alimuamsha mtoto aje anisalimie maana kuna zahanati alimpeleka na alipatiwa dawa ila aliacha deni tu pale zahanati, ilibidi nitoe pesa aende kulipa hilo deni maana afya ya mtoto ni ya muhimu zaidi ya vyote. Kingine ni kuhusu yule mtoto mdogo Elly, kwakweli kwa jinsi nilivyokuwa namuangalia ananikumbusha zamani kabisa kipindi cha udogo wako, wewe ulikuwa ni mtoto mpole na mchangamfu basi ndio alivyo yule Elly, mwanangu mimi naomba jambo moja tu hata kama Sia humpendi basi mpende yule mtoto, nakuomba ukubali kupima DNA na Elly”
“Umemaliza mama?”
“Ndio, nimemaliza nakusikiliza wewe sasa”
“Kwanza kabisa siwezi kwenda kupima DNA na Elly, nikifanya hivyo inamaana sijiamini. Pili ngoja nikuulize mama, inamaana Ellyn i mwanangu halafu Erick sio mwanangu?”
“Mmmh mimi sijasema Erick sio mwanao, kwanza itakuwaje Erick asiwe mwanao jamani! Erick si kazaliwa na mkeo, sasa itakuwaje sio mwanao? Ninachohitaji mimi ni Elly kupata haki sawa na wenzie wote, una watoto pale kuna Angel, Erick, Erica, Ester na sasa Elly awepo kwenye familia”
“Kwa misingi ipi mama?”
“Ellyn i mtoto wako ambaye umezaa na Sia”
“Mama, mimi ndio mwanaume ambaye Sia anadai amezaa nae, ila mimi nakataa mbele ya vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kuwa sijazaa na Sia mimi.”
“Ila mwanangu unakumbuka tabia zako vizuri wewe, ni wadada wangapi waliokuwa wakilalamika kwangu kuwa wana mimba zako sembuse Sia ambae muda wote alikuwa na wewe! Je kama akitokea mdada mwingine na mtoto utakataa kuwa sio mwanao wakati ulikuwa muhuni sana wewe!”
“Ni kweli mama, yani siwezi kukataa kuwa sikuwa muhuni, kama uhuni nimeufanya sana tu, ila niliufanya sababu ya stress nilikuwa siwezi kumpata mwanamke nimpendaye ndiomana nilikuwa nafanya ule uhuni, kuna wanawake wakija kusema Erick tulizaa na wewe naweza nikakubali ila sio Sia, unajua nini Sian i mwanamke ambaye alikuwa akiniganda sana. Na toka nimetoka Afrika kusini na kuanza kuishi na Erica kw aupendo ile ikawa mwisho wa mimi na Sia yani sikuwa na ukaribu nae tena, alikuwa akifanya kila mbinu lakini ilishindikana kuwa na mimi, halafu leo useme Sia kazaa na mimi tena mtoto ambaye ni umri sawa na watoto niliozaa na Erica, hapana kwakweli Sian i muongo tena muongo namba moja. Kuna mwanamke mmoja angesema hivyo ningesema labda maana kipindi kile Erica alinikatalia kabisa hadi ndoa na mimi ni mwanaume ila yule mwanamke alikuwa akijua kila kitu kuhusu mimi na Erica hadi siku namuacha nikamwambia mimi na wewe basi maana nimerudi kwa Erica wangu, yule mwanamke alikubali kwa roho moja na hajawahi kunitafuta tena hadi leo kwani anajua kuwa nina familia yangu ila kwanini Sia anakuwa hivi jamani! Kwani wanaume wameisha duniani au kitu gani?”
Mama yake akapumua kidogo na kusema,
“Haya, mfano huyo mwanamke aseme pia ana mtoto wako utasemaje?”
“Haiwezekani sababu yule mwanamke nilikuwa nae na aliweka kijiti cha miaka mitatu, na wakati niko nae ilikuwa ni mwaka wa pili, mama katika maisha yangu kitu mimba nilikuwa nakihofia sana na kukuheshimu kwani nilitambua wazi kuwa Erica akiona nina watoto wengi basi hatonikubali, kwahiyo nilikuwa makini sana”
“Sawa mwanangu ila mimi hoja yangu bado ni moja tu, ukapime DNA na Elly”
“Mama, tafadhari hilo swala kwangu halikubaliki. Yani hiyo kitu haipo, labda ukapime wewe na ukikuta mnafanana basi jua kuwa ni mwanao na sio mwanangu sababu mimi sijazaa na Sia”
“Sasa hayo matusi mwanangu, yani unanitusi mama yako. Inamaana mimi nimezaa na Sia? Yani wewe mtoto loh! Mitoto mingine tunabebaga change tu tumboni”
Kisha mama yake akanyanyuka na kuondoka zake, inaonyesha alikuwa amekasirika ila baba Angel wala hakujali zaidi zaidi aliendelea na kazi zake tu.

Madam Oliva alimpelekea Erica kama alivyoahidi na Erica alikula pale, kisha walipomaliza kumsuka alimwambia kuwa anampeleka ofisini kwa baba yake ili aondoke na baba yake maana yeye alidai kuwa kuna kazi anataka kuifanya.
Basi aliondoka na Erica pale huku akimsifia kuwa kapendeza sana hadi kabadilika, basi Erica alikuwa akifurahi sana kuambiwa vile, yule madam nae alikuwa akifurahi kuona Erica anafurahi ndipo Erica alipomwambia,
“Madam, wale wafanyakazi wako mule wanafki”
“Wamefanyaje tena?”
Erica alianza kumueleza moja baada ya jingine ambalo wafanyakazi wale walikuwa wakisema na kuelekeza kabisa yupi kasema lipi na yupi kaongea lingine, kiukweli yule madam alichukia sana,
“Yani badala ya kufanya kazi wanafanya kazi ya kunisema!”
“Tena mwenzao alipowakatisha wakasema anasemwa raisi sembuse wewe!”
Yani madam Oliva alizidi kuchukia kwakweli na kuona kuwa wafanyakazi wake wabaya, basi alienda na Erica hadi ofisini kwa baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa amekaa tu maana hata yeye kichwa chake kilikuwa kimevurugwa ila alipomuona binti yake alimsifia sana kuwa kapendeza kisha akamshukuru madam Oliva na kumuuliza pale,
“Eeeeh ndio pesa ngapi hapo?”
“Aaaah hii leo nimempa ofa”
“Kumbe ofa!! Jamani madam kwanini lakini!”
“Hamna jamani, hii ni ahadi yangu kwake, na sio kwa leo tu kwani siku zote akiitaji kusuka basi nitampeleka saluni kwangu na atasuka bure kabisa”
Basi baba Angel alicheka tu, kwavile hata yeye alichoka aliamua kuondoka kwahiyo aliagana na madam Oliva halafu yeye kuelekea kwake huku madam akirudi kwenye saluni yake.
Basi Erica kama kawaida alianza kumsimulia na baba yake maneno ambayo wale wadada wa saluni walivyokuwa wakiongea na jinsi na yeye alivyomueleza madam Oliva,
“Aaah mwanangu, unajua utakuwa umewafanya hao wadada wafukuzwe kazi!!”
“Ila baba, mimi sijasema kwa ubaya, nimesema tu ili madam Oliva ajue kuwa wafanyakazi wake ni watu wa aina gani!”
“Mmmh ila Erica mambo yako jamani!”
Baba Angel alicheka na kutikisa kichw atu huku wakielekea nyumbani.
Walipofika nyumbani, kila mtu alikuwa akimsifia Erica kuwa kapendeza sana na kumfanya hata yeye afurahie sana zile sifa alizokuwa anapewa.
Basi waliongea ongea kidogo pale halafu Erica alienda chumbani kwake halafu mama yake alimfata na kumuuliza,
“Eeeh Erica, nipe habari za huko”
Erica kama kawaida alimuelezea kila kitu yani hakuacha hata kimoja, kisha akamwambia,
“Wale wasusi wanasema madam yupo kutafuta hela ila kapewa hela na baba kaikataa”
“Hela ya nini?”
“Si ya kunisuka mimi, eti kasema ni ofa”
“Kheee kumbe!!”
“Ndio mama, kwahiyo nimesukwa bure”
“Haya sawa mwanangu, mimi nashukuru kwa ujumbe”
Mama Angel alijua kuwa mwanae lazima atamwambia kila kitu, sababu ya kumuuliza ni kujiridhisha kuwa madam Oliva sio mtu mbaya katika maisha yao, na kwa yale maongezi ya mwanae hakuona ubaya wa madam huyo sababu ameambiwa kuwa huyo madam yupo kwaajili ya kutafuta pesa tu.
 
SEHEMU YA 236

Basi usiku wa siku hii, baba Angel aliongea na watoto wake maana Erica alienda kuomba kuwa hiyo safari ya ufukweni iwe kesho, na kwavile alijihisi uchovu sana akaona hakuna tatizo kwahiyo aliwaambia tu kuwa kesho yake wataenda huko ufukweni kutembea, ila ilikuwa nu furaha kubwa. Basi siku hiyo walilala huku wakiwaza uhuru ambao kesho yake watakuwa nao.
Basi kulipokucha, baada ya kazi za hapa na pale ndio walienda kujiandaa sasa na walipokuwa tayari ndio walienda kuchukua ruhusa mapema naye aliwaruhusu na kuwapa pesa kwaajili ya matumizi ya huko watakapokuwa kutembea ila baba yao aliwaambia,
“Ila kule ni kuzuri sana mwisho wa wiki, sema leo siku ya kawaida mtakuta kumepooza sana”
“Aaaah baba, sisi hatuna tatizo ni bora tukashuhudie maji tu”
Basi akawaruhusu na wao wakaondoka kisha pale nyumbani alibaki na mkewe tu huku wakiongea na kupanga mambo mbalimbali.
Muda huu mama Angel ndio alikuwa na simu ya mume wake, basi ujumbe mara ukaingia kwenye simu ya mume wake,
“Baba Elly, mbona unafanya hivyo?”
Moja kwa moja mama Angel alitambua kuwa aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni Sia, basi alimuangalia mumewe na kumuuliza,
“Eeeeh mume wangu huyu Sia ana ajenda gani za kukuita baba Elly?”
Akampa simu mumewe ambapo naye aliangalia ule ujumbe na kumwambia mke wake,
“Aaaah si mjinga huyu, hutambui hilo mke wangu. Naomba usifatilie mambo ya huyu”
“Ila amekazana sana mume wangu?”
“Achana nae, yani yeye ilimradi kapata namba zetu basi anaona cha kufanya ni kutusumbua tu, usimjali kwa lolote huyu mtu mke wangu”
“Na akija tena hapa nyumbani!”
“Hawezi, nishamwambia mlinzi kuwa sitaki kuiona ile takataka hapa nyumbani kwangu, hebu tufanye vitu vya muhimu mke wangu. Eeeh watoto wote wameondoka, leo tutakula nini?”
“Mmmh hata sijui halafu naona uvivu kupika leo hatari”
“Hakuna tatizo mke wangu, basi leo nitakupikia naamini utapenda chakula changu”
Mama Angel alicheka na kumkumbusha kitu mume wake,
“Ndio unipikie kama ugali aliopika dada yako nyumbani kwetu, na maharage yenye macho”
Baba Angel alicheka sana, yani alicheka muda huo na kusema,
“Yani Tumaini kashasahau ujue kama alikuwa hajui kupika, saivi anajiona ndio mwenyewe wakati aliumbuka ukweni. Ila kwenu sio watu wazuri, yani kumfanyia vile dada yangu dah! Haya sasa nikupikie nini mke wangu?”
“Chohote utakachokipenda wewe basi nami nitakipenda tena leo nimepikiwa na mume wangu basi nitakulaje!”
Wakacheka pale na kuendelea na mambo mengine.

Wakina Erick walifika ufukweni walikokuwa wakienda, basi baada ya kufika pale Junior akawaambia,
“Jamani, mimi nitatembea na Vaileth huku nikimuonyesha mandhari ya ufukwe halafu nyie kaka na dada ongozaneni huko kwingine sio tuanze kufatana fatana”
Erick na Erica wakaguna ila wakakubaliana nae tu na moja kwa moja Junior aliongozana na Vaileth ila kwakweli Vaileth hakutaka kuongozana na Junior sema tu hakutaka Erick na Erica watambue chochote kile.
Vaileth na Junior waliongozana huku Junior akijifanya kumuonyesha Vaileth baadhi ya vitu vya ufukweni, kisha alimuomba wakae mahali kwenye mchanga ili amuonyeshe vizuri, na walipokaa tu alianza maongezi nae,
“Kwanza kabisa Vaileth, ni kwanini umenichukia?”
“Hivi unadhani kuna mtu anaeweza kufurahia ujinga Junior, sikia umenidanganya mimi kuwa unanipenda kumbe una wanawake zako kibao. Najua unanifanyia yote haya sababu unaniona mimi mjinga kwakuwa ni mtu mzima halafu nimekupenda wewe kijana mdogo”
“Ngoja nikukatishe kuhusu umri wako, kwanza kabisa tambua kuwa umri ni namba tu, mapenzi hayaangalii umri wala nini. Halafu unaweza kuona mimi ni mdogo ila nikawa natambua mambo mengi sana katika mapenzi kutokana na niliyopita. Siwezi kukataa hili, ni kweli mimi nilikuwa muhuni sana na nilikuwa na wanawake wengi, ila nilipokupata wewe nikasema kwanini nihangaike na wanawake wengine wakati wewe nakupenda! Sasa yule msichana niliachana nae kitambo sana na alisema kuwa ana mimba yangu na anahitaji kuitoa, basi nilimpatia pesa za kuitoa na hapo nikamwambia kuwa mimi na yeye ndio basi. Sasa hata namshangaa kunitafuta tena sijui damu zinamtoka, kwanza kabisa mimba alikuwa nayo yeye na sio mie, halafu ni yeye ndio aliyeenda kutoa, sasa anamlalamikia nani kuwa damu zinamtoka? Achana na yule msichana, kwanza nilimwambia kuwa mimi nina mke aniheshimu ila hataki ndiomana kafanya huo ujinga, jamani Vai nakupenda sana”
“Mmmh kwa mtindo huu ndio tutakuwa kama mama na baba kweli kule nyumbani! Wale wanapendana kwa dhati na wala baba hana uhuni kabisa”
“Sikia nikwambie, mama yangu nilimsikia akiongea na baba na walikuwa wakiongea kuhusu bamdogo huyo, nasikia alikuwa ni malaya tena malaya koko, hata mbwa mwenyewe akasome”
“Jamani Junior, punguza ukali wa maneno”
“Aaah basi, ila usione watu wametulia kwenye ndoa zao ukadhani wameibuka tu, penzi la kweli linatengenezwa na maelewano mema na masikizano, sasa unanifungia mlango kabisa hutaki hata kusikia upande wangu naongea kuhusu nini au nitajitetea vipi ila unabaki kuumia moyo na kunilaumu. Jamani Vaileth mimi nakupenda sana”
“Mmmh lakini swala la kusema baba alikuwa muhuni nakukatalia”
“Haya, endelea kukataa tu ila wanaomfahamu wenyewe wanasema, kuwa alikuwa ni kiwembe balaa kinakata kulia na kushoto, unaambiwa akiwa anatembea na wewe mdada na ukamtambulisha rafiki zako basi jua wote hao atawapitia”
“Duh!!”
“Mbona mimi mstaarabu sana, ila maisha huwa yanabadilisha mtu. Muangalie sasa, katulia na ndoa yake, hanywi pombe na unaambiwa alikuwa analewa yule hadi anazima”
“Junior! Nani kakwambia maneno hayo?”
“Yani licha ya kumsikia mama ila kuna mama mmoja hivi, sijui alikuwaga mwanamke wa zamani wa bamdogo basi huwa nikikutana nae ananiambia mambo mengi sana ya bamdogo kipindi hiko”
“Kwahiyo na yeye alimvumilia tu! Yani mwanaume analewa hadi anazima, anatembea na rafiki zako wote, bado alimvumilia tu”
“Si alimpenda, tena sio marafiki tu hata ndugu zako ikiwezekana anatembea nao. Unajua ukiona mwanaume wa hivyo tambua kabisa hakupendi kwani mwanaume anayekupenda atawaheshimu ndugu zako, atawaheshimu rafiki zako na atakuheshimu na wewe pia. Yule mmama nilimwambia kuwa basi hakukupenda, ila yule mama anavyoongea kwa uchungu hata nina mashaka nae”
“Ni mama gani huyo?”
“Siku moja nitakuonyesha, nikimuona tu nje ya geti basi nitakuita ili tuongee nae, kiukweli utabaki unamuangalia tu. Ila sijui alinihadithia mimi tu au huwa anawahadithia wengi sijui. Kiukweli siwezi kumueleza bamdogo yale maneno najua atachukia sana”
“Ila kwakweli imenishangaza sana, kwahiyo wewe unanipenda kweli?”
“Vaileth jamani, mimi ninakupenda sana tu, kiasi kwamba hata siwezi kumtamani mwanamke mwingine zaidi yako. Naomba unisamehe na tuanze kurasa mpya ya mapenzi yetu”
Vaileth alitabasamu tu na kumfanya Junior atambue kuwa pale ameshasamehewa kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwani alitamani mno kusamehewa na Vaileth.
 
SEHEMU YA 237

Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao.
Kwakweli kile kibao kilimuingia Samir, kiasi kwamba aliamua kukimbia tu kwani angeendelea kusimama mahali hapo basi angepigwa tena na huyu bibi na alimtambua vizuri mambo yake, hivyobasi alikimbia, basi bibi alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, kwakwlei kwa wakati huo Angel alijiandaa kupigwa tu kwani alijua wazi kuwa atapigwa sana na bibi yake huyu, ila walipoingia ndani bibi alimkalisha Angel chini na kumuuliza,
“Una uhakika kuwa huyo Samir anakupenda?”
Erica alinyamaza kimya tu huku akiangalia chini kwa aibu, kisha bibi yake akamwambia tena,
“Mjukuu wangu, huyo Samir hakupendi wala nini hebu jiulize anayekupenda kweli anaweza kukimbia sababu ya kupigwa kibao kimoja? Mtu akikupenda huwa tayari kwa lolote lile, kuna kijana mmoja aliitwa Bahati basi alikuwa akimpenda dada mmoja hivi na kumfatilia sana, yani yule kijana alikuwa tayari hata kumwagiwa maji ya moto sababu ya mwanamke, yule kijana aliwahi kukaa rumande sababu ya mwanamke, hakuwa na kosa ila alikaa rumande sababu ya upendo wake tu kwa mwanamke”
“Kheee bibi, sasa kwanini aliwekwa rumande?”
“Ndugu wa mwanamke hawakumtaka, kwahiyo alivyokuwa hataki kuondoka hadi aonane na mwanamke ndipo walipomuweka rumande ila badae walimuhurumia sana na kumuachia huru. Kijana huyo alikuwa akihudumia familia ya mwanamke kama familia yake akiwaletea kuku na samaki, kijana huyo alikuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine ambaye huyo dada alimzaa kabla, yani huyo kijana alikuwa na upendo wa dhati tena upendo mkubwa sana”
“Bibi, vijana kama hao wapo?”
“Wapo ndio, msubirie wa kwako ila sio huyu Samir anakuongopea tu, kibao kimoja kakimbia vile, hata hajali kuwa nitakupiga wewe au nini! Nakwambia ingekuwa huyo Bahati angetaka apigwe yeye badala yako, usimfikirire Samir mjukuu wangu hakupendi wala nini. Haya nipe na simu nikaiweke”
Basi Angel aliitoa ile simu na kumpa bibi yake ili aiweke, kisha bibi aliinuka yani Angel kwakweli hakuamini kama kapona kipigo toka kwa bibi yake maana alihisi muda huo angepigwa vibaya sana ila hakupigwa wala nini zaidi ya kuambiwa kuwa Samir hafai kabisa kwake.
 
SEHEMU YA 238

Erick na Erica nao walikuwa wakitembea tembea pembezoni mwa maji huku wakichezea maji na kukimbizana, basi Erica akasema,
“Jamani, mimi huwa nikimuona Sarah yupo karibu na wewe basi roho huwa inaniuma sana”
“Kwanini?”
“Hata sijui kwakweli”
“Sikia basi tufanye kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Mimi na wewe tupeane ahadi ya jambo moja ambalo wewe hutolifanya katika maisha yako na mimi sitolifanya katika maisha yangu”
“Jambo gani”
“Iwe hivi, yani mimi nisiwe na rafiki yoyote wa kike zaidi yako yani wewe uwe ndio rafiki yangu na kila kitu kwangu, na wewe usiwe na rafiki yoyote wa kiume zaidi yangu yani mimi niwe kila kitu kwako”
“Unamaanisha hata kuongea nao tusiongee nao!”
“Unaweza kusalimiana nao tu ila ukiona wanaleta maongezi mengi unaachana nao na mimi iwe hivyohivyo, unajua na mimi naumia sana moyo nikimuona yule Bahati na unavyoongea nae vizuri kwakweli naumia sana. Sisi ni mapacha, yatupasa tupendane”
“Kweli kabisa, kwahiyo tule kiapo?”
“Ndio”
“Sasa kiapo hiko tunakulaje?”
Twende pale kwenye ukingo wa bahari nikuelekeze cha kufanya”
Basi Erick na Erica wakaongozana hadi kwenye ukingo wa bahari na kwenda kuelekezana namna ya kula kiapo.

Muda huu Tumaini alikuwa ametoka kwenye shughuli zake ila njiani alimuona Sian a kumfanya asimamishe gari ili aongee nae maana mama Erick alishampigia simu kwa kumwambia kuwa inatakiwa wamshawishi baba Angel kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia.
Basi alishuka kwenye gari na kusimama nae nje huku akiongea nae,
“Eeeh Sia, nimesikia ishu za kwenda kupima DNA sijui Erick na mtoto wako, jamani Sia rafiki yangu mbona una makubwa wewe, unajua wazi mtoto sio wa Erick, kitu gani kinakusumbua lakini”
“Tumaini, najua huelewi uchungu ambao upo katika moyo wangu ndiomana unasema hivyo”
“Huo uchungu ni uchungu gani wa miaka hiyo hadi leo! Inamaana wewe huwezi kupata mwanaume zaidi ya Erick, kwani Sia una kasoro gani wewe hadi ukose mwanaume? Unachong’ang’ania kwa Erick ipo siku utakipata”
“Ndio, nataka sana anioe”
“Hilo swala la Erick kukuoa hebu lifute katika mawazo yako, halipo na kamwe halitakuwepo. Unajua na mimi nimeolewa kwahiyo naujua uchungu wa mume, usitake Erica aone ndoa yake chungu eti sababu yako Sia. Hebu acha wenzio wafurahie ndoa yako, sijui umeibuka wapi wewe”
“Sijaibuka ila nampenda sana Erick”
“Oooh tena kabla sijasahau, Erick alinipigia simu kasema…..”
Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,
“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”
Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale.


Basi madam Oliva alifika na Erica saluni na kumuweka pale huku akiwaelekeza wasusi namna ya kumsuka nao walianza jambo lile, huku muda huo madam akiwaaga kuwa anaenda kwanza kuangalia chuo chake, kisha alimuuliza Erica,
“Nikirudi nikuletee nini? Maana leo itabidi ule huku”
“Chochote tu”
“Sawa, nitakuletea chips kuku basi”
“Sawa, asante”
Erica alitabasamu halafu madam Oliva alitoka. Alipotoka tu wale wasusi waliokuwa wakimsuka Erica walianza maongezi, kwanza kabisa walimuuliza Erica,
“Huyu madam ni ndugu yako?”
“Hapana, ila ni mwalimu wa kaka yangu”
“Ooooh sawa”
Kisha mwenzie akasema,
“Jamani, huyu madam leo alivyo na furaha utafikiri kitu gani. Halafu naona huyu mtoto kampenda sana”
“Inaonekana, maana sio kawaida yake. Asubuhi kapita kuwa anamleta mtoto tumsuke, alivyokuwa anatuambia kuhusu huyo mtoto basi nikajua mtoto mdogo sana kumbe binti tu. Sijui muusuke taratibu, msimsumbue, msimvute nywele, mpeni anachotaka”
Wakaanza kucheka huku mmoja akisema,
“Kwani jamani yule madam ana mume yule?”
“Mume hana, eti anasema yeye yupo kutafuta pesa tu hana shida na mume wala shida ya kuolewa”
“Ila ana mpenzi au?”
“Yani kwa kifupi yule madam hana mpango kabisa na wanaume, yani yeye anasema anawaza pesa tu ndio ya muhimu kwake.”
“Na kama pesa ni anaitafuta kweli, maana yule kaajiriwa halafu ana biashara zake. Ana chuo chake cha kompyuta, ana hii saluni na ana shule yake ya kujifunza ushonaji”
“Kweli yupo vizuri ila kuna umuhimu wa kuwa na mwanaume katika maisha, mtu anaishi vipi jamani bila mwanaume! Tamaa zake za kimwili anazimaliza vipi?”
“Hapo sasa, au mwenzetu hana tamaa za kimwili jamani! Kuna mambo mengine ndiomana mtu unakuwa na hasira muda wote, kwanza toka nimfahamu huyu madam ndio leo namuona anacheka”
Mwingine akadakia,
“Usikute kashaonja tamu ya asali”
Mmoja akawanyamazisha wenzie,
“Badilisheni mazungumzo jamani, kumbukeni mnayemsema katuajiri na anafanya turinge mjini”
“Kheee bwana eeeh anasemwa raisi sembuse yeye!!”
Basi wakacheka na kuendelea na maongezi mengine.
 
SEHEMU YA 239

Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa muda huo, akaja mama yake kama ambavyo aliongea nae kwenye simu jana yake basi alimkaribisha na kumsalimia pale kisha kuanza maongezi nae ambapo mama yake alianza kuongea,
“Mwanangu sikia, naomba niache niongee kwanza halafu zamu yako ikifika ndio utasema yani usinikatishe wakati naongea”
“Sawa mama”
“Ni hivi, Sia alinipigia simu kuwa mtoto anaumwa, kwakweli na mimi ni mama halafu na mimi nimepitia mazingira ya kulea mtoto bila ya baba kwahiyo najua uchungu wake na ninajua ni hali gani inakuwa. Nimekulea wewe, nimehangaika na wewe kipindi hiko baba yako hana hata habari hata wewe mwenyewe unakumbuka wazi kuwa baba yako umefahamiana nae ukiwa mkubwa kabisa unajitambua tena ukiwa unatangatanga huko baada ya kufukuzwa shule. Kiukweli nilipatwa na uchungu kusikia mtoto mdogo anaumwa na mama yake hana pesa, ilibidi niende. Nilipofika pale nilimkuta mtoto kalala, yani nilienda kwa kuelekezwa na Sia mwenyewe, na nilivyofika alimuamsha mtoto aje anisalimie maana kuna zahanati alimpeleka na alipatiwa dawa ila aliacha deni tu pale zahanati, ilibidi nitoe pesa aende kulipa hilo deni maana afya ya mtoto ni ya muhimu zaidi ya vyote. Kingine ni kuhusu yule mtoto mdogo Elly, kwakweli kwa jinsi nilivyokuwa namuangalia ananikumbusha zamani kabisa kipindi cha udogo wako, wewe ulikuwa ni mtoto mpole na mchangamfu basi ndio alivyo yule Elly, mwanangu mimi naomba jambo moja tu hata kama Sia humpendi basi mpende yule mtoto, nakuomba ukubali kupima DNA na Elly”
“Umemaliza mama?”
“Ndio, nimemaliza nakusikiliza wewe sasa”
“Kwanza kabisa siwezi kwenda kupima DNA na Elly, nikifanya hivyo inamaana sijiamini. Pili ngoja nikuulize mama, inamaana Ellyn i mwanangu halafu Erick sio mwanangu?”
“Mmmh mimi sijasema Erick sio mwanao, kwanza itakuwaje Erick asiwe mwanao jamani! Erick si kazaliwa na mkeo, sasa itakuwaje sio mwanao? Ninachohitaji mimi ni Elly kupata haki sawa na wenzie wote, una watoto pale kuna Angel, Erick, Erica, Ester na sasa Elly awepo kwenye familia”
“Kwa misingi ipi mama?”
“Ellyn i mtoto wako ambaye umezaa na Sia”
“Mama, mimi ndio mwanaume ambaye Sia anadai amezaa nae, ila mimi nakataa mbele ya vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kuwa sijazaa na Sia mimi.”
“Ila mwanangu unakumbuka tabia zako vizuri wewe, ni wadada wangapi waliokuwa wakilalamika kwangu kuwa wana mimba zako sembuse Sia ambae muda wote alikuwa na wewe! Je kama akitokea mdada mwingine na mtoto utakataa kuwa sio mwanao wakati ulikuwa muhuni sana wewe!”
“Ni kweli mama, yani siwezi kukataa kuwa sikuwa muhuni, kama uhuni nimeufanya sana tu, ila niliufanya sababu ya stress nilikuwa siwezi kumpata mwanamke nimpendaye ndiomana nilikuwa nafanya ule uhuni, kuna wanawake wakija kusema Erick tulizaa na wewe naweza nikakubali ila sio Sia, unajua nini Sian i mwanamke ambaye alikuwa akiniganda sana. Na toka nimetoka Afrika kusini na kuanza kuishi na Erica kw aupendo ile ikawa mwisho wa mimi na Sia yani sikuwa na ukaribu nae tena, alikuwa akifanya kila mbinu lakini ilishindikana kuwa na mimi, halafu leo useme Sia kazaa na mimi tena mtoto ambaye ni umri sawa na watoto niliozaa na Erica, hapana kwakweli Sian i muongo tena muongo namba moja. Kuna mwanamke mmoja angesema hivyo ningesema labda maana kipindi kile Erica alinikatalia kabisa hadi ndoa na mimi ni mwanaume ila yule mwanamke alikuwa akijua kila kitu kuhusu mimi na Erica hadi siku namuacha nikamwambia mimi na wewe basi maana nimerudi kwa Erica wangu, yule mwanamke alikubali kwa roho moja na hajawahi kunitafuta tena hadi leo kwani anajua kuwa nina familia yangu ila kwanini Sia anakuwa hivi jamani! Kwani wanaume wameisha duniani au kitu gani?”
Mama yake akapumua kidogo na kusema,
“Haya, mfano huyo mwanamke aseme pia ana mtoto wako utasemaje?”
“Haiwezekani sababu yule mwanamke nilikuwa nae na aliweka kijiti cha miaka mitatu, na wakati niko nae ilikuwa ni mwaka wa pili, mama katika maisha yangu kitu mimba nilikuwa nakihofia sana na kukuheshimu kwani nilitambua wazi kuwa Erica akiona nina watoto wengi basi hatonikubali, kwahiyo nilikuwa makini sana”
“Sawa mwanangu ila mimi hoja yangu bado ni moja tu, ukapime DNA na Elly”
“Mama, tafadhari hilo swala kwangu halikubaliki. Yani hiyo kitu haipo, labda ukapime wewe na ukikuta mnafanana basi jua kuwa ni mwanao na sio mwanangu sababu mimi sijazaa na Sia”
“Sasa hayo matusi mwanangu, yani unanitusi mama yako. Inamaana mimi nimezaa na Sia? Yani wewe mtoto loh! Mitoto mingine tunabebaga change tu tumboni”
Kisha mama yake akanyanyuka na kuondoka zake, inaonyesha alikuwa amekasirika ila baba Angel wala hakujali zaidi zaidi aliendelea na kazi zake tu.

Madam Oliva alimpelekea Erica kama alivyoahidi na Erica alikula pale, kisha walipomaliza kumsuka alimwambia kuwa anampeleka ofisini kwa baba yake ili aondoke na baba yake maana yeye alidai kuwa kuna kazi anataka kuifanya.
Basi aliondoka na Erica pale huku akimsifia kuwa kapendeza sana hadi kabadilika, basi Erica alikuwa akifurahi sana kuambiwa vile, yule madam nae alikuwa akifurahi kuona Erica anafurahi ndipo Erica alipomwambia,
“Madam, wale wafanyakazi wako mule wanafki”
“Wamefanyaje tena?”
Erica alianza kumueleza moja baada ya jingine ambalo wafanyakazi wale walikuwa wakisema na kuelekeza kabisa yupi kasema lipi na yupi kaongea lingine, kiukweli yule madam alichukia sana,
“Yani badala ya kufanya kazi wanafanya kazi ya kunisema!”
“Tena mwenzao alipowakatisha wakasema anasemwa raisi sembuse wewe!”
Yani madam Oliva alizidi kuchukia kwakweli na kuona kuwa wafanyakazi wake wabaya, basi alienda na Erica hadi ofisini kwa baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa amekaa tu maana hata yeye kichwa chake kilikuwa kimevurugwa ila alipomuona binti yake alimsifia sana kuwa kapendeza kisha akamshukuru madam Oliva na kumuuliza pale,
“Eeeeh ndio pesa ngapi hapo?”
“Aaaah hii leo nimempa ofa”
“Kumbe ofa!! Jamani madam kwanini lakini!”
“Hamna jamani, hii ni ahadi yangu kwake, na sio kwa leo tu kwani siku zote akiitaji kusuka basi nitampeleka saluni kwangu na atasuka bure kabisa”
Basi baba Angel alicheka tu, kwavile hata yeye alichoka aliamua kuondoka kwahiyo aliagana na madam Oliva halafu yeye kuelekea kwake huku madam akirudi kwenye saluni yake.
Basi Erica kama kawaida alianza kumsimulia na baba yake maneno ambayo wale wadada wa saluni walivyokuwa wakiongea na jinsi na yeye alivyomueleza madam Oliva,
“Aaah mwanangu, unajua utakuwa umewafanya hao wadada wafukuzwe kazi!!”
“Ila baba, mimi sijasema kwa ubaya, nimesema tu ili madam Oliva ajue kuwa wafanyakazi wake ni watu wa aina gani!”
“Mmmh ila Erica mambo yako jamani!”
Baba Angel alicheka na kutikisa kichw atu huku wakielekea nyumbani.
Walipofika nyumbani, kila mtu alikuwa akimsifia Erica kuwa kapendeza sana na kumfanya hata yeye afurahie sana zile sifa alizokuwa anapewa.
Basi waliongea ongea kidogo pale halafu Erica alienda chumbani kwake halafu mama yake alimfata na kumuuliza,
“Eeeh Erica, nipe habari za huko”
Erica kama kawaida alimuelezea kila kitu yani hakuacha hata kimoja, kisha akamwambia,
“Wale wasusi wanasema madam yupo kutafuta hela ila kapewa hela na baba kaikataa”
“Hela ya nini?”
“Si ya kunisuka mimi, eti kasema ni ofa”
“Kheee kumbe!!”
“Ndio mama, kwahiyo nimesukwa bure”
“Haya sawa mwanangu, mimi nashukuru kwa ujumbe”
Mama Angel alijua kuwa mwanae lazima atamwambia kila kitu, sababu ya kumuuliza ni kujiridhisha kuwa madam Oliva sio mtu mbaya katika maisha yao, na kwa yale maongezi ya mwanae hakuona ubaya wa madam huyo sababu ameambiwa kuwa huyo madam yupo kwaajili ya kutafuta pesa tu.
 
Back
Top Bottom