Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 202

Siku hiyo mchana alifika rafiki wa Erica, yani Samia na alikuwa ameleta tena mikanda ya ngumi yani hiyo mikanda ambayo bibi yao alihisi kuwa walikuwa wakiangalia ndio kwanza Samia aliileta siku ya leo na alipokelewa na rafiki yake na kukaribishwa vizuri tu, basi Samia alikuwa akiongea mambo mengi sana na Erica moja wapo alimuuliza kuhusu Erica,
“Huyu kaka yako ni vipi lakini Erica? Mbona hapendi kuongea na watu?”
“Mmmh huyo mzoee tu ndio zake hizo”
Basi aliongea mambo mengi sana na siku hii Erica aliitumia kumtambulisha Samia kwa mama yake ambaye nae alionekana kumfurahia ila tu hakujua kama Samia ndio huwa anawaletea watoto wake mikanda ya ngumi, basi Samia wakati anaaga akamwambia mama Angel,
“Mama, siku moja naomba umruhusu Erica aje na kwetu”
“Hakuna shida, atakuja na kaka zake”
“Ni vizuri hata hivyo, nitafurahi sana. Mimi naenda”
“Haya, karibu tena”
Ila wakati Samia anatoka basi Junior leo alijitolea kwenda kumsindikiza Samia, wakati Erica kaishia getini ni moja kwa moja Junior alimsindikiza Samia kituoni kwenda kupanda gari la kurudi kwao kwani Samia alikuwa yupo huru sana nyumbani kwao na hakufungiwa kama ambavyo Erica alikuwa akifungiwa.
Basi Junior alikuwa akimsindikiza huku akiongea nae mambo mbalimbali,
“Kwenu mpo wangapi Samia?”
“Wawili tu, mimi na kaka yangu”
“Oooh! Ila unaonekana wewe ni binti mpole sana, mkarimu na muongeaji mzuri”
“Asante sana”
“Sema ningependa tuwe tunawasiliana zaidi, una simu?”
“Hapana, labda simu ya kaka”
“Sawa hakuna tatizo Samia, usijali nimekuelewa”
Basi alimsindikiza hadi Samia alipopanda gari na yeye kurudi nyumbani kwao pale, ila lile tukio la Junior kumsindikiza Samia lilimchukiza sana Vaileth ukizingatia Junior alikuwa kijana ambaye haaminiki kabisa.

Siku hiyo usiku wakati wa kulala, kawaida ya Junior alienda chumbani kwa Vaileth kulala ila alimuona kuwa Vaileth amechukia na kumuuliza ambacho kimemchukiza,
“Mbona unaonekana huna furaha leo”
“Unaona ulichofanya kipo sawa, mbona siku zote huwa humsindikizi yule mtoto lakini leo umemsindikiza”
“Jamani Vai, ushasema yule ni mtoto sasa mimi wa nini jamani!”
Basi Junior alianza kumpapasa papasa Vaileth ili aweze kumsahaulisha lile wazo la yeye kumsindikiza Samia.
Mara wakasikia mlango ukigongwa na moja kwa moja walihisi ni bibi yao tu, basi kama kawaida Junior alikimbilia chooni kujificha, na Vaileth alienda kufungua mlango ila aliyeingia alikuwa Erica ila cha kushangaza moja kwa moja Erica alikimbilia chooni kwa Vaileth na huko alibambana na Junior na kumfanya Erica apige kelele kama kawaida yake.


Mara wakasikia mlango ukigongwa na moja kwa moja walihisi ni bibi yao tu, basi kama kawaida Junior alikimbilia chooni kujificha, na Vaileth alienda kufungua mlango ila aliyeingia alikuwa Erica ila cha kushangaza moja kwa moja Erica alikimbilia chooni kwa Vaileth na huko alibambana na Junior na kumfanya Erica apige kelele kama kawaida yake.
Yani Junior muda ule ule alimkimbilia Erica na kumziba mdomo kisha kutoka nae kwenye chumba cha Vaileth ambapo Erick alivyokuwa anakuja na mama Angel walikutana na Junior akiwa kamshikilia Erica, basi mama Angel akauliza,
“Kwani tatizo nini jamani?”
“Nadhani bahati mbaya, tumekutana hapo njiani na Erica tukagongana”
“Jamani na nyie usiku huu mnaenda wapi jamani!”
Basi mama Angel akamchukua Erica toka mikononi mwa Junior na kumpeleka chumbani kwake yani chumbani kwa Erica, ila muda huo Junior alikuwa na wasiwasi sana kuwa Erica anaweza kusema ukweli ukizingatia ni mbeya yani alihisi kila kitu kinaenda kuharibika, basi wakati Erica yupo na mama yake muda ule ule Junior alienda kuzima umeme wa nyumba nzima ili wote washughulikie umeme na washindwe kuongea na Erica, na kweli umeme wa nyumba nzima ulipokatika yani mama Angel alihisi kiwewe kwa mtoto wake mchanga kuwa giza, hivyobasi alimuacha Erica pale na kwenda kukimbilia chumbani kwa mtoto wake mdogoila muda huo huo Junior nae aliingia chumbani kwa Erica na kumwambia,
“Ole wako uropoke ulichokiona leo”
Kisha akatoka na kurudi tena kwenye soketi kubwa na kurudisha umeme kwahiyo hawakujua kuwa tatizo ni kitu gani mpaka umeme kukatika gafla vile kwa nyumba nzima.
 
SEHEMU YA 203

Mama Angel alikuwa akilalamika tu kwa mume wake,
“Ni kitu gani kimetokea leo jamani, kwanini umeme ukatike gafla hivi! Yule fundi wako hakutengeneza vizuri”
“Nitamuita kesho aje kuangalia ila sidhani kama kuna tatizo mke wangu maana alitengeneza vizuri tu”
“Sasa kama hakuna tatizo ni kwanini ukatike gafla hivi! Si kuna jenereta jamani tena ametuunganishia la moja kwa moja kuwa ukikatika wa kawaida basi jenereta liwake, kwakweli mimi binafsi sielewi hii hali jamani! Sio kawaida”
“Basi mke wangu usijali, kesho nitamuita fundi atengeneze, usiwe na wasiwasi”
“Sawa, na lile swala la Junior na Angel kwenda kusoma kompyuta umelishughulikia?”
“Ooooh umenikumbusha kitu, ngoja niwasiliane na huyu mtu”
Basi baba Angel alichukua simu yake na kumpigia mtu aliyekuwa akimsema, mtu huyo alikuwa ni madam Oliva, alishawahi kuongea nae na huyu madam alishawahi kumueleza kuwa ana sehemu yake ambapo anawafundisha watu kozi ya kompyuta, yani baba Angel hakujali ule ni usiku wala nini ila nia yake ilikuwa ni kumpa jibu linaloeleweka mke wake,
“Hallow baba Erick, mbona usiku!!”
“Samahani mwalimu, nilikuwa naulizia kile kituo chako cha kufundishia kompyuta, nina vijana wangu nataka kuwaleta”
“Ooooh hakuna tatizo, walete tu Jumatatu nitakuwepo na kuwaonyesha mazingira, walete tu”
“Sawa, asante. Usiku mwema”
Basi baba Angel aliagana na huyu madam na kumpa mkewe jibu kuwa Jumatatu atawapeleka Junior na Angel, basi mama Angel nae akamzogodoa pale mumewe kidogo,
“Ndio usiku huu na wewe, si ungempigia kesho tu!!”
“Mmmh mke wangu wewe nakujua mwenyewe, ningesema sijafatilia lazima ungeongea yako muda huu, uanze kusema ingekuwa sina mtoto mdogo ningeenda mwenyewe, haya mama nimefatilia sema sikuulizia vizuri tu na mwalimu ndio huyo niliyekuwa naongea nae”
“Haya nimekuelewa mume wangu hakuna tatizo”
Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.

Jumapili hii kama kawaida walijiandaa kwa kwenda Kanisani, na kama ilivyokuwa kwa wiki iliyopita basi leo waliondoka vile vile Junior, Angel, Erick na Erica ila leo Erick aliwapeleka wenzie kwenye kanisa lingine kabisa kwani yeye ndio aliyekuwa akiendesha gari, ila Erica alichukia sana,
“Yani wewe ukiamua kitu ndio hicho hicho”
Junior akasema,
“Muache, huyo ndio baba mwenye nyumba, kwahiyo ndio mwenye maamuzi, huwezi kwenda kinyume nay eye la sivyo uhame nyumba”
“Aaaargghh”
Basi walishuka na kwenda kwenye hilo Kanisa ambalo Erick aliwapeleka wenzie, kwahiyo kwa siku hiyo waliabudu kwenye hilo Kanisa.
Baada ya ibada walitoka na moja kwa moja kuingia kwenye gari na safari ya nyumbani ikaanza, ila njiani Erica aliona watu anaowafahamu na kushangaa kuona wameongozana,
“Jamani, yule si Bahati na Abdi wale!!”
Erick akadakia,
“Ndio wenyewe”
“Kheee au ni ndugu!”
“Itakuwa, ndio uone kuwa naona mbali”
Basi Erica hakuendelea tena kuongea ila mbele kidogo walimuona Elly na mama yake, ila Erick akataka kuongeza mwendo sema gari likazimika gafla na kumfanya Erick kuchukia sana basi Junior alimuuliza,
“Kwani tatizo ni nini Erick?”
“Hata sielewi, limezimika gafla tu”
“Basi tushuke, tuliangalie kidogo”
Ikabidi washuke ili waangalie tatizo ni nini, ila wakati wanashuka basi Elly na mama yake nao walifika eneo lile, naye mama yake Elly akamwambia Erick,
“Yani huwezi kunikimbia mimi, ona ulitaka kuongeza mwendo ila gari imesimama kwaajili yangu. Nilitaka tu kukusalimia, na hiyo gari haijaharibika wala nini ni nzima kabisa ila iligoma tusalimiane”
Angel nae alimua kushuka kwenye gari na kumuuliza mama Elly,
“Kwani mama una tatizo gani? Nakumbuka mara ya kwanza nilikuona kwetu ambapo Samir alikunasa kibao”
Elly akauliza kwa mama yake,
“Yani mama kuna mtu alikunasa kibao?”
“Achana na hayo mambo mwanangu, tufikirie vitu vya muhimu. Ukiwaona hawa uwaone kama ndugu zako”
“Kivipi mama?”
“Kuna siku nitakaa chini na kuzungumza na wewe mambo ambayo huyajui kabisa wala huyafikirii kabisa ila jua kwamba hawa ni ndugu zako”
Yani Erick ndio alizidi kuchukia huku akitamani hata kumtukana yule mama ila alimuangalia tu na kurudi kwenye gari na alipojaribu kuwasha ni kweli liliwaka yani hakuna sehemu ambayo ilikuwa inamatatizo kwenye gari wala nini. Basi wote wakaingia kwenye gari na Junior aliuliza wakati Erick akiendesha lile gari tena,
“Kwani yule mama alikuwa akiongelea vitu gani maana sijamuelewa hata kidogo”
“Ni bora usimuelewe hivyo hivyo maana ukimuelewa utaharibu siku yako”
Junior alimuangalia tu Erick kwa lile jibu ila pia alijiuliza ni kwanini Erick ameonekana kuchukia zaidi baada ya kumuona yule mama na hakupata jibu ila waliendelea tu kwenda nyumbani.

Muda huu mama Elly aliongozana na mwanae hadi kwenye duka ambalo Steve alikuwa akiuza, kwanza kabisa alimuuliza mwanae,
“Katika maisha yako, mfano ukawa tajiri na mali nyingi ni nani wa kwanza utakayemfikiria?”
“Ni wewe mama yangu, hakuna mtu mwingine yoyote zaidi yako”
“Mfano watu wakinibeza na kunichukia na kunitenga, je wewe utanichukuliaje?”
“Mama, nilishakwambia nab ado nakwambia hata dunia nzima ikukatae, hata dunia nzima ikikutenga bado mimi nitakuwa sambamba na wewe, nakupenda sana mama yangu yani wewe ndio maisha yangu”
“Nakupenda pia mwanangu”
Basi mama Elly alimkumbatia mwanae na kuingia nae kwenye lile duka, kiukweli Steve alipowaona hata alikumbuka ushauri wa bosi wake tu kuwa Jumapili awe anapumzika, yani kilichomfanya leo kufungua duka ndio kitakachompambanisha na huyu mwanamke, kisha alimuuliza,
“Na wewe umefuata nini tena?”
“Hivi huwa huelewi nilichofuata hapa? Hapa nimefuata mali za mwanangu”
“Mali za mwanao kivipi? Unajua sikuelewi, mwanao huyo mwenye hizi mali ni mwanao gani? Huwa unamsema Erick au huyu Elly?”
“Kwani wewe unahisi ni mwanangu gani?”
“Sijui, wewe ndiye unayejua maana ulinitambulisha kuwa huyu ndio mtoto wako na mara ukasema Erick ni mtoto wako, vipi mwenzetu ulizaa mapacha?”
Elly naye alimuuliza mama yake,
“Kwani mama una mtoto mwingine zaidi yangu?”
“Achana na huyu mwanangu, ila hili duka ni lako. Hii ni mali yako”
“Kivipi mama?”
“Mwanangu si nilikwambia kuwa mimi ni mama yako na nitafanya kila kitu kukufurahisha katika maisha yako, na katika jitihada zangu basi kuna hili duka. Natumaini umelipenda, hili duka ni mali yako mwanangu, nishakuja hapa na wewe mara nyingi tu hata nashangaa kwanini unashangaa jambo hili, nataka ujue kuwa hili duka ni mali yako na baada ya mwezi huu nitakukabidhi kila kitu kinachohusiana na hili duka, yani hadi huyu mfanyakazi atakuwa chini yako”
Kisha Sia alimshika mkono Elly na kuondoka naye, huku Steve akibaki anamuangalia tu na kumshangaa.
 
SEHEMU YA 204

Leo wakina Erick walivyofika nyumbani tu, kuna mgeni alienda kumtembelea Erick kama ambavyo alimuahidi na mgeni huyu alikuwa ni Sarah ambapo Vaileth alimkaribisha vizuri tu na moja kwa moja alisema kuwa anamuhitaji Erick, naye Erick alifika kusalimiana nae ila hata Erick hakuamini kama Sarah angeenda kweli kumtembelea kama ambavyo alikuwa akisema,
“Kheee umekuja kweli Sarah”
“Ndio, ulidhani nadanganya? Haya ahadi yangu iko pale pale, nimekuja kunuona mtoto na nimebeba zawadi za mtoto”
“Haya karibu”
Basi moja kwa moja Erick alienda kumuita mama yake na kumueleza juu ya ujio wa rafiki yake ambaye ameenda kumuona mtoto,
“Kheee mwanangu, rafiki yako yupi huyo?”
“Anaitwa Sarah!”
“Kumbe ni msichana! Haya mwambie aje”
Basi Erick akaenda kumkaribisha Sarah, ila kiukweli mama Angel alipomuona Sarah alijikuta akimpenda sana kwani Sarah alionekana ni binti mchangamfu, muongeaji na mcheshi sana, basi akamkaribisha vizuri sana na moja kwa moja Sarah alimkabidhi zawadi za mtoto,
“Ooooh wow, nimefurahi sana unaonekana ni mcheshi sana”
Sarah alikuwa akitabasamu tu kwani ndio kitu alichokipenda zaidi na kuongea kwahiyo alisema,
“Napenda sana watoto, wakati Erick kaniambia amepata mdogo wake nikatamani sana kuja kumuona maana mimi kwa mama yangu nimezaliwa peke yangu, napenda sana watoto. Anaitwa nani?”
“Anaitwa Ester”
“Oooh jina zuri sana jamani, na mtoto mwenyewe ni mzuri kwakweli nimempenda”
“Hata mimi nimekupenda sana”
Basi mama Angel alitumia muda mrefu sana kuzungumza na Sarah maana alijikuta kampenda binti huyu, yani alikuwa akihisi raha tu kuongea nae kwa muda wote.
Jioni ilipofika Sarah aliaga, na Erick nae aliomba ruhusa ili aweze kumsindikiza Sarah ambapo mama yake alikubali Erick amsindikize.
Mama Angel alibaki mwenyewe huku akitabasamu tu kwa maongezi ya Sarah, alikuja bibi na kuanza kuongea na mwanae,
“Katika wageni wote wanaokujaga hapa nyumbani nahisi huyu amekukosha”
“Yani mama, huyu Sarah yani huwezi amini nimetamani hata angekuwa mwanangu pia, mtoto anaongea vizuri huyu, yani maneno yake yana kituo na yanaeleweka halafu nio mcheshi sana”
“Haya usijali lakini maana ndio mkwe wako”
“Kheee mkwe kivipi?”
“Unadhani huo ukaribu na Erick ni wa kawaida?”
“Hamna mama, Erick hana mambo hayo ujue, ila hata hivyo hapo badae nikipata mkwe kama Sarah nitafurahi sana nimempenda sana, mama hebu nivutie huo mfuko nione kamletea mtoto zawadi gani!”
Basi mama yake alimvutia mfuko ambao alienda nao Sarah, yani mama Angel alifungua ule mfuko na kujaa tabasamu katika sura yake baada ya kuona zawadi ya Sarah kwa mtoto kisha akamwambia mama yake,
“Mama, ona alichokileta huyu Sarah”
“Kheee kaleta mdoli jamani!”
“Tena mdoli wa pinki na nyeupe, hivi huyu mtoto kajuaje kama napenda wadoli na ninaipenda hii rangi!”
“Si nimekwambia mkwe wako huyo! Ila mdori mzuri na unavyopendaga wadori nahisi umefurahi sana. Ila siku hizi naona hupendi kama zamani”
“Ni kweli ila huyu Sarah atakuwa amerudisha upendo wangu kwa wadori unajua watoto wangu wote hakuna anayependa wadori hata mmoja, huyo Erica ndio kwanza yeye ni karata basi karata na yeye, huyo Angel anachopenda naye anajua mwenyewe. Kwakweli huyu Sarah karudisha tabasamu usoni mwangu”
Mama Angel alionekana kumfurahia sana Sarah hata mama yake alimuelewa kwa ile hali aliyokuwa nayo ya kumfurahia Sarah, yani katoa hadi ruhusa kwa Erick kuwa ampeleke Sarah sababu kampenda sana.

Basi Erick akiwa kwenye gari wakati anampeleka Sarah kituoni ila akamwambia kuwa atampeleka hadi kwao na kumfanya Sarah afurahi zaidi kwani aliona sasa safari yake itakuwa vizuri zaidi,
“Oooh Erick jamani, leo nitaota kwakweli. Ila kwenu mna upendo sana haswaa mama yako yani nimempenda bure, oooh sijawahi kufikiria kama ningemkuta mama mwenye upendo kiasi hiki yani mama ambaye nimetumia muda mrefu sana kuzungumza nae, kwakweli Erick nimempenda sana mama yako”
“Hata yeye anaonekana amekupenda sana, huwa sio kawaida ya mama kuongea na rafiki zetu kwa kiasi kile, kwahiyo wewe utakuwa umeugusa moyo wake”
Basi Sarah alifurahi sana kwani kile ndio kitu alichokuwa anakitaka, alitaka kupendwa na familia ya Erick maana alishampenda Erick kwahiyo alitaka familia ya Erick imkubali pia, basi alimuuliza swali lingine,
“Ila mbona dada zako sikuwaona?”
“Aaaah wanapenda sana kulala ndiomana hujawaona, ila usijali kuna siku ukija utawaona tu”
“Ila najua watakuwa na upendo kama mama yenu, kuna yule mmoja nilimuona kwa mbali siku ile niliyowakuta na yule mama pale getini kwenu ila kwenu inaonekana mna upendo sana, sema natamani pia kumfahamu huyo pacha wako”
“Usijali utamfahamu tu”
“Halafu nataka awe rafiki yangu, safari ijayo nikija nitamletea zawadi yeye kwani nataka niwe nae karibu zaidi”
“Mmmh yani wewe Sarah, sikuwezi kwakweli unajitambua mwenyewe tu”
Basi mpaka walifika nyumbani kwakina Sarah ambapo naye Sarah alimuomba Erick hata akamsalimie mama yake tu kwani alijua na mama yake atafurahi sana kwa salamu ya Erick, ilibidi Erick nae ashuke na kwenda kumsalimia mama yake Sarah, basi walimkuta tu akiendelea na mambo yake mengine ndani ya nyumba yake, ila Sarah alipofika na kumtambulisha Erick kwa mama yake alishangaa kuona mama yake akifurahi sana ila alitoa machozi kwenye macho yake kitu ambacho hata Sarah hakuelewa ni kwanini mama yake alionekana kufurahi ila alilia, basi yule mama moja kwa moja alienda kumkumbatia Erick na alimkumbatia kwa muda mrefu sana huku akitoa machozi, baada ya hapo ndio alimkaribisha,
“Karibu sana Erick, karibu nyumbani kwangu”
Sarah alimuuliza mama yake,
“Mama, mbona inaonekana una furaha halafu unalia?”
“Sarah! Huwezi jua mwanangu, ila hili jina limenikumbusha mbali sana, yani mbali sana kuna siku nitakueleza vizuri. Karibu sana Erick nyumbani kwangu, karibu sana mwanangu. Muda wowote utakaojisikia kufika basi unakaribishwa”
Yani Sarah alimshangaa sana mama yake, yani jina tu ndio limtoe machozi, kwakweli Sarah hakumuelewa kabisa mama yake kwa hilo.
Basi Erick alipomaliza kusalimia alikuwa akiaga ila yule mama hakukubali Erick aondoke bila ya kula chochote kwenye nyumba yake na kumwambia,
“Naomba, ule japo kidogo tu ili utie baraka kwenye nyumba yangu. Nimekupenda bure kijana”
Muda ule yule mama alishandaa chakula na kumfanya hata Sarah aanze kumlazimisha Erick kula kidogo ambapo Erick alikaa na kula kidogo tu kisha aliaga tena na kuondoka, basi Sarah na mama yake walimsindikiza hadi nje kwenye gari yake huku wakimuaga mara mbili mbili basi Erick alipanda zake kwenye gari na kuondoka zake ila hata yeye hakuelewa ni kwanini yule mama alionekana kafurahi ila alikuwa akitoa machozi kwa wakati mmoja, na kwanini alimkumbatia kwa muda mrefu sana, kwakweli Erick hakuelewa kabisa.
 
SEHEMU YA 205

Siku hii Erick alifika nyumbani kwao akiwa ameshiba tayari kwahiyo hakuweza kula tena na mama yake alimuuliza swali moja tu,
“Umemfikisha Saraha salama”
“Ndio mama, na mama yake amefurahi sana”
“Ooooh sawa mwanangu”
Basi Erick alienda chumbani kwake ila Erica alijiuliza sana kuhusu huyo Sarah ni nani hadi mama yake amuulizie vile, muda wa kulala ni moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kumuuliza,
“Huyo Sarah ndio nani?”
“Ni rafiki yang utu wa shule, leo alikuja kumuona mama na mtoto”
“Mmmh! Jamani mbona haya mambo sijawahi kuyasikia kabla, kwani nini kinaendelea kati yako na huyo Sarah?”
“Hakuna kitu, yule ni rafiki yang utu yani mimi na yeye tumezoeana kawaida kabisa yani ile kirafiki, usinifikirie vibaya”
“Halafu inakuwaje mama aseme ulimfikisha salama? Kwahiyo ulimpeleka hadi kwao? Jamani huyo Sarah ni nani? Natamani sana kumfahamu”
“Usijali utamfahamu tu”
Basi Erica alitoka zake chumbani kwa kaka yake, na kumfanya Erick achukue simu yake ambayo alikuta namba za Sarah zimempigia sana, ikabidi nay eye ampigie,
“Nilikuwa nauliza Erick umefika?”
“Ndio nishafika, ila na mimi nilikuwa na swali”
“Niulize tu”
“Mbona mama yako alikuwa akilia?”
“Hata mimi najiuliza sijui kwanini, ila usijali nitampeleleza na ataniambia ukweli tu.”
“Sawa, ila mama yako ni mtu mzuri sana hata mimi nimekupenda”
“Kama yeye alivyokupenda ujue, yani mama kakupenda sana Erick. Basi kesho kama kawaida kwenye siti yetu ile”
“Sawa, usiku mwema”
Erick aliagana na Sarah kwani hakuwa na maongezi naye sana wala nini.

Kulipokucha kama kawaida waliondoka wote na kwenda kwenye shughuli zao hata baba Angel aliondoka pia ila baada ya muda kidogo alirudi kwa lengo la kuwachukua Angel na Junior kwenda nao huko kwenye chuo cha yule madam.
Basi aliondoka nao na kuwasiliana na yule madam hadi kwenye kile chuo, ambapo Angel na Junior walipelekwa kwanza kuzoea mazingira, huku madam akiongea na baba Angel,
“Kwanza madam samahani sana kwa kukupigia simu usiku”
“Unadhani kuna tatizo basi! Mimi mwenyewe bachela, sijaolewa wala nini”
“Kheee hujaolewa madam! Nilijua wewe ni mke wa mtu?”
“Hapana sijaolewa, wanaume wenyewe nyie hamueleweki”
“Aaaah jamani, wengine tunaeleweka”
“Sema wewe unaeleweka sio wengine, usione hadi leo nipo hivi nishapitia milima na mabonde ya mahusiano hadi nilikuwa chizi mimi ila kwasasa nimechoka nikasema acha niishi mwenyewe, hata usijali wewe nitafute muda wowote tu mimi napatikana. Ukiona nipo hotelini au kwenye mgahawa basi ujue nimeenda mwenyewe tu kushangaa shangaa na kupoteza muda maana sina hata wa kunitoa matembezi”
Kuna muda baba Angel alimuangalia huyu madam na kumuhurumia kwani alikuwa ni mzuri tu hata alishangaa jinsi anavyolalamika kuwa mapenzi yamemtenda sana, ila bado alimpa moyo,
“Ila usikate tamaa madam maana mume wako yupo mahali anaandaliwa kwahiyo usijali”
“Jamani huyo mume anaandaliwa hadi lini? Na mimi mwanadamu ujue na nina mahitaji yangu muhimu ya kimwili, sasa huyo mume wanaandaliwa tu, watu hadi tutakufa na utamu wetu”
Baba Angel alicheka ila aliamua kubadili stori kwani aliona stori zile zinaweza kupelekea katika mambo mengine, kwahiyo aliona ni vyema kwa muda huo kubadili stori tu,
“Madam, hapa nimeleta hao vijana wangu wawili ila nahitaji uangalifu wako mkubwa sana kwa hao watoto si unajua dunia imeharibika hii”
“Usijali kitu, walimu hapa wapo vizuri sana, muda mwingi mimi nashinda kule shuleni kwakina Erick maana ndio ninakofundisha halafu mimi ndio mwalimu wa taaluma”
“Oooh upo vizuri sana madam, nimefurahi sana”
“Ila hujaniambia kuwa wewe napaswa muda gani kukupigia simu na muda gani sipaswi kukupigia simu!”
Baba Angel alicheka kidogo na kumwambia,
“Kwa matatizo ya watoto hakuna tatizo nipigie tu muda wowote ila sio usiku maana nakuwa nimelala halafu mimi nina mke”
“Ooooh sawa, hakuna tatizo”
Basi baba Angel muda huu na yule madam walikuwa wamesimama nje ya gari kwani baba Angel alikuwa akiwasubiria watoto wake waonyeshwe kidogo mazingira na aondoke nao kwa siku hiyo halafu kesho ndio waende kuanza kwenda shule, basi akiwa anaongea na yule madam alishangaa sana kwa muda huo kutokea Sia, ambaye alipowaona alicheka sana na kutikisa kichwa halafu akasema,
“Unajua Erick hiyo tabia nilijua umuiacha, kumbe bado unayo! Nicheke mie, mbona Erica ana kazi sana jamani!”
Kwakweli baba Angel alitamani hata kumnasa vibao huyu mwanamke.

Basi baba Angel muda huu na yule madam walikuwa wamesimama nje ya gari kwani baba Angel alikuwa akiwasubiria watoto wake waonyeshwe kidogo mazingira na aondoke nao kwa siku hiyo halafu kesho ndio waende kuanza kwenda shule, basi akiwa anaongea na yule madam alishangaa sana kwa muda huo kutokea Sia, ambaye alipowaona alicheka sana na kutikisa kichwa halafu akasema,
“Unajua Erick hiyo tabia nilijua umeiacha, kumbe bado unayo! Nicheke mie, mbona Erica ana kazi sana jamani!”
Kwakweli baba Angel alitamani hata kumnasa vibao huyu mwanamke.
Hadi Oliva aliona jinsi sura ya baba Angel ilivyobadilika hadi akamuuliza,
“Kwani unamfahamu huyu mwanamke?”
Sia nae akadakia na kusema,
“Asinifahamu kwanini? Mimi ndio mkewe wa kwanza kama ulikuwa hujui”
Oliva alizidi kushangaa halafu baba Angel pia alizidi kuwa na hasira kupita maelezo, mara Junior na Angel walifika pale maana walishaelekezwa na kesho yake ndio walikuwa wanatakiwa kuanza, basi baba Angel akaona ni vyema aondoke na watoto wale tu maana la sivyo ataweza kuanza kuharibiana siku zizuri na yule mwanamke, ikabidi wakina Angel nao waingie kwenye gari hata hawakuelewa ila baba yao aliondoka gari sema kitu pekee walichojiuliza ni kuhusu yule mwanamke aliyekuwepo chini kweani walishawahi kumuona wakati gari imegoma halafu Erick alikuwa na hasira nae sana, na leo ni baba yao halafu pia Angel alishawahi kumshuhudia huyu mwanamke akinaswa kibao na Samir kwahiyo kuna mambo hakuelewa kabisa.
 
SEHEMU YA 206

Kwakweli hata madam Oliva alibaki akishangaa tu kwani baba Angel alionekana kuchukia sana na hakuongea kitu kingine chochote zaidi ya kuwaambia wanae wapande kwenye gari na kuondoka nae, ila hapo aliposimama madam Oliva basi nae Sia aliendelea kusimama na kumfanya Oliva amuulize kwa makini zaidi,
“Unajua dada sijakuelewa vizuri, ulikuwa mke wa yule baba kivipi?”
“Sikiliza nikwambie, mimi ndiye nilikuwa mke wa yule, unajua yule anaitwa Erick, kama uliwahi kumsikia mwanae mmoja aitwaye Erick, Erick basi ndio mtoto ambaye nimezaa nae ila mtoto yule haujui ukweli kuwa mimi ndiye mama yake mzazi na ananikataa hadi kecho”
“Kheee makubwa, huyo Erick ni mwanafunzi wangu”
“Kumbe!! Anasoma shule gani kwasasa?”
Yule madam akamtajia bila kujua hilo ni jambo baya kwani huyu mama anamfatilia sana Erick, ila yeye alimtajia kwa uzuri tu, kisha Sia akaendelea kumwambia,
“Unajua wewe ni mwanamke nadhani unaweza ukanielewa kidogo tu juu ya haya nitakayokueleza, mimi na huyu Erick tumeishi kama mke na mume na mambo mengi sana tumeshauriana. Kwetu walimfahamu wote na kwao walinifahamu yani hakuna ndugu yake asiye nifahamu na hakuna ndugu yetu asiyemfahamu ila Erick aliamua kuniacha gafla na kuwa na yule mke aliyemuoa, kwakweli unaweza kujua ni jinsi gani niliumia, mimi kweli wa kuachwa naye? Nimemvumilia Erick mimi kwa shida na raha, nikiamini kuna siku nitakula nae raha za maisha, nilikuwa namfumania mimi na wanawake mara zote namsamehe, Erick alikuwa ni mlevi hakuna mfano, anaenda huko analewa hadi anajitapikia ila mimi naenda kurua nguo zote alizozitapikia, kusaisha chumba chake, nampikia supu yani kila cha kumfanya arudi katika hali ya kawaida, hebu fikiria nimetumia muda wangu wa kiasi gani kwaajili ya penzi lake? Naomba tu ufikirie na useme kama nimekosea kukwambia ukweli hapa”
“Ila mbona umesema Erica ana kazi?”
“Nimehisi anakutongoza pia, maana huyu mtu kwa kutongoza wanawake ndio zake, huyo Erica ndio mke wake, ila kiukweli nakwambia Erica bado hamjui Erick, kwakweli Erica hamjui Erick ninayemjua mimi ila ipo siku huyu Erica atamjui Erick ni mtu wa aina gani? Kama alikuwa akiona wenzie wanateseka kwenye ndoa basin a yake ipo njiani kuteseka, mimi nimekwambia ukweli ili kama una mpango wa kumkubali ujue jambo hilo. Nimemaliza”
Basi Sia aliondoka na kumuacha Oliva akimshangaa hadi mwisho wa safari.
Basi Oliva alimuangalia sana Sia hadi alipoishia kisha alianza kujiuliza mwenyewe,
“Mwanaume kamfanyia vitu vya ajabu, alikuwa mlevi, alikuwa na wanawake anamfumania nao ila bado alimsamehe, sasa mwanaume kaoa mwanamke mwingine ila bado anamzungumzia inaonyesha kuwa bado anampenda tena sana tu, mmmh huyu Erick ana kitu gani? Lazima kuna kitu cha ziada anacho sidhani kama ni pesa tu ila kuna kitu huyu Erick anacho kwanini huyu mama aongee kama mtu aliyechanganyikiwa ilihali anaonekana kuwa na akili timamu? Lazima kuna kitu cha ziada ambacho Erick anacho, natamani kukifahamu, sitaki kufahamu ukweli kuhusu mtoto wao sijui watoto wao watajijua wenyewe ila nataka kufahamu kuhusu huyu baba ana kitu gani cha ziada ambacho wanaume wengine wamekosa? Nitajua tu, mimi ndio Oliva bhana”
Basi yule madam alienda zake kwenye ofisi zake moja kwa moja kuendelea na mambo yake.

Baba Angel moja kwa moja aliwapeleka Angel na Junior nyumbani na baada ya kuswashusha tu, yeye aliondoka tena kwakweli Angel na Junior hata hawakuelewa kwanini, wakaingia ndani ambapo walipoingia tu Angel alidakwa na mama yake na kuanza kuulizwa maswali,
“Mmerudi na nani sasa?”
“Baba ndio katurudisha”
“Mbona hata hajaingia ndani?”
“Sijui mama kwanini ila katushusha tu na kuondoka zake”
“Jamani baba Angel mara nyingine sijui vipi, ngoja nitampigia simu. Ila chuo hiko kizuri alichowapeleka? Mmekipenda?”
“Eeeeh ni pazuri mama, waliokuwepo wanapasifia halafu hata mazingira yake ni mazuri”
“Oooh nafurahi kusikia hivyo”
Kisha mama Angel alirudi ndani kwa mtoto maana alikuwa analia, basi alimchukua mwanae na kuanza kumnyonyesha huku akiongea na mama yake,
“Ila mama, uzazi wa sasa nimeufurahia sana, kumbe kuzaa mtoto mmoja kuna raha yake. Mapacha nao raha yao wakikuwa jamani, yani wakiwa wadogo hadi unapata kizunguzungu”
Basi mama yake akacheka na kumwambia,
“Ndio kuna raha sana ya kuwa na mtoto mmoja, ila kipindi kile una mapacha kuna muda nilikuwa nakuona unatamani kulia, ukinyonyesha huku na huyu anataka halafu kuna muda wote wawili wanataka ziwa moja ndio pale unapata kichaa, wakianza kutambaa ndio wanaanza mabalaa zaidi”
“Oooh mama, yani nilikuwa Napata kiwewe, ila Erick wakati mdogo alikuwa mtundu sana hadi nilikuwa nahisi uchizi, unamkataza hili anashika lile, unamkataza lile anarudi kwenye hili huku dada yake anafanya uharibifu tu. Hivi mtu umelea watoto wako kwa shida hivyo halafu mtu anatokea kirahisi tu anakwambia hawa watoto sio wako”
“Mmmmh kivipi mwanangu? Yani umlee Ester hapo halafu mtu aseme sio mtoto wako?”
“Huwa inatokea hiyo mama, hujawahi kusikia? Tuachane na habari hizo, hivi mama swali hili nimewahi kukuuliza zamani nab ado nitaendelea kukuuliza, hivi Derick ni kweli alikuwa mtoto wa baba?”
“Ndio, kwanini unauliza hivyo?”
“Jamani, ukoo mzima hatufanani na matendo ya Derick”
“Huwezi jua labda katoa kwenye ukoo wa mama yake huko ila ndio hivyo Derick ni ndugu yenu, tena mlifatana tu kuzaliwa wewe na Derick, yani usikatae katika ukoo hamuwezi wote mkafanana tabia lazima kuna mmoja anakuwa na tabia zake na mambo yake ya ajabu ajabu. Ila bado siri ya mtoto anayo mama yani mama ndio anajua mtoto ni wa nani, ila nimejaribu kumuelewa mama Derick maana hadi mwisho anadai kuwa yule mtoto ni wa baba yenu kwahiyo usikatae ni ndugu yako”
“Mmmmh sawa mama, ila kuna vitu nilikuwa na mashaka sana juu ya Derick”
“Kama vitu gani? Ila kuna kitu nahisi kipo kati yako na Derick ila hujawahi kuniambia mama yako sababu ya usiri wako, kuna kitu hata mimi nahisi, nakumbuka vizuri siku umerudi sijui mlienda kwenye madawa ya kienyeji na dada yako, nakumbuka vizuri ingawa kuna mambo sikuelewa. Erica, kwakweli wewe umenificha mengi sana mama yako, ndiomana kuna muda huwa nakwambia kuwa usimshangae sana mwanao Angel, maana kuna mambo kachukua kwako kama kuwa msiri sana, ila usiri wenu hauna maana, mimi nampenda sana huyu Erica mdogo jamani mtoto hana siri huyu na atafanya tutambue mambo mengi sana. Haya nidokezee mwanangu leo ya kuhusu wewe na Derick, unajua huwa nasikia juu juu sijui ulitoa mimba yake sijui nini na nini kiukweli huwa sielewi”
“Mmmmh mama, naomba tuachane na hayo na tujadiliane vitu vya msingi, yalishapita hayo”
Mama Angel hakupenda kukumbusha mambo ya zamani ambayo yalipita na yalimuumiza sana kwahiyo hakupenda kuyakumbushia.

Muda huu baba Angel moja kwa moja alienda nyumbani kwa dada yake, na kweli alimkuta dada yake na kuanza kuongea nae, yani kilichompeleka kwa dada yake lilikuwa ni swala zima la Sia, kwahiyo alienda kwa dada yake ili ajue cha kufanya,
“Karibu sana Erick, naona leo umenikumbuka”
“Si oleo tu, mimi huwa nakukumbuka siku zote, ila leo nimekuja sababu ya matatizo kidogo”
“Yapi hayo?”
“Kiukweli kuna huyu mwanamke aitwaye Sia, yani sijajua cha kufanya nae au ni kitu gani anahitaji kutoka kwangu unajua sasa kaja kwa kasi ya ajabu na pia naona kama atavuruga amani ya nyumba yangu na anaweza kumvuruga mke wangu pia, kama unavyomjua wifi yako ni mgumu sana kuchuja mambo yani yeye anaweza kuchukulia mambo kama anavyoambiwa, kwakweli huyu Sia ananiumiza kichwa sana”
“Kivipi kaka, unajua sikuelewi, huyu Sia anakuumiza vipi kichwa?”
Basi baba Angel aliamua kumueleza tu kwa kifupi matukio ambayo Sia anayafanya, maana kuna mengine Tumaini hakuyaelewa, basi alimueleza pia la kuhusu Erick na pia kuhusu duka na jinsi ambavyo alimkuta siku hiyo,
“Ni wazi kuwa huyu mwanamke anafatilia kila njia ninayopita kwenye maisha yangu, nahitaji kujua anataka kitu gani kwangu? Kwanini ananifanyia hivi, kweli kabisa nisiishi kwa amani sababu yake jamani eeeh!!”
“Pole mdogo wangu, pole sana hata sikutambua hayo! Hivi huyu Sia ana matatizo gani jamani, ni kuchanganyikiwa au kitu gani na kama ni kuchanganyikiwa basi kitu gani kilichomchanganya hiko? Yani kwanini awe hivyo jamani, mbona Sia hakuwa hivyo! Loh!! Amenisikitisha sana kwakweli, ila kaka nakuahidi kuwa nitafanyia kazi hilo swala maana nina mawasiliano yake kwahiyo usijali mdogo wangu”
“Nitashukuru kwa hilo, yani huyu kiumbe ananikosesha amani ujue, sina amani nikimuona wala sina furaha, mwambie aniache na familia yangu nifurahie kama siku zote. Nimeishi na mke wangu na watoto wangu kwa upendo sana siku zote wala sikuwahi kupatwa na maswahibu yake, nakuomba sana dada yangu nisaidie kwa hilo”
“Usijali”
Basi baba Angel aliaga na kuondoka zake, ila muda huu alimua kupitia dukani ili amchukulie mke wake zawadi ingawa hakusema ni zawadi, aliona duka moja la nguo na vitu vya urembo kwa wanawake, aliamua kuingia kwenye duka hilo na kukutana na mwanamke na mwanaume wakihusika kuuza duka hilo, basi aliwasalimia pale na kuanza kuongea ongea nao kama ushauri wa zawadi ya kumpelekea mke wake, basi yule mwanaume akamshauri,
“Mpelekee gauni”
“Kheee gauni?”
“Ndio, tena hilo hapo ni zuri sana natumai atalifurahia”
Basi mwanamke akadakia,
“Unaonyesha tu hilo hapo unajua mke walivyo jamani! Gauni litamtosha kweli hili, eti kaka mkeo yukoje kwani?”
“Mmmh mwili wake hauna tofauti na wako ila wewe umemzidi kidogo unene”
“Oooh basi hili gauni alilokuonyesha baba Emma litamtosha”
“Basi nitoleeni”
Baba Emma alilitoa lile gauni, kweli lilikuwa ni zuri sana na linavutia machoni ila tu baba Angel hakujua kama kweli mkewe angelipenda hilo gauni, basi alipolilipia yule mwanaume akamwambia mwanamke,
“Mama Emma, mtolee risiti basi”
Ndipo baba Angel alihisi kama wale ni mke na mume, basi aliuliza,
“Kumbe nyie ni mke na mume?”
“Ndio, sisi ni wanandoa”
“Oooh inapendeza sana kufanya kazi pamoja, nimeipenda hii”
Na wao walicheka tu kwa jinsi yeye alivyofurahi, basi baba Angel alichukua ule mzigo wake na kuwaambia,
“Jamani nampelekea mke wangu, akiipenda hakika basi hili ndio litakuwa duka langu kumchukulia zawadi kwasasa”
Walifurahi sana na baba Emma alimkaribisha sana pale dukani na baba Angel aliondoka muda ule kiukweli aliondoka na tabasamu ingawa siku yake hiyo iliharibiwa na Sia ila kwa muda huo alijikuta akiwa na furaha na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 207

Baba Angel alipofika tu nyumbani, moja kwa moja alienda chumbani ambapo mke wake nae alienda na swali la kwanza alimuuliza,
“Kheee na leo ulienda wapi yani ile kushusha mizigo tu na kuondoka, ulienda wapi?”
“Jamani mke wangu! Unataka kunilaumu sasa, unadhani mimi niende wapi? Wivu ushakuanza hivyo”
“Wivu lazima kwa mtu ninayekupenda kama wewe, nisipokuonea wewe wivu nimuonee nani tena!”
“Haya, ni hivi niliporudi na wakina Angel niliitwa ofisini ila nilipotoka kidogo tu nikakumbuka kuwa sijakuchukulia zawadi mke wangu kwa siku za hivi karibuni kwahiyo nikaamua kupita kwenye duka moja hivi na kukuchukulia zawadi hii”
Alimpa mama Angel ule mzigo ambapo alifungua kwakweli alionekana kufurahi sana na kujaribisha muda ule ule, na alipomaliza alimsogelea mume wake na kumkumbatia huku akimwambia,
“Jamani jamani, nimeipenda hii zawadi sijui nikwambiaje? Unajua nimekaa nikawaza kuhusu gauni la mtindo huu hata nisijue pa kulipata, jamani mume wangu umejuaje? Kwakweli nimefurahi sana, kweli Erick unanifaa”
Baba Angel nae alifurahi kuona mkewe kafurahia ile zawadi maana ndio kitu alichokuwa akikihitaji kumuona mkewe akifurahia zawadi aliyompelekea.
“Asante sana mume wangu, oooh kwa bahati mbaya chakula cha leo kimeshapikwa na usiku tayari ila niambie kesho unahitaji kula chakula gani?”
“Yani wewe mke wangu kwa kutenda mambo kwa matukio sikuwezi, haya nahitaji pilau”
“Sawa, nitapika mwenyewe hakuna tatizo”
“Ila mke wangu si bado upo kwenye uzazi jamani! Usitake kuniletea makubwa na mama mkwe, cha kufanya mwambie mama apike”
Walianza kucheka kwa pamoja na siku hiyo ikawa ni furaha sana kwa upande wao.

Leo Angel alikuwa akiwasiliana na Samir kuhusu mambo mbalimbali ila kuna muda Samir alimtafuta Angel na kumwambia,
“Yani Angel kuna kazi kidogo nafanya ila nahitaji kuongea nawe kwa muda kidogo ili tupange mambo yetu”
“Sawa hakuna shida, kwahiyo utanitafuta muda gani?”
“Kwenye saa sita usiku basi nitakupigia ili tuongee Angel, kumbuka nakupenda sana”
Basi Samir alikata simu na muda huo ilikuwa ni saa tatu usiku, na sio kawaida ya Samir kusema kuwa anakazi kwa muda huo basi Angel alijiuliza mno kuwa itakuwa ni kazi gani kwa muda huo ila hakupata jibu kabisa, baada ya nusu saa alipigiwa simu na Mussa na kuanza kuongea nayo ila kwa sauti ndogo sana ili asisikike kabisa hata na mtu anayepita nje ya chumba chake,
“Oooh Angel unaongea sauti tamu sana, kwakweli una sauti nzuri sijapata sikia duniani”
“Mmmmh jamani Mussa!”
“Ndio hivyo Angel ila mbona siku hizi mara nyingi hupokei simu zangu wala jumbe zangu huzijibu?”
“Unajua nini, kiukweli mimi nina mahusiano na Samir, na siku ile hajapenda kabisa na kasema nisiwasiliane tena na wewe”
Mussa akacheka kidogo na kusema,
“Hivi Angel, huyo Samir unamfahamu vizuri wewe! Mimi na Samir ni ndugu siwezi kumsingizia kwa chochote ila Samir hakufai kabisa”
“Kwanini?”
“Samir ni muhuni sana Angel, yani Samir sidhani kama kuna mwanamke huwa anaacha kumpitia, sikai nyumba moja na Samir ila namfahamu alivyo, haya leo umewasiliana nae?”
“Ndio ila kasema kuna kazi anafanya muda huu na atanitafuta saa sita”
“Oooh pole sana Angel, mwenzio Samir yupo na mwanamke muda huu. Nimemshuhudia kwa macho yangu maana leo nipo kwao, siku ukifika kwakina Samir utaelewa ni maisha gani wanaishi, maisha yao ni ya kujiachia sana kiasi kwamba Samir hufanya anachojisikia yeye, pole Angel muda huu Samir yupo na mwanamke ndiomana kasema atakutafuta saa sita”
“Jamani kumbe Samir ndio muongo hivyo!! Basi inatosha Mussa naomba nilale tu kwa muda huu”
Yani Angel alijikuta amechukia sana, hivyo aliamua kuzima simu kabisa na kulala tu kwani alijikuta kuwa na hasira.

Yani toka siku ambayo Vaileth alibambwa na Erica, alijikuta akikosa amani kabisa kwenye moyo wake, hivyo siku hiyo karibia na muda wa kulala aliamua kwenda chumbani kwa Erica ili kuongea nae.
Alimkuta Erica akiwa ananyoosha sare zake za shule,
“Kheee mdogo wangu Erica leo umechelewa kunyoosha nguo?”
“Nimechelewa kweli, ila yote hii ni uvivu, yani leo nimetoka shule na kuona uvivu kabisa, nikajikuta nimelala kwa muda mrefu”
“Ndiomana sikukuona na wenzio, nikusaidie basi mdogo wangu”
Erica alimpa pasi na Vaileth alianza kunyoosha nguo za Erica, huku Erica akitabasamu tu na kukaa kitandani kwake akiendelea kupanga daftari zake, yani kwa siku hiyo Erica alionekana kujishughulisha sana basi Vaileth alipomaliza kunyoosha nguo za Erica hata Erica nae alionekana kumaliza kupanga daftari zake, basi Vaileth alianza kuongea nae,
“Mdogo wangu Erica, kwanza kabisa naomba msamaha kwa kile ulichokikuta chumbani kwangu, hakuna chochote kinachoendelea kati ya mimi na Junior tafadhari usimwambie mama”
“Dada sikia, mimi naweza kuwa mtoto mdogo ni kweli bado mdogo ila kuna mengi sana nayatambua na kuyajua kwani siku hizi tunajifunza vitu vingi sana. Sijui ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea kati yako na Junior ila ninachojua ni kuwa nilimkuta chooni kwako na pia alikuja kunikataza nisiseme na leo umekuja wewe kunikataza nisiseme”
“Sio hivyo mdogo wangu, jaribu kunielewa jamani Erica”
“Ila dada mbona nimekuelewa jamani, una wasiwasi wa bure tu ila mimi nishakuelewa sana tu hata usiwe na wasiwasi. Mimi ni mbea kweli ila hilo sijamwambia mama na wala sitomwambia sababu niliyonayo ni moja tu?”
“Ipi hiyo mdogo wangu?”
“Unajua nakuhurumia sana, kuna siku niliwahi kuona ukimsimulia mama kuhusu maisha ya kwenu kwakweli nilikuonea huruma sana, na mimi sitopenda wewe ufukuzwe kwasababu yangu, ilimradi umeacha ushirikina basi sina tatizo na wewe ila kuna jambo moja tu ngoja nikwambie dada yangu”
“Jambo gani hilo?”
“Unajua sababu ya baba kumchukua Junior aje kuishi hapa?”
“Sijui”
“Sawa, najua mambo mengi ya Junior umesikia kwa familia hapa wakiongelea, ila swala la baba kumchukua Junior lilikuja baada ya kumkuta Junior ameingia guest na mwanamke, tena mwanamke mwenyewe alikuwa ni mkubwa kushinda hata mama yake yani mama yetu mkubwa, kwakweli baba alisikitika sana ndiomana alimchukua Junior”
Kidogo Vaileth alishtuka na kuona kuwa kutembea na wanawake wakubwa kupita umri wake ni kawaida ya Junior, kwakweli kwa upande mwingine roho ilimuuma kiasi kwamba alishindwa hata kumjibu Erica na kujikuta tu kajiinamia, basi Erica akamuuliza,
“Mbona umepooza gafla dada yangu?”
“Aaaah hamna kitu”
“Basi nikuombe kitu kwa leo dada”
“Kitu gani?”
“Naomba kwa leo ulale humu chumbani kwangu tafadhari, mimi sitakusemea kwa mama kuhusu lile swala”
Vaileth akafikiria ila hakuwa na budi zaidi ya kukubali tu kulala na Erica mule chumbani kwa Erica, yani siku hiyo alilala kwa mawazo sana kwani alijua lazima Junior alikuwa akimngoja chumbani kwake.
Mpaka kulivyokucha wakati Erica akijiandaa ndipo na yeye alipoamka na kwenda kuanza kazi zake za siku hiyo.
 
SEHEMU YA 208

Moja kwa moja Vaileth alienda jikoni na kuanza kufanya kazi halafu kuanza usafi ila alishangaa kumkuta Junior sebleni akisinzia, yani inaonyesha Junior alimtafuta sana usiku wa jana, ila hakuweza kuongea nae kivile kwani muda huo kila mmoja ndani alikuwa kaamka na anajiandaa kwa mambo ya siku hiyo.
Basi mama Angel nae alitoka na kumkuta Junior pale sebleni akamshtua,
“Kheee Junior, vipi mwanangu leo una nini?”
Junior akashtuka pale na kumsalimia mama yake mdogo kisha moja kwa moja kuinuka pale kwenye kochi na kuelekea chumbani kwake, yani alipitiwa na usingizi pale ila lengo kubwa la kukaa pale ni kumuona Vaileth akiingia maana alihisi kuwa Vaileth alikuwa nje ya nyumba hiyo kwa siku hiyo na kumfanya hata yeye aumie sana moyo.
Basi mama Angel akiwa pale sebleni kwake, alishangaa kusikia simu ya mezani ikiita na kujiuliza,
“Asubuhi yote hii jamani nani tena anapiga?”
Moja kwa moja alienda kupokea ile simu na kuongea nayo,
“Mbona leo Angel hupatikani, tatizo ni nini?”
“Kheee nani wewe?”
Simu ile ikakatika na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa Angel hapatikani kivipi? Wakati anatambua wazi kuwa mwanae hana simu! Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kufungua mlango ila alimkuta binti kajiinamia, alipomuinua kichwa aligundua kuwa Angel alikuwa akilia.

Simu ile ikakatika na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa Angel hapatikani kivipi? Wakati anatambua wazi kuwa mwanae hana simu! Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kufungua mlango ila alimkuta binti kajiinamia, alipomuinua kichwa aligundua kuwa Angel alikuwa akilia.
Ikabidi mama Angel akae pia karibu na mwanae na kumuuliza kwa makini kitu kinachomfanya alie,
“Wewe Angel nini kinakuliza mwanangu?”
“Mama, kichwa kinaniuma sana”
“Jamani Angel yani kichwa kinakuumza ndio unakazana kulia badala ya kuja kuniambia! Haya jiandae hapo nimpigie baba yako akupeleke hospitali”
Angel aliinuka na mama yake alikuwa akimsaidia kujiandaa, kiukweli Angel hakuwa akisumbuliwa na kichwa wala nini ila alizna kusumbuliwa na swala zima la mapenzi kwani moyo wake uliuma sana baada ya kusikia kuwa Samir ana mwanamke mwingine na ndiomana alisema kuwa kuna kazi anafanya, basi mama Angel alipomaliza kumsaidia Angel kujiandaa muda huo alienda kumpigia simu baba Angel ambaye alikuwa katoka ili ampeleke Angel hospitali.
Basi Angel alibaki ndani kwake na kujiuliza kuwa atapima nini hospitali wakati haumwi kweli? Aliwaza ila mama yake alirudi muda huo na kumwambia baba yake anakuja muda sio mrefu kwahiyo Angel alitoka sebleni kumsubiri.
Baada ya muda kidogo tu baba Angel alifika maana huyu baba alikuwa akisikia mtoto anaumwa basi akili yake ilichanganyikana kabisa kabisa, akafika na kumchukua Angel na kuondoka nae kwenda hospitali huku njiani akimuhoji maswali kadhaa,
“Hiko kichwa mwanangu kimeanza muda gani?”
“Tangia usiku baba ila asubuhi ndio nikaona kama kinazidi, ila muda huu kimepoa”
“Ooooh ila hata kama kimepoa, lazima twende hospitali. Ngoja nikupeleke kwa rafiki yangu ni daktari mzuri sana”
“Sawa baba, ila kwasasa kichwa kimepoa kabisa”
“Hata kama mwanangu, hospitali ni lazima”
Ikabidi Angel awe mpole tu maana kayataka mwenyewe na kwajinsi mama yake alivyosema kuwa Angel anaumwa basi baba yake ilimlazimu tu amfikishe hospitali na kumpima kabisa hata kama anasema kuwa amepona.

Baba Angel alifika na mwanae hospitali, moja kwa moja alisogea karibu na chumba cha daktari ila alikuwa na mgonjwa na baada ya muda kidogo yule mgonjwa alitoka ila Angel alimuangalia sana yule mgonjwa na kugundua kuwa ni mwanafunzi aliyewahi kusoma nae kwenye ile shule ambayo alihamishwa, basi baba yake aliingia nae mule kwa daktari ambapo baba yake na yule daktari walianza kusalimiana huku baba Angel akimtania daktari,
“Mmmh kuna binti mdogo ndio nimepishana nae katoka humu, ila ugonjwa unaonekana kama yale magonjwa yetu ya kipindi kile, vipi na yule?”
“Aaaah yule, tushamaliza mchezo”
“Khaaa usiniambie bhana, hujaacha tu!!”
“Ndio kazi yangu mjini hapa, ila mimi nipo vizuri kaulize wote niliowahi kuwafanyia miaka hiyo kama hawana watoto kwasasa? Mimi nipo vizuri na najiamini”
“Ila yule binti ni mdogo?”
“Aaaah na mwanaume wake mwenyewe ni mdogo pia, kaja kali alia hapa, ikabidi niwadai kiasi kidogo tu, halafu wanafunzi hawa wajinga sana siku hizi”
Kisha daktari akamuangalia Angel na kumwambia,
“Soma mama, usitutie aibu wazazi wako, wewe bado mdogo. Mapenzi yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, wewe soma. Nadhani umenisikia, haya unasumbuliwa na nini?”
“Ni kichwa ila kwasasa kimepona”
Basi yule daktari akampima pima vitu baadhi ila aliona ni vyema apate muda kidogo wa kuzungumza na Angel, basi alimuomba baba Angel awapishe kidogo,
“Hebu nipishe kidogo na mgonjwa wangu”
“Mmmmh usianze mambo yako, mwanao huyo ujue!”
“Aaaah na wewe jamaa huniamini!! Ningekuwa sio mtu mzuri basi ningepita na mkeo, yule alikuwa chombo halafu alikuwa rika langu, sasa nianze kuhangaika na watoto wetu jamani! Nitakuwa sina akili basi!”
Baba Angel alitoka nje na kumuacha daktari akiongea na Angel pale ofisini,
“Eeeeh kichwa kilianzaje kuuma?”
“Mmmh ila daktari usimwambie baba”
“Simwambii, nieleze tu kichwa kilianzaje kuuma?”
“Sijui ni sababu nililia sana, mimi nina mpenzi wangu ila nimeambiwa kuwa ananisaliti”
“Angel, wewe ni binti mdogo sana nan i mapema mno kuanza kujihusisha na maswala ya mapenzi, mbona umeanza kulia mapema hivyo! Ukifika miaka thelathini wewe si ndio itakuwa balaa! Mapenzi ni matamu sana ila ukianza kwa muda sahihi ingawa bado kuumizwa kupo pale pale hata uwe na miaka hamsini, ila ninachoongelea hapa mwanangu wewe bado ni mdogo sana mambo ya mapenzi usijihusishe nayo”
“Ila nampenda”
“Ni kweli unampenda, umesikia anakusaliti, hujashuhudia kumbuka ila umesikia na umeumia hivyo je siku ukishuhudia kwa macho yak ohayo itakuwaje? Haya hilo sio tatizo sana, ila bado unasoma je siku ukibeba mimba ya huyo mtu itakuwaje? Nadhani na wewe umemuona binti aliyetoka humu, nimetoka kumtoa mimba yule, unajua madhara ya kutoa mimba? Unaweza usizae maisha yako tena na unaweza ukapoteza maisha. Kitu cha msingi hapa ninachotaka kukwambia ni kuwa, huyo mwanaume anakuzalisha halafu anakuacha kwenye mataa yani unabaki ukishangaa tu, mbele husongi wala nyuma hurudi, hivi unadhani ukizalishwa nani atakutaka tena!! Hakuna kitu kinachoshusha thamani ya mwanamke kama kuzalia nyumbani tena na mtu asiyeeleweka, kwanza thamani yako inashuka na uzuri wako unapungua, kuna watu wa maana watakuwa wanakuhitaji kwa kipindi hiko ila wakijua kama una mtoto basi watakukimbia. Sasa kwanini uharibu maisha yako kwa starehe ya muda mfupi, kitu gani hupati kwenu Angel? Nina uhakika unapewa kila kitu unachohitaji, sasa huyo mwanaume anataka kukulaghai kwa kitu gani? Kwa mapenzi ya dhati, je baba yako hakupendi? Mama yako hakupendi? Mapenzi yapo na hayaepukiki ila ni bora kuyangoja katika wakati sahihi ila sio sasa Angel. Una umri gani kwanza?”
“Miaka kumi na sita”
“Ooooh jamani Angel kumi na sita!! Wewe bado mdogo sana Angel, usiwaze mapenzi mwanangu, yatakuumiza tu kwasasa. Zingatia elimu ndio jambo la msingi kwasasa katika maisha yako, wanaume huwa tupo tu”
Basi yule daktari alijitahidi pale kumwambia Angel maneno ya busara na kweli kwa kiasi kikubwa sana Angel alielewa na hapo daktari alimuita tu baba Angel ili kuondoka na mwanae, baba Angel aliuliza,
“Sasa mwanangu anasumbuliwa na nini?”
“Oooh ana msongo wa mawazo huyo anakaa sana nyumbani, hebu uwe unampeleka peleka kidogo kutembea mtoto”
“Asante kwa ushauri ndugu yangu”
Waliagana pale, kisha baba Angel aliondoka na mwanae ambapo kwenye gari alimuuliza kama siku hiyo anaweza kwenda kusoma kozi ya kompyuta, naye Angel alikubali kwani kiukweli hakuwa na ugonjwa wowote ule ila alijigelesha kwa mama yake kwani hakutaka kumwambia kitu kinachomliza.
Baba Angel alifika nyumbani na kumtaka Junior nae ajiandae halafu aliwapeleka chuo ila aliwataka muda wa kurudi wakodi tu usafiri wa kuwarudisha nyumbani maana alikuwa na mambo mengi ya kufanya kwa siku hiyo kwahiyo hakudhani kama ataweza kuwafata.
Alipowafikisha chuoni, yeye akaondoka zake.
Ila akiwa njiani alimuona Sia akiwa anavuka barabara, alitikisa kichwa tu, alitaka kusimama ila hakuona kama ni vyema kwani Sia mwenyewe akili zake alikuwa akizijua mwenyewe kwahiyo baba Angel hakusimama wala nini ukizingatia hakutaka hata kufahamu kwa muda huo Sia alikuwa akielekea wapi.
 
SEHEMU YA 209

Sia alikuwa akielekea mahali ambapo alipanga kukutana na Tumaini, na kweli walionana na kuanza kuzungumza mambo mawili matatu yani Tumaini hakutaka kukutana nae nyumbani kwake kwahiyo alimpigia simu na kumtaka kuwa wakutane mahali na ndio huko walipokutana, Sia alianza kumwambia kumbe aliliona gari la baba Angel wakati likipita,
“Nimemuona Erick akipita na gari yake, kwakweli amekuwa na roho mbaya sana siku hizi hata kunisalimia loh!”
“Tena kilichonifanya nije kuongea na wewe ni kuhusu huyo Erick, kwani Sia wewe una nini? Kitu gani unataka kwa Erick?”
“Ngoja nikukumbushe mambo machache Tumaini, unakumbuka kipindi naanza mahusiano na Erick alikuwa na hali gani? Unakumbuka? Najua kuwa unakumbuka vizuri sana, ni wewe uliyekuwa ukinionea huruma sana na kunipa moyo kuwa ipo siku Erick atabadilika tu, nilimtambulisha Erick kwa wazazi wangu wote wawili, baba yangu siku anakufa ananiachia usia kuwa mwanangu Sia usije ukamuacha Erick maana huyu ndio mume wako, mama yangu nae siku anakufa ananiambia hivyo hivyo, nimeteseka mimi kwenye mapenzi ya Erick, nimemfumania mara ngapi na wanawake? Mara nyingi sana ila nikamsamehe na kuendelea na mahusiano yetu, mara ngapi Erick alilewa hadi kuzima kabisa na mimi ndiye nilikuwa napigiwa simu na kuanza kuhangaika kumrudisha nyumbani, mara ngapi Erick alikuwa akijitapikia sababu ya pombe na ni mimi pekee ambaye nilikuwa nikifua zile nguo na kufuta yale matapishi yake, kwanini Erick hakutaka kunirudishia upendo wangu? Kwanini Erick hakunipa kile ninachostahili? Mimi ni mwanadumu, nina moyo na nyama na damu ila kwanini Erick kanifanyia hivi! Sema wewe ungepitia katika hali yangu ungefanyeje?”
Tumaini akapumua kidogo na kumwambia,
“Ila Sia, hayo mambo si yalishapita?”
“Yalipita machobni ndio ila sio kwenye moyo wangu, unajua kila ninapoenda kwenye makaburi ya wazazi wangu nalia kitu gani? Sina furaha ya mapenzi mimi toka kipindi kile, nilitumia muda wangu na maisha yangu yote kwa Erick, ni wanaume wangapi mimi niliwakataa sababu ya Erick? Ni mimba ngapi mimi nilitoa sababu ya Erick, unajua Tumaini wewe ni mtu unayefahamu mengi niliyopitia nikiwa na Erick, basi kaa katika nafasi yangu”
“Mmmmh sawa, kwahiyo unataka Erick akufanyie nini?”
“Nahitaji Erick anipende na anijali kama mkewe, yeye ndio kaharibu maisha yangu kwa sehemu kubwa sana, sina furaha mimi sababu yake, siku zote Erick yupo katika akili yangu na ninampenda sana”
“Mmmmh haya makubwa nashindwa hata kuwaza, halafu nasikia unasumbua kuwa Erick ni mtoto wako? Kivipi ni mtoto wako?”
“Hilo tuliache kwanza, ila pale Erick atakapokubali kunifanya mimi kama mkewe basi na mimi nitafunguka kila kitu kuhusu watoto na kuhusu mimi binafsi, kumbuka hata mimi nilikuwa mjamzito kipindi yule Erica akiwa mjamzito, na mimi mimba yangu ilimpenda sana Erick, kiukweli huwezi fikiria ila niliumia sana moyo siku ya ndoa ya Erick na Erica. Kwakweli nitasema nab ado nitasema, Erica hakupaswa kuolewa na Erick maana hajapitia yale ambayo nimepitia mimi, jamani nimeteseka mimi kwa penzi la Erick halafu kirahisi tu mnasema nimuache Erick, hilo halitawezekana labda nife, na hata kama nikifa naamini bado mzimu wangu utaendelea kumsumbua Erick”
“Duh! Ila bado sijakuelewa Sia, kwahiyo unataka Erick akuoe uwe mke wa pili?”
“Itapendeza zaidi, yani siku nikiolewa na Erick nitafurahi sana”
“Mmmmh mbona pagumu hapo, unajua ndoa za Kikristo ni ndoa za mke mmoja na mume mmoja?”
“Kwaajili yangu hiyo sharia ipuuzwe kwanza, jamani mimi ninachotaka ni Erick kuwa mume wangu basi!! Sitoacha kumsumbua, katika maisha yote hadi naingia kaburini mpaka siku atakayokubali kuwa mume wangu”
“Ila mapenzi hayalazimishwi Sia”
“Ni kweli mapenzi hayalazimishwi, ila muulize Erick kati yangu na yeye ni nani alimfata mwenzie? Alinifata mwenyewe na kuniambia Sia nakupenda sana, kiukweli na mimi nilidata kutongozwa na Erick na kufanya nimkubali haraka haraka, nilipoanza nae mahusiano kitu pekee nilichokuwa naogopa ni kuachana nae, ndiomana nilimkazania Erick kwa maisha yangu yote, sikuwa na mwanaume mwingine yoyote mimi zaidi ya Erick, yani yeye ndio maisha yangu na kila kitu kwangu. Wazazi wangu wote walikufra wakisema kuwa Erick ndio mume wangu na mimi nilikula kiapo cha kutokumuacha Erick kamwe naye analitambua hilo, siwezi kumuacha Erick kabisa”
“Haya, basi nieleze ukweli kuhusu mtoto”
“Nimekwambia ukweli nitrakwambia siku Erick atakapoamua kuniweka mimi kama mke wake, ukiongea na Erick hebu mueleze ni jinsi gani nampenda, hebu mueleze ni jinsi gani nilivyopigani apenzi lake, hebu mkumbushe kila kitu nilichofanya nikiwa nay eye. Nampenda sana Erick, sijui kama kuna mtu anaweza kunishauri chochote kile”
Tumaini akapumua tena na kusema,
“Kwakweli Sia sina hata la kusema ujue, ila swala uliloliomba kwa Erick najua litakuwa gumu sana maana Erick anampenda sana Erica, kwa umuonavyo Erick yupo tayari kugombana na kila mtu katika ulimwengu huu lakini sio Erica, yani Erick hata hajali kuwa mimi ni dada yake wa pekee, yani naweza kupotea kama simkubali Erica, hata mama Erick mwenyewe hana sauti kwa mwanae juu ya yule mwanamke, kama kupenda basi Erick naweza kumpa medali maana ni amependa kupitiliza kwakweli, sasa hilo swala lako mbona halitawezekana Sia! Sijui itakuwaje!”
“Sikia Tumaini, mwambie Erick hata anioe kisiri siri tu, mimi nitafurahi na nitaacha kumsumbua”
“Kwahiyo uwe unyumba ndogo”
“Sina tatizo, ilimradi Erick awe mume wangu”
“Nitajaribu ila siwezi kukuhakikishia kuwa hilo swala litafanikiwa maana Erick namtambua vizuri kwa jinsi anavyompenda yule mke wake”
Basi Tumaini aliongea ongea na Sia pale na kuamua kuagana nae.
Muda huu Tumaini moja kwa moja aliondoka na kuelekea nyumbani kwa kaka yake, kwani alitaka pia kwenda kuona tena wifi yake huku maneno ya Sia nayo yakichanganya akili yake maana hata hakujua ataanzia wapi kumshauri kaka yake kuhusu Sia.

Junior na Angel walisoma vizuri tu siku hiyo na walipomaliza waliondoka kueleka nyumbani, ila baba yao aliwaambia kuwa wakodi usafiri ambapo walipotoka waliongea kuhusu hilo,
“Baba kasema tukodi usafiri wa kuturudisha nyumbani”
“Angel, katika jamii kuna baadhi ya mambo unajifunza kwa kukutana na watu mbalimbali, hivi muda wote tukizunguka kwenye magari tutajifunza nini na muda gani? Hebu tupande daladala tu Angel”
“Sawa, na mimi nakubaliana na wewe kuhusu hilo”
Basi walienda hadi stendi ya daladala na kusubiri daladala moja wapo na kupanda, walienda kukaa siti ya nyuma kabisa maana ndio ilikuwa tupu, basi mara mbele kidogo alipanda mdada ambaye nae alienda kukaa siti ya nyuma kabisa ila mdada huyu alipowaangalia Angel na Junior aliwafahamu na kuwashtua na wao ndipo waliposhtuka na kumuangalia kwa makini,
“Kheee Husna?”
“Ndio mimi, za siku Angel kwanza sijaamini kabisa kama kuna siku ningekutana nawe kwenye daladala”
“Nipo, za siku”
“Nzuri, hivi Samir bado unawasiliana nae?”
“Mmmmh wewe nawe, tumekutana tu umeanza habari za Samir, mimi huwa siwasiliani nae na hata sijui yuko wapi”
“Kheee basi bhana, kumbe Samir alikuwa anatembea na Warda”
“Mmmh Warda?”
“Ndio, kale kabinti Fulani hivi umekasahau na wewe!! Nasikia ndio Samir alikuwa akitembea nacho”
Basi Angel akafikiria kitu na kumkumbuka binti ambaye alionana nae hospitali na ndio huyo huyo Warda, basi alimjibu Husna kuwa anamkumbuka na Husna aliendelea kumpa habari,
“Za chini ya kapeti sasa, nasikia Warda ana mimba ya Samir, ila kile kisichana kama hakitaenda kutoa sijui”
“Mmmh Husna nawe, umepata wapi hizo habari?”
“Mimi taifa kubwa wewe, sio kama yule shoga yako Yusra sijui nae kafia wapi siku hizi, ila mimi ni taifa kubwa yani habari zote lazima zipitie kwangu zichujwe halafu ndio zisambazwe”
Angel akapumua kidogo ila yeye na Junior walikuwa wamefika hivyobasi walishuka na kumuacha Husna akiendelea na safari yake.
Junior na Angel waliposhuka, basi Angel alimuuliza Junior,
“Vipi Husna huyu hujampitia kweli wewe?”
“Aaaah tayari, si umemuona kanikaushia leo kamejifanya kama hakanifahamu vile, yani wasichana bhana mna vituko”
“Mmmh ila na wewe umezidi kaka yangu jamani, nasikia hata Yusra umempitia?”
“Ndio, hiko ni kipimo cha uanaume na sio vituko wala nini, ila Yusra katulia sana tofauti na huyu Husna mapepe sana. Ila zile stori zenu nilikuwa nazisikia, yani Warda kaninyima mimi kaenda kumpa Samir dah!”
“Kheee kumbe na huyo Warda umewahi kumtongoza?”
“Naacheje sasa? Msichana mrembo vile, naacheje kumtongoza, yani darasani ulipona wewe tu sababu dada yangu basi ila wengine wote nimetongoza na wengi nimepita nao”
“Mmmmh jamani!”
“Kawaida tu hiyo”
Basi Angel aliendelea kuongea na Junior pale ila bado kichwa chake kilikuwa kimevurugwa tu na mambo hayo ya Samir na Warda.
 
SEHEMU YA 210

Basi Tumaini pale anaongea ongea na mama Angel ila lengo lake kwa muda huo ni kumuona kaka yake, huku bibi Angel akiulizia habari za wajukuu zake pamoja na mwanae,
“Jamani mpange siku mje kunitembelea nyumba nikirudi”
“Sawa mama, hakuna tatizo tutakuja tu”
Basi baba Angel aliporudi Tumaini alifurahi sana na muda alipotaka kuondoka alimtaka kaka yake amsindikize, ilibidi baba Angel amrudishe Tumaini na gari yake kwani siku hiyo Tumaini hakutembea na gari basi wakiwa njiani ndipo Tumaini alipoanza kumwambia kuhusu Sia,
“Erick bhana, huyo Sia amekataa kunieleza kuhusu mtoto akisema ni siri yake, ila hayo mambo ya mtoto sidhani kama ni kweli ila nadhani Sia anayaweka ili kuongeza chumvi kwenye mboga yani ili matakwa yake yakubalike kirahisi”
“Matakwa gani?”
“Ni hivi, Sia anataka umuoe pia ilia ache kukufatilia wewe na familia yako”
Yani hadi baba Angel alipaki gari pembeni kwanza ili aongee na dada yake kwani kidogo habari hizo zilimchanganya, kwanza aliuliza tena,
“Anasemaje?”
“Anasema umuoe”
“Kheee huyo mwanamke ana wazimu eeeh! Kama alishindwa kipindi kile kuzuia ndoa yangu na Erick kabla sijamuoa Erica basi hawezi kwa kipindi hiki, kwanza nimuoe kwa misingi ipi? Na kwanini nimuoe?”
“Anasema kuwa umempotezea muda wake mwingi sana na amefanya vitu vingi sana na wewe, kwahiyo anahitaji utimize ulichomuahidi maana hadi wazazi wake wanakufa wameacha hiyo ahadi kwake pia kuwa wewe ndio mume wake”
“Unajua dada, kuna mambo kwenye ujana ni wengi sana huwa wanafanya, kiukweli sikutegemea kama Sia atakuwa chizi namna hii yani amekuwa mtu wa kushusha thamani yangu kwa ujinga wake, yeye kama alifanya mambo mengi kwaajili yangu si alitaka mwenyewe? Na nilimwambia kuwa sitaki ugomvi nae na wala sitaki kuachana nae kwa kugombana, nakumbuka nilijenga kaburi la baba yake na mama yake, ni mimi ndiye niliyekuwa nalisha familia yao, sasa huyu mwanamke anataka nini tena? Mara ngapi huyu Sia kanifumania na wanawake, tena mbele ya wanawake hao nilimwambia kuwa sikupendi ila bado alijiliza liza, mara ngapi nililewa na kumwambia kuwa sikupendi, ila bado alijiliza liza kwangu, unajua huyu mwanamke ni chizi, na ningejua mapema haya kwakweli nisingewahi hata kumtongoza, kwanza nilimtongoza kwa kumjaribu tu na nilimwambia wazi kuwa mimi nina stress kwani kuna mwanamke ninayempenda sana hanitaki, jamani hakuna nilichowahi kumdanganya Sia. Alichofanya kwangu chochote basi aliamua tu kufanya kama ambavyo mimi niliamua kulisha familia yao na nilivyoamua kumjengea makaburi ya wazazi wake, umuulize Sia kama kwao walikuwa na nyumba inayoeleweka? Nyumba yao ilikuwa inakaribia kuwazika wakiwa ndani ila niliwahurumia na kuamua kuitengeneza nyumba ile yani ilibomolewa kabisa na kuanzwa upya hadi nyumba yao ikawa inaonekana ni nyumba mtaani kwaajili yangu, anataka kusema nini huyo mwanamke?”
“Oooh kumbe! Yote hayo nilikuwa siyajui ila Erick kwa kifupi hayo ndio yanayomfanya Sia akung’ang’anie, mwenzio anaamini kuwa ulikuwa ukimpenda ndiomana uliweza kufanya yote hayo!”
“Ninayempenda mimi ni Erica, naweza kuwa sijafanya kitu kwakina Erica ila sababu hawakuwa na uhitaji huo, kwakina Sia nimefanya sababu ya huruma tu, ila ninayempenda ni Erica. Kumbuka Erica ndio kabadili tabia yangu mimi tena kwa asilimia zote, nilikuwa mlevi ila sinywi tena, nilikuwa mvuta sigara mimi ili sivuti tena, nilikuwa mpenda wanawake mimi ila wote nawaona kwangu walikuwa wapiti njia hata nikikutana nao sishtuki. Mbona wanawake wote niliowahi kuwa nao, nikikutana nao basi huwa tunaongea vizuri tu maana kila mtu na maisha yake na familia yake, kwanini Sia? Kuna analolitaka kwangu, mwambie kuhusu swala la mimi kumuoa asahau kabisa tena sio kumuoa tu hata kuishi nae asahau kabisa, nampenda sana mke wangu, yani Erica ndio kila kitu katika maisha yangu, tena mwambie aelewe hata kama Erica asingekuwa anazaa bado ningempenda na kumjali na kumthamini sana, huo upuuzi asiniletee kabisa, mwanamke mjinga huyo”
Kisha baba Angel alimrudisha dada yake ila alionekana kuchukizwa sana, halafu akarudi nyumbani kwake.

Leo karibia na muda wa kulala, Erica alitamani kupata mtu wa kuongea nae kwanza kabla ya kwenda kulala, basi aliamua kwenda chumbani kwa kaka yake, alipofika alifungua mlango kama kawaida na kumkuta kaka yake yupo kuongea na simu hana hata habari, basi akasogea karibu na kumuuliza,
“Unaongea na nani Erick?”
“Ni Sarah, ngoja nikupe umsalimie”
Basi Erick alimkabidhi ile simu Erica ambapo muda ule ule Sarah alimsalimia Erica,
“Mambo wifi yangu wa ukweli”
Erica alikaa kimya tu na kumfanya Sarah aongee tena,
“Wifi, wifi upo?”
“Nipo”
“Mambo wifi yangu? Siku ile nilipokuja ulikuwa umelalala ila nitakuja tena usijali kitu chochote kile wifi yangu na nitakuletea zawadi yako”
“Haya”
Kisha Erica alimkabidhi Erick simu yake ila kiukweli alikuwa ameumizwa sana na ile simu kwani aliondoka mule chumbani kwa Erick bila hata ya kuaga. Hakuwa na raha kabisa, moja kwa moja akapata wazo la kwenda chumbani kwa Vaileth basi akaongoza na kwenda chumbani kwa Vaileth alivyofika aliingia na kukutana na Vaileth akiwa anajiandaa kuoga,
“Kheee umechelewa leo dada?”
“Na kweli nimechelewa, ila mbona umekuja muda huu?”
“Leo ni zamu yangu ya kuja kulala chumbani kwako dada, kwahiyo ndio nimekuja hivi”
Vaileth hakuwa na jinsi zaidi ya kumkubalia tu Erica kuwa alale nae chumbani mule basi akamwambia,
“Karibu ila mimi naenda kuoga”
“Sawa dada, hakuna tatizo”
Basi Erica alijifunika shuka la Vaileth wakati Vaileth ameingia bafuni, muda kidogo mule ndani aliingia Junior na kwenda kitandani moja kwa moja kwani alijua ni Vaileth ndio amelala pale kitandani basi akaanza kusema,
“Mpenzi jamani, sijui jana ulienda kulala wapi ukanipa mawazo kweli mke wangu, unajua nakupenda sana”
Kisha Junior alianza kumpapasa Erica akijua ni Vaileth, yani muda ule ule Erica alijifunua shuka na Vaileth nae alitoka chooni yani Junior alibaki kushangaa tu.

Basi Erica alijifunika shuka la Vaileth wakati Vaileth ameingia bafuni, muda kidogo mule ndani aliingia Junior na kwenda kitandani moja kwa moja kwani alijua ni Vaileth ndio amelala pale kitandani basi akaanza kusema,
“Mpenzi jamani, sijui jana ulienda kulala wapi ukanipa mawazo kweli mke wangu, unajua nakupenda sana”
Kisha Junior alianza kumpapasa Erica akijua ni Vaileth, yani muda ule ule Erica alijifunua shuka na Vaileth nae alitoka chooni yani Junior alibaki kushangaa tu.
Ila muda ule ule Junior aliamua kumuwahi kumziba Erica mdomo kwani alijua ambacho kingefatia kwa muda ule ni Erica kupiga kelele kisha akamwambia,
“Erica nakuomba tafadhali usipige kelele yoyote mdogo wangu, nakuomba sana.”
Kisha akamuachia mdomo na Erica akamuangalia Vaileth na kumuuliza,
“Dada, si ulikataa wewe kumbe kweli!!”
Junior akamziba tena mdomo na kumwambia,
“Erica nakuomba mdogo wangu jamani usipige kelele basi, ngoja nitakueleza ukweli unaoutaka, kwani unahitaji kufahamu kitu gani?”
“Mmmmh nashangaa tu kuona mna mahusiano”
“Sikia mdogo wangu, mimi na Vaileth tunapendana tena sana, nampenda sana Vaielth”
“Unaniahidi nini kwa huyu dada Vai?”
“Nakuahidi kuwa nikianza maisha yangu nitamuoa”
“Mmmh!”
“Kweli Erica, niamini. Halafu nakuomba usimwambie mama kwasasa, ngoja muda muafaka ufike nitamwambia mwenyewe ila sio kwasasa, nakuomba sana Erica. Kuanzia leo wewe ndio mdogo wangu mpendwa yani, unataka zawadi gani mdogo wangu ila usimwambie mama kabisa”
“Mmmmh! Nataka simu yani na mimi nikiwa na simu nitafurahi sana”
“Sawa mdogo wangu, nitatimiza hitaji lako, nivumilie kidogo tu. Nakununulia simu na laini mdogo wangu si unataka tu kupiga na kutumiana ujumbe na wanafunzi wenzio?”
“Ndio”
“Basi nitakununulia mdogo wangu, leo lala tu humu mdogo wangu. Usitusemee kwa mama eeeh!”
Kisha Junior akainuka na kuondoka ambapo Vaileth nae alikazana kuomba msamaha Erica ili asiwasemehe maana Erica alijulikana nyumba nzima kwa umbea na huwa akipata jambo lazima alitangaze, kwahiyo Vaileth alihofia sana ila Erica nae alimuaga kuwa anaenda kulala chumbani kwake na kumuacha mule chumbani huku Vaileth akiwa na mawazo sana.
 
SEHEMU YA 211

Usiku wa leo, Angel alitumiwa jumbe nyingi sana na Samir akiulizwa tatizo ni nini ila hakuzijibu kabisa kwani moyo wake ulikuwa ukiumia sana kwa kile alichosikia kuhusu Samir, basi kuna ujumbe wa Samir uliingia, Angel alifungua na kuusoma,
“Nadhani Angel unataka kusikia kuwa nimekufa ndio itakuwa furaha yako, ila hata nikifa jua kwamba nakupenda sana”
Moyo wa Angel ulidonda kidogo na kuanza kumjibu Samir zile jumbe zake,
“Wewe Samir ni muongo, unadai unanipenda mimi wakati una mahusiano na mwanamke mwingine, kumbe Samir ulikuwa na mahusiano na Warda hadi ukampa mimba na mmeenda kutoa jamani Samir!! Dunia haina siri na yote nimeyapata, au kwavile mimi nashinda ndani ndio ukahisi sitajua chochote kuhusu wewe!! Nimejua kila kitu Samir”
Basi baada ya ujumbe ule, Samir aliamua kupiga simu kabisa ila Angel hakupokea na Samir kuamua kutuma ujumbe,
“Jamani mpenzi wangu Angel, nani amekwambia maneno hayo jamani!! Nakupenda sana mpenzi wangu, nani kakwambia!”
“Sio nani kaniambia ila jua ukweli wote naujua”
“Angel hakuna ukweli hapo jamani, kwanza Warda gani unamzungumzia wewe! Angel jamani kwanini huniamini kuwa wewe ndiye mwanamke nimpendaye!”
“Saizi unajifanya Warda humjui!! Si yule tuliyekuwa tukisoma nae shule ile tuliyohama, usinifanye mjinga Samir, nishasikia uchafu wako wote”
“Unajua Angel, ukisikiliza maneno ya watu tu basi mapenzi hayawezi kwenda wala nini, kiukweli mimi huyo Warda mara ya mwisho nimemuona siku niliyohama shule, sina mazoea nae ya aina yoyote ile iweje niwe na mahusiano nae!! Angel mpenzi wangu, inatakiwa mimi na wewe tupate wasaa tuonane na tuzungumze, tafadhali Angel nakuomba kama utaweza kuja kwetu itakuwa ni vizuri zaidi”
“Kheee kwenu nitakuja vipi mimi? Kwanza hapa nyumbani tu siruhusiwi kutoka”
“Hujaanza kwenda chuo?”
“Nimeanza”
“Basi nielekeze unaposoma Angel, nakupenda sana mpenzi”
Angel nae alimuelekeza Samir sehemu ambayo anasoma, ila siku hiyo hakuwasiliana nae sana kama siku zote kwani baada ya kuwasiliana nae kidogo tu aliamua kulala.

Kulipokucha kila mmoja alienda kwenye mambo yake kama kawaida ila leo Vaileth hakuwa na raha kiasi kwamba hata mama Angel alitambua hilo na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
“Kheee Vai umekumbuka sana kwenu nini?”
“Hamna kitu mama”
“Mbona umepooza sana, sio kawaida yako ujue”
“Hamna mama, nipo sawa tu”
Basi mama Angel hakuongea zaidi ila alimuona Vaileth kuwa hayupo sawa wala nini, muda huu alienda kuongea na mama yake na kumwambia,
“Ila leo Vaileth anaonekana hayupo sawa”
“Ni kawaida ya wadada wa kazi, siku akiamka na visirani vyake ndio kama hivyo, mchukulie kawaida tu mwanangu. Halafu unajua mimi nakaribia kurudi kwangu maana maswala ya uzazi wako nishamaliza”
“Jamani mama, nimekuzoea ujue”
“Ni kweli, ila ni wakati wa nyie kuja kwangu sasa. Unajua sisi wazazi sio kitu kizuri kukaa sana kwa watoto kwanza tunawanyima uhuru, naelewa kuna mambo mumeo anatamani kukufanyia ila anashindwa sababu yangu na ukizingatia haya maadili ya kiafrika ndio kabisa yani, nishakuhudumia uzazi na mtoto kashachangamka vya kutosha, kwanza nimekaa sana, sikutakiwa kukaa kwa siku nyingi hivi. Ni wakati wa kurudi kwangu”
“Mmmmh sawa mama, ila nitakukumbuka sana”
“Usijali mwanangu, nitazidi kuwaombea na tutazidi kuwasiliana, kwahiyo Jumamosi hii naondoka”
“Nimekuelewa mama yangu”
Ilibidi tu mama Angel akubaliane na maamuzi ya mama yake, ila mama Angel alimwambia kitu,
“Hivi mama, mbona mama Erick yuko hivi jamani!! Kashindwa hata kuja kuniona kweli!!”
“Kheee mwanangu, mkwe halaumiwi, kwanza akija kukuona au asipokuja kukuona anakupunguzia nini au anakuongezea nini? Mambo mengine hata sio ya kuumiza kichwa, tufikirie mambo ya maana katika maisha yetu kuwa nifanye kitu gani, niwe nani, nijiboreshe vipi, ila maswala ya kuwaza mtu Fulani hajaja kuniona utapata vidonda vya tumbo bure. Muangalie mumeo, anakupenda sana huyu mwanaume, muangalie na umshikilie, kumbuka baba yake alikuwa kipingamizi kikubwa sana hata baada ya ndoa yenu nina uhakika yule mzee kuna mengi kayatenda nyuma ya pazia huko, si unaona hata alivyokufa kiajabu ajabu, ila sio swala la kushangaa wala nini, katika maisha huwezi kupendwa na kila mtu na huwezi kuchukiwa na kila mtu, halafu kitu kingine mtu kuja kukuona au kutokuja kukuona sio kipimo cha upendo wala nini, mwingine atakuja kukuona kwa lengo la kukusanifu na mwingine kumbe kuna vitu katingwa navyo ila usimfikirie vibya, yule mama tulishamaliza tofauti nae, kumbuka hadi unaolewa na mwanae, nadhani ni yeye alikuwa na furaha sana utafikiri kitu gani na anampenda Angel hadi kesho bila kujali kuwa hajafanana na mtoto wake, tatizo lake tu hajui kulea watoto ila usimfikirie vibaya, mkweo yule. Tena ukiweza, yani ukipona zako, jibebe na zawadi mpelekee kumuona yeye, mtu akikutendea baya hebu mtendee wema uone itakavyokuwa”
“Asante mama, ndiomana wewe ni mama yangu kuna muda una maneno ya busara sana”
“Kwahiyo kuna muda mwingine naongea ujinga?”
“Hapana mama, sina maana hiyo, wewe ni mama bora kwangu umekuwa ukinifundisha kila siku na ndiomana mpaka leo nipo , nimeolewa, naishi na familia yangu ila ni kwa juhudi zako mama, umepambana sana juu yangu, sijui ingekuwaje”
Kisha mama Angel alimsogelea mama yake na kumkumbatia huku akimwambia,
“Nakupenda sana mama”
“Nakupenda pia mwanangu”
Basi waliongea mambo mengi sana kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 212

Muda wa Angel na Junior kutoka chuoni ulifika ila siku hii walitoka mapema zaidi, basi walivyofika nje ya chuo Junior akamwambia Angel,
“Leo, nataka niende kidogo kwa mama sasa sijui utarudi nyumbani mwenyewe?”
“Nitarudi ndio, kwanza nishazoea”
“Ila kumbuka hatujamwambia yule dereva atufate halafu leo hatujapewa hela ya kukodi usafiri, je utapanda daladala? Au tumpigie simu dereva aje?”
“Hapana bhana, nitapanda daladala, na mimi huwa natamani sana kupanda daladala ili kujua raha yake, halafu usijali kitu”
Basi wakaongozana Angel na Junior hadi kituo cha daladala ambapo Junior alikuwa akingoja Angel apande daladala kwanza, ila Angel alimwambia kuwa asijali lolote, ikabidi Junior apande daldala ya kuelekea kwao na kuondoka huku akiamini kuwa Angel nae atapanda daldala na kuondoka sababu alikuwa akingoja daldala yenye siti, ile Junior kuondoka Angel alishikwa bega, kugeuka nyuma alimkuta Samir ambaye alikuwa akitabasamu, basi Angel alimuuliza,
“Umejuaje kama niko hapa stendi?”
“Unajua nimefika hadi pale kwenye chuo chenu, nikawaona wewe na Junior mmesimama nje, basi nikaanza kuwafata nyuma hadi hapa stendi”
“Jamani una vituko wewe”
“Yani kitu Mungu akipanga basi kitafanyika tu, hebu ona leo jamani yani tumepangiwa kabisa tuwe pamoja”
“Aaaah acha maneno yako Samir”
“Kweli Angel, itapatikana wapi siku kama ya leo? Naomba ukapaone tu nyumbani kwetu”
“Hapana, nitachelewa sana nyumbani”
“Huchelewi Angel, kwani mimi nitahakikisha nakukodia usafiri hadi kwenu, na hapa nakodi usafiri ili tuwahi kwetu”
Basi muda huo huo Samir akaita bodaboda na kupanda yeye na Angel halafu safari ikaanza kuelekea kwakina Samir.

Junior alienda kwao moja kwa moja, shida yake ni kuongea na mama yake ili aweze kumpatia pesa za kumnunulia Erica simu kama ambavyo alimuahidi, basi alimkuta mama yake akiendelea na kazi zake kama kawaida, ila mama Junior alifurahi sana kumuona mwanae na kusema,
“Ooooh leo mwanangu Junior umenikumbuka jamani! Kweli Mungu mkubwa, karibu mwanangu”
Mama Junior alimfata mwanae na kumkumbatia kisha kumkaribisha ndani, ambapo Junior aliingia na kuanza kuongea nae,
“Kwanza vipi za huko mwanangu?”
“Ni nzuri tu mama”
“Kweli naona”
“Ila nimekuja mara moja tu hata mamdogo sijamuaga ujue”
“Ooooh wewe nawe! Kwanini lakini?”
“Aaaah mama ni hivi, unajua sio vizuri kwa mimi kila hela nimuombe mamdogo na bamdogo wakati mama yangu upo, sasa wanafunzi wote tuliomaliza kidato cha nne pale shuleni tumeandaa kama sherehe fulani ya kusherekea pamoja, sasa nikafikiria na kuona ni vyema nije nikwambie mama yangu, tafadhari naomba unisapoti kwa hilo mama”
“Kheee kwahiyo inahitajika pesa ngapi?”
“Elfu hamsini mama”
“Mmmh Junior jamani! Elfu hamsini sherehe gani hiyo? Kuna mtu anaoa ni michango ya harusi au kitu gani?”
“Jamani mama, mbona hivyo lakini, lini nimewahi kuja kukuomba kitu cha namna hii!!”
Mume wa mamake nae alikuwepo, basi alisikia maongezi ya mke wake pamoja na Junior na yeye alienda pale ambapo Junior alimsalimia kisha yule baba akasema,
“Mama Junior, mtoto wetu huyu kwanza kwasasa hatuna majukumu yoyote kwake, kwanini tusimpe anachokihitaji!”
“Aaaah naona hela ndefu!”
“Hela ndefu elfu hamsini jamani!”
Kisha huyu baba alimuangalia Junior na kumwambia,
“Usijali mwanangu nitakupa laki moja ya hiyo shughuli yenu na nitakupa elfu ishirini ya nauli”
“Oooh asante sana baba, nashukuru sana”
Basi yule baba alienda ndani na kutoa zile hela na kumkabidhi Junior, kwakweli Junior alifurahi sana wala hakuendelea kukaa kwao kwani muda ule ule aliamua kuaga na kuondoka zake.
Pale alibaki mama Junior na mumewe ambapo alimuuliza,
“Kheee unajua umenishangaza leo, imekuwaje?”
“Unajua kuna siku nilipita ofisini kwa Erick, kiukweli alinisema sana, natakiwa kumlea Junior kama mwanangu wa kumzaa na si tofauti na hapo, nikiangalia mimi nimeishi na Junior ila sijawahi kumpa yale mapenzi ya baba kwa mtoto, acha nianze sasa”
“Ooooh sawa, nimekuelewa, na pia nashukuru sana kwa kumjali mwanangu.”
Mama Junior alifurahi pia kwa siku hiyo ingawa aliona kama mwanae kamdanganya kuhusu uhitaji wake wa ile hela.

Samir alifika na Angel nyumbani kwao na kumkaribisha vizuri sana, kwa muda huo hapakuwa na mtu mwingine kwakina Samir zaidi yam dada wa kazi tu, ila Angel alihofia kwenda chumbani kwa Samir kwani alihisi kwenda chumbani kwa Samir basi ndio tiketi ya kulala na Samir,
“Hapana Samir, sijapanga kulala nawe”
“Kwani nani kakuambia Angel kuwa ukiingia chumbani kwangu basi utalala na mimi!! Jamani Angel, tende tu mara moja ukaone chumba ambacho mpenzi wako analala”
“Mmmh hapana Samir”
“Kwahiyo Angel hunipendi eeeh!!”
“Nakupenda sana Samir ila kwa leo hapana, nakuomba Samir jamani tafadhari, naogopa”
“Sasa unaogopa nini?”
“Naogopa kufanya mapenzi”
“Aaaah Angel acha hizo jamani! Kwani nani kakwambia kuwa tukiingia tutafanya mapenzi jamani!! Mimi nakupenda, najua mapenzi yapo muda maalum ukifika basi tutafanya hadi tuchoke ila kwasasa twende tukaongee tu faragha kidogo”
Angel akafikiria kwa muda, pia akafikiria maneno ya bibi yake na kumfanya ahofie, aliwaza pia akipata mimba itakuwaje? Na bibi yake alimwambia kuwa akizalia nyumbani basi anapunguza thamani yake, Angel akafikiria kidogo na kuogopa kuingia chumbani kwa Samir ila bado Samir alikuwa akimlazimisha, ikabidi amuahidi kitu kingine,
“Mpenzi wangu Samir naomba nikuahidi hili, tukikutana tena basi siku hiyo ndio tutakuja wote na kuingia chumbani kwako kwa maongezi ila kwasasa Samir hapana, kwanza nitachelewa kurudi nyumbani na itakuwa balaa kwa mama”
“Sawa, basi kaa kidogo hapa sebleni ili tupate hata juisi na tuongee ongee kidogo”
Angel alikaa na kuanza kuongea pale na Samir huku yule mdada wa kazi wakina Samir akiwaletea juisi, kwahiyo walikuwa wakinywa huku wakiongea, ila maongezi ya muda ule yalikuwa yakimshawishi sana Angel na kujikuta akitamani kuwa karibu zaidi na Samir,
“Tungeingia chumbani leo kidogo tu ningekuonyesha mapenzi yangu kwako, nisingelala nawe ila ningekuonyesha mapenzi yangu”
Basi Samir akawa akimueleza Angel vitu ambavyo angemfanyia wakiwa chumbani, kisha akamsogelea na kuanza kumbusu, kwakweli Angel alikuwa kalegea kabisa muda huo, mara mlango wa sebleni ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni mdogo wake Samir ambaye alikuwa ametoka shule ila alipowaona pale aliwasalimia na kushtuka kidogo alipomuona Angel na kusema,
“Dada, wewe si ndio dada yake Erica?”
Angel alikaa kimya ila alihisi aibu kidigo na kumwambia Samir kuwa aondoke tu na aelekee kwao, basi Samir akamwangalia mdogo wake na kumwambia,
“Na wewe hebu nenda kabadili nguo huko, kaone vile ni umbea tu”
Samia alienda chumbani kwake huku Angel nae akiinuka na kutoka nje ambapo Samir alitoka nae huku akimwambia,
“Ndiomana Angel nilisema kuwa twende chumbani mpenzi wangu, ila umekataa”
“Tutaenda safari nyingine, ila kwasasa nahitaji kurudi nyumbani yani ninavyochelewa ndio balaa”
Basi waliondoka na Samir alikodi usafiri ambao uliwapeleka moja kwa moja nyumbani kwakina Angel.
 
SEHEMU YA 213

Moja kwa moja Junior alienda kwenye duka la simu na huko alinunua simu kwaajili ya Erica na simu kwaajili ya Vaileth maana nae Vaileth toka amepokonywa ile simu na bozi wake mama Angel basi hakuwa na simu tena, kwahiyo Junior hakumkuta na simu kwahiyo aliona ni vyema amnunulie simu ili muda mwingine awe anawasiliana nae tu kama chumbani kwake hakuna mtu, basi alienda na kununua laini za zile simu na moja kwa moja kurudi kwa mamake mdogo.
Basi Junior alifika na moja kwa moja alielekea chumbani kwake na kuweka zile simu ila baada ya muda kidogo alimsikia mamake mdogo akimuita, basi alienda kumsikiliza,
“Junior, umerudi na Angel eeeh! Na mbona leo mmechelewa sana?”
“Kheee Angel hajafika kwani?”
“Anafika vipi wakati siku zote huwa manarudi pamoja!”
“Nilijua kashafika mamdogo, unajua mimi nilipitia kidogo nyumbani na nilimuacha Angel akija huku”
“Kheee kwahiyo Angel alikuwa akirudi mwenyewe”
“Ndio mamdogo”
“Kheee kapitia wapi jamani!!”
“Sijui mamdogo ila nilimuacha aje nyumbani”
“Ngoja nijiandae twende huko chuoni”
Muda huo huo Angel nae aliingia, kwakweli mama yake alikuwa na hasira sana na kwenda kumnasa kibao Angel halafu ndio akamuuliza,
“Ulikuwa wapi muda wote?”
“Jamani mama unanionea bure tu, leo dereva hakuja kutufata maana tulisahau kumwambia wakati tunaenda, halafu sina simu kusema nimpigie, sina hela ya kusema nikodi usafiri, hela kidogo niliyokuwa nayo niliamua kupanda daladala ila njiani liliharibika ndio tukasubiri litengenezwe na ndio nimerudi muda huu, samahani mama”
“Samahani mwanangu, sikufahamu hilo mwanangu, pole sana. Ila nitajua cha kufanya kuhusu usafiri”
Basi Angel moja kwa moja alienda chumbani kwake huku akishukuru sana njia aliyofundishwa na Samir ili kumdanganya mama yake kwa siku hiyo na mamake amemuelewa kweli kumbe kamdanganya.

Baba Angel akiwa ofisini kwake, akikamilisha kamilisha kazi zake ili afunge ofisi maana siku hiyo alitaka afunge mapema na awahi kurudi nyumbani kwake, basi alipigiwa simu na mtu wa mapokezi,
“Bosi, kuna mgeni hapa anahitaji kukuona”
“Mwambie aingie”
Yule mgeni alipoingia, kwakweli baba Angel alishangaa sana kwani alikuwa ni Sia, basi alimuangalia ka hasira na kumuuliza,
“Shida yako nini ofini kwangu?”
“Usiseme ofisini kwako ila sema ofisini kwetu maana chako ni change na change ni chako, mimi na wewe ni wanandoa”
“Hivi una wazimu wewe Sia?”
“Sina wazimu ila kumbuka ni muda gani umepoteza katika maisha yangu! Miaka miangapi tulikuwa pamoja, mimba ngapi umenilazimisha kutoa? Mara ngapi umeshiriki nami tendo la ndoa? Yani hilo tendo ndio tumefanya mar azote hadi kwenye gari, sasa nashindwaje kusema kuwa mimi ni mke wako? Yani Erick huwezi kukwepa hili, mimi ni mkeo tu, nilikataa wanaume wengi sana kwaajili yako, mimba ulizonitoa umefanya nifuje yani urembo wangu wa awali utoweke, hata sikujua kama nitazaa tena ni mapenzi ya Mungu tu hata nimepata mtoto mmoja, hivi Erick utaniambia nini wewe nikuelewe? Tena shukuru sana kwa miaka yote hii nimekuacha umeishi kwa amani, ila nisingekuacha wewe, nilitakiwa nikuharibie hata siku ya ndoa yako, umenitumia sana mimi. Baba yako aliongea nami mara ya mwisho kwa maneno mengi sana, hivi unajua kuwa baba yako alikufa kwenye mikono yangu nikiwa nimemshika, unajua aliongea nini na mimi? Unajua ni mangapi baba yako amenisaidia ili mimi niwe na wewe? Kwakweli Erick huna cha kunikwepa, sema kwa muda huu hiki sio kilichonileta hapa, kuna siku nitaongea mengi sana ya moyoni ili jamii ijue”
“Kheee tuseme bado una mengine!!”
“Tena mengi tu, ila kwa muda huu hakijanileta hiko kitu”
“Nini kimekuleta, sema haraka nataka nikamuwahi mke wangu”
Sia akacheka kwa muda na kusema,
“Huyo Angel, nimemuona akiwa kwenye bodaboda na mwanaume, tena mwanaume mwenyewe ni Samir, usiulize nimemfahamu vipi Samir ila namfahamu ndani na nje yule mtoto, kwahiyo nimemuona binti yako akiwa nae pamoja, chunga sana usipokuwa makini yule Angel nae atazalia nyumbani kama mama yake, najua unampenda sana mtoto huyu tena nadhani unampenda kuliko hata baba yake mzazi angefanya kwake, ila ndio hivyo anapotea yule mtoto, na mkimfahamu Samir vizuri mtaona kama mnavyofanya siri kwa Angel kuhusu ndugu zake ni vizuri au si vizuri, mimi nina siri nyingi sana ila nipo makini sana nikiona kuna tatizo linataka kutokea basi naingilia kati ili tatizo hilo lisiibuke, nakwambia tena kuwa makini sana Angel na Samir mambo ni moto yani kama mahaba yamewapata haswaaa, nina hofia Angel asije kuwa kama mimi kwa siku za mbeleni, apoteze uzuri wake sababu ya mwanaume na mwisho wa siku ajute kwani Samir hatoweza kumuoa yeye na ataoa mwanamke mwingine na hapo ndio kutakapoibua tatizo. Ukitaka fatilia na usipotaka potezea, ila mimi ujumbe nimeshakufikishia, kwaheri”
Sia aliondoka na kumuacha baba Angel mule ofisini akimuangalia tu Sia hadi alipotokomea, kiukweli hata hamu ya kufanya kazi ilimuisha kabisa na kujikuta akiwaza kwa muda kisha akafunga kazi na kuondoka zake.

Moja kwa moja Junior alienda chumbani kwa Erica na kugonga ambapo Erica alimkaribisha kisha alimpa ile zawadi ya simu ambayo alimuahidi, kwakweli Erica alifurahi sana, kwani lengo lake ilikuwa ni kutaka kufanana na Erick maana alimuona Erick anajifanya simu inampa umakini sana, alimshukuru sana Junior,
“Asante sana Junior”
“Usijali, ila mimi na wewe ahadi yetu ni pale pale kuwa tuendelee kufanya siri”
“Sawa na ahadi nyingine pia ibaki pale pale kuwa ukijipanga utamuoa dada Vai”
“Ndio nitamuoa mdogo wangu, nakuahidi hilo, lazima nitamuoa Vai hakuna tatizo”
“Hapo tutaelewana, sipendi kumuona akilia wala akisononeka”
“Sawa mdo wangu, nakuahidi kuwa nitamfanya Vaileth kuwa na furaha muda wote”
Basi Junior alifurahi pale na kumuachia ile simu Erica kisha akaondoka zake.
Ilikuwa ni furaha sana kwa Erica kupata ile simu na alijisemea kuwa atajitahidi kuitunza siri ile”
Basi alikaa na kuanza kuibonyeza bonyeza.

Mama Angel muda huu alikuwa amekaa sebleni akiangalia Tv maana ni muda hajafanya hivi, ila alishangaa kusikia kuwa kuna mgeni amefika, alipomuangalia mgeni mwenyewe alishangaa kumuona Elly yani hapo aliwaza moja kwa moja lazima Elly atakuwa kaenda na Sia, kiukweli uoga ulimshika kidogo na kuinuka huku akimuuliza Elly,
“Umekuja kufanya nini?”
“Nahitaji kumuona Erica”
Naye Erica alikuwa akitoka ndani akielekea hapo sebleni, hata yeye alishangaa kumuona Elly kwani hakumtegemea kwa siku hiyo na kwa muda huo.
Ila Elly alivyomuona Erica, alimkimbilia na kumkumbatia yani kile kitendo kilizidi kumuogopesha mama Angel kwani alijua ni wazi yule Elly katumwa na Sia ila tu hakujua ni tukio gani litaendelea.
 
SEHEMU YA 214

Naye Erica alikuwa akitoka ndani akielekea hapo sebleni, hata yeye alishangaa kumuona Elly kwani hakumtegemea kwa siku hiyo na kwa muda huo.
Ila Elly alivyomuona Erica, alimkimbilia na kumkumbatia yani kile kitendo kilizidi kumuogopesha mama Angel kwani alijua ni wazi yule Elly katumwa na Sia ila tu hakujua ni tukio gani litaendelea.
Basi akasogea karibu ya Erica na Elly na kuwaachanisha pale kisha akamfokea Elly,
“Muda huu nyumbani kwangu umekuja na nani?”
“Nimekuja na mama yangu, yupo nje ananisubiria”
Mama Angel alizidi kuchukia na kumwambia Elly,
“Haya, toka kwenye nyumba yangu sasa hivi”
Erica alimuuliza mama yake,
“Kwanini unamfokea mama?”
“Mama yake na huyu sio mtu mzuri kabisa, Elly ondoka katika nyumba yangu”
Elly hakubisha na moja kwa moja alitoka nje na kuelekea nje ya geti ambako kulikuwa na mama yake kisha akamwambia mama yake,
“Mama Erica kanifukuza”
“Usijali mwanangu, ipo siku atajutia. Muda utafika, usijali mwanangu, twende nyumbani”
Kisha mama Elly aliondoka na Elly, muda huu mama Angel alikuwepo getini pia maana alimfata Elly kwa nyuma, kwakweli alichukia sana na kurudi ndani kwake akiwa na chuki ila bado Erica alikuwa pale sebleni akishangaa kwani alishangaa pia kwa muda huo Elly alienda kwao kufanya nini na nani aliyemfikisha Elly nyumbani kwao kwani alikuwa anatambua wazi kuwa Elly hapafahamu hapo nyumbani kwao, basi mama yake akamuangalia na kumwambia,
“Erica, kuanzia leo sitaki ukaribu wako wowote na Elly”
“Kwanini mama?”
“Sidhani kama nina majibu kwa muda huu, nenda ukale huko ukalale”
Mama Angel alitulia tu huku akiwa na hasira za kutosha.

Baba Angel nae alirudi akiwa na hasira pia, ila huyu baba hata kama aliambiwa kitu cha ukweli na Sia bado hakuweza kumfokea Angel yani yeye aliona kumfokea Angel ni kama kumfanya ajihisi vibaya, ila pia alikuwa na hasira kwa yale maneno ambayo aliambiwa na Sia,kitu hiko kilimfanya alipoingia ndani basi moja kwa moja alienda chumbani kwake ila badae alikumbuka kuhusu Angel na kuinuka ili akaulizie, wakati anataka kutoka akakumbana na mkewe mlangoni kwani pia alikuwa amemfata chumbani,
“Vipi tena baba Angel?”
“Huyu Angel yupo?”
“Yupo ndio, sasa aende wapi jamani!”
Baba Angel akapumua kidogo na kurudi kukaa ambapo mkewe alimuuliza tena kama kuna tatizo,
“Kwani una tatizo gani mume wangu?”
“Hapana sina tatizo, nadhani ni kazi tu hizi zinanisumbua”
“Halafu ngoja nikwambie kitu yani leo nimemuona Vaileth hana raha kabisa, sijui kakumbuka kwao!”
“Oooh nimekumbuka, nilimuahidi kuwa nitampatia pesa za kumuwezesha yeye kuwatumia wazazi wake ili warekebishe nyumba yao maana alisema kuwa inavuja”
“Sasa mume wangu hiyo pesa utakuwa unamkopesha au?”
“Kwani pesa ngapi mke wangu? Ni milioni mbili, kumbuka Vaileth anakaa na familia yetu hapa, ngoja tumfurahishe ili azidi kumpenda familia yetu na kuishi nayo vizuri”
“Sawa mume wangu hakuna tatizo, halafu hivi tutamkabidhi lini Angel akaunti yake?”
“Hata sasa hakuna tatizo”
“Hapana, bado. Unajua Angel ana akili moja mbovu sana, nadhani tukimkabidhi mapema hivi tutalia pia, naona tumuache tu kwanza, na akihitaji pesa aombe kwetu”
“Sawa, umeongea sahihi mke wangu”
Ila siku hiyo baba Angel alisikia akili kuchoka kweli ila hakumuuliza mkewe chochote kuhusiana na kile alichoambiwa kuhusu Angel, sema tu alifurahi moyoni mwake kuona kuwa Sian i muongo na mwanae hajafanya ujinga wowote.

Leo Junior alienda kulala chumbani kwa Vaileth na kumpatia ile zawadi ya simu, kwakweli Vaileth alifurahi sana na kumwambia Junior,
“Kweli nimeamini kuwa Junior unanipenda”
“Ndio, mimi nakupenda sana Vaileth, yani jua nakupenda wala usiumizwe kichwa juu ya jambo lolote lile”
“Ila nasikia wewe ni muhuni!”
“Hiyo zamani, ila sio sasa”
“Ila Junior bado kijana wewe!”
“Kwani ujana ni kitu gani ikiwa mtu umeamua? Mimi kwasasa nimeamua kukupenda wewe na nitakupenda siku zote, yani Vaileth elewa kuwa wewe ni mke wangu kabisa, lazima nikuoe”
Vaileth alitabasamu na kujihisi rah asana, yani siku hiyo ndio alilala vizuri zaidi na Junior kwa kumshukuru kwa zawadi ya simu.

Basi Angel usiku huu alikuwa akiwasiliana tu na Samir na kumueleza vile mama yake alivyomuamini,
“Kweli wewe Samir ni kiboko jamani, yani yale uliyosema nimueleze mama amekubali kwa urahisi sana”
“Si nilikwambia Angel, unajua unapokua unatakiwa kujua ni uongo gani wa kumpa mzazi wako ili uweze kufanikisha mambo yako. Basi Angel, kuna siku mimi na wewe tutatoka na kwenda kufurahi wala mama yako hatojua chochote kile”
“Ooh asnte sana Samir, ila huyo Samia ndio mdogo wako?”
“Ndio”
“Oooh ni rafiki wa Erica huyo, hebu kaa nae asije akasema umbea”
“Usijali, asubuhi kabla hajaenda shule nitaongea nae maana muda huu kalala halafu yule akilala huwa haelewi kitu”
Basi waliwasiliana kwa muda mrefu sana na wote kulala ikiwa ni usiku sana, kitendo kile kilimfanya hata Samir asishtuke asubuhi kwenda kumfata mdogo wake na kumpa onyo kwani naye alilala sana.

Kama kawaida wanafunzi wote walienda shule na wengine kwenye dhughuli zao za kila siku, ila wakati Erica yupo shuleni basi rafiki yake Samia alimfata na kuanza kuongea nae,
“Jana bhana wakati natoka shule, ile kufungua mlango wa sebleni si nikamkuta kaka na mwanamke, ila yule mwanamke alikuwa na aibu hatari, ila unajua alikuwa nani?”
“Ni nani?”
“Dada yako, yule umenitambulisha siku ile yule Angel, kumbe ndio mwanamke wa kaka”
“Haiwezekani kabisa, jamani mama yetu ni mkali sana, unataka kuniambia dada Angel alikuja kwenu? Haiwezekani utakuwa umemfananisha”
“Haya, shauri yako ila sijamfananisha wala nini ni mwenyewe kabisa yani, yule ni dada yako na aliponiona kanionea aibu sana hata swali langu hakujibu maana nilimuuliza kama ni dada yako ila hakujibu kwa aibu”
“Ila Samira mmmh! Nadhani mimi na wewe tunafanana kwenye umbea jamani, yani mimi hadi nyumbani wananichukia eti”
“Mimi je!! Yani baba ndio huwa hataki hata nimuone na mwanamke kaongozana nae maana lazima nimpelekee habari mama”
Basi wakacheka pale na kurudi darasani kuendelea na masomo sasa, ila siku hiyo ilikuwa siku fupi kwani ilikuwa ni siku ya Ijumaa.

Wakati wa kutoka shule, kama kawaida Erick alikaa kiti kimoja na Sarah, kwa kipindi hiki Sarah alikuwa kamzoea sana Erick na alimfanya kuwa ni mtu wake wa karibu na kuzungumza nae mambo mengi sana, basi Erick akamkumbusha swali kuhusu mama yake kuwa kwanini alilia siku ile,
“Eeeeh kwanini mama yako alilia?”
“Tena afadhari umeniuliza, basi nimemuuliza mama kwanini umelia? Unadhani kanijibu? Hajanijibu chochote ila kasema anataka akuone tena”
“Kheee anataka kuniona tena!!”
“Ndio, basi kesho nitakuja tena kwenu ili unisindikize, sawa Erick”
“Mmmh sawa hakuna tatizo, nitafanya hivyo”
“Yani mimi napenda sana kuwa karibu na wewe Erick, furaha yangu ni kuwa karibu na wewe”
“Ila sisi bado ni wadogo na wewe ni mtoto wa kike Sarah hutakiwi kuwa hivyo!”
“Mama yangu, alinifundisha jambo moja la kutokukaa na kitu moyoni na kama mtu nimempenda basi nimwambie mapema, kwahiyo nimelelewa hivyo na nimekuwa kwa stahili hiyo”
“Haya”
“Kwahiyo unasemaje kuhusu mimi?”
Gari ilikuwa imefika kwakina Erick, hivyobasi Erick alishuka nyumbani kwao na moja kwa moja kuingia ndani ila alimkuta mama yake ambaye kwa siku hiyo alimuuliza swali,
“Sarah hajambo!”
Erick alishangaa pia na kumjibu mama yake,
“Hajambo”
“Anakuja lini tena kututembelea?”
“Kasema kesho mama, kumbe umemkumbuka!”
“Ndio, binti mcheshi vile ndio nisimkumbuke kweli! Namkaribisha sana nyumbani kwangu”
Erick akatabasamu na kwenda ndani ila Erica alikuwa mahali na alisikia vile mama yake alivyokuwa akimsifia Sarah, kiukweli hakupenda kabisa, na muda huu alienda chumbani kwa Erick ambaye alikuwa akibadilisha sare za shule, basi Erick alimuangalia Erica na kumwambia,
“Naona leo umenikumbuka mdogo wangu”
“Niite jina langu ndio inapendeza zaidi”
“Khaaaa ila wewe jamani!! Haya karibu ndani Erica”
“Ngoja ngoja nikupe maji, nasikia dada Angel jana alikuwa kwakina Samia, sijui ana kaka yake basi huyo kaka yake kumbe anatembea na dada Angel”
“Kheee ndio maji hayo?”
“Ndio, huu ni umbea na umbea ni kama maji usipounywa utauoga”
“Ila wewe mdogo wangu una vituko sana jamani!! Yani wewe una vituko umepitiliza, una uhakika? Huyo Samia nae mbea kama wewe”
Erica alinyanyuka na kuondoka bila hata ya kumuaga kaka yake kwani alikuwa ashachukia kwani hapendi kupeleka habari halafu isisikilizwe. Ila Erick alibaki akisikitika tu kidogo na kusema,
“Yani huyu Erica jamani kama kazaliwa uswahili, kwa hali hii hajazaliwa uswahilini, hivi angezaliwa uswahilini kama wengine ingekuwaje jamani! Dah huyu mdogo wangu jamani, lakini nampenda sana”
Basi Erick alimuangalia tu Erica anavyotoka huku akionekana kuwa amechukia.
Moja kwa moja Erica alienda chumbani kwake, ila akatamani akamueleze habari hiyo mama yake ila akakumbuka maneno ya Erick kuwa una uhakika? Ikabidi tu akae kimya, kisha akainuka na kwenda jikoni ambako alianza kumsaidia Vaielth kazi mbalimbali huku akimwabia,
“Kesho nitapika mimi, kuna kitu nataka kujaribisha kupika”
“Umefundishwa tena na Elly?”
“Hapana, halafu nimemkumbuka Elly sana, yupo kama ndugu yangu yule ila sijui kwanini mama hampendi Elly, tena kasema hataki urafiki wangu na Elly kabisa”
“Mdogo wangu usilazimishe kitu ambacho mama hapendi, fanya kile tu anachopenda ili uishi nae vizuri na kwa usalama”
“Ila nina jambo nataka kuongea yani nisiposema hili naweza kupatwa na vidonda vya tumbo”
“Jambo gani tena?”
Basi akaanza kumuelezea vile alivyoelezwa na Samia shuleni kuhusu dada yake Angel kwenda kwakina Samia, kwakweli Vaileth aliogopa kwani aliona hata siri yao itafichuliwa tu,
“Kwahiyo hilo ndio jambo ambalo ungekaa nalo ungepata vidonda vya tumbo Erica?”
“Ndio, yani sikuweza kukaa nalo kabisa”
“Ila Erica nakuomba, kuhusu mimi na Junior usiseme”
“Usijali, wala sisemi kwanza Junior kanipa simu basi usijali yani siwezi kusema kabisa”
Basi Vaileth akapumua kidogo na kuendelea na kazi zake.
 
SEHEMU YA 215

Leo baba Angel wakati anatoka tu ofisini kwake, alikutana na rafiki yake wa muda mrefu sana na kuanza kusalimiana pale, kisha wakaona ni vyema kutafuta hata hoteli na kuongea mawili matatu,
“Khaaa umebadilika Erick”
“Si unajua ukubwa tena!! Hata wewe umebadilika ndugu yangu jamani! Nikikumbuka kipindi kile dah! Kweli miaka inaenda na maisha yanaenda sana. Vipi familia yako kwasasa Juma?”
“Oooh Alhamdulilah, nina mke na watoto watano kwasasa”
“Oooh hongera sana, na mimi nina mke na watoto wanne, kwahiyo umenizidi mmoja”
Juma alicheka na kuendelea kukumbushana mambo ya zamani,
“Hivi unamkumbuka Rahim?”
“Aaaah namkumbuka ndio”
“Yule jamaa sasa, ana watoto kama uchafu jamani, nina uhakika hata watoto wake wengine hajui walipo”
Baba Angel alikaa kimya kidogo kwani huyu Rahim aliyezungumziwa hapa ndio baba halisi wa Angel, basi alitulia kwa muda na kusema,
“Tuachane na habari za huyo mtu”
“Ila yeye huwa anakutaja sana tena huwa anasema kuwa anakutafuta sana sijui anakutafutia nini”
“Achana na huyo mtu kwakweli, historia yake ni ndefu sana”
“Haya bhana, ila sasa inatakiwa tutembeleane ili uweze kufahamu familia yangu nami niifahamu familia yako ndugu yangu”
Basi wakati wanaongea pale, kuna mtu alisogea na kukaa karibu yao, Erick alishtuka kidogo ila alipomuangalia akagundua kuwa ni Dora basi alirudi kawaida na kuongea nae,
“Kheee Dora, karibu, leo upo hotelini kumbe!”
“Unajua nawashangaa, kumbe nyie watu mnafahamiana?”
“Ndio, huyu ni Juma ni rafiki yangu kitambo sana”
Juma alikuwa akitabasamu na kusema,
“Hata mimi na huyu Dora tunafahamiana, vipi Dora lakini za siku? Yale mambo yako umeacha siku hizi!”
“Mmmh jamani nimeokoka ujue, siku hizi nimeokoka sina mambo ya kijinga kabisa. Hapa hotelini kwenyewe nimepita tu kidogo ili leo nile chakula cha hapa yani nimejikuta tu nimekikumbuka ila kuna mtu ananivuruga sana”
Baba Angel akamuuliza,
“Mtu gani huyo shemeji yangu?”
“Aaaah ni Sia huyo shemeji, yani mwanamke ananivuruga yule hatari”
Baba Angel alishtuka ila Juma nae alishtuka kidogo sema hakuonyesha sana mshtuko wake, basi baba Angel akamuuliza tena Dora,
“Anakuvurugaje tena huyo Sia?”
“Yani acha tu shemeji, ila huyu mwanamke kuna siku nitarudi Dora wa zamani na nitamshikisha adabu, nadhani hanifahamu vizuri”
“Mmmmh umeokoka Dora ujue!”
“Ni kweli nimeokoka ila sio mtu akiokoka basi ndio apandwe hadi kichwani, yani kuna siku huyu Sia atasema kweli wewe ni Dora maana nitamvuruga kupota yeye alivyoivuruga familia yangu”
Baba Angel alibaki tu kumuangalia Dora kwani na yeye akiwaza jinsi Sia anavyoivuruga familia yake alikosa raha kabisa, basi wakajikuta wakianza kuongea tu habari zingine kwani za Sia ziliwachanganya wote.

Baba Angel alipoagana na rafiki yake Juma pamoja na Dora, aliamua sasa kurudi nyumbani kwake, ambapo aliporudi tu mkewe alimfata chumbani kuongea nae kwani hakumwambia kuwa mama yao amepanga kuondoka Jumamosi ambayo ndio kesho, basi akaanza kuongea nae,
“Oooh sorry mume wangu, ni hivi nilisahau kukwambia tu ila mama alisema kuwa ataondoka Jumamosi yani kesho”
“Aaaah hapana haiwezekani, mama Angel jamani ndio mambo gani hayo? Kwahiyo mama ataondoka bila zawadi?”
“Sijui ila ndio kasema hivyo”
“Haiwezekani kumruhusu mama aondoke bila ya zawadi, kumbuka mama ameacha kazi zake nyingi sana, ametumia muda wake mwingi tu kutuhudumia hapa halafu tumuache tu aondoke bila zawadi! Hapana kabisa haiwezekani”
“Sasa tutafanyaje mume wangu!”
“Inabidi uongee nae na umshawishi ili mama akubali kuondoka Jumapili na kesho niende kumtafutia zawadi, mwambie tena Jumapili nitampeleka mwenyewe, tafadhari mama Angel ongea na mama kuhusu swala hilo jamani, haiwezekani tumuache mama aondoke bila zawadi”
“Si unamjua yule mama lakini, akisha amua lake basi ameamua”
“Hata kama mama Angel, nakuomba mke wangu ongea na mama tafadhari, nakuomba sana”
“Sawa basi, ngoja nikaongee nae”
Mama Angel alionoka mule chumbani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mama yake ambapo alimkuta akipanga panga nguo zake kwaajili ya safari, basi mama Angel alianza kuongea nae,
“Oooh mama, sikia mama yangu naomba uondoke Jumapili”
“Kwanini sasa niondoke Jumapili? Na mimi nimepakumbuka kwangu”
“Naelewa mama ila ukiondoka Jumapili itapendeza”
“Kwanini iwe Jumapili na sio kesho?”
“Sikia mama, yani sikumueleza baba Angel kuwa unaondoka Jumamosi, sasa leo nimemwamboia kaniomba sana uondoke Jumapili na kasema kuwa atakupeleka yeye mwenyewe hadi nyumbani, mama tafadhari nakuomba kuhusu hilo”
“Si unajua nimeshapanga lakini jamani! Mimi nataka kuondoka, nahitaji kwenda kwangu”
“Naelewa mama ila nakuomba juu ya hilo tafadhari mama yangu nakuomba”
“Ila na wewe Erica jamani uking’ang’ania kitu loh! Haya basi nitaenda hiyo Jumapili mnayotaka nyie”
“Asante sana mama yangu”
Mama Angel alifurahi sana na muda huo aliamua kwenda kumpa taarifa hiyo mume wake kuwa mama yao kakubali kuondoka Jumapili.

Usiku wa leo, Erick aliamua kwenda chumbani kwa Erica kwani alijua kuwa alimkera mdogo wake kwakutokumsikiliza kwani mdogo wake alipenda sana kusikilizwa na kwavile alimtambua vizuri basi hakuwa na budi kumfata ili akamjulie hali.
Alimkuta amekaa tu na amejiinamia, basi Erick alisogea na kumuuliza,
“Una tatizo gani kwani mdogo wangu Erica?”
“Sina tatizo lolote”
“Aaaah mimi nakufahamu vizuri sana Erica, najua kuwa una tatizo, najua kuwa muda ule ulichukia sababu sijakusikiliza, nisamehe mdogo wangu ila nakuomba usiende kumwambia ukweli mama kuhusu swala hilo maana halina uhakika”
“Mbona sijamwambia mama hata hivyo nimesema simwambii chochote”
“Ni bora uende kumuuliza Angel mwenyewe kuliko kumwambia mama”
“Nimekuelewa Erick, ila niache nipumzike”
“Aaah mambo hayo yameanza lini jamani Erica? Naomba tucheze karata”
Erica aliposikia vile alifurahi sana na kwenda kutoa karata ili waweze kucheza na muda huo huo walianz akucheza zile karata, na kama kawaida walicheza sana karata na kulala kule kule chumbani kwa Erica.
Kilichowashtua asubuhi ni sauti ya mama yao ambaye alikuwa akiita akiwa sebleni, basi Erick alikurupuka na moja kwa moja kwenda alipoitwa na mama yake ambapo alipewa kazi yak wend akusafisha gari lao, ila siku zote Erick sio mtu wa kubisha kazi yoyote anayopewa, hivyo basi alizunguka nyuma ya nyumba yao kwaajili ya kwenda kuosha gari, ila alipofika alimkuta Junior nae akiosha gari jingine ambapo Junior alipomuona Erick alimlalamikia kidogo,
“Yani mama anachofanya sio sawa kabisa, utafikiri ni watu wasiokuwa na hela jamani! Hivi anashindwa nini kupeleka hizi gari car wash zikaoshwe huko mpaka tuoshe hapa nyumbani jamani!”
Ila hii ni kawaida kwa mama maana anasema tuzoee maisha yote, tena kipindi cha nyuma hapa hata mdada wa kazi hakuwepo basi Jumamosi kama hii ni mwendo wa kazi tu yani mtafanya kazi hadi mkome, ikifika mchana utakuta tumelala tu maana mama huwa kuna kazi zingine anazigungua muda huo huo, tena hajaibuka hapa na kazi yake ya kusafisha madirisha, utaniambia akianza, yani mama ni wa kumzoea tu”
“Yani anafanya kamavile watu wasiokuwa na pesa jamani! Hapo Angel atakuwa anasafisha ndani na Erica atakuwa anaosha vyombo, yani huyu mamdogo nimemshindwa tabia kwakweli”
Erick alicheka na kusema,
“Hamna, Erica ameambiwa kusafisha uwanja leo na vyombo vinaoshwa na Angel halafu Vaileth yupo jikoni kwani nyumba alishasafisha”
“Oooh yani huyu mamdogo jamani dah!”
Basi waliosha magari yale pale huku wakiongea mambo mbalimbali tu.
 
SEHEMU YA 216

Wakati Junior na Erick wakiendelea kuosha magari, mara alienda Erica na kumwambia Erick,
“Weeee kimwanamke chako kimekuja”
“Nani huyo?”
“Sijui anaitwa Sarah”
Erick alishangaa sana kusikia kuwa Sarah amefika kwa muda huo maana ilikuwa bado mapema sana, basi akamwambia Erica,
“Mwambie nakuja, ngoja nimalizie”
Erica akaondoka zake, Sarah alikuwepo kasimama tu maana alimkuta Erica anasafisha uwanja ndio akamwambia kuwa amekuja kumtembelea Erick, basi Erica alivyorudi pale akamwambia,
“Kasema umsubirie anakuja”
“Nipeleke alipo nikamuone”
Basi Erica aliongozana na Sarah hadi kule nyuma ambako alikuwepo Erick akiosha gari, ila Sarah alivyomuona Erick alimkimbilia na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Erick tabia mbaya, napiga simu yako tangu jana hata hupokei, nakutumia meseji hata hunijibu jamani!”
“Ngoja nimalize kazi kwanza”
Basi Erick alijitoa kwenye mikono ya Sarah na kuendelea kuosha gari ila kiukweli lile swala la Sarah kumkimbilia Erick na kumkumbatia lilimuumiza sana Erica na kujikuta gafla akimchukia sana Sarah, kwani muda ule ule aliondoka zake, hata kule kusafisha uwanja hakuendelea tena kwani moja kwa moja alienda chumbani kwake na kwenda kuoga kisha kubadili nguo na kujilaza kitandani maana alikuwa na hasira.

Muda huu Angel alimaliza kuosha vyombo na kuamua kurudi chumbani kwake, ila aliporudi akakutana na jumbe toka kwa Samir,
“Jamani Angel nimekumiss hadi nahisi kuumwa”
“Mmmh jamani Samir”
“Kweli yani, nakuja kwenu muda sio mrefu”
“Ila Samir unajua kama kwetu geti kali?”
“Najua bhana, ila nakuomba Angel fanya juu chini nikuone tu mpenzi wangu nakuomba Angel, nakupenda sana”
“Kwahiyo unakuja muda gani?”
“Nakuja muda sio mrefu nitakwambia”
Basi Angel akajiandaa pale kwani alijua wazi kuwa Samir anaweza hata akakodi pikipiki ili awahi na kweli baada ya muda kidogo tu ujumbe wa Samir ukaingia kwenye simu ukisema,
“Angel, njoo nje basi mara moja tu”
Basi Angel akatoka chumbani kwake, ila pale sebleni alimkuta bibi yake na mama yake ambapo mama yake alimuuliza,
“Unaenda wapi Angel?”
“Aaaah kuna kitu nakiangalia hapo nje ya geti tu”
Basi Angel akatoka nje ila kiukweli hakupenda vile mama yake anavyomfatilia sana kwenye mambo yake, muda kidogo bibi yake Angel nae akamwambia mama Angel,
“Eeeeh mwanangu, na mimi ngoja nikatembee kidogo nje ya nyumba yako yani sijawahi kutembea tembea hata kidogo jamani!”
“Kheee kwahiyo mama unaenda kutembea nje ya geti?”
“Ndio, nione na mandhari ya nje kabla sijaondoka, maana kuondoka kwenyewe kwenye gari, nitaangalia muda gani hiyo mandhari!”
“Sawa mama”
Basi bibi yake Angel nae akainuka na kutoka, ila alipotoka nje ya geti akamkuta Angel na Samir ndio wamekumbatiana, basi aliwasogelea karibu na kuwaachanisha, kiukweli Angel aliona aibu sana ila bibi yake alimuangalia Samir na kumwambia,
“Wewe si ni Samir jamani!!”
Angel alishangaa kuwa bibi yake kamfahamu vipi Samir!!


Basi bibi yake Angel nae akainuka na kutoka, ila alipotoka nje ya geti akamkuta Angel na Samir ndio wamekumbatiana, basi aliwasogelea karibu na kuwaachanisha, kiukweli Angel aliona aibu sana ila bibi yake alimuangalia Samir na kumwambia,
“Wewe si ni Samir jamani!!”
Angel alishangaa kuwa bibi yake kamfahamu vipi Samir!!
Ila Samir alionekana kuona aibu sana na kumsalimia bibi huyu,
“Shikamoo”
Halafu akageuka na kuondoka zake yani hata nyuma hakuangalia tena, basi bibi Angel alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, huku akitikisa kichwa chake aliingia nae ndani hadi chumbani kwake ambapo mama Angel nae aliwaona na kuwafata nyuma, basi bibi Angel alimkalisha Angel kwanza na kumuuliza,
“Hivi unamfahamu vizuri Samir?”
Angel alikuwa kimya tu, mama yake akadakia,
“Samir tena!!”
“Nimemkuta nae nje”
“Kheee jamani Angel jamani, kwanini lakini!”
Mama Angel akashikwa na hasira na kusogea karibu na Angel kisha kumnasa vibao kama vitatu ambapo alikatishwa na bibi yake Angel kwa kumwambia,
“Kupiga mwanangu sio suluhisho, unajua mara nyingine sipendi makosa ambayo niliyafanya kwenu yakajirudia ila kuna wakati naona ni heri kumpiga mtoto ili kuweka akili yake sawa, ila kwa muda huu tuongee tu na Angel”
Kisha bibi yake Angel alimuangalia Angel na kumwambia,
“Angel, katika wamama ambao hawawezi kulea mtoto bila kumpiga basi mimi ni namba moja, yani hivi mama yenu anavyowapiga huwa anawagusa tu, maana mimi nikiamua huwa napiga hatari, uliza mama zako wote wakupe habari zangu, halafu kitu kingine ujinga sipendi kabisa. Unajua wakati mama yako akilalamika sikujua ni kwanini analalamika mpaka nilipokuona leo, unajua ningetaka kukupiga basi ningekupiga sana pale na hakuna wa kunizuia yani tambua hilo kabisa. Ila ninachotaka sasa ni kukufundisha kuhusu maisha, upo tayari kunisikiliza”
Kwa aibu Angel alijibu kuwa yupo tayari kumsikiliza basi bibi yake akaanza kuongea,
“Mara nyingi nimekuwa nikija chumbani kwako na kuongea nawe kuhusu mahusiano, Angel wewe bado ni binti mdogo sana usitake kuharibu maisha yako mapema kiasi hiki! Unafikiri ni kitu gani kinachofanya mwanaume akufate fate hivyo? Ni huko chini ndio kunamfanya aje mara kwa mara, na akikupata huko basi thamani yako ndio inapoanzia kushuka na itashuka kila siku, akikupa mimba ndio kabisa yani thamani yako itakuwa chini kabisa, unatakiwa ujithamini, jiheshimu na ujipende. Angel wewe ni binti mzuri sana ila kujiachia kwako kwa wanaume basi uzuri wako utapotea, thamani yako itapotea na utaonekana sio chochote wala sio lolote. Angel acha ujinga mjukuu wangu, acha ujinga kabisa, mimi huwa siongei jambo moja mara mbili. Nadhani umenielewa, nenda chumbani kwako tu”
Muda huu mama Angel alikuwa kajiinamia tu kwani alijikuta akiwa na hasira sana juu ya mwanae, haswaaa baada ya kusikia kuwa alikuwa na Samir, ila Angel alipoondoka alikaa chini na mama yake na kumuuliza,
“Kwani mama huyu Samir unamfahamu au wamejitambulisha kwako?”
“Namfahamu vizuri yule mtoto, unajua bibi yake ni rafiki yangu sana, yani Samir na Angel wamepishana mwaka mmoja tu, nakumbuka siku yule binti anapata uchungu nilikuwa kwao na hadi anajifungua nilikuwepo. Baada ya hapo alikuwa akiulizwa kuhusu baba wa mtoto anabaki kulia tu”
“Kheee kwahiyo Samir baba yake ni nani?”
“Simjui ila baba yake Samir nasikia alikuwa ni muhuni sana, alikuwa na mahusiano na wanawake wengi, yani yule binti alikuwa akilia tu. Ila kwasasa ana maisha yake, kaolewa na anaishi na mumewe, ila ana watoto wawili tu, sema huyu wa pili ndio huwa simjui ila ni wakike na hawa watoto basi baba zao ni tofauti, sasa Angel anataka maisha ya namna hii jamani!! Maisha ya kuishi na kila mtoto na baba yake!! Sio maisha kabisa, unajua njia ulizopita wewe naona haka katoto kako nako kama kanataka kupitia, unatakiwa kuwa makini sana kumfundisha huyu mtoto ili asipitie kwenye hizo njia”
“Nimekuelewa mama”
“Nafurahi kama umenielewa, ila itakuwa vizuri zaidi kama nikienda kuishi na Angel nyumbani kwangu hadi matokeo yatakapotoka”
“Oooh mama, hilo ni wazo zuri sana. Nashukuru kwa hilo, yani huyu Angel yupo kuniumiza kichwa tu ila hilo ni wazo zuri mama, unapoondoka basi utaondoka nae, ngoja nikamwambie ajiandae kabisa maana kesho safari”
Kwakweli mama Angel alifurahi sana kwa Angel kwenda kukaa kidogo na bibi yake kwani aliona kidogo tabia ya Angel inaweza kutengemaa maana hata yeye aliharibika akili alivyoenda chuo ila kwa mama yake alikuwa akikaa sawa na kufata maadili ya mama yake.
 
SEHEMU YA 217

Angel alitulia chumbani kwake huku akifikiria siku hiyo alivyobambwa, ila akaja kuletewa taarifa na mama yake kuwa ajiandae maana ataondoka na bibi yake,
“Aaaah mama jamani, nyie si mmenitoka kunitoa kwa bibi yule!”
“Sitaki maneno mengi Angel, jiandae hapo ulipo na ujue kabisa kesho unaondoka na bibi yako”
Kisha mama yake akatoka na kumfanya Angel abaki amekasirika sana kwani bibi yake huyo alimfahamu vizuri sana, basi akachukua simu yake na kumtumia ujumbe Samir,
“Mwenzio nimeambiwa kuwa kesho nitaondoka na bibi, jamani umeniponza Samir, yule bibi alivyomkali yani itakuwa ngumu kwetu kuonana”
“Usijali Angel, tutaonana tu. Maana huyo bibi ni kama bibi yangu ila najua kuonana kwetu kutakuwa kwa masharti sana ila usijali”
“Sawa, yani nimekosa hata amani halafu kumkatalia mama siwezi”
“Sawa mpenzi nimekuelewa kabisa, usijali kitu”
Basi Angel aliamua tu kufanya maandalizi kama alivyoambiwa na mama yake ila kiukweli hakupenda kwenda kuishi kwa bibi yake kwani alielewa malezi ya bibi yake huyo yalivyokuwa.
Wakati akiendelea kujiandaa, mara aligonga Vaileth mlango wake na kumkaribisha kisha Vaileth alianza kuongea nae,
“Angel nasikia kesho unaondoka na bibi, ni kweli?”
“Ndio hivyo, yani nitakoma maana huyo bibi namfahamu fika alivyo na mambo yake”
“Ooooh pole mdogo wangu, jinsi huyu bibi anavyojua kufatilia mambo yani hadi nakuhurumia”
“Yani acha tu, nimechukia hapa balaa, wewe umewasikia au?”
“Ndio, nimewasikia wakiongelea basi nikamsema mmmh nimeanza kuwa Erica sasa kusikiliza yasiyonihusu”
Angel alicheka na kusema,
“Yani kale kaErica sijui tabia ya umbea katoa wapi jamani, mtoto ni mbea yule sijapata kuona, baba sio mbea, mama sio mbea ila yeye sasa akipata jambo anawashwa mdomo balaa”
“Mmmh Angel una maana gani sasa?”
“Aaaah sina maana yoyote, ila Erick na Erica kiukweli kabisa hawafanani, si sura wala sio matendo yao maana Erick ni mstaarabu, muelewa na mpole, ila Erica sasa uwiii ni mbea, anapenda kufatilia mambo ya watu, akisikia tu watu wanaongea kidogo basi yeye kashayabeba, yani yule mtoto jamani!”
“Labda kuna ndugu yenu yuko hivyo, maana mbona Erica kafanana sana na mama yako! Yani kafanana nae sana kasoro huo umbea”
“Aaaah aliyefanana na mama ni mimi bhana na sio Erica”
Basi Vaileth akacheka tu, halafu Angel akaendelea kuongea,
“Ila licha ya hivyo jamani Erica ni mbea hadi huwa siongei nae mara kwa mara wakati ni mdogo wangu ningekuwa napanga nae vitu vingi ila umbea wake hadi unakera”
Vaileth alicheka na kumuacha Angel aendelee kujiandaa.

Erick alipomaliza kuosha gari yani siku hiyo anaonekana hata hakupenda Sarah kwenda nyumbani kwao, basi alimwambia asubiri aende kuoga kwahiyo Sarah alimsubiri kule kule nje walipokuwa wakiosha magari, muda huo hata Junior alishaingia ndani na kujiandaa ila muda kupita bila ya Junior wala Erick kurejea Sarah alijiuliza kuwa tatizo ni nini, ila alipotaka kuinuka tu alifika pale Junior na kusema,
“Kheee bado upon je jamani mtoto mzuri dah! Karibu ndani jamani”
Basi Sarah aliongozana na Junior hadi ndani ambapo muda huu walimkuta mama Angel sebleni na baada ya kumuona tu Sarah alitabasamu ambapo Sarah nae alitabasamu kisha akaenda kumkumbatia huku akimuuliza,
“Eeeeh za kwenu Sarah!”
“Nzuri tu, mama anakusalimia”
“Oooh wow, naomba ukirudi usalimie pia binti yangu. Vipi lakini za tangu siku ile”
“Ni nzuri kabisa”
“Nafurahi kusikia hivyo na nimefurahi kukuona kwa leo, kumbe kweli Erick alivyosema kuwa unakuja, oooh nimefurahi sana”
“Na mdogo wangu hajambo!”
“Hajambo, kachangamka sana kwasasa”
Basi bibi Angel akaja na mtoto Ester amembeba maana alikuwa ameamka, basi yule bibi alivyofika pale Sarah alimsalimia vizuri sana na akahitaji pia kumsalimia mtoto ambapo bibi alimpa ili amsalimie ila leo wakati Sarah amekaa na yule mtoto akasema,
“Yani mama jamani huyu mtoto amekufanana hatari, leo ndio nimemuangalia vizuri, ni wewe mtupu”
Mama Angel alikuwa akitabasamu tu ila bibi Angel aliongezea na kusema,
“Ila kweli Ester kakufanania sana jamani, yani Ester kakukopi vile ulivyo hapa mwanangu umejizaa”
Mama Angel akamchukua mtoto wake huku akimuangalia vizuri na kutabasamu na wote walijikuta wakitabasamu na kufurahi.

Erick alijua wazi kuwa mdogo wake amechukia sana siku hiyo, kwahiyo alivyomaliza kujiandaa alienda moja kwa moja chumbani kwa Erica na alimkuta amejilaza, basi alianza kuongea nae kwa kumuamsha,
“Erica, Erica jamani Erica”
Erica alishtuka na kukaa kwanza huku akimsikiliza kaka yake,
“Sasa Erica umechukia nini jamani mdogo wangu!”
“Hapana sijachukia mbona”
“Erica, mimi nakufahamu vizuri sana na najua umechukia baada ya kumuona Sarah, hebu nisikilize hili kwanza”
Erica alikaa vizuri na kumsikiliza kaka yake,
“Sikia Erica, katika maisha yangu basi wewe ndiye ndugu yangu bora sana, kumbuka tumezaliwa wote na tumenyonya wote, tumecheza wote michezo yote inayojulikana, ukilia nipo, nikilia upo, nakuonea huruma na unanionea huruma. Jamani uwepo wa Sarah ndio ukuondoe amani jamani Erica! Kumbuka mimi ni nani kwako, kumbuka jinsi tulivyo mimi na wewe, yani Sarah ni mpita njia tu, tena ningependa awe rafiki yako maana ni rafiki yangu pia, akiwa rafiki yako utaona kuwa hana matatizo yoyote yale, usiwaze vibaya mdogo wangu nakupenda sana”
Kisha Erick alimsogelea mdogo wake na kumkumbatia, kitendo hiko kilimfanya Erica ajihisi vizuri, kwani katika maisha yake alikuwa akipenda sana kujihisi kuwa anapendwa ndiomana hata swala la kuwa mtoto wa mwisho alilifurahia sana kwani aliona atakuwa akipendwa mno na wazazi wake, huku wakimsikiliza na kumthamini yeye, ila baada ya kupata mdogo wake aliamua kuishi kwa kutokudeka ila bado anapenda sana kugundua kuwa anapendwa sana kwahiyo alifurahi, kisha Erick alimuomba kuwa waende pamoja kuongea na Sarah ambapo Erica alikubali na wakaenda pamoja.
Basi waliongea na Sarah pale mambo mbalimbali hadi Sarah alipoaga na mama Angel kumwambia tena Erick kuwa ampeleke, ila Sarah alikuwa akipenda sana ule muda way eye kuwa peke yake na Erick kwahiyo siku hiyo hakufurahi sana kwani aliona kama Erica anambania vile.
Muda wa kuondoka, bado Erick alimuangalia Erica na kumtaka wamsindikize kwa pamoja Sarah, kwahiyo siku hiyo walipanda kwenye gari watatu yani Erick, Erica na Sarah na siku hiyo Sarah alikaa siti ya nyuma kwani pale mbele isingewezekana kukaa watatu.
Moja kwa moja walienda hadi kwakina Sarah yani siku hiyo kwenye gari ilikuwa ni kimya kimya, tofauti na ile siku ya kwanza ambayo walikuwa wakiongea mambo mbalimbali wakati wapo Erick na Sarah tu.
Walifika nyumbani kwakina Sarah na walimkuta mama Sarah ambaye alipowaona kama kawaida alishindwa kujizuia machozi yake kwa Erick, kwani alimsogelea na kumkumbatia huku akilia, na leo alilia kwa muda mrefu kidogo kwahiyo Sarah na Erica walisimama pembeni tu wakimuangalia jinsi yule mama alivyomkumbatia Erick huku akilia, na baada ya hapo aliwalazimisha kuingia ndani kwake ili kupata chochote cha kula, ila leo Erica aliweka mgomo na kudai kuwa wana haraka sana kwahiyo ilibidi wage tu na kuondoka zao.
Wakiwa ndani ya gari Erica alimuuliza Erick,
“Kwahiyo hata siku ile ulipokwenda kumsindikiza huyo Sarah ulikula kwao? Naona tu maana hata leo bila ya mimi ulitaka kukubali, ushasahau mama huwa anasemaje?”
“Mmmh jamani Erica, mbona hata Sarah anakula kwetu kwanini sisi tushindwe kula kwao?”
“Kula sehemu ni mpaka mama akubali, uoni mimi nilikuwa nakuja na visheti nyumbani! Ingawa nilikula vingine kisirisiri ila mama alinisema sana na nilimuahidi kutokurudia tena, sisi tutakula kwakina Sarah mpaka pale mama atakapomfahamu vizuri mamake Sarah”
“Mmmh wewe nawe kwa kukuza maneno hujambo”
Basi waliendelea tu na safari na kurudi nyumbani kwao.

Baba Angel alirudi nyumbani kwake na kama alivyokuwa amemuahidi mke wake basi alirudi na zawadi ya kumpa mama yao, ambapo moja kwa moja alienda kumkabidhi zawadi hizo, hata bibi Angel alizifurahia sana kisha baba Angel sasa moyo wake ukawa mweupe kumruhusu mama yao,
“Sasa mama, moyo wangu mweupe kabisa nakuruhusu”
“Kumbe mlinikataza sababu ya zawadi jamani watoto wangu! Mmesumbuka jamani!”
“Hamna mama hata usijali kitu, inapaswa kufanya hivi kwako maana umetuhudumia sana hapa nyumbani, umetulea, umeacha mambo yako mengi sana kwaajili yetu kwahiyo yatupasa kufanya hivi mama”
“Haya, nashukuru sana wanangu”
Basi baba Angel alirudi chumbani kwake kwani alikuwa amechoka, mke wake alimfata na kumpa habari kuwa Angel ataondoka kesho na mama yao,
“Jamani, tunampa tena mama mzigo wa Angel?”
“Hamna, mama atakaa nae vizuri tu, naomba ukubali hilo mume wangu. Naelewa mama yangu alivyo”
“Hata mimi namuelewa sana”
“Unajua leo mama kamkuta Angel na Samir getini kwakweli kachukia sana, halafu anamfahamu vizuri sana Samir, hamfai mtoto wetu, nasikia baba yake ni muhuni sana kwahiyo lazima Samir atakuwa na tabia za baba yake. Halafu siku ile ulisema kuna mtu unamfananisha na Samir ni mtu gani?”
“Oooh nitakuonyesha tu siku moja, utamuona ila unamfahamu sema humfahamu kivile ni rafiki yangu”
“Oooh hapo sawa, nikajua ni ndugu yako”
Baba Angel alicheka kwa muda kidogo na kusema,
“Ila huyo rafiki yangu sio muhuni kwahiyo hawezi kuwa baba wa Samir”
“Na kweli maana duniani ni wawili wawili, ila hata hivyo mara nyingine unakuta mtoto na baba wanafanana kwa mbali sana kama wewe na baba yako mlivyokuwa”
“Oooh umenikumbusha yule mzee wangu, alikuwa ni mzee mtata, ila nilimpenda jamani baba yangu, dah angekuwepo hadi leo aangalie wajukuu zake”
“Na hivi Angel alivyokuwa anavutia unadhani baba yako anagejistahi amuache!”
“Mmmh ushaanza hivyo na maneno yako ya kijinga, hata kama baba alikuwa na tabia mbaya ila bado asingeweza kumtamani mjukuu wake, kwani Angel ni kama mjukuu wake pia. Halafu kumbuka japo fadhila za baba yangu jamani, kumbuka baba ndio alisimamia harusi yetu yote yani yeye ndiye aliyegharamia kila kitu, kumbuka pia wakati unajifungua hawa mapacha wetu ni baba yangu ndio alikuwa karibu”
“Ila Erick hujui tu, mimi nafahamu mambo mengi sana ila sikuweza kukwambia kwani sikutaka ugombane na baba yako, hujui tu ni kwanini baba yako aligharamia harusi yetu na kuhusu kuwepo wakati najifungua ilibidi iwe vile kwani ni yeye aliyekupa kazi wewe kwahiyo hakukuwa na namna zaidi yayeye kuwepo. Namshukuru kwa mazuri aliyotufanyia, ila Erick baba yako alikuwa ni kichomi, hujui ni nini alikuwa akiongea na mimi kila alipokutana nami, kuna mengi yapo kwenye moyo wangu nadhani nikisema utaona kamavile namkosea heshima marehemu mkwe wangu. Ngoja niishie hapo”
“Ndio bora uishie hapo maana sio vizuri kuwaongelea vibaya marehemu”
Muda huo waliamua kubadili mongezi na kuendelea na maongezi mengine ya jinsi ya kumfikisha mama yao nyumbani kwa siku ya kesho.
 
SEHEMU YA 218

Basi usiku wa leo Angel alikuwa na mawazo tu ya kwenda kuishi kwa bibi yake yani alimtambua vizuri bibi yake huyu basi alikuwa akiongea mambo mbalimbali na Samir kwenye simu,
“Jamani Smair ndio kesho hivyo naenda kwa bibi”
“Hakuna namna Angel, najua wazi ukikataa basi watakuhisi vibaya sana, tutakuwa tukiwasiliana tu kama kawaida na kuonana tutakuwa tukionana kwani nitakuwa nakuja chuo”
“Ila nahisi bibi atakuwa na tabia Fulani kama za shangazi, maana hadi ilikuwa nikichelewa kurudi shule dakika mbili tu lazima niwe na maelezo ya kutosha ingawa nilikuwa narudi na dereva, huyu bibi si ndio balaa”
“Wala usihofu kitu mpenzi wangu”
Wakawasiliana sana kwa muda huo na kama kawaida waliongea sana hadi mwisho wa siku walilala muda ukiwa umeenda sana.
Kulipokucha, Angel alikuja kushtuliwa na mama yake maana tayari ilikuwa pamekucha halafu yeye alikuwa bado amelala, basi mama yake akamwambia.
“Wewe Angel hebu amka ujiandae kuondoka”
“Kheee mama ndio mapema hivi!!”
“Ndio, mambo yote asubuhi”
Basi Angel aliinuka na kujinyoosha halafu alienda kuoga na kujiandaa baada ya kutoka alimkuta bibi yake alishajiandaa na baba yake kwahiyo alipotoka tu aliaga ndugu zake na moja kwa moja kutoka nje pamoja na bibi yake na baba yake kwaajili ya safari yani Angel alikuwa amepanda kwenye gari huku amepooza sana na safari ilikuwa ikiendelea.

Basi siku hii wakina Erica walivyoenda Kanisani, mama Angel alimuagiza dreva wao akamtafutie zawadi kwaajili ya mama mkwe wake kwani naye alitaka wakamshtukize mama mkwe wake, nyumbani alibaki yeye na Vaileth basi walikuwa wakiongea mambo mbalimbali,
“Hivi Vaileth mwanaume uliyezaa nae yuko wapi?”
“Mama, alikataa mimba ikiwa ndogo kabisa yani nilijihisi kama nimetengwa basi nilihangaika na ile mimba hadi kujifungua, mtoto wangu ni wakike, alipofikisha miaka mitatu yule mwanaume akatokea na kumtaka mtoto, basi nyumbani wakamwambia alipe faini, ila alijigeresha kufanya hivyo basi bibi yangu akaniambia kuwa nimpeleke kwake kwani yule mwanaume anaweza akamuiba, basi ndio mtoto nilimpeleka kwa bibi ndio kule mlikonikuta, maana nilikuwa nikienda kufanya kazi namuacha kwa bibi na ndio ipo hivyo hadi leo na ameshazoea mazingira ya kule kwa bibi, kwasasa ndio ana miaka mitano”
“Oooh, hapo nimekuelewa, kwahiyo huyo mwanaume hajakutafuta tena?”
“Hajanitafuta, nasikia kwanza ameoa ila mkewe hazai ndiomana alikuja kumchukua mtoto, nasikia anamtaka mtoto ila hataki kulipa faini”
“Jamani kuna wanaume vichomi sana loh! Kwasasa angalia maisha yako tu Vaileth”
“Ndio hivi dada”
Basi Vaileth aliendelea na mambo mengine, kisha yule dereva alirudi na zawadi ambazo mama Angel alimuagiza basi aliziweka vizuri na kujiandaa huku akimsubiria mumewe arudi.
Na baada ya muda kidogo tu baba Angel alirudi na mama Angel akamuomba waende kumuona mama mkwe wake,
“Kheee umekumbuka nini mke wangu?”
“Hamna nataka nikamuone tu”
“Ila mtoto bado mdogo”
“Aaaah sio mdogo huyu, mbona kakua sasa, twende tukamuone tu kidogo halafu tutarudi nishajiandaa na nishamuandaa mtoto”
Basi baba Angel hakuweza kukataa kwani muda huo huo aliondoka na mke wake kuelekea kwa mama yake ambapo kulikuwa na umbali kidogo na pale walipokuwa wakiishi.
Basi walipofika hata mama yule alishangaa sana kwani hakuamini kama wangeenda na ukizingatia hawajamwambia,
“Kheee jamani kweli mmeamua kunishtukiza mweeeh!!”
Kisha aliakaribisha ndani na walimsalimia vizuri sana ila alijihisi aibu maana tangu mama Angel ajifungue hakwenda kumuona, basi akamwambia,
“Erica mwanangu nisamehe bure tu, ila mlinikera kipindi kile kwa kitendo chenu cha kumchukua Angel bila ridhaa yangu”
“Tusamehe kwa hilo mama”
“Nishawasamehe tayari na nimefurahi kweli kuja kwenu kuniona”
Kisha Erica akampa mama mkwe wake zawadi ambazo alimtuma dereva, kwakweli huyu mama alifurahi sana kupokea zile zawadi ila akasema,
“Jamani, natakiwa mimi nimletee mjukuu wangu zawadi ila mimi ndio nimeletewa jamani!”
“Usijali mama”
Basi aliaenda kuziweka zile zawadi ndani, huku baba Angel akimwambia mama Angel,
“Naona ulitaka kunishtukiza na mimi jamani hata kuniambia kuwa umemnunulia mama zawadi!!”
Mama Angel alitabasamu tu, kisha bibi Angel alirudi na kuendelea kuongea nao ambapo baada ya muda kidogo tu walimuaga kuwa wanaondoka maana walichelewa kwenda na vile vile kule palikuwa ni mbali na kwao ila hakuwazuia kwani pia alifurahi kuwaona tu.

Siku hii ilikuwa ni kama kuwaachia ukumbi wakina Erica maana walivyotoka Kanisani walikuwa na furaha sana, ukizingatia wazazi wao wote hawakuwepo, basi waliweka mikanda ya ngumi sasa na kuanza kuangalia, ile mikanda ambayo ililetwa na Samia, basi walikuwa wakiongea pale ambapo Junior alianza kusema,
“Ila jamani bora bibi kaondoka, maana yule bibi alikuwa mnoko balaa”
Wote walikuwa wakicheka, basi Vaileth akasema,
“Yani mimi niliposikia anaondoka nilichekelea, ila sasa kazi ipo kwa Angel jamani mbona balaa kwake”
“Na kweli balaa, yule bibi yetu tunamfahamu vizuri sana, yani kule lazima Angel aumie moyo. Ila jamani tuache utani, yule bibi ndio kamfananisha Erica, huwa tunajiuliza Erica katoa wapi umbea ila ni kwa yule bibi”
Walicheka wote ila Erica alinuna, huwa hapendi kusemwa semwa kwa kitu anachokifanya kweli, kisha akainuka zake na kwenda chumbani kwake ila wenzie waliendelea kuangalia tu ule mkanda hadi wazazi wao waliporudi ndio waliposhtuka na kuzima tv.
Basi mama Angel cha kwanza kabisa alimuulizia Erica maana alijua lazima angekuwa pale anaangalia tv ila akaambiwa kuwa yupo chumbani,
“Mmmh mtakuwa mmemkorofisha mwanangu nyie, haiwezekani make hapa halafu yeye ajifungie chumbani”
Basi alienda kumlaza mtoto na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erica ambapo alimkuta kajilaza, akamuamsha na kuanza kuongea nae,
“Mwanangu, tatizo ni nini? Unaumwa?”
“Hapana mama, eti wanasema mimi umbea nimeutoa kwa bibi”
“Aaaah wajinga hawa, nani huyo aliyekuwa anakwambia hivyo!”
“Junior huyo mama”
“Aaaah achana nae, halafu mwanangu jana hujanipa habari ya kwakina Sarah ulivyorudi nimehisi kama unajambo maana ulikuwa unakuja chumbani kunichungulia na kuondoka, eeeh niambie mwanangu”
“Mmmh mama, tulivyofika kwa kina Sarah basi mama yake Sarah akamkimbilia Erick na kumkumbatia halafu akaanza kulia yani alilia kwa muda mrefu sana”
“Mmmmh mbona unanishangaza Erica, kwanini alilia sasa?”
“Sijui mama, halafu baada ya hapo akaanza kutulazimisha tule chakula ila mimi nilikataa na kumtaka Erick tuondoke basi ndio tukarudi nyumbani”
“Oooh natakiwa nimfahamu huyo mama yake Sarah”
Mara simu ya Erica ilianza kuita, basi mama yake alimuangalia na kuuliza,
“Nini hiko kinaita kama simu?”
Erica alibaki kimya akimuangalia mama yake.
 
SEHEMU YA 219

Mara simu ya Erica ilianza kuita, basi mama yake alimuangalia na kuuliza,
“Nini hiko kinaita kama simu?”
Erica alibaki kimya akimuangalia mama yake.
Ilibidi mama yake amuulize kwa ukali kwani ile simu ilizidi kuita,
“Nimekuuliza nini hiko kinaita kama simu?”
Basi mama yake alikuwa kama anataka kumpiga, katika vitu ambavyo Erica alikuwa akiogopa ni kupigwa basi kwa haraka haraka aliitoa ile simu na kumpa mama yake huku akimwambia,
“Mama nisamehe”
“Haya, umetoa wapi hii simu, nani kakupa simu Erica unajua wewe ni binti mdogo sana!”
“Kanipa kaka Junior?”
“Una uhakika kakupa Junior! Kakupa kwa misingi ipi, yani kwanini Junior akupe simu utumie?”
“Mama, baada ya kumuona Erick akiwa na simu nami nilitamani simu basi kaka Junior akaenda kuninunulia”
“Kheee kumbe na Erick ana simu!! Kaitoa wapi na yeye?”
“Ni baba ndio alimnunulia”
“Aaaah humu ndani jamani, yani mtu lazima upatwe na ugonjwa wa moyo. Haya lete hiyo simu na huyu Junior atanieleza ni kitu gani kimemfanya hadi akununulie simu”
Erica alimkabidhi mama yake ile simu ambapo mama yake alitoka kwa hasira na kumuita Junior na kuanza kumfokea kwanini kamnunulia simu Erica, yani Junior alianza kuwa na mashaka kuwa huenda Erica kasema ukweli wote ila ilibidi anywamaze tu, basi mama Angel alimsema sana na kuondoka zake.
Moja kwa moja Junior alienda kuongea na Erica ili kumuuliza vizuri,
“Imekuwaje Erica hadi umekamatwa na simu?”
“Kaka ile simu hukunitolea mlio, leo imeita basi mama kasikia, yani sikuwa na watu wa kunipigia simu ila leo kuna mtu alikuwa akipiga ndio mama kasikia”
“Kwahiyo umemuelezea kila kitu?”
Erica akamwambia vile alivyomwambia mama yake, basi Junior alitabasamu na kusema,
“Kwasasa nimekupenda bure Erica, yani hujasema kuhusu hili oooh asante sana, yani nimekupenda mno mdogo wangu. Usijali acha mama aichukue hiyo simu ila nitakuwa nakuletea vitu vizuri vizuri mara kwa mara”
“Ila unajua Erick atachukia sana baada ya mimi kumsemea kwa mama kuwa ana simu!”
“Aaaah usijali kwani hata hivyo mama angejua tu, sababu baba angemwambia. Usijali mdogo wangu, kesho tu nitakuletea zawadi yako”
Basi Erica alitabasamu tu na kumfanya Junior aondoke akiwa na furaha sana kwani kwake ilikuwa raha mno kwa kugundua kuwa Erica hajasema ukweli.

Mama Angel alienda chumbani moja kwa moja kuongea na mume wake ambaye kutokana na uchovu aliokuwa nao basi alikuwa amelala muda huo, ilibidi mama Angel amuache tu mumewe apumzike kwani hata yeye alitambua ni kiasi gani ambavyo mumewe amechoka kwa siku hiyo.
Ila aliona jambo la msingi kwanza ni kwenda kumpokonya Erick simu aliyoambiwa kuwa anatumia, basi alitoka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erick ambapo alimkuta Erick ndio anatumia ile simu ambayo aliificha baada ya mama yake kuingia,
“Erick nimekuona na hiyo simu, haya ilete”
Ilibidi Erick aitoe na kumkabidhi mama yake, kisha mama yake akamuuliza,
“Baba alikununulia simu kwa misingi ipi?”
“Ili niwasiliane nae”
“Uwasiliane nae muda gani wakati muda wote tunaonana hapa nyumbani, mwanangu yawapasa kuwa makini na masomo yani kwasasa kitu muhimu katika maisha yenu ni elimu na sio mambo ya simu. Tunakutegemea wewe ndio mlezi wa familia, wewe ndio wa kuwaangalia dada zako halafu wewe ndio unafanya ujinga wa kutumia simu kweli!! Achana na mambo ya simu jamani! Nadhani umenielewa”
“Nimekuelewa mama”
Kisha mama Angel alitoka na kurudi chumbani kwake ila muda sio mrefu Erica alienda chumbani kwa Erick ili kumuomba msamaha, alimkuta Erick kajiinamia tu kwani mama yake amechukua simu wakati ndio alitaka kumjibu ujumbe Sarah, basi Erick alimshtua pale na kumwambia,
“Naomba unisamehe Erick”
“Umefanya nini kwani?”
“Mama leo kanibamba na simu basi nikamwambia ukweli kuwa hata wewe unayo”
“Dah! Erica wewe ni mtu wa ajabu sana, unajua mama hajasema ni nani kamwambia wala nini, nilijua ni baba kaamua kumwambia mama ukweli kumbe ni wewe! Hata hivyo nadhani baba alimwambia mama siku nyingi tu ila hakutilia maanani sema leo ulipomwambia wewe ndio kaelewa, jamani Erica mambo yako sijui hata nikufananishe na nini jamani!”
“Ila nisamehe jamani Erick”
“Nishakusamehe hatabusijali mdogo wangu”
Kwasasa Erica alifurahi na kumuaga kaka yake kisha kurudi chumbani kwake kulala.

Usiku wa leo ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa upande wa Junior, kwanza bibi yao hakuwepo tena halafu Erica hakusema ukweli licha ya kukamatwa na simu, basi Junior kama kawaida alienda chumbani kwa Vaileth huku akisifia sana siku ile,
“Yani Vaileth hujui tu jinsi mimi na wewe tunavyopendana, hata Mungu anatambua hili ndiomana tunaachiwa nafasi kubwa ya kuwa pamoja”
Vaileth akatabasamu na kuuliza,
“Kivipi?”
“Kwanza bibi hayupo, halafu unajua nini leo Erica alibambwa na simu na mamdogo yani leo ndio ingekuwa siku mbaya kabisa kwetu kwa jinsi Erica alivyokuwa mbea halafu maneno yake yanavyoaminika kwenye nyumba hii, ni hivi Erica kamdanganya mamdogo kwahiyo tupo huru kabisa”
“Mmmh siamini, kwahiyo Erica hajasema ukweli?”
“Ndio, nadhani kaanza kukua sasa kwahiyo kaanza kujitambua”
Basi wakafurahi sana na siku hiyo walilala huku wakitabasamu muda wote kwani walikuwa na furaha sana.
Kulipokuchja, Vaileth aliamka na kumuacha Junior bado amelala chumbani kwake, basi alienda kusafisha nyumba ila baada ya muda kidogo mama Angel alimfata Vaileth na kumuuliza,
“Umemuona Junior ametoka?”
“Hapana mama”
“Jamani, yuko wapi huyu mtoto asubuhi yote hii!! Nina shida nae halafu nadhani chumbani kwakwe hayupo, kafunga mlango na nimeita sana. Ngoja nikaulize kwa mlinzi kama kamuona kutoka”
Basi mama Angel alienda nje na moja kwa moja Vaileth alienda chumbani kwake kumkurupua Junior ili arudi kwake,
“Weee Junior, mama anakutafuta huko hebu amka”
Basi Junior aliinuka na kujinyoosha kisha kuamka halafu kutoka ila alipokuwa nje tu akakutana na mamake mdogo ila Junior alijegeresha kidogo ambapo mama Angel alimuuliza,
“Ulikuwa wapi wewe?”
“Nilienda ile sebule nyingine, nilikuwa nasoma soma magazeti”
“Mmmh mbona macho yako yanaonyesha kuwa ndio umetoka kuamka?”
“Kumbe nilisinzia kule mamdogo, nisamehe bure”
“Haya nenda kajiandae mara moja, kuna mahali nataka nikuagize”
Basi Junior alienda kujiandaa na alipomaliza alienda na kuagizwa na mama yake mdogo, ila alipomuagiza palikuwa ni ofisini.
Junior alivyoondoka tu, mama Angel alipigiwa simu na dada yake,
“Jamani! Leo mapema yote hii dada umeniota au?”
“Hapana mdogo wangu, ila nimemkumbuka tu Junior jamani nimeshangaa nikipatwa na mawazo kweli kuhusu Junior, yuko hapo niongee nae”
“Oooh samahani dada, kuna mahali nimemuagiza”
“Asubuhi hii ni ofisini nini?”
“Ndio ni ofisini, kwenye ile ofisi iliyokuwa ya baba yake, kuna kitu cha muhimu walikuwa wakikihitaji na mimi ndio nilikuwa nafahamu, sasa si unajua uzazi tena sijaweza kwenda ndio nimemtuma Junior”
“Mmmh wewe nawe ulikuwa ukifahamu nini, nakumbuka ile ofisi ulifanya kazi za kujitolea tu na hata hukufanya kwa muda, ila dah! Nimekumbuka kitu jamani”
“Kitu gani?”
“Unajua ile ofisi ilitakiwa iwe ya Junior kwasasa, jamani kweli maisha yanabadilika sana, nakumbuka wakati nina mimba ya Junior basi mume wangu alikuwa akifurahi sana huku akinishika tumbo langu na kusema huyu ndio mrithi wangu ila leo hii dah!”
“Aaaah dada jamani! Kila kitu ni Mungu anapanga, na kama ofisi ilitakiwa kuwa ya Junior basi amini kuwa siku moja itarudi mikononi mwa Junior, hata mimi sikujua kama naweza kutafutwa na watu wa ile ofisi hadi nimemtuma Junior, elewa kila kitu Mungu anajua ni kwanini kimetokea”
“Naelewa, ila jamani maisha haya, kuna mambo nikikumbuka huwa machozi yananitoka tu”
“Jamani dada, usiseme hivyo. Nadhani inatakiwa tupate muda wa kuzungumza zaidi, basi njoo kwangu”
“Sawa nitakuja mdogo wangu”
Basi wakaagana pale kisha mama Angel alienda kuendelea na kazi zingine.
 
Back
Top Bottom