Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 276

Ila Erica alivyotoka chumbani kwa Vaileth moja kwa moja alienda bustanini maana alimuona Junior akielekea huko basi alimkuta na kuanza kuongea nae,
“Umemfanya nini dada Vai?”
“Kwanini?”
“Nimemkuta macho yamemvimba, kanidanganya kuwa macho yanamuuma ila anavyoonekana ni kuwa amelia sana”
“Mmmh mimi sijui kitu”
“Halafu kitu kingine, siku ile Samia amekuja amesema kuwa ulimpatia laki tano”
“Mmmh huyo Samia chizi eeeh!”
“Ndio kasema, pia kasema wewe hakupendi wala nini ila kuna mwanaume mwingine kwenye nyumba yetu ndio anampenda”
“Haya sasa umeona kama Samia ni chizi, anamaanisha kuwa anampenda Erick”
Hapo Erica akashtuka kidogo na kuuliza tena,
“Unasema?”
“Ndio hivyo anampenda Erick, sasa unashtuka nini? Samia ni msichana na Erick ni mvulana, tatizo liko wapi wakipendana? Hutaki wifi wewe? Ndio nyie ambao huwa mnagombana na mawifi zenu bila sababu”
“Kwani mimi nimesema jambo lolote”
“Hata kama ila nakuelewesha”
“Ila umebadili mada tu, umemuhonga Samia laki tano!!”
Vaileth akaenda kule bustanini pia maana alikuwa anataka kufagia kidogo na kuweka mazingira safi, kwahiyo alisikia haya maneno ya mwishoni na kumfanya aelewe zaidi kuwa kwanini Junior aling’ang’ania kumsindikiza Samia siku ile, kwahiyo Vaileth akazidi kupata ushahidi.
Basi alisogea pale na Junior alimsalimia ila hakumuitikia yani moyoni mwake alikuwa na kinyongo sana.

Kisha muda wa kwenda kanisani leo wote walijiandaa na kwenda Kanisani kama kawaida ya nyumba hii, na leo ni nyumba nzima waliondoka na kwenda Kanisani.
Huku nyumbani alifika Derrick ambaye alikaribishwa na mlinzi tu na kwenda kukaa kwenye kibaraza kwani familia nzima hii haitakuwepo kwa siku hiyo.
Basi alikaa pale kwenye kibaraza hadi akasinzia pale pale, ila wakati amesinzia akajiwa na ndoto na hiyo ndoto aliona watu wengi wamemzingira huku wakisema mwizi huyooo, mwizi huyooo piga pia, Derrick alishtuka sana huku akihema, akaamka na kujisemea,
“Ila mimi sio mwizi, mimi siibi na simpori yoyote ila wanatoa kwa hiari yao, nitakuwaje mwizi sasa?”
Akaona hapo hata hapamfai kuendelea kusinzia sababu alikuwa na mambo yake mengi tu ya kufanya basi aliinuka na kumuaga mlinzi na kuondoka zake.
Wakati anaondoka ndipo akakutana na Tumaini ambaye nae alikuwa akienda mahali hapo, ila alikuwa ameongozana na rafiki yake kwa muda huo basi akamuuliza Derrick,
“Kheee Derrick, leo ulikumbuka kuja kwa dada yako!”
“Ndio, nilitaka kumsalimia maana nimemkumbuka sana ila sijawakuta”
Huyu rafiki yake Tumaini alishtuka kidogo na kumuuliza Derrick,
“Kaka, hunikumbuki?”
“Nikukumbuke kwani tumesoma wote?”
“Hapana sio hivyo, mimi nakukumbuka vizuri ulinitapeli wewe”
“Kuwa na adabu mwanamke, hivi unavyoniona nina muonekano wa kitapeli? Kuwa na heshima”
Kisha akamuaga Tumaini na kuondoka zake, ambapo yule dada alimwambia Tumaini,
“Huyu kaka ni tapeli, yani alinitapeli mimi kila kitu nilichokuwa nacho”
“Lazima umemfananisha, unajua anafanya kazi gani huyu? Unajua elimu yake, hawezi kuwa tapeli hata kidogo”
“Namkumbuka vizuri dada, alinitapeli huyu”
“Haiwezekani nakwambia, wewe nawe ujue tunaenda nyumbani kwa dada yake kwenye ofisi yake anatafuta mtu wa kumsaidia ndio nakupeleka wewe unaanza kumuita kaka yake tapeli, hebu usije sema hivyo mbele yake kabisa”
Ila sasa hata na wao waliposogea kwa mlinzi waliambiwa vile vile kuwa wale watu bado wapo Kanisani na siku hiyo walichelewa sana kutoka Kanisani tofauti na siku zingine, waliwasubiri pia na kuchoka ikabidi waondoke zao tu.

Siku ya leo, walipotoka Kanisani baba Angel aliamua kuwapeleka wote kwenda kula hotelini, yani siku hiyo alikuwa na furaha sana ya kumaliza ujenzi wake wa kile kiwanda kidogo, kwahiyo alikaa na familia yake na kuagiza nao chakula ambapo walikuwa wakila huku wakifurahi, kasoro Vaileth ambaye muda mwingi alikuwa kimya kwani alikuwa akifikiria laki tano yake, ila walipomuuliza sababu ya kuwa kimya kiasi kile alisingizia kuwa siku hiyo hakuamka vizuri tu.
Basi walikuwa wanakula huku wakiongea mambo mbalimbali ndipo Junior alipoingizia swala la kumuona Derrick ufukweni,
“Halafu mamdogo, tulimuona mjomba Derrick mahali anacheza ile michezo ya kitapeli”
“Michezo gani?”
“Ule mchezo wa karata tatu”
Baba Angel alishtuka kidogo na kusema,
“Hivi ule mchezo bado upo!! Kwahiyo kuna watu wanapeliwa bado kwa ule mchezo, nakumbuka zamani sana utakuta mtu anatapeliwa hadi nguo”
“Hata hapo ilikuwa hivyo hivyo, unajua bamdogo mjini kila siku washamba wanaongezeka, yani kuna watu hawajui kama ile ni michezo ya kitapeli”
“Hivi mmesema Derrick, mna uhakika nyie mnamfahamu Derrick?”
“Tumemuita na kumuita, akasogea na kuuliza tunafanya nini halafu akaondoka”
Mama Angel alikaa kimya tu kwani alishawahi kuambiwa tabia ya kaka yake huyo kwa siku hizo kwahiyo akajikuta hana cha kusema, mumewe akamuangalia na kumuuliza,
“Kwahiyo unaamini haya maneno ya watoto?”
“Tutaongea zaidi tukirudi nyumbani ila sio muda huu”
Yani mama Angel alikatisha yale maneno ya kuhusu ndugu yake, mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake basi akafungua na kusoma,
“NImekuja kwenu nimekaa sana hadi nimechoka, by Derrick”
Mama Angel akashtuka kidogo kwani kwa tabia ya utapeli aliyosimuliwa kuhusu Derrick akajikuta akihofia kuwa isikuwa Derrick kamtapeli hadi mlinzi wao ila akaona ni vyema asiwaze hayo sana sababu atashindwa kukaa vizuri mahali pale na kufurahi na familia yake.
Basi waliendelea tu na mazungumzo mengine hadi pale walipomaliza na kufurahi.

Sia akiwa katika harakati zake za biashara, anakutana na Dora na kumsimamisha kisha kuanza kuongea nae,
“Leo sijakusimamisha kwa ubaya Dora maana hapo ulipo tayari ushakunja sura jamani, pole sana”
“Kwani mimi nimesema kuwa umenifananisha kwa shari? Hata hivyo niambie ulichonisimamisha, kwanza upo kwenye biashara saa hizi hukwenda kwenye ibada leo?”
“Leo sijaenda, yani mimi kwenda kuna watoto wa Erick, wakiniona kanisani wanaona kama mzuka vile”
“Jamani! Mbona una mambo ya ajabu Sia, kwani wale watoto wanakufahamu?”
“Tuachane na habari hiyo, Kwa kifupi ni hivi, mdogo wako kapewa dawa na yule mwanamke”
“Kivipi?”
Sia alianza kumueleza toka yule madam Oliva alivyokuwa akimtaka Erick, na jinsi ambavyo alimpelekea Erick viatu halafu mama Angel akavipeleka kwa Steve,
“Kheee kumbe ndio ilivyokuwa!”
“Ndio hivyo”
“Jamani kwanini mdogo wangu mmemuonea hivi!! Hivi kweli haiwezekani kwa yeye kumpenda mwanamke anayemtaka mpaka mumkorogee madawa, kuna kipindi mtaharibu akili ya mdogo wangu”
“Mmmh usiniseme mimi, mseme huyo wifi yako mpya”
“Simtambui kama ni wifi yangu”
“Hata mimi hujawahi kunitambua ingawa nimezaa na kaka yako, yani wewe Dora una matatizo sana”
“Ila samahani, unapafahamu nyumbani kwa huyo mwanamke?”
“Napafamu ndio”
“Nakuomba basi unipeleke ili nikaongee nao mwenyewe”
Sia alikubali kumpeleka na aliweka vitu vyake vizuri kisha yeye na Dora waliondoka eneo lilena kwenda nyumbani kwa madam Oliva.
Walifika pale na kugonga geti ambapo mlinzi wa nyumba ile alienda kufungua mlango, ila macho ya Diora na yule mlinzi yalipokutana kila mmoja alionekana kupata mshangao dhidi ya mwenzie.

Sia alikubali kumpeleka na aliweka vitu vyake vizuri kisha yeye na Dora waliondoka eneo lilena kwenda nyumbani kwa madam Oliva.
Walifika pale na kugonga geti ambapo mlinzi wa nyumba ile alienda kufungua mlango, ila macho ya Dora na yule mlinzi yalipokutana kila mmoja alionekana kupata mshangao dhidi ya mwenzie.
Waliangaliana kwa makini sana, ila mwisho wa siku Dora alijihisi vibaya kwani huyu mlinzi wa madam Oliva alikuwa ni mtoto wa James ambaye alizaa na msichana wa kazi, maana alimuuliza,
“Unaitwa nani kijana?”
“Naitwa James”
“Imekuwaje hadi umekuwa mlinzi?”
“Unajua mimi naishi na mjomba, sasa kila kitu namtegemea mjomba, nikaona ni vyema nitafute kazi ila Mungu mwema ndio nikapata kazi mahali hapa”
Kwakweli Dora aliacha hadi kufikiria kilichompeleka mahali pale na kujikuta akimuangalia kwa makini sana huyu kijana kwani moyo ulikuwa ukimuuma sana, basi Sia alimuuliza,
“Inamaana huyu ni James, mtoto wa James!”
Dora aliitikia kwa kichwa tu kisha Sia akamwambia,
“Mimi nilishawahi kukwambia haya, nadhani leo umenielewa ni kitu gani nilichokuwa nazungumzia, unaishi kwenye nyumba nzuri, una maisha mazuri, unafanya utakacho ila watoto wa huyo mtu wanaishije? Je wanalalamikaje kwa Mungu. Haya kama wamefikia hatua ya kuwa walinzi ni mara ngapi wamelalamika kwa Mungu, na wakati wewe unaouwezo wa kuwasaidia?”
Basi Dora akamuangalia yule kijana na kumuandikia namba yake kwenye karatasi kisha akampatia na kumwambia,
“Naomba utanitafuta”
Halafu Dora akaondoka, ikabidi Sia nae aondoke zake maana aliyempeleka alikuwa ameondoka kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 277

Dora alirudi nyumbani kwake na kujifikiria vitu vingi sana, kuna muda alihisi machozi yakimtoka na kusema,
“Ingawa mwishoni James hakunifanyia vitu vizuri ila alikuwa akiniambia nikumbuke watoto wake, alikuwa akimtaja James, Junior na Jasca, kwanini nimekuwa mbinafsi kiasi hiki!! Kwani wokovu ndio unatufundisha hivi? Neno la Mungu ndio linafundisha hivi kudhurumu mali ya mtu! Si wanasema mtu mwenye dhuruma hatouona ufalme wa Mungu, eeeh Mungu naomba unisamehe”
Basi akafikiria pale cha kufanya kwani aliona ni wazi anawajibu wa kuwasaidia watoto wale ili na wao waishi kama Jesca na watambuane maana ni mali za baba yao wote watatu.
Wakati akifikiria hayo, simu yake ya mkononi ilianza kuita na alipoangalia aliona namba ngeni na kupokea na kuanza kuongea nayo,
“Ni Sia anaongea hapa”
“Eeeh Sia unasemaje?”
“Unajua ni jambo gani lilitupeleka pale? Yani ulipomuona yule kijana umesahau kila kitu, mdogo wako karogwa wewe!”
“Unajua naweza kukazana kumfatilia huyo aliyemroga mdogo wangu wakati mimi kuna dhambi nimefanya na ninazifumbia macho, acha kwanza nijisafishe na dhambi yangu hii”
“Kheee haya, ila mimi nilikwambia ukanipuuzia. Kuna muda unaona unaishi kwa amani sana ila kuna mtu umedhuruma nafsi yake na kila siku analia kwaajili yako”
“Kwaheri maana wewe nawe ukianza humalizi”
Dora alikata ile simu huku akiendelea kutafakari mambo mbalimbali.

Familia ya mama Angel, kwa muda huu wote walikuwa wakirudi nyumbani huku wakiongea mambo mbalimbali kwenye gari, ila njiani mama Angel alikuwa akiangalia nje na alimuona Derrick kasimama na mdada halafu Derrick akaondoka muda huo magari yalikuwa kwenye foleni kwahiyo mama Angel alikuwa akiona karibia kila kitu kilichoendelea, mara alimuona yule dada akilia hadi kukaa chini, ndipo alipomuomba mumewe asimamishe gari pembeni kwanza ili akaongee na yule mwanamke, na kweli magari yaliporuhusiwa baba Angel alisimamisha pembeni halafu mama Angel alishuka na kumfata yule mwanamke aliyeonekana amechanganyikiwa,
“Vipi dada tatizo ni nini?”
“Nimetapeliwa dada, yani kuna mbaba nilisimama nae hapa kumbe ni tapeli, kanitapeli kila kitu hadi hela ya nauli”
“Yani kakutapeli kivipi?”
“Yule kaka nimetoka nae mbali kidogo, kaniambia kuwa yeye huwa anawasaidia watu kuongeza kipato chao, basi aliniambia vitu vingi sana hadi tumefika hapa akaniambia nimpe mkoba wangu na simu yangu nami sijui vipi nikampatia ila alipoondoka ndio nimegundua kuwa nimetapeliwa hapa sijui hata nyumbani narudi vipi”
“Duh pole sana”
Kisha mama Angel akampa yule mdada elfu tano ili iweze kumsaidia kama nauli ya kurudi, basi alirudi kwenye gari ya mume wake na safari iliendelea.

Usiku huu baba Angel aliona vyema kuuliza kuhusu mkewe kwenda kuongea na yule mwanamke, kuwa ni kitu gani kilimfanya aende kuongea na yule mwanamke, basi alimwambia tu kuwa yule mwanamke alikuwa katepeliwa ila hakusema kama tapeli mwenyewe ni Derrick kwani aliamini kuwa aliyemuona Derrick alikuwa ni yeye mwenyewe, basi alimulezea mumewe tu lile tukio la yule mwanamke, basi baba Angel akasema,
“Ila tamaa ya kupata hela kwa haraka haraka ndio inayofanya wengi watapeliwe, ukianza kufatilia utaona wengi kweli walitamani hela za haraka. Ila mke wangu kuna tatizo lingine”
“Lipi hilo”
“Sikukwambia sijui, ila ni hivi Steve hajaenda ofisini kabisa, nilimpigia simu akapokea madam Oliva, kwahiyo Steve yupo kwa madam Oliva”
“Kheee jamani huyu mwanamke ni nyoka, kwahiyo ndio alitaka akuweke wewe hivyo jamani!! Si ningekuwa chizi mimi loh!! Ila pale dukani itabidi tumpe mtu mwingine, la sivyo huyo Steve atahonga duka letu kwa huyo madam wake”
“Mmmh sijui, ila tutafanya hivyo”
Basi waliaongea ongea pale na kuamua tu kulala kwa muda huo.

Angel kama kawaida alimuomba bibi yake simu na kuanza kuwasiliana na wale watu wake aliokuwa akiwasiliana nao sana, yani kitu pekee ambacho huwa kinamfanya kuomba simu kwa bibi yake ni kuwasiliana na Samir, na huwa akiipata hiyo simu anaanza kumtumia ujumbe Samir,
“Samir”
“Oooh niambie malaika wangu, unajua Angel nakupenda sana”
“Jamani Samir unafanya nihisi hakuna mwanaume tena katika ulimwengu huu mwenye mapenzi kama wewe, ukimtoa baba yangu”
“Ni kweli kwa waliobaki hakuna kweli, tumebaki wachache sana. Ila Angel siku za mbeleni huko tutaishi pamoja na kuwa mke na mume”
“Nitafurahi sana Samir”
“Vipi na shule bado hujatajiwa”
“Sijatajiwa ila baba alisema kuwa naweza leo kwenda kufanya usahili”
“Basi ukienda kuwa makini sana Angel ili unitajie hiyo shule maana nataka tusome pamoja ili niwe nakulinda kipenzi changu”
“Mmmh Samir una vituko sana”
Mara simu ya Angel ilianza kuita, alipoangalia ni Mussa aliyekuwa anapiga, ila kwavile alipenda zaidi kuwasiliana na Samir, kwahiyo hakupokea ile simu ya Mussa na kuendelea kuwasilina na Samir.

Kesho yake mapema kabisa, baba Angel alijiandaa na kwenda ofisini kwake, kisha alienda kwenye ujenzi wake ambapo alitaka kufanya sherehe kidogo ya ufunguzi wa jingo lake hilo ila alitaka kumshtukiza tu mke wake kwahiyo hakutaka kumwambia ni kitu gani kitaendelea.
Basi alipomaliza hapo, kuna mwalimu aliwasiliana nae kuhusu Angel kwenda kufanya usahili basi alipoondoka hapo alienda kumfata Angel ambaye alifanya ule usahili na kumrudisha nyumbani, ila wakati wa kurudi simu ya Angel ilianza kuita maana siku hiyo alisahau kumrudishia bibi yake, basi baba yake alisimamisha gari pembeni na kuanza kumuuliza Angel,
“Nasikia simu inaita?”
Angel hakuwa na jibu, basi baba yake akamwambia,
“Hebu nipe hiyo simu niione”
Angel hakuwa na namna zaidi ya kutoa ile simu ili baba yake aweze kuiona, basi baba Angel alichukua ile simu na kuiangalia kwakweli ilikuwa ni simu ya gharama sana, akamuuliza,
“Hii simu umepewa na nani Angel?”
“Samahani baba, nilipewa na babu”
“Na babu? Babu yupi huyo?”
“Nilimfahamu kwa bibi kule nilipokuwa, ndio akaniletea hii simu”
Kwakweli baba Angel aliiangalia sana ile simu ila hakuongea jambo lingine lolote na kurudisha ile simu kwa Angel, kisha safari iliendelea ambapo alimfikisha Angel kwa bibi yake halafu yeye akarudi katika ujenzi wake ili kupanga na baadhi ya vijana kuwa mahali hapo atafanikisha vipi kwaajili ya sherehe yake fupi ya ufunguzi wa kiwanda chake, basi alipanga nao pale na kisha kuondoka zake kurudi nyumbani, kiukweli alikuwa amechoka sana siku hiyo kutokana na matembezi aliyokuwa nayo.

Kulipokucha leo kabla baba Angek hajaondoka aliona ni vyema kwanza akiongea na mke wake, basi alianza kuongea nae pale kuhusu Angel,
“Halafu mama Angel unajua mwanao anamiliki simu ya aina gani?”
“Eeeh ya aina gani?”
“Mwanao anamiliki simu ya gharama sana, niliwahi kuulizia zile simu wanauza milioni, mbili nimemuuliza tu nani kampatia ile simu kasema baba yake kule kwa bi I yake alipokuwa yani kwa mama yangu, kwakweli nimesikitika na kushindwa hata kuongea lolote”
“Kheee na mama yangu nae kamuachia simu jamani wakati niliongea nae!”
“Kuongea na mama hakusaidii kitu ila hapa naona cha muhimu ni wewe kuongea na Angel”
“Niongee nae nini sasa?”
“Yule ni mtoto wa kike na wewe ndio mama, tafuta siku na uongee na mtoto ukweli”
“Unamaana nimuelezee kuhusu uhalisia wake”
“Aaaah sijasema hivyo maana hayo ni maamuzi yako, ila ninachoongelea hapa ni ile hali ya mama kuongea na mtoto wake wa kike”
“Unajua sikuelewi mume wangu, niongee nae kuhusu nini?”
“Sikia nikwambie, kaa chini na Angel mueleze ukweli wote kuhusu mahusiano, najua umepitia changamoto nyingi pia kwahiyo unaweza kumueleza mtoto wako hata kwa kuto kusema ni wewe yani ukasema kuna rafiki yako yalimpata haya na haya na haya, mueleze ukweli mtoto ajue kuhusu mahusiano kwanza, hata ukimueleza ukweli kuhusu uhalisia wake na bila kumueleza ukweli kuhusu mahusiano basi atatembea na hao unaosema ndugu zake maana ataona ni kawaida, sasa kaa na echini mwambieukweli jinsi mahusinao yalivyo hata yakimtokea puani bado atakumbuka kuwa lakini mama alisema, kwani tukiendelea kumthibiti kuhusu simu bila kumwambia ukweli napo ni kazi bure, utamzuia na simu hii kuna jamaa atamnunulia simu nyingine. Angel ni bvinti mzuri tena mzuri sana ila akiharibikiwa basi ule uzuri wake hautoonekana kwani kila sehemu atakuwa akielezewa kuhusu sifa mbaya, mama Angel kaa chini na mtoto”
“Nitajitahidi mume wangu, kwani sitaki mtoto aharibikiwe”
“Maana naona kuna wanaume wameanza kuichanganya akili yake kiasi kwamba nahisi ana mawazo yupi ni yupi katika maisha yake, na ikiwa tukiona kuna mwanaume anamfatilia sana mtoto wetu basi hatuna budi kufatilia uhalisia wa huyo mwanaume ingawa ni ngumu sana kuchunga kila mwanaume anayemfatilia mtoto wetu. Ila mueleze mtoto ukweli ili aweze kujilinda na kujichunga”
Mama Angel alimuelewa vyema kabisa mume wake, kwahiyo alikubaliana nae na kile alichokuwa akikisema na kusema kuwa atakitekeleza.
 
SEHEMU YA 278

Usiku wa leo, Vaileth bado aliamua kuwa mbali kabisa na Junior kwani kila akifikiria kuhusu laki tano ambayo Junior aliichukua kwake na kukumbuka aliyoyasikia kuwa alipeleka hela hiyo kwa mwanamke, alijikuta akiwa hana furaha tena na Junior kiasi cha kufanya amchukie sana, ila kabla hajalala alitumiwa ujumbe na Junior,
“Vaileth mpenzi wangu, nifanye nini ili uweze kunielewa, sijui hata nikuelezeje ila mama yangu si mkweli”
“Oooh mama yako si mkweli, kwahiyo mama yako kapanga na Samia au? Halafu usiniongezee hasira Junior”
“Basi, ila niambie nifanye kitu gani kwasasa uweze kunisamehe”
“Nirudishie laki tano yangu, sitaki maneno mengine”
“Sawa hakuna tatizo, hiyo hela nitakupatia tu hakuna tatizo”
Vaileth hata hakuendelea kuwasiliana nae zaidi ya kutafuta usingizi tu muda huo ila akapigiwa simu na ndugu yake Prisca na kuipokea,
“Unajua nini Vai, natamani kuja kwenye hiyo nyumba kukuona ila naogopa na ninaona aibu”
“Pole sana, kwa yale mambo lazima uone aibu”
“Kwanza hongera sana, nasikia matusi uliyofanya kijijini huko”
“Matusi gani tena?”
“Si umerekebisha nyumba ya wazazi, nasikia wameweka bati na wamerekebisha kote yani nasikia pamependeza nyumbani kweli, halafu mjomba kawasaidia kuvuta umeme kwa ile hela”
“Oooh swala zuri sana, kwahiyo nyumbani kuna umeme kwasasa?”
“Ndio, unajua nguzo za umeme zilipita pale pale ila sababu ya pesa ndiomana hawakuvuta, halafu nyumba ya bati zilizooza na umeme wa kazi gani? Ila Vai umefanya kazi kubwa sana, hongera mdogo wangu umefanya jambo la akili. Ila ngoja nikuulize, zile pesa ndio mshahara au kitu gani? Na mimi natamani kupata kazi za ndani jamani, kwa miezi michache tu umeweza kufanya kitu cha namna ile nyumbani!! Oooh na mimi nitafute kazi za ndani sasa”
“Sikia kwanza, ile pesa sio mshahara ila ile pesa nimepewa na wazazi hapa, nilipowaambia tu kuhusu nyumbani basi wakanipatia ile pesa, tena mama aliituma mwenyewe kwa mama nyumbani kupitia simu ya mjomba, tuliwasiliana nao na kutuma ile pesa, kwakweli hii familia wananipenda sana na wananilea sana, kwakweli nawapenda”
“Haya, ila nasikia kule kijijini kuna mkaka mwalimu anafundisha shule ya jirani, toka kaambiwa kuhusu wewe basi anasema ukirudi tu anakuoa, kwahiyo jiandae na ndoa”
“Jamani ndugu yangu, usinichekeshe mie, ngoja nilale halafu tutaongea vizuri siku nyingine unajua ni usiku huu!”
“Najua ndio, ila huu ni muda mzuri wa kukupata hewani ila hakuna tatizo usiku mwema”
Basi Vaileth alikata ile simu ila hakutaka kutilia maanani kuhusu huyo kijana mwalimu wala nini zaidi ya kufikiria mambo mengine na kulala tu.

Leo baba Angel kabla ya kwenda ofisini, alipitia kwanza kwenye ujenzi wake kuangalia maandalizi ya ufunguzi yatakavyokuwa maana alishaongea nao, kwahiyo alienda tu kuangalia na kupanga zaidi,
“Ila bosi, kukipambwa kidogo hapa nje basi shughuli itapendeza zaidi”
“Kwahiyo kuna umuhimu wa kutafuta mpambaji?”
“Ndio, kuna umuhimu wa kufanya hivyo”
“Mimi sijuani sana na watu wengi, basi mtanitafutia mtu mnayeona anafaa na kumpa hii kazi”
“Oooh kuna baba mmoja hivi anaitwa Babuu ni hatari kwa mapambo, yani akikupambia mahali lazima ubaki mdomo wazi”
“Basi nitafutieni huyo Babuu na muelekezeni tunachotaka halafu mtaniambia gharama zake”
“Sawa, hakuna tatizo juu ya hilo”
“Nataka ile siku ikifika mimi na familia yangu yote tuwe hapa na nitaongea machache kidogo kwani hiki ni kiwanda changu cha kwanza kufungua na ninahitaji kifanye vizuri”
“Usijali bosi, kwanza eneo umepata zuri na kubwa, lazima kiwanda kitafanya vizuri sana”
Basi alikubaliana na huyu kijana na kutembelea tembelea baadhi ya vifaa alivyoviweka kwani kuna watu aliwaweka watengeneze bidhaa ambazo zitakuwepo siku ya ufunguzi na kufanya watu wafahamu bidhaa zake, basi alipomaliza aliondoka zake na kuelekea kazini kwake.
Ila leo alipoingia ofisini tu kuna mgeni alikuja ofisini kwake, mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi akamuuliza,
“Kheee Sia, umefata nini kwani?”
“Sijaja kwa nia mbaya ila nimekuja kukupa habari flani hivi”
“Habari gani?”
“Shemeji yako Derrick ni tapeli”
“Kivipi?”
“Ni hivi, Derrick ana michezo ya kitapeli na wengi sana kawatapeli na kuwaliza, mimi mwenyewe alitaka kunitapeli, nikamuangalia na kumuuliza Derrick mbona mimi nakufahamu vizuri sana, yani unataka kunitapeli kweli! Basi akaona aibu na kuondoka, kwakweli Derrick sio mtu mzuri kwasasa”
“Duh!! Ila kwanini umekuja kuniambia hayo?”
“Nimekuja kukwambia ili nyie mjue cha kufanya na huyu ndugu yenu, unajua utapeli sio sifa nzuri eeeh!! Tapeli hana tofauti na mwizi, ila tofauti yake ni kuwa yeye hapori bali unampa mwenyewe na mwizi anaphora ila tapeli ni kama mwizi tu kwani anakuumiza kimaisha na kisaikolojia, kwahiyo mnatakiwa mjue cha kufanya”
“Sasa cha kufanya ni kipi hapo?”
“Sikia nikwambia, kwasasa unaona hakuna cha kufanya ila hii ni sifa mbaya ambayo haitaishia kwa Derrick tu bali itasambaa hadi kwenye familia yenu, hebu angalia ulivyo na pesa na jina zuri mjini halafu Derrick anamtapeli mtu na kusikika kuwa yule ni shemeji wa Erick, unajua sio sifa nzuri kabisa hiyo. Hebu kuweni makini na ndugu yenu, yule Derrick ni msomi, na mpaka kawa vile lazima kuna kitu kimemfanya awe vile, msikubaliane na ile hali kabisa, nyie mnasali siku hizi na uzuri ni kuwa mnatambua jinsi gani nguvu za giza zinafanya kazi, mkomboeni ndugu yenu”
“Kheee ulivyoongea kwa uchungu, sawa mama nimekuelewa”
“Jamani, leo mbona nitalala huku nikitabasamu, Erick umeniita mama!! Asante sana”
Baba Angel alicheka tu huku akitikisa kichwa, basi Sia aliinuka na kumuaga baba Angel huku akimwambia,
“Naomba ufanyie kazi hilo nililokwambia, msimuache Derrick aendelee kupotea, ha[endi kuwa vile, msaidieni”
Sia akaondoka zake, ila kuna muda kama aliona kuwa Sia anazungumza ukweli kuwa wanapaswa kumsaidia Derrick, ila kwavile siku ile alikuwa na mambo mengi ya ufunguzi wa kampuni yake ambao karibia unafanyika basi ndio kitu alichofikiria zaidi.

Leo, mama Angel alikuwa amekaa sebleni na Erick wakiangalia Tv, kidogo ilikuwa ni tofauti kidogo kwani mara nyingi Erick sio mpenzi wa kuangalia Tv, basi kulikuwa na kipindi cha mahusiano na kuna mtu alipiga simu kuwa ameachwa na mpenzi wake, alipomaliza kuongea kwenye simu, wale watangazaji wakaanza kudadavua sasa ambapo mmoja akasema,
“Jamani kuachw akunauma tena sana”
Mwingine akadakia,
“Ni kweli kunauma ila inatakiwa ifikie hatua watu waone kuachwa au kuachana ni kawaida tu, sasa mtu mmekutana kimjini mjini asikuache kwasababu gani? Akipata mpya anayefaa anakuacha tu, mtu mwenyewe mmekutana na meno yote mdomoni, asikuache umezaliwa nae tumbo moja huyo? Ni pacha wako hadi asikuache”
Wale watangazaji walikuwa wakicheka sana huku wakiongea kwa furaha, basi Erick alimuangalia mama yake na kumuuliza,
“Kwani kuna mahusiano ya kimapenzi kwa watu waliozaliwa tumbo moja au mapacha?”
“Mmmh mahusiano ya kimapenzi? Haiwezekani maana ni ndugu”
“Sasa hawa mbona wanasema kuwa mtu ambaye hujazaliwa na tumbo moja au mtu ambaye sio pacha wako ni lazima akuache, sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na mahusiano”
“Hujaelewa hapo mwanangu, ni hivi katika mahusiano kuacha na kuachwa ni kawaida kwani mtu anahitaji apate mtu wa kuridhika nae, anaweza kuona tabia ambazo hazifai kwake na akakuacha, ila ndugu kuachana ni ngumu, sio kimahuano ya kimapenzi bali kimahusiano ya kindugu, kuachana ni vigumu sana kwani ni ndugu wanajuana toka watoto na damu zao zimewaunganisha, kwa undugu wa mapacha ndio ngumu kabisa kuutenganisha. Ila kuna usemi usemao ndugu wakigombana chukua jembe ukalime kwahiyo mambo ya ndugu kidogo ni mambo ambayo yana gusa sana”
“Kwahiyo mama ndugu hawawezi kuwa wapenzi”
“Jamani Erick, uliona wapi ndugu wakawa wapenzi jamani! Kuna baadhi ya kabila tu ndio zinaruhusu mabinamu kuoana ila ndugu kuwa wapenzi ni kinyume kabisa”
“Ila mama, ukisoma kwenye Biblia unaona kuwa mtu wa kwanza kuumbwa ni Adam halafu akafatia Eva, hiyo inamaanisha kuwa duniani wote ni ndugu hivi ni kweli ndugu hawaoani? Au Mungu aliumba watu wengine tofauti na hao kwanza?”
“Kheee wewe mtoto usinitie kiungulia mie, mambo ya uumbaji nitayajulia wapi jamani, kwanza nenda kaoshe ile gari pale nje maana unaongea sababu huna kazi za kufanya kwasasa”
Basi Erick aliinuka na kwenda kuosha gari ambalo mama yake alimwambia ila bado alikuwa na maswali yake ambayo mama yake hakuwa na majibu na hayo maswali.
Wakati akiosha gari lile, alienda Erica kule ambapo kaka yake alikuwa akiosha gari, alimnyatia kwa nyuma na kumwagia maji na kufanya Erick ashtuke sana, kisha walianza kukimbizana na kusahau hata kile alichokuwa akifanya.
Walikuwa wakikimbizana huku kila mmoja akipata maji anamvizia mwenzie na kummwagia, kitendo hiko kilifanya kummwagia maji baba yao ambae alikuwa ndio amerudi,
“Nyie watoto vipi kwani?”
“Samahani baba”
‘Hebu njooni hapa”
Erica na Erick walisogea kwa baba yao ambaye alianza kuongea nao,
“Haya, huo mchezo wa kumwagiana maji mmeutoa wapi?”
“Baba, nilikuwa naosha gari ila Erica akaja nyuma yangu na kunimwagia maji”
“Eeeh Erica kwanini umefanya hivyo?”
“Baba, zamani tulipokuwa watoto basi mimi na Erick tulikuwa tukicheza michezo mingi sana ila siku hizi huwa simuelewi Erick maana muda mwingi kama ananikwepa basi ndio nikaamua kuja kuanzisha mchezo wa kummwagia maji”
Baba Angel alitikisa kichw akama kusikitika kidogo halafu akacheka na kusema,
“Yani nyie watoto mnaakili mbovu sana, hebu cheki mlivyolowa chapachapa jamani. Haya Erick acha tabia ya kumkwepa mdogo wako, uwe unaongea nae na kucheza nae”
Basi Erica akasema,
“Tena ni vyema baba kama mimi na Erick tukisoma shule moja kama zamani”
“Hilo tutaliongelea pia, Erick wewe ndio mlinzi wa dada yako na sio mtu wa kumkwepa. Haya nendeni mkabadilishe nguo”
Basi waliingia ndani na baba yao nae aliingia ndani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mke wake na kuongea nae,
“Kesho, naomba uwaandae vijana wetu wote maana kuna mahali tunaenda halafu tutaenda kumpitia na Angel, na mama kwenda nae hiyo sehemu”
“Ni wapi huko?”
“Aaaah utajua tu mke wangu, ni surplise”
Basi mama Angel hakuongea zaidi, aliwafata tu watoto na kuwaambia kuwa wajiandae kuna mahali wataenda siku ya kesho.
Kulipokucha, kila mtu alijiandaa kama walivyoambiwa kisha safari ikafanyika ya kwenda kumfata Angel ila kwa bahati mbaya hawakumpata Angel maana alikuwa kaondoka na bibi yake, kuna mahali walienda basi mama Angel akamwambia mumewe,
“Unaona sasa mambo yako ya kushtukiza, hatujawapata wala nini ni bora watu kuwaandaa kwanza”
“Sawa, hakuna tatizo nitawapeleka wao siku nyingine”
Kisha waliondoka pale na kuelekea kwenye safari yao.
 
SEHEMU YA 279

SEHEMU YA 280

SEHEMU YA 281

Moja kwa moja walifika kwenye kile kiwanda ambacho baba Angel alikuwa amejenga, na palikuwa pamepambwa sana na kumfanya mama Angel afurahi kwani ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kuwa yeye na mume wake siku moja wamiliki kiwanda chao, na akajua kuwa kiwanda kile ndio ufunguzi wa wao kuwa na viwanda mbalimbali.
Basi baba Angel aliwatembeza kwenye kile kiwanda huku akiwaelekeza mambo mbalimbali, basi mama Angel akamwambia,
“Ila umekosea sana kutokutushirikisha, unajua ungetushirikisha basi ingekuwa rahisi kwa ndugu zetu wote kuwepo mahali hapa”
“Hakuna tatizo, kuna siku nitafanya sherehe mahali hapa, na ndugu wote nitawaalika”
Basi mama Angel na familia nzima walifurahi na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali, muda huu baba Angel aliingia tena kiwandani ili kuelekezana kidogo na aliamua kumchukua Erick kwani kuna kitu aliwahi kuambiwa kuhusu Erick kwahiyo alitaka kusikia kwanza mawazo yake.
Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,
“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”
Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel.

Kwanza kabisa mama Angel alijikuta akikosa ujasiri kabisa, kisha akamwambia Erica aende mbali ili yeye aweze kumwambia yule mwanaume aondoke, ila Erica akasita na kumwambia mama yake,
“Mama, kuna kitu nataka nikwambie”
“Uniambie nini? Ondoka nimekwambia ondoka upesi”
Mama Angel aliongea kwa ukali na kufanya mtoto wake aondoke kwa unyonge sana kwani hata alichokuwa anataka kusema kwa mama yake hakuweza kusema tena, kisha Rahim akamwambia mama Angel,
“Mtoto hafai kufanyiwa ukali namna hiyo, hebu angalia ulivyomfananisha sura na alivyoondoka kwa unyonge, hivi roho haikusuti kumfokea hivyo!!”
“Na wewe ondoka, mambo ya familia yangu hayakuhusu”
“Yananihusu maana hata mimi ni baba yao pia”
“Mjinga wewe, hebu ondoka zako huko”
Rahim hakuondoka ila alivuta kiti na kukaa karibu na mama Angel kisha akasema,
“Nilimuangalia sana huyu mtoto kafanana na wewe jamani, yani kafanana na wewe sana. Nikajikuta nikimuuliza jina lake, aliponiambia Erica moyo wangu ulidunda na kumuuliza mama yako yuko wapi akasema yupo mahali hapa, nikamuomba anilete kwa mama yake”
“Naomba uende Rahim”
“Niende kivipi Erica, kwani mimi nina ugomvi na wewe jamani!! Inakuwaje utake kunifukuza hivyo!!”
“Naomba tu uende, sina matatizo na wewe. Kwanza hapa nipo na familia yangu”
“Una hofu na Erick, kwani Erick hanifahamu? Angekuwa hanifahamu ni vizuri sana ila ananifahamu kwa uzuri tu, sasa nakushangaa wewe Erica kutaka kuwa na hasira kiasi hiko jamani. Huna sababu ya kunichukia wala sababu ya kunifukuza, mtoto wangu Angel yuko wapi nimemkumbuka sana, natumai kakua sana”
“Sahau kama kuna mtoto ulizaa na mimi”
“Kwamaana hiyo Angel alikufa!!”
“Kheee usinichulie Rahim, naomba uniache na watoto wangu kwa amani”
“Oooh nilijua Angel amekufa, ngoja nikwambie jambo ambalo sikuwahi kukwambia na wala hukuwahi kulijua nadhani, ingawa mimi nina watoto wengi sana kwasasa, ila mtoto pekee aliyekaa katika akili yangu ni Angel unajua kwanini?”
Mama Angel alikaa kimya tu, basi Rahim aliendelea kuongea,
“Unajua mwanaume unaweza ukawa na wanawake wengi sana ila katika maisha yako kuna mwanamke unaona kabisa kagusa maisha yako, basi katika maisha yangu si wake niliooa na kuacha, si wanawake nilioishi nao ila bado huwa nakufikiria wewe kwani uliyagusa maisha yangu Erica, ulikuwa ni mwanamke ambaye ulifaa kuwa na mimi nadhani ningekuwa nawe kwasasa ningekuwa zaidi ya hapa, na wala pengine nisingezaa hovyo kama hivi.Erica, nina kila sababu ya kumfikiria Angel na kumpenda Angel sababu nilimpenda mama yake ambaye ndio wewe. Erica wewe ni mwanamke wa tofauti sana, umeumbiwa upendo tena upendo wa dhati, kwakweli huwa siachi kukufikiria katika maisha yangu….”
“Naomba unyamaze Rahim, sitaki kukusikia unachotaka kuongea, naomba uende”
“Hivi unafikiri namuogopa Erick? Kwani hajui ni jinsi gani nakupenda? Anajua vizuri sana, naelewa ni kwanini kakung’ang’ania hadi leo hataki kukuacha, una mapungufu yako ila wewe una sifa bora za mwanamke ambazo mtu yoyote atapenda mkewe awe hivi, kwanza wewe ni mzuri kiasi kwamba hata kukutambulisha kwa watu kuwa huyu ni mke wangu unaonekana umefanya jambo la maana, wewe ni mtafutaji, una upendo, una huruma, unajali, huchepuki, ukiwa na mwanaume unampenda kweli. Aliyenivuruga hadi nikaachana na wewe namlaani hadi kesho ni yule mwanamke waliyenitafutia kuoa ndio chanzo yule, ila mimi nakupenda Erica hadi kesho na imani yangu inaniambia kuwa ipo siku mimi na wewe tutaungana na kuwa kitu kimoja, tutaishi pamoja tukilea mtoto wetu katika maadili mema”
Mama Angel alikuwa na hasira akasimama ili aondoke, ila mumewe muda huo huo akasogea eneo lile ila na yeye alipomuona Rahim alijikuta akichukia sana kiasi kwamba hata hakumsalimia zaidi ya kumwambia mke wake aende kwenye gari na aliwafata watoto wake nao kuingia kwenye gari kisha alimwambia Erick awapeleke nyumbani ambapo alifanya hivyo kwahiyo alibaki yeye tu na watu pale kiwandani hakutaka watoto wake wahisi kitu chochote kile.
 
SEHEMU YA 282

Baba Angel alipomaliza ndipo alipomfata Rahim na kumtaka kuondoka,
“Naomba uondoke sehemu yangu”
“Kwakweli Erick unasikitisha sana, mwanaume gani wewe ambaye muda wote una mashaka na mkeo? Kumbuka huyo unayemuona mkeo nimezaa nae mimi”
“Hiyo ya kuzaa nae sio sababu Rahim, sikia nikwambie unajua mimi nilikuwa nawe vizuri tu na nikakwambia uwe unakuja kwangu kwaajili ya wewe kucheza na mtoto ili akuzoee halafu ukataka kufanya nini nyumbani kwangu?”
“Najua nilitaka kufanya makosa, ila Erick wewe ni mwanaume una wasiwasi gani lakini? Unampenda Erica na anakupenda, unajua hawezi kushawishika kijinga, tatizo lako ni nini lakini?”
“Unajua wewe akili yako naona imeliwa na hivyo virusi vya ukimwi kichwani!”
“Nani kakwambia kuwa mimi nina virusi, unajua usiongee kitu ambacho huna ushahidi nacho. Kwani virusi ni kitu gani katika maisha, watu wanaishi navyo na wanadundika tu hapa tunayemuongelea ni Erica. Hebu sikia Erick, wewe ulikuwa rafiki yangu na matendo yetu yaliendana kwa asilimia mia moja, kwahiyo kubadilika kwako kwasasa hakukubadilishi wewe unabaki kuwa Erick siku zote, ni kweli umemuoa Erica, mmelea mtoto wangu, umezaa nae watoto wengine, ila tambua kuwa hata mimi bado nampenda Erica, ungeelewa hilo basi ungekaa na mimi na kunishauri kisaikolojia na sio kunikwepesha na familia yako”
“Hivi utake kumbaka mke wangu halafu nikuache karibu na familia yangu nina wazimu au ni kitu gani! Kwanza Rahim naomba uende”
“Yuko wapi mwanangu Angel?”
“Laiti kama nikikaa na huyo Angel nikamueleza yale maovu yako basi hatokaa kukutaka uwe baba yake kamwe, hivi si wewe mwenyewe uliyesema Angel angekuwa sio mtoto wako basi ungemtamani kimapenzi kisa ni mzuri sana, hivi Rahim kwanini hukui jamani!! Kwasasa wewe ni baba tena una watoto lukuki, hivi nikae chini na kumueleza Angel maovu yako moja mbili tatu atakutamani wewe uwe baba yake!!”
“Nadhani hukunielewa, kwani nilivyosema vile ndio nilimaanisha kuwa namtamani, hivi naweza kutembea na mtoto wangu mimi!! Sio mtoto wangu tu, hivi hata mtoto wa rafiki yangu na jamii yangu naweza tembea nae wakati na mimi nina watoto wadogo! Mambo mengine uwe unayatafakari kwanza, sawa tuseme nilisema hivyo, au hata ningembaka mtoto wangu mwenyewe je hilo lingebadilisha chochote kuwa mimi ndiye baba yake mzazi? Na siwezi kufanya hivyo mimi, Erick una watoto wako sasa, nahitaji mtoto wangu hilo tu basi”
“Naomba uende”
“Naenda ila weka akilini kuwa nahitaji mtoto wangu, siku nikiamua kutumia nguvu basi familia yako nzima nitaitikisa”
halafu Rahim akaondoka zake, kiukweli baba Angel hakuwa na furaha kabisa na moyo wake uliingia simanzi gafla na muda huo huo akaacha tu maagizo kwa mtu halafu yeye akaondoka zake.

Siku hii baba Angel aliamua kuita bodaboda na kuondoka nayo kuelekea nyumbani kwake, alipofika tu alioga na moja kwa moja kujilaza, hakuongea kitu chochote na mkewe na kumfanya hata mama Angel kujihisi vinaya maana lile tukio la kufatwa na Rahim hakulipenda pia, basi alikaa karibu na mumewe pale alipokuwa amelala na kufikiria mambo kadhaa ambayo aliwahi kufanyiwa nyuma na Rahim,
“Alinidanganya ananipenda, nikampa moyo wangu nami nikampenda, nikampa mapenzi yangu, nikapata mimba yake na akakubali kila kitu kuwa atanitunz na kunihudumia na kuahidi kunioa, nilijificha na mimba ile maana alisema nitakuja nitakuja ila hakutokea, baadae nyumbani wakajua, nikabahatika kujifungua na ahadi yake kwangu iliendelea nitakuja ila hakuonekana, akanipa sharti gumu ambalo sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku ataniambia vile maana tulikubaliana kuoana hata bomani sababu ya utofauti wa dini zetu, akaniambia nibadili dini, nikamfikiria mwanangu, nikafikiria aibu niipataye kwa kuzaa nje ya ndoa, nikafikiria jinsi ninavyojificha ili ndugu wasijue, nikaona ni bora nikubali ili anioe niepukane na aibu, nikakubali na kumwambia kuwa nipo tayari kubadili dini unioe ili tuishi na kulea mtoto ila alinibadilikia, ndio kwanza hakutaka tena mawasiliano na mimi, hakutaka tena kumuhudumia mtoto hakutaka tena kusikia chochote kuhusu mimi, maisha yakawa magumu sana kwa upande wangu maana kila mahali nanyooshewa kidole, nimemaliza chuo na zawadi ya mtoto, nikashindwa kwenda kutafuta kazi maana mtoto alikuwa bado mdogo na mimi sina mbela wala nyuma yani sikuwa na msingi wowote wa maisha, niliona dunia inanicheka, niliona dunia inanitenga, niliwaza kwanini nastahili adhabu hii wakati hakuna baya nililowahi kuliwaza kwa huyu mwanaume, anizalishe na bado anidhalilishe na kunifanya nioenekane sina thamani yoyote katika maisha, muda wote macho yangu yalijaa machozi, nilimshika mwanangu na kulia nae sana, kuna muda nilijiona kuwa mimi ni mwanamke mpumbavu sana kwa kumuamini mwanaume, ila alinionyesha mapenzi na nikaamini kuwa ananipenda. Katika kukata kwangu tamaa, alirudi kwangu Erick na sasa alirudi akiwa mpya kabisa na kunipa mapenzi yote na kuchukua jukumu la ubaba kwa mtoto wangu Angel, ananipenda na anampenda mtoto wangu ila bado aliona kuna umuhimu wa Angel kumtambua baba yake halisi, ni kitu gani tena Rahim alitaka kunitenda kwenye nyumba ya mume wangu?? Na bado aliweka na vitisho kuwa kama atashindwa kwangu basi atafanya kwa mwanangu, ambaye ni mtoto wake mwenyewe, Rahim kawa ni mwanaume wa ajabu sana katika maisha yangu. Najuta kumfahamu, sijui ni kwanini nilikutana nae. Moyo wangu unajawa na machozi tena, ameivunja furaha ya mume wangu ambaye ananipenda sana, nitakuwa mgeni wa nani mimi, sijapanga haya katika maisha yangu ila sijui kwanini yananifata jamani!!”
Alikuwa akilia huku akiongea hayo, na muda huu alilia hadi mumewe alisikia na kumfanya baba Angel aamke na kukaa na mkewe kisha alimkumbatia na kumwambia,
“Usijali mke wangu, mimi na wewe tunapendana na hilo ndio la msingi kwetu, watoto ni ziada yetu ili kukamilisha furaha ya nyumba yetu. Usijali mke wangu, hata mimi nafikiria vingi pia, usidhani nimechukia kwani siwezi kuchukia sababu ya hili ila tu sijafurahishwa nalo ila Mungu ni mwaminifu atatusaidia na kujua ni jinsi gani tutaweza kushinda na kuvuka hapa tulipo”
Basi alikumbatiana pale na mume wake na kuona kidogo moyo wake ukirudisha tabasamu na furaha basi mumewe akamuomba kuwa apumzike kidogo naye alifanya hivyo.

Kulipokucha, wakati baba Angel akijiandaa kwenda ofisini akapata ukumbe kutoka kwa madam Oliva,
“Kuna jambo nahitaji ushauri kutoka kwako”
Baba Angel alishangaa tu ila hakujibu kitu kwenye ule ujumbe bali alimaliza kujiandaa kisha kumuaga mkewe pale na kwenda kazini.
Mama Angel alibaki nyumbani na familia yake, ila muda kidogo Erica alienda kukaa na mama yake na kumuuliza mama yake,
“Kwani mama, yule baba wa jana ni nani?”
“Aaaah ya jana si yalishapita mwanangu, sidhani kama ni vyema kuyazungumzia”
“Yalipita ndio, ila sikuelewa mama hebu ona jinsi tulivyorudi nyumbani inaonyesha hata haikupangwa iwe vile, baba karudi badae na pikipiki, sijaelewa vitu vingi vya jana. Halafu yule baba alivyokuwa akiongea na mimi mmmh!”
Mama Angel alishtuka kidogo na kumuuliza,
“Aliongea nini na wewe?”
“Kwanza, aliponiona alishtuka halafu akaniita, akaniambia unafanana sana na mwanamke mmoja ambaye nampenda sana, nikamshangaa”
“Mmmh! Akasemaje tena?”
“Ndio akasema unaitwa nani, nikamwambia naitwa Erica, akasema mimi ni mzuri sana, halafu akauliza mama yako yuko wapi, nikasema ulipo ndio akasema nimlete ulipo. Ni nani yule mama?”
“Mmmh Erica, achana na hizo habari ila ukikutana tena na yule mtu akikuita usiende tafadhari”
“Halafu mama, nisamehe jana sikukwambia alinipa na hii hapa hela”
“Kheee alikupa na hela? Wewe ulianza kuongea nae muda gani na alikuwa hela ya nini?”
“Aliniambia kuwa mimi ni mzuri sana, ananipongeza kwa kuzaliwa mzuri ndio akanipa na hii hela”
“Mbona hukusema?”
“Niliogopa mama kukwambia pale wakati ulishaniambia niondoke”
Kisha Erica akatoa zile pesa na kumfanya mama yake ashangae sana kwani zilikuwa ni nyingi tu, akachukua zile pesa kwa mwanae na kwenda chumbani kwake bila kuongea kingine na mtoto wake, hata Erica alibaki sebleni akishangaa tu.
Mama Angel aliingia chumbani huku machozi yakimtoka, akakumbuka mara ya kwanza kutekwa akili yake na Rahim ilikuwa ni katika pesa, yani Rahim alikuwa ni mwanaume ambaye alimpa sana pesa, kwahiyo alipoona Rahim kumbe kampa mwanae pesa, aliumia sana moyoni mwake na kujisemea,
“Hivi Rahim ana nini lakini jamani, kwanini ampatie mwanangu pesa? Tena pesa nyingi namna hii jamani!!”
Mama Angel aliihesabu hela ile aliona kuwa ilikuwa ni laki mbili halafu kwenye zile hela kulikuwa na kadi yenye namba za simu za Rahim,
“Sasa kamuwekea namba huyu mtoto wangu ili amtafute au nini jamani? Mbona kuna wanaume wana laana jamani loh!!”
Kwakweli mama Angel alisikitika sana kwa alichokifanya Rahim.
 
SEHEMU YA 283

Baba Angel akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zake za hapa na pale, mara alifika madam Oliva ila kiukweli baba Angel kwa kipindi hiki alikuwa akimuogopa sana madam Oliva maana hakumuamini tena, ila alimkaribisha tu na kuongea nae,
“Jamani baba Erick, kama unanikwepa vile, hebu sahau yote yaliyopita”
“Haya, niambie”
“Ningependa tupate mahali tuzungumze maana kuongelea ofisini swala hili kidogo sio vizuri, naomba chagua mahali gani ambapo patatufaa ili tuzungumze, sina nia mbaya na wewe baba Erick, usinifikirie vibaya tena. Ni wapi sasa tutakaa na kuzungumza”
“Basi nitakwambia”
“Mmmh jamani, hukawii kusema kuwa umesahau wewe”
“Hapana, sisahau wala nini au utanikumbusha muda nikiwa natoka kazini. Leo nitatoka kwenye saa kumi”
“Sawa nitakukumbusha basi”
Kisha madam Oliva akaondoka zake, na baba Angel akaendelea na shughuli zake zingine.
Muda wa kutoka ni kweli madam Oliva alimkumbusha tena, basi akamwambia mahali pa kukutaniana ambapo kweli alivyotoka ofisini alienda mahali hapo na kukutana na madam Oliva kisha kuanza kuongea,
“Haya, niambie ni kitu gani ulikuwa unataka kunieleza?”
“Kwanza kabisa, ni kweli nilikuwa nakutaka yani nisikatae, mimi ni mtu mmoja ambaye huwa napenda kusimamia ukweli hata kama ukichukia au vipi ila ni vyema nimeongea ukweli. Sababu ya kukutaka unajua ni nini?”
“Eeeh ni nini?”
“Nilikuwa naona fahari sana ukimsifia mke wako mbele yangu, yani wewe ni mwanaume unayejiamini na ni wanaume wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivyo, kingine ni yule mwanamke Sia, yani jinsi alikuwa anakuhitaji ndio kitu pekee kilichofanya nikutake pia ili na mimi nipate hicho ambacho wanawake wenzangu wanang’ang’ania kutoka kwako. Na nimetumia madawa mengi sana kukupata ila imeshindikana, kiukweli nguvu iliyokuwepo kati yako na mke wako ni kubwa sana. Kitu kingine mimi nilikuwa simjui Steve wala sikuwa namfatilia habari zake kumbe ni rafiki yangu wa facebook kwa miaka mingi sana na siku zote huwa ananitumia ujumbe lakini simjibu sababu mimi nilikuwa naangalia maisha yangu tu. Kumbe huyu Steve alikuwa akinipenda kwa muda mrefu sana ila hakujua ni jinsi gani anaweza kunipata, kwa kupitia vile viatu ambavyo nilikutegeshea wewe basi Steve akaanza kuhaha kunitafuta, na sasa mimi na yeye tupo pamoja. Naweza sema ni nguvu ya dawa imetumika ila na nguvu ya mapenzi imetumika pia, sababu kwanini vile viatu asingevaa mtu mwingine zaidi ya Steve?”
Baba Angel alicheka kwanza kwani akiifikiria historia ya Steve hakudhani kama kuna nguvu ya mapenzi hapo, kwani Steve alishawahi kula tunda ambalo Sia aliliweka dawa ili apendwe na yeye ila akala Steve na Steve kuanza kuishi na Sia, kwahiyo yeye aliona ni mauzauza ya Steve tu, madam Oliva akamuuliza,
“Mbona unacheka?”
“Hapana, nafurahia tu mapenzi yako na Steve”
“Sasa ushauri niliokuita kukuomba ni huu, nahitaji kufunga ndoa na Steve, nahitaji wewe na mke wako ndio muwe wasimamizi wetu”
Baba Angel akashtuka kwanza na kumwambia madam Oliva,
“Swala la nyie kufunga ndoa ni jema, ila swala la mimi na mke wangu kuwa wasimamizi wenu naomba unisamehe tu kwa hilo maana halitawezekana”
Madam Oliva alijaribu kumshawishi pale baba Angel ila alikataa kabisa kwa wao kuwasimamia ndoa yao.

Mama Angel akiwa chumbani kwake muda huu huku akipanga namna ya kumueleza mumewe kuhusu Erica kupewa hizo pesa, alishangaa tu kupokea simu kutoka namba ngeni akaanza kuongea nayo,
“Mimi ni Sia, usinikatie simu ni jambo nataka kuongea na wewe”
“Jambo gani hilo?”
“Mumeo, muda huu yupo hotelini na madam Oliva, kuwa makini sana la sivyo unampoteza. Ni kheri umpoteze kwangu kuliko kwenye mikono ya mamba ya yule mwanamke”
Kisha Sia akakata simu, kwakweli mama Angel kama akili yake ikagoma hivi kwani hakujua ni kwanini mumewe aweze kwenda hotelini na Oliva baada ya kujua mambo mengi sana kuhusu madam Oliva, kisha akaamua kumpigia mumewe simu kwa muda huo, na mumewe alipokea,
“Upo wapi baba?”
“Samahani mke wangu sikukwambia, kuna hoteli hapa nimepita mara moja”
“Umepita kufanya nini? Nakuomba nyumbani mume wangu”
“Sawa, narudi muda sio mrefu. Nakupenda sana mke wangu”
Basi mama Angel alikata ile simu huku akitafakari mambo kadhaa.

Muda huu Erick alikuwa amekaa kwenye bustani basi Erica alienda kuongea nae na kumwambia kuhusu mbaba aliyempatia pesa,
“Yule baba wa jana mliyemuona amekaa pale na mama, alinipa hela jana laki mbili pamoja na kadi yenye namba zake za simu”
“Kheee ili iweje? Viko wapi hivyo vitu?”
“Nimempa mama leo, unajua nilishangaa sana alivyonipa”
“Alisema anakupa ili iweje?”
“Kwanza alinisifia huyo balaa, akasema kuwa mimi ni mzuri sana, akasema nina sura nzuri ya upole, na macho ya kuvutia kisha akanipa hela ya kusema kuwa ni hela ya kunipongeza kwa uzuri niliokuwa nao”
“Hao ndio wababa wasiofaa, ndio mafataki hao mdogo wangu ila nakupongeza swala moja la kwenda kumkabidhi hiyo hela mama, nakupongeza sana na siku nyingine mtu kama huyo akikupa hela kata kabisa”
“Sawa sawa, halafu baba alisema usiwe unanitenga jamani Erick!!”
“Sikutengi na nitaongea na baba ili tusome pamoja kama zamani, najua baba atanielewa tu”
“Oooh hapo nimefurahi sasa, ila kama baba alisita siku ile”
“Sikumsisitiza tu, ila subiri nimwambie vizuri basi baba atakuleta tu shuleni kwetu”
Hili swala Erica alionekana kulifurahia sana.

Baba Angel alifika nyumbani, ila wakati anaongea na mama Angel wala hakumuuliza sababu ya kupitia hotelini ila alimweleza tu vile ambavyo Erica amepewa hela na Rahim, kwakweli baba Angel alisikitika sana na kusema,
“Katika watu wapuuzi namba moja duniani basi ni Rahim, sijui lini akili yake itakaa vizuri na kuwaza kutenda matendo mema. Hebu ona mimi naishi vizuri na Angel nampenda na kumuhudumia, ila yeye bila aibu ameanza swala la kumuhonga mwanangu kweli!! Hebu naomba hiyo kadi yake nimuulize vizuri alipo ili nikaongee nae, sitaki ujinga kwa watoto wangu”
Basi baba Angel alichukua ile kadi na kuwasiliana na Rahim ambaye alimtajia alipo na muda huo huo baba Angel aliamua kuondoka nyumbani kwake ila hakupanda gari bali alikodi pikipiki tu na kuondoka nayo, hata mama Angel aliona ni vyema asingemwambia mume wake kwani alimuona hasira aliyokuwa nayo baada ya kuambiwa hayo.

Alifika mahali alipo Rahim, na kumkuta akicheka tu na kutikisa kichwa,
“Hivi Rahim jamani mbona una akili mbovu wewe!! Kwahiyo umeona vyema kabisa kumuhonga binti yangu na kumpa namba zako za simu?”
“Kwani tatizo liko wapi Erick? Nimempa binti yako pesa, laki mbili tu? Nimempa na namba zangu za simu ili niwe nawasiliana nae hata mara moja moja, wewe je? Unamuhonga binti yangu kila siku zaidi ya kila kitu maana nasikia hadi kuna baadhi ya biashara zako zinasimama kwa jina la binti yangu, na kila siku unampigia simu binti yangu, kati ya mimi na wewe nani mwenye nia mbaya na mtoto wa mwenzie”
“Hivi una akili kweli wewe!!”
“Nina akili ndiomana nafanya haya”
“Sitaki uwe karibu na binti yangu, tena hata Angel sitaki uwe karibu nae”
Rahim akacheka na kusema,
“Unajua Erick utawadanganya wengine tu ambao hawakujui vizuri ila sio mimi ninayekujua ndani na nje, utamdanganya huyo huyo Erica wako ndani, unajua kabisa Angel sio mwanao ila unajifanya unampenda kufa, hadi mali zako umemuandikisha, lengo lako ni nini? Nikikwambia unatembea na Angel utawezaje kukataa wewe?”
Kiukweli baba Angel alichukia zaidi na kujikuta akishindwa hata kumjibu na zile hela hakumrudishia na muda huo huo akaondoka huku Rahim akiwa anacheka sana.

Baba Angel alienda moja kwa moja stendi na kupanda kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alikuwa akiwaza moyoni mwake,
“Hivi wanaume wote wanaolea watoto ambao sio wao huwa wanapatwa na adhma hii ambayo naipata mimi? Kwanini inakuwa hivi lakini, kila nikutanapo na huyu mtu kwasasa ni kuichosha tu akili yangu”
Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,
“Dah!!”
Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,
“Habari baba”
Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana.

SEHEMU YA 284

SEHEMU YA 285

SEHEMU YA 286

Moja kwa moja walifika kwenye kile kiwanda ambacho baba Angel alikuwa amejenga, na palikuwa pamepambwa sana na kumfanya mama Angel afurahi kwani ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kuwa yeye na mume wake siku moja wamiliki kiwanda chao, na akajua kuwa kiwanda kile ndio ufunguzi wa wao kuwa na viwanda mbalimbali.
Basi baba Angel aliwatembeza kwenye kile kiwanda huku akiwaelekeza mambo mbalimbali, basi mama Angel akamwambia,
“Ila umekosea sana kutokutushirikisha, unajua ungetushirikisha basi ingekuwa rahisi kwa ndugu zetu wote kuwepo mahali hapa”
“Hakuna tatizo, kuna siku nitafanya sherehe mahali hapa, na ndugu wote nitawaalika”
Basi mama Angel na familia nzima walifurahi na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali, muda huu baba Angel aliingia tena kiwandani ili kuelekezana kidogo na aliamua kumchukua Erick kwani kuna kitu aliwahi kuambiwa kuhusu Erick kwahiyo alitaka kusikia kwanza mawazo yake.
Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,
“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”
Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel.

Baba Angel alienda moja kwa moja stendi na kupanda kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alikuwa akiwaza moyoni mwake,
“Hivi wanaume wote wanaolea watoto ambao sio wao huwa wanapatwa na adhma hii ambayo naipata mimi? Kwanini inakuwa hivi lakini, kila nikutanapo na huyu mtu kwasasa ni kuichosha tu akili yangu”
Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,
“Dah!!”
Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,
“Habari baba”
Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana.

Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,
“Dah!!”
Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,
“Habari baba”
Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana.
Basi alimuitikia salamu yake,
“Salama MAnka, umekuwa mmama siku hizi”
“Hata wewe umekuwa mbaba, unajua sikutegemea kama ningekutana na wewe jamani”
“Mungu ni mwema wakati wote”
“Unaenda wapi? Yani sikutegemea kukutana nawe kwenye daladala, vipi gari iko wapi? Najua wewe upo vizuri kitambo sana”
“Aaaah nimeamua tu”
“Nilienda kumuona mtoto wetu yupo kwa bibi yake”
Baba Angel alishtuka kiasi kwani alishangaa kuwa hakumuuliza chochote kuhusu mtoto ila huyu mwanamke alisema mhivi, ila baba Angel hakuongeza neno lingine lolote, basi kituo kilichofuta baba Angel alikuwa anashuka na kumuaga yule mwanamke ila yule mwanamke alishuka pia, kwahiyo pale kituoni walikuwa pamoja, kisha baba Angel alisogea nae pembeni na kumwambia maana alihisi pengine mwanamke huyu ana neno na yeye,
“Niambie Manka”
Huyu mama alianza kulia na alimsogelea baba Angel na kumkumbatia tena alilia kwa muda mrefu, basi baba Angel akamwambia,
“Unajua tupo njiani?”
“Najua ndio, ila ni wapi nitakupata mimi na kukueleza uchungu nilionao juu yako”
Baba Angel akashtuka na kumuangalia vizuri huyu mwanamke, ila ilikuwa kwenye mida ya saa tatu usiku kwahiyo kulikuwa na giza kiasi kwamba sio rahisi kuangaliana labda iwe kwenye mwanga ila baba Angel alimuangalia na kumuuliza,
“Kwani tatizo ni nini? Una shida gani?”
“Natamani siku moja uje nyumbani kwangu, uje kumuona mtoto wako”
Baba Angel akashtuka sana na kuuliza,
“Mtoto wangu!!”
“Ndio, mtoto wako. Najua ni mimi ndiye nilitaka kuwa na wewe ila sababu nilikuwa nakupenda, uliposema upo kujipooza kwangu sikukataa ila nilipopata mimba niliogopa kukwambia kwani ulikuwa na mtindo wa kupeleka mwanamke hospitali akachomolewe mimba yake na mimi sikutaka hilo kwani nilitaka mwanangu adumu na mimi”
“Unajua unanichanganya Manka?”
“Sikuchanganyi ila nakwambia ukweli, nina mtoto wako. Roho inaniuma kwa mwanangu kujua kwamba hana baba halafu anae roho inaniuma sana”
“Sikuelewi, yani sielewi chochote”
“Huwezi kunielewa hadi siku ukate shauri na kuja nyumbani kwangu kumuona mtoto wako”
Mara simu ya baba Angel ilikuwa inaita, kuangalia ni mkewe alikuwa akipiga basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,
“Uko wapi mume wangu? Usiku huu ujue!”
“Nakuja, nipo stendi tu hapa usijali”
Basi baba Angel alikata simu na kuamuangalia Manka, kisha akamwambia
“Inatakiwa tupate siku ili tuweze kuzungumza kuhusu hilo swala”
“Hilo ndio jambo jema Erick, nitafurahi sana. Nimekuwa na uchungu, na majonzi na kulia siku zote. Roho inaniuma sana, sio kosa langu kwa mwanangu kukosa baba ila ni kosa la mapenzi yangu kwako, nilikupenda, nilikuthamini na ndiomana mtoto wetu namlea kwa upendo wa hali ya juu kiasi kwamba sitaki hata kumgusa mtoto huyu, nampenda sana ndio kila kitu katika maisha yangu”
Basi baba Angel alimpa tu kadi yenye namba zake ili waweze kuwasiliana, basi Manka aliichukua ile kadi na kumkumbatia baba Angel tena hakutaka kumuachia kabisa huku akimwambia,
“Nakupenda sana Erick, katika maisha yangu sijawahi kumpenda mwanaume yoyote kama wewe. Nakupenda na daima nitakupenda”
Baba Angel alijitoa kwenye mikono ya yule mwanamke ila bado yule mwanamke alikuwa kamshikiria basi baba Angel akamwambia,
“Samahani Manka, natakiwa niwahi kurudi nyumbani unajua nina familia yangu, kwasasa mimi ni mume wa mtu na nina watoto, natakiwa kurudi kwangu, tutaongea tena”
Manka alionekana kulia sana tena alilia kwa muda mrefu halafu ndio alimuachia baba Angel na kumuaga, basi baba Angel aliondoka zake na moja kwa moja alichukua pikipiki na kwenda nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa kimebeba mawazo ya kutosha.

Baba Angel alipofika nyumbani kwake na kuingia chumbani aliona ni vyema akaoge ili apumzishe akili yake na mawazo kwani alijiona kuwa na mawazo mengi sana, kwahiyo alihisi akioga basi atapata nguvu na kuweza kuichanganya vyema akili yake.
Basi alitoa nguo zake na kuzitundika halafu yeye akaenda kuoga, muda ule mama Angel nae akaingia chumbani ila alihisi kusikia harufu ya manukato mengine katika shati la mume wake, basi alilichukua karibu na kulinusa na kugundua kuwa lazima kuna mtu mumewe alikuwa nae, alianza kuwaza huenda akawa madam Oliva, ila akakumbuka kuwa mwanzoni ndio alitoka kwa madam Oliva na alibadili nguo wakati akienda tena kuonana na Rahim, akajiuliza tena labda hakwenda kuonana na Rahim bali alikutana tena na madam Oliva, wakati akiangalia lile shati la mume wake, kuna kitu kilimstaajabisha sana, kwani aliona midomo ya mwanamke yenye rangi kwenye hilo shati kwahiyo rangi ya midomo ilibaki kwenye shati la mume wake, hapo mama Angel ilimuuma sana na kujikuta akitoa machozi huku akikumbuka maneno ya dada yake kuwa unajifanya unamuamini sana huyo mwanaume eeeh! Ila alijifuta yale machozi kwani bado hakuona kama ni vyema kumuhisia vibaya mume wake ingawa kuna vitu vimejionyesha wazi kabisa, aliwaza kuwa mumewe akitoka amuulize vizuri maana hakuelewa, moyo mwingine ukamtaka asimuulize ila amchunguze, ila aliona kufanya vile ni kuzidi kuumia kwenye moyo wake, wakati anawaza hayo mumewe nae alitoka bafuni na kumkuta mke wake na lile shati mikononi mwake, akamfata karibu na kumkumbatia ila mke wake akajisogeza na kufanya amuulize,
“Tatizo ni nini mke wangu?”
“Nieleze kuhusu shati lako, nasikia harufu ya manukato mengine na kuna rangi ya mdomo kwenye shati lako. Je umeanza kunisaliti mume wangu?”
“Hapana, na sina sababu ya kufanya hivyo. Ngoja nikwambie ukweli, kuna mwanamke nilikutana nae njiani ila tunafahamiana hata na wewe unamfahamu sababu tumesoma nae, basi aliponiona ndio alinikumbatia nadhani rangi ya midomo yake ikashika shati langu”
“Kwahiyo alijilaza kifuani kwako?”
“Hata sijui nikueleze vipi mke wangu unielewe ila ndio kama nilivyokwambia”
“Huyo mwanamke ni nani?”
“Ni yule Manka, ambaye tulisoma nae”
“Aaaah yule alikuwa binti mzuri sana darasani”
“Hapana, wewe ndio ulikuwa mzuri darasani”
Mama Angel akatabasamu kwani aliona raha kusifiwa na mume wake, na kujikuta akimsamehe tu kwa kosa lile kisha akamuuliza mambo ya alipotoka,
“Kwahiyo ulionana na Rahim?”
“Dah! Nimeonana nae, ila ni pasua kichwa hatari nikikwambia alichoniambia kwa hakika utanionea huruma mke wangu”
“Pole jamani, kakwambiaje kwani?”
Baba Angel alimueleza maneno ambayo aliongea na Rahim, kiukweli hata mama Angel alijihisi vibaya sana, roho yake iliumia mno na kujikuta akisema,
“Katika maisha kuna makosa ambayo mtu uliwahi kuyatenda, basi ukifika kwenye maisha mengine unatamani upate ufutio wa kufuta makosa yako, jamani mimi hii dhambi ya kuwa na Rahim naona inanitesa maisha yote, hadi sijielewi. Mara nyingine sielewi kwanini Angel alikuja kwenye maisha yangu”
Mumewe akamziba mdomo na kumwambia,
“Shiiiii usiseme hivyo mke wangu tafadhari, Angel ni baraka kwetu. Usiwaze hayo kabisa, hapa tunayemuongelea ni chizi mmoja anayeitwa Rahim ambaye amekosa akili ya kutafakari na kujifikiria na sio Angel ambaye ni malaika asiyetambua lolote maana yeye sio kosa lake kuwepo katika maisha yetu”
“Ila jamani, Rahim ana mambo ya karaha sana. Hivi ndio wananikazania kweli nimwambie Angel huu ujinga wa baba yake mzazi?? Bado kwakweli, ngoja nijipange ndio nitamwambia. Na vipi ile hela yake ulimrudishia?”
“Oooh hata sijamrudishia chochote”
Baba Angel alichukua suruali yake na kukuta ile hela ya Rahim ipo tu ila ile kadi ya Rahim haikuwepo ndipo alipogundua kuwa Manka badala ya kumpa kadi ya namba zake yeye za simu ila alimpa kadi yenye namba za Rahim za simu, hapo aliwaza kiasi ila hakumwambia ukweli wa hilo mke wake kwani hata alichoongea na Manka hakumwambia wala nini, basi mama Angel akasema,
“Basi hizi pesa tuziache tu maana hata sio wa kuonana nae tena yule mtu atatufanya tusiwe na raha ya maisha bure kwa ujinga wake”
Basi wakakubaliana vile kuwa wasimfatilie tena Rahim wala nini atazidi kuwaumiza kichwa, kisha walienda kula na kuamua kulala tu kwani muda nao ulikuwa umeenda.
 
SEHEMU YA 287

Junior alikuwa chumbani kwake ila hakuwa na raha kabisa, kitendo cha yeye kukosa ukaribu tena na Vaileth kilimuumiza sana, aliwaza ni jinsi gani anaweza kuipata tena hiyo laki tano ili aweze kumpa Vaileth na aweze kusamehewa. Kuna jambo lilimjia kichwani mwake, aliona kesho yake alifanyie kazi jambo hilo, kwahiyo alilala akiwa na mawazo sana kichwani mwake siku hiyo.
Basi kesho yake palipokucha kabisa alijiandaa na kutoka huku akisema kuwa anaenda matembezi tu, akaenda sehemu mbali mbali kuangalia uwezekano wa kupata pesa ila ikawa ni ngumu sana sema kuna kitu alikumbuka kwani alikumbuka kuwa kuna ofisi mamake mdogo aliwahi kumtuma na kule ofisini walionekana kumsifia sana, basi akafikiria na moja kwa moja kwenda kwenye ile ofisi, kisha akaomba kuonana na yule bosi ambaye alionekana kumsifia sana ingawa yule bosi alichukua namba za Junior ila hakumtafuta Junior, basi Junior aliingia pale kwenye ile ofisi na kukutana na yule bosi, basi akamsalimia pale na kuanza kuongea nae,
“Samahani, mama yangu ni mgonjwa sana yani inatakiwa milioni moja kwa tatizo lake ila nimejikakamua kutafuta laki nne bado laki sita sijui utanisaidiaje baba yangu”
“Aaaah jamani, kalazwa wapi mama yako?”
“Kalazwa Muhimbili”
“Anaumwa nini kwani?”
“Ana uvimbe umeota kwenye kizazi ndio wanataka kumfanyia upasuaji”
“Aaaah mbaya sana hiyo, kwakweli inasikitisha sana. Sikia una simu hapo?”
“Ndio ninayo”
“Ngoja nikurushie basi pesa kwenye simu yako, naitoa benki na kukurushia moja kwa moja halafu wewe utaenda kuitoa, dah nimesikitika sana. Utaniambia hali ya mama yako basi, nikipata muda tutawasiliana ili nije kumuona”
Basi yule baba alimuuliza Junior namba zake za simu na wakati huo huo alimrushia fedha kwenye simu yake na pia akatoa laki moja na kumkabidhi Junior, kisha akamwambia
“Hii itakusaidia saidia nauli na mambo mengine madogo madogo, na hiyo itakayo baki huko itakusaidia katika mahitaji mengine madogo madogo ya mgonjwa, usisite kuja kuniambia lolote litakaloendelea. Mpe pole sana mama yako, dah nimeumia sana”
Junior alimshukuru yule baba na kuondoka zake pale ofisini.
Yule baba kwakweli alisikitika, alimuita mwenzie ambaye alikuja na kuongea nae,
“Unajua huyu mtoto wa James kaja leo sababu mama yake kalazwa hospitali yani walikosa laki sita tu za kuweza kumsaidia mama yake”
“Jamani dah!! Mtoto wa James wa kuteseka hivi jamani!!”
“Ndio hivyo, kwakweli nimetoa hela yangu bila kujielewa na kumpa kijana huyu, nikikumbuka baba yake alivyokuwa jamani!! Roho imeniuma sana”
“Basi utamuulizia vizuri alipolazwa mama yake ili twende tukamuone, ila si ulisema huyu mtoto anaishi na Erica, unajua maisha anayoishi Erica siku hizi sio ya kukosa laki sita jamani”
“Familia zinaficha mengi hizi huwezi jua kinachoendelea kwakweli, ila nimeumia sana”
“Kwakweli pole yake, jinsi James alivyokuwa akijitoa kwenye matatizo ya watu dah!! Ukiachana na ulevi na uhuni wa James ila alikuwa akijitoa sana”
“Nakumbuka wakati mama yangu anaumwa moyo, sina mbele wala nyuma, James alitoa hela ya mfukoni kwake na kulipia gharama zote za mama kwenda kutibiwa India, kiasi kwamba mama alipokuja kusikia kifo cha James alilia sana kama kafiwa na mwanae wa kumzaa, kwakweli James ni mfano wa kuigwa alikuwa na roho nzuri sana”
Basi walikazana kumsifia tu James huku wakiumia sana kwa swala la kusikia kuwa mama Junior anaumwa.

Junior alienda kutoa pesa huku akiangalia katumiwa na yule baba kwenye simu yake, alichekelea sana na kufurahi sana,
“Wow, kumbe kanitumia milioni moja!! Jamani sikujua kama naweza kupata fedha kirahisi namna hii dah!!”
Alifurahi sana na kuitoa ile pesa, yani alikuwa akitabasamu tu njia nzima ila aliwaza jambo moja kuwa yule bosi akimpigia je kutaka kujua hali ya mama yake? Akaona kitu chema ni kuzima simu hata kwa siku tatu ili asiwasiliane kabisa na huyo bosi kwani hakuwa tena na jibu la kumpa, basi alikuwa akirudi kwao huku akijisemea,
“Yani nafanya yote haya sababu ya mapenzi tu dah!! Nampa mama yangu ugonjwa, ili tu kumridhisha mwanamke! Aliyeleta mapenzi aiseee katuweza, tena kaniweza kweli mtu kama mimi, Vaileth ananipa kila kitu lakini sijui ni kitu gani kinanitamanisha kwingine jamani!! Ila nitatulia kwasasa, maana huu uongo jamani umezidi, eti mama ana uvimbe sijui nilipanga saa ngapi kuongea vile! Kweli mimi nina akili sana”
Alikuwa akitabasamu huku akirudi kwao, na alipofika ni moja kwa moja alienda chumbani kwake kwanza kuweka zile pesa.
Halafu alitoka na kwenda kwenye bustani ambako alimkuta Erick amekaa na kuanza kuongea nae,
“Siku hizi unapenda sana maeneo haya eeeh!!”
“Huwa napenda sababu Napata muda mzuri wa kutafakari mambo mbalimbali”
“Hivi ni mambo gani zaidi huwa unatafakari Erick ikiwa hapo huna mwanamke wala huwazi kuhusu mwanamke, maana huwazi kuhusu Samia wala Sarah yani sijui ukoje wewe ndugu yangu”
“Mimi huwa nawaza kuhusu maisha tu”
“Sasa maisha yamefanyeje ikiwa huwazi vyema kuhusu kupata mwanamke au kuwa na mwanamke?”
“Sasa mwanamke wa nini katika maisha yangu? Mama yangu na dada zangu wananitosha”
“Hivi wewe mzima kweli, huyo mama yako na dada zako ndio watakupa utamu”
“Halafu Junior naomba ukiwa unaongea na mimi kwanza jua kabisa unaongea na mdogp wako, ongea na mimi mambo ya kunijenga sio mambo ya kijinga kama hayo ya wanawake”
“Sasa mambo ya kukujenga kama yapi?”
“Hivi unajua kama wewe ni mwanaume, na sisi wanaume ndio tunaotegemewa katika maisha, yani hapo uniambie mdogo wangu, biashara Fulani inalipa, au kuna biashara nimefikiria ambayo ikifanywa hivi na hivi inaleta faida kubwa, au mdogo wangu kuna mtu nimesikia anauza kiwanja”
“Kwahiyo sisi tunaweza kununua kiwanja? Tunaweza kufanya biashara?”
“Hakuna kitu kinachoshindikana, halafu kitu kama hatuwezi na wazo letu ni zuri si tunamshirikisha baba hapo, kama anaona inawezekana kufanywa na sisi basi atatushika mkono tu kutusapoti ili tufanikishe na kama tukishindwa kabisa na akiona wazo la maana basi analishikiria yeye. Unajua ni nani alimwambia baba kuhusu swala la kujenga kiwanda? Ni mimi mwenyewe nilimwambia baba jinsi ninavyofikiria kichwani na mwisho wa siku baba kafanya kweli ingawa wazo hili nilimwambia miaka mitatu iliyopita, kwahiyo kujitoa na kuwaza ya maana ni muhimu sana”
“Mmmh dogo una mambo sana, ngoja niendelee kukaa nawe ili kuikomaza akili yangu maana naona una mawazo mapana sana kushinda hata mimi kaka yako”
Basi alianza kuongea nae kuhusu mambo ya shule maana hakutaka kuambiwa kuhusu vitu vingine asivyoweza kuelezea.

Baba Angel leo akiwa kazini kwake, alitulia ila alikuwa na mawazo kiasi huku akifanya kazi zake, basi yule rafiki yake Juma alienda kumtembelea na kuongea nae mawili matatu pale,
“Hivi swala nililokwambia umelifanyia kazi?”
“Swala gani?”
“Nimekwambia kuwa mchukue yule kijana wako, weka pale kiwandani hata kwa mwezi mmoja halafu uangalie kiwanda chako kitafanyaje”
“Dah!! Sijalifanyia kazi ujue”
“Yani Erick unakaa na fursa halafu unashindwa kuitumia kweli! Unajua kijana wako ni fursa yule, tena karibia anafungua shule inatakiwa uwe nae makini kwasasa ili hata akiwa anaenda shule basi kipindi cha mwisho wa wiki unamchukua na kumtumia, yule kijana ana akili sana, yupo vizuri sana kichwani”
“Nashukuru kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi hakuna tatizo”
“Nitakuja tena nadhani kesho alasiri ili kuangalia ulipofikia”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi aliagana nae na yeye kuondoka zake, baba Angel alifikiria kwa makini na kuona ni vyema kumtumia mtoto wake huyo katika maendeleo yake, alijisemea,
“Ila ni kweli, Erick ana akili sana, halafu anajitambua sijui kapata wapi ufahamu aliokuwa nao ila nadhani ni malezi ambayo tumempa. Siku zote huyu mtoto amekuwa akinishauri vitu vya maana sana, natakiwa kufanyia kazi swala hili na kesho nitaenda nae kiwandani na kumuacha huko, nitaanza kumjaribisha tu hadi azoee kwanza ndio nadhani itakuwa rahisi kwake kutoa mawazo yake, ila namuhurumia mwanangu bado mdogo, awaze biashara na masomo dah!!”
Ila aliona ni vyema kufanya hivyo kwani itakuwa ni bora kwa maisha yao na maisha ya kijana wao.
Alipomaliza kazi zake baba Angel aliamua kwenda nyumbani kwake mapema, ila alipokuwa njiani alifikiria kuhusu mke wake, akafikiria kwa yale yote yaliyopita ni vyema akamchukulia zawadi mke wake na iwe rahisi kwa yeye kuanza kumpeleka Erick kiwandani na hata mkewe asikatae kuhusu hilo, basi moja kwa moja alienda kwenye lile duka la baba Emma na mama Emma na kuongea nao,
“Nimekuja leo tena kuchukua zawadi ya mke wangu”
Mama Emma akawahi na kusema,
“Leo zamu yangu kumchagulia mkeo zawadi”
Ila baba Emma akasema,
“Mke wangu, wewe tulia tu. Ngoja kwanza tumuulize muhusika. Eti zile zawadi ambazo huwa nakuchagulia huwa mkeo hazipendi?”
“Oooh huwa anafurahia sana, na azisifia kuwa ni nzuri”
“Basi na leo nikuchagulie au unasemaje?”
“Ndio, hakuna tatizo”
Basi baba Emma alimuangalia mkewe na kusema,
“Eeeh umeona sasa, mimi ndio noma kwenye kuchagua zawadi”
Basi baba Emma alimchagulia baba Angel kiatu na kumpatia kisha akamwambia,
“Leo mpelekee zawadi ya hiki kiatu au unaonaje?”
Baba Angel alikiangalia kile kiatu na kumuuliza baba Emma,
“Kheee umejuaje kama mke wangu anavaa namba hii ya kiatu? Maana umeniachagulia kiatu kizuri na cha kumtosha kabisa”
“Nimekisia tu, hata sikujua kama kitamtosha”
Basi baba Angel alilipia ile pea ya viatu na kuondoka nayo kwenda nyumbani kwake.
Alipofika tu alipokelewa na mke wake kama kawaida na waliingia ndani huku wakiongea mambo mbalimbali na alimpa mkewe ile zawadi aliyomtafutia, kwakweli mama Angel alijaribisha na kufurahi sana kwani kiatu kile kilimpendeza na kilimkaa vizuri sana mguuni hata mumewe aliona ni namna gani kile kiatu kilivyompendeza mkewe, basi mama Angel alimshukuru sana mumewe ila leo hakusita kumuuliza,
“Samahani mume wangu, unajua sijawahi kukuuliza hivi. Mbona siku hizi umekuwa noma sana kwenye kuchagua zawadi yani kila zawadi unayoniletea ni balaa jamani!!”
“Nitakupa siri ya kunifanya niwe hivi mke wangu, nitakupeleka duka ambalo linauza vitu hivi vya kijanja”
“Yani kila unachoniletea nikivaa kinanipendeza hatari, ona hiki kiatu sasa, dah yani mume wangu ni noma. Asante sana”
Baba Angel alifurahia sana kuona mkewe anafurahia zawadi ambazo yeye anampelekea.

Usiku wa leo Junior alimtumia ujumbe Vaileth akimwambia,
“Vai, mke wangu naomba leo uje chumbani kwangu”
“Nikome kabisa, tena unikome nani mke wako? Mkeo ni huyo ambaye ulichukua laki tano kwangu na kumpelekea, nimekaa kimya usifikiri siumii mtu mzima mie, naumia vizuri sana”
“Samahani mke wangu, naomba unisamehe, ila nataka nikukabidhi ile laki tano”
“Niletee ila siji chumbani kwako”
“Basi nifungulie mlango, nije”
“Junior, usifikiri utanidanganya kama siku zote, kwakweli nikiona unanidanganya nipo radhi kwenda kulala sebleni kama ukigoma kutoka”
Basi Junior aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Vaileth, kikuweli alitamani sana kuwa nae pamoja, basi alifika pale na kuingia mule chumbani kwa Vaileth na kuanza kumwambia,
“Nisamehe Vai jamani mpenzi wangu”
“Junior, mimi sio mtoto ujue. Yani mimi ni mtu mzima na nina mtoto tayari, kwahiyo maswala ya kukaa na kudanganywa na mwanaume kila leo siwezi tena, usinidanganye wala kunitania naomba kila mmoja awe na maisha yake. Naomba kama huna cha maana nenda zako tu”
Junior akatoa zile hela na kukaa kitandani, ila muda huu hata Vaileth alipunguza ule ukali wake na kuanza kuongea taratibu na Junior, alimwambia,
“Kumbe umezileta kweli!”
“Sikia Vaileth, nakupenda na wala sikudanganyi, unasikiliza watu wanachosema ila hakuna ukweli wowote, mimi sijaenda kumuhonga mtu yoyote hiyo hela jamani”
“Kwahiyo mama yako nae ni muongo!”
“Ndio ni muongo, humjui mama yangu wewe. Mimi ndio namjua mama kuwa anaweza kufanya kitu gani, yani yale mambo kayatengeneza tu kwani anahisi kuna kitu kinaendelea baina yangu na yako kwahiyo lazima aniharibie, mimi kweli kuna biashara nilienda kufanya na hii hela ndiomana imekuwa hivi Vaileth. Na kukuhakikishia haya, ni kwamba ile biashara niliyofanya nimepata na faida kwahiyo nimekuletea mtaji na faida”
“Kheee kumbe!!”
“Hesabu hizo hela”
Vaileth alizihesabu na kukuta ni laki nane, alifurahi sana hata aliamini maneno ya Junior kuwa alikuwa akifanyia biashara ile pesa, yani siku hii alisahau kama hata aligombana nae maana aliongea nae vizuri sana na kuendelea kuhadiana nae mambo mbalimbali.
 
SEHEMU YA 288

Kulipokucha tu, baba Angel alienda kumuamsha Erick ambaye alijiandaa halafu moja kwa moja alienda nae kwenye kiwanda chake na kumwambia,
“Mwanangu, wewe ndio mtoto wa kiume kwenye familia, na wewe ndio wa kuwashikiria dada zako. Leo nimekuleta huku kiwandani ili nikuache na hawa wafanyakazi halafu utembelee kila kitu na uangalie ni kipi kipunguzwe na kipi kiongezwe, kumbuka hii ni biashara ya familia kwahiyo lazima tuiendeleze. Badae nitakuja kukuchukua mwanangu, natumai umenielewa”
“Nimekuelewa baba”
Basi baba Angel alimuacha Erick hapo halafu yeye alienda ofisini kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Kwenye mida ya saa tisa, alifika yule rafiki yake Juma na kuanza kuongea nae,
“Umefata wazo langu?”
“Ndio, nimempeleka leo mwanangu na kumuacha pale kiwandani nitamfata muda sio mrefu”
“Basi, twende wote ili na mimi nikaangalie kidogo”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi baba Angel aliweka vitu vyake vizuri halafu akatoka akiwa ameambatana na Juma, ila walipofika nje ya ofisi kuna jambo liliwashangaza sana, kwani alimuona Sia ambaye anaonekana alitaka kwenda pale ofisini ila alipowaona alikimbia sana utafikiri kaona kitu cha ajabu.

Baba Angel aliona kuwa ile sio hali ya kawaida, kwani siku ya kwanza alifikiria ni sababu ya yeye, alihisi pengine Sia alimuogopa yeye ila leo alihisi kuna jambo ambalo Sia analikimbia kwa Juma, basi alimuangalia Juma na kumuuliza,
“Unamfahamu yule mwanamke?”
“Aliyekimbia?”
“Ndio, unamfahamu?”
“Unajua sijamuona vizuri kwahiyo siwezi kusema kama namfahamu au la sema alivyokuwa akikimbia kuna mtu nimemfananisha nae, kwani anaitwa nani?”
“Anaitwa Sia, na wewe unamfananisha na nani?”
Waliingia kwenye gari huku Juma akiwa hajajibu swali lolote aliloulizwa hapo na baba Angel, ambapo aliamua kumuuliza tena,
“Unamfahamu huyo Sia?”
“Hapana, simfahamu Sia, sina kumbukumbu ya jina hilo katika maisha yangu”
Basi baba Angel alianza kuendesha gari huku akimuuliza,
“Ila umemfananisha na nani sasa?”
“Dah!! Niliyemfananisha nae hata sipendi kumuongelea, unajua katika maisha tunapitia mambo mengi sana na vikwazo vingi sana kuna wakati mtu hadi unasema sijui ilikuwaje”
Alionekana kusikitika sana, swala la kumfanya baba Angel apende kufahamu kwa undani zaidi, basi alimuuliza tena,
“Jamani Juma, unajua wewe ni rafiki yangu mkubwa sana, naomba niambie unamfananisha na nani? Alikuwa akiitwa nani huyo mtu?”
“Alikuwa akiitwa Baby”
“Baby? Kuna mtu anakuwa na jina hilo jamani!!”
“Yani yeye alisema kuwa alipozaliwa kwao walizoea kumuita Baby, Baby na mwisho wa siku hilo ndio likawa jina lake”
“Kwahiyo na shuleni alitumia jina hilo hilo?”
“Ndio, hata rafiki zake aliowahi kunitambulisha kipindi hiko walikuwa wakimuita Baby”
“Duh!! Unajua ndio nasikia kwako!”
“Ndio lilikuwa jina lake hilo”
“Haya niambie basi alikufanya nini?”
“Kwakweli sipo tayari kuongelea hilo kwasasa, nisamehe rafiki yangu nitafute tu siku nyingine”
“Basi kesho nitakutafuta, unajua mtu unapopata habari mbalimbali unaweza kujifunza na vitu mbalimbali. Inawezekana nisijifunze mimi ila wakajifunza watoto wangu”
“Ila Erick jamani, unapenda kupata habari. Basi kesho nitakuelezea, kwasasa tumuongelee Erick mdogo tu”
Na kwa bahati walikuwa wamefika kiwandani na kushuka, moja kwa moja walimfata Erick ofisini ila hakuwepo, basi walimuulizia alipo na kumkuta yupo kiwandani pia akiwajibika, basi baba yake alimuita ofisini na kuanza kuongea nae.
Ni Juma ndio alianza kumuuliza maswali Erick mdogo,
“Umeionaje kazi mwanetu, unaonaje kiwanda?”
“Kipo vizuri na kazi inaenda vizuri”
“Na vipi mbona usiwe ofisini mpaka tukakukuta kule kwenye mashine?”
“Ni hivi, muhusika yani mwenye mali lazima uonyeshe kuwa kazi yako unataka ifanywe vipi, kwahiyo nahitaji kuwa mfano bora kwa wafanyakazi wote wa hapa kiwandani, pia sijataka wajihisi vibaya kwa kusimamiwa na kijana mdogo”
Baba Angel na Juma waliangaliana kisha baba Angel akamwambia mwanae,
“Muda umeenda sasa, kesho nitakuleta tena na kila siku atakuwa dereva anakuleta huku kwani kuanzia sasa hiki kiwanda kipo chini ya usimamizi wako”
Erick alitabasamu na kufurahi sana, kisha alienda kuweka sawa na kuondoka na baba yake pamoja na Juma.

Moja kwa moja waliondoka pale na njiani Juma alishuka na kuwaacha ndani ya gari kisha Erick na baba yake wakiendelea na safari huku baba yake akimuuliza baadhi ya maswali ya kiwandani na alifurahishwa na majibu ya mtoto wake,
“Oooh najivunia sana kuwa na mtoto mwenye akili”
“Nami najivunia sana kuwa na baba mwerevu”
Basi walikuwa wakitabasamu tu na safari ikiendelea hadi walipofika nyumbani ambapo baba Angel alienda chumbani na kuanza kuongea na mke wake,
“Eeeeh vipi Erick huko kiwandani”
“Kwakweli mke wangu tuache masikhara ila huyu mtoto ni jembe kweli tumepata, mtoto wetu ana akili sana”
“Itakuwa karithi kwangu huyu”
“Mmmh!!”
“Sasa unaguna nini jamani, mume wangu?”
“Inamaana mimi sina akili?”
“Hapana sina maana hiyo, ila Erick atakuwa karithi kwangu akili”
“Hukawii kusema na Erica karithi kwangu umbea”
Wakacheka tu, kisha baba Angel aliongea tena,
“Vyovyote vile ila Erick ni zawadi tuliyopewa na Mungu, na huyu atawalinda na kuwalea dada zake”
“Kweli kabisa mume wangu”
Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, basi akaichukua kuangalia na kuona aliyekuwa anampigia ni madam Oliva, basi akamtazama kwanza mkewe na kupokea ile simu,
“Halafu unajua kama watoto washachaguliwa shule nzuri tu za sekondari”
“Nishawatafutia shule mbona”
“Aaaah kumbe! Nilijua bado”
“Mmmh umesahau kuwa ni wewe ndio ulikuwa ukinielekeza shule ya kuwapeleka watoto!!”
“Ooooh nilisahau, yani mapenzi anayonipa Steve hadi sikumbuki jamani, yani Steve ananipenda hadi najiogopa. Hivi ni kweli mtu anaweza kukupenda hivi maishani?”
“Usiku mwema”
Baba Angel akakata ile simu na kuamuangalia mkewe ambaye alikuwa akingoja kwa hamu kusikia kutoka kwa mumewe kuwa ni kitu gani alikuwa akizungumzia,
“Alikuwa ananiambia tu shule walizochaguliwa Angel na Junior, ila kwavile nishawatafutia shule zingine basi tena”
“Ila mbona kama nahisi kuna mazungumzo mengine?”
Baba Angel akakumbuka kitu na kusema,
“Oooh nimekumbuka, hivi biashara yetu kule itafungwa hadi lini? Itabidi tutafute mtu wa kukaa kwenye ile biashara”
“MMmmh nani sasa?”
“Ngoja mke wangu, kuna mtu namfikiria ngoja nitamtafuta kuongea nae”
“Nani huyo?”
“Nitakwambia tu, ila nadhani atafaa katika kuendeleza gurudumu la biashara yetu”
“Sasa si umtaje?”
“Nikimtaja lazima utakataa”
“Mmmh usiniambie kuwa mtu huyo ni Derrick, tafadhari usimfikirie Derrick kabisa yani”
“Jamani mke wangu!!”
Baba Angel hakutaka kuendelea kuongelea mambo yale zaidi zaidi aliamua tu waendelee na mambo mengine na kwenda kulala tu.

Kulipokucha, baba Angel aliondoka na Erick kama kawaida na kwenda kumuacha kiwandani ila leo alimuomba dereva akamfate Erick muda wowote ambao Erick atamwambia kuwa aende kumfata, kisha baba Angel akaenda zake ofisini kwake.
Ila alivyofika ofisini alikumbuka tukio la jana yake la Sia kumkimbia Juma, akajiambia,
“Nahitaji kujua ukweli, ila inaweza kuwa ukweli ninachohitaji kujua? Nahitaji kujua huyo Baby alimtenda nini Juma, na je Sia ndio anaweza kuwa huyo Baby? Mmmh sidhani lakini”
Akampigia simu Juma na kuongea nae,
“Vipi tutaonana leo tuongee kidogo”
“Labda uje huku karibia na kwangu”
“Sawa nitafika huko kwenye saa nane au saa tisa alasiri”
Basi wakakubaliana, kisha akaendelea na kazi zake ila muda kidogo madam Oliva alifika ofisini kwa baba Angel na kuanza kuongea nae,
“Mbona jana ulinikatia simu? Ulihisi wivu?”
“Sasa wivu wa nini?”
“Wivu wa kusikia kuwa Steve ana mapenzi hadi shetani anaogopa?”
Baba Angel alitikisa kichwa na kumwambia madam Oliva,
“Unajua unataka kunichekesha tu, sasa mapenzi ya Steve kwako yanitie wivu kwasababu ipi? Mimi nina mke wangu na ninampenda sana sasa tatizo liko wapi?”
“Basi huo upendo wako kwa mke wako ni cha mtoto maana Steve ni ananipenda zaidi ya neno lenyewe kupenda, sijawahi kupendwa hivi katika maisha yangu yote”
“Ila upendo wa uhalisia ni mzuri sana kuliko upendo wa dawa, umemchanganya kijana wa watu akili zote pale alipo hazifanyi kazi halafu upo hapa kunieleza na kujitapa kuwa Steve anakupenda sana, kweli akili zako zipo sawa mwalimu?”
“Kheee kweli nimeichanganya akili yako hadi leo umeniita mwalimu! Ni kweli mimi ni mwalimu tena mwalimu ninayeijua taaluma yangu vizuri kabisa, ndiomana sipendi kukaa ndani ya uongo na kuwa mwalimu sio shida kwani wote sisi ni binadamu tuna hisia na mawazo tofauti tofauti”
“Sijui unazungumzia nini?”
“Huwezi kujua hadi mwalimu nikae chini na kukuelewesha ni kitu gani namaanisha, ngoja nikamuwahi mume wangu muda huu. Nitakuja kwaajili ya mipango ya harusi”
Kisha madam Oliva akainuka na kuondoka, basi baba Angel alitikisa kichwa na kusema,
“Sasa hili ni tatizo lingine nimezua nikitoa Sia jamani mmmh!! Yani hili ni tatizo kabisa kabisa”
Baba Angel akaamua tu kuendelea na kazi zake, muda wake ulipofika alifunga kazi na kuwasiliana na rafiki yake Juma na kwenda kuonana nae.
 
SEHEMU YA 289

Baba Angel alifika walikopanga kuonana na Juma, kwahiyo walikaa katika moja ya migahawa huku wakiongea ongea ambapo bado baba Angel alikuwa kisisitiza kujua hizo habari za Baby,
“Kwanini umekazana hivyo? Unazani yule mwanamke aliyekimbia ndio atakuwa Baby?”
“Hapana sijui, hata hivyo yule mwanamke haitwi Baby, bali anaitwa Sia. Yani natamani tu kujua kuhusu huyo Baby sijui kwanini ila natamani kujua”
“Ipo hivi, Baby alikuwa ni mwanamke ambaye nilimpenda sana, nilimthamini sana huwezi amini nilimpeleka kwa ndugu zangu wote, yani hakuna mtu kwetu ambaye hakumfahamu Baby, lakini yeye alinitambulisha tu kwa rafiki zake na kuogopa kunipeleka kw awazazi wake wala ndugu zake akisema kuwa yeye bado mdogo. Ila nilikuwa nae sababu sikutaka kumkosa kabisa, nakumbuka nilihitaji kumuoa ila Baby alisema haiwezekani kwani mimi na yeye tupo na dini tofauti, nisikudanganye Erick sababu ya Baby mimi nikabadili dini na kumuomba akanitambulishe kwa wazazi wake ili tuoane, akadai kuwabado hajafikia wazo la kuolewa ni mapema mno kwake, tukaendelea tu na mahusiano, kitendo alichonifanyia Baby ni kupata mimba yangu na kwenda kuitoa huku akisema hajajiandaa kuzaa na mimi, kwakweli niliumia sana, nikaona kuwa Baby ni mwanamke asiyenifaa alianza kukata mawasiliano na mimi, na mwishowe alikuja kuniambia kuwa kuna mpenzi wake kampata na wanapenda sana, mimi nimsahau kabisa, niliumia sana moyo na hapo Baby aliondoka katika maisha yangu sikuwa nae tena. Ilipita kama miaka mitatu au minne nikakutana na Baby akiwa amejawa na machozi usoni, nilimuuliza tatizo ni nini? Aliniambia katendwa sana na mapenzi, kiukweli nilimuhurumia. Nisikudanganye, kipindi hiko nilikuwa nipo kwenye harakati za kuoa huyu mke niliyemuoa sasa, ila nilikuwa radhi kuahirisha ndoa kwaajili ya Baby, na niliondoka nae na kwenda nae nyumbani kwangu tulikaa huko kwa siku mbili huku tukiwa na furaha sana na kufurahia maisha, nilimwambia Baby kuwa nitamuoa na alikubali kubadili dini yeye na kusema kuwa ataitwa Johari, nilifurahi sana alipotaja jina hilo. Ila alipoondoka kwangu akabadilika kabisa, hakutaka tena mawasiliano na mimi, akasema nisimtafute tena, niliumia sana na kufanya maamuzi ya haraka kumuoa Johari tena bila ya sherehe wala nini. Baada ya miezi michache, Baby aliniletea picha za harusi yake, niliumia sana, kiukweli alipendeza sana, nikatamani yule mwanaume aliyemuoa Baby ningekuwa mimi. Ila kuna kitendo kimoja alinifanyia Baby cha kuniumiza zaidi ya nilivyoumia mwanzo, yani huyu Baby huyu ni zaidi ya nilivyomjua. Ila sitasema ni kitu gani alinitenda”
“Mmmh alikufanyeje jamani, kitu hiko kinaweza kuwa msaada baina yangu na yako”
“Kwani unamfahamu huyo Baby?”
Baba Angel akafikiria kidogo, ni kweli hakumfahamu huyo Baby, ila alishangaa kwanini alitaka kujua habari zake, alimuwaza Sia kuwa amfikirie kuwa ni Baby kidogo alikuwa na mashaka na kumwambia Juma,
“Unajua nini nilikuwa nataka niangalia kama yule Sia ndio anaweza kuwa Baby, ila naona wazo langu linagoma. Unajua yule Sia nimewahi kuwa nae kwenye mahusiano, ila ana maisha halisia sana, na katika maisha yake kitu pekee anachokitaka ni kupendwa yani yeye analilia kupendwa usiku na mchana hadi anaenda kwa waganga”
“Mmmh basi hawezi kuwa Baby huyo, kwani Baby alikuwa hayo mambo ya waganga anayapinga kabisa. Nishawahi kumshawishi kufanya hivyo wakati kuna mambo yangu yamekwama ila Baby alikataa kabisa”
“Kumbe na wewe unaendaga kwa waganga?”
“Jamani Erick, tumekuja kuongelea nini na wewe unasema nini tena!! Unajua kuna baadhi ya mambo unaona hayaendi, ukiangalia kushoto hola, kulia hola unaona ni vyema nikatafute kinga kidogo, hatuendi kuroga ila kutafuta vya kutusaidia”
“Mmmh!”
“Tuachane na hizo stori jamani Erick, mimi nitaanza kukueleza bure mambo usiyopaswa kuyajua. Niambie kuhusu Erick”
Basi waliongea pale na kuagana halafu baba Angel alienda kumfata mwanae maana dereva alisema kuwa hakupigiwa simu na Erick.

Akiwa njiani baba Angel kuna mambo alikuwa akiyafikiria kichwani mwake, kwa muda huo mambo ya Sia na Baby hakuyaweka akilini ila alichoweka akilini ni kuhusu rafiki yake Juma kusema kuwa huwa ana tabia ya kwenda kwa waganga basi akajisema,
“Mmmmh ni kweli Juma amenipa wazo zuri sana ila sio wa kumuamini sana na yeye, akinigueka na kwenda kumroga mwanangu je!! Natakiwa kuwa na mipaka na huyu mtu sasa”
Basi moja kwa moja alienda kiwandani na kumkuta Erick akiwa hana habari kabisa kama anatakiwa kurudi nyumbani, basi baba yake alimwambia akamilishe na kuondoka.
Wakiwa kwenye gari alimsema kwanza,
“Unatakiwa kuwa na kiasi cha kazi Erick, sio muda wote ufanye kazi. Nimejaribu kuongea na mmoja hapo nasikia chai hunywi wala chakula cha mchana huli, sasa utaishi maisha gani jamani mwanangu Erick eeeh!! Na leo nimeona hata muda wa kuondoka huna habari nao, mwanangu kazi ipo tu ila mwili nao unatakiwa kupumzika ndiomana kuna muda wa kulala ila kufanya miili yetu ipumzike, mwanangu usifanye nijute kukuweka kiwandani, niahidi kuwa utabadilika”
“Nitabadilika baba, samahani”
“Yani usirudie tena kitu hiko, hebu angalia kumbe hujala tangia asubuhi jamani. Hapana Erick sitaki hii kitu tena”
“Sawa baba nimekuelewa”
Basi walifika nyumbani na kama kawaida baba Angel alienda chumbani ila muda huu Erick alienda chumbani kwake na kumkuta Erica ndio yupo mule kweye chumba chake, basi alikaa kitandani na kumuuliza,
“Vipi leo Erica mbona upo chumbani kwangu?”
“Unajua kukumiss! Nimekumiss sana Erick, ila umechoka na umenyong’onyea sana inaonyesha una njaa wewe”
“Ni kweli nina njaa sana”
“Kheee halafu leo tumepika chapati na rosti ya maini, sasa itakuwaje?”
“Duh!! Sitashiba, sijala toka asubuhi halafu mnipe chapati sijui na rosti la maini jamani mtafanya nile chambati hizo kama mbuzi na mimi kutafuna sana siwezi. Nikuombe kitu Erica?”
“Niombe tu”
“Naomba kanisongee ugali, nakuomba tafadhari”
Basi muda huo huo Erica alienda jikoni na kubandika sufuria na kwaajili ya kusonga ugali, basi Vaileth nae alienda jikoni na kumkuta Erica ndio anakorogea uji na kumuuliza,
“Kheee nini unapika?”
“Nataka kusonga ugali kwaajili ya Erick, njaa inamuuma sana”
“Oooh nyie mapacha mnajaliana hadi raha jamani”
Erica alitabasamu na kumwambia Vaileth,
“Dada, niangalizie samaki humo kwenye friji unipakie na viungo nimkaangie”
Basi Vaileth alifanya vile na Erica alipomaliza alimuweke kile chakula Erick na zile mboga yani samaki wa kukaanga na rosti ya maini, basi Erick alitoka tu chumbani na kuanza kula kile chakula, kwakweli alikuwa na njaa kiasi kwamba alikula chakula chote huku akifurahi na kumsifia sana dada yake kwa upishi wake,
“Ndiomana baba huwa anasema, kwakweli Erica kwenye mapishi wewe ni kiboko”
“Mmmh njaa hiyo, kwani ugali nao una utaalamu?”
“Ndio una utaalamu, kuna watu hawajui kusonga ugali, sio niseme watu tu hata mimi mwenyewe siwezi kusonga vizuri hivi kama ulivyosonga wewe, yani mtu unakula ugali unaona kabisa umeiva, ugali laini na mzuri, mwingine sasa anasonga ugali mgumu kama jiwe”
Erica alicheka, ila muda huo kuna mgeni alikuwa amefika ndani kwao ila hawakumuona mpaka alipowasogelea pale mezani na kumuuliza Erick,
“Ushawahi kuona mtu kasonga ugali mgumu kama jiwe?”
Wakamuangalia na kumsalimia kwa pamoja,
“Shikamoo shangazi”
Alikuwa ni shangazi yao Tumaini, aliitikia ila alionyesha kuwa hakuwa na furaha kabisa, kisha akamwambia Erica,
“Kaniitie mama yako, maana nimefika muda sana tu”
Basi Erica alienda kumuita mama yao ambaye kwa muda mfupi tu alifika ila alishangaa kwa muda ule kumuona wifi yake akamkaribisha,
“Karibu wifi ila mbona muda huu!! Kwema kweli huko?”
“Kwema ndio, kuna mahali nilikuwepo sio mbali na hapa kwahiyo wakati naondoka nikasema ni vyema nije kuwasalimia kidogo”
“Oooh karibu sana na umefanya vizuri”
“Ila ndio nataka kuondoka”
“Jamani, ngoja nimuita basi kaka yako”
“Aaaah usimuite, twende nje mara moja”
Basi mama Angel alitoka na wifi yake ila kufika kule nje wifi yake alimwambia,
“Unajua sikupanga kabisa kuja huku, ila nilipokuwa sio mbali na hapa kiasi kwamba sikujihisi vizuri kuondoka bila kuja kuwasalimia, ila kumbe Mungu alikuwa na maana halisi ya kunileta mimi huku”
“Unamaanisha nini?”
“Hivi Erica, kweli kabisa wewe wa kuwaletea watoto mambo ambayo yalifanyika miaka ya nyuma kabisa kabla hawajazaliwa? Watanionaje mimi kuwa shangazi yao sijui kupika au?”
“Unajua sikuelewi”
“Hunielewi kitu gani, umewaambia watoto wako kuwa mimi sijui kupika. Umewaambia kuwa niliwahi kusonga ugali mgumu kama jiwe, kwakweli sijapenda na sijapenda kabisa, Halafu alimtia singi yani alimsukuma kichwa kwa mkono, kisha akapanda gari lake na kuondoka zake.
Mama Angel hakuelewa chochote kwani hakuwepo sebleni wakati watoto wakiongea hayo, kumbe naye Tumaini kajihisi tu bila hata ya kusemwa wala nini.

Usiku huu, Angel alikuwa na simu yake ambapo kwa muda huu alinyata tu na kuichukua chumbani kwa bibi yake ambaye alikuwa amelala na yeye wazo lake lilikuwa ni kuwasiliana na Samir, basi aliwasha simu yake na kujaribu kumpigia Samir ambaye alimpigia yeye, basi alianza kuongea nae,
“Unajua nimekumbuka hata sauti yako, jamani Samir karibu hata uje unione tu”
“Basi kesho kutwa yani Jumamosi nitajitoa muhanga na kuja huko hata usijali kipenzi changu”
Wakati akiendelea kuongea nayo mara alisikia kama mlango wa bibi yake ukilia, kwahiyo alishtuka sana na kufanya simu ianguke chini na ilianguka vibaya sana kiasi kwamba ilipasuka kwenye kioo, yani roho ilimuuma sana, alipoona pametulia aliiokota simu yake na kujaribi kuiwasha iliwaka ila ilikuwa kama na ukungu kwa mbali sababu ya kioo kupasuka, alikosa raha kabisa, ujumbe wa Samir uliingia kwenye simu yake,
“Tatizo ni ni mpenzi?”
“Yani nilisikia kama bibi basi simu si ikanianguka, imepasuka kioo yani simu yangu imeondoka shoo yote”
“Oooh pole, utanitajia basi aina ya simu ili niangalie uwezekano wa kuitengeneza”
Basi Angel akamwambia kuhusu simu yake na Samir alimuahidi kuitengeneza, alimwambia kuwa hiyo kesho kutwa ataenda kuitengeneza.
Basi Angel aliirudisha ile simu kwa bibi yake na kumkuta amelala hana hata habari, basi na yeye alirudi chumbani kwake na kulala sasa, aliwaza kiasi kuhusu simu yake ila aliamini kuwa Samir atafanikisha hilo la kumtengenezea simu yake.

Leo jioni wakati Samir yupo kwao, alikuwa na mawazo kiasi basi mdogo wake alianda karibu na kumuuliza,
“Kwani kaka unawaza nini?”
“Unajua nini nina hitaji laki mbili ya haraka, sijui naipata vipi”
“Oooh kaka, unaahidi kunipa nini nikikupatia hiyo laki mbili”
“Halafu wewe jamani, hiyo laki mbili utaitoa wapi sasa eeeh!!”
Kisha Samir aliachana na mdogo wake na kuondoka zake, kwenda kwenye matembezi yake, ila siku jioni hii alikutana na Hanifa, na kumshangaa pale,
“Kheee Hanifa una mimba?”
“Sasa unashangaa kitu gani kwani ni jambo la ajabu kwa mwanamke kubeba mimba?”
“Hapana sio jambo la ajabu ila wewe bado mdogo”
“Usitake nicheke mie, mdogo!! Kwani mimba nimejipa au? Si ndio nyie nyie wanaume mmenipa!”
“Kwahiyo kumbe ulifanya mtihani wa mwisho ukiwa na mimba!!”
“Ndio, nilikuwa najibana ila kipindi kile ilikuwa bado ni ndogo, yani Samir unavyoshangaa utafikiri huajwahi kumpa mwanamke mimba!! Unafikri habari zako na Warda hatuzijui? Wewe si ulimpa mimba Warda na umeenda kumtoa”
“Kheee jamani, watu mnayatafutaga maneno hata sijui huwa mnayatafuta wapi jamani, nani kakwambia maneno hayo?”
“Unadhani ni siri hiyo? Sio siri kabisa, bora mimi ninayeenda kuzaa kuliko huyo aliyetoa. Najua na huyo Angel nae atapata mimba yako tu na utamtoa kama kawaida sababu unaogopa aibu na kwenu huna cha kumjibu yule baba yako mshika dini lakini ana watoto wengi”
Samir hakutaka kuongea sana na huyu Hanifa, kwanza alimuona wazi maisha yamempiga kwa kubeba mimba, kwahiyo aliachana nae na kuondoka zake.

Usiku wa leo, Junior akiwa chumbani kwa Vaileth walijikuta wakiongea mambo mengi sana ya maisha yao basi Vaileth alimdadisi pia,
“Kwanini simu yako unaizima Junior? Kuna wanawake zako eeeh unaogopa watakupigia?”
“Hapana, ila kuna watu sitaki wanipate hewani”
“Mmmh mimi nina hisia mbaya, maana wewe Junior hata huaminiki”
“Haya, iwashe hapo iache hewani hadi asubuhi uone kama kuna mwanamke wa kunitafuta”
Basi Vaileth aliiwasha ile simu ya Junior, ila muda ule ule kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, jina la mtu ujumbe lilitokea Samia, basi Vaileth alifungua ule ujumbe na kuusoma,
“Junior, nimekumiss. Kesho nitakupa kweli ila naomba uniletee laki mbili halafu ndio nitakupa”
Vaileth alimtazama Junior kwa gadhabu kubwa sana.

Kisha alimtingisha na kumwambia,
“Sikumpa Samia hela yoyote, nilienda kufanyia biashara, utumbo gani huu kaandika huyo Samia wako!”
Junior alichukua ile simu na kusoma ujumbe wa Samia, kwanza moyo wake ulidunda kiasi kisha akamuangalia Vaileth na kumwambia,
Vai mpenzi wangu, sijui nikuelezeje ili upate kunielewa, haka katoto kametumwa na mama lazima mama yangu ndio kakatuma kufanya ujinga kama huu. Hakuna kinachoendelea baina yangu na Samia”
“Unanifanya mimi mjinga eeeh!! Narudia, mimi sio mtoto Junior wa kunidanganya kila siku kwanini lakini Junior? Naomba uwe mkweli ili angalau nikuelewe maana naona unanichanganya tu”
“Jamani Vai mpenzi, huo ndio ukweli”
“Junior, hivi unajua umri wangu kwasasa? Unajua mimi na wewe tumepishana miaka mingapi? Unajua ni mangapi nimepitia hadi leo? Junior sio mdogo mimi, naelewa mengi tu, niambie ukweli sio unafanya kazi ya kunificha ficha na kunidanganya”
“Vaileth, sina cha kukwambia zaidi ya niliyokwambia”
“Sasa basi, kwa siku ya kesho sitaki kukuona ukitoka hata kwenda dukani, nataka ukae hapa hapa nyumbani, nimechoka na uongo wako Junior”
“Nimekubali, sitatoka wala sitaenda popote mpenzi wangu”
Junior alijua ni jinsi gani Vaileth amechukia, kwahiyo alikuwa akimbembeleza tu.
 
SEHEMU YA 291

Samir alimfata mdogo wake ambaye alikuwa amekaa sebleni huku ameshikilia simu yake, alimuuliza,
“Haya mpango wako wa kupata laki mbili umeishia wapi?”
“Aaaah tatizo kaka huniamini, halafu huyu mjinga nae sijui kakwama wapi, kila muda anasema anakuja anakuja”
“Ni nani huyo? Unajua mdogo wangu una vituko sana wewe!!”
“Ngoja kaka nikwambie, kuna huyu mtu ananifatilia kweli yani ananitongoza, mara ya kwanza nilimwambia niletee laki tano akaniletea, na sasa nimemwambia laki mbili”
“Mmmmh hiyo tabia umeipata wapi Samia? Mtoto mdogo hivyo umeanza kupenda hela, unajua sikukuelewa kabisa, lakini kama ni ujinga huo hapana kwakweli”
“Sio ujinga kaka, kwani kuna chochote nafanya nae jamani!! Mimi nachukua hela yake tu, nafanya kamavile baba alivyonifundisha”
“Aaaah yani baba ndio anakufundisha na wewe ujinga wake jamani!! Ila amakweli baba tunae loh!! Haya na huyo anayekufatilia ni nani?”
“Anaitwa Junior, ni ndugu yake na Erica”
“Wewe mjinga wewe, kaone vile. Junior atakubaka wewe, hakuna mtu mwenye akili mbovu kama Junior, wewe mtoto ukoje lakini. Hebu acha kuwaza ujinga, kaone vile, ndiomana watoto huwa mnakatazwa simu maana naona simu inakupa kichaa hiyo. Mjinga wewe”
Kisha Samir akaondoka zake, maana hakupenda kile kitu kilichosemwa na mdogo wake, ni kweli hakuwa na pesa ila hakutaka ipatikane kwa njia hiyo.

Angel akiwa ametulia kwa bibi yake, muda huu alikuwa akiangalia simu yake huku akiwaza kama kuna uwezekano wa kupona kioo cha simu yake, yani akawaza sana basi akaamua kumtumia ujumbe Samir maana alimuahidi kutengeneza ile simu,
“Sasa Samir vipi mbona hujanipa jibu?”
“Dah samahani, yani nimeulizia matengenezo ya kioo kwa hiyo simu ni laki mbili, ila samahani kwasasa nimepungukiwa kidogo na hela ila nitaitengeneza tu”
Angel alimuitikia ila alionekana kukosa furaha kabisa kwani aliona wazi ile simu ikiendelea inazimika kabisa, ila akakumbuka kuwa jana yake alimtafuta na Ally na alimwambia swala lile, basi akataka kumtafuta tena ila muda ule ule ujumbe wa Ally uliingia kwenye simu yake,
“Angel nimeulizia matengenezo ya hiyo simu nimeambiwa ni laki mbili, nikutumie ukaitengeneze au nije niifate niipeleke kwa fundi akaitengeneze”
“Njoo uifate tu, maana mimi sitaweza kwenda popote”
“Kwanini usimwambie bibi yako kuwa unaenda kuitengeneza simu halafu kesho nije nikuchukue twende kwa fundi”
“Ngoja nitajaribu”
Basi Angel akakubaliana hivyo na Ally, na kuinuka ili akaongee na bibi yake kuhusu swala hilo, ila alipofika tu kwa bibi yake ni bibi yake ndio alianza kuongea,
“Yani hawa wamenishtukiza tu, inabidi kesho nikakutane na wenzangu kwenye kikoba, yani kuna watu wa mikopo ndio inabidi tukawajadili kesho”
“Sawa bibi hakuna tatizo”
“Na wewe utakuwa unafanya nini?”
“Mimi natabaki nimelala tu bibi”
Basi Angel hakuona haja ya kuomba ruhusa kwa bibi yake kwani aliona ni nafasi iko wazi kabisa ya yeye kuweza kutoka.

Baba Angel na Erick muda huu waliungana na wengine mezani kupata chakula cha usiku kwanza, kwani Erica alipika chakula cha kuweza kuliwa na familia nzima, na siku hiyo alipika pilau, basi baba Angel alikula huku akisifia,
“Kheee kweli tumekuza, yani binti yangu umekuwa hadi unaweza kupika pilau tamu namna hii!! Ndiomana Erick kagoma kula pote hadi tufike nyumbani”
Basi Erica alikuwa kitabasamu tu huku akimshukuru baba yake kwa zile sifa alizompa, wote ndani walikula na kusifia kile chakula, basi kila mmoja aliposhiba siku hiyo walimshukuru sana kisha kila mmoja alielekea kwenye mambo yake.
Baba Angel na mama Angel waliingia chumbani ambapo mama Angel cha kwanza aliuliza,
“Hereni nilizokuagiza mume wangu ziko wapi?”
“Aaaah nimekuja nazo pea mbili, ila unatakiwa kuchagua moja maana nyingine itakuwa ya Erica”
“Mmmh umemkumbuka mwanao eeeh!! Anajua nini ndiomana kawapikia pilau leo!!”
Baba Angel alicheka tu na kutoa zile hereni, basi mama Angel alizishika na kusema,
“Zote ni nzuri na zinapendeza sana”
“Kwahiyo umechagua hereni zipi mpenzi?”
“Aaaah nimezipenda zaidi hizi hapa, nimezipenda sana”
Basi alichukua na kuzijaribu kisha akajiangalia kwenye kioo na kujiona kuwa kapendeza sana, basi alimshukuru mume wake na kumwambia,
“Yani asante sana, ila siku hizi umekuwa noma katika kuchagua zawadi mume wangu, dah nimezipenda hizi hereni sana”
“Ooooh nimefurahi kusikia hivyo mpenzi, basi lete hizo nimpelekee Erica sasa”
Basi mama Angel alimkabidhi zile hereni na moja kwa moja baba Angel alienda nazo kwa Erick kwanza kwani alitaka kumuuliza jambo kwakuwa yeye alisahau,
“Eti Erick, hizi hereni ndio alichagua yule mama au yule baba?”
“Ni yule mama ndio alichagua hizi, kumbe mama kapenda zile alizochagua yule baba eeeh!!”
“Ndio, kazipenda zile mama yenu. Chukua mpelekee Erica”
Basi baba Angel alitoka ila alikuwa akishangaa sana kwanini vitu akichagua yule baba Emma basi hutokea mkewe akavipenda sana vitu hivyo kama hizo hereni, basi alirudi ndani na kuongea na mke kidogo,
“Mke wangu, hivi wewe unapenda nini?”
“Mmmh mimi napenda vitu vingi sana ila cha kwanza kabisa ni wewe”
“Aaaah jamani, asante mke wangu. Yani nilikuwa namaanisha kwenye zawadi unapenda nini?”
“Napenda kila zawadi unayoniletea haswaa zawadi unazoniletea siku hizi, nazipenda sana. Kama hizi hereni uwiiii jamani sijui mume wangu umejuaje kuwa nitafurahi namna hii kwa hereni hizi!”
Basi baba Angel alitabasamu tu,ila kwa muda huo waliamua tu kulala.

Kulipokucha, baba Angel alikumbuka jambo kuhusu Juma kutaka kuja kuonana na mtoto wake basi akaita familia yake na kuongea nao,
“Jamani, leo ni Jumamosi. Wiki ijayo shule zinafunguliwa, kwahiyo nisipofurahi kwasasa nanyi watoto wangu basi itakuwa ngumu sana kufurahi tena, kwahiyo naomba mjiandae leo tutaenda ufukweni kutembea”
Wote walifurahia tena walifurahi sana, mama Angel aliuliza,
“Mimi na Ester je?”
“Naye tunaenda nae, kwani tatizo liko wapi mke wangu? Tunaenda na Ester wetu kufurahi”
Baada ya hapo kila mmoja alijiandaa kwaajili ya hiyo safari ambayo baba yao ameipanga.
Walipomaliza walipanda kwenye gari, basi wakati baba Angel akijiandaa kutoa ile gari kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake, alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Juma,
“Ndio nipo njiani nakuja, leo nakuja na mke wangu”
Baba Angel hakutaka kuongea chochote wala hakutaka kumwambia mke wake kwani anajua wazi mkewe akijua atakazana wabaki ili wawapokee hao wageni, kwahiyo moja kwa moja aliondoa gari na kuelekea ufukweni.

Angel aliwasiliana na Ally na kujiandaa kabisa, basi Ally alifika muda ambao bibi Angel hakuwepo nyumbani kwahiyo Angel alitoka na moja kwa moja alipanda kwenye bajaji ya Ally na kuanza kuelekea kwa fundi ili Angel akatengenezewe simu yake, basi alikuwa akiongea nae,
“Yani Angel mimi nakupenda sana, nipo tayari kufanya chochote kwaajili yako ili tu wewe ufurahi”
“Ila ile kauli ya mamangu mkubwa kuwa sisi ni ndugu uliichukuliaje?”
“Aaaah mimi nimechukulia tu kama mtu kaongea kama kuongea kwani huo undugu mimi na wewe utatokea wapi? Tupo tofauti kabisa yani, mimi ninachojua nakupenda basi”
“Ila mimi nina mpenzi”
“Huyo mpenzi wako angekuwa wa maana basi yeye ndio angeingia dhamana ya kutengeneza simu yako, ila mimi ndiye ninayekupenda kwa dhati”
Angel hakujibu kitu kwani lengo lake ni ile simu ipone tu ili isizimike maana alijua ikizimika basi ndio mawasiliano hakuna tena.
Walifika kwa fundi na moja kwa moja kumkabidhi ile simu kwaajili ya matengenezo, ila Ally alimuomba kitu Angel,
“Wakati simu inatengenezwa hapa, twende pale tukapate vinywaji kidogo”
Angel alikubali na walitoka kwa yule fundi huku Ally akiwa amemshika mkono Angel ila pale nje Angel alishtuka kidogo kwani alimuona Samir ambaye inaonyesha alikuwa akienda kwa fundi yule yule, ila Samir aliwakaribia na kumuuliza Ally,
“Nani yako huyu?”
Ally nae alijibu kwa kujiamini,
“Huyu ni mpenzi wangu, kwani vipi?”
Samir alionekana kuwa na hasira sana, kwani muda ule ule alikunja ngumi na kumshindilia Ally puani.

Ally alionekana kuchukia na yeye ila kabla hajafanya lolote, alishtukia akipigwa teke na Samir hadi akaanguka chini, yani ni Angel ndio alienda kumsaidia kuinuka pale chini, Samir alitaka kumshindilia teke lingine pale chini ila Angel akamzuia,
“Wewe Samir ukoje wewe yani hata huulizi jamani eeeh!!”
“Niulize mara ngapi? Si amejibu kuwa ni mpenzi wako!”
“Kumbe Samir hujui akili zangu eeeh!! Yani umeshindwa kuniuliza mimi mwenyewe!! Sasa kuanzia leo sikutaki”
Kisha Angel alimsaidia Ally pale chini kuinuka, ila Samir alikuwa kama katengenezewa kidonda vile basi akamsogelea Angel na kuanza kumuomba msamaha,
“Samahani Angel mpenzi hii hali haitajirudia”
“Mjinga wewe, siwezi kuwa na mahusiano na mwanaume bondia, hebu nipishe huko sikutaki na usinitafute tena”
Bado Samir hakuelewa kabisa, na kuamua kumpigia magoti Angel ili aweze kusamehewa na Angel ila bado Angel alikuwa mgumu kufanya hivyo na alimwambia Samir aachane nae kabisa, yani Angel aliona kamavile siku yake imeharibika kwani aliingia kwa yule fundi na kumuomba simu yake ambayo bado hakuanza kuitengeneza ila Angel alitoka nayo na kuanza kuondoka, ikabidi Ally amfate na kuingia nae kwenye bajaji halafu wakaondoka huku akimuuliza,
“Sasa Angel mbona umetoa simu kwa fundi kabla ya kutengenezewa”
“Nimeghairi sitaki tena itengenezwe”
“Oooh jamani Angel, nakuomba jambo moja basi tupitie hapo upate japo simu ya mawasiliano kwa hii laki mbili maana nipo nayo kwaajili yako”
Angel hakujibu kitu ila Ally alipita nae dukani na kununua nae simu nyingine ambayo walinunua kwa laki mbili na elfu ishirini kwani ndio simu angalau ambayo Angel alionyesha kuipenda na kuvutiwa nayo.
Wakati wanatoka kwenye duka lile, Angel alimuona mama mmoja ambaye yule mama ashawahi kumuona mara kadhaa ila yule mama alionekana kuongea jambo na Ally na kumpatia Ally pesa kidogo.
Basi wakati wanaondoka, Angel alimuuliza Ally,
“Kwani yule mama ni nani?”
“Ni mama yangu mdogo yule, huwa kuna kazi zake ananipa ndio katoka kunipatia pesa. Sasa Angel mimi ndio nitakuwa mpenzi wako eeeh!! Usikatae Angel tafadhari, nakupenda sana”
“Ndio utakuwa mpenzi wangu, ila sharti langu ni moja usiniletee habari za kufanya ngono”
“Mmmmh!!”
Kuna jambo Ally aliwaza kichwani,
“Mapenzi bila ngono inawezekana kweli!!”
Ila hakusema ili Angel asifikirie vingine, bali alimjibu,
“Hakuna tatizo ila tu ni vyema tuwe tunapata muda mzuri wa kubadilishana mawazo na kuambiana mambo mbalimbali”
“Sawa hakuna tatizo juu ya hilo”
“Nakupenda sana Angel”
“Asante, wewe ni kijana mstaarabu nimependa ulichofanya leo, hukuonekana kumjibu vibaya yule aliyekupiga, hukuonekana kutaka kumrudishia wala nini, nakuona kuwa ni kijana mwema. Ila kuhusu mapenzi inabidi unisubiri maana mimi ninasoma,subiri nimalize masomo yangu”
“Sawa sawa, hakuna tatizo Angel.”
Basi walifika hadi kwa bibi yake Angel na Ally alimuaga hapo Angel na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 292

Tumaini, kuna mahali alikuwa ametoka muda huu ila njiani alimuona Sia na kuamua kusimamisha gari ili kuongea nae, alifanya hivyo mara kwa mara sababu ni mtu ambaye alikuwa rafiki yake kabla,
“Sia, Sia”
Sia akasogea karibu na kusalimiana nae,
“Unajua kuna wakati huwa najiuliza kuwa Tumaini huwa ananikumbuka kweli”
“Kwanini nisikukumbuke sasa?”
“Sijui basi tu, umetoka wapi kwani muda huu?”
“Kuna mahali nimetoka nikataka kwenda kwakina Erica nikawasalimie kidogo maana kuna ujumbe nilikuwa nao kwaajili ya Erica ila njiani kabla sijafika nikakutana na Derrick akaniambia katoka huko, kuwa wenyewe hawapo”
“Kheee wameenda wapi?”
“Nasikia wameenda kutembea, Derrick alisema kuwa alienda huko alikuwa na maongezi na Erick sijui ila hajawakuta, basi nikaamua kuondoka, nimemwambia Derrick tuondoke wote kagoma, kasema kuwa ana safari zake”
“Mmmh huyo Derrick na huo utapeli wake sijui kama hajaliza mtu huko kwa Erick!!”
Sia akacheka, kisha Tumaini akamuuliza,
“Na wewe umetoka wapi?”
“Nimetoka huko kufanya maovu”
Tumaini akatikisa kichwa kidogo na kusema,
“Kweli umetoka kufanya maovu maana mambo yako siku hizi ni zaidi hata ya neno lenyewe maovu, hivi kwanini Sia umekuwa hivyo unajua sio Sia yule niliyemfahamu miaka kadhaa iliyopita, niliyekuwa namsaidia katika mambo mbalimbali hadi nikajiingiza kugombana na Erica kama nami namgombea Erick kumbe kwaajili ya kukuonea huruma wewe, yuko wapi yule Sia wa siku zote?”
“Siku mtakayokubali kuniweka mimi kama mmoja wa familia yenu basi nitaonekana kwenu kiundugu na nitakuwa nanyi bega kwa bega tukisaidiana mambo mbalimbali ila mkiendelea na kunitenga basi na mimi nitawatenga”
“Ila unajua wewe ni mwezi mchanga yani huwa sikuelewi kabisa, nilikuwa nakusalimia tu kaendelee na maovu yako”
Kisha Tumaini akarudi kwenye gari yake na kuendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake.

Angel alitulia ndani, ila kwa upande mwingine aliona ni vyema kwa yeye kupata simu mpya, maana atamficha bibi yake na kumuacha abaki na ile nyingine, na alishukuru muda huo bibi yake hakuwepo nyumbani wala nini, kwahiyo alirudisha ile simu kwa bibi yake na kuijaza chaji hii nyingine na kuweka laini yake, ambapo muda mfupi tu alipokea ujumbe toka kwa Samir,
“Angel umenikataa sababu ya kumpiga ngumi yule kijana au sababu ya kukosa laki mbili?”
“Aaaargh umeniudhi bhana, sitaki ujinga mie”
“Ila kumbuka Angel tunapendana sana”
“Sijali kitu, ninachojali ni kumpata mwanaume wa kawaida na sio bondia”
“Mmmmh Angel jamani, usinifanyie hivyo”
Ila Angel hakumjibu chochote kwani yeye alikuwa akifikiria vitu vingine kabisa, aliona kuwa ile itakuwa ni adhabu kwa Samir na kumfanya asije kurudia siku nyingine kufanya alichokifanya.
Basi akamtumia ujumbe Ally,
“Yani hii simu ni nzuri hiyo hadi raha, haina vitu vigumu kama ile niliyokuwa naitumia”
“Oooh, ndio simu za gharama zina mambo mengi zile ndiomana wanaziuza bei sana. Ila hiyo ni nzuri na rahisi kutumia, sasa jiunge whatsapp uwe unanitumia picha zako”
“Mmmmh!! Ngoja nitafanya hivyo basi hakuna tatizo”
Muda kidogo bibi yake alirudi na kumuita Angel, ambapo Angel alienda kwa bibi yake,
“Mjukuu wangu ulikuwa umelala?”
“Ndio bibi, si unajua nipo mwenyewe maana hata Maria hayupo”
“Kheee kumbe bado hajarudi toka jana!! Mmmh kashapata mwanaume wa kumdanganya yule, haya nimeleta chakula kwahiyo hakuna kazi ya kupika”
Angel alitabasamu kwani hata wazo la kupika hakuwa nalo, basi bibi yake alitoa chakula na kumfanya Angel aulize,
“Umetoa wapi hiki chakula bibi?”
“Kule tulipofanya kikao leo tuliandaliwa chakula, kimebaki sasa kila mtu kabeba nikaona kwanini nisibebe mie! Nikajibebea zangu tuepuke bajeti”
“Jamani bibi, umenikumbusha mama tulienda hotelini akabakisha chakula weeee akaomba mfuko na kufunga chakula chake”
“Kheee mama yako nae, kwa hela zote zile bado anakumbuka chakula chake. Ila ni vizuri, hata wewe uwe hivyo sio unaacha acha chakula kizembe”
Walikula pale na walipomaliza, Angel alienda chumbani kwake sasa ila akajikuta akikumbuka kitu, alimkumbuka yule mama aliyekuwa akiongea na Ally, akakumbuka kuwa kuna siku yule mama aliwahi kupigwa kibao na Samir, halafu Erick alikuwa hampendi kabisa yule mama, basi akajiuliza,
“Yule mama ni nani? Mmmh!”
Ikabidi aachane na hayo na kuamua kulala tu.

Muda huu baba Angel na familia yake walikuwa wamerudi nyumbani na walikuwa wamechoka sana kutokana na mambo yote yaliyofanyika siku hii.
Basi walijiandaa kulala ndipo baba Angel aliposhika simu yake na kukutana na jumbe mbalimbali moja ya jumbe zilizokuwepo ilikuwa ni ujumbe toka kwa Juma, ujumbe huu ulimshtua kidogo hadi alimsomea mkewe,
“Kuna ujumbe kanitumia Juma, kiukweli umenishtua hapa”
“Ujumbe gani?”
“Ngoja nikusomee, umetoka kwa yule rafiki yangu Juma”
Basi baba Angel alianza kumsomea mkewe ule ujumbe,
“Mmmh kiukweli kilichonipata leo hapo nyumbani kwako hadi najuta, ungeniambia mapema kuwa hutokuwepo kuliko hivi ndugu yangu, nimekuja na mke wangu leo ila sijakukuta wewe wala familia yako, halafu nakupigia simu hupokei. Ila hilo sio swala la muhimu, kinachoniuma ni mtu ambaye nimekutana nae hapo na akajitambulisha kuwa yeye ni mnajimu, huwezi amini katutapeli mimi na mke wangu milioni tatu hivi hivi jamani. Yani tumerudi nyumbani ndio tumegundua utapeli wa huyu jamaa!! Kwakweli sijafurahishwa kabisa na hiki kitendo cha huyu mtu tena kwenye geti lako, nasikitika sana”
Baba Angel akamuangalia mkewe na kumuuliza,
“Inawezekana akawa Derrick kweli!!”
“Mmmh, ngoja nikamuulize mlinzi, ila nahisi ni Derrick tu. Kwanini anafanya hivi lakini jamani!! Aaarggh!”
Basi mama Angel akataka kutoka ili akamuulize mlinzi, ila mumewe alimrudisha na kwenda yeye mwenyewe kuuliza kwa mlinzi.
Alimkuta mlinzi getini na kumuuliza,
“Ni watu gani walikuja leo?”
“Mmmh walikuja yule baba wa siku ile na mama mmoja hivi waliwaulizia niliposema hampo waliamua kuondoka”
“Ni nani walikutana nae nje ya geti? Au ni nani mwingine alikuja?”
“Mmmh sijui kwakweli maana mimi nilikuwa ndani ya geti wakati wanaondoka”
“oooh sawa, usiku mwema”
Baba Angel alirudi kwa mkewe na kumwambia alichosema mlinzi, halafu akasoma tena ule ujumbe wa Juma na kumuuliza mke wake,
“Kwani mnajimu ndio mtu gani?”
“Ni mtu mwenye elimu ya nyota, haya sasa hadi rafiki yako katapeliwa si huwa unasema wanaotapeliwa si wenye tamaa ya mali!!”
“Sasa unadhani ni kitu gani kilichomfanya Juma na mkewe watapeliwe? Nadhani huyo mtu kawadanganya kuwa yeye ni mtaalamu wa nyota na kawadanganya kuhusu nyota zao maana matapeli wengi sana huwa wanatumia hiyo. Ila najiuliza, hiyo milioni tatu wameitoa vipi nao!!”
“Dah!! Ila matapeli ni wabaya sana, natamani kumjua tapeli mwenyewe. Kama sio Derrick sijui yani”
Basi waliamua tu kwa muda huo kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda sana.
Kulipokucha familia nzima ilijiandaa na leo na kwenda Kanisani kwahiyo hapo nyumbani hakuna mtu ambaye alibaki zaidi ya mlinzi wao tu.

Muda huu bibi Angel alitoka na mjukuu wake Kanisani, wakati wapo njiani kuna mama mmoja walikutana nae ambaye alionekana kumfahamu bibi yake Angel basi aliwasalimia pale na kuuliza,
“Kheee huyu ndio mtoto wa Erica, yule aliyekuwaga anamficha ndani!”
Bibi Angel akaona huyu anamletea mada zisizoeleweka, basi akambadilishia mada na muda huo huo wakaondoka zao.
Walipofika tu nyumbani, wakaandaa chakula na kuanza kula basi Angel akamuuliza bibi yake,
“Kwani bibi, mama alikuwa ananificha mimi?”
“Aaaah achana na yule mwanamke aliyeuliza pale ni chizi”
“Mmmh bibi!!”
Mara alifika Mage na kuwakuta wanakula pale, walimkaribisha naye alikaribia huku akisifia,
“Nina mguu mzuri sana, mimi ni mkulima halisi. Hebu Angel kanipakulie na mimi chakula”
Angel akaenda kumpakulia na kumletea, ambapo Mage alianza kula na kusema,
“Mmmh hiki chakula kapika nani?”
“Angel huyo”
“Mmmh Angel nawe hata sio mpishi hodari kama mama yako, ila kitamu kiasi chake ila mama yako ni noma”
“Ukitaka pishi la Erica basi upikiwe na Erica mdogo mbona utajing’ata vidole, mtoto mdogo ila anajua kupika balaa”
Angel hakupenda ile sifa ambayo alipewa Erica na kuachwa yeye dada mtu, kwahiyo alivyomaliza kula tu aliamua kwenda zake chumbani kwake, halafu pale sebleni bibi yake na mamake mkubwa walikuwa wakiongea,
“Kwanza mama samahani, najua swala hili hulipendi hata kidogo ila sina budi kukuletea tena naomba msaada wako”
“Swala gani tena?”
“Mama, mimi ni dada. Mimi ndiye mkubwa wa hii familia na ndiye muhimili, natakiwa kusimama imara kwaajili ya wadogo zangu. Ni kweli Derrick kazaliwa nje ya ndoa ila bado ni mtoto wa baba yetu yani bado ni ndugu yetu, mama nahitaji msaada wako kama mzazi wetu”
“Sasa msaada gani unataka kutoka kwangu”
“Itakuwa vyema sana ukituita watoto wako wote hapa na kutufanyia kikao na sisi tuweze kuzungumza, nahitaji sana mimi na familia tushirikiane kumuokoa Derrick anahangamia mama. Yani Derrick ni tapeli haswaa na wala sio wa kusingiziwa”
“Sasa, Mage jamani unaniingiza kwenye mambo yasiyonihusu kabisa. Hivi mimi ni mtoto wa baba yenu au kitu gani?”
“Hapana mama ila wewe ni mama yetu, tafadhari mama nakuomba sana fanya hivi kwaajili yetu mama yengu jamani nakuomba sana”
“Naomba nisikujibu kwa leo, nitakujibu siku nyingine ngoja nifikirie kwanza”
Muda kidogo simu ya bibi Angel iliita basi aliipokea na kuongea nayo kw amuda kidogo, alivyokata alimuangalia mwanae na kusema,
“Jamani, watu wengine wana majaribu sana. Eti wananipigia leo kuwa kesho kuna kitchen party na mimi natakiwa nikaongee jamani, sasa nitaenda kuongea nini? Na nitajiandaa muda gani? Haya ni makwazo sasa”
“Mmmh mama jamani, hebu nenda tu. Itakuwa katika kufikiria huko wametambua kuwa kuna mama wa maadili hapa ndiomana wamekuita, wasamehe kw akukushtukiza tu ila nenda mama”
“Aaaah washanichanganya tayari, ukiwa unaondoka naomba mwambie yule dada msusi wa barabarani aje anisuke kama hana mteja leo”
“Mmmh utapendeza mama, hadi na kusukwa, sipati picha. Upige picha tu huko nije kuziona mie”
Basi Mage alimuaga mama yake na kuondoka zake, na bibi Angel alienda kumpa Angel taarifa hiyo ila ilikuwa ni furaha kwa Angel kwani hakupenda vile bibi yake anavyomchunga sana.
 
SEHEMU YA 293

Familia ya mama Angel waliporudi nyumbani, moja kwa moja walifikia kula chakula na kukaa huku wakitafakari mambo mbalimbali wakati huo Erick na Erica walienda kuandaa vitu vyao vizuri maana kesho yake ilikuwa ni shule zinafunguliwa.
Basi mama Angel alikuwa katulia tu na mgeni akafika pale kwao alikuwa ni Tumaini ambaye walianza kuongea nae,
“Naona leo hakuna umbea uliowaambia watoto”
“Mmmh wifi jamani, umbea gani mimi niliusema jamani!!”
“Haya, tuachane na hayo, jana nilikuwa nakuja hapa ila nikaambiwa hampo, nilikuwa na ujumbe wako”
“Ujumbe gani?”
“Kuna mwalimu mmoja hivi alikuwa akimfundisha Angel pale nyumbani kwangu anaitwa mama Sarah, sasa juzi nimekutana nae, sijui ikawaje nikakuongelea akasema anakufahamu sijui mlisoma wote”
“Mmmmh nani huyo?”
“Mimi simjui jina lake ila najua tu jina la mama Sarah, ila namba zake zile zingine kabadili ndio kanipa kadi yake nikuletee ili awasiliane na wewe, anasema kuwa ana mengi sana ya kuongea na wewe”
Basi Tumaini akatoa pochi yake ili aweze kutoa hiyo kadi ili amkabidhi mama Angel, ila alipekua na kushtuka kisha akajiuliza,
“Mbona hiyo kadi siioni tena”
“Kwani uliiweka wapi?”
Tumaini akatafakari kwa muda na kusema,
“Ooooh nimekumbuka, jana nilipokutana na Derrick aliniomba chenchi ya elfu kumi, nadhani wakati nampa ndio nikampa na kadi. Ila mmmh mbona na hela za kwenye hii pochi sizioni”
“Kwani ulikuwa na pesa ngapi?”
“Nilikuwa na laki moja kwenye pochi, naona hii elfu ishirini tu. Tatizo ni nini jamani!!”
“Kwani Derrick ulikutana nae wapi?”
“Nilikutana nae njiani wakati nakuja huku na ndiye aliyeniambia kuwa katoka huku pia ila hajawakuta”
Kengele ikalia kwenye kichwa cha mama Angel kuwa Derrick lazima kamtapeli hadi Tumaini, yani alishangaa sana kwa Derrick kumtapeli Tumaini wakati alikuwa ni mtu wake wa karibu sana, ila alisikitika na kushindwa kusema chochote kwa wakati ule ambapo Tumaini nae akaendelea kuongea,
“Jamani, jana sijafungua hii pochi muda mwingine wowote zaidi ya muda wa kumpa Derrick chenchi Derrick tu, inamaana nimekutana na chumaulete au?”
“Pole sana”
“Unajua sielewi, ngoja niende nyumbani kwangu”
Yani Tumaini akaondoka muda huo huo.
Basi mama Angel alienda kumueleza mumewe kuhusu tukio la Tumaini,
“Yani nahisi aliyewatapeli wakina Juma ni huyo huyo Derrick tu”
“Dah!! Huyo Derrick sasa ni tishio, bila kufanya kitu mapema itakuwa balaa, yani katoka kutapeli milioni tatu, halafu akaenda kutapeli elfu themanini dah!! Huyu Derrick amezidi sasa”
Baba Angel alitulia kimya kwa muda kwanza akifikiria ni kitu gani anweza kufanya ili kumuokoa Derrick kutokana na ile tabia aliyojiingiza nayo.

Usiku wa leo, Angel alikuwa akiwasiliana na Ally na kumwambia kuwa bibi yake kesho anaenda kwenye sherehe,
“Oooh hilo ni swala zuri sana kwangu, basi kesho nitakuja kukuona ili tuongee mawili matatu”
“Ila kama nilivyokwambia kuwa na mimi tutaongea kawaida tu, hakuna cha ngono”
“Mbona nimekubali hilo Angel, mimi nakupenda na nipo tayari kukusubiri hadi umalize shule. Shida yangu ni kuongea na wewe tu”
Angel alikubali, ila muda huo kulikuwa na jumbe kadhaa za kutoka kwa Samir, sema Angel hakujibu kabisa, basi Samir akatuma ujumbe mwingine,
“Angel umenichunia ila sijui kosa langu kwako, sema siwezi kuacha kukupenda, nitakulinda siku zote, siwezi kuacha huyo fedhuli aharibu maisha yako. Mtu mwenyewe dereva wa bajaji, hana hadhi yako Angel jamani. Mimi ndiye mwanaume ninayekuafaa, nakupenda sana”
Angel hakumjibu, ndio kwanza aliaendelea kuwasiliana na Ally kwani aliona Ally ni mwanaume mstaarabu sana na ni mwanaume anayesikiliza kwahiyo kwake ilikuwa ni vyema zaidi kuwasiliana na Ally.
Basi muda wa kulala ulipofika aliona ni vyema kulala tu, kuhusu hii simu mpya ya Angel aliyokuwa nayo, bibi yake hakujua kabisa swala hili maana ile nyingine alikuwa akiiona tu chumbani kama kawaida.

Kulipokucha, Erick na Erica walienda shuleni kama kawaida kwenye zile shule ambazo wanasoma, ila Erick alivyofika shuleni alipokelewa kwa shangwe kubwa sana na Sarah, yani Sarah alionekana kumfurahia sana Erick,
“Halafu nina zawadi yako”
“Mmmh zawadi gani?”
“Nitakupa tu hata usijali ila nitakupa kesho, sema nilikukumbuka sana Erick jamani!”
Erick alikuwa akicheka tu, na moja kwa moja alienda darasani ila Sarah nae alienda kwenye darasa lile lile alilosoma Erick na kumfanya Erick amuulize,
“Jamani Sarah, wewe si unaingia kidato cha tatu?”
“Unajua nini kilichotokea? Nitakwambia tu ila kwasasa jua kuwa tunasoma wote”
“Ulifeli?”
“Hapana, sijafeli na siwezi kufeli”
“Sasa kwanini imekuwa hivi!!”
“Siwezi kukaa mbali na wewe Erick, nipo tayari kurudia kidato”
“Kheee mambo gani haya, sijawahi kusikia katika maisha yangu jamani!!”
“Erick nawe jamani, mimi naweza kuendelea au kurudia ila ni wewe ndiye unayeweza fanya niendelee au nirudie”
“Kwahiyo unataka nifanye kitu gani?”
“Nitakwambia, usijali”
Kiukweli Erick alikuwa akimshangaa sana Sarah, alimuangalia tu bila kummaliza.

Bibi Angel alijiandaa na kuondoka zake, muda huu Angel alibaki nyumbani mwenyewe na muda kidogo tu akafika Ally kanakwamba alikuwa mahali akisubiri bibi Angel atoke tu, basi alifika ndani na kugonga kisha Angel akamkaribisha.
“Kheee umejuaje kuwa bibi kashaondoka?”
“Nimehisi tu Angel”
Basi aliingia ndani kwakina Angel na kumkumbatia Angel ila Angel alijitoa na kumwambia,
“Sio wakati sahihi wa kunikumbatia”
“Wakati sahihi ni upi mpenzi wangu?”
“Mmmh sipendi kukumbatiwa”
“Haya yaishe, nimekuletea tunda kama ishara ya upendo wangu kwako, naomba ung’ate kidogo tunda hili”
Basi angel alichukua lile tunda na kung’ata kidogo ila gafla alikuwa kama mtu aliyekunywa kilevi na kuanguka, basi Ally akamnyanyua ila wakati anataka kutoka naye tu alitokea Samir.

Basi angel alichukua lile tunda na kung’ata kidogo ila gafla alikuwa kama mtu aliyekunywa kilevi na kuanguka, basi Ally akamnyanyua ila wakati anataka kutoka naye tu alitokea Samir.
Ambaye hata hakuuliza na wakati huo huo kuanza kumshambulia Ally, ni alimpiga siku hii hadi Ally alianguka chini na kuanza kutoa damu puani, kisha Ally alijitahidi kuinuka na kumuacha Samir akimshughulikia Angel halafu yeye alitoka nje na kuondoka zake ingawa alikuwa kaumia vibaya sana maana Samir alimpiga hovyo hovyo bila kujali kitu chochote.
Kisha Samir, akamlaza Angel vizuri kwenye kiti huku akijaribu kumpa huduma ya kwanza,
“Umepatwa na nini Angel, amka mpenzi wangu.”
Samir alijitahidi pale huku akiwaza moyoni mwake,
“Kwani huyu kijana alitaka kumfanya nini Angel? Bibi yake Angel yuko wapi? Kwanini imekuwa hivi? Inamaana nisingetokea basi huyu kijana angekuwa kambaka Angel au? Kwanini Angel unaruhusu jambo kama hili katika maisha yako!”
Basi Samir alikaa pale na Angel huku akimsikilizia Angel aweze kuamka maana alikuwa kama mtu aliyelewa sana kiasi kwamba haelewi kinachoendelea na hata akishtuka anaongea kilevi na kuendelea kulala yani hapo ndio palimchanganya zaidi Samir.
Ukapita muda mrefu sana huku Samir akiwa amekaa huku kichwa cha Angel amekiegamizia kwenye miguu yake na kuwa kama akimbembeleza Angel aamke.
Muda huu mlango ukafunguliwa, na kuingia bibi yake Angel, kulikuwa na zile damu zilizoanguka toka kwa Ally chini, na kumfanya bibi yake Angel asielewe kitu kabisa, pale sebleni alivyomkuta Samir kamlaza Angel vile halafu kuna damu damu pembeni yao hakuelewa, alimuangalia Samir kwa gadhabu sana,
“Wewe mjinga, umebaka mjukuu wangu!”
“Hapana bibi”
Bibi alimuinua Samir na Angel kuachwa pale chini, yani bibi alikuwa na khasira sana kiasi kwamba alijikuta akichukua mwiko na banio jikoni kwake na vyote viliishia katika mwili wa Samir, ni alimpiga tena alimpiga sana na hakutaka hata kumuachia, kila Samir alipotaka kujitetea wala bibi hakuelewa jambo kwani yeye alipiga tu tena popote, na kumfanya Samir aanguke kisha akaenda kukanyaga mguu wa Samir na kufanya mguu ule uteguke, yani Samir akaona kuendelea kujitetea kwa huyo bibi ni kujitafutia balaa, basi akajikongoja na kufanikiwa kujiengua toka mikononi mwa yule bibi, yani bibi Angel alikuwa na hasira sana.
“Kambaka mjukuu wangu hadi kazimia!! Hivi Angel akipata mimba hapa nitasemaje mimi?”
Bibi akambeba Angel hadi chumbani kwake, akamvua nguo zote na kumkagua, akakuta mjukuu wake hakuingiliwa kimwili ni hiasia zake tu sababu aliona zile damu pale chini kwenye sebule yake na hakujua kuwa zile damu ni za kitu gani.
Basi akamchukua mjukuu wake na kwenda kumuogesha, alipofanya vile tu ikawa Angel karudiwa na ufahamu wake huku akishangaa kuwa ni kitu gani kimetokea, alishangaa kwa muda na kumuuliza bibi yake,
“Kwani nini bibi?”
“Aaaah sielewi, pia, wewe mtoto utaniua kwa presha. Hizo shule na zianze tu maana siwezi kwakweli”
Kisha bibi alimuacha Angel apumzike maana hata alipokuwa akimuuliza naye Angel alikuwa haelewi, basi bibi alimuacha na kwenda kufunga milango yake vizuri na kwenda kulala huku akitafakari kuwa ile hali sio hali ya kawaida kabisa kwake, yani kuna kitu kingine aliwaza, na kumfanya akose raha kabisa.

Kulipokucha, Angel anajifikiria pia kuwa ni kitu gani ambacho kimetokea ila hapati jibu yani kama kumbukumbu zake, zimefutika hivi. Mara akapokea ujumbe toka kwa Samir,
“Unaendeleaje Angel? Mimi naumwa sana mguu, unanivuta sana kutokana na kile kipigo nilichopata jana toka kwa bibi yako, ila bado nakupenda sana Angel”
Pale ndio Angel akashtuka kusikia kuwa Samir kapigwa sana, basi akamuuliza,
“Unajua Samir sielewi kitu, naomba nieleweshe kwani imekuwaje? Ulikuja muda gani huku kwetu hadi bibi akakupiga?”
“Ipo hivi Angel, mimi nilikaa nyumbani ila nilijiona nikikosa amani kabisa katika moyo wangu, nikasema lazima nije nikuone bila kuhofia uwepo wa bibi yako wala nini. Nimefika hapo kwenu na kukuta ni kimya sana, sijui ni kitu gani kilichoniambia kuwa niingie ndani kwenu bila kugonga sehemu yoyote, nikamkuta yule mwanaume wa siku ile ambaye alisema ni mpenzi wako kakubeba halafu hujitambui kabisa, sijui alitaka kukupeleka wapi ila mimi niliingiwa na hisia mbaya sana jumlisha na wivu, nilihisi alitaka kukubaka kwani alionekana kuwa na uchu sana na wewe, basi nilipata hasira sana na kuanza kumpiga hadi mwisho alikimbia, ukabaki wewe na mimi, nikajaribu kukuamsha wapi hukuamka wala nini kwahiyo nilikaa na wewe hapo sebleni kwenu. Nikijaribu kukubembeleza na kufanya kila ninachojua ili uamke, ndio akatokea bibi yako ambaye naye alinihisi vibaya, kwakweli kanipiga vibaya mno sijategemea kuwa huyu bibi ndio angenipiga kiasi hiki jamani!!”
“Kheee pole jamani Samir, pole sana”
“Asante, ila na wewe unaendeleaje?”
“Mimi naendelea vizuri kabisa, pole Samir na asante kwa kuniokoa”
Basi Angel aliwasiliana na Samir na kuonyesha kuwa anamuhurumia sana, ila kuna tukio la mwisho alilikumbuka, akakumbuka kuwa Ally alimpa tunda ambapo alipoling’ata tu alipatwa na usingizi wa ajabu, basi hapo akawaza kuwa huenda Ally kuna kitu aliweka kwenye lile tunda ndiomana lilimfanya vile, hakutaka kumtafuta Ally wala kuongea nae kuhusu kitu chochote kile.
 
SEHEMU YA 294

Leo, wakati Erick yupo darasani, Sarah nae alikuwa katika darasa lile kama jana yake tena alikuwa karibu kabisa na Erick, kwakweli Erick hakupenda kwani alijua wazi hata itakapofikia kwa dada yake yani Erica kuhamishiwa hapo basi hatopenda ule ukaribu wake na Sarah, kwahiyo akajaribu kuongea nae ili aende kwenye darasa lao kama kawaida,
“Sarah, niambie ni kitu gani unataka nifanye ili uweze kuendelea na kidato unachosoma?”
“Nahitaji uniambie kuwa unanipenda, basi nitaweza kusonga mbele maana mimi ninakupenda sana”
“Lakini Sarah, hivi unajijua kuwa wewe nib ado mdogo na hutakiwi kuwa na mawazo ya namna hiyo kabisa”
“Mimi sio mdogo, naweza kuwa mdogo wa umri ila sio mdogo wa mawazo na akili. Mama yangu ananifundisha kuwa halisi na kuishi maisha yenye uhalisia, kwahiyo siwezi kuwa kinyume na uhalisia, nakupenda tena sana na ninahitaji na wewe unipende vile vile.”
“Kwahiyo nikikwambia nakupenda ndio utaweza kuendelea na kidato cha tatu?”
“Ndio, naomba unipende Erick”
“Basi nakupenda, naomba uendelee na masomo yako, usifanye makosa ukaja kujutia milele”
Yani Sarah alihisi raha sana kuambiwa na Erick kuwa anapendwa, basi alimkumbatia kwafuraha na hapo akakubali kuondoka kwenda kwenye darasa lingine, ila Erick alikuwa akimshangaa sana, alishangaa mno kuwa Sarah anatoa wapi kiburi cha kufanya kile alichokuwa anakifanya, basi kuna mwanafunzi mmoja alimfata Erick na kumwambia,
“Unabahati sana ya kuongea na huyu binti?”
“Kwani huwa haongei?”
“Hapana, ila anachagua sana watu wa kuongea nao kutokana na kwao kuwa na hadhi”
“Kivipi?”
“Hii shule ni ya babu yake Sarah, halafu mama yake Sarah ni mtoto wa kipekee sana kwao na hivyo kuishi maisha Fulani na huyu Sarah ya kumdekeza sana, unavyomuona huyu Sarah hakuna mwalimu hata mmmoja anayemfokea wala kumpiga wala kumpa adhabu na ndio hivyo hivyo anavyoishi kwao, kwakweli unabahati sana. Nilikuwa nasikia maongezi yenu, una bahati sana ya kupendwa na huyu binti, kwanza ni mzuri, kwao wana hela, ana umbo zuri na mcheshi. Ukimuacha binti kama huyu basi kutakuwa na kitu unakitafuta”
Erick alimuangalia huyu mwanafunzi na kutokumjibu kwa muda huu kwani angeyajua mawazo ya Erick wala asingejisumbua kuongea maneno mengi vile kuhusu Sarah.

Baba Angel wakati anakamilisha kazi zake, akafuatwa ofisini na rafiki yake juma na kumkaribisha vizuri tu kisha akaanza kuongea nae,
“Karibu, na pole sana kwa yaliyokupata nyumbani kwangu”
“Dah!! Erick umenifanyia dhambi sana ni bora ungeniambia mapema kuwa haiwezekani kuliko kwa nililolipata nyumbani kwako. Ila cha kwanza kabisa, Erick mdogo anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri tu”
“Kwahiyo yupo kiwandani kwasasa?”
“Hapana, unajua shule zimefunguliwa nimeacha mwanangu aende shule, kiwandani atakuwa anaenda mara moja moja”
“Unajua kuna wakati unachekesha sana Erick, hivi unashindwa nini kufikiria lasilimali ambayo Mungu amekupatia? Ndio kwanza wiki hii wamefungua shule, mara nyingi huwa wiki hii haichanganyi sana na masomo, mimi nilijua utamuachia wiki hii kiwandani halafu wiki ijayo ndio aanze shule, ila hata angeanza shule bado kungekuwa na nafasi nzuri tu ya yeye kwenda kiwandani hata kukaa kwa nusu saa kiwandani ni jambo jema kwake. Usipoteze hiyo bahati”
“Juma sikia, mimi nawapenda sana wanangu. Najua mali zote nilizokuwa nazo bila elimu ni kazi bure, kwahiyo ni bora mwanangu apate elimu kwanza”
“Yani mimi ndio ningepata hazina hii basi Mungu anajua ni jinsi gani ningeitumia, haya elimu ni muhimu ngoja nikuulize ni kwanini watu wanasoma?”
“Ili kuondokana na ujinga”
Juma akacheka kwa muda na kusema,
“Ngoja nikwambie, nenda chuo chochote uliza hata watu kumi kwanini wanasoma. Asilimia kubwa watakwambia ili wapate kazi nzuri na walipwe vizuri badae, wengine watakwambia ilia pate heshima kuwa ni msomi. Hakuna anayesoma na kusubiri kukaa kukaa tu bila kazi, nenda kwa wasomi wasiokuwa na kazi utawakuta wapo kuilalamikia serikali, nimesoma lakini hakuna ajira, bora hata nisingesoma. Hakuna mtu anayepoteza muda wake shuleni halafu asipate kitu, kwahiyo tunasoma ili tupate kazi nzuri na kupata hela. Sasa Erick yupo vizuri kichwani, ana mawazo mazuri, kwanini bado unamng’ang’aniza na shule? Muache afanye maujuzi yake uingize kipato”
“Juma, nisikie kwanza, unajua mimi nilipoanza na mke wangu kipindi yeye kamaliza chuo na mimi nilikuwa na pesa sana, kiukweli niliumia sana moyo ni kweli nina pesa lakini mke wangu kanizidi elimu, sitaki jambo kama hili lijirudie kwa watoto wangu. Kuna kipindi mimi nilikuwa naendelea na biashara zangu huku najiendeleza kielimu, yani ukisoma akili inapevuka na unawaza mambo makubwa zaidi, ni kweli unaweza kuwa na mawazo mazuri ila yale mawazo yako yaongezee na elimu kwa hakika utayafurahia sana. Kwa upande wangu mimi bado elimu ni bora sana”
“Amakweli upele hukuota asiye na kucha”
“Hebu tuachane na hayo, haya niambie ulitapeliwa vipi milioni tatu?”
“Dah!! Yani hadi aibu, yule mtu alisema yeye ni mnajimu anashghulika na maswala ya nyota na kusema kuwa kwa siku ile nyota kwa upande wetu imekaa kimafanikio, na chochote nitakachotoa kwa nyota basi nitapata mara kumi sababu nyota ya siku hiyo kwa upande wangu ilikuwa katika asilimia kumi. Unajua mwanzoni nilikuwa na mashaka naye, ila akasema kama una elfu kumi hapo lete nikuonyeshe jinsi nyota itakachokujibu leo. Basi tukampa elfu kumi na akaiinua juu na kusema naomba nyota mtu huyu mjibu muda huu ya kuwa unatoa asilimia kumi, cha kushangaza kabisa kwenye mfuko wangu ikapatikana laki moja, kwenye mfuko ule niliotoa elfu kumi,kiukweli nilitamani sana. Ndipo tulipoamua kutoa ile milioni tatu ndani ya gari tukitarajia kupata milioni thelathini, aliuliza tunakaa wapi tukamtajia, basi akaichukua ile milioni tatu na kuipandisha juu akasema ewi milioni tatu sikia kwa nyota ya leo inayozalisha asilimia kumi basi naomba ukamzalishie huyu mtu aliyetoa kwa moyo wake. Wakifika tu nyumbani kwao basi hiyo milioni tehalathini ipatikane kwao, tulifurahi sana na pale alituambia tukae kama dakika tano ndio tuondoke, basi tulikaa pale dakika tano wakati yeye kaondoka ndipo na sisi tulipoondoka, tuliporudi nyumbani ndio tulijua kuwa tumetapeliwa maana haikuwepo milioni thelathini wala ile laki moja nayo haikuwepo”
“Dah!! Pole sana, huyo jamaa nadhani anatumia mazingaombwe. Nakumbuka kipindi kile shule ya msingi kuna majamaa walikuwa wanakuja shule mnachanga kiingilio kwenda kuwaangalia, basi mara wanaonyesha mtu kala ndizi moja halafu anaanza kujisaidia ndizi, au karatasi zinachanwa chanwa kwenye kopo halafu zinageuka na kuwa hela. Dah pole sana ndugu yangu jamani”
“Asante nashukuru, basi hayo ndio yaliyonipata hapo nyumbani kwako, ila ngoja niondoke kwa muda huu kuna mahari nataka kuwahi. Ila ndugu yangu itabidi unichangie nusu hasara”
“Ngoja nikajadiliane na mke wangu kuhusu hilo”
“Duh wewe jamaa yani, kila kitu nikajadiliane na mke wangu, ila hata mimi ningemuoa Baby nadhani ningekuwa hivyo hivyo. Kwaheri”
Basi Juma akaondoka zake na kumuacha baba Angel akiendelea na kazi zake zingine.

Baba Angel aliporudi nyumbani kwake anaamua kumueleza mkewe kuhusu kisa kilichompata Juma na mke wake hapo nyumbani kwao, kwakweli hata mama Angel anasikitika sana na kusema,
“Inamaana Derrick kafikia hiyo hali ya kutapeli kwa mazingaombo?”
“Ndio, unadhani bila mazingaombo atawapata wangapi wa kuwatapeli, lazima awadanganye kidogo ili wamuamini halafu awatapeli. Ila mke wangu huwa siku zote ndio inavyokuwaga ukitaka kupata pesa ya bure bila kuifanyia kazi ndio mambo kama haya unatapeliwa, yani wapi hapo unaweka milioni tatu unapata milioni thelatini jamani!! Tena ndani ya wiku moja, tamaa ndio inayofanywa tutapeliwe. Nadhani sasa utakubaliana na mimi”
“Ni kweli tamaa ila tamaa imeletwa na hali ngumu ya maisha”
“Hata kama, inatakiwa mtu ujiulize kwanza, yani naweka milioni tatu Napata milioni thelathini? Ipo siku atakutana nao tena na kuwaambia kuwa siku hiyo nyota inazalisha kwa asilimia mia moja, ukiweka milioni tatu unapata milioni mia tatu, na bado kuna watakaomuamini na kuwekeza kwake kwenye mazingaombwe. Kwakweli Mungu atusaidie tu. Watoto wanaendeleaje mke wangu?”
“Wapo salama, walienda shule vizuri na wamerudi vizuri”
“Erick alisema kwasasa yupo tayari kusoma na Erica, nimekosa tu muda wa kuwahamisha”
“Aaaah waaache hivi hivi hata usisumbuke, kama kusoma wanasoma tu vizuri hakuna tatizo, mimi naona ni vyema sana wanavyosoma hizi shule tofauti kumbuka Erica ni mbea sana anaweza akamkwaza kaka yake bure”
“Ngoja wakisema tena basi ndio nitalifanyia kazi ila kwasasa wacha niwaache tu wasomo walivyozoea.”
Kwa muda huo waliamua tu kulala kwani ilikuwa ni usiku tayari.
Kulipokucha tu, baba Angel anajiandaa zake kama kawaida mapema kabisa na kumuaga mke wake ila leo anamuuliza,
“Nikuletee zawadi gani?”
“Mmmh!! Niletee gauni”
“Ooooh umechagua gauni, basi hakuna tatizo nitakuletea mke wangu”
Basi anambusu na kuondoka zake, ila muda huu watoto nao ndio waliondoka kwenda shuleni, basi baba Angel alipotoa gari lake nje ya geti kuna mtu alimuona kajibanza pembezoni mwa ukuta wake, basi akatoka kwenye gari na kumfata mtu huyo akamkuta ni Sia,
“Una nini lakini wewe mwanamke? Ni kitu gani kinakuleta kuja kuchungulia nyumbani kwangu?”
“Naomba unisamehe bure tu”
Halafu leo Sia hakuongea maneno mengi kwani muda huo huo aliondoka zake na kuamuacha baba Angel akimuangalia tu huku akimsikitikia.

Leo madam Oliva, anaamua kwenda na Steve madukani ili kumfanyia manunuzi ya baadhi ya vitu kama nguo, na kweli walibahatika kupata walichokuwa wanakitaka, ila wakati wanaondoka walikutana na Dora ambaye alichukia sana na kuanza kusema,
“Hivi wewe Steve mdogo wangu akili yako lini itakuwa jamani!! Kwanini wanawake wanakuvuta na madawa kila siku, yani wewe umekuwa ni mtu wa kuvutwa na madawa tu kwanini lakini?”
“Sijavutwa na madawa mimi ila nimempenda mwenyewe, ni mimi ndiye niliyeanza kumpenda Oliva kwahiyo hayo madawa unayasema wewe”
“Kwahiyo unaona raha mwenyewe kwa hayo maisha ya kwenda kufanyiwa shopping na mwanamke wakati wewe ndio unatakiwa kufanya hivyo. Hivi unajiita mwanaume kweli kwa hali hiyo!”
Madam Oliva naye akaongea,
“Wifi jamani usiwe na jazba kiasi hiko, kaka yako akimpenda mtu unatakiwa na wewe kukubali sio kupinga tu muda wote, haya unapinga umemtafutia kaka yako mwanamke wa kuwa nae? Unajua mara nyingine unapinga ila fikiria maisha ya hao watu. Steve ananipenda na mimi nampenda kwani tagtizo liko wapi tukiwa pamoja? Tatizo liko wapi tukiamua kuoana? Yani unataka tu kukuza mambo ila haya ni mambo ya kawaida kabisa, acha kuwa na mawazo mgando ndugu yangu, wivu kidonda ukizidisha utakonda”
“Kwahiyo mimi nina wivu?”
“Acha hizo jamani wifi”
Kisha madam Oliva aliondoka na Steve na kwenda kupanda gari yao na kuondoka zao, kwakweli Dora alibaki akiwaangalia kwa gadhabu tu ila kuna kitu alifikiria na kusema,
“Sikumpenda James, ila niliamua kumkomesha sababu yeye alinikomesha kwa kunilewesha na kunibaka na kunikana kwa watu kuwa hawezi kuwa na mwanamke kama mimi. Nikaamua kumkomesha na kumuendea kwa mganga ambapo nilichukua dawa na kumuwekea, alipoitumia akanipenda sana kiasi hata mkewe alipotaka talaka ilikuwa jambo rahisi tu, na hadi mimi na yeye tuakaamua kuoana na hadi sasa nina mtoto naye, kwakweli haya mambo ni makubwa ila yanawezekana. Kiukweli nimeumia ila nadhani hata ndugu wa James kwa kipindi kile waliumia sana tu, inatakiwa sijui nifanyeje jamani. “
Aliongea kwa muda na kauamua kuondoka eneo lile.
 
Back
Top Bottom