Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 296

Erica alikuwa anakaribia kutoka shule, alifika rafiki yake Samia na kumsisitiza kuhusu Junior kumpatia yeye pesa,
“Mmmh Junior nae, ana tamaa sana yule halafu muhuni sana”
“Namjua vizuri yule kaka yako halafu mimi simpendi wala nini, yani simpendi kabisa”
“Tena uwe unamshushua kabisa”
“Ila nina ujumbe wangu huu naomba ukamkabidhi Erick”
Samia alimpa Erica ule ujumbe ambapo ulikuwa ndani ya bahasha, na juu ya bahasha hiyo iliandikwa Erick, basi Erica alikubali kuwa barua hiyo ataifikisha,
“Nitafurahi sana ukimpatia ujumbe wangu huo, halafu mwambie kuwa nasubiria barua kesho toka kwake kwahiyo atakuagiza wewe”
“Sawa, hakuna tatizo”
Erica aliiweka ile barua ila kiukweli alitamani sana kujua ni kitu gani kilikuwa kimeandikwa kwenye ile barua, alitamani sana afike nyumbani mapema ili aangalie kuna ujumbe gani.
Erica alipofika nyumbani tu, cha kwanza alienda chumbani kwake na kabla hata hajavua zile sare za shule alifungua kwanza ile barua na kuanza kuisoma,
“Kwako Erick, najua utastaajabu sana kwa hii barua yangu fupi, inawezekana si kawaida kwako kuambiwa na mwanamke neno nakupenda, kwakweli nimevumilia sana ila nimeshindwa, nakupenda sana Erick, nahitaji uwe mpenzi wangu. Tafadhari naomba unijibu”
Basi Erica alisoma mara mbilimbili na kusema,
“Kheee hivi huyu Samia ana wazimu au kitu gani? Yani kabisa kaka chini na kuandika barua kama hii kwa Erick jamani!! Sasa ngoja nimjibu, mjinga kabisa huyu msichana”
Akachukua peni na karatasi na kuanza kuandika jibu kwa Samia, ila alijifikiria na kusema,
“Ila Samia atasema mbona muandiko sio wangu?”
“Ngoja nikampelekee Erick mwenyewe aamue mwenyewe, akikubali tu basi nauvunja undugu leo”
Akatoka chumbani kwake na moja kwa moja akaingia chumbani kwa Erick ambapo alikuwa akibadilisha nguo, yeye mwenyewe Erica alipoingia alishtuka na kumwambia
“Jifunike jamani Erick”
“Na wewe kwanini unapenda kuingia chumbani kwangu bila hodi!”
“Mmmh yani hadi mimi nigonge hodi jamani!! Sijazoea hayo”
Basi Erick alijifunga taulo na kukaa ili kusikiliza ujumbe ambao umeletwa na Erica,
“Samahani, Samia kanipa barua yako ila sijaweza kuvumilia nimeifungua na kuisoma ndio nimekuletea, naomba nisamehe”
“Ingekuwa siijui tabia yako ya umbea sawa, ila naijua fika tabia yako”
“Jamani Erick, ndio maneno gani hayo!!”
Erick alichukua ile barua na kusoma ule ujumbe, alisikitika sana na kumuangalia Erica kisha akamuuliza,
“Nishauri nimuandikie jibu gani?”
“Sina ushauri ila usirogwe kukubali maana leo nitavunja undugu baina yetu”
“Kwanini sasa?”
“Kwanini!! Inamaana umesahau ahadi yetu au!!”
“Ahadi yetu naikumbuka, ni kuwa nisiwe na rafiki wa kike na wewe usiwe na rafiki wa kiume, haya huyu sio rafiki anaomba kuwa mpenzi. Kwani wewe unaweza kuwa mpenzi wangu?”
Erica alichukia kwa swali hilo, aliinuka na kuondoka zake na kumfanya Erick ajue kuwa amemkera kwa swali alilomuuliza.

Baba Angel leo wakati anarudi nyumbani kwake, alimuona Derrick njiani, tena akiwa amesimama na mtu yani hapo akili ikamcheza kuwa Derrick anataka kumliza mtu huyo, basi akasimamisha gari, akashuka na kumfata karibu halafu akamuita yani Derrick alishtuka kama mtu aliyeshtuliwa toka usingizini kiasi kwamba hata hakuweza kuongea tena na yule mtu ila Erick alimvuta mkono pembeni na kuongea nae,
“Derrick, hiki unachokifanya sio kabisa na kitakupeleka pabaya”
“Najua ushasikia vingi kuhusu mimi, hata wewe unaweza kuwa mmoja kati ya watu wanaonichukia”
“Sikuchukii kabisa, na nikuchukie kwasababu ipi? Naomba twende mahali tuongee kidogo”
Basi wakapanda kwenye gari, na kweli walishuka mahali na kupata sehemu nzuri na kukaa kisha kuanza mazungumzo ya hapa na pale,
“Kwanza kabisa Derrick ni kitu gani kikubwa kinakusumbua?”
“Sijui nikuelezeje upate kunielewa, ni hivi katika dunia mimi ni kiumbe nisiyekuwa na bahati kabisa”
“Huna bahati kivipi?”
“Kwanza kabisa, mimi nimeanza kukataliwa toka nipo tumboni mwa mama yangu, nimezaliwa sijapata mapenzi ya baba kabisa, nimepelekwa nyumbani kwa baba nasikia tukatimuliwa, toka hapo ndugu wa baba hawanipendi ni wachache tu wanaonaoniona kama mmoja wa familia yao. Nimekazana nitoke kimaisha, mama yangu kapata tabu ya kunisomesha na kweli nimefika chuo, nimehangaika kupata kazi, nikapata kazi ila hiyo kazi nimefukuzwa, hivi ni maisha gani nitakayoishi mimi? Kwanini dunia inanifanya hivi!! Ndiomana nikaamua nichague aina nyingine ya maisha kwani hata mimi natamani nimuhudumie mama yangu, nae aishi vizuri na ashukuru kunizaa”
“Unajua Derrick umekata tamaa mapema sana, yani elimu yako hupendezi kabisa kufanya kazi ya kitapeli, hivi kweli umetafuta kazi kote imeshindikana? Kuna siku hata umewahi kuja kwangu na kusema shemeji nisaidie angalau nipate kazi?”
“Hivi nakuja vipi kwako ikiwa mkeo ambaye nina undugu nae, hataki hata kuniona. Yani mimi sijui ni gundu sijui ni kitu gani. Katika maisha yangu ni kweli nilikuwa muhuni sana ila hakuna kitu ambacho sikupenda kama kutoa mimba, ila kuna mwanamke aliivuruga akili yangu kwa kutoa mimba yangu, huyu alikuwa ni mwanamke wa kwanza kumpa mimba na alikuwa wa kwanza kuitoa mimba yangu, kiukweli aliivuruga sana akili yangu, toka hapo huwa nahisi akili ikiwehuka tu. Kuna mwanamke nimezaa nae, na siku zote najua mtoto ni wangu kumbe mtoto mwenyewe katupa mababa wawili, yani wanawake jamani dah!! Ameona sieleweki ndio anasema yule mtoto sio wako, nimeumia sana, ila najua yule ni mwanangu ila tu sababu wanawake wanaangalia sehemu yenye maslahi zaidi”
“Kwahiyo huyo mtoto yuko wapi?”
“Najua basi, yule mwanamke alihama na watoto wake, roho iliniuma sana kila siku naenda kumlilia mwanangu, nilimpa jina la mama yangu ila yeye kampa jina lake analolijua mwenyewe. Yote hii sababu sijapata maslahi tu”
“Toka uanze kutapeli hujapata maslahi tu!!”
“Sijui ni kitu gani, sijui ni laana sijui ni nini. Yani mimi huwa natapeli hela za maana ila hakuna kitu cha maana ninachofanya”
“Unapotea ndugu yangu, yani unapotea kabisa. Kiukweli Erica kanibadilisha mimi ila ilikuwa rahisi sababu na mimi niliona ile njia niliyokuwa napita haikuwa njia sahihi kwa mimi kuendelea nayo, unajua kuna vitu vingine badala vikuendeleze vinakutia umasikini tu, unapata pesa ya laana kwa uongo ila pesa hiyo hiyo unayopata unaenda kumalizia kwa wanawake, haya hayo maendeleo utayatoa wapi?”
“Ni kweli kabisa, ila hii laana imeletwa na yule mwanamke aliyetoa mimba yangu”
“Basi achana na hayo, kama upo tayari naomba kesho niache mambo yangu nikupeleke kwenye maombia. Upo tayari?”
“Mmmmh!!”
“Nini sasa Derrick?”
“Utanipeleka kwenye maombi, utanipa na kazi? Maana hata niombewe na wachungaji wote duniani, na mshekhe nao waungane wote, ila kama sina kazi mwendo utakuwa ni huu huu wa kutapeli tu”
“Dah!! Yani wewe jamani!! Nitakupatia na kazi, ila sasa huwezi kufanya kazi vizuri kama hujaamua kuacha kabisa haya unayoyafanya”
Basi wakakubaliana pale kuwa wataonana kesho yake ili kuweza kuzungumza na kwenda huko kwenye maombi.
 
SEHEMU YA 297

Baba Angel leo aliporudi nyumbani kwake hakumwambia mkewe swala la yeye kuonana na Derrick kwani alijua wazi kuwa mkewe hawezi kukubali swala la kuongozana na Derrick kutokana na mambo ambayo Derrick huwa anayafanya.
Basi baba Angel alienda kuoga, muda huu mama Angel alipigiwa simu na dada yake Bite na kupokea,
“Erica, nipigie”
Simu ikakatika, mama Angel alipotaka kupiga akagundua kuwa simu yake haina salio, basi akachukua simu ya mume wake ili kupigia dada yake, ila alipoichukua tu simu ya mumewe kuna ujumbe uliingia katia simu ile,
“Erick, asante sana kwa hii pesa uliyonipa. Mtoto wetu Elly hajambo na muda huu ameshalala, anawaza masomo yake tu. Kumbuka nakupenda sana, by Sia”
Mama Angel alisoma ule ujumbe mara mbilimbili na aliona ukimuumiza tu, basi aliufuta na hata kumpigia simu dada yake hakumpigia tena kwani alishakuwa na hasira kwa muda huo.
Basi mumewe alivyotoka bafuni wala hakumwambia kitu chochote zaidi ya kuendelea na mambo mengine ila moyo ulikuwa ukimuuma sana ikabidi aulize tu maana alishindwa kuvumilia,
“Mara ya mwisho kuonana na Sia ilikuwa ni lini?”
Baba Angel akahisi tu kuna kitu ambacho mkewe lazima kawa na mashaka nacho, basi akaamua kumueleza vile ilivyokuwa jinsi Sia alivyomkimbia Juma na jinsi Juma alivyomueleza, na jinsi yeye alivyoenda kutafuta ukweli kwa Sia,
“Ni hivyo mke wangu, hakuna lingine zaidi ya hayo”
“Sawa, nimekuelewa, napenda sana vile unavyokuwa muwazi kwangu”
“Nisipokuwa muwazi kwako nitakuwa muwazi kwa mtu gani sasa? Mimi nakupenda mke wangu na daima itabaki hivyo”
Mama Angel alifurahi sana na kwa muda huo hakulala na kinyongo tena.

Asubuhi wakati wamejiandaa kwenda shuleni, ndipo Erick alipompa Erica karatasi na kusema ni jibu la Samia, basi Erica alilichukua na kuliweka kwenye begi, basi alipoingia kwenye gari la shule tu akaifunua ile karatasi ndani ya begi na kusoma, iliandikwa kwa maneno machache sana,
“SIKUTAKI, by Erick”
Erica alitabasamu na kuchekelea sana jibu lile kisha akafunga vizuri ile karatasi na alipofika shuleni tu alimkabidhi Samia, ambaye alimuuliza kwanza,
“Ila Erick alikuwaje baada ya kuona ile barua yangu?”
“Sijui, maana mimi huwa sifatilii mambo yasiyonihusu”
“Mmmmh hata huu ujumbe hujasoma?”
“Kwanza kanipa asubuhi hii, niliweka kwenye begi moja kwa moja, sijui hata kaandika nini na yeye”
Samia hakusoma kwani na yeye moja kwa moja akaweka kwenye begi lake na kumtaka Erica waende darasani,
“Kheee mbona hujasoma?”
“Nitasoma mwenyewe tu”
Basi wakaenda darasani ila ukweli wa ile barua alikuwa anafahamu kila kitu kilichoandikwa humo ila akajifanya tu hafahamu chochote kile.
Baada ya vipindi kuisha, Erica na Samia waliagana halafu kila mmoja aliondoka kwani walikuwa wakipanda gari tofauti za shule.

Erick wakati wamepanda gari ya kuelekea nyumbani, kama kawaida Sarah alienda na kukaa karibu yake huku akiongea nae mambo mbalimbali,
“Kwahiyo kwasasa Erick wewe ni mpenzi wangu”
Erick alikaa kimya tu, kisha Sarah akaendelea kusema,
“Kuna zawadi nimekuletea Erick”
“Zawadi gani?”
“Ila nataka umpelekee mama yako”
“Mmmmh!! Nini tena?”
Basi Sarah alitoa mfuko kwenye begi lake na kumkabidhi Erick ambaye aliuweka vizuri tu, kisha Erick alimuuliza Sarah,
“Kwani ni kitu gani hiki?”
“Ni zawadi tu lakini ya mama yako, yani mama mkwe wangu”
“Mmmh!!”
“Unaguna nini jamani Erick, mimi nakupenda tena nakupenda sana. Nahitaji kuwa pamoja na wewe hadi mwisho wa maisha yani wewe pekee ndio uje kuwa mume wangu, nipo tayari kufanya chochote na wewe”
Kwakweli Erick hakuwa na kitu cha kusema, na kwa wakati huo alifika kwao na kushuka.
Moja kwa moja Erick alipoingia ndani tu alimkuta mama yake yupo sebleni akamsalimia na kumwambia,
“Mama, kuna zawadi yako nimepewa na Sarah nikuletee”
“Oooh jamani Sarah, nimemkumbuka sana sijui lini atakuja tena kuniona jamani, dah binti ana roho ya upendo sana”
Kisha Erick alitoa ule mfuko na kumkabidhi mama yake, ambaye alishukuru sana halafu Erick alienda zake chumbani kwake kubadilisha sare zake za shule na kuoga.

Baba Angel alitoka kwenye kazi yake na kupitia kiwandani, sababu aliwasiliana na Derrick ila hakuweza kumpata hewani kwahiyo aliamua tu kwenda kwenye kiwanda chake ili aangalie maendeleo ya kile kiwanda, alikuta kipo kawaida tu basi akamuita ambaye huwa anasimamia pale na kumuuliza,
“Eeeh shughuli zinakwendaje hapa”
“Ziko vizuri tu, ila yule kijana wako alikuwa hatari sana”
“Hebu niambie kwanza”
“Yule kijana wako akija hapa kiwandani kama mwezi hivi basi tena!! Yani mambo yatanyooka hatari, ila tatizo lake hali chakula cha hapa sijui kwanini”
“Aaaah yule hajazoea kula mbali na nyumbani”
“Basi kama utaweza, kuna kuwa na mtu maalum wa kumletea chakula, nakwambia baada ya mwezi utafurahi na roho yako”
“Dah!! Hapo ni mpaka shule zifungwe, mwanangu anasoma siwezi kumkatishia masomo sababu ya biashara zangu, ngoja nitavumilia tu. Ila siku hizi nitakuwa nakuja kila siku mimi mwenyewe”
Wakaongea pale, kisha baba Angel akatembelea biashara yake kwa uzuri kabisa na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake, ila njiani gari lake lilisimamishwa na aliyesimamisha alikuwa ni Juma basi akasimama halafu Juma akapanda na kumwambia,
“Bila shaka unaelekea nyumbani kwako!!”
“Ndio, naelekea nyumbani kwangu”
“Basi twende wote, yani nilipoona gari lako linapita nimejikuta tu namkumbuka kijana wako Erick natamani sana kumuona”
Kiukweli baba Angel alianza kuwa na mashaka na rafiki yake Juma kwahiyo hakutaka huyu Juma kuwa na ukaribu na mtoto wake yoyote yule, basi akaamua kumdanganya tu kwa muda huo,
“Aaaah unajua watoto wangu hii wiki ya kufungua shule wanatokea kwa bibi yao”
“Kheee bibi yao yupi?”
“Yule mama wa mama yao yani mama mkwe wangu, kwahiyo watoto wote wapo huko sie tunalea tu kichanga chetu”
“Dah!! Nilitaka kwenda kumuona Erick ila basi tena, utaniambia siku watakayorudi. Utanishusha mbele tu hapo”
Basi waliendelea na maongezi mengine hadi alipofika anaposhuka, yani baba Angel alipumua kidogo ila bado hakumuelewa rafiki yake kwanini anataka ukaribu ule na mtoto wake!! Alikosa jibu kabisa yani.
 
SEHEMU YA 298

Mama Angel alikuwa ndani akiitathimini zawadi ambayo amepewa na Sarah, basi aliangalia na kusema,
“Yani huyu mtoto kama alikaa katika akili yangu, sijui kafikiria nini kunipa zawadi kama hii jamani maana nilikuwa nafikiria sana kwenda kununua hiki kitu na mimi nitamshtukiza mume wangu kwa zawadi pia itakayotokana na hii”
Kisha akaweka ile zawadi yake vizuri na kwenda chumbani kwa Erick ambapo alimkuta amekaa tu akiandika kwa muda huo,
“Oooh mwanangu unajisomea, vizuri sana. Ila mwambie Sarah nimefurahia sana zawadi yake, yani ni binti mwenye upeo wa hali ya juu”
“Sawa mama nitamwambia”
“Unajua ni zawadi gani amenipa?”
“Sijui!”
“Sasa mbona hujaniuliza? Yani wewe!! Angekuwa Erica basi kitambo tu kashajua ni zawadi gani nimepewa mama yake. Amenipa zawadi ya kitenge, ni kitenge kizuri hicho, kina rangi nzuri sana, nitakuosha nikiwa naenda kukishona”
Erick alitabasamu tu kisha mama yake alimtakia kujisomea kwema halafu yeye aliondoka na kwenda chumbani kwake.
Muda huu baba Angel nae alikuwa amewasili basi waliongea mengi ambapo alimueleza pia kuhusu rafiki yake Juma kuulizia kuhusu mtoto wao,
“Mmmh usimuamini sana huyo mtu mume wangu, kwanza ameweza kuishi na Johari jua kuna tabia kafanana na Johari, kumbuka Johari ni rafiki yangu ila alikuwa ni chanzo kikubwa cha mimi na wewe kuwa mbalimbali na kuchukiana”
“Nakumbuka”
“Kwahiyo Juma, inawezekana hata akatumwa na mke wake, sio wa kuwaamini sana wale”
“Ni kweli, sitaki kuwaamini sana, ni vile vile kama ambavyo huwa simuamini Dora ingawa anadai kabadilika kwa asilimia kubwa ila bado huwa nashindwa kumuamini moja kwa moja”
Wakaongea ongea na muda huo waliamua tu kulala maana hapakuwa na jambo lingine la kufanya ila bado baba Angel hakumwambia mkewe kile alichoongea na Derrick.

Nyumbani kwakina Samia, siku hii Samia hakwenda shuleni alikuwa kajikalia nje huku akilia, basi mama yake alimuona na kwenda kumuuliza,
“Tatizo nini Samia?”
“Mama, kuna mwanaume nampenda sana halafu yeye kaniambia hanitaki”
Huyu mama alikaa chini kwani alijua mwanae atakuwa na matatizo ya kisaikolojia, kwahiyo aliamua kuongea nae kwa utaratibu,
“Samia, umeanza lini hayo mambo ya kupenda wanaume jamani!!”
“Mama, sio kosa langu nimejaribu kuvumilia ila nimeshindwa, nampenda sana”
“Kwahiyo leo hujaenda shule kwasababu hiyo?”
“Ndio mama, nampenda sana sijui nifanyeje”
“Pole mwanangu, ila inabidi nikupe darasa la kutosha kuhusu mapenzi na akili yako ikae sawa.”
Samia akampa mama yake na lile karatasi ambalo kaandikiwa na Erick kuwa hatakiwi, basi mama yake akalichukua na kulisoma, kisha akainuka kwa gadhabu kubwa sana na kumuuliza Samia kwa ukali,
“Kwahiyo huyo mwanaume anaitwa Erick?”
“Ndio mama, anaitwa Erick”
Mama Samia alizidi kupandwa na hasira kiasi kwamba, alianza kumpiga mwanae tena alimpiga hovyo hovyo hadi Samia akazimia.

Samia akampa mama yake na lile karatasi ambalo kaandikiwa na Erick kuwa hatakiwi, basi mama yake akalichukua na kulisoma, kisha akainuka kwa gadhabu kubwa sana na kumuuliza Samia kwa ukali,
“Kwahiyo huyo mwanaume anaitwa Erick?”
“Ndio mama, anaitwa Erick”
Mama Samia alizidi kupandwa na hasira kiasi kwamba, alianza kumpiga mwanae tena alimpiga hovyo hovyo hadi Samia akazimia.
Ila huyu mama hakuonyesha kujali wala nini ila alionekana kuwa na hasira zilizopitiliza, basi alitokea Samir na kumuuliza mama yake kinachomfanya kuwa na hasira kiasi kile,
“Kwani kuna nini mama?”
Kisha Samir akainama kama kumuamsha mdogo wake, ila mama yake akasema,
“Achana nae huyo ataamka mwenyewe”
“Khee mama, kamavile hujatuzaa wewe!! Kama vile hukutuzaa wawili tu kama mboni za macho yako!! Siku zote mama ndio mwenye uchungu na watoto wake tofauti na baba, hivi usipotujali wewe unadhani ni nani atatujali? Usipotupenda wewe ni nani atatupenda? Angalia baba ana watoto kibao, na kiukweli hakuna anayempenda sababu ni wengi mno kwahiyo wote anatuona kawaida, ila wewe ndiye mama yetu, ndiye pekee tuliyebakiwa nae, na wewe hutupendi tena kweli!! Tutakuwa wageni wa nani sisi?”
Haya maneno yalionekana kumuingia sana mama yao, ambaye alikaa chini na kujikuta akianza kulia tena akilia kwa uchungu mpaka Samir ikabidi amfate sasa mama yake, muda huu hata Samia alikuwa kazinduka, kwahiyo Samir alimuingiza Samia ndani na mama yao aliingia ndani kisha alianza kuongea nae,
“Kwani mama tatizo ni nini?”
“Unajua mdogo wako kaanza tabia mbaya, kaanza tabia ya kupenda wanaume, unajua ni mdogo sana huyu kufanya huo ujinga!! Nilitaka kukaa na echini ili nianze kumueleimisha, ila kilichonichefua zaidi ni hilo jina la mwanaume anayemtaka”
“Kheee jina gani mama?”
“Muulize mwenyewe, si huyo hapo”
Samia alijibu huku kajiinamia chini,
“Anaitwa Erick”
“Kheee kwahiyo mama, tatizo sio Samia kuanza tabia ya wanaume ila tatizo ni hilo jina la Erick!!”
“Ndio, sitaki kulisikia hilo jina katika nyumba yangu hii, halafu wewe Samia hayo mambo ya kupenda wanaume umeanza lini? Mbona hukuwa hivyo wewe!!”
Samir akajibu,
“Huyu naona kichwa chake kinaharibiwa na mawazo anayopewa na baba, maana baba ndio anamwambia aombe hela kwa wanaume”
“Oooh jamani, huyu mwanaume huyu loh anataka kuniharibia watoto tu kama yeye alivyoharibika, haya nipeni presha kwahiyo na wewe Samir unampenda nani?”
“Kuna mdada nampenda sana anaitwa Angel”
“Kheee kumbe na wewe tayari, jamani nyie watoto vipi jamani. Haya hiyo Angel na wewe ni vipi? Mnajua msinichanganye kabisa akili yangu, hebu watoto nyie mkue katika misingi imara, nawafundisha mambo mbalimbali halafu mnafanya ujinga, haya wewe Samia unampenda mtu anaitwa Erick unataka nini katika maisha yako? Unaakili kuwa kuna ndoa hapo kati yako na huyo kiumbe? Na wewe Samir huna hata aibu unampenda mwanamke anaitwa Angel, aaah jamani nyie watoto msifanye nijute kuwazaa jamani.”
“Ila mama kwani mimi kuwa na Angel kuna ubaya gani jamani, nampenda na yeye ananipenda”
“Haya, ubini wa huyo Angel ni nani?”
“Anaitwa Angel Erick”
“Ptuuuu nishasema sitaki kusikia hilo jina hapa nyumbani kwanfu, nyie watoto nadhani hamnijui vizuri mie mama yenu ila dawa tenu inachemka jikoni”
Basi mama yao aliinuka na kuondoka zake ilionyesha ni jinsi gani hilo jina la Erick lilimtia hasira sana.
Ila muda huo huo baba yao nae alirudi na kuwakuta watoto wake sebleni wakiwa wamejikunyata, ila huyu baba huwa anampenda sana Samia, kwahiyo alisogea karibu na kumuuliza,
“Tatizo nini mwanangu?”
Samir alijibu,
“Tatizo Erick”
Baba yao akashtuka sana,
“Erick!! Hilo jina limekuja vipi nyumbani kwangu humu?”
“Mama kampiga Samia sababu Samia anampenda kijana mmoja aitwae Erick, mama kasema hataki kusikia hilo jina humu ndani”
“Ila jamani watoto wangu hata mimi msije kunitajia hilo jina tafadhari, yani watu wenye majina hayo huwa hawana ubinadamu kabisa, wana roho mbaya kama za wanyama. Sikieni watoto wangu, mimi huwa nawafundisha yaliyomema na mazuri, hebu achaneni na hao vichwa panzi. Haya msisononeke wala msihuzuke sababu ya mama yenu kuwapiga sijui kuwafanya nini badala yake nendeni mkajiandae halafu twende tukatembee maeneo huko”
Basi baba yao akaenda zake ndani ila hakuongea chochote wala kumuuliza chochote mke wake kwani ndio walikuwa na utaratibu huo kwa siku zote.
 
SEHEMU YA 299

Baba Angel alikuwa akiendelea na kazi zake mbalimbali ila leo alifatwa ofisini na madam Oliva, akahisi ndio mambo yale yale anataka kuyaanza tena madam Oliva, ila leo alikuja na ujumbe mpya, baada tu ya salamu alianza kuongea na baba Angel,
“Hivi mtoto wenu Angel mmemlea vipi?”
“Kivipi?”
“Unajua binti yule bado mdogo sana, kwa mila zetu za kiafrika yule binti bado mdogo jamani. Sio wa kuanza kugombewa na wanaume”
“Kugombewa na wanaume!! Kivipi? Sikuelewi”
“Sikia nikwambie, kuna siku nilikuwa naende kwenye mizunguko yangu, nikamuona Angel mahali akiwa amesimama na mwanaume, ile sehemu ilikuwa ni kwa fundi simu, mara alitokea kijana mwingine na gafla alianza kumpiga yule kijana hadi chini sikuelewa kitu pale ila Angel aliongea ongea na yule kijana alionekana kumpigia magoti kama kumuomba msamaha ila gafla yule kijana mwingine na Angel wakaondoka, wakapanda bajaji wakaenda zao. Nilienda kuuliza imekuwaje ndio nikasikia kuwa wale vijana walikuwa wakimgombea Angel, kwakweli kama mzazi nimeumia sana sijajisikia vizuri kabisa yani. Angel katika lile rika lake sio sawa kuanza kugombewa na wanaume”
“Unajua sikuyajua hayo kwakweli, Angel yupo kwa bibi yake, amewezaje kutoka na kwenda kukutana na mwanaume!! Ni kweli haya mambo yanasikitisha sana, hata mimi kama mzazi wake sijapenda kwakweli ila madam una uhakika ni Angel?”
“Hivi mimi nije kumsingizia Angel ili nipate faida gani? Au nije niseme wakati sio Angel niliyemuona ili iweje sasa? Siwezi kufanya kitu cha namna hjiyo, nimekuja kukwambia kuhusu Angel sababu ni Angel niliyemuona, na mimi kama mzazi nimeumia ndiomana nimekuja kukwambia”
“Haya mwalimu, unashauri nini kifanyike sasa?”
“Cha kuwashauri, shule ambaye utampeleka Angel kidato cha tano mpeleke shule ya misheni yani zile shule zenye muongozo wa kidini halafu umuache chini ya uangalizi wa masister, muokoe mwanao, msaidie kwasasa maana ni wengi watamsifia kuwa mzuri ila hawana lengo zuri na maisha yake, kwahiyo ni bora kumuweka makini mapema sana”
“Nashukuru kwa ushauri wako madam, una ushauri mzuri ila na mimi ngoja nikuambie jambo. Naomba mpe uhuru Steve, imezidi sasa, yani hadi namuhurumia, mpe uhuru wake, ebu muache akupende mwenyewe ndio upendo wenye raha ila sio huo upendo wa kufugana ndani, mpe uhuru wake”
“Nimekusikia”
“Nawaza, ingekuwaje ndio ungenipata mimi, wewe mwanamke sio mzuri ujue, yani familia yangu sijui ingekuwa kwenye wakati gani. Samahani nimewaza kwa sauti”
Madam Oliva aliinuka na kuondoka zake, tena siku hii hakuaga inaonyesha maneno ya mwisho ya baba Angel yalimuingia vizuri kwenye akili yake.

Mama Angel akiwa nyumbani leo huku akiendelea na mambo mengine alipata ugeni ambao hakuutarajia kabisa, alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana aliyeitwa Johari, basi alimkaribisha sana na kuanza kuongea nae,
“Kheee Johari jamani, leo umekuja kwangu!”
“Ndio, unajua nimekukumbuka sana shoga yangu, ni kweli mengi sana yamepita baina yetu kiasi cha kufanya tusiwe na ukaribu vizuri ila kiukweli nimekukumbuka sana”
“Karibu sana”
“Na wewe karibu sana nyumbani kwangu, mumeo anapajua ni wapi naishi na mume wangu. Siku ile tumekuja hatujawakuta mimi nikasema hakuna tatizo cha msingi nimepajua nikaona basi nitafunga safari tu mwenyewe na kuja kukutembelea”
“Karibu sana, kuwa huru rafiki yangu”
“Eeeh saivi una watoto wangapi mwenzangu?”
“Wanne, yule wakwanza Angel, wapili ni mapacha kuna Erick na Erica na wa tatu ni huyu wa mikononi”
“Oooh, mimi ninao watano kwasasa, nimekuzidi mmoja”
Wote wakacheka na kuendelea na mazungumzo mengine,
“Kwahiyo watoto wako wote upo nao?”
“Mmmmh mwenzangu unafikiri maisha ya kutangatanga nayo ni maisha!! Wanawake tuna siri nyingi sana ni Mungu tu anatufichia hizi siri tulizokuwa nazo na vifua vyetu, kwa kifupi nina watoto sita ila yule mkubwa alichukuliwa na baba yake yule mwalimu kwahiyo anaishi na baba yake”
“Inamaanisha huyo mtoto mumeo hamjui?”
“Anamjua ila kuna siri nyingi tu wee acha tu”
“Mmmh Johari jamani hujaacha kwani kuhangaika jamani! Si ulisema umeridhika na mumeo wewe?”
“Nadhani Erica hunielewi, ni kwamba wanawake tuna siri nyingi sana, nina ndugu yangu kaolewa na ana watoto ila wale watoto hata sio wa mume wake, tena kila mtoto ana baba yake, ila mumewe hajui kitu yani anajua watoto ni wake, huwa ananiambia Johari naomba nisife mapema maana kufa na siri hizi naona nitaenda kuchomwa moto”
Johari akacheka, kisha mama Angel akamwambia,
“Ila sio vizuri hivyo, hajamfanyia sawa mume wake, angemwambia ukweli tu”
“Wewe unaweza kumwambia ukweli mumeo kuhusu kila kitu! Kuna vitu mtu huna namna ni lazima umdanganye tu mumeo, unadhani aseme ukweli halafu aende wapi na watoto? Atawaeleza nini wakati wamekuwa wakijua yule ni baba yao? Yani unakufa na tai shingoni shoga yangu”
“Mmmh jamani siwezi kumficha mume wangu kitu cha namna hiyo, kwahiyo wewe unaweza mficha mumeo kitu cha namna hiyo?”
“Erica hujui tu wanaume nao wana siri hao halafu wanamaudhi hatari kwahiyo huwa tunavumiliana tu maana ndio misingi ya ndoa ilivyo ni kuvumiliana”
“Ni kweli kuna kuvumiliana ila usiwe tena na mambo ya kusaliti ndoa yako, ujinga ni zamani, mtu ukiamua kutulia unatulia moja kwa moja”
“Haya, kilichonileta kwako ni wewe unipatie mawazo mbalimbali ya biashara, nahitaji kufanya biashara ila mtu wa kunishika mkono ndio sijampata”
“Sawa hakuna tatizo, kama una muda kesho kutwa nitafute ili nikupeleke mahali, utafurahi kwa wazo utakalolipata huko”
“Ila usimwambie mume wangu, nataka nifanye mwenyewe yani mume wangu asielewe kitu chochote”
“Kheee Johari hadi kuhusu biashara unamficha mumeo!”
“Shauri yako wewe, kuwa mjinga tu mwambie mwanaume kila kitu ila atakapokugeuka atakuacha mtupu kabisa, mwanaume sio ndugu yako, sio baba yako wala mama yako, usijifanye kumuamini mwanaume kwa asilimia mia moja, unatakiwa kumuamini nusu nusu”
“Duh!!”
“Shangaa tu, habari ndio hiyo, utaona anakupenda, anakujali, anakuthamini ila anachofanya nyuma ya pazia ukikijua unaweza ukafa kwa presha, hebu usimuamini hivyo mwanaume. Ila sijaja kukuvunjia ndoa, sema tu nakufundisha misingi ya ndoa na vile wanawake tunavyotakiwa kuishi, wanaume wenyewe wanasiri kibao, wacha na sisi tufiche siri zetu”
Basi wakaongea mengi na kukumbushana mambo mengi sana, mwisho wa siku Johari aliaga kuwa anaondoka, ila mama Angel alishindwa kumsindikiza mbali sababu muda huo mtoto alikuwa akilia sana na hakuweza kutembea na mtoto wake, kwahiyo ilibidi aagane nae tu.
 
SEHEMU YA 300

Wakati Johari anatoka nje ya geti la mama Angel, yani baada ya hatua kama mbili hivi alishikwa bega, akageuka na kumuona mwanamke kasimama nyuma yake basi akasimama pia na kuanza kusalimiana na yule mwanamke kisha wakaanza kuongozana nae, ndipo yule mwanamke akajitambulisha kwa Johari,
“Samahani, ngoja nijitambulishe kwako, mimi naitwa Sia”
“Oooh sawa sawa, na mimi naitwa Johari”
“Naona umetoka kuonana na Erica, ni rafiki yako eeeh!”
“Ndio ni rafiki yangu tena sana, toka utotoni. Umejuaje kama nimetoka kumuona yeye”
“Nilivyokuona umetoka tu hapo getini basi nikahisi hivyo, hivi Angel yupo kwani?”
“Mmmh halafu sijamuuliza ila nasikia watoto wake wapo kwa bibi yao”
“Hivi unajua kama yule Angel sio mtoto wa mume wake huyu rafiki yako!”
“Mmmh kivipi?”
“Mwenzangu, mwanadamu mnyime chakula lakini sio maneno, unaweza ukatunza siri miaka nenda miaka rudi ila kuna siku ukweli unabumburuka wazi kabisa, mtoto sio wa Erick wala nini natumai Erick unamjua yani mume wake na Erica”
“Namjua ndio, nimesoma nao wote wawili”
“Oooh kweli nyie ni marafiki sana, ila duh Erica msiri jamani hadi wewe rafiki yake hujui loh!! Yule Angel sio mtoto wa Erick, yule Angel ana baba yake anaitwa Rahim, tena baba yake ana asili ya kipemba sijui kiarabu yani ni mshombeshombe hivi, ni mzuri sana ndiomana hata huyo mtoto ni mzuri sana”
“Mmmmh yani sikuelewi”
“Ndio hivyo, hata mtoto mwenyewe hajui kama kafichwa”
“Erick je!”
“Erick anajua ukweli sijui hajui maana huwa anajipumbaza, mtoto hafanani nae hata ukucha ila anasema mtoto wangu wa kwanza, hadi kote wanamuita baba Angel wakati sio mtoto wake yule, maana mtoto yule ana baba yake yupo tu”
“Unajua nashangaa kitu gani, Erica ni rafiki yangu mkubwa tu. Nilipozaa mara ya kwanza sieleweki sina mwanaume wa kunioa, alibaki ananishangaa na kusema bora kusoma, haya sasa kasoma kiko wapi? Kaenda kuzaa mtoto wa kwanza na mwanaume mwingine, je mimi na yeye tuna tofauti gani? Yani mimi na yeye tupo sawa sawa kasoro majina tu. Ila wanawake sisi loh!! Tena usikute ananisisitiza kutulia halafu labda hata huyu mtoto wa mwisho sio wa mume wake”
“Mmmh hilo sijui, atakuwa wa nani sasa?”
“Chunguza tu, mbona na huyu mtoto nimejaribu kumshika pale hafanani na Erick wala Erica”
“Mmmh ngoja nichunguze na hilo, nikipata ukweli nitafurahi sana”
“Kwani wewe kitu gani kinakufanya umfatilie?”
“Humjui tu rafiki yako, ana majivuno sana yani anajiona kuwa yeye ndio mwanamke wa pekee katika ulimwengu huu. Yani yeye haoni kitu chochote zaidi ya kujiona yeye yupo juu, sijui anapendwa, sijui anapesa, anaringa sana yule mwanamke”
Muda huu walifika kwenye stendi ya daladala na kupeana namba za simu ili wawe wanawasiliana, kwakweli Johari alishangaa sana baada ya kufikiria ile siri ya rafiki yake.

Kweli leo, wakina Samir walienda kutembea na baba yao, na kweli kwao ilikuwa ni ajabu sana siku hii maana sio kawaida kwa familia hii kabisa, kwahiyo alienda na watoto wake kwenye hoteli moja kula na kunywa, wakaagiza chakula pale na kuanza kula na vinywaji wakinywa huku baba yao akiwaambia watoto wake ni kiasi gani anawapenda,
Basi Samir alimuuliza baba yao,
“Mmmh baba kwahiyo unatupenda sisi kuliko watoto wako wote?”
“Kuna mwaka ambao watoto wangu wote nitawaweka pamoja, unajua mkubwa ana umri gani?”
“Hatujui baba?”
“Ana miaka ishirini na nne, yani mimi nina binti mkubwa kabisa wa kumuozesha, siku ya harusi yake nitachukua watoto wangu wote hadi wale ninaokataliwa kuwa nao”
“Kheee kuna watoto wengine unakataliwa kuwa nao!!”
“Yani mwanangu Samir, ngoja nikwambie haya, katika maisha yako usije ukarogwa kuwa na mwanamke asiyekuwa na akili, atakusumbua sana, asilimia kubwa ya wanawake niliozaa nao hawana akili, mwanamke msomi alikuwa ni mama yenu na mwanamke mmoja hivi ila yule dada alikuwa msomi halafu kumbe ni kichaa, nimezaa nae mtoto nimemuhudumia vizuri mtoto kaenda kumpa jina analolitaka yeye, kampeleka mwanangu Kanisani na kibaya zaidi kampa mwanangu baba mwingine”
“Kheee baba!!”
“Ila huwa nawaambia kuwa siku zote mtu hukumbuka asiliyake tu, waache wamlee malaika wangu ila ipo siku atarudi kwenye himaya yangu, na kipindi hiko watajiona wajinga sana sababu wamenisaidia kulea na hawatopata kitu toka kwa mwanangu. Kuna wanawake vichaa sana, ndiomana mwisho wa siku nikaamua tu kutulia na kumuoa mama yenu”
“Ila baba kwanini ukawa na wanawake wengi hivyo!!”
Ila baba yao kuna watu aliwaona na kuwafahamu basi akaaga watoto wake kwa muda na kwenda kuwasalimia watu hao.
Alienda kwenye ile meza na kukaa na kuanza kuongea nao kwa kuwasalimia,
Unanikumbuka ndugu Bahati”
“Nakukumbuka vizuri sana, wewe tena”
“Naona upo na mkeo”
“Ndio, nipo na mke wangu si unajua mara moja moja lazima nifurahi na familia yangu”
“Siku hizi umeacha mawazo ya yule kivuruge wako?”
“Aaaah sio habari za kuongelea hapa jamani, hebu karibu tuongee mambo mengine”
Basi baba Samir alimuangalia huyu Bahati halafu akamuangalia mke wa Bahati na kumwambia,
“Naona shemeji umefanya jitihada kubwa sana za kumbadilisha mumeo, hongera kwa hilo”
“Asante”
Kisha alimuangalia mumewe na kumwambia,
“Inatakiwa tuondoke sasa maana muda wetu wa kukaa hapa umeisha”
Basi walimuaga baba Samir pale na kuondoka zao, kwahiyo ilibidi arudi kwa watoto wake tu ambapo alikaa nao kidogo na kuondoka nao.

Baba Angel leo aliporudi nyumbani kwake, aliamua kuongea na mke wake kile alichoambiwa kuhusu Angel, kwakweli mama Angel alishtuka sana,
“Nani kakuletea hayo maneno baba Angel?”
“Hapana sitasema ni nani ila ni mtu ambaye anamfahamu vizuri sana Angel, mke wangu inatakiwa tuwe makini sana na mtoto”
Basi muda ule ule mama Angel aliamua kumpigia simu mama yake ili kujua ni kitu gani kinaendelea kuhusu mtoto wake, muda ule ule mama yake nae alipokea simu na kuanza kuongea nayo,
“Tena afadhari umenipigia mwanangu, nilikuwa nataka kukupigia muda tu ni kuhusu huyu Angel”
“Kafanyaje mama?”
“Unajua hadi kuna muda sielewi cha kufanya, hivi unajua huyu ni binti mkubwa sio sawa nimfunge kamba au nitembee nae kila mahali kwa kuhofia kuwa atafanya ujinga”
“Vipi tena mama?”
“Ni hivi, kuna siku hapa ilikuwa patashika, nilitoka kidogo tu kwenda kwenye shughuli huko, narudi namkuta Angel kazimia huku yule kijana asiyejielewa yule Samir yuko pembeni yake, kwakweli nilichukia sana nilimpiga mno kijana wa watu. Mungu anisamehe tu, huyu mtoto wenu ananitia dhambi haswaaa, kumbe sijui kuna kijana mwingine alifika nae kampa Angel tunda lenye madawa ili ambake, jamani huyu mtoto huyu anataka kunitia dhambi unajua nimepatwa na mawazo hadi nikajikuta sijawapigia simu kwa wakati”
“Duh!!”
“Tena hiyo haitoshi maana, ile simu Angel nilimpokonya kumbe kanunuliwa simu nyingine na mwanaume mwingine. Yani Erica huyu mtoto wako kwakweli kanishinda tabia, nitapiga nimuumize jamani”
“Oooh asante mama kwa kuniambia, ngoja nijadiliane na baba yake hapa tujue cha kufanya”
“Yupo ila nikampe simu uongee nae”
“Hapa mama hata sitaki kuongea nae, ataniumiza kichwa tu, ngoja baba yake niongee nae. Asante mama, usiku mwema”
Mama Angel aliagana na mama yake kisha akamuangalia mumewe na kumwambia,
“Yani uliyoambiwa kuhusu Angel ni ukweli mtupu hadi nahisi kichwa kuvurugika hapa, hivi tufanyeje sasa?”
“Nimeshauriwa kuwa tumpeleke kwenye shule za misheni na tumuache chini ya uangalizi wa masister”
“Naona hiyo ni nzuri, na akitoka shule nitakaa nae na kumueleza maana huyu mtoto anajitia kichwa rungu jamani khaaa sijapata kufikiria kama angekuwa anawaza ujinga kiasi hiki jamani Angel, kwahiyo sasa tutaenda lini kumchukua?”
“Nadhani keshokutwa twende kumchukua, au nitaenda mimi mwenyewe hakuna tatizo”
“Sawa nimekuelewa, ila kule kwa Tumaini alishika adabu yule, kweli mama saivi kazeeka jamani, kweli Angel wa kumshinda bibi yake kweli!! Kweli mama kaanza kuchoka loh!”
“Miaka inaenda, mama yangu ndio kabisa nadhani hata muda wa kumfokea mjukuu hana kabisa, yani huyu Angel akikaa kwa mama yangu hata mwezi kwa tabia zake hizi basi angerudi na mimba maana mama hana muda wa kufatilia kabisa”
Wakajadiliana pale na kuamua kufanya mambo mengine tu kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 301

Usiku wa leo, Erica alienda chumbani kwa kaka yake na kumuuliza,
“Kwani Samia ulimjibu nini?”
“Mmmh Erica hujaona nilichomjibu Samia kweli!”
“Sijaona ndio, maana mimi niliweka tu ile barua kwenye mkoba na kumpelekea”
“Nilimwandikia kuwa hata na mimi nampenda”
“Mmmh mbona leo hajaja shule basi!”
“Sasa asipokuja shule nahusika vipi hapo?”
“Inaonyesha ulimjibu vibaya kwahiyo kaumia moyo ndiomana hajaja shule”
“Hayo ni mawazo yako Erica, ila mimi nimemwambia kuwa nampenda”
“Kwahiyo upo tayari kuwa mpenzi wake?”
“Erica, mimi bado ni kijana mdogo, je huwa husikii mafundisho ambayo mama huwa anatufundisha? Mama katufundisha nini kuhusu mapenzi? Mapenzi yapo, na muda muafaka ukifika basi yatakuja yenyewe tu bila kulazimishwa, kwasasa mimi bado ni kijana mdogo na wewe bado ni binti mdogo, hapa maana yangu ni hii hata wewe usiingie vishawishi vyovyote vile vya kujiingiza kimapenzi na mtu yoyote yule maana bado ni binti mdogo, mapenzi yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo. Tukae na msemo huo wa mama”
“Ila mimi nishawishike kivipi, yani kitu gani kitanishawishi?”
“Ni kweli hakuna cha kukushawishi na ndio usishawishike, mabinti wengi hudanganywa na pesa, sasa wewe ni nani wa kukudanganya na pesa ikiwa baba yetu anahenyeka kwaajili yetu hakuna kitu ambacho tuakosa hapa nyumbani, haya kuhusu upendo familia nzima tunakupenda, kama mimi nakupenda sana mdogo wangu sasa kitu gani kitakushawishi?”
“Ila kwani imekuwaje mpaka Samia akuandikie wewe kuwa anakupenda sana?”
“Achana na Samia, hajafunzwa maadili yule maana angekuwa amefunzwa maadili basi asingeweza kufanya alichokifanya, ila Erica wewe uishi hivyo hivyo maana siku nikute sijui kuna mkaka anakufatilia sijui yani nitamfanya kitu gani, kwahiyo kuwa makini sana mdogo wangu”
“Sawa, nimekuelewa”
Kisha Erica aliinuka na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kwenda kulala.

Leo Erick akiwa darasani, muda wa mapumziko alifatwa na Sarah na kuanza kuongea nae,
“Ila Erick mbona muda mwingi unaonekana kama una mawazo sana?”
“Aaaah ni kawaida, binadamu lazima uwaze mambop mbalimbali”
“Lakini wewe umezidi jamani, sikia mama yangu kakukumbuka kweli, vipi kesho njoo basi nyumbani kwetu”
“Mmmh siwezi”
“Jamani!! Au nije mimi kukuchukua, najua mama yako hawezi kukataa kuhusu swala hili, najua lazima atakubali, kwani kuna ubaya gani Erick kuja kwetu!”
“Ngoja nikuulize Sarah, hivi ni malezi gani ambayo mama yako amekupatia wewe? Kwa kifupi yani unaishije na mama yako nyumbani?”
“Sijui nikwambie vipi ila mama yangu ananipenda sana, huwa anasema mimi ni mtoto ambaye kazaa na mwanaume aliyempenda sana, ndiomana mara kwa mara huwa tunaenda kwenye kaburi la baba na kulipalilia na kukaa kidogo huko, kwakweli mama yangu ananipenda sana”
“Unajua kupika wewe?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Kufua je? Unajua kuosha vyombo?”
“Mmmh ndio unanipima ili ujue kama nafaa kuolewa au sifai au ni kitu gani?”
“Hapana, mikono yako Sarah ni laini sana kiasi kwamba sidhani kama kuna kazi yoyote huwa unafanya nyumbani kwenu”
“Mmmh tusijadili hayo, ila nitakueleza vizuri kuhusu mimi”
Kengele ya kurudi darasani ililia ilibidi waachane na kila mmoja kuelekea kwenye darasa lake.

Leo Johari akiwa nyumbani kwake, mumewe akamuomba jambo moja,
“Hivi yule mke wa Erick si unapafahamu kwao?”
“Ndio napafahamu”
“Naomba unipeleke”
“Kwani unataka kwenda kufanya nini?”
“Nataka kwenda kumuona mtoto wa Erick aitwaye Erick, kuna jambo la muhimu sana mke wangu juu ya huyu mtoto tunatakiwa kuwa nae karibu mtoto huyu ni mali kubwa sana”
“Mmmh uwe nae karibu anakuhusu?”
“Hata kama, mtoto wa mwenzio ni mtoto wako, kuna vitu ukiviona kwa mtoto unatakiwa kuwa makini sana lkwani leo na kesho utafaidika pia”
“Mmmh, haya twende lini?”
“Nahitaji twende leo”
Ilibidi Johari ajiandae kisha yeye na mumewe waliondoka na kwenda moja kwa moja hadi kwa bibi Angel na hapo walimkuta Angel na bibi yake, basi waliwasalimia na kuanza kuongea nao mawili matatu, ambapo Juma aliulizia pia kuhusu watoto wa Erick,
“Eti Erick mdogo yupo?”
“Mmmh hayupo”
“Ila si washatoka shule!! Maana leo ni Ijumaa”
“Hawaishi mahali hapa, wapo kwao”
“Mmmh kumbe! Lakini mbona baba yao aliniambia kuwa wapo huku”
Mara alifika mgeni kwenye nyumba ile, na huyo mgeni alikuwa ni mama Junior, ila cha kushangaza yani kila mtu pale alibaki kustaajabu kwani mama Junior alisogea karibu na Juma na kumkunja kama anataka kupigana nae.

Mara alifika mgeni kwenye nyumba ile, na huyo mgeni alikuwa ni mama Junior, ila cha kushangaza yani kila mtu pale alibaki kustaajabu kwani mama Junior alisogea karibu na Juma na kumkunja kama anataka kupigana nae.
Basi bibi Angel alisogea pale na kumuweka mama Junior pembeni huku akimuuliza,
“Kwani tatizo kitu gani Bite?”
Mama Junior alimuangalia Juma kwa gadhabu sana na kumwambia,
“Ulidhani hatutakutana?”
Mama yake akamuuliza tena,
“Kwani amekufanyeje? Hebu shusha presha kwanza mwanangu”
Mama Junior alikaa chini na kusema,
“Huyu baba amenifanyia roho mbaya sana, sikia mama nadhani kila mara huwa unaniuliza ni kwanini sifatilii mali za marehemu James wakati nilizaa nae, basi chanzo ni huyu hapa”
“Yani yeye kafanya nini?”
“Hivi mama unajua kuwa huyu ni rafiki mkubwa sana wa marehemu James, alinipa maneno machafu sana huyu. Namchukia simpendi kabisa na sitaki hata kumuona”
Juma akasema,
“Naomba unisamehe, sikujua haya”
“Mjinga wewe, ambacho hukujua ni kitu gani?”
Mama Junior alikuwa na hasira sana, basi Johari akaanza kumtuliza pale,
“Lakini dada Bite, ongea vizuri ili tukuelewe”
“Mjinga nini wewe, si umuulize vizuri mumeo ndio umuelewe”
Basi kwasababu ya hasira alizokuwa nazo mama Junior ilibidi wakina Johari waage tu na kuondoka zao.
Pale ndani, mama Junior alibaki na mama yake, na hapo bibi Angel akamwambia Angel akalete maji ili mama Junior ashushe hasira zake, basi alimletea maji na kuyanywa kwanza, ila hakutaka kuongea kwa muda huo na kuomba muda kidogo apumzike kwahiyo alienda kulala kidogo.
 
SEHEMU YA 302

Basi Johari na mumewe wakati wanaondoka, waliulizana,
“Kwani wewe umemfanya nini huyu dada?”
“Unajua sikuweza kuunganisha matukio, kumbe huyu ni dada yake Erica?”
“Ndio, tena kutoka huyu basi ndio akafatia Erica, tena kwenye familia yao basi Erica na huyu ndio wanapendana sana”
“Dah!! Mimi sikujua kabisa”
“Kwani mambo gani ulimfanyia?”
“Sikia nikwambie kwa kifupi, huyu mwanamke alimuomba mumewe talaka kwa madai kuwa mumewe kaathirika, na aliomba ile talaka kwa madaha kabisa, nakumbuka ile kesi ya talaka ni mimi ndio nilikuwa nampeleka James mhakamani, ikaendeshwa ile kesi hadi ikabidi waachane kwa talaka sasa, ila kiukweli James alimpenda sana huyu mke wake, sema mimi niliumia mno kwa jinsi huyu mwanamke alivyoamua kumfanyia mumewe, alikosa hata utu kitu kidogo tu mwanaume mwenyewe umeathirika, kiukweli James alioa yule mwanamke mwingine sio kwasababu alimpenda ila ni sababu ilimbidi tu kufanya vile ndiomana aliamua kuoa. Cha kushangaza, yule yule mwanasheria aliyekuwa anashadadia ishu ya talaka ndio mwanaume aliyemuoa huyu mwanamke, si inamaana kwamba ni kitu ambacho walipanga? Yani huyu hakuona njia nyingine yoyote kwa mumewe zaidi ya kuomba talaka? Kwakweli alinikera sana, ilitakiwa agaiwe na yeye sijui urithi sijui nini na nini, basi na mimi nikatafuta wanasheria wangu wenye figusu hadi hakupata kitu hata baada ya msiba wa James, yani hakuna kitu alichoambulia ila kosa ni langu mimi, ila nilifanya sababu huyu mwanamke alinikera sana, hakuwa wa kumfanyia vile rafiki yangu. Sema sikujua kama nitakuwa nafahamiana nae”
“Hujamfanyia vizuri hata kidogo, kwanza yeye na huyo mumewe ndio wanajua ndani walikuwa wanaishije? Na iweje mwanaume akaathirika wakati mwanamke hana, ni wazi kuwa mwanaume huyo hakutulia, unaweza kumlaumu sana huyu lakini nadhani ni kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao ndiomana ikawa hivyo ilivyokuwa. Huyu dada ninamjua kitambo sana, hana hayo mambo kabisa, kwa kifupi huyu dada sio muhangaikaji, itakuwa huyo mwanasheria alionyesha nia ya dhati na yeye akaona nisihangaike sana bora nipate wa kutulia nae, unamlaumu bure tu. Halafu ulikazania hivyo mali za rafiki yako ulitaka azipate nani sasa? Ulikuwa na malengo gani? Huyu dada na huyo mumewe si wana mtoto lakini?”
“Unajua badae nilitambua kosa langu ila sikuwa na la kufanya wala nini labda turudie tena kesi, ni hivi yule mwanamke aliyekuwa anaishi na James kwa kipindi hiko, walikuwa katika ndoa na wana mtoto pia, aliongea na mimi nimsaidie ili aweze kumiliki mali za mume wake maana ni haki yake, alikuwa anahofia kwa watu kutokea na kuzitaka zile mali”
“Na yeye ana roho mbaya, utafikiri yeye ndio alikuwa wa kwanza kuolewa? Tena wewe mwenyewe ndio ufanye jitihada ili mtoto wa huyu dada nae apate haki yake”
Muda huu walikuwa wakiendelea tu na safari yao ya kurudi nyumbani kwao.

Baba Angel leo alirudi mapema nyumbani kwake, maana kuna jambo alikuwa amelipanga kwenye kichwa chake na kuna safari alikuwa ameipata, kwahiyo aliona ni vyema kwenda kuzungumza na mkewe kwanza,
“Natakiwa kusafiri, nitakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja”
“Mmmmh mwezi mmoja!! Jamani, itakuwaje hapa sasa?”
“Mama Angel, kwani ni mara ya kwanza kwa mimi kusafiri? Si huwa nasafiri mara kwa mara? Ila kuna kitu nataka kukiweka sawa kwanza”
“Kitu gani hiko?”
“Nitahakikisha Angel nishampeleka kwenye ile shule maana nasikia masomo yameshaanza, halafu Junior nae aende shule ingawa sio mbali sana na hapa ila ni bweni, akasome huko aache ujinga wa hapa nyumbani. Nitaacha maelekezo ya kutosha kwa Erick ili angalau mwisho wa wiki hata mara moja au mbili aende kiwandani”
“Kwani hiyo safari ni ya muhimu sana eeeh!”
“Ndio ni ya muhimu na itatuingizia hela nyingi, kwanza kesho naenda kumchukua Angel halafu napitia nae kununua baadhi ya vifaa yani asifikiri atakaa nyumbani maana ni shule moja kwa moja, uzuri ndio shule aliyofanya usahili, nikifika namkabidhi kwa sister ambaye atafatilia nyendo zake zote”
“Kheee kwahiyo Angel shule lini?”
“Kesho kutwa, naenda kumkabidhi shuleni, kwahiyo Jumatatu ataanza kuingia darasani”
“Sijui atafurahi, sijui atachukia!”
“Tusifikirie hilo kwasasa, ila tufikirie elimu ya Angel”
“Sawa, nimekuelewa ila safari yako imekuwa gafla sana nitakukumbuka mno jamani mume wangu”
“Wasiwasi wako nini, bado sijasafiri”
Mama Angel alionea tu kwa huruma kwani aliona wazi kuwa atamkumbuka sana mume wake kwani ameshamzoea na muda mwingi wanakuwa wapo wote.

Usiku wa leo Erica alimfata Erick na kuanza kumwambia habari za Samia maana alikutana nae shuleni,
“Nasikia Samia alipigwa na mama yake hadi akazimia”
“Mmmh kwanini sasa?”
“Si alimwambia mama yake ukweli kuwa anakupenda wewe, basi mama yake kamwambia hataki kabisa kusikia jina lako likitajwa katika masikio yake”
“Kwahiyo Samia amekoma eeeh!!”
“Sasa umefurahia jamani! Kumbuka Samia anakupenda”
“Tena mama yake kafanya vizuri sana kumpiga, ni utaratibu wa wapi huo kwa binti mdogo kama Samia kumtaka kimapenzi kijana mdogo kama mimi! Yani bora kapigwa ili akili imkae sawa”
“Ila cha kushangaza sasa, anasema ingawa amepigwa ila hatoacha kukupenda wewe”
Erick alitabasamu kisha Erica akamwambia,
“Hatujacheza siku nyingi karata, basi leo tucheze karata”
“Ila leo nimechoka sana”
“Ndio najua kama umechoka, basi tucheze japo mchezo mmoja tu”
Erick akakubali na kuanza kucheza karata, walipokuwa wakicheza zile karata ziliwanogea na kujikuta wakilala humo humo chumbani tena wakiwa hawana habari kabisa.
Leo mama Angel alienda chumbani kwa Erick maana alikuwa akitaka kuongea nae kuhusu baba yake, aliwakuta wakiwa wamelala tena hawana habari huku karata zile zikiwa pembeni, yani mama yao alitikisa kichwa na kuwaamsha,
“Nyie, hebu amkeni yani nyie mbona mna akili mbovu kiasi hiko!! Erica huna chumbani kwako wewe hadi unakuja kujilaza kwenye chumba cha kaka yako?”
“Nisamehe mama”
“Halafu mambo ya karata si niliwakataza mimi, kwanini hamsikii kitu nyie watoto mna matatizo gani kwani?”
“Tusamehe mama”
“Haya inukeni hapo, wajinga nyie”
Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake ila kwavile mama yake alizichukua karata alijua wazi hawezi kuzipata tena, na ukizingatia mtu ambaye alikuwa akimletea karata ni Abdi ambaye hawasomi pamoja tena, basi alisononeka sana na kumuacha mama yao akizungumza na Erick mule chumbani.
 
SEHEMU YA 303

Siku hii Johari alipigiwa simu na Sia na kwenda kukutana nae na kuongea nae mambo mengi,
“Sikia nikwambie, nataka nikuonyeshe mwanaume ambaye amezaa na Erica yule Angel”
“Mmmmh! Ila wewe nawe una mambo lakini!”
“Hapana, unajua kuna umuhimu wa huyu mwanaume kupata haki yake, kuna umuhimu wa huyu kumtambua mtoto wake”
“Ila duh wewe una mambo zaidi, kuna mambo mimi huwa najua ila mengine huwa sijui, ila wewe unamjua hadi mwanaume aliyezaa na Erica!”
“Namjua ndio nataka nikakuonyeshe, tena twende leo leo”
“Ila unataka kunionyesha ili iweje?”
“Umjue, ili hata pengine utaweza kumwambia ukweli huyo mwanaume”
“Aaaah mtihani mzito huo, haya nipeleke”
Mara simu ya Johari ikaanza kuita, kuangalia ni mama Angel basi akapokea na kuanza kuongea nayo,
“Unakumbuka lakini Johari, ni leo njoo mara moja nikupeleke mapema si unajua kuwa nina mtoto mdogo”
“Oooh naelewa ndio, nakuja muda sio mrefu”
Basi Johari aliamua tu kumuaga Sia na kuachana nae kwa muda huo, kiukweli Sia hakupenda kwani alitaka Johari amtambue mwanaume aliyezaa na mama Angel.

Basi Johari alienda kwa mama Angel na kufanikiwa kwa muda ule ule kuondoka pale nyumbani kwani mama Angel hakutaka kuchelewa ukizingatia alikuwa na mtoto mdogo, basi walipokuwa kwenye gari kuna swali Johari alimuuliza mama Angel,
“Hivi Erica unajua kuwa sisi tulikuwa marafiki wakubwa sana, tulipendana na kufanya mambo mengi sana, ila imekuwaje siku hizi tupo mbalimbali au kisomo ndio kimetutenganisha? Huniambii siri zako, haupo karibu na mimi hata sijui tatizo ni nini?”
“Ni kweli Johari ulikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana, ulinifanyia mambo mengi ila nilisamehe. Sema kitu kimoja ambacho sikipendi katika maisha yangu ni kuwa sipendi rafiki mnafki yani wewe Johari ni rafiki yangu ila ni mnafki yani hushindwi kunizunguka wewe, halafu mwenyewe unajionea sawa kabisa, sijui ni urafiki wa aina gani huo”
“Hayo yalikuwa ni mambo ya zamani Erica, kwasasa tumekuwa watu wazima na tuna familia, tunahitaji watoto wetu waishi vizuri na wapatane kama ndugu ila mama zao tukiwa mbalimbali hivi sio picha nzuri ujue! Ila wewe Erica kuna rafiki yako ambaye unamuona sio mnafki kweli!”
“Yupo ndio, nina rafiki anaitwa Fetty yani yeye maisha yake ni uhalisia, halafu sio mnafki kwangu, huwa ananifundisha na kunielekeza mambo mengi sana, nikifanya vizuri atanipongeza, nikikosea ataniambia tena kwa utaratibu ila mnafki, ukikosea anaenda kukusema kwa watu ili akuharibie zaidi sasa unapata faida gani? Yani mimi huwa sipendi unafki”
“Mmmh nimeacha mambo ya unafki jamani Erica, eeeh unanipeleka wapi?”
“Tena nimekumbuka, ngoja tupitie hapo stationary nikununulie daftari na peni, nakupeleka huko kuna semina ya ujasiliamali, nikikuelekeza mimi naweza nikakupoteza ila ukienda kwenye semina afadhari utapata mwanaga wa mambo mbalimbali, ndiomana nimekuharakisha leo sababu tangazo lao nililisikia”
Basi walifika kwenye duka na kusimama, kisha wakashuka na kwenda kununua hivyo vitu, wakati wanaondoka kuna mwanamke ambaye mama Angel alifahamiana nae, alifika na kumsalimia mama Angel, na yeye alimsalimia halafu akaondoka na Johari, wakapanda kwenye gari ila Johari akamuuliza,
“Nani huyo?”
“Ni mwalimu wa shule wanayosoma watoto wangu, ila ni mnafki sana yani sikujua kama anaweza kujivika moyo wa kijasiri namna hiyo na kunisalimia”
“Mmmmh kwanini?”
“Nikikueleza mambo yake utashangaa, kwa kifupi alitafuta dawa sijui kwa mganga wa kienyeji huko na kumuwekea mume wangu ili amtege yani amchukue kimoja, ila Mungu sio Athumani, ile dawa akaitumia mwanaume mwingine basi ndio kamganda hatari, namshangaa hata anapata moyo wa kunisalimia”
“Duh! Ila wanadamu wabaya sana, hata mimi kuna mwanamke huyo aliachwa na mumewe, hana mbele wala nyuma ila nashangaa sana eti naye alitaka kumuwekea dawa mume wangu ili ampate, yani katika maisha tunakutana na watu wa ajabu jamani”
Basi walifika kwenye hiyo semina, mama Angel alilipa kiingilio kwaajili ya rafiki yake na kumuacha hapo kwani kuna mahali alitaka kupitia halafu ndio arudi nyumbani kwake kwaajili ya mtoto wake.
Moja kwa moja mama Angel alipitia sehemu aliyotaka kwenda, ilikuwa ni kwa fundi ambaye alimpelekea kitenge amshonee maana alikuwa akitaka kupata sare ya kitenge kile, yani alishona nguo yake na shati la mumewe, kilikuwa ni kitenge ambacho alipelekewa zawadi na Sarah.
Basi wakati yupo kwa yule fundi ndipo alikutana na mtu ambaye wanafahamiana kwa zamani, wakasamiana pale alichukua bidhaa zake na walitoka nje wakiongea kiasi,
“Unajua mara ya mwisho tumekutana ni pale hospitali yani wewe Erica jamani, bado tu unatuchukia sababu ya mjinga mmoja”
“Sio hivyo Babuu ila siku ile nilikuwa na mambo mengi sana, unafanya nini siku hizi?”
“Najishughulisha na mapamba, napamba vizuri sana, sijisifii ila ukitaka utaona kazi zangu”
Basi Babuu alichukua simu yake na kuanza kumuonyesha mama Angel baadhi ya picha za mapambo ambayo huwa anafanya, kwakweli yalikuwa mazuri sana, ila kuna picha ilimshtua kidogo na kumuuliza Babuu huku akimuonyesha ile picha,
“Inamaana ni wewe ndio ulipamba mahali hapa?”
“Ndio ni mimi”
“Khaaa unajua hiki ni kiwanda changu na mume wangu, yani kumbe mpambaji ulikuwa ni wewe, kwakweli palipendeza sana. Mbona sikukuona?”
“Aaaah kumbe!! Mimi huwa nikimaliza shughuli zangu naondoka, naacha vijana tu ambao ndio hutandua mapambo, ila ningejua kabla basi ningesubiri hata nikusalimie”
Mama Angel akatabasamu tu, kisha Babuu aliendelea kuongea,
“Unajua nini, katika maisha mtu unapitia katika mambo mbalimbali, ila yote huwa yapo kwaajili ya kujifunza. Ila huwa sisahau kamwe, siku ambayo nililala rumande sababu ya uzurulaji tena uzurulaji wenyewe nilikamatwa baada ya kutoka kukuona wewe, nilikuomba nikalale guest ukakataa na kutaka nirudi nyumbani basi nikarudi na kukamatwa na askari usiku ila wewe ulihisi nimeenda kwa wanawake zangu, natoka na uchafu wangu rumande, moja kwa moja chuoni kwenu nakutana na rafiki yako yule Dora ananipa maneno ya kejeli na karaha, huwa sisahau hii siku katika maisha yangu jamani”
“Yamepita jamani, nisamehe”
“Ila ni funzo kwangu na kwako pia, tena kwako ndio ujifunze vizuri hata mumeo ndani usije ukamfanyia vile kama ulivyonifanyia mimi, yani wewe hisia zako zinapokupeleka basi ndio huko huko, hujali kuwa hiki kitu ni cha kweli au cha uongo ila wewe upo tu kukazana na misimamo yako, kwakweli hapo ujirekebishe”
“Mmmmh yameisha na maisha yameendelea, ila nashukuru hujakaa na kinyongo kwangu”
“Ni kweli sina kinyongo ila mimi ni tofauti na ulivyonifikiria, nilikuwa mkweli kwako, nilikupenda na kukujalia na leo pengine ndio ungekuwa mke wangu, ila naona Mungu alipanga iwe hivi”
Mama Angel aliona kuendelea kuongea na Babuu pale basin i kuanza kukumbusha mambo yaliyopita kwa sana, ikabidi tu amuage kwani alimwambia kuwa ana mtoto mdogo, basi Babuu nae akaagana nae ila akampa kadi ya namba zake ili wawe wanawasiliana, kisha mama Angel aliingia kwenye gari yake na kuondoka.
 
SEHEMU YA 304

Basi baba Angel alifanikiwa kwenda kumfata Angel na kumueleza lengo mama yao kuwa ni kumpeleka Angel shule, basi akaondoka nae na kupanda nae kwenye gari kisha akampa barua ya kukaribishwa shuleni na kumwambia,
“Sasa tunaenda dukani kununua vyote vilivyoandikwa hapo, kwaajili ya wewe kwenda shule’
“Kwani shule naenda lini baba?”
“Kesho nakupeleka shule”
“Duh baba!!”
Baba Angel wala hakuongea zaidi, na moja kwa moja walianza kuingia madukani na kununua vitu mbalimbali kama vifaa vya shule.
Walipomaliza, wakati wanaondoka walikutana na madam Oliva ambapo aliwasalimia na kutaka kuongea kidogo na baba Angel, basi Angel aliingia kwenye gari na wao kubaki pale nje,
“Mmmh Erick, sio muda wote nikitaka kuongea na wewe basi naongea ujinga! Hapana, kuna muda nataka kuongea na wewe mambo ya maana”
“Mambo gani hayo?”
“Ni hivi, hili jambo ni leo leo nimeliona kwa nyakati tofauti, kwanza nimemuona yule Sia akiwa na mwanamke mmoja hivi wakionekana kama wakijadili kitu halafu kuna mahali tena nimemuona mkeo na huyo mwanamke wakiongea na kufurahi inaonyesha ni marafiki, yani hili ni swala la leo leo. Mimi ni mwalimu na kwa bahati naweza kumsoma mtu hata kama simfahamu, naweza kuongea nae kidogo tu nikamsoma. Kwanza ni hivi Sia sio mtu mzuri katika familia yako, yani yule yupo kwa lengo la kuiangusha familia yako, kwanza kumbuka anakupenda sana na inamuuma sana kuona kuwa unafuraha na mke wako, kwahiyo anafanya juu chini ili furaha hiyo isiwepo, kuna muda utaona kama anaongea nawe vizuri ila sio mtu mzuri na kama ni mtu mzuri basi hayo anayosema kayaficha angewaweka wazi. Halafu kitu kingine huyu mwanamke niliyemuona na Sia anaonekana macho juu juu sana, nilipomuona na mkeo nimeshtuka, hadi nilienda kumsalimia mkeo, nadhani hajaelewa ni kwanini nimeenda kumsalimia ila ni sababu ya yule mwanamke, mwambie mkeo awe nae makini sana asije akalia badae. Hata kama ni rafiki yake ila awe nae makini sana, asimuamini kwa asilimia zoyte ataumia moyo wake bure”
“Oooh nimekusikia, ila sijui huyo mwanamke ni nani?”
“Ukimuuliza mkeo, atamjua ni nani. Muulize mwanamke ambaye mlikutana na madam Oliva ukiwa nae, alivaa gauni rangi ya nyeusi lenye maua ya njano, na kichwani kasuka yeboyebo halafu kajitanda ushungi kiasi atamkumbuka tu”
“Sawa, hakuna tatizo. Nashukuru kwa hilo.”
“Utaniambia shule unayompeleka Angel, niwe namtembelea”
“Sawa, nitakwambia”
Kisha akaagana nae na akaenda kumuaga Angel pia na kuondoka zake.

Baba Angel na mwanae walirudi nyumbani sasa, ila muda huu walimkuta mama Angel tayari yupo nyumbani huku akishughulika na mapishi maana alijua wazi mwanae anakuja halafu kesho yake mwanae ataenda shuleni kwahiyo hatokuwa hapo nyumbani, licha ya hasira alizokuwa nazo dhidi ya mwanae ila akaona vyema kumpikia mwanae chakula ambacho huwa anakipenda sana.
Kwahiyo walivyofika tu, waliwapokea na kuongea kidogo kisha Vaileth na Erica walienda kuandaa chakula ili waweze kula kwa pamoja, na kweli walikaa siku hiyo kama familia wakila na kufurahi.
Baada ya hapo, mama Angel alienda na Angel chumbani kwa Angel ili kumsaidia kuweka vitu vyake vizuri kisha alianza kuongea nae,
“Sikia Angel, nilitamani tupate wasaa wa kuzungumza hata kwa wiki moja ila nahitaji zaidi usome, nenda shule ujifunze vitu vingi uweze kupanua akili yako na fikra zako”
“Asante sana mama”
“Haya, na hizo simu ulizokuwa unatumia kwa bibi yako ziko wapi?”
Angel hakujua kama mama yake angekumbuka hizo simu, kwani kwa mawazo yake aliona vyema kama usiku wa siku hiyo aweze kuwasiliana na Samir na kumueleza kuhusu yeye kupelekwa shule maana hakumwambia chochote kwahiyo hata kwa upande wake ilikuwa gafla kidogo, na muda mama yake anamuuliza aliogopa kukataa na kuamua kutoa zile simu kumkabidhi mama yake, yani mama Angel alisikitika na kumuangalia mwanae huku akipokea zile simu, aliziweka pembeni na kuzungumza nae,
“Hivi Angel mfano ndio ungebakwa siku hiyo? Ungepata mimba ingekuwaje?”
Angel alikaa kimya tu, kisha mama yake akaongea,
“Sijui sijawahi kuongea na wewe, ila hata kama sijawahi nina uhakika bibi yako ameshakufundisha haya mara nyingi tu, Angel ukimaliza kidato cha sita naomba uje uniambie kuwa mama nimekuwa mkubwa sasa naomba unipe simulizi ya maisha, basi nitakupa simulizi inayohusu maisha yangu mwenyewe na wala sio ya mtu mwingine. Mwanangu sio kila anayekwambia anakupenda ukahisi anamaanisha, katika maisha tumezingirwa na maadui kila kona, kwahiyo mwingine ana lengo la kukuangamiza. Haya, huyo kijana unamfahamu vizuri? Angekubaka ingekuwaje? Niambie kwanza umefahamiana vipi na huyo kijana aliyetaka kukubaka?”
“Mama, kwanza naomba unisamehe ila yule kijana ni dereva bajaji, siku moja niliamua kurudi kwa shangazi kwa miguu ndio nilikutana nae akanipa lifti basi ndio nikazoeana nae hapo. Halafu ni kijana ambaye aliwahi kukuleta wewe hapa nyumbani, nikaja kumpa hela kama unakumbuka”
“Mmmh sikumbuki, kwahiyo ulimfahamu kwa njia hiyo, je hukuona kama kuna kitu kibaya anaweza kukufanyia ukizingatia humfahamu vizuri?”
“Sikujua mama, alikuwa anaongea vizuri sana. Ila siku aliyogombana na Samir, nilimuona na yule mama ambaye mara nyingi anakuja hapa nyumbani, hata Erick hampendi yule mama, nilimuona akimpa pesa, halafu Samir nae aliniambia kuwa alipoenda hospitali alimuona yule mama akienda kumuona, Samir pia huwa hampendi yule mama sijui tatizo ni nini ila huwa anasema kuwa yule mama ni mbea sana, na akasema kuwa Ally atakuwa katumwa na yule mama”
“Mmmh anaitwa nani huyo mama?”
“Simjui, ila muulize Erick atakwambia jina la huyo mama”
Ila mama Angel alihisia kitu, sema tu aliendelea kumpa nasaha mtoto wake na kumsaidia kupanga vitu pale na mwisho wa siku aliondoka na zile simu kwenda nazo chumbani kwake kwahiyo Angel hakuweza kuwasiliana na Samir kuhusu kwenda kwake shuleni.

Kulipokucha, wote kwa pamoja waliakaa sebleni na kula chakula cha asubuhi kwa pamoja kumuaga Angel na kumtakia masomo mema, kisha Angel na baba yake wakaondoka na kuanza safari yao.
Wakati Angel anaondoka na baba yake, wakiwa kwenye gari ndipo Angel alipomwambia baba yake kuwa kuna kitu kasahau kununua jana,
“Tafadhari baba, naomba ninunue leo”
“Jamani Angel unataka kwenda na vingapi shuleni mwanangu?”
“Hiko kimoja tu baba, ni cha muhimu sana”
“Haya tumesahau kitu gani?”
“Nahitaji poda baba”
“Khaaa ila watoto wakike jamani!! Haya ngoja tupitie dukani hapo”
Basi walifika kwenye duka na kushuka kisha Angel alienda kuchagua poda aitakayo halafu baba yake akawa anailipia, wakati huo kuna mbaba alisikika akimuongelesha Angel,
“Umekuwa mkubwa Angel”
Baba Angel pia alisikia na kuamua kugeuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyekuwa akiongea na Angel.

Basi walifika kwenye duka na kushuka kisha Angel alienda kuchagua poda aitakayo halafu baba yake akawa anailipia, wakati huo kuna mbaba alisikika akimuongelesha Angel,
“Umekuwa mkubwa Angel”
Baba Angel pia alisikia na kuamua kugeuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyekuwa akiongea na Angel.
Aliomuona aliyekuwa akiongea na Angel alipumua kidogo, kisha aliwafata pale karibu na yule baba alimsalimia pale baba Angel kisha baba Angel hakutaka maneno mengi sana na kuondoka na Angel ila yule baba alimsimamisha na kumuuliza,
“Samahani, kwani muda huu unampeleka wapi?”
“Anaenda shule huyu”
“Hongera sana, wewe ni mwanaume wa pekee. Mwanzoni sikufikiria kama ungefanya hivi kwa huyu mtoto, nilijua ni mimi tu mwenye uwezo wa kuwa na mapenzi nae, hongera sana”
Baba Angel alimuangalia tu na hakujibu kitu ila alipanda kwenye gari na mwanae na kuondoka zao.
Wakiwa kwenye gari, Angel alimuuliza baba yake,
“Kwani baba huyu tuliyekutana nae ni nani?”
“Anaitwa Bahati, ni rafiki wa zamani kidogo. Alikuona zamani ndiomana ameshangaa kuwa umekuwa mkubwa”
“Mbona anasema kuwa hakufikiria kama ungefanya hivi kwangu?”
“Angel mwanangu, kuna vitu katika maisha havitakusaidia kwa wakati huu, kwahiyo sio lazima kuvijua, nimekutajia tu anaitwa nani ili umtambue. Na siku nyingine ukimuona basi umjue”
“Sawa baba”
Safari ikaendelea, ila kuna mahali kidogo gari ilisimama katika foleni, na Angel alimuona mtu akivuka barabara, basi alimuuliza baba yake,
“Baba, samahani, yule anaitwa nani?”
“Kwani unamfahamu?”
“Namfahamu kidogo”
“Yule, anaitwa Sia, unamfahamu vipi?”
“Kuna stori nimemsimulia mama, basi ukirudi mwamabie huyo mtu aliyekwambia Angel anaitwa Sia”
Baba Angel kidogo alishtuka na kumuuliza mwanae,
“Ni stori gani?”
Kwani alimfahamu vizuri sana Sia, ila kwavile Angel alikuwa huru kuongea kila kitu na baba yake, basi alimsimulia baba yake kila kitu toka alipokutana na Ally na jinsi alivyotaka kumtengenezea simu na jinsi Ally alivyopigwa na Samir, kwahiyo alimsimulia baba yake kila kitu ambaye alisikitika tu kwa kusikia yale,
“Nilimuuliza Ally, akasema kuwa huyu mwanamke ni mamake mdogo ila nimekuwa nina mashaka sana na huyu mwanamke, na vile alivyoniambia Samir ndio kabisa baba, nimekuwa na mashaka nae.”
“Ila mwanangu, cha kujifunza hapo ni kuwa usimuamini mtu kupitiliza, yani wewe fanya mambo yako mengine na usiwe na imani na mtu kupitiliza kwani huwezi jua kuwa huyo mtu anakuwazia vitu gani”
Baba Angel aliongea na mwanae kule na kujaribu kumuelekeza vitu na mambo mbalimbali ya maisha huku akiendelea kumpeleka shuleni.
 
SEHEMU YA 305

Muda huu, mama Angel alikuwa akimpangia vizuri mumewe nguo za safari kwani alijua wazi kuwa, mumewe akitoka huko basi atamalizana na Junior na kuondoka kwenye hiyo safari yake.
Wakati akipanga nguo, aliambiwa kuwa kuna ugeni, basi aliamua kuacha na kuongea kwanza na mgeni huyo, alipofika alikuta ni rafiki yake Fetty amefika kumsalimia, basi alimkaribisha na kwenda kukaa nae bustanini kwani alikuwa na mazungumzo nae,
“Kwanza Erica za siku?”
“Nzuri tu, vipi wewe na familia yako na ndoa yako?”
“Kwakweli namshukuru Mungu maana naendelea vizuri, unajua nilikata tamaa yani sikuwa na raha kabisa jinsi mume wangu alivyobadilika na kuanza tena kukutaja wewe. Ingawa najua wazi hawezi kuwa na wewe ila nilikuwa naumia sana kwa alichokuwa anakifanya”
“Pole sana ndugu yangu, kwakweli hata mimi mwenyewe nilikuwa sielewi wakati maisha yamebadilika na kila mtu na maisha yake. Ila hongera kwa kufanikiwa kumuweka katika mstari”
“Unajua nini, na mimi bado kidogo tu nianze kuhangaika maana nilichoka. Mwanaume haeleweki hata kidogo, ndiomana nilikuwa natoka kwangu bila kuaga na kwenda kufanya mambo yangu, ila kuna mama nimekutana nae, kiukweli amenifundisha mambo mazuri sana na amenifungua akili yangu. Nikajiuliza ni wapi nakosea? Kwanini mume wangu akakumbuke alipotoka na kuacha kunikumbuka mimi? Nikaona kuwa lazima kuna kitu nakosea, na sikuona kama ni vizuri kumchukia mume wangu, basi nilianza kujirekebisha, cha kwanza sikutaka tena kuanza mabishano na mume wangu maana mimi nilikuwa na hiyo tabia, akipanda basi na mimi napanda, ila yule mama alinishauri vyema sana, nikaanza kujishusha na kuwa mpole, kiasi kwamba hata siku moja mume wangu aliniuliza, hivi ni wewe Fetty niliyekuzoea au kaja Fetty mwingine? Sikuwa namjibu vibaya mume wangu na nimefanya upendo wake kwangu unawili sasa. Huwezi amini kwasasa tunaishi kwa maelewano sana, yani hakuna tatizo kati yetu. Ila kilichonileta leo sasa unajua ni nini?”
“Niambie”
“Ni hivi, kwanza nilitaka kukushudia hayo kuhusu mimi na mume wangu ila pili, nataka kukwambia kuhusu yule mwanamke aliyekuwa anakusumbua sana wewe akili kipindi unakaribia kwenye ndoa yako na Erick”
“Mmmh unamsema Sia huyo!”
“Ndio huyo huyo, kwanza Sia anaonekana kuwa na matatizo ya kisaikolojia, halafu kila anayetambua yupo karibu na wewe anaanza kumwambia kuhusu Angel. Hebu fikiria, kakutana na mimi siku hiyo akaanza kuniambia sijui Angel sio mtoto wa Erick, yani nilimuangalia na kutamani kumzaba vibao, hata kama sio mtoto wa Erick basi yeye inamuhusu nini? Kwanza siri ya mtoto aijuaye ni mama. Akaanza kuniambia, naomba nikupeleke kwa baba mzazi wa Angel, yani kiukweli yule mwanamke sio mtu mzuri na mambo yako wewe yanamuhusu nini na anayajuaje?”
“Kwahiyo na wewe unaamini kuwa Angel sio mtoto wa Erick?”
“Mmmh sio naamini, bali mimi ukweli naujua vizuri, halafu huwezi amini hii kitu ni leo mume wangu ndio kaniambia sijui alikutana na Angel pamoja na Erick, basi alivyorudi nyumbani akasema, ana furaha sana. Nikamuuliza kwanini, akasema kuwa sikudhani kama Erick angeweza kumpenda vile Angel ukizingatia sio mtoto wake kabisa, siku zote nilikuwa nataka kumlea Angel ila kwa upendo niliomuona nao Erick basi naamini Erica ana furaha sana kuwa nae”
“Kumbe ulikuwa hujui!”
“Ndio nilikuwa sijui, ila mimi siku zote nakwambia ni mbea sana sema sifatilii mambo yasiyonihusu, sasa yeye kumwambia kila aliyekuwa karibu yako ni nini? Tumaini anaujua ukweli?”
“Mmmh! Nadhani anajua, familia ya wakina Erick ipo tofauti sana, wana upendo wale. Yani Tumaini licha ya ukorofi wake ila ana upendo mkubwa sana kwa watoto, na ukimpelekea mtoto wako usifikiri atamtenga na watoto wake, anajua sana kulea. Hata Angel aliishi nae kipindi akisubiria mitihani ya mwisho”
“Basi tulia, nitajua cha kufanya na huyu Sia. Nataka kujua ni kwanini anapenda kufatilia mambo yako na anapata faida gani, najua Tumaini hawezi kumfokea sababu ni shoga yake, il hilo jambo la Sia limeniuma na kufanya nije siku ya leo kukueleza hayo”
“Nashukuru sana, nami nimeelewa vizuri tu, hakuna tatizo”
Waliongea na mambo mengine mbalimbali na kisha kuagana ambapo Fetty aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake.

Jioni ya leo wakati baba Angel anarudi toka kumpeleka mwanae shuleni, moja kwa moja alipitia nyumbani kwa Sia, ambapo alimkuta, kama kawaida Sia alikuwa akitabasamu alipomuona na kutaka kwenda kumkumbatia ila alipomsogelea baba Angel alimdaka Sia kwa kibao kwenye shavu, ambacho kilimfanya Sia hadi aanguke chini na kuanza kujiliza,
“Jamani, kwani nimefanya nini?”
Alikuwa akilia huku akishikilia shavu lake, baba Angel aliinama pale chini na kumwambia,
“Wewe mjinga si nilishakwambia achana na familia yangu”
Kisha baba Angel aliinuka na kumpiga teke Sia, teke lile lilimsukuma Sia kidogo na kumfanya ahisi hata maumivu ya lile teke, basi akainuka taratibu,
“Kumbe una hamu Erick ya mimi kuanza tena kuifatilia familia yako, yani kuja kunipiga hivi kweli!!”
“Hivi unafikiri mambo yako uliyoyafanya siyajui, hivi wewe wa kwenda kupanga na mtu ili ambake mtoto wangu! Una akili kweli wewe!! Tena nadhani hela zangu mwenyewe nilizokuwa nakupa ndio ulikuwa unaenda kufanyia huo uovu wako, unaniletea ukichaa wako mimi!!”
“Nisamehe bure tu, ila mimi sijafanya hivyo kwa kutaka kumuharibia mwanao ila mimi namuokoa yule mtoto asije kutembea na kaka yake, unajua Samir ni kaka yake?”
“Kaka yake kivipi?”
“Samir ni mtoto wa Rahim, ndiomana nilikuwa nafanya Angel awe mbali na Samir”
“Halafu abakwe na kijana uliyemuandaa wewe!!”
“Hapana, yule kijana asingembaka kihivyo”
“Unajua wewe mwanamke ni kichaa eeeh!! Sikia nikwambie, Angel ni mtoto wangu na kama huyo Samir ni mtoto wa Rahim basi ndio vizuri atakuwa na Angel maana Angel ni mtoto wangu, unajifanya hamnazo, basi mimi ndio hamnazo zaidi yako”
“Usiwe hivyo Erick, hebu fikiria wewe watoto wako usikie wameoana utajisikiaje? Kumbuka Rahim hajapenda kuwa na watoto kila mahali imetokea tu, na kuhusu huyo Angel ni nyie ndio mmemfuga ili asimjue baba yake, sio vizuri hivyo. Na mimi nitamwambia ukweli Rahim”
Baba Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu zaidi, kisha akamsogelea na kumzaba vibao visivyokuwa na idadi halafu akamkunja na kumwambia,
“Ole wako, mjinga wewe nitakutia ngeu. Jitie tu akili zimekuruka”
Halafu baba Angel akaondoka zake na kumuacha tu Sia pale akilia huku akishika mashavu yake.

Baba Angel alifika nyumbani kwake usiku, na akamuita Junior na kumwambia kuwa kesho yake ataenda kununua nae vitu na kwenda kumkabidhi shuleni, hapakuwa mbali ila ilikuwa ni shule ya bweni.
Kisha alipomaliza ndio alienda kuongea na mke wake, kwa wakati huo hata hakuwa na ya kuongea mengi kwani alikuwa na uchovu mwingi alimwambia tu mkewe kuwa siku ya kesho kutwa ndio angesafiri sababu sehemu yenyewe anatakiwa Jumatano, mkewe alimuelewa na hakuwa na tatizo nae juu ya hilo,
“Kwahiyo utasafiri na ndege au basi?”
“Nitasafiri na basi tu”
“Sawa, hakuna tatizo basi”
Muda huu waliamua tu kulala kutokana na uchovu.
Basi kulipokucha, baba Angel alijiandaa na moja kwa moja kuondoka na Junior kwenda kununua nae mahitaji yani Junior hakudhani kama ingewezekana kweli kwa siku hiyo kupelekwa shuleni ila hakujua vizuri baba Angel huwa akiamua lake basi ameamua tu.
 
SEHEMU YA 306

Leo, Elly hakwenda shule sababu aliona kama mama yake hana hali nzuri, alimua kukaa nae nyumbani tu,
“Elly jamani kwanini hukwenda shule?”
“Mama unanificha tu ila nakuona kuwa haupo sawa kabisa, angalia mashavu yako yalivyovimba hivyo, toka jana huniambii ukweli ila mama haupo sawa”
Mama Elly aliinama chini na kulia ambapo mtoto wake alimsogelea karibu ili kujua kinachomliza mama yake,
“Kwani tatizo nini mama?”
“Unajua sikufikiria kumpata mtoto mwenye kujali na mwenye upendo kama wewe Elly, kwakweli mwanangu upo tofauti sana. Ni kweli sipo sawa ila hii sio sababu ya kukufanya wewe usiende shuleni jamani!!”
Mara simu ya mama Elly iliita na kuongea nayo pale, na baada ya kuikata alimuangalia mwanae na kuinuka,
“Sasa nimepata nguvu, unajua nini sina hela mwanangu halafu Amina nae si unaona kuwa anahitaji matibabu kwasasa, sema kuna jambo limetokea”
“Jambo gani mama?”
“Yule dada yangu wa mkoani, amesema kesho nimsafirishe Amina, na yeye atampokea kwahiyo sasa ngoja nimuandae Amina kwaajili ya safari”
Alienda kujiandaa kwa muda huo bila ya kujali kuwa kavimba mashavu au la ila alijiandaa haraka haraka na kwenda kumtafutia mkoba Amina wa kuwekea nguo zake ili aweze kumsafirisha vizuri.

Muda huu Tumaini alienda nyumbani kwa mama Angel kuongea nae mawili matatu maana kuna ujumbe aliupata ndio alikuwa amemletea ujumbe huo,
“Niambie wifi yangu”
“Kheee leo naona umekuja na furaha hadi kuniita wifi!!”
“Aaaah jamani, kawaida tu ila nina maongezi na wewe. Tupate mahali tuzungumze maana humu ndani kwako siku hizi naogopa, hivi Erica yupo?”
Mama Angel alicheka na kumjibu wifi yake,
“Erica yupo shuleni, anaogopewa eeeh! Ila twende sebule ya juu kule”
Basi wakaenda zao hadi sebule ya juu na kuanza kuzungumza,
“Kwanza kabisa yule mama Sarah ulimtafuta?”
“Kheee umesahau wewe kuwa ulitapeliwa na Derrick sijui hela pamoja na namba ya huyo mama Sarah!”
“Dah eti nilisahau jamani loh! Basi nimepata habari za mama Sarah, unajua mimi sio mbea ila huwa naletewa habari tu usije sema Erica karithi kwangu, akuuu Erica karithi kutoka kwenye ukoo wako”
“Aaaah jamani, haya habari gani hizo?”
“Ni hivi, nasikia mama Sarah alikuwa akiishi na mwanaume ila huyo mwanaume alikufa, toka hapo yule mama Sarah nasikia kazi yake ni kuiba waume za watu tu”
“Mmmh!!”
“Sasa nina mashaka, kama anakufahamu basi kuwa makini sana na mumeo maana kwa niliyoyasikia kumuhusu nikanyoosha mikono juu”
“Ila hivi nafahamiana nae kweli!!”
“Anadai anafahamiana na wewe, kingine kilichonileta sasa”
“Eeeh kipi hiko?”
“Kuna kijana mmoja ni dereva bajaji, alikuja nyumbani kwangu jana, akisema kuwa alikuwa na mahusiano na Angel, halafu kuna siku sijui Angel alipoteza fahamu basi akambeba ili kumsaidia ila akatokea kijana ambaye alidai kuwa na mahusiano na Angel pia, yule kijana akampiga sana hadi alikuwa amelazwa, ndio ametoka, kaja jana nyumbani kwangu akiwa anachechemea. Unajua sijaelewa kabisa ndiomana leo nimekuja huku”
“Kheee, ngoja nikusimulie yaliyotokea yani hadi tumeamua kumpeleka Angel shule mapema kabisa”
Basi mama Angel alianza kumsimulia toka alipowasiliana na mama yake na jinsi Angel alivyomsimulia, kisha akamwambia,
“Ila nahitaji kuonana na huyo kijana ili niongee nae vizuri maana kuna mambo nataka kumuuliza”
“Yupo tu, na uzuri napafahamu hadi nyumbani kwao, anaishi na bibi yake. Hata sielewi alianza lini mahusiano na Angel jamani, mambo haya loh!!”
Walizungumza tena, ila Tumaini alipigiwa simu kwahiyo muda huo huo akaaga na kuondoka zake.

Tumaini, leo hakutembea na gari kwahiyo akiwa njiani kuna mtu alimsimamisha na alipomuangalia mtu huyo alikuwa ni Sia, basi alianza kumsalimia pale na kumuuliza,
“Mbona umejitanda hivyo? Unajua hadi sikukufahamu!”
Sia akajifunua kagha alizokuwa kajifunikiza kiasi,
“Kheee mbona umevimba mashavu hivyo!”
“Mambo ya mdogo wako hayo?”
“Ni Erick ndio kakufanya hivyo jamani!Imekuwaje tena? Hayo mambo yalikuwa zamani, imekuwaje kwani?”
“Yani hata mimi simuelewi, nilikuwa nyumbani kwangu ila kuna kijana mmoja hivi huwa anakuja kunisaidia baadhi ya kazi nyumbani kwangu, mara akaja Erick, sijui akafikiria nini kuhusu mimi na yule kijana, jamani alianza kunipiga vibao visivyokuwa na idadi. Sijui kwanini Erick ananifanyia hivi! Ana maisha yake kwasasa, ana mke na watoto ila kwanini ananionea wivu mimi!!”
“Unajua sikuelewi Sia, yani Erick akuonee wivu wewe?”
“Kama huamini mpigie hapo simu muulize kama jana hajaja kwangu na kunipiga?”
Kwakweli Tumaini hakuyaamini maneno ya Sia kabisa, basi alichukua simu yake na kumpigia kaka yake, alivyosalimiana nae tu alimuuliza,
“Eti, Erick, nasikia jana ulienda nyumbani kwa Sia na kumpiga sana”
“Huyo mwanamke ni kichaa, najua lazima kakuletea hayo maneno akifikiri kuwa wewe ni mtetezi wake, tena mwambie akiendelea nitamkata miguu yake kabisa”
Simu ikakatika, kisha Tumaini alimuangalia Sia na kumuuliza,
“Kwani ulimfanya nini?”
“Nimfanye nini unadhani? Ni ile tu mimi kumtetea yule mkaka basi ndio imekuwa tatizo, yani kama kaka yako ananipenda si anioe tu nijue moja kuliko kunifanyia hivi mtoto wa watu mie, na mimi nastahili kupendwa, nastahili kudekezwa kama anavyomdekeza Erica”
“Mmmh pole sana”
“Asante, ila naomba unisaidie namba ya mama Erick tena”
“Unataka kumueleza huu ujinga?”
“Hapana, ni vitu vingine kabisa. Aliniambia niwe namwambia maendeleo ya Elly shuleni, naomba namba yake tena maana mimi nimebadili simu ile nyingine iliharibika”
“Mmmh!”
Tumaini aliguna ila alimpa namba na kuagana nae, kisha kila mmoja kuelekea kwenye safari yake aliyokuwa akienda.
Ila Tumaini aliondoka hapo huku akijiuliza maswali mengi sana,
“Yani sielewi, kweli kabisa Erick ampige huyu mwanamke sababu ya wivu! Hapana kuna kitu kingine huyu mwanamke kakifanya, lazima ni hivyo”
Wakati Tumaini akiendelea mbele, kuna mahali alimuona kaka yake akiwa kasimama na mwanamke, basi hakusita kumfata na kumsalimia, kidogo kaka yake akajiuma uma midomo na kumtambulisha Tumaini,
“Aaaah huyu ni mdogo wangu anaitwa Tumaini, halafu mdogo wangu huyu ni wifi yako anaitwa Mariam”
Tumaini akaitikia pale na kumvuta kidogo kaka yake pembeni huku akidai anataka kuongea nae kidogo,
“Kaka Deo jamani hapana kwakweli, kwanini kutufanyia hivi wanawake? Unajua na mimi ni mwanamke tena nimeolewa na ninaumia sana kuona mwanamke mwenzangu anafanyiwa kinyume. Kweli unapata ujasiri gani wa kunitambulisha kuwa yule ni wifi wakati mimi namjua mama Junior?”
“Sikia nikwambie kitu, siku zote hutakiwi kuwa upande wa wifi yako ila unatakiwa kuwa upande wa kaka yako. Hiko ndio kitu ambacho ulikuwa ukigombana na Erick kipindi kile, sababu ukiwa tayari na uelewano na wifi Fulani basi unaona ndio maisha ya uwifi yameishia hapo ila hapana, mwache kaka yako awe huru na afanye anachojisikia”
“Sio kwa stahili hii, kumbuka umeoa, na licha ya kuoa yule mwanamke anavumilia sana kukulelea mitoto uliyozaa huko, badala na wewe utulie ndio kwanza unafanya mambo ya ajabu. Tena hata Junior humlei wewe maana alikuwa akimlea mwenyewe na sasa analelewa na Erick ila mitoto yako anailea pale kwa upendo kabisa, unawezaje kumsaliti mwanamke kama yule?”
“Mambo ya ndani huwezi kuyajua wewe, fanya yako niache na maisha yangu”
Tumaini alimuangalia kaka yake kwa gadhabu sana kiasi kwamba aliondoka hapo bila hata kumuaga huyo wifi mpya aliyetambulishwa na kaka yake, yani alijikuta tu akisikitika kuhusu wifi yake aliyemzoea.
 
SEHEMU YA 307

Baba Angel alipomaliza kumkabidhi Junior shuleni, alitoka pale na moja kwa moja kwenda shuleni kwakina Erick ili kumchukua Erick na hapo ilibidi apate ruhusa toka kwa madam Oliva, maana alikuwa ni mwalimu wa nidhamu na ilikuwa ni zamu yake kwa wiki hiyo, basi baba Angel alienda ofisini kwake na kuongea nae,
“Ila swala langu umelifanyia kazi?”
“Swala gani tena?”
“Si lile la mkeo na yule shoga yake?”
“Dah ndio unanikumbusha ujue, yani mimi mambo ya wanawake huwa sifatilii sana wala nini. Kwahiyo nipe ruhusa mwalimu, halafu nikuombe kitu kama siku kukiwa hakuna masomo jioni naomba umpe ruhusa Erick ili dereva aweze kumchukua”
“Kwani atakuwa anaenda wapi?”
“Ni kwenye kiwanda changu, nahitaji Erick awe anasimamia japo kwa ufupi tu, najua kuwa anasoma na masomo yanambana sana ila nahitaji awe anapata muda angalau hata dakika kumi na tano kuwepo kiwandani kwaajili ya kufunga mahesabu”
“Oooh hayo ni mambo ya maendeleo na ni mazuri sana, ila kuna kitu naomba nikusaidie”
“Kitu gani?”
“Mara moja moja niwe nampeleka Erick huko kiwandani na nimsubiri amalize na kumrudisha nyumbani ili pia kutunza muda wake vizuri wa kimasomo na kutokupoteza uelekeo”
“Mmmh haya hakuna tatizo”
“Kwahiyo tunaanzia leo, yani hapa naacha mtu ili na mimi nikaone kidogo huko kiwandani”
Basi baba Angel hakuona kama ni tatizo, akaamua kuondoka na madam Oliva huku akiambatana na Erick hadi kiwandani ambapo walionyeshana pale, na baba Angel alimuelekeza Erick cha kufanya kipi akiwa hayupo, na mambo mbalimbali kisha wakaondoka na hivyo ikambidi baba Angel kumpitisha kwanza madam Oliva nyumbani kwake.
Walifika hadi kwa madam Oliva ambaye aliwakaribisha vizuri kabisa,
“Karibuni jamani, sio vizuri kuishia nje, karibuni hata ndani kwangu mnywe japo maji”
Baba Angel alikumbuka siku ambayo yule madam alimwekea dawa, na kujikuta akigoma tu na kudai kuwa wanaharaka sana, muda huo huo Steve nae aliyeonekana kuwa alitoka ndio alikuwa akirudi tu taratibu akitembea, kwahiyo alipoona gari pale getini alisogelea ili kuangalia ni nani, akakutana na baba Angel sasa ambapo baba Angel alimsikitia Steve tu alipomuona ila hakuongea kitu zaidi ya kuaga na kuondoka zake.
Wakiwa njiani Erick alimuuliza baba yake,
“Ila baba, sijakuuliza swali hili hivi duka letu kule limeishia wapi? Halafu huyu si ndio alikuwa akiuza duka letu?”
‘Ndio, ila huyu hauzi tena, natafuta mtu mwingine ila muaminifu wa kufanya hivyo, sema bado sijampata kwahiyo duka limefungwa tu”
“Niruhusu mimi nitafute mtu”
“Kheee utampatia wapi wewe?”
“Niruhusu tu baba, utaona na duka litafanya vizuri”
“Nakuamini mwanangu, basi muda huu twende kwanza tukatembelee pale dukani ingawa muda umeenda ila nitakuelekeza vichache pale na utaweza kujua cha kufanya”
Kisha safari kwa muda huo ikawa ni moja kwa moja hadi dukani ambako alikuwa akiuza Steve na kumfanya baba Angel amuelekeze vizuri mwanae pale, kwahiyo muda walioondoka kurudi nyumbani ilikuwa ni muda umeenda sana na kulikuwa na uchovu haswaa kwa baba Angel ambaye alikuwa na mizunguko sana kwa siku hiyo.

Walipofika nyumbani, ni moja kwa moja kujindaa tu kulala kwahiyo vitu vingi baba Angel hakuongea na mke wake hadi palipokucha, ni mama Angel aliyemuamsha mumewe mapema maana walishaongea kuhusu hiyo safari, basi aliamka na kwenda kuoga na kujiandaa kisha walikaa kidogo na kuongea,
“Hivi unajua mume wangu hatujaongea mambo mengi sana?”
“Ni kweli ila hii safari nayo ni ya gafla sana”
“Ila kwanini umechagua kupanda basi na sio ndege?”
“Nikirudi kutoka hiyo safari utajua vizuri mke wangu ni kwanini sijapanda ndege, wenyeji watanipokea kutoka kwenye basi na sio ndege”
“Sawa nimekuelewa”
Muda ulifika na baba Angel kutaka kuondoka, kwani tayari alishaongea na dereva ila mkewe alimwambia,
“Subiri kidogo tuondoke wote, maana nitakusindikiza hadi stendi kuu”
“Mke wangu jamani, baki tu na mtoto”
“Hapana, siwezi kubaki na kuacha bila kukusindikiza”
Ilibidi baba Angel akubali tu ingawa hakutaka kumchosha mke wake, kwahiyo waliondoka pale kuelekea stendi, walipofika moja kwa moja mama Angel alimsindikiza mumewe kwenye basi alilotakiwa kupanda ila kwa bahati nzuri au mbaya, lile basi lilikuwa ndio basi ambalo Sia alimpakiza yule mtoto Amina, kwahiyo wakati Sia anashuka kutoka kumuweka Amina kwenye siti ndio akakutana na baba Angel na mama Angel mlangoni, basi Sia akasema,
“Jamani Erick kama ulikuwa unakuja kusindikizwa na mkeo si ungeniambia tu ili nisihangaike kuja kukusindikiza?”


Ilibidi baba Angel akubali tu ingawa hakutaka kumchosha mke wake, kwahiyo waliondoka pale kuelekea stendi, walipofika moja kwa moja mama Angel alimsindikiza mumewe kwenye basi alilotakiwa kupanda ila kwa bahati nzuri au mbaya, lile basi lilikuwa ndio basi ambalo Sia alimpakiza yule mtoto Amina, kwahiyo wakati Sia anashuka kutoka kumuweka Amina kwenye siti ndio akakutana na baba Angel na mama Angel mlangoni, basi Sia akasema,
“Jamani Erick kama ulikuwa unakuja kusindikizwa na mkeo si ungeniambia tu ili nisihangaike kuja kukusindikiza?”
Wote walijikuta wakimshangaa Sia, ni pale baba Angel aligundua kuwa huyu mwanamke ana matatizo ya akili, ila gari nalo lilikuwa linataka kuondoka, basi baba Angel akasogea karibu na mkewe na kumwambia,
“Tafadhari mke wangu usimsikilize huyo mwanamke, ona kama mgonjwa wa akili anaongea peke yake, nakuomba kwa muda huu urudi tu nyumbani”
Akambusu na yeye kupanda ndani ya lile basi halafu likaondoka maana ilikuwa kama linamsubiria yeye, basi mama Angel nae alikuwa akirudi kwenye gari yao ila Sia alimfata kwa nyuma na kuongea nae tena,
“Unajua kuna muda huwa unahisi mimi ni kama chizi ila kuna muda huwa unahisi naweza kuwa naongea ukweli, pole sana sababu hunielewi ila ukitafakari utanielewa vizuri sana”
Mama Angel hakumjibu na kwenda hadi walipoacha gari lao, na kutaka kufungua mlango ili apande ila kabla hajafungua ule mlango, Sia alienda mbele yake, hadi ikabidi aongee,
“Kwani una matatizo gani wewe?”
“Matatizo unayo wewe ambaye hujiamini”
“Unajua wewe, kweli una kichaa. Sasa mimi nisijiamini kwa lipi? Hebu sogea hapo nipande”
Sia alisogea ila mama Angel alipofungua tu mlango na yeye alifungua wa nyuma na kupanda pia, mama Angel hakutaka kuongea sana na kuondoa gari lile mahali pale, maana yeye alivyoamua kumsindikiza mumewe aliondoka na mumewe tu kwahiyo hawakuondoka na dereva.
Basi alifika mahali akasimamisha akapaki gari pembeni sasa na kumuuliza Sia,
“Kwani tatizo lako ni nini? Kitu gani unahitaji toka kwangu?”
“Kwani hujui? Ninahitaji kuwa mke mwenzio, ni hivi Erick hataki kunioa sababu anajua kuwa wewe utachukia na kudai talaka ndiomana anaogopa kufanya hivyo, ila wanawake tuwe na huruma jamani hebu tuhurumiane, kubali Erick anioe na mimi ili nami niwe na mume”
Mama Angel akacheka kidogo na kumuuliza,
“Kwani huyo wa kukuoa ni mimi au Erick?”
“Ni Erick”
“Sasa mbona unakuja kuniomba mimi? Unajua una wazimu wewe eeeh! Ngoja nikwambie, nahisi hujui kuhusu mimi vizuri, kwenye ukoo wetu hakuna mambo ya uke mwenza, yani sahau kabisa kuwa utaolewa ikiwa mimi nipo ndani yani sahau kuhusu hilo. Halafu jambo lingine, wewe ni mwanamke wa aina gani ambaye huelewi neno sikutaki? Huyo Erick ulikuwa nae na alikufanyia vituko vyote vya dunia ila ukajifanya unapenda sana, saivi unaaanza kuhangaika kama paka shume. Hivi unadhani ujinga uliokuwa ukifanyiwa na Erick anaweza kunifanyia mimi? Sikia nikwambia, kama mwanamke unatakiwa uishi kwa kujitambua sio kuendeshwa kama toy, wewe unaona kabisa kwa matendo ya huyu mwanaume hakuna upendo hapa bado unakomaa tu kumfatilia, na mpaka leo hujakata tamaa, hivi ni mwanamke wa aina gani wewe?”
“Mimi ni mwanamke wa kawaida tu kama wanawake wengine, sikia nikwambie Erica, nimejua kuteseka kipindi nikiwa kwenye mahusiano na huyo Erick, muulize kanitoa mimba ngapi? Muulize mara ngapi nimemfumania na nikamsamehe tu, muulize ni mara ngapi alikuwa akinikosea ila nikimuuliza ananipiga mimi, ila sababu nilimpenda basi nilivumilia kila kitu, nilikuwa naenda kwao mimi, nasafisha chumba chake, nafua kila kitu chake, nikiamini kuwa kuna siku nitaishi nae kama mke na mume, usinilaumua wala usinione mjinga. Mbona wewe umezaa na Rahim? Si uliamini atakuoa pia, yani maisha ndivyo yalivyo kwahiyo usinishangae mimi”
“Kwahiyo kama nilizaa na Rahim ndio unataka nimkazanie huyo Rahim anioe? Akili zako ziko wapi Sia? Mtu ukishafanya kosa moja basi usitake kulirudia kosa hilo, ukianguka unainuka na kujikung’uta kisha maisha yanaendelea”
“Ungetambua hayo basi ungemuonyesha Angel baba yake”
“Baba yake gani sasa? Angel ni mtoto wa Erick, hutaki nenda kachote maji uoge ili upate nguvu za kuendelea kubisha”
“Kwahiyo Rahim?”
“Huyo unamjua wewe, ila mama wa Angel ni mimi na baba wa Angel ninayemtambua ni Erick. Kama Angel ulimzaa wewe basi itakuwa baba yake ni Rahim ila kwa niliyemzaa mimi ni mtoto wa Erick”
“Yani unajibu kwa madaha kiasi hiko!”
“Ndio, naomba ushuke tu kwenye gari yangu kiroho safi wala sitaki kugombana na wewe”
Na kweli leo Sia hakubisha wala nini kwani moja kwa moja alishuka kwenye lile gari na mama Angel aliendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 308

Vaileth hakufanya kazi yoyote siku hiyo maana alikuwa na kibarua cha kumbembeleza mtoto Ester tu, ukizingatia mama yake alijua kuwa atawahi kurudi ila haikuwa hivyo, alichelewa kurudi, basi wakati akimbembeleza ndipo alikuja shangazi yao na wakina Erica yani Tumaini, kwahiyo alimkuta Vaileth akimbembeleza mtoto,
“Kheee mama yake yuko wapi?”
“Alitoka asubuhi kwenda kumsindikiza baba, maana baba leo kasafiri”
“Loh! Hawa nao jamani, halafu mbona safari za kimya kimya hizo hata hawasemi loh!”
Basi alikaa kimya na kumtaka mtoto na yeye akimbembeleza mtoto yule, basi akamwambia Vaileth akalete vitu vitu vya kuchezea mtoto ili amzubaishe navyo, ambapo Vaileth alifanya vile, na kati ya vile vitu alikuwepo na mdori ambaye aliwahi kuletwa na Sarah, basi Tumaini alipomshika yule mdori alijikuta akikumbuka kitu,
“Mbona kama namjua huyo mdori, au nilikuwepo wakati wakinunua!”
Vaileth alisikia na kujibu,
“Hapana, huyo mdori aliletwa na binti mmoja hivi anaitwa Sarah ni rafiki mkubwa sana wa Erick”
“Oooh sawa, nashukuru kufahamu”
Basi akawa anambembeleza mtoto kwa kumchezeshea yule mdori ni kweli mtoto alinyamaza huku akiangalia jinsi yule mdori alivyo, alicheza cheza nae pale yule mtoto hadi mwisho akalala pale pale na hata Tumaini nae alijihisi uchovu na kulala pia kwenye kochi.
Mama Angel aliporudi aliwakuta pale sebleni na kumshtua wifi yake, wakasalimiana pale,
“Ila wewe, unawezaje kwenda kumsindikiza mumeo na kuacha mtoto mdogo hivi nyumbani!”
“Jamani, kwahiyo hakuna nitakachoweza kumfanyia mume wangu sababu nina mtoto mdogo!!”
“Hapana sina maana hiyo, ila kwanini usingeenda nae tu! Mtoto Amelia sana huyu”
Basi mama Angel alimchukua mwanae ambaye alimka pia kwa muda huo na kwenda nae chumbani ili kumnyonyesha mwanae, na kweli alienda na kumnyonyesha huko halafu mwanae akalala na kumuacha chumbani amelala kisha akatoka tena sebleni ambapo wifi yake akamuuliza,
“Kwani ulipotoka kumsindikiza mumeo ulipitia wapi?”
“Sijapitia popote, ila kuna chizi mmoja kanichelewesha sana”
“Chizi gani huyo?”
“Si huyo Sia, jamani kwa kifupi ni kwamba nimemchoka Sia, yani nimemchoka kabisa, ana mambo ya ajabu sana tena hajifikirii wala nini”
“Hata mimi alikuwa rafiki yangu ila kwasasa nimemchoka pia, natumai hajakuharibia siku yako. Naomba Mungu akusaidie uweze kupambana na huyu adui maana naona Sia kawa adui yako kabisa”
“Amen, Mungu anisaidie tu kwakweli. Ananiandama na watoto wangu balaa, akianza balaa zake unaanza kuwaza ni kwanini nimemfahamu huyu kiumbe jamani.”
“Pole sana, tuachane na huyo mtu kwasasa. Ngoja nikuulize tu, hivi huwa unaongea na dada yako Bite”
“Kuongea kuhusu nini?”
“Naomba umshauri dada yako atafute mwanasheria kwaajili ya kusimamia mali za Junior, unajua Junior nae anastahili kupata urithi wake. Nimefikiria sana juu ya hilo nikaona nije kuongea nawe hivyo, ukizingatia kwa niliyoyaona jana”
“Yapi hayo?”
“Sikwambii kwa ubaya, ila jana nimekutana na kaka Deo akiwa kasimama na mwanamke mwingine, halafu bila aibu amanitambulisha kwa huyo mwanamke kuwa ndio wifi yangu, kwakweli nimeumia sana, maana mimi ni mwanamke, na dada Bite namfahamu vizuri sana, ni mwanamke mwenye roho nzuri na asiye na makuu ni kwanini amfanyie hivi basi! Nimeumia, naona pale hakuna chochote atakachoambulia Junior maana kaka yangu siku zote hajamuhesabia Junior kama mwanae, ni tatizo pia kwa wifi yangu ukizingatia hajazaa na kaka Deo, kiukweli nimemuonea huruma sana mama Junior, msaidie kwa hili”
“Nashukuru sana, ila kwanini baadhi ya wanaume wapo hivi jamani!! Hivi mtu kama dadabyangu ndio wa kumfanyia ujinga kiasi hiko kweli!! Masikini, mwanamke wa watu ni mpole na asiye na makuu ila hana bahati na mapenzi kabisa, sijui kwanini yani”
“halafu kitu kingine ambacho naona wazi kaka Deo hajamfanyia sawa mama Junior, ni ile hali ya kumkataza kufanya kazi, ili tu amlelee watoto wake, masikini dada yako ni mpole na ana utu, akakubali hiyo hali na kukaa tu bila kazi. Naona cha muhimu pia ni kumsaidia apate kazi, kumsaidia pia apate urithi wa mumewe maana yule alikuwa ni mke halali wa ndoa licha ya talaka ile”
“Unajua katika maisha kuna mambo tunayafanya halafu badae tunakuja kujutia sana na kujiuliza kuwa tumeanzaje kufanya mambo ya namna hii. Ila kabla ya kwenda kufungua nae kesi, nitamtafuta kwanza Dora na kuongea nae ili nisikia anasemaje juu ya hatma ya mali za watoto”
“Hapo sawa kabisa, ila Dora atakubali kurudisha kwa amani kweli?”
“Kumbuka Dora kaokoka kwasasa, natumaini atakubali tu, tukiona anabisha basi tutatumia hata viongozi wa kanisa lake kumshauri. Ila kaka yako anachofanya sio sawa kabisa, ndiomana dada yangu hakutaka kuolewa tena, bora angeishi kwa maisha aliyojiamulia kuliko hiko alichofanywa na kaka yako”
“Ila sio ndio mtuchukie ukoo mzima, halafu usimwambie ukweli kuhusu hayo, yani mwambie tu unashughulika kwaajili ya Junior”
“Siwezi kumwambia kuhusu hayo, mambo ya mapenzi, unaweza sema hapa halafu ugeukwe na uonekane ni mnafki na una lengo la kubomoa ndoa yao. Ila nitashughulika na hayo maana roho inaniuma pia”
Waliongea pale na Tumaini aliamua kuaga na kuondoka zake.

Jioni ya siku hii wakati Erica amerudi tu kutoka shuleni, muda mfupi Junior nae alirudi na kumfanya mama Angel amshangae,
“Wewe Junior jamani, si jana ndio umepelekwa shule wewe!!”
“Ni kweli mamdogo ila kiukweli bamdogo kanichukua haraka haraka sana, kuna vitu nilisahau. Kwahiyo kesho nitatokea hapa kwenda shuleni”
“Kheee Junior jamani”
Basi Junior alienda chumbani kwake, muda kidogo Erick nae alirudi basi mama yake alimuita na kuongea nae,
“Kwahiyo Erick ulipitia kiwandani?”
“Ndio mama”
“Ngoja nikwambie kitu mwanangu, sio kila siku ndio uwe unapitia kiwandani. Kumbuka una masomo na pia unahitaji muda wa kupumzika, sijui unanielewa”
“Nakuelewa mama”
“Vipi Sarah hajambo!”
“Leo sijaonana nae, hajafika shule leo”
“Oooh labda anaumwa jamani, basi na kesho asipokuja utaniambia Erick. Sawa mwanangu”
“Sawa mama”
Kisha Erick akaenda chumbani kwake kubadilisha sare za shule, muda huo huo akafatwa na dada yake ambaye alipoingia tu alimuuliza,
“Kwanini mama anapenda sana kumuulizia Sarah?”
“Sijui ila nadhani ni kwavile Sarah ni mcheshi na ana upendo ndiomana mama anamuulizia”
“Mama kajuaje kama Sarah ana upendo?”
“Si kwa zile zawadi ambazo Sarah huwa anampa mama”
“Mmmmh zawadi gani hizo?”
“Umeona kitenge alichovaa mama Juzi! Basi alipewa zawadi na Sarah”
“Mmmh!”
“Ndio hivyo, hutaki!! Unadhani sisi ambavyo hatumkumbuki mama kwa zawadi ndio watu wan je nao wapo hivyo? Wenzetu wanamkumbuka mama yetu, kwahiyo tujirekebishe”
“Haya nimekusikia, ila mimi sina hela za kumnunulia mama zawadi, nitafanyeje sasa? Naona Sarah atakuwa akiishi maisha ya kujiachia sana kama anayoishi Samia, ila mimi nafugwa sana hadi sina raha kabisa”
“Jamani Erica, raha gani unayoita wewe lakini eeeh!”
“Sikia nikwambie, Samia ana simu na anawasiliana na mtu amtakaye, akitaka mahitaji yake anapewa hela na anaenda kununua mwenyewe, kwahiyo anazunguka mwenyewe madukani na kununua atakacho ni tofauti na mimi. Nipo shuleni ila utakuta sina hata mia, kisa tu kila kitu nakula cha shule, yani siwezi kununua hata pipi, ni Samia tu huwa ananiletea zawadi mara za pipi, biskuti na keki ila mimi sina hela ya kumnunulia hata maji, mama ananipa maisha ya manyanyaso sana”
“Utaona ni manyanyaso kwasasa, ila ukikua utaona kuwa mama alikuwa akikuweka katika misingi imara, ni kweli huna hela ila huwa hutamani hela hata ukute mtu kaianhgusha ndiomana ile laki mbili ulikuja kumkabidhi mama, ni kitu gani utake mama asikununulie? Ila usijali, nitaongea na mama ili awe anakupa hata mia tano ya kulinda begi lako la shule”
“Oooh hilo swala zuri sasa, na mimi nitaweza kumnunulia mama zawadi kama huyo Sarah”
Kisha Erica alitoka, ila ilionekana wazi hakupenda kabisa mama yake kuonekana kumsifia sana Sarah, kwahiyo aliona kama Sarah anapendwa zaidi na mama yake.
 
SEHEMU YA 309

Usiku wa leo, Junior alienda kulala chumbani kwa Vaileth huku akilalamika kuhusu shule,
“Sijui ni kwanini wamenipeleka shule ya kulala huko huko, mimi siwezi sijui wana mpango nifeli hawa!”
“Hamna Junior, wanakuandalia mazingira mazuri sana, ila kwasasa unaona kama wanajisumbua ila wanakuandalia mazingira mazuri sana kwa wewe kuweza kusoma na kufika mbali. Usiwe kama wakina sisi”
“Ila mimi sitaweza kusoma nikiwa nalala shule, yani nalala mbali na wewe ndio kusoma gani huko? Nataka niwe nalala karibu na wewe ndio nitasoma vizuri zaidi”
“Mmmh sijui wewe na mamako mdogo, mtaelewana wenyewe ila asitufumanie tu maana nadhani iatakuwa ni balaa sijui nitarudishwa kijijini mweeeh!”
“Usijali, muone hivihivi huyu mamdogo na ukali wake, ila ni mpole sana hakuna mfano kwahiyo hata akitufuma atatusamehe tu”
Basi kwa siku hiyo walilala vizuri kabisa, na kulipokucha, Junior alienda kujiandaa na kuondoka zake kwenda shuleni, hakupita kumuaga mama Angel wala nini, ni moja kwa moja alienda shuleni tu.

Mama Angel alitulia nyumbani kwake na kuwasiliana na mume wake kumuuliza kuhusu huko alipoenda, na alipompigia simu tu alipokea na kuanza kuongea nae,
“Nisamehe mke wangu kwa kutokukwambia kuwa nimefika, huku mtandao unasumbua sana”
“Dah pole jamani”
“Halafu kuna baridi sana, kitu kingine sikukwambia asante sana kwa hizi shati ulizoniwekea yani leo nimevaa hii ya kitenge kila mtu ananisifia kuwa nimependeza sana, asante mke wangu”
“Asante pia mume wangu, ila kuwa muangalifu huko. Nakupenda sana”
Basi akaagana nae, na kuweka simu pembeni, muda huu alisogea Vaileth karibu na kumwambia mama Angel,
“Mama, hongera sana.”
“Hongera ya nini?”
“Huwa siku zote natamani kusema ila nashindwa, kwakweli maisha yenu yapo vizuri sana yani nyie mnapendana hadi shetani mwenyewe anaogopa”
Mama Angel akacheka na kumwambia Vaileth,
“Usijali na wewe siku moja utampata mwanaume wa ndoto zako, ambaye atakupenda na kukujali kwa kila hali”
“Asante mama”
Ila kabla hajakaa sawa, alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Dora yani kabla mama Angel hajachukua hatua ya kumfata Dora tayari Dora alishafika nyumbani kwake.
Basi akaamua kwenda nae kwenye bustani ili kufanya nae mazungumzo,
“Bora leo umenikumbuka Dora”
“Mmmh kilichonileta hapa sasa mmmh!”
“Nini tena?”
“Unajua nahitaji kukaa na dada yako ili tujue cha kufanya na watoto wa marehemu wote wapate haki zao, maana kuna wangu Jesca, kuna wa dada yako, Junior na kuna yule James. Nahitaji wapate haki zao”
“Kwakweli Dora umebadilika ndugu yangu, tena umebadilika sana tu.”
“Unajua kitu gani? Kama kawaida yangu ya kutaka kuanza shari na mwanamke anayeishi nae Steve, ila nilivyofika mlangoni kwa yule mwanamke shari yote iliniisha maana nilimuona mtoto wa James ndio kawa mlinzi, kweli baba yao atakuwa anafurahi huko alipo? Hata kama wafu hawasikii chochote ila hiki nilichofanya naona sio kizuri kabisa mbele za Mungu hata mbele za wanadamu”
“Ila ni vizuri kama umeamua hivyo, kwa tupange sasa itakavyokuwa ili wote kupata haki yao na kama kusimamiwa basi wasimamiwe na mama zao”
“Naona wanaweza kujisimamia labda Junior sababu anasoma ila huyo James kwakweli, roho imeniuma sana kumkuta ni mlinzi”
Wakajaribu kuongea cha kufanya pale na kufikia muafaka wa kuona kuwa kipi bora na kipi kifanyike.

Siku hii Erica aliporudi kutoka shule, alimfata mama yake na kumwambia,
“Mama, kwani Erick hajakwambia?”
“Kuniambia kuhusu nini?”
“Jana nilikuwa naongea nae, wenzangu shule mama wanakujaga na hela ila mimi utakuta sina hata mia ya maji. Pale shule mbona duka lipo ila siwezi kununua hata pipi, basi Erick akasema atakwambia ili uwe unanipa angalau mia tano”
Mama Angel alicheka na kusema,
“Kweli umejanjaruka, naona ile laki mbili imekutoa ufahamu mwanangu. Toka lini ukadai hela wewe! Shule unayosoma, maji ya kunywa yapo, chai mnapewa, chakula cha mchana mnapewa tena kizuri tu haya unataka hela ya nini? Ule pipi umekuwa mtoto?”
“Sio hivyo mama, wenzangu wote wanakuja na hela shuleni na wanaweza kununua chochote kile. Ni kweli tunakunywa chai ila muda mwingine mtu unatamani soda”
“Sasa kama unatamani soda si uwe na kopo lako unamimina juisi unaenda nayo shule”
“Ila mama jamani! Haya basi”
Erica aliondoka zake na kwenda chumbani kwake, ila Vaileth alimsogelea mama Angel na kumwambia,
“Mama, ila ni vizuri ungekuwa unampa hela hata kidogo”
“Hela ya nini sasa huyu? Kwanza bado mdogo halafu kila kitu shule anakipata”
“Ni kweli ila shuleni kuna vishawishi mama, mbona Angel mlikuwa mkimpa hela?”
“Kheee muulize Angel kama kuna hela huwa anapewa hapa nyumbani! Labda apewe na baba yake”
“Ila mama, ukitaka mtoto wa kike asiwe katika vishawishi basi jaribu kumfanya asiwe na uhitaji wa lazima nje, mfano kitu kidogo kinaweza kumtia kwenye vishawishi Erica, ndiomana kipindi kile mnalalamika kuhusu ile shule na kusema kuwa Erica anaongea sana na vijana sababu wanampa mahitaji ayatakayo, haya niliongea na Angel kidogo tu akanielezea kuwa yule mwanaume alienda kutengenezewa simu sababu yule mwanaume alisema laki mbili anayo na mwisho wa siku akataka kumbaka Angel, ila mambo kama hayo si Angel angekuwa wazi tu kwenu! Naomba usinifikirie vibaya mama ila nasema sababu naelewa wazi inavyokuwa. Hivi huyo Sarah ambaye huwa unamsifia kuwa mtoto anajiongeza, ni nani huwa anampa pesa ya kufanya ayafanyayo?”
“Mmmmh!! Ila sipendi kumzoesha mwanangu hela, ila basi nitakuwa nampa japo mia tano aliyosema. Ila huyu Erica lengo lake ni kuagiza karata tu, yani akishakuwa na hela atanunua karata lazima maana anapenda sana kucheza karata”
Basi muda huo Erick nae aliwasili kutoka kiwandani sababu alikuwa anatoka shule na kupitia kiwandani kwanza halafu ndio anarudi nyumbani, baada ya salamu mama Angel alimuuliza kuhusu Sarah,
“Vipi leo Sarah amekuja?”
“Hajaja mama, nahisi labda atakuwa anaumwa”
“Jamani masikini, unapafahamu kwao?”
“Napafahamu ndio, si nishawahi kumrudisha kwao”
“Basi tufanye hivi, kama hadi kesho hajaja shule itabidi usiende kiwandani kesho, ukitoka tu njoo nyumbani ili twende kumuona Sarah nyumbani kwao”
“Mmmh mama!”
“Ndio, hakuna cha kuguna. Kwahiyo itakuwa hivyo, jitahidi kesho tufanye hivyo”
“Sawa mama”
Basi Erick akaenda kuendalea na mambo yake mengine kwani alikuwa amechoka.
 
SEHEMU YA 310

Siku ya leo Erick alipokuwa yupo shuleni, wakati muda unakaribia kutoka aliitwa na madam Oliva ambaye alimtaka waende kiwandani,
“Aaaah leo siendi madam”
“Kwanini?”
“Nataka kuwahi nyumbani”
“Sio nilivyokubaliana hivi na baba yako, basi twende leo halafu kesho ndio usiende, sawa”
Erick hakuweza kumkatalia madam hata hivyo kule kiwandani hakuwaambia kuwa siku hiyo hatoenda kwahiyo aliondoka tu na madam kuelekea huko kiwandani.
Basi walivyofika, Erick aliingia kiwandani wakati huo madam Oliva alikuwa amekaa nje ya gari lake huku akiangalia angalia mazingira ya pale, mara kuna mtu alisogea na kumsalimia,
“Habari”
“Nzuri tu, sijui tunafahamiana?”
“Hapana hatufahamiani, mimi naitwa Rahim na wewe unaitwa nani mwenzangu?”
“Mimi naitwa madam Oliva, ni mwalimu wa sekondari”
“Oooh, katika maisha yangu nilitamani sana kuoa mwalimu ila sikupata bahati hiyo unajua kwanini nilitamani kuoa mwalimu?”
“Kwanini?”
“Kwasababu mwalimu ni mtu ambaye ana maadili na huwa anafundisha vyema watoto, ana muda wa kutosha wa kuangalia watoto na pia muda wa kutosha wa kuela mume na familia sababu mwalimu habanwi sana kwenye kazi yake, tofauti na kuoa mke nesi au daktari kwani kidogo tu mara nipo shifti ya usiku, mara natakiwa siku mbili kazini yani mimi ningepata bahati ya kukutana na mwanamke mwalimu kwa hakika ningeoa upesi sana”
Basi madam Oliva alitabasamu tu, na kumuangalia vizuri Rahim aliyekuwa akiendelea kumpa sifa,
“Kwanza wewe licha ya kuwa mwalimu maana kuwa mwalimu ni sifa toshelezi ya kumfanya mwanaume apate hamu ya kukuoa, sasa nikitoa swala la kuwa mwalimu, pia wewe ni mwanamke mrembo sipati picha enzi za udogo wako, kwakweli madam wewe ni mrembo sana, una sura nzuri na umbo zuri la kuvutia, umevaa kiheshima na una vutia kwakweli”
“Dah! Hizo sifa zote kwema?”
“Kwema tu, najua ushanisoma tayari, maana mnaupeo wa kuelewa vitu zaidi ndiomana mkapendelewa na kuwa walimu wetu”
“Jamani leo kweli nimekutana na mtu maana sio kwa sifa hizi, nimekuwa mwalimu kwa kipindi chote hiki ila sijawahi pata mtu wa kunisifia kiasi hiki na kufanya nijivunie kwa kazi yangu”
“Kwanza kuna mwalimu kweli anaweza kukaa bila kuolewa? Yani akose mume wa kumuoa? Labda aamue tu, kila mwanaume anapambana apate mwanamke mwalimu na aoe mwanamke huyo, vipi madam umeolewa?”
“Khaaa jamani, mimi sijaolewa ila naishi na mwanaume”
“Oooh sifa nyingine ya mwalimu ni hiyo hapo, kuwa mkweli katika maisha. Hongereni sana walimu, Mungu kawabariki kwa kila idara. Chukua hii kadi yangu ili tuwe tunawasiliana kwa mambo mengi tu, mfano biashara na kushauriana kwani ushauri wa mwalimu huwa ni ushauri bora zaidi ndiomana mnafanya watoto wapanuke akili na kuwa viongozi wakubwa. Sifa zote zipo kwenu walimu, kwaheri”
Madam Oliva alichukua zile namba huku akitabasamu tu maana alipewa sifa zilizopitiliza kabisa.
Rahia alipoondoka tu, Erick nae alitoka kisha madam Oliva alimrudisha Erick kwao halafu yeye kwenda nyumbani kwake.

Erick alipoingia alimkuta mama yake ameshajiandaa na swali aliloulizwa kwanza lilikuwa,
“Sarah amekuja shule leo?”
“Hajaja”
“Na mbona umechelewa?”
“Nilipita kiwandani mama”
“Ila wewe dah! Haya hata usiende kubadili nguo, tutoke sasa hivi twende kumuona Sarah”
Erick hakubisha kitu chochote ila aliacha tu begi lake la shule pale sebleni na kuondoka na mama yake ambaye alimuachia Vaileth maagizo ya mtoto ambaye alikuwa amelala kwa muda huo.
Basi waliondoka na moja kwa moja walienda mpaka kwakina Sarah, na kushuka. Waligonga mlango kuna mdada alienda kufungua mlango na kuwakaribisha, Sarah walimkuta amekaa sebleni huku kajifunika na blanket halafu kuna picha alikuwa akiangalia, ila alipomuona Erick aliinuka na kwenda kumkumbatia kwa furaha yani alifurahi sana kwa Erick kwenda kumtembelea. Basi walimsalimia pale, na kumuuliza hali yake,
“Yani naumwa halafu mama nae hayupo”
“Sasa ulienda hospitali?”
“Sijaenda, sababu mama hayupo”
“Khaaa jamani, itabidi twende muda huu huu”
Mama Angel akataka muda huo huo wampeleke Sarah hospitali ila Sarah akasema,
“Dada alinipa dawa, ila nilikaa hapo nikiangalia picha ya marehemu baba yangu na nilivyomuona Erick ndio nimejihisi kupona kabisa”
Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.

Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.
Mama Angel alimuangalia Sarah kwa makini sana na kumuuliza,
“Kwahiyo huyu ndio marehemu baba yako?”
“Ndio, ni marehemu baba yangu”
“Umewahi kumuona?”
“Sijawahi, mama aliniambia kuwa alikufa pindi tu nilipozaliwa”
“Mmmmh!”
“Mbona unaguna mama? Ila baba yangu alinipenda sana kwani mama anasema kuwa hata hii nyumba baba aliijenga kwaajili yangu hata kabla sijazaliwa, na biashara nyingi za familia ni yeye aliziweka kwaajili yangu yani hakutaka mimi nipate shida, natamani sana angekuwepo baba yangu maana alinipenda sana”
Mama Angel akamuangalia kwa makini Sarah na kumtaka muda huo waende nae hospitali tu huku akili yake ikiwaza vitu vingi sana kutokana na ile picha aliyoiona.
Basi waliondoka na Sarah kuelekea hospitali ambapo alichukuliwa vipimo na kugundulika kuwa ana malaria, kwahiyo alipewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Basi mama Angel na Erick wakamrudisha Sarah nyumbani kwao ambapo alikuwepo msichana wa kazi tu akiishi nae sababu mama yake hakuwepo, ila mama Angel alitamani sana waondoke na Sarah ili akamuhudumie kwani aliona kuwa Sarah anahitaji kupata huduma ya karibu zaidi, sema Erick akamzuia mama yake,
“Ila mama, utamchukuaje Sarah bila ruhusa ya mama yake? Ungempata mama yake hewani basi ungeongea nae kwanza ila sio kujichukulia tu maamuzi”
“Basi mwanangu nimekuelewa”
Kisha mama Angel alimuuliza yule msichana wa kazi wakina Sarah kama ataweza kukaa na mgonjwa vizuri,
“Nitakaa nae tu mama, hakuna tatizo”
“Nitajitahidi kesho mchana nije kumuona pia hali yake inaendeleaje”
“Sawa, nashukuru sana”
Basi mama Angel na Erick ikabidi wage pale kwakina Sarah na kuondoka zao, basi wakiwa kwenye gari Erick akamuuliza mama yake,
“Mbona mama ile picha ya marehemu baba yake Sarah imekushtua sana?”
“Unajua ni mtu ninayemfahamu sana, sijui hata nikwambiaje ila kwa kifupi Sarah ni ndugu yenu”
“Mmmh mama, ndugu yetu kivipi?”
“Kama ile picha aliyonionyesha ni kweli basi elewa kuwa Sarah ni ndugu yenu”
Erick alishangaa na kumuangalia mama yake bila ya kummaliza, kisha akamwambia,
“Ndiomana ulikuwa uking’ang’ania tukamuuguze nyumbani!”
“Hapana hiyo sio sababu ila tu nilitaka kuwa nae karibu sababu ni mgonjwa”
“Hapana mama nadhani ni sababu unahitaji kujua zaidi kuhusu baba yake Sarah, ila ni marehemu kumbuka”
“Ndio ni marehemu kwani mimi nimesema yuko hai! Hebu endesha gari na wewe, hivi unajua muda umeenda sana na tangu tuondoke nyumbani hatujarudi mpaka muda huu, sijui mwanangu kaliaje huko jamani”
“Atakuwa Amelia sana ila Erica yupo atambembeleza”
“Unamuamini sana Erica eeeh! Ndiomana ulitaka kuja kumuombea niwe nampa mia tano! Hebu elewa jambo moja, yule ni mtoto wa kike, naogopa kumzoesha hela”
Hapo Erick hakuongea neno lolote zaidi ya kuendelea kuendesha gari tu.

Erica alikuwepo nyumbani akimbembeleza mdogo wake tu, ni kweli siku hii mama yao alichelewa sana kwenye hiyo safari aliyoenda na Erick, basi Erica akawa anamuuliza Vaileth,
“Kwani walienda wapi?”
“Nilisikia kuwa wameenda kumuona Sarah”
“Kafanyeje huyo Sarah?”
“Nasikia anaumwa”
“Ila mama nae jamani loh! Mtoto analia hivi”
“Ngoja nikubebeshe labda atatulia”
Basi Vaileth alimbebesha Erica yule mtoto, na kweli alivyombeba mgongoni alitulia na alionyesha kubembelezeka hata kulala alianza kulala sasa, na alivyotulia vizuri, Erica aliweza kukaa na kuangalia Tv.
Muda kidogo mama Angel na Erick walirudi na kumkuta Erica akiwa kambeba mtoto mgongoni,
“Oooh Erica mwanangu, kweli umekuwa mama. Pole eeeh!”
Kisha mama Angel akamchukua mtoto na kwenda nae chumbani, halafu Erick akaenda pia chumbani kwake ambapo alipakuta pamepangwa vizuri kabisa, akaenda kuoga kwanza ili akale maana hakula chochote kile toka ameondoka na mama yake, basi alienda kula na kumkuta Erica akiwa pale mezani,
“Nilikuwa nakusubiri tu, nikasema usipotoka basi nakuja kukufata mwenyewe humo chumbani kwako maana mmeondoka bila kula”
“Ni kweli, na nilikuwa nahisi njaa hatari ila nilikuwa navumilia tu”
“Anaendeleaje huyo Sarah”
“Tulimpeleka hospitali, tumemkuta ana malaria.”
Basi Erick alikuwa anakula, kisha mama yao nae anaenda kula, basi anakula pale huku akiongea ongea nae ila alikuwa na mawazo sana huku akitamani kumwambia mume wake kuhusu alichokipata kwakina Sarah.
 
SEHEMU YA 311

Mama Angel alipomaliza tu kula alienda chumbani na kujilaza huku akifikiria mambo kadhaa, akachukua simu yake na kumpigia mume wake ili ampe ujumbe, simu ile ikapokelewa ila mumewe aliongea katika hali ya usingizi sana,
“Kumbe ushalala mume wangu?”
“Muda umeenda huu mama Angel”
“Haya usiku mwema”
Basi akakata simu na kuanza kufikiria mambo kadhaa, kwanza kuhusu Sarah na yule aliyemuona kwenye picha,
“Hivi inawezekana kweli marehemu mzee Jimmy akawa ndio baba mzazi wa Sarah!! Mmmh natakiwa kuonana na mama Sarah ili nimuulize vizuri. Ila si mpaka mwisho wakina Erick walisema kuwa baba yao ana matatizo ya uzazi!! Anaweza kuwa na mtoto kweli halafu watoto wake wasijue? Halafu kwanini Sarah aseme baba yake kafa baada ya yeye kuzaliwa, jamani mbona mzee Jimmy kaacha hata wajukuu wake wamekuwa kuwa, maana nakumbuka kifo chake wakina Erica walikuwa darasa la tano! Inakuwaje Sarah awe kabla hajazaliwa? Mmmh!”
Alichoka sana kufikiri ila alishangaa siku hiyo akiwa hana usingizi hata kidogo, aliamua kuchukua simu ya mwanae Angel ile iliyopasuka kioo, aliiwasha nayo ikawaka, na moja kwa moja alifungua data na kuingia kwenye facebook ya mtoto wake ili aangalie alikuwa akiwasiliana na nani, ila aliona mtu ambaye mwanae aliwasiliana nae sana alikuwa ni Samir, tena sio kwa kutumia facebook maana inaonyesha walitumia ujumbe wa kawaida kwa sana kwenye mawasiliano yao. Basi alikuwa akiangalia tu taarifa mbalimbali za kwenye mtandao, ndipo alipoona mtu kaandika ujumbe, unaosema,
“Jamani mwenzenu simuelewi mume wangu, akiwa yupo nyumbani ataniita majina yote mazuri, mara mke wangu, mara mpenzi yani hadi huwa Napata raha sana, ila akiwa mbali sasa balaa nikimpigia simu muda wowote hata usiku wakati amelala utasikia ananiita mama Fulani, yani haniiti mke wangu kama nyumbani”
Mama Angel akapumua kidogo, na kuangalia wachangiaji walichosema,
“Ukiona hivyo ujue unaibiwa, mumeo anaogopa kukuita mke wangu maana mchepuko atajua kama ana mke, kumbuka sio michepuko yote wanaojuaga kuwa huyu mtu kaoa au ana mke, wengine hawajui kwahiyo anazidi kumficha”
“Tena mimi wangu utakuta unampigia anajifanya amelala kumbe anachepuka, jamani wanaume hawa Mungu atusaidie tu”
“Pole sana, hapo jua tu kuna watu wanakusaidia”
“Tena mwingine akiona unamsumbua usiku anaamua kuzima na simu kabisa, yamenikuta hayo. Poleni wanawake wenzangu”
Mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa muda huo kwani akizingatia ni muda mfupi tu katoka kumpigia mume wake simu na alionyesha kuwa amelala halafu hakumuita mke wangu kama siku zote bali alimuita mama Angel, basi alijikuta akishikwa na wivu na kuchukua tena simu ili kumpigia, jibu lililokuja,
“Mtumiaji unayempigia hapatikani kwasasa, tafadhari jaribu tena badae”
Yani hapo ndio alihisi kuibiwa kabisa, na usingizi ndio ukakata kabisa alijikuta akishindwa kulala hadi panakucha yani hakuwa na usingizi hata kidogo.

Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, mama Angel aliamua kumpigia tena simu mume wake ambaye kwa muda huo alipokea na kuanza kuongea nae,
“Mume wangu, ilikuwaje ukazima simu yako?”
“Yani jana nilichoka sana halafu simu kumbe iliisha chaji kwahiyo ikajizima yenyewe, samahani mama Angel”
“Na hiyo mama Angel vipi? Mbona sikuelewi?”
“Jamani mke wangu, hunielewi nini tena?”
Hapo mama Angel alitabasamu kiasi na kumwambia,
“Unajua mara nyingine napata mashaka, vile ukishindwa kuongea nami kwenye simu!”
“Mashaka ya nini tena mke wangu jamani!! Siku zote hizi hujanizoea tu eeeh!! Nawezaje kufanya ujinga kwako? Usiniwazie tofauti mke wangu, tujenge maisha yet utu. Vipi watoto lakini wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, ila kuna jambo nahitaji tuongee ukirudi mume wangu maana nadhani kwasasa wala hatutoelewana”
Sababu mumewe alikuwa anawahi kwenye shughuli zake za huko, ikabidi waagane tu maana hakukuwa na namna tena.
Mchana wa siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda kumuona tena Sarah, na alipofika alimkuta Sarah anatapika na kupata habari kuwa alitapika sana hata asubuhi ya siku hiyo, basi alimsaidia pale na kukaa nae ndani kwa muda, kisha akamuomba yule msichana wa kazi ili amruhusu yeye kuondoka na Sarah,
“Naomba uniruhusu niende na Sarah ili nikamuuguze nyumbani kwangu”
“Mmmh hapana mama, siwezi kukubali maana watanisema sana ukizingatia nimeachiwa mimi dhamana ya kumuangalia Sarah”
“Ila anaumwa sana, eti Sarah unasemaje kuhusu mimi kukuchukua ukaugulie nyumbani kwangu eeeh!”
“Nipo tayari, hapa dada hata haniangalii vizuri”
Basi dada yake akamuangalia na kusema,
“Jamani Sarah, kweli sikuangalii vizuri mimi!”
“Sina maana hiyo, ila nikienda kwa huyu mama nitapata nafuu kwa haraka sana, kumbuka mama yangu hayupo na mimi napenda kuwa karibu na mama, halafu mama yangu hayupo unadhani ni nani anaweza kunipa mapenzi ya mama zaidi ya huyu aliyejitolea? Mimi nawafahamu ni watu wenye roho nzuri, nipe ruhusa tu niende dada Siku”
“Mmmh jamani sijui yani”
Mama Angel ikabidi amtoe uoga,
“Sikia Siku, tutaenda wote hadi nyumbani kwangu ambapo atabaki Sarah ili nimuhudumie kwa ukaribu, yani wewe upafahamu nyumbani kwangu ili usiendelee kuwa na mashaka nami”
Basi Siku akakubali na kuenda kumuandalia Sarah nguo chache kisha kuondoka nao mapaka nyumbani kwa mama Angel.
Walifika pale, walikaribishwa vizuri kabisa na Vaileth kisha baada ya muda kidogo Siku aliondoka tu kurudi kule nyumbani kwa mama Sarah.
 
SEHEMU YA 312

Leo Erick anawahi kutoka shule sababu alishaomba ruhusa kwa mwalimu wake, hivyobasi alivyoondoka tu moja kwa moja alienda kwenye duka la baba yake, na kuanza kuangalia vizuri ila wakati yupo pale dukani alifika yule rafiki wa Steve yani yeye alienda kwaajili ya kumtembelea rafiki yake maana siku zote alifika na kukuta duka limefungwa, basi alivyomkuta Erick ndio alianza kuongea nae,
“Steve ni rafiki yangu sana”
“Aaaah, basi Steve kapata kazi sehemu nyingine. Na hapa tunatafuta mtu”
“Jamani hata mimi nafaa jamani, sina kazi mimi”
“Unaitwa nani kwani?”
“Naitwa Rama”
“Oooh ila majina ya Rama, naona wengi ni wastaarabu. Basi fanya hivi, kesho nitakuja hapa dukani niletee wadhifa wako yani cheti chako, barua ya serikali ya mtaa wako na barua yako ya maombi ya kazi, nitaipitisha ili Jumatatu uanze kazi”
“Dah! Nashukuru sana, yani sasa hivi naenda kufanya hivyo vitu. Yani mimi nahangaika tu siku zote hizi sina kazi”
“Basi ndio umepata kazi, ila kuwa muaminifu kama jina lako”
“Hata hivyo mimi ni muaminifu kweli, hivyo vitu hata leo leo ningevileta”
“Ila naona muda umeenda, nitachelewa nyumbani. Jitahidi iwe kesho halafu ndio nitakuonyesha na vitu ndani tunafanyeje”
“Asante sana”
Kisha Rama akaondoka muda huo ili kwenda kushughulikia vitu hivyo.
Erick aliangalia angalia vizuri kwenye lile duka na wale walinzi ambao baba yake aliwaweka, kisha akataka kuondoka basi wakati anatembea ili aite bodaboda aondeke nayo, alishangaa akishikwa bega, alipogeuka alikuwa ni Sia amemshika bega, Erick akachukia sana na kusema,
“Ni wewe kimama tena!!”
“Najua Erick unanichukia sana, ila ungepata kuona nafsi yangu jinsi gani napata faraja hata kuongea nawe tu, ungenielewa”
“Unataka nikuelewe kuhusu nini? Kuwa wale ninaoishi nao sio wazazi wangu? Na wewe ndiye mama yangu au nini?”
“Bado una mambo hayo tu Erick jamani, achana na mambo hayo ya mwaka jana, zama zimebadilika hizi. Ni hivi Erick, endelea kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wako ila na mimi usinichukie kiasi hiko, nipende na kunijali, sio kosa langu mimi kufanya yote haya ninayoyafanya, ipo siku utanielewa ni kwanini nafanya haya niyafanyayo, naomba unisamehe sana”
“Achana na mimi bhana”
“Nitaachana nawe ila niambie kuwa umenisamehe, Erick sitaki kuwa kikwazo katika mafanikio yako ila nataka kuwa chachu ya wewe kufanikiwa zaidi, achana na yote yaliyopita Erick mwanangu”
“Hapo ndio unaponikera, nani mwanao?”
“Mtoto wa mwenzio ni wako, kwahiyo wewe ni kama mwanangu. Nakuona wewe ni kama Elly, usinichukie Erick”
“Kwaheri”
Erick alishaita bodaboda na kupanda kisha aliondoka nayo sababu tu hakutaka kuendelea kumsikiliza Sia.
Basi Erick anarudi hadi nyumbani kwao, ila alipofika tu sababu ya uchovu ni moja kwa moja alienda chumbani kwake na kujilaza, yani leo alisahau hata kwenda kula au kuvua sare za shule kwani alihisi kichwa chake kuchoka sana.

Muda huu mama Angel alikuwa sebleni pamoja na Erica sababu Sarah alikuwa amelala, ila Erica alikuwa akimlalamikia mama yake,
“Yani mama ndio kumuweka Sarah nilale nae kweli?”
“Kwani kuna ubaya gani jamani! Sarah ni mgonjwa unataka alale peke yake, akizidiwa je!”
“Ila mama, aaargh jamani”
Erica akaondoka na kwenda tena chumbani kwake, muda kidogo alifika Junior na mama Angel kumshangaa,
“Kheee Junior, umerudi tena!”
“Mamdogo, leo ni mwisho wa wiki, nitaenda tena shule Jumatatu”
“Sasa hiyo ni shule ya bweni au ni shule ya kutwa?”
“Jamani mamdogo, yani wanafunzi wote wa karibu wameondoka leo, ni wale wa mbali tu ndio wamebaki, halafu na mimi nibaki kweli wakati naishi karibu hapa”
“Haya, nimekuelewa”
Kisha Junior moja kwa moja alienda jikoni kwani alijua huko lazima atamuona Vaileth na kweli alimkuta akiwa ndio anamalizia kupika, basi akaenda nyuma yake na kumbusu halafu akamwambia,
“Unajua siwezi kukaa shule kwa siku nyingi zaidi maana mawazo yangu yote ni juu yako”
Vaileth alitabasamu tu, mara ikasikika sauti ya mama Angel,
“Vai, hiko chakula bado tu!”
“Ndio namalizia mama”
Mama Angel tayari alishafika jikoni na kumuuliza Junior,
“Na wewe Junior, kituo cha kwanza jikoni kuna nini?”
“Ni njaa mamdogo, nahisi njaa sana”
“Khaaa wanafunzi wa bweni jamani mna vituko sana, haya Vai andaa hiko chakula ili wote wapate kuja kula”
Kisha Junior akatoka, na mama Angel akatoka pia kwenda kumchukua Sarah chumbani ili aweze kula chakula.
Alijua Erica atamkuta chumbani pia ila Erica hakuwepo mule chumbani, basi alikaa na Sarah na kumwambia,
“Twende basi ukajaribishe kula chakula nilichokuandalia”
“Mmmh hata sijisikii kula”
“Hapana Sarah, ule japo kidogo upate nguvu binti yangu”
Mama Angel akatoka na kwenda kumletea chakula Sarah na kuanza kujaribu kumlisha pale ni kweli alikula, tena alikula vizuri tu na baada ya kushiba sasa aliongea nae kidogo na kumruhusu apumzike halafu yeye akatoka na kuondoka zake, hakuwa na tatizo na wanae kwani alijua ni lazima wangeshuka na kula chakula tu.

Erica aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili kumuelezea, ila alimkuta akiwa amelala tena bado hajavua hata sare za shule, basi alimshtua na Erick aliamka,
“Wewe Erick, nini tena?”
“Dah!! Nimechoka sana jamani”
“Kwahiyo hata kula hujala jamani, halafu sikujua maana ningekuja kukuamsha muda sana”
Basi Erick ndio aliinuka na kuanza kubadili zile sare za shule,
“Khee unabadili nguo hata huniambii nikupishe?”
“Sasa unipishe kitu gani? Kuna kipi hukijui katika mwili wangu”
Erica alicheka tu na kuinuka, kisha akamwambia,
“Utanikuta sebleni”
Basi Erick alienda kuoga na baadae alishuka kwenda kula chakula na baada ya hapo aliongozana tena na Erica kwenda chumbani kwake, basi Erica alianza kumwambia,
“Mama, anaupendeleo sana”
“Kafanyaje kwani?”
“Mama kamleta Sarah hapa nyumbani”
“Mmmh kamleta Sarah?”
“Ndio, kumbe hujui! Basi mama kaja na Sarah leo, ila anavyomjali huyo Sarah tofauti na sisi, yani Sarah kaenda kulishwa chakula sababu anaumwa halafu kamuweka nilale nae mimi”
“Unasema kweli mama kamleta Sarah hapa nyumbani? Kakubaliana na mama yake kweli?”
“Sijui ila ndio Sarah yupo hapa nyumbani, kwakweli mimi siwezi hata kwenda kulala huko chumbani bora nikalale sebleni tu”
“Aaaah jamani usifanye hivyo”
“Mimi sikubali, mama angetaka aneomba ushauri kwanza kwangu mwenye chumba sio kujiamulia tu mwenyewe na maamuzi yake”
Kisha Erica akainuka na kusema,
“Usiku mwema”
“Kwahiyo ndio unaenda kulala sebleni?”
“Ndio, siwezi kwenda kulala chumbani kwangu”
“Hapana usiende kulala sebleni, tafadhari baki humu chumbani tulale wote”
Erica nae aliona ni jambo jema, kwahiyo alibaki humo chumbani kwa Erick na muda huo wakalala wote.
 
SEHEMU YA 313

Kulipokucha, mama Angel alienda kumuangalia Sarah ajue hali yake ila alimkuta ameanza kupona maana hata nuru usoni mwake ili onekana, basi alimsalimia pale na kuongea nae kidogo,
“Eeeh unajisikiaje, unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri mama”
“Vipi huyu Erica ameshaamka nini”
“Sijui, kwani Erica huwa analala humu?”
“Ndio, huwa analala humu”
“Basi sikumuona maana nililala mwenyewe tu kama nyumbani”
“Kwahiyo nyumbani kwenu napo umezoea kulala mwenyewe eeeh!”
“Ndio, mama huwa anasema mimi ni mlalavi yani nalala vibaya kwahiyo nisilale na mtu, huwa nalala mwenyewe tu”
“Oooh basi sawa, labda Erica kajiongeza. Asubuhi hii nikuandalie nini?”
“Mmmh labda supu ya kuku na chapati”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi mama Angel alienda jikoni na kuandaa hiko chakula mwenyewe, yani Erica alimkuta mama yake akiandaa hiko chakula,
“Ndio chakula chetu hiko leo mama?”
“Cha mgonjwa hiki, si unajua Sarah anaumwa?”
“Najua ila na mimi nitakula hiko hiko unachomuandalia Sarah”
Mama Angel hakusema neno maana alimtambua wazi mtoto wake huyu kwa ubishi, basi alimuita Vaileth tu na kumtaka aandae supu ya nyumba nzima ili wote wapate kunywa supu hiyo.

Mida ya saa nne asubuhi, Erick alijiandaa na kumuaga mama yake ila kwa muda ule Erica nae aling’ang’ania aondoke na Erick maana hakutaka kukaa hapo nyumbani wala nini.
Basi mama yake alimruhusu tu bila kujua kuwa Erica amechukia uwepo wa Sarah pale nyumbani kwao.
Baada ya kuondoka tu, ni Vaileth ndio alienda kumwambia ukweli,
“Unajua nini mama, mwenzio Erica kachukia uwepo wa Sarah”
“Jamani haka katoto sijui nani kakafunza roho mbaya mweeeh!”
Kisha mama Angel alienda kuongea na Sarah ambaye bado alikuwa chumbani na alitoka kuoga tu kwa muda huo,
“Unajionaje hali kwa muda huu Sarah?”
“Nimepona, maana hata nimeweza kuoga. Ila kwanini Erick hajaweza kuja hata kuniona huku chumbani!”
“Kheee hakuja kukuona! Nadhani sababu ya majukumu yake, ila atawahi kurudi na atakuja kukuona”
“Sawa, ila mama mbona ulishangaa sana kuona picha ya marehemu baba yangu?”
“Aaaah kuna mtu nimemfananisha nae, hivi huko kwenye kaburi la baba yako mmeanza kwenda lini?”
“Toka mwaka juzi, huwa tunaenda mara kwa mara na mama na kufanya usafi kwenye kaburi la baba”
“Huyo baba yako aliitwa nani?”
“Mama, aliniambia kuwa baba anaitwa Jimmy”
Hapo kidogo mama Angel akashtuka na kuhisi pengine kuna ukweli ila bado ilimchukua ngumu sana kuamini, akamuuliza baadhi ya maswali Sarah na mwisho wa siku aliamua kutoka nae sebleni ili wakae waangalie hata vipindi mbalimbali kwenye luninga.

Siku akiwa anafanya kazi zake, mara alifika pale mama mkubwa wa Sarah yani dada yake na mama Sarah, na alienda pale kwa lengo la kumuona Sarah, kwakweli aliogopa sana ukizingatia katoa ruhusa ya Sarah kwenda kuhudumiwa pengine,
“Haya Saraha yuko wapi?”
Siku alikuwa akitetemeka kwani alimjua huyu alivyo mkali,
“Nisamehe mama”
“Nikusamehe kitu gani? Yuko wapi Sarah?”
Ikabidi amueleze ukweli wote wa jinsi ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumpa Sarah ruhusa,
“Hivi wewe Siku una akili kweli, hata kama umeshindwa kumuuguza mtoto si ungenipigia simu hata mimi nije nimchukue jamani! Ila ni vyema alijitokeza huyo msamalia mwema, yani wewe huna maana kabisa, mdogo wangu anakuhudumia bure, anakupa kila kitu halafu unashindwa kumuuguza mtoto wake kweli!! Shwain, haya nipeleke huko kwa msamalia mwema”
Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,
“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”
Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel.


Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.
Mama Angel alimuangalia Sarah kwa makini sana na kumuuliza,
“Kwahiyo huyu ndio marehemu baba yako?”
“Ndio, ni marehemu baba yangu”
“Umewahi kumuona?”
“Sijawahi, mama aliniambia kuwa alikufa pindi tu nilipozaliwa”
“Mmmmh!”
“Mbona unaguna mama? Ila baba yangu alinipenda sana kwani mama anasema kuwa hata hii nyumba baba aliijenga kwaajili yangu hata kabla sijazaliwa, na biashara nyingi za familia ni yeye aliziweka kwaajili yangu yani hakutaka mimi nipate shida, natamani sana angekuwepo baba yangu maana alinipenda sana”
Mama Angel akamuangalia kwa makini Sarah na kumtaka muda huo waende nae hospitali tu huku akili yake ikiwaza vitu vingi sana kutokana na ile picha aliyoiona.
Basi waliondoka na Sarah kuelekea hospitali ambapo alichukuliwa vipimo na kugundulika kuwa ana malaria, kwahiyo alipewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Basi mama Angel na Erick wakamrudisha Sarah nyumbani kwao ambapo alikuwepo msichana wa kazi tu akiishi nae sababu mama yake hakuwepo, ila mama Angel alitamani sana waondoke na Sarah ili akamuhudumie kwani aliona kuwa Sarah anahitaji kupata huduma ya karibu zaidi, sema Erick akamzuia mama yake,
“Ila mama, utamchukuaje Sarah bila ruhusa ya mama yake? Ungempata mama yake hewani basi ungeongea nae kwanza ila sio kujichukulia tu maamuzi”
“Basi mwanangu nimekuelewa”
Kisha mama Angel alimuuliza yule msichana wa kazi wakina Sarah kama ataweza kukaa na mgonjwa vizuri,
“Nitakaa nae tu mama, hakuna tatizo”
“Nitajitahidi kesho mchana nije kumuona pia hali yake inaendeleaje”
“Sawa, nashukuru sana”
Basi mama Angel na Erick ikabidi wage pale kwakina Sarah na kuondoka zao, basi wakiwa kwenye gari Erick akamuuliza mama yake,
“Mbona mama ile picha ya marehemu baba yake Sarah imekushtua sana?”
“Unajua ni mtu ninayemfahamu sana, sijui hata nikwambiaje ila kwa kifupi Sarah ni ndugu yenu”
“Mmmh mama, ndugu yetu kivipi?”
“Kama ile picha aliyonionyesha ni kweli basi elewa kuwa Sarah ni ndugu yenu”
Erick alishangaa na kumuangalia mama yake bila ya kummaliza, kisha akamwambia,
“Ndiomana ulikuwa uking’ang’ania tukamuuguze nyumbani!”
“Hapana hiyo sio sababu ila tu nilitaka kuwa nae karibu sababu ni mgonjwa”
“Hapana mama nadhani ni sababu unahitaji kujua zaidi kuhusu baba yake Sarah, ila ni marehemu kumbuka”
“Ndio ni marehemu kwani mimi nimesema yuko hai! Hebu endesha gari na wewe, hivi unajua muda umeenda sana na tangu tuondoke nyumbani hatujarudi mpaka muda huu, sijui mwanangu kaliaje huko jamani”
“Atakuwa Amelia sana ila Erica yupo atambembeleza”
“Unamuamini sana Erica eeeh! Ndiomana ulitaka kuja kumuombea niwe nampa mia tano! Hebu elewa jambo moja, yule ni mtoto wa kike, naogopa kumzoesha hela”
Hapo Erick hakuongea neno lolote zaidi ya kuendelea kuendesha gari tu.
 
SEHEMU YA 314

Erica alikuwepo nyumbani akimbembeleza mdogo wake tu, ni kweli siku hii mama yao alichelewa sana kwenye hiyo safari aliyoenda na Erick, basi Erica akawa anamuuliza Vaileth,
“Kwani walienda wapi?”
“Nilisikia kuwa wameenda kumuona Sarah”
“Kafanyeje huyo Sarah?”
“Nasikia anaumwa”
“Ila mama nae jamani loh! Mtoto analia hivi”
“Ngoja nikubebeshe labda atatulia”
Basi Vaileth alimbebesha Erica yule mtoto, na kweli alivyombeba mgongoni alitulia na alionyesha kubembelezeka hata kulala alianza kulala sasa, na alivyotulia vizuri, Erica aliweza kukaa na kuangalia Tv.
Muda kidogo mama Angel na Erick walirudi na kumkuta Erica akiwa kambeba mtoto mgongoni,
“Oooh Erica mwanangu, kweli umekuwa mama. Pole eeeh!”
Kisha mama Angel akamchukua mtoto na kwenda nae chumbani, halafu Erick akaenda pia chumbani kwake ambapo alipakuta pamepangwa vizuri kabisa, akaenda kuoga kwanza ili akale maana hakula chochote kile toka ameondoka na mama yake, basi alienda kula na kumkuta Erica akiwa pale mezani,
“Nilikuwa nakusubiri tu, nikasema usipotoka basi nakuja kukufata mwenyewe humo chumbani kwako maana mmeondoka bila kula”
“Ni kweli, na nilikuwa nahisi njaa hatari ila nilikuwa navumilia tu”
“Anaendeleaje huyo Sarah”
“Tulimpeleka hospitali, tumemkuta ana malaria.”
Basi Erick alikuwa anakula, kisha mama yao nae anaenda kula, basi anakula pale huku akiongea ongea nae ila alikuwa na mawazo sana huku akitamani kumwambia mume wake kuhusu alichokipata kwakina Sarah.

Mama Angel alipomaliza tu kula alienda chumbani na kujilaza huku akifikiria mambo kadhaa, akachukua simu yake na kumpigia mume wake ili ampe ujumbe, simu ile ikapokelewa ila mumewe aliongea katika hali ya usingizi sana,
“Kumbe ushalala mume wangu?”
“Muda umeenda huu mama Angel”
“Haya usiku mwema”
Basi akakata simu na kuanza kufikiria mambo kadhaa, kwanza kuhusu Sarah na yule aliyemuona kwenye picha,
“Hivi inawezekana kweli marehemu mzee Jimmy akawa ndio baba mzazi wa Sarah!! Mmmh natakiwa kuonana na mama Sarah ili nimuulize vizuri. Ila si mpaka mwisho wakina Erick walisema kuwa baba yao ana matatizo ya uzazi!! Anaweza kuwa na mtoto kweli halafu watoto wake wasijue? Halafu kwanini Sarah aseme baba yake kafa baada ya yeye kuzaliwa, jamani mbona mzee Jimmy kaacha hata wajukuu wake wamekuwa kuwa, maana nakumbuka kifo chake wakina Erica walikuwa darasa la tano! Inakuwaje Sarah awe kabla hajazaliwa? Mmmh!”
Alichoka sana kufikiri ila alishangaa siku hiyo akiwa hana usingizi hata kidogo, aliamua kuchukua simu ya mwanae Angel ile iliyopasuka kioo, aliiwasha nayo ikawaka, na moja kwa moja alifungua data na kuingia kwenye facebook ya mtoto wake ili aangalie alikuwa akiwasiliana na nani, ila aliona mtu ambaye mwanae aliwasiliana nae sana alikuwa ni Samir, tena sio kwa kutumia facebook maana inaonyesha walitumia ujumbe wa kawaida kwa sana kwenye mawasiliano yao. Basi alikuwa akiangalia tu taarifa mbalimbali za kwenye mtandao, ndipo alipoona mtu kaandika ujumbe, unaosema,
“Jamani mwenzenu simuelewi mume wangu, akiwa yupo nyumbani ataniita majina yote mazuri, mara mke wangu, mara mpenzi yani hadi huwa Napata raha sana, ila akiwa mbali sasa balaa nikimpigia simu muda wowote hata usiku wakati amelala utasikia ananiita mama Fulani, yani haniiti mke wangu kama nyumbani”
Mama Angel akapumua kidogo, na kuangalia wachangiaji walichosema,
“Ukiona hivyo ujue unaibiwa, mumeo anaogopa kukuita mke wangu maana mchepuko atajua kama ana mke, kumbuka sio michepuko yote wanaojuaga kuwa huyu mtu kaoa au ana mke, wengine hawajui kwahiyo anazidi kumficha”
“Tena mimi wangu utakuta unampigia anajifanya amelala kumbe anachepuka, jamani wanaume hawa Mungu atusaidie tu”
“Pole sana, hapo jua tu kuna watu wanakusaidia”
“Tena mwingine akiona unamsumbua usiku anaamua kuzima na simu kabisa, yamenikuta hayo. Poleni wanawake wenzangu”
Mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa muda huo kwani akizingatia ni muda mfupi tu katoka kumpigia mume wake simu na alionyesha kuwa amelala halafu hakumuita mke wangu kama siku zote bali alimuita mama Angel, basi alijikuta akishikwa na wivu na kuchukua tena simu ili kumpigia, jibu lililokuja,
“Mtumiaji unayempigia hapatikani kwasasa, tafadhari jaribu tena badae”
Yani hapo ndio alihisi kuibiwa kabisa, na usingizi ndio ukakata kabisa alijikuta akishindwa kulala hadi panakucha yani hakuwa na usingizi hata kidogo.

Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, mama Angel aliamua kumpigia tena simu mume wake ambaye kwa muda huo alipokea na kuanza kuongea nae,
“Mume wangu, ilikuwaje ukazima simu yako?”
“Yani jana nilichoka sana halafu simu kumbe iliisha chaji kwahiyo ikajizima yenyewe, samahani mama Angel”
“Na hiyo mama Angel vipi? Mbona sikuelewi?”
“Jamani mke wangu, hunielewi nini tena?”
Hapo mama Angel alitabasamu kiasi na kumwambia,
“Unajua mara nyingine napata mashaka, vile ukishindwa kuongea nami kwenye simu!”
“Mashaka ya nini tena mke wangu jamani!! Siku zote hizi hujanizoea tu eeeh!! Nawezaje kufanya ujinga kwako? Usiniwazie tofauti mke wangu, tujenge maisha yet utu. Vipi watoto lakini wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, ila kuna jambo nahitaji tuongee ukirudi mume wangu maana nadhani kwasasa wala hatutoelewana”
Sababu mumewe alikuwa anawahi kwenye shughuli zake za huko, ikabidi waagane tu maana hakukuwa na namna tena.
Mchana wa siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda kumuona tena Sarah, na alipofika alimkuta Sarah anatapika na kupata habari kuwa alitapika sana hata asubuhi ya siku hiyo, basi alimsaidia pale na kukaa nae ndani kwa muda, kisha akamuomba yule msichana wa kazi ili amruhusu yeye kuondoka na Sarah,
“Naomba uniruhusu niende na Sarah ili nikamuuguze nyumbani kwangu”
“Mmmh hapana mama, siwezi kukubali maana watanisema sana ukizingatia nimeachiwa mimi dhamana ya kumuangalia Sarah”
“Ila anaumwa sana, eti Sarah unasemaje kuhusu mimi kukuchukua ukaugulie nyumbani kwangu eeeh!”
“Nipo tayari, hapa dada hata haniangalii vizuri”
Basi dada yake akamuangalia na kusema,
“Jamani Sarah, kweli sikuangalii vizuri mimi!”
“Sina maana hiyo, ila nikienda kwa huyu mama nitapata nafuu kwa haraka sana, kumbuka mama yangu hayupo na mimi napenda kuwa karibu na mama, halafu mama yangu hayupo unadhani ni nani anaweza kunipa mapenzi ya mama zaidi ya huyu aliyejitolea? Mimi nawafahamu ni watu wenye roho nzuri, nipe ruhusa tu niende dada Siku”
“Mmmh jamani sijui yani”
Mama Angel ikabidi amtoe uoga,
“Sikia Siku, tutaenda wote hadi nyumbani kwangu ambapo atabaki Sarah ili nimuhudumie kwa ukaribu, yani wewe upafahamu nyumbani kwangu ili usiendelee kuwa na mashaka nami”
Basi Siku akakubali na kuenda kumuandalia Sarah nguo chache kisha kuondoka nao mapaka nyumbani kwa mama Angel.
Walifika pale, walikaribishwa vizuri kabisa na Vaileth kisha baada ya muda kidogo Siku aliondoka tu kurudi kule nyumbani kwa mama Sarah.

Leo Erick anawahi kutoka shule sababu alishaomba ruhusa kwa mwalimu wake, hivyobasi alivyoondoka tu moja kwa moja alienda kwenye duka la baba yake, na kuanza kuangalia vizuri ila wakati yupo pale dukani alifika yule rafiki wa Steve yani yeye alienda kwaajili ya kumtembelea rafiki yake maana siku zote alifika na kukuta duka limefungwa, basi alivyomkuta Erick ndio alianza kuongea nae,
“Steve ni rafiki yangu sana”
“Aaaah, basi Steve kapata kazi sehemu nyingine. Na hapa tunatafuta mtu”
“Jamani hata mimi nafaa jamani, sina kazi mimi”
“Unaitwa nani kwani?”
“Naitwa Rama”
“Oooh ila majina ya Rama, naona wengi ni wastaarabu. Basi fanya hivi, kesho nitakuja hapa dukani niletee wadhifa wako yani cheti chako, barua ya serikali ya mtaa wako na barua yako ya maombi ya kazi, nitaipitisha ili Jumatatu uanze kazi”
“Dah! Nashukuru sana, yani sasa hivi naenda kufanya hivyo vitu. Yani mimi nahangaika tu siku zote hizi sina kazi”
“Basi ndio umepata kazi, ila kuwa muaminifu kama jina lako”
“Hata hivyo mimi ni muaminifu kweli, hivyo vitu hata leo leo ningevileta”
“Ila naona muda umeenda, nitachelewa nyumbani. Jitahidi iwe kesho halafu ndio nitakuonyesha na vitu ndani tunafanyeje”
“Asante sana”
Kisha Rama akaondoka muda huo ili kwenda kushughulikia vitu hivyo.
Erick aliangalia angalia vizuri kwenye lile duka na wale walinzi ambao baba yake aliwaweka, kisha akataka kuondoka basi wakati anatembea ili aite bodaboda aondeke nayo, alishangaa akishikwa bega, alipogeuka alikuwa ni Sia amemshika bega, Erick akachukia sana na kusema,
“Ni wewe kimama tena!!”
“Najua Erick unanichukia sana, ila ungepata kuona nafsi yangu jinsi gani napata faraja hata kuongea nawe tu, ungenielewa”
“Unataka nikuelewe kuhusu nini? Kuwa wale ninaoishi nao sio wazazi wangu? Na wewe ndiye mama yangu au nini?”
“Bado una mambo hayo tu Erick jamani, achana na mambo hayo ya mwaka jana, zama zimebadilika hizi. Ni hivi Erick, endelea kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wako ila na mimi usinichukie kiasi hiko, nipende na kunijali, sio kosa langu mimi kufanya yote haya ninayoyafanya, ipo siku utanielewa ni kwanini nafanya haya niyafanyayo, naomba unisamehe sana”
“Achana na mimi bhana”
“Nitaachana nawe ila niambie kuwa umenisamehe, Erick sitaki kuwa kikwazo katika mafanikio yako ila nataka kuwa chachu ya wewe kufanikiwa zaidi, achana na yote yaliyopita Erick mwanangu”
“Hapo ndio unaponikera, nani mwanao?”
“Mtoto wa mwenzio ni wako, kwahiyo wewe ni kama mwanangu. Nakuona wewe ni kama Elly, usinichukie Erick”
“Kwaheri”
Erick alishaita bodaboda na kupanda kisha aliondoka nayo sababu tu hakutaka kuendelea kumsikiliza Sia.
Basi Erick anarudi hadi nyumbani kwao, ila alipofika tu sababu ya uchovu ni moja kwa moja alienda chumbani kwake na kujilaza, yani leo alisahau hata kwenda kula au kuvua sare za shule kwani alihisi kichwa chake kuchoka sana.
 
Back
Top Bottom