Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 315

Muda huu mama Angel alikuwa sebleni pamoja na Erica sababu Sarah alikuwa amelala, ila Erica alikuwa akimlalamikia mama yake,
“Yani mama ndio kumuweka Sarah nilale nae kweli?”
“Kwani kuna ubaya gani jamani! Sarah ni mgonjwa unataka alale peke yake, akizidiwa je!”
“Ila mama, aaargh jamani”
Erica akaondoka na kwenda tena chumbani kwake, muda kidogo alifika Junior na mama Angel kumshangaa,
“Kheee Junior, umerudi tena!”
“Mamdogo, leo ni mwisho wa wiki, nitaenda tena shule Jumatatu”
“Sasa hiyo ni shule ya bweni au ni shule ya kutwa?”
“Jamani mamdogo, yani wanafunzi wote wa karibu wameondoka leo, ni wale wa mbali tu ndio wamebaki, halafu na mimi nibaki kweli wakati naishi karibu hapa”
“Haya, nimekuelewa”
Kisha Junior moja kwa moja alienda jikoni kwani alijua huko lazima atamuona Vaileth na kweli alimkuta akiwa ndio anamalizia kupika, basi akaenda nyuma yake na kumbusu halafu akamwambia,
“Unajua siwezi kukaa shule kwa siku nyingi zaidi maana mawazo yangu yote ni juu yako”
Vaileth alitabasamu tu, mara ikasikika sauti ya mama Angel,
“Vai, hiko chakula bado tu!”
“Ndio namalizia mama”
Mama Angel tayari alishafika jikoni na kumuuliza Junior,
“Na wewe Junior, kituo cha kwanza jikoni kuna nini?”
“Ni njaa mamdogo, nahisi njaa sana”
“Khaaa wanafunzi wa bweni jamani mna vituko sana, haya Vai andaa hiko chakula ili wote wapate kuja kula”
Kisha Junior akatoka, na mama Angel akatoka pia kwenda kumchukua Sarah chumbani ili aweze kula chakula.
Alijua Erica atamkuta chumbani pia ila Erica hakuwepo mule chumbani, basi alikaa na Sarah na kumwambia,
“Twende basi ukajaribishe kula chakula nilichokuandalia”
“Mmmh hata sijisikii kula”
“Hapana Sarah, ule japo kidogo upate nguvu binti yangu”
Mama Angel akatoka na kwenda kumletea chakula Sarah na kuanza kujaribu kumlisha pale ni kweli alikula, tena alikula vizuri tu na baada ya kushiba sasa aliongea nae kidogo na kumruhusu apumzike halafu yeye akatoka na kuondoka zake, hakuwa na tatizo na wanae kwani alijua ni lazima wangeshuka na kula chakula tu.

Erica aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili kumuelezea, ila alimkuta akiwa amelala tena bado hajavua hata sare za shule, basi alimshtua na Erick aliamka,
“Wewe Erick, nini tena?”
“Dah!! Nimechoka sana jamani”
“Kwahiyo hata kula hujala jamani, halafu sikujua maana ningekuja kukuamsha muda sana”
Basi Erick ndio aliinuka na kuanza kubadili zile sare za shule,
“Khee unabadili nguo hata huniambii nikupishe?”
“Sasa unipishe kitu gani? Kuna kipi hukijui katika mwili wangu”
Erica alicheka tu na kuinuka, kisha akamwambia,
“Utanikuta sebleni”
Basi Erick alienda kuoga na baadae alishuka kwenda kula chakula na baada ya hapo aliongozana tena na Erica kwenda chumbani kwake, basi Erica alianza kumwambia,
“Mama, anaupendeleo sana”
“Kafanyaje kwani?”
“Mama kamleta Sarah hapa nyumbani”
“Mmmh kamleta Sarah?”
“Ndio, kumbe hujui! Basi mama kaja na Sarah leo, ila anavyomjali huyo Sarah tofauti na sisi, yani Sarah kaenda kulishwa chakula sababu anaumwa halafu kamuweka nilale nae mimi”
“Unasema kweli mama kamleta Sarah hapa nyumbani? Kakubaliana na mama yake kweli?”
“Sijui ila ndio Sarah yupo hapa nyumbani, kwakweli mimi siwezi hata kwenda kulala huko chumbani bora nikalale sebleni tu”
“Aaaah jamani usifanye hivyo”
“Mimi sikubali, mama angetaka aneomba ushauri kwanza kwangu mwenye chumba sio kujiamulia tu mwenyewe na maamuzi yake”
Kisha Erica akainuka na kusema,
“Usiku mwema”
“Kwahiyo ndio unaenda kulala sebleni?”
“Ndio, siwezi kwenda kulala chumbani kwangu”
“Hapana usiende kulala sebleni, tafadhari baki humu chumbani tulale wote”
Erica nae aliona ni jambo jema, kwahiyo alibaki humo chumbani kwa Erick na muda huo wakalala wote.

Kulipokucha, mama Angel alienda kumuangalia Sarah ajue hali yake ila alimkuta ameanza kupona maana hata nuru usoni mwake ili onekana, basi alimsalimia pale na kuongea nae kidogo,
“Eeeh unajisikiaje, unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri mama”
“Vipi huyu Erica ameshaamka nini”
“Sijui, kwani Erica huwa analala humu?”
“Ndio, huwa analala humu”
“Basi sikumuona maana nililala mwenyewe tu kama nyumbani”
“Kwahiyo nyumbani kwenu napo umezoea kulala mwenyewe eeeh!”
“Ndio, mama huwa anasema mimi ni mlalavi yani nalala vibaya kwahiyo nisilale na mtu, huwa nalala mwenyewe tu”
“Oooh basi sawa, labda Erica kajiongeza. Asubuhi hii nikuandalie nini?”
“Mmmh labda supu ya kuku na chapati”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi mama Angel alienda jikoni na kuandaa hiko chakula mwenyewe, yani Erica alimkuta mama yake akiandaa hiko chakula,
“Ndio chakula chetu hiko leo mama?”
“Cha mgonjwa hiki, si unajua Sarah anaumwa?”
“Najua ila na mimi nitakula hiko hiko unachomuandalia Sarah”
Mama Angel hakusema neno maana alimtambua wazi mtoto wake huyu kwa ubishi, basi alimuita Vaileth tu na kumtaka aandae supu ya nyumba nzima ili wote wapate kunywa supu hiyo.
 
SEHEMU YA 316

Mida ya saa nne asubuhi, Erick alijiandaa na kumuaga mama yake ila kwa muda ule Erica nae aling’ang’ania aondoke na Erick maana hakutaka kukaa hapo nyumbani wala nini.
Basi mama yake alimruhusu tu bila kujua kuwa Erica amechukia uwepo wa Sarah pale nyumbani kwao.
Baada ya kuondoka tu, ni Vaileth ndio alienda kumwambia ukweli,
“Unajua nini mama, mwenzio Erica kachukia uwepo wa Sarah”
“Jamani haka katoto sijui nani kakafunza roho mbaya mweeeh!”
Kisha mama Angel alienda kuongea na Sarah ambaye bado alikuwa chumbani na alitoka kuoga tu kwa muda huo,
“Unajionaje hali kwa muda huu Sarah?”
“Nimepona, maana hata nimeweza kuoga. Ila kwanini Erick hajaweza kuja hata kuniona huku chumbani!”
“Kheee hakuja kukuona! Nadhani sababu ya majukumu yake, ila atawahi kurudi na atakuja kukuona”
“Sawa, ila mama mbona ulishangaa sana kuona picha ya marehemu baba yangu?”
“Aaaah kuna mtu nimemfananisha nae, hivi huko kwenye kaburi la baba yako mmeanza kwenda lini?”
“Toka mwaka juzi, huwa tunaenda mara kwa mara na mama na kufanya usafi kwenye kaburi la baba”
“Huyo baba yako aliitwa nani?”
“Mama, aliniambia kuwa baba anaitwa Jimmy”
Hapo kidogo mama Angel akashtuka na kuhisi pengine kuna ukweli ila bado ilimchukua ngumu sana kuamini, akamuuliza baadhi ya maswali Sarah na mwisho wa siku aliamua kutoka nae sebleni ili wakae waangalie hata vipindi mbalimbali kwenye luninga.

Siku akiwa anafanya kazi zake, mara alifika pale mama mkubwa wa Sarah yani dada yake na mama Sarah, na alienda pale kwa lengo la kumuona Sarah, kwakweli aliogopa sana ukizingatia katoa ruhusa ya Sarah kwenda kuhudumiwa pengine,
“Haya Saraha yuko wapi?”
Siku alikuwa akitetemeka kwani alimjua huyu alivyo mkali,
“Nisamehe mama”
“Nikusamehe kitu gani? Yuko wapi Sarah?”
Ikabidi amueleze ukweli wote wa jinsi ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumpa Sarah ruhusa,
“Hivi wewe Siku una akili kweli, hata kama umeshindwa kumuuguza mtoto si ungenipigia simu hata mimi nije nimchukue jamani! Ila ni vyema alijitokeza huyo msamalia mwema, yani wewe huna maana kabisa, mdogo wangu anakuhudumia bure, anakupa kila kitu halafu unashindwa kumuuguza mtoto wake kweli!! Shwain, haya nipeleke huko kwa msamalia mwema”
Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,
“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”
Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel.


Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,
“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”
Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel.
Kwakweli mama Angel alimshangaa sana, huku akimuangalia kwa makini huyu mwanamke ambaye alionekana kuwa na gadhabu sana, basi mama Angel alimuuliza,
“Kwani tatizo nini dada?”
Yule mama aliongea huku akibana pua na kuiga alichoongea mama Angel,
“Kwani tatizo nini dada? Hivi una akili wewe mwanamke, yani unaweza hata kuthubutu kumchukua mtoto wa dada yangu umlee na hiyo roho yako mbaya! Muone vile, sikupendi kabisa”
“Nimefanyaje? Sikuelewi?”
“Hunielewi eeeh!! Sio wewe uliyekuwa ukishangaa shangaa pindi ukifika ofisini kwa Erick! Sio wewe ambaye kipindi kile nilitaka kukuraluwa halafu ukatetewa na Sia!!”
Huyu mama akacheka kwanza na kusema,
“Mimi ndio Linah, haya huyo Sia kikowapi? Kaolewa na Erick au kaishia wapi? Sikupendi wewe”
Mama Angel akajaribu kuvuta kumbukumbu ila kumbukumbu zake ziligonga mwamba kabisa, akaona kuwa anatakiwa kutumia busara tu kwa muda huo maana hakumuelewa kabisa huyu mtu anamaanisha nini.
Basi alirudi sebleni na kukaa ambapo wale nao waliingia, kisha yule mama alienda kumshika mkono Sarah ili aondoke nae, ila Sarah aligoma,
“Mimi sitaki kuondoka”
“Kheee una wazimu wewe au kitu gani? Sasa hutaki kuondoka, ni kwenu hapa?”
“Sio kwetu ila naridhika nikikaa hapa, hata nimepata amani ya moyo na nimeanza kupona, nitarudi kesho”
Yule mama akamuangalia mama Angel na kumuuliza,
“Umemfanya nini mtoto wangu wewe Erica na uchawi wako?”
Mama Angel alikuwa nyumbani kwake ila alinyamaza kimya kabisa na alishindwa kusema jambo lolote kwani hakumuelewa huyu mtu kabisa.
Huyu mwanamke alionekana yupo kwa shari mahali hapo na kwenda kumbeba Sarah kinguvu na kutoka nae nje halafu alimwambia mama Angel,
“Mimi na wewe hatujamalizana, kama siku ndio kwanza imeanza na nitahakikisha unanikumbuka vizuri, mjinga sana wewe mwanamke”
Halafu akatoka na kuondoka akiwa na Sarah pamoja na yule msichana Siku maana yule msichana hakuongea neno lolote lile zaidi ya kufanya vile alivyo amriwa tu.

Mama Angel kwakweli alipumua kidogo na kuinuka kwenda chumbani kwake maana yale yalikuwa maswahibu kwake, alijaribu kuwaza sana bila hata ya kupata jibu, alijiuliza sana lakini hakupata jibu,
“Linah! Linah ndio nani mbona simkumbuki jamani! Nimewahi kuonana nae wapi?”
Akakumbuka pia huyu msichana kamtaja Sia, hapo akaona kuna ulazima wa kumtafuta Sia ili aweze kujua huyu mwanamke ni nani kabla hajamrudia tena maana kwa ule muda mchache hakumuelewa kabisa.
Leo alichukua simu yake na kumpigia Sia, kitendo ambacho hajawahi kukifanya kutokana na akili ya Sia,
“Kheee leo Erica umenipigia! Kweli maajabu, kuna nini tena jamani?”
“Nina maongezi na wewe”
“Oooh nije kwako? Nakuja sasa hivi, utamwambia basi mlinzi aniruhusu niingie”
Muda ule ule Sia alikata simu yani hakusikiliza maelezo mengine wala nini inaonyesha alifurahi kusikia kuwa mama Angel ana mazungumzo nae.
Basi mama Angel akajiweka sawa na kusema,
“Najua si jambo jema kuzungumza na Sia ila kwa hili natakiwa kuzungumza nae tu, natakiwa nimtambue huyu mwanamke mapema, maana simkumbuki kwa lolote lile jamani”
Baada ya muda mfupi tu alipokea simu toka kwa mlinzi akiulizwa kuwa amruhusu Sia nae alisema amruhusu basi alitoka nje na kukutana na Sia na moja kwa moja alienda nae kwenye bustani yake kuzungumza nae,
“Najua utashangaa sana kwanini nimekuita”
“Kweli nashangaa hadi muda huu bado nashangaa, upendo ulionionyesha leo ni mkubwa”
“Kheee jamani wewe mwanamke, hivi huna mashaka kuwa nitakudhuru?”
“Wapo wakuwa na mashaka nao ila sio mtu kama wewe, nikiitwa na yule Oliva lazima ningeomba usaidizi wa kusindikizwa, ila wewe hapana jamani huwezi kunidhuru. Niambie tu ulichoniitia hata hivyo mimi sio adui yako kabisa, ila adui yako ni mapenzi”
“Mapenzi ndio adui yangu!! Khaaa tuachane na habari hizo kwanza, kuna kitu nataka nikuulize”
“Kitu gani?”
Mama Angel alimueleza kwa kifupi tu kuhusu mtu aliyekuja hapo nyumbani kwake na kusema anaitwa Linah, hakumuelezea tu kuhusu Sarah kuwa alienda kumchukua au nini ila alimuelezea kile alichotaka kufahamu kuhusu Linah,
“Unajua nimejaribu kumkumbuka ila simkumbuki kabisa, sema kasema kuwa alitaka sijui kuniburuza ofisini ila nikaokolewa na wewe”
“Kheee yani kumbe yule Linah mkorofi ndio kapajua hapa kwako!! Mbona pole sana”
“Eeeeh nielekeze vizuri”
“Kipindi cha zamani hapo, wakati mwanao Angel akiwa mdogo sijui ulitumwa na Erick kuja ofisini kumchukulia Angel bima ya afya, ila yule secretary akasema subiri, na mara akaja Linah na kukusukuma, ni kidogo tu ungebamiza kichwa hiko ila kwa bahati nilitokea nyuma yako na kukudaka”
Hilo tukio mama Angel aliaweza kulikumbuka na kusema,
“Aaaah kumbe!! Ndio yule mdada alikuwa baunsa?”
“Ndio huyo huyo, na ni baunsa kweli yani, siku ile nisingetokea kukutetea lazima ungerudi kwenu na ngeu, maana yule pale ofisini kote walikuwa wanamuhenya”
“Sasa nimekumbuka, ila mimi kosa langu nini kwani hadi leo?”
“Kosa lako si kumchukua Erick! Kwani hujui ni kwanini tunakuchukia jamani? Ni sababu ya Erick tu, yani Erick ndio tatizo wa yote haya”
“Hebu leo tuongee vizuri kwanza, maana hadi sijamuelewa huyu Linah kabisa”
“Ngoja nikueleze kwa kifupi, na miaka hiyo ya nyuma niliwahi kukwambia, ni hivi Erick hakuna rangi ya mwanamke aliyoiacha, aliyejichubua kidogo, aliyejichubua sana, aliyekuwa hasilia wote kapita nao, mwembamba, mnene, mrefu, mfupi, saizi ya kati wote kapita nao yani Erick hakuna mwanamke aliyeacha, sema wengine tulikuwa tukimvumilia tu huku tukijipa moyo kuwa ipo siku atatuoa, kama mimi na wengi waliamini nitaolewa na Erick ila haikuwa hivyo”
Sia akapumua kidogo na kuendelea,
“Sasa kuhusu Linah, pale ofisini mwanamke ambaye alitembea na Erick halafu alikuwa na nguvu sana na wote ofisini walimuogopa alikuwa ni Linah, yani yeye ndio kila mtu pale ofisini alikuwa akimuogopa kasoro mimi ambaye wengi walihisi ndio nitakuwa mke halali wa Erick, kama kuhusu mimba, Erick kashatutoa sana mimba, kiukweli Erick unamuona mstaarabu tu kwasasa ila kama watoto naye angekuwa na kijiji chake kwasasa, ila katoa wanawake wengi sana mimba, na wengi walikuwa wakikubali maana alikuwa anasema ukiendelea na hiyo mimba naachana na wewe, basi tukajikuta tunakuwa watumwa kwa Erick. Yani ilikuwa unamkuta na Kitabu chake kidogo kina tarehe za siku za wanawake zake kama ni siku zake vile, yeye hadi anakukumbusha ukachome sindano za majira. Kwakweli Erick alikuwa akijijali yeye na hisia zake tu, sasa kilichotokea ni kwamba, baada ya sakata lako kila mtu pale ofisini alikuwa hakufagilii wala nini, ila kuna jambo baya sana lilitokea maana Erick alirudi na kutufukuza wote kazi, yani wote na akaajili watu wengine kwahiyo watu wengi walikosa kazi sababu yako akiwepo na huyo Linah, na hadi anaondoka pale kazini alisema nikija kumkamata huyo Erica nahisi atanitambua vizuri”
“Duh jamani, sasa mimi nahusika na nini hapo?”
“Wewe huhusiki ila ni kwamba mtu anakuwa na kinyongo tu na kuhisi kuwa wewe ndio chanzo, ila una pesa Erica, basi usibabaishwe na huyo Linah, halafu mumeo akirudi hebu mwambie akae sawa na wanawake wote aliowapitia ili ajue kaacha doa gani”
“Duh!”
“Usishangae, haya mambo ndio yalivyo, unajua mara nyingine mtu unafanya jambo katika maisha ila hujui madhara yake sema badae yanapokutokea puani ndio uanjua kuwa ulichokuwa unafanya hakikuwa sawa. Katika wanawake wote wa Erick basi mimi ndio nilikuwa namba moja maana nilijulikana na familia yake nzima, mama yake, baba yake, huyo dada yake Tumaini ndio alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na anajua ni mangapi nimepitia kwa mdogo wake, ni kweli natenda mambo ya karaha ila huyo Tumaini hawezi kusema sana kwani anajua ni mangapi nimepitia, huyo Erick pia ataishia kunipiga tu ila hawezi kunifanyia kitu kibaya maana ingawa kwa ubaya wangu ninaoufanya ila bado kuna mazuri yangu ambayo akiyafikiria moyo wake unamsuta sana”
“Mmmh!”
“Usigune Erica, kumbuka Erick alikuwa ni mlevi sana anaweza akajitapikia balaa basi mimi nitamtoa nguo na kuanza kuzifua na kusafisha pote alipotapika, kuna siku alitapikia gari yake nilifanya usafi kwenye gari ila kamavile hakutapika kabisa, kwakweli nilikuwa najitoa sana kwa Erick nikiamini kuwa yeye ndio atakuja kuwa mume wangu na nitaishi nae kwa furaha na amani”
Mama Angel akaona hapo ataletewa stori zingine kabisa, basi aliamua kumkatisha Sia kwa kumshukuru kwa kumuelezea kuhusu Linah kisha akamuaga,
“Kheee jamani ndio hata kwenda ndani kwako kula hakuna!”
“Mimi sikukuita uje kula ila nilikuita kwasababu hiyo”
Ila mama Angel alijua wazi kuwa Sia alikuwa akipenda sana pesa basi alienda ndani na kumtolea pesa kidogo na kumpa, basi Sia akatabasamu na kuondoka zake, kisha mama Angel akaenda zake ndani sasa.
 
SEHEMU YA 317

Erick alikuwa na Erica kwenye lile duka la baba yao, na muda kidogo yule Rama alifika na vile vitu alivyokuwa ameagiziwa na Erick,
“Oooh ndio umeniletea wasifu wako eeeh!”
“Ndio, kama ulivyoniagiza jana”
Basi Erick alifungua ile bahasha na kupitia pitia, basi Rama alikuwa akimuangalia Erica jinsi alivyokuwa akiangalia angalia vitu pale dukani, akamuuliza Erick,
“Samahani, ndio shemeji yule nini!”
“Mmmh kivipi?”
“Yani yule ndio mtu wako? Yani mpenzi wako?”
Erick akacheka kwanza na kumwambia,
“Hey, sababu nasimamia duka hapa ndio unaniona mkubwa, jamani mimi bado mdogo sina hayo mambo kabisa. Yule ni mdogo wangu, ni pacha wangu, mimi na yeye tumezaliwa mapacha”
“Aaaah naomba unisamehe”
Kisha Erick akamuita Erica karibu na kuanza kumtambulisha kwa Rama,
“Si unaona hata majina yetu yanavyoendana? Sababu sisi ni mapacha”
“Nisamehe, ila kwenu ni wazuri sana, maana huyu pacha wako ni mzuri sana”
Erick alishika ule wasifu wa yule kaka na kumwambia kuwa Jumatatu aende kuanza kazi, ila yule kaka akamwambia,
“Hata kesho naweza kuanza tu hakuna tatizo”
“Sawa, basi kesho njoo uanze kazi, kila kitu nitakuonyesha leo. Halafu kesho nitapitia kidogo kukuangalia”
Basi akaanza kumuelekeza vitu pale dukani na kuweka vizuri kila kitu, na walipomaliza Erick alitaka kufunga tu duka maana alikubaliana na Rama kuanza kesho ila Rama akamwambvia,
“Hapana, ngoja tu leo niimalizie hapa ili hata wateja wajue kuwa duka limerudi sasa na litakuwa wazi siku zote”
“Oooh sawa, sasa watakaokusaidia kuuza, maana Steve alikuwa na wadada wawili humu dukani, yeye ndio anajua alikowapata maana sisi tulikuwa tunamtambua yeye. Na kitu kingine hao watu wewe ndio unajua cha kufanya nao, kwahiyo kama utataka wale wa Steve sawa, au kama utatafuta wengine napo sawa, ila tu biashara isonge mbele. Ukiwatafuta nitakuja kuwakagua pia”
Rama aliitikia tu maana hakuwa na namna zaidi ya kumuheshimu mtu huyu ingawa alikuwa mdogo kwake ila alikuwa na pesa za kumfanya yeye amuheshimu sana tu.
Basi Erick alipomaliza aliondoka na Erica kwenda nae kiwandani.

Walifika kiwandani nankutembea nae sehemu mbalimbali kisha Erick alienda ofisini sasa kufanya kazi za pale ambazo zipo ila muda huo Erica alikuwa akizunguka zunguka tu nje ya kiwanda kile, na mara akakutana na yule baba aliyekutana nae siku ile ya uzinduzi ambaye alimpa pesa na kadi ya mawasiliano,
“Erica hujambo!”
Erica akashtuka kidogo na kumuitikia,
“Sijambo shikamoo”
“Leo hapa kiwandani umekuja tena na mama yako?”
“Hapana, nimekuja na kaka”
“Oooh unanikumbuka vizuri, siku ile nilikupa pesa na kadi yangu ya mawasiliano”
Erica aliitikia kwa kichwa tu kuwa anamkumbuka, kisha yule baba akasema tena,
“Mbona hukunitafuta au zile pesa hazikukutosha?”
“Kheee, mimi pesa za nini zile? Nilimpa mama hela zote na ile kadi”
“Wa wapi wewe mtoto eeeh! Mbona wa ajabu hivyo, kwani huna matumizi ya pesa? Una simu?”
“Hapana sina simu”
“Basi mimi nitakununulia simu nzuri sana, unajua wewe ni binti mzuri sana”
Erica akatabasamu, basi yule baba akasema,
“Khaaa kumbe wewe katoto umerithi hadi dimpozi za mama yako, hakika wewe ni mrembo sana. Yani ndio nyie ambao mmezaliwa mkazalika, wewe mtoto ni mzuri sana, unavutia sipati picha ukiwa mkubwa huko utakuwaje? Ila kiukweli nimevutiwa sana na wewe”
Erica alikaa kimya sasa maana hata hakujua ni kitu gani ajibu kwa huyu mtu aliyekuwa akimsifia kiasi huki, basi yule baba akatoa pesa zingine na kumapa Erica ila Erica alikataa zile pesa,
“Chukua tu, mama mwambie kuwa anko Rahim ndio kanipa hizi hela, unafikiri atagomba! Yani atafurahi tu”
“Hapana, mimi sina matumizi ya hela”
“Wewe mtoto mbona wa ajabu sana, huna matumizi ya hela kivipi? Kwanza dada yako Angel yuko wapi?”
“Yupo shule, anasoma boarding”
“Kheee ndio wamemkumbizia huko mwanangu!”
“Mwanao!!”
Mara alifika pale Erick na kumuita,
“Erica”
Basi akageuka na kumuaga yule baba na kumfata Erick,
“Nani yule, na ulikuwa unaongea nae nini?”
“Si yule wa siku ile, alikuwa ananipa tena hela ila nimekataa”
“Haya, twende tukakae wote ofisini yani wewe mambo yako hata sijui huwa unafikiria nini”
Moja kwa moja Erica aliongozana na Erick hadi ofisini na kumuacha yule baba akiwa amesimama tu pale nje ya ile ofisi na alisimama pale kwa muda kidogo kisha akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 318

Erica na Erick walimaliza na kutoka ofisini kurudi nyumbani kwao, walipokuwa kwenye gari Erica alilalamika kuhusu Sarah,
“Jamani mimi na leo nitalala sebleni”
“Hapana utalala chumbani kwangu, usiwaze kulala sebleni wakati chumbani kwangu papo”
“Sawa, hakuna tatizo. Kheee kaka hebu angalia yule ni nani?”
Ilibidi Erick asimamishe gari pembeni, na walimuona mjomba wao Erick akiwa amezingirwa na vijana kama kumi hivi huku wengine wakisogea, basi ilibidi washuke kwenye gari na kufata karibu ili wajue tatizo ni kitu gani,
“Jamani kuna nini?”
“Nyie watoto mtatusaidia nini hata mnauliza kuna nini?”
Ila Derrick alipoona hawa watoto wa dada yake aliwasogelea karibu na kuanza kuwaomba msaada,
“Nisaidieni wangu, nahadhirika leo”
“Kwani tatizo ni nini?”
“Wananidai laki moja”
Yani Erick kwakweli hakuona kama ni jambo jema kwa mjomba wao kudhalilika sababu ya laki moja, basi kwa bahati alikuwa nayo kwenye gari ikabidi atoe na waondoke pale na mjomba wao, huku wale watu wakidai siku hiyo wangemfunza adabu, Erick aliondoa gari lile na kumuuliza,
“Kwani mjomba tatizo ni nini? Kwanini udhalilike kiasi hiko, mbona nasikia wewe umesoma sana tu”
“Ni kweli mwanangu, yani hata mimi sielewi, sijui nina laana sijui ni kitu gani. Ila nashukuru sana mmenisaidia maana leo hata sijui ningefanyeje jamani”
Basi kuna mahali akafika na kuhitaji wamshushe na kuwaomba hata nauli, basi Erick akatoa elfu kumi na kumpatia mjomba wao nauli na kuagana nae.
Ila wakati Erick anaendelea kuendesha ile gari akagundua kuwa mafuta yalikuwa yameisha na kumwambia dada yake,
“Aaaah siku makini, unajua mafuta haya hayawezi kutufikisha nyumbani, ngoja tupitie pale kituo cha mafuta tuweze kuongeza mafuta”
“Bora umekumbuka maana linetuzimikia katikati ya barabara ndio balaa”
Basi walipita kwenye kituo cha mafuta na kuweka gari yao ili ijazwe mafuta, kisha mama wa makamo ndio alifika dirishani na kuwauliza,
“Ya pesa ngapi?”
“Ya elfu arobaini”
Basi yule mama aliwatilia mafuta na baada ya hapo kuwadai hela, ila cha kushangaza Erick hakuwa na pesa yoyote ile yani alijipekua ila hakuwa na pesa kabisa, Erica alimuuliza,
“Kwani imekuwaje?”
“Unajua sielewi kabisa hata sielewi imekuwaje ila pesa hakuna”
Yule mama alisikia akaona hawa watamkimbia basi akawahi kuingiza mkono wake kwenye gari na kuchukua funguo, kisha akawaambia,
“Nipeni pesa yangu ndio muondoke hapa”
Basi Erick akaamua kumsihi yule mama,
“Sikia mama, naomba turuhusu halafu mimi nitakuletea hiyo hela yako”
“Unachekesha sana, hivi nyie vijana wa siku hizi mkoje eeh! Mnacheza na kazi za watu sio, umekuja na gari zuri sijui umeaizma wapi, umekuja na kimwanamke chako, kwahiyo ukataka kukionyesha kuwa una hela, weka mafuta ya elfu arobaini halafu hela yenyewe huna, sichezi hapa, nina watoto wakubwa kushinda nyie, nipeni hela yangu ndio muondoke kabla sijawaitia watu hapa”
Erick alimuangalia Erica, ikabidi washuke tu kwenye gari ili wajadiliane pembeni, basi Erica akasema,
“Basi tumpigie simu mama au baba”
“Tutawapigia na nini? Mimi huwa sina simu toka mama alivyotupokonya, nikiwa ofisini basi nawasiliana nao kwa simu ya ofisi, ila sasa tupo njiani tutafanyaje jamani!”
“Kwanza imekuwaje huna hela? Yani imekuwaje tuseme tuwekewe mafuta bila hela?”
“Sijui kama unaweza kunielewa, ni hivi wakati natoka nyumbani nilikuwa na laki moja kwenye gari maana baba aliniambia kuwa niwe natembea na pesa kiasi ili likitokea tatizo niweze kupata ufumbuzi, sasa na kule kiwandani kuna laki tatu nimetoka nayo leo maana hatukuifanyia mahesabu na ilikuwepo pale maana wanunuzi wetu wengi wanalipia kwa kutumia hundi. Nilipanga na meneja wa pale kuwa kesho nitaenda tuifanyie mahesabu kwahiyo nikaondoka nayo na niliiweka kwenye wallet, tulivyofika pale ambapo mjomba alizingirwa na lile tatizo la laki moja, nikaona isiwe kesi ndio nikatoa ile laki moja ya kwenye gari na kuwapa wale halafu tukaondoka na mjomba, sasa wakati mjomba anashuka alivyokuwa anaomba nauli ndio nikamtolea elfu kumi kwenye wallet na kumpa, ila nashangaa hapa sina kitu kwenye wallet, ni tupu kabisa, hakuna hata mia”
“Duh!! Sasa ni kitu gani hiki?”
“Yani sielewi, ukisikia kuumbuka ndio leo jamani, sijui tutapata wapi msaada”
Yule mama alikuwa akiwafata mara kwa mara na kuwaambia maneno ya karaha, yani wakawaza cha kufanya pale hadi basi, kisha Erica akasema,
“Au tufanyeje, tukodi bodaboda halafu mmoja wetu aende nyumbani kuchukua hela”
“Umewaza vyema ila itatugharimu sana”
“Najua ila ni bora kuliko aibu na dhahma hii”
“Lakini nani ataenda nyumbani na nani atabaki hapa?”
“Mimi hapa naweza kubaki tu”
“Hapana, siwezi kuruhusu ubaki tu hapa au uende mwenyewe nyumbani na bodaboda”
“Kwanini sasa?”
Mara Erick alimuona kama mtu anayemfahamu, basi alimfata na kumsalimia, alikuwa ni Juma ambaye alikuwa akipita hapo kwenye kituo cha mafuta,
“Kheee Erick, nimefurahi sana kukuona.”
“Samahani baba, nilikuwa na shida. Unaweza kutuazima elfu arobaini”
“Ya nini kwani?”
Erick alimsimulia kifupi tu kuwa wanadaiwa hela ya mafuta hapo, walikwenda kujaza mafuta bila kuangalia pesa kama ipo, kwakweli Juma aliamua kumpa Erick hiyo hela maana huwa anampenda sana huyu mtoto, basi Erick alimshukuru pale na kwenda kumlipa yule mama ambaye alitoa funguo kwa masimango pia,
“Ndio muache tabia hii jamani, hiki kituo cha mafuta sio cha baba yenu”
Basi walimshukuru tena yule Juma na kuagana nae ambapo sasa walielekea nyumbani.

Mama Angel alishangaa sana kwa jinsi watoto wake walivyochelewa kurudi ila walimsimulia kila tukio mama yao,
“Kheee jamani, mlianzaje kumpa hela mjomba yenu?”
“Sasa tungefanyaje mama? Alikuwa na matatizo”
“Ni kweli yule ni mjomba wenu ila ana matatizo sana, mjomba wenu ni tapeli kwahiyo hizo hela ni yeye kazichukua kimazingaombwe”
“Kwahiyo si kweli kwamba wale walikuwa wakimdai laki moj?”
“Inawezekana ikawa kweli ila tapeli siku zote hana shukrani, sasa nyie mmemsaidia kwa upendo halafu yeye kawatapeli jamani, poleni sana wanangu”
Ila mama Angel hakupenda kabisa kile kitendo ambacho kimefanywa na Derrick.
Yani Erica na Erick hakuna hata mmoja aliyeulizia habari za Sarah kuwa yuko wapi wala nini, zaidi zaidi walienda kula na moja kwa moja kwenda kulala ambapo Erica alienda kwanza chumbani kwake, na vile hakumkuta Sarah ndio akafurahi na kulala humo kwa furaha.

Usiku wa leo, kama kawaida Junior alikuwa amelala chumbani kwaVaileth huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Hivi kweli Junior utanioa?”
“Ndio, nitakuoa Vai. Niamini, nimedhamiria kuwa na wewe”
“HIvi kweli umeacha kabisa kufikiria wanawake zako wengine?”
“Wa kazi gani sasa wakati wewe upo”
Mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, ila Vaileth aliomba ausome huo ujumbe, na Junior alimpa bila tatizo,
“Hellow Junior, mbona umenipotezea hivi? Natuma ujumbe hunijibu, nakupigia simu hupokei, kwanini unanifanyia hivi Junior?”
Basi Vaileth alimuangalia Junior na kutabasamu kwani alitambua kuwa kwasasa Junior anampenda kiasi cha kusahau wanawake zake wengine wote.

Kulipokucha, mama Angel alikuwa kaamka na kuwataka wote mule ndani wajiandae kwaajili ya kwenda ibadani, na kweli wote walijiandaa kwa siku hii hadi Vaileth maana alitaka kuondoka na watu wote.
Basi mama Angel alipokuwa akitoka ndani, alishangaa kumuona yule Linah akiingia getini kwake, inamaana siku hii alirudi tena, halafu alikuwa kaongozana na mwanamama mwingine mwenye mwili mkubwa zaidi hadi mama Angel alishikwa na uoga kiasi, ila walipomsogelea tu kabla hawajaongea chochote, wakina Junior nao walitoka ndani na kusogea pale ila cha kushangaza yule Linah alipomuona Junior alishangaa sana na kusema,
“Junior!! Kheee unaishi hapa!”
 
SEHEMU YA 319

Basi mama Angel alipokuwa akitoka ndani, alishangaa kumuona yule Linah akiingia getini kwake, inamaana siku hii alirudi tena, halafu alikuwa kaongozana na mwanamama mwingine mwenye mwili mkubwa zaidi hadi mama Angel alishikwa na uoga kiasi, ila walipomsogelea tu kabla hawajaongea chochote, wakina Junior nao walitoka ndani na kusogea pale ila cha kushangaza yule Linah alipomuona Junior alishangaa sana na kusema,
“Junior!! Kheee unaishi hapa!”
Junior alikaa kimya tu, ila huyu mama alisogea na kumshika Junior mkono halafu akatoka nae nje ya geti kabisa huku yule mmama mwingine akimfata kwa nyuma, kwakweli hii hali ilikuwa inamshangaza mama Angel hadi akakosa cha kusema kwa muda huo, alibaki anashangaa tu basi Erica akasema,
“Mama unashangaa hivyo unajua yule mwanamke ni nani?”
“Mmmh! Inamaana wewe unamjua? Ni nani?”
“Mmmh sitaki kusema hapa nitaonekana mbea”
Muda huo Vaileth alienda ndani maana alihisi kutokuelewa kabisa, kwahiyo pale alibaki Erica na mama yake maana Erick alisogea kule getini alikopelekwa Junior, basi mama Angel alimuuliza vizuri,
“Ni nani kwani?”
“Yule mama ni mwanamke wa Junior”
Mama Angel alishangaa sana hadi alihisi akili yake kugoma kufanya kazi,
“Yani Junior akawe na mahusiano na mwanamke mtu mzima vile kushinda hata mama yake!!”
“Ndio hivyo”
“Hebu mshike mtoto nenda nae ndani”
Kisha mama Angel alienda moja kwa moja nje ili ajue ni kitu gani wale wanawake wameenda kuongea na Junior, alipofika nje aliwaona wale wanawake wakiingia kwenye bajaji na Junior wakiondoka nae, kwakweli alishangaa zaidi na kumuuliza Erick ambaye nae alisimama akiwashangaa,
“Umeelewa kitu gani mwanangu?”
“Sielewi kitu, nimesikia tu yule mama analalamika kwa Junior kuwa kwanini anapiga simu halafu Junior hapokei, sijui anatuma jumbe ila hazijibiwi na Junior ndio wakambeba na kuondoka nae”
“Kheee makubwa haya”
Mama Angel alirudi ndani hata Erick nae alirudi ndani ila kiukweli kwa muda huo hakuwa tena na hamu hata ya kwenda ibadani kwani alihisi akili yake kuvurugika vilivyo, kuna muda alijipa moyo kuwa Junior angerejea tu ila badae akaona hapana anatakiwa kujitoa muhanga na kwenda kumfatilia Junior, hivyo alimuomba mwanae Erick waende pamoja kwahiyo hapakuwa tena na safari ya ibadani,
“Ila mama tutaenda kuwafata wapi?”
“Yule mwanamke ni mama mkubwa wa Sarah, kwahiyo twende kwakina Sarah ndio tutajua pa kuwapata”
Basi Erick alikubali kwahiyo mama Angel alienda kubadili nguo kisha akawaaga wakina Erica na kuondoka na Erick.

Vaileth alimfata Erica na kumuuliza vizuri maana alihisi lazima kuna jambo Erica anatambua kuhusu wale wanawake,
“Erica naomba uniambie ukweli, kumbuka mimi ni mwanamke mwenzio”
“Ila humu ndani si huwa mnaniita mimi kambea?”
“Hapana, mimi sijawahi kukusema vibaya kwa hiyo tabia yako, nakuomba Erica uniambie ukweli”
“Ni hivi, yule mmama aliwahi kuwa na mahusiano na Junior”
Yani hata Vaileth mwenyewe alishangaa sana na kuuliza,
“Kheee mmama wote yule?”
“Nakumbuka nishawahi kukwambia kuwa Junior aliwahi kuwa na mahusiano na wamama wakubwa kushinda hata mama yake, basi ndio kama vile”
“Jamani Junior, kwanini lakini?”
“Kwanza ungetakiw akushangaa kwa Junior kukufata wewe, maana ni kijana mdogo ila kakufata wewe na anajifanya anakupenda sana kuliko chochote kile. Jiulize kwanza wewe Junior umempita umri gani? Na alipata wapi ujasiri wa kukufata wewe?”
“Mmmh Erica unaongea kama na wewe ni mtu mzima? Inaonekana unatambua mengi sana”
“Ndio, sababu mimi ni mbea na umbea wangu unafanya nitambue mambo mengi sana, na vingine hata huwezi kudhani na unaweza kujiuliza kuwa huyo mama nimemjuaje? Ila mimi namjua huyo mama na nilionyeshwa na huyo huyo Junior”
“Kheeee!!”
“Kwa kifupi, Junior anapenda kuwa na mahusiano na wanawake waliomzidi umri, sijui ni kwanini ila ndio tabia yake, hata baadhi ya watu waliniambia hivyo kuwa Junior anatembea na wanawake wakubwa sana. Naona kukupata wewe imekuwa furaha kwake, yani wewe unajiona mkubwa ila Junior anaona kamavile upo sawa nae. Ila jitafakari kama Junior anakufaa”
Yale maneno yalimuingia Vaielth kwenye akili yake, na kujikuta akiinuka pale sebleni na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.

Mama Angel na Erick walifika nyumbani kwakina Sarah na hawakumkuta mtu yoyote, nyumba tu ilikuwa imefungwa, yani hapo ndio mama Angel hakuelewa kabisa, basi hakuwa na namna zaidi ya kumwambia mwanae warudi nyumbani tu kwani alitaka kwenda kufikiria zaidi kitu cha kufanya.
Wakiwa njiani, alimuona Sia ameongozana na mtoto wake Elly basi mama Angel alimwambia Erick asimamishe gari kisha akashuka na kumuita Sia ambapo Sia alifika na kumsalimia, Elly nae akamsalimia mama Angel,
“Shikamoo”
Sia akadakia na kumwambia Elly,
“Shikamoo nani? Sema shikamoo mama”
Basi Elly akarudia tena,
“Shikamoo mama”
Mama Angel aliitikia tu kwani hakutaka kufanya mabishano yoyote na Sia kwa muda huo, kisha akamvuta pembeni na kumwambia yale yaliyojiri kwani alimtambua fika Sia kuwa ni mtu wa matukio mbalimbali,
“Samahani, kwanza nashukuru kukuona. Nyumbani kwangu kumetokea tatizo”
“Tatizo gani?”
Mama Angel akamsimulia jinsi Linah na mwenzie walivyokuja na jinsi alivyoambiwa na Erica na jinsi walivyoondoka na Junior hapo kwake, basi Sia akasikitika na kusema,
“Naona kwasasa unauona umuhimu wangu Erica, mimi ni kama maji usiponinywa basi utanioga tu”
Erica hakutia neno hapo maana alikuwa akihitaji msaada kwaajili ya Junior, kisha Sia akaongea tena,
“Ipo hivi, kwa habari ambazo nimezisikia, Linah ana stress bora hata zangu afadhari, kiukweli huyu Erick huyu katutianuchizi haswaa, yani nasikia Linah aliona kuwa wanaume wakubwa hakuna mwenye mapenzi ya kweli ndio hapo alipoanza kutembea na vivulana vidogo. Namshukuru Mungu sijafikia huko maana ni kujidhalilisha, kwahiyo inawezekana kabisa kuwa alikuwa na mahusiano na Junior ukizingatia Junior ni kavulana kahuna sana, kamerithi kwa baba yake kale, ila uhuni utamtesa kama huyo babake mdogo Erick. Ila mimi nitakusaidia na Junior atarudi nyumbani”
“Nashukuru sana ndugu yangu”
“Kheee makubwa, nimekuwa ndugu yako leo, yani mimi adui yako namba moja leo nimekuwa ndugu!! Kweli maisha yanabadilika”
“Tuachane na hayo yaliyopita bhana, unajua nimeshangaa sana kwa Junior kuwa na mahusiano na mmama mkubwa vile!”
Sia akacheka na kusema,
“Ama kweli inachekesha na kuhuzunisha kwa wakati mmoja, mwanamke anatembea na baba halafu miaka ijayo anakuja kutembea na mtoto jamani maisha haya. Ila hata Erick alikuwa hivyo, alikuwa anatembea na wadada wakubwa kwa wadogo, usimshangae sana Junior”
“Mmmmh! Hayo mambo yalishapita ndugu yangu”
Ila kwa stahili hii naamini kuna siku utakubali Erick anioe mimi na wewe yani wote tuishi pamoja, yani mimi kinachonitesa ni mapenzi, kilichoondoa akili yangu ni mapenzi. Nimejaribu sana kumtoa Erick katika akili zangu, fikra zangu na mawazo yangu lakini nashindwa kabisa, muda wote nakumbuka mapenzi yake, nakumbuka alivyokuwa akinijali, nakumbuka alivyokuwa akinibembeleza, licha ya maudhi machache aliyokuwa nayo Erick ila ni mwanaume ambaye anajua sana kupenda, kila muda namuwaza Erick”
Mama Angel alipumua tu ila hakusema neno lolote lile, zaidi zaidi aliagana nae,
“Natumaini utanifanyia hiyo kazi, asante sana”
“Usijali ila kitu kimoja tu ningetaka kutoka kwako, uwe unaniruhusu hata nije nyumbani kwako kumsalimia Erick, tafadhali msinifanyie kama mlivyomfanyia Rahim kutokumuona kabisa mwanae na hadi sasa hajui anafananaje, nipeni ruhusa ya kuja kumsalimia Erick”
“Hapo ndio mimi na wewe hatuelewani, hebu kuwa muwazi, kwahiyo Erick ni mwanao na Elly ni mwanangu? Na imekuwaje hiyo?”
“Sijui jinsi ya kukueleza ila Erick ni mwanangu na Elly ni mwanangu pia”
“Yani kama binadamu ana akili tatu basi wewe imebaki moja tu ya kukuongoza kwenye mambo madogo madogo, hebu sikia kwanza, nilibeba mimba, nilienda hospitali nikiwa na mume wangu kupima, nikagundulika nimebeba mapacha tena wa kike na wa kiume. Nilijifungua ingawa kwa operesheni lakini salama kabisa na nilikabidhiwa watoto wangu na ndio hao nawalea hadi sasa. Nakumbuka wewe ulibeba mimba ya mtoto mmoja, haya iweje una mtoto wako na bado unang’ang’ania mtoto wangu?”
“Ipo siku Erica utaitambua akili yangu vizuri, ila ukipaniki utajitesa na kujisumbua mwenyewe. Hata mimi kuna vitu vingine sielewi, najua kwamba Erick ni mwanangu ila sijui ni kwanini ananichukia maana nahisi huyo mtoto akiambiwa mtu wa kwanza kumuua duniani ataanza na mimi. Hivi kwanza hamumuoni kwamba hafanani na nyie ndani kwenu, mtoto ana roho mbaya huyo kama mkaanga sumu, mtoto ana akili mbovu huyo kupita maelezo, mpe malezi yote, msomeshe dini zote ila hapo utagonga mwamba, najua siku moja utakuja kunililia kuhusu huyo mtoto, utasema kuwa nilikwambia na maneno yangu yatatimia”
“Ushindwe na ulegee”
Kisha mama Angel aliondoka zake na kurudi kwenye gari ila Erick hakushuka kabisa hata kumsalimia huyu mama ndio kwanza alimuuliza mama yake,
“Kwani mama ulikuwa unaongea nini na yule mmama?”
“Aaaah kuna mambo nilikuwa namwambia”
“Simpendi kabisa, yani simpendi”
“Naelewa ni kwanini humpendi ila usimjali maneno yake maana huyu mwanamke ni watu waliochanganyikiwa na maisha. Hata usimjali kitu”
Basi wakaendelea na safari na kurudi nyumbani.
 
SEHEMU YA 320

Mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwake kupumzika kwani aliona akili yake ikigonga mwamba, alifikiria kuhusu Junior bila ya jibu kisha alianza kufikiria kuhusu maneno ya Sia na kujisemea,
“Yule mwanamke ni mgonjwa tena ni mgonjwa sana, huwezi kukazana kusema mtoto ni wako halafu unamuombea mabaya muda wote, hakuna mzazi anayemuombea mabaya mwanae. Nadhani kuna kitu anataka kukijenga kwetu, anataka tumchukie mtoto wetu halafu mwishowe tujutie kwa kitendo hiko. Sasa maneno yake yameingia kulia na kutokea kushoto, nitampenda Erick na yeye ndio atakayeangalia dada zake”
Basi wakati akifikiria hayo, akapigiwa simu na huyo huyo Sia, ikabidi apokee na kuanza kuongea nayo,
“Nimefanikiwa kufika nyumbani kwa Linah, ni kweli kabisa yupo na Junior na analalamika kuwa Junior kampotezea, eti huwa anampigia simu halafu hapokei anamtumia ujumbe halafu hamjibu. Kwakweli hata mimi imeniuma kwa mtoto mdogo kama Junior kuwekwa kinyumba na hili zee, sijapenda kabisa. Sasa nitajitahidi Junior nirudi nae leo, sema sasa tafuta pa kumpeleka maana hili limama litamfata tena”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi akakata ile simu na kuanza kufikiria kwa muda huo kuwa Junior akirudi tu basi arudi shuleni tu kwa siku hiyo.
Na kweli jioni ya siku hiyo Junior aliletwa na Sia, kiukweli Junior alikuwa mpole sana kiasi cha kushindwa kuongea lolote, mama Angel akamwambia,
“Kajiandae nikupeleke shule, muda huu huu”
Junior hakubisha zaidi ya kwenda kujiandaa, halafu Sia alitoka nje kwenda kuongea na mama Angel,
“Nashukuru sana kwa kazi uliyofanya ya kunirejeshea mwanangu”
“Usijali, ingawa nimepambana, na nimetumia uongo wa hali ya juu najua Linah akijua atachukia sana ila mimi kunipata hawezi”
Ikabidi mama Angel ampe tu pesa kidogo Sia kama shukrani kwake, kisha Sia akaondoka halafu mama Angel alimfata Junior na kumtaka waondoke nae ampeleke shule, yani Junior hakuweza kubisha wala kupinga kutokana na mambo yaliyotokea siku hiyo.
Basi wakati wanatoka mama Angel alimwambia mlinzi wake kutokuruhusu tena watu asiowafahamu ndani kwake,
“Natumai umenielewa, kama wale walioingia asubuhi, tafadhari usiruhusu tena watu kama wale”
“Sawa mama nimekuelewa”
Basi mama Angel akaondoka na Junior kuelekea shuleni kwakina Junior.

Wakiwa kwenye gari alimsema sana,
“Kwakweli Junior unatia aibu, kijana mdogo kama wewe kwenda kuhangaika na wamama walioshindikana kiasi kile jamani!”
“Nisamehe mamdogo”
“Sio nisamehe, kwakweli umenikera sana. Na hayo maswala yako ya kurudi rudi nyumbani siyataki hata kidogo, nikikuta umerudi tu bila sababu tutagombana Junior, nadhani umenielewa”
“Nimekuelewa mamdogo”
“Loh unachefua kabisa, mmama wote yule. Ptuuu mtoto mchafu wewe aaarrghhh yani sijui hata cha kukufanya, ukasome tu mjinga wewe. Umenichefua sana”
Basi alimfikisha Junior shuleni na kumuacha hapo kisha yeye akawa anarudi, ila njiani kuna mtu alimuona na kumfananisha na mtu ambaye aliwahi kusoma nae ila hakusimamisha gari kumsalimia kwani mtu huyo alionekana kuwa na haraka sana.
Moja kwa moja mama Angel alirudi nyumbani kwake akiwa amechoka na mambo ya Junior kwa siku hiyo, muda kidogo alipigiwa simu na mume wake,
“Nasikia umeanza kushirikiana na Sia”
“Mmmh kushirikiana nae kivipi?”
“Kwani umeongea nae nini leo na kitu gani kakusaidia?”
“Mume wangu, ngoja niingie chumbani nikusimulie ilivyokuwa”
Basi mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwake, na kuanza kuongea na mume wake sasa, ambapo alimueleza mlolongo mzima, kuanzia habari za Sarah hadi mambo ya Linah,
“Hadi masikio yanauma kusikiliza hayo mambo, unajua sijaelewa kituhata kimoja ulichoniambia. Ni kwamba baba yangu alikuwa na mtoto mwingine? Yani Sarah ni mtoto wa baba yangu?”
“Sijui mimi, ila ndio picha niliyoikuta nyumbani kwakina Sarah”
“Dah!! Hiyo habari sidhani kama ina ukweli wowote, baba yangu alikuwa na matatizo ya uzazi, na kwenye kaburi lake mbona kuna watu ambao tuliwaweka kwaajili ya kufanya usafi na kuangalia na hawajawahi kutuambia kama wamewahi kuwaona hao watu. Hapo kuna kitu mke wangu, kwa hayo mambo naomba hata huyo mtoto Sarah uwe mbali nae kwa muda kwanza maana nashindwa kuelewa kabisa”
“Na habari ya huyo Linah ambaye alikuwa mwanamke wako, ndio alikuja ili kunipiga na mwenzie sijui, ila ndio hivyo wamemkuta Junior ambaye alikuwa akitembea nae”
“Hiyo ndio sijaielewa hata kidogo, nina hakika huyo Linah kwasasa ni mtu mzima wa kutosha tu, hivi akatembee na Junior kweli!! Mbona dunia ina mambo kiasi hiki”
“Kwahiyo wewe hujashangaa swala la huyo mwanamke kutaka kunipiga ila umeshangaa swala la yeye kutembea na Junior?”
“Yote nimeshangaa mke wangu, ila kwasasa nitaongeza ulinzi hapo nyumbani, watu wa kijinga jinga wasiwe wanafika kabisa hapo”
“Haya sasa, lingine ni kuhusu huyo shemeji yako Derrick unayemtetea siku zote, ni hivi kawatapeli watoto wako laki nne”
“Sikuelewi”
Mama Angel akamuelezea vile ambavyo yeye alielezewa na watoto wake,
“Ila mbona kama ndio hivyo kafikia hatua mbaya sana huyo Derrick, halafu kwa mtindo huo inamaana Derrick anatumia chumaulete eeeh!! Maana sio kwa kuvuta hela kwa aina hiyo”
“Ndio hivyo, mimi nilikwambia wazi kuwa Derrick sio mtu mzuri, haya sasa hii hela utailipa wewe”
“Khaaaa mama Angel lakini dah!! Utafikiri akaunti zangu huzijui? Nenda katoe hela kwangu uweke hapo ilipopotea”
“Ila nimeona vyema kukwambia”
“Ni vizuri kuniambia ila nakuamini mke wangu, tena nakuamini sana. Na ninahangaika kwaajili yenu yani wewe na watoto wetu kwahiyo vitu vyangu, pesa zangu na kila kitu changu kipo juu yenu”
Mama Angel aliongea na mumewe na badae kuagana nae kwaajili ya kulala, ila alipomaliza kuongea na mumewe alikaa na kujitafakari,
“Hivi wanaume kama huyu Erick wapo kweli duniani, yani mara nyingine anaongea na mimi naona kama naota vile. Ni kweli nimeolewa na mwanaume mwenye upendo kiasi hiki!! Hii ni bahati kwangu, inapaswa mimi kumshukuru Mungu. Jumapili ijayo nitaandaa sadaka ya shukrani kwaajili ya mume wangu, nitamshukuru Mungu kwa kunipatia huyu mume katika maisha yangu.”
Kisha mama Angel akaamua kulala tu kwa muda huo, ila wakati amelala kuna wazo lilimjia yani alijikuta akitamani kuujua ukweli kuhusu Sarah kuwa mtoto wa mzee Jimmy, yani alijikuta tu akitamani kutambua hayo. Basi akaona ni vyema kesho yake aende kutembelea kaburi la mzee Jimmy ambaye alikuwa ni baba mkwe wake.

Vaileth alienda kulala ila hakuwa na raha kabisa, alijikuta akikaa tu chumbani na kulia kwa muda mrefu sana, alijiona kuwa na mkosi, alijiona kukosa bahati kabisa, aliwaza ni kitu gani afanye ila alikosa jibu kabisa kuwa ni nini afanye, wakati analia na kuumia, simu yake iliita na alipoangalia aliona ni Junior anapiga, kwakweli hakutaka kupokea ila moyo ulikuwa unamuuma sana na kuamua kupokea ile simu,
“Naomba unisamehe mpenzi wangu Vaileth, najua ni jinsi gani umeumia na ni jinsi gani nimekukera”
“Kwakweli Junior naomba tuachane tu, yani kila mtu apite na mambo yake, kwakweli siwezi kuendelea na wewe”
“Kwa kosa gani nililolifanya? Yule mama simtaki kabisa ila huwa anatumia mabavu muda wote, tatizo mamdogo nae hana nguvu hivi kweli anamuacha mwanamke baunsa vile anitoe tu jamani! Yule mama ndio ule ujumbe uliousoma usiku uliopita akilalamika kuwa sipokei simu zake, na alichonifanya aliponichukua ni Mungu tu anajua, sitakwambia kwasasa ila ipo siku nitakwambia. Kuna yule mama huwa tunamchukia sana hapo nyumbani ila ndiye aliyenisaidia, kwakweli yule mama ana mbinu za ajabu sana hata nilishangaa kama nitaweza kupona kwenye mikono ya yule mama maana usiku wa leo sijui ningekuwaje mimi Junior. Sirudii tena upuuzi wa namna hii, naomba unisamehe Vaileth”
“Nimekusamehe ila sikutaki tena Junior”
“Nimeambiwa nisirudi hovyo hapo nyumbani ila kwaajili yako nitarudi tu, siwezi kuishi bila wewe Vaileth. Nisamehe tafadhari”
Mara mlango wa Vaileth uligongwa, alishtuka sana na kuweka simu mbali, na kwenda kufungua tena mgongaji alikuwa ni mama Angel,
“Kheee usiku huu unaongea na simu Vai, ndio umeanza kudanganywa tena na wanaume eeeh! Kuwa makini sana siku hizi magonjwa mengi na unaweza kudhani unapata wa maana kumbe unaangukia kwenye mikono ya wazee”
Vaileth aliangalia chini tu kwa aibu, kisha mama Angel akamwambia,
“Kesho itabidi uamke asubuhi sana sababu kuna mahali nataka kwenda kwahiyo nitaenda mapema ili niwahi kurudi maana kule ni mbali sana, kwahiyo utaamka asubuhi kwaajili ya kukaa vizuri na mtoto”
“Sawa mama”
Kisha mama Angel aliondoka na kurudi kulala.
Ila ni tofauti na jinsi ambavyo walipanga kwani kesho yake mama Angel alijikuta akiamka saa mbili asubuhi na sio kama alivyopanga, basi aliamka na uchovu kiasi na kwenda moja kwa moja jikoni kumfokea Vaileth,
“Jamani, wewe hata kuniamsha?”
“Niesamehe mama, hata mimi nilipitiliza yani nimeamka wakati wakina Erick wanaondoka”
“Khaaa huu usingizi gani jamani loh! Sasa nitafanyeje? Itabidi niende kesho halafu nitamwambia Erick ndio aniamshe”
Basi wakakubaliana pale kuwa aende kesho yake.
 
SEHEMU YA 321

Leo Erick alipomaliza masomo yake kama kawadia alienda kushtuliwa na madam Oliva ili waende kiwandani yani madam Oliva nae ilionyesha kuwa maeneo ya kule kiwandani ameyapenda maana kila siku alikuwa akitaka kumsindikiza Erick.
Basi alienda hadi kiwandani na moja kwa moja Erick alivyoingia kiwandani pale nje alibaki madam Oliva huku akiangaza angaza mazingira ya pale, alishikwa bega na kushtuka kiasi, alipogeuka alikuta ni baba wa siku ile yule Rahim, basi alianza kuongea nae,
“Oooh madam, ulishangaa sijakupigia simu eeeh!”
“Ndio, hujanitafuta”
“Aaaah yani sijui vipi, nilikuwa natamani sana kukutafutaila nikajua utakuwa upo na jamaa yako na hawezi kufurahi akisikia kuna mwanaume mwingine amekupigia simu”
Madam Oliva alitabasamu tu, kisha Rahim aliendelea kuongea,
“Una mtoto madam?”
“Ndio ninaye mmoja”
“Wa kike au wa kiume”
“Ni wa kiume”
“Hupendi kuwa na mtoto wa kike?”
“Napenda ila naona kama umri umepita”
“Aaaah umri umepita wapi, mbona wewe bado kijana mdogo yani bado unadai wewe. Sikia sasa, una mpango gani na huyo jamaa yako?”
“Tuna mpango wa kuoana”
“Oooh vizuri sana, nafurahi kusikia hivyo. Sikia madam, nahitaji ukiwa na muda wako wa ziada nitafute mimi kuna mambo ya muhimu sana nataka kuongea na wewe”
Kisha Rahim akatoa pesa na kadi yake ya mawasiliano na kumkabidhi madam Oliva huku akitabasamu, basi madam Oliva alipokea na kuagana na Rahim, baada ya kuondoka alijisemea,
“Jamani wanaume wa namna hii walikuwa wapi kipindi cha ubinti wangu? Mwanaume hata hufahamiani nae vizuri anakuhonga kweli! Mwanaume mzuri, shombeshombe, mrefu, ana mwili mzuri halafu hakufahamu vizuri lakini ana kuhonga mweeeh walikuwa wapi enzi zangu hawa! Hivi akinitongoza kama huyu namkataaje kwa mfano? Yani hapo mambo ya Steve mbona yatasahaulika kabisa, kwanza hana kazi yule namlea na kumlisha mwenyewe. Nilitongozwa na huyu ajue namuacha kwenye mataa na ujinga wake”
Madam Oliva alikuwa akijisemea huku akitabasamu, yani alionekana kuwa na furaha sana.
Erick alipotoka aliondoka nae mpaka kwao na kumuacha karibia na njia ya kwao halafu yeye akaenda nyumbani kwake.
Kisha Erick moja kwa moja akaenda kwao ila akakutana getini na Sia, kwakweli Erick hakumpenda kabisa huyu mama, basi Sia alipomuona Erick alitabasamu na kufurahi sana kisha akamsogelea ili amkumbatie ila Erick alimsukuma hadi chini, yani Sia alianguka ila alisonya na kusema,
“Liangalie vile, toto lina roho mbaya kama mkaanga sumu”
Ila Erick hakumjali wala nini zaidi zaidi aliingia ndani kwao, basi Sia aliinuka huku akijikung’uta na kulalamika sana halafu akaondoka zake.

Usiku wa leo, mama Angel alimuomba Erick amuamshe asubuhi ili aweze kuondoka kwani alijua akipanga yeye mwenyewe tena itakuwa mambo kama ya jana yake.
Basi wakakubaliana muda ambao atamuamsha na kweli palivyokucha tu Erick alienda kumuamsha mama yake ambapo aliamka na kuanza kujiandaa halafu alienda kumuamsha Vaileth ili aweze kubaki vizuri na mtoto.
Alipomaliza kujiandaa, alimuaga Vaielth na kuondoka zake, kwakweli ilikuwa ni safari ndefu kiasi maana alitumia kama masaa sita hivi kufika kwenye kaburi la mzee Jimmy, alisogea pale kwenye kaburi, ni kweli palikuwa pamesafishwa vizuri na palikuwa pamewekwa maua na mishumaa hata yeye mwenyewe akasema,
“Lazima kuna wa ziada wanaofanya haya licha la yule mlinzi”
Mara akashikwa bega, na kusikia sauti ikimuita,
“Erica”
Alishtuka sana kwani hakutegemea kwa muda huo kumpata mtu aliyemfahamu yeye kwa jina lake la Erica.

Alipomaliza kujiandaa, alimuaga Vaielth na kuondoka zake, kwakweli ilikuwa ni safari ndefu kiasi maana alitumia kama masaa sita hivi kufika kwenye kaburi la mzee Jimmy, alisogea pale kwenye kaburi, ni kweli palikuwa pamesafishwa vizuri na palikuwa pamewekwa maua na mishumaa hata yeye mwenyewe akasema,
“Lazima kuna wa ziada wanaofanya haya licha la yule mlinzi”
Mara akashikwa bega, na kusikia sauti ikimuita,
“Erica”
Alishtuka sana kwani hakutegemea kwa muda huo kumpata mtu aliyemfahamu yeye kwa jina lake la Erica.
Basi mama Angel aligeuka na kukutana na bi.Aisha, ni mwanamke ambaye alionana nae kwa kipindi kirefu sana ila alimfahamu kutokana na maneno yake ya busara, alimsalimia kisha bi.Aisha akamuuliza,
“Unanikumbuka lakini?”
“Nakukumbuka ndio, wewe ni bi.Aisha”
“Wow, vizuri sana, nilijua utakuwa umesnisahau maana mimi na wewe mara ya kwanza kufahamiana ilikuwa ni siku ya harusi yako, na baada ya hapo tukawa karibu kiasi hadi kipindi nilipoondoka kwa mzee Jimmy ndio ikawa mwisho kuonana”
“Nakumbuka ndio”
“Umekuja huku Erica, kuangalia kaburi la mkwe wako!! Kwakweli Hongera sana maana una moyo wa kipekee mno”
“Asante, lakini hakuna sababu ya mimi kushindwa kuja kutembelea kaburi la baba mkwe, ni kwamba hatukupanga tu kufanya hivi ndiomana”
“Pole sana, kwa ujinga wote aliokufanyia mzee Jimmy, ila bado umepata nguvu ya kusema hakuna chochote”
“Ujinga gani?”
“Inamaana hujui alichokifanya kwako? Ndio sababu hata mimi ya kutokuendelea tena kuishi naye, sitaki kusema mengi ila utayajua yote”
“Ujinga gani, tafadhali mama niambie ni kitu gani”
“Sijui kama ni hivi ambavyo nilimsikia akiongea na yule daktari, kwanza watoto wako wanaendeleaje? Nauliza kwa wale mapacha?”
“Wanendelea vizuri tu, kwani ni kitu gani?”
Hapo mama Angel alishgtuka zaidi na kutamani kujua kuwa ni kitu gani,
“Sijui nikwambie nini Erica, ila kuna siku nilikuwa nyumbani kwa mzee Jimmy, alikuwa na rafiki yake mmoja ambaye alikuwa ni daktari, alikuwa akiongea nae kuwa ukiaribia kujifungua basi ampe kazi Erick yani aondoke kabisa ili swala zima la kujifungua alisimamie yeye, halafu kuna sindano sijui za aina gani aliongea na yule daktari kuwa awachome hao mapacha wako pindi watakapozaliwa tu, halafu nilisikia kuwa hizo sindano zitawasumbua sana watoto wako kiasi kwamba utahitaji msaada wake, na nia yake ni kukukomesha wewe. Kwakweli nilisogea pale na kumzaba mzee Jimmy kibao kwani kila nikikumbuka jinsi mtu unavyobeba mimba kwa shida, na kuzaa kwa shida halafu mtu ana mpango wa kuchoma sindano zisizofaa watoto wako ili tu kukutesa, sikupenda kabisa nilijikuta nikilia kwa uchungu na kumuuliza kwanini anataka kukufanyia roho mbaya kiasi kile, ila hakunijibu kitu halafu ulipokaribia kujifungua ni kweli alimuondoa Erick, nilipatwa na wazo baya sana na pale nilipoamua kuondoka kwa mzee Jimmy maana sikutaka kuendelea kushuhudia mambo kama yake. Huwa mara nyingi nakuja huku kaburini yani nawaza kuwa naweza kufa na siri hii bila ya wewe kujua ukweli. Ila kweli watoto wako wanaendelea vizuri”
Mama Angel akapumua kidogo na kujibu,
“Wanaendelea vizuri ndio”
“Umewachunguza? Labda dawa aliyowapa inafanya kazi taratibu, naogopa sana mimi, naogopa kwakweli.”
“Ila siwaoni kama wana tatizo lolote, sababu nawaona ni kawaida kabisa”
“Pole sana Erica, hivi unakumbuka ajali uliyoipata pindi ukiwa unakaribia kujifungua na ndipo ukawaishwa hospitali?”
Mama Angel akakumbuka kidogo, ni kweli ilikuwa ni ajali mbaya sana kwake yani ilibakia kidogo tu angeweza kupoteza hata maisha, akajibu,
“Nakumbuka ndio, huwa siwezi kusahau lile tukio maana dereva wangu alikufa”
“Basi ile ajali ilipangwa na mzee Jimmy”
“Jamani kwanini lakini aliamua kunifanyia hivi!! Kwani kosa langu ni nini, hakujua kama akiniumiza mimi basi anamuumiza mtoto wake?”
“Hilo mzee Jimmy hakujali, huyu mzee kafa na laana nyingi sana, nikikueleza mambo mengi aliyoyafanya juu yako unaweza ukahisi moyo wako kuvuja damu hata ukatamani kufukua kaburi lake upigepige mifupa yake, Mzee Jimmy hakuwa mtu mzuri kwako kabisa, alisimamia harusi yenu ila alikuwa na mambo yako, nikikwambia kitu alichokipanga hata unaweza kulia hapa”
“Unajua mama unanitisha sana, kuna mwanamke mmoja alikuwa na mahusiano na Erick, yule mwanamke kaibuka kipindi hiki na kudai kuwa pacha mmoja sio mtoto wangu, kuwa ni mtoto wake, yani hadi alimwambia hivyo mwanangu na alimchanganya sana, mpaka mwanangu anakuwa na mawazo mno”
“Hebu tulia, tuliza akili, kama unalea watoto wako na hakuna tatizo lolote uliloliona huenda mambo ya mzee Jimmy hayakufanikiwa. Ila huyo asikufanye ukose raha ya maisha inawezekana yupo kwenye kiapo cha kukutesa na mzee Jimmy, yani hiyo inawezekana kabisa ni mambo ya kukutesa kisaikolojia wewe na familia yako. Kama watoto wako ni wazima wa afya basi achana na dhana yake kuwa mtoto sio wako, sasa mtoto sio wako kivipi wakati ulijifungua mapacha?”
“Ndio hapo huwa nashangaa sana mama”
Bi.Aisha alijaribu kumwambia mama Angel maneno ya busara ili aweze kufanya vizuri, alimshauri pia,
“Nakuomba huku kuja kutembelea kaburi la mzee Jimmy uwe unakuja na Erick au Tumaini, usije mwenyewe maana huyu mzee haaminiki hata kidogo, ni kweli amekufa ila kaacha watu gani nyuma yake? Kumbuka mwanadamu anaweza kukuangamiza sababu ya pesa, je kawaachia pesa ngapi ya kufanya ujinga? Ni kweli amekufa ila ahadi walizoahidiana bado zinaishi. Kwa muda huu nakuomba tu ugeuze na uondoke maana hata mimi binafsi siwezi kuridhika kukuacha wewe huku kwenye kaburi la mzee Jimmy”
Mama Angel alisikia mausia ya huyu mama, hivyobasi aliamua kuagana nae na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 322

Vaileth akiwa nyumbani na mtoto, alishangaa tu kuona Junior amefika mahali pale,
“Kheee Junior si untakiwa kuwa shule wewe!!”
“Ni kweli natakiwa kuwa shule ila sijihisi kabisa kukaa shuleni ilihali hujanisamehe Vaileth”
“Hapana, mimi siwezi tena kuwa na wewe Junior”
Basi Vaileth aliinuka na kwenda kumlaza mtoto kwenye kitanda chake pale sebleni maana alikuwa amelala, kwahiyo alimlaza pale ili iwe rahisi kwake kumsikia pindi atakapoamka.
Alipomlaza tu, nyuma yake alienda Junior na kuanza kumpapasa huku akijaribu kumpa maneno matamu, yani Vaileth alishindwa hata kusema chochote kile na kujikuta na yeye akimpa sapoti Junior na moja kwa moja walienda chumbani na kulala huko.
Hapa sebleni alifika mama Junior kwa muda huo, alishangaa kumkuta mtoto kalazwa pale, basi alijaribu kuita ila hakuitikiwa,
“Wenyewe! Mama Angel, Vaileth. Kheee humu ndani leo hakuna mtu zaidi ya huyu mtoto mdogo Ester jamani eeeh!!”
Basi mtoto nae alianza kulia, ikabidi amchukue na kuanza kumbembeleza, akataka kwa muda huo ampigie simu mama Angel ili kumpa hiyo taarifa, ila kabla hajapiga ndipo Vaileth alitoka ndani na kwenda pale sebleni,
“Kheee wewe Vaileth nakuita muda wote huitiki ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa naoga mama, nisamehe”
“Mjinga wewe, halafu umemlaza mtoto hapa sebleni akiibiwa je?”
“Nilijua haiwezi kuwa hivyo sababu kuna mlinzi getini”
“Mjinga sana wewe, usirudie hiki kitu tena, yuko wapi mama Angel?”
“Kuna mahali kaenda asubuhi sana ila kasema ni mbali na atachelewa kurudi”
“Jamani aaargh. Ngoja niende chooni kwanza”
Basi mama Junior akainuka na kwenda chooni, muda huo Junior nae alitoka taratibu na kumbusu Vaileth halafu akaondoka ili mama yake asimuone na asitambue kuwa alifika mahali hapo.
Junior alivyofika getini alimshukuru sana yule mlinzi,
“Asante sana kwa ujumbe ulionipa leo kuwa mamdogo hayupo, nashukuru sana wewe ni rafiki wa kweli. Naomba wote wakina Erick wasijue kama leo nilirudi hapa”
Kisha akampa mlinzi elfu kumi halafu akamuaga na kuondoka zake akielekea shuleni.
Njiani alikutana na Sarah pamoja na mama yake, basi Sarah akambulisha Junior kwa mama yake ila mama yake akasema,
“Namfahamu huyu mbona”
Junior aliona aibu tu na kuangalia chini, kisha mama Sarah akamwambia Junior,
“Wewe bado ni kijana mdogo sana, zingatia masomo yako achana na watu wazima utalia. Nimepata habari zako achana na watu wazima nakwambia. Yule ni dada yangu namjua vizuri, wewe ni mtoto mdogo sana Junior”
Basi Junior akawaaga pale na kuondoka zake maana aliona huyu mama atazungumza mengi kwani alishawahi kumuona mara kadhaa akiwa na Linah.

Njiani mama Angel alijiuliza sana, kuwa alienda kwenye kaburi la mzee Jimmy kufanya nini sasa ikiwa hakufanya chochote zaidi ya kukutana na bi.Aisha tu!! Pia alijiuliza kuhusu swala la watoto wake kuchomwa sindano, alijiuliza sana ni sindano ya nini na je alikuwa na lengo gani kufanya hivyo? Ila kilichompa tumaini ni kuona kuwa watoto wake hawana tatizo lolote lile maana aliona wapo kawaida na wanaishi kawaida kabisa, basi alikuwa akiendesha gari huku akiwaza mambo mengi sana.
Alipokuwa anakaribia nyumbani kwake, ilikuwa ni jioni kabisa, hata giza kwa mbali lilianza kuonekana, ila alimuona Sia na kusimamisha gari lake kisha akashuka na kumuita,
“Sia”
Sia alisogea karibu na kumsikiliza, kisha akamsalimia na kumuuliza,
“Umetoka wapi muda huu Erica? Mumeo hayupo na bado unanyonyesha, au Junior kakorofisha tena?”
“Hapana, ila nilienda kwenye kaburi la mzee Jimmy”
Sia akashtuka kidogo na kumuuliza,
“Umepata nini huko?”
“Nimegundua vitu vingi sana, hivi Sia mzee Jimmy alikulipa kiasi gani cha kuisumbua akili yangu?”
“Mmmh jamani, sijalipwa na mzee Jimmy mimi”
“Haya ni kipi kinakufanya uwe unasema Erick ni mtoto wako?”
“Kheee muda gani nimesema hivyo kuhusu Erick jamani!! Ni mtoto wangu tokea lini?”
“Khaaa kumbe wewe ni mwezi mchanga, kwaheri”
Mama Angel alirudi kwenye gari yake na kuondoka zake, yani alikuwa akishangaa gafla jinsi Sia alivyobadilisha maana ya kitu ambacho kila siku anakiongelea, kuwa Erick ni mwanae halafu siku hii kakataa kabisa, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kusikitika.
Kwanza alijiuliza sana, maana angekuwa na mtu angesema Sia anakataa sababu ya yule mtu ila alikuwa mwenyewe na Sia amekataa katakata kwamba hajwahi kusema hivyo, yani aliondoa gari huku akisikitika sana.

Mama Angel aliingia nyumbani kwake kwenye mida ya saa moja maana ilikuwa ni safari ndefu na alichoka sana, basi moja kwa moja alienda kuoga tu na kurudi kula, kisha Vaileth alimweleza kuhusu ujio wa mama Junior,
“Alikuja hapa mama Junior, ila amekaa sana alipoona hurudi akaamua kuondoka”
“Jamani dada yangu masikini, kanikuta na mambo mengi leo hatari, nitawasiliana nae hakuna tatizo. Ila umeshinda salama na mtoto!! Naona kalala muda huu”
“Ndio, nimeshinda nae salama, na alivyorudi Erica basi imekuwa rahisi zaidi maana Erica anajua sana kubembeleza mtoto yani kama amewahi kuwa na mtoto vile”
“Mwanamke yule, mwanangu ni mwanamke kamili maana naona vitu vyote vifanywavyo na mwanamke basi Erica anavimudu”
Basi mama Angel alipomaliza kula, aliinuka na kupitia chumbani kwa Erick ili kumuangalia kama yupo macho basi azungumze nae kidogo kuhusu kiwandani, ila alipoingia chumbani kwake alimkuta yupo hoi kabisa huku akiwa na makaratasi ya mahesabu pembeni yake, mama Angel alisikitika kiasi,
“Masikini mwanangu jamani, tunampa mzigo mkubwa sana kushinda umri wake hebu ona alivyochoka hapo!”
Na kweli Erick hakuwa hata na habari, basi akamuacha kwanza na kusema kuwa kesho atawahi kuamka ili aongee nae kwanza kwani alipanga kumwambia kuwa awe anapumzika siku zingine yani sio kila siku awe anaenda kiwandani.
Kisha mama Angel alienda zake kulala tu kwa muda huo, ila kabla usingizi haujampitia vizuri simu yake iliita alipoiangalia aliona ni mumewe anapiga, basi akaipokea simu ile,
“Erica, nasikia leo ulienda kwenye kaburi la marehemu baba, kwanini umeenda bila ya kuniambia?”
“Samahani mume wangu, ila kuna kitu nilitaka kugundua ukweli, nilitaka kujua kama kweli Sarah na mama yake wanaenda kule kaburini mara kwa mara”
“Na ukweli huo ungeupata wapi?”
“Kwa wale walinzi”
“Haya, wamekwambia chochote?”
“Sijaongea nao sababu nilikutana na bi.Aisha yule mmama aliyeamua kuishi na baba yako kipindi kile ambacho baba yako alilalamika kuwa ni mpweke”
“Na mkazungumza vitu gani?”
“Vitu vingi sana ila kikubwa kaniambia kuwa nisiwe naenda kule mwenyewe, kasema niende na wewe au na Tumaini, sijui ni kwanini ila kasema hivyo tena akanitaka niondoke muda huo huo kwahiyo hata kaburini sikusogea zaidi ya kuondoka tu. Nisamehe sana mume wangu”
“Haya, nimekusamehe. Ila kuna jambo mke wangu nataka unisaidie sijui utaweza”
“Jambo gani?”
“Nataka kesho uende ofisini kwangu, kuna faili nitakuelekeza uniangalizie, nataka uniangalizie wewe. Sijui utaweza?”
“Nitaweza ndio, hakuna tatizo”
Basi alikubaliana na mume wake na moja kwa moja kuamua kulala tu kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 323

Siku hii Erick alienda shuleni kama kawaida ila Sarah nae alifika siku ya leo maana alisema kuwa anaendelea vizuri, basi muda wa mapumziko moja kwa moja Sarah alimfata Erick na kuanza kuongea nae,
“Ila Erick tabia mbaya, kweli kabisa nimekuja kuishi kwenu hata kupata moyo tu wakuja kuniona!!”
“Nilikuwa na mambo mengi sana”
“Nikwambie kitu ninachotamani kwasasa?”
“Kitu gani?”
“Natamani kubeba mimba yako”
Erick alishtuka sana, na kusema,
“Hivi Sarah una wazimu au ni kitu gani? Ni malezi gani wewe uliyolelewa”
“Kwanini?”
“Huoni kama haupo sawa na mtoto wa kiafrika, hivi utasema unatamani kubeba mimba yangu kwa umri huo!! Na bado unasoma, hivi unafikiria maisha yako ya baadae?”
“Unajua niliwahi kuongea na mama yangu, aliniambia kuwa kuna mambo ukifikiria maisha yako ya badae basi huwezi kuyafanya ila mambo hayo yanafanya maisha yako ya badae kuwa bora na imara zaidi”
“Kama mambo gani?”
“Mama, huwa ananiambia kuwa hakuwa na mpango wa kunizaa mimi kabisa. Ukizingatia alikuwa bado hajaolewa na hakujua ni kipindi gani angeolewa, na aliniambia fika kuwa alijua wazi baba yangu asingeweza kumuoa yeye, nilimuuliza kwanini akasema kuwa ataniambia tu. Ila kuna mtu alimshawishi kuzaa na baba, na baada ya kubeba mimba yangu basi maisha yake yalibadilika moja kwa moja, akaanzishiwa biashara, akafunguliwa miradi mbalimbali na ile nyumba tunayoishi ya kisasa ni matokeo ya kunizaa mimi, kwahiyo maisha ya mama yangu yamebadilika baada ya kupata ushawishi wa kunizaa mimi”
“Sikuelewi, ngoja nikwambie kitu Sarah. Kwasasa zingatia masomo, kama mapenzi yapo tu. Yalikuwepo na yataendelea kuwepo”
“Yani furaha yangu itatimia pindi nikibeba ujauzito wako”
Yani Erick alimuangalia bila kummaliza, kwa bahati nzuri kengele ya darasani ililia basi ikabidi wote waingie tu darasani.

Mama Angel alienda ofisini kwa mume wake na kufanya yote ambayo mume wake alimuelekeza, na alipomaliza aliweka vizuri na kuondoka kwani alikuwa ameacha mtoto wake nyumbani.
Ila wakati anatoka tu kwa muda huo, akakutana na mtu nje ya ofisi ila ni mtu ambaye anafahamiana nae, basi alisimama na kusalimiana nae,
“Oooh leo nimefurahi sana kukuona Erica”
“Haya, vizuri ila mimi nataka kuwahi”
“Subiri kwanza nikwambie kitu, mwanangu anaumwa”
“Pole sana”
“Mbona huniulizi anaumwa nini?”
“Eeeeh anaumwa nini?”
“Ngoja nikwambie, unajua sijui ni kitu gani kipindi kile mimi na wewe tulipandikiza kati yetu, nakumbuka nilikupenda sana kiasi cha kuanza hata kupagawa sababu ya kukupenda wewe. Sasa nina mwanangu ambaye kachukua jina langu, anaitwa Bahati na yeye, sijui alionana wapi na mtoto wako Erica, basi mwanangu anaugua sana moyo wake maana anampenda sana mwanao Erica, halafu hata mwanao anaonekana kumuelewa mwanangu”
“Bahati, hebu acha ujinga wako, usitake kuharibu watoto. Hivi watu wengine mnaleaje watoto wenu lakini? Mimi watoto wangu kwa umri ule huwezi kusikia akikwambia natamani mtu, sijui nataka kuwa na mpenzi sijui nini na nini, hivi wenzangu ujasiri huo wa kufundisha watoto wenu ujinga mmeutoa wapi? Nina uhakika hao watoto wako watakuwa wamefundishwa huo ujinga kwa mama zao maana Fetty hawezi kubaliana na hayo mambo. Mkanye mwanao, tena akimuona mahali mwanangu basi iwe kama muhalifu kaona kituo cha polisi, kwaheri”
Mama Angel aliingia kwenye gari na kuondoka zake.
Basi alivyofika tu nyumbani kwake, akapigiwa simu na rafiki yake Fetty,
“Ndugu yangu yani huwezi amini yaliyonipata leo”
“yapi tena hayo?”
“Jamani si nimekutana na Derrick, basi nikafurahi mwenyewe sababu hatujaonana siku nyingi, basi nikakumbatiana nae pale, jamani kuja kuangalia pochi yangu kulikuwa na elfu sitini yote haipo basi hata sielewi kama nimeibiwa na Derrick au kitu gani”
“Duh pole sana ndugu yangu, ngoja nitafatilia ili nijue kama ni Derrick”
Alishindwa kumtaja moja kwa moja ingawa tabia ya Derrick ilianza kumkera sasa maana alitapeli hadi watu wa karibu, basi akajisemea,
“Yani huyu Derrick kawa mbaya jamani, anatapeli kila mtu”
Vaileth akasogea na kumwambia,
“Kuwa makini mama ili asije akakutapeli hata wewe”
“Weee amtapeli nani? Hawezi kunitapeli mimi maana nina akili zangu timamu”
“Hata hao anaowatapeli mama wanaakili zao timamu, yani yeye akija anajua mtu kama wewe akutapeli vipi ni kuwa nae makini tu”
Basi mama Angel aliachana na Vaileth pale na kwenda chumbani kwake tu kupumzika muda huo.
Ila baada ya muda aliwaza kuwa bora siku hiyo hiyo angemaliza na swala la yeye kuchukua hela kwenye akaunti ya mume wake kwaajili ya kulipa ile ambayo ilitapeliwa na Derrick, kwahiyo akaona ni vyema aondoke muda huo kuichukua ili Erick akirudi amkabidhi hela hiyo.
Basi alimpigia simu mume wake kumpa hiyo taarifa,
“Ndio, nataka kwenda leo kuchukua ile hela mume wangu”
“Ila si nilishakurubhusu jamani mke wangu, hata usijali”
Basi wakati anaongea na mumewe kwenye simu alisikia sauti ya pili kama ikimuuta mumewe,
“Erick, njoo tujadiliane kuhusu hiyo simu”
Basi mama Angel akaguna na kusema,
“Mbona hiyo sauti ya kike?”
“Mke wangu jamani, tusiishi hivyo kwakutokuaminiana jamani, hapa huwa wananitania tu kuwa mke wangu ananichunga sana, ndiomana umemsikia huyo mama akisema hivyo”
Basi mama Angel aliridhika na kuagana na mumewe.
Baada ya hapo alijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye ATM kutoa hiyo pesa ili amkabidhi Erick.

Kama kawaida Erick alienda kiwandani akiwa na madam Oliva, basi moja kwa moja alienda kiwandani huku madam Oliva akiwa nje ya kiwanda kama kawaida, basi Erick alishughulika mule kiwandani basi kama kawaida pale nje alipokuwa madam Oliva, alipita Rahim na kuanza kuongea nae,
“Mbona hata kunipigia simu hakuna ile usiku?”
“Aaaah niliona nikupigie muda wa mchana”
“Una wasiwasi gani kwani tunaongea kuhusu nini? Kuwa huru nipigie muda wowote ule. Halafu nikuombe tu jambo huna muda tuweze kuonana na kuongea vizuri mwisho wa wiki hii?”
“Muda ninao”
Ila leo Erick aliwahi kutoka kiwandani na kumkuta madam Oliva amesimama na Rahim, basi Erick alijikuta akichukia tu maana toka siku ambayo alipewa maelezo kuwa yule alimpa hela Erica basi alijikuta akiwa na hasira nae sana, kiasi alisogea pale bila ya kumsalimia, madam Oliva alimfokea,
“Erick, tabia ya wapi hiyo ya kutokusalimia?”Rahim akauliza,
“Na huyu anaitwa Erick?”
“Ndio, anaitwa Erica”
“Ni mtoto wa Erick na Erica?”
“Ndio, unawafahamu kumbe?”
“Ila jamani kuna watu wanapenda kugelezea sana, yani yule Erick kaona kuna mtoto kapewa jina kama langu basi na yeye akaamua kumpa mwanae jina lake, wanachekesha sana hawa watu. Haya wewe kijana mbona unaonekana una kiburi sana?”
Erick alikaa kimya tu bila ya kusema chochote kile,
“Mmmh sijawahi kuona mtoto mwenye kiburi hivi jamani ila nikiamua nitakunyoosha mjinga wewe”
Erick alimwambia madam Oliva,
“Madam naomba twende nyumbani”
“Erick mbona hivyo? Mbona unaonekana kuwa na hasira sana?”
Erick hakumjibu hata mwalimu wake, ila cha kushangaza, Erick aliondoka pale na moja kwa moja kuchukua pikipiki na kwenda nayo nyumbani kwao yani hata hakufatilia chochote kile, yani madam Oliva na Rahim walibaki kumshangaa tu, ila madam Oliva akamwambia Rahim,
“Ila usijali kuhusu huyu mtoto, mimi ni mwalimu wake wa nidhamu na nitamnyoosha, siku zote huwa namuona ni mtoto mwenye heshima sana ila sijawahi kufikiria kama ana kiburi kiasi hiki!!”
Kisha madam Oliva aliagana pia na Rahim kwani hakuipenda kabisa tabia ambayo imeonyeshwa na Erick.
 
SEHEMU YA 324

Mama Angel alikuwa muda huo ndio amerudi nyumbani baada ya kutoka Atm kuchukua hiyo pesa, basi alivyokuwa anataka tu kuingia getini kwake akashtuliwa na Derrick maana muda huo hakutembea na gari sababu aliona achukue tu usafiri wa haraka kwenda na kurudi, basi alisimamishwa na Derrick na kusimama na kuanza kuongea nae,
“Muda huu kweli nyumbani kwangu jamani!!”
“Halafu nilikuwa napita tu, sema nikakuona nikasema sio vizuri nisije kukusalimia”
Mara simu ya Derrick iliita kidogo na kukata, kisha akaitoa mfukoni na kutoa karatasi la vocha basi akasema,
“Oooh dada, samahani naomba nisaidie shilingi mia hapo nikwangulie hii vocha, yani huyu mtu ananisaka sana, halafu simu yangu imeisha hela, nilinunua hii vocha na kuiweka maana sikuwa na cha kukwangulia”
Mama Angel hakuona tatizo la kumpa Derrick shilingi mia akwangulie vocha, basi alimpa na muda ule ule Derrick alimuaga ila mama Angel alimuuliza,
“Kheee wewe kama ulikuwa na lengo kweli la kunisalimia mbona hutaki kwenda kusalimia watoto wangu? Au unaogopa utapeli wako ulioufanya kwao?”
Ila Derrick hakusema neno na alianza kuondoka, mama Angel alishtuka pia na kujiuliza,
“Hivi hajanitapeli na mimi kweli!!”
Akaangalia kule alipomtolea mia na kukuta hana hela yoyote ile.


Ila Derrick hakusema neno na alianza kuondoka, mama Angel alishtuka pia na kujiuliza,
“Hivi hajanitapeli na mimi kweli!!”
Akaangalia kule alipomtolea mia na kukuta hana hela yoyote ile, kwakweli alishangaa sana basi alianza kumuita Derrick ila Derrick hakuitika wala nini, ndipo alipoamua kumkimbilia ila mbele kidogo Derrick alipanda pikipiki na kuondoka zake, kwakweli mama Angel alichoka kabisa, hakuwa na namna zaidi ya kuingia tu getini, alifika ebleni na kupumua kwa nguvu sana hata Vaileth alifika na kumuuliza,
“Vipi mama? Ni salama?”
“Yani leo ndio nimeamini ule msemo usemao lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja, yani huwezi amini, leo leo nimekutana na Derrick hapo nje ya geti na amenitapeli jamani!! Huyu Derrick ni mzima kweli dah!”
“Pole mama, amekutapeli vipi?”
“Sikia nikwambie, ndio kwanza nimerudi kutoka ATM nikakutana na Derrick hapo getini akidai alikuwa anapita ila kaona vyema asogee kunisalimia, mara simu yake ikaita mara moja na kukatika yani kama mpigaji alikuwa akimbeep vile, mara akatoa vocha na kuniomba mia haraka haraka akwangulie vocha, yani sikuwa na wazo kwamba anaweza kunitapeli kwa kutumia ile mia jamani, nikaitoa na kumpa, kakwangulia pale na kuanza kuondoka, nikamuuliza mbona anaondoka bila kuingia ndani kusalimia wanangu? Nikamuuliza au unaona aibu sababu umewatapeli, ila hakunijibu kitu nikashtuka na kuangalia kwenye mkoba, kwakweli hela zote hazipo yani Derrick kanilamba pesa yote hivi hivi yani. Sielewi ni kitu gani hiki jamani!”
“Mama, huyo sio tapeli pekee bali anatumia pia chumaulete”
“Kheee chumaulete tena!! Ndio inakuwaje hiyo naisikiaga tu”
“Yani mtu anakuja kukuomba hata hamsini na ukimpa tu basi hela zako zote anavuta, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nauza duka la mjomba, sasa mambo ya chumaulete yakakazana hatari, yani mtu unauza, anatokea mteja huyo anataka kitu halafu hela yake unatakiwa kumpa chenji basi ukimpa tu utakuta kakomba hela zote”
“Kheee sasa si hasara hiyo? Sasa mlifanyaje?”
“Ni kweli ni hasara tena hasara kubwa sana, ila pale kijijini tuligundua kitu. Yani tuligundua nguvu ya mkaa kwa chumaulete, yani ikawa kila mtu anaweka kipande cha mkaa kwenye droo ya pesa au kwenye pochi ya kuhifadhia pesa, basi chumaulete akija hawezi kuvuta zile hela sababu ya nguvu ya mkaa”
“Mmmmh yani mkaa tu!! Sasa mkaa ndio una nguvu gani?”
“Sijui, ila ni mambo ya imani haya mama. Ila huwezi amini ni kweli ukiweka mkaa kwenye hela zako basi huyo chumaulete hawezi kuvuta pesa zako, yani walizidi ilifikia kipindi mtu unatembea na kipande cha mkaa hata kwenye mfuko wa sketi yako au suruali yako maana chumaulete unaweza kukutana nae popote pale, na mara nyingine ukamsaidia kwani unaweza kujua kuwa ana tatizo kweli kumbe mwenzio yupo kazini, basi mkaa ndio ilikuwa komesha yao”
“Kwakweli tabia ya Derrick imeniogopesha, nitaanza na mimi kutembea na mkaa jamani!! Ila huyu Derrick dawa yake inachemka jamani, haiwezekani asumbue kiasi hiki”
Basi mama Angel aliinuka zake na kwenda chumbani ila hilo swala la yeye kutambeliwa na Derrick aliona akimwambia mumewe atamcheka kwahiyo aliona vyema kukaa nalo kimya bila kusema lolote lile kwa mumewe.

Leo usiku, Erick alikuwa amechoka kiasi kwahiyo baada ya kula tu alienda kulala. Muda huu Erica nae alitoka chumbani kwake na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erick sababu kuna jambo alitaka kumueleza, ila alipofika alimuona Erick akiota huku akiweweseka na kutaja jina la Erica,
“Jamani Erica, aaaah Erica”
Erica akamshtua pale kaka yake,
“Kheee wewe unalala hadi unaota na kuongea, haya ni kitu gani hiko hadi unitaje ndotoni?”
Erick alikaa huku akiwa kimya kwa muda maana alikuwa akitafakari ndoto yake, basi Erica alimshtua tena na kumuuliza,
“Ulikuwa unaota kuhusu nini?”
“Mmmh acha tu Erica ni ndoto tu hata sijui ni kuhusu nini!”
“Unajua sijawahi kuona ukiota ndoto hadi unaongea namna hiyo, ila nitakachokwambia si ndio uataota unaongea hadi asubuhi”
“Kitu gani hiko Erica, niambie tafadhari”
“Hata sikwambii”
Kisha Erica akainuka na moja kwa moja kutoka kwenye kile chumba cha kaka yake, basi Erick alibaki kumuangalia tu na kujiuliza kuwa anataka kumwambia kitu gani ila hakupata jibu ya kitu hiko.

Kulipokucha Erick alienda shuleni kama kawaida, ila alipopanda kwenye gari tu alikaa na Sarah ambapo Sarah alionekana kufurahi sana,
“Siku hizi sikupati kwenda shule wala kurudi, una mambo mengi sana Erick”
“Ni kweli nina mambo mengi”
“Ila wewe ni mwanaume uliyetulia sana, shuleni kuna wasichana wengi mno ila Erick hujaonyesha kuvutiwa hata na mmoja wapo jamani! Ila mimi nakuahidi kujitunza hadi pale utakaponizawadia”
“Halafu Sarah kuna kitu hujui kati yetu”
“Kitu gani?”
“Mama aliniambia kuwa inawezekana mimi na wewe ni ndugu kwahiyo kuna uwezekano wa asilimia tisini kuwa wewe ni ndugu yangu”
“Hapana haiwezekani kabisa, siwezi kuwa ndugu na mwanaume nimpendaye namna hii, hivi Erick unajua ni jinsi gani nakupenda lakini”
“Tupo kwenye gari la shule Sarah, hebu jiheshimu na maneno yako basi”
Walifika shuleni na moja kwa moja Erick alienda darasani ila aliitwa na madam Oliva, kwahiyo ilibidi aende kumsikiliza, kwakweli leo madam Oliva hakumchekea kama siku zote anavyofanyaga, alirudisha ukali wake ule aliokuwa nao kabla hajamfahamu baba wa Erick na kuanza kumpenda, basi Erick alivyokuwa pale huyu madam alimuamuru kupiga magoti, ilibidi Erick apige magoti tu kisha madam Oliva alimuuliza,
“Unajua kwanini nimekupigisha magoti?”
“Sijui”
“Sasa mbona umepiga?”
“Ningekataa ungesema nina kiburi ndiomana nimepiga magoti kama ulivyosema”
“Ni kweli una kiburi Erick, mbona hukuwa hivyo wewe!! Ulikuwa kijana mtulivu na mwenye heshima, ila kwasasa umekuwaje? Ni kitu gani kimekukumba Erick?”
Erick alikaa kimya tu, kisha madam Oliva aliendelea kuongea,
“Sasa nakupa onyo la mwisho, kwakweli ukionyesha tabia kama ile tena utaniona mbaya kabisa, sipendi watoto wasiokuwa na nidhamu. Haya inuka nenda darasani”
“Asante”
Kisha Erick aliinuka na kwenda zake darasani, ila siku hii alivyotoka shule aligoma kwenda kiwandani yani yeye hakutaka kwenda tena na madam Oliva kwahiyo akamdanganya tu kuwa siku hiyo mama yake alimwambia kuwa asiende kwahiyo kwa siku hiyo moja kwa moja alirudi nyumbani kwao.

Mama Angel alipomuona Erick mapema siku hiyo akajua sababu hakumpatia ile pesa ambayo alitapeliwa na Derrick, basi alianza kumuuliza mwanae,
“Mbona leo hujaenda?”
“Basi tu mama”
“Ila hata hivyo nilitaka kuja kuongea na wewe kuwa uwe unaangalia na siku za kwenda sio kila siku kila siku maana utashindwa kufanya vizuri kwenye masomo yako”
“Nimekuelewa mama, ila mimi kuna kitu sikipendi”
“Kitu gani?”
“Kila siku ninapoenda kiwandani basi madam Oliva anaambatana na mimi, kwakweli sitaki haya mambo kabisa mama. Niwe naenda mwenyewe tu”
“Mmmh yule madam nae kiherehere kweli yani, sikia basi dereva atakuwa anakuja kukuchukua, ila siku za kwenda kiwandani iwe Jumatatu, Jumatano na Ijumaa napo sio unakaa kwa muda mrefu, yani jitahidi usitumie muda mrefu sana kiwandani”
“Sawa mama, nimekuelewa mama yangu”
Kisha Erick akaenda zake ndani, basi mama Angel akajijadili kuwa kwanini huyo madam Oliva ameanza pia kumfatilia mtoto wake,
“Jamani hawa watu loh! Wameanza tena kumfatilia mwanangu jamani! Sijui vipi”
Basi baada ya muda kidogo Erica nae alirudi kutoka shule, na alivyofika tu alianza kumsimulia mama yake,
“Yani mama leo wakati tunarudi tukiwa kwenye basi la shule, njiani nilimuona anko Derrick, uwiii kuna mtu kamtapeli maana yule mtu alikuwa akimlalamikia sana. Ila mama hivi hamjapata tu cha kufanya na huyo anko?”
“Tufanye kitu gani?”
“Ngoja mama, nitamuwekea mtego halafu nyie mtajua cha kufanya”
“Mmmh Erica mtego!! Sasa mtego gani utakuwa nao wewe?”
Erica alicheka tu na kwenda zake ndani kubadili sare za shule.
 
SEHEMU YA 325

Muda wa kulala ulipofika, mama Angel moja kwa moja alienda zake kulala ila kabla ya kulala alipigiwa simu na Sia, basi akaipokea simu ile,
“Mambo vipi Erica?”
“Salama tu”
“Hivi mumeo unajua alipo na anafanya nini?”
“Mmmh yupo kikazi kwani vipi?”
“Kuna mwanamke nasikia umewahi kusoma nae, ilikuwa kipindi mpo shule wewe na Erick, huyo dada aliitwa Manka, unamkumbuka?”
“Mmmmh Manka? Oooh nimemkumbuka, alikuwa ni mweupe sana”
“Ndio, sasa nasikia yule amewahi kuwa na mahusiano na Erick”
“Unazungumzia nini wewe?”
“Basi nakwambia kuwa huyo Erick yupo na Manka kwasasa, wanakula raha yani hakuna cha kazi wala nini. Hivi wewe hushtuki eeeh! Sio kawaida ya Erick kusafiri muda mrefu hivi na kukuacha mkewe, kwanza kakuacha ili iweje? Mwenzio kakuzalisha ili yeye apate upenyo wa kuwa pamoja na Manka”
“Kiukweli sikuelewi kabisa”
“Sikia nikwambie, siku moja mdadisi huyo rafiki yako Jofari kuhusu Manka na Erick”
“Kheee unamfahamu hadi Johari!”
“Ndio namfahamu, sasa unadhani huyo Manka ningemfahamu vipi? Huna mashaka ndugu yangu eeeh? Ni kweli una rangi nzuri ila mwenzio Manka ni mweupe, na asilimia kubwa ya wanaume wanapenda wanawake weupe sana, najua wewe sio mweusi yani siwezi kukuweka kwenye weusi ila mwenzio Manka ni mweupe peee, na yale macho yake ya gololi, unadhani Erick anaweza kupindua pale?”
“Usinichanganye mie”
Mama Angel aliikata ile simu kwani aliona Sia akimchanganya tu kwa muda huo, basi alivyokata simu akaanza kumkumbuka vizuri huyo Manka,
“Mmmh hivi huyu Manka si ndio kipindi kile tunasoma alisema kuwa ana mahusiano na Erick hadi mimi nikaogopa kuwa pamoja na Erick! Mmmh Johari si ndio alikuja kunipa maneno kuwa Erick yupo na Manka hadi wamepelekana kutoa mimba jamani! Ila mbona Erick hajawahi kugusi hata mara moja kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na Manka?”
Akainuka na moja kwa moja akasogea kwenye kioo na kujiangalia kisha akasema,
“Mimi sio mbaya, hivi huyu Sia ana wazimu wa kusema Manka ni mzuri sana sababu ni mweupe sana? Kwani nani kasema kuwa weupe ndio uzuri? Asinibabaishe mie nishindwe kulala kwa amani nianze kuwaza mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu”
Kisha aliamua moja kwa moja kulala, yani kwa muda huo hata mume wake hakumpigia simu wala nini kwani aliona maneno ya Sia ni kumuweka roho juu juu tu.

Siku hii mama Angel alikaa nyumbani kwake akiwa amejichokea kiasi kidogo, kwahiyo alijikuta akijiwa na usingizi tu kwenye kochi, mida ya mchana akafikiwana mgeni na kushtuliwa pale na Vaileth basi akaamka na kumkuta huyo mgeni ni Juma, basi alimkaribisha vizuri sana na moja kwa moja Juma alianza kuulizia maendeleo ya Erick,
“Anaendeleaje kijana wetu Erick?”
“Yupo salama kabisa, ameenda shule”
“Na kiwandani huwa anaenda?”
“Ndio, ila nimemwambia awe anaenda mara moja moja, ili athiathiri masomo yake”
“Oooh ni vizuri, ila shemeji naomba nikuulize swali la kizushi”
“Uliza tu”
“Hivi kwa mtoto Erick hukuchepuka kweli? Mmmh mbona nahisi kama sio damu ya Erick hii”
“Kheee ndio swali gani hilo sasa? Nampenda mume wangu na tangia niingie kwenye hii ndoa basi huko unakoita kuchepuka hakuna nafasi katika maisha yangu yote. Kwahiyo unataka kusema mtoto Erick sijazaa na mume wangu? Kumbuka wapo mapacha, kwahiyo hii pacha nilichepuka eeeh!”
“Aaaah shemeji, mimi nimeuliza tu”
“Haya, basi nilichepuka na wewe”
“Jamani shemeji ndio yamekuwa hayo? Unajua mimi sio kwamba sikufahamu wewe, nakufahamu vizuri sana, hata mtoto wa kwanza sio wa jamaa, hilo nafahamu”
“Kheee umetumwa wewe au?”
“Sio kutumwa, mimi nakufahamu vizuri Erica, kama uliweza kutembea na shemeji yako yani mume wa dada yako ndio utashindwa kuchepuka kwenye ndoa yako?”
“Naomba uende mjinga wewe, naona huna jambo la kuongea na mimi. Kama ningekuwa hivyo usemavyo si hata wewe ningekukubali, mjinag wewe. Toka nyumbani kwangu”
Mama Angel alichukizwa na kujikuta akimfukuza tu, basi Juma alianza kumuomba msamaha na kusema kuwa ni utani,
“Nisamehe jamani shemeji yangu, sikujua kama una hasira kiasi hiki, naomba unisamehe”
“Naomba uende tu kwa amani, tusiharibiane siku tafadhari”
Basi Juma alkamuaga mama Angel na kuondoka zake.

Siku hii ya Ijumaa pia Erick hakutaka kwenda kiwandani na madam Oliva, basi alikaa hadi mwisho huku akipanga aende kwanza kwao halafu kama akiweza basi kwa siku hiyo abadili tu nguo na kwenda kiwandani sababu siku hii waliwahi kutoka shule, ila walivyopanda kwenye gari la shule kurudi nyumbani, leo Erick hakukaa siti moja na Sarah, ila Erick alivyofika kwao na kushuka ni hapo ambapo Sarah nae alishuka.
Basi wakiwa pale nje ya geti, Erick alimuuliza Sarah,
“Mbona umeshuka sasa?”
“Kiukweli nimemkumbuka mama yako, nahitaji kumsalimia tu ndio nirudi nyumbani”
“Kheee makubwa, ila kama nilivyokwambia kuwa mimi na wewe ni ndugu”
“Hilo kwangu sijali ila ninachojali ni kuwa nakupenda sana”
Erick hakubishana nae, basi moja kwa moja aliingia nae ndani kwao, na kumuacha sebleni akiwa na mama yake, basi Sarah alikuwa akiongea na mama Angel,
“Yani nimejikuta nimekukumbuka sana, basi nimeona leo nije nikusalimie mara moja tu halafu niende nyumbani”
“Oooh nashukuru sana kwa kunikumbuka”
“Ila mimi sio mkaaji sana mama”
“Oooh basi, Erick atakurudisha hakuna tatizo”
Na muda kidogo Erick alitoka ndani maana alitaka kwenda kiwandani, ila alipofika tu sebleni kabla hajamwambia mama yake lengo lake la kutaka kwenda kiwandani, aliambiwa na mama yake kuwa ampeleke Sarah nyumbani kwao,
“Hakikisha unamfikisha ndio unarudi, natumai unanielewa mwanangu”
Ilibidi Erick amuitikie tu mama yake na hata hakumwambia lengo lake kwani alijua wazi kuwa anaweza akachelewa na kushindwa kwenda kiwandani sababu kwakina Sarah na kiwandani zilikuwa ni sehemu mbili tofauti na zilikuwa mbalimbali.
Basi akatoka na Sarah na kuondoka nae kwenda nae nyumbani kwao, basi Sarah akawa akimuuliza,
“Ila mbona siku hizi Erick kama unanikwepa hivi, unajua sijui tatizo ni nini?”
“Hakuna tatizo”
Walifika nyumbani kwakina Sarah, basi Erick alimtaka Sarah ashuke ila Sarah alitaka kushuka nae kwanza ikabidi ashuke nae na kwenda nae ndani kwake, amabpo cha kwanza Erick aliulizia alipo mama yake Sarah,
“Kwani mama yako bado hajarudi?”
“Alirudi ila jana kasafiri tena, ila safari hii hatokawia kurudi”
“Aaaah sawa, basi mimi naenda”
“Unaenda wapi tena Erick? Naomba twende wote chumbani kwangu mara moja”
Erick aliogopa na kuinuka, kisha akatoka nje ambapo Sarah alimfata na kumuuliza,
“Kwani Erick wewe sio mwanaume?”
“Mimi sio mwanaume ndio maana mimi bado ni mdogo, kwahiyo mimi ni mvulana”
“kheee wawapi wewe lakini, mbona unakuwa mshamba hivyo?”
“Acha niendelee na ushamba wangu”
“haya, nikusubiri hadi miaka mingapi? Nikusubiri hadi umalize kidato cha nne?”
Sarah alikuwa akiongea na Erick huku kalegeza macho haswaa, yani kwa muda ule ilibidi tu Erick amuage na moja kwa moja alienda kupanda gari na kuondoka, badala ya kwenda kiwandani, ni moja kwa moja alienda kwenye duka lao ambapo alimuweka Rama kuuza lile duka.
Alipofika pale dukani alimkuta Rama akiangalia simu yake, na kugundua kuwa Rama alikuwa akiangalia mtandao wa facebook huku akisikitika, basi Erick alimuuliza,
“Sasa unasikitika nini?”
“Kuna huyu mtu nimemuona huku, yani nasikitika haswaa”
“Mtu gani?”
Rama akamuonyesha Erick ile picha, katika picha ile kulikuw ana binti mdogo tu halafu kasimama na mbaba, ila yule mbaba Erick alimfahamu, ila alimuuliza Rama ni kitu gani kinamsikitisha haswaa,
“Mbona ni picha ya kawaida, ila kwanini umesikitika hivyo?”
“Ni picha ya kawaida ndio ila huyu baba lazima atakuwa na mahusiano na huyu binti aliyepiga nae picha”
“Kwanini?”
“Huyu baba namjua vizuri, aliwahi kuwa shemeji yangu ila ni muhuni hatari, na umuonapo hapo kaathirika tayari, yani yeye anajivunia uzuri wake na pesa yake, kampa dada yangu ukimwi huyu baba, halafu hana aibu hata kidogo anatembea na wasichana wadogo kwa wakubwa, ndiomana nasikitika sana kwani namsikitikia huyu binti”
Erick alimuuliza ilia pate uhakika wa anachokihisi, alimuuliza,
“Kwani huyo baba anaitwa nani?”
“Anaitwa Rahim, nasikia kwasasa kaoa mke daktari tena mkewe nasikia ni mpole sana, ametulia ni mwanamke mwenye stara na heshima zake. Anaitwa Maimuna, ni mwanamke mpenda dini na anayeheshimu watu wote ila dada huyu hajapata bahati kabisa ya kuolewa na hiki kimeo yani namuhurumia sana. Hii picha ya kawaida ila kwa tabia za huyu mwanaume hata sio kawaida hapa lazima kuna kitu kinaendekea”
“Duh! Kumbe”
Basi Erick aliendelea na mambo mengine pale dukani ila kwa taswira ya haraka haraka ni kuwa huyu Rahim anamtaka pia Erica maana haikuwa kawaida kwa jinsi ambavyo kila akimuona Erica kutaka kumpatia pesa.
 
SEHEMU YA 326

Erick alipomaliza alirudi tu nyumbani kwao, na siku hii alikaa na mama yake na kumueleza tu kwa kifupi kuhusu huyo Rahim, yani vile alivyotaka kumpa Erica pesa, na jinsi anavyokuwa akiongea na madam Oliva, na jinsi alivyoambiwa na Rama, basi mama yake na hivi huwa anamchukia Rahim ndio akachukia maradufu na kumwambia mwanae,
“Tena Erick kuwa makini sana mwanangu, bora umemgundua, naomba ukae mbali na mtu huyo, hata kumsalimia usimsalimie hivyo hivyo, sitaki kabisa uwe karibu naye, ni mtu mbaya sana huyo”
“Sawa mama nimekuelewa, hata mimi nilihisi kuwa si mtu mzuri kabisa, kwajinsi ambavyo huwa anaongea na Erica, nikahisi kuwa yule sio mtu mzuri kwenye maisha yetu kabisa”
Erick akakubaliana na mama yake kuwa awe anamkwepa Rahim kabisa na hata kumsalimia asiwe anamsalimia, mama Angel alifanya hivi sababu alihofia ikiwa Rahim atapata ukaribu na Erick, basi atamwambia ukweli kuhusu Angel na yeye hakutaka hilo.
Muda wa kulala ulipofika kila mmoja alienda kulala na siku hiyo asubuhi na mapema Erick aliamka na kujiandaa halafu akaenda kiwandani sababu hakuenda kwa siku zote hizi akaona ni vyema aende siku hiyo.

Jumatatu ilipofika, kama kawiada Erick alikuwa shule na alivyomaliza masomo tu, madam Oliva alimuita ili waende nae kiwandani, Erick alikuwa akikataa ila madam Oliva akamlazimisha sana, ikabidi Erick akubali tu maana hakuwa na namna tena.
Waliondoka na madam Oliva hadi kiwandani, na kama kawaida wakati Erick ameenda kufanya kazi, huyu madam alibaki nje na baada ya muda pale nje alifika Rahim na kuanza kuongea nae,
“Aaaah madam na wewe ni mzushi sana, tumekubaliana vizuri kabisa kuwa tutakutana mwisho wa wiki hii, sasa mbona umezingua?”
“Dah!! Naomba unisamehe bure, ni kweli tulipanga kukutana ila mume wangu mtarajiwa alinibana haswaa hakutaka nitoke hata kidogo. Leo sikupanga kuja huku ila nikasema ngoja nije ili niweze kuonana na wewe na kuongea na wewe”
“Yani umeniangusha sana, huwa najua walimu sio waongo, ila wewe umenidanganya, yani nimesubiri simu yako hadi nikahisi kuchanganyikiwa”
“Nisamehe tafadhari”
“Haya, tutakutana lini tena na tutakutana wapi? Hapa sio mahali pazuri kwa mimi na wewe kukutana, inatakiwa tupate sehemu nzuri ili tuzungumze kwa upana zaidi, ni wapi tutakutana sasa?”
“Mmmh sijui, popote tu utakapopenda”
“Nielekeze shule unayofundisha ili siku nije nikuchukue muda wa kutoka halafu twende mahali tukayajenge”
Madam Oliva alianza kumuelekeza Rahim ili afahamu shule anayofundisha, muda kidogo Erick nae alitoka kiwandani na alitaka waende nyumbani.
Ila alipofika pale na kumuona Rahim kama kawaida hakumsalimia wala nini, basi madam Oliva alichukia sana na Rahim akamwambia madam,
“Si mwalimu wa nidhamu wewe!! Ndio mnavyowafundisha hivi shuleni kudharau wakubwa?”
Erick hakusema chochote ila aliondoka, na kama kawaida aliita pikipiki na kuondoka nayo kwenda nyumbani kwao.Erick aliingia nyumbani kwao na wala hakusema kitu chochote cha siku hiyo zaidi ya kufanya mambo mengine tu ambayo huwa anayafanya siku zote hadi muda wa kulala na moja kwa moja kwenda kulala.
Kulipokucha tu alijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida.

Erick alipofika tu shuleni aliitwa na madam Oliva, na kwenda kisha madam Oliva akamwambi,
“Natumaini unaelewa ni kitu gani umefanya”
Erick alikaa kimya tu, kwani hakuwa muongeaji wa sana, na tabia hii ilifanya wengi kumuona kuwa ana kiburi, kisha madam Oliva alisema tena,
“Ila wewe Erick una kiburi sana, si nilikuonya wewe ila jana umeenda kurudia kitendo kilekile, halafu kuna habari nyingine nimesikia kuwa una mahusiano ya kimapenzi na Sarah, nadhani ndio kitu kinachochangia kukufanya uwe na kiburi kiasi hiko. Hivi hujui mambo kama hayo yanakatazwa shuleni? Yani mimi huwa nakutetea sababu naelewana na wazazi wako, ila hakuna atakayeweza kufurahi akisikia mambo kama haya. Leo nitakuchapa fimbo tatu, ila jirekebishe, kwanza uwe na adabu na pia umuone Sarah kama dada yako, mambo ya kusikia tena una mahusiano nae sitaki kuyasikia. Haya inuka nikuchape”
katika vitu ambavyo Erick alikuwa havipendi ni kuchapwa viboko, ni sababu nyumbani kwao sio mtoto mbishi kwahiyo hata viboko hajawahi kuchapwa na mama yake wala na baba yake.
Kwahiyo swala la kuambiwa kuwa achapwe viboko lilikuwa gumu sana kwake, basi akamwambia madam Oliva,
“Madam nina ombi moja”
“Ombi gani hilo”
“Kabla ya kunichapa viboko naomba uniruhusu nimuite mama yangu nae asikie mashtaka haya halafu akuruhusu kunichapa”
“Unasemaje wewe! Mjinga kabisa”
Madam Oliva aliinuka kwa hasira na kumcharaza fimbo moja ya nguvu sana Erick, ila kitendo kile kilimfanya Erick aanguke na kupoteza fahamu.

Madam Oliva aliinuka kwa hasira na kumcharaza fimbo moja ya nguvu sana Erick, ila kitendo kile kilimfanya Erick aanguke na kupoteza fahamu.
Hapo madam Oliva akashikwa na wasiwasi sana, basi akaanza kumpatia Erick huduma ya kwanza, na baadhi ya walimu walienda kumsaidia, ila walipoona kuwa hazinduki ikabidi wampeleke hospitali.
Madam Oliva alijieleza kuwa mtoto kaanguka tu mwenyewe, aliogopa kusema kamchapa maana alijua kama akipatwa na matatizo itakuwa ni tatizo kubwa zaidi, basi yule daktari akawaambia kuwa wamuite mzazi wa yule mtoto, ilibidi tu madam Oliva ampigie simu mama Angel na kumuelekeza hospitali waliyokuwepo ili afike.
Kwakweli madam Oliva alihisi yupo kwenye wakati mgumu sana, huwa anaadhibu watoto ila ilikuwa tofauti kwa huyo mtoto, wakati amekaa na mawazo akapigiwa simu na Rahim, ilibidi aende nayo pembeni kuongea nayo,
“Vipi madam, nimepita hapa karibu na shule yenu, nije kukusalimia?”
“Dah nina matatizo mwenzio, nipo hospitali kwasasa”
“Hospitali? Unafanya nini tena? Nielekeze ni hospitali gani nije”
Madam Oliva alimuelekeza vizuri kabisa ila hakuwa na amani katika moyo wake hata kidogo kwani alijua wazi ukweli ukigundulika basi itakuwa ni tatizo kubwa sana kwake, yani alikuwa akifanya maombi yote ili Erick azinduke tu.

Kwakweli mama Angel toka amepata ile simu kuwa aende hospitali alihisi kuchanganyikiwa kabisa, hakujielewa maana hakujua huko hospitali kuna tatizo gani.
Basi alimuacha mtoto kwa Vaileth na kuondoka zake hadi huko hospitali, kwanza alimkuta madam Oliva akiwa nje kasimama na Rahim, akapatwa na hasira kuona madam Oliva kamuitia Rahim akataka kuondoka, ila madam Oliva akamkimbilia bila kujua kuwa anataka kuondoka sababu ya Rahim,
“Mama Angel mbona kama unataka kuondoka? Ni Erick amelazwa”
Hapo moyo wa mama Angel ulilia paaa, yani alihisi kama kapewa habari gani vile, na kutaka kuonyeshwa mwanae, basi moja kwa moja alipelekwa kwa daktari ambaye alianza kuongea nae,
“Samahani, mwanao ana tatizo la kuanguka?”
“Ninachotaka ni kumuona mwanangu, niambieni ukweli nini kimetokea kwa mwanangu? Naomba mniambie”
“Inasemekana mwanao alianguka gafla shuleni, na bado tunampatia huduma ila tumekuita ili tuweze kupata historia ya ugonjwa”
“Hakuna historia hiyo kwa mwanangu wala kwenye ukoo wetu hakuna kitu cha namna hiyo, nionyeshe Erick tafadhari”
Basi moja kwa moja daktari akampeleka mama Angel katika chumba alicholazwa Erick, pale mama Angel alimsogelea mwanae na kumshika mkono yani alijikuta tu akitokwa na machozi mengi kama maji, ila muda huo huo Erick nae alifumbua macho na kusema,
“Nakupenda sana mama”
Kwakweli mama Angel alifurahi sana na kumkumbatia mwanae huku akisema,
“Asante Mungu, asnte Mungu, asante Mungu”
Yani ndio kauli aliyokuwa akiitamka, ila madaktari walijaribu kumpima Erick na kugundua kuwa hana tatizo lolote lile.
Kwahiyo walimpa ruhusa huku wakimtaka aende siku nyingine kwaajili ya uchunguzi, muda huu ndio daktari na mama Angel waliangaliana na kukuta ni watu wanaofahamiana,
“Kheee kumbe ni wewe Erica”
“Ndio ni mimi, unajua hata sikufikiria pia kuwa ni wewe”
“Nakumbuka kipindi kile ulikuwa bado binti mdogo, saivi umekuwa ila sura yako haipotei yani bado umzuri vile vile”
Mama Angel aliona bora aagane nae tu huyu daktari ili asije kuzungumza mengine bure mbele ya mtoto, basi akaagana nae na kuondoka.
Pale nje bado madam Oliva alikuwa kasimama na Rahim, yani hata hakujua kuwa mtoto kazinduka, ila alivyowaona alitaka kuwafata ila mama Angel aliongozana haraka na Erick na kupanda gari ili kuelekea nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 327

Madam Oliva akiwa amesimama pale na Rahim akasema,
“Simuelewi mbona kachukia hivyo au mwanae kamwambia ukweli”
“Kwani ukweli ni nini?”
“Ni hivi, nilikuwa nimechukizwa sana na tabia yake ya jana, basi leo nikaamua kumuadhibu tena nilimchapa fimbvo moja tu ndio akaanguka na kupoteza fahamu, sasa sielewi tatizo ni nini. Ila nimekoma mimi, unadhani nitarudia tena kuchapa mtoto wa mtu! Kamwe sirudii mimi, yani nilikuwa naiona rumande inakuja jamani”
“Aaaah pole ila usingefungwa wala nini?”
“Mmmh unasemaje? Unadhani mtoto angekufa huyu kuna ambaye angeniamini kuwa ni bahati mbaya?”
“Najua Erica angekusamehe”
“Kheeee sio kwa watoto wake, yani yule mwanamke chezea vyote ila sio watoto wake na wala sio mume wake. Kumbe unamjua eeeh!”
“Namfahamu ndio, tuachane nae tuongee yetu. Vipi sasa twende tukayajenge”
“Yani leo sipo vizuri, akili yangu imevurugika kabisa, sina amani sina raha, hapa kwenyewe narudi kazini tu nachukua ruhusa na kwenda nyumbani kwangu, yani siwezi kwenda popote, nilikuwa naongea na wewe hapa kuendelea kujipa moyo tu na matuamaini ila ungeingia katika moyo wangu na kuona hali yake ilivyokuwa basi ungenielewa nasema kuhusu kitu gani. Tutaenda kuzungumza vizuri siku nyingine”
Na alipomaliza kusema hayo, aliamua tu kuagana na Rahim na kurudi zake shuleni kwanza kuchukua ruhusa ila Rahim hakupenda maana siku hiyo alitaka apate muda mzuri wa kuongea nae.

Mama Angel akiwa kwenye gari na mwanae akamuuliza,
“Erick sio kawaida ujue, usione nimeondoka tu na wewe hospitali bila kuuliza vizuri, lazima kuna tatizo mwanangu. Niambie tatizo ni nini? Imekuwaje hadi uanguke?”
“Mama, kwakweli sikumbuki vizuri ila mara ya mwisho nakumbuka ni madam alinichapa fimbo”
Mama Angel alisimamisha gari na kuliweka pembeni kwanza, halafu akamuuliza mwanae kwa makini,
“Alikuchapa fimbo? Kisa nini?”
Erick alimuelezea mama yake jinsi ilivyokuwa hadi madam Oliva akamchapa fimbo,
“Aaaargh ningejua mapema jamani, ngoja”
Kisha mama Angel akageuza gari na moja kwa moja kwenda hadi shuleni kwakina Erick, na moja kwa moja alienda kwenye ofisi ya mwalimu mkuu kumlalamikia,
“Shule zipo nyingi, ila mzazi nimeamua kugharamikia kumleta mwanangu hapa ilia je kupata elimu bora, sio aje kupata fimbo, haya leo mlimchapa mwanangu akazimia, na siku mkiniulia kabisa mtoto?”
“Mama Erick, naomba upunguze jazba”
“Sio nipunguze jazba, kwakweli siwezi kukubaliana na hali kama hii kabisa, natupa hela zangu nyingi sana hapa shuleni, nimeishi na mwanangu kwa miaka yote hii, hana kiburi, sio jeuri wala sio mbishi, sijawahi kumchapa hata kumpiga kibao sijawahi, halafu leo unaenda kumchapa mwanangu tena bila hata ya kuniuliza mzazi wake jamani!!”
“Tusamehe bure mama Erick, kwanza mimi sielewi kitu ni nini kimetokea kwani?”
“Muulize huyo mwalimu wako madam Oliva”
“Oooh amekuja hapa muda sio mrefu kuchukua ruhusa, kasema hajisikii kukaa ofisini kwa siku ya leo”
“Basi ndio huyo kanichapia mwanangu hadi kazimia, nahisi mwanangu hayupo sawa kabisa. Kumbuka natoa pesa nyingi kwa elimu ya mwanangu halafu mnataka kuniulia mwanangu kweli!”
“Naomba utusamehe bure mama Erick, huyo madam Oliva nitaongea nae vizuri”
“Nitawafungulia kesi mimi maana ushahidi upo”
Huyu mkuu wa shule aliamua kuendelea kumbembeleza mpaka pale mama Angel aliporidhika na kuondoka na mwanae, ila wakati wanarudi nyumbani ndani ya gari tu akampigia simu mume wake, hadi Erick aliomba tu gari aendeshe yeye maana aliona mama yake ataleta balaa bure.
Basi akamuacha Erick aendeshe huku yeye akiongea na mume wake,
“Sasa huyo Oliva ametaka kutuulia mtoto leo”
“Kafanyaje?”
“kampiga mtoto hadi kazimia, hivi nimetoka hospitali na ndio naenda nyumbani na Erick, yani sijapenda kabisa tabia aliyoifanya madam Oliva”
“Sawa, mke wangu nashukuru kwa taarifa”
Kisha baba Angel alikata simu, ambacho mama Angel hakufahamu ni kuwa baba Angel ndio alichukia zaidi yake, yani alichukia mno, alitamani hata huyo madam Oliva angekuwa karibu yake kwa muda huo.

Madam Oliva alirudi nyumbani kwake ila bado alikuwa na mawazo kiasi, basi alikaa na Steve ambapo Steve alimuuliza tatizo ni nini, aliishia tu kumwambia,
“Wewe acha tu”
Muda kidogo simu yake ya mkononi ikaita, kuangalia akaona mpigaji ni baba Angel, yani hapo akapatwa na mashaka makubwa sana, ila aliipokea ile simu ambapo baba Angel alianza kumwambia maneno yake aliyojisikia kuyasema kwa muda ule,
“Sijapenda kabisa, unataka kuniulia mwanangu? Hivi unajua kama mtoto wa kiume ninaye mmoja tu!! Hivi unajua kama yule ndio mtoto wa kuwaangalia dada zake, unataka kumuua ili mimi nibakiwe na nini?”
“Naomba unisamehe, haikuwa kusudio langu, naomba unisamehe sana, yani mimi nilikuwa tu nataka kumfunza adabu ila ikawa vile”
“Umfunze adabu kwa lipi alilokukosea?”
“Sikia nikwambia, huwa naenda na mwanao kiwandani, ila kule nilikuwana na baba mmoja anaitwa Rahim na tulikuwa tunaongea maswala ya biashara, ila mwanao huwa akinikuta na yule baba huwa hamsalimii kabisa na nikimuuliza ananiangalia kwa dharau na kuondoka zake, sasa leo nikasema ngoja nimchape kiboko ili ajifunze heshima, jamani fimbo moja tu hata sijui imekuwaje hadi kuwa vile”
“Mjinga wewe, kwanza aliyekwambia uwe unaenda kiwandani na mwanangu ni nani? Halafu kitu kingine, wewe si ndio ulikuwa ukililia kuolewa wewe na kusema kuwa unataka kuolewa na Steve, haya huyo uliyekutana nae unayezungumza nae kuhusu biashara wa nini? Utakufa na ukimwi wewe, tamaa zitakuponza, umesoma lakini kajinga. Mwenzio ana ukimwi yule anafanya kazi ya kuusambaza tu, usije kumuua Steve wa watu bure kwa ujinga wako, umemtundika midawa hata kutoka hawezi halafu unataka kumletea na maradhi. Mjinga kweli wewe”
Madam Oliva alikaa kimya kwa muda kisha akasema tena,
“Nasamehe tafadhari”
Halafu baba Angel alikata ile simu, Steve alimuangalia madam Oliva na kumuuliza kuwa anaomba masamaha wa kitu gani, ikabidi madam Oliva amsimulie kila kitu jinsi ilivyokuwa kwa siku hiyo.
Steve alishangaa kwa muda ila akasema,
“Dah iliwahi kunitokea hiyo siku moja wakati nikiwa mvulana mdogo, kuna mtu alinikorofisha basi nikamzaba kibao, uwiii si akaanguka na kupoteza fahamu yani nilihisi kuchanganyikiwa, mpaka alipokuja mama yake, ndio akazinduka, ndio mama yake akaniambia kuwa mwanae huw ahapigwi. Yani toka siku hiyo nilikuwa naogopa kupiga watu hovyo balaa”
“Ooooh pole, basi ndio yaliyonipata leo”
Kisha madam Oliva aliinuka na kwenda chumbani basi alifikiria kwa muda maneno ambayo baba Angel alimwambia mwishoni kuwa Rahim ameathirika, akajiangalia kwa muda na kusema,
“Hivi baada ya miaka yote hii kujitunza, nije kupata ukimwi kizembe namna hii dah!”
Akapumua kwa muda na kuamua kujilaza tu kwa muda huo.

Muda huu mama Angel akiwa nyumbani huku Erick akiwa ameenda kupumzika, mara akapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Sia, sababu alimruhusu siku ile basi mlinzi hakuwa akimkatalia tena kuingia ndani, na yeye akaongea nae kawaida tu ili kujua shida yake,
“Nimekuja kumuona Erick”
“Ili iweje?”
“Nasikia alizimia, na mimi kama mama nina wajibu wa kujua kuwa mwanangu anaendeleaje?”
“Dah! Yani wewe sijapata kuona mimi, huwa nakutafakari sana ila nakosa jibu kabisa. Anaendelea vizuri. Una lingine”
“Ndio lipo, mwanao Elly anakusalimia”
“Naona umeamua kuja kuniachanganya muda huu, hebu Sia acha kunitia kichaa, niliyonayo kichwani yananitosha. Naomba utoke”
Sia hata hakubishana leo kwani muda huo huo aliofukuzwa, alijiongeza na kuondoka zake.
Alipoondoka, mama Angel alipumua kiasi yani aliona ni afadhari kaondoka, ila baada tu ya kuondoka, alisogea Vaileth mahali pale na kumuuliza mama Angel,
“Samahani mama, kwani huyu mwanamke huwa anakuja kwako mara kwa mara kufanya nini?”
“Aaaah achana nae huyu”
“Mmmh kama namfahamu”
Mama Angel akashtuka kidogo na kumuuliza kwa makini,
“Unamfahamu? Kivipi?”
“Ila sina uhakika kuwa ni yeye”
“Niambie tu unavyomuhisi”
“Ni hivi, mimi nina babu yangu ni mganga wa jadi, sema siku hizi sina mawasiliano nae ya karibu sana kutokana na dawa aliyokuwa anataka kunifanyia nami nikaikataa hiyo dawa. Nakumbuka kipindi nikiwa mdogo huyu mwanamke nimewahi kumuona mara kadhaa kwa babu, inasemekana alikuwa akichukua dawa ya kumdhibiti mwanaume ila dawa sijui ilikosewa ikaenda kwa mwanaume mwingine, na hilo swala likamsumbua sana, huwa nahisi kama ni yeye vile, najua hanikumbuki ila mimi namuhisi”
“Huyo babu yako yuko wapi?”
“Anaishi Bagamoyo”
“Oooh sawa, nitafatilia tu kujua kuwa ni yeye au wanamsingizia. Ngoja nikuulize na wewe, inamaana kipindi kile ndugu zako ndio walichukua dawa kwa huyo mganga?”
“Hapana, mganga yule walimpata hapahapa mjini, hata nilikuwa simfahamu hadi siku waliyonipeleka”
“Ila Vai unaonaje kuhusu maswala ya uganga?”
“Mmmh hata sielewi, ila mimi uganga kiukweli siupendi. Naomba nikaendelee na kazi zingine”
Vaileth aliona ataulizwa maswali mengine ambayo atashindwa kujieleza, kwahiyo aliamua kwenda jikoni na mama Angel alimruhusu kufanya hivyo.

Usiku wa leo, Erica anaamua kwenda chumbani kwa Erick maana kama hakuelewa vile wakati mama yake akizungumza, akamfatya ili aujue ukweli,
“Kwani leo kimetokea nini Erick?”
Erick alimsimulia jinsi ilivyokuwa, ila katika maelezo ya Erick hakuna hata sehemu moja aliposema kuwa sababu za kupigwa na madam Oliva zimehusishwa pia na swala la yeye kuwa na mahusiano na Sarah. Yani alikuwa akielezea tu kutokumsalimia Rahim,
“Kale kamadam jamani loh! Yani angaejua huyo mtu asivyopendwa kwetu nahisi angeelewa ni kwnaini hujamsalimia”
“Ndio hivyo, yani akanipiga kiboko hiko ila nashangaa ni kwanini nimezimia kwa fimbo moja tu!”
“Ila na yeye kwanini kakuchapa? Na hospitali nao wamesema kwanini umezimia?”
“Hawajasema tatizo ni nini ila nadhani tatizo ni kuchapwa, ila kwanini nizimie baada ya kuchapwa kiboko kimoja tu! Ni kweli sijawahi kuchapwa na mama wala na baba ila sijafikiria kuwa naweza kuwa na tatizo nikichapwa mimi. Nitachunguza tu na kujua kuwa tatizo ni nini”
“Mimi nitakusaidia kuchunguza, hata usijali. Ila leo nitalala humu humu chumbani kwako ili usije kuzimia tena bure, lazima nikuangalie”
Erick alicheka sana, ila hakusema neno lolote lile, kwani hata yeye alifurahi kwa swala la Erica kulala chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 328

Siku hii, mapema kabisa Vaileth alikuwa ameshaamka ila aligundua kuwa Erick na Erica hawakuamka kwenda shuleni, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica aligonga ila hakuitikiwa, akafungua mlango na kukuta Erica hayupo humo, basi akaenda chumbani kwa Erick aligonga ila hakuitikiwa, akafungua mlango na kukuta Erick na Erica wamelala tena wakiwa hawana habari kabisa, alisikitika huku akiwaangalia mara mbilimbili na kusema,
“Hawa si kaka na dada hawa? Tena mapacha, maajabu haya jamani, ndio ulalaji gani huu?”
Akafikicha macho yake vizuri na kuwasogelea kisha aliwashtua, kwakweli walishtuka sana toka usingizini, halafu Vaileth alimuuliza Erica,
“Mbona umelala humu leo? Na vipi huendi shule?”
“kwani saa ngapi saa hizi?”
“Saa moja na nusu hii”
“Kheeee!”
Kisha Erica alimuangalia Erick na kumuuliza,
“Kwahiyo igtakuwaje, na wewe hutoenda shule?”
“Tushachelewa, haiwezekani kwenda shule, nitaenda kiwandani tu leo”
“Basi tutaenda wote kiwandani, ngoja nikajiandae”
Erica aliinuka, yani Vaileth aliwaangalia sana wala hawakuonekana kuwa na wasiwasi wa aina yoyote ile kila kitu kwao ilikuwa ni kawaida kabisa, basi Vaileth nae alitoka mule chumbani ila alikuwa akitafakari sana huku akijisemea,
“Mmmh haya ni malezi mabovu, watoto wa Kiswahili ukawalee kizungu ndio madhara yake haya, yani watoto wanalala pamoja kama sio dada na kaka vile mmh!!”
Kisha akaenda jikoni kuandaa chai.

Erisk alishaenda kuongea na mama yake kuhusu kwenda kiwandani kwa siku hiyo, basi walipomaliza kujiandaa na Erica walienda kunywa chai na kumuaga mama yao kisha kwenda kiwandani, basi mama Angel alikuwa amekaa huku akimbembeleza mwanae mdogo, Vaileth alienda karibu yake na kumuuliza,
“Mama, mbona hujamwambia Erica aende shule basi?”
“Wamechelewa kuamka, watoto wale mapacha wana mambo yakufanana ndiomana hata huwa sijiumizi kichwa changu”
“Hivi Erick na Erica umeanza kuwatenga chumba wakiwa na umri gani?”
“Yani nyumba ambayo nilikuwa naishi mwanzoni, nilipenda watoto wangu wote walale pamoja na walikuwa wanalala pamoja, ila badae Angel alisema kuwa Erick ni mtoto wa kiume na atawachungulia, basi tulipohamia hapa nikawahamisha kila mtu na chumba chake, ila ilikuwa ni ngumu sana kwa Erick na Erica kulala kwenye vyumba vyao, yani kama hujamkuta Erick kwenye chumba cha Erica basi utamkuta Erica kwenye chumba cha Erick hadi nikaanza kuwafanyia ukali, kidogo ikasaidia ila baba yao hakupenda ukali ninaoufanya kwa watoto, yani ni wao wenyewe ndio walivyoona wamekuwa basi ndio hivyo kila mmoja analala kivyake”
“Halafu jana nilisikia ukisema kuwa Erick alipigwa shuleni hadi akazimia, kwahiyo huyo mwalimu alimpiga hovyohovyo?’
“Alimpiga fimbo moja”
“Hujawahi kumchapa Erick?”
“Nimchape kwa kosa gani? Yani humu ndani kwangu hakuna watu waoga kama watoto wangu, ni waoga balaa, tena Angel ile ukishika fimbo tu basi utaona chozi na kuomba msamaha balaa, kuhusu Erick ndio kabisa, sijawahi kumpiga hata kibao, huwa nafoka tu ila sijawahi kuwapiga”
“Wanaraha kukupata wewe, jamani mama yangu uwiii hata akikuita hukuitika sababu hukusikia, utashtukia tu mkong’oto huo wa nguvu hadi unasahau jina lako, jamani kuna wamama wanapiga haswaaa, ila nadhani wewe sio mpigaji ndiomana hata Angel huwa anakusumbua sana”
“Niliwahi kumpiga Angel siku ile, ambayo nilijifungia nae chumbani, ila nilikuwa nalia sana. Yani mimi kumuadhibu mtoto siwezi jamani, sijui kwanini ila siwezi, nitawafundisha vyote ila sio viboko”
Vaileth alimuangalia tu ila hakusema neno lingine lolote lile, kisha akaenda kufanya mambo mengine.

Mchana wa siku hiyo, alifika mgeni pale nyumbani kwa mama Angel, alifika Juma na kumkuta mama Angel na kuanza kuongea nae,
“Unajua kilichonileta?”
“Kipi hicho, mimi nitajuaje? Nimekuwa mfalme njozi?”
“Una majibu sana, ila nimekuja kumuona Erick anaendeleaje? Nimepata habari zake za kuzimia”
“Kheee jamani, hiyo habari ndio imeenea kiasi hiko?”
“Hakuna kitu kinaweza kumpata Erick halafu mimi nisijue”
“Kwakuwa wewe ni nani kwa Erick? Wewe ndio mzazi wake au kitu gani?”
“Hapana, ila hujui tu jinsi ninavyomfatilia huyu mtoto kwa karibu. Na huwa namwambia hata rafiki yangu Erick kuwa kapata mtoto haswaa, yani ni mtoto ambaye anatakiwa kumtumia katika biashara zake, unajua Erick ni kijana mwenye akili sana. Msimpoteze kwa kumuweka shuleni”
“Unamaana gani?”
“kama hayo yaliyotokea, basi muachisheni shule halafu muache akae kiwandani kwa mwezi mmoja tu makini uone kama hamjafungua kiwanda kingine, na mtanishukuru sana. Huyo mtoto ni kichwa kingine kabisa”
“Haya sawa, ngoja nikuulize je wewe unafaidika na nini kumfatilia hivyo Erick?”
“Hata mimi mwenyewe sijui nafaidika na nini ila natamani kumfatilia kwa karibu sana, natamani kumfahamu vizuri, natamani kujua mengi kuhusu yeye. Mnisamehe bure tu ila nataka kumfahamu Erick zaidi”
“Kheee makubwa jamani! Hapa ndio uchawi unapoanzia, yani uache kufatilia watoto wako ufatilie mwanangu kweli? Usione kama watoto wako wana akili, uone akili za mwanangu kweli?”
“Usinifikirie vibaya, wakati ujenzi unaendelea niliwahi kufika pale kiwandani na kukutana na vijana wenu wawili. Junior na Erick, ila kwanini nilikuja hadi kumwambia rafiki yangu kuhusu Erick? Ni kutokana na vile nilivyokuwa nikiongea nae, niliweza kumsoma kuwa ni mtoto mwenye kipawa cha ajabu sana, ni mtoto mwenye akili kubwa sana. Natamani muone kile ambacho mimi nakiona kwa Erick ila sijui kwanini hamuoni hili jamani dah! Kwahiyo yuko wapi leo?”
“Kaenda kiwandani”
“Basi naenda huko, niongee nae japo kidogo tu”
Muda huo huo Juma akaondoka zake, ila mama Angel alimuangalia na kujiuliza sana kuwa kwanini huyu anaonekana kutaka kumjua zaidi Erick yani hapo hakumuelewa kabisa.

Siku ya leo kwenye madam Oliva anadatwa shuleni na Rahim, kwakweli alishangaa ujio wake na kwenda kuongea nae,
“Mmmh madam, najua saivi ni muda wa kupata chakula cha mchana, naomba leo twende tukapate wote chakula cha mchana”
Madam Oliva hakuona kama ni tatizo, ilimradi ni chakula cha mchana basi alikubali na moja kwa moja kupanda kwenye gari ya Rahim na kwenda nae kwenye moja ya hoteli ambapo kila mmoja aliagiza chakula alichokitaka na kuanza kula, basi Rahim alianza kuongea nae,
“Katika maisha yangu sikuwa naelewa neno kupenda lina maana gani, yani nilikuwa nashangaa tu wale wanaosema nimependa sana hadi nimeachwa nahisi kuchanganyikiwa, yani nilikuwa nawashangaa mno. Unajua kwanini? Naomba leo nikueleze kidogo tu kuhusu maisha yangu”
Moja kwa moja madam Oliva akajua hapo ndio muda ambao Rahim anahitaji kumtongoza, yani alielewa kuwa Rahim atasema hakuwahi kupenda ila kampenda yeye, kwahiyo alitegesha masikio yake kumsikiliza kwa makini sana,
“Nakusikiliza Rahim”
“Kwanza mimi nimeishi sana Marekani, mimi nilikuwa natongozwa sana na wanawake, na walikuwa wakinipa pesa ili nitembee nao, sikuwa napenda kabisa yani nilikuwa natembea nao ilimradi tu. Sikukaukiwa na hela mimi maana kwetu kulikuwa ni sehemu yenye hela na wanawake zangu wengi walikuwa ni wenye hela na walikuwa wakinipa wenyewe. Siku moja nikiwa nimerudi nyumbani, nilimkuta binti mmoja ambaye nilitambulishwa, kiukweli nilipomuona moyo wangu ulidunda sana na kujikuta nikitamani kuwa nae karibu. Njia pekee ya kumvuta yule mwanamke ilikuwa kwakutumia pesa, ila baada ya muda niliona moyo wangu kuanza kumuhitaji sana, basi nikamshawishi kulala nae kwakujua kuwa hamu yangu kwake itaisha, ni kweli nililala nae na nilimfaidi haswaaa, halafu katika siku hizo hizo akabeba mimba yangu ila niliamua kumpotezea taratibu, na kumpa vigezo vigumu ili aachane na mimi, kiukweli alikuwa akiumia sana tena sana kwa niliyokuwa namfanyia, ila imani yangu iliniambia kuwa mwanamke nikimzalisha ni ngumu sana kuniacha, kwahiyo nilijua ni wazi kuwa hawezi kuniacha kwa vyovyote vile. Ila huwezi amini yule dada aliolewa na mtoto wangu akampa jamaa mwingine, ila cha kushangaza sasa kila muda najikuta nikizidi kumpenda huyu mwanamke yani nampenda sana ingawa tayari ni mke wa mtu”
Madam Oliva alikaa kimya tu akimuangalia, halafu alishangaa kushtuliwa na swali hili,
“Hivi mama yake na yule kijana Erick anaishi wapi? Unapafahamu?”
“Napafahamu ndio”
“Naomba unipeleke”
Madam Oliva alimuangalia ila hakumuhoji zaidi ya kukubali kumpeleka kwani hata yeye alijua atapata muda wa kuongea na mama Angel kuhusu Erick.
Basi aliinuka na kuondoka na Rahim kuelekea kwa mama Angel.
Walifika kwa mama Angel na mlinzi aliwafungulia geti na kuwakaribisha, basi waliingia ndani na muda huo mama Angel alikuwa ametoka nje ila Rahim alipomuona mama Angel alimkimbilia na kumkumbatia.

Walifika kwa mama Angel na mlinzi aliwafungulia geti na kuwakaribisha, basi waliingia ndani na muda huo mama Angel alikuwa ametoka nje ila Rahim alipomuona mama Angel alimkimbilia na kumkumbatia.
Mama Angel alimtoa Rahim katika mwili wake ila Rahim hakutoka kwani alikuwa amemkumbatia kwa nguvu sana, yani lile tukio lilimshangaza, madam Oliva, Vaileth na hata mlinzi maana wote muda huo walikuwa hapo nje.
Basi mama Angel alipopata upenyo wa kuondoka kwenye mikono ya Rahim, yani alijikuta muda huo akikimbilia ndani kwake, yani hakutaka kuongea chochote kile, alikimbilia chumbani moja kwa moja na kufunga mlango huku akihofia kuwa huenda Rahim akawaeleza kitu pale nje, ila aliogopa kutoka tena nje ya nyumba yake.
Ila pale nje napo, Rahim alipoona mama Angel kakimbilia ndani, alimgeukia madam Oliva na kumtaka waondoke bila hata kuongea chochote kile.
Yani madam Oliva alishangaa tu na kumfata kwa nyuma, basi akaondoka nae, ambapo moja kwa moja Rahim alimrudisha madam Oliva kwenye ile shule anayofundisha, ila madam Oliva akamuuliza,
“Kuna nini kinaendelea? Sijakuelewa?”
“Kusoma hujui, hata picha nayo huoni? Ila asante sana, nashukuru kupafahamu mahali pale, asante sana”
Kisha Rahim hakutaka kuongea zaidi na kumtaka tu madam Oliva ashuke ambapo alishuka halafu yeye aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 330

Siku hii watoto walienda shule kama kawaida, ila Erick leo hakupanda basi la shule, kwahiyo alimuomba tu dereva wao ampeleke shule. Alifika na kuingia darasani ila alifatwa na Sarah na kuanza kuongea nae,
“Erick sijakuona jana nini tatizo? Hata juzi sijakuona, halafu leo hujapanda basi la shule”
“Nakuomba ukae mbali nami Sarah”
“Kwanini?”
“Hivi unajua kuwa juzi nimechapwa na madam Oliva kwasababu yako”
“Kheee kwasababu yangu?”
“Ndio, nilichapwa hadi nikazimia”
“Kheee kumbe mwanafunzi aliyezimia ni wewe Erick! Yani madam Oliva anakupiga wewe hadi unazimia kwasababu yangu?”
“Ndio, kasema asinione tena karibu na wewe”
“Aaaah tulia, dawa ya huyo madam inachemka, amekaa hapa shuleni kwa muda mrefu na kupendwa na wengi ila kwasasa kapoteza sifa yake na atajutia sana tu”
“Kivipi?”
“Subiri, utaona tu”
Sarah aliinuka na kuondoka zake, kwahiyo Erick alibaki akimtazama tu bila ya kummaliza.

Madam Oliva, siku hii alimuita Erick ili aongee nae kuhusu kwenda kiwandani ila Erick aligoma na kusema kuwa hatoenda,
“Baba, kaniambia kuwa nisiwe naenda, nitaenda kwa zile siku anazozisema yeye tu”
“Kheee mnaharibu biashara lakini ujue”
“Wapo watu wakusimamia, huwa naenda tu mimi ila watu wapo”
“Ila wewe mtoto ni mbishi, hata sijui walikupata kwa kipindi gani? Hivi na wazazi wako huwa unawabishia kiasi hiki au?”
“Madam, nimekwambia siendi tena kiwandani hayo maswala ya ubishi ni yako. Hakuna mzazi wangu niliyewahi kumbishia kitu chochote kile”
Basi Erick akaondoka, kwakweli madam Oliva hakupenda kabisa ila hakuweza tena kumuadhibu Erick, muda huu aliamua tu kurudi nyumbani kwake.
Leo hakutembea na usafiri wake, basi njiani alikutana na Sia ambaye alianza kumuongelesha kwa kutikisa kichwa,
“Yani wewe madam una mambo ya ajabu sana, umpende A utegeshe dawa, umpate B halafu unajifanya ndio umezama kwa huyo B”
“Kwani tatizo lako ni nini?”
“Tatizo langu analijua, muulize mimi ni nani kwake? Yeye ni baba wa mtoto wangu”
“Kheee makubwa, mbona mwenyewe hajawahi kuniambia mambo kama hayo?”
“Atakwambia muda gani na umemfanya bwege? Hivi unajisikiaje kumfuga mwanaume ndani kwako? Yani badala ya yeye kuwa mwanaume basi wewe ndio unakuwa mwanaume, yani yeye akae ndani tu ukirudi akupikie, wewe ule na kutundika miguu juu. Unajisikiaje madam? Kumbuka ni mtoto wa mwanamke mwenzio yule, hebu mwache Steve asimame kwenye nafasi yake kama mwanaume na afanye vile wanaume wengine wafanyavyo”
“Unajua huwa sikuelewi kabisa, unataka nini Sia?”
“Nimekwambia muache Steve asimame kwenye nafasi yake, acha kumfuga namna hiyo jamani, na yeye anahaki ya kutambua ukweli wa maisha, yani ataendelea hivyo hadi lini? Mpunguzie dozi bhana mtoto wa watu”
Kisha Sia akaondoka zake, ila hakusema chochote kuhusu kupigwa kwa Erick inaonekana hakujua kama ni madam Oliva ndiye aliyempiga Erick.
Madam Oliva alifika kwake akiwa amechoka kiasi na kukaa sebleni, ila Steve alikuwepo na alikuwa ameshapika na kuandaa chakula basi madam Oliva akacheka na kukumbuka yale maneno ya Sia, kisha akamuangalia Steve na kumwambia,
“Nimeambiwa nikupunguzie dozi”
“Dozi gani?”
“Eti sio kawaida kwa mwanaume kukaa nyumbani na kufanya kazi za mwanamke”
“Aaaah achana nao bhana, mimi nimeridhika na nitakuhudumia mke wangu”
Madam Oliva alitikisa kichwa tu, ila alihisi lazima kuna kitu hakipo sawa kwa Steve maana alikuwa akishinda nyumbani tu labda amwambia siku kuwa watoke ila bila ya hivyo alishinda nyumbani tu na alifanya kazi zote za nyumbani pale kama kupika, kufua, kusafisha nyumba hata kuosha vyombo.
Usiku wa siku hiyo madam Oliva alipigiwa simu na Erick, basi aliipokea na kuanza kuongea nae,
“Hivi wewe mwanamke una kichaa au kitu gani?”
“Kwanini lakini, kwanini upeleke watu wa ajabu ajabu nyumbani kwangu? Nadhani hunijui, nishakuona ukiifatilia sana familia yangu ila nitakukomesha”
“Kheee jamani, sikuelewi ujue”
Ile simu ilikatika na kumfanya madam Oliva abaki kuwa na maswali maana hakufikiria kama kile kitu ni cha kuchukia kiasi kile.
Basi Steve alikuwa akimuuliza pale imekuwaje,
“Yani hata nikikueleza huwezi kuelewa, ila leo nimekutana na Sia anadai kuwa wewe na yeye mna mtoto”
“Yule mwanamke ni kichaa ujue, nimelea mimba, nimehudumia kila kitu, ila kumbe mtoto mwenyewe ana mababa sijui wangapi, mara aseme mtoto wangu, mara wa Erick, mara sijui wa nani huko, mara nikute kuna jamaa anamdai mtoto, halafu mtoto mwenyewe, wakati mchanga lkaletwa mwingine na baada ya siku chache kaletwa mwingine na kubadilishwa jina, kwakweli yule mwanamke huwa haeleweki hata kidogo”
“Kheee imekuwaje, inawezekanaje kwanza? Mbona ni tofauti sana?”
“Ndio hivyo, yule mwanamke anajijua mwenyewe na anajua mwenyewe ni kitu gani alifanya mpaka imekuwa hivi ilivyukuwa. Twende tukalale tu mke wangu, achana na mambo hayo”
Basi madam Oliva alielekea tu kulala bila kuwaza mengine katika akili yake.

Leo Erick alipoenda shuleni, alifatwa tena na Sarah darasani na kuanza kuongea nae,
“Erick, tayari nishampa funzo madam Oliva”
“Funzo gani?”
“Utaona tu, hii shule ni ya baba yangu na ilijengwa kwaajili yangu, inaendeshwa kwaajili yangu halafu atokee mtu wa kunifanyia vitu visivyoeleweka kweli!”
“Kumbe shule hii ni mali yako?”
“Ndio, mimi sio mtu wa mchezo mchezo Erick, nakupenda sio sababu ya mali zenu hapana, yani nakupenda tu, kama mali basi niameachiwa za kutosha na baba halafu kumbuka kuwa mimi ni mtoto pekee kwa mama yangu”
“Je huyo baba yako hakuwa na watoto wengine?”
“Mama kasema hata kwa baba mimi ni mtoto pekee ndiomana kaniachia hizi mali zote”
“Hongera sana”
“Asante, hakuna wa kukatisha mahusiano yetu Erick. Acha sisi tupendane na mwisho wa siku tuje tuishi pamoja kwa furaha”
Erick alitabasamu tu kwani alijua wazi kuwa hawezi kumpenda Sarah hata iweje kwani alikuwa akimuona kawaida tu, basi Sarah aliamua sasa kwenda darasani kwake.

Kuna ujumbe madam Oliva aliupata kwa siku hiyo alihisi akili yake kuchanganyikana kabisa, basi akabeba mkoba wake na kuondoka, njiani akakutana tena na Sia ambaye alimuuliza,
“Mbona leo upo kama umechanganyikiwa”
“Nina haki ya kuchanganyikiwa kwakweli, nimefanya kazi kwenye ile shule kwa miaka mingi sana. Halafu leo kwasababu za kijinga tu eti nimesimamishwa kazi, yani huyu Erick huyu!”
“Erick yupi?”
“Si kale katoto kenye roho mbaya”
“Kheee Erick amenza kufanya roho mbaya hadi kwa watu baki jamani! Ngoja leo nitaenda huko naona Erica hamfunzi vizuri adabu huyu mtoto”
Yani Sia hakuuliza imekuwaje wala nini zaidi zaidi akapanga hivyo tu, basi moja kwa moja alienda nyumbani kwake.
Siku hii Elly aliwahi kurudi kisha Sia alimwambia Elly amsindikize mahali,
“Wapi mama?”
“Kuna mahali nataka kwenda kumuonyesha mtu mmoja asiyejua kulea watoto ajue ni jinsi gani watoto wanapaswa kulelewa”
“Kheee haya mama”
Basi Elly alijianmdaa vizuri na kuondoka na mama yake.

Muda huu Erick alikuwa amerudi nyumbani kwao, ila mama Angel alimtuma sababu alihitaji vocha na simu yake haikuwa na hela,
“Kaninunulie vocha mwanangu, nitakaa ndani ya geti kusubiria”
“Kheee mama ndani ya geti? Kwani si naleta tu!”
“Nina haraka nayo sana”
Basi Erick aliondoka na kwenda dukani, wakati anarudi kufika tu getini akamuona Sia, kiukweli hakupenda kumuona wala nini, basi Sia akasogea ili amuongeleshe ila kabla hajasema neno lolote, Erick alimsukuma Sia na kumuangusha chini, kitendo kile kilimkera sana Elly na hapo hapo alijikuta akimvaa Erick na kuanza kupigana nae.
 
SEHEMU YA 331


Basi Erick aliondoka na kwenda dukani, wakati anarudi kufika tu getini akamuona Sia, kiukweli hakupenda kumuona wala nini, basi Sia akasogea ili amuongeleshe ila kabla hajasema neno lolote, Erick alimsukuma Sia na kumuangusha chini, kitendo kile kilimkera sana Elly na hapo hapo alijikuta akimvaa Erick na kuanza kupigana nae.
Mama Angel alisikia kile kishindo cha Sia kuanguka, kwahiyo alitoka nje kwa haraka kujua ni nani anaanguka ndipo alipokutana Elly akimpiga Erick kwani Erick hakuwa mtu wa kupigana kwahiyo alikuwa amesimama tu, basi mama Angel alienda na kumsukuma Elly kisha akamnasa kibao na kumwambia kwa ukali,
“Unawezaje kupigana na mtu ambaye hapigani na wewe?”
Kisha mama Angel alimuangalia Sia, halafu akamsogelea na kumnasa kibao na kumwambia,
“Chezea vyote na sio watoto wangu”
Mama Angel akamshika mkono Erick na kuingia nae ndani, kwahiyo pale nje alibaki tu Elly na mama yake, ambapo waliangalia kisha Elly akamwambia mama yake,
“Yani mama umeshindwa kabisa kunitetea kwa yule mama?”
“Sasa mwanangu hata mimi mwenyewe nimeshindwa kujitetea maana nilikuwa namshangaa tu yule mwanamke, baada aulize chanzo ni kitu gani anavamia tu watu na kuwachapa makofi, ila ipo siku atajutia jambo hili”
“Utamfanyaje mama?”
“Si unajua huwa mama yako hakuna kitu kinachonishinda, basi subiri tu utaona picha lenyewe litakavyoenda, anamuona huyu Erick kama dhahabu ila atalia kilio mbuzi kachoka”
Kisha Sia akaondoka na mtoto wake muda huo.

Mama Angel nae akiwa ndani alimfokea Erick,
“Na wewe unakuwa kama mzembe jamani, unaachaje mtu akupige namna ile?”
“Mama, mimi huwa sipendi ukorofi na hujanifundisha hivyo”
“Oooh sawa, hata hivyo nimeogopa sana jamani, ungezimia na pale mwanangu je!”
“Jamani mama, inamaana mimi nitakuwa nazimia hata nikiguswa kidogo tu!!”
“Sina maana hiyo mwanangu, haya nipe hiyo vocha”
Erick aliangalia vizuri na kugundua kuwa hiyo vocha ameiangusha nje ya geti lao, akamwambia mama yake,
“Dah! Nadhani pale wakati yule ananitingisha na vocha ilianguka pale, ngoja nikaifate mama”
“Hapana, kaa hapo naenda kuifata mwenyewe”
Mama Angel aliinuka na kutoka, basi alipotoka tu nje ya geti wakati anaangalia ile vocha na kuinama ili aiokote, alishangaa kuna mtu kainama pia na kushika mkono wake, kwahiyo alipoinuka aligongana nae macho kwa macho mtu huyo alikuwa ni Rahim,
“Kheee Rahim!”
“Ndio ni mimi, nipo hapa kipenzi changu. Mwanamke wa roho yangu”
“Kwenda zako huko”
Mama Angel aliinuka sasa, ila Rahim alimwambia,
“Kumbuka mimi ndiye mwanaume wa kwanza kabisa kukupa heshima wewe ya kuwa mama, halafu unapokumbuka mabaya yangu basi jaribu kukumbuka na mazuri yangu. Wanawake wangapi huwa wanapewa mimba na kutelekezwa kabisa yani mwanaume hata hajali kuwa una kiumbe chake, ila mimi wakati umeniambia kuwa una mimba yangu, nilikutumia pesa ya kupanga chumba na kununua kila kitu ndani na bado nilikuwa nakujali kwa kukutumia pesa kila mara, hata ulipojifungua bado nilikuwa nakujali Erica, ila tatizo lako wewe ni kukazana kuwa lazima nikuoe ndio ikawa tatizo kwangu sababu kwa kipindi hiko sikuwa na maamuzi sahihi ila ukiniambia kwasasa Erica nakuoa tu tena bila ya kipingamizi”
“Unajua usitake kuniletea uchizi hapa, jisahaulishe tu mambo yako, ni kweli ulikuwa ukinitumia pesa ila ulisahau jambo moja tu kuwa utu ni bora kuliko kitu. Nimekaa mimi, nimedhalilishwa mimi, nimechekwa mimi, nimeitwa majina yote mabaya sababu tu ya kumbeba Angel, na bado baba wa mtoto nikikwambia kitu unanijibu vibaya, hivi ulikuwa unawaza hata kwa mbali ni uchungu gani niliokuwa naupata kwa yale majibu yako? Naomba Rahim niache kwa amani, niache niishi vyema na familia yangu”
“Na mimi kamwe sitokuacha kwa amani, yani hilo sahau kabisa, tena nikome nakwambia”
“Bado, nitakuja tena”
Rahim alimsogelea mama Angel na kumbusu kwenye paji la uso, lile tukio lilikuwa la haraka kidogo kwahiyo hata mama Angel hakujipanga nalo, ila muda huo huo aliamua tu kuingia ndani halafu Rahim nae alirudi kwenye gari yake, kumbe kwa muda huo Tumaini nae alikuja akija hapo kwa mama Angel ila alipoona vile alijibanza mahali, kwahiyo Rahim aliporudi kwenye gari tu alimfata na kumuuliza,
“Kuna nini kinaendelea kati yako na Erica?”
“Kwani wewe ni nani?”
“Mimi ni wifi yake”
“Oooh ni dada yake Erick, yule ulikuwa bonge kipindi kile unakula kila kitu, ila saivi umekuwa mmama na mwili umekupendeza, sio kipindi kile, binti ila bonge shavu hilo utafikiri…”
Tumaini alimkatisha na kumuuliza,
“Kwani wewe ni nani?”
“Sijui unijui au kiburi tu au umenisahau? Au nimezidi kuwa mtanashati, maana kila siku nazidi kuchanganya macho ya wanawake, usikute na wewe umeanza kuchanganyikiwa na mimi”
“Vipi wewe?”
“Mimi naitwa Rahim, mimi ndio mwanaume wa kwanza kabisa kuwa na Erica, mimi ndio nilimfundisha Erica nini maana ya mapenzi, mimi ndio nilimfanya awe mama kwa umri ule, mimi ndiye niliyemfanya, apate mtoto mzuri hadi kuchukuliwa na makampuni mbalimbali kwa matangazo. Mimi ni mzuri na ninajivunia hilo”
“Mbona unajisifia kama mwanamke?”
“Ukitaka kujua uanaume wangu tafadhari twende chumbani”
“Mjinga wewe”
Tumaini akaondoka zake, na wala hakuingia tena kwa mama Angel, naye Rahim akaondoka zake pia.

Tumaini alivyofika tu nyumbani kwake, alimpigia simu mdogo wake na kumueleza kile alichokikuta kwenye nyumba yake,
“Kiukweli nimeshindwa hata kuingia, usidhani nakuharibia ndoa ila nakwambia ukweli halisi.”
“Nimekuelewa na wala siwezi hisi kuwa unaniharibia ndoa, sababu najua jinsi gani Erica anavyonipenda, hakuna kiumbe yoyote wa kukatisha mbele yake halafu akanisahau mimi”
“Na alivyombusu je?”
“Itakuwa ni bahati mbaya, Tumaini hujaingia kwenye moyo wa Erica wewe. Yule hata umchane chane, basi damu yake itaanguka chini na kuandika Erick”
“Mmmh siwawezi”
“Na hakuna anayetuweza hata mmoja, mimi na Erica tunapendana, kwahiyo hakuna kiumbe yoyote wa kukatisha kwenye penzi letu. Kama kuna mwanamke alinikosa mimi kwa kipindi kile basi asitegemee kunipata kwa kipindi hiki, na kama kuna mwanaume alimkosa Erica kwa kipindi kile asitegemee kumpata kwa kipindi hiki, namuamini sana mke wangu na kumthamini”
“Haya basi yaishe, mbea mimi kukuletea huo ujumbe”
“Hujafanya vibaya kuniambia ila tu nilikuwa nakusahihisha kuwa huyo jamaa hawezi kuharibu penzi langu na Erica sababu sisi tuna nguvu iliyopo ndani ya mioyo yetu”
Tumaini hakuwa na la kuongeza zaidi ya kumuaga tu kaka yake, ila mumewe alikuwepo siku hii basi alimsikia kwenye yale maongezi na kumuuliza vizuri, na yeye alianza kumuelezea kuaznia mwanzo hadi jinsi alivyojibiwa na Erick,
“Kheee huyo Rahim bado tu anamfataga mdogo wangu?”
“Kumbe unamfahamu”
“Namfahamu ndio, ila Erick hajakosea ni kweli kabisa ukimchana Erica basi damu yake itaanguka chini na kuandika Erick. Kwakweli mdogo wangu ni amependa tena kapitiliza, hakuna hata mmoja wa kumbabaisha”
“Mmmh ila wanavutia na mapenzi yao, hivi na wewe unanipenda hivyo kweli mimi!”
“Kwani ushawahi kunifumania?”
“Sijawahi? Ila ndio kusema huna wanawake wa nje?”
“Mwanaume yoyote ambaye hujawahi kumfumania jua kuwa huyo anakupenda sana, kama mwanaume ana wanawake nje ila anamficha mkewe yani anafanya juu chini mkewe asijue basi huyo mwanaume anaupendo wa dhati na mkewe, na hataki mke wake atambue kitu cha namna hiyo. Kwahiyo ukiishi na mwanaume bila kumfumania, acha kumuwazia mawazo potofu maana anakupenda sana kiasi hawezi fanya ujinga mbele yako”
“Kwahiyo wewe una wanawake wengine huko eeeh!”
“Hapana sina maana hiyo ila nilikuwa nakuelekeza tu, wanawake wengine mimi wanini jamani wakati nakupenda wewe mke wangu! Tumetoka mbali Tumaini, acha kunihisia vibaya, jua mumeo nakupenda sana na hakuna wa kukuzidi”
Hapo Tumaini alifurahi sana na kutabasamu kwa furaha aliyokuwa nayo, maana kitu ambacho kilikuwa kinamfanya achukie mapenzi ni ile hali ya kusalitiana.

Mama Angel aliongea na simu kwa muda mrefu sana maana alikuwa akiongea na dada yake Mage, kwahiyo aliongea nae kwa muda mrefu sana, na alipomaliza kuongea alisinzia kwa muda huo.
Alishtuka usiku sana, basi akachukua simu yake na kuona kuwa siku hii hakumtafuta mume wake hewani, ikabidi ampigie simu muda huo, simu iliita sana ikakatika, basi akapiga tena na mumewe akapokea ila akiwa katika hali ya usingizi,
“Mke wangu mbona usiku huu!”
“Aaah nimekukumbuka tu mume wangu, usiku mwema”
Basi mama Angel aliridhika kwa muda huo na kukata ile simu kisha na yeye akalala sasa.
Asubuhi kulivyokucha tu baada ya wakina Erick kwenda shuleni, muda kidogo alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni madam Oliva, alimshangaa kwa kwenda ila alimkaribisha kwanza na kumwambia,
“Baada ya kunipigia mwanangu hadi kuzimia, na kuniletea mgeni wa maajabu, leo umekuja bila aibu?”
“Kwanza naomba unisamehe, sikuwa na lengo la kumchapa Erick azimie, nilimchapa fimbo moja tu hata nashangaa alizimia sijui tatizo ni nini? Na nyie wazazi mna makosa, kwanini msingesema tangu mwanzo kuwa mtoto wenu ni mgonjwa? Yani na nyie pia mna matatizo, ila naomba unisamehe sana”
“Nimekusamehe ila kama mwanangu angepatwa na matatizo zaidi sidhani kama ningesikiliza huo msamaha wako”
“Asante, na pia nisamehe kwa kumleta yule mgeni, sikujua kama mna ugomvi wenu, nilijua ni kawaida tu ndiomana nikamleta. Naomba unisamehe na hilo pia”
“Nimekusamehe, haya sema kilichokuleta”
“Ni hivi, nilimchapa Erick siku ile kwa makosa mawili, moja la kutokumsalimia yule baba ila sikuelewa kumbe mna ugomvi wenu, na la pili kuwa na mahusiano ya kimapenzi shuleni wakati mapenzi shuleni yamekatazwa”
“Unamaana gani? Yani mwanangu ana mwanamke shuleni?”
“Ndio, ana mahusiano na Sarah”
“Mmmh hainiingii akilini hiyo”
“Ndio hivyi, Erick ana mahusiano ya kimapenzi na Sarah, na nilimsema pia siku ile kuwa azingatie masomo bado mdogo mapenzi yatampoteza. Sasa kilichotokea, Sarah kafikisha maneno kwenye uongozi wa shule na mimi nimesimamishwa kazi”
“Sikuelewi, yani usimamishwe kazi kwa maneno ya mwanafunzi! Uache kusimamishwa sababu ya kumpiga Erick ila usimamishwe sababu ya Sarah!”
“Ndio, unajua Sarah ile ni shule ya marehemu baba yake, kwahiyo kamuachia mali nyingi sana Sarah, yani Sarah anajivunia sana, yule mtoto hachapwi wala hafanywi kitu chochote, mama yake mwenyewe anamlea yule mtoto kama Mungu mtu nakwambia”
“Mmmh!!”
“Jinsi unavyomuona Sarah, hawezi kufua hata nguo yake ya ndani ila walimu tukiongea tunaonekana kuwa tunapiga kelele, kwahiyo nimesimamishwa kazi. Kilichonileta hapa, ingawa nimesimamishwa kazi ila bado Erick ni kama mwanangu lazima nimuhurumie, ongea nae mwambie mapenzi na shule ni vitu viwili tofauti yani yeye akazane tu na masomo wala asiangalie mapenzi yatampoteza”
Mama Angel akapumua kidogo na kusema,
“Haya nimekusikia ingawa nimeshangaa sana”
“Ndio hivyo, kuwa makini na mtoto wako. Mfunze yaliyomema bado mdogo sana, ndio kwanza kidato cha pili”
“Nimekusikia mwalimu nakuahidi kuwa nitaongea nae, ila nikiweza pia nitaenda kuongea na uongozi wa pale shuleni, na hata nitaongea na Sarah na wewe utarudi shuleni kama kawaida kwani najua Sarah ni muelewa yani ni mtoto wa kumuelewesha tu”
“Nashukuru kwa hilo”
Leo madam Oliva wala hakuongea mengine zaidi ya hayo, kisha akaaga na kuondoka zake.

Erica alitoka shule kabla ya kaka yake, kwahiyo alimkuta mama yao na kumsalimia pale, ambapo mama yao alimuuliza,
“Jipya la shuleni leo?”
“Mmmh hakuna jipya mama, ila njiani nimemuona mama yake Samia”
“Wewe unamfahamu mama yake Samia?”
“Hapana, ila alisimamisha gari ya shule na Samia akashuka akisema ni mama yake”
“Kwahiyo ni hilo tu leo mwanangu? Niambie kama kuna lingine”
“Mmmh lingine sina uhakika nalo”
“Lipi hilo?”
“Yule mnayemsemaga Samir Samir kuwa anamsumbua dada Angel nahisi ni kaka yake Samia”
“Mmmh!! Samir na Samia wana undugu?”
“Ndio mama, maana hata Samia huwa anamtajataja, halafu tabia za Samia na tabia za huyo Samir kama zinafanana”
“Tabia gani hizo?”
“Mmmh mama jamani, leo unanikaba na maswali hadi nashindwa kujieleza”
“Kheee makubwa, Erica wewe ndio ushindwe kujieleza kweli!! Hapana haiwezekani hiyo kabisa, hebu niambie ukweli”
“Ni hivi mama, huwa nawasikia kuwa Samir anamsumbua dada Angel mara kwa mara, na imetokea kuwa Samia anamsumbua Erick mara kwa mara na leo kanipa….. Aaah mama hakuna kitu”
“Mjinga wewe, yani habari umenianzishia halafu unataka kuikatisha hebu nipe alichokupa”
Erica alitoa barua nyingine aliyopewa na Samia kuwa amletee Erick, kisha mama yake akamtaka akabadili nguo tu kwa muda huo, basi Erica akaondoka zake ila alitaka kujua hitimisho la yeye kuikabidhi ile barua kwa mama yao.

Muda huu Erick alikuwa chumbani kwake, basi mama yake alimfata na kuanza kuongea nae,
“Erick mwanangu ni kitu gani kinaendelea shuleni?”
“Hakuna kitu mama”
“Ni nini kinaendelea kati yako na Sarah?”
“Mmmh hakuna kitu mama”
“Nimepata habari kuwa una mahusiano na Sarah, mwanangu mahusiano na shule ni mbaya sana. Je ni kweli una mahusiano nae?”
“Hapana mama, ila ngoja nikwambie ukweli, ni kwamba Sarah aliniambia kuwa ananipenda sana ila nilimwambia kuwa siwezi kuwa nae”
“Kheee watoto wa siku hizi jamani, mna mambo sana sijapata kufikiria kama mna mambo kiasi hiki. Sikia mwanangu nikwambie jambo, kata hivyo hivyo usijihusishe na mapenzi kabisa, zingatia masomo, wazazi wenu tunahitaji msome na mfike mbali kielimu ila mkiendekeza mapenzi mtaishia njiani. Hivi kesho si Ijumaa!! Naomba mwambie Sarah aje hapa nyumbani, nina maongezi naye halafu nitaongea nanyi wote ili muwe kitu kimoja”
“Sawa mama”
“Ila zingatia, yoyote anayekufata kwa habari za mapenzi usikubali”
Kisha mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake, ila baada ya muda mfupi tu alifatwa na Erica ambaye alimuuliza mama yake,
“Mbona hujamwambia Erick kuhusu barua ya Samia niliyokupa?”
“Una uhakika gani kuwa sijamwambia?”
“Nilikaa pale mlangoni kwake wakati ukiongea nae, nilikuwa nasikiliza”
Ilibidi mama Angel acheke na kusema,
“Dah!! Hivi huo umbea wa hivyo Erica umeutoa wapi jamani kheee yani mtoto mbea sijapata kuona, kwahiyo uliupoona naenda kuongea na Erick basi na wewe ukanyata ili usikilize hayo maongezi, loh! Hebu nenda kalale huko”
Basi Erica aliondoka zake, na muda huo mama Angel alimpigia simu mumewe na kumueleza hayo ya watoto wake,
“Jamani huyu Erick kaanza kuwa kama Erick wewe, kurithisha watoto majina nako ni balaa”
“Kawaje kwani?”
“Anatongozwa na watoto wa kike, ila tofauti ya wewe na yeye ni moja tu. Mwenzio hawakubali”
“Kwani mimi nilikuwa nawakubali?”
“Ndio, tusizungumze hayo maana utachukia bure. Sasa huyu Erica jamani ni mbea yani kama mtoto wa Sia”
Mama Angel alikuwa akiongea huku akicheka sana, basi mumewe akasema,
“Mmmh usimuite mtoto kama mtoto wa Sia, yule Sia sio mzima kwenye akili yule na hafai hata kuwa mama yani hata yule Elly namuhurumia kwakweli”
“Haya mume wangu, ila unarudi lini? Nimekukumbuka mwenzio, sina raha ujue na sijazoea kuishi mbali na wewe, yani nahisi kama kuna kitu kimepungua katika maisha yangu”
“Hata mimi nimekukumbuka sana mke wangu ila nitakaporudi kwa hakika utafurahi sana, kwani nitakuja kivingine wala hatutohangaika tena kufanya kazi muda wote bali tutafanya kwa afya kwa tu”
“Sawa nakusubiri”
“Nisubiri tu, unajua ni jinsi gani nakupenda mke wangu”
Hapo mama Angel alikuwa anahisi amani sana moyoni mwake kila alipoambiwa na mumewe kuwa anapendwa, ni mara kwa mara mumewe alisema hivi ila kwa mama Angel mara zote aliona kama ni kitu cha muhimu sana katika maisha yake.

Asubuhi ya leo mama Angel aliona ajitahidi yeye mwenyewe kwenda kiwandani ilia one ni kitu gani kinachoendelea, basi alijiandaa na kuondoka zake.
Alipofika pale kiwandani kwakweli alishangaa kwani kila mfanyakazi aliendelea na mambo yao tu kwani msimamizi wao alichelewa kufika, mama Angel alichukia na kumfata mlinzi,
“Hivi hapa huwa wanafika muda gani? Yani huyo msimamizi anakuja muda gani?”
“Mara nyingi anafika saa tatu au saa nne”
“Kwahiyo muda huo ndio hawa wafanyakazi wanaanza kufanya majukumu yao?”
“Ndio, sababu hawawezi kufanya chochote bila kuelekezwa cha kufanya”
“Hivi kiwanda kitaendelea kweli kwa mambo kama haya jamani!”
“Unajua mwanzoni wakati Erick anakuja kila siku kidogo ilikuwa afadhali na walikuwa wakifanya kazi kwa bidii ingawa wanachelewa ila wanahakikisha hadi muda Erick anafika basi wanakuwa wametimiza malengo ya Erick. Unajua Erick ana hasira sana, kuna mfanyakazi Fulani alimfukuza kazi hapa bila hata kumsikiliza vizuri, ila asipokuja ndio kama hivi”
“Aaaah jamani, majitu mazima haya ndio yakasimamiwe na Erick kweli!! Ngoja aje huyo kiongozi wao nimpe habari, na kila siku asubuhi nitakuwa nakuja mwenyewe, huu ni ujinga, kiwanda hakiwezi kuendelea kwa ujinga huu”
Mama Angel alienda kukaa pembeni kwanza akimsubiria kiongozi wa hapo afike, na baada ya muda alifika, ila kwakweli hakutegemea ujio wa mama Angel kwahiyo aliogopa kiasi, kisha mama Angel alimpa masharti anayoyataka pale nakumwambia kuwa atakuwa anaenda kila asubuhi kuangalia vile walivyofanya,
“Kumbe kuna umuhimu sana wa kuja Erick mahali hapa! Sasa tumeweka wafanyakazi wa kazi hgani? Mbona kutaka kurudishana nyuma jamani! Naomba ratiba izingatiwe, sitaki hiki kiwe kiwanda cha kwanza na cha mwisho, nataka maendeleo kutoka hapa, msiniletee ujinga mimi.”
Kisha mama Angel alienda nae yule kiongozi ndani ya kiwanda na kukagua vizuri mambo yanavyoendelea pale, alikagua kila kitu na aliporidhika na mahesabu ndio aliondoka muda ule.
Kwakweli alivyoondoka yule kiongozi alipumua kidogo na kumfata mlinzi,
“Wewe lazima kuna kitu umemwambia huyu mama”
“Nimwambie nini mimi? Sina undugu nae, siwezi kumwambia chochote”
“Ila huyu mama mzuri sema anaonekana kuwa na roho mbaya sana, yani hacheki wala nini. Nadhani ndio kamlandisha yule mwanae Erick maana kale katoto kagumu hatari, siku ile laki tatu tu sababu haikuwa na mahesabu ya kueleweka akaondoka nayo, yani katoto kale ni balaa. Ila ngoja tupige kazi”
“Ndio bosi, ni kheri kuendelea na kazi maana ndio zinazotufanya tucheke hizi”
“Usiniite bosi bhana, mabosi wenye viwanda vyao. Niite jina langu tu”
“Sawa Yuda”
“Eeeeh hapo sawa”
Kisha alienda kuendelea na kazi kama kawaida ila kwa siku hiyo aliweza kutambua ukali wa mama Angel.

Siku hii mapema kabisa, Erica na Erick walienda shuleni, wakati Erick yupo shuleni alifatwa na Sarah kama kawaida na yeye alimpa ujumbe wa kuonana na mama yake.
“Jamani, mama mkwe kanikumbuka eeeh!”
Erick alikuwa kimya tu maana hakuwa na cha kumjibu kwa muda huo, halafu Sarah aliendelea kuongea,
“Hivi unajua ni kiasi gani nakupenda Erick?”
“Tuachane na mambo hayo jamani Sarah, kuna vitu vya muhimu vya kujadili na sio mapenzi”
“Ila mimi nakwambia ukweli kuwa nakupenda sana, siku moja nitaenda na wewe kwenye kaburi la baba yangu, najua atafurahi kuona binti yake nimepevuka na kufikia hatua ya kupenda”
Erick aliamua kwenda darasani tu kwani maongezi ya Srah hayakumvutia hata kidogo.
Walipotoka shule, leo kama ambavyo walipanga ni kuwa Sarah alishuka na Erick na moja kwa moja kwenda naye ndani kwao na alimkuta mama yao yupo ndani na alionekana muda sio mrefu katoka kufika mahali hapo, basi mama Angel alimkaribisha na kuanza kuongea nae kama mama, alimfundisha kwa kiasi maswala ya madhara ya mapenzi shuleni na jinsi mwanamke unavyokuwa ukimtongoza mwanaume,
“Ipo hivi binti yangu, mtoto wa kike unapomtongoza mwanaume kwanza kabisa unadharaulika, hakuna mwanaume anayependa kutongozwa na mwanamke. Unaishusha heshima yako, kama mwanaume anakupenda mwache aje akwambie mwenyewe, umejifunzia wapi kumueleza mwanaume mambo kama hayo?”
“Mama, mimi sijakurupuka kufanya hivi ni kutokana na malezi ambayo mama amenipa. Huwa ananiambia kuwa nikimpenda mtu ni bora kuwa muwazi, kumueleza mtu huyo mapema kuwa nampenda ili awe anajua kuliko kuishia kumuonyesha kama nampenda tu, inatakiwa ajue kwani itamfanya yule mtu apate urahisi wa kuwa na mimi kwani ataona ni jinsi gani nimejivika ujasiri wa kumueleza ukweli kuwa nampenda sana”
“Muulize vizuri mama yako alikuwa akikufundisha hayo kwa misingi ipi maana sifikirii kama mama yako alikuwa na hiyo nia ambayo wewe unaisema. Ngoja nikwambie kitu kingine, kuhusu Erick. Kwanza kabisa ile picha ya baba yako kama unakumbuka nilishtuka sana nilipoiangalia, na kama yule ndio baba yako basi wewe na wakina Erick ni ndugu sababu yule ni babu yao”
Sarah alishtuka sana na kusema,
“Hapana, baba yangu alikuwa ni mtu wa nje na hakuwa na ndugu hapa nchini”
“Ngoja nisiongee mengi zaidi, kesho ni Jumamozi naomba niletee mama yako ili niongee nae, Natumai amerudi”
“Ndio, amerudi jana”
“Basi kesho naomba uje nae niongee nae kwani najua nikiongea nae atanielewa zaidi na yeye kukuelekeza itakiwa vizuri zaidi”
“Sawa nitamwambia tu”
“Sawa, ila weka akilini mwako kuwa mtoto wa kike kumtongoza mwanaume hiyo haifai kabisa, unaondoa thamani yako kama mwanamke, yani hutaonekana kabisa, unatakiwa kuwa makini kwa yote uyafanyayo. Sarah wewe ni binti mzuri sana, Mungu atakujaalia na utapata mume mzuri mwenye moyo wa upendo. Mimi nakupenda ndiomana nimekuita na kukueleza haya, nakupenda sana sijui kwanini ila nakupenda na sipendi upotee kabisa, napenda uje kuwa mwanamke bora hapo badae, uwe ni mwanamke wa kuigwa na wengine. Natumaini Sarah unanielewa ninayoyasema”
“Ndio nimekuelewa”
Sarah aliamua kuaga kwani lile swala la kuambiwa kuwa ana undugu na Erick hakulipenda kabisa, na bado akajiapia kuwa hata kama ana undugu na Erick bado hakutaka kuacha kumpenda kama mpenzi wake.
Kisha mama Angel alimtaka Erick kumsindikiza Sarah nyumbani kwao, ila Erica nae alitokezea na kusema kuwa na yeye anaenda ikabidi waende wote wawili kumsindikiza Sarah.
 
SEHEMU YA 332


Walifika nyumbani kwakina Sarah na kukaribishwa vizuri kabisa, mama Sarah alionekana kufurahi sana kwa yeye kumuona Erick na kusema,
“Umekuja tena!! Nimefurahi sana Erick, karibuni nyumbani kwangu”
Walimsalimia pale ila hakutaka kukaa sana na kuamua kuaga muda huo na kuondoka zao.
Basi Sarah alienda na mama yake chumbani na kumuelezea kuhusu kuitwa kwake na mama Angel,
“Kaniambia kuwa anataka kuongea na wewe”
“Mmmh kuhusu nini lakini? Kwani ananifahamu?”
“Hakufahamu ila amesema kuna mambo anahitaji kuongea na wewe kuhusu mimi”
“Mmmh umefanya nini tena huko Sarah mtoto wangu jamani!”
“Sijafanya kitu mama, si unanifahamu vizuri huwa sina ugomvi na mtu yoyote yule”
“Nakuelewa mwanangu, hakuna tatizo. Kesho jioni tutaenda wote”
Sarah alikubaliana na mama yake kuwa wataenda kesho yake jioni.

Erick na Erica wakati wanarudi kwenye gari, Erick alimuuliza,
“Mbona leo umekazana kuwa na wewe unataka kumsindikiza Sarah?”
“Ni hivi, nishasema kuanzia sasa nitaanza kukulinda, nishasema kiwandani tutaenda wote, na ukiwa unaenda mahali basi tutaenda wote hakuna tatizo”
Njiani wakamuona Elly na mama yake, basi Erica akasema,
“Simamisha nimsalimie Elly”
“Kumbe hujui? Elly alitaka kupigana na mimi, Elly ni mkorofi”
“Kheee mbona haonekani, karithi kwa mama yake basi maana hata mama yake ni mkorofi kumbe hadi wakina Samia wanamjua”
“Kheee wewe nawe una habari zote, wanamjua vipi?”
“Nasikia huwa anafatilia familia yao balaa ila mama yao ndio huwa namtimua kwani hataki kufatiliwa nae, nasikia mama yao na wakina Samia hapendi marafiki kabisa. Halafu nimekumbuka jana Samia alinipa barua yako ila mama kaichukua”
“Mmmh mama kajuaje?”
“Aliniuliza na mimi nilimwambia ukweli maana sikuweza kumficha”
“Ila wewe…. Ngoja nisiseme sana”
Basi walirudi moja kwa moja nyumbani kwao na walimkuta mama yao akiendelea na mambo mengine tu.
Usiku ule kila mmoja alilala kwa usalama kabisa, kulivyokucha, mama Angel aliamka na kumtaka Erick ajiandae ili aende nae kiwandani kwa asubuhi ile, basi moja kwa moja walienda kiwandani ila siku hii walikuta wafanyakazi wamefika mapema sana na wameanza kufanya kazi zao mbalimbali, basi mama Angel alimtaka Erick amuelekeze yeye ambacho huwa anafanya, kwani alitaka afahamu ili aanze kusimamia yeye mwenyewe na mwanae awe makini na masomo.

Jioni ya siku hii, Sarah aliongozana na mama yake hadi nyumbani kwa mama Angel kwani alitaka kufahamu kitu ambacho huyo mama alimuitia, ila walifika na kutokumkuta, hata Sarah akashangaa imekuwaje hawajamkuta wakati jana yake alimsisitiza kuwa aende na mama yake.
Kwa kawaida mama Sarah huwa hapendi kupoteza muda sehemu moja, basi muda ule ule ambavyo hawajamkuta muhusika akaamua kumwambia mwanae kuwa waondoke, kwahiyo waliwaaga tu wakina Vaileth, ila wakati wanataka kutoka ndio muda huo huo mama Angel na Erick walikuwa wamerudi, kwakweli mama Sarah alipomuona mama Angel alishangaa na kusema,
“Kumbe ni Erica!!”

Kwa kawaida mama Sarah huwa hapendi kupoteza muda sehemu moja, basi muda ule ule ambavyo hawajamkuta muhusika akaamua kumwambia mwanae kuwa waondoke, kwahiyo waliwaaga tu wakina Vaileth, ila wakati wanataka kutoka ndio muda huo huo mama Angel na Erick walikuwa wamerudi, kwakweli mama Sarah alipomuona mama Angel alishangaa na kusema,
“Kumbe ni Erica!!”
Mama Angel alimshangaa kwa muda kidogo yani alikuwa kama amemsahau, kisha mama Sarah akamwambia mama Angel,
“Tuseme hunikumbuki mimi! Hunikumbuki kuwa tumesoma wote? Unajua wewe hubadiliki”
Mama Angel aliposikia kuwa tumesoma wote akajua lazima litazuka la kuzuka hapo, kwani ana mashaka sana na watu ambao amesoma nao basi akamvuta mkono mama Sarah na kwenda nae pembeni kuzungumza nae, halafu akamuuliza,
“Hebu nikumbushe?”
“Mimi ni Manka, tuseme umenisahau?”
“Oooh ni Manka, umenenepa ndiomana nimekusahau. Kwahiyo wewe ndio mamake Sarah?”
“Ndio ni mimi, Sarah ni binti yangu wa pekee”
“Sawa, ngoja tuongee kidogo”
Mama Angel alisogea na mama Sarah hadi kwenye bustani, kisha alikaa nae kwenye viti vya hapo na kuanza kumuuliza maswali,
“Hebu niambie ukweli, Sarah ni mtoto wa nani?”
Mama Sarah akashtuka sana na kumuuliza,
“Kwanini umeuliza hivyo? Uliwahi kuongea na Johari hivi karibuni?”
“Kuongea nae kuhusu nini? Hakuna chochote nilichoongea na Johari ila nimekuuliza tu”
“Sikia kwanza nikwambie kitu, kwanza kabisa sikujua kama ni wewe ndiye uliolewa na Erick yani sikujua chochote kabisa, ni mpaka nilipokutana na Johari na akanieleza kuwa uliolewa na Erick hata sikuwa najua”
“Imekuwaje? Erick anaingiaje hapa? Kwani Erick ndio baba wa Sarah?”
Mama Sarah akashtuka tena huku akijibu kwa wasiwasi kidogo,
“Hapana sio Erick”
“Basi baba wa Sarah ni nani?”
“Kwanza niambie kwanini unataka kumjua baba wa Sarah?”
“Ni hivi, kipindi Sarah anaumwa nilikuja nyumbani kwako nakukuta akiangalia picha, aliniambia kuwa ni picha ya baba yake mzazi, nikataka kuiona, kwakweli niliona ni mtu ninayemfahamu, ndiomana nimehitaji kuongea na wewe je kweli mzee Jimmy ndio baba wa Sarah?”
“Sasa unataka ukweli gani hapo?”
“Na kwanini umwambie Sarah kuwa baba yake hakuwa na mtoto mwingine zaidi yake na umwambie kuwa baba yake hakuwa na ndugu?”
“Ndio nakiri kumwambia hivyo, ila ni sababu tu sikutaka mtu yoyote kunifatilia. Kwani wewe unamfahamu mzee Jimmy kama nani?”
“Yule ni mkwe wangu, mimi ni mke wa Erick na mzee Jimmy ni baba mzazi wa Erick”
Mama Sarah alionekana kushangaa sana kwani jambo hili yeye hakulifahamu kabisa,
“Kheee inamaana mzee Jimmy na Erick ni ndugu?”
“Ndio, ni mtu na mtoto wake. Ndiomana nikashangaa sana kuona ile picha halafu Erick hajui chochote, mzee Jimmy alikuwa na watoto, mzee Jimmy alikuwa na ndugu ila sijui ni kitu gani ulipanga kuhusu mzee Jimmy na wewe”
Mama Sarah alionekana kuinama kwa muda na kufuta machozi, ambapo mama Angel alimuuliza kwa ukaribu zaidi,
“Kwanini unalia?”
“Sijui hata nikwambie kwanini nalia, ila najuta mimi”
“Unajuta nini?”
“Ngoja nikwambie jambo moja ambalo hulijui wala hujawahi kulihisi”
“Niambie”
“Nakumbuka wakati tunasoma, mimi nilikuwa ni binti niliyesiwa kwa urembo shuleni, ni wengi walinisifia na wanaume wengi walinitaka kimapenzi, ila alipofika Erick pale shuleni nilijikuta nikivutiwa nae sana. Basi niligundua kuwa Erick anakuhitaji wewe sikupenda, ila nikatumia ule udhaifu wako wa ukimya kusema kuwa Erick ananitaka, na kwa msaada wa Johari hakika tuliweza kukusambaratisha wewe na Erick kipindi tupo shuleni. Nakiri wazi baada ya kumaliza shule pale, niliwahi kukutana na Erick na kuanza mahusiano nae, ila siku zote aliniambia wazi kuwa anakupenda sana sema niliamini ipo siku angenipenda na mimi kwani niliamini kuwa mimi ni mweupe na mzuri kushinda wewe, ila haikuwa hivyo, nilibeba mimba ya kwanza, Erick alikazana hadi ile mimba nikaitoa, nilibeba mimba ya pili nayo ikawa vilevile. Ikafikia kipindi Erick akanikataa kabisa akidai kuwa kampata mpenzi wa moyo wake ila bado sikukata tamaa, na ndio kuna kipindi wakati namfatilia Erick nikakutana na huyu mzee Jimmy, hata sikujua kuwa ni baba wa Erick ila nilipanga nae vitu vingi sana”
Mama Sarah akainama tena na kulia, basi mama Angel akasogea karibu yake na kumbembeleza huku akimuuliza kwa makini,
“Ndio ukazaa na mzee Jimmy?”
“Sijui, yani sijui ila kwa kifupi tu nilitembea na mzee Jimmy na nilitembea na Erick ila usiniulize kuhusu Sarah ni mtoto wa nani”
Mama Angel akapumua kiasi, akamuangalia mama Sarah bila ya kummaliza, yani alikaa kimya kidogo bila ya kujua cha kuongea kisha akasema,
“Je mzee Jimmy alitambua kuwa ulishawahi kuwa na mahusiano na Erick?”
“Ndio alijua, ila kuna kitu kilitokea hapo katikati kabla ya kuzaliwa Sarah! Hapana jamani mzee Jimmy hawezi kuwa baba wa Erick”
Mama Sarah aliinama huku akilia, basi mama Angel aliendelea kumbembeleza ili amweleze ukweli,
“Kulia hakutakusaidia bali ukweli ndio utakuweka huru, niambie ukweli. Mimi sitachukia, hata kama kuna kitu kilitokea kati yako na Erick bado siwezi kuchukia kwani ni mambo ya zamani”
“Erica, sipo sawa. Siku nikiwa sawa nitakuja kuongea nawe vizuri sana, yani sikufikiria haya, nitakutafuta”
Mama Sarah aliinuka na kwenda kumfata mwanae kisha akaondoka nae, yani mama Angel alibaki akimshangaa tu na kuingia zake ndani.

Mama Angel alienda chumbani kwake huku akijiuliza maswali kadhaa bila ya majibu ya aina yoyote,
“Huyu Manka anamaanisha nini? Mbona Erick hajawahi kutaja hata mara moja kuwa alikuwa na mahusiano na Manka! Nadhani alichofanyiwa Manka na mzee jimmy ni kile alichokuwa akitaka kunifanyia mimi, yani alitaka kutembea na mimi wakati nipo na Erick, yule mzee ana wazimu sana, ingawa marehemu huwa hasemwi vibaya ila mzee Jimmy hapana jamani, kwahiyo Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy! Nina uhakika hawezi kuwa wa Erick, ila mmmh usikute Manka nae kazaa huko ila kambebesha mzee Jimmy sababu aligundua kuwa ana pesa, ila haya mambo jamani kama sielewi elewi hivi loh!”
Mama Angel aliamua kwenda kuoga tu kwa muda huo, ila alipotoka alikuta simu yake inaita na kuichukua ili kuongea nayo, alikuta ni mumewe anapiga, basi akaona pia ni muda wa kumuuliza mumewe,
“Aaaah mke wangu mbona nimepiga sana?”
“Nilikuwa kuoga, ngoja nikuulize kitu. Kumbe uliwahi kuwa na mahusiano na Manka?”
“Aaaah nani kakwambia hayo maneno?”
“Hii dunia ni ndogo sana mume wangu, hakuna kitu unaweza fanya kisijulikane”
“Naomba unisikilize mke wangu, mpenzi wangu, kipenzi cha roho yangu naomba unisikilize kwa makini. Mambo yote mimi na wewe tutayazungumza vizuri nikirudi, naomba na namuomba Mungu asije kuibuka shetani wa kukuchanganya hiyo akili yako. Nakuomba mke wangu tena nakuomba sana, kwasasa usisikilize maneno ya mtu yoyote yule, subiri nirudi halafu tutaongea kwa kina na tutajua cha kufanya ila naomba neno lolote la mtu lisiingie kwenye akili yako”
“Jamani, yote hayo yanatoka wapi? Mimi nimekuuliza tu”
“Kwani mke wangu sikujui vizuri wewe!! Nakujua vizuri sana, kitu kidogo kama hiki kinaweza kuanza kukuliza mke wangu, naomba usisikilize maneno ya mtu yoyote, mimi ndiye mwenye kauli na ndio inafaa kunisikiliza. Natumaini umenielewa mke wangu, tafadhari usisikilize chochote”
Kisha baba Angel akambadilishia mkewe mada, ambapo waliongea hadi alipokata simu, kwakweli mama Angel alijiuliza, kwanini mumewe kawahi kusema kuwa asisikilize ya watu,
“Mmmh au kuna ukweli? Ila ngoja nisijiumize moyo mie, nimsubiri tu mwenyewe akirudi atanieleza vizuri”
Mama Angel nae kwa muda huo aliamua kulala tu.

Kulipokucha, wakina Erick walijiandaa na kwenda Ibadani ila siku hii walienda Erick na Erica tu maana mama yao alibaki nyumbani hata Vaileth nae alibaki nyumbani ila Vaileth akamwambia mama Angel,
“Mama, ni wiki ya tatu hii hujaenda Ibadani!”
“Mmmh halafu kweli eeeh!”
“Ndio ni kweli mama, najua huwa unapenda sana Ibada hata sijui nini kimekupata”
“Mmmh ngoja niende basi, ila mimi jamani mtoto ananipa uvivu sana”
“Mimi nipo nyumbani mama, unaweza kuniachia tu”
“Na wewe hutaki kwenda Ibadani?”
“Mimi nitaenda wiki ijayo mama”
Mama Angel hakujiuliza sana zaidi zaidi alienda kujiandaa na kuondoka zake kwenda Ibadani, baada ya muda mfupi tu pale nyumbani alifika Junior, kumbe Vaileth alikuwa akimbembeleza mama Angel aende Ibadani ili yeye apate muda mzuri wa kuwa na Junior, basi Junior akaanza nae,
“Unajua nilivyopokea simu yako usiku nikajua ni wazi umenimiss sana, hadi kutaka nije?”
“Yani sijui nisemeje, kila muda toka jana nakuwaza tu. Nimejitahidi kujizuia wapi jamani! Nakuhitaji Junior, yani leo najikuta nakuhitaji sana”
Basi moja kwa moja Junior na Vaileth walienda chumbani kufanya mambo yao, na walikaa huko hadi ule muda walipoona ni karibia na walioenda kwenye Ibada wanarudi.
“Dah! Ila Vai natamani kama leo ningelala hapahapa ila siwezi sababu sitaki mama mdogo agundue chochote kati yetu”
“Hata mimi sitaki agundue ila nimeridhika sasa, kwakweli nilikuwa na hali mbaya sana, nilitamani uje jana ila Erica cha umbea ndio tulikuwa nae hapa nyumbani, nikaona yule atasema tu. Anaweza asiseme yote ila la wewe kuja akasema tu”
Basi Junior akajiandaa na kula kabisa kisha kuondoka zake kurudi shuleni kwao.

Erick na Erica wakiwa wanarudi huku wameambatana na mama yao, na dereva muda huo alikuwa ni Erick, basi njiani walimuona Derrick akiwa amezingirwa na watu halafu kama kuna mabishano vile, basi Erica akamwambia mama yao,
“Mama, sio anko Derrick yule?”
Mama Angel alimuangalia vizuri na kujithibitisha kuwa ni yeye,
“Ndio ni yeye, sijui kakumbwa na nini?”
“Itakuwa watu wanaomdai wale”
“Mmmmh!!”
“Kwanini tusiende kumsaidia?”
Erick akasema,
“Kheee Erica hukumbuki kama ndio huyu alifanya tutukanwe sana pale kwenye kituo cha mafuta sababu alikomba hela zote!”
Mama Angel nae akasema,
“Jamani eeeh ingawa tumetoka kusali ila kwa Derrick hapana jamani, yani pale hata haijulikani ni kweli au ndio njia ya utapeli. Huyu mjomba wenu, sikuwaambia sijui, alinikuta getini siku hiyo na kuniomba shilingi mia ili akwangulie vocha, niliona jambo la kawaida tu, ila kufumba na kufumbua hela zote nilizochukua zilikuwa zimeisha. Erick naona umepunguza mwendo, hebu endesha turudi nyumbani, hivi Derrick mnamfahamu vizuri au mnamsikia tu.”
Erick aliongeza mwendo na moja kwa moja kwenda nyumbani tu, na walimkuta Vaileth ndio kwanza kaanza kupika chakula alichoambiwa aandae, yani yeye alipika chakula cha upesi cha kula Junior tu, halafu kile alichoambiwa aandae muda huo ndio alikuwa anakiandaa, basi mama Angel alimkuta ndio anaandaa,
“Kheee wewe Vaileth, muda wote ulikuwa unafanya nini?”
“Mtoto mama, leo Ester kasumbua kweli”
“Nimekuelewa, haya Erica kamsaidie basi”
Vaileth alipumua kwani alijua Erica akienda kumsaidia ndio atapumzika kabisa ukizingatia Erica alipenda sana kupika.
Baada ya muda chakula kilikuwa tayari na walikaa kwaajili ya kula huku wakiongea mambo mbalimbali na ule utamu wa kile chakula.
“Oooh mwanangu Erica, kila siku unazidi kunifurahisha juu ya upishi wako, hakika wewe ni mwanamke kamili”
Basi Vaileth akaongea leo,
“Ni kweli Erica yupo vizuri sana, ila unaweza kushangaa anaolewa halafu mumewe anaenda kuhangaika na wanawake wengine wakati mkewe wanajua kupika hivi”
Mama Angel alimuuliza Vaileth,
“Unamaana gani Vai?”
Maana yeye alihisi anasemwa yeye na mume wake, basi Vaileth aliamua kumuomba msamaha tu.

Jioni ya siku hiyo wakati mama Angel katulia zake, alipokea simu kutoka kwa dada yake Mage, basi dada yake alianza kumwambia,
“Ni hivi nasikia Derrick kapigwa na kuumizwa vibaya sana, kwahiyo yupo hospitali kwasasa”
“Kheee, mambo hayo yametokea wapi?”
Mage alimtajia na kumfanya mama Angel kushangaa zaidi kwani kumbe pale walipomuona Derrick kazingirwa ndio hapo ambapo alikuwa anapigwa, kwahiyo alishangaa sana, basi alimuuliza tu dada yake mahali ambapo Derrick amelazwa basi maana ile ilikuwa ni habari mbaya kidogo ukiacha yale matendo ya Derrick ya siku zote.
Muda huu mama Angel alimua tu kulala kwani hakutaka kichwa chake kuendelea kufikiria mambo kama hayo ya kumkosesha usingizi tu.
Kulipokucha tu, mama Angel alijiandaa na kwenda hospitali kwanza kumuona Derrick kwani hata akikataa bado ni ndugu yake wa damu.
Alifika hospitali, alimkuta pale mama mzazi wa Derrick ambaye alifurahi kumuona mama Angel,
“Siamini Erica umekuja kumuona kaka yako!”
“Ndio nimekuja mama, yani huyu ni kaka yangu haijalishi ni kipi kimewahi kupita kati yetu ila bado ni kaka yangu”
“Nafurahi kuona ulimsamehe, ila ana hali mbaya sana”
Basi mama Angel alisogea kumuangalia na kweli Derrick alikuwa na hali mbaya sana, yani alionekana kupigwa sana, basi alikaa pale na mama Derrick huku wakiongea,
“Ila Derrick atapona tu”
“Natumaini atapona, jana nilikuwepo hapa na yule dada yenu mkubwa Mage. Kwakweli huyu amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu, toka Derrick akiwa mdogo hadi leo, mshikilieni sana huyu dada yenu. Ameondoka usiku sana jana, tulikubaliana leo ataleta chakula cha mchana”
“Oooh sawa, basi na mimi nitajitahidi nije tena jioni ule muda wa kuangalia wagonjwa”
Basi wakaongea pale, na muda wa kuangalia wagonjwa uliisha kwahiyo walitoka nje ambapo mama Derrick hakutaka hata kuondoka zaidi ya kumsindikiza kidogo tu mama Angel,
“Basi jioni mama nitakuja kumuona”
“Sawa hakuna tatizo, Mungu amsaidie mwanangu apone jamani”
“Atapona tu, Mungu ni mwaminifu”
Kisha mama Angel alipanda kwenye gari akielekea kiwandani kwani ndio alikuwa na lengo hilo kwanza kwa muda huo, ingawa mumewe hakujua kama mkewe kaanza ratiba za kwenda kufatilia kiwanda ila mama Angel aliamua kufanya hivi kwaajili ya usalama wa mali zao na kiwanda chao, alijua angemwambia mumewe asingekubali ukizingatia mtoto wao bado ni mdogo.

Moja kwa moja mama Angel alienda kiwandani na kukuta walifika na kuanza kufanya kazi, kwahiyo ule msisitizo wa siku ile inaonyesha uliwafanya sasa kuzingatia muda wa kwenda kazini na kufanya kazi kwa ufasaha zaidi, basi alimuita yule kiongozi wa pale na kuongea nae,
“Yuda, kama kuna kitu chochote kinatakiwa au kuna mapungufu yoyote tafadhari kwasasa muwe mnaniambia mimi”
“Sawa mama”
“Ile Jumamosi nilifanya mahesabu na Erick, na alinielekeza mambo mbalimbali. Sasa nahitaji kufanya mahesabu na wewe pia, usinione hivi ni mwanamke ila mahesabu kichwani kwangu yapi vizuri sana”
Mama Angel alikuwa akimwambia hivi ili kama kumpa tahadhari kwanza kuwa mahesabu anatakayomfanyia yawe halisia maana hata yeye anaelewa mahesabu yalivyo, basi Yuda alienda na mama Angel ofisini na kuanza kuonyeshana na kumuelekeza mahesabu, alimfanyia mahesabu yote kisha mama Angel alimuuliza,
“Kuna laki mbili hapa imepelea na kuna laki tatu inazunguka tu, hizi hela ni vipi?”
“Aaaah mama, hiyo laki tatu ndio ile ambayo Erick aliondoka nayo siku ile”
“Haya, na hii laki mbili?”
“Aaaah hii aaah hebu subiri kidogo mama”
Yuda aliondoka na kwenda kuongea na baadhi ya wafanyakazi, kwahiyo mama Angel alikaa pale akisubiri majibu.
Basi Yuda aliita pale wafanyakazi kama watatu wa pale kiwandani na kuanza kuongea nao,
“Jamani huyu mama ni hatari, hafai kabisa bora hata bosi Erick arudi, huyu mama ni nuksi kushinda hata mtoto wake. Unajua kagundua kuhusu ile laki mbili!! Huwezi amini kaanza na mimi mahesabu ya tangia tumeanza kiwanda”
“Duh!! Ndiomana mmetumia muda mrefu sana?”
“Ndio, hata cha mchana sijala sababu ya kuelekezana nae jamani, yani mama anauliza hadi mia imeenda wapi, haka kamama sijui kabila gani jamani! Mtu ana hela lakini hela ndogo ndogo anataka kuzichunguza hadi basi. Tujipange sasa, hiyo laki mbili tuseme nini?”
“Halafu tutaipata wapi tena?”
“Mshahara ukitoka mwisho wa mwezi huu, tuchangishane tuilipe hiyo hela ya watu ila saivi niambieni cha kusema ili iwe rahisi kumtuliza”
“Sikia Yuda, mwambie kuwa kuna sehemu tuliagiza mzigo ila wamezingua na wamesema wataturudishia hela. Mdanganye kuwa tulisikia wanauza kwa bei nzuri ndiomana tukaagiza”
“Mmmh akiniuliza wapi itakuwaje?”
“Mmmh tafuta maneno na wewe, weka hata uongo hapo. Mwambie tushaandikishiana mwisho wa mwezi huu hela hiyo inalipwa”
“Sijui kama atanielewa jamani dah! Mama ni mtata huyu hatari”
Basi Yuda akaenda kuongea nae kama alivyokubaliana na wenzie,
“Haya hayo maandishi kuwa mnalipana mwisho wa mwezi huu yakowapi?”
“Oooh nimesahau nyumbani mama ila kesho nitakuja nayo”
Mama Angel alisikitika kidogo, kisha alimsisitiza kuwa kesho yake angehitaji kuyaona hayo maandishi, kisha mama Angel alizunguka kiwandani pale na alipomaliza aliondoka zake na kupata wazo kuwa aende kwanza kutembelea na lile duka lao maana hakujua chochote kinachoendelea ukizingatia Erick aliongea nae juu juu tu.
Basi alienda katika lile duka na kumkuta Rama, ambapo naye alimuuliza mahesabu ya pale kisha Rama alianza kumuonyesha na kumuelekeza ilivyo, mama Angel kuja kushtukia ni usiku ushaingia, hakwenda hospitali wala nini na alikuwa amechoka sana, hata kula chakula alikuwa hajala, basi kwa muda huo moja kwa moja alirudi nyumbani kwake tu.
 
Back
Top Bottom