Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 333

Kwakweli siku hii mama Angel alichoka sana, hakushinda na mwanae, alishinda kwenye biashara tu, basi alienda kuoga na kula chakula, kisha muda huo Erick alienda kuongea na mama yao,
“Mama, ulienda kiwandani leo?”
“Ndio nilienda mwanangu, nimechokaje jamani maana nilikuwa nafanya mahesabu na yule Yuda”
“Uligundua upotevu wa laki mbili?”
“Kheee kumbe na wewe ulijua? Mbona hukusema sasa?”
“Sikusema ndio ila niligundua muda tu, tatizo wale huwa wananiona mimi mtoto sana ndiomana sikuwauliza”
“Ila mwanangu unatakiwa ujiamini maana ile ni mali ya baba yenu, mkishindwa kuisimamia ni nani ambaye angeisimamia?”
“Ndiomaana zile laki tatu niliamua kuondoka nazo mama”
“Nimekuelewa mwanangu, ila unatakiwa kutetea mali ya baba yako kwa nguvu zako zote, watapoteza laki mbili, kesho milioni, kesho kutwa mtaji mzima na kiwanda kitafungwa, inatakiwa kuwa makini sana”
“Sawa mama”
Basi mama Angel alifurahi kwa kuona kuwa mwanae ana akili sana, muda huu aliinuka na kwenda chumbani huko aliamua kumpigia simu Tumaini ili kumpa taarifa kuhusu kuumwa kwa Derrick,
“Jamani, nini kimempata tena?”
“Nasikia kapigwa sana, kuna watu kakutana nao wamempiga sana”
“Au aliwafanyia kama alivyonifanyia mimi?”
“Mmmh sijui ila kapigwa sana na kwasasa yupo hoi hospitali”
“Dah! Itabidi kesho nijitahidi niende kumuona”
“Hata mimi kesho nitaenda tena, ila ndio hivyo Derrick hana hali nzuri kabisa”
Tumaini alishukuru kwa taarifa, na kwa muda huo mama Angel aliamua tu kulala kwani alikuwa amechoka kwa kiasi Fulani.
Kulipokucha tu, mama Angel alipokea simu kutoka kwa dada yake Mage,
“Ila Erica una tabia mbaya wewe, jana jioni umeahidi kwenda kumuona mgonjwa ila hujaenda”
“Ni majukumu dada yalinibana”
“Basi jitahidi leo, na jitahidi umuandalie mgonjwa chakula atakachokula usiku, muandalie tu mtori au chakula chochote kilaini”
“Sawa dada nimekuelewa”
Mama Angel alikata ile simu, ila kiukweli leo alikuwa amechoka na alitaka kutumia muda kidogo kuwa na mtoto wake kwahiyo aliona ni vyema asienda kiwandani kwa siku hii, anajua tu kule sababu hawajui lazima wajishughulishe kwani watahisi muda wowote ule ataenda.
Basi akaona ni vyema kwenda kutafuta vya kupika kwaajili ya kumpelekea mgonjwa jioni hospitali.
Kwenye mida ya saa tatu asubuhi, mama Angel aliondoka nyumbani kwake na kwenda sokoni, alipomaliza tu kununua mahitaji yake akakutana na Sia,
“Kheee kumbe na wewe huwa unakuja sokoni!”
“Jamani, kwani mimi nina nini cha kufanya nisije sokoni?”
“Aaah nimekuuliza tu, vipi mume amesharudi?”
“Bado”
“Huna wasiwasi? Unaibiwa huko, shauri yako nakwambia, wanaume wenyewe hata hawaaminiki hawa haswaa kwa mwanaume kama Erick unamuamini vipi? Yani kama hujaletewa binti mwenye mimba nyumbani kwako sijui”
“Nitolee balaa mie”
Mama Angel aliondoka zake na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake.

Muda huu Tumaini alikuwa anatoka nyumbani kwake, ila alifika mgeni pale nyumbani na mgeni huyo alikuwa ni mama Sarah,
“Kheee mama Sarah, karibu ila mimi nilikuwa natoka”
“Jamani, nilikuwa nina maongezi na wewe. Unaenda wapi kwani?”
“Mmmh kuna kijana nilisoma nae, sasa nasikia kapigwa sana na amelazwa hospitali, ndio naenda kumuona, yani nasikia yupo kwenye hali mbaya sana”
“Kheee, basi twende wote”
“Hakuna tatizo”
Basi Tumaini aliondoka na mama Sarah na moja kwa moja walienda hospitali huko, kisha walienda kwenye wodi aliyolazwa Derrick, hadi pale kitandani ilikuwa ni wodi ya mgonjwa mmoja mmoja, kwahiyo kwa muda huo alikuwepo Derrick na mama yake ambaye naye alifika kumuona mwanae, basi wakafika na kumpa pole ila mama Sarah alishtuka kidogo na kuuliza,
“Jamani huyu sio Derrick huyu!!”
“Ndio mwenyewe, kumbe unamfahamu?”
Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,
“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”
“Ndio, ni kaka yangu wa damu”

Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,
“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”
“Ndio, ni kaka yangu wa damu”
Mara mama Sarah akaonekana kama mtu aliye na kizunguzungu na kutaka kama kuanguka ni Tumaini ndio alimdaka kwa haraka.
Wote walimshangaa kuwa ana matatizo gani, mama Angel alimshika mkono na kutoka naye nje akamuuliza,
“Tatizo nini Manka?”
Mama Sarah alipumua kisha akasema,
“Acha tu kama ilivyo, utamwambia mama Leah nimeondoka. Kwaheri”
Kisha mama Sarah aliondoka zake, kwakweli mama Angel alimshangaa sana na kurudi wodini ambapo Tumaini alimuuliza vizuri,
“Kwani imekuwaje?”
“hata sijui, kaniaga tu na kuondoka”
Mama Derrick akasema kuwa,
“Au na yeye katapeliwa na mwanangu jamani, yani huyu Derrick dah!!”
“Usiwaze hayo mama, kwasasa tusifikirie utapeli wa Derrick ila tufikirie namna ya kupona kwa Derrick.”
Waliongea kidogo pale kisha waliaga ambapo walipotoka nje, Tumaini alimuuliza mama Angel,
“Inamaana Derrick ni tapeli!! Inamaana siku ile alinitapeli eeeh! Ndiomana nilihisi hivyo”
“Ni kweli ni tapeli ila nadhani anatumia dawa maana sio hali ya kawaida, utashangaa anakuazima tu hela ndogo na ukimpatia utakuta amekomba hela zote za kwenye mkoba wako”
“Aaaah kumbe, halafu kitu kingine hebu tuongee kikubwa, yule shoga yule yani mama Sarah nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa anafahamiana na wewe, sema namba yake ndio akaichukua Derrick. Ila leo nimeshangaa sijui mlishaonana? Halafu kuna nini kinaendelea kati yake na Derrick?”
“Mmmh hata sijui”
“Hajakwambia chochote kwani ulivyotoka nae nje?”
“Si nilikwambia pale, hakuna alichoniambia zaidi ya kuniaga tu”
“Oooh nilijua unanificha sababu ya mama yake Derrick pale, au Derrick ndio baba mzazi wa Sarah?”
“Mmmh! Kwani unamfahamu vizuri yule mwanamke?”
“Namfahamu kiasi tu sio kivile, ila huwa haongei habari za kuwa na mume wala baba yake Sarah, ndiomana nimehisi hivi, labda hakutegemea kukutana nae, hebu fatilia usikute Sarah ni shangazi yako!!”
Halafu Tumaini akaagana na mama Angel ambapo muda huu mama Angel moja kwa moja aliondoka na kurudi nyumbani kwake, na yeye alikuwa akijiuliza tu bila ya kupata jibu.

Mama Angel aliwakuta wanae muda huu wanakula, basi na yeye alienda kujimwagia na kujumuika nao, kisha akawaambia hali ya mgonjwa,
“Jamani wanangu sikuwaambia ni hivi, mjomba wenu Derrick kalazwa, hospitali kumbe siku ile tulipomuona akapatwa majanga pale, nasikia walimpiga sana. Nimetoka kumuona leo hospitali anaendelea vizuri”
“Oooh masikini jamani, ndiomana nilikuwa nasema tukamsaidie ila wewe mama na Erick mlikataa na kusema kuwa tusimsaidie atatutapeli, niliona yale mazingira sio rafiki kwake. Ila bora anaendelea vizuri, Mungu amsaidie apone”
“Mmmh leo Erica naona una huruma sana”
“Ndio mama, yule ni mjomba wetu, lazima niwe na huruma naye”
Muda huu Erick hakuongea jambo lolote lile, walimaliza kula na kila mmoja alienda chumbani kwake, ila Erica moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Mbona hujasema chochote kuhusu mjomba kulazwa”
“Sasa ulitaka niseme nini jamani!”
“Hata utoe pole kwa mama , kwani yule ni kaka yake mama”
“Ila katutapeli laki tatu”
“Kumbuka kuna watu kawatapeli hela nyingi kuliko hizo, ila kapatwa na matatizo unatakiwa kuwa na huruma naye”
“Mimi sina huruma naye labda mpaka atakapoacha utapeli wake”
“Mmmh wewe nawe, halafu ngoja nikuulize, hivi siku ile alivyokuja Sarah na mama yake ulimuelewa mama yake Sarah na mama?”
“Sikuwaelewa ila inaonyesha kuwa ni watu wanaofahamiana ndiomana mama anasema kuwa Sarah ni ndugu yetu”
“Ila habari ya Sarah kuwa ndugu yetu nimeipenda sana”
“Kwanini?”
“Sababu ataacha kukusumbua wewe, toka lini ndugu wakawa wapenzi? Hakuna mila za kihivyo, mimi sitaki Sarah awe mpenzi wako, kwahiyo kama ni ndugu yetu ni afadhali sana yani”
Erick alikaa kimya tu, kisha Erica alimuuliza,
“Kwani hujapenda kwa Sarah kuwa ndugu yetu?”
“Vyote kwangu sawa tu, awe ni ndugu yetu, au asiwe ndugu yetu ila bado mimi siwezi kuwa na mahusiano naye”
“Kwahiyo utakuwa na mahusiano na nani? Au utamkubali Samia?”
“Hakuna, kwani umesahau kiapo chetu Erica hadi unaniuliza maswali kama hayo? Leo nimechoka halafu nina usingizi sana, muda sio mrefu nalala”
Erica ilibidi amuage kaka yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kulala.

Mama Angel alijikuta akiwaza kuhusu mama Sarah, alijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu,
“Kwanini ashtuke vile na kutaka kuzimia? Je Derrick ni nani katika maisha yake au alikuwa na mahusiano na Derrick? Je Sarah ni mtoto wa nani? Wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick? Ila hawezi kuwa wa Erick bhana, hilo nakataa maana angeniambia mapema tu. Ila ni wa nani? Au ndio mtoto ambaye Derrick huwa anamsema? Sielewi jamani, kuna nini kati ya Manka na Derrick, au kipindi anampenda sana Erick akakutana na Derrick akamdanganya kama alivyonidanganya mimi? Mmmmh!!”
Mama Angel aliwaza sana bila hata ya jibu lolote na kuamua kulala, ila alishtuliwa na simu kutoka kwa mume wake na kuamua kupokea ile simu,
“Kumbe Derrick kalazwa? Ndio Tumaini kanipigia simu kuniambia leo, mke wangu umeshindwa kuniambia kweli?”
“Nisamehe mume wangu jamani, sijui hata nimeghafilika vipi ila ndio hivyo kalazwa”
“Una mawazo gani Erica? Sio hali ya kawaida, kwanza jana kutwa nzima hatujawasiliana na leo nisingekutafuta basi inamaana ingepita bila ya sisi kuwasiliana, tatizo ni nini mke wangu?”
“Hakuna tatizo”
“Nimekwambia kuwa habari za wakina Manka, sijui wakina nani zisikupe presha mke wangu, yote nikirudi tutazungumza kwakina, nakuomba usiwe na mawazo kwasababu hiyo”
“Sina mawazo yoyote hata usijali kuhusu mimi mume wangu”
Basi wakaongea mengi kwa usiku ule, kisha kuagana na mama Angel kuamua kulala sasa kwa uzuri zaidi.

Leo Erick alivyoenda shuleni tu alifatwa na Sarah ambaye alianza kuongea nae,
“Erick, mbona unaonekana kunikwepa sana?”
“Sikukwepi, ila Sarah hivi unajua kama sisi ni ndugu?”
“Hilo nishalikataa kabisa, siwezi kuwa na undugu na wewe Erick, ninachojua ni kimoja tu kuwa nakupenda sana”
“Duh!”
Muda wa kipindi ulianza kwahiyo ikabidi Sarah aende darasani, kwahiyo Erick alibaki huku akishangaa tu maana hakumuelewa Sarah kwakweli.
Basi waliendelea na masomo kama kawaida, ila siku hiyo mchana Erick alifatwa darasani kuwa anaitwa halafu alitoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa walimu na kukuta ni Sia yuko pale ambapo Sia aliwaomba walimu nafasi kidogo aweze kuzungumza na Erick maana alijitambulisha yeye kama mama mdogo wa Erick, kwanza kabisa Erick aliulizwa,
“Je unamfahamu huyu? Ni mamako mdogo?”
Erick aliitikia tu maana angekataa basi siku hii angemfanya Sia aumbuke sana, basi akatoka nae nje na kwenda kuzungumza nae,
“Kwanza kabisa asante Erick, nilijua utanikana”
“Hapana, nazijua akili zako ndiomana nimekubali, ushindwi kuangua kilio ofisini”
Leo Sia alicheka kiasi na kumwambia Erick,
“Kilichonileta hapa ni kitu kimoja, nimeona bora nije shule nikwambie hili, ni hivi nasikia kuna mwanaume anaitwa Juma anapenda sana kukufatilia. Tafadhari Erick kaa mbali na mtu huyu maana si mtu mzuri kwako”
“Kivipi?”
“Ipo siku nitakaa na wewe na kuongea nawe vizuri zaidi ila yule mtu si mtu mzuri kwako”
“Kwahiyo kwasasa hujaja na hoja kusema kuwa wewe ni mama yangu?”
“Siku zote uongo hujitenga na ukweli, na kitu kama ni ukweli basis i kulazimisha maana kuna kipindi kitajidhihirisha chenyewe. Kuna upendo ambao watu wanaita ni upendo wa asili, je huna upendo huo juu yangu? Kama unao basi mimi ni mama yako, ila kama huna huo upendo juu yangu basi mimi si mama yako, ila hata kama mimi si mama yako bado ninajukumu la kukulinda na kukutunza, nakuomba uwe mbali kabisa na Juma. Sikujua mapema kuwa anakufatilia ila sasa imejua”
“Umejuaje?”
“Yule Juma ana mke wake, na yule mke wake ni rafiki yangu mkubwa na ni rafiki wa mama yako pia. Nimejikuta nikimpenda na kuongea nae mambo mengi sana, kwahiyo kuwa makini sana na Juma, jiepushe nae na ikiwezekana ukimuona mkimbie kabisa. Yangu ni hayo tu, sina mengine wala sina la ziada, kwaheri”
Sia alienda ofisini na kuwashukuru walimu kwa kumruhusu kuongea na Erick halafu aliondoka zake, kwakweli Erick alikuwa akishangaa tu kwanza alishangaa jinsi huyu Sia alivyoongea kiustaarabu siku ya leo, basi alikuwa akienda darasani huku akisema,
“Ingawa kaongea na mimi kiustaarabu ila hiki kimama sikipendi jamani, yani sikipendi kabisa”
Akaenda zake darasani na kuendelea na masomo yake kama kawaida.

Mama Angel akiwa kiwandani leo, bado alitaka maelezo ya ile laki mbili, basi Yuda aliileta ile laki mbili na kumkabidhi huku akisema kuwa yule mtu amemlipa, haikuwa kweli ila Yuda alikopa ile hela mahali ili aweze kumlipa huyu mama na kuepuka lawama,
“Oooh kumbe wameleta, basin i vizuri kumbe ni waaminifu”
“Halafu Erick mtoto atakuja lini tena kiwandani?”
“Atakuja tu ila mwanangu nimeona bora akazanie masomo kwanza kwani ndio ya muhimu kuliko vitu vyote”
“Unaonekana unapenda shule eeeh!”
“Ndio napenda sana, napenda watoto wangu wawe wasomi wa kimataifa”
Waliendelea kufanya kazi huku mama Angel akipita kukagua kagua eneo lake, muda kidogo wakati anajiandaa kutoka, mule ofisini alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Juma kwani alijua kuwa siku hiyo angemkuta humo ofisini, ila alimkuta mama Angel, ikabidi tu akae na kuanza kuzungumza nae,
“Halafu sikutegemea kama ningekukuta wewe”
“Ndio umenikuta sasa, karibu”
“Asante, ila si una mtoto mdogo wewe huoni kama ukija huku unamkosesha mtoto haki yake?”
“Yani uzuri ni kuwa mtoto wangu amezoea kila kitu, kwahiyo anakunywa maziwa analala, na sio msumbufu hadi wakati narudi”
“Hata kama ila mtoto anahitaji jasho la mama kwa ukaribu sana”
“Aaaah hayo mambo ilikuwa zamani, ila kwasasa wanawake tumeamka”
“Sawa, sikupingi. Yuko wapi Erick?”
“Yupo shule, unadhani atakuwa wapi?”
“Yani alikopigwa hadi akazimia bado umemrudisha tena! Nina mashaka na wewe, ni mzazi wa aina gani usiye na huruma na mtoto wako?”
“Sikuelewi”
“Hivi umeshindwa kufikiria kweli, ni bora hata ungemuahamisha shule, kuliko kumrudisha shule hiyo hiyo. Hata hivyo hiki sio kilichonileta”
“Haya sema kilichokuleta”
“Ni hivi, nilipanga na Erick kuwa Jumamosi ningekuja kumchukua ili twende mahali ila nilishindwa, basi namuomba Jumamosi hii, tena ni vizuri nimekukuta na wewe mama yake, naomba ruhusa kwako”
“Haiwezekani, siwezi kumrudusu mwanangu kwenda sehemu nisiyoijua”
“Kumbe tatizo ni wewe kutokupajua tu!! Basi naomba twende wote siku hiyo, tafadhari nakuomba. Natumaini utatendea kazi ombi langu, kwaheri”
Juma aliinuka na kuondoka yani hakutaka hata kusikia jibu la mama Angel kama kakubali au kakataa ila yeye alihakikisha tu kuwa ameshamwambia na kama anataka na yeye aongozane nao.

Mama Angel alirudi nyumbani kwake muda huu akiwa amejichokea kiasi Fulani, baada ya kuoga na kula alienda kuongea na Erick kuhusu Juma,
“Nakuomba mwanangu jambo moja, najua nilikwambia ila narudia tena naomba mwanangu usiwe karibu na Juma, hata akufate wapi mkwepe, naona sio mtu mzuri kweko”
“Halafu leo mama, alikuja yule mwanamke nisiyempendaga shuleni”
“Nani huyo? Sia?”
“Ndio huyo huyo”
Mama Angel akachukia hapo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani Sia alimwambia mtoto wake, ila Erick alimwambia vile ambavyo alizungumza na Sia mpaka mama Angel alishangaa na kusema,
“Yani Sia ndio kaja kukwambia hayo maneno! Huo urafiki wa Sia na mke wa Juma umeanza lini hadi waambiane kila kitu jamani! Mmmmh unajua mtu unaweza kuzungukwa hapa hapa bila hata kujijua wala kutambua kuwa ni kitu gani kinachokusumbua kumbe ni mtu wako wa karibu. Haya mwanangu hata kama huwa unamchukia ila hilo alilokwambia ni bora zaidi, tafadhali kaa mbali na Juma”
Kisha akamuaga mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na huko alimpigia simu mumewe na kumwambia tu habari za Juma, ila hakumwambia kuwa alienda kiwandani kwani hakutaka mumewe ajue kuwa huwa anaenda kiwandani,
Huyu Juma ana wazimu eeeh! Kwahiyo alikuja tena hapo nyumbani?”
“Ndio alikuja”
“Sijui kaingiliwa na nini jamani na huyo Juma, anaacha kufatilia watoto wake anakazana kufatilia watoto wa wenzake”
“Tuachane na hayo, jamani mume wangu unarudi lini? Nimekukumbuka sana ujue”
“Nitarudi tu mke wangu usijali ila siku ya kurudi sitakwambia maana nataka nikushtukize tu”
“Ushaniambia tayari maana mshtukizo hata mtu haambiwi kabisa, huwa inatokea tu”
Baba Angel akacheka, na kuongea zaidi kidogo na mke wake kisha waliagana na kulala huku mama Angel anawaza kukikucha tu aende kwanza kiwandani maana alitakuwa kwasasa anataka kujua kila kitu.
Basi kulivyokucha, alijiandaa kwaajili ya kutoka ila muda ule ule alifika mama Junior, na kumfanya mama Angel ashangae maana ni asubuhi sana, basi alienda kukaa nae kwenye sebule yao nyingine na kuongea nae maana pale ndio kwanza Vaileth alikuwa akifanya usafi,
“Kheee dada mbona asubuhi asubuhi?”
“kwani na wewe hii asubuhi yote unaenda wapi?”
“Naenda kazini dada”
“Kivipi? Hebu nieleweshe vizuri”
Mama Angel alimwambia kuwa huwa anaenda kiwandani kuangalia jinsi kiwanda kinavyofanya kazi, na kufatilia wafanyakazi wa pale, na hata alimuelezea toka kaanza kufatilia ni makosa mangapi kayagundua,
“Ni vizuri sana sio vibaya ila huwa unaondoka muda gani na kurudi muda gani?”
“Asubuhi halafu narudi jioni”
“Aaaah Erica hebu wacha ujinga, una mtoto mdogo wewe ujue!! Sikia, unachofanya sio kibaya ila panga muda wako vizuri uwe unawahi kurudi kumnyonyesha mtoto na kukaa nae karibu, jamani unafanya kama wale wanawake ambao hawana waume kwahiyo wanapambana wenyewe ili watoto wale, ndio huwa wanafanya kazi muda wote hata muda wa kulea watoto haupo, unadhani Erick akisikia hili atafurahi? Hawezi kufurahi hata kidogo, amehangaika, ameteseka ili mke wake na watoto mtulie, amehitaji mtoto ili utulie nyumbani kulea mtoto ila wewe ndio kama biashara umeanza leo jamani Erica eeeh! Usiwe hivyo jamani mdogo wangu”
“Haya nimekuelewa, asubuhi yote hii ya nini?”
“Jana bhana, kuna binti kaja kunililia usiku mwenzangu ana mimba ya Junior”
Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia dada yake,
“Kheee sasa umeamua nini?”
“Niamue nini zaidi ya kumshauri akatoe”
“Hapana dada usifanye hivyo, unajua kutoa mimba ni sawa na dhambi ya kuua tu. Muache azae mtoto wake”
“Unakumbuka kipindi chako nini?”
“Nakumbuka ndio, muacheni azae, wala hata usimtoe hiyo mimba. Kwanza wewe mwenyewe una kitoto kimoja tu halafu ndio uanze kutoa mimba za wakwe zako kweli? Muache azae tu”
“Haya, ila kuna mengine”
“Yapi hayo?”
“Kuhusu shemeji yako jamani, si kuna kimwanamke alikipata huko sijui wapi ndio kikawa kinamsumbua akili, hadi nilikuja siku ile ili nikueleze dukuduku langu, ila sasa akili ikacheza, siku hiyo kachelewa kurudi nikamuanzishia kilio kama cha msiba, yani nilikumbuka msiba wa baba kabisa, kwani amerudia tena kuwasiliana na yule mwanamke mbele yangu! Kwani kachelewa tena kurudi!!”
“Mmmh dada, kwa kilio tu au kuna mengine ulimfanyia?”
“Ukiona mumeo anakusumbua niambie nikueleze, ila ndio hivyo Deo saibvi katulia ila sitaki tena kukaa nyumbani, nataka kuanza kazi kwakweli nimechoka kukaa nyumbani, kwahiyo natafuta kazi”
“Hilo la kutafuta kazi ni wazo zuri dada, tena kuna rafiki yake baba Angel nitakuunganisha nae, hukusema tu mapema ila kwasasa usijali mambo ni moto. Ila bado hujaniambia mbona umekuja asubuhi sana?”
“Nilijua sitokukuta, maana mara nyingi tu napoiga simu naambiwa kuwa umeondoka”
“Huwa unapiga ya mezani wewe, ila hata hivyo Derrick kalazwa, sijui umepata habari au dada Mage alisahau kukwambia?”
Mama Junior alishangaa kidogo, na kusema kuwa siku hiyo itabidi waende wote kumuona Derrick maana hata wafanyeje bado ni ndugu yao tu.

Tumaini akiwa anaelekea katika shughuli zake, akakutana njiani na Dora na kuanza kuongea nae na kumpa taarifa kuhusu kulazwa kwa Derrick,
“Jamani masikini, kafanyaje tena?”
“Kumbe hujui? Derrick alikuwa ni tapeli ila dada yake yani Erica alikuwa akimfichia siri”
“Ila unajua kuna kitu huwa sielewi”
“Kitu gani?”
“Ni kuhusu Derrick na Erica, kwahiyo wale ni ndugu kabisa?”
“Ndio ndugu, baba mmoja wale”
“Unajua nini?”
“Nini?”
“Kipindi tupo chuo, kuna kipindi Fulani Erica alikuwa anatembea na Derrick, si unajua Erica alikuwa ni rafiki yangu sana ila tukaja kugombana badae kwa mambo madogo tu, basi Erica alikuwa anatembea na Derrick”
“Mmmh kwahiyo alikuwa ni mpenzi wake kabisa?”
“Ndio, alikuwa nae sasa nashangaa kusikia kuwa ni ndugu”
“Ila Erica anaonekana kuwa mpole sana, sidhani kama alitembea nae”
“Weeee ana upole gani yule! Niulize mimi listi ya wanaume aliotembea nao, ninaowajua tu ni wengi hatari, kuna kijamaa kilikuwa kinaitwa Babuu katembea nacho, kilikuwa kimasikini hatari ila Erica ndio alikufa alioza, mwenzio Erica katembea na George na aliachwa na George sababu hakuwa bikra”
“Mmmh unajua George na Erick ni ndugu kwa upande wa mama yake Erick huko!”
“Kheee basi hekaheka za Erica sio za nchi hii, kuna kipindi alijikuta kagonganisha ndugu watatu yule na wote katembea nao, huyo Derrick unayesema ni ndugu yake katembea nae, halafu kuna jamaa nadhani unamjua siku ya harusi ya Erick na Erica aliongea maneno mengi kiasi, yule jamaa anaitwa Bahati, kwasasa anaishi na Fetty basi yule Erica katembea nae, usimuone vile huwa kuna mambo namtetea tu. Ni kweli ni mpole ila kwenye swala la uhuni na yeye alikuwa muhuni”
“Kumbe!! Ndiomana alipatana na wewe, nikamshangaa msichana mpole vile kuwa na urafiki na wewe! Bora hata Fetty kidogo hakuwa na makuu chuoni ila wewe mmmh nilishangaa sana”
“Siku zote mwizi anatembea na mwizi mwenzie, ila kwasasa nimeokoka hayo mambo nimeacha jamani hata umbea huu sikutakiwa kukwambia, eeeh Mungu nisamehe”
Tumaini alicheka sana na kumuuliza,
“Ila hiyo listi ya wanaume wa Erica uliijuaje?”
“Mmmh unajua mimi nina dhambi nyingi jamani, namshukuru Mungu ni mwaminifu na anasamehe, la sivyo mimi nisengesamehewa jamani. Unajua nilikuwa namuonea sana huruma Erica akilia kuhusu mapenzi halafu hivi vidume vikijidai vyenyewe kwa kuumiza moyo wa Erica, yani siku niliyogundua nimeatirika basi nilimfata mmoja baada ya mwingine na kutembea nae, yani kila aliyemuumiza Erica nami nilihakikisha namuumiza na ukimwi”
“Ndiomana ukaamua kumuambukiza na baba yangu! Mwanamke mbaya wewe hata hufai”
“Mmmh tuachane na habari hizo Tumaini ila baba yako ndio aliniambukiza mimi. Nisamehe kwa hilo”
“Mbaya wewe na sidhani kama dhambi zote umesamehewa, hata huo ulokole wako nina mashaka nao. Kajinga kweli wewe”
Dora akaona yataanza marumbano pale bure, kwahiyo akaamua kuagana na Tumaini tu ila aliahidi kuwa ataenda kumsalimia Derrick pia.
Baada ya Dora kuondoka, kwakweli Tumaini alijiuliza sana,
“Kumbe watu wanatoka mbali eeeh! Ndiomana Erica alipata yule mtoto wa kiarabu kumbe na yeye alikuwa na mambo sana”
Basi akachukua simu yake na kumtumia mdogo wake ujumbe,
“Habari Erick, nasikia Erica kabla ya kukutana na wewe alishatembea na wanaume zaidi ya watano”
Muda kidogo akapokea ujumbe kwa Erick,
“Hata angetembea na dunia nzima bado ningempenda tu tena sana.”
Kisha akapiga simu ambapo Tumaini akapokea,
“Ila dada yangu kwani una matatizo gani? Ulisikia kuwa mwanamke akiwa ametembea na wanaume wengi haolewi wapi? Si ilimradi apate anayependana nae tu”
“Kheee yameisha basi, mimi nilikuwa nasema tu”
“Unajua kuna muda huwa sikuelewi, unampenda Erica ila unaniambia maneno kama haya, unataka niachane nae au ni kitu gani? Dada yangu nakuomba umuheshimu mke wangu, nampenda sana na unalijua hilo, mimi Erica nampenda hata niambiwe wale watoto wote sio wangu kazaa na wanaume wengine huko bado nitampenda na watoto nitawapenda yani usijisumbue kupata habari huko na kuniambia”
“Basi yameisha wala sitokwambia tena mambo kama haya”
“Halafu hizo tabia za umbea sijui umezitoa wapi? Utakuwa unaongea sana na Sia wewe ndiomana, naomba usiniletee tena umbea wa kuhusu mke wangu, nampenda jinsi alivyo na huwezi jua nimempendea nini”
“Nimekuelewa Erick, hata mimi nampenda Erica yani hata sijui naanzaje kukuletea umbea wa aina hii, naomba unisamehe”
“Kila siku na mke wangu tunajiuliza Erica mdogo katoa wapi umbea kumbe katoa kwako, naomba usiniambie tena habari za hivi, tuwe tunaongea mambo mengine tu”
“Nisamehe, nimekuelewa”
Tumaini alikata simu na kupumua kiasi kisha akasema,
“Kweli mapenzi ya kweli yapo, kuna muda hadi nahisi Erick karogwa jamani, si kwa kupenda huku mmmh! Ila hata mimi mume wangu ananipenda jamani, niache wivu loh!”
Akaendelea na safari yake ya kwenda kwenye shughuli zake.

Mama Angel alimuomba dada yake wapiti kwanza kiwandani halafu ndio waende hospitali maana hakutaka siku hiyo aipitishe bila kwenda kuangalia shughuli za kiwanda zimekwendaje.
Basi walienda hadi kiwandani, kwa mara ya kwanza mama Junior aliweza kuona kile kiwanda kilivyo,
“Jamani mdogo wangu, mmejitahidi sana”
“Asante”
Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamo
na kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,
“Wewe si mama yake na Junior?”
“Ndio ni mimi”
Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama.
 
SEHEMU YA 334

Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,
“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”
“Ndio, ni kaka yangu wa damu”
Mara mama Sarah akaonekana kama mtu aliye na kizunguzungu na kutaka kama kuanguka ni Tumaini ndio alimdaka kwa haraka.
Wote walimshangaa kuwa ana matatizo gani, mama Angel alimshika mkono na kutoka naye nje akamuuliza,
“Tatizo nini Manka?”
Mama Sarah alipumua kisha akasema,
“Acha tu kama ilivyo, utamwambia mama Leah nimeondoka. Kwaheri”
Kisha mama Sarah aliondoka zake, kwakweli mama Angel alimshangaa sana na kurudi wodini ambapo Tumaini alimuuliza vizuri,
“Kwani imekuwaje?”
“hata sijui, kaniaga tu na kuondoka”
Mama Derrick akasema kuwa,
“Au na yeye katapeliwa na mwanangu jamani, yani huyu Derrick dah!!”
“Usiwaze hayo mama, kwasasa tusifikirie utapeli wa Derrick ila tufikirie namna ya kupona kwa Derrick.”
Waliongea kidogo pale kisha waliaga ambapo walipotoka nje, Tumaini alimuuliza mama Angel,
“Inamaana Derrick ni tapeli!! Inamaana siku ile alinitapeli eeeh! Ndiomana nilihisi hivyo”
“Ni kweli ni tapeli ila nadhani anatumia dawa maana sio hali ya kawaida, utashangaa anakuazima tu hela ndogo na ukimpatia utakuta amekomba hela zote za kwenye mkoba wako”
“Aaaah kumbe, halafu kitu kingine hebu tuongee kikubwa, yule shoga yule yani mama Sarah nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa anafahamiana na wewe, sema namba yake ndio akaichukua Derrick. Ila leo nimeshangaa sijui mlishaonana? Halafu kuna nini kinaendelea kati yake na Derrick?”
“Mmmh hata sijui”
“Hajakwambia chochote kwani ulivyotoka nae nje?”
“Si nilikwambia pale, hakuna alichoniambia zaidi ya kuniaga tu”
“Oooh nilijua unanificha sababu ya mama yake Derrick pale, au Derrick ndio baba mzazi wa Sarah?”
“Mmmh! Kwani unamfahamu vizuri yule mwanamke?”
“Namfahamu kiasi tu sio kivile, ila huwa haongei habari za kuwa na mume wala baba yake Sarah, ndiomana nimehisi hivi, labda hakutegemea kukutana nae, hebu fatilia usikute Sarah ni shangazi yako!!”
Halafu Tumaini akaagana na mama Angel ambapo muda huu mama Angel moja kwa moja aliondoka na kurudi nyumbani kwake, na yeye alikuwa akijiuliza tu bila ya kupata jibu.

Mama Angel aliwakuta wanae muda huu wanakula, basi na yeye alienda kujimwagia na kujumuika nao, kisha akawaambia hali ya mgonjwa,
“Jamani wanangu sikuwaambia ni hivi, mjomba wenu Derrick kalazwa, hospitali kumbe siku ile tulipomuona akapatwa majanga pale, nasikia walimpiga sana. Nimetoka kumuona leo hospitali anaendelea vizuri”
“Oooh masikini jamani, ndiomana nilikuwa nasema tukamsaidie ila wewe mama na Erick mlikataa na kusema kuwa tusimsaidie atatutapeli, niliona yale mazingira sio rafiki kwake. Ila bora anaendelea vizuri, Mungu amsaidie apone”
“Mmmh leo Erica naona una huruma sana”
“Ndio mama, yule ni mjomba wetu, lazima niwe na huruma naye”
Muda huu Erick hakuongea jambo lolote lile, walimaliza kula na kila mmoja alienda chumbani kwake, ila Erica moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Mbona hujasema chochote kuhusu mjomba kulazwa”
“Sasa ulitaka niseme nini jamani!”
“Hata utoe pole kwa mama , kwani yule ni kaka yake mama”
“Ila katutapeli laki tatu”
“Kumbuka kuna watu kawatapeli hela nyingi kuliko hizo, ila kapatwa na matatizo unatakiwa kuwa na huruma naye”
“Mimi sina huruma naye labda mpaka atakapoacha utapeli wake”
“Mmmh wewe nawe, halafu ngoja nikuulize, hivi siku ile alivyokuja Sarah na mama yake ulimuelewa mama yake Sarah na mama?”
“Sikuwaelewa ila inaonyesha kuwa ni watu wanaofahamiana ndiomana mama anasema kuwa Sarah ni ndugu yetu”
“Ila habari ya Sarah kuwa ndugu yetu nimeipenda sana”
“Kwanini?”
“Sababu ataacha kukusumbua wewe, toka lini ndugu wakawa wapenzi? Hakuna mila za kihivyo, mimi sitaki Sarah awe mpenzi wako, kwahiyo kama ni ndugu yetu ni afadhali sana yani”
Erick alikaa kimya tu, kisha Erica alimuuliza,
“Kwani hujapenda kwa Sarah kuwa ndugu yetu?”
“Vyote kwangu sawa tu, awe ni ndugu yetu, au asiwe ndugu yetu ila bado mimi siwezi kuwa na mahusiano naye”
“Kwahiyo utakuwa na mahusiano na nani? Au utamkubali Samia?”
“Hakuna, kwani umesahau kiapo chetu Erica hadi unaniuliza maswali kama hayo? Leo nimechoka halafu nina usingizi sana, muda sio mrefu nalala”
Erica ilibidi amuage kaka yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kulala.

Mama Angel alijikuta akiwaza kuhusu mama Sarah, alijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu,
“Kwanini ashtuke vile na kutaka kuzimia? Je Derrick ni nani katika maisha yake au alikuwa na mahusiano na Derrick? Je Sarah ni mtoto wa nani? Wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick? Ila hawezi kuwa wa Erick bhana, hilo nakataa maana angeniambia mapema tu. Ila ni wa nani? Au ndio mtoto ambaye Derrick huwa anamsema? Sielewi jamani, kuna nini kati ya Manka na Derrick, au kipindi anampenda sana Erick akakutana na Derrick akamdanganya kama alivyonidanganya mimi? Mmmmh!!”
Mama Angel aliwaza sana bila hata ya jibu lolote na kuamua kulala, ila alishtuliwa na simu kutoka kwa mume wake na kuamua kupokea ile simu,
“Kumbe Derrick kalazwa? Ndio Tumaini kanipigia simu kuniambia leo, mke wangu umeshindwa kuniambia kweli?”
“Nisamehe mume wangu jamani, sijui hata nimeghafilika vipi ila ndio hivyo kalazwa”
“Una mawazo gani Erica? Sio hali ya kawaida, kwanza jana kutwa nzima hatujawasiliana na leo nisingekutafuta basi inamaana ingepita bila ya sisi kuwasiliana, tatizo ni nini mke wangu?”
“Hakuna tatizo”
“Nimekwambia kuwa habari za wakina Manka, sijui wakina nani zisikupe presha mke wangu, yote nikirudi tutazungumza kwakina, nakuomba usiwe na mawazo kwasababu hiyo”
“Sina mawazo yoyote hata usijali kuhusu mimi mume wangu”
Basi wakaongea mengi kwa usiku ule, kisha kuagana na mama Angel kuamua kulala sasa kwa uzuri zaidi.

Leo Erick alivyoenda shuleni tu alifatwa na Sarah ambaye alianza kuongea nae,
“Erick, mbona unaonekana kunikwepa sana?”
“Sikukwepi, ila Sarah hivi unajua kama sisi ni ndugu?”
“Hilo nishalikataa kabisa, siwezi kuwa na undugu na wewe Erick, ninachojua ni kimoja tu kuwa nakupenda sana”
“Duh!”
Muda wa kipindi ulianza kwahiyo ikabidi Sarah aende darasani, kwahiyo Erick alibaki huku akishangaa tu maana hakumuelewa Sarah kwakweli.
Basi waliendelea na masomo kama kawaida, ila siku hiyo mchana Erick alifatwa darasani kuwa anaitwa halafu alitoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa walimu na kukuta ni Sia yuko pale ambapo Sia aliwaomba walimu nafasi kidogo aweze kuzungumza na Erick maana alijitambulisha yeye kama mama mdogo wa Erick, kwanza kabisa Erick aliulizwa,
“Je unamfahamu huyu? Ni mamako mdogo?”
Erick aliitikia tu maana angekataa basi siku hii angemfanya Sia aumbuke sana, basi akatoka nae nje na kwenda kuzungumza nae,
“Kwanza kabisa asante Erick, nilijua utanikana”
“Hapana, nazijua akili zako ndiomana nimekubali, ushindwi kuangua kilio ofisini”
Leo Sia alicheka kiasi na kumwambia Erick,
“Kilichonileta hapa ni kitu kimoja, nimeona bora nije shule nikwambie hili, ni hivi nasikia kuna mwanaume anaitwa Juma anapenda sana kukufatilia. Tafadhari Erick kaa mbali na mtu huyu maana si mtu mzuri kwako”
“Kivipi?”
“Ipo siku nitakaa na wewe na kuongea nawe vizuri zaidi ila yule mtu si mtu mzuri kwako”
“Kwahiyo kwasasa hujaja na hoja kusema kuwa wewe ni mama yangu?”
“Siku zote uongo hujitenga na ukweli, na kitu kama ni ukweli basis i kulazimisha maana kuna kipindi kitajidhihirisha chenyewe. Kuna upendo ambao watu wanaita ni upendo wa asili, je huna upendo huo juu yangu? Kama unao basi mimi ni mama yako, ila kama huna huo upendo juu yangu basi mimi si mama yako, ila hata kama mimi si mama yako bado ninajukumu la kukulinda na kukutunza, nakuomba uwe mbali kabisa na Juma. Sikujua mapema kuwa anakufatilia ila sasa imejua”
“Umejuaje?”
“Yule Juma ana mke wake, na yule mke wake ni rafiki yangu mkubwa na ni rafiki wa mama yako pia. Nimejikuta nikimpenda na kuongea nae mambo mengi sana, kwahiyo kuwa makini sana na Juma, jiepushe nae na ikiwezekana ukimuona mkimbie kabisa. Yangu ni hayo tu, sina mengine wala sina la ziada, kwaheri”
Sia alienda ofisini na kuwashukuru walimu kwa kumruhusu kuongea na Erick halafu aliondoka zake, kwakweli Erick alikuwa akishangaa tu kwanza alishangaa jinsi huyu Sia alivyoongea kiustaarabu siku ya leo, basi alikuwa akienda darasani huku akisema,
“Ingawa kaongea na mimi kiustaarabu ila hiki kimama sikipendi jamani, yani sikipendi kabisa”
Akaenda zake darasani na kuendelea na masomo yake kama kawaida.

Mama Angel akiwa kiwandani leo, bado alitaka maelezo ya ile laki mbili, basi Yuda aliileta ile laki mbili na kumkabidhi huku akisema kuwa yule mtu amemlipa, haikuwa kweli ila Yuda alikopa ile hela mahali ili aweze kumlipa huyu mama na kuepuka lawama,
“Oooh kumbe wameleta, basin i vizuri kumbe ni waaminifu”
“Halafu Erick mtoto atakuja lini tena kiwandani?”
“Atakuja tu ila mwanangu nimeona bora akazanie masomo kwanza kwani ndio ya muhimu kuliko vitu vyote”
“Unaonekana unapenda shule eeeh!”
“Ndio napenda sana, napenda watoto wangu wawe wasomi wa kimataifa”
Waliendelea kufanya kazi huku mama Angel akipita kukagua kagua eneo lake, muda kidogo wakati anajiandaa kutoka, mule ofisini alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Juma kwani alijua kuwa siku hiyo angemkuta humo ofisini, ila alimkuta mama Angel, ikabidi tu akae na kuanza kuzungumza nae,
“Halafu sikutegemea kama ningekukuta wewe”
“Ndio umenikuta sasa, karibu”
“Asante, ila si una mtoto mdogo wewe huoni kama ukija huku unamkosesha mtoto haki yake?”
“Yani uzuri ni kuwa mtoto wangu amezoea kila kitu, kwahiyo anakunywa maziwa analala, na sio msumbufu hadi wakati narudi”
“Hata kama ila mtoto anahitaji jasho la mama kwa ukaribu sana”
“Aaaah hayo mambo ilikuwa zamani, ila kwasasa wanawake tumeamka”
“Sawa, sikupingi. Yuko wapi Erick?”
“Yupo shule, unadhani atakuwa wapi?”
“Yani alikopigwa hadi akazimia bado umemrudisha tena! Nina mashaka na wewe, ni mzazi wa aina gani usiye na huruma na mtoto wako?”
“Sikuelewi”
“Hivi umeshindwa kufikiria kweli, ni bora hata ungemuahamisha shule, kuliko kumrudisha shule hiyo hiyo. Hata hivyo hiki sio kilichonileta”
“Haya sema kilichokuleta”
“Ni hivi, nilipanga na Erick kuwa Jumamosi ningekuja kumchukua ili twende mahali ila nilishindwa, basi namuomba Jumamosi hii, tena ni vizuri nimekukuta na wewe mama yake, naomba ruhusa kwako”
“Haiwezekani, siwezi kumrudusu mwanangu kwenda sehemu nisiyoijua”
“Kumbe tatizo ni wewe kutokupajua tu!! Basi naomba twende wote siku hiyo, tafadhari nakuomba. Natumaini utatendea kazi ombi langu, kwaheri”
Juma aliinuka na kuondoka yani hakutaka hata kusikia jibu la mama Angel kama kakubali au kakataa ila yeye alihakikisha tu kuwa ameshamwambia na kama anataka na yeye aongozane nao.

Mama Angel alirudi nyumbani kwake muda huu akiwa amejichokea kiasi Fulani, baada ya kuoga na kula alienda kuongea na Erick kuhusu Juma,
“Nakuomba mwanangu jambo moja, najua nilikwambia ila narudia tena naomba mwanangu usiwe karibu na Juma, hata akufate wapi mkwepe, naona sio mtu mzuri kweko”
“Halafu leo mama, alikuja yule mwanamke nisiyempendaga shuleni”
“Nani huyo? Sia?”
“Ndio huyo huyo”
Mama Angel akachukia hapo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani Sia alimwambia mtoto wake, ila Erick alimwambia vile ambavyo alizungumza na Sia mpaka mama Angel alishangaa na kusema,
“Yani Sia ndio kaja kukwambia hayo maneno! Huo urafiki wa Sia na mke wa Juma umeanza lini hadi waambiane kila kitu jamani! Mmmmh unajua mtu unaweza kuzungukwa hapa hapa bila hata kujijua wala kutambua kuwa ni kitu gani kinachokusumbua kumbe ni mtu wako wa karibu. Haya mwanangu hata kama huwa unamchukia ila hilo alilokwambia ni bora zaidi, tafadhali kaa mbali na Juma”
Kisha akamuaga mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na huko alimpigia simu mumewe na kumwambia tu habari za Juma, ila hakumwambia kuwa alienda kiwandani kwani hakutaka mumewe ajue kuwa huwa anaenda kiwandani,
Huyu Juma ana wazimu eeeh! Kwahiyo alikuja tena hapo nyumbani?”
“Ndio alikuja”
“Sijui kaingiliwa na nini jamani na huyo Juma, anaacha kufatilia watoto wake anakazana kufatilia watoto wa wenzake”
“Tuachane na hayo, jamani mume wangu unarudi lini? Nimekukumbuka sana ujue”
“Nitarudi tu mke wangu usijali ila siku ya kurudi sitakwambia maana nataka nikushtukize tu”
“Ushaniambia tayari maana mshtukizo hata mtu haambiwi kabisa, huwa inatokea tu”
Baba Angel akacheka, na kuongea zaidi kidogo na mke wake kisha waliagana na kulala huku mama Angel anawaza kukikucha tu aende kwanza kiwandani maana alitakuwa kwasasa anataka kujua kila kitu.
Basi kulivyokucha, alijiandaa kwaajili ya kutoka ila muda ule ule alifika mama Junior, na kumfanya mama Angel ashangae maana ni asubuhi sana, basi alienda kukaa nae kwenye sebule yao nyingine na kuongea nae maana pale ndio kwanza Vaileth alikuwa akifanya usafi,
“Kheee dada mbona asubuhi asubuhi?”
“kwani na wewe hii asubuhi yote unaenda wapi?”
“Naenda kazini dada”
“Kivipi? Hebu nieleweshe vizuri”
Mama Angel alimwambia kuwa huwa anaenda kiwandani kuangalia jinsi kiwanda kinavyofanya kazi, na kufatilia wafanyakazi wa pale, na hata alimuelezea toka kaanza kufatilia ni makosa mangapi kayagundua,
“Ni vizuri sana sio vibaya ila huwa unaondoka muda gani na kurudi muda gani?”
“Asubuhi halafu narudi jioni”
“Aaaah Erica hebu wacha ujinga, una mtoto mdogo wewe ujue!! Sikia, unachofanya sio kibaya ila panga muda wako vizuri uwe unawahi kurudi kumnyonyesha mtoto na kukaa nae karibu, jamani unafanya kama wale wanawake ambao hawana waume kwahiyo wanapambana wenyewe ili watoto wale, ndio huwa wanafanya kazi muda wote hata muda wa kulea watoto haupo, unadhani Erick akisikia hili atafurahi? Hawezi kufurahi hata kidogo, amehangaika, ameteseka ili mke wake na watoto mtulie, amehitaji mtoto ili utulie nyumbani kulea mtoto ila wewe ndio kama biashara umeanza leo jamani Erica eeeh! Usiwe hivyo jamani mdogo wangu”
“Haya nimekuelewa, asubuhi yote hii ya nini?”
“Jana bhana, kuna binti kaja kunililia usiku mwenzangu ana mimba ya Junior”
Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia dada yake,
“Kheee sasa umeamua nini?”
“Niamue nini zaidi ya kumshauri akatoe”
“Hapana dada usifanye hivyo, unajua kutoa mimba ni sawa na dhambi ya kuua tu. Muache azae mtoto wake”
“Unakumbuka kipindi chako nini?”
“Nakumbuka ndio, muacheni azae, wala hata usimtoe hiyo mimba. Kwanza wewe mwenyewe una kitoto kimoja tu halafu ndio uanze kutoa mimba za wakwe zako kweli? Muache azae tu”
“Haya, ila kuna mengine”
“Yapi hayo?”
“Kuhusu shemeji yako jamani, si kuna kimwanamke alikipata huko sijui wapi ndio kikawa kinamsumbua akili, hadi nilikuja siku ile ili nikueleze dukuduku langu, ila sasa akili ikacheza, siku hiyo kachelewa kurudi nikamuanzishia kilio kama cha msiba, yani nilikumbuka msiba wa baba kabisa, kwani amerudia tena kuwasiliana na yule mwanamke mbele yangu! Kwani kachelewa tena kurudi!!”
“Mmmh dada, kwa kilio tu au kuna mengine ulimfanyia?”
“Ukiona mumeo anakusumbua niambie nikueleze, ila ndio hivyo Deo saibvi katulia ila sitaki tena kukaa nyumbani, nataka kuanza kazi kwakweli nimechoka kukaa nyumbani, kwahiyo natafuta kazi”
“Hilo la kutafuta kazi ni wazo zuri dada, tena kuna rafiki yake baba Angel nitakuunganisha nae, hukusema tu mapema ila kwasasa usijali mambo ni moto. Ila bado hujaniambia mbona umekuja asubuhi sana?”
“Nilijua sitokukuta, maana mara nyingi tu napoiga simu naambiwa kuwa umeondoka”
“Huwa unapiga ya mezani wewe, ila hata hivyo Derrick kalazwa, sijui umepata habari au dada Mage alisahau kukwambia?”
Mama Junior alishangaa kidogo, na kusema kuwa siku hiyo itabidi waende wote kumuona Derrick maana hata wafanyeje bado ni ndugu yao tu.

Tumaini akiwa anaelekea katika shughuli zake, akakutana njiani na Dora na kuanza kuongea nae na kumpa taarifa kuhusu kulazwa kwa Derrick,
“Jamani masikini, kafanyaje tena?”
“Kumbe hujui? Derrick alikuwa ni tapeli ila dada yake yani Erica alikuwa akimfichia siri”
“Ila unajua kuna kitu huwa sielewi”
“Kitu gani?”
“Ni kuhusu Derrick na Erica, kwahiyo wale ni ndugu kabisa?”
“Ndio ndugu, baba mmoja wale”
“Unajua nini?”
“Nini?”
“Kipindi tupo chuo, kuna kipindi Fulani Erica alikuwa anatembea na Derrick, si unajua Erica alikuwa ni rafiki yangu sana ila tukaja kugombana badae kwa mambo madogo tu, basi Erica alikuwa anatembea na Derrick”
“Mmmh kwahiyo alikuwa ni mpenzi wake kabisa?”
“Ndio, alikuwa nae sasa nashangaa kusikia kuwa ni ndugu”
“Ila Erica anaonekana kuwa mpole sana, sidhani kama alitembea nae”
“Weeee ana upole gani yule! Niulize mimi listi ya wanaume aliotembea nao, ninaowajua tu ni wengi hatari, kuna kijamaa kilikuwa kinaitwa Babuu katembea nacho, kilikuwa kimasikini hatari ila Erica ndio alikufa alioza, mwenzio Erica katembea na George na aliachwa na George sababu hakuwa bikra”
“Mmmh unajua George na Erick ni ndugu kwa upande wa mama yake Erick huko!”
“Kheee basi hekaheka za Erica sio za nchi hii, kuna kipindi alijikuta kagonganisha ndugu watatu yule na wote katembea nao, huyo Derrick unayesema ni ndugu yake katembea nae, halafu kuna jamaa nadhani unamjua siku ya harusi ya Erick na Erica aliongea maneno mengi kiasi, yule jamaa anaitwa Bahati, kwasasa anaishi na Fetty basi yule Erica katembea nae, usimuone vile huwa kuna mambo namtetea tu. Ni kweli ni mpole ila kwenye swala la uhuni na yeye alikuwa muhuni”
“Kumbe!! Ndiomana alipatana na wewe, nikamshangaa msichana mpole vile kuwa na urafiki na wewe! Bora hata Fetty kidogo hakuwa na makuu chuoni ila wewe mmmh nilishangaa sana”
“Siku zote mwizi anatembea na mwizi mwenzie, ila kwasasa nimeokoka hayo mambo nimeacha jamani hata umbea huu sikutakiwa kukwambia, eeeh Mungu nisamehe”
Tumaini alicheka sana na kumuuliza,
“Ila hiyo listi ya wanaume wa Erica uliijuaje?”
“Mmmh unajua mimi nina dhambi nyingi jamani, namshukuru Mungu ni mwaminifu na anasamehe, la sivyo mimi nisengesamehewa jamani. Unajua nilikuwa namuonea sana huruma Erica akilia kuhusu mapenzi halafu hivi vidume vikijidai vyenyewe kwa kuumiza moyo wa Erica, yani siku niliyogundua nimeatirika basi nilimfata mmoja baada ya mwingine na kutembea nae, yani kila aliyemuumiza Erica nami nilihakikisha namuumiza na ukimwi”
“Ndiomana ukaamua kumuambukiza na baba yangu! Mwanamke mbaya wewe hata hufai”
“Mmmh tuachane na habari hizo Tumaini ila baba yako ndio aliniambukiza mimi. Nisamehe kwa hilo”
“Mbaya wewe na sidhani kama dhambi zote umesamehewa, hata huo ulokole wako nina mashaka nao. Kajinga kweli wewe”
Dora akaona yataanza marumbano pale bure, kwahiyo akaamua kuagana na Tumaini tu ila aliahidi kuwa ataenda kumsalimia Derrick pia.
Baada ya Dora kuondoka, kwakweli Tumaini alijiuliza sana,
“Kumbe watu wanatoka mbali eeeh! Ndiomana Erica alipata yule mtoto wa kiarabu kumbe na yeye alikuwa na mambo sana”
Basi akachukua simu yake na kumtumia mdogo wake ujumbe,
“Habari Erick, nasikia Erica kabla ya kukutana na wewe alishatembea na wanaume zaidi ya watano”
Muda kidogo akapokea ujumbe kwa Erick,
“Hata angetembea na dunia nzima bado ningempenda tu tena sana.”
Kisha akapiga simu ambapo Tumaini akapokea,
“Ila dada yangu kwani una matatizo gani? Ulisikia kuwa mwanamke akiwa ametembea na wanaume wengi haolewi wapi? Si ilimradi apate anayependana nae tu”
“Kheee yameisha basi, mimi nilikuwa nasema tu”
“Unajua kuna muda huwa sikuelewi, unampenda Erica ila unaniambia maneno kama haya, unataka niachane nae au ni kitu gani? Dada yangu nakuomba umuheshimu mke wangu, nampenda sana na unalijua hilo, mimi Erica nampenda hata niambiwe wale watoto wote sio wangu kazaa na wanaume wengine huko bado nitampenda na watoto nitawapenda yani usijisumbue kupata habari huko na kuniambia”
“Basi yameisha wala sitokwambia tena mambo kama haya”
“Halafu hizo tabia za umbea sijui umezitoa wapi? Utakuwa unaongea sana na Sia wewe ndiomana, naomba usiniletee tena umbea wa kuhusu mke wangu, nampenda jinsi alivyo na huwezi jua nimempendea nini”
“Nimekuelewa Erick, hata mimi nampenda Erica yani hata sijui naanzaje kukuletea umbea wa aina hii, naomba unisamehe”
“Kila siku na mke wangu tunajiuliza Erica mdogo katoa wapi umbea kumbe katoa kwako, naomba usiniambie tena habari za hivi, tuwe tunaongea mambo mengine tu”
“Nisamehe, nimekuelewa”
Tumaini alikata simu na kupumua kiasi kisha akasema,
“Kweli mapenzi ya kweli yapo, kuna muda hadi nahisi Erick karogwa jamani, si kwa kupenda huku mmmh! Ila hata mimi mume wangu ananipenda jamani, niache wivu loh!”
Akaendelea na safari yake ya kwenda kwenye shughuli zake.

Mama Angel alimuomba dada yake wapiti kwanza kiwandani halafu ndio waende hospitali maana hakutaka siku hiyo aipitishe bila kwenda kuangalia shughuli za kiwanda zimekwendaje.
Basi walienda hadi kiwandani, kwa mara ya kwanza mama Junior aliweza kuona kile kiwanda kilivyo,
“Jamani mdogo wangu, mmejitahidi sana”
“Asante”
Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamo
na kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,
“Wewe si mama yake na Junior?”
“Ndio ni mimi”
Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama.

Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamo na kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,
“Wewe si mama yake na Junior?”
“Ndio ni mimi”
Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama. na pale pale alijikuta yeye na yule mama wakianza kupigana vibao hadi alipotokea Rahim na kuwaamulia maana wote wawili alikuwa akiwafahamu.
Rahim aliwauliza pale,
“Kwani mna matatizo gani nyie?”
Mama Junior akaongea,
“Hata namshangaa huyu mwanamke, simjui, hanijui halafu kanivamia tu na kuanza kunipiga vibao”
Rahim alimuangalia yule mwanamke na kumuuliza,
“Weee Linah, kwani tatizo ni nini?”
“Mwambie huyo mwanamke akamuulize mtoto wake Linah ni nani?”
“Khee makubwa, mtoto wangu aanze kufahamiana na watu wazima kama wewe!”
Mama Angel nae alifatwa na mlinzi kwahiyo alitoka pale nje kuangalia kuna nini na kumkuta Rahim ndio yupo kati akiwaamulia watu hawa, basi mama Angel akasema kwa msahangao,
“Kheee ni wewe tena!!”
Mama Junior akamuuliza,
“Kwani unamfahamu?”
“Dada, dunia ina makubwa hii unaweza kuzimia mambo mengine ukiyajua, eti huyu mtu mzima na ukubwa wake alikuwa na mahusiano na Junior”
Yani pale Rahim nae aliuliza,
“Kwani huyo Junior ana umri gani?”
Linah aliondoka huku akisonya tu, na mama Angel akamwambia Rahim,
“Junior na Angel wamepishana mwaka mmoja tu”
“Khaaa, huyu Linah mbona katia aibu hivyo?”
Rahim aliwaacha pale mama Junior na mama Angel halafu yeye alimfata Linah alipoelekea.
Basi mama Junior alimuomba tu ndugu yake waondoke muda huo maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa, basi mama Angel alienda kukamilisha kazi kidogo na kuondoka na ndugu yake ambapo moja kwa moja alienda nae kwenye mgahawa na kuagiza chakula pale huku wakiongea kidogo, basi mama Junior akauliza tena,
“Inamaana yule mwanamke mtu mzima ndio alikuwa akitembea na Junior?”
“Ndio! Sasa dada unashangaa nini wakati wewe mwenyewe uliwahi kusema kuwa Junior anatembea na wamama wakubwa”
“Yani nilikuwa najua ni wale wanawake wa kumzidi miaka kumi au kumi na mbili, kumbe anatembea na wanawake wanaoweza kumzaa kabisa jamani eeeh!! Sasa yule si Junior ni kama mtoto wake watatu au wanne, ana nini huyu Junior lakini jamani!”
“Usijali dada, Junior tutamdhibiti tu na atakaa sawa kama watoto wengine, kwasasa nimempiga marufuku hata kurudi nyumbani, nimemwambia akae shuleni huko na akazane na masomo, hakuna cha mwisho wa wiki wala nini, sitaki ujinga wa kurudi nyumbani kabisa, naona akiwa nyumbani ndio anawaza ujinga zaidi”
“Yani Junior jamani dah!! Sasa mama mkubwa vile kweli, halafu halina adabu linafika na kuanza kuninasa vibao, nikasema huyu hajui kichaa changu nikaanza kumnasa vibao pia, yani yule mwarabu koko wako asingetokea basi mimi na yule mwanamke tungechapana pale”
Mama Angel alicheka na kusema,
“Jamani dada eti mwarabu koko!”
“Ndio ni mwarabu koko yule, yani hajali chochote hata kuja kuamulia naona kajitoa kweli. Halafu huku kafata nini au kajua kuwa unakuja huku siku hizi!!”
“Hapana, ila nyumbani kwao sio mbali na hapa yani kwao kabisa. Hivi dada asingetokea yule kweli mngepigana?”
“Naona Erica unanisahau, jamani mimi huwa sitaki ujinga, anianzae nammaliza, yani sitaki ujinga kabisa, na hata ule mwili wake usingenitisha tungepigana vizuri kabisa pale, mimi ni mpole sana ila huwa sipendi mtu anitanie. Unadhani ndio kama wewe, ambaye unapigwa halafu unaangalia tu yani Erica dah sijui umerithi wapi huo upole”
Basi wakaongea kidogo na kupanga kwenda hospitali kumuona mgonjwa kama ambavyo walipanga.

Moja kwa moja, Rahim alimfata Linah na kuanza kuongea nae akiwa njiani tu,
“Najua ulipata aibu ndiomana ukaondoka, ila kama unajua ni kitu cha aibu uliwezaje kuwa na mahusiano na mtoto mdogo hivyo!!”
“Sijui yani, sijui ni kuchanganyikiwa yani sijui halafu najikuta nikimpenda hatari”
“Kwani huyo mtoto ana nini cha ziada ambacho watu wazima hatuna?”
“Mmmh Rahim niache mie, hivi asiyejua kuwa umeathirika ni nani? Labda mgeni na wewe, naomba uniache tu tafadhari, uliniumiza vya kutosha. Nikajua nitafurahia maisha na huyu mtoto ila naye kumbe mama yake anakataa mapenzi yetu”
“Haya ni lini umesikia kuwa nimeathirika? Ukimwi sio mwisho wa maisha, si unaniona bado nadundika, watakufa hao wasiumwa na mimi nitaendelea kubaki na uzima wangu. Ukimwi sio kifo, ila ukimwi ni ugonjwa ambao unakufanya binadamu ujifunze kula vizuri na kuishi vizuri. Pole kwa kuhangaika na watoto wadogo huku ukijua hilo ndio suluhisho la mapenzi, kwanza mwanangu hajambo?”
“Mjinga wewe, mwanao siku hizi anaendesha bajaji, usiniulize tena ukimuhitaji haswaa nitafute sio kukutana njiani na kuniuliza ujinga”
Linah aliondoka zake, ila Rahim alimuangalia na kutikisa kichwa huku akisema,
“Hawa wanawake huwa wanachekesha sana, si kipindi kile aling’ang’ania kuwa mtoto anaweza kumtunza mwenyewe bila msaada wangu, haya imekuwaje sasa mtoto anaendesha bajaji? Wanawake ni watu wapuuzi sana, ila mwanangu atanitafuta tu, hiyo bajaji ikimchosha atakuja kunitafuta”
Kisha akaondoka zake na yeye kuendelea na mambo yake mengine.
 
SEHEMU YA 335


Erick leo aliwahi kurudi nyumbani tofauti na siku zingine na alimkuta Vaileth akiwa amesinzia tu sebleni, kisha alipoingia Erick alishtuka na kumuuliza,
“Imekuwaje leo mapema hivi?”
“Kichwa kinanigonga sana ndio nikaomba ruhusa na kuondoka zangu, ndiomana nimewahi kurudi”
“Pole sana, ila itakuwa una mawazo mengi sana. Sijui huwa unawaza vitu gani ila nakuona kuwa una mawazo mengi sana, cha kufanya uwe unakunywa maji mengi ndio yatakusaidia kutengeneza kichwa vizuri”
“Eti eeeh! Asante kwa ushauri wako, ngoja nikapumzike kidogo”
Erick alikuwa akiondoka ila ile simu ya mezani nyumbani kwao ilianza kuita na muda huo Vaileth alimuomba Erick apokee mwenyewe ile simu, moja kwa moja Erick alienda kupokea ile simu na kweli mpigaji alikuwa ni Srah,
“Jamani Erick nini shida? Nimesikia kuwa umeondoka unaumwa?”
“Ndio, ni kichwa”
“Pole sana, nikitoka tu shule nakuja kukuona jamani, pole sana”
Halafu ile simu ilikatika kisha Erick aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.
Ila baada ya kama nusu saa hivi, mara alifika Sarah mahali pale inaonyesha na yeye aliomba ruhusa hata hakungoja watoke,
Alifika na kumuuliza Vaileth kuwa Erick yuko wapi,
“Ameenda chumbani kwake kulala”
“Chumba chake kiko wapi?”
“Ukipandisha hapo, mlango utakaotizamana nao upite halafu ingia chumba kinachofatia ndio cha Erick”
“Asante”
Vaileth hakutaka kufatilia sana kwani aliona kuwa Sarah kwa kipindi hiko alikuwa akiishi hapo kama mwanafamilia.
Sarah alipoingia alimkuta Erick amelala, akaona akimuamsha atamsumbua, basi na yeye alienda kujilaza pembeni yake.

Mama Angel na mama Junior walifika hospitali kwaajili ya kumuona Derrick, kwakweli leo kidogo maendeleo ya Derrick yalionekana kwani aliweza hata kufumbua macho yake, basi walimtazama pale na kuanza kumuuliza mama yake,
“Ila kwasasa anakula vizuri mama?”
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwakweli, kwasasa Derrick anaendelea vizuri”
“Mchana wa leo aliletewa chakula na dada Mage?”
“Hapana, Mage alimletea asubuhi, na cha jioni hii kimetoka nyumbani kwangu ila mchana alileta yule mwanamke ambaye siku ile alitaka kuanguka halafu akadakwa na wifi yako”
Mama Angel aliguna kwani alielewa kuwa huyo mwanamke ni nani, alielewa kuwa ni Manka, ila hakuelewa kuna nini kinaendelea kati ya Manka na Derrick, basi aliitikia tu na kuendelea kuuliza habari zingine za ndugu yao.
Muda kidogo alifika Dora nae kwenda kumuona mgonjwa yule, kwakweli mama Junior hakupenda kumuona Dora kabisa ila Dora alimsalimia mama Junior na kuwasalimia wote mahali hapo kisha akaomba mara moja akazungumze nje na mama Junior huku mama Angel akiwa shahidi kwani alimtambua jinsi mama Junior alivyokuwa na hasira, kwahiyo hakutaka kuanza nae shari.
Walimuaga mama Derrick pale na kutoka nje kwenda kuzungumza,
“Kwanza kabisa dada yangu samahani, najua mimi na wewe hatujapata muda mzuri wa kukaa na kuongea na pengine unanichukia bure tu hujui ni nini kipo kati yangu, sijui unanielewa?”
“Wewe endelea tu”
“Kwasasa nimeokoka, najitahidi kuacha maovu ambayo nilikuwa nayafanya nyuma”
“Unachekesha wewe, unacheza na wokovu, mtu kama wewe unaokokaje?”
Mama Angel akamkatisha dada yake,
“Dada, msikilize kwanza”
“Ni hivi, kipindi kile ni kweli nilifanya makosa, nakiri wazi nilienda kwa mganga na kuchukua dawa za kumteka James, ila kilichonifanya nifanye vile ni kimoja tu. Siku tumetoka mimi, Erica na James, basi James akanifanya ninywe sana pombe, hata Erica alipoondoka alimuahidi kuwa atanirudisha nyumbani ila haikuwa hivyo, badala yake alinipeleka kwenye chumba na kuniingilia kimwili tena mbele na nyuma, halafu akanitupa njiani, kiukweli niliumia sana tena sana, nakumbuka nilimfungulia kesi ila alishinda sababu ya pesa zake, na akawa akinikana kila sehemu kuwa hajawahi kuwa na mimi na sio yeye aliyenifanyia mimi vile, ukizingatia ile kesi alishinda, hujui tu ni jinsi gani niliumia moyoni mwanangu. Ni kweli mimi nilikuwa nahangaika na wanaume ila sikuwa najiuza mimi kwamba unikute nimejisimamisha barabarani ili waninunue hapana, ila nilikuwa na wale walionitaka tu. Halafu kitu kingine ni kuwa hakuna nilichokuwa naogopa kama kufanya mapenzi kinyume na maumbile, nilikuwa naogopa sana, halafu James alinifanyia unyama kama huu. Niliumia sana, ndipo nilipokuwa sawa nikasema James lazima nimfundishe funzo, ndipo nilipoenda kwa mganga kuchukua dawa na kumpatia James, na hapo ndipo alipoanza kunipenda hatari. Sasa ulipomuacha hakuwa na namna zaidi ya kunioa mimi tu. Unajua miaka ilipopita James alirudia tabia yake ya umalaya, yani ile tabia ipo kwenye damu yake jamani ndiomana naomba kila siku ili mwanangu Jesca asije akarithi tabia yangu wala ya baba yake, nahitaji mwanangu awe mtoto mwema kama watoto wengine. Ni marafiki wa James ndio walionikazania kuwa nishikilie mali zote ndiomana imekuwa hivi, naomba unisamehe sana tafadhari, halafu kitu kingine ambacho hujui ni kuwa James alikufa akiwa guest na mwanamke, naomba ukiwa unaomba kata hiko kitu kwa mtoto wako yani asijekuwa kama hivyo. Nisamehe dada yangu, hii hali ya kutangatanga na maisha ndio inafanya watu tuache utu kwakweli, nipo tayari kukaa chini ili tuwagawie watoto wote mali sawa kwa sawa, maana yupo na yule James, yule mtoto ambaye James alizaa na mdada wako wa kazi, naomba tuzingatie hilo pia”
Mama Junior akapumua kidogo na kusema,
“Kumbe kuna wakati huwa unaweza kuongea kwa busara namna hiyo?”
“Nimebadilika mimi, nazidi kumuomba Mungu anibadilishe zaidi kuna tabia naomba azitoe kabisa katika maisha yangu ili nibaki safi”
“Khee makubwa, ila nimekuelewa nadhani tutakaa kuongea vizuri kwa mama Angel, tupange tu siku ya kufanya hivyo”
Basi wakapanga siku ya kuonana tena na kuagana kwa muda huo, kisha mama Nagel alimrudisha dada yake nyumbani kwake moja kwa moja halafu yeye kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake pia.

Erica nae alipotoka shuleni tu, kitu cha kwanza leo ilikuwa ni kumuulizia Erick maana kuna habari alikuwa nayo, alimuuliza Vaileth,
“Eti dada, Erick amesharudi?”
“Ndio muda tu tena anaumwa”
Basi Erica hata hakusikiliza maelezo mengine kwani moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick, akamuona Erick amelala huku Sarah yuko pembeni yake, yani Erica alijikuta akijawa na hasira sana na kitu pekee alichowaza muda huo ni kwenda chooni na kuchukua maji kisha kuja kuwamwagia pale kitandani Erick na Sarah, kwakweli walishtuka sana na wa kwanza kushtuka alikuwa ni Sarah ambaye aliuliza,
“Nani katumwagia maji?”
Srick nae alishtuka kumuona Sarah yuko pale kitandani na kuuliza,
“Sarah umefika muda gani?”
“Muda tu Erick, nilipomaliza kuongea na wewe tu niliomba ruhusa na kuondoka”
Erica alikuwa akiwaangalia tu, basi Erick akamuuliza,
“Kwahiyo Erica ndio umetumwagia maji!”
“Ndio, umesahau ahadi yetu Erick!”
Basi Erick ukizingatia alikuwa anaumwa na yale maji aliyomwagiwa na Erica alijikuta akianza kutetemeka na hakuweza kulala tena pale kitandani kwani kulikuwa kumelowa, basi huruma ikamshika Erica ilibidi amsaidie kumtoa pale na kumpeleka chumbani kwake, basi Sarah akataka naye aingie ila Erica alimzuia,
“Kwani una nini wewe? Utanikatazaje kumuona kaka yako!”
“Sitaki ndio”
“Au unamtaka kaka yako!”
Erica alimnasa kibao Sarah kwa maneno haya, ila Vaileth alisikia ule mzozo mwanzoni kabisa kwahiyo alienda kuingilia, wakati Sarah akitaka kumrudishia Erica, tayari Vaileth alikuwa pale kuwaamulia na kuwaachanisha ambapo alimtaka Sarah aondoke tu, kwakweli Sarah aliondoka ila alikuwa na hasira sana kwa muda huo na kusema kuna siku atamkomesha Erica.

Mama Angel aliporudi nyumbani kwake tu alipewa taarifa kuhusu kuumwa kwa Erick,
“Kheee jamani, kumbe mwanangu anaumwa”
Basi akataka kwenda moja kwa moja chumbani kwa Erick ila Erica alimwambia kuwa yupo chumbani kwake, mama Angel hata hakuuliza sababu zaidi ya moja kwa moja kwenda huko chumbani kwa Erica ili kumuangalia Erick na kweli alimkuta anaumwa sana na muda huo alikuwa akitetemeka kabisa, basi alimchukua na kumbembeleza pale ili aende nae kwanza hospitali, kwahiyo aliondoka nyumbani akiwa yeye na Erica kwani yeye alikaa kuendesha gari huku Erica akiwa amekaa na Erick hadi hospitali kwahiyo nyumbani alibaki tu Vaileth na mtoto Ester.
Mama Angel alivyofika hospitali, moja kwa moja alimpeleka Erick kwa daktari halafu Erica alibaki nje tu.
Muda kidogo simu ya mama Angel ilikuwa ikiita na Erica ndio alikuwa na ile simu kwahiyo alipokea muda huo huo,
“Hallow”
“Mama yupo kwa daktari na Erick”
“Kheee kuna nini kwani?”
“Erick anaumwa”
“Khaaa jamani, ndiomana moyo wangu unaumia. Niambie ni wapi nije sasa hivi”
“Kwani wewe nani?”
“Nielekeze nije”
“Mimi sijui ni hospitali gani hii, mama ndio anajua”
Halafu Erica alikata simu na kuangalia ile namba ila ilikuwa ni namba tu bila jina, basi hakujali kitu na kuendelea kukaa pale akisubiri mama yake atoke ili amuulize vizuri.
Ila muda kidogo simu nyingine ikaita ila sasa hivi aliyepiga alikuwa ni madam Oliva, ila Erica hakutaka tena kupokea simu kwani alijua wazi mama yake akimkuta kapokea zake nyingi basi atachukia.

Vaileth akiwa na mtoto nyumbani, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni Sia kwa kipindi hiko Sia alikuwa hazuiliwi kwenda pale kwahiyo mlinzi alikuwa akimruhusu tu.
Basi alifika pale na kumuuliza Vaileth kuwa Erick kapelekwa hospitali gani,
“Mmmh sijui maana mama wakati anaondoka hajasema kuwa anampeleka hospitali gani, ila umejuaje kama anaumwa?”
“Nilimpigia simu mama yenu ila ilipokelewa na Erica mdogo ambaye akaniambia kuwa wapo hospitali ila hakusema ni hospitali gani, ndiomana nimekuja hapa moja kwa moja”
“Hata mimi sijui ila naomba nikuulize swali mama yangu maana wewe ni mkubwa kwangu kwahiyo ni kama mama tu”
“Uliza tu, ila sina mtoto mkubwa kama wewe”
“Haya sawa, ila kwanini unapenda sana kufatilia hii familia haswaa unapenda sana kumfatilia Erick kwanini?”
“Ngoja nikujibu tu kwa kifupi, katika maisha mtu huwa unapitia mambo mengi sana ambayo unaweza kuwa huyapendi ila inabidi uyapitie sababu ya kitu Fulani, kwa kifupi ni kuwa Erick ni mwanangu”
“Mmmh mwanao? Kivipi?”
“Ni mwanangu wa kumzaa”
“Kheee makubwa, inamaana sio mtoto wa hii familia au ni kitu gani?”
“Sijui, yani sijui hata nikuelezeje. Ngoja nikwambie tena, mimi nilipanga na mtu kubadilisha mtoto wakati najifungua, ila sijui ilikuwaje maana mtoto walisahau kumbadilisha ila nadhani sababu Mungu alitaka kidogo mtoto wangu anuse jasho langu, basi mtoto akiwa na miezi mitatu kasoro akabadilishwa ndio hapo nilipewa mtoto wa huyu mama yenu nimlee na yeye alipewa mtoto wangu”
“Mmmh!!”
“Ila usimwambie mama yenu habari hii, yani Erick katolewa kwenye mikono yangu akiwa na miezi mitatu kasoro ndio nikaletewa Elly nimlee. Kipindi hiko Erick nilimpa jina la Steve ila alivyoletwa huku alibadilishwa hadi jina ili nisimfahamu ila siku zote damu yako ni damu yako tu”
“Kwahiyo wewe hukutamani kuwa na mtoto wako mwenyewe?”
“Sikia, tulipanga abadilishwe kipindi akizaliwa tu na nilijua hivyo maana wakati namchukua sikujua kama ni mtoto wangu kumbe ndio wangu ila alikuwa ni mlizi sana, yani alikuwa analia mno na kunifanya nikeshe usiku, kuna muda mwingine nilikuwa namuacha alie tu bila kuhangaika nae, ila wakaja kuniambia kuwa hawakuweza kumbadilisha wakati mdogo sijui mama Angel alizimia wakati wa kujifungua na bibi mtu alikuja kung’ang’ania watoto wapimwe kwanza, kwahiyo wakati mtoto ana miezi mitatu kasoro ndio wakaniomba ili wakambadilishe, mimi nikiwa nyumbani nikaletewa mtoto mwingine hapo nikaambiwa kazi imeisha. Sikujua kama na yeye nitampenda maana ni wazi sio wangu ila alikuwa tofauti sana alikuwa mtulivu sio mliaji hovyo yani nimemlea Elly kwa raha sana ndiomana nampenda sana”
“Inamaana mama anajua kuhusu hilo?”
“Hajui kitu ndiomana nakwambia kuwa usimwambie, yani siku Erick akikubali nitakuonyesha hadi alama ambayo nilimuweka kabla hajaondolewa katika mikono yangu, hiyo alama nilimuweka kwenye makalio. Akikubali basi ataonyesha, nimemlea mwanangu kwa mwezi miwili sio kwamba sijamlea”
“Ila kwanini ulikubali abadilishwe?”
“Usiombe umasikini ukutawale katika maisha, yani yote hii ni umasikini uliokithiri. Ila kitu kimoja tu ambacho nafanya sawa ni kuhakikisha kuwa Elly namlea katika misingi na maadili mazuri, sina pesa ila Elly anasoma shule nzuri na sitaki apate shida kwani najua hata mwanangu huku analelewa vizuri. Najua ipo siku Erick atanikubali ila hata asiponikubali basi niwe napata japo nafasi ya kumuona tu”
Kwakweli Vaileth alipumua tu maana hakuelewa kabisa, ila alitamani kujua kwa undani zaidi kuhusu maneno ya yule mwanamke, yani aliona ni ngumu sana kwa mtoto kubadilishwa hata kwa mwezi mmoja halafu mwenye mtoto asigundue chochote.

Kwenye mida ya saa tano usiku, walirudi kutoka hospitali na kumkuta Sia pale nyumbani kwao akitaka kujua hali ya Erick ila mama Angel hakupenda kabisa na kumtimua huku akimwambia kama anahitaji kujua chochote kuhusu Erick basi aende kesho yake, kwa kipindi hiko Sia hakuwa mbishi kabisa kwani kwa muda huo huo aliotimuliwa aliondoka zake.
Mama Angel alimpeleka Erick chumbani kwake na kugundua kuwa kitanda cha Erick kina maji na kuuliza imekuwaje, basi Erica alitaka kujielezea ila Erick alisema,
“Nilikuwa na kiu, nikamuagiza Erica aniletee maji, ila alivyonipa mkono ukaniteleza na kile kikombe kikaangukia kitandani”
“Kheee basi, ukalale kwa Angel?”
“Hapana mama, bora nilale kwa Erica”
Mama Angel hakusema neno na moja kwa moja alimpeleka mwanae chumbani kwa Erica na ile ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Erica, kwanza kutetewa na Erick na pia kwa mama yao kukubali Erick kwenda kulala kwake.
Kwa muda huo mama Angel alikuwa amechoka sana, alienda kuoga na kumchukua mwanae, huku akiwaza kwa muda jinsi ambavyo hampi haki inavyotakiwa mtoto huyo maana kutwa kucha anahangaika tu na kumuacha mtoto na mdada wake wa kazi, alikuwa amechoka na muda huo akaamua kulala tu.
Kulipokucha alienda kumuangalia Erick ila alimkuta Erica nae akigoma kwenda shule sababu Erick anaumwa ila akaona ni vyema amlazimishe na hivyo Erica akajiandaa na kwenda shule.
Basi Erica alivyoondoka alitoka zake sebleni huku akilalamika,
“Yani Erica leo ameniletea akili mbovu sana, asiende shule sababu Erick anaumwa kweli!! Khaaaa jamani, mimi kwangu utaenda tu sijali huo upacha wala nini, hakuna maswala ya akiumwa mmoja eti mnaumwa wote, nilimuachia siku ile basi akajua na leo nitamuachia, kajinga kweli haka”
Basi Vaileth akaona ni muda muafaka wa kumuuliza mama Angel maswali yake kwani hata yeye hakuelewa yale maneno ya Sia,
“Mama, unajua siku zote anajiuliza hivi Erick na Erica ni mapacha au ni watoto waliofatana?”
“Kheee jamani Vaileth siku zote upo ndani humu na hujui kama Erick na Erica ni mapacha? Kama ni watoto waliofatana nimewaza vipi kuwazaa hivyo walivyo? Ingeonekana kidogo wamepishana sio hivyo wako sawa kabisa”
“Samahani mama kwa maswali haya, uliwazaa kwa kawaida au kwa kisu?”
“Kwa kisu yani, halafu damu zilinitoka nyingi sana, nilizimia na kuzimia, nakuja kukabidhiwa watoto siamini macho yangu kuona wanangu wakiwa wazuri na nyuso za furaha ila kile kidonda kilinitesa sana ndiomana sikuwa na hamu tena ya kuzaa”
“Kheee pole sana mama, uzazi wako wote ni kisu au hao tu?”
“Jamani, huoni Ester nimejifungua kawaida? Sijui ni sababu ni mmoja, ila wapo wanaozaa mapacha kawaida tu ila mimi walikuwa wanene sana”
“Ila kuhudumia mapacha ni kazi sana, ulikuwa na msichana wa kazi mama?”
“Hapana, hapakuwa na msichana wa kazi kwangu, yani kidonda kilinisumbua. Kipindi najifungua baba yenu hakuwepo kwahiyo aliyenipeleka hospitali ni baba mkwe wangu ila nilipojifungua nilirudi nyumbani, baada ya wiki mbili mume wangu alirudi ila sababu kidonda kilikuwa kikinisumbua sana ilibidi awakatie watoto hati ya kusafiria na tukaondoka nao wote kwenda Afrika Kusini kwaajili ya matibabu yangu, yani watoto tulisafiri nao wakiwa na wiki tatu tu. Ila tulikaa sana huko, tulirudi na watoto wakiwa wakubwa kabisa”
“Kheee kwahiyo mlisafiri na Angel?”
“Ndio maana na yeye alikuwa ni mdogo kwa kipindi hiko, basi kule watoto wangu waliishi vizuri sana, na nilipata huduma nzuri sana, huwezi amini kila kitu alikuwa akifanya mume wangu, yani tumeishi hivyo kwa maisha yote. Ila nilipopona nilikuwa nafanya mwenyewe na tumaishi huko kwa miaka kama mitatu yani tumerudi watoto wakiwa wakubwa kabisa na walizoea maisha ya kule ila walikuja kuzoea na huku. Kwakweli toka uzazi ule sikufikiria kama nitakuja kuzaa tena”
“Ila hawakuwa walizi sana watoto wako?”
“Halafu hawa watoto kama walijua hali ya mama yao vile, hawakuwa walizi hata kidogo, wakishiba tu wanalala hoi yani hawakuwa na tatizo kabisa”
Vaileth akapumua tu, yani toka hapo hakuelewa ila aliweza kuhisi kuwa Sia ana matatizo kidogo kwenye kichwa chake ndiomana kaweza kumwambia maneno kama yale, hakujua ni kitu gani kilimsumbua Sia ila hakuhisi kama Sia ni mzima kichwani.

Muda huu mama Angel alitoka nje na Erick akimwambia kidogo wapate mwanga wa asubuhi, kwahiyo walikaa kwenye kibaraza chao, muda kidogo tu alifika madam Oliva kwakweli huyu madam alifurahi sana kwa siku hiyo kumkuta mama Angel nyumbani kwake, ila kabla hajaongea chochote alifika Sia ambaye alienda pale kumuona Erick ila alivyomkuta madam Oliva alichukia sana na kumuuliza,
“Umefata nini hapa?”
Madam Oliva alibaki kumuangalia tu kwani alimshangaa kumuuliza hivyo wakati nyumbani pale sio kwake, basi Sia akasema tena,
“Au Steve kakutuma uje kumuangalia mtoto wake?”
Madam Oliva alishangaa na kuuliza,
“Mtoto wake?”

Madam Oliva alibaki kumuangalia tu kwani alimshangaa kumuuliza hivyo wakati nyumbani pale sio kwake, basi Sia akasema tena,
“Au Steve kakutuma uje kumuangalia mtoto wake?”
Madam Oliva alishangaa na kuuliza,
“Mtoto wake?”
Sia akajibu kwa haraka,
“Ndio, Erick ni mtoto wa Steve”
Mama Angel alimuangalia na kumuuliza,
“Hivi wewe Sia, leo umekunywa dawa zako za mwezi mchanga? Naona kile kichaa chako kinaanza tena. Mlinzi njoo unitolee huyu kiumbe tafadhari”
Basi mlinzi alifika na kumtoa Sia, ila Erick nae aliamua kwenda ndani kwani kwa kawaida huwa hampendi huyu mama kabisa.
Basi pale nje alibaki mama Angel na madam Oliva ambapo madam Oliva naye alikaa chini pale kibarazani na kuanza kuongea na mama Angel, kwanza kabisa alianza kuongea kuhusu Sia,
“Hivi yule mwanamke ana wazimu au ni kitu gani? Mtoto gani anaemsema ni wa Steve?”
“Achana na yule mwanamke, ni mwezi mchanga yule”
“Na kwanini unamchekea? Nadhani ingekuwa mimi wala asingekanyaga nyumbani kwangu maana muda wote ni kuongea mambo yasiyoeleweka tu kuhusu wewe”
“Nishamzoea tayari, achana nae tu”
“Sijui baba Erick alikwambia au alisahau! Ni hivi kuna siku nilikuona na rafiki yako nikaja kukusalimia, nia yangu ni kuhakikisha kuwa yule rafiki yako ndio yule ninayemdhania au la, nikakuta ni yeye. Yani yule rafiki yako nilimkuta akiongea na huyu Sia na wakipanga mambo mbalimbali na pale nikasema yule sio rafiki mzuri kwako kwani siku zote huwa hata huyu Sia naona sio mzuri kwako”
“Kheee leo naona unafunguka sana madam, haya niambie ujio wako”
“Ujio wangu ni kutaka ukaniombee msamaha shuleni, najua wewe ukiniombea msamaha basi nitarudishwa kazini. Natamani sana kurudi kwenye kazi yangu maana mimi kufundisha kupo kwenye damu, nisaidie nisije nikawa chizi mie”
“Sawa hakuna tatizo, nitaenda na kuongea na uongozi wa shule”
“Asante sana, hizi siku zote nilikuwa nahitaji kuja kuzungumza na wewe kuhusu hilo swala ila kila nikija sikukuti yani leo ndio nimekubahatisha”
“Nina mgonjwa mwenzio, kaka yangu kalazwa, alipigwa huko basi yupo hospitali”
“Jamani masikini dah! Kalazwa wapi?”
Mama Angel alimueleza, basi madam Oliva alimuomba siku mama Angel akiwa anaenda awasiliane nae ili aweze kwenda nae,
“Yani nimejikuta tu naingiwa na imani jamani, utaniambia basi twende wote kumuona”
“Sawa hakuna tatizo nitakushtua”
madam Oliva alimuachia tena mama Angel namba zake kisha akamuaga na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake.

Leo Erica akiwa shuleni, muda wa mapumziko alikaa pembeni akiongea na rafiki yake Samia ambapo Samia alianza kumuhadithia mambo ya nyumbani kwao,
“Mmmh leo mama na baba bado kidogo tu wapigane”
“Duh!! Kisa nini?”
“Sijui imekuwaje ila nimewasikia asubuhi wakizozana, mama akilalamika kwa baba, yani wewe mwanaume umelala kweli unawewesika unaanza kutaja wanawake zako kweli? Sijui Erica jamani umenikera kweli leo. Niliguna kusikia jina lako, kweli baba yangu alale akiweweseka akitaja jina lako!!”
Kisha Samia alikuwa anacheke kidogo, basi Erica akamwambia,
“Itakuwa ni Erica mwingine maana hilo jina ni la watu wengi sana. Ila jamani nyumbani kwetu hata mara moja sijawahi kumsikia mama akigombana na baba”
“Itakuwa labda wanajificha huko, hata mimi sikuwahi kuwasikia ila leo ndio nimesikia wakizozana hivyo yani kidogo tu wangepigana ila mama alitoka maana alikuwa anaenda kazini. Unajua kama mama yangu ni daktari?”
“Aaaah kumbe!! Kwahiyo nyumbani kwenu hamna hata shida!”
“Ndio, ila mkali huyo balaa. Siku ile aliipata barua aliyonijibu Erick jamani nilipigwa na mama hadi nikazimia, akaniambia hataki tena kusikia nikija jina la Erick pale nyumbani kwetu. Kwanza barua Erick umempa?”
“Nilimpa ndio kwani ilikuwa inahusu nini?”
“Nilimuandikia jinsi mama alivyonichapa, jamani mama yangu ana hasira sana hadi basi. Ila mimi nampenda Erick sijui nifannyeje?”
“Kama umekatazwa na mama yako naomba uache, wazazi wana busara zaidi na akikukataza kitu basi ameona kasoro yake”
“Kwahiyo Erick ana kasoro?”
Kengele ya darasani ililia na wote wakarejea kwenye darasa ili kuendelea na vipindi.
 
SEHEMU YA 339

Siku hii mama Angel alijiandaa kama kawaida na kwenda kiwandani kwake, basi alifanya shughuli zote za kiwanda na kuwahi kuondoka, ila nje alikutana na Rahim ambapo Rahim huyu alimsimamisha na kuanza kuongea nae,
“Erica, leo naomba unisikilize wala sitaongea na wewe maneno ya karaha”
“Haya sema unataka nini?”
“Naomba kitu kimoja tu, nahitaji mwanangu Angel anifahamu, nahitaji afahamu ndugu zake, nina watoto wengi wakubwa kwa wadogo, naogopa isije kuwa balaa badae kwa watoto wangu kuoana”
“Si ulisema mtoto akikua atakutafuta mwenyewe wewe! Imekuwaje leo?”
“Hapana Erica, kuna muda mtu unasema kit utu ila badae roho yako inauma kwa kile ulichokisema, nakuomba sana, nakuomba Angel anifahamu baba yake. Nipo tayari kulipa kila kitu ambacho Erick amemuhudumia binti yangu Angel”
Mama Angel alimuangalia bila kumjibu kitu chochote halafu aliondoka zake na muda huo moja kwa moja alielekea nyumbani kwake.
Alishangaa siku hii kufika nyumbani alipoambiwa na Erica kuwa amerudi shule sababu anajihisi vibaya,
“Nini tena mwanangu?”
“Tumbo linaniuma mama”
“Kheee nyie watoto jamani, ndio mmeanza majanga haya kila siku tena!!”
Basi mama Angel akampatia mwanae dawa za maumivu, akasubiri kama tumbo litaendelea kumuuma basi ampeleke hospitali ila Erica hakulalamika tena tumbo ila hata mama Angel hakujua ukweli kama Erica alirudi sababu ya kuumwa tumbo tu au alikuwa na mambo mengine ila hakufatilia.
Kesho yake Erica alienda shule kama kawaida, na siku zote alienda kama kawaida yani lile tumbo lililalamikiwa siku moja tu na wala hakulalamika tena.

Siku hii mama Angel akiwa anatoka kwenye mambo yake, alimuona Sia njiani, akaamua kusimama ili na yeye amuulize kuhusu kupigwa na Erick, basi alisimamisha gari na kumuita ambapo Sia akasema,
“Nilitaka nishangae hiyo roho mbaya umeanza lini kiasi cha kutokutaka kuniona wakati unajua nimepokea kipigo toka kwa mwanao!”
“Ushaanza lawama jamani, mimi nakuuliza tu unaendeleaje na ilikuwaje maana hata sielewi ni kitu gani kinaendelea kwakweli”
Basi Sia alianza kumueleza jinsi Erick alivyoenda na kumpiga na maneno aliyoyaongea, kisha Sia akamwambia mama Angel,
“Naomba leo nikwambie ukweli wa kwanini nakazana kusema kuwa Erick ni mwanangu”
“Eeeeh niambie huo ukweli niusikie, huenda nikakuelewa kuliko kila siku kuanza kutupiana maneno”
“Ipo hivi, mzee Jimmy aliongea na mimi kuwa anataka kubadilisha watoto yani mtoto wangu akupe wewe na mtoto wako anipe mimi, nilimuuliza kwanini alisema kuna kitu anataka kugundua, akanilipa na hela nyingi sana, sababu ya shida zangu nikakubali tu. Sijui siku uliyopelekwa hospitali ni siku ambayo na mimi niliitwa hospitali yani nilifanyiwa operesheni bila ya kuwa na dalili zozote za kujifungua ilimradi tu mtoto atoke, na kweli nilijifungua ila nikamsikia mzee Jimmy akilalamika kuwa umejifungua watoto wa kike tupu, sijui alikuwa akinichanganya akili sijui ni kitu gani, maana alisema yeye hitaji lake ni mtoto wa kiume ndio ana kazi nae, ila nikashangaa nimeletewa mtoto wa kiume, basi nilirudi nae nyumbani kwangu nikijua ni mtoto wako ila yule mtoto alikuwa akilia sana. Ila alivyofika miaezi kama mitatu hivi mzee Jimmy akaniambia kuwa kipindi kile hawakubadilisha maana sijui alienda pale hospitali mama yako na akang’ang’ania awashike wajukuu wake mwenyewe, kwahiyo alisema anataka kubadilisha kwa kipindi hiko, nilimuuliza si utagundua maana mtoto wangu ni wa kiume na wako ni wa kike? Akasema alikosea kuangalia kumbe watoto wako mmoja wa kiume na mwingine ni wa kike, basi tulienda hospitali na mwanangu alichukuliwa baada ya muda nikaletewa mtoto ambaye niliambiwa ni mtoto wako, yani chanzo cha ugomvi wangu na Steve pia ni kuhusu mtoto kuwa kwanini mtoto wa mwanzoni alikuwa ni tofauti na mtoto wa pili? Ndio hapo alipochukia na kuondoka ila sikujali sababu nilikuwa na pesa. Baada ya siku chache mzee Jimmy alisema mmesafiri na kwenda Afrika kusini na watoto wenu, aliniambia nitafurahi sana kwani mwanangu atakuwa na maisha mazuri sana, na jina la Elly kwa mwanangu ni yeye ndiye aliyelitoa alisema sababu ni mjukuu wake, ila anahitaji Elly akikua afanye kisasi kwenu sababu mtamkataa. Sasa baada ya kifo cha mzee Jimmy, roho ilikuwa inaniuma sana, nilitamani Elly awajue wazazi wake halisi na Erick anijue mzazi wake halisi, ndiomana kila siku nasema kuwa Erick ni mwanangu”
“Oooh leo nimekuelewa Sia na nimekuelewa vizuri sana tena sana, ila hapo nadhani kuna kitu kimejificha. Sidhani kama mzee Jimmy alikuwa na lengo la kunikomesha mimi maana aliyekukomesha ni wewe tena kakukomesha vibaya sababu hata huwezi jua mtoto wako wa kweli yuko wapi na huyo Elly ni mtoto wa nani, ila kitu kingine usikute Elly ndio mtoto wako halisi”
“Kwanini?”
“Ni hivi, mimi nilivyojifungua kwa kisu sikuwa katika hali nzuri, kiasi kwamba Erick alikuwa akinihurumia sana na kuona kuwa nahitaji matibabu ya hali ya juu, watoto wakiwa hawajatimiza hata mwezi tulisafiri nao kwenda nje kwaajili ya matibabu na tulikaa huko kwa miaka kama mitatu hivi, haya huyo Erick kabadilishwa muda gani? Hebu jitafakari tena kuna kitu mzee Jimmy alikuficha, yani marehemu huwa asemwi vibaya ila naweza kumsema vibaya yule mzee Jimmy, mzee ni mpuuzi sana yule dah! Ndiomana sikuwahi kumpenda ingawa alikuwa ni mkwe wangu. Ngoja tu niwahi nyumbani kwangu”
Mama Angel aliamua kumuaga Sia na kuondoka zake kwenda nyumbani kwake yani hata hakumsikiliza zaidi.

Siku ya Ijumaa kama ambavyo mama Angel alipanga na madam Oliva, basi moja kwa moja alimfata ili waende nae hospitali na yeye alikubali kweli kwenda hospitali kumuona huyo Derrick.
Walivyofika hospitali walikuta hata Derrick karuhusiwa siku hiyo kwahiyo ndio wanajiandaa kwaajili ya kuondoka, ila muda kidogo alifika mama Sarah ambapo alipofika tu madam Oliva alionekana kuchukizwa sana kumuona mama Sarah, kiasi kwamba alimsogelea kwa hasira na kumkunja yani pale hospitali wote walikuwa wakishangaa tu lile swala.

Walivyofika hospitali walikuta hata Derrick karuhusiwa siku hiyo kwahiyo ndio wanajiandaa kwaajili ya kuondoka, ila muda kidogo alifika mama Sarah ambapo alipofika tu madam Oliva alionekana kuchukizwa sana kumuona mama Sarah, kiasi kwamba alimsogelea kwa hasira na kumkunja yani pale hospitali wote walikuwa wakishangaa tu lile swala.
Mama Angel akakumbuka kitu na kwenda karibu na kuwaachanisha kisha alimvuta madam Oliva pembeni na kumwambia,
“Madam, wewe ni mwalimu tafadhari usijiondolee sifa yako kwa hizi fedheha, ni aibu kubwa sana kwa mwalimu kama wewe kuonekana kupigana na mtu au kurushiana maneno na mtu njiani”
Basi madam Oliva alipumua kidogo na kusema,
“Kwaheri, siwezi kukaa tena hapa hospitali”
Ila mama Nagel alielewa na kumruhusu tu aondoke kwani madam Oliva alishamsimulia kila kitu kwahiyo muda huo alikuwa ameunganisha matukio tu.
Derrick nae alishangaa kumuona mama Sarah kwani hakumuona kabla sababu mama Sarah alifika kipindi Derrick akiwa hoi kabisa na tangu kapata unafuu hakufika tena hadi siku hii ndio alionekana tena kwenda kumsalimia, basi Derrick akamwambia mama Sarah,
“Manka, wewe mwanamke ni mjinga sana umekuja kufanya nini hapa?”
Wote wakamuangalia kisha mama yake akamkataza na kumwambia,
“Laiti ungejua kuwa mwanamke huyu alijitolea kukuhudumia wala usingemsema”
“Kwani niliomba msaada wake? Hamjui tu huyu mwanamke ana akili mbovu kiasi gani, hamjui tu nawaambia”
Basi mama Sarah hakutaka kuongea mengi na kutaka kuondoka zake, ila Derrick alisema anahitaji kuongea na mwanamke huyo ambapo walitoka nje, kisha kupanda kwenye gari na safari ikafanyika hadi nyumbani kwakina Derrick, na huko walitoa upenyo kidogo wa mama Sarah kuongea na Derrick,
“Samahani Manka, mtoto wangu yuko wapi?”
“Samahani Derrick, huujui ukweli tu”
“Ukweli upi?”
“Hukuzaa na mimi, kiukweli sina mtoto wako”
“Sikuelewi Manka, najua wazi ile mimba ilikuwa ni yangu ila mtoto wangu ulienda na kumpa baba mwingine sababu ni tajiri na mimi ni masikini ukaona sifai, ila Manka nina kila sababu ya kumfahamu mtoto wangu na pia kuna kila sababu ya mtoto wangu kunifahamu mimi. Unajua kwanini nimepigwa sana?”
“Sijui?”
“Sababu mimi ni tapeli, unajua kwanini mimi ni tapeli?”
“Sijui”
“Sababu yako Manka, nimejaribu kufanya kazi tofauti tofauti ila bado malengo yangu ya kuwa tajiri hayakutimia, pale waliponifukuza kazi ndio wakaitibua kabisa akili yangu kwani malengo yangu ni kuwa tajiri ili nikikutana na wewe uone kweli Derrick amebadilika, nasema wazi kuwa wewe Manka ndio sababu ya kunifanya mimi niwe tapeli, kwakweli Manka ni asilimia kubwa sana umechangia katika kuharibu maisha yangu. Nadhani unamkumbuka yule mwanamke aliyekukunja pale hospitali, nina uhakika unamkumbuka sana tu”
“Namkumbuka ndio”
“Yule mwanamke alinipenda sana ila nilimuacha kwaajili yako Manka, ila wewe ukanifanyia mambo ya ajabu sana kwa kwenda kuuza mtoto kwa mwanaume mwingine, kwakweli sikupenda kabisa ulichofanya wala nini”
“Unanilaumu bure tu, unaacha kujilaumu kuhangaika kwako na wanawake unakazana kunilaumu mimi, kuna kitu nilichokuwa nahitaji kwako kwa kipindi hiko, ukikaa chini na kutafakari utakijua, ila sijaja kukuona ili unipe lawama zako, kwaheri”
Manka aliinuka na kutoka nje ambapo aliwaaga na wakina mama Angel ila mama Angel alimfata mama Sarah ili amuulize vizuri, alimuuliza,
“Inamaana Sarah ni mtoto wa Derrick?”
“Hapana, ila baba wa Sarah hakuhusu”
Mama Sarah hakuangalia hata nyuma alivyolitoa jibu hilo kwani moja kwa moja aliondoka zake, basi mama Angel alibaki akimshangaa tu kwa muda kidogo kisha akarudi tena nyumbani kwakina Derrick ila hakutaka kukaa sana aliongea kidogo tu na kusema anahitaji kuongea kidogo na Derrick pia ili amuage.

Mama Angel aliingia kuongea na Derrick kwa muda huo, basi alimuuliza swali la kwanza kabisa,
“Huyu Manka ndiye mwanamke uliyezaa nae?”
“Ndio ni yeye, ila mtoto kamkabidhi mwanaume mwingine”
“Dah pole sana, ila usijali nitafatilia jambo hili. Na vipi kuhusu mtoto wa Oliva, wewe ndiye baba au?”
“Mimi ndiye baba wa mtoto wa Oliva, ila sijui ni utoto sijui ni kitu gani, unajua kipindi kile sikuwa na kazi yoyote, bora yako hata ulikuwa ukifanya kazi kwa shemeji yako halafu akaja Erick na kukukomboa tofauti na mimi nilikuwa na shida sana, nikaona nikichukua majukumu ya kulea mtoto itakula kwangu, wakati huo Manka nae akisema ana mimba yangu basi ikabidi Oliva nimtoe sadaka, ila sikupenda ni umasikini tu”
“Duh!! Huu umasikini ungekuwa una sauti basi ungeongea maana watu mnafnaya mambo ya kijinga halafu mnasingizia umasikini, kubali tu ulifanya makosa na sio kusingizia umasikini. Mimi nitajaribu kupoteza muda wangu na kwenda kuongea na Manka pia kwenda kuongea na Oliva”
“Dah!! Utakuwa umenisaidia sana, nataka wanangu watambue uwepo wangu”
Basi mama Angel kwa muda huo aliamua kumuaga na kuwaaga wote kwenda zake nyumbani kwake kama kawaida.
Alipofika alikuta watoto wake wote wameenda kulala, basi alimuuliza Vaileth,
“Mbona wanalala mapema sana hawa viumbe wangu?”
“Sijui ila namuona Erica kama hizi siku za karibuni kabadilika kiasi, tofauti na ambavyo huwa akirudi shule anaanza kueleza habari mbalimbali ila toka siku ile karibu akiumwa na tumbo basi amekuwa akirudi tu anaishia huko huko chumbani kwake, akitoka ni kula kidogo na kurudi chumbani kwake, bora hata Erick, ila hata Erick kaniambia kuwa Erica alimfukuza chumbani kwake wakati akitaka kwenda kumuuliza tatizo linalomfanya awe mpole kiasi hiko”
“Kheee anamfukuza hadi kaka yake?”
“Ndio, sijui ana tatizo gani”
“Jamani huu ubusy nao loh!! Nakosa hata muda wa kukaa na watoto kuuliza tatizo ni nini, hebu nikamuangalie kwanza”
Basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica na kumuamsha kisha kumuuliza kitu gani kinachomsumbua ila Erica alijibu kuwa hana tatizo lolote na yupo sawa kabisa tu, basi mama Angel alimuacha pale mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kujipumzisha.
Basi muda kidogo akapigiwa simu na rafiki yake Johari na kuanza kuongea nae,
“Kwakweli nakushukuru sana shoga yangu kule uliponipeleka, nimeweza kufungua mawazo yangu na sasa natengeneza vitu vyangu mwenyewe na kuvisambaza”
“Oooh hongera sana, hiyo ni habari njema kwakweli”
“Nakwambia shoga sasa hivi na mimi nitakuwa juu kabisa ya kinara, yani sasa hivi nitakufikia ila tutakuwa na sifa tofauti maana wewe ni hela za mumeo lakini mimi ni hela zangu nilizozitolea jasho”
“Jamani Johari hata mimi nachakarika sio kujikalia tu nyumbani”
“Uchakarike wapi? Wenzio tulizaa tukaacha na kupumzika huku tukiwaza vya kufanya, sasa wewe bado unazaa kweli kuna kuchakarika hapo? Kila utakapokuwa maziwa tu yanakuchuruzika”
“Hayo mambo yalikuwa kwa mama zetu sio karne hii ndugu yangu, hakuna mwanamke wa kujibweteka. Watu na watoto migongoni wanachakarika sembuse mimi”
Basi wakaongea pale na kuagana, ila mama Aliwaza kitu kuhusu ofisi yake ambayo hakwenda kwa kitambo kidogo, akaona bora kesho yake ajitahidi aende kuangalia ofisi yake inaendeleaje nayo, hakutaka kujibweteka ndiomana alikuwa akichakarika.

Kulipokucha tu, mama Angel alijiandaa moja kwa moja na kwenda kiwandani kwani alishapanga siku hii aende kiwandani halafu akaangalie na ofisi yake ipo katika hali gani, kwahiyo alivyomaliza shughuli za kiwanda moja kwa moja aliamua kwenda kwenye ofisi yake ili kuangalia mambo yanaendaje kwenye ofisi yake, basi alifika pale na wafanyakazi wake walifurahi sana kisha aliingia ofisini na kuanza kuangalia kazi zake moja baada ya nyingine, alitumia muda mrefu kidogo, kiasi kwamba alipanga siku hiyo awahi kurudi nyumbani kwake ukizingatia ni Jumamosi lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alikuta kazi nyingi zikiwa zinamsubiria, kwahiyo aliendelea nazo tu kwa muda huo.
Muda kidogo alipigiwa simu na mume wake na kupokea ile simu,
“Uko wapi mama Angel?”
“Oooh sikukwambia mume wangu, nimekuja mara moja kwenye ofisi yangu huku”
“Mama Angel, mimi kukuagiza mara moja ofisini kwangu sikuwa na maana kuwa muda wote unatakiwa kuwa ofisini, hebu tenga muda vizuri mke wangu, kuna watoto pale wanahitaji malezi yako ya karibu sana, na kuna mtoto mdogo Ester anahitaji maziwa yako muda wote, kweli kumuacha mtoto mdogo vile muda wote jamani mke wangu!”
“Nisamehe sikukwambia ila Ester nilimkamulia maziwa”
“Jamani mke wangu kwanini lakini? Wanawake ambao waume zao hawajiwezi wahangaike halafu na wewe uhangaike kweli jamani dah!”
“Nisamehe mume wangu”
“Oooh yani katika vitu vyote basi ni swala la kuomba msamaha, jamani Erica nakusifu kwa hilo ni rahisi sana kwako kuomba msamaha bila ya kujali uzito wa tatizo wala nini. Hivi unajua kinachoendelea kwa Erica mdogo!”
“Kitu gani hiko?”
“Unaona sasa, hata mwanao anasumbuliwa na kitu gani hujui sababu unakosa muda wa kuongea nae kama mama umuelekeze mema yanayotakiwa. Ni hivi kumbe Erica kakua, yani kamfata Sia ndio ambaye anampa maelekezo ya kufanya kitu gani na kitu gani ila wazazi hatujui chochote. Mke wangu naomba muda huu funga hizo kazi zako, rudi nyumbani waangalie watoto wangu, nahitaji watoto wetu wapate malezi bora”
Mama Angel akapumua, kwanza kidogo habari ya Erica ilimchanganya, basi aliagana na mumewe na kufunga kazi halafu akaondoka muda ule ule.

Mama Angel alikuwa njiani akifikiria sana, kuwa mwanae amekuwa halafu kashindwa kumwambia yeye na kwenda kumwambia Sia!! Kwakweli hapa alishangaa sana, alipokuwa anakaribia nyumbani kwake alikutana na Sia njiani, basi akasimamisha gari ili amuulize vizuri,
“Yani mwanangu kakua kaja kukwambia wewe?”
“Usishangae, siku zote mtoto huangalia sehemu ambayo ataweza kupata msaada kwa urahisi zaidi”
“Kwahiyo kwako ndio sehemu ya urahisi kwake kupata msaada kuliko mimi mama yake?”
“Sijui, ila nadhani kuna kitu huelewi kuhusu mwanao, anapenda sana kusikilizwa, anapenda sana kupewa kipaumbele na sio kuachwa nyuma nyuma, aliniambia kuwa akikwambia chochote huwa unamshushua sana ndiomana ameogopa kukwambia hili. Kwa kifupi ni kuwa mwanao kakua, mimi kama mzazi nimetumia muda wangu vizuri tu katika kumuelekeza swala zima la ukuaji na swala zima la kujistiri, kwakweli aliondoka akiwa na furaha na uelewa wa hali ya juu”
“Haya asante”
Mama Angel alirudi kwenye gari na kuanza kuelekea nyumbani kwake.
Wakati amefika nyumbani kwake, kuna mtu alimkuta ndio anatoka, mtu huyo alikuwa ni wifi yake Tumaini, basi alishuka kwaajili ya kumsalimia pale, wakaongea mawili matatu,
“Mbona mapema sana wifi yangu?”
“Unajua nimekuja muda sana huku nyumbani kwako ila hukuwepo na nilijua leo nitakukuta nyumbani”
“Ni kweli ungenikuta ila sijui hata nikueleze vipi, majukumu haya ndugu yangu”
“Mmmh na wewe jamani, hayo majukumu ni majukumu yapi? Kusimamia watu nayo ni majukumu, mbona kutaka kujitia kazi ambazo zinakuzidi nguvu jamani! Mtoto unamuacha na Vai kila siku, kuwa na msichana wa kazi imekuwa tatizo? Tena wakati mwingine unaondoka asubuhi sana na kurudi usiku, sio siri wifi yangu jirekebishe, hatukatai watu tunakuwa na majukumu ila wakati mwingine tunatakiwa kuwa makini na majukumu yetu tunayoyafanya, wewe ni mama na unatakiwa kuwa makini sana katika ulezi wako”
“Nimekuelewa wifi yangu ila nipo makini”
“Wapi ndugu yangu? Makini!! Ungeshindwa kujua kuwa mtoto wangu kwasasa amekuwa mkubwa kweli?”
“Unajua Erica huwa nazungumza nae mambo mengi sana kiasi hata sielewi ni kwanini hajaniambia kuhusu hilo swala jamani, unaweza kunilaumu bure tu lakini mtoto mwenyewe ndio tatizo”
“Hapana na wewe kutokuwa makini, kwanza kwa kipindi chote hiki si ungekuwa ukijitafuti mwanangu bado tu kukua, mwanangu bado tu. Kuna watoto wanakua wakiwa darasa la sita, wengine la saba ila Erica kachelewa kiasi ingawa hajachelewa sana ila ungekuwa unajiuliza kama mama, na mtu kama Erica ungekuwa umemfundisha baadhi ya mambo kiasi kwamba angeona na kukufata wewe moja kwa moja. Unajua shuleni wanajifunza mengi sana, basi yeye kashajua mambo mbalimbali ndiomana alivyoona kaona bora akamwambie mama anayemsikiliza. Halafu kitu kimoja ambacho hujui kuhusu Sia, yani yeye akijua mtu huyu anapenda sana kusikilizwa basi atajifanya kumnyenyekea na kuwa nae karibu kiasi kwamba mtu huyo lazima awe anaenda kwake tu sababu ananyenyekewa sana, humsomi mwanao, unaacha mpaka machizi wajue kuhusu mwanao”
“Nisamehe wifi yangu tafadhari”
Aliamua kuagana nae maana Tumaini alisema kuwa ana haraka kwahiyo aliagana nae na yeye kuingia ndani kwake.

Mama Angel alipoingia ndani tu, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambapo hakumkuta chumbani kwa muda huo na kutoka kumuuliza Vaileth,
“Kwani Erica yuko wapi?”
“Oooh yupo kule bustanini na Erick”
Basi mama Angel akatoka na kwenda bustanini na kukuta kweli Erica na Erick wamekaa ila walivyokaa kama watu ambao sio ndugu kabisa, halafu kama maadui vile kwani walikaa mbalimbali, basi alipofika aliwasalimia pale na kuwaauliza kwanini wamekaa vile mbalimbali, Erick alimjibu mama yao,
“Mama, sijui kwanini jamani ila Erica anafanya kazi ya kunikwepa tu sijui hata tatizo ni kitu gani, nilimfata chumbani kwake ili niongee nae ndio akaja huku, nimemfata napo ananikwepa”
“Sawa, naomba niongee kidogo na Erica, wewe nenda tu ndani Erick”
Basi Erick aliondoka na mama Angel alisogea karibu na mwanae na kuanza kuongea nae, kwanza alianza kumuelekeza kuhusu ukuaji na pia alimuelekeza kuhusu swala zima la kujiweka katika usafi, kisha kuanza kumuuliza,
“Mwanangu kwanini lakini hukuniambia kama umekua?”
“Niliogopa mama”
“Uliogopa nini sasa?”
“Ungesema nimeanza umbea tena maana ulisema nisikuletee tena maneno ya umbea”
Ilibidi mama Angel afanye kazi ya kumuelimisha mtoto wake kuwa kwanini alisema vile na kuzidi kumuelekeza mtoto wake jinsi ya kuishi vyema na wazazi,
“Yani mzazi ndio mtu wa kwanza wa kujua chochote kinachoendelea katika maisha yako, haya ni kwanini unamkwepa hivyo Erick?”
“Yule mama kaniambia kuwa, nikiwa kwenye hali hii natakiwa kuwakwepa kabisa wanaume, sababu ukikaa nao karibu watagundua ndiomana namkwepa Erick”
“Dah! Mwanangu unahitaji kupata somo la ziada kwakweli ili uweze kuielewa hiyo hali uliyokuwa nayo, ila usijali tupo pamoja”
Kisha mama Angel alianza kumuelekeza mwanae namna ya kuendenda katika hali kama ile na jinsi ya kuishi na watu wote, na alimfundisha kutambua kuwa ile ni hali ya kawaida tu sema inahitaji usafi tu ili kuepuka harufu mbaya, na pia kuepuka magonjwa mbalimbali maana mtu ukiwa msafi ni ngumu kupatwa na magonjwa mengine kwahiyo kuna baadhi ya magonjwa yanaepukika kwa usafi tu”
“Sawa mama, nimekuelewa”
Basi mama Angel alimtoa hofu yoyote ambayo Erica alikuwa nayo, kisha ndio akaenda ndani sasa kufanya mambo yake mengine.

Usiku wa leo, Erick alienda tena kuongea na Erica ili ajue ni kwanini Erica alikuwa akimkwepa sana kwa kipindi hiko, alimkuta muda huo akiandaa nguo ya kuvaa kesho yake, basi alianza kuongea nae,
“Kwanini Erica ulikuwa unanikwepa? Kwanini ulikuwa ukinifukuza humu chumbani kwako?”
“Samahani Erick, naomba unisamehe bure, ila sikuwa najihisi vizuri”
“Yani ulishindwa kuniambia kama unaumwa? Ni mara ngapi unaniambia mambo yako Erica halafu ushindwe tu kuniambia kuwa unaumwa!”
“Sio ugonjwa kama ugonjwa ila nilikuwa naumwa ukubwa”
“Kheee ukubwa ndio nini?”
“Kama hujui potezea”
“Mmmh ndio kubunja ungo nini!”
“Toka zako bhana, mimi sipendi mtu aniambie hivyo”
“Basi sirudii tena, ila unaendeleaje kwasasa?”
“Naendelea vizuri tu, natafuta nguo ya kuvaa kesho kwenye ibada, njoo unisaidie basi”
Moja kwa moja Erick alimsaidia Erica kuchagua nguo ya kuvaa, na nguo aliyomchagulia ni ile ambayo aliwahi kumnunulia kwani alipenda tena kumuona katika nguo hiyo, kwahiyo walikubaliana kuwa kesho yake atavaa nguo ile, na muda ule Erick aliondoka na kurudi chumbani kwake.
Kulipokucha kama kawaida walijiandaa vizuri kabisa na kwenda Kanisani, siku hii waliondoka wote pale nyumbani hata Vaileth aliondoka pia kwahiyo hakuna mtu ambaye alibaki nyumbani kwa muda huu.
Ila leo ibadani kila mtu alikaa sehemu yake, muda kidogo Erica aliinuka ili kwenda maliwatoni, ila muda mwingi Erick alikuwa akimuangalia Erica kwahiyo alikuwa kama anaangalia muda alioinuka na muda atakaorudi.
Erica moja kwa moja alienda maliwatoni, ila wakati anatoka kufika njiani tu kuna mtu alimshtua na kumsimamisha, alipogeuka mtu huyu alikuwa ni Bahati, basi alianza kusalimiana nae,
“Kheee unafanya nini hapa kanisani?”
“Huwezi amini, nimekaa kwetu nimejikuta nakufikiria sana, basi nikasema leo nije tu hapa angalau nikuone. Kidogo moyo wangu umeridhika”
“Oooh sawa, basi mimi naenda”
“Hapana, usiende, naomba tuongee kidogo”
Basi Bahati akamvuta mkono Erica na kutoka nae pale kwenye eneo la kanisa kidogo na kuanza kuongea nae,
“Unajua nakupenda sana, nahitaji uwe mpenzi wangu”
“Kheee jamani, mimi haya mambo sijazoea kabisa, ni maneno gani unaniambia hayo?”
“Nahitaji uwe mpenzi wangu Erica, nakupenda sana”
Muda huo huo alitokea Erick mahali pale maana alikuwa akimtafuta Erica baada ya kuona kachelewa kurejea ndani ya Kanisa, basi alifika na kumshika mkono yani hakuongea kitu chochote zaidi ya kwenda nae tena Kanisani tu kwa muda huo.

Wakati wanarudi nyumbani, mama Angel alimuona madam Oliva kwahiyo aliwaacha watoto wake kwenye gari waendelee na safari ya kurudi nyumbani halafu yeye akashuka na kumfata madam Oliva,
“Oooh bora nimekuona hapa muda huu”
“Kuna mahali nimetoka, halafu kuna kitu nilikuwa nasubiria hapa”
“Najua hatukupata muda mzuri wa kuongea ile juzi, naomba tusogee kidogo pale kwenye mgahawa naomba muda wako kidogo tuzungumze”
Madam Oliva alikubali na moja kwa moja walienda kwenye mgahawa wa hapo karibu na kukaa huku wakianza kuzungumza,
“Kwanza kabla ya yote, kuna kitu nilihisi siku ile. Nadhani yule ndio mwanamke aliyeharibu penzi lako na Derrick, je nipo sawa?”
“Ni sawa kabisa”
“Ila kwasasa una maisha yako, umelea mwanao nina hakika umesamehe hayo yaliyopita, ila jamani kwanini ulimkunja tena?”
“Mama Erick, yani yule mwanamke alinitenda vibaya sana. Kwanza kawa mpole ila alikuwa na nyodo sana yule mwanamke”
“Haya tuachane na habari zake, vipi Derrick anaweza kumuona mtoto wake?”
“Yule ni mwanangu na sio mtoto wa Derrick, mtoto yule anatumia jina la mbele la babu yake yani baba yangu, anaitwa Paul Paul, kiukweli huyo Derrick sitambui kama nilizaa nae katika maisha yangu ila ninachotambua ni kuwa kuna msumbufu mmoja nilikutana nae katika maisha, sina muda nae kabisa na simtaki tena”
“Naelewa kabisa kuhusu hilo, ila kuna umuhimu wa mtoto kumfahamu baba yake”
“Mama Erick hebu jaribu kidogo kukaa nafasi yangu. Eeeeh nimekumbuka kitu, yule Rahim aliniambia kuwa amezaa na wewe, nina uhakika mtoto aliyezungumziwa ni Angel, je anamfahamu baba yake? Ingekuwa anamfahamu, je Rahim angekuwa analalamika hadi leo kuhusu Angel? Wanawake tunapitia mengi sana ndiomana kuna muda tunafanya maamuzi magumu hata kuyafikiria, kwakweli mimi niache tu na furaha yangu ila Derrick asahau kabisa kama kuna mtoto yoyote alizaa na mimi”
Mama Angel alipumua kidogo kwani yale maneno yalimuingia vilivyo ukizingatia ni kweli yeye hataki hata kidogo Angel afahamiane na baba yake, yani yupo radhi Angel asimfahamu baba yake maisha yote, sababu tu ya mambo ambayo bado anayakumbuka katika akili yake kuwa ni mabaya na hakupaswa kutendewa na Rahim ila yeye mwenyewe alikuwa kumbembeleza mwenzie ampeleke mtoto kwa baba yake, ila maneno ya sasa yalimuingia kwenye kichwa vilivyo na kuamua kuacha kwanza, alimwambia
“Madam, hata sikulazimishi wala nini nilikuwa naongea tu. Najua alifanya makosa sana juu ya hilo, kutelekeza mtoto wake jamani! Kwakweli hajafanya vizuri kabisa”
“Ndio hivyo, kwasasa nataka kuandaa harusi yangu na Steve, nahitaji mimi na Steve tuanze kuishi rasmi kama mke na mume”
“Ila naomba nikushauri kitu”
“Kitu gani?”
“Kwanza kabisa mtafutie shughuli ya kufanya, si vizuri mwanaume kushinda nyumbani siku nzima kufanya shughuli za mwanamke, afanye kama kusaidia ila sio ndio kusema inakuwa kazi yake moja kwa moja. Msaidie kwa hilo ndugu yangu”
Haya maneno yalimuingia madam Oliva na kuahidi kuwa atayafanyia kazi, basi waliagana na kuondoka zake.

Mama Angel aliona ni vyema kama siku hiyo hiyo akiitumia pia kuonana na mama Sarah ili kuongea nae kuhusu mtoto wa Derrick, basi akachukua bodaboda pale na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwa mama Sarah.
Alimkuta mama Sarah yupo nje akimwagilia maua yake, basi alimsogelea na kumsalimia, kisha kumuomba kidogo waongee,
“Mama Sarah, nina maongezi na wewe kidogo tu. Nakuomba kidogo tukae mahali tuweze kuzungumza”
“Kuzungumza kuhusu nini?”
“Mmmh kuhusu baba mzazi wa Sarah”
“Wewe anakuhusu nini huyo baba mzazi wa Sarah?”
“Nataka kufahamu ukweli”
“Ukweli upi?”
“Je baba mzazi wa Sarah ni Derrick?”
“Hapana, baba mzazi wa Sarah ni mume wako”
Mama Angel alijikuta akipumua tu kwa nguvu maana kama kitu kiligonga kwenye moyo wake.

Alimkuta mama Sarah yupo nje akimwagilia maua yake, basi alimsogelea na kumsalimia, kisha kumuomba kidogo waongee,
“Mama Sarah, nina maongezi na wewe kidogo tu. Nakuomba kidogo tukae mahali tuweze kuzungumza”
“Kuzungumza kuhusu nini?”
“Mmmh kuhusu baba mzazi wa Sarah”
“Wewe anakuhusu nini huyo baba mzazi wa Sarah?”
“Nataka kufahamu ukweli”
“Ukweli upi?”
“Je baba mzazi wa Sarah ni Derrick?”
“Hapana, baba mzazi wa Sarah ni mume wako”
Mama Angel alijikuta akipumua tu kwa nguvu maana kama kitu kiligonga kwenye moyo wake.
Mama Angel alimuangalia tena mama Sarah na kumuuliza tena,
“Unasema Sarah ni mtoto wa nani?”
“Inamaana hujanisikia au? Sarah ni mtoto wa mume wako, Sarahni mtoto wa Erick, unataka nini lingine nikujibu?”
Mama Angel akapumua tena na kumuuliza mama Sarah tena,
“Hivi wewe si ndio umemuonyesha Sarah kuwa baba yake ni mzee Jimmy? Halafu saa hizi unasema ni mtoto wa Erick, wakati huo huo inasemekana kuwa ni mtoto wa Derrick. Lipi ni lipi?”
“Mimi ndio mama mzazi wa Sarah, na hao wanaume wote watatu nimetembea nao, na mimi ndiye ninayejua ukweli halisi wa Sarah. Ukweli ni kuwa huyu ni mtoto wa Erick, nimemaliza. Kama imekuuma chukua chupa saga halafu meza vipande vyake”
Mama Angel alikaa kimya kwa muda halafu mama Sarah aliendelea kuongea,
“Kwanza wewe sio wa kushangaa kuhusu mimi na Erick, mbona mahusiano naye nilianza kitambo sana, kwani mimba ngapi za Erick nilizotoa? Yani wewe unaongea kama unatapika tu, hata hukutakiwa kufata ushahidi kwangu. Jiongeze tu huyu ni mtoto wa Erick ndiomana anakupenda na wewe unampenda, ndiomana akikuletea vitu unafurahi sababu damu ya Erick unayempenda ipo ndani yake, na mimi nampenda sababu nampenda Erick na kumpenda siachi wala usijidanganye kusema kuwa nimemuacha Erick, maana nikikutana nae lazima nikumbushie enzi”
Safari hii mama Angel hakujibu kitu wala hakusema neno zaidi ya yeye kuondoka zake tu, aliondoka moja kwa moja na kwenda kusimamisha bodaboda na kuelekea nayo nyumbani kwake kwani alichoka mwili na roho kwakweli.

Mama Angel alifika nyumbani kwake na kuwakuta wanakula, walimkaribisha mama yao nae alienda kujumuika nao kula ila alionekana kuwa na hasira sana, ilibidi Erica amuulize mama yake,
“Mbona mama unaonekana haupo sawa?”
“Ni kweli sipo sawa mwanangu, matatizo tu ya dunia”
“Nini mama?”
“Aaaaah msijali kitu”
Kisha mama Angel alikula kidogo tu na kuondoka zake kuelekea chumbani na kwenda kuoga maana siku hii alitangulia kula kabla ya kuoga, ila akiwa chumbani kwake, leo kwa mara ya kwanza alifatwa na Erick mdogo ambaye alienda kumuuliza mama yake kuwa tatizo ni kitu gani kumbe hata yeye aliona tofauti ya mama yake ukilinganisha na siku zote,
“Kwani mama tatizo ni nini? Unaonekana huna raha, yani kama una dukuduku moyoni tatizo ni nini?”
“Kuna mtu nilienda kuongea nae leo ila alichonijibu sijapendezewa kabisa”
“Mtu gani na alikujibu nini mama?”
“Yani mama Sarah ana tabia mbaya, najuta kumfahamu yule mwanamke, kanichefua kabisa”
“Mmmh kafanyaje kwani mama?”
“Wewe bado mdogo Erick, kuna mambo hutakiwi kuyatambua kwasasa, kwahiyo neneda kalale tu”
“Lakini mama….”
Simu ya mama Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga ni mume wake, ilibidi Erick atoke na kumuacha mama yake akipokea ile simu na kuanza kuongea nayo;
“Kheee mke wangu mbona leo unaongea kama mgonjwa?”
“Dah! Nilienda kuongea na Manka bhana aka….”
Mumewe akamkatisha na kumwambia,
“Tafadhari usiniambie alichokwambia Manka maana sitaki hata kukisikia ila mke wangu tafadhari naomba uwe na amani katika moyo wako, acha kuwaza vitu tofauti ambavyo havipo kabisa. Unababaishwa na maneno ya Manka ya kazi gani hayo? Muone Manka ni mjinga kama wajinga wengine, umeweza kupotezea maneno ya Sia, ndio maneno ya Manka yatakuumiza kichwa kweli mke wangu! Hebu achana nayo, hata hivyo mimi karibia narudi kwahiyo usijali kitu”
Kidogo mama Angel akawa na furaha na kuongea vizuri na mume wake kwa wakati huo.
 
SEHEMU YA 341

Kulivyokucha, leo wakati Sarah akijiandaa kwenda shule, mama Sarah nae alijiandaa na kwenda nae pamoja huku akimwambia kuwa anataka kumtambulisha kwa huyo mwanafunzi mgeni aliyempeleka, ila alipofika shuleni tu alipigiwa simu na Sia kuwa waonane, ikabidi amuache Sarah aingie shuleni halafu yeye alienda kuonana na Sia ambapo alifika kwenye mgahawa wake, basi alianza kuongea nae,
“Biashara yangu ndio hii ya mgahawa, ilikuwa inaenda vizuri sana ila hapa katikati ikasita kidogo kwani nilikuwa sifanyi vizuri kutokana na kipigo nilichopata”
“Kipigo tena? Ulipigwa na nani?”
“Yani siku hiyo nikiwa hapa mgahawani, alikuja Erick mdogo yani mtoto wa Erica, uwiiii sijui alisikia maneno gani kwa mama yake, yani alinipiga ngumi hizo balaa, nilianguka akanipiga mateke yasiyokuwa na idadi, baada ya hapo mwili wangu ukawa dhaifu sana maana nilikuwa naumwa mbavu na mwili wote”
“Duh pole sana, yani Erick huyo ndio kakupiga kiasi hiko?”
“Ndio, Erick huyo, kanipa kipigo sana. Kanidhalilisha mno hadi nikashangaa kwanini ameamua kunifanyia hivi alivyonifanyia jamani, kwakweli sina raha kabisa kwa hiki ambacho Erick kanifanyia”
“Oooh pole sana”
“Sasa, nimefatilia uhamisho kule shule aliyokuwa anasoma Elly, nimeambiwa ana deni la laki tatu, yani hata sielewi, na biashara bado haijakaa sawa.”
“Oooh pole jamani, ila hiyo sio tatizo maana nitalipa. Nielekeze tu shule ambayo alikuwa akisoma Elly awali au twende wote ili nikamalize mambo yote”
“Ngoja basi niache vizuri hapa”
“Au nielekeze tu”
Ilibidi Sia amuelekeze tu mama Sarah, ambapo alipoondoka muda huo moja kwa moja alienda hadi shule ambayo Elly alikuwa akisoma awali, na kumaliza kila kitu huko.
Ila wakati anakaribia kuondoka alikutana na mwalimu wa nidhamu wa pale shuleni ambaye alikuwa ni mwalimu Haruni, ila walivyoonana tu waliweza kukumbukana,
“Kumbe Haruni unafundisha siku hizi?”
“Ndio, je wewe uliacha ualimu?”
“Hapana sijaacha, ila mara nyingi huwa nafundisha mara moja moja kwa watoto wanaohitaji kufundishwa twisheni za binafsi yani mimi ndio huwa nafanya mambo hayo”
“Kheee madam, yanalipa?”
“Tena sana tu, kumbuka najitoa kwenda kumfundisha mtoto mmoja tu kwahiyo nalipwa hela ndefu, hata hivyo nina miradi yangu mingi tu. Na pia nina shule yangu”
“Hongera sana, wengine bado tumegangamala na kazi za kuajiriwa ndugu yangu”
“Ila vipi, hujaoa hadi sasa?”
“Aaaah historia ndefu sana, ila na wewe yule mbaba wako nadhani atakuwa mbabu siku hizi bado upo naye?”
“Acha zako hizo jamani”
“Nipe mawasiliano yako basi, tuwe tunawasiliana Manka”
Basi mama Sarah alimpa Haruni namba yake, kisha waliagana na muda huo mama Sarah kuondoka zake kuelekea shule aliyompeleka Elly yani aliamua tu kufata utaratibu ingawa angeweza kumuhamisha tu na utaratibu huo walimu wenyewe ndio wangefatilia.
Alipofika shuleni aliomba kuitiwa Elly na pia aliomba kuitiwa Sarah, basi walipofika aliwatambulisha pale ili wafahamiane, kwakweli Sarah alionekana kufurahi sana kumfahamu Elly basi waliongea kidogo na kurudi kila mmoja kwenye darasa lake.

Leo mama Angel alijiandaa kwenye mida ya saa nne ili aende kwenye ofisi yake, basi kama kawaida alimuachia mtoto Vaileth halafu yeye aliondoka zake kuelekea kwenye kazi yake. Alipoondoka tu ndipo Vaileth alipoweza kuwasiliana na Junior na kumwambia kuwa mama yao katoka, na kweli baada ya muda mfupi tu Junior alifika pale nyumbani,
“Unajua nini Vai, yani nimepanda pikipiki ili niwahi hii nafasi, kasema anarudi muda gani?”
“Nadhani ni jioni ndio atarudi, hata akiwahi tutamfanyia ujanja, cha muhimu uwe umemuelekeza vizuri mlinzi”
“Nimemuelekeza ndio kuwa akiwa anakuja tu anitonye, yani hii nafasi sijataka kuiacha kabisa, huwezi amini nilivyotoroka shule leo sababu yako Vai, kwakweli nakupenda sana jamani”
Basi kama kawaida mtoto aliachwa pale sebleni na wao walienda chumbani ili kukumbushiana mambo yao ambayo huwa wanayafanya.
Muda wakiwa chumbani, alifika Tumaini pale na kukuta mtoto akilia, basi aliingia na kumchukua huku akiita Vaileth ila kimya kilitawala maana Vaileth alikuwa ndani, basi akawa anajiuliza,
“Jamani, huyu binti kaenda wapi kwani na kuacha mtoto loh! Ndiomana watu huwa hawaamini mabinti kama hawa jamani”
Muda kidogo Vaileth alifika na kumsalimia Tumaini,
“Shikamoo shangazi”
“Mjinga sana wewe, ulikuwa wapi na kuacha mtoto akilia hapa?”
“Nilikuwa kuoga shangazi”
“Haya, yuko wapi huyu mamake?”
“Kaenda kazini”
“Aaaah jamani, kashaanza tena mambo ya kwenda kazini kweli dah!! Yani huyu jamani”
Basi muda ule ule Tumaini alimpigia simu kaka yake na kuanza kuongea nae,
“Hivi mama Angel si ulishamwambia swala la yeye kukaa nyumbani na kulea watoto”
“Ndio nilimwambia hivyo”
“Basi na leo katoka na kuacha huyu mtoto mdogo akiwa na Vai tu hapa, nimekuta Vai kaenda kuoga na mtoto analia tu. Unajua kuna wakati unatakiwa kuwa mkali kwa Erica, bila hivyo utalia nakwambia”
“Ngoja nikwambie kitu dada yangu, weka akilini hiki ninachokwambia. Hakuna kitu ambacho kinatendwa na Erica halafu mimi nisijue au hakuna kitu ambacho kinafanywa na mimi halafu yeye asijue, kwahiyo kama umekuta ameondoka hapo nyumbani ujue kuwa ameniambia hilo na mimi mwenyewe ndio nimemruhusu kufunya hivyo”
“Ila nimekuta mtoto akilia jamani Erick”
“Mimi na Erica tumefahamiana kabla ya huyo mtoto, kwahiyo usiwe na wasiwasi maana mke wangu ajua kile anachokifanya”
“Kheee, haya sitakwambia tena kuhusu chochote. Yani Erick kuna mambo huwa sitaki kukwambia sababu hiyo hiyo, yani utafikiri mtu uliyerogwa jamani, huwa unaongea kama unatapika. Nishachefukwa hapa, kwaheri”
Tumaini aliinuka kwa hasira na kumuaga Vaileth ambapo vaileth alimbembeleza mtoto na alipolala akarudi tena chumbani alipokuwa na Junior na kuanza kuongea nae,
“Jamani huyu shangazi yenu nae ana visa sana, ila inavyoonekana baba anamjua vizuri”
“Kafanyaje tena?”
“Kampigia simu baba, halafu kaweka sauti kubwa kwahiyo nilikuwa nasikiliza kila kitu, kamlalamikia kuhusu mama jamani kashushuliwa balaa”
Vaileth akawa anacheka huku akimsimulia yale maongezi,
“Tatizo la shangazi yule sijui vipi. Wale wanapendana kwahiyo mambo mengi lazima waambizane, anafikiri mama anakurupuka tu kuondoka hapa bila ya kuongea chochote na mume wake? Yani shangazi yule nae loh! Ngoja tumalizie halafu nile niondoke asije akanikuta bure maana akianzaga na yeye balaa”
vaileth alikuwa akifurahi tu kwani kwa kipindi hiko alijikuta akipenda sana kuwa karibu na Junior kuliko kitu chochote.

Mama Angel alipomaliza kazi zake, alijiandaa vizuri kurudi zake nyumbani kwake kwani hakutaka agundulike kuwa aliondoka nyumbani kwake, basi alipokuwa akitoka ofisini kwake, kabla hajapanda kwenye gari yake akashikwa bega, kugeuka akamkuta Rahim ndio kamshika bega, akamuangalia kwa dharau sana kwani kwa kipindi hiko alijikuta akizidi kumchukia,
“Una shida gani na wewe?”
“Shida yangu ni wewe Erica, napenda utambue ni jinsi gani nakupenda Erica”
“Sikia kwanza, naomba unisikilize kwa makini, sitaki huo ujinga wako wa kunipenda, niache kama nilivyo na maisha yangu. Nina mume wangu, na wewe una mke wako, hayo maswala ya kupendana yanatoka wapi? Sitaki huo ujinga Rahim, sitaki kabisa, achana na mimi”
“Sawa, ila vipi kuhusu mtoto wetu Angel?”
Mama Angel alimsonya Rahim na kuingia kwenye gari lake halafu akaondoka zake kwani hakutaka kuongea nae kabisa na aliona akimchefua tu kwa wakati huo.
Wakati anatembea na gari yake, alipita karibu na mgahawa wa Sia, na kusimama kumsikia kwa muda huo ana jipya gani la kumueleza,
“Oooh naona umesimama ili kuangalia naendeleaje? Unajua wewe huwa roho mbaya unaiigiza tu ila huiwezi hata kidogo Erica, huiwezi roho mbaya wewe yani unaiigiza tu”
“Unaongelea nini?”
“Ila usijali, sitakusumbua tena kuhusu Elly maana amepata mfadhili na atasomeshwa maisha yote, sema lingine”
“Kheee bado una hayo hayo tu jamani, unaendeleaje lakini? Nimekuona ndiomana nimesimama ili nikusalimie”
“Naendelea vizuri tu hata usiwe na wasiwasi juu yangu”
“Haya, kwaheri”
Mama Angel aliondoka na gari lake kwa muda huo na kurudi moja kwa moja nyumbani kwake tu, alimkuta Vaileth ametulia na mtoto sebleni maana muda huo Junior alikuwa ameshaondoka, basi alimsalimia pale na kuanza kuongea nae,
“Vipi leo hajasumbua huyu?”
“Aaaah hajasumbua mama, ila kuna muda nilienda kuoga akaamka na kuanza kulia, basi alifika shangazi Tumaini na kuchukia sana”
“Kheee pole, najua lazima kakufokea sana”
“Aaaah sio kunifokea ila alikuulizia, nilipomwambia haupo akachukia zaidi na kumpigia simu baba ila akaweka sauti kubwa”
Kisha Vaileth alimueleza kile ambacho alisikia baba Angel akiongea na Tumaini yani hadi mama Angel alicheka na kumchukua mwanae kwenda nae chumbani, alikaa na kujitafakari kwa muda kidogo na kusema,
“Ila mume wangu ananipenda sana jamani, yani hakutaka dada yake aniseme ingawa sikumuaga ila kanitetea kuwa nilimuaga, kwakweli Erick ananipenda sana”
Muda huo huo akaamua kumpigia simu mume wake ili aombe msamaha kwanza,
“Naomba unisamehe kwa kutoka bila kukuaga”
“Usijali, kabla hujaomba huo msamaha tayari nimeshakusamehe”
“Unarudi lini mume wangu”
“Sikwambii ni lini maana nitakuja kukushtukiza tu mke wangu kwahiyo usijali kitu”
“Jamani, nimekukumbuka sana”
Wakaongea mengi mno kwenye simu, muda kidogo wakina Erica walirudi kutoka shule na moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa mama yake na kuanza kuongea nae,
“Yani mama, Samia jana kaniambia vitu vingi sana na leo karudia tena”
“Vitu gani hivyo?”
“Eti anasema majina ya wakina Erica hawajatulia, nimempinga ila leo karudia tena”
Kisha Erica alimsimulia ambacho alisimuliwa Samia toka kwa bibi yake,
“Achana na mambo ya Samia mwanangu atakuumiza kichwa tu, kwanza hiyo shule nitakuhamisha maana huyo Samia anakuchochea tu ili uwe mbea zaidi ya hapo ulipo kwasasa”
“Kwahiyo niytahamia shule gani mama?”
“Nitakwambia tu”
Erica alitoka chumbani kwa mama yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.

Usiku wa leo mama Sarah akafikiria jambo na kuongea na Sarah,
“Hivi mwanangu, Ijumaa ya kesho nikimchukua Elly awe analala huku kwetu mwisho wa wiki utafurahi?”
“Oooh mama nitafurahi sana kwakweli, hata mimi natamani sana Elly aje hapa kwetu, nimempenda bure”
Mama Sarah alikubaliana na Sarah kuwa kesho yake ataenda kuongea na mama Elly ili Elly aende kulala hapo nyumbani kwake.
Palipokucha tu wakati Sraah ameenda shuleni naye alijiandaa na moja kwa moja kwenda kwenye mgahawa wa Sia na kuongea nae kuhusu siku hiyo kumchukua Elly ili akalale nyumbani kwake,
“Oooh hilo siwezi kupinga ingawa nitammisss sana Elly ila siwezi kupinga”
“Basi badae nitakuja nyumbani kwako kwaajili ya kumchukua”
Wakakubaliana hivyo na mama Sarah aliondoka zake, ila njiani alikutana na Johari ambapo alisimama na kuanza kuongea nae,
“Kumbe upo? Hivi ulishaonana na Erick?”
“Mmmh nionane nae wapi mwenzangu? Sijamuona halafu kasafiri ila nimeonana na Erica, mwanzoni unajua sikujua kama Erica na Erick ni mke na mum, kumbe walioana na watoto wanao wa kutosha tu”
“Ndio, wale walikuwa wanapendana kweli. Nikikumbuka figisu tulizoweka juu yao ila hazikufua dafu kwani ndio kwanza walitafutana na kuoana. Ila unajua siku ile ulivyosema umezaa na Erick sikuelewa eti!”
“Nimezaa nae ndio, nina mtoto wa kike ambaye baba yake mzazi ni Erick, kiukweli mambo ambayo Erick alinifanyia na nilivyokuwa nampenda nilijikuta kila nikisikia jina Erick najikuta nikilia tu jamani”
“Pole sana maana na wewe ulipenda ndugu yangu, ila mapenzi haya loh! Ila bora ulizaa nae”
“Sema sijui kama atakubali mtoto”
“Mwambie akapime damu na mtoto”
“Uwiiii huyo Erick umesikia kwanza alivyondondocha kwa huyo Erica! Kwani unafikiri ndio mimi tu aliyezaa nae! Kazaa na wanawake kibao ila watoto wote Erick amewakataa sababu tu hataki kumkera mke wake, yani Erick hataki hat kumsomesha mtoto wake mwenyewe kisa ni mtoto wa nje ya ndoa na anaogopa kumkera mke wake. Kwahiyo hiyo kupima damu hataki, yani hataki kitu chochote kile, anachokitaka yeye ni mke wake tu”
“Duh! Jamani rafiki yangu Erica kampa nini mume wake anipe ushauri na mimi nimpe wa kwangu?”
“Ila huyu Erick nimepanga kumkomesha, yani hatokuja kunisahau katika maisha yake yote. Lazima nimlize nakwambia”
“Utamfanya nini?”
“Wewe tulia, kuna mikakati nimeshaanza kuifanya, yani hakuna kitu ambacho kinashindikana kwangu ujue, nitamkomesha Erick najua hadi siku hiyo atakaa chini na kusema Manka umeniweza”
“Mmmmh nidokezee basi”
“Wewe tulia tu, nitakwambia vizuri mambo yalivyo”
Waliongea mambo mengine tu na kuagana kwa muda huo kisha kila mmoja alienda sehemu yake.

Mama Angel alikuwa akiongea na Vaileth kuhusu usafi wa mule ndani maana maua yalianza kunyauka sababu hayakumwagiliwa maji vizuri,
“Jamani Vaileth maua yangu yanakufa ujue, kesho nikumbushe ili iwaambie Erick na Erica wakamwagilie maua”
“Kweli mama, ila na pale nje ya geti kuna vile vimajani vimeota pembeni haviweki sura nzuri mahali pale”
“Ni kweli, tena umenikumbusha kitu. Ngoja niende nikaving’oe maana baba yenu akniambia atarudi muda wowote, sitaki akute kuna taswira mbaya pale nje.”
“Ila si ungeweka mtu tu mama wa kufanya hiyo kazi”
“Aaaah mtu wa nini, naona mwenyewe naweza kufanya kile kitu acha tu nikafanye mwenyewe maana sehemu yenyewe hata sio kubwa wala nini”
“Au basi niende mimi”
“Hapana usijisumbue”
Kisha mama Angel akamuachia pale mtoto na kumwambia akianza kulia amuite, halafu yeye akatoka zake hadi nje ya geti lake na kuanza kung’oang’oa yale majani yaliyojiotea hovyo pale nje.

Muda huu Rahim alikutana njiani na mdam Oliva na kusimama akianza kuongea nae,
“Oooh madam nimefurahi kukuona”
“Aaaah wewe hufai kabisa, yani baada ya kunifatilia kwa muda mrefu nilijua lengo lako ni kutaka kunitongoza kumbe lengo lako ni kuwa karibu na Erica duh! Nilishangaa sana”
Rahim alicheka kwa ile hoja ya madam Oliva, kisha alimwambia,
“Aaaah ningetaka kukutongoza mbona ningekwambia siku ile ile, ila mimi nampenda sana Erica, na kwakweli leo umenikumbusha kitu, ngoja niende kwake hata nimuone tu moyo wangu uridhike”
“Kheee makubwa hayo jamani”
Basi waliachana pale na moja kwa moja Rahim alielekea nyumbani kwa mama Angel.
Rahim alifika pale kwa mama Angel na alipomuona pale nje alifurahi sana, basi alimfata pale alipokuwa anang’oa nyasi na kusimama nyuma yake huku akimkumbatia yani mama Angel alishangaa sana na kuinuka ila bado Rahim alimsogeza karibu kwenye mwili wake na kumkumbatia, muda huo huo baba Angel alifika pale akiwa kwenye pikipiki kwahiyo aliona vizuri kilichotokea pale.

Rahim alifika pale kwa mama Angel na alipomuona pale nje alifurahi sana, basi alimfata pale alipokuwa anang’oa nyasi na kusimama nyuma yake huku akimkumbatia yani mama Angel alishangaa sana na kuinuka ila bado Rahim alimsogeza karibu kwenye mwili wake na kumkumbatia, muda huo huo baba Angel alifika pale akiwa kwenye pikipiki kwahiyo aliona vizuri kilichotokea pale.
Baba Angel alichukia sana, alifika pale karibu na kumpiga teke Rahim, alipogeuka alimpiga ngumi ya pua ambayo ilimpa kizunguzungu Rahim hadi akaanguka chini, kisha alimpiga mateke yasiyokuwa na idadi pale chini, kwa muda huo kulikuwa na Sia naye alikuwepo eneo lile kumbe, kwahiyo alisogea karibu ya Rahim na kumuomba baba Angel amsamehe,
“Jamani Erick, kwanini lakini?”
Baba Angel alionekana kuwa na hasira sana na yule mtu, ila muda ule Rahim nae akainuka na kusema,
“Erick, nimekuachia sio kwamba siwezi kupambana na wewe ila muda haujafika wa mimi kupambana na wewe, kwakweli wewe ni mwanaume mpumbavu unaacha mambo yako na kuja kupigana na mwanaume mwenzio sababu ya mwanamke? Unashindwa kujiuliza mimi nimekuja kufanya nini hapa kama si yeye aliyeniambia nije? Unashindwa kujiuliza hilo? Mwanamke umemuoa, unampa kila kitu, unalea na mtoto wake wa nje ya ndoa, unamthamini na kumjali ila bado yupo kumkumbuka Rahim tu, ila hujiulizi hivyo zaidi ya kufika na kuanza kupambvana na Rahim, kuwa makini sana mimi nitakupoteza wewe kwa ujinga kama huu. Unadhani kukuchia Angel umtunze ndio nimeshindwa kumtoa kwako? Sijaamua tu, mtunze na ukimaliza nitakuja kumchukua rasmi na kamwe hatokumbuka uwepo wa baba chizi kama wewe”
Baba Angel alimuangalia huyu Rahim na kupatwa na hasira zaidi hata kutaka kwenda kupambana nae tena ila mkewe alimshika mkono na kumkataza kufanya hivyo basi Rahim alicheka sana na kusema,
“Si unaona mkeo anakukataza kuja kupambana na tamu yake, endelea kuwaza kuwa unapendwa sana na huyo mwanamke wakati ana sababu zake za kuwa karibu na wewe”
Mama Angel hakumuachilia mume wake, alimsihi waingie ndani, alimuomba sana mumewe waingie ndani, basi baba Angel alikubali na waliingia ndani kwahiyo pale nje alibaki tu Rahim na Sia, basi Sia akamwambia Rahim,
“Ila wewe kiboko, unaongea maneno ya kuchoma hayo”
“Kwani unadhani nimeongea uongo? Yule mwanamke ananipenda kufa, yani pale hakuna anachoelewa kwa mumewe zaidi ya kunielewa mimi”
“Duh! Ulimpa nini mpaka akakupenda kiasi hiko?”
“Ni mapenzi tu, mimi nipo vizuri kimapenzi kushinda huyo Erick. Mimi najua kumuweka mwanamke katika mstari”
“Sasa kwanini alikuacha?”
“Ana ubavu huo wa kuniacha? Nilimzingua na kumuacha ndio akakimbilia kwa huyu bwege Erick, na kwenda kumpa hata yule mtoto Angel, na alivyomjinga, kamlea Angel, kamsomesha na kumuandikisha kwenye biashara zake akiamini kuwa Angel akija kusikia kuhusu baba yake mzazi basi hatomtaka huyo baba mzazi, kumbe anakosea sana. Mimi ni baba mzazi wa Angel, na ipo siku yule mtoto atarudi kwenye himaya yangu, muache tu na ujinga wake alee mtoto, amtunze na ampe haki yote halafu ataona picha ya badae”
“Duh! Ila nimekupenda bure, unajua siku zote huwa nakuona tu ila sikufahamu kwa undani zaidi, yani nimekupenda bure, nipe mawasiliano yako ili tuwe tunawasiliana”
Basi Rahim akampa Sia mawasiliano yake na muda huo kila mmoja aliondoka zake.
 
SEHEMU YA 342

Mama Angel na baba Angel wakiwa chumbani bado baba Angel alionekana na hasira sana dhidi ya Rahim kuwa pale nyumbani kwake,
“Nani kamuita leo Rahim?”
“Mimi sijui mume wangu hata mimi nimeshtuka tu kumuona pale nje”
“Na wewe nini kilikupeleka pale nje?”
“Nilienda kung’oa majani ambayo yameota pale karibu na geti letu”
“Toka lini Erica umefanya hivyo? Ulishindwa hata kuweka kibaria wa kufanya hivyo jamani mke wangu, mbona kutaka kuniumiza moyo sababu ya huyu mtu jamani. Mpaka lini tutakaa na kupigania mapenzi mke wangu?”
“Naomba unisamehe”
“Kuniomba msamaha sio suluhisho, nimekuuliza lini tutaacha haya mambo eeeh! Nimeamua kuwa mume mwema kwako, usidhani sioni wanawake huko, ila najiuliza nifate nini kwao wakati mke wangu ana kila kitu! Halafu nakupenda sana, kwahiyo siwezi kwenda kutafuta magonjwa huko wakati wewe upo, ni kweli wapo wanaonishangaa sana ila mimi sioni aibu kuelezea kuwa nampenda sana mke wangu wakati wowote ule ila kwanini mtu kama huyu Rahim unamchekea? Bado unampenda?”
Mama Angel alishtuka sana kwani hakutegemea kuulizwa swali kama hili na mume wake, alimuangalia na kumwambia,
“Jamani Erick, kweli kabisa nimpende Rahim kwa lipi? Kwa yote aliyonitendea jamani! Tukiacha yote bado ukweli upo wazi kuwa wewe ndiye mwanaume nikupendaye kwa dhati, nakupenda mume wangu. Hata ukisema nizae watoto kumi kwaajili yako basi nitazaa tu, sipendi kuona ukikwazika jamani, na mimi sijapanga kitu na huyo Rahim”
“Sasa kwanini afike muda tu ambao wewe upo nje hapo?”
“Kwakweli sijui mume wangu, nahisi shetani anataka kutugombanisha tu”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni madam Oliva, basi mama Angel alipokea ile simu na kuweka sauti kubwa ili mumewe ajue ni nani anaongea nae maana alishaona mume wake kaanza kumuwekea mashaka,
“Samahani mama Angel, mzima lakini”
“Bila samahani, mimi ni mzima”
“Leo njiani nilikutana na yule jamaa ambaye ulichukia sana nilipomleta kwako”
“Nani huyo?”
“Yule Rahim, ila muda nimekutana nae akasema amekukumbuka anakuja nyumbani kwako. Sasa muda huo sikuwa nyumbani halafu sikuweka vocha kwenye simu ndiomana saivi nimeamua nikupigie simu ili umzuie mlinzi wako asimkaribishe maana sidhani kama yule ana lengo zui na ndoa yako”
“Asante kwa taarifa madam”
“Haya asante pia, jioni njema”
Basi alikata ile simu na kumuangalia mume wake, ambapo baba Angel moja kwa moja alimuuliza mama Angel,
“Inamaana siku hizi huyu madam amaekuwa rafiki yako?”
“Aaaah huwa nawasiliana nae mara moja moja tukiambizana mambo mbalimbali ya maisha”
“Duh! Kweli maisha yanabadilika sana, ila ni vizuri kupunguza idadi ya maadui”
Basi kwa muda huu walianza kuongea vizuri sasa na kuulizana kuhusu mambo mbalimbali ya huko alipotokea, halafu mama Angel alimuuliza mumewe kuwa amuandalie chakula gani kwa siku hiyo aliyofika,
“Labda chapati na rosti ya maini”
“Sawa mume wangu”
Basi mama Angel alitoka na kumtuma Vaileth ili akanunue maini aweze kumuandalia mume wake, kwahiyo muda huo huo Vaileth alitoka ili akanunue hayo maini wakati huo mama Angel alibaki akianza kufanya maandalizi ya kumpikia mumewe kitu alichokihitaji.

Vaileth alienda mpaka buchani na kununua alichokuwa ameagizwa, ila wakati anatoka buchani alikutana na Sia, na kusimama ili kumuuliza tena,
“Vipi mwanao Erick umemfatilia tena?”
“Mmmh yule mtoto unadhani ni mwanangu basi!! Leo nimemkataa kabisa yule mtoto simtaki tena jamani, ila sijui nini kilitokea ila yule mtoto si mwanangu”
“Kwanini?”
“Unajua alikuja kwenye mgahawa wangu na kunipiga sana, alinipiga ngumi na mateke, halafu leo nimemshuhudia baba yenu akimpiga mtu ngumi na mateke tena kampiga haswaaa kama Erick alivyonipiga mimi, yule ni damu yake, siwezi kuzaa toto lenye akili za kijinga kama lile jamani”
“Kheee kumbe baba kapigana leo? Ndiomana alienda moja kwa moja chumbani hata kuongea nae sijaongea nae”
“Basi kuna majanga aliyafanya balaa, ila…. Aaaah nenda tu ipo siku nitakupa siri hiyo hadi utakaa mdomo wazi”
“Siri gani tena?”
“Nenda tu”
Vaileth alijitahidi kumshawishi pale ila hakumwambia lolote kwahiyo ilibidi aondoke tu, wakati anakaribia kwao, alikutana na kijana mmoja aliyemsimamisha, huyu kijana alionekana rika limepishana kidogo na wakina Erick ila hakumuamkia Vaileth wala nini ni sababu ya mwili mdogo aliokuwa nao ulifanya wengi waone huenda akawa ni mdogo, basi yule kijana akamwambia,
“Samahani dada, eti Erica yupo ndani?”
“Mmmh wewe ni nani kwani? Erica atakuwepo maana nahisi kasharudi shule, ila wewe ni nani?”
“Mwambie Bahati, kwakweli dada ngoja nikwambie kitu. Yule Erica nampenda sana jamani, sijui nimwambiaje na nimpataje! Nimekuona nae mara nyingi maeneo ya Kanisa pale, nampenda sana Erica”
“Kheee jamani, hiyo unaniambia ni ngumu kumeza hatari, yani unampenda Erica, uwiiii unatafuta balaa wewe”
“Balaa gani sasa?”
“Baba Erica hapendi kabisa ujinga na masikhara kwakweli, naomba tu uache kumfatilia Erica maana atakupoteza”
Kisha Vaileth aliachana na yule kijana pale na moja kwa moja kuingia ndani na kupeleka kile alichoagizwa halafu kuendelea na mapishi ambapo alikuta Erica kweli alishafika nyumbani na alikuwa jikoni kusaidiana na mama yake katika kuchoma chapati,
“Kheee kumbe Erica usharudi shule?”
Mama Angel akajibu,
“Kasharudi, hapa yupo kumtengenezea baba yake chapati yani alivyosikia karudi kafurahi sana”
Basi wakawa wanacheka huku wakiendelea na yale mapishi.

Usiku wa leo, Rahim alienda zake mahali na huko aliagiza pombe na kunywa maana alihisi kichwa chake hakipo sawa yani alijihisi kuwa na mawazo sana kwa muda huo.
Wakati anakunywa, kuna mtu alifika na kukaa karibu yake, kumuangalia mtu huyo alikuwa ni Bahati mkubwa, basi mtu huyu alianza kuongea nae,
“Tatizo nini Rahim, mbona unakunywa pombe kiasi hiko? Hujui kama pombe ni haramu?”
“Naomba achana na mimi, yani mimi ukikuta nimeamua kuwa hivi ujue nachanganywa akili na mtu mmoja tu”
“Nani huyo?”
“Erica, ananichanganya sana akili huyu mwanamke”
“Khaaaa jamani kumbe!! Ndugu yangu nakumbuka miaka mingi iliyopita tuligombana mimi na wewe sababu ya huyo mwanamke, ukapata bahati mwenzangu ya kuwa nae sababu ya pesa ulizokuwa nazo na kila kitu chako, ila mimi nilikosa hiyo bahati ingawa nilikuwa na mapenzi ya dhati. Bahati ile uliichezea ni kama ulikuwa ukichezea shilingi kwenye tundu la choo, ikadumbukia kwahiyo hukuwa tena na hiyo bahati, mwanamke akakukataa hakukutaka tena maisha yake yote. Laity ungejua yule binti kaaibika vipi sababu yako hata usingejifanya muda huu unalewa kwaajili yake, yule mwanamke kapigwa kwao yule, alikuwa anaficha mtoto ndani maana ni aibu kwani mtoto hakuwa na baba, aliogopa kuwaambia ndugu sababu ya aibu, kiukweli kateseka sana kutokana na familia aliyokuwa nayo. Sasa akatokea huyo waliyependana na kuwa pamoja, mimi pia nilimpenda sana na niliwasumbua sana mumewe ila namshukuru sana mke wangu ni mtu mwenye akili sana, ni mwanamke mcha Mungu, na mwenye akili ya dini, huwezi amini alihangaika sana na mimi ila akanifanyia dua na sasa wala siwezi kumsumbua tena Erica na mumewe. Wewe ndugu una nini lakini?”
“Achana na mimi wewe, sisi hatufanani kabisa. Wewe hujawahi kupendwa na Erica, ila mimi nilipendwa na Erica hebu tofautisha hilo kwanza. Wewe ulitaka kubadili dini ili umuoe Erica ila Erica alitaka kubadili dini ili aolewe na mimi, hebu tofautisha mimi na wewe kabisa. Yule ni wangu, kumbuka kwanza nimezaa nae, mtoto wa kwanza kabisa kwa Erica ni mtoto wangu, sikumbaka Erica ila ni mapenzi yake akaamua kuwa na mimi na kuzaa na mimi kwa mapenzi yake, ukiona mwanamke hadi anaamua kuzaa na mwanaume jua anampenda sana. Siwezi sema Erica anampenda sana Erick sababu hakuna dalili yoyote ile. Erica kaamua kuolewa na Erick na kuzaa nae sababu Erick alionyesha upendo kwa mtoto wetu yani pale sio kumpenda Erick ila ni sababu ya Angel. Ukitaka jaribu kufatilia maisha anayopewa Angel na wale vikaragosi wengine ambao hawajulikani mwanzo wala mwisho wake ndio utajua kuwa Erick anapendwa sababu ya mtoto wangu”
“Duh!”
“Ndio hivyo, kwahiyo ukiwa unaongea usiongeee tu ilimradi, tena ngoja nikuhakikishie jambo moja kuna kipindi Erica atarudi kwangu na nitafunga nae ndoa. Na tutazaa mtoto mwingine”
“Khaaaaa!”
“Shangaa sana ila hivyo ndivyo ilivyo, yule mwanamke ananipenda sana mimi. Sina shida, acha ninywe pombe ili akili yangu izidi kuchangamka, hakuna kitu cha maana nitakachoambiwa na wewe kikaragosi”
Bahati hakuwa na sababu ya kuendelea kuongea na huyu mtu kwani aliona ni kujisumbua tu ukizingatia hakuna alichokuwa anaambiwa akaelewa moja kwa moja. Basi akaondoka zake na kumuacha pale akiendelea kunywa pombe zake.

Kulipokucha, Elly alikuwa nyumba ni kwakina Sarah, kwakweli ilikuwa ni ajabu sana kwake kulala kwenye nyumba nzuri vile, na alifurahia mandhari ya ile nyumba, basi waliamka wote na kwenda kunywa chai huku mama Sarah akimwambia Elly,
“Yani Elly ujisikie amani kabisa kukaa hapa nyumbani kwangu, sina hiyana mimi na wala sina tatizo lolote mimi”
“Sawa, nashukuru sana”
“Najua pia unatamani kama hata tungeweza kutoka na kutembea kidogo”
Sarah akadakia na kumwambia mama yake,
“Mama, kwanini tusiende ufukweni leo?”
“Umeniambia swala jema sana, ngoja twende ufukweni, basi mtajiandaa badae twendeni tukatembee”
Ilikuwa ni furaha sana ile habari kwa upande wa Elly kwani yale maisha aliyafurahia sana, basi muda huo huo mama Sarah alisikia simu yake aliyoiacha kwenye kochi ikiita, basi akainuka na kwenda kuipokea, alikuta ni Sia ndio aliyekuwa anampigia, basi aka[pokea,
“Jamani za huko, mmeamkaje?”
“Salama kabisa, hofu kwako”
“Salama, basi jana nilipita karibu kwenye nyumba ya Erica kumbe Erick ndio amerudi jana”
“Weeee kumbe!! Ngoja nimpigie simu”
Mama Sarah alikata ile simu ya mama Elly na kuanza kutafuta namba ya Erick ila akakumbuka kuwa hakuwa na ile namba kwenye simu, basi muda huo alienda chumbani kwake na kuchukua mkoba wake mmoja ambao anakumbuka kuna siku alikutana na Erick halafu alimpa namba zake za simu, akapekua na kukuta ile kadi basi akabonyeza zile namba na kupiga ambapo muda kidogo tu ile simu ilipokelewa,
“Kheee Erick umerudi kimya kimya, nina shida ya kuonana na wewe”
“Oooh unataka kuonana na mimi wapi?”
“Kwanza unajua unayeongea nae?”
“Sijajua, ni nani wewe?”
“Mimi Manka, nina shida sana ya kuonana na wewe”
“Sawa, tuonane wapi sasa?”
“Badae naenda na watoto wangu ufukweni, basi tukutane huko”
“Muda gani na ufukwe gani?”
“Ngoja nikutumie ujumbe basi, maana mkeo asije akasikia”
Basi mama Sarah alikata ile simu na moja kwa moja kutuma ujumbe kwenye ile namba kuhusu muda wa kukutana na ufukwe wa kukutana.
Kisha mama Sarah aliwafata watoto wake na kuwaambia muda wa kwenda kutembea na ufukwe wa kwenda, na wote walifurahi bila ya kujua ni kwanini mama yao kapanga kile kitu.

Leo baba Angel alitulia kidogo na kuona ana kila sababu ya kwenda kiwandani ili kuangalia maendeleo ya kiwanda,
“Naona hadi Jumatatu nitakuwa nimepoteza vingi sana”
“Basi nenda na Erick maana anatambua vingi sana pia”
“Oooh sawa, nitaenda nae. Si ndio wanamwagilia maua? Basi nenda kamwambie kuwa nitatoka ne”
Mama Angel alitoka na kwenda kuwafata watoto wake ambapo walikuwa wanamwagilia maua, aliwakuta wapo kumwagiana maji huku wakikimbizana na kucheza,
“Ila nyie jamani loh! Ndio kumwagilia maua huko”
“Mama Erick ndio mchokozi, ndio kaanza kunimwagia maji”
“Hamna mama, ni Erica huyo”
“Mmmeanza sasa, haya Erick utajiandaa kwenda na baba yako kiwandani”
“Sawa mama”
Basi Erica alimuangalia Erick na kumwambia,
“Naomba niletee zawadi ukienda”
Erick alicheka tu na mama yao akaondoka na kuwaacha hapo, kwahiyo Erick alimalizia pale kumwagilia maua na kwenda kujiandaa ili kuondoka na baba yake kwenda kiwandani.
Na alipomaliza tu kujiandaa aliondoka na baba yake, basi baba Angel alikuwa akimuuliza maswali mbalimbali,
“Eeeeh mwanangu, hebu niambie zile siku ulizokuwa unakuja kiwandani, nasikia upo vizuri sana kwenye maswala ya kiwanda”
Mara kuna mbaba walimuona mbele kidogo na Erick alimwambia baba yake,
“Yule mzee ni mteja wetu mzuri sana pale kiwandani, kwakweli anatuungisha sana”
“Kheee upo vizuri mwanangu hadi wateja unawajua?”
Basi baba Angel alisimamisha gari na kushuka kwenda kumsalimia huyo mteja ambaye ni mteja mkubwa sana, basi walisalimiana pale na kufurahi sana,
“Nashukuru sana kwa kuwa mteja wetu mzuri”
“Hata hivyo bidhaa zenu zipo vizuri sana na zinapendwa sana, ila hongera sana maana huyu kijana wako yupo vizuri sana”
“Asante”
Basi waliongea kidogo na kuagana ambapo walirudi kwenye gari na kuanza kuondoka, basi baba Angel alimuuliza mwanae kuwa yule mteja anaitwa nani,
“Huwa wanamuita mwarabu, sema wakina Yuda ndio wanalijua jina lake halisi”
“Anaonekana yupo vizuri sana”
“Ni yupo vizuri kweli, halafu ana upendo sana. Yani mara nyingi akifika kiwandani lazima aulizie kuhusu mimi, nishafika hadi kwenye biashara zake, ana biashara kubwa sana inaonekana ana hela sana”
“Inaonekana hivyo, ila ni vizuri mwanangu kuwafahamu wateja wetu, umekuwa vizuri sana”
Basi moja kwa moja walienda zao kiwandani na kuanza kupeana maelekezo ya vitu vilivyopita.

Mama Angel leo akiwa nyumbani kwake, alifatwa na rafiki yake Johari basi alimkaribisha vizuri sana na kuanza kuongea nae, ila alienda kuongea nae kwenye bustani yao ili wapate na upepo wa nje kidogo,
“Kwanza kabisa asante sana kwa kule ulikonipeleka maana nafanya biashara kwasasa hadi najishangaa”
“Hongera kwa hilo”
“Unajua sikujaribu hapo kabla sababu moja, utakuta watu wanasema hawa wajasiriamali wanakufundiaha halafu ukitoka hapo huwezi lolote unakaa tu nyumbani, ila sasa nilivyofika pale alipita mama mmoja na kutufundisha kwakweli yale mafundisho yaliniingia akilini, alisema wengi hawafanikiwi sababu moja, akishatoka hapa anataka ajaribu kila kitu kwa wakati mmoja na mwisho wa siku anaona ni kujisumbua tu anaamua kuacha, utakuta anataka atengeneze mafuta, sabuni za aina zote, vikoi, tambi sijui mishumaa mara keki vyote kwa wakati mmoja halafu akija badae anajibu yale mambo hayalipi, hebu niwaambie wanawake wenzangu mjaribu kwanza kujikita sehemu moja mtafute soko na uhakika itakutoa tu, ndipo unapoongezea vingine, ila ukitaka vyote kwa wakati mmoja lazima uone hasara maana mtaka vyote hukosa vyote. Basi mafundisho yakaendelea, nilipotoka hapo nikasema ngoja nikomae na sabuni ya maji, uwiiii huwezi amini yani ndani ya muda mfupi nimekuwa na soko kubwa sana na ninaenda kusambaza sehemu mbalimbali. Kwakweli shoga yangu ubarikiwe sana kwa hili la kunitoa tongotongo mwenzio”
“Nimefurahi kusikia hivyo, siku hizi wanawake ni kuinuana kwakweli maana uchumi wa sasa sio wa kutegemea kuletewa tu. Sema watu wengine huwa wanafikiria ni masikhara, ni kweli akisemacho utakuta mtu anahudhuria kila darasa la ujasiliamali ila kusema ngoja nifanye hiki nilichofundishwa sasa, nikomae nacho hakuna, ila utamkuta leo alienda hapa kesho yupo hapa. Na hata biashara zipo hivyo, mwingine akisikia vitunguu vinalipa basi kashahamia kwenye vitunguu, korosho zinalipa huyo kwenye korosho, akiambiwa kuna madini yanalipa sana, huyo kwenye madini mwisho wa siku kila biashara anaona ni mbaya kwake sababu hajui afanye nini, kitu jua kwanza faida na hasara zake basi utaweza kukabiliana nacho ila kuvamia vamia kila kitu utashangaa tu wenzio wamesonga mbele”
Basi waliongea mengi sana na kuendelea kushawishiana mambo mengi, ndipo Johari alipoanza kumueleza na habari za Manka pia,
“Nasikia Manka alikuja kukwambia kuwa kazaa na Erick!”
“Jamani habari za Manka, hata sizitaki ila bado sijamuuliza mume wangu ili aniambie ukweli”
“Mimi sijui na wala sitaki kuwa chanzo cha kukugombanisha tena na mume wako Erica, nakumbuka kipindi cha nyuma nilifanya mambo sio mazuri kabisa hata roho yangu ilinisuta tena sana. Siwezi sema kuwa mtoto kweli ni wa Erick au la maana yule Manka nae haaminiki kabisa”
“Eti eeeh!!”
“Sijui kwakweli, ila ngoja niende nitakuja tena siku nyingine”
Basi Johari alimuaga mama Angel na kuondoka zake.
Alipofika njiani Johari alikutana na Sia na kuanza kusalimiana nae,
“Naona umetoka kwa rafiki yako”
“Eeeeh nimetoka kwa rafiki yangu”
“Ila nahitaji sana kukufahamisha kuhusu mwanaume aliyezaa na rafiki yako yule mtoto wake wa kwanza”
“Mmmh unadhani nahitaji kumfahamu basi? Hata sihitaji kumfahamu kwakweli. Kwaheri”
Johari aliondoka yani Sia alishangaa sana kujibiwa vile na Johari ila alijua kuna maneno tu atakuwa kaambiwa na mama Angel.

Mama Sarah akiwa ufukweni na watoto wake, basi akapigiwa simu na ile namba ambayo alikuwa akimpigia Erick,
“Na mimi nipo ufukweni, upo sehemu gani nije”
“Niambie wewe ulipo nije maana nipo na watoto hapa, ngoja nije tuzungumze kwanza ndio tutakutana nao”
Basi alielekezwa alipo na moja kwa moja aliwaaga watoto wake na kuondoka zake, muda huo Sarah na Elly walikuwa wakiongea kuhusu mambo mbalimbali,
“Elly una mwanamke wewe?”
“Mmmh mwanamke? Hapana, kwanza nasikia wanawake wanapenda sana hela sasa mimi nitampa hela gani mwanamke?”
Basi Sarah alicheka sana, na kumuuliza tena,
“Ushawahi kufanya mapenzi?”
Elly akashtuka sana na kumuangalia vizuri Sarah kisha akamwambia,
“Hapana, naogopa kabisa. Wewe je?”
“Aaaah hapana sijawahi kabisa ila nasikia ni mchezo mzuri sana halafu raha”
“Mmmmh umesikia wapi? Nani kakwambia?”
“Kwenye simu yangu huwa naona watu wakifanya, kuna video nyingi huwa natumiwa. Tukifika nyumbani nitakuonyesha”
“Mmmh nasikia huo ni mchezo mbaya sana, mtu mkubwa akikukuta hata unaangalia hizo video basi utapigwa sana”
“Kwahiyo tukiangalia nani atatupiga huyo?”
“Mama yako”
Sarah akacheka na kusema,
“Sijawahi kupigwa hata kibao na mama toka nimezaliwa, na hii simu wala mama yangu huwa haishiki kuangalia chochote kile ninachokiangalia yani mama yangu kaniacha huru kuangalia chochote na kuwasiliana na yoyote ninayetaka”
“Kheee basi mama yako anakupenda sana, ila hata mimi mama ananipenda sana sema nikikosea lazima aniadhibu ili nisirudie tena”
“Basi itakuwa mimi huwa sikosei maana mama huwa hanipigi, ananipenda sana”
Wakaongea mengi na kukubaliana kuangalia hizo video pindi wakirudi nyumbani.

Mama Sarah moja kwa moja alienda kukutana na yule mtu ambaye alifikiria kuwa ni Erick ila alivyofika pale hakukuta kuwa ni Erick alishangaa sana kuona ni mtu mwingine, basi yule mtu alimfata karibu na kujitambulisha kwake,
“Habari, naitwa Rahim.”
“Kheee mbona sio Erick?”
“Kweli mimi sio Erick, utakuwa umekosea namba ila hiyo sauti yako ilinichanganya sana na kuhamisha kabisa ufahamu wangu nikajikuta nahitaji kukufahamu zaidi”
Basi Rahim alitabasamu, kiukweli mama Sarah alihisi akipata raha sana kumuona, basi Rahim alisogea karibu yake na kushika kiganja cha mkono wa mama Sarah, yani hii kitu Rahim alikuwa akiijua vizuri sana kuwa tabasamu lake na mikono yake ilikuwa ikimaliza sana wanawake, kwani wengi walipenda kuona Rahim akitabasamu sababu ya mpangilio mzuri wa meno yake, ambayo yalivutia sana kuyaangalia na pia walipagawa mno alipowashika mikono kwani mikono ya Rahim ilikuwa ni milaini sana, kwahiyo mama Sarah nae alijihisi akisisimka sana huku akimuangalia tu Rahim bila ya kusema lolote, basi Rahim alimshtua tena kwa kumwambia,
“Mbona umeduwaa?”
“Hapana, basi tu”
“Unajua sauti yako ilinichanganya sana, halafu nimekuona kuwa wewe ni mzuri sana. Unavutia kwakweli”
Mama Sarah alitabasamu tu, kisha Rahim alimwambia tena,
“Manka, naomba unipeleke nyumbani kwako nipafahamu”
Kwakweli mama Sarah hakuwa na pingamizi kabisa juu ya hilo, basi akaondoka ili kwenda kuongea na watoto wake kuwa waende nyumbani.
Ila walipofika pale, Elly alionyesha kumshangaa Rahim na kusema,
“Kumbe mnafahamiana?”
Mama Sarah alimuangalia Rahim, na Rahim alikuwa akimuangalia Elly maana hata hakumkumbuka.
 
SEHEMU YA 344

Mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwaajili ya kuongea na mume wake kuhusu hilo swala la kuishi na huyo binti,
“Mmmh wewe umeamua nini mama yangu?”
“Sijui nakusikiliza wewe tu”
“Mimi sina tatizo, ila tu hakikisheni mnapafahamu vizuri anapotokea huyo binti tusijeleta matatizo bure hapa nyumbani”
“Sawa hakuna tatizo, basi nitamwambia amlete kesho”
“Hakuna tatizo”
Mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoangalia ule ujumbe ulitoka kwa rafiki yake Johari, basi akausoma,
“Leo, nimekutana na Manka, alikuwa kaongozana na watoto wake anaenda nao mahali. Ila nimeongea nae kidogo tu na bado akisisitiza kuwa yule mtoto ni wa Erick, cha kushangaza sasa, alikuwa kaongozana na mtoto mwingine wa kiume, akasema naye ni wa Erick pia, mmmh sijui labda Manka alizaa mapacha au ni kitu gani sikuelewa hapo!”
Mama Angel alisoma ule ujumbe mara mbilimbili kisha alimuangalia sana mume wake bila ya kusema chochote kile, ila baba Angel alihisi tu kuna kitu hakipo sawa kwa mkewe, basi akamuuliza,
“Tatizo nini mke wangu?”
“Sijui ila najiona sipo sawa kabisa”
“Kwanini wajiona hivyo?”
“Baba Angel, unajua swala la Manka linaniumiza kichwa sana, yani kila nikifikiria naona kichwa changu kikizunguka mno”
“Kwanini lakini?”
“Nahitaji tu kujua ukweli, ni kweli Manka ulizaa nae au la”
“Jamani, sijazaa na Manka huo ndio ukweli au unataka tukutane na huyo Manka tumuulize vizuri?”
“Ndio, hiyo itakuwa nzuri zaidi”
“Sina namba zake”
“Mimi najua anapoishi”
“Duh! Haya tutaenda basi mke wangu”
Baba Angel anamjua mkewe vizuri kuwa akitaka jambo basi anataka lifanyike muda huo huo hata sio wa kusema nisubiri kwanza, maana inaonyesha alitaka sana kujua ukweli wa mtoto wa mama Sarah.

Mama Sarah akiwa kwenye sherehe, muda ule ule akapigiwa simu na Rahim na kuanza kuongea nae,
“Unajua natamani hata leo kuja nyumbani kwako”
“Ila mimi sipo nyumbani, nimekuja huku na familia yangu kuna sherehe ya kuzaliwa ya wajina wangu”
“Oooh sawa, kwanini basi tusikutane leo unipeleke huko kwako Manka? Naomba tukutane, waache watoto huko halafu tutawafata, niambie ulipo nije kukuchukua”
Basi Manka hakuona tatizo lolote alikubaliana na Rahim na kumuelekeza mahali alipo, ambapo baada ya muda kidogo tu Rahim alimpigia simu kuwa kafika, basi alienda kuwaaga watoto wake kuwa atawafata badae.
Akatoka na kuondoka na Rahim huku wakiongea mengi tu,
“Huyo wajina wako umempelekea zawadi gani ya siku yake ya kuzaliwa?”
“Unajua wamenishtukiza tu hata sijajua nimchukulie zawadi gani”
“Kwahi huwa anapenda nini? Ana umri gani?”
“Aaah bado mdogo ana miaka mitano”
Wakati wanapita mahali waliona kuna duka la nguo na vifaa vya watoto, hivyo Rahim alienda kusimamisha gari maeneo yale na kumtaka mama Sarah wakachague zawadi, basi walishuka na kwenda dukani kuchagua zawadi ambapo zile zawadi zote zililipiwa na Rahim na kumfanya mama Sarah afurahi sana.
Ila Rahim alipenda sana ukarimu wa yule muuzaji pale dukani, basi akamuachia kadi yake ya mawasiliano na kumtaka wawasiliane.
Kisha mama Sarah na Rahim waliendelea na safari ya kwenda nyumbani kwa mama Sarah.

Huku mama Angel na mumewe walijiandaa kwaajili ya kwenda nyumbani kwa mama Sarah ili wakaongee nae, na kweli waliondoka hapo na kuanza safari.
Walipofika kwa mama Sarah walishangaa kumuona mama Sarah akiingia ndani kwake na Rahim.

Walipofika kwa mama Sarah walishangaa kumuona mama Sarah akiingia ndani kwake na Rahim.
Mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa muda kisha baba Angel akamwambia mkewe,
“Sasa mama watoto, kweli ndio mtu wa kwenda kumfatilia huyu atuambie ukweli kabisa!! Hebu mambo mengine tuache tu kama yalivyo, hebu tuondoke zetu”
“Kwani ni kitu gani hiki? Umeelewa mume wangu?”
“Sijaelewa na wala sina shida ya kuelewa, ila mke wangu nishakwambia mara nyingi kuwa maneno ya Manka usiyasikilize, ni sawa tu na maneno ya Sia, yani usiwasikilize kabisa. Mimi ndio nakwambia kuwa sijazaa na Manka, niamini mimi, kama nimezaa nae kwanini nikatae eeeh!! Siwezi kukataa kitu ambacho nimekifanya kweli, sijazaa na Manka, na kwa ujinga ule ambao ameanza wa kushirimiana na Rahim hata sina haja ya kufahamu zaidi kitu kinachoendelea, tuondoke tu hapa mke wangu”
Basi wakaamua kuondoka, ila baba Angel hakwenda moja kwa moja nyumbani na mke wake bali alienda nae hotelini ili kupata chakula kidogo na kuongea mawili matatu maana ni siku nyingi alikuwa kasafiri, basi walifika pale na kuagiza chakula huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Nakumbuka kipindi hiko wakati nakufukuzia, hata hukutaka kunielewa kabisa, ulikazana na swala moja tu kuwa mimi ni muhuni sana wakati wala sikuwa muhuni wa kiasi hiko ila tatizo la kunikataa ndio likazaa swala la mimi kuwa muhuni, kwahiyo mara nyingine mke wangu unihurumie tu na tuendelee kuaminiana”
“Nakuamini mume wangu, ila hawa wanawake wananipa presha hatari”
“Wasikupe presha mke wangu maana mimi na wewe tunapendana kiukweli kabisa, kwahiyo hao vikaragosi wasikubabaishe”
Wakati wanaongea pale, alifika eneo lile Fetty na kukaa karibu nao na kuwasalimia pale,
“Nawaona wapendanao jamani, yani nyie mnapendana hadi shetani anawaogopa”
Mama Angel na baba Angel wakatabasamu, na kusalimiana nae pale kisha mama Angel alimuuliza,
“Umekuja mwenyewe huku?”
“Hapana, nilikuja na mume wangu ila kuna mtu kamuita mara moja si unajua wafanyabiashara muda wote wanawaza biashara tu, kwahiyo ametoka kwenda kumpa mzigo mtu mzigo ndiomana kaniacha hapa sababu atarudi”
“Ila nimefurahi leo kusikia kuwa ulikuja hapa na mumeo”
“Ndio, mume wangu kabadilika sana siku hizi. Kwakweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu maana tabia ya Bahati imekuwa mpya kabisa”
“Hongera sana”
Kisha Fetty alimuangalia baba Angel na kumwambia,
“Shemeji kumbe ulisafiri?”
“Ndio, umejuaje?”
“Kheee jamani, mimi nisijue kweli! Hata kama Erica asingeniambia basi ningejua tu, na huu umbea nisijue kweli jamani! Haiwezekani”
“Mmh yani wewe Fetty ni mbea hatari”
“Mimi tena shoga yangu ni balaa, ila ngoja nigeukie kwako shemeji, unajua nini kuna mama alikuwa anakufanyia sana usafi huko ulipokuwa, alikuwa akifanya usafi mara kwa mara kwenye chumba chako, anaitwa Juli, yule mama ni rafiki yangu sana, kwahiyo alikuwa akiniambia mengi sana”
“Eeeeh bhana eeeeh sikuwezi kwakweli, nyie wanawake ni noma sana jamani, yani yule mama kule unamfahamu kwahiyo mlikuwa mkiulizana kuhusu mimi!”
“Ndio lazima nimuulize, ili nijue mwenendo mzima wa shemeji yangu kule ulipokuwa”
Fetty aliongea huku akicheka na kuendelea na maongezi mengine, baada ya muda kidogo Bahati nae yani mume wa Fetty alifika na kuwasalimia pale ila alimtaka mkewe waondoke muda ule ule, kwahiyo ilibidi wawaage na kuondoka zao.
Mama Angel na mumewe nao walikaa kwa muda kidogo na kuamua kuondoka kurudi nyumbani kwao kwani waliona pia muda umeenda.

Usiku wa leo, Fetty alimuuliza mume wake kilichopelekea kutaka kuondoka mapema kiasi kile, basi mumewe alianza kumueleza,
“Ni hivi mke wangu, kwanza huwa sipendi kukuficha kitu chochote, nina uhakika unanijua kushinda hata ninavyojijua, ni mwanamke wa pekee sana kwangu maana ulijitoa kunivumilia kwa kila hali ukiamini kuwa kuna siku nitakuwa sawa kabisa, ni hivi mke wangu, yule Erica ni mwanamke ambaye nilimpenda sana, huwa napenda kusema hili kuwa sehemu kubwa ya mabadiliko katika maisha yangu basi ni sababu ya Erica tu, mimi sikuwahi kupikia jiko la gesi bila Erica kuniletea, mimi sikuwaza kuwa na biashara kubwa kubwa hivi maana sikuwa na mtaji wa aina yoyote, mimi nilikuwa mvuvi tu, yani navua samaki na kupata shilingi mbili tatu ila ziliishia kwa matumizi ya nyumbani na matumizi yangu binafsi maana ingawa sikuwa na mbele wala nyuma ila bado nilitegemewa sana na familia yangu. Erica alikuja kwenye maisha yangu kwa lengo la kunibadili kabisa, maana alinipa mtaji na hapo niliweka mabwaya ya samaki, na kufungua bucha langu mwenyewe, na kweli biashara ilikuwa nzuri sana, akanipa tena mtaji, nikaweka kuku na kufanya biashara ya kuku ambayo ilinilipa sana. Nilijitajidi kufanya kwa bidii ili kumfurahisha Erica, kwani nilihitaji niwe kama aina ya wanaume anaopenda yeye. Na kweli nikapata kiwanja na kujenga nyumba, na kununua gari lengo kubwa ni kuishi na Erica kwa masiha ambayo najua alikuwa akiyatamani kwa kipindi hiko. Kwanza kwa hayo tu natakiwa nimpende Erica kufa na kupona, nampenda sana, huwa sikufichi juu ya hili, huwa nakwambia wazi”
“Naelewa mume wangu”
“Ujue chanzo cha mimi kuachana na Erica, ni madawa ya kishirikina waliyonifanyia hadi nikamuoa yule mke niliyemuacha Nasma, nasikia Erica ilimuuma sana, naweza kuhisi kidogo maumivu yake yalivyokuwa, kuna wakati hata huwa nalia”
“Najua mume wangu, hayo mambo yanavyokuumiza, ila swali nimekuuliza lingine ila umeanza kunipa historia yako na Erica wakati swali langu hata halihusu historia yenu”
“Hivi umeniulizaje?”
“Nimekuuliza kwanini baada ya kukuta nimekaa na Erick na Erica pale ukadai tuondoke upesi upesi? Hilo ndio swali, nina uhakika hayo majibu yako hata hayapo katika swali”
“Ngoja nikujibu, ni sababu bado nampenda, halafu sipendi kuona akiwa na Erick. Najizuia hisia zangu ndiomana kwasasa sipendi kuwa nao karibu wala kuwa karibu yake, najua baada ya miaka kupita itakuwa pia ni historia katika maisha yangu ila kwasasa acha niwe na amani mke wangu, ukikaa walipokaa wale usishangae naondoka. Nalinda ndoa yetu, na mke wangu huwa unanifanyia dua nzuri sana, kwanini nianze na tamaa na wanawake wengine mie? Kwakweli hapana, nitabaki na wewe tu”
Hapa kidogo Fetty alikuwa na amani kwani alitumia muda wake wa kila siku kuweza kumrejesha mumewe katika mstari anaouhitaji.

Leo kama kawaida, watoto walienda shuleni, kwahiyo Elly alivyotoka shule hakurudi kwakina Sarah kwani moja kwa moja alienda kwenye mgahawa wa mama yake na kuamua kurudi nae nyumbani,
“Ila mama kuishi kule dah!”
“Kwani kuna nini mwanangu?”
“Hawana maadili mama, hawaendi Kanisani wala nini. Kwanini umekubali nikaishi kule mama yangu?”
“Mwanangu kila kitu kinafanywa sababu ya shida tu, unadhani nafurahi basi kukuacha wewe uteseke? Natamani ningekuwa na pesa basi ningekulea mwenyewe bila kumtegemea mtu yoyote ila sina pesa mwanangu”
“Basi jana, tulienda kwenye sherehe ila mama alituacha huko kwanza, jamani mama watu walivaa nguo za ajabu hizo balaa eti ndio uzungu, halafu sherehe yenyewe ya mtoto ila watu walivaa nguo za ajabu”
“Kheee mwanangu, waswahili husema ukimchunguza bata sana huwezi kumla, kwahiyo mambo mengine acha kama yalivyo ila cha msingi ulelewe ili upate maisha mazuri”
“Sawa mama nimekuelewa”
Wakiwa wanakaribia nyumbani, walikutana na madam Oliva, ila Elly hakujua kama kuna tatizo kati ya madam Oliva na mama yake maana yeye alijua ni mwalimu wake tu,
“Mama, huyu ni mwalimu wangu madam Oliva, madam na huyu ni mama yangu”
Ila alishangaa bila kusalimiana, kisha Sia alimvuta pembeni madam Oliva na kuanza kuongea nae,
“Hivi wewe ulishamwambia Steve kuwa mwanae anamkumbuka huku!!”
“Unajua wewe kweli ni mwezi mchanga, yani kadri siku zinavyoenda napata kukufahamu zaidi. Sasa mtoto wa Steve au wa Erick?”
Sia hakumwambia kitu, ila alirudi kwa mwanae na kumshika mkono kisha waliendelea kurudi nyumbani kwao.

Siku ya leo Erick aliporudi nyumbani kwao alimpelekea hoja nyingine baba yake, na hiyo hoja ilikuwa ni kutaka kuhama shule,
“Kwanini unataka kuhama Erick?”
“Siipendi tena ile shule”
“Aaaah basi ngoja nifikirie kuhusu hilo swala”
Kisha baba Angel alienda kuongea na mke wake kuhusu swala la Erick kutaka kuhama shule,
“Kwanini anataka kuhama sasa?”
“Sijui anasema haipendi tu ile shule”
“Unajua nini mume wangu, kuna mambo tunapokuwa na watoto tunatakiwa kuwa na kiasi chao, Erick anataka kuhama shule kwasababu gani? Au ni sababu ya huyo Elly aliyepelekwa pale, kwani huyo Elly anamsumbua kitu gani Erick?”
“Oooh Elly mtoto wa Sia? Ndio kapelekwa kusoma hapo?”
“Ndio si unamjua Sia ni mkorofi, huwa anatafuta sababu tu ya kutugombanisha”
“Sasa nimeelewa kwanini Erick anataka kuhama, nitafanyia kazi hilo swala lake, ila ngoja nitaongea nae kwanza”
Kisha Erica alifika kumuita mama yake maana mgeni alifika, mama Angel akatoka ndani na kukuta mgeni mwenyewe ni mama Junior akiwa ameambatana na yule msichana ambaye amedai kuwa ana mimba ya Junior, ilibidi tu amakaribishe na kuongea nae kidogo halafu alienda kumuonyesha chumba cha vaileth na kumwambia Vaileth kuwa atakuwa akilala nae, Vaileth aliguna ila alikubali tu ingawa alijua itakuwa ngumu sana kufanya mambo yake kwenye chumba hiko.
Kisha mama Junior akamuaga ndugu yake, kwahiyo mama Angel alimtoa ndugu yake huku wakizungumza kidogo,
“Yani nashukuru sana mdogo wangu kwa kunipokea huu mzigo, kwahiyo inabidi tutafute hela ya faini kwasasa”
“Ila Junior hawezi kuoa, maana bado anasoma”
“Ndio, hata hivyo huwezi kumlazimisha amuoe labda hampendi au vipi, ila huyu binto akae kae hapa hadi kujifungua maana kwao wameshamsusa hivyo”
Basi waliongea kidogo na moja kwa moja waligana halafu mama Angel aliingia ndani na moja kwa moja kwenda cbumbani kwa vaileth ili kuongea na yule binti,
“Unaitwa nani kwanza maana hata sijakuuliza”
“Naitwa Daima”
“Oooh Daima, sawasawa, karibu sana itaishi vizuri tu hapa. Nikikaa vizuri tutaenda wote kwenu ili niitambue familia yako”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi mama Angel hakuwa na tatizo nae na alimuacha hapo na kwenda kuendelea na mambo mengine.

Usiku wa leo wakati Vaileth ndio kaingia kulala na huyu Daima pembeni yake basi alianza kumuhoji maswali,
“Kwahiyo hiyo mimba ya nani?”
“Ya Junior”
Vaileth alimeza mate kidogo na kuendelea kumuuliza,
“Junior mwenyewe anajua?”
“Ndio anajua ila mara zote huwa ananikatia simu, kwetu wamechukia ndiomana wamenipeleka kwao. Basi mama yake ndio kanileta huku, ila jana nililala kwakina Junior”
“Duh! Ila kwenu nako watachukuaje maamuzi ya kukupeleka kwa mwanaume tu?”
“Weee kwetu, hawataki mtu uzalie nyumbani, yani hawataki kabisa, mama yangu ni mkali sana, baba yangu nae ni makali sana, hawataki haya mambo kabisa, sina namna zaidi ya kukubaliana na hali halisi tu”
“Ila umemaliza shule?”
“Nimeishia kidato cha nne, ndio nimepata hii mimba ya Junior kwahiyo sijaweza tena kuendelea na shule”
“Una miaka mingapi kwani?”
“Aaaah mimi niliwahi shule tu, sababu nilikuwa na mwili mkubwa sana. Ikabidi tu niwahishwe shule. Wazazi wangu ni wakali sana, na mimi kwetu ni mtoto wa kwanza, hakuna aliyekubali jambo hili ndiomana imekuwa hivi”
“Ila Junior unampenda? Anakupenda?”
“Ninampenda kweli Junior, ila sina uhakika na yeye kama ananipenda kama mimi ninavyompenda. Nampenda sana Junior, yani sana, na hiki kitoto chetu kikiwa cha kiume nitakiita Junior”
Vaileth alimuangalia ila kiukweli hakupenda kabisa, sema alikuwa anavumilia tu maana hakuwa na namna yoyote ya kufanya, sema moyo ulimuuma sana alijikuta siku hii akilala huku machozi tu yakimtililika, halafu akamtumia ujumbe Junior,
“Hivi Junior unanipenda kweli?”
Muda huo huo Junior alijibu ule ujumbe,
“Aaaah Vai, mpenzi wangu jamani. Nisipokupenda wewe nimpende nani tena!!”
“Na Daima je?”
Ujumbe ule ulikawia kidogo kujibiwa na kumfanya Vaileth apate maumivu zaidi katika moyo wake, ila badae ujumbe ule ulijibiwa,
“Jamani mambo gani tena hayo, huyo Daima simtambui maana ninayekutambua ni wewe tu Vai wangu na ninakupenda sana”
Vaileth hakujibu huu ujumbe kwa muda huu na kuamua tu kulala kwani alikuwa na mawazo sana.
Kilivyokucha, Vaileth alimuamsha Daima ili wakafanye kazi za mule ndani,
“Kheee mimi nina mimba ujue, nitafanyaje kazi mimi?”
“Kwani mimba ni ugonjwa? Ulisikia watu wakiwa na mimba hawafanyi kazi?”
“Ndio, mama anasema mwanamke mjamzito anatakiwa kupumzika, kwahiyo mimi siwezi kufanya kazi sana mimba yangu isije ikatoka bure wakati mwanangu namuhitaji sana”
Vaileth alimuangalia Daima bila ya kummaliza, kisha yeye akainuka na kwenda zake jikoni kuanza kazi za mule ndani.

Leo shuleni, muda wa mapumziko kama kawaida ya Erica na rafiki yake Samia, walikaa pamoja na kuanza kuongea mambo ya nyumbani kwao, ambapo Samia alimuuliza kwanza Erica kama baba yake amerudi,
“Hivi baba yako kasharudi Erica?”
“Ndio karudi, ila mimi hiwa napenda sana baba akiwepo sababu ni mtu anayenisikiliza sana kuliko mama”
“Oooh na mimi basi baba ndio hunisikiliza sana kuliko mama, unajua mama yangu ni daktari eeeh kwahiyo muda mwingi anakuwa kwenye kazi, mara shifti ya asubuhi, mara ya ya usiku yani mama yangu haeleweki. Ila nyie mnakuwa muda mwingi sana na mama yenu”
“Ni kweli ila mama hapendi masikhara kabisa, kuna vitu unaogopa kabisa hata kumwambia mama ila baba akiwepo unamuambia tu. Eeeh niambie kuhusu baba yako na mama yako basi”
“Basi bhana, unajua ile Jumapili baba aliondoka nyumbani, halafu alijua mama atakuwa shifti ya usiku, kumbe hakurudi hadi Jumatatu asubuhi yani jana, sijui ilikuwaje huko lakini dada yetu yule wa kazi kanieleza kidogo tu, inaonyesha baba kaanza na mwanamke mwingine”
“Mmmmh mmejuaje?”
“Si kwasababu alikuwa akimjibu mama vibaya, yani alikuwa akimjibu tu ilimradi, dada akaniambia inaonekana baba kaanza na mwanamke mwingine”
“Ila baba yako ni noma sana”
“Kweli ni noma sana baba yangu, ila baba yangu anapenda wanawake huyo balaa”
“Umejuaje?”
Kengele ya darasani iligonga, ikabidi waende darasani kuendelea na vipindi vya siku hiyo.

Baba Angel aliamua kwenda na mkewe kiwandani baada ya mkewe kumwambia kuwa alikuwa akienda wakati yupo safarini, basi walimuacha pale nyumbani mtoto, Vaileth na yule Daima halafu wao waliondoka moja kwa moja na kwenda kiwandani.
Walifika na kufanya kazi za kiwanda huku wakielekezana mambo mbalimbali,
“Unajua kuna muda naelewa ni kwanini wanawake ni wasaidizi wa wanaume”
“Kwanini?”
“Sababu mpo kufanya pale tunapokwama, kwakweli wewe mke wangu umekuwa ni sehemu kubwa sana kwangu. Sikuamini wakati naelezwa vyote ulivyovifanya hapa kiwandani, kumbe nilikuacha msimamizi mzuri na hodari”
Mama Angel alitabasamu tu kwa sifa alizopewa na mume wake.
Basi wakati wakiendelea na kazi za hapa na pale, ndipo kuna mgeni alifika pale kiwandani, mgeni huyo alikuwa ni Juma, baba Angel alitoka na kuongea nae vizuri tu,
“Unajua nini, nilikuwa napita hapo, sasa nikaona ni vyema nipitie hapa. Kumbe Erick umerudi kimya kimya jamani!!”
Baba Angel alicheka tu, kisha Juma aliendelea kuongea,
“Na vipi mkeo nae anaendeleaje?”
“Nipo nae kiwandani”
“Oooh haya, hongera zenu. Leo sina mengi ila ukirudi mpe salamu zangu Erick”
Juma aliaga na kuondoka zake kisha baba Angel akarudi kuendelea na kazi zake na kawaida.
Waliporidhika wakaona ni vyema kurudi nyumbani, ila wakati wanarudi baba Angel alianza kumwambia mke wake,
“Hivi mke wangu, huyo Daima aliyekuja sijui mwenye mimba ya Junior, ushafanya utaratibu wa kufahamu wanapoishi wazazi wake? Au dada yako kashafanya hivyo?”
“Mmmh hata sijui, ngoja nimpigie kwanza mama Junior nijue”
Muda ule ule mama Angel alimpigia simu mama Junior, na alipokea simu na kuanza kuongea nae,
“Samahani dada, unapajua wanapoishi wazazi wa huyu msichana uliyemleta kwangu, huyu Daima?”
“mmmh hapana, hilo ni kosa nimefanya, yani alipokuja kumbwaga rasmi hata sijauliza wanapoishi wala nini”
“Jamani dada jamani. Hivi tukipata matatizo je! Mtu mwenyewe ni mjamzito, kama unavyojua mimba zilivyo.”
“Naelewa mdogo wangu, nisameheni bure”
“Basi, ngoja nikamuulize ili ikiwezekana kesho anipeleke huko kwa wazazi wake”
Mama Angel aliagana na dada yake na kukata ile simu kisha akamwambia mumewe,
“Nitaongea na yule msichana ili anipeleke kesho kwa wazazi wake niwafahamu”
“Ooooh sawa kama ni hivyo, maana si vizuri kuishi na mtoto wa mtu bila kujua kwao. Ila unajua kuna vitu sielewi”
“Vitu gani?”
“Hivi mtoto wako akipewa mimba na kijana, mfano kama binti yetu Erica au Angel, hivi mzazi unawezaje kuchukua hatua na kwenda kumsokomeza huyo binti yako kwenye familia ya huyo kijana ambayo huijui vizuri wala nini!”
“Mmmh hapo pagumu, ila huwezi jua ni kwanini mzazi mpaka kafikia hatua hii, labda kashamkanya binti yake sana ila mtoto hajasikia”
“Mfano hapafahamu nyumbani kwao huyo kijana ataenda wapi huyo binti yako? Au ukimpeleka huko napo akifukuzwa itakuwaje?”
“Mmmmh sielewi”
“Kwani sheria inasemaje?”
“Hivi nikuulize wewe, mfano wale mabinti wote uliokuwa ukiwapa mimba wangeletwa kwenu ingekuwaje?”
“Oooh tuachane na habari hizo mke wangu, tuongee mambo mengine. Unawaonaje watoto wetu?”
“Nawaona wapo sawa tu”
“Na Erica na ukuaji wake umemfatilia vizuri?”
“Ngoja nikwambie kitu kuhusu Erica, yule mtoto tumempata ni mbea tu yani umbea kwake ni moto moto, ila Erica hana tabia chafu hata moja, halafu ninachompendea ni kimoja tu ukimkataza kitu harudiii tena”
“Na Erick je!”
“Yule nimempatia jina jipya, yani Erick ana kisirani sana, ila tukitoa hiko kisirani ni mtoto mzuri sana na mwerevu sana, kwakweli nampenda sababu hata yeye ukimkataza kitu hakai arudie tena hiko kitu”
Baba Angel alifurahi kusikia wasifu wa watoto wake, wakaendelea na safari na kurudi nyumbani kwao.
Walipoingia ndani, moja kwa moja mama Angel alienda jikoni na kumkuta Vaileth kambeba mtoto mgongoni huku akipika,
“Kheee kwanini umefanya hivyo Vai?”
“Alikuwa analia mama”
“Sasa kwanini usingempa yule Daima ambembeleze?”
“Mama, huyo Daima kasema kuwa yeye hawezi fanya kazi yoyote sababu ni mjamzito”
“Kheee makubwa, kwahiyo yuko wapi?”
“Aliamka tu kula, ila karudi tena kulala”
“Ndio huwezi kufanya zile kazi ngumu, lakini hii ya kukaa na mtoto tu jamani, kuosha vyombo napo anashindwa? Au kapewa mapumziko? Khaaa huyu kanishinda tabia, haya mlete huyo mtoto”
Basi mama Angel akamchukua mwanae na kwenda nae chumbani.
 
SEHEMU YA 345

Leo jioni Tumaini alikutana njiani na mama Sarah kwahiyo walianza kusalimiana maana ni muda mrefu sana hawakuonana,
“Kheee jamani mama Leah, nyumbani kwangu sio mbali na hapa, naomba twende ukapafahamu”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi wakaongozana huku wakiongea mambo mbalimbali ikiwemo na lile swala la mama Angel,
“Hivi Erica unafahamiana nae vipi maana sikufatilia”
“Erica nimesoma nae kabisa, halafu unajua sikujua kitu kumbe na Erick ni ndugu yako kabisa”
“Ndio ni mdogo wangu, unamfahamu pia?”
“Ndio, nilisoma shule moja na Erica na Erick ila walifukuzwa sababu ya utovu wa nidhamu maana walileta mapenzi shuleni”
“kheee ni Erica ndio mlikuwa mnasoma nae!”
“Ndio, yani utovu wa nidhani ulifanya Erica na Erick wafukuzwe shule, ila nawafahamu vizuri sana na wao wananifahamu vizuri sana. Jina langu halisi ni Manka”
“Oooh kumbe!! Nafurahi kukufahamu leo zaidi”
Basi moja kwa moja walifika nyumbani kwa mama Sarah ambapo alimkarisha ndani na hapo walimkuta Sarah amekaa maana alishatoka shuleni, basi aliwasalimia pale nakuendelea na mambo yake, alikuwa akiangalia Tv huku akichezea simu na alikuwa makini nayo sana.
Mama Sarah alimtambulisha Sarah pale kwa Tumaini,
“Huyu ndio binti yangu mpendwa, mwanangu wa pekee ninampenda sana. Huyu ndio Sarah”
“Oooh kumbe Sarah mwenyewe ndio huyu! Nafurahi sana kumfahamu”
“Sarah, huyu ni rafiki yangu anaitwa mama Leah”
“Sawa mama, nashukuru kumfahamu”
Basi mama Sarah alimuaga kidogo Tumaini pale kuwa anaenda kuweka mkoba na kumwambia msichana wake wa kazi amletee juisi Tumaini, kisha akaondoka na kwenda kuweka mkoba wake.
Tumaini alibaki akimuangalia Sarah pale, akamuuliza,
“Upo busy na simu Sarah, kwani unafanyaje?”
“Nipo instagram yani kuna vitu vingi vya kuchekesha sana”
“Mmmh!! Unajua bado mdogo sana wewe! Kwahiyo huwa unaangalia hiyo instagram muda wote?”
“Ndio, yani mimi facebook nipo, whatsapp na istagram, ila mara nyingine huwa naangalia video youtube”
“Duh!! Wewe Sarah wewe bado mdogo sana kufanya vitu hivyo”
Mama Sarah nae alitoka chumbani kwake na kukuta yale mazungumzo kati ya Sarah na Tumaini, basi akamuuliza Tumaini,
“Unasema bado mdogo nani na kwanini?”
“Nasema huyu Sarah bado mdogo katika kuchezea simu hivyo”
“Mmmh na wewe kama mtu wa kale jamani, mimi mwanangu namlea kizungu, acha afahamu mambo mengi mapema wala haitamsumbua hapo badae, ni mtaalamu wa simu balaa”
Tumaini hata hakutaka kukaa sana na kuamua kuaga, basi wakati mama Sarah akimsindikiza akarudia tena kumwambia,
“Ila mama Sarah, yale sio malezi ya mtoto. Nimekaa muda mchache sana ila nimeweza kuona malezi ambayo Sarah amekuwa nayo, sio malezi mazuri”
“Jamani kwanini?”
“Mwnao kanywa juisi pale ila kashindwa kutoa kile kikombe wala nini, ndio kwanza anachezea simu tu hadi yule mdada wenu kuja kutoa”
“Ila yule Siku ile ni kazi yake, namlipa mshahara kwasababu ya kazi ile, kwanini mwanangu ahangaike”
“Haya, na kuhusu simu”
“Kuhusu simu ni kuwa mwanangu anaishi kizungu, nimemlea hivyo toka mdogo. Huwezi amini ila yule mtoto hata kumpiga kibao sijawahi kumpiga”
“Dah!! Hayo sio malezi kabisa mama Sarah haijalishi una pesa kiasi gani ila hayo sio malezi kwa mtoto. Siku nakuomba poteza muda wako uje kwangu nikufundishe jinsi ya kumlea mtoto, muwahi huyo Sarah, huko sio kumpenda bali ni kumuharibu tu”
Tumaini aliagana nae na kuondoka zake muda huo.

Usiku wa siku hiyo, mama Angel alimuita Daima na kuongea nae kuhusu wazazi wake na kumtaka kuwa kesho yake ampeleke kwa wazazi wake ili akawafahamu,
“Sawa, hakuna tatizo, nitakupeleka”
“Si mama yako na baba yako wapo?”
“Wapo ndio, tena kesho hata baba atakuwepo nyumbani maana mara nyingi huwa anapumzika siku hiyo”
“Sawa, kesho utajiandaa ili twende”
Basi mama Angel alivyomaliza kuongea nae alienda tu kwa mume wake muda huo ili waweze kulala, ila mume wake akaongea nae jambo lingine,
“Unajua nini, kuna mteja Fulani hivi Erick alinitambulisha nasikia anajulikana kwa jina moja la mwarabu, nimejaribu kufatilia nasikia ni mteja wetu mkubwa sana, nahitaji kuwa nae karibu zaidi ikiwezekana hata siku tumualike hapa kwetu kupata chakula cha jioni pamoja”
“Ooooh hiyo ni zuri, tena tutamualika yeye na mke wake, kama ni mteja mkubwa basi inatakiwa tumkirimu zaidi ili kuendelea kuweka alama nzuri ya kuwa mteja kwetu”
“Sawa mke wangu, kesho nitaenda kwanza ofisini kwangu kule halafu nitaenda kiwandani ambapo nitaondoka na Yuda ili tukapafahamu vizuri kenye biashara za yule mzee”
Hapo sawa mume wangu”
Wakaongea mengi sana na mwishowe waliamua tu kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda.

Kulipokucha, mama Angel alifanya tu shughuli zake kwanza na kumtaka Daima ajiandae ili waende nae huko kwao, na kweli baada ya muda mchache Daima alishajiandaa na kuanza safari ya kumpeleka mama Angel nyumbani kwao.
Walipofika nyumbani kwakina Daima, mama Angel alipaki gari yake pembeni na kwenda sasa kuingia ndani ya hiyo nyumba, ambapo aliyewakaribisha alikuwa ni mama yake Daima, moja kwa moja waliingia sebleni ambapo palikuwa na baba yake Daima ila mama Angel alipomuangalia alishangaa maana ni mtu ambaye anamfahamu.

Walipofika nyumbani kwakina Daima, mama Angel alipaki gari yake pembeni na kwenda sasa kuingia ndani ya hiyo nyumba, ambapo aliyewakaribisha alikuwa ni mama yake Daima, moja kwa moja waliingia sebleni ambapo palikuwa na baba yake Daima ila mama Angel alipomuangalia alishangaa maana ni mtu ambaye anamfahamu.
Basi alimuangalia kwa makini, ila baba Daima alimuwahi na kumkaribisha nyumbani kwake,
“Karibu sana, hapa ndio nyumbani kwangu, eti Daima umetoka wapi na mgeni huyu?”
Daima alikuwa kimya tu, kisha mama Angel akamwambia baba Daima,
“Kwanza sikujua kama huyu ni mtoto wako Babuu, kumbe una binti mkubwa kiasi hiki jamani!!”
“Aaaah mkubwa wapi huyu mjinga, shule mmemshinda, ana ukubwa gani hapo alipo”
“Si kamaliza kidato cha nne huyu!!”
“Amalize wapi wakati mwaka jana kafanya mtihani wa kumaliza kidato cha pili amefeli, kwahiyo tulikuwa nae nyumbani nikifikiria kumrudisha tena shule akaanze kidato cha kwanza”
“Mmmh ila hebu tuongee vizuri, kwanza sikujua kama ni binti yako huyu. Samahani sana, ila nilimwambia kuwa leo nahitaji kufahamu wazazi wako”
“Kwani wewe umemfahamu vipi huyu Daima?”
“Huyu, kaletwa tu nyumbani kwangu na dada yangu kuwa wazazi wake mmembwaga kwake na kusema kuwa ana mimba ya kijana wetu”
Baba Daima akashtuka sana,
“Kheee ana mimba!!”
Akainuka na kusogea karibu na Daima na kumzaba vibao vitatu na kusema,
“Wewe mjinga, shule umefeli halafu umeenda kubeba mimba!!”
Mama Daima ilibidi aingilie kati maana wakati mumewe ameanza kuongea na mama Angel alitoka kidogo, ila aliposikia mumewe akimzaba vibao mtoto wao ikabidi atoke ili akamuamulie, basi akamtuliza pale mumewe na kumkalisha pembeni,
“Kwani tatizo nini mume wangu?”
“Tatizo nini? Yani kumbe huyu mjinga ana mimba na hujaniambia chochote”
“Punguza jazba kwanza mume wangu nikueleze vizuri yaliyopo”
Baba Daima alitulia huku akingoja maelezo,
“Ni hivi, mtoto humu ndani alianza kuumwa, hataki kula chakula, anachagua chagua, nikaamua kwenda nae hospitali na ndio nikagundua kuwa ni mjamzito, kwakweli nilichanganyikiwa kwani nilijua ungegungua ingekuwa balaa, ila nilipanga kukwambia. Nilimbana mimba ya nani, ndio akanitajia huyo kijana wa kuitwa Junior, basi nikamtaka anipeleke kwao, yani nishaenda nae huko kwakina Junior mara kadhaa ila niliona huyo mama Junior haeleweki ndio nikaamua kumbwagia pale mtoto hadi atakapojifungua”
“Khaaa hivi na wewe mke wangu una akili kweli eeeh!! Mambo mengine unatakiwa kunishirikisha mimi mwenyewe. Haya wewe Daima, hebu kaa vizuri hapo, una mpango gani na hiyo mimba?”
“Nahitaji kuwa na mtoto baba”
Baba Daima alisikitika sana na kusema,
“Yani kumbe nilikuwa nakusomesha bure tu, huna maana hata moja, mjinga wewe”
“Nisamehe baba”
“Kwahiyo una mpango gani na huyo mjinga mwenzio?”
“Nahitaji anioe baba, nahitaji awe mume wangu”
“Kweli wewe mtoto ni tahira wa mwisho sijapata kuona, unajua kama unanichefua zaidi”
Basi mama Angel aliamua kutuliza kidogo pale na kuelezea azma yake iliyompeleka mahali pale basi baba Daima akasema,
“Kwa leo muache hapa huyu binti yangu, nishauriane na halmashauri ya kichwa changu kwanza halafu kesho tutamleta huko nyumbani kwako”
Mama Angel hakuwa na maneno zaidi, basi aliaga tu na muda huo baba Daima aliinuka kwenda kumsindikiza mama Angel wakati huo Daima kabaki na mama yake ndani.
Basi walipofikia gari ya mama Angel, baba Daima akamwambia,
“Unajua mara nyingine ni bora kuoa yule uliyepanga toka mwanzo kumuoa katika misha kwani itasaidia na kujikuta mambo mengi sana mkifanana, ila haya maswala ya kuoa tu ili kutimiza sheria ndio madhara yake haya”
“Kwanini?”
“Kwakweli, wewe ndio ulikuwa mke wangu. Wewe ndio ulikuwa mwanamke wa maisha yangu”
“Aaaah Babuu hayo yalishapita, tuyaacha bhana. Una maisha yako na mimi nina maisha yangu, namuheshimu mume ambaye Mungu amenipatia na wewe muheshimu mke ambaye Mungu amekupatia”
“Namuheshimu mke wangu tena namuheshimu sana, tatizo lake ni moja tu tumeishi kipindi chote lakini huwa ananiogopa yani mambo mengi sana huwa haniambii ukweli kabisa hata sijui ana matatizo gani, tofauti na jinsi ulivyokuwa wewe”
“Mwambie vile unavyopenda mbona atabadilika tu, yeye sio malaika kusema agundue ni kitu gani unapenda kutoka kwake. Mwambie ili naye afanye vile unavyotaka wewe”
“Ila tuache masikhara Erica, unazidi kupendeza kwakweli, nakumbuka miaka hiyo wakati nakutana na wewe ukiwa binti mdogo sana, kwakweli mapenzi yaliniwehesha, wala sikusikia wala kuhema juu yako, kwakweli Erica nilikupenda sana na bado nakupenda ila namuheshimu mke wambaye Mwenyezi Mungu amenipatia kama ulivyosema kwani kila kitu kinachotokea katika maisha yetu basi ni Mungu ndiye anajua kwanini kimetokea”
“Hapo sasa ni sawa, na tutaenda sambamba. Ila usimfokee sana na mtoto, tutajua tu cha kufanya kama wazazi tutaungana na kuwa letu moja”
“Sawa sawa nimekuelewa”
Basi wakaagana na moja kwa moja mama Angel alipanda kwenye gari na kuondoka zake.

Mama Angel akiwa njiani alimuona rafiki yake Dorah, basi alisimamisha gari na kumpakia huku akiongea nae,
“Kwani unaenda wapi muda huu?”
“Naenda hapo mbele, kuna shule ndio anasoma binti yangu”
“Aaaah sawa, ngoja nikupeleke basi”
“Aaaah vizuri hivyo, utakuwa umenisaidia. Eeeeh nimekumbuka kitu Erica”
“Kitu gani hiko?”
“Jumapili nilimuona Rahim mahali akiwa ameongozana na mwanamke Fulani hivi ila namkumbuka mwanamke huyo”
“Ni mwanamke gani?”
“Mwanamke mmoja hivi, kipindi wakati nipo na mzee Jimmy alikuwa nae pia, nakumbuka wakati mzee Jimmy kajigundua kuwa ameathirika alikuwa akinilaumu sana mimi, alinisema sana kuwa nimemuambukiza. Ila kuna siku moja wakati nimeolewa niliwahi kumuuliza mzee Jimmy ni kwanini alikuwa akishutumu kuwa mimi ndio nimempa ukimwi wakati alikuwa na mwanamke mwingine? Huyo dada eeeh nimekumbuka jina lake anaitwa Manka, basi mzee Jimmy aliniambia katika wanawake wastaarabu aliowahi kukutana nao basi ni Manka, maana mara zote alizokutana nae kimwili basi Manka alikuwa akitoa kinga na kumvisha, kwahiyo 1alisema Manka hawezi kumuambukiza yeye ukimwi. Ila Jumapili nimemuona huyo Manka akiongozana kwa madaha na Rahim, laiti angejua kuwa ameenda kuuzoa ugonjwa hata asingetembea nae kwa madaha”
“Kheee kumbe, ila Rahim nae anausambaza hatari”
“Yule tabia yake kama ile yangu ya kipindi kile, ila ataacha tu”
Basi mama Angel alimfikisha Dora kwenye shule aliyokuwa anasoma binti yake na kuagana nae.

Baba Angel leo alienda ofisini kwake kwanza, halafu alitoka ili aende kiwandani, ila wakati yupo njiani kuna mtu alimuona na kumshangaa kidogo maana hakutegemea kama angemuona mitaa hiyo, basi akasimamisha gari ili kumsalimia maana alimuheshimu huyu mama, alikuwa ni bi. Aisha, basi akamsalimia pale na kuanza kuongea nae machache,
“Nilimuona mkeo kaja kule kaburini kwa mzee wenu, tafadhari usimruhusu tena mkeo kwenda kule peke yake”
Baba Angel aliona ni vyema kama akimuuliza vizuri kuhusu hilo, basi alisogea nae karibu na gari lake na kuanza kumuuliza,
“Kwani mama tatizo ni kitu gani?”
“Sikia nikwambie, ni kweli mzee Jimmy alikuwa ni baba yenu na aliwapenda sana watoto wake, yani ni kweli kabisa aliwapenda, ila huyu mzee naweza sema ni mzee ambaye alikuwa na tabia chafu ya kujaribu kufanya vitu ambavyo huwa vina matokeo mabaya badae ila tu huwa anajaribu kuona kama itakuwa anavyofikiria”
“Kivipi, sikuelewi”
“Ni kweli kunielewa itakuwa ngumu sana, mimi sikujua ni kipi kipo kati ya mkeo na baba yako mzazi, ila badae nikagundua kuwa baba yako alikuwa akimpenda sana mkeo, yani hata siku ya harusi yako alitamani yeye ndio amuoe mkeo, kile kitendo cha wewe kumpiku yeye kilimuuma sana. Ila hili sidhani kama lilikuwa tatizo sana, kwani mzee Jimmy umri ulienda na alikuwa na kila sababu ya kuacha wewe na mkeo mfurahie ndoa yenu. Ila sijui nini tena kilimuingia na kuanza kufikiria kufanya ujinga”
“Ujinga gani?”
“Erick, ukiwa na muda naomba ufike nyumbani kwangu na tuongee mengi sana. Nahitaji kuongea nawe kwa kirefu kuhusu baba yako, najua kuna mengine nayajua lakini wewe huyajui wala nini. Kwanza watoto wenu wale mapacha wanaendeleaje?”
“Wanaendelea vizuri tu”
“Basi nashukuru kwa hilo, maana katika vitu vyote ni wale watoto ndio huwa wananipa mashaka. Ila tutaongea vizuri tu”
Kwakweli baba Angel alitamani siku hiyo hiyo asikie kila kitu, yani alijikuta akiwa tayari kuacha mambo yote ambayo alikuwa akiyafatilia siku hiyo ili akamsikilize huyu mama, basi alimuomba ampeleke huko kwake ili akamwambie ukweli,
“Hapana Erick sio leo, nitagfute kwa siku yako”
Basi yule mama alimpa tu baba Angel namba yake ya simu ili waweze kuwasiliana, baada ya hapo yule mama aliondoka zake.
Kwakweli baba Angel alienda kiwandani ila mawazo yote ni kwa huyo mama kwani alitamani kuujua ukweli wa mambo yote ulivyo.

Usiku wa leo, mama Angel anamueleza mumewe kuhusu kilichojiri wakati wa yeye kumpeleka Daima kwao,
“Kumbe baba yake Daima ni mtu ambaye namfahamu”
“Unamfahamu kivipi?”
“Ni ndugu yake na Rahim, alinikumbuka basi tumeongea pale na wamesema kuwa watakuja kesho kwahiyo mtoto wao nimemuacha huko”
“Dah! Kesho”
“Ndio, kesho kwani kuna tatizo gani mume wangu?”
Basi baba Angel alimueleza kuhusu bi.Aisha alivyokutana nae njiani, alimueleza yote ambayo aliongea na yule mama, kisha akamwambia mke wake,
“Yani nilichokuwa nawaza ni kuwa kesho nifanye juu chini ili niende kwa yule mama na kumsikiliza kile anachokijua kuhusu baba yangu”
“Dah! Kweli mume wangu, ila kesho kuna ugeni jamani, naomba twende wote keshokutwa, usiniache peke yangu kusikiliza hao wageni mume wangu”
“Nimekuelewa mke wangu, basi sitaenda kesho, tutaenda wote keshokutwa maana nahisi hayo maneno hata wewe unatakiwa kuyasikiliza”
Wakakubaliana kwenda wote kwa siku ya kesho kutwa, ila muda huo mama Angel aliona ni vyema kumwambia dada yake ili nae afike kesho yake wakati wazazi wa Daima wanafika ili waweze kuzungumza kuhusu Daima na Junior,
“Sawa mdogo wangu nitakuja, nashukuru sana. Kwakweli umefanya jambo la akili sana, yani hata sikufikiria kabisa kuhusu swala hilo”
“Tupo pamoja dada”
Kisha kwa muda huo baba Angel na mama Angel waliamua kulala tu.

Usiku huu Vaileth aliamua kumpigia simu Junior ili aongee nae vizuri kuhusu Daima maana leo Daima hakuwepo kwahiyo akaona kuwa ataongea nae vizuri,
“Hebu nieleze ukweli Junior, huyu Daima ana mimba yako au sio yako?”
“Kwani wewe Daima huyo umemfahamu vipi?”
“Usiniulize Junior ila niambie ukweli, ninachotaka kujua ni ukweli tu”
“Huyo Daima hana mimba yangu”
“Kwahiyo mimba aliyokuwa nayo ni ya nani?”
“Ngoja nikwambie ukweli Vai, ni kwamba niliwahi kuwa na mahusiano na huyo Daima ila ni zamani kidogo, nikaachana nae ila ndio akawa analazimisha tuendelee na mahusiano, kama unakumbuka kuna siku ulikuta ujumbe kwenye simu yangu wa mwanamke akisema kuwa katoa mimba na damu nyingi zimemtoka, basi ni huyo Daima, ila hakuwa na mimba bali aliongea tu. Kuna siku aliniambia kwavile simtaki basi atasingizia kuwa ana mimba yangu ili mimi nilazimishwe kuwa nae, kiukweli Daima hana mimba na wala hana mimba yangu, huyo binti ni malaya na nilishaachana nae zamani sana”
“Mmmmh Junior”
“Kweli hiki ninachokwambia, simpendi Daima wala nini, ninayekupenda ni wewe. Nasubiri nimalize shule ili mimi na wewe tuoane na tuwe mke na mume rasmi, usisikilize habari za watu wagombanishi Vai, nakupenda sana mpenzi wangu”
“Mmmh!”
“Usigune Vai, nakupenda sana mwenzio, tena sana. Ipo siku nitaongea mbele ya hao watu wote na mbele ya mama yangu kuwa nakupenda sana wewe, achana na maneno yasiyo na maana mpenzi wangu na tuendelee kupendana tu”
Basi wakaongea pale na mwisho wa siku wakaagana na kila mmoja kulala tu.
Kulipokucha tu, Vaileth aliamka na kuanza kazi za hapa na pale kama kawaida yake, ila siku hiyo mapema kabisa mama Junior alifika na kumkuta Vaileth ndio anamalizia usafi,
“Kheee upo vizuri Vai, kumbe ndio unamalizia usafi muda huu!”
“Ndio mama, shikamoo. Karibu”
Basi mama Junior alimsubiria pale Vaileth amalize kudeki na kuingia nae ndani, ambapo mama Angel ndio alikuwa akipika chakula cha asubuhi,
“Kheee dada, ndio umekuja asubuhi asubuhi!”
“Ndio, yani hujui tu nimelala nikiwa na mawazo kiasi gani, jamani huyu Junior ataniua mimi. Mara nyingine ni bora hata uwe na watoto wawili na kuendelea kidogo kichwa kitatulia lakini akiwa mmoja tu dah”
“Dada, unaweza ukawa na wengi ila nao wote wakakusumbua, cha muhimu ni kumuomba Mungu tu”
Kisha walikaa pale na kuandaa chakula cha asubuhi na kuanza kula,
“Yu wapi shemeji?”
“Ametoka, ila atarudi tena maana nilimuomba na yeye awepo”
“Oooh hapo sawa sawa”
Basi wakaendelea na majukumu mengine ya siku hiyo.

Baba Angel alijitahidi kumaliza majukumu yake mengine ili akawawahi hao wageni na kuwasikiliza maana mkewe alishaongea nao na walisema wataenda kwenye mida ya saa nane, kwahiyo kwenye saa saba baba Angel alitoka zake kwenye shughuli zake na kuanza kuelekea nyumbani kwake, ila njiani alimuona yule mteja muarabu ambaye alipanga kukutana nae rasmi ila hakuweza kuonana nae siku aliyoenda, basi akasimama na kuanza kumsalimia pale huku wakiongea mawili matatu,
“Tulijaribu kukufata kwenye duka lile ulilotuelekeza ila ulikuwa umeondoka”
“Kweli mimi ni mtu wa mihangaiko sana, si unajua sisi wafanya biashara tulivyo hatutulii sehemu moja”
“Dah! Basi tukakukosa bhana”
“Hakuna tatizo lakini, tuwe tunawasiliana ndio itakuwa rahisi zaidi kuonana”
“Sawa, sawa”
Baba Angel leo alichukua mawasiliano ya huyu mwarabu ili awe anawasiliana nae mwenyewe, basi akaagana nae na kwenda nyumbani kwake.
Na alivyofika tu nyumbani, na wale wageni nao walifika, yani baba Daima, mama Daima pamoja na Daima mwenyewe.
Basi waliwakaribisha pale na kuanza kuongea nao, wakati huo Vaileth alikuwa akiwaletea vinywaji pale ili washushie wakati wa maongezi, na maongezi hayo aliyaanza baba Daima,
“Unajua kwanza nimeshtuka sana ile jana kugundua kuwa binti yangu ni mjamzito, yani kilichotuleta hapa ni kujua hatma ya hii mimba”
Baba Angel aliongea nae,
“Cha kwanza kabisa tujue, mimba hiyo ina umri gani?”
Mama Daima akajibu,
“Ina miezi mitatu kwasasa, ni mimi mwenyewe ndio nilienda hospitali na Daima na kugundua kuwa ni mjamzito”
Basi baba Angel akaendelea kuongea,
“Sawa, tuongee kama wazazi sasa, hatutaki baya litokee kwa mtoto wenu wala baya litokee kwa mtoto wetu. Hawa ni watoto wetu, inatakiwa sisi wazazi tujue jinsi ya kufanya”
“Ila ni vizuri kama na huyo mwanaume angekuwepo hapa ili atujibu vizuri”
“Baba Daima, wewe ni mwanaume mwenzangu nadhani unaelewa fika haya mambo yalivyo. Jamani mimi kwanza kabisa naomba msamaha kwaajili ya Junior, ila kwasasa yupo shuleni, na sisi kama wazazi tutakuwa bega kwa bega nanyi kwa jambo hili”
“Kivipi? Kumbuka huyo Junior kaharibu maisha ya mwanangu maana mwanangu ana mimba sasa, je atamuoa? Tunahitaji hili jibu kutoka kwake”
“Sawa, hakuna tatizo. Inabidi kikao kijacho awepo na Junior, mimi nitaenda kumfata Junior shuleni ili Jumapili awepo hapa na kikao hiko kifanyike akiwepo ila kwanza wazazi tupate muafaka”
“Hakuna muafaka wa wazazi tupu hapa, nataka kauli ya kijana kwanza ndio niendelee kuongea kama baba. Yupo tayari kumuoa mwanangu? Nikijua ndio nitasema ninachotaka kusema”
Baba Angel alipumua kidogo ila hakutaka kufanya marumbano pale, ikabidi wakubaliane kuwa Jumapili ataitwa Junior ili kusema pia kuhusu kumuoa Daima au la.
Baada ya maongezi hayo, waliwakaribisha mezani ili waweze kula chakula, na kweli walikaa mezani na kula, huku wakinywa juisi, ila wakati wa kula baba Daima akasema,
“Hii juisi nimekunywa tangu mwanzo nikashindwa kuongea, ila naomba niulize muda huu. Hii juisi imetengenezwa na mama mwenye nyumba eeeh!!”
Baba Angel alimuangalia baba Daima na kumuangalia mke wake kisha akauliza,
“Kwanini?”
“Nishawahi kunywa juisi ilitotengenezwa naye”
“Ni kweli nimetengeneza mimi”
Mama Angel alisema ili kukatisha yale mazungumzo kidogo, kisha baba Daima akasema,
“Ni nzuri sana kwakweli, hongera sana”
“Asante”
Basi walivyomaliza kula, waliongea ongea kidogo na kuamua kuondoka ila Daima waliamua kumuacha hadi hiyo Jumapili ambayo wataenda kufanya kikao kingine,
“Ila huyu Daima abaki tu hadi hiyo Jumapili”
“Hakuna tatizo, tutakuwa nae hapa tu”
Kisha mama Daima na baba Daima wakaaga tena na kuondoka zao.
 
SEHEMU YA 346

Ila mama Daima na baba Daima walivyotoka tu nje ya geti, kuna mwanamke alikuwa karibu na pale, na kumuita baba Daima pembeni kwahiyo mama Daima alisimama tu kuwasubiri maana hakuelewa yule mwanamke kamuitia nini mume wake,
“Samahani, najua hunijui”
“Sikujui ndio”
“Mimi naitwa Sia, ila kuna kitu nimekiona kwako”
“Kitu gani?”
“Wewe si umekuja kwaajili ya binti yako mwenye mimba ya Junior?”
“Ndio, tatizo nini kwani?”
“Huyu mama mwenye nyumba, ana mtoto anaitwa Angel, huyo mtoto baba yake anatamani sana kumuona ila huyu mama hataki kabisa mtoto amfahamu baba yake anamficha, kwahiyo ongea nae labda wewe atakuelewa”
“Kwani wewe ni nani na huyo baba yake Angel”
“Aaaah….. mimi aaaah…. Mimi ni msamalia mwema tu ambaye namuhurumia Angel na ninapenda amtambue baba yake wa halali”
“Sikia nikwambie kitu, huyo baba Angel unayemsema ni ndugu yangu kabisa, anaitwa Rahim. Sasa sisi wenyewe wenye ndugu hatuna tatizo ila wewe jirani inakuuma nini? Angel kafanana sana na baba yake, kuna kipindi yeye mwenyewe atamtafuta baba yake halali”
“Ndio, tatizo lenu wanaume hilo mpaka mnakosa haki yenu sababu ya mambo hayohayo, sijui mpoje. Hivi unajua kama mtoto akishajazwa ujinga na mama yake basi huwezi ukampata kamwe, yani wewe badala upigani haki ya ndugu yako unasema kuwa Angel atamtafuta mwenyewe baba yake. Umemuona huyo Angel au unaongea tu kujifurahisha?”
“Kwanza nikuulize, wewe unamfahamu vizuri huyo Rahim? Amekwambia kuwa anashida na huyo mtoto kwasasa?”
“Asingekuwa na shida basi asingekuja hapa na kupigwa na Erick”
Baba Daima akacheka sana na kumwambia Sia,
“Wee unachekesha sana, Erick ndio wa kumpiga Rahim? Hebu uwe unafikiria kwanza kabla ya kuongea huo utumbo”
Halafu baba Daima alimfuta karibu mke wake na kuondoka nae.

Leo walipofika nyumbani tu, mama Daima alishindwa kuvumilia na kujikuta akimuuliza mumewe kuhusu mama Angel maana aliona wana ukaribu zaidi,
“Samahani mume wangu, kwani yule ni nani?”
“Yupi huyo?”
“Yule mama Angel?”
“Oooh leo umeniuliza, ngoja nikwambie kwa kifupi. Yule anaitwa Erica, ni msichana mwenye bahati ya kupendwa sana”
“Kivipi?”
“Aaaah naona tutaweka mada ndefu bure, ila siku ukikutana na kaka yangu Rahim muulize Erica ndio nani katika maisha yake basi atakwambia mengi sana”
“Sikuelewi, kwahiyo wewe uliwahi kunywa juisi ya kutengenezwa na yeye wakati yupo na kaka yako?”
“Mengine nikiongea mke wangu utatafuta tu njia za kuumiza moyo wako ambazo hazina umuhimu wowote”
“Aaaah niambie tu, kwani si yatakuwa ni mambo yaliyopita zamani, mimi wa nini tena? Nahitaji tu kujua na kumtambua vizuri huyo mwanamke”
“Kwanza ulimuona yule mwanamama ambaye aliniita pale nje ya geti? Ngoja nikwambie alichokuwa anasema”
Basi akamuelezea kile ambacho alikuwa akiongea na Sia, baada ya hapo akamwambia mke wake,
“Tena nitampigia simu Erica kumweleza kuhusu hili, maana sijaelewa kama yule mwanamke ana maana gani kwake”
“Kwahiyo Erica kazaa na Rahim? Au huyu Erica ndio yule niliyekuwa nasikia habari zake kipindi kile pale kwa mama yako mkubwa”
“Habari gani?”
“Si nilisikia huyo Erica katembea na nyie wote, yani hakujua kama nyie ni ndugu au ni yupi?”
“Mmmh tuachane na hayo mke wangu, tuongee mambo mengine tu”
Basi mama Daima hakuwa na maneno zaidi.

Mama Junior nae aliaga na kuondoka zake, walikubaliana tu kuonana hiyo Jumapili,
“Kwahiyo shemeji utamfata Junior huko shuleni”
“Ndio, hata usijali shemeji yangu”
Basi aliwaaga pale na kuondoka zake, muda ule ule baba Angel akakumbuka pia kuhusu bi.Aisha basi akamwambia mke wake,
“Kwanini tusimuulize yule bi.Aisha muda huu alipo ili kama yupo nyumbani kwake tumfate na tuweze kuongea nae”
“Mmmh tutaondoka muda huu? Ila kama muda umeenda?”
“Sio sana mke wangu, kwanza wakina Erica karibia wanarudi kwahiyo watakuwepo tu hapa nyumbani. Ngoja nimpigie sasa hivi nimsikie”
Baba Angel alichukua simu yake na kumpigia bi.Aisha ambapo baada ya muda mfupi tu alipokea,
“Unaongea na Erick hapa mama, samahani uko wapi leo maana nilihitaji sana kuonana na wewe ili tuweze kuongea”
“Oooh kwa leo haiwezekani, labda kesho”
“Aaaah sawa mama, basi kesho nitakutafuta”
“Jioni ndio itakuwa vizuri maana nitakuwa nimerudi nyumbani”
“Sawa, mama yangu kwaheri”
Basi baba Angel aliagana na huyu mama na kumpa ujumbe mkewe kuwa wataenda tu kesho,
“Basi asubuhi nitaenda kwanza kwenye shughuli zangu halafu jioni nitakuja kukufata ili twende kwa huyo mama”
“Sawa, hakuna tatizo”
Kisha baba Angel aliamua kupumzika kidogo kwa siku hiyo ili kupumzisha mawazo yake kwanza.

Usiku wa siku hiyo, simu ya mama Angel ilianza kuita, alipoiangalia alikuta ni baba Daima ndio anapiga, basi akaamua kupokea na kuanza kuongea nae, alimuelezea kuhusu mtu aliyekutana nae nje ya geti lao, na kumpa tahadhari kuhusu mtu huyo, basi alipomaliza kuongea mama Angel akamwambia mumewe,
“Hii sasa imezidi jamani, huyu Sia amezidi mno”
“Kafanyaje tena?”
Mama Angel alianza kumuelezea kile ambacho alikuwa akiongea na baba Daima, kisha akamwambia mumewe,
“Kwakweli hii tabia ya Sia inavuka mipaka sasa, yani tusipokuwa makini atafata hata wasiostahili kufatwa”
“Sasa tufanyeje mke wangu”
“Naona ni bora tukutane na huyu mtu tuongee nae ilia ache hii tabia, kwakweli ananikera sana mimi”
“Sasa mke wangu tukakutane na yule chizi wa kazi gani?”
“Hapana, inabidi tuonane nae tu. Kwakweli mimi ananichosha sana, tena inabidi tuwe pamoja”
“Basi mke wangu tufanye hivi, kesho asubuhi twende wote tukaongee nae, halafu nikakurudisha nyumbani na kwenda kwenye shughuli zangu halafu jioni nitakufata tena kwaajili ya kukutana na yule bibi”
“Sawa sawa, hapo nimeridhika sasa”
Kwahiyo wakakubaliana asubuhi kwabisa kwenda nyumbani kwa Sia kwanza.

Kulipokucha kama ambavyo walipanga kwenda kwa Sia, walijiandaa kwa kila kitu na kumuacha mtoto kwenye mikono ya Vaileth, halafu wao waliondoka.
Basi walikuwa wakiongea mengi tu kwenye gari,
“Ila mume wangu jamani, hadi ukapajua kwa Sia!”
“Mtu anatusumbua kiasi hiki ndio nisijue nyumbani kwake kweli? NIliona ni lazima nipajue tu”
Mama Angel alicheka tu na safari yao ikaendelea.
Walifika nyumbani kwa Sia, na kushuka kwa pamoja ili waende kugonga, ila walipokuwa wanakaribia mlango walishangaa kuona Sia akiwa anatoka ndani kwake huku kaongozana na bi.Aisha.

Walifika nyumbani kwa Sia, na kushuka kwa pamoja ili waende kugonga, ila walipokuwa wanakaribia mlango walishangaa kuona Sia akiwa anatoka ndani kwake huku kaongozana na bi.Aisha.
Basi mama Angel ndio alianza kuongea,
“Jamani bibi mwenyewe tunayesema tutamfata badae si ndio yule pale anatoka nje na Sia jamani?”
“Ndio mwenyewe, swali ni kuwa anafanya nini nyumbani kwa Sia?”
“Ndio hapo sasa?”
Ila walipoangalia tena yule bi.Aisha ilikuwa kama kaingia ndani tena maana hakuonekana pale nje, ni Sia ndio alibaki peke yake, basi walimsogelea na bila ya salamu walianza kumuuliza, ni mama Angel ndio aliyeanza kumuuliza,
“Yule bibi uliyeongozana nae muda mfupi uliopita yuko wapi?”
“Yupi huyo?”
“Yule uliyekuwa umeongozana nae”
“Khaaaa unaugua macho au, nimeongozana na mtu saa ngapi jamani?”
Baba Angel ilibidi aingilie kati na kuluuliza,
“Yule bi.Aisha uliyekuwa umeongozana nae”
“Jamani, ndio nani huyo?”
“Halafu Sia, hebu acha huo uchizi wako, ni nani uliyekuwa umeongozana nae muda mfupi ulipita?”
“Unajua mnaweza kusema mimi chizi ila na mimi nawaona nyie ndio machizi maana mnaniuliza kuhusu mtu nisiyemfahamu kabisa yani, sasa mimi nimeongozana na mtu gani kuja nje? Na nimetoka nae wapi?”
“Umetoka nae ndani kwako humo?”
“Kheeee niondoleeni balaa, humu ndani nilikuwa naishai mimi, mwanangu Elly na watoto watatu wa ndugu zangu ambao wote hao watatu nimewapeleka kwa mama zao, halafu Elly siku hizi huwa karibia na mwisho wa wiki analala kwa mamake mdogo huko, sasa nyie mnanieleza kuwa niliongozana na mtu ni mtu gani huyo?”
“Unajua Sia achja kutuchezea akili, tukuone kabisa uongozane na mtu halafu ukatae kweli? Hebu kuwa mstaarabu basi”
“Hivi mnachokifanya nyie ni ustaarabu? Mmefika hapa hakuna cha salamu wala nini zaidi ya kuniuliza mtu niliyetoka nae ndani, nitoke na mtu gani mimi? Ndiomana nawashangaa. Ila karibuni na sijui niwasaidie nini”
“Haya hakuna tatizo, ngoja tu tuongee na wewe kitu kilichotuleta hapa”
“Kitu gani?”
“Tena ngoja nikwambie vizuri Sia, hili ni onyo la mwisho, sitorudia tena kukwambia chochote kile, sikia hatujakwambia utusaidie kumtafuta baba mzazi wa Angel, mimi ndio baba yake Angel na imeisha hiyo sitaki lingine lolote la ziada zaidi ya hilo, naomba kuanzia leo sitaki kusikia kwa mtu yoyote sijui umemsimamisha na kuanza kuongea nae kuhusu Angel najua unajua ni kitu naweza kukufanya, tafadhari kaa mbali na mtoto wangu, sitaki kukusikia tena ukisema lolote kwa mtu yoyote kuhusu Angel, nikisikia tu sitakuja kuongea na wewe kwa maneno bali nitaongea nawe kwa vitendo, mjinga sana wewe”
Kisha baba Angel alimshika mkono mke wake na kurudi nae kwenye gari kwaajili ya kwenda nyumbani.

Na kweli walianza safari ya kurudi nyumbani kisha baba Angel alimuuliza mkewe kuhusu kuonana na bi.Aisha,
“Hivi tuendelee na wazo la kuonana na bi.Aisha?”
“Mmmh sijui, yani sielewi, kwanza ameenda kufanya nini kwa Sia?”
“Hilo sio tatizo sana, ila kwanini ajifiche? Inaonyesha katuona ndio kaenda kujificha, na hapo lazima tuwe na mashaka nae”
“Kama kumsikiliza nenda tu halafu utaniambia”
“Kwanza alisema jana haiwezekani kumbe ndio yupo kwa huyu chizi, naona ndio kalala huku huku, labda wana undugu sijui ila kwanini atukimbie?”
“Na kwanini Sia agome kuwa hamfahamu?”
“Yani hapo ndio penye utata, ila hata sijui kama nitaenda kumsikiliza”
Basi walirudi nyumbani na mama Angel alishuka halafu baba Angel alienda kwenye shughuli zake.
Mama Angel aliingia ndani kama kawaida alimkuta Vaileth kabeba mtoto mgongoni huku akiendelea na shughuli zingine, mama Angel hakuongea chochote na Vaileth kwani moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kumfata Daima ambaye alikuwa yupo kuchezea simu, mama Angel alitikisa kichwa kidogo na kumuuliza,
“Daima unaendeleaje?”
“Sijambo, shikamoo”
“Marahaba, hivi unadhani unachofanya ni sahihi? Mfano unaishi kwako, hutofanya chochote sababu ya mimba? Ni kweli mimba zinakuwaga na mtindo Fulani wa usumbufu ila kwako imezidi jamani, ndio hata kukaa na mtoto kidogo huwezi wakati mwenzio akiendelea na kazi zake?”
“Samahani mama, naogopa mimba yangu itatoka”
“Nani alikwambia mwanamke akifanya kazi mimba inatoka?”
“Wanasema tusiiname, tusifanye kazi yoyote mpaka kujifungua”
“Hizo ni mimba zenye matatizo, mfano wale wenye watoto wadogo na anaishi mwenyewe na ana mimba, unadhani wale watoto wake anawalea nani? Haya mimba inahitaji mazoezi, bora hata ungekuwa unatembea tembea ila unalala na simu tu muda wote ndio mimba gani hiyo wewe binti? Ndiomana mama yako hakutaki nyumbani, kumbe hujielewi kabisa wewe”
Kisha mama Angel alimuacha na kwenda kumchukua mtoto kwa Vaileth na kwenda nae chumbani kwake.

Baba Angel alipomaliza shughuli zake, aliamua kupita shuleni kwakina Erick na kumchukua Erick ili kwenda nae kiwandani, na kweli aliongozana nae hadi kiwandani na kuanza kufanya zile kazi za kiwanda huku wakiongea kuhusu mambo mbalimbali.
Baada ya kumaliza mambo yote, wakati wapo ofisini, baba Angel aliuliza pia kuhusu duka,
“Nilishampata muuzaji mpya, yupo vizuri sana baba, kwakweli ni mkarimu na ana upendo kwahiyo wateja wengi wanapenda kuhudumiwa nae”
“Ooooh upo vizuri sana mwanangu, basi leo tukitoka hapa tutapitia huko”
Walikubaliana na muda mfupi tu walivyotoka pale kiwandani walianza safari ya kwenda dukani.
Ila walivyofika tu dukani, kuna mtu baba Angel alimuona akitoka dukani, ni mtu aliyemfahamu ila hakujua ni kitu gani ameenda kufanya pale dukani, basi moja kwa moja walipoingia dukani na kutambulishwa kuhusu Rama alianza kumuuliza,
“Samahani, yule aliyetoka dukani muda mfupi uliopita unafahamiana nae?”
“Hapana, ila aliwahi kuja kununua bidhaa mahali hapa, na alinunua nyingi tu. Basi tokea hapo kawa mteja mzuri kwani mara nyingi anakuja kununua bidhaa mahali hapa”
“Sawa, kuna kitu huwa anaongea na wewe?”
“Si mara zote, ni leo tu ndio kaniuliza kama naridhika kuwa hapa nilipokuwa, nami nilimjibu kuwa naridhika kwani kwakweli sehemu hii inanisaidia sana kwenye mambo yangu mengi tofauti na nilivyokuwa nimekaa bila ya kuwa na kazi ya aina yoyote ile”
“Sawa nimekuelewa”
Kisha baba Angel alifatilia mahesabu na kila kitu pale dukani, halafu yeye na Erick waliondoka zao kurudi nyumbani.
Njiani, Erick alimuuliza baba yake,
“Kwani yule aliyetoka ni nani?”
“Aaaah sijui, nilikuwa namuulizia tu”
“Kafanana na yule ambaye alikuwa anampa Erica hela?”
“Kheeee kashawahi kumpa tena!!”
“Ila Erica alikataa”
Basi baba Angel alitulia tu na moja kwa moja kurudi nyumbani kwao.

Leo Elly alipotoka shuleni, moja kwa moja alirudi akiwa na Sarah hadi nyumbani kwakina Sarah, basi walikuwa wakiongea mambo mengi sana ya kuhusu shule na kila kitu.
Walimkuta mama yao nyumbani akiwa tu na shughuli zake,
“Bora Elly umekubali kuja leo”
“Ni mimi ndio nimemlazimisha mama, eti leo Ijumaa halafu anasema kuwa aje Jumamosi, nimemwambia weee tutaenda tu wote leo, ndio nimerudi nae”
“Hivyo ni vizuri hata mimi nimefurahi ila leo sitakuwepo nyumbani maan akuna sherehe ya wenzangu inaanza saa mbili usiku kwahiyo kwenye saa moja moja nitaondoka hapa”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Basi moja kwa moja Elly nae alisalimiana vizuri na mamake Sarah na kwenda ndani.
Muda ulipofika, mama Sarah alikuwa kashajiandaa na kuondoka zake kwenda kwenye hiyo sherehe, kwahiyo ndani alibaki Elly, Sarah na Siku.
Muda kidogo Siku nae alimwambia Sarah,
“Kuna mgeni wangu hapo barabarani tu, naenda kuongea nae na nitarudi badae”
“Mmmh saa ngapi dada?”
“Usijali, kwani unaogopa nini na Elly yupo humu ndani”
Basi Siku nae akatoka zake kwahiyo ndani alibaki Elly na Sarah tu, walikuwa wakiangalia luninga muda huo, ila Sarah akamwambia Elly,
“Eeeeh nimekumbuka, ngoja nije nikuonyeshe zile video, unajua hadi nina mikanda yake kabisa”
“Mmmmh mikanda yake?”
“Ndio”
Sarah alisogea na kuweka mkanda kwenye video na ule mkanda ulianza kuonyesha muda ule ule,
“Kheee Sarah! Ni vitu gani hivyo jamani?”
“Si unaona mwenyewe wanavyofanya hapo? Ndio mapenzi hayo?”
“Mimi naogopa kuangalia Sarah, watu hao wapo watupu kabisa”
“Ndio yanavyofanywa, mapenzi hayafanywi na nguo”
Elly alikuwa akiangalia kwa uoga, yani alikuwa anaangalia huku anaangalia kama kuna mtu anatokea kuwaona wakiangalia kitu cha namna hiyo, naye Sarah alielewa ile hali ya uoga ya Elly, basi alizima tv na kutoa ule mkanda, halafu akainuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na baada ya muda alirudi na kumuita Elly,
“Twende chumbani kwangu”
“Kufanya nini?”
“Kuangalia ule mkanda maana nako nina video, halafu hujawahi kuingia chumbani kwangu eeeh!”
Elly alikuwa na uoga ila aliinuka na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Sarah ambapo ule mkanda ulikuwa ukiendelea, kisha Sarah akamwambia Elly,
“Kwanini na sisi tusivue nguo ili tujaribu wanachokifanya?”
Yani kwa muda huu Elly hata hakuweza kujibu kitu chochote ila alijikuta tu akivua nguo na mwisho wa siku alijikuta akiwa amelala na Sarah.
Kilichokuja kuwashtua ni hodi iliyopigwa, ni hapo Sarah alipogundua kuwa Siku amerudi, basi Elly alikuwa na wasiwasi sana,
“Usijali Elly, ni Siku huyo ngoja nikamfungulie”
Sarah alijifunga taulo na kwenda kumfungulia Siku, ambaye aliingia na kufunga mlango wala hakuongea kitu kwani moja kwa moja alienda chumbani kwake, kisha Sarah alirudi alipokuwa Elly, kwakweli Elly alionekana kuona aibu kwani ni kitu ambacho alikiona kwa mara ya kwanza na ni kitu ambacho alikifanya kwa mara ya kwanza, ila muda kidogo alimuona Sarah kainama huku akilia, basi alimfata karibu na kumuuliza,
“Unalia nini Sarah, nimekuumiza? Nisamehe tafadhari, nisamehe sana sikujielewa kwakweli naomba unisamehe”
“Usijali, nalia sababu nimeharibu usichana wangu, unajua kufanya hivi ni kuharibu usichana, kwahiyo mimi sio msichana mdogo tena”
“Nisamehe Sarah! Ila hizi video ni mbaya, naomba tusiangalie tena. Nisamehe Sarah”
Elly aliinuka na kwenda chumbani kwake, na hapo hata Sarah alienda kuoga sasa.
 
SEHEMU YA 347

Kwakweli huu ulikuwa ni usiku wa mawazo sana kwa Elly kwani hakutegemea kutokea kwa kile kilichotokea, alibaki tu anakijutia katika moyo wake, alikumbuka pia mausia ya mama yake kuwa anatakiwa kuwa makini sana, basi alikuwa akijisemea,
“Ila mama kanionya sana juu ya mambo haya, sijui kwanini nimefanya hivi jamani! Sarah kaniponza halafu atanichukia na kunifanya nianze kujilaumu mwenyewe”
Yani hakuwa na raha hadi panakucha bado hakuwa na raha kabisa.
Siku hii aliitwa tu kwenda kunywa chai maana hata hakutoka chumbani sababu roho yake ilikuwa ikimsuta sana, basi akatoka na kwenda kunywa chai ila hakuongea sana kwani alipomaliza tu kunywa chai alitoka nje na kwenda kukaa peke yake, huko Sarah alimfata na kuanza kuongea nae,
“Mbona upo hivyo Elly?”
“Nisamehe sana Sarah, najihisi vibaya, najihisi ni mkosaji”
“Hujanikosea chochote, kumbuka ni mimi ndiye niliweka ule mkanda na sababu kubwa nilitaka kujaribu ile kitu ingawa nilijua kuwa itaharibu usichana wangu”
“Ila nimekuumiza nisamehe”
“Usijali, ni kweli nimeumia ila nasikia ndio inavyokuwaga kwa siku ya kwanza”
“Naogopa mama akijua itakuwa ni tatizo kubwa sana”
“Hata usijali, hii ni siri baina ya mimi na wewe, hatojua mama wala Siku, yani ni mimi na wewe tu. Hata usijali, sisi sio wa kwanza kufanya huu mchezo, dunia nzima wanafanya”
“Ila dah nimeogopa”
“Kwani haikuwa nzuri eeeh!! Hebu niambie na wewe ulivyojisikia, nilikuwa nakuona hadi ulibadilika yani”
Elly hapa alicheka tu kwani hata maelezo hakuwa nayo kabisa, na baada ya hapo walianza kuongea kawaida tu kama walivyotambulishwa kuwa ni ndugu kwahiyo walianza kuongea kindugu na kirafiki hata mama Sarah alipowaona alifurahi sana na kusema kwa hakika Sarah kapata ndugu yake.
Muda kidogo mama Sarah alijiandaa na kutoka kwahiyo aliwaacha wale watoto wakiwa na mambo yao pale nje, kwake ilikuwa ni furaha sana.
Wakati alipokuwa njiani alipitia kwenye biashara ya Sia na kuanza kuongea nae mawili matatu,
“Yani Elly ni mtoto mzuri sana, wanapendana na Sarah hadi raha jamani, yani Elly na Sarah wanapendana hadi raha”
“Ooooh hiyo ni nzuri sana”
“Halafu unajua ni ndugu wale eeeh!!”
“Kivipi?”
“Sarah ni mtoto wa Erick, halafu Elly pia ni mtoto wa Erick”
“Kumbe ulizaa kweli na Erick?”
“Ndio, ingawa hawataki kukubali huo ukweli, ila Erick anatambua wazi kuwa mtoto ni wake. Yani Elly na Sarah kama wanajuana vile ni ndugu kabisa maana wanapendana sana”
“Oooh hiyo ni habari njema, nimefurahi sana kusikia habari hiyo”
“Basi mimi nimepitia tu kukusalimia, kwaheri”
Mama Sarah aliondoka zake.

Muda kidogo pale alipokuwa Sia, alifika Tumaini na kumwambia,
“Nimemuona mama Sarah kaondoka hapa, kumbe mnajuana?”
“Ndio, yani mwanamke ana moyo wa upendo sana yule. Bora hata ingekuwa ni yeye ndio kaolewa na Erick”
“Kivipi?”
“Amezaa na Erick yule, yani kama unamfahamu huyo Sarah basi ni mtoto wa Erick”
“Duh! Haiwezekani, sijawahi kumfahamu kabla. Sikia nikwambie kitu Sia, wanawake wa Erick karibia wote nilikuwa nawafahamu, yani kila mwanamke wake alikuwa akinitambulisha, huyo mama Sarah hapana kwakweli”
“Na wewe kama umerogwa na huyo Erica, unavyomtetea kaka yako loh! Ila huyu mama Sarah ana roho nzuri sana”
“Kakufanyia nini?”
“Kamchukua mwanangu Elly anaishi nae na anamsomesha”
“Kwahiyo Elly anaishi nyumbani kwa huyu mama na yule binti yake?”
“Ndio, mbona kama umeshtuka vile”
“Sijashtuka tu ila nasikitika sana, hata kama umechoka kulea mwanao ila sio kwenda kumpeleka akalelewe na yule mama, hajui kulea watoto yule, umemuona huyo mwanae Sarah! Ila sababu Elly ni wa kiume hakuna tatizo, ila mama Sarah hajui kulea watoto yule”
“Naona nimekuambukiza tabia ya kufatilia maisha ya watu, pole utachukiw akama mimi bure”
Tumaini akaona kuendelea kuongea na huyu mtu ni kujiumiza akili yake tu, basi akaamua kuondoka zake maana muda huo alikuwa akielekea nyumbani kwa baba Angel.

Leo Erick na Erica walikuwa wakifanya usafi wa nje ya nyumba yao, kung’olea majani kwenye maua na kumwagilia maua, kwahiyo Tumaini alipofika aliwakuta ndio wanafanya hiyo kazi, aliwasalimia pale na kusema,
“Hapa kweli kaka yangu amezaa watoto jamani, ninachowapendea nyie ni kujishughulisha, mpo vizuri sana kwenye kazi, sio kama dada yenu Angel ni mvivu hakuna mfano loh!”
Akawaacha hapo nje na kuingia ndani, basi na wao wakaanza kuongea,
“Ila kweli Erick, sisi ni wachapakazi ujue, na tutakuwa vizuri sana tukiwa wakubwa”
“Sisi ni wakubwa tayari au wewe bado sio mkubwa”
Erica alikaa kimya kidogo, na Erick aliendelea kuongea,
“Kwani wewe Erica sio mkubwa? Kumbuka uliwahi kuniambia kuwa unaumwa ugonjwa wa kikubwa. Kama uliumwa ugonjwa wa kikubwa inamaana umeshakuwa mkubwa tayari, kwahiyo sisi ni wakubwa yani tunaendelea kukua tu”
“Kwahiyo na wewe ushakuwa mkubwa?”
“Ndio, si unaona sauti yangu imeanza kubadilika siku hizi”
“Imekuwa mbaya, inataka kufanana na sauti ya baba”
Walianza kucheka huku wakitaniana,
“Mbona na wewe umekuwa na manyonyo kama mama”
“Sitaki Erick, nitaenda kukusemea kwa mama sasa hivi”
“Basi yaishe, halafu ujue huwa sipendi uchukie Erica! Najua nimekuudhi, nifanye nini ili ufurahi”
“kaninunulie karata”
“Sawa, nitafanya hivyo”
Erick alimpa Erica ahadi ya kumnunulia karata kwani Erica alipenda sana kucheza karata.

Tumaini aliingia ndani na kukutana na mama Angel yupo pale na mtoto wake, basi akamkaribisha vizuri kabisa, naye alifika na kukaa kisha akamuita Vaileth na kumuagiza juisi,
“Kaniletee juisi Vai, maana najua humu ndani huwa hapakosi juisi”
Mama Angel akacheka na Vaileth alienda kumletea na kumkabidhi, kisha mama Angel akamtuma Vaileth,
“Halafu kamuite yule Daima, mwambie aje kunywa chai, jamani huyo mtu loh!”
Vaileth aliondoka, na Tumaini alianza kuulizia,
“Kwani Daima ndio nani?”
“Mwenzangu kuna makubwa hapa, yani weee acha tu. Ni hivi kuna binti kapewa mimba na Junior, basi wazazi wa huyo binti walienda kumbwaga nyumbani kwa mamake Junior, ila kaka yako kawaka hatari imebidi mama Junior aje kuomba huyu binti aishi huku”
“Kheee, huo ujinga mimi ndio siutaki, yani siwezi kukubali kabisa”
Basi Daima alitoka na moja kwa moja alienda mezani kunywa chai, na alipomaliza alienda sebleni kumsalimia mgeni aliyefika, ila Tumaini alipomuona alimshangaa kidogo na kumuuliza,
“Kheee kwani ulimaliza shule wewe?”
“Amalize wapi? Nasikia kidato cha pili alifeli, na sasa ndio huyo mjamzito”
“Nilijua tu, wewe mtoto unanikumbuka mimi?”
Daima alitikisa kichwa kuwa hamkumbuki,
“Ndio, ujinga wako ndio unafanya usinikumbuke. Mimi huwa sipendi ujinga, na nilijua tu utaishia njiani wewe mtoto”
“Unamfahamu vipi huyu mtu wifi yangu?”
“Unajua mimi, sijui nikoje yani ila nikiona watoto wanafanya mambo ya ajabu huwa naumia sana hata kama sio watoto wangu na wala sio watoto wa ndugu yangu, ila naumia kwani najua hata mzazi wa huyo mtoto akigundua ujinga anaoufanya mwanae lazima ataumia sana, sasa huyu binti nishawahi kukutana nae kama mara tatu hivi akiwa na rafiki zake wawili. Siku ya kwanza niliwakuta kwenye daladala, wamekaa siti ya nyuma na mimi ndio nikawa mtu wa nne kukaa kwenye ile siti ya nyuma, walitoa simu na kuanza kuonyeshana sijui video gani na muda huo huo walikuwa wakipiga stori za wanaume, sijui wewe mwanaume wako mzuri sijui nini na nini, kama mzazi niliumia sana, niliwaambia nakumbuka vizuri kabisa, nyie watoto elimu ni bora kuliko hayo mnayoyafanya, wanaume hawatawafikisha popote zaidi zaidi mtapata mimba na kuacha shule, niliwasema sana ila walikuwa tu wakinibinulia midomo yao michafu. Siku nyingine nilimuona na hao rafiki zake wawili, ni muda wa darasani ila wenyewe wamekaa chini ya mti eti wamechoka shule, kiukweli siku ile nilitamani kuwapiga kabisa, na niliwasema sana. Siku nyingine, haka katoto kalivaa nguo za nyumbani nikakakuta na mwanaume, nikamwambia si mwanafunzi wewe! Nikamwambia kwa mshangao, wewe ni mtoto mdogo sana. Akaniambii mtoto mdogo ulinizaa wewe? Una cheti changu cha kuzaliwa? Umeniona nimezaa sare za shule hapa? Achana na maisha yangu, nilijihisi vibaya sana siku ile. Ila haya ndio matokeo yake, haya hunikumbuki wewe mtoto?”
Daima aliinama chini kwa aibu, kisha Tumaini aliendelea kuongea,
“Huo ndio mshahara wa kiburi chako, kione vile sura ilivyokushuka kama umevaa sidiria ya mama nibebe vile”
“Mmmh basi yanatosha wifi yangu, haya Daima rudi ulipokuwa huko chumbani”
Daima akaondoka kwa aibu sana na kuelekea chumbani kwa Vaileth tu maana alipatwa na aibu muda ule.
Kisha Tumaini akamwambia mama Angel,
“Halafu msiwe mnakubali kirahisi rahisi hivyo kuwa ni mimba ya Junior, waambieni wazazi wake wakakae nae huko hadi mtoto azaliwe mkampime damu, maswala ya kutuchanganyia mada hatutaki, kwanza Junior amemsingizia tu. Ni kweli Junior ana tabia mbaya ila huyu binti kazidi sana”
“Sawa sawa, ni bora na wewe uje kwenye kikao cha kesho”
Ikabidi mama Angel amwambie kilichoongelewa mwanzo na hicho kikao cha kesho muda wake,
“Ooooh nitakuja ndio, kama wameshindwa kumlea binti yao vizuri wasituletee matatizo bure sisi hatutaki ujinga kabisa maana huu ni ujinga. Mimi nitawaeleza wazazi wake ujinga wa huyu mtoto wake, na vile vyenzake sijui kama navyo shule haijawashinda”
Wakaongea mengi sana kuhusu malezi ya watoto yani inaonyesha ile tabia ya Daima ilikuwa imemchukiza sana Tumaini.

Leo wakati baba Angel anarudi kutoka kwenye kazi zake, njiani alimuona mama Sarah, ikabidi asimame na kumuita,
“Manka”
Aliitika na kusogea, na kutaka kumkumbatia baba Angel ila baba Angel alimkinga na mikono kwa maana kuwa hakutaka kukumbatiwa, mama Sarah akamwambia,
“Yani Erick ndio hata kunikumbatia hutaki jamani”
“Kwani tatizo ni nini? Kwani usiponikumbatia utauguwa?”
“Kheee Erick, umepewa nini na huyo mwanamke jamani!”
“Usiniulize kuhusu mke wangu, kwanza nashukuru sana nimekuona leo. Hivi kwanini ulimwambia mke wangu huo uzushi wako? Nimezaa na wewe muda gani?”
“Erick na wewe hebu ongea kama mwanaume basi, kwani wewe sio mwanaume? Kwani wewe huwezi kumpa mwanamke mimba?”
“Nisikie, mimi ni mwanaume niliyekamilika vizuri kabisa ila najua wazi kuwa sijazaa na wewe Manka”
“Unakataa vipi wakati tumezaa mtoto Sarah pamoja jamani”
“Tena ukome kabisa Manka, najua tulikuwa na mahusiano ndio ila sijazaa na wewe, na kama ungekuwa na mtoto wangu basi asingekuwa umri wa huyo Sarah, lazima angekuwa ni mkubwa sana kushinda hata watoto wangu, ila unaniletea mtoto rika la watoto wangu halafu unasema tumezaa? Hebu akili yako ifanye kazi basi, acha kunizushia ujinga”
“Sawa, nilishaambiwa kabla kuwa ni tabia yako kukataa watoto wa nje kwahiyo hata Sarah unamkataa sababu unamuogopa mke wako”
“Hayo mambo ya kumuogopa mke wangu hata hayakuhusu, ila sitaki unizushie, mwanamke mbaya sana wewe, ushamdanganya mwanao kuwa ni mtoto wa baba yangu”
“Ila mimi sikujua kama mzee Jimmy ni baba yako”
“Mjinga wewe, kwaheri”
Baba Angel aliingia kwenye gari yake na kuondoka zake kwani hakutaka tena kumsikiliza mwanamke huyu.

Jumapili ya leo ni Erica na Erick tu pamoja na baba yao ndio walienda Kanisani.
Kisha walipotoka, baba yao aliwaacha karibia na nyumbani halafu yeye akaenda shuleni kwakina Junior ili kumfata Junior.
Basi Erick na Erica muda huu walikuwa wakitembea kuelekea nyumbani kwao, ndio njiani walikutana na Abdi akiwa ameongozana na Bahati, pale Erica alishangaa sana na kuwauliza,
“Kwani nyie ni ndugu?”
Bahati alijibu,
“Ndio, mimi ni kaka na huyu ni mdogo wangu”
“Aaaaah kumbe!!"”
Basi Abdi alianza kimsalimia Erica pale ila Erick alikuwa kimya tu kanakwamba hamfahamu Abdi wala huyu Bahati hajawahi kumuona.
Basi Erica aliongea nao kidogo na kuondoka na kaka yake, ila leo Erick hakusema chochote hadi ilibidi Erica amuulize mwenyewe,
“Mbona leo hujasema kitu?”
“Sasa ulitaka niseme kitu gani?”
“Mmmh haya basi, ila yanayoendelea nyumbani unayaelewa kuhusu yule msichana wa kuitwa Daima?”
“Sijui”
“Mmmh yani Erick mambo yako loh! Yule ana mimba ya Junior, ndiomana baba kamfata Junior leo shuleni. Sipati picha siku ikiwa wewe ndio umempa mwanamke mimba"
“Erica unasemaje!!”
“Aaaah hamna kitu, twende ndani”
Erick hakusema kitu kingine zaidi ya kuingia ndani tu.
Walipoingia walikuta kuna ugeni tayari pale kwao kwani mama Daima na Baba Daima walishafika, mama Junior nae alishafika kwahiyo muda huo walikuwa wakimsubiri baba Angel tu na Junior.

Baba Angel aliondoka na Junior na kuanza safari ya kuelekea nae nyumbani, ila Junior alimuuliza,
“Kwani kuna nini bamdogo?”
“Utajua huko huko nyumbani, twende tu”
Basi wakawa wanaendelea na safari tu.
Ila walivyofika getini kuna mgeni nae aliwasili mahali pale, baba Angel alionekana kuchukia sana kumuona yule mgeni nyumbani kwake, alishuka kwa hasira toka kwenye gari.

Ila walivyofika getini kuna mgeni nae aliwasili mahali pale, baba Angel alionekana kuchukia sana kumuona yule mgeni nyumbani kwake, alishuka kwa hasira toka kwenye gari yake.
Moja kwa moja alimfata yule mgeni na kumuuliza,
“Umefata nini hapa nyumbani kwangu Linah?”
Linah nae alionekana kishtuka kwani ni kitu ambacho hakukitegemea pia, basi baba Angel akamwambia,
“Naomba uondoke muda huu kwa amani tu, nilishakwambia wewe mwanamke sitaki unifatilie tena”
Ambacho baba Angel hakuelewa vizuri ni kuwa yule mwanamama alimfata Junior mahali pale na wala hakumfata yeye, ila Linah hakujibu kitu zaidi zaidi aliondoka mahali pale.
Baba Angel alirudi kwenye gari na kupiga honi, kisha kuingiza gari ndani na pale alishuka pamoja na Junior halafu wakaingia ndani.
Kwakweli Junior alishtuka sana kumuona Daima mahali pale alitamani hata kukimbia ila hakuweza maana wote walikuwa wakimuangalia yeye, ilibidi awasalimie tu na kukaa pale kwenye kile kikao huku akiwa na hofu, kwanza baba Angel alimtambulisha Junior pale na kuruhusu kikao kiendelee, baba Daima alianza kwa kumuuliza swali Junior,
“Wewe Junior kidume, unamtambua hutu Daima?”
Junior aliitikia kwa kichwa tu hata mama yake akamfokea muda huo,
“Huna mdomo Junior au ni kitu gani? Kwanini uitikie kwa kichwa?”
“Samahani, namfahamu ndio”
“Eeeeh unamfahamu kama nani?”
Hapo Junior alinyamaza kimya kwa muda, hadi mama yake akamfokea tena ndio akasema,
“Namfahamu kama rafiki yangu tu”
“Unafahamu kama ana mimba?”
“Hapana sifahamu”
Baba Daima akamuangalia Daima na kumwambia aongee neno,
“Junior leo unasema hufahamu kama nina mimba na wakati siku zote tupo pamoja”
“Sifahamu kama una mimba Daima”
“Hufahamu kivipi wakati mimba ni yako!”
Ikawa kama kuna ubishano kidogo, ikabidi baba Angel aingilie kati na kumwambia Junior,
“Junior usikatae wakati kitu kipo wazi kabisa, tumekuita hapa ili utuambie kama utamuoa Daima au utafanyeje kulea mtoto wenu”
“Mimi siwezi kumuoa Daima”
Wote wakamuangalia na jibu lile lilimfanya baba Daima awe na hasira zaidi,
“Kwahiyo umeharibu maisha ya mwanangu halafu unakuja na jibu kama hilo! Huyu binti yangu ukitaka utamuoa usipotaka utamuoa maana ushamjaza mimba tayari”
“Ngoja niongee ukweli ulivyo jamani, ni kweli jilikuwa na mahusiano na Daima, na alipata mimba kweli akaniomba hela aende kutoa hiyo mimba. Mimi nilimdanganya mama yangu na hiyo hela nikampa yeye akatoe mimba, ila baada ya kumpa hela nikamfumania na jamaa mmoja hivi, nilichukia sana nikamwambia Daima mimi na wewe basi. Toka siku ile sikufatilia habari zake, alinitumia ujumbe sijui katoa mimba na damu inamtoka sana, sikumjibu. Toka hapo nilikuwa simjibu ujumbe wake wowote. Halafu sasa kaibuka na kusema kuwa ana mimba yangu, hilo nakataa kabisa maana hiyo mimba sio yangu.”
Baba Angel alipumua kidogo maana hawa ni watoto wadogo ila wanaongea mambo makubwa sana, akamuuliza tena Junior
“Unakataa vipi kuwa sio yako? Labda hakutoa?”
“Ingekuwa ndio ile mimba ya kipindi kile basi ingekuwa ni kubwa sana, sio kama hivyo. Mimi na Daima tuliachana siku nyingi sana, hiyo mimba naikataa na siwezi kumuoa Daima.”
Muda huo huo Tumaini nae aliwasili na kukuta ndio Junior anamalizia kuongea, yani na yeye alidakia palepale bila hata ya salamu,
“Jamani msimlazimishe Junior kuoa huyu mwanamke, hii ndio inaitwa asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Ndugu zangu kwa habari zenu”
“Kheee jamani dada kwanini umeanza na maneno bila ya salamu?”
“Salamu nimeitoa kama hivyo, ila huyu binti nyie msimtetee kabisa”
Muda uleule alianza kueleza jinsi anavyomfahamu Daima, kwahiyo walibaki tu kushangaa na Daima aliendelea kuona aibu, kwakweli mama Daima alichukia sana na kumuuliza mwanae,
“Daima, hebu tueleze ukweli hiyo mimba ni ya nani?”
“Siwezi kudanganya, hii mimba ni ya Junior”
“Mwanangu sema ukweli”
“Huo ndio ukweli mama”
Basi baba Angel akaamua kusema,
“Sisi wote hatuujui ukweli, basi iwe hivi wazazi wa Daima nendeni tu na binti yenu halafu tutajitahidi kwa kila hali kusaidiana na ninyi, mtoto akizaliwa tutaangalia kama kafanana na Junior au la. Mnasemaje kwa hilo?”
Baba Daima alijihisi aibu sana na kweli alikubaliana na hali ya kumchukua Daima mahali hapo ila Daima aligoma huku akilia sana, alidai kuwa wazazi wake wanaweza kumdhuru nyumbani maana kabeba mimba nje ya ndoa na vilevile kabeba mimba akiwa mdogo, alikuwa akilia sana hadi mama Angel aliingiwa na huruma na kusema waache akakae kae hapo kwanza kwani hakuna kitu alichomaliza mahali hapo ila tu walitaka kuwa na ushirikiano na wazazi wake, baba Daima aliafiki hilo swala.
Kwahiyo walimaliza kikao na wale wengine kuanza kusambaratika wakati huo Junior akikazana kuwa alale hapo na kuondoka kesho kwenda shuleni, pia hawakuona kama ni wazo baya na wakaruhusu abakie pale nyumbani tu kwa siku hiyo.
 
SEHEMU YA 348

Baada ya wageni kuondoka, baba Angel alikaa na Junior na kumsema sana,
“Ulianza lini hiyo tabia Junior?”
“Naomba mnisamehe, ila sijui kwanini nimekuwa hivi, ni kwavile nilihisi kuwa sipendwi na mtu yoyote ndiomana nikaanza kuzunguka na wanawake ili wanipende”
“Junior jamani, hadi mama yako uliona hakupendi?”
“Mama siku zote anawapenda wale watoto wa baba, kitu kidogo tu alikuwa akitishia kunifukuza nyumbani”
“Mmmh Junior, kwa stahili hiyo ungeweza kweli kumdanganya kitu mama yako ili upate pesa ya kwenda kumtoa mimba mwanamke?”
“Badae niligundua kuwa mama yangu ananipenda sana na nilianza kujutia mambo yote niliyokuwa nikimtenda, nilijutia sana na kujiona mjinga maana mama ananipenda sana. Kuna mengi najutia katika maisha yangu kama swala la kutembea na wanawake wakubwa sana”
“Kheeee ulifikia hatua hiyo?”
“Ndio, yule tuliyemkuta getini nilikuwa natembea nae na alikuwa akinilea”
Baba Angel alishtuka sana yani kama hakuelewa vile kilichokuwa kikiongelewa, alimuuliza kwa makini,
“Inamaana umewahi kuwa na mahusiano na yule Linah?”
“Ndio bamdogo, ila najutia kwasasa”
“Jamani, yule si amemzidi hata mama yako yule! Tena ana watoto wakubea kushinda wewe, mbona mambo ya aibu haya Junior! Ulianzaje kwanza, yani sielewi ulianzaje?”
“Nisamehe bamdogo, kuna binti fulani nilikuwa namfatilia ila hakunitaka, basi siku hiyo yule mama aliniambia kuwa anataka kunifundisha namna ya kutongoza, ndio siku hiyo hiyo ndani kwake nikaanza nae”
Baba Angel alipumua na kusema,
“Junior, unatakiwa kuwq makini sana, zingatia masomo yako na uache mambo ya kijinga. Fikiria maisha yako ya mbele, sitaki kusikia tena mambo kama haya yanatokea kwakweli sitaki.”
Kisha baba Angel akamruhusu Junior kwenda, halafu yeye alienda ndani kwa mke wake ili amuage kidogo aweze kutoka,
“Unataka kwenda wapi kwani baba Angel?”
“Aaaah nikapunge upepo tu wa nje, nataka ninyooshe nyooshe miguu.”
“Mambo ya leo yamekuchosha eeeh mume wangu, ila ndio ukubwa huu. Tunatakiwa kupambana tu, hakuna namna ila sitakuruhusu kwa muda huu kutoka mwenyewe, ukitaka tutoke wote twende tukatembee tembee”
Baba Angel hakupinga hilo swala zaidi ya kukubali kutoka wote akiwa na mke wake.

Mama Angel na baba Angel wakatoka na kuanza kutembea tembea, walikutana njiani na Sia, alionekana katoka kwenye shughuli zake na alisogea kuwasalimia,
“Naona leo mmeamua kuangalia mazingira ila mbona muda umeenda sana?”
“Tumeamua tu kwakweli kutembea tembea”
“Ni vizuri kuliko kukaa tu ndani, ndiomana mengi yanayotendeka hamyaoni”
Pale walipokuwa wamesimama kulikuwa na nyumba ya wageni jirani yake, walimuona mama mtu mzima akiingia na kijana mdogo mule ndani, basi wakati wakishangaa Sia akasema,
“Sasa mnashangaa nini, mbona hiyo ni kawaida sana siku hizi. Mnaona kama mama na mtoto ila wale ni mtu na mpenzi wake”
“Duh!”
“Sasa na wewe Erick unashangaa nini jamani, mbona na wewe ulikuwa unatembea na dada zako na walikuwa wakorofi sana wakijua utawaoa. Umemsahau Linah!”
Baba Angel akakumbuka kitu na kusema,
“Nimekumbuka, kumbe Linah alikuwa akitembea na Junior!”
Sia akadakia,
“Na msipokuwa makini na huyo Junior humo ndani kwenu pia mtalia, mimi nikiongea huwa naonekana mzushi. Kwaherini”
Baba Angel na mama Angel nao hata hawakutaka kuendelea na matembezi yao kwani muda huo huo walirudi nyumbani kwao tu.

Usiku wa leo Vaileth hakuwa na raha kabisa kwa kitendo cha Daima kuachwa pale maana alikuwa akitaka yule Daima aondoke na wazazi wake, basi alikuwa akimuangalia tu yule Daima akijilaza kitandani, mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Vaileth, alipoangalia ujumbe ule ulikuwa ukitoka kwa Junior,
“Mpenzi wangu Vai, najua unanipenda nami nakupenda sana, naomba uje chumbani kwangu tuongee kidogo japo kwa dakika tano tu, nakuomba sana mpenzi wangu. Sijaweza kuja huko chumbani kwako maana nimeambiwa ndio unalala na huyo kiberenge, nakuomba mpenzi wangu, nakuomba sana uje kunisikiliza”
Kiukweli Vaileth hakutaka kuongea tena na Junior ila badae moyo ulimuuma sana kwani alihisi ni jinsi gani alimpenda Junior, ilibidi anyanyuke na aende chumbani kwa Junior.
Alifika na kuingia, kisha Junior aliinuka na kufunga mlango, wala hakuongea kitu na Vaileth kama alivyomwambia kuwa anamuita kwaajili ya maongezi zaidi zaidi alimpapasa na mwishowe wakalala pamoja.
Walipomaliza, Vaileth alinyanyuka na kuvaa upesi,
“Junior siwezi kulala humu chumbani kwako, maana tunaweza kujisahau na kulala hadi asubuhi”
“Nimekuelewa Vai wangu ila nimeridhika, najua bado kitambo kidogo tu mimi na wewe tutaishi pamoja kwa furaha”
Basi Vaileth kabla hajatoka, Junior alimsogelea na kumbusu, kwakweli ile hali ilimfanya Vaileth aone kuwa anapendwa sana na Junior.
Basi Vaileth alitoka na kurudi chumbani kwake, ila muda huu alimkuta Daima amekaa huku akilia tu, basi alimsogelea karibu na kumuuliza,
“Unalia nini Daima?”
“Najutia maisha yangu mimi, najutia sana. Niliamini zile kauli za nakupenda nakupenda. Niliamini Junior alinipenda kweli yani leo Junior wa kunikana mbele ya wazazi wangu? Imeniuma sana”
“Kwani ni kweli ulitoa mimba ya Junior?”
“Sijawahi kutoa mimba mimi na wala sijawahi kumuomba Junior hela ya kutolea mimba, na yeye ndio kanifanya mimi nianze umapepe”
“Kivipi?”
“Junior ndio mwanaume wangu wa kwanza, nilimkubali baada ya kuona wenzangu wote wana wanaume, niliacha kufata mambo ya dini mimi na kuendekeza ujinga. Nadhani hata mama yangu analia sana muda huu kwani hakutegemea kuwa angepata yale maelezo kuhusu mimi, nilikuwa nikiwa naenda shule najitanda juba mimi, ila nilipoanza na Junior alisema sipendezi nikijitanda basi nikaanza kuacha taratibu na mwishowe nikafanana na rafiki zangu wale wawili, tukawa hatuendi shule tunaenda tu huko kujirusha, Junior akinihitaji muda wowote ananipata na alisema kuwa ananipenda sana, katika maisha yake hakuna mwanamke atakayekuja kumuoa zaidi yangu yani aliniambia kuwa mimi ndio mwanamke wa maisha yake ndiomana nikaanza kiburi, ila alipokuwa akinizingua ndipo rafiki zangu walipokuwa wakiniunganisha na wanaume wengine ia bado moyo wangu ulimpenda sana Junior. Niliwahi kumuuliza nikibeba mimba itakuwaje? Akasema ni vizuri maana mama yake hana mtoto mwingine kwahiyo atafurahi kupata mjukuu, sikuwa na mashaka mimi, hata nilipofeli bado Junior alinitia moyo, nashangaa toka nilipomwambia nina mimba yake ndipo alipoanza kupiga chenga, ndiomana mama aliponibana nikaamua kumpeleka kwa mama Junior maana Junior aliwahi kunipeleka hadi pale, na mama yake alinipokea vizuri kabisa. Eti leo Junior amenikana na kunifanya nionekane kuwa mwanamke malaya sana, sawa Mungu atanilipia mimi, kama nimemsingizia Junior hii mimba basi naomba nife na mimba yangu, roho inaniuma sana”
Daima alikuwa akilia kwa uchungu sana muda huu hata Vaileth alimuonea huruma ingawa na yeye alitoka kufanya uchafu na Junior ila kwa muda ule alichukua jukumu la kuanza kumbembeleza.
Basi alimbembeleza pale na mwishoe alitulia na kulala, na Vaileth nae akalala.
Ila palipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuamka leo na kumtaka Vaileth amuonyeshe kazi za mule ndani, na alipoonyeshwa moja kwa moja alienda kuosha vyombo wakati Vaileth akisafisha nyumba.

Erick akiwa shuleni kwenye muda wa mapumziko alifatwa na Elly na kuanza kuongea nae,
“Erick, naomba sehemu yoyote tuliyokosana tusameheane. Tuishi kwa upendo”
“Sawa hakuna tatizo, tutaishi vizuri”
“Kwanza Erica hajambo? Nimemkumbuka sana yule dada yangu”
“Hajambo kabisa”
Muda kidogo alifika Sarah pale walipokuwa wanaongea, basi alikaa karibu ya Elly, na kuanza kumsalimia Erick halafu akaongea na Elly,
“Erick mambo? Jamani Elly kwanini uliondoka jana, mimi nilitaka leo tuje wote shuleni. Unaonaje ukianza kukaa kwetu moja kwa moja?”
“Tatizo mama yangu atabaki mpweke sana”
“Halafu Erick mbona nimekusalimia haujaitikia? Au umeona wivu mimi kuongea na Elly?"
“Wivu? Sasa wivu wa nini? Tatizo Sarah unaongea sana, unanisalimia wakati huo huo unaongea na Elly sasa ulitaka nikujibu vipi?”
“Haya basi, mambo vipi? Mama hajambo?”
“Poa, hajambo kabisa”
“Nampenda sana yule mama maana anaupendo wa kweli, nampenda sana. Ukirudi mwambie. Saivi nawapenda sana watu wanne”
Erick na Elly walimuuliza kwa pamoja,
“Wakina nani hao?”
“Baba yangu, mama yangu, mama yake Erick, halafu nampenda sana na Elly”
Elly alitabasamu ila Erick alikuwa kimya tu na kuinuka zake na kuondoka, basi Sarah akamuangalia Elly na kumwambia,
“Usimjali yule, alifikiri nitasema kuwa nampenda na yeye, sasa nimpende kwa lipi jamani! Hata simpendi”
Kengele ya kurudi darasani ililia na wote wakarudi zao darasani.

Leo mama Angel pale nyumbani alishangaa sana jinsi Daima alivyokuwa akijibidiisha na kazi, yani alitaka afanye kila kazi hadi alikuwa akimzuia kazi zingine, aliamua kumuita na kumuuliza,
“Mbona upo hivyo leo?”
“Sitaki kuwa mzembe”
“Kivipi?”
“Naomba uniache nikae kae hapa, nakuomba mama”
Halafu alianza tena kulia, kwakweli mama Angel hakumuelewa kabisa ilibidi aache tu kumuuliza kwa muda huo na kumuacha akiendelea na mambo mengine.
Muda kidogo baba Angel alirudi kwakweli leo aliwahi kurudi kuliko siku zote na akapitiliza chumbani, ikabidi mama Angel amfate mume wake na kwenda kumuongea nae,
“Tatizo ni nini baba Angel mbona unaonekana haupo sawa?”
“Kwakweli mwili wangu haupo vizuri kabisa, najihisi kuchoka sana”
“Au homa?”
“Hapana ni uchovu tu, nahitaji kupumzika”
Basi alipumzika, wakati huo mama Angel alienda kumuandalia mumewe kitu ambacho alihisi huenda mumewe akala.

Elly alipotoka shule moja kwa moja alipita kwenye biashara ya mama yake na kumsalidia pale kisha kurudi wote nyumbani, njiani alikuwa akimuuliza mama yake,
“Mama samahani, eti mapenzi ni nini?”
Sia alishtuka kidogo na kumuangalia Elly kisha akamwambia,
“Kwanza sikutegemea kama ungeniuliza swali kama hilo Elly, kweli mtoto wa nyoka ni nyoka pia. Jinsi ulivyokuwa unaonekana mtakatifu halafu leo unaniuliza mapenzi ni nini!”
“Sijakuuliza kwa ubaya mama, nimekuuliza kwa wema tu”
“Sawa, mapenzi ni kupendana. Watu wanapendana na kuwa pamoja katika mahusiano ya kimapenzi”
“Na kufanya mapenzi ni nini?”
Sia alishtuka tena na kumuuliza Elly,
“Hebu niambie Elly ni nini unachotaka kujifunza? Usijiingize katika michezo michafu, sitaki kuwa kati ya wamama wenye malezi mabaya kwa watoto wao.”
“Jamani mama, nimekuuliza sababu nataka kujua”
“Kufanya mapenzi ni kitendo cha kuingiliana kimwili, mara nyingi ni kati ya mwanaume na mwanamke. Kitendo hiki huitwa tendo la ndoa, ni vyema likafanywa baada ya ndoa kwani kabla ya hapo kuna mambo yanaweza kuwa ni majuto kwako. Mfano msichana anaweza kupata mimba”
Elly akashtuka sana na kumuuliza mama yake,
“Kwahiyo ni lazima mwanamke apate mimba?”
“Inawezekana ndio kama mtu amefanya mapenzi bila ya kutumia kinga halafu kama mwanamke yupo katika siku za hatari za kupata mimba huwa hivyo. Ila kwanini umeniuliza maswali hayo Elly?”
“Hapana mama, nimekuuliza tu mama yangu sina maana nyingine yoyote”
Basi wakaongozana na mama yake hadi nyumbani, muda kidogo simu ya mama Elly iliita na alipopokea, ilisikika sauti ya kike aliyejitambulisha ni Sarah na kuomba kuongea na Elly basi mama Elly alimpa Elly simu,
“Niambie Sarah”
“Huwezi amini, eti nimekaa tu nikakukumbuka hadi nimemuomba mama namba ya mama yako”
“Aaaah kumbe!”
“Ndio hivyo, wewe hujanikumbuka?”
“Nimekukumbuka pia, tutaonana shule kesho”
“Muombe mamako ruhusa ili kesho turudi wote nyumbani”
“Sawa nitafanya hivyo, usiku mwema”
Elly aliamua kukata simu na kumuaga Saraha, basi mama Elly alimsogelea mwanae na kumuuliza,
“Vipi huyo Sarah ndio mpenzi wako?”
“Hapana mama, ni dada yangu yule. Ni mtoto wa mama aliyejitolea kunisomesha”
“Oooh kumbe ndio Sarah wa Manka?”
“Ndio mama”
“Oooh samahani kwa kukwambia hivyo mwanangu, alikuwa anasemaje?”
“Unajua pale huwa hakuna mtu wa kuongea nae kwahiyo mimi kuwa pale alifurahi sana, ananiambia nikuombe ruhusa ili kesho nirudi nae kwao”
“Sawa hakuna tatizo, mwanangu jitahidi usimuudhi huyo binti maana anapendwa na mama yake hatari, jitahidi uwe unamsikiliza, fanya kile anachokitaka, yani ukiona kitu kinamfurahisha basi mfanyie hata kama anapenda kuimbiwa jifunze kuimba mwanangu, ndio tunawategemea kwasasa, yani fanya kila kitu kumfurahisha. Ishi nae kama ndugu yako kabisa, usimkere wala kumuudhi”
“Sawa mama nimekuelewa”
Basi Sia aliampa mwanae mausia ya kutosha kuhusu kuishi na Sarah.

Usiku huu, kila chakula ambacho mama Angel alimjaribisha mumewe alitapika chakula hicho, basi hakuwa na namna zaidi ya kutaka kumpeleka hospitali tu.
Basi alijiandaa kisha yeye na Erick mdogo pamoja na baba Angel waliondoka pale nyumbani, wakati huo ni Erick mdogo ndio alikuwa akiendesha gari kuelekea hospitali.
Walifika hospitali na kumshusha mgonjwa, sababu hakuwa na hali nzuri alitakiwa kupata matibabu ya haraka sana kwa wakati huo.
Basi waliingia nae moja kwa moja kwenye chumba cha daktari na kumlaza kitandani huku mama Angel kasimama akimuangalia mumewe kwa huruma, muda huo nesi nae alikimbia kwenda kumuita daktari ili aende kumuhudumia yule mgonjwa maana daktari alitoka kidogo.
Daktari alivyoingia tu, moja kwa moja macho yake yalimuangukia mgonjwa na kusema,
“Khaaaaa kama mgonjwa mwenyewe ndio huyu, simuhudumii mimi”
Ile kauli ilimshtua na kumchanganya sana mama Angel, ambaye aligeuka na kumuangalia yule dokta aliyetoa hiyo kauli ila macho yao yaligongana, dokta akasema kwa mshangao,
“Kheeee mama Angel!!!”

Basi waliingia nae moja kwa moja kwenye chumba cha daktari na kumlaza kitandani huku mama Angel kasimama akimuangalia mumewe kwa huruma, muda huo nesi nae alikimbia kwenda kumuita daktari ili aende kumuhudumia yule mgonjwa maana daktari alitoka kidogo.
Daktari alivyoingia tu, moja kwa moja macho yake yalimuangukia mgonjwa na kusema,
“Khaaaaa kama mgonjwa mwenyewe ndio huyu, simuhudumii mimi”
Ile kauli ilimshtua na kumchanganya sana mama Angel, ambaye aligeuka na kumuangalia yule dokta aliyetoa hiyo kauli ila macho yao yaligongana, dokta akasema kwa mshangao,
“Kheeee mama Angel!!!”
Mama Angel alimuangalia kwa makini, ni mtu ambaye wanafahamiana nae sana, basi akamuuliza,
“Kwanini dokta hutaki kumuhudumia mume wangu?”
“Kumbe ndio mume wako huyo?”
“Ndio ni mume wangu”
“Samahani, ila nadani nikimuhudumia mimi naweza kumfanya kitu kibaya”
Basi alimuangalia nesi na kumuomba akamuite dokta mwingine ili akamshughulikie, kwakweli mama Angel hakuelewa mantiki ya huyu dokta kugoma, basi nesi alienda kumuita dokta mwingine.
Ni kweli baba Angel alikuwa akiugulia kwa maumivu sana ila huyu dokta wala hakuonyesha kushtuka kabisa, hadi pale alipoenda dokta mwingine kisha mama Angel alitoka nje pamoja na huyu dokta wakati yule mwingine akimuhudumia baba Angel.
Ingawa hali ya baba Angel haikuwa nzuri ila bado mama Angel alihitaji kujua ni kwanini huyu dokta hataki kumuhudumia mumewe, basi alimsogelea na kumuuliza,
“Dokta Maimuna, kwani unamfahamu mume wangu?”
“Kwanza nisamehe kwa mimi kukataa kumuhudumia, ila sikutegemea kumuona yule kiumbe kabisa”
“Niambie basi alikufanya nini?”
“Sitakuficha sana, ni hivi nimewahi kuwa na mahusiano na mume wako”
Mama Angel alishtuka sana, ila dokta aliendelea kuongea,
“Kwasasa ningekuwa na mtoto mkubwa sana ambaye pengine angekuwa labda kaolewa tayari sababu alikuwa wa kike, huyu mjinga alikuwa akinitoa sana mimba. Nilipopata mimba ile nilikaa kimya ili nijizalie kimwanangu, hili jina lilikuja na madawa yake kayaweka kwenye juisi akanipa ninywe, mwishowe ile mimba ya miezi saba ilitoka na kitoto kilikuwa kimekufa. Nililia sana, huyu Erick ni muuwaji. Ningekusimulia mengi sana ila niache tu kwasasa.”
Dokta Maimuna aliondoka zake na kumuacha mama Angel pale akiwa kaduwaa tu maana hakufikiria jambo lile hata kidogo.
Basi yule dokta aliyekuwa akimuhudumia mumewe alitoka na kumpa taarifa mama Angel,
“Kuna chakula mumeo alikula hakikuwa salama kwake, kilikuwa kama na sumu kiasi, nimemchoma sindano na kumtundikia dripu, atakuwa sawa tu”
Basi mama Angel alienda kumuangalia ambapo muda huu alikuwa kapelekwa wodini, basi mama Angel alimtazama mumewe huku akijiuliza,
“Kwanini kila mwanamke ana sifa mbaya juu ya mume wangu jamani!”
Kidogo tu baba Angel alianza kutapika, tena alitapika sana, baada ya hapo mama Angel alimuita tena daktari ambapo baada ya kumuangalia alimwambia mama Angel,
“Usijali kuhusu kutapika, kwanza ni bora ametapika kwani sumu ndio ilikuwa inatoka hivyo.”
Basi dokta akamuelimisha pale, na kutoka kwenda kuendelea kuhudumia wagonjwa wengine.

Usiku wa leo, mama Sarah aliwaaga watoto wake kuwa anaenda kwenye mkesha, kwakweli kipindi hiki hata Sarah alimshangaa mama yake maana haikuwa kawaida yake kabisa kwenda kwenye mikeha, basi kila mmoja alienda chumbani kwake kulala ila baada yamuda kidogo, Sarah alienda chumbani kwa Elly, na kuingia ndani, alimkuta Elly ndio anatafuta usingizi kwa muda huo basi alimuomba Elly aende nae chumbani kwake,
“Mmmh hapana Sarah”
“Jamani Elly utaniudhi ujue”
Elly akakumbuka maneno ya mama yake, basi akamuangalia Sarah na kukubali kwenda nae chumbani kwake ambapo walipofika tu Sarah alifunga mlango na kuvua nguo zote halafu akamuwekea Elly zile video walizokuwa wakiangalia siku ile na kumwambia,
“Elly angalia tena ili unifanyie kama siku ile”
“Ila unajua kama sio vizuri kufanya hivyo?”
“Kivipi?”
“Vaa nguo Sarah, hiyo ni tabia mbaya tena ni dhambi”
Muda huo Elly alikuwa akiangalia pembeni yani alikuwa akiona hata aibu kumuangalia Sarah ila Sarah hakujali, ndio kwanza aliweka zile video vizuri na kumtaka Elly aangalie zile video, na zilivyoanza Elly alijihisi hali yake kubadilika kwakweli kani alishikwa na hisia za hali ya juu kabisa, basi Sarah nae alikuwa akimsogelea huku akiwa mtupu kabisa na kuanza kuondoa nguo za Elly, yani Elly alijikuta akifanya tena na Sarah kile kitendo ambacho aliamini kuwa ni kitendo kibaya.
Basi walipomaliza Elly akachukua nguo zake ili kuvaa ila Sarah alimzuia na kumwambia kuwa wakaoge pamoja,
“Mmmh Sarah!!”
“Ndio twende tukaoge wote, unaogopa nini kwani Elly jamani!!”
Sarah alimshika mkono Elly hadi bafuni na wakaoga, kisha kurudi na kuvaa nguo, kwa muda huo Sarah alikataa Elly asiondoke kwanza kwani alitaka kuongea nae kidogo, basi alianza kumuuliza Elly,
“Eeeeh una mpango gani na mimi?”
Elly akashtuka na kuuliza,
“Mpango gani kivipi?”
“Kwani hujui kama mimi na wewe kwasasa ni wapenzi? Niambie utanioa au?”
“Sarah naogopa mimi, mama yako kanichukua kama mtoto wake”
“Unadhani mama yangu atakataa? Nikitakacho mimi haiwezekani mama yangu akakataa kwani ananipenda sana”
“Muda umeenda sana Sarah! Tutaongea tena kesho”
Elly alimuomba Sarah ili aweze kumruhusu akalale, ila mwishowe Sarah alimruhusu tu kwenda kulala, ila Sarah hakupata usingizi kwani alikuwa anawaza huenda Elly hampendi ndiomana hana jibu la moja kwa moja kwake, yani alijikuta akipitiwa na usingizi wakati pamekucha kabisa, ilikuwa hivyo hata kwa upande wa Elly ambaye alijihisi vibaya sana kwa kile kilichotokea na kumfanya akose usingizi kwa wakati, yani ile kunakaribia kukucha ndio akapitiwa na usingizi pia.
 
SEHEMU YA 349

Erick alikuwa amepitiwa na usingizi ndani ya gari, alikuja kushtuka pamekucha tayari, kwenye gari ndio kulikuwa na simu ya baba yake, ambayo ilianza kuita, basi Erick akaivuta na kuipokea ili amwambie kuwa baba yake amelazwa, ila kabla hajasema kitu yule mpigaji alianza kuongea,
“Erick nimekukumbuka sana, ila wanawake wako wakiamua kukuroga utakuwa chizi wewe, kwataarifa yako mimi nishakuja kwa mganga huku jiandae tu.”
Halafu simu ikakatika, kwakweli Erick alibaki akishangaa sana.
Aliiangalia sana ile simu na bila ya kupata jibu lolote lile, aliamua kuchukua peni na karatasi na kuandika ile namba pembeni kwani alitamani sana kumfatilia yule mtu ili ajue tatizo ni kitu gani.
Alipomaliza tu kuandika ile namba, alifika pale mama yake na kumsalimia kisha akamwambia,
“Naona mwanangu leo tumekesha hospitali, pole sana hutoweza kwenda shule"
“Cha muhimu ni hali ha afya ya baba, anaendeleaje?”
“Mungu kasaidia kwakweli, anaendelea vizuri, asubuhi hii inawezekana tukaruhusiwa kwenda nyumbani”
Yani muda huu mama Angel hata hakukumbuka kuhusu mtoto nyumbani maana alijikuta mawazo yote ni juu ya mumewe, na vile alivyoambiwa alipewa sumu ndio hakuwa na imani kabisa ya kumuacha mahali hapo, basi muda kidogo alimuona dokta Maimuna akitoka ambapo huyu dokta alipomuona mama Angel alimfata na kuongea nae,
“Pole sana, nasikia mumeo alipewa chakula chenye sumu, pole sana”
“Asante”
“Kuwa makini sana, najua mumeo humjui vizuri ila kwa zile tabia zake nina uhakika ana maadui wengi sana, kwahiyo kuwa nae makini asile hovyo. Tena bora mmewahi kuja hospitali la sivyo tungekuwa tunaongea mengine sasa”
“Dah sijui nani kamfanyia hivi”
“Huwezi kumjua kwa kufikiria tu ila inatakiwa kuwa makini sana. Halafu kipindi kile si ulikuwa na mimba wewe!! Mtoto yuko wapi?”
“Yupo nyumbani’
“Haya, nenda kamchukue mumeo huko ataruhusiwa muda sio mrefu ukaangalie mtoto wako, mimi naenda nyumbani maana zamu yangu imeisha. Kwaheri”
Dokta Maimuna aliondoka zake, na mama Angel nae alienda kumfata mume wake.

Leo Erica hakwenda shule pia, kwani ndio alibaki kulea mdogo wake toka usiku na hadi asubuhi, yani alikuwa yupo vizuri na kulea hadi Vaileth alimshangaa na kumwambia,
“Kwakweli Erica utakuwa mlezi mzuri, hadi nimekupenda bure. Maana toka usiku alipoondoka mama yako upo na mtoto tu, hongera sana”
Erica alikuwa akitabasamu yani alifurahia kile alichokuwa anaambiwa na Vaileth, muda huu Daima alikuwa akishughulika tu na kazi za hapa na pale.
Basi muda kidogo, mama Angel, Erick na baba Angel walirudi kutoka hospitali kwahiyo pale nyumbani walifurahi sana, mama Angel alienda kwanza kumshughulikia mume wake kisha alirudi kwaajili ya mwanae mdogo,
“Masikini mwanangu jamani, ila kusingekuwa na watu nyumbani, hakuna namna ningeondoka nae tu”
Vaileth akamwambia,
“Ila mama, Erica yupo vizuri sana. Tangu umeondoka yeye ndio yupo na mtoto tu hadi muda huu”
“Jamani, wanangu hadi kwenda shule leo imeshindikana jamani!!”
Basi mama Angel alimchukua mwanae na kwenda nae chumbani.
Kwakweli alikuwa akimuangalia mumewe sana huku akimuhurumia ila alimuacha apumzike kwanza.

Leo Sarah na Elly hawakuenda shule maana walichelewa kuamka halafu walikuwa na uchovu, mama Sarah hakuelewa kitu kwani jana yake hakuwepo, alienda kwenye mkesha na kukawia sana kurudi kwahiyo aliporudi hata hakufatilia kama watoto walienda shule au la maana yeye alienda kulala moja kwa moja kutokana na uchovu aliokuwa nao.
Kwenye mida ya saa tatu asubuhi ndipo Sarah na Elly walipokaa na kuweza kupata kifungua kinywa, ndio muda huo naye mama yao alitoka chumbani na kuwasalimia pale,
“Kheee nyie vipi, mbona hamjaenda shule?”
Sarah ndio akamjibu mama yake,
“Jana tulijisahau mama, tuliangalia sana sinema tukachelewa kwenda kulala, kitendo hiko kimefanya tuchelewe kuamka leo”
“Oooh sawa, ila msirudie tena kuangalia sinema hadi usiku sana, jamani leo nimechoka sana”
“Kwani mama ulienda kwenye mkesha wapi?”
“Aaaah huko mbali kidogo, ila nimechoka sana, ngoja ninywe chai ili nirudi kulala kwanza maana nimechoka sana”
Na kweli alikunywa chai pale na kwenda zake chumbani.
Basi walikaa kaa pale ila Sarah nae alijihisi uchovu na kuwa na usingizi kwahiyo aliamua kwenda kulala pia, ni Elly ndio alibaki pale sebleni huku akiwa na mawazo mengi sana, kwani alikuwa akijutia kile alichokifanya usiku.
Muda huu wakati anaangalia sinema ila haelewi kitu sababu ya mawazo, alifika Siku na kumuuliza Elly kinachoendelea kwenye ile sinema ila Elly hakuelewa kitu,
“Kheee unaonekana una mawazo sana Elly, unawaza nini kiasi hiko?”
“Dah! Sijui kwakweli”
“Wewe ni mtoto mdogo hata majukumu hujayaanza, halafu wewe ni mzuri mweeeh!”
Elly alikaa kimya tu, kisha Siku aliendelea kumwambia,
“Au hakuna mtu aliyewahi kukusifia kuhusu uzuri wako? Unajua pale wakati unafika sikuona uzuri wako ila umeishi hapa kidogo tu ndio nimekuona kuwa wewe kijana ni mzuri sana”
“Ila wanawake ndio wanaosifiwa kwa uzuri na sio wanaume”
“Khaaa jamani, kama mwanaume mzuri lazima apewe sifa zake, kwakweli wewe ni mzuri sana Elly, halafu jina lako ni zuri sana”
Kwakweli Elly hakujibu kitu muda huu ila alimuaga Siku kuwa na yeye anaenda kulala kwa muda huo.

Muda huu alifika Tumaini pia kuja kumuona kaka yake maana alipigiwa simu kuwa alikuwa anaumwa, basi alifika kumuona na kuongea nae kidogo, muda huu baba Angel alikuwa sebleni tu amejilaza kwenye kochi, basi alifika pale na kumsalimia na kumpa pole,
“Pole sana mdogo wangu jamani, pole sana. Kwanini nini cha zaidi jamani?”
“Yani hata sielewi”
Basi mama Angel alimwambia wifi yake kuhusu daktari alichokisema, basi Tumaini alisikitika sana na kusema,
“Kwasasa kuwa makini sana Erick, yani usile chochote kile. Kwanza ni kitu gani umekula hadi imekuwa hivyo?”
“Hata sielewi, nakumbuka nilikula matunda yaliyokatwakatwa tu”
“Nani alikuletea?”
“Yani aliyeniletea huwa ananiletea siku zote hata sijui imekuwaje, ila sidhani kama ni matunda yale ndio yamesababisha hali kama hii, sielewi kwakweli”
“Kuwa makini sana kwasasa”
“Nitajitahidi kwa hilo dada yangu”
Wakaongea mengi sana, na mwishowe Tumaini aliaga na kuondoka zake.
Alipokuwa anaondoka kuelekea stendi, njiani akakutana na Sia na kusimama na kuanza kumsalimia,
“Naona leo umetoka kumsalimia nduguyo”
“Ndio, alikuwa anaumwa”
Sia alishtuka kidogo na kuuliza,
“Alikuwa anaumwa nini tena?”
“Yani alikuwa hoi nakwambia, ndio Erica alimuwahisha hospitali jana, kumbe sijui wapi huko walimlisha sumu”
“Jamani, nani huyo mwenye wazo la kumpa sumu Erick jamani, kwanini lakini?”
“Sijui kwakweli, nadhani wanataka kummaliza kaka yangu”
“Ila nitafatilia mwanzo mwisho hadi nijue ni nani, huwa sishindwi kitu mimi nikiamua, kwakweli nimeumia sana. Ila Tumaini zamani tulikuwa vizuri sana, ukiacha tofauti zetu najua ungeniambia mapema sana kuhusu hali ya Erick, yani hadi nikutane na wewe kweli!!”
“Aaaah acha mambo ya zamani, wewe ndio umeharibu ukaribu wangu nawe kwa maneno yako yasiyokuwa na mwanzo wala mwisho”
“Nisamehe kwa yote yaliyotokea ndugu yangu, ni mapenzi ndio yalinifanya niwe hivi nilivyokuwa. Tatizo langu nilimpenda sana kaka yako na nilijiaminisha kuwa ndiye atakuja kuwa mume wangu, ila kadri siku zinavyoenda naona haiwezekani. Ila bado siwezi kuwa na ubaya na Erick, kanisaidia vitu vingi sana wala siwezi kufurahia Erick apatwe na mabaya, niamini kuwa nitashughulikia hilo hadi nitajua ukweli wa nani alitaka kumdhuru Erick wangu”
Basi Tumaini aliongea nae kidogo tu na kuondoka zake.

Usiku wa leo, mama Angel alipokuwa chumbani na mumewe aliamua kumuuliza maswali kadhaa kuhusu uwepo wa dokta Maimuna, basi alimuuliza,
“Mume wangu samahani, yule dokta Maimuna unamfahamu?”
“Yule Maimuna namfahamu ndio, na sikujua kama ni dokta kwasasa”
“Anasema kuwa ulimpa tunda ale na kusababisha mimba yake ya miezi saba kutoka, je ni kweli?”
“Unajua mtu ukiwa na tabia Fulani basi kila kitu kikitokea katika maisha lazima utasingiziwa tu. Nilisema toka nakuoa kuwa nitajitahidi kuwa mkweli, na nitajitahidi kukueleza kila kitu kwa upana zaidi, ngoja nikueleze kwa kifupi”
“Eeeeh nasikiliza”
“Ni hivi, niliwahi kuwa na mahusiano na yule Maimuna kiukweli, tena kwa kipindi hiko nilimuona kuwa ana akili kwani alikuwa akiwaza sana ya mbeleni. Alikuwa anasoma, na yeye ndio alilalamika kupata mimba ya kwanza kabisa, basi mimi sikuwa na budi zaidi ya kumpeleka kwa rafiki yangu yule dokta ambaye anatoa sana mimba. Tena mimba ya Maimuna ndio ilikuwa mimba ya kwanza mimi kupeleka mwanamke kutoa mimba sababu ya yeye kusema haitaki mimba, ingawa kwa kiasi Fulani alinisaidia kwani hata mimi kwa kipindi hiko sikufikiria kufanya majukumu ya kutunza mtoto. Tumewahi kutoa mimba tatu na Maimuna, nikamshauri atumie dawa za uzazi wa mpango ila akakataa katakata, nakumbuka akapata mimba tena na hiyo hakuniambia hadi ilipokuwa kubwa kabisa, katika mambo yote nisingeweza kutoa mimba kubwa vile, akaniagiza matunda na nilikuwa namuhudumia vizuri tu. Nilienda kumchukulia matunda sehemu aliyoniagiza na nilipofika nayo tu alianza kuyala, ila muda ule ule tumbo lilianza kumuuma na kumuwahisha hospitali, alijifungua kabisa mtoto mfu. Basi toka hapo Maimuna akanichukia kupita kiasi, nilijaribu kumuomba msamaha na kumuelewesha ila hakutaka kunisikiliza, maelewano baina yangu na yake yalikatika hapo. Tukaachana kabisa, sasa itakuwaje nahusika kutoa hiyo mimba kubwa”
Mama Angel akapumua kidogo na kusema,
“Mmmh ila wewe ni noma jamani, wewe Erick hapana kwakweli. Hivi umesababisha mimba za wanawake wangapi zitoke? Au umewatoa mimba wanawake wangapi?”
“Mimi mwenyewe huwa najutia kile kitendo tena huwa najutia sana, ila hawa wanawake walikuwa wakinitaka wenyewe, na mimi nilikuwa sipo vizuri kichwani yani nilikuwa na mawazo hadi basi, nikawa nawakubali tu. Lakini hakuna mwanamke hata mmoja ambaye sikuwahi kumwambia kuwa nampenda sana Erica, yani walikuwa na mimi ila waliamini siku akirudi Erica katika maisha yangu basi nitawageuka kabisa na kuwakataa, na huo ndio ulikuwa ukweli halisi maana moyo wangu upo kwa Erica tu. Nakupenda mke wangu, madhaifu yangu yaliyopita usifanye yanikandamize kwasasa, mimi nakupenda sana Erica wangu”
“Mmmh, nimekusikia”
Mama Angel hakuendelea tena kuhoji, ila alihisi tu kuna siku ataletewa watoto wa nje ingawa baba Angel alikuwa hakubali kuwa ana mtoto wa nje, sema mama Angel alihisi tu kuna siku ataletewa mtoto lazima.
Kwa muda huo waliamua kulala tu, kwani ilikuwa ni usiku sana.

Leo Elly na Sarah walienda shule kama kawaida ila Elly alikuwa na mawazo sana yani hakuwa na raha kama siku zote ambavyo huwa anakuwaga, ile hali hata Erick aliigundua na kwenda kumuuliza tatizo ni nini,
“Kwani unaumwa Elly?”
“Hapana, ila sijihisi vizuri natamani nirudi nyumbani”
“Nenda kaombe ruhusa sasa, ili upate amnai ya moyo”
“Wataniruhusu eeeh!”
“Ndio”
Basi Elly aliondoka na kwenda kuomba ruhusa, ni kweli walimruhusu muda huo huo kwenda nyumbani kwao.
Elly alipoondoka, moja kwa moja alienda kwenye biashara ya mama yake na kumkuta pale kisha alimsalimia na kuanza kuongea nae,
“Mbona mapema sana leo mwanangu Elly?”
“Yani sijihisi vizuri sijui kwanini, moyo unaniuma sana ndiomana nimeamua kurudi”
“Kheeee unahisi homa?”
“Hapana mama, ila natamani kukutana na watu mbalimbali sijui kwanini ila moyo wangu unaniuma sana”
“Haya, nisaidie kwa wateja maana naona umeamua”
Basi Elly alikuwa akimsaidia mama yake kuhudumia wateja wao pale kwenye mgahawa.

Leo Erica akiwa shuleni, kama kawaida alianza kuongea na rafiki yake Samia akiambiwa kuhusu kilichotokea nyumbani kwakina Samia,
“Yani siku hizi nyumbani kwetu jamani, sijui baba kawaje”
“Kwani vipi?”
“Ni hivi, mara mama alipoondoka juzi kwenda kazini ule usiku, kuna simu nilimsikia baba akiwasiliana nayo, halafu akatoka pia na kurudi jana asubuhi. Basi unaambiwa acha asemwe na mama jamani maana alirudi muda ambao mama amesharudi, yani mama alichukia sana, tabia ya baba imeanza kumkera sana mama”
“Duh! Poleni sana, huyo baba yenu kaanza tabia mbaya kwakweli”
“Asante, yani hafai hata kidogo, namuonea huruma sana mama yangu jamani”
Wakaongea pale mambo mengi sana, hadi muda wa kurudi darasani.
Ulivyofika muda wa kutoka darasani kama kawaida wanafunzi wote walielekea kwenye gari za kurudi nyumbani kwao.
Gari walilopanda wakina Erica, kuna mahali lilipata pancha, kwahiyo dreva alishuka kubadili tairi ila Erica aliamua kuondoka tu kwani ilikuwa ni mitaa ya nyumbani kwao.
Ndipo alipopita karibu na mgahawa wa Sia, ila leo Elly alipomuona Erica alimkimbilia na kumkumbatia sana hata Erica alimshangaa sana Elly kufanya vile, alijitoa kwake na kumuuliza,
“Tatizo ni nini Elly?”
“Nimefurahi sana kukuona Erica, moyo ulikuwa unaniuma ila nilipokuona nimefurahi sana hata maumivu ya moyo wangu yamepungua”
Basi Erica akamsalimia kidogo mama Elly na kutaka kuondoka, ambapo Elly aliamua kumsindikiza huku akimuuliza baadhi ya mambo,
“Erica samahani, hivi unajua kupika?”
“Najua ndio, umesahau huwa nakuja kumuuliza mama yako kuhusu mapishi ili nami nikapike?”
“Nakumbuka ndio, kufua je na kuosha vyombo?”
“Najua ndio, kwanini unaniuliza hivyo?”
“Nimekuuliza tu, una simu wewe?”
“Uwiiii mama yangu hataki kabisa nimiliki simu, yani huwa akinikuta na simu ni balaa. Kasema hadi nikue, mimi najiona nimekua ila kwa mama bado ananiona kuwa ni mdogo sana”
“Je unaangaliaga sinema gani ukiwa nyumbani?”
“Mmmh leo Elly unaniuliza maswali gani? Mimi nikiwa nyumbani mara nyingi mama anapenda kuangalia sinema za Kiswahili sijui kwanini huwa anapenda hivyo basi na mimi naangalia, halafu kaka anapenda za ngumi, basi nazo huwa naangalia, akija dada Angel anapenda zile tamthilia za wazungu basi huwa nazo naangalia, kwahiyo mimi sina ninachopenda zaidi ya kufanya wanachopenda wao. Kitu pekee ninachofurahia kufanya muda wote ni kupika tu”
“Sawa, ila mama yenu kawalea vizuri sana, hongera zake kwakweli”
“Hata wewe mama yako kakulea vizuri”
Elly akatabasamu tu na Erica alikuwa amefika kwao, basi aliagana na Elly na moja kwa moja yeye akaingia nyumbani kwao.

Muda Erick nae kafika kwao ndio akamuona Elly na Erica wakiagana, basi alipofika alimuita Elly muda huo Erica alishaingia ndani, Elly alisogea kisha Erick alimuuliza,
“Wewe si ulisema unajihisi vibaya wewe!”
“Ni kweli, ila kwasasa nipo vizuri”
“Baada ya kumuona Erica sio!!”
“Mmmh inawezekana, unajua Erica ana maneno yenye busara sana”
“Kushinda Sarah”
“Sijawashindanisha ila ni kwavile Erica nimemzoea zaidi kushinda Sarah”
Kisha Elly aliamua kumuaga Erick kwani alihisi kuwa huenda wakagombana bure muda huo.
Erick aliingia ndani na kusalimia wazazi wao kisha moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambaye alikuwa akibadili sare za shule kwa muda huo, kwahiyo alipomuona Erick alishtuka kidogo nankumwambia,
“Uwe unagonga mlango mara nyingine Erick, utakuja kuona visivyoonekana bure”
“Kama vinini?”
Erica akacheka tu na kumuuliza Erica,
“Haya leo ni kitu gani kimefanya uje moja kwa moja chumbani kwangu”
“Nataka kujua ulikuwa unaongea nini na Elly”
“Khaaa kumbe ulituona, alikuwa ananiuliza tu kama najua kupika, kufua na kuosha vyombo”
“Ili iweje? Yani alijua iwe nini sasa?”
“Sijui ila kamsifia sana mama yetu kuwa ana malezi mazuri”
Basi Erick akaondoka kuelekea chumbani kwake, yani Erica alimuangalia tu bila ya kusema kitu zaidi ya moja kwa moja kwenda kuoga.

Elly alikuwa anarudi kwenye mgahawa wa mama yake huku akiwa na furaha kwa kuongea na Erica kwa siku hiyo.
Basi alifika tu pale kwenye mgahawa, muda kidogo wakafunga mgahawa na mama yake na kuondoka kurudi nyumbani, basi walipofika wakaanza kuongea ongea,
“Kwanza mwanangu niambie nini tatizo leo?”
“Hakuna tatizo ila nilikukumbuka tu”
“Mmmh jamani mwanangu”
“Kweli mama, unadhani siwezi kukukumbuka?”
“Unaweza mwanangu ila kama kuna tatizo naomba uniambie, usinifiche mimi ni mama yako”
Muda kidogo walifikiwa na wageni mahali pale, wageni wale ilikuwa ni mama Sarah na mwanae Sarah, basi na siku ile ndio Sia alitambulishwa vizuri kwa Sarah kisha wakasema kilichowapeleka pale ni sababu Elly aliondoka shule kwa kuaga kuwa anaumwa, kwahiyo mama Sarah aliposikia akaamua kwenda na mwanae kumuona Elly. Basi alimuuliza pale kuwa hali yake ikoje kwa muda huo,
“Naendelea vizuri kabisa”
Basi Sia akadakia na kuwaambia,
“Huyu nae mtoto wa mama hana looote, alinikumbuka tu”
Basi wakaongea ongea kidogo pale na kuaga ila muda huu hawakumlazimisha Elly kuondoka nae.

Usiku wa leo wakati madam Oliva katulia ndani na Steve, alipigiwa simu na ndugu yake,
“Jamani, Paul kakukumbuka ujue, yani anaumwa”
“Khaaaa jamani, Paul mkubwa hivyo aumwe sababu ya kunikumbuka mimi kweli!”
“Ndio, hivyo kasema kesho anakuja”
“Haya, mwache aje tu sina pingamizi mie”
Basi simu ilipokatika alianza kumwambia Steve,
“Nasikia mwanangu kanikumbuka sana, nimewaambia wamuache tu aje.”
“Bora ili na mimi nikamfahamu”
Madam Oliva akatabasamu kidogo na kusema,
“Usijali utamuona Paul wangu, mtoto mpole sana. Huwa nampenda sana mwenyewe”
Basi Steve alikuwa na hamu sana ya kumuona Paul maana siku zote anaambiwa sifa za Paul tu.
Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.
Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana.

Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.
Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana.
Kwakweli madam Oliva alishangaa sana basi aliwaangalia kwa muda kisha, aliwasogelea halafu Paul alienda kumkumbatia na yeye na kumsalimia kisha alimuuliza,
“Yani Paul ulimpita mama hapa ukaenda kumkimbilia mwingine! Kwanini?”
“Sababu ni baba yangu”
“Baba yako? Nani kakutambulisha?”
Wakakaa kwenye kochi sasa ili kusikiliza maelezo, yani madam Oliva alitaka kuelewa imekuwaje, ingawa ni kweli Steve ni baba mlezi sababu yeye yupo naye ila kajuana vipi na Paul? Madam Oliva alihitaji kujua,
“Kwani mmefahamiana vipi?”
Basi Steve alianza kuelezea,
“Unajua sikutegemea kama kuna siku nitakutana tena na huyu kijana, kuna mahali alikuwa akiishi nami nilikuwa nikiishi huko, basi mara kwa mara huyu kijana nilikuwa namuona akipita, nilijikuta nikimpenda sana kwani kila nikimuangalia naona karibia kila kitu naendana nae, nilimpenda sana, ni mpole na nilikuwa naongea nae mara nyingi. Aliniambia yeye ana mama lakini hana baba, nikamwambia basi mimi ndio nitakuwa baba yako. Kwahiyo siku zote alikuwa akiniita baba na tulikuwa tukipendana sana mpaka sikumuona tena, niliumia sana lakini sikuwa na namna yoyote ile. Siku zote ulipomuongelea Paul sikujua kama unamuongelea Paul huyu, jamani yani huyu ni mwanangu kabisa haijalishi chochote ila ni mwanangu”
Madam Oliva alitabasamu kwani alijihisi vyema kuona mumewe mtarajiwa kawa na mapenzi ya hali ya juu na mtoto wake Paul, basi akamuuliza na Paul
“Umejihisije mwanangu baada ya kumuona huyu?”
“Yani nimejihisi furaha sana mama, nimefurahi sana. Mimi hapa siondoki, nitakuwa nasoma huku huku nikae na baba yangu"
Yani kile kitendo wote kiliwashangaza sana jinsi upendo kati ya Paul na Steve ulivyokuwa hadi mama mdogo wa Paul yani mdogo wake na madam Oliva alikuwa akishangaa, kisha madam Oliva alitumia muda huu kumtambulisha Steve kwa mdogo wake,
“Huyu ni mdogo wetu wa mwisho, anaitwa Mary. Na huyu ni shemeji yako anaitwa Steve”
Basi Mary na Steve wakasalimiana pale na kuanza kuongea mambo mengine yaliyopo.

Leo ilikuwa ni siku ya sikukuu ya kiserikali kwahiyo hawakwenda shule, Erick na Erica walibaki nyumbani tu na kufanya zile shughuli mbalimbali ila baba Angel alimtaka Erick aende kiwandani ila leo alimtaka aende na Erica maana aliona bora wawe wawili huku akiwasisitiza wasile chakula hovyo, kwahiyo walijiandaa na kuondoka zao.
Mama Angel aliongea na mumewe,
“Mmmh saivi unahofia chakula cha hovyo eeeh!”
“Yani hata sielewi, unajua mimi kumuwekea mashaka mtu ni mara chache sana. Nakumbuka hata madam Oliva alikuwa akiniletea chakula kipindi kile nakula, angeamua kunidhuru basi naye lazima angenidhuru tu maana nilikuwa nakula bila ya wasiwasi wowote ule.”
“Kweli angeamua angekupata kiurahisi, ila baba Angel huyu mtoto kakua sasa na mimi nahitaji kurudi kwenye shughuli zangu nifanye kama zamani, unajua kuna mambo mengine hayaendi eeeh sababu mwenyewe sipo”
“Naelewa mke wangu, basi uwe unafanyaje! Yani uwe unaenda halafu saa ngapingapi unarudi sio unazamia hukohuko hadi jioni au usiku, yani hapo ndio kwenye tatizo na kufanya nione huyu mtoto hapati malezi mazuri. Kipindi cha hawa mapacha wetu, kwakweli mke wangu ulilea hawa watoto tena uliwalea sana, ila kwanini kuwe na tatizo katika kumlea huyu mmoja? Jitahidi mke wangu, kama pesa mbona na mimi natafuta sana! Haya hadi watoto nao wapo vizuri, inatakiwa mambo mengine tupunguze”
“Sawa nimekuelewa, ngoja nikakuandalie chakula”
Basi mama Angel alienda jikoni, na kumkuta Daima akiwa anajaribu kupika pale,
“Kheee Daima jamani mbona kujichosha hivi?”
“Mimba sio ugonjwa”
“Kheeee sio hivyo, nadhani umeninukuu vibaya siku ile nilipokwambia mimba sio ugonjwa, ni kweli mimba sio ugonjwa ila mimba inahitaji uangalifu wa hali ya juu maana ukikosea kidogo unaweza kupoteza mtoto au wote kwa pamoja, ndiomana mama mjamzoito anaopaswa kutazamwa kwa jicho la tatu. Yani kuna kazi za kufanya ukiwa mjamzito ila zingine unaachana nazo. Kama kazi za kuinama sio nzuri kwa afya yako na mimba yako”
“Sawa lakini mimi nahitaji kufanya kazi, sitaki kujibweteka tu”
“Usifanye kazi ngumu, ukiwa mjamzito kuna mambo inatakiwa uyaepuke hata kama unayapenda sana. Ni kweli kusema huwezi fanya chochote sababu ya mimba inakuwa ni tatizo lingine ila vilevile ukiwa mjamzito huwezi kufanya kila kitu kama ambavyo mtu ambaye si mjamzito hufanya. Unatakiwa kujilinda wewe na kumlinda mtoto ajaye. Haya acha hapo niendelee mwenyewe”
Daima aliacha pale ila alienda sehemu nyingine kutafuta kazi nyingine ya kufanya ni kwavile tu hakutaka tena kukaaa kaa na kulala lala bila kazi yoyote wakati hata hapo anaishi kwa bahatinasibu maana anawaza akirudishwa kwao itakuwaje tena na ile mimba yake.

Erick na Erica wakiwa kiwandani, kama kawaida Erick aliendelea na kazi za kiwanda ila Erica alikuwa akizunguka zunguka tu.
Siku hiyo alifika yule mteja wao mkubwa, yule mwarabu na kukutana nje na Erica, basi alianza kuongea nae,
“Natamani sana kumfahamu mama yako?”
“Kwanini?”
“Una heshima sana halafu inaonekana umefanana nae”
“Asante sana, ni kweli nimefanana na mama. Kwetu tupo wa nne ila mimi nimefanana sana na mama. Yupo dada yangu anaitwa Angel, nina kaka yangu Erick, na mimi ni Erica halafu kuna mdogo wetu wa mwisho ambaye bado ananyonya anaitwa Ester”
“Ooooh natamani sana kuwaona kwakweli, ila nyie wengine mbona majina yenu yameanzia na E halafu huyo dada yenu peke yake jina limeanzia na A, kwanini?”
“Sijui, naona pengine wazazi walitaka majina yetu yaanzie na A ila walivyotuzaa sisi walitupa majina yao maana baba na mama wanaitwa Erick na Erica, halafu sisi walituzaa mapacha, naona ndio herufi E ilipoanza”
“Aaaah nimekupenda bure wewe mtoto, nitakuwa babu yako yani ukiniona uwe unaniita babu. Halafu uwe jnanitambulisha kwa ndugu zako kama huyo dada yako Angel nae nimejikuta nikitamani sana kumfahamu, naamini utanitambulisha”
“Ndio, sema dada Angel yupo shule anasoma ya kulala huko huko”
“Akirudi utamwambia babu anataka kukusalimia, halafu mtanipigia simi hapa nitakuja hapa hapa kiwandani. Ukienda tu kwa meneja mwambie mpigie babu mwarabu atanipigie”
“Sawa hakuna tatizo”
“Ngoja niingie kwanza, yani nimekupenda bure”
Basi yule mwarabu alienda moja kwa moja ofisini kwaajili ya kuagiza bidhaa zake.

Elly nae alikuwa muda mwingi na mama yake, na alipata muda pia wa kuzungumza nae na kwa siku hii alizungumza nae vitu vingi sana,
“Kwani mama mwanamke anajigundua vipi kuwa mjamzito?”
“Mmmh Elly, mbona unanitisha na maswali yako?”
“Nahitaji tu kujua mama, nipo kujifunza.”
“Sawa, kwanza kabisa mwanamke anakuwa hapati siku zake yani zinakata hadi atakapojifungua, hiyo ni nia ya kwanza kabisa mwanamke kujihisi kuwa ni mjamzito. Ila kwa njia ya haraka ni kupima mkojo”
“Kivipi?”
“Mwanamke anaweza kwenda hospitali kupima, ila vile vile kuna vipimo vya kupima mimba nyumbani, yani mtu anaweza akanunua kipimo hiko kwenye duka la madawa na kwenda kupima nyumbani”
“Aaaah, kwahiyo akifika anasema nataka kipimo cha kupimia mimba?”
“Kheee wewe Elly, mbona unataka kujua vingi sana. Niweke wazi mwanangu kuna nini kinaendelea ili nijiandae, kama umeshamjaza mtu huko mimba nijue mapema. Ila nishakukataza habari za uzinzi mwanangu, au umeanza uzinzi?”
“Hapana mama, sina mambo hayo kabisa”
“Unauliza sana kuhusu mimba, napata wasiwasi”
“Jamani mama, nimeuliza tu nataka kujua, maana hapo badae natarajia kuwa daktari wa wanawake”
“Oooh vizuri mwanangu utatusaidia mengi maana wanawake tuna magonjwa mengi sana”
“Naelewa mama, na je mimba inazuiliwaje?”
“Mmmmh!! Kwa kutumia kinga na kwa mwanamke kutumia uzazi wa mpango. Ila Elly niambie ukweli tu kama umeanza uzinzi”
“Hapana mama, nilisema hadi nikiwa mkubwa”
“Mmmh unanipa mashaka na haya maswali yako”
“Sikuulizi tena mama”
Basi Elly aliinuka na kwenda ndani ila alikuwa akiwaza kitu kuwa lazima akamshawishi Sarah ili wanunue kipimo cha mimba na wajaribu kupima, ila alikuwa akiogopa sana moyoni mwake.

Wakati wa kurudi nyumbani, Erick na Erica waliamua kupitia kwanza dukani ili kuangalia mambo yanavyoendelea kwenye duka lao.
Basi walimkuta Rama akiendelea na kazi zake kama kawaida, Erick alifatilia baadhi ya mambo na kuona kuwa yapo sawa, ila kabla hawajaondoka kuna mtu alifika pale na kuanza kuongea na Rama, mtu huyo walipomuangalia vizuri alikuwa ni Rahim ila hawakuonyesha kama wamemuona kwani waliendelea na mambo mengine tu, alipoondoka ndipo Erica alipomfata Rama na kumuuliza,
“Unamfahamu yule uliyekuwa unaongea nae?”
“Aaaah yule ni mteja, tena ni mteja mzuri sana halafu inaonyesha ana mtoto mdogo sana kwasasa maana siku ya kwanza kuja alichukua nguo za mtoto mkubwa ila siku hizi huwa anachukua nguo za watoto wadogo inaonyesha ana watoto wadogo sana kwasasa”
“Aaaah kumbe, namjua yule ila sikujua kama ana watoto wadogo”
Basi Erick na Erica wakamuga Rama na kuondoka zao, ila kabla hawajafika mbali walimuona Juma akielekea hapo dukani, ikabidi Erick asimamishe gari na ashuke kwenda kumsalimia maana ni kitambo sana hajaongea nae, ingawa wazazi wake walikuwa wakimkataza kuongea na Juma ila Erick hakuona tatizo lolote kufanya hivyo. Alimsogelea na kumsalimia,
“Ooh Erick, nimefurahi sana kukuona. Naamini ni pacha wako Erica ndio kakushawishi kuja kunisalimia”
“Hapana ni mimi mwenyewe, kwanini unasema hivyo?”
“Naelewa moyo wa Erica ulivyo, ana upendo sana huyo binti ndiomana nasema kuwa ni yeye aliyekushawishi kuja kunisalimia”
Erick alicheka tu ila leo hakuongea nae sana, muda kidogo alimuaga na kurudi kwenye gari lao na kuendelea na safari huku akimwambia Erica,
“Ni kwanini watu wengi hukuona wewe kuwa na roho nzuri sana?”
“Ndio ukweli huo mimi nina roho nzuri”
“Na mbona ulitumwagia maji kitandani mimi na Sarah wakati ulijua wazi kuwa Sarah anaumwa?”
“Sikumuamini Sarah ndiomana, namuona macho juu juu sana”
“Kivipi?”
Erica aliamua kubadilisha mada hadi pale walipofika nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 350


Usiku wa leo, Daima alikuwa amekaa huku akilia tu Yani ilionekana kwa kiasi kikubwa sana anajutia mambo ambayo aliyafanya, basi Vaileth akawa anambembeleza, akakumbuka kipindi yeye alipobeba mimba na shule kumshinda, alikumbuka hilo na kujihisi vibaya sana,
“Pole sana Daima kiukweli nakuhurumia maana nimewahi kupitia hiyo kama yako”
“Mimi imezidi kwakweli, hakuna hata wa kunibembeleza, Junior hanipigii simu, mama na baba nao wala hawana habari na mimi, nimekuwa kama kifaranga aliyeachwa kwenye mvua, nateseka mimi”
“Pole sana, ila wewe na Junior si ilikuwa mnapendana sana!”
“Tena sana hata sijaamini kuwa kuna siku itakuwa hivi, yani Junior atanikana kabisa hata kuongea maneno ya uongo juu yangu. Sikufikiria kabisa kama kuna siku kama hii katika maisha yangu”
“Unachotakiwa kufanya ni kuamini kuwa hayo mambo yamepita na uangalie mambo mengine ya kufanya, kama kumlea mwanao”
“Kumlea bila ya baba, wakati baba yake yupo”
“Kwani wasiwasi wako nini? Mtoto akizaliwa walazimishe wakampime damu”
“Mmmh hawajataka kupima kipindi hiki ndio watakubali mtoto akizaliwa?”
“Watakubali tu hata usijali”
Basi siku walijikuta wakiongea sana hadi wakachelewa muda wa kulala.
Kulipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuinuia bila kujali kama usiku hakulala wala nini kwani moja kwa moja alienda kufanya usafi na kutaka kudeki ila mama Angel alimkuta na kumkataza kufanya hivyo, kisha akaongea nae,
“Unajua Daima kwakweli mimi nashangaa sana kuwa imekuwaje hadi umekuwa hivyo, sikuelewi ujue”
“Hunielewi nini mama?”
“Kwanini unajipa kazi zenye uwezo wa kutoa mimba yako, narudia leo sitaki kuona ukifanya kazi ngumu”
Basi mama Angel alienda kumtayarishia mumewe chakula ambaye alikula na kumuaga mke wake maana alitaka kidogo kwenda ofisini kwake.

Baba Angel alipofika ofisini tu, muda mfupi alifikiwa na mgeni na kumkaribisha maana mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi alimuuliza kitu kilichompeleka pale ofisini kwake,
“Umefata nini Sia?”
“Nataka kufanya utafiti juu ya aliyekupa sumu”
Baba Angel alicheka sana na kumuangalia kwa makini,
“Hayo maswala ya utafiti umeyaanza lini? Na nani aliyekwambia kuwa nilipewa sumu?”
“Nilikutana na Tumaini akaniambia hivyo, nilikuwa natamani kuja kukuona nyumbani kweko ila kuna muda huwa namuhofia sana mkeo maana na yeye huwa anabadilika kama kinyonga yani mambo yake huwa hayaeleweki kabisa”
“Haya mambo ya uchunguzi umesomea wapi?”
“Hivi nikiamua kuchunguza langu naanzahe kushindwa kwa mfano? Sikujua kipaji changu toka utotoni, yani sikujua kama nina kipaji cha upelelezi ila ni kipaji changu hiki. Nimekigundua ukubwani, ni kweli sijasomea ila naweza kufanya kwa njia za kawaida na nikagundua chanzo cha tatizo kama wachunguzi wengine”
“Ni kipi ulichowahi kukigundua wewe?”
“Hivi mimi ningemjua vipi Rahim aliyezaa na Erica yule mtoto wenu Angel? Ningemjua vipi Bahati aliyempenda sana Erica na sasa anaishi na rafiki kipenzi wa Erica? Ningejua vipi maovu ya Dora na ulokole wake fake?”
“Kheee umenishinda tabia, haya chunguza basi nani kanipa sumu”
“Niambie kwanza sehemu unazokumbuka kula chakula kabla ya kuanza kuumwa? Au kwa urahisi niambie ulipokula siku kabla hujaanza kuumwa”
“Aaaah nilikunywa maji tu na matunda”
“Maji uliyatoa wapi na matunda hayo uliyatoa wapi?”
“Maji ni hapa hapa ofisini, yale ambayo wote hapa huwa wanakunywa. Matunda kuna mama mmoja yuko hapo nje ya ofisi yetu huwa anatuletea matunda wote hapa na hata kwenye ofisi zingine halafu namuamini hawezi kunifanyia kitu chochote kile kibaya kwani ni mama mtu mzima kabisa”
“Inawezekana sio yeye ndio ila yote hayo nitayapata baada ya kuchunguza”
“Mmmh yani Sia akili zako huwa unazielewa mwenyewe”
Basi muda ule Sia alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alicheka tu na kuendelea na kazi zake kama kawaida.

Sia alitoka nje na kujaribu kunywa maji pale ofisini kwa baba Angel kisha akatoka nje na kumfata mama mtengeneza matunda na kuanza kuzungumza nae kirafiki,
“Vipi biashara inalipa hii eeeh!”
“Kiasi chake inalipa, sema haiwezi kutosheleza mahitaji yote sema inasaidia”
“Ila hata sijajitambulisha dah! Naitwa Sia au mama Elly, na wewe mwenzangu unaitwa nani?”
“Nimezoeleka kwa jina moja la mama Juli”
“Unajua mimi najishughulisha na shughuli za mama lishe, nina mgahawa wangu, kwakweli kwa kiasi chake napata pata vifaida jamani”
“Hongera na wewe”
“Aaah niambie ukweli basi, biashara inalipa hii?”
“Kiasi chake tu sio sana”
“Mmmh hutaki kuniambia ukweli sababu unahisi na mimi nitakuja kufanya hii biashara nini!"
Huyu mama akacheka kidogo na kumwambia Sia,
“Hamna ningekwambia ukweli, siwezi kukuficha. Ningepata faida sana kama ningekuwa na vitendea kazi vya kutosha ila sababu bado sijawa vizuri sana ndiomana”
“Pole, kuna mahali wanakopesha wafanyabiashara wadogo wadogo, kwanini tusiende huko ili upanue biashara yako?”
“Ningeenda ila kuna mama mmoja alikuja hapa na ameniahidi kuniongezea mtaji na amenihakikishia kabisa”
“Una bahati sana wewe, hongera. Ilikuwaje hadi aseme atakupa mtaji unajua sio kitu cha kawaida hiko?”
“Kweli hata mimi sikuamini kabisa, yule mama aliniletea matunda ya aina mbili alisema niyaoshe vizuri nimpelekee bosi Erick na yeye atanilipa, nilifanya vile na bosi aliyasifia sana”
Sia alishtuka kidogo ila hakutaka huyu mama agundue mshtuko wake, akamuuliza tena
“Baada ya hivyo tu ndio akakuahidi kukuongezea mtaji?”
“Ndio alisema yeye husaidia wasiojiweza, ila nakumbuka mara ya mwisho alisema atakuja tena Ijumaa”
“Yani kesho?”
“Ndio kesho atakuja, alisema kwenye mida ya saa saba au saa nane atakuja”
“Kwakweli hiyo ni bahati, hongera sana”
Basi waliongea pale, Sia alimueleza vizuri mambo yake ya chakula na alikuwa muwazi kwa huyu mama ili naye awe muwazi kwake,
“Yani kuna wanawake tuna shida sana jamani, mfano mimi mwanaume aliniacha basi mtoto nahangaika nae mwenyewe tu dah!! Tunashida sana wanawake, bora na nyie ambao kidogo mliolewa zamani”
“Tuolewe wapi? Tena mimi ndio nina mkosi wa kutosha tu, historia yangu utakaa chini kabisa kuisikiliza”
“Inasikitisha eeeh!”
“Sio kusikitisha tu, yani hata haieleweki, kuna mambo nikikusimulia unaweza sema ni makusudi ila ndio hali halisi ya maisha yangu, nina mtoto mmoja tu na mtoto mwenyewe ni majanga”
“Duh!!”
“Nitakusimulia siku nyingine maana naona tushakuwa ndugu”
“Haya, ngoja niende”
Basi Sia aliagana na huyu mama na kuondoka zake ila kimoyomoyo alipanga kwenda tena kesho yake ili amuone huyo mtu wa kumpa mtaji huyu mama.

Baba Angel alipomaliza kazi zake maana siku hii hakukaa sana kwenye kazi yake, aliamua kuondoka mapema, moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani kwake maana alikuwa ana uchovu kiasi, ila alipigiwa simu na mke wake,
“Upo wapi muda huu?”
“Nipo njiani narudi nyumbani”
“Samahani, nimepata taarifa kuwa Derrick hali yake imebadilika, kama utaweza pitia nyumbani kwao basi”
“Sawa, hakuna tatizo”
Baba Angel aliamua kwa muda ule ule kugeuza gari na kuanza kuelekea kwakina Derrick, ni kweli alipofika alimkuta mama Derrick akilia tu kiasi kwamba hata yeye aliingiwa na wasiwasi, alienda kwa haraka kuangalia tatizo, alimkuta Derrick kalala tu yani hata hatingishiki, alimuuliza mama Derrick tatizo ni nini,
“Sijui mwanangu ndio anakufa, sijui ni kitu gani sijui ni nini”
“Kwani imekuwaje?”
“Sijui, nimekuja kumuamsha Derrick haamki wala nini, mwanangu Derrick jamani”
Baba Angel aliomba usaidizi pale na walimbeba Derrick na kumpakia kwenye gari kisha ikafanyika safari ya kumpeleka hospitali.
Kufika kule, kweli hali yake haikuwa nzuri kiasi kwamba alikimbizwa moja kwa moja kwa wagonjwa mahututi.
Basi walikaa pale nje ila mama Derrick alikuwa akilia muda wote, basi baba Angel alimpigia simu mkewe ili kumpa taarifa kuwa Derrick kapelekwa hapo hospitali,
“Kwakweli hali yake si njema ila madaktari wanamuhudumia”
“Tatizo ni nini kwani?”
“Sijui maana hata mama yake nae hana maelezo mazuri kabisa yani, ngoja nisikilizie atakachokisema daktari”
Basi baba Angel alipokata simu aliitwa na daktari na kuagizwa baadhi ya dawa zingine za kumpatia Derrick, kwahiyo alitoka na kwenda kununua hizo dawa, wakati anatoka kwenye duka lile la madawa, alikutana na vijana wawili yani Elly na Sarah ambao walimsimamisha na kumsalimia,
“Kheee nyie mmetoka wapi?”
“Aaaah tumetoka na sisi hapo duka la madawa”
“Kwani mnafahamiana?”
“Ndio mama zetu ni marafiki”
Baba Angel aliwaaga ila alijiuliza kidogo kwani alimtambua Elly kuwa ni mtoto wa Sia, na aliambiwa Sarah kuwa ni mtoto wa Manka, basi alijiuliza,
“Kheee urafiki wa Sia na Manka umetokea wapi? Mmmh hawa wanawake hawa, usikute wanapanga ujinga wao”
Basi akaondoka zake kuelekea hospitali kwaajili ya kumuwahishia yule mgonjwa dawa.

Usiku wa siku hiyo wakati baba Angel amerudi, mkewe alimuuliza hali ya mgonjwa na alisema kuwa anaendelea vizuri,
“Kwani tatizo ni nini?”
“Unajua mama yake mwanzoni hakuwa na majibu mazuri ila sasa badae baada ya kumuuliza vizuri zaidi ndio akaweza kuniambia kidogo maana hali ya mgonjwa ilikuwa afadhari”
“Alisema tatizo ni nini?”
“Alisema kuwa, chanzo ni jana Derrick alikuwa akilia sana, alipomuuliza tatizo ni nini alisema kuwa roho inamuuma sana sababu anajua wazi ana watoto ila hajawahi kuwatia machoni watoto hao hata mara moja. Kwahiyo yeye alikuwa akiumia sana moyo wake”
“Kheee kumbe ndio sababu?”
“Inawezekana maana unaambiwa alikuwa akilia sana, na ndio leo alipolala akalala, maana kila walipomuasha hakuamka wala kuitikia ndio mpaka tumemkimbiza hospitali tena dokta alisema tungechelewa tu ingekuwa balaa”
“Duh!”
Mama Angel alisikitika sana ila aliamua kulala tu kwa muda huo.
Kulipokucha, baba Angel hata hakutaka kwenda popote kwa siku hiyo kwani kuna karatasi alirudi nazo nyumbani aliona bora azifanyie kazi akiwa nyumbani.

Sia kama ambavyo alipanga siku hii kwenda ofisini kwa baba Angel ili kumchungulia yule mama ataonana na mtu gani wa maana maana alihisi huyo mtu ndio atakuwa aliyemuwekea sumu baba Angel.
Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah.


Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.
Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana.
Kwakweli madam Oliva alishangaa sana basi aliwaangalia kwa muda kisha, aliwasogelea halafu Paul alienda kumkumbatia na yeye na kumsalimia kisha alimuuliza,
“Yani Paul ulimpita mama hapa ukaenda kumkimbilia mwingine! Kwanini?”
“Sababu ni baba yangu”
“Baba yako? Nani kakutambulisha?”
Wakakaa kwenye kochi sasa ili kusikiliza maelezo, yani madam Oliva alitaka kuelewa imekuwaje, ingawa ni kweli Steve ni baba mlezi sababu yeye yupo naye ila kajuana vipi na Paul? Madam Oliva alihitaji kujua,
“Kwani mmefahamiana vipi?”
Basi Steve alianza kuelezea,
“Unajua sikutegemea kama kuna siku nitakutana tena na huyu kijana, kuna mahali alikuwa akiishi nami nilikuwa nikiishi huko, basi mara kwa mara huyu kijana nilikuwa namuona akipita, nilijikuta nikimpenda sana kwani kila nikimuangalia naona karibia kila kitu naendana nae, nilimpenda sana, ni mpole na nilikuwa naongea nae mara nyingi. Aliniambia yeye ana mama lakini hana baba, nikamwambia basi mimi ndio nitakuwa baba yako. Kwahiyo siku zote alikuwa akiniita baba na tulikuwa tukipendana sana mpaka sikumuona tena, niliumia sana lakini sikuwa na namna yoyote ile. Siku zote ulipomuongelea Paul sikujua kama unamuongelea Paul huyu, jamani yani huyu ni mwanangu kabisa haijalishi chochote ila ni mwanangu”
Madam Oliva alitabasamu kwani alijihisi vyema kuona mumewe mtarajiwa kawa na mapenzi ya hali ya juu na mtoto wake Paul, basi akamuuliza na Paul
“Umejihisije mwanangu baada ya kumuona huyu?”
“Yani nimejihisi furaha sana mama, nimefurahi sana. Mimi hapa siondoki, nitakuwa nasoma huku huku nikae na baba yangu"
Yani kile kitendo wote kiliwashangaza sana jinsi upendo kati ya Paul na Steve ulivyokuwa hadi mama mdogo wa Paul yani mdogo wake na madam Oliva alikuwa akishangaa, kisha madam Oliva alitumia muda huu kumtambulisha Steve kwa mdogo wake,
“Huyu ni mdogo wetu wa mwisho, anaitwa Mary. Na huyu ni shemeji yako anaitwa Steve”
Basi Mary na Steve wakasalimiana pale na kuanza kuongea mambo mengine yaliyopo.

Leo ilikuwa ni siku ya sikukuu ya kiserikali kwahiyo hawakwenda shule, Erick na Erica walibaki nyumbani tu na kufanya zile shughuli mbalimbali ila baba Angel alimtaka Erick aende kiwandani ila leo alimtaka aende na Erica maana aliona bora wawe wawili huku akiwasisitiza wasile chakula hovyo, kwahiyo walijiandaa na kuondoka zao.
Mama Angel aliongea na mumewe,
“Mmmh saivi unahofia chakula cha hovyo eeeh!”
“Yani hata sielewi, unajua mimi kumuwekea mashaka mtu ni mara chache sana. Nakumbuka hata madam Oliva alikuwa akiniletea chakula kipindi kile nakula, angeamua kunidhuru basi naye lazima angenidhuru tu maana nilikuwa nakula bila ya wasiwasi wowote ule.”
“Kweli angeamua angekupata kiurahisi, ila baba Angel huyu mtoto kakua sasa na mimi nahitaji kurudi kwenye shughuli zangu nifanye kama zamani, unajua kuna mambo mengine hayaendi eeeh sababu mwenyewe sipo”
“Naelewa mke wangu, basi uwe unafanyaje! Yani uwe unaenda halafu saa ngapingapi unarudi sio unazamia hukohuko hadi jioni au usiku, yani hapo ndio kwenye tatizo na kufanya nione huyu mtoto hapati malezi mazuri. Kipindi cha hawa mapacha wetu, kwakweli mke wangu ulilea hawa watoto tena uliwalea sana, ila kwanini kuwe na tatizo katika kumlea huyu mmoja? Jitahidi mke wangu, kama pesa mbona na mimi natafuta sana! Haya hadi watoto nao wapo vizuri, inatakiwa mambo mengine tupunguze”
“Sawa nimekuelewa, ngoja nikakuandalie chakula”
Basi mama Angel alienda jikoni, na kumkuta Daima akiwa anajaribu kupika pale,
“Kheee Daima jamani mbona kujichosha hivi?”
“Mimba sio ugonjwa”
“Kheeee sio hivyo, nadhani umeninukuu vibaya siku ile nilipokwambia mimba sio ugonjwa, ni kweli mimba sio ugonjwa ila mimba inahitaji uangalifu wa hali ya juu maana ukikosea kidogo unaweza kupoteza mtoto au wote kwa pamoja, ndiomana mama mjamzoito anaopaswa kutazamwa kwa jicho la tatu. Yani kuna kazi za kufanya ukiwa mjamzito ila zingine unaachana nazo. Kama kazi za kuinama sio nzuri kwa afya yako na mimba yako”
“Sawa lakini mimi nahitaji kufanya kazi, sitaki kujibweteka tu”
“Usifanye kazi ngumu, ukiwa mjamzito kuna mambo inatakiwa uyaepuke hata kama unayapenda sana. Ni kweli kusema huwezi fanya chochote sababu ya mimba inakuwa ni tatizo lingine ila vilevile ukiwa mjamzito huwezi kufanya kila kitu kama ambavyo mtu ambaye si mjamzito hufanya. Unatakiwa kujilinda wewe na kumlinda mtoto ajaye. Haya acha hapo niendelee mwenyewe”
Daima aliacha pale ila alienda sehemu nyingine kutafuta kazi nyingine ya kufanya ni kwavile tu hakutaka tena kukaaa kaa na kulala lala bila kazi yoyote wakati hata hapo anaishi kwa bahatinasibu maana anawaza akirudishwa kwao itakuwaje tena na ile mimba yake.

Erick na Erica wakiwa kiwandani, kama kawaida Erick aliendelea na kazi za kiwanda ila Erica alikuwa akizunguka zunguka tu.
Siku hiyo alifika yule mteja wao mkubwa, yule mwarabu na kukutana nje na Erica, basi alianza kuongea nae,
“Natamani sana kumfahamu mama yako?”
“Kwanini?”
“Una heshima sana halafu inaonekana umefanana nae”
“Asante sana, ni kweli nimefanana na mama. Kwetu tupo wa nne ila mimi nimefanana sana na mama. Yupo dada yangu anaitwa Angel, nina kaka yangu Erick, na mimi ni Erica halafu kuna mdogo wetu wa mwisho ambaye bado ananyonya anaitwa Ester”
“Ooooh natamani sana kuwaona kwakweli, ila nyie wengine mbona majina yenu yameanzia na E halafu huyo dada yenu peke yake jina limeanzia na A, kwanini?”
“Sijui, naona pengine wazazi walitaka majina yetu yaanzie na A ila walivyotuzaa sisi walitupa majina yao maana baba na mama wanaitwa Erick na Erica, halafu sisi walituzaa mapacha, naona ndio herufi E ilipoanza”
“Aaaah nimekupenda bure wewe mtoto, nitakuwa babu yako yani ukiniona uwe unaniita babu. Halafu uwe jnanitambulisha kwa ndugu zako kama huyo dada yako Angel nae nimejikuta nikitamani sana kumfahamu, naamini utanitambulisha”
“Ndio, sema dada Angel yupo shule anasoma ya kulala huko huko”
“Akirudi utamwambia babu anataka kukusalimia, halafu mtanipigia simi hapa nitakuja hapa hapa kiwandani. Ukienda tu kwa meneja mwambie mpigie babu mwarabu atanipigie”
“Sawa hakuna tatizo”
“Ngoja niingie kwanza, yani nimekupenda bure”
Basi yule mwarabu alienda moja kwa moja ofisini kwaajili ya kuagiza bidhaa zake.

Elly nae alikuwa muda mwingi na mama yake, na alipata muda pia wa kuzungumza nae na kwa siku hii alizungumza nae vitu vingi sana,
“Kwani mama mwanamke anajigundua vipi kuwa mjamzito?”
“Mmmh Elly, mbona unanitisha na maswali yako?”
“Nahitaji tu kujua mama, nipo kujifunza.”
“Sawa, kwanza kabisa mwanamke anakuwa hapati siku zake yani zinakata hadi atakapojifungua, hiyo ni nia ya kwanza kabisa mwanamke kujihisi kuwa ni mjamzito. Ila kwa njia ya haraka ni kupima mkojo”
“Kivipi?”
“Mwanamke anaweza kwenda hospitali kupima, ila vile vile kuna vipimo vya kupima mimba nyumbani, yani mtu anaweza akanunua kipimo hiko kwenye duka la madawa na kwenda kupima nyumbani”
“Aaaah, kwahiyo akifika anasema nataka kipimo cha kupimia mimba?”
“Kheee wewe Elly, mbona unataka kujua vingi sana. Niweke wazi mwanangu kuna nini kinaendelea ili nijiandae, kama umeshamjaza mtu huko mimba nijue mapema. Ila nishakukataza habari za uzinzi mwanangu, au umeanza uzinzi?”
“Hapana mama, sina mambo hayo kabisa”
“Unauliza sana kuhusu mimba, napata wasiwasi”
“Jamani mama, nimeuliza tu nataka kujua, maana hapo badae natarajia kuwa daktari wa wanawake”
“Oooh vizuri mwanangu utatusaidia mengi maana wanawake tuna magonjwa mengi sana”
“Naelewa mama, na je mimba inazuiliwaje?”
“Mmmmh!! Kwa kutumia kinga na kwa mwanamke kutumia uzazi wa mpango. Ila Elly niambie ukweli tu kama umeanza uzinzi”
“Hapana mama, nilisema hadi nikiwa mkubwa”
“Mmmh unanipa mashaka na haya maswali yako”
“Sikuulizi tena mama”
Basi Elly aliinuka na kwenda ndani ila alikuwa akiwaza kitu kuwa lazima akamshawishi Sarah ili wanunue kipimo cha mimba na wajaribu kupima, ila alikuwa akiogopa sana moyoni mwake.

Wakati wa kurudi nyumbani, Erick na Erica waliamua kupitia kwanza dukani ili kuangalia mambo yanavyoendelea kwenye duka lao.
Basi walimkuta Rama akiendelea na kazi zake kama kawaida, Erick alifatilia baadhi ya mambo na kuona kuwa yapo sawa, ila kabla hawajaondoka kuna mtu alifika pale na kuanza kuongea na Rama, mtu huyo walipomuangalia vizuri alikuwa ni Rahim ila hawakuonyesha kama wamemuona kwani waliendelea na mambo mengine tu, alipoondoka ndipo Erica alipomfata Rama na kumuuliza,
“Unamfahamu yule uliyekuwa unaongea nae?”
“Aaaah yule ni mteja, tena ni mteja mzuri sana halafu inaonyesha ana mtoto mdogo sana kwasasa maana siku ya kwanza kuja alichukua nguo za mtoto mkubwa ila siku hizi huwa anachukua nguo za watoto wadogo inaonyesha ana watoto wadogo sana kwasasa”
“Aaaah kumbe, namjua yule ila sikujua kama ana watoto wadogo”
Basi Erick na Erica wakamuga Rama na kuondoka zao, ila kabla hawajafika mbali walimuona Juma akielekea hapo dukani, ikabidi Erick asimamishe gari na ashuke kwenda kumsalimia maana ni kitambo sana hajaongea nae, ingawa wazazi wake walikuwa wakimkataza kuongea na Juma ila Erick hakuona tatizo lolote kufanya hivyo. Alimsogelea na kumsalimia,
“Ooh Erick, nimefurahi sana kukuona. Naamini ni pacha wako Erica ndio kakushawishi kuja kunisalimia”
“Hapana ni mimi mwenyewe, kwanini unasema hivyo?”
“Naelewa moyo wa Erica ulivyo, ana upendo sana huyo binti ndiomana nasema kuwa ni yeye aliyekushawishi kuja kunisalimia”
Erick alicheka tu ila leo hakuongea nae sana, muda kidogo alimuaga na kurudi kwenye gari lao na kuendelea na safari huku akimwambia Erica,
“Ni kwanini watu wengi hukuona wewe kuwa na roho nzuri sana?”
“Ndio ukweli huo mimi nina roho nzuri”
“Na mbona ulitumwagia maji kitandani mimi na Sarah wakati ulijua wazi kuwa Sarah anaumwa?”
“Sikumuamini Sarah ndiomana, namuona macho juu juu sana”
“Kivipi?”
Erica aliamua kubadilisha mada hadi pale walipofika nyumbani kwao.

Usiku wa leo, Daima alikuwa amekaa huku akilia tu Yani ilionekana kwa kiasi kikubwa sana anajutia mambo ambayo aliyafanya, basi Vaileth akawa anambembeleza, akakumbuka kipindi yeye alipobeba mimba na shule kumshinda, alikumbuka hilo na kujihisi vibaya sana,
“Pole sana Daima kiukweli nakuhurumia maana nimewahi kupitia hiyo kama yako”
“Mimi imezidi kwakweli, hakuna hata wa kunibembeleza, Junior hanipigii simu, mama na baba nao wala hawana habari na mimi, nimekuwa kama kifaranga aliyeachwa kwenye mvua, nateseka mimi”
“Pole sana, ila wewe na Junior si ilikuwa mnapendana sana!”
“Tena sana hata sijaamini kuwa kuna siku itakuwa hivi, yani Junior atanikana kabisa hata kuongea maneno ya uongo juu yangu. Sikufikiria kabisa kama kuna siku kama hii katika maisha yangu”
“Unachotakiwa kufanya ni kuamini kuwa hayo mambo yamepita na uangalie mambo mengine ya kufanya, kama kumlea mwanao”
“Kumlea bila ya baba, wakati baba yake yupo”
“Kwani wasiwasi wako nini? Mtoto akizaliwa walazimishe wakampime damu”
“Mmmh hawajataka kupima kipindi hiki ndio watakubali mtoto akizaliwa?”
“Watakubali tu hata usijali”
Basi siku walijikuta wakiongea sana hadi wakachelewa muda wa kulala.
Kulipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuinuia bila kujali kama usiku hakulala wala nini kwani moja kwa moja alienda kufanya usafi na kutaka kudeki ila mama Angel alimkuta na kumkataza kufanya hivyo, kisha akaongea nae,
“Unajua Daima kwakweli mimi nashangaa sana kuwa imekuwaje hadi umekuwa hivyo, sikuelewi ujue”
“Hunielewi nini mama?”
“Kwanini unajipa kazi zenye uwezo wa kutoa mimba yako, narudia leo sitaki kuona ukifanya kazi ngumu”
Basi mama Angel alienda kumtayarishia mumewe chakula ambaye alikula na kumuaga mke wake maana alitaka kidogo kwenda ofisini kwake.

Baba Angel alipofika ofisini tu, muda mfupi alifikiwa na mgeni na kumkaribisha maana mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi alimuuliza kitu kilichompeleka pale ofisini kwake,
“Umefata nini Sia?”
“Nataka kufanya utafiti juu ya aliyekupa sumu”
Baba Angel alicheka sana na kumuangalia kwa makini,
“Hayo maswala ya utafiti umeyaanza lini? Na nani aliyekwambia kuwa nilipewa sumu?”
“Nilikutana na Tumaini akaniambia hivyo, nilikuwa natamani kuja kukuona nyumbani kweko ila kuna muda huwa namuhofia sana mkeo maana na yeye huwa anabadilika kama kinyonga yani mambo yake huwa hayaeleweki kabisa”
“Haya mambo ya uchunguzi umesomea wapi?”
“Hivi nikiamua kuchunguza langu naanzahe kushindwa kwa mfano? Sikujua kipaji changu toka utotoni, yani sikujua kama nina kipaji cha upelelezi ila ni kipaji changu hiki. Nimekigundua ukubwani, ni kweli sijasomea ila naweza kufanya kwa njia za kawaida na nikagundua chanzo cha tatizo kama wachunguzi wengine”
“Ni kipi ulichowahi kukigundua wewe?”
“Hivi mimi ningemjua vipi Rahim aliyezaa na Erica yule mtoto wenu Angel? Ningemjua vipi Bahati aliyempenda sana Erica na sasa anaishi na rafiki kipenzi wa Erica? Ningejua vipi maovu ya Dora na ulokole wake fake?”
“Kheee umenishinda tabia, haya chunguza basi nani kanipa sumu”
“Niambie kwanza sehemu unazokumbuka kula chakula kabla ya kuanza kuumwa? Au kwa urahisi niambie ulipokula siku kabla hujaanza kuumwa”
“Aaaah nilikunywa maji tu na matunda”
“Maji uliyatoa wapi na matunda hayo uliyatoa wapi?”
“Maji ni hapa hapa ofisini, yale ambayo wote hapa huwa wanakunywa. Matunda kuna mama mmoja yuko hapo nje ya ofisi yetu huwa anatuletea matunda wote hapa na hata kwenye ofisi zingine halafu namuamini hawezi kunifanyia kitu chochote kile kibaya kwani ni mama mtu mzima kabisa”
“Inawezekana sio yeye ndio ila yote hayo nitayapata baada ya kuchunguza”
“Mmmh yani Sia akili zako huwa unazielewa mwenyewe”
Basi muda ule Sia alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alicheka tu na kuendelea na kazi zake kama kawaida.
 
Nzuri. Hongera. Ntaanza mwanzo. Ila unarudia rudia kupost.

Asantee sana... Ila sio kurudiarudia mkuu.

Simulizi kwangu imeunganishwa, mtunzi aliiweka kila kipande kianze na "ilipoishia". Ndio sabb unaona.. But ukiisoma utazoea na utaskip
 
SEHEMU YA 351

Sia alitoka nje na kujaribu kunywa maji pale ofisini kwa baba Angel kisha akatoka nje na kumfata mama mtengeneza matunda na kuanza kuzungumza nae kirafiki,
“Vipi biashara inalipa hii eeeh!”
“Kiasi chake inalipa, sema haiwezi kutosheleza mahitaji yote sema inasaidia”
“Ila hata sijajitambulisha dah! Naitwa Sia au mama Elly, na wewe mwenzangu unaitwa nani?”
“Nimezoeleka kwa jina moja la mama Juli”
“Unajua mimi najishughulisha na shughuli za mama lishe, nina mgahawa wangu, kwakweli kwa kiasi chake napata pata vifaida jamani”
“Hongera na wewe”
“Aaah niambie ukweli basi, biashara inalipa hii?”
“Kiasi chake tu sio sana”
“Mmmh hutaki kuniambia ukweli sababu unahisi na mimi nitakuja kufanya hii biashara nini!"
Huyu mama akacheka kidogo na kumwambia Sia,
“Hamna ningekwambia ukweli, siwezi kukuficha. Ningepata faida sana kama ningekuwa na vitendea kazi vya kutosha ila sababu bado sijawa vizuri sana ndiomana”
“Pole, kuna mahali wanakopesha wafanyabiashara wadogo wadogo, kwanini tusiende huko ili upanue biashara yako?”
“Ningeenda ila kuna mama mmoja alikuja hapa na ameniahidi kuniongezea mtaji na amenihakikishia kabisa”
“Una bahati sana wewe, hongera. Ilikuwaje hadi aseme atakupa mtaji unajua sio kitu cha kawaida hiko?”
“Kweli hata mimi sikuamini kabisa, yule mama aliniletea matunda ya aina mbili alisema niyaoshe vizuri nimpelekee bosi Erick na yeye atanilipa, nilifanya vile na bosi aliyasifia sana”
Sia alishtuka kidogo ila hakutaka huyu mama agundue mshtuko wake, akamuuliza tena
“Baada ya hivyo tu ndio akakuahidi kukuongezea mtaji?”
“Ndio alisema yeye husaidia wasiojiweza, ila nakumbuka mara ya mwisho alisema atakuja tena Ijumaa”
“Yani kesho?”
“Ndio kesho atakuja, alisema kwenye mida ya saa saba au saa nane atakuja”
“Kwakweli hiyo ni bahati, hongera sana”
Basi waliongea pale, Sia alimueleza vizuri mambo yake ya chakula na alikuwa muwazi kwa huyu mama ili naye awe muwazi kwake,
“Yani kuna wanawake tuna shida sana jamani, mfano mimi mwanaume aliniacha basi mtoto nahangaika nae mwenyewe tu dah!! Tunashida sana wanawake, bora na nyie ambao kidogo mliolewa zamani”
“Tuolewe wapi? Tena mimi ndio nina mkosi wa kutosha tu, historia yangu utakaa chini kabisa kuisikiliza”
“Inasikitisha eeeh!”
“Sio kusikitisha tu, yani hata haieleweki, kuna mambo nikikusimulia unaweza sema ni makusudi ila ndio hali halisi ya maisha yangu, nina mtoto mmoja tu na mtoto mwenyewe ni majanga”
“Duh!!”
“Nitakusimulia siku nyingine maana naona tushakuwa ndugu”
“Haya, ngoja niende”
Basi Sia aliagana na huyu mama na kuondoka zake ila kimoyomoyo alipanga kwenda tena kesho yake ili amuone huyo mtu wa kumpa mtaji huyu mama.

Baba Angel alipomaliza kazi zake maana siku hii hakukaa sana kwenye kazi yake, aliamua kuondoka mapema, moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani kwake maana alikuwa ana uchovu kiasi, ila alipigiwa simu na mke wake,
“Upo wapi muda huu?”
“Nipo njiani narudi nyumbani”
“Samahani, nimepata taarifa kuwa Derrick hali yake imebadilika, kama utaweza pitia nyumbani kwao basi”
“Sawa, hakuna tatizo”
Baba Angel aliamua kwa muda ule ule kugeuza gari na kuanza kuelekea kwakina Derrick, ni kweli alipofika alimkuta mama Derrick akilia tu kiasi kwamba hata yeye aliingiwa na wasiwasi, alienda kwa haraka kuangalia tatizo, alimkuta Derrick kalala tu yani hata hatingishiki, alimuuliza mama Derrick tatizo ni nini,
“Sijui mwanangu ndio anakufa, sijui ni kitu gani sijui ni nini”
“Kwani imekuwaje?”
“Sijui, nimekuja kumuamsha Derrick haamki wala nini, mwanangu Derrick jamani”
Baba Angel aliomba usaidizi pale na walimbeba Derrick na kumpakia kwenye gari kisha ikafanyika safari ya kumpeleka hospitali.
Kufika kule, kweli hali yake haikuwa nzuri kiasi kwamba alikimbizwa moja kwa moja kwa wagonjwa mahututi.
Basi walikaa pale nje ila mama Derrick alikuwa akilia muda wote, basi baba Angel alimpigia simu mkewe ili kumpa taarifa kuwa Derrick kapelekwa hapo hospitali,
“Kwakweli hali yake si njema ila madaktari wanamuhudumia”
“Tatizo ni nini kwani?”
“Sijui maana hata mama yake nae hana maelezo mazuri kabisa yani, ngoja nisikilizie atakachokisema daktari”
Basi baba Angel alipokata simu aliitwa na daktari na kuagizwa baadhi ya dawa zingine za kumpatia Derrick, kwahiyo alitoka na kwenda kununua hizo dawa, wakati anatoka kwenye duka lile la madawa, alikutana na vijana wawili yani Elly na Sarah ambao walimsimamisha na kumsalimia,
“Kheee nyie mmetoka wapi?”
“Aaaah tumetoka na sisi hapo duka la madawa”
“Kwani mnafahamiana?”
“Ndio mama zetu ni marafiki”
Baba Angel aliwaaga ila alijiuliza kidogo kwani alimtambua Elly kuwa ni mtoto wa Sia, na aliambiwa Sarah kuwa ni mtoto wa Manka, basi alijiuliza,
“Kheee urafiki wa Sia na Manka umetokea wapi? Mmmh hawa wanawake hawa, usikute wanapanga ujinga wao”
Basi akaondoka zake kuelekea hospitali kwaajili ya kumuwahishia yule mgonjwa dawa.

Usiku wa siku hiyo wakati baba Angel amerudi, mkewe alimuuliza hali ya mgonjwa na alisema kuwa anaendelea vizuri,
“Kwani tatizo ni nini?”
“Unajua mama yake mwanzoni hakuwa na majibu mazuri ila sasa badae baada ya kumuuliza vizuri zaidi ndio akaweza kuniambia kidogo maana hali ya mgonjwa ilikuwa afadhari”
“Alisema tatizo ni nini?”
“Alisema kuwa, chanzo ni jana Derrick alikuwa akilia sana, alipomuuliza tatizo ni nini alisema kuwa roho inamuuma sana sababu anajua wazi ana watoto ila hajawahi kuwatia machoni watoto hao hata mara moja. Kwahiyo yeye alikuwa akiumia sana moyo wake”
“Kheee kumbe ndio sababu?”
“Inawezekana maana unaambiwa alikuwa akilia sana, na ndio leo alipolala akalala, maana kila walipomuasha hakuamka wala kuitikia ndio mpaka tumemkimbiza hospitali tena dokta alisema tungechelewa tu ingekuwa balaa”
“Duh!”
Mama Angel alisikitika sana ila aliamua kulala tu kwa muda huo.
Kulipokucha, baba Angel hata hakutaka kwenda popote kwa siku hiyo kwani kuna karatasi alirudi nazo nyumbani aliona bora azifanyie kazi akiwa nyumbani.

Sia kama ambavyo alipanga siku hii kwenda ofisini kwa baba Angel ili kumchungulia yule mama ataonana na mtu gani wa maana maana alihisi huyo mtu ndio atakuwa aliyemuwekea sumu baba Angel.
Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah.

Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah.
Sia alishangaa kidogo na kujiuliza kama kweli mama Sarah anaweza kufanya kitu cha kumdhuru baba Angel, alijiuliza sana bila ya jibu lolote.
Alitulia pale hadi mama Sarah alipoondoka ndipo alipoenda tena pale kwa mama Juli na kumsalimia kisha alianza kuongea nae,
“Nikaona gari inaondoka hapa wakati nipo kwa mbali, ndio huyo tajiri wako nini?”
“Ndio ni yeye, yani mama ana roho nzuri sana yule”
“Kwahiyo kakwambia atakupa huo mtaji?”
“Ndio kaniambia hivyo, kwakweli nafurahi sana kukutana nae”
“Hajamuulizia bosi Erick?”
“Aaaah hajamuulizia leo sijui kwanini ila hajamuulizia, hata hivyo anasema kuwa ni rafiki yake sana”
“Kwahiyo huo mtaji ameshakupa?”
“Kaniambia atakuja tena Jumatatu kwenye mida ya saa nane au saa tisa”
Sia alijaribu kupeleleza zaidi ila hakupata jibu la moja kwa moja, basi aliagana na yule mama na kuondoka zake, ila bado alijiuliza sana kuwa ni kweli mama Sarah ndiye aliyetaka kumdhuru baba Angel? Alikisa jibu kabisa, alijiuliza zaidi kila muda
“Amdhuru kwasababu gani? Sababu alizaa nae na amekataa mtoto au ni kitu gani? Lazima kuna kikubwa kati ya huyu Manka na Erick”
Muda huu aliona ni vyema kurudi kwenye biashara yake tu, na aliporudi aliendelea na kazi zake kama kawaida ila muda kidogo alifika pale mama Sarah na alimkaribisha na kuongea nae vizuri tu kama hakuna kitu,
“Unajua nilikuja mwanzoni nikakukosa, ndio nimekuja tena. Unadhurula sana wee mwanamke”
“Si unajua tena nipo kwenye kutafuta ndiomana”
“Huko kutafuta kwenye uzurulaji ni kutafuta kupi?”
“Aaaah ni kuhangaika tu na maisha”
“Haya sawa ni vizuri kuhangaika”
“Ni kweli, mna raha nyie wenzetu ambao maisha mmeyapatia”
Mama Sarah alicheka na kusema,
“Katika ujana unatakiwa kuwa makini sana na kupanga maisha yako kwa mpango kamili, kuna vitu ukikosa kuvifanya ujanani basi uzeeni utaona kila mtu mbaya kwako. Maisha yakikuendea kinyume katika njia uliyopo unatafuta njia nyingine ili kujiinua. Nikwambie siri ya mafanikio yangu”
“Eeeh niambie”
“Mimi nilimpenda sana Erick na nilikuwa na mahusiano nae, maana mimi ni mwanamke mzuri tena ninajfuraha, ila Erick alikuwa na mambo mengi sana na alijua wazi hawezi kudumu na mwanamke mzuri kama mimi tena ninajiamini na uzuri wangu. Kuachana na Erick kuliniumiza sana ila hakukuwa sababu ya mimi kutokusonga na kuanzisha maisha mengine. Nilianza mahusiano na mwanaume mmoja hivi, yeye hakuwa akihonga hela wanawake ila mimi alikuwa akinihonga tena sana tu, ila wakati huo sio kwamba niliachana moja kwa moja na Erick hapana, nikikutana nae tunamalizana kama kawaida na ilikuwa ni furaha kwangu ila badae nikaona ni ujinga kwani natakiwa kupanga maisha yangu. Ndipo nilipopata baba mmoja hivi, alinipenda, alinijali na kunihudumia nilifanya chochote alichotaka na ndio chanzo cha utajiri wangu”
“Kheee hongera, baba gani huyo?”
“Aliitwa mzee Jimmy”
Sia akashtuka hata mama Sarah aliona mshtuko wake na kumuuliza,
“Mbona umeshtuka hivyo?”
“Aaaah sio kitu, kwahiyo Sarah baba yake ni nani?”
“Yoyote kati ya hao ni baba yake maana nilikuwa nao wote”
“Kheee”
“Badae nitakuja kumfata Elly nyumbani kwako, kwaheri”
Muda huo mama Sarah aliondoka zake.

Kwenye mida ya saa moja kasoro, Sia alikuwa amekaa nje na mwanae Elly huku akiongea nae,
“Halafu mama Sarah alisema kuwa atakuja kukuchukua wewe, nashangaa mpaka muda huu hajaja”
“Ila mama mbona napafahamu vizuri wanapoishi, naweza kwenda mwenyewe sio mpaka nije kuchukuliwa”
“Ila mwanangu huoni ufahari eeeh! Unakuja kuchukuliwa na gari, hapa mtaani watu walikuwa wakituona tupotupo tu, wengine wakisema nawezaje kukusomesha shule za gharama ila kwasasa naona wameshindwa kusema zaidi maana kila mara magari yanakuja hapa. Ila mwanangu toka juzi nakuona kama una mawazo sana”
“Aaaah mama, usijali kuhusu mimi mbona nipo kawaida tu”
“Haya mwanangu yani mimi nilikuwa nakuona kama haupo sawa vile ila kama una tatizo lolote usisite kuniambia maana mimi ndio mama yako hakuna mtu mwenye mama wawili duniani, ni mama mmoja tu”
“Nimekuelewa mama lakini....”
Mama Sarah alifika muda ule ule na kusalimiana nao pale, kisha akamtaka Elly waondoke wote,
“Yani leo Sarah kaniambia nisipomshawishi Elly kwenda nae nyumbani basi na mimi sitotoka kwenda popote, halafu nataka nitoke sasa”
Elly akawaza kidogo ila mama yake akamshawishi ajiandae na aende, kiukweli Elly alikuwa akiogopa sana.
Basi alijiandaa na kuondoka na mama Sarah na moja kwa moja mama huyu alianza safari huku akiongea mambo mbalimbali na Elly,
“Hivi unamjua baba yako mzazi?”
“Simjui na hata sitaki kumjua, mama aliniambia kuwa baba alinikataa toka siku nazaliwa, alisema kuwa sijafanana nae”
“Oooh pole mtoto mzuri, hivi ukija kugundua kuwa ni mpango wa mama yako ili usimjue baba yako utafanyaje?”
“Sidhani kama mama anaweza fanya kitu kama hiko juu yangu, naamini mama ananipenda sana na sidhani kama ana mpango huo wa kufanya mimi nisimjue baba yangu”
“Je wewe una mpango wowote wa kukataa mtoto wako?”
Elly akashtuka kiasi na kukaa kimya kwa muda kisha akajibu,
“Aaah mimi siwezi, aaah siwezi kumkana mtoto wangu”
“Hivi unajua kuwa unaweza kupata mtoto kwa umri huo?”
Elly akatetemeka na kuogopa, alihisi labda Sarah kapima mimba, alijikuta tu jasho likimtoka na kukosa hata majibu, muda kidogo simu ya mama Sarah ilianza kuita na akaipokea, ilionekana aliyempigia alikuwa akimsubiria, basi aliongeza mwendo na walipofika nyumbani tu alienda kujiandaa na kuwaaga halafu akaondoka zake.

Leo Elly alishindwa hata kula vizuri kwani alikuwa na mawazo sana, alipomaliza moja kwa moja alienda chumbani kwake huku akiwaza sana yani aliogopa mno.
Akiwa chumbani kwake mida ule alienda Sarah mule chumbani na kumfanya Elly aogope zaidi na kitu cha kwanza alimuuliza Sarah,
“Umepima mimba Sarah?”
“Unaonekana unaogopa sana Elly, kwani mimba ni kitu gani? Usiwe muoga kiasi hiko Elly”
“Niambie kwanza Sarah”
“Hivi tulienda wote hadi duka la madawa kununua kipimo pamoja, ukaniacha nirudi nacho mwenyeww nyumbani unadhani naweza pima peke yangu? Hapana siwezi, nilikuwa nataka nawe uwepo ndio nipime, jana umeahidi kuja kulala kwetu ila hukuja ndiomana leo nilimuomba mama aje akulazimishe mwenyewe uje. Haya niambie tupime mimba au tusipime?”
“Mmmh Sarah naogopa sana, natamani kujua ila naogopa sana kwani hata nikiujua ukweli bado sitaweza kuuchukulia maana naogopa sana, moyo wangu unatetemeka kwa mawazo”
“Basi tusipime kwanza hadi tuanze kuwa na wasiwasi, ila hata hivyo kuna kitu shuleni walisema wataongea na watoto wa kike kuhusu afya na uzazi kwa mwanamke, kwahiyo nikisikiliza nitapata cha muhimu zaidi ya kupima. Naomba ushushe presha"
Elly akapumua kidogo, na afadhari akawa sawa, ndipo Sarah alipomvuta mkono na kumtaka aende nae chumbani kwake, kwakweli hili swala lilikuwa ni mtihani mkubwa kwa Elly na aligoma kukataa kwani familia hii ndio ilimpa kila kitu kwa wakati huo, hata mama yake alimfundisha kuwa asimkasirishe Sarah kabisa.
Akaenda nae chumbani kwa Sarah, na kama siku zote Sarah alihitaji kwahiyo ilibidi Elly afanye vile Sarah alivyotaka, baada ya hapo aliamua kurudi chumbani kwake, ila katika mambo yote tatizo lake lilikuwa sehemu moja tu, alijikuta akiwaza sana kuhusu mimba yani hakujua kama Sarah akiwa na mimba itakuwaje juu yake.
Aluporudi chumbani tu kabla ya kujilaza alishangaa kusikia mlango ukigongwa, moja kwa moja alihisi ni Sarah tena basi aliinuka na kwenda kufungua ila hakuwa Sarah kwani aliyeingia alikuwa ni Siku ambaye moja kwa moja alimziba mdomo Elly na kuingia nae chumbani kwa Elly na kufunga mlango kisha akamwambia,
“Elly najua kama wewe ni mwanaume rijali, najua kama wewe ni mwanaume uliyekamilika. Mimi ni siki nyingi sana sijafanya chochote, nakutamani siku zote hizi, nitakufundisha mapenzi. Kwangu utajua mapenzi ni nini na utazidi kuwa mwanaume wa ukweli”
Elly akaogopa ila Siku alianza kumpapasa Elly, kwakweli wazo la Elly muda huo lilimwambia kuwa yote yale ni umasikini wa nyumbani kwao na hakuwa tayari kufanya chochote na huyu dada yao ila alijua yule mdada akiendelea kumpapasa basi atajikuta akifanya makosa tena, hivyo basi alionekana kukubali halafu akamwambia Siku,
“Kuna kitu nahitaji muda huu halafu tutafanya kwa raha”
“Kitu gani?”
“Nahitaji kunywa maji”
“Ngoja nikakuletee”
“Hapana nisubiri hapa hapa nikanywe”
Elly alitoka mule chumbani kama anaenda jikoni kunywa maji ila moja kwa moja alienda chumbani kwa Sarah, na kwa uzuri Sarah hakufunga na funguo mlango wake basi Elly akaingia na kufunga kisha moja kwa moja alienda kulala pembeni ya Sarah maana Sarah nae muda huo alikuwa amelala hoi kabisa.
Kulipokucha, Sarah anashtuka na kumkuta Elly kalala pembeni yake, basi anamuamsha na kumuuliza,
“Kheee Elly ulirudi kulala humu?”
“Ndio, nilijikuta siwezi kulala mwenyewe”
“Oooh umeanza kunipenda eeeh”
Elly alikaa kimya kwa muda ila badae aliitikia na kumfanya Sarah afurahi sana, basi Elly akatoka kinyemela na kurudi chumbani kwake kwani muda huo hata Siku hakuwepo humo tena.

Basi leo Erica anakumbuka kuwaeleza wazazi wake kuhusu yule mwarabu, baba Angel aliposikia vile aliona ni vyema kama siku hiyo waendw wote kwa pamoja kwenye biashara ya huyo mwarabu na waweze kumualika kwao kwa chakula cha jioni kwa siku nyingine. Basi mama Angel akauliza,
“Jamani na mimi?”
“Ndio na wewe mke wangu”
“Hapana, huyo baba si ana hamu ya kunifahamu itakuwa vyema kama hatonifahamu kwa wakati ili mkimualika kwwnye chakula cha jioni aweze kufika na atanifahamia huku nyumbani”
“Ila mke wangu una akili sana wewe jamani, ndiomana nikakuoa kwakweli, haya Erick na Erica mjiandae tuweze kwenda huko”
Walijiandaa na kisha kuondoka hapo nyumbani kwahiyo pale alibaki mama Angel, Daima, Vaileth na Ester.
Kama kawaida Daima alikuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali kwakweli ile hali ilikuwa ikimkera sana mama Angel hadi alianza kujiuliza kuwa huyu binti ana lengo gani,
“Daima unataka hiyo mimba itoke?”
“Hapana mama”
“Sasa kwanini unafanya vitu nilivyokukataza? Nani kakutuma upinde mgongo hapo kwenye kibaraza na udeki, nani kakutuma?”
Daima alikuwa kimya kwa muda, kisha mama Angel akaendelea,
“Nina madekio ya kusimama, ila wewe umeenda kuchukua tambala na kusafishia ili tukueleweje?”
“Tambala linafuta vizuri mama”
“Unajua usinichefue, nitakurudisha kwenu wewe, sitaki ufanye ujinga hapa kwangu”
Daima alianza kulia tena alilia sana hata mama Angel alimshangaa na kushindwa hata kumbembeleza zaidi zaidi alimuita Vaileth na kumwambia kuwa ambembeleze,
“Vai, mbembeleze mwenzio huyo, mimi siwezi jamani”
Kisha mama Angel alienda zake ndani na kuendelea na mambo mengine.

Ile habari ya kuhusu mzee Jimmy ilikuwa imeshtua kwa kiasi fulani Sia, na siku ya leo aliamua kwenda kwa Tumaini ili kumueleza habari hiyo kwani alijua ndio pekee anaweza kumsikiliza.
Moja kwa moja alienda kwa Tumaini na alimkuta na kuanza kuongea nae,
“Nina habari ndugu yangu na inaniwasha hatari”
“Habari gani? Na wewe kwa umbea hujambo ndugu yangu”
“Mmh sio umbea tu, natumai unamfahamu mama Sarah?”
“Yule mwalimu?”
“Ndio huyo huyo, alikuwa mwalimu wa kujitegemea ila yule hajasomea ualimu”
“Kheee wewe jamani unafahamu mambo mengi sana ya watu”
“Aliniambia yeye mwenyewe”
“Mmmh ila wewe, haya kaja kukwambia tena kuwa mtoto wake ni wa Erick?”
“Hapana, ila nimepata mapya”
“Yapi hayo?”
“Kumbe mama Sarah alikuwa akitembea na baba yenu mzee Jimmy, jana kaniambia vizuri na ile mali aliyokuwa nayo ni mambo ya mzee Jimmy”
“Mmmh ila wewe hukawii kuniambia hata mtoto wake ni mdogo wetu”
“Hajaniambia kuhusu mtoto ila habari ndio hiyo, usinifikirie vibaya, nimekuletea ujumbe tu”
Basi muda kidogo aliaga na kuondoka zake, moja kwa moja alielekea kwenye biashara zake sasa.
Alipofika tu alimkuta mama Sarah yuko hapo akimsubiria, basi akamwambia,
“Ila na wewe unahangaika umeacha biashara hapa sijui ukaenda wapi?”
“Sikuwa mbali sana nilikuwepo tu kufata madeni yangu”
“Wamekulipa sasa?”
“Ahadi kibao, ndiomana huwa sipendi kukopesha chakula, mtu akishakula, akienda chooni anasahau kila kitu loh”
Mama Sarah akacheka tu na kumwambia Sia,
“Unahangaika sababu hukupanga misingi imara ya maisha yako”
“Aaaah maisha mara nyingine inatokea tu”
“Hapana inatakiwa kupanga, mfano kabla ya kupata mtoto inatakiwa kupanga nazaa na nani? Mwanangu ataishi vipi? Atasomaje na atakula nini? Mavazi je, unataka mwanao awe vipi, maisha ni kupanga”
“Kwahiyo wewe ulipanga?”
“Ndio, mimi nilipanga na niliyezaa nae niliona ni sahihi, nilizaa na mzee Jimmy, ona maisha yalivyoninyookea, nina nyumba tatu na zote nimeachiwa na mzee Jimmy, nina shule mbili, nina viwanja na mashamba. Mwanangu Sarah hawezi kupata shida sababu baba yake kamuachia mali za kutosha”
“Kheee hongera sana”
“Asante, nilipita tu kukusalimia. Kwaheri”
Mama Sarah aliondoka zake, yale maneno yalimpa mchecheto Sia yani alijikuta akiamani kuyapeleka kwa Tumaini, na muda huo huo aliondoka na kwenda tena hadi kwa Tumaini na hata Tumaini alimshangaa kwani giza lilishaanza kuingia kwa muda huo,
“Mmmh Tumaini, kuna mambo duniani. Baba yenu aliwaachia vitu gani vya kurithi?”
“Kivipi?”
“Mama Sarah sasa, kaachiwa nyumba tatu na mzee Jimmy, shule kubwa kubwa mbili, viwanja vya kutosha na mashamba kibao. Mzee Jimmy alikuwa tajiri sana, halafu kumbe Sarah ni mdogo wenu halali”
“Mmmh Sia nani kakwambia hayo maneno?”
“Yeye mwenyewe mama Sarah”
“Duh!! Haya, asante kwa taarifa”
Sia aliamuaga Tumaini na kuondoka zake kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 352

Usiku wa leo Tumaini alijiuliza sana juu ya habari alizopewa na Sia, na kujiuliza kwanini baba yao alifanya siti hadi anakufa bila kuwaambia ukweli wowote ule, alijiuliza sana bila ya jibu, akaamua kulala tu siku hii.
Jumapili ile kama kawaida Tumaini alienda kwenye Ibada, ila alipotoka akakutana na mama Sarah na kusalimiana nae pale, ila hakuweza kubaki na jambo lile moyoni, aliamua kumuuliza tu,
“Mama Sarah, kwanini usituambie mapema kuwa Sarah ni damu yetu?”
“Kivipi?”
“Mzee Jimmy ni baba yetu mzazi mimi na Erick”
Mama Sarah alijifanya kushtuka kamavile ni kitu ambacho hakukijua kabla, alimuuliza Tumaini
“Kwani nani kakwambia hayo maneno?”
“Siwezi kumtaja ila kwanini hutuambii ukweli kama Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy!”
“Yani hata mimi nashangaa maana huyo mzee hata aimfahamu jamani, yuko wapi kwani?”
“Baba yetu alishakufa”
“Oooh poleni sana, simjui huyo mzee”
“Humjui wapi wakati kakuachia nyumba tatu sijui, shule mbili, na viwanja na mashamba, humjui wapi? Hilo la kukuachia mali sio tatizo ila tatizo kwanini umfiche ndugu yetu!”
“Unajua nashangaa tu hapa, mimi sijui chochote jamani mama Leah. Nani kakwambia hayo maneno jamani!”
“Kwaheri”
Tumaini hakumtajia mama Sarah kuwa Sia ndio kamwambia hayo maneno, na akaagana nae muda huo na kuondoka zake.

Jumatatu ya leo, baba Angel anaamua kumuaga mkewe na kwenda zake ofisini, ila mama Angel nae anamuahidi kuwa badae na yeye ataenda huko huko ofisini,
“Sawa mke wangu”
Basi baba Angel akaondoka muda huo na kwenda ofisini.
Mama Angel akafanya majukumu mengine, ila pia alikumbuka kuhusu ndugu yake aliyekuwa hospitali basi alijiandaa pia na kwenda kumuona. Ila siku hii alitoka nyumbani kwake bila usafiri kwani hakujihisi kuendesha gari siku hii na pia hakutaka kumuita dereva wao, kwahiyo aliondoka hapo kwake mpaka stendi na kuchukua daladala kwenda mpaka hospitali.
Akiwa njiani kwenda kumuona Derrick, alikutana na Rahim basi Rahim alianza kumsemesha,
“Erica, bado una kisirani na mimi hutaki hata kunisalimia?”
“Achana na mimi”
“Nimeachana na wewe na wala sitokuwa nikikusumbua kama zamani kwani nimepata mchepuko wa Erick”
“Mchepuko wa Erick!”
“Nilijua kama hilo jambo lazima likushangaze sana, ndio mchepuko wa Erick alijisahau na kunipigia mimi simu basi ndio nipo nae”
Mama Angel alielewa vizuri kuwa huyu Rahim anazungumzia nini maana walimuona siku akiwa na mama Sarah, ila hakutaka kuongea nae sana zaidi zaidi alimuaga tu,
“Mimi nina haraka bhana, namuwahi mgonjwa wangu”
“Au wivu umekujaa?”
Mama Angel hakumjibu kitu zaidi zaidi alienda kuingia kwenye hospitali aliyokuwa akienda kumuona Derrick.
Mama Angel aliingia moja kwa moja kwenye wodi aliyoelekezwa, ni kweli Derrick alikuwa na hali mbaya kwani hata kuongea hakuweza, basi aliongea kidogo na mama Derrick pale
“Ila saivi hali yake unaionaje?”
“Mbona afadhari, alikuwa na hali mbaya sana. Bila mumeo kwa hakika tulikiwa tunampoteza huyu mtu”
Basi mama Angel aliongea kidogo na kuondoka zake, ila aliona ni vyema kwa muda huo kupitia ofisini kwa mume wake. Kwahiyo alichukua tu usafiri wa pikipiki kwa muda huo maana hakutaka tena kukutana na Rahim njiani.
Basi alivyofika ofisini hata mumewe alishtuka kidogo kwani hakujua kama ataenda muda huo,
“Unajua sikujua kama ungekuja muda huu?”
“Nilipita hospitali kumuona Derrick nikaona ni vyema nipitie kukuona mume wangu. Au nimefanya vibaya?”
“Hapana hujafanya vibaya mke wangu, hii ni ofisi yako na ukumbuke uliniambia kuwa utakuja”
“Ndio mume wangu, ila nakuomba kwasasa uwe makini na chakula huku usile hovyo”
“Sili tena mke wangu”
“Nahitaji nirudi nyumbani halafu nikuletee chakula”
“Hapana, hata leo nitawahi kutoka. Nenda kaniandalie chakula kizuri tu nikirudi nitakuja kula maana najua mke wangu kwa mapochopocho ni hatari”
Mama Angel alitabasamu na kumuaga mumewe, ila wakati yupo njiani alikutana na mama Sarah, yani mama Sarah ndio alimuona mama Angel na kusimama nae njiani akimsalimia ila mama Angel alikuwa na hofu kiasi na mtu huyu, kiasi kwamba mama Sarah alicheka na kumwambia mama Angel,
“Acha uoga wewe, una wasiwasi sana unahisi nitamuiba mumeo? Jiamini”
“Mbona najiamini sana tu”
“Hapana hujiamini, muda wote unahisi kuibiwa mumeo, kwanza pole sana. Ila kumbuka kunguru hafugiki, yule Erick ni kama kunguru tu”
Mama Angel aliamua tu kuondoka kwani hakutaka kuongea zaidi na mtu huyu.

Sia alijibanza pembeni kama kawaida, kwenye mida ya saa tisa kasoro alionekana tena mama Sarah akienda kwa yule mama na walionekana wakiongea kwa kirefu sana.
Mama Sarah alipoondoka tu, Sia alienda kwa yule mwanamke ili kumuuliza vizuri,
“Naona na leo bosi wako alikuja!”
“Mbona unamfatilia sana, na wewe unataka msaada wake nini nimwambie?”
“Hapana, mimi nilikuwa napita tu hapa ndio nikakuona naye”
Sia akaona leo hakuna ushirikiano sana kwa huyu mama, akaamua tu kumuaga na kuondoka zake.
Moja kwa moja alirudi kwenye biashara zake ila alishangaa sana kumkuta mama Sarah pale alisalimiana nae kisha mama Sarah alimuuliza,
“Umetoka wapi?”
“Kwenye mihangaiko yangu tu”
“Mihangaiko ya kutafuta umbea”
Sia alishtuka kidogo na kujibu kwa kujibalaguza,
“Hapana bhana”
Mama Sarah alicheka kwa kejeli kisha akamnasa kibao Sia na kumwambia,
“Unanifatilia ili iweje?”
Sia alikuwa akishangaa tu kwani hakutegemea kama mama Sarah angemgundua.

Sia alishtuka kidogo na kujibu kwa kujibalaguza,
“Hapana bhana”
Mama Sarah alicheka kwa kejeli kisha akamnasa kibao Sia na kumwambia,
“Unanifatilia ili iweje?”
Sia alikuwa akishangaa tu kwani hakutegemea kama mama Sarah angemgundua.
Mama Sarah akamuangalia tena na kumzaba Sia kibao kingene kisha akamwambia,
“Kumbe ndiomana biashara yako haikui sababu kutwa kucha kufatilia maisha ya watu, haya ulikuwa unanifatilia ili iweje?”
Sia aliona aibu kiasi na kuamua kumuomba mama Sarah ili wakazungumze pembeni ambapo mama Sarah alikubali hilo ingawa alikuwa na hasira sana, basi Sia alianza kumuomba msamaha,
“Kwanza naomba unisamehe sana kwa kukufatilia, sijui ni vipi umenigundua ila naomba unisamehe sana”
“Mimi ni mtu makini sana na hufanya vitu kwa umakini zaidi, nilikugundua toka siku nimekuona unachungulia pale karibu na ofisi ya Erick”
Sia akapumua kidogo maana kumbe alionekana akichungulia, akaendelea kumuomba msamaha,
“Nisamehe sana”
“Na ulivyokuwa mjinga sasa, kila ninachokuambia unapeleka makatambuga yako kwa mama Leah kumwambia nilichosema, mimi ni mtu makini sana na kila kitu huwa nafanya kwa akili. Usidhani kila nilichokwambia ni cha kweli, bali nilitaka kupima kiwango chango cha umbea. Niambie sasa kilichokufanya uanze kunifatilia ni kitu gani?”
Sia hakuwa na namna nyingine hivyobasi akaona ni vyema tu amwambie ukweli,
“Ni hivi, nilipewa taarifa na Tumaini kuwa Erick ameumwa gafla, na hospitali walisema kuwa alinyweshwa sumu, ni hapo nilipoanza kufatilia kuwa hiyo sumu kapewa na nani? Nilipofatilia alichokula ndio nikagundua kuwa amekula matunda ya yule mama, ndipo nilipoanza kumfatilia na kukukuta wewe”
“Kwahiyo unahisi kuwa mimi ndio nilimuwekea Erick hiyo sumu?”
“Hapana, ila bado nilikuwa nachunguza”
“Lazima ulinihisi na ndiomana ulikuwa ukifika pale muda ninaoenda mimi tu. Haya ulipogundua kuwa ni mimi ulichukua uamuzi gani?”
“Mimi nilikuwa bado nachunguza kwani sikuamini kuwa wewe unaweza kufanya hivyo”
Mama Sarah akacheka kidogo na kumuuliza tena Sia,
“Sasa kwanini hukuja kuniuliza mwenyewe? Usijiumeume kuwa bado ulikuwa ukichunguza, ile siku ya kwanza wakati una mashaka nami, ungekuja kuniuliza, ila kwanini hukufanya hivyo? Hakika wewe sio rafiki, wewe ni mnafki sana”
“Nisamehe ndugu yangu”
“Haya, huyo Erick anakulipa nini kwa kumsaidia uchunguzi?”
“Hanilipi chochote ila nimefanya tu sababu nampenda Erick”
“Wewe nawe hebu nitolee balaa mimi, unampenda Erick huko kumpenda vipi? Unadhani unaweza kuwa nae? Ni bora mimi, kwanza Erick kuzaa na wewe nahisi huwa anajutia sana, hueleweki hapo ulipo, yani hueleweki kitu chochote”
“Sieleweki lakini Erick alikuwa mpenzi wangu na tulipendana sana”
“Jidanganye, hivi wanawake wa Erick unaweza kujifananisha nao? Umeniona mimi vizuri, huyo Erica mwenyewe haingii ndani kwangu kwa uzuri, yani hata shule alikuwa anaogopa balaa akisikia mwanaume ananifatilia mimi basi yeye anajiweka kando, akawa anajifanya binti mlokole maana hakuna wa kumchagua. Watu tupo na uzuri wetu”
Sia hakumjibu hapa kwani hakutaka kubishana na huyu ukizingatia bado anahitaji msaada wake, kwahiyo alichokifanya yeye ni kuzidi tu kumuomba msamaha.
“Nisamehe sana naomba yaishe”
“Sasa sikia nikwambie na uweke akilini, hakuna kitu sipendi katika maisha yangu kama kufatiliwa, hata mimi na ndugu zangu huwa hatufatiliani yani kila mtu na mambo yake. Iwe nimemuwekea sumu kweli au sijamuwekea sitaki unifatilie kabisa, nadhani umenielewa!”
“Nimekuelewa ndio, sitorudia”
“Haya, mjinga wewe. Nenda kaendelee kuuza biashara yako ya kijinga, biashara haikui sababu ya umbea, unaacha kutafuta masoko huko upo makini kwenye kufatilia yasiyokuhusu”
Sia alimuangalia tu mama Sarah ambaye kwa muda huo aliondoka zake na kuendelea na mambo yake mengine.

Yani leo Sia alirudi nyumbani huku akijiuliza vitu vingi sana,
“Hivi yule ana maanisha nini? Kwahiyo mimi mbaya jamani, mbona huyu mwanamke ana ringa sana dah!!”
Muda kidogo Elly nae alirudi toka shuleni, basi Elly alivyopumzika tu kidogo, Sia akamuuliza mwanae,
“Eti Elly mwanangu, mimi mama yako sio mzuri?”
“Aaaah mama, wewe ni mzuri sana. Nani anakusema vibaya mama yangu?”
“Hakuna, nimekuuliza tu”
Basi Sia akaweka vitu vyake vizuri, ila siku hiyo umeme ulikatika na wakaamua kuwasha tochi ya kwenye simu, ilibidi Sia aende dukani kununua mshumaa kwa muda huo.
Basi alifika dukani na kununua mshumaa, ila wakati anarudi kuna mbaba mmoja alimsimamisha na kuanza kuongea nae,
“Samahani, unaishi wapi?”
“Hapo juu kidogo”
“Sijawahi kukuona mitaa hii, naomba nikusindikize kidogo”
Sia hakuona tatizo na alianza kusindikizwa na huyu mbaba basi yule baba alianza kumsifia Sia,
“Sijapata kuona mwanamke mzuri kama wewe”
Sia alianza kucheka, tena alicheka sana na kumwambia huyu baba,
“Hivi nyie wanaume mna matatizo gani? Huwa mnasifia hata vitu visivyokuwepo, Nitolee balaa mie:”
Sia aliachana na yule mbaba na kutembea haraka haraka kurudi nyumbani kwake, ila alipofika tu na umeme nao ukarudi kwahiyo mshumaa wao ulipona kutumika kwa siku hiyo.

Siku ya leo walivyoenda shule, muda wa mapumziko, Sarah alimfata Elly na kumuita pembeni kisha kuongea nae,
“Kuna mahali nataka kwenda kesho itabidi unisindikize”
“Tukitoka shule?”
“Hapana, tutaomba ruhusa kabla hata ya kutoka shule kuna vitu vingine ni muhimu kuwahi zaidi”
“Mmmh ni wapi huko?”
“Utapajua tu hiyo kesho, kwani una tatizo gani?”
“Hapana kitu”
Basi Sarah akaondoka zake, kipindi hiki Sarah hata hakuwa karibu na Erick kama ilivyokuwa hapo mwanzo, basi Elly alivyorudi Erick alianza kumuuliza maana kwa kipindi hiki walikuwa wakiongea vizuri tu na sio ugomvi kama zamani,
“Kwani ni kitu gani ambacho huwa unaongea na Sarah?”
“Unajua nini, Sarah kawa dada yangu yani mimi nipo chini ya malezi ya mama yake”
“Aaaah hapo nimeelewa sasa”
Wakaendelea na vipindi kama kawaida, muda wa kutoka shule ulivyofika Erick alitoka leo ila hakutaka kupanda gari la shule, kwahiyo alitoka na wale wanafunzi ambao huwa wanapanda daldala.
Moja kwa moja alipanda daladala la kurudi kwao, wakati anashuka kwenye ile daladala alikutana na Sia, ila Erick alitaka kumpita tu, sema Sia alimsimamisha na kuanza kuongea nae,
“Erick unataka kunipita tu bila ya salamu, sio vizuri hivyo. Mimi sio mbaya wako ujue”
Basi Erick akamsalimia na kutaka kuondoka ila Sia alimzuia na kumwambia,
“Utaondoka tu Erick, ila ngoja nikwambie. Majina ya Erick ni watu wakarimu sana halafu hawana hasira kama wewe ufanyavyo”
“Kwahiyo unataka kusema nini leo? Kuwa Erick sio jina langu au ni kitu gani?”
“Hapana, sina maana hiyo. Sikia Erick, kuna vitu vingi sana vipo nyuma ya pazia na wewe huvijui ila siku ukivijua utaona kuwa mimi nilikuwa naongea nawe mambo ya maana. Ila nilisema kuwa naacha umbea, ngoja ninyamaze”
Wala Erick hakutaka kuongea nae zaidi kwani muda huo huo na yeye aliondoka zake kwaajili ya kurudi nyumbani kwao.

Kwenye mida ya mchana, wakati baba Angel yupo ofisini, mke wake alienda kumpelekea chakula cha mchana, kwakweli alifurahi sana kwani alitamani sana kwa mkewe kuanza kumfanyia hivyo,
“Leo nimefurahi sana mke wangu, naona jinsi gani unanijali mume wako”
“Ndio nakujali sababu nakupenda sana”
“Kula mume wangu, leo nipo kwaajili yako. Nikitoka hapa nitapitia kidogo kwenye ofisi yangu”
“Ila usikawie sana, sio ndio urudi nyumbani usiku sana”
“Hapana nitageuza mapema tu”
Wakaongea pale kisha baba Angel alipomaliza kula, mama Angel alibeba vyombo na kumuaga mumewe kisha akaondoka zake.
Muda kidogop tu, kuna mgeni alifika kwenye ofisi ya baba Angel alimshangaa kidogo ila mgeni huyo alikuwa ni mama Sarah,
“Kheee Manka, umejuaje hapa ninapofanyia kazi?”
“Hakuna kitu ambacho mtu uamue kukigundua halafu usikigundue, hakuna hiyo kitu kabisa”
“Haya lipi limekuleta? Ni kuhusu mtoto tena?”
“Siwezi kukwambia kuhusu mtoto maana wewe kama umerogezewa na mkeo kuwa ukatae watoto wa nje wakati pia wewe ni mwanaume rijali”
“Haya, kipi kimekuleta? Mambo ya mimi na mke wangu yaache kama yalivyo”
Mama Sarah alitoa kontena dogo na kufunua, lile kontena lilikuwa na nyama ya kuchoma, pilipili pembeni na ndimu, kisha akamwambia,
“Nimekuletea nyama, najua uchu wako ulivyo kwenye nyama. Najua sijawahi fika hapa ila leo nikasema nije na kitu cha tofauti kwako kama siku yangu ya kwanza kuingia kwenye ofisi yako, karibu sana”
“Asante, mke wangu katoka hapa muda si mrefu na aliniletea chakula kizuri sana nimekula na nimetosheka, asante sana”
“Ila hajakuletea nyama ya kuchoma, una wasiwasi gani kwani? Hii ni nyama tu, unaweza ukawa unatafuna huku unaendelea na kazi zako yani unaweza fanya kama unatafuna karanga”
“Huo utakuwa ni uroho maana mimi nishashiba, ila kawape wengine wenye uhitaji”
Kisha baba Angel akachukua ule mfuniko wa pembeni na kufunika kile chakula, mama Sarah alimuangalia na kutabasamu tu kisha akamwambia,
“Ngoja nikwambie kitu Erick, kwa manufaa yako na yangu, ila sanasana manufaa yako. Mimi ni kweli kabisa niliwahi kuwa na mahusiano na mzee Jimmy, sikujua kama ni baba yako hadi pale Erica aliponiambia ukweli, roho iliniuma si utani kitendo cha kumchanganya baba na mtoto kwakweli niliumia sana, ila nilijikaza tu. Sikutaka iwe hivi ila ni katika mpangilio wa maisha tu. Ni hivi Sarah ni damu yenu haijalishi ni wako au wa baba yako ila ni damu yenu, halafu Sarah anampenda sana mwanao Erick mdogo huoni kama ni tatizo hilo? Ni laana kwa mtu kutembea na ndugu yake. Kuwa makini sana, hii ni kwa manufaa yako”
“Sawa, je Erick anampenda Sarah? Yani huyo Sarah ndio kakwambia wewe kuwa anampenda Erick?”
“Ndio, Sarah mwenyewe kaniambia jinsi anavyompenda Erick, ila Erick anamkwepa Sarah, sema huwezi jua watakapokutana vizuri”
“Hivi una akili wewe?”
“Kwanini?”
“Mtoto mdogo kama Sarah kapata wapi ujasiri wa kuja kukueleza mama yake kuwa mimi nampenda Fulani?”
“Hebu nitolee balaa hapa na wewe, Sarah ana udogo gani yule? Yupo kidato cha tatu ana udogo gani? Hata kama nilimuwahisha shule ila bado sio mdogo wa kuelewa chochote, kuna makabila huko binti akimaliza darasa la saba tu unakuta kashaolewa. Haya tuache mambo ya makabila, wewe hadi ulifukuzwa shule sababu ya mapenzi na ulikiri wazi kwa walimu kuwa unampenda sana Erica, ulikuwa na umri gani? Si ulikuwa kidato cha pili wewe? Kupenda kuna umri unadhani?”
“Sina maana kuwa hawezi kupenda, ila nakuuliza kapata wapi ujasiri wa kukwambia hayo?”
“Kwanini asiniambie, mimi ni mama yake, ni mshauri wake, ananiambia ili nimwambie kama huyo mtu anamfaa au hamfai. Nyie watu vipi lakini, hamjui kulea watoto eeeh! Unatakiwa kuweka wazi mtoto aelewe kila kitu na awe wazi kwako kwa kila kitu, unamficha ficha mtoto kila kitu unadhani hayo ndio maisha? Kwa mtoto kama Erick kutokujua chochote kuhusu uanaume wake hayo sio maisha, hebu fundisheni watoto wawe wazi kwa kila kitu. Halafu muwape watoto wenu uhuru”
“Aiseee hongera sana kwa hilo, mimi ni mwafrika na nitalea watoto wangu hivyo, nitawakataza mabaya na kuwafunza mema tu. Maswala ya kuanza kuwafundisha waniambie wanaowapenda hapana kwakweli, siwezi na sitoweza”
“Shauri yako, ila ndio nimeshakwambia hivyo akili kichwani mwako, kusuka au kunyoa. Nyama zangu umekataa. Ila nitaziacha hapa, utampa yoyote utakayejisikia”
Mama Sarah alimuaga baba Angel na kuondoka zake kwa muda huo.

Baba Angel alipotoka kazini, moja kwa moja alielekea nyumbani kwake, alifika getini na kuingiza gari yake ndani, ila akakumbuka ule mzigo wa mama Sarah aliomuachia ofisini, basi kwavile alifika nao nyumbani, akaona kuingia nao ndani kwake itakuwa balaa kwa mkewe, basi moja kwa moja alienda kumpa mlizi wao ambae alishukuru sana. Kisha baba Angel akaenda zake ndani, na kumkuta mkewe akiongea na dada yake Tumaini, basi alimkaribisha na kuongea nae mawili matatu,
“Tena bora umenikuta maana shida yangu ni wewe”
“Ipi tena hiyo?”
“Sijui tukaongee wenyewe! Au na mama Angel awepo?”
“Kwani ni kuhusu nini?”
“Ni kuhusu mama Sarah”
Baba Angel alifikiria kidogo na kuona ni vyema wakaongee na mkewe asikie kwani hapo alishasikia ni kuhusu nani, halafu asiposhirikishwa ataona kuna kitu anafichwa.
Basi wakaondoka wote watatu na kwenda kwenye bustani ambapo Tumaini aliongea kile alichoambiwa na Sia, na vile alivyokutana na mama Sarah na jinsi mama Sarah alivyosema, kwakweli baba Angel alishangaa sana na yeye ilibidi aseme tu ukweli kuhusu mama Sarah alivyofika siku hiyo ofisini kwake na kile alichokisema, yani mama Angel alishangaa sana,
“Kwahiyo Sarah anamtaka Erick? Malezi gani hayo?”
“Ndio anasema yupo kwenye malezi ya kumuweka wazi mtoto kwa kila kitu na watoto wapate uhuru”
Tumaini akasema,
“Kumuweka mtoto wazi kwa kila kitu ni vizuri ila sio wazi kwa kila kitu jamani, yani kuna wazazi hawajui uwazi unaopaswa kumueleza mtoto. Na huo uhuru kwa mtoto unapaswa kuwe na miopaka, huyo Sarah muda wote yupo na simu ndio uhuru gani ule zaidi zaidi kumfundisha mtoto tabia mbaya, mitandao yote ya kijamii Sarah yupo, anaangalia vitu vya ajabu sana, nilimkuta siku ile nilisikitika sana kwa mtoto mdogo kama Sarah kuwa makini vile na simu sikupenda kwakweli. Kama kweli Sarah ni damu yetu atupe wenyewe tumlee asituharibie mtoto wetu jamani”
Walikaa kimya kwa muda, kisha Tumaini akaongea tena,
“Yani yule mtoto Sarah anaonekana kuwa muelewa, inatakiwa tumuwahi mapema hivi maana tukichelewa itakula kwetu jamani, tunatakiwa kuwa makini sana. Ikiwezekana tumfate huyo mama Sarah tufanye nae kikao na atueleze ukweli kuhusu Sarah, nipo tayari kumlea”
Yani Tumaini alionekana kuchukizwa sana ila baba Angel na mama Angel walikuwa kimya kabisa, kisha mama Angel aliwaza kitu na kumuuliza baba Angel,
“Ulisema Manka alikuletea nyama ofisini, umeziweka wapi? Sijui ni kwanini nimewaza hili?”
“Kwakweli nimekuja nazo hadi hapa nyumbani na nimempa mlinzi wetu”
“Aaaah kwanini lakini?”
“Sasa ningeingia nazo ndani ungenielewa?”
“Sio hivyo, kuna mambo tunatakiwa kuyaepuka. Hebu kumbuka vile viatu ambavyo uliletewa na madam Oliva ofisini kwako, mimi nikavichukua na kumpelekea Steve, nini kimetokea kwa Steve sasa? Hasikii haelewi kitu ingawa anadai sio madawa yaliyomfanya ampende madam Oliva. Haya leo umeenda kumpa nyama mlinzi, kama na yeye aliweka madawa je? Ni bora ungetupa tu”
“Nilijihisi vibaya kutupa chakula”
Mama Angel akamuacha pale Tumaini na kaka yake, halafu yeye moja kwa moja alienda kwa mlinzi wao ili kumwambia kama zile nyama anazo basi ampatoe, yani alipofika pale getini ndio kwanza alimkuta mlizni akimalizia zile nyama,
“Kheee umezimaliza zote!”
“Sijui bosi kazitoa wapi, ni nzuri hizo sijapata kuona”
Mama Angel alishindwa la kuongea zaidi zaidi ya kupeleka jibu kuwa vimeshaliwa, na muda huo huo Tumaini nae aliaga na kuondoka zake huku akisisitiza swala la kufanya kikao kwaajili ya kujua hatma ya Sarah.

Usiku wa leo wakati Vaileth na Daima wamelala, simu ya Vaileth ilianza kuita na alipoiangalia akaona kuwa ni Junior ndio anapiga ile simu, akapokea na kumwambia,
“Tuma meseji nitakujibu”
Halafu akakata ile simu, muda kidogo uliingia ujumbe toka kwa Junior,
“Nimekukumbuka sana Vai wangu, nashindwa kufanya chochote sababu yako. Halafu siku hizi hapo sio pazuri tena kama zamani maana nikija tu huyo mjinga nae ananiona.”
“Pole sana, ndio maisha yalivyo”
“Wewe hujanikumbuka Vai?”
“Nimekukumbuka pia”
“Sikia, naongea na mlinzi nakuja mara moja”
“Usiku huu Junior!!”
“Ndio, nimekukumbuka sana”
Kisha ujumbe mwingine toka kwa Junior ukaingia,
“Sikia Vai, nakuja muda huu nitaongea na mlinzi na utanikuta kwenye bustani”
Vaileth aliwaza kidogo na kukosa jibu kabisa, ila vile vile alishindwa kulala mpaka pale aliposikia kuitwa na mama Angel, basi Vaileth akaiweka simu kwenye meza ya pale chumbani na kwenda alipoitwa na mama Angel.
Moja kwa moja mama Angel alienda nae kwenye chumba kile cha kumbembelezea Ester na kumwambia amshikie Ester wakati akimkorogea maziwa,
“Yani leo maziwa yangu yamekuwa machache sana, Ester hashibi kabisa, nishikie kwanza maana anapiga kelel tu chumbani halafu baba kalala”
Kwahiyo Vaileth alimshika mtoto na kuanza kumbembeleza huku mama Angel akimuandalia Ester maziwa mengine ya kopo, huku akiongea ongea na Vaileth, kwakweli Vaileth alikuwa akiitikia tu ila hata hakupenda kabisa.

Daima akiwa anajigeuza geuza tu kitandani, akasikia simu ya Vaileth ikiita pale mezani, aliinuka kuiangalia kwani muda mrefu sana alitamani kujua ni mtu gani anayewasiliana na Vaileth kila mara, alipoitazama simu aliona jina lililotokea ‘Junior’ akashtuka sana na kujiuliza,
“Kwahiyo Junior ndio anampigia huyu dada? Ili iweje?”
Akaamua kupokea bila ya kuongea chochote, alaimsikia Junior akisema,
“Njoo hapa kwenye bustani nishafika tayari”
Daima alikata ile simu na kuirudisha pale mezani, kisha alinyata na kutoka chumbani hadi kwenda kutoka mlango wa nje, hawakumgundua sababu walikuwa vyumbani pia, basi moja kwa moja Daima alienda nyuma kwenye bustani ni kweli alimkuta Junior amekaa akimsubiri Vaileth, na alipofika mwanzoni kabla Junior hajaangalia vizuri alimwambia,
“Nimekutumia meseji muuuda kuwa utoke ila mpaka nimekupigia simu ndio umekuja”
Kwakweli Daima alimtazama Junior na kuanza kulia, Junior alipomuangalia vizuri aliona ni Daima, kwakweli Junior alishtuka kwani hakutegemea, basi akamkwepa ila Daima alikuwa akimfata kwa kilio,
“Wewe Daima, hebu nyamaza huko, mambo gani haya unataka kufanya?”
Daima akamdaka Junior kwa nguvu na hakutaka kumuachia, alitaka Junior amwambie ukweli kuwa kamuita Vaileth wa kazi gani,
“Niambie ukweli Junior, una mahusiano na yule dada wewe, muda wote unawasiliana nae”
“Hamna mimi huwa nawasiliana nae kuhusu wewe”
“Hamna usinidanganye Junior ni mpenzi wako”
“Niachie bhana Daima”
“Sikuachii Junior, nataka watu wote humu ndani wajue sababu ya wewe kunikataa mimi. Kumbe ni sababu ya huyo mdada!”
Akamshika kwa nguvu, Junior akajitahifi kutoka ila wapi, ndipo Junior alipoamua kumnasa kofi mbili za nguvu Daima hadi mwenyewe alimuachia na kuanza kupiga kelele kwa nguvu sasa, Junior alikimbia na kutoka nje ya geti kisha akamwambia mlinzi kuwa amfichie siri.
Kelele zile za Daima ziliwashtua wote mule ndani, kaisi kwamba wote waliamka, na kukimbilia bustanini ila Vaileth hakukimbilia bustanini moja kwa moja kwani alikimbilia chumbani kwake, na kuchukua simu yake akakutana na ujumbe toka kwa Junior,
“Futa meseji zetu zote, futa namba yangu ya simu, futa kila kitu. Sitaki jambo hili lijulikane kwa muda huu”
Yani Vaileth alikuwa akitetemeka na kufuta kila kitu kisha akaiacha simu pale mezani na yeye kutoka nje kujua kuna nini, alimkuta baba Angel na mama Angel ndio wamemzunguka Daima, ila Erick na Erica nao hata hawakutoka, basi Daima alikuwa akiulizwa kilichomtoa nje na kumpigisha kelele,
“Ni Junior alikuwa mahali hapa”
“Junior!! Alikuja kufanya nini?”
“Mama na baba, naomba mjue kuna kitu kinaendelea kati ya Junior na huyu dada humu ndani”
“Kivipi?”
Daima alianza kuelezea ilivyukuwa hadi simu ya Junior aliyopokea toka kwenye simu ya Vaileth, walishangaa na kumuangalia Vaileth, muda huo huo mama Angel alimshika mkono Vaileth na kumwambia,
“Twende ukanipe simu yako niangalie”
Vaileth alienda nae hadi ndani na mama Angel alichukua simu ya Vaileth ila hakuona hata namba ya Junior, basi alimuangalia Vaileth na kumuuliza,
“Umefuta?”
“Muda gani mama?”
“Mbona ulichelewa kutoka wakati kuna kelele?”
“Nilikuwa namlaza vizuri mtoto mama, sijafuta chochote hata nashangaa tu”
Mama Angel alitoka tena nje na moja kwa moja kwenda kwa mlinzi na kumuuliza,
“Eti Junior alikuja leo?”
“Junior? Hapana, hajaja Junior leo”
Moja kwa moja mama Angel alihisi kuwa Daima atakuwa na matatizo, alirudi na kumwambia mumewe amuache tu yeye na Daima,basi mumewe alienda zake chumbani kuendelea na usingizi, mama Angel alikaa kidogo na Daima na kumwambia,
“Unampenda sana Junior eeeh!!”
“Ndio nampenda sana”
“Haya nenda kalale kwanza, halafuy kesho tutawasiliana vizuri”
Basi mama Angel aliingia ndani na Daima na kufunga mlango vizuri maana alihisi kuwa Daima hayupo sawa kwenye kichwa chake.
 
SEHEMU YA 353

Kulipokucha, wakina Erick walijiandaa na kwenda shuleni yani wao hata hawakuelewa chochote kile ambacho kiliendelea usiku, basi mama Angel na baba Angel waliongea kidogo kuhusu Daima,
“Naona tumrudishe kwa wazazi wake”
“Hata mimi naona hivyo, tutawaita tu tuongee nao vizuri maana huyu ameanza kuchanganyikiwa jamani”
“Ni kweli mke wangu, ngoja nijiandae niende kazini”
“Badae nitakuja huko, leo nitakuletea chakula pia. Tafadhari usile popote pale nakuomba”
“Naelewa mke wangu, siwezi kula sehemu yoyote ile”
Baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kuelekea kwenye kazi yake, muda huu mama Angel aliendelea na mambo mengine ila alichogundua siku hii ni kuwa Daima hakuweza hata kula alikuwa akilia tu kwa muda mwingi, basi alimfata kuongea nae,
“Daima, tatizo ni nini jamani?”
“Inaniuma sana, kuona Junior amenikana sababu ya huyu dada humu ndani na hakuna mtu anayenielewa. Huyu dada anatembea na Junior”
“Unajua nini Daima, mara nyingine uwe na ushahidi na unachokiongea, tupo hapa na Vaileth toka mwaka jana, na tumeishi nae vizuri kabisa, hawezi kufanya ujinga kama huo. Hebu shusha presha au unataka tukurudishe kwenu?”
“Hapana, msinirudishe nyumbani”
“Haya, kula chakula basi”
Yani Daima alienda kulak wa kujivuta vuta tu sababu hata hakutaka, mama Angel aliendelea na mambo mengine.
Ila kuna simu ikaingia kwake, na alipopokea alikuwa ni mama yake na Derrick akimwambia kuwa hali ya afya ya Derrick imebadilika kwa muda huo,
“Naomba mwanangu uje, hata sijui cha kufanya”
“Ila madaktari si wapo kumuhudumia mama?”
“Wapo ndio ila hali ya Derrick ni mbaya sana”
“Sawa nakuja huko”
Mama Angel ilibidi aweke mambo yake sawa na muda huo huo akajiandaa na kuondoka zake kuelekea hospitali.

Kama ambavyo walipanga, Sarah na Elly walitoka shule muda huo ambapo Sarah ndio aliomba ruhusa na hawakuweza kumkatalia kwahiyo waliondoka na moja kwa moja Sarah alimtaka Elly waende nyumbani kwao na wakina Elly kwanza ili wakabadilishe nguo, basi walienda na Sarah alivaa nguo zingine alizozibeba kwenye begi, halafu Elly nae ikabidi abadilishe nguo na kuondoka na Sarah.
Elly alikuwa akimuuliza Sarah,
“Tunaenda wapi lakini?”
“Ni mahali Fulani hivi, nataka nikachome sindano ya uzazi wa mpango, nahitaji waone kuwa mimi ni mkubwa maana nitawaambia kuwa wewe ni mdogo wangu. Halafu wewe useme umemaliza kidato cha nne sio kuniletea mambo yako ya kitoto toto”
“Mmmh, sindano ya uzazi wa mpa ngo Sarah! Ili iweje?”
“Ili iweje? Si ili nisipate mimba? Au unataka nipate mimba?”
Elly alitulia na kuendelea na ile safari, na kweli walifika kwenye duka moja kubwa la madawa ambapo kwa upande wa duka hilo walikuwa wakitoa huduma hiyo, Sarah alijiandikisha kuwa ana miaka kumi na nane, na alimdanganya vitu vingi yule nesi,
“Mara ya mwisho kuona siku zako ilikuwa lini?”
“Aaaah ni juzi tu hapo”
“Aaaah basi, hapo sawa”
Basi yule nesi alimchoma sindano Sarah bila kuzingatia vitu vingine.
Muda huu Elly alikuwa nje akihofia kiasi yani hakuelewa cha kufanya na kujikuta akiinuka na kuanza kuondoka.

Mama Angel alifika hospitali na kuangalia hali ya Derrick kweli ilionekana kubadilika, na alikuta mama Derrick kuna dawa kaandikiwa kuwa akamnunulie Derrick, kwahiyo muda huo huo mama Derrick alimkabidhi mama Angel lile karatasi la dawa, basi mama Angel aliondoka na kwenda kununua hizo dawa.
Alipotoka kununua dawa, alishangaa kumuona Elly, basi alimsimamisha na kumtaka aondoke nae, ambapo Elly alipanda kwenye gari ya mama Angel basi akaanza kumuuliza,
“Muda huu wa masomo, wewe unafanya nini huku?”
“Aaaah kuna rafiki yangu nilimsindikiza kununua dawa?”
“Yuko wapi na anaumwa nini?”
“Aaah….aaaah….hapana, ni mimi ndiop naumwa”
“Mbona unajiuma uma sana”
Elly alishindwa kumjibu mama Angel, walifika hospitali na mama Angel alisimamisha gari, ila alishuka na Elly kwani alijikuta kuwa na maswali mengi ya kumuhoji huyu kijana, alikumbuka alichokifanya Tumaini kwa Daima, kwahiyo aliona ni vyema na yeye kuuliza vizuri kuhusu elimu ya huyu kijana.
Moja kwa moja aliingia nae kwenye wodi aliyolazwa Derrick na kusogea kwenye kitanda cha Derrick, ila Elly kwa ile hali ya Derrick aliyoiona ilimfanya asikitike sana na kujikuta akitoa machozi huku akimsogelea Derrick kitandani. Machozi ya Elly yalianguka kwenye kiganja cha mkono cha Derrick cha kushangaza Derrick alifumbua macho na kutabasamu.

Moja kwa moja aliingia nae kwenye wodi aliyolazwa Derrick na kusogea kwenye kitanda cha Derrick, ila Elly kwa ile hali ya Derrick aliyoiona ilimfanya asikitike sana na kujikuta akitoa machozi huku akimsogelea Derrick kitandani. Machozi ya Elly yalianguka kwenye kiganja cha mkono cha Derrick cha kushangaza Derrick alifumbua macho na kutabasamu.
Na muda huo huo Derrick aliyekuwa akihangaika mwanzoni pale kitandani aliweza kukaa halafu akamkumbatia Elly, yani kila mtu alikuwa akishangaa pale kuwa ni kitu gani, Derrick alimkumbatia Elly huku machozi yakionekana kumtoka tena yalikuwa ni machozi ya furaha maana yalimtoka huku akicheka, mama Derrick pamoja na mama Angel walikuwa pembeni tu wakishangaa kile ambacho kimetokea.
Kisha Derrick alikaa vizuri pale kitandani sasa yani kwa kuishusha miguu yake chini huku akimtaka Elly akae pembeni yake ambapo Elly alifanya hivyo.
Mama Derrick aliamua kumuuliza Derrick,
“Nini kimekutokea mwanangu?”
“Mama, kwa hakika nimepona kabisa”
“Inaonekana kweli umepona ila nini kimekutokea?”
Muda huo alifika daktari pia aliyekuwa akishangaa kuona hali ya Derrick ikiwa imetengemaa vile, na Derrick aliomba aandikiwe ruhusa aende nyumbani, basi daktari alijaribu kumuangalia kidogo pale hakuona kama ana tatizo lolote, kwahiyo alimuandikia tu ruhusa, na muda huo Derrick aliomba waondoke wakiwa wameongozana na Elly.
Basi mama Angel ikabidi ndio awarudishe nyumbani kwakina Derrick sababu bado alikuwa akijiuliza sana ni kitu gani kimetokea baina ya Derrick na yule mtoto Elly? Hakuelewa kabisa.
Waliondoka hadi nyumbani, ila muda wote Derrick alionekana akimuangalia sana Elly, mpaka wanaingia ndani hakuna aliyekuwa anamuelewa Derrick, ila kabla ya yote walipoingia tu mama Derrick alihitahi kujua kilichokuwa kimetokea, ni kweli kafurahi kwa mwanae kupona, ila alitaka kujua ni kitu gani kimetokea, basi Derrick aliakaa na kuanza kuwaambia,
“Nilikuwa naumwa sana, nilikuwa na hali mbaya sana ila muda wote niliokuwa kitandani nilikuwa naletewa picha ya huyu mtoto, yani ndio picha halisi iliyokuwa ikinijia, kuna muda nilipata ndoto kuwa atafika na kuangusha machozi yake kwenye kiganja changu. Sijawahi kumuona huyu mtoto, ila nazungumza kwa uhakika kabisa, huyu ni mwanangu, sijui mama yake kama ni Oliva au Manka ila huyu ni mwanangu”
Mama Derrick na mama Angel waliangaliana bila ya majibu, kisha mama Derrick alimuuliza mama Angel,
“Kwani wewe umemtoa wapi huyu mtoto?”
“Namfahamu huyu, tena namfahamu vizuri sana, sasa leo nilikuta mahali na ni muda wa shule ndiomana nikamchukua kuongozana nae ili nimuulize kwanini hayupo shule na ni muda wa shule? Maana nilijifunza kitu mtoto wa mwenzio ni mtoto wako pia, kwahiyo nilitaka nimuhoji vizuri sababu namfahamu”
Kisha mama Angel alimuangalia Derrick na kumwambia,
“Ila mbona huyu mtoto sio wa Oliva wala wa Manka, ni wa mtu mwingine kabisa”
“Sijali, ila ninachojua ni kuwa huyu ni mwanangu”
Derrick alimuangalia Elly na kumuuliza,
“Kwani baba yako mzazi yuko wapi? Na kwanini ulitoa machozi kwangu pengine hiyo itasaidia hawa kuamini kuwa wewe ni mwanangu”
Yani Elly alikuwa kama kapigwa na butwaa vile, basi akasema,
“Mimi sina baba, mama aliniambia kuwa baba alikimbia kipindi nimezaliwa tu. Halafu mimi nilipokuona sijui hata imekuwaje ila nilijikuta tu nikitokwa na machozi na kukusogelea karibu”
“Unaona? Wewe ni mwanangu, hata mama yako anatakiwa atambue kuwa wewe ni mwanangu, mwambie mama yako kuwa nimemuona baba yangu”
Mama Angel akapumua kidogo na kumuuliza Derrick,
“Unamjua mama wa huyu mtoto lakini?”
“Hata awe nani lakini huyu ni mwanangu, na nimefurahi kumuona kabla ya kifo changu. Naomba mtoto kwa leo au kesho uniletee mama yako hapa nimfahamu”
Mama Angel alishindwa kabisa kuongea na muda huo akamwambia Elly kuwa aondoke nae tu waende kwa huyo mama yake ili kumueleza yaliyojiri, yani Derrick hakutamani hata yule mtoto aondoke, na alimuomba mama Angel amletee tena yule mtoto kwani ni mtoto wake, kwakweli mama Angel hakuwa na usemi zaidi kwani alihisi huenda Derrick ameanza kuchanganyikiwa.

Basi mama Angel aliondoka na Elly na moja kwa moja walienda nae kwenye biashara ya Sia, kwakweli Sia alishangaa kumuona mama Angel yupo pamoja na Elly basi aliwafata na kumwambia mama Angel,
“Naona sasa umekubali kuwa Elly ni damu yenu?”
“Dah! Wewe jamani, kumbe huyu Elly ni mtoto wa Derrick”
“Wa Derrick kivipi? Kwanza Derrick gani?”
“Yule ndugu yangu”
“Yule tapeli? Mimi nikazae na tapeli nina kichaa au ni kitu gani?”
Mama Angel akamueleza vile ilivyokuwa hadi kusema kuwa Elly ni mtoto wa Derrick, hata ile habari Sia nae ilimchanganya kidogo ila akasema,
“Haiwezekani hiyo, tena haiwezekani kabisa, huyu mtoto sio wa huyo tapeli ila ngoja nifanye uchunguzi wangu”
Mama Angel alimuangalia kisha akamuangalia Elly na kumwambia,
“Natumai unatufahamu ndugu zako sasa, unafahamu wazi baba yako alipo”
Halafu mama Angel aliondoka zake na kumuacha Sia akiwa na mawazo mengi sana.

Muda huu nyumbani kwa mama Angel kulikuwa na mzozo kati ya Vaileth na Daima maana Daima hakutaka kukubali kwakweli, aliona ni wazi kuwa Vaileth anatembea na Junior halafu anajigelesha, basi alimfata alipokuwa na kuanza kumwambia kwa shari kamavile anataka kupambana nae,
“Mwanamke mtu mzima kama wewe huoni haya kutembea na mtoto mdogo kama Junior”
“Kutembea nae kwenda wapi?”
“Unajifanya huelewi au? Unaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Junior? Wadanganye wengine humu ndani ila sio mimi niliyeona simu yako”
Daima aliongea sana kama kumkujeli Vaileth, ndipo Vaileth alipomwambia,
“Unajua Daima, wewe ni mdogo sana kwangu halafu ukizingatia na hiyo mimba unatakiwa utulie na ulee mimba usubirie kuzaa. Halafu kuhusu mimi kuwa na mahusiano na Junior kwani wewe inakusumbua nini ikiwa Junior alitamka mbele ya watu wote hapa kuwa hakutaki tena!! Halafu mimi na mwanamke, na Junior ni mwanaume kwahiyo tukiwa pamoja tatizo ni kitu gani?”
“Hivi una akili timamu wewe mdada au umepagawa, yani unajisifia kabisa na uanaona sawa kwa wewe kutembea na Junior?”
“Sioni tatizo ndio”
Daima akachukia sana na kumvamia Vaileth mwilini maana alitaka kupigana nae, kwa bahati nzuri mama Angel nae alikuwa karidi muda huo na kuwaamulia huku akimsema Vaileth,
“Jamani Vai, wewe ni mkubwa wa kutosha tu. Hivi ukapigana na mtu kama Daima kweli?”
“Mama, mimi sikuwa nikipigana nae ila ni yeye ndio alikuja kunivaa mimi.”
“Tatizo ni nini kwani?”
Mama Angel akawakalisha chini ili wamuelezee tatizo ni nini hadi kupelekea wao kupigana namna ile, Daima alianza kuelezea,
“Mama, nadhani ile usiku hamkunielewa. Nampenda sana Junior, ni kweli hii mimba ni ya Junior ila Junior kanikataa mimi sababu ya huyo mdada huyo, huyu Vai ana mahusiano na Junior na kwangu kakubali wazi kabisa”
Mama Angel akamuangalia Vaileth na kumuuliza,
“Eti Vai ni ya kweli haya?”
“Mama, hata mimi nabaki kushangaa tu hapa, sijui huyu msichana ana matatizo gani jamani yani sielewi kabisa, Junior alikuwepo hapa siku zote kama kuwa nae si ningekuwa nae jamani! Mimi sina mahusiano na Junior”
Daima akadakia,
“Sema ulichokuwa ukiniambia mimi kuwa Junior ni mwanaume na wewe ni mwanamke kwahiyo lazima muwe pamoja”
Basi mama Angel akawaambia,
“Sitaki mzozo jamani, sitaki mzozo kabisa. Muda umeenda sasa ila nadhani kabla ya muda wa kulala kufika tutakuwa tumepata suluhisho, ila sitaki mzozo wowote kuendelea”
Basi moja kwa moja, mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake tu kwa muda huo.

Mama Angel aliingia chumbani kwake yani kwa matukio ya siku hiyo alijikuta kichwa chake kikiwa kimejawa mawazo tu yasiyokuwa na majibu mwanzo hadi mwisho, kwanza alifikiria kuhusu mtoto Elly, akafikiria kuhusu Sia akidai kuwa Erick ni mwanae, pia akafikiria yaliyotokea kwa Derrick siku hii,
“Mmmh hivi Sia hakuwa na mahusiano na Derrick kweli, nina mashaka nae maana hata haeleweki”
Muda kidogo baba Angel nae alirudi kutoka kazini na kumkuta mke wake pale nyumbani, basi alimuuliza ni kwanini hakwenda kazini kwake siku hiyo, mama Angel alimsimulia yote ambayo yametokea siku hii, yani baba Angel alibaki akistaajabu na kushangaa sana,
“Kwahiyo Derrick amepona baada ya kumuona Elly”
“Ndio hivyo”
“Halafu Derrick anadai kuwa Elly ni mtoto wake?”
“Yani hapo ndio kwenye utata maana Sia anakataa katakata kuwa kwenye mahusiano na Derrick, sasa ni kivipi Derrick adai kuwa Elly ni mtoto wake?”
“Ila mke wangu nawe umesahau akili za Sia zilivyo? Anaweza kukataa kumbe kweli, na ukweli wote utakuta anaujua kuwa alikuwa na mahusiano na Derrick hadi kumzaa Elly, hivi unasahau alivyokuwa anazusha hapa kuwa Erick ni mwanae! Tena anakomaa kabisa na kukazana hadi mtoto akakosa imani na raha, akamaliza hayo akaanza kukazana kuwa Elly ni mtoto wangu hadi kwa mama habari ilifika, yule Sia ni mgonjwa wa akili kwahiyo usimuamini moja kwa moja, kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa alizaa na Derrick”
“Je Steve ni vipi?”
“Mke wangu, yule Sia haeleweki ujue, ukimuwaza sana utapata kichaa bure, cha muhimu siku tumshikilie na atuambie ukweli. Ila kama Derrick anasema yule ni mtoto wake huenda ikawa kweli, ujue damu ni nzito kuliko maji eeeh! Ndiomana huyo Elly na Derrick wamejikuta tu wameweza kuungana, hizo habari tuziache kwanza ila tutajua tu ukweli wa mambo”
“Sawa, mume wangu sasa kuhusu Daima ndio kuna balaa”
“Kafanyaje tena”
Mama Angel akamsimulia jinsi ambavyo alikuwa akitaka kupigana na Vaileth,
“Khaaa huo ni ujinga, tena ni ujinga sana hebu wapigie simu wazazi wake waje wachukue mzoga wao, anataka mimba imtoke hapa halafu iweje kwetu!”
“Ndio hapo sasa”
Basi mama Angel alichukua simu na moja kwa moja alimpigia baba Daima ila aliyepokea simu alikuwa ni mama Daima, alisalimiana nae na kuongea nae,
“Samahani, huyu mtoto wenu mje mumchukue maana hapa anataka kuleta balaa, au kama hamuwezi kuja basi mimi nimlete”
“Aaaah usimlete kwanza, ngoja baba yake atawapigia simu akirudi. Siwezi sema chochote, baba yake ndio ataamua kitu gani kiendelee”
“Mmmh haya”
Mama Angel alikata ile simu na kuongea kidogo na mume wake, kisha kumwambia kuwa anaenda kumuandalia chakula kwa muda huo.
“Unajua nataka chakula gani leo?”
“Eeeh nikuandalie nini?”
“Usisumbuke sana mke wangu, niandalie tu ugali na samaki, nitafurahi sana kwani sijala siku nyingi chakula hiki”
Basi mama Angel alienda kuandaa kile chakula, na kilivyoiva walikaa wote mezani na kula kile chakula, kasoro Daima hakutaka chakula kile kwahiyo alipika anachokipenda na kukaa pale kuanza kula, hawakuwa na tatizo nae sana kwani wanaelewa jinsi gani mimba zinavyosumbua, ila yeye mwenyewe alianza kusema,
“Nikiwa mzima tu huwa sipendi kula ugali na huwa siupendi kabisa ugali, halafu na hali hii ndio nikale ugali kweli!! Hapana aisee hiko chakula sikipendi kabisa”
“Kwanini hupendi ugali?”
“Huwa nakiona kama ni chakula cha kimasikini, yani mimi hakinipi ladha kabisa”
Mama Angel hakumuhoji zaidi kwani yale majibu yalimtosha kabisa na kumfanya asiendelee kumuhoji.
Walimaliza kula, na kila mmoja kwenda moja kwa moja kwenye vymba vyao vya kulala tu.

Usiku ule kwakweli Vaileth alishindwa hata kulala mule chumbani kwani kidogo tu alikuwa akitupiwa maneno na Daima, yani aliona kama ule usiku ni mbaya sana kwake, na hakuweza kubishana na Daima kwavile alihofia ile hali ya mimba aliyokuwa nayo.
Basi Vaileth kwa kuepusha shari, kwa muda huo aliamua kwenda tu sebleni na alilala sebleni kwa siku hiyo. Aliamka mapema sana na kuanza usafi kwani hakutaka wajue kuwa alilala sebleni kwa siku hiyo, yani kwakweli uwepo wa Daima ulikuwa ukimkosesha raha kabisa na alijikuta hana furaha hata kidogo.
Wakina Erica walitoka pale na kwenda shule kama kawaida, baba Angel nae alitoka ila siku hii alimwambia mkewe kuwa asimpelekee chakula sababu atawahi kurudi nyumbani tu.
Kwahiyo mama Angel alikaa tu nyumbani, ila akakumbuka kitu kuwa mama Daima alisema kuwa baba Daima angepiga simu usiku wa jana ila hakupiga simu kabisa, basi aliamua tena kuchukua simu asubuhi ile na kuwapigia,
“Inamaana hukunielewa au kitu gani? Huyu mtoto wenu inatakiwa arudi kwenu kama mimba tutalea huko huko akiwa kwenu”
“Si nilikwambia baba yake atakupigia simu!”
“Hakupiga sasa”
“Basi subiri tu atakupigia tu, kwani unaharaka na kitu gani jamani!”
Mama Daima alikata simu, kwakweli mama Angel alichukia sana kwa majibu ya mama Daima kwani walionekana ni watu wasiojali kabisa.

Leo baba Angel alitoka mapema kazini kwake kama alivyopanga ila kabla ya kwenda nyumbani aliamua kwenda kupitia mahali kumchukulia mke wake zawadi, basi aliamua moja kwa moja kwenda katika lile duka ambalo huwa anamnunulia zawadi mama Angel ila leo alikuwepo mama Emma tu, kwani mumewe hakluwepo,
“Kheee jamani, ukatukimbia kabisa”
“Aaah nilisafiri ndiomana sikuonekana, na mumeo yuko wapi?”
“Nae kasafiri, hata hayupo wala nini”
“Aaaah kumbe!!”
“Nimekuja kumchukulia mke wangu zawadi tena leo”
“Nitamchagulia zawadi nzuri kabisa, na hakika ataipenda sana”
Basi mama Emma alimchagulia viatu, na baba Angel alipoviangalia aliona kweli ni vzuri na vitamfaa mke wake, moja kwa moja akakubali kufungiwa viatu vile na kurudi navyo nyumbani.
Alifika pale na kula kwanza, halafu alipoingia chumbani akamwambia mke wake,
“Leo nataka usiku tutoke, tutaenda kula pamoja chakula cha usiku hotelini”
“Familia nzima?”
“Familia nzima ya kazi gani? Hii ni mimi na wewe tu mke wangu, hii ni kwaajili yetu tu. Natamani sana tuwe tunakumbuka mapenzi yetu siku zote za maisha yetu”
Mama Angel alifurahi sana, ilivyofika jioni wakati watoto wamerudi, alienda kuongea na Erica kwaajili ya kumuachioa mtoto na baada ya hapo alimuandalia mtoto maziwa na kila kitu kisha alienda kujiandaa, ila alipomaliza kujiandaa ndipo mumewe akamtolea vile viatu, basi mama Angel alifurahi na kumshukuru mumewe pale halafu akavijaribisha na kutembea navyo kidogo tu, mumewe akamwambia,
“Hivyo viatu ndio utavivaa tunapotoka leo”
“Mmmh mume wangu, naomba unisamehe ila viatu hivi vinanibana”
“Vinakubana? Mbona ni namba yako kabisa hii!”
“Hata mimi nashangaa mume wangu, ila vinanibana”
Basi baba Angel hakutaka kumlazimisha mkewe kuvaa viatu vinavyombana, zaidi zaidi alimchagulia viatu vingine na akavivaa viatu hivyo na kufurahi kwa pamoja tu.

Kwenye mida ya saa moja usiku, mama Angel na baba Angel walitoka zao na kuwaacha pale nyumbani, wenyewe moja kwa moja walienda kwenye hoteli na kuanza kuongea kidogo kisha waliagiza chakula na kuanza kula huku wakiongea,
“Huoni raha mke wangu, tukipata muda kidogo na kutoka kuja sehemu kama hii tukiongea na kukumbuka mapenzi yetu yalivyokuwa”
“Huwa nafurahi sana, sababu sisi tunapendana kila siku, tunaletewa chokochoko, maneno mbalimbali ila bado tunapendana kwakweli Mungu ni mwema sana katika maisha yetu na anatufanya tuzdidi kupendana sana”
“Ndio, sio sababu tuna watoto basi muda wote ni kukaa nyumbani na watoto, muda mwingine tunakuwa peke yetu kama hivi, tunazidi kuweka mapenzi yetu kwenye viwango vingine”
Basi wakati wanaendelea na maongezi, simu ya mama Angel iliita na kuangalia mpigaji alikuwa ni baba Daima, basi alipokea na kuanza kuongea nae,
“Nimepata habari mnasema kuwa tuje kumchukua mtoto wetu?”
“Ndio mje mumchukue Daima, kwakweli siwezi kuendelea kuishi nae nyumbani”
“Hilo haliwezekani kabisa, yule mtoto kapewa mimba na kijana wenu. Tumejadiliana hapa kama familia tunasema kuwa hilo haliwezekani yani tunachongoja hapa ni nyie kuleta posa na kumchukua jumla”
“Hivi una akili kweli?”
“Ndio nina akili kwani unadhani mimi ni chizi”
“Unajua kama unaongea kama unatapika, huyu ni mtoto wenu”
“Kuongea kama kutapika ndio kuongea vipi? Ni mtoto wetu ndio ila kapewa mimba na kijana wenu, au tufungue kesi na kijana wenu aende miaka thelathini jela”
“Kwa uanafunzi gani aliokuwa nao Daima? Yani ajineng’eneshe huko halafu useme utamfunga kijana wetu miaka thelathini jela, fungua hiyo kesi ila uje kuchukua mtoto wako huku”
“Siji kumchukua, na tunasubiri posa tu. Huyu kijana wenu atake atamuoa Daima, asitake atamuoa Daima, mimi sio kama wazazi wengine ambao watoto wao wanazalishwa na vidume halafu wao wanatulia tu. Huyo mtoto mtaoa mtake msitake”
“Ndiomana nikakuuliza una akili kweli wewe?”
“Nisingekuwa na akili ungeweza kukubali niwe mwanaume wako wa kwanza”
Hii kauli ilimshtua baba Angel maana simu ilikuwa kwa sauti kubwa, baba Angel alichukua ile simu na kumwambia baba Daima,
“Naona unataka kunipanda kichwani sasa, kwaheri”
Akakata ile simu na kumwambia mkewe,
“Ujinga wa namna hii huwa siupendi kabisa, haya ni matztizo kabisa ujue, ukoo hausogei yani unazunguka hapo hapo, inakuwaje huyu Junior akatembee na mdada ambaye ni mtoto wa mtu wako wa zamani! Yani ukoo hausogei mwisho wa siku tunapata matatizo tu”
“Nisamehe kwa hilo, ila ukoo wetu hausogei toka mwanzo, fikiria mimi nimeoana na wewe, Tumaini kaolewa na Tonyo wakati huo Tumaini ni dada yako upande wa baba halafu Tony ni kaka yangu, tunakuja upande wa Dada Bite, kaolewa na Deo. Wakati Deo ni kaka wa Tumaini kwa mama yake halafu Dada Bite ni dada yangu, yani ukoo hausogei kweli hata ukienda kushtaki unaenda kushtaki wapi ikiwa kila mmoja atajifanya anakufahamu sana”
“Ni muda wa kusogeza ukoo wetu, huyu Daima tunamfuta kwani kubeba mimba ni kitu gani? Wangapi wanazalia kwao huko? Kama kweli mtoto wetu tutalea kama si kweli watalea wenyewe, ila Daima wao tunamrudishia”
“Ila weka akilini kuwa inasemekana Junior ana mahusiano na Vaileth, kama ni kweli je inakuwaje? Utawabariki waoane?”
“Aaaah watajijua wenyewe, ila hata hivyo Vaileth si wa ukoo wetu. Yani habari za huyo baba Daima zimenichanganya kidogo, kwani si ndio ndugu wa Rahim huyo? Nakumbuka vizuri sana”
Mama Angel aliangalia chini na kuamua kubadilisha mada ingawa baba Angel alikazana na msimamo wake kuwa atakaporudi nyumbani kwake basi atamrudisha Daima kwao.

Huku nyumbani, Erica alimbeba mtoto Ester moja kwa moja hadi chumbani kwa kaka yake na kuanza kuongea nae,
“Umeona Ester alivyomzuri, halafu kafanana sana na mimi hadi raha”
“Si amefanana na mama huyu, halafu na wewe umefanana na mama, ila unajua sana kulea mtoto hongera”
“Asante, napata ujuzi ili miaka ijayo na mimi niweze kulea mwanangu”
“Utakayezaa na nani?”
“Na mume ambaye Mungu atanijaalia”
“Mmmmh!! Ila mimi bado nipo na msimamo wangu ule ule, sijui kama katika maisha yangu nitakuja kuoa yani sijui kama nitakuwa na mke”
“Kwanini Erick huwa unasema hivyo?”
“Sababu nimpendae hawezi kuwa mke wangu kamwe”
“Kwanini? Unampenda nani kwani Erick?”
“Unataka kunisaidia kumpata?”
“Unadhani nitakusaidia umpate? Ndio kwanza nitafanya kila jitihada usimpate”
“Kwanini?”
“Nasikia wanaume wakianza maswala ya mapenzi wanasahau ndugu zao na kuthamini wanawake zao, yani mwanaume anaweza hata kumkana mama yake au dada yake, si unamuona Junior anavyomsumbua mama yake sababu ya mapenzi! Yani nikimjua huyo mwanamke nitafanya juu chini usimpate”
Erick alicheka na kumuuliza tena,
“Kwahiyo unataka nimpende nani?”
“Usimpende yeyote zaidi yangu mimi”
“Khaaaa, wewe nakupenda ndio ila wewe ni ndugu yangu tena ni pacha wangu. Natakiwa nikitaka kuwa na mahusiano niwe na mwanamke ambaye si ndugu yangu ila nyie ndugu zangu nitaendelea kuwapenda tu kama kawaida”
“Mmmmh kwahiyo unataka kusema unampenda nani ambaye hutoweza kumuoa?”
Erick akacheka na kutaka kusema neno, ila wakasikia mzozo sebleni, ni mzozo kati ya Vaileth na Daima, ikabidi waende na kukuta hawa watu wakipigana, tena Daima akionekana kuwa na hasira sana kwani ndiye aliyekuwa akimshambulia Vaileth, basi Erick aliamua kuwatenganisha sababu Erica alikuwa kashika mtoto ila kule kutenganisha hakukusaidia kitu kwani kidogo Daima aliponyoka kwenye mikoni ya Erick na kumvaa tena mwilini Vaileth na kuanza kumpiga, ila Vaileth aliogopa kupigana nae ili kuepusha matatizo kwani alijua wazi kwa tatizo la yule akipigana nae anaweza kuzua tatizo zaidi, Erick akamshikilia Daima, muda huu Daima alijitahidi kujitoa kwa Erick alishindwa, sasa kilichofatia ni kuanza kutukana, aliwatukana matusi kama wanaoga vile, na ile nyumba hawakuzoea matusi, kitendo hiko cha Daima kutukana kilimchukiza sana Erick, hivyobasi Erick alijikuta akimzaba Daima vibao viwili vya nguvu huku akimwambia,
“Nyamaza, usituletee ujinga humu ndani”
Muda huo huo wazazi wao nao waliwasili kwahiyo waliona Erick alivyomzaba vibao Daima, basi Daima alikaa chini na kuanza kulia huku akisema kuwa nyumba yote ile yani Erick, Erica na Vaileth wamemchangia na kuanza kumpiga, baba Angel hakutaka kusikiliza zaidi kwani muda ule ule alimwambia Vaileth akalete nguo zote za Daima, basi Daima alianza kuomba msamaha pale kuwa abaki,
“Hapana huwezi kubaki hapa ,si salama tena kwako kwa hali yako hiyo. Usituletee balaa”
“Naomba mnisikilize basi”
“Tukusikilize nini, kama wamekuchangia wote na kukupiga si balaa hilo!! Sitaki matatizo mimi”
Vaileth alileta zile nguo za Daima na muda huo huo baba Angel alimchukua Daima na kuondoka nae kwani aliamini kuwa Daima anapafahamu kwao kwahiyo atamuonyesha tu, hakutaka kwenda na mke wake kwani aliona ni vyema kwa mke wake kukaa na mtoto wao mdogo ambaye wamemuacha muda kidogo.
Basi mama Angel alibaki pale na kuanza kuuliza vizuri ambapo Erica alimuelezea jinsi Daima alivyokuwa akitukana,
“Sitaji hayo matusi mama maana na mimi nitakuwa nimetukana, ila hafai kabisa huyu mtu”
Basi walikuwa wakiongea tu pale huku mama Angel akimngoja mumewe arudi kwanza ndipo waweze kwenda kulala.
 
SEHEMU YA 354

Baba Angel aliondoka na Daima huku akimtaka amuelekeze wanapoishi, basi Daima alienda nae na kumuelekeza sehemu nyingine kabisa, na walipofika alidai sio hapo na kumuelekeza sehemu nyingine na muda ule ulikuwa ni usiku yani hadi baba Angel alichukia sana na kuanza kumfokea,
“Una matatizo gani wewe binti, kwanini uananizungusha hivi mtu mzima kama mimi? Hebu acha ujinga huko nionyeshe kwenu nikupeleke la sivyo nakuacha popote”
Daima akamuelekeza sehemu nyingine baba Angel, walienda na kufika hiyo sehemu, kisha Daima alimuonyesha nyumba ambayo wanatakiwa kuingia, basi wakashuka kwenye gari maana baba Angel alitaka amkabidhi huyu binti kwa wazazi wake kabisa.
Kabla ya kuingia kwenye hiyo nyumba, baba Angel alishtuka kidogo kwani mbele ya ile nyumba paliandikwa pembezoni yake, ‘LODGE’
Baba Angel alishtuka sana na kumuangalia Daima kwa hasira,
“Yani wewe mjinga unanileta Lodge?”
Baba Angel kwa hasira akamnasa kibao Daima, muda huo Daima alianza kupiga kelele nyingi,
“Ananibaka, ananibaka”
Watu wa karibu walifika eneo lile na kuanza kumshangaa baba Angel.


Kabla ya kuingia kwenye hiyo nyumba, baba Angel alishtuka kidogo kwani mbele ya ile nyumba paliandikwa pembezoni yake, ‘LODGE’
Baba Angel alishtuka sana na kumuangalia Daima kwa hasira,
“Yani wewe mjinga unanileta Lodge?”
Baba Angel kwa hasira akamnasa kibao Daima, muda huo Daima alianza kupiga kelele nyingi,
“Ananibaka, ananibaka”
Watu wa karibu walifika eneo lile na kuanza kumshangaa baba Angel.
Kwakweli kwa muda huo baba Angel hakujua cha kufanya na aliona kuna wananchi wengine wakija na gadhabu huko akaona isiwe shida, ilibidi afanye maamuzi ya haraka kichwani maana aliona hapo kujitetea itashindikana, muda ule ule aliingia kwenye gari na kuondoa gari lake kwahiyo alimuacha Daima akiwa pale pale na wale watu huku baadhi yao wakirushia mawe gari la baba Angel, ila alifanikiwa kuondoka kabisa eneo hilo.
Daima ndio alibaki pale na wale watu huku akilia na kusema kuwa yule baba alimkuta njiani na kumpa lifti halafu alikuwa akimlazimisha kufanya nae mambo machafu, kwahiyo walimuhurumia sana, halafu msamaria mwema mmoja akajitokeza ili kwa usiku huo Daima aweze kulala kwake halafu kesho yake ndio aweze kurudi nyumbani kwao.
Basi yule mama alienda na Daima nyumbani kwake, ila Daima alionekana kulia tu,
“Nyamaza binti, cha kushukuru ni kuwa hakuweza kukubaka. Yani wanaume ni wajinga jamani. Sasa mbaba mtu mzima vile atake kwenda kulala na wewe kitoto kidogo? Wewe si sawa tu na binti zake jamani! Mbona haya mashikolo mageni”
Mama mwingine akamuuliza Daima,
“Kwahiyo yule baba humjui? Na usiku huu ulitoka wapi binti?”
Daima alikuwa akilia na kuanza kuwaelezea,
“Yani mimi nina mikosi sana, kuna nyumba ya ndugu yangu Fulani nilikuwa nakaa, basi mtoto wake wa kiume akanitaka kimapenzi nikamwambia mimi siwezi maana wewe ni ndugu yangu. Akachukia na kusema maneno ya uongo kwa wazazi wake, ndipo waliposema usiku huu huu nirudishwe kwetu, sikuwa na tatizo maana kwetu kupo. Nikapanda kwenye gari na yule kijana, akanipeleka mahali na kunitupa huko halafu yeye akaondoka yani nikakosa uelekeo, ndio akaja huyu baba na kusema kuwa atanisaidia, basi nikapanda kwenye gari yake ila ndio hivyo akawa anataka kunibaka ndani ya gari, nikamuomba tutafute chumba kwani nilijua akitafuta chumbva naweza pata msaada kwa wananchi. Tukafika pale, ndio akanishika mkono na kunilazimisha kuingia nikawa nakataa ndio akaninasa kibao, ikabidi nipige kelele”
Daima alikuwa akiwaonyesha alama ya kibao kwenye shavu lake, na kweli alitokwa na alama kwani baba Angel alimzaba kwa hasira sana, basi wale wamama walimuhurumia sana Daima na kulaani vikali vitendo vya wanaume huku wakisema,
“Yani wanaume ni wanyama, hawafgai kabisa wana roho mbaya sana, hebu ona binti mdogo hivi kafanyiwa unyama na wanaume”
“Nikwambie wanaume ni viumbe hatari sana, tunaishi nao tu duniani ila wanaume jamani, ptuuuuu. Siwataki hata kidogo”
Basi walimbembeleza Daima pale na kumtaka kwenda kulala tu kwa muda huo huku wakimuahidi kuwa kesho yake watamsaidia kumpeleka kwa wazazi wake, Daima alitulia tu ila alielewa madhara ya uongo alioutengeneza pale.

Baba Angel alirudi nyumbani kwake usiku sana, tena alirudi huku akionekana kama akili yake ikikosa mawasiliano vile, alimkuta mkewe tu ndio yupo kumsubiri, alivyorudi mama Angel alifurahi kwa uwepo wake na kwenda nae moja kwa moja chumbani huku akimpa pole na kumuuliza kilichomfanya na kumchelewesha vile,
“Wazazi wa Daima walikuwa wakigoma kumchukua mke wao nini?”
“Yani bora hata ningefika kwa hao wazazi wa Daima kuliko alichonifanyia huyo Daima”
“Kakufanyaje tena?”
“Jamani, kanizungusha mji wote kila mahali tukifika sio hapo kwetu, ananionyesha pengine, hadi nikachukia sasa, akanipeleka ehemu moja hivi kumbe ni Lodge, khaaaa kushuka kwenye gari naona lodge nikachukia sana, na kumnasa kofi Daima, weee asianza kupiga kelele kuwa nataka kumbaka, watu wakajaa, siunjaua wananchi tena wanione na mtoto mdogo kama Daima wangenielewa wapi, niliamua tu kufanyua akili ya haraka haraka hata sikuongea kitu zaidi ya kupanda kwenye gari na kuondoka, wananchi wale walipiga mawe gari langu lakini sikujali, kwakweli huyo Daima sitaki hata kumuona na hapa nyumbani kwangu asije tena mtajuana mambo yenu na huyo mtoto wenu wenyewe, mtajua wewe na dada yako mtakachokifanya kwa huyo Daima kwakweli nimeshindwa, khaaaa huyu mtoto hapana aiseee”
“Dah! Pole sana mume wangu, pole kwa hayo yaliyokupata, bora ningempeleka mwenyewe. Mtoto mjinga sana huyo jamani loh! Sikutegemea kama angefanya kitu cha namna hiyo”
Mama Angel aliamua kutumia muda huo kumtuliza mume wake, kwani alitambua wazi kuwa mambo hayo yamemchanganya sana mumewe, basi akamtuliza pale hadi mwishowe wakaamua kulala tu.

Leo wakiwa shuleni, karibia na muda wa kutoka, siku hii hakukuwa na masomo mengi kwahiyo wanafunzi walikuwa wakiongea ongea tu, basi kwa muda huo Erick alikaa na Elly huku wakizungumza kwani siku hizi hawakuwa na zile tofauti zao hata kidogo na walikuwa wakiongea vizuri tu.
Elly alijikuta akimuelezea Erick kuhusu kile kitendo cha mjomba wao kusema kuwa yeye ni mwanae,
“Duh!! Inawezekana ikawa kweli Elly, kwani wewe unaonaje?”
“Sijui, ila mwenye ukweli ni mama maana mama ndio pekee anayejua baba halisi wa mtoto”
“Ila mama yako anasemaje?”
“Nimejaribu kumdadisi sana hataki kuniambia ukweli, anachokisema yeye ni kuwa yule mtu sio baba yangu”
“Sikia Elly nikwambie kitu, yule mama ni mama yako ila ana mambo mengi sana ya ajabu huwezi kuyajua ila mama yako ana mambo mengi sana ya ajabu. Ukiona moyo wako unamkubali baba huyo basi ujue ni kweli ni baba yako, kwani kwa kipindi kifupi tu nilichomfahamu mama yako nimegundua kuwa ni mtu anayeweza kukazania ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli, yani utakuta anakazania kabisa, hata ugomvi wangu na yeye ni sababu ya swala lake la kunizushia maneno ya uongo, siku hizi mbona kaacha mwenyewe, kwa kifupi Elly kuwa makini sana na mama yako. Wewe mkazanie huyo kuwa ni baba yako na ipo siku atakwambia ukweli tu”
“Tena baba mwenyewe anaonekana kuwa na upendo sana, kwakweli huwa napenda sana kuwa na baba, nimekosa mapenzi ya baba kabisa. Mama angekubali hata angeniruhusu nikakae kule na baba ila mama yangu namfahamu mwenyewe”
Wakati wanaendelea kuongea pale, alifika Sarah na kumtaka Elly kuwa waondoke wote,
“Elly si unajua leo ni Ijumaa!! Inabidi uende nami nyumbani kwetu ili tukawe huko”
Erick akamwambia Elly,
“Ningekuwa mimi ningeenda kutumia huu muda wa mwisho wa wiki kukaa na baba yangu”
Sarah alimuangalia Erick na kumwambia,
“Mbona una wivu sana wewe! Kwahiyo nikiwa na Elly roho inakuuma sana? Pole eeeh! Ulikataa bahati, pole sana”
Sarah akamshika mkono Elly, na kwakweli Elly hakubisha kwani bado elimu yake ilimtegemea mama yake Sarah, basi aliondoka nae. Na Sarah aliamua kuondoka nae muda ule kwavile hakutaka kupanda nae kwenye gari la shule ndiomana akafanya vile, Erick nae akaamua siku hii asipande usafiri bali moja kwa moja amfate Erica tu shuleni kwao na waweze kurudi wote nyumbani.

Mama Angel leo aliamua kwenda moja kwa moja kumuangalia tena Derrick kuwa anaendeleaje, basi alienda kumuangalia na kumkuta Derrick akiwa mzima kabisa, na muda huo alimkuta akimwagilia bustani ya mboga mboga,
“Oooh kaka yangu umemaua kulima mboga mboga?”
“Yani nimeona ni vyema nijishughulishe kidogo maana kukaa tu hakuna faida yoyote ile nitakayoipata ukizingatia nimepona. Ila nimemkumbuka sana mtoto Elly”
“Usijali, nitakuja nae tena tu”
“Yule ni mtoto wangu, nina watoto wawili mimi, na yule ni mmoja wapo”
“Ila yule sio mtoto wa Oliva au Manka, ni mtoto wa Sia yule”
“Kheeee yule Sia chizi?”
“Kheee kumbe unamjua? Ndio huyo huyo”
“Aaaah yule mjinga, inawezekana hata aliiba mtoto. Bora mngenitajia mama mwingine ila kwa yule Sia yule, hapana aisee yule mwanamke hana mtoto nina uhakika asilimia mia moja kuwa Elly ni mtoto wangu, huyo Sia tukimbana atatueleza ukweli ila Elly ni mtoto wangu”
Mama Angel hakuwa na cha zaidi cha kuongea na Derrick, basi alimuaga tu kwa muda huo na kuondoka zake.
Akiwa njiani alikutana na mama Sarah na kumsimamisha huku akianza kuongea nae,
“Sikia Manka, tunataka kuja kwako ili tujadiliane vizuri kuhusu mtoto Sarah”
“Kheee una wazimu nini wewe, ujadiliane na nani kuhusu Sarah?”
“Tunataka kujua ukweli wa mtoto huyu, kama ni wa mzee Jimmy, Erick au Derrick”
“Mjinga sana wewe, mimi ndio mama mzazi wa Sarah, na mimi ndio mwenye uwezo wa kuwaambia kuwa yule mtoto ni wa nani. Ningetaka hayo basi ningekuja mwenyewe huko kwenu ili tujadiliane nanyi, ila sina haja mfahamu chochote kile”
“Unajua acha kichaa weee mwanamke, ulisema wazi kuwa Sarah anampenda Erick na unajua wazi kama Sarah na Erick wakiwa pamoja ni shida sababu ni ndugu hata iweje, ikiwa Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick bado ni tatizo kwani ni ndugu, tunahitaji kujadiliana ili watoto watambuane kuwa ni ndugu na waujue ukweli halisi wa mambo”
“Hayo mambo hayakuhusu, kwanza sidhani kama nina muda mchafu wa kukaa na kujadiliana na wewe kuhusu huo ujinga”
Mama Sarah aliondoka zake, basi mama Angel aliona ni vyema kwa muda huo aende moja kwa moja kwa wifi yake Tumaini ili kuongea nae kuhusu hilo swala, yeye alitamani hilo swala liishe ili yote yawe peupe kabisa.
Basi alifika kwa Tumaini na kumkuta na kumueleza yale yaliyojiri kwa siku hiyo, akamueleza pia alivyokutana na mama Sarah na walivyozungumza,
“Yule mtoto kuna utata maana hata Derrick anasema mtoto wa mama Sarah ni wake”
“Kheeee kuna wanawake wa ajabu sana duniani, mtoto mmoja ana mababa watatu! Duh sio haki kwakweli, kuna wanawake hawajitambui. Huyo mama Sarah ni hajitambui kwakweli”
“Sasa tutafanya nini?”
“Nenda kamwambie Erick kuwa Jumapili tunaenda huko kwa mama Sarah, yani yule mwanamke atake au asitake lazima tujadiliane nae kuhusu hili, asituchezee kabisa, na kama Sarah sio wetu basi atuweke wazi, kuliko kusema watoto wanapendana halafu watoto hao ni ndugu ana maana gani? Kwahiyo anataka ndugu watembeleane? Asituletee matatizo sie”
Mama Angel akakubaliana na Tumaini kuwa Jumapili wataenda kwa mama Sarah kujadiliana nae kuhusu hilo swala.

Erick kama alivyopanga, moja kwa moja alienda kwenye shule anayosoma Erica kwahiyo aliondoka na Erica bila kupanda basi la shule, waliongozana kurudi nyumbani huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Eeeeh uliahidi kuninunulia karata Erick, nahitaji karata”
Basi Erick alipitia dukani na kumnunulia dada yake karata, basi pale dukani kuna watu walisikika wakisema,
“Siku hizi kuna mambo ya ajabu sana, watoto wadogo utakuta washaanza kupendana yani hapo kamununulia karata ili amuhonge”
Mwingine akacheka na kusema,
“Kheee hadi kwa karata jamani, mabinti hawana thamani siku hizi”
Yale maneno waliyasikia vizuri sana, cha kustaajabu, Erick alimuacha Erica pale na kusogea kwa wale waliokuwa wakiongea na kumpiga ngumi yule aliyesema kuwa mabinti hawana thamani siku hizi, na mzozo ulianzia pale maana huyu alikuwa ni mama mtu mzima halafu Erick katumia nguvu kufanya vile, yule mama alianza kumsema Erick na wote pale walianza kumshambulia kwa maneno,
“Una laana wewe, utampigaje mtu mkubwa hivi, huyu si kama mama yako tu! Mitoto ya siku hizi mpaka mara nyingine unawaza kuifanya supu ujinywee zako unenepe, sio kuzaa watoto punguani kama huyu”
“Unavuta bangi au?”
Wale wamama wakaambizana kuwa wamchangie Erick ili wamfundishe adabu basi walianza kumzoga zoga pale, yani Erica alikuwa akilia tu na kumuombea msamaha kaka yake, ila muda huo wakati wale wanawake wamesema wamchangie, Erick alikuwa katikati yao na wala hakuonyesha kuwa anaogopa chochote kile, basi Erica alienda pale katikati na kuana kumsihisi kaka yake,
“Waombe msamaha tuondoke”
“Siwaombi msamaha, kwani walichokuwa wakikisema ni kizuri, waache wanipige tu halafu ndio watajua kuwa mimi ni mtu wa aina gani”
Kuna baadhi ya wanawake waliogopa na kuna wegine walitaka kumuadhibu ili kile kiburi chake kiishe kabisa, cha kushangaza kati yao hakuna aliayeanza kumpiga Erick bali walikuwa wamemzingira tu huku wakimpa maneno mbalimbali,
“Unajivunia huo urefu, wenzio wanajivunia akili sio urefu”
“Wazazi wako wana mikosi kwa kukuleta mtoto kama wewe, hufai duniani wala akhera”
Ila kuna mama alitokea pale na kuwaomba wale wamama wamsamehe tu Erick, na kumtoa pale katikati ya wale wamama na kumtaka aopndoke, kwahiyo Erick aliondoka na dada yake.
Yule mama aliwaambia,
“Jamani wamama wenzangu, hawa watoto wa siku hizi maradhi kibao yamewajaa, usikute ni kifo chake, unajaribu kumpiga unashangaa yupo chini amekufa, halafu inaanza kesi ya mauwaji tutakimbiana hapa mjue, hebu muecheni tu. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, naomba tusimfunze sisi wanawake, ila tuache wanaume wenzie ndio wamfundishe”
Wale wamama waliongea sana ila hakuna hata mmoja aliyejua ni kwanini walishindwa kumpiga yule kijana yani walibakia tu kumtupia maneno lakini hakuna aliyeweza kumpiga, na hakuna aliyejua ni kwanini yule kijana alionyesha kujiamini sana kupita chochote kile.

Mama Daima alichukia sana kwa yale maelezo aliyopewa na Daima, maana wale wamama walimrudisha kwao tu na kusema kuwa alitaka kubakwa, sasa walipoondoka ndipo Daima alipomwambia mama yake kuwa aliyetaka kumbaka alikuwa ni baba Angel na kumfanya mama yake achukie sana kwa hilo.
Mida ya jioni, mama Daima aliondoka nyumbani kwake, akaenda moja kwa moja nyumbani kwa mama Angel na kumkuta mama Angel amakaa na mwanae Erica kwenye kibaraza maana Erica alitaka kumuhadisia mama yake ya siku hiyo kuhusu Erick, ila yule mama alivyofika pale bila hata salamu alianza kusema mambo ambayo ameyatunza kwenye moyo wake, kwanza alifunga kibwebwe na kuanza kusema,
“Hata kama mwanangu ni muhuni sio kwa hili mlilotaka kumfanyia, yani kijana wako atake kumbaka na mumeo nae atake kumbaka”
“Kheee wewe mama una akili lakini, si uulize sio unakuja kupaniki tu”
“Niulize kitu gani? Mnatabia mbaya sana nyinyi, huyo mumeo kakosa wanawake wote wanaojiuza huko hadi atake kumbaka binti yangu, tuseme wewe humtoshelezi mumeo mpaka atake kumbaka binti yangu? Mnachefua sana, wewe na tabia zako chafu nimekusitiri tu, umetembea na ukoomzima wa mume wangu ila unadhani hatujui kwa kukaa kimya kukusitiri tu maana tunaona tukisema tutakuabisha sana mjinga wewe. Kumbe hata hujifikirii hata kidogo, hujui baya wala hujui vibaya, mwanamke mbaya wewe na mchafu loh!”
“Umemaliza?”
‘Sijamaliza bado”
Akaendelea kuongea, basi mama Angel alimuangalia Erica na kumtuma,
“Kalete maji ya kunywa ndani”
Erica alienda na muda kidogo alikuja na maji, basi mama Angel akamwambia mama Daiam,
“Najua utakuwa unaishiwa na pumzi sababu ya kuongea sana, maji hayo hapo utakuwa unashushia kidogo kidogo”
“Puanguani nini wewe, aliyesema anataka maji ya kunywa nani? Nakueleza tabia mbaya za mumeo unajifanya huelewi”
“Ungekuja kuuliza kistaarabu ningekujibu”
Basi mama Angel akamvuta mkono Erica na kuingia nae ndani kwahiyo walimuacha mama Daima anaongea pake yake pale nje.
Kwakweli mama Daima alichukia sana na kuendelea kusema maneno machafu pale, muda huu Erick mdogo alikuwa nyuma ya nyumba yao, aliposikia zile kelele za mama Daima alisogea karibu, basi mama Daima kumuona Erick akamsogelea na kumkunja huku akisema,
“Eeeeh tena ndio wewe wewe uliyetaka kubaka mwanangu”
Akaanza kumwambia maneno yake ambayo yalimchukiza sana Erick, na yule mama hakujua hasira alizonazo Erick ila alishtukia tu akipewa ngumi hiyo ambayo ilimpeleka hadi chini, kiasi kwamba alianza kutoka damu mdomoni, halafu Erick hata hakujali aliingia ndani, yani mama Daima aliona ile nyumba ina magaida, kwa muda huo aliamua kuondoka huku akijifunika mdomo wake ambao ulikuwa ukitoa damu.

Usiku huu wakati baba Angel yupo ndani na mkewe alielezewa kuhusu mama Daima kwenda pale na kuanza kutukana, yani kitu ambacho mama Angel hakukijua ni kuwa mama Daima alipigwa ngumi na Erick, muda wakati anamuhadithia mumewe, simu yake ilianza kuita na kupokea allikuwa ni baba Daima,
“Kwakweli sijapenda kwa kitendo mlichomfanyia mke wangu”
“Kitendo gani”
“Mke wangu kaja huko kwa ustaarabu kuwaeleza kuhusu alichokisema binti yetu, kweli mlichokifanya kwa mwanetu mnaona kipo sawa?”
“Sikia baba Daima, angekuja kwa ustaarabu mbona tungeelewana, sasa mkeo kaja na matusi”
“Ndio mumpige ngumi ya mdomo hadi mke wangu kuanza kutokwa na damu mdomoni”
“Kheee mwenye uwezo wa kumpiga ngumi mkeo hadi damu ni nani?”
“Unajifanya hujui, si huyo kijana wako humo ndani. Huyo jambazi mnayemfuga humo ndani”
“Khaaa jamani, hapana aiseee, Erick hawezi kufanya hivyo”
“Muulize akwambie alichomfanya mke wangu, mtoto wako ana roho mbaya sana huyo. Halafu kwanini mmefanya hivi kwa binti yangu mjue tunaheshimiana sana!”
Mama Angel aliamua kumueleza kilichojiri hadi baba Angel kumuacha pale na kuondoka zake,
“Haya wale wananchi wangeamua kumpiga mume wangu na kumdhuru, si ingekuwa ni tatizo kubwa sana. Kwakweli huyo binti yako hafai na usipokuwa makini unaweza hata kugombana na baadhi ya majirani kwa uongo wake”
“Ulishindwa nini kumueleza mke wangu mambo hayo?”
“Muulize mkeo jinsi alivyokuja kwangu, muulize akamwambie maneno aliyoyasema’
Basi baba Daima alikata ile simu na muda ule alianza kuongea na mumewe,
“Jamani inawezekana kweli kwa Erick kufanya hivyo?”
“Hata mimi nashangaa kwakweli, inawezekana Erica anajua ngoja nikamuulize maana kama Erica anajua ataniambia ukweli zaidi kuliko Erick”
Basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambaye alificha karata zake baada ya mama yake kuingia,
“Umeficha nini Erica?”
“Hakuna kitu nimeficha mama”
“Yani wewe mtoto wewe, hebu niambie jana tulivyoingia ndani na mimi nikaenda chumbani nini kilitokea? Yule mama aliyekuwa akiongea aliondoka muda gani?”
“Mimi nilikuwa sebelni mama, Erick alikuwa nje, basi nikasikia kama yule mama anaongea na Erick halafu nikachungulia na kuona yule mama kamkunja Erick ila muda ule ule Erick alimsindika ngumi hiyo yule mama hadi alianguka chini na damu zilikuwa zikimtoka yani alipoinuka alikimbia na kuondoka zake”
“Mbona hukuniita sasa”
“Mmmh Erick angechukia zaidi, ila unadhani hilo tukio ni la kwanza kufanywa na Erick? Leo leo kafanya balaa huko njiani”
“Balaa gani?”
Erica hakumueleza mama yake kuwa walienda kununua karata, bali alisema kuwa Erick alienda kumnunulia juisi, basi akamwambia maneno waliyokuwa wakiongea wale wamama na Erick kwenda kumpiga mama mmoja wapo, na jinsi ilivyokuwa, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kusema,
“Hapana aiseee, Erick wangu hawezi kufanya hivyo”
“Usikatae mama, ndio kafanya hivyo huyo Erick wako hata usimkatalie”
Mama Angel akakumbuka pia Sia alivyolalamika kuwa kapigwa sana na Erick hadi mbavu zilimuuma kipindi hiko, ila bado mama Angel aliona hiyo ni ngumu sana kwa mwanae.
Basi akaondoka na kumuacha Erica alale halafu akaenda kwa mumewe na kumuelezea hayo,
“Mmmh itabidi kesho niongee na kijana wangu, asije kuleta balaa bure, huo ubondia kautoa wapi?”
“Kautoa kwako, maana nawe mkorofi”
“Hapana sijafikia huko”
“Ila cha kurithi kinazidi”
“Hata kama, sio kawaida hii kuna tatizo kwa mtoto wetu lazima tujue kuwa tatizo ni kitu gani”
Basi wakaongea na muda huo kuamua tu kulala.

Jumamosi ya leo, Steve anaongea na mtoto Paul kuwa waende kwenye matembezi naye, kwakweli Steve alijikuta akipatana sana na mtoto huyu, yani alipatana nae kupita maelezo ya kawaida, alikuwa kama mwanae kabisa, ana alifanya mambo yote pamoja nae, kitendo kile kilimfanya madam Oliva kuhisi furaha sana moyoni mwake.
Basi muda ulipofika Steve pamoja na Paul walijiandaa na kwenda kwenye matembezi ambapo walienda sehemu mbalimbali yani Steve aliona fahari kwake kutambulisha kuwa Paul ni mtoto wake.
Katika kwenda sehemu mbalimbali ndipo alipoamua kwenda na Paul nyumbani kwao, na hapo walimkuta mamake Steve akifanya tu shughuli zake, kwakweli alishangaa sana kuwaona na kuwakaribisha, basi waliongea ongea pale ila huyu mama aliashindwa kujivunga na kusema,
“Steve, huyu mtoto unajua kuwa umefanana nae sana!”
“Hata mimi nimeona, duniani wawili wawili”
“Au ndio yule wa kipindi kile!”
Steve alicheka na kumwambia mama yake,
“Huyu ni mwanangu, kutoka kwa Oliva”
Mama Steve alishtuka kidogo, na kumvuta mkono Steve na kwenda kuongea nae pembeni,
“Inamaana hujaanza leo na huyo Oliva, mna muda mrefu eeeh!”
Steve alicheka, na mama yake aliendelea kuongea,
“Sema ukweli mwanangu, naona wazi kuwa huyu ni mjukuu wangu kabisa”
Steve aliamua kumdanganya mama yake kuwa ni kweli alikuwa na madam Oliva tangu zamani na wamezaa pamoja huyo mtoto Paul, kwakweli mama Steve alifurahi sana na kumwambia Steve kuwa siku zote alikuwa akimpinga madam Oliva ila kwa hilo anamkubali kwa mikoni miwili.
Basi mama Steve akamfata Paul na kumkumbatia huku akimwambia,
“Karibu nyumbani mjukuu wangu”
Kisha mama Steve alienda kukamata kuku nje, na kuanza kumuandaa kwani alitaka kumfurahisha mjukuu wake, yani alikuwa na furaha sana kuona mtoto wake ana mtoto kweli.
Paul naye alifurahi sana, ila kitu ambacho Paul hakukielewa ni kuhusu Steve kama ni baba yake kweli au ni baba yake kwavile anaishi na mama yake, yani hapo ndio hakuelewa kabisa.
Mama Steve alimaliza kuandaa ile kuku na kuiweka mezani ili wote waweze kula, basi Steve alishangaa tu pale kuwa na ile kuku ya kuchomwa, halafu kuna mchuzi wa samaki na wali, akauliza,
“Mbona mama hiyo kuku umemuwekea Paul peke yake?”
“Ndio ni ya mjukuu wangu, nataka ale afurahi na yeye kwa uwepo wa bibi yake”
Basi Steve akacheka tu na kuendelea kula kile chakula kilichoandaliwa na mama yake.

Baba Angel alienda zake kiwandani leo na alienda na Erick basi walipomaliza mambo yote, aliamua kwa siku hiyo kwenda na Erick kwenye moja ya mgahawa ili kuweza kuzungumza nae,
“Mwanangu nimesikia habari zako, umeanza lini ubondia?”
“Ubondia baba! Kivipi?”
“Si nasikia kila anayekuchokoza huko unampiga tu utakavyo”
“Oooh baba, naomba unisamehe”
“Unajiamini vipi kupambana na watu wote, umesahau kuwa wewe ulichapwa na madam Oliva fimbo moja na ukazimia?”
“Nakumbuka baba, ila sijui kwanini siku hizi yani nikishikwa na hasira najiona kuwa na nguvu za ajabu sana”
“Mmmh, utakuwa na tatizo mwanangu, nadhani utakuwa na mapepo”
“Hapana baba, sina mapepo mimi wala nini. Huwa watu wakinikera ndio nakuwa hivyo”
Baba Angel aliamua kuzungumza na mwanae namna ya kuheshimu watu wote, na madhara ya kugombana na watu, alimuelekeza vingi ili mwanae aweze kuacha hiyo tabia maana hata yeye binafsi hakuelewa kuwa tabia hiyo mtoto wake kaitoa wapi.
Walielewana kisha kufanya safari ya kurudi nyumbani.

Usiku wa siku hiyo, mama Angel alikumbuka kumwambia mumewe kile ambacho alijadiliana na Tumaini kuhusu mama Sarah,
“Kwahiyo ndio kesaho tukazungumze na huyo mwanamke”
“Ndio, bora mambo haya kuyaweka sawa, huyu mwanamke ni vyema gtumfate wote ili atwambie ukweli, kumbuka alimwambia Tumaini kuwa hata mzee Jimmy hamfahamu kabisa, kwahiyo tunatakiwa kuwa makini na maneno yake”
“Sawa nimekuelewa mke wangu, kwahiyo kesho tutampitia Tumaini na kuondoka nae kwa pamoja, nimekuelewa vizuri sana”
Kisha mama Angel alimuuliza mumewe kama aliongea na mtoto wao Erick, na mumewe alimueleza ambacho aliongea nae, muda kidogo ilipigwa simu kutoka kwa baba Daima na akalalamika kuwa mkewe kalazwa anaumwa juu ya ngumu aliyopewa na Erick.
Kwakweli hawakutaka kufikiria sana kuhusu hilo.

Jumapili kama walivyopanga, walijiandaa vizuri kabisa na kumpitia Tumaini kisha kufanya safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Sarah.
Walifika pale na kukaribishwa ndani ila waliambiwa kuwa mama Sarah hayupo kwani aliyewakaribisha alikuwa ni Siku yani mdada wa kazi wa mama Sarah, siku hii mama Sarah hakurudi toka ameondoka jana yake jioni, halafu Elly nae leo aliondoka asubuhi asubuhi kwenda Kanisani kwahiyo pale alibaki Siku na Sarah tu. Ikabidi waulizie uwepo wa Sarah,
“Sarah yupo ndani kalala, analalamika tumbo linamuuma sana”
Mama Angel alijikuta akijiwa na moyo wa huruma tu, kwani huwa akisikia mtoto anaumwa anasikia kuteseka sana moyoni, basi akahitaji kwenda kumuona.
Ikabidi yeye na Tumaini huku wakiongozana na Siku wakaenda hadi chumbani kwa Sarah na kumkuta amekaa huku akilalamika tumbo, walipoingia tu alianza kutapika, wakati wanamuhamisha ili wamfute yale matapishi walikuta kuna damu nyingi sana zinamtoka.
 
Back
Top Bottom