Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 409


Walipofika mlango wa kuingia ndani, Samir alikuwa kafungua mlango akitoka basi bibi Angel alishtuka sana kumuona Samir na kumuuliza baba Angel kwa mshangao,
“Ni nani huyu!?”
Baba Angel alimshangaa pia mama yake na kumuuliza,
“Kwani unamfahamu mama?”
“Hapana, ila ni nani?”
“Aaaah historia ndefu mama, nitakwambia tu karibu ndani”
Bibi Angel aliingia ndani ila jicho lake halikuganduka kwa Samir kwani alijikuta akimuangalia sana na kabla ya yote alitaka kutambulishwa kwa Samir kwanza kuwa ni nani, ikabidi baba Angel amuulize mama yake kuwa anafikiria ni kitu gani.
“Kwani mama unafikiria ni nani maana uleshtuka sana na bado unamuangalia?”
Bibi Angel alikuwa akiongea kiutaratibu na mwanae sasa,
“Weee mbona huyu kijana kafanana sana na baba yako! Yani kipindi cha ujana wao ndio alikuwa hivi hivi, yani huyu ni mzee Jimmy mtupu”
“Mmmmh mama!”
“Ndio, hamjawahi kuona picha za baba yenu za ujana wake? Alikuwa hivi hivi, yani kila kitu khaaa, hebu niambie ni nani?”
Baba Angel alipumua kidogo, akakumbuka mambo ya mtoto wa Jack, akakumbuka jinsi Rahim alivyosema huenda yeye na Rahim wana undugu, basi akafikiria kidogo na kusema, hapana kisha akamuuliza mama yake,
“Mama,kwani mzee Jimmy alikuwa na mtoto mwingine?”
“Mmmh yule baba yenu alikuwa na matatizo ya kizazi haswaaa, awe na mtoto mdogo hivyo!! Mimi nilijua huenda ukasema kuwa huyo ni mtoto wako, ulizaa huko nje maana nyie watoto wa kiume mna mambo sana, mwanamke akiolewa ajue tu kuna siku mambo yataripuka yani muda wote awe tayari kwa chochote. Kwahiyo huyo kijana ni mtoto wa nani?”
“Ni mtoto wa rafiki yangu mama”
Bibi Angel akaomba kutoka nje kidogo na baba Angel, kisha alienda nae moja kwa moja kwenye bustani ambapo bibi Angel alimuuliza baba Angel,
“Hebu niambie ukweli mwanangu, huyu mtoto sio damu yako kweli?”
“Mmmh sijui mama”
“Naomba kamuulize vizuri mama wa huyu mtoto, hamfahamiani kweli?”
“Aaaah mama, huyo mamake niliwahi kuwa na mahusiano nae zamani”
“Inawezekana ikawa ni damu yako ila alikuficha maana sisi wanawake tunamatatizo sana ikiwa mwanaume kakuudhi, mara nyingi unaamua kumfanya mtoto ni wako peke yako sababu baba yake alikuumiza sana. Hebu muulize vizuri ila nina uhakika asilimia mia moja kuwa hii ni damu yako, ingekuwa mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kuzaa tena baada ya wewe basi ningesema huyu ni mtoto wake ila mzee Jimmy alipata matatizo ya kizazi, halafu usifikirie ni mtloto wa mdogo wake mzee Jimmy labda ndio kamzaa huyo mtoto hapana, mzee Jimmy kwao alizaliwa peke yake ndiomana alikuwa na mali nyingi sana kwani ukoo mzima walikuwa wakimthamini yeye, na babu yao alikuwa ni mwenye pesa nyingi kwenye kijiji chao, kwahiyo alimtoa mjukuu wake kule na kumpa mali nyingi sana. Kwahiyo, nina uhakika asilimia mia moja kuwa hii ni damu yako”
Yani baba Angel alipumua ila alijiona kuwa na mawazo zaidi, maana kama Samir ni damu yake, je ataweza vipi kuliweka sawa swala hilo? Na je ni kivipi ikiwa yeye na mamake Samir waliachana sababu ya yeye kumsababishia yule mwanamke mimba itoke!! Alijikuta akikaa kimya kwa muda huku akimtazama mama yake ambaye alimwambia tena,
“Ukoo wenu sio mkubwa, kusanya vitoto vyako, bile mwenyewe katika mstari. Kwangu upo peke yako, kwa baba yako mpo wawili tu, kusanya hao ndio ndugu zenu wa badae. Nimemaliza, ila yule ni mjukuu wangu”
Kisha bibi Angel akauliza alipo Angel ili akamsalimie, yani baba Angel alimpeleka mama yake huku akiwa na mawazo sana juu ya kile ambacho mama yake amekiongea kwake kwa muda huo.

Basi baba Angel alirudi sebleni huku akimuangalia sana Samir, yani kwa muda huu alimuangalia sana hakuweza hata kummaliza, alijiuliza maswali mengi sana kuwa kama kweli Samir ni mtoto wake ila hakupata jibu la moja kwa moja.
Basi bibi Angel alipotoka alimtaka mwanae amsindikize kidogo, ingawa alikuwa na gari ila alitaka mwanae amwendeshe kidogo ambapo baba Angel alitoka kumsindikiza mama yake.
Wakiwa kwenye gari, bibi Angel alirudia tena yale maneno yake,
“Wakati wa kutoka tena nimemuangalia sana yule kijana, aaaah yule ni mwanao lazima ni mwanao Erick”
“Mmmh ila mama, siku ya kwanza nakutana na yule kijana nilimfananisha sana na jamaa fulani hivi”
“Acha kujidanganya Erick, labda kama unajifananisha nae mwenyewe, yule mtoto ni damu yako.”
Baba Angel alikaa kimya ila mama yake aliendelea kuongea,
“Jumamosi nitakuuliza kama tayari ushaongea na mama wa mtoto, akigoma nenda kapime damu na mtoto yule maana ni damu yako”
Yani baba Angel alishindwa kuongea kwakweli na kukaa kimya tu, mpaka pale mama yake aliporidhika basi yeye alishuka na kurudi nyumbani kwake ambapo tayari ilikuwa ni usiku.
Mama Angel alimuuliza mumewe kitu ambacho mama yake alishangaa kumuona Samir,
“Alishangaa sana halafu alikuwa kama anakunong’oneza kitu, mara ukatoka nae nje ni kitu gani hiko”
“Aaaah mama alikuwa kiuliza ugonjwa wa Angel, mbona alishaacha kumshangaa Samir yani yeye alichokuwa akishangaa ni kuwa yule kijana anafanya nini hapa nyumbani kwetu. Nilipomwambia ni mtoto wa rafiki yangu akaridhika”
“Aaaah kumbe!! Eeeeh umemwambia Angel alikuwa akiumwa nini?”
“Hivi mama Angel, mwanzoni kabisa nilipomuona Samir nilikwambia namfananisha na nani?”
“Mmmmh hata hukuniambia ila ulisema kuwa kuna mtu anafanana nae tena ulisema mtu huyo namfahamu ila hukuniambia hadi leo kuhusu huyo mtu”
“Aaaah nilifikiri nilimtaja?”
“Hapana, ni nani uliyekuwa ukimfananisha na Samir?”
“Aaaah ni Rahim”
“Rahim wapi? Yule mtoto hata hafanani na Rahim sijui na yeye kachomekewa”
Halafu mama Angel alianza kucheka ambapo baba Angel akamuuliza,
“Kama wewe ulivyonichomekea Angel?”
“Mmmh jamani yamekuwa hayo tena!! Wewe si ulimkubali Angel ilihali unafahamu kila kitu!! Tuachane na hayo mume wangu, tujadili maswala ya watoto”
“Eeeeh Angel anaendeleaje”
“Hajambo kabisa, anaendelea vizuri”
Baba Angel hakutaka kuongea sana kwa muda huo kwani aliona akili yake kama imevurugika hivi, kwahiyo aliamua tu kulala.

Leo baba Angel alimuita Samir mapema kabisa kwenye bustani yao na kuanza kuongea nae,
“Eti Samir, huwa baba yako unamuonaje yule?”
“Sijawahi kumuelewa tangu nilipokuwa mtoto, sijui kama ni baba yangu yule”
“Kwa mfano mama yako akakutambulisha baba yako mwingine utafanyaje?”
“Nitafurahi tu, maana yule baba hata huwa simuelewi”
“Jiandae, kuna mahali nataka kwenda na wewe”
Basi Samir alijiandaa kisha alitoka na baba Angel na moja kwa moja baba Angel alienda na Samir nyumbani kwa Tumaini, wakati huo alikuwa amemtumia ujumbe Tumaini kuwa amuangalie sana huyu kijana ambaye anaenda nae nyumbani kwake.
Walipofika ni kweli Tumaini nae aliguna na kuwasalimia pale kisha alimvuta nje kaka yake na kumuuliza,
“Erick, ndio matunda yako yameanza kuonekana nini?”
“Kivipi?”
“Unafikiri mchezo!! Wale wanawake wote uliokuwa ukiwapa mimba kipindi kile na kuwatoa, wapo ambao walitunza”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Hii damu yetu hii, umekuja kunionyesha shangazi yangu eeeh!!”
“Aaaah sio hivyo, unaona kafanana na nani huyo mtoto?”
“Kuna picha za baba akiwa mvulana mdogo yani hivyo hivyo kama huyo kijana. Siku nikienda kule nyumbani nitaenda kuzipekua, Erick kwakweli una damu kali mdogo wangu”
“Hivi hujawahi kumuona huyu kijana eeeh!!”
“Sijui kama nimewahi kumuona, nahisi sijawahi kumuona ila nimefurahi kumjua. Kumbe tuna kijana mkubwa hivi, nilijua Erick ndio mkubwa pekee”
“Aaaah Tumaini acha zako bhana”
“Halafu sikukwambia, jana kuna maeneo nilikuwepo halafu akapita Erick nikasikia wanasema duh yule kijana ni hatari sana, mwengine akasema anacheza kungfuu huyo, duh sikusema kitu maana hawakujua kama wanayemuongelea ni damu yangu”
“Mmmh dada, mambo ya Erick yaache kwanza. Nilimleta huyu kijana umuone basi”
“Nimemuona na nimemkubali kuwa ni wa kwetu”
Hapo baba Angel hakuwa na usemi zaidi basi walirudi ndani ambapo Tumaini alienda kuwaandalia chakula ili waweze kula pale nyumbani kwake.
Walipoanza kula tu, simu ya baba Angel iliita ikabidi atoke nje na kuipokea maana aliyekuwa akipiga ni Jack,
“Samahani Erick, naona kila siku hatuelewani. Ni hivi, mtoto huyu kuna binti alimpa mimba, yule binti kajifungua leo, ile familia wanahitaji twende kujitambulisha. Ndiomana siku zote hizi nilikuwa nakukazania ili ujue kuwa mtoto wako anahitaji kutambua kwamba ana baba yake”
Baba Angel akapumua kidogo na kusema,
“Nimekuelewa Jack, mmepanga kwenda lini?”
“Wiki ijayo”
“Sawa hakuna tatizo, tutaenda wote. Nishtue tu siku ikifika”
Basi baba Angel alikata ile simu na kurudi ndani kuendelea kula, na baada ya muda waliondoka zao.

Jioni ya leo, Angel alitoka na kwenda kukaa kwenye bustani yao ambapo Erica nae alienda kukaa nae karibu na kuongea nae,
“Unaendeleaje dada?”
“Sarah yuko wapi?”
“Amelala, ila nimekuuliza unaendeleaje?”
“Kwani nilikuwa naumwa?”
“Ndio, si ulikuwa na mimba wewe imetoka!”
“Mama amekwambia?”
“Hapana”
“Ila umepata wapi hiyo habari?”
“Nimeota”
“Umeanza mambo yako ya ndoto, haya hiyo mimba ni ya nani ilikuwa?”
“Nimeota kuwa ulipata mimba ya Samir, siku ile mliyosababisha moto. Halafu baada ya kugundua, baba na mama wakakukimbizia kwa bibi ambapo kuna siku hukula na ukikuwa ukilia sana, ukahisi kizunguzungu na kuanguka hakuna aliyejua, ulizinduka ukiwa mwenyewe chumbani, bibi akakuuliza ukasema uitiwe baba ndio baba akaitwa ukapelekwa hospitali na kukuta mimba imetoka”
“Kheee nimekuvulia kofia wewe mtoto jamani, hebu niambie kwenye ndoto zako unaona mimi nitaolewa na nani?”
“Niliwahi kuota kuwa wewe unaolewa na huyo huyo Samir ila kuna utata mkubwa sana ulitokea maana kila mtu alikuwa akipinga kuoana kwenu na wakidai kuwa nyie ni kama ndugu”
“Ni kama!! Kwahiyo sisi sio ndugu?”
“Sijui kitu, nakueleza vile nilivyoota”
“Wewe Erica, unapata wapi uwezo wa kuota vitu vyote hivyo?”
“Hata mimi sijui, kuna ndoto zingine hata kusema huwa naogopa maana zinakuwa na makubwa ndani yake”
“Kama ndoto gani?”
“Kama ndoto ya kuhusu mimi na Erick”
“Eeeeh wewe na Erick mmefanyaje?”
“Ipo siku nitakwambia ila sio leo. Sema pole sana dada yangu, haya ni mapito tu, kuna muda utazoea na kusahau kama kuna kitu cha namna hii kimepita katika maisha yako”
“Wewe bado mdogo ila mara nyingine una maneno ya busara sana. Yani Sarah ndio mvivu kama mimi jamani, hebu kamuamshe”
Basi Erica alienda ndani kumuamsha Sarah ambaye aliamka na kutoka na Erica hadi kwenye bustani, halafu Angel alimwambia Sarah
“Yani wewe unapenda kulala jamani, utapata wapi muda wa uwaza maendeleo? Muda wa kuwaza mahali pa kupatia pesa?”
“Kwanini niwaze vyote hivyo dada?”
“Kwanini?”
“Mimi kwetu ni mtoto wa pekee, baba yangu aliniachia mali nyingi sana, hapa unavyoniona nina nyumba tatu, nina mashamba makubwa matatu, nina ile shule kubwa sana. Baba yangu alikuwa akinipenda sana, na hakutaka nipate shida duniani, namshukuru mama kwa kunitafutia baba kama yule”
“Mama yako akiviuza je?”
“Angeviuza wakati nipo mdogo ila sio kwasasa hivi nikiwa mkubwa hivi, mama hana kiburi cha kufanya chochote bila ridhaa yangu. Ila kwa jinsi ninavyowapenda Erick na Erica basi najitolea kugawana nao mashamba yangu yani kila mmoja atachukua moja moja”
“Kheee na mimi je dada mkubwa?”
“Wewe nitakupa nyumba”
Walicheka pale, walijua ni maongezi tu ya kumaliza siku yani hakuna aliyetilia maanani yale yote yaliyokuwa yakizungumzwa mahali pale.
 
SEHEMU YA 410


Usiku wa leo, Erick akiwa chumbani kwake alifatwa na Erica ambaye alianza kuongea nae, kwanza alimuita
“Erick”
Erick akageuka maana alikuwa akiangalia sehemu nyingine, kisha akasema,
“Erica umenishtua sana yani sijui nimehisi vipi”
“Pole sana, leo ulikuwa wapi?”
“Aaaah kwanini umeuliza hivyo? Mbona siku zote huniulizi?”
“Aaaah nimekuuliza leo tu”
“Kama kawaida nilikuwa kiwandani”
“Umemfanya nini yule meneja wa pale kiwandani?”
“Mmmh!! Umeanza mambo yako hivyo Erica!! Sijamfanya kitu ila nimempa onyo basi”
“Duh!! Ila Erick mambo yako ni hatari sana”
“Kwahiyo siku hizi unaniogopa Erica?”
“Hapana, ila watu wanakuogopa Erick”
“Achana nao Erica, njoo ukae hapa karibu tuongee ya maana basi”
Erica alisogea karibu na kukaa kitandani pamoja na kaka yake ambapo Erick alikaa kimya kwa muda bila kuongea chochote na kumfanya Erica amuulize,
“Mbona huongei kitu sasa?”
“Sijui ni nini, nashangaa siku hizi ukiwa karibu yangu nashindwa kukwambia chochote kile Erica, sijui tatizo ni nini”
“Pole”
“Je unaweza kunifanyia tena kama siku ile?”
Erica alihisi kusisimka mwili mzima na kuinuka kisha akamuacha kaka yake mule chumbani mwenyewe kwani hakutaka tena kutenda kile kile alichokitenda na kaka yake.

Kulivyokucha, mama Angel alimtaka mumewe anywe chai kwanza kabla ya kwenda ofisini, basi walikaa mezani na kuanza kuzungumza,
“Hivi yule dokta Jimmy si mlipanga kukutana baba Angel, ungemkumbusha kabisa ili tujue ni wapi tutakutana nae”
“Nitamuuliza ila lazima twende na madam Oliva maana yule dokta haaminiki ujue, asije kutufanyia kitu mbaya”
Erick alikuwa akipita ila mama yake alimuita ili nae anywe chai kwanza,
“Si unaenda kiwandani mwanangu!!”
“Ndio mama”
“Njoo unywe chai kwanza halafu ndio utaenda huko”
Basi Erick alikaa pale na kunywa chai huku baba Angel na mama Angel wakiendelea kuongea ambapo mama Angel alisema,
“Simpendi dokta Jimmy”
Baba Angel akadakia,
“Nadhani hunifikii mimi mke wangu, ningekuwa na uwezo wa kumfanya chochote dah basi tu. Ila muache atupe siri kwanza”
“Najua unachuki nae sana ila anagalia usitende dhambi”
Waliongea pale, kisha baba Angel aliondoka zake, halafu Erick nae aliondoka zake kuelekea kiwandani.

Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa siku ya leo, alifuatwa na yule bibi muuza matunda ambaye huwa siku zote yupo hapo akiuza matunda yake, basi aliingia ofisini kwa baba Angel na kumwambia,
“Leo, nimekuletea zawadi”
“Kheee zawadi gani?”
Bibi alitoka nje na kumkaribisha mgeni aliyeambatana nae na kumwambia baba Angel,
“Haya sasa, Juli huyu hapa”
Baba Angel alifurahi kiasi na kusalimiana na yule Juli huku akiongea nae mambo mbalimbali,
“Yani kumbe Juli, siku zote hizi nipo na mama yako mzazi hapa”
“Unajua nilishangaa sana siku ile wakati naongea nawe kwenye simu kwa kupitia simu ya mama. Ndiomana nimerudi nikamwambia mama cha kwanza kabisa naomba unipeleke kwa boss Erick ili nikamsalimie”
“Oooh vizuri sana, nafurahi kusikia hivi”
Muda kidogo alifika mgeni mwingine kwenye ofisi ya baba Angel, mgeni huyu alikuwa ni Juma ambaye alifika na kuwasalimia kisha kuanza kuongea pale,
“Yani dunia ina mambo yaliyojificha sana, mimi sikujua kama kuna ndugu yangu huyu. Nafurahi kukufahamu Juli”
Walipongezana pale, kisha Juli alihitaji kupafahamu nyumbani kwa baba Angel sababu aliwahi kuongea na mke wake,
“Nahitaji kumfahamu na yeye anifahamu maana kipindi kile alinihisi vibaya sana”
“Sawa, basi nikitoka tu ofisini hapa tutaenda wote nyumbani kwangu”
Kisha Juli na mama yake walitoka kwanza kumsaidia mama yake kuweka matunda vizuri kwanza, halafu baba Angel alibaki pale na Juma huku wakiongea,
“Unajua Erick ni bondia sana”
“Umeanza Juma”
“Kweli, nilimshuhudia pale dukani kwako akimpiga mtu mmoja dah!! Erick ni bondia, ana nguvu ambazo niliwahi kusikia kuwa babu yangu anazo”
“Kwahiyo bado una wazo kuwa Erick ana husiana na wewe!!”
“Hapana, nimesema tu. Siwezi sema nahusiana na Erick maana mimi sijawahi kuwa na mke wako hata mara moja”
“Haya, ngoja nimalize kazi kwanza”
Baba Angel alimaliza kazi zake na moja kwa moja kuondoka na Juma, pamoja na Juli na mama yake kuelekea nyumbani kwake.

Muda huu Erick alikuwa dukani kwa baba yake ambapo alikuwa akiongea na Rama kuhusu kilichoendelea baada ya siku ile,
“Kitu gani kilitokea? Wale watu walirudi tena?”
“Hapana, sikuwaona wala nini”
Muda kidogo kuna mteja alifika pale dukani kwa baba Angel na kuanza kuulizia baadhi ya vitu, ila Erick alimfata huyu mtu na kumuuliza,
“Jina lako nani?”
“Kwani unanijua?”
“Nakujua ndio, unaitwa nani?”
Huyu mtu alihofia kidogo na kutoka mule dukani kwa kasi halafu akaondoka zake, ila kitu ambacho hakukifahamu ni kuwa Erick alikuwa akimfatilia kwa nyuma, alipofika tu nyumbani kwake alishangaa nuona Erick nae amefika basi huyu mtu aliogopa hata kutoka ndani ya gari lake, ila Erick alisogea karibu na gari la huyu mtu na kuvuta mlango ambao ulifunguka na kumtoa huyu mtu nje, akamkaba na kumuuliza tena,
“Ni nani wewe?”
“Aaaah, mimi ni dokta”
“Dokta huna jina?”
“Naitwa dokta Jimmy”
“Huwa nasikia baba akikutaja taja sana sijui umemfanyia nini na siku ile ambayo baba alitekwa ni wewe nilikukuta lile eneo la tukio”
Kisha Erick alimpa ngumi ya mdomo dokta Jimmy kiasi cha kumfanya kuanza kutoa damu mdomoni ila Erick hakujali kitu chochote kile zaidi ya kumshindilia ngumi nyingine, halafu akamwambia,
“Maswala ya wewe kufatilia familia yangu sitaki kabisa kusikia, nikiona baba akilalamika tena kuhusu wewe utanitambua mjinga mmoja wewe”
Kisha Erick alimpiga mtama dokta Jimmy na kumfanya aanguke chini halafu alienda na kumpiga teke ambalo lilienda kumuangusha karibu na getini kwake. Halafu Erick akaenda kupanda pikipiki yake na kuondoka maana kwa kipindi hiko alikuwa akitumia zaidi usafairi wa pikipiki.

Usiku wa leo, baba Angel anapigiwa simu na Jack ambapo anapokea na kuanza kuongea nae,
“Tutaenda kumuona kesho, kwahiyo sio Jumamosi bali ni kesho”
“Sawa hakuna tatizo, utaniambia muda na mahali pa kuelekea”
“Nakutumia kwenye ujumbe”
Muda kidogo ujumbe ulitumwa ambapo baba Angel aliusoma na kufuta ujumbe ule kwani hakutaka mkewe aone ule ujumbe wa kwenye ile simu. Kisha aliendelea na maongezi mengine na mke wake,
“Kwahiyo yule wa leo ndio alikuwa Juli yule aliyekuwa akikufanyia usafi?”
“Ndio, ni yule, ndiomana siku ile nilikwambia mke wangu usiwe na mashaka, huyu ni mama mwenye heshima zake. Ndiomana na yeye ametaka kuja kukusalimia”
“Yule Juma nae ana kiherehere, sasa kilichomleta na yeye ni kitu gani?”
“Unajua yule ni ndugu yake!! Yani ni ndugu yake kabisa, kwahiyo usishangae kwa yeye kuja pamoja nao wale”
“Sasa mbona alikuwa na haraka sana ya kuwaharakisha wenzie kuondoka?”
“Aaaah yule Juma mzoee tu hata usiwe na shaka nae”
Waliongea ongea kupoteza muda tu kwa usiku ule.

Muda huu baba Angel alijiandaa, kisha akaondoka nyumbani kwake na kumpigia simu Rahim huku akimwambia mahali pa kukutana, yani bado alikuwa na imani kuwa yule mtoto ni mtoto wa Rahim.
Wakakutana na kisha kukutana na Jack na mtoto wake halafu wakaanza kuondoka, Rahim aliamua kuuliza,
“Kwani tunaenda wapi?”
“Huyu kijana kazalisha bhana, ndio tunaenda kumuona mtoto kama wazazi”
“Kheee na mimi ndio nimewekwa kwenye kundi la wazazi?”
“Ndio kwani kuna ubaya, hebu ona mtoto ulivyofanana nae Rahim yani ni wewe mtupu”
“Halafu huyu kijana hata hamjanitajia anaitwa nani”
Jack aliyekuwa kimya tu, akasema
“Anaitwa Derrick”
Baba Angel akashtuka kidogo maana hakujua jina la huyu mtoto, akamuuliza kwa makini Jack,
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa Derrick, nilimpa jina ili aendane na wewe. Kwahiyo ni Derrick Erick”
“Duh!”
Baba Angel alipumua tu na walifika mahali walipokuwa wanaenda, ila muda wote huyu kijana Derrick alikuwa kimya kabisa, inaonyesha hata yeye hakuwaelewa hawa watu maana aliambiwa mmoja ni baba yake ila hakuona huyu mtu akijali lolote.
Walipoingia kwenye hiyo nyumba ndipo Rahim alipopatwa na mshtuko, mara kuna mama alitoka ndani ya ile nyumba na kusogea karibu na Rahim kisha akamnasa kibao yani kila mtu alikuwa akishangaa kwanini huyu mama kamnasa kibao Rahim.

Walipoingia kwenye hiyo nyumba ndipo Rahim alipopatwa na mshtuko, mara kuna mama alitoka ndani ya ile nyumba na kusogea karibu na Rahim kisha akamnasa kibao yani kila mtu alikuwa akishangaa kwanini huyu mama kamnasa kibao Rahim.
Kisha yule mama alianza kumwambia Rahim,
“Mjaa laana wewe, ulimkimbia mwanangu toka akiwa na mimba haya leo nini kimekuleta?”
“Dah!! Nisamehe”
“Nani akusamehe? Mjinga sana wewe, umekuja kufanya nini? Ndio umekuja kumuona mjukuu wako? Na mjukuu mwenyewe alivyokufanana ni balaa”
Basi huyu mama alimshika mkono Rahim na kumuingiza ndani na hawa wengine walibaki kushangaa tu kuwa ni kitu gani kinaendelea.
Moja kwa moja Rahim aliingizwa ndani ambapo palikuwa na binti amepakata mtoto mchanga akimnyonyesha, huyu mama alimwambia Rahim
“Haya sasa, umemuona binti yako na mjukuu wako!! Maana huyu binti hujawahi kumuona toka mama yake akiwa na mimba ya miezi sita, ukakimbia mazima, haya muone sasa”
Rahim alibaki kutoa mimacho tu, huyu mama aliangalia wale waliokuja na Rahim na kumtambua Erick,
“Kheee Erick!! Mbona leo makubwa haya, unanikumbuka mimi lakini? Umekuwa mbaba siku hizi!”
“Nakukumbuka ndio, wewe si mama mdogo wa Sia”
“Oooh kweli unanikumbuka jamani, umemtoa wapi huyu kiumbe mjinga aliyekimbia mtoto wake!! Mwanaume mjinga sana huyu, hivi mtu unawezaje kukimbia mtoto wako eeeh!! Haya angalia sasa hadi linaona aibu”
Sasa ilibidi Erick aulize vizuri,
“Kwahiyo, huyu kijana ndio amezaa na huyu binti”
Akimuonyeshea Derrick, hapo yule mama akamuangalia na Derrick pia maana hakuwahi kumuona, basi alihamaki na kusema,
“Kheee mbona kijana mwenyewe kafanana na huyu mjinga Rahim? Inamaana watoto wa Rahim mmetembeleana na kuzaa!”
Huyu mama alipiga makofi na kucheka kisha akakaa chini na kusema,
“Dunia ndogo hii, huwa watu mnaona dunia ni kubwa sana huenda mkajificha na maovu yenu ila hii dunia ni ndogo sana. Ona kilichotokea sasa, watoto wa baba mmoja mjinga wameenda kuzaa na kuendeleza kizazi, na mimi nawaambia hivi wajukuu zangu mmepata baraka zote kutoka kwangu, mtaoana tu hakuna cha ndugu wala nini, hii ndio dawa ya wanaume wakware”
Kwakweli Rahim alikuwa kimya tu ni kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi yani alikuwa ni kama anashangaa kila kitu kinachoongelewa, kisha yule mama akaongea tena,
“Yani Rahim limekushuka shuu, umekuwa mdogo kama piritoni hapo ulipo mbele huchezi na nyuma hutikisiki, ulikuwa unanikera nikikukumbuka wewe mjaa laana loh!! Nasema hivi mjukuu wangu hata mahari sitaki, semeni tu lini mnaenda kuanza kuishi pamoja. Liacheni libaba lenu hili lililojaa laana mpaka kwenye unyayo, mjinga sana wewe, hodari kuwaambia wanawake wakuzalie halafu hodari kwa kukimbia watoto.”
Yani kwa ufupi hata walishindwa kufanya mazungumzo yoyote pale, Rahim alimshika mkono baba Angel na kutoka nae nje ili waweze kujadiliana maana hakuelewa kabisa,
“Unajua hapa nilipo sielewi kitu?”
“Kwani huyu mama unamjua kweli?”
“Ndio, niliwahi kuwa na mahusiano na binti yake, nakumbuka vizuri nilimuacha akiwa mjamzito”
“Kheee basi shughuli ipo”
“Ila huwezi amini, Erica ndio alifanya mimi nimuache huyu mwanamke”
“Halafu na Erica mwenyewe ulimuacha akiwa na mimba, nahisi una aleji na wanawake wenye mimba wewe”
“Lakini yule mama sio muelewa, kaniparamia tu kuwa yule ni mtoto wangu pia. Mmmmh au kweli yule kijana ni mtoto wangu!! Naanza kupata mashaka, inabidi mniruhusu nikapime na yule kijana, ila kama wote ni watoto wangu nitafanyaje? Mbona kichwa kinaniuma jamani. Ya Angel na Samir hayajaisha halafu linaibuka hili lingine uwiiii mimi jamani nitajificha wapi. Naondoka Erick”
Rahim alimuacha baba Angel pale na kuondoka zake maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa kwa muda huo, baba Angel nae alijikuta akikosa maamuzi sahihi na kutaka kuondoka ila aliamua kumuita Jack kwanza na kuongea nae pale nje,
“Samahani Jack, mimi naomba niende”
“kwahiyo unaniacha peke yangu na mtoto!!”
“Hivi Jack, hukusikia kile kilichokuwa kinaendelea au kitu gani?”
“Nimesikia vizuri, alikuwa akisemwa yule mwenzio kwani ni wewe uliyekuwa unasemwa? Ukweli wa mtoto tunao mimi na wewe”
“Hapana, ukweli unao wewe. Si unaona hata yule mama alipomuona kijana wako Derrick kashtuka na kusema ni mtoto wa Rahim, ni wazi kuwa mwanao kafanana sana na Rahim. Hebu jaribu kuchunguza hili”
“Nichunguze kitu gani wakati mimi najua kuwa baba wa mtoto ni wewe!!”
“Basi Jack, naomba uniruhusu niondoke halafu kesho tutaonana na tutaongea vizuri, sawa”
Jack hakuitikia ila alimuangalia tu baba Angel ambaye aliondoka zake kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 411


Baba Angel alipotoka pale moja kwa moja alipitia kiwandani na kuanza kukagua maana ni muda mrefu hakuja kwenye kiwanda chake, mara nyingi alikuwa ofisini kwake kwahiyo huku kiwandani ni Erick tu ndio alikuwa anakuja.
Basi alitembelea na kwenda kuongea na meneja wa kiwanda chake yani Yuda, alimkuta mkononi kafunga hogo yani mkono unaning’inia tu, ikabidi baba Angel amuulize,
“Tatizo nini Yuda?”
“Kwani hujaambiwa?”
“Niambiwe na nani?”
“Shughuli ya Erick hii”
“Kheee Erick!! Ilikuwaje tena?”
“Dah!! Sina hata cha kusema, ila bora hapa ofisini uwe unakuja mwenyewe, zamani tulikuwa tunaona Erick mpole sana kumbe ni tofauti hakuwa mpole wala nini. Humo kiwandani wafanyakazi wote hao wanamuogopa Erick balaa”
“Kwani ilikuwaje?”
“Aaaah mimi sijui ila alinikunja mkono tu na kusema ananipa onyo, yani mkono umeniuma sana, nimeenda hospitali ndio nimefungwa hilo hogo”
“Duh!! Pole sana. Kwakweli sikuwa nafahamu hayo kabisa”
“Yani mwanao siku asipokuja basi wafanyakazi wote hapa huhisi kufanya sherehe, mwanao ni mkali hatari”
“Ila naona kiwanda kimeendelea, ufanisi wa kazi umeongezeka”
“Ni kweli, Erick hataki masikhara kabisa, mtu akiharibu kumwambia sitaki kukuona kazini kesho kwake ni kawaida, kwahiyo wafanyakazi wengi wamekuwa makini. Kwa hilo nampongeza sana ila apunguze ukali wake”
Baba Angel aliahidi pale kuwa atazungumza na kijana wake, kisha alivyoondoka hapo moja kwa moja alienda dukani kwake napo kuangalia kuwa kuna nini kinaendelea katika duka lake.
Basi alivyofika kule alimkuta Rama na kumuuliza maendeleo ya pale,
“Bosi, jana kuna mteja alikuja hapa na alikuwa akiulizia bidhaa vizuri tu. Mara alitokea Erick na kumfata yule mteja huku akimuuliza kuwa anaitwa nani, yule mteja naona aliogopa na kuamua kuondoka ila Erick alimfatilia na pikipiki yake, sijui ni kitu gani kilitokea huko ila Erick hakurudi tena hapa”
“Khaaa sasa Erick kavuka mipaka sasa, ubondia hadi kwa wateja jamani!”
“Ndio hivyo bosi, na sijui kwanini Erick hakumtaka yule mteja. Mbona wengine huwa anawahudumia mwenyewe na huwa wanampenda sana na kumuulizia kila wanapokuja ila nashangaa sana kwa mteja wa jana”
Baba Angel hakutaka kuongea sana ila aliona kuwa kuna ulazima wa yeye kuongea vizuri na Erick maana aliona kuwa amevuka mipaka. Kwahiyo aliondoka hapo dukani na kuelekea nyumbani kwake.

Baba Angel alifika nyumbani kwake wakati giza tayari lilikuwa limeshatanda, ila alivyofika tu moja kwa moja alihitaji kuongea na Erick, kwahiyo aliulizia kuwa Erick yuko wapi,
“Khaaaa mbona Juma alikuja kumfata Erick muda ule ule ulipoondoka wewe”
“Kheee kaenda nae wapi? Mbona hajaniambia?”
“Nikajua mliongea maana jana mlikuwa wote, kwahiyo Juma aliondoka na Erick na bado Erick hajarudi hapa nyumbani”
“Duh!! Na Samir je?”
“Samir aliondoka pia, alisema anaenda kwa mama yake”
“Aaaah mbona hajaniaga na yeye!!”
“Unadhani mtoto wa mwenzio ni sawa na mtoto wako!! Yeye anajichukulia maamuzi yake mwenyewe, nadhani mimi kaniaga sababu nilikuwa hapa nyumbani”
“Aaaah sawa hakuna tatizo, kama mama yake na baba yake wamepatana basi sawa”
“Hivi yule dokta Maimuna anajua kweli kama sisi ndio wazazi wa Angel?”
“Sidhani kama anajua, kumbuka hata sisi tumejua baada ya kuwaona kwenye mahafali, kwahiyo sidhani kama anajua”
Basi wakaacha ile mada na kuendelea na mambo mengine, hadi baba Angel aliamua kulala bado Erick alikuwa hajarudi, ilibidi mama yake tu ndio amsubiri kwanza arudi nyumbani.

Erick alifika nyumbani kwenye mida ya saa tano usiku, kwakweli mama yake hakupenda na alimsema kwa tabia hiyo,
“Sijapenda kabisa Erick, siku hizi umefanya kama mazoea ya kunirudia usiku kwanini lakini?”
“Nisamehe mama”
“Huangalii muda huko unapokuwa? Unafanya roho yangu iwe juu juu muda wote, yani sijapenda kabisa kabisa, halafu mtu mwenyewe uliyeondoka nae ni Juma, kumbe hata ruhusa kwa baba yako hajaomba. Hiyo tabia isijirudie tena”
“Sawa mama”
Basi moja kwa moja Erick alipitiliza chumbani kwake, alioga na kulala ila muda kidogo Erica alienda chumbani kwa Erick na sahani ya chakula kisha akamuamsha na kumtaka ale,
“Umejuaje kama sijala Erica?”
“Najua tu kama hujala, mama kakusema na wewe hupendi kusemwa. Una hasira za karibu sana Erick, ila mimi nakuomba ule hiki chakula nilichokuletea”
Basi Erick alikaa na kaunza kula kile chakula huku akiongea na dada yake,
“Mlienda wapi leo Erick?”
“Aaaah yule jamaa unajua ananipelekaga kwenye vitu vya hatari sana”
“Vitu gani?”
“Tulienda huko kwenye mizinga ya nyuki eti kumsaidia kupakua asali”
“Mmmh nyuki hawajakuuma kweli?”
“Wala hawajaniuma, nilikuwa naogopa ila nikajipa ujasiri tu, kisha akanielekeza cha kufanya basi nikawa nafanya nae”
“Hukuogopa kweli!! Nyuki naogopa mimi”
“Hamna hata hawafanyi kitu, tutapanga siku twende pamoja”
“Sawa Erick”
Erick aliendelea kula ila kuna muda alikuwa akiona uvivu kubeba kijiko na kula chakula, basi Erica akajitolea kumlisha kwa muda huo kwani alikuwa akijua wazi kuwa kaka yake hajashiba kile chakula, muda kidogo akaingia baba yao mule chumbani kwa Erick na kumkuta Erica ndio akimlisha Erick chakula, kiukweli baba Angel alichukia sana na kuwauliza,
“Ndio mambo gani hayo?”
“Erick amechoka kubeba kijiko baba, ndio namsaidia kumlisha”
“Huyo wa kumpiga kila mtu ndio achoke kubeba kijiko tu! Nyie watoto jamani, msitutie simanzi wazazi wenu, kumbuka tunawapenda sana. Hii imezidi sasa ila nitajua tu cha kufanya, haya Erica nenda chumbani kwako.”
Ikabidi Erica aache kumlisha Erick na kuondoka zake kisha baba Angel alimwambia Erick,
“Kesho nina maongezi na wewe”
halafu baba Angel alitoka zake na kurudi chumbani kwake tu kwa muda huo.

Baba Angel alimwambia mkewe ndani,
“Ni bora tu ningeendelea kulala kuliko niliyoenda kuyashuhudia huko”
“Yapi tena hayo?”
“Nimekuta Erica akimlisha chakula Erick, jamani hawa watoto kwasasa wamevuka mipaka. Hivi hawakufanya kweli hawa?”
“Mmmmh inawezekana wamefanya, labda tunafuga viwapenzi humu ndani, aibu yetu ni kubwa mno.”
“Sasa tufanyaje mama Angel?”
“Mmmh sijui yani watoto wananipa mawazo hawa hatari”
“Unaonaje tukimtafutia Erica shule ya bweni huko awe harudi hapa nyumbani maana naona hii ya kurudi inampa kiburi sana”
“Mmmmh hiyo ya bweni si ndio atarudi na akili kama za dada yake Angel, maana karudi na msemo wake tumefundishwa kujiamini, yani mitoto isiyojua kutafakari ni shida tupu”
“Basi, ngoja tufikirie mambo mengine, maana naona akili yangu haifanyi kazi vizuri kabisa”
Baba Angel aliamua kulala tena kwa muda huo, ila muda kidogo alikuwa akipigiwa simu, alipoangalia aliona ni Jack ndio aliyekuwa akipiga ile simu basi alikuwa akiikata na mwisho wa siku akaizima kabisa maana ulikuwa ni usiku na hakutaka mkewe amfikirie vibaya.

Asubuhi na mapema, baba Angel kama alivyopanga alimuita Erick ili aongee nae kuhusu swala lake la kupiga hadi wateja na swala la kupiga Yuda,
“Erick mwanangu, nimeenda jana kiwandani nimemkuta Yuda ana hogo, tatizo ni nini kwani? Kwaniniumempiga?”
“Baba, yule Yuda alikuwa na mtindo mchafu, alikuwa akitoa bidhaa kwa njia za panya na kwenda kuziuza huko. Sasa nilipomgundua ndio nikampa onyo”
“Kwahiyo pale umempa onyo!!”
“Ndio, sijampiga yule, nimempa onyo tu”
“Duh!! Ila Erick sijapenda, unapiga hadi wateja”
“Mteja gani baba?”
“Juzi dukani, nasikia umemtisha sana mteja”
Simu ya baba Angel ilianza kuita muda ule kwahiyo baba Angel aliacha kuongea na Erick kwanza na kupokea ile simu na kuanza kuongea nayo maana aliyekuwa akipiga alikuwa ni madam Oliva,
“Hivi unakumbuka kuwa ni leo ndio tulipanga kuonana na dokta Jimmy!”
“Oooh umenikumbusha, yani nilishasahau, ngoja nimtafute nijue pa kukutana nae.”
“Pa kukutana nae wapi? Huyo dokta Jimmy yupo hoi nyumbani kwake”
“Anaumwa nini tena?”
“Nimempigia simu anasema kuwa kuna mtu kampiga sana, kwahiyo hali yake sio nzuri hata ongea yake ni ya shida”
“Duh!! Na yeye kapata kiboko yake kumbe!! Ila ni jambo la muhimu sana kuongea nae”
“Ndio hivyo haiwezekani ila yeye anasisitiza kuusema ukweli wote, nadhani tu tupange siku twende kwake ili tukaongee nae pale pale wala huo ugonjwa usiwe kisongizio”
Basi madam Oliva alikata ile simu halafu baba Angel alitabasamu kidogo maana kusikia kuwa dokta Jimmy kuna mtu kampiga kwake ilikuwa amani, ukizingatia alijikuta huyu dokta hampendi tu kwa yale aliyomtendea. Kisha baba Angel akauangali Erick na kumuuliza tena,
“Eeeeh hatujamalizana, kwanini umpige mteja”
Erick alimsimulia baba yake ilivyokuwa hadi alivyomfata huyo mteja, yani baba Angel alijikuta baada ya maelezo haya akifurahi sana, hata hakumuuliza swala lingine Erick ila moja kwa moja alienda kwa mke wake na kuongea nae,
“Hatimaye zile dawa walizozifanya kwa watoto wetu zimeenda kuwarudi wenyewe”
“Kivipi?”
“Nasikia Erick kampa kichapo dokta Jimmy kiasi kwamba dokta Jimmy hawezi kwenda popote pale, anaongea kwa shida tu. Hakuna siku niliyofurahi kama leo, nilikuwa nahitaji sana dokta Jimmy aingie kwenye anga za Erick na hatimaye kaingia na kapata kichapo chake. Kumbe yeye ndio alikuwa mteja”
“Mmmh alikuwa mteja kweli au alikuwa na mambo yake!! Mbona bora jamani, simpendi yule baba hatari”
Baba Angel alicheka tu na kwenda kujiandaa kwaajili ya kutoka tu kwa muda huo.

Baba Angel alienda moja kwa moja ofisini kwake kwa muda huo ila alipofika tu alianza kupigiwa tena simu na Jack,
“Kwani uko wapi baba Derrick”
“Duh!! Nishakuwa baba Derrick tayari”
“Acha masikhara jamani, sasa unadhani nimezaa na nani mimi? Unajua unanichanganya sana Erick jamani!!”
“Basi yaishe, nipo ofisini kwangu muda huu”
“Ila kwanini unanifanyia hivi Erick? Kwanini lakini, simu zangu unakata, hutaki kuongea na mimi unachonifanyia sio kizuri kabisa. Naomba nielekeze ofisini kwako basi ili niweze kuja tuzungumze”
“Sawa nakuelekeza, huwezi potea maana sio mbali wala nini”
“Sawa, hakuna shida nasubiri”
Basi baba Angel akamtumia Jack maelekezo ya ilipo ofisi yake kisha aliendelea na kazi zake.
Ila mpaka muda baba Angel anamaliza kazi zake hakuweza kumuona Jack wala nini, akaamua kumpigia simu mwenyewe ili aongee nae,
“Mimi ndio nataka kuondoka Jack, au utakuja kesho?”
“Kesho utakuwepo ofisini?”
“Hapana, kesho nitakuwepo nyumbani labda uje kesho kutwa”
“Basi nielekeze nyumbani kwako”
“Aaaaah hiyo ni ngumu Jack, unajua mke wangu hajui kitu chochote kuhusu mimi na wewe!”
“Ila ndio anapaswa kujua hivyo, una nini lakini Erick jamani. Tena nyumbani kwako ndio itakuwa vizuri ili nimlete Derrick aonane na ndugu zake”
“Aaaah Jack, sikia basi, tutawasiliana tu kesho halafu mimi kesho kutwa nitakufata mwenyewe tuongee”
“Kwani kuna nini nikija nyumbani kwako Erick?”
“Sio kwasasa Jack, nakuomba sana utakuja siku nyingine. Mimi na wewe tutaongea Jumatatu”
Baba Angel alikata ile simu na kupumua kidogo huku akisema,
“Huyu mwanamke anataka kuniletea balaa huyu, anataka kukumbusha mambo ya zamani yaliyopita, namshangaa kuzidi kukazana kuwa mtoto ni wangu wakati picha halisi ya yule mtoto inaonekana kuwa ni mtoto wa Rahim. Au ananichezea mchezo huyu na Rahim wana lengo la kugombanisha ndoa yangu!”
Baba Angel aliamua kufunga kazi na kuondoka zake kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.

Erick, leo alikuwepo tu nyumbani na dada zake akiongea nao kuhusu vitu mbalimbali maana leo ilionyesha kuwa ana furaha tofauti na siku zingine, hata Angel alimuuliza Erick,
“Mbona leo una furaha sana?”
Sarah akasema,
“Huyu anatakiwa kuwa na furaha siku zote maana amezungukwa na wadada, anakosaje furaha? Na sasa nimeongezeka na mimi?”
Angel alimuuliza Sarah,
“Yale mashetani yako ya kumtaka Erick umeyaacha eeeh!!”
“Aaaah nitamtaka vipi wakati nijua ukweli kuwa ni ndugu yangu!! Sina sababu ya kuendelea kumtaka ndugu yangu. Ila jamani tuongee ukweli, Erick ni mzuri jamani halafu ana mwili wa kiume”
“Mmmmh na wewe Sarah una mambo, kwani kuna wanaume wana mwili wa kike?”
“Ndio, wapo wengine wamelegea sana”
“Mfano kama nani?”
Erick aliamua kuwabadilishia stori, yani siku hii walionekana kuwa na furaha sana. Hata mama Angel alipowaangalia alihisi raha moyoni mwake kwani siku zote alikuwa akitamani kuona watoto wake wakiwa na furaha, hasa alikuwa akipenda kuona wakipatana sana na Sarah maana hata Sarah alimuweka kama moja ya familia yake, kwahiyo ile hali aliifurahia sana.
Muda kidogo alifika mgeni ambaye alikuwa ni Sia, basi mama Angel aliamua kwenda kuongea nae ili kujua ni kitu gani kimemleta pale kwake,
“Eeeeh Sia, niambie”
“Nimekutana na Manka”
“Eeeh anasemaje?”
“Unajua Manka ni kama amechanganyikiwa kwasasa eeeh!! Hajielewi kabisa yule mwanamke, bado anakazana kuwa Sarah ni mwanae pia wakati Sarah ni mtoto wa Oliva”
“Ila na wewe muda mwingine umezidi, kama siku ile ulichokifanya hata sijakipenda, mtu gani umemkuta tu hapa madam basi kuropoka ndio moto, yani wewe mambo yako jamani unajijuaga mwenyewe”
Mara simu ya Sia ilianza kuita na hapo baada ya Sia kuongea nayo tu akamuaga mama Angel na kuondoka zake.

Usiku wa siku hii baba Angel na mama Angel walikuwa chumbani wakijadili kuhusu kesho yake,
“Mmmh kesho twende Kanisani mume wangu, unajua hatujaenda siku nyingi!!”
“Halafu kweli mke wangu, hatujaenda siku nyingi kweli sijui siku hizi tumepatwa na kitu gani”
“Watoto leo walikuwa wamepatana sana hadi raha, nimefurahi kwa wanangu kuongea vizuri na Sarah”
“Aaaaah yule mtoto yupo vizuri, mwanzoni hakufundishwa vizuri tu. Saivi nimemuona amekuwa na adabu sana”
Walijikuta wakiongea mengi tu kwa siku hii na kuamua kulala.
Kulipokucha tu, mapema kabisa baba Angel alipata ujumbe kwenye simu yake na kuamua kuusoma, ujumbe ule ulitoka kwa Jack ukisema,
“Jana, nilikuja ofisini kwako nimekufatilia hadi nyumbani kwako. Nashukuru sana nimepafahamu nyumbani kwako kwahiyo nitarajie kwa siku yoyote na muda wowote kuja hapo, mwambie kabisa mke wako kuhusu uwepo wangu”
Baba Angel alishtuka kidogo na kutoka nje kisha akampigia simu Jack ambaye alipokea na kuanza kuongea nae,
“Una nini lakini Jack? Wewe ni mwanamke muelewa, kwanini unataka kufanya ujinga wa namna hiyo?”
“Huu sio ujinga, kwanini hutaki mkeo ajue ukweli? Kwanini unaficha Erick? Mimi nitaendelea kumficha huyu mtoto hadi lini?”
“Naomba tukutane tuongee Jack”
Jack akakata ile simu, baba Angel akafikiria kwa muda kidogo kama kweli amwambie mkewe kuhusu swala lile, yani hakuelewa hapo.
Baba Angel alirudi chumbani ambapo mke wake alikuwa akijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye Ibada, kisha baba Angel alikaa kwanza ambapo mkewe alimuuliza,
“Tatizo ni nini mume wangu? Jiandae basi twende”
“Unafikiri najisikia! Yani sijui leo nipoje”
“Sio leo upoje, kwasasa huwa sikuelewi maana kuna simu Fulani hivi huwa unaongea nayo kwa siri halafu ukimaliza kuongea nayo huwa sikuelewi kabisa, huwa sikuulizi tu ila najua wazi kuwa haupo sawa, tatizo ni kitu gani”
“Basi njoo tukae ili tuweze kuzungumza kuhusu hili jambo”
Mama Angel alikaa ila baba Angel alimwambia mama Angel kuwa wakanywe chai kwanza halafu ndio waongee vizuri kuhusu hilo analotaka kumwambia, kwakweli mama Angel alimshangaa sana mumewe.

Leo mamake Samir yani dokta Maimuna alijiandaa na Samir kwani alitaka mwanae ampeleke huko kwa wazazi wa Angel ambapo ndio alikuwa akiishi huko, Samir alikubali. Kisha na mama yake waliondoka kwao na kuanza safari ya kwenda kwakina Angel.
Samir na mama yake walifika pale ila mama yake alishangaa kidogo maana pale alikuwa akipafahamu vizuri sana, ila hakuongea kitu chochote kile na moja kwa moja wakagonga geti na kuingia ndani.
Na hapo walifika kugonga mlango wa ndani hodi, alitoka Erica na kuwafungulia ila wakati wanaingia tu ndipo Jack nae alipofika mahali pale na mtoto wake Derrick.

Samir na mama yake walifika pale ila mama yake alishangaa kidogo maana pale alikuwa akipafahamu vizuri sana, ila hakuongea kitu chochote kile na moja kwa moja wakagonga geti na kuingia ndani.
Na hapo walifika kugonga mlango wa ndani hodi, alitoka Erica na kuwafungulia ila wakati wanaingia tu ndipo Jack nae alipofika mahali pale na mtoto wake Derrick.
Kisha Maimuna na Jack walitazamana kwa muda kidogo ambapo Jack alimwambia Maimuna,
“Wewe si ndio dokta Maimuna!!”
“Ndio ni mimi”
Basi Maimuna na Jack walikumbatiana pale, muda huo Erica nae alikuwa anaendelea kuwakaribisha kiasi kwamba baba yake na mama yake walikuwa wakishangaa kuwa huyu Erica anawakaribisha wakina nani, baba Angel akainuka kwenda kuangalia kuwa ni kitu gani kinaendelea, alipomuona Jack na Maimuna moyo wake ulifanya paaa, na kilichomshtua zaidi ni kumuona Jack maana hakutegemea kama Jack angefika pale kwao, basi alitoka nje kwa haraka ili aweze kuongea nao ila mkewe nae alikuwa ametoka pia.
Kwahiyo hakuwa na namna zaidi ya kuwakaribisha tu, ila baba Angel alijua wazi kuwa lazima hapo kitanuka tu na hakutaka watoto wasikie, kwahiyo aliwaomba hawa wakaongee kwenye bustani ambapo Mimuna aliuliza,
“Kwani unajua kilichotuleta? Yani mfano mimi unajua ni kitu gani kimenileta?”
“Hapana, ila twendeni tukaongee pale maana hata nimeshangaa kuwa mnafahamiana”
Waliongozana tu mpaka kwenye bustani, muda huo wote mama Angel alikuwa akishangaa tu kwani hakuelewa chochote kile kilichokuwa kikiendelea.

Wakina Samir pamoja na yule Derrick ilibidi tu waingie ndani na kukaa pale sebleni pamoja na wenzao wengine, huku Derrick akijitambulisha kwao hawa halafu na wao wakijatambulisha majina yao kwake,
“Nashukuru kuwafahamu”
Basi Samir akamwambia Derrick,
“Dah!! Umefanana sana na baba yangu, yani baba yangu ni kopi yako kabisa”
Angel nae akadakia,
“Kumbe na wewe umeona eeeh!! Kafanana sana na baba yako, halafu na yule ndugu yako Muddy kafanana nae sana.”
Derrick alicheka tu jinsi alivyofananishwa na watu wale kisha akawaambia,
“Huyo mnayemsema nimeonana nae na kila mtu ananifananisha nae, mwanzoni nilikuwa simjui basi watu wengi walikuwa wakisema kuwa nafanana na Rahim nilibaki kuwashangaa tu ila kwasasa nimemjua na kweli nina fanana nae”
Samir akamuuliza,
“Au ni ndugu yetu wewe, maana mimi ni mtoto wa Rahim!”
“Aaaah, baba yangu mimi anaitwa Erick”
Wote ndani walishtuka na kumuangalia vizuri, pale alikuwepo na Sarah ambaye alishangaa kwa sauti na kusema,
“Kheeee, mbona wewe kama mwarabu!!”
Kisha Sarah akajijibu mwenyewe,
“Ila hata dada Angel nae ni mwarabu.”
Samir akasema,
“Watoto wababa wote ni waarabu kasoro mimi tu”
Ndipo Erica alipouliza,
“Kwani da Angel ni mtoto wa baba yako pia?”
Angel aliamua kubadilisha mada na kuwauliza wanapenda sinema gani ili waweze kuangalia kwa muda huo kuliko kuongelea yale waliyokuwa wakiongelea maana hakuona kama yana umuhimu kwa muda ule.

Walipofika kwenye bustani mama Angel aliwakaribisha pale ila alihitaji utambulisho hasa kwa Jack maana hakumfahamu, baba Angel aliomba kuwa akaongee pembeni kidogo na Jack ila Jack aligoma na kusema,
“Pembeni tukatafute nini Erick? Hukuamini kama nitakuja nyumbani kwako au nini? Sina nia ya kuharibu familia yako ila nina nia ya mwanangu kuwatambua ndugu zake”
Hapo baba Angel aliamua kuwa mpole tu, kisha alimuuliza Maimuna,
“Na wewe dokta!”
“Mimi nilikuja hapa na mwanangu Samir, nia yangu ni kuangalia sehemu aliyokuwa anaishi, nimeshangaa kukuta kuwa alikuwa anaishi hapa. Kumbe yule Angel niliyekuwa namsikia ndio mtoto wa Rahim!!”
Mama Angel alijibu tu kwa taratibu,
“Ndio”
“Kumbe mlizaa na mume wangu, mbona ulikuwa ukificha jambo hili mama Angel! Siku zote ulikuwa rafiki yangu mkubwa sana, ila nilishangaa siku uliyomuona mume wangu pale hospitali ukapotea kimoja.”
Halafu dokta Maimuna akamuangalia Jack na kumuuliza,
“Mwanao yuko wapi?”
“Si ndio yule niliyekuwa nimeongozana nae! Nadhani yupo kule kunisubiria, huyu ndio mwanaume niliyezaa nae”
Kwakweli mama Angel alikuwa haelewi kitu kwa muda huo, alikuwa akimuangalia tu mume wake ambapo baba Angel aliamua kusema,
“Sikia Jack, umechukua uamuzi wa haraka sana kufika nyumbani kwangu, kwanza sijajiridhisha kuwa yule ni mwanangu. Dokta Maimuna, wewe ni daktari, nenda kamthaminishe yule mtoto vizuri uone kama kafanana na mimi. Mtoto kafanana na Rahim kwa kila kitu halafu uje nyumbani kwangu na kusema kuwa ni mwanangu! Nilikwambia tuongee kwanza Jack ila ukawa mbishi, hivi unadhani kwa stahili hii ndio kitu gani utakuwa umefanya sasa?”
Dokta Maimuna alipumua kidogo kwanza, na kuwaangalia ambapo mama Angel aliuliza,
“Mnajua siwaelewi, hebu nielewesheni”
“Ni hivi, mimi nilikuwa na mahusiano na Erick kipindi yupo Afrika kusini na aliniacha na ujauzito halafu akaja huku, nilizaa mtoto na kumlea mwenyewe, na sasa mtoto amekua anamuhitaji baba yake, ndio nimemleta”
Mama Angel alimuangalia vizuri huyu dada, alijikuta akikumbuka kipindi akiwa chuo aliwahi fatwa na Tumaini na kuambiwa kuwa baba Angel yani Erick anamchumba Afrika Kusini na amepanga kumuoa mchumba wake huyo, kisha alimuonyesha picha, alimkumbuka vilivyo ingawa kwa kipindi hiki alikuwa kanenepa nenepa ila sura yake haikubadilika sana, alimtazama na kumtazama baba Angel kisha akamuuliza,
“Ndio huyu mwanamke ambaye nilikuwa naonyeshwa picha zake na Tumaini?”
“Mke wangu, hayo tutazungumza wenyewe, ngoja tumalize haya kwanza”
Jack alijibu,
“Ndio ni mimi, nilikuwa nawasiliana mara kwa mara na huyo wifi yangu Tumaini, kwanza anafahamu wazi kuwa mimi nina mtoto wa ndugu yake”
Mama Angel alipumua kwanza na kuamua kukaa kimya kwa muda, kisha baba Angel akasema,
“Tumekusikia, ila mbona mtoto hajafanana na mimi? Siwezi kumkubali mpaka pale nitakapopima nae vinasaba”
Hapo dokta Maimuna aliyekuwa kainama tu alikohoa kwanza na kufanya washtuke kidogo kisha akasema,
“Jamani sijui nisemaje, sijui kama naweza kueleweka, sijui kama manaweza kunielewa. Naomba nisamehewe kwanza”
“Kwanini”
“Sikutegemea kama kuna siku kama hii itatokea katika maisha yangu, ila nilitegemea kuwa kuna siku nitasema ukweli kabla sijaingia kaburini, naomba mnisamehe sana”
“Kwani tatizo ni nini Maimuna?”
“Naomba unisamehe sana Jack, nisamehe dah sikutegemea jambo kama hili”
“Jambo gani?”
“Kwanza sikujua kama umezaa na Erick, sikujua kabisa, huyu ni mwanaume niliyekuwa namchukia maisha yangu yote. Nakumbuka stori za mimi na wewe hatujawahi kuwaongelea kuhusu wanaume waliotuzalisha maana walikuwa ni wabaya kwetu, ila naomba unisamehe Jack”
“Kwani ni kitu gani?”
“Naomba tu niseme ingawa sikutegemea kama nitasema siku ya leo ila pia sitegemei kwa mtu mzuri kama Jack kuumbuka kwa makosa yangu”
“Sema nikusikie Maimuna”
“Niliwahi kuwa na mahusiano na Erick hapo kabla, ila alinifanyia kitu kibaya sana, nilipata mimba ya kwanza akasababisha ikatoka, nikapata mimba ya pili napo akaniletea ujinga wake wa machungwa na mimba yangu ikatoka. Nikamchukia sana Erick, yeye pamoja na wanaume wengine nikajikuta nayachukia mapenzi kupita maelezo, ila akaja mwanaume mmoja wa kuitwa Rahim ambaye alionyesha kunipenda sana tena sana, nakumbuka kipindi hiko nilikuwa nipo kwenye mafunzo ya vitendo. Rahim akanipa mimba na kuniacha kwenye mataa, aaah nilichukia sana, nikiwa na mimba yangu nikamfumania Rahim na wanawake mara tano, nilikosa amani ya moyo, sikumpenda hata kidogo, nikahisi kama moyo wangu umeingia donge zito, huwezi amini nilikuwa natamani hata mimba itoke, sikufikiria kama nitampenda mtoto ambaye nitakuwa nimezaa na Rahim. Nikaitwa na mjomba wangu mmoja ana hospitali Afrika Kusini kwani aliambiwa kuwa nina msongo wa mawazo, alisema niende kule ili akili yangu ikae sawa, na nifanye kazi pale kwenye hospitali yake na kweli nilikuwa pale na kufahamiana na Jack. Huyu Jack alikuwa akija mara kwa mara pale hospitali na nilikuwa naongea nae sana, na yeye alikuwa akisema jinsi mwanaume alivyomtenda ila hakusema kama ana hasira nae, sema nilihisi tu kuwa atakuwa na hasira nae. Siku ambayo Jack aliletwa akiwa na uchungu mkali, ni mimi niliyempokea hospitali na kumpeleka leba, ila na mimi nilishikwa na uchungu muda ule na kupelekwa chumba kingine kwaajili ya kusaidiwa, kweli sikukawia kujifungua ila muda niliojifungua ndio muda aliojifungua Jack, watoto wetu walikuwa wakihudumiwa na dokta mmoja wa kuitwa Samir, nilijikongoja na kumfata kwenye sehemu ya watoto kumbuka nilikuwa ni mtu wa pale kwahiyo nilikuwa na kibali cha kuingia popote, nilipofika nilimng’ang’ania dokta Samir anipe mtoto wangu, basi alinipa ila mimi nilimkazania yule wa Jack kwani nilijua wazi sababu yule mtoto simjui uhalisia wake basi nitamlea kiukweli kweli, na mwanangu alelewe vizuri na Jack ambaye anaonekana bado ana mapenzi na baba mtoto wake. Hata dokta Samir alinishangaa sana ila nilimtunuku kwa kumoa mwanangu jina lake”
Baba Angel akamkatisha kidogo dokta Maimuna na kumwambia,
“Inamaana Samir ndio mtoto wa Jack, halafu mtoto wa Jack ndio mtoto wako”
“Ndio, naomba mnisamehe sana”
Baba Angel alipumua kwanza maana kama hakuelewa kitu vile, kwakweli Jack alikuwa akishangaa sana huku akimuangalia dokta Maimuna na kumwambia,
“Sikuelewi”
Mama Angel nae akadakia,
“Yani mimi ndio sielewi chochote kinachozungumzwa hapa, kwahiyo Samir ni mtoto wako Erick? Kila siku unasema kuna mtu unamfananisha nae kumbe ni mwanao!!”
“Aaaah mke wangu tutaongea vizuri, ngoja tumalize hili kwanza.”
Kwa busara baba Angel aliona ni vyema hapo wamuache dokta Maimuna na Jack waongee wenyewe na wakubaliane wenyewe sababu wao ndio wahusika wakuu wa watoto wao na ndio wanajua ni kitu gani kilichotokea.

Baba Angel alienda pembeni na mke wake huku akiongea nae kwa taratibu,
“Natumaini mke wangu utanielewa”
“Sio nitakuelewa, nishakuelewa ila sijui kwanini Tumaini kanificha kuhusu hili”
“Sio wewe tu hata mimi nilikuwa sijui, nadhani hakutaka kuweka mgogoro baina yetu. Mengine tutaongea vizuri zaidi tukiwa chumbani, ngoja wayaweke sawa wenyewe”
“Kwahiyo, Samir ni mtoto wako?”
“Tutaongea vizuri”
“Mmmmh makubwa haya, dunia ina mambo sio ya kitoto duh!!”
“Usijali mke wangu tutaongea tu”
“Ila bado najiuliza, kwahiyo Rahim alimuoa dokta Maimuna huku akiamini kuwa Samir ni mtoto wake!!”
Basi Dokta Maimuna aliwaita kuwa kashamaliza kuyapanga na Jack, walirudi pale na kusikilizana nao, baba Angel aliwauliza,
“Mmefikia muafaka?”
“Ndio, mwanangu mimi ni mtoto wa Jack, na mtoto wangu ndio mtoto wenu na Jack. Kwamaana hiyo Samir ni mtoto wako na Jack. Nimemuelewesha Jack, sikumchukua kwa ubaya Samir, nimejitahidi kumpa mapenzi yote na kumlea kama mama kwani najua wazi kuwa hata mwanangu nae anapendwa vizuri na kulelewa vizuri. Kama shule nzuri Samir nimempeleka na mapenzi yote nilimpatia kama mama, hata mkimuuliza Samir atawaambia kwanza nina uhakika hawezi kuamini kama mimi sio mama yake mzazi”
Mama Angel aliuliza,
“Ila ngoja nikuulize dokta, ulipata ujasiri gani wa kuchukua mtoto wa mwenzio na kulea wewe halafu kuacha mtoto wako kwa mwenzio, yani ulijiamini nini? Na siku zote Rahim alijua kuwa Samir ni mtoto wake? Kwani wewe na Rahim mlioana kwa kipindi gani?”
“Sidhani kama maswali yako hayo ni muda muafaka wa kuyajibu, kumbuka mtoto wa kwanza nimezaa na Rahim, nimembadili bila ya yeye kujua, alivyorudi badae alirudisha mapenzi kwangu na kumuhudumia mtoto ingawa alikuwa na mke wake, ila hapo nilizaa nae mtoto wa pili ndipo alipoamua kumuacha mkewe na kunioa mimi, sijawahi kumwambia ukweli kuhusu Samir, siku zote anajua kuwa mtoto ni wa kwake, ila mtoto sio wake nilimbadilisha. Sikumjua baba wa Samir kuwa ni wewe, nadhani ningemjua nisingeweza kumuiba wala nini. Nisameheni kwa hiki kilichotokea. Haya tuzungumze yangu, ila sijui kama kunahitajika maelezo maana mambo yamegeuka zaidi ukizingatia huyo Angel ni mtoto wa Rahim ila kalelewa na wewe Erick, wakati huo Samir ni mtoto wako ila kalelewa na Rahim, hapo sijui nini kitatendeka. Ila kwa ushauri wangu, naomba jambo hili nilichukue kisaikolojia, sio jambo la kukurupuka kuwaambia watoto, nitajua jinsi nitakavyoongea na Samir na nina uhakika atanielewa ila sijui kama atakubali kuniacha mimi, halafu Jack utaongea na mtoto wako ila cha muhimu usimwambie kuwa mimi simpendi, mwambie nilikosea, nitakwambia jinsi ya kumwambia ili aweze kuelewa, halafu mimi na wewe Jack tutakutana na watoto wetu na tutaongea nao vizuri kabisa. Kwahiyo kazi ni kwako Erick kumkubali mwanao, na huyo Rahim nitaenda kuongea nae na kumuelewesha pia kuhusu huyu mtoto wake wa ukweli. Naomba kwa leo yaishie hapa, Jack nenda na Derrick kama ulivyokuja nae na mimi naondoka na Samir kama nilivyokuja nae, halafu tutakutana tena, tusiongee chochote hapa tutachafua tu hali ya hewa”
Waliweza kumuelewa huyu dokta Maimuna, na walikubaliana nae vizuri kabisa kwahiyo kwa muda huo waliweza kila mmoja kuondoka na mwanae na kusema kuwa wataenda kuongea vizuri wakiwa nyumbani kwao.
Baba Angel na mama Angel kwa siku ya leo bado hawakuwa sawa kabisa, baba Angel alimuomba mke wake kuwa watoke kidogo kwaajili ya mazungumzo yani waende mbali kidogo kama walivyokuwa wakifanya kipindi cha katikati, kwani aliweza kuona ni jinsi gani mke wake alivyokosa amani juu ya jambo lile jambo.

Mama Angel na baba Angel walitoka na kwenda kwaajili ya maongezi, kwahiyo moja kwa moja walienda kwenye hoteli na kuagiza vinywaji huku wakinywa, baba Angel alimuomba msamaha tena mke wake,
“Naomba msamaha kwa hili lililotokea, natumai umenielewa mke wangu”
“Hakuna tatizo nimekuelewa mbona. Hivi mimi nishindwe kukuelewa kwa hili kweli!! Ulinikubali mimi nikiwa na mtoto wa mwanaume mwingine, halafu mimi nisindwe kukuelewa wewe kuwa na mtoto mwingine nje wakati tabia yako ya mwanzo naijua fika ilivyokuwa. Mtoto angekuwa mdogo hapo sawa, ningekuuliza imekuwaje mume wangu hadi ukaenda kuzaa na mwanamke mwingine ndani ya ndoa yetu? Ila mtoto ni mkubwa yule, naulizaje sasa? Nimekubali kwa mikono miwili kuwa ni mtoto wetu na tutaishi nae tu hakuna tatizo”
“Nimefurahi kusikia hivyo mke wangu, unajua nini ni mama ndio alinishtua kuhusu Samir, baada ya kusema kafanana sana na mzee Jimmy enzi za ujana wake, mama alisisitiza nimfatilie Samir ili nijue ukweli wake maana mama alihisi kuwa Samir ni mtoto wangu kabisa”
“Aaaah kumbe ndio siku ile!”
“Ndio, yani ile siku mama alinikazania sana nimueleze ukweli kuhusu Samir, hata nilipomwambia kuwa ni mtoto wa rafiki yangu, bado hakunielewa kabisa”
“Haya, sasa utaenda kumuelewesha, najua atafurahi. Hatimaye tumeongeza mtoto mwingine wa kiume maana tulikuwa na Erick pekee ila bado natumaini kuwa Erick atabaki kuwa mtoto wako wa pekee au nakosea?”
“Ni kweli, nampenda mwanangu Erick na nitawapenda wote pia. Sasa ngoja nikwambie jambo lingine”
Baba Angel alimuelezea mke wake kuhusu ile safari ambayo alienda na Rahim na kukutana na yule binti aliyezalishwa na yule kijana Derrick, mama Angel alishtuka sana na kusema,
“Kheee huyo Rahim kama alichangayikiwa juu ya Samir na Angel basi kwasasa ndio atachanganyikiwa maradufu, duh mbona ni hatari sana”
“Ni hatari kweli, ila hata kwetu hakuna usalama mke wangu. Kumbuka Angel ni mwanangu halafu Samir ni mwanangu pia na wale watoto wanapendana kama na wao walipewa dawa aliyopewa Erick na Erica dah!! Sijui hata tunafanyeje?”
“Na nijuavyo akili zao wale, wakijua ukweli tu basi tujue ndio mimba ya pili ipo mlangoni, inatakiwa tufanye juhudi za mapema kunusuru hili jambo. Mimi ndio hata sielewi, nikiwafikiria Erick na Erica ndio napata kichaa kabisa yani”
“Mmmh turudi nyumbani mke wangu, hakuna ninachoelewa hapa kwa muda huu kwakweli”
Waliongea kidogo kisha kuinuka na kurudi nyumbani tu.

Kulivyokucha siku ya leo, baba Angel alienda zake ofisini kwake kama kawaida na kuanza kazi zake ila muda kidogo alifika pale Erick akiwa na sare za shule na kuanza kuongea nae,
“Erick, leo vipi mbona upo hapa muda huu na sio shuleni?”
“Aaaah baba kuna jambo nataka tuongee”
“Jambo gani hilo?”
“Unajua leo shuleni, asubuhi kabisa kaja yule sijui mamake Sarah, yule ambaye alikuwa akija na Sarah kipindi kile”
“Eeeh alikuwa akitaka nini?”
“Aliniita ofisini na kuanz akuongea na mimi, tulibaki wawili tu yani mimi na yeye”
“Alikuwa anasemaje sasa?”
“Ameniambia kuwa, katika maisha yake hakuwahi kufikiria jambo ambalo limetokea kwake. Anasema alikuwa akiamini kuwa Sarah ni mwanae ila kaambiwa kuwa mwanae ni Elly na kapewa uhakika, anasema kwamba bado anajipa moyo kuwa Sarah ni mtoto wake yani anaamini kuwa alijifungua watoto mapacha sababu mpaka leo haijulikani wazazi wa Sarah wako wapi, ila kaniuliza swali moja ambalo nilishindwa kumjibu kwakweli”
“Swali gani?”
“Kaniuliza kuwa ikitokea mimi na Sarah ni mapacha je mimi nitafanyaje? Yani kama Erica sio pacha wangu, sijamuelewa ana maanisha nini? Kwani Sarah ni mtoto wa nani na kwanini imekuwa hivi?”
Baba Angel alipumua kwanza kwani hapa aliona ni pagumu sana kwake kisha akasema,
“Huyo mwanamke lazima atakuwa na wazimu tu sio bure, nyie wote ni watoto wangu yani wewe na Erica”
“Na Sarah je? Maana mama huwa anasema kuwa Sarah ni mwanae!”
“Ndio huwa anasema hivyo sababu Sarah ni mtoto wa mjomba wenu Derrick, kwahiyo kama ni mtoto wa kaka yake basi na yeye ni mtoto wake pia. Usijali maneno ya huyo mama, ni amechanganyikiwa”
“Basi Sarah mama yake ni nani?”
“Huyo huyo mama Sarah ndio mama yake na Sarah, achana na hayo mwanangu. Ndio kimekutoa shule hiko?”
“Ndio baba, yani nimejikuta nakosa amani kabisa. Nampenda sana dada yangu Erica”
Baba Angel akaguna na kuinuka kisha akamwambia Erick,
“Nikurudishe shule mwanangu, achana na hayo mambo”
“Hapana, siwezi kurudi tena shule muda huu, acha tu niende kiwandani”
“Basi twende wote”
Baba Angel alikamilisha kazi zake pale na kuondoka na kijana wake kuelekea nae kiwandani.
 
SEHEMU YA 412


Baba Angel na Erick walifika kiwandani na kuanza kufanya kazi mbali mbali za pale kiwandani huku wakipitia mafaili mbalimbali, kwakweli baba Angel alikuwa akipenda utendaji kazi wa mtoto wake, kwani vitu vingi vilienda kwenye mstari hapo kiwandani sababu ya Erick, na waliweza kuingiza faida kubwa sababu ya ufanisi wa kazi wa Erick.
Ilipofika jioni, simu ya baba Angel iliita, alipoangalia aliona ni dokta Jimmy anapiga basi akatoka nayo nje ya ofisi na kupokea,
“Ndio nakusikia”
“Nakuomba kitu kimoja Erick”
“Kitu gani?”
“Naomba fanya mpango ili mwanao Erick aweze kulala na pacha wake”
“Una kichaa nini wewe!!”
“Ili tumuokoe huyo mtoto bila ya hivyo ni hatari, hujui tu alichokifanya leo”
“Kwani kafanyaje tena?”
“Erick naomba unisikie, tiba ya ubondia wa mwanao ni kulala na dada yake tu, hapo tutakuwa tumemaliza kazi ila hivi ni kazi bure, mwanao hafai huyo”
“Kwani kafanyaje?”
“Mwanao ataua watu huyo ujue, nakuomba ukubaliane nami ili tuweze kumnusuru mtoto wako”
“Nitolee ujinga mie, siwezi kukubali huo uchafu hata kidogo”
Kisha baba Angel alikata simu bila hata kujua kuwa ni kitu gani cha ajabu kimefanywa na Erick siku hiyo ila baba Angel hapo alipumua kidogo kwani aliweza kujua kuwa siku ile Erick hakulala kimapenzi na Erica.

Jioni ya leo, Junior aliamua kutoka na mke wake Vaileth kwaajili ya matembezi, yani toka wafunge ndoa ndio siku hiyo ambayo waliamua kutoka kwa pamoja, kwahiyo walienda kuangalia mazingira mengine na kuongea pamoja huko, mtoto aliachwa na bibi ambaye alikuwepo tu nyumbani kwa Junior kwa siku hiyo, walitafuta mahali kwenye bustani nzuri na kukaa kwaajili ya maongezi,
“Ila Junior umejua kusumbua akili yangu wewe dah!! Hadi leo huwa siamini kama tumeoana, hata huwa siamini kama unanipenda”
“Aaaah mimi nakupenda Vai, achana na yale mambo ya utoto”
“Ila huo utoto sijuiutakuisha lini?”
“Kwanini?”
“Haya, tupo pamoja hapa ila macho yako yapo kule unaangalia nini Junior?”
Junior alikaa kimya kwa muda na kumjibu mke wake,
“Mbona hakuna kitu ninachoangalia”
“Acha masikhara yako Junior, nimekuona vizuri ukiangalia kule, sijui unatazama kitu gani. Yule mwanamke kageuka mgongo tuila macho yote yamekutoka kwake”
“Aaaah sijui unaweza kunielewa Vai, yani ni kawaida ya wanaume kupepesa macho ila mimi na wewe tupo pamoja, hata mimi sijui nilikuwa naangalia nini”
Vaileth akageuka tena kuangalia mahali ambapo Junior alikuwa akiangalia ila macho yake yaligongana na macho ya Daima, kwahiyo kwa muda wote Junior alikuwa akitazamana na Daima, kile kitendo kilimkera sana Vaileth na kumfanya ainuke kwa hasira,
“Unaenda wapi sasa mke wangu?”
“Naenda nyumbani”
“Kwahiyo unaenda nyumbani na kuniacha mimi hapa!! Haya, nenda tu”
Vaileth alimuangalia Junior na kuamua kukaa ila kiukweli ile tabia ya Junior kwa siku hiyo hakuipenda kabisa, muda kidogo walipokaa Daima alisogea kuwasalimia akiwa ameongozana na kijana mwingine, Junior alipomuangalia yule kijana akagundua kuwa ni ndugu yake yule James.

Vaileth alimuangalia Junior na kuamua kukaa ila kiukweli ile tabia ya Junior kwa siku hiyo hakuipenda kabisa, muda kidogo walipokaa Daima alisogea kuwasalimia akiwa ameongozana na kijana mwingine, Junior alipomuangalia yule kijana akagundua kuwa ni ndugu yake yule James.
Yani pale Junior alibadili muonekano wake kwakweli, halafu Daima na James wakaka pale ambapo Daima alimtambulisha James kwa Junior,
“Huyu ni mchumba wangu anaitwa James”
“Mjinga wewe, huyu ni ndugu yangu”
“Kumbe ni ndugu yako!! Napo sio mbaya sana maana kumbe sijaenda mbali na ukoo wako”
“Wewe mwanamke una kichaa au kitu gani?”
James ilibidi aingilie kati na kuuliza,
“Mbona Junior imeonekana kupaniki sana, huyu uliyenaye ni nani?”
“Huyu ni mke wangu”
“Kheee mmefunga ndoa kabisa?”
“Ndio ni mke wangu wa ndoa”
“Jamani, ndio kimya kimya ndugu yangu. Kweli hatupendani loh!! Ila sisi ni ndugu Junior, yani uwe unakumbuka hili muda wote”
“Aaaah ilikuwa haraka ila huyu mwanamke uliyenaye hafai”
Daima alikuwa akicheka tu na kusema,
“Sasa sifai nini?”
“Aliwahi kuwa na mimi huyu”
“Kwani nikiwahi kuwa na wewe ndio nini? Wewe ni mume wa mtu sasa, na mimi nipo na James ambaye ni mume wangu mtarajiwa kwani tatizo ni nini?”
Junior alimuangalia Vaileth na kumtaka kuwa waondoke mahali hapo maana alijiona akizidi kupatwa na hasira, kwani hakutegemea kama hapo wangekutana na Daima, ila kabla ya kuondoka walibadilishana tena mawasiliano na James maana hata iweze bado wao ni ndugu tu.

Baba Angel na Erick, walimaliza mambo yao na kuanza kurudi nyumbani ila baba Angel hakumuuliza chochote mwanae juu ya kitu gani amekufanya kama ambavyo dokta Jimmy alisema.
Wakiwa njiani, gari yao ilisimamishwa na aliyesimamisha alikuwa ni Juma ambaye alishuka kwenye gari yake na kwenda kuongea nao,
“Yani hapa ndio nilikuwa nakuja huko kiwandani, ila nimekutana nanyi njiani, bora nimewawahi”
“Ndio, kuna tatizo gani Juma”
“Kuna kitu naombva, naomba kesho Erick ukanisaidie kule kwenye mizinga yangu ya nyuki ili tupakue asali”
“Kheee hao nyuki wapo vizuri, tayari asali nyingine!!”
“Hata mazingira yangu yapo vizuri, nakuomba sana Erick. Ila kama tungepata na kijana mwingine ingependeza zaidi”
“Sawa nimekuelewa”
Kisha wakaamuaga Juma pale na baba Angel alianza kuondoka na mwanae huku akimuuliza,
“Kwahiyo kesho huendi shule Erick?”
“Nitaenda tu baba, usiwe na mashaka na mimi. Nina akili za kuzaliwa”
“Kweli naona ila elimu nayo ni muhimu sana”
“Kwanza nashukuru nimalize shule, yani nimechoka kusoma hatari”
“Ila Erick ulikuwa unapenda shule wewe, sijui shetani gani limekukumba tena. Usiwe kama mimi baba yako, ilibidi nijiendeleze shule kidogo nikiwa hivi mkubwa maana mimi niliacha shule nikiwa kidato cha pili”
“Kheee kwanini sasa baba? Mlishindwa ada au kitu gani? Mbona babu anaonekana kuwa alikuwa na mali nyingi toka siku nyingi!”
“Acha tu mwanangu, mapenzi kwa mamako yaliniponza mimi baba yako. Nilikuwa nampenda sana, tena sana muda wote nilikuwa darasani namuwaza, yeye, ila nilipomwambia alinitolea nje, niliumia sana. Na hivyo niliamua kufanya kwa vitendo, ikawa tatizo bhana kuna kirafiki chake Fulani huwa anaongea nacho hadi leo si kikapeleka umbea kwa bibi yenu, akaja shule kufoka tukafukuzwa shule. Nilikuwa naishi na mamdogo, alichoka kwa utukutu wangu wa kunihamisha shule kila siku, alisema hanipeleki tena shule, basi nikaanza kuishi mitaani, hapo ujue wala sikuwa namfahamu baba yangu wala nini, kumbe mama na baba waligombana wakati mimi mdogo kwahiyo mimi nikaishi na mama na kuwajua ndugu wa mama tu. Siku hiyo katika mahangaiko yangu si nikaenda kuomba kazi mahali kumbe ndio kwa baba yangu, kwanza aliponiona tu alishtuka huwezi amini hiyo siku ndio ikabadilisha maisha yangu. Ila mmmh sijui kwanini nakwambia yote haya!”
“Ni vizuri umeniambia baba ili nami nijue mapenzi yanafanyaje kazi”
“Aaaah ila wewe acha bhana tabia ya kumpenda dada yako, yule ni pacha wako ujue”
Hapo Erick alikaa kimya kwanza kwani haya maneno ya mwisho yalimuingia baba yake, alijikuta akimuuliza kuhusu kitu kingine,
“Huyo rafiki wa mama aliyekuwa mbea ni nani?”
“Ni mke wa Juma, yani mke wa Juma ni rafiki mzuri sana wa mama yako ila alikuwa ni mbea sana yule mwanamke”
“Aaaaah kwahiyo alisababisha wewe na mama msiweze kuwa pamoja kwa wakati?”
“Ndio, yani yeye ndio chanzo hadi mimi nikaacha shule yani mambo mbalimbali ila Mungu ni mwema tumesahau hayo”
“Aaaah hujasahau baba, ungesahau usingekumbuka kuyasema”
“Si tunayasema tu kupoteza siku”
“Unajidanganya baba, hata hujayasahau”
Baba Angel alicheka tu, muda huo walikuwa wamefika nyumbani kwao kwahiyo waliingia ndani tu moja kwa moja.

Kwakweli hii kitu aliyoifanya Junior leo, haikumpendeza kabisa Vaileth aliweza kuhisi kuwa bado Junior alikuwa na mapenzi na Daima, kwahiyo aliondoka nae bila ya kuongea chochote kile hadi walipofika nyumbani kwao.
Wakati wa kulala, Vaileth alishindwa kuvumilia na kuamua kumuuliza Junior kuhusu Daima,
“Kama ulikuwa ukimpenda Daima, ni kwanini ulimkana wakati amekuja na mimba hadi ukasababisha balaa kwake?”
“Hivi unaona Daima ni mwanamke anayejielewa? Sikuwa na namna zaidi ya kumkana tu”
“Kwahiyo kati ya mimi na Daima ungeambiwa uchague basi ungemuoa Daima au?”
Junior alicheka na kusema,
“Ila Vai mke wangu, maswali mengine unauliza wakati jibu unalo”
“Jibu lipi hilo, niambie basi, ungemuoa Daima au?”
“Kwani hapa nimemuoa nani? Si inamaana nakupenda wewe au ni nini?”
Simu ya Junior ilianza kuita ambapo aliipokea na mpigaji alikuwa Erick, yule ndugu yake mtoto wa baba Angel,
“Niambie Erick”
“Kesho unaenda wapi kaka?”
“Hapana, nipo nyumbani tu”
“Kuna kazi, nataka tukaifanye wote”
“Oooh, vizuri sana. Basi utaniambia pa kukutana”
Junior alikata ile simu na kumuangalia mke wake na kumwambia,
“Ila Erick yupo vizuri sana, yani huwa ananikumbuka sana kaka yake”
“Haya vizuri”
Vaileth aliamua kulala tu kwa muda huo, hata Junior nae aliamua kulala.

Leo kama ambavyo Erick alipanga na Junior, aliweza kukutana nae na moja kwa moja kwenda shambani kwa Juma kwaajili ya kumsaidia kuhusu ile mizinga,
“Oooh Erick kumbe umekuja na kijana”
“Ndio nimekuja nae, nilikuonea huruma jana uliponipigia na kusema kuwa itabidi uje na mke wako”
“Hata hivyo nimekuja nae, ila ni muoga sana hataki hata kupaka dawa ili tuingie yani anaogopa nyuki balaa”
“Aaaah yuko wapi nikamsalimie”
Juma akamuongoza hadi alipo mke wake ambapo Erick alimsalimia yule mke wa Juma kisha Juma alianza kupanga nao jinsi ya kufanya kazi siku hiyo.
Wakajiandaa na wote wakaingia kwenye kazi, muda huo mke wa Juma alikuwepo tu sehemu ya nje akiangalia angalia kwani yeye alikuwa akiogopa sana nyuki.
Wakati wakiendelea na kazi, Juma alishangaa tu gafla hamuoni tena Erick, ikanidi amuulize Junior kuwa Erick amekwenda wapi,
“Yuko wapi tena Erick?”
“Sijui katoka kaenda wapi”
Juma aliamua kumuangalia Erick kuwa kaenda wapi, katika kumtafuta tafuta akamuona Erick amemshika mke wake mkono huku akiongozana nae, kwakweli Juma hakuelewa kuwa Erick anaenda wapi na mke wake yule, akawaita ila kitu cha kustaajabusha eneo lile walitokea nyuki wengi sana na kumvamia mke wa Juma, kwakweli kitendo kile kilimstaajabisha sana Juma ikabidi akimbie eneo lile na kwenda kumuokoa mke wake kutoka kwa wale nyuki ila kitu cha kwanza alijikuta akishikwa na hasira sana kwani alihisi kuwa lazima Erick amefanya kile kitu kwa kudhamiria kabisa, basi aliposogea pale na kumtoa mkewe kwa wale nyuki maana yeye alikuwa akijua kitu cha kufanya ukizingatia ameshafuga sana nyuki. Basi akamsogelea Erick na kumnasa kibao, hapo ndio aliharibu akili ya Erick kabisa na hata hakutegemea kama Erick angefanya kitu cha namna ile alichokifanya pale.

Erick alirudi nyumbani kwao kama kawaida, na kwenda moja kwa moja kuoga alipotoka tu alikuta ndio wapo kula kwahiyo na yeye aliungana nao mezani kwaajili ya kupata kile chakula cha usiku, basi pale mambo yalikuwa yakizungumzwa mbalimbali huku wakiendelea kula ila hakuna mahali hata sehemu moja ambayo Erick alisema jambo lolote.
Alipomaliza kula tu moja kwa moja alirudi chumbani kwake, baada ya muda mfupi Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kumuuliza maana alimuona hana raha kabisa,
“Tatizo nini Erick, au umechukia kwa mama kukukataza jana kulala chumbani kwetu?”
“Aaaah hamna klitu”
“Najua kama ulichukia Erick, ila unajua kama mama ana mashaka sana na sisi yani mama hatuamini kabisa, anahisi kuna kitu sio cha kawaida ambacho tutakifanya tukiwa pamoja”
“Aaaah huwa sipendi wanifikirie vibaya, ni kweli nina hisia nyingi sana na wewe Erica, ila nashukuru Mungu amekupa upeo mkubwa sana maana bila ya hivyo basi tungekuwa tumetenda zaidi ya kile tulichokifanya. Naomba unisamehe tu, ila mama huwa hajui ni kwanini napenda kulala karibu yako Erica”
“Najua kuwa ulikosa amani, basi leo najitolea mimi kuja kulala humu chumbani kwako. Kwa leo tutalala wote Erick”
“Nitafurahia sana, asante kwa hilo”
Basi Erica hakutoka kweli mule chumbani kwa Erick kwani alilala pembeni yake na wote wakashikwa na usingizi kwa muda huo.

Baba Angel akiwa na mkewe chumbani wakiwa wanajiandaa kwaajili ya kulala, muda kidogo simu ya baba Angel iliita na kumfanya aipokee simu ile kwani mpigaji alikuwa ni Juma kwahiyo alitaka kusikia kuwa tatizo ni kitu gani,
“Yani hapa tulipo ndugu yangu tupo hospitali”
“Kheee vipi tena?”
“Alichotufanya Erick ni Mungu tu ndio anajua”
“Kwani kafanyaje?”
“Njoo utuone, hapa nimebakisha sauti tu ya kuongea kwakweli, mtoto huyo hapana, kuanzia leo hata simtaki tena”
Baba Angel alishangaa sana, hata mama Angel alishtuka kwakweli na kuulizia vizuri ambapo alipewa yale maelezo ambayo baba Angel alipewa na Juma, walijikuta wakitazamana,
“Kwani imekuwaje tena?”
“Hata sijui”
“Twende tukamuulize Erick”
Walijikuta wakiinuka kwa pamoja hadi chumbani kwa Erick, walipofungua mlango waliona Erick amelala na Erica kwenye kitanda kimoja tena wakiwa hawana habari sema hakuna lolote baya walilokuwa wakifanya, ni kila mmoja alilala kivbyake na uzuri walikuwa wamevaa nguo zao za kulali, ila mama Angel alitaka kumtimua Erica ambapo mumewe alimsuia na kurudi tu chumbani kwa muda huo na kuanza kuongea,
“Kwanini umenikataza nisimuamshe Erica, wakitenda dhambi je?”
“Hiyo dhambi wakitaka kuitenda wataitenda tu, kwani sehemu zote tunaenda nao pamoja? Wakiamua mbona tumeisha, hata tusitake kufatilia sana mke wangu tutalia tu, sema tujue jinsi ya kuweza kumdhibiti Erick”
“Sasa atakuwa amefanya mambo gani?”
“Sijui, unajua hata kuhusu mambo aliyosema dokta Jimmy sijafatilia wala nini yani, kesho mapema tutaenda hospitali kumuona huyo Juma. Tena hata tusimuulize Erick ila tutakuja kuongea nae baada ya kutoka hospitali”
Mama Angel alikubali ila kishingo upande kwani alilala huku mawazo yake yote yakiwa juu ya watoto wake maana hakuelewa kabisa kitu ambacho kingetokea baina yao.

Kulivyokucha tu, mapema kabisa baba Angel na mama Angel walijiandaa na kwenda hospitali ambapo Juma alikuwa kalazwa na mkewe, na kweli waliwakuta wana hali mbaya kiasi, basi walisogea na kuanza kuongea na Juma,
“Imekuwaje kwani?”
“Mtoto wako kanifanyia fujo jana sikutegemea kabisa”
“Kwani kafanyaje?”
“Kwanza kamchukua mke wangu, sijui kampeleka sehemu yenye nyuki, anajua mwenyewe alichokifanya maana wale nyuki walianza kumshambulia mke wangu, na hapo ikawa ni hatari nami nikawasambaratisha maana nishafuga nyuki sana naelewa, ila nilichukia maana mke wangu aliakuwa kaumia, basi nikamzaba Erick kibao, jamani sitaki kusema ilivyokuwa, hapa nilipo hakuna rangi ambayo nimeacha bila kuiona kwakweli, nimepigwa na Erick mimi tena nilikuwa sijielewi kabisa, bila yule ndugu yake aliyekuja naye basi mimi ningekuwa marehemu. Mwanao hafai kabisa tena hafai”
“Dah!! Pole sana”
Baba Angel na mama Angel walisikitika, kisha walienda kumuona na mke wa Juma yani Johari na kusikitika pia, basi waliongea kidogo tu pale na Juma na kukubaliana nae kuwa watakuwa wakienda kuwaangalia mara kwa mara na wataenda kuongea na mtoto wao.
Baba Angel na mama Angel waliporudi nyumbani waliambiwa kuwa wakina Erick wameenda shuleni kwahiyo wakasema kuwa watamuuliza tu siku akipumzika nyumbani.

Siku hii baba Angel akiwa ofisini kwake, alifatwa na madam Oliva na kumkaribisha na kuanza kuongea nae,
“Kheee kumbe kuna baraka inakuja eeeh!!”
Madam Oliva akacheka tu maana tumbo lilikuwa limetangulia mbele kabisa, kisha madam Oliva akasema,
“Yani nikizaa mtoto wa kiume tena, siwezi hata kwa bahati mbaya kumpa jina Erick”
“Kwanini?”
“Yani majina ya Erick nyie ni watu wa ajabu sana”
“Kivipi?”
“Unajua mwanao kafanya maajabu sana shuleni, na sasa ana wiki nzima hajakanyaga kabisa shuleni halafu wewe Erick mwenzie hata kuulizia kuwa imekuwaje hakuna, unajua mwanao yupo darasa gumu kabisa kwasasa”
Baba Angel alipumua kwanza na kumuuliza vizuri madam Oliva,
“Sikuelewi madam”
“Sikuwepo kazini, unajua siku hizi sio mara kwa mara mimi kwenda shuleni, nasikia alifika siku hiyo mamake Sarah yule Manka ambaye ndio mmliki wa pili wa ile shule, sasa sijui akaenda kuongea na Erick ofisini unaambiwa kila mtu alishangaa kusikia yule mama akipiga kelele, walipoenda walimkuta akipokea kichapo toka kwa Erick, na kila mwalimu aliyeingilia naye alipigwa vibaya sana, hata walinzi walijaribu kumkamata nao walipigwa vilevile, kwakweli Erick hafai halafu wewe hata hujaja shuleni wala nini, huna haja ya kufahamu maendeleo ya mtoto wako wala nini. Tulitamani kumshtaki ila kila mtu anamuhurumia maana Erick bado ni kijana mdogo, mwanao ameanza kuvuta bhangi?”
“Unajua bado nashangaa”
“Twende shuleni ndio ukashangae vizuri zaidi”
Basi baba Angel aliamua kufunga kazi tu na moja kwa moja kuondoka na madam Oliva kuelekea nae shuleni ili kujua kisa na mkasa.

Walifika pale shuleni na moja kwa moja baba Angel alifika ofisini na walimu wote wa pale walianza kumsimulia baba Angel kila ambacho mtoto wake amekifanya, kwakweli alistaajabu na kuuliza,
“Chanzo ni nini kwani?”
“Sidhani kama kuna anayetambua chanzo ni nini? Alifika bosi wetu hapa na kuhitaji kuongea na Erick, waliingia kwenye ofisi hiyo kwaajili ya maongezi, baada ya muda mfupi tu tulimsikia yule bosi akipiga kelele, yani kila aliyeenda kuzuia alipewa kichapo cha hali ya juu, hata walinzi walipigwa jamani, kwakweli huyu Erick hafai na alituacha hapa na kuondoka, toka siku hiyo Erick hajafika tena shule hadi leo”
Hapo baba Angel akakumbuka vizuri jinsi ambavyo Erick alienda ofisini kwake na ilikuwa mapema sana, akakumbuka jinsi maelezo ya Erick ambavyo yalikuwa hayana mashiko wala nini ila hakuwa na cha kufanya kwa muda ule zaidi ya kuwasikiliza walimu tu,
“Sisi kama shule tunahitaji kumfukuza shule huyu mtoto Erick, hatuwezi kuishi na mwanafunzi wa dizaini hii”
“Jamani nawaomba walimu, msimfute shule mtoto wangu, kumbukeni huu ndio mwaka wake wa mwisho, naomba tu aweze kumaliza shule hapa salama”
“Njia nyingine ni kuwa, mtoto wako hatotakiwa shuleni hadi siku ya mtihani wa mwisho, kama umeafikiana na hilo tukubaliane hapa”
“Dah!! Mwanangu atakosa masomo, si atafeli huo mtihani jamani!! Naomba mmuhurumie mwanangu”
“Hatuwezi fuga mabondia hapa shuleni, na hiyo njia ya pili ni tumekupendelea maana kilichopo ni kumfukuza shule kabisa. Na hiyo njia ya pili itafanikiwa endepo Erick akikubali kuja kuomba msamaha hapa shuleni”
Baba Angel akafikiria kwa muda na kuona wazi kuwa anatakiwa kumshawishi mtoto wake kuja kuomba msamaha mahali hapo, kwahiyo alikubaliana na walimu kuwa atampeleka Erick kwenda kuomba msamaha, aliamini kuwa walimu wanaweza kumfikiria adhabu nyingine Erick maana aliona swala hili kidogo litaathiri mwenendo wa Erick shuleni.
Basi walipomaliza pale, baba Angel aliondoka huku ameongozana na madam Oliva ambapo madam Oliva alimuuliza,
“Kwani Erick amekuwaje tena? Mbona alikuwa mtoto mzuri tu, ni kitu gani kipo kati yake?”
“Hata najua basi madam! Yani pale nilikuwa nashangaa tu, jinsi Erick alivyokuwa muoga halafu leo hii naambiwa kafanya kitu cha namna hiyo, kwakweli nimebaki nimeduwaa tu”
“Nakumbuka mimi niliwahi sababisha matatizo kwa Erick, ila sikutegemea kabisa, nilimchapa fimbo moja tu halafu akazimia yani hapo ilikuwa ni mwisho kwa mimi kupiga watoto. Nakumbuka hadi Erick kazinduka na kuendelea na masomo alikuwa ni mtoto mzuri tu, huwezi mkuta hata akibishana na mwanafunzi mwenzie shuleni hata sijui ni mdudu gani kamkumba Erick jamani dah!”
“Yani ambavyo huelewi madam na sisi ni hivyo hivyo”
Ila baba Angel alijikuta akitamani kumueleza madam Oliva kuhusu dokta Jimmy alichokifanya kwa Erick na Erica wakati wadogo akajikuta akisita tu na kutokumwambia chochote kile, hadi wanaagana hakuongea nae chochote kuhusu hilo jambo.

Usiku wa leo, baba Angel alimsimulia mke wake kuhusu kile alichokifanya Erikc shuleni, kwakweli waliamua kumuita kwa pamoja chumbani kwao ili waweze kuongea nae maana waliona kuzidi kukaa kimya ni kuendelea kufanya tatizo liwe kubwa zaidi.
Erick alienda chumbani kwa wazazi wake ambapo walimkalisha na kuanza kuongea nae, baba Angel alimuuliza kwanza,
“Erick, mara ya mwisho wewe kwenda shule ilikuwa ni lini?”
“Siku ile niliyokuja mapema ofisini kwako”
“Kwanini hukwenda tena shule Erick?”
“Baba sikia, nilikuwa shule siku ile kama kawaida, alikuja yule mama wa kuitwa Manka au mama Sarah akaniita nami nilitii na kwenda kuongea nae. Alichokuwa akiniambia ofisini sasa, kwanza aliongelea kuhusu Sarah, sijui Sarah sio mwanae sijui anahisi Sarah ni mtoto wa familia yetu ila akajijibu mwenyewe kuwa haiwezekani kwani mimi na Erica tulikuwa ni sehemu ya mtego, nikamuuliza mtego kivipi ndipo aliponiambia kuwa mimi nimepewa dawa ili nimtake dada yangu Erica kimapenzi, na pale nitakapofanya mapenzi na dada yangu basi ndio undugu wetu utakuwa umekwisha, nilimuuliza kwanini ilifanyika hivyo, akasema ili kuwakomesha wazazi wetu, halafu akasema kuwa wewe baba ni malaya sana, hapo ndio alinikera zaidi. Akamalizia kwa kusema mimi nimepewa dawa nitembee na dada yangu ili nisirithi umalaya wa baba. Nasema wazi nilichukia mno, nilijikuta nikipandwa na hasira za ajabu na hapo ndio nikafanya fujo pale shuleni ila haikuwa lengo langu wala haikuwa dhamitra yangu, niliogopa kuwaambia kwani najua wazi mngechukia sana, ila najua hadi mmeniuliza ni lazima mmejua ukweli”
Baba Angel na mama Angel walipumua kwanza maana haya mambo kwao yalikuwa makubwa sana, kisha mama Angel alimuuliza Erick,
“Kwahiyo wewe ni kweli huwa unapatwa na hisia kwa ndugu yako Erica?”
Hapa Erick alijibu kwa kichwa kumaanisha kuwa ni kweli, baba Angel na mama Angel walipumua tena na kumtaka mtoto wao kwenda kulala ila kabla ya kuondoka baba Angel alimwambia Erick,
“Basi Erick nakuomba jambo moja tu, naomba twende wote shule ukawaombe msamaha walimu ili uweze kufanya mtihani wa mwisho, halafu tutatafuta twisheni ya wewe kupata masomo yaliyokupita shuleni, sijui umeielewa hiyo?”
“Nimekuelewa baba, hakuna tatizo”
Kisha wakamruhusu Erick kuondoka kwa muda huo.
Baba Angel na mama Angel waliangaliana kwa muda bila ya kusema chochote halafu mama Angel akasema,
“Kwahiyo hawa watu kitendo cha kufahamu udhaifu wa watoto wetu imekuwa tatizo jamani? Kwanini dah!! Sielewi kwakweli”
“Je unaona kampiga kihalali au kakosea?”
“Ila yule Manka nae amezidi mdomo acha apate adabu kidogo, kumbuka amejaribu kukuua mara mbili yule kiumbe, mwache tu akomeshwe kwasasa”
Wakaikatisha mada hiyo na kuamua tu kulala.

Kulivyokucha, baba Angel alimwambia mkewe kitu ambacho alifikiria kwa wakati huo,
“Mke wangu, hivi kwanini tusiende kwa dokta Jimmy tu. Nina hakika kipo ambacho anacho cha kuongea na sisi”
“Hapo sawa mume wangu, twende lini sasa?”
“Leo yani muda huu, jiandae twende”
Mama Angel alijiandaa kwa muda huo kisha yeye na mume wake waliondoka hapo kwao na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea kwa dokta Jimmy.
Walipofika tu kwa dokta Jimmy, kuna mtu walimuona akitoka kwenye nyumba ya dokta Jimmy na kufanya washtuke sana kwani ni mtu ambaye walimfahamu na hawakufikiria kama ana ukaribu wowote na dokta Jimmy.

Walipofika tu kwa dokta Jimmy, kuna mtu walimuona akitoka kwenye nyumba ya dokta Jimmy na kufanya washtuke sana kwani ni mtu ambaye walimfahamu na hawakufikiria kama ana ukaribu wowote na dokta Jimmy.
Baba Angel alienda kuweka gari pembeni kwa haraka ili kumuwahi yule mtu waweze kumuuliza vizuri, ila yule mtu nae aliingia kwenye gari yake na kuondoka zake, mama Angel na baba Angel wakatazamana, kisha baba Angel akamuuliza mkewe,
“Huyu baba Emma kafata nini huku kwa dokta Jimmy?”
“Mmmmh hata sijui”
“Au wana undugu?”
“Sidhani kabisa kuhusu hilo, ila huwezi jua maana hawa shemeji yao ni dokta pia kumbuka hilo, ila sijui kwakweli. Sema nimeshangaa sana”
“Kama mimi, hili jambo limenishangaza haswa yani, mpaka muda huu sielewi kitu”
Basi wakashauriana kiasi kisha wakashuka kwenye gari na kuelekea ndani kwa dokta Jimmy ambapo waligonga lile geti na kufunguliwa kisha kuingia ndani na kumuulizia dokta Jimmy,
“Hapana, dokta ametoka”
“Ametoka? Si alisema anaumwa?”
“Ndio, hali yake bado sio nzuri na ameenda hospitali kwaajili ya matibabu zaidi”
“Kheee kwahiyo hayupo”
“Ndio hayupo”
Baba Angel alichukua simu yake na kuanza kumpigia dokta Jimmy ila simu iliita sana bila ya kupokelewa, basi ilibidi tu waage na kuondoka.
Walipotoka kwenye lile geti, waliona kuna gari ya kukodi imemleta mtu pale, walisimama na kuangalia wakaona huyo mtu anayeshuka alikuwa ni Manka huku akiwa na majeraha, ila Manka nae alipowaona alionekana kuchukia sana na kuwafata karibu akiwaambia,
“Mnaona mtoto wenu alichonitenda?”
Na kweli Manka alionekana kuwa na majeraha kwenye mwili wake, hasa usoni ingawa ni majeraha ambayo yalionyesha kuanza kupona, kisha Manka akasema,
“Mimi Manka, nitahakikisha mtoto wenu anaenda jela kwa hili alilonifanyia”
“Pole sana”
“Pole haitoshi, wala pole sio msaada kwangu. Nilikuwa na dada yangu Linah mimi yani nilikuwa nikipata tatizo lolote ni yeye ambaye ananisaidia, sasa amekufa halafu mtoto wangu naye mmemchukua maana najua tu kuwa yupo kwenu. Ila hiki mnachonifanyia ipo siku kitawarudi”
“Kwani kosa letu ni nini Manka?”
“Kosa lenu ni kuzaa mtoto mwenye roho ya kigaidi, halafu wewe Erick uende ukafate barua ya marehemu Linah alikuachia huko hadi leo hujaifata. Kwaherini”
Halafu Manka aliingia nyumbani kwa dokta Jimmy kwahiyo walijikuta wakimuangalia kwa muda tu pale, halafu wakarudi kwenye gari yao.
Waliongea kwa muda kuhusu cha kufanya ila waliona vyema kwa muda huo warudi tu nyumbani kwao.

Angel na wadogo zake leo walikuwa nyumbani ambapo Sarah na Erica ndio waliingia jikoni na kupika siku hii maana Sarah bado alikuwa kwenye kujifunza kupika.
Wakati wanaandaa chakula mezani, alifika shangazi yao na kumsalimia pale kisha kumkaribisha mezani ambapo alikaa nao na kula nao, leo hata Erick alikuwepo nyumbani kwahiyo na yeye alikuwa akila tu. Shangazi yao aliwauliza kuhusu wazazi wao ambapo walisema kuwa wametoka,
“Kheee jamani hata leo Jumamosi wametoka!”
“Tena wametoka asubuhi kabisa”
Basi waliendelea kula huku shangazi yao akisifia baadhi ya vitu kwenye chakula kile,
“Hizi tambi kapika nani?”
“Mambo ya Erica hayo shangazi”
“Ooooh tamu sana, ila Erica leo hujaunga vizuri haya maini”
Angel alicheka na kusema,
“Ni mambo ya Sarah hayo”
Tumaini alicheka, aliangalia yale maini akajikuta akikumbuka mbali sana, muda ule ule Erica akasema,
“Msishangae jamani kuona nyanya zimesimama peke yake, Sarah anajifunza kupika”
Wote walikuwa wakicheka, Tumaini aliangalia kwa makini jinsi ile mboga ilivyokuwa yani alijikuta akicheka kisha akamuangalia Sarah na kumwambia,
“Usijali mtoto mzuri ipo siku utaweza kupika na utapika vizuri kama Erica, hata utasahau kama ilikuwepo siku ambayo ulipika nyanya zikiwa zimesimama dede huku vitunguu vikielea”
Walicheka tena huku wakiendelea kula kile chakula.
Kabla ya kumaliza, Tumaini alipigiwa simu na kwenda nje kuipokea ile simu na kuwaacha pale ndani ambapo baada ya kumaliza tu waliweza kutoa vyombo huku Angel akisema kuwa wajiandae kutengeneza chakula kingine cha usiku, Erick akasema,
“Ila apike Erica”
“Mmmh wewe nawe, kama humu ndani kuna mpishi mmoja tu!! Cha usiku nitapika mimi na Sarah”
Muda kidogo shangazi yao alirudi ndani na kumuita Erick pambeni kuongea nae kwanza,
“Mwanangu Erick, kuna mahali naomba unisindikize”
“Wapi huko shangazi?”
“Unajua wamenishtua tu, sikujua kama nitaenda leo, ingekuwa Jumatatu ni bora ningeenda na mjomba wako ila sehemu yenyewe siwezi kwenda mwenyewe na wamepanga kunidhulumu wale, nisipoenda leo itakuwa balaa”
“Sawa, shangazi ngoja nikajiandae basi”
Erick alienda ndani kujiandaa na baada ya muda alitoka na shangazi yake ili waweze kuondoka, basi nje Tumaini alianza kuwaza,
“Mmmh sijui tukakodi bajaji maana si unajua kama sijaja hata na gari”
“Usijali shangazi, twende kwa pikipiki”
Basi Erick alienda kuitoa pikipiki yao na kupanda na shangazi yake kisha kuondoka kwa maelekezo ya shangazi yake kuhusu mahali wanapoelekea.

Walifika sehemu ambayo ndio shangazi mtu alikuwa akielekea, basi akamwambia Erick kuwa sio mbali kutoka pale, ila ilibidi awasiliane na mtu kwanza, aliwasiliana nae na yule mtu alifika pale alipokuwa Tumaini na Erick, yule mama alimwambia Tumaini,
“Kheee ulivyosema lazima nije na kijana wa kiume nilijua unakuja na baunsa, kumbe upo na kijana wa shule kabisa”
“Ndio, ila mwanaume ni mwanaume. Najua peke yangu watanizingua wale ila wakiona mwanaume wataogopa”
“Ila wamejipanga hao, hadi huruma, yani leo roho imeniuma hadi nimeamua kukuita, bila aibu wanagawana tu vipande vya shamba lako, halafu wapo wengi sana. Ila nitambulishe kwa mwanao huyo, ndio wa kwanza nini!!”
“Aaaah si unajua mimi sina mtoto wa kiume, ila huyu ni mtoto wa kaka yangu kabisa, kwahiyo hii ni damu yangu, anaitwa Erick”
“Kheee kumbe, na mimi naitwa mama Erick”
“Mmmmh wewe nawe kila leo kumbadilisha mtoto wako majina, ukiniona na Leah hapa utajifanya mama Leah”
Walicheka tu na kuendelea na safari wakati huo Tumaini na huyu mama walikuwa wakitembea huku Erick akiwafata nyumba taratibu na pikipiki yake.
Walifika eneo la shamba ambapo Erick sasa aliweka pikipiki pembeni na kuanza kuwafata wale waliokuwa wakimegeana sehemu, walifika pale na Tumaini akawauliza,
“Jamani mbona mnamega shamba langu bila ya kunishirikisha?”
“Sikia mama, serikali imeamuru watu wenye mashamba makubwa yapunguzwe”
“Mbona sijasikia hilo tangazo?”
“Sio lazima usikie, kwahiyo sisi tupo kazini”
Tumaini aliangalia na aliona wazi kuwa hakuna cha kufanya, alimuangalia yule mwenzio na kumwmabia,
“Sasa nifanyeje?”
“Hao, labda uwape pesa si unaona wapo na migambo, yani kwenye shamba lako wamejipanga haswaa, bora hata mashamba mengine walikuwa wachache, na muhusika akija na mwanaume wanaweza kuelewana nae, ila wewe na hako kakijana kako sijui katakusaidia nini”
“Kwahiyo hela ngapi?”
“Muite pembeni huyo umuulize”
Basi akamuita yule aliyekuwa akiongea nae ili amuulize vizuri kama ni pesa awape pesa ngapi,
“Mimi nakuombeni kitu kimoja, mngeniachia shamba langu mbona nalishughulikia vizuri tu”
Yule mama mwingine akasema,
“Nilisikia serikali ikisema walioacha mashamba kama mapori ndio wanyang’anywe ila huyu ndugu yangu anajitahidi kwakweli, analifanyia usafi hili shamba kila mara ndiomana mnaona ni safi na mmeweza kupima”
“Hili shamba pia ni moja kati ya mashamba yanayopaswa kugawiwa kwa wananchi”
Basi Tumaini akasema,
“Kwani mnataka pesa ngapi ili niwape muweze kuachia shamba langu?”
“Sijui wenzangu watasemaje, ngoja nikajadiliane nao”
Akasogea kidogo kwa wenzie na kurudi kuwapa ujumbe,
“Wamesema maana huu ujumbe ni wa serikali kwahiyo wakipuuza ni kama wanajitafutia matatizo, ila wamesema kama ukiwapa milioni mbili basi wataahirisha zoezi”
Yule mama pamoja na Tumaini walishtuka kwa pamoja,
“Milioni mbili!!”
“Jamani hili shamba nilinunua au nilipewa bure!”
“Mama, hatupo kwenye mabishano hapa, kama hutaki basi hili shamba litakatwa vipande na kuuzwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji wa viwanja”
Halafu yule baba akaelekea kule kwa wenzie na kuendelea kupima, yani Tumaini alihisi kuchanganyikiwa na kumuangalia mwenzie na kuuliza tena,
“Nifanyeje mama Kulwa jamani!!”
“Nina uhakika kama wangekuwa wachache halafu ungekuwa na mwanaume mkubwa wale mbona wangeacha eneo lako maana hakuna tatizo, hujawahi kuacha pori hapa, halafu kitu kingine hiyo milioni mbili ni kubwa sana jamani loh!! Si hata ukaanze kununua tofali hapa, hata kama mtu una pesa sio kununua shamba moja mara mbili mbili”
“Yani nakumbuka miaka hiyo ya nyumba hili shamba loto ndio nilinunua kwa hiyo bei halafu leo hii niitoe tena kunusuru kwa hawa wazulumaji jamani, bora hata ningekuja na mume wangu”
Wakati huo Erick alikuwa tu pembeni akitathimini lile eneo la shamba maana lilikuwa ni kubwa halafu lilivutia, ila alipomuangalia shangazi yake alimuona kuwa hayupo kawaida na kusogea karibu kumuuliza ambapo Tumaini aliamua kumueleza ukweli wa kila kitu, ila hapo alishangaa gafla kuona Erick akibadilika halafu alienda kuwafata wale watu kwenye lile eneo na kutoa amri moja tu kwao, walipobisha aliwapa kipigo hiko hadi Tumaini alijikuta akishika kichw ana kutokutaka kutazama tena, yani aliangalia chini tu maana hakuamini kile kilichokuwa kinatokea.
Ndani ya dakika tano palikuwa kimya kabisa pale shambani yani hapakuwa na kelele ya mtu yeyote maana wale watu wote hawakuonekana kabisa.
Kisha Erick alirudi kwa shangazi yake na kumuuliza,
“Kuna lingine?”
“Mmmh hapana shangazi”
“Je hiyo milioni mbili ya kuwapa hawa ulikuwa nayo?”
“Yani mwanangu, hapa nilikuwa na mawazo hatari hata sikujua cha kufanya, yani nilikuwa nataka kwenda kujaribu kuongea na mjomba wako.”
“Haya shangazi, nilikuwa nakwambiaje. Nenda tafuta hizo hela uje ujenge hata chumba kimoja hapa hawataweza kuvamia tena”
Tumaini na yule mama walimuangalia kwa makini Erick ambaye alikuwa akielekea kwenye bodaboda yake kwa ishara kuwa alitaka waondoke, basi Tumaini akainuka na kuanza kufatana nae, alimuaga yule mama na kuondoka akiwa na Erick yani Tumaini hakuelewa kitu chochote kwakweli.
Njiani alimuomba tu Erick amfikishe yeye nyumbani kwake halafu ndio Erick arudi kwao.
 
SEHEMU YA 413


Tumaini alianza kumsimulia mumewe kuhusu kitu alichokifanya Erick kwakweli hata mumewe alishangaa jambo hilo,
“Erick katoa wapi hizo nguvu?”
“Hata najua basi, yani nimebaki kushangaa hadi niliinamisha kichwa chini kwa uoga, yani Erick alikuwa kama wale wakaka wa kwenye sinema za kivita”
“Duh!! Katoa wapi hayo mapambano Erick?”
“Hata najua basi!! Yani nilibaki kushangaa tu na kustaajabu kwakweli, yani Erick sio mtu wa kawaida nakwambia”
Mara kidogo simu ya Tumaini iliita, aliangalia na kukuta yule rafiki yake mama Kulwa ndio alikuwa akipiga, akapokea na kuongea nae,
“Kheee huyo kijana wako nimemfananisha na babu mmoja kijijini kwetu, yani huyo babu alikuwa ni tishio”
“Babu gani?”
“Kuna huyo babu ilikuwa ni balaa, babu alikuwa na nguvu huyo akianza kupiga anachakaza kabisa, kwakweli nimemuogopa tena sana. Nimemuogopa kabisa”
“Yani mimi nimebaki mdomo wazi hadi muda huu sielewi ujue, sijawahi sikia kama mtoto wa kaka yangu yupo hivi, sijawahi sikia kabisa hayo mambo. Nimeshangaa kama wewe tu ulivyoshangaa”
“Tutaongea vizuri ukija tena huku”
Kisha yule mama alikata simu na hapo mume wa Tumaini alimwambia kuwa apige simu kwa baba Angel ili kuuliza vizuri kuhusu Erick
“Usikute wamemuweka kwenye shule ya ubondia”
“Mmmh inawezekana”
Tumaini alimpigia simu moja kwa moja mdogo wake na kumueleza hayo ambaye alishangaa pia ila hakushangaa sana kwani tabia ya Erick kwa siku hizo aliifahamu vizuri sana.

Mama Angel na baba Angel baada ya kuambiwa yale na Tumaini, waliona leo pia wapime kuhusu mtoto wao, je ataenda kulala kwakina Erica au atalala peke yake? Na kama akilala peke yake ni kitu gani kitatokea? Walitaka kutambua jambo hilo kwanza.
Basi muda wa kulala, mama Angel alienda kumchungulia Erick chumbani kwake na kweli hakumkuta na moja kwa moja alijua lazima Erick kalala chumbani kwakina Erica, basi mama Angel nae alienda kwakina Erica na kweli alimkuta Erick kalala na siku hii hata Sarah hakuwepo inamaana Sarah alilala kwenye chumba chake, basi mama Angel alimuamsha Erick pale,
“Weee inaka upesi, nenda kalale chumbani kwako huko. Usiniletee balaa mie”
Erick aliinuka na kwenda kulala chumbani kwake, kisha mama Angel alirudi chumbani kwake lakini kwa siku hii walijikuta siku nzima wakitumia kumchungulia Erick chumbani kwake ni kitu gani huwa kinatokea.
Walichoona ni kuwa Erick hakulala kabisa alikuwa akijigeuza geuza tu, kumbe Erick akitoka kupambana huko halafu akalala mwenyewe basi huwa anakosa usingizi kabisa yani kila walipoenda kuchungulia walimkuta Erick akiwa macho .
Kulivyokucha, mama Angel na baba Angel walijadiliana,
“Jamani huyu mtoto unajua hajalala usiku mzima!”
“Hii inaonekana itakuwa kawaida yake, ndiomana huwa anataka kulala na Erica”
“Mmmmh kwanini inakuwa hivi lakini?”
“Yani hapa, lazima tupate tiba ya tatizo la kijana wetu maana naona tatizo linakuwa kila siku, yani kila siku tatizo ni kubwa zaidi”
“Yani hapa ni huyo huyo dokta Jimmy ndio tumshikilie maana hapa hakuna cha kufanya kama hatujajua dawa ya tatizo”
“Dawa aliyosema dokta Jimmy si mimi wala si wewe unayeweza kuikubali, maana dokta Jimmy anataka mimi na wewe tukubali Erick na Erica walale pamoja kimapenzi, hivi kweli waliwapa watoto wetu dawa kwa lengo la kutuumiza!! Hivi binadamu wapoje jamani”
“Dah!! Mume wangu, naomba leo twende kanisani, siku hizi tunasahau sana kusali labda ndiomana tunapatwa na majanga kila siku, twende kwenye ibada leo”
“Sawa, umesema jambo jema, tutaenda familia nzima”
“Ngoja nikaandae chai ili tule kwa pamoja twende”
Mama Angel alienda kuandaa chai na aliita watoto wake wote pamoja huku wakinywa chai na akiwaambia kuhusu kwenda Kanisani, akasema Sarah,
“Ila mimi huwa sina nguo za kwenda nazo Kanisani”
Erica akamwambia Sarah,
“Na wewe, si utavaa zangu, siku zote unavaa za kwangu tatizo lako ni nini?”
“Hivi kumbe mnavaliana eeeh!!”
“Ndio, miili yetu inaendana halafu hadi viatu tunavaliana”
“Kumbe!! Basi vizuri hivyo, Sarah utavaa nguo za Erica”
Mama Angel alimtazama Erick ambaye ndiye pekee ambaye hakuongea wala kucheka pale mezani na alionekana akila kwa taratibu sana kuliko siku zote, mama Angel alimuangalia na kumuuliza,
“Na wewe vipi mwenzetu?”
Kabla Erick hajajibu rara kuna sauti ilisikika nje kwa nguvu na walipoisikiliza kwa makini mama Angel na baba Angel walijua moja kwa moja kuwa ile sauti ilikuwa ni sauti ya Rahim,
“Wewe wa kuitwa Erick unayejiita baba Angel kuja hapa nje upesi”
Baba Angel alishangaa kwakweli na kutoka nje, ila ile kitu ilifanya wote pale mezani kuanz akuinuka na kutoka nje ili wajue kuwa kuna kitu gani kinaendelea.
Rahim alikuwa amesimama kwa hasira huku amemshika mkono Samir, basi baba Angel alipotoka tu akamwambia,
“Wewe baba Angel feki nipe Angel wangu na umchukue Samir wako”
“Rahim, hebu twende pembeni kuongea, unaongea vitu visivyo na maana unawafaidisha watoto tu”
“Nawafaidisha kitu gani? Wanatakiwa kujua ukweli, nyie watoto, huyu Samir ni kaka yenu yani ni mtoto ambaye baba yenu kazaa na mwanamke mwingine halafu huyo Angel ni mwanangu mimi, yani mimi nilizaa na mama yenu kabla ya huyu baba yenu”
Hapo baba Angel alishikwa na hasira sana basi alijikuta akimsogelea Rahim na kumnasa kibao cha nguvu sana, kile kibao kilimfanya Rahim amtumie Samir kwa pembeni maana alikuwa na hasira sana kwa yale aliyoambiwa ukizingatia kamlea sana Samir bila kujua kuwa analea mtoto wa baba Angel kama ambavyo baba Angel amelea mtoto wake.
Rahim alimvamia baba Angel na kumpa mtama ambao ulimuangusha chini baba Angel ila kabla hajaanza kumshambulia, Rahim alishtukia akikabwa na kuinuliwa juu juu yani kile kitendo kila mtu alikishangaa sana, kitendo hiko kilifanywa na Erick, yani kila mtu alibaki akishangaa, hapo mama Angel alijikuta akijiwa na huruma ya Rahim alivyokunjwa na Erick, basi alisogea karibu ili kumzuia Erick ila alishangaa akisukumwa vibaya sana na Erick yani hapo mtoto wao alikuwa amebadilika kabisa, mlinzi wao nae alisogelea alimpa ngumi moja na kumfanya aanguke huko na kupoteza fahamu, yani kwa jinsi alivyokuwa amemkaba Rahim ni wazi alikuwa akitaka kummaliza kabisa, baba Angel aliona ile ni balaa, basi alijaribu kusogea karibu ila alipoona Erick akitaka kumpiga hadi yeye akaogopa na kurudi nyuma, hapo akili ya haraka ikamjia na kwenda kumvuta Erica ambaye alikuwa pamoja na wakina Angel wakimshugulikia mama yao ambaye ameanguka, baba Angel alimuomba Erica,
“Nakuomba nenda kamzuie kaka yako, ataua yule”
Erica akaenda mbele kabisa, ila bado Erick hakumuachia Rahim wala nini kiasi cha kumfanya Rahim kutokwa na jasho jingi sana, basi Erica akili yake ikacheza haraka na kwenda nyuma ya Erick na kumkumbatia, muda huo huo Erick alimuacha Rahim chini ambaye alianguka na kupoteza fahamu kabisa, basi Erica alimpeleka moja kwa moja Erick ndani na alimpa glasi moja ya maji, kisha aliongozana nae mpaka chumbani kwake, yani Erica hakutaka kuongea na Erick kwa muda huo wala nini zaidi ya kumtaka alale na kupumzika tu, kwakweli Erick alikuwa na hasira sana ila baada ya kukaa kidogo na Erica aliweza kulala na hapo ndio Erica alitoka sasa.

Kila mtu pale nje alikuwa haelewi kwakweli, ilibidi tu baba Angel na Samir wamkimbizie Rahim hospitali maana tayari waliona kuwa hali yake sio nzuri kutokana na kule kukabwa sana na Erick.
Mama Angel alikuwa amekaa na Angel, Sarah na Erica ambapo Angel aliuliza,
“Kwani Erick ana tatizo gani jamani?”
“Mmmmh sijui, labda muulizeni Erica mtu wa ndoto ndio atakuwa anajua”
Erica akasema,
“Siku nyingine Erick huwa anaweza kujizuia hasira zake ila leo toka asubuhi anaonekana kuwa alikuwa na hasira sana, itakuwa kuna kitu hakipo sawa kwake toka usiku”
Yani siku hii hata walisahau kama walipanga kwenda kwenye Ibada maana walihisi kila kitu kimevurugika kabisa, walihisi mambo yameenda ndivyo sivyo, walijadiliana sana ila hawakufikia muafaka wa majadiliano yao.
Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwake huku akijiuliza sana,
“Hivi huyu Erick ndio hizo sindano au kuna kitu kingine kati yake? Mbona amekuwa wa ajabu kiasi hiki!! Tutapata kesi sisi kama hatujachukua hatua kwa haraka sana”
Mama Angel akawaza kitu kingine ambacho walimzuia Erick kulala chumbani kwa Erica, waliwaza pengine ndio hasira zile maana inaonekana wazi hakuna mtu aliyekuwa akimsikiliza wakati kwa kawaida Erick aliwaogopa sana wazazi wake, ila hapo walimshangaa kwakweli maana Erick aliwabadilikia hadi wao.
Mama Angel aliamua kujilaza maana alihisi mgongo wake kuuma kwa kile kitendo cha Erick kumsukuma, pale alivyojilaza alipitiwa na usingizi kabisa.

Baba Angel alirudi nyumbani kwake na moja kwa moja kwenda chumbani kuongea na mke wake,
“Kwanza anaendeleaje huyu mtu?”
“Anaendelea vizuri, tumekutana na Maimuna pale kasema atakuja kutueleza vizuri ilivyokuwa ila ametaka nimuache pale na familia yake”
“Ila mambo naona kama yanazidi kuwa magumu, hivi ulitegemea kweli kama Erick angenisukuma hivi au angekutishia wewe kukupiga?”
“Unajua sielewi, kila nikifikiria lile tukio nahisi kuchanganyikiwa”
“Mume wangu, kiukweli tunahitaji msaada, tena msaada wa nguvu. Hebu jaribu tena kumpigia dokta Jimmy”
Baba Angel alimpigia dokta Jimmy simu ambapo mud aule ule ile simu ilipokelewa na dokta Jimmy,
“Ndio Erick, tena afadhali umenipigia maana nilitaka kukupigia muda sio mrefu”
“Eeeeh dokta nakusikiliza”
“Nasikia mlikuja kwangu ila mkanikosa, naomba kesho fanya juu chini mje tafadhari maana hili jambo ni lazima tulichukulie hatua kwasasa”
“Jambo gani tena?”
“Si jambo la watoto wenu hao, naomba mje”
“Sawa tutakuja”
Walikata simu, ila waliona ni vyema kwenda ili kujua mbivu na mbichi, juu ya kitu kinachoendelea kati yao na kati ya watoto wao.
Muda kidogo ule mlango wa chumbani uligongwa, walipomkaribisha mgongaji aliingia Erick yani baba Angel na mama Angel walitazamana, ila Erick alifika na kuwaomba msamaha wazazi wake,
“Baba na mama naomba mnisamehe sana, hata sijui ilikuwaje. Naomba mnisamehe sana”
“Usijali, tumekuelewa. Kuwa na amani tu Erick”
Baba Angel na mama Angel hawakutaka kuongea mengi sana wala kumuuliza maswali mengi Erick.

Leo mapema kabisa, baba Angel na mama Angel walijiandaa kwa pamoja na kuondoka kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy.
Walipofika moja kwa moja walikaribishwa ndani ambapo dokta Jimmy walimkuta amekaa kwenye bustani yake, kwahiyo walimfata alipo na kuanza kuongea nae kuhusu kinachoendelea, dokta Jimmy alianza kuwaambia,
“Hivi mnajua kama watoto wenu wale wanatakiwa kuwa na mwenzao!”
Mama Angel na baba Angel walishangaa na kuuliza,
“Mwenzao kivipi?”
“Nadhani hamnielewi, ila kabla ya yote kuna kitu kikubwa sana ambacho hamfahamu kuhusu watoto wenu”
Baba Angel na mama Angel walishtuka na kumuangalia kwa makini dokta Jimmy

Walipofika moja kwa moja walikaribishwa ndani ambapo dokta Jimmy walimkuta amekaa kwenye bustani yake, kwahiyo walimfata alipo na kuanza kuongea nae kuhusu kinachoendelea, dokta Jimmy alianza kuwaambia,
“Hivi mnajua kama watoto wenu wale wanatakiwa kuwa na mwenzao!”
Mama Angel na baba Angel walishangaa na kuuliza,
“Mwenzao kivipi?”
“Nadhani hamnielewi, ila kabla ya yote kuna kitu kikubwa sana ambacho hamfahamu kuhusu watoto wenu”
Baba Angel na mama Angel walishtuka na kumuangalia kwa makini dokta Jimmy.
Kisha baba Angel alimuuliza,
“Kipi ambacho hatufahamu ikiwa kuhusu dawa tunafahamu?”
“Lipo ambalo hamfahamu, sio kuhusu dawa tu ila kuna jambo ambalo hamfahamu”
“Tuambie ni jambo gani?”
“Ngoja nimuite huyu mtu kwanza, hajui kitu ila nahitaji nae ajue”
Dokta Jimmy aliinuka na kwenda kumuita mtu huyo ambaye alikuwa ni Manka, alifika pale na kuwasalimia maana hakujua kama wamekuja hapo nyumbani kwa dokta Jimmy, kisha dokta Jimmy akauliza,
“Kwani Sarah yuko wapi Manka?”
“Yupo kwa hao japo, hao ndio wananiharibia mtoto wangu”
“Samahani, Manka. Hawa hawamuharibu mtoto wako maana yule ni mtoto wao”
Manka pamoja na mama Angel na baba Angel walibaki wakishangaa na kumuuliza kwa pamoja dokta Jimmy,
“Kivipi?”
“Yule Sarah ni mtoto wenu wewe Erica na Erick”
Baba Angel na mama Angel waliangaliana kwa muda na kuuliza,
“Inamaana Erica na Erick sio watoto wetu? Au kuna mmoja kati yao sio mtoto wetu?”
Manka nae alimuuliza dokta Jimmy,
“Unazungumzia kitu gani dokta? Sikuelewi ujue!”
“Naomba mnisikilize kwa makini, msiyaingilie haya maelezo ili nisikosee kuwaelezea, nisikilizeni kwa makini sana”
“Mmmh!!”
Walijikuta wote watatu wakiguna, kisha dokta Jimmy alianza kuelezea,
“Ni hivi, mzee Jimmy alikuwa na mahusiano na Manka, na kwa hakika alimpenda sana ila sehemu ambayo hakumuelewa Manka ni pale Manka alipodai kuwa ana mimba yake wakati mzee Jimmy anakumbuka wazi kuwa siku zote alilala na Manka kwa kutumia kinga, ila hakukataa kwani Manka alikazana kuhusu jambo hilo. Kuna siku mzee Jimmy alimuwekea mtego Manka, na hapo alitambua ukweli halisi wa mtoto wa Manka wakati huo Manka akiwa na mimba kubwa sana, kwakweli mzee Jimmy alichukia mno, ingawa alijua wazi kuwa mimba si yake ila alichukia zaidi kumjua muhusika wa ile mimba. Tulikuwa na mpango na mzee Jimmy wa kubadilisha watoto yani tulitaka mtoto wa Sia tumbadilishe na mtoto wa Erica ila hapo kuna mtu alituletea dawa ndipo mzee Jimmy aliona hiyo dawa itakuwa ni bora zaidi kwani Erica na Erick mtaumia moyo sana pale watoto wenu watakapotakana kimapenzi, roho yake ilikuwa ikiumia sana kwa kile kitendo cha Erick kutomsikiliza na kuamua kumuoa Erica, na swala la Erica kumkataa lilimuumiza sana alijikuta akiumia sana moyo wake na ndiomana alifikia hili swala la kumbadilishia Erica mtoto. Wakati Erica anakaribia kujifungua, mzee Jimmy aliamua kumtuma mbali Erick ili asiweze kushuhudia kile tulichokuwa tunataka kukifanya. Erica alipoletwa hospitali moja kwa moja tulimpeleka kwenye operesheni ila ukweli ni kwamba Erica alijifungua mapacha watatu badala ya wawili, na hapo mmoja alikuwa wa kiume na mwingine alikuwa wa kike, hapo kidogo hata sisi tulipagawa ila akili ya mzee Jimmy ilikuwa ikifanya kazi haraka kupita maelezo kwani muda huo hata Manka nae alikuwa kajifungua ila alijifungua mtoto wa kiume, yani akili ya mzee Jimmy ilimtoa yule mtoto wa kiume wa Manka na kumuweka pembeni halafu tukamchukua mtoto mmoja wa Erica ingawa ni wa kike tukamuweka kwa Manka, ili Erica asijue chochote kile, ukizingatia alishaambiwa kuwa ana mapacha wa kike na wa kiume tumboni. Basi kilichofanyika pale ni kuwaweka watoto alama na kwenda kuwaweka sehemu ya watoto ambapo baada ya muda mfupi alifika mama yake mzazi na Erica akitaka kuona wajukuu zake, ilibidi tu tumuonyeshe basi muda ule mzee Jimmy akasema kuwa kitakachoendelea ni ule mpango wetu wa sindano tu, ndio tulipowarudisha tukawadunga sindano zetu basi, alipozinduka Erica tukamkabidhi mtoto wake, wakati huo mtoto wa Manka yupo mafichoni. Yule mtoto nilimlea mwenyewe pamoja na mtoto wa Oliva, ila nilikuja kumkabidhi Sia wakati mtoto ana miezi mitatu kasoro hivi maana mzee Jimmy alikuwa akimuhudumia pia Sia sababu alibeba mtoto wa Manka, na alimpa Manka mtoto wa Erica ili mali zote atakazoziandikisha kwa mtoto basi zirudi kwenye familia yake. Naomba mnisamehe na pia mumsamehe mzee Jimmy, ila Sarah ni mtoto wenu pia”
Kiukweli Manka alikuwa ameinama huku akilia tu wakati huo baba Angel na mama Angel walikuwa wakishangaa maana hii habari iliwashangaza sana, yani baba Angel alijiuliza sana dhumuni la baba yake bado hakupata jibu kabisa, kisha Manka alianza kumwambia dokta jimmy,
“Yani siku zote unanichekea kumbe kuna ujinga wewe na mzee Jimmy mmenifanyia dah!! Kwanini lakini jamani!”
“Nisamehe Manka, ila na wewe ulizidi kumdanganya yule mzee mtoto wa kwake wakati sio wa kwake, yule mzee mwenzio hata hakuwa na uwezo wa kuzalisha tena ndiomana alikugundua mapema tu kuwa kuna mahali umebeba ile mimba basi akaanza kukufatilia”
Baba Angel akamuuliza dokta Jimmy,
“Bado kwetu hujamaliza, kwahiyo ndio Erica na Erick mkawachoma sindano?”
“Ndio, tena Erick tulimchoma mbili ila yeye iwe rahisi zaidi kumpenda dada yake, na kwa nguvu ya ile sindano tuliamnini kama Erick akimshawishi kidogo dada yake basi wangefanya maana inafanya kazi pia kwenye mwili wa Erica”
“Dah!! Mna dhambi sana nyie watu, sasa kwanini jamani, kwanini lakini eeeh!!”
“Sio mimi ila ni mzee wako, alikuwa na lengo la kuwakomesha”
“Ila amekomesha na ukoo wake, kwakweli nimechukia sana. Halafu unasema sio kosa lako wakati wewe usingekubali najua isingewezekana maana baba huo utaalamu wa kuchoma sindano autoe wapi? Wewe ni mbaya sana dokta Jimmy, wewe na baba yangu ni mashetani”
“Tusamehe bure Erick, ila njia pekee ya kumuokoa mwanao na huo ubondia wake ni kuhakikisha kuwa hao mapacha wawili wanalala pamoja kimapenzi”
“Wewe dokta hebu nitolee huo upuuzi wako mie, mmefanya ujinga halafu unaendelea kutuambia ujinga”
“Sio ujinga Erick, ni tiba kwaajili ya watoto wako”
Mama Angel aliyekuwa amekaa kimya kidogo, aliinuka kwa muda huo na kumzaba kibao dokta Jimmy kisha akasema,
“Ni mjinga sana wewe daktari, kwakweli hapa nilipo nina hasira sana na wewe”
Kisha mama Angel alimzaba kibao cha pili na kusema,
“Hiko ni kibao cha kukumbusha yale uliyonitendea, hivi kabla ya kufanya hayo mlijaribu kufikiria maumivu tutakayoyapata kwenye mioyo yetu? Kwanza nimekereka sana kwanini mtoto wangu mumchukue wakati mdogo?”
Dokta Jimmy akajieleza kwa kifupi,
“Mwanao alichukuliwa ili kuandikishwa kiurahisi mali za babu yake”
Mama Angel alimzaba kibao kingine yule dokta na kusema,
“Kwani asingepewa hizo mali angekufa? Hizi ni binadamu gani nyie ambao mlikosa utu kabisa, ni viumbe gani nyie?”
Mama Angel alijikuta akipandwa na hasira sana, hivyo kuanza kumkaba dokta Jimmy yani ni baba Angel tu ndio aliyemtoa na kuondoka na mke wake kwani kwa muda ule wote walikuwa na hasira na dokta Jimmy.

Manka alibaki pale akilia kama mtu aliyefiwa kabisa, alilia sana alijikuta akikumbuka msiba wa dada yake vizuri, alilia akikumbuka maneno ya dada yake, yalikuwa yakimjia kichwani kwake,
“Manka, usidhani hao wanakupenda, hao ni wanafki na hawakupendi wala nini. Ipo siku utakumbuka maneno yangu kuwa hao hawakupendi, haiwezekani watu wanaokupenda wanakuwa kwako kwaajili ya maslahi yao tu na kukutuma kufanya kazi zao za ajabu ajabu, hawakupendi hao, ipo siku utaniambia”
Manka alijikuta akipaza sauti na kusema,
“Uko wapi Linah, uko wapi dada yangu? Leo imefika ile siku uliyosema kuwa nitaumbuka basi ndio leo nimeumbuka mimi Manka, yule mtoto niliyekuwa naringia kila mahali sio mtoto wangu, mtoto ambaye niliteseka katika kulea, mtoto ambaye niliogopa hata kumuangushia kofi langu, nakuja kugundua sio mtoto wangu. Naumia mimi kushinda nilivyokuwa nahisi mwanzo kuwa nilizaa mapacha ila kwasasa maumivu yangu ni maradufu, yule aliyelelewa maisha ya kimasikini hadi nikaamua kumsaidia na bado nikamuadhibu kwa kutembea na mwanangu kumbe ndio mwanangu”
Manka alilia kama mtoto mdogo, hata huyu dokta Jimmy hakuweza kumbembeleza, maana kila aliposogea Manka alijibu kwa ukali,
“Niache, shetabi mkubwa wewe. Toka mbele yangu shetani”
Ni wazi kuwa Manka alikuwa na hasira sana, yani leo alilia kushinda siku aliyolia kwenye kaburi la mzee Jimmy, alijikuta akisema,
“Kwanini lakini mzee Jimmy umenifanyia hivi? Si bora ungekataa tu kuwa mtoto wako simtaki halafu ungeniacha na mwanangu ningejua jinsi ya kumlea, sasa mwanangu wa ukweli hanitaki na huyu wa uongo hanitaki pia”
Yani kelele alizokuwa akipiga Manka hadi watu walianza kuzunguka nyumba ya dokta Jimmy huku wakitaka kuingia na kujua kuna nini, basi dokta Jimmy kwa haraka haraka alienda kuchukua dawa na kumpulizia Manka ambaye alianguka chini na kupoteza fahamu, kisha akambeba na kumpeleka ndani ya nyumba kabisa.

Mama Angel alijikuta akishindwa hata kuongea kitu, alikuwa tu akifikiria toka siku ya kwanza kukutana na Sarah na jinsi alivyoona yeye na Sarah wameendana damu, akakumbuka zawadi ambayo Sarah alimletea wakati katoka kujifungua, akakumbuka ucheshi wa Sarah, akajikuta machozi yakimtoka kila alipokumbuka jinsi Sarah alivyomshawishi Elly ambaye ni binamu yake kutembea nae, mama Angel alijikuta akipatwa na maumivu kwa hilo, aliona ni vyema angelea mwenyewe watoto wake wote. Akawaza pia kuhusu dawa ambayo wameambiwa kuwa mtoto wake Erick na Erica wamepewa, alijikuta akizidi kuumia moyo maana anaambiwa suluhisho ni Erick na Erica kulala pamoja kimapenzi, moyo wake unavuja machozi haelewi kabisa, anaanza kuhisi laana ya yeye kulala na ndugu yake yani Derrick ndio ambayo imerudi kwa watoto yani mtoto wake kulala na mtoto wa Derrick halafu matukio yamefanana kwa kiasi Fulani kwani Sarah nae alipata mimba ya Elly na kuitoa kwa njia ya kujizuia kupata mimba, alijikuta akisema,
“Hii ni laana”
Alianza tena kulia kwa sauti, ilibidi baba Angel apaki gari pembeni na kuanza kumbembeleza mke wake,
“Laana ya nini mke wangu? Haya mambo yaache tu tutagundua ufumbuzia juu ya kitu cha kufanya, usiumie moyo mke wangu, hata mimi naumia vile vile ila Mungu ni mwema hata hapa bado anatupigania”
“Roho inaniuma Erick, kwanini lakini kwanini mzee Jimmy anifanyie haya? Ni sababu ya ile milioni kumi au kuna lingine? Ile hela yote aliichukua Dora hata mzee Jimmy anatambua hilo ila kwanini anifanyie hivi, kaniumiza sana tena sana”
“Pole mke wangu, mimi na wewe wote tumeumia yani hujaumia peke yako, cha msingi ni kumuomba Mungu atupe subira na busara ili tujue cha kufanya maana akili zetu zimefika mwisho kabisa kwenye swala la kufikiria kuhusu haya mambo”
Baba Angel alijitahidi kumnyamazisha mke wake, yani hata yeye alikuwa na uchungu ila alitakiwa kupooza uchungu wake ili waweze kufika nyumbani salama, mama Angel sasa ilikuwa kama leo kapata uthibitisho maana siku zote alipokuwa akisikia kuwa watoto walipewa dawa, aliona kama masikhara, sasa leo aliona kumbe ni kweli kuna tatizo kubwa sana juu ya watoto wake.
Njia nzima alikuwa akilia tu, yani hakuwa na amani mama Angel kabisa.

Wakiwa nyumbani siku hii, Angel na wadogo zake waliamua tu kula kwa muda huo kwani waliona wazazi wao wamekawia kuja, walikula huku akiongea kidogo ambapo Angel alimuuliza Sarah,
“Hivi huwa unamkumbuka mama yako Sarah?”
“Ndio huwa namkumbuka sana tu, yule ni mama yangu na siwezi kupingana na hilo. Akijirekesbisha basi mimi nitaenda kuishi nae, ila kiukweli natamani kama mama yenu ndio angekuwa mama yangu, ningefurahi sana”
“Aaaah usijali, mama ana upendo, huwa anapenda watu wote yani yeye ndio kazaliwa hivyo kwa upendo”
Muda kidogo mama Angel na baba Angel waliingia yani mama Angel alishindwa kujizuia kabisa kwani moja kwa moja alienda kumfata Sarah alipo na kumkumbatia huku akilia tena alilia sana hata watoto wake wote walimshangaa mama yao, alimshika na kusema,
“Nakumbuka maneno ya marehemu baba yangu siku anakata roho akiwa mikononi mwangu aliniambia nichunge sana maana binadamu ni wabaya, anaweza akakuchekea machoni kumbe moyo I anakupalia makaa.”
Akakumbuka jinsi mzee Jimmy alivyojitolea kugharamia harusi yake na mume wake, yani mzee Jimmy aligharamia kila kitu kwenye ile sherehe na kweli ilifana, yani mama Angel hakufikiria kama kuna siku ambayo mzee Jimmy angetenda jambo kama lile, licha ya mabaya ambayo mzee Jimmy alikuwa akiyafanya ila hakufikiria kama angefanya kitu cha namna ile. Alimkumbatia sana Sarah na kumwambia,
“karibu nyumbani mwanangu, hapa ni nyumba ni kwenu. Mimi na mama yako kabisa na hawa ni ndugu zako kabisa”
Alimfata Erick na Erica na kuwavuta kwa pamoja kisha akawakumbatia na kusema,
“Naomba mumpokee Sarah ni ndugu yenu kabisa”
Akamvuta na Angel huku akisema yale maneno tena, kwakweli ilikuwa ni kitu cha kustaajabisha kwa upande wa watoto ila walikuwa wakiitikia tu huku wakimuangalia mama yao maana walishindwa cha kusema wala kufanya kwa muda huo.
Mama Angel aliporidhika ndipo alipoenda nyumbani kwake kumalizia machungu yake sasa.
Angel na wadogo zake walikuwa wakishangaa pale ila mara Erica akawaambia,
“Ndio, Sarah ni pacha wangu”
Angel alimuangalia na kumuuliza,
“Kivipi?”
“Tulizaliwa watatu ila Sarah walimuiba, hii kitu imenijia mara kadhaa ila nilikuwa siiielewi na sasa nimepata kuielewa”
“Kheee kwahiyo Sarah….!! Hata sielewi mwenzenu, haya Sarah karibu kwenye familia yetu. Haya mambo ya kuiba watoto mmmh”
Kisha walitoa vyombo pale na wote kwa pamoja kuelekea vyumbani kwani kila mmoja alikuwa na mawazo yake, haswa Sarah hakuna kitu ambacho alielewa kwa wakati ule ndiomana alikuwa akishangaa tu.

Usiku huu baba Angel alijaribu kuongea na mke wake ili akimtaka waweze kwenda kula chakula maana alionekana kutokuwa sawa kabisa, basi alianza kuongea nae,
“Kwanza kabisa mke wangu ni jambo la kumshukuru Mungu kuweza kuwafahamu watoto wetu wote”
“Na kuhusu swala la Erick na Erica?”
“Hili ni tatizo ila sio tatizo sana sababu tumejua ukweli na tutaweza kukabiliana nao, ni kujua tu jinsi ya kukabialiana nao”
“Au tuwaambie ukweli Erick na Erica kuwa walipewa dawa wakati wadogo!”
“Mmmh sijui kama itakuwa sahihi ila ikiwezekana inabidi tu tuwaambie ukweli maana najua hata wao wanashangaa ile hali waliyokuwa nayo, nina uhakika hata wao inawachanganya sana. Ni ngumu kwa kaka na dada kushikwa na hisia za kimapenzi kama wao, basi moja kwa moja hapa inatakiwa waujue ukweli ila tutapanga namna ya kuwaambia ukweli huo”
“Tusubiri wafanye mitihani basi”
“Hapo ni sawa mke wangu, ila kwa muda huu naomba twende kula chakula kwa pamoja halafu ndio tutakuja kulala, kumbuka toka mapema tupo kwa yule mjinga Jimmy, yani yule ni sawa tu na dokta feki jamani hadi kero kumfahamu”
Mama Angel aliinuka na moja kwa moja kwenda na mumewe sebleni na kuandaa chakula kisha kuanza kula, kidogo mlinzi wao aliwagongea mlango basi walimfungulia na kuongea nae,
“Vipi tatizo nini?”
“Yani bosi mbavu zinaniuma sana”
“Kheeee imekuwaje tena!! Nakumbuka Erick alikupiga ngumi usoni”
“Aaaah mama, Erick hafai yani sio mtu wa kawaida kabisa. Leo alikuwa akipita getini nikamwambia Erick ulinipiga sana hadi nilipatwa na kizunguzungu, jamani baada ya kumwambia hayo sikuamini kwani alinipiga ngumi moja kwenye mbavu zangu hapa hadi muda huu zinaniuma”
“Khaaa huyu Erick kafikia pabaya jamani”
Ila baba Angel na mama Angel hawakutaka kuongea mengi sana kwani kwa muda huo huo walimuahidi yule mlinzi kuwa kesho watampa pesa za kuweza kwenda kuangalia hali yake ya afya.

Siku ya leo, mama Angel aliamua kuwaita wanae wote maana aliona ni vyema kuweka sawa kuhusu swala la Sarah kuwa ni ndugu yao ili watoto wake wasijiulize sana kuhusu jambo hilo, basi alianza kuongea nao,
“Jamani watoto wangu, najua jana mmenishangaa sana ila hata mimi hii kitu ilinishangaza ndiomana nilijikuta kama nimepagawa vile, mimi mama yenu wakati wa kujifungua uzao wa pili kumbe nilijifungua mapacha watatu ambapo sikutambua hili wala nini, nilijua tu ni wawili yani huyu Erica na Erick kumbe ilikuwa ni watatu, nasikia babu yenu ndiye aliyempeleka pacha mmoja na kumbadilisha na mtoto halisi wa Manka ambaye ndio mnamtambua kama mama yake Sarah, kitendo kile kilifanya Sarah akulie kule na ni yeye ndiye aliyempa jina Sarah, ni jina la mama yake mzazi, kwahiyo Sarah kapewa jina la nyanya yake. Hivyobasi naomba mumtambue Sarah kama ndugu yenu, najua kwako Sarah ni ngumj sana ila ndio hivi ilivyokuwa”
Sarah akauliza,
“Na mama yangu yule anayajua haya? Yuko wapi kwasasa? Na mwanae halisi ni nani?”
“Mtoto halisi wa mama yako ni Elly ambaye ni binamu yenu halafu mamako amejua kila kitu, hata yeye hii habari imemchanganya sana”
“Ningependa nimuone najua atakuwa amelia sana”
“Usijali Sarah, nitakupeleka alipo maana ndiye aliyekulea na kukufikisha hapo ulipo”
“Inamaana yule niliyeonyeshwa kwenye picha kuwa ndio baba yangu ni babu yangu?? Inamaana lile kaburi tunaliendaga na mama kumtembelea baba ni la babu na ndiye aliyefanya yote haya?”
“Ndio ni yeye”
“Ila mama aliniambia kuwa baba alinipenda sana, unajua sielewi eeh yani sielewi kabisa”
Mama Angel aliamua kukaa pembeni na Sarah ili kuweza kumuelewesha kilichopo, ni kweli siku zote Sarah alitamani kuwa mtoto kabisa wa mama Angel ila hakufikiria kama itakuwa kwa namna hiyo.
Mama Angel alipoongea kidogo na Sarah aliamua kumpigia Manka simu kwanza ili Manka aweze kuongea na binti yake, ila ile simu iliita tu bila ya kupokelewa yani hapakuwa na matumaini yoyote ya kupokelewa kwa ile simu ilibidi mama Angel aache tu na kumuahidi Sarah kuwa wataenda kumtembelea.
Wakati huo alifika Sia akiwa ameongozana na Elly, kwahiyo walimkaribisha tu.

Dokta Maimuna aliwasiliana na Jack kuwa ampeleke yule Derrick mdogo nyumbani kwake, ili waweze kuongea nae kidogo.
Basi Jack alijiandaa na Derrick na kuondoka nae wakielekea nyumbani kwa Rahim.
Walifika pale, ila Rahim bado alikuwa kitandani kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa Erick, basi Rahim alikiwa hajiwezi kabisa.
Dokta Maimuna aliomba kidogo Jack ampe nafasi ili aweze kuongea na Derrick, ambapo Jack hakubisha na kuwaach kwaajili ya maongezi, basi walianza kuongea pale ambapo dokta Maimuna alimwambia Derrick,
“Ni hivi, wewe ni mtoto wangu na wala mamako sikujua mambo haya, unajua tena hizi hospitali nazo kumbe walituchanganyia watoto, mimi wakanipa mtoto wa mamako halafu mamako wakampa mtoto wangu ambaye ndio wewe”
Derrick alimuangalia na kumwambia,
“Sikuelewi”
“Kwani mama yako hajakwambia?”
“Kaniambia ila na yeye sijaweza kumuelewa”
Basi dokta Maimuna pale aliamua kutumia njia mbalimbali ili kufanya Derrick aelewe ujumbe ila ni kwa kiasi kidogo sana Derrick aliweza kuelewa.
Ilibidi dokta Maimuna akamuomba Jack kuwa wajaribu kupanga siku hizi wawe wanakaa karibu na watoto wao wa ukweli yani yeye Jack awe karibu na Samir halafu Derrick awe karibu na yeye dokta Maimuna,
“Mmmh sijui kama Derrick ataweza, unajua huyu mtoto hajazoea na hajawahi kuishi na mtu mwingine tofauti na mimi!”
Hapo dokta Maimuna alimtazama kwa makini na kutaka kuleta maelezo mengine, ila muda kidogo mahali pale alifika mkwe wa dokta Maimuna yani baba mzazi wa Rahim yani yule Mwarabu, mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Derrick mdogo kwakweli yule mwarabu alijikuta akisimama kama dakika kumi bila kuongea huku akimshangaa tu Derrick.

Baba Angel leo alipotoka ofisini tu, basi moja kwa moja aliamua kupitia kule alipokuwa akiishi marehemu Linah kwaajili ya ile barua.
Alifika na kumkuta yule msichana wa kazi ambaye baada ya salamu tu alienda kumletea baba Angel ile barua ambaye aliifungua na kuanza kuisoma palepale ila ule mstari wa kwanza ulimshtua na kumfanya aache kuisoma ile barua.

Alifika na kumkuta yule msichana wa kazi ambaye baada ya salamu tu alienda kumletea baba Angel ile barua ambaye aliifungua na kuanza kuisoma palepale ila ule mstari wa kwanza ulimshtua na kumfanya aache kuisoma ile barua.
Kisha baba Angel alianza kuangalia mara mbili mbili na kumuita yule mdada wa kazi akamuuliza,
“Unauhakika hii barua imeandikwa na marehemu Linah?”
“Ndio, na hakuna aliyeiona yani wewe ndio wa kwanza kuifungua, nisingekiuka kile ambacho alikisema, niliishi nae kama mama yangu mzazi”
“Aaaah sawa, hakuna tatizo. Kwaheri”
Baba Angel aliiweka ile barua na kwenda kuisoma nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake alienda kuoga na kumuomba jambo mkewe kuwa anhitaji utulivu kiasi kwahiyo alienda kwenye sebule yao nyingine na kuifungua ile barua na kuanza kuisoma, nayo ilianza,
“Najua tu hii barua umeipokea na kuanza kuisoma mbele za watu wakati mimi nataka uisome sehemu iliyotulia”
Baba Angel akapumua na kuanza kuisoma tena ile barua kwa makini zaidi,
“Erick, nilikupenda sana na hili siwezi kubisha maana nilikupenda halafu niliamini kuwa wewe utakuja kuwa mume wangu, niliamini katika nguvu nilizokuwa nazo kiasi kwamba niliweza kupambana na wanawake wengi uliokuwa nao, kwa kipindi hiko ni mwanamke wako mmoja tu ambaye alinishinda kwenye mapambano naye alikuwa ni Sia, sio kwamba alinishinda kwa ubavu hapana maana ubavu huo hakuwa nao na kama ningeamua basi ningemchakaza kwa dakika ingawa nguvu alikuwa nazo. Ila hakuna mtu aliyekuwa na maneno ya karaha kama Sia, alikuwa na maneno ya kukera na yale ya kuumiza moyo kiasi kwamba ukitaka kumpiga unajikuta umeishia njiani maana hujui ni wapi uanzie kugombana na Sia, alikuwa na mtindo wa kuuma na kupuliza. Ni yeye alinishinda ila niliamini kama hujamuoa yeye basi utanioa mimi. Siku nakutana na Sia akaniambia wazi kuwa umeoa, tena umeoa mwanamke mwingine kabisa ambaye niliwahi kutaka kumpiga pia, niliumia moyo ila niliacha maisha yaendelee. Nilipoachana na wewe niliwahi kuwa na mausihano kadhaa ila mahusiano yale hayakuzaa matunda kwani wanaume wote walikuwa ni waongo na hawakuwa na mapenzi ya kweli, ndipo nilipompata kijana Junior, sikufikiria kama ningeweza kuwa na mahusiano na mtoto mdogo kama Junior, ila kuna siku nilienda disko kujirusha na ndio huko nilipokutana na Junior kwa mara ya kwanza, kila nilipokuwa nikicheza alikuja nyuma yangu na tukacheza wote, baada ya hapo tulikunywa sana pombe, muda wa kuondoka sikuweza hata kuendesha gari langu sababu ya ulevi, basi Junior akaamua kunirudisha nyumbani kwangu, ila Junior hakuondoka bali nililala nae hadi asubuhi, ni akili za pombe ndio zilinituma kufanya vile ila baada ya hapo ndio mapenzi yangu kwa Junior yalipozaliwa, nilimpenda, nilimjali na kumthamini, kikubwa zaidi kila nilipomuhitaji alikuja kuwa na mimi. Ndiomana alipogeuka nilikuwa tayari kutumia nguvu ili kumrudisha Junior mikononi mwanangu, roho imeniuma sana baada ya kujua kuwa Junior alikuwa ni mtoto wa ndugu yangu James, huyu James nilikuwa napatana nae sana, na tena amenisaidia vitu vingi sana, sikutegemea kabisa kama mimi ningechukua maamuzi ya kutembea na mwanae tena kumpenda kupita kiasi yani kupita maneno. Ni kweli nilibahatika kupata mimba ya Junior katika umri mkubwa huu, niliamua kumzalia mwanaume niliyempenda kwa dhati ila nilipogundua kuwa ni mwanangu niliona aibu sana sikujua pa kuiweka sura yangu, na ndio wazo la kutoa mimba liliponijia kichwani. Niliamua kunywa dawa za kutoa mimba, na kuna mahali walinishauri kitu cha kufanya, sikutaka kwenda hospitali kwasababu zangu mwenyewe ambazo hata nikifa nitakufa nazo moyoni mwangu. Damu ni nyingi sana zimenitoka siku zote hizi hadi mara ya mwisho nilikupigia simu ila hadi muda huu hujatokea Erick nadhani utapata tu ujumbe kuwa Linah amekufa, kwa upande Fulani habari ya kifo changu itafurahisha sana familia yako. Ila kuna jambo kubwa sana ambalo limejificha katika familia yako pia, sio kila kitu mtu utajua, vingine huwezi kuvijua, yani kuna jambo zito mno. Mchunguze vizuri binti yako Erica utagundua kuwa naongelea nini, nilikutana mara kadhaa na huyo mtoto ila niliweza kumsoma, mchunguze vizuri kijana wako Erick utagundua, na utakapogundua hayo yatakuumiza sana, utakosa raha na amani katika moyo wako ila itakubidi kuukubali ukweli halisi wa kinachoendelea. Erick, ni wazi nilikupenda sana, yote niliyokuwa nafanya kwako chukulia tu ni kama changamoto za maisha, ni kama changamoto ulizozipata kwa Sia ila najua mtu huyu kwasasa amekuwa mtu wa karibu kwako na unaongea nae vizuri. Hata nikifa usiache kuja kutembelea kaburi langu mara kwa mara, nadhani nitakuwa nafurahi huko nilipo kwa kukuona ukinijali hata kama nimekufa. Ila narudia jambo hili, wachunguze vizuri watoto wako hawa, kuna jambo kubwa sana limejificha kati yao, kuna kitu kikubwa sana kati ya watoto wako hawa wawili namaanisha huyo Erick na Erica, Ila kuna rafiki yako dokta usisahau kumtafuta kwaajili ya watoto wako hawa halafu kitu kikubwa jihadhari sana na mwanao Erick kula ndizi, kuna kitu kiliwekwa kwa kupitia ndizi mbivu kwa yeye, kwaheri”
Ile barua iliisha na baba Angel alipumua huku akiiangalia mara mbili mbili huku akijiuliza maswali kadhaa,
“Anamzungumzia rafiki yangu dokta yupi? Nina marafiki wengi ni madokta lakini sio dokta Jimmy maana hajawahi kuwa rafiki yangu na kwamwe hatokuwa rafiki yangu. Na matatizo ya watoto wangu anazungumzia matatizo ya sindano au kuna mengine tena? Mmmh bora angekuwa hai ningemuuliza vizuri”
Baba Angel aliikunja ile barua na moja kwa moja kwenda kuiweka chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 415 ......... MWISHO


Usiku wa siku hii waliitumia kama familia kwaajili ya kumuaga Erick, ila baba Angel alikuwa na mashaka sana kuwa kama mwanae wamemtangaza basi itakuwa ni ngumu sana kuweza kutoroka hapo nchini, Erica alimuangalia baba yake na kumuuliza,
“Baba, una mashaka na safari ya Erick?”
“Kiukweli sina raha kabisa”
“Hapana kuwa na amani tu, ataondoka salama”
Basi Erick kusikia vile, alimvuta Erica pembeni na kuongea nae,
“Ila je nitaweza kuishi bila kukuona wewe kabisa kwa siku zote?”
“Kwani umeambiwa kuwa hutoniona siku zote? Kuna siku utaniona tu hata usijali, nenda tu huko kwa usalama wako Erick. Mimi mwenyewe binafsi sitaki upatwe na matatizo yoyote yale”
“Sawa nimekuelewa, ila nitakukumbuka sana”
“Najua hilo Erick, ila jiokoe kwanza kwa haya yaliyopo”
Basi wakarudi na kula kwa pamoja na kuagana nae maana kesho yake ndio alikuwa akianza safari yake, kwa siku hii Sarah na Erica walilala nae pamoja tena.

Muda wa safari tu ulipofika, baba Angel aliondoka na Erick mpaka uwanja wa ndege na kukutana huko na Jack, kisha akaongea na Jack pale jinsi ya kumsaidia mtoto wake ambapo kuna namba za mtu wa kumsaidia ambazo Jack alimpa kisha muda ulipofika moja kwa moja Jack na Erick walimuaga vizuri baba Angel na wenyewe wakaondoka.
Baba Angel alikaa pale akiangalia angalia na muda ulipofika aliamua kuondoka ambapo moja kwa moja alienda kukutana na mtu ambaye alipewa namba na Jack, basi alikutana na yule mtu ambaye aliwasiliana nae, basi yule mtu alimsalimia baba Angel na kujitambulisha jina lake,
“Mimi naitwa Ayubu au baba Yusra, karibu sana”
“Asante, mimi naitwa Erick au baba Angel. Nashukuru sana kukufahamu”
“Jack alinieleza mambo mengi tu kuhusu yanayokusibu”
Kidogo simu ya yule Ayubu ilianza kuita, basi baada ya kuongea nayo ndio akamuangalia baba Angel na kumwambia,
“Oooh kuna jirani yangu mahali Fulani nasikia ameuwawa, leo wamenikumbuka na wanahitaji nifanye uchunguzi wa hiyo kesi ili mtuhumiwa akamatwe”
“Ooooh sasa itakuwaje?”
“Hapo pagumu kidogo, ila unaonaje twende nyumbani kwangu ili ukapafahamu”
Baba Angel alikubali na kwenda pamoja na huyu Ayubu ili apafahamu nyumbani kwake.
Kufika nyumbani kwa Ayubu alishangaa kuona binti wa Ayubu akimfahamu yeye vizuri sana,
“Nakufahamu ndio, wewe si baba yake Angel!!”
“Ooooh kumbe unamfahamu Angel?”
“Ndio namfahamu nilisoma nae yule”
“Aaaah, nafurahi kujua hilo. Nitamwambia basi”
Kisha baba Angel aliagana pale na Ayubu huku wakitegemea tena kuonana kwani Ayubu ndio alikuwa anataka kwenda kwenye huo msiba.

Baba Angel alirudi nyumbani kwake lakini moja kwa moja alijua wazi kuwa yule Ayubu ameitiwa msiba wa Moses ila hakutaka kumuonyesha mshangao mapema, alitaka tu akimaliza hayo mambo ndio aweze kuongea nae.
Usiku wa siku ile baba Angel alipigiwa simu na Ayubu kisha kuanza kuongea nae,
“Jirani yangu anaitwa Moses, mazingira ya kesi yake yanafanana na ambayo amenielezea Jack, je ndio kesi ambayo mwanao anahusika”
“Mmmmh tuonane kwanza ili tuongee vizuri”
“Usijali, nataka niweke sawa haya mambo, kama ni yeye niambie ili nijue jinsi nitakavyowajibu kuhusu ushahidi wangu”
“Ngoja basi nimuulize vizuri halafu nitakujulisha”
Baba Angel alikata ile simu huku akiwaza kwa muda na kuamua kumpigia Jack ila kwa muda huo Jack hakupatikana hewani, aliamua kumtafuta kwenye mtandao wa kijamii na kumpata kisha akamuuliza,
“Yule Ayubu kaniuliza swali ambalo ni kweli kabisa muhusika ni Erick, je nikubali? Haiwezi kuwa tatizo badae yani labda watumie kama ushahidi?”
“Hapana usijali, yule ni ndugu yangu kabisa hawezi kukufanyia kitu kibaya, nishamueleza kuhusu mimi na wewe, hawezi kufanya ubaya, wewe mueleze tu kila kitu naye atajua namna ya kukuepusha na hilo janga”
Ndipo baba Angel alipopata ujasiri wa kuwasiliana tena na yule mtu na kumwambia kuwa mwanae ni kweli ingawa hana uhakika kama kahusika kwa asilimia mia moja,
“Basi ngoja nitajua jinsi ya kufanya, usijali kitu chochote. Kuwa na amani tu”
Basi baba Angel alikata ile simu, ila kiukweli hakuwa na raha kabisa yani mambo hyote alikuwa akiyafanya ilimradi tu.

Wakati mitihani ilipokaribia, ilibidi baba Angel ampeleke Erica akaishi kwa dada yake yaani Tumaini ili iwe rahisi maana kule kwa mama yake ni mbali sana, ingekuwa ngumu kwa Erica kwenda shule na kufanya mtihani.
Basi waliongea kidogo pale na dada yake,
“Hayo mambo yataishia wapi?”
“Sijui dada yangu kwakweli ila Mungu anisaidie tu”
Kisha baba Angel aliondoka kwa dada yake, ila njiani alikutana na Sia na kuanza kuongea nae kwani anajua fika kuwa Sia anafahamu vitu vingi sana, kwanza Sia alianza kumuuliza baba Angel,
“mbona hewani hupatikani?”
“Simu yangu ilipotea”
“Halafu nyumbani kwako hampo familia nzima!”
“Aaaah matatizo tu, nipe khabari maana najua wewe huwa hupitwi”
“Na kweli sipitwi, nilikutana na Manka, yupo kama mtu aliyechanganyikiwa vile. Nasikia Moses amekufa, halafu mke wa Moses nae kachanganyikiwa sana”
“Duh!! Dokta Jimmy anaendeleaje maana simpati hewani”
“Huyo ndio hajulikani kabisa, ni wa kufa leo au kesho, hali yake ni mbaya sana kupita maelezo ya kawaida”
“Duh!!”
Hapa baba Angel ndio aligundua kuwa Erick hakumuua siku ile dokta Jimmy bali ameenda kummaliza Moses na shahidi wa mambo yote yale ni Manka tu ndiomana yupo kama kachanganyikiwa basi baba Angel aliona ni vyema kuongea na Manka pia huku akisaidiana na Ayubu katika kumsafisha mwanae.

Baada ya miezi miwili, baba Angel alimtafuta Manka ambaye alikuwa kama watu waliopungukiwa na akili, hata yeye mwenyewe binafsi alimuhurumia sana, ila alikaa chini na kuongea nae,
“Unajua sina amani, sina furaha moyoni, siwezi kuishi tena na Sarah maana kawapenda sana halafu pia siwezi kuishi na Elly, najihisi vibaya sana katika moyo wangu. Natamani ingetokea kitu moja kikubwa kifanyike hata niweze kuishi pamoja na wanangu hata niwe nawaona tu”
“Usijali, lazima tuhakikishe kuwa tutafanya kitu. Ngoja nikuulize, kesi ya kifo cha Moses imeishia wapi?”
“Ni wazi aliyeua ni mwanao, ila ulichokifanya Erick unakijua mwenyewe, leo hii inasemekana kuwa Moses kajiua mwenyewe, halafu dokta Jimmy alipata ajali eti ajali ndio imemuweka kitandani hadi umauti!!”
“Khaaa dokta Jimmy amekufa?”
“Ndio, dokta Jimmy amekufa, tumetoka kumzika kama wiki mbili zilizopita, hakuna mwenye amani ya moyo kabisa.”
“Yule mtoto ambaye dokta Jimmy alikuwa akimlea, yule wa madam Oliva kaishia wapi?”
“Yule mtoto kachukuliwa na Oliva mwenyewe, kwanza unajua kama huyo Oliva alishajifungua tayari!!”
“Kumbe!!”
“Ndio, amepata mtoto wa kike, na yule mtoto wake ameenda kuishi nae. Yule mtoto anaitwa Jimmy. Ila mimi na yule anaitwa Sia ndio hatuna bahati kwakweli, mimi sijui naishia wapi najiona kabisa nimefikia ukingoni”
“Pole sana”
“Kuna shamba kubwa sana, Sarah alipewa na mzee Jimmy ila Sarah hajawahi kuliona shamba hilo, siwezi kumdhurumu, nashukuru nimekutana nawe twende nikakuonyeshe shamba hilo”
Baba Angel alikubali tu na muda huo huo waliondoka na kuelekea kwenye hilo shamba huku wakiongea vitu mbalimbali,
“Ila kwanini ulitaka kuniua Manka?”
“Nisamehe ila nilikuwa natumwa tu kufanya vile, nilijua hawa watu niko nao pamoja kumbe wananing’onga na kunicheka”
Walifika kwenye lile shamba na baba Angel alipata kuliona, kwakweli lilikuwa kubwa sana na kumfanya baba Angel afikirie kitu cha kufanya na lile shamba.
Aliongea nae kidogo tu na kuahidi kumtafuta tena.

Baba Angel, leo alihama na familia yake kutoka kwenye nyumba ya mama yake maana kulikuwa na nyumba yake nyingine ambayo ndio aliimalizia kuijenga, basi walifurahi na kwa pamoja waliondoka na kuhamia huko, ila sehemu waliyohamia walikuta na baba Emma nae na familia yake ndio wamehamia sehemu hiyo hiyo.
Basi siku hiyo alikutana nae huku baba Emma akilalamika,
“Yani yule dokta Jimmy amekufa bila mimi kujua ukweli wa watoto wangu walipo!! Roho inaniuma sana”
“Pole sana, ila Mungu akitaka ukweli uujue basi utaujua tu maana hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”
“Ila naumia sana, huyu dokta Jimmy nitamchukia hadi naingia kaburini”
Baba Angel alijaribu kumpa moyo pale kisha kuendelea kuwa majirani wazuri pale kwao.
Baba Angel aliamua kutimiza lile wazo la Jack na kuamua pia kuishi sehemu moja Derrick na Samir maana alijenga sehemu nyingine ya kuweza kuishi hawa watoto wa kiume ili pale pale maeneo ya nyumbani kwake. Alifanya hivi ili asiwe nao mbali na hawa ukizingatia Jack ndio alikuwa akiishi na Erick.
Pia baba Angel alimwambia mama Sarah arudi kwenye nyumba yake ambapo mara moja moja Sarah alikuwa akimtembelea maana bado ni mlezi wake ila mama Sarah alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa haswaa kwa swala la Elly kutokumkubali huku akizamia kwa baba yake Derrick.

Miaka mitano inapita na kufanya waanze kusahau yale machungu ambayo yalitokea baina yao, leo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye familia yao kwani ilikuwa ni siku ambayo Erick alirudi kutoka Afrika Kusini akiwa ameongozana na Jack, yani ilikuwa ni furaha sana kwa familia hii na wote walikuwepo nyumbani kwaajili ya kumkaribisha Erick tena katika maisha yao.
Siku hii Angel alikaa na Samir na kuanza kuongea nae,
“Angel, sikia nikwambie kitu yani mimi naona kabisa sitaweza bila wewe kuwa mke wangu. Ila nafasi ya mimi na wewe kufunga ndoa ipo wazi kabisa, sababu wewe ni mtoto wa Rahim na mimi ni mtoto wa Erick, mama zetu ni tofauti kabisa, je kwanini tusiweze kuoana?”
“Mmmmh ngoja tumuombe baba, anaweza akakubali”
Walijipanga na siku hii Angel aliweka ombi hili kwa baba yake kuwa anaomba yeye na Samir wafunge ndoa,
“Hapana haiwezekani Angel”
“Baba, inamaana mimi sitaolewa miaka yote maana mtu ninayempenda ni Samir halafu hakuna kizuizi kati yangu na Samir, kwanini isiwezekane?”
“Ngoja nikajadiliane hayo maswala na mama yenu”
Baada ya shughuli ya siku ile baba Angel alienda kumwambia mama Angel kuhusu watoto wao ila mama Angel alikubali kiurahisi kabisa, kisha kesho yake wakamtaka Angel na Samir waende kuongea na Rahim kuhusu swala lao la hiyo ndoa.

Angel alimuomba Erick aweze kumsindikiza katika kumpa ujumbe Rahim juu ya ndoa yake na Samir maana Samir aliogopa kwenda kusema ukizingatia alikuwa akimuogopa sana Rahim toka siku aliyotaka kumuua.
Angel alikutana njiani na Rahim na kuanza kumwambia kuhusu dhamira yake,
“Naomba mimi na Samir tuweze kufunga ndoa, nampenda na yeye ananipenda”
“Haiwezekani, aibu niliyoipata kwa Derrick inatosha msije kuniletea na nyie aibu”
“Aibu kivipi? Baba kule amekubali ukizingatia mimi na Samir sio ndugu”
“Nitolee balaa Angel, Samir nimemlea kama yeye haoni undugu wenu basi alete masikhara kwangu nitamfanyia kitu kibaya asiweze kusahau maisha yote”
Mara Erick akamwambia Rahim,
“Unasemaje wewe?”
Rahim alimuangalia Erick na kumuona kabadilika sura huku mishipa ikiwa imemsimama yani Rahim aliogopa sana alikumbuka siku aliyokabwa na Erick, kwahiyo kwa kujihami akajikuta akianza kukimbia, ila kwa bahati mbaya hakuangalia upande wa pili wakati anavuka barabara kwa kukimbia hadi akagongwa na gari.


Rahim alimuangalia Erick na kumuona kabadilika sura huku mishipa ikiwa imemsimama yani Rahim aliogopa sana alikumbuka siku aliyokabwa na Erick, kwahiyo kwa kujihami akajikuta akianza kukimbia, ila kwa bahati mbaya hakuangalia upande wa pili wakati anavuka barabara kwa kukimbia hadi akagongwa na gari.
Kilikuwa ni kitendo cha gafla sana, ikabidi Angel na Erick wasogee pale alipokuwa Rahim na kuomba msaada wa kupelekwa hospitali ila haikuchukua muda kwani majibu yalipatikana pale pale kuwa Rahim ameaga dunia, basi Angel alianza kupigia simu watu mbalimbalikuwapa ile taarifa huku akimwambia Erick,
“Na wewe umezidi na misuli yako, kwa stahili hii jamani si utaua wengi wewe!”
“Aaaah sikutaka ila sikupenda ile kauli yake”
“Hata kama, uwe unajitahidi kujizuia, Erick umerudi jana tu halafu leo umezua balaa jamani loh!!”
Wakaenda nyumbani ambapo baba Angel na mama Angel walielezewa na Angel ilivyokuwa na moja kwa moja walijua kuwa uoga wa Rahim kwa Erick ndio umesababisha yote yale ila hawakuwa na cha kufanya maana tayari msiba ulishatokea.

Ikawa ni majonzi ya kifo cha Rahim lakini kilichosababishwa na Erick, huku ikisemekana kuwa ni ajali ndio iliyomuua Rahim, hapo walilia sana hasa watoto wa Rahim na baba Angel kuzidi kuona madhara yaliyopo kwa Erick, kiukweli hakujua cha kufanya na Erick.
Siku ya mazishi ya Rahim, na Manka alikuwepo kwahiyo baada ya mazishi tu baba Angel aliamua kwenda kuongea na Manka kuhusu Erick, alikuwa akihisi huenda hata dokta Jimmy alikuwa amemuachia siri ya kufanya Erick apate nafuu, ila Manka alimwambia kuwa dawa ni moja tu yani Erick alale na Erica ndio nguvu za Erick zitakuwa sawa, kwakweli baba Angel bado roho ilimuuma sana kwa kuweza kufikiria jinsi Erick na Erica walale kimapenzi wakati ni watoto wake wote wawili.
Ila wakati anataka kuondoka, Manka alimpa ujumbe ambao alipewa na Sarah,
“Sarah kaniambia kuwa kapata mchumba, atakuja kukutambulisha ili aolewe”
“Kheee watoto wa siku hizi wanawahi”
“Mwache awahi tu, huyu mtoto alianza mapepe mapema sana, bora tu aolewe ila mimi najitolea kuishi nao yeye na mchumba wake nyumbani kwangu”
“Kama wakiamua kuishi kwao je?”
“Basi nitahamia huko, mimi ni mpweke sana. Halafu ngoja nikwambie kitu kingine ambacho hujui kuhusu mimi”
“Kitu gani hiko?”
“Mimi ni mwathirika”
Hili baba Angel alilijua vizuri kabisa maana huyu alitembea na Rahim ambaye alishaathirika kitambo sana ila tu alijifanya kushangaa kanakwamba hakujua kitu,
“Oooh pole na hongera kwa ujasiri wako wa kusema, kuwa muathirika sio mwisho wa maisha, bado unanafasi kubwa sana ya kusonga mbele”
“Asante ila najua aliyeniambukiza”
“Nani huyo?”
“Huyu huyu marehemu Rahim, alijifanya ananipenda kumbe yupo kwaajili ya kunipa maradhi tu, ila Mungu alivyosasa ona yeye kafa kwa ajali tena ya kujitakia mwenyewe maana alikuwa anakimbilia wapi sijui”
“Mmmmh haya yaishe, tutaonana tena siku nyingine”
Siku hizi Manka alikuwa mpole sana, kwanza alionekana kama mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri na hakuona tatizo kuongea lolote na sehemu yoyote ile.

Baba Angel alirudi nyumbani kwake huku akikuna kichwa chake kwa mawazo aliyokuwa nayo, basi aliongea na mke wake kile ambacho aliambiwa na Manka,
“Unajua Manka anasema tatizo la Erick linaweza kumalizwa na Erica tu”
“Hivi kwa mfano tukamtafutia Erick msichana mwingine itakuwaje?”
“Mmmh unatafuta balaa mama Angel, tutamsafirisha wapi tena akiharibu? Anaweza kuua huyu mtoto ujue. Tujifunze kutokana na makosa”
“Sasa itakuwaje? Tutakubali watoto wetu walale pamoja kimapenzi?”
“Aaaah hiyo ngumu ila ngoja tutafakari”
Waliamua tu kulala kwa muda huo.
Kulivyokucha tu, Sarah aliwafata na kuwapa taarifa kuwa anataka kwenda kumtambulisha mchumba wake kwao, walikubali tu hawakuwa na pingamizi juu ya hilo.
Kisha baba Angel alienda kumfata Erick ambaye hana siku nyimgi toka arudi, aliongea nae kirafiki tu amsikie majibu yake,
“Erick, hebu niambie kitu. Leo ndugu yako Sarah amesema kuwa analeta mchumba wake kumtambulisha, je wa kwako utamleta lini?”
“Kwani na Erica kashamleta wa kwake?”
“Hapana”
“Nitamleta pindi Erica akimleta mtu”
Baba Angel aliitikia tu ila alijaribu kusoma kitu na kwenda kuongea na mke wake kisha wakapanga mpango.

Kwenye mida ya jioni, Sarah alileta mchumba wake nyumbani kwao na walimkaribisha vizuri sana, huyu alikuwa ni mtoto aliyelelewa na madam Oliva, ila ni mtoto wa Sia na Steve yani Paul.
Baba Angel na mama Angel hawakuwa na pingamizi kabisa juu ya mapenzi ya hawa watu.
Kisha baada ya Paul kuondoka, baba Angel aliondoka pia ili kwenda kujaribu kile anachoona kinafaa zaidi, alienda hadi nyumbani kwa Bahati na Fetty na kuongea nao juu ya kijana wao Bahati aje kwake kujitambulisha kama mchumba wa Erica, alimuahidi kumlipa ila hakumwambia kwanini anataka iwe hivyo, hilo lilikuwa swala rahisi sana kwa Bahati mdogo kwani alikubali kiurahisi ukizingatia anampenda sana Erica.
Baba Angel alipomaliza hapo alirudi nyumbani na kumpa ule ujumbe mke wake, ambaye aliafikiana nae na wakapanga kesho yake kuwa wampange Erica aweze kukubali wakati Bahati anaenda kujitambulisha maana hawakutaka kuchelewesha mambo.
Halafu wakapanga lingine sasa,
“Hili likifanikiwa tu, basi moja kwa moja tutaenda kuongea na baba Emma ili tumchukue yule Emmanah awe na Erick au unasemaje?”
“Hapo sawa kabisa baba Angel, yani yule Emmanah umelenga haswaaa, tujitahidi Erick aweze kumkubali kwakweli”
Basi walipanga mpango wao kwa namna hiyo.

Kulipokucha tu, mama Angel akamuita Erica na kumpanga ila Erica alikuwa akipinga vikali kuhusu swala hilo,
“Kwanini mmefikia huko mama?”
“Tunataka kumuokoa kaka yako”
“Nadhani mnataka kumuangamiza, mnajua madhara ya hiko mnachokitaka?”
“Usiwe mkaidi Erica, naomba ukubali”
Erica alikubali lakini kishingo upande.
Jioni ya siku hii, alikuja Bahari kama mchumba wa Erica yani alikuja kujitambulisha na baba Angel aliwaita watoto wake wote ili wamshuhudie mchumba wa Erica, basi baba Angel alianza kutoa ule utambulisho, kitu cha kushangaza Erick aliinuka huku akiwa na gadhabu kali sana, alimkunja Bahati na kumtwika ngumi ambayo ilimpeleka Bahati chini yani ilibidi tu Erica ndio aende kuingilia kati ila Bahati alikuwa na hali mbaya sana ikabidi wamkimbizie hospitali kwa tiba ya haraka yani kila kitu hapo nyumbani kwao kilivurugika.

Wakati baba Angel yupo hospitali kwaajili ya matibabu ya Bahati, ndipo alipokutana na mke wa Moses ambaye alidai kuwa mwanae yupo hapo hospitali pia,
“Kheee pole sana, kafanyaje kwani?”
“Kapata ajali, kapoteza damu nyingi sana yani sijui nifanyeje na anatakiwa kuongezwa damu”
Baba Angel alijitolea kufanya hivyo, ila walienda kumchukua damu yake na kukuta na damu ya yule kijana haziendani, ila mara baba Emma nae alionekana pale akisema kachanganyikiwa maana mwanae kapata ajali pia na anatakiwa kuongezwa damu ila yeye haendani nae damu yake, ila daktari akawaita wote wawili maana kila mmoja damu ilionekana kuonda kwa mwingine, yani baba Emma alifanana damu na mtoto wa Moses halafu baba Angel alifanana damu na Emmanuel, basi waliwaongezea damu na watoto wakendelea vizuri.
Ikawa kila wanapoenda hospitali wanakutana, huku wakina Bahati na mkewe Fetty nao wakienda kumtazama mtoto wao.

Siku hii, Erica alimuita baba yake na mama yake na kuanza kuongea nao,
“Kwani baba na mama tatizo lenu ni nini?”
“Tatizo letu ni kuwa tunaogopa wewe na Erick kuwa pamoja kimapenzi, ndiomana tunafanya jitihada zote kuweza kuweka mambo sawa”
“Ila kabla hamjaendelea na hiso jitihada zenu, nakuomba baba nenda kamtafute yule rafiki yako dokta Noah mwambie akwambie ukweli”
Baba Angel alishangaa sana ila alikubali kufanya vile, na kweli siku ile ile aliamua kumtafuta dokta Noah na kuanza kuongea nae, hata dokta Noah alimshangaa baba Angel na kumuuliza,
“Nani kakwambia kuwa mimi nina ukweli?”
“Binti yangu Erica”
“Dah!! Ila naogopa”
“Hapana, niambie tu.”
“Ngoja nitapanga siku nitakuita mahali utakutana na wengine, na hapo nitasema ukweli ila mnilinde maana sina cha kufanya”
“Nitakulinda, nahitaji tu ukweli”
Baba Angel alimuahidi dokta Noah kuwa atamlinda maana alimwambia kuwa atausema ukweli wote ulivyo.

Siku hiyo dokta Noah alimuita baba Angel na mama Angel, walijiandaa na kwenda alipowaita ila walishangaa sana kufika kule kumkuta baba Emma, mama Emma, mke wa Moses pamoja na Juli, kisha dokta Noah alianza kuongea,
“Samahani sana kwa hiki nitakachowaambia”
“Bila samahani, sisi tutakusikiliza”
“Miaka ya nyumba iliyopita wakati Erica akiwa mjamzito, nilimsikia mkwe wake na dokta mwenzangu wakipanga mipango mibaya juu ya wale watoto, kwanza walipanga mipango ya kuwabadilisha na badae walipanga mipango ya kuwachoma sindano, roho iliniuma sana kwani nilijua wazi hao watoto wakiwa wakubwa watakuwa ni mwiba kwa wazazi wao. Naomba mnisamhe hiki ambacho nitakachowaambia, kuna huyu dada anaitwa Juli, enzi hizo alikuwa na maisha magumu sana na alikuwa akitaka atoe mimba, ila badae alipanga akijifungua atupe mtoto, ila alijifungua watoto mapacha mmoja wakike na mwingine wa kiume, nilimuomba asiwatupe, nikaenda kuwahifadhi na ndipo muda naenda kuwahifadhi nilikuta Erica ameshajifungua wale watoto wake, ila alijifungua mapacha watatu tofauti na tulivyojua mwanzo, yani hata sikufikiria mara mbili bali nilimbadili yule mtoto wa kiume na mtoto wa Erica muda huo huo. Ila sikutaka mtoto wa Erick aende kuishi maisha ya shida, na hivyo nikawaweka pembeni na kupewa mgonjwa wa kujifungua ambaye alikuwa ni wewe Neema, kiukweli hukujifungua mapacha ila ulijifungua mtoto mmoja, nami nikamchukua mtoto wako na kukuwekea wale wawili ambapo mmoja ni mtoto wa Juli na mwingine ni mtoto wa Erica, nikaondoka na mtoto wako ambaye sikutaka apate shida pia, basi mke wa Moses alipojifungua nikamuongezea na mtoto mwingine ambapo na yeye alionekana kuwa kajifungua mapacha, hii kitu imenitesa kwa miaka yote hii. Niliandika hadi kwenye Kitabu changu cha kumbukumbu, kila siku nilitamani kusema ukweli ila niliogopa. Nilijua kuwa wote mngenichukia, sikufanya kwa nia mbaya ila kitendo changu cha kubadilisha mtoto wa Erica ndio kimezaa yote haya. Naomba mnisamehe sana”
Baba Angel alipumua kiasi na kumuuliza,
“Inamaana hata dokta Jimmy na mzee Jimmy hawajui hiki ulichokifanya?”
“Hakuna aliyekuwa anajua zaidi yangu”
“Yani kumbe wengine wanabadilisha huku watoto na wewe unabadilisha huku, mnajua nyie mnaweza fanya wazazi wakawa machizi!”
“Nisamehe Erick, ila nilifanya kwaajili ya kukomboa kizazi chako”
“Kwahiyo Erick sio mwanangu?”
“Ndio, Erick na Emmanah ni mapacha, ni watoto wa Juli ambaye alishindwa kuwalea”
“Duh!!”
Baba Emma nae aliuliza vizuri,
“Kwahiyo na mimi mwanangu ni nani?”
“Ni mtoto wa Moses, anaitwa Abraham ndio mtoto wako wewe”
Mke wa Moses nae alikuwa akishangaa na kuuliza,
“Kwahiyo sikujifungua mapacha?”
“Ndio, ulijifungua mtoto mmoja tu”
“Ile hospitali ndiomana mnapenda kutufanyia upasuaji kumbe mnayenu mnayoyajua nyie”
“Ishafungwa ile hospitali kwa ujinga wao”
“Naomba mnisamehe maana nilitaka kuokoa watoto wa Erick”
“Aaaah hata kama, ila kwanini uingilie na kubadilisha watoto wa wengine? Hapo ndio sijakupenda”
Basi mama Angel alimuangalia Juli na kumuuliza,
“Na wewe kulikoni kutaka kutupa watoto? Ulizaa na nani kwanza?”
“jamani maisha dah!! Najua hata hivyo watoto wenyewe hawawezi kunikubali. Nilizaa na mtu mmoja anaitwa Yuda”
“Khaaa alipokea kichapo toka kwa Erick huyo loh!! Ni halali yake kumbe, alikataa mimba eeeh!!”
“Ndio alikataa ndio chanzo cha mimi kuanza kutangatanga”
Ila wote walijikuta wakimjadili vibaya dokta Noah, kasoro baba Angel, mama Angel na Juli. Ila sababu dokta Noah alisema ukweli baba Angel aliamua kuchukua hatua pale pale na kurudi nyumbani kwake huku akiruhusu Erica na Erick kuwa pamoja maana aliona Erick atazidi kuharibu na kuharibikiwa.
Ila Erica bado alishikilia msimamo wake ule ule kuwa hakuna kitu mpaka ndoa ifanyike, kwakweli hili swala lilikuwa ni jambo la aibu kwa baba Angel ila alikubaliana nao wote kufunga ndoa na kufanya sherehe ya kifamilia.

Na kweli walifunga ndoa na kufanya sherehe ya kifamilia, yani baba Angel alikuwa akiona aibu sana ila siku aliyofunga ndoa Angel na Samir, ndio siku aliyofunga ndoa Sarah na Paul halafu Erica na Erick nao walifunga ndoa siku hiyo. Baba Angel hakutaka wengi wajue, ila habari ilimfikia Sia ambaye alifika na kuongea na baba Angel,
“Unajua kuna vitu mtu unaweza kuvizuia weee ukajikuta unashindwa ila badae mapenzi yakachukua nafasi yake, unaamini kuwa mapenzi yana nguvu sana?”
“Ndio ninaamini, hata kwa madam Oliva na Steve ilikuwa hivi hivi, tulijua ni dawa tu kumbe na mapenzi nayo yalikuwa na nguvu zake hadi mtu kajikuta anatengeneza dawa”
“Umeona kwa watoto, umewalea siku zote katika misingi ya dini sijui ikawaje ukateleza kumbe nguvu ya mapenzi inataka kuchukua nafasi yake”
Baba Angel akacheka na kumwambia Sia,
“Mjinga wewe, saivi na mke wangu tunarudi tena kwenye maombi”
“Mungu hakutaka mumsumbue kwa maombi yenu ya kuombea watoto watengane wakati kuna nguvu ya mapenzi kati yao”
“Mjinga sana wewe”
“Ila tuache masikhara Erick, kwakweli mapenzi yana nguvu”
Baba Angel alicheka tu, ila zile sherehe zilipoisha aliwapatia wote watoto wake nyumba za kuishi halafu yeye nyumbani kwake alibakia na mke wake pamoja na mtoto wao Ester.

Leo, baba Angel alienda kumtembelea Erick pamoja na Erica huku akiwa ameongozana na dokta Noah, ambapo alikaa na kuongea nao ukweli wote ila ilikuwa ni ajabu sana kwani Erick hakuchukia kama siku zote jinsi anavyofanya ila tu alimpongeza huyu dokta kwa kile alichokifanya kwao, huku akimsifia sana Erica,
“Licha ya dawa tulizopewa ila bado Erica ni mwanamke jasiri sana, kwani ameweza kunitoa katika hali hii mara nyingi sana. Kwakweli Erica anahaki ya kupewa sifa ya kuwa mke mwema”
Basi baba Angel alimuuliza mwanae kwa masikhara,
“Eti Erick, mapenzi yana nguvu?”
“Ndio baba yana nguvu sana, yani wao walipanga vile halafu mapenzi yakapanga vingine. Unafikiri kwanini huyu dokta alitubadilisha! Ni sababu ya nguvu ya mapenzi, hakubadilisha kwa akili yake ila nguvu ya mapenzi ilimsukuma, alihisi uchungu kwa rafiki yake kufanyiwa fedheha”
“Ila bado Erick utabaki kuwa mwanangu wa pekee”
“Hata wewe baba utabaki kuwa baba yangu wa pekee”
Erick na baba Angel walikumbatiana pale.

MWISHO

 
😳😳😳🙏🙏🤓🤓 dahhh ila mtunzi wa hili jambo kiukweli kawaza sana yaani story imepangwa vizuri ngoja niongeze bando🇨🇦🇨🇦
 
Back
Top Bottom