Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Abdallahking

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2018
Posts
3,985
Reaction score
10,840
Simulizi: NINI MAANA YA MAPENZI
Mwandishi: ATUGANILE MWAKALILE
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES


SEHEMU YA 1

Alikuwa binti mpole ila muongeaji sana, aliyelelewa katika mazingira ya dini, nyumba yao ilijihusisha zaidi na maswala ya dini kiasi kwamba hakutaka kujihusisha na maswala ya mapenzi kwa umri mdogo kwani akiangalia dada zake wote walikuwa kwenye ndoa zako, kwahiyo ndoto yake yeye ilikuwa ni kumaliza shule, kuanza kazi kisha kupata mchumba na kuolewa. Ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto wanne, wakike watatu na wakiume mmoja tu.

Alikuwa na dada yake mmoja ambaye alipatana nae sana na kipindi hicho dadake huyo ndoa yake ilikuwa bado changa kwani ndio kwanza alitoka kuolewa, alikuwa akipenda kupiga nae stori na mara zote dadake alikuwa akimshauri kuwa makini sana na vijana,

“Erica mdogo wangu, nakupenda sana. Naomba uwe makini sana na vijana, ni wadanganyifu. Unatuona dada zako, tumejiheshimu hadi tumeolewa, ni fahari kwetu na heshima kwa familia. Alitangulia dada yetu Maria, nimefata mimi. Najua na wewe utaenda katika mtiririko unaofaa. Usikubali kushawishiwa kijinga na wanaume”

“Dada Bite najua unanijua vizuri mdogo wako, hayo mambo sina. Ndio kwanza nipo kidato cha pili”
“Ndio upo kidato cha pili, yani hiko kidato ndio asilimia kubwa huharibikia hapo kuwa makini sana”
“Usijali kuhusu mimi dada”

Walikuwa wakiongea vizuri sana kirafiki kama marafiki wa kawaida vile lakini ilikuwa ni mtu na dada yake. Beatrice alimrudisha mdogo wake nyumbani kwao baada ya kutoka kumsalimia kwani mama yao alikuwa anampenda sana binti yake huyo na alikuwa anamuona bado ni mdogo kutembea mwenyewe.
 
SEHEMU YA 2

Erica alikuwa na rafiki aliyeitwa Johari, na alimpenda sana na kupiga nae stori za kila aina ila tofauti ya Erica na Johari ni kuwa Johari alikuwa mapepe sana, ila Erica alikuwa mpole sana yani yeye ni uongeaji tu.

Wakiwa darasani siku hiyo aliletwa kijana mgeni kwenye darasa lao, kwa hakika Yule kijana alikuwa ndio amehamia hapo shuleni, ila alipoingia tu macho yote yalianguka kwake. Mwalimu akamtambulisha Yule kijana kwa wanafunzi wote,
“Huyu ni mwenzenu anaitwa Erick mpokeeni vizuri”

Darasa lote wakaguna na kumuangalia Erica kiasi cha kumtia aibu Erica na kuangalia chini, hadi mwalimu akawauliza walichoguna, mmoja akajibu

“Tumeguna sababu kuna pacha wake humu anaitwa Erica”
Wakaangua kicheko wote, mwalimu akawatuliza,

“Kufanana majina ni kawaida tu, kwani hamjawahi kusikia hayo majina? Acheni habari zenu za ajabu, haya mpokeeni mwenzenu huyo”

Kisha mwalimu akamkabidhi Yule kijana kwa wavulana wenzie halafu yeye akaondoka zake. Johari akamuangalia Erica na kumwambia,

“Umesikia jina la Yule kijana?”
“Nimesikia ndio”
“Sasa mbona hujafurahia?”
“Nifurahie nini sasa?”

“Mmmh kijana mzuri vile, macho yake ya kuvutia kama anaita, halafu kafanana jina na wewe, huoni kama ni bahati hiyo”
“Johari, tafadhali achana na habari hizo kwangu”

“Mmmh wewe nae na ulokole wako, yani hiyo chance ya kufanana jina ningeipata mimi basi leo leo ningemfata Yule kijana. Ila Yule kijana mzuri jamani loh kama ameshushwa, lazima nitembee nae, nitampitia tu”
“Johari jamani hivi hatuwezi kuangelea habari zingine zaidi ya hizo?”

“Haya mama Mchungaji, leo umekusanya sadaka kiasi gani?” Erica alikaa kimya kwani tayari alikuwa ameshachukia kutokana na watu kuguna pindi tu Yule kijana wakati anatambulishwa na vile ambavyo Johari amemwambia.
 
SEHEMU YA 3

Muda wa kurudi nyumbani ulifika na Erica alirudi nyumbani kwao na kufanya shughuli zake kama kawaida, alipokaa na kutulia alishangaa picha ya Yule kijana ikimjia kichwani na jinsi Johari alivyokuwa akimsifia kuwa Yule kijana ni mzuri sana.

“Mungu wangu, sitaki kumfikiria Yule kijana, kwanini nimfikirie jamani? Sijawahi kumfikiria kijana yoyote maishani mwangu, kwanini nimfikirie Yule, hapana sitaki”

Alitulia ila bado picha ya Yule kijana ilikaa kwenye mawazo yake na alikuwa akijisemea moyoni kuwa Yule kijana ni mzuri kweli hata alipoletwa darasana kidogo moyo wake ulipatwa na mshtiko kuwa kijana mzuri vile katoka wapi ila bado alijipa moyo wa kupambana na zile hisia kwani hakutaka kabisa maswala ya mapenzi huku akifikiria ushauri aliopewa na dada yake.

Usiku akiwa amelala, alimuona Erick kwenye ndoto zake, tena aliona kamavile ana mahusiano na Erick, alishtuka sana.
“Jamani mimi ni mtoto wa kike nitaanzaje kumwambia mwanaume nampenda? Kwanza sio utamaduni wetu, hata hivyo sitaki kumpenda, nataka nisome nimalize shule name nije kuolewa na kupata heshima kama dada zangu. Erick ondoka kwenye akili yangu”

Kwavile ilikuwa pamekucha tayari, ikabidi aamke na kujiandaa kwa ajili ya kwenda shule.

Erica alifika shuleni na asilimia kubwa ya wadada walionekana wakimuongelea Erick tu kuwa ni kijana mzuri aliyefika shuleni kwao,

“Jamani Yule kaka ni mzuri, hadi natamani anitongoze. Yani akithubutu kunitongoza wala sitalaza damu”
“Unangoja hadi akutongoze subiri uone, mi nitamtongoza mwenyewe”
“Kujidhalilisha huko”

“Hata kama mwenzangu, unaweza ukasubiri mwisho wa siku ukakuta mwenzio kashawahi. Hapa shule kuna wasichana wazuri eti, unafikiri Yule Erick atafikiria kukufata wewe? Aache kufikiria wakina Miriam, wakina Manka akufikirie wewe thubutuuu”

Erica alisikiliza kwa makini sana na kuona ni jinsi gani Erick alikuwa akigombewa shuleni kwao, na kuondoa kabisa tumaini la kuweza kuwa hata karibu na huyo Erick ila upande mwingine wa roho yake alifurahia maana kuwa mbali na kijana ambaye ameanza kumpenda kutamuwezesha yeye kutimiza ndoto zake za kumaliza shule kwanza.

Stori nyingi shuleni hapo zilikuwa ni kuhusu huyu kijana mpya aliyefika yani kila binti alihitaji kumpata huyu kijana.
 
SEHEMU YA 4

Zilipita wiki mbili, ilikuwa siku ya Jumamosi siku hiyo hawakwenda shule, Erica alikuwa nyumbani. Akachukua kioo na kujiangalia, kisha akasema

“Mimi ni msichana wa kawaida sana, sina uzuri wa kupendwa na kijana kama Yule. Hawezi kunipenda mimi, natakiwa kumsahau na kumtoa kwenye akili yangu”

Akajiwa na mgeni alikuwa ni rafiki yake Johari, akamkaribisha vizuri sana kisha akaanza kupiga nae stori ila stori za Johari mara zote ni kuhusu wanaume, na umbea ila siku hiyo stori yake kubwa ilikuwa ni kuhusu Erick, ingawa stori za vile Erica alikuwa hapendezewi nazo ila kwavile zilimuhusu Erick alikuwa akizisikiliza,

“Basi bhana, si nimefatilia nyumbani kwao Yule Erick, loh wana hela hao balaa”
“Kumbe”
“Ndio hivyo, halafu nasikia shuleni kuna wadada kama wane wamebambwa na mwalimu walimuandikia Erick barua za mapenzi”

“Kheee, wewe umepona kweli?”
“Hahaha mimi nimtongoze kwa barua nina wazimu au? Mi nitamtongoza live kabisa, tuangaliane ana kwa ana. Hapo ndio nitajua kama ana aibu au la”
“Kwahiyo utamtongoza lini?”
“Nipe mwezi, nataka nimzoee zoee kwanza”
“Je akikukataa”
“Najua atanikataa, ila kwangu hata ile kumtongoza tu napo ni raha”

Erica alikuwa anamshangaa sana huyu rafiki yake ambaye yeye alikuwa akijionea kila kitu kuwa kawaida kabisa.
 
SEHEMU YA 5

Jumatatu yake, siku ya shule kama kawaida ila leo kidogo Erica alichelewa shule. Sasa muda anaingia darasani kwa kunyata akajikuta amekumbana kikumbo na Erick maana nae alikuwa anatoka kidogo, Erica alinyanyua macho yake na kumwangalia Erick kisha akamwambia,

“Samahani”
“Hamna shida usijari”
Erica alienda kukaa ila mwili wake ulipatwa na msisimko mkubwa sana vile alivyokumbana kikumbo na Erick.
Alikaa huku akihema, rafiki yake Johari alimfata na kumuuliza,
“Mbona unahema sana, vipi wewe?”
“Nilichelewa shule leo”

“Ndio uheme hivyo sababu ya kuchelewa? Nimekuona vizuri, uligongana kikumbo na Yule mkaka mzuri”
“Ni bahati mbaya tu”

“Sawa, ila umeona macho yake? Jamani macho ya Yule kaka yanaita, kama anakwambia njoo njoo uwiii jamani natamani hiyo nafasi ya kugongana nae ningeipata mimi maana ningemkumbatia pale pale”
“Ushaanza hivyo Johari, kwanza mimi sina uzuri huo wa kuwa na Yule mkaka”

“Kwani wewe una ubaya gani sasa? Kwanza hapa shuleni hujirembi hufanyi nini ila bado unapendeza, usijidharau Erica wewe ni mzuri, ila tu Yule Erick niachie mimi”

Wakacheka tu na kuendelea na kazi zingine za darasani.
 
SEHEMU YA 6

Muda wa mapumziko siku hiyo Erica hakutoka sababu kuna kazi alikuwa anaimalizia kufanya, kwahiyo alikaa anaandika wakati wanafunzi wengine wako nje. Mara alisikia kuna sauti imefika na kumsalimia,
“Mambo”

Erica alinyanyua macho yake na kumuangalia aliyekuwa anamsalimia, alikuwa ni Erick kitu ambacho kilimfanya Erica kukosa ujasiri kidogo huku sauti yake ikitetemeka tetemeka na kuitikia,
“Safi”

Halafu akarudisha macho yak echini huku akiendelea kuandika,
“Mbona hujatoka kupumzika?”
“Kuna kazi ya kuandika naifanya”
Erica alikuwa anamjibu huku macho yake yapo kwenye daftari tu hakutaka kutoa nafasi ya kumtazama Erick kwani aliogopa kijana Yule kubaki kwenye akili yake. Ila Erick aliendelea kuongea,
“Samahani ile asubuhi, unajua ni kosa langu ndiomana tumegongana. Nilikuwa siangalii mbele”
“Hapana ni kosa langu”

“Sio lako ni langu, naomba unisamehe Erica”
Erica akainua macho yake sasa na kumtazama Erick vizuri kwani hakutambua kama huyu mkaka angeweza kumuita kwa jina lake, kwa mawazo yake yeye alijua huyu kijana halijui jina lake. Ila wakati ameinua macho yake, alifika Johari na kaunza kumsalimia Erick,
“Mambo vipi Erick”
“Safi”

“Mbona hujatoka kwenda kunywa chai?”
“Nilimuona Erica amejiinamia hapa, ndiomana nikaja kumuuliza kwanza yeye kuwa kwanini hajaenda mapumziko”
“Ana kazi huyu, nikusindikize basi utembee tembee kidogo mazingira ya shule”
“Sawa, ila ngoja nimuulize kitu Erica”

Erica alivyosikia aulizwe kitu akashtuka kidogo na mapigo ya moyo kumuenda kwa kasi maana tayari alikuwa anampenda huyu kijana ila alikuwa akipambana na hisia zake ili aweze kuishi bila mahusiano mpaka atakapomaliza shule, Erica akainua macho yake kisha Erick akamuuliza,
“Utakula nini mama nikuletee?”
Kiukweli Erica aliona aibu sana na kukataa kuwa asimletee chochote ila Erick alisisitiza kuwa atamletea chochote kisha akatoka na Johari.

Erica alijikuta kama akiganda kwa muda hivi kwani akili yake iliruka kabisa kwa wakati huo kila alipoifikiria kauli ya Erick kuwa utakula nini mama nikuletee yani alijikuta ufahamu ukikatika kabisa.
 
SEHEMU YA 7


Muda wa kutoka ulipofika, Erica alifatwa tena na Erick huku akimkabidhi mfuko,
“Nimekununulia juisi na keki ila kwavile muda wa darasani ulikuwa umefika sikuweza kukuletea tafadahari pokea”
Erick alimshika mkono Erica na kumfanya apokee ule mfuko huku akitoa asante ambayo hata haikusikika vizuri maana sauti yake ilikumbwa na tetemeko la gafla.

Erica alifika nyumbani kwao akianza kuwa na mawazo maradufu kuhusu Erick,
“Hapana Erick usinipende mimi tafadhali, sio mimi usinipende”

Alijikuta akiongea peke yake maana alianza kushikwa na hofu ukizingatia yeye tayari ameshampenda Erick halafu Erick ameanza kumuonyeshea hisia ambazo ni hakika atakuwa naye anampenda, “Sipo tayari kuwa na mahusiano yoyote, natakiwa nisome nimalize shule, nianze kazi nipate mume niolewe kama dada zangu. Hapana sitaki kuwa na mahusiano shuleni”

Aliwaza hayo ila muda wote aliokaa mwenyewe sura ya Erick ilimjia machoni pake na kumfanya akose raha kabisa, alimfikiria Erick muda mwingi sana na hata usiku alipolala alimuona Erick kwenye ndoto zake.

Siku hiyo alienda shuleni ilikuwa ni siku ya michezo, wanafunzi walikaa mbalimbali kwa lengo la kucheza, mara Erick akamfata Erica na kumpa kipande cha karatasi halafu akaondoka zake, Erica alifungua ule ujumbe ulindikwa “I LOVE YOU” alishtuka sana na kutetemeka, rafiki yake Johari alifika na kutaka kujua kuwa kile kikaratasi kimeandikwa nini.

Siku hiyo alienda shuleni ilikuwa ni siku ya michezo, wanafunzi walikaa mbalimbali kwa lengo la kucheza, mara Erick akamfata Erica na kumpa kipande cha karatasi halafu akaondoka zake, Erica alifungua ule ujumbe ulindikwa “I LOVE YOU” alishtuka sana na kutetemeka, rafiki yake Johari alifika na kutaka kujua kuwa kile kikaratasi kimeandikwa nini.
Erica akaona kwamba Johari atakichukua na kukisoma, hivyo akakitumbukiza mdomoni na kukitafuna, Johari alimwangalia sana rafiki yake na kumwambia,

“Loh Erica jamani yani umekitafuna kweli? Niambie basi rafiki alikuwa amekuandikia nini?”
“Eti alikuwa anaomba daftari langu la Kiswahili”
“Mmmh kama ndio hivyo mbona umekitafuna?”
“Sasa kwani wewe unahisi nini?”
“Mbona unapaniki rafiki yangu? Mimi nimeuliza tu kuwa hicho kikaratasi kilikuwa kinahusu nini?”
“Kwahiyo unahisi alikuwa ananitongoza au?”
Johari alianza kucheka sana kisha akamwambia rafiki yake,
“Hebu nitolee vituko mie, huyo Erick anavyotongozwa na wasichana wote hapa shuleni aanze kukutongoza wewe kwa lipi? Mtu mwenyewe binti mlokole, hata vijana wanakuogopa”
Erica alinyamaza kimya tu ila maneno ya Johari yalimuingia vilivyo, alikuwa akimuangalia Erick kwa mbali alivyokuwa amezungukwa na wadada akicheka nao.
 
SEHEMU YA 8

Erica siku hiyo alikuwa na mawazo sana kiasi kwamba alikuwa kama mgonjwa na kuamua kwenda kuchukua ruhusa kwa mwalimu na kurudi nyumbani, alienda nyumbani kwao kama mgonjwa siku hiyo akijiuliza maswali kadhaa kuwa ni kweli kile ambacho Erick alikiandika kwenye kikaratasi alikuwa anamaanisha? Na kama alikuwa anamaanisha mbona alikuwa akiongea na kucheka na wanawake wengine, na pia maneno aliyoyasema rafiki yake yalimuondoa katika hali ya kupendwa kabisa na Erick.

Akiwa njiani kurudi kwao alikutana na rafiki wa dada yake akiwa kabeba mtoto mgongoni, akamsalimia. Huyu rafiki wa dada yake alianza kumuuliza maswali
“Vipi Erica mbona mapema sana leo?”
“Najisikia vibaya Da Rehema”

“Pole, ila mdogo wangu soma. Usiwaendekeze wanaume, unaona hapa, wengine tunahangaika na watoto migongoni, wengine nyumbani wanalialia. Hatujaolewa hadi leo tunatanga na njia tu, mdogo wangu soma, achana na mapenzi kabisa yani wewe jail masomo yako tu”
“Asante dada”

Erica aliachana na huyu dada ila maneno ya dada huyu yalimuingia kwenye akili yake, na kumfanya ile hali ya kujihisi homa iishe katika mwili wake na kuanza kujihisi yuko salama kabisa, alifika nyumbani na mamake alimuuliza kuwa nini tatizo ilibidi ajifanye kuwa tumbo linauuma sababu kwa wakati huo hakuwa na hali ya homa kabisa.

Kesho yake shuleni alikwenda akiwa na hali mpya, fikra za mapenzi alizifuta kabisa katika akili yake. Alipofika alikutana na rafiki yake Johari,
“Vipi wewe jamani mbona jana ulipotea tu?”
“Nilikuwa najihisi vibaya, tumbo lilikuwa laniuma”
“Kwahiyo ukaomba ruhusa?”
“Ndio”

“Ila wewe kuruhusiwa ni lazima maana walimu wanajuaga kuwa wewe si muongo”
Basi Erica alikuwa akiulizia masomo yaliyompita jana, kwani wazo la mapenzi lilipotea kabisa kwenye akili yake kwa wakati huo.
Muda wa mapumziko akiwa anaandika kazi ya jana, alikuja Erick na kukaa karibu yake kisha akamuuliza,
“Jana uliondoka mapema sikukuona tena?”
“Kwani ulikuwa unanitafuta?”
“Hapana, ila nilikuangalia tu sikukuona. Vipi nikakuletee nini nje?”
“Sitaki chochote”

“Mbona unaongea kwa hasira?”
“Hivi nimeongea kwa hasira eeh! Samahani ila sitaki chochote”
Ilibidi Erick aondoke zake ila Erica alifanya vile sababu hakutaka tena kujihusisha na maswala ya mapenzi aliona angeharibu maisha yake.
Alipokuwa amekaa pale muda kidogo Johari alirudi, na kama kawaida alianza kuongea aliyoyaona nje,
“Mwenzangu nimemuona Manka anamuongelea Erick, mmmh Yule mtoto kwa weupe ule na uzuri ule atamuopoa tu Erick”

“Kwahiyo Manka anamtaka Erick?”
“Aaah nasikia Erick ndio anamtaka Manka halafu Manka nae anampenda Erick, mmh nangoja nione tu picha la malavidavi litakavyoenda”
Kiukweli maneno haya yalimchoma Erica vilivyo ingawa hakutaka habari za Erick tena ila swala la kuambiwa kuwa Erick anamtaka Manka na inaonyesha Manka anampenda Erick zilimchanganya vilivyo ukizingatia akijiangalia yeye na Manka alimuona Manka kuwa na mvuto zaidi kwani yeye hakujiweka kabisa kwenye kundi la wasichana wanaovutia.
 
SEHEMU YA 9

Muda wa kutoka shule, aliweza kumshuhudia Erick akiwa ameongozana na Manka yani hapo moyo wake ukalia kabisa, alihisi kupasuka moyo na kuanza kuwa na wivu ila alijipa moyo asiendelea kumuonea wivu Erick,
“Mwanamke yeyote atakaye kuwa nae ni sawa, sitaki kumpenda”

Alirudi nyumbani kwao ila alionekana kuwa na mawazo sana, alimkuta mama yake na hakuweza kumwambia chochote ukizingatia bado binti mdogo atamwambiaje mama yake kuhusu mapenzi, alijiuliza tu moyoni,

“Mapenzi ni nini? Kwanini najisikia hivi kwa Erick? Kwanini nimeumia moyo kumuona Erick yupo na Manka? Aaah sitaki mapenzi jamani, siku zote nafundishwa ubaya wa mapenzi ila kwanini nijisikie hivi kwa Erick? Natamani Erick aniambie ananipenda, ila hapana hawezi kuniambia hilo neno. Mmmh na kile kikaratasi alichoniandikiaga je? Hapana labda alimuandikia mwingine ndio akajisahau na kunipa mimi”

Alikuwa akijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe kisha kuamua kufanya kazi zake za shule na mambo yake ya masomo.
Usiku wa siku hiyo mamake alimuita na kumwambia,
“Mwanangu Erica, umemuona Aisha?”
“Sijamuona, kafanyaje kwani?”

“Shule imemshinda kabeba mimba, tafadhari Erica usinitie aibu ya aina hiyo maana sijui sura yangu nitaiweka wapi”
“Mama jamani mimi naweza kufanya hivyo!”

“Mwanangu, kidato cha pili ndio kidato cha watoto kuota mapembe maana huwa hamsikilizi nyumbani wala walimu shuleni, na wengi shule inawashinda hapo. Mwanangu usinitie aibu, soma kama dada zako, maliza upate kazi ndio uolewe. Yani watoto wako uzae ndani ya ndoa, maswala ya kurukaruka na vijana hapana, tena ikitokea kuna kijana anakusumbua huko sijui nakupenda sijui nini na nini njoo uniambie mwanangu. Wewe niambie halafu mimi nitajua nifanye nini na huyo kijana, sitaki maswala ya mtu kukuchezea binti yangu. Umenielewa!”
“Sawa mama nimekuelewa”

Kisha akamuaga mama yake na kwenda kulala.
 
SEHEMU YA 10


Akiwa amelala, Erica alijiona yuko mahali ufukweni halafu Erick yupo pembeni yake na akimuonyesha mapenzi ya hali ya juu na kumfanya apagawe zaidi. Akashtuka kutoka usingizini akihema hema,
“Shindwa shetani, sitaki maswala ya mapenzi, sitaki kupenda jamani”

Alikaa chini ila wazo la ile ndoto likafanya kazi kwenye akili yake na kuanza kujihisi akitamani kuwa karibu na Erick ila alipingana vikali na wazo hilo.
Kulipokucha kama kawaida alijiandaa na kwenda shuleni, ile anafika tu shuleni akashangaa kumuona Erick akiwa ameongozana na Manka, hakupendezwa na ile kitu kabisa, kisha Erick akaenda upande mwingine halafu Manka akasogea alipo Erica na kumsalimia,
“Erica mambo”
“Poa”
“Mbona leo sio mchangamfu?”
“Kawaida tu, nipo kawaida”
“Ngoja nikuulize kitu”
“Niulize”

“Hivi mimi na Erick tunapendezana eeh!”
Hili swali Erica hakulipenda kabisa, ila kwavile alitaka kumuonyesha Manka kuwa yupo kawaida aliamua kulijibu,
“Mnapendezana, ndio shemeji nini?”
Manka akacheka na kujibu,

“Hapana, ila nina mpenzi wangu kafanana na Erick huyo ndio nilikuwa nataka kujua kama tunapendezana”
“Mmmh Manka jamani, si useme ukweli tu kama ndio shemeji”
Manka akacheka na kumuacha Erica halafu yeye akaelekea darasani kwao, ila Erica aliweza kuelewa pale kuwa Erick na Manka wameshakuwa na mahusiano tayari ukizingatia toka jana amjibu vibaya Erick wala hakuonekana kumfata akimuuliza chochote kile.

“Alikuwa ananipima tu jana, sijui kajua kuwa nampenda kwahiyo anataka kucheza na hisia zangu? Simtaki na sitaki kupenda”
Aliingia zake darasani na kumuona Erick akiwa anazungumza jambo na Johari, alipita kama hawaoni vile maana alienda moja kwa moja kukaa sehemu yake.
 
SEHEMU YA 11

Johari alimfata Erica na kuanza kuongea nae,
“Umeniona pale nilikuwa nimekaa na Erick?”
“Nimekuona ndio”
“Basi mwenzangu, Erick alikuwa ananitongoza”
“Mmmh anakutongoza?”
“Ndio, Erick alikuwa ananitaka yani anasemaje hapa shuleni wasichana wote hakuna anayenifikia mimi kwa uzuri”
“Mmmh sasa wewe umemjibu vipi?”
“Nimemkataa”
“Mmmh Johari wewe umemkataa? Unakumbuka ulisema utamtongoza mwenyewe Erick sasa umepata bahati hiyo amekutaka mwenyewe kweli umkatae”

“Nimemkataa ndio, unafikiri Erick mwenyewe ni mzuri kivile, wala wa kawaida tu”
“Ila jana ulisema alimtongoza Manka”

“Kumbe Erick alimwambia Manka kuwa aje aniambie mimi kuwa ananipenda ila Manka nae anamtaka Erick hajaja kuniambia ndiomana Erick kaamua aniambie mwenyewe leo”
Ikabidi Erica amueleze rafiki yake vile ambavyo aliambiwa na Manka na kuhisi kuwa Manka na Erick washakubaliana,
“Hana lolote huyo Manka, anajivunia ule weupe wake tu. Erick ananitaka mimi ila nimemkataa”

Ilibidi Erica akubaliane na ukweli wa Johari kuwa Erick anamtaka yeye, na moja kwa moja alihisi kuwa Erick ni kijana muhuni na anataka kuchzea wasichana tu ndiomana anawatongoza tongoza hovyo.

Muda kidogo wasichana wote wakaitwa na mwalimu wa malezi pale shuleni alikuwa ni mmama wa makamo, aliwaita na kuanza kuongea nao kuhusu maadili,

“Hivi kweli kabisa msichana unamuandikia barua mvulana ya kumtaka kimapenzi, hamjui kuwa mnajiharibia maisha yenu! Mapenzi yapo tu na mtayakuta mkimaliza shule, hawa vijana wasiwababaishe kabisa, mtu anayekupenda hawezi kukuharibia masomo, atasubiri umalize shule kwanza. Ni aibu kubwa sana kwa jamii ya kiafrika haswaa ya kitanzania kwa mtoto wa kike kumtongoza mvulana. Muache hiyo tabia mnatutia aibu. Leo siwataji wahusika wa tabia hii ila safari ijayo msipojirekebisha nitawataja, hiyo tabia ikome kabisa mnatutia aibu”

Yule mama malezi wao aliwaelekeza vilivyo na kufanya wenye kuelewa waelewe ila wasioelewa kwao ilikuwa ni anapiga makelele tu.
 
SEHEMU YA 12

Muda wa kuondoka leo Erica aliongozana na Johari,
“Unajua madam alikuwa anawasema wakina nani pale”
“Wakina nani?”

“Mwenangu Manka kabambwa na barua kamuandikia Erick kuwa anampenda yani Manka bhana hadi ameshindwa kuniambia mimi ukweli kuwa Erick ananipenda mimi kumbe alishamwandikia barua ya kumtaka”
“Ila mimi hizo hbari za Erick sizitaki”
“Mmmh na mfano akija kukutongoza na wewe?”

“Naenda kumsemea kwa mama yani asithubutu kabisa kabisa. Anafanya wanawake kama mpira eeh kila anayetaka anabutua, kwakweli anikome ingawa najua hawezi kunitongoza mimi”

“Mmmh huwezi jua ya Mungu mengi, ila unatakiwa kuwa na msimamo shoga yangu. Wanaume wana tamaa, yani kama Erick anatamaa sana, mtu mgeni lakini anatamani wanawake hapa shuleni balaa. Yani kuwa makini”
Waliachana kisha Erica kurudi nyumbani kwao na kujiuliza kuwa ni kwanini rafiki yake alikuwa anamsisitiza kuwa awe makini maana yeye aliona kawaida tu na wala hakufikiria kama Erick anaweza kumtongoza ila rafiki yake alivyomtahadhalisha ni balaa.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya Ijumaa na iligubikwa na michezo mbalimbali pale shuleni kwao, Erica alikuwa darasani mwenyewe na rafiki yake Johari walikuwa wakipiga stori za hapa na pale. Muda kidogo aliingia mule darasani Erick akiwa ameongozana na rafiki yake Musa walikaa mbele kidogo na walipokaa Erica na johari.

Wakati maongezi yao yanashamili mara Erick aligeuka na kuita,
“Erica”
Erica alimuangalia Erick ila hakumuitikia, kisha Erick akamuita tena Erica na muda huu Erica alivyomuangalia akamwambia,

“Erica nakupenda”
Moyo wa Erick ulienda kwa kasi sana, na kumfanya asijibu chochote ila Erick alisema tana,
“Erica nakupenda”
 
SEHEMU YA 13



Erica alimuangalia Erick ila hakumuitikia, kisha Erick akamuita tena Erica na muda huu Erica alivyomuangalia akamwambia,
“Erica nakupenda”
Moyo wa Erica ulienda kwa kasi sana, na kumfanya asijibu chochote ila Erick alisema tena,
“Erica nakupenda”
Erica alijihisi vibaya moyoni maana lile swala la kutongozwa mbele ya rafiki yake Johari na mbele ya Musa hakupendezwa nalo, alinuka na kutoka nje kwa aibu, cha ajabu wala rafiki yake Johari hakumfata alipotoka, alikaa peke yake mpaka muda wa kwenda nyumbani.
Leo aliondoka akiwa ameongozana na wanafunzi wengine huku ameweka begi lake mgongoni, mara akavutwa begi na kuwa kama mtu aliyevutwa kwa nyuma, alipogeuka alimuona Erick halafu alikuwa akimuangalia kwa jicho la hamasa sana, huku akiongea kwa sauti kama ya kunong’oneza na yenye mtetemeko ndani yake,
“Erica nakupenda”
“Sitaki uniambie maneno hayo Erick, nitaenda kusema kwa mama”
Kauli hii ilimchekesha Erick na kufanya aanze kucheka, kisha akamuuliza,
“Sasa Erica kukupenda wewe kunahusiana vipi na kwenda kumwambia mama yako? Mimi nakupenda wewe Erica, naomba nielewe”
Erica akaona hii sasa itakuwa ngoma nzito aliamua kukimbia na kumwacha Erick akiwa ameduwaa pale maana Erica alienda kujichanganya na wanafunzi wengine katika mlolongo wa kwenda nyumbani.
Alifika kwao huku sauti ya Erick ikimjia kichwani kuwa Erica nakupenda, aliwaza sana na kutafakari ila uoga nao ulikuwa unamshika vilivyo.
Siku hiyo hadi wakati wa kula chakula cha usiku bado sauti ya Erick ilifanya kazi vilivyo masikioni mwake, hadi akaamua kuwahi kwenda kulala lakini usingizi haukumpata mapema kwani alikuwa akisumbuliwa na sauti ile ile ya Erick.

 
SEHEMU YA 14


Kesho yake akiwa ametulia nyumbani kwao alienda rafiki yake Johari na kumkuta pale na kusalimiana nae kisha kuanza stori za hapa na pale,
“Eeeh jana uliishiana vipi na Erick?”
“Shiiii, punguza sauti mama yupo ndani atasikia”
“Mmmh umemkubalia nini? Sema ukweli Erica”
“Jamani si upunguze sauti nimekwambia, tubadilishe stori kwanza”
“Ila wewe si ulisema akikutongoza utakuja kumwambia mama yako, saivi unasema nipunguze sauti umemkubali nini?”
Mara mama yake Erica alitoka ndani na kuuliza,
“Kitu gani hicho?”
Johari alijibu haraka haraka,
“Kuna kijana mama anaitwa Erick kaja shuleni na amemtongoza Erica halafu huyo kijana anatongoza kila msichana shuleni”
“Amemtongoza?”
“Ndio kamtongoza”
“Yani nyie watoto mmeanza habari za kutongozana kweli? Hayo ndio mambo mnayojifunza huko shuleni, na udogo huo mshaanza kutongozana. Erica niambie hayo maneno ni kweli?”
Erica alikaa kimya na kuinamia chini, mama yake alimuuliza tena ila Erica alinyamaza tu. Mama yake akamsogelea na kumnasa kibao,
“Wewe Erica si naongea na wewe, unaniletea upunguani eeh! Yani binti mdogo hivyo unatongozwa shuleni unaacha kusema kwa mama yako? Na Jumatatu tutaenda wote shuleni nikamuone huyo shababi wa kutongoza tongoza hovyo”
Huyu mama alionekana amechukia vilivyo kisha akaondoka zake, Erica alimuangalia kwa gadhabu sana Johari na kumwambia kuwa aondoke zake.
“Ondoka kwetu”
Johari hakubisha kitu chochote na kuinuka kisha akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 15


Siku ya Jumapili, mama Erica alienda na Erica kanisani na baada ya ibada alimpeleka kwa mchungaji,
“Naomba umuombee mwanangu, ni binti mdogo ila anatakwa kutekwa na ulimwengu wa uzinzi”
Mchungaji alimuangalia Erica na kumuuliza,
“Umesimama wapi binti yangu? Unataka kuharibu usichana wako?”
Erica hakujibu chochote, mchungaji akamuomba mama Erica awapishe ili wapate kuongea kidogo na Erica, basi mama Erica alifanya hivyo. Na baada ya maombi mchungaji alianza kuongea na Erica,
“Ni kweli umeanza uzinzi Erica?”
“Hapana baba”
“Unajua kama uzinzi ni dhambi?”
“Najua na sijafanya uzinzi mimi”
“Sasa imekuwaje mamako aseme umeanza uzinzi?”
“Kuna kijana mmoja shuleni amenitongoza, sijamkubali ila rafiki yangu kaja kusema nyumbani kuwa nimetongozwa”
“Kidato cha pili mnaanza kutongozana jamani!”
“Sikuwa na lengo la kumkubali, tafadhali mchungaji ongea na mama anielewe. Mimi sio mtoto mbaya”
“Sawa nitaongea naye, ila kumbuka kuwa hata kwenye biblia Mithali 4:13 inasema “Mkamate sana elimu, usimuache aende zake” Kuwa makini na masomo yako mwanangu”
“Nimekuelewa”
Basi mchungaji aliahidi kupata siku na kuzungumza na mama yake Erica kwahiyo muda huo akamruhusu kuondoka.
Erica alirudi na mama yake nyumbani ila alimuona mama yake kama hakuwa na furaha kabisa kwa siku hiyo na hakujua ni kitu gani mama yake anakipanga moyoni mwake.

 
SEHEMU YA 16


Jumatatu kama kawaida Erica alijiandaa na kwenda shuleni, ila nay eye hakuwa na furaha kabisa siku hiyo kutokana na vile alivyosemewa na Johari na jinsi alivyosemewa na mama yake kwa mchungaji wao.
Akiwa amekaa darasani mara alikuja kuitwa na mwalimu, na kuongozana nae kuelekea ofisini. Alipoingia tu moyo wake ulishtuka sana kwani alimkuta mama yake na mwalimu wa nidhamu. Kwakweli raha ilizidi kumuisha kabisa kwani hakujua kuwa mama yake ameenda kufanya nini,
“Haya sogea huku Erica”
Erica alisogea kwa mwalimu na kuanza kumsikiliza,
“Ni kijana gani aliyekutongoza?”
Erica alikaa kimya kwani aliogopa kusema kwa kuhofia ni aibu kwa Erick, ila mama yake alimuangalia kwa gadhabu sana, na kumsogelea mwenyewe halafu akamnasa tena kofi,
“Hebu mtaje huyo mwendawazimu mwenzako”
Mwalimu nae akashika bakora kuwa asipotaja atamuadhibu, mwalimu akataka kumchapa bakora. Erica aliamua kusema,
“Lakini hakuna mtu aliyenitongoza”
Mama yake akawaka kwa hasira,
“Kwahiyo mimi ni chizi? Nimekuja kuleta habari za uongo, hebu muiteni rafiki yake Johari aje kuthibitisha ujinga wa huyu”
Mwalimu alimuangalia Erica na kumuamuru apige magoti, kisha mwalimu mwingine alienda kumuita Johari.
Alipofika aliulizwa kuhusu mwanaume aliyemtongoza Erica,
“Ni Erick mwalimu, ila msinitaje”
“Hebu toa ujinga wako hapa, na umuite huyo Erick upesi”
Basi Johari akatoka na kwenda kumuita Erick ambaye alishangaa kufika ofisini na kukuta kuna mmama amekaa huku walimu wawili wakiwa wamesimama na viboko vyao halafu Erica kapigishwa magoti.
Alipofika nae aliamriwa kupigwa magoti na kuulizwa kama ni kweli amemtongoza Erica,
“Ni kweli mwalimu ila sijamwambia kwa lengo baya ni kweli nampenda”
“Nyamaza upesi, unajua kupenda wewe? Ndio nyie mnaoanzaga kuharibu maisha ya wenzenu bado mapema kabisa, unakubali kirahisi rahisi tu.”
Wale walimu walimuomba mama Erica aondoke maana walisema watamshughulikia huyo Erick, kisha wakamwambia Erica ainuke na kwenda darasani.
Kiukweli Erica alishikwa na moyo wa huruma sana, kwani walimu wale walianza kumuadhibu Erick kwa viboko pale pale, basi Erica akasema
“Mwalimu lakini Erick hajanitongoza”
“Nyamaza upesi na wewe, unataka adhabu tukupe wewe eeh! Haya Erick tongoza tongoza nenda darasani, adhabu yako apate huyu kipenda roho”
Erick aligoma na kuwaambia walimu,
“Mimi ndio naye stahili kuadhibiwa kwani ni kweli nilimwambia Erica kuwa nampenda, ingawa sikuwa na nia mbaya. Na ninampenda kweli”
“Nyamaza wewe kijana, Erica toka upesi nenda darasani. Na siku nyingine mtu akikutongoza shuleni uje useme kwa walimu na sio kwenda kusema nyumbani. Mnawapanikisha sana wazazi”
Erica alitoka mule ofisini ila alijawa na roho ya huruma sana, alirudi darasani ila roho ilikuwa inamuuma mno.

 
SEHEMU YA 17


Erica alikuwa kimya kabisa darasani huku watu wakitamani kumuuliza kuwa imekuwaje kule ofisini walipoitwa, ila walishindwa sababu Erica alionekana kuchukizwa sana.
Baada ya masaa mawili, Erick alirudi darasani na kuchukua begi lake kisha akaondoka zake. Yani Erica alitamani kumuuliza kuwa imekuwaje kuwaje, ila hakuweza kufanya hivyo ila Erick alipotoka tu Johari nae alimfata nyuma kumuuliza,
“Pole Erick, imekuwaje tena?”
“Sikujua kuwa Erica ni msichana mjinga kiasi hiki. Kumbe ulijua kuwa atanisemea kwa mama yake kwanini hukuniambia?”
“Ila mimi nilikwambia Erick usimtongoze Erica yani kaniingizia matatizo na mimi, nimeshangaa tu ofisini naitwa nithibitishe eti amesema wakati unamtongoza mimi nilikuwepo. Yani Erica ni muuwaji kwakweli, pole sana Erick. Kwahiyo imeishiaje?”
“Aaah walimu nao wale sijui vipi yani hawaelewi kuna kupenda”
“Kwahiyo umekubali kabisa kuwa kweli ulimtongoza?”
“Kwanini nikatae sasa wakati ni kweli nimemtongoza! Sikuona sababu ya kukataa ukizingatia ni kweli nampenda Erica, wanaweza sema ni akili za kitoto ila kutoka moyoni kabisa nampenda Erica”
“Jamani ukaamua ujitoe muhanga hivyo! Ungekataa kuwa hukumtongoza”
“Siwezi kukataa kitu ambacho nimefanya kweli ila nimeshangaa walimu waliponiambia kuwa Erica amemwambia mama yake kuwa mimi natongoza wasichana hovyo shuleni, jamani toka nimekuja kwenye shule hii sijawahi kumtongoza msichana yeyote Yule, hata shule nilizotoka sijawahi kumtongoza msichana ila Erica nimejikuta yupo moyoni mwangu ila ameniponza”
“Duh pole sana, kwahiyo walimu wamechukua uamuzi gani?”
“Wamesema nikamuite mzazi wangu, wewe rudi darasani yani acha tu”
Erick aliondoka na kumuacha Johari akirudi darasani, ila Joharia alienda moja kwa moja alipokaa rafiki yake na kujaribu kuzungumza nae,
“Jamani Erica usinichukie. Mimi ni rafiki yako ujue, nimefanya yote haya kukuokoa tu”
“Sasa umeniokoa nini na umemuingiza kijana wa watu kwenye matatizo”
“Matatizo gani? Sikia nikwambie, pale nimemfata Erick na kumuuliza kinafki tu. Akasema kuwa alikutongoza mbele yangu ili roho iniume kuwa anakutaka wewe wakati kashanitongoza na mimi. Halafu anasema amekubali ofisini ili wewe umuonee huruma na siku zijazo umkubali ili amalize machungu yake kwako. Yani wanaume ni wapumbavu sana.”
Erica maneno ya Johari yalimuingia kwa kiasi Fulani kwani aliweza kuona kuwa pengine ni kweli Erick alikuwa akimjaribu tu na swala la Erick kukubali ofisini inawezekana ni sababu anahitaji tu amuonee huruma ili mwisho wa siku baada ya zile adhabu amkubali.

 
SEHEMU YA 18


Erica alirudi nyumbani kwao ila hakutaka kumuuliza mama yake kuwa aliongea maneno gani shuleni kwao kwani alijua kama angemuuliza basi angeanzisha mada upya, ila mamake akamuita mwenyewe,
“Yule kijana mwanangu, walimu wamesema lazima atafukuzwa shule”
“Atafukuzwa shule?”
“Ndio, nimemsemea na swala lake la kutongoza kila binti hapo shuleni kwenu. Yani kijana mzuri vile halafu anakuwa na matendo ya ajabu, anajivunia uzuri wake. Yani vijana wa vile huwa hawafai, kazi yao ni kuchezea chezea wasichana”
Erica hakutaka kuchangia mada yoyote kabisa alibaki tu kumsikiliza mama yake kisha kwenda chumbani kwake, ila alikuwa anajiuliza sana kama kosa alilolifanya Erick lina haki ya yeye kufukuzwa shule.
Siku hiyo hakupata usingizi kabisa maana alijikuta akiwaza kuhusu Erick tu na kile kilichotokea siku hiyo hadi panakucha alijiandaa tena na kwenda shuleni.
Aliangalia darasani huku na huku hakumuona Erick, akajikuta akianza kujihisi vibaya katika moyo wake. Akainuka na kutaka kutoka nje ya darasa kidogo akamuona Erick akiwa ameongozana na mama wa makamo alihisi ni mama yake Erick, alitamani sana kujua kuwa ni kitu gani kinaenda kuzungumzwa ofisini.
Alitoka vizuri darasani na kuwa kama anaelekea uwani, ila hakwenda uwani kwani alienda nyuma ya ofisi ya walimu ili kusikiliza kilichokuwa kinajadiliwa.
Alianza kusikia walimu wakiongea na Yule mama ila sauti ya Erick haikusikika,
“Mwanao kaonyesha nidhamu mbovu hapa shuleni hivyobasi tunamsimamisha masomo”
“Jamani walimu, mpeni nafasi nyingine sidhani kama mwanangu atarudia hiko kitu baada ya adhabu yote mliyompa”
Erica alikuwa makini sana kule nyuma akisikiliza, mara alihisi kama kuna mtu kamshika kiuno, akageuka haraka na kumuangalia alikuwa ni Erick.
 
SEHEMU YA 19




Erica alikuwa makini sana kule nyuma akisikiliza, mara alihisi kama kuna mtu kamshika kiuno, akageuka haraka na kumuangalia alikuwa ni Erick.
Ila Erick alikuwa akitabasamu tofauti na Erica alionyesha sura ya kuchukizwa sana kwani hakutegemea kushikwa kiuno na Erick, basi kabla hajasema chochote Erick alimsogelea na kumbusu, kitendo kile kilimzubaisha kidogo Erica kisha Erick akamwambia,
“Najua sitakuona kwasasa maana hii shule ndio basi tena! Ila nimekubusu kama ishara ya upendo wangu kwako”
Erica alikuwa kimya tu, basi Erick akasogea na kumbusu tena ila kwa bahati mbaya wakabambwa na mwalimu wa nidhamu,
“Kheeee yani kesi bado haijaisha mnafanya mambo ya ajabu huku, haya piga magoti”
Wakapiga magoti huku Erica akitetemeka sana na kuanza kumuomba msamaha mwalimu,
“Mwalimu naomba msamaha”
“Msamaha gani niutoe kwa mambo ya kijinga kama hayo? Mimi ni mwalimu wa nidhamu mnataka watu wafikirie nini kwenye shule yetu ikiwa wanafunzi mnafanya vitendo vya ajabu hivyo!”
Erick nae akaongea,
“Lakini mwalimu hakuna kibaya ulichotukuta tunafanya, mimi nimembusu tu Erica”
“Hebu nyamaza na wewe, haya inukeni hapo twendeni ofisini mkapate adhabu yenu”
Basi wakainuka pale kisha mwalimu akaongozana nao hadi ofisini,
“Nimewakuta hawa wajinga nyuma ya ofisi hapo wanabusuana”
“Kheee nyie watoto mna nini lakini? Ni mapenzi gani hayo? Kwakweli sina mjadala hapa, Erick shule basi, na wewe Erica kesho uje na mzazi wako. Mama Erick hakuna cha kusikiliza kutoka kwako, hatutaki vijana wa kuharibu mlolongo wa shule hapa, naomba uondoke na mtoto wako, barua hii hapa nilishawaandalia”
Mama Erick aliona mwanae kamtia aibu sana, kwahiyo akaondoka nae na Erica alitakiwa kwenda kwao muda ule ule kuita mzazi wake.

 
SEHEMU YA 20


Erica aliondoka akiwa na mawazo sana maana hata hakuelewa kuwa mama yake atamueleza kitu gani sababu ni picha mbaya tayari, alifika kwao na kunyata kuingia ndani ila mama yake alimuona na kumuuliza,
“Wewe vipi una matatizo gani wewe? Na mbona mapema hivi?”
Erica alianza kujiuma uma kwani hakuelewa ni jinsi gani amueleze mama yake kuwa anahitajika shuleni na amekutwa na Erick.
“Wewe Erica wewe mbona husemi chochote, kuna tatizo gani mbona mapema?”
“Walimu wamesema nije nikuite”
“Mungu wangu, umefanya ujinga gani tena Erica mwanangu jamani eeh! Niambie ujinga gani umefanya?”
“Sijafanya chochote mama”
“Haiwezekani hujafanya chochote niitwe shuleni kwenu, sema umefanya nini?”
“Sijafanya chochote mama”
“Usiniletee uchizi wako kabisa, tunaenda huko shuleni kwenu sasa hivi, unajua kama una mtihani wa taifa wewe? Unafanya ujinga kweli? Ngoja nijiandae twende”
Yule mama alitumia muda mfupi sana kujiandaa kisha kuanza kukokotana na Erica kwenda shuleni, kwakweli kile kitendo kilikuwa ni cha aibu sana machoni pa Erica.
Walipofika shuleni, wakati mama Erica anaingia getini akielekea ofisini, Erica alirudi nyuma na kujificha kisha akatumia njia za panya kuondoka. Kwahiyo mama Erica alijikuta akiingia mwenyewe ofisini.
Erica alirudi tena nyumbani na kujifungia chumbani kwake akilia, kwakweli alilia sana nah ii aliiona kuwa ni siku mbaya sana kwake kwani kaonekana ni msichana mbaya mwenye tabia mbaya, roho ilimuuma sana.


 
Back
Top Bottom