Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 21


Mama Erica alirudi nyumbani akiwa na hasira sana kwanza kwa kile alichoambiwa mwanae kakifanya na pia kuhusu swala la mwanae kumkimbia shuleni. Aliingia ndani na kumkuta Erica sebleni akijiliza, kwakweli mama Erica alimshika Erica na kuanza kumpiga sana,
“Umenitia aibu sana wewe mtoto, nitaiweka wapi sura yangu hii. Yani siku zote najivunia wanangu wametulia ni wasomi halafu wewe unataka kuharibu sifa ya familia kweli? Sijapenda ulichokifanya Erica, na umesimamishwa masomo mjinga wewe, sijui utafanyaje na kuna mtihani wa kidato cha pili”
Erica alilia sana hadi alikosa raha kabisa kwa kulia, akaenda kujifungia chumbani kwake akilia, yani siku hiyo hakutoka tena nje ukizingatia alionekana ni msichana mstaarabu halafu gafla kaonekana ni msichana asiye na maadili kabisa, alijikuta akiyachukia mapenzi na kukosa raha kabisa.
Mama Erica, alipiga simu kwa Bite ili washauriane kuhusu Erica, naye Bite aliamua kwenda ili akajue imekuwaje.
Baada ya mazungumzo na mama yao aliamua kwenda kuzungumza na mdogo wake,
“Pole mdogo wangu Erica”
“Nisameheni dada ila sijafanya chochote kibaya”
“Naelewa ila niambie ukweli jinsi ilivyokuwa ili nijue jinsi ya kukusaidia”
Erica aliamua kumueleza kitendo cha yeye kwenda nyuma ya ofisi ili kusikiliza alichokuwa anaambiwa mzazi wa Erick na jinsi Erick alivyokuja nyuma yake na kumbusu kisha mwalimu kuwakuta,
“Dada sijafanya chochote kibaya, hata mimi nilikuwa nikimshangaa tu kunibusu ila nimeshangaa walimu kuchukua maamuzi mazito sana kwangu”
“Sawa mdogo wangu nimekuelewa basi usiwe na mawazo sana”
“Mawazo lazima dada, nipo kidato cha pili natakiwa kufanya mtihani”
“Si bado namba za mitihani hamjaandikisha?”
“Ndio ila nitafanyaje?”
“Usijali nitakufanyia mpango haraka iwezekanavyo na tutaenda kuishi wote kule kwangu hadi umalize kidato cha nne na kumaliza masomo yoko yote vizuri ila niahidi tu kuwa hutoniangusha. Yani maswala ya mapenzi hayatakuwepo kwenye akili yako”
“Dada nataka kusoma, sitaki habari za mapenzi kabisa nataka kusoma”
“Basi usijali, ngoja niongee na mama. Tutaondoka leoleo maana mama inaonyesha amechukizwa sana asije akafanya kitu kibaya bure, ngoja twende ili mama nae apunguze mawazo”
“Sawa dada nimekuelewa”
Basi Bite aliamua kwenda kuongea na mama yao ili kuangalia namna ya kumsaidia mdogo wake huyu.

 
SEHEMU YA 22


Erica alichukuliwa na dada yake kisha akatafutiwa shule nyingine na kuanza masomo yake huko, kwakweli alijikuta akifikiria zaidi masomo na kuyachukia mapenzi kwani yalishamwekea doa na sifa mbaya, hakupenda ile kitu ijirudie katika maisha yake ya kwenye shule hiyo mpya kwahiyo alijitahidi kusoma kwa bidii na kujiweka mbali na watoto wa kiume kwani kila aliporudi nyumbani dadake alikuwa akimuhusia kuhusu mapenzi kuyaanza mapema yanavyoumiza moyo,
“Kwahiyo dada ni kipindi gani kizuri kuanza mapenzi?”
“Usifikirie hayo kwasasa mdogo wangu, kipindi kizuri ukikua utakijua tu ila kwasasa usifikirie chochote kuhusu mapenzi yani wewe fikiria elimu yako tu. Mapenzi yapo na utayakuta huko mbele, kwasasa fikiria masomo”
“Sawa dada”
“Na kama kuna jambo lolote unakumbana nalo huko shuleni usisite kuniambia, nieleze mimi ni dada yako na nimepitia mengi nayajua”
Erica alimuelewa sana dada yake huyu na aliona anafanya yote haya sababu anamuhurumia kwahiyo ikabidi asome kwa bidii, hata akaachana na marafiki wote aliokuwa nao awali zaidi ya kufatilia masomo yake.

Erica alimaliza kidato cha nne na matokeo yalitoka alikuwa amefaulu vizuri tu na kuchaguliwa kuendelea na masomo yake kwenye shule ya bweni ya wasichana, alifurahi maana aliona huko kutamsaidia zaidi kutokujihusisha na maswala ya mapenzi.
Dada yake alimfanyia mipango yote ya kuweza kuanza shule na alianza shule aliyopangiwa, ila muda ambao marafiki aliokutana nao kule wakiwa wanaongelea mada za mapenzi kwenye kichwa chake inamjia picha ya mtu mmoja tu ambaye ni Erick hadi mara nyingine anawaza kuwa Erick atakuwa wapi, kuwa nay eye je anaendelea na shule? Kwenye moyo wake aliona ni kweli anampenda Erick na aliamini ipo siku atakutana tena na Erick halafu Erick atamtongoza tena na kuanza mahusiano,
“Sijui kwanini huyu Erick hatoki kwenye akili yangu, ni siku nyingi lakini Erick bado kaganda kwenye akili yangu. Kuna siku nitamuona tena kweli? Kama Erick alikuwa ananipenda kweli nina hakika nay eye atakuwa anasubiri tukutane tena tukiwa wakubwa”
Ndio mawazo yake yalivyokuwa yakimueleza maana moyo wake ulimpenda Erick vilivyo.


 
SEHEMU YA 23


Shule ilifungwa na wanafunzi walikuwa wakirudi likizo, alipanda kwenye basi na wanafunzi wengine, ila siti aliyokaa yeye alipakana na kijana mmoja ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi anarudi kwao likizo, Yule kijana alianza kwa kumuongelesha Erica,
“Naitwa John, sijui mwenzangu unaitwa nani”
“Naitwa Erica”
“Oooh jina zuri sana, unajua safari ni ndefu mno bora tuzoeane tu. Unaishi sehemu gani?”
Erica alianza kuzungumza na yule John na kujikuta wakiongelea habari nyingi za hapa na pale ila mwisho wa siku John akamuomba Erica namba za simu,
“Sina simu”
“Mmmh huna simu mdada wa kidato cha tano?”
“Ndio sina simu, shuleni wanakataza. Nyumbani ndio kabisa, dadangu aliniambia nikimaliza kidato cha sita ataninunulia”
“Sasa itakuwaje? Mi napenda tuendelee kuwasiliana”
“Sijui itakavyokuwa, tutawasiliana tu siku nyingine tukionana ila simu mimi sina”
John akafungua begi lake la mgongoni na kutoa simu,
“Nina simu mbili, naomba uchukue hii moja tuwe tunawasiliana, natamani niwe na mawasiliano na wewe ya karibu sana Erica. Tafadhali naomba usikatae”
“Mmmh sasa wewe unaniamini nini mimi hadi kunipa simu?”
“Moyo wangu umekuamini Erica, tafadhali chukua simu hii tuwe tunawasiliana nakuomba, laini ipo nitakuwa nakupigia hata kama ukikosa vocha uwe unaniambia nikurushie”
John alimbembeleza sana Erica naye Erica aliona John ana moyo wa kipekee sana yani kumpa simu mtu asiye mfahamu vizuri ni kitu cha ajabu sana. Baada ya kubembelezwa sana Erica alikubali simu ile kwani kiukweli hata yeye alitamani sana kumiliki simu ila tu kwao walikuwa wanamzingua kumnunulia kwahiyo bahati ya kupewa simu na Yule kijana ilikuwa ni nzuri sana kwake ukizingatia Yule ni mwanafunzi mwenzie kwahiyo aliona katoa kwa upendo tu.

 
SEHEMU YA 24


Erica alifikia nyumbani kwao maana mama yake alisema likizo awe anarudi nyumbani, kwahiyo ile simu aliyopewa na John aliificha chumbani kwake.
Ila likizo yake alikuwa akishinda sana chumbani kiasi kwamba mama yake akajua ni sababu ya kushinda sana shuleni kumbe alikuwa makini akiwasiliana kwa njia ya ujumbe na John, ila kila mama yake alipomuita aliificha ile simu. Alikuwa akiwasiliana na John kiasi kwamba aliona kuwa anaanza kumpenda John hata akasahau kama kuna mtu wa kuitwa Erick kwenye kichwa chake,
“Unajua Erica wewe ni msichana mrembo sana, natamani siku moja uje kuwa mke wangu”
“Jamani John mmmh!”
“Tupange kuonana kabla ya kurudi shule”
“Sasa tutaonana wapi?”
“Kuna sehemu nzuri sana mitaa ya Kigamboni, nitakwambia na tutaonana mapema sana halafu utarudi kwenu jioni”
“Sijui kama nitaweza, sijui kama nitapewa ruhusa”
“Kwanini wasikuruhusu binti mkubwa tu!”
“Kwetu ni watu wa dini sana, mama yangu ni mlokole yani hataki nitoke kabisa hata sijui nitamuagaje”
“Huwezi kumwambia unaenda kusalimia ndugu zako?”
“Yani mimi kutoka nyumbani labda dada yangu akijaga kunichukua kuwa twende nae mahali, na kusalimia ndugu wote anakujaga kunichukua yeye. Yule dada yangu aliyekuja kunipokea stendi”
“Sasa tutaonana vipi Erica?”
“Sijui”
“Hutaki kujifunza mapenzi wewe?”
“Mmmh naogopa ujue”
“Usiogope nitakufundisha”
Erica aliitwa na mama yake ikabidi aache simu na kwenda kumsikiliza,
“Mwanangu Erica mbona toka umerudi unajifungia tu chumbani au bado una mambo yale yale yaliyopita mwanangu? Yaliyopitwa si ndwele jamani Erica”
“Hapana mama sijifungii sababu hiyo nakuwa tu nimechoka”
“Kuwa mkweli mwanangu, yani nimeomba likizo urudi hapa nyumbani. Maana toka kipindi kile chote umekaa kwa dada yako, nikaona mwanangu umeenda mbali sana, nikaomba urudi hapa ili nikae kae na wewe japo kidogo ila tangu umerudi ni kujifungia ndani tu hadi sielewi kuwa una tatizo gani?”
“Hapana mama sina tatizo lolote”
“Basi uwe unakuja tunaongea ongea kidogo, hujanimiss mama yako jamani! Hutaki kuongea kidogo na mama yako huoni ni furaha hiyo”
“Nimekuelewa mama ila hata rafiki zangu wa mtaani nimewakumbuka, natamani nikawasalimie”
“Ukawasalimie nini watoto mapunguani wale, Yule rafiki yako Johari unajua kama ana mtoto!”
“Ana mtoto?”
“Ndio ana mtoto shule ilimshinda, yani kaendekeza mapenzi mwishowe ana mtoto. Nilikutana nae siku hiyo anaenda kliniki kachakaa hatari, ndiomana mwanangu nakwambia usome, hao rafiki zako hata sio watu”
“Ila mama ningeenda kuwasalimia tu”
“Unataka ukamsalimie nani Johari? Nitakupeleka kwao maana mimi pia nahitaji kwenda mitaa ya kule kwao kesho”
Erica ilibidi tu akubaliane na mama yake maana sharia za mama yake zilikuwa zinambana kiasi kwamba alikosa hata raha ya kufanya mambo yake mengine.

 
SEHEMU YA 25


Kesho yake kama alivyopanga na mama yake walienda kwakina Johari, mama yake alikuwa anaongea na mama Johari halafu Johari alibaki kuongea na Erica,
“Kheee Johari kumbe una mtoto kweli?”
“Ndio rafiki yangu nina mtoto”
“Shule tena!!”
“Unadhani kuna cha shule hapa, nalea tu. Ila unajua aliyenizalisha?”
“Nani?”
“Geuka nyuma umuone anakuja”
Erica akageuka, alipomuona alishangaa sana maana hakuamini kabisa.


“Kheee Johari kumbe una mtoto kweli?”
“Ndio rafiki yangu nina mtoto”
“Shule tena!!”
“Unadhani kuna cha shule hapa, nalea tu. Ila unajua aliyenizalisha?”
“Nani?”
“Geuka nyuma umuone anakuja”
Erica akageuka, alipomuona alishangaa sana maana hakuamini kabisa.
Alimuangalia tena na kumuangalia Johari kisha akamuuliza kwa mshangao,
“Johari umezaa na mwalimu wa nidhamu!”
“Ndio hivyo rafiki yangu”
“Sasa nidhamu iko wapi hapo ikiwa mwalimu anazaa na mwanafunzi? Huyu mwalimu alisababishwa hadi nifukuzwe shule sababu ya busu la Erick tu ila leo umezaa nae! Inamaana ulikuwa na mahusiano na mwalimu?”
“Erica yani acha tu haya mambo haya sijui nikuelezeje ila acha tu”
Mama yake Erica alimfata Erica na kushangaa pia uwepo wa Yule mwalimu, ila Erica hakumficha mama yake ni pale pale alimpasulia kuwa mtoto wa Johari ni wa Yule mwalimu,
“Kheee baba kumbe tulijua unatuchungia wanetu kumbe wewe ndio fisi loh!”
Kisha mama Erica akaondoka na Erica na kurudi nae nyumbani, walipofika tu akaanza kumpa tena sharia zake,
“Hapa nyumbani hutoenda popote zaidi ya kwenda shuleni shule zikifunguliwa, na nitauliza walimu wako kama umefika shuleni. Ole wako uniletee upuuzi kama wa mwenzio Yule sijui hiko kitoto chako utakiweka wapi, sitaki ujinga mimi”
Kwa maneno haya ya mama yake aliona itakuwa ni vigumu kabisa hata kuonana tena na John ingawa alikuwa akiwasiliana nae kwenye simu.

 
SEHEMU YA 26


Aliwasiliana na John kwa hakika hakuweza kukutana nae hadi likizo inaisha ila wakaahidiana aende na simu shuleni ili wawe wanawasiliana kinyemela kwani aliamini kuwa wapo wanafunzi wenye simu, alikubaliana nae kufanya hivyo.
Siku ya kurudi tena shuleni ilifika na alifatwa alfajiri na dada yake ili akapandishwe kwenye basi la kwenda shuleni, katika harakati za kuwahi akajikuta akisahau simu yake chumbani na aligundua wakati ameshapanda basi la kwenda mkoa.
Kwakweli alipatwa na gadhabu sana na kuwaza ikiwa mama yake ataiona hiyo simu itakuwaje maana hakuwa na uhakika wa haswa kuwa wapi ameiacha,
“Sijui nimeisahau vipi jamani, si John ataona kuwa namfanyia makusudi? Sijui imekuwaje nimesahau ile simu”
Alifika hadi shuleni akiwa na mawazo ya kusahau simu yake tu huku akisubiri likizo nyingine akienda nyumbani kwao, ila ilikuwa tofauti kwani likizo iliyofuata dada yake naye alikuwa kwenye mkoa huo na kumwambia kuwa atakuwa nae kwenye likizo nzima kwahiyo hakuweza kurudi nyumbani mpaka tarehe ya kufungua akarudi tena shuleni, alipatwa na mawazo sana ila mwisho wa siku akaamua kuachana na wazo hilo na kuona kama ni bahati basi anaweza akaja kukutana tena na Yule John kwa sehemu nyingine.
Alimaliza kidato cha sita na dada yake alihudhuria kwenye mahafali yake na kumwambia kuna zawadi amemuandalia ambapo wakati wakirudi nyumbani atampatia.
Na kweli kipindi anarudi dada yake akamkabidhi simu na laini na kumwambia kuwa kafurahishwa nae sana kuweza kumaliza shule na kumzawadia hiyo simu,
“Najua ulikuwa unatamani sana kumiliki simu, hiyo hapo utatumia na nilishamwambia mama amekubali pia”
“Asante sana dada”
Basi safari ilifanyika hadi wakafika nyumbani na kumkabidhi kwa mama yake, kisha dada yake kuelekea nyumbani kwake.
Sababu walifika usiku alikuwa amechoka sana, hivyo alifikia kuoga, kula na kulala.

 
SEHEMU YA 27


Kulipokucha akakumbuka kuhusu simu yake aliyoiacha nyumbani kwao hapo, akajiuliza kuwa aliiacha sehemu gani na je bado itakuwa nzima au mbovu akaanza kutafuta mule chumbani, alitafuta sana ila hakuipata, muda kidogo mama yake akamuita, alitoka na kumsalimia
“Unaonekana upo busy sana, unatafuta nini?”
“Hamna kitu mama”
“Mmmh mpaka leo Erica bado unamficha mama yako jamani, najua unachotafuta ni simu”
Erica akashtuka kidogo maana hakudhania kuwa mama yake anajua kuhusu ile simu, alibaki anamtazama tu na mama yake aliendelea kuongea,
“Umekuwa msichana mkubwa sasa na karibia utaenda chuo kikuu, mwanangu nilikuwa nafanya yote kukulinda ila bado nikashangaa umepata ujasiri wa kuhongwa simu! Mwanangu mwanaume aliyekuhonga simu hakukutakia mema na maisha yako, na Mungu ni mkubwa sana ukaisahau, unajua uliisahau wapi?”
Erica aliangalia tu chini, na mama yake aliendelea kuongea
“Uliisahau hapo kwenye meza ya kula chakula. Nilijua tu ni wewe umeiacha maana humu ndani tunakaa san asana wawili, sasa unajua kilichotokea kwenye ile simu?”
“Sijui”
“Basi ile simu ilianza kuita na hukuweka mlio zaidi ya mtetemeko tu, nilisikia kitu kikiungurumisha mezani, nikakuta anapiga mtu aitwaye John maana uliandika jina hilo. Nikataka nipokee nijue mbivu na mbichi kama ujuavyo mama yako sipendi kinishinde chochote, ila kwa bahati mbaya muda huo nilikuwa nimeweka ndoo maji ili nideki na ile simu iliniponyoka na kuingia kwenye maji”
Erica alishangaa sana, huku akitamani kujua nini kiliendelea kwahiyo alimuuliza mama yake,
“Kwahiyo ndio ikafa hapo?”
“Hapana, niliitoa na kuifungua nilitaka niweke ile laini kwenye simu nyingine ila wakati natoa ile laini kwenye ile simu ilivunjika, yani laini ilivunjika kabisa, na simu nimeiacha ndani nadhani imekuwa kopo sasa. Haya mwanangu uliitoa wapi na John ni nani?”
Erica aliona sasa ni njia pekee ya kujitetea maana mama yake hajajua ukweli wowote wa ile simu,
“Ile simu haikuwa yangu mama, ila kuna rafiki yangu wakati tunarudi aliisahau kwenye begi langu na bahati mbaya alisafiri kabla yangu kwahiyo alisema nimpelekee shuleni, na mimi nikaisahau hata sikujua nimeiacha sehemu gani”
“Kheee kumbe ni ya rafiki yako? Na huyo John?”
“Hata simjui mama, huniaminigi tu mama ila mimi sina mambo hayo, unamuona Yule mwalimu aliyesingizia kuwa kaniona mimi na Erick, kiko wapi sasa ndio kamzalisha Johari, mama kuna watu hawapendi tu maendeleo yangu, hayo mambo sina”
“Jitunze mwanangu, jitunze nije kula mahali yako nzuri. Uwe mtoto mwema na mzuri, umalize shule uolewe, mama zenu tulijitunza ndiomana hadi leo tupo kwenye ndoa zetu”
“Sina mambo hayo mama hata usinifikirie vibaya, mimi mwenyewe nataka nisome na nipate kazi halafu ndio niolewe. Sitaki kuchezea maisha yangu mama”
“Sasa huyo mwenzio ulimalizana nae vipi?”
“Nilimueleza dada Bite, na alimlipa Yule mwenzangu, ndiomana akaninunulia na mimi simu”
“Kwasasa tumia tu simu ila wasiliana na wasichana wenzio sio wakina John, sijui Erick hapana utaharibu maisha yako”
“Jamani mama, sina mambo hayo”
Erica aliona sasa amefaulu ule mtihani wa kutokuaminiwa na mama yake ingawa alijua wazi hawezi kuwasiliana tena na John, pia hakujua kama ingetokea siku aneonana tena na Erick, watu hawa alishawatoa kwenye akili yake ingawa mara moja moja alipatwa na mawazo kuwahusu ila bado hakujua ni yupi amchague kati yao maana wote walimvutia.

 
SEHEMU YA 28


Erica kwasasa alikuwa nyumbani tu na alijiona kuboreka sana ukizingatia hakuwa na wa kuwasiliana nae na hakuwa na cha kufanya zaidi ya kufanya kazi za nyumbani na kuangalia televisheni tu.
Siku hiyo akiwa anaangalia televisheni usiku akaona kipindi kinaitwa cha rafiki nakutafuta, akavutiwa nacho. Ilikuwa kwenye saa tano usiku na aliona watu wakiandika namba zao za simu kuwa wanatafuta marafiki wa kuwasiliana nao, akaona ni vyema nae aangalie hapo, ndipo alipoinyaka namba moja na kuandika kwenye simu yake kisha kujaribisha kuipiga, akashangaa ile namba ikiita akaogopa na kukata. Muda kidogo ile namba ilianza kupigwa, ikaita hadi kukatika, ikaanza kuita tena akaamua kuzima televisheni na kwenda chumbani kwake kupokea, ilikuwa ni sauti yam kaka,
“Hallow, mambo umenibipu”
“Samahani, niliona namba yako kwenye tv ndio nikaijaribisha”
“Aaah unapenda kuchat”
“Ndio”
“Unaitwa nani?”
Erica akajiuma uma akajikuta akiropoka tu jina,
“Naitwa Irene, na wewe je?”
“Mimi kama jina langu lilivyotokea kwenye screen naitwa Babuu”
“Aah sawa”
“Basi tuwe tunachat”
Yule kijana akamuaga pale Erica na kukata simu, kwakweli Erica alihema kiasi na kuona kumbe wale watu wanaotafuta marafiki wanakuwaga wa kweli yeye alijua ni watu uongo, ila alishangaa kuona akiongea ni mtu kweli. Aliamua kulala sasa maana hakuwa na kingine cha kufanya.
 
SEHEMU YA 29



Alipoamka asubuhi tu alikutana na ujumbe kwenye simu yake kutoka kwa Babuu,
“Hellow Irene, mambo vipi?”
Akatabasamu, ila kwavile hakuwa na vocha alisema kuwa mpaka anunue vocha ndio ataweka ili awasiliane nae, kwahiyo akaamka vizuri na kwenda kufanya kazi zingine za pale nyumbani kwao.
Kwenye mida ya saa nne asubuhi alisikia simu yake inaita na kwenda kuiangalia, aliona akiwa Babuu anapiga, akapokea kwa uoga,
“Mambo Irene?”
“Safi tu”
“Mbona nakutumia sms zangu hujibu jamani, tatizo nini mama?”
Erica alianza kujiuma uma na kuamua kuongea,
“Simu haikuwa na salio ila nikiweka salio nitakujibu”
“Usijali, ngoja nikuungie kifurushi”
Simu ilikatika, na muda mfupi Erica aliona ameungiwa kifurushi kwenye simu yake, na kubaki tu,
“Wow huyu mkaka hata hanijui masikini ya Mungu jamani ila ameniungia kifurushi loh ngoja niwasiliane nae”
Akaanza kutumiana ujumbe na Babuu kwa njia ya ujumbe alijikuta akitumia simu mara kwa mara kuandika ujumbe kwa kuwasiliana na huyo babuu alishangaa sababu ni mtu ambaye alikuwa kila muda lazima awezeshe kuchat nae.

Toka Erica afahamiane na Babuu ilikuwa ni muda wote kuwa na simu yake, alikuwa na hiyari akale chakula chumbani ili atumie simu yake kuwasiliana na Babuu kwa njia ya ujumbe,
“Nakupenda Irene”
“Mmmh utanipendaje na hujawahi kuniona!”
“Irene, moyo ni kitu cha ajabu sana. Ni kweli sijawahi kukuona ila huwezi amini, kila siku nakuona kwenye ndoto zangu. Nakupenda Irene, naimani wewe ndiye mwanamke unayefaa kuwa mke wangu”
“Mmmh Babuu jamani”
“Kweli kabisa, ila sijui kama wewe utanipenda mimi. Mwenzio nakupenda”
“Kwani wewe upoje?”
“Mimi ni mfupi kiasi na mweusi kiasi”
“Mmmh”
“Mbona unaguna?”
“Kiukweli wanaume wafupi na weusi huwa siwapendi”
“Kwanini?”
“Basi tu siwapendi”
“Jamani Irene usinifanyie hivyo, basi tupange siku moja tuonane kwa hakika nitaridhika hata nikikuona”
“Hakuna shida tutaonana ila mi naona bora tuendelee kuwasiliana tu hivi hivi, yani wanaume wafupi halafu weusi siwapendagi hata kidogo”
“Sawa ila siku zote Irene utakaa katika moyo wangu, nakupenda sana”
Erica alijikuta akiwaza sana kuhusu muonekano wa Babuu, alivutiwa na mawasiliano ya Babuu yalivyo ila hakuvutiwa na jinsi Babuu alivyomwambia kuwa yupo hivyo.
“Aaah hapana siwezi kumpenda hata kama yeye ananipenda vilivyo ila mimi kumpenda siwezi. Yani mi napenda mwanaume awe mrefu halafu awe na maji ya kunde, nikimpata kama huyo nitafurahi sana”
Akawaza pale, akakumbuka mwanaume aliyekuwa vile alivyokuwa anapenda yeye alikuwa ni Erick,
“Mmmh kweli Erick alikuwa ninavyopenda mimi ila je Erick alinipenda kweli? Erick alitongoza wadada wengi shuleni, inawezekana Johari aliongea ukweli kuwa Erick alitaka kunichezea tu. Ila hivi mimi nitapata mpenzi kweli? Natamani na mimi niwe na mpenzi, nipate mwanaume nimpende na badae aje kuwa mume wangu nitafurahi sana, sijui kama nitampata? Muda wote nipo nyumbani ndani, hata njiani sionekani, kuna dalili yoyote ya kupata mwanaume kweli? Labda nikienda chuo”
Aliwaza sana ila hakupata majibu.
 
SEHEMU YA 30



Babuu aliendelea kusisitiza kuhusu swala la kuonana na Erica ambaye yeye alimjua kwa jina la Irene sababu ndio jina alilojitambulisha nalo kwake, ilibidi Erica amwambie jinsi ilivyokuwa ngumu kwa yeye kutoka nyumbani kwao,
“Jamani Irene si umesema ndio umemaliza kidato cha sita wewe?”
“Ndio”
“Sasa watakukataza vipi na ushakuwa mkubwa? Huwezi kusema unataka kwenda kumtembelea rafiki yako?”
“Hata sijui nyumbani nitasemaje maana kama ni rafiki wa hapa mtaani mama atasema twende wote”
“Wewe hupendi kutembea ufukweni?”
“Napenda”
“Basi mimi nataka tukutane ufukweni, yani tuonane tu nitaridhika. Najua kunipenda huwezi Irene ila tuonane tu basi ili tufahamiane kwa sura”
“Sawa ila kwetu nitaagaje?”
“Ngoja nikufundishe, leo mwambie mamako kuwa kuna rafiki yako anaumwa na kesho mmepanga kukutana na wenzio ili mkamuone hospitali, na hakika atakuruhusu tu. Mwambie rafiki yako ambaye hamjui yeye mliyesoma nae bweni huko, mtaje yeyote”
“Basi nitajaribu”
“Haya utaniambia ili kesho nijiandae kukutana na wewe malaika wangu”
“Mmmh!”
“Usigune bhana, wewe ni malaika wangu”
“Ila si nimekwambia sitaki”
“Nisamehe bure ni moyo wangu ndio king’ang’anizi, ila naomba tuonane tu Irene”
Basi Erica akajaribu tu kuongea na mama yake kamavile alivyoelekezwa ila mama yake alimkubalia hata yeye mwenyewe akashangaa kuwa mama yake mbona kawa mwepesi vile kukubali.
“Nitakupa na nauli mwanangu, ni vyema kuwa na ushirikiano hivyo na wenzio”
“Asante mama”
Erica alifurahi sana, yani siku hiyo alilala huku akitabasamu.


 
SEHEMU YA 31


Kesho yake alijiandaa vizuri kabisa, na kwenda kumuaga mama yake ambaye kweli alimpa nauli kama alivyomuahidi maana alijua ni kweli anaenda hospitali kumuona mwenzao anayeumwa ila ukweli ni kuwa Erica alikuwa anaenda kuonana na Babuu.
Erica alifika hadi eneo ambalo alipanga kukutana na Babuu, akampigia simu alipo ila alishangaa Babuu akimwambia Erica.
“Nishakuona tayari, nakuja hapo sasa hivi”
Erica akashangaa kwani Babuu alikuwa hamjui Erica kwa sura halafu kamwambia nimeshakuona, akashangaa amemuona vipi, akiwa anashangaa mara kuna mtu alimshika began a kumuita,
“Irene”
Aligeuka na kumuangali, ila Erica alipigwa na bumbuwazi kiasi kwamba hakuweza kuongea chochote kwa wakati huo.


Erica akashangaa kwani Babuu alikuwa hamjui Erica kwa sura halafu kamwambia nimeshakuona, akashangaa amemuona vipi, akiwa anashangaa mara kuna mtu alimshika began a kumuita,
“Irene”
Aligeuka na kumuangali, ila Erica alipigwa na bumbuwazi kiasi kwamba hakuweza kuongea chochote kwa wakati huo.
Babuu alimuuliza Erica,
“Mbona unashangaa?”
Erica alikuwa kimya kwenye mshangao, na baada ya muda alimuuliza,
“Si ulisema wewe mfupi?”
“Ndio mimi ni mfupi, kwani nina urefu gani?”
“Si ulisema wewe ni mweusi?”
“Ndio mimi ni mweusi kwani nina weupe gani?”
Erica alikuwa kwenye mshangao bado kwani Babuu aliyekuwa akimfikiria sio huyu aliyemuona kwenye macho yake, Babuu huyu alikuwa ni kijana anayevutia sana na alivutia macho yake kiasi cha kumfanya Erica hata aone aibu kumtazama.
Ila Babuu alimshika mkono Erica na kwenda kukaa nae mahali pale pale ufukweni ili waongee mawili matatu, na waliongea kweli ila Erica alitumia muda mwingi sana kumuangalia Babuu kiasi kwamba hata Babuu aliposema kuwa ni muda wa kuondoka ilikuwa ngumu sana kwa Erica kukubaliana na hilo ila kila alipokumbuka kwao ilibidi tu atake kuondoka na yeye. Ila aliamua kumwambia Babuu ukweli wa jina lake,
“Babuu mimi sio Irene, ila naitwa Erica. Nilikudanganya tu”
“Usijali Irene, ooh sorry Erica, ila nimezoea kukuita Irene, usijali jina sio tatizo kwangu”
“Sawa hamna shida hata ukiniita hilo Irene sio tatizo”
Walienda hadi kwenye stendi ya daladala ambapo Babuu alihakikisha Erica kapanda basi ya kwenda kwao halafu akampa na nauli, kisha yeye kuondoka zake.
Yani Erica mule kwenye daladala alijikuta akiwaza kuhusu Babuu tu, alimuwaza sana Babuu hadi anafika nyumbani kwao.

 
SEHEMU YA 32


Alipoingia ndani, mama yake alimuuliza,
“Mbona umechelewa?”
“Foleni mama”
“Kwani ni hospitali gani?”
“Ni Muhimbili”
“Anaendeleaje”
“Hajambo anaweza akaruhusiwa kesho”
“Eeeh Mungu ni mwema kwakweli, nimekuwa nikimuombea jamani bora aruhusiwe tu”
Erica aliongea ongea pale kidogo na mama yake kisha kwenda chumbani ila mawazo mengi yalikuwa kwa huyu mtu anayeitwa Babuu.
Alioga na kula huku akiwaza sana, alitamani Babuu amtongoze tena na kusema iwapo itatokea hiyo nafasi basi atamkubali haraka iwezekanavyo,
“Hivi mkaka mzuri vile kweli anakosa wanawake hadi atafute kwenye tv? Mbona mkaka mzuri Yule”
Ujumbe kutoka kwa Babuu ukaingia,
“Wewe ni msichana mrembo sana, macho yangu yalitamani muda wote yakutazame wewe, kwa hakika nakupenda. Tafadhali Erica usinikatae utanitesa”
Erica aliusoma ujumbe huu mara mbili mbili, kisha akamjibu,
“Ni kweli kabisa unanipenda Babuu?”
“Nakupenda sana tena sana Erica”
“Na mimi nakupenda pia”
Inaonyesha Babuu hakuamini kabisa kwani alipiga na simu ili kuhakikisha kuwa anayewasiliana nae kwenye ujumbe ni Erica na leo kamjibu kuwa anampenda pia, walianza kuongea kwenye simu ila Erica alikuwa na aibu sana na kumuomba Babuu kuwa waendelee kuongea kwa njia ya ujumbe. Ikabidi Babuu akate na waendelee kwa njia ya ujumbe,
“Unajua furaha niliyo nayo hadi siamini kama kweli umenikubalia Erica, nakupenda sana naahidi kukupenda siku zote za maisha yangu”
“Nakupenda pia Babuu”
“Sijawahi kumpenda msichana yeyote katika maisha yangu, wewe ni msichana wa kwanza kabisa. Nakupenda sana, naimani nitadumu na wewe mpaka mwisho wangu”
Erica alikuwa akitabasamu tu na alijikuta akiwasiliana na Babuu hadi usiku wa manane wa siku hiyo.

 
SEHEMU YA 33


Kesho yake aliamka saa mbili na nusu asubuhi hadi mama yake akamshangaa maana sio kawaida yake kuchelewa hivyo kuamka, huwa akichelewa sana basi ni saa moja asubuhi kwahiyo kuamka saa mbili na nusu siku hiyo ilikuwa ajabu kidogo.
“Leo mwanangu umechelewa kuamka?”
“Leo usingizi ulikuwa mtamu mama nahisi ndiomana nimechelewa kuamka”
Alifanya shughuli zake ila alionekana kuwa na furaha sana hata mama yake akashangaa kuwa mtoto wake kuwa na furaha vile ni kitu cha ajabu.
Siku hiyo alifika dada yake Bite kumsalimia mama yao, kwahiyo nay eye alipata muda wa kuongea nae kidogo kama kawaida yake,
“Dada, hivi mapenzi ni nini?”
“Mapenzi ni kitu flani hivi ambacho unajisikia moyoni kuwa unampenda mtu Fulani halafu mtu huyo nae anakupenda wewe. Yani mapenzi ni kupendana, ila raha ya mapenzi ni kupendwa. Kupendwa raha mdogo wangu asikwambie mtu”
“Na utajuaje kama mtu anakupenda?”
“Anakujali, anakusikiliza na ana hisia na wewe”
“Mmmh ni hivyo tu?”
“Maelezo marefu bhana, kuna mtu anakupenda nini mdogo wangu?”
“Hamna dada nimeuliza tu, na hivi unajuaje kama unampenda mtu Fulani?”
“Unajisikia moyoni kuwa unampenda halafu unakuwa na wivu na mtu huyo yani inakujaga tu automatically”
Erica alimsikiliza dada yake ila kama alikuwa anamuelewa na kama alikuwa hamuelewi kwani kwa muda huo mawazo yake ni Babuu tu.
Na aliendelea kuwasiliana na Babuu siku zote ila kuonana nae ilikuwa ngumu sababu ya kukosa ruhusa ya kutembea tembea kutoka kwao.

 
SEHEMU YA 34


Erica alibahatika kuchaguliwa chuo kwahiyo alikuwa na harakati za kuanza chuo ambapo ilimlazimu kukaa hosteli, kitu ambacho kwa upande mwingine alikipenda sana kwani aliona kuwa atakuwa huru sasa na kuonana na Babuu na akajiona atapanga vingi sana akiwa anaonana na Babuu.
Alimuona Babuu kama ni kijana pekee katika maisha yake, akampenda kupita maelezo ya kawaida hata siku zilivyoenda na Babuu kumuomba mapenzi hakuwa na sababu ya kumkatalia kwani ameshakuwa ni mpenzi wake wa muda mrefu, na walionyesha kupendana sana.
“Pole Erica ila nimefurahi sana mimi kuwa mwanaume wa kwanza kwako, naahidi kukupenda siku zote za maisha yangu”
“Asante Babuu, natumaini wewe ndiye mume wangu”
Walijikuta muda mwingi sana wakiongea kuhusu maswala ya mapenzi yao tu, mpaka watu wengine aliokuwa analala nao Erica kwenye chumba walikuwa wakishikwa na wivu ila pale chuo alipata rafiki aliyeitwa Dora na walipatana sana.
Miezi mitatu tangu aanze chuo alienda kumtembelea dada yake Bite, ila leo dada yake alimpa usia mpya kabisa,
“Mdogo wangu, usikubali kulala na mwanaume mpaka uolewe”
Alimuitikia dada yake lakini huo usia alishauvunja kwa kulala na Babuu kwani aliamini ndiye mwanaume ampendaye ukweli.

Alimtambulisha Babuu kwa rafiki yake Dora, baada ya Babuu kuondoka rafiki yake alimuuliza,
“Yule Babuu anjishughulisha na nini?”
“Yupo tu, aliishia kidato cha nne na alishindwa kuendelea na masomo kwahiyo kuna shughuli shughuli anajishughulisha nazo”
“Unajua rafiki yangu unaenda kuwa na shahada, yani mwanaume wa kidato cha nne hakufai tena”
“Una maana gani?”
“Aaah usinifikirie vibaya, ila Babuu hatokufaa tena”
“Mimi nampenda Babuu na ninaamini kuwa yeye ndiye mwanaume bora kwangu”
“Mmmh haya, ila mimi nimesema tu usinifikirie vibaya”
Erica hakupenda huo ushauri maana aliona kwa Babuu amefika na hakutaka mwanaume mwingine zaidi ya Babuu.
Jioni ya siku hiyo kama kawaida Babuu alienda tena kumtembelea Erica kwenye hosteli yao,
“Babuu huchoki kunitembelea, mchana si ulikuwa huku huku?”
“Ndio Erica hivi nawezaje kuchoka kumuona kila muda msichana nimpendae? Sichoki sababu nakupenda na muda mwingi nahitaji kuwa na wewe Erica”
“Naelewa na mimi najisemea tu kiukweli nafurahi sana unavyokuja mara kwa mara kuniona, unafanya niamini kweli Babuu unanipenda”
Walijikuta wanaongea sana hadi usiku kabisa,
“Mmh Erica leo nimechelewa?”
“Umechelewa sana mpenzi, na usafiri saivi haukatishi huku sijui utafanyaje mpenzi?”
“Usijali nitafika tu nyumbani, mbona siku nyingine nafika”
“Lakini huchelewagi kama leo”
“Au niende pale kwenye nyumba ya wageni nikalale”
“Usiniudhi Babuu, sasa kwenye nyumba ya wageni pale ukalale na nani? Bora uende kwenu, mi siafikiani na swala la wewe kwenda kulala nyumba ya wageni vishawishi ni vingi”
Erica alionyesha kuchukizwa kiasi, ikabidi Babuu amuahidi kuwa atarudi kwao kwa njia yoyote ile. Basi akambusu kisha wakaagana na kuanza kuondoka.
Erica alirudi hosteli ila usiku huo ilikuwa ajabu sana maana Babuu hakumtafuta kabisa hata kuwasiliana nae hakuwasiliana nae na kufanya Erica ashangae maana haikuwa kawaida yao, ikabidi amtumie ujumbe ila ujumbe wake haukujibiwa, na alipiga simu ila simu yake haikupokelewa kwa mara ya kwanza Erica alipata maumivu ya mapenzi moyoni mwake maana hakuelewa ni kwanini Babuu hakutaka kupokea simu yake, alimtafuta vilivyo ila Babuu hakupokea simu yake kabisa.
Siku hiyo hata usingizi hakuupata kabisa yani hakuweza kulala sababu ya mawazo, alijikuta akifikiria sana kuwa Babuu kapatwa na majanga gani au kapitia nyumba ya wageni kama alivyosema yani alijikuta akiwa na mawazo lukuki.



 
SEHEMU YA 35


Kesho yake alivyofika chuoni tu, kutokana na mawazo yake alijikuta akigongana na mkaka mmoja kitendo kilichofanya aangushe vitabu vya Yule kaka, ikabidi ainame na kuanza kumuokotea huku akimuomba msamaha,
“Samahani sana”
“Bila samahani, najua ni bahati mbaya tu. Ila ni vizuri tukafahamiana”
“Sawa, naitwa Erica nipo mwaka wa kwanza”
“Sawa, naitwa George nipo mwaka wa tatu. Ni vizuri kufahamiana, na kama hivyo upo mwaka wa kwanza unapata urahisi wa kusaidiwa na mimi. Halafu mimi ni waziri wa michezo”
“Aaaah sawa, nashukuru kukufahamu”
Basi George akamuomba Erica namba ya simu ili wawe wanawasiliana, kisha Erica aliendelea na harakati zake za kuwahi kipindi.
Baada ya kipindi tu alitafutwa na George na kumuita mgahawani waweze kula pamoja na kuongea ongea, Erica alienda kumsikiliza ingawa alikuwa na mawazo sana kipindi hiko kuhusu Babuu.
Alifika mgahawani na kumkuta George yupo mahali pale, na kumuagizia chakula
“Umejuaje napenda chakula hicho?”
“Nimejua tu, unajua kuna vitu tunavyo sisi watoto wa kiume. Yani Mungu katuumba na upeo wa ajabu sana, huwezi jua ila nimejua kwa kukuangalia tu kuwa unapenda chakula gani”
“Mmmh basi wewe ni noma”
Chakula kililetwa na walianza kula huku wakiongea habari za pale chuoni,
:”Chuo unakionaje?”
“Ni kizuri, unajua ndoto zangu ilikuwa ni kusoma chuo hiki kwahiyo kitendo cha ndoto zangu kutimia kwasasa kimenifurahisha sana”
“Na hujapotea, hiki ni chuo bora kati ya vyuo vyote. Na daima hutoa watu bora, ndoto zako za badae ni nini baada ya hapa?”
“Nikimaliza, nitatafuta kazi”
“Kwahiyo unawaza kuajiriwa?”
“Ndio, sasa nitawaza nini zaidi?”
“Ila nyie watoto wa kike hamna tatizo, sisi watoto wa kiume ndio watafutaji wa haswaaa. Mi nikimaliza chuo naenda kuendeleza biashara zangu, kwahiyo kazi itakuwa ni akiba tu, yani labda mshahara wangu wa kwenye kazi ni kumpa mke wangu pesa hizo atumie labda saluni au matumizi yake mengine kwani najua biashara zangu zinalipa sana”
“Kumbe una biashara?”
“Ndio, mimi nasoma huku naendeleza biashara zangu kwahiyo nikimaliza chuo ndio nitazisimamia vizuri zaidi”
“Hongera sana, ni vijana wachache sana wanaofanya hivyo”
“Vijana wanaofanya hivi ni wale wanaofikiria maisha yao ya badae, najua badae nahitaji mke wangu na watoto wasipate tabu kabisa. Nataka kuishi nao maisha ya kifahari”
“Mmmh mkeo atakuwa na raha sana”
“Kawaida tu, lazima mke apate raha na afurahie maisha. Ila ukiwa na shida yoyote Erica usisite kuniambia”
Walicheka na kuongea mengi sana kisha kuagana na kuahidi kuendelea kuwasiliana mara kwa mara.

 
SEHEMU YA 36


Erica alirudi hosteli na siku hiyo alijiandaa na kurudi kwao kumsalimia mama yake maana alimkumbuka tayari na ukizingatia ilikuwa ni mwisho wa wiki, alifika na kumsalimia mama yake kisha kuongea nae mawili matatu.
“Umemuona rafiki yako Johari?”
“Sijamuona”
“Kachakaa jamani, yani kachakaa vilivyo. Unajua nyinyi mabinti mnajiingizaga kwenye mambo mengine bila ya kufikiria kwa makini, haya sasa huyo mwalimu ni anampa nini zaidi ya kumuongezea mikosi tu”
“Jamani mama kwanini unasema hivyo?”
“Unajua Yule mwalimu alifukuzwa kazi sababu hakuonyesha maadili mazuri shuleni pale, hana kazi nyingine wala biashara yani yupo yupo tu. Rafiki yako Johari kajidumbukiza haswaa na atajutia maisha yake yote. Unajua unapoamua kuwa na mwanaume angalia mwanaume mwenye faida na wewe, kwanza kabisa awe msomi, ajue kutafuta pesa, asitegemee kazi tu maana kuna leo na kesho akifukuzwa kazi, ujasiliamali utawawezesha ila wanaume ambao wapo wapo tu sio wanaume wa kupoteza nao muda kwakweli. Mwanangu kuwa makini, chagua mwanaume sahihi katika maisha yako, ukipata mwanaume wa kukuoa uangalie vigezo hivyo nilivyosema”
Erica aliongea ongea na mama yake pale ila badae alipokaa na kujifikiria aliona kuwa sifa anazozisema mama yake basi zote zipo kwa George,
“Mmmh ndio kusema George anafaa kuwa mume wangu jamani!”
Aliwaza sana, na upande mwingine akamfikiria Babuu,
“Mmmh kuna Babuu, tulipendana sana ila mbona hanitafuti tena hewani? Ila Babuu hana sifa anazozisema mama, sio msomi kama mimi nitakavyokuwa na shughuli zake hazieleweki kabisa, ila George yupo sawa, halafu nahisi ananipenda na atanitongoza tu”
Alijikuta akimlinganisha George na Babuu ila hakuelewa atafanyaje fanyaje maana bado alikuwa akimpenda Babuu ila aliona kuwa George ndio mwanaume anayemfaa kwani ana sifa zote zilizotajwa na mama yake.

 
SEHEMU YA 37


Erica alienda tena chuoni ila aliendelea kuwasiliana na George, sema tu toka siku ile hakuweza kumpata Babuu hewani kabisa na kumfanya kuhisi kuwa Babuu ana msichana mwingine ila kwavile alimpata George kuwasiliana nae aliona faraja kiasi.
Na siku hiyo George aliomba kuonana nae kwenye vimbweta vya pale chuoni, na alikutana nae na kuzungumza,
“Hivi Erica una mpenzi?”
Erica akacheka na kujibu,
“Hapana, sina mpenzi”
“Oooh Mungu ni mwema kunikutanisha na wewe”
Wakati anaongea na George pale, aliangalia pembeni gafla akamuona Babuu akiwa na nguo zile zile ambazo alivaa siku ile usiku na alionekana akimtafuta yeye mwenyewe.


Wakati anaongea na George pale, aliangalia pembeni gafla akamuona Babuu akiwa na nguo zile zile ambazo alivaa siku ile usiku na alionekana akimtafuta yeye mwenyewe.
Erica aliona Babuu atamuharibia hapo, ikabidi aombe udhuru kidogo kwa George kisha akaondoka zake na kwenda sehemu nyingine kwani hakutaka kabisa kuonana na Babuu.
Kwa bahati nzuri Babuu alikutana na Dora na kumsalimia kisha kumuuliza kuhusu alipo Erica,
“Mmmh hata sijui, sijaonana nae leo. Kwanini usimpigie simu yake?”
“Simu yangu imezimika”
“Na mbona upo hivyo una tatizo gani?”
“Nilipata matatizo, niliwekwa selo na nimetoka leo. Moja kwa moja nimekuja hapa ili nionane tu na Erica halafu niende kwetu”
“Pole kwa matatizo, ila na wewe ulishindwa kwenda kwanza kwenu ndio uje huku kumtafuta Erica?”
Babuu alijiangalia na kweli akajiona kuwa ni mchafu mchafu, kwa aibu akaamua kumuaga Dora na kuondoka zake. Dora alimuangalia Babuu na kumsikitikia,
“Kijana mzuri ila tatizo hajasoma. Mmmh! Pole yake”
Kisha akaondoka zake na kuelekea hosteli ya kwa kina Erica.

 
SEHEMU YA 38


Alimkuta Erica amejiinamia tu nje ya hosteli yao,
“Vipi Erica?”
“Safi tu”
“Umemuona Babuu?”
“Sitaki hata kumuona huyo mtu”
“Bora usitake kumuona, yani kaja mchafu huyo balaa, eti anasema aliwekwa selo”
“Selo?”
“Ndio, alikuwa rumande nadhani alikamatwa na polisi. Ndio mwanaume wa kuwa naye huyo loh hapana jamani, sio saizi yako kabisa, hakufai”
Mara simu ya Erica ilianza kuita alipoiangalia alikuwa ni George anapiga, akapokea
“Erica mbona hukurudi tena au nilikuwa nakuboa na maswali yangu?”
“Hapana George, tumbo liliniuma gafla nikarudi hosteli”
“Aaah pole sana, naomba nielekeze hosteli uliyopo nije”
Basi ikabidi Erica amuelekeze George alipo kisha akakata simu, ila alitaka kumdanganya Dora ambapo Dora alimshtukia kabla hajamdanganya,
“Mmmh usinidanganye Erica, nimeona sura yako unataka kunidanganya, bora uniambie ukweli tu. Ni nani huyo ulikuwa unazungumza nae?”
“Humjui”
“Nimekusikia unamuelekeza hapa hosteli, nasubiri nimuone nimjue”
“Mmmh na wewe Dora loh!”
“Nini sasa kwani vibaya? Mimi na wewe tumeanza kufichana Erica?”
“Hapana, basi utamuona”
Wakaendelea na maongezi mengine, na baada ya muda mfupi George alifika pale walipo Erica na Dora, ikabidi Erica amtambulishe kwa Dora kuwa ni rafiki yake,
“Na huyu ni kaka yangu anaitwa George”
“Mmmh Erica! Kaka yako!”
“Mmmh wewe nae Dora jamani, karibu George”
George alikuwa akicheka tu kwa kuwasikiliza wale mabinti wawili, kisha baada ya muda kidogo Dora aliaga na kuondoka zake kwani alijua anatakiwa kuwapa nafasi ya kuongea hawa wawili.
Alipoondoka tu, George alimuomba Erica kuwa ampeleke hospitali,
“Hapana George nimeshapona”
“Najali afya yako Erica jamani”
“Usijali nimeshapona”
“Sawa, kuna jambo napenda kukuomba”
“Jambo gani hilo?”
“Napenda kuanzia sasa mimi na wewe tusiwe marafiki tu bali tuwe wapenzi na badae uje kuwa mke wangu”
Erica alikaa kimya kidogo kwani neno hili alikuwa akilitamani muda sana, ila hakuweza kujibu kwa muda huo huo sababu ya aibu.
George akamwambia tena,
“Naomba nikuachie muda utafakali swala hilo kwani najua ni gafla tu nimekwambia, Erica tutawasiliana badae”
Basi George alimuacha Erica na kuondoka zake, ila angejua ukweli kuwa Erica alishamkubali toka kitambo tu na alikuwa akingoja kauli tu kuwa anampenda ila pale pale alishindwa kumjibu.
 
SEHEMU YA 39


Usiku wa siku hiyo alikuwa akiona simu yake ikipigwa na Babuu ila hakupokea kabisa, yani Babuu alipiga na kupiga ila Erica hakupokea badala yake muda huo alikuwa akiwasiliana na George kwa njia ya ujumbe kuwa amekubali kuwa mpenzi wake, kwahiyo kwenye moyo wake alianza kumuweka George na vile alihisi kuwa Babuu ni msaliti hakumtaka tena kuonana na Babuu wala kuwa na Babuu. Basi wakaahidiana na George kuonana kesho yake ili kuongea vizuri zaidi.
Na kweli kesho yake wakaonana na kuongea mengi zaidi, George alitaka kupima uaminifu wa Erica na kumuomba simu yake kidogo,
“Naomba simu yako kidogo, nikae nayo tukiwa tunazungumza”
“Mmmh kwanini?”
“Niangalie tu picha zilizopo, na wewe shika ya kwangu”
George akampa Erica simu yake naye Erica akampa George simu yake ila kimoyomoyo alishukuru sababu alikuwa amefuta picha zote alizowahi kupiga na Babuu pale tu alipoumia moyo na kuhisi kuwa Babuu anamsaliti kwahiyo hakukuwa na chochote cha Babuu.
Wakati George ameshika ile simu ya Erica akiangalia angalia picha zilizomo mara uliingia ujumbe kwenye simu ile, na ilionekana umetoka kwa Babuu, George akaufungua ule ujumbe na kuusoma;
“Erica mpenzi wangu, nakupigia simu ila hupokei sijui tatizo ni nini. Lakini mwenzio nilipatwa na matatizo, siku ile nilipokuwa natoka kuonana na wewe, nilikamatwa na polisi kwa uzurulaji. Basi niliwekwa rumande hadi walipokuja kunitoa, ila niligoma kwenda nyumbani hadi nikaja chuoni kwenu ila sikukukuta. Nielewe Erica, usinifikirie vibaya bado nakupenda sana”
George alisoma mara mbili mbili ule ujumbe, kisha aliufuta kabisa na kumuangalia Erica kisha akamuuliza tena,
“Ni kweli Erica hujawahi kuwa na mpenzi kabla yangu?”
Erica alikaa kimya kidogo ila akona ni vyema amwambie ukweli maana ipo siku Babuu atatokea halafu atashindwa kujieleza,
“Ngoja nikwambie ukweli, nilikuwa na mpenzi wa kuitwa Babuu ila alinisaliti na kwenda kuwa na wengine nikaamua kuachana nae”
“Je huyo Babuu hukufanya nae chochote?”
Erica alijifikiria sana kuhusu hilo, ila ikabidi ajibu kuwa hajawahi kufanya chochote na Babuu. George aliposikia vile alifurahi sana, na kuinuka kisha akamkumbatia Erica na kumwambia,
“Nakuomba unipende mimi tu, achana na mawazo ya Babuu huyo kabisa. Na ninakuomba kitu kimoja, futa namba zake kwenye simu yako”
Erica alichukua simu yake na kufanya hivyo na kuzidi kumfurahisha zaidi George kiasi ya kwamba George alimuahidi kumpenda mpaka mwisho wa maisha yake.
Ingawa Erica alifuta namba zote za Babuu kwenye simu yake ila ni wazi kuwa George hakuridhika kwani kesho yake alikuja na laini mpya na kumpa Erica kuwa atumie laini hiyo na aivunje ile ya zamani, kwahiyo alichokifanya Erica ni kukopi majina tu kisha kutaarifu ndugu zake wa karibu kuwa kabadilisha namba ya simu. Hakuona kama ni tatizo kufanya vile sababu alishamuingiza George moyoni mwake na aliamini kuwa ndiye mume wake wa badae.

 
SEHEMU YA 40


Erica alionekana kuwa na furaha sana, hata alipoenda chuo rafiki yake aliweza kugundua furaha yake,
“Niambie ukweli Erica”
“Mmmh sijui nikwambie”
“Niambie bhana”
“Yule George kuanzia sasa ni shemeji yako”
“Mmmh nilihisi tu, ila anakufaa sana Yule”
“Kwanini?”
“Ni mrefu, mtanashati, msomi kwakweli ndio mwanaume anayekufaa ila sio wakina Babuu”
“Hahaha achana na habari za huyo Babuu sitaki hata kumuona kwasasa”
“Kwanini?”
“Msaliti Yule, aliondoka akaenda kulala guest”
“Ila una uhakika gani kama amekusaliti?”
“Nahisi tu ni msaliti bhana, tuongelee habari za George maana nampenda haswaaa”
“Hata kwa Babuu ulisema hivyo hivyo”
“Mmmh Dora jamani, ngoja nikuulize kitu hivi mapenzi ni nini?”
“Mapenzi ni kupendana”
“Yani kupendana kiaje?”
“Mapenzi ni kumpenda na yeye akupende”
“Kama mimi na George”
Dora alicheka tu na kugundua kuwa ni penzi jipya ndiomana linauliziwa sana, muda kidogo George alimpigia simu na kuhitaji kwenda nae kwenye chakula cha mchana.

 
Back
Top Bottom