Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 135


Alipokuwa kwao alifikiria sana, na kuanza kuhisi huenda maneno aliyoyasema Fetty yana ukweli kuwa huenda Derick ndio amesambaza habari mbaya kuhusu yeye,
“Itakuwa ni Derick tu maana ndio aliyeshuhudia wale vijana waliotaka kunibaka, jamani kwanini ananifanyia hivi wakati ni ndugu yangu! Na habari kubwa anayotaka kueneza kuhusu mimi ni ipi?”
Akawaza sana na kusema,
“Mungu wangu, asije akaeneza kuwa nimetoa mimba, jamani nitaweka wapi sura yangu mimi Erica? Najuta kumfahamu huyu mtu, ni kwanini nimempata ndugu wa aina hii?”
Aliwaza sana, na kusema kuwa kesho yake ataenda kumtafuta Derick ili aongee nae na aache kumfanyia vitu vya ajabu kiasi hiko kama kumsambazia vitu vya uongo, kiukweli Erica hakuwa na raha kabisa na alijiona akikosa amani moyoni mwake kila siku maana ni kama liliibuka jipya kila siku, usiku ulifika na mama yake alimuuliza kuwa imekuwaje amerudi tena kutoka chuoni, alisema uongo wake wa kumkumbuka ila kiukweli chuo kile kilianza kumchosha kwa kipindi hiko.
Kesho yake alienda chuoni na alimtafuta Derick hewani ili aonane nae, na kweli Derick alikubali kuonana nae na kwenda kuongea nae,
“Derick kwanini lakini umeamua kunifanyia hivi? Kweli kabisa wewe ni wa kueleza habari mbaya kunihusu mimi?”
“Habari gani Erica?”
“Wewe umewaambia watu kuwa mimi nilibakwa na wanaume wane sijui, jamani Derick, unajua fika kuwa sikubakwa, kweli ni wa kunisambazia habari za hivyo?”
“Erica, kwani habari hizo ni za uongo”
“Ndio ni uongo, kwani wewe hukuona kama sikubakwa?”
“Kama hukubakwa mbona ulikubali twende kupima mimba na magonjwa ya zinaa? Erica, unaweza kumdanganya mtoto ila sio mimi, na kila leo unajiliza liza, hata hivyo habari hizo zilizagaa kipindi kile kile hata sijagundua kuwa wewe ni ndugu yangu”
“Sasa umepata faida gani kwa mfano kunisema hivyo? Unataka watu wanichukie eeh! Unajua wewe ni muuwaji?”
“Hivi uuwaji wangu mimi unaweza kufikia uuwaji wako wa kutoa mimba? Nyie kwenu ni wauaji ndiomana mamako hakunitaka”
“Hivi wewe Derick unaongea au unaropoka? Jamani siku ile da Mage si amesema maneno ambayo mimi na wewe hatukuyajua kabisa, kwanza kumbuka ulilala na mimi bila ridhaa yangu, halafu unataka nionekane malaya, hivi ukoje Derick, wewe ni mtoto wa baba kweli? Labda baba alisingiziwa tu”
Derick akacheka kwa kejeli na kusema,
“Mamako hajanipa haki zangu sababu naye akikazania kuwa mimi ni mtoto wa kusingiziwa, sikia nikwambie Erica, siku niliyogundua kuwa wewe ni ndugu yangu nimekuchukia balaa. Katika watoto wa baba nampenda dada Mage tu sababu amekuwa name bega kwa bega maisha yote, hivi wewe ulishindwa kuzaa hadi kwenda kutoa ile mimba kama sio mchezo wako? Hata kama nilifanya mapenzi nawe kwa bahati mbaya ila si ungezaa tu na tungeendelea kufanya iwe siri maana kama mapenzi tumefanya kweli”
“Basi yaishe, tushakuwa ndugu sasa naomba yaishe. Niheshimu kama dada yako”
“Nitaanza kukuheshimu pale tu nitakaposema kuwa ulitoa mimba na watu wote wajue rangi yako halisi, maana unaonekana binti mpole kumbe hakuna lolote”
Erica alihisi kuchanganyikiwa kabisa maana huyu ndugu yake hakumuelewa hata kidogo aliona akimchanganya tu akili hata akajiuliza kuwa baba yao alianzaje kuzaa nje mtoto wa aina ile asiyekuwa na akili ya utu hata kidogo.
“Hivi Derick, undugu wa wewe na mimi uko wapi? Hivi unajua kuwa mimi ni dada yako?”
“Tena nitasambaza kuwa huna aibu umelala na kaka yako hadi ukapata mimba na mimba hiyo ukaenda kutoa, yani Erica utapata sifa chafu sana kutoka kwangu. Unafikiri maisha niliyoishi mimi niliyafurahia? Mama yangu alipata shida sana sababu ya mama yako na tena alisema baba alikataa nisilelewe pale sababu mkewe alikuwa na mtoto mdogo, umefanya nikose upendo wa baba, halafu unajishauwa nini? Nataka upate uchungu nilioupata mimi wa kuishi bila upendo wa baba”
“Derick unadhani utapata faida gani kufanya hivyo? Au maisha uliyoishi wewe kutaka wengine wayaishi kutakufaidisha nini? Sasa mimi nahusika vipi na kuteseka kwako? Wakulaumiwa sio mimi ni baba”
“Sikia Erica, mimi nimeteseka sana sababu sijawahi kupata upendo wa baba, kila mwanaume aliyetaka kumuoa mama yangu haikuwezekana sababu mama ana mtoto ambaye ni mimi, baba amemfanya mama yangu asifurahie kama kuna kitu kinaitwa ndoa maishani mwake, nimeteseka sana mimi, na wewe ukaenda kutoa mimba kama ambavyo baba alitaka mimba yangu itolewe”
“Sasa ulitaka nizae mtoto wa laana, tena bora hata mimba yako ingetolewa tusingeletewa machizi kama wewe duniani”
“Mimi chizi eeeh! Subiri, uchizi wangu utauona vizuri, hiki chuo kitakuwa kichungu sana kwako”
Erica alimshangaa sana huyu Derick yani hakumuelewa kabisa, Yule Derick akaondoka zake kisha Erica nae akaondoka zake na kurudi hosteli huku akiwa na mawazo mengi sana maana akili yake alihisi ikiruka kabisa.

 
SEHEMU YA 136

Alifika hosteli na kukaa kwenye kitanda chake huku akiwa na mawazo mengi sana akachukua simu yake na kuiwasha ambapo alikutana na ujumbe toka kwa Rahim,
“Mbona kimya mpenzi? Kwani una tatizo gani? Nieleze”
Ilibidi aanze kumjibu kuwa hana tatizo ila kiukweli alihisi moyo wake kuuma sana, na alijihisi kuwa na matatizo mengi sana ila hakuweza kuyaweka wazi.
Akapokea na ujumbe mwingine toka kwa Tumaini,
“Kesho nitakuja hosteli hapo, nina shida nyingine na wewe”
Aliisoma bila ya kujibu maana akili yake ilikuwa imevurugwa kabisa, muda huo Bahati nae alikuwa akimpigia, akaamua kupokea,
“Erica, hupokei simu zangu siku hizi, kwani una tatizo gani mpenzi?”
“Sina tatizo”
“Erica, nakuhisi tu kuwa hauko sawa mpenzi wangu”
“Nipo sawa”
Erica alivyoona maswali mengi sana akaamua kukata ile simu ya Bahati na hata alipompigia tena hakupokea kabisa.
Muda kidogo akaona ujumbe toka kwa Erick,
“Ndio mumeo alikukataza nini kuchat na mimi maana toka siku ile kimya?”
“Sio hivyo Erick”
“Naomba nikuulize kitu”
“Niulize tu”
“Je dada yangu amejua chochote kuhusu mimi na wewe? Je amejuwa kama tulishawahi kuwa na mahusiano”
“Hapana, ila tu nilimwambia kuwa nakupenda”
“Sitaki ajue Erica maana atakuchukia sana, na sitaki dada yangu akuchukie. Ameniambia kuwa kuna kitu ataniambia kuhusu wewe, ndiomana nilitaka kujua kama umemwambia chochote”
Erica akawaza kwanza kuwa ni kitu gani Tumaini anataka kumwambia Erick, alihisi tumbo kumsokota na kuamua kwenda kwanza chooni.
Alitoka chooni na kumtumia tena ujumbe Erick,
“Ni vitu gani hivyo anavyotaka kukwambia?”
“Sijui ila kaniambia vinakuhusu wewe”
Erica alishindwa hata kuendelea kuwasiliana na kuamua tu kulala huku akisubiri kesho kitajiri kitu gani.
 
SEHEMU YA 137

Kulipokucha alijiandaa kwaajili ya kwenda chuo kwanza alishasahau kama Tumaini alisema kuwa ataenda kuonana nae, yeye kwenye mida ya saa nne akaenda zake chuo, wakati akipita maeneo ambayo wanachuo walikaa vikundi vikundi aliweza kuhisi ni jinsi gani wanamsema maana walionekana kumuangalia sana hadi akajishtukia yani kamavile ni mtu aliyetenda mambo ya ajabu kweli katika jamii, aliingia kwenye kipindi, ingawa hakuwa na marafiki ila aliona ni jinsi gani watu walivyomkwepa, alihisi kutakuwa na habari mbaya zaidi zimesambazwa kuhusu yeye, alijisikia vibaya sana.
Kipindi kilipoisha alirudi hosteli, na moja kwa moja alienda kitandani kwake na kujilaza, ila hakulala usingizi, alijifunika shuka tu na huku akilia, alijisikia vibaya sana watu kuonekana dhahiri wanamnyanyapaa utafikiri ni kitu gani kipo kwake.
Wakati amejilaza, alifika Fetty chumbani kwake na kumuita,
“Erica, kuna mgeni wako nje”
Erica alijifuta machozi yake vizuri ndani ya shuka kisha kushuka kitandani kuongozana na Fetty,
“Ni mgeni gani huyo?”
“Utamuona tu, pole Erica naona ulikuwa unalia. Najaribu kuyahisi maumivu yako pole sana, kwakweli habari zinazoenea kuhusu wewe si nzuri kabisa”
“Habari gani nyingine?”
“Inasemekana Erica una ukimwi”
Kwakweli Erica alihisi moyo wake ukijaa machozi ila hakutaka kujionyesha kwa Fetty kama zile habari zimemuumiza kiasi gani, alifika kwa aliyekuwa mgeni wake akamtazama alikuwa ni Bahati.
Kwakuwa Erica alikuwa na maumivu sana moyoni mwake, alimsogelea Bahati na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka. Mara gafla alisikia mtu akipiga makofi, kumuangalia mtu Yule alikuwa ni Tumaini akamwambia,
“Nimekupiga na picha Erica, namtumia Erick sasa hivi”
Erica alikuwa ameduwaa tu huku macho yake yakiwa yamejaa machozi.
 
SEHEMU YA 138



Kwakweli Erica alihisi moyo wake ukijaa machozi ila hakutaka kujionyesha kwa Fetty kama zile habari zimemuumiza kiasi gani, alifika kwa aliyekuwa mgeni wake akamtazama alikuwa ni Bahati.
Kwakuwa Erica alikuwa na maumivu sana moyoni mwake, alimsogelea Bahati na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka. Mara gafla alisikia mtu akipiga makofi, kumuangalia mtu Yule alikuwa ni Tumaini akamwambia,
“Nimekupiga na picha Erica, namtumia Erick sasa hivi”
Erica alikuwa ameduwaa tu huku macho yake yakiwa yamejaa machozi.
Ila Tumaini aliendelea kuongea,
“Usijilize Erica, ujinga wako wote leo unafika sehemu husika”
Bahati hakupendezewa na kitendo cha kumuona Erica akiwa amejawa machozi kiasi kile, alimshika mkono na kwenda nae barabarani kisha akakodi bajaji na kwenda nae ufukweni kwani alijua jinsi gani Erica aliyapenda maeneo ya ufukweni, na hata hivyo alijua tu Erica hayupo sawa kwa wakati huo.
Walifika na kukaa kwenye michanga, ni kweli Erica hakuwa sawa kabisa, Bahati alimuuliza,
“Nini tatizo Erica?”
“Najiona kama sina faida tena hapa duniani, sina thamani ya kuishi”
“Kivipi ukose thamani Erica?”
“Sipendwi tena, watu wote hawanipendi kwa maneno ya uongo. Natamani hata kufa”
“Erica jamani usiseme hivyo, siku zote jua kuna Bahati wako anakupenda sana hata iweje. Kwanza ni maneno gani waliyokutangazia?”
“Wamezusha eti mimi nilibakwa yani habari imeenea chuo kizima na wamesema kuwa mimi nina ukimwi, kwakweli sina raha mimi bora hata nife”
“Erica usinichekeshe yani utamani kufa sababu ya habari hizo, wamesema umebakwa, hayo ni maneno tu hata kama kweli ulibakwa ndio nini sasa? Wanasema una ukimwi, kwani unao kweli? Hata kama unao kwani utawaambukiza wao? Utaniambukiza mimi, yani maneno kama hayo ningekuwa ningeambiwa mimi ningewashushua kwakweli, Erica ngoja nikwambie kitu, wewe hata uwe malaya dunia nzima wakufahamu sababu ya umalaya ila mimi sikuachi. Wewe hata uwe na ukimwi na vipimo vyote vionyeshe kuwa una ukimwi, mimi sikuachi. Nakupenda Erica, na ninakupenda kweli yani kupita yeyote Yule aliyewahi kukwambia kuwa anakupenda”
Erica alimuangalia Bahati na kumshangaa kwakweli maana alikuwa anaongea maneno kama mfu, yani alishangaa kuwa Bahati ni mwanaume wa aina gani ambaye hakati tamaa kwake, yani yeye anamuimbia wimbo wa nakupenda kila siku.
Bahati alimshauri Erica asirudi hosteli bali aende kwao akapunguze mawazo,
“Ila nataka kuchukua na nguo zangu hosteli”
“Inamaana kwamba hutaki tena kukaa hosteli?”
“Sitaki ndio, bora nikae nyumbani, hata kile chuo chenyewe sikitaki natamani hata kuhama”
“Hivi inawezekana kuhama chuo?”
“Nitaenda kuulizia, kwakweli Bahati nahitaji akili yangu ipumzike. Najua nimebakiza mwaka mmoja ila sitaki kumalizia pale chuoni, bora nihame”
“kama inawezekana, sina pingamizi mimi. Ilimradi wewe ukiridhika basi na mimi nimeridhika”
Akakubaliana nae arudi kwanza hosteli akachukue nguo zake, na alirudi hosteli kwenye mida ya saa moja jioni, Bahati alibaki kwenye bajaji akimsubiria, siku hiyo Bahati alikuwa na hela kwahiyo haikuwa shida kwa yeye kukodi bajaji.
 
SEHEMU YA 139

Erica aliingia hosteli na moja kwa moja alienda kwenye chumba alichokuwa analala, na kubeba nguo zake huku zingine akiziweka kwenye mkoba, ilibidi wenzie wa kwenye chumba hicho wamuulize,
“Vipi Erica mbona unabeba nguo zote, unahama?”
“Mmmh hapana, nitarudi tu. Nataka nikabadilishe baadhi ya nguo”
Akawaaga pale na kutoka, alikutana na Fetty nje ambaye alimuuliza pia,
“Vipi Erica unahama?”
“Nataka nikapumzike kidogo nyumbani”
“Ila Erica hata mimi kama ningekuwa wewe kweli tena ningeenda kupumzika, jamani yani wanaume wengine sio wa kutembea nao kabisa, lete begi nikusaidie”
Erica alimpa begi lake ambapo Fetty alimsaidia kubeba huku wakielekea nje, na Fetty akiendelea kuongea,
“Yani Derick shetani kabisa Yule, unajua amesema eti umetoa mimba”
“Nimetoa mimba!”
“Ndio, kasema umetoa mimba jamani Derick anakuchafulia sifa zako balaa, ila shoga yangu siku nialike tukutane na Derick yani siku hiyo nitamchamba sitamuacha chochote yani mwanaume mzima hovyo. Naomba namba yako Erica”
Ikabidi Erica ampatie huyu Fetty namba yake, kisha akafika kwenye bajaji na kuagana nae ambapo Erica alipandisha mabegi yake na kuondoka na Bahati.
Alifika kwao kwenye mida ya saa tatu usiku, na kumfanya mamake ashangae sana alipoenda na mabegi, kwa wakati huo alikuwa ameshaagana na Bahati.
“Kheee vipi wewe na mabegi?”
“Nimechoka kukaa hosteli mama”
“Sasa utaweza kutoka huku nyumbani kila siku kwenda chuo?”
“Nitaweza mama”
“Kwani tatizo ni nini Erica mbona unaonekana huna raha mwanangu?”
Erica alishindwa kujizuia kwa mama yake na kuangusha machozi, ilibidi mama yake ambembeleze na kumuuliza kwa makini, Erica aliamua kumueleza mama yake baadhi ya maneno yanayomliza huku yale ya ukweli akiyaficha,
“Mama, hivi Yule Derick kwanini alikuwa mtoto wa baba?”
“Kafanyaje kwani?”
“Analalamika kuwa mimi ndiye nilimfanya akose upendo wa baba sababu hata nyumbani mligoma kumuhudumia sababu nilikuwepo mimi”
“Kwani nani amekukutanisha na huyo mwanaharamu?”
“Dada Mage ndio kanifahamisha kuwa Yule ni mtoto wa baba”
“Aaah Mage nae, hanaga akili Yule ndiomana akaolewa na choka mbaya. Sasa huyo Derick ndio anakuumiza kichwa hadi unalia mwanangu?”
“Silii sababu ya Derick ila ninalia sababu ya maneno ya uongo aliyoeneza juu yangu eti nipate uchungu kama alioupata yeye kwa kukosa upendo wa baba”
“Maneno gani hayo?”
“Derick katangaza chuo kizima, na habari zimeenea kote sababu mimi sio muongeaji, eti ametangaza kuwa mimi nilibakwa na nina ukimwi”
“Kheee mtoto ana wazimu huyo eeh! Ukimwi aache kuupata mama yake kwa umalaya wake, uje uupate wewe”
“Yani mama chuo kizima wananinyanyapaa”
“Unajua wanaume nao mara nyingine sijui akili zao zipo kwenye makalio yani hata hawajifikiriagi, unamsaliti mkeo unaenda kuzaa na mwanamke mwingine basi msaliti na mwanamke mwenye akili timamu, unaenda kumsaliti na chizi na unazaa nae, yani baba yenu sijui alikuwa na akili gani, Yule mwanamke hana akili hata kidogo ndiomana nilimtimua hapa na vitoto vyake, mwanamke ni tahira Yule. Nyumba yangu mwenyewe halafu anakuja na mitoto yake hana hata aibu, Yule mwanamke ni malaya wa kutupwa., halafu anajifanya kama yeye ni mke kwenye familia hii yani atoe amri anavyojisikia, nikasema sitaki kuona uchafu wake wala watoto wake. Sikufanya kosa kuwatimua kwakweli, ona shetani alilolikuza sasa, hivi ndio linatumika kuharibu furaha ya mtoto wangu! Nyamaza Erica wangu, mama yako najua mwanangu hujawahi kubakwa na huna ukimwi, maneno ya hao watu yasikuumize”
“Mama hujui tu, chuo chote wananinyooshea vidole, halafu kanizushia kuwa nilitoa mimba”
“Hivi anataka nini huyo mtoto jamani! Kwanini kukuzushia habari za kijinga namna hii. Baba Mage, unaona ujinga uliofanya kwenda kuzaa na matahira, mwanetu anadhalilika sasa bila sababu, Erica naomba kesho nikakutane na huyo Derick, mbwa mkubwa huyo”
Erica akaona mama yake akienda kukutana na Derick itakuwa soo kubwa zaidi, akamuomba jambo moja mama yake,
“Mama, usiende ila mimi nataka kuhama chuo”
“Umebakiza mwaka mmoja tu mwanangu”
“Ndio huo mmoja nataka nikamalizie kwenye chuo kingine”
“Yani yote haya kayataka babako, yani wanaume hawaelewagi tu kama mwanamke unayezaa nae inabidi umtambue uelewa wake mapema sana, sio kila mwanamke ni wa kuzaa nae, ndio mwisho wa siku kuzaa na matahira kama hao. Yani hilo litoto litakuwa na akili za mama yake na labda limeambiwa lifanye visasi, unafikiri babako angezaa na mwanamke makini ningegoma kulea mtoto? Hata kama kwetu hawakutaka ila nisingegoma kulea, ila siwezi kulea toto la mwanamke tahira kama mama yake Derick. Siku ukimuona huyo mama utagundua maneno yangu, huyo mama hajisomi yani yupo yupo tu. Ila mwanangu, kuhama kunataka pesa hiyo pesa nitatoa wapi kwa kipindi hiki?”
Erica akafikiria akaona ni kweli kuhama kunahitaji pesa, ila aliamua kwenda chumbani tu kujifikiria vizuri zaidi.

 
SEHEMU YA 140


Alienda kuoga na kurudi kulala maana siku hiyo kichwa chake kilikuwa kibovu sana na alifikiria mambo mengi sana, aliwaza kuwa afanye kitu gani kwa muda huo, akapata wazo la kuongea na dada yake ampe namba za mama yake Derick ili akazungumze na mama yake Derick kwani hata kuhama chuo bado isingekuwa suluhisho kwake ikiwa bado kuna sifa mbaya kuhusu yeye zitazungumzwa, akawaza pia pesa ya kuhama chuo ataipata wapi maana aliwaza vitu vingi sana ambavyo vitamuingia gharama ikiwa pia ni kujaribu kuhonga ili apate nafasi ya kuhamia chuo kingine, aliwaza sana.
Alichukua simu yake na kumpigia dada yake,
“Samahani dada Mage, nilikuwa naomba namba ya mama yake Derick”
“Si ungemuomba Derick!”
“Jamani dada, ukiona hivyo nina shida nayo, nataka kumshtukiza tu Derick”
“Sawa, nakutumia basi”
Kisha Mage akakata simu na kumtumia Erica namba ile, Erica alifurahi sana kuipata huku akiwaza kama akimpigia huyo mama atakubali kukutana nae? Hakutaka kufikiria sana, akaamua kumpigia tu, kisha mama Derick akapokea na kumsalimia, kisha aliulizwa kuwa ni nani,
“Mimi ni rafiki wa Derick mama, nina shida na wewe sijui naweza kuja nyumbani kesho kuonana nawe?”
“Unaonekana ni binti mpole sana, karibu nyumbani”
“Basi nielekeze mama, ila sitaki Derick ajue kama nakuja”
“Hakuna shida mwanangu”
Kisha Yule mama alimuelekeza Erica anapoishi na Erica alimuahidi kwenda kesho, baada ya hapo akakata simu na kufurahi sana kwani shida yake kwa muda huo ni kuonana na huyo mama yake Derick na kuongea nae maana hakuelewa kabisa kwanini Derick anafanya vile.
Alipokuwa anataka tu kulala aliamua kuingia kwenye mtandao kidogo ili kuangalia kama kuna chochote kipya kinaendelea, muda huo huo akapokea ujumbe toka kwa Rahim,
“Mpenzi kimya sana, tatizo nini au una shida gani?”
Erica akafikiria ila akaona ni vyema amwambie Rahim kuhusu swala lake la kuhama chuo,
“Yani Rahim nina mawazo sana, chuo ninachosoma kinanipa kero. Wanafunzi hawanipendi sababu tu sina urafiki nao, wananitangazia mambo mabaya hadi sina furaha”
“Jamani mpenzi wangu pole, ila kama sehemu haikupi furaha si uhame tu!”
“Natamani kuhama kweli ila tatizo pesa maana najua itakuwa gharama sana”
“Erica mpenzi wangu, unajua mimi nipo kwaajili yako na nimekwambia kuwa ukiwa na shida yoyote usisite kuniambia, kweli kitu kama hicho ni cha kukupa mawazo mpenzi wangu? Sikia, wiki hii nitakutumia pesa, natumai itakutosha katika shughuli za kuhama. Kwani ada anakulipiaga nani au ni mkopo?”
“Sina mkopo, ada analipaga mjomba na hela za matumizi nazo ananipaga”
“Sawa, na umebakiza miaka mingapi kumaliza? Je ada ni shilingi ngapi?”
“Ni mwaka mmoja tu, ada ni milioni moja. Najua ada mjomba atanilipia ila swala la kuhama chuo hawezi kunishughulikia”
“Je wewe mwenyewe utaweza kujishughulikia uhamisho?”
“Nitaweza Rahim, nimechoshwa na masimango”
“Basi usijali mpenzi, aiki hii nitakutumia hela itakayokusaidia mambo ya uhamisho na matumizi kidogo”
“Nashukuru sana”
Kwakweli Erica alishangazwa sana na Rahim maana kwake kutoa pesa hakukuwa tatizo hata kidogo, alijisemea mwenyewe tu
“Jamani huyu mwanaume ananipenda hadi naogopa, nikimwambia mama kuhusu huyu mwanaume ni atamkubali asilimia mia moja ila nitawezaje kumuacha Bahati maana ni king’ang’anizi hakuna mfano, nitapata tu njia ya kumuepuka Bahati ila kwasasa nijitunze kwaajili ya Rahim natumai yeye ndio atakuwa mume wangu”
Aliagana na Rahim pale kwa njia ya ujumbe na kulala zake, huku akiwa na tabasamu zito usoni.
 
SEHEMU YA 141


Kesho yake alijiandaa kama alivyopanga kuonana na mama yake Derick, aliwasaliana nae kisha kuondoka kwao mpaka sehemu aliyoelekezwa akawasiliana nae tena na kufika hadi nyumbani kwakina Derick na kukutana na huyo mamake Derick na kumsalimia kisha Yule mama akamkaribisha vizuri sana na kwenda kukaa nae ndani.
“Karibu sana binti yangu, natumaini wewe ni mchumba wa mwanangu”
Erica akacheka tu kisha akamwambia,
“Hapana mama, ila mimi nasoma na Derick naitwa Erica ni mtoto wa mzee Joseph ambaye pia ni baba wa Derick”
“Kheee kumbe mtoto wa Jose!! Nani amekupa namba yangu na imekuwaje umetaka kuonana na mimi?”
“Sina nia mbaya mama, maana nakuchukulia wewe kama mama yangu. Mwanzoni sikujua kama Derick ni ndugu yangu na kujikuta tukiwa kwenye mahusiano ila badae nikajua kama Derick ni ndugu yangu, nikamwomba tusahau yaliyopita kati yetu na tuchukuliane kama ndugu. Ila anachonifanyia Derick chuoni ndio kilichofanya nije hapa”
“Kwanza mwanangu, nafurahi sana umekuwa mkweli maana Derick aliwahi kunieleza kuwa kuna msichana alikuwa na mahusiano nae na amegundua kuwa ni mtoto wa babake. Nimefurahi umekuwa mkweli kwa hilo, pole kwa hayo maana tatizo ni kwetu wazazi kutowaweka wazi watoto wetu. Haya niambie sasa tatizo lingine ambalo Derick anakufanyia chuoni”
Erica alimshukuru huyu mama kwa kuwa muelewa kwanza, kisha akamueleza jinsi Derick alivyomsambazia yeye kuwa alibakwa na kumsambazia kuwa ana ukimwi na kumsambazia kuwa ametoa mimba na jinsi wanavyomnyooshea kidole na kumuita malaya,
“Na amesema atafanya mpaka nione chuo kichungu ili nipate uchungu alioupata yeye kwa kukosa mapenzi ya baba, kwakweli mama mimi sijui kosa langu, ananiumiza sana, yeye ni ndugu yangu wa kuwa karibu na mimi ila yeye ndio anafanya kuniumiza mimi yani sina raha kabisa, chuo nakiona kichungu kweli, watu wananinyanyapaa sina raha wala amani”
“Kwanza pole sana mwanangu, sikia nikwambie mimi siwezi kumtuma Derick afanye huo upuuzi kwanza kabisa huwa sipendi mabinti kama nyie mpitie maisha ambayo nilipitia mimi. Ngoja nikwambie kwa kifupi kuhusu mimi na utaweza kuelewa ni maisha gani niliyopitia, ilifikia hatua ya kuitwa malaya na majina yote mabaya na iliniuma sana ila mwanangu sipendi kuona mwingine anaopitia maisha haya”
Erica alitulia kwa makini akimsikiliza mama yake Derick,
“Derick sio mwanangu wa kwanza, ila mtoto wangu wa kwanza yupo na nilizaa nikiwa shuleni. Mwanangu thamani ya mwanamke inapungua sana akizaa yani mwanamke ukiwa na mtoto kisha Yule baba mtoto hakutaki tena ujue itachukua muda mrefu sana kumpata mtu sahihi wa kukupenda wewe na mwanao, kiukweli mwanaume aliyenipa mimba wakati nasoma alinikimbia na kufanya nikose uelekeo ila nikasaidiana na nyumbani kumkuza Yule mtoto, nikapata mwanaume wa kuishi nae ila alionekana wazi hampendi mwanangu huku akinilazimisha nimzalie na yeye, nilizaa nae ila akanikimbia hapo nikawa na watoto wawili wasio na baba, sifa mbaya juu yangu zikaanza nikajisikia vibaya sana. Ndipo nikakutana na Jose, na aliniambia kuwa ana mke ila aliahidi kunioa mimi pia, nikawa tayari ili angalau nipate baba wa kulea watoto wangu, alinipangia chumba ikawa ni faraja kwangu ndipo nikazaa nae Derick, nikamwambia sababu ameahidi kunioa anipeleke nyumbani kwake mkewe anijue, akagoma, basi nikamvizia siku anaenda kwake nikamfata nyuma na kwenda hakuweza kunifukuza, nikaenda kuwachukua na wanangu kuishi nao pale ila mama yako alinitukana sana majina yote mabaya aliniita na siku hiyo alinifukuza mimi na wanangu na kusema nata Yule mtoto hamtambui, nilichukia sana nikakaa na ile chuki kwenye moyo wangu, wakati wangu wanakuwa siku zote niliwaambia nilivyomchukia mama yenu na ninyi haswa Derick nilikuwa naongea nae sana habari hizi sababu alikuwa baba yake nahisi ndiomana Derick anakuchukia ila saivi ni mtu mzima naelewa, nimejifunza kuwa halikuwa kosa la mama yenu maana naye alikuwa akitetea penzi lake, ila mimi ndio niliyeharibu maisha yangu toka mwanzo kwa kuchanganya mapenzi na shule. Nilikuwa naumia sana kuitwa malaya kwakuwa na watoto watatu wenye baba tofauti halafu baba wote hawataki watoto wao ila Jose alikuwa tofauti sana kwani alikuwa anamtuma mwanae mkubwa Mage aniletee hela za matumizi hadi kifo chake bado Mage aliendelea kuniangalia hadi nilipohama pale nilipokuwa nakaa. Erica nisamehe mimi maana ndio nimeweka chuki hiyo kwa mwanangu, ila nitaongea na Derick na hatokuumiza tena”
“Pole mama kwa yote hayo yaliyokupata, najua hukupenda yakupate hayo ila ni bahati mbaya tu, yani mimi natamani kuhama hata chuo”
“Hata usihame chuo mwanangu, nitaongea nae Derick atanielewa tu. Sitaki maisha niliyopitia mwingine ayapitie. Ila kuwa makini sana mwanangu, nitafurahi siku ukinialika nije kusherekea harusi yako”
Kiukweli Erica alimpenda sana huyu mama kwa jinsi alivyokuwa akiongea, na ilionyesha jinsi gani alikuwa akiyajutia makosa aliyoyafanya.
“Nafurahi sana kuongea na wewe, sikutegemea kama ungekuwa mzuri kwangu kiasi hiki”
“Usijali mwanangu, hata hivyo nimeongea tu na wewe bila hata kinywaji chochote! Dah sio vizuri kwakweli, unakunywa nini mwanangu?”
“Aaah usijali mama”
“Niambie bwana, unakunywa nini? Hutoondoka hapa bila kunywa kinywaji kwenye nyumba yangu”
“Basi maji tu yananitosha”
“Sawa, ngoja nikakuletee”
Mama Derick aliinuka na kutoka nje, Erica akasikia mlio wa meseji kwenye simu yake, akachukua na kufungua akakuta Rahim kamtumia meseji ya kawaida kabisa,
“Hellow kipenzi changu, tayari nimekutumia pesa kwaajili ya kuhama chuo. Ukiingia facebook utaona nimekutumia taarifa za kuchukua pesa hiyo, nimekutumia milioni tatu, isipotosha utaniambia. Nakupenda sana, saizi nalala. Byee”
Erica alisoma mara mbili mbili huu ujumbe na alijiona kama anaota vile, alichukua simu yake nyingine na kufungua mtandao kweli alikuta ujumbe wa Rahim wenye taarifa zote za msingi za kuipata pesa hiyo, yani alihisi kimuhemuhe kabisa tayari ile hela ilishamchanganya.
Mama Derick alirudi na maji ya dukani, Erica aliyapokea kisha kumuaga huku akimshukuru sana,
“Sasa mbona mapema hivyo mwanangu?”
“Nahitajika chuo mama, ila tutaendelea kuwasiliana”
“Sawa mwanangu ila usihame chuo, nitaongea na Derick halafu mwambie mama yako nilishamsamehe kwa yote na yeye anisamehe kwa yote.”
Erica aliaga na kuondoka, kwakweli alikuwa na harakati sana, kwani muda huo akili ilikuwa ikiwaza zile pesa alizotumiwa na Rahim tu.



 
SEHEMU YA 142


Akiwa njiani kuelekea benki, kuna gari ilisimama karibu yake na kwenye hiyo gari alishuka Mrs.Peter yani mama yake na Rahim, kisha akasalimiana na Erica pale na kumkumbatia,
“Umenitupa mwanangu”
“Sijakutupa mama”
“Ngoja nikutambulishe basi”
Kisha Yule mama alimuita binti aliyekuwa nae kwenye gari kisha Yule binti akashuka, kisha Mrs.Peter akamwambia Yule binti,
“Salma, huyu anaitwa Erica ni kama binti yangu. Mimi sinaga mtoto wa kike kwahiyo kumpata huyu imekuwa bahati sana kwangu, ni mwanangu pia huyu kwahiyo ni wifi yako”
Neno la wifi yako lilimshangaza kidogo Erica ila alitulia kusikia zaidi, kisha mrs.Peter akageuka kwa Erica na kuendelea na utambulisho,
“Erica, huyu anaitwa Salma ni mkwe wangu yani ni mchumba wa Rahim”
Erica alionyesha mshangao wa wazi wazi,
“Mchumba wa Rahim? Kwani Rahim ana mchumba?”
“Najua lazima ushangae, ila Rahim kampigia simu baba yake kuwa amtafutie mchumba si unajua Rahim kutongoza hawezi, ndio baba yake kamtafutia huyu na tumemtumia Rahim picha kasema amempenda. Hivyo ndio nampeleka na nyumbani kwangu akapafahamu”
Erica alihisi kama masikio yameziba asikii vizuri maana hakuelewa kabisa.


“Erica, huyu anaitwa Salma ni mkwe wangu yani ni mchumba wa Rahim”
Erica alionyesha mshangao wa wazi wazi,
“Mchumba wa Rahim? Kwani Rahim ana mchumba?”
“Najua lazima ushangae, ila Rahim kampigia simu baba yake kuwa amtafutie mchumba si unajua Rahim kutongoza hawezi, ndio baba yake kamtafutia huyu na tumemtumia Rahim picha kasema amempenda. Hivyo ndio nampeleka na nyumbani kwangu akapafahamu”
Erica alihisi kama masikio yameziba asikii vizuri maana hakuelewa kabisa.
Mpaka Yule mama alimshtua tena Erica maana alionekana kushangaa sana,
“Unashangaa eeeh! Ipo hiyo ya kutafutiana wachumba, ulikuwa hujui? Inafanywa sana na wazazi kama mtoto hawezi kutafuta, unajua Rahim amekuwa eeh! Anatakiwa kuwa na mwanamke”
“Sawa mama, nashukuru kumfahamu”
Kisha Erica akampa mkono Yule dada ila ni mkono wa kinafki kwani kiukweli alikuwa anaumia sana moyoni mwake, na hapo hapo akaaga na kuondoka, akaiweka akili yake sawa kuwa asilie muda huo ila akaenda kwanza benki alipokuwa anaenda kuchukua hizo pesa alizotumiwa na Rahim.


 
SEHEMU YA 143



Erica alipochukua zile pesa akarudi nyumbani kwao moja kwa moja, ila aliwaza sana kuwa ni kwanini mwanaume kama Rahim anafikia hadi kiwango cha kumtumia pesa halafu huku kuna mwanamke mwingine amesema atafutiwe, akawaza sana akaona kichwa kinamuuma tu kwa kuwaza, akapigiwa muda huo simu na Bahati,
“Erica upo sawa?”
“Nipo sawa ndio”
“Nahisi kama unatakiwa uwe sehemu upigwe na upepo kidogo, hisia zangu zinasema haupo sawa. Kwani uko wapi sahizi”
“Nipo nyumbani”
“Twende beach basi”
“Muda huu jamani!! Si saa kumi na moja hii”
“Ndio kwani kuna ubaya gani, si hata tukikaa nusu saa itatosha mpenzi wangu!”
“Mpaka nijiandae, kuondoka hapa saa kumi na moja”
“Ndio ukiwa tayari niambie, nije nikufate na pikipiki. Kuna rafiki yangu kaniachia pikipiki yake leo nitembee tembee nayo”
Erica alikubali tu kwani kweli alihitaji apate mahali atakapotuliza akili yake kidogo kwani aliona ikivurugika haswaaa maana kila alipomfikiria Rahim alikosa raha, akainuka na kujiandaa kisha akampigia simu Bahati na ilionyesha hakuwa mbali na kwao maana muda huo huo alifika na kumchukua kisha wakaenda ufukweni.
“Ulikuwa unanisubiria nini mitaa ya nyumbani, maana muda huo huo umefika”
“Yani muda nakupigia simu nipo mitaa ya kwenu, nikasema kama utakuwa chuo basi ningekufata, unajua ni jinsi gani nakupenda Erica! Najua hujui sababu ungejua basi ungeona hata dunia yote hii ipo chini yako kwa upendo wangu kwako. Nakupenda Erica yani hadi nahisi neno lenyewe la nakupenda halitoshi kueleza hisia zangu kwako. Niambie nifanye nini ili unipende pia”
Erica akacheka kisha akamwambia,
“Kwani leo umetambua kuwa sikupendi?”
“Erica sikia nikwambie, hata ukinieleza mara ngapi kuwa hunipendi ila moyo wangu utasema kuwa wewe ni wangu na umeumbwa kwaajili yangu, Erica siku moja nitakuwa na pesa kama hao wenye majumba na magari, nakupenda sana na wala sitokuacha nikiwa hivyo kwani sikuzote wewe utabaki kuwa thamani yangu”
Erica alisikiliza maneno ya Bahati ambaye alikuwa tofauti kabisa na wanaume wengine, ila aliamua kumpinga kidogo,
“Ila wanaume wote ndio zenu, nakupenda, nakupenda kumbe hakuna lolote. Siku moja unakuja kunisaliti, nyie wanaume sio watu kabisa, nyie ni waongo maradufu, hamuaminiki”
“Erica, sikatai kuna wanaume waongo duniani ila wakweli nao wapo. Katika wanaume wakweli mfano wapo ni mimi, Erica hakuna chochote ninachoweza kukudanganya wewe, nitaona wasichana mbalimbali ila wewe ni zaidi ya wote, najua umona wanaume wengi, au umeona wengi kwa rafiki zako ama kwa ndugu zako wakiwa ni waongo ila sio mimi Erica, najua maneno yangu utayaamini tu ipo siku, maana mimi hata nikizeeka bado nitakupenda wewde hadi naingia kaburini”
Kwakweli Erica alimuona Bahati kuwa mwanaume wa ajabu sana kati ya wanaume wote aliokuwa nao tatizo ni moja tu, hakuwa na upendo hata kidogo kwa huyu Bahati. Akajifikiria jambo na kuamua kumuuliza kitu Bahati,
“Ngoja nikuulize”
“Niulize tu”
“Unajua mimi sipendi kazi yako ya uvuvi wa samaki, sasa ni kitu gani unaweza kufanya kuboresha biashara yako ili angalau uwe na thamani”
“Erica, kwasasa sina pesa ila uvuvi unalipa vizuri tu. Nikipata pesa nitaboresha kazi yangu, kwanza nitatafuta eneo, nitanunua friji kubwa ya kuhifadhi samaki na nitakuwa nauza kwa watu wengi sana, nitapata faida kubwa sababu navua mwenyewe. Na nikiendelea vizuri naanza kufuga samaki wengine sababu kuwahudumia najua”
“Ungetaka kama kiasi gani?”
“Kwa kuanzia nikipata kama milioni mbili nitakuwa mbali sana. Kwanini umeniuliza hivyo Erica?”
“Aaaah hamna kitu”
Wakaaongea ongea mambo mengine na muda ulikuwa umeenda hivyo Erica akasema arudi kwao maana anaelewa kuwa mama yake atakuwa amerudi tayari.
 
SEHEMU YA 144



Na kweli alifika kwao na kumkuta mama yake anakula, akamuita,
“Eeeeh umegfikia wapi swala lako la kutaka kuhama chuo?”
“Bado mama, ila nadhani nisihame tu”
“Hata mimi nilitaka nikushauri hivyo mwanangu, angalia mjomba wako anavyojitoa kwaajili yako halafu asikie umehama chuo atasemaje? Usihame chuo mwanangu, huyo Derick nitamtafuta mama yake na nitamwambia ni vibaya anavyofundisha watoto”
Erica aliamua kumwambia mama yake jinsi alivyomtafuta mama yake Derick na jinsi alivyosema kuwa atamkanya mtoto wake,
“Mama kumbe Yule mama wala hana hata roho mbaya, usimchukie mama ni baba alimlagkai kuwa atamuoa mke wa pili. Usimchukie mama Derick, kasema msameheane”
“Wewe nae ni mtoto hata huelewi ila nishamsamehe, hivi unadhani kutembea na mume wa mtu ni sifa? Eti aliahidiwa kuolewa mke wa pili, aondoe mashetani yake hapa, aseme lingine ila aongee tu na huyo shetani wake”
“Amesema ataongea nae, ila usimchukie mama”
“Kwahiyo unataka nimchukie baba yenu au? Wanawake hawajielewi hawa, nisingemtoa kitimutimu angejizalisha watoto kama kumbikumbi hapa. Hebu kula ukalale huko usiniletee habari za vichaa”
Yule mama akainuka zake kisha Erica alikula pale na kwenda kuoga kisha akaenda kulala, kwakweli hata hakutamani kuingia kwenye mtandao na wala hakuzitamani hela za Rahim maana yeye alishaanza kumkaribisha kwenye moyo wake halafu anakuja kugundua mambo ya ajabu, hakutaka kabisa kumfikiria.
Kulipokucha alijiandaa asubuhi, akaweka vitabu vyake vizuri kwa lengo la kwenda chuo, ila alitaka kufanya kitu cha kushtukiza kwa Bahati.
Aliondoka kwao na kwenda moja kwa moja hadi kwa Bahati, na kweli lilikuwa jambo la kushtukiza kwani Bahati hakufikiria kama Erica angeenda kwake kwa muda huo,
“Karibu mpenzi wangu, naona leo umeamua kunishtukiza”
“Nawahi chuo ila nimeona ni vyema nipitie hapa, nina zawadi yako”
“Zawadi!!”
“Ndio zawadi yako”
Erica akatoa bahasha kubwa kidogo na kumkabidhi Bahati,
“Nini hiki Erica?”
“Utafungua nikiondoka, ngoja niwahi chuo”
Bahati alitaka kumsindikiza ila Erica alikuwa ameenda na bodaboda kwahiyo akatoka na kumuaga Bahati kisha akapanda bodaboda na kuondoka.
Bahati alipata kimuhemuhe cha kufungua ile bahasha, akaifungua akashangaa ni hela kwakweli Bahati alishangaa sana, akaanza kuzihesabu akakuta ni milioni mbili na laki tano.
“Kheee kwahiyo Erica ameamua kunipa hela ili nifanye vizuri hii biashara! Jamani huyu mwanamke ni ananipenda tena ananipenda sana ila hataki tu kujionyesha. Erica bila ya chochote kile naahidi kukupenda maisha yangu yote, najua unafanya haya ili nifanane na aina ya wanaume ambao unatamani kuwa nao. Sitakuangusha Erica, nitafanya kazi kwa bidii hadi ujisikie fahari kunitambulisha kwa rafiki zako kuwa mimi ndiye mume wako. Nakuahidi Erica, nitakupenda hadi pumzi yangu ya mwisho.”
Bahati alijikuta akisema peke yake tu kama mjinga maana si kitu alichokitegemea kabisa.
 
SEHEMU YA 145


Erica alienda chuo maana alikuwa na kipindi ila alipomaliza kipindi tu alipanda gari na kurudi nyumbani kwao kwani kiukweli hakutaka kukaa maeneo ya chuo kabisa, alijisikia amani kutoa zile pesa na kumpa Bahati,
“Sababu kasema anataka kuboresha biashara yake, acha aboreshe. Mimi nitabaki nah ii laki tano ila nayo hata siitamani sijui hata nifanyie kitu gani, yani mwanaume kanichefua Yule amefanya niione dunia chungu kuliko uchungu wenyewe”
Akamsikia mama yake anajiongelesha ongelesha sebleni akaenda kumsikiliza,
“Yani mwanangu safari hii kikoba kitanitokea puani”
“Kwanini mama?”
“Unajua nategemeaga biashara yangu ya vitambaa ila vimebuma yani wengi nimewakopesha hawajalipa, halafu dadako Bite toka amepata mimba yani hakuna msaada tena kwangu, kila ukipigia simu habari yake ni mimba mimba yani kama wimbo wa taifa. Huyo Mage ndio sio wa kumtegemea kabisa, mtoto wa kiume sasa, ninae kama sina ni hana msaada wowote toka anaishi kwa mjomba wake. Yani nahisi kukwama, sijui mwezi huu nitapata hela wapi ya kupeleka kwenye kikoba, maana ni kesho hapo na ukichelewa kupeleka faini”
“Kwani ni sh ngapi mama?”
“Si elfu hamsini, yani hapa sielewi kabisa”
Erica aliondoka pale sebleni na kuelekea chumbani, mama yake alijua mwanae kamdharau, ila baada ya muda Erica alirudi na kumkabidji mama yake hela,
“Laki mbili hiyo mama, najua itakusaidia”
“Kheee wewe mtoto wewe jamani Mungu akuweke, Erica hujaanza kazi ila nakula matunda yako mapema hivi. Ukianza kazi si nitanenepa mimi jamani, Erica mwanangu, nakupenda sana jamani”
Mama Erica alifurahishwa sana na ile hela kwani hakuitegemea pia, na wala hakumuuliza kuwa kaitoa wapi. Erica alirudi zake chumbani kwake na kujilaza.
Alipokuja kushtuka ilikuwa tayari saa mbili usiku, akakutana na ujumbe wa kawaida kutoka kwa Rahim,
“Mpenzi hata salamu jamani! Facebook huingii kabisa, nini tatizo Erica kipenzi changu? Unajua nakupenda sana, ingia basi facebook tuchat kidogo”
Erica alisonya kisha akachukua simu yake na kuingia facebook kuona kuwa huyu Rahim ana kipi kipya, akakutana na ujumbe wa Rahim
“Nimefurahi umeingia facebook mpenzi, najua umechukizwa na vitu visivyokuwa na uhalisia. Mama aliniambia kuwa kakutana na wewe sijui kakutambulisha msichana walionitafutia”
Erica alipumua kidogo, kisha akamtumia ujumbe pia,
“Ndio, Rahim kumbe unanidanganya tu hunipendi wala nini!”
“Hivi Erica kama ningekuwa sikupendi ningekuwa nahangaika na wewe kiasi hiki ili iweje? Wasichana wangapi wananitaka mimi huku nilipo ila kwanini nahangaika na wewe?”
“Sijui mwenyewe una maana gani?”
“Najua huelewi mambo ya familia yangu, yule mwanamke wameshauriana wenyewe kumtafuta sababu mama yangu huwa anafikiria kuwa mimi siwezi kutongoza na wanaona umri unaenda, wanataka nioe ila mimi ninayekutaka ni wewe. Sitarudi nchini mpaka umalize chuo, sijataka kuwakatalia kwani sitaki kuanza kuumizana nao vichwa kwasasa, sijamwambia mama kama ni wewe nikupendae sababu mama yangu namjua ataanza kukusumbua. Yule ni mama yangu namjua vizuri sana Erica, wewe unamjua kwa juu juu ila mimi namjua vizuri sana Erica. Tambua kwamba wewe ndiye mwanamke nikupendaye na ninafanya vyote hivi sababu ya upendo wangu kwako, jitunze Erica nakupenda sana”
Kwakweli Erica hakuelewa hata ajibu nini kwa Rahim, alisoma ule ujumbe mara mbili mbili huku akijaribu kutafakari ila alishindwa amjibu kitu gani huyu Rahim, akamuuliza tena,
“Kwahiyo Yule msichana humpendi?”
“Erica nielewe ninaposema nakupenda wewe, hakuna msichana mwingine yeyote ninayempenda zaidi yako, ila nakuomba usiwe karibu kabisa na mama yangu, atakupa presha za bure, yani jitenge na mama yangu. Ukimuona A, basi wewe pita B. Nielewe mimi Erica, mimi ndiye ninayekupenda na si mwinginewe”
Erica alianza kulainika kwa maneno yale ya Rahimu maana alijisikia vizuri sasa kuwa Rahim anampenda ila hela ndio alishazigawa tayari, ila kabla hajamuandikia Rahim ujumbe mwingine wowote alimuandikia,
“Nitakutumia pesa nyingine kwaajili ya matumizi yako ya hapa na pale Erica, tambua nakupenda sana. Mapenzi mengi huvunjika kwa kusikiliza maneno ya watu ila nakuomba usisikilize maneno ya watu bali angalia vitendo vyangu mimi”
Alijikuta akiwasiliana nae kwa muda mrefu sana hadi pale alipoamua kumuaga na kulala.



 
SEHEMU YA 146


Alipoamka alikuwa akijifikiria sana, huku akijiuliza kama Rahim anampenda kweli au la, alikosa jibu kabisa huku kichwani mwake akishindwa kumtoa Erick ila akishindwa pia kumtafuta hewani maana alihisi kuwa Tumaini alimwambia mambo mengi sana maana toka siku ile hakuona tena meseji kwenye simu yake kutoka kwa Erick wala kwenye facebook yake.
Alijiandaa na kwenda chuo kama kawaida, alipotoka tu kwenye kipindi aliitwa na Derick, aliamua kwenda kumsikiliza,
“Erica, naomba unisamehe na tuanze maisha mapya. Nimetambua makosa yangu”
“Nishakusamehe tayari, ila kama umetambua makosa yako ni vizuri”
“Sasa nitakulinda dada yangu, nitakutunza sitapenda kuona wakikusema vibaya. Nisamehe sana”
“Usijali nishakusamehe”
“Ila dada yangu, naomba ujitulize. Usituamini sana sisi wanaume, tuna maneno matamu kushinda asali ila ni waongo wa kupindukia, dada yangu napenda tuishi kindugu na endapo utakuwa na swala lolote la kunishirikisha mimi niambie tu nitakuwa nawe bega kwa bega, au hatakama unahitaji kuniuliza kama mwanaume yupi anakufaa nifate nitakuambia. Ila dada yangu usirudie tena kutoa mimba ni hatari kwa afya yako, hebu jihurumie dada yangu isije siku ukashindwa hata kuzaa kumbe sababu ya kutoa mimba”
“Nimekuelewa”
Kiukweli hizi mada za kutoa mimba Erica hakuzipenda kabisa, aliamua tu kumuaga Derick pale na kumuahidi kuwa watakuwa wakiwasiliana vizuri tu.
Erica aliondoka akielekea nyumbani kwao ila hakuwa na sababu tena za kuhama chuo kile akajisemea kuwa hatohama ila atamdanganya Rahim kuwa amehama ili Rahim asione kuwa pesa yake imeenda bure.
Alifika nyumbani kwao na kuongea ongea kidogo na mama yake ila kwakuwa usiku ulikuwa umefika akaona vyema aende kulala, ila kabla ya yote aliingia kwanza facebook ili kuangalia kama kuna jipya, alipofungua tu akakutana na ujumbe wa Rahim,
“Nimetoka sasa hivi kukutumia milioni mbili, najua itakutosha kwasasa.”
Erica alitabasamu na kuona kweli kuwa Rahim anampenda ingawa hataki mama yake ajue, akamshukuru sana na kuongea nae mambo mengi sana,
“Erica, kaa mbali na mama yangu. Namjua mama yangu alivyo, sipendi kuumia moyo, mama huniambia kitu hata nisipomuuliza, halafu namuamini sana, naomba ukae mbali na mama yangu”
“Ila hata nikiwa nae karibu kwani nitafanya nini?”
“Mama akijua una mahusiano na mimi atakufatilia kila nyendo zako, unaweza kusimama na mwanafunzi mwenzio tu ila mama akajua ni mchumba wako, akiniambia nitaumia sana na nitakuchukia Erica, naomba ujitenge na mama yangu name niendelee kukuamini. Najua unanipenda, naomba ukae mbali na mama yangu”
“Sawa, nimekuelewa Rahim nitafanya hivyo”
“Hata swala la kukutana na wewe, sikumuuliza ila aliniambia tu ilivyokuwa na jinsi sura yako ilivyoonyesha mshangao hadi akaniuliza kuwa kuna nini baina yetu ila nikamwambia sina mazoea na wewe, tafadhali kaa mbali na mama yangu. Sitaki uumie moyo, sitaki uniumize moyo”
“Nimekuelewa Rahim”
Alizungumza nae sana kisha akamuaga kuwa analala, na akalala.
 
SEHEMU YA 147


Kulipokucha alijiandaa kama kawaida kwenda chuo ila siku hiyo hakuwa na vipindi chuoni aliamua kwenda kwanza benki kuchukua pesa ambayo Rahim alimtumia, alifika na kuzitoa kisha kutaka kurudi tena kwao ila kabla hajapanda basi alipigiwa simu na Bahati akimuomba afike mahali ambako yeye yupo, naye Erica alienda kwani alijua asipoenda basi Bahati angefika nyumbani kwao,
“Nimekuita hapa kukuonyesha mahali nilipopatafuta kwaajili ya biashara yangu”
“Aaah kumbe! Ndio umepata kwa haraka hivyo!”
“Ndio, kuna mama mmoja nampelekeaga samaki ndio kanipatia eneo hilo, nimemwambia kuwa nataka kufanya biashara na mchumba wangu. Amefurahi sana, twende yupo pia, akakufahamu”
Basi Erica akaongozana na Bahati hadi kwenye eneo hilo na kuingia ndani, mama mwenye eneo alifika na Bahati kuanza kumtambulisha Erica kwa Yule mama,
“Mama, huyu anaitwa Erica ni mchumba wangu yani mke wangu mtarajiwa”
Muda huo mapigo ya moyo ya Erica yalikuwa yakienda kwa kasi sana kwani mama Yule alikuwa ni Mrs.Peter yani mama yake na Rahim.


Basi Erica akaongozana na Bahati hadi kwenye eneo hilo na kuingia ndani, mama mwenye eneo alifika na Bahati kuanza kumtambulisha Erica kwa Yule mama,
“Mama, huyu anaitwa Erica ni mchumba wangu yani mke wangu mtarajiwa”
Muda huo mapigo ya moyo ya Erica yalikuwa yakienda kwa kasi sana kwani mama Yule alikuwa ni Mrs.Peter yani mama yake na Rahim.
Huyu mama aliuona uoga aliokuwa nao Erica, akamuuliza
“Mbona hivyo Erica?”
Ndio Bahati akashangaa kuwa wanafahamiana,
“Kumbe mnafahamiana?”
Mrs.Peter akajibu,
“Ndio, yani huyu Erica ni kama binti yangu vile. Nimefurahi sana kuona mko pamoja, Erica bingti yangu mshike sana huyu kijana. Anakutajaga sana ila sikujua kama anayekutaja ni wewe, huwa anasema anakupenda sana, hadi anatamani dunia yote ijue ni jinsi gani anakupenda. Mshike sana huyu”
Erica aliitikia tu ila kinafki kwani haikutoka moyoni, hakutaka hata kuendelea kuangalia mandhari ile kwani aliaga kuwa anawahi chuo na akaondoka na kurudi kwao huku akiwa na mawazo mengi sana.
Alifika kwao na kuwaza sana, aliwaza kuwa aanze yeye kumtafuta Rahim na kumwambia au aache kwanza kinuke ndipo atafute njia za kujitetea, alikuwa anawaza kuwa hata kujitetea atajiteteaje, aliwaza sana bila ya jibu.
Mama yake aliporudi alimfata kuongea nae,
“Mama nina rafiki yangu mmoja hivi kapatwa na matatizo, sasa anaomba ushauri”
“Matatizo gani?”
“Ana mchumba wake yupo nje ya nchi na huyo mchumba wake anamjali haswaa yani kama hela anamtumia na kila kitu, ila sasa kuna mwanaume hapa nchini ni anamfatilia hadi kero, kuna siku alikuwa kwenye matembezi yake Yule mwanaume nae alienda mara gafla akakutana na mamake Yule mchumba wake wan je ya nchi, sasa anawaza kuwa afanye nini maana Yule mchumba wake ataambiwa na mama yake”
“Huyo rafiki yako nae ni chizi, yani ni chizi kabisa namba moja. Mtu unapata mwanaume anayekujali na pesa anakutumia halafu unaanza kuzunguka na hawa vinuka mkojo wakusaidie nini kwanza kama sio utahira huo? Unajua wanasema unaposhikwa shikamana, sasa huyo rafiki yako atakula jeuri yake. Ila na wewe mwanangu wakati wenzio wanapata wanaume nje ya nchi kwanini wewe hupati? Kwani una kasoro gani mwanangu jamani!”
“Mama utamjua tu mchumba wangu hata usijali”
“Usije ukanitambulisha Yule muuza samaki, kwakweli Erica nitakunyofoa macho hayo. Sitaki ujinga kabisa, tafauta na wewe wanaume wan je ya nchi ndio wanakuwaga na hela”
“Mama jamani, kwahiyo kwako hela ni bora kuliko mapenzi ya kweli!”
“Hebu nitolee balaa za mapenzi ya kweli, tumepitia haya mambo ndiomana nakupa ushauri wa kumng’ang’ania mwenye hela. Mimi nilimpenda baba yenu ingawa alikuwa fukara ila sababu ya upendo wa kweli nikaowana nae, ona sasa alichokuja kunifanyia, kujitia yeye mashuhuri wa kuoa wake wawiliwawili wakati bila mimi asingepata heshima hii iliyomfanya ajidai duniani. Mwanangu unaweza ukawa na fukara na akakusaliti na unaweza ukawa na mwenye pesa na akakusaliti sasa bora kusalitiwa na mwenye pesa haiumi sana ila kusalitiwa na fukara inauma mwanangu asikwambie mtu”
“Sawa mama nimekuelewa, kwahiyo ushauri wako kwahuyo rafiki yangu”
“Huyo sina ushauri kwake, atachagua mwenyewe kusuka au kunyoa. Wenzie wanatafuta wanaume kama hao wenye pesa halafu yeye anachezea bahati. Yani ingekuwa enzi zangu nipendwe na mwanaume mwenye pesa yani njiani hata salamu ya mwanaume mwingine nisingeiitikia”
“Mmmh mama hata salamu ya baba usingeitikia?”
“Achana na mambo hayo bhana”
“Sasa mama kwahiyo hakuna ushauri kwa huyo rafiki yangu?”
“Sina ushauri maana hayo matatizo ni ya kujitakia. Ngoja nifanye shughuli zangu mie, ushauri kuwapa watu wasiokuwa na akili sitaki”
Mamake aliondoka, Erica nae alienda chumbani kwake, akawaza sana kuwa hata mama yake kamtoa akili,
“Kwani kosa langu mimi ni nini? Najifikiria sana ila sijui kosa langu kabisa, kosa langu ni kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi au kosa langu ni nini? Na kwanini kila neema inapokuja kwangu linatokea jambo la kuharibu neema hiyo, kosa langu ni nini haswaa? Erick nimemkosa na huyu Rahim nimkose pia jamani! Yani mwanaume pekee anayekuwa na mimi bega kwa bega ni Bahati, sielewi kwakweli”
Aliamua kulala tu ingawa hakuwa na usingizi kwa muda huo ila aliamua kujilaza.
 
SEHEMU YA 148


Ilipofika usiku aliingia kwenye mtandao huku akiwaza kama Rahim ameshapata habari ila siku hiyo aliwasiliana vizuri sana na Rahim, ikionyesha kwamba habari hajapata, akawa anamuomba Mungu mamake Rahim asahau na asimwambie ukweli Rahim, kitu pekee ambacho alisisitizwa na Rahim kwa siku hiyo ni kuwa asome basi na sio swala lile kabisa, hakuulizwa.
Aliendelea na mawasiliano na Rahim na hakuna siku ambayo Rahim alimuuliza chochote kuhusu Bahati na kuhisi kuwa huenda mama yake Rahim hajamwambia chochote.
Dada yake alikuwa kajifungua kwahiyo alikuwa akihudumiwa pale nyumbani kwao, muda mwingi alijikuta akimdadisi dada yake kuhusu shemeji yake maana hakumuamini,
“Dada. Kwahiyo Yule msichana wako wa kazi ndio umemuacha na shemeji”
“Ndio, maana mume wangu atashindwa kwenda kazini anatakiwa kuhudumiwa kila kitu, kufuliwa nguo, kupigiwa pasi, kupikiwa lazima Yule mdada abakie”
“Ila pia na huku kuna kazi, kumuangalia mtoto, kumuhudumia, kufua nguo za mtoto. Kwanini usingekuja nae huku akusaidiage?”
“Unayosema ni kweli ila kule mume wangu nae anatakiwa kuhudumiwa, kuna msichana nimeagiza atakuja kunisaidia hapa nyumbani”
“Kwahiyo utakaa hapa hadi uzazi uishe?”
“Kwani mdogo wangu vipi? Hutaki kuniona hapa nyumbani au? Nakuzibia nini hapa? Mbona shughuli zote anafanya mama, kwani ni wewe unatumwa kufanya kazi za hapa”
“Hapana dada, ila nasikiaga wanaume kipindi wake zao wakitoka kujifungua hupenda sana kutembea na wasichana wa kazi”
“Ushindwe na ulegee, sio kwa mume wangu mimi. Kashindwa kunisaliti kote huko ulaya alikokuwa, aje kunisaliti na msichana wa kazi? Hiko kitu hakunaga, mume wangu ana kinyaa sana hawezi tembea na msichana wa kazi”
“Dada, ila wanaume si wa kuwakatalia sana maana hata msichana wa kazi naye ni mwanamke kama wewe”
“Weee mtoto wewe, ujue mimi ni mkubwa wako na mapenzi nimeyajua kabla yako, au kwavile ulibeba mimba ya Yule taahira ndio unazani mapenzi yapo hivyo? Kwanza wewe mdogo wangu sijui ukoje, huna kinyaa, hivi kweli wewe wa kwenda kutembea na Yule mwanaume? Loh! Uchafu mtupu, mwanaume huendani nae hata kidogo, yani wewe mdogo wangu wewe, ndiomana unahisi kusalitiwa tu. Wanaume masikini na wachafu wachafu ndio wanaosaliti ila sio wanaume wasomi na waliondelea”
“Mmmh dada, haya yaishe”
Erica hakutaka kumwambia vitu vingi dadake kuhusu shemeji yake, ila alikuwa na hisia mbaya sana kuhusu shemeji yake maana hakumuamini kabisa. Ila alimshangaa sana dada yake kuwa na imani vile na mume wake.
 
SEHEMU YA 149


Erica alikuwa akienda chuo akitokea nyumbani kwao, walipokuwa wanakaribia kumaliza mwaka wa pili walitakiwa kutafuta sehemu watakayo fanya mafunzo kwa vitendo, na kwa bahati alipata kwenye ofisi ya shemeji yake James. Alifurahi ila akafikiria sana namna itakavyokuwa hapo ofisini kwa shemeji yake, ni kweli kapata sehemu ya mafunzo ila mtihani uliopo ni kuwa kwenye mafunzo hayo ni kwa shemeji yake ambaye amekuwa akimtaka, ila kwavile alishajisemea kuwa hatotembea na mume wa dada yake akaamua kushikiria msimamo wake huo huo.
Kwahiyo walipofunga chuo, walihamia kwenye mafunzo kwa vitendo, na alikuwa akienda mara kwa mara kama alivyohimizwa na dada yake.
Siku hiyo shemeji yake alimuita ofisini,
“Mbona unanikwepa sana Erica? Au ule uongo wako ndio unafanya unikwepe sana siku hizi!”
“Hapana shemeji”
“Si ulininyima ukaenda kuwapa wale mabwege, ila nakutamani mtoto wewe”
Erica alikuwa kimya tu ila shemeji yake aliendelea kumuongelesha,
“Basi naomba siku tutoke Erica wangu jamani”
Erica bado alikuwa kimya kabisa kwani hakujua hata amjibu nini huyu shemeji yake ukizingatia ndio yupo kwenye ofisi yake akiendelea na mafunzo, aliwaza kuwa ni kitu gani kinaweza kumfanya huyu shemeji yake asimsumbue kabisa.
Akaona akifika nyumbani atapata wazo kuwa afanye kitu gani ila kwa muda huo hakuweza kumjibu shemeji yake. Muda wa kuondoka ulipofika, shemeji yake alimkazania kuwa ampe lifti ya kumpeleka nyumbani na akamuangalie na mtoto, kwa bahati kuna mtu alitokea na kumuita shemeji yake kwahiyo yeye akaondoka na kwenda nyumbani.

Aliwaza sana maana ndio kwanza alikuwa na siku ya tatu kwenye ile ofisi ila shemeji yake kashamuanzishia tamaa, akawaza sana kuwa atafanya kitu gani, akapata wazo moja kuwa amuombe Bahati awe anaenda ofisini kumchukua ili shemeji yake akose hata ile nafasi ya kusema kwamba nikupe lifti kumbe ana mambo yake mengine.
Akampigia simu Bahati na kumwambia hilo swala, kwakweli hilo swala lilikuwa ni swala la furaha sana kwa Bahati na alijiona kuwa ana bahati kama jina lake maana hiyo nafasi aliihitaji sana na kipindi hiko akaipata,
“Erica, nitakuwa nafunga biashara zangu mapema ili nije kukuchukua mpenzi wangu. Nashukuru kwa kuniamini”
Erica alikubaliana nae muda wa kwenda kufatwa pale ofisini na kumuelekeza ofisi ilipo, maana yeye toka siku ile amuone mrs.Peter hakutaka tena kwenda kwenye ofisi ya Bahati ili kumuepuka na vile ambavyo Rahim hakumuuliza kulimfanya kuona kuwa Rahim hajaambiwa chochote kuhusu yeye.
Na siku zote alikuwa akiwasiliana kawaida tu na Rahim na hakuthubutu kumwambia kuwa kwa kipindi hiko yupo kwenye mafunzo ya vitendo kwani alihisi labda atazua maswali mengi sana kwa Rahim.
Kesho yake alienda ofisini kwa shemeji yake kama kawaida, ila muda wa kutoka alifika Bahati na kumfanya yeye aondoke nae, shemeji yake akamuita,
“Erica, jana umenikimbia tusiongozane na leo tena unakimbia. Kwanini unafanya hivyo?”
“Aaaah shemeji kuna mtu huwa anakuja kunichukua”
“Mtu gani huyo?”
“Ni mchumba wangu”
Kisha Erica akamuaga shemeji yake na kuelekea nje, kitendo ambacho kilimfanya James kutoka pia ili kuona ni nani huyo anayeenda kumchukua Erica, alichukia sana baada ya kumuona ni Bahati maana hakumpenda kijana huyo toka siku ya kwanza aliyomuona na Erica.
Ila swala la shemeji yake kuchukia halikumfanya Erica ajali chochote kwani yeye cha msingi yupo salama tu, akaenda nyumbani kwao.

 
Back
Top Bottom