Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 261


Wakaingia ndani, Erica akaona kuna wababa watano, kisha kuna mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele ambapo Yule meneja alimwambia Erica kwa taratibu,
“Yule wa mbele ndio mkurugenzi mkuu”
Erica alipomuangalia vizuri, akagundua ndio Yule mzee Jimmy.
Alijikuta akiishiwa nguvu kabisa ila bado alisimama ili kujua hatma yake, alimsikia Yule meneja akimtambulisha Erica kwa wale wakurugenzi,
“Huyu anaitwa Erica, ndio mama wa Yule mtoto”
Kisha meneja akatambulisha majina ya wale wakurugenzi kwa Erica, ila alishangaa kuona mzee Jimmy hata hakushtuka wala hakujifanya kumfahamu zaidi zaidi walimuuliza baadhi ya maswali kisha Mzee Jimmy akasema,
“Binti, Jumamosi saa nne asubuhi umlete huyo mtoto wako tuje tumuangalie vizuri na tukusainishe mikataba yetu”
Erica alikubali, kisha wakamruhusu kuondoka. Kwakweli alivyotoka nje ya ile benki ndio aliweza kupumua sasa, huku akiliangalia lile jingo refu la ile benki. Alikuwa amekubali tu ila hakujua kwakweli kama itakuwa rahisi maana Yule mzee alishaonyesha kumtaka.
Erica alirudi ofisini akiwa hana raha kabisa, James alimuita na kumuuliza kuwa imekuwaje alipotoka maana alimdanganya kuwa anaenda hospitali,
“Mbona unaonekana huna furaha?”
“Hamna mbona nipo kawaida tu”
“Erica, nakufahamu wewe pengine kupita hata unavyojifahamu au umeanza tena kumuwaza Yule mwanaume wako?”
“Hapana”
Kisha Erica akaenda kuendelea na kazi zake ila muda huo ndio alianza kumfikiria Erick sasa, alitamani kujua Erick anaendeleaje, aliinuka na kutoka nje kisha kupiga ile namba aliyopewa usiku, ila alipopiga aliambiwa kuwa Erick aliruhusiwa kurudi nyumbani na aliendelea vizuri, muda huo Erica aliamua kupiga namba ya Erick, na kweli iliita na kumfanya afurahi sana kisha Erick akapokea simu,
“Unaendeleaje Erick?”
“Salama kabisa, unanijali hadi kunijulia hali!”
“Ndio nakujali Erick”
“Hivi kweli unanipenda Erica?”
“Ndio nakupenda sana Erick”
Muda huo kumbe James alikuwa nyuma ya Erica kwahiyo lile neno la mwisho alilosema Erica alilisikia vizuri sana, akamfokea Erica hadi akaangusha simu
“Yani unaacha kufanya kazi unaanza kuongea maswala ya mapenzi ofisini? Haya Erica, nifate ofisini kwangu”
Erica aliinama kuokota simu yake kisha akamfata nyuma James kuelekea ofisini kwake ila kwa mara ya kwanza aliweza kuona sura ya James ikichukia sana na kuonyesha hasira za waziwazi, Erica alipofika James alianza kuongea,
“Erica, kipi kimekufanya uwepo hapa ofisini?”
“Ni kazi bosi”
“Sasa kazi ya kuongea na simu na kumwambia mtu unampenda ndio iliyokuleta hapa ofisini?”
“Nisamehe bosi”
“Aaah umenikera sana, mimi napenda kazi, muda wa kazi fanya kazi, na muda wa madudu yako huko fanya madudu sikuzuii ila sio ofisini kwangu. Erica katika wafanyakazi wangu umekuwa namba moja kuomba udhuru mara leo sijui imekuwaje, mara nampeleka mtoto kliniki, mara naenda kumfungulia mtoto akaunti, mara tumbo linaniuma siji, mara naenda hospitali yani umefanya kama ofisi hii ni ofisi ya baba yako sasa yani unafanya unavyotaka wewe na sio anavyotaka mwenye ofisi. Ushemeji wa mimi na wewe unaishia nyumbani lakini sio ofisini, ndiomana watu huwa hawaajili ndugu zao sababu ya mambo kama haya yani kazi haziendi na ndugu akitoa taarifa lazima umsikilize hata kama hiyo taarifa ni uongo. Nimekuvumilia sana Erica, na sasa naomba nikwambie kuwa nimekusimamisha kazi”
“Jamani shemeji nihurumie”
“Nishakwambia, ushemeji ni nyumbani, ila nikiwa ofisini sina ushemeji na wewe. Yani uharibu kazi zangu kwa dhana ya ushemeji? Kuna umuhimu gani wa kumuajiri mtu asiyejielewa kama wewe? Yani huna akili hata kidogo, unabebwa ila hubebeki, unataka ufanyiwe nini ubebeke? Erica, nishafanya upande wangu hata Mungu mwenyewe anaona ila kwasasa nimechoka, na ninamaanisha kuwa nimekusimamisha kazi”
Erica akapiga magoti kwa shemeji yake huku akilia na kuzidi kuomba msamaha,
“Naomba unisamehe bosi, haitajirudia tena”
“Mwambie huyo uliyekuwa unamwambia kuwa unampenda sana akutafutie kazi ila kwangu umesimamishwa kwasasa, mpaka pale nitakapoamua mimi kukurudisha tena kazini”
Erica alikazana kuomba msamaha ila shemeji yake alishaamua kwani alichukizwa sana na ile simu ya Erica ya kusema ‘nakupenda sana Erick’ yani muda wote alijikuta hilo neno likiimba kwenye kichwa chake kama mziki, kwahiyo hakuweza tena kuendelea kumuona Erica hapo ofisini, kwahiyo Erica ilibidi ainuke na kwenda kuweka sawa kazi zake kisha kudhikabidhi na kuondoka.
Alikuwa na mawazo sana, alihisi kama kichwa chake kitavurugika tena maana hakujua kuwa amekosa kazi atafanya nini tena, maana lile swala la kwenda kazini tu lilikuwa likifariji moyo wake.
Akiwa kwenye daladala alichukua simu yake na kuiangalia, aliiona kioo hakitamaniki kabisa maana aliiangusha sana na kumfanya akose raha zaidi ila akaiwasha na ikawaka, akaona ni vyema imewaka ingawa imevunjika kioo ila swala la kuwaka lilikuwa ni bora kwake maana hakutaka kutumia hela yoyote ya mtoto wake kwaajili ya kununua simu ukizingatia kazi tena ndio ilikuwa basi, sasa akianza kujiendekeza kutumia hela za mtoto itakuwaje? Alishukuru tu vile simu inawaka.
 
SEHEMU YA 262

Alifika nyumbani kwao hata mama yake alishangaa jinsi mwanae alivyowahi sana siku hiyo,
“Mbona leo mapema zaidi?”
“Mama nimesimamishwa kazi”
“Kheee James kakusimamisha kazi au nini?”
“Ndio”
“Chanzo nini?”
“Alinikuta naongea na simu”
“Wewe nae, unaongea na simu ofisini jamani! Hata hivyo simu tu ndio usimamishwe kazi! Ni kawaida yako kuongea na simu au?”
“Halafu mama sikuongea ofisini, nilitoka nje kumbe na yeye alikuja nyuma yangu na akanisikia kuwa naongea na simu ndio balaa”
“Mmmh ngoja ninyamaze mie nisiongee sana maana sizijui sharia za hiyo ofisi ila kuongea na simu mara moja tu jamani loh! Tulia mwanangu, haikuwa ridhiki yako, kuna mahali Mungu kakuandikia, hata usiwe na mawazo sana. Si unaniona mama yako eeeh! Nimekuwa mpole siku hizi, sitaki tena kufanya makosa ya mwanzo kwako mwanangu, nahitaji ukae kwenye mstari ulionyooka. Tulia mwanangu, kama ridhiki yako ipo basi ipo tu”
“Asante mama”
Kisha Erica alienda chumbani kwake, kwavile alihisi kama kuvurugwa vurugwa akaamua kulala.
Ilikuwa jioni sana akastuliwa na mlio wa simu yake, kuangalia mpigaji alikuwa ni Erick, akapokea na kuongea nae,
“Mbona muda ule ulikata simu gafla Erica?”
“Aaah muda ule, aaah simu iliniponyoka ikaanguka”
“Aaah pole, haijaharibika kweli!”
“Imevunjika kioo tu, ila sio sana”
“Pole sana Erica, unafanya nini muda huu?”
“Nimejilaza tu”
“Mwanetu yuko wapi?”
Erica alijihisi fahari sana baada ya Erick kumuita mtoto wa Erica mwanetu kwamaana hiyo Erick alikuwa amemkubali mtoto wa Erica, alijibu kwa furaha sana,
“Yupo kwa bibi yake”
“Aaah sawa, haya pumzika mama. Nitakutafuta tena. Msalimie sana mtoto wetu”
Kisha Erick alikata simu ila kwenye moyo wa Erica ilikuwa ni furaha sana maana hakutarajia kama ingekuwa rahisi vile kwa Erick kumkubali Angel, alijikuta akisema,
“Kweli kabisa ukweli humuweka mtu huru, na ukisema ukweli Mungu nae atakusimamia. Kwakweli Mungu kanisimamia ingawa nilitoa ukweli wa kuumiza ila mungu kanisimamia. Asante Mungu”
Erica aliinuka sasa na kwenda kumchukua mtoto kwa mama yake kisha kuendelea na mambo mengine mpaka muda wa kulala.
 
SEHEMU YA 263

Kulipokucha aliendelea na shughuli zake zingine, ila alipochukua simu yake alikuta kuna ujumbe kutoka kwa Dora,
“Erica, nakuomba mara moja. Njoo nyumbani”
Kwavile mwenzie alikuwa anaumwa, Erica aliamua kwenda kumuaga mama yake kwanza ili apate ruhusa ya kwenda,
“Haya, kazi umesimamishwa. Unaenda wapi? Ndio kutafuta kazi nyingine?”
“Hapana mama, kuna rafiki yangu anaumwa ndio niende kumuona”
“Na uwahi kurudi sio maswala ya kunirudia usiku hapa wakati haupo kazini”
“Sawa mama”
Kisha Erica akamaliza shughuli zake na kwenye mida ya saa sita alijiandaa na akaondoka zake kwenda kwakina Dora.
Alifika na kumkuta leo Dora kachangamka tofauti na ile juzi aliyofika kumuona, akamuuliza kama anaendeleaje na Dora alimwambia kuwa anaendelea vizuri kabisa.
“Ila nilichokuitia hapa ni yale yale, nakuomba msaada Erica, nahitaji kupata haki yangu. Wewe ndio shahidi pekee uliyebaki, unajua nimeenda kwenye ile hoteli tuliyoenda kula kuku wamenikana kabisa, hata Yule muhudumu aliyetuhudumia nikawa namkumbusha hadi matukio yaw ewe kukataa pombe na kutaka soda ila amenikana kabisa na kusema hajawahi kuniona na hawezi kutoa ushahidi kwenye kesi za uongo. Nimeenda kule club ila napo wamenikana kabisa, hapa pale tulipoenda kulala na shemeji yako wamenikana. Jamanai Erica najua watu hawa wamepewa pesa ndiomana hawawezi kuwa upande wangu, sasa mtetezi wangu umebaki wewe tu”
“Dora, samahani yani mpaka hivi sasa kesi yenu bado inanipa maswali mengi maana wewe unavyonielezea vingine na shemeji nae anavyonielezea vingine”
“Anasemaje kwani?”
Erica akaanza kumuelezea vile ambavyo ameelezewa na James, ila ambacho hakumwambia ni kuwa tu James amesema kuwa ana sura nzito, yani hilo ndio hakumgusia ila yote aliyoelezewa na James alimwambia.
“Khaaa Erica, Yule shemeji yako ni muuwaji jamani, yani ametunga story kiasi hiko? Sikatai kweli napenda kunywa ndio nibaki kunywa peke yangu? Na je ni nanai aliyekuwa ananinunulia pombe? Erica nilikuwa na akili zangu timamu hadi tunaingia chumbani naelewa ila ndio nikalala sababu ya pombe na shemeji yako akatumia mwanya huo kunifanya vibaya na kwenda kunitupa. Au alijua nimekufa kwahiyo alinitupa ili kuepuka ushahidi? Hapana kwakweli shemeji yako mtu mbaya sana.”
Muda kidogo Dora aliitwa nje kwahiyo alitoka na kumuacha Erica pale ndani, kwakweli Erica bado alijiuliza maswali bila ya jibu, ukumbuke kashamuudhi shemeji yake ofisini halafu asimame kwenye kesi amtetee Dora si atachukiwa zaidi tena sio na shemeji yake tu bali hata dada yake atamchukia maana Yule ni mume wake.
Wakati akitafakari hayo, kuna ujumbe uliingi kwenye simu yake, alipouangalia ulikuwa unatoka kwa mzee Jimmy,
“Hujambo binti mzuri Erica, naomba leo tuonane jioni saa kumi. Kuna mambo nahitaji kuongea na wewe kabla ya kesho kusaini mkataba”
Erica aliguna na kushindwa kujibu huo ujumbe kabisa kwani alihisi kama unamuongezea mawazo tu. Alikaa kimya kwa muda, ila akapokea ujumbe mwingine toka kwa mzee Jimmy,
“Mbona hujanijibu mtoto mzuri? Juwa bila mimi hakuna chochote kinachoweza kufanyika, nahitaji kuongea nawe maswala ya biashara. Unajua kama hii ya mwanao kuwa balozi ni swala la biashara? Basi kutana na mimi tujadiliane maswala haya, nijibu tafadhari”
Erica alikuwa kimya tu maana hakujua kuwa ni kitu gani amjibu maana aliona akimchanganya tu, Dora akarudi ndani na kuanza kuongea na rafiki yake
“Yani kuna watu wana mambo ya ajabu sana, unajua mimi nilipopatwa na matatizo juzi basi nilipelekwa kwanza kwa mamangu mdogo halafu ndio kuletwa nyumbani kwahiyo mamdogo anajua kila kitu kilichonipata. Jamani mwanamke Yule unajua kanitangazia kwa watu yani mpaka anawaambia msimuone hajaenda kazini ana majanga ya kubakwa, jamani kweli kabisa huyo ni ndugu au muuwaji?”
“Pole mwaya, ila si mamako mdogo kabisa huyo?”
“Ndio ila ni mbeya balaa hadi kwenye ukoo wanamtengaga sababu ya umbea, sasa kunitangazia mimi nimebakwa ndio anapata faida gani sasa? Kunichafulia jina tu mtaani hapa, halafu huyo shemeji yako ajiangalie. Erica ngoja nikwambie kitu, nikishindwa kwenye kesi mimi, huyo shemeji yako nitamuendea hata kwa mganga, kama amezoea kusumbua wengine basi sio mimi”
“Kheee Dora, bado una imani za waganga tu?”
“Hebu na wewe nitolee maswali ya kijinga huko, kuna mtu kwenye dunia hii haendi kwa mganga? Wewe mwenyewe na familia yako mnaendaga ila mmefanya siri.”
“Mmmmh kwahiyo hata kaka yangu ungemroga wewe eeeh!”
“Ningeamua hata nisingeshindwa sema kwavile kaka yako mwenyewe ana hela za mawazo wala siwezi kujisumbua, ila angekuwa dizaini ninayotaka mimi ningemroga ndio kwanini nikufiche? Watu wanaroga huko na wanafanikiwa, maisha haya bila kujikinga kinga ni ngumu kufanikiwa”
“Mmmmh leo umeniambia makubwa Dora, hata sikukufikiria. Ila kiukweli mimi sijawahi kwenda kwa waganga toka nizaliwe hata sijui kukoje”
“Basi siku nikupeleke”
“Hapana shoga yangu, mimi namuamini Mungu tu”
“Ambaye hamuamini Mungu nani? Hao waganga wenyewe wanamuamini Mungu, yani usijidanganye kuwa waganga hawana Mungu, hata wao wanamuamini Mungu ndiomana wapo”
“Mmmh haya rafiki yangu, ila kwa hilo nimekushindwa tabia”
“Hebu acha ujinga na wewe Erica jamani”
Muda huo simu ya Erick ilikuwa ikiita anaikata sababu mpigaji alikuwa ni mzee Jimmy na hakuwa tayari kuongea nae ingawa hata hakujua hatma ya mwanae na swala la kuwa nalozi wa benki. Kisha Erica aliamua kumuaga rafiki yake ila bado Dora alimsisitizia kuwa akamtetee mahakamani siku ya kesi, Erica alimpa moyo Dora kuwa ataenda ila kiukweli Erica alianza kukata tamaa ya kwenda kwenye kesi kabisa, na vile mwenzie alivyosema maswala ya kwa mganga ndio yakamvuruga kabisa.
Basi Dora akaamua kujiandaa vizuri ili kumsindikiza Erica maana leo alidai kuwa na nguvu kabisa tofauti na siku ile alikuwa na maumivu.
 
SEHEMU YA 264


Basi wakawa wanatembea njiani wakielekea kituoni, gafla kuna gari ilikuja na kusimama mbele yao, kioo kiliposhushwa ni mzee Jimmy ambapo alimsalimia Erica,
“Hellow Erica”
Dora alimwambia Erica kwa sauti ya chinichini,
“Erica wewe matawi, hadi unafahamika na huyu mzee”
Erica alimuangalia Yule mzee na kuitikia salamu yake kisha akamuamkia, Yule mzee akamuitikia na kumuuliza,
“Mbona hupokei simu zangu?”
“Simu yangu imeharibika spika”
“Aaah si ungeniandikia hata ujumbe, twende basi kwenye mazungumzo”
Erica hakushindwa kujitetea hapo ila akamwambia Dora kuwa waende wote, yani Dora kwa Yule mzee alijikuta akisahau kabisa mambo yaliyompata na kukubali kuongozana na Erica.
“Nipo na huyu sasa itakuwaje?”
“Basi, twendeni wote”
Basi wote wakaingia kwenye gari ya mzee Jimmy na safari ikaanza, moja kwa moja walifika mjini kwenye duka kubwa la simu kisha Erica akaambiwa achague simu anayoitaka, Erica alisema yoyote, Yule mzee akachagua simu na kulipa pale milioni moja keshi kisha Erica akakabidhiwa ile simu, alimshukuru Yule mzee na kuwataka warudi tena kwenye gari kisha safari ikaendelea hadi kwenye hoteli Fulani ambapo walishuka na kukaa mahali kisha Yule mzee aliwaambia waagize vinywaji halafu yeye aliinuka kama kuna mtu anaenda kuongea nae. Waliagiza vinywaji, kisha Dora alimuangalia Erica na kumwambia,
“Unajua Erica una bahati sana, huyu mzee umemjuaje?”
“Tena nilimjua siku ileile niliyotoka kwenu alitaka kunipa lifti kwa gari yake”
“Aaah rafiki yangu una bahati, umeogea mpendwa pendwa nini?”
“Ndio nini?”
“Aaah tuachane na hayo, ila rafiki yangu una bahati. Jamani mzee tajiri huyu, ni ana hela uchafu halafu hana hata familia ya kumuumiza kichwa maana watoto wake wote wakibwa, ni ana watoto wawili tu. Mzee ana hela huyu Erica, uwiii yani huyu unamwambia akujengee nyumba tena anakujengea ya kifahari, unamwambia akununulie gari, anakununulia gari la kifahari, unamwambia nifungulie ofisi yani ukiwa na huyu mzee hata kazi kwa shemeji yako unaacha”
“Dora, umejuaje habari za huyu mzee?”
“Namfahamu huyu mzee ni tajari hapana”
“Watoto wake wako wapi?”
“Sijui, sijawahi kuwaona nasikia wana malingo sana. Sitaki kuwafahamu ila baba yao ni hatari, mzee tajiri huyu Erica. Kama anakutaka wala usijifikirie mkubali upesi”
“Mmmh kwakweli mimi nina mwanaume wangu nampenda sana anaitwa Erick”
“Na wewe Erica unaleta habari za vijana, ulisikia wapi vijana wakawa na mapenzi ya kweli? Kitu wazee wanajua kupenda, wanajua kuhonga yani hadi raha. Erica kweli rafiki yangu kama huyu mzee anakutaka usimkatae”
Muda kidogo mzee Jimmy akarudi na kuanza kuongea nao,
“Mbona mmeagiza juisi tu!”
Dora akacheka na kutaka kuagiza pombe ila Erica aliwahi na kumwambia mzee Jimmy,
“Huwa hatutumii vileo ndiomana tumeagiza juisi”
“Aaah vizuri lakini”
Kisha mzee Jimmy alianza kuongea pale pale tena bila hata ya kumuhofia Dora,
“Sasa Erica, mwanao unahitaji awe balozi wa benki yetu. Mimi ndio mkurugenzi mkuu wa benki ile, kama ukifanya ninavyotaka mimi basi mkataba wa mwanao dau lake litakuwa mara tatu ya lilivyo sasa.”
Erica alikuwa kimya huku akiinama chini na kujiuliza kuwa Yule mzee anataka mambo gani tena, kisha Yule mzee akaendelea kuongea,
“Sijaona shida ya kuongea mbele ya rafiki yako, binti unaitwa nani kwanza”
Dora bila hiyana alitaja jina lake upesi upesi,
“Naitwa Dora”
“Unanifahamu mimi?”
“Nakufahamu ndio hadi nyumbani kwako”
“Sawa, basi vizuri. Sasa Dora, nadhani unajua kuwa kila mwanadamu kaumbwa na kitu cha muhimu sana, kila mwanadamu kaumbwa na hisia. Rafiki yako nampenda na sijaona shida yoyote ya kuongea hivi mbele yako”
Erica alihisi moyo wake ukienda mbio kwani alizidi kuona kama huyu mzee hana nia njema kwake, kisha Yule mzee akamtazama tena Erica na kumwambia.
“Erica, huwa sinaga tabia ya kupindisha pindisha maneno yangu. Mimi nakutaka, kama utakubali kuwa name siku zote sawa ila kama hutaki kuwa name siku zote basi naomba kwa leo tu unipe hilo tunda lako hakika moyo wangu utafarijika”
“Hapana kwakweli, sipo tayari kwa chochote”
Dora akamkata jicho Erica na kumfinya kidogo, Erica alimuangalia Dora na kusema tena,
“Namaanisha nisemayo Dora, sipo tayari”
Yule mzee Jimmy alimuangalia Erica kisha akasema,
“Erica nakupa muda ujifikirire kuhusu swala hilo, naenda kuongea na muhudumu wa chumba, hatuchukui muda mrefu ni dakika tano tu. Ilimradi roho yangu isuuzike”
Kisha Yule mzee akasimama na kuondoka, Dora akamuangalia Erica na kumwambia,
“Erica usiwe mjinga, kwa huyu mzee ni hela nje nje, hutaki bahati wewe? Watu wengine mkoje? Yani unapewa bahati hutaki, ona mzee wa watu alipita kukununulia hadi simu tena ya gharama ila bado unaleta ubishi wa kulala nae mara moja tu! Kwani anaondoka nayo?”
“Ingekuwa tatizo ni kuondoka nayo nadhani hata wewe usingekuwa unalalamika kubakwa na shemeji, ila tatizo ni utu na heshima. Yule mzee ni sawa na mzazi wangu, hata hivyo nina mpenzi wangu nampenda sana. Siwezi tena kufanya makosa ya namna hii, kama shida ni simu hii hapa akifika mpe”
Erica alimpa Dora ile simu kisha yeye akainuka na kuondoka zake, Dora alijaribu kumsihi asiondoke ila Erica hakusikiliza usia wa Dora, alitoka nje ya ile hoteli na kusimamisha bodaboda kisha kuondoka nayo.
 
SEHEMU YA 265


Erica aliondoka hadi stendi kisha kupanda daladala na kuelekea kwao, ambapo alifika kwao na kumkuta mama yake amekaa na Angel kisha akaanza kumlalamikia,
“Erica kweli kwenda kumuangalia rafiki yako hadi muda huu mwanangu? Unajua sipendi upatwe na matatizo?”
“Nisamehe mama, haitajirudia tena”
“Kwenye kuomba msamaha ni mwepesi hatari ila mambo unayoyafanya hayaendani na msamaha unaoomba. Ila nimekusamehe, usirudie tena kuchelewa nyumbani”
“Sawa mama”
Erica alienda chumbani kwake ila aliwaza sana kuwa Yule baba kwanini atake kumfanyia vile,
“Jamani au mzee kaathirika Yule anataka wa kwenda naye? Dora nae na ujinga wake hata maumivu ya kubakwa hayajaisha vizuri ila Yule mzee akimtaka analala nae, jamani nilikuwa mjinga nikisaka penzi la kweli ila sio kwa mzee mwenye umri wa mzazi wangu, hapana kwakweli jana mama aliniambia, kama ridhiki yangu ipo ipo tu”
Aliamua kulala tu maana hakutaka hata kuwasiliana na mtu yeyote.
Kesho yake ilikuwa ni Jumamosi siku ambayo aliambiwa kuwa aende kule benki ila alivunjika moyo jana na kusema kuwa hatoenda tena maana Yule mzee asingekubali asaini mkataba ukizingatia alishakataa kutembea nae, kwahiyo aliendelea na kazi zake tu.
Kwenye mida ya saa nne, alipigiwa simu na Yule meneja wa benki,
“Erica habari, mbona hujafika mpaka saa hizi na mtoto?”
Erica akawa anajiuma uma tu maana alishajipa jibu mwenyewe, kisha Yule meneja aliendelea kuongea,
“Fanya haraka ufike na mtoto, wakurugenzi wameshakaa kwenye kikao, ndio nimeitwa na nimeulizwa kuhusu wewe”
“Basi nakuja sasa hivi”
Erica alijiandaa haraka haraka na kumuandaa mwanae, akahisi kuwa labda Yule mzee hawezi kusababisha mwanae asipewe mkataba ndiomana wamemuita tena.
Alipomaliza kujiandaa, kwa bahati mama yake alikuwa ametoka kwahiyo hata yeye ikawa rahisi kwake kujiandaa na kuondoka haraka, aliita gari ya kukodi kisha aliondoka na usafiri huo hadi benki.
Alipofika alishuka na mwanae, ila kabla hajaingia benki alikutana na Babuu akiwa ametoka kwenye ile ile benki,
“Kheee Erica, kumbe huyu ndio mwanao?”
Erica aliitikia kwa aibu tu kuwa Yule ndio mwanae,
“Kheee mbona kafanana fanana na Rahim? Kwahiyo Erica umezaa na Rahim?”
Erica akawa kimya tu, muda huo huo alitoka John kumbe nae alikuwa ndani kwenye benki hiyo, akamkuta pale Erica, Babuu na yule mtoto wa Erica. Naye akashangaa na kusema,
“Huyo mtoto mbona kafanana fanana na Rahim?”
 
SEHEMU YA 266


Alipofika alishuka na mwanae, ila kabla hajaingia benki alikutana na Babuu akiwa ametoka kwenye ile ile benki,
“Kheee Erica, kumbe huyu ndio mwanao?”
Erica aliitikia kwa aibu tu kuwa Yule ndio mwanae,
“Kheee mbona kafanana fanana na Rahim? Kwahiyo Erica umezaa na Rahim?”
Erica akawa kimya tu, muda huo huo alitoka John kumbe nae alikuwa ndani kwenye benki hiyo, akamkuta pale Erica, Babuu na yule mtoto wa Erica. Naye akashangaa na kusema,
“Huyo mtoto mbona kafanana fanana na Rahim?”
Erica alikuwa akiangalia chini tu, John akamtazama Erica na kumsalimia
“Mambo Erica”
Erica akajibu,
“Poa”
kisha John akauliza vizuri,
“Kwani mtoto wa nani huyu?”
Babuu akamtazama John na kumuuliza,
“Kumbe unamfahamu Erica?”
“Ndio namfahamu, alikuwa ni msichana wa kwanza kumpenda. Nilimpenda sana msichana huyu”
“Kheee Erica, ndugu wawili sasa tumekutana kwenye mlolongo mmoja. Haya sasa, mtoto huyu kufanana na Rahim ni wake?”
John akamuuliza Babuu kwa mshangao,
“Sijakuelewa Babuu, unamaanisha nini?”
Erica akaona hawa watu watamchanganya akili ni watafanya achelewe kuingia ndani, akaachana nao pale nje akambeba mwanae na kuingia zake ndani ya benki, hakutaka kujua nyuma walijadili vitu gani ila tu alijua kama angeendelea kusikiliza hoja zao basi angechanganyikiwa kabisa. Walijaribu kumuita ila kwavile Erica alishadhamiria kutokuendelea kusikiliza hoja zao ikabidi aingie zake ndani ya benki.

Alivyofika alienda kwenye ofisi ya meneja moja kwa moja ambapo wafanyakazi wa pale walionyesha kufurahi sana walipomuona mtoto wa Erica kwa macho yani mubashara na sio kwa picha tena.
Alifika ofisini kisha meneja akamkaribisha na Erica kukaa na mtoto wake, Yule meneja alitabasamu na kumsifia mtoto wa Erica,
“Kwa hakika huyu mtoto anastahili kuitwa jina ulilomuita, yani una mtoto mzuri sana hongera”
“Asante”
Erica alikuwa akitabasamu kisha Yule meneja aliendelea kuongea,
“Ila hata wewe ni mzuri, naona huyu mtoto kachukua uzuri wako, sasa yeye na ushombeshombe ndio kazidi uzuri”
Erica alikuwa akitabasamu tu ila muda huo alikuwa akisubiri kupewa mkataba wa kusaini kwaajili ya mtoto wake maana alihisi itakuwa rahisi kama kule dukani. Kisha meneja akamwambia tena,
“Erica, sijui umechelewa wapi wakati ntulipanga tangu saa nne! Muda ule nakupigia simu, wakurugenzi walikuwa kwenye kikao yani sijui unechelewea wapi ila hakijaharibika kitu, Mkurugenzi mkuu amenipa hii bahasha amesema ukifika nikupatie maana ina maelekezo humo na kasema wiki ijayo ndio uje na mtoto maana wenyewe kuna mahali wameenda.”
Yule meneja akamkabidhi Erica ile bahasha ambapo Erica alijiuliza kama apokee ile bahasha au afanyaje, na akaona asipopokea lazima Yule meneja atajua kuwa kuna kitu hapo, ikabidi apokee tu na kumuaga Yule meneja.
Kisha akatoka na kuwaaga wale wengine, alipofika nje alishukuru kuona John na Babuu walishaondoka kwahiyo ilikuwa furaha kwake maana hakutaka tena mtu wa kumuumiza kichwa, kisha akapanda gari na mwanae na kuondoka kurudi kwao.
 
SEHEMU YA 267


Alifika nyumbani ambapo mama yake alikuwa bado hajarudi, Erica alikaa sebleni na kufungua ile bahasha, kwanza kabisa ilitoka ile simu ya jana ambayo alinunuliwa na mzee Jimmy,
“Uwiii Mungu wangu yani ile simu kanipa tena!”
Akaendelea kufungua na kukuta kuna bahasha ndogo, akaichukua na kufungua hela zikaanguka kutoka kwenye ile bahasha, mwanae alikuwa anacheza cheza ila kuona zile hela akaenda kuziokota na kuanza kuzichezea,
“Wewe Angel, acha hela hizo”
Mtoto bado alikuwa akichezea zile hela yani kwenye ile bahasha hapakuwa na kitu kingine zaidi ya zile hela na simu, wakati akimwambia mwanae aache zile hela, mama yake aliingia na kushangaa,
“Kheee hela zote hizo Erica umezitoa wapi?”
Erica akamnyang’anya kwanza mtoto zile hela huku akijifikiria namna ya kumjibu mama yake maana hata hakujua kama alitoka siku hiyo, alipomaliza kuziokota mama yake akamuuliza tena,
“Erica, hizo hela umezitoa wapi?”
“Mama, subiri nikwambie. Kuna mbaba mmoja huwa ananitongoza ila nimemkataa ila leo nimeshangaa kamtuma kijana alete bahasha kwangu, yani Yule kijana kaja kagonga geti na kunipa hii bahasha kisha akasema imetoka kwa mzee Jimmy, ndio nimeichukua kufungua ndio nikaona hiyo simu halafu kulikuwa na bahasha nyingine ndani ndio kulikuwa na hizo hela”
“Kheee huyo mzee ana maana gani? Hebu lete hiyo simu niione”
Erica akampa mama yake ile simu, mama yake akahamaki sana,
“Hizi simu si ndio wanazisema za gharama sana, jamani huyo mzee anataka nini kwako mwanangu?”
“Sijui mama”
“Hebu hesabu na hizo hela”
Erica akaanza kuhesabu zile hela na kumwambia mama yake,
“Ni milioni mbili mama”
“Kheeee mbona makubwa haya, yani mtu akupe simu ya gharama hivi na pesa zote hizo, anataka nini huyo mzee jamani? Hao ndio wenye mpango mbaya na watoto wetu, huwa sipendi ujinga wa namna hiyo kabisa, huo ni ujinga. Anatuona sisi tuna dhiki sana eeeh kwahiyo anataka kukuteka kwa hela zake, umesema alimtuma kijana kuja hapa?”
“Ndio mama”
“Dah! Hebu nipe hivyo vitu kwanza, akikutafuta utaniambia amesemaje maana najua lazima akutafute”
Erica alirudisha zile hela kwenye bahasha na simu kwenye ile bahasha kubwa kisha akampa mama yake, ambapo mama yake alionekana kuchanganywa nay ale mambo kabisa kwani alienda chumbani kwake na ile bahasha bila kusema chochote.
Erica alienda chumbani na mwanae, akajilaumu sana kufungua ile bahasha sebleni,
“Zile hela si ningeenda kuweka kwenye akaunti ya mwanangu jamani, mama naye loh! Kama hajasema turudishe sijui maana mama ana sheria huyu balaa”
Akawaza ila akaendelea na mambo mengine.
 
SEHEMU YA 268

Jioni ilipofika, Erica akapokea ujumbe kutoka kwa mzee Jimmy,
“Natumaini zawadi zangu umezipata na umezipenda, sasa hiyo ni rasharasha tu, mvua yenyewe itakuja. Naomba tukutane kwenye ile hoteli ya juzi, nina hamu sana na wewe binti yangu. Njoo kwenye mida ya saa mbili usiku”
Erica alifikiria sana akasema,
“Hivi huyu mzee ana akili kweli, si nimemwambia kuwa nimeolewa sasa ataanzaje kusema kuwa tukutane kwenye hiyo hoteli? Mmmh mambo haya ni makubwa, ngoja nikamwambie mama tu”
Erica akaenda kumueleza mama yake na kumuonyesha ule ujumbe, mama yake alisikitika sana,
“Inamaana Erica, ushawahi kulala na huyo mzee?”
“Hapana mama”
“Na kwanini aseme tukutane kwenye hoteli ya juzi? Kumbe ndiomana juzi ulichelewa nyumbani?”
“Hapana mama, sijawahi kulala nae”
“Hizi laana hapana sizitaki katika maisha yangu umesikia eeeh! Huwa namuomba Mungu mwanangu upate mume wa kukuoa, mume mwenye akili timamu na mapenzi ya dhati, mume mwenye hofu ya Mungu. Sijamuomba Mungu upate mababa ya kukuingiza majaribuni, sasa jiandae twende huko hotelini”
“Jamani mama”
“Hakuna cha jamani, usiniletee ujinga kabisa mimi, sijakulea kijinga hivi.”
Ikabidi Erica aende kujiandaa na kumuandaa mtoto wake, kisha mama yake alimuita yani alishajiandaa huyu mama na kumwambia Erica aite gari linalompelekaga liwapeleke,
“Sasa mama, mwenye gari atataka pesa”
“Nitamlipa bhana, sitaki ujinga ujue, mambo ya kijinga namna hii siyataki na siku nyingine mizigo ya kijinga hivi usipokee”
Kisha Erica akaita ile gari na kupanda na mama yake hadi kwenye ile hoteli kisha mama yake akamwambia Erica apeleke mzigo ule mapokezi na awaambie wampatie Yule mzee akifika, Erica alienda kupeleka huku mama yake akimuangalia kwa makini akimkabidhi Yule wa mapokezi na kusainishana kisha Erica kurudi kwa mama yake na kupanda tena gari kurudi nyumbani.
Walipofika mtoto wa Erica alikuwa kashalala, mama yake akamwambia kuwa akamlaze mtoto halafu yeye aende aongee nae, alivyomlaza alirudi sebleni na kumsikiliza mama yake,
“Sikia Erica, kipindi nakuzaa kila mtu alikupenda sana, yani ulikuwa mtoto wa pekee kwangu na wala sikutegemea kama ingetokea ungezaa nje ya ndoa maana nilijua ungeolewa kwanza ndio ungezaa ila haikuwa hivyo, basi nimekubaliana na matokeo lakini sio kwa stahili hii ambayo inaendelea sasa, Erica sina hela ila nimetumia hela yangu kurudisha mizigo ya huyo firauni maana najua wanaume wanaotumiaga hela hivi wana lengo gani, siku zote hawana lengo jema. Kama mtu ana lengo jema, kwanini asiseme nipeleke kwa wazazi wako nijitambulishe nikuoe, kwani tatizo liko wapi kama hela anazo! Ila anazitumia hela hizo kukuchimbia kaburi, halafu licha ya hivyo, ushasema huyo ni mtu mzima lazima ana familia yake, anaicha na nani familia yake hadi kuja kwako? Huwa sipendagi ujinga wa namna hii kabisa, siku nyingine wakikuletea waambie warudishe walipoutoa, maana pesa zina haribu sana fikra za watu najua hata huyo aliyekupa mimba ulimvumilia sababu ya pesa, pengine hata ulijua kuwa matendo yake hayafai ila pesa ikakuzugisha. Mwanangu jifunze kumsoma mtu kabla ya matatizo hayajakutokea, huu ujinga siutaki tena katika nyumba yangu”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Sio kunielewa tu, fanyia kazi nilichosema”
“Sawa mama”
Basi Erica akaagana na mama yake na kwenda kulala, alisikia simu yake ikiita ila hakuipokea wala kuiangalia maana alijua ni Yule mzee anapiga, na hakutaka kuongea nae kabisa maana kwa muda huo alitaka kumuwaza Erick tu maana ndio alianza kumuamini kuwa ni mwanaume anayempenda kweli.
 
SEHEMU YA 269


Kulipokucha akachukua simu yake na kuangalia, akakuta aliyekuwa anapiga ni Erick, akajisikia vibaya sana, na kuamua kwenda kutafuta vocha ili ampigie.
Akajiandaa kwaajili ya kutoka, ila mama yake akamuuliza,
“Erica, asubuhi yote hii? Unaenda wapi?”
“Naenda dukanini mama kununua vocha”
“Aaah chukua chupa basi, na mimi ukaninunulie soda”
Basi Erica akachukua na chupa kisha kuondoka, alifika dukani na kununua vocha ila lile duka hakupata soda ambayo mama yake alikuwa amemuagiza ikabidi aende kwenye duka lingine la barabarani.
Wakati yupo pale dukani akinunua soda aliyoagizwa, alifika mama wa makamo kwenye gari, alisimamisha gari yake na kuomba achukuliwe maji dukani, ikabidi Erica amchukulie na kumpatia, Yule mama akamshukuru sana Erica na kumuuliza,
“Unaitwa nani binti?”
“Naitwa Erica”
“Wow, jina zuri sana. Nimekupenda bure, una moyo wa kipekee maana nilikuwa naona uvivu haswaa kushuka kwenye gari na kuagiza maji, halafu mwenye duka nae ana wateja wengi ila wewe na huruma yako umenichukulia maji dukani na kuniletea, asante sana”
“Usijali”
“Basi kama hutojali binti, naomba namba yako”
Erica akampa Yule mama namba yake kisha kuagana nae, halafu Yule mama akaondoa gari yake na kuondoka zake, Erica akachukua soda dukani na kurudi kwao.
Mama yake alimuuliza kwanini kachelewa,
“Sikukuta soda uliyoniagiza duka la karibu ilibidi niende maduka yale ya barabarani mama”
“Nikajua umeanza tena mambo yako ya kukutana na wazee”
Basi Erica aliingia chumbani kwake na kuweka vocha kisha kutaka kumpigia Erick, ila kabla hajapiga kwa Erick, simu yake ikaita na mpigaji alikuwa Erick kwahiyo alivyokuwa anawaza kumpigia Erick ndivyo Erick nae alivyokuwa anampigia, kwahiyo hilo swala lilifanya moyo wa Erica kujawa tabasamu,
“Erica, mbona jana usiku hukupokea simu yangu?”
“Nilikuwa nimelala ndiomana”
“Basi badae nitakupigia, kuna mambo nahitaji tuongee”
“Sawa, hakuna tatizo”
Kisha Erick akakata simu na kumuacha Erica akibaki na tabasamu tu, gafla akapokea ujumbe kutoka kwa mzee Jimmy,
“Erica, sijapenda kurudisha zawadi ambazo nimekupatia yani sijapenda kabisa”
Erica hakujisumbua kujibu huo ujumbe wala nini, kisha mamake akamuita na kumuaga kuwa anaenda kanisani, kama kawaida Erica alibaki nyumbani na mwanae maana bado hakupata muhamko wa kwenda kanisani kwani bado hakuwa huru kueleza kuhusu mtoto aliyenaye na ukizingatia kule kanisani kwao walimjua vilivyo.
Wakati yupo nyumbani kwao akapokea ujumbe toka kwa Dora,
“Nakuja kwenu Erica”
Akajua lazima kuna jambo ndiomana Dora anakuja, basi alitulia akimsubiria.
Muda kidogo akapigiwa simu na dada yake Bite, na baada ya salamu dada yake alimuuliza,
“Wewe Erica, umemfanya nini shemeji yako?”
“Jamani dada, sijamfanya kitu chochote, kwani kasemaje?”
“Erica mdogo wangu mbona umekuwa na tabia mbaya kiasi hiki jamani! Kesho nitakuja kuongea na mama”
“Ila dada unanionea hakuna nilichofanya kweli tena”
“Unabebwa hubebeki, unataka mtu afanyaje? Nasikia umeanza urafiki na watu wa ajabu ajabu na kuna mambo umemfanyia shemeji yako, sikutegemea kweli mdogo wangu ungefanya hivi tena kwa shemeji yako mume wa dada yako! Sikutegemea kwakweli”
Bite akakata simu na kufanya Erica abaki na maswali kweli maana hakuna kibaya alichofanya kwa shemeji yake zaidi yay eye kusimamishwa kazi, alishangaa kusikia kibao kinamgeukia, alijiuliza kuwa ni kitu gani hakupata jibu kabisa.
 
SEHEMU YA 270

Baada ya muda Dora alifika kweli, kisha Erica akamkaribisha vizuri tu ndani kwao.
Akamsalimia pale na kuanza kumuuliza maswali mawili matatu kwa kilichotokea juzi,
“Eeeh Dora, uliondoka pale?”
“Erica, naanzaje kuondoka kwa mfano? Ila Erica shoga yangu una bahati jamani sijapata kuona, mwenzio natamani nipate bahati kama zile ila sibahatiki ila wewqe bahati kama ile unaichezea, kweli upele humuota asiye na kucha”
“Sasa Dora, kutakwa na mtu mzima Yule ndio bahati”
“Kwani utu uzima wake unakuathiri nini? Ng’ombe hazeeki maini upo! Halafu watu siku hizi hawaangalii utu uzima wanaangalia pochi”
“Kwahiyo wewe ulitulia tu kumsubiri”
“Sikia Erica, kwavile uliondoka mimi ilibidi nimsubiri mzee wa watu maana nilimuhurumia ukizingatia alisema kuwa ana ugumu, halafu masikini mzee wa watu alishakodi chumba, Erica una dhambi wewe loh! Kwani ungelala nae mara moja tu kingeharibika kitu gani?”
“Hivi Dora unafikiri mimi naweza kusikiliza ushauri wako tena! Labda niwe chizi, wewe ndio ulifanya nikaachana na mpenzi wangu Babuu, wewe ndiye uliyechochea mapenzi ya mimi na George na wewe ndio ukafanya nilale na George wakati unajua wazi anataka mabikira. Unadhani nasahau? Ni kweli nimekusamehe ila kusahau siwezi”
“Mmmh Erica jamani! Basi tuachane na hayo, juzi bhana Yule mzee alinyong’onyea sana nilipomwambia kuwa umeondoka na simu aliyokununulia umeiacha, alipooza hadi nikamuonea huruma, basi nikamwambia nipo mimi nitakuliwaza, akafurahi basi nikaenda nae kwenye chumba alichokodi. Ile hoteli ni nzuri Erica dah nzuri sana, basi bhana jamani Yule mzee nikampa mambo hayo sio ya nchi hii, yani nilitumia ufundi wangu wote kwa kujua kuwa angenipa ile simu aliyokununulia wewe. Ila tulipomaliza cha kushangaza hakunipa ile simu akasema ile simu ni yako na lazima ikufikie, niliumia sana. Basi akatoa pesa, burungutu la fedha, nikajua nimelamba bhana, loh mzee Yule sijaamini amenipa laki tu halafu hela zote karudisha, niliumia halafu akaniambia angekuwa Erica, hizi hela zote ningempa. Jamani Erica una nini mwenzangu na mimi unigawie eeeh! Mbona bahati kama hizi sizipatagi mimi? Ila hata hiyo laki nashukuru maana wanaume wangu akikuhonga laki sijui umfanyie nini ila Yule baba dakika chache tu kanipa laki, ila mihela ile nilikuwa na hamu nayo dah!”
Erica alimuangalia Dora na kumsikitikia kwakweli maana alimuona anaongea kama mtu asiyejitambua, Dora alipoona Erica asemi chochote akamuuliza tena,
“Vipi ile simu alikuletea?”
“Aliniachia bahasha kwenye benki yao, nilipofika nyumbani nilikuta kaweka simu na milioni mbili”
Dora akawaka kwa mshangao,
“Milioni mbili!!”
“Ndio milioni mbili”
“Jamani shoga yangu, naomba kidogo basi”
“Mama aliniona wakati nafungua kwahiyo hela na simu tulirudisha mapokezi kwenye hoteli aliyosema tukutane”
“Yani Erica na mamako mmerudisha hela milioni mbili! Mtakufa masikini nyie, tangu lini hela ikarudishwa?”
“Mama yangu hataki kabisa huo ujinga”
“Uwiii angekuwa mama yangu anavyopenda hela yani ningeozeshwa kwa huyo mzee hata mke wa mbali tu inatosha. Sasa Erica tufanye kitu”
“Kitu gani?”
“Basi kubali kulala na Yule mzee mara moja tu tuuage umasikini”
“Hivi unaakili wewe Dora? Yani unaongea kama uliishia la saba, yani mwanaume umelala nae wewe halafu na mimi nikalale naye inakuja kweli hiyo?”
“Kwani tatizo liko wapi? Mbona George aliwahi kuwa mpenzi wangu na wewe ukalala nae”
“Kuhusu George sikujua maana ulinificha ila sio kuhusu Yule mzee, hata hivyo simtaki kama hela zake akae nazo tu”
“Hivi Erica unajihakikishia nini maisha haya? Kwani Yule mzee akilala na wewe itakuwaje? Ataondoka nayo? Si itabaki kwako kama kawaida? Ningekuwa mimi ndio wewe, ningetumia hii fursa hatari, swala la kusoma nimesoma ndio nikijua nitapata kazi nzuri ila wapi, kazi zenyewe manyanyaso tu halafu mshahara mdogo ila mzee kama Yule anatoa tu hela, jamani Erica tafadhali mkubali Yule mzee”
Mamake Erica aliingia ndani na kuwaka,
“Amkubali nani?”
Kisha akamuangalia vizuri Dora na kusema,
“Khaaa kumbe wewe changudoa ndio umekuja tena kwangu! Haya toka, ondoka upesi sitaki kukuona”
Ikabidi Dora ainuke na kuanza kutoka, Erica akataka kumsindikiza ila mama yake akamkataza,
“Na wewe unataka kwenda wapi? Kalisha makalio yako chini mjinga wewe”
Ilibidi Erica akae kwa kusikiliza maneno ya mama yake, alianza kusema,
“Ndiomana dadako kanipigia simu, jamani Erica umeanza na urafiki na huyu firauni kweli? Ikiwa kweli maneno aliyoniambia dada yako tutaonana wabaya kwakweli”
“Maneno gani hayo mama”
“Umeniudhi sana, ngoja nikapumzike, labda badae nitasema”
Kisha mamake Erica alifunga mlango wa kutoka nje na funguo halafu funguo kwenda nazo chumbani kwake akimaanisha kuwa hataki Erica atoke.

Erica naye aliingia chumbani kwake huku akitafakari jinsi mama yake alivyomtimua Dora, ila hakumlaumu sana maana maneno ya Dora kama mama yake kayasikia vizuri basi ana haki ya kumtimua maana sio maneno ya busara kabisa.
Ilikuwa ni jioni na wakasikia mlango wao ukigongwa, kwa maana hiyo kulikuwa na ugeni, mama Erica alitoka na funguo ili akafungue mlango muda huo Erica naye alikuwa nyuma ya mama yake ili kuchungulia ni nani aliyekuwa anagonga.
Baada ya kufungua mlango, akamsikia mama yake akisema,
“Kheee Mwajuma hadi kwangu kweli!”
Erica alisogea kumuona huyo Mwajuma, alishangaa kumuona Mrs.Peter yani mama yake na Rahim akiwa ameongozana na Babuu.
 
SEHEMU YA 271



Baada ya kufungua mlango, akamsikia mama yake akisema,
“Kheee Mwajuma hadi kwangu kweli!”
Erica alisogea kumuona huyo Mwajuma, alishangaa kumuona Mrs.Peter yani mama yake na Rahim akiwa ameongozana na Babuu.
Alishangaa vile ambavyo mama yake alionekana kumfahamu Mrs.Peter, kisha mama yake aliendelea kuongea pale pale mlangoni kabla hata hajawakaribisha vizuri,
“Eeeeh kilichokuleta nyumbani kwangu ni nini?”
“Kheee tulia mama weee, hata kilichonileta si wewe , nimekuja sababu ya binti yako huyo anayechungulia. Tusiondoleane ladha mapema hivi”
Mamake akageuka na kumuangalia Erica ambaye alisimama tu akiwaangalia na kumuuliza,
“Unawajua hawa?”
“Ndio mama”
Kisha mamake Erica akaachia mlango waingie ndani ila hakuwakaribisha wala nini na ile ilionyesha kwamba hawa watu wana ugomvi wa siku nyingi.
Mrs.Peter alipita na kukaa kwenye kochi, Babuu alimsalimia mama yake Erica na kukaa pia, ila mama yake Erica alikuwa na chuki bado za wazi wazi kabisa, walipokaa alimuuliza tena mrs.Peter,
“Kilichokuleta?”
“Usiniulize mimi, muulize huyo binti yako. Erica mbona unasimama tu, njoo umwambie mama yako kilichotuleta”
Erica akasogea na kusema,
“Karibuni ila hata mimi sijui kilichowaleta”
Mrs.Peter aliwaka kwa msahangao,
“Hujui kilichotuleta? Mtoto mbaya wewe sikutegemea”
Mama Erica akamwambia,
“Weee hakuna mtoto mbaya duniani, usiniitie mwanangu mbaya, uishie hapo hapo na useme kilichokuleta”
“Kwanza usinifikirie vibaya, sijasema mbaya kwa kumaanisha ni mbaya, kila mmoja anajua kuwa Erica ni mzuri hata kichaa akimuona Erica atasema kuwa dada huyu ni mzuri na si kwamba ni msichana wa kujiremba ndio uone uzuri wake hapana ila Erica ni mzuri asilia. Sasa niliposema mbaya sikumaanisha ubaya unaoufikiria wewe, ila alichofanya kwangu ndio kimefanya nimuite mbaya”
“Haya kafanyaje?”
“Erica namfahamu, na sijamfahamu juzi wala jana ni kipindi kirefu sana namfahamu ila mwanao anatumia uzuri wake vibaya, kwanza mtoto muongo huyu yani kazaa na mwanangu halafu kashindwa kuniambia kuwa kazaa na mwanangu kweli? Tena nilikutana nae hadi kliniki akanidanganya kuwa mtoto aliyembeba ni wa dadake kumbe ni mjukuu wangu ila hakutaka nimuone jamani Erica kweli wewe wa kunifanyia hivyo!”
Erica alitazama chini tu kwa aibu kisha Mrs.Peter aliendelea kuongea,
“Yote tisa kumi, yani Erica kumbe umekuwa na mahusiano na wanangu wote kweli? Rahim na John, na licha ya hivyo hata huyu ndugu yao Babuu umekuwa na mahusiano nae, kweli hiyo? Yani uzuri wako ndio unafanya uchanganye ndugu jamani”
Erica alibaki kimya, kisha mamake alimuangalia na kumfokea,
“Hebu njoo ukae hapa, usitusimamie kama mlingoti na useme kama yasemwayo ni ya kweli?”
Erica alienda kukaa kwa aibu ila hakusema chochote, kisha mamake akaendelea,
“Kweli umezaa na mtoto wa huyu mwanamke? Na kweli ulikuwa na mahusiano na watoto wake wote?”
Erica alikuwa kimya tu, kisha Mrs.Peter akaongea,
“Anaona aibu kusema ukweli, ila kaumiza sana mioyo ya watoto wangu, na kama anabisha basi niwalete wote na akatae mbele yao kuwa sikuwa na mahusiano nao. Haya mfano tosha ni huyu Babuu yupo hapa akatae kama hajawahi kuwa na mahusiano nae, na mtoto aliyenaye kazaa na mwanangu Rahim”
Kwakweli Erica aliona amepewa aibu iliyopitiliza maana hakufikiria kama mama yake hata amewaza kuwa mwanae amewahi kuwa na mahusiano na wanaume wengi vile zaidi ya Yule aliyemoa mimba, ila anajielezaje hapo, aliona aibu sana na kushindwa kuongea kabisa ila mama yake alimfokea sana ikabidi aongee,
“Jamani vitu vingine mtanilaumu bure tu, nisameheni bure. Sipendi kuongelea maswala ya hao wanaume labda tuongelee kuhusu mtoto tu”
Mrs.Peter akadakia,
“Kwanza mtoto mwenyewe yuko wapi? Maana kwa mtindo huu usikute hata mwanangu anabambikiwa, familia moja ushatembea na watatu je huko nje? Wewe mtoto ni shimo la taka, usikute wanangu hawa wameona mwarabu mwarabu wakamfananisha na Rahim labda hata sio wa Rahim, kama wanaume ulikuwa nao wengi. Mlete kwanza huyo mtoto nimchunguze kama ni wa mwanangu kweli”
Erica akataka kuinuka akamchukue mtoto maana alikuwa kalala, ila mama yake alimzuia na kusema,
“Weee Erica, kalisha mbaliga zako chini huwa sitaki ujinga mie, mtoto hapa hali, havai, halali au kitu gani mwanao hapati?”
“Anapata kila kitu mama”
“Sikieni, huwa sipendi dharau. Halafu wewe Mwajuma umekuja na kufoka mwanangu muongo sijui hakukwambia kama ana mtoto wa mwanao, ngoja nikuulize swali. Kwanini usimuulize huyo mwanao kama kweli kazaa na Erica? Si ungemuuliza kwanza mwanao upate uhakika, eti mlete mtoto nimchunguze, mjukuu wangu hachunguzwi umesikia eeeh! Tena naomba muondoke kwa amani kabisa, mkiwa na uhakika kuwa ni wa kwenu karibuni ila sio leo ya kumchunguza mwanangu sawa! Mtoto hachunguzwi huyu, Erica tulia hapo mwanangu, hata mimi wanangu hamkuchunguzwa iweje mjukuu wangu achunguzwe? Mwanangu wewe sio changudoa wa kusema humjui baba wa mtoto sijui hadi achunguzwe, leo utachunguza kwa macho, kesho utaomba kupima DNA na mtoto, sio kwa mjukuu wangu tafadhali, ondokeni”
“Sasa mama Mage unakuwa mkali hivyo kwa lipi? Hivi wewe ukiambiwa mwanao wa kiume ana mtoto sehemu hutotaka kumchunguza huyo mtoto?”
“Nitamuuliza mwanangu kwanza, akikubali basi mtoto nitamkubali. Kwahiyo wewe nenda ukamuulize mwanao, maswala ya kuchunguzwa kwa mwanangu sio kazi yako. Nora hata baba mtoto ndio angesema nakuja kumchunguza mtoto ila wewe unikome. Nimesema tokeni kwenye nyumba yangu”
Wakati huo aliongea kwa ukali sana ilibidi Mrs.Peter na Babuu wainuke na kutoka maana mwenye nyumba alishaonyesha kuchukizwa vilivyo.
 
SEHEMU YA 272

Sasa walibaki ndani wawili kama kawaida, Erica na mama yake, kisha Erica akamuuliza mama yake,
“Ila mama kwanini umegoma wasimuone mtoto?”
“Sijagoma wasimuone mtoto ila kauli zao ndio zimefanya nigome, Erica nimewazaa, nimewalea, niwatunza hadi mmekuwa wakubwa, haiwezekani mtu aniletee fadheha kwenye nyumba yangu mwenyewe, eti anataka amchunguze mtoto, yeye kama nani? Sijui bibi, si akamuulize mwanae huko kama ana mtoto huku au la! Wenzie hawasemagi wamchunguze, angeomba kuona mjukuu wake, angeletewa na ndio hapo angemchunguza yani kashamkubali hata moyo wa kumletea unakuwa nao, ila mtu kashaweka mashaka umletee amchunguze ili iweje? Na wewe Erica, kweli kabisa ulikosa watu wote hadi kwenda kuzaa na mtoto wa Yule mwanamke? Jamani simpendi dah!”
“Kwani kakufanya nini mama?”
“Unajua Yule Mwajuma ndio dada wa mama yake Derick”
Erica alishangaa hapo na kukumbuka alipoambiwa na Babuu kuwa alienda kwenye mahafali maana kulikuwa na ndugu yake, ndio akakumbuka kuwa ni Derick ndio ndugu wa Babuu, alibaki tu kushangaa kwa mama yake na kumuuliza kuwa alimfanyeje,
“Kheee kumbe ni ndugu na wakina Derick, sasa alikufanya nini mama?”
“Yule mwanamke hana akili kabisa, kipindi nagombana na mdogo wake hadi nikamfukuza hapa, jamani jamani mwanamke alinitukana huyu sijapata kuona, nadhani kipindi kile kungekuwa na simu ndio ningeyaoga matusi kabisa. Kuna kikundi Fulani cha wanawake, tulikuwa vizuri kweli kwenye kukopeshana na kwenye michango nilikuwa vizuri si ndio aliponifahamia. Kile kikundi tulikuwa tunakutana kwa wiki mara nne, na kilikuwa imara kweli jamani kila nikikutana nae mwanamke Yule ni matusi tu, Yule mama hana hata simile, yeye ni kutukana tu. Mdogo wake alifikia mahali akakubaliana na matokeo ila Yule mwanamke ni kutukana tu, kuna kipindi hadi tulipigana hadi nikamshangaa kuwa mapenzi ya mdogo wake yeye anayaingilia nini. Halafu ubaya zaidi, uwiii Yule Mwajuma ni mbea jamani haijapata kutokea, ni mbea na mnafki, alinitangazia maneno ya uongo hadi wanawake wote kwenye kikundi wakanichukia, nikaona kikundi kichungu ila sababu nilikuwa natetea kuhusu mume wangu, sikuachana na mume wangu ila niliachana na kile kikundi maana lengo lake lilikuwa niachane na mume wangu ili mdogo wake achukue nafasi yangu”
“Kheee makubwa hayo mama”
“Yani Yule Mwajuma sina hamu nae kabisa, halafu watu huwa wanamuamini maneno yake sijui kwanini, ila Yule mwanamke hafai, alifanya niache na hela zangu kwenye kile kikundi maana mama yako nina hasira sana, mwenyekiti ilibidi aniletee walipokuwa wakivunja kikundi huku akisema kuwa mwajuma anahitaji kupafahamu kwangu maana inaonyesha mdogo wake hakutaka kumleta maana hapendi shari ila huyu mwanamke sidhani kama kajirekebisha si unamuona hata leo kaja kishari shari na kimbeambea, simpendi hasirani sijui umeanzaje na wewe kuzaa na mtoto wake aaah!”
Kisha mama Erica akainuka na kwenda chumbani kwake, kwavile jioni iliingia ikabidi Erica aanze kufanya kazi za pale kwao za jioni kama kuandaa chakula cha usiku na vitu vingine huku akiwaza sana.

Usiku wakati wa kulala, Erica aliamua kusikiliza redio kwani alijiona hayupo sawa kabisa, akahisi pengine akisikiliza mahubiri kama mama yake anavyomshauri ataweza kupata amani kiasi, alipowasha tu akamsikia Yule muhubiri akisema,
“Hakuna kitu chema kama kuomba toba mbele za Mungu, toba inatuweka karibu na Mungu. Hakuna mwanadamu aliyekamilika, sote tuna mapungufu, tunatakiwa kuomba toba mbele za Mungu. Toba inafuta makosa yetu na tunakuwa wapya baada ya toba, kumbuka kutubu mbele za Mungu wetu”
Mara simu ya Erica ikaanza kuita, ikabidi azime redio ili apokee ile simu, alipoiangalia alikuta ni Babuu ndio anapiga, akapokea ile simu na kuongea nayo,
“Erica, unajua sikukutegemea kabisa kama unaweza kufanya hivyo, kweli umezaa na Rahim?”
“Sasa wewe mpaka umefikia hatua ya kumleta mama yake Rahim ulikuwa huna uhakika au ni nini?”
“Nakuuliza kwa upendo tu, yani Erica umenichanganya na ndugu zangu wote? Unajua nimemuuliza mamdogo kuwa kamjuaje mama yako ndio kaniambia kuwa Derick ni ndugu yako, nikashangaa sana ikabidi nimpigie Derick simu kumuuliza akasema kuwa naye aliwahi kulala na wewe. Khee Erica, ulilala hadi na ndugu yako? Kaka yako wa damu? Umeshindikana Erica”
Erica aliamua kukata ile simu maana aliona inamletea kizunguzungu tu, alivyokata tu akapokea ujumbe toka kwa Derick, ilikuwa ni mara ya kwanza leo maana hakuwasiliana nae kwa muda mrefu sana. Akafungua ule ujumbe na kuusoma,
“Haya sasa kiko wapi, Derick malaya malaya, kumbe wewe ndio malaya, kweli Erica wa kutembea na ukoo mzima kweli? Nasikia umezaa na Rahim, hivi huoni aibu? Utasingizia kwangu nilikunywesha pombe, haya na hao wengine walikunywesha pombe? Mbona mwanamke hujiheshimu wewe? Heshima ya mwanamke iko wapi kwako? Kweli mwanamke mzuri asiye na akili zitakazoumia ni sehemu zake za siri, kumbe Erica wewe ni malaya kiasi hiko? Tena ni malaya koko, najuta kuwa na ndugu wa dizaini yako.”
Huu ujumbe uliumiza sana moyo wa Erica na hisia zake na hata hakujua kosa lake lipi maana kwa kipindi chote alikuwa akitafuta penzi la dhati kumbe alitembea na ndugu kwakweli aliumia sana roho, alilia sana alipomaliza kusoma ule ujumbe, alijikuta akisema,
“Ooooh Mungu wangu, hivi ni mimi tu ndiye mkosaji dunia nzima? Hivi ni mimi tu mwanamke nisiye na akili dunia nzima? Kwanini lawama zote napewa mimi, hawa wanaume mbona na wenyewe hawajilaumu jamani”
Alilia sana, akasikia ujumbe mwingine unaingia kwenye simu yake, kuangalia umetoka kwa Babuu, akausoma,
“Erica una laana wewe, kutembea na kaka yako ni laana hiyo, na kuniacha mimi ni laana pia. Ujue mimi ndio nilikuwa mwanaume wako wa kwanza, hukutakiwa kuniacha ila swala la kuniacha mimi ukajipatia laana ya milele, na itakutafuna hadi unaingia kaburini”
Erica alizima simu yake na kujikuta akilia sana, akakumbuka mahubiri aliyotoka kuyasikia kwenye simu kuwa ni vizuri kufanya toba, alipiga magoti chini na kuanza kutubu akisema,
“Eeeeh Mwenyezi Mungu, najua nimekutenda mengi mabaya, nimefanya makosa mengi sana ila yote sababu sikuona anayenipenda kwa dhati. Naumia moyoni, nilipenda siku moja na mimi niwe na mume wangu, na maisha yangu na watoto wangu tukifurahi pamoja ila sikupenda maisha yangu yawe ya majuto kiasi hiki. Naomba Mungu wangu nisamehe kwa yote niliyoyatenda, naomba laana ninazopewa zisinipate. Amen”
Akalia sana maana mambo yale yalichanganya akili yake, alipomaliza kulia alipanda kitandani na kulala.
 
SEHEMU YA 273

Palipokucha aliendelea na shughuli zake za hapa na pale, mama yake nae alimuangalia na kumuuliza,
“Weee mbona macho yamekuvimba hivyo?”
“Hamna kitu mama”
“Umevimba sababu ya jana kuitwa malaya? Kwani ni kweli ulitembea na ndugu wote? Najua bado una mawazo ila ukitulia njoo uniambie kila kitu mama yako, unieleze kila kitu usinifiche chochote hata kama kibaya mimi kukijua nieleze tu na nitakwambia cha kufanya, usiwe na mawazo sana mwanangu”
Erica alimuitikia mama yake pale kisha kuendelea na kazi zake zingine, mchana wa siku hiyo alifika dada yake Bite na kukaribishwa na mama yao, akakaa sebleni, kisha Erica akafika na kumsalimia dada yake, alipomuitikia tu alimtupia leseni ya udereva,
“Haya, leseni yako hiyo hapo”
Erica alipokea bila kusema chochote kwani bado alikuwa na mshangao kuwa leseni si alitakiwa akachukue mwenyewe, sasa imekuwaje kuletewa na dada yake? Kisha dada yake akamwambia,
“Haya, kalete funguo za gari langu”
Erica akainuka na kwenda kuleta funguo za gari, kisha akaja nazo na kumkabidhi dada yake, ambapo dada yake alimuangalia mama yao na kumwambia,
“Unaona mama, unaona”
“Nimeona mwanangu”
“Maana tungesema tu ingekuwa kama tunamsingizia, labda tungemuona James muongo ila unaona uthibitisho huu!”
“Naona”
“Haya Erica, shemeji yako alikupa shilingi ngapi ukasome udereva?”
“Laki tatu”
“Na alikupa shilingi ngapi umpeleke mtoto kliniki?”
“Laki moja”
“Haya, na alikupa pesa ngapi ya kwenda kumfungulia mtoto akaunti?”
“Laki mbili”
“Unaona mama, yani huyu Erica huyu loh!”
“Naona mwanangu, yani hata sijui niseme kwa lugha ipi Erica apate kunielewa”
Kwakweli Erica alikuwa kwenye mshangao tu maana hakuelewa kuwa mambo yote yale yametoka wapi, akaendelea kumsikiliza dada yake akiongea,
“Erica si wewe mwenyewe uliniambia kuwa James alitaka kukubaka ila ukatumia ujanja kumtoroka? Wewe mwenyewe uliniambia kuwa shemeji yako alikuwa anakwambia anakupenda, sasa kiko wapi leo? Unaenda kutangaza shida za nyumbani kwetu kwa shemeji yako kweli? Nilikuonea huruma mdogo wangu kukaa nyumbani bila kazi, nikakuombea kazi kwa shemeji yako halafu umeenda kufanya ujinga kwenye kazi jamani! James aliniuliza kuwa uliyezaa nae yuko wapi? Nikamueleza ukweli na akakuhurumia haswaaa ndio hadi kukupa kazi, kumbe wewe umetumia swala hilo kama nafasi ya kujiachia kwako, kazini unaenda kwa kupenda, mara uende mara usiende, ukifika kazini unaanza kueleza shida za nyumbani sijui mama ana matatizo, sijui hatuna pesa yani umenitia aibu haswaaa Erica. Umeenda kumuomba hela ya kumpeleka mtoto kliniki, kweli jamani Erica wa kuomba hela ya kliniki kwa James? Kwani ndio baba wa mtoto wako huyo? Halafu unaenda kuomba hela ukasomee udereva, kweli Erica hujui kuendesha gari wewe? Yani sababu Yule ni shemeji yako ndio amekuwa kitega uchumi kwako? Haya leseni shemeji yako alipie, mara hela ya kumfungulia mtoto akaunti, Erica hivi James ni mume wako au mume wangu mimi? Mbona sikuelewi wewe mtoto jamani eeeh! Yote tisa kumi, kumbe gari nimeliacha hapa imekuuma roho hatari hadi kumuomba shemeji yako funguo ili uendeshe wewe, jamani si ungeniomba hata mimi mwenyewe! Nadhani una yako kwa shemeji yako Erica. Haya sasa shemeji yako kakufuma unaongea na simu ya mapenzi ofisini kakusimamisha kazi halafu umemuenezea maneno kwa wafanyakazi pale eti shemeji yakokambaka rafiki yako ndiomana umeacha kwenda ofisini, Erica wa kumpakazia shemeji yako vitu kama hivyo kweli? Tena nasikia umejipanga kwenda mahakamani kutoa ushahidi kuwa shemeji yako kambaka rafiki yako maana tayari mshafungua na kesi, hivi kumchafulia huko jina mume wangu kwanini Erica? Sijapenda kwakweli, sijapenda kabisa, haya kata sasa maana ushahidi wote upon a vithibitisho vipo”
Kwakweli Erica hakujua aanzie wapi na aishie wapi maana hakuelewa jinsi shemeji yake alivyoweza kuyatunga maneno kiasi kile, yani kwa jinsi dada yako alivyoongea akaona hata aseme vipo bado ataonekana muongo, alikaa kimya, mama yake akamfokea
“Wewe Erica wewe, si unajua sana kunitia aibu haya kata na haya sasa. Na huyo rafiki yako aliyebakwa na shemeji yako ni nani?”
“Ni Yule Dora mama”
“Hivi una akili wewe, (Kisha akamuangalia Bite na kumwambia) Huyo Dora ndio lile changudoa lililoletwa na kaka yenu hapa, hivi ukae na Yule kiumbe upange nae jinsi ya kumtafutia kesi shemeji yako!”
“Ila mama, ni kweli alimbaka”
“Nyamaza kenge wewe, hivi Yule Dora ni wa kubakwa Yule? Wapo wa kubakwa ila sio Yule dora, hata aseme amebakwa na wanaume kumi ni wazi ametaka mwenyewe. Na hata angetaka mwenyewe, shemeji yako si mchafu kiasi hiko. Haya sasa, hizo hela ulizokuwa unachukua kwa shemeji yako sijui nyumbani kuna shida ziko wapi?”
“Sina mama”
“Yani nimezaa kopo kopo jamani, Erica nilijua wewe ni msomi mahali wa kuikomboa familia yako kumbe nililipa ada ya bure tu. Kwanza mahafali hukusherekea, halafu nyumbani umeniletea shahada ya mtoto, umeenda kuzaa na mtoto wa adui yangu, na sasa unaanza kufanya mambo ya ajabu kwa shemeji yako. Nilikuuliza mimi kwanini umesimamishwa kazi, ukasema ooh simu sijui shemeji kanionea kumbe unaongea mambo ya mapenzi ofisini”
“Sio hivyo mama”
Mama yake akawa mkali sasa na kuinuka, kisha akamuuliza,
“Sio hivyo nini?”
“Amenisingizia”
“Wewe mwenyewe umeleta funguo hapa, na umekubali kupokea pesa saivi unasema ana kusingizia? Una akili kweli wewe?”
“Akili ninazo mama”
Mama yake akamzaba kofi lililompelekea Erica ajihisi kama kizunguzungu maana lilishuka kwa nguvu sana kwenye uso wake, alijikuta akisema kwa uchungu sana,
“Unanionea mama”
“Nakuonea nini na nilishakuonya toka siku ya kwanza umesema unaenda kuanza kazi kwa shemeji yako!”
Mama yake akamzaba kofi lingine, Erica akainuka na kukimbilia chumbani kwake akajifungia mlango na kulia sana, alijiona kama mtu asiyekuwa na bahati katika maisha, alilia kwa muda mrefu hata mtoto wake alipoamka alimkuta mama yake akilia na kumfanya Yule mtoto nae kuanza kulia.
 
SEHEMU YA 274

Bite alibaki na mama yake sebleni ila Bite akamuaga mama yake,
“Mama, ngoja niende kuangalia familia yangu mie mambo hya hapa nyumbani siyawezi. Ila kaa sana na huyu Erica, aache mambo ya kumsingizia shemeji yake na kutuweka ubaya kwenye familia”
“Usijali mwanangu”
Bite aliondoka zake, mama yao alipoona Erica hatoki chumbani na muda ulienda alishikwa na huruma kwa binti yake ikabidi aende kumgongea,
“Erica mwanangu, toka chumbani tuongee vizuri. Unajua mama yako nilikupiga sababu ya hasira”
Basi Erica alitoka ila macho yake yalivimba kwa kulia maana hakuwa na furaha hata kidogo, mama yake alimuhurumia sana, hakupenda tabia ya mwanae aliyoambiwa ila alimuonea huruma maana hakuna mtoto kati ya watoto wake aliyekuwa na sura ya upole kama Erica, kwahiyo muda wote ukiambiwa kafanya chochote lazima uhisi kasingiziwa ndiomana mama yake alijua anajitetea tu sababu anajua ana sura ya upole, akamuita na kumuuliza tena,
“Yaliyosemwa na dada yako ni kweli?”
“Mama, si kweli hakuna ukweli hata mmoja”
“Sasa funguo za gari la dada yako ulikuwa wafanya nazo nini? Na hizo hela ulizokubali kupewa alikupa za nini?”
Ingawa Erica alikuwa na hasira ila alijaribu kumueleza mama yake kwa kifupi ilivyokuwa hadi akapewa zile hela na funguo za gari, ila hakumueleza tu kuhusu kubakwa kwa Dora na simu aliyokuwa akiongea nayo.
“Ila Erica mwanangu si nilikukataza wewe, nilikwambia bora kazi utafute sehemu nyingine ila sio kwa shemeji yako Yule. Umeyaona leo? Na nisingekupiga hapa dadako angeona nakuendekeza, ila muache afurahi na wakafurahi na mumewe. Nisamehe mwanangu, siku hizi nitakuwa nachunguza habari zote nitakazo zisikia kuhusu wewe, kuanzia leo hata shemeji yako aseme kuwa urudi ofisini kwake kufanya kazi hakuna kurudi? Kama hujapata kazi kaa hapa hapa nyumbani tutakula kama kawaida kitakachopatikana, sawa? Ila hakuna tena kwenda kufanyakazi kwa James”
“Sawa mama, nimekuelewa”
“Basi usilie tena mwanangu, nisamehe mama yako. Sawa mama eeeh! Unataka kula nini leo usiku nikuandalie mwanangu”
“Chochote tu”
“Basi usilie tena mwanangu jamani, sawa eeeh!”
“Sawa”
Kisha Erica akarudi tena chumbani ila mtoto alimuacha na mama yake maana mama yake alisema abakie na mjukuu wake muda huo acheze cheze nae.

Usiku ulipoingia aliamua kuwasha simu yake maana ni tangu alipoizima jana yake na ndio aliiwasha muda huo ila ilipowaka tu kuna jumbe ziliingia mfululiza, jumbe moja wapo ilitoka kwa Erick ikisema,
“Nakutafuta mpenzi wangu Erica mbona hupatikani? Nini tatizo? Basi naomba kesho uwe hewani, nitakupigia simu mchana”
Alifurahi sana kuona jumbe ya Erick, akachukua simu ili ampigie muda huo ila akashangaa kuwa salio halitoshi na kukumbuka kuwa salio aliloliweka alilimaliza, akaona ujumbe toka kwa mzee Jimmy,
“Erica, umenizimia simu sio vizuri ujue. Katika maisha yangu hakuna binti niliyetokea kumpenda kama wewe, ila kwa mara ya kwanza nimetoa zawadi kubwa lakini imerudishwa unataka nikufanyie nini Erica ili unipe angalau mara moja tu! Ila mimi sio mtu wa kukata tamaa na nitakutafuta tu”
Huu ujumbe ulimkera sana, na muda tu alipomaliza kuusoma mzee Jimmy alianza kumpigia simu, Erica akaona afanye jambo moja tu la kuzima simu tena na kujisemea kuwa angeiwasha kesho yake mchana muda ambao Erick angempigia simu.
Aliamua kulala ila kulipokucha tu aliamua kuwasha simu yake kwa kuhisi kuwa pengine Erick angemtafuta kuanzia asubuhi, ila alipowasha tu alipokea ujumbe kutoka kwa Rahim na kushangaa sana maana ni siku nyingi,
“Erica ingia kwenye mtandao kuna mambo nataka kujadili na wewe”
Erica akafikiria na kuhisi pengine ni mambo ya msingi, akaamua kuwasha ile simu yake nyingine kisha kuingia kwenye mtandao na alipoingia tu alipokea ujumbe kutoka kwa Rahim,
“Erica sijapenda, si nilikwambia kuwa usimueleze chochote mama yangu? Nini kimekufanya ukamueleza mama yangu?”
“Sijamueleza mbona”
“Mama yangu sio mjinga Erica, na kajuaje kama mimi na wewe tuna mtoto eeeh! Erica, kwanini umemueleza mama yangu?”
Kwakweli Erica bado hakumuelewa kabisa Rahim kuwa ni kwanini hapendi mama yake ajue ukweli, na akaona kuendelea kubishana nae ni kupoteza wakati akaamua kutoka kwenye mtandao na kuzima simu ile ila baada kama ya nusu saa alipokea ujumbe wa kawaida toka kwa Rahim,
“Erica unajifanya una kiburi, sasa subiri kiburi chako kitakuponza”
Kwakweli bado hakuelewa maana alihisi tu kuchanganywa na mambo, ikiwa asubuhi bado akiwa anatafakari ule ujumbe aliotumiwa na Rahim akapigiwa simu na Dora,
“Erica, nakuomba hapa nje kwenu mara moja”
Erica alijua tu ni kuwa Dora amekuja kumfata maana ile ndio ilikuwa siku ya kesi, akaamua kwenda nje ili kumwambia kuwa hatoweza kwenda nae.
Akatoka nje, alivyofungua geti tu akamuona Dora ambaye alimvutia kwa nje na gafla akamuona mzee Jimmy akija yani kumbe Dora alimpeleka mzee Jimmy kwakina Erica.
 
SEHEMU YA 275


Erica alijua tu ni kuwa Dora amekuja kumfata maana ile ndio ilikuwa siku ya kesi, akaamua kwenda nje ili kumwambia kuwa hatoweza kwenda nae.
Akatoka nje, alivyofungua geti tu akamuona Dora ambaye alimvutia kwa nje na gafla akamuona mzee Jimmy akija yani kumbe Dora alimpeleka mzee Jimmy kwakina Erica.
Erica akapigwa na butwaa, halafu Dora akamvutia mkono hadi kwa mzee Jimmy ambapo mzee Jimmy alitaka amuinguze Erica kwenye gari kinguvu, ila bila kutegemea Erica alianza kupiga kelele za kuita mama yake kama anakabwa vile,
“Mama, mama, mama nakufa huku mama”
Mzee Jimmy akaogopa sana na kumuacha Erica kisha akaingia kwenye gari yake na kuondoa gari, mama Erica alitoka na kukuta gari ya mzee Jimmy ikiishia huku pale yupo Dora na Erica, sababu kitendo cha mzee Jimmy kuondoka kilikuwa cha gafla kwahiyo bado walikuwa wamesimama palepale.
Mama Erica alipotoka alijua labda Dora alimkaba mwanae, akamfata Dora na kumpiga vibao vya kutosha kisha akamshika Erica mkono na kumuingiza ndani.
Alikaa nae na kumuuliza,
“Wewe mtoto umefata nini nje asubuhi yote hii? Na Yule malaya kakufanya nini?”
“Mama, Yule Dora kweli kama ulivyoniambia ni rafiki mbaya, ngoja nikueleze kwanza chanzo cha Dora na mimi kuwa karibu.”
Erica akamueleza mama yake alivyomsamehe Dora, na akamueleza jinsi walivyofika ofisini pia akamueleza kisa cha shemeji yake kutaka kwenda nae kutembea mpaka alivyomualika Dora na kuwakimbia na hadi Dora alivyomuelezea kuwa amebakwa,
“Sasa leo ndio siku ya kesi ya Dora, alivyosema nitoke yupo nje kwetu nikajua anataka nimsindikize kwenye kesi, nikatoka ili nimwambie kuwa sitoenda tena, ndio nikashangaa kuwa alikuja na mzee Jimmy, sijui walikuwa na lengo gani ila Yule mzee alitaka kunipakia kwenye gari lake ndio nikapiga zile kelele, na zile kelele ndio zilimfanya Yule mzee apande gari na kukimbiza gari yake”
“Khaaa kumbe! Huyo mzee anakutakia nini mwanangu jamani? Yani hana hata haya jamani, na huyo Dora mwanangu sio rafiki yani sio rafiki kabisa, ningemuona kipindi mnasoma ningekwambia mapema mwanangu kuwa huyo sio rafiki, hakufai mwanangu. James nae kweli kabisa alimbaka Dora? Mweeeh ila wanaume nao sio wa kuwakatalia sana kuwa hawajafanya maana akili zao wanazijua wenyewe. Erica mwanangu, kuanzia sasa mimi ndio rafiki yako yani usifanye chochote bila kunishirikisha mimi maana mimi ndio mama yako na mimi ndio najua ni vitu gani nilipitia hadi kukupata wewe, najua hata wewe hutopenda kuona Angel akiumia au akipotea, ndio hivyo hivyo na kwangu, sipendi kukuona ukiumia au ukipotea.”
“Sawa mama nimekuelewa ila yote haya ni sababu nilimsamehe Dora ndio nikawa nae karibu tena, ila nisingemsamehe yote haya yasingetokea, nilisikiliza yale mahubiri kuwa ni vizuri kusamehe”
“Erica, ni kweli kusamehe ni vizuri sana ten asana kwani hata kwa Mungu ni mengi tunayatenda ila Mungu ni mwaminifu huwa anatusamehe. Ila kiubinadamu swala la kusema huyu ni binadamu ana akili za kibinadamu liko pale pale, kusamehe ni vizuri ila usirudi nyuma tena kusema kwamba huyu mtu kabadilika maana huwezi jua ya mbele, kusamehe ni kuzuri maana kama kuna cha kumsaidia utamsaidia tofauti na mtu ambaye hujamsamehe huwezi kumsaidia. Sasa wewe kumsamehe Dora si kosa ila kosa lako ni kumfanya Dora kuwa rafiki yako tena wakati unajua fika Dora ni mtu wa aina gani? Na licha ya hivyo, umeweza kujionea, bado ana tamaa na anaweza kukuingiza kwenye mdomo wa mamba Yule, kuwa makini mwanangu, mamako nakupenda ndiomana naongea haya”
“Asante mama”
Erica alitabasamu na kumuitikia mama yake maana aliona siku hiyo mama yake amempa maneno ya faraja kuliko siku zote.

Akaendelea na kazi zake za hapa na pale, kisha badae alipomlisha mwanae na kumuacha akicheza na bibi yake, akaingia chumbani na kuchukua simu yake ambayo kwa kipindi hiko ilikuwa kama hakimu maana alitumiwa ujumbe wa lawama na kuhukumiwa tu, alichukua ili kuangalia kama Erick amemtafuta, ila alikutana na ujumbe toka kwa mzee Jimmy.
“Siamini Erica umenidhalilisha kiasi hiki, Erica umenidhalilisha kweli kwa kosa lipi? Unajua nilitaka kufanya nini kwako? Unajua nilitaka kuongea nini na wewe? Unajua mimi nina wadhifa gani hadi umenidhalilisha kiasi hiki? Sitasahau kamwe ulichokifanya leo wewe binti maana hata sikufikiria kama unaweza kutenda kama hivi.”
Erica hakujua hata ajibu vipi huo ujumbe wa mzee Jimmy na kubaki kimya tu, muda kidogo sasa ndio akapigiwa simu na erick, pale alijawa na tabasamu zito sana na kuanza kuongea nae,
“Upo sehemu nzuri Erica, kiasi kwamba tunaweza kujadili ishu za mimi na wewe?”
“Ndio nipo sehemu nzuri tu, tunaweza kuongea”
“Sawa, najua sijawahi kukuuliza maana kidogo akili yangu ilishikwa na sintofahamu ila naomba nikuulize sasa”
“Niulize tu”
“Naomba unieleze kwa kifupi kuhusu Angel, yani mwanaume uliyezaa nae yuko wapi? Ana mpango gani? Anasemaje kuhusu mtoto ili nijue tunaanzia wapi na tunaishia wapi”
Erica akapumua kidogo maana hakuelewa kuwa aanzie kumueleza Erick sehemu gani ila aliamua kuanza popote tu ilimradi ujumbe ufike kwa Erick,
“Mwanaume niliyezaa nae Angel, alinilaghai na nikahisi kuwa ananipenda ila nilipozaa tu aligeuka kuwa mbogo na hakutaka mtoto ajulikane na familia yake hata yeye tangu nizae huyu mtoto sijawahi kumtia tena machoni pangu yani kwa kifupi hata mtoto hajawahi kumuona tangu azaliwe. Nina mengi sana ya kuongea Erick ila nasikia uchungu kila nikifikiria”
“Aaaah pole sana Erica, pole sana huyo mwanaume hana akili kabisa yani kuumiza moyo wa malkia wangu kiasi hiko! Sijapenda, na ulipomuuliza kuhusu swala la kuja kumuona mtoto alisemaje?”
“Mwanzoni alikuwa ananiambia nitakuja nitakuja, ila saivi inaonyesha hiyo kuja ni ndoto tu maana hata huduma za mtoto kasitisha. Erick, naomba unisamehe ila sijui hata nisemaje uelewe ninavyojutia”
Erick alimsikia Erica akilia na kweli alijisikia huruma sana na kumwambia,
“Tafadhali Erica acha kulia na futa hayo machozi yako maana mfariji wako nipo. Kwahiyo kwa kifupi Angel hana baba?”
“Naweza sema hivyo Erick maana baba yake hamjali tena”
Erica akawa analia tena, Erick akamwambia,
“Nimesema Erica acha kulia mpenzi wangu. Kumbuka mara ya mwisho shuleni nilikubusu kuonyesha ishara ya mapenzi yangu kwako, ni kweli nilikupenda Erica, nakupenda na nitaendelea kukupenda. Hivyobasi swala la Angel kutokuwa na baba hata lisikuumize kichwa, naomba kuwa baba yake”
Erica alikaa kimya kwani yale maneno kama yaliingia kwenye moyo wake na kuugusa vilivyo kwani hakuamini kabisa, mpaka Erick aliongea tena,
“Erica, unanisikia kweli? Naomba kuwa baba wa Angel.”
“Erick sijui niseme nini, nadhani ungepasua moyo wangu na kuona furaha niliyonayo moyoni mwangu hata ungeshangaa, Erick nakubali uwe baba wa mwanangu kwa asilimia zote”
“Wow Erica, sikia nikwambie kitu kingine.”
“Niambie tu”
“Naomba huyo Angel umuandikishe majina yangu, namaanisha maana hata kwenye mali zangu nay eye atakuwa mmoja wapo kama mwanangu, na hata nikifa basi atakuwa mrithi wa mali zangu”
Kwakweli hili swala lilichanganya akili ya Erica, yani hakuelewa kama Erick anaongea kwa kumaanisha au ni kitu gani na kujikuta hata akishindwa kumjibu, Erick akasema tena,
“Nadhani nimekupa swali gumu, ila nakupa muda ufikirie na fikiria maisha ya badae ya mtoto wetu. Waswahili husema ukipenda boga penda na uwa lake, mimi napenda uwa la boga kama ndio boga lenyewe, nakupenda wewe Erica na ninampenda Angel, pengine hao waliopita kwako hawakujua thamani yako ni nini ila mimi naijua na sitajivunia kuwa wa kwanza kwako ila nitajivunia kuwa wa mwisho kwako. Nakupenda Erica”
“Nakupenda pia Erick”
“Sikia Erica nikwambie kitu, ni mengi sana tumepitia mimi na wewe, kutokuwa karibu kumesababishwa sana na maneno ya watu. Sitaki kukubali kauli ya kusema kuwa watu wanaopendana hawadumu na hawaishii pamoja, najua inawezekana kama tukiamua kuwa na jambo moja. Erica najua ushafanya yako machafu mengi tu ila kwavile moyo wako haukuwa na msimamo, na mimi nishafanya yangu machafu mengi tu sababu moyo wangu haukuwa na msimamo pia. Usikae kusikiliza ya watu sijui Erick alikuwa malaya, sijui Erick alikuwa anabadilisha wasichana kama nguo, hayo yaache yalipita ila sasa tuangalie ukurasa mpya wa maisha yetu”
“Sawa Erick nimekuelewa, sitasikiliza ya watu tena”
“Napenda kurudia hili, najivunia kuwa wa mwisho kwako Erica, mimi ndio najua thamani yako. Nakupenda sana”
“Nakupenda sana pia Erick”
Kisha Erick akakata ile simu yani Erica alijikuta akijilaza kidogo kitandani huku akimfikiria Erick, alijikuta akifikiria kuwa yeye, Erick na Angel wameongozana wakifurahi na kucheza pamoja, alijilaza kitandani akiwaza kwa furaha hata hakutaka kuinuka kwani Erick alitawala tu kwenye kichwa chake kwa muda huo.

ITAENDELEA
 

ukhty khadija The Hurricane Chabrosy leechan de ommykhan Shupavu Shabdullah loviesundy nyakisese bubblymolly famad AlmasMAlmas mwanaspotiapp MENO YA KUKU Lengutee Msichana wa jana unprejudiced Gwappo Mwakatobe Lewis18 G'taxi Authority subadesubking Joseph lebai ikhatibu Depal Interlacustrine Region helment chrisbleez femalepilot Nuhu39 Smart911 benjamin ayombo kitalembwa joefrancy jKingSenior kanonb song 16 binti mapozi EnnoMX Nimetoka Katavi kaka kaka kax bedui Jr Teta kuchikubwa Baharia wa Buza mkulima2 crix pronto Mkatauzi KigaKoyo mpasta MR KUO charrote babu chilau Secret Man Mtende Mine eyes Teleshkova Hades yna2 NEIMAA Keijay Lex luther kipanta SangaweJr Jovet Litro qim SIFUGIKI Mnazareth chabeen ummul khaulaty mgaka ivan1212 josephat mugisha longola FrankMakeps Mdex jonoma elvas kizeze mandella DENAMWE Cappuccino Troisième Ceil mlyn Mkare_wenu Machmadem bioto yona raphael lameckkawawa denhoo manji h cariha havanna Muigai Jr Nyabhakangala kukumsela Mkulima Jr majangatz ELY NE Ibanga 53 Tonyblair asahd kidawisee fj44556 Angrybird muyakb24 Matts Reptilia Majjipolo 3lly da rophet creaty gal rehanishabani Franky Samuel Mr no MR MO CONFIDENCE meshack mnyambwa Active Dayone paul samky assey dumejeuri Joseparty manyanga21 dluv Enguraruu m.k Usher raymond Joharia Laurent apolinary network search von tosy Req qinglong Chemagati anunnaki kashata mactal project planner Blackninja Queen M NOHEMBRE Magema jr makedonia benybeny Super AMOLED kisukari Sweta LA Tanzania client3 AMBURIA uhaale Bruno mbunda Don Clericuzio makubia Isinika Chiefmzala Mshuza2 Lordrank Elly Kiwango Rural Swagga sinyora Ochumeraa edson ominic Jr Da'Vinci Disneyland Bayser17 Ben Kaozlee Sangomwile Thadeo sijaona fred tarimo sophiere Ukwaju stable Behaviourist Clkey bugza Mhariri Boqin Phlagiey Mkulungai
 

ukhty khadija The Hurricane Chabrosy leechan de ommykhan Shupavu Shabdullah loviesundy nyakisese bubblymolly famad AlmasMAlmas mwanaspotiapp MENO YA KUKU Lengutee Msichana wa jana unprejudiced Gwappo Mwakatobe Lewis18 G'taxi Authority subadesubking Joseph lebai ikhatibu Depal Interlacustrine Region helment chrisbleez femalepilot Nuhu39 Smart911 benjamin ayombo kitalembwa joefrancy jKingSenior kanonb song 16 binti mapozi EnnoMX Nimetoka Katavi kaka kaka kax bedui Jr Teta kuchikubwa Baharia wa Buza mkulima2 crix pronto Mkatauzi KigaKoyo mpasta MR KUO charrote babu chilau Secret Man Mtende Mine eyes Teleshkova Hades yna2 NEIMAA Keijay Lex luther kipanta SangaweJr Jovet Litro qim SIFUGIKI Mnazareth chabeen ummul khaulaty mgaka ivan1212 josephat mugisha longola FrankMakeps Mdex jonoma elvas kizeze mandella DENAMWE Cappuccino Troisième Ceil mlyn Mkare_wenu Machmadem bioto yona raphael lameckkawawa denhoo manji h cariha havanna Muigai Jr Nyabhakangala kukumsela Mkulima Jr majangatz ELY NE Ibanga 53 Tonyblair asahd kidawisee fj44556 Angrybird muyakb24 Matts Reptilia Majjipolo 3lly da rophet creaty gal rehanishabani Franky Samuel Mr no MR MO CONFIDENCE meshack mnyambwa Active Dayone paul samky assey dumejeuri Joseparty manyanga21 dluv Enguraruu m.k Usher raymond Joharia Laurent apolinary network search von tosy Req qinglong Chemagati anunnaki kashata mactal project planner Blackninja Queen M NOHEMBRE Magema jr makedonia benybeny Super AMOLED kisukari Sweta LA Tanzania client3 AMBURIA uhaale Bruno mbunda Don Clericuzio makubia Isinika Chiefmzala Mshuza2 Lordrank Elly Kiwango Rural Swagga sinyora Ochumeraa edson ominic Jr Da'Vinci Disneyland Bayser17 Ben Kaozlee Sangomwile Thadeo sijaona fred tarimo sophiere Ukwaju stable Behaviourist Clkey bugza Mhariri Boqin Phlagiey Mkulungai
Tuko pamoja mkuu.
 
SEHEMU YA 276

Mama yake alifanya kumuita tu ila Erica alienda kwa mama yake akiwa amejawa na tabasamu, huku mama yake akimuuliza kuwa amefurahi nini ila bado alikuwa na tabasamu tu hadi usiku ulipoingia alikuwa akitabasamu muda wote.
Basi usiku akashika simu yake ili atume ujumbe kwa Erick, akashangaa akikuta ujumbe mwingine toka kwa Dora,
“Yani Erica ndio umefurahi sasa kwa shemeji yako kukutwa hana hatia juu yangu wakati unajua fika kuwa shemeji yako alinibaka. Ndio msamaha gani ulionipa huo Erica? Msamaha wa visasi?”
Erica aliamua kumjibu Dora maana aliona sasa anataka amuwekee mazoea yasiyo na maana,
“Dora sikia, niliposema nimekusamehe sikusema kuwa tuendelee kuwa kama zamani, tena nilikwambia wazi kuwa nimekusamehe ila hutokuwa rafiki yangu tena. Naona unataka kunipanda kichwani, sikukutuma ukanywe pombe na shemeji yangu, sikukutuma ulewe hadi usahau kwenda kwenu. Inawezekana shemeji alikubaka kweli au hakukubaka maana mtu mwenyewe ulikuwa umelewa, mtoto wa kike unakunywa pombe kama kichaa, utafikiri hukusoma, tena unikome sitaki mazoea ya kijinga, ukaribu na wewe ni mwisho sitaki unizoee tena”
Akatuma ujumbe huo kwa Dora kisha akamtumia ujumbe Erick kuwa amekubali mtoto wake atumie majina ya Erick, basi Erick akampigia simu kwani alikuwa na furaha sana ya jibu lile,
“Ni swala la haraka Erica ili mtoto apate na kadi ya bima ya afya, yani ukishakamilisha tu, nitakuelekeza mahali upeleke cheti cha kuzaliwa na picha za mtoto ili washughulikie”
“Sawa Erick, kesho tu nitaanza kushughulikia”
“Sawa ila naomba nikuombe swala lingine”
“Niombe tu Erick”
“Erica, ukiangalia mapenzi yetu mwanzoni kabisa yalivunjwa na rafiki yako, naomba usiwe na marafiki wa aina hiyo. Ukiwa na swala linakutatiza bora uniambie mimi, naomba niwe rafiki yako”
“Erick, nishaachana na habari ya marafiki kwasasa, kwahiyo swala unalosema kuwa wewe uwe rafiki yangu sio ombi maana wewe ni rafiki yangu tayari”
“Kumbuka nakupenda Erica”
Kisha Erick akakata simu, kwakweli Erica alijihisi kama yupo ndotoni, maswala hayo aliogopa kumshirikisha mama yake maana alihisi kuwa huenda angemkataza wakati yeye moyo wake umeridhia kumbadilisha mwanae majina, kwani alipenda sana mwanae apate kuthaminiwa kama watoto wengine.
Wakati anatabasamu akapokea ujumbe toka kwa Dora,
“Erica kumbuka ni mambo mangapi nimefanya na wewe, ni mambo mangapi nimekushirikisha ila leo hii unaongea kama mtu anayetapika? Asante sana Erica, ila kumbuka unachomtendea mtu nawe utatendewa vilevile tena na zaidi”
“Usinitishe na ujinga wako, tena ukome kuniletea mababu nyumbani kwetu. Huyo mzee Jimmy tembea nae mwenyewe, simtaki na wala benki kwake siendi tena”
Erica aliona anamzingua tu huyu, akaamua kuweka simu pembeni na kulala.
 
Back
Top Bottom