Trimmer
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 2,443
- 4,007
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni ya jana usikuNYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NANE: “ok! malipo yangu yaliyobakia” alisema Deus, huku anamtazama Sheba, ambae pia alikuwa anatabasamu, “una uhakika kuwa unahitaji fedha pekee, au na kitu zaidi unahitaji kwa mschana mrembo kama mimi?” aliuliza Sheba kwa sauti laini na tulivu, “huu sio wakati wa utani, mpaka sasa sijajua narudi vipi mpaka tarakea kilomita ishirini kwa mguu begi la kilo hamsini mgongoni…” alisema Deus na kabla hajamaliza kuongea, akakatishwa na mlio wa simu ya kwenye dash board ya gari, wote wawili wakatazama kwenye kioo cha screen yenye upana wa sentimeta thelathini kwa kumi na tano..…….ENDELEA…
Wakaona jina la mpigaji kuwa ni Atshen, Sheba akaipokea mara moja, “kazi nzuri Deus, dakika chache kabla ya muda ulio ahidi, nina zawadi kubwa kwako kwa kazi nzuri uliyoifanya” alisema Atshen kwa sauti yenye kujawa na furaha ya wazi, “Sheba, mpatie hiyo funguo ya ile nyumba ya kule Kisarawe, msetie GPS itakayomfikisha pale, kisha muelekeze password na umuelekeze namna ya kufungua mlango, mpatie fedha zote za kitanzania ulizo nazo kwenye gari” alisema Atshen na kumfanya Deus ajitabasamulie moyoni, “mwisho bwana Deus, hilo gari ni la kwako, unaweza kubadili namba za sajili kwa kuweka plate namba iliyopo kwenye buti, nakutakia safari njema na mafanikio mema, naamini safari ijayo tutafanya kazi nzuri zaidi” alisema Atshen, na kabla hajakata simu, Deus akaachia tabasamu la wazi kabisa, “asante sana boss” alisema Deus, huku anageuka na kutazama mandhari ya gari lile kwa ndani.
Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Deus alieona kama vile ametimiza ndoto yake ya kumiliki BMW S7, hata baada ya kukamilisha makabidhiano ya kila kitu ambacho alitakiwa kukabidhiwa, yaani begi jingine la fedha, lililokuwepo ndani ya buti, ambazo sio tu zilizidi milion hamsini ya kukamilisha kwenye malipo yake ya millioni mia moja, ila zilizidi mara dufu.
Pia alikabidhiwa funguo za nyumba, kadi ya gari, password ya kufungulia nyumba ambayo aliambiwa anaenda kuimiliki na mwisho ikafuata zamu ya kushangaa, ni baada ya kuona linashushwa sanduku toka kwenye buti la gari, nao wakafungua na kukagua mzigo ambao ulikuwa na vijitofari hamsini vya dhahabu, kila kimoja kikiwa na uzito wa kilo moja, “ina maana huu ndio mzigo niliokuwa na usafirisha na sio yule mwanamke kama nilivyoambiwa?” aliuliza Deus, ambae kwa malipo aliyopewa, na kazi aliyoifanya aliona inalipa.
Saa mbili kasoro dakika tano, ndio muda ambao, Deus, alianza safari kuelekea tarakea, huku wakina Sheba wakiingia porini, kuufuata mpaka wa kenya ambako wangekuta gari, ambalo wangelitumia mpaka Nairobi, ambako wange panda ndege ya kuelekea Ethiopia, “wacha nikapumzike Arusha mjini, kesho nirudi na barabara ya dodoma kupitia ngorongoro, siwezi kupitia njia ile ile lazima nitakamatwa” aliwaza Deus, ambae kutwa nzima alikuwa katika misuko suko, pia alihitaji kupumzika, sababu siku iliyopita alikesha kwenye kitumbua cha Neela, “nitakutunza kwa nguvu zangu zote” aliwaza Deus, huku anatazama Dash board ya gari lile na kwa bahati nzuri, macho yake yakatuwa kwenye geji ya mafuta, iliyosoma kuwa imebakiza robo ya tank. nitaweka pale njia panda ya himo” alijisemea Deus, huku anaendelea kuyoyoma kuitafuta tarakea.********
Naam pale mrina hotel, mwanaume mtu mzima, mwenye kubeba sanduku dogo jeusi, anaibukia kwenye ukumbi mkubwa ambao ulitawaliwa na watu waliokuwa wanapata vinywaji kwenye meza zao, huku wamekaa kwa mtindo wa wawili wawili mpaka watatu na zaidi, huku meza nyingi zikiwa zime tawaliwa na wanawake.
Yani kwa kifupi ni kwamba ungekuta meza chache sana zina wanaume watupu, ambao licha ya kupata vinywaji, pia macho yao yangekuwa yanakodoa kodoa kwenye meza nyingine ambazo wanawake watupu au wanawake walikaa mmoja mmoja kwenye meza yake au wanawake walio kuwa wanajipitisha pitisha kwa wanaume hao, ukiachilia wale ambao walikuwa wamekaa na wanaume wao, wakipata vinywaji na mbuzi wa kuchoma
Lakini anapoibuka tu yule mwanaume mtu mzima, ghafla wakainuka wanawake kama wanne hivi, toka kwenye meza tofauti tofauti na kumfuata, “karibu baba, chumba ninacho” alisema mmoja na mwingine akadakia, “leo sijafanya kazi kabisa baba, wewe ndio wa kwanza” yule jamaa, ambae alionekana kushangazwa na mapokezi yale, aligeuka kuwatazama wanawake wale, huku anaendelea kutembea, “ukitaka miguu yote nitakupa offer elfu ishirini” alisema mwingine, lakini yule jamaa hakuwajali, alizidi kutembea kuelekea mapokezi, ambako kulikuwa kunauzwa pombe.
Baada ya kuona mgeni yule hakuwa na mpango nao, wale wanawake wakageuka na kurudi kwenye viti vyao, na kumuacha yule jamaa akizidi kuelekea mapokezi, “sasa amekuja kufanya nini hapa? au ni mchuna ngozi” aliongea mmoja kati wanawake wale na kumalizia kwa msonyo mrefu, huku anajikalisha kwenye kiti kimoja, karibu na meza moja iliyokaliwa na wanaume wawili walikuwa wana kunywa pombe taratibu.
Yule mwanamke, alieonyesha kuwa na hasira, akamtazama yule mwanaume mtu mzima, ambae sasa alikuwa amesha fika mapokezi, nakutamani kuachia tusi jingine, sijuwi kwanini alimkasirikia kiasi hiki, lakini kabla hajaongea lolote, akasikia toka kwa wale jamaa, walikaa pembeni yake, “afadhari mzee mipango huyooo anapiga simu” alisema mmoja wao, kwa sauti yenye furaha na matumaini, “nani huyo Mduma nini” aliuliza mwenzie, “sasa je, huyu jamaa ukiona anakupigia simu ujuwe muda sio mrefu unakamata mkwanja” alisema yule wa kwanza na hapo hata yule mwanamke pia akavutika na kugeuza uso wake kuwatazama.
Akamuona mmoja wao akiwa ameishika simu yake, ambayo aliipokea na kuiweka sikioni, “niambie Mduma” alisema yule jamaa na kutulia kidogo, akisikilizia upande wa pili, ilikuwa vigumu kwa mtu wa pembeni kusikia upande wapili ulikuwa unasema nini, zaidi angemsikia huyu jamaa akijibu kwa minguno na maneno mafupi, “ndiyo…. mhmh!... yes nipo hapa…..yupoje…” hapo angeuliza huku anatazama kule mapokezi “mshua flani hivi, anamkoba mweusi….basi imeisha hiyo nyie fanyeni faster” alimaliza kuongea yule jamaa na kukata simu, “vipi Chao, jamaa anasemaje?” aliuliza yule mwenzie, “si nilikuambia jamaa hakosi mchongo, anasema yule dingii pale counter, anae jiwe moja kubwa ni kinyama, ametoka nalo jioni hii melerani, sasa haitakiwi apande nalo ndege, lazima lirudi kwetu, kisha tulivushe Kenya tukapige hela mingi” alisema yule alieitwa Chao, “kwahiyo tunafanyaje?” aliuliza kwa sauti yenye shauku yule mwingine, tuliza mshono chalii, inabidi kwanza tujuwe chumba chake halafu baadae tusemenae, yani unaambiwa anao mzigo wa maana” alisema Chao huku wakitazama kule mapokezi.
Naam wakati wawili hawa wanaendelea na maongezi yao, yule mwanamke hakuwepo tena kwenye kiti chake, nadhani alienda kukaribisha mgeni mwingine.*******
Naam nusu saa tu ilipita toka gari la polisi, lenye kikundi cha koplo Othman liondoke Mombo ajalini, wakina Cheleji nao wakaingia na gari lao, wakikuta tayari moto umesha zimwa, na magari yakianza kupita, tayari walikuwa wamesha pewa taarifa na Ulenje, ambae aliwasisitiza kuongeza speed waliwahi BMW jeusi, kabla halija vuka mpaka, pia aliwagawa mara mbili wengine wawahi mpaka wa tarakea, huku wengine wakiwahi mpaka wa Namanga, ambayo ndiyo mipaka pekee inayoweza kutumiwana na watu hao wanao watafuta.
“Nadhani tumeona picha halisi ya mtu tunae mfuatilia, hakika sio wa mchezo” tukikutana nae tuna msalimia kwa risasi nyingi sana” alisema Cheleji, wakati safari inaendelea, huku Dereva wake akimsikiliza, “ sita ruhusu nikose mkwanja hata iweje” alisema Cheleji, kwa sauti ya kukamia kweli kweli, huku gari likizidi kushika mwendo.*******
Saa mbili na nusu za usiku, njia panda ya himo, lilionekana gari dogo jeusi aina ya BMW S7 jeusi, likitokea upande wa Rombo na kuiacha njia ya kwenda Moshi na kuifuata ya kwenda dar, mwanzo nilitaka kushangaa, kwanini Deus, ameamua kurudi Dar es salam, lakini mshangao unamalizika muda mfupi baadae, baada ya kuona gari lile likichepuka na kuingia kwenye kituo cha mafuta.
Naam dakika mbili baadae, wakati Deus akiwa amesimama pale kwenye kituo cha mafuta anaweka mafuta kwenye gari lake, mara ikasikika ngurumo ya gari lilikuwa lina lalamika barabarani, lilipita pale usawa wakituo cha mafuta kwa speed kali sana na kwenda kupunguza mita chache kabla ya kuikuta njia panda ya himo na bila hata kuonyesha taa elekezi, yani enducator, kuwa linakata kona kulia likaingia mazima na dereva akakanyaga mafuta kwa nguvu, akitokomea upande wa Rombo, “hawa jamaa usikute wamesha sikia huko boda kuna mzigo unavushwa” alisema mmoja kati ya wahudumu wa pale kwenye kituo cha mafuta, ambao walilitambua gari lile kuwa la Polisi, sio kwa rangi zake au maandishi ya ubavuni, pia mkao wa watu waliokuwa nyuma ya gari ilikuwa ni kitambulisho tosha kuwa lilikuwa gari la polisi, Deus alijitabasamulia moyoni.
Gari lilibugia mafuta tank nzima, kisha akafanya malipo na kuingia kwenye gari lake, kisha akaondoka zake kuelekea moshi.********
Mwanaume mtu mzima, alipofika mapokezi, ambapo palikuwa na mschana mrembo kweli kweli alitulia na kusalimia. “habari dada yangu” ilikuwa ni sauti ya kirafiki, “nzuri tu karibu” aliitikia na kukaribisha, “asante sana, nahitaji chumba chenye usalama” alisema yule jamaa na kumfanya yule mschana wa mapokezi atabasamu kwa mshangao, “umekuja na mke wa mtu au?” aliuliza yule mrembo kwa sauti ya kunong’ona huku tabasamu likiwa limeshamili usoni mwake.
Yule jamaa nae akatabasamu kidogo, “hapana, ninahitaji kulala mpaka asubuhi kisha nikapande ndege kuelekea dar” alisema yule jamaa na hapo akaweza kumuona yule mrembo wa mapokezi akimtazama kwa macho yenye kiulizo kidogo, “samahani anko, ni mara yako ya kwanza kufikia hapa?” aliuliza yule mhudumu, huku anapekuwa kitabu chake cha wageni, “yah! ni mara yangu ya kwanza pia kufika arusha” alijibu yule jamaa, na kumfanya mhudumu atabasamu kidogo, “ok! nitakupa namba saba upande wa pili, kule tulivu kidogo, ila bei ya kulala ni elfu ishirini” alisema yule mschana, huku anasogeza kitabu mbele ya yule jamaa ambae sasa ilikuwa ni zamu yake kushangaa, alishangaa bei ya chumba kuwa ni ndogo sana, wakati yeye alikuwa anahitaji hotel ya daraja la juu. “una uhakika kitanifaa hicho chumba kweli?” aliuliza yule mwanaume mtu mzima, “siyo vibaya kama utaenda kutazama mwenyewe” alisema yule mwanamke mhudumu, na hapo akatazama kushoto na kulia kutazama mtu wa kumsindikiza huyu mwanaume kwenda kutazama chumba.
“Nitampeleka mimi” ilisikika sauti toka pembeni yao, wote wakatazamana na yule jamaa akamuona mwanamke mmoja kati ya wale walio mpokea kwa matangazo ya kibiashara, wala usijali, sijaja kibiashara utanipatia hela ya soda tu, alisema yule mwanamke ambae ni wazi alikuwa alisha juwa kuwa yule mzee amemkumbuka kuwa ni mmoja kati wanawake walio kuwa wamempokea hapo awali, “sawa haina shida twende ukanionyeshe” alisema yule jamaa, na kuanza kuongozana na yule mwanamke, kulifuata korido lenye vyumba kushoto na kulia, ninani huyu mtu, na amebeba nini…..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
Shukrani mkuuHii ni ya jana usiku
Tunasubiri ya kututuliza hasira baada ya jana kutufanya tukeshe bila kitu😅🤣Hii ni ya jana usiku
tupia ya asubuhi basi mbona unaremba sanaHii ni ya jana usiku
Una hadithi nziri ila sasa umekuwa zaidi ya mgawa dawa moja kwa siku ila nusu kidonge jitahid ndugu hata epsod mbili uwe unatuwekea japo tunajuwa una majukum yako yanakubana nduguNYUMA YA MLANGO WA ADUI

AmeenMungu akibariki kipaji chako
PamojaNice
Nitajitahidi mkuuUna hadithi nziri ila sasa umekuwa zaidi ya mgawa dawa moja kwa siku ila nusu kidonge jitahid ndugu hata epsod mbili uwe unatuwekea japo tunajuwa una majukum yako yanakubana ndugu