Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NANE: “ok! malipo yangu yaliyobakia” alisema Deus, huku anamtazama Sheba, ambae pia alikuwa anatabasamu, “una uhakika kuwa unahitaji fedha pekee, au na kitu zaidi unahitaji kwa mschana mrembo kama mimi?” aliuliza Sheba kwa sauti laini na tulivu, “huu sio wakati wa utani, mpaka sasa sijajua narudi vipi mpaka tarakea kilomita ishirini kwa mguu begi la kilo hamsini mgongoni…” alisema Deus na kabla hajamaliza kuongea, akakatishwa na mlio wa simu ya kwenye dash board ya gari, wote wawili wakatazama kwenye kioo cha screen yenye upana wa sentimeta thelathini kwa kumi na tano..…….ENDELEA…

Wakaona jina la mpigaji kuwa ni Atshen, Sheba akaipokea mara moja, “kazi nzuri Deus, dakika chache kabla ya muda ulio ahidi, nina zawadi kubwa kwako kwa kazi nzuri uliyoifanya” alisema Atshen kwa sauti yenye kujawa na furaha ya wazi, “Sheba, mpatie hiyo funguo ya ile nyumba ya kule Kisarawe, msetie GPS itakayomfikisha pale, kisha muelekeze password na umuelekeze namna ya kufungua mlango, mpatie fedha zote za kitanzania ulizo nazo kwenye gari” alisema Atshen na kumfanya Deus ajitabasamulie moyoni, “mwisho bwana Deus, hilo gari ni la kwako, unaweza kubadili namba za sajili kwa kuweka plate namba iliyopo kwenye buti, nakutakia safari njema na mafanikio mema, naamini safari ijayo tutafanya kazi nzuri zaidi” alisema Atshen, na kabla hajakata simu, Deus akaachia tabasamu la wazi kabisa, “asante sana boss” alisema Deus, huku anageuka na kutazama mandhari ya gari lile kwa ndani.

Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Deus alieona kama vile ametimiza ndoto yake ya kumiliki BMW S7, hata baada ya kukamilisha makabidhiano ya kila kitu ambacho alitakiwa kukabidhiwa, yaani begi jingine la fedha, lililokuwepo ndani ya buti, ambazo sio tu zilizidi milion hamsini ya kukamilisha kwenye malipo yake ya millioni mia moja, ila zilizidi mara dufu.

Pia alikabidhiwa funguo za nyumba, kadi ya gari, password ya kufungulia nyumba ambayo aliambiwa anaenda kuimiliki na mwisho ikafuata zamu ya kushangaa, ni baada ya kuona linashushwa sanduku toka kwenye buti la gari, nao wakafungua na kukagua mzigo ambao ulikuwa na vijitofari hamsini vya dhahabu, kila kimoja kikiwa na uzito wa kilo moja, “ina maana huu ndio mzigo niliokuwa na usafirisha na sio yule mwanamke kama nilivyoambiwa?” aliuliza Deus, ambae kwa malipo aliyopewa, na kazi aliyoifanya aliona inalipa.

Saa mbili kasoro dakika tano, ndio muda ambao, Deus, alianza safari kuelekea tarakea, huku wakina Sheba wakiingia porini, kuufuata mpaka wa kenya ambako wangekuta gari, ambalo wangelitumia mpaka Nairobi, ambako wange panda ndege ya kuelekea Ethiopia, “wacha nikapumzike Arusha mjini, kesho nirudi na barabara ya dodoma kupitia ngorongoro, siwezi kupitia njia ile ile lazima nitakamatwa” aliwaza Deus, ambae kutwa nzima alikuwa katika misuko suko, pia alihitaji kupumzika, sababu siku iliyopita alikesha kwenye kitumbua cha Neela, “nitakutunza kwa nguvu zangu zote” aliwaza Deus, huku anatazama Dash board ya gari lile na kwa bahati nzuri, macho yake yakatuwa kwenye geji ya mafuta, iliyosoma kuwa imebakiza robo ya tank. nitaweka pale njia panda ya himo” alijisemea Deus, huku anaendelea kuyoyoma kuitafuta tarakea.********

Naam pale mrina hotel, mwanaume mtu mzima, mwenye kubeba sanduku dogo jeusi, anaibukia kwenye ukumbi mkubwa ambao ulitawaliwa na watu waliokuwa wanapata vinywaji kwenye meza zao, huku wamekaa kwa mtindo wa wawili wawili mpaka watatu na zaidi, huku meza nyingi zikiwa zime tawaliwa na wanawake.

Yani kwa kifupi ni kwamba ungekuta meza chache sana zina wanaume watupu, ambao licha ya kupata vinywaji, pia macho yao yangekuwa yanakodoa kodoa kwenye meza nyingine ambazo wanawake watupu au wanawake walikaa mmoja mmoja kwenye meza yake au wanawake walio kuwa wanajipitisha pitisha kwa wanaume hao, ukiachilia wale ambao walikuwa wamekaa na wanaume wao, wakipata vinywaji na mbuzi wa kuchoma

Lakini anapoibuka tu yule mwanaume mtu mzima, ghafla wakainuka wanawake kama wanne hivi, toka kwenye meza tofauti tofauti na kumfuata, “karibu baba, chumba ninacho” alisema mmoja na mwingine akadakia, “leo sijafanya kazi kabisa baba, wewe ndio wa kwanza” yule jamaa, ambae alionekana kushangazwa na mapokezi yale, aligeuka kuwatazama wanawake wale, huku anaendelea kutembea, “ukitaka miguu yote nitakupa offer elfu ishirini” alisema mwingine, lakini yule jamaa hakuwajali, alizidi kutembea kuelekea mapokezi, ambako kulikuwa kunauzwa pombe.

Baada ya kuona mgeni yule hakuwa na mpango nao, wale wanawake wakageuka na kurudi kwenye viti vyao, na kumuacha yule jamaa akizidi kuelekea mapokezi, “sasa amekuja kufanya nini hapa? au ni mchuna ngozi” aliongea mmoja kati wanawake wale na kumalizia kwa msonyo mrefu, huku anajikalisha kwenye kiti kimoja, karibu na meza moja iliyokaliwa na wanaume wawili walikuwa wana kunywa pombe taratibu.

Yule mwanamke, alieonyesha kuwa na hasira, akamtazama yule mwanaume mtu mzima, ambae sasa alikuwa amesha fika mapokezi, nakutamani kuachia tusi jingine, sijuwi kwanini alimkasirikia kiasi hiki, lakini kabla hajaongea lolote, akasikia toka kwa wale jamaa, walikaa pembeni yake, “afadhari mzee mipango huyooo anapiga simu” alisema mmoja wao, kwa sauti yenye furaha na matumaini, “nani huyo Mduma nini” aliuliza mwenzie, “sasa je, huyu jamaa ukiona anakupigia simu ujuwe muda sio mrefu unakamata mkwanja” alisema yule wa kwanza na hapo hata yule mwanamke pia akavutika na kugeuza uso wake kuwatazama.

Akamuona mmoja wao akiwa ameishika simu yake, ambayo aliipokea na kuiweka sikioni, “niambie Mduma” alisema yule jamaa na kutulia kidogo, akisikilizia upande wa pili, ilikuwa vigumu kwa mtu wa pembeni kusikia upande wapili ulikuwa unasema nini, zaidi angemsikia huyu jamaa akijibu kwa minguno na maneno mafupi, “ndiyo…. mhmh!... yes nipo hapa…..yupoje…” hapo angeuliza huku anatazama kule mapokezi “mshua flani hivi, anamkoba mweusi….basi imeisha hiyo nyie fanyeni faster” alimaliza kuongea yule jamaa na kukata simu, “vipi Chao, jamaa anasemaje?” aliuliza yule mwenzie, “si nilikuambia jamaa hakosi mchongo, anasema yule dingii pale counter, anae jiwe moja kubwa ni kinyama, ametoka nalo jioni hii melerani, sasa haitakiwi apande nalo ndege, lazima lirudi kwetu, kisha tulivushe Kenya tukapige hela mingi” alisema yule alieitwa Chao, “kwahiyo tunafanyaje?” aliuliza kwa sauti yenye shauku yule mwingine, tuliza mshono chalii, inabidi kwanza tujuwe chumba chake halafu baadae tusemenae, yani unaambiwa anao mzigo wa maana” alisema Chao huku wakitazama kule mapokezi.

Naam wakati wawili hawa wanaendelea na maongezi yao, yule mwanamke hakuwepo tena kwenye kiti chake, nadhani alienda kukaribisha mgeni mwingine.*******

Naam nusu saa tu ilipita toka gari la polisi, lenye kikundi cha koplo Othman liondoke Mombo ajalini, wakina Cheleji nao wakaingia na gari lao, wakikuta tayari moto umesha zimwa, na magari yakianza kupita, tayari walikuwa wamesha pewa taarifa na Ulenje, ambae aliwasisitiza kuongeza speed waliwahi BMW jeusi, kabla halija vuka mpaka, pia aliwagawa mara mbili wengine wawahi mpaka wa tarakea, huku wengine wakiwahi mpaka wa Namanga, ambayo ndiyo mipaka pekee inayoweza kutumiwana na watu hao wanao watafuta.

“Nadhani tumeona picha halisi ya mtu tunae mfuatilia, hakika sio wa mchezo” tukikutana nae tuna msalimia kwa risasi nyingi sana” alisema Cheleji, wakati safari inaendelea, huku Dereva wake akimsikiliza, “ sita ruhusu nikose mkwanja hata iweje” alisema Cheleji, kwa sauti ya kukamia kweli kweli, huku gari likizidi kushika mwendo.*******

Saa mbili na nusu za usiku, njia panda ya himo, lilionekana gari dogo jeusi aina ya BMW S7 jeusi, likitokea upande wa Rombo na kuiacha njia ya kwenda Moshi na kuifuata ya kwenda dar, mwanzo nilitaka kushangaa, kwanini Deus, ameamua kurudi Dar es salam, lakini mshangao unamalizika muda mfupi baadae, baada ya kuona gari lile likichepuka na kuingia kwenye kituo cha mafuta.

Naam dakika mbili baadae, wakati Deus akiwa amesimama pale kwenye kituo cha mafuta anaweka mafuta kwenye gari lake, mara ikasikika ngurumo ya gari lilikuwa lina lalamika barabarani, lilipita pale usawa wakituo cha mafuta kwa speed kali sana na kwenda kupunguza mita chache kabla ya kuikuta njia panda ya himo na bila hata kuonyesha taa elekezi, yani enducator, kuwa linakata kona kulia likaingia mazima na dereva akakanyaga mafuta kwa nguvu, akitokomea upande wa Rombo, “hawa jamaa usikute wamesha sikia huko boda kuna mzigo unavushwa” alisema mmoja kati ya wahudumu wa pale kwenye kituo cha mafuta, ambao walilitambua gari lile kuwa la Polisi, sio kwa rangi zake au maandishi ya ubavuni, pia mkao wa watu waliokuwa nyuma ya gari ilikuwa ni kitambulisho tosha kuwa lilikuwa gari la polisi, Deus alijitabasamulia moyoni.

Gari lilibugia mafuta tank nzima, kisha akafanya malipo na kuingia kwenye gari lake, kisha akaondoka zake kuelekea moshi.********

Mwanaume mtu mzima, alipofika mapokezi, ambapo palikuwa na mschana mrembo kweli kweli alitulia na kusalimia. “habari dada yangu” ilikuwa ni sauti ya kirafiki, “nzuri tu karibu” aliitikia na kukaribisha, “asante sana, nahitaji chumba chenye usalama” alisema yule jamaa na kumfanya yule mschana wa mapokezi atabasamu kwa mshangao, “umekuja na mke wa mtu au?” aliuliza yule mrembo kwa sauti ya kunong’ona huku tabasamu likiwa limeshamili usoni mwake.

Yule jamaa nae akatabasamu kidogo, “hapana, ninahitaji kulala mpaka asubuhi kisha nikapande ndege kuelekea dar” alisema yule jamaa na hapo akaweza kumuona yule mrembo wa mapokezi akimtazama kwa macho yenye kiulizo kidogo, “samahani anko, ni mara yako ya kwanza kufikia hapa?” aliuliza yule mhudumu, huku anapekuwa kitabu chake cha wageni, “yah! ni mara yangu ya kwanza pia kufika arusha” alijibu yule jamaa, na kumfanya mhudumu atabasamu kidogo, “ok! nitakupa namba saba upande wa pili, kule tulivu kidogo, ila bei ya kulala ni elfu ishirini” alisema yule mschana, huku anasogeza kitabu mbele ya yule jamaa ambae sasa ilikuwa ni zamu yake kushangaa, alishangaa bei ya chumba kuwa ni ndogo sana, wakati yeye alikuwa anahitaji hotel ya daraja la juu. “una uhakika kitanifaa hicho chumba kweli?” aliuliza yule mwanaume mtu mzima, “siyo vibaya kama utaenda kutazama mwenyewe” alisema yule mwanamke mhudumu, na hapo akatazama kushoto na kulia kutazama mtu wa kumsindikiza huyu mwanaume kwenda kutazama chumba.

“Nitampeleka mimi” ilisikika sauti toka pembeni yao, wote wakatazamana na yule jamaa akamuona mwanamke mmoja kati ya wale walio mpokea kwa matangazo ya kibiashara, wala usijali, sijaja kibiashara utanipatia hela ya soda tu, alisema yule mwanamke ambae ni wazi alikuwa alisha juwa kuwa yule mzee amemkumbuka kuwa ni mmoja kati wanawake walio kuwa wamempokea hapo awali, “sawa haina shida twende ukanionyeshe” alisema yule jamaa, na kuanza kuongozana na yule mwanamke, kulifuata korido lenye vyumba kushoto na kulia, ninani huyu mtu, na amebeba nini…..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Hii ni ya jana usiku
 
Una hadithi nziri ila sasa umekuwa zaidi ya mgawa dawa moja kwa siku ila nusu kidonge jitahid ndugu hata epsod mbili uwe unatuwekea japo tunajuwa una majukum yako yanakubana ndugu
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TISA: “Nitampeleka mimi” ilisikika sauti toka pembeni yao, wote wakatazamana na yule jamaa akamuona mwanamke mmoja kati ya wale walio mpokea kwa matangazo ya kibiashara, wala usijari sijaja kibiashara, utanipatia hela ya soda tu, alisema yule mwanamke ambae ni wazi alikuwa ashajua kuwa yule mzee amemkumbuka kuwa ni mmoja kati ya wanawake walio kuwa wamempokea hapo awali, “sawa haina shida twende ukanionyeshe” alisema yule jamaa na kuanza kuongozana na yule mwanamke, kulifuata korido lenye vyumba kushoto na kulia, ni nani huyu mtu na amebeba nini…..…….ENDELEA…

Huyu ni anaitwa bwana Hassan Simba, ni mfanya biashara wa madini nae ni kama bwana Atshen, anafanya biashara bila vibali vyovyote, tofauti ni utaifa wao, huyu ni mtanzania na biashara zake hazikuwahi kuhusisha umwagaji wa damu kama ilivyo kwa bwana Atshen ambae utaifa wake ni Ethiopia.

Leo akiwa amepigiwa simu na mchimbaji mmoja mdogo mdogo wa pale melerani, akamwambia aje Arusha haraka, kuna mzigo mkubwa umepatikana, nae akachukuwa ndege kwa haraka na kuwahi Arusha kisha merelani ambako alikutana na jiwe kubwa la tanzanite lenye uzito wa kilo moja na robo, ambalo alilinunua kwa bei rahisi mno, yaan million mia mbili na hamsini, ikiwa ni gharama ndogo sana kulinganisha na gharama halisi ya jiwe lile la thamani, gharama ambayo ukiifananisha nayo ungeweza kusema umenunua ng'ombe kwa bei ya kuku, pengine ni kutokana na ukaribu wao na uteja wa kudumu wenye uhakika.*********

Naam huko jijini Dar es salaam, bwana Uleje, alikuwa anapokea simu za mara kwa mara toka kwa bwana Kadumya, “kaka Fanya hima mzigo upatikane, tutapoteza fedha nyingi sana” alisema Kadumya na kuzidi kumtia wazimu bwana Ulenje, “kaka vijana wapo kazini na nina amini muda wowote watalifikia gari” alisema Ulenje kwa kujiamini na hata alipokata simu moja kwa moja akapiga kwa Cheleji.

Simu haikuita sana, ilipokelewa mara moja, “mpo wapi Cheleji?” aliuliza Ulenje, “afande tupo kwa Sadara hapa, tumesha pita moshi tunaelekea Arusha” alijibu Cheleji, ambae sauti yake ilisikika, sambamba na ngurumo ya gari, ilionyesha wazi walikuwa wanaendelea na safari, “jitahidini kuwahi kabla hawajavuka mpakani” alisisitiza Ulenje, ambae hakuishia hapo na vipi kuhusu, wakina Othuman umewasiliana nao?” aliuliza Ulenje, ambae aliamini kuwa akifanikiwa kulipata lile gari lazima atajipatia fedha ndefu pamija na lile gari la kifahari, “sijawasiliana nao, ila tayari wamesha elekea Tarakea” hilo lilikuwa jibu la Cheleji, kabla hawajagaana kwa Ulenje kusisitiza taarifa za mara kwa mara.

Naam mara baada ya kukata simu, akabofya namba ya Othman, kwa lengo la kuipiga, lakini kabla haijaanza kuita ile namba ikajitoa kwenye kioo na simu yake hiyo kuanza kuita, alipotazama jina, alikuwa ni Othman akaipokea mara moja na kuiweka sikioni, “niambie Othman, vipi mmesha fanikiwa kulikamata hilo gari?” aliuliza Ulenje, kwa sauti yenye shauku kubwa, “afande mpaka tupo tarakea, hakuna dalili ya uwepo wa lile gari, kuna watu wanasema kuna gari lilionekana, lakini hawana uhakika kama ni lenyewe, maana tayari giza lilikuwa limeshaingia, ila wanasema limesha rudi upande wa himo na kitu cha kushangaza hatuja kutana nalo” mh! inamaana wameshindwa kuvukia tarakea na sasa wanatafuta mpaka mwingine wakuvukia?, endelezeni msako, kumbukeni kuna fedha ndefu sana inawasubiri” alisisitiza Ulenje ambae bado alikuwa na matumaini ya kulipata lile gari, na yeye kujipatia fedha nyingi sana na lile gari la kifahari (bossi wake pia analiwaza hilo gari 😅😅 sijui tuwaambie kuwa mwenzao kasharudi😅 ila acha tuendelee.******

Naaaam bwana Simba akiwa anatembea taratiu nyuma ya mwana dada huyu mfupi kiasi mwenye makalio makubwa, alievalia kaptula fupi ya jinsi, ambayo haikuweza kuhifadhi mapaja manene ya mwanamke huyu mweupe mwenye kunyoa kiduku kichwani mwake, alitazama makalio ya mwanamke yule akapandisha macho yake mpaka mgongoni, kisha shingoni na kichwani ni kama alikuwa anathaminisha kitu flani, “anafaa kuliwa, ila sina uhakika na usalama wa mzigo wangu” aliwaza mzee Simba, akiwa ameshikilia sanduku lake dogo jeusi.

Wakiwa wanatembea kuelekea upande wa vyumbani, waliufikia mlango wa kutokea uwani, ndipo mzee Simba alipomuona yule mwanamke anasimama ghafla na mbele yake, “babaangu sikiliza sikujuwi wala hunijuwi na sijuwi una mzigo gani hapo ulipo, nilikuwa nimekaa kwenye meza moja jirani na wanaume fulani, mmoja wao akaongea kwa simu, wakasema umetoka melerani na una mzigo, hivyo wanataka kukuibia, na hawa jamaa jinsi walivyo wanaweza kukuuwa kabisa, fanya unachoweza ondoka sehemu hii haraka sana” alisema yule mwanamke kisha akageuka na kuanza kutembea kuelekea upande wa uwani, “dada subiri kwanza” alisema mzee Simba na yule dada akasimama na kumtazama mwanaume huyu mtu mzima, ambae alimuona akiwa anaingiza mkono mfukoni na kuibuka na kitita cha fedha, “asante sana kwa msaada wako” alisema yule mzee huku anachapua noti kadhaa, za elfu kumi kumi na kumpatia yule mschana, “asante sana, babangu, ila jitahidi uondoke hapa, wale watu ni wakatili kinyama” alisisitiza yule mwanamke huku anapokea ile fedha.

Hapo likabakia swala moja kwa mzee Simba, atatokaje mahali pale, maana ni wazi kuna mtu alishaanza kumfuatilia, “hivi kuna njia nyingine ya kutokea hapa?, maana?” aliuliza mzee Simba, na kabla hajamaliza kuuliza tayari mwanamke alikuwa na jibu lake, “twende huku babangu” alisema yule mwanamke, huku akiongoza kwenye mlango wa kutokea uwani, na mzee Simba akafuata.

Walitembea kwa pamoja, wakiibukia kwenye eneo la uwani, ambako kulikuwa na vyumba vingi, wao hawakuhangaika na chumba hata kimoja, walienda moja kwa moja kwenye malango wa kutokea nje, “tupite hapa, ukatokee barabara ya Stendi ndogo, kisha uwahi barabarani uchukuwe hata boda boda ukimbie, alisema yule mwanamke wakati wanavuka ule mlango na kuibukia nje, wakati huo tayari mzee Simba tayari alikuwa amesha tawaliwa na uoga mkubwa sana.******
Naam Deus Nyati, akiwa ndani ya BMW S7 gari la ndoto yake, sasa alikuwa anaingia Arusha mjini, huku mara kwa mara akikagua dash board ya gari lake, ambayo kwenye screen yake palionyesha ramani ya GPS, iliyochukukuliwa kwa mfumo wa setelite, iliyoonyesha vyema mitaa na barabara za jiji la Arusha.

Kijana wetu Deus, akatazama hotel iliyopo karibu na barabara ya ngorongoro, akaiona hotel imeandikwa Mrina Hotel, “hapo hapo patanifaa” alijisemea Deus, huku anatazama mbele anakoelekea, akiona Bango pembeni ya barabara, limeandikwa Sakina Hotel, Deus ambae alikuwa katika mwendo mdogo, hakuijali ile hotel zaidi ya hapo anaingiza mkono mfukoni na kuibuka na simu yake ambayo ilikuwa na masaa mengi hajaiwasha, wakati huu alikuwa anapandisha mpando wa kuingia mianzini.******

Naam baada ya kuhakikisha yule mzee mwenye sanduku dogo jeusi amesha toka pale mapokezi, nakupotelea kwenye korido, akiongozana na yule mwanamke, ambae ni mmoja kati ya wanawake wanaofanya kazi ya kuburudisha wanaume, ndipo kijana Chao akainuka na kuelekea mapokezi, “oya sister kuna mzee wangu mmoja amevaa shati la blue, ameenda chumba namba ngapi?” aliuliza Chao, akijidai kufahamiana na mzee Simba, “hoo yule mzee mwenye sanduku jeusi, ameenda kukagua chumba namba saba” alijibu yule mschana, ambae sasa alikuwa anatoa vinywaji kwenda kwa mhudumu alieagizwa na mteja.

Hapo Chao hakupoteza hata dakika, akatoka pale mapokezi nakuelekea upande ule wa kirido la vyumbani, ambako licha ya kufika pale na kutazama huku na huku, lakini hakumuona yule mwanaume mtu mzima, hapo Chao akatambea kwa haraka mpaka kwenye mlango wa chumba namba saba, Chumba ambacho aliambiwa kuwa, yule mzee mwenye sanduku jeusi ameenda kukikagua.

Chao alifika mbele ya chumba kile ambacho mlango wake ulikuwa wazi, hivyo akajionea kwa macho yake, chumba kikiwa tupu, sio yule mzee wala yule mwanamke, wote hawakuwepo ndani ya chumba, “pumbavu ameondoka huyu, alisema Chao huku anatoa simu haraka na kupiga namba ya Mduma, nayo ikaanza kuita nae akasikilizia huku anaufuata mlango wa kutokea nje.*******

Naam wakati huo huo, lilionekana gari dogo aina ya Toyota Alteza, likikatiza kwa speed mitaa ya setendi kuu, likitokea upande wa Ngarenalo, na kupotelea upande wa barabara kuu iendayo moshi, huku ndani yake wakionekana vijana wanne ambao wao binafsi ilikuwa ngumu kuonana kutokana na wingu la moshi wenye harufu kali sana, moshi ambao chanzo chake ni sigara bwege ambazo, zilikuwa zinavutwa mle ndani ya gari lile dogo, “kamua babake, tukachukuwe vyetu, yule fala nimemuona kwa macho yangu anaondoka na lile jiwe” alisema mmoja wao aliekaa seat ya pembeni ya Dereva kwa sauti yenye lafudhi ya kiarusha
, iliyo changanyika na ulevi wa sigara bwege, “niamini Chalii, sekunde tu, tunatimba hapo Mrina” alisema Dereva wa gari lile, dogo jeusi, lenye sauti kubwa katika ngurumo yake.

Naam wakati safari imeshika kasi, huku sigara bwege zikiendele kuvutwa ndani yagari, mala simu ya Mduma ikaita, nae akaitoa mfukoni, na kuipokea, “niambie baba la baba” alisema Mduma, wakati huo gari lao limeshika mwendo kweli kweli, “fanyeni faster jamaa amesanuka, nazani atakuwa anatafuta usafiri asepe” alisikika Chao toka upande wa pili wa simu, alie onekana wazi kuwa, alikuwa anatembea kwa speed, kwa jinsi alivyo kuwa ana hema mfurulizo, mfukuzie wa boya, sisi tuna kuja huko” alisema Mduma, kabla kukata simu, na kumsisitiza Dereva aongeze speed, nae akufikilia mala mbili, wala ya kuwa walikuwa wamesha karibia barabara kuu, nakwamba wataingia barabara kuu, na kukata kona upande wa kulia, kuelekea upande wa stendi ndogo, ambako ndiuo maeneo ya karibu ya Mrina hotel kule ambako liko wino lao.******

Wakati huo huo kwenye kichochoro cha upande wa kulia wa jengo la Mrinda hotel, kilicho funikwa na giza nene, bwana Simba akiwa nyumba ya mschana alie mpa habari za watu wanao panga kumpora malizake, walitembea kwa haraka kuelekea upande wa barabarani, huku bwana Simba mwenyewe akiwa ametawaliwa na ofu kubwa sana, “hivi hapa ninaweza kupata usafiri wa ufika Moshi usiku huu?” aliuliza mzee Simba ambae sauti yake ilikuwa ime tawaliwa na kitetemeshi, “usafiri mwingi sana, ila kuwa makini, maana inaonyesha yule kaka anawenzake na wapo njiani wanakuja” alisema yule mwanamke, huku wakiwa wanakaribia mwisho wajengo lile la hotel, ambako palionekana kuwa na mwanga, ..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom