Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TATU: toka aliponiambia kuwa kuna mizigo itasafiri leo kuja songea sijaona hata ujumbe wake na simu yake haipatikani kabisa” alisema mzee Nyati na kuendelea kusema “ila kama nitapata mawasliano yake au akiwasha simu, nitamueleza kila kitu” alisema mzee Nyati, kwa sauti ambayo ilimaanisha alichokuwa anakisema, “ok! kabla hatujaondoka tunaomba tukuulize kitu kama hutojari” alisema yule luten kanal, huku akimtazama mzee Nyati kwa macho yenye vipimo vya kung'amua uongo na ukweli…..….…….ENDELEA…

“bila shaka unaweza kuuliza” alijibu mzee Nyati, “ok! tunahitaji kufahamu kama Deus ana miliki gari aina ya BMW S7, jeusi” alisema Luten kanal, “mh! hajanieleza kama amenunua ila ninachojua gari la aina hiyo ni gari la ndoto yake, alipanga kununua mara akirudi toka DRC” alijibu mzee Nyati, lakini hapo hapo nikama alikumbuka jambo, “lakini ndio kwanza amerudi jana sidhani kama atakuwa amenunua, labda leo hii aanze mpango wa kulinunua” alisema mzee Nyati akionyesha mashaka yake, “ok! basi kama utapata taarifa zake unaweza kutujulisha” alisema kanal na kumpatia namba yake mzee Nyati na kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka zao wakimuacha mzee Nyati akiwa sindikiza kwa macho na walipotoweka tu akaanza kuandika ujumbe kwenye simu yake.********

Naam, twende kilomita kumi kusini mwa mji wa kibaha, kwenye barabara ya vumbi iendayo wilaya ya kisarawe, tunaliona BMW S7 jeusi likienda kwa mwendo wa kasi ya kawaida likielekea upande wa kisarawe, lakini linapofika maeneo ya relini linapunguza mwendo zaidi na kutembea mwendo mdogo zaidi huku dereva akitazama zaidi pembeni mwa barabara upande wa kulia kwake.

Gari linatembea mita kama mia mbili mbele, kwa mwendo ule mdogo, mpaka walipoikuta barabara ndogo yenye upana wa mita tatu na nusu au nne hivi barabara ambayo mwanzo Deus aliitilia mashaka, lakini alipotazama keenye GPS akaona kuwa hapo ndipo palipo kusudiwa, akakata kona upande wa kulia na kuendesha gari kufuata upande ule wa barabara, ambapo alitembea mita mia nne mbele na kujikuta mbele ya nyumba moja ambayo haijakamilishwa ujenzi wake.

Deus kwa kufuata maelekezo aliyopewa na Sheba, aliingiza gari ndani na kuingia ndani ya jengo lile, aliendelea kufuata maelekezo ya sheba mpaka alipojikuta ndani ya nyumba iliyopo ardhini, ambayo aliambiwa kuwa sasa ni ya kwake, “nipumzike kidogo nikanunue gari dogo kwaajili ya kuzugia” alisema Deus, ambae alioga na kuandaa chai kidogo na vitafunwa ambayo asilimia kubwa ni kwenye vifurushi, yani mifuko na makopo ambavyo hununuliwa kwenye maduka makubwa (Super market).

Naam Deus akiwa anapata chai akatumia muda huo kupekuwa zile bahasha toka kwa madoctor wa UN yani yule wa Kenya, na yule Burundi, ambamo mulikuwa na noti kadhaa za dollar mia mia za kimarekani, pia kulikuwa na zawadi ya simu nzuri ya kisasa na saa ya mkononi, ambayo ilikuwa na uwezo wa kuunganisha mawasiliano na kupiga picha nzuri, ikiwa na camera yenye megapics 5.7, baada ya hapo Deus Nyati alianza kuhesabu fedha alizo zivuna kwa siku ya jana pekee.

Zilikuwa ni zaidi ya million mia mbili na hamsini, fedha ambayo kama angetulia angeweza kufanyia mambo makubwa zaidi, ukiachilia malipo yake aliyoyapata kule MONUSCO, na mishahara yake ya miezi tisa ambayo ilikuwa katika account yake binafsi, ambayo ilikuwa inakaribia milion kumi na tano.

Baada ya hapo Deus akaingia kwenye moja ya chumba ambacho alielekezwa kuwa ndio cha kwake, kwa maana ya chumba maalumu chenye kila kitu, akajilaza kitandani na kufungua simu yake ambayo aliizima jana saa tisa jioni.

Naam ile anafungua simu tu, ikaanza kupokea ujumbe toka kwa baba yake, ile anaufungua na huku jumbe nyingine zikaanza kumiminika kwa fujo, nyingi zikiwa namba ngeni, ilimshangaza sana Deus, maana siku zote simu yake inakuwa hewani lakini hakuwa anapokea jumbe nyingi kiasi hiki, tena sio za kawaida pekee, ila pia ni jumbe za whatsapp pia, lakini Deus hakuangaika na sms nyingine akafungua ile iliyotoka kwa baba yake.

“Deus, jeshi lina kutafuta, wameagiza uliport makao makuu kabla ya saa mbili asubuhi, ni chaguo lako, kuendelea na kazi au kufanya mambo mengine, maana bado una nguvu na uwezo wa kuanza maisha mapya, muhimu umeshajionea mwenyewe, yaliyonitokea mimi na wewe yamekutokea” ulisema hivyo ujumbe ule toka kwa baba yake.

Naam ujume huo ndio uliomfanya aanze kufungua jumbe mbali mbali kwenye simu yake, zikiwa ni zile za simu kawaida na zile za whatasapp, “private Deus Nyati, unatakiwa kureport makao makuu ya jeshi kwaajili ya kurudiwa kwa hukumu yako, imeagizwa kesho saa moja kamili uwe mbele ya ofisi ya CDMP” ulisema ujumbe mmoja wapo kati ya nyingi ambazo zilizoingia kwenye simu yake.

Deus alifungua tena jumbe nyingine kadhaa, zote zikiwa na maneno sawa na jumbe ile ya kwanza, tofauti ni kwamba zilikuwa zimetoka kwenye idara mbali mbali za pale makao makuu ya jeshi, kama vile COT na zinginezo, “dah! nini hii, au hawajardhika na adhabu waliyonipatia” aliwaza Deus, ambae akitazama fedha alizo kuwa nazo, angeweza kuishi maisha mapya bila kutetereka, huku akijiwekea vitega uchumi kadhaa na kabla hata hajamaliza kusoma sms zilizopo, ikaingia nyingine toka kwa baba yake, akaifungua haraka, nayo ilikuwa inasema, “Deus, mbona maswali ni mengi sana, BMW S7 linahusiana nini na wewe, kwani ulishanunua?” swali hilo lilimshtua sana Deus, ambae kabla hajajiuliza hata swali moja, mara akaona simu yake inaanza kuita, kutazama mpigaji, “dah! baba amejua kuniotea” alijisemea Deus, huku anabofya simu yake kuipokea, “shikamoo baba” alisalimia Deus kwa sauti tulivu kama kawaida yake, “marhaba Deus, vipi ulisha kutana na wenzako?” aliuliza mzee Frank kwa sauti fulani, iliyokosa utulivu, “hapana mzee ndio kwanza sasa nawasha simu toka jana, hivyo habari nimeipata toka kwako” alisema Deus, kwa sauti ile ile tulivu, “kwahiyo sasa hivi upo wapi?” aliuliza mzee Frank, kwa sauti ile ile iliyokosa utulivu, “nipo dar lakini hii sehemu hata mimi siifahamu vizuri” alisema Deus.

Hapo wakaongea mawili matatu, huku mzee Frank akimsisitiza Deus kuwa makini na uamuzi wowote ambao atauchukua, japo yeye alimshauri kuachana na kazi ya jeshi, akiamini kuwa licha ya majeshi yote kuwa na misingi mizuri lakini kuna baadhi ya watu wamekosa uaminifu na kutanguliza sifa zao binafsi, hasa linapokuja swala la kuchukuwa hatua za kinidhamu, “lakini baba nitajitahidi tukutane siku za hivi karibuni, maana kuna jambo tunatakiwa kuzungumza” alisema Deus, “ni kuhusu BMW S7?” aliuliza mzee Frank, safari hii aliongea kwa sauti tulivu, “ndiyo baba, tutalizungumza kwa kina tukikutana” alisema Deus, ambae baba yake alishamzoea katika uongeaji wake wa sauti ya taratibu.

Naam walimaliza maongezi yao na mwisho wakaagana na kukata simu, halafu Deus akaizima kabisa.******

Naam saa nne asubuhi makao makuu ya jeshi la ulinzi bado askari Deus Frank Nyati hakuwa amepatikana, makamanda wakuu wa jeshi hilo lenye kuheshimika afrika, walikuwa wameshindwa kupata jibu sahihi juu ya jambo hilo, maana waziri wa ulinzi nae alikuwa anasubiri jibu la kupatikana kwa askari huyo ili apeleke kwa rais.

Wakati huo tayari baadhi ya watu walisha chukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwa pamoja na Brigedia SS Chawe, ambae alikuwa nyumbani kwake anafunga mizigo tayari kuelekea Mtwara ambako angekuwa ni kingozi wa kamand ya askari wa nchi kavu wa kanda ya kusini.

Ukiachia hilo, pia tayari kitengo cha mafunzo na utendaji kivita walisha tuma askari wanne, kwenye makampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika, ilikuona waagizaji wangapi wamenunua gari aina BMW S7 hapa nchini.

Lakini kila kampuni waliyoenda waliambiwa kuwa BMW S7, bado haijaanza kuuzwa kama mtumba na katika ukaguzi wa mtandao waliweza kuona magari ya aina hiyo yaliyowahi kuagizwa mwisho ni S6 na siyo zaidi ya hapo, “labda nendeni pale poster kwenye kampuni ya BMW” sehemu karibu zote walishauriwa hivyo.

Saa nane mchana askari hawa wanne walijikuta kwenye jengo la utawala la BMW, “karibu maafisa niwasaidie tafadhari” alisema meneja wa kampuni ile, “sisi ni maafisa wa jeshi la ulinzi toka makao makuu ya jeshi, tupo hapa kuangalia orodha ya watu walionunua gari aina ya BMW S7 hivi karibuni” alisema askari mwenye cheo kikubwa kuliko wenzake, huyu alikuwa ni yule major wa msaidizi wa mkuu wa kitengo cha mafunzo na utendaji kivita, “mh! boss hilo gari unalosema… hebu tuone kwenye kitabu” alisema yule meneja huku anavuta daftari moja kubwa maarufu kama counter book, “yani kwa kumbu kumbu zangu, ni kwamba toka hili gari liingie sokoni….” alisema yule jamaa, huku akiendelea kufunua kurasa za kitabu kile na kwenda kukwama kwenye kurasa moja, “yes ni magari nane tu yameingia nchini, nayo ni yaliagizwa na watu maarufu” alisema yule meneja ambae alitaja majina ya waagizaji.

Katika majina aliyoyataja hakuwepo Deus Frank Nyati, baada yake kulikuwa na wafanya biashara wakubwa na viongozi wa kisiasa, hapa kuwa na msanii wala mwanamichezo au mtu binafsi wa kawaida, “mh! sasa hii imekaaje?” aliuliza mmoja wao wakati wanaondoka zao, ni baada ya kuwa wameaga pale BMW, “lakini habari za mwanzo zinasema kuwa toka Deus asajili whatsapp alikuwa ameweka picha ya gari lile” alisema mwingine huku mwenzao akidakia, “isitoshe afande huyu amefika jana tu, hilo gari amelinunua lini na saangapi, ni wazi kabisa yule askari hajamiliki hilo gari” alisema yule askari na kuzidi kuaminishana kuwa Deus hakuwa huyo muuwaji wa Arusha.*****

Yap! siku ya kwanza ilikatika, Deus akiwa amejipumzisha ndani ya jengo lile chini ya ardhi, sana alitoka kidogo na kwenda kutafuta bidhaa kwaaji ya kuandaa vyakula alivyo vizoea, alinunua vitu kama mchele, unga viungo kama vile nyanya vitunguu maji, hoho na vinginevyo vingi.

Pia alinunua vifaa vya kufanyia usafi wa mzingira, kama vile jembe, fyekeo koleo na vitu vingine vingi, kama msumeno nyundo na misumari, kisha akarudi nyumbani kwake.

Naam siku ilipita, sio Jeshi au polisi waliompata Deus, siku ya pili nayo ikapita, huku Deusi akifanya kazi ndogo ikiwa ni pamoja na kununua gari dogo la kubeba mizigo maarufu kama kirikou, huku akitengeza matuta kadhaa na kupanda mboga mboga, ndani ya week moja tayari mimea ilisha anza kumea, huku tayari Deus alikuwa amesha tengeneza banda la kuku na kufanya mazingira ya nyumbani kwake yaonekane kama kweli anaishi mtu, tena mwenye maisha duni, Deus akitumia muda wa Asubuhi na jioni, kufanya mzoezi ya utimamu wa mwili na mapigano.

Naam week tatu baadae ikiwa ni week ya kwanza ya mwezi wapili week ya tatu jeshi la polisi, lilisha kubari kuwa ni vigumu kumpata muuwaji mwenye BMW jeusi, wengine waliamini kuwa pengine muuwaji alitokea Kenya, huku jeshi la ulinzi na vyombo vingine vya usalama vikiamua kuweka pembeni swala la Deus, kwamba endapo atapatikana sawa na asipopatika ni sawa maana tayari alisha hukumiwa kundolewa kazini, ni week ya tatu toka Deus azime simu yake ya mkononi, hii ni ijumaa ya week ile, mida ya saa kumi na mbili za jioni, Deus akiwa mazoezini mara akapokea simu ni kwa namba ile ya kwenye gari, ambayo sasa aliiunganisha kwenye ile simu aliyopewa na wale madoctor. .…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NNE: wengine waliamini kuwa pengine muuwaji alitokea Kenya, huku jeshi la ulinzi na vyombo vingine vya usalama vikiamua kuweka pembeni swala la Deus, kwamba endapo atapatikana sawa na asipopatikana ni sawa maana tayari alisha hukumiwa kundolewa kazini, ni week ya tatu toka Deus azime simu yake ya mkononi, hii ni ijumaa ya week ile, mida ya saa kumi na mbili za jioni, Deus akiwa mazoezini mara akapokea simu, ni kwa namba ile ya kwenye gari, ambayo sasa aliiunganisha kwenye ile simu aliyopewa na wale madoctor. .…….ENDELEA…

“hallow Dereva kuna mzigo wa kilo mia moja, kilomita mia tisa themanini na mtu mmoja, malipo yako shilingi million mia mbili” ilisikaka sauti ya kiume toka upande wapili wa simu.

Kwanza Deus aliachia tabasamu la kimya kimya, huku anajiuliza million mia mbili kwaajili ya mzigo wa aina gani, lakini akahisi pengine uelekeo ni mgumu sana ndio maana fedha imekuwa kubwa sana, “ok! taja uelekeo tafadhari” alisema Deus kwa sauti tulivu, “dar, Songea mpaka likuyufusi, mpakani na msumbiji” ilisema ile sauti ya kiume upande wapili wa simu.

Mpango wa safari ulimsisimua sana Deus, maana ukiachia kujipatia fedha, pia ataenda kukutana na baba yake, “sheria zako kabla sijakupa za kwangu” alisema Deus, ambae sasa alikuwa amelowa jasho kama amenyeshewa na mvua, kwaajili ya mazoezi, “moja usifungue mzigo, mbili mzigo ufike salama ni hizo tu, sasa nasikiliza toka kwako” alisema yule mwanaume upande wapili wa simu,

Ukweli Deus hakuwa na sheria zozote zaidi ya ile ya kutokujuana majina na kuto kuingia na bunduki kwenye gari lake, pamoja na ile ya hakuna mpango juu ya mpango” ambazo alizitunga akiwa safarini Arusha baada ya kuamsikia sheba pia hizo habari za sheria, na hapo ndipo alipoona kuwa kuna umuhimu wa kuwa na sheria zake binafsi zitakazo msaidia katika kazi hii mpya, ambayo malipo yake ni makubwa sana, “ok! tuta tumia sheria namba moja mpaka tatu na nne” alisema Deus kwa namna ya ubunifu, ilikuifanya kazi yake iwe na heshima fulani, “nifafanulie kijana” alisema huyo mtu ambae uongeaji wake, ulionyesha wazi kuwa ni mtu mwenye fedha nyingi.

Hapo Deus kwa ubunifu kubwa sana, akaanza kutaja sheria zake huku akizipa namba, “namba moja, hakuna kujuana majina, namba mbili malipo ni mkononi na hakuna mkopo, namba tatu, hakuna matumizi ya bunduki kwenye gari langu, na sheria namba nne, hakuna mpango juu ya mpango” alisema Deus, ambae sasa alikuwa anaingia ndani ya lile jengo chakavu, ambalo sasa lilikuwa limefungwa camera za ulinzi kila kona na kwa siri kubwa sana, kiasi cha kuto kuonekana kirahisi, “sawa nimekubari, lakini hakikisha usalama wa mzigo na abiria wako” alisema huyo mtu ambae kutokana na sheria za Deus hakupaswa kutaja jina lake, “sawa nitajie siku na saa ya kuanza safari” alisema Deus, kwa sauti yake tulivu huku akiwa anamaliza kuingia ndani nyumba ya chini na kuchukuwa kijitabu cha kumbu kumbu na kalamu ya wino na kuanza kuandika zile sheria zake kwa kufua namba kama alivyo zitaja, “safari inaanzia mwenge jijini Dar es salaam, muda saa mbili kamili za usiku, saloon ya mama P, mita kumi na tano, kusini mashariki toka ilipo benk ya NMB” alisema yule mwanaume.

Wakati huo Deus alikuwa anaandika sheria zake nyingine zaidi ya zile zamwanzo, “ok! mpango umekubarika, lakini zingatia sheria namba nane, simamia muda sahihi” alisema Deus, huku anaandika hiyo sheria namba nane, akimaliza na sheria namba tisa, nidhamu ndani ya gari lake baada ya hapo akaingi chumbani kwake ambako kuna bafu na choo kwaajili ya kwenda kujiandaa na safari.*******

Naam!, sasa tupo barabara ya kilwa, maeneo ya saba saba huko Temeke, lilionekana gari aina ya ford ranger likiingia upande wa kushoto wa barabara na kuambaa ambaa pembezoni mwa ukuta wa uwanja wa saba saba, kisha linaenda kusimama mita kama mia moja hivi, eneo ambalo lilikuwa na magari kadhaa, yakiwepo magari makubwa ya mizigo na ya mafuta, pia yalikuwepo magari madogo.

Lile Ford Range, linaenda kusimama pembeni ya gari jingine dogo aina ya Toyota Noah la rangi nyeusi, hapo hapo mlango wa Toyota Noah unafunguliwa, anashuka kijana mmoja na begi dogo anaweka na kusogea kwenye lile gari aina ya ford Ranger, ambalo bado lilikuwa lina unguruma, sasa tunaona kioo cha Dereva kina shushwa,“kilo ishirini hizi, boss amesema week ijayo anataka mzigo wake” alisema yule kijana, huku anakabidhi lile begi kwa dereva ambae sasa tunapata kumuona dereva huyo mwenye muonekano wa utu uzima, “nimeongea nae, amesisitiza hilo ila asiwe na wasi wasi, nadhani ananifahamu kuwa nina mawakala wengi sana” alisema yule dereva mtu mzima, huku anapokea lile begi na kuliweka kwenye seat ya pembeni yake, yani seat ya abiria wa mbele, kisha akapandisha kioo cha gari na kugeuza gari kisha akaondoka zake, akiacha lile gari jeusi aina Toyota noah likiwa lesimama pale pale na yule alieshuka alikuwa ameshaingia tena kwenye gari na kufunga mlango.

Naam Ranger liliingia barabara kuu na kuelekea upande wa mjini, huku dereva wa gari lile akiendesha gari kwa kasi nakuja kusimama kwenye maungio ya barabara ya kilwa na Mandera, ambapo palikuwa na foleni ndefu kiasi, na hapo ndipo dereva huyu mtu mzima alipofungua lile begi lake na kuzamisha mkono ndani yake, kisha akaibuka na bando moja kubwa sawa na mkate wa buku mbili, lililofungwa kwa mifuko ya plastic, ambayo ilikuwa inaangaza kile kilichopo ndani yake, ambacho kwa muonekano wa kawaida ni kama unga fulani mweupe mfano wa maziwa ya unga, dereva akaupekuwa zaidi na kutazama ndani kulikuwa na bando nyingine nne kama lile.

Dereva anatabasamu huku anatoa simu yake na kupiga namba ya mtu flani, ambayo haikuchelewa kupokelewa, “oya! mzigo umeingia, fanya faster uje uuchukue usambaze kwa vijana” alisema yule dereva, “poa poa, kesho nije home?” aliuliza mvulana upande wa pili wa simu, “hapana tukutane Rozana kwenye ile bar ya Sun city” alisema dereva kabla ya kukata simu na kupiga simu nyingine, wakati huo magari yanaanza kutembea taratibu.

Simu ilipokelewa mara moja, na maongezi yalikuwa kama yale ya mwanzo, akafanya hivyo kwa watu kadhaa na mpaka analiacha lile eneo la foleni, tayari alishaongea na watu wanne, akiwataka kukutana nao hapo Sun City bar.

Huyu anaitwa Issa Simba ni ndugu wa damu kabisa na Hassan Simba, mwanaume mtu mzima wa Arusha, tofauti ya Hassan na Issa ni utendaji wa biashara zao, wakati Hassan alikuwa anasimamia biashara zake binafsi, lakini Issa yeye alikuwa anafanya kazi chini ya mtu na mbaya zaidi ni biashara ngumu sana, ni biashara ya dawa za kulevya.*******

Saa mbili kasoro dakika tano za usiku, maeneo ya mwenge dar es salaam, ndani ya saloon moja kubwa sana ya kike, yenye bango kubwa nje yake lililoandikwa MAMA P, ndani walionekana wanawake wanne, wote wakiwa wenye muonekano wa kuvutia, wawili wenye umri wa miaka kati ya ishirini na mbili mpaka ishirini na tano, waliovalia nguo ambazo zilionyesha wazi kuwa ni wahudumu au wafanyakazi wa saloon hii yenye kila sifa ya kuwa saloon ya VIP, kutokana na muonekano wake wa ndani.

Wanawake hao wawili, walikuwa wanatoa huduma kwa wateja wao, ambao ni wanawake wawili, mmoja mtu mzima aliekuwa anamalizia kuosha nywele, na mwingine alikuwa ni mwanamke wa kati ya umri wa miaka thelathini, ambae alikuwa kwenye kikausha nywele, mambo hayo yaliendelea huku wakisindikizwa na music muzuri wa taratibu.

Nje ya saloon hiyo nzuri, anaonekana mwanamke mmoja mwenye muonekano mzuri wa sura na umbo matata, aliesimama nje ya saloon hii ya matawi ya juu karibu kabisa na gari dogo aina ya Toyota Lav 4 J, akiwa anaongea na simu, “hiyo hiyo inatosha sihitaji hela nyingi” alisema yule mwanamke, ambae hata muonekano wake ungeshindwa kukuaminisha kuwa ana umri wa miaka thelathini na tano, “na vipi ratiba yako kesho inasemaje, maana nina hamu na wewe” iliskika sauti ya kiume toka upande wa pili wa simu.

Na hapo yule mwanamke ambae muonekano wake, ulimtambulisha kuwa ni mwanake ambae hela ndogo ndogo haimsumbui, yani alikuwa na uhakika wa kushika fedha muda wowote anaohitaji, “sikia Ezze baby wangu, kama ujuwavyo, mimi muda wote nipo free, hata ukitaka kulala nyumbani kwangu ni sawa tu, hapo ni wewe tu na mke wako” alisema yule mwanamke ambae aliitwa kwa jina la Emmy, mwenye kumiliki umbo moja matata sana lenye mfano wa namba nane yenye duara dogo upande wa juu, duara kubwa upande wa chini, “wala usijari huyu mjinga hawezi kunizidi akili zangu, nitajua cha kufanya” ilisikika sauti ya bwana Eze, iliyojaa majigambo, kabla hawajaagana na kukata simu.

Huyu anaitwa Emmy Eduard Msigala, au mama Specioza, mwenye asili ya watu wa Njombe, mama wa mtoto mmoja wakike aliemzaa miaka kumi na moja iliyopita na bwana Simon Kajange, ambae sasa ni mkurugenzi wa shirika la mapato, kwasasa Specioza alikuwa anasoma darasa la nne shule ya bweni ya waschana huko Bagamoyo.

Mwanamke huyu anaezeeka na uzuri wake, licha ya kumiliki saloon hii kubwa ya kisasa, ambayo wateja wake ni wanawake wenye uwezo mkubwa wakifedha, wakiwepo wake wa matajiri, wanawake maarufu kama vile wanamusic wanasiasa na viongozi wa serikali, waigizaji na wanawake wafanyabiashara, pia alikuwa na maduka ya nguo za kike, nguo manukato, mikoba na viatu vya kike, pia alikuwa ana maduka ya mavazi ya watoto.

Chanzo kingine cha fedha cha mama P, anaemiliki jumba la kifahari huko mbezi bichi ni mwanaume wake wa sasa, bwana Ezekiel Ndimbo, ambae ni mfanya biashara za magendo na Mihadarati, siyo yeye peke yake hata baba P, yani bwana Kajange pia bado alikuwa anatoa fedha za matunzo kwa binti yake, japo ilikuwa ni kwasiri kubwa, maana familia yake haikuwa inatambua juu ya uwepo wa binti huyo aliefanana na mama yake kwa kiwango kikubwa sana.

Naaam! mara baada ya kumaliza kuongea na simu, mama P alitazama sasa kwenye simu yake, “mh! ndio kwanza saa mbili kasoro dakika tano” alisema mama P, huku anavuta hatua kuingia ndani ya saloon, lakini hakufanikiwa kuufikia mlango akaona mwanga mkali wa taa za gari unammulika, akageuka kutazama lile gari, akaliona subari forester jeusi likiwa linakuja usawa ule, akalitazama huku akijaribu kulifananisha kama ndilo lenyewe au la.

Gari lile lilipofika usawa wa saloon yake, ndipo alipogundua kuwa ndilo alilokuwa analifahamu, lilikuwa ni gari la matumizi ya nyumbani la mpenzi wae wa zamani, yani baba P ambae ni bwana Simon Kajange, gari ambalo mara zote huwa analitumia kuja kukutana na yeye, siyo tu kwa kuleta matumizi ya mtoto ambayo mara nyingi hupitia benk, ila pia kuna siku ambazo, wawili hawa huamua kupasha kiporo, “mh! mbona amekuja bila taarifa huyu mwanaume?” alijuliza mama P, huku anageuka na kulitazama lile gari, ambalo lilikuwa linasimama mbele ya saloon yake.

Hapo hapo kioo cha dereva kikashushwa, na mama P, akaweza kumuona baba P, yani mkurugenzi wa TRA, bwana Simon Kajange, alie tawaliwa na tabasamu pana, “mbona ghafla baba P” aliuliza mwanadada Emmy, huku anasogelea gari lile usawa wa mlango wa dereva, “kwani siruhusiwi kukutembelea bila kutoa taarifa?” aliuliza bwana Simon, huku anatazama saa yake mlangoni, “saa mbili kasoro dakika moja, mbona anakiuka sheria zake mwenyewe, itakuwaje sheria za..” alijiwazia bwana Somon Kajange na hata kabla hajamaliza kumsimanga mtu, ghafla akashtuka kusikia ngurumo nyepesi ya gari, nyuma ya gari lake. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Kongole bro
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO: “mbona ghafla baba P” aliuliza mwanadada Emmy, huku anasogelea gari lile usawa wa mlango wa dereva, “kwani siruhusiwi kukutembelea bila kutoa taarifa?” aliuliza bwana Simon, huku anatazama saa yake mlangoni, “saa mbili kasoro dakika moja, mbona anakiuka sheria zake mwenyewe, itakuwaje sheria za..” alijiwazia bwana Simon Kajange na hata kabla hajamaliza kumsimanga mtu, ghafla akashtuka kusikia ngurumo nyepesi ya gari nyuma ya gari lake. …….ENDELEA…

bwana Simon na mama P, wakatazama nyuma ya Subaru na wote wakaliona gari dogo aina BMW S7 likiwa liesimama nyuma ya gari lile kwa kugeuziana mgongo, Simon akatazama saa yake, “saa mbili kamili, shuka pakiza mzigo” alisema Simon akitazama kwenye seat ya nyuma, ambako kulikuwa na kijana wa kiume, alikuwa ametulia kimya muda wote huku yeye anafungua buti la gari lile, yule kijana akashuka toka kwenye gari na kuzunguka nyuma ya gari na kuinua buti la gari lile aina ya Subaru, na wakati huo huo buti la BMW likaonekana likiinuka lenyewe.

Yule jamaa akaanza kutoa mabegi makubwa, mabegi ambayo yanauwezo wa kuingiza hata jozi hamsini za nguo na kuweka kwenye buti la BMW, yalikuwa ni mabegi manne yenye uzito mkubwa kiasi, baada ya kumaliza hivyo, akaenda kwa dereva wa Subaru, yani bwana Simon ambae mida hii bado alikuwa anaongea na mzazi mwenzie, “vipi Emmy unaonaje leo kama tutalala pamoja na kujadiliana juu ya maisha ya baadae ya bnti yetu?” aliuliza Simon, huku anamtazama Emmy kwa jicho lenye ushawishi na tabasamu la ulaghai, Emmy nae akatabasamu, “mh! jamani baba P, unadhani nitasemaje, kwani nina uwezo wakukukatalia sasa, labda uniambie nitakukuta wapi” alisema Emmy kwa sauti yenye kijiaibu cha kiutani, maana alishajua anachoitiwa usiku huo, ukweli siyo mjadala ila kinatakiwa kitumbua cha mwanamke huyo ambae midume kibao ilikuwa inamtolea macho na kumfukuzia bila mafanikio.

Naaam kabla Simon hajajibu, tayari yule kijana alishawafikia, “boss tayari” alisema yule kijana, na hapo Simon hakiujibu kitu, akashuka toka kwenye gari akiwa na begi dogo mkononi, akaanza kutembea kuelekea kwenye BMW upande wa mlango wa dereva, Emmy akiwa nyuma yake.

Naam Simon na Emmy walipoufikia tu mlango BMW S7 wakaona kioo kinashushwa na hapo wote wawili wakaweza kumuona kijana mdogo mpole mwenye uso unaoeleza sifa tabia na uwezo wa kijana huyu kuwa ni kijana mtulivu sana na mwenye nidhamu ya hali ya juu, “shikamoni” ilikuwa ni sauti tulivu yenye upole wa hali ya juu, toka kwa kijana Deusi, kama ilivyo sura yake, macho ya mwana dada Emmy aliekuwa pembeni ya mzee Kajange yaliganda kwa kijana huyo na kuanza kumkagua kuanzia usoni mpaka kifuani na mikono yake, ambapo aliweza kujionea umbo la kiume lililokaa vyema la kijana huyo, ambae alikuwa amevalia tishet na suruali ya kaki, “marahaba kijana, hongera kwa kufuata sheria ya muda” alisema mzee Kajange kwa sauti iliyojaa uchangamfu na utani.

Deus akatabasamu kidogo, “ni tabia yangu Kufuata sheria na taratibu nilizoweka zilizowekwa na mteja na nitakazo ziweka” alijibu kwa sauti yake ile ile tulivu huku anatazama mbele bila kuwatazama wawili hawa, hawakujuwa kuwa alikuwa anawatazama kupitia kioo cha kuangalizia nyuma kilichopo katikati ya gari akipata nafasi ya kumuona huyo mwana dada alietoa macho ya matamanio juu yake,

“Ok! malipo ya mwanzo haya hapa kama tulivyo kubaliana na malipo ya pili utayapata mara tu utakapofikisha mzigo” alisema mzee Kajange, huku anamkabidhi Deus lile begi dogo mkononi, Deus alipokea na kufungua zip akatazama kilichopo ndani, “ni kilo moja siyo?” aliuliza huku anafunga zip na kutupia begi nyuma, “hakika wala haina shida” alisema Kajange, wakati huo Emmy bado anamtazama Deus kwa macho yaliyojaa matamanio, “ok! abiria wangu aingie” alisema Deus, huku anatazama saa ya mkononi mwake, ilikuwa saa mbili na dakika saba.

Hapo Kajange akamtazama kijana wake ambae alikuwa ameshika mabegi mawili mkononi, moja kama lile alilopewa Deus, na jingine la mgongoni, wengi wanaita laskert, akamuonyesha ishara aingie kwenye gari na yule jamaa akazunguka upande wa abiria wa mbele, “unatarajia kufika saa ngapi?” aliuliza Kajange, huku anamtazama Deus, ambae sasa alikuwa anaseti GPS kwa mfumo wa settlite, “kama hakuna tatizo ni masaa nane tu” alisema Deus, huku anamaliza kuset GPS na kupandisha kioo cha gari, huku gari linaanza kundoka taratibu huku Kajange na Emmy wanalisindikiza kwa macho mpaka lilipotoweka machoni pao., “yap! sasa nitatulia, waje tu nawasubiri kwa hamu” alisema bwana Kajange huku ana mgeukia Emmy, “sasa tukutane Sistafada hotel tusherehekee usiku wa leo” alisema Kajange, akionyesha mwenye tabasamu pana la ushindi, “kwani ule mzigo gani?” aliuliza Emmy kwa sauti ya mshangao wakawaida, “usiwe na haraka, nitakusimulia baadae,” alijibu Kajange, ambae leo aliaga nyumbani kwake kuwa anasafirisha mzigo ule mpaka morogoro na atarudi kesho asubuhi, “sawa basi ngoja nifunge saloon nitakukuta Sistafada” alijibu Emmy Eduward mama mwenye shepu yake mjini, ambae hata wavulana wadogo umtolea macho ya uchu.*******

Naam leo tena tunamuona bwana Hassan Simba, ni toka aachane na kijana Deus, week chache zilizopita, tunamuona ndani ya gari lake aina ya Toyota Nadia, ndani yupo na watu wengine watatu, yani mke wake na watoto wawili wadogo wakiume, mkubwa akiwa na miaka saba na mdogo akiwa na miaka miaka mitatu, walikuwa wanatoka ilala wanakuja buguruni safari ya nyumbani kwao, hakika bwana Hassan Simba na mke wake walionekana kuwa wenye furaha, walikuwa wakiongea hili na lile na kucheka kwa pamoja huku wakisaidiwa watoto wao.

Lakini wakati wanakaribia buguruni Rozana, mke wa bwana Simba akaona kitu, “hivi yule siyo shemeji kweli?” aliuliza mke wa bwana Hassan, huku akionyesha gari aina ford Ranger, lililokuwa lina chepuka mbele yao kutoka barabara ya kutokea buguruni shelli na kuelekea upande wa sokoni, ambapo lilipita kwenye barababra inayo tenganisha nyumba za jeshi la polisi na upande wa soko kuu la buguruni, “ni yeye huyo, sijuwi anaenda wapi” alisema bwana Hassan kwa sauti ya tahadhari kama vile amehisi jambo lisilo la kawaida kwa ndugu yake, huku anapunguza mwendo, macho ameyaelekeza kule liliko gari la ndugu yake, ambalo lilienda nakusimama ubavuni mwa Sun city Pub, “hapana, ngoja kwanza” alisema bwana Hassan huku anawasha taa ya upande wa kushoto kuonyesha kuw alikuwa anaingia upande huo wa kushoto.

Naam bwana Hassan aliingia upande wa kushoto, na kwenda kusimamisha gari lake mita kadhaa nyuma ya gari la ndugu yake, ambae sasa waliweza kumuona bwana Issa alikuwa amesha shuka kweny gari na begi dogo mkononi mwake, akiingia ndani ya Sun City, ni kama vile alikuwa anamsubiri aingie tu, ili na yeye amfuate, maana Issa alipo potelea ndani ya bar na yeye akashuka toka kwenye gari, “nisubirini nakuja sasa hivi” alisema Hassan huku anaondoka kuelekea ndani.

Hassan alipofika ndani ya bar hii, ambayo mida hii ya saa mbili na nusu ilikuwa imechangamka sana, watu walikuwa wengi kwenye meza zao, wakipata vinywaji na vyakula huku wakiburudishwa na miziki mbali mbali iliyopigwa kwa sauti ya juu mwenyewe hakuijali burudani ile wala kuwatazama watu wale walikuwa wakiendelea na buruani zao, yeye alitazama kushoto na kulia kumtafuta ndugu yake ambae alikuwa ametoweka machoni pake, “ahwezi kuwa hadharani” alijisemea Hassan, huku anatembea kuelekea upande wa kushoto ambako kulikuwa na watu wachache kidogo na mwanga afifu.

Ni kweli hisia za Hassan zilikuwa sahihi, kwamba Issa atakuwa upande huu, maana alimuona Issa akiwa kwenye meza moja na vijana wawili, ambao alikuwa anawapatia vibando flani flani, ambavyo waliweka kwenye mikoba yao na kuondoka zao, wakimjacha Issa kama vile anamsubiria mtu mwingine na yeye akamsogelea huku amekunja uso wake kwa hasira, “Issa, hii ni ya Songoro?” aliuliza Hassan mara baaa ya kumfikia.

Issa Simba anashtuka vibaya sana na kumtazama ndugu yake na macho yao yanapokutana Issa anatazama chini kama vile anajisuta moyoni, “lakini haina shida, nipo makini kwa kila ninachokifanya” alisema Issa, wakati huo kuna kijana anafika pale mezani, “nadhani sijachelewa kaka” anasema yule jamaa na hapo Issa anatoa bando kwenye begi na kumkabidhi yule kijana, “hakikisha unaleta mzigo kwa wakati” alisema Issa na jamaa anaondoka zake.

Walimsindikiza kwa macho mpaka aliposogea mbali kiogo, kisha Hassan akamtazama Issa, “sikia Issa ni vyema kama utaachana na Uredi, yule jamaa amewatendea vibaya sana watu anaoshirikiana nao” alisema Hassan kwa sauti ya upole, akionyesha ameamua kutumia busara kumuokoa ndugu yake, “lakini nitaishije mjini, hebu ona nimejenga hapa mjini, nina gari zuri, familia yangu inaishi maisha mazuri, binti yangu anasoma shule nzuri, nitawezaje bila hii?” aliuliza Issa kwa sauti ya kulalamika iliyojaa utetezi wakinyonge, “Issaaaaa mara ngapi na kuambia kuwa tutashiriki kwenye biashra zangu au nitakupatia mtaji ufanye biashara zako mwenyewe hata hizo unazofanya sasa” alisema Hassan, ambae lengo lake siyo kumtoa ndugu yake toka kwenye biashara haramu ya dawa za kulevya ila ni kumtoa kwa Uredi Songoro, mtu ambae hakuwa na msamaha pale unapoenda nae tofauti.

Hapo bwana Issa simba alitulia kidogo kama anajadili mpango wa ndugu yake kichwani, kisha akainua kichwa na kumueleza kaka yake kuwa amekubaliana nae, “lakini wacha nimalizane nae kisha niachane nae kabisa” alisema Issa na hapo wakaagana na Hassan akaondoka zake kutoka nje kuungana na familia yake.********

Naam wa ndani ya chumba namba sita cha gorofa ya tano hapa Sister Fada Hotel, walionekana bwana Kajange na bi Emmy, wakiwa wamekaa kwenye sofa la watu wawili, lililpo mbele ya meza ndogo ya kioo iliyobeba wine ya #Mbogo_land stater, inayotengenezwa nchini Mbogo Land, ikiwa ni zao la matunda ya miti asili yenye sifa kubwa ya kurutubisha nguvu na kuongeza hamu ya kushenyetana, matunda ambayo hutumiwa sana na wanyama kama Tembo, nyati faru, nyani na sokwe, pia bila kusahau swala na wengine wadogo wadogo wadogo hasa msimu wa kuzaliana, wale askari wa wanyama polisi wanafahamu hiyo.

Tahadhari, licha ya utamu na ulevyaji wa pombe hii yanye ladha kama maziwa na chokleti, ambayo haina harufu mbaya hata kidogo, haifai kunywa na mwanamke yeyote asie mpenzi wako, hata dada au binamu yako maana litatokea jambo bila kupenda kama ambavyo sasa tuna weza kuwaona wapenzi hawa wawili, ambao walivaa nguo za ndani pekee huku wakiendelea kunywa pombe hii pekee yenye utamu, “hivi baby ulisema ule ni mzigo wa nini?” aliuliza Emmy, akiwa amejiegemeza kifuani kwa Kajange ambae muda mfupi uliopita wametoka kukamilisha mzunguko wa kwanza wakupeana dudu.

“Zile ni fedha” alisema bwana Simon Kajange, ambae mkono wake wakushoto ulikuwa umekamata grass ya wine, huku vidole vyake vya mkono wa kulia vikiwa vimepenya kwenye nywele tim tim za Emmy, eneo la kisogoni na kufanya kama anamkuna fulani hivi, “weee fedha, inawezekanaje?” aliuliza Emmy kwa mshangao mkubwa huku akiinuka toka kifuani kwa Kajange na kumtazama usoni kwa macho yaliyojaa mshangao wakuto amini, “yes! tena sio shilingi ni noti za dollar mia mia” alisema Kajange kwa sauti fulani ya kujiachia kwa raha na furaha za mafanikio, “sijaelewa Simon, sasa umezipeleka wapi na yule kijana dereva ni nani?” aliuliza Emmy, ambae kiukweli alitamani sana kumfahamu yule kijana aliemuona leo ndani ya BMW jeusi.

bwana Kajange alipele grass ya wine mdomoni, na kupiga funda moja kisha akashusha pumzi kwanguvu, “yule kijana simjuwi kwa jina ni moja ya sheria zake, maana hata mimi hakuhitaji kunijuwa jina, unaweza kumuita Dereva, tena ume nikumbusha inabidi nimpigie kupata taarifa zao kwamba wamefika wapi?” alisema Kajange huku anachukua simu na kutafuta namba iliyoandikwa Dereva, wakati huo Emmy au mama Specioza akitazama kwa umakini namba ile ambayo kiukweli ilimshangaza sana “04472574?” aliuliza Emmy, kwa mshangao, “yani kiukweli hata mimi nilishangaza sana mara ya kwanza nilipoiona” alisema Kajange huku anapiga ile namba. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Karibu na huku Its Pancho
 
Deus alitakiwa kubadilisha gari kwa kwenda msafara mwingine.
Hilo BMW S7, linasakwa kila kona na vyombo vya Usalama.
Ingependeza pia angesafiri usiku.
Free from askari.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SITA: “yule kijana simjui kwa jina, ni moja ya sheria zake maana hata mimi hakuhitaji kunijua jina, unaweza kumuita Dereva, tena umenikumbusha inabidi nimpigie kupata taarifa zao kwamba wamefika wapi?” alisema Kajange huku anachukua simu na kutafuta namba iliyoandikwa Dereva, wakati huo Emmy au mama Specioza akitazama kwa umakini namba ile ambayo kiukweli ilimshangaza sana “04472574?” aliuliza Emmy kwa mshangao, “yani kiukweli hata mimi nilishangaza sana mara ya kwanza nilipoiona” alisema Kajange huku anapiga ile namba. …….ENDELEA…

Simu haikuita hata kwa sekunde mbili ikapokelewa, “unazidi kunifurahisha Dereva, yani upo makini sana” alisema Kajange huku anaachia kicheko cha raha, “ni kawaida yangu boss, ndio maana hata mimi napenda kila kitu kiende kama kilivyopangwa” ilikuwa ni sauti tulivu upande pili wa simu, sauti ambayo ilisikika vyema na kuvuja toka kwenye simu ile na kusababisha Emmy asisimkwe kiasi cha mwili kuota vipele ya baridi, “ok! mupo wapi mida hii?, tumeshaiacha mikumi, tunaitafuta luaha” alijibu Deus, huku maneno yake yakimfurahisha bwana Kajange, wakati sauti hiyo ikizidi kumsisimua Emmy na kumfanya azidi kutamani kukumbatiwa na kijana dereva, “ok! nawatakia safari njema” alisema Kajange kabla ya kukata simu.

Naam wakati Kajange anaweka simu mezani, Emmy akaiwahi haraka kuipokea na kuitazama ile namba ya Dereva, “sasa huu ni mtandao gani tena?” aliuliza Emmy, ambae lengo lake sio kutazama tu, ila ni kuzikalili zile namba za Dereva, ambazo hazikumpa shida kutokana na uchache wake, “sasa umesahau kunieleza kuhusu hela unapeleka wapi?” aliuliza Emmy, huku anaweka simu mezani, “hooo usiwe na haraka Emmy, nakuelekezea” alisema bwana Kajange na kuanza kueleza habari kamili.

Hapo naomba turejee tahadhari ya sehemu ya kwanza kabisa, ambayo inaeleza kuwa kisa hiki na matukio yaliyopo ni yakubuni haya husiani na mtu wala kitu chochote hata kama utaona kina fanana na tukio unalolijua.

Ukweli ni kwamba, bwana Kajange ambae ni mkurugenzi wa shirika la mapato alikuwa amejikusanyia fedha nyingi sana ambazo alikuwa anazibadili kwa mfumo wa dollar na kuziweka nyumbani kwake, fedha ambayo alikuwa anaikusanya kwa kutumia watu mbali mbali, ambao pia alikuwa anawagawia fedha kidogo, kwaajili ya kutatua shida zao ndogo ndogo, huku yeye akihofia kuweka benk, maana angeuzwa maswali na kufanya aanze kufuatiliwa na vyombo vya usalama, ni kutokana na uwingi wake.

Ndani ya miezi nane, tayari Kajange alikuwa amekusanya fedha nyingi sana, fedha ambayo kiukweli hata yeye mwenyewe ilibidi achukuwe likizo ili kuweza kuzihesabu, na alitumia siku tano kutwa kucha tena akitumia machine ya kuhesabia fedha kama zile za benk.

Naam mpaka anamaliza, alikuwa amepata hesabu ya fedha nyingi ambazo kwa thamani ya fedha ya Tanzania ni zaidi billion miambili ishirini na tano, hiyo ni fedha ya mtu mmoja aliyoipata kwa njia za kuibia serikali kwenye kukusanya kodi, wizi ambao ulipunguza mapato ya serikali kwa kiwango kikubwa, kiwango ambacho kilipelekea serikali kuanza uchunguzi wa siri wakitumia usalama wataifa na Takukuru, ambao kwa bahati walibaini kuwa licha ya kuwa na wezi wengi pale TRA, lakini pia kiasi kikubwa cha fedha kinaibiwa na mkurugenzi, hivyo wakaanza kumchunguza kwa siri kubwa.

Walikagua kwenye account zake za benk lakini hakukuwa na fedha ambazo walizikadiria kuwa anazikwapua serikalini, wakatazama kwenye account za watu wake wa karibu, kama vile mke wake watoto na hata mwanamke aliezaa nae na account ya mtoto wake wa nje ya ndoa , lakini hakukuwa na fedha iliyo kisiwa kuwa atakuwa ameibia serikali, zaidi wangekuta million tatu nne na sio zaidi ya hapo.

Lakini serikali haikurudi nyuma, ikaingia katika upelelezi wa ndani zaidi na kubaini kuwa fedha inatunzwa ndani ya nyumba ya afisa yule wa TRA, lakini watu wanasema kuwa kuishi na watu vizuri ni akiba, kuna mtu mmoja alimdokeza bwana Kajange kuwa siku inayofuata yaani jumamosi muda wowote angevamiwa nyumbani kwake na takukuru, ambao watakuwa wanashirikiana na jeshi la Polisi kwaajili ya msako mkubwa sana ambao asingeweza kuchomoka hata kidogo.

Hapo sasa bwana Simon Kajange, akaanza kuhaha kukutafuta namna ya kutorosha fedha, ambapo aliikumbuka account yake ambayo ipo kwenye benk moja kubwa huko ufaransa, lakini swali likaja, ataziwekaje maana nilazima aweke kwa kuziweka kwenye account yoyote ya benk ya hapa nyumbani na kuzituma kwenda kwenye account yake huko ufaransa.

Lakini tatizo likaja lile lile, endapo ataweka fedha kiasi kile kwenye account yoyote ya benk hapa Tanzania lazima watu wangezuia account na kuchunguza uhalali wa upatikanaji wa fedha zile, na yeye kukamatwa na kufungwa miaka mingi sana kwa kwa kosa la ufisadi, hivyo njia ambayo ilikuwa imebakia ni kusafirisha fedha hizo kwenda nchi jirani na baadae kuzituma ufaransa kwa benk za nchi hizo, na njia rahisi ambazo zingetuma fedha hizo bila kuhoji, zingejali kodi na makato mbali mbali bila kutaka kujua chanzo cha fedha hizo ni nchi ambazo uchumi wake ni mdogo kama ilivyo msumbiji.

Hapo Kajange aliweka mipango yake sawa, akawasiliana na watu wake wa Msumbiji, ambao walisema wangempokea kwenye mpaka wa likuyu kusini mwa mji wa songea, swala likaja mzigo utasafiri vipi, maana tayari kuna watu walishajua kuwa kunafedha nyingi itasafirishwa.

Baada ya lisaa lizima la kutafuta usafiri wa uhakika wenye usalama, ndipo alipopewa namba ya kijana Deus Nyati alietambulishwa kama Dereva wa BMW, aliempatia namba ya Deus hakukosea maana saa kumi na moja za afajiri Deus alikuwa anaingia songea mjini akitokea mpaka wa songea na msumbiji, ambako tayari alikuwa ameshamuacha yule kijana na mzigo wake na wakapokelewa na wenyeji wao, na kuingia msumbiji huku yeye akirudi Tanzania katika wilaya ya songea, sehemu ambayo alikuwa ameipita lisaa limoja lililopita, Deus alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa wazazi wake.

kwakifupi ni kwamba alikutana na wazazi wake na kukaa nao kwa week nzima, huku akiwa amesha msimulia baba yake kila kitu na kumueleza shughuli yake ya sasa ya usafirishaji, huku akieleza kuwa lengo lake ni kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi na kuachana nayo, kisha aangalie mambo mengine, sababu ilikuwa ni kazi inayomuhitaji kuvunja sheria kwa kiwango kikubwa sana.

Mzee Frank, alimueleza kijana wake kuwa ajitaidi aachene na kazi hiyo anayoifanya, asije akagundulika na kulazimika kutoroka nchi ya Tanzania, kitu ambacho kitakuwa ni kibaya sana kwao, sababu Tanzania ndiyo nchi pekee yenye usalama kwao, maana hawawezi kurudi nchini kwao ambako yeye mzee Frank anahesabika kama mmoja kati ya watu hatari wenye mpango wa kupindua nchi, “na kama ujuavyo bwana Chitopelah kwa sasa ni waziri wa ulinzi, ni rahisi sana kutuangamiza ilikuweza kutimiza malengo yake, na pengine kujitengenezea sifa, na heshima kubwa, huku akijenga kuaminiwa na mfalme.*******

Naam, ilikuwa ni siku ya juma tano, week nne toka taarifa za kufukuzwa kazi kwa Deus Nyati, mida ya saa tatu usiku, siku hiyo mfalme Elvis Mbogo, alikuwa ndani ya chumba chake anapekuwa makabati ya kumbu kumbu binafsi za wafalme, yani kumbu kumbu na mipango iliyoandikwa na wafalme kwa mikono yao wenyewe, ndipo mfalme mwenye umri mdogo kupata kuitawala #mbogo_land, akaipata kumbu kumbu ya kushangaza iliyo andikwa na king Eugen wa 25 ambae ni baba yake king Eric wa 2, ambae ni babu wa king Elvis wa kwanza, mfalme wa sasa wa #mbogo_land.

Usiku huu king Elivs wa kwanza katika kupekuwa kwake alikutana na karatasi hiyo iliyoandikwa “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini na waliojitolea kwa kiwango kikubwa kuilinda nchi na kukulinda wewe, lakini siwezi kuibadilisha akili yako kabla sijakamatwa na kuuwawa, wacha leo niikimbie nchi yangu ninayo ipenda, lakini nakuaidi uwe wewe au kizazi chako, kitakumbuka maneno yangu, nikiweza nitaipigania nchi yangu mimi au kizazi changu” ujumbe huu ulimtisha sana king Elvis na tatizo ni kwamba ujumbe haukuelekeza unatoka kwa nani kwenda kwa nani au ulenga jambo gani.

Baada ya kuutazama kwa muda fulani akauweka pembeni na kuachana nao, akipanga kuukalia chini siku nyingine.********

Siku mbili baadae, ikiwa ni siku ambayo bwa Issa alitakiwa kupeleka fedha kwa bwana Uredi Songoro, lakini mpaka mida hii alikuwa bado hajakamilisha kiasi cha fedha alichotakiwa kuwakilisha kwa boss huyo wa mihadarati, ni kiasi cha milllion hamsini, na asingeweza kuwakilisha fedha nusu kwa bwana Songoro, na kwa kufanya hivyo, Issa simba aliomba week moja kwa Songoro kwaajili ya kukusanya zaidi, na hapo sasa tunafika pale tulipoanzia, yaani ndio tunaanza mkasa wetu. Naam! Katika kitu pekee ambacho anacho mtunzi Edgar Mbogo ni kuweza kuianza stori katikati kisha akarudisha kumbukumbu nyuma akaja kuunga pale pale alipokaachia kwa episode nyingi bila kuchanganya mtukio, kwa hili aaah apewe mau yake kwa kweli,sasa hapa ndio tunaanza rasmi mkasa wetu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapahapa jamii forums
 
Back
Top Bottom