Nephew
JF-Expert Member
- Jun 29, 2014
- 256
- 295
Weka vitu mtaalam Abou Shaymaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😅😅Kuna watu palivyotajwa Mrina hapa walifuraaaahii wenyewe🤣🤣
Ha ha haKuna watu palivyotajwa Mrina hapa walifuraaaahii wenyewe🤣🤣
Kongole broNYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NNE: wengine waliamini kuwa pengine muuwaji alitokea Kenya, huku jeshi la ulinzi na vyombo vingine vya usalama vikiamua kuweka pembeni swala la Deus, kwamba endapo atapatikana sawa na asipopatikana ni sawa maana tayari alisha hukumiwa kundolewa kazini, ni week ya tatu toka Deus azime simu yake ya mkononi, hii ni ijumaa ya week ile, mida ya saa kumi na mbili za jioni, Deus akiwa mazoezini mara akapokea simu, ni kwa namba ile ya kwenye gari, ambayo sasa aliiunganisha kwenye ile simu aliyopewa na wale madoctor. .…….ENDELEA…
“hallow Dereva kuna mzigo wa kilo mia moja, kilomita mia tisa themanini na mtu mmoja, malipo yako shilingi million mia mbili” ilisikaka sauti ya kiume toka upande wapili wa simu.
Kwanza Deus aliachia tabasamu la kimya kimya, huku anajiuliza million mia mbili kwaajili ya mzigo wa aina gani, lakini akahisi pengine uelekeo ni mgumu sana ndio maana fedha imekuwa kubwa sana, “ok! taja uelekeo tafadhari” alisema Deus kwa sauti tulivu, “dar, Songea mpaka likuyufusi, mpakani na msumbiji” ilisema ile sauti ya kiume upande wapili wa simu.
Mpango wa safari ulimsisimua sana Deus, maana ukiachia kujipatia fedha, pia ataenda kukutana na baba yake, “sheria zako kabla sijakupa za kwangu” alisema Deus, ambae sasa alikuwa amelowa jasho kama amenyeshewa na mvua, kwaajili ya mazoezi, “moja usifungue mzigo, mbili mzigo ufike salama ni hizo tu, sasa nasikiliza toka kwako” alisema yule mwanaume upande wapili wa simu,
Ukweli Deus hakuwa na sheria zozote zaidi ya ile ya kutokujuana majina na kuto kuingia na bunduki kwenye gari lake, pamoja na ile ya hakuna mpango juu ya mpango” ambazo alizitunga akiwa safarini Arusha baada ya kuamsikia sheba pia hizo habari za sheria, na hapo ndipo alipoona kuwa kuna umuhimu wa kuwa na sheria zake binafsi zitakazo msaidia katika kazi hii mpya, ambayo malipo yake ni makubwa sana, “ok! tuta tumia sheria namba moja mpaka tatu na nne” alisema Deus kwa namna ya ubunifu, ilikuifanya kazi yake iwe na heshima fulani, “nifafanulie kijana” alisema huyo mtu ambae uongeaji wake, ulionyesha wazi kuwa ni mtu mwenye fedha nyingi.
Hapo Deus kwa ubunifu kubwa sana, akaanza kutaja sheria zake huku akizipa namba, “namba moja, hakuna kujuana majina, namba mbili malipo ni mkononi na hakuna mkopo, namba tatu, hakuna matumizi ya bunduki kwenye gari langu, na sheria namba nne, hakuna mpango juu ya mpango” alisema Deus, ambae sasa alikuwa anaingia ndani ya lile jengo chakavu, ambalo sasa lilikuwa limefungwa camera za ulinzi kila kona na kwa siri kubwa sana, kiasi cha kuto kuonekana kirahisi, “sawa nimekubari, lakini hakikisha usalama wa mzigo na abiria wako” alisema huyo mtu ambae kutokana na sheria za Deus hakupaswa kutaja jina lake, “sawa nitajie siku na saa ya kuanza safari” alisema Deus, kwa sauti yake tulivu huku akiwa anamaliza kuingia ndani nyumba ya chini na kuchukuwa kijitabu cha kumbu kumbu na kalamu ya wino na kuanza kuandika zile sheria zake kwa kufua namba kama alivyo zitaja, “safari inaanzia mwenge jijini Dar es salaam, muda saa mbili kamili za usiku, saloon ya mama P, mita kumi na tano, kusini mashariki toka ilipo benk ya NMB” alisema yule mwanaume.
Wakati huo Deus alikuwa anaandika sheria zake nyingine zaidi ya zile zamwanzo, “ok! mpango umekubarika, lakini zingatia sheria namba nane, simamia muda sahihi” alisema Deus, huku anaandika hiyo sheria namba nane, akimaliza na sheria namba tisa, nidhamu ndani ya gari lake baada ya hapo akaingi chumbani kwake ambako kuna bafu na choo kwaajili ya kwenda kujiandaa na safari.*******
Naam!, sasa tupo barabara ya kilwa, maeneo ya saba saba huko Temeke, lilionekana gari aina ya ford ranger likiingia upande wa kushoto wa barabara na kuambaa ambaa pembezoni mwa ukuta wa uwanja wa saba saba, kisha linaenda kusimama mita kama mia moja hivi, eneo ambalo lilikuwa na magari kadhaa, yakiwepo magari makubwa ya mizigo na ya mafuta, pia yalikuwepo magari madogo.
Lile Ford Range, linaenda kusimama pembeni ya gari jingine dogo aina ya Toyota Noah la rangi nyeusi, hapo hapo mlango wa Toyota Noah unafunguliwa, anashuka kijana mmoja na begi dogo anaweka na kusogea kwenye lile gari aina ya ford Ranger, ambalo bado lilikuwa lina unguruma, sasa tunaona kioo cha Dereva kina shushwa,“kilo ishirini hizi, boss amesema week ijayo anataka mzigo wake” alisema yule kijana, huku anakabidhi lile begi kwa dereva ambae sasa tunapata kumuona dereva huyo mwenye muonekano wa utu uzima, “nimeongea nae, amesisitiza hilo ila asiwe na wasi wasi, nadhani ananifahamu kuwa nina mawakala wengi sana” alisema yule dereva mtu mzima, huku anapokea lile begi na kuliweka kwenye seat ya pembeni yake, yani seat ya abiria wa mbele, kisha akapandisha kioo cha gari na kugeuza gari kisha akaondoka zake, akiacha lile gari jeusi aina Toyota noah likiwa lesimama pale pale na yule alieshuka alikuwa ameshaingia tena kwenye gari na kufunga mlango.
Naam Ranger liliingia barabara kuu na kuelekea upande wa mjini, huku dereva wa gari lile akiendesha gari kwa kasi nakuja kusimama kwenye maungio ya barabara ya kilwa na Mandera, ambapo palikuwa na foleni ndefu kiasi, na hapo ndipo dereva huyu mtu mzima alipofungua lile begi lake na kuzamisha mkono ndani yake, kisha akaibuka na bando moja kubwa sawa na mkate wa buku mbili, lililofungwa kwa mifuko ya plastic, ambayo ilikuwa inaangaza kile kilichopo ndani yake, ambacho kwa muonekano wa kawaida ni kama unga fulani mweupe mfano wa maziwa ya unga, dereva akaupekuwa zaidi na kutazama ndani kulikuwa na bando nyingine nne kama lile.
Dereva anatabasamu huku anatoa simu yake na kupiga namba ya mtu flani, ambayo haikuchelewa kupokelewa, “oya! mzigo umeingia, fanya faster uje uuchukue usambaze kwa vijana” alisema yule dereva, “poa poa, kesho nije home?” aliuliza mvulana upande wa pili wa simu, “hapana tukutane Rozana kwenye ile bar ya Sun city” alisema dereva kabla ya kukata simu na kupiga simu nyingine, wakati huo magari yanaanza kutembea taratibu.
Simu ilipokelewa mara moja, na maongezi yalikuwa kama yale ya mwanzo, akafanya hivyo kwa watu kadhaa na mpaka analiacha lile eneo la foleni, tayari alishaongea na watu wanne, akiwataka kukutana nao hapo Sun City bar.
Huyu anaitwa Issa Simba ni ndugu wa damu kabisa na Hassan Simba, mwanaume mtu mzima wa Arusha, tofauti ya Hassan na Issa ni utendaji wa biashara zao, wakati Hassan alikuwa anasimamia biashara zake binafsi, lakini Issa yeye alikuwa anafanya kazi chini ya mtu na mbaya zaidi ni biashara ngumu sana, ni biashara ya dawa za kulevya.*******
Saa mbili kasoro dakika tano za usiku, maeneo ya mwenge dar es salaam, ndani ya saloon moja kubwa sana ya kike, yenye bango kubwa nje yake lililoandikwa MAMA P, ndani walionekana wanawake wanne, wote wakiwa wenye muonekano wa kuvutia, wawili wenye umri wa miaka kati ya ishirini na mbili mpaka ishirini na tano, waliovalia nguo ambazo zilionyesha wazi kuwa ni wahudumu au wafanyakazi wa saloon hii yenye kila sifa ya kuwa saloon ya VIP, kutokana na muonekano wake wa ndani.
Wanawake hao wawili, walikuwa wanatoa huduma kwa wateja wao, ambao ni wanawake wawili, mmoja mtu mzima aliekuwa anamalizia kuosha nywele, na mwingine alikuwa ni mwanamke wa kati ya umri wa miaka thelathini, ambae alikuwa kwenye kikausha nywele, mambo hayo yaliendelea huku wakisindikizwa na music muzuri wa taratibu.
Nje ya saloon hiyo nzuri, anaonekana mwanamke mmoja mwenye muonekano mzuri wa sura na umbo matata, aliesimama nje ya saloon hii ya matawi ya juu karibu kabisa na gari dogo aina ya Toyota Lav 4 J, akiwa anaongea na simu, “hiyo hiyo inatosha sihitaji hela nyingi” alisema yule mwanamke, ambae hata muonekano wake ungeshindwa kukuaminisha kuwa ana umri wa miaka thelathini na tano, “na vipi ratiba yako kesho inasemaje, maana nina hamu na wewe” iliskika sauti ya kiume toka upande wa pili wa simu.
Na hapo yule mwanamke ambae muonekano wake, ulimtambulisha kuwa ni mwanake ambae hela ndogo ndogo haimsumbui, yani alikuwa na uhakika wa kushika fedha muda wowote anaohitaji, “sikia Ezze baby wangu, kama ujuwavyo, mimi muda wote nipo free, hata ukitaka kulala nyumbani kwangu ni sawa tu, hapo ni wewe tu na mke wako” alisema yule mwanamke ambae aliitwa kwa jina la Emmy, mwenye kumiliki umbo moja matata sana lenye mfano wa namba nane yenye duara dogo upande wa juu, duara kubwa upande wa chini, “wala usijari huyu mjinga hawezi kunizidi akili zangu, nitajua cha kufanya” ilisikika sauti ya bwana Eze, iliyojaa majigambo, kabla hawajaagana na kukata simu.
Huyu anaitwa Emmy Eduard Msigala, au mama Specioza, mwenye asili ya watu wa Njombe, mama wa mtoto mmoja wakike aliemzaa miaka kumi na moja iliyopita na bwana Simon Kajange, ambae sasa ni mkurugenzi wa shirika la mapato, kwasasa Specioza alikuwa anasoma darasa la nne shule ya bweni ya waschana huko Bagamoyo.
Mwanamke huyu anaezeeka na uzuri wake, licha ya kumiliki saloon hii kubwa ya kisasa, ambayo wateja wake ni wanawake wenye uwezo mkubwa wakifedha, wakiwepo wake wa matajiri, wanawake maarufu kama vile wanamusic wanasiasa na viongozi wa serikali, waigizaji na wanawake wafanyabiashara, pia alikuwa na maduka ya nguo za kike, nguo manukato, mikoba na viatu vya kike, pia alikuwa ana maduka ya mavazi ya watoto.
Chanzo kingine cha fedha cha mama P, anaemiliki jumba la kifahari huko mbezi bichi ni mwanaume wake wa sasa, bwana Ezekiel Ndimbo, ambae ni mfanya biashara za magendo na Mihadarati, siyo yeye peke yake hata baba P, yani bwana Kajange pia bado alikuwa anatoa fedha za matunzo kwa binti yake, japo ilikuwa ni kwasiri kubwa, maana familia yake haikuwa inatambua juu ya uwepo wa binti huyo aliefanana na mama yake kwa kiwango kikubwa sana.
Naaam! mara baada ya kumaliza kuongea na simu, mama P alitazama sasa kwenye simu yake, “mh! ndio kwanza saa mbili kasoro dakika tano” alisema mama P, huku anavuta hatua kuingia ndani ya saloon, lakini hakufanikiwa kuufikia mlango akaona mwanga mkali wa taa za gari unammulika, akageuka kutazama lile gari, akaliona subari forester jeusi likiwa linakuja usawa ule, akalitazama huku akijaribu kulifananisha kama ndilo lenyewe au la.
Gari lile lilipofika usawa wa saloon yake, ndipo alipogundua kuwa ndilo alilokuwa analifahamu, lilikuwa ni gari la matumizi ya nyumbani la mpenzi wae wa zamani, yani baba P ambae ni bwana Simon Kajange, gari ambalo mara zote huwa analitumia kuja kukutana na yeye, siyo tu kwa kuleta matumizi ya mtoto ambayo mara nyingi hupitia benk, ila pia kuna siku ambazo, wawili hawa huamua kupasha kiporo, “mh! mbona amekuja bila taarifa huyu mwanaume?” alijuliza mama P, huku anageuka na kulitazama lile gari, ambalo lilikuwa linasimama mbele ya saloon yake.
Hapo hapo kioo cha dereva kikashushwa, na mama P, akaweza kumuona baba P, yani mkurugenzi wa TRA, bwana Simon Kajange, alie tawaliwa na tabasamu pana, “mbona ghafla baba P” aliuliza mwanadada Emmy, huku anasogelea gari lile usawa wa mlango wa dereva, “kwani siruhusiwi kukutembelea bila kutoa taarifa?” aliuliza bwana Simon, huku anatazama saa yake mlangoni, “saa mbili kasoro dakika moja, mbona anakiuka sheria zake mwenyewe, itakuwaje sheria za..” alijiwazia bwana Somon Kajange na hata kabla hajamaliza kumsimanga mtu, ghafla akashtuka kusikia ngurumo nyepesi ya gari, nyuma ya gari lake. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
KinakujaMkuu tupe kipande cha mwisho.
Muda unakwenda au utatupia usiku wa manane tukiwa tunakoroma?!Kinakuja
Kwa leo inatosha pumziken mapema kesho j3Muda unakwenda au utatupia usiku wa manane tukiwa tunakoroma?!
Karibu na huku Its PanchoNYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO: “mbona ghafla baba P” aliuliza mwanadada Emmy, huku anasogelea gari lile usawa wa mlango wa dereva, “kwani siruhusiwi kukutembelea bila kutoa taarifa?” aliuliza bwana Simon, huku anatazama saa yake mlangoni, “saa mbili kasoro dakika moja, mbona anakiuka sheria zake mwenyewe, itakuwaje sheria za..” alijiwazia bwana Simon Kajange na hata kabla hajamaliza kumsimanga mtu, ghafla akashtuka kusikia ngurumo nyepesi ya gari nyuma ya gari lake. …….ENDELEA…
bwana Simon na mama P, wakatazama nyuma ya Subaru na wote wakaliona gari dogo aina BMW S7 likiwa liesimama nyuma ya gari lile kwa kugeuziana mgongo, Simon akatazama saa yake, “saa mbili kamili, shuka pakiza mzigo” alisema Simon akitazama kwenye seat ya nyuma, ambako kulikuwa na kijana wa kiume, alikuwa ametulia kimya muda wote huku yeye anafungua buti la gari lile, yule kijana akashuka toka kwenye gari na kuzunguka nyuma ya gari na kuinua buti la gari lile aina ya Subaru, na wakati huo huo buti la BMW likaonekana likiinuka lenyewe.
Yule jamaa akaanza kutoa mabegi makubwa, mabegi ambayo yanauwezo wa kuingiza hata jozi hamsini za nguo na kuweka kwenye buti la BMW, yalikuwa ni mabegi manne yenye uzito mkubwa kiasi, baada ya kumaliza hivyo, akaenda kwa dereva wa Subaru, yani bwana Simon ambae mida hii bado alikuwa anaongea na mzazi mwenzie, “vipi Emmy unaonaje leo kama tutalala pamoja na kujadiliana juu ya maisha ya baadae ya bnti yetu?” aliuliza Simon, huku anamtazama Emmy kwa jicho lenye ushawishi na tabasamu la ulaghai, Emmy nae akatabasamu, “mh! jamani baba P, unadhani nitasemaje, kwani nina uwezo wakukukatalia sasa, labda uniambie nitakukuta wapi” alisema Emmy kwa sauti yenye kijiaibu cha kiutani, maana alishajua anachoitiwa usiku huo, ukweli siyo mjadala ila kinatakiwa kitumbua cha mwanamke huyo ambae midume kibao ilikuwa inamtolea macho na kumfukuzia bila mafanikio.
Naaam kabla Simon hajajibu, tayari yule kijana alishawafikia, “boss tayari” alisema yule kijana, na hapo Simon hakiujibu kitu, akashuka toka kwenye gari akiwa na begi dogo mkononi, akaanza kutembea kuelekea kwenye BMW upande wa mlango wa dereva, Emmy akiwa nyuma yake.
Naam Simon na Emmy walipoufikia tu mlango BMW S7 wakaona kioo kinashushwa na hapo wote wawili wakaweza kumuona kijana mdogo mpole mwenye uso unaoeleza sifa tabia na uwezo wa kijana huyu kuwa ni kijana mtulivu sana na mwenye nidhamu ya hali ya juu, “shikamoni” ilikuwa ni sauti tulivu yenye upole wa hali ya juu, toka kwa kijana Deusi, kama ilivyo sura yake, macho ya mwana dada Emmy aliekuwa pembeni ya mzee Kajange yaliganda kwa kijana huyo na kuanza kumkagua kuanzia usoni mpaka kifuani na mikono yake, ambapo aliweza kujionea umbo la kiume lililokaa vyema la kijana huyo, ambae alikuwa amevalia tishet na suruali ya kaki, “marahaba kijana, hongera kwa kufuata sheria ya muda” alisema mzee Kajange kwa sauti iliyojaa uchangamfu na utani.
Deus akatabasamu kidogo, “ni tabia yangu Kufuata sheria na taratibu nilizoweka zilizowekwa na mteja na nitakazo ziweka” alijibu kwa sauti yake ile ile tulivu huku anatazama mbele bila kuwatazama wawili hawa, hawakujuwa kuwa alikuwa anawatazama kupitia kioo cha kuangalizia nyuma kilichopo katikati ya gari akipata nafasi ya kumuona huyo mwana dada alietoa macho ya matamanio juu yake,
“Ok! malipo ya mwanzo haya hapa kama tulivyo kubaliana na malipo ya pili utayapata mara tu utakapofikisha mzigo” alisema mzee Kajange, huku anamkabidhi Deus lile begi dogo mkononi, Deus alipokea na kufungua zip akatazama kilichopo ndani, “ni kilo moja siyo?” aliuliza huku anafunga zip na kutupia begi nyuma, “hakika wala haina shida” alisema Kajange, wakati huo Emmy bado anamtazama Deus kwa macho yaliyojaa matamanio, “ok! abiria wangu aingie” alisema Deus, huku anatazama saa ya mkononi mwake, ilikuwa saa mbili na dakika saba.
Hapo Kajange akamtazama kijana wake ambae alikuwa ameshika mabegi mawili mkononi, moja kama lile alilopewa Deus, na jingine la mgongoni, wengi wanaita laskert, akamuonyesha ishara aingie kwenye gari na yule jamaa akazunguka upande wa abiria wa mbele, “unatarajia kufika saa ngapi?” aliuliza Kajange, huku anamtazama Deus, ambae sasa alikuwa anaseti GPS kwa mfumo wa settlite, “kama hakuna tatizo ni masaa nane tu” alisema Deus, huku anamaliza kuset GPS na kupandisha kioo cha gari, huku gari linaanza kundoka taratibu huku Kajange na Emmy wanalisindikiza kwa macho mpaka lilipotoweka machoni pao., “yap! sasa nitatulia, waje tu nawasubiri kwa hamu” alisema bwana Kajange huku ana mgeukia Emmy, “sasa tukutane Sistafada hotel tusherehekee usiku wa leo” alisema Kajange, akionyesha mwenye tabasamu pana la ushindi, “kwani ule mzigo gani?” aliuliza Emmy kwa sauti ya mshangao wakawaida, “usiwe na haraka, nitakusimulia baadae,” alijibu Kajange, ambae leo aliaga nyumbani kwake kuwa anasafirisha mzigo ule mpaka morogoro na atarudi kesho asubuhi, “sawa basi ngoja nifunge saloon nitakukuta Sistafada” alijibu Emmy Eduward mama mwenye shepu yake mjini, ambae hata wavulana wadogo umtolea macho ya uchu.*******
Naam leo tena tunamuona bwana Hassan Simba, ni toka aachane na kijana Deus, week chache zilizopita, tunamuona ndani ya gari lake aina ya Toyota Nadia, ndani yupo na watu wengine watatu, yani mke wake na watoto wawili wadogo wakiume, mkubwa akiwa na miaka saba na mdogo akiwa na miaka miaka mitatu, walikuwa wanatoka ilala wanakuja buguruni safari ya nyumbani kwao, hakika bwana Hassan Simba na mke wake walionekana kuwa wenye furaha, walikuwa wakiongea hili na lile na kucheka kwa pamoja huku wakisaidiwa watoto wao.
Lakini wakati wanakaribia buguruni Rozana, mke wa bwana Simba akaona kitu, “hivi yule siyo shemeji kweli?” aliuliza mke wa bwana Hassan, huku akionyesha gari aina ford Ranger, lililokuwa lina chepuka mbele yao kutoka barabara ya kutokea buguruni shelli na kuelekea upande wa sokoni, ambapo lilipita kwenye barababra inayo tenganisha nyumba za jeshi la polisi na upande wa soko kuu la buguruni, “ni yeye huyo, sijuwi anaenda wapi” alisema bwana Hassan kwa sauti ya tahadhari kama vile amehisi jambo lisilo la kawaida kwa ndugu yake, huku anapunguza mwendo, macho ameyaelekeza kule liliko gari la ndugu yake, ambalo lilienda nakusimama ubavuni mwa Sun city Pub, “hapana, ngoja kwanza” alisema bwana Hassan huku anawasha taa ya upande wa kushoto kuonyesha kuw alikuwa anaingia upande huo wa kushoto.
Naam bwana Hassan aliingia upande wa kushoto, na kwenda kusimamisha gari lake mita kadhaa nyuma ya gari la ndugu yake, ambae sasa waliweza kumuona bwana Issa alikuwa amesha shuka kweny gari na begi dogo mkononi mwake, akiingia ndani ya Sun City, ni kama vile alikuwa anamsubiri aingie tu, ili na yeye amfuate, maana Issa alipo potelea ndani ya bar na yeye akashuka toka kwenye gari, “nisubirini nakuja sasa hivi” alisema Hassan huku anaondoka kuelekea ndani.
Hassan alipofika ndani ya bar hii, ambayo mida hii ya saa mbili na nusu ilikuwa imechangamka sana, watu walikuwa wengi kwenye meza zao, wakipata vinywaji na vyakula huku wakiburudishwa na miziki mbali mbali iliyopigwa kwa sauti ya juu mwenyewe hakuijali burudani ile wala kuwatazama watu wale walikuwa wakiendelea na buruani zao, yeye alitazama kushoto na kulia kumtafuta ndugu yake ambae alikuwa ametoweka machoni pake, “ahwezi kuwa hadharani” alijisemea Hassan, huku anatembea kuelekea upande wa kushoto ambako kulikuwa na watu wachache kidogo na mwanga afifu.
Ni kweli hisia za Hassan zilikuwa sahihi, kwamba Issa atakuwa upande huu, maana alimuona Issa akiwa kwenye meza moja na vijana wawili, ambao alikuwa anawapatia vibando flani flani, ambavyo waliweka kwenye mikoba yao na kuondoka zao, wakimjacha Issa kama vile anamsubiria mtu mwingine na yeye akamsogelea huku amekunja uso wake kwa hasira, “Issa, hii ni ya Songoro?” aliuliza Hassan mara baaa ya kumfikia.
Issa Simba anashtuka vibaya sana na kumtazama ndugu yake na macho yao yanapokutana Issa anatazama chini kama vile anajisuta moyoni, “lakini haina shida, nipo makini kwa kila ninachokifanya” alisema Issa, wakati huo kuna kijana anafika pale mezani, “nadhani sijachelewa kaka” anasema yule jamaa na hapo Issa anatoa bando kwenye begi na kumkabidhi yule kijana, “hakikisha unaleta mzigo kwa wakati” alisema Issa na jamaa anaondoka zake.
Walimsindikiza kwa macho mpaka aliposogea mbali kiogo, kisha Hassan akamtazama Issa, “sikia Issa ni vyema kama utaachana na Uredi, yule jamaa amewatendea vibaya sana watu anaoshirikiana nao” alisema Hassan kwa sauti ya upole, akionyesha ameamua kutumia busara kumuokoa ndugu yake, “lakini nitaishije mjini, hebu ona nimejenga hapa mjini, nina gari zuri, familia yangu inaishi maisha mazuri, binti yangu anasoma shule nzuri, nitawezaje bila hii?” aliuliza Issa kwa sauti ya kulalamika iliyojaa utetezi wakinyonge, “Issaaaaa mara ngapi na kuambia kuwa tutashiriki kwenye biashra zangu au nitakupatia mtaji ufanye biashara zako mwenyewe hata hizo unazofanya sasa” alisema Hassan, ambae lengo lake siyo kumtoa ndugu yake toka kwenye biashara haramu ya dawa za kulevya ila ni kumtoa kwa Uredi Songoro, mtu ambae hakuwa na msamaha pale unapoenda nae tofauti.
Hapo bwana Issa simba alitulia kidogo kama anajadili mpango wa ndugu yake kichwani, kisha akainua kichwa na kumueleza kaka yake kuwa amekubaliana nae, “lakini wacha nimalizane nae kisha niachane nae kabisa” alisema Issa na hapo wakaagana na Hassan akaondoka zake kutoka nje kuungana na familia yake.********
Naam wa ndani ya chumba namba sita cha gorofa ya tano hapa Sister Fada Hotel, walionekana bwana Kajange na bi Emmy, wakiwa wamekaa kwenye sofa la watu wawili, lililpo mbele ya meza ndogo ya kioo iliyobeba wine ya #Mbogo_land stater, inayotengenezwa nchini Mbogo Land, ikiwa ni zao la matunda ya miti asili yenye sifa kubwa ya kurutubisha nguvu na kuongeza hamu ya kushenyetana, matunda ambayo hutumiwa sana na wanyama kama Tembo, nyati faru, nyani na sokwe, pia bila kusahau swala na wengine wadogo wadogo wadogo hasa msimu wa kuzaliana, wale askari wa wanyama polisi wanafahamu hiyo.
Tahadhari, licha ya utamu na ulevyaji wa pombe hii yanye ladha kama maziwa na chokleti, ambayo haina harufu mbaya hata kidogo, haifai kunywa na mwanamke yeyote asie mpenzi wako, hata dada au binamu yako maana litatokea jambo bila kupenda kama ambavyo sasa tuna weza kuwaona wapenzi hawa wawili, ambao walivaa nguo za ndani pekee huku wakiendelea kunywa pombe hii pekee yenye utamu, “hivi baby ulisema ule ni mzigo wa nini?” aliuliza Emmy, akiwa amejiegemeza kifuani kwa Kajange ambae muda mfupi uliopita wametoka kukamilisha mzunguko wa kwanza wakupeana dudu.
“Zile ni fedha” alisema bwana Simon Kajange, ambae mkono wake wakushoto ulikuwa umekamata grass ya wine, huku vidole vyake vya mkono wa kulia vikiwa vimepenya kwenye nywele tim tim za Emmy, eneo la kisogoni na kufanya kama anamkuna fulani hivi, “weee fedha, inawezekanaje?” aliuliza Emmy kwa mshangao mkubwa huku akiinuka toka kifuani kwa Kajange na kumtazama usoni kwa macho yaliyojaa mshangao wakuto amini, “yes! tena sio shilingi ni noti za dollar mia mia” alisema Kajange kwa sauti fulani ya kujiachia kwa raha na furaha za mafanikio, “sijaelewa Simon, sasa umezipeleka wapi na yule kijana dereva ni nani?” aliuliza Emmy, ambae kiukweli alitamani sana kumfahamu yule kijana aliemuona leo ndani ya BMW jeusi.
bwana Kajange alipele grass ya wine mdomoni, na kupiga funda moja kisha akashusha pumzi kwanguvu, “yule kijana simjuwi kwa jina ni moja ya sheria zake, maana hata mimi hakuhitaji kunijuwa jina, unaweza kumuita Dereva, tena ume nikumbusha inabidi nimpigie kupata taarifa zao kwamba wamefika wapi?” alisema Kajange huku anachukua simu na kutafuta namba iliyoandikwa Dereva, wakati huo Emmy au mama Specioza akitazama kwa umakini namba ile ambayo kiukweli ilimshangaza sana “04472574?” aliuliza Emmy, kwa mshangao, “yani kiukweli hata mimi nilishangaza sana mara ya kwanza nilipoiona” alisema Kajange huku anapiga ile namba. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums