Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI: mschana aliempa habari za watu wanaopanga kumpora mali zake, walitembea kwa haraka kuelekea upande wa barabarani, huku bwana Simba mwenyewe akiwa ametawaliwa na hofu kubwa sana, “hivi hapa ninaweza kupata usafiri wa ufika Moshi usiku huu?” aliuliza mzee Simba ambae sauti yake ilikuwa imetawaliwa na kitetemeshi, “usafiri mwingi sana ila kuwa makini, maana inaonyesha yule kaka anawenzake na wapo njiani wanakuja” alisema yule mwanamke, huku wakiwa wanakaribia mwisho wa jengo lile la hotel ambako palionekana kuwa na mwanga, ..…….ENDELEA…

Naaam mara walipofika mwisho wa ile chochoro, yule mwanamke akasimama, akifuatiwa na mzee Simba ambae pia alisimama nyuma ya yule mwanamke, “sasa babangu, nadhani nimesha kusaidia vya kutosha, mimi naishia hapa cha kufanya wewe kimbilia hapo mbele ukivuka tu kona ya hapo mbele utatokea stendi, kuna magari na boda boda mimi nakushauri chukuwa boda boda mpaka mianzini ukapande gari, ila kama una ishirini na tano au thelathini boda boda anakupeleka mpaka moshi” alisema yule mwanamke huku akimtazama mzee Simba, ambae kiukweli hakuwahi kutegemea kama leo angekutana na dhahama kama hii, “asante sana dada yangu, wacha niwahi kabla hao wenzake hawajafika, nikija siku nyingine nitakutafuta, kwaajili ya shukrani zaidi” alisema mzee Simba huku anachungulia na kutazama kushoto na kulia, kuangalia kama sehemu ile ina usalama, “usiwe na shaka babaa hapa nipo kama nyumbani kwangu utanikuta tu” alisema yule mwanamke ambae bado alikuwa pale kizimbani.

Ukweli mzee Simba aliona eneo lile la mbele ya hotel kuwa ni salama kabisa, yani hapa kuwa na mtu wa kumtilia mshaka yoyote zaidi ya kuwaona watu waliokuwa wanaingia na kutoka pale hotelini, hapo akashika mkoba wake vyema na kuanza kutembea kwa haraka kutoka kwenye ile chochoro akiibukia eneo la mbele la hotel ile maarufu mjini Arusha, akikifuata kichochoro cha mbele yake ambacho kingempeleka mpaka barabara kuu ya Monduri ambako kuna stendi ndogo.*******

Yap! wakati huo huo Kijana Deus akiwa anakaribia njia panda ya kuelekea stendi kuu ameshikilia simu yake mkononi ana taka kubofya kiwashio, ndipo ghafla mbele yake likaingia gari dogo aina ya Toyota Altezza lililo kuwa katika speed ya ajabu, ambalo liliingia na kukamata uelekeo wa kule anakoelekea yeye na kujikuta akakinyaga brake za ghafla ili asiligonge lile gari, ambalo aliweza kuliona linamuacha kwa mwendo ule ule wa kasi ya ajabu, “hii ndiyo Arusha” alijisemea Deus huku anaachia brake na kukanyaga mafuta kidogo kuendelea na safari yake, “dah! angeligonga gari langu sidhani kama ningemuacha” aliwaza Deus, ambae kwa kuona kilichotokea alijuwa kuwa kama asipokuwa makini anaweza kujikuta akisababishiwa ajali, hivyo ni vyema angeachana na simu na kuiwasha baadae atakapo kuwa amesha jipumzisha kwenye hotel, ambayo kwa mujibu wa GPS yake ilikuwa mita chache toka pale alipokuwepo, kwa ushauri huo aliojipa Deus akaiweka simu kwenye seat ya pembeni.

Deus aliendesha gari lake kwa tahadhari na uangalifu mkubwa akihofia kusababishiwa ajali, na wakati huo akiliona kwa mbali lile gari dogo, linapunguza mwendo na kuingia upande wa kushoto wa barabara kwenye njia ambayo kwa mujibu wa GPS ambao ni mpangilio maalumu wa kuonyesha sehemu, walioanzisha hiyo wanaitwa Global Positioning System, ilimuonyesha kuwa na yeye alikuwa anatakiwa upande huo huo.

Deus akaongeza mwendo kuifuata ile barabara, ambayo ilikuwa mita chache mbele yake, barabara ambayo aliifikia sekunde chache sana baadae, alipoifikia akakata kushoto ambapo mita chache mbele yake aliweza kuona jengo kubwa lililoandikwa Mrina Hotel, siyo hivyo tu aliweza kuliona pia lile gari lililompita wakati ule nakutaka kumsababishia ajali, gari ambalo lilionekana kuwa limeingia muda mfupi uliopita, maana sasa aliweza kuona milango yote minne ya gari lile inafunguliwa na wanashuka watu wanne huku wawili kati yao wakitupa vipisi vya sigara na kisha kuanza kutembea kuelekea kwenye lango la hotel “mh! ni sehemu sahihi kweli hii” alijiuliza Deus, huku anaendesha gari lake taratibu akipishana na watu mbali mbali waliokuwa wanaingia na kutoka pamoja na magari.

Deus akiwa anaendesha gari lake taratibu, huku anatafuta sehemu ya kuegesha mara akawaona wale vijana wanne waliokuwa wanaelekea kwenye jengo la hotel, wakisimama ghafla kumtazama mwanaume mmoja mtu mzima, aliebeba sanduku dogo jeusi, ambae alikuwa anatembe kwa kasi kuja upande wa pili wa jengo la hotel, akipita usawa wa gari lake lilikuwa linatembea taratibu.

Deus ambae mwanzo hakuwajali watu wale, akawaona wanaanza kumfuata yule mwanaume mtu mzima, ambae pia nikama aliwaona watu wale na kuanza kuongeza mwendo, kuja usawa wa gari, kitu ambacho kilimlazimu Deus kusimama kabisa ilikuepuka kusababisha ajali ya kugonga mtu.

Hapo sasa Deus akaweza kushuhudia juhudi za yule mwanaume mtu mzima ambae ni mzee Simba, ziligonga mwamba maana aliweza kuwaona wale jamaa wa nne wakianza kumkimbiza yule mtu mzima, ambae pia hakutaka kuzubaa, nae akatoka mbio dhaifu.

Hakika mazoezi binafsi ni kitu muhimu sana, maana huyu mwanaume mtu mzima hakuweza hata kulivuka gari la Deus, tayari alijikuta mikononi mwa wale jamaa wanne, “we! boya unadhani unaweza kutukimbia sisi” alisema mmoja wao huku akimnyang’anya lile sanduku, yule mzee alionekana kuwa na wasi wasi na uoga mkubwa huku sura ya kinyonge na kukata tamaa ikimtawala,

Kitendo kile kilimuumiza sana Deus, ambae hakutaka kujiingiza kwenye jambo lile ambalo aliliona kama vile halikumhusu, “hii ndiyo R chuga wewe hatuishi kizembe” alisema mwingine huku akimsukuma kwa nguvu yule mzee, ambae alienda kujibamiza kwenye BMW S7, “khaaa! imezidi sasa” alisema Deus, huku anaweka gia katika sehemu ya kuegesha wakati huo anamuona yule aliemsukuma yule mzee, akimfuata pale kwenye gari na kumkwida yule mzee akimkandamiza kwenye gari, “sikia we fala, funga mdomo wako na utulie hivyo hivyo, “alisema yule mmoja huku anaingiza mkono wake wakulia kwenye mfuko wa suruali wa yule mtu mzima na kuibuka na kitita cha fedha akakiweka kwenye mfuko wake.

Deus alifungua mkanda seat na kufungua mlango wakati huo yule mkabaji akizamisha tena mkono kwenye mfuko mwingine wa suruali ya mtu mzima na kuinuka na simu, “we boya rudi ndani ya gari faster” alisema mmoja kati ya wale wanne, huku anamsogelea Deus kwa haraka huku ameinua mkono kwa lengo la kutandika ngumi kijana huyu ambae umoja wa maaifa wameliweka jina lake kwenye orodha yao.

Ukweli kijana huyu, hakuwa na bahati maana kabla hata hajarusha ngumi yake, tayari alisha kutana na kitu kizito kilichotuwa usawa wa mgongo wa pua na kumtupa hatua kadhaa nyuma, huku wenzake wakigeuka kumtazama kwa mshtuko kubwa wasiamini kama amepigwa au amegongwa na boda boda, kisha kwa macho yaliyojaa hasira na mshangao wakamtazama Deus, “ase we fala unaleta maniaje tena, hivi unatujuwa sisi” alisema yule aliemshika yule mzee, huku anamuachia mzee mtu mzima na kuingiza mkono wake usawa wa kiuno, ambap aliibuka na kisu kirefu maarufu kama sime, kilichokuwa kinang’ara kwa makali yake na wenzake wawili, ukiacha yule alieshika sanduku, nao wakatoa visu vinavyo fanana na kile cha mwenzao, ambae ni Mduma, huku Deus akiwa anawatazama tu.

“sikilizeni wakubwa, sina ugomvi na nyie, ila nilitaka niwaambie msiguse gari langu” alisema Deus, kwa sauti ya upole yenye utaratibu wa kidaktari, ambayo haikuwashtua wakina Mduma, “oyaaa, acha kuongea ujinga babake, kama vipi weka mazaga yote juu ya boneti kisha tambaa zako” alisema Mduma huku anamsogelea Deus, ni wazi aliamini kuwa Deus amekuwa mpole kwaajili ya vile visu walivyoshika, “sikia bro, sijapenda kuumiza mtu mwingine zaidi, ni vyema mukakaa mbali na gari langu, ila mukini lazimisha nitafanya” alisema Deus, wakati huo bwana Simba akiwa amesimama pembeni anawatazama kwa macho ya uoga mfano wa paka anae subiria chakula kianguke toka mezani.

Neno la Deus nikama lilikuwa dharau kwa Mduma, ambae aliinua mkono juu akivuta lile nusu panga na kulishusha kuelekea begani kwa Deus, “hebu kaa chini we kim…” kabla hata mduma hajamaliza kuongea alichokusudia kuongea, aliweza kushuhudia yule jamaa akivuta hatua moja mbele kumkaribia zaidi na kuudaka mkono wake ambao aliuzungusha kwa nguvu na kwa ghafla, kitendo kilicho sababisha mduma mwenyewe zunguke kwa nguvu na kabla hajakaa sawa alihisi kitu kizito kikitua usawa wa kifua chake, huku mlio kama wa kuvunjika kwa mbao au kijiti kikavu ukisikika na yeye kwenda chini kama kiroba akinyimwa kupiga kelele ya aina yoyote kwa mkandamizo wa mguu, uliokita shingoni kwake huku akinyang’anywa lile panga lake, ambalo ndilo lililo tumika kuwageuza bucha wenzake.

Yani ndani ya muda mfupi watu waliokuwepo eneo la mbele la hotel pamja na mzee Simba walikuwa wameshuhudia tukio ambalo kama kuna aliewahi kuliona basi ni kwenye filamu za kikorea japan au china au hata ile ya sara dini part 3, kilikuwa ni kipigo kizito kipigo cha paka jizi, kipigo ambacho kilitumia muda mfupi sana, kipigo ambacho kilimfanya mzee Simba abakie anamtazama Deus kwa mshangao, nikama alikuwa anajiuliza kama Deus nae alikuwa anafuata sanduku lake ama sivyo, na kama ndiyo hivyo basi hatima yake ni mbaya zaidi kuliko ile ya mwanzo, maana sio kwa kipigo kile ambacho alikiona kwa macho yake, ambacho hata mimi sijaona kama itakuwa vyema kukielezea, kwa kunusuru wale mwana JF mwenye ugonjwa wa moyo.

Naam tayari watu walikuwa wanaanza kusogelea kwenye tukio huku kelele za chini chini zikianza kusikika, “ameuwa, kauwa” hawa kuwa watu waliokuwepo pale nje pekee, wapo pia waliotokea nani, “ni vyema kama utaacha kunitazama na ukachukuwa kila kilichochako, kisha ukaondoka eneo hili” alisema Deus, huku anatazama gari lake kama vile analikagua kuhakiksiha halijaumia sehemu, liwe tayari kwa safari mpya, ukweli asingeweza kukaa tena pale Arusha japo n ikama tukio lile lilichukuliwa kawaida na wenyeji, wakidhania kuwa ulikuwa ni ugomvi wa walevi.

Wakati huo mzee Simba, akiwa analiokota sanduku lake na kisha akamfuata Mduma, ambae sasa alikuwa amelala chini, huku anatokwa na damu puani na mdomoni, akampekuwa na kuchukuwa fedha yake na simu yake, kama vile alikuwa anafanya juhudi ya kumuwahi Deus, alie kuwa anaingia kwenye gari ili waondoke pamoja.

Ni kweli ile fumba na kufumbua tayari mzee Simba alishafungua mlango wa seat ya abiria wa mbele, na kufunga mlango, “kijana naomba unipeleke Dar es salaam, nitagharamia kuanzia mafuta na gharama nyingine zozote zitakazojitkeza wakati wote wa safari” alisema yule mtu mzima kwa sauti ya kuomboleza, akonyesha wazi kuwa anaamini kuwa Deus ndie mtu pekee anaeza kumfikisha Dar es salaam.

Hapo Deus akahisi kama vile kazi ya usafirishaji, inaenda kuwa kazi yake mpya, “unadhani mzigo wako na thamani yako inaweza kuwa sawa na lita mia moja za petrol?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu huku anafunga mkanda wa kwenye kiti, “kijana taja gharama kiasi cha fedha unachohitaji” alisema mzee Simba, akionyesha kuhitaji sana usafiri wenye usalama wa kijana huyu,msomaji wangu nakukumbusha tena kuwa simulizi yetu bado haijaanza, huu ni utangulizi tu wa bwana Deusi Frank Nyati ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Jamaa niliishiwa na bando ila nilikusudia kuunga sehemu ya 70 na 71 polen kwa usumbufu naleta sehem ya saa 72 kbla ya kulala leo
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MOJA: Hapo Deus akahisi kama vile kazi ya usafirishaji, inaenda kuwa kazi yake mpya, “unadhani mzigo wako na thamani yako inaweza kuwa sawa na lita mia moja za petrol?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu, huku anafunga kanda wa kwenye kiti, “kijana taja gharama kiasi cha fedha unacho hitaji” alisema mzee Simba, akionyesha kuhitaji sana usafiri wenye usalama wa kijana huyu..…….ENDELEA…


“nakupa offer ya kuchagua kwasababu nipo njiani kuelekea dar” alisema Deus, kwa sauti tulivu wakati huo baadhi ya watu walionekana wakianza kupiga simu kituo cha polisi kutoa taarifa juu ya tukio lile “million hamsini mpaka dar” alisema mzee Simba, wakati huo anaonekana Chao kati ya lile kundi la watu, akiwatazama kwa mshangao wenzake waliokuwa wamelala pale ardhini, “ok! imekubaliwa, ila mashariti yangu ni kwamba, 1)hakuna bunduki ndani yagari, 2)hakuna kujuwana majina, 3)hakuna mpango ndani ya mpango 4)malipo ni mkononi” alisema Deus, huku anatazama nyuma kwa kutumia Side mirror, ambako pia kulikuwa na watu wachache washangaaji, “funga mkanda wa kiti muda wote uwapo safarini” alisema Deus huku anaingiza gia ya uwani, kisha akakanyaga mafuta taratibu, kurudi nyuma utadhani hakuna alichokifanya eneo lile.


Deus aligeuza gari kutazama alikotoka yani kule stendi ndogo ya kwenda monduri, kisha akakanyaga mafuta kuelekea upande huo, nadhani hata wale watu waliokuwepo pale waliushangaa mwendo wa dereva yule, ambae aliendeshesha taratibu, usingewaza kama ametoka kufanya mauwaji ya kinyama, hata alipofika njia panda ya kuingia barabara kuu ya monduri, akasimama kupisha gari la polisi aina ya land rover Deffender, lililokuwa linakatiza kwa speed, kuelekea njia panda ya Namanga, huku askari sita wakionekana nyuma yake wakiwa wamevalia nguo za kiraia.


Baada ya lile gari kupita tu, Deus nae akakanyaga mafuta kuingiza gari barabarani, kisha kukamata upande wa Monduri, ikiwa ni kwa mwendo wa taratibu kama vile hakukuwa na jambo lolote lililotokea, ambapo dakika mbili baadae tayari yana onekana magari mawili aina ya Toyota Land Cruizer two (2) mali ya jeshi la polisi, ambayo nyuma yapo wazi na kutuwezesha kuona askari watano kila gari, wakiwa na silaha zao mkononi, yakiwa katika mwendo wa kasi sana, yaliingia stendi ndogo na kukata kona kuelekea Mrina hotel na kwenda kusimama karibu na kundi la watu, lililokuwa limezunguka sehemu ya mbele ya hotel ile kubwa.


Naam polisi wanashuka haraka na kutawanyika katika eneo lile huku wengine waki wakisogelea katika sehemu ambayo raia walikuwa wameizunguka na kuanza kuwasogeza wale wanachi pembeni ili waweze kufanya kazi yao.


Sasa basi mara baada ya kufanikisha kuwasogeza wananchi na kuacha eneo lile wazi, gari moja la polisi likasogea na kumulika taa zake pale ilipokuwa ile miili, hapo kila polisi alionekana akitazama pembeni huku anashika sehemu ambayo aliiona inafaa kushika kwa wakati ule huku wanatazama pembeni, wapo walioshika vichwa vyao, wapo walioziba midomo yao kwa mshangao, pia wapo walioshika viuno vyao, huku sura zao zikionyesha wazi kuwa katika simanzi.


Hakika ilitisha sana hii, maana waliweza kuona vijana wanne wakiwa wamelala chini, huku majeraha makubwa yanaonekana kwenye miili yao, huku karibu wote ikiwa ni maeneo ya tumboni na kwenye shingo zao, wakibakia kama mbuzi wanao subiri kuchunwa ngozi, “sijawahi kuona tukio la kinyama kama hili” alisema askari polisi mmoja mwenye cheo cha inspector, “halafu imekuwaje Mduma ameuwawa kinyama na namna hii” aliuliza polisi mwingine mwenye cheo cha sajent kwa sauti ya chini kidogo, huku akijaribu kuutazama mwili wa Mduma ambae alikuwa amelala chini na wenzake huku visu vyao vikiwa vimezagaa pembeni yao, “inaonyesha mapambano yalikuwa makali sana, na walikutana na kundi la watu wenye uwezo mkubwa wa kupambana” alisema yule inspector huku anageuka kutazama upande walioko wale raia, “kuna yoyote ambae anaweza kutupatia dondoo za tukio?” aliuliza insp, lakini hakuonekana mtu yoyote kujaribu kuelelezea,


Hapo inspector akarudia tena, “jamani sio kwamba tunahitaji shahidi ila tunataka kujuwa tunaanzia wapi uchunguzi” alisema inspector akiwatoa hofu raia wale, na hapo ndipo akajitokeza raia mmoja na kupaza sauti “wameondoka na gari jeusi, wameelekea upande wa kisongo” ndivyo ilivyosikika ile sauti na mwingine akadakia, “tena wanaenda taratibu sana watakuwa wanaenda kambini monduri”


Huyu wa pili alileta maono ndani ya vichwa vya askari kwamba muuwaji ni askari wa jeshi la ulinzi, maana upande wa monduri ndiyo sehemu yenye makambi mengi ya jeshi la ulinzi. “bakia hapa hakikisha miili inakaguliwa vizuri na inafikishwa Mount Meru, mimi na gari moja tuna wafuata huko huko” alisema yule askari mwenye cheo cha inspector, huku anakibilia kwenye gari. pamoja na askari waliokuja na gari lile, kisha safari ikaanza mara moja kufuata barabara ya Monduri.*******


Yap! saa tatu na nusu za usiku, mida ambayo CP Ulenje akiwa nyumbani kwake, anasubiri taarifa toka kwa vijana wake juu ya msako wa BMW jeusi, huku akiwa amejawa na shauku kubwa sana ya kusikia kuwa wameshalipata gari na sasa wanaenda kupata mamilioni ya fedha, pamoja na gari zuri sana la kisasa.


Wakati CP Ulenje anawaza hayo, mara akasikia simu yake ikaita na alipoitazama akaona jina la mpigaji kuwa ni koplo Cheleji, akaipokea haraka, na kuweka sikioni, “niambie Cheleji, mmelipata gari” aliuliza Ulenje kwa sauti yenye mumkali, “afande mpaka sasa bila bila, tumefika mpaka namanga, lakini hakuna gari wala dalili ya gari, tumeuliza kama wameliona gari tunalolitafuta wakasema halijaonekana, sasa tupo njiani tunarudii Arusha mjini hatukai tuna rudi dar” alisema Cheleji, “upuuzi, mmelipotezaje hilo gari?” alipiga kelele Ulenje kiasi kwamba hata mke wake aliekuwa chumbani alishtushwa na sauti ya mumewe, lakini haikuwa ajabu kwake, maana alisha wahi kusikia mara nyingi sana hasa wakati ambao kuna jambo haliendi sawa huko kazini. “fanyeni haraka nyie wapuuzi, sijuwi tutafidiaje mafuta tuliyopoteza” alisema Ulenje na kukata simu, kisha akapiga simu nyingine kwenda kwa Erasto Kadumya.*******


Taarifa za tukio la Mrina hotel zilianza kusambaa kwa kasi kubwa sana, hasa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakieleza jinsi mauwaji yalivyotokea na kwamba kijana mmoja anae hisiwa kuwa ni askari wa jeshi la ulinzi wa moja kati ya makambi yaliyopo huko Monduri aliekuwa anamuokoa mtu mmoja alievamiwa na majambazi au wanyang’anyi, huku wengine wakieleza muonekano wa mpiganaji yule mwenye uwezo mkubwa wa kimapigano, ambae amewafyekelea mbali vijana wanne ambao ni kati ya vijana wa arusha mjini wanaosifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukeleza matukio ya kiharifu pale mjini Arusha na vitongoji vya jirani.


Mkuu wa wajeshi la polisi mkoa wa Arusha, pia alitangaza na kuthibitisha tukio hilo, lakini alisema kuwa muuwaji bado anaendelea kutafutwa, taarifa za mwanzo zinasema kuwa tayari polisi wameenda kwenye makambi kadhaa ya jeshi la ulinzi na kufanya magwaride ya utambuzi wa sura, lakini hawakufanikiwa, pia waliuliza kama kuna askari mwenye kumiliki gari kama lile, lililloonekana kwenye tukio, lakini baada ya uchunguzi wa mfupi wa gari hilo aina ya BMW S7, wakagundua kuwa ni ghari la gharama kubwa, toleo la mwaka mmoja kabla, gari ambalo ni adimu na gharama kubwa kulipata, hivyo kwa mfanyakazi wa daraja la kati wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, asingeweza kumiliki, sababu gari hilo alikuanza kuuzwa kama gari la mtumba……….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Mambo yanazidi kupamba moto
 
Usijal haina haja pia shukran kwa support yako mkuu, naleta episode moja kwaajili yako soon 🙏🙏
Nafurahisha na ukarim wako wa kututoa mawazo ya maisha magum kwa kutupa hadithi zenye kupendeza kwa sisi wasomaji pia kujitoa bila kutanguliza tamaa mbele hakika toka moyoni nakuombea mungu akupe zaidi ya unavyotupa sisi faraja ya kututoa mawazo ya pilika za kila siku ubalikiwe mkuu
 
Pamoja mkuu
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI: pia waliuliza kama kuna askari mwenye kumiliki gari kama lile lililloonekana kwenye tukio, lakini baada ya uchunguzi mfupi wa gari hilo aina ya BMW S7, wakagundua kuwa ni gari la gharama kubwa, toleo la mwaka mmoja kabla, gari ambalo ni adimu na gharama kubwa kulipata, hivyo kwa mfanyakazi wa daraja la kati wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania asingeweza kumiliki, sababu gari hilo halikuanza kuuzwa kama gari la mtumba……….ENDELEA…


Hivyo ni wazi kabisa muuwaji hakuwa askari wa jeshi la ulinzi na siyo tu kwa kufuatilia gari, hata kwa kukusanya askari wa vikosi vyote, vilivyopo Monduri na kuwa kagua mmoja baada ya mwingine kwa msaada wa baadhi ya watu waliokuwepo kwenye eneo la tukio, lakini pia hawakupata mtu anae fanana na muuwaji zaidi ya kuwapata askari kadhaa wanaofanana na muuwaji huyo, lakini ilielezwa kuwa askari wale muda wote walikuwa pale kambini wakiendelea na majukumu yao ya kila siku.


Taarifa hiyo ilimshtua sana Ulenje ambae sasa ndio alifahamu kuwa aliwatuma vijana wake kwa mtu ambae sio kwamba tu wale askari wa mombo, hata hawa wakina Cheleji, wangepoteza maisha na yeye kubakia katika wakati mgumu, wa kujibu maswali ambayo majibu yangepatika kwa yeye kufukuzwa kazi na kuswekwa lumande miaka kadhaa.


Taarifa hiyo ya habari, pia ili gonga kichwani mwa baadhi ya makamanda wa jeshi la ulinzi, akiwepo Major general Mbike, ambae mwanzo hakuwaza lolote, ila baada ya kupigiwa simu na msaidizi wake ambae ni Major na kumueleza jambo, “afande umesikia hiyo inshu ya Arusha?” aliuliza yule Major, “unawezaje kuhangaika na habari za Arusha wakati una habari ya kuifuatilia?” aliuliza Mbike, ambae alionesha wazi kusongwa na mambo kichwani mwake, “afande we nijibu kama umesikia vizuri hiyo habari” alisema tena Major, “nime sikia major, si una zungumzia habari ya hayo mauwaji mrina hotel?” alisema Mbike kwa sauti ya kukeleka, “hayo hayo afande, hebu ingia whatsapp halafu tafuta namba ya Deus, kisha tazama profile picha yake” alisema Major na hapo bila kuuliza lolote Mbie akakata simu.


Naam sekunde chache baadae Mbike alijikuta akitabasamu huku anatazama picha ya BMW S7, iliyowekwa kama picha ya jarida la kijana Deus, sambamba na maandishi, SIKU MOJA, “isiwe kweli, hii isiwe kweli, ni tatizo kubwa sana” aliongea Mbike kwa sauti ya chini, huku anapiga simu kwa major, simu ambayo ilipopokelewa tu, Mbike akatoa maelekezo, “waambie watu wa Songea wafuatilie kama Deus alinunua gari kama hilo na kama ndiyo tuingize watu mtaani kumsaka huyu dogo haraka iwezekanavyo, kabla ajafanya mambo mengi zaidi” alisema Mbike na kukata simu”.*******


Naam saa kumi na moja na robo za alfajili, ndiyo mida mbayo gari aina BMW S7 lilikuwa lina simama nje ya nyumba moja kubwa ya kifahari, maeneo ya kibwegele, kilomita kama sita hivi toka barabara ya morogoro, maeneo ya kibamba njia panda ya shule, huku wakionekana watu watatu, wawili vijana wenye miili iliyojengeka na mmoja ni mwanaume mtu mzima, huku kati ya wale vijana wawili mmoja akiwa ameshika begi dogo.


Mzee Simba akiwa na sanduku lake mkononi akashuka toka kwenye gari huku miguu yake inatetemeka kutokana na mwendo uliotembewa na lile gari kwa muda wote wa safari, mzee Simba analitazama gari lake, kisha anamtazama Deus, ambae alionekana ametulia nyuma ya kiongoza gari, yani stearing, wakati mwingine unaweza kuita mshikanio, kama vile ndio kwanza anaingia kwenye gari, usingedhania kuwa amesafiri mikoa zaidi tano kwa msaa kumi na sita.


Mzee Simba kama vile hakuwa anaamini alicho kishuhudia, akatazana saa yake kwenye simu, “dah! siamini kama ni kweli haya yametokea, yani tume zunguka toka arusha singida, Dodoma, Morogoro mpaka Dar, kwa masaa tisa” alisema yule mzee kwa sauti iliyoonyesha mshangao wa hali ya juu, Simba, tutasimama hapa tukikutazama mpaka saa ngapi? Hebu niambie kama mzigo umefika salama tumalize biashara” alisema yule mzee kwa sauti kavu japo ilikuwa katika utulivu, “mzigo umefika japo nilikutana na changamoto kidogo” alisema mzee Simba, huku anafungua sanduku lake, ambalo ndani yake kulikuwa na jiwe kubwa lenye kung’aa kwa rangi ya blue na pia kulikuwa na bando kadhaa za fedha, akachambua bando tano “mzigo wetu huu hapa” alisema mzee Simba, huku anamkabidhi fedha Deus, ambae alipokea na kuziweka kwenye seat ya pembeni yake, yani ya abiria wa mbele.


Baada ya hapo Deus akaingiza gia tayari kuondoka, lakini bwana Simba akamzuia kidogo, ni kama kuna kitu alisahu, “kijana subiri kidogo, alisema mzee Simba na Deus akasitisha kuondoa gari, Simba akasogelea gari, “nadhani hii ni biashara yako siyo?” aliuliza mzee Simba, “ndiyo karibu kama unakazi yoyote” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, “hakika nitakaribia, anyway, naitwa Simba, sijuwi mwenzangu nani na unapatikana wapi kama nitakuhitaji” aliuliza mzee Simba.


Deus alitabasau kidogo, “mzee ukitaka biashara ziendelee kumbuka sheria zangu kama mimi nitavyofuata za kwako, maana naona umesahau sheria yangu ya hakuna kujuana” alisema Deus, kwa sauti tulivu huku ana bofya kwenye ile screen ya kwenye dash boar na kufungua sehemu ambayo imeandikwa Call yenye kialama cha simu zile za mezani, kisha ikaibuka namba flani ya simu, “utanipata kwa namba, 04472574, muda wowote” alisema Deus, huku mzee Simba akiandika ile namba na alipomaliza kaondoa gari huku anapandisha kioo cha gari lake.


Mzee Simba na wenzake watatu walilisindikiza kwa macho lile gari mpaka lilipotoweka machoni mwao, na wakati huo ndio wakati ambao, yule mzee alikumbuka jambo, “BMW” alinong’ona yule mzee huku akionekana kuoanisha tukio fulani, halafu ghafla akamtazama “mzee simba, hivi habari inayosambaa kwenye vyombo ya habari toka jana usiku inahusiana na huyo kijana?” aliuliza yule mzee, alieonekana kushtushwa na kile alichokihisi, “ilikuwa zaidi ya hatari, nadhani sasa safari zangu za kibiashara zipo salama” alisema mzee Simba, ambae alikuwa anahifadhi ile namba kwenye simu yake akindika jina dereva, japo haikuwa na mfanano na namba ya kawaida ya simu.


Simba aliwasimulia kilichotokea na jinsi alivyo nusulika kuporwa mali yake na vijana wahuni wa Arusha, baada ya kusaidiwa na kijana huyu ambae moja ya taratibu zake ni kuto kuhusisha majina katika shuguri zao, akaeleza pia kijana yule alivyo waangamiza wale vijana wanne ndani ya muda mfupi na kisha kuanza safari yao ya kuja dar wakipitia barabara ya ngorongoro, “he! masaa tisa inamaana siyo tu kupigana ila hata kuendesha gari” alisema mzee yule kwa sauti yenye mshangao wa kishabiki na kukubari ubora wa kijana yule, “nivyema nikiwa na namba ya kijana huyo” alisema yule mzee huku anatoa simu yake akiihitaji namba ya simu ya dereva ambayo alitajiwa huku wanaingia ndani ya jengo lile jipya, ambalo lilikuwa linakaliwa na kijana mdogo alishika nafasi kama muangalizi wa nyumba hiyo mpya.


Waliiingia ndani na kumaliza biashara yao, mzee Simba hakutaka kukaa na mzigo ule ambao ulibakia kidogo ugharimu maisha yake, baada ya hapo mzee Simba aliingia kwenye mchumba kimoja, ambacho ni maalumu kwaajili yake pale anapohitaji kuja kupumzika huku na kujilaza kidogo akipunguza usingizi wa usiku kucha kabla hajaenda nyumbani kwake, ambako wanajua kuwa mpaka sasa bado yupo Arusha, huku yule mzee na wenzake wakiwa wanaondoka zao kwa gari lao aina ya Toyota V8, “huyu kijana mbona sikuwahi kumfahamu, ikiwezekana nitamfanya afanyie kazi kwangu kabisa” alisema yule mzee ambae pengine tunaitaji kufahamu kwa jina.


Huyu anaitwa Lumen Manyonyi, yeye ni mfanyabiashara na kama ilivyo kwa bwana Hassan Simba, tofauti ni kwamba bwana Manyonyi siyo kuwa na biashara zisizo na vibari, ila pia alikuwa anafanya biashara katika mazingira hatarishi sana, mara kwa mara alishaingia kwenye mashambulizi ya kutupiana risasi na wafanya biashara wapinzani wake, na hii ni kwaajili ya aina za biashara ambazo alikuwa anazifanya.


Ukichilia kununua chochote chenye thamani, kwa bei ya chini na kukiuza kwa bei ya juu, pia alikuwa tayari kudhulumu mtu yoyote ili apate anacho kitaka hata wakati mwingine ikitakiwa kutoa roho ya mtu mwingine.*******


Naam saa kumi na mbili na robo, gari aina ya lan rover puma, mali ya jeshi la ulinzi lilionekana likitimua vumbi kwenye barabara ya vumbi ya mtaa wa Making’ina, likitokea upande wa Chandamali, huku watu watatu wakiwa ndani yake wote wakiwa ni askari wa jeshi la ulinzi, mmoja akiwa na cheo cha luten kanali, mwingine akiwa ni sajent na mwingine akiwa ni private, ambae alikuwa ndie Dereva.


Gari lile lililionekana kuwa na haraka sana, lilienda moja kwa moja mtaa wa Shuleni, na kuingia kwenye eneo la mbele la nyumba moja kubwa yenye hadhi ya kawaida, lilisimama kati kati ya magari mawili moja likiwa ni Toyota Corolla 110 lililotengenezwa nchini uingereza, lililosimama nyuma ya land rover mia na tisa, pia likiwa ni kutoka uingereza, wakashuka askari wawili yani yule Luten Kanal na sajent, huku dereva akiwa amebakia ndani ya gari.


Yule sajent aliusogelea mlango, wakati yule luten kanal akiwa amesimama hatua chache toka kwenye ngazi za mlango, akimtaza Sajent alie panda ngazi na kuufikia mlango, lakini kabla hajagonga mlango akasikia michakato ya nyayo za binadau toka upande wa kulia wa nyumba ile, “karibu makamanda” ilikuwa ni sauti ya kiume toka upande huo wa kulia wa nyumba ile, wote wakageuka na kutazama upande huo, Macho yao yanakutana na mtu mwanaume mtu mzima, alie valia viatu vyeusi vyenye shingo ndefu, yani buti, suruali ya kaki yenye mifuko pembeni, kama nguo za jeshi zilivyo pia tishti la kijani, lililo lowa vibaya sana, ungegundua kuwa ni jasho, baada ya kuna want usoni mwake na mikononi, alimo kuwa anavuja jasho.


“Hooo! asante sana, bila shaka ni mzee Frank Nyati?” aliuliza yule Luten Kanal kwa sauti iliyojawa na uchangamfu, “yes ndiyo mimi, karibu sana” alijibu mzee Nyati kwa sauti ya uchangamfu pia, “baba kama mtoto, kumbe na wewe ni mtu wazoezi pia” alisema luten kanal, huku anamtazama mzee Nyati kuanzia juu mpaka chini, “yah! bila hivi, chai haipitishingoni mwangu, naona mumenitembelea asubuhi asubuhi, vipi ni kuhusu Deus tena?” aliuliza mzee Nyati, “ndiyo bwana Nyati, tunahitaji kufahamu sehemu alipo kijana wako au kupata mawasliano yoyote ambayo yanaweza kutuunganisha nae” alijibu Luten kanal.


Hapo mzee Nyati alitulia kidogo, kama vile anatafakari jambo na kabla hajasema jambo, “sina uhakika kama huko aliko hajafahamu kama anatafutwa na jeshi la ulinzi na sina uhakika kama atahitaji kuendelea kuwa jeshini” alisema mzee Nyati, “mzee tunafahamu kuwa ni jambo baya lilifanyika kwa Deus, lakini kinachotaka kufanyika sasa nikurekebisha makosa, kijana anatakiwa saa moja awe makao ni muhimu ukatusaidia tuwasiliane nae” alisema luten kanal, kwa sauti yenye kuhitaji kuweka sawa kila kitu, “ukweli ndugu yangu, mpaka sasa sijapata mawasiliano ya Deus, toka aliponiambia kuwa kuna mizigo itasafiri leo kuja songea, sijaona hata ujumbe wake na simu yake haipatikani kabisa” alisema mzee Nyati, na kuendelea kusema “ila kama nitapata mawasliano yake au akiwasha simu, nitamueleza kila kitu” alisema mzee Nyati kwa sauti ambayo ilimaanisha alichokuwa anakisema, “ok! kabla hatujaondoka tunaomba tukuulize kitu kama hutojari” alisema yule luten kanal, huku akimtazama mzee Nyati kwa macho yenye vipimo vya kung'amua uongo na ukweli…..….…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Aamiyn nanyi pia mubarikiwe
 
Ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…