Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Tunasubiri kisa cha Deus na Veronika wacha kujishebedua.
Leo Simba inacheza ikiisha meshi weka mwendelezo.
 
Hivi ukiacha hii hadithi na ile ya asali haitiwi kidole, ni hadithi gani umeisimulia.
Nataka nizifuatilie.
Pia nataka kujua kama utasimulia hadithi nyingine baada ya hii kuisha.
Ziko nying na baada ya hii kuna ambayo inakuja
 
Huyu atakuwa Yanga tu huyu.
Hapo tusubiri hadi keshokutwa akitulia labda.
Vikundi fc, ni shida sana yaani.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TISA: Deus anachokiona kwa Emmy kinamfanya atoe macho kwa mshangao, maana anamuona mwanamke yule akiwa amepembua lile taurlo na kubakia uchi wa mnyama, “jamani Dereva, sasa tutakaaje humu ndani bila kujuana majina?” aliuliza Emmy kwa sauti ya kujidekeza huku anainama kwa kubinua makalio yake akiacha wazi sehemu hiyo aliyojaliwa kuliko sehemu nyingine, mwana dada huyu mwenye umbo la kushawishi jambazi kurudisha kisu mfukoni, anachukua chupi aina bikini kwenye box aliloleta Deus na kuitazama kama vile anaikagua……….ENDELEA…

Hapo Deus anatoa macho ya mshangao, sio kwa kugundua kuwa atalipwa laki tatu kwa kuleta boxi lenye chupi, ila pia Deus anashangaa kitendo cha mwanamke huyu kupembua nguo zake mbele yake, “mimi sio mkaaji nahitaji malipo yangu, niwahi kazi nyingine” alisema Deus kwa sauti tulivu na ya upole huku anamtazama yule mwana dada ambae sasa alikuwa anaivaa ile nguo ndogo nyekundu, ambayo ilikuwa kivutio tosha kwenye kiuno chake, “wanakulipa kiasi gani nikulipe mara mbili kwaajili ya kazi yangu nyingine? hiyo itakuwa ni usiku kucha” aliuliza Emmy kwa sauti iliyojaa mahaba huku anainama tena na kuchukua shidiria kwenye lile box, huku macho ya Deus aliekuwa anamtazama kama vile hamtazami yakiweza kuona viji kamba kamba vilivyo potelea kwenye maungo ya mwana dada huyu mwenye umbo namba nane nayo ni yarangi nyekundu.

“sheria namba nne, hakuna mpango pacha, tunatatakiwa kumaliza mpango uliopo kisha tuingie kwenye mpango mwingine” alijibu Deus, kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, “sawa! Hata hivyo najua hautochukuwa muda mrefu kumaliza hiyo kazi nyingine” alisema Emmy, ambae sasa alikuwa anageuka na sidiria yake mkononi na kumtazama Deus kwa macho lembuzi yaliyo jaa hali fulani kama sio ya ulevi basi mahaba au vyote kwa pamoja, akimpa nafasi kijana wetu kutazama kitumbua cha buku kilicho tuna ndani ya kitambaa kidogo cha bikini kiasi cha kufanya muhogo uzidi kuchipua na kujitutumua ndani ya suruali yake, “sawa, maliza kwanza mpango uliopo” alisema Deus japo kwa Sauti tulivu, lakini ilikuwa yenye kusisitiza huku anamtazama Emmy, ambae sasa alikuwa anavaa sidiria kuficha manyonyo yake yaliyotuna vizuri na nakujaa vyema kifuani kwake.

Emmy alivaa sidiria kisha akaufuata mkoba wake uliopo kitandani, hata wakati wa kuuchukuwa, aliinama kwa mtindo fulani ambao, dah! ni Deus pekee ndie alievumilia, zaidi ya hapo angekuwa rafiki yangu nani huyuuuuu…, sidhani kama mpaka dakika hii kisu kingekuwa nje ya kifuko chake,

Sekunde chache zilitumika kutoa kitita cha noti za elfu kumi kumi toka kwenye mkoba ule, “sawa malipo yako haya hapa, je sasa tunaweza kuongea?” aliuliza Emmy huku anamsogelea Deus na kumkabidhi zile fedha, “yah! taja muda, aina ya mzigo, route na sheria zako” alisema Deus huku anaweka fedha mfukoni bila kuhesabu.

Hapo Emmy akamsogelea Deus na kusimama mbele yake kabisa, yani mita sifuri kabisa kiasi cha kifua cha mwanamke huyu kugusa kifua cha Deus, “muda wowote usizidi saa tano, rout ni hapa hapa hotelini chumbani kwangu, sheria za kwako wewe, hakuna mzigo zaidi ya mimi mwenyewe, kazi yako ni kunipa raha usiku kucha, nitajie garama yako” alisema Emmy au mama P, huku anaiweka mikono yake mabegani kwa Deus, kisha akaizungusha na kumkumbatia kwa hisia akilaza kichwa chake kifuani, huku Emmy akihisi dudu inamgusa maeneo ya tumbo lake.

Deus alitabasamu kidogo, “hapo sheria namba kumi inakataa, siruhusiwi kufunua au kuchungulia mzigo” alisema Deus, huku anamshika Emmy na kumtoa taratibu kifuani kwake, “basi sawa, iwe nje ya biashara, nakuhitaji kama rafiki, maana toka siku ile nimekuona sikuwahi kuacha kukutamani mpaka leo hupo mbele yangu, je unataka uniache na kiu yangu mpenzi?” aliongea Emmy kwa sauti ya kubembeleza iliyoonyesha ni kweli alikuwa anahitaji dudu ya kijana wetu usiku ule.********

Wakati hayo yanaendelea upande wa nje nako bado magari yaliyobeba vikundi vya vijana wa Songoro wakiongozwa na Songoro mwenyewe vilizidi kusogea upande wa shekilango, na sasa yalikuwa yamesha karibia zaidi, kama lilivyokuwa kwa bwana Eze ambae alikuwa anaendesha gari huku uso ameukunja kwa hasira, njia nzima anajisemesha mwenyewe, “sijui nimfanyaje huyu mseng.. yani nitawaambia wamfir..” alijisemea Eze huku akiendelea tena kuongea peke yake, alisema kuwa, “leo Emmy, nitamtomb.. mpaka asubuhi, si anajifanya ananyege za kicheche”*****

Naaaam turudi Songea, nyumbani kwa askari mtoro wa MLA luten kanal Frank Nyati, ambako bado alikuwa sebuleni na wageni wake watatu, sasa tayari mke wake alikuwa amesha waletea kahawa ambayo walikuwa wanainywa taratibu huku wakiendelea na maongezi, “afande Frank, kuna huyu Deus Nyati, ni kijana wako?” aliuliza sajent Ngasa, “Deus ni kijana wangu, nadhani pia mutataka kujua yupo wapi na anafanya nini” alisema Frank na wote watatu wakakubaliana nae kwa kuitikia kwa vichwa vyao.

Na hapo mzee Nyati akawatazama wale wageni wake kama vile anapima uaminifu wao, kisha akawaleza, “Deus ameachishwa kazi ya jeshi kwa kosa la utovu wa nidhamu, japo baadae iligundulika kuwa maamuzi yalifanyika kwa haraka bila kikao kikuu cha maamuzi kukaliwa na wao kuamua kumtafuta Deus, ambae hawakufanikiwa kumpata mpaka leo” alieleza mzee Frank huku wakiendelea kunywa kahawa yao, “hivi ni kwanini hawakumpata, inamaana Deus hakusikia kama anatafutwa na jeshi? na kama alisikia kwanini hakwenda kureport kazini?” aliuliza captain Amos Makey.

“Deus hakutaka tena kujiunga tena na jeshi, hivyo alikwepa makusudi kabisa kwenda makao makuu ya jeshi” alieleza Frank ambae kabla hawajaongea chochote wageni wake akawahi “najua mutauliza anafanya nini kwa sasa, pengine sasa amejiunga na UMD kama kisasi cha kusingiziwa kwangu” alisema mzee Frank na kuwafanya wageni wake wacheke kidogo.

Kicheko hicho kilimtambulisha mzee Frank kuwa, alichokisema ni kweli, “ondoeni shaka, Deus nimemlea kwa maadili mzuri hawezi kufanya hivyo na kwa sasa Deus yupo dar es salaam ametulia anafikiria nini cha kufanya baada ya kuondolewa jeshini” alisema mzee Frank na hapo likaja swali jingine, “lakini mzee unadhani hawa watu hawawezi kutumia sababu ya wewe kusingiziwa uhaini, kumshawishi Deus kujiunga nao huku akihofia kukuambia lolote kwa kuhofia utamzuia?” aliuliuliza Captain Amos Makey,

Naaaam hapo Frank akajibu swali hilo, “hilo ni kosa kubwa kwao na pengine likapeleka mwisho wa mpango wao, hata wao wanalijua hilo, hivyo hawawezi kufanya hivyo hata kidogo” alisema Frank na kuendelea kuwaeleza, “mimi nawashauri jambo moja, nivyema mkaweka macho yenu kwa James maana hisia zangu ni kwamba, walipandikiza chuki kati ya James na serikali, ili waweze kumtumia James hapo baadae na pengine baadae yenyewe ndiyo hii” alisema Frank akiwa mwenye kujiamini na uhakika mkubwa wa kile anachokisema, “ushauri mzuri afande frank, inabidi tumueleze General Sixmund, tumueleze juu ya hilo, halafu tutakushirikisha maamuzi yao” alisema captain Amos.

Baada ya hapo wakaagana na kupeana namba za simu, wakitumia line za Tanzania ambazo walipewa mara baada ya kuingia ubalozini, “afande Frank, wacha sisi twende zetu, nadhani kama kuna lolote ambalo utapenda kushiri na sisi, basi utatujulisha” alisema captain kabla hawajaondoka.*****

Yap! sasa turudi dar es salaam kule sisterfada Hotel, ghorofa ya tatu, chumba namba nane, ambako bado tunamuona mzee James, ambae ni tajiri na mfanya biashara mkubwa sana katika ukanda huu wa Africa Mashariki kusini na kati, akiwa amekaa kwenye kochi anatetemeka kwa uoga, mitutu miwili ime elekezwa kichwani, huku askari wawili walioshika bunduki hizo wakisubiri amri toka kwa mkuu wao, yani bwana Kadumya ya kufyatua risasi, “subirini kwanza” alisema Kadumya, ambae pia alikuwa amekaa kwenye kochi anavuta sigara yake na glass ya pombe mkononi mwake, “kwanza inabidi tupate picha ya pamoja, inayo muonyesha huyu mzee anaongea na waasi ambao anashirikiana nao kupindua nchi ya #mbogo_land, baada ya hapo tumuuwe” alisema Kadumya.

Na baada ya hapo akageuza uso wake, kuwatazama wale askari wawili waliosimama upande wa dirishani, dirisha pana lenye upana mkubwa uliotawaliwa na kioo bila nondo yoyote, zaidi ni panzia ambalo lilikuwa limefungwa, pembeni na kuacha dirisha wazi na kuwafanya wale vijana wawili wenye silaha aina ya H&K G95 5.56MM, waweze kuona nje vyema kabisa, “oya dogo hebu tupige picha kisha mtumie Kafuru aweke kwenye tovuti yetu ya uvumi” alisema Kadumya na hapo askari mmoja akaweka silaha mgongoni kwa kutumia mkanda maalumu kwaajili ya kubebea bunduki, yani tring lifle, kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya kisasa nzuri sana kwa kupigia picha.*******

Naam wakati hayo yanaendelea ghorofa namba tatu, huku ghorofa ya nne Emmy akiwa anasubiri jibu toka kwa Dereva na kabla Deus hajatoa jibu lolote mara ghafla mlango ukasukumwa kwa nguvu na fujo, Deus na Emmy wakatazama mlangoni na kuona vijana wawili wakiingia na bastora mikononi mwao, huku mtutu wameielekeza kwa Deus, “khaaaa! bunduki tena?” aliuliza Deus kwa sauti iliyoonyesha kuchukizwa na kitendo kile huku anageuka kumtazama Emmy, maana alihisi Emmy ametumwa kumpanga na kumuingiza katika mtego ule.

Lakini anamuona Emmy akiwa katka hali ya mshangao na mshtuko mkubwa uliochanganyika na bumbuwazi, “majambazi” alisema Emmy kabla hajazinduka toka kwenye bumbuwazi na kuanza kukimbilia kitandani, ambako alichukua shuka na kujifunika haraka, “nani jambazi we kahaba, unamuacha mumeo halafu unakuja kujificha huku na huyu boya, tena usikute hata lile gari umemnunulia wewe” alisema mmoja kati ya wale vijana wawili, akimueleza Emmy huku akiwa amesimama na bostora yake mkononi, akiwa ameielekeza kwa Deus kama mwenzie alivyofanya, “inamaana Eze ndiyo kawatuma kufanya hivi?” aliuliza Emmy kwa sauti ya mshangao akionyesha kushangazwa na kilichotokea, “hebu kaa kimya wewe, za mwizi arobaini na leo ndiyo arobaini yenyewe” alisema tena yule muongeaji sana wakati huo mlango unafungwa na mtu aliekuwa nje ya chumba hicho, “samahani jamani nimesha maliza kazi yangu, nawatakia jioni njema” alisema Deus huku anageuka akitaka kuondoka,

“we fala unaenda wapi we mjinga, tutapasua ubongo wako sasa hivi” alisema Inocent, na hapo nikama inzi kwenye uchafu jinsi wale vijana wawili walivyo msogelea Deus kwa fujo na bastora zao mikononi, kitendo ambacho kilikuwa ni kama kumkosea kijana wetu, “oi oi oi, kwanza naombeni msinionyeshee bastora zenu” alisema, Deus ambae mara zote huamini anapokuwa karibu na bunduki ya aina yoyote, lazima matatizo yangetokea, “oya mbona huyu bwege anajifanya mjuaji, hebu mtulize kwanza akae chini amsubiri boss yupo njiani” alisema Inno, ambae kabla hajamaliza tayari yule mwenzie alikuwa ameshainua bastora yake akiigeuza kitako chake kwaajili ya kumgonga Deusi kichwani.

Lilikuwa kosa kubwa sana kwao maana hawakuamini kilichotokea, hasa pale walipomuona Deusi akiyumba pembeni na kupisha kile kipigo cha kitako cha bastora, kilichopita hewani kwa nguvu, huku Innocent ambae alikuwa ametoa macho ya mshangao, akishangaa mkono wake ukipapaswa na ile anapata wazo la kuminya trigger tayari mkono haukuwa na kitu.

Wakati huo yule alietaka kumpiga Deus na kitako, anakaa sawa ili amdhibiti Deus, akashtuka akipigwa ngumi moja nzito sana ya uso, iliyomtupa chini na kumzimisha pale pale, ile Inocent anataka kumvamia Deus, akajikuta anatazamana na mtutu wa bastora, “nimekuambia usininyooshee bunduki” alisema Deus kwa sauti tulivu huku akimalizia kwa kushusha kitako cha bastora kwenye paji la uso wa Inocent, ambacho kilikita kwa nguvu na kumpeleka chini kijana huyu, ambae alikata mawasiliano ya ubongo na sehemu nyingine za mwili akaenda chini kama gunia lililo tupwa toka ndani ya gari… …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISI: Wakati huo yule alietaka kumpiga Deus na kitako anakaa sawa ili amdhibiti Deus, akashtuka akipigwa ngumi moja nzito sana,ya uso, uliliyomtupa chini na kumzimisha pale pale, ile Inocent anataka kumvamia Deus, akajikuta anatazamana na mtutu wa bastora, “nimekuambia usininyooshee bunduki” alisema Deus kwa sauti tulivu, huku akimalizia kwa kushusha kitako cha bastora kwenye paji la uso wa Innocent, ambacho kilikita kwa nguvu na kumpeleka chini kijana huyu ambae alikata mawasiliano ya ubongo na sehemu nyingine za mwili akaenda chini kama gunia lililo tupwa toka ndani ya gari… …….ENDELEA…

Deus akataka kuufuata mlango, lakini anaukaribia akaona mlango unafunguliwa, ni wazi wale waliokuwa nje mmoja wao alikuwa anataka kuingia ndani, “vipi mbona kama kuna…” ilisikika sauti ya mwanaume huku akitokeza uso pale mlangoni kwa maana ya kuchungulia, lilikuwa kosa kubwa kwake mchunguliaji, maana hakupewa hata nafasi ya kuuliza kuna nini, Deus akiukita mlango kwa mguu, akiukanyaga kwa nguvu kama vile anaufunga na kufanya mlango umbamize huyu jamaa kwa nguvu sehemu ya kichwa, akapiga ukelele wa maumivu huku anajirudisha koridoni na kumpa nafasi kijana Deus ya kufunga mlango, kisha akamtazama mama Spesioza, matokeo ya uvunjifu wa sheria namba tatu, (hakuna bunduki)” alisema Deus, kwa sauti ya upole huku anatembea kulifuata dirisha, lililokuwa limefunikwa kwa panzia.

Akiwa anamtazama huyu kijana mpole na mtaratibu mwenye kivutia, kijana ambae sura yake uongeaji wake ni tofauti na matendo yake, alionekana akifunua panzia na kufungua dirisha lile kubwa la kioo, ambalo lilifunguka kwa mtindo wa mlango wa daladala, yani kwa kusogeza pembeni.

Mwanzo Emmy, alidhania kuwa dereva anataka kuchungulia nje, lakini alishangaa kumuona kijana yule, mwenye mapigo ya kijambazi akichungulia nje kisha akapita dirishani, hapo Emmy akatoa macho kwa mshangao, “ghorofa ya nne, masikini kijana mzuri anaenda kujiua mwenyewe” aliwaza Emmy, akiwa mwenye uoga na wasi wasi juu ya kile kilichotokea mbele ya macho yake na huku kinachoenda kumtokea dereva wake ambae sasa alishapotelea nje.

Emmy akasogea dirishani haraka na kuchungulia chini, ambako aliweza kumuona kijana wetu, akiwa amekanyaga jofu la kiyoyozi, A/C box la ghorofa linalofuata, yani ghorofa namba tatu, huku baadhi ya watu waliopo chini kabisa wakionyesha kule juu alikokuwa Dereva, ni kama walikuwa wanamshangaa kijana huyu kwa mchezo wa hatari anaoufanya.

Wakati Emmy anaendelea kumshangaa Deus, huku nako mlango ukasikika ukijaribiwa kufunguliwa na mtu toka nje, hapo Emmy akakumbuka kuwa anahitaji kuvaa haraka nguo zake, maana muda mfupi ujao chumba kile kina geuka ukumbi wa makusanyiko, hivyo mwili wake ungegeuka wa maonyesho.*********

Naaaam nje ya jengo, yanaonekana magari matatu yakiingia kwa fujo na kusimama mbele ya hotel ile sisterfada, wakati magari mawili yakiwa ni Songoro na vijana wake, gari la tatu lilikuwa ni gari la bwana Ezekiel, “wapo wapi hao vijana wako Eze?” aliuliza Songoro akiwa mwenye jazba na hasira huku anaficha bastora yake kiunoni, kama vijana wake ambao walihifadhi SMG zao ndani ya makoti marefu ya mvua, ungeshangaa kuona watu wanavaa namna ile wakati hapakuwa na hata dalili ya mvua, “chumba namba nane, ghorofa ya nne” alijibu Ezze huku anatembea kuelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya hotel.

Kitendo bila kuchelewa, Songoro akawatazama vijana wake, “wanne wanifuate na nyie wengine mfuateni Eze,alisema Songoro, huku anaanza kutembea kueleka upande wa maegesho ya magari ya ndani.

Hapo wale vijana wakajigawa kwa haraka kama walivyo elekezwa na Songoro, hivyo kundi kubwa lilimfuata Eze aliekuwa amesha likaribia lango la kuingilia ndani ya hotel na huku vijana wanne wakimfuata yeye Songoro, “oya dogo simama ukaguliwe kwanza unaenda wapi?” ilisikika sauti ya mlinzi alieongea huku anamsika mkono mzee Eze, sijui kwanini alimuita dogo au ufupi nao ni utoto.

Haikuwa bahati ya mlinzi yule wa kampuni ya ulinzi ya kujitegemea, maana alichomoka kijana mmoja kati ya wale saba waliokuwa wanamfuata Eze na kumfyatua mtama yule mlinzi, ambae alielea elea angani na ile anafika chini akakutana na kisigono cha buti kama la kuendeshea farasi, kilichokita kwenye mbavu zake na kumfanya aachie kilio cha uchungu wa maumivu.

Kitendo kile ni kama kiliwashtua watu waliokuwepo eneo lile na kuwafanya wang’amuke kuwa kuna ujio wa watu wasio wakawaida pale hotelini, hivyo wakaanza kutimua mbio wakikimbia huku na huko wakitafuta njia ya kutokea, ni wazi walidhania kuwa watu hawa ni majambazi, maana ukiachilia kuingia kwa fujo na ubabe pale hotelini, pia mara baada ya kuingia hotelini tu, wakatoa silaha zao kwenye makoti yao ya mvua na kuanza kutembea kumfuata bwana Eze, ambae alikuwa anatembea kwa haraka kuifuata lift.

Huko nje bwana Songoro akiwa na uchungu na hasira, iliyogubikwa na hamu ya kumnasa kijana dereva wa BMW jeus, ambae amemfanyia dharau kubwa sana siku iliyopita, alitembea kwa haraka kueleka upande wa maegesho ya magari, “huyu jamaa atakuwa amefumaniwa na mke wa mtu” ilisikika sauti ya mtu mmoja toka upande ule ule, lakini mbele kidogo ya jengo la hotel, lakini Songoro hakujarli mambo ya kufumaniwa, alicho jali nikufika kwenye maegesho na kumsubiri dereva ambae kwa vyovyote lazima gari atakuwa ameliegesha humo, “we unadhani atakuwa amefanya nini zaidi ya kufumaniwa, yani apande ghorofa bila sababu” isikika sauti nyingine ya kiume safari hii ikiambatana na kicheko.

Lakini bado sauti ile haikumshawishi Songoro kwenda kutazama upande ule, aliendelea kutembea sambamba na vijana wanne ambao bado walikuwa wameficha bunduki zao kwenye makoti yao ya mvua, ambao sasa walikuwa wameshalifikia geti la kuingilia kwenye nagesho ya magari ya ndani, “utakufa we bwege, acha uzinzi” alisikika mmoja kati ya wale watu wenye kumtazama mgoni akipaza sauti kubwa.

Hapo Songoro akasimama ghafla ni wazi kuna jambo alihisi, maana aligeuka haraka na kutazama kule ilikokuwa inatokea sauti ya wanaume, nao wakawaona vijana wawili wamesimama wanatazama juu ghorofani, sehemu ambayo wao wasingeweza kuiona, kutokana na sehemu waliyokuwepo, kwa maana ilikuwa ni ubavuni mwa jengo lile.

Wote wakavutika kwenda kuona kilichokuwa kina tazamwa na vijana wale wawili na Songoroa ndie aliekuwa wa kwanza kuanza kutembea kuelekea upande huo huku vijana wake wakimfuata.

Naam wakati huo huo chumba namba namba nane cha ghorofa namba tatu, hapa Sisterfada, ambako zoezi la upigaji picha zilikuwa zinamalizika akasikika Kadumya, “sasa ndio wakati wako wa kusali sala zako za mwisho kama una dini, kama hauna basi waombe babu zako wakupokee” alisema Kadumya huku anatoa bastora yake kwenye mfuko wa ndani wa koti la suit pamoja na mtutu wa kiwambo cha kuzuia sauti na kuanza kufunga kwenye mtutu wa bastora yake aina ya Beretta 92 toka Italy pasipo kumtazama mzee James ambae alikuwa anatetemeka kwa uoga, kijana mmoja akiwa dirishani na yule mwingine anatuma picha kwa Enock kafulu, ambae angetimiza lengo lao kwenye mtandao wao wa uvumi na propaganda.

Kadumya alipomaliza kufunga kiwambo cha kuzuia sauti, akaikoki bastora tayari kumuuwa mzee James, ambae sasa alikuwa anakaribia kujikojolea kwa uoga aliokuwa nao, “boss naona chini kuna watu wanatazama huku kama vile kuna kitu wanaonyeshanana huku, kama vile kuna kitu wanaonyesha hivi” alisema yule kijana aliekuwa bado dirishan.

Hapo Kadumya akashtuka na kumtazama James, kwa macho yaliyojaa tahadhari, “pumbavu james, ina maana ulitutega na kutuchoma kwa MLSA?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya chini na kutembea kuelekea dirishani, na moja kwa moja akatazama nje ambako aliweza kuona watu wawili wakitazama kule juu kama vile kuna kitu wanaonyeshana, “mh! mbona kama hawana madhara yoyote” alisema Kadumya, huku anageuka, “boss ni vyema ukaangalia tena” alisema yule kijana mwingine, wakati huo James anawatazama kwa umakini huku anaomba utokee muujiza wowote aweze kuepuka kifo hiki.

Kadumya anasimama na kugeuka nyuma, kisha anatazama kule chini na sasa anawaona watu watano wengine wakiongezeka, hawa ni tofauti na wale wa kwanza ambao walikuwa wamevaa nguo za kaiwaida tu tofauti na hawa waliovalia makoti marefu meusi, na wao walitazama kule juu walikokuwepo wao, huku mmoja wao kama vile ana walekeza kitu ambacho kipo kule juu, “hebu fungua dirisha, haraka tuwasikie wanaongea nini” alisema Kadumya, ambae alionekana kuingiwa na tahadhari ya kwamba kinachosema kule chini kinahusiana na wao, maana jamaa walikuwa wanaonyesha usawa ule ule waliokuwa wao.

Naam wakati yule jamaa mwenye bunduki anafungua dirisha, huku Kadumya anawaona wale jamaa watano wanatoa SMG kwenye makoti yao, “washenzi wanatoa bunduki washambulie” alipiga kelele Kadumya na bila kujiuliza mara yule kijana akakoki bunduki yake na ile anaielekeza dirishani, akasikia “pah! pah! pah! pah!” milipuko ya risasi mfululizo ikitokea kule chini, huku ghafla akipigwa kikumbo kimoja kikubwa sana na kuangukia ndani huku bunduki yake ikimtoka mkononi na kuangukia mita chache pembeni.

Kadumya na wengine waliokuwa mle ndani kwa macho yao wanamuona kijana mmoja akiwatazama kwa mashangao, huku mvua ya risasi ikiwa inaendelea kulindima upande wa nje, hapo Kadumya bila kuuliza anainua bastora yake na kuielekezea alipokuwa yule kijana, ambae kwa wepesi wa ajabu sana anamshika yule alie anguka nae chini na kumgeuza kwa haraka, akimfanya kama kinga, wakati huo tayari kadummya alikuwa ana minya kidole chake mara mbili, akiluhusu risasi kuchomoka kwenye mtutu wa bastora. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MOJA : Kadumya na wengine waliokuwa mle ndani, kwa macho yao wanamwona kijana mmoja akiwatazama kwa mashangao huku mvua ya risasi ikiwa inaendelea kulindima upande wa nje, hapo Kadumya bila kuuliza anainua bastora yake na kuielekezea alipokuwa yule kijana, ambae kwa wepesi wa ajabu sana, anamashika yule alie anguka nae chini na kumgeuza kwa haraka, akimfanya kama kinga, wakati huo tayari kadummya alikuwa ana minya kidole chake mara mbili akiruhusu risasi kuchomoka kwenye matutu wa bastora. …….ENDELEA…

Wakati anaruhusu risasi kadumya, alitamani kuizuia risasi japo moja tu kutoka kwenye mtutu wa bastora yake, lakini hakuwa na uwezo huo, zaidi ya kuwa mmoja wa mashuhuda wa kifo cha askari wake huyo ambae alizipokea risasi zote mbili mgongoni, kutahamaki tayari wengine wawili walishainua bunduki zao na kuzielekeza kwa kijana huyu ambae tayari alikuwa amesha uachia mwili wa yule aliepigwa risasi na kubiringika kama tairi la gari kuelekea usawa wa bunduki iliyoangushwa na yule kijana ambae sasa ni mfu, huku milipuko kadhaa ya risasi, ikisikika mule chumbani na kufanya mzee James azidi kutetemeka kwa uoga, maana tayari chumba kilishageuka uwanja wa vita, tena vita kubwa, aliweza kuona miale ya cheche za moto ikitokea sakafuni, ikiwa ni ya mikito ya risasi zilizomkosa kijana huyu mvamizi wa mambo yasio muhusu, wakati huo huo, yule mwingine ambae ni mpiga picha akiwa anatoa bunduki yake mgongoni kwaajili ya kuikoki huku bwana Kadumya akiwa anaweka sawa bastora yake kutafuta malengo ya sahihi ya kumlenga kijana huyu, ambae mpaka sasa hakuweza kumtambua kama ni moja wa askari wa MLA au MLSA.

Lakini kanali mtoro wa jeshi la serikali ambae sasa anajiita General Erasto Kadumya, pamoja na shuhuda mwingine ambae ni mkimbizi tajiri kuliko wakimbizi wote duniani, bwana James Kervin, waliweza kushuhudia kijana huyu mwenye uharaka kama mwanga wa tochi akikaa sawa, huku tayari bunduki ikiwa mkononi mwake.

Hapo ni kitendo bila kuchelewa ikasikika “pah! pah!” tayari risasi mbili zilikuwa zimesha toka kwenye mtutu wa HECKLER &KOCH G95, ikifuatia vijana wawili washambuliaji mikono yao ikishindwa kudhibiti bunduki zao mzuri toka ujerumani na kuziacha zikianguka chini, huku wao wakishikilia sehemu mbali mbali za miili yao, wakati mmoja akishikilia bega la mkono wa kulia, mwingine alishilia sehemu ya paja la mguu wa kulia huku akienda chini.

Kuona hivyo Kadumya anaweka sawa bastora yake, kumuelekea kijana yule alieingilia dirishani na kuachia risasi mbili mfululizo, lakini anakuwa amechelewa maana tayari kijana huyu anakuwa ameshamrukia mpiga picha ambae tayari alikuwa amesha koki bunduki yake, hivyo teke moja zito la kifuani lililomtupa na kwenda kujibamiza ukutani, linamfanya aachie risasi mfululizo, yaani rapid, bahati nzuri mtutu ulikuwa umeelekea juu, hivyo akakung’uta zenge la ghorofa ile ya tatu huku akiwa amepoteza fahamu na kidole kikiwa kime ng’ang’ania kifyatulio mpaka risasi zilipokoma, kikawaida risasi thelathini zkipigwa kwa mtindo huu, huchukuwa sekunde tatu mpaka tatu na nukta kumi, kuisha kabisa.

Ilimshangaza sana Kadumya, hakutegemea kuona mtu mwepesi namna ile, pengine angetaka kufanana na luten kanal mmoja mtoro mkimbizi, toka MLA, lakini haikutosha kumkatisha tamaa Kadumya ambae alikumbuka kuelekeza bastora yake kwa kijana huyu machachali, lakini alikuwa ameshachelewa tayari, kijana alikuwa hewani anakuja usawa wake huku amevuta ngumi moja nzito ambayo alipoipeleka usoni mwake alihisi maumivu makali kama amepigwa na nyundo ya kilo kumi akifuatiwa na giza kutanda usoni mwake sambamba na nyota za kijani. “siku nyingine wafundishe vijana wako matumizi mazuri ya silaha nzuri kama hii” kwa mbali Kadumya alisikia maneno hayo huku akizidi kupoteza nguvu ya mwili wake.

Hapo kijana yule ambae matendo yake ni tofauti kabisa na sura yake, akaichukua bastora ya Kadumya na kutoa kimkebe cha risasi ambacho kilionyesha bado kina risasi za kutosha, akaurudisha na kuielekeza kwa mpiga picha ambae bado alikuwa amepoteza fahamu, akageuka kwa yule aliemtandika mkono ambae sasa alijua anauwawa, hivyo akaanza kukimbilia mlangon kwa lengo la kutoka nje, akamuwahi kwa risasi ya mguu kisha amuongeza na yule mwingine aliemchapa risasi ya mguu mara ya kwanza.

Mzee James akiwa ubavuni mwa kochi, mwanzo alidhania kuwa huyu jamaa ni shushu wa MLA au MLSA alietumwa kuja kumuokoa, lakini akashangaa kumuona kijana yule akiweka bastora mezani na kuanza kuusogelea mlango, hapo akajua kuwa akimuacha kijana huyu atoke, basi atafikia mikononi mwa hawa UMD, maana wengine walikuwepo pale nje kwahiyo huu ndio msaada wake wa kutokea hapa hata kwa gharama yeyote.*******

Yap! Songea mjini, maeneo ya msamala karibu na stend kuu, mita kama mia moja toka Nyumban lodge, anaonekana bwana Chiropo akiwa amekaa juu ya pikipiki anaongea na simu huku macho yake yapo kwenye lango la hotel ile, “muheshimiwa wameshaingia hotelini, lakini mpaka sasa ni kwamba ujio wao huku tanzania hawajafika kwa leongo la kushiriki zoezi lolote la pamoja la kijeshi, ila ukweli ni kwamba wamekuja kuchunguza juu ya UMD” alisema Chiropo kwa sauti ya chini kidogo, “mh! ulifanikiwa kusikia maongezi yao?” iliuliza sauti ya upande wa pili wa simu, “nilisikia mwanzo mpaka mwisho” alisema Chiropo na kueleza jinsi maongezi ya wakina mzee Frank na wale askari wa MLA, “Nyati amesema kuwa kuna mtu yupo serikalini anahusika na mipango yote ya kikundi cha UMD” alieleza Chiropo, “mpuuzi Nyati, ndio maana sikutaka awe hai mpaka leo, nilijuwa atakuwa tatizo hapo baadae, lakini ameshachelewa, hivi karibuni kila kitu kinaenda kuisha” ilisikika sauti ile, ambayo ni wazi alikuwa bwana Chitopela, “lakini muheshimiwa, inaonyesha wanaanza kugundua mambo mengi, hata mpango wa kuwauwa wale watu muhimu wa MLA na MLSA, Nyati ameuzungumizia” alisema Chiropo.

Hapo ile sauti upande wa pili wa simu, yani ya Chitopela, ikasikika ikiachia kicheko cha dharau, “imekula kwao, wakati wao wanaweka vikao vya siri tayari mambo yanakamilika huko dar es slaam, tena watachanganyikiwa watakapo muona James akiwa amekaa na wanamapinduzi wa ukweli kwenye picha moja wanapata mvinyo” alisema Chitopela huku akiendelea kucheka.

Naam baada ya maongezi mawili matatu, Chitopela akiwa amemsisitiza Chiropo, kuwafuatilia watu hao kila hatua watakayo kanyaga.*******

Naam tukirudi hoteli Sisterfada, kule chini kabisa ya jengo hili la ghorofa, mida hii palikuwa pamesha chafuka, watu walikuwa wanakimbizana hovyo ovyo, nikutokana na milindimo ya risasi iliyosikika, hasa ile ya bwana Songoro na vijana wake, ambao walipoona dereva BMW jeusi ameingia kwenye dirisha la moja ya vyumba vya ghorofa namba tatu, nao wakaelekea ndani moja kwa moja kwenye lift, huku songoro anapiga simu kwa Ezze, “waambie hao malofa waende ghorofa la tatu haraka” alisema kwa ukali bwana Songoro huku wanaingia kwenye lift na kubofya kitufe kilicho andikwa namba tatu, huku wakiwa wameshikilia bunduki zao mikononi.

Hakika ungesema ni tukio la kwenye filamu, lakini ukweli lilikuwa ni tukio halisi lenye kutisha, maana ni matukio adimu sana hapa nchini, unaweza kuliona hilo kwa jinsi maeneo ya jirani na hotel hii ya sisterfada yalivyoshtushwa na kupata taharuki, kutokana na milindimo ya risasi iliyosikika usiku ule.

Mida hii CP Ulenje alikuwa nyumbani kwake anasubiria taarifa ya kufanikiwa kwa mpango wa kumnasa kijana dereva aliendesha BMW jeusi lililoshiriki kutorosha dhahabu, japo hawakuwahi kumfahamu kwa sura hapo mwanzo, mara Ulenje anapokea simu toka makao makuu ya polisi, “hallo Ulenje, hebu paleka askari wilaya ya kinondoni, (kwa sasa ubungo) wakaungane na askari wa huko kuna uvamizi kwenye jengo la sisterfada hotel maeneo ya sinza” hiyo ndiyo taarifa ambayo alipewa Ulenje kisha simu ikakatwa.

Nae pasipo kuhisi kuwa tukio hilo ni la washirika wake, akapiga simu kwa OC FFU, na kumpa maagizo ya kupeleka askari Sinza, huku yeye akitulia nyumbani kusubiria taarifa za kukamatwa kwa dereva na pengine kuokotwa kwa mwili wa kijana huyo *******

Naaam wakati huo bwana Eze ambae alikuwa anawaza kwenda kumuua mtu anaetembea na hawara yake, akaona amri ya Songoro haikuwa na maana kwa wakati huo zaidi ya kile kilichomleta hapa Sisterfada.

Eze akiwa na kundi la vijana saba wa Songoro, anaufikia mlango namba nane ambapo anawakuta vijana wake wawili wakiwa wamesimama, pembeni yake yeye anashika kitasa cha mlango namba nane na kukinyonga kwa hasira kwa maana ya kufungua mlango, lakini mlango unakuwa umefungwa kwa ndani, “nyie washenzi hebu fungueni mlango, mbona mme jifungia mlango, munamfnya nini mke wangu?” alipiga kelele Eze sambamba na kugonga mlango kwa ngumi na mateke, “boss nadhani anaekusikia ni shemeji tu” alisema mmoja kati ya wale vijana kwa sauti ya kinyonge, huku mwenzie akiwa anashikilia kichwa kwa maumivu, nadhani ni yule aliebamizwa na mlango, “wakina Ino wapo wapi na huyo fala?” aliuliza Eze kwa sauti yenye hasira kali, “wapo ndani lakini sidhani kama wanakusikia” alijibu yule jamaa.

Hapo Eze akaona kama anazinguliwa, akamtazama mmoja kati ya wale vijana aliokuja nao ambae ni Said, “fungua mlango” alisema Eze kwa sauti yenye uzito wa amri, hapo bila kuchelewa Side akakoki SMG yake ya mwaka 57, akiweka risasi kwenye chemba, lakini kabla haja elekeza mtutu kwenye kwenye kitasa wote wakaona mlango unafunguliwa na akajitokeza Emmy, “yaani unawatuma watu wanifuatilie, kwahiyo huniamini” aliongea Emmy kwa sauti ya kulalamika huku machozi yana mtoka, Eze akapitiliza ndani kama vile hakuyajari maneno ya Emmy, “hebu ona umesababisha watu wapigane, mpaka mtoto wa watu anatokea dirishani, je kama angeanguka ungepata faida gani?” aliuliza Emmy, lakini Eze alionekana kutoa macho ya mshangao akiwatazama vijana wake wawili waliokuwa wamelala sakafuni hawajitambui, “ina maan huyo hawara yako ndio amewafanyia hivi watu wangu?” aliuliza kwa ukali Eze, “jamani baby nani kasema ni hawara yangu, yule ni dereva msafirishaji nilisahau kitu salooni nikamtuma aniletee, waulize wafanyakazi wangu watakuambia” alisema Emmy kwa sauti ya kulalamika.

Hapo kidogo Eze akapoa kidogo, “inamaana sio mpenzi wako?” aliuliza Eze kwa sauti iliyopoa kidogo huku wakina Side wakianza kujumlisha maelezo ya Emmy kwamba kijana huyo ni dereva msafirishaji, “hata jina simfahamu, yeye nilimwagiza tu” alisema Emmy, ambae alikuwa anaachia kilio cha uongo na ukweli, “sasa hapa umekuja kufanya nini?” aliuliza Eze huku anazungusha macho mle chumbani, “mimi mara nyingi tu huwa nakuja kulala hapa mwenyewe, hasa nikitaka kubadilisha mawazo” alisema kwa kulalamika Emmy, na kumfanya Eze atazame chini kwa aibu, “nifuateni” ilisikika sauti ya Side, akiwaeleza wale wenzake, huku anakimbia kutoka nje, na kuelekea kwenye lift, ambayo ilionyesha ilikuwa inapanda juu, na sasa ilikuwa ghorofa yapili. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
mkuu leo umetukosha sana huu ndio mwendo unaotakiwa kwenda nao kila siku uwe unatupia vipande vitatu kama hivi sio ile kimoko unatokomea na ww ushasema una stori nyingi za kuleta humu sasa kuwa unabania nini kwa kuteletea kimoja kimoja..fanya kama hivi leo vipande vitatu poa sana..
 
mkuu leo umetukosha sana huu ndio mwendo unaotakiwa kwenda nao kila siku uwe unatupia vipande vitatu kama hivi sio ile kimoko unatokomea na ww ushasema una stori nyingi za kuleta humu sasa kuwa unabania nini kwa kuteletea kimoja kimoja..fanya kama hivi leo vipande vitatu poa sana..
Kwahy tukutane kesho tushushe tatu kama leo au sio?
 
Hiyo kanuni namba 8 ya kutofungua mzigo sijaipenda upande wa emmy
 
Back
Top Bottom