NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA TISA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA NANE:- alisema Songoro, kwa sauti yenye ubabe ndani yake, mpaka hapo ACP Ulenje aliona wazi kuwa anaenda kuharibikiwa kabla jua hailijachomoza, hivyo ni lazima achukue maamuzi magumu “sawa bwana Songoro, pengine umejipanga, ila itabidi nikuongezee nguvu ya askari na silaha” alisema Ulenje kwa sauti tulivu mfano wa mtu alie kubaliana na msimamo wa Songoro, “hapo sasa ndio umeongea point, sasa nakutana nao wapi hao askari?” aliuliza Songoro, akionyesha kufurahia mpango wa Ulenje, hakujua kuwa kilichopangwa na Ulenje ni zaidi ya mipango yake ya kikatiri aliyowahi kuifanya… ENDELEA..
“umesema mpo ndani kidogo upande wa kulia pembeni mwa reli?” aliuliza Ulenje, “ndiyo, kuna kinjia fulani hivi, tena naona kuna alama za matairi ya gari, inaonyesha njia inayotumika sana” alijibu Songoro pasipo kujua kuwa anaelekeza hatari kuja upande wake, “sawa sawa subiri hapo mpaka vijana wangu watakapo kuja” alisema Ulenje, na Songoro akakubari mara moja akidhania kuwa Ulenje kubari kufuata anavyotaka yeye.******
Ndani ya golden house kwa mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mtoto wa king Eric wa pili na Malkia Doctor Irene, ambae sasa alikuwa ametulia huku macho yake kwa mpenzi wake huyu ambae hadithi ya kukutana kwao inapendeza na kusisimua zaidi ya ile ya #UMEKOSEA_LAKINI_TAMU, akmwambia “aya mke wangu, sasa nakusikiliza, hebu fafanua unachowaza” alisema Elvis kwa sauti ya upole.
Na hapo Vaselisa akaanza kuongea kwa ile sauti yake tamu, kama kinubi cha mfalme Suleiman, “mume wangu, kwanza kumbuka kuwa wewe na general Sixmund, ndio watu pekee munao endesha huu mpango wa siri, kwa maana hiyo hakuna mwingine ambae anafahamu juu ya hilo, na mpaka sasa tayari mumeshatilia mashaka makubwa juu ya njama kubwa iliyofanyika wakati wa operation ya kwanza ya mwaka 92, ambayo iliendeshwa na huyo huyo Chitopelah, ambae hajui kama kuna watu wameshaipata orodha ya askari na wanausalama walioshiriki katika operation ile….” Wakati malkia Vaselisa anaendelea kueleza anachokihisi, mara simu binafsi ya king Elvis ikaanza kuita.
King Elvis akaichukua simu haraka na kuitazama, akaona kuwa mpigaji alikuwa ni major General Sixmund, hii hakujiuliza mara mbili, akaipokea mara moja na kuweka sauti ya wazi ili wote wawili wasikie kitakacho ongelewa, “ndiyo Sixmund, kuna jipya lolote?” aliuliza Elvis kwa sauti iliyojaa shahuku, “mtukufu mfalme, licha ya kuwepo kwa habari mbaya, ila pia kuna habari njema” alisema Sixmund, nae akianza kama alivyoanza Chitopelah muda mfupi uliopita, “anza na hizo mbaya” alisema Elvis, ambae safari hii, alionekana kuwa na wasi wasi mara mbili, akihofia kupewa taarifa kama zile za Chitopelah, ambazo zingethibitisha kuwa ni kweli kuna waasi ndani ya serikali yake.
Naam, Major General Sixmund akaanza kueleza huku mfalme Elvis na malkia mwenye umri mdogo kuliko malkia wote kwa kipindi hicho, wakisikiliza kwa umakini, “mtukufu mfalme, taarifa mbaya ni kwamba, kati ya watu ishirini na tano katika orodha ya wanausalama walioshiriki operation ya mwaka 92, watu ishirini na tatu wote wametoweka katika mazingira ya kutatanisha, kama sio kifo basi ni kuacha kazi ghafla na kupotea kabisa, huku tukikosa kumbu kumbu muhimu zote za watu wale” alieleza Sixmund, na hapo mfalme akamtazama mke wake, ambae pia alikuwa anamtazama kwa mshtuko na mshangao, “Habari njema ni kwamba kati ya wawili walio salia, ambao Habari zao zimeatikana ni Waziri Chitopela ambae katika mpango wetu, tumepanga kutomuhoji chochote, maana yeye ndie aliekuwa kiongozi wa zoezi lile, hatuna uhakika kama mahojiano yetu na yeye hayatoleta madhara katika taifa letu” alisema Sixmund.
Na hapo Elvis akadakia, “na huyo mwingine ni nani na yupo wapi?” aliuliza Elvis aliekuwa na shauku kuu, “huyo mwingine ni sajent taji Ashraff Kibwana wa MLA, na baadae MLSA, ambae alitoweka miezi michache baada tu ya kumalizika kwa operation ile ya kuondoa waasi, na ameanza kuonekana miaka michache iliyopita huku magharibi katika nje ya kitongoji cha Komwe, anaishi kama mkulima muhamiaji masikini” alieleza Sixmund, ambae pia alieleza kuwa tayari wamesha tuma askari kwaajili ya kwenda kufanya nae mahojiano, “tunaamini kuwa huyo atakupatia majibu sahihi tunayo yahitaji” aliitimisha Sixmund, na hapo Elvis akamtazama mke wake kama vile anawazo fulani lenye mashaka akilini mwake, ni sawa na mke wake ambae pia alikuwa anamtazama kama yeye, “ok! katika hali yoyote, Ashraff apatikane, mimi nipo njiani, nieleze nikukute wapi nataka kusikia mahojiano kwa masikio yangu” alisema Elvis wakati huo yeye na mke wake walikuwa wameshainuka toka kitandani na kuelekea kwenye kabati la nguo za kawaida ambazo mara nyingi huzitumia katika matembezi yao binafsi na ya siri.
Kitu cha kujua msomaji ni kwamba kuna wakati ambao Elvis na Vaselisa, huwa wanakuwa na tamaa ya kufanya matembezi wakiwa kama raia wa kawaida, hivyo huvaa kikawaida na kuingia kwenye gari kisha kuondoka zao kuelekea mitaani hasa nyakati za usiku, ambako utembea sehemu mbali ikiwemo kwenye viunga ya bustani za TT City, ambako hupenda kutumia sehemu zile kufanyia utani wa kimapenzi na michezo ya wapenda nao, vitu ambavyo walivifanya sana wakiwa Tanzania miaka michache iliyopita. *******
Yaaap! Kilomita zaidi ya nane toka njia panda ya kisarawe na kibaha, magharibi mwa kisarawe ndani ya msitu wa Kazi Msumbwi katika machimbo ya kokoto laini na mchanga, bado wakina Kadumya wanaonekana wakiwa wamesimama na magari yao mawili wanasubiria wenzao ambao tayari walikuwa wamesha karibia.
Muda wote bwana Kafulu, ambae siku za nyuma alikuwa anajiita JJD, alikuwa anawaza kuhusu kitu kilicho mtokea kule makabe na kuona kama alidhalilishwa vibaya sana, hasa akikumbuka jinsi ambavyo alionyesha umwamba mbele ya Veronica na kijana Deus, ambae dakika chache baadae akamchapa kama mtoto na kuondoka na Veronica akiwa amechukua fedha ambazo zingesaidia katika mpango wa mapinduzi, “mshenzi sana huyu, hakutaka kuniachia nifungue kitumbua toka kwenye box mimi mwenyewe, aliwaza Kafulu ambae baada ya kuwaza kwa muda akapata wazo, “mkuu mimi na wazo ambalo litatusaidia kumpata yule Dereva na Veronica pamoja na fedha zetu” alisema Kafulu, akimueleza Kadumya aliekuwa amesimama pembeni yake wote wanavuta bangi, “mpango gani huo Kafulu?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya tabu kidogo kutokana na kuubana moshi wa bangi mdomoni na puani.
Hapo Enock Kafulu akaanza kueleza mpango wake ambao ulikuwa ni kujifanya wateja wapya na kumpigia simu Deus, wakimueleza sehemu ya kuchukuwa abiria au mzigo, “ili akiingia hapo, tayari askari wetu watakuwa wanamsubiri kuwaweka chini ya ulinzi” alieleza Kafulu na hapo likaonekana tabasamu usoni kwa Kadumya, “upo sawa kabisa Enock, tena safari hii ni vyema kama tukitumia simu yako” aliunga mkono Kadumya ********
Naaaam, Songea mkoani Ruvuma, giza lilikuwa limetanda kweli kweli, mji ulikuwa kimya kabisa, ni wazi watu walikuwa wamelala mida hii ya usiku mkubwa, lakini basi nyumbani kwa mzee Frank Nyati iliyopo mtaa wa Making’inda, bado tunamuona mzee huyu akiwa ametulia sebuleni na simu yake sikioni, ni wazi alikuwa anampigia mtu fulani ambae hakuwa na mpango wa kupokea simu hiyo, “kwanini huyu mpuuzi hapokei simu, lazima ajue kuwa MLA wapo dar kuwa saidia na kwamba kila anachokifanya ni kwaajili ya nchi yake ya asili nchi ya baba yake nchi ya babu zake” alijisemea mzee Frank, ambae mpaka sasa alikuwa ameshapiga simu zaidi ya mara kumi bila kupokelewa.
Hali hiyo pia ilikuwa huko kinyerezi dar es salaam, katika nyumba ya bwana James, mtaa ulikuwa kimya kabisa, japo baadhi ya nyumba za jirani na nyumba ya bwana James, walionekana watu wakiwa wanachungulia katika madirisha yao, lakini ni katika hali ya umbea tu kuona kitu kinachoendelea kwa wale askari wa jeshi la ulinzi walio zunguka uzio wa jengo la bwana James.
Lakini upande wa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa imepewa ulinzi mkali sana, sasa tuna waona watu ishirini, yani askari kumi na sita wa MLA, askari wa jeshi la Tanzania na bwana James wakiwa na familia yake, bwana James akiwa anapiga simu ya binti yake ambayo iliita muda mrefu bila kupokelewa, kitu ambacho kilikuwa kinampatia wasi wasi mkubwa juu ya usalama wa binti yake, “isijekuwa yule kijana ameshapatana na wale washenzi awapatie Veronica kwa malipo, aliwaza mzee James huku anawatazama watu wengine mle ndani.
Askari walikuwa busy na mipango yao, mke wake alikuwa na binti yao Caroline wamekaa kwenye kochi moja wanasinzia kutokana na kulemewa na usingizi, “lazima nifanye jambo kabla mambo hayajawa mabaya zaid na binti yangu kufikishwa kwenye mikono ya UMD” aliwaza mzee James huku anainuka toka kwenye kochi na kuelekea chumbani akiwa na simu yake mkononi. *******
Naaaam! Sasa turudi Visegese, sasa tuyaona magari yale Matano ya polisi, manne yakiwa ni magari ya viongozi wakuu wa jeshi hilo ngazi ya mkoa, yaliyokuwa yanakatiza eneo lenye kibarabara hafifu kilicho tokomea upande wa kulia wa barabara na gari la nne katika msafara ndani yake yupo bwana Ulenje, ambae anaonekana akibofya bofya simu yake kwa namna ya kuingia kwenye sehemu ya miito iliyopita, anaonekana kukwama kwenye namba zilizo ambatana na jina la Cheleji, na bwana Ulenje anaipiga namba ile ambayo inaita kwa muda mfupi kisha inapokelewa, “ndiyo afande” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, “sikia Cheleji, kuna kazi ya kufanya” alisema Ulenje, na kuanza kutoa maagizo kwa askari wake huyu anaemuamini kuliko wote.
Wakati huo sisi tunaachana na magari yale, tunaelekea upande kulia wa barabara, tuna fuata ile barabara ndogo ambayo mbele tuna wapita wakina Songoro waliokuwa wamesimama sehemu wakipata mapumziko ya kuvuta sigara bwege, huku Songoro mwenyewe akinywa pombe yake, kila mmoja wao akiwa na silaha yake mkononi, maongezi yao yalikuwa ni namna watakavyo muadhibu Dereva wa BMW na kummalizia kwa kifo chenye maumivu makali, “dogo anabahati sana, yani tunge mnasa pale hotelini angejisahau hata yeye mwenyewe kwa kitu ambacho tungemfanyia” aliongea Side kwa namna ambayo ungesema anazungumzia kukamata kuku wa kisasa, hakika wangejua nadhani wangeachana na mpango wao na kufuata maelezo ya Ulenje.
Tunaachana na wakina Songoro, tunasogea mbele zaidi umbali kama wa mita mia mbili, ambapo pana nyumba ya chakavu yenye kuzungukwa na mashamba madogo ya mboga mboga yaliyostawisha mboga mboga vizuri kabisa, tunaingia ndani ya nyumba hii moja kwa moja chini kabisa eneo la sebuleni hakuna mtu yoyote, tunaelekea chumbani kwa Deus ambako safari hii kabla hatujaingia ndani, mara mlango unafunguliwa na wanatokea wapenda nao wawili, waliokutana kwa mara ya kwanza na kuzindua penzi lao katika siku hii ya kwanza, safari hii tunamuona Deus alievalia bukta pekee bila tishert akiwa amembeba kifuani mwanadada mrembo Veronica alievalia truck suti na tishert nyingine, sura zao zikiwa zimetawaliwa na matabasamu ya furaha, macho yao yanatazama kwenye simu ambazo zilikuwa zimetulia, nao wanaishia kwenye makochi, Deus anamlaza Veronica kwenye kochi kubwa na yeye anakaa pembeni, lakini Veronica anajiinua kidogo na kujilaza kwenye mapaja ya Deus.
Naaam ile wanaanza kumiminiana wine kwenye grass mara simu ya Deus inaanza kuita, safari hii sio ile simu yake binafsi, ni simu ya kazi, Deus anaitazama akijaribu kuangalia kama ni mteja anaemfahamu au mpya, anaona kuwa ni mteja mpya, Deus anaichukuwa simu kwa tahadhari kubwa huku anajiuliza isije kuwa ni wakina Kadumya wameamua kutumia namba ngeni ili wajaribu kupanga mipango yao fake kwaajili ya kumnasa awapatie Veronica na Fedha, na pengine kumuangamiza kwasababu amesha jua wao ni wakina nani.
Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji, lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA MDAU, COMMENT LIKE VINAMPA HAMASA MTUNZI YA KULETA HUU MKASA KWAN NDIO ATAJUA KUWA KUNA WATU WANAFUATILIA...
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA TISA:- Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wapili wa simu, na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo, Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA…
Kijana ambae sio tu kwa kuwa amemsaidia kutoka mikononi mwa watu ambao walipanga kumfanyia kitu kibaya, ila pia ni mtu ambae amekuwa Rafiki yake kwa muda mrefu japo hawakuwahi kukutana mwanzo, na leo ikiwa siku yao ya kwanza kukutana amejikuta amezama kwenye penzi lake pasipo kujari tabia yake ya kuuwa bila kujiuliza mara mbili, “hoooo! Samahani kijana nilisahau, lakini nakuahidi sitovunja sheria hata moja” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima, “ok! nafasi ya mwisho, ongea mpango bila kuvunja sheria” Veronica alimsikia Deus akiongea kwa sauti ile ile tulivu, japo hakujua anaongea na nani, ila kiukweli alijua anaongea na mteja wake maana tayari alisha sikia mambo ya sheria.
“kijana sijui nisemeje maana siwezi kujitambulisha kama ilivyo sheria yako namba moja, ila ninahitaji uniletee binti yangu kwa kiasi chochote unachohitaji” ilisikika ile sauti ya mtu mzima yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu ni wazi hakutaka watu wengine wamsikie, “sehemu ya kumchukuwa na sehemu ya kumpeleka?” aliuliza Deus Frank Nyati, mwenye jina la utani, msafirishaji au mchoraji, “sehemu ya kumchukua ni pale ulipompeleka na sehemu ya kumleta ni kinyerezi mwisho nyumbani kwangu, hapo Deus akajua kuwa anaongea na bwana James Kelvin, akamtazama Veronica ambae alikuwa amelala pajani mwake huku macho ameyaelekeza kwake, macho yao yalipokutana, Veronica akajitabasamulisha na Deus nae akatabasamu, “mpango umekataliwa, nitakua navunja sheria namba 4” alisema Deus, kwa sauti ile ile kama hataki vile, kisha akataka kukata simu, lakini kabla hajakata simu mzee James akawahi, “subiri kijana, kuna mpango gani mwingine juu ya binti yangu?” aliuliza mzee James kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa alikuwa amesha changanyikiwa kusikia vile, maana Sheria namba nne inasema hakuna mpango juu ya mpango.
Ukweli ni kwamba, ilikuwa ni vigumu kwa Deus, kuingia mpango wa biashara juu ya Veronica ambae ukiachilia kuwa katika hatari ya kuvamiwa na kushambuliwa muda wowote huku baba yake akikosa msaada wa kumlinda, na pia alishapanga kuwa asingefanya kazi ile tena, na ili apate nafasi ya kuishi kama mtu wa kawaida, maana kamafedha tayari alikuwa nayo, lakini kubwa zaidi ni kwamba, mschana huyu kwa sasa ni mpenzi wake na wameshaingia katika makubaliano ya kuchumbiana.
Deus akamtazama tena Veronica, ambae bado alikuwa anamtazama kama vile aamini kama mtu alie kuwa ana wasiliana nae kila siku ndie huyu mbele yake, na kwamba anaenda kuwa mpenzi wake wa siku zote, hakufikiria kuhusu kile anachoongea kwenye simu ya kwamba kina muhusu yeye, “tayari huyo yupo kwenye mpango uliotangulia, siwezi kubadiri mpango wa mwanzo” alisema Deus, kwa sauti ile ile, ambayo kama unafahamu matendo yake ungesema ile sauti ni ya kuigiza, na siyo sauti yake halisi, lakini ukimtazama usoni, ungejua kuwa Deus anaupole ni waasili.
Maneno yale ni kama yalimshtua zaidi mzee James, ambae ni wazi alihisi kuwa tayari binti yake alikuwa katika mpango wa kupelekwa kwa wakina Kadumya kama alivyo hisi mwanzo, “nakuomba kijana, nipo tayari kukulipa mara tano zaidi ya malipo uliyoaidiana na hao washenzi” ni Deus pekee ndie aliekuwa anasikia sauti ya mzee James aliekuwa analalamika, “mzee nimesema siwezi kuingiza mpango juu ya mpango mwingine, huwa nasimamia sheria zangu” Veronica alimsikia mpenzi wake huyu akiongea kwa sauti ya upole kama vile hakumaanisha alichokisema, “jamani mchoraji wangu si umkubalie tu, mbona kama mteja wako anakuomba sana” alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyojaa mahaba makubwa, Deus anamtazama huku anatabasamu nakukata simu.
Lakini ile anakata simu na wakati huo, simu hiyo hiyo ikaanza kuita tena, “bado hujamalizana na mteja wako, huyooo anapiga tena” alisema Veronica huku anaachia tabasamu la kivivu, kama unge waona wawili hawa basi ungejua kuwa bado muda ilikuwa ni mapema sana.
Deus akaitazama namba ya mpigaji wake, ambae mwanzo alijua kuwa ni mzee James, yani baba wa binti huyu, lakini alipotazama ile namba haikuwa na mfanano wowote na ile namba ya mwanzo, akaipokea na kuiweka sikioni. Na wakati huo huo ikasikika simu ya Veronica nayo inaanza kuita, Veronica anaitazama anaona kuwa ni baba yake ndie aliekuwaa anapiga, Veronica akamtazama Deus, kama vile anamuomba apokee simu, nae akamuonyesha ishara ya kwamba apokee, wakati huo nayeye simu ilikuwa sikioni na macho kwenye kioo cha TV kubwa kwenye kona ya kulia ya sebule, ambapo kijana wetu aliweza kuona kipande cha camera na mbili, kukiwa na watu kumi waliosimama nje ya magari yao, mawili huku bunduki zao zikiwa mikononi. ********** Naam huko #Mbogo_land, ndani ya mtaa tulivu unaonakaliwa na viongozi wenye hadhi ya kipekee, kama vile wajumbe wa kamati za serikali, mawaziri na wazee wa mabaraza mbali mbali, ulikuwa kimya kabisa, kama ulivyokuwa mji mzima wa Treach Town, moja kati ya majiji ya kifahari duniani, ikiwa namba mbili kwa starehe kutoka kwa jiji la paris, na jiji la kwanza kwa usafi na utajiri duniani.
Nalo lilikuwa kimya kabisa, maana tayari watu walikuwa wameshalala, hata kama ulilala masaa kumi na mbili ya mchana, lakini ifikapo saa nane za usiku, lazima utapatwa na japo kalepe ka usingizi, labda kama ukiwa na kazi ya kufanya au mafunzo maalumu ya kuvumilia uchovu wa usingizi, japo mida hiyo lazima utahisi kitu fulani mwilini mwako, japo inakuwa tofauti kwa mtu aliepo bar.
Nyumbani kwa Waziri Chitopela, mambo yalikuwa tofauti kidogo, yeye licha ya kuhisi usingizi mkali, lakini bado alijitahidi kunywa pombe yake na kuendelea na mipango yake ya kimapinduzi, huku anasuka properganda moja kubwa, ambayo ingeshtua nchi nzima ya #mbogo_land, lengo ni kutoa nafasi kwa majeshi yake yafanikishe lengo.
Naam sasa bwana Chitopela, anaonekana akimaliza kuandika kitu fulani kwenye computer mpakato yake na kutuma kwa mtu fulani, kisha akachukua simu yake na kuipiga, simu haikuita sana ikapokelewa, “afadhari Chilopo umetambua kuwa leo sio siku ya kulala” alisema Kadumya mara baada ya simu kupokelewa, “siwezi kulala mkuu wakati najua siku za mapinduzi zinakaribia” alisikika Chilopo kwa sauti yenye kuelemewa na uzito wa usingizi, “ok! changamka tufyetue mabomu mawili mazito, tayari nimesha kuwekea kwenye email yako” alisema Chitopelah na Chilopo akakubaliana nae, “bila shaka mkuu, inatekelezwa sasa hivi” alisema Cholipo, sambamba na sauti ya kuliza kwa kitanda, ikionyesha wazi kuwa Chilopo alikuwa ananyanyuka toka kitandani, “ok! nakutakia mafanikio bwana Chilopo, Waziri wa Habari ajae” alisema Chitopela kabla ya kukata simu.
Ile anakata simu, bwana Chitopela, kabla hajaweka simu mezani akaisikia ikitekenye mkono wake, kwa mtetemo wa muito, akaitazama kuona mpigaji, nae alikuwa ni Kobwe, mkuu wa kombania A, ya batallion ya UMD, akaipokea maea moja, “niambie Kobwe, natarajia kusikia habari njema” alisema Chitopelah, kwa shauku, ndio mkuu habari njema ni kwamba sasa ndio tunaingia sehemu ya makutano na wakina Kadumya” ilisikika sauti toka upande wa pili, hapo Kadumya akatazama saa yake, ilikuwa inasoma saa nane, “mwendo mzuri bwana Kobwe, nasubiri taarifa zaidi za kazi” alisema Chitopela, kabla ya kukata simu.*********
Naaam, wakati huo huo, magaharibi mwa TT City, barabara ya kutokea Komwe, katika mashamba yaliyopo pembezoni mwa mto Bhumbu za Kwala, magari manne ya kijeshi yalionekana yakitembea kwa kasi ya nguvu, Askari mtoro wa MLA staff sajent Ashlaff Kibwana akiwa mwenye hofu kubwa na pasipo kuamini kile kinacho mtokea, alikuwa amekaa ndani ya gari zuri la kijeshi, lenye muonekano wa gari la ki VIP, pembeni askari wawili wenye bunduki zao, aina ya Uzi, pia nyuma kabisa walikuwa askari wawili wenye bunduki kama hizo, na seat ya mbele ya abiria pia kulikuwa na askari mwenye bunduki, hakika licha ya MLA kumueleza mzee Ashlaff, kuwa hawakuwa na lengo baya kwake na kwa familia yake, ambao walikuwa kwenye gari la nyuma yake, lakini ulinzi na ujio wa askari hawa wajeshi ambalo hapo mwanzo aliwahi kulitumikia.
Dakika ishirin baadae, tayari magari yale yalikuwa yamesha ingia mjini, nae bwana Ashlaff akitazama mitaa ya jiji lile ambalo kwa miaka mingi hakuwa na uwezo wa kutembea akiwa huru, safari inaenda moja kwa moja mpaka Mtaa wa Sizwe, ni mmoja kati ya mitaa tulivu katika jiji la Trench Town na wenye sifa ya kukaliwa na viongozi wakubwa wa ulinzi na usalama.
Moja kwa moja magari yanaenda kusimama mbele ya lango kubwa la chuma lililoshikizwa kwenye kuta kubwa na imara, ukuta licha ya kuwa mrefu na wenye ulinzi wa umeme, lakini pia kulikuwa na askari kadhaa MLA, waliokuwa wamesimama nje ya lango lile na bunduki zao mikononi.
Lango linafunguliwa na magari yote yanaingia ndani, ambako pia wanakutana na magari mengine ya kifahari zaidi kasoro gari moja dogo ania ya Toyota caldina, huku wakionekana askari kadhaa wenye bunduki wakiwa wamesimama imara wakitazama pande zote za ukuta ule pasipo kuhangaika na magari yale yaliyokuwa yanaingia.
Mzee Ashlaf ambae hakuwa na pingu wala kibanio cha Kamba, licha ya kuwa alihakikishiwa usalama wake, lakini bado alionekana kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake na familia yake, mzee huyu anaona magari yana simama, askari wanashuka mara moja, “mzee kumbuka upo na familia yako, hatutaki kuipa wasi wasi na mashaka yoyote familia yako, hivyo utafuata kile tunacho kueleza bila kujaribu kufanya ujanja wowote” alisema askari aliekuwa amekaa seat ya mbele ya gari lile alilopanda Ashlaf, ambae kwenye kosi za shati lake jeusi la sare za uvamizi wa usiku, ungeona nyota mbili kila upande, ikimtambulisha kuwa ni mwenye cheo cha luten.
Hapo bwana Ashlaf anatazama kwenye gari la nyuma na kuwaona mke wake na Watoto wake wakiwa wanashuka toka kwenye gari na kusimama pembeni ya gari lile, huku wakionekana kushangaa, kwa maana ya kutokujua kinachoendelea, ila nyuso zao zilionyesha kuwa na uoga kwa kiasi kikubwa, “bila shaka, afande, lakini naomba msiushishe familia yangu kama mlivyofanya kwa wengine” alisema Ashraff ambae alionekana kutokuwa na imani na wana MLA hawa, “ondoa shaka na ushuke kwenye gari” alisema yule luteni wa MLA kwa sauti ya chini, ni wazi hakutaka mke na watoto wawili wa bwana Ashraf wasikie maongezi yao.
Naaam bwana Asraff ana shuka toka kwenye gari, na wakati huo huo anamuona askari mmoja wa kike akija mbele ya mke wake na Watoto wake na kuwaongoza kuelekea ndani ya jengo lile, na wakati huo huo wakati wao wanaingia ndani, wanapishana na kanali Jastin, “safari itaishia hapa, hatuendi LS Base, mpelekeni kwenye chumba cha mahojiano” alisema kanali Jastin Johnson, kisha akarudi ndani ya jengo lile la kifahari, usingefikilia kuwa ni jengo linalomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hii ya kifalme.******
Naaaam! Sasa turudi njia panda ya kisarawe, ambapo tuna wakuta askari wa jeshi polisi, PT yani Polisi Tanzania, wakiwa bado wamekaa kwa vikundi, huku wengine wakiwa wametafuta sehemu za kujiegesha na wengine wakianza kusinzia kabisa kutokana na muegesho ule.
Tofauti na kundi dogo la askari kumi na tano, ndani ya jeshi hili linalo aminiwa na serikali, walio kuwa wamesimama pembeni kabisa katika vikundi vidogo vidogo wakiendelea kuwasha mienge ya sigara na bangi, na ndio wakati ambao koplo wa polisi Cheleji, aliekuwa na koplo Othman alikuwa anamaliza kuongea na simu, “kaka kimeumana” alisema Cheleji, huku anaweka simu mfukoni na kutoa mkebe wa risasi kwenye bunduki yake, akaitazama kama ina risasi, akagundua kuwa ilikuwa nazo lakini chache, nadhani alizitumia kuwashambulia wakina Deus kule barabara ya malamba mawili, “vipi mkuu anasemaje?” aliuliza Othman, kwa sauti yenye shauku, huku anamtazama Cheleji aliekuwa anaweka ule mkebe wa risasi kwenye kifuko kilichopo kiunoni mwake na kutoa mkebe mwingine uliosheheni risasi, “kuna kazi relini inabidi ikafanyike” alisema Cheleji, huku anaupachika mkebe wa risasi kwenye bunduki yake.
Wakati wanaongea hayo, wakati huo huo, wakayaona magari yanaingia pale njia panda, yakitokea upande wa kibaha, hakuna alieuliza ni magari ya nani, tayari walishajua ujio wa wakuu wao, hivyo haraka sana wakajikusanya mbele ya magari yale kwaajili ya kusikiliza amri za matarajio.
Dakika mbili baadae tayari viongozi walio tangulia na askari pale njia panda, walikuwa wameshaanza kutoa taarifa za mwanzo kwa mkuu wa polisi kanda ya dar es salaam, “afande mpaka sasa uelekeo wa waharifu ni kazimzumbwi, hatuna uhakika kama huku walikoelekea ndiko kwenye makazi yao au wamekimbilia kwasababu ya kujificha kwa muda” alisema yule Assistant inspector, “vipi kuhusu yule mualifu Deus Nyati, yule Dereva mwenye gari jeusi, kuna taarifa zozote za kufahamu sehemu alipo kwa sasa?” aliuliza CP Nyambibo, huku Ulenje na wenzake wakiwa wanasikiliza taarifa zile, “afande zaidi ya taarifa za kuonekana barabara ya maramba mawili hakuna taarifa nyingine ya kuonekana kwake” alisema yule inspector.
Hapo Kamanda Nyambibo akawatazama wenzake, yani makamanda wa polisi mikoa, “mnashaurije sasa?” aliuliza Nyambogo, akiwazama kwa zamu, “afande nashauri tusi jiziuke na hawa wenye magari peke yao, muhimu zaidi ni yule dereva wa gari jeusi” alisema kamanda Ulenje, lakini Nyambibo akaonekana kutokukubaliana na wazo hilo, “ujue Ulenje mpaka sasa Deus Nyati hajawa hatari kama walivyo hao jamaa, kwasababu mpaka sasa wamesha uwa polisi, lakin Deus amekuwa akitukikimbia tu” alisema CP Nyambibo na Ulenje akaona ndio nafasi ya kutoa ushauri, ambao utawapotosha wenzake na kuwaokoa wakina Kadumya, hivyo haraka sana akadakia, “naitakuwaje kama Deus Nyati ni mshiraka wa hao wengine, huoni kama tukimpata yeye itatusaidia kuwapata hao wengine?” alisema Ulenje.
Hapo Ulenje akamuona CP Nyambibo akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo na mshangao, nao wakaonekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile, ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa
jamii forums