Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

huyu Chitopella atakuwa ni Mmaviya mwenzangu kabisa.
Yaani ni uhakika kabisa
 
Kwamba "Kamanda" ni mzembe kiasi Cha kutekwa na kundi la Sangolo!!!
Basi UMD ninaenda kumteka Carolina🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃😂🤣😂😂😂😂🤣😂
Wahi ukamfariji maana dr kashachojolewa kule hadi baba simu azipokelewi 😀😀😀
 
Ngoja tuvute subira, pengine weekend hii tukaimaliza simulizi yote,,
 
General Kadunya,eti umejuaje kama tupo huku!.

Ogopa sana,kupambana na mtu mwenye mahesabu.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA SABA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA SITA:- Turudi nyumbani kwa Deus, ambako sasa pale sebuleni hatuoni mtu zaidi ya nguo zilizo zagaa pale chini, nguo ambazo muda uliopita zilikuwa zime valiwa na Deus mwenyewe na mwanadada Veronica, hebu twendeni chumbani kwa Deus, labda walihamia huko, tunapiga hatua za taratibu kukifuata chumba cha Deus, ambacho kwa bahati kipo wazi, tunapoingia ndani ya chumba nako hakuna mtu, lakini wakati tuna jiuliza wapo wapi, ……. ENDELEA…

Mara tuna sikia sauti ya maji toka bafuni yakimwagika toka kwenye bomba la juu sambamba na sauti za watu wakiongea kwa sauti za kubembelezana, “ona damu, yani tumefanya siku ya kwanza tu kukutana” ilisikika sauti ya kulalamika ya kike, nayo ni sauti ya doctor Veronica alieongea kwa deka kama vile alikuwa analia, “pole Vero, sikujua kama utaumia” ilisikika sauti ya kiume yenye utulivu unaofaa kubembelezea, “lakini si ungefanya juu juu, sasa wewe umefanya kabisa ona sasa” ililalamika sauti ya kike ambayo tunaijua kabisa kuwa niya yule mwanamke mrembo Veronica, huku maji yakiendelea kumwagika, “pole Vero, lakini haiwezi kuuma tena” alisema Deus, kwa sauti yenye mbembelezo wa mtoto mchanga, hatuwezi kuwachungulia, maana niwazi walikuwa wanaogeshana, “hata kama lakini, ndio unifanye kabisa” alisema Veronica kwa kulalamika na kudeka kweli kweli, “samahani lakini nilijua unafurahia, ndio maana ukaniambia nikufanye” ilikuwa ni sauti ya Deus Nyati yenye kubembeleza kweli kweli, “kwani we hukujua nilisema vile kwasababu nilizidiwa na utamu?” aliuliza Veronica kwa sauti yake ile ile yenye ukudeka na kulalamika.

Hapo ikasikika sauti ya kicheko cha mguno kinacho zuiliwa toka kwa Deus, “lakini wewe si unajijua ulivyo mzuri, ningewezaje kujizuia?” aliuliza Deus kwa sauti ile ile ya mwanzo yenye kubembeleza, “hata kama siungejizuia, halafu ungenikataza na mimi” alisema Veronica huku safari hii ikiwa ni zamu yake kujizuia kucheka, hapo kikafata kicheko kidogo cha kivivu toka kwa Deus, “ni ngumu sana kufanya hivyo, nilikosa ujasiri huo” alisema Deus, huku maji yakiendelea kumwagika mule ndani., “hai! mchoraji bwana, usiniguse huko unanitekenya, nitajisafisha mwenyewe, au unataka nizidiwe halafu unifanye tena” ilikuwa sauti ya Doctor Veronica James, yenye mshtuko wa mtekenyo,, iliyo ambatana na kicheko cha kivivu, “utaki kupata raha tena?” ilikuwa sauti tulivu yenye kujaa utani ya Deus Nyati.

Niwazi sasa walikuwa katika mahaba mazito, “hiiii ebu ona jamani, yani inaanza tena kutamani, kwahiyo nikupa tena utanifanya?” aliuliza Veronica, ambae niwazi kuna kitu alikuwa anakiona mbele yake huko ndani ya bafu, “sidhani kama nitaweza kupata ujasiri wa kukataa” alijibu Deus na wote wakacheka, “lakini wewe ni jasiri sana, unaweza kujizuia, sema unajiendekeza tu” alisema Veronica kwa sauti fulani ya mfano wa mtu anae sisimulia wa na kitu fulani, “nikuambie kitu Vero, wewe ungekuwa ni silaha, basi ndiyo pekee ambayo ingeweza kuniuwa kirahisi” alisema Deus kwa sauti tulivu, huku maji yanaendelea kumwagika, “kwanini?” iliuliza sauti ya Veronica yenye kutetemeka kwa msisimko, “yani kwangu, wewe ni rahisi kupambana na Platoon ya askari wa miguu bila bunduki kuliko kujizuia kupambana na hisia zangu juu yako” alisema Deus, na kikasikika kicheko cha kivivu, toka kwenye midomo ya Veronica alieonyesha kuwa alikuwa katika msisimko mkubwa, “jamani Deus, kwahiyo unanipenda sana?” aliuliza Vronica kwa sauti ile ile yenye kusisimka, “nakupenda zaidi ya sana unayoitaja” ilijibu sauti ya Deus, yenye utulivu mkubwa.

Sasa unafuata ukimya mfupi, ukifwatiwa na mguno wa msisimko, “unaona sa..a..sa, naanza kutamani tena, wakati bado sijapona” alisikika Veronica, kwa sauti yenye msisimko mkubwa, “hoooo pole Pacha, nilikuwa na kusafisha tu” alisema Deus, na Veronica akadakia, “hapana usiache kwanza bwana, mwenzio nasikia raha” lisikika sauti ya Veronica, ambayo iliyo onyesha wazi kuwa, anahitaji kitu fulani, “ukizidiwa je, si utaniambia tena nikufanye?” aliuliza Deus, kwa sauti ile ile nzito na tulivu, “ndiyo, kwani dhambi wewe si umesema utanioa” alisema Veronica kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa anaendelea kufanyiwa kile alichokuwa anafanyiwa mwanzo, huku sauti ya kulala mika ikoma na kubakia sauti ya kusikilizia utamu.

Kinapita kimya cha dakika nzima, tunasikia sauti mihemo mizito na miguno ya utamu, hapo nakosa la kufanya zaidi ya kuwapisha wawili hawa waendelee kufanya wanachokifanya, taratibu natoka mle chumbani narudi sebuleni ambako nakuta simu zote mbili zinaita, yani simu ya Deus Nyati ile binafsi na jina la mpigaji linaonekana ni baba, na simu ya Veronica, ambayo pia jina la mpigaji ni baba, hakuna cha kufanya, vyema kwenda kuangazia sehemu nyingine, lakini kabla sijaondoka namsikia Veronica akiomba kitu kwa Deus, “mwenzio nataka tena, lakini fanya taratibu nisiumie” ilikuwa ni sauti iliyozidiwa na utamu, “una uhakika Vero?” iliuliza Sauti nzito na tulivu ya Deus, “sina lakufanya Deus, wewe ndiyo mwenye mali, fanya tu” alisema Veronica, ikionyesha wazi kuwa dakika chache zijazo wanaingia kwenye milindimo, hebu tuwapishe tena.********

Naaam saa saba na nusu za usiku, kuanzia jeshi la polisi la nchini Tanzania, TSA, na Jeshi la ulinzi, wote walikuwa katika msako wa kundi la UMD, na kijana Deus Nyati, ambae mpaka sasa waliamini anamshikilia mwanadada Veronica, alieshiriki wizi wa mabilioni ya fedha katika benk ya uhifadhi ya mali za wananchi, wakati maafisa na wapiganaji wakiwa porini huko misegese, huku viongozi wa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama walikuwa maofisini wakitafiti na kupokea taarifa za matukio muhimu ya kile kinacho endelea katika msako na Maisha binafsi ya watuhumiwa.

Upande wa pili yani nchini Mbogo land, MLA na MLSA, wote walikuwa kazini, japo kwa #mbogo_land, ilikuwa operation ya siri, ambayo iliongozwa na kikundi teule toka MLA ARU, yani Amoured Recce Unity, toka LS Base, yani Lion Skull Base, nao walikuwa katika pilika za uchunguzi wa kujua nani ni mratibu na mfadhiri halisi wa UMD ndani ya serikali ya mfalme King Elvis, japo mpaka sasa mapigano makubwa yalikuwa nchini Tanzania, na mbaya zaidi UMD walionekana kujikita tanzania mapema sana, kuliko kwao, na kitu ambacho mfalme Elvis, alikuwa anakifikiria sana kwa wakati huu ni kwamba, watu ambao wameonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao ni wale ambao, miaka iliyopita walionekana kuwa ni waasi, watu ambao walikimbia kifo nchi kwao, yani bwana James Kelvin na kanali wa zamani wa MLA Frank Nyati, walioonyesha ushirikiano mkubwa sana kupingana na UMD.

Tuanze magharibi mwa Kisarawe, njia panda ya kibaha na maneromango, ambapo tunayaona magari mengi sana ya polisi yakiwa yamesimama, huku polisi wakiwa katika mikao ya kuzagaa katika eneo lile la njia panda, wapo waliosimama kwa vikundi vikundi, wapo walio kuwa katika kikundi kutoka na urafiki, wapo walijikusanya kimajukumu, kwa maana ya kulinga kwa vyeo na madaraka, waliokuwa wakijadiriana, juu ya taarifa muhumi na mpango wa kazi, ili watakapo fika viongozi wao wangazi za juu waweze kuwapa taarifa nzuri ambazo zingeweza kutoa mwanzo mzuri wa msako na mapambano dhidi ya hao watu wenye magari mawili aina ya Land rover Puma walioshambulia wenzao na kusababisha vifo na majeruhi.

Wapo waliojikusanya kwaajili ya utumiaji wa sigara na vitu vingine kama hivyo, pia wapo waliojikusanya kwaajili ya maongezi na kusimuliana kila mmoja aliyo yapitia katika msako huo, ila pia kulikuwa na waliokuwa wamesimama kila mmoja peke yake akiongea au kuchati, ni wazi walikuwa wanawaeleza, familia zao au ndugu jamaa na marafiki juu ya ugumu wa kazi ya usiku ule.

Ukiachana na hao, pembeni kabisa walionekana koplo Cheleji na koplo Othman, wakijadiliana swala fulani kwa umakini mkubwa sana, “kama ni kweli hawa jamaa wapo huku, inatakiwa tufanye jambo ili kuwazuia hawa wasiende huko” alisema Cheleji kwa sauti ya chini, “lakini si umesikia kuwa mkuu anakuja, ngoja afike ili atupe muongozo” alishauri Othman, “ni sawa, ila yeye alikuwa ameshanieleza kuwa tukiona tunawakaribia tufanye tukio la kuwasubirisha hawa wenzetu ili wakina Kadumya wapate nafasi ya kusogea mbele zaidi” alisema Cheleji, wakati huo askari waliokuwa nao kwenye magari yao wakiwa wamesimama pembeni kidogo, nao kwa vikundi huku wengi kati yao wakiwa ni wavutaji wa sigara, walikuwa wanaongea ili na lile juu ya msako ule ambao unaweza kuwa msako mgumu kuwahi kuushuhudia toka wameingia jeshi.

Wakati hayo yanaendelea njia panda ya Maneromango, wakati huo huo kilomita saba mbele, magari mawili aina ya Land Rover puma yalikuwa yanazidi kuchanja mbuga, kuelekea ndani zaidi ya msitu wa Kazi mzumbwi, huku mara kwa mara Kadumya aliekuwa seat ya mbele, akiwasiliana na captain Kobwe kujua wameshafikia wapi, maana kwa jinsi hali ilivyokuwa ni muhimu sana kwao kuungana nao, “tumesha ingia kwenye barabara uliyosema, na sasa tunavuka daraja la nne” alisema Kobwe ambae alionyesha wazi kuwa, walikuwa wamesha sogea kwa kiasi kikubwa, “ok! sisi tunatafuta sehemu ya kuwasubiria, maana mafuta tuliyonayo muda wowote yanakata” alisema Kadumya aliekuwa katika gari la mbele kabisa.

Na baada ya kukata simu, walitembea kama mita mia mbili, kisha wakachepuka upande wa kulia na ambako kulikuwa na barabara inayoende kwenye machimbo ya kifusi cha mchanga na kokoto laini, sehemu ambayo ilikuwa mita kama mia nne hivi, toka barabarani. ******

Naaam wakati mambo yanaendelea kuwa moto moto na kikundi cha UMD kombania A lililo ongozwa na kapten Kobwe likiwa lina karibia kuingia kituo cha makutano, assembly Area, huku bwana Chitopela akiwa nyumbani kwake na yeye anaendelea kupokea taarifa za majeshi yake ambayo yalikuwa safarini kuelekea dar es salaam kuongeza nguvu ya kumsaka kijana Deus Nyati aliekuwa na fedha walizo tegemea kuzitumia kulipia gharama za usafirishaji wa silaha, pia kumpata doctor Veronica mtoto wa James, ambae kupatikana kwake na kuuwawa, kungesaidia sana kuichonganisha serikali na wananchi, pia kuichafua serikali ya #mbogo_land kimataifa na kuifanya kazi yao kuwa nyepesi, napengine kuonekana kuwa wanacho kifanya kinastahili, “hivi huyu Sixmund ana inshu gani na mfalme?” alijuliza Chitopelah wakati anaendelea kunywa pombe na kuperuzi mtandaoni kuona matokeo ya habari za uzushi walizo zipost, “hapana huyu kuna kitu anakifanya, tena kinaweza kuwa namadhara kwangu na kwa mpango mzima, haiwezekani watume watu tanzania kwa siri kiasi kile bila hata kunijulisha” aliwaza Chitopelah huku anajaribu kufikiri kwa kina.

Naaam baada ya kufikiri kwa dakika kadhaa, huku akiuliza maswali kadhaa wa kadhaa, akapata jibu moja, “ni vyema nikifanya jambo ambalo litamchafua Sixmund, hata kama kuna jambo analifanya basi asitishe kila kitu huku akihangaika kujisafisha” aliwaza Chitopelah, huku anachukuwa simu yake na kubofya namba ya mfalme, namba ya simu binafsi namba ambayo hupigwa na watu wachache sana muhimu.*********

Naaaam, wakati huo huo major general, Sixmund, alikuwa sebuleni kwake akiwa tayari ameshatuma orodha ya wanausalama walioshiriki msako wa waasi ndani ya serikali kwa mkuu wa kambi ya fuvu la simba, huku na yeye akijaribu kutazama nakala hiyo aliyokuwa nayo kuona kama anaweza akaona majina ya watu wanaoweza kuwapata kwa haraka ili kuweza kufanya mahojiano nae, ilikupata dondoo za mtu alieshawishi kuuwawa kwa watu muhimu kiusalama nchi #Mbogo_Land, lakini kwa upande wake, katika orodha ile yenye watu ishirini na tano, wengi kati yao walikuwa wamesha acha kazi ya jeshi hawajulikani walipo, na wengine walikuwa wametoweka kwa namna ya kustaajibisha.

Katika watu ishirini na tano, hapakuwa na taarifa za kueleweka wala kusaidia katika kuzuia mapinduzi na kuangamiza kundi la UMD, yani kama siyo kuacha jeshi na kutoweka ghafla basi ni kufa kifo cha ghafla, mtu pekee aliekuwa anapatikana kirahisi, katika orodha hii ni mkuu wa operation hiyo alieandikwa kwa jina la kanali Dickson Chitopela, ambae baadae alipanda vyeo na mwishoni kuwa Waziri wa ulinzi, ikiwa ni matokeo ya sifa alizojizolea katika operation ya kuondoa waasi ndani ya serikali, “hii imekaaje, mbona kama kuna kitu ambacho serikali haikufahamu mapema” aliwaza Sixmund, na wakati huo huo simu yake ikaita.

Six akaitazama na kuona kuwa mpigaji alikuwa ni kanali Jastin Johnson, mkuu wa kambi la LSB Lion Skull Base, sixmund akaipokea mara moja, ndiyo Jastin, nipe Habari, “afande kazi haikuwa ndogo, ukweli ni kwamba, katika watu ishirini na tano katika orodha hii, ni mtu mmoja tu ambae mwanzo alionekana kuwa taarifa zake ndiyo zinapatikana kwa uwazi, nae ni mheshimiwa Chitopela, wengine wote kama siyo kuacha jeshi au kutoroka basi walitoweka au kufa katika namna za kutatanisha” alieleza kanali Jastin.

Japo Sixmund alishaliona hilo tokea mwanzo, lakini bado alikuwa na hamu ya kusikia zaidi toka kwa kanali Jastin, “lakini afande hatukuishia hapo, katika kuangalia angalia kwetu, tumegundua kuwa, huyo ambae ni namba kumi na tatu kwenye orodha” alisema Jastin na Sixmund akatupia amacho yake kwenye jina la kumi na tatu katika orodha, “huyu anaitwa staff sajent Ashraf Kibwana, yeye anapatika magharibi nje kabisa ya kitongoji cha komwe, kwa taarifa zilizopo ni kwamba, miaka kumi na saba iliyopita, alitoweka ghafla na kuja kuibuka tena kwa siri, miaka mitatu iliyopita, akiwa anaishi kama muhamiaji masikini, na mbaya zaidi hataki ndigu zake wajue ujio wake” alisema Justin, na kuendelea kueleza kuwa, mpaka dakika hii tayari askari sita wapo njiani wanaenda kumchukua mzee, iwe kwa hiyari au kwa nguvu kwaajili ya kufanya nae mazungumzo, “tunaamini anaweza kuwa ni mmoja wa wapelelezi wa kundi hilo haramu” alisema Jastin, akiwa amemaliza kutoa taarifa yake muhimu.

Naaam taarifa hii ilikuwa nzuri sana kwa Sixmund, ambae sasa aliona ni mwanga mzuri wa kumpata mtu anaeratibu mipango yote ya UMD, Pamoja na kumfahamu kiongozi wa kundi hilo, ambae waliamini wakimtia nguvuni tayari watakuwa wamesha lidhibiti kundi zima, “sawa bwana Jastin, mawasiliano ni muhimu sana, ni lazima nihudhurie mahojiano na huyu bwana Ashraf” alisema Sixmund kabla ya kukata simu.

Wakati huo huo, Mbogo land, katika jiji la handaki, ndani ya Ngome ya dhahabu, kwa king Elvis, bado mfalme huyu kijana kuwahi kutokea katika utawala wa nchi hii ndogo na tajiri, alikuwa macho anasubiria taarifa toka kwa Major General Sixmund, juu ya nini wamekipata kwenye orodha ya wanausalama waliohusika katika Operation ya kuwaondoa waasi nchi humo iliyofanyika mwaka 1992, “naamini tutafanikiwa kumpata kiongozi wao na kuzima mipango ya mapinduzi” alisema malkia Vaselisa kwa sauti tamu yenye kuliwaza, ambae sasa alikuwa ameegemeza kichwa chake kwenye kifua cha mume wake, “hata mimi naamini hivyo, lakini hatujui mpango wao wakuingiza silaha umekaaje, na kwamba watapitishia wapi” alisema Elvis ambae ni wazi alikuwa ameshtushwa na jinsi mambo yanavyoenda, “lakini mpaka sasa umeshajua kambi yao ipo wapi, na kama kama ujuavyo, hata kama wakipata silaha nzuri kiasi gani, bila kuwa na askari hawawezi kufaya chochote, cha msingi ni kuteketeza kambi lao” alisema malikia Vaselisa, muuza bagia za kunde wa zamani.

Hapo King Elvis, mteja wa zamani wa bagia za kunde, aliinua uso wake huku akitabasamu, ni wazi alikuwa amepata wazo zuri sana, “ujue mke wangu katika vitu ambavyo nimefanikiwa katika Maisha yangu, ni kuwa na mke kama wewe, yani unawaza kwa haraka sana, utadhania umepitia mafunzo ya kijeshi kwa ngazi za juu” alisema Elvis, akimalizia kwa kuweka mdomo wake kwenye paji la uso la mke wake nakupiga busu zito, kisha akachukuwa simu yake ambayo ile chukua tu, nayo inaanza kuita na mpigaji alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani, yani Mheshimiwa Dickson Chitopelah, hakika ilimshtua sana Elvis, ambae alimtazama mke wake ambae pia alishaona jina la Chitopela, nao wakatazamana, “vipi mume wangu mbona kama umeshtuka sana” aliuliza Malikia Vaselisa, huku anamtazama mume wake, “unadhani hii simu itakuwa na Habari gani, mbona kama inanipa wasi wasi” alisema Elvis kabla hajaipokea na kuweka sauti ya wazi…..……. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA NANE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA SABA:- Hapo King Elvis, mteja wa zamani wa bagia za kunde, aliinua uso wake huku akitabasamu, ni wazi alikuwa amepata wazo zuri sana, “ujue mke wangu katika vitu ambavyo nimefanikiwa katika Maisha yangu, ni nokuwa na mke kama wewe, yani unawaza kwa haraka sana, utadhania umepitia mafunzo ya kijeshi kwa ngazi za juu” alisema Elvis, akimalizia kwa kuweka mdomo wake kwenye paji la uso la mke wake, nakupiga busu zito kisha akachukua simu yake ambayo ile kuchukua tu nayo inaanza kuita, na mpigaji alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani, yani Mheshimiwa Dickson Chitopelah, hakika ilimshtua sana Elvis, ambae alimtazama mke wake, ambae pia alishaona jina la Chitopela, nao wakatazamana, “vipi mume wangu, mbona kama umeshtuka sana” aliuliza Malikia Vaselisa huku anamtazama mume wake, “unadhani hii simu itakuwa na Habari gani, mbona kama inanipa wasi wasi” alisema Elvis kabla hajaipokea na kuweka sauti ya wazi…..ENDELEA….

Na hapo ikasikika sauti iliyojaa nidhamu na heshima toka upende wa pili wa simu “salaaam ewe mfalme wa Mbogo Land” huyo alikuwa ni Waziri Chitopelah, “salaam Waziri chitopelah” aliitikia mfalme Elvis, huku anatazamana na mke wake, “asante mtukufu mfalme kwa kupokea simu yangu kwaajili ya usalama wa taifa letu” ilisikika sauti iliyojaa utiifu ya bwana Chitopelah, “ni Habari gani ambazo umekusudia kunipatia bwana Chitopelah?” aliuliza Elvis, alie onekana kuwa katika hali ya mstuko, “mtukufu kuna habari mbili, moja ikiwa mbaya kwa usalama wetu na nyingine ikiwa njema kwa usalama wetu, naomba nianze na hii mbaya” alisikika Chitopelah, na hapo mfalme na mke wake Vaselisa wakatega masikio kwa umakini.

Chitopelah akaanza kueleza, “mtukufu, imebainika kuwa, kuna uwepo wa mamluki ndani ya serikali yako tukufu, ambao wanatusaliti na kusaidia upangaji wa mapinduzi wakisaidiana na UMD” alisikika Chitopelah, na kumfanya Elvis na mke wake watazamane kwa macho ya mshangao, huku kila mmoja akiwaza sawa na mwenzie, “yanajirudia mambo ya mwaka 92” wakati wanawaza hayo, Chitopelah, alikuwa kimya akisikilizia matokeo ya taarifa ile, “unasema, yani Pamoja na usalama wote tulionao lakini bado UMD wamejipenyeza ndani ya Serikali?” aliuliza king Elvis akionyesha mstuko wa hali ya juu.

Naam pengine hapo ndipo Chtopela alipokuwa anapahitaji, “mtukufu, ukweli ni kwamba ni rahisi sana kwa mamluki kuingia serikalini yaani kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, kwasababu wahusika ni viongozi wakubwa na watu muhimu walio aminiwa na serikali yako tukufu” maneno ya Chitopelah yalionyesha wazi kumvuruga Elvis, ambae alimtazama tena mke wake lakini akashangaa kumuona mwanamke huyu mrembo, akiwa anatabasamu na kutikisa kichwa kwa masikitiko, ilimshangaza Elvis, “kuna mmoja aliefahamika Chitopelah?” aliuliza Elvis, ambae mpaka sasa, alionyesha mshtuko wa wazi kabisa, “mtukufu hilo ndilo lililonifanya nikupigie simu, ikiwa ni habari njema kwamba, nahitaji kibali cha kuunda kikundi kidogo, ambacho kitachunguza na kuwakamata wote wanaohusika, kwasababu hatuwezi kutoa taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi” alisema Chitopeah kwa sauti yenye kujaa utiifu, “sawa kibali kimetolewa, fanya hivyo haraka iwezekanavyo, nahitaji majibu” alisema king Elvis, kabla ya kukata simu.

Hapo mke wake akacheka kwa nguvu kiasi cha Elvis kushangaa, “unacheka nini Vaselisa, unajua kuwa nchi ipo katika wakati mgumu wa kiusalama?” aliuliza Elvis kwa sauti yenye kuonyesha kutokumuelewa mke wake, “hivi unashindwa kufahamu kuwa kinataka kujirudia kilichotokea mwaka 92?” aliuliza malikia Vaselisa, huku akimtazama mume wake kama vile anataka kuhakikisha anamuelewa anachoongea.

Nikweli kabisa alicho kiongea Vaselisa, kwamba kuna kitu kinataka kujirudia katika utawala wake kama kile kilichowahi kutokea miaka ishirini iliyopita, lakini ni kitu gani kinamchekesha mke wake, “ndiyo inajirudia, lakini kinacho kuchekesha ni kitu gani?” aliuliza Elvis, ambae licha ya kumwamini mke wake, lakini kwa hili ni wazi hakumuelewa mke wake, zaidi alimuona kuwa analeta utani kwenye jambo muhimu, “mume wangu, huwezi kuona kuwa hii njama ya pili kuondoa watu muhimu katika serikali na kuuchafua utawala wako kama ilivyokuwa kwa babu Eugen” alisema Malkia Vaselisa, lakini Elvis hakuonekana kukubaliana nae moja kwa moja.

Maana mfalme huyu alitulia kwa sekunde kadhaa, kabla hajaongea neno, “hata kama ilitokea mwaka 92, lakini haiwezi kuwa sawa na hii, hasa katika kipindi kama hiki ambacho serikali inatilia mashaka msako ule wa mwanzo, ni wazi sasa tunahitaji kuwapata watu waliopo ndani ya serikali wanao shirikiana na waasi” alisisitiza king Elvis, na kumfanya mke wake atikise kichwa kwa masikitiko, “mume wangu, unapaswa kutuliza akili katika kipindi kigumu, wewe ni sawa na mgonjwa ambae hajapata tiba sahihi ya ugonjwa wake, mgonjwa ambae anapokea kila ushauri na kuutumia katika kujitibu pasipo kujua kuwa wasio mpenda nao wanatumia nafasi hiyo hiyo kumuangamiza” alisema Vaselisa kwa sauti tulivu yenye kubembeleza, “una maana gani Vaselisa, unadhani nimechanganyikiwa kiasi hicho?” aliuliza Elvis, ambae ni kama alianza kukasilika.

Ni kama mke wake alishaliona hilo, akaachia tabasamu laini huku anamtazama mume wake, tabasamu ambalo halijawahi kumuacha salama king Elvis toka alipo kutana na Vaselisa kwa mara ya kwanza wakiwa wanamiaka mitano, mpaka leo hajawahi kulizoea na kuliona la kawaida, “mume wangu si unajua huwa sipendi ukasirike?” aliuliza Vaselisa huku anapitisha mkono wake taratibu, juu ya kifua cha mume wake huyu ambae ni mfalme pekee mwenye umri mdogo kwa wakati huo, “najua, lakini nashangaa leo” alisema Elvis, huku sauti yake ikiwa imepoa kabisa, “basi sasa ndio ujue kuwa lengo langu sio kukukasirisha, ila nikukusaidia, kama inavyokuwa siku zote” alisema Vaselisa, ambae ukimuona hapa kitandani unaweza kusema anajiandaa kwenda kwenye mualiko mkubwa na wakipekee, yani alikuwa amependeza vibaya sana, na kitu cha kuvutia zaidi ambacho msomaji utakiwa ukifahamu ni kwambanmalkia Vaselisa, alikuwa amejipaka mafuta nazi pekee, ndiyo mafuta ambayo uyatumia wakati wakulala, lakini ungesema ametumia vipozi zaidi kumi na unga wa mapambo wa rangi saba tofauti, na ile midomo yake milaini ungesema amejipaka king’arisho cha midomo, wao wanaita “lip shine”*********

Naaaam wakati huo kilomita kama arobaini, magharibi mwa TT City, yani Treanch Town City, nje ya kitongozji maarufu cha Komwe la Mwanamtama, kutokana na urefu wa jina la kitongoji hicho chenye jina la mwanamke maarufu Mwanamtama aliepata kuishi miaka mingi iliyopita aliejaaliwa kuwa na kipanda uso kikubwa kuliko mwanamke yoyote aliewahi kutokea #mbogo_land, walifupisha na kuita Komwe.

Usiku huu, kitongoji kilikuwa tulivu sana ni wazi watu walikuwa wamelala, maana usiku ulikuwa mkubwa sana, hapa kuonekana mtu wala magari yaliyokuwa yakizurula usiku ule, achana na Kijiji, twende magharibi zaidi, ambako ukiachilia mapori mkubwa na misitu ya kati, tunakutana na mashamba makubwa makubwa ya ngano na mahindi, ambayo pia katikati au pembeni ya shamba ungeona Nyumba kubwa yenye kupembeziwa na mabanda ya mifugo, “kupembeziwa ni neno ambalo linatumika kuwakirisha kile kilicho shikizwa pembeni ya kitu kingine.

Lakini tofauti na mashamba hayo makubwa, pia pembezoni mwa mto bhumbu (korodani) la Chifu Kwala, ni mto mkubwa kiasi, uliopewa jina hilo la Korodani za Chief Kwala, mwishoni mwa karne ya 18, miaka michache kabla ya uvaamizi wa wadachi katika nchi zinazoizunguka Mbogo land ni baada ya Chiefu huyo wa kiyao, aliekuwa anasafiri toka magharibi mwa Tanzania, kabla hata haijaitwa Dueustche ost – afrika ambayo baada ya kuchukuliwana waingeleza ikaitwa Tanganyika, jina lililotokana na ziwa Tanganyika, na baadae kuitwa Tanzania baada ya muungano, akielekea wilayani tunduru, akikwepa majeshi ya kingoni yaliyokuwa yamechukua eneo la kaskazini mwa milima ya matogoro.

Sehemu hii ambayo ilikuwa na wenyeji wapole na wastaarabu, wenye ukarimu na wapenda amani, ndiyo ilikuwa sehemu pekee ambayo wasafiri wengi waliweza kupumzika na kupata chakula, sasa siku hiyo Chiefu kwala, au Ache Kwala, kama unavyoweza kumwita, aliamua kuoga kidogo ndani ya mto huo, na kwa habati mbaya wakati anaoga baadhi ya wasaidi wake wakike walienda kuchota maji muda huo na kuona korodani za Chief, toka siku hiyo mto ukaitwa jina hilo, bhumbu za Kwala.

Hapo mtoni kuna shamba moja lenye mazao yaliyostawi vyema, japo mkazi au wakazi wa nyumba hii ndogo hafifu iliyo jengwa kwa Udongo na kuezekwa kwa makuti ya minazi, walionekana kujihusisha na uvuvi, kwasababu kulikuwa na nyavu pale nje, ila hapakuwa na mtu yoyote zaidi alie onekana pale nje kama ilivyo kule kitongojini, ni wazi kuwa wenyeji walikuwa wamelala, hapo ghafla tunaona askari wa MLA waliovalia sale nyeusi, wakiibuka toka vichakani kushoto kulia na mbele ya nyumba hii, huku wakiizuka na kujipanga kwa ulinzi na bunduki zao aina ya Uzi gun ya mwaka 2008.

Kitendo cha haraka, askari wanatembea kwa kunyata wakipeana majukumu na maeneo ya ulinzi kwa kutumia ishara za kivita, vilivyo husisha vidole vya mikono, ishara zilizo wagawa askari hawa, na kila mmoja akikaa kwenye sehemu yake, kila kona ya nyumba ile, huku askari wanne wakiusogelea mlango ambao walipoaribu kuufungua taratibu nao ukafunguka, na askari wakaingia kwa kunyata huku tochi zao zikiwa zimetangulia mbele na kuangazia mule ndani, “hamkuwa na haja ya kunyatia, nilikuwa najua ipo siku mutanifikia ndio maana sikukimbia nilipo hisi ujio wenu” ilisikika sauti toka upande wa kulia wa chumba kile, wote wanageuka upande ule, ambapo wanamuona mwanaume mmoja mtu mzima akiwa amesimama kwenye kizingiti cha mlango kilichokuwa kimezibwa kwa kipande cha shuka chakavu.

Makamanda wa kikundi maalumu cha uchunguzi wa kivita, kila mmoja akashangaa moyoni mwake, huku wote bila kupepesa wakiwa bado wameelekeza bunduki zao kwa mwanaume huyo, unatakiwa kutulia hivyo hivyo, usijiguse sehemu yeyote” alisistiza mmoja kati ya wale askari wanne waliongingia ndani, huku bunduki imemkodolea yule mzee aliekuwa anawatazama kwa macho ya kukata tamaa, “chochote mutakacho nifanya naomba musiidhuru familia yangu” alisema yule mwanaume mtu mzima kwa sauti ya kukata tamaa, “staff sajent Ashraf Kibwana, sisi hatupo hapa kukudhuru ila tunahitaji ujisalimishe na hii itasaidia familia yako kuwa salama” alisema mmoja kati ya wale askari walioingia ndani, “inamaana hamtonifanya kama mulivyo wafanya wengine?” aliuliza mzee yule kwa sauti yenye mashaka, “tunahitaji kuondoka na wewe kwaajili ya mahojiano, ili kujuwa kilicho tokea mwaka 92 pamoja na kujua kilicho watokea askari wenzio walioshiriki katika operation ya kuondoa waasi, hii ni siri na kwa faida ya taifa” alisema yule askari wa MLA, “nyie mmetumwa na nani, serikali yenyewe au Waziri Chitopelah?” aliuliza bwana Ashraff kwa sauti yenye mashaka, “hili ni agizo toka kwa mfalme Elvis, hivyo unatakiwa kuongozana na sisi” alisema yule askari.

Nivkama kauli hiyo iliibua matumaini kwa mzee huyu, ambae kwa mara ya kwanza aliachia tabasamu, kama ni kweli nipo tayari, lakini naomba munihakikishie usalama wangu na familia yangu” alisema yule mzee, kwa sauti yenye kuchangamka kdogo, “bila shaka, tutaondoka na familia yako, lakini kumbuka kuwa usijaribu kuleta ujanja wowote” alisema yule askari.*********

Yaaaap! Magari Matano yaliyopo katika msafara wa makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la polisi kanda maalumu ya kipolisi ya dar es salaam, yalionekana yakikatika mapori ya misegese, maeneo ya relini, huku katika gari manne yaliyokuwepo katikati ya magari matatu ya walinzi yaliyojipanga kwa mtindo wa moja mbele mawili nyuma, gari la nne katikati lilikuwa ni gari la RPC ilala, bwana Robart Ulenje, ambae muda wote alikuwa anaongea na simu kutoa maelekezo kwa watu ambao kwa namna moja au nyingine, ni washirika wake nje ya taratibu za kiuongozi wa jeshi la polisi.

Naaaam, ukiachilia kuongea na simu mara kwa mara, pia Ulenje alikuwa anafikiria sana kuhusu uwepo wa kundi dogo la bwana Uled Songoro, katika maeneo haya ya msitu wa misegese, akimsaka kijana shupavu na mjuzi wa vita Deus Nyati, “huyu mjinga hajui anamsaka nani, lazima kitamkuta kitu ambacho kitamfanya akimbilie msaada wa polisi, ambao watamuweka chini ya ulinzi na kunisababishia matatizo” aliwaza Ulenje huku anabofya namba ya Songoro na kuipiga.

Bahati nzuri simu iliita na kupokelewa mara moja, “niambie Ulenje, kuna jipya” aliuliza Songoro kwa shauku kubwa, “Songoro upo wapi sasa hivi?” aliuliza Ulenje, “nipo kichakani nimejibanza, nasubiri kwanza magari ya polisi yapite, vipi kuna inshu?” aliuliza Songoro, “Songoro nataka kujuwa sehemu mulipo” alisema Ulenje, ambae alionyesha kuto kuhitaji maongezi mengi, “nipo ndani kidogo kutoka barabarani, karibu na reli” alisema Songoro, na hapo Ulenje akashusha pumzi kidogo, kama vile ana jambo fulani muhimu anataka kumueleza Songoro.

“sikia Songoro, ni vyema kama utaondoka eneo hili, kwasababu jeshi la polisi lote la dar es salaam lipo huku, hebu subirini sisi tupite, kisha nyie muondoke, vinginevyo kitawakuta kitu ambacho sitokuwa na msaada kwenu” alisisitiza Ulenje wakati anaongea na simu, “hivi Ulenje unanichukuliaje wewe, nyie watafuteni hao wapuuzi wenu, mimi namsaka yule mjinga, mpaka nimtie mkononi” ilisikika sauti ya upande wa pili wa simu iliyojaa majisifu na kujitia umwamba, “Songoro hebu nikuulize kitu, hapo unavijana wangapi?” aliiuliza Ulenje, “hapa nina watu kama tisa na mimi mwenyewe wa kumi” alijibu Songoro upande wapili wa simu, “wanamafunzo gani ya kijeshi?” aliuliza Ulenje, na hapo kikafuata kicheko kikali cha dharau, “inamaana Ulenje ndio umenidharau kiasi hicho, kwamba watu wangu hawawezi kupambana na huyu mtoto?” aliuliza Songoro, ambae alionekana wazi kuwa kile kicheko chake, kilikuwa cha hasira, “sikia Songoro, sio kwamba nakudharau, ila ukweli ni kwamba, hao vijana ulio nao hawawezi kupambana na Dereva, cha kufanya wewe rudi mjini hii kazi niachie mimi” alisema Ulenje, kwa sauti iliyojaa maombi.

Lakini ilikuwa ni kama kupigia mbuzi gitaa, Sogoro hakuonyesha dalili yoyote ya kukubariana na Ulenje, “Ulenje, wewe shida yako nini, mimi najua ninachofanya, wewe endelea na mipango yako na mimi napambana kivyangu” alisema Songoro, kwa sauti yenye ubabe ndani yake, mpaka hapo ACP Ulenje, aliona wazi kuwa anaenda kuharibikiwa kabla jua ailijachomoza, hivyo nilazima achukue maamuzi magumu, “sawa bwana Songoro, pengine umejipanga, ila itabidi nikuongezee nguvu ya askari na silaha” alisema Ulenje, kwa sauti tulivu mfano wa mtu alie kubaliana na msimamo wa Songoro, “hapo sasa ndio umeongea point, sasa nakutana nao wapi hao askari?” aliuliza Songoro, akionyesha kufurahia mpango wa Ulenje, akujuwa kuwa kilichopangwa na Ulenje ni zaidi ya mipango yake ya kikatiri aliyowai kuifanya……..……. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Mkuu, tutegemee lini Tena kuupata mwendelezo wa matukio ya "UMD"
🙈🙈🙈🙈
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA NANE:- alisema Songoro, kwa sauti yenye ubabe ndani yake, mpaka hapo ACP Ulenje aliona wazi kuwa anaenda kuharibikiwa kabla jua hailijachomoza, hivyo ni lazima achukue maamuzi magumu “sawa bwana Songoro, pengine umejipanga, ila itabidi nikuongezee nguvu ya askari na silaha” alisema Ulenje kwa sauti tulivu mfano wa mtu alie kubaliana na msimamo wa Songoro, “hapo sasa ndio umeongea point, sasa nakutana nao wapi hao askari?” aliuliza Songoro, akionyesha kufurahia mpango wa Ulenje, hakujua kuwa kilichopangwa na Ulenje ni zaidi ya mipango yake ya kikatiri aliyowahi kuifanya… ENDELEA..

“umesema mpo ndani kidogo upande wa kulia pembeni mwa reli?” aliuliza Ulenje, “ndiyo, kuna kinjia fulani hivi, tena naona kuna alama za matairi ya gari, inaonyesha njia inayotumika sana” alijibu Songoro pasipo kujua kuwa anaelekeza hatari kuja upande wake, “sawa sawa subiri hapo mpaka vijana wangu watakapo kuja” alisema Ulenje, na Songoro akakubari mara moja akidhania kuwa Ulenje kubari kufuata anavyotaka yeye.******

Ndani ya golden house kwa mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mtoto wa king Eric wa pili na Malkia Doctor Irene, ambae sasa alikuwa ametulia huku macho yake kwa mpenzi wake huyu ambae hadithi ya kukutana kwao inapendeza na kusisimua zaidi ya ile ya #UMEKOSEA_LAKINI_TAMU, akmwambia “aya mke wangu, sasa nakusikiliza, hebu fafanua unachowaza” alisema Elvis kwa sauti ya upole.

Na hapo Vaselisa akaanza kuongea kwa ile sauti yake tamu, kama kinubi cha mfalme Suleiman, “mume wangu, kwanza kumbuka kuwa wewe na general Sixmund, ndio watu pekee munao endesha huu mpango wa siri, kwa maana hiyo hakuna mwingine ambae anafahamu juu ya hilo, na mpaka sasa tayari mumeshatilia mashaka makubwa juu ya njama kubwa iliyofanyika wakati wa operation ya kwanza ya mwaka 92, ambayo iliendeshwa na huyo huyo Chitopelah, ambae hajui kama kuna watu wameshaipata orodha ya askari na wanausalama walioshiriki katika operation ile….” Wakati malkia Vaselisa anaendelea kueleza anachokihisi, mara simu binafsi ya king Elvis ikaanza kuita.

King Elvis akaichukua simu haraka na kuitazama, akaona kuwa mpigaji alikuwa ni major General Sixmund, hii hakujiuliza mara mbili, akaipokea mara moja na kuweka sauti ya wazi ili wote wawili wasikie kitakacho ongelewa, “ndiyo Sixmund, kuna jipya lolote?” aliuliza Elvis kwa sauti iliyojaa shahuku, “mtukufu mfalme, licha ya kuwepo kwa habari mbaya, ila pia kuna habari njema” alisema Sixmund, nae akianza kama alivyoanza Chitopelah muda mfupi uliopita, “anza na hizo mbaya” alisema Elvis, ambae safari hii, alionekana kuwa na wasi wasi mara mbili, akihofia kupewa taarifa kama zile za Chitopelah, ambazo zingethibitisha kuwa ni kweli kuna waasi ndani ya serikali yake.

Naam, Major General Sixmund akaanza kueleza huku mfalme Elvis na malkia mwenye umri mdogo kuliko malkia wote kwa kipindi hicho, wakisikiliza kwa umakini, “mtukufu mfalme, taarifa mbaya ni kwamba, kati ya watu ishirini na tano katika orodha ya wanausalama walioshiriki operation ya mwaka 92, watu ishirini na tatu wote wametoweka katika mazingira ya kutatanisha, kama sio kifo basi ni kuacha kazi ghafla na kupotea kabisa, huku tukikosa kumbu kumbu muhimu zote za watu wale” alieleza Sixmund, na hapo mfalme akamtazama mke wake, ambae pia alikuwa anamtazama kwa mshtuko na mshangao, “Habari njema ni kwamba kati ya wawili walio salia, ambao Habari zao zimeatikana ni Waziri Chitopela ambae katika mpango wetu, tumepanga kutomuhoji chochote, maana yeye ndie aliekuwa kiongozi wa zoezi lile, hatuna uhakika kama mahojiano yetu na yeye hayatoleta madhara katika taifa letu” alisema Sixmund.

Na hapo Elvis akadakia, “na huyo mwingine ni nani na yupo wapi?” aliuliza Elvis aliekuwa na shauku kuu, “huyo mwingine ni sajent taji Ashraff Kibwana wa MLA, na baadae MLSA, ambae alitoweka miezi michache baada tu ya kumalizika kwa operation ile ya kuondoa waasi, na ameanza kuonekana miaka michache iliyopita huku magharibi katika nje ya kitongoji cha Komwe, anaishi kama mkulima muhamiaji masikini” alieleza Sixmund, ambae pia alieleza kuwa tayari wamesha tuma askari kwaajili ya kwenda kufanya nae mahojiano, “tunaamini kuwa huyo atakupatia majibu sahihi tunayo yahitaji” aliitimisha Sixmund, na hapo Elvis akamtazama mke wake kama vile anawazo fulani lenye mashaka akilini mwake, ni sawa na mke wake ambae pia alikuwa anamtazama kama yeye, “ok! katika hali yoyote, Ashraff apatikane, mimi nipo njiani, nieleze nikukute wapi nataka kusikia mahojiano kwa masikio yangu” alisema Elvis wakati huo yeye na mke wake walikuwa wameshainuka toka kitandani na kuelekea kwenye kabati la nguo za kawaida ambazo mara nyingi huzitumia katika matembezi yao binafsi na ya siri.

Kitu cha kujua msomaji ni kwamba kuna wakati ambao Elvis na Vaselisa, huwa wanakuwa na tamaa ya kufanya matembezi wakiwa kama raia wa kawaida, hivyo huvaa kikawaida na kuingia kwenye gari kisha kuondoka zao kuelekea mitaani hasa nyakati za usiku, ambako utembea sehemu mbali ikiwemo kwenye viunga ya bustani za TT City, ambako hupenda kutumia sehemu zile kufanyia utani wa kimapenzi na michezo ya wapenda nao, vitu ambavyo walivifanya sana wakiwa Tanzania miaka michache iliyopita. *******

Yaaap! Kilomita zaidi ya nane toka njia panda ya kisarawe na kibaha, magharibi mwa kisarawe ndani ya msitu wa Kazi Msumbwi katika machimbo ya kokoto laini na mchanga, bado wakina Kadumya wanaonekana wakiwa wamesimama na magari yao mawili wanasubiria wenzao ambao tayari walikuwa wamesha karibia.

Muda wote bwana Kafulu, ambae siku za nyuma alikuwa anajiita JJD, alikuwa anawaza kuhusu kitu kilicho mtokea kule makabe na kuona kama alidhalilishwa vibaya sana, hasa akikumbuka jinsi ambavyo alionyesha umwamba mbele ya Veronica na kijana Deus, ambae dakika chache baadae akamchapa kama mtoto na kuondoka na Veronica akiwa amechukua fedha ambazo zingesaidia katika mpango wa mapinduzi, “mshenzi sana huyu, hakutaka kuniachia nifungue kitumbua toka kwenye box mimi mwenyewe, aliwaza Kafulu ambae baada ya kuwaza kwa muda akapata wazo, “mkuu mimi na wazo ambalo litatusaidia kumpata yule Dereva na Veronica pamoja na fedha zetu” alisema Kafulu, akimueleza Kadumya aliekuwa amesimama pembeni yake wote wanavuta bangi, “mpango gani huo Kafulu?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya tabu kidogo kutokana na kuubana moshi wa bangi mdomoni na puani.

Hapo Enock Kafulu akaanza kueleza mpango wake ambao ulikuwa ni kujifanya wateja wapya na kumpigia simu Deus, wakimueleza sehemu ya kuchukuwa abiria au mzigo, “ili akiingia hapo, tayari askari wetu watakuwa wanamsubiri kuwaweka chini ya ulinzi” alieleza Kafulu na hapo likaonekana tabasamu usoni kwa Kadumya, “upo sawa kabisa Enock, tena safari hii ni vyema kama tukitumia simu yako” aliunga mkono Kadumya ********

Naaaam, Songea mkoani Ruvuma, giza lilikuwa limetanda kweli kweli, mji ulikuwa kimya kabisa, ni wazi watu walikuwa wamelala mida hii ya usiku mkubwa, lakini basi nyumbani kwa mzee Frank Nyati iliyopo mtaa wa Making’inda, bado tunamuona mzee huyu akiwa ametulia sebuleni na simu yake sikioni, ni wazi alikuwa anampigia mtu fulani ambae hakuwa na mpango wa kupokea simu hiyo, “kwanini huyu mpuuzi hapokei simu, lazima ajue kuwa MLA wapo dar kuwa saidia na kwamba kila anachokifanya ni kwaajili ya nchi yake ya asili nchi ya baba yake nchi ya babu zake” alijisemea mzee Frank, ambae mpaka sasa alikuwa ameshapiga simu zaidi ya mara kumi bila kupokelewa.

Hali hiyo pia ilikuwa huko kinyerezi dar es salaam, katika nyumba ya bwana James, mtaa ulikuwa kimya kabisa, japo baadhi ya nyumba za jirani na nyumba ya bwana James, walionekana watu wakiwa wanachungulia katika madirisha yao, lakini ni katika hali ya umbea tu kuona kitu kinachoendelea kwa wale askari wa jeshi la ulinzi walio zunguka uzio wa jengo la bwana James.

Lakini upande wa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa imepewa ulinzi mkali sana, sasa tuna waona watu ishirini, yani askari kumi na sita wa MLA, askari wa jeshi la Tanzania na bwana James wakiwa na familia yake, bwana James akiwa anapiga simu ya binti yake ambayo iliita muda mrefu bila kupokelewa, kitu ambacho kilikuwa kinampatia wasi wasi mkubwa juu ya usalama wa binti yake, “isijekuwa yule kijana ameshapatana na wale washenzi awapatie Veronica kwa malipo, aliwaza mzee James huku anawatazama watu wengine mle ndani.

Askari walikuwa busy na mipango yao, mke wake alikuwa na binti yao Caroline wamekaa kwenye kochi moja wanasinzia kutokana na kulemewa na usingizi, “lazima nifanye jambo kabla mambo hayajawa mabaya zaid na binti yangu kufikishwa kwenye mikono ya UMD” aliwaza mzee James huku anainuka toka kwenye kochi na kuelekea chumbani akiwa na simu yake mkononi. *******

Naaaam! Sasa turudi Visegese, sasa tuyaona magari yale Matano ya polisi, manne yakiwa ni magari ya viongozi wakuu wa jeshi hilo ngazi ya mkoa, yaliyokuwa yanakatiza eneo lenye kibarabara hafifu kilicho tokomea upande wa kulia wa barabara na gari la nne katika msafara ndani yake yupo bwana Ulenje, ambae anaonekana akibofya bofya simu yake kwa namna ya kuingia kwenye sehemu ya miito iliyopita, anaonekana kukwama kwenye namba zilizo ambatana na jina la Cheleji, na bwana Ulenje anaipiga namba ile ambayo inaita kwa muda mfupi kisha inapokelewa, “ndiyo afande” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, “sikia Cheleji, kuna kazi ya kufanya” alisema Ulenje, na kuanza kutoa maagizo kwa askari wake huyu anaemuamini kuliko wote.

Wakati huo sisi tunaachana na magari yale, tunaelekea upande kulia wa barabara, tuna fuata ile barabara ndogo ambayo mbele tuna wapita wakina Songoro waliokuwa wamesimama sehemu wakipata mapumziko ya kuvuta sigara bwege, huku Songoro mwenyewe akinywa pombe yake, kila mmoja wao akiwa na silaha yake mkononi, maongezi yao yalikuwa ni namna watakavyo muadhibu Dereva wa BMW na kummalizia kwa kifo chenye maumivu makali, “dogo anabahati sana, yani tunge mnasa pale hotelini angejisahau hata yeye mwenyewe kwa kitu ambacho tungemfanyia” aliongea Side kwa namna ambayo ungesema anazungumzia kukamata kuku wa kisasa, hakika wangejua nadhani wangeachana na mpango wao na kufuata maelezo ya Ulenje.

Tunaachana na wakina Songoro, tunasogea mbele zaidi umbali kama wa mita mia mbili, ambapo pana nyumba ya chakavu yenye kuzungukwa na mashamba madogo ya mboga mboga yaliyostawisha mboga mboga vizuri kabisa, tunaingia ndani ya nyumba hii moja kwa moja chini kabisa eneo la sebuleni hakuna mtu yoyote, tunaelekea chumbani kwa Deus ambako safari hii kabla hatujaingia ndani, mara mlango unafunguliwa na wanatokea wapenda nao wawili, waliokutana kwa mara ya kwanza na kuzindua penzi lao katika siku hii ya kwanza, safari hii tunamuona Deus alievalia bukta pekee bila tishert akiwa amembeba kifuani mwanadada mrembo Veronica alievalia truck suti na tishert nyingine, sura zao zikiwa zimetawaliwa na matabasamu ya furaha, macho yao yanatazama kwenye simu ambazo zilikuwa zimetulia, nao wanaishia kwenye makochi, Deus anamlaza Veronica kwenye kochi kubwa na yeye anakaa pembeni, lakini Veronica anajiinua kidogo na kujilaza kwenye mapaja ya Deus.

Naaam ile wanaanza kumiminiana wine kwenye grass mara simu ya Deus inaanza kuita, safari hii sio ile simu yake binafsi, ni simu ya kazi, Deus anaitazama akijaribu kuangalia kama ni mteja anaemfahamu au mpya, anaona kuwa ni mteja mpya, Deus anaichukuwa simu kwa tahadhari kubwa huku anajiuliza isije kuwa ni wakina Kadumya wameamua kutumia namba ngeni ili wajaribu kupanga mipango yao fake kwaajili ya kumnasa awapatie Veronica na Fedha, na pengine kumuangamiza kwasababu amesha jua wao ni wakina nani.

Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji, lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA MDAU, COMMENT LIKE VINAMPA HAMASA MTUNZI YA KULETA HUU MKASA KWAN NDIO ATAJUA KUWA KUNA WATU WANAFUATILIA...

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHINI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA TISA:- Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wapili wa simu, na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo, Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA…

Kijana ambae sio tu kwa kuwa amemsaidia kutoka mikononi mwa watu ambao walipanga kumfanyia kitu kibaya, ila pia ni mtu ambae amekuwa Rafiki yake kwa muda mrefu japo hawakuwahi kukutana mwanzo, na leo ikiwa siku yao ya kwanza kukutana amejikuta amezama kwenye penzi lake pasipo kujari tabia yake ya kuuwa bila kujiuliza mara mbili, “hoooo! Samahani kijana nilisahau, lakini nakuahidi sitovunja sheria hata moja” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima, “ok! nafasi ya mwisho, ongea mpango bila kuvunja sheria” Veronica alimsikia Deus akiongea kwa sauti ile ile tulivu, japo hakujua anaongea na nani, ila kiukweli alijua anaongea na mteja wake maana tayari alisha sikia mambo ya sheria.

“kijana sijui nisemeje maana siwezi kujitambulisha kama ilivyo sheria yako namba moja, ila ninahitaji uniletee binti yangu kwa kiasi chochote unachohitaji” ilisikika ile sauti ya mtu mzima yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu ni wazi hakutaka watu wengine wamsikie, “sehemu ya kumchukuwa na sehemu ya kumpeleka?” aliuliza Deus Frank Nyati, mwenye jina la utani, msafirishaji au mchoraji, “sehemu ya kumchukua ni pale ulipompeleka na sehemu ya kumleta ni kinyerezi mwisho nyumbani kwangu, hapo Deus akajua kuwa anaongea na bwana James Kelvin, akamtazama Veronica ambae alikuwa amelala pajani mwake huku macho ameyaelekeza kwake, macho yao yalipokutana, Veronica akajitabasamulisha na Deus nae akatabasamu, “mpango umekataliwa, nitakua navunja sheria namba 4” alisema Deus, kwa sauti ile ile kama hataki vile, kisha akataka kukata simu, lakini kabla hajakata simu mzee James akawahi, “subiri kijana, kuna mpango gani mwingine juu ya binti yangu?” aliuliza mzee James kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa alikuwa amesha changanyikiwa kusikia vile, maana Sheria namba nne inasema hakuna mpango juu ya mpango.

Ukweli ni kwamba, ilikuwa ni vigumu kwa Deus, kuingia mpango wa biashara juu ya Veronica ambae ukiachilia kuwa katika hatari ya kuvamiwa na kushambuliwa muda wowote huku baba yake akikosa msaada wa kumlinda, na pia alishapanga kuwa asingefanya kazi ile tena, na ili apate nafasi ya kuishi kama mtu wa kawaida, maana kamafedha tayari alikuwa nayo, lakini kubwa zaidi ni kwamba, mschana huyu kwa sasa ni mpenzi wake na wameshaingia katika makubaliano ya kuchumbiana.

Deus akamtazama tena Veronica, ambae bado alikuwa anamtazama kama vile aamini kama mtu alie kuwa ana wasiliana nae kila siku ndie huyu mbele yake, na kwamba anaenda kuwa mpenzi wake wa siku zote, hakufikiria kuhusu kile anachoongea kwenye simu ya kwamba kina muhusu yeye, “tayari huyo yupo kwenye mpango uliotangulia, siwezi kubadiri mpango wa mwanzo” alisema Deus, kwa sauti ile ile, ambayo kama unafahamu matendo yake ungesema ile sauti ni ya kuigiza, na siyo sauti yake halisi, lakini ukimtazama usoni, ungejua kuwa Deus anaupole ni waasili.

Maneno yale ni kama yalimshtua zaidi mzee James, ambae ni wazi alihisi kuwa tayari binti yake alikuwa katika mpango wa kupelekwa kwa wakina Kadumya kama alivyo hisi mwanzo, “nakuomba kijana, nipo tayari kukulipa mara tano zaidi ya malipo uliyoaidiana na hao washenzi” ni Deus pekee ndie aliekuwa anasikia sauti ya mzee James aliekuwa analalamika, “mzee nimesema siwezi kuingiza mpango juu ya mpango mwingine, huwa nasimamia sheria zangu” Veronica alimsikia mpenzi wake huyu akiongea kwa sauti ya upole kama vile hakumaanisha alichokisema, “jamani mchoraji wangu si umkubalie tu, mbona kama mteja wako anakuomba sana” alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyojaa mahaba makubwa, Deus anamtazama huku anatabasamu nakukata simu.

Lakini ile anakata simu na wakati huo, simu hiyo hiyo ikaanza kuita tena, “bado hujamalizana na mteja wako, huyooo anapiga tena” alisema Veronica huku anaachia tabasamu la kivivu, kama unge waona wawili hawa basi ungejua kuwa bado muda ilikuwa ni mapema sana.

Deus akaitazama namba ya mpigaji wake, ambae mwanzo alijua kuwa ni mzee James, yani baba wa binti huyu, lakini alipotazama ile namba haikuwa na mfanano wowote na ile namba ya mwanzo, akaipokea na kuiweka sikioni. Na wakati huo huo ikasikika simu ya Veronica nayo inaanza kuita, Veronica anaitazama anaona kuwa ni baba yake ndie aliekuwaa anapiga, Veronica akamtazama Deus, kama vile anamuomba apokee simu, nae akamuonyesha ishara ya kwamba apokee, wakati huo nayeye simu ilikuwa sikioni na macho kwenye kioo cha TV kubwa kwenye kona ya kulia ya sebule, ambapo kijana wetu aliweza kuona kipande cha camera na mbili, kukiwa na watu kumi waliosimama nje ya magari yao, mawili huku bunduki zao zikiwa mikononi. ********** Naam huko #Mbogo_land, ndani ya mtaa tulivu unaonakaliwa na viongozi wenye hadhi ya kipekee, kama vile wajumbe wa kamati za serikali, mawaziri na wazee wa mabaraza mbali mbali, ulikuwa kimya kabisa, kama ulivyokuwa mji mzima wa Treach Town, moja kati ya majiji ya kifahari duniani, ikiwa namba mbili kwa starehe kutoka kwa jiji la paris, na jiji la kwanza kwa usafi na utajiri duniani.

Nalo lilikuwa kimya kabisa, maana tayari watu walikuwa wameshalala, hata kama ulilala masaa kumi na mbili ya mchana, lakini ifikapo saa nane za usiku, lazima utapatwa na japo kalepe ka usingizi, labda kama ukiwa na kazi ya kufanya au mafunzo maalumu ya kuvumilia uchovu wa usingizi, japo mida hiyo lazima utahisi kitu fulani mwilini mwako, japo inakuwa tofauti kwa mtu aliepo bar.

Nyumbani kwa Waziri Chitopela, mambo yalikuwa tofauti kidogo, yeye licha ya kuhisi usingizi mkali, lakini bado alijitahidi kunywa pombe yake na kuendelea na mipango yake ya kimapinduzi, huku anasuka properganda moja kubwa, ambayo ingeshtua nchi nzima ya #mbogo_land, lengo ni kutoa nafasi kwa majeshi yake yafanikishe lengo.

Naam sasa bwana Chitopela, anaonekana akimaliza kuandika kitu fulani kwenye computer mpakato yake na kutuma kwa mtu fulani, kisha akachukua simu yake na kuipiga, simu haikuita sana ikapokelewa, “afadhari Chilopo umetambua kuwa leo sio siku ya kulala” alisema Kadumya mara baada ya simu kupokelewa, “siwezi kulala mkuu wakati najua siku za mapinduzi zinakaribia” alisikika Chilopo kwa sauti yenye kuelemewa na uzito wa usingizi, “ok! changamka tufyetue mabomu mawili mazito, tayari nimesha kuwekea kwenye email yako” alisema Chitopelah na Chilopo akakubaliana nae, “bila shaka mkuu, inatekelezwa sasa hivi” alisema Cholipo, sambamba na sauti ya kuliza kwa kitanda, ikionyesha wazi kuwa Chilopo alikuwa ananyanyuka toka kitandani, “ok! nakutakia mafanikio bwana Chilopo, Waziri wa Habari ajae” alisema Chitopela kabla ya kukata simu.

Ile anakata simu, bwana Chitopela, kabla hajaweka simu mezani akaisikia ikitekenye mkono wake, kwa mtetemo wa muito, akaitazama kuona mpigaji, nae alikuwa ni Kobwe, mkuu wa kombania A, ya batallion ya UMD, akaipokea maea moja, “niambie Kobwe, natarajia kusikia habari njema” alisema Chitopelah, kwa shauku, ndio mkuu habari njema ni kwamba sasa ndio tunaingia sehemu ya makutano na wakina Kadumya” ilisikika sauti toka upande wa pili, hapo Kadumya akatazama saa yake, ilikuwa inasoma saa nane, “mwendo mzuri bwana Kobwe, nasubiri taarifa zaidi za kazi” alisema Chitopela, kabla ya kukata simu.*********

Naaam, wakati huo huo, magaharibi mwa TT City, barabara ya kutokea Komwe, katika mashamba yaliyopo pembezoni mwa mto Bhumbu za Kwala, magari manne ya kijeshi yalionekana yakitembea kwa kasi ya nguvu, Askari mtoro wa MLA staff sajent Ashlaff Kibwana akiwa mwenye hofu kubwa na pasipo kuamini kile kinacho mtokea, alikuwa amekaa ndani ya gari zuri la kijeshi, lenye muonekano wa gari la ki VIP, pembeni askari wawili wenye bunduki zao, aina ya Uzi, pia nyuma kabisa walikuwa askari wawili wenye bunduki kama hizo, na seat ya mbele ya abiria pia kulikuwa na askari mwenye bunduki, hakika licha ya MLA kumueleza mzee Ashlaff, kuwa hawakuwa na lengo baya kwake na kwa familia yake, ambao walikuwa kwenye gari la nyuma yake, lakini ulinzi na ujio wa askari hawa wajeshi ambalo hapo mwanzo aliwahi kulitumikia.

Dakika ishirin baadae, tayari magari yale yalikuwa yamesha ingia mjini, nae bwana Ashlaff akitazama mitaa ya jiji lile ambalo kwa miaka mingi hakuwa na uwezo wa kutembea akiwa huru, safari inaenda moja kwa moja mpaka Mtaa wa Sizwe, ni mmoja kati ya mitaa tulivu katika jiji la Trench Town na wenye sifa ya kukaliwa na viongozi wakubwa wa ulinzi na usalama.

Moja kwa moja magari yanaenda kusimama mbele ya lango kubwa la chuma lililoshikizwa kwenye kuta kubwa na imara, ukuta licha ya kuwa mrefu na wenye ulinzi wa umeme, lakini pia kulikuwa na askari kadhaa MLA, waliokuwa wamesimama nje ya lango lile na bunduki zao mikononi.

Lango linafunguliwa na magari yote yanaingia ndani, ambako pia wanakutana na magari mengine ya kifahari zaidi kasoro gari moja dogo ania ya Toyota caldina, huku wakionekana askari kadhaa wenye bunduki wakiwa wamesimama imara wakitazama pande zote za ukuta ule pasipo kuhangaika na magari yale yaliyokuwa yanaingia.

Mzee Ashlaf ambae hakuwa na pingu wala kibanio cha Kamba, licha ya kuwa alihakikishiwa usalama wake, lakini bado alionekana kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake na familia yake, mzee huyu anaona magari yana simama, askari wanashuka mara moja, “mzee kumbuka upo na familia yako, hatutaki kuipa wasi wasi na mashaka yoyote familia yako, hivyo utafuata kile tunacho kueleza bila kujaribu kufanya ujanja wowote” alisema askari aliekuwa amekaa seat ya mbele ya gari lile alilopanda Ashlaf, ambae kwenye kosi za shati lake jeusi la sare za uvamizi wa usiku, ungeona nyota mbili kila upande, ikimtambulisha kuwa ni mwenye cheo cha luten.

Hapo bwana Ashlaf anatazama kwenye gari la nyuma na kuwaona mke wake na Watoto wake wakiwa wanashuka toka kwenye gari na kusimama pembeni ya gari lile, huku wakionekana kushangaa, kwa maana ya kutokujua kinachoendelea, ila nyuso zao zilionyesha kuwa na uoga kwa kiasi kikubwa, “bila shaka, afande, lakini naomba msiushishe familia yangu kama mlivyofanya kwa wengine” alisema Ashraff ambae alionekana kutokuwa na imani na wana MLA hawa, “ondoa shaka na ushuke kwenye gari” alisema yule luteni wa MLA kwa sauti ya chini, ni wazi hakutaka mke na watoto wawili wa bwana Ashraf wasikie maongezi yao.

Naaam bwana Asraff ana shuka toka kwenye gari, na wakati huo huo anamuona askari mmoja wa kike akija mbele ya mke wake na Watoto wake na kuwaongoza kuelekea ndani ya jengo lile, na wakati huo huo wakati wao wanaingia ndani, wanapishana na kanali Jastin, “safari itaishia hapa, hatuendi LS Base, mpelekeni kwenye chumba cha mahojiano” alisema kanali Jastin Johnson, kisha akarudi ndani ya jengo lile la kifahari, usingefikilia kuwa ni jengo linalomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hii ya kifalme.******

Naaaam! Sasa turudi njia panda ya kisarawe, ambapo tuna wakuta askari wa jeshi polisi, PT yani Polisi Tanzania, wakiwa bado wamekaa kwa vikundi, huku wengine wakiwa wametafuta sehemu za kujiegesha na wengine wakianza kusinzia kabisa kutokana na muegesho ule.

Tofauti na kundi dogo la askari kumi na tano, ndani ya jeshi hili linalo aminiwa na serikali, walio kuwa wamesimama pembeni kabisa katika vikundi vidogo vidogo wakiendelea kuwasha mienge ya sigara na bangi, na ndio wakati ambao koplo wa polisi Cheleji, aliekuwa na koplo Othman alikuwa anamaliza kuongea na simu, “kaka kimeumana” alisema Cheleji, huku anaweka simu mfukoni na kutoa mkebe wa risasi kwenye bunduki yake, akaitazama kama ina risasi, akagundua kuwa ilikuwa nazo lakini chache, nadhani alizitumia kuwashambulia wakina Deus kule barabara ya malamba mawili, “vipi mkuu anasemaje?” aliuliza Othman, kwa sauti yenye shauku, huku anamtazama Cheleji aliekuwa anaweka ule mkebe wa risasi kwenye kifuko kilichopo kiunoni mwake na kutoa mkebe mwingine uliosheheni risasi, “kuna kazi relini inabidi ikafanyike” alisema Cheleji, huku anaupachika mkebe wa risasi kwenye bunduki yake.

Wakati wanaongea hayo, wakati huo huo, wakayaona magari yanaingia pale njia panda, yakitokea upande wa kibaha, hakuna alieuliza ni magari ya nani, tayari walishajua ujio wa wakuu wao, hivyo haraka sana wakajikusanya mbele ya magari yale kwaajili ya kusikiliza amri za matarajio.

Dakika mbili baadae tayari viongozi walio tangulia na askari pale njia panda, walikuwa wameshaanza kutoa taarifa za mwanzo kwa mkuu wa polisi kanda ya dar es salaam, “afande mpaka sasa uelekeo wa waharifu ni kazimzumbwi, hatuna uhakika kama huku walikoelekea ndiko kwenye makazi yao au wamekimbilia kwasababu ya kujificha kwa muda” alisema yule Assistant inspector, “vipi kuhusu yule mualifu Deus Nyati, yule Dereva mwenye gari jeusi, kuna taarifa zozote za kufahamu sehemu alipo kwa sasa?” aliuliza CP Nyambibo, huku Ulenje na wenzake wakiwa wanasikiliza taarifa zile, “afande zaidi ya taarifa za kuonekana barabara ya maramba mawili hakuna taarifa nyingine ya kuonekana kwake” alisema yule inspector.

Hapo Kamanda Nyambibo akawatazama wenzake, yani makamanda wa polisi mikoa, “mnashaurije sasa?” aliuliza Nyambogo, akiwazama kwa zamu, “afande nashauri tusi jiziuke na hawa wenye magari peke yao, muhimu zaidi ni yule dereva wa gari jeusi” alisema kamanda Ulenje, lakini Nyambibo akaonekana kutokukubaliana na wazo hilo, “ujue Ulenje mpaka sasa Deus Nyati hajawa hatari kama walivyo hao jamaa, kwasababu mpaka sasa wamesha uwa polisi, lakin Deus amekuwa akitukikimbia tu” alisema CP Nyambibo na Ulenje akaona ndio nafasi ya kutoa ushauri, ambao utawapotosha wenzake na kuwaokoa wakina Kadumya, hivyo haraka sana akadakia, “naitakuwaje kama Deus Nyati ni mshiraka wa hao wengine, huoni kama tukimpata yeye itatusaidia kuwapata hao wengine?” alisema Ulenje.

Hapo Ulenje akamuona CP Nyambibo akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo na mshangao, nao wakaonekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile, ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom