Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA SITA:- Pale mapokezi hakuwaona kabisa wale jamaa wanne, wala jamaa wa mapokezi au meneja wa hotel, “wameenda wapi hawa jamaa” aliuliza Cheleji, akimuuliza mmoja wa askari aliekuwepo pale eneo la mapokezi, “wameelekea chumba cha kuongozea camera” alijibu yule askari huku akionyesha upande wenye chumba cha kuongozea camera za usalama wa jengo hilo…..….ENDELEA…

Cheleji alitoka haraka na kuelekea upande ule alio onyeshwa, yani kwenye chumba chenye camera za usalama za hotel nzima.********

Naam! sasa turudi mbezi mwisho, stendi ya malamba mawili mtaa bado umechangamka, wafanya biashara wadogo wadogo waliojaa pembezoni mwa barabara wanaendelea kuwahudumia wateja wao sauti za matangazo toka kwenye speeker zinasikika zikinadi bidhaa mbali, ikiwa ni pamoja na simu usajiri wa line za simu na bidhaa nyingine nyingi, sauti za music na kelele za watu toka kwenye bar za jirani zilisikika, magari boda boda na waenda kwa miguu nao walizidi kupilikisha mtaa.

Mita mia mbili toka lilipo jengo la Benk ya uhifadhi, BMW jeusi toleo la kisasa kabisa (kwa wakati huo) linaonekana likiwa limesimama, huku bado likiwa katika muungurumo, japo kama haukuwa makini usingesikia ngurumo hiyo hafifu ya gari hilo la kisasa, zaidi ungegundua kwa taa ambazo zilikuwa zinawaka kwa mwanga hafifu.

Ndani ya gari hilo la kisasa, yupo kijana Deus peke yake, ambae anatoa simu yake ndogo na kufungua, hapo anakutana na jumbe kadhaa za whatsap, ana bofya huku anatabasamu, nikama alijua mtumaji ni nani, hata anapofungua application ile ni kweli anakutana na jumbe kadhaa toka kwa pacha, “nita jibu baadae, ngoja kwanza ni mpigie baba” anajisemea Deus huku anaodoa ile sehemu ya whatsap na kupiga kwenda sehemu ya miito na kuipiga namba ya baba yake.

Simu inaita kwa sekunde chache kisha inapokelewa, “Deus, vipi tena usiku huu, kuna tatizo?” aliuliza mzee Frank akionekana wazi kuwa hakuwa na dalili yoyote ya mtu ambae ametoka usingizini, “usiku vipi baba wakati hujalala bado?” aliongea Deus, kwa sauti ya utani, “ok! tuyaache hayo kuna jipya gani huko dar?” aliuliza mzee Frank, “nikuhusu mzee James, yule tajiri, alietoroka #mbogo_land, mwaka 1992” alisema Deus, na kuanza kumsimulia mkasa wote ulivyokuwa.

Wakati Deus anasimulia mkasa wake na baba yake, sisi twendeni ndani ya jengo la benk, ambako tunaingia tukiongozana na vijana watatu wenye kuvaa makoti makubwa ya baridi na sox vichwani mwao, wanatembea kwa kwaharaka huku wamekumbatia mikono yao maeneo ya vifuani mwao kama vile wameshikilia vitu fulani, lakini sisi tunatangulia kuingia ndani kabla yao.

Ndani ya jengo lile kubwa kiasi, shughuli zinaendelea kama kawaida, watu wapo kwenye mistari ya kusubiria huduma, anaonekana mschana mmoja mrembo mwenye uso uliojaa wasi wasi akiwa amekaa kwenye kiti kimoja kati ya vingi vya kusubiria huduma, macho yake yakiwa yanazunguka kuwatazama wateja waliopo kwenye foleni ya kusubiria huduma, baadae macho yake yanakwama kwa kijana mmoja, aliebeba begi lenye ukubwa wa kipimo cha kati, aliekuwa kwenye ile foleni ya kusubiria huduma akiwa mtu wa saba toka dirishani.

Wakati huo huo wanaingia vijana watatu wenye makoti mazito ya baridi na kofia za sox vichwani mwao, kila mmoja anashtuka na kabla hawajafanya lolote, wanamuona kijana wa mwisho kuingia anasimama mlangoni na mwingine anakimbilia mwishoni mwa ukumbi ule mdogo na kusimama karibu na main switch, huku mmoja akisimama katikati ya ukumbi na wote kwa pamoja wakafungua zip za makoti yao na kutoa bunduki, kisha yule wakatikati akaelekeza juu na kuminya trigger.

Hapo ukasikika mlipuko mkubwa wa risasi, “wote lala chini” alipiga kelele mmoja na mwingine pia akadakia, “lala chini pumbavu” alisema mwingne na mwingine akadakia, huku watu wakihangaika kujilaza chini kwa uoga kama vile mwanadada Veronica alivyofanya, alilala chini kwa haraka, yeye na wenzake wakiwa wametawaliwa na uoga wa hali ya juu.

Naaaam Veronica akiwa amelala pale chini, pamoja na wengine, anaweza kumuaona mmoja kati ya wale vijana watatu waliokuwa wameshikilia mitutu ya bunduki akienda moja kwa moja mpaka kwa yule mtu mwenye begi la kipimo cha kati toka kwenye kampuni ya bwana Lumen Manyonyi na kuchukua lile begi, “wekeni sura zenu chini” alisema yule aliechukuwa begi lile huku anatembea kusogelea kule alikokuwepo Veronica na wakatia anamkaribia yule wa mlangoni akapiga kelele, “oya fanyeni haraka polisi wanakuja” sauti hiyo ya juu, iliambatana na tukio la ghafla la kuzimika kwa taa za mule ndani.

Giza lilitanda, kimya kilitawala, hofu zilizidi mioyoni mwa watu, ndio wakati ambao Veronica alihisi begi linawekwa karibu yake, kisha vikasikika vishindo ya watu kutoka nje ya jengo lile, huku vishindo vingine vikiingia ndani, “polisi tulieni hivyo hivyo” ilisikika sauti ya kikakamavu, toka kwa mmoja kati ya wale waliongia na sekunde chache taa zikawashwa.

Naam mwanga ukatanda mle ndani watu walianza kuonana wazi wazi, kila mmoja aliweza kuwaona polisi wanne waliovalia sale zao mpya za kipolisi, majambazi watatu hawakuwepo mule ndani, mateka wa muda mfupi walijiona sasa wapo salama nao wakaanza kuinuka, “bilion kumi, za boss” alipiga kelele mmoja kati ya wale wateja, huku akikaribia kuangua kilio huku ana nyayuka toka chini.

Veronica nae akanyanyuka na lile begi, hakuna aliekumbuka kulitazama, maana hakukuwa na hata mmoja aliewaza kuwa begi lile liliachwa mule ndani, “subiri utatoa maelezo yako kituoni, kwa sasa tokeni nje kupisha ukaguzi” alisema mmoja kati ya wale polisi na hapo watu wakaanza kutoka kwa fujo mule ndani, huku Veronica akijichanganya na watu hao akiwa na begi lake, hata polisi nao walitoka na watu wale, hakika mambo yalifanyika kwa muda mfupi sana.

Turudi mita mia mbili, liliposimama BMW S7, ndani yake kuna Deus Nyati, ambae licha ya kusikia mlipuko wa risasi ambao moja kwa moja alijua kuwa mteja wake anahusika, yeye aliendelea kuongea na simu, “kwa hiyo baba, unatakiwa kuwa makini sana, kama wameanza na mzee James, pengine wakaja kwako pia” alisema Deus huku anatazama saa kwenye dash board ya gari lile la kifahari, ilikuwa imeshatimia saa nne na dakika mbili, “sidhani kama wananihitaji mimi, lengo lao lilikuwa ni kuniuwa na sio kunitumia baadae” alijibu bwana Frank na wakati huo Deus analiona land rover puma, likipita pale alipo na kuondoka zake likitokomea upande wa barabara kuu ya morogoro, “ok! baba ninapaswa kuondoka sehemu hii muda wangu umeisha” alisema Deus, huku anakata simu, ambayo aliitazama kwa sekunde kadhaa kama vile anajiuliza au anajishauri kitu fulani, “nitamjibu nikifika home” alijisemea Deus huku anaweka simu kwenye dash board.

Naaam ile anakanyaga cruitch ili aingize gia namba moja mara akasikia mlango wa gari seat ya abiria unafunguliwa kisha akaingia mwanamke, mwanamke ambae kama tukisema mrembo sidhani kama inatosha, labda niseme ni mzuri kuliko wote ambao Deus aliwahi kuwaona kwa macho yake, japo aliweza kumuona mwanamke huyu akimtazama kwa macho ya uoga na wasiwasi, lakini haikusababisha kuondoa uzuri asilia wa mwanmke huyu aliekuwa na begi mkononi, “sheria namba nane imeshavunjwa, mume shindwa kwenda na muda” alisema Deus kwa sauti tulivu huku anatazama mbele na mikono yake akishika kiongoza gari, yani mshikanio, “sheria ngapi za nchi mumevunja mpaka unajali kuhusu muda?” aliuliza yule mwanamke kwa sauti ya chini kama vile anajaribu, maana wasi wasi mwingi ulionekana ndani yake, wakati huo anafunga mlango, “ni vyema ukaweka hilo begi lako set ya nyuma na ukafunga mkanda kuliko kuongea ukiwa hujui unacho ongea” alisema Deus.

Naaam Veronica anaweka begi seat ya nyuma, na kufunga mkanda huku anamtazama kijana huyu, wenye sura ya upole ya kupendeza yenye kushangza na umbo la kusisimua, ambalo kila mwanamke angependa kujilaza kifuani kwake nyakati za usiku, ambae sasa alikuwa anakanyaga crachi na kuingiza gia namba moja, kisha gari linaondoka taratibu kuingia barabarani.

Safari inanza kimya kimya, huku kila mmoja akiwaza la kwake moyoni mwake, “hivi demu mkali kama huyu anawezaje kuwa jambazi, yani amekosa kabisa mwanaume wa kumhudumia au tamaa za kutajirika haraka haraka?” alijiuliza Deus huku akijizuia kumtazama Veronica ambae pia alikuwa anawaza yake , “masikini kijna wa watu mzuriiii lakini jambazi, hivi ukikutana nae mchana akikutongoza si unaweza kusema umepata mwanaume?” alijiuliza Veronica huku akimtazama kijana huyu kwa jicho la wizi.

Naaam kila mmoja akiwa katika mawazo yake, mala ghafla wanasikia ving’ora vya magari ya polisi, wote wanashtuka na kushikwa na wasi wa..….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Naaam ile anakanyaga cruitch ili aingize gia namba moja mara akasikia mlango wa gari seat ya abiria unafunguliwa kisha akaingia mwanamke, mwanamke ambae kama tukisema mrembo sidhani kama inatosha, labda niseme ni mzuri kuliko wote ambao Deus aliwahi kuwaona kwa macho yake, japo aliweza kumuona mwanamke huyu akimtazama kwa macho ya uoga na wasiwasi, lakini haikusababisha kuondoa uzuri asilia wa mwanmke huyu aliekuwa na begi mkononi, “
Hatimae wamekutana pacha na pacha wake ila je? Watajuana? Tukutane sehemu Inayofuata tujue nini kimeendelea na simulizi yetu iko mwisho, baada yake tunayo nyngne ni bandika bandua wenye stress hapa ndipo kuna tiba yao.
 
Hatimae wamekutana pacha na pacha wake ila je? Watajuana? Tukutane sehemu Inayofuata tujue nini kimeendelea na simulizi yetu iko mwisho, baada yake tunayo nyngne ni bandika bandua wenye stress hapa ndipo kuna tiba yao.
Muuza vyombo wa Daslam na mwanafunzi wa chuo wa mkoani Mbeya .Full kupigana kamba yani Mchoraji na Pacha wake😂🙌
 
Mkuu kongole,chuma kimefikia climax mwaga moto kwa wingi.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA SABA:- Safari inanza kimya kimya, huku kila mmoja akiwaza la kwake moyoni mwake, “hivi demu mkali kama huyu, anawezaje kuwa jambazi, yani amekosa kabisa mwanaume wa kumuhudumia au tamaa za kutajirika haraka haraka?” alijiuliza Deus, huku akijizuia kumtazama Veronica ambae pia alikuwa anawaza yake , “masikini kijna wa watu mzuriiii lakini jambazi, hivi ukikutana nae mchana akikutongoza si unaweza kusema umepata mwanaume?” alijiuliza Veronica huku akimtazama kijana huyu kwa jicho la wizi.

Naaam kila mmoja akiwa katika mawazo yake, mara ghafla wanasikia ving’ora vya magari ya polisi, wote wanashtuka na kushikwa na wasi was..….ENDELEA……..

Huku kila mmoja likiwa na askari kadhaa nyuma yake, wenye silaha mabegani mwao huku magari yale mawili yakiwa yamewasha ving’ora vyenye taa nyekundu za tahadhari, ambayo yana wapita kwa speed kali huku Deus akilazimika kusogeza gari pembeni kuipisha miamba hii ya usalama wa raia na mali zao, ambao aliweza kuona kwa kutumia side mirror wakielekea moja kwa moja kwenye benk ya hifadhi ya mali za wanachi.*****

Naam twendeni kwanza Kinyerezi mwisho, nyumbani kwa mzee James, ambako kabla haujafikia uzio wa jengo lake kubwa usiku wa leo unakutana na magari mawili ya jeshi la ulinzi, yakiwa yamesimama mbele ya lango la uzio wa jengo hili, na kama ukitazama vizuri utaweza kuona askari waliosimama kuzunguka uzio wa jengo hili mikononi wana bunduki zao aina ya SMG, wakiwa wamesimama kwa kuachiana mita kumi kumi wapo makini kutazama chochote kinachokuja.

“dah! Haya mambo yameenda kwa haraka sana, huyu fala amewezaje kupata ulinzi kwa haraka namna hii” alisema Bwana Kadumya, ambae alikuwa na wenzake sita ndani ya gari, kati yao watatu walikuwa wamejeruhiwa, mmoja amekufa na wawili walikuwa wazima, wapo ndani ya gari lao aina ya Land Rover puma, lililosimama mita mia mbili na hamsini toka nyumbani kwa mzee James, “mkuu mimi nadhani ile mbinu nyingine ya kumtumia yule binti yake inafaa zaidi” alisema mmoja kati ya wale vijana waliokuwa nae ndani ya gari ambao ni wazima, “geuza gari twendeni Makabe” alisema Kadumya huku anatoa simu yake na kupiga namba ya Enock Kafuru.

Simu haikuita muda mrefu ikapokelewa, “ndiyo mkuu” alisikika Kafuru toka upannde wa pili wa simu, “nipe taarifa za huko, vipi mume fanikiwa” aliuliza Kadumya, wakati huo dereva anageuza gari na kuendesha kuelekea barabara kuu, “mkuu mambo yanaenda vizuri, mpaka sasa mzigo upo njiani unakuja, wahi sherehe” alisika luten mtoro wa MLA Kafulu, akiongea kwa sauti yenye kujiamini, “sawa Kafulu, sasa hakikisheni hao wote munawaweka chini ya ulinzi na muna wazuia mpaka ninapofika” alisema Kadumya ambae pia aliongeza jambo jingine, “halafu kabla ya yote wakija tu mchkueni video huyo mwanamke na video itumwe kwa baba yake, iambatane na ujumbe mzito wenye maumivu ambao utamfanya ajilete yeye mwenyewe” alisisitiza Kadumya, “nifanya kama ulivyosema mkuu” aliitikia Enock Kafulu.

“na vipi kuhusu huyu mwingine?” aliuliza Enock Kafulu, “huyo kenge sina inshu nae, labda nikute tu mwili wake, ila cha kuzingatia afe katika maumivu makali sana, kwa maana alisababisha hasara kubwa kilo hamsni ya dhahabu” alisema Kadumya kabla ya kukata simu, huku safari yao inaendelea na sasa walisha kamata barabara ya kuelekea mbezi kupitia malamba mawili.********

Naam magari mawili aina ya defender, yanasimama mbele ya jengo la Benk ya uhifadhi, ambalo kwa sasa eneo la mbele lilikuwa lime jaa watu waliokuwa wanashangaa na kusimuliana juu ya tukio lililotokea muda mfupi uliopita, polisi wale ambao idadi yao walikuwa kumi na mbili, wanagawana majuku kwa haraka, kundi moja la watu sita likibakia nje na kundi jingine likiingia ndani pamoja na askari mwenye nyota mbili, yani inspector, akiongozana na askari mwenye cheo cha sajent.

Ndani wanakuta kuna watu wachache ambao ni wafanya kazi wa benk ile, tuna watambua kutokana na sare zao za mashati meupe na suruali nyeusi pamoja skaff zao shingoni, “nani mkubwa wenu?” aliuliza yule afisa mwenye nyota zake mbili mabegani, “mimi hapa ni meneja” alijibu mwanamke mmoja mtu mzima, “nini kimetokea, maana imeripotiwa kusikika kwa mlipuko wa risasi?” aliuliza yule afisa mara baada ya yule mwanamke kumfikia karibu yake,

“kaka nikama mlivyoona pale mwanzo, walikuja majambazi kama mulivyo waona walivyokuwa wanakimbia, wakati ule munakuja” alisema yule mwanamke na kumfanya yule polisi aliekuwa na wenzake atoe macho kwa mshangao, “sajent, kwani kuna askari waliokuja huku?” aliuliza yule inspector huku anamgeukia sajent ambae pia alikuwa katika mshangao.

Hapo wote wawili wakawageukia wale askari wengine waliokuwa nao, ambao ni kama walijua kuwa wanaulizwa kama wanajua lolote juu ya askari waliofika hapa mwanzo, maana kila mmoja alikataa kwa kutikisa kichwa, hapo askari mwenye nyota mbili na sajent wakatazama tena kwa mshangao, “vipi kaka, kwani hamkuwa nyie muliokuja hapo mwanzo? lakini sawa ila mutakuwa mume wapita polisi wenzenu hapo nje, maana walitoka walipokuwa wamewatoa raia nje” alisema yule mwanamke, ambae hapo mwanzo alijitambulisha kama meneja.

Ukweli iliwashangaza sana askari hawa, maana wao ndio askari wa kituo cha karibu cha hapa mbezi, na ndio askari waliokuwa doria na walikuja mara moja baada ya kupigiwa simu na kuelezwa juu ya kusikika kwa milipuko ya risasi toka kwenye benk ya uhifadhi, “dada una uhakika kuwa waliokuja walikuwa polisi?” aluliza yule inspector, kwa namna fulani ya kutiliashaka maneno ya meneja, “ndiyo walikuwa wamevaa magwanda na buti mapya kabisa, tena bunduki kama hizo walizobeba wenzenu” alisema yule meneja kwa msisitizo akionyesha anajua anachokisema.

Hapo polisi hawa wawili waliosomea uongozi kwa ngazi ya juu katika vyuo mbali mbali vya kipolisi, wakatazamana na kuuliza kwa ishara ya macho, ni kama walikuwa wanaulizana waanzie wapi.

Naam sekunde chache za kujiuliza ziliisha kwa kitendo cha ghafla cha inspector kutazama juu kwenye dali ambako aliona camera kadhaa kila kona ya jengo lile, hakika kwa sasa Elimu ni muhimu zaidi ya miaka ya nyuma, ambapo kwa kila jambo hata jambazi anatakiwa awe ameenda shule, maana miaka hii ulinzi umekuwa wasayansi zaidi, ukishindwa shule ya kawaida bora hata akasomee ujambazi kama unashule, vinginevyo utakamatwa siku yako ya kwanza tu, kabla hata hajamaliza siku zake arobaini.

“hizi camera mnaongozea wapi?” aliuliza inspector huku anamtazama yule mwanamke mtu mzima, “pale kwenye computer zile pale” alisema yule mama meneja huku anaonyesha meza moja iliyopo kwenye kona kabisa juu yake ikiwa na computer moja, hakukuwa na mtu yoyote mbele ya computer ile, “ina tunza kumbu kumbu kwa muda gani?” safari hii aliuliza sajenti, huku wanatembea kuelekea kwenye ile meza upande wa sehemu za mahesabu, ina hard disc mbili, kila moja ina Tela bite 5000, na huwa ina tunza kumbu kumbu za week nzima, alisema yule meneja na wakati huo walifika na kuanza kukagua matukio yaliyo tokea muda mfupi uliopita.*******

Yap! sasa twendeni SisterFada hotel, tuanze Chumba namba nane cha ghorofa namba nne, ambako wasi wasi ulikuwa umetanda kwa wapenzi wawili, yani bwana Eze na mpenzi wake wa pembeni bi Emmy Eduward, japo wasi wasi wao ulikuwa na sababu ya mambo mawili tofauti, wakati Emmy akiogopeshwa na hali iliyojitokeza ya muda mfupi uliopita hapa hotelini, milindimo ya risasi na mafumanizi ya watu wenye bunduki.

Wakati huo huo Eze, ambae alilazimika kuendelea kubakia pale Hotelini kutokan na agizo la polisi, alikuwa anawaza juu ya mke wake, kwamba ata mwambia nini atakaporudi nyumbani kwa kuchelewa, maana hata uondokaji wake nyumbani haukuwa mzuri, huenda kukawa na kipigo huko.

Wakati huo huo tukishuka flow ya chini kabisa kwenye chumba cha kuongozea camera za ulinzi, tuna waona wale wanausalama wanne toka TSA, wakiwa na meneja wa hotel na mtu wa mapokezi, na vijana wengine wawili ambao, ndio wahusika wa chumba kile, wanaendelea kuzipitia video za kuanzia saa mbili na nusu.

Tayari walisha ona baadhi ya matukio ya pale hotelini, ikiwa ni pamoja na makundi ya watu walioingia na silaha na wale waliotoka wakiwa wamebeba mwili wa mwenzao, pamoja na kijana alietoka akiwa na tajiri James, “huyu hebu kwanza simamisha hapo” alisema mwanausalama mmoja, wakati walipo muona kijana mmoja akikatiza mapokezi na kuelekea upande wa lift, “mzoom huyo alie shika box” alisema yule mwana usalama, yule kijana alie kuwa anaongoza ile video akafanya kama alivyo elekezwa na kuikuza ile video na kuipata picha ya kijana huyo, japo haikuonekana vyema, “hebu mtafute kwenye camera nyingine” anasema mwana usalama na kijana yule muongozaji anaanza kusaka video kwenye camera za ghorofa nyingine.

Wakati wote wakiwa makini wanafuatilia Video kwenye kioo cha computer mara mlango unafunguliwa anaingia askari polisi mwenye cheo cha Koplo, “samahani jamani nimechelewa kidogo” alisema yule koplo huku anafunga mlango na kuwasogelea pale mezani, “umechelewa kwani umeitwa humu ndani?” anauliza mmoja kati ya wanausalama wa TSA, “naitwa Koplo Cheleji, ni kiongozi wa polisi waliopo hapa” alijitambulisha Cheleji, “simamisha hapo hapo, nadhani hii hapa ni nzuri zaidi” alisema mwanausalama” wakati wanaitazama video ya kijana yule yule, alieonekana anaingia chumba namba nane cha ghorofa ya nne.

Sasa akiwa anatoka kwenye chumba namba nne cha ghorofa ya tatu akiwa na mzee James, “inaonekana yeye amemteka mzee James, je ametumwa na serikali au?” alisema mwanausalama mmoja na mwenzake akapinga, “sidhani kama ni hivyo, mbona kama huyu kijana ni yule askari aliekuwa anatafutwa na jeshi la ulinzi miezi miwili iliyopita?” aliuliza yule mwanausalama na wote wakatazama vyema kwenye computer.

“kweli bwana, ni yeye hebu chukua picha iende makao makuu ya jeshi wakamtambue kisha kipatikane kibali cha kumsaka” wakati huo huo vikundi hivi viwili visakwe haraka” alisema mmoja kati ya wale wanausalama, ambae alionekana ndie mkubwa wao, huku wakimalizia kutazama video zile zilizo chukuliwa kwa camera za usalama mpaka lilipoonekana BMW S7 jeusi likiondoka pale hotelini, “mkuu, sasa tunaweza kusema kuwa, huyu ndie yule dereva wa BMW jeusi aliefanya mauwaji ya majambazi kule Arusha” alisema mmoja wao, huku wakiendelea kufanya taratibu za kuchapisha nakara moja ya picha ya kijana huyu.

Hapo Cheleji akiwa amesisimkwa mwili akatoka mara moja mule chumbani, akiwaacha wale wanausalama wakiendelea na taratibu za kupata picha na kuhamisha ile video kuiweka kwenye computer mpakato waliyokuja nayo ndani ya sanduku dogo walilokuja nalo.******

Yap! sasa kikosi cha watu kumi na sita kilikuwa tayari kwa safari, wanasubiri amri ya kuondoka, ndipo captain Amos Makey, aliposikia simu yake inaita akaitoa mfukoni na kutazama jina la mpigaji.

Alikuwa ni luten kanali Frank Nyati, hapo Amos akakaipokea haraka na kuiweka sikioni, “ndiyo afande Frank kuna jipya lolote?” aliuliza captain Amos kwa sauti ya chini kidogo, “jipya lipo, tayari mambo yameanza huko dar, UMD walijaribu kumteka James, bahati yake kuna mtu alimsaidia, hivyo kuna umuhimu wa kuijulisha serikali ya #mbogo_land, ili wampatie ulinzi, vinginevyo watahitajia kumuua bwana James” alisema mzee Frank, kwa msisitizo, “afande nashukuru kwa taarifa, ila kiukweli hivi sasa tupo safarini tunaelekea dar lengo lilikuwa ni kwenda kumchukua mzee James baada ya kusambaa kwa picha zake akiwa na askari waasi wa UMD, alisema Amos, ambae baada ya kumaliza kuongea na mzee Frank akapiga simu kwa general Sixmund, ambae pia hakuchelewa kupokea simu yake, ikionyesha nae alikuwa macho mpaka muda ule, akampata taarifa za utekwaji nyara mzee James.*******

Naam safari ilikuwa ya kimya kimya, gari hili lilipita barabara ya goba mpaka njia panda ya makabe, ambapo lilikata kushoto na kufuata barabara ya makabe kupitia msakuzi, huku wote wawili wakiwa kimya, kila mmoja akiwaza la kwake, “hii kazi ndiyo kazi yangu ya mwisho, kama msafirishaji haramu, maana ninakabiliana na hatari nyingi sana, na pengine nikaingia kwenye orodha ya watu hatari wanao tafutwa hapa nchini” aliwaza Deus, huku akizidi kukanyaga mafuta kwenye barabara hii ya vumbi yenye kutawaliwa na mawe madogo dogo, japo kwa gari hili hayakusikika kabisa.

Veronica ambae muda wote alikuwa anamtazama kijana huyu, ambae kila muda ulivyozidi kwenda wakiwa pamoja ndani ya gari, akazidi kuuona muonekano mzuri wakijana huyu mwenye sura ya upole na umbo la kimazoezi, kifua kipana na mikono iliyokazabkwa push up, “hivi ni kweli nikifika wataniacha au ndiyo wata nikamata na mimi” aliwaza Veronica huku anamtazama Deus kwa macho ya wizi, ila huyu kaka anonekana kama ana huruma kidogo, pengine yeye anaweza kuwaaambia wenzake wanachilie” aliwaza Veronica ambae mpaka sasa bado alikuwa anahisi kuwa Deus ni mshrika wa wale waliomteteka mchumba wake John John Daud.

“kwa hiyo kaka yangu, nikishawapa hili begi lenu, muna muachia John?” aliuliza Veronica huku anamtazama huyu kijana asiefanana na kazi anayoifanya, “mpaka sasa umesha vunja sheria mbili, kumbuka hakuna kujuana majina, pia mimi sijui lolote, kazi yangu ni kukufikisha eneo la tukio tu” alisema Deus, kwa sauti yake tulivu, huku macho ameyakaza mbele. .….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom