Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
- Thread starter
- #661
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA SABA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA SITA:- “hallow!! Vero, upo wapi mwanangu?” ilisikika sauti ya mama Vero toka upande wa pili wa simu ikifuatiwa na saut ya mzee James, “upo salama Vero, hebu tuambie upo wapi tuwalete polisi waje kukuchukua” hapo Veronica alie shindwa kujibu anamtazama Dereva aliekuwa anaendesha gari kimya kimya, “dada mbona huongei jamani, ni kweli upo na Deus Nyati?” hilo lilikuwa swali toka kwa Carloline na ndilo swali lililo mfungua mdomo mwana dada Veronica, “Deus Nyati ndio nani huyo?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojawa na mshangao…..ENDELEA…..
Hapo Deus alishtuka kidogo, sio kwa sababu ya kujulikana kwa Veronica yupo na yeye, hilo alilijua wazi kuwa tayari kuna baadhi ya polisi,l wanafahamu kuwa Veronica yupo ndani ya BMW S7, tatizo ni wamejuaje kuwa dereva wa BMW anaitwa Deus Nyati, simjui huyo Deus Nyati” alisema Veronica, “sasa kama haupo na huyo upo wapi na upo na nani?” aliuliza mzee James, hapo Veronica akamtazama Deus ambae alimuona amekaa kwa utulivu kwenye kiti cha dereva anaendesha gari taratibu kuisogelea nyumba moja ambayo niwazi haikumaliza ujenzi, japo mazingira yake kwa nje ilionyesha wazi kuna mkulima anaishi ndani yake, “kuna kaka mmoja amenisaidia, nachotaka mujue ni kwamba JJ ni jambazi yeye na wenzake waliniteka, akalazimisha niende nikachukue hela benk, halafu alitaka anibake lakini huyu kaka akanisaidia” alisema Veronica kwa sauti yenye deko na lalamiko ndani yake, “tutaongea baadae Vero, kwa sasa tuambie upo wapi na huyo kijana ni nani?” alisema mama Vero na hapo Vero akamtazama tena dereva ambae alikuwa ameelekeza macho mbele kwa utulivu mkubwa, alionyesha wazi kuwa maongezi yale hayakuwa yakimhusu.
Kitu ambacho Veronca hakukijuwa ni kwamba, dereva wake alikuwa anawaza na kuwazua, ambavyo ameweza kubainika kuwa yeye ndie dereva wa BMW s7, japo alipanga kazi hii ilikuwa ya mwisho, yani ya kumchukuwa Veronica benk na kwamba angeachana na biashara hii, lakini sio kwa mtindo huu, “mama nyie tambueni hivyo kuwa nipo salama, mengine tutaongea baadae kwa sasa siwezi kuwaambia kwasababu hamuwezi kuwatumia polisi, baadhi yao wanasaidiana na majambazi, msinipige mpaka niwapigie mimi” alisema Veronica na kukata simu, huku anatazama mbele ambako gari lilikuwa linaingia kwenye kibanda cha gari kwenye ile nyumba isiyo malizika.
Veronica anashangaa wasi wasi unaongezeka, maana niwazi hapa porini kwenye nyumba hii chakavu ndio mwisho wa safari yao, anashindwa kuuliza maana hakuwa na chaguzi, ukichukulia hapa alipo asingeweza kuondoka mwenyewe, maana sio tu kwaajili ya msitu uliopo, ila pia asingeweza kujua aeleeke wapi ili afike nyumbani kwao, na kilicho mtisha zaidi tabia ya upole ya kijana huyu.
Naam wakati anaendelea kujiuliza mara doctor Veronica anashangaa kuona gari linaanza kuzama ardhini taratib mfano wa watu waliopo kwenye lift, lakini kila walipozama ndipo alipoanza kuona mwanga kama vile wanashukia kwenye jengo la kisasa lenye umeme, na hata wanapofika chini anaweza kuona gari dogo aina ya Suzuki la kubebea mzigo likiwa katika maegesho ya kisasa kabisa, “bibie usiku huu utapumzika hapa wakati tunaangalia namna ya kukufika nyumbani kwenu, maana sio wewe wala sio mimi ambae atasalimika endapo tutakutana na wale polisi wanao wasaidia adui zetu” alisema Deus huku anatoa mkanda wa kiti gari likiwa bado lina unguruma.******
Naam! Sasa twendeni dar es salaam airport, ambapo wanaonekana maafisa kadhaa wa jeshi, wamesimama eneo zinaposimama ndege za VIP, mita kadhaa nyuma yao yanaonekana magari manne aina ya Toyota V8 meusi yenye namba za ubalozi wa mbogo land sambamba na magari mengine mawili ya jeshi la ulinzi yanye rangi za kijani na fito nyeupe lenye maandishi mekundu yakiwa katika herufi mbili tu, MP huku askari wacheche ambao ni wazi kabisa kuwa ni polisi wa jeshi, ambao pamoja na wakuu wao walikuwa wanaitazama ndege moja ndogo ya shirika la ndege la nchini #mbogo_land, ambayo hutumiwa na mabalozi wa nchi hiyo waliopo nchi Tanzania, wafanyakazi na familia zao, ikiwa inamesimama sehemu ya VIP upande wa jeshi la ulinzi la Tanzania linalohusika na mambo ya anga, ndege ambayo ndiyo kwanza ilikuwa inazima engine.
Yap! mlango wa ndege unafunguliwa, mlango ambao ndiyo ngazi moja kwa moja ikifuatiwa na kuonekana kwa vijana kumi na sita waliobeba mabegi yao wakishuka toka kwenye ndege hiyo ya kisasa na moja kwa moja kuelekea waliposimama maafisa wa jeshi la ulinzi wanapo wafikia, yule wa mbele ambae ni captain Amos Makey anasalimia kijeshi, ni baada ya kuona kati ya wenyeji wake watatu, ukiachana na mteule daraja la pili na luten, pia palikuwa na major, ambae ni mkubwa kwa cheo ukilinganisha na cheo cha captain cha Amos.
Kwa kifupi ni kwamba, jeshi dunia nzima ni moja, hata kama akiwa ni komandoo wa marekani, mwenye cheo cha private, atapokea amri ya toka kwa koplo wa msumbiji au Tanzania, endapo watakutana katika majukumu ya kijeshi na aendapo atakataa kutekeleza jukumu, basi atashitakiwa kwa sheria za kijeshi, “jambo captain Makey, habari ya #mbogo_land” aliitikia yule Major, ikiwa ni haki yake kabisa kupokea salut hii ya captain wa MLA, “huko tumeacha salama, matatizo ni haya ambayo yametuleta huku na tunajitahidi kuyadhibiti” alisema captain Amos Makey huku wanapeana mikono na wale makamanda wenzao.
Naam baada ya kupokelewa na kusalimiana wakina makey wakaingia kwenye magari aina ya Toyota V8, na safari ikaanza kuelekea kinyerezi, huku mbele ikiongoza land rover 110, la MP na jingine kama hilo likiwa nyuma huku askari wa jeshi hili imara la Tanzania, wakiwa wananing’inia na silaha zao mikononi. ******
Naam! Wakati kikundi cha Amoured Rece Troop, yaani ART, wakiwa wanaingia Tanzania, mfalme Elvis akiwa nyumbani kwake chumbani kitandani na malikia Vaselisa, wanajadiri hili na lile, mara akapigiwa simu toka kwa mkurugenzi wa idara ya habari na mawasiliano ya ikulu ya Golden House, nae akiwa na mke wake wakajua lazima kutakuwa na jambo jipya limetokea, “vipi kuna jambo gani tena?” aliuliza mfalme akisahau hata kutoa salamu ya kifalme, “mtukufu mfalme, kuna habari toka kwenye ile kurasa ya uchochezi na proper ganda iliyotuma habari za James kuwa mfadhiri wa UMD, ni vyema kama ukiiona” alisema msemaji huyo wa ikulu, “hawa watu bwana, wamekuja na jambo gani tena?” aliuliza Elvis huku anainuka toka kitandani na kusogelea sehemu ambayo wanaweka simu, hasa nyakati za usiku, “mtukufu mfalme, kuna habari tatu lakini kiukweli hazina ukweli wowote” alisikika mkurugenzi wa habari, wakati huo king Elvis, alikuwa anachukua simu mezani, huku mke wake akiwa anainuka na kumfuata mume wake.
Naam Vaselisa alimfikia mume wake na kumkuta anabofya simu yake kubwa kuingia kwenye mtandao aliotajiwa, mtandao ambao mara zote umekuwa ukitoa habari sizopendeza za serikali ya #MBOGO_LAND, yani habari zenye kuichafua nchi hiyo, nyingi zikiwa ni uvumi na uongo, “nadhani wanajaribu kuichonganisha serikari na raia” alisikika mkurugenzi wa habari, "vipi mliwahi kuangalia chanzo cha habari hii kinapatikana wapi?" aliuliza king Elvis, huku mke wake akichukua simu toka kwa mfalme huyo kijana na kupekuwa kurasa ambayo mume wake alikusudia kuipekuwa, "mtuku mfalme, hilo tulilifanya siku za nyuma sana, tukagundua kuwa kurasa hii ilisajiliwa na mtu ambae alikuwa tanzania, lakini muhusika aliesajiri kurasa hii licha ya kutumia utambulisho bandia, lakini pia aliwahi kuitumia kurasa hii akiwa sehemu mbali mbali, ikiwa pamoja na hapa nchini, ila mara nyingi tanzania, hata hizi post za leo amezipost akiwa tanzania" alisema kurugenzi na hapo wakaongea mawili matatu kabla ya hawajakata simu na mfalme kuungana na mke wake kusoma zile habari za kuchochezi, huku mara kwa mara akipokea simu toka kwa wasaidizi wake, yani mawaziri na wakurugenzi, pamoja na wazee wa baraza waliokuwa wakimpatia habari za makala ya kichochezi iliyopostiwa usiku huu mtandaoni.**********
Yaap! Veronica anashuka toka kwenye gari na kumfuata mweji wake aliekuwa anatembea, kueleka kwenye mlango uliokuwa mbele yao upande wa kushoto, Veronica alitembea nyuma ya mwenyeji wake huku amekumbatia mkoba wake, begi la fedha wakiwa wameliacha kwenye gari.
Veronica anamuona dereva kijana mwenye sura ya upole akiwa anaufikia mlango na kuufungua, wote wanaingia ndani ambapo wanaibukia ndani ya sebule moja nzuri ya kifahari yenye ukumbi wa chakula na jiko, bar ndogo na kila kinachohitajika, "hoooo! plan nzuri, unaishi na nani hapa?" anauliza Veronica huku anakaa kwenye kochi, wakati mwenyeji wake anasimama mbele ya friji na kukinga maji ya kunywa, "nipo peke yangu, na zaidi yangu hapa tanzania ni wewe tu ndie unae pajua hapa" alisema Deus huku anamaliza kukinga maji na kuyagugumia, kisha anamgeukia mgeni wake na kwa msaada wa mwanga wa taa za pale sebuleni, wote wawili wanapata nafasi ya kutazamana na kuonana vyema, ikiwa ni baada ya kukaa kwenye mwanga hafifu toka wamekutana. …..…. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums