SIMULIZI: "The Godfather"

SIMULIZI: "The Godfather"

SEHEMU YA SABA:

Mheshimiwa waziri katika serikali inayomaliza muda wake, mgombea katika nafasi ya uraisi ambae amekatwa jina lake dakika za mwisho kabisa alikua mzee wa totoz kwelikweli, tulimfuatilia na kufahamu ratiba zake kadhaa, lakini jamaa alikua kama ana kismart hivi maana tulikua tunapishana nae sana. Kupitia Inno tukafanikiwa kufahamu weakness ya jamaa, jamaa alikua ana mahusiano ya kudumu na mwanadada mrembo sana wa kuitwa Kidawa, Kidawa alikua Kidawa kweli kweli, slay queen wa kwenda.

Niliona si haba kama nitaanza na Kidawa na kupitia yeye atatupatia mheshimiwa. Shetani akawa upande wetu maana Kidawa alikua mjamzito na alikua na clinic yake maalumu pale aghakhan hospitali, ana shida gani Kidawa wa watu, acha afaidi pesa ya mheshimiwa. Niliegesha gari pembeni ya gari ya kidawa , nikasubiri kwa masaa kadhaa ili amalizane na daktari wake , baada ya muda nikamuona Kidawa akitoka ndani ya jengo la hospitali akiwa anajizoazoa, ujauzito ulimpendeza Kidawa, macho yalipata tulizo kwa picha nzuri niliyokua naitazama.

Kwa mwendo wa kivivu alifungua mlango wa gari lake na kuliondoa maeneo ya maegesho. Sikua na papara, nilijua tu kwa mda ule zaidi ya kupitia sehemu akapate chakula, hakuna mahala pengine ataelekea, lazma atahitaji mapumziko, nilichohitaji ni dakika chache za maongezi nae, na niliona si vyema kuongea na mjamzito akiwa na njaa , acha apate msosi kwanza. Nilimfata kwa tahadhari, Kama nilivyowaza ndivyo ilivyokua, Kidawa alipitia mgahawani kupata chakula, nilimsubiri hadi alipomaliza na safari yetu ya kurudi nyumbani ilianza.

Kwa tahadhari ileile niliendelea kumfuatilia hadi katika makazi yake upanga . Ile nyumba ilikua ni mfano wa nyumba ya kisasa, ilikua na kila kitu kinachohitajika kuwepo katika nyumba, kwa muonekano ule ulinipa taswira ya kua nipo sehemu sahihi kwani mheshimiwa alimpa thamani Kidawa kiasi cha kumpa maisha ya gharama namna ile. Nilisubiri geti lifunguliwe na nihakiki kua pale ndipo anapoishi mrembo yule wa mheshimiwa kisha nikapotea maeneo yale.

Nilihitaji kufahamu vitu vichache vya Kidawa, hakuna mrembo asie na siri, na sikuchelewa sana kuipata, jioni ya ile siku nikiwa katika ziara zangu zisizo rasmi niliona gari aina ya crown ya kijivu ilitoka ndani ya nyumba ya mheshimiwa, ndani ya gari alikuwepo Kidawa na kijana wa makamo mwenye muonekano wa kijana wa kisasa. Sikuchelewa nikaamua kuwaungia tela, msafara wetu uliishia club moja maarufu sana kwa kipindi kile.

Haikuhitaji kua na elimu ya shahada kujua kua ile mikao ya mama kijacho na kijana wa kisasa ilikua ni ya kimapenzi, niliwaacha wafurahie usiku wao, mimi ni nani wa kuzuia watu kufurahia maisha yao, nikajipa mahangaiko kidogo ya nafsi kutaka kujua ule mzigo wa mama kijacho utakua wa muheshimiwa kweli au wa kijana wa kisasa, nilijicheka mwenyewe, tangu lini nimeanza biashara ya udaku jamani.

Saa sita usiku ulinikuta katika sebule maridhawa ya bibie Kidawa, kijana wa kisasa waliachana na Kidawa pale club baada ya kumkodia usafiri wa kumfikisha nyumbani, na yeye akapotelea gizani, sikutaka kuhangaika nae, niliyemuhitaji ni Kidawa, hakukua na mlinzi kwa usiku ule, nadhani Kidawa hakutaka mashahidi kwa yale anayoyafanya na hivyo alilazimika kumpumzisha mlinzi, kwa tahadhari nikiwa nimeegesha gari yangu mita chache toka makazi ya kidawa , nilijongea geti la mrembo yule, kwa kutumia zana zangu maalum nilifanikiwa kufungua geti na kuingia hadi ndani.

Nilimkuta mrembo akiwa kajilaza kihasara pale sebuleni, chupa kadhaa za pombe zikiwa sakafuni kudhihirisha kua palikua na hekaheka si kitoto, nilikionea huruma kitoto kilichopo tumboni mwa mwanamke yule mrembo asiyejielewa. Nikachukua maji kwenye jokofu na kumuamsha mrembo wa mheshimiwa, Kidawa alikurupuka akawa anataka kukimbia, nikamuamuru atulie na akae chini.

Nilimueleza juu ya niliyoyashuhudia, nikamwambia kua kama anahitaji taarifa zake za ufuska na ulevi zisimfikie mheshimiwa aanze kuropoka anayoyajua kuhusu mheshimiwa. Nilihitaji kufahamu makazi ya kudumu ya mheshimiwa kwa pale dar, shule wanazosoma wanae, marafiki zake ni kina nani, mali anazomiliki kama anafahamu na aina ya magari anatumia.

Ndani ya dakika chache nikawa nimepata taarifa nyingi kuliko nilivyowaza na zaidi ya kua mheshimiwa amedhamiria kuingia Ikulu kwa heri au kwa shari, kwahiyo atahakikisha anagombea kupitia upinzani na ameshaanza kufanya taratibu za kuhama chama , ilikua imebaki siku ya kutangazwa rasmi .

Hio ilikua taarifa muhimu sana, ama kweli tulicheza karata muhimu sana, mheshimiwa anamthamini na kumuamini kimada kiasi cha kumuelezea mipango yake ya kisiasa. Kwa mwendo wa tahadhari niliiacha nyumba ya kimada wa mheshimiwa na kutokomea kusikojulikana.
 
SEHEMU YA NANE:

Ratiba ya mheshimiwa kwa mujibu wa Kidawa alikua nje ya nchi, kwa akili yangu ya kujiongeza nikafahamu tu kua mheshimiwa anatafuta wadhamini kwa ajili ya harakati zake za kisiasa, ama kweli alidhamiria kuingia Ikulu. Nikaona si dhambi kama tutamsaidia mheshimiwa kurudi nyumbani mara moja kuja kutujulia hali wananchi wake, eee ...nami nishakua mwananchi ndugu zangu , natokea Singida ....

Mheshimiwa alikua anamiliki shamba la kufuga wanyama mkoani Lindi lenye ukubwa wa kutosha kujenga shule mbili za msingi, mbili za sekondari, zahanati na nyumba za watumishi . Nilijaribu kufuatilia serikali ya kijiji kwa kutumia njia zangu za mkato na kubaini kua lile shamba mheshimiwa alipewa kama zawadi na serikali ya kijiji, kwa kipoozeo kidogo kwa uongozi wa Kijiji kwa ahadi ya kua shamba darasa, kubwa na la kushangaza hakuna mwanakiji alieruhusiwa kuingia shambani mule wala kulisogelea, labda walitakiwa kujifunza ndotoni.

Nilikua na kijana wangu Inno, tulifanikiwa kuruka ukuta na kuingia ndani ya like shamba, palikua na wanyama waliofugwa kisasa kabisa, ng'ombe walistawi na kunona . Kwa vile hapajawahi kua na rabsha kabla na pia palikua ni kijijini hapakua na ulinzi wa kutisha, na hata kama walikuwepo walikua katika kuridhika kua wamepata kazi ya bure, wanalala wanaamka , miaka inakatika hapana tukio wanaanza kulinda kwa mazoea. Tulitafuta sehemu ya kunywea maji, lita mbili za dawa ya kuua magugu ilitosha kuleta maafa. Hatukua na haraka ya kuondoka eneo lile, kwa kutumia kivuli cha wapima barabara, ilitusaidia kusalia siku tatu zaidi pale kijijini ili kupata majibu ya kazi yetu.

Jioni ya siku iliyofuatia minong'ono ilianza kuzagaa kua palikua na ugonjwa umezuka shambani kwa mheshimiwa. Zaidi ya ng'ombe elfu tatu walikua wamefariki, tulipongezana na kijana wangu tukachomoka bila ya kuaga mtu, hatukua na mda wa kupoteza . Japo Kidawa alisita kutupa uhakiki wa kutosha kuhusu umiliki wa mheshimiwa katika kiwanda Cha magodoro kilichopo Chanika nje kidogo ya manispaa ya jiji la dar es salaaam, kwa kutumia upepelelezi wetu tulimudu kubaini kua mheshimiwa alikua ana umiliki kwenye kile kiwanda.

Kwa mwendo wa kijasusi tulifanikiwa kufika kiwandani saa nane usiku, kwa kutumia njia za maji machafu tulifanikiwa kuingia hadi sehemu ya ndani ya kiwanda na kusababisha shoti ya umeme, tulitega umeme ujiongeze baada ya lisaa tangu tutoweke kiwandani hapo na kusababisha moto mkubwa kuwahi kushuhudia, Kuna matukio unayasababisha halafu unakuja kuona uhalisia wake unakua unapingana na nafsi yako kama ni wewe umeshiriki hilo tukio.

Tukio la moto nililishuhudia kwenye taarifa ya habari ya saa mbili, kiwanda kilikua kimeungua kimebaki majivu, hakuna walichomudu kuokoa, iliniuma kua tuliua watu nane maskini kama mimi wasio na hatia, ila hakukua na namna ilibidi mapambano yaendelee. Nilipata taarifa kupitia Kidawa kua mheshimiwa anaingia baada ya siku mbili , tulijipanga imara na Inno kumpokea.

Tulikua tumetega kilometa chache kabla ya kuingia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. Ile siku ya kumpokea mheshimiwa waziri anaemaliza muda wake ulikua umewadia. Tulihitaji kuonana nae kabla hajajiudhuru nafasi yake ya uwaziri na kutangaza nia ya kuhama chama maana tulihofia hekaheka za waandishi wa habari kwa kipindi hicho. Tuliusindikiza msafara kwa mbali hadi uliposhia katika hotel ya Kilimanjaro, nadhani alikua anakutana na watu wake muhimu, tulihitaji tupate picha za walau watu watatu anaokutana nao.

Niliingia mle hotelini baada ya msafara wa mheshimiwa kuingia, nilichukua chumba ili iwe rahisi kufuatilia matukio kwa kadri yatakavyoendelea bila ya kutiliwa hofu. Nilikua na muonekano nadhifu ndani ya suti kali ya nyeusi ya mtaliano brand ya 'mrkotyin' ...tabasamu langu la kuchanua la kuzuzua warembo lilifanya nipewe kipaumbele na uchangamfu pale mapokezi na kisha kukabidhiwa funguo za chumba changu.

Inno alibaki kwenye gari kwa ajili ya kupata picha mnato ya kila mtu atakayetoka mle hotelini baada ya nusu saa hadi masaa mawili mbele. Nilitaraji hata kama wanajadili ukombozi wa dunia lazma watakua wamemaliza ndani ya masaa mawili. Nimemsindikiza sana general kwenye hivi vikao vya wanasiasa, nilijua lazma wataagiza chakula ukizingatia mheshimiwa ametoka safarini atakua hajala kitu cha maana , nami niliamua kuagiza chakula, nilifahamu kutokana na ule ugeni wa ghafla sehemu ya jiko watakua hawakujipanga kwaio patakua na ucheleweshaji wa oda za vyumbani na hapo ndipo nilipotaka kuweka nongwa zangu.

Nilitoa oda iliyokuja kuletwa baada ya lisaa lizima, niliigiza kukasirika kwelikweli, dada alieleta oda alikua anaomba radhi kwa kuchelewa na kunieleza kua palikua na msururu wa oda kutokana na ugeni wa ghafla pale hotelini , niliuliza ina maana hao wageni ndio wanasababisha mimi nishinde njaa? Akanijibu nisamehe sana kakangu , hua inatokea mara chache sana , ila mara nyingi hua wanapiga simu siku mbili kabla ila leo wametushtukiza sana, ni vile tu ni waheshimiwa mawaziri na pia wanajuana na mwenye hii hotel maana na yeye yupo kwenye kikao la sivyo tungeikataa oda. Mimi mwenyewe zamu yangu imeshaisha lakini nimelazimishwa kusalia ili kuongeza nguvu.

Nikamruhusu dada aende na kumpatia dola kumi kwa ahadi ya kuja chumbani kwangu akimaliza zamu yake nina maongezi nae muhimu. Nilikua nimepata taarifa muhimu kwa mda mfupi sana ya kua pale wanakutana mara kwa mara na kwamba wapo mawaziri wengine na wafanyabiashara ambao wapo kwenye mpango wa kukitoa chama tawala madarakani, ila nilichokiona ndani ya muda mfupi ni wao kukosa umoja na kua na tamaa. Palikua na haja gani ya mrundikano wa vyama na pia hao mawaziri kuungana kumsapoti mwenzao kwenda chama kingine cha upinzani ilihali pana chama kikuu cha upinzani kinachosapotiwa na Jaji na Padre ambacho kilikua kinapigiwa chapuo kushinda, nikaja kupata hofu pengine hawa nao ni mamluki wa chama tawala ndani ya kofia ya upinzani.
 
Nitag pls

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TISA:

Mapambazuko yalinikuta nyumbani kwangu Mbezi, kwa jitihada kubwa za Inno tulifanikiwa kumdaka mmiliki wa Kilimanjaro hotel, tulikua na ushahidi wa video wa sehemu kubwa ya mambo yanayofanyika kwa siri ndani ya hotel yake chini ya usimamizi wake, binti aliyeleta chakula ambaye alikua amenieleza mengi na ziada kuhusu unyanyasaji wa kingono wanaokutana nao hotelini hapo na biashara ya ngono inayofanywa kidigitali kwa mabinti kuuzwa kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa, kwa vitisho vya kwamba ukikataa unafukuzwa kazi na kupewa sifa mbaya kiasi cha kushindwa kuajiriwa tena kwenye sekta ya hoteli, binti aliongea kwa uchungu sana, dola kumi ilifanya kazi yake kamilifu.

Niliahidi kumsaidia ili aondoke mahala hapo akiwa na ripoti safi , na ahadi ya kumtafutia kazi Zanzibar, nimeshakua na connections kadhaa kwa hiyo lilikua ni suala la simu kadhaa, binti alihoji kama mimi ni mwanausalama, nikaona si haba kujipa cheo, naaaaam...nikajivika cheo mujarabu, na kumuomba ajaribu kufanya namna awepo katika listi ya wanaoenda kutoa huduma kwa chumba cha waheshimiwa, na kwa juhudi aliyoionesha binti akatunukiwa hiyo nafasi pia kwenda kutoa huduma ya kukanda miili ya waheshimiwa, kwa siri nikampa camera ndogo mfano wa kifungo na kukichomeka kwenye blauzi yake.

Binti alifanya kazi yake yakinifu, na ilikua na msaada mkubwa kwani alitueleza jambo la aibu la mheshimiwa la kupenda kuwaingilia vijana wadogo wa kiume wanaoajiriwa hotelini hapo kama kivuli tu, ila lengo kuu hutumika kwa kazi maalumu. Chumba cha massage kilibeba siri nzito, naaam, mmiliki wa hotel alitoa macho kwa mfadhaiko baada ya kuona siri zao zikiwa nje . Kama kawaida tulimpa machaguo kadhaa, kwanza atoe vibali vya wafanyakazi wake wote wanaotaka kuhama hotelini kuanzia mda huo, tulifanya hivyo ili kuficha uhusika wa nani alirekodi ile video. Na pili , tulimwambia ahakikishe anatupa ushirikiano kwa kila vikao vinavyofuatia vya umoja wao la sivyo ile video ataikuta mtandaoni, na la tatu ni kukomesha ile biashara haramu inayoendelea pale hotelini kwake ya kutuharibia taifa letu la kesho.

Ndugu tajiri alitoa ushirikiano sana, maana ile video sio tu itamfarakanisha na washirika wake bali itachafua hoteli yake na kumshusha kibiashara. Na alijua katika siasa hakuna rafiki wa kudumu, kwa hiyo ndugu waziri asingevumilia kuchafuka na akamuacha salama, lazma angemmaliza kibiashara na hata kumuua. Hakua na machaguo mengi yaliyobaki, tulimwambia tutampa nafasi ya pili kama tu atatupa ushirikiano wa kutosha. Ana siku mbili za kuchagua kua na sisi au kumlinda waziri, ila tulimuacha na tafakuri ya kwamba kama tulifanikisha waziri kuahirisha ziara ya nje na kumfikia hadi hotelini, basi hata yeye hayupo salama, na tunapo pa kuanzia kumuandama, video chafu mikononi mwetu...msichana alikua smart maana alihakiki vitu vichache vitakavyothibitisha kwamba ile video ilichukuliwa hotelini hapo vinaonekana kwenye video ikiwemo mashuka, kadi za kufungulia mlango na simu ya mezani yenye logo ya hotel.

Tulimpa namba maalumu ambayo haiwezi kufuatiliwa na kujulikana inatumika mahala gani, ya kutuma ujumbe pale atakapopata taarifa yenye mashiko, kwa utaratibu uleule aliokuja nao wa kuwekwa kwenye buti, alirudishwa hadi katika ufukwe wa Coco Beach akapunge hewa kidogo, kukaa kwenye buti na joto la dar si mchezo. Hatukumuacha hivihivi, tulimpa kichapo cha dakika kadhaa kufidia ufedhuli wa kuharibu vijana wetu wa kizazi kijacho, kwa ahadi ya kuwafidia vijana wa watu na wale mabinti waliodhulumiwa utu wao kwa kuwapa ongezeko la pesa wakati wa kuwalipa stahiki zao, na kuahidi kututumia stakabadhi za malipo, tuliahidi kutomuandama sana kama ataahidi kutoenda kinyume .

Tayari tulishaupata mtandao mzima wa bwana Padre na washirika wake, Hadi wakati huo nilikua na hakika kua tumemtangulia general kwa sehemu kubwa sana, tulifanikiwa kumfahamu rafiki wa general kupitia maadui zake. Maana mtandao mzima wa akina Padre walikua wanafanya kazi chini ya mgombea wa upinzani mwenye ushirika na waziri anaekaribia kumaliza muda wake ambae yupo mbioni kuhama chama....tuliona ni wakati muafaka wa kujaribu mitambo yetu .....
 
SEHEMU YA KUMI:

Kupitia maelezo na ushahidi wa video toka kwa bwana tajiri mmiliki wa Kilimanjaro hotel, tulipata taarifa nyingi sana zinazomuhusu ndugu mgombea anaemaliza muda wake, sio tu kuhama chama bali alitakiwa apambane kufa na kupona ili aingie ikulu. Alitakiwa ahakikishe anaanzisha maadamano ya kupinga matokeo ya chama kitakachoshinda kwa kuwahonga vijana pesa ili waingie barabarani kufanya machafuko.

Malengo yao makubwa ni kupata ushawishi mkubwa wa baadhi wa wanajeshi wenye tamaa, kuligawa jeshi kwa ahadi lukuki ya kwamba wamsimike yeye kama Raisi baada ya vuguvugu la uchaguzi litakaloacha wananchi wengi wa Tanzania wakimbizi. Na pia wameahidi kumpa mdhamini umiliki wa eneo kubwa sana la uzalishaji wa dhahabu ikiwemo Geita kwa namna atakavyowasaidia kufika ikulu.

Wadhamini waliamua kucheza karata muhimu sana, 'divide and rule', walijua nguvu ya machafuko katika siasa, waliona fursa katika nchi ya Kongo. walishachoshwa na maigizo ya amani ya Tanzania. Naijua Vita, nimeishiriki, nimeiishi, sikua tayari kuona taifa la kupendeza kama Tanzania linaingia kwenye migogoro kwa tamaa za wachache.Tanzania imenipa mahala naweza kupaita nyumbani, nina mamia ya ndugu zangu wanyarwanda na Waburundi waliostirika baada ya kukimbilia Tanzania. Kwa pamoja na ndugu yangu Inno tuliamua kua wazalendo, niliamua kuchagua upande sahihi kwa wakati huo.

Nilikua na ushahidi wa kutosha , na mashahidi wa kutosha ambao walikua kwenye himaya yangu bila ya wao kujijua . Kwa msaada wa ndugu tajiri wa hotel, niliomba appointment ya kuonana na mgombea aliepita kupitia chama tawala. Nilihitaji ampe mwaliko pale hotelini kwake, na ahakikishe kua hakuna mshirika wake atakayetambua juu ya kikao changu na ndugu mgombea.

Siku ya makutano na mgombea ikawadia, kama kawaida tulikua pamoja na ndugu yangu Inno. Tulishafika hotelini masaa manne kabla ili kuona kama kutakua na aina yoyote ya usaliti kwa upande wa mmiliki wa hotel. Nilijua lazma atakua na hofu kuwasaliti wenzie na pengine angeamua kutuuza. Baada ya kuhakiki kua palikua na amani zote, nilijongea katika chumba husika, nikiwa makini na camera za ulinzi za pale hotelini, kofia yangu ya pama ilinisaidia kuficha uso wangu kwa namna fulani. Nilibadilika kutoka muonekana wa siku za nyuma wa kijana mwenye muonekano nadhifu, hadi kua kijana makini mwenye muonekano wa katatanisha kiasi.

Kwa tahadhari nilikifikia chumba alichokuwepo mgombea, Inno alikua garini pamoja na bwana tajiri, tulifanya hivyo ili kuhakiki usalama wangu, wanasiasa hawaaminiki, kukuuza ni dakika sifuri, bwana tajiri kushirikiana na wanasiasa kwa mambo mengi tayari kunamfanya kua kwenye kundi la watu wasioaminika. Inno alimhakikishia kua hatodhurika, ila usalama wake utategemea na usalama wangu kule ndani.

Nilikifikia chumba cha bwana mgombea, nikagonga na mlango ukafunguliwa na mgombea mwenyewe, katika sharti nililotoa ni kumkuta mgombea akiwa peke yake. Nilipenda ujasiri wake na kuona nia ya dhati ya kuyavaa mashindano. Kwa macho ya udadisi nilifanikiwa kugundua kivuli kwenye mlango wa maliwato. Nilikaa kwa utulivu, kisha nikamuomba mheshimiwa mgombea amuamuru mlizi wake binafsi atupishe, sipo hapo kumdhuru. Kama ningekua na nia ovu nisingehitaji usaidizi wa mmiliki wa hotel maana ingenifanya nitambulike mapema.

Ndugu mgombea alikua mtu wa kutabasamu, akamuamuru mlinzi wake atupishe, mlinzi , kipande cha mtu kilichokosa umakini akatoka maliwato na kwa jicho la hasira akaniangalia na kuamua kutupisha, hakwenda mbali sana, alisimama nje ya mlango wa kile chumba, niliona si haba naweza anza mazungumzo yangu.

Nilikua na nakala ya kila ushahidi nilioukusanya, nilitunza nakala halisi mahala ambapo ni mimi na Inno ndio tunafahamu. Mheshimiwa akanimiminia kinywaji kwenye bilauri, akanywa kisha akanipatia, nadhani alijua tu nafahamu kua biashara ya kuuza siri haina kuaminiana. Nikampatia nakala za video pamoja na picha , na sauti za kurekodi za kila kikao kilichofanyika hotelini hapo. Nikamwambia sipo hapo kuuza siri, bali nahitaji ajira ya kudumu ya kua mlinzi wake binafsi, na sipo peke angu, bali tupo wawili na mwenzangu yupo mahala si mbali sana na hapa hotelini akisubiria majibu toka kwangu.

Mheshimiwa alinitazama kwa tahadhari, akaniuliza nimemfanyaje huyu mzee tajiri hadi akawasaliti wenzie, nikamwambia hayo ni makubaliano yangu na tajiri kua sitosema, nilihitaji azingatie ajenda za kikao chetu. Mheshimiwa mgombea akanambia kua anajua anapigwa vita na wenzie wa chama chao ila hakufahamu ni kwa ukubwa wa kiwango kipi. Tulipeana mikono na kuniambia kua atawasiliana nami atakapokua tayari, ulinzi wake unafata utaratibu maalumu lakini kwa namna nilivyokusanya ushahidi ataona namna gani tutafanya kazi.

Kwa tahadhari ileile niliyoingia nayo nikaitumia kuondoka hotelini hapo, hata Inno hakujua nilitoka mda gani. Niliingia chumba cha kubadilisha nguo za wafanyakazi wa hotel na kuvaa mavazi ya wapishi, nguo zangu niliziweka kwenye mkoba maalumu na kutoka mahala hapo kama vile mpishi wa hotel. Nilimpigia Inno baada ya kufika kilometa kadhaa kutoka hotelini, Inno alimuachia ndugu tajiri na kunifata nilipo huku akiwa na mshangao nimepitaje lango kuu la hotel na ilihali alikua makini kuangalia kila anayeingia na kutoka hotelini hapo.
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA:

Kama tulivyotaraji ndivyo ilivyokua, mgombea wa chama Tawala aliekatwa jina kwa kura za wajumbe, swahiba wa bwana tajiri wa hotel, danga la bibie Kidawa alitangaza kuhama chama Tawala na kuhamia chama cha upinzani ambacho kilikua kinakua kwa kasi. Umaarufu wa chama cha upinzani alichohamia bwana mgombea aliesaliti kambi ulitokana na kuongozwa na mwanasiasa mahiri zao la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania aliyetimuliwa kwa kashifa ya kua mamluki wa chama Tawala.

Ile taarifa ilitukuta katika majukumu ya kila siku ya kujenga taifa, sikua nimeachana na general rasmi, wanasema waweke maadui zao karibu na marafiki zako karibu zaidi. Kwangu niliamua kucheza karata dume, hata Inno nilimuweka karibu lakini kwa tahadhari, utakuja kunielewa baadae. Sio kila jambo langu Inno alilifahamu ingawa nilijitahidi kufahamu mambo yake karibia yote. Nilihitaji ndugu mgombea wa chama Tawala achukue nchi na kuapishwa kua Raisi ndipo nimuoneshe general makali yangu.

Hadi hapo sikua na shaka kua mgombea anayemtumia general ni yule aliyehama chama na kuhamia upinzani. Nikajipongeza kwa kumzidi general kwa hatua nane zaidi. Tulipangiwa majukumu yetu kama madereva wa mgombea baada ya kupita chuo cha taifa cha udereva 'NIT'...tulipitishwa kozi ya muda mfupi ya mwezi mmoja na kuanza majukumu yetu rasmi. Vuguvugu la uchaguzi lilikua limeshika hatamu. Nafasi yangu ya udereva ilinipa muda mwingi wa kukaa na mheshimiwa mgombea, tukijadili haya na yale, majukumu ya general tuliyafanikisha kwa wakati pia maana tulikua na zamu katika kumuendesha mheshimiwa, katika kupeana zamu huko ndipo pengo lilipoonekana kati yangu na Inno lililopelekea mvurugano mkubwa baadae.

Vuguvugu lilianzia kwa Inno kupoteza mzigo muhimu sana wa general. Ilitoka kazi nikiwa njiani na mheshimiwa kuelekea dodoma kwenye ziara ya kufanya kampeni. Kutokana na namna tulipangiana kufanya kazi na Inno, kwa wakati huo alikua amebaki dar kuendelea kumla kisogo general. Niliwasiliana nae katika njia zetu za siri na kumpa taarifa ya kazi, kuna raia wa Ethiopia aliyekua anatakiwa kuingia nchini kinyemela na kufikishwa kwa general. Hadi wakati huo huyo raia alikua Kisumu nchini Kenya, mamlaka za Kenya zilikua zimepata taarifa za uwepo wake nchini mwao na ilifanyika doria ya usiku na mchana kumsaka . Tulihitajika kumvusha hadi Arusha kwa general kwa njia zozote tutazoona inafaa, kwangu nilimshauri atumie bahari kupitia Mombasa hadi dar es salaam kuepukana na ukaguzi wa mipakani.

Ni njia rahisi sana na salama ya kuvusha magendo kwa kutumia meli za mizigo, na kisha kupakua mizigo muhimu kabla ya kufika bandari ya dar, kuihamishia kwenye mitumbwi ya wavuvi na kuingia mjini kama wavuvi ambapo ulinzi unakua mdogo sana, ukaguzi na umakini unakua kwenye meli kubwa na maboti kwa angalizo la kua hakuna mzigo wa maana utakaopita baharini kwa njia tofauti na hiyo.

Nikiwa katika chumba changu cha mapumziko jijini dodoma baada ya mizunguko ya kutwa ya kampeni, simu ya general iliita. Swali la kwanza ilikua kwanini simu yangu inasoma kua nipo dodoma wakati natakiwa kua Kenya nikifuatilia mzigo wake. General alinipiga kwenye mshono, sikua na jibu la harakaharaka, katika kubabaika na jibu, akaniambia uliyemtuma amepoteza mzigo wangu muhimu, nauhitaji kabla jua halijazama kesho.

Jasho jembamba lilinitoka, ama tulikua tumecheza karata dume na sasa imeturamba. Nikapambana kumpigia Inno hakua anapatikana hewani, ikiwa na maana kua Inno amekamatwa pamoja na mzigo, na kama amekamatwa, naanzia wapi kumtafuta Inno pamoja na huo mzigo, nilikua tayari kumpotezea general mazima na kuingia rasmi vitani nae, ila nafsi iliniuma maana sikua nafahamu wapi Inno alipo.

Katika vitu ambavyo sikutakiwa kukosea ni kuongeza adui mwingine kwa wakati huo, tena adui anayekaribia kushika nchi. Nilimgongea mheshimiwa mlango , bahati ikawa kwangu hakua amepumzika. Nikaomba kuteta nae mawili matatu. Nilijitahidi kumuelewesha kwa kifupi kuhusu hatari inayomkabiri Inno, mheshimiwa alinisikiliza kwa makini na kuniruhusu kwenda kumtafuta Inno kwa sharti la kurudi kazini baada ya wiki moja, hakua na maswali mengi nilishukuru kwa hilo kwani sikua tayari kujielezea sana kwake.

Kwa uchunguzi wangu wa harakaharaka niligundua kua Inno hakutumia ushauri niliomwambia, Inno aliingia Kenya kwa ndege na alikua katika jaribio la kuondoka na mzigo nchini Kenya kwa kutumia usafiri binafsi kupitia Isebania, mpakani mwa Kenya na Tanzania, uliopo upande wa kaskazini mwa Tanzania ili atokee mkoani Mara aunganishe hadi Arusha. Inno aliangalia wepesi wa safari na sio hatari iliyozungukwa na safari.

Inno alibaki kua ndugu pekee niliekua nae kwa kipindi kile, kulelewa pamoja na general ,maisha magumu ya msituni, kua na historia zenye ulinganifu kwa asilimia kadhaa, kuongea lugha moja ya nyumbani, kukosa wazazi kulitufanya tuleane. Nilikua ni kama kaka kwa Inno, alikua mdogo wa thamani sana. Hakuna kitu chochote kilichokua na thamani kwa wakati huo zaidi ya Inno, pamoja tuliamua kuukimbia mkono wa general, lakini kabla hatujapiga hatua zaidi mkono ule dhalimu ulitudaka na kuturudisha nyuma kwa kasi. Nilitakiwa kuitafuta hiyo package ya general, kwa kufa na kupona lazma Inno apatikane pia.

General alimtuma Tolu na jamaa mwingine aliyeitwa gody kwa ajili ya kuongeza nguvu, kitendo Cha kuambiwa kua Tolu atakuwepo kwenye hio 'rescue mission' kilinipa hofu, Tolu ni mtu hatari sana, hatokei kwa misison za kitoto, kwa akili ya kujiongeza nikajua kua Kenya kimenuka, nami sikwenda kitoto, nilijikoki kadri niwezavyo na kuanza safari yangu ya kufa na kupona kwenda kumsaka ndugu yangu wa ukubwani, bwana Innocent.
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI:

Niliingia Mombasa saa kumi na mbili asubuhi, niliamua kusafiri alfajiri sababu ya kukwepa doria, magendo mengi yanapita usiku wa manane, na hivyo kufanya msako wa mara kwa mara baharini mida ya usiku kwa askari wapenda rushwa, nilikua nimebeba silaha nzito kwahiyo nilitakiwa kutumia akili ya ziada kuziingiza Kenya. Nilichepuka kilometa kadhaa kabla ya kuingia bandari ya Mombasa na kuvusha mzigo kwa kutumia mtumbwi hadi Kwale mjini.

Kwa kutumia gari ya kukodi, na kwa msaada wa jamaa aliyenivusha, hawa ni wavuvi wa mchongo, maisha yao wanayaendesha kwa kuvusha magendo kwa asilimia kubwa, uvuvi ilikua ni geresha tu, nilifanikiwa kupata gari ndogo ya kubebea samaki,tulijaza silaha zangu kwenye sanduku maalumu la mbao na kisha kulitanguliza mbele, ikifuatiwa na shehena ya samaki iliyokua kwenye sanduku maalumu lililojaa mabarafu, safari ya kuitafuta Kisumu ilianza.

Nilikua nimewasiliana na kina Tolu kwa code maalumu, hatukutaka kuuza mission maana hadi wakati huo tulijua doria itakua kubwa kusaka washirika wa Inno. Aliekamatwa ni kiongozi hatari wa kundi la vuguvugu nchini Ethiopia aliekua anatafutwa na mamlaka za nchi hiyo. Serikali ya Kenya ilikua inamtaka pia maana jamaa alihusika sana kwenye uuzaji wa silaha na biashara nyingine za magendo ukanda wa Africa Mashariki. Isingekua umuhimu wa Inno kwangu ningeacha tu jamaa akavune alichopanda, nimeshuhudia jinsi biashara ya silaha inavyofanywa kinyambisi na kujaribiwa uzito wa silaha na ubora wake kwa kufumua vichwa vya mateka wa vita, ila sikua nimemalizana na general, acha nifanye anavyotaka.

Niliingia Kisumu usiku sana, tulikua njiani kwa zaidi ya masaa kumi na tano, niliwakuta kina Tolu kwenye kijumba chakavu nje kidogo ya mji wa Kisumu panaitwa Muhoroni. Kwa msaada wa mwenyeji wetu ambae alishaanza kufuatilia lile sakata, tulifanikiwa kupata mawili matatu juu ya taarifa za kutekwa kwa Inno.

Kwa taarifa tu za juu juu ni kua kesho ndio siku ambayo Inno na yule jamaa wa Ethiopia walikua wanasafirishwa kwenda kukabidhiwa kwa mamlaka za Ethiopia. Ilikua ndio nafasi pekee ya kuwaokoa na ilikua ni mission ya hatari sana, tulitakiwa kulala pale hadi majira ya saa kumi alifajiri , nikawaambia hapana, zege halilali, tunaondoka mda huohuo kuweka doria mpakani, tukisubiri masaa yakatike lazma nao watatanguliza watu wachache wa kusafisha njia, itakula kwetu.

Nilichojaaliwa ni uwezo wa kujenga hoja, hatukua na cha kupoteza ,ni heri kuwahi kuliko kuchelewa, tukaamsha hadi mpakani. Tulitafuta sehemu ya kuweka kambi kilomita chache kabla hujafika mpakani, eneo la mpakani liliathiriwa kwa kiasi kikubwa na ukame, palikua na vijichaka vya kusuasua, tulivaa mavazi meusi ambayo yangetubeba na muonekano wa giza, pamoja na kujifunika mashuka maalumu yenye muonekano wa udongo wa mahala pale, hayo mashuka tulipatiwa na mwenyeji wetu ambaye huyatumia wakati wa kuvuka mpaka.

Baada ya masaa manne tuliona gari ya jeshi kwa mbali, wote tukaangaliana, kwa hesabu za harakaharaka yalikua yamebaki masaa mawili mbele ili msafara upite, ikimaanisha kua nilikua sahihi kuwaza kuhusu kutumwa wasafisha njia, tulikua tayari kwa lolote. Lile gari la wanajeshi lilipita kwa kasi, kwa mbele likasimama na wanajeshi baadhi wakashuka , wakasambaa na kuanza ukaguzi kwa maeneo ya karibu na mpaka, kwa kile ambacho hatukukitegemea jamaa waliweka kambi eneo la mpakani. Hadi wakati huo pakafanya idadi ya wanajeshi kumi na nne pamoja na wale nane tuliowakuta .

Niliweka sawa silaha yangu aina ya DENEL NTW - 20, silaha adhimu toka South Africa, ina uwezo wa kudungua hadi kilomita 1 na zaidi, inategemea na uwezo wa shabaha yako, ugunduzi wa bwana Denel Mechem, niliona na wenzangu wakiandaa silaha zao, palikua na bunduki aina tano tofauti pale, mabomu ya kurusha na mabomu ya moshi, kwa idadi jumla tulikua watano, watatu toka Tanzania na wawili tuliwakuta Kenya.

Masaa mawili mbele tukaona msafara wa magari mawili ya jeshi, hapo ndio nilielewa kwanini general alihitaji mimi na Tolu tuwepo. Tuligawana makundi mawili, nilibaki na wale wakenya wakati Tolu akisogea mbele na Gody kwa mtindo wa kutambaa na tumbo. Tungeweza kuwamaliza wale wanajeshi mapema waliotangulia , ila ukimya wao wakati msafara unafanya mawasiliano kusogea mbele zaidi ungefanya root ibadilike, au siku zisogee mbele na ulinzi uzidi kuimarishwa, hatukua na muda zaidi wa kupoteza , ilikua ni lazma tumalize mchezo siku ilele kabla hapajakucha.

Tulisubiri msafara usogee ndani ya kipimo changu , kwa kutumia kifaa cha kuweza kuona mbali, niliweza kuona mateka wawili wakiwa wamefunikwa vichwa, nikafahamu kua wanaweza wakawa mizigo yetu tuliyoifata. Nikajaribu kukagua wanajeshi waliobaki labda kuna namna watakua wametufanyia mchezo maana ilikua michezo yetu Burundi kubadili muonekano wa mateka kupumbaza maadui. Kwa ishara ya mwanga wa tochi mara mbili tulianza kushambulia msafara kama nyuki, risasi zilitembea kama mvua, ilikua ni ghafla mnoo, mimi nilicheza na kuwapunguza waliokua wamening'inia kwenye magari , nikafuatia na madereva wa gari zote mbili, wanajeshi wengine waliruka kwenye magari na kupambana kuzuia risasi zisiwafikie mateka.

Tolu na Gody kwa pamoja waliwashambulia wanajeshi waliokua mpakani, ilikua ambush ya kushtukiza na hawakuitegemea maana walishasafisha njia kwahiyo walikaa kizembe wakisubiri kukabidhi mzigo. Ndani ya dakika kumi risasi zilitembea kama mvua, Kuna mwanajeshi wa Kenya alituotea na bomu la kurusha , mmoja kati ya vijana tuliyekua nae akaliwahi na kulirusha mbali , lililipuka na kufanya mtikisiko wa kuogofya, nilishamalizana na wale waliotakiwa kudunguliwa, tulilisogelea gari lilikuwepo mateka kwa mtindo wa kupeana migongo ,hiyo inasaidia kujilinda zaidi na adui.

Tulifanikiwa kuwaokoa mateka na kuwamalizia wanajeshi wawili waliokua wamejeruhiwa na risasi, mmoja alikua anapambana kufanya mawasiliano ya kupata msaada wa wanajeshi zaidi, nilimtwanga risasi ya kichwa na story yake ikaishia pale. Niliwaacha wale wakenya walinde package na kwenda kutoa msaada kwa akina Tolu, ndani ya dakika ishirini zaidi tukawa tumefanikisha kuweka hali ya usalama, tulijua hatutomudu kutoboa tena Kenya, tulikiwasha usiku ule ule hadi Kisumu. Kwa msaada wa mwenyeji wetu tuliwapatia Inno na yule Muethiopia huduma ya kwanza na kukiwasha hadi Mombasa kwa kutumia usafiri wa lori la mizigo.

Inno alikua anashukuru njia nzima , siamini kama umekuja kuniokoa kaka... nilijua sitokuona tena....kuna namna ya upendo niliuona kwa Inno ulinikumbusha ndugu zangu Rwanda, Ni jinsi gani unapata faraja kuonana na nduguyo ambae hukutaraji kumuona tena. Kwa Mara ya kwanza nilitamani kurudi Rwanda. Kwa namna ileile niliyoingia Mombasa niliitumia pia kuondoka nchini Kenya maana nilijua mipakani kutakua hapafai wakijua tutafanya kosa lilelile alilofanya Inno. Hawakujua wanadeal na mtu wa aina gani. Ile siku ndio lilitoka jina la 'Godfather'...."master of missions, master of plans and master of actions"
 
Back
Top Bottom