SIMULIZI: "The Godfather"

SIMULIZI: "The Godfather"

SEHEMU YA KUMI NA TATU:

Tuliingia jijini salama, general aliamuru Tolu ahakikishe kua Inno na 'package' wanafika salama Arusha, sikua na shaka na utendaji wa Tolu. Tulifanya utaratibu wa kuondoka dar kwa kutumia usafiri binafsi, ilitafutwa gari maalumu ya kubeba mizigo iliyokua na uwazi wa kutosha kulala mtu mzima katikati ya bodi ya nyuma na sehemu ya dereva ambayo huwezi kuiona kwa jicho la kawaida. Nyuma ya bodi ilipakiwa shehena ya magodoro, mzigo ulijaa ukashona, jamaa tulimuwekea mtungi wa hewa kwa ajili ya kupumua, ngoma ikalala hadi Arusha.

Nilijipa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurudi rasmi kibaruani kwangu kwa mheshimiwa. Nilikua natoka matembezi ya hapa na pale, kwa mbali nikaona kuna pikipiki inanifungia mkia, sikua na hakika sana ikanibidi kufanya kitu. Nilikua kwenye foleni nikitokea kurasini kuelekea Mbezi, wakati nakaribia mataa ya Tazara nikafanya jaribio la pata potea, nilisubiri taa zikaruhusu nikakunja kulia kama naelekea mjini, nikaona jamaa wa pikipiki akijihakiniza kukunja kona kunifuata pia, nadhani alijua nitaendelea kutumia Mandera road. Nikanyoosha mbele kidogo na kuingia kulia nikaweka kambi zilipokuwepo ofisi za NHIF zamani.

Jamaa hakua smart, alinifata na kunipita na kwenda kuweka kambi kwa mbele, hadi hapo nikajua tu jamaa ananifatilia. Nilishuka kwenye gari na kuingia ndani ya zile ofisi za bima, ikawa bahati kwangu nikakuta watu kadhaa wapo kwenye utaratibu wa kupewa huduma, nikapoa kwa muda kwenye benchi nikisubiri kuona jamaa atafanya nini.

Baada ya kama dakika kumi nikaona Ile pikipiki inajongea mahala nimeegesha gari yangu kwa tahadhari , na kwa haraka akainama na kuweka kifaa na kupotea kwa kasi. Sikua na shaka ya kua atakua ametumwa kuniwekea kifaa cha kufuatilia mienendo yangu, ila nikajipa angalizo . Niliita bodaboda na kupotea mahala pale, nilipiga simu garage maarufu iliyopo Tabata na kuwaomba wakanichukulie gari langu kwa ajili ya marekebisho madogomadogo ili nimudu kulitumia safarini.

Nilisubiri hadi usiku wa saa nane na kuamua kua utakua muda muafaka wa kulifata gari langu, napenda utulivu na pia ulikua mda sahihi kuhangaishana na wanaotaka kuhangaika nami maana hapana foleni na pia itaepusha kudhuru raia wema wasio na hatia. Ile garage ilikua na mlinzi mzee sana, kwa mda nimefika alikua amelala hana habari, nikaona nisimsumbue bali nimuongezee masaa ya kulala kwa kumpulizia dawa ya usingizi, wazee sio watu wakusumbuliwa jamani, na kwanini wanaajiri walinzi wazee kulinda mali za mamilioni, sijawahi kufahamu.

Niliingia na kukagua kile kifaa kama bado kipo, nikakuta bado kipo na kinafanya kazi, gari yangu haikua imefanyiwa chochote hadi muda huo, nikaitoa na kuongoza uelekeo wa Kawe beach. Nikiwa maeneo ya Mwananchi nikaona kuna gari inakuja uelekeo wangu kwa kasi, nikanyoosha hadi Ubungo mataa jamaa bado wapo na mimi, nikaingia kulia kuitafuta Mwenge jamaa bado wanakomaa ,nikasema kumekucha....

Magari yalikua machache sana barabarani hivyo kufanya utulivu kiasi na kuonana kwa umakini, walijua kufata mchoro wangu na waliingia bila hodi, ilikua ni suala la muda kuawaambia karibu. Maeneo ya beach yalikua tulivu sana kwa muda huo wa saa nane, niliegesha gari yangu gizani mahala ambapo haliwezi kuonekana kwa urahisi sikuhitaji usumbufu na walinzi.

Jamaa waliweka kambi umbali wa kilometa moja toka nilipokuwepo, kwa tahadhari nikashuka na kurudishia mlango wa gari, nikajificha chini ya gari na kutulia. Dakika chache nikaona kivuli kikijongea mahala nilipokuwepo, kikifuatiwa na kingine, kwa msaada wa mbalamwezi nilihesabu vile vivuli na kuona idadi ya watu wanne. Niliwasubiri hadi wasogee karibu, mmoja wao akafungua mlango wa gari upande wa dereva, najua alihamaki kuona patupu, kabla hajafungua mdomo nilimvuta uvunguni , pigo moja la nguvu lilitosha kumnyamazisha.

Mwenzie alikuja kwa kunyata huku akiita jina la yule aliyetangulia, hakujua kua mwenzake alikua anawasaidia malaika kuchochea kuni ahera, maana kwa hizi mishe zetu pepo tutaisikia tu. Alikaribia gari lakini katika kusita , sikumchelewesha nikamchana na kisu mshipa unaounganisha unyayo na mguu, alipiga yowe na kuanguka kama zigo, nikamshindilia bisu la shingo na kumuacha akitapatapa na roho yake.

Waliobaki wakawa katika kuhaha, nilichomoka uvunguni mwa gari kwa kasi ya umeme, nikamuotea mmoja wa wale mabwana kwa risasi ya kifua, yowe ya uchungu lilimtoka, aliyebaki alijaribu kutimua mbio, sikumpa nafasi ya kupiga hatua, nilimuwahi na ngumi mbili matata zilizomfanya atepete , nikawasachi na zaidi ya simu na bunduki nne hawakua na chochote. Sikua na muda wa maziko maana kwa ile milio ya risasi nilijua itakua imewashtua walinzi, acha polisi wetu wapate cha kuwaweka bize kwa siku mbili tatu, niijua hawawezi pata chochote maana bunduki niliyotumia ilikua ya magendo,nikambeba majeruhi wangu na kupotea eneo hilo baada ya kuing'oa kile kifaa na kukiweka kwenye mfuko wa suruali wa mmoja wa zile maiti.

Nilimfikisha mgeni wangu Mbezi na kumfungia chumba maalumu, zile simu nilizizima kwa hofu ya kama zitakua zinasoma location. Nilirudisha gari na kumkuta babu yangu mlinzi akiendelea kukoroma, nilihakiki kama patakua na chochote cha kutia shaka kwenye gari nikaona amani asilimia mia. Nilimpulizia dawa nyingine babu ya kumuwezesha kupata ahueni ya usingizi baada ya lisaa lizima ambayo itamfanya akiamka zaidi ya kuhisi uchovu hakuna tofauti yoyote ataiona mwilini mwake. Nilipotea maeneo ya garage Kama sijawahi kuwepo, kwa usafiri wa pikipiki niliyoisimamisha njiani nilimudu kufika kwangu Mbezi mapema kabla hapajakucha.
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE:

Sikua na papara na mgeni wangu, nilimuacha apate usingizi wa kutosha, nilifanya majukumu yangu ya asubuhi ikiwemo mazoezi, usafi binafsi na wa nyumba . Majira ya saa mbili kamili nikaingia chumba nilichomuhifadhi jamaa. Alikua kaamka anahangaika kujitoa kwenye kiti nilichomfunga, nikamwambia usijihangaishe ndugu, 'save your energy , you might need it'.

Jamaa aliniangalia kwa hofu, nadhani ile picha ya ufukweni bado alikua nayo kichwani, alikua anawaza nitakachomfanya au sijui alimkumbuka mwanamke wake kua hatomuona tena, mi hayanihusu hayo. Niliandaa zana zangu za kazi , na vifaa vya kumfanyia bianadamu usafi wa mwili. Nilimuinua jamaa na kiti chake akawa anaangalia dari, nilichukua kitambaa na kumfunika mdomo,nilichukua mafuta ya petrol kwenye dumu la lita tano na kumshindilia mdomoni.

Jamaa alitoa macho kama anakata roho, nilimpa dakika tatu za kuvuta hewa, kisha nikarudia zoezi kwa dakika moja na zaidi. Nilipomuachia na kuonesha dalili ya kutaka kurudia kwa mara ya tatu jamaa huku akipambana kupumua kwa kasi na akiwa ametoa jicho hadi sentimeta ya mwisho akanionesha ishara ya mkono kua niache kumtesa. Mimi ni nani nisiwe msikivu kwa kiumbe wa Mungu, nikavuta kiti nikamwambia tuanze maongezi yetu.

Nilimwambia jamaa sidhani kama itafaa kujitambulisha, hadi mnanifuatilia nadhani mnanifahamu, ila ingekua vyema kama ungejitambulisha. Akanambia kua wametumwa na bwana Juma ,mlinzi binafsi wa mgombea wa Uraisi, wametumwa kuniteka ili niwaambie wapi nilipokua wiki nzima. Nilijikuta nimecheka kwanza, niliona jicho la husda la bwana Juma tangu siku ya kwanza naenda kuongea na mheshimiwa hotelini, nilikua na mtafutano wa nafsi wa kufahamu iwapo bwana yule ananichunguza kwa matakwa yake binafsi au ya bosi wake?

Nilimwambia anieleze waliyoyafahamu kuhusu mimi hadi wakati huo, nilikua nimeshachunguza zile simu na kuzikagua kama zitakua na kifaa chochote cha kufuatilia mahala tulipo,sikuona chochote, baada ya kuona hazina madhara, niliziacha wazi ili nione kama naweza kung'amua chochote, hadi muda huo hakuna simu iliyoita katika zile simu, nikagundua kua zile zilikua simu maalumu kwa ajili ya ile kazi tu, jamaa alijipanga kupambana na mimi, ni vile tu hakua smart since day one.

Kupitia mateka wangu niligundua kua hawakua wamefika mbali katika upelelezi wao, na hata ile kuniotea mara ya kwanza ni kwa sababu jamaa anajua aina ya gari natumia na kwa kushirikiana na askari wa barabarani aliweza kuninasa kwenye rada zake. Kwa hilo nilimpongeza, ila nadhani angeokoa maisha ya vijana wake kama angetumia askari haohao wa barabarani kuniweka kizuizini na kunipata kirahisi, maana katika vitu nilikua najiepusha ni kuichokonoa serikali waziwazi. Ndio maana nachelea kusema jamaa hakua smart kabisa.

Niliwasiliana na jamaa yangu wa garage na kumwambia kua nahitaji kubadilisha rangi ya gari yangu. Jamaa hakua mtu wa maswali, niliifata gari jioni ya siku hiyo, nilikua na plate number za aina tatu tofauti pale nyumbani, nikabandika mojawapo na kuipa gari yangu muonekano mpya. Nilishaona nuksi za ile gari na hivyo nikaona ni wakati muafaka wa kuiiuza na kutafuta gari nyingine. Kwa msaada wa jamaa yangu wa garage niliuza ile gari na kununua gari nyingine aina ya Noah, niliona itanifaa kwa mishemishe zangu.

Akuanze mmalize, nilimalizana na mateka wangu na kwenda kumtupa bonde la mto msimbazi. Jioni yake ilinikuta Hongera bar, bar moja maarufu kwa kipindi kile pale Sinza. Kwa kiasi nilikua nimeifahamu ratiba ya mgombea uraisi ,alikua ni mtu wa ibada sana, siku ya ijumaa huitumia kwa ibada na kukutana na viongozi wa kidini pamoja na familia. Kwa vyovyote vile bwana Juma atakua anajipongeza kwa ratiba ngumu ya wiki nzima. Ijumaa ilikua mapumziko ya bwana Jumaa, ingawa alikua kijana wa kiislamu lakini kwake ijumaa ilitumika kufanya ufuska wa kutosha na kuwatambishia watu jinsi alivyotakata na kufahamiana na wakuu wa nchi.

Dada poa wa Sinza walijua kuitafuna pesa ya bwana Jumaa, nami niliona sio vibaya kuanzia hapo . Niliegesha gari katika garage bubu upande wa pili wa barabara , magari yalitapika utadhani sikukuu, watu walijazana kutumia pesa zao. Nilipata meza sehemu iliyojificha ambayo naweza kumuona kila anayeingia na kutoka na kumuomba muhudumu aniletee kinywaji, nilikipiga taratibu huku nikisindikizwa na mziki wa bolingo wakati huohuo nikitazama uumbaji wa Mungu, maana walipita kila aina ya warembo, kila mmoja akijaribu kunasa mawindo nami nilikua mawindoni.

Haikupita kitambo kabla sijamuona mtarajiwa wangu, alikua amezungukwa na warembo watatu, walikua wamelewa haina mfano. Niliwaacha wamelewa kwa kiasi cha kutojielewa, ilipofika saa nane usiku bwana Jumaa na warembo wake walinyanyuka kwa ajili ya kwenda kupumzika. Mtaa wa nyuma na pale bar palikua na gest bubu , nilimshangaa yule bwana kwa kuyaweka maisha yake rehani kwa kulala katika kagesti uchwara kama kile. Niliwaacha wakachukua chumba, nami nikachukua chumba kinachofuatia.

Ulevi haujawahi kumuacha mtu salama, yule bwana na wale dada poa watatu walichokumbuka ni kuingia chumbani , kurudishia mlango na kujitupa kitandani, hata mlango hawakukumbuka kufunga. Nilielewa sasa kwanini dada poa walimpenda bwana Jumaa, sasa mtu anakunywesha pombe za bure na michemsho ya kutosha na unalala mahala walau pana pangaboi na kunguni wa kuhesabu wasiokera, na hakuna anachokufanya hadi asubuhi, unaachaje kumshobokea jamani.

Niliingia mle chumbani na kumkokota bwana Juma hadi chumbani kwangu, sikutaka kuwasumbua dada zetu, majukumu yao mazito jamani. Nilimfunga bwana Juma kwenye kakiti cha mbao kalikokua mle chumbani, nilimsaidia kumvua viatu na soksi, nilimvua tisheti alilovaa na kumshindilia mdomoni, nilichukua plaizi na kuanza kung'oa kucha yake ya dolegumba , jamaa aliruka kama kang'atwa na siafu, na kutua chini kama furushi na kujikuta amevunja hadi kiti cha watu, bwana Jumaa muharibifu sana, si angeruka taratibu tuuu, ona kamtia hasara mwenye gesti sasa. Nikamsalimu yule bwana, 'Asalaam Aleykuuum bwana Jumaaa'
 
Hatari.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Come on come NANA , STORI TAMU SANA GO ON GO ON
 
Nitaandika, sijapata utulivu, halafu sijawahi katisha story labda sio mfuatiliaji wa story zangu....tutamalizia siku si mingi, mepita tu kuwasalimu
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI:

Niliingia Mombasa saa kumi na mbili asubuhi, niliamua kusafiri alfajiri sababu ya kukwepa doria, magendo mengi yanapita usiku wa manane, na hivyo kufanya msako wa mara kwa mara baharini mida ya usiku kwa askari wapenda rushwa, nilikua nimebeba silaha nzito kwahiyo nilitakiwa kutumia akili ya ziada kuziingiza Kenya. Nilichepuka kilometa kadhaa kabla ya kuingia bandari ya Mombasa na kuvusha mzigo kwa kutumia mtumbwi hadi Kwale mjini.

Kwa kutumia gari ya kukodi, na kwa msaada wa jamaa aliyenivusha, hawa ni wavuvi wa mchongo, maisha yao wanayaendesha kwa kuvusha magendo kwa asilimia kubwa, uvuvi ilikua ni geresha tu, nilifanikiwa kupata gari ndogo ya kubebea samaki,tulijaza silaha zangu kwenye sanduku maalumu la mbao na kisha kulitanguliza mbele, ikifuatiwa na shehena ya samaki iliyokua kwenye sanduku maalumu lililojaa mabarafu, safari ya kuitafuta Kisumu ilianza.

Nilikua nimewasiliana na kina Tolu kwa code maalumu, hatukutaka kuuza mission maana hadi wakati huo tulijua doria itakua kubwa kusaka washirika wa Inno. Aliekamatwa ni kiongozi hatari wa kundi la vuguvugu nchini Ethiopia aliekua anatafutwa na mamlaka za nchi hiyo. Serikali ya Kenya ilikua inamtaka pia maana jamaa alihusika sana kwenye uuzaji wa silaha na biashara nyingine za magendo ukanda wa Africa Mashariki. Isingekua umuhimu wa Inno kwangu ningeacha tu jamaa akavune alichopanda, nimeshuhudia jinsi biashara ya silaha inavyofanywa kinyambisi na kujaribiwa uzito wa silaha na ubora wake kwa kufumua vichwa vya mateka wa vita, ila sikua nimemalizana na general, acha nifanye anavyotaka.

Niliingia Kisumu usiku sana, tulikua njiani kwa zaidi ya masaa kumi na tano, niliwakuta kina Tolu kwenye kijumba chakavu nje kidogo ya mji wa Kisumu panaitwa Muhoroni. Kwa msaada wa mwenyeji wetu ambae alishaanza kufuatilia lile sakata, tulifanikiwa kupata mawili matatu juu ya taarifa za kutekwa kwa Inno.

Kwa taarifa tu za juu juu ni kua kesho ndio siku ambayo Inno na yule jamaa wa Ethiopia walikua wanasafirishwa kwenda kukabidhiwa kwa mamlaka za Ethiopia. Ilikua ndio nafasi pekee ya kuwaokoa na ilikua ni mission ya hatari sana, tulitakiwa kulala pale hadi majira ya saa kumi alifajiri , nikawaambia hapana, zege halilali, tunaondoka mda huohuo kuweka doria mpakani, tukisubiri masaa yakatike lazma nao watatanguliza watu wachache wa kusafisha njia, itakula kwetu.

Nilichojaaliwa ni uwezo wa kujenga hoja, hatukua na cha kupoteza ,ni heri kuwahi kuliko kuchelewa, tukaamsha hadi mpakani. Tulitafuta sehemu ya kuweka kambi kilomita chache kabla hujafika mpakani, eneo la mpakani liliathiriwa kwa kiasi kikubwa na ukame, palikua na vijichaka vya kusuasua, tulivaa mavazi meusi ambayo yangetubeba na muonekano wa giza, pamoja na kujifunika mashuka maalumu yenye muonekano wa udongo wa mahala pale, hayo mashuka tulipatiwa na mwenyeji wetu ambaye huyatumia wakati wa kuvuka mpaka.

Baada ya masaa manne tuliona gari ya jeshi kwa mbali, wote tukaangaliana, kwa hesabu za harakaharaka yalikua yamebaki masaa mawili mbele ili msafara upite, ikimaanisha kua nilikua sahihi kuwaza kuhusu kutumwa wasafisha njia, tulikua tayari kwa lolote. Lile gari la wanajeshi lilipita kwa kasi, kwa mbele likasimama na wanajeshi baadhi wakashuka , wakasambaa na kuanza ukaguzi kwa maeneo ya karibu na mpaka, kwa kile ambacho hatukukitegemea jamaa waliweka kambi eneo la mpakani. Hadi wakati huo pakafanya idadi ya wanajeshi kumi na nne pamoja na wale nane tuliowakuta .

Niliweka sawa silaha yangu aina ya DENEL NTW - 20, silaha adhimu toka South Africa, ina uwezo wa kudungua hadi kilomita 1 na zaidi, inategemea na uwezo wa shabaha yako, ugunduzi wa bwana Denel Mechem, niliona na wenzangu wakiandaa silaha zao, palikua na bunduki aina tano tofauti pale, mabomu ya kurusha na mabomu ya moshi, kwa idadi jumla tulikua watano, watatu toka Tanzania na wawili tuliwakuta Kenya.

Masaa mawili mbele tukaona msafara wa magari mawili ya jeshi, hapo ndio nilielewa kwanini general alihitaji mimi na Tolu tuwepo. Tuligawana makundi mawili, nilibaki na wale wakenya wakati Tolu akisogea mbele na Gody kwa mtindo wa kutambaa na tumbo. Tungeweza kuwamaliza wale wanajeshi mapema waliotangulia , ila ukimya wao wakati msafara unafanya mawasiliano kusogea mbele zaidi ungefanya root ibadilike, au siku zisogee mbele na ulinzi uzidi kuimarishwa, hatukua na muda zaidi wa kupoteza , ilikua ni lazma tumalize mchezo siku ilele kabla hapajakucha.

Tulisubiri msafara usogee ndani ya kipimo changu , kwa kutumia kifaa cha kuweza kuona mbali, niliweza kuona mateka wawili wakiwa wamefunikwa vichwa, nikafahamu kua wanaweza wakawa mizigo yetu tuliyoifata. Nikajaribu kukagua wanajeshi waliobaki labda kuna namna watakua wametufanyia mchezo maana ilikua michezo yetu Burundi kubadili muonekano wa mateka kupumbaza maadui. Kwa ishara ya mwanga wa tochi mara mbili tulianza kushambulia msafara kama nyuki, risasi zilitembea kama mvua, ilikua ni ghafla mnoo, mimi nilicheza na kuwapunguza waliokua wamening'inia kwenye magari , nikafuatia na madereva wa gari zote mbili, wanajeshi wengine waliruka kwenye magari na kupambana kuzuia risasi zisiwafikie mateka.

Tolu na Gody kwa pamoja waliwashambulia wanajeshi waliokua mpakani, ilikua ambush ya kushtukiza na hawakuitegemea maana walishasafisha njia kwahiyo walikaa kizembe wakisubiri kukabidhi mzigo. Ndani ya dakika kumi risasi zilitembea kama mvua, Kuna mwanajeshi wa Kenya alituotea na bomu la kurusha , mmoja kati ya vijana tuliyekua nae akaliwahi na kulirusha mbali , lililipuka na kufanya mtikisiko wa kuogofya, nilishamalizana na wale waliotakiwa kudunguliwa, tulilisogelea gari lilikuwepo mateka kwa mtindo wa kupeana migongo ,hiyo inasaidia kujilinda zaidi na adui.

Tulifanikiwa kuwaokoa mateka na kuwamalizia wanajeshi wawili waliokua wamejeruhiwa na risasi, mmoja alikua anapambana kufanya mawasiliano ya kupata msaada wa wanajeshi zaidi, nilimtwanga risasi ya kichwa na story yake ikaishia pale. Niliwaacha wale wakenya walinde package na kwenda kutoa msaada kwa akina Tolu, ndani ya dakika ishirini zaidi tukawa tumefanikisha kuweka hali ya usalama, tulijua hatutomudu kutoboa tena Kenya, tulikiwasha usiku ule ule hadi Kisumu. Kwa msaada wa mwenyeji wetu tuliwapatia Inno na yule Muethiopia huduma ya kwanza na kukiwasha hadi Mombasa kwa kutumia usafiri wa lori la mizigo.

Inno alikua anashukuru njia nzima , siamini kama umekuja kuniokoa kaka... nilijua sitokuona tena....kuna namna ya upendo niliuona kwa Inno ulinikumbusha ndugu zangu Rwanda, Ni jinsi gani unapata faraja kuonana na nduguyo ambae hukutaraji kumuona tena. Kwa Mara ya kwanza nilitamani kurudi Rwanda. Kwa namna ileile niliyoingia Mombasa niliitumia pia kuondoka nchini Kenya maana nilijua mipakani kutakua hapafai wakijua tutafanya kosa lilelile alilofanya Inno. Hawakujua wanadeal na mtu wa aina gani. Ile siku ndio lilitoka jina la 'Godfather'...."master of missions, master of plans and master of actions"
Maua Yako nana yaan nasoma najiona mm ndio godfather kumbe pisi Kali tu
 
Back
Top Bottom