SIMULIZI: "The Godfather"

SIMULIZI: "The Godfather"

SEHEMU YA NNE:

Nilipewa maelezo machache na kunifanya niwe na picha ya kile kinachokuja mbele yangu, jioni ya ile siku ilikuja gari na kunichukua hadi makazi mapya yaliyopo Monduli nje kidogo ya manispaa ya Arusha. Palikua na nyumba kubwa yenye mahitaji yote muhimu ikiwemo chumba cha mazoezi yaani gym na uwanja mkubwa wa mpira.

Kulipokucha asubuhi na mapema, nilikuja kuamshwa na kuambiwa natakiwa uwanja wa mazoezi ndani ya dakika kumi, mi ni mwanajeshi kamili kasoro gwanda, dakika kumi ni nyingi sana, dakika sita zilinitosha kujiandaa na kufika uwanja wa mazoezi, tukifanyishwa mazoezi ya kawaida ikiwemo kukimbia, baada ya mda wa dakika kadhaa akaja mwalimu rasmi wa mazoezi, tukipigishwa zoezi la kufa mtu, ni push ups za kutosha hadi unatamani kulia, mazoezi ya jeshi yalinisaidia kwa kiasi fulani kwenda sawa na program ya mwalimu.

Baada ya uwanjani tukahitajika kuingia gym kwa ajili ya ukakamavu zaidi, ikifuatiwa na shule ambayo ilikua ni mtindo wa brush, tulifundishwa mada muhimu tu ambazo zitatusaidia katika harakati zetu, kumbuka niliingia jeshi la waasi nikiwa na miaka tisa kwahiyo ile nafasi ya kusoma ni kama sikuipata, ingawa kwa juhudi binafsi wakati nipo Burundi nilipambana nikajua kusoma ,kuandika na kuongea lugha zaidi ya tano, nilijua ipo siku zitanifaa mbeleni.

Mafunzo yaliendelea ikiwemo mafunzo ya silaha ikianziwa na pistol hadi sniper rifle, hilo somo kwangu lilikua ni marudio maana nimeshafanya field katika ushiriki wangu wa vita Rwanda na Burundi, hapa yalikua ni marudio tu. Ilikua ni lazma hayo masomo yatolewe maana pale palikua na mchanganyiko wa watu mbalimbali na background mbalimbali.

Baada ya mafunzo yote hayo yalifutia mafunzo ya mapigano, hapo sikua mwenyeji sana, kule nilipotoka bunduki ilitumika kuokoa mda, ni nadra sana unakaribiana na adui kwa sentimeta chache za kukuwezesha kurushiana ngumi, mara nyingi tulikua tunafanya ambush kwaio bunduki ilikua first priority. Nilikua makini katika hili somo maana nilihitaji kujifunza kila kitu kwa umakini ili niweze kutimiza malengo yangu.

Baada ya miezi minne ya mazoezi magumu na masomo makini tulifanikiwa kumaliza. Tulianza arobaini ila tuliomaliza tulikua kumi na nane. Siku ya kumaliza ndio tulifanikiwa kumuona tena General, na yule jamaa kipande alienifata kambini ambae nilikuja kufahamu kua jina lake anaitwa Tolu. Waliobakia katika idadi ya arobaini wapo waliopata majeraha wakiwa katika mazoezi na kulazimika kuahirisha hadi wakati mwingine na wanne walitaka kutoroka wakaishia kulambwa risasi.

Kazi yangu ya kwanza nakumbuka ilikua kwenda kumteka tajiri mmoja hivi mkubwa tu hapa nchini na kuamuliwa kua anatakiwa kufikishwa nchini Congo. Kazi yangu haikuniruhusu kuuliza maswali ,nilikua a delivery guy...'pick and deliver mission'...hakuna maswali. Tulifatilia ratiba ya yule mdosho tukaipata , tulimtegea wakati anatoka bank tukamlia ambush, zilikua gari mbili zinazofanana zikamfungia tela moja mbele nyingine nyuma. Jamaa alikua na bastola kwenye gari, akawa anahangaika kuikoki, kabla risasi hazijafika kwenye chemba tulikua tushamfikia, mwenzangu niliekua nae akampiga dereva na kitako cha bunduki, ilikua missions ya 'pick and deliver' ....no casualties, one witness wa kufikisha taarifa kwa wahusika.

Tukamzuga na madawa ya kulevya jamaa akazima, tukamtia kwenye buti huko asituletee usiku, tukasepa na jamaa hadi Congo, tulikua na vitambulisho halali vya kitanzania , kadi za benki hadi kadi za kupiga kura. Kwa kipindi hicho nilikua nafahamika Kama Jonas Mkumbi, mzaliwa wa Singida. Ile mission ulienda poa, swala la jamaa atarudi vipi Tanzania na nini walimfanya halikua langu, nilitakiwa kurudi mara tu baada ya kumfikisha sehemu husika.

Nilikua na umri wa miaka kumi na saba lakini yale mazoezi yalinipa muonekano wa kijana wa makamo. Niliendelea kupokea kazi na kuzifanya bila ya kuhoji maswali , kwa zaidi ya miaka nane nilifanya kazi za bwana General za kuteka watu na kuwafikisha mahala husika, tuliteka wanasiasa, wafanyabiashara, watu wa mataifa ya nje na hata watumishi wa Mungu. Kama kawaida, nafanikisha mission nachukua changu, siulizi maswali. Nilifanikiwa kujiimarisha kiuchumi na kua sehemu nzuri zaidi, nilijua mwisho wa zile kazi hua ni kupotezwa katika mazingira ya kutatanisha kwa hiyo sikukaa kizembe, nilipambana nikatengeneza cycle yangu ninayoiamini .

Kwa mara ya kwanza nilitamani kua huru, na ili umtangulie maarifa adui yako lazma ujue taarifa zake zote. Nilikua nimedhulumiwa utoto wangu na haohao kina general, sikukubali waudhulumu ujana wangu na utu uzima wangu...nilianza taratibu kumchunguza general, na kwa kuanzia nilihitaji kujua ni nani wapo kwa cycle yake, nilipanga kuanzia hapo.
 
Baada ya kichapo cha IHEFU...basi tuendelee...
 
SEHEMU YA TANO:

Kitu cha kwanza ilikua ni kupata mfuasi, kosa ambalo walilifanya kina General ni kutoa kazi kwa pair, mimi nilikua napangwa na Inno tangu siku ya kwanza, kuna namna tulianza kumatch. Katika hustle za hapa na pale tulifanikiwa kuelezana mawili matatu kuhusu wapi tumetokea na historia kiasi za familia zetu.

Inno alitolewa Burundi wakati wa mapigano, familia yake iliuawa na General na yeye kuchukuliwa na General na kulelewa na kisha kuingizwa katika mfumo wake. Ingawa General hakua anamuonesha kua alihusika na vifo vya wazazi wa Inno, haikumzuia Inno kuufahamu ukweli kupitia dereva wa General ambae Inno alipewa kazi ya kumuua, kabla hajakata roho , dereva aliropoka kua 'hata wewe haupo salama, unayemuita uncle sio ndugu yako bali muuaji wa wazazi wako ukiwa na miaka miwili'...

Maelezo ya Inno yaliifanya mission yangu kua rahisi sana, kwa pamoja tulipanga kuutafuta uhuru wetu. Baada ya masiku kadhaa ,kazi nyingine ikatoka, tukaambiwa tukamteke Padre wa kanisa katoliki ambae alijizolea umaarufu sana kwa mahubiri yake. Tulishiriki ibada kama waumini wengine, mda wa kutoka nikaingia ofisini kwa Padre nikiomba kuongea nae maongezi binafsi, tulishafanya uchunguzi na kubaini mlango wa dharura unaotokea nyuma ya kanisa ambapo pana uzio wa michongoma.

Sikuhitaji kufahamu madhumuni ya ule mlango, ila kwa wakati ule ulikua msaada wetu mkubwa. Hakukua na mda wa kupoteza, nilimwambia Padre achague moja, nimtwange risasi palepale halafu niondoke kama hakikutokea kitu, maana bunduki yangu ilikua na kiwambo cha kuzuia sauti au afate maelekezo yangu ili aendelee kuishi maana walionituma wamenihakikishia kua wanamaongezi nae tu mafupi kisha atarudi kuendelea na huduma ya kutuombea wenye dhambi.

Padre akiwa katika kutetemeka huku akionesha ishara ya msalaba akanambia atafata maelekezo yangu, nikamwambia fungua huo mlango wa dharura tuondoke, alipigwa na butwaa ni jinsi gani meufahamu maana wanaofahamu huo mlango hawazidi watatu hapo parokiani, na ukiwa mle ofisini panaonekana shelf kubwa lenye vitabu vya kila aina vya kidini na falsafa, hapana dalili ya mlango wa dharura.

Akiwa katika kuzubaa, nilimshtua na kofi matata huku nikiwa nimemtolea macho, kwa haraka akatoa remote kwenye mtoto wa meza akaibonyeza lile shelf likaanza kujisogeza. Nikamuamuru azime simu na aiache hapohapo ofisini mahala ambapo haitaonekana kwa urahisi. Mlango ukawa wazi tukapita akauridishia na kubonyeza tena remote control ukajirudi kama awali, kwa nje ulikua una muonekano wa ukuta tu wa kawaida, aliyefanya matengenezo alitumia akili sana, kwa hilo nampa sifa zake lakini kwa jicho la kijasusi niliweza kung'amua utofauti wa ukuta na mng'ao wa rangi katika kipande kidogo cha ile sehemu na kisha kutambua kua ule ni mlango wa dharura baada ya kugonga gonga na kuona utofauti wa mlio kati ya ukuta halisi na ukuta wa mbao ulionakshiwa na kufanana kila kitu na ukuta halisi.

Padre alitakiwa kufikishwa Kibaha kabla ya jioni ya ile siku kwa hiyo nilikua na mda wa kutosha kufanya nilichopanga. Inno alikua dereva wakati mimi nilikua na Padre siti ya nyuma, tulitoka nae kiungwana kabisa bila ya mtu yeyote kuhisi chochote. Safari yetu iliishia Mbezi katika nyumba niliyokua nimeiandaa kwa shughuli zangu rasmi katika mapambano ya kujiweka huru.

Baada ya dakika arobaini na tano tulifika mjengoni , tukamshusha Padre na kuingia nae ndani. Inno alimfunga kwenye kiti na mahojiano yalianza, hakua mtu ambae tulihitaji kutumia nguvu katika mahojiano, nafahamu wapo watumishi wa Mungu majasusi lakini huyu hakua hata na mfanano nao, alikua na hali ya kuridhika, kakitambi kwa mbali na muonekano wa kutakata.

Nilimpa options mbili tu ndugu yetu , atupe ushirikiano kwa hiari au tutumie nguvu. Nilihitaji kufahamu ni kwanini anahisi ametekwa maana najua hawezi kumfahamu General, kwahiyo hapakua na haja ya kuanza kumuhoji kama anamfahamu , General yeye ni mtu wa kupokea oda tuu, wapo wanaotoa hizo oda. Padre akanieleza inawezekana ni sababu ya mahubiri yake kuhusu aina ya mgombea ambae alipenda waumini wake wamchague, akasema kua tangu wakati huo amekua akipokea vitisho sana kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo na ndio sababu ya kuweka mlango wa dharura.

Nilikua namfahamu huyo mgombea kupitia runinga, huo mwaka Tanzania palikua na vuguvugu la uchaguzi na palikua na mchuano mkali kati ya wagombea wawili, mmoja akitokea chama Tawala na mwingine chama kikuu cha upinzani. Ndugu Padre alikua anampigia chapuo mgombea wa upinzani nadhani ndio akasababisha huo mtafaruku kwa upande wake.

Sikua mtu wa siasa sana, ila naamini katika siasa safi, 'let the best man win'... nimeshafanya kazi za wanasiasa nikiwa Burundi kwahiyo natambua nguvu ya kutumia madaraka vibaya kuumiza wengine. Niliamua kumsaidia Padre na pia kujisaidia mwenyewe, lakini nikajipa angalizo kua daima mwenye nguvu sio mwenzio, kwahiyo nilicheza nafasi ya kinyonga kusubiri upi upande sahihi wa kuwepo wakati najitafuta, nilihitaji back up ya mtu mwenye mamlaka ili kuhimili mkono wa General.
 
SEHEMU YA SITA

Ndugu Padre alitoa ushirikiano wa kutosha, alitupa mwanga wa jinsi siasa za Tanzania zinafanyika, ingawa palikua na ule muonekano wa nje wa nchi yenye amani, lakini amani ilipatikana kwa kutoligusa tabaka Tawala, nilishajionea kwa vitendo kwani nimehusika kudeliver watu wengi kwa General ambao walikua na uhusiano wa moja kwa moja na siasa.

Maelezo yalitushibisha kwa kile tulichokikusudia, nilijua tu hatodhurika zaidi ya usafi wa hapa na pale wa viungo vyake vya mwili , kwa hiyo nilimfikisha anapohusika kwa sharti kua asije ongea kuhusu kile tulichoongea pale kwangu, kama nimempata leo ,nitampata tena hata akiweka milango ya dharura elfu kumi. Padre alinielewa na rasmi nikamuingiza kwenye mfumo wangu baada ya kunipatia majina kamili na mahali ambapo ninaweza wapata wahusika baadhi wanaopambania mgombea yule wa upinzani apite.

List ilikua ni ndefu, wapo hadi watu wa usalama ambao walikua wamechoka na utawala wa chama kimoja kwa mda mrefu, watu walihitaji mabadiliko lakini hapakua na mwenye ujasiri wa kumfunga paka kengele, kwahiyo wote walijificha nyuma ya pazia huku wakimsapoti mgombea yule wa upinzani wakiwa gizani. Nilichokuja kugundua ni kua ndugu Padre alitolewa kafara, na ile kofia yake ya dini alihisi hawezi kuguswa.

Nilikuja kufahamu kupitia Inno siku mbili baadae kua Padre amesharudishwa kwenye makazi yake ila mwendo ni kama umebadilika, nikawaza aina ya usafi waliomfanyia Padre wa watu , nikajikuta nasikitika tuuu. Watu wanaweza hisi hatuna huruma ila kuna namna ukishaingia kwa hizi kazi unapambana kufanikisha majukumu yako ambayo wakati mwingine yataleta ulemavu au kifo kwa yule aliekusudiwa, kwetu inakua ni siku tu nyingine ofisini.

Nilikua nimepata kwa kuanzia, nikaanza kuwasaka wale niliotajiwa na Padre mmoja mmoja kwa nyakati tofauti. Nilianzia kwa Jaji wa mahakama kuu, huyu aliingia kwenye mfumo wa mgombea kwa ahadi ya kupewa ujaji mkuu na mgombea baada ya kushinda. Kazi yake ilikua kuhakikisha kesi zote za mgombea pamoja na chama anazitolea hukumu kwa wakati sahihi na kwamba matokeo yanakua kwa upande wa chama. Sikufahamu alijiamini nini maana ni kama uhusika wake ulianza kujulikana mapema tu kwa namna alivyokua mwiba na kesi za chama Tawala. Nikaona si vibaya nikamtembelea bwana Jaji nipate vifungu kadhaa toka kwake.

Usiku wa saa nne na madakika kadhaa yalinikuta nyumbani kwa Jaji, huyu bwana alikua akiishi Tabata Kinyerezi, nyumba yake ilizungushiwa ukuta mrefu pamoja na nyaya za umeme. Kibao cha 'Kaa mbali ukuta huu unalindwa na Z.Z security hakikukosekana. Nilikua na zana zangu za kazi, umbali wa sentimeta chache kutoka ulipo ukuta palikua na mti mkubwa tu wa mwembe kwa ndani, niliparamia ule ukuta kwa tahadhari, nilizifika nyaya na kuzikata kwa kutumia kifaa maalumu, nikatandika blanket maalumu ambalo linazuia umeme kunifikia, niliruka na kuingia ndani kupitia ule mti wa mwembe, kwa mwendo wa paka nikamfikia mlinzi, sikua na haja ya kuongeza idadi ya dhambi kwa watu ambao hawajanikosea, nilimpa pigo moja takatifu mlinzi aliekua anasinzia akaanguka chini kama roba, nilimsaidia kumdaka ili anguko lake lisifanye kelele. Baada ya uchunguzi wa muda mfupi kua hapakua na mbwa wala myama mwingine hatarishi, nilijongea nyumba ya Jaji kwa tahadhari.

Dakika ishirini zilinitosha kufanya ziara kwenye vyumba vyote vya nyumba ya mheshimiwa Jaji...kwa tahadhari ileile nikabaini chumba anacholala mheshimiwa yeye na mkewe. Nilinyata na kumuamsha bwana Jaji, kwa tahadhari nikamuwekea kidole cha kuonesha anatakiwa akae kimya huku nikiwa nimemuelekezea mkewe bastola, sikutaka kuacha ushahidi ili hata bwana Jaji atakapopiga yowe baada ya mimi kuondoka ionekane ni uzee tu umemnyemelea hakuna kiumbe yeyote aliyeingia mle ndani.

Kwa taratibu tukaongozana yeye akiwa mbele mimi nyuma, moja kwa moja hadi chumba chake cha kusomea. Nikamwambia bwana Jaji karibu, samahani kwa kukujia bila appointment, na samahani kwa kukata nyaya yako juu ya ukuta, hakikisha unarekebisha pakishakucha wezi wasije kukuotea. Yule bwana alikua katika hamaki, nikamwambia hebu relax , ningekuja kukuua usingekua unapumua hadi sasa...

Nikamwambia lengo langu kua nataka kujua mpango wa chama chao jinsi gani wamejipanga kukitoa chama tawala madarakani. Yule bwana alihamaki, yaani mahangaiko yote yale kumbe ni kuhusu chama tawala, sijui alijua watu aliokula rushwa zao na akaenda kinyume nao walikua wamemfata, atajua mwenyewe....nilimwambia sina mda wa kupoteza aanze kuongea au nimrambe risasi.

Yule bwana akanieleza mipango yao na jinsi walivyojipanga, majukumu aliyopangiwa na idadi ya watu walioahidi kuwasaidia. Kwa kiasi fulani akawa ameniridhisha na majibu yake. Kwa sharti la kutoripoti polisi wala kuongea popote nikaahidi kutomsumbua tena yeye wala familia yake, ila nilimpa angalizo kua akijaribu kufungua mdomo wake hakuna atakaemlinda hata akiweka wanajeshi getini. Nikamwambia alale chini bila ya kutikisika, sio kwa mahangaiko yale niliyompa na kile kitambi, kwa namna ileile niliyoingia nikaitumia kuondoka mahala pale.

Kupitia Jaji nikawa nimepata kitu kipya, sio tu watu baki bali hata wanasiasa wengine toka chama Tawala ambao walikatwa wakati wa kinyang'anyiro cha mchujo kwa siri waliamua kusapoti chama cha upinzani kwa ahadi kua watapata teuzi mbalimbali baada ya wapinzani kupita. Niliona si hoja kumtembelea kiongozi mmoja wa chama tawala nikajifunze uzalendo kiasi .
 
Stori tamu , sana go on go go NANA
 
Back
Top Bottom