BssU
Senior Member
- Nov 13, 2018
- 126
- 213
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
True hii Story kweli imenishangaza maana mambo mengi yaliyopo humu yanauhalisia au ukweli ndani yake mfano: Suala la ushirikiano wa kijeshi na North Korea katika masuala ya Air defense na marekebisho ya baadhi ya Rada (kuziupgrade) kiasi fulani yananifanya niione hii story imebase on the True story Hongera mtunzi unakipaji hakikaPredictable: sio mbaya sana, maana haifanani na bongo movie
Relatable: sikujua kama hiki ni kizungu halali, lakini nimekuelewa. This is the worst part of the story, kuna vitu viko open sana vinahusisha yanayoendelea katika mazingira halisi, mfano ujenzi wa uwanja wa ndege
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwaka huu lazima nijue kikorea aisee.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]The President And I(Mimi Na Rais)- Sehemu Ya Kumi Na Mbili
Lello Mmassy  February 12, 2019

Stanley Macha Ahojiwa. Askofu Begere Amvuruga Julius Kebwe
“Macha, mimi si mpelelezi wa shauri lako hili, lakini kwa heshima uliyokuwa nayo ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama nimekuja mwenyewe. Nimekuja kusikia kutoka kwako mwenyewe, nataka uniambie ni nini kilikusibu, na utueleze kwa mapana ipi ilikuwa nia ya wewe na wenzako kutaka kumpindua Rais halali wa nchi yetu aliyechaguliwa kidemokrasia na kwa kufuata matakwa ya Kikatiba na anayeungwa mkono karibu na watu wote.
Mlikusudia nini na unashiriki wewe na nani? Ni vyema ukasema yote na kuwataja wenzako kabla njia nyingine hazijaanza kutumika’’, Alikuwa ni Inspekta Mabubi Majita akimhoji Stanley Macha kwa mara ya kwanza huku akimshushia na mkwara kidogo.
Stanley Macha alichukuliwa na kuwekwa ndani ya nyumba maalumu ya siri ya Idara ya Usalama wa Taifa Stanza, wenyewe wakiita‘safe house’ iliyopo karibu na fukwe za bahari katika eneo linalofahamika kama Khanama akiwa ameshikiliwa huko kwa kosa la uhaini kwa kushirikiana na Joe.
Pamoja na nyumba hii kuwa maeneo ya makazi wanapoishi matajiri na viongozi wa ngazi za juu serikalini, hakuna aliyekuwa anafahamu matumizi yake na wala hakuna aliyewahi kuitilia shaka. Hata baadhi ya viongozi wa juu wa serikali hawakuwa wanafahamu kazi yake zaidi ya maafisa usalama walioingia na kutoka mara kwa mara kwa shughuli maalumu.
Kabla ya kutumia njia za mateso, Jeshi la Polisi liliamua kujaribu mbinu za kidiplomasia kwani wanafahamu wazi ugumu wa kumfanya mwanausalama kusema lolote ambalo hataki kusema. Kuna wanausalama wengi hufa kwa mateso bila kusema hata tone la siri ambayo kwao wanaona haipaswi kumfikia mtu asiyepaswa.
Inspekta Majita alikuwa maarufu na mashuhuri sana katika kufuatilia masuala ya kiuchunguzi. Ni miongoni mwa ma afisa wa jeshi la Polisi watatu tu Stanza waliopata mafunzo nchini Pakistan, Cuba, Marekani na Israeli. Nchi zote katika nyakati tofauti.
Mathalani, Inspekta Majita ni miongoni mwa wataalamu wachache walioitwa kuunda kikosi cha kuchunguza tukio la ulipuaji wa balozi za Marekani katika nchi za Afrika ya Mashariki yaani Tanzania na Kenya mwaka 1998. Ni baada ya tukio lile Marekani ilimpa nafasi ya kwenda kuongeza ujuzi katika shirika lao la uchunguzi, Federal Bureau of Investigation maarufu kama FBI.
Inspekta Majita alikuwa ni mrefu, watoto wa mjini wangesema amepanda hewani, alipenda kufuga ndevu nyingi na kuvuta sana sigara hasa anapokuwa kwenye kazi maalumu. Alipendelea pia kuvaa shati lenye mikono mirefu na kisha kuikunja huku akivaa mkononi saa yake inayotumia mapigo ya moyo kutembea. Sauti yake ilikuwa nzito sana na yenye kukwaruza, hali hii ilichangiwa na uvutaji sana sigara uliopitiliza tangu akiwa mtoto wa miaka 16 tu.
Majita hakuwa muongeaji sana na hakuonekana mara kwa mara, hata serikalini na kwenye taasisi za kiusalama, wanausalama wenzake humuita Kakakuona, kwasababu kuonekana kwake kulikuwa kwasababu maalumu na kwa kazi maalumu tu. Alipendelea kufanya kazi bila kuonekana na watu wala vyombo vya habari.
Inspekta Majita hakuwa na magenge ya marafiki ndani au nje ya taasisi za usalama, alipendelea kuwa na mahusiano ya kikazi pekee. Tabia hii ilisababisha asioe na hakuwa na mtoto. Kwasababu hiyo hakuwa amezoeana na Stanley Macha hata kidogo japo walikuwa wakijuana na mara kadhaa Stanley Macha akiwa kama bosi wake alishawahi kumtuma kazi kadhaa na alizitekeleza vyema.
Stanley Macha anamfahamu fika inspekta Majita na uwezo wake. Leo ni zamu yake kuwekwa kitimoto.
“Majita, unajua unachofanya hapa ni kutaka kukamua maji kutoka kwenye mwamba. Hakuna mpango kama huo”, Macha alimjibu Majita wakiwa wamekaa meza ya mahojiano.
“Labda mimi ni nabii Mussa, huwezi kujua Macha. Nahitaji maji yatoke kwenye mwamba niwanyweshe wana wa Mungu. Rais Costa anahitaji majibu sasa, ukisema hakukuwa na mpango kama huo mimi siwezi kukuelewa na Rais hawezi kunielewa pia”, Majita nae alijibu kwa utaratibu huku akipuliza moshi wa sigara kutoka puani.
“Unajua nilitii na kuwa mkimya kwa sababu nilitaka kujiridhisha lakini ukweli ni kuwa mimi na Joe tulikuwa katika mpango wa kumpima Pius kama kweli yupo thabiti katika kumlinda na kumtetea Rais na Bahati nzuri matokeo ndio haya tumeona alivyo”, Macha alimjibu Majita.
“Macha stop that nonsense man. Both you and I know that is not it. Unampima mnadhimu mkuu wa Jeshi kama ana utii kwa Rais? Unampima kwa kibali cha nani? Kwanini? Kwanini umpime kwa njia hiyo?” Majita aliuliza huku akisimama na kuelekea dirishani.
“Majita zipo sababu nyingi. Kwanza ikumbukwe Pius yupo nafasi ya pili baada ya mkuu wa Majeshi na labda siku moja au siku za usoni yeye atashikilia nafasi hiyo kubwa ndani ya jeshi. Kwa kumbukumbu tu, mipango ya uasi wa jeshi miaka miwili iliyopita Pius alikuwa karibu na mkuu wa kikosi cha mizinga pamoja na anga ambao ilikuja kuthibitika kuwa ndiyo waliokuwa wapanga mipango ya kutaka jeshi liasi.
Ni mimi na Joe ndio tuliuzima mpango ule, unajua historia hiyo. Pius sasa hivi anahusika katika misheni ya kisualama ya Korea Kaskazini, yeye ndiye atakuwa akihusika sana kama kiungo ni muhimu tukajua ama kwa hakika yupo thabiti kumtetea Rais na kulitetea taifa na hana tamaa”, Macha alimalizia utetezi wake wa kuungaunga usio hata na kichwa wala miguu.
“Macha, wewe ndio ulinipendekeza kwa mara ya kwanza kwenda Cuba kusomea haya mambo. Ukanipeleka na Israel na Pakistan. Sasa leo unaponigeuza poyoyo unanikosea sana bosi wangu. I need the truth and only truth. Haya rudia tena”. Majita alimjibu Macha huku akiwa dirishani anaangalia nje. Hakuwa hata anamwangalia, alimpa kisogo. Majibu ya Macha yalimkera.
“Majita, unataka kuamini kweli kuwa mimi naweza kupanga njama za kumpindua Rais Costa? Kwasababu zipi? Ili nipate nini? Mimi nilimnusuru kwenye tukio la kwanza halafu tena leo nipange kumpindua? Come on guys mnanikosea sana. Hata Joe mnamkosea sana anafanya kazi kubwa iliyowashinda wote kwenye serikali hii”, Macha nae alijibu kwa dharau.
“Kama kweli ilikuwa ni kumpima Pius kwanini simu yako uliifanyiaHard reset? Kwanini taarifa zako za simu na za mawasiliano hazipatikani popote. Umezifuta. Faili hili hapa zimetoweka dakika tatu kabla ya kusimamishwa kwenye korido za Ikulu kwa kumtumia kijana wako Daudi.
Amefuta mpaka kwenye server za idara. Nikaagiza kufanyike hard backup nikakuta hakuna kitu. Kila kitu umefuta halafu unaniambia haukuwa mpango wenye nia mbaya? Macha ninakuheshimu, don’t push me to the corner that you would not wish for. Heshima ninayokupa itunze”, Majita aliongea kwa hasira jambo lililomshtua Macha.
“Majita, I have worked in intelligence community since I was in high school, keep that in mind. Maswali unayoniuliza hayana maana. Kuhakikisha taarifa zangu zipo salama ni kosa? Kwani hiyo si kanuni namba moja uliyofundishwa?”, Macha nae alijibu mapigo kwa kufoka.
“Sio ndani ya muda mfupi namna ile toka ujulikane mpango wako ovu” Majita alijibu.
“Kwa hiyo unasemaje”, Macha alijibu kwa hasira
“You are leaving me with no option than applying enhanced interrogation techniques on you Macha. I know both you and I do not wish for that”, Majita alijibu.
“Nimeihudumia serikali hii kwa miaka 30. Nimemlinda na kumtetea Rais Costa kwa mwaka wa 12 sasa. Kama hii ndiyo gharama ya uaminifu wangu kwa Mh Rais na kwa taifa hili, basi nipo tayari kuilipa”. Macha alijibu kwa kupayuka huku Inspekta Majita akiwa anatoka nje na kutotaka kumsikiliza.
“I will show you some love and you’ll fall in love with the show. I will be back to say hello soon”, Inspekta Majita alijibu na kutupa kipisi cha sigara chini na kisha kutoka.
**********************************
조에서 뭐 들었 니? o-eseo mwo deul-eoss ni? (Umesikia lolote kutoka kwa Joe?). Rais Kim alimuuliza Waziri En wakiwa wamesimama kibarazani kwenye jumba la Ryongsong, makazi maalum ya Rais Kim.
아니요, 그들이 베이징에 안전하게 도착했다고 확인되었지만 그의 탁월함aniyo, geudeul-i beijing-e anjeonhage dochaghaessdago hwag-indoeeossjiman geuui tag-wolham(Hapana Kamaradi, japo nilithibitishiwa kuwa walifika salama Beijing), Waziri En alijibu huku akiwa ameinamisha kichwa kidogo.
이것은 어색합니다. 코스타 대통령은 핵무기에 대한 생각을 좋아하지 않았습니까? igeos-eun eosaeghabnida. koseuta daetonglyeong-eun haegmugie daehan saeng-gag-eul joh-ahaji anh-assseubnikka? (Hii ni ajabu sana, au Rais Costa hakupenda wazo letu la silaha za kinyuklia?) Rais Kim alionesha mashaka yake kwa ukimya wa serikali ya Stanza.
나는 그의 탁월함을 확신하지 못한다.naneun geuui tag-wolham-eul hwagsinhaji moshanda. (Sina hakika Kamaradi), Waziri En alijibu kiufupi.
그것을 찾으십시오 . Joe와 논의한 내용이 여전히 유효한지 알고 싶습니다. geugeos-eul chaj-eusibsio. Joewa non-uihan naeyong-i yeojeonhi yuhyohanji algo sipseubnida. (Fuatilia na uje unihakikishie kuwa tuliyoyaongea na kuyapanga na Joe yapo katika mchakato au kuna mabadiliko yoyote), Rais Kim alimalizia.
Waziri En aliondoka.
******************************
Toka siku ile Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge bwana Kinyamagoha afukuzwe na Rais kwa sababu ya kushindwa kusukuma kwa nguvu muswada uingie bungeni wa kubadili umri wa mtu kugongea u Rais kutoka miaka 40 mpaka 55, hakuwahi hakuonekana hadharani tena.
Alitoka pale na moja kwa moja alielekea kijijini kwao Kwamchae ili kwenda kufanyiwa “maarifa”. Kama kuna mtu dunia hii aliamini uchawi na uganga basi Kinyamagoha aliongoza.
Aliamini misukosuko ile ni kwasababu mwaka huu hakuwa ametoa kafara. Kafara ya Kinyamagoha ilihusisha watoto wachanga wasiozidi umri wa siku moja. Kinyamagoha akishirikiana na baadhi ya manesi anaowalipa pesa nyingi aliua watoto hasa wakati mama anapokuwa anajifungua. Wakati ule huhakikisha kwa namna yoyote hata kwa kumziba mtoto asipumue ama vinginevyo basi huua mtoto kama sehemu ya hitaji la waganga wake.
Baada ya kuua na mama aliejifungua kuambiwa na kuhuzunika nesi hujifanya anaenda kumsafisha ili wamfunge kwa mazishi lakini kabla ya humchanja yule mtoto na kutoa damu kiasi ambayo kuikinga na kupelekwa kwa Kinyamagoha kisha kuipekea kwa mganga.
Iikuwa ni ngumu kuamini hasa kutokana na tabia ya Kinyamagoha kupenda kuandaa makongamano ya dini akihusisha maaskofu ama mashehe. Tena mara kadhaa utamuona akiwa misikiti mbalimbali akishiriki swala ya Ijumaa ama kusaidia vituo vya watoto wasiojiweza.
Kinyamagoha alikuwa fisi ndani ya ngozi ya kondoo. Lakini pia, Kinyamagoha alikuwa ni kama alama ya wanasiasa walio wengi na hata wanajamii walio wengi kwa ujumla. Wengi walikuwa na dini zao lakini hawakuacha kushiriki masuala ya kishirikina au vinginevyo, kama si ya kishirikina basi waliendelea kutekeleza dini zao za asili, maarufu kama dini za Kiafrika zinazohusisha uganga na matambiko ya aina mbalimbali
********************************
“Tunamshuru sana Mh. Rais na serikali yake kwa kukubali kutoa kibali cha Ujenzi wa hospitali kubwa kule Kilungululu. Hii siyo tu inaonyesha nia njema ya Rais katika kuunga mkono jitihada za kanisa, lakini pia nia yake njema ya kutaka wananchi wa Stanza wapate huduma bora za afya.
Ni rai yangu basi waamini wenzangu kumuunga mkono Mh. Rais hata katika mambo mengine anayoyafanya ambayo ni tija kwa taifa letu. Hii tabia ya kumzodoa, kumkatisha tamaa na kumtusi tuiache, haisaidii wala haijengi.
Wapo wanaosema hafuati sheria wala katiba, tena haheshimu utawala bora. Mimi nasema Roma haijajengwa kwa siku moja, tutafika huko. Sasa hivi sio muda wa kufanya siasa, ni muda muafaka sasa wengine wote tuweke mikoba yetu na ya vyama vyetu chini tushirikiane na tuunge mkono juhudi njema za Mh Rais anazofanya kwa maslahi ya taifa letu. Hata nafsi tatu za Mungu hutenda kazi pamoja, kama kila moja ingekuwa ina kazi ya kumkosoa mwenzake basi hata leo tungekuwa hatujakombolewa”, Askofu Damian Begere aliendelea.
Ilikuwa ni siku ya Jumapili akiwa katika ibada ya kiaskofu akitoa mahubiri yake kikanisa huitwahomilia. Hakuna aliyeamini kama kweli maneno yale anayatamka Askofu Begere. Watu kanisani walikuwa wakinong’onezana sana wakiulizana kulikoni. Hakuna aliyemzoea askofu Begere na mahubiri ya mtindo ule yenye sifa kedekede kwa Rais Costa. Waswahili husema usilolijua ni sawa usiku wa giza.
Kama ilivyo ada, baada ya ibada ya misa Askofu hutoka nje ya saktestia(chumba maalumu cha Padri au Askofu kujiandaa kabla na baada ya ibada) na kisha kusalimiana na baadhi ya watu na kuongea nao mawili matatu.
Julius Kebwe, kiongozi mkuu wa siasa za upinzani nchini Stanza alienda kumsalimu Muhashamu baba Askofu Damiani Begere.
“Tumsifu Yesu Kristu baba Askofu”, Julius alisalimia huku akibusu pete ya askofu.
“Milele amina Julius. Haujambo?” Askofu Begere aliitikia huku akitabasamu.
Askofu Begere na Julius ni marafiki wakubwa. Urafiki wao ulianza tangu Julius akiwa kiongozi wa chama cha kitume cha wanafunzi wakatoliki mashuleni kijulikanacho kamaSYCMS (Stanza Catholic Movement for Students). Ni kutokea huko askofu Begere alimkuza Julius tena akitaka amfanye aingie seminari na kuwa padri lakini Julius alikataa.
Baada ya Julius kuingia kwenye siasa, askofu Begere amekuwa msaada mkubwa sana katika kumtia moyo na kumpa ushujaa na kumtaka kutoogopa kusimamia anayoamini ila tu iwe haki na kweli. Askofu Begere ni mtoa hamasa mkuu kwa Julius.
“Baba leo umeniacha njiani. Sijakuona kabisa”, Julius alianza kumtania askofu Begere.
“Siku zetu zinakaribia kwisha Juli”, Askofu Begere nae alijibu kiujanja kwani alijua Julius anamaanisha na kulenga nini.
“Lakini siku zikikaribia kwisha si ndo mnatakiwa wazee mtuachie wosia?” Julius nae alidodosa harakaharaka.
“Sometimes, you need to compromise for a greater cause”, askofu Begere alijibu kiutu uzima.
“Should I compromise as well?”, Julius nae alihoji.
“Njoo nyumbani tuzungumze Julius”, Askofu Begere alimwalika Julius kwenye makazi yake.
Julius alitabasamu na kumuhakikishia askofu kuwa ataenda kuonana nae kesho yake siku ya Jumatatu. Maswali ya Julius yalimwingia Askofu Begere na hakika aliona alichoongea kinajifunga sana na uhalisia wake na uhalisia wa mambo pia. Ila angefanyaje?
Anataka aonane na Julius.
*************************************
Joe alimwita Habibu asogee karibu na simu yake ili aweze kusoma mazungumzo watakayokuwa wanaandikiana Joe na huyo mtu mwingine kupitia game ya Clash Royale.
“Hii application inaitwaje Joe?”, Habibu alipoona tu kwanza aliuliza.
“Mapema kwa sasa wewe kufahamu ila subiri tuone kama atajibu kwanza”, Joe alimjibu Habibu huku akiwa ameandika salamu akisubiria jibu.
“Na huyu unayewasiliana nae ndio anaitwa Saddam Hussein?”, Habibu alihoji kwa mshangao.
“Hapana. Hilo ni jina analotumia huku”, Joe alijibu na ghafla ile salamu yake ilijibiwa.
“Aisee nimekwama na sijui naanzia wapi. Nimeambiwa Meshack nae kashapigwa pini, vipi Tigerwamempeleka wapi?” Joe aliandika kwenye ujumbe.
“Tiger yupo kama sio nyumba namba 3 basi ni wamempeleka red square”. Yule mtu alieandikwa kama Sadam Hussein alimjibu Joe kwa ujumbe.
Muda wote huo Habibu nae alikuwa akifuatilia mawasiliano yale akiwa ameachwa njiapanda asijue Joe anaongea na nani ila alijua nyumba namba 3 na red square ni kati ya nyumba za siri za Idara ya Usalama wa Taifa Stanza, kizungu wanaziitasecret detention facilities au kama zinatumika kwa kuhifadhi mtu kwa ajili ya usalama wake huitwa ‘safe houses.’
Alijaribu kuuliza Tiger ndio nani lakini Joe alimwambia atamwambia asijali.
“Kwa hivyo haujapata kujua chochote kinachoendelea kwa Tiger?”, Joe alihoji.
“Ndio, si unajua Sabinasi ndio sasa kapewa kitengo? Anajiona yeye niIgor Kostyukovu, pumbavu sana. Taarifa anazificha balaa”, Yule mtu alieandikwa kama Saddam Hussein alijibu.
Igor Kostyukovu ndio mkuu wa Idara ya Inteligensia ya Taifa la Urusi. Mmoja kati ya jasusi nguli duniani.
“Hakikisha familia yangu haiguswi Saddam. Wewe sasa ndiye uliebakia kunisaidia kumalizia kugurudumu hili. Nimeshapoteza mengi na siwezi kurudi nyuma maana haitosaidia tena. This time around ni mimi ama yeye.” Joe aliandika.
“Sawa Che, lakini huoni kama hakuna namna nyingine? Kwanza nakuomba mwache Habibu arudi. Hakuna sababu ya kumuharibia maisha huyo kinda”, Yule aliyejiita Sadam aliandika.
Joe alimwangalia Habibu aliekuwa akisoma kila kitu. Habibu alipoona ameangaliwa alitikisa kichwa kuashiria kuwa hataki kurudi na anataka awe pamoja na Joe.
“Una hakika Habibu”, Joe alimuuliza.
“Ndiyo”, Habibu alijibu na kupeleka macho kwenye simu ya Joe ili aone maongezi yataendeleaje?
“Habibu hayupo tayari kurudi Stanza.Ameamua kuendelea na mkakati huu”. Joe alimuandikia Saddam.
“Che, nitakurudia baadae kidogo” Saddam aliandika na kutoka hewani.
“Tiger na Che ndio kina nani?”, Habibu alihoji baada ya kuona la Sadam Hussein hajibiwi.
“Tiger ni Stanley Macha na Che Guevara ni mimi”, Joe alimjibu kiufupi.
“Na huyo Sadam Hussein je?” Habibu aliuliza kwa hamu kubwa.
“Sadam Hussein ni Gideon”, Joe alijibu na kumwacha Habibu hoi asiamini alichosikia.
*******************************
Gideon Kalumanzila, mshauri wa karibu na kipenzi cha Rais Sylvester Costa na Joseph Kaduma ni marafiki wa siku nyingi. Urafiki wao haukuwa ukifahamika sana miongoni mwa wengi katika serikali ya Rais Costa. Hii ilitokana na ukweli kwamba ni watu waliokuwa wakisukuma agenda nyingi nyuma ya pazia katika serikali ya Stanza hivyo waliafiki kutokuweka wazi urafiki wao.
Ilikuwa ni ngumu kufatilia uhusiano wao na kujua umeanzia wapi maana kwenye rekodi zao hakuna mahali inaonekana kufahamiana kwa namna yoyote ile. Kuanzia makabila yao, shule walizosoma, vyuo na nchi walizowahi kuishi hakuna mahusiano hata kidogo. Ni hali hii iliwapa nafasi nzuri sana ya kusukuma mambo serikalini na mtu asijue kabisa kama ni nguvu ya pamoja.
Si hivyo tu, hata mitazamo yao mbele ya viongozi wenzao wa Stanza ilitofautiana sana. Yeye Gideoni alionekana kama mtu mwenye kuunga mkono kila haja ya Rais Costa wakati Joe yeye huhoji kila suala na wakati mwingine kupingana na Rais Costa.
Si mara moja wala mbili Gideon alionekana kumchongea Joe kwa Rais Costa ili achukuliwe hatua za kinidhamu katika masuala mbalimbali. Ni yeye aliyeshauri na kushupalia haswa Joe avuliwe ubalozi na kupewa kesi ya uhujumu uchumi iliyomtesa kwa miaka miwili. Jambo hili lilifanyika kwa umaridadi mkubwa ili Gideon azidi kuwekwa karibu na Rais Costa.
Kwa macho ya nje, Gideon alifanikiwa sana kujitenga na Joe na hakika kama tungekuwa kwenye medani za kishushushu basi Gideon alifuzu viwango vyote vya kuitwaundercover agent. Joe alihakikisha Gideon hagunduliki hata kwa thumni na hilo walifanikiwa sana.
Watu hawa walijuana vipi?
Ilikuwa ni katika miaka ya 1991 wakati Joe akichukua shahada ya Uzamili katika Diplomasia ya Kimataifa kutoka chuu kikuu chaWarwick huko Uingereza na Gideon akichukua shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Siasa kutoka chuu kikuu cha Melbourne huko Australia walipokutana katika fainali za kombe la dunia la mchezo wa Rugbyzilizofanyika Ufaransa.
Gideon akiwa miongoni mwa waliounda kikosi cha timu ya Australia yeye Joe alikuwa ni mmoja wa kamati ya ufundi kwenye timu ya Uingereza. Ni katika mechi ile ambayo Australia waliibuka mabingwa wa dunia kwenye mchezo wa Rugby na kwa shauku kubwa Joe alipenda kujua muafrika mmoja tu aliyekuwa akiunda timu ile iliyoibuka na ushindi alitokea wapi.
Joe, alishangaa alipojua kuwa Gideon ni Mstanza. Gideon alikuwa ni Mstanza pekee labda mpaka nyakati hizi aliewahi kushiriki kombe la dunia la mchezo wa Rugby na timu yao kuibuka kidedea.
Ni baada ya mechi ile Joe aliongea na Gideon na kuanzisha mahusiano ya kirafiki. Japo hawakuwa wakiwasiliana mara kwa mara lakini mahusiano yao yalidumu. Ni Joe alieanza kurudi Stanza na kuingia serikalini. Baada ya miaka mitano Joe akiwa kwenye mkutano wa kimataifa Brusells Ubelgiji alikutana na Gideon kwenye moja ya migahawa ambapo wakati huo Gideo alikuwa Ubelgiji akifanya tafiti.
Joe aliongea kwa kirefu sana na Gideon juu ya siasa za Stanza na ni hapo Joe alivutiwa sana na mitazamo ya Gideon juu ya maendeleo ya nchi za kiAfrica. Alimsihi Gideon arudi Stanza na angefanya kila jitihada kumfanya awe mshauri wa Rais kwani aliona kabisa mawazo yake yangeisaidia Stanza kwa namna nyingi.
Gideon alirudi Stanza na kuteuliwa kuwa mshauri mdogo wa Rais Costa katika masuala ya kimataifa kwa ushawishi wa Joe. Wakati huo urafiki kati ya Rais Costa na Joe ulikuwa katika viwango vya hali ya juu labda kuliko mtu yeyote katika serikali ya Rais Costa.
Mienendo ya siasa na uendeshwaji wa nchi ya Stanza vilimchosha sana Gideon. Aliona ni bora arudi zake ughaibuni akaendelee na mambo yake kuliko kukaa kwenye nchi ambayo ushauri wa kitaalamu unaonekana ni takataka na badala yake umbea ndio unathaminiwa.
Joe alimsihi Gideon kuwa hapaswi kuondoka badala yake yafaa abaki ili wasaidiane kurekebisha hali ya utawala nchini Stanza. Ni hapo ndipo walipokubaliana namna bora ya kufanya.
Wakati wakiwa katika mpango ule ndipo Rais Costa alipoanzisha mpango wa yeye kuendelea kubaki madarakani kwa muhula wa tatu kwa kupeleka marekebisho ya katiba bungeni. Joe alipingana nae na kusababisha chuki dhidi yake na Rais Costa.
Joe alimsisitiza Gideon hata katika hali ile asiache kuwa karibu na Rais Costa na kuhakikisha analinda urafiki na ukaribu wake na Rais hata hapo muda muafaka utakapofika. Gideon alifanikiwa sana katika hilo na hakika kama kuna watu Rais Costa anawahusudu basi Gideon ni nambari moja.
Ni Gideon na Stanley Macha waliohakikisha wanamrudisha Joe kwenye picha na kumfanya aongoze ujumbe kule Korea Kaskazini. Baada ya yote kutokea ni yeye Gideon amebakia kama kimbilio la mwisho na mtu pekee anaeweza kuifanya misheni hii ya kumtoa Rais Costa madarakani ikamilike ama ishindikane. Gideon Kalumanzila, macho yote ya Joe, Habibu na Stanley Macha yanamwangalia yeye.
***********************************
Joe na Habibu waliendelea kubaki katika ardhi ya China. Walichagua kupumzika katika mgahawa waShenang, uliojengwa pembezoni mwa mto Chachiu ambao una vivutio vingi ikiwemo aina mbalimbali za ndege na maua.
Pamoja na kuwa katika msukumo mkubwa wa kiakili kufikiria ni hatua gani wangefuata baada ya mpango wa awali kukwama, Joe na Habibu waliamua kupumzika katika eneo hilo kusafisha akili zao na kupata mawazo mapya.
Wakati wakiendelea na tafakuri na kupata chakula cha mchana, Joe alisikia milio miwili tofauti katika simu yake kuashiria kuingia kwa jumbe mbili kwa mifumo miwili tofauti jambo lililomshtua kidogo.
Kupitia program ya Clash Royale, alipokea ujumbe kutoka kwa Gideon ulioandikwa kwa kifupi tu ‘’I have got an idea, let the movie begin. The plan B is taking off’’. Gideon alikuwa amemrudia Joe kama alivyomuahidi hapo awali.
Wakati Joe akiendelea kutafakari ujumbe wa Gideon, alikumbuka kuwa kuna ujumbe mwingine uliingia katika simu yake. Alipangusa kioo cha simu yake kwa kushusha chini na aliona ujumbe kutoka kwa Waziri En ukimuuliza ni nini kinaendelea na kwanini hawajasikia kutoka Stanza tangu waondoke Korea Kaskazini.
Ujumbe wa Waziri En ulitumwa kwa njia mahsusi, ni simu ya Joe peke yake iliwezeshwa kwa codesmaalumu ambazo ingeweza kupokea ujumbe akiwa sehemu yoyote duniani bila kujali kuwa ana mtandao au hana, hata kama amezima simu yake. Ujumbe ungekuja na mhuhusika akishausoma, basi ungetoweka katika simu yake. Ili aweze kujibu, ingempasa abofye namba maalumu alizopewa na kujibu kisha ujumbe wake ungefutika pia na kutoacha aina yoyote ya hustoria kuwa watu wao walishawasiliana.
Joe alikuwa na jumbe mbili za kujibu kutoka watu wawili muhimu katika kuleta matumaini mapya ya mkakati wa kuleta mabadiliko ya kiutawala nchini Stanza.
********************************
Gideon Amepata Plan Gani? Joe Amepokea Taarifa Zipi Kutoka Kwa Waziri En?.Sehemu Ya 13 Itakujia Ijumaa.
USISAHAU KU 'LIKE' NA KU 'FOLLOW' Ukurasa wetu
Sent using Jamii Forums mobile app