Simulizi:The President and I(Mimi Na Rais)

Hyo speed yako ni kubwa sana mkuu, super speed. Mimi nasoma kwa vituo sana, sijui ni kukosa muda au vipi. Japo nimejiwekea utaratibu kuwa walau kwa siku nisome hata page mbili za kitabu kwa siku ambazo nakuwa nimebanana
Namshukuru Mungu kwa hili nasoma speed mno..
Nililelewa kwenye familia ya ki islam while mm ndio mkristo pekee since nina 6yrs so biblia nilikua naiona nikienda sunday tu tena ilikua marachache sana kwenda. So nikawa na hamu nijue visa vilivyomo mule but siwez kuipata. Nilipoanza form one ndio nikarudi kwa wazazi wakristo so nikawa na passion mno kusoma simulizi za mule.
So siku niliyoipata nilianza Mwanzo hadi Ufunuo though ufunuo nilikua naruka coz ni ngumu kidogo kuelewa. But niliimaliza na mpaka leo ipo kichwani kasoro vifungu tu ndio sijui

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Hyo speed yako ni kubwa sana mkuu, super speed. Mimi nasoma kwa vituo sana, sijui ni kukosa muda au vipi. Japo nimejiwekea utaratibu kuwa walau kwa siku nisome hata page mbili za kitabu kwa siku ambazo nakuwa nimebanana
Pia kutokua na ubize mkubwa kuna changia. Ukipigwa na mchoko wa mchana lazima usome kidogo

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
The President And I(Mimi Na Rais) -Sehemu Ya Kumi Na Tano

Joe Amchezesha Gideon Nafasi Ya "Kiungo Namba 8" Kwenye Misheni

Wazir En baada ya kuwasiliana na Joe siku ile ilimbidi apeleke mrejesho kwa Rais Kim. Alimweleza Rais Kim kila kitu kama alivyoelezwa na Joe. Rais Kim alionekana kushangaa na kuchukizwa na kitendo cha Pius.

“그런 다음 두 가지를 진행해 봅시다.” geuleon da-eum du gajileul jinhaenghae bobsida (Basi tuendelee na mpango wetu namba mbili), Rais Kim alimwambia Waziri En.

“동지, 대안 2는 매우 위험합니다. 윌은 아프리카 전역과의 외교 관계에 영향을 미칠지 모른다” dongji, daean 2neun maeu wiheomhabnida. wil-eun apeulika jeon-yeoggwaui oegyo gwangyee yeonghyang-eul michilji moleunda (Kamaradi, mpango namba mbili ni hatari sana. Unaweza kuathiri mahusiano yetu ya kidiplomasia na bara zima la Africa). Waziri En alionyesha shaka yake.

“En 위험을 완화하는 것은 당신의 일입니다” En wiheom-eul wanhwahaneun geos-eun dangsin-ui il-ibnida (Ni kazi yako kuzuia hizo hatari zisitokee En), Rais Kim alisisitiza.

Waziri En hakuwa na namna zaidi ya kwenda kuanza utekelezaji wa mpango namba mbili.
********************************

Baada ya Pius kuwasili Stanza jana yake na kuwapa mrejesho Rais Costa na jopo lake, waliamua sasa kuwasiliana na Korea ili Rais Costa atoe mrejesho kwa Rais Kim juu ya ugeni ule alioutuma.
Wakiwa wamekaa kwenye meza ya nusu mduara asubuhi ya saa nne kwa saa za Stanza, huku wakiitazama screen kubwa iliyopo mbele yao waliunganishwa kwenye simu ya video (Video Call) kutoka Ikulu ya Korea Kaskazini, Ryongsong.

“Mr. President, it is nice to hear from you” (Mh. Rais ninafuraha kusikia kutoka kwako), Rais Kim alianza mazungumzo kwa kiingereza cha kuunga unga.

“It is my pleasure too Comrade” (Ni furaha yangu pia Kamaradi), Rais Sylvester Costa alijibu.

Rais Kim alitambulisha ujumbe aliokuwa nao kwa upande wake kuwa ni Waziri En, anaehusika na masuala ya kigeni, Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la Korea Kaskazini pamoja na Makamanda wengine wawili wa ngazi za juu wa Jeshi la Ukombozi la Korea Kaskazini.

Kwa upande wake Rais Costa alimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Stanza Jenerali Ernest Nduta, Mshauri maalum wa Rais Gideon Kalumanzila, Mkuu wa Idara ya Usalama Wa Taifa Stanza Sabinasi Paulo na Pius Kihaka, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi na Mjumbe katika msafara ule wa Korea.

“Where is Joseph Kaduma and Habibu Chamchua?” (Wapo wapi Joseph Kaduma and Habibu Chamchua?) Rais Kim aliuliza kwa mshangao kama vile hafahamu kinachoendelea.

“They are both assigned with other tremendously important matters Mr President, but nothing to worry about. We can still proceed” (Wote nimewapa tena majukumu mengine ya muhimu Mh. Rais, lakini hakuna cha kuogofya. Tunaweza kuendelea), Rais Costa alijibu kwa haraka.

Maongezi yalianza na Rais Costa alikiri kupokea mrejesho wa mazungumzo yote. Rais pamoja na timu yake walikubaliana na matakwa yote ya Korea isipokuwa tu kuanzisha uzalishaji wa silaha za nyuklia nchini Stanza. Suala hilo lilipingwa vikali na Rais Costa na timu yake.

Rais Kim hakutaka kusisitiza kutiwa saini makubaliano kulingana na nyaraka alizopokea kwani alifahamu wazi kuwa nyaraka zote hazikufikia serikali ya Stanza na kwa kufanya hivyo ingeweza kuleta hali ya sintofahamu katika kikao kile muhimu. Hakuonesha uharaka wa kutiwa sahihi makubaliano yale.

“Mr. President, I am afraid that by not providing us with the secret location and access to uranium so that we can process nuclear in Stanza, we will not be able to support you with what you requested from us”. (Mh. Rais nina shaka kuwa bila ninyi kutupa sisi nafasi ya kujenga ngome yetu huko ya kuzalisha silaha za kinyuklia hatutaweza kuwapa msaada wowote mlioomba), Rais Kim alisisitiza.

“Mr. Presient, Pius is our top rank military commander, second in rank after the Chief of Defence Forces, he specifically advised against that being part of the deal, didn’t he? (Mh Rais, Pius ni kiongozi mkubwa katika jeshi letu, mtu wa pili kimamlaka baada ya Mkuu wa majeshi, yeye alishauri kutohusisha ujenzi wa kinu cha nyuklia Stanza kama sehemu ya makubaliano. Ama sivyo?). Gideon aliona atumie mwanya huo kuzidi kumwaribia Pius, wazungu huita ‘’reputation damage’’ mbele ya Rais Costa.

Alijua fika Pius alishiriki kuhawahamasisha wenzake wakubali nyuklia izalishwe Stanza la sivyo Joe asingekubali. Kitendo cha yeye kuja na kusema sio yeye bali ni Joe aliona ni uongo wa kujipendekeza kwa Rais Costa na hivyo swahi hilo aliliuliza makusudi ili Rais Kim ‘afunguke’ mbele ya watu wote na iwe aibu kwa Pius.Kwa vyovyote vile alikuwa hataki Pius apewe nafasi ya ukuu wa mejeshi.Aliuliza swali la kinafiki.

“We are not here to discuss who said what, but to make final decisions and move forward” (Hatuko hapa kujadili nani alisema nini bali kufanya makubaliano ya mwisho na kuendelea mbele), Waziri En alijibu.

Kikawaida na kiutawala katika mazungumzo kama yale Rais humjibu Rais na ni dharau mtu wa kawaida kumtupia swali Rais ndio maana Waziri En alidakia kujibu na sio Rais Kim.

“I propose that we use today’s meeting as a learning point of the position of both our brother countries. We should perhaps call for another bilateral meeting after discussing it in detail. What do you think gentlemen?” (Nadhani kikao cha leo tukichukulie kama kikao cha kukiri kupokea mrejesho kutoka kwenu na kujua msimamo wa nchi zetu marafiki, halafu baadae tuitishe kikao kingine baada ya kujadili kwa kina. Mnaonaje?). Jenerali Ernest Ndutta alishauri baada ya kuona hakutakuwa na muafaka.

“I would recommend that too” (Sawa, ningependekeza hilo pia) Mkuu wa Majeshi wa Korea Kaskazini alijibu.

Rais Kim na Rais Costa ambao ni wenyekiti wenza wa kikao kile walikubaliana na mapendekezo ya wakuu wao wa majeshi na kukubaliana kuahirisha kikao kile.

Mjala ulifungwa na mkutano ule uliofanyika kwenye mfumo maalumu wa kieletroniki unaotumia kioo kikubwa cha video ulifungwa.

“Suala la silaha za nyuklia hapana aisee”, Rais Costa aliongea baada ya video kukatwa.

“Ni suala nyeti”, Jenerali Ernest Nduta aliunga mkono kwa kukazia.

“Nduta, nadhani kikao hiki chafaa kukutaarifu. Kwanza niseme umehudumu taifa hili kwa juhudi, weledi na uaminifu mkubwa kwa muda wote wa utumishi wako. Najua umechoka na kuna wakati uliniomba upumzike mimi nikakulazimisha uendelee, lakini sasa hata mimi nakuonea huruma. Nimeonelea nikukubalie ombi lako la kupumzika na kumteua Pius kushika nafasi yako. Sijui hilo unalionaje?” Rais Costa aliongea kwa upole na unyonge sana.

Alikuwa akimpa taarifa Jenerali Arnest Nduta ya kutaka kumpumzisha kutoka kwenye nafasi yake ya Ukuu Wa Jeshi kama walivyojadili na kukubaliana jana yake na Gideon.

“Mh. Rais nashukuru sana. Ni kweli umri umenikimbia na kama unavyoona kadiri miaka inavyozidi kwenda changamoto ni nyingi, si sawa na ile miaka yetu. Kwa hivyo mimi sioni tatizo kabisa. Pius ni askari hodari na mwenye weledi, ataliongoza vyema jeshi letu”, Jenerali Ndutta alijibu.

“Ninafurahi kuwa umepokea suala hili kwa mtazamo chanya. Wapo wengine huwa hawapendi kustaafu utumishi wa umma kwasababu wanapenda kuendelea kutumikia’’. Nashukuru kwa utumishi wako’’, Rais Costa alimjibu.

Wote walisimama na Jenerali Ndutta kwa ukakamavu mkubwa alisimama na kupiga saluti kuashiria heshima yake kwa Rais Costa. Rais Costa naye alipokea salamu ile ya kijeshi kwa kupiga saluti na kisha kushusha mkono na kumpa Jenerali Ndutta.

Wengine wote walifuata kwa kumpa Jenerali Ndutta mkono wa heshima.

“Pius najua wewe ni kijana na bado damu inachemka, naomba alipoishia Jenerali Ndutta wewe nyoosha kwa spidi zote. Nataka jeshi la kisasa.” Rais Costa alisisitiza.

“Mh Rais!” Pius Kihaka alijibu kwa kifupi akiwa bado haamini kuwa anaukwaa Ukuu wa Majeshi bila matarajio yoyote.

Wote walikubaliana waandae mpango maalumu wa ustaafu na kuachiana madaraka ili kila kitu kiende bila mawimbi.

“Mtakapokuwa tayari mtaniambia nilitaarifu taifa”, Rais Costa aliagiza.

“Sawa Mkuu”, wote walijibu kwa pamoja.

Rais alinyanyuka na kutoka na kisha kila mmoja alitoka.

Gideon alishika korido ya kuelekea ofisini kwake, Sabinasi alitoka kabisa akielekea ofisi za Idara ya Usalama na Ndutta na Pius walitoka kurudi makao makuu ya jeshi.
***************************************

Gideon akiwa anakaribia kuingia ofisini kwake alimuona Sara, mke wa Rais Costa.

“Mmemaliza kikao? Nahitaji kumuona baba Brian”, Sara alimuuliza Gideon.

“Ndiyo shemeji, tumemaliza nadhani Mh. Rais atakuwa ameelekea ofisini kwake. Lakini mbona nimeona kwenye habari BBC kuwa kongamano linaendelea na wewe nakuona hapa?” Gideon aliuliza kinafiki.

“Shemeji acha tu, huyu Costa tatizo lake la kusikiliza maneno ya watu wengi mwisho atapotezwa” Sara alimjibu Gideon.

“Embu ingia ofisini shemeji uniambie kulikoni”, Gideon alimwingiza Sara ofisini kwake.

Gideon ni mjumbe wa bodi wa shirika la Sara mke wa Rais Costa linalojihusisha na vijana walioathirika na madawa ya kulevya. Ni kawaida Sara kuingia ofisini kwa Gideon kutaka ushauri na mambo mengine mengi ya utendaji wa shirika. Ni katika mahusiano hayo walitokea kuzoeana sana na hata kupelekea Sara na Alicia mke wa Gideon kuwa marafiki wakubwa.

“Hebu shemeji nieleze, kulikoni?” Giden alihoji huku akikaa kwenye kiti.

“Costa kanirudisha ananiambia amesikia mimi nataka kumpindua sijui, kuwa nashirikiana na Macha na Joseph. Mimi hawa watu hata ukaribu nao sina, unajua nimeshangaa sana?” Sara alianza kutiririka.

“Sasa wewe ukamwambiaje?”, Gideon alihoji.

“Nimwambie nini? Kwani mimi nataka kumpindua ili iweje? Nilimwambia kama kupindua ningepindua ndoa yetu baada ya yeye kuanzisha mahusiano na yule Malaya wake’’, Sara alijibu kwa ghadhabu.

“Mmmmmh. Unajua nini shemeji, nilivyosikia na naomba usinitaje lakini” Gideon alianza kujihami.

“Sikutaji bwana we, mbona la Ketina sikukutaja kabaki kunitolea macho tu. Niambie ehee”, Sara alijibu Kiswahili Swahili.

“Nilivyosikia ni kuwa shutuma hizi sio nini wala nini ni namna ya kukuandaa ili akutaliki amuoe Ketina. Yani anakutengezea mazingira akuache kwa kosa la kutaka kushirikiana na waliotaka kumpindua ili aoane na Ketina”, Gideon alipigilia msumari kama alivyoelekezwa na Joe.

“Unasema? Shemeji ya kweli hayo?” Sara aliuliza kwa mshangao.

“Kwani nilipokwambia juu ya Ketina shemeji yangu si ulinikatalia hivi hivi mpaka ulivyothibitisha mwenyewe? Sina sababu ya kukudanganya shemeji” Gideon aliendelea kumwaga sumu kwenye uhusiano ambao tayari ulikuwa katika hali ya kuhitaji dawa.

“Kwani huu mpango wa kumpindua ni kweli?” Sara alihoji.

“Ninavyosikia ni kweli si unaona Macha kawekwa ndani na hivi karibuni atakutana na Rais kukiri. Ila sasa kuna wengine hawajulikani bado”, Gideon alijibu.

“Laiti ningewajua ningewasaidia, huyu Costa ni mpuuzi sana. Sikuwahi kufikiria kuwa anaweza akawa na mpango wa kipumbavu namna hiyo dhidi yangu. Nimeishi nae kwa miaka 30 sasa tangu akiwa hana kitu hata mavazi na chakula alishindwa kuifadhili familia. Aniache mimi nimemkosea nini? Eti shemeji nimemkosea nini mimi? Sasa ni mimi au Ketina. Hilo nitahakikisha kwa maji au damu.” Sara alionekana mwenye ghadhabu huku machozi yakionenaka kwa mbali.

“Shemeji, shemeji, shemeji basi usilie mtu ataingia hapa iwe tatizo. Ninachokuomba usimweleze chochote kwanza wakati huu ambao hatuna Uhakika sana na taarifa zozote, mimi nitaendelea kukutaarifu kila kinachoendelea na huyu kimada wake. Lakini pia nitafuatilia kuthibitisha ikiwa ni kweli kulikuwa na jaribio la mapinduzi na nitakumegea siri nikiwa na taarifa za uhakika zaidi’’, Gideon alimjaza Sara upepo huku akimvuta taratibu katika mpango wa kumng’oa Rais Costa bila Sara yeye kujua moja kwa moja.

“Sawa Shemeji. Ila bora huu mpango ungefanikiwa. Wasipompindua wao nitampindua mimi, I swear! Siwezi kukubali kudhalilishwa hata baada ya kumlea na kumfanya Costa kuwa Costa!” Sara alijibu kwa hasira na kutoka ofisini kwa Gideon.

Gideon hakuamini mapokeo aliyoonesha Sara. Alijua ni Dhahiri kuwa ikiwa Sara angekengeuka na kumdokeza Rais Costa kuhusu mazungumzo yale basi angekuwa kwenye hatari kubwa, lakini kama angeendelea kuwa mwanamke shupavu anayemfahamu basi huu ulikuwa ni ushindi kwa kambi yao.

Alichukua simu na kuingia kwenye game ya Clash Royale na kumtaarifu Joe kila kilichotokea.

“Sadam, Tiger is a living genius”, Joe alimjibu Gideon akimsifia Macha kwani mpango mzima kuanzia ule wa Gideon kutumwa kumtonya Sara mahusiano ya Rais Costa na Ketina mpaka Joe kumtaja Sara kwenye maongezi yao yote na hivyo kumfanya anahusika ili Rais Costa aanzishe ugomvi na mkewe, mpaka Gideon kufanya alivyofanya ni mchoro makini uliochorwa na Macha kabla ya misheni kuanza.

“Che, hata Tiger akifa leo nitampigia saluti nyingi sana”, Gideon nae alijibu.

“Sasa tunakaribia kumpata Sara. Huyu tutaenda nae taratibu kazi yake ipo mwishoni. Bahati Mbaya mtu pekee anayeifahamu kazi hiyo ni Tiger, hivyo hakikisha unapata nafasi ya kuonana nae kumpa hizo taarifa ili akueleze namna ya kumtumia Sara”, Joe alimalizia kuandika ujumbe na kuutuma kwa Gideon.
******************************************

Meshack aliwasili mji mkuu wa Stanza, Peron akitokea jimbo alilopangiwa kama afisa usalama baada ya kupamguliwa na Sabinas.

Aliwasili kwa ajili ya kazi moja tu kuhakikisha Sylvanus hapandi ndege kuelekea China kwa ajili ya kumuua Joe. Meshack alijua fika si rahisi Joe kumkwepa Sylvanus kwani ni muuaji hatari na mahiri lakini pia hakuwa na hakika ni kwa vipi atammudu Sylvanus, aliujua umahiri wake katika medani za kijasusi na ulinzi.

Aliwasili jijini Peron na kitu cha kwanza alichofanya ni kusubiri giza liingie. Siku aliyowasili kesho yake ndiyo haswa siku waliyokuwa wanasafiri kikosi kazi kilichotumwa kwenda kumuua Joe nchini China. Kikosi kile kilikuwa kinaondoka na ndege ya saa 12 asubuhi. Meshack alijua wazi anahitajika siyo tu kumnyamazisha Sylvanus lakini pia kuhakikisha haijulikani kama ni yeye.

Ilipotimia mishale saa tatu usiku hivi Meshack alitoka akiwa amevaa koti jeusi la baridi, raba nyeusi na jinzi nyeusi. Alivaa kofia nyeusi na shati la kijivu, na hakubeba silaha ya moto zaidi ya kisu kikali kidogo kilichokuwa na uwezo wa kujikunja na kuwa kama kiberiti. Mfukoni hakubeba kitambulisho chochote zaidi ya pesa kidogo.

Mchana wa siku hiyo Meshack alishinda akifanya mazoezi ya mikono (push ups) hivyo mikono yake ilikuwa imevimba kwa kujazia. Alibeba barakoa ya skii, hii ni aina ile kofia ambayo hufunika kichwa na uso na kuacha macho tu. Akiitunza kwenye mfuko wa koti pamoja na glavu nyembamba za kuvutika kama mpira zinazofanana na zile zinazotumika hospitalini. Meshack alitoka na kuanza kuzunguka mjini.

Meshack alijua tabia za Sylvanus. Alimjua ni mtu anayependa sana kucheza kamari kwenye mahoteli makubwa makubwa hasa Casino. Alifahamu kuwa usiku wa siku kama ile ni lazima angemkuta kwenye moja ya Casino akicheza kamari.

Japo aliifahamu hulka ile lakini alijua Sylvanus ni mtu mwenye machale, yaani haikuwa kazi rahisi kumnasa kwani ni mtu aliyesomea na kubobea katika kusoma mazingira na kukwepa kila inapowezekana. Hilo lilimpa wasiwasi Meshack.

Kama alivyowaza, Meshack aliingia New Continental Casino na alipotupa macho kwa mbali akiwa ndani ya kofia yake na miwani alimwona Sylvanus kwa mbali akicheza kamari. Kama ilivyokawaida, vile Meshack anaingia tu Sylvanus ni kama alihisi jambo akanyanyua uso na kaunza kuangaza macho.

Haraka Meshack aligeuza sura na kuangalia kaunta na kuanza kuelekea kuchukua kinywaji. Meshack alichukua kinywaji na kujibanza mahali alipohakikisha kuwa anamuona Sylvanus lakini Sylvanus hamuoni yeye.

Wakati akichukua simu ili aweze kumtaarifu Joe kuwa yupo kwenye misheni aliyomuomba hakuamini alichokisikia.

“Meshack”, mtu alimgusa bega kwa nyuma huku akiita jina lake.

Meshack alichanganyikiwa kwani aliamini kabisa kwa jinsi alivyovyaa hakuna mtu angeweza kumfahamu. Haraka Meshack alirusha macho kwenye machine ya kamari aliyokuwa anacheza Sylvanus, hakuamini, Sylvanus hakuwepo pale. Meshack aliishiwa nguvu.
*************************************
Nani Amemwita Meshack?Meja Byabato Imekuwaje?Yote Utayafahamu Wiki Ijayo.

the Legend☆
 
Lol..tutaachika kwa hii story yaani mpk wiki ijayo.?[emoji19]
Asante ndugu mwandishi wacha tuwe wapenzi wavumilivu chee km sadam[emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu natumbua macho mno kuona muendelezo niliishia sehem ya 9 naomba mnitag au ndo ishaisha?👀
 
Back
Top Bottom