FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #201
KaribuMkuu naweka kambi ya kudumuuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KaribuMkuu naweka kambi ya kudumuuu.
Nimerudi mkuuMkuu febiani umetuacha mbnona
Tunakusubiria mkúuu
Punguza hasira kiongozi.Oyaa endelea kutupa muendelezo basi..kama ulikuwa na mpango wa kuuza usingetuletea humu
DoneMkuu ukiweka mwendelezo utanistua
mbona ni kawaida yake, simulizi zake huwa amalizi naona huwa anaziweka kama matangazo ya kibiashara zaidiDah. Mtoa simulizi sijui kaingia wapi!!!???
Ngoja niamie huku kupunguza arosto ZA KULE KWINGINE fabiani BABUYAHADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
"Mnaweza kujiuliza kwamba inakuwaje niwe hivi na bado Justin aweze kunitambua? Jibu ni rahisi sana kwanza ni kwa sababu jina langu halisi mpaka hili ambalo nilikuwa nalitumia kwenye kazi alikuwa analijua lakini pia yeye ndiye ambaye alinifundisha hii michezo ya kuweza kubadili sura"
"Bosi unamaanisha huyu mtu mnafahamiana kabla ya hapa?" mwanaume mmoja aliuliza kwa mshangao
"Sio tumefahamiana bali tulikuwa marafiki wakubwa sana tena zaidi hata ya neno sana ndiyo maana hata niweje kwenye maisha yake yeye kunitambua mimi ni kazi rahisi sana. Kwenye shingo yangu nina alama nyeusi hapa ambayo kwa bahati mbaya sana ni yeye mwenyewe ndiye aliniumiza hivyo mimi siwezi kujificha mbele yake hata nikiwa vipi lakini je mnataka kujua pia kwamba alifanikiwaje kujua kwamba mimi bado nipo hai na bado ninaishi?" Robert aliongea huku akiwa anacheka na kumpiga piga mgongoni Nicole kwa sababu alikuwa karibu na alipokuwepo. Hakuna hata mmoja ambaye alijibu chochote kwa sababu kila mmoja alibakia anamwangalia mwenzake usoni, Robert alisogea mbele yao wote na kujichoma sindano ndogo shingoni ambapo ngozi ilijitanua kidogo akaivuta kwa nje na kuivua ile sura ambao alikuwa anaonekana nayo kwa muda mrefu sana kitu ambacho kiliwashangaza sana wote ambao walikuwa humo ndani wasiamini kile ambacho walikuwa wanakiona kwani mbele yao hakuwa mzee kama walivyokuwa wanamuona bali alikuwa na umri wa takribani miaka arobaini sita hivi.
"Justin alifanikiwa kunipata kwa sababu kuna msaliti humu ndani na ananisikiliza mpaka wakati huu ambao mnanisikiliza aliamua kuuza taarifa zangu" alikuwa anaongea akiwa siriasi sana huku akiwa amemkazia macho Hezroni ambapo bwana mdogo alianza kujitetea mapema.
"Bosi mimi siwezi kufanya jambo kama hili na unalijua hilo" kijana huyo alikuwa anatetemeka sana wakati huo Robert aliitoa bastola na kuielekezea kwa bwana mdogo huyo na kuwafanya wote wabaki wameduwaa.
"Najua Hezroni wewe hauwezi kunisaliti kwa namna yoyote ile lakini je ni nani unahisi ambaye ananisaliti mimi?" aliongea kwa sauti kali akiwa anawasogelea watu hao mbele yao huku akiwa anaikoki bastola yake. Aliigeuza ghafla sana na kuielekezea pale alipokuwepo Nicole na kumpiga risasi mkononi, mkono ambao Nicole aliutumia kuitoa bastola moja kwenye droo lakini aliwahiwa kwa sababu Robert alikuwa anajua muda sana kila alichokuwa anakifanya. Alicheka sana huku akiwa anamsogelea Nicole akiwa ameegamia meza anavuja damu kwa maumivu makali sana bastola ikiwa chini.
"Hili jambo nilikuwa nalijua mapema sana Nicole kwamba wewe ni msaliti na hapa nilitaka kuwadhihirishia wenzako kwamba wewe unatusaliti sisi kwani kama ningefanya maamuzi bila wao kuona unacho kifanya basi wangepoteza imani na mimi kwa kuhisi siwaamini kabisa lakini sio kweli kwa sababu hata baadhi ya akaunti zangu za benki wote mna uwezo wa kuingia na kutoa pesa sasa utasema vipi siwaamini?"
"Kitu kimoja ambacho ulifanya makosa kwenye kazi yako ni kushindwa kujua kwamba server za hiyo mitambo ambayo mlikuwa mnaitumia nilikuwa na mifumo yake yote kwenye simu yangu hivyo kila ambacho mlikuwa mnakifanya ilikuwa ni lazima mimi niipate taarifa mapema sana kwenye simu yangu. Kwa muda mrefu sana kwenye dark web kuna picha zangu zilisambazwa na aina mbali mbali za sura za kufake ikiwemo hii ambayo huwa naitumia kwamba kama kuna mtu atakuja kuniona mahali basi aripoti kwa watu hao atajipatia pesa za kitanzania taslimu Bilioni moja. Je unahisi nilikuwa sijui Nicole?"
"Hayo yote niliyafahamu mapema ndiyo maana baadae baada ya kufanya na mimi kazi kwa muda ukaamua kuanza kuuza siri zangu huku ukiwaambia kwamba unanifahamu na muda wowote unaweza ukanikamatisha kwao lakini ukawa unahitaji malipo kwanza ila nao waligoma kwa kutaka kwanza uthibitisho na ndiyo sababu siku ile ulilazimisha sana kupiga picha na mimi ambapo picha hiyo uliitumia kuwatumia kama ushahidi na baada ya hapo wakakuahidi kukupatia milioni mia tano kwanza ambayo kweli walikulipa na milioni miatano nyingine wangekupa ukinikamatisha kwenye mikono yao. Hivyo uliwapa taarifa za namna ya kunipata lakini kwenye ile nyumba kubwa hukutaja kwamba ndipo tunaishi kwa sababu ulijua wazi kwamba ningejua mhusika ni wewe lakini hata wewe mwenyewe bado ulikuwa na wasiwasi ukiamini kwamba wanaweza kukuua wakikukuta hivyo ukataka kujitoa nje ya msala na kunipakazia mimi"
"Mimi sishangaia sana kwa sababu naelewa pesa inaweza kununua nafsi ya mtu ila kitu ambacho kilinikera sana ni kuhatarisha maisha ya Hezroni kwa sababu kama mtu yule wakati anarudi angemkuta basi alikuwa anamuua moja kwa moja na hata wewe mwenyewe angekutafuta kuja kukuua. Huwezi ukala pesa ya Justin halafu ukaishi hata kama umemfanyia ni kazi, yule mchaga anaipenda pesa kuliko hata maisha yake yeye mwenyewe"
"Lakini licha ya hayo yote Nicole bado nilichagua kukupa nafasi nyingine bila kukuuliza wala kukuchukulia hatua yoyote ile nikiamini kwamba huenda ungeweza kubadilika lakini ni wazi kwamba haukuwa kabisa tayari kubadilika hata tulipo fika hapa bado umeamua kutuuza tena kwa mara nyingine, je bado unahitaji mimi nikuache hai?" Robert alimpatia mwanamke huyo maelezo kumuonyesha kwamba alikuwa na uhakika sana na taarifa zake wala hakuwa anabahatisha hivyo mrembo huyo alitakiwa sana kulielewa jambo hilo kwamba wenzake waliamkia pale ambapo yeye anakilaza kichwa chake ili kupumzika.
"Bosi unamaanisha nini kusema kwamba ametuuza na hapa?" mwanaume mmoja aliuliza akiwa anaanza kupata mashaka.
"Ametoa taarifa kuna watu wanakuja hapa muda huu kutuchukua"
"Oooooh nooooooooo" mwingine alipingana na hilo jambo akiwa anafunua pazia kuangalia nje, kwa mbali sana aliona msafara ukiwa unakuja kwa kasi sana kuelekea kwenye jengo hilo. Walipatwa na hasira sana, mwanaume mmoja alimsogelea mwanamke huyo na kuitoa bastola ambapo alimtandika risasi nyingi sana mwilini huku akiwa anaomba msamaha kwamba asingeweza kurudia tena juu ya jambo hilo lakini alikuwa amechelewa sana hivyo walitakiwa kupotea haraka sana na ndicho walicho kifanya hata ile simulizi ya historia ya maisha ya Robert kabla ya siku ile hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaihitaji tena maisha yao yalikuwa ya mhimu kwanza.
Walitokea upande wa pili na kutokomea eneo hilo huku Hezroni akiwa amekaa kwenye komputa mpakato yake wakiwa kwenye gari na kusababisha shoti kubwa sana ndani ya ile sehemu na wakati watu wale wanafika pale ulitokea mlipuko mkubwa sana ambao uliliteketeza jengo hilo kazi nzuri iliyokuwa imefanywa na Hezroni hivyo hata wavamiaji ambao walikuwa wanaongozwa na Justin hawakusimama tena eneo hilo wakawa wametoweka haraka sana maana polisi wangeingia sehemu hiyo muda wowote ule.
Kikao kizito kiliitishwa usiku sana ndani ya WE ARE BROTHER'Z TECH COMPANY. Ethan Kamau ndiye alikuwa bosi wa kampuni hiyo kubwa sana ya teknolojia, alikuwa na uraia wa nchi ya Kenya na hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anamfahamu hata katibu mkuu kiongozi hakuwahi kumuona mwanaume huyo hata siku moja zaidi ya kuishia kuwasiliana naye kwenye simu tu.
57 sina la ziada.