HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
Raisi alibaki kwenye ofisi yake ambapo alisimama na kuifungua simu yake, aliifungua picha ya mwanamke huyo Mariana Amboni kisha pembeni akawa anaiangalia picha kubwa ya mkurugenzi Cleopatra Gambo. Alicheka sana mheshimiwa, wanawake hao walikuwa wanaicheza karata moja ngumu sana ambayo huenda bila msaada mkubwa wa Anelia Baton asingeweza kuing'amua haraka kisha akaitoa simu yake.
"Mpango umebadilika, vijana utakutana nao kesho lakini mimi na wewe tunatakiwa kukutana muda huu ndani ya Kilimanjaro Hotel kwenye chumba namba 101 haraka sana" hakutaka hata kusubiri jibu upande wa pili akaikata simu hiyo na kutoka ndani ya ofisi yake.
Ndani ya nusu saa baadae usiku wa manane sana mheshimiwa alikuwa ndani ya chumba ambacho alikuwa ameahidi kuwepo, alikuwa upande wa dirishani akiwa anaangalia chini ya jengo hilo kubwa ambapo aliona msafara wa gari mbili ukiwa unaingia ndani ya eneo hilo, alitabasamu.
Ulinzi ulikuwa ni mkali sana ndani ya hilo eneo ambapo mwanaume ambaye alikuwa anafika hapo alikaguliwa sana na walinzi wake ambao alikuja nao walibaki nje kisha yeye akaingia ndani kukutana na bosi wake akiwa na begi ya laptop mkononi.
Walikumbatiana na kusogea kwenye meza kubwa kisha wakakaa hapo. Mwanaume ambaye alifanikiwa kufika ndani ya hiyo sehemu ndiye yule ambaye alipigiwa simu na mheshimiwa kwamba anamhitaji haraka sana aweze kufika Tanzania na ndiye ambaye kesho yake alitakiwa kuwepo kwenye kikao na wanaume watano ambapo mmoja alipotea ambaye ni ULIMBOKA.
"Bosi ni usiku sana saivi, kuna usalama kweli?"
"Hapana kungekuwa na usalama ningehitaji tuonane asubuhi. Kuna kazi ambayo inatakiwa kufanyika haraka sana kabla hakujapambazuka" mheshimiwa aliongea akiwa anaitoa karatasi ndogo kwenye mfuko wake na mwanaume yule aliipokea kwa mashaka sana akiwa anamwangalia mheshimiwa.
"Hiyo ni address na namba ya nyumba najua kupitia hiyo unaweza kuidukua nyumba hiyo ukapata taarifa za siri za mmiliki na kila kinacho endelea hapo sio?"
"Ndiyo mheshimiwa kama tu mmiliki wa nyumba aliweka taarifa zake hata kama ni kwa siri sana inawezekana kuzipata"
"Itachukua dakika ngapi?"
"Tatu tu"
"Do it" huyo mwanaume licha ya kuwa mtu hatari sana lakini pia alikuwa ni mdukuzi wa kutisha mno ambaye alikuwa amefanya kazi nyingi sana za hatari ila ni wanadamu wachache sana ambao walikuwa wanalifahamu hilo au kuufahamu ukweli kuhusu mtu huyo.
"Mmiliki wa hili eneo anaitwa Mariana Amboni, ni mwanajeshi mstaafu kwa sasa na ni mama wa mtoto mmoja ambaye hakuna taarifa yake yoyote"
"Umesema ana mtoto mmoja?"
"Ndiyo bosi na huyo mtoto ndiye ameandikwa kama mmiliki wa hiyo nyumba" mwanaume huyo aligeuza laptop yake ili mheshimiwa aweze kujionea mwenyewe.
"oooooh fu**k na kuhusu familia?"
"Ana ndugu mmoja japo kwenye hiyo sehemu ambayo inaonyesha family tree pamewekwa kivuli, hii ina maana kwamba taarifa za huyu ndugu yake zimefichwa"
"Hahaha hahahah hahahah kwenye nchi hii ni nani ambaye anajiamini kuweze kunifanya mimi mpuuzi kiasi hiki?" mheshimiwa alicheka na kuongea kwa jazba sana huku akiendelea yeye mwenyewe.
"Oooooh Cleopatra son of a b***" alitukana tusi zito sana kwenda kwa mkurugenzi. Huyo mwanamke hapo taarifa za CDF zilionyesha kwamba hakuwa na uwezo wa kuzaa na wala hakuwa na ndugu yeyote lakini taarifa za siri zilikuwa zina eleza kwamba mwanamke huyo alikuwa mama wa mtoto mmoja na alikuwa na ndugu mmoja ambapo wote walikuwa ni siri nzito sana.
kisha akakumbuka tena CDF alimwambia kwamba kuna taarifa zilikuwa zinadai kwamba mwanamke huyo aliwahi kuonekana na Domimic Sawa Sawa. Maana yake ni kwamba kulikuwa na mawili, kama sio kuzaa na Dominic Sawa Sawa basi alikuwa amemlea mtoto wa Dominic Sawa Sawa kwa siri kubwa sana na huenda ndiyo sababu ya yeye kuweza kustaafu jeshi na kutohitaji maisha yake yaje kuwa wazi tena.
"Ina maana mtoto mmoja wa Dominic Sawa Sawa yupo hai? Oooooh shiiiiiit!" alitamka huku akiwa anabamiza chupa kubwa ya wine chini kwa hasira sana. Alikuja kulitambua hilo akiwa amechelewa sana mheshimiwa na ndio wakati ambao alianza kuelewa kwamba ni kwanini ilitoka taarifa kama ile kwenye gazeti ili kumtaka kupiga goti hadharani na kuomba msamaha, ilikuwa ni kwa sababu mtu huyo alikuwa amerudi kuchukua kile ambacho wao walimbebea. Mwanaume aliyekuwa kwenye laptop yake hata yeye baada ya kusikia jambo hilo lilimshtua sana.
"Bosi hili jambo haliwezekani kabisa"
"You fAILED ME BIG TIME BOY" alimgeukia mwanaume huyo na kumkwida shingoni akiwa anamtamkia kwa hasira sana kwamba alimfelisha sana.
"Bosi kila kitu kilifanyika kama ilivyokuwa inatakiwa"
"Mpaka leo tusingekuwa hapa mpuuzi mkubwa wewe kama kazi ilifanyika kwa usahihi kama unavyotaka kuanza kunidanganya hapa. Mimi na wewe tutalizungumza hili kwa marefu ili unipe sababu za msingi za mimi kutowaua ninyi nyote wapuuzi wakubwa, for now huyo mwanamke nakupa masaa mawili awe kwenye mkono wako vinginevyo nakuua wewe" alitamka kwa msisitizo mkubwa sana mheshimiwa huku akiwa anabeba kofia yake na kutoka ndani ya chumba hicho kwa hasira kali sana kwa sababu vijana wake walionekana kufanya kazi kipumbavu sana kitu ambacho hakukubaliana nacho hivyo kabla ya asubuhi alitoa amri kwamba mwanamke huyo awe amepatikana vinginevyo kijana wake huyo ndiye alitakiwa kufa kwenye mikono yake hivyo ilikuwa ni kwake kuchagua cha kufanya.
Mkurugenzi baada ya kushindwa kuelewana na mdogo wake wakati ambao alipigiwa simu akiwa anatoka kwenye kambi kuu ya jeshi la nchi alirudi nyumbani kwake kuweza kulala lakini hakupata hata lepe la usingizi kwa sababu moyo wake ulikuwa unamuenda mbio sana na alikuwa anaumia sana kwa kile ambacho alikuwa amekifanya, alijihisi hatia kubwa sana ndani ya moyo wake na kuona amemkosea sana mdogo wake hivyo alitamani kumpigia simu ili amuombe msamaha.
Aliamka kutoka kitandani na kuipiga namba nyingine ya siri sana ambayo ilikuwa ni ya chumbani kwa mdogo wake. Simu iliita mpaka ikakata, alipiga kwa mara ya pili lakini bado haikupokelewa. Moyo wake ulianza kwenda mbio sana asijue kwamba shida ilikuwa wapi hivyo akalazimika kupiga simu kwa walinzi wa mdogo wake lakini hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anapokea simu. Alishtuka sana Cleopatra Gambo, hilo halikuwa jambo la kawaida bali kulikuwa na hatari ambayo ilikuwa inajieleza mbele ya macho yake na kwenye moyo wake. Alivaa haraka sana na kuchukua silaha kisha akatoka nje na kuwataka vijana wake waondoke naye kwani kulikuwa na dharura ya mhimu sana wakati huo hivyo msafara wa gari tatu ukaingia barabarani ukiwa kwenye kasi mno.
55 inafika mwisho.