Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA PILI
Mkuu wa gereza alimsogelea mwanaume huyo huku akiwa anatabasamu sana lakini baada ya kufika na kumkagua mtu huyo aliikunja sura yake vibaya kwa ghadhabu kubwa.

"Wewe ndiye mpuuzi mmoja ambaye umenifanya mpaka usiku huu nishindwe kulala na mwanamke wangu nikae nikikusubiri hapa? Siwezi kuacha hili lipite, nakuhakikishia lazima ukalipe kwa hili mpuuzi mkubwa wewe. Niliwahi kuapa kwamba watu ambao walikuwa kwenye gereza hili walikuwa wanatosha na sikuwahi kuhitaji kuletewa mtu mwingine ila wewe umefanya kosa la aina ile ile ambalo sikuwa nahitaji litokee na hatimaye umeletwa huku sehemu ambayo hatakiwi kuhifadhiwa mwanadamu wa kawaida, je unajua ni kipi kitakupata kwenye maisha yako bwana mdogo? Niamini mimi ni bora wakati wa kiangazi ungeenda kuishi jangwani sehemu ambako hakuna hata maji ila sio kuletwa sehemu kama hii" aliongea akiwa anamzunguka mwanaume huyo ambapo alimtwisha rungu la chuma mgongoni lakini mwanaume huyo alibaki ameganda tu hivyo hivyo bila kutamka neno lolote lile wala kutikisika.

"Una familia?" kwa mara ya kwanza mwanaume huyo aliitoa sauti yake ambayo ilikuwa nzito sana na ya kukwaruza kwa mbali akionekana wazi kwamba alikuwa anamlenga ni kiongozi huyo wa hilo gereza. Alihisi aliisikia vibaya kiasi kwamba akawageukia vijana wake lakini aligundua kwamba mwanaume huyo alikuwa amemlenga ni yeye mwenyewe. Alishikwa na hasira kali mno kitu ambacho kilimfanya atoe bastola yake na kumpiga risasi mbili za kwenye mapaja mwanaume huyo mpaka akashindwa kusimama na kuishia kupiga magoti huku akiwa anauma meno kwa maumivu makali sana ambayo alikuwa anayapata wakati huo.

"Mpuuzi mkubwa wewe kijana, wewe hapo ndiye mtu ambaye unathubutu kuliingiza jina la familia yangu kwenye huu upuuzi wako? ulitakiwa kuisoma historia ya maisha yangu ya nyuma. Nina historia mbaya sana ya haya maisha mpaka leo kuwa kiongozi kwenye gereza kama hili ni bahati nasibu kwa sababu mimi nilitakiwa kuwa miongoni mwa wafungwa ambao wangekuwa wanayaishi maisha magumu ila mimi ndiye kiongozi kwenye sehemu kama hii. Ukajifunze maana ya jina langu la pili la Gambino nililipataje, kaisome familia yenye historia ya jina hilo huko Marekani kisha utagundua kwamba umefanya kosa kunijibu nikiwa naongea" aliongea kwa hasira huku akiwa anairudisha silaha yake kwenye mfuko wake ambao uliunganishwa na ganda lake kisha akawageukia vijana wake.

"Hatakiwi kulala kwa masaa arobaini na nane, apitie mateso makali ila hakikisheni hafi na hizo risasi atakaa nazo kwa muda mwilini akili imkae ndipo ataelewa kwamba huku sio kwa ajili ya watoto wa mama ambao wakiguswa tu wanataka kuwalilia mama zao na kuhitaji kunyonya. Akimaliza hiyo adhabu ndipo aanze kupatiwa matibabu kidogo kidogo" alitamka huku akiwa anageuka na kuelekea kwenye ofisi yake, muda ulikuwa umeenda sana hivyo alihitaji kurudi ili akajiandae kupumzika maana kazi ya kumpokea mfungwa huyo ilikuwa imekamilika tayari.

Mwanaume huyo akiwa ndani ya maumivu makali kwenye mwili wake, aliunyanyua uso wake ambao haukuwa na nuru hata kidogo kuangalia juu ya ukuta wa kuingilia kwenye vyumba ambavyo walikuwa wanahifadhiwa wafungwa mbali mbali, huko aliona maandishi makubwa tena yakiwa yameandikwa GEREZA LA DOMINIC. Baada ya kuliona jina hilo, kuna picha nyingi zilikuwa zinapita kwenye kichwa chake kwa kasi sana kiasi kwamba zilianza kumuumiza mpaka akayafumba macho yake, alipokuja kushtuka wanaume walikuwa wapo nyuma yake wakimnyanyua kwa nguvu huku wakimpiga na vitako vya bunduki zao kumtaka aelekee sehemu ambayo yangekuwa makazi yake mapya kwa wakati huo.

Luka Gambino baada ya kufika kwenye ofisi yake alisogea mpaka kabatini ambako alitoa chupa ya pombe na kuanza kuinywa kwa pupa akionyesha kutoridhika na kauli ya mwanaume ambaye muda mfupi uliokuwa umepita alitoka kumpokea kwa makamanda wa jeshi. Akiwa anainywa hiyo pombe yake aliingia msaidizi wake akiwa na bahasha mkononi mwake.

"Kuna kingine umesahau?"
"Ndiyo bosi"
"Sikio langu ni lako" alimaanisha anamsikiliza.

"Kuna hizi taarifa za mtu huyu zimefika muda sio mrefu, kuna mtu amezileta inaonekana zilisahaulika, pia kuna frashi ndogo inasemekana kwamba kuna taarifa zote za mtu huyo hivyo itakuwa ni jambo la busara kama tutafanikiwa kuweza kuzipitia na kuweza kumjua kiundani ukiachana na zile taarifa fupi ambazo zilikuja mwanzo" mheshimiwa baada ya kumsikia kijana wake anaongea hayo maneno, alisogea kwenye kiti na kumpa ishara kijana huyo kuelekea ukutani ambako kulikuwa na skrini kubwa ili aweze kumchambulia taarifa hizo na maelekezo yake yaliyokuwepo ndani.

"Remy Claude ndilo jina lake linalo daiwa kuwa la kuzaliwa lakini jina lake ambalo linafahamika sana kwa watu wake ni Menace likiwa na maana ya muuaji wa hatari. Mwaka huu anaingia mwaka wa thelathini na sita tangu azaliwe, hakuna alama yoyote ambayo inaonyesha kwamba alizaliwa wapi na lini ila taarifa zilizopo ni kwamba ni mtoto wa mtaani ambaye maisha yake hayana mwanzo bali mwisho wake utakuwepo."

"Ni kiongozi wa genge la hatari sana la kihalifu ambalo linajulikana kwa jina la SARAFU KUMI NA TANO (FIFTEEN COINS). Hizo sarafu kwa mujibu wake ni kwamba zilishapotea hivyo anazitafuta na haijulikani kwamba hizo sarafu zina maana gani kwa sababu jina la genge hilo linaonekana lilibadilika baada tu ya yeye kuanza kuliongoza"

"Watu ambao alikuwa anawaongoza kwenye genge hilo wanadaiwa kwamba kwa sasa wote wamekufa kwa kuuawa na mtu pekee ambaye amefanikiwa kuishi ni yeye ambaye ndiye alikuwa kiongozi. Ni genge la kimafia ambalo limesababisha athari kubwa sana kwa taifa yakiwepo mauaji ya kutisha, kuliyumbisha taifa kiuchumi lakini ilidaiwa kwamba pia genge hilo lilikuwa likisambaza madawa ya kulevya mitaani na kuwatumikisha vijana wengi kwa kuwaachisha masomo na kuwaingiza kwenye biashara hiyo huku wote ambao walikuwa wanapingana na genge hilo walikuwa wanaishia kuuawa na wanawake kubakwa hovyo hovyo" msaidizi wa mkuu wa gereza aliacha kwanza kuichambua na kuisoma taarifa hiyo huku jasho likiwa linamtoka kwenye uso wake. Yalikuwa ni maelezo ya juu tu lakini yalikuwa ni maelezo mazito sana ambayo hayakuwa na usalama mkubwa kwa walikokuwa wanaelekea. Alikunywa maji na kuikuza picha kubwa ya mwanaume ambaye walikuwa wanamuongelea hapo akiwa ndani ya suti safi na begi lake huku kwenye kichwa chake akiwa na nywele nyingi za kutosha kisha akaendelea tena.

"Baada ya jambo hili kutokea na kuwa kubwa mtaani ndipo serikali ilitengeneza mazingira ya kuweza kumkamata mtu huyu. Kumkamata haikuwa kazi rahisi kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye pesa na jina hivyo ulikuwa unahitajika ushahidi wa kutosha ili kumpata kwani kazi yake alikuwa anaifanya kwa usahihi na umakini sana. Hali hiyo ilipelekea maafisa wengi kupoteza maisha kwa wale ambao walikuwa wanaingia kwenye njia zake ili kuweza kumtafutia ufumbuzi mtu huyo na ndipo shirika la usalama la nchi lilipo amua kumvalia njuga kisawa sawa baada ya kukerwa na kupotea kwa maofisa wengi ambao walikuwa wanapewa kazi ya kuweza kumfuatilia mtu huyu"

"Sentinel Nexus Intelligence Agency (SNIA), shirika letu la usalama wa taifa chini ya mkurugenzi Cleopatra Gambo lilimteua mwanamke mrembo Anelia Baton kuweza kuifanya kazi ya kufanikiwa kumuweka karibu mwanaume huyo ili kujua njia zake zote ambazo alikuwa anazitumia kwenye biashara yake kwa ujumla lakini bila kusahau kuweza kuuangamiza mtandao wake wote ili ikiwezekana akamatwe ama kuuawa japo serikali ilikuwa ikimhitaji zaidi awe hai kwani angekuja kuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa hapo baadae"

Sehemu ya pili inafika mwisho.

Wasalaam,
Iko njema sana
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA TATU
"Mwanamke huyo ambaye alikuwa na urembo usio elezeka na umbo ambalo dunia ilipata kustaajabu ule urembo wa asili usio na kasoro yoyote ile kwa mwanadamu, mwanamke ambaye alikuwa na taaluma ya udaktari ndiye mpelelezi ambaye aliwekwa chambo mezani kuweza kumpata mhalifu Remy Claude. Taarifa za siri kuhusu mwanamke huyu (confidential information) hazitaji wazi kwamba alitumia njia gani kuweza kuingia huko ila ni kwamba njia hii iliweza kuzaa matunda kwa ukubwa sana na kufanikiwa kuliangusha genge hili hatari hapa nchini. Penzi likaliokoa taifa kutoka kwenye hatari ya kuweza kuyumbishwa na kuteketezwa na genge hilo" mkuu wa gereza baada ya maelezo hayo aliguna kidogo na kumtaka msaidizi wake aweze kumuonyesha picha ya mwanamke ambaye alikuwa anaongelewa hapo.

Alisimama kutoka pale alipokuwa ameketi na kusogea mpaka kwenye ile skrini, aliigusa na kuikuza ile picha ya huyo malaika ambaye alikuwa anazungumziwa hapo, hakuamini alichokuwa anakiona, bado hakuwa kwenye fahamu zake kuweza kuamini kwamba taifa la Tanzania lilikuwa na mwanamke mrembo wa namna hiyo, hilo ni jambo ambalo kwake lilikuwa ni gumu kuamini.

"Unataka kuniambia huyu binti ni mzaliwa wa hili taifa?"
"Ndiyo bosi, kama sio hivyo wasingeweza kumtumia kwenye kazi nyeti namna hii"
"Mhhhh natamani nipate bahati ya kuja kuutumia hata usiku mmoja kitandani na mwanamke huyu. Baada ya hapa hakikisha unamtafuta kwa gharama yoyote ile"

"Lakini bosi, japo taarifa zake zinadaiwa kuwa za siri huyu mwanamke lakini kuna sehemu hapa inaonyesha alama ya X kwenye picha yake ikiwa ni kama tafsiri ya kwamba huenda alishakufa"
"Hapana, mpaka tuhakikishe hilo, kama angekuwa amekufa basi wangeonyesha moja kwa moja kwenye hizo taarifa huyu atakuwa yupo hai na anaishi mahali kwa starehe kabisa"

"Sawa bosi, nitafanya hivyo"
"Ebu malizia maelezo ya huyu mtu kisha mimi nikalale, umekuwa usiku mrefu sana leo"

"Baada ya mwanamke huyo kufanikiwa kutoa taarifa zote za mtu huyu ambaye serikali ilikuwa inamtafuta kwa miaka kumi bila mafanikio hatimae kikosi maalumu kiitwacho HOLY TRINITY (UTANO MTAKATIFU) huku wao wakipenda kujiita TULIKUFA TUKIWA HAI, kilitumwa kwenda kumchukua mtu huyu sehemu ambayo walielekezwa kwamba alikuwepo"

"Hicho kikosi umewahi kukisikia au unakifahamu?" mkuu wa gereza alishtuka kusikia jina kama hilo kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupata kulisikia jina la namna hiyo ndiyo maana aliamua kuingilia maelezo ya kijana wake.

"Hapana bosi, imeandikwa (confidential) hizi taarifa zao hakuna mtu ambaye anatakiwa kuzijua wala kuwajua, nadhani wakubwa ndio watakuwa na majibu sahihi kwamba hiki kikosi ni kipi na kilianzishwa kwa ajili ya jukumu lipi"
"Endelea"

"Watu hawa wapo watano tu ambapo kiongozi wao ni mwanamke, hawa ndio ambao walifanikiwa kumkamata mwanaume huyu baada ya pambano la muda mrefu na baada ya hapo walimzidi nguvu kwa sababu inadaiwa kabla alikula chakula chenye sumu ya kulegeza mwili hivyo walifanikiwa kumkamata na kuteketeza watu wake wote na ndipo alipelekwa mahakamani kwa kosa la kuua watu kumi kwa makusudi pamoja na uhalifu wa hilo genge lake, akahukumiwa miaka sitini jela. Akiwa kwenye gereza la kwanza aliua askari watano na wafungwa wenzake kumi na watano na ndipo ikaamuliwa aletwe huku baada ya kupata kipigo kikali sana kutokana na ujeuri ambao alikuwa nao"

Habari ya mwanaume huyo namna alivyoweza kukamatwa na utambulisho wake uliokuwa mezani ulikuwa umeishia hapo, uliletwa ili mkuu wa gereza aweze kujua mtu ambaye alikuwa amemuweka kwenye mkono wake alikuwa mtu wa namna gani. Baada ya kufanikiwa kumaliza maelezo hayo na kuangalia picha ambazo zilikuwepo kwenye frashi ambayo walikuwa wamepewa waliiona video moja, ilikuwa ni video ya dakika mbili tu ambayo walitakiwa kuiangalia kwa umakini sana kabla ya kuacha kila kitu ambacho kilikuwepo.

Kwenye video walikuwa wanaonekana wanaume sita ambao kwa mwonekano tu walikuwa ni makomando kutokana na magwanda ambayo yalikuwa kwenye miili yao wakiwa wamemzunguka mwanaume mmoja ambaye alikuwa amejifunika uso wake huku akiwa ameipa kamera mgongo na kwenye mwili wake akiwa amevaa mavazi meusi. Kwenye mkono wake mwanaume huyo alikuwa ameishika sindano ya kushonea viatu huku komando mmoja akiwa amemuweka chini ya ulinzi.

Katika moja kati ya makosa makubwa ambayo komando huyo aliyafanya ni kumsogelea karibu mtu huyo ambaye alifanya jambo la ajabu na la kushtua. Aliugeuza mkono ambao ulikuwa na sindano kwa nguvu, wakati anageuka baada ya kupiga mahesabu na kugundua kwamba mtu ambaye alikuwa na silaha alikuwa na uwezo wa kumfikia pale alipokuwepo. Komando huyo baada ya kupata mshtuko aliachia risasi ambayo alichelewa kuiachia kwa sababu mtu huyo alikuwa amefika karibu na usawa wa bunduki hivyo risasi ikaenda hewani wakati huo mkono wake uligeuzwa vibaya ambapo alichomwa chomwa sindano nyingi kwenye mkono wake ambazo ziliishia shingoni.

Alichanwa chanwa shingo vibaya kisha sindano ikazamishwa ndani ya shingo na ilipokuja kutolewa, koromeo halikuwa likifaa kabisa. Alishuka chini taratibu akiwa amejishika shingoni hata silaha yenyewe hakuwa na uwezo wa kuishika tena, hali yake ilikuwa mbaya mno na dakika za yeye kuwa hai zilikuwa zinahesabika muda wowote alikuwa anaenda kupoteza maisha yake. Hata wenzake walibaki kwenye mshangao mkubwa maana lilikuwa ni jambo ambalo lilifanyika kwa haraka kiasi kwamba hawakuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo.

Waligadhabika kwa hali ambayo ilikuwa imemtokea mwenzao, alijifyatua mmoja kwa kasi na buti lake zito ambalo lilimpata mwanaume huyo kifuani lakini hakutetereka wala kurudi nyuma. Komando yule alitua mguu wake chini na kuirusha ngumi kali ambayo ilimpuliza mwanaume yule kwenye uso wake kisha akageuka na mateke ambayo yalikuja mfululizo. Ni teke moja tu lilizama tena kifuani ila lingine wakati linakaribia mwanaume huyo alilizuia kwa kutumia sindano ambayo ilikuwa kwenye mkono wake.

Sindano hiyo iliuchana mguu wake kwa maumivu mno kiasi kwamba wakati anataka kugugumia kwa hayo maumivu makali alijisahau, alipigwa ngumi mbili za haraka kwenye kifua chake. Alibaki amesimama tu akiwa ameyatoa macho yake kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kujongea, kuhema wala kuongea. Mkuu wa gereza aliisimamisha video hiyo kwa mshangao mkubwa sana akasogea karibu zaidi ili kuweza kuangalia kwa usahihi kwamba ni kipi kilifanyika. Alicho kishuhudia ni kwamba ngumi ambazo zilitua kwenye kifua cha yule komando zilimletea madhara kiasi kwamba moyo wake ulisimama kufanya kazi hivyo akawa hana namna ya kuishi. Video ilipo ishia pale ambapo ilikuwa imefikia, komando yule alidondoka chini akiwa tayari ni wa juzi

Sehemu ya 3 niseme baaasi.

Wasalaam.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA NNE
Hakutaka hata kukaa tena, alihitaji kuona kwamba ni kipi ambacho kilikuwa kinaenda kutokea hata kwa wale wanne ambao walikuwa wamebaki pale. Hao walimchangia wote, uzembe mdogo tu uliwapoteza wenzao wawili kiwepesi mno hali ambayo hawakuwa tayari kuendelea kuiruhusu iweze kutokea hata kwao. Ujio wao ulikuwa mzito, walimpiga ngumi nyingi mwanaume yule kiasi kwamba alishindwa kuhimili hivyo alidondoka mpaka chini ambapo alitua kwa mkono mmoja na alipo nyanyuka alikuwa ameukunja mkono wake mmoja na sindano yake kwenye mkono wa kushoto.

Alifanya mauaji ya kikatili sana kwa watu hao ambapo aliwaua makomando wawili kwa kuwachana chana sehemu za shingoni huku komando mmoja akimzamishia sindano hiyo kwenye mdomo wake na kuisindikiza na ngumi kali ambayo ilimfanya mwanaume huyo kuimeza sindano hiyo kwa lazima. Alihangaika sana akiwa anapiga kelele lakini aliishia kujichomeka kwenye nondo ambayo ilikuwa ukutani akiwa anakimbia kimbia kila sehemu kutokana na maumivu makali ambayo alikuwa ameyapata hivyo mmoja ndiye pekee alikuwa amebakia hapo.

Mwanaume huyo alijisachi kwenye kiuno chake, hakuwa na kitu zaidi ya kisu kimoja tu na hapo ndipo akakumbuka kwamba aliyekuwa na bastola ni mmoja tu ambaye alikuwa wa kwanza kufa. Aliangalia umbali wa ile bastola ilipokuwa imeangukia, hesabu ziligoma asingeweza kuiwahi maana adui yake ambaye walimfuata hapo ndiye alikuwa karibu zaidi na hiyo bastola. Njia pekee ambayo alikuwa amebakiwa nayo ni kumvamia mwanaume huyo na kisu ambacho kilikuwa kwenye mkono wake.

Alisogea nacho kwa spidi lakini mwenzake alikuwa amempigia hesabu za muda mrefu kwani wakati anakaribia mwanaume huyo alichomoa bastola kwenye kiuno chake kisha aliipigiza kwa nguvu kwenye buti lake kuikoki vizuri na alipokuja kuinyanyua tena, risasi sita ziliishia kwenye kichwa cha komando ambaye alikuwa amebakisha hatua moja tu kumfikia mwanaume huyo. Baada ya kuhakikisha amewaua wote sita, aligeuki sehemu ambayo bila shaka hakujua kama kuna kamera, akakitoa kitambaa ambacho kilikuwa kimemfunika uso wake.

Sura ambayo Luka Gambino aliiona ilimshtua sana. Alikuwa ni Remy Claude, mwanaume ambaye muda mchache uliokuwa umepita yeye ndiye alikuwa amempokea ili aanze kuitumikia miaka yake sitini akiwa ndani ya hilo gereza ambalo lilikuwa linatajwa kutokuwa kabisa na haki za binadamu, mtu akiwa huko hakuwa na thamani yeyote ile na wala hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaruhusiwa kuweza kumuona eneo hilo kwa namna yoyote ile. Huo ndio ulikuwa utangulizi wa Remy kwa mkuu wa gereza la Dominic, gereza ambalo haikujulikana kwamba ni kwanini lilikuwa linamtoa machozi mwanaume huyo ambaye kwenye video alionekana kutokuwa na ubinadamu ndani yake. Huyo ndiye mtu ambaye alisisitizwa kwamba asije akamtoa kwenye hiyo minyororo bila kuwa na uhakika na usalama wake binafsi lakini pia na usalama wa watu wote ambao walikuwa wanapatikana ndani ya eneo hilo.

Mfungwa huyo alikuwa anatakiwa kuja kutoka gerezani akiwa na miaka tisini na sita kwa hukumu yake ya miaka sitini ilivyokuwa inajieleza. Remy Claude, The Menace.

SNIA HEAD QUARTERS
Nje kabisa ya mji, yalipokuwepo makao makuu ya shirika la usalama la nchi ya Tanzania, kulikuwa na kikao kizito sana ambacho kilikukwa kinaendelea. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo madam Cleopatra Gambo alikuwa na kikao na msaidizi wake pamoja na vijana wake ambao walikuwa ni mhimu hususani kwa kazi kubwa ambayo walikuwa wametoka kuifanya muda sio mrefu. Alikuwa nao hapo kwa ajili ya kujadili hatua ambazo walikuwa wamezipiga na kujua ni kipi ambacho kilikuwa kinatakiwa kufuata kwenye huo mpango wao.

"Tumefanikisha kazi kubwa sana ya kuweza kumkamata mtu ambaye alikuwa anadaiwa kuwa hatari mno kwa hili taifa, maisha ya wananchi wetu yalikuwa yanayategemea maamuzi yetu magumu ili kulifanikisha hili na kwa pamoja niseme kwamba tumefanya kazi nzuri sana. Nitumie nafasi hii kuweza kumpongeza kila mmoja wenu kwa kukamilisha kazi hii na kwa sasa nawapeni likizo ya mwezi mmoja kila mtu akaitumie ndani ya nchi anayo ipenda au na familia yake. Kuna swali?" mama huyo aliyatoa maelezo yake kwa watu sita ambao walikuwa wanamwangalia mbele yake.

Mmoja alikuwa ni msaidizi wake Henry Mawenzi, huku wengine watano ambao walikuwa wamebakia ni kikundi cha kutisha ambacho hakuna mtu alikuwa anaujua uhalisia wake HOLY TRINITY maarufu kama TULIKUFA TUKIWA HAI. Hicho ndicho kikosi ambacho kilifanikisha ukamatwaji wa mwanaume aliyepata kuitwa Remy Claude, walikuwa ni vijana wapelelezi ambao walikuwa wanafanya kazi ndani ya idara ya usalama wa taifa chini ya mkurugenzi Cleopatra Gambo.

"Kiongozi mimi sioni kama kuna muda wa kupumzika, kwa sababu nina mashaka sana na kitu ambacho kimefanyika, nadhani kuna sehemu sisi hatupo sawa na kama tutakuwa sawa basi ni wazi kuna mambo tumeyafanya bila kuweza kuujua uhalisia wake na huenda kwa baadae inaweza kuwa tatizo kubwa kama tusipo chukua hatua stahiki mapema" msaidizi wake aliongea akiwa kama mtu ambaye hakuridhika na hatua zote ambazo zilikuwa zimefanywa mpaka kumfikisha mwanaume yule gerezani.

"Kitu gani kinakupa mashaka sana kiasi hicho bwana Henry?"

"Kuna vitu vingi sana, kwanza kwa maelezo ambayo yametolewa kwenye historia ya mtu huyu sidhani kama tungefanikiwa kumpa kiwepesi namna hii. Mtu ambaye tumemtafuta kwa miaka kumi bila kufanikiwa kumtia nguvuni, unahisi inawezekana vipi kumkamata kienyeji tu namna hii? Simaanishi kwamba nina wasiwasi na kazi nzuri ambazo vijana wameifanya hapana, bali najaribu kupima aina ya mtu ambaye tumemkamata na namna tulivyo mkamata na namna mambo yalivyo fanyika mpaka wakati huu"

"Bado sijaelewa pointi yako ya msingi iko wapi"
"Nahisi huyu mtu atakuwa amejikamatisha mwenyewe"
"Una uhakika kabla ya kuja hapa haujanywa hata kidogo?"
"Sijawahi kutumia pombe wala kilevi chochote kwenye maisha yangu na unalijua hilo kiongozi"
"Sasa kwanini unaanza kuongea mambo ya ajabu kama unaota? kwa uelewa wako unahisi mtu mwenye akili timamu anaweza kujikamatisha akiijua kabisa adhabu ya hatari kama ile ambayo ilikuwa mbele yake? alijua kabisa kwamba mambo yakienda mrama anapelekwa ndani ya lile gereza ambalo halizijui hata haki za wanadamu ndiyo maana wanapelekwa watu wa aina yake, kwahiyo unataka kuniambia kwamba yote hayo aliyafanya makusudi? Unaweza ukaniambia ni kitu gani hasa kimekufanya uweze kufikiria mambo kama hayo?"

"Kiongozi najua ni furaha kubwa kumkamata mtu wa aina hii, hili litatupa sifa kubwa nchini na hata nje ya mipaka ya nchi akiwemo mheshimiwa raisi lakini tumejiuliza sababu ya msingi na lengo la msingi la kumkamata mtu huyu limetimia? jibu linaweza kuwa hapana. Kumkamata huyu mtu ni jambo moja na kukamilisha malengo yetu ni suala jingine kabisa. Huyu mtu historia ya maisha yake ina kona kona nyingi mpaka anakuja kuwa kiongozi wa hilo genge, ukiangalia ni aina ya mtu ambaye alikuwa anachagua hata watu wa kuwaua na sio kila mtu hivyo tunaweza kusema hakuwa hatari kwa taifa bali alikuwa ni hatari kwa maisha ya watu fulani pekee, sasa swali ni kwanini?"

"Kama nadharia yangu itakuwa sahihi basi huenda bado hakuna kitu ambacho tunakijua kuhusu huyu mtu na kama tutakijua basi tunaweza kuijua sababu nzuri zaidi ya kwanini yeye aliishi maisha haya na kwanini alimuua kiongozi wa kwanza wa hilo genge kisha akaingia yeye. Hapo mnaweza kuja kuniamini kwamba huenda huyu mtu alikuwa na ajenda zake kuweza kufanya haya yote ambayo sisi tunahisi ndiyo tumeyafanya. Tunaweza kuwa tunahisi kwamba tumefanikisha kazi kumbe tunaishi kwenye mtego wake yeye na tunaifanya ni kazi yake mwisho wa siku akatugeuza sisi wajinga"

Mr Henry mbona kama anataka kutuchanganyishia habari naye! Kwamba bwana mkubwa alijikamatisha ili akateseke? Aaaah bhana! Wewe unaonaje?

4 inaishia hapa.

CIAO.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA PILI
Mkuu wa gereza alimsogelea mwanaume huyo huku akiwa anatabasamu sana lakini baada ya kufika na kumkagua mtu huyo aliikunja sura yake vibaya kwa ghadhabu kubwa.

"Wewe ndiye mpuuzi mmoja ambaye umenifanya mpaka usiku huu nishindwe kulala na mwanamke wangu nikae nikikusubiri hapa? Siwezi kuacha hili lipite, nakuhakikishia lazima ukalipe kwa hili mpuuzi mkubwa wewe. Niliwahi kuapa kwamba watu ambao walikuwa kwenye gereza hili walikuwa wanatosha na sikuwahi kuhitaji kuletewa mtu mwingine ila wewe umefanya kosa la aina ile ile ambalo sikuwa nahitaji litokee na hatimaye umeletwa huku sehemu ambayo hatakiwi kuhifadhiwa mwanadamu wa kawaida, je unajua ni kipi kitakupata kwenye maisha yako bwana mdogo? Niamini mimi ni bora wakati wa kiangazi ungeenda kuishi jangwani sehemu ambako hakuna hata maji ila sio kuletwa sehemu kama hii" aliongea akiwa anamzunguka mwanaume huyo ambapo alimtwisha rungu la chuma mgongoni lakini mwanaume huyo alibaki ameganda tu hivyo hivyo bila kutamka neno lolote lile wala kutikisika.

"Una familia?" kwa mara ya kwanza mwanaume huyo aliitoa sauti yake ambayo ilikuwa nzito sana na ya kukwaruza kwa mbali akionekana wazi kwamba alikuwa anamlenga ni kiongozi huyo wa hilo gereza. Alihisi aliisikia vibaya kiasi kwamba akawageukia vijana wake lakini aligundua kwamba mwanaume huyo alikuwa amemlenga ni yeye mwenyewe. Alishikwa na hasira kali mno kitu ambacho kilimfanya atoe bastola yake na kumpiga risasi mbili za kwenye mapaja mwanaume huyo mpaka akashindwa kusimama na kuishia kupiga magoti huku akiwa anauma meno kwa maumivu makali sana ambayo alikuwa anayapata wakati huo.

"Mpuuzi mkubwa wewe kijana, wewe hapo ndiye mtu ambaye unathubutu kuliingiza jina la familia yangu kwenye huu upuuzi wako? ulitakiwa kuisoma historia ya maisha yangu ya nyuma. Nina historia mbaya sana ya haya maisha mpaka leo kuwa kiongozi kwenye gereza kama hili ni bahati nasibu kwa sababu mimi nilitakiwa kuwa miongoni mwa wafungwa ambao wangekuwa wanayaishi maisha magumu ila mimi ndiye kiongozi kwenye sehemu kama hii. Ukajifunze maana ya jina langu la pili la Gambino nililipataje, kaisome familia yenye historia ya jina hilo huko Marekani kisha utagundua kwamba umefanya kosa kunijibu nikiwa naongea" aliongea kwa hasira huku akiwa anairudisha silaha yake kwenye mfuko wake ambao uliunganishwa na ganda lake kisha akawageukia vijana wake.

"Hatakiwi kulala kwa masaa arobaini na nane, apitie mateso makali ila hakikisheni hafi na hizo risasi atakaa nazo kwa muda mwilini akili imkae ndipo ataelewa kwamba huku sio kwa ajili ya watoto wa mama ambao wakiguswa tu wanataka kuwalilia mama zao na kuhitaji kunyonya. Akimaliza hiyo adhabu ndipo aanze kupatiwa matibabu kidogo kidogo" alitamka huku akiwa anageuka na kuelekea kwenye ofisi yake, muda ulikuwa umeenda sana hivyo alihitaji kurudi ili akajiandae kupumzika maana kazi ya kumpokea mfungwa huyo ilikuwa imekamilika tayari.

Mwanaume huyo akiwa ndani ya maumivu makali kwenye mwili wake, aliunyanyua uso wake ambao haukuwa na nuru hata kidogo kuangalia juu ya ukuta wa kuingilia kwenye vyumba ambavyo walikuwa wanahifadhiwa wafungwa mbali mbali, huko aliona maandishi makubwa tena yakiwa yameandikwa GEREZA LA DOMINIC. Baada ya kuliona jina hilo, kuna picha nyingi zilikuwa zinapita kwenye kichwa chake kwa kasi sana kiasi kwamba zilianza kumuumiza mpaka akayafumba macho yake, alipokuja kushtuka wanaume walikuwa wapo nyuma yake wakimnyanyua kwa nguvu huku wakimpiga na vitako vya bunduki zao kumtaka aelekee sehemu ambayo yangekuwa makazi yake mapya kwa wakati huo.

Luka Gambino baada ya kufika kwenye ofisi yake alisogea mpaka kabatini ambako alitoa chupa ya pombe na kuanza kuinywa kwa pupa akionyesha kutoridhika na kauli ya mwanaume ambaye muda mfupi uliokuwa umepita alitoka kumpokea kwa makamanda wa jeshi. Akiwa anainywa hiyo pombe yake aliingia msaidizi wake akiwa na bahasha mkononi mwake.

"Kuna kingine umesahau?"
"Ndiyo bosi"
"Sikio langu ni lako" alimaanisha anamsikiliza.

"Kuna hizi taarifa za mtu huyu zimefika muda sio mrefu, kuna mtu amezileta inaonekana zilisahaulika, pia kuna frashi ndogo inasemekana kwamba kuna taarifa zote za mtu huyo hivyo itakuwa ni jambo la busara kama tutafanikiwa kuweza kuzipitia na kuweza kumjua kiundani ukiachana na zile taarifa fupi ambazo zilikuja mwanzo" mheshimiwa baada ya kumsikia kijana wake anaongea hayo maneno, alisogea kwenye kiti na kumpa ishara kijana huyo kuelekea ukutani ambako kulikuwa na skrini kubwa ili aweze kumchambulia taarifa hizo na maelekezo yake yaliyokuwepo ndani.

"Remy Claude ndilo jina lake linalo daiwa kuwa la kuzaliwa lakini jina lake ambalo linafahamika sana kwa watu wake ni Menace likiwa na maana ya muuaji wa hatari. Mwaka huu anaingia mwaka wa thelathini na sita tangu azaliwe, hakuna alama yoyote ambayo inaonyesha kwamba alizaliwa wapi na lini ila taarifa zilizopo ni kwamba ni mtoto wa mtaani ambaye maisha yake hayana mwanzo bali mwisho wake utakuwepo."

"Ni kiongozi wa genge la hatari sana la kihalifu ambalo linajulikana kwa jina la SARAFU KUMI NA TANO (FIFTEEN COINS). Hizo sarafu kwa mujibu wake ni kwamba zilishapotea hivyo anazitafuta na haijulikani kwamba hizo sarafu zina maana gani kwa sababu jina la genge hilo linaonekana lilibadilika baada tu ya yeye kuanza kuliongoza"

"Watu ambao alikuwa anawaongoza kwenye genge hilo wanadaiwa kwamba kwa sasa wote wamekufa kwa kuuawa na mtu pekee ambaye amefanikiwa kuishi ni yeye ambaye ndiye alikuwa kiongozi. Ni genge la kimafia ambalo limesababisha athari kubwa sana kwa taifa yakiwepo mauaji ya kutisha, kuliyumbisha taifa kiuchumi lakini ilidaiwa kwamba pia genge hilo lilikuwa likisambaza madawa ya kulevya mitaani na kuwatumikisha vijana wengi kwa kuwaachisha masomo na kuwaingiza kwenye biashara hiyo huku wote ambao walikuwa wanapingana na genge hilo walikuwa wanaishia kuuawa na wanawake kubakwa hovyo hovyo" msaidizi wa mkuu wa gereza aliacha kwanza kuichambua na kuisoma taarifa hiyo huku jasho likiwa linamtoka kwenye uso wake. Yalikuwa ni maelezo ya juu tu lakini yalikuwa ni maelezo mazito sana ambayo hayakuwa na usalama mkubwa kwa walikokuwa wanaelekea. Alikunywa maji na kuikuza picha kubwa ya mwanaume ambaye walikuwa wanamuongelea hapo akiwa ndani ya suti safi na begi lake huku kwenye kichwa chake akiwa na nywele nyingi za kutosha kisha akaendelea tena.

"Baada ya jambo hili kutokea na kuwa kubwa mtaani ndipo serikali ilitengeneza mazingira ya kuweza kumkamata mtu huyu. Kumkamata haikuwa kazi rahisi kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye pesa na jina hivyo ulikuwa unahitajika ushahidi wa kutosha ili kumpata kwani kazi yake alikuwa anaifanya kwa usahihi na umakini sana. Hali hiyo ilipelekea maafisa wengi kupoteza maisha kwa wale ambao walikuwa wanaingia kwenye njia zake ili kuweza kumtafutia ufumbuzi mtu huyo na ndipo shirika la usalama la nchi lilipo amua kumvalia njuga kisawa sawa baada ya kukerwa na kupotea kwa maofisa wengi ambao walikuwa wanapewa kazi ya kuweza kumfuatilia mtu huyu"

"Sentinel Nexus Intelligence Agency (SNIA), shirika letu la usalama wa taifa chini ya mkurugenzi Cleopatra Gambo lilimteua mwanamke mrembo Anelia Baton kuweza kuifanya kazi ya kufanikiwa kumuweka karibu mwanaume huyo ili kujua njia zake zote ambazo alikuwa anazitumia kwenye biashara yake kwa ujumla lakini bila kusahau kuweza kuuangamiza mtandao wake wote ili ikiwezekana akamatwe ama kuuawa japo serikali ilikuwa ikimhitaji zaidi awe hai kwani angekuja kuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa hapo baadae"

Sehemu ya pili inafika mwisho.

Wasalaam,
🙏🙏
 
Back
Top Bottom