Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

121.
Macho yakamtoka pima akiwa haamini kile anachokiona nyuma yake kinakuja pale mbele.

“Simeria?” Akaita kwa sauti ya chini Dokta Ice.

“Ndiye Simeria. Mkeo wa zamani, Ice.” Uzo akamwambia Dokta Ice wakati mwanamama aliyeitwa Simeria akisogea upande wake wa kushoto na kusimama. “Lakini sasa, si mkeo tena.” Akamgeukia Simeria, naye yule mwanamke akamgeukia na kupeana ndimi zao kwa sekunde kadhaa kitu kilichomfanya Dokta Ice kutaka ardhi ifunguke naye aingie, kisha ijifunge naye afie huko.

“Nini kimekubadilisha Simeria?” Akauliza kwa uchungu Dokta Ice.

“Hamna. Ni maisha tu! Nilitakiwa kuwa nawe ili yatimie haya. Umenifundisha folmura nyingi sana. Na sasa ni muda wangu kwenda nazo.” Akajibu Simeria.

“Kwa hiyo mapenzi yote yale, yalikuwa ni maigizo?” Akauliza tena na Uzo alikuwa kimya wala hakutaka kuingilia ule ugomvi.

“Heri yawe maigizo ya kutisha ama ya mapenzi, tunaweza kukumbwa na hisia za kweli. Lakini hayakuwa maigizo hayo, bali yalikuwa maigizo ya vichekesho. Yaani unaweza kufa, mtu asiamini kama umekufa kwa sababu ni ucheshi.” Akajibu Simeria na kumfanya Ice kusikitika. “Una swali lingine kabla hujafa?” Akauliza tena Simeria lakini Dokta Ice alikuwa kimya kainamisha kichwa chake asijue aulize nini. “Baby,” Simeria akamuita Uzo.

“Naam, honey.” Akaitika yule mwanaume mwenye umri kati ya miaka arobaini hadi arobaini na sita.

“Huyo ni wenu. Naomba nianze kazi yangu.” Akaongea yule mwanamama ambaye naye si haba. Licha ya kuwa na umri kati ya miaka thelathini na sita hadi arobaini, lakini alikuwa kama msichana wa kileo kutokana na mavazi pamoja na mikwatuo aliyokuwa anajikwatulia.

“Okay baby.” Uzo alimuitikia na kisha mwanamke yule akajipeleka na kukutanisha ndimi zao tena kwa mahaba makubwa hadi baadhi ya walinzi wakawa wanaona aibu kuwaangalia. Walipomaliza tendo hilo la aibu, Simeria akaanza kuelekea kule ilipo mitambo.

“Simeria.” Akaitwa na Dokta Ice. Mwanamke yule akageuka na kurudi tayari kwa kumsikiliza.

“Merice….” Akalitaja jina hilo kwa kigugumizi. Ni wazi alitaka kuuliza lakini hakutaka kupata majibu anayoyafikiria.

“Merice nini? Mbona humalizii sentensi?” Akauliza kwa ngebe Simeria.

“Merice, mtoto wetu. Naye yuko wapi?” Ikambidi amuulizie mwanaye pekee wa kike ambaye inasemekana alikufa kwenye ajali mbaya ya gari akiwa na mama yake, lakini mama yake kaonekana, je mwanaye?

Simeria akamsogelea Dokta Ice hadi wakakaribiana nyuso zao.

“Si mwanao tena.” Akaongea maneno hayo na kuchapa vidole vyake na kutoa sauti kama ya kuita kitu fulani kije. Ndipo mlango ukafunguliwa na akatokea mwanamke mmoja mrefu na mwenye nywele mwanana akiwa kavalia mavazi ya kijeshi. Dokta Ice akawa kakodoa macho yake asiamini kile anachokiona.

“Umemuharibu hata mwanao wa kumzaa Simeria?” Aliongea Dokta Ice baada ya kushuhudia uso wa Merice ambaye naye alikuwa katika muonekano wa kutocheka wala kutambua lolote kuhusu wazazi na watu wengine.

“Ni wako huyu Uzo.” Simeria badala ya kuongea na Dokta Ice, akamruhusu Uzo, yule mwanaume wake mwingine afanye anachoweza kumfanya Dokta Ice. Naye Uzo bila haya, wakati Simeria anaondoka eneo lile, akampiga kofi kwenye makalio yake na mwanamke yule alitabasamu kana kwamba kile ni kitendo cha kawaida sana.

“Watakuua tu siku moja Simeria. Kama ulivyoniua mimi.” Dokta Ice aliongea lakini Simeria hakujibu lolote bali kupotea kabisa eneo lile.

“Turudi kwenye biashara yetu Dokta.” Aliongea Uzo huku anaanza kusogea mbele ya Dokta Ice.

“Sina biashara na wewe Uzo.” Akajibu mapigo Dokta Ice.

“Unayo. Na tambua hata kama huwezi kuongea sasa, tutakufanya utapike yote. Nadhani unalitambua hilo vema sana.” Uzo alibwabwaja. “Nachotaka kujua, ni huyu mwanajeshi uliyemtorosha, anaubora gani na ulitumia folmura ipi?” Akauliza.

“Hahahaaaa.” Dokta Ice akacheka kwa sauti kabla ya kutulia na kumuangalia Uzo. “Unamuogopa sana eeh! Ni hatari sana huyo, mara mia na hawa niliyowatengeneza.” Akaongea kwa furaha Dokta Ice.

“Sijakuuliza uhatari wake. Nimekuuliza kitu kingine kabisa.”

“Unajua sheria za udaktari, huruhusiwi kutoa siri za ugonjwa au mbinu za kutibu ugonjwa. Nipo hapa kama daktari. Kwa hilo hutopata.” Akajibu Ice.

“Okay. Na kuna risasi ulikuwa unazitumia kule kwako….” Uzo ni kama alikuwa kasahau kitu. Akakatisha yale maneno. “Na nilitaka kusahau, ni mkeo ndiye alituambia nyumba yako ya siri.” Akaongea maneno hayo baada ya kujishtukia.

“Si mke wangu. Ni malaya wetu.” Akaongea Dokta Ice na kumfanya Uzo acheke.

“Leo ni malaya?” Akauliza kwa mshangao.

“Kama unaweza kumpiga matako na akacheka tu, unadhani yupo salama akilini huyo?” Maneno hayo yakamfunga mdomo Uzo.

“Hayakuhusu.” Mwishowe akaongea. “Nachotaka sasa ni kujibu nachokuuliza.” Akaongea kwa ukali zaidi.

“Oooh! Umekuwa mbogo pia? Napenda ukiwa na hasira kuliko ukijidai mwema.” Akaongea huku katabasamu Dokta Ice. “Hata hivyo, hutaambulia lolote.” Akaongeza na kumfanya Uzo amfate pale kwenye kiti na kumchapa ngumi moja ya nguvu.

“Nahitaji majibu. Na siyo porojo zako.” Akaongea Uzo kwa hasira.

“Uzo rafiki yangu. Umesahau kuwa tulisomea wote upelelezi? Umesahau yale mateso yote tuliyoshiriki kwa pamoja ili tuseme kambi yetu iko wapi? Hivi tulisema kweli?” Akamuuliza lakini hakumpa nafasi ya kujibu. “Nadhani unaelewa unachokifanya ni kujisumbua tu kwani sitosema lolote.” Akamaliza.

“Ipo njia ya kusema.” Uzo alipoongea hayo, akafanya ishara ya mkono wake na Dokta mmoja alifungua mlango ule aliotokea Simeria na aliingia eneo lile akiwa kabeba sahani iliyofunikwa kwa bakuli la bati.

Akaenda hadi kwa Uzo na kuifunua sahani na hapo ikaonekana sindano ambayo muhimili wake uliundwa kwa chuma na ulikuwa na muonekano kama wa bastola. “Pinnacle.” Akaongea Uzo akiwa kakamata ile sindano huku anaingalia. “Nadhani jina la sindano hii uliipa wewe kwa sababu ya maumivu yake na ulevyaji wake. Ni muda wa wewe kuelewa maana ya pinnacle.”

“Kama niliitengeneza mimi, basi najua jinsi ya kuihimili.” Akajibu Dokta Ice na kabla Uzo hajasogea pale alipokuwa kakalishwa, Dokta Ice akarusha teke lake na kumpiga sehemu za siri Uzo na kwa taharuki ya hatari, akajirusha kwa nyuma huku kiti bado kikiwa mgongoni kwake, akadondokea mgongo na kukifanya kiti kile kivunjike na wakati huo karibu yake kulikuwa kuna mwanamaabara mmoja aliyepigwa mtama wa kushtukiza jambo lililofanya adondoke na kumpa nafasi Dokta Ice asimame naye huku kamkaba.

“Mkileta papara tu! Navunja shingo ya huyu mbwa wenu.” Akawachimba mkwara na wakati huo wanajeshi wawili, mmoja aliyekuja na Dokta Ice na mwingine Merice, mtoto wake wa kumzaa, wote walikuwa wamemuoneshea bastola.

“Msifanye lolote.” Aliongea Uzo kuwaelekeza wale wanajeshi lakini kitendo cha kushtukiza sana





“Kama niliitengeneza mimi, basi najua jinsi ya kuihimili.” Akajibu Dokta Ice na kabla Uzo hajasogea pale alipokuwa kakalishwa, Dokta Ice akarusha teke lake na kumpiga sehemu za siri Uzo na kwa taharuki ya hatari, akajirusha kwa nyuma huku kiti bado kikiwa mgongoni kwake, akadondokea mgongo na kukifanya kiti kile kivunjike na wakati huo karib yake kulikuwa kuna mwanamaabara mmoja aliyepigwa mtama wa kushtukiza jambo lililofanya adondoke na kumpa nafasi Dokta Ice asimame naye huku kamkaba.
 
122.
“Mkileta papara tu! Navunja shingo ya huyu mbwa wenu.” Akawachimba mkwara na wakati huo wanajeshi wawili, mmoja aliyekuja na Dokta Ice na mwingine Merice, mtoto wake wa kumzaa, wote walikuwa wamemuoneshea bastola.

“Msifanye lolote.” Aliongea Uzo kuwaelekeza wale wanajeshi lakini kitendo cha kushtukiza sana alikifanya Uzo, kitendo ambacho hamna aliyekitegemea, hata Dokta Ice.

ENJOY.

Wakati anawasihi wanajeshi wake wasifanye lolote, kwa kasi ya ajabu alichomoa bastola yake na kugeuka alipo Dokta Ice na kumpiga risasi ya bega Dokta yule na kumfanya amuachie yule mwanamaabara na kugugumia kwa maumivu.

“Ulisahau kuwa nilisomea usalama wa taifa, Dokta Ice. Ina maana umesahau?” Aliuliza huku ametabasamu Uzo wakati huo yule mwanamaabara alikuwa anapepesuka huku akitoka eneo lile la Dokta Ice.

Macho ya Dokta Ice yakawa yanamuangalia Merice, mwanaye pekee wa kike. Kisha akatabasamu na kukumbuka miaka kumi na tisa nyuma walipompata mwana yule.

Yeye na mke wake, Simeria walikuwa wanagombania jina la kumpa. Dokta Ice alitaka kumpa jina la ukoo wao na Simeria alitaka kutoa jina toka ukoo wao, hivyo ikawa vurugu na patashika japo kulikuwa hamna gomvi bali utani na masikhara mengine.

“Basi tufanye kitu mke wangu.” Aliongea Dokta Ice baada ya mvutano mdogo.

“Nataka kiwe kitu cha maana.” Naye Simeria akaongea.

“Unaonaje tukaunga majina yetu, kisha tukapata jina moja la kumpa huyu mtoto.” Akatoa wazo ambalo halikupingwa kabisa na Simeria kama yale mawazo ya mwanzo.

“Tumuitaje sasa kwa majina yetu?”

“Icemeri?” Jina hilo likapingwa vibaya na Simeria. Dokta Ice akaendelea kutoa majina na majina kupitia muunganiko wa majina yao lakini Simeria alikataa. “We’ unataka jina gani?” Ikabidi Ice amuulize Simeria.

“Merice. Yaani Meri la kwanza ni langu na Ice la mwisho ni lako. Hiyo ‘i’ ni yangu na yako pia. Unaonaje?” Simeria akatoa wazo na kumfanya Dokta Ice atabasamu.

“Limepita hilo, sina la kusema wala kuongeza.” Akaongea Dokta Ice na wote wakawa wamekubali kumpa Merice hilo jina. Leo anamtazama Merice mwingine kabisa, Merice aliyeathiriwa na C.O.D.EX.

“Utasema tu ni folmura gani imeitumia na zile risasi zako ni kemikali gani zile.” Sauti ya Uzo ikamtoa mawazoni Dokta Ice ambaye alikuwa anaenda pale alipokuwa kakaa huku mkono wake mmoja ukiwa umeshika jeraha alililopigwa risasi.

“Uzo Buzzin,” Akaita Dokta Ice na kumfanya Uzo amuangalie mtu anayemuendea huku kakamata sindano yake. Macho yake yalimtazama vema Dokta Ice na yaling’amua jambo fulani la hatari. “Umesahau kuwa tumefundishwa na njia za kumshinda adui ambaye ameshindikana.” Akaongeza maneno yake Dokta Ice.

“Usifanye huo ujinga Dokta.” Akaonya Uzo huku akiongeza kasi ya kwenda pale alipokuwepo Dokta.

“Merice. Wewe ni mtoto mwema, kumbuka hilo.” Maneno hayo yalitoka wakati huo Merice naye alikuwa anamtazama baba yake. Kabla Uzo hajafika alipokuwa kakaa Dokta Ice, Dokta yule aliikunja shingo yake upande wa kushoto, kisha kwa nguvu sana akaizungushia upande wa kulia na kuifanya ilie kama kipande cha mti kilichovunjika.

Uzo akasimama ghafla na kumtazama Dokta Ice aliyekuwa kakodoa macho yake. Tayari alikuwa kajinyoga bila kamba wala mikono. Ni mbinu walizowahi kufundishwa wakiwa usala wa taifa, hivyo ndivyo alivyosema.

“Mjinga sana Dokta Ice. Umeona bora ufe kuliko kusema ukweli. Hongera sana. Wewe ni shujaa wangu wa mwisho.” Uzo akageuka nyuma na alimuangalia Merice ambaye naye alikuwa kama hajielewi baada ya kuona tukio lile. Alikuwa kama kapatwa na mshtuko baada ya kushuhudia kile kifo. Macho yake bado yakawa kwa Dokta Ice lakini hajui ni kwa nini hali ile ilimtokea.

“Merice.” Akaitwa na Uzo na Merice akamtazama yule bwana. “Chukueni hiyo maiti na kuipeleka maabara. Yawezekana ubongo wake tukaupandikiza kwa mtu mwingine na kugundua alichotuficha.” Maneno hayo hayakusubiriwa na wale wanajeshi wawili bali mwili wa Dokta Ice kubebwa na kupelekwa maabara.

****

Macho ya Idris Iris yalibaki kwenye kioo cha kompyuta yake akiwa haamini kama Dokta Ice ndiye Yule aliyekuwa anashiriki upuuzi wa kuwaua watu ambao yeye hakuwafahamu lakini kwa asilimia fulani aliamini wale walikuwa wazazi wake.

“Haiwezekani.” Idris alibwata kwa sauti ya juu kidogo na kumfanya muhudumu wa ndege ilea je na kumtuliza kwa sababu kwenye ndege hakuhitajiki kelele za namna ile. “Sawa mkuu.” Alijibu kiuanajeshi baada ya kuuambiwa kuwa haihitajiki kelele ndani ya ndege.

Muhudumu wa kike alitabasamu baada ya kugundua kuwa yule ni mwanajeshi na kamjibu kwa heshima ya jeshi.

Idris akaachana na ile video ambayo iliishia Dokta Ice anachukua kompyuta iliyokuwepo juu ya pambo moja lililozungukwa na taa mule chumbani. Akafungua video nyingine ambayo ilionekana pale kwenye kompyuta yake. Ilipofunguka, Dr. Ice ndiye alionekana na alikuwa anaongea mengi sana kwa lugha ya Kiingereza.
 
123.
“Iris. Kama bado hujaelewa video za mwanzoni, basi naomba uelewe sasa. Dokta Boucher na Jesabel walikuwa ni marafiki zangu sana. Walikutana nyumbani kwangu kwenye siku ya kuzaliwa ya mke wangu. Ilikuwaa maraya pili, hapo wakaanza mahusiano yao ambayo yalipelekea hadi ndoa kufungwa. Baadaye wakapata mtoto wa kiume ambaye kwao alionekana kaja kwa mengi na ndipo wakamuita Best.” Video ile ilianza kueleleza kwa maneno hayo. Ikazidi kuendelea huku Iris akiweka umakini wake zaidi ya mwanzo. “Walipouawa, mengi yalionekana lakini hakuna ambaye alikuwa tayari kushuhudia maafa yakimtokea. Walinyamaza wote.

Lakini sasa nataka ulimwengu ujue ni nini kilitokea na ni siri gani waliyonayo hadi wanadiriki kuua madaktari wazuri baada ya kupata wengine. Lakini kabla sijakupa siri hiyo, tambua kuwe Best ni wewe na Bouncher na mkewe ndio wazazi wako.” Idris akavuta pumzi kabla hajaendelea kuangalia.

“Sasa nakupa siri,” Hapo Idris akatega mwili na akili vyote kwa pamoja. “C.O.D.EX ni sumu moja matata sana katika mwili wa binadamu. Hapo mwanzo waliwekewa watu wenye akili zao kabisa. Ilikuwa inambadilisha binadamu na kuwa kama Shetani. Maumivu ambayo alikuwa anayapata huyu mtu anayeingiziwa hii kemikal, hamna ambaye aliweza kuyavumilia. Wengi walikufa na hata waliopona, nao walikuwa si watu bali ni silaha za hatari. Baadaye makao makuu ya C.O.D.EX, yalivunjwa kwa sababu yalikuwa kinyume na haki za binadamu. Miaka kumi mbele ndipo yakafunguliwa tena na kuna baadhi ya wanajeshi tayari tumekwishawajenga. Mimi, baba yako na mke wangu ndio tulipewa jukumu la kutengeneza kemikali hizi na badala ya kuwamiminia binadamu, tuliwawekea maiti au wafu.” Manenno hayo yakamfanya Idris ajihisi kufa tena baada ya kusikia kuwa waliwekewa wafu.

“Ina maana nilikufa?” Akajiuliza lakini hakuwa na jibu zaidi ya kuendelea kuangalia ile video.

“Lakini siyo marehemu wote ambao walikuwa wanatengenezwa kwa hii kemikali na si wote waliweza kuhimili hii kemikali, na ndipo hapo tulipoamua kuwa tunaua wale watu imara katika mapambano na wenye akili nyingi sana. Hao tuliowaua tuliweza kufanikiwa sana tena sana tu. Kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo sana. Baada ya C.O.D.EX kufanikiwa kwa asilimia nyingi sana, ndipo waliamua kumuua Baba yako na Mama yako na baadae kumuua mke wangu na mtoto wangu. Wewe nilikabidhiwa mimi lakini pia walikunyweshwa madawa ya kukukata uhai wako ukiwa na miaka kumi na saba.” Iliendelea kuelezea video ile huku Idris akiwa makini sana. “Sikutaka uwe kundi la wanajeshi wale makatili, nikakutenga kabisa. Miaka minne mbele ndipo tukaanza kuwajaribu wanajeshi wetu, tukafanikiwa na mwaka huu tukawaita Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi, wakaanza kuwafanyia majaribio lakini wanajeshi hawa yaonekena wameumbwa kwa ajili ya kufanya maangamizi na si kuokoa. Hapo ndipo nikapata wazo la kukutumia wewe kwa kukuwekea hizo kemikali lakini ukiwa na uwezo wa kuwa na huruma na kutunza kumbukumbu. Kwa sasa huna kumbukumbu zako, lakini jinsi unavyokwenda, utakuja kukumbuka yote ya nyuma, tangu ukiwa mtoto.” Aliendelea Dokta Ice kuongea mengi ya muhimu kuhusu C.O.D.EX lakini kubwa zaidi alimsisitiza Idris ajifiche sana huko aendako.

“Kwa hiyo umeamua kunipoteza?” Akaiuliza ile video kana kwamba yaweza kumjibu. “Kwa hiyo mimi ni mwanajeshi mwenye huruma, na ni mwanajeshi mwenye kumbukumbu na kibaya zaidi, mimi ni mwanajeshi niliyepotezwa?” Akajiuliza tena. “Sawa. Acha nipotee. Kama nitapotea, basi mimi si mwanajeshi niliyepotezwa bali mwanajeshi aliyepotea. I am A Missing Soldier, they have to find me..” Akamaliza hayo huku anafunga kopyuta yake na kutulia.

****

Saa saba mchana ndani ya Jiji la Dar es Salaam ndege ya Shirika la Ethiopia ambayo iliwachukua baadhi ya wateja walioshuka na ndege toka Marekani, ilitua katika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere. Idris Iris alionekana akishuka taratibu huku kakamata mabegi yake mawili, moja likiwa la kompyuta na lingine la nguo chache. Aliitazama ardhi ya Tanzania kwa makini na kutafakari machache kabla hajachukua jukumu la kwenda sehemu ya ukaguzi.

“Idris Iris. Karibu sana Tanzania.” Sauti ya kike ilimuongelesha Idris huku mwanadada huyo akimkabidhi ‘passport’ yake Idris.

“Ahsante sana…..” Idris alionesha kidole chake akitaka mwanadada yule ajitambulishe jina lake baada ya yeye kuishia njiani. Aliongea Kiswahili fasaha sana. Dokta Ice aliweza kumpachika chipu inayoweza kumbadilisha mwanjeshi yule na kuongea lugha yoyote ile.

“Naitwa Miss Timasi.” Akamjibu mwanadada huku tabasamu pana likiwa limepamba uso wake.

“Sawa Miss Timasi. Nadhani kuna ndege yangu ambayo napaswa kuipanda hadi Arusha.” Akaongeza Idris.

“Ipo tayari Idris. Nenda mlango ule na kisha utawakuta walinzi ambao utapanda nao ndege hadi Arusha. Huko nenda kaishi salama. Na hapa nilikuwa nasubiri ujio wako tu. Kesho, nami nitaanza kuhudumia wakazi wa Arusha.” Akaongea Timasi huku bado tabasamu lake likiwa bado limekamata namba.

Timasi alikuwa ni mwanamke wa makamo, miaka kati ya ishirini na tisa hadi thelathini na tatu, ndio ilitosha kumkadiria. Alikuwa na rangi ya kahawia, na nywele nyeusi huku macho yake yakiwa yanapendeza kwa rangi kali ya udhurungi. Alipendelea kupaka midomo yake rangi ya damu ya mzee na kuzungushia wanja mweusi na kuufanya uso wake uzidi kupendeza kama malaika wa duniani.

Siku hiyo yeye ndiye alikuwa anawagongea mihuri ya wasafiri mbalimbali wanaoingia na kutoka Tanzania, na ndiye yeye aliyetoa mamlaka ya Idris kwenda ambapo ndege yake binafsi inamsubiria.

“Ahsante sana dada. Na karibu Arusha.” Alishukuru Idris na kuanza kwenda kwenye mlango alioelekezwa na Timasi. Baada ya kutoka, aliweza kuelekea ilipokuwepo ndege aliyoandaliwa, nayo ilimchukua na kuanza kwenda katika Jiji la Arusha.





Timasi alikuwa ni mwanamke wa makamo, miaka kati ya ishirini na tisa hadi thelathini na tatu, ndio ilitosha kumkadiria. Alikuwa na rangi ya kahawia, na nywele nyeusi huku macho yake yakiwa yanapendeza kwa rangi kali ya udhurungi. Alipendelea kupaka midomo yake rangi ya damu ya mzee na kuzungushia wanja mweusi na kuufanya uso wake uzidi kupendeza kama malaika wa duniani.
 
124.
Siku hiyo yeye ndiye alikuwa anawagongea mihuri ya wasafiri mbalimbali wanaoingia na kutoka Tanzania, na ndiye yeye aliyetoa mamlaka ya Idris kwenda ambapo ndege yake binafsi inamsubiria.

“Ahsante sana dada.” Alishukuru Idris na kuanza kwenda kwenye mlango alioelekezwa na Timasi. Baada ya kutoka, aliweza kuelekea ilipokuwepo ndege aliyoandaliwa, nayo ilimchukua na kuanza kwenda katika Jiji la Arusha.

****

ENDELEA

Uwanja wa kawaida sana uliopo Jijini Arusha, uliweza kumpa tofauti kubwa sana Idris. Alipotoka, huko Marekani, kulikuwa na maisha matamu sana na yenye utajiri mwingi kuliko Tanzania. Lakini hayo yote hayakumfanya Idris Iris kukataa kuja kuishi katika Jiji lile ambalo yasemakana kwa Tanzania, ndilo lenye gharama za juu katika maisha yake hasa kwenye vyakula na malazi.

“Tanzania. Kwa nini nimekuja huku?” Akajiuliza Idris wakati anatoka uwanja wa ndege na kuelekea sehemu ambayo aliona gari aina ya Audi nyeusi na ya gharama ikiwa imepaki kwa ajili yake. “Kwa sababu ni sehemu ya amani na naweza kufanya mambo yangu huku bila wasiwasi.” Akajijibu mwenyewe na wakati huo gari ile iliyokuwa inamsubiri yeye, ilijifungua mlango yenyewe ile sehemu ya abiria, na Idris alikwea ndani yake tayari ya kupelekwa maeneo ambayo atakuwa anaishi.

****

Baada ya kifo cha Dokta Ice, huko Marekani pakazuka mtafaruku mkubwa kati ya mashirika ya kijasusi na kipelelezi pamoja na serikali ambayo iliingilia yale mambo na kuyafanya kuwa kama kisasi. Kitendo cha Dokta Ice kufa akiwa anakataa katukatu wale wanajeshi wasitumiwe kwa ajili ya kuangamiza wasiyokuwa wana hatia, kiliweza kuyafanya mashirika ya upelelezi kukubaliana naye na walisikitika sana kuona mtetezi yule amekufa na kapewa mamlaka mtu mwingine ambaye naye hana huruma hata chembe. Mwanamama Simeria, mke wa zamani wa Dokta Ice na sasa ni kimada wa Uzo, akapewa jukumu la kuunda wanajeshi wengine kama wale wa Dokta Ice tena wakiwa bora Zaidi na wenye roho mbaya sana.

“Nasema sisi kama FBI, hatuwezi kuona huu ufilauni wenu unafanyika bila kuupigia kelele.” Alilalamika Afisa mmoja wa FBI wakati wa kikao chao na serikali ya Marekani.

“Bwana Bastian, hatupo hapa kubishana na wewe. Tupo hapa utuambie upo ndani au nje, kuhusu hawa wanajeshi. Huna mamlaka ya kukataa ambacho tumekianza. Kwanza wewe ni mpelelezi tu, mambo ya jeshi ni ya serikali.” Akaongea Waziri wa Ulinzi ambaye ndiye alikuwa muongeaji mkuu wa serikali ya Marekani.

“Sasa mliniita hapa ili iweje?” Akauliza Mkuu wa FBI ambaye kitambulisho chake kilisomeka kwa jina la Bastian Winch.

“Kukupa heshima yako tu! Usijekuona kama tunakutenga. Na kama hutaki hii heshima, tutatuma C.O.D.EX mmoja tu nyumbani kwako. Atatafuna hadi kale kachanga kako.” Maneno yalimtoka Uzo, mkuu anayesimamia projekti nzima ya C.O.D.EX.

Bastian akagwaya baada ya maneno hayo. Akamuangalia kwa macho makali sana yule bwana anayeitwa Uzo.

“Bwana Ally. Upo nasi au nawe hadi tukwambie kama tulivyomwambia Bastian.” Swali hilo likamgeukia mkuu wa CIA ambaye yeye alijulikana kama Ally Ahmed Ally. Bwana yule akamtazama Bastian, akatikisa kichwa kushoto na kulia, kasha akawaangalia wale wachimba mkwara.

“Nitakuwa nanyi japo Bastian yupo sahihi Zaidi.” Akawajibu wale mabwana na hapo hapo kwa pamoja wakasimama na kupeana mikono ya kheri kwenye kazi yao ya kushirikiana kuua na kushambulia mataifa mengine kwa kutumia wanajeshi waliyoundwa kwa kemikali za C.O.D.EX.

“Mi nadhani tumekubaliana kwa pamoja japo kwa kutumia nguvu kidogo.”Akaanza tena Uzo baada ya kukaa kwenye sehemu zao. “Hilo halina shaka, mtatuelewa baadae maana yetu. Hii ni Marekani, lazima tudhihirishe nguvu zetu hapa duniani. Na moja ya kufanya hivi, ni kuunda jeshi ambalo litapigana vita kwa nguvu na kushinda vita hiyo.” Akaongeza.

“Lakini kuna tatizo nimelipata Uzo.” Bastian, kutoka FBI akakatisha maelezo ya kibabe toka kwa Uzo.

“Tatizo gani Bast…” Akataka kujua.

“There’s a missing soldier.” Akajibu akimaanisha kuwa, kuna mwanajeshi kapotea.

“Ni kweli Bast… Mwanajeshi huyo aliyepotea, aliundwa na Dokta Ice na ni yeye ndiye anajua yupo wapi. Na tulipofatilia ni wa aina gani, tukagundua ni kama binadamu tu! Yeye anahuruma na pia hayupo kama hawa anaowatengeneza Simeria. Kwa hiyo sidhani kama ni tatizo kwetu.” Akajibu kwa kujiamini.

“Siyo tatizo?” Akauliza kwa mshangao Ally, mwana CIA.

“Ndio. Kwani yeye kaumbwa kama binadamu tu.”

“Lakini ni zao letu lile. Veje leo awepo mahali kwingine na hatushtuki na tunaona hamna tatizo kabisa.” Akaongeza Ally.
 
125.
“Unataka ushauri nini Ally.” Ikabidi Uzo aulize baada ya kukabwa sana mbele ya Waziri wa Ulinzi ambaye alionekana kuwa upande wa Ally na Bastian.

“Tumtafute, na tumrudishe eidha awe mfu au hai. Silaha kama ile ikiingia China, Urusi au Korea, hakika wataiboresha Zaidi na watatisha sana.” Akajibu Ally.

“Hiyo ni kazi yako wewe CIA, kumtafuta.” Akajibu Uzo.

“Hapana. Mwanajeshi hutafutwa na wanajeshi wenzake. Sisi kazi yetu ni kuwatafutia mahali alipo tu! Kumkamata ni kazi yenu.”

“Unataka kumaanisha nini?”

“Tutakuonesha alipo, kasha utatuma C.O.D.EX wako.”

“Hawa si kazi yao. Hawatafuti mtu mmoja bali hawa ni wa kupambana vita tu.”

“Wale mateka mliowaua walikuwa ni vita?” Akauliza Bastian.

“Naomba hayo usiyaingize hapa Bast..” Akang’aka Uzo.

“Sasa usikatae na kutetea mambo ambayo hayana makalio wala kucha.” Bastian naye akatuna mbele ya Uzo. Uzo naye akabaki anamtazama Bastian kwa macho ya hasira.

“Tutatuma C.O.D.EX endapo tutajua wapi alipo huyu mwanajeshi.” Ikabidi Waziri wa Ulinzi akubali jukumu hilo ambalo Uzo alikuwa kama anataka kulikimbia.

“Ahsante Muheshimiwa.” Akanena Ally kwa furaha.

“Lini mtakuwa mmempata?” Akauliza Uzo.

“Wiki moja tu.” Ally wa CIA akajibu na kwa majibu hayo, yakawafanya wote walidhike na habari zingine zikaanza kujadiliwa hasa katika kuvamia nchi mbalimbali na majaribio ya silaha zao.

*****

Siku tatu nzima, Idris alikuwa anashinda ndani bila kwenda sehemu yoyote. Chakula na kila kitu vilikuwa ndani ya jumba kubwa na la kifahari lililopo Jijini Arusha. Sura yake haikutawaliwa na tabasamu hata kidogo, kila muda alitaka kujua mengi ya dunia. Aliangalia taarifa za habari na vipindi vya burudani kila siku ili kujifunza kuishi sawa na maisha ya binadamu wa leo.

Pia kila mara alikuwa anasoma nyaraka nyingi ambazo aliachiwa na Dokta Ice. Aliweza kugundua mengi sana ambayo yalikuwa nyuma ya pazia. Aligundua mtandao mzima wa mauaji ya watu huko Marekani na aliweza kujua jinsi gani Jeshi la C.O.D.EX linavyotengenezwa. Ndani ya nyaraka hizo, pia kulikuwa na madhumuni chanya na hasi ya C.O.D.EX na pia watu pekee ambao wanaweza kusimamisha mpango huo, ni UN.

“Hawa UN nawapataje? Na wataelewa kweli nia yangu? Au wanaweza kunifanya kitoweo hawa na kuniletea matatizo zaidi.” Akaendelea kujiwazia kisha macho yake yakarudi kwenye runinga ambayo ilikuwa sebuleni kwake. Akajikuta anaitazama kwa muda kabla ya kufanya maamuzi. “Ila kwani mimi na shida gani? Nina kila kitu humu ndani, kwa nini nisifurahie maisha haya badala ya kuanza kuwaza mambo yatakayonifanya nipotee duniani kabisa au kufanywa muuaji baada ya kurudishwa tena Marekani. Acha nifurahie utamu wa Tanzania.” Maneno hayo ndio yakawa mwisho wa kusoma mafaili mengi aliyoachiwa na Dokta Ice, akayakusanya na kuyahifadhi mahali na kisha taratibu akaanza kujifunza mambo mengi ya kidunia.

Aliangalia video mbalimbali za starehe kama kucheza muziki, kuimba, kufanya mapenzi, na pia aliendelea kujifunza mengi ambayo hakuyajua kwa kupitia video hizo. Ndani ya wiki moja, tayari aliamini kuwa yupo tayari kuanza kuyatumia mambo aliyojifunza.

Shauri la kwanza alitaka mtu ambaye anaweza kumsindikiza katika kufanya mambo yake. Idris alihitaji rafiki wa karibu ambaye wangeweza kufurahi kwa pamoja na kutumbua mali ambazo alikuwa kawekewa na Dokta Ice.

Akiwa kakaa sebuleni kwake, akawa anawaza na kuwazua ni nani anaweza kuwa rafiki yake wa karibu? Dereva wake au nani? Dereva hakumtaka kabisa kwa sababu si kazi yake kumtambulisha jiji. Yeye alitaka rafiki ambaye kidogo anaijua dunia na mambo yake hasa anasa.

“Timasi.” Akajikuta anataja jina hilo baada ya kumkumbuka mwanadada mrembo aliyemuona uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na kisha kumgongea visa ya kuishi Tanzania, kabla hajaenda Arusha akitokea Marekani.

Haraka baada ya mawazo hayo, akachukua koti lake la leiza na kutoka nje haraka ikiwa ni mchana wa saa saba. Akabonyeza rimoti ndogo iliyokuwa imeungwa na funguo za nyumba, mlango mkubwa wa bati ukaanza kufunguka kwenda juu na hapohapo ukaonekana uzio mkubwa ambao ulikuwa na magari yapatayo nane na yote ni ya kifahari.

Gari nyekundu aina ya ferrarri, ndiyo ilimvutia siku hiyo. Akaingia ndani yake na kuitoa nje. Akabofya rimoti yake na ule mlango wa varanda, ukajifunga, naye Idris akachoma mafuta yaliyomo kwenye gari lake hadi uwanja wa ndege.

****

“Hellow mrembo.” Sauti ya Idris ilichombeza mbele ya Timasi ambaye hakumuona kama amekuja pale uwanja wa ndege ambapo alihamishiwa. Uso wa Timasi ukanyanyuka na kisha kupambwa kwa tabasamu mwanana.

“Wapi leo Idris.” Akauliza Timasi akitaka kujua Idris anataka kwenda safari ya wapi.

“Oooh! Leo nataka kwenda na wewe mahali.” Akajibu mwanaume kwa bashasha. Timasi akamuangalia kwa mshangao na kisha akatabasamu kama kawaida yake.

“Unataka kwenda wapi na mimi?” Akauliza Timasi.

“Popote pale tulivu tukajiliwaze.”

“Hahaaa. Am sorry my dear.” Maneno hayo ya samahani yalimtoka Timasi huku kanyanyua mkono wake na kumuonesha pete aliyovaa.

“Ouch. Sorry too my dear. Sikujua hilo. Kwa hiyo wewe ni Mrs nani?” Akauliza Idris.

“Mrs. Sema.” Akajibu Timasi huku bado tabasamu mwanana likiendelea kuupamba uso wake.

Wakati wote huo wanaongea, kulikuwa hamna wateja wa kuwahudumia lakini wakiwa katika maongezi, mara walisikia kelele kali ya mshangao na ya kike. Wote wakageuka kwa haraka kuangalia kule sauti ile kali ilipotokea.

Macho yakamtoka Timasi baada ya kumuona mtoto wa kike ambaye alipiga kelele zile. Idris naye akawa kwenye kizungumkuti akiwa haamini kama anaona jini au anaangalia filamu ya maigizo na muda ukifika itakwisha na kugundua kuwa yalikuwa maigizo. Wote watatu na wafanyakazi wengine wakawa katika mshangao wa aina yake.







“Mrs. Sema.” Akajibu Timasi huku bado tabasamu mwanana likiendelea kuupamba uso wake.

Wakati wote huo wanaongea, kulikuwa hamna wateja wa kuwahudumia lakini wakiwa katika maongezi, mara walisikia kelele kali ya mshangao na ya kike. Wote wakageuka kwa haraka kuangalia kule sauti ile kali ilipotokea.
 
126.
Macho yakamtoka Timasi baada ya kumuona mtoto wa kike ambaye alipiga kelele zile. Idris naye akawa kwenye kizungumkuti akiwa haamini kama anaona jini au anaangalia filamu ya maigizo na muda ukifika itakwisha na kugundua kuwa yalikuwa maigizo. Wote watatu na wafanyakazi wengine wakawa katika mshangao wa aina yake.

ENDELEA.

“Timasi?” Sauti ileile iliyopiga kelele na kuwafanya watu wapigwe na butwaa, ndio pia iliita jina la Timasi kwa nguvu.

“Limasi?” Naye Timasi akaita kwa nguvu na kuanza kutoka sehemu ile ya dawati la kuhudumia wateja na kuanza kwenda kule ambapo yupo mtu aliyemuita Limasi. “Ooooh! Dada huyoo.” Akawa anamfuata Limasi huku katanua mikono yake kwa kutaka kumkumbatia.

Bado macho ya Idris yalikuwa hayaamini yanachokiona. Katika kumbukumbu zake hakuwahi kuwaza kuwa kuna watu wanaweza kufanana namna ile. Limasi na Timasi walikuwa wanafanana kila kitu, hadi aina ya nguo na vipodozi wanavyopaka, walikuwa wanaendana sana. Idris akatikisa kichwa na kufuta macho yake ili aone kama amelala au yupo macho, lakini alipoangalia, aliweza kuona picha ya wawili wale wakiwa wamekumbatiana kwa furaha kubwa.

“Mbona unakuja kimyakimya dada?” Timasi akamuuliza Limasi baada ya kuachiana.

“Nilitaka nikusapraizi dada yangu. Yaani hapa siamini kama ni wewe. Shemeji yangu, handsome langu, mzima?” Limasi aliyeonekena wa maneno mengi, alianza uchokozi wake.

“Mzima, ndio sababu ya mimi kuhamia Arusha toka Dar. Ila twende kwanza nyumbani. Maana wewe ulivyo chiriku, sitamaliza hapa.” Maneno hayo yalienda sambamba na Timasi kuchukua baadhi ya mizigo ya dada yake na kuanza kuivuta hadi pale kwenye dawati analofanyia kazi. Wakati huo Idris bado alikuwa anawatazama asiweze kuamini kama kweli duniani kuna watu wa aina ile.

“Idris. Huyu ni pacha wangu. Yeye ni Doto na mimi ni Kulwa. Anaitwa Limasi. Alikuwa India miaka saba sasa. Kasomea huko elimu yake ya juu.” Timasi akamtoa mawazoni Idris ambaye alikuwa bado anamtazama Limasi.

“Nimesomea Sheria, na nimesoma hadi ‘School of Law’ na nina muhuri na naweza mengi tu.” Aliongea kwa tambo Limasi. Idris akawa mtu wa kutabasamu kwa mbwembwe za Limasi.

“Limasi. Huyu anaitwa Idris. Alitokea Marekani wiki iliyopita. Kaishi sana huko na sasa kaamua kurudi nyumbani. Leo kaja kunitembelea kwa sababu mimi ndiye nilimpokea na kuthibitisha passport yake ya kusafiria.” Timasi akamtambulisha Idris kwa Limasi.

“Nafurahi kukufahamu Limasi.” Sauti nzito ilimtoka Idris.

“Mmmmh! Gentleman. Nafurahi pia kukufahamu.” Akaongea Limasi kwa pozi nyingi sana.

“Ngoja niage kwa sababu muda wangu umekwisha pia. Nataka twende nyumbani. Idris unaweza kutupeleka?” Akauliza Timasi huku anaelekea ofisini kwa mkuu wake ili amuage.

“Sure. Naweza.” Akajibu Idris wakati huo Timasi alikuwa ameingia ndani ya ofisi.

****

Huko makao makuu ya CIA wiki ilikatika na hakuna matokeo yoyote ambayo yalionekana kuhusu Idris Iris. Walitumia mitambo yao yote ya Satelite na camera za CCTV ili kuona kama watampata mwanaume huyo, lakini hawakufanikiwa hata chembe. Nchi zote za Ulaya zilitazamwa. Asia na mabara yote makubwa pamoja na baadhi ya nchi za Afrika, yalipitiwa na msako mkali wa CIA na mashirika mengine ya kipelelezi, lakini hawakuweza kumuona Idris.

“Nipe maendeleo Ally.” Uzo alikuwa anawasiliana na aliyepewa jukumu la kumsaka Idris.

“Hamna kitu Uzo.” Akajibu Ally.

“Afrika umeangalia au umepuuzia.” Akauliza tena Uzo.

“Nimeangalia Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Morocco, Tunisia, Algeria lakini sijaona kitu.” Akajibu Ally.

“Sasa atakuwa wapi? Kama Afrika, hatuwezi kuwafuata sana. Najua hawezi kuwa nchi za kipumbavu kama zile. Hapo atakuwa amepelekwa nchi zenye uwezo wa kutengeneza silaha tu!” Akaongea Uzo.

“Sasa kama ataingia mikononi mwa hao, huoni kama ni hatari?” Akauliza swali ambalo ndio sababu ya yeye kupewa jukumu la kumtafuta Idris. Badala ya Uzo kujibu swali lile, akakata simu.

****

“Idris. Yaonekana unapesa sana. Umetoa wapi?” Limasi akamuuliza Idris ambaye alikuwa anawapeleka nyumbani kwao kwa gari yake aina ya Ferrarri.

“Baba yangu alikuwa Daktari huko Marekani. Baada ya kufa, akaacha mali nyingi sana huku na kule ili baadae nichague niishi wapi. Nikaona bora nije kwetu tu ili niendeleze biashara zangu nilizokuwa nafanya huko.” Akajibu.

“Kwa hiyo unafanya biashara gani?” Limasi akachimbua.

“Aaagh na wewe mwanasheria embu tulia mwenzako aendeshe gari.” Timasi akaingilia baada ya kuona maswali yanazidi kipimo.

“Sasa dada si nataka kumjua rafiki yetu?” Akadeka Limasi.

“Hamna shida Timasi. Mimi na kampuni ya usafirishaji wa kwenye maji. Nasafirisha mizigo pamoja kupokea pia, huko Mtwara na Mombasa.”

“Ohoo! Hiyo safi sana. Na umeoa?” Akauliza tena Limasi. Timasi akashusha pumzi ya nguvu na ni wazi swali lile aliliona la ajabu.

“Bado sana.” Akajibiwa kwa kifupi. Limasi akakaa kitako na kumshangaa Idris.

“Kivipi handsome kama wewe, tajiri kama wewe na mtaalamu kama wewe, uliyeishi Marekani na msomi mwenye kampuni kubwa ya usafirishaji, usiweze kuoa?” Maneno yakamwagika toka kinywani mwa Limasi. Bado Timasi alikuwa anatamani afike nyumbani ili maongezi yale yaishe, lakini haikuwa rahisi.

“Hamna Limasi. Kila kitu huenda kwa mipango tu. Nadhani nitaoa sasa.” Akajibu Idris na kumuangalia Limasi ambaye alikaa upande wake wa kushoto na Timasi akiwa nyuma kafura kwa tabia za dada yake.

“Utamuoa nani?” Akauliza kwa hamasa Limasi. Kabla hata Idris hajajibu, akazidi kuendeleza maswali yake na maneno mengi. “Kama dada yangu nitafurahi sana. Lakini naye kaolewa ila nina rafiki pia anapenda kuolewa na Mtanzania. Au tayari wifi tunaye, nisijekuwa najipendekeza hapa.”

“Jamani Limasi, si utulie dada?” Kwa unyonge Timasi akamuhasa dada yake ambaye alikuwa bingwa wa kuzogoa ndani ya Ferrari.

“Dada, siongei na wewe. Hapa naongea na shem wangu mpya. Eti Idris, shemeji langu, utamuoa nani?” Akazidi kuonesha ujuaji wake.

“Natamani wewe ndiye nikuoe.” Akajibu Idris. Mshtuko wa moyo ukampata Limasi. Mapozi yakamuisha. Akatazama pembeni ya kioo na aibu fulani ya kike ikamchukua.

“Eheee! Endelea sasa. We’ si kiboko ya kuungia wenzako, linywe hilo sasa.” Timasi akaongea huku akicheka.

“Vipi. Mbona kama umepoa ghafla? Kuna tatizo?” Akauliza Idris. “Au nimekukwaza Limasi.” Maswali yakaendelea bila kikomo lakini Limasi alikuwa kimya na hakuongea tena hadi anafika nyumbani walipopanga kufika.
 
127.
“Idris, ahsante sana kwa kutufikisha nyumbani. Hapa ndio kwetu na dada yangu karudi, unaweza kuwa unakuja kumchukua.” Aliongea Timasi huku katabasamu lakini Limasi alimtazama kwa macho ya ghadhabu baada ya kusikia maneno yale.

“Dada naomba uniteme.” Limasi aliyeoonekana ni mjanja mjanja, alimbwatukia Timasi kwa hasira.

“Linywe mama. Umeyataka mwenyewe. Idris, mchumba huyu, nakuachia.” Timasi akazidi kupamba maongezi na wakati huo akifungua mlango tayari kwa kutoka ndani ya gari. Lakini badala ya Limasi kumuaga Idris Iris, naye alifungua mlango wa Ferrari ile matata na kwa hasira akabamiza mlango wake na kwenda anapopaswa kuishi. Idris akabaki anamshangaa mrembo yule matata.

“Idris. Mzowee dada yangu kwa leo tu. Namjua mimi.” Dada mtu ikabidi amtetee Limasi kwa kile kitendo.

“Usijali Timasi. Kawaida tu!” Akaonesha urijali wake.

“Okay. Karibu basi nyumbani kwangu. Mbona hutoki humo?” Akauliza Timasi akiwa anachungulia kwenye kioo cha gari, upande aliokuwa kakaa Limasi.

“Hamna shida, kwa leo nitaishia nje. Siku zingine nitakuja kula hadi ugali.” Alijibu Iris

“Haya baba. Kwa kheri eeh.” Timasi aliongea hayo na kuanza kuondoka lakini Idris alimuita tena na kumpa kadi yeke ya biashara ambayo inamawasiliano yake yote.

“Kwa lolote, usisite kuniambia.” Aliongea hayo wakati anampa kadi hiyo Timasi ammbaye aliipokea na kuanza kuelekea ndani kwake.

*****

“Lim, sasa ni nini kumfanyia vile Idris?” Timasi alimuuliza dada yake Limasi ambaye alikwishazowea kumuita Lim au dada. Maongezi hayo yalianza baada ya Idris kuondoka na Timasi kuingia ndani.

“Sina haja ya mapenzi. Majanaume mashenzi kama nini, Tim.” Aliongea Limasi huku anafungua kabati na kuanza kuweka mikoba yake aliyotoka nayo safari.

“Sasa kwani kakutongoza?” Akauliza Timasi.

“Sasa hadi uambiwe nakupenda au kupelekwa bichi na kununuliwa midoli ndio ujuwe hapa unatongozwa? Embu acha kuwa kama kipofu asiyesikia.” Alibwabwaja Limasi.

“Lakini mbona umepaniki ghafla sana?” Akaulizwa tena.

“Sitaki maswala ya mapenzi masikioni mwangu.”

“Ila unataka midomoni mwako. Uwe unawaungia watu eeh. Umekuwa kuwadi wewe?”

“Tim.” Akafoka huku anamuoneshea kidole dada yake. “Nakuomba sana tu! Mimi siyo kuwadi.” Ni wazi alikuwa na hasira Limasi.

“Basi ungetulia garini, sio kubwabwaja kama ndege wa asubuhi.” Timasi akaendelea kumpa somo lakini dada yake safari hii hakuwa akichangia lolote. “Halafu mbona ni HB tu! Kwa nini usimfikirie?” Akamaliza kwa maneno hayo huku anatoka nje na Limasi akageuka na kumuangalia kwa macho makali dada yake. Akaufuata mlango na kuufunga kwa kuubamiza huku msonyo mrefu ukifuatia.

“Kama Handosome, si umchukue wewe.” Akamaliza kwa maneno hayo na kuendelea kufanya mengine.

****

Muda wa saa nne usiku, ndani ya ukumbi mmoja wa starehe Jijini Arusha, Limasi na Timasi ambaye aliamua kwenda na dada yake katika ukumbi huo, walikuwa kwenye furaha kubwa ya kucheza muziki. Limasi licha ya usomi wake, lakini alikuwa ni mtu wa kupenda sana mambo ya starehe. Alimaliza tofauti zake na dada yake, kisha akamuomba usiku huo waweze kwenda katika ukumbi huo ambao ulikuwa maarufu sana pale Jijini Arusha kwa kutoa burudani.

Timasi akiwa kakaa kwenye kaunta anakunywa sprite ya kopo, alikuwa anamuangalia dada yake jinsi anavyocheza peke yake katikati ya ukumbi ule. Timasi akaamua kutoa pochi yake yenye simu na kuchukua kadi ya biashara aliyopewa na Iris, kisha akamtumia ujumbe ambapo wapo na dada yake. Iris akajibu kuwa anafika hapo muda si mrefu.

Limasi akiwa anakinyonga kiuno chake kwa ustadi mkubwa, akawafanya vijana na wazee wakware waanze kumtolea mate kwa tamaa eidha ya kucheza naye, au kufanya naye ngono. Limasi aliendelea kuyarudi mayenu huku akijipapasa kimahaba na kufanya watu wazidi kumtamani.

“Naweza cheza na wewe?” Sauti mwanana ilisikika masikioni mwa Limasi. Akamuangalia aliyemwambia hayo, uso wake ukatua kwa Iris aliyekuwa kavaa mavazi ya ukijana na kifua chake kipana kuonekana vema, lakini hilo halikumshawishi Limasi.

“Hapana. Huwa napenda hivi. Waweza kwenda kucheza na dada pale kaunta.” Akajibiwa hivyo Iris na Limasi, akasogea mbali naye akimuacha Iris aende kwa Timasi na kukaa kisha kuagiza kinywaji kimoja cha kileo.

“Achana naye huyo. Namjua sana katika wanaume. Si mrahisi kihivyo. Huwa hapatani na wanaume.” Akamtetea dada yake, Timasi.

“Hamna shida Timasi. Nimemuelewa.” Akajibu kilijari.

Baada ya kauli hizo za kufarijiana, walianza kuongea haya na yale kuhusu biashara na maisha mengine kwa ujumla huku wakiwa wamesahau kabisa kuhusu Limasi na mtindo wake wa kucheza kimahaba.

Wakiwa wamezama kimaongezi, mara kelele zinasikika ukumbini. Vijana wanakuwa kama wamepagawa ndani ya ukumbi. Walipotazama, walishuhudia Limasi akiwa kazunukwa na vijana wapatao kumi na wote walionekana wapo katika kulewa. Limasi alikuwa katika hali ya uoga na wale vijana ambao wengine walikuwa vifua wazi, walionekana wanataka kufanya naye jambo.

“Kaa hapahapa Timasi.” Akaongea Iris na kusimama tayari kwa kwenda pale alipo mrembo Limasi.





“Hamna shida Timasi. Nimemuelewa.” Akajibu kilijari.

Baada ya kauli hizo za kufarijiana, walianza kuongea haya na yale kuhusu biashara na maisha mengine kwa ujumla huku wakiwa wamesahau kabisa kuhusu Limasi na mtindo wake wa kucheza kimahaba.

Wakiwa wamezama kimaongezi, mara kelele zinasikika ukumbini. Vijana wanakuwa kama wamepagawa ndani ya ukumbi. Walipotazama, walishuhudia Limasi akiwa kazunukwa na vijana wapatao kumi na wote walionekana wapo katika kulewa. Limasi alikuwa katika hali ya uoga na wale vijana ambao wengine walikuwa vifua wazi, walionekana wanataka kufanya naye jambo.

“Kaa hapahapa Timasi.” Akaongea Iris na kusimama tayari kwa kwenda pale alipo mrembo Limasi.

ENDELEA.

“Hapana Iris, hao ni wakorofi wa Arusha. Usiende, watakuumiza bila sababu.” Alibwata kwa woga Timasi huku anajaribu kumvuta Iris asiende kwenye lile tukio.

“Kwa hiyo tuache dada yako anafanyiwe upuuzi?” Akauliza swali hilo ambalo lilimfanya Timasi amuachie mkono wake yule mwanaume aende kufanya alichokusudia.

Iris akaenda hadi katikati ya ukumbi ule ambapo Limasi alikuwa kazungukwa na vijana wa Kiarusha wengine wakiwa wamekamata chupa za vilevi vyao.
 
128.
“Kila kitu kipo sawa vijana?” Iris akaongea kiuungwana ambapo wale vijana wa kiume waligeuka na kumuangalia aliyeongea hayo.

“Hayakuhusu braza. Kaa mbali na hii kitu.” Kijana mmoja mwembamba na mdogo kiumbo, akiwa kavalia kata mikono kama la wacheza kikapu, alibwatuka kwa lafudhi ya Kiarusha.

“Mnataka shilingi ngapi ili mumuache dada yangu.” Iris aliongea tena safari hii akiingiza mkono wake kwenye suruali yake ya kitambaa na kutoa kiasi kadhaa cha fedha na kuanza kuhesabu.

“Tunataka zote hizo, pamoja na huyu kuku tumbambie mpaka turidhike.” Kijana mwingine aliongea huku akipora kiasi kile cha fedha na kukifutika mbele ya sehemu zake za siri.

“Okay. Kwa upendo tu, chukueni hizo fedha na kumuacha huyo dada aendelee kucheza muziki peke yake.” Akashauri Iris.

“Unasemaje wewe bwege?” Kijana mwingine aliyekuwa kifua wazi na kakamata chupa kubwa ya mvinyo, alijitunisha huku anamfata Iris ambaye alitabasamu bila kupenda. “Hivi wewe unazijua charii za ara ama huzijui wewe.” Aliendelea yule kijana mwenye chupa ya mvinyo huku anazidi kutuna kila anapopiga hatua. Alivutia kwa kumuangalia na mwili wake mdogo lakini anajaribu kuutunisha.

“Dogo, bora ukalale kama umelewa na kuchoka.” Maneno yakamtoka Iris na bila kuuliza, yule kijana wa Arusha aliruka kwa haraka na kutaka kumpiga chupa ya kichwani Iris, lakini mwanaume yule alisogea pembeni kidogo tu, na kijana wa watu akapitiliza. Iris hakufanya makosa, akamsukuma kwa mguu kijana yule na kumfanya aende mbele kichwa kichwa na kwa kasi ya ajabu.

“Limasi. Toka hapo njoo huku kama hutaki kuchezewa na hawa madogo.” Iris aliongea lakini pale Limasi alipotaka kutoka katikati ya kundi la wahuni wa Arusha, akajikuta hapati njia ya kutokea na wakati huo, ukumbi mzima ulikuwa kimya na milango yote ikafungwa ili asitoke wala kuingia mtu. “Yoyote atakayejaribu kukugusa, namtengua mkono. Nadhani kila kijana kaelewa nachomaanisha.” Maneno hayo yakampa ujasiri Limasi na kuamua kuanza kutoka katikati ya kundi lile. Alipomfikia kijana mmoja, kijana yule akajaa mbele yake na kumzinga ili aispite. Iris akaenda hadi pale kijana alipozinga na kumshika bega kijana yule. “Muache apite.” Akaongea kwa utaratibu Iris.

“Huyu ni wetu braza. Huwa hatuogopi kitu sisi.” Aliongea kijana yule na kumshika mkono Limasi, lakini alichokutana nacho, nadhani hadi leo anakihadithia kwa wajukuu.

Iris alimtoa mkono wa yule kijana kwenye mwili wa Limasi, na kisha akaunyanyua juu kama refa wa ubondia akitangaza mshindi. Baada ya hapo, akamtwanga ngumi kali ya kwapa yule kijana. Alilia kwa sauti ya juu lakini haikumfanya Iris ashindwe kurudisha mkono wa kijana kwa kasi na kuuzungusha nyuma ya mgongo wake na kuubana vema.

“Nilikwambiaje dogo?” Akaulizwa kijana wa Arusha.

“Niache. Nasema niachee. Kaka ananiumiza huku.” Kijana yule alipiga ukelele mzito na sijui kaka yake alikuwa nani, lakini mara alitokea jamaa mmoja mrefu na mwenye mwili kiasi na kuruka teke la juu lililomkuta Iris kifuani na kumfannya amuachie yule dogo na kurudi nyuma kidogo.

Idris akakaa sawa na kumtazama yule kaka mtu ambaye alikuwa kavaa kapero na mdomoni mwake akiwa anatafuna bazuka.

“Kaeni mbali madogo. Muone nachomfanya huyu bwege.” Aliongea yule aliyeitwa kaka na wale vijana walisogea pembeni huku wakinong’onezana maneno ya kumsifu kaka mtu kuwa anapiga ngumi kama Donnie Yen.

Macho ya Iris yakawa makini zaidi kwa Donnie Yen wa Arusha ambaye naye bila uoga, alifyatuka kama risasi na kuruka teke la juu ambalo Iris alilikwepa lakini kijana yule ni kama alijua kuwa litakwepeka teke lake, akawa karusha ngumi ya haraka ambayo ilimkuta Iris kwenye shavu la kulia. Donnie Yen akatua chini kwa sarakasi ndogo lakini haikuwa kama alivyofikiria, Iris alikuwa amekwishafika nyuma yake na akamnyanyua jamaa yule kwa roba kali. Jamaa akawa ananing’inia juu kwa roba ya mkono mmoja. Lakini katika hali ya kushangaza, yule dogo mwenye chupa ya mvinyo alitokea kwa nyuma yake na kumtwanga Iris chupa ile ya mvinyo hadi ikapasuka.

Iris akamuacha Donnie Yen na kumtazama aliyemtwanga na chupa. Akamuona dogo yule na kipande cha chupa ambacho alitaka kukitumia kama silaha. Iris akamuwahi na kumshika mkono wenye chupa kisha akauminya hadi dogo akaiachia chupa ile, kisha akampa kofi zito lililomfanya apige kelele kama kafiwa.

Kelele hiyo ikawafanya wale vijana wengine wasogee na kuanza kufanya vurugu lakini Iris aliweza kuwamudu kwa kuwakamata na kuwatengua mikono yao. Ilikuwa ni kimuhe muhe ndani ya ukumbi ule wa starehe. Aliyejaribu kumpiga ngwara, Iris alimkanyaga hukohuko chini na kusababisha maumivu makali katika miili yao.

Dakika tano zilitosha kwa Iris kuwafanya wale vijana wawe wamekamata mikono yao kwa maumivu makali sana. Akamuendea yule kijana aliyechukua pesa zake na kuzitoa kule alipoziweka.

“Nilikwambia, chukua na ondoka, ukajifanya unajua. Sasa umekosa vyote.” Akamaliza kwa kumtisha kama anampiga ngumi ya uso, kijana yule akaziba uso na Iris hakupiga usoni bali kwenye mkono alioutengua. Kilio kikamzidi kijana aliyechukua hela.

Akamfata Donnie Yen ambaye alikuwa kakamata shingo yake na anagugumia kwa maumivu makali ya roba mbaya ya kijeshi.

“Wafundishe vijana wako tabia njema badala ya huu upuuzi.” Akamaliza kwa kumpiga kofi zito Donie Yen. Akasimama na kuanza kuondoka eneo lile akiacha ukumbi mzima unampigia makofi.

“Kapiga wababe wa Arusha leo.” Sauti za baadhi ya watu zilisikika lakini Iris hakuzifatilia na badala yake akaenda hadi kwa Limasi.

“Upo salama Limasi?” Akamuuliza, na mwanadada yule badala ya kujibu, alimkumbatia Iris.

“Nipo salama Iris.” Akajibu kwa sauti ya chini na wakati huo, Timasi alisogea hadi eneo la tukio na kuwataka waondoke haraka kabla ukumbi hujajaa wahuni wengine.

Safari ya watatu wale iligotea nyumbani kwa Idris ambapo Timasi na Limasi walianza kuongea haya na yale hasa kuhusu vurugu ambazo zilitokea kwenye ukumbi. Maongezi yalikuwa ya huruma na saa nyingine ya kufurahisha hasa kwa sababu hakuna aliyedhurika sana.

“Idris, niliona yule dogo alikupiga kwa chupa, vipi kakupa jeraha?” Akauliza Timasi huku anaenda pale alipokuwepo Idris na kutaka kumtazama kama alipatwa na jeraha lolote lakini Idris alikataa sana kuonesha sehemu ambapo alipigwa kwa chupa kwa sababu palishajirudisha katika hali yake muda mrefu sana.

“Hapana Timasi, nipo salama tu! Kuwa na amani.” Idris aliongea hayo kwa haraka huku anaelekea lilipo jokofu la vinywaji na kutoa kinywaji chake. “Mtatumia vinywaji gani jamani?” Akauliza Idris.

“Hatuna hata hamu ya vinywaji, tunaomba kwanza twende nyumbani tu! Siku nyingine tutakuja kukutembelea.” Akajibu Timasi.
 
129.
“Basi hamna shida. Na ni tayari usiku sana. Ngoja niwapeleke.”

“Sawa Idris.” Majibu hayo yakawafanya vijana wale watoke ndani ya jengo mwanana na la kifahari la Idris na kwenda kwenye gari ambalo liliwapeleka nyumbani wanapoishi Timasi na Limasi.

“Usiku mwema Idris.” Akaaga Timasi huku anashuka ndani ya gari la Idris huku akimuacha dada yake akiwa bado kakaa ndani, sehemu ya mbele ya gari lile.

“Nawe pia Timasi.” Akajibu Idris na Timasi akawaacha wawili ndani ya gari.

“Idris…” Akaita kwa kusua kidogo Limasi lakini aliendelea na kilichombakiza ndani ya gari la Idris. “Kwanza naomba unisa….” Kabla hajasema maneno hayo, Idris alimuwahi na kumuwekea mkono wake mdomoni akikamkataza asiseme neno alilokusudia.

Limasi akamuangalia Idris kwa macho ya aibu na wakati huo taratibu Idris alitoa mkono wake na kisha kwa pamoja wakabaki wanaangaliana kwa macho fulani ambayo yalielezea ni nini kinachotaka kutokea.

Taratibu Iris alianza kusogeza kichwa chake kwenye kichwa cha Limasi. Limasi bado alikuwa hajafanya maamuzi sahihi ya kwamba naye asogee au abaki palepale. Mawazo hayo ndiyo yaliyomfaya ajikute kaganda hapohapo hadi kichwa cha Iris kikamfikia na kujikuta analambwa midomo yake na ulimi wa Iris. Hapo ndipo alishtuka na kutoka kwenye mawazo yake ya nini afanye na kisha akatanua midomo yake mitamu hata kwa kuiangalia, na kuruhusu ulimi wa Iris uzame ndani zaidi ya midomo yake. Wakajikuta wameingia kwenye dunia nyingine tofauti sana. Dunia ambayo iliwasisimua kuanzia nywele hadi kucha, visogo hadi visigino.

Ndimi zao ziliendelea kubadilishana nafasi kwenye vinywa vyao na wakati huo Iris alikuwa akijaribu kupapasa pia mapaja ya moto ya mwanadada Limasi. Limasi pia hakuwa nyuma, alikuwa akiingiza vidole vyake kwenye masikio ya Iris na kufanya tendo lile liende kwa utamu wa kipekee. Hadi dakika tatu zinatimia, ndipo waliamua kuachana kugandana midomo yao na kubaki wakiangaliana.

“We’ ni mtamu sana.” Ikabidi Iris ndiye atoe ukimya uliotawala kwa sekunde kadhaa na maneno hayo yalimfanya Limasi aone aibu na kutazama pembeni.

“Id, naomba niende kwanza nyumbani maana hapa naweza kuondoka na wewe nisipoangalia.” Akaongea Limasi akiwa bado na aibu.

“Kwani mimi kuondoka na wewe ni tatizo, Lim?” Naye Idris alifupisha jina la Limasi kama Limasi naye alivyofupisha lake kwa kumuita Id.

“Hapana. Ila kwa leo naweza kugombana na Dada kwa kuondoka wakati tulishafika hadi nyumbani.” Maneno hayo hayakuwa sahihi kwenye kichwa cha Idris, lakini mwanaume yule alielewa kuwa kwa mila za Kitanzania, hamna msichana ambaye huweza kukubali kirahisi siku hiyohiyo akalale na mwanaume, labda iwe biashara yake. Ila unaweza kulala naye au kushinda naye ndani, baada ya siku moja.

“Sawa Lim.” Akakubali Idris. “Kwa hiyo nikufuate lini uje ukae kwangu siku nzima.” Akatupa kete nyingine muhimu.

“Nitakupa taarifa kwenye simu, siwezi kukujibu hapa.” Limasi akaivunja ile kete iliyotupwa na Idris kwa jibu hilo.

“Sawa. Nasubiri mlio wako wa simu.” Idris akakubali huku anampatia kadi yake ya biashara Limasi ambaye aliipokea na kabla hajatoka garini, Idris alimvuta tena na kumuingizia tena ulimi wake kinywani. Wakabadilishana tena ndimi zao na ndipo Limasi aliposhuka garini na kwenda ndani ya nyumba anayoishi.





“Sawa Lim.” Akakubali Idris. “Kwa hiyo nikufuate lini uje ukae kwangu siku nzima.” Akatupa kete nyingine muhimu.

“Nitakupa taarifa kwenye simu, siwezi kukujibu hapa.” Limasi akaivunja ile kete iliyotupwa na Idris kwa jibu hilo.

“Sawa. Nasubiri mlio wako wa simu.” Idris akakubali huku anampatia kadi yake ya biashara Limasi ambaye aliipokea na kabla hajatoka garini, Idris alimvuta tena na kumuingizia tena ulimi wake kinywani. Wakabadilishana tena ndimi zao na ndipo Limasi aliposhuka garini na kwenda ndani ya nyuba anayoishi.

ENDELEA.

Akiwa na dada yake, Limasi alikuwa haamini kama aliweza kuingia mkenge kirahisi namna ile na kujikuta anachukua busu laini na nyevu la Idris.

“Yaani Tim mimi hata sijui nilikuwaje. Akili yote ilinihama.” Akawa anamuhadithia dada yake huku yupo kitandani kakamata mto wake na Timasi alikuwa akimtazama huku tabasamu hafifu likiupamba uso wake. “Nilikuwa napata msisimko wa ajabu ambao hadi sasa kama siiuelewi vile. Sijui kanipa nini yule mwanaume.” Maneno hayo yakamfanya Timasi naye akae kwenye kitanda cha Limasi na kuzishika nywele za dada yake kwa kuzilaza kwa nyuma.
 
130.
“Lim. Hayo ndio mapenzi. Ndivyo yalivyo. Uhamisha akili na hupoteza kabisa kujiamini. Na saa nyingine, hata ngvu za mwili. Damu yote hujaa msisimko, unaopoteza nguvu kilaini. Kwa hiyo, usijali sana, ndivyo yalivyo na nafurahi kwa wewe kuingia huko tena. Naimani Idris ni mtu sahihi kwako.” Limasi alimuangalia dada yake kwa macho ya huruma, au tuseme macho ya kudeka.

“Dada naogopa kuumia mimi. Tayari waliniumiza hawa watu, na huyu akiniumiza mimi nitaishi kweli?” Safari hii aliongea huku akitamani kutoa machozi.

“Idris, ndilo chaguo sahihi. Wale wengine kumbuka niliwahi kukuonya. Ila huyu, nakuhakikishia, upo sehemu sahihi na utafurahia mapenzi.” Akajibiwa Limasi.

“Kaniomba niende kwake. Sijui niende lini.”Akachomekea na suala la kwenda kwa Idris.

“Sema anakuja keshokutwa. Ndio anatoka huko Afrika Kusini. Akija na ukasalimiana naye, unaweza kwenda hata mwezi mzima.” Timasi akamuelezea kuhusu kuja kwa mume wake ambaye yupo Afrika Kusini. Na maneno hayo yakampa faraja Limasi kwani alianza kujihisi hali ya kumpenda Idris kwa siku hiyohiyo moja. Hapo ndipo ule usemi wa mapenzi ni kama magugu maji, unapanda asubuhi, saa sita unakuta yametapakaa kiwanja kizima. Unatimia.

“Mwezi nzima. Sasa si bora nihamie.” Akaongea huku anacheka Limasi ambaye kwa muda mfupi tu! Ule ukanjanja wake ulipotea na alikuwa msichana mwenye hekima.

“Kuwa huru Lim. Wala usiogope, Namuamini sana Idris, yaani namuamini kuliko wale wengine. Jitahidi kumtunza awe wako pekee.” Akaongeza maneno mengine ambayo yalikuwa kama msumali wa mwisho kwenye kugongelea hisia za mapenzi kwenye moyo wa Limasi.

Hadithi ikawa hiyohiyo usiku huo hadi wakapitiwa na usingizi wakiwa hapohapo kwenye kitanda cha Limasi.

*****

HUKO Marekani, hali ilizidi kuwawia ugumu baada ya kutompata Idris Iris ambaye alikuwa Tanzania. Walipeleleza kila mahali lakini hawakupata jibu la alipokuwepo Idris. Waliweza kuchukua kamera za barabarani pamoja na za uwanja wa ndege ambao Iris alikwenda, lakini hamna walichoshuhudia. Waliangalia hadi pass za wasafiri wa wiki nzima ndani ya Marekani, lakini hawakumuona Idris wala jina ambalo walihisi ndilo analotumia.

“Mmefikia wapi Ally?” Alifoka kwenye simu Uzo baada ya mkuu wa CIA kupokea simu yake.

“Hamna kitu Uzo. Naomba unipe muda wa kuendelea kumtazama. Na pia kama unavideo za Dokta Ice, naomba uzilete hapa ili tuchunguze mambo kadhaa.” Akaongea Ally.

“Video zipo hadi za siku yake ya kufa. Hilo halina tatizo. Baada ya nusu saa, zitakuja hapo kwa ndege maalumu.” Maneno hayo yalienda sambamba na Uzo kukata simu na kumfanya Ally atoke ofisini kwake na kwenda kusimama kwenye kioo kikubwa ambacho kiliungwa kwenye kompyuta na kuonesha nchi nzima ya Marekani. Wafanyakazi wengi walikuwa wanaendelea kucharaza kompyuta zao, yote ni katika utendaji wao wa kazi.

Wakati hayo yanaendelea kujiri ndani ya Jiji la New York huko Marekani, ndani ya Jiji la Arusha, Tanzania, Idris alikuwa anapapasa kiuno hadhimu cha mwanadada Limasi ambaye alikuwa bado kalala na kajifunika shuka jeupe lililotandikwa kwenye kitanda cha Idris. Usiku mmoja uliopita, ni kelele na lugha za mapenzi ndizo zilizuka kwenye nyumba kubwa ya Idris. Idris aliendelea kuchezea kiuno cha Limasi ambacho kilikuwa kimefunikwa kwa shuka.

“Bwana niache nilalee.” Sauti ya puani ilimtoka Limasi baada ya kuona kashikashi za Idris zinazidi kwenye kiuno chake.

“Kwani nimekukataza jamani.” Naye Idris akajibu.

“Sasa ndio nini hivyo?” Akaendelea kuuliza kwa sauti yake ya puani.

“Basi tu, napenda hivi.” Akajibu tena Idris.

“Je nikifanya hivi.” Limasi akakatika kwa minato na kuzidi kumfanya Idris ahisi yupo dunia nyingine ya kisasa kuliko ile ya sasa hivi ambayo maisha magumu kuliko chuma.

“Ndio maana napapasa hapo kwa sababu jana mambo yaliyokuwa yanatokea, sikuyaelewa kabisa ni kwa sababu gani. Ni hichi ndio kilikuwa kinahusika?” Akafunguka yake Idris.

“Unaonaje kwani?” Safari hii Limasi alinyanyuka kabisa na kufunua shuka walilokuwa wamejifunika. Miili yao ambayo ilikuwa inangozi pekee, ikaonekana na macho yao kwa pamoja walikuwa wanaona jinsi ngozi zao zilivyobarikiwa.

“We’ ni mzuri Lim.” Maneno hayo yakamfanya Limasi asogee kwa Idris na kumlaza kifudifudi, kisha akampandia kwa juu kama farasi na kusogeza kinywa chake hadi kwenye kinywa cha Idris. Tendo la kuchukuliana mate, likapamba moto.

“Id, nimekuheshimu hadi hapa nipo katika kifua chako. Sipo hivi, ila unastahili zawadi hii. Lakini sijui mimi nastahili zawadi gani toka kwako.” Akaongea baada ya kunyonyana ndimi kwa dakika kadhaa huku bado akiwa kamdandia kama farasi.

“Huna unachostahili zaidi ya hicho kidoleni.” Maneno yalimtoka Idris na kumfanya Limasi atazame kwenye kidole chake. Hapo alikutana na pete ndogo lakini imenakwishiwa na jiwe la almasi inayopendeza sana.

“Id?” Akauliza huku katanua midomo yake. “Hii umeweka saa ngapi.” Bado alikuwa haamini. “Na kwa nini……” Akashindwa kumaliza kauli yake baada ya Idris kumvuta kwake na kuanza kunywa kinywaji cha mapenzi. Na mwisho wa yote, walijikuta wakilia kilio cha utamu, utamu ambao uliwafanya waahidiane mambo kibao ambayo sidhani kama wangekuwa hawapo katika dunia hiyo, wangepeana kizembe hivyo.

****

Baada ya mwezi mmoja. Si CIA, FBI wala C.O.D.EX waliokuwa wanataarifa za mwanajeshi aliyepotea (A missing Soldier). Wote walishindwa kutambua ni wapi alipokuwepo Idris Iris. Walichoka na kushindwa kabisa kuendelea kumtafuta mwanaume yule ambaye kwa wakati huo, alikuwa amefanya harusi kubwa sana na kumuoa rasmi Limasi.

Harusi ilikuwa kubwa sana Jijini Arusha. Kila ambaye aliweza kuhudhuria, alikubali harusi ile licha ya upande wa Idris kuwakilishwa na watu wachache sana akiwepo dereva wake pamoja na marafiki wa dereva huyo ambao walisimama kama ndugu wa Idris.

Kwa upande wa Limasi, alikuwa ni mwenye furaha kila mara. Familia za wazazi wake, zilifika katika harusi ile. Na ndugu wa mume wa Timasi nao walifika kunogesha harusi ile iliyokuwa babu kubwa jijini.

“Kwanza napenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa pumzi leo, hadi nimesimama hapa kwenu. Bila yeye, mimi si kitu,” Sauti ya Limasi ilipaa baada ya kupewa wasaha wa kuongea. “Pili nimshukuru dada yangu Timasi, yeye ndiye kila kitu kwangu hasa baada ya wazazi wetu kuondoka duniani. Yeye na mumewe, wamekuwa bega kwa bega hadi nikafika hapa leo. Mume wangu Idris, umekuja kuwa wa muhimu sana kwangu. Nakuahidi nitakuheshimu na kukutunza daima. Hilo ndilo kubwa. Wazazi wangu popote walipo, juweni kuwa nawapenda sana na nimewakumbuka sana.” Kimya kikatawala wakati wa maneno hayo machache. “Pia ndugu wa baba na mama na wageni wote mliofika, sina cha kuwapa zaidi ya upendo wangu kwenu. Nawapenda sana jamani.” Watu wote ndani ya ukumbi wakanyanyuka na kupiga makofi kwa maneno hayo machache aliyoyaongea Limasi.
 
131.
Upande wa mwanaume, pia Idris aliongea na kuhadithia historia ya uongo kuhusu wazazi wake. Wapo walioguswa na wapo waliosikitika sana na kuamua kumpa pole. Hivyo ndivyo harusi ya Idris na Limasi ilivyochukua nafasi katika Jiji la Arusha na wakati huo, mashirika ya kipelelezi na kijasusi, yakiwa yanamtafuta kwa udi na uvumba.

****

“Uzo, umeona hii video?” Ally Ahmed Ally, Mkuu wa CIA, alikuwa anacheza video ambayo ilikuwa inaonesha jinsi Uzo alivyokuwa anamlazimisha Dokta Ice ataje mambo aliyoyafanya. Video hiyo ndio ilionesha kifo cha Dokta Ice pia.

Walikuwa wamekutana kwa mara nyingine ili kupata muelekeo sahihi wa kumsaka Idris na siku hiyo, Ally alikuwa ana ahueni juu ya majibu ya kile wanachokitafuta.

“Hiyo video, mimi nilikuwepo, halafu unaniuliza kama nimeiona tena? We’ vipi bwana?” Alibwata Uzo.

“Yawezekana ukaigiza filamu lakini ukuwahi kuiangalia, ndio maana nimekuuliza.” Akaongea Ally.

“Nenda kwenye mada husika Ally.” Waziri wa Ulinzi ambaye alikuwepo wakati anatoa majukumu ya kumsaka Idris, aliongea na kumfanya Ally asimame na kwenda pale kwenye video.

“Sikilezeni hapa kwa makini alichokiongea Dokta Ice.” Akacheza video ile baada ya kuongea maneno hayo.

“Unajidanganya. Mimi ndiye alpha na omega kwenye kutengeneza hiyo kemikali na kuifanya iwe bora zaidi. Nilioshirikiana nao, wote mliwaua. Bado mimi ni jiwe la pembeni.” Maneno hayo ya kwanza yakasikika toka kwenye video, Wote waliokuwepo kwenye mkutano wakawa kimya zaidi.

“Una uhakika Ice?” Swali la Uzo pia likasika

“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Jibu hilo likamfanya Bastian, Mkuu wa FBI kurudisha mgongo wake kwenye kiti.

“Inaonekana unapajua sana Tanzania. Hamna kitu wale, tukiamua kuiangamiza ni dakika tano tu.” Ally hakutaka kuendelea kucheza video ile hadi mwisho bali kuirudisha tena nyuma hadi kwenye maneno aliyoona ni picha ya kuanzia kwenye upelelezi wake.

“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Akacheza sehemu hiyo kama mara saba kwa kuirudisha rudisha nyuma. Waliokuwepo kwenye kikao wote wakawa wameelewa anachomaanisha Ally.

“Unataka kusema Soldier yupo Tanzania?” Akauliza Uzo na wakati huohuo, Ally alirudi kwenye kiti chake na kukaa kabla hajajibu.

“Hapana. Nachotaka kukwambia, hivi sasa kaoa pia, huko Tanzania. Na hamna mpango wa yeye kurudi huku.” Akajibu Ally.

“Kwa hiyo unaushauri nini Ally?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.

“Tanzania ni marafiki zetu sana. Na hawana uwezo wowote wa kutupiga wala kutengeneza silaha kama ile. Kwa nini tusimuache tu?”

“Yule ni zao letu bwana.” Akawaka Uzo. “Tukimuacha halafu akitoka kwenda nchi nyingine je?” Akazidi kupayuka.

“Kwa hiyo tufanyaje Uzo?” Akauliza Bastian, mkuu wa FBI.

“Tukachukue kilicho chetu.” Akajibu kifupi.

“Kwa sasa anauraia wa Tanzania. Anajulikana ni Mtanzania aliyeishi Marekani. Ni ngumu kumrudisha.” Akatiririka Ally.

“Wapelelezi wa kule wanasemaje kuhusu huyu mwanajeshi wetu?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.

“Niliongea na Shirika la Siri la Kipelelezi la kule, wakaniambia wao hawawezi kumkamata mtu wa aina ile kabla ya kupata ruhusa toka kwa Rais wao. Tuliwatumia na video za jinsi mwanajeshi yule anavyofanya kazi. Wakasema watamuangalia asifanye ujinga wowote na yaonekana anatabia njema tu.” Akajibu Ally.

“Hamna tabia njema, yule arudishwe tu huku.” Akabwabwaja tena Uzo.

“Walipoongea na Rais, wakaambiwa kuwa jamaa anatakiwa arudishwe Marekani, kweli. Lakini hawataki waajeshi wetu waende kule kumkamata, wakasema watamkamata wenyewe.” Akaongeza Ally.

“Wataweza. Kuna mtu anaweza kumkamata yule Tanzania?” Akauliza Bastian kwa mshangao.

“Ndio. Rais wao alisema anamtu wake anamuamini sana katika hilo.” Akajibu Ally.

“Mh! Ni nani huyo?” Waziri wa Ulinzi akakaa kitako kusikia mtu ambaye hadi Rais wa nchi anamuamini.

“Wanamuita ‘The Undercover Agent’ au Agent Zero.” Akajibu Ally na kuendelea. “Wanasema huyo ndiye tegemeo la nchi ya Tanzania…” Hakumaliza, Waziri wa Ulinzi akamsitisha maelezo yake.

“Basi, namjua huyo. Hamna kitakachoshindikana.” Waziri akaongea.
 
132.






“Wataweza. Kuna mtu anaweza kumkamata yule Tanzania?” Akauliza Bastian kwa mshangao.

“Ndio. Rais wao alisema anamtu wake anamuamini sana katika hilo.” Akajibu Ally.

“Mh! Ni nani huyo?” Waziri wa Ulinzi akakaa kitako kusikia mtu ambaye hadi Rais wa nchi anamuamini.

“Wanamuita ‘The Undercover Agent’ au Agent Zero.” Akajibu Ally na kuendelea. “Wanasema huyo ndiye tegemeo la nchi ya Tanzania…” Hakumaliza, Waziri wa Ulinzi akamsitisha maelezo yake.

“Basi, namjua huyo. Hamna kitakachoshindikana.” Waziri akaongea.

ENDELEA.

IKULU, TANZANIA.

Kijana mwenye mwili mdogo lakini uliyokaa kimazoezi, alikuwepo ndani ya chumba cha mazoezi kwenye Ikulu tukufu ya Tanzania. Alinyanyua vyuma vidogo na vikubwa kwa nyakati tofauti na aliweza kwenda kwenye mashine ya kutafutia pumzi ambayo alikuwa anakimbia juu yake. Jasho lililowanisha fulana yake ya mikono mirefu na rangi ya kijivu lakini hakuonekana kukoma kufanya mazoezi hayo licha ya kuchoka kwake hata kwa kumuangalia.

Alipomaliza mazoezi hayo ya pumzi pamoja na kunyanyua vyuma, alienda kwenye ‘punching bag’ na kuanza kulipiga ngumi pamoja na mateke makali ambayo yalikuwa yanaenda kwa mitindo mbalimbali anayoijua yeye ni wapi alijifunzia.

“Agent.” Ndilo jina ambalo mwanadada wa Ikulu alimuita. Naye bwana yule mfanya mazoezi aliacha kulitwanga lile dubwasha na kumfuata yule kimwana.

“Ndio mrembo.” Akanguruma huku anamtazama yule mwanadada ambaye si haba pia ukimuita mrembo.

“Rais anataka kukutana na wewe.” Akampa ujumbe wake huku bado kasimama mbele ya Agent.

“Wewe hutaki kukutana na mimi?” Agent akamuuliza huku tabasamu lake la kichokozi likipamba uso wake. Yule mwanadada akatazama eneo moja la pembeni na lililojuu ya paa ya Ikulu ile. Naye Agent akatabasamu bila kuangalia eneo lile ambalo lilikuwa nyuma yake. “Huwa sifanyi mazoezi yangu huku kamera zinanitazama. Hiyo kamera nimeshaizima zamani sana. Hapo waliokuwa wananitazama, wanaona napiga ‘push up’ bila kuchoka. Kwa hiyo ondoa shaka mrembo.” Akaongeza Agent safari hii akishika kidevu cha yule mwanadada.

“Bwana wewe, siyo hivyo, mi nimeolewa.” Dada yule aliongea kwa sauti ya chini na ya kuogopa kidogo.

“Sawa, kwani kuolewa kunakataza mimi nisikushike kidevu au kuku…” Agent aliongea hayo huku anasogeza midomo yake na kugusanisha na midomo ya mwanadada yule ambaye naye bila aibu, alianza kutanua midomo yake mwanana kama pipi.

“Agent.” Sauti kali ilisikika kabla hawajafanya kitendo kile cha aibu kwa Mwafrika. Agent akaangalia alipoitwa na wakati huo mwanadada mrembo alipatwa na mshtuko na kuondoka haraka eneo lile. “Wanawake utawaacha lini wewe?” Akauliza tena bwana aliyemuita. Agent akawa anakuna nywele zake za kisogoni bila kujibu lolote.

“Nasikia umeniita mkuu.” Akajitutumua kujibu asichoambiwa.

“Ndiyo. Na nimemtuma huyu mwanadada aje akuite lakini naona ulianza kutumbua mali zisizo zako. Acha ujinga huo Agent, ni wake za watu hawa na wanajiheshimu. Uwe unajiheshimu hata mara moja moja. Siyo kwa kuwa wadhaifu kwa mwili kama wako, basi ndio uwatese kwa tabia zako.” Rais wa Tanzania alionesha wazi kukasirishwa na tabia za Agent.

“Bahati mbaya mkuu.” Alijitetea Agent.

“Nyamaza.” Lakini alikatishwa na sauti kali ya Rais na kumfanya Agent yule anywee kama mchicha ndani ya sufuria lenye maji ya moto. “Twende huku.” Akaongeza Rais akimtaka waongozane hadi ofisini kwake.

“Sijaoga bado.” Akaongea Agent huku anaangalia kilipo chumba cha kujisafi.

“Kwa hiyo ulikuwa unataka uogeshwe na huyu mwanamke?” Akamjibu Rais na Agent hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda pale mlangoni aliposimama Rais wake. Akamuona yule mwanadada aliyetaka kumbusu busu nyevu akiwa ndani ya aibu nzito. Akashusha pumzi ya nguvu. “Ni sekretali wangu. Muheshimu kama dada yako au mama yako mdogo, kama unataka, kachukue wapishi huko nje. Huyu sitaki hata umguse.” Akaongeza Rais huku anamtazama Agent.

“Kwa nini sasa Mkuu.” Agent aliongea huku akiwa anataka kucheka kwa sababu ya mkwara wa Rais wake ambao ulionekana kama unambania kuwa na yule mwanadada.

“Kaolewa na mtoto wa kaka yangu. Na hii kazi kaombewa na kaka yangu. Na pia, akiwa na mahusiano na jitu kama wewe, atatoa baadhi ya siri ambazo hupaswi kuzitambua. Umenielewa?” Akajibu Rais na kumfanya Agent anywee hasa kwa ule uhusiano wa Rais na yule mwanadada.

“Samahani dada eeh.” Agent alimuomba msamaha bila kuficha.

“Hilo ndilo la msingi. Sasa nisikie tena hata umemuita lodge zenu za shilingi elfu kumi na tano.” Akaongea tena Rais huku anaingia kwenye ofisi yake.

Agent wakati naye anaingia ofisini, akamtazama tena yule mwanadada, wakakutanisha macho yao na Agent akamkonyeza na kumfanya mwanadada yule atabasamu na kuendelea kucharaza kiparaza cha kompyuta yake.

*****

“Nimekuita hapa kwa jambo moja Agent.” Rais alianza kuongea mbele ya kijana aliyemuita ofisini kwake na wakati huo, ofisi nzima ilikuwa imefungwa na baadhi ya mitambo ya kutotoa sauti nje ilifunguliwa ili kile kinachoongelewa kiwe siri ya wawili tu.

“Ndio mkuu wangu.” Akakaa kitako tayari kwa kumsikiliza mkuu wa Nchi yake.

“Kuna mwanajeshi mpotevu, wao wanamuita ‘a missing soldier’. Lakini wamempatia Tanzania na anaonekana anakula raha zake huko Arusha.” Akaanza maelezo hayo na Agent alionekana akiwa makini kumsikiliza.

“Ni mwanajeshi wa wapi na kwa nini usitume wanajeshi wakamkamata?” Akauliza Agent kabla ya kumuacha Rais kuendelea.
 
Back
Top Bottom