KIONJO
Alishusha pumzi ndefu na sekunde hiyo hiyoakazama kwenye tafakari huku kauli za bosi wake zikijirudiarudia akilini mwake na punde akagutushwa na mlio wa simundogo aina ya Motorola C113, akaipokea na kuiweka sikionihuku akipima utulivu wa upande wa pili
"je ne paux pas croire tu as ete si negligent au point de gâchertout le plan,et maintenant nous sommes exposés au grand jour.il ne reste plus que le monde nous brûle" Alifoka mtu yule aliyepiga simu na kumfanya mpokeaji kutetemeka kwa hofuhuku akichakata ni jibu lipi atatoa kuzima lawama na tuhuma nzito zilizopelekea mpango kuharibika kwa uzembe wa bwana huyu.
"J'ai déjà commencé à résoudre le problème et je te garantisqu'avant ce soir , tu recevras de bonnes nouvelles, madame"alijitutumua kujibu bwana yule kwa sauti ya unyenyekevu huku naye akitumia lugha ya kifaransa kujibu tuhuma zile huku akimhakikishia jua halitazama bila mwanamama huyo hajapata habari ya kumfurahisha.
"pour la négligence que tu as commise, tu as deux options maintenant:démissionner et mourir d'une mort doulureuse.J'attends ta réponse immediatement" alifoka mwanamama yule huku akitoa machaguo mawili kwa yule bwana kwamba kabla jua halijazama awe ametekeleza wazo la yeye kufa pasipo maumivu au asubiri na kukaidi kisha kufa kifo cha mateso, hakika ni machaguo yaliyofanya koo lake likauke kwa hofu.
"madame,donne-moi une autrechance ,c'etait juste un accident,cela ne se reproduira plus, fais-moiconfiance"alijitutumua tena huku akiomba nafasi ya pili ili asahihishe makosa yake.
"if you want second chance kill me, if not do as i say and remember my eyes are on each step you hit, take that on your head and dont try me Rest in Paradise Director......tititititi" simu ilikatwa na kumuacha mtu yule akivuja jasho la kutosha huku kiyoyozi kikiendelea kukifanya chumba kuwa cha baridi na hewa safi, mzee yule akazama katika tafakuri nzito huku akihesabu kila pumzi inayoingia na kutoka alijutia sana kujingiza katika mtandao huo na alichakata kila wazo linalopita kichwani mwake na mwisho akaivuta kompyuta mpakato yake na kuwahi nyumbani kwani mahali hapo hapakuwa salama, ilimchukua dakika kadhaa kufika kwake huku ofisini akiaga kuwa anakwenda hospitali na hajisikii vizuri huku msafara wake ukijipnga tayari kwa kuondoka.
"Mama Johnson leo hajaenda kazini?" Lilikuwa ni swali aliloulizwa mlinzi ambaye alijikuta akibabaika kujibu, kupitia taswira ya macho ya yule mlinzi ilionekana kuna kitu hakiko sawa alishuka na kupitiliza kwenye jumba lake moja kwa moja, jumba lilimlaki kwa ukimya akapitiliza mpaka chumbani nako hakukuta mtu zaidi ya kitanda kilichokuwa kimetandikwa vizuri.
"atakuwa wapi huyu mwanamke.....nina sekunde chache sana kabla hawa jaharibu mpango wangu" alichukua kompyuta yake na diski mweko kisha kwa haraka akaunganisha na intaneti na kuyatuma mafaili kadhaa kwenye barua pepe kisha akafuta kila kitu na kupiga magoti akikielekea kitanda na muda huo huo mwili ulimsisimka kwani kwa jasusi mbobevu kama huyo kunusa hatari inayokuja mbele yake ni sawa na pua kunusa manukato yenye harufu nzuri.
vishindo vya buti kama wavaazo wanajeshi kulimfanya afumbue macho huku masikio yake ya kihesabu kila hatua miguu inapokanyaga katika chumba kile kikubwa na kipana. Almanusura akimbie kwa alichokiona mbele yake koo likamkauka ghafla na kumfanya ahisi miguu haina nguvu kwani sura ya mwanamke mrembo na mpole ulikuwa mbele yake huku ukiwa katika hali ya ukatili, bwana yule akatizama picha iliyokuwa ukutani ikiwaonesha watu hao wakiwa na furaha na tabasamu la mahaba kisha akamtazama mwanamke aliyeko mbele yake.
"mama johnson unafanya nini na hao ni akina nani mkewangu?"aliuliza mkurugenzi wa idara ya ujasusi huku akiwatazama kwa zamu wanaume wanne ambao hakuwa akiwafahamu na alibaki akijiuliza wameingiaje ndani humo huku nje kuna ulinzi mkali wa vijana wa idara ya ujasusi ya nchini humo SNR.
************************************
KWA SHILINGI BUKU TU UNAIPATA HADI MWISHO USIUKOSE UHONDO WA SIMULIZI HII